ABDULLAH IBN SABA` NA NGANO NYINGINEZO
Kimetungwa na: ALLAMAH SAYYID MURTADHA AL- ASKARI
Kimetarjumiwa na: Al-Akhi Ramadhani Kanju Shemahimbo P.O. Box 107 DAR ES SALAAM TANZANIA.
i
ŠHaki ya kunakili imehifadhiwa na: AL - ITRAH FOUNDATION
ISBN # 9987 - 665 - 30 - 6
Kimeandikwa na: Sayyid Murtadha Al - Askari
Kimetarjumiwa na: Al-Akhi Ramadhani Kanju Shemahimbo S. L. P. 1017 Email: info@alitrah.org Website: www.alitrah.org Kupangwa katika kompyuta na: Ukhti Pili Rajabu.
Toleo la kwanza: Oktoba 2004 Nakala:1000 Kimetolewa na kuchapishwa na: Al-Itrah Foundation P. O. Box 1017 Dar-es-Salaam, Tanzania Simu: +255 22 2110640 Fax: +255 22 2113107 Email: info@alitrah.org Website: www.alitrah.org
ii
NENO LA MCHAPISHAJI
Kitabu kilichoko mikononi mwako, ni tarjuma ya kitabu cha Kiingereza, kwa jina la"Ibn Saba and other myths" (Ibn Saba na ngano nyingine) kilichoandikwa na Sayyid Murtadha Al - Askari Kitabu hiki kimeandikwa na Mwanachuoni mkubwa, mwanahistoria na mtafiti. Kitabu hiki kinahusu ngano ya Ibn Saba mtu ambaye hajawahi kuishi katika ulimwengu huu. Lakini mtu huyu ambaye amepachikwa jina la Abdullah Ibn Saba, amesukwa kwa maneno katika vitabu vya historia mpaka watu wakaamini kwamba kweli alikuwepo mtu kama huyu, na baya zaidi, watu wakapotoshwa kwamba huyu ndiye aliyeanzisha Ushia. Ili kuwatoa watu katika dhana hii potofu Mwanachuoni huyu mahiri amefanya utafiti wa kina na kuthibitisha pasina shaka yoyote kwamba hajakuwepo mtu kama huyu duniani. [Itabidi wale wanaoshikilia dhana hii, kama hawataki ukweli, wamtafute Ibn Saba mwingine lakini sio huyu tena]. Kutokana na ukweli huu tumeona tukitoe kitabu hiki kwa lugha ya Kiswahili ili kizidishe mwanga wa elimu kwa Waislamu wazungumzaji wa Kiswahili ili kuondokana na dhana hii potofu. Na hili ndilo lengo kubwa la Taasisi yetu ya 'Al-Itrah Foundation' katika kuwahudumia Waislamu, hususan wazungumzaji wa Kiswahili. Tunamshukuru Ndugu yetu al-Akhy Ramadhani Kanju Shemahimbo kwa kukubali jukumu hili la kukifanyia tarjuma kitabu hiki. Vile vile tunawashukuru wale wote walioshiriki kwa njia moja au nyingine hadi kufanikisha kuchapishwa kwa kitabu hiki. Ni matumaini yetu kwamba kitabu hiki kitakuwa ni mwanga kwa wasomaji wetu na kuzidisha upeo wao wa elimu katika dini. Mchapishaji: Al-Itrah Foundation S. L. P. 1017 Dar-es-Salaam.
iii
YALIYOMO. i. ii. iii.
Dibaji ya Mchapishaji………………………………....................... ix Maelezo ya Mtunzi……………………………….............................x Wasifu wa Mwandishi……………………………. ..........................1 Hatua zilizochukuliwa……………………………............................1 Mtu wa Elimu na Vitendo………………………..............................2 Taasisi na Mashirika ya Kiislam………………….. ........................5
iv.
Maoni ya Dr. Hamid Hafni Dawood: (Profesa wa lugha ya Kiarabu katika chuo Kikuu cha Cairo)…………….. .................................10 Ukweli nyuma ya uwongo…………………………........................10
v. vi.
Maoni ya: Sheikh Mahmood Abu Riyya………............................13 Maoni ya: Al-Sheikh Jawad Mughniah (Mwanazuoni wa Kishiah)…………………………………….....................................15 Maoni ya:Profesa James Robinson D.L.H.D.D Glasgow, U.K…………………………………………………………...............17 Mpendwa Sayyed Murtadha Al-Askari………………...................17
.
vii.
1.
UTANGULIZI…………………………………………….............................20 Ngano ya 'Abdullah Ibn Saba'……………………………........................ 20
2.
ASILI YA NGANO HII YENYEWE……………………….......................... 20 Seif ni nani (Wasifu Mfupi)………………………………........................... 21 Jeshi la Usama………………………………………………....................... 22 Saqifa, ukumbi wa Bani Saidah……………………………....................... 22 Kuhusu ukumbi wa Saqifa Banu Saidah kwa Mujibu wa vyanzo sahihi……………………………………………….................... 23
3.
DIBAJI…………………………………………………………..................... 24 Vipi na kwa nini kitabu hiki kimekuja………………………...................... 24 Ngano ya Abdullah Ibn Saba'…………………………………...................25 Mukhtasari wa kile kinachojulikana kutoka kwa Wanahistoria….............
4.
ASILI YA NGANO YENYEWE NA YA WASIMULIAJI WA NGANO HII…….....................................................................................................28 Muhammad Rashid Ridha…………………………………….................... 28 Abdul Fida ( Kafa 732H.L. 1331 AD)………………………….................. 28 Ibn Athir (Kafa 630H.L - 1229 A.D)………………………........................ 28
iv
Ibn Kathir ( Kafa 774 H.L - 1289.A.D)………………………......................29 Ibn Khaldun……………………………………………………..................... 29 Muhammad Farid Wajdi…………………………………….........................29 Al-Bustani……………………………………………………….................... 29 Ahmed Amin…………………………………………………….................... 30 Hasan Ibrahim…………………………………………………................... 32 Van Flotten (volten) (Johannes 1818-1883)……………………............. .33 Nicholson, Reynold alleyne (1868-1945)……………………….................33 Ensaiklopidia ya Kiislamu………………………………………...................33 Donaldson, M. Dewight…………………………………………. ................ 34 Well Housen Juliua (184-1918)………………………………….................35 Mirkhand katika kitabu chake Rawzatus Safa…………………................35 Ghiathud din (Kafa 940H.L. - 1455A.D)...………………………................35 Tabari na chanzo chake………………………………………….. ...............36 Ibn Asakir (Kafa 571H.L- 1086A.D)…………………………… ..................36 Ibn Bardan (Kafa 1346 H.L. 1851A.D)………………………….................36 Ibn Abibakr (Kafa 741H.L- 1256A.D…………………………….................37 Sa'd Afghani…………………………………………………….....................37 Dhahabi (Kafa 784H.L-1263 A.D)…………………………….....................37 5.
SEIF IBN UMAR AT-TAMIMI (Kafa baada ya 170A.H)………………...39
6.
UCHUNGUZI KUHUSU SEIF NA SIMULIZI ZAKE……………………… 40 Seif ni nani………………………………………………………....................40 Vitabu vya Seif……………………………………………….........................40 Tathmini ya maandishi ya Seif…………………………………...................41
7.
JESHI LA USAMA…………………………………………………………....44 Ngano ya Seif…………………………………………………......................44 Masimulizi ya wengine mbali na Seif………………………………............44 Ulinganisho…………………………………………………..........................45 Baadhi ya Masahaba watambulishwa………………………….................46 Busara za Muhammad katika kitanda chake cha mauti…………............47
8.
SEIF NA SAQIFAH………………………………………….........................49 Uchunguzi juu ya ukweli wa Ngano kuhusu Saqifa kama zilivyandikwa na Seif………...........................................................................................51
v
Msimuliaji wa Ngano……………………………………………...................51 Tukio la Saqifa na wanahistoria wangine mbali na Seif…………………...51 Saqifa na Abubakr………………………………………………...................51 Je Mtume alieleza nia yake kwa maandishi?……………………..............52 Kifo cha Mtume s.a.w.w…………………………………………..................55 Hawa wagombea kabla ya mazishi ya Mtume s.a.w.w………….............57 Mgombea wa pili wa urithi wa Mtume s.a.w.w…………………................58 Mgombea aliyefaulu…………………………………………….. .................59 Kiapo cha hadhara………………………………………………..................62 Baada ya kiapo cha utii…………………………………………...................63 Mazishi ya Mtukufu Mtume s.a.w.w……………………….........................63 Hifadhi katika nyumba ya Fatimah……………………………...................64 Mwisho wa matukio pale kwenye kiapo………………………...................68 9.
MAONI YALIYOTOLEWA NA WATU MBALI MBALI KUHUSU HICHO KIAPO CHA UTII …………………………………………........... ..70 Fadhl Ibn Abbas………………………………………………......................70 Abdullah Ibn Abbas………………………………………….........................70 Salman Farsi……………………………………………………...................71 Umma Mistah……………………………………………………...................71 Abu Dhar…………………………………………………………..................71 Miqdad……………………………………………………………................. 71 Bibi mmoja kutoka Bani Najjar …………………………………................ 72 Abu Sufian………………………………………………………...................72 Wito wa Abu Sufian- Enyi wana wa Abd Manafi………………................72 Mu'awiyah………………………………………………………....................75 Khalid Ibn Said………………………………………………….....................75 Sa'd Ibn Ubaidah………………………………………………….................76 Umar………………………………………………………….........................78 Tathmin ya simulizi ya Seif…………………………………….. .................78
10.
RIDDAH (Uasi)…………………………………………………………….....84 Uasi katika Uislamu……………………………………………. ..................84 Waasi wakati wa Mtume s.a.w.w………………………………. ............ .. 84 vi
Uasi wakati wa Abubakr………………………………………................ .. 85 11.
MALIK IBN NUWAIRA…………………………………………………........90 Ngano ya Maliki kwa Mujibu wa Seif…………………….......................... 93 Kiini cha ngano za Seif………………………………………...................... 95 Ni nani hawa Sa’b,Atyya na Uthman………………………........................95 Kwa nini Ngano za Seif ni za uwongo……………………........................95 Maandishi ya Ngano za Seif……………………………………..................96 Ulinganisho……………………………………………………….................. 96
12
NGANO YA ALA IBN HAZRAMI………………………………………… ...99 Seif anatueleza kuhusu Ala Ibn Hazrami…………………….....................99 Asili ya ngano ya Seif…………………………………………....................101 Ngano ya Ala kutoka kwa wengine mbali na Seif……………….............101 Vita dhidi ya waasi (ulinganishaji na Hitimisho)………………................101
13.
HAUW-AB NCHI YA MIJIBWA…………………………………………….104 Chanzo cha ngano ya Seif……………………………………...................104 Ni nani alibwakiwa na Mbwa hapo Hauwab?……………………............104
14.
KUUSAHIHISHA MTI WA FAMILIA YA ZIAD……….109 Kiini cha ngano ya Seif……………………………………….....................110 Ilivyoelezwa na wengine mbali na Seif…………….................................110
15
NGANO YA MUGHAIRA IBN SHU'BA…………………………………... 111 Wanahistoria wengine………………………………………….................. 113 Asili ya ngano ya Seif…………………………………………....................116
16.
KIFUNGO CHA ABU MAHJAN…………………………………………...118 Simulizi ya Seif………………………………………………….................. 120 Asili ya ngano ya Seif………………………………………….................. 120
17.
SIKU ZA SEIF…………………………………………………………….....123 Siku ya Ng'ombe…………………………………………..........................123 Vyanzo vya ngano za Seif……………………………………....................123 Siku za Armath, Aqwas na Emas………………………………................124 Chanzo cha ngano ya Seif……………………………………...................124
vii
Siku ya Jarathim…………………………………………….......................124 18.
MASHAURIANO NA KIAPO CHA UTII KWA UTHMAN………………..128 Ngano ya mashauriano kutoka kwa wengine mbali na Seif…. ...........128 Ushauri na Umar………………………………………………...................129
19.
QUMMAZBAN MWANA WA HURMUZAN KWA MUJIBU WA SEIF…136 Ngano kama ilivyoelezwa na wengine mbali na Seif…………...............136
20.
MIJI ILIYOBUNIWA NA SEIF……………………………………………...139 Doluth……………………………………………………...........................139 Tawous…………………………………………………………....................140 Je'rana na Na'man……………………………………………....................140 Qorduda……………………………………………………….....................140 Mto Utt…………………………………………………………....................140 Irmathi Aghwath na Amas ……………………………………................ 141 Altheni, Thanya Talkerab, Al-Qodais Al-maqr, Wayakhord Walaja na Alhawafi….............................................................................141
21.
SEIF NA TAREHE ZA KADHIA HIZO……………………………...........143
22.
HITIMISHO …………………………………………………………….........145
viii
Dibaji ya mchapishaji (Chapa ya Kiingereza)
Islamic Thought Foundation (Taasisi ya Fikra za Kiislam) ni taasisi ya msaada inayojihusisha na uchapishaji wa vitabu na majarida ya Kiislam katika lugha tofauti. Taasisi hii imechapisha karibu vitabu 50 kwa Kiarabu, Kiingereza, Kijerumani, Kifaransa, Kihindu, Kijapani, Kiurdu, Kituruki, na Kiswahili . Kitabu hiki "Abdullah ibn Saba" ambacho kipo mikononi mwako sasa ni utunzi wa mwanazuoni mashuhuri Bw.Sayyid Murtadha Al-Askari. Ni (utunzi) wa kipekee na wenye mwanga wa namna yake wenye kuweza kuondoa shaka miongoni mwa madhehebu tofauti za Kiislamu na kuzileta karibu zaidi pamoja. Kitabu hiki kimepokelewa vizuri na kusifiwa na wanazuoni wote Sunni na Shi'ah na mustashirki wa Magharibi vilevile, kama inavyoweza kuonekana kwenye mapokezi yao yaliyomo kwenye kurasa za utangulizi za chapa hii. Taasisi ya Fikra za Kiislam imeamua kuchapisha nakala mpya ya "Abdullah ibn Saba" kwa sababu mbili. Kwanza, kitabu kinadhihirisha ukweli juu ya matukio ya awali ya kihistoria ya Uislam ambayo kwa mara ya kwanza yanatoa mwanga juu ya mabadiliko yaliyofanywa wakati wa matukio haya. Pili, kitabu cha namna hii ni hatua muhimu, ya kawaida na ya msingi katika kuleta umoja miongoni mwa madhehebu za Kiislam. Taasisi inatumaini kwamba wasomaji wanaopenda kujua na watafutaji wa ukweli watayaona haya yaliyomo humu ni yenye faida.
ix
Bismi llahi r- Rahmani r- Rahiym Kwa jina la Allah Mwingi wa Rehma Mwenye Kurehemu. Shukurani zimwendee Muumba wa Ulimwengu, na salamu na amani kwa mitume Wake na kwa Mtume Muhammad (rehma na amani juu yake na kizazi chake) na wateule wa nyumba yake. Hii, ikiwa ni chapa ya tatu ya kitabu hiki kwa lugha ya Kiingereza (ya kwanza kwa Kiswahili) imetolewa kwa wale wanaotafuta ukweli kuhusu historia ya Uislamu, hususan wafuasi wa watu wa nyumba ya Mtume (s.a.w.w.).Tunamuomba Allah atusaidie na kutuongoza tufanikiwe na kufanya vitendo vinavyompendeza Yeye.
Mwandishi.
x
ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO
WASIFU WA MWANDISHI Sayyid Murtadha Al - Askari alizaliwa katika mji mtukufu wa Samarrah (Iraq), mwezi 8 Jamadu Thani, 1332 (A.H). Alisoma katika Hauza (Kituo cha Theolojia ya Kiislam), na katika Muharram ya 1350 (A.H) alihamia kwenye mji mtukufu wa Qum huko Iran na akaishi hapo mpaka 1353 (A.H). Huko Qum, yeye na marafiki zake wawili, Ayatullah Sheikh Murtadha Haeri na Sayyid Ahmad Sajjadi walijifunza sheria ya dini na kanuni zake kutoka kwa walimu mashuhuri na viongozi wa kidini, kama vile: Ayatullah Sayyid Shehabul-Din Marashi Najafi (R.A) na Ayatullah Sheikh Muhammad Husein Shari'at-Madar‌.. Allamah Sayyid Murtadha Al-Askari pia alijifunza masomo mbalimbali ya itikadi pamoja na Imam Khomeini (R.A.), masomo ya tafsiri pamoja na Sheikh Mirza Khalil Kamrei na maadili pamoja na Ayatullah Sheikh Mahdi Shahidi (msimamizi wa Shule ya Razawi). Inafahamika wazi kwamba Ayatullah Sheikh Mahdi Shahidi alikuwa katika Shule ya Razawi kwa miaka miwili, kisha akaenda Hauza Feyziyeh. Kwa kweli , alichukua jukumu muhimu katika utengenezaji wa hadhi ya Allamah Askari na alikuwa ndiye mshauri wake hasa. Hatua zilizochukuliwa kuimarisha mfumo wa elimu wa Hauza. Allamah Askari, wakati wa masomo yake katika Hauza hii, alifikia uamuzi kwamba marekebisho fulani ni lazima yafanywe kuhusu mfumo wa kielimu wa Kituo hiki. Kwa sababu hii, yeye pamoja na baadhi ya wanafunzi wa Hauza hii wenye moyo walifanya jitihada kuunda upya mfumo wa elimu wa Haudha hii. Walijaribu kuandaa upya programu za kielimu kwa namna ambayo kwamba Hauza iweze kufanya jukumu la uhakika kwa uwezo wake wote na kutimiza wajibu wake kwa ummah wa Kiislamu. Baadhi ya masomo yaliyojadiliwa katika mpango wao au mfumo wa elimu uliopendekezwa ni: Somo la tafsiri, somo la ngano, na somo la uchambuzi linganifu wa maoni ya Kiislamu sambamba na somo la sheria ya kidini (fiqh) na kanuni na taratibu zake. Mfumo huu wa elimu ulioshauriwa pia ulihusu: Jinsi ya kutoa hutuba; jinsi ya kuandika na kuhariri sawasawa; na jinsi ya kufundisha kazi za kijamii kwa wanafunzi wa theolojia pamoja na mkazo juu ya kujifunza na kufanya tafiti mbalimbali kuhusu hali ya Waislamu katika jamii tofauti na kuwaonyesha namna ya kukielimisha na kukifunza kizazi cha baadae chenye kukubali ushauri na kilichotaalamika cha Waislamu halisi ili kupata Ummah bora wa Kiislamu. Uamuzi huu ulifanywa wakati wa kipindi cha mamlaka ya Ayatullah Uzma Sheikh Abdul-Karim Haeri, mwasisi wa kituo maarufu cha Theolojia ya Kiislamu cha Hauza Ilmiyyah, Qum. Baadaye, Allamah Askari alirudi nyumbani kwake kwenye asili yake nchini Iraq, 1
ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO
kwenye mji mtukufu wa Samarrah ili kuendelea na masomo yake ya kidini mpaka 1366 A.H. hadi kufikia kiwango cha 'Al-Kifayeh' pamoja na Sheikh Habibullah Eshtehardi. Masomo haya yaliendelea mpaka mwanzoni mwa Vita Kuu ya Pili. Mtu wa Elimu na Vitendo Tangu alipokuwa na umri wa miaka 15, Allamah Al-Askari alionyesha shauku kubwa katika historia, na safari za wavumbuzi wa dunia. Kwa matokeo ya juhudi zake alilimbikiza habari katika nyanja hii ambayo ilikuwa ni zaidi ya kiwango cha kawaida cha elimu miongoni mwa wenzie wa darasani. Baada ya kuyasoma maandishi ya wanafunzi wa Ayatullah Shirazi juu ya Sheria ya Tumbaku na kile walichokiandika watu wa Magharibi kuhusu nchi za Kiislam katika vitabu vyao vya kumbukumbu za kila siku, alichambua tarehe ya uvamizi wa wakoloni kwenye nchi za Kiislam. Kwa ujuzi na akili yake, aliyatambua malengo ya uovu ya wakoloni ya kusambaza milki yao ya kielimu na kiutamaduni katika ulimwengu wote wa Kiislam na kuufichua utambulisho wao sahihi.Uvamizi wa kisomi haujamalizika bado hata pamoja na mwisho wa milki ya moja kwa moja ya wakoloni juu ya nchi za Kiislam na bado unaendelea kwa kificho. Aligundua pia jitihada za hatari za kuhusisha kwa makusudi fikra sahihi na maoni ya Kiislam na fikra za kisasa za Kimagharibi na matokeo yake katika kubadili sura halisi ya Uislamu katika mawazo ya vizazi vya baadae. Allamah Askari alikuwa miongoni mwa wasomi wa Kiislamu wa awali wa Iraq waliogundua sababu halisi ya programu za kielimu zilizoandaliwa na washauri wa kigeni katika shule za serikali kwa vijana wa nchi za Kiislam. Baada ya uchunguzi makini, alielezea tofauti kubwa kati ya programu za kielimu za nchi kama Ujerumani, Ufaransa, Japani, n.k., na programu za zile nchi zilizomilikiwa na muktadha wa vitabu vyao vya kiada. Kutokana na tofauti hizi, aligundua kwamba moja ya sababu kubwa za kuwa nyuma kwa nchi za Kiislam ni hii mipango ya kielimu na mafunzo. Ndiyo maana akaziita shule zetu 'kiwanda cha kuandaa waajiriwa wa baadae,' kwa sababu shule wakati ule zilianzisha waajiriwa wa kazi zisizo na sulubu 'white-collar employees' ambao wangefanya chochote kutekeleza amri za mamlaka kuu na programu katika jamii bila hoja wala majibizano. Allamah Askari pia aliuona ukosefu wa uhusiano kati ya Hauza hiyo na vyuo vikuu vya kisasa, hizi nguzo kuu mbili muhimu za jamii ya Kiislamu. Hauza ilitengwa na kujihusisha na kuwafunza wanafunzi kuwa mabingwa wa ujuzi na walimu wa baadae wa Hauza na si kingine chochote; na vyuo vikuu pia vilikuwa na mwelekeo 2
ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO
wa Kimagharibi na walikuwa wageni kwenye jamii yao ya Kiislam. Kwa hiyo, kulikuwa na haja ya harakati (chama) za kuondoa mkwamo huu na kufuta utengano na unyonge huu. Allamah Askari alianzisha harakati hii wakati ule Vita Kuu ya Pili ilipoihatarisha Iraq na watu wake. Harakati yake ya kwanza ya kitamaduni ilikuwa ni kuandaa mikutano ili kuwajulisha watu na kuwaelimisha. Wakati huo huo, alianzisha shule ya kuwasomesha vijana na alipanga namna ya masomo yeye mwenyewe, kisha akaifanya shule hii kama sehemu ya mpango wake mkubwa. Katika shule hii, baadhi ya wanazuoni, kama vile Sheikh Mirza Najmu-Din Sharif Askari, Sheikh Hassan Kumeil, Sayyid Jafar Shahrestani na Sheikh Mahdi Hakim walifundisha. Wakati akianzisha na kupanga, Allamah Askari kama mwana mageuzi mwingine yeyote yule katika karne zilizopita, alipambana na upinzani wa kijinga na wa kizamani. Hivyo aliona ni bora kuandika kitabu kuhusu utamaduni wa Kimagharibi na uvamizi wa kisomi katika nchi za Kiislamu na akasanifu mipango mbalimbali kupambana na uvamizi huu. Baadhi ya mipango hiyo ilikuwa ni: a) Kuasisi shule za kisasa za kuelimisha kizazi kichanga na kuwatambulisha kwenye utamaduni na elimu ya Kiislam. b) Kuasisi shule nyingine zenye wahitimu waliobobea katika dini ya Kiislamu ambao wanaweza kuhamishia elimu yao kwa jamii. c) Kuchapisha vitabu na majarida ya Kiislamu. Kitabu chake hiki kilipokwisha, alikiita; 'Maradhi ya Jamii na Matibabu Yake'. Baada ya muda, alirudi Iraq na kuishi katika mji mtukufu wa Kazimayn ili kupata mazingira bora ya kutibu baadhi ya maradhi ya jamii yaliyokuwepo kwa utamaduni wa Kiislamu. Hapa alimtembelea Profesa Ahmad Amin (Mwandishi wa kitabu'Mageuzi katika Uislam') na kwa kubadilishana alimpa kitabu chake. Katika kukutana huku kulikotokea mwaka 1363 A.H. wanazuoni wakubwa wawili hawa walifikia makubaliano ya kuanzisha shule ya maandalizi. Marhum Ahmad Amin alikubali jukumu la kubuni muundo wa shule kwa msaada wa Allamah Askari na kumtia moyo kwake. Mwishowe shule hii ilianzishwa hapo Kazimayn na waliiita 'Muntada Al-Nashr'. Mara tu baadae, shule hii ilijiunga na jamii ya 'Muntada Al- Nashr' au 'Kituo cha uchapishaji' cha Najaf ili kupata kibali cha kazi kutoka serikalini haraka iwezekanavyo. Kwa kuhakikishiwa uanzishwaji wa shule hii, Allamah Askari alirudi Samarrah. Lakini kwa vile Ahmad Amin alikabiliana na matatizo kadhaa, alimkaribisha tena kuishi Kazimayn, kuwa mkuu wa shule na kuweka taratibu 3
ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO
mbalimbali kueneza utamaduni wa Kiislamu. Baada ya kukamilika kwa sehemu ya kwanza ya mpango huo ambao ulikuwa mafanikio ya muundo wa shule, Allamah Askari aliamua kutekeleza sehemu ya pili ya mpango wake, yaani, kupata kibali cha ujenzi wa taasisi, kama ile shule ya theolojia iliyokuja kuanzishwa baadae huko Baghdad, ili kuifundisha dini ya Kiislamu na kufunza watu wenye akili. Kwa kukamilika kwa sehemu ya pili ya mpango wake, Allamah Askari alianza awamu mpya katika maisha yake ya kidini. Alirudi Samarrah na kutumia miaka miwili kupata fiqhi iliyochanganuliwa kutoka kwa Profesa wake Ayatullah Eshtehardi.Wakati huohuo, aliandika na kuhariri vitabu mbalimbali juu ya historia ya fikra za Kiislamu. Aligawanya matokeo yake katika sehemu nyingi zitokanazo na sura tofauti za uundwaji wa fikra za Kiislamu tokea mwanzo kabisa wa kujitokeza kwa Uislamu mpaka mwisho wa ugavana wa Bani Abbas. Baadhi ya vikwazo vigumu kwenye maendeleo ya utafiti wake vilikuwa: ngano mbalimbali zilizokubaliwa na Waislamu walio wengi zilipoteza kuaminika kwake baada ya uchunguzi wa kina, kwa mfano, zile ngano kutoka kwa Ummul-Mu'minin (Ayisha), Abu Huraira, Ibn Abbas, Aun Ibn Malik na kadhalika. Matokeo ya utafiti huu na uchunguzi yalikuwa safi sana kwa vile Allamah Askari aliona udhaifu wa ngano hizi kwa uthibitisho usiopingika. Nyingi ya ngano hizi zilikuwa hazina msingi, hasa ngano ya 'Abdullah Ibn Saba' na 'Masahaba Mia na Hamsini wa Uongo'. Kwa matokeo ya ugunduzi wa utafiti huu muhimu, baadhi ya mambo yanayofahamika yaliyokubalika kwa watu kwa karne, yalipoteza kusadikika kwake, na msingi wa maandishi na ngano za Tabari au wana-historia mashuhuri wengine hazikuungwa mkono. Vitabu vya kwanza vya Allamah Askari vilivyochapishwa kuhusu matokeo haya ya utafiti mwaka 1375 A.H. vilikuwa 'Abdullah Ibn Saba' na 'Pamoja na Dr. Alwardi'. Ingawa Allamah Askari alitumia muda wake mwingi kwa kujifunza na kuandika, hakuacha harakati zake za kidini na kijamii. Punde baadae, aliamua kuendeleza shughuli zake kwa dhahiri kabisa na akaanzisha shule na Haudha mbalimbali za dini za kipekee. Hakuguswa hata kidogo na vikwazo na matatizo yaliyokuwepo. Kwa hiyo, alihamia Iran na akamtembelea mmoja wa wenye mamlaka (ya kidini) wa wakati wake Ayatullah Sayyid Agha Husein Burujerdi (R.A.). Katika mkutano huu walikuja kukubaliana kuanzisha Hauza maalum ya kidini huko Qum na Allamah Askari akiwa ndiye mkuu wake. Lakini utata wa hali ya kisiasa huko Iran kwa wakati ule na nguvu ya migongano kati ya Ayatullah Kashani na wafuasi wake kwa upande mmoja, na Dr. Mussadiq na wafuasi wake kwa upande mwingine, vilimlazimisha arudi Iraq na kuishi huko Kazimayn. Alianza kutengeneza Hauza ya kidini katika mji huo lakini hakuweza kukamilisha kazi hiyo kwa sababu ya vikundi mbalimbali vya upinzani. Hivyo alianza kujenga shule nyingine, Shule ya Imam Kadhim (A.S.) ambayo ilikuwa imara hadi wakati wa mapinduzi ya tarehe 14,Julai,1968.
4
ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO
Taasisi na Mashirika ya Kiislamu Baada ya kuona ueneaji wa shughuli za vyama vya kidunia kama vile: vyama vya Kikomunisti na cha Baathi, na ongezeko la mashambulizi ya mpangilio ya kipropaganda za wamisionari (wa Kikristo) katika kiwango chake cha juu yakidhihiri katika shule na taasisi zao, kama Taasisi ya Watawa wa Chalde (Rahebat Alkaldan) na Taasisi ya Watawa wa Bikra Maria (Rahebat Maryam Al-Uzra), Allamah Askari alikusanya nguvu zake zote na pamoja na ndugu zake katika dini na marafiki kutoka Najaf na Baghdad na chini ya usimamizi wa moja kwa moja wa Marhum Ayatullah Sayyid Muhsin Hakim, akaanzisha makabiliano makali kabisa ya kisiasa na kisomi na vyama hivyo na wamisionari. Sasa, mbali na wajibu wake wa kidini, ilibidi akubali majukumu ya shughuli za kisiasa pia. Kwa sababu hii, Allamah Askari alikwenda kwenye jimbo la Al-Bayyaha la Baghdad kama mwakilishi wa wenye mamlaka na kutoka hapo na kuendelea alikwenda kwenye jimbo la Karradeh Mashariki (huko Baghdad). Yeye na wafuasi wake walidhamiria kulitumia jimbo hili kama kituo chao kikuu cha kuanzishia harakati na kufanya mabadiliko kwenye mji wote wa Baghdad. Mwanzo wa harakati za Kiislamu ulikuwa kutoka ndani ya 'Hussainiya' ( sehemu ambazo kifo cha kishahidi cha Imam Hussein kinaombolezewa). Katika wakati wa Allamah Askari, kikundi cha wanafunzi wa kidini (kwa namna ya waombolezaji wa Imam Hussein (a.s.) waliandamana wakati Marhum Dr. Dawud Al-Attar aliyekuwa kiongozi wao,alikiongoza kikundi hicho kutoka "Shule ya Imam Kadhim" kwenda Kazimayn na kwenye Kuba la Imam Kadhim (a.s.). Harakati hii ilichukua kasi katika miaka michache iliyofuata. Ni jambo linalothibitika kwamba Allamah Askari alikuwa na majukumu makubwa katika harakati ya Kiislamu. Harakati hii ilikusanya Iraqi, Makuba matukufu ya Baghdad, Karbala na Najaf, na ardhi ya Mtume na Maimamu. Imani ya Allamah Askari ilikuwa ndiyo dhamana ya maendeleo ya juhudi na harakati. Harakati za Kiislamu inakuwa na nguvu tu kama imeundwa katika shirika au taasisi ya Kiislamu siyo na mtu asiyejua. Pili, harakati hiyo isiingiliwe na maoni binafsi. Matokeo yake, Sayyid Hebatul-Din Shahrestani aliasisi 'Kituo cha Kiislamu cha Utoaji Sadaka na Allamah Askari alikuwa ndiye mtu wa kwanza baada ya Hebatul-Din Shahrestani aliyekuja kuwa mkuu wa kituo hiki. Kabla ya kuanzishwa kwa kituo hiki, Allamah Askari alikuwa tayari amekwisha anzisha kituo kingine kwa jina la "Jumuiya ya Mwongozo wa Kiislam", lakini aliondoka kwenye jumuiya hiyo kwa sababu ya baadhi ya migogoro kati ya uongozi. Na Allamah Askari akiwa mkuu wa "Kituo cha Kiislamu cha Utoaji Sadaka", kituo hiki kilianzisha miradi mbalimbali. Baadhi ya huduma muhimu sana za kituo hiki katika uwanja wa utamaduni zilikuwa kule kuanzishwa kwa vituo vya elimu ya Kiislamu. Kutokana na vituo hivi kilijitokeza kizazi kilichovutika kidini waliokubali 5
ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO
baadhi ya majukumu mazito ya jamii ya Kiislamu, na wakashiriki katika harakati tukufu ya Iraqi, n.k. Majina ya baadhi ya vituo hivi vya kielimu ya Kiislam ni:
Shule za Imam Jawad huko jimbo la Karradeh Mashariki, Baghdad. Shule zote hizi ziliongozwa na Dr. Dawud Al-Attar.
Shule za Baghdad -Baghdad, ziliongozwa na Abdul-Rahim Shawki. Rawdhat al-Zahra - Chekechea ya watoto. Al-Zahra Shule ya Wanawake huko Kazimayn. - Shule hizi ziliongozwa na Shahid Bint-al-Huda Sadr, marehemu dada yake Ayatullah Shahid Sayyid Muhammad Baqir Sadr. Shule za Imam Sadiq - huko jimbo la Basra. Zikiongozwa na viongozi wa kidini wa Basra na mkuu wake alikuwa ni Sayyid Muhammad Abdul-Hakim. Sekondari ya juu ya Imam Baqir huko Hellah. Ikiongozwa na Sheikh Ali Samakeh. Sekondari ya juu ya Imam Hasan huko Diwaniyah. Ilianzishwa na Sheikh Muhammad Mahdi Shams Al-Din na ikaongozwa na 'Kituo cha Kiislamu cha Utoaji Sadaka'. Kituo cha Elimu kwa Wanawake huko Numaniyyah - katika jimbo la Kute. Kilianzishwa na Sayyed Qassim Shobba na kuongozwa na 'Kituo cha Kiislamu cha Utoaji wa Sadaka'. Kwa kutaja baadhi ya michango yake ya kijamii, mtu anaweza kuangalia uanzishwaji wa kituo cha kliniki cha "Mostosef Al-Ri'ayeh Al-Islamiyyah" (kituo cha afya cha Kiislam) katika jimbo la Karradeh Mashariki ya Baghdad mwaka 1382 A.H., na kituo kingine cha afya kwa jina hilohilo katika jimbo la Kazimayn ili kuuguza na kutibu wanafunzi wa kidini wa Kiislamu, wenye kuzuru kwenye makuba matukufu na masikini. Alidhamiria pia kutengeneza hospitali kubwa iitwayo "Hospitali ya Imam Hussein". Lakini mpango mkubwa na muhimu sana wa Allamah Askari ulikuwa ni kuanzisha shule ya theolojia huko Baghdad mwaka 1384 A.H. ili kuanzisha chuo kikuu kikubwa zaidi cha Kiislam chenye masomo yote ya taaluma. Baada ya kutokeza kwa chama cha Baath, ambao ni makafir (wasioamini) na utawala wake juu ya mambo ya Iraqi, Allamah Askari chini ya uongozi wa Ayatullah Hakim (R.A) na wafuasi wengine walionyesha upinzani wao kwa huo utawala wa 6
ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO
Baath. Matokeo yake, chama cha Baath kilitoa amri ya kukamatwa kwa Allamah Askari na ilimbidi aondoke Iraqi mwaka 1389 A.H. na kwenda Lebanon. Hii nchi ya baadae, pamoja na viongozi wengine wa kidini kama Sayyed Musa Sadr, mkuu wa Bunge Kuu la Kiislamu la Shi'ah, Muhammad Hussein Fazlullah na Sheikh Muhammad Mahdi Shams Al-Din waliendeleza upinzani wao dhidi ya utawala wa Iraqi. Lakini alipogundua kwamba nia ya utawala wa Iraqi ilikuwa ni kumkamata au kumteka nyara huko Lebanon, aliondoka nchini humo na akarudi Iran. Siku hizi, Allamah Askari, bila ya kujali umri wake wa uzee, anajitolea muda wake mwingi kushughulika na upeo mpana wa uandishi wake. Mengi ya maandishi yake hayajachapishwa bado na yeye (kama inavyotegemewa) bado anakerwa na matukio ya sasa hivi na anaweka juhudi zake zote bila unyimi kutetea dini ya Uislamu na kupeperusha bendera tukufu ya Uislamu kwenye nchi zote za Kiislamu. Huko Iran, Allamah Askari alitumia muda wake mwingi kusoma, kuendesha uchunguzi na kuchapisha vitabu. Pia, alifanikisha huduma mbalimbali za kijamii na kiutamaduni zikiwemo: a) Kuanzishwa kwa Baraza la Kisayansi la Kiislamu mwaka 1398 A.H. b) Kuchapishwa kwa vitabu vya kiada vitakavyo fundishwa katika Hauza za kidini. Miongoni mwa vitabu hivi mtu anaweza kurejea: i. Ta'alim Al-Lugha til arabiyyah (jinsi ya kufundisha lugha ya Kiarabu). ii. Al-Amthila wa Sarf Mir. iii. Al-Tassrif. iv. Al-Hidayah Fi Al-Nahaw. v. Qhawa'id Al-Imlah. vi. Tahdhib Al-Balaghah. vii. Al-Mantiq wa Manahij - Al-Bahth Al-Ilmi. viii.Tahdhib Sharh Ibn Aqil (cha kuchapishwa). ix. Tahdhib Al-Mughni. x. Muntakhab Hiliat Al-Mutaqin. xi. Al-Manhad Al-Muqtarrah Lisanawat Al-Arba (Mpango uliokusudiwa wa masomo ya kufundishwa kwa miaka minne) Majina ya vitabu vilivyochapishwa na Allamah Askari. Uchapishaji wake ni kama hivi hapa chini.
7
ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO
* Utafiti juu ya Qur'ani Tukufu - katika juzuu 3. 1) Qur'ani Tukufu wakati wa utume wa Mtukufu Mtume Muhammad (s.a.w.) na baada ya utume wake. 2) Qur'ani Tukufu na ngano za kidini ( chategemea kuchapishwa) 3) Qur'ani Tukufu na simulizi za Ahlu'l-Bayt [kizazi kitukufu cha Mtukufu Mtume (s.a.w.)] - chategemea kuchapishwa. *Utafiti katika theolojia ya Kiislam (kufundisha Uislamu). 1. Kufundisha Uislamu (kimechapishwa). 2. Maadili na kanuni za Kiislamu (kimechapishwa). 3. Muntakhab Al-Adiyah (dua zilizoteuliwa) - kimechapishwa. 4. Sheria katika Uislamu (cha subiri kuchapishwa). 5. Siasa katika Uislamu juu ya amri za kiserikali (cha subiri kuchapishwa). 6. Maoni ya Uislamu ndani ya Qur'ani Tukufu, juzuu tatu. i) Maoni ya Kiislamu toka siku ya kwanza ya kuumbwa hadi Qiyamah (kimechapishwa). ii) Tabia na mwenendo wa Mitume na Maimamu (cha subiri kuchapishwa) iii) Sheria za mwisho za kidini ( za kuchapishwa). *Ma'alim al-Madrassatayn (kigezo cha madhehebu mbili) katika juzuu nne. 1) Utafiti na uchunguzi wa madhehebu mbili (makatib) juu ya masahaba wa Mtume na Maimam (a.s.) 2) Utafiti na uchunguzi wa madhehebu mbili juu ya Rasilimali ya Sheria za Dini ya Kiislam (kimechapishwa). 3) Athari za kusimama kwa Imam Hussein katika kuhuisha sunnah za Mtukufu Mtume (kimechapishwa) 4) Maendeleo ya fikra za madhehebu mbili na makabiliano yao na maka8
ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO
bila ya Mongoli na shutuma zao kwa kizazi kitukufu cha Mtume toka karne ya 2 A.H. mpaka karne ya 12 A.H. (kitachapishwa) *Ensaiklopidia ya uchunguzi ili kutakasa sunnah ya Mtume kutokana na ngano potovu zilizohusishwa kwake: i) Ngano (simulizi) za Ummul-Mu'minin (Ayisha) - sehemu za maisha yake, juzuu ya1 (kimechapishwa). ii) Ngano za Ummul-Mu'minin (Ayisha) - uchunguzi wa simulizi zake, juzuu ya 2 (cha tegemewa kuchapishwa). iii) Abdullah Ibn Saba na ngano nyinginezo, juz. 1(kimechapishwa). iv) Abdullah Ibn Saba na ngano nyinginezo, juz. 2(kimechapishwa). v) Abdullah Ibn Saba na ngano nyinginezo, juz. 3( kuchapishwa). vi) Masahaba
mia
na
hamsini
wa
uwongo
kama
Ghamim,
juz.1(kimechapishwa). viii) Masahaba mia na hamsini wa uwongo pamoja na wa makabila mwengine, juz. 3(cha kuchapishwa). ix) Wasimuliaji wasio Sahihi (cha kuchapishwa). x) Aina mbalimbali za uwongo na waongo (cha kuchapishwa). xi) Ngano za Wayahudi na ngano za wakana-mungu na wapiga chuku (cha kuchapishwa). xii) Baadhi ya sifa na tabia za Mtume (s.a.w.) na kizazi chake kitukufu. xiii) Wasifu wa wale masahaba ambao walimuona Mtume (s.a.w.) na kupokea toka kwake (cha kuchapishwa) xiv) Wasifu wa wale masahaba waliomuona Mtume(s.a.w.) lakini hawakupokea toka kwake (cha kuchapishwa) xv) Wasifu wa wale masahaba ambao hawakumuona Mtume(s.a.w.) na hawakupokea toka kwake (kuchapisha). *Mfululizo wa vitabu vilivyoandikwa kwa Kifursi kuhusu dhima ya Maimam (A.S.) katika kuhifadhi mafundisho ya Uislam: 1. Istilahi za Kiislam (kimetafsiriwa kwa Kiarabu) 2-7 Ni kuhusu mambo muhimu kabla na baada ya Uislam. 8. Mtazamo mfupi kuhusu tabia na mwenendo wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) katika jamii za Waarabu kabla ya Uislam
9
ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO
9. Sunnah baada ya Mtume(s.a.w.). 10) Madhehebu za Kiislam. 11) Uimam (uongozi) kwa mtazamo wa madhehebu mbili: amri za Mtume (s.a.w.), watekelezaji na viongozi na walinzi wa Uislam. 12) Imani katika Tawhid (upweke wa Allah) kwa mtazamo wa madhehebu mbili. 13) Maelezo ya kanuni mbalimbali za Kiislam. 14) Wajibu wa Imam katika kuhuisha Sunnah.
MAONI YA DR. HAMID HAFNI DAWOOD, PROFESA WA LUGHA YA KIARABU KATIKA CHUO KIKUU CHA CAIRO. UKWELI NYUMA YA UWONGO Kumbukumbu ya kuzaliwa Uislam ya 1300 imekwisha sherehekewa. Katika wakati huu baadhi ya waandishi wetu wasomi wamewashutumu Mashi'ah eti kwa kutokuwa na maoni ya Kiislam. Waandishi hao walivutia maoni ya watu dhidi ya Shi'ah na wakasababisha hitilafu kubwa miongoni mwa Waislam. Badala ya busara na elimu, maadui wa Shi'ah walifuata imani na upendeleo wao wenyewe waliouchagua, kuufunika ukweli, na kuwashutumu Mashi'ah eti kuwa ni wenye itikadi za kidhana n.k. Hivyo Elimu ya Kiislam ilipata taabu sana, kwa kuwa maoni ya Shi'ah yalikandamizwa sana. Kwa matokeo ya shutuma hizi, kupotea kwa Elimu ya Kiislam kulikuwa kukubwa kuliko hasara waliyoipata Mashi'ah wenyewe kwa sababu chanzo cha maarifa haya ya sheria, ingawa ni kitajiri na chenye manufaa, kilitelekezwa, ikaishia kwenye kuwa na elimu finyu. Lakini! Huko nyuma watu wetu waliosoma walidhuriwa, vinginevyo tungeweza kunufaika kutokana na maoni mengi ya Ki-Shia. Yeyote anayetaka kufanya utafiti katika maarifa ya sheria ya Kiislam lazima aangalie rejea za Ki-Shia na zile za Sunni vilevile. Hakua Imam wa Ki-Shia Jafar al-Sadiq (aliyefariki mwaka 148 H.L), mwalimu wa Maimam wawili wa Ki-Sunni? yaani Abu Hanifah al-Nu'man Ibn al-Thabit (aliyekufa mwaka 150 H.L.) na Abu 'Abdullah Malik Ibn Anas (aliyekufa mwaka 179 H.L.). Abu Hanifah alisema, "Bila ya ile miaka miwili Nu'man angeangamia," akiashiria ile miaka miwili aliyonufaika kutokana na elimu ya al-Imam Jafar as-Sadiq. Malik pia alikiri wazi wazi kabisa, kwamba hajakutana na mtu yeyote aliyebobea 10
ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO
sana katika maarifa ya sheria ya Kiislam zaidi ya al-Imam Jafar as-Sadiq. Bado watu wasomi kama hao, kwa bahati mbaya walizidharau taratibu za utafiti kwa kunufaisha malengo yao. Hivyo elimu haikufunuliwa kwao kikamilifu, na walisababisha tofauti kubwa kati ya Waislam. Ahmed Amin alikuwa mmoja wa wale walionyimwa mwanga wa elimu, wakabakia katika giza, ingawa hata hivyo mshumaa wa Ushia ulikuwa ukiwaka daima na hakukuwa na mwanga mwingineo. Historia imelinakili doa hili katika joho la Ahmad Amin na marafiki zake, ambao walifuata kwa upofu madhehebu moja maalum. Katika makosa mengi yaliyofanywa na yeye, kubwa kabisa linaelezwa katika ngano ya 'Abdullah Ibn Saba'. Hii ni moja ya simulizi zinazosimuliwa ili kuwashutumu Mashia kwa uasi (wa kidini) na matukio yaliyopita. Mtafiti mashuhuri wa kisasa, mstahiki Sayid Murtadha al-Askari, katika kitabu chake amethibitisha kwa ushahidi thabiti, kwamba 'Abdullah Ibn Saba' alikuwa ni wa kubuni, na kwa hiyo ni uongo mkubwa kusema yeye alikuwa ndiye mwanzilishi wa Ushia. Sayyid Murtadha al-Askari ameshughulika sana katika historia na amethibitisha kutokana na rejea za Kisunni kwamba maadui wa Mashia ni wa uongo. Tangu siku za mwanzoni za Uislam hadi sasa, ngano kama zile za kuhusu 'Abdullah Ibn Saba' zilizoelezwa na Seif Ibn Umar, ziliaminika kama zilitoka kwenye vyanzo vya uhakika, lakini katika kitabu hiki, utafiti mkubwa sana umefanywa kuhusu ngano hizi, ili kuwezesha kupatikana kwa ukweli juu yao. Mwenyezi Mungu ameagiza kwamba watu waliosoma waufichue ukweli bila ya kujali lawama wanazoweza kupata. Mtangulizi katika nyanja hii ni mstahiki mtunzi wa kitabu hiki,ambaye amewafanya wasomi watafiti wa Kisunni kukipitia kitabu cha historia cha Tabari,(Historia ya Mataifa na Wafalme) na kuchekecha zile ngano sahihi kutoka zile za uongo. Ngano ambazo zilibakia bila kubadilishwa na kugeuzwa kwa karne kama Maneno ya Mwenyezi Mungu. Mwandishi mstahiki huyu, kwa ushahidi mwingi, ameuondoa utando au utata kutoka kwenye matukio yale ya kihistoria, na kwa njia bora kabisa akaufichua ukweli, kwa kiasi ambacho baadhi ya mambo yanaonekana yakushitusha. Bila shaka, baadhi yao yanaonekana kushangaza, kwani yanapingana na imani ya kipindi cha uhai wa mtu, na urithi wetu wa kidini - kwa umri wa karne nyingi. Lakini tunapaswa kuutii ukweli hata kwa kuonekana ugumu kiasi gani. "Haki ni bora ifuatwe" Ili kujua yote inahusu nini, mtu inambidi kusoma kitabu hiki na kuchunguza kwa makini matukio ambayo kwamba kuna maoni tofauti; kama vile: "Jeshi la Usama." "Kifo cha Mtukufu Mtume" "Ngano ya Saqifah" 11
ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO
Yote ambayo yamechunguzwa na mwandishi. Wakati Mtume wa Mwenyezi Mungu alipokaribia kufa, baadhi ya watu waliondoka kwenye Jeshi la Usama bila ruksa, na wakarudi Madina kwa matumaini ya kupata kazi za nyadhifa. Mwandishi anawatambulisha watu hawa kwetu. Akiwa kwenye kitanda cha mauti yake, Mtume alitaka kufanya wosia lakini watu wengine wakapuuza haja hii, na wakaiita "kuweweseka kwa mtu anayekufa". Pengine walikuwa wanahofia uwezekano wa kumtambulisha kwake al-Imam Ali kama mshika makamu wake. Mwandishi anaufichua ukweli kuhusu matukio haya. Ni nini Umar alikuwa nacho kichwani mwake kukataa kifo cha Mtukufu Mtume? Kwa nini alikuwa anawatishia kuwaua wale waliokuwa wakieneza habari za kifo cha Mtume? Wakati al-Imam Ali, binamu yake Mtume, ami yake Abbas na watu wazima wanaosha mwili wa Mtukufu Mtume, Umar na Abu Ubeydah kwa haraka sana wakaja Saqifah (chumba chenye baraza yenye paa) na kuwataka watu watoe kiapo chao kwa Abu Bakr. Ambapo kama wangengojea mpaka mazishi ya Mtume yakaisha, Ali ndiye mtarajiwa pekee wa ushika makamu wa Mtume, na Bani Hashim hawakumjua mtu mwingine. Mtunzi, chini ya vichwa vya habari vitatu hivi vilivyotajwa kabla, ameuchuja ukweli kutokana na uongo, wema kutokana na ubaya, mpaka ameufikia ukweli ulio dhahiri; na kwa sababu ya utafiti wake, milango ya ulaghai na udanganyifu imefungwa daima kwa wala njama. Masomo mengine katika kitabu hiki yanaonyesha ukweli kwa uwazi kabisa, kwamba hivi karibuni, mabadiliko makubwa katika historia ya Uislam yatatokea. Ningependa kuweka maswali matatu kwa wasomaji kabla sijamalizia makala yangu: 1. Je hivi sahaba wa karibu wa Mtume anaweza kufanya kosa? 2. Je tunaweza kukosoa kazi yake? 3. Je, tunaweza kusema kwamba sahaba mtukufu wa Mtume ni mnafiki au asiyeamini (kafir)? Majibu kwa maswali mawili ya kwanza ni dhahiri, lakini jibu kwa la tatu liko kinyume - siyo kwa sababu nina chuki na ninasema kitu kilicho kinyume na mantiki - -la hasha, ninayo sababu ya msingi na ya kimantiki, kwani kutoamini na unafiki kunatoka moyoni, na hakuna yeyote ila Allah (swt) anayejua yaliyomo kwenye mioyo yetu na siri za wanadamu. Ninafurahi kutoa heshima kubwa kwa kitabu hiki na mtunzi wake mstahika, mtafiti aliyebobea Sayyid Murtadha Askari. Nimeridhishwa pia na Bw. Murtadha Rizvi Kashmir (mchapishaji) ambaye amekitoa kitabu hiki katika sura ya kupendeza, ametimiza wajibu wake, huduma kwa Uislam. Jukumu hili litabeba uzito zaidi katika kuhuisha historia halali ya Kiislam. 12
ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO
Dr. Hamid Hafni Dawood 12thOctober,1961 Cairo - Misri. Makala hiyo hapo juu imeandikwa na mwanachuoni wa Kisunni, ambaye ameukata mzizi wa ushabiki na kugombana kwa nia tu ya kuzozana. MAONI YA SHEIKH MAHMOOD ABU RIYYA
Mmoja wa Ulamaa wa Misri Bwana Abu-Riyya ametuma barua ifuatayo kwa Allamah Sayyed Murtadha Al-Askari na kuomba nakala ya ya kitabu cha Abdullah Ibn Saba. Profesa Sheikh Murtadha Al - Askari, Najaf, Iraq Utukufu na amani ya Allah uwe juu yako Hivi karibuni kulikuwa na mjadala miongoni mwa kikundi cha wanazuoni wa Kiislam juu ya mada tofauti, yakiwemo maandishi yenye maana ya wanasayansi na watunzi ambayo ni yenye faida kwa Waislam. Mmoja wa washiriki alikitaja kitabu chenye thamani "Abdullah Ibn Saba" ulichoandika wewe na ambacho ndani yake umezungumzia bayana kwa mara ya kwanza kuhusu baadhi ya mambo mapya na ambayo ndiyo maana nimeshawishika sana kujifunza zaidi kuhusu kitabu hicho na nikategemea kupata nakala moja kwa moja kutoka kwako. Bila shaka nitakuwa na deni kwako, ikiwa utaweza kunitumia nakala. Naomba nitangulize shukurani zangu za dhati Amani na Utukufu wa Allah uwe juu yako. Mahmood Abu Riyya Misri, Jimbo la Al-Khabirah Rajab 20, 1380 Hijiria June 11, 1960.
13
ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO
Baada ya kupokea na kukisoma kitabu alituma barua ifuatayo kwa Ayatullah AlAskari na Kuthibitisha yale yaliyokuwemo ndani ya kitabu hicho.
Mpendwa Profesa Murtadha Al-Askari Amani na Utukufu wa Allah na Rehma Zake ziwe juu yako. Ningependa kuchukua nafasi hii kusema maneno kidogo juu ya kitabu chako "Abdullah Ibn Saba." Nimekisoma mara moja na ninakusudia kukisoma tena hivi karibuni. Ngoja niseme kwamba umetumia mtazamo mpya na wa kitaalam juu ya suala hili katika utafiti na mijadala yako, ambao haujatumiwa na mtu mwingine yeyote kabla. Nakupongeza kwa uaminifu na kwa dhati kweli kweli, kwani Allah amekujaalia wasaa wa kufuatilia mjadala huu na amekuongoza kufichua mambo ambayo hakuna mwingine aliyeyazungumzia katika karne 14 zilizopita. Matokeo ya utafiti wako yanathibitisha ubishi wa mwanasayansi wa Kizungu, Wales, aliyesema, "Historia moja kwa moja ni mwandamano wa uongo." Kwa bahati mbaya inaoana na historia ya Uislam iliyoandikwa kwa shauku ya chuki na ubaguzi kwa nyakati tofauti. Hii ni kweli kwa kiwango fulani kwamba inaleta umuhimu sasa wa kuanza uchunguzi wa historia wa makusudi na wa kina. Hasa, kitabu chako "Abdullah Ibn Saba" ndiyo chanzo juhudi kama hiyo ya utafiti. Tumshukuru Allah (swt) kwamba uliipata fursa hii na namuomba Allah (swt) akupe nguvu na moyo wa kuendelea katika njia hii bila woga, kufichua mambo bila kusita, na akuongoze katika kutumia kipaji na fasaha yako katika mijadala yako na kuomba kwamba wasomaji wako nao wafanye vivyo hivyo katika kulifahamu hilo jambo, hasa kuhusu Abu Bakr na Umar kwa vile hatuwezi siku zote kustahimili ukweli wa wazi. Kwa kufunga, naomba nizitume salamu zangu za kweli kwako. Utukufu na Neema za Allah (swt) ziwe juu yako.
Wako wa kweli, Mahmood Abu Riyyah Misri, Jimbo la Al-Khabirah Rajab 20, 1380 Hijiria - 1961.
14
ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO
MAONI YA AL - SHEIKH JAWAD MUGHNIYYAH (MWANACHUONI WA KISHIAH) "Kila kitu katika dunia hii kinabadilika isipokuwa maandishi dhidi ya Shiah. Kwa kila mwanzo una mwisho, isipokuwa shutuma dhidi ya Mashiah. Kila hukumu inaungwa na ushahidi, isipokuwa hukumu dhidi ya Shiah. Kwa nini? Kwani Mashiah ni wakorofi au wachochezi wenye vurugu ambao wanapenda tu kuwavuruga watu?" Jibu hili hapa. Katika Karne ya Pili ya Enzi ya Uislam (H.L.), aliishi mtu aliyeitwa Seif Ibn Umar at-Tamimi. Aliandika vitabu viwili: 1. al-Fatuh wal Reddah. 2. al-Jamal wal Masiiri Ayishah wa Ali. Alifanyia kazi malengo mawili katika vitabu vyake viwili: 1. Kubuni ngano bila msingi. 2. Kunukuu matukio katika njia ambayo kwamba ukweli ulionekana kama uongo, na uongo ukaonekana kama ukweli. Alibuni Masahaba kwa ajili ya Mtume kama vile Suiir, Hazhaaz, Ott, Humaiza n.k. Alinukuu ngano zake kwa namna ambayo zilionekana kama zimesimuliwa na watu ambao walikutana na masahaba hawa. Miongoni mwa mashujaa wake wa kubuni ni 'Abdullah Ibn Saba', ambaye anadhaniwa kuwahi kusimulia hadithi kuhusu Mashia; ngano zote dhidi ya Mashia zilizoandikwa na wana historia zimetokana na Seif. Baada ya Seif, wana historia walivikubali vitabu vyake kama vya kweli tupu. Tabari alikuwa mwanahistoria wa kwanza aliyetegemea vitabu vya Seif. Wanahistoria wengine, Ibn Athir na Ibn Asakir, miongoni mwao, walimfuata Tabari kiupofu. Seif alibuni ngano na akachanganya matukio sahihi lakini chanzo pekee cha ngano zake zote ni vitabu vyake mwenyewe 'al-Fatuh' na 'al-Jamal Hiki kitabu 'Abdullah Ibn Saba' kinathibitisha kwamba maelezo hayo hapo juu ni ya kweli na kazi ya mtunzi wake mwenye elimu, ni kuonyesha ukweli kama ulivyokuwa, bila ya kuuharibu kwa kuupamba sana. Hakuna hata mtu mmoja mwenye elimu anayeweza kukataa, au kushuku chochote kile ambacho Sayyid Murtadha al-Askari ameandika kwa sababu kitabu chenyewe kinatokana na ushahidi wa kimantiki na hakuna anayeweza kukataa mantiki na usemi wa dhahiri. Nimekijadili 'Abdullah Ibn Saba' na watu wengi, lakini nimewajibu kama wasomi waliopita walivyofanya, isipokuwa kwamba nimefanya rahisi kwao kuelewa, kwamba, niliamini kuwepo kwa 'Abdullah Ibn Saba'. Sasa, msomi mzuri sana Sayyid 15
ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO
Murtadha al-Askari, ameibadili kabisa ngano hiyo, na akathibitisha kwamba 'Abdullah Ibn Saba' ni wa kubuni. Ninaweza kusema kwamba hiki ni kitabu cha kwanza cha Kiarabu kilichochunguza historia kisayansi. Mtunzi amefanya huduma kubwa siyo tu kwa ajili ya dini, elimu na Ushia, bali kwa Uislam. Ameufunga mlango kwa wale ambao walitaka kuuvuruga umoja wa Waislam, na kwa wale Sunni wanaopata ujasiri kutokana na ngano zao za uongo. Leo ushahidi wao wa kwanza na wa pekee, ngano za Ibn Saba na Ibn Sauda zilizobuniwa na Seif zimethibitishwa kuwa ni za uongo. Mohammed Jawad Mughniyyah Lebanon.
16
ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO
MAONI YA PROFESA JAMES ROBINSON D. Ltt., D. D. Glasgow, U. K. Mpendwa Sayyid Murtadha al-Askari, Ilikuwa ni katikati ya mwezi wa Agosti iliyopita nilipopokea kutoka kwako nakala za vitabu vyako viwili, 'Abdullah Ibn Saba' wa Asatir Ukhra, na Khamsun wa-mi'a Sahabi Mukhtalq, al-Qasim al-Awwal. Wakati nilipokuandikia napenda niseme kwamba sasa ni mzee na siko mwenye afya njema, kwa hiyo, nitahitaji muda wa kuvipitia vitabu hivi. Imenichukua mudu mrefu kuliko nilivyotegemea; lakini nimevisoma vitabu hivi mara mbili kwa shauku kubwa, na ingawa ningependa kuandika kwa kirefu kiasi, nahisi ni lazima niandike kuelezea kufurahishwa kwangu na njia iliyochukuliwa na utaalam makini ulioonyeshwa katika vitabu viwili hivi. Kwa umri wangu siwezi kutazamia kwa kujiamini kuwa na uwezo wa kuandika na hivyo naona nisichelewe zaidi nisijejikuta sina uwezo tena wa kuandika. Katika kitabu cha kwanza nimependa yale maelezo ya kina ya ngano ya jadi ya 'Abdullah Ibn Saba' na Sabaiyyah (wafuasi wa Ibn Saba), ikifuatiwa na mjadala mzito wa waandishi (wa zamani na wa sasa) huko Mashariki na Magharibi na mielekeo ambayo waliitegemea. Ile jedwali iliyoko ukurasa wa 43 ni yenye msaada sana katika kuonyesha vyanzo vikuu vya habari kuhusu Seif na ngano zake na jinsi waandishi wa baadae walivyotegemea juu ya moja au nyingine kati ya hizi. Kisha inakuja orodha ya baadhi ya waandishi waliotoa maoni yao juu ya tathmini ya ngano za Seif, kutoka kwa Abu Dawud (kafa 275 - maandishi yanasema 316 kimakosa) kwa Ibn Hajar (kafa. 852 ). Kama wote wanavyozungumza kwa kukosoa, kwa kutumia maneno kama "dhaifu", "ngano zake zimeachwa," "Haina thamani", "Muongo", "Anashukiwa kuwa Zandiki" n.k. Wanakubaliana katika kuthibitisha huko kutokuaminika, au hata uongo wa ngano hizo. Hii ni hoja nzito kabisa. Katika kuchunguza maoni ya waandishi juu ya wasimuliaji mbali mbali, nimegundua kwamba wote hawakubaliani. Lakini hapa hakuna kutokukubaliana ambako kunamfanya mtu ashangae kwa ninni waandishi wa baadae wamekuwa tayari hivyo kukubali taarifa za Seif. Lakini ningependa kutoa maoni juu ya Tabari ambaye hana wasiwasi katika kumnukuu Seif. Historia yake (kitabu chake), siyo kitabu cha historia kwa namna ya uandishi wa kisasa, kwani lengo lake kuu linaonekana lilikuwa ni kuandika habari zote alizokuwa nazo bila kulazimika kutoa maoni juu ya tathmini yake. Mtu, kwa hiyo, yuko tayari kuona kwamba baadhi ya taarifa zake siyo za kuaminika kuliko nyingine. Hivyo, pengine tunaweza kumsamehe kwa kutumia njia ambayo haikubaliki siku hizi. Ametoa angalau lundo la habari. Inabakia kwa wanazuoni watambuzi kama wewe mwenyewe kupambanua kati ya kweli na batili. Katika kujadili idadi fulani ya mambo yaliyotajwa na Seif, hoja hiyo inaendeshwa katika namna inayofaa, kwanza kutoa maelezo ya Seif na kisha kuyalinganisha na 17
ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO
maelezo yaliyotolewa na wengine. Ulinganishaji huu makini unashughulika na vyote, habari zenyewe na sanadi, na inaonyeshwa kwamba Seif mara nyingi ananukuu watu wasiojulikana. Hii inaleta swali kwamba kwa nini hata mmoja wao asinukuliwe na wasimuliaji wengine, na inamuongoza zaidi mtu kufikiria kwamba Seif amewabuni. Shutuma hii kali ni dhana ya maana kwa kumlinganisha Seif na wengine. Imeonyeshwa kwamba Seif anazo ngano zenye kutokea kwa maajabu ambazo ni vigumu kuziamini, kama vile mchanga wa jangwani kuwa maji kwa ajili ya majeshi ya Waislam, bahari zigeuke kuwa mchanga, ng'ombe wanazungumza na kuwajulisha Waislam walipokuwa wamefichwa, n.k. Katika wakati wa Seif ilikuwa inawezekana kwake kufanikiwa kutengeneza ngano na historia kama hizo, lakini wakati huu mwanafunzi makini kwa kawaida huziona ngano kama hizo haziwezekani kabisa. Hoja zenye nguvu pia hutumika kuonyesha jinsi habari za Seif kuhusu Ibn Saba na hao Sabaiyya siyo za kuaminika kabisa. Mwandishi anadokeza kwamba baadhi ya mutashirki wameegemeza uchunguzi wao juu ya taarifa za Seif, mambo kama ile idadi kubwa ya watu waliouawa kwenye vita vya awali vya Waislam, wazo la kwamba Myahudi asiyejulikana, Abdullah Ibn Saba, yangeweza kuwa kishawishi cha kuwapotosha Masahaba wa Mtume kutoka kwenye imani yao, na kimekuwa kishawishi kikuu katika kuwaamsha watu kuasi dhidi ya Uthman na kusababisha kifo chake, na kuchochea mapigano yaliyofanywa na Ali pamoja na Talha na Zubayr. Hii inaweza kuwa kweli kwa baadhi, lakini haikuwa kweli kwa wote. Hili ni dhahiri kutokana na makala kuhusu Abdallah Ibn Saba katika chapa ya kwanza na ya pili za Ensaiklopidia ya Uislam. Seif alitumia muda mwingi kutengeneza mashujaa kutoka Tamim, kabila ambalo Seif alifuatilizia nasaba yake, lakini Sir William Muir zamani sana alieleza jinsi Tamim walivyokuwa wasalimu amri kwa majeshi ya Ukhalifa wa awali katika wakati wa kile kinachoitwa kuritadi. Sir Thomas Arnold anaweza kuonekana akivuta nadhari kwenye ukweli kwamba ule ushindi wa manzo haukuwa hazikuwa hasa kwa madhumuni ya kueneza imani, kwa ajili ya kupanua eneo la utawala wa Waislam. Katika kitabu cha pili inavutwa nadhari kwenye ukweli kwamba Seif ambaye aliishi katika robo ya kwanza ya karne ya pili ni wa Tamim, moja ya makabila ya Mudar ambao waliishi Kufa (Iraq). Hii inamsaidia mtu kuchunguza mwelekeo wake na athari zinazopelekea kwenye hekaya hii. Kuna mjadala wa Dini ya zamani ya waajemi. Moyo na ushabiki wa chama unasemekana kuendelea kutoka wakati wa Mtume, mpaka ule wa Bani Abbas. Seif alitetea makabila ya kaskazini, akibuni mashujaa, washairi wanaosifu hao mashujaa wa makabila, masahaba wa Mtume kutoka kabila la Tamim, vita na mapigano yasiyo na ukweli, mamilioni waliouawa na idadi kubwa ya mateka kwa nia ya kuwatukuza hao mashujaa aliowabuni. Mashairi yaliyohusishwa na kwa mashujaa wa kubuni yalikuwa ya kuwatukuza makabila ya Mudar, kisha Tamim, kisha Ibn 'Amr, kabila dogo Seif alilofuatilizia asili 18
ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO
yake. Seif aliwataja watu wa Mudar kama viongozi wa vita ambavyo viliongozwa na watu wa makabila mengine, viongozi wake wa uongo wakati mwingine wakiwa watu wa kweli, wakati mwingine majina yalitokana na ubunifu wake. Inasemekana kwamba udanganyifu wa habari zake ulikuwa kwa sehemu fulani wa kugeuza imani ya wengi na sehemu fulani kuwapa wasiokuwa Waislam dhana potofu. Alikuwa fundi sana katika udanganyifu wake kiasi kwamba ulionekana kama historia halali. Huu ni mukhtasari mfupi wa uongo ambao kwamba Seif alikuwa na hatia. Sehemu kuu ya kitabu inaelezea kwa kirefu kuhusu watu ishirini na watatu, wakitoa mifano ya maandishi ya Seif na kuonyesha jinsi alivyotofautiana na waandishi halali siyo tu katika habari bali pia katika sanadi kwa kutumia majina ya watu ambao hawapo. Kazi hiyo imefanywa kwa maelezo makubwa ikitoa hoja nyingi mno dhidi ya tegemeo la Seif mbali na waandishi mashuhuri wanaoweka habari katika maandishi yao. Vitabu viwili vya Seif vinachunguzwa kuonyesha kwamba siyo vya kutegemewa kama maandishi mengine ambayo watunzi wa baadae wamenukuu kutoka kwake. Huu ni uchunguzi unopenyeza sana uliofanywa kwa utambuzi makini na ukosoaji wa hali ya juu sana. Ninashukuru sana kwa kuweza kupata fursa ya kutumia muda mwingi wa kutosha kuchunguza hoja ambazo zinanivutia kama zenye kuridhisha sana, na nina hakika kwamba wote wanaochunguza vitabu hivi kwa uwazi wa fikra watakuwa tayari kuthamini nguvu ya hoja hizo. Pamoja na shukrani nyingi sana kwa kunitumia vitabu hivi, na ninaomba samahani kwa, kutokana na umri wangu pamoja na udhaifu mwingine kwa sababu ya uzee, kuchukua muda mrefu katika kukujibu. Wako mwaminifu, James Robinson.
19
ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO
UTANGULIZI NGANO YA 'ABDULLAH IBN SABA' Wanahistoria wanasema kwamba Myahudi anayeitwa 'Abdullah Ibn Saba' alibadilishwa kuwa Mwislamu katika wakati wa Khalifa Uthman, ili kutimiza malengo yake kwa amani kwa kufanya maadui ndani ya Ummah wa Kiislam. Huyu 'Abdullah Ibn Saba alieneza mawazo yafuatayo miongoni mwa Waislam. a) Kufufuka kwa Mtume. b) Mitume wote walikuwa na warithi - mrithi wa Mtume Muhammad ni Ali, binamu yake na mkwewe. Amenyan'ganywa cheo chake kitukufu na khalifa Uthman, na kwa hiyo ni muhimu kuasi dhidi ya Uthman kwa fadhila ya Ali. Abdullah Ibn Saba aliunda kundi lililoitwa Sabaia (wafuasi wake Ibn Saba), na kundi hili liliasi na kumuua Uthman, khalifa wa tatu. Pia walifanya fitna kati ya majeshi ya Ali na Talha, adui yake, wakati makubaliano ya amani yalikuwa yakitegemewa katika Vita vya Jamal karibu na Basra. Hawa Sabaia ambao walikuwa wameandikishwa kwenye majeshi yote, walianza kurusha mishale mapema asubuhi moja bila kungojea amri yoyote kutoka kwa amirijeshi, na hivyo waliianzisha vita. Kwa hiyo, Myahudi huyu alikuwa ndiyo chanzo hasa cha fitina hizi na vita miongoni mwa Waislam, na ndiye mtu aliyeeneza wazo la kufufuka kwa Mtume Muhammad, na wazo la Ali kuwa mrithi wa Mtume miongoni mwa Waislam. ASILI YA NGANO YENYEWE Kisa cha 'Abdullah Ibn Saba' kina zaidi ya karne kumi na mbili sasa. Wana-historia na waandishi, mmoja baada ya mwingine wakakiandika, na kuongeza zaidi na zaidi juu yake. Wanahistoria wote wanakubali kwamba ngano hii ilisimuliwa kwanza kabisa na Seif. Wana-historia wafuatao waliinukuu moja kwa moja kutoka kwa Seif: 1) Tabari. 2) Dhahabi - aliisimulia pia kutoka kwa Tabari. 3) Ibn Abi Bakr - amenukuu pia kutoka kwa Ibn Athir 15, ambaye amenukuu kutoka kwa Tabari. 4) Ibn Asakir. Wafuatao wamenukuu katika mzunguuko (siyo moja kwa moja toka kwa Seif): 20
ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO
5) Nicholson kutoka kwa Tabari 2. 6) Ensaiklopidia ya Uislam kutoka kwa Tabari 2. 7) Van Floton kutoka kwa Tabari 2. 8) Wellhauzen kutoka kwa Tabari 2. 9) Mirkhand kutoka kwa Tabari 2. 10) Ahmad Amin kutoka kwa Tabari, na kutoka kwa Wellhauzen. 11) Farid Wajdi kutoka kwa Tabari 2. 12) Hassan Ibrahim kutoka kwa Tabari 2. 13) Saeed Afghani kutoka kwa Tabari 2, na kutoka kwa Abi Bakir 3, Ibn Asakir 4, na Ibn Badran 21. 14) Ibn Khaldoun kutoka kwa Tabari 2. 15) Ibn Athir kutoka kwa Tabari 2. 16) Ibn Kathir kutoka kwa Tabari 2. 17) Donaldson kutoka kwa Nicholson 5, na Ensaklopidia 6. 18) Ghiathud Din kutoka kwa Mirkhand 9. 19)
Abulfada kutoka kwa Ibn Athir 15.
20)
Rashid Redha kutoka kwa Ibn Athir 15.
21)
Ibn Badran kutoka kwa Ibn Asakir 4.
22)
Bostan kutoka kwa Ibn Kathir 16.
Orodha hiyo hapo juu inatoa ushahidi kwenye ukweli kwamba ngano ya 'Abdullah Ibn Saba' imeanzishwa na Seif na kusimuliwa kwa mara ya pili kutoka kwa Tabari. Kwa hiyo, tabia na historia ya Seif ichunguzwe na kuchambuliwa kwa uangalifu mkubwa. SEIF NI NANI? (WASIFU MFUPI) Seif Ibn Umar Tamimi aliishi katika karne ya pili ya zama za Uislam (karne ya 8 A.D.) na akafa baada ya mwaka 170 A.H. (750A.D.). Aliandika vitabu viwili. 1) al-Futuuh wal Ridhah - ambacho ni historia ya kipindi kabla ya kifo cha Mtukufu Mtume mpaka Khalifa wa tatu Uthman alipochukua madaraka kama mtawala wa ulimwengu wa Kiislam. 2)
al-Jamal wal Masiiri Ayishah wa Ali - ambacho ni historia toka kuuawa kwa Uthman mpaka vita vya Jamal. Vitabu hivi viwili vimejaa msisimko mwingi kuliko ukweli; baadhi ya ngano za 21
ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO
kubuni, na baadhi ya matukio ya kweli ambayo, kwa makusudi, yameandikwa kwa namna ya dhihaka. Kwa vile Seif alizungumza juu ya baadhi ya masahaba wa Mtume, na pia akabuni baadhi, ngano zake zimeathiri historia ya Uislam wa awali. Baadhi ya waandika wasifu kama vile watunzi wa Usudulghabah, Istiab na Isabah na wana-jogorafia kama vile watunzi wa Mujami-ul Buldan na Al-ruwzumi'tar wameandika maisha ya baadhi ya masahaba wa Mtume, na wakataja majina ya sehemu ambazo zimo tu kwenye vitabu vilivyoandikwa na Seif. Kwa sababu hii, maisha na tabia ya Seif lazima yachunguzwe kwa makini na kwa uangalifu. Matokeo ya uchunguzi wa maisha ya Seif yanaonyesha kwamba Seif alikuwa mkana habari za Mungu na msimuliaji ngano asiyeaminika. Ngano zilizosimuliwa na yeye ni zenye mashaka na zote au sehemu zake ni za kubuni. Zifuatazo ni baadhi ya ngano alizosimulia yeye: 1.
JESHI LA USAMA:
Mtume aliandaa jeshi la kwenda Syria. Kiongozi wa jeshi hili alikuwa ni Usama. Kabla ya safu ya mwisho haijaondoka mpakani mwa mji wa Madina, Mtukufu Mtume akafa. Usama akamtuma Umar kupata idhini kutoka kwa Abu Bakr mrithi wa Mtume. Umar pia alibeba ujumbe kutoka kwa baadhi ya Ansari wakishauri kwamba jemedari Usama abadilishwe. Abu Bakr aliusikia ujumbe huo, akaruka, na akamkamata Umar kwenye ndevu zake, akamfedhehesha kwa kusema, "Mtume alimfanya Usama kuwa jemedari, mimi sitambadilisha." Akaamuru kuondoka haraka kwa jeshi la Usama na kumlaani Umar akisema, "Msiba uwe juu yako." Wanahistoria wa wakati huo wameliandika tukio hilo kwa tofauti kabisa. 2.
SAQIFA, UKUMBI WA BANI SAIDAH:
Siku ile ile aliyokufa Mtume (s.a.w.), Seif anasema, Muhajirina wote walimuunga mkono Abu Bakr kama mrithi wa Mtume, isipokuwa wale walioukataa Uislam. Habari za kuchaguliwa Abu Bakr zilimsisimua sana Ali kiasi kwamba alitoka, akiwa amevaa shati lake tu. Akapeana mikono na Abu Bakr kirafiki na baadae nguo zake zilipoletwa akazivaa, akakaa chini kando ya Abu Bakr. Seif anaendelea, akisema kwamba Abu Bakr alidai kuwa na shetani katika moyo wake na kwamba Waislam lazima wamuangalie, na wamzuie kutenda dhulma kwake. Seif alisimulia ngano saba za kuhusu Saqifah. Walikuwepo mashujaa watatu katika ngano hizi, wakiwemo miongoni mwao Masahaba wa Mtume. Majina yao hayakutajwa mahali popote isipokuwa kwenye ngano za Seif. Upekee huu unamfanya mtu kufikiri, na kutilia shaka ukweli wa ngano zenyewe. Wakati vitabu vya kuaminika, vinavyokubaliwa na viongozi wa Sunni vikitazamwa, mkengeuko wa Seif toka kwenye ukweli, katika kuandika matukio ya Saqifah, unaweza kuwa tayari kugundulika. 22
ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO
KUHUSU UKUMBI WA SAQIFA BANU SAIDAH KWA MUJIBU WA VYANZO SAHIHI Katika kitanda chake cha umauti, Mtume Muhammad alitaka kuandika wosia. Umar akampinga, na baadae alitoa vitisho dhidi ya watu kama watathubutu kueneza habari za kifo cha Mtume mpaka Abu Bakr alipofika. Kisha ghafla Umar akanyamaza. Wakati familia ya Mtume wakihangaika na ibada za mazishi, Kundi la Ansari lilikusanyika ndani ya ukumbi kumchagua Sa'd Ibn Ubada kama mrithi wa Mtume. Umar, Abu Bakr na marafiki zao walikimbilia kwenye ukumbi huo kujiunga na mkutano huo. Mwishowe, uchaguzi ulikamilika kwa kuchaguliwa Abu Bakr. Kundi hilo kisha ndipo likaenda Msikitini kutoa kiapo cha utii cha Waislamu wote kwa Abu Bakr. Wakati wote huu mwili wa Mtukufu Mtume ulilazwa ndani ya nyumba yake na familia ya Mtume tu na mtu mmoja wa Ansari ndiyo waliokuwepo. Baada ya kiapo cha utii kwa Abu Bakr katika ukumbi na Msikitini kilipokwisha, watu walikwenda kwenye nyumba ya Mtume na wakajiunga na sala za mazishi. Mwili wa Mtume ulilala kwenye kitanda chake cha mauti toka Jumatatu mchana hadi Jumanne usiku mazishi yalipofanyika. Familia ya Mtume tu ndiyo iliyohudhuria mazishi. Al-Imam Ali na Bani Hashim (binamu zake Muhammad), hawakutoa ridhaa ya kuchaguliwa Abu Bakr kama mrithi wa Mtume, na walichukua hifadhi kwenye nyumba ya Fatima, binti ya Mtume. Umar alikwenda nyumbani hapo kuwachukua kuwapeleka Msikitini kutoa kiapo cha utii kwa Abu Bakr. Lakini walikataa kumuunga mkono Abu Bakr kwa kipindi chote cha uhai wa Bibi Fatima. Baada ya miezi sita Ali na Bani Hashim hatimae wakatoa ridhaa yao na kiapo baada ya kufariki Fatima. Matukio yote hayo hapo juu, uamuzi juu yao kutoka kwa Ibn Abbas, Abu Dhar, Miqdad, Abu Sufyan, Mu'awiyyah na Umar Ibn Khatab, mukhtasari juu ya maisha ya Sa'd Ibn Ubadah katika umri wake wa uzeeni, na ulinganisho baina ya maandishi ya Seif na yale ya kutoka kwenye vyanzo vya kuaminika, yamekusanywa katika kitabu hiki cha sasa. Kinaonyesha jinsi Seif alivyoandika wasifu za masahaba wa Mtume kuiridhisha serikali ya wakati huo na kufaa maoni ya watu wa kawaida. Seif alighushi ili kuunga mkono ushahidi wake na kulinda maoni yake, ili kuidhihaki historia ya Kiislam. Kwa karne nyingi ngano za Seif zilikuwa zikionekana kama ndiyo historia ya Uislam. Ni wakati wa kufichua vyanzo vya hizi ngano za uongo za Seif na watu wa aina yake, ili kuuonyesha Uislam kama ulivyo hasa, kwa kujifunza ngano za kweli kuhusu Muhammad, familia yake na masahaba. Tusimtetee Seif na simulizi zake, au kuzilinda kwa jina la ngano za Kiislam. Vinginevyo, tutaudhuru Uislam kwa kupinga uenezaji wa ukweli wa Uislam.
23
ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO
DIBAJI VIPI NA KWA NINI KITABU HIKI KIMEKUJA Mnamo mwaka 1949(1369H.L.), nilikuta ngano za Uislam zenye mashaka ndani ya vitabu vya historia ya Kiislam. Hizi nilizikusanya kutoka kwenye vyanzo tofauti. Baada ya uchunguzi makini niliridhika kwamba baadhi yao zimezushwa kwa malengo maalum. Kisha nilihisi wajibu wa kutekeleza kuzitangaza. Nilipanga maelezo yangu ili kutengeneza kitabu cha kuitwa ngano za Seif. Msomi mkubwa, mashuhuri ndugu Sheikh Radhi Aali Yasin, mwandishi wa kitabu 'Sulhul Hasan' alinihimiza kuendelea na kazi hiyo, na akanishauri kitabu hicho nikipe jina la 'Abdullah Ibn Saba' , na mimi nikakubali kwa furaha sana. Maandishi ya maelezo hayo yaliwekwa kwa miaka saba mbali na ndugu zangu wasomi wachache, hakuna aliyeyajua. Nilikuwa na wasiwasi kwamba ningeamsha hisia za watu wa Mashariki, kwani yalikuwa kuhusu matukio katika wakati wa Mtume mpaka mwaka 36H.L. Vitabu vya historia vya miaka hiyo vilikubaliwa kama kweli tupu na bila shaka watu walikuwa na imani juu yao, na walijifunza kutoka humo juu ya wahenga wetu wa kale wa Uislam. Mjadala huu unavunja misingi ya kihistoria juu yake ambayo wanahistoria wameegemeza vitabu vyao. Unaonyesha jinsi gani zisivyoaminika baadhi ya ngano za Kiislam, na kukanusha usahihi wa baadhi ya vyanzo. Msomaji ataona kwamba mjadala huu haukukomea kwenye ngano za 'Abdullah Ibn Saba' tu, bali katika mazungumzo haya, itaonekana kwamba viko vyanzo vingine vingi visivyoaminika. Kwa sababu hii, nilihofia mpaka nilipogundua kwamba waandishi wengine wawili walikwisha jadili (kwa maandishi) baadhi ya sehemu zake. Ndipo nikaanza kuchapisha kitabu changu. Nimetaja tu vile vitabu vilivyokuwa vimeandikwa kabla ya mwaka wa 500 H.L.
Murtadha al-Askari Baghdad, 1955 A.D. 15 Ramadhan,1375.
24
ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO
NGANO YA ABDULLAH IBN SABA Kwa miaka elfu moja wana-historia wamekuwa wakiandika ngano za kushangaza kuhusu 'Abdullah Ibn Saba' na wafuasi wake - Sabaia a) b)
Abdullah alikuwa ni nani, na nani walikuwa Sabaia - wafuasi wake? 'Abdullah alisema nini, na ni nini alichokifanya?
MUKHTASARI WA KILE KINACHOJULIKANA KUTOKA KWA WANAHISTORIA Myahudi kutoka Sana'a (Yemen) alijifanya kama aliyesilimu na kuwa Mwislamu katika wakati wa Uthman, Khalifa wa tatu na akapanga njama dhidi ya Uislam na Waislam. Alisafiri nje kwenye miji mikubwa kama: Kufa, Basra, Damascus, na Cairo, akihuburi imani ya Kufufuka kwa Mtukufu Mtume Muhammad, kuwa kama kurudi kwa Isa (Yesu) duniani hapa, kabla ya Siku ya Qiyammah. Alihubiri pia wazo la unabii, na akadai kwamba al-Imam Ali alikuwa ndiye mrithi wa haki wa Mtume Muhammad akimshutumu Uthman kwa kupora kwa dhulma nafasi ya al-Imam Ali. Aliwasisitiza watu kwa bidii sana kumuua Khalifa Uthman, ambaye baadae aliuawa. Wanahistoria walimuita Myahudi huyu, 'Abdullah Ibn Saba' , kama shujaa wa ngano hizo. Alijulikana kama Ibn Amatus-Sawda, ikiwa na maana ya mtoto wa mtumwa wa ki-Negro. 'Abdullah alituma ujumbe wake kwenye miji mingi akijifanya kuhubiri imani ya kweli ya Kiislam kuhimiza mema, na kukataza mabaya, akiwahimiza watu kuasi dhidi ya magavana wao na hata kuwauwa. Katika orodha ya wafuasi wa 'Abdullah Ibn Saba wamo baadhi ya masahaba wema wa Mtukufu Mtume, kwa mfano, Abu Dhar pia na baadhi ya Tabi'in, kama Malik Ashtar. Katika wakati wa Imam Ali, watu wawili Talha na Zubair, waliasi dhidi ya Imam Ali wakidai kuadhibiwa kwa wauaji wa Uthman. Kwa sababu ya hili, Vita vya Jamal vikapangwa. Imam Ali na wapinzani wake wawili wakakubaliana kwenye sulhu, lakini baadhi ya Sabaia, yaani wale waliokuwa na hatia ya kumuua Uthman, hawakutaka ugomvi huo usuluhishwe kwa sababu majina yao yalikuwa yamefichuliwa. Hivyo, wale Sabaia kwa siri wakajiandikisha kwenye majeshi yote; jeshi la Imam Ali na lile jeshi lililoasi. Wakati wa usiku ambapo kila mtu alikuwa anaota kuhusu ule mkataba wa amani utakaofanyiwa makubaliano siku inayofuata, wala njama hawa wakaanza kurusha mishale pande zote. Kama matokeo ya hili, Vita vya Jamal vikaanza bila ya ruksa wala kujua kwa ma-amirijeshi wa pande zote mbili. Kabla ya kujadili ngano ya Abdullah Ibn Saba kwa kirefu, inafaa kuwachunguza wale watu ambao majina yao yamo kwenye orodha ya wa-Sabaia:
25
ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO
1) 2) 3) 4) 5) 6) 7)
Abu Dhar. Ammar Ibn Yasir. Muhammad Ibn Hudhaifa. Abdur-Rahman Adis. Muhammad Ibn Abubakr, - mwana wa Khalifa wa kwanza. Sa'sa'a Ibn Suhan Abdi. Malik Ashtar.
1) Abu Dhar (Jundub Ibn Junadih) Ghifari: Yeye ni mtu wa tatu katika orodha ya watangulizi wanne waliokuwa wa kwanza kuukubali Uislam. Alikuwa Muumini wa Mungu mmoja hata kabla ya kusilimu kwake. Alitangaza imani yake juu ya Uislam huko Makkah katika Msikiti Mtukufu Baitul Haram. Maquraishi walimtesa karibu ya kufa lakini aliokoka akaishi, na kwa maagizo ya Mtume Muhammad, alirudi kwenye kabila lake. Baada ya vita vya Badr na Uhud, alirudi Madina na akaishi hapo mpaka alipokufa Mtume. Kisha Abu Dhar alipelekwa Sham (Damascus) ambako hakuweza kukubaliana na Mu'awiyah. Baadae, Mu'awiyah alilalamika kuhusu Abu Dhar kwa Uthman, Khalifa wa tatu, naye alimpeleka uhamishoni Abu Dhar kwenda Rabaza ambako baadae alikufa. Simulizi nyingi zimeandikwa kuhusu Abu Dhar kutoka kwa Mtukufu Mtume. Wakati mmoja alisema: "Chini ya mbingu ya rangi ya samawati, na juu ya ardhi, hakuna aliye mnyoofu na mkweli kuliko Abu Dhar." 2) Ammar Ibn Yasir: Alikuwa akijulikana kama Abuyaqzan. Alikuwa mmoja kati ya kabila la Bani Tha'laba na alihusiana na Bani Makhzum. Jina la mama yake lilikuwa Sumayya. Yeye na wazazi wake walikuwa watangulizi katika kuukubali Uislam, na alikuwa wa saba katika kutamka imani yake. Wazazi wake waliuawa baada ya kuteswa na kabila la Quraishi kwa sababu ya kuingia katika Uislam. Zipo ngano sahihi zilizosimuliwa na Mtukufu Mtume kuhusu Ammar, kama vile, "Ammar amejawa na imani". Alipigana katika upande wa Imam Ali katika vita vya Jamal na Siffin, na aliuawa katika medani ya vita akiwa na umri wa miaka 93. 3) Muhammad Ibn Hudhaifa (akiitwa Abul Qasim): Baba yake alikuwa Utba Ibn Rabi'a al-Abshami na mama yake alikuwa Sahlah, binti ya Suhail Ibn Amr Ameryyah. Alizaliwa huko Ethiopia katika wakati wa Mtume. Baba yake aliuawa shahidi huko Yamama, hivyo, Uthman alimchukua kama mtoto wa kupanga. Uthman, wakati wa utawala wake, alimpa ruksa ya kwenda Misri ambako aliasi dhidi ya Uqba Ibn Ameir, yule msaidizi wa Madina, Abdullah Ibn Abi Sarh (mtu wa 10 kuwa Gavana wa Misri) aliyekuwa amekwenda Madina, na alikuwa haruhusiwi kuingia tena Misri. Muhammad Ibn Hudhaifa alifaulu na akawa ndiye Gavana mpya, kisha alihamasisha askari mia sita chini ya Abdur26
ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO
Rahman Ibn Adis, kupigana na Uthman huko Madina. Baada ya Imam Ali kuwa Khalifa, alimruhusu Muhammad kubakia kama Gavana wa Misri. Wakati Mu'awiyah akiwa njiani kuelekea Siffin alikwenda Misri, Muhammad alimzuia kuingia Fostat. Lakini Mu'awiyah alifunga mkataba na Muhammad. Chini ya mkataba huu Muhammad Ibn Hudhaifa na Abdur-Rahman Ibn Adis, pamoja na watu 29 waliondoka Cairo ili kuwa salama kutokana na Mu'awiyah, lakini baadae Mu'awiyah aliwakamata na kuwafunga. Muhammad aliuawa akiwa jela huko Damascus na mtumwa wake mwenyewe Mu'awiyah aitwaye Rushdain. Muhammad alikutana Mtume. 4) Abdur-Rahman Ibn Adis Balavi: Alikuwa mmojawapo wa watu waliohudhuria kwenye mkataba wa Shajara. Alishiriki katika vita vya Misri, na baadhi ya ardhi ya Misri ilikuwa chini ya ulinzi wake. Alikuwa ndiye kamanda wa jeshi lililotumwa kutoka Misri kwenda kupigana na Uthman. Alitekwa na Mu'awiyah na akafungwa huko Palestina. Baada ya kufanikiwa kutoroka alikamatwa tena na akauawa. Alipata fursa ya kukutana na Mtume. 5) Muhammad Ibn Abubakr: Mama yake alikuwa Asma binti Umais Khathamyiah, mke wa Jafar Ibn Abi Talib. Baada ya Jafar kuuawa shahidi, Asma aliolewa na Abubakr na akamzaa Muhammad. Imam Ali alimchukua kama mtoto wa kupanga baada ya kufa Abubakr. Muhammad alikuwa kamanda wa jeshi la askari wa miguu katika vita vya Jamal. Alikuwepo vilevile katika vita vya Siffin. Imam Ali alimteuwa kama Gavana wa Misri, na aliichukua kazi yake tarehe 15/9/37 H.L. Mu'awiyah alituma jeshi chini ya uongozi wa Amr Ibn Al-Aas kwenda Misri mwaka wa 38, waliopigana na kumteka Muhammad na kisha wakamuua. Mwili wake ulitiwa kwenye tumbo la punda aliyekufa na kuchomwa moto. 6) Sa'sa'a Ibn Souhan Abdi: Bwana huyu alikuwa mzungumzaji mzuri na alisilimu wakati wa Mtume. Alipigana katika vita vya Siffin wakati Mu'awiyah alipoikamata Kufa. Mu'awiyah alimhamisha Sa'sa'a kwenda Bahrain ambako ndiko alikofia. 7) Malik Ashtar al-Nakhai: Alikutana na Mtume na alikuwa mmoja wa Tabi'in waaminifu. Alikuwa ndiye mkuu wa kabila lake, na baada ya kupata jeraha kwenye moja ya macho yake katika vita vya Yarmuuk, alikuja kujulikana kama Ashtar. Katika vita vya Jamal na Siffin, alikuwa pamoja na Imam Ali na walipata ushindi mkubwa. Katika umri wa miaka 38, aliteuliwa kuwa Gavana wa Misri, lakini akiwa njiani kuelekea huko, karibu na Bahari Nyekundu (Red Sea), alikufa baada ya kula asali iliyochanganywa na sumu iliyopangwa na Mu'awiyah. Hizo hapo juu ni wasifu fupi za baadhi ya Waislam mashuhuri. Inasikitisha kwamba baadhi ya wana-historia walidai kwamba walifuata Myahudi asiyejulikana. Baada ya kulijua hili, tujaribu sasa kuchanganua dhamira za ngano za Abdullah Ibn Saba. 27
ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO
ASILI YA NGANO YENYEWE NA YA WASIMULIAJI WA NGANO Ni karne kumi na mbili zimepita tangu wanahistoria walipoanza kuandika kuhusu Abdullah Ibn Saba. Mtu anaweza kwa shida sana kuona mwandishi asiyezungumza kuhusu yeye ikiwa anaandika kuhusu masahaba, Waislam ambao walikutana na Mtume. Tofauti kati ya maandishi ya wanahistoria wa zamani na wa sasa wa Uislam wanapozungumzia kuhusu ngano za Abdullah Ibn Saba - ni kwamba hawa wa sasa wamechagua njia ya kisasa ya mchanganuo wa uandishi, ambapo wale wa zamani walikisimulia kisa hicho kwa lugha ya Hadith (nukuu ya semi za Mtume). Kuisoma na kuichunguza ngano hii kwa ufasaha, hebu na tuwatafute wasimuliaji walioongea na, au walioandika juu yake. 1)
MUHAMMAD RASHID RIDHA
Miongoni mwa waandishi wa kisasa ni Muhammad Rashid Ridha, ambaye katika Kitabu chake al-Sunna wal Shiah (uk. 4-6), anasema: "Ushiah ulibuniwa na Abdullah Ibn Saba. Alidai kwamba ameikana imani yake ya Kiyahudi na amesilimu na kuwa Mwislamu. Alitia chumvi sana kuhusu Ali, mrithi wa nne wa Mtume Muhammad, na akabuni Ushia kwa jina la Ali. Kubuni Ushia kulikuwa mwanzo wa vurugu katika mambo ya kidini na ya kidunia ya umma wa Muhammad, kwa kuzua tofauti kati ya Waislam." Kisha Ridha akaipindisha ngano kumfaa yeye binafsi, na kama mtu anataka kujua mwanzo wa ngano hii, Muhammad Rashid Ridha anakiri akisema, "Yeyote anayetazama ngano zinazohusu vita vya Jamal katika kitabu cha historia cha Ibn Athir kwa mfano, atagundua kiwango cha athari za uovu wa Sabaia katika majeshi ya pande zote, wakati sulhu ilikuwa inatarajiwa (rejea juz.ya 3, uk. 96, 103)." Hivyo chanzo cha habari cha Sayid Rashid kilikuwa kitabu cha historia cha Ibn Athir. 2)
ABDUL FIDA (KAFA 732 H.L. - 1331A.D.)
Abdul Fida katika kitabu chake al-Mukhtasar, anasema: "Nimefanya mukhtasari katika kitabu changu yale ambayo Sheikh Izzid-Din Ali, anayejulikana kama Ibn Athir Jazari, aliyoandika katika kitabu chake kamili." Hivyo vyanzo vya waandishi hao wawili hapo juu vilikuwa ni Ibn Athir. 3)
IBN ATHIR (KAFA 630 H.L. - 1229 A.D.)
Ibn Athir ameitaja ngano hii miongoni mwa matukio yaliyotokea katika miaka ya 30 -36 H.L. Haelezei chanzo cha ngano hizi isipokuwa kwenye utangulizi wa kitabu chake Tarikh al-Kamil (kilichochapishwa Misri, 1348 H.L.), akisema: "Nimeziona ngano hizi katika kitabu cha Abu Jafar al-Tabari," Hicho kitabu kamili cha historia cha Tabari (17) ndiyo Msahafu wa Waislam wa historia, kitabu pekee cha kutegemewa miongoni mwa Waislam wanaokirejea wakati jambo lolote lenye mashaka 28
ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO
likitaka kuchunguzwa. Tabari ameandika ngano nyingi katika sehemu tofauti za kitabu chake, kuhusu tukio moja; lakini nimezipanga upya ngano hizi chini ya kichwa cha habari makhsusi na nimechagua ngano iliyokamilika zaidi kwa kila tukio. Kuhusu Masahaba nimenukuu ngano zao vilevile hasa kama Tabari (17) alivyoziandika kwenye kitabu chake, na isipokuwa maelezo ya ufafanuzi yasiyoingiliana na nukuu hizo. Huyu ni Ibn Athir (3) ambaye kutoka kwake Muhammad Rashid (1) na Abul Fida (2) wameazima ngano zao.Huyu Ibn Athir (3) ameandika hasa kile at-Tabari (17) alichoandika. 4)
IBN KATHIR (KAFA 774 H.L. - 1289 A.D.)
Ibn Kathir katika kitabu chake Al-Bidaia wal Nihaya juz. 7, akimnukuu Tabari anasema: "Seif Ibn Umar amesema kwamba chanzo cha uasi dhidi ya Uthman kilikuwa ni Abdullah Ibn Saba aliyejifanya ni Mwislamu na akaenda Misri kueneza ngano za uongo." Kisha Ibn Kathir anaiandika ngano kamili ya Abdullah Ibn Saba, ikiwemo vita vya Jamal. Anasema katika ukurasa wa 246: "Huu ni mukhtasari wa kile ambacho Abu Jafar Ibn Jarir Tabari (17) (Mola Amrehemu) alichokiandika." 5)
IBN KHALDUN
Mwana-falsafa wa wana-historia katika kitabu chake al-Mubtada wal Khabar amewataja Sabaia katika Matukio ya Nyumba (kifo cha kishujaa cha Uthuman) na Jamal. Kisha katika juz. 2, uk. 425 wa kitabu chake, anasema: "Huu ni mukhtasari wa matukio ya Jamal kutoka kwenye kitabu cha Abu Jafar Tabari (17) kwa sababu anategemewa sana na kuaminiwa sana kuliko wanahistoria wengine pamoja na Ibn Qutaybah." Pia, katika uk.457, anasema: "Hili ni neno la mwisho kuhusu umakamu wa Kiislam, na watekaji wa ki-maasi na vita. Baada ya hili yatakuwa makubaliano na Mkutano (al-Jamaat) miongoni mwa Waislam. Nimechukua dondoo hizi kutoka kwenye kitabu cha Muhammad Ibn Jarir at-Tabari (17) kama kilivyo cha kutegemewa sana, na hakiwakosoi Masahaba na Tabi'in." 6)
MUHAMMAD FARID WAJDI
Muhammad Farid Wajdi katika kitabu chake Ensaiklopidia chini ya neno: Atham na chini ya Vita vya Jamal, pia katika wasifu wa Ali Ibn Abi Talib, ameitaja ngano ya Abdullah Ibn Saba na katika uk. 160, 168 na 169, anatueleza kwamba chanzo chake cha habari ni kutoka kwa Tabari (17). 7)
AL-BUSTANI
Katika Ensaiklopidia yake chini ya jina Abdullah Ibn Saba, anasema: "Abdullah Ibn Saba anasema Ibn Kathir………." 29
ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO
8)
AHMAD AMIN
Mmoja wa wanahistoria wa leo ambaye ametumia mbinu ya uchambuzi ya kuandika ngano hizo ni Ahmed Amin. Katika kitabu chake Fajrul Islam kuhusu Waajemi1 na athari zao katika Uislam, anaandika: "Tofauti kuu kati ya dini ya Mazdak na dini nyinginezo ilikuwa ni ile dhana yao ya kisoshalisti (kijamaa). Dini ya Mazdak iliamini usawa wa mwanadamu kwa kuzaliwa na kueleza kwamba ni lazima kwa hiyo, wawe na fursa sawa katika namna yao ya maisha. Aliyaona mambo ya muhimu sana katika usawa wa mwanadamu kuwa ni mali na wanawake, haya yakiwa ndiyo chanzo cha migogoro. Hivyo alisema wanawake na mali vilikuwa ni sawa kwa wote. Wanaume wa hali ya chini walichukua fursa ya mafunzo ya Mazdak na wakasababisha matatizo mengi. Wafuasi wake walivamia kwenye nyumba, wakigawana miongoni mwao wenyewe, wanawake na vitu. Hii iliendelea kwa muda mrefu kiasi kwamba watoto hawakujua baba zao ni nani, na akina baba hawakuweza kutambua watoto wao." Ahmed Amin anaendelea akisema, "Namna hii ya maisha ilitwaliwa na Kerman (Uajemi ya Kusini) ambako dini hii ilikuwa bado ikitumika katika enzi za ufalme wa Amawy." "Kutokana na hili" anasema Ahmed Amin, "tunaona kufanana kwa dhana ya Abu Dhar na Mazdak kutokana na mgawano wa mali unavyohusika." "Abu Dhar", anasema Tabari, "alisimama huko Damascus (Sham) akisema, "Enyi watu matajiri, gawaneni fedha zenu na maskini", na akasoma Aya hii ya Qur'ani: "Wabashirie adhabu iliyo chungu wale wanaohodhi dhahabu na fedha na wala hawazitumii katika Njia ya Mwenyezi Mungu. Siku zitakapochomwa katika moto wa Jahannam na kwazo vikachomwa vipaji vya nyuso zao na mbavu zao na migongo yao." (Qur'ani 9:34). Abu Dhar alirudia nukuu hii mara kwa mara kiasi kwamba watu masikini wakachukulia kwamba ni wajibu kwa watu matajiri kugawa fedha zao, na wakawakera sana matajiri mpaka wakamlalamikia Abu Dhar kwa Mu'awiyah, Gavana wa Syria, naye akamuamuru Abu Dhar kwenda Madina kumuona Khalifa Uthman. "Ewe raia wa Damascus, kwa nini ulimi wako unalalamika sana?" Akauliza Uthman. "Watu matajiri hawapaswi kuweka fedha zao kwa ajili yao peke yao tu", akasema Abu Dhar.
1Kabla ya Ahmad Amin, Rashid Ridha ameandika ngano hii katika kitabu chake, as-Sunna wa Shia.
30
ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO
"Tunaona kutokana na hayo hapo juu", anasema Ahmad Amin, "kwamba dhana ya Abu Dhar ilikuwa karibu sana na ile ya Mazdak kuhusu mali." Lakini Abu Dhar amepata wapi wazo hili? Tabari anajibu: "Ibn al-Souda alikutana na Abu Dhar na akashauri dhana hii ya kijamaa, katika mkutano na Abu Darda2 na Ubada Ibn Samit, lakini hawa wa baadae hawakudanganyika na walimchukua Ibn al-Souda mpaka kwa Mu'awiyah na kumwambia huyu ndiye mtu aliyemshawishi Abu Dhar kukuchosha.3 Ahmed Amin anaendelea: "Tunajua pia kwamba Ibn al-Souda alijulikana kama Abdullah Ibn Saba aliyekuwa Myahudi kutoka Sana'a (Yemen). Alijifanya kuwa Mwislamu katika wakati wa Uthman, na akajaribu kuibomoa dini ya Waislam kwa kueneza dhana zenye madhara." Hili tutalijadili baadae. "Abdullah Ibn Saba", anaendelea Ahmed Amin, "alisafiri kwenda kwenye miji mingi katika Bara Arabu kama vile: Basra, Kufa, Damascus na Cairo. Anaweza kuwa ameipata dhana hii ya kijamaa kutoka kwa wafuasi wa Mazdak huko Iraq au Yemen. Hivyo, Abu Dhar alijifunza hiyo kutoka kwake." Ahmed Amin aliandika pambizoni mwa kitabu chake hivi: "Rejea Tabari Juz. 5, uk. 66 na kuendelea." Katika ukurasa wa112 Ahmed anamalizia kwamba: "Mashia waliwaona Ali na wanae kama ni watakatifu, kama walivyofanya wahenga wao wa Kiajemi na Wapagani kuhusu Wafalme wao wa utawala wa Sasanid." Ahmed Amin alikuwa mwaminifu wa ahadi yake aliposema, "tutazijadili dhana za Abdullah Ibn Saba zenye madhara baadae." Ahmed Amin katika ukurasa wa 254, akizungumzia juu ya madhehebu tofauti anasema: "Mwishoni mwa uongozi wa Uthman, baadhi ya vikundi vya siri, vilivyotawanyika kila mahali, viliasi dhidi ya Uthman, vikijaribu kumnyan'ganya madaraka na kumpa mtu mwingine. Miongoni mwa vikundi hivi vingine vilikuwa vikiomba kuungwa mkono kwa ajili ya Ali, nguvu kuu nyuma ya kitendo hiki katika Basra, Kufa na Damascus ilikuwa ni Abdullah Ibn Saba. Alisema: " Kila Mtume ana mrithi na Ali ndiye mrithi wa Mtume Muhammad. Ni nani dhalimu zaidi kuliko yule mtu ambaye amepora nafasi ya Ali kwa dhulma?" Alilisisitiza hili mpaka Uthman akauawa. "Hatuna budi", anasema Ahmed Amin, "kuijadili ngano hii kwani madhehebu matatu yalizuka kama matokeo yake, nayo ni Shia, n.k." 2 Walijulikana kama Wafuasi wa Mtume (Masahaba). 3 Ngano hii ni ya uongo na ilitungwa na Abdullah Ibn Saba, Abu Dhar kamwe hakuhubiri dhidi ya watu matajiri, mazungumzo yake yalimlenga Mu'awiyah na ufalme wake, ambao walitwaa mali za watu kwa nguvu na Abdullah Ibn Saba akajaribu kulifunika jambo hilo kwa kutunga ngano hizi.
31
ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO
Katika mlango unaohusu Shia katika ukurasa wa 266-278, anasema kwamba ile dhana ya kuja kwa mara ya pili kwa Nabii Eliyah ni ya Wayahudi. Abdullah Ibn Saba alijifunza hili kutoka kwa Wayahudi. Shia waliitwaa kutoka kwa Abdullah Ibn Saba kukubaliana na dhana zao kuhusu Mahdi aliyetarajiwa kuja na kuujaza haki ulimwengu . Ushia ni kimbilio la kuhifadhi wale wanaotaka kuubomoa Uislam kwa kificho cha mapenzi kwa watu wa nyumba ya Mtume. Myahudi yeyote au Mkristo anaweza kuelezea maoni yake kuhusu Uislam kupitia kwenye Ushiah, kama ile dhana ya Kiyahudi kuhusu kuja kwa mara ya pili kwa Eliyah.4 Katika ukurasa wa 277, anasema: "Kwa mujibu wa Wellhouzen, Ushia unatokana zaidi na imani za Kiyahudi kuliko za Kifursi, kwa sababu Abdullah Ibn Saba alikuwa Myahudi." Kwa maneno mengine, Ahmed Amin anasema kwamba Mashia walipata imani zao juu ya umakamu wa Ali, na kuja kwa mara ya pili kwa Watakatifu na Mahdi, kutoka kwa Ibn Saba, yaani, toka kwa Myahudi. Abu Dhar alipata fikra zake za kikomunisti kutoka kwa Ibn Saba. Ibn Saba alijifunza ukomunisti kutoka kwa watu wa Mazdaki ambao waliishi katika wakati wa utawala wa Amawiy. Mazdak alikuwa Mfursi, na Wafursi waliwatukuza wafalme wao. Vivyo hivyo Mashia wanawatukuza Maimamu wao. Ushiah ni kificho kwa wale wanaotaka kuuvunja Uislam kwa chuki na wivu. Ni hifadhi pia kwa mtu yeyote anayetaka kuanzisha dini ya Kiyahudi, Ukristo au imani ya Kizoroasta katika Uislam, Tunaona kwamba fikra zote hizi zinatoka kwa Abdullah Ibn Saba, ambazo Ahmed Amin amezichukua kutoka kwa Tabari na Wellhouzen. Tutaona kwamba Wellhouzen pia, ameziandika kutoka kwa Tabari (17). 9)
HASAN IBRAHIM
Mwanahistoria mwingine wa siku hizi ambaye amechukua njia ya uchambuzi katika kitabu chake Islamic Political History (Historia ya Siasa za Kiislam), ni Dr. Hasan Ibrahim. Baada ya kutazama hali ya Uislam mwishoni mwa Ukhalifa wa Uthaman anasema: "Mazingira yalikuwa tayari kuvikubali vitendo vya Sabaia. Mmoja wa Masahaba wa Mtume anayejulikana sana kwa uchamungu wake na uadilifu, alikuwa mmoja wa viongozi wa wasimulizi, akiitwa Abu Dhar Ghafari. Alikuwa ni bwana huyu aliyesababisha matatizo, kama alivyoathiriwa na propaganda zenye uchochezi za Abdullah Ibn Saba, na akampinga Uthman na Gavana wake huko Syria, Mu'awiyah. Abdullah Ibn Saba alikuwa Myahudi aliyejifanya kuwa Mwislamu na alisafiri kwenda Hijaz, Kufa, Syria na Misri. Dr. Hassan Ibrahim amechukua ngano hii kutoka juz.1,uk.2859 ya Tabari (17). katika ukurasa 349 anasema, "Abdullah Ibn Saba alikuwa mtu wa kwanza kuwaongoza watu dhidi ya Uthman, na kusababisha yeye kupinduliwa."
4 Inasikitisha kwamba kitabu cha Ahmed Amin, Fajrul Islam na Historia ya Siasa za Kiislam cha Hassan E. Hassan ndiyo vitabu pekee kuhusu fikra za Kishia kwenye vyuo vikuu vya Magharibi.
32
ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO
Katika pambizo ya kitabu chake alimrejea Tabari mara nne kuhusu ngano ya Abdullah Ibn Saba. Pia anarejea kwa Tabari mara kumi na mbili kuhusu ngano hii katika kitabu chake. Bado amejiepusha kunukuu kile Tabari alichoandika katika kitabu chake kuhusu Sabaia, ingawa hata hivyo shujaa katika ngano zote ni huyo huyo - Abdullah Ibn Saba. Mpaka sasa tumeona jinsi wanahistoria wa Kiislam walivyonukuu kutoka kwenye kitabu cha historia cha Tabari (17) kuhusu Sabaia 10)
VAN FLOTTEN (VOLTEN) (JOHANNES 1818-1883)
Katika kitabu chake Arabian Rule and Shiah and Israilyat in Amawid Time, (Sheria ya Kiarabu na Shiah na Uyahudi katika Wakati wa Bani umayyah), kilicho tafsiriwa na Dr. Hassan Ibrahim na Muhammad Zaki Ibrahim (chapa ya 1 Misri, uk. 79) anasema kuhusu Shiah: "Hawa Sabaia, wafuasi wa Abdullah Ibn Saba walimuona Ali kama mtu mwenye haki ya urithi wa Mtume katika wakati wa Uthman." Kisha anarejea kwa Tabari(17) kwenye pambizo ya uk. 80 katika kitabu chake. 11)
NICHOLSON, REYNOLD ALLEYNE (1868-1945)
Katika kitabu chake The History of Arabian Literature (Historia ya fasihi ya Kiarabu) Cambridge, uk. 215, anasema, "Abdullah Ibn Saba aliasisi jamii ya Sabaia. Alitokea Sana'a huko Yemen. Inasemekana kwamba alikuwa Myahudi ambaye, katika wakati wa Uthman, aliingia Uislam. Alikuwa kwa kweli ni msafiri, mmisionari fisadi, aliyejaribu kuwapotosha Waislam. Alianzia Hijazi, na akaenda Basra, Kufa na Syria. Hatimae aliishi Misri. Aliamini katika kuja kwa mara ya pili kwa Mtume." Akasema, "Watu waliamini kuja kwa mara ya pili kwa Yesu, lakini wakapinga kuja kwa mara ya pili kwa Mtume Muhammad, ingawa hii imetajwa katika Qur'ani. Aidha, Mwenyezi Mungu ametuma mitume zaidi ya elfu moja, na kila mmoja wao alikuwa na msaidizi na mrithi. Ali ndiye mrithi wa Mtume Muhammad wa mwisho wao." Kisha katika pambizo ya kitabu chake anamrejea Tabari (17), na kuuonyesha ukurasa wenyewe. 12)
ENSAIKLOPIDIA YA KIISLAM
Katika Ensaiklopidia hii, iliyoandikwa na baadhi ya mutashirki, ngano hiyo imeandikwa kama ifuatavyo: "Kama tunataka kuangalia tu kile Tabari na Maghrizi walichoandika, tunasema kwamba moja ya mambo Ibn Saba aliyokuwa akiyahubiri ilikuwa ni kuja kwa mara ya pili kwa Muhammad. Hii ilikuwa ndiyo nadharia -- kwamba kwa kila Mtume yupo mrithi, na Ali ndiye mrithi wa Muhammad. Hivyo, kila Mwislamu, kwa hiyo, lazima amsaidie Ali kwa maneno na vitendo." Inasemekana kwamba Abdullah Ibn Saba alituma wamisionari nchi nzima kuhubiri nadharia yake hiyo. Yeye mwenyewe binafsi alikuwa miongoni mwa wale walioondoka toka Misri kuelekea Madina katika mwezi wa Shawwal 35 H.L., April, 656 A.D. Ensaiklopidia hii inarejea kwa Tabari 33
ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO
na Maghrizi, Tabari aliishi miaka 300 baada ya ngano yenyewe, na Maghrizi miaka 800. Tabari anataja majina ya wale aliowanukuu, lakini Maghrizi hataji. Kwa hiyo maandishi ya Maghrizi hayafikiriwi kama ni ya kuaminika kama yale ya Tabari, aliyeishi miaka 500 kabla ya Maghrizi. Tutaandika kuhusu Maghrizi baadae. 13)
DONALDSON, M. DEWIGHT.
Katika kitabu chake The Shiah Articles of Faith, (Shuruti za imani za Kishia) tafsiri ya Kiarabu katika uk. 85 anasema: "Kumbukumbu za awali zinatuonyesha kwamba yale madai ya wafuasi wa Ali, kuhusu urithi wake hayakuwa ya kisiasa tu, bali waliamini kwamba urithi wa Ali ulikuwa wa majaaliwa ya kimungu. Bado mtu wa ajabu anaweza kufikiriwa kuhusika sana na imani hiyo. Katika wakati wa utawala wa Uthman, Abdullah Ibn Saba alianzisha harakati za kuubomoa Uislam, kama inavyosemwa na Tabari." Donaldson hakunukuu moja kwa moja kutoka kwa Tabari, lakini kwa mujibu wa pambizo ya uk. 59 katika kitabu chake, amenukuu kutoka kwenye Ensaiklopidia ya Kiislam iliyotajwa hivi punde na kutoka kwenye kitabu History of Arabian Literature. Tumeeleza mapema kwamba wao wenyewe wamenukuu kutoka kwa Tabari (17) 14)
WELLHOUSEN JULIUS (1844 - 1918)
Katika uk.56-57 katika kitabu chake Sabaian and the Spirit of Prophethood, anasema: "Kikundi kiliundwa huko Kufa, kinachoitwa Sabaian, na kikundi hiki kilifanya mabadiliko makubwa katika Uislam. Mbali na mafundisho ya Qur'ani, walihubiri utakatifu wa Mtume Muhammad. Sabaians waliamini kwamba Muhammad alikufa kimwili lakini siyo kiroho, kwamba roho yake ni tukufu, na iko hai daima milele." Kama katika nadharia ya kupata mwili - incarnation, wanasema kwamba roho ya Mungu imepandikizwa kwenye Mitume yake na kupita kwa manabii wote, mmoja kwenda kwa mwingine, na kwamba baada ya Muhammad, ilipitishwa kwa Ali na kisha kwa kizazi chake. Hawakuona kwamba Ali alikuwa sawa na Makhalifa waliomtangulia na walikuwa warithi wa Muhammad, bali waliwaona Makhalifa wale ni batili. Walimtangaza Ali kama mrithi pekee, mtakatifu, na wa haki wa Mtume Muhammad, na utii kwake ulikuwa uonekane kama utii kwa Mwenyezi Mungu. Wellhousen pia amesema kwamba inafahamika kwamba hawa Sabaian wanapata jina lao kutoka kwa Ibn Saba, Myahudi wa Yemen, na chini ya kichwa 'wakereketwa wa Sabaia na Wanaoamini juu ya Uhamisho wa roho' - kutoka kiumbe kwenda kiumbe. Anasema,: "Hawa wakereketwa wanayo majina tofauti yasiyofaa kutajwa, lakini majina hayo yote yalithibitisha kwamba wamekwenda kombo wamepotoka." Seif Ibn Umar Tamimi anasema: "Sabaian tokea mwanzoni walikuwa wakorofi, kwa kumuua Uthman, na kuanzisha vita vya wenyewe kwa wenyewe‌‌.. Wengi wao walikuwa watumwa wasiokuwa Waarabu. Waliamini juu ya kupita kwa roho kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine, hasa roho ya Muhammad kuhamia kwa Ali, kisha kizazi cha Ali, kwa Fatima, binti ya Mtume, 34
ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO
waliwakataa hawa Sabaia, hivyo walimfuata Muhammad al-Hanafiyah, mtoto wa Ali lakini siyo kwa Fatima. Hawa Sabaia walimfuata Aba Hashim mtoto wa Muhammad al-Hanafiyah, mtu asiyestahili kama baba yake. Aba Hashim alimteuwa mwanae Muhammad Ibn Ali Abbasy. Hivyo urithi wa Ali ulitoka kwake kwenda kwenye ufalme wa Bani Abbas. Bani Abbas, kama Sabaia, ni wa asili ya Kufa. Makundi yote yaliasi dhidi ya Waislam Waarabu na wafuasi wao walikuwa ni watumwa wa ki-Iran." Wellhousen anamrejea Seif mara mbili katika ngano hii katika pambizo ya kitabu chake. Hivyo ni wazi kwetu kwamba ameichukua ngano hii kutoka kwa Tabari (17) mwanahistoria wa kwanza kumtaja Seif. Hivyo, tumeandika juu ya wanahistoria waliomtaja Tabari, moja kwa moja au vinginevyo, wakati wa kuandika hii ngano ya Ibn Saba. Wapo waandishi wengine ambao hawakumtaja mwandishi wa asili wa ngano hii ya Ibn Saba. Lakini katika sehemu nyingine katika vitabu vyao wamemtaja Tabari au vitabu vilivyonukuu kutoka kwa Tabari kama vile: 15)
MIRKHAND KATIKA KITABU CHAKE - RAWZATUS-SAFA.
16)
GHIATHUD DIN (KAFA 940H.L. - 1455 A.D.)
Mtoto wa Mirhand, katika kitabu chake Habibus Siyar, amenukuu kutoka kwa baba yake kama inavyotajwa kwenye utangulizi wa kitabu chake. Wanahistoria wote hapo juu wamenakili kutoka kwa Tabari (17). 17)
TABARI NA CHANZO CHAKE
Abu Jafar Muhammad Ibn Jarir Tabari Amuli (kafa 310 H.L. - 825 A.D.). Katika kitabu chake Tarikhul Umam wal Muluuk (Historia ya Mataifa na Wafalme), Tabari amenakili ngano ya Sabaia pekee kutoka kwa Seif Ibn Umar Tamimi. Anarejea tu kwenye baadhi ya matukio ya mwaka wa 30H.L. kama ifuatavyo: "Katika mwaka huo huo (i.e. mwaka wa 30 H.L) tukio la kumhusu Abu Dhar lilitokea. Mu'awiyah alimtoa Abu Dhar kutoka Sham (Damascus) kwenda Madina. Mambo mengi yanasemwa kuhusu tukio hilo, lakini sipendi niyaandike. Sari ameniandikia juu ya wale wanaotafuta visingizio juu ya Mu'awiyah, kutokana na matukio yanayomhusu Abu Dhar. Shuaibhas alimweleza Sari kwamba Seif alisema, "Wakati Ibn Sawda alipofika Shaam (Damascus) alikutana na Abu Dhar na akamweleza kitu ambacho Mu'awiyah alikuwa anakifanya.' Na Tabari anaisimulia ngano ya Sabaia kama ilivyosemwa na Seif, na anamalizia ngano ya Abu Dhar kwa maneno yafuatayo, 'Wengine wamesema mengi kuhusu hii ngano(ya kufukuziwa uhamishoni kwa Abu Dhar), lakini ninasita kuwataja.' Juu ya matukio ya miaka hiyo (30 - 36 H.L.), Tabari anaandika hii ngano ya Ibn 35
ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO
Saba na wale Sabaia, mauaji ya Uthman (Khalifa wa tatu) na Vita vya Jamal kutoka kwa Said Seif akiwa ndiye mmoja tu aliyeweza kunakili toka kwake. Tabari anasimulia ngano yake kutoka kwa Seif kupitia watu wawili, 1. Ubaidullah Ibn Sa'id Zuhri kutoka kwa ami yake Ya'qub Ibn Ibrahim na kisha toka kwa Seif. Kutoka kwenye sanadi hii ngano zikaanza "nimesimuliwa" au "tumesimuliwa". 2. Sari Ibn Yahya kutoka kwa Shuaib Ibn Ibrahim toka kwa Seif. Tabari akinakili kutoka kwenye vitabu viwili, al-Futuuh na al-Jamal kutoka kwa Seif, ameanza na "Aliniandikia", "Alinisimulia", na "Katika barua aliyoniandikia". Mpaka hapo tumeshughulika na chanzo cha Tabari. 18)
IBN ASAKIR (KAFA 571 H.L. - 1086 A.D)
Ibn Asakir anaandika kutoka kwenye chanzo kingine. Ndani ya kitabu chake The History of Damascus (historia ya Damascus) wakati akiandika wasifu wa Talha na Abdullah Ibn Saba, ameandika sehemu za ngano ya Sabaian, kupitia kwa Abul Qasim Samarqandi kutoka kwa Abul Hussein Naquur kutoka kwa Abu Tahir Mukhallas toka kwa Abubakr Ibn Seif toka kwa Sari toka kwa Shuaib Ibn Ibrahim kutoka kwa Seif. Kwa hiyo, wa mwanzo ni Sari, mmoja kati ya sanadi ambazo Tabari amenakili toka kwao. 19)
IBN BARDAN (KAFA 1346 H.L. - 1851 A.D.)
Ibn Bardan ameandika ngano katika kitabu chake Tahdhib bila kutaja majina ya watu ambao amenakili kutoka kwao.Ameandika baadhi ya ngano ya Ibn Saba katika kitabu chake bila ya kuwataja waanzilishi wake. Lakini katika wasifu wa Ziad Ibn Abih amemtaja Tabari kuhusiana na ngano za Seif (juz.5, uk.406). 20)
IBN ABIBAKR (KAFA 741 H.L. - 1256 A.D.)
Ibn Abibakr anacho kitabu kinachoitwa at-Tamhid, ambacho baadhi ya waandishi wamenakili kutoka humo. Kitabu hicho kinahusu mauaji ya Khalifa Uthman na katika utangulizi wake hili jina la al-Futuuh, la kitabu cha Seif limetajwa, vilevile na jina la Ibn Athir. Ibn Athir amenakili kutoka kwa Tabari na Tabari kutoka kwa Seif. Mpaka hapa ngano za Seif zina vyanzo vikuu vitatu: 1) Tabari (kafa 310H.L. - 825 A.D.); 2) Ibn Asakir (kafa 571 H.L. - 1086 A.D.); 3) Ibn Abibakr (kafa 741H.L. - 1256 A.D.). Baadhi ya waandishi wamenakili kutoka kwenye rejea moja, wengine kutoka viwili, 36
ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO
na wengine kutoka kwenye vyote vitatu. 21)
SA'ID AFGHANI
Katika kitabu chake Aisha and Politics (Aisha na Siasa), Sa'id Afghani ameandika baadhi ya ngano za Sabaian chini ya vichwa vifuatavyo: "Mtume dhidi ya Uthman na Matokeo yake." "Ibn Saba Shujaa wa Siri wa Kuogopesha" "Uchunguzi wa Maafikiano" na "Njama." Anawataja pia hawa Sabaia katika mlango mwingine wa kitabu chake. Rejea yake kuu ni Tabari, akifuatiwa na Ibn Asakir, kisha Tamhid ya Ibn Abibakr. Anamtegemea zaidi Tabari kuliko mwingine yeyote, akitoa kama sababu yake kule kumuamini kwake Tabari alikonako, akisema kwamba Tabari anategemewa zaidi, na kwamba wanahistoria wote waliopita walimuamini. Kisha anasema, "Kwa kiasi nilivyoweza, nimenukuu kutoka kwenye kitabu cha Tabari vile hasa kilivyokuwa." 22)
DHAHABI (KAFA 784 H.L. - 1263 A.D.)
Kuna sanadi nyingine ya ngano ya Ibn Saba inayoitwa maandishi ya Dhahabi. Ameandika baadhi ya sehemu za ngano hii katika kitabu chake The History of Islam (Historia ya Uislam) juz.2, uk.122 - 128, ambamo ameonyesha kuuawa kwa Uthman miongoni mwa matukio ya mwaka wa 35H.L. Anaanza kama ifuatavyo: "Na Seif Ibn Umar amesema kwamba Atyya amesema, kwamba Yazid al-Faq-asi alisema wakati Ibn Sawda alipokwenda Misri‌‌" Dhahabi ameandika pia ngano nyingine iliyosimuliwa na Seif kwa maelezo zaidi kuliko Tabari. Baadae, ameandika mukhtasari wa kile Tabari alichokiandika. Asili ya ngano hizo zilizoandikwa na Dhahabi kuhusu Sabaia na nyinginezo, inaweza kupatikana kwenye utangulizi wa kitabu chake. 1)
Vitabu kama vile al-Futuuh cha Seif, ambacho kutoka humo Dhahabi amepata habari muhimu kwa ajili ya kitabu chake.
2)
Vitabu ambavyo kutokana navyo amepata kile alichokiandika kama mukhtasari.
3)
Vitabu anavyorejea mara kwa mara, kama vile Tabari.
Kwa vile Dhahabi amekitaja kitabu cha al-Futuuh cha Seif na aliishi katika karne ya 8 ya zama za Uislam basi hiki kitabu cha al-Futuuh lazima kiwe kilikuwa kinapatikana mpaka kufikia wakati huo. Kwa mukhtasari tunaweza kusema kwamba wanahistoria wote hawa waliotajwa, 37
ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO
wamechukua ngano zao na kisa cha Abdullah Ibn Saba kutoka kwa Seif. Wanne wa wanahistoria hawa: Tabari, Ibn Asakir, Ibn Abibakr na Dhahabi wamechukua ngano zao moja kwa moja toka kwa Seif. Hiyo chati kwenye ukurasa ufuatao inaonyesha sanadi ambazo kwazo kisa cha Sabaia kimeandikwa kutoka kwa msimuliaji wa asili - Seif.
38
ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO
SEIF IBN UMAR AT-TAMIMI (KAFA BAADA YA 170 A.H)
ADH-DHAHABI
AT-TABARI
(748 A.H)
R.A
IBN ABI BAKR
(310 A.H)
ENCYCLOPAEDIA
NICHOLSON
OF ISLAM
VAN
J.WELL
MIR KHUND
FLATON
HAUSEN
(903 A.H.)
IBN ASAKIR
(741A.H)
IBN KATHIR (747 A.H)
IBN
(571 A.H)
IBN AL-
KHALDUN
ATHIR
(808 A.H)
(630A.H)
GHIYATH AD-DIN (940 A.H)
ABU`L FIDA (732 A.H.)
AHMAD AMIN D.M. DONALDSON
RASHID RIDA (135 A.H)
FARIDWAJDI
39
HASAN IBRAHIM
IBN BADRAN (1346 A.H)
SA’ID
AL AFGHANI
ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO
UCHUNGUZI KUHUSU SEIF NA SIMULIZI ZAKE
SEIF NI NANI? Kwa mujibu wa Tabari, juz.1,uk.1749, na Europe and Lubabul Ansab, juz.1,uk.49, jina kamili la Seif lilikuwa ni Seif Ibn Umar al-Tamimi al-Usayyadi. Kwa mujibu wa Jamharatul Ansab, uk. 199, na al-Ishtiqaq cha Ibn Duraid, uk. 201 - 206, jina la Usayyad lilikuwa ni Amr Ibn Tamimi. Kwa sababu Seif alikuwa ni kizazi cha Amr amechangia zaidi sana kuhusu matendo ya kishujaa ya Bani Amr kuliko wengine. Imeandikwa "Usady" katika kitabu cha Nadim, Fihrist, badala ya Osayyad. Imesimuliwa ndani ya Tahdhibul Tahdhib, al-Burjumi wal Sa'ady au al-Zaby. Kama hii ingekuwa kweli inadhihirisha tu kwamba hili kabila la Burjum na Usayyad walikuwa na namna ya makubaliano (mkataba wa amani n.k.) kati yao kwa vile Burjun na Usayyad hawakuwa ndugu wa karibu hata kama tutaamini kwamba makabila yote haya yalikuwa kizazi cha Bani Tamimi. Imeandikwa katika Tahdhibut Tahdhib, Khulasatut Tahdhib na Hidayatul Arifin kwamba Seif alitokea Kufa na akaishi Baghdad. Kwa mujibu wa KhulasatutTahdhib, Seif alikufa mwaka wa 170H.L. Imeandikwa ndani ya al-Tahdhib, "Nimeuona mwandiko wa Dhahabi akisema kwamba Seif alikufa wakati wa utawala wa Harun al-Rashid." Ismail Pasha katika kitabu chake al-Hidaia, anasema, "Yeye (Seif) alikufa Baghdad wakati wa utawala wa Harun al-Rashid katika mwaka wa 200 na al-Rashid alikufa mwaka wa 193." Hakuna mwingine yeyote aliyesema hivyo, wala Ismail Pasha hakuonyesha rejea ya taarifa yake. VITABU VYA SEIF Kwa mujibu wa al-Fihris na al-Hidaia, Seif aliandika vitabu viwili: 1) al-Futuuh al-Kabir wal Ridhah. 2) al-Jamal wa Masiri Aishah wa Ali. Na kwa mujibu wa al-Lubab, Tahdhib na Kashful-Zunuun, Seif aliandika kitabu kimoja tu "al-Futuuh". Tabari katika kitabu chake ameandika kutoka kwenye vitabu viwili vya Seif, alFutuuh na al-Jamal katika mpango wa majina ya watu wanaohusika kwenye hilo 40
ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO
tukio, lakini hakufanya marejeo kwenye vitabu vya Seif. Dhahabi katika historia yake ya al-Kabir; na Ibn Asakir katika al-Tamhid wameandika kutoka kwa Seif kwa mujibu wa majina ya watu wanaohusika katika hilo tukio na wamefanya marejeo kwenye vitabu vya Seif. Wanahistoria maarufu kabisa ambao wameandika kuhusu masahaba wa Mtume ni Ibn Abdul Birr, Ibn Athir, Ibn Hajar na Dhahabi. Wanahistoria hawa wameandika majina ya mashujaa waliobuniwa na Seif pamoja na majina ya Masahaba wa kweli wa Mtume. Wanajogorafia kama al-Hamawi, katika Mujam yake; na al-Him'iari katika al-Ruuz wametaja majina ya sehemu zisizopo zilizobuniwa na Seif. Abdul Mumin ameandika sehemu za Seif kutoka kwa al-Hamawi. Mtu wa mwisho, tuliyempata, aliyesema kwamba alikuwa anacho kitabu cha Seif mkononi mwake ni Ibn Hajar (kafa 852H.L.). Yule mwandishi wa al-Isabah. TATHMINI YA MAANDISHI YA SEIF. 1. Yahya Ibn Maiin (k. 233H.L.), amesema kuhusu Seifi “mapokezi yake ni dhaifu na hazifai." 2. Nasai (k.303H.L.) katika sahih amesema, "mapokezi yake ni dhaifu, zisithaminiwe kwa sababu hakuwa wa kutegemewa na hakuwa mwaminifu." 3. Abu Dawuud (k.316H.L.), "Hana thamani, ni muongo." 4. Ibn Abi Hatam (k.327H.L.), "Wamezitelekeza mapokezi yake." 5. Ibn al-Sakan (k.353H.L.), "Ni dhaifu." 6. Ibn Udai (k.365H.L.), "Ni dhaifu, baadhi ya mapokezi yake ni maarufu bado nyingi ya ngano zake zinatweza na hazifuatwi." 7 Ibn Hibban (k.354H.L.), "Katika mapokezi yake, ametaja majina ya watu waaminifu, lakini wanasema alishutumiwa kwa uasi na ngano za kuzua." 8. Hakim (k.405H.L.), "mapokezi yake zimetelekezwa, alishutumiwa kwa uasi." 9. Katib al- Baghdad‌ 10. Abin Abd al-Bir (k.463H.L.) alisimulia kutoka kwa Abi Hayan kwamba "mapokezi yake Seif zilitelekezwa, tulikuwa tukizitaja kwa ajili ya elimu tu." 11) Safiud Din (k.923H.L.) "Alionekana dhaifu." 12) Firuuzabadi (k.817H.L.) katika Tuwalif ametaja, "Seif pamoja na hao wengine akisema ni dhaifu." 13) Ibn Hij'r (k.852H.L.), baada ya mapokezi yake mamoja kutajwa, "kwamba imesimuliwa na wasimuliaji dhaifu, dhaifu zaidi yao wote, ni Seif." 41
ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO
Haya ndiyo maoni ya waandishi wa wasifu juu ya Seif na ngano zake. Sasa hebu tuziangalie ngano zenyewe. Na kwa kufanya hivyo itabidi turejee kwenye kitabu cha historia cha Tabari miongoni mwa vingine kwa sababu kina tarehe za mwanzo kuliko vinginevyo na kilichorejewa zaidi katika vitabu vya historia. At-Tabari amesimulia nyingi ya ngano za Seif akinakili kutoka kwenye vitabu vyake viwili, alFutuuh wal Radah na al-Jamal. Pia amesimulia kutoka kwenye mapokezi yake kuhusu Saqifa na kifo cha Uthman. Hivyo kuzifany mapokezi yake ni rejea mashuhuri, zinazotajwa kwenye historia zote za Kiislam hadi leo hii. Tutaiangalia historia ya Tabari kwanza na kisha wasimuliaji wengine waliomtegemea Seif katika simulizi zao na tutalinganisha na kutofautisha ngano zake na nyinginezo ili kujua ni mbinu gani alizotumia katika kuzighushi na tathmini ya ngano zake.
42
ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO
1. TUKIO LA JESHI LA USAMA KAMA LILIVYOSIMULIWA NA SEIF NA WENGINEO MBALI NA SEIF ULINGANISHO
43
ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO
JESHI LA USAMA Tabari (juz.3.uk.212, juz.1,uk.1849-50 EUR), na Ibn Asakir (juz.1,uk.427), kuhusu matukio ya mwaka 11 wa Hijiria, historia iliyoandikwa ya Jeshi la Usama iliyosimuliwa na Seif ni kama ifuatavyo: NGANO YA SEIF "Mtume wa Mwenyezi Mungu, kabla ya kifo chake, alikusanya pamoja jeshi chini ya uongozi wa Usama. Umar Ibn Khatab alikuwemo ndani ya jeshi hilo. Kabla ya jeshi hilo halijatoka hata nje ya mipaka ya mji wa Madina, Mtume wa Mwenyezi Mungu akafariki. Usama akamtuma Umar kwenda kwa mrithi wa Mtume (Khalifa) kuchukua ruksa ya jeshi hilo kurudi Madina. Masahaba wa Mtume, waliokuwemo kwenye jeshi hilo, walimwambia Umar amuombe Abubakr amuondoe Usama na achague kiongozi mwingine." Abubakr akaruka mbele na kumkamata Umar kwenye ndevu zake akisema, "Ewe Ibn Khatab, mama yako akalie kwenye kitanda chako cha mauti. Alikuwa ni Mtume mwenyewe aliyemchagua Usama kuwa kiongozi wa jeshi, bado unanitaka mimi nimuondoe na nichague mtu mwingine badala yake." Abubakr kisha akaliamuru jeshi kuondoka na akawaangalia wakiondoka, akiwaaga akisema, "Nendeni, Mwenyezi Mungu akuangamizeni kwa mauaji na tauni." Hii iliyopita imesimuliwa na Seif kuhusu jeshi la Usama. Lakini wengine wamesema ngano yenyewe ni kama ifuatavyo: MASIMULIZI YA WENGINE MBALI NA SEIF. Katika mwaka wa 11 wa Hijiria, siku ya Jumatatu, kukiwa kumebakia siku nne za mwezi wa Safar, Mtume aliwaamuru watu wajiandae kwa vita na Warumi. Siku iliyofuata alimuamuru Usama kuongoza jeshi hilo akimwambia, "Nenda sehemu ambayo baba yako aliuawa shahidi, na uwashambulie." Siku ya Jumatano Mtume mwili ukawa na joto kali na maumivu ya kichwa. Siku iliyofuatia, Alhamisi, Mtume mwenyewe akatengeneza bendera ya vita na akamkabidhi Usama. Usama aliichukua bendera na akaondoka Madina, akipachagua Jurf kama sehemu ya kambi. Wakubwa wa makundi ya Muhajir na Ansari, Abubakr, Umar Ibn Khatab, Abu Ubaydah Jarrah, Sa'd Waqqas Said Ibn Azid na wengineo waliamriwa kuunda jeshi chini ya uongozi wa Usama. Kwa vile Usama alikuwa kijana mdogo sana, kulikuwa na vipingamizi kuhusu kufanywa kwake kiongozi wa jeshi kwa kupendelewa kuliko wale watu wazima wa Waislamu Muhajir. 44
ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO
Mtume wa Mwenyezi Mungu akavisikia vipingamizi hivi na akatoka nje ya nyumba yake, kichwa chake kikiwa kimefunikwa na kitambaa, na taulo mabegani mwake, kwa vile alivyokuwa mgonjwa. Alivyopanda juu ya mimbari akawaambia watu akisema, "Ni habari gani hizi nilizosikia kuhusu Usama, ambaye amechaguliwa kuwa kamanda. Mlifanya upinzani kwa baba yake sasa mnampinga yeye. Wallahi Usama ana uwezo wa kushika nafasi hii, kama alivyokuwa baba yake." Mtume kisha akashuka kutoka kwenye mimbari, na Waislam waliokuwa wanakwenda kambini huko Jurf wakasema kwa heri. Afya ya Mtukufu Mtume ilizidi kuzorota, na Usama alimtembelea wakati Mtume alipokuwa hana uwezo wa kuongea aliweza tu kumbusu Usama busu la kwa heri. Jumatatu iliyofuata, Mtume alipata nafuu, na alimpokea Usama, akisema, "Nenda, kila la kheri juu yako." Usama alirudi kambini na kuamuru msafara kuondoka. Alipokuwa anataka tu kupanda farasi wake, ujumbe ukaja kutoka kwa mama yake ukisema Mtume ni mgonjwa sana. Usama, Umar na Abu Ubaydah walirudi Madina, na siku ile ile Mtume akafariki. Baada ya kifo cha Mtume, wakati Abubakr alipokuwa Khalifa, alimuamuru Usama kuchukua kazi ile ile kama alivyoamrishwa na Mtume, (Ibn Asakir, juz.1, uk.433). Katika ukurasa wa 438 Ibn Asakir pia anasema, "Abubakr alimwambia Usama kwamba Mtume alikwishatoa maagizo yote muhimu, na haongezi chochote juu yake." Abubakr hakuwasikiliza wale waliomshauri msafara ule uakhirishwe. ULINGANISHO Ulinganisho kati ya njia hizo mbili hapo juu za uandishi. Kuna baadhi ya mambo yanayofaa kutajwa juu ya uandishi wa Seif. Anasema: 1) “Jeshi hilo lilikuwa likivuka mpaka wa Madina wakati Mtume anafariki.� Seif aliuongeza msitari huu katika kitabu chake kuficha ukweli kwamba kulikuwa na ucheleweshaji uliozuia jeshi hilo kuondoka; na hapakuwa na vurugu kutoka kwa hao wakorofi waliosababisha kukawia huko.Bado katika wakati akiwa na fahamu kamili Muhammad alikasirika kwamba jeshi limekawizwa, na akarudia amri yake ya awali, "Jeshi la Usama lazima liondoke." 2) Seif anasema, "Wakati Usama aliposikia kwamba Mtume amekufa alimtuma Umar kwa mrithi wa Mtume wa Mwenyezi Mungu kupata ruksa ya kurudi kwa jeshi hilo Madina." Maelekezo mengine yanasema, "Usama alisikia kwamba hali ya Mtume ilikuwa mbaya sana, hivyo akaenda Madina na Umar, Abubakr na Abu Ubaydah. (Wengine wanasema Abu Ubaydah hakuwa pamoja nao.) Baada ya kifo cha Mtume, na baada ya kuchaguliwa kwa Abubakr huko Saqifa, na uchaguzi wake wa mwisho hapo Msikitini, ndipo akashughulika na jeshi la Usama." Hapa tena Seif anarudisha nyuma urithi wa Abubakr, kuufanya uonekane 45
ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO
3)
kwamba alichaguliwa kuwa mrithi (Khalifa) kabla ya kifo cha Mtume. Seif anasema, "Ansar walimuomba Abubakr kumuondoa Usama na kuchagua kamanda mwingine wa jeshi hilo." Ibn Asakir (juz.1,uk.438) na wanahistoria wengine wanasema, "Muhajirina wa mwanzo walimuomba Mtume ambadilishe Usama." Hapa tena Seif amebadilisha jina la wapendekezaji kutoka Muhajir kwenda Ansar kuridhisha Serikali ya wakati huo ambayo ilikuwa ya kundi la Muhajirina. Seif anasema: "Abubakr alimpa Usama maelekezo kumi." Wanahistoria wengine wanasema:Abubakr alisema kwamba Mtume alitoa maagizo muhimu na hakuwa na haja ya kuongeza chochote juu yake." Seif anasema: "Abubakr alimshika Umar kwenye ndevu zake kwa sababu alileta ujumbe wa Ansar," ingawa mjumbe hawezi kulaumiwa. Seif anasema, "Abubakr alililaani hilo jeshi na akategemea wataangamizwa kwa tauni." Seif akiwa ni muasi alitaka kufanya dhihaka ya Uislam kama dini, na vile vile kumfurahisha Khalifa wa wakati wake. Ngano zilizozushwa na Seif hazina msingi, na mashujaa waliotajwa ndani yake hawakuwapo kamwe kwani walikuwa ni utungo tu wa fikira zake. Tutaelezea kwa ufasaha zaidi baadae.
BAADHI YA MASAHABA WATAMBULISHWA Wakati umefika sasa kwetu kuwatambulisha kwa ufupi Masahaba tuliowataja mpaka hapa wa 1 na wa 2. Hakuna haja, kwa kweli, ya kusema chochote kuhusu Abubakr na Umar, Makhalifa wa kwanza na wa pili wanaofahamika sana. 3)
Abu Ubaydah Jarrah Amer, mwana wa Abdullah Ibn Jarrah na Umaymah, binti ya Ghunm Ibn Jabir. Abu Ubaydah alikuwa mmoja wa waliosilimu mwanzoni kabisa kuingia Uislam kutoka kabila la Quraish, na alihama mara mbili kutoka Makkah. Abubakr alimfanya kamanda wa jeshi lililotumwa kwenda Syria. Alikufa kwa tauni na akazikwa huko Jordan.
4)
Sa'd Waqqas, Abu Ishaq, mtoto wa Malik, kutoka kwenye familia ya Zuhra ya kabila la Quraish. Alikuwa mtu wa saba kuingia Uislam. Alishiriki katika Vita vya Badri na vita vingine vyote vilivyofanywa na Mtume. Alikuwa Mwislam wa kwanza kutupa mshale kwa maadui, kamanda mkuu wa majeshi yaliyoteka Iraq. Umar alimchagua kuwa Gavana wa Kufa. Sa'd alikuwa mmoja wa wajumbe sita wa kamati iliyoteuliwa kumchagua Khalifa baada ya Umar. (Alikuwa ni Umar aliyeamuru kamati hiyo ianzishwe mara moja baada ya kuchomwa vibaya na Abu Lulu). Sa'd alirudi kwenye makazi yake Aqiq karibu na Madina, baada ya Uthman kuuawa. Alikufa wakati wa utawala wa Mu'awiyah na alizikwa Baqi kwenye makaburi ya Madina.
5)
Said Ibn Zaid. Anatoka kwenye ukoo wa Adi wa kabila la Quraishi, na ni binamu yake Umar Ibn Khatab. Umar alimuoa Atikah, dada yake Said, naye Said akamuoa Fatimah, dada yake Umar. Said na Fatimah waliingia Uislam kabla 46
ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO
ya Umar. Wakati Umar aliposikia kwamba dada yake amekuwa Mwislamu, alikwenda nyumbani kwake, na akampiga makofi kwa nguvu sana uso wake mpaka ukaanza kutoka damu. Umar alisikitika sana kwa kitendo chake cha pupa, na papo hapo yeye mwenyewe akaukubali Uislam. Said alikufa mwaka wa 50 au 51 H.L. na alizikwa Madina. 6)
Usama. Baba yake Usama alikuwa ni Harithah, mtumwa aliyeachwa huru na Mtume Muhammad. Mama yake alikuwa Ummu Ayman, mtumwa wa Muhammad aliyemuacha huru. Usama alizaliwa mwanzoni mwa Uislam, na alikufa wakati wa utawala wa Mu'awiyah.
BUSARA ZA MUHAMMAD KATIKA KITANDA CHAKE CHA MAUTI Katika dakika zake za mwisho za maisha yake Mtume alifanya maajabu, aliwaondoa watu wazima wote na kumuacha Ali pekee Madina. Alisisitiza kuwapeleka Viongozi wa vikundi wote kwenda Syria, mbali na moyo wa Uislam, na akamuweka mtu ambaye wazazi wake ni watumwa, kuwa kiongozi wa watu wazima hao. (Hili litaelezwa baada ya kuyachunguza matukio yaliyotukia baada ya Mtume wa Mwenyezi Mungu kufariki.)
47
ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO
2. SEIF NA TUKIO LA SAQIFAH KAMA ILIVYOELEZWA NA SEIF NA WENGINEO MBALI NA SEIF ULINGANISHO
48
ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO
SEIF NA TUKIO LA SAQIFAH Ngano ya mjadala na mabishano ya mwanzoni huko Saqifah yanayohusu urithi wa Abubakr kama Khalifa wa Mtume ni moja kati ya ngano za kuvutia zilizosimuliwa na Seif ambayo inahitaji uchunguzi makini. Seif anasema: 2.1) Isabah (juz.2,uk. 230). "Wanasema kwamba Qa'qa Ibn Umar amesema, 'Wakati Mtume wa Mwenyezi Mungu alipokuwa anakufa, nilikuwepo. Mtu mmoja alikuja Msikitini wakati wa sala ya mchana, na akawaambia baadhi ya watu kwamba Ma-Ansari wanakwenda kumchagua Sa'd Ibn Ubaydah kwa kauli moja, kama Khalifa, na kupuuza mkataba wa Mtume wa Mwenyezi Mungu. Muhajirina waliguswa sana na hili.'" 2.2) Tabari (juz.3,uk.201). Matukio ya mwaka wa 11. Msimuliaji alimuuliza Amr Ibn Huraith, 'Ulikuwepo wakati Mtume wa Mwenyezi Mungu alipofariki?' Jibu lilikuwa ndiyo. Swali la pili lilikuwa, 'Ni siku gani Abubakr alichaguliwa?', na jibu likawa, 'Siku hiyohiyo alipokufa Mtume, kwa sababu watu hawakutaka kuchangukana ingawa kwa nusu siku.' Kisha akauliza, 'Kulikuwa na upinzani wowote?' 'Hapana, ulitoka kwa waasi tu au wale waliokaribia kuwa waasi,' 'Kuna jamaa yeyote wa Muhajiriin aliyempinga?' aliulizwa tena, na jibu likawa, 'Hapana, wote walitoa kiapo cha utii kwa Abubakr kwa hiari kabisa, mmoja baada ya mwingine.'" 2.3) Tabari, kuhusu Ansar kumuunga mkono Sa'd Ibn Ubaydah, na kumkataa: kwao Abubakr, anasema: "Zahhak Ibn Khalifah amesema kwamba Hubab Ibn Munzir alisimama na upanga mkononi mwake, akisema, "Mimi ni gongo la kuegemewa juu yake, mimi ndiyo jiti ambalo ngamia wanajikunia pale mahali wanapolala. Mimi ndiyo mti mkubwa ambao chini yake wanatafuta kivuli na hifadhi. Siogopi madhara kutoka kwenye upepo wowote. Mimi ndiye baba wa watoto wa simba ndani ya zizi lao." Umar akaruka haraka mbele na kuugonga upanga huo kutoka mkononi mwa Hubab. Umar akauokota huo upanga na kumshambulia nao Sa'd Ibn Hubab, na watu wengine waliokuwa wakimpinga Sa'd, walimuunga mkono Abubakr, kumsaidia kushinda uchaguzi huo. Uungaji mkono wa Ansari kwa Sa'd ulikuwa ni kosa kama lile la wakati wa ujahilia wa kabla ya Uislam. Bahati nzuri, Abubakr alimpinga Sa'd kwa nguvu na akayumbisha uungaji mkono wa watu kuja kwake. Wakati watu walipomshambulia Sa'd, mtu mmoja alipiga kelele kwamba ameuawa. Umar akasema, 'Mwenyezi Mungu amuue, ni mnafiki.' Kisha Umar akauchukua upanga huo na kuuvunja kwenye jiwe." 49
ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO
2.4) Tabari (baada ya ngano hiyo hapo juu): Mubashshir amesema kwamba Jabir amesimulia kwamba "Sa'd alimwambia Abubakr, 'Enyi Muhajir mlikuwa na wivu juu ya nafasi yangu kama mkuu wa nchi, na kwa wewe Abubakr, ulinilazimisha nikutii, kwa msaada wa kabila lako mwenyewe.' Muhajirina wakajibu, 'Kama tulikulazimisha kuondoka kwenye mkusanyiko ulikuwa na haki ya kutupinga, lakini tunakulazimisha kubaki ndani ya mkusanyiko. Sasa kama utapinga chombo cha jumla ya Waislam, utakatwa kichwa.'" 2.5) Tabari. "Ali alikuwa nyumbani kwake wakati habari zilipomfikia kwamba watu wametoa kiapo cha utii kwa Abubakr. Akiwa bado kwenye nguo yake ya usiku, alikurupuka kutoka nje, kwenda mara moja kwa Abubakr, na wakapeana mkono naye. Baadae, aliletewa nguo zake na akazivaa." 2.6) Tabari: "Abubakr alitoa hotuba mbili ndefu siku iliyofuatia kifo cha Mtume wa Mwenyezi Mungu. Alizungumzia zaidi juu ya mashaka ya dunia, maangamio ya mwanadamu, na Siku ya Qiyammah. Alisisitizia sana shetani aliyekuwa naye akisema, 'Kuna shetani wa maovu aliyeko ndani yangu. Niepukeni wakati nguvu hii ya uovu inaponizidi, ikiwa nitakuwa sipori tu mali zenu, bali hata nafsi zenu.'" 2.7) Tabari: Mubashshir Ibn Fuzail alisimulia kwamba Jubair (mlinzi wa Mtume) alisema kwamba baba yake alisema: "Khalid Ibn Saiid Ibn Aas alikuja Madina kutoka Yemen, mwezi mmoja baada ya Mtume wa Uislam kufariki. Alikuwa amevaa koti la hariri alipokutana na Umar na Ali. Umar akakemea, "Chaneni koti la Khalid vipande vipande kwani amevaa hariri wakati wa amani.' Khalid akageuka na akaongea na Ali, akisema, 'Ewe Abul Hasan, Enyi wana wa Abd Manafi mmeachia urithi wa Mtume, hivyo mmeshindwa. Enyi wana wa Abd Manafi ni ninyi tu mnaostahili kuwa warithi wa Mtume.' Umar akasema, 'Ewe Khalid, Mungu aukate ulimi wako; waongo daima watatumia maneno yako dhidi ya Uislam, na hii hatimae itakuwa dhidi yao wao wenyewe.' Umar baadae akamweleza Abubakr kuhusu kukutana kwake na Khalid. Muda mrefu baadae, Umar alimzuia Abubakr kumuweka Khalid kuwa kamanda wa jeshi linalopigana dhidi ya waasi. Umar alimwambia Abubakr kwamba Khalid alikuwa mbaya, ambaye alisema uongo ambao umesababisha mnon'gono daima na kwa hiyo msaada wake usihitajike. Abubakr alimpeleka Khalid Syria kama msaidizi wa Kamanda wa Jeshi huko Tima; kwani Abubakr alimsikiliza Umar nusunusu."
50
ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO
UCHUNGUZI JUU YA UKWELI WA NGANO KUHUSU SAQIFA KAMA ZILIVYOANDIKWA NA SEIF. 1) Msimamo na tabia ya wasimuliaji. 2) Yaliyomo kwenye ngano za Seif. a) Seif amenakili ngano yake ya kwanza kutoka kwa Qa'qa Ibn Amr at-Tamimi. Lakini Qa'qa ni mtu wa bandia aliyebuniwa na Seif, na ni katika kitabu cha Seif tu ndimo anamotokea. Hakuna dalili ya Qa'qa mahali pengine popote ila katika vitabu vile ambavyo waandishi wake wananakili kutoka kwa Seif. Baada ya Seif, kwa bahati mbaya, wanahistoria wengine na waandishi wametaja sehemu, viwanja vya vita, mashairi na shughuli za kijamii za kumhusu Qa'qa, na wamemtaja kama mmoja wa masahaba wa Mtume (tazama masahaba wa bandia). Seif ameandika ngano yake ya nne kutoka kwa Mubashshir, ambaye jina lake haliwezi kupatikana popote, ila ndani ya ngano za Seif. Sakhr ni mtu mwingine wa bandia aliyebuniwa na Seif, na alitokea katika ngano za mwisho za Seif. Seif alimtambulisha kama mlinzi wa Mtume, na bado jina lake halionekani popote katika habari za watu mashuhuri iitwayo "Nani ni nani". b) Yaliyomo kwenye ngano za Seif. Seif alikuwa mahiri katika kutoa ngano za uzushi kama za kweli na katika kupotosha ngano za kweli kukidhi haja yake. Mfano mmoja ni anaposema, "Siku ile ambayo Mtume alikufa, mtu mmoja alikuja Msikitini na kusema, "Watu wanakwenda kumchagua Sa'd kama mrithi wa Mtume na kuvunja mkataba wa Mtume.' Katika kuisoma hii, mtu anapata picha kwamba Mtume alichagua mrithi kabla hajafa, na kwamba lile kundi la Ansari lilikuwa linamsaliti Mtume." Seif vilevile anasema kwamba Usama alimtuma Umar kwa Abubakr baada ya kusikia habari za kifo cha Mtume. Kwa kusema hivi anataka kujulisha kwamba Abubakr alikwisha chaguliwa tayari kama Khalifa kabla Mtume hajafa. MSIMULIAJI WA NGANO Ule mkutano muhimu huko Saqifa, uliopelekea kuchaguliwa kwa Abubakr kama Khalifa, ulikuwa ni jiwe la pembeni la madaraka kwa ajili ya Khalifa na Mu'awiyah. Seif, msimuliaji wa ngano, alipindisha matokeo ya mkutano huu kukidhi maoni yake binafsi. Tutayatazama matukio ya mkutano huo, yaliyoandikwa na wanahistoria wasomi wa Sunni kabla ya kuchunguza maandishi ya Seif juu yake. TUKIO LA SAQIFAH NA WANAHISTORIA WENGINE MBALI NA SEIF SAQIFAH NA ABUBAKR Maandalizi kwa ajili ya mkutano wa Saqifa yalianza kabla ya kifo cha Mtukufu Mtume. Akiwa kwenye kitanda chake cha mauti, Mtume alijaribu kuwaondoa 51
ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO
kwenye Makao Makuu ya Umma wa Kiislam wale Wakuu wa Vikundi, na akamuweka Ali peke yake hapo Madina. Aliwaamuru kwa kurudiarudia viongozi hao waondoke Madina na kujiunga na vikosi viendavyo kwenye Uwanja wa Vita huko Syria (Sham). Walipuuza amri ya Mtume na kwa makusudi kabisa wakakawiza uondokaji wa jeshi hilo mpaka Mtume akafariki. Katika muda huu wa ucheleweshaji, lilitokea tukio la ajabu lililobadilisha mwelekeo wa historia. JE? MTUME ALIELEZA NIA YAKE KWA MAANDISHI? Dakika za mwisho za Mtume zilikuwa zinakaribia. Madina ilikuwa katika hali ya hofu. Kila mmoja alihisi kwamba yule kiongozi wa mwanadamu, alikuwa anaiaga dunia milele. Mtukufu Mtume alikuwa na mpango kwa ajili ya muda huu kwa wakati; ilikuwa akilini mwa Mtume awaweke mbali na Madina wale Wakuu wa vikundi, lakini walikataa kuondoka. Wao pia walikuwa na mpango, na walikuwa wakiyaangalia matukio kwa karibu sana. Walimzuia Mtume kuacha hati kwa Waislam kwa ajili ya uongozi wa mwanadamu. Kwa mujibu wa Tabaqat cha Ibn Sa'd juz.2,uk.243-244, Umar Ibn Khatab mwenyewe anasema, "Tulikuwa kando ya Mtume na wanawake walikuwa wamekaa nyuma ya pazia, kisha Mtume wa Mwenyezi Mungu akasema, 'Niosheni na maji mifuko saba ya ngozi iliyojaa, na nileteeni wino na karatasi kusudi niweze kuwaandikia ujumbe utakaokuzuieni msipotee.' Wale wanawake wakasema, 'Mleteeni Mtume wa Mungu hicho anachokitaka.'" Maghrizi anasema kwamba haya yalisemwa na Zainab binti ya Jahash, mke wa Mtume, na wanawake aliokuwa nao. Umar akasema, 'Niliwaambia wanawake hao wanyamaze kimya, kwamba walikuwa ndiyo wanawake waliofumba macho yao na kujidai kulia wakati Mtume alipokuwa mgonjwa, lakini waliomkalia kooni alipokuwa mzima." Wakati huo, Mtume akawaambia wale wanaume, 'Wanawake ni bora kuliko ninyi." Katika Tabaqat, juz.2,uk.242, Ibn Sa'd ameandika kwamba Jabir alisema, "Mtume, katika kitanda chake cha mauti, alitaka karatasi na kalamu ili aweze kuandika ujumbe kwa watu wake, akiwapa maagizo nini cha kufanya, kusudi kwamba wasiweze kupotea au kupotoshwa. Lakini watu walikusanyika hapo na kufanya ghasia mpaka Mtume akaliacha wazo lake hilo." Katika Musnad Hanbal, juz.1,uk.293, (sherehe ya Ahmad Shakir, Ngano 2676), Ibn Abbas alisema, kifo cha Mtume kilipokaribia alisema, "Nileteeni fupa la bega la kondoo, na nitawaandikia ujumbe. Kisha baada ya kifo changu, hakuna watu wawili watakaotofautiana baina yao." Wale waliokuwepo walipiga makelele mengi na mwanamke mmoja akauliza, "Hamuoni kwamba Mtume ataandika wosia?" Ibn Abbas mahali pengine alisema kwamba Mtume katika maradhi yake ya mwisho, alisema, "Nileteeni karatasi na wino niwaandikie ujumbe, ili kwamba hamtapotea baada ya kifo changu." Umar Ibn Khatab akasema kwamba kulikuwa bado 52
ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO
kuna miji, kama vile mji fulani na fulani, ya kuteka, na kwamba Mtume hatakufa mpaka awe ameichukua yote. Kama anakufa watasubiri kurudi kwake kama Bani Israil walivyomngojea Musa. Zainab, mke wa Mtume kwa muda huu, akasema, "Hamuwezi kuona kwamba Mtume atatengeneza wosia?" Kisha pakawepo na kelele kubwa na ghasia na Mtume akasema, "Tokeni, nyote," kisha mara moja akafariki. Kutoka kwenye matukio tuliyotaja, na yale ambayo tutayaandikia, inakuwa wazi kwamba licha ya udhaifu (wa afya) wa Mtume kabla ya kifo chake, aliitisha wino na karatasi, lakini wale waliokuwepo wakasababisha ghasia kubwa kiasi kwamba Mtume akaliacha ombi lake. Maelezo yetu yanayofuata yanaonyesha kwamba kwa sababu ya mabishano ya makusudi na yasiyo na maana, Mtume hakuwa na njia nyingine ila kuliacha wazo lake hilo. Katika kitabu cha Sahih Bukhari, Ibn Abbas alisema, "Oh Alhamisi! Siku gani hii." Alikuwa na huzuni kiasi kwamba machozi yaliyotoka machoni mwake yalitiririka kwenye mchanga uliokuwa chini yake. Pale ugonjwa wa Mtume wa Mwenyezi Mungu ulipozidi, Mtume akasema, "Nileteeni karatasi na wino ili niwaandikie ujumbe, utakaokuokoeni na kupotea nitakapokuwa nimeondoka." Kisha pakawa na mabishano mengi na majadiliano miongoni mwa wale waliokuwepo pale, ingawa kusingekuwa na mabishano mbele ya Mtume. Wengine wakasema kwamba Mtume alikuwa anaongea kwa kuweweseka. Kisha Mtume akasema, "Niondokeeni, nitahitaji faragha kwa muda huu." Katika sehemu nyingine Ibn Abbas amemtambulisha yule mtu aliyetamka kauli hiyo. Anatuambia katika kitabu cha Sahih Bukhari kwamba Mtume katika kitanda chake cha mauti alisema, "Msipoteze muda. Ngojeni niwaandikie jambo la kuwaokoeni msipotee." Umar ambaye alikuwa miongoni mwa mkusanyiko huo akasema, "Maradhi yameizonga akili ya mtu huyu, Qur'ani, Kitabu cha Allah, kipo pamoja nasi, na kinatosha." Kisha likaanza zogo na mabishano. Mtume alikasirika na akasema, "Tokeni nje, msibishane na kupingana mbele yangu." Katika vitabu: Musnad Hanbal na Tabaqat, imeelezwa kama ifuatavyo: "Waliongea upuuzi mwingi mpaka ukamfanya Mtume ahuzunike." Baadae Ibn Abbas alikuwa akisema, "Ulikuwa ni muda mfupi wa msiba mkubwa kwamba walipozungumza upumbavu walimzuia Mtume kuandika ujumbe huo." Katika ngano zote za hapo juu, hakuna yeyote ila Umar aliyetajwa kama ndiye aliyemzuia Mtume kuandika ujumbe huo. Umar ndiye aliyewaambia wanawake, "Nyie ni wake za mtu." Alikuwa ni Umar aliyewakemea kwa ukali wake za Mtume, akizungumza nao kwa namna isiyo ya adabu. Umar alitoa kauli hii ya kifedhuli kwa wanawake hawa pale waliposema, "Leteni karatasi na wino, Mtume anataka kuandika." Umar ndiye aliyesema, "Kama Mtume atakufa nani ataiteka miji ya Warumi?" Umar ndiye mtu, ambaye baada ya kuona wengi wanapendelea kukidhi ombi la Mtume na kumletea karatasi na wino, akasema, "Maradhi yamemzidi 53
ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO
mtu huyu. Anaweweseka. Qur'ani, Kitabu cha Allah kipo pamoja nasi - kinatosha." Alikuwa ni Umar aliyesema kwamba Mtume anaweweseka. Kwa maongezi kama hayo alifanikisha lengo lake kwa sababu hata kama wengine waseme, kwa nini Mtume hakusisitiza kuchagua mtu kwa maandishi? Tutambue hata hivyo kwamba hata hati ya maandishi isingekuwa na thamani sana, kwa sababu kwa shutuma za Umar wangesema maandishi hayo yamefanywa wakati anaweweseka na akiwa hajui anachokifanya. Hili limesimuliwa pia na Ibn Abbas. Kwa mujibu wa mapokezi kutoka kwa Ibn Abbas, mtu mmoja alimfuata Mtume na akamuuliza kama alikuwa bado anahitaji hiyo karatasi na wino. Mtume akajibu, "Baada ya hili kisha kuna nini?" Ikimaanisha kwamba baada ya mtu kusema kwamba anaweweseka itachukuliwa kwamba kitu chochote alichoandika kitakuwa hakina thamani, kwa sababu kiliandikwa wakati wa weweseko. Inaweza kuonekani kwamba Umar aliufanya mpango wake wa kifitna kwa werevu sana kwa kutoa kauli ile; na kwamba alimzuia Mtume kuandika ujumbe wa kuwaokoa Waislam kutokana na kupotea baada ya kifo chake. Baada ya maelezo hayo hapo juu pengine Umar angeulizwa swali lifuatalo, " Ulithubutu kumshutumu Mtume kuzungumza akiweweseka, kwa nini basi hukupinga wosia wa Abu Bakr alioutolea imla wakati wa kuweweseka?" Katika Tabaqat, juz.4,uk.52, Abubakr akiwa kwenye kitanda chake cha mauti, alimpokea Uthman peke yake. Alimwambia aandike, "Kwa Jina la Mwingi wa Rehma, huu ni wosia wangu. Pendekezo kwa Waislam kutoka kwangu mimi Abubakr Ibn Quhafa." Mara kufika hapa alipotelewa na fahamu, hivyo Uthman akaendelea kuuandika wosia, kwa majisifu hayo hayo, kama ifuatavyo, "Nimeamua kumfanya Umar kuwa mrithi wangu, Khalifa wangu. Nimewafanyieni vizuri." Kufikia hapa Abubakr akazinduka na kusema, "Nisomee tena kile ulichoandika." Uthman akafanya hivyo, na Abubakr kisha akasema, "Allah Akbar. Uliogopa kwamba ningekufa bila ya kupata fahamu, Waislam wangekuwa hawana Khalifa, na wangepotea." Uthman akaitika, na Abubakr akasema, "Mwenyezi Mungu akulipe vema kwa msaada ulioutoa kwa Waislam na Uislam." Umar angeulizwa, jibu lako ni lipi kwa wosia wa Abubakr?" Umar alikuwa nyumbani kwake, akiwa amezunguukwa na marafiki zake, akiwa amevalia na kusubiri kutokea kwa mtumwa wa Abubakr akileta huo wosia, ambao yaliyomo ndani yake yangefanywa rasmi. Umar aliipokea barua hiyo, na kisha akaihutubia hadhara hiyo hivi, "Sikilizeni enyi watu! Tiini kile ambacho Khalifa wa Mungu amesema. Khalifa anasema amewafanyieni vizuri." Umar huyu huyu, aliyemzuia Mtume kuandika wosia wakati wa maradhi yake ya mwisho na akasema, "Mtu huyu anaweweseka - kinatutosha Kitabu cha Mwenyezi Mungu," sasa anaikubali barua ya Abubakr, iliyoandikwa katika kitanda chake cha mauti kwenye hali ya kuweweseka. Ibn Abbas kwa kweli alikuwa na haki ya kulia mpaka mchanga uliokuwa ardhini ukaloa kwa machozi.
54
ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO
KIFO CHA MTUME (S.A.W.W.) Wakati wa mchana siku ya Jumatatu, Mtukufu Mtume alifariki chumbani kwake huko Madina. Umar alikuwepo, na Abubakr alikuwa kwenye makazi yake, Sanh, ambako ni maili moja kutoka Madina. Umar na Mughirah walipewa ruksa ya kuingia kwenye chumba ambamo mwili wa Mtume ulikuwa umelala. Umar akafunua nguo iliyokuwa imefunika uso wa Mtume, akisema, " Mtume amezimia." Mughirah akamwambia Umar wakati wanatoka chumbani humo, "Lakini unajua kwamba Mtume wa Allah alikuwa amekufa." Umar akamwambia, "Unadanganya, Mtume hakufa. Wewe ni mkorofi. Mtume wa Allah kamwe hatakufa mpaka awaangamize wanafiki wote." Umar aliwatisha wale wote waliosema Mtume amekufa, kwa vifo vyao wenyewe. Akatangaza, "Baadhi ya wanafiki wanadhani Mtume wa Allah amekufa, hakufa. Amekwenda kwa Mola kama vile Musa alivyofanya kwa siku arobaini. Watu walifikiri Musa alikufa lakini alirudi na hivyo Mtume wa Allah atarudi,na atakata mikono na miguu ya wale ambao walifikiri amekufa." Umar akasema, "Nitamkata kichwa yeyote anayesema kwamba Mtume wa Allah amekufa, Mtume amepaa Mbinguni." Ibn Makhtum Amr Ibn Qais ndipo akasoma kifungu cha Qur'ani kinachosema, "Muhammad ni Mtume kama wale waliokufa kabla yake. Mtageukia kwenye njia zenu za zamani kwa sababu amekufa? Yeyote mwenye kugeuka nyuma hamdhuru chochote Mwenyezi Mungu, lakini Mwenyezi Mungu atawalipa waumini." Abbas, ami yake Mtume akasema, "Mtume wa Mwenyezi Mungu kwa hakika amekufa, nimeuona uso wake na umefanana na nyuso za watoto wa Abdul Muttalib waliokufa." Kisha akawauliza watu, "Hivi Mtume alisema chochote kile kwenu kuhusu kifo chake? Kama ndivyo, tafadhali tujulisheni." Watu wakajibu kwamba hawajui chochote. Kisha akamuuliza Umar, "Unajua chochote?" Lakini Umar akajibu kwamba hakujua chochote. Ndipo Abbas akawahutubia watu akisema, "Shuhudieni, kwamba hakuna hata mmoja anayejua chochote ambacho Mtume amekisema kuhusu kifo chake. Naapa kwa Mola, ambaye ni mmoja tu na hakuna anayefanana kama Yeye, kwamba Mtume wa Allah amekufa." Umar bado alikuwa anarindima kwa hasira na kufanya vitisho, lakini Abbas aliendelea akisema, "Mtume wa Mwenyezi Mungu, kama mtu mwingine yeyote anapaswa kufa na kupata maradhi; na amekufa. Mzikeni bila kukawia. Hivi Mungu anatuua sisi mara moja, na amuue Mtume wake mara mbili? Kama unayosema ni kweli, Allah anaweza kumfufua toka kaburini. Mtume wa Allah amemuonyesha mwanadamu njia sahihi ya kwenye ustawi na uongofu katika uhai wake." Umar aliendelea kukemea, na sasa alikuwa anatokwa na povu mdomoni kwa ukali wake. Salim Ibn Ubaid ndipo akaenda kwa Abubakr na kumueleza kinacho tokea. Alikuja Madina na akamuona Umar amesimama pale na kutishia watu, akisema, "Mtume wa Mwenyezi Mungu yuko hai. Hakufa. Atatoka chumbani kwake na kuwakata mikono wale wanaoeneza uongo juu yake, atawakata vichwa, atawanyonga." Pale Umar alipomuona Abubakr, alitulia; Abubakr akamtukuza 55
ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO
Mungu akisema, "Kwa wale wanaomuabudu Mungu, Mungu yuko hai, lakini kwa wale wanaomuabudu Muhammad, Muhammad amekufa." Kisha akasoma kutoka kwenye Qur'ani, "Muhammad alikuwa ni Mtume. Kabla yake wamepita mitume wengi." Umar akauliza kama hicho kilikuwa ni kifungu kutoka kwenye Qur'ani na Abubakr akathibitisha kwamba ndivyo. Lakini hotuba ya Mughira, kule kusoma toka kwenye Qur'ani kwa Amr Ibn Qais na Abbas, ami yake kufafanua, vilishindwa kumshawishi Umar kwamba Mtume alikuwa amekufa, lakini akamsikiliza Abubakr kwa ukimya. Hebu na tusikie simulizi kutoka kwa Umar mwenyewe. "Ninaapa kwa Allah, nilipomsikia Abubakr akisoma ile Aya magoti yangu yalilegea hivyo kwamba nilianguka chini, nisiweze kuamka, na nilitambua kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu amekufa." Hivi alikuwa Umar siku hiyo, amechanganyikiwa kwa kumpoteza Mtume wa Mungu, kwamba mpaka akashindwa kujimiliki mwenyewe; na ni kweli kwamba alikuwa mwenda wazimu siku hiyo kama baadhi ya wanahistoria walivyoandika? Hatuyaamini mambo haya, kwani tunaijua sababu nyuma ya kuubadili ukweli. Ibn Abil Hadid anasema, "Wakati Umar alipokijua kifo cha Mtume, akawa na wasiwasi kama kutakuwa na mabishano kuhusu mrithi wa Mtume. Aliogopa kwamba kundi la Ansari au wengineo wangepata madaraka, hivyo akazusha mashaka na akaonyesha ukaidi wa kukubali kifo cha Mtume, kama ulinzi wa Imani mpaka kufika kwa Abubakr." Ibn Abil Hadid alikuwa sawa, kwa sababu Umar aliogopa kwamba Ali angeweza kushinda uchaguzi huo. Kulikuwa na wagombea watatu tu wa urithi huo, na Umar alimuunga mkono mgombea wa tatu, ambaye ni Abubakr. Wagombea watatu hao walikuwa ni: 1)
Ali Ibn Abi Talib, aliyekuwa akiungwa mkono na wafuatao: a. Bani Hashim, ule ukoo wa Mtume. b. Abu Sufian, kiongozi wa upinzani kabla ya kubadilika kuwa Mwislamu c. Khalid Ibn Saeed Amawi, Bara Ibn Azib Ansari, Salman, Abu Dhar, Miqdad na masahaba mashuhuri wengine wa Mtume wa Mwenyezi Mungu.
2.) Sa'd Ibn Ubaidah Ansari: ambaye alikuwa mgombea wa kabila la Khazraj (kundi la Ansari). 3) Abubakr ambaye waungaji mkono wake walikuwa Umar, Mughira Ibn Shu'ba, na Abdur-Rahman Ibn Auf. Ali na Abubakr walikuwa na nafasi nzuri ya kushinda uchaguzi huo, kwa vile mgombea wa pili alitoka kundi la Ansari na hakuwa na uungwaji mkono kutoka kwa Muhajirina. Kama Ali angekuwepo kwenye 56
ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO
uchaguzi huo baada ya mazishi ya Mtume, angeweza kupata kura nyingi zaidi ya Abubakr, kwa sababu Muhajirina, Ansari na kabila lote la Abd Manafi walikuwa upande wake. Kwa hiyo yote yale aliyofanya Umar (Abu Hafsa), kabla na baada ya kifo cha Mtume, yalisababishwa na woga wake kwamba Ali angewekwa madarakani. Ukweli ni huu: Kama kifo cha Mtume kimemchanganya sana Umar, angebakia na kusaidia kwenye maandalizi ya mazishi, badala ya kusema kwamba Mtume hakufa, na kukimbilia Saqifah kuchagua mrithi wa Mtume. Ibn Hisham anasema, "Wakati Umar na Abubakr (masheikh wawili hawa) walipojua kifo cha Mtume, Umar alimwambia Abubakr, "Twende tukaone Maansari wanafanya nini?" Mwili wa Mtukufu Mtume ulikuwa umelala chumbani mwake na kwa mujibu wa Tabari, Umar na Abubakr walimwacha Ali kando ya kitanda cha Mtume, akimtayarisha kwa mazishi, na wakaenda Saqifah. Wakiwa wamo njiani, walikutana na Ubaidah Jarrah na akaenda nao Saqifah. Ma-Ansari walikuwa Saqifah na wakaungwa na Muhajirina, hakuna yeyote, ila ukoo wake, waliomsaidia katika matayarisho ya mazishi ya Mtume. Abi Zuwaib Huzali anasema, "Nilifika Madina na kuwakuta watu wanalia na kutoka machozi kama vile mwanzoni mwa hija. Nikauliza sababu, wakaniambia kwamba Mtume alikuwa amekufa. Niliharakisha kwenda Msikitini lakini sikukuta mtu pale. Mlango wa chumba cha Mtume ulikuwa umefungwa, na nikaambiwa kwamba alikuwa yupo chumbani mwake na familia yake ikiwa imemzunguuka. Nikauliza watu wote walikuwa wamekwenda wapi, na nikaambiwa kwamba wamekwenda Saqifa kujiunga na Ansari. Watu pekee waliobaki nyumbani kwa Mtume kumtayarisha kwa mazishi walikuwa, ami yake Abbas, Ali Ibn Abi Talib, Fadhil Ibn Abbas, Qathm Ibn Abbas, Usama Ibn Haritha na mtumwa wake Saleh. Ali akiwa amevaa shati tu, alimbeba Mtume kifuani kwake. Abbas, Fadhl na Qathm walimsaidia Ali kumgeuza Mtume. Usama na Saleh walimmwagia maji, na Ali alimuosha Mtume. Uas Ibn Khawali Ansari alisimama karibu, akiangalia." HAWA WAGOMBEA KABLA YA MAZISHI YA MTUME (S.A.W.W) Kampeni ya nyumba hadi nyumba kwa ajili ya mrithi wa Mtume ilianza kabla ya mazishi yake. Ali alikuwa mmoja wa wagombea hao. Ibn Sa'd ameandika katika Tabaqat yake kwamba Abbas alimwambia Ali, "Nitapeana mikono na wewe hadharani kama ishara ya kiapo cha utii, na kuwahimiza wengine kufanya vivyo hivyo." Masoud anasema kwamba Abbas alimwambia Ali, "Ngoja nikupe mkono wa kiapo ewe mwana wa ndugu yangu, ili kwamba pasiwe na mgogoro kuhusu wewe kuwa mrithi wa Mtume." Dhahabi na wengine wanasema kwamba Abbas alisema, "Ngoja nikupe mkono wa kiapo, ili kwamba watu waseme kwamba ami yake na 57
ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO
familia yake wameushika mkono wa mpwawe; na mara uchaguzi utakapo kwisha hauwezi kufutwa." Jawhari anasema kwamba Abbas alimlaumu Ali baadae, akimwambia, "Wakati Mtume alipokufa, Abu Sufiani na mimi tulikujia, tukikutaka umuache mkuu wa ukoo na mimi mwenyewe tupeane mkono na wewe. Kabila la Bani Hashim wangefanya vivyo. Pindi makabila ya Abd Manafi na Bani Hashim yangekuwa upande wako, urithi wako ungesimama imara. Lakini ulituambia tuakhirishe jambo hili mpaka baada ya mazishi ya Mtume." Tabari anasema kwamba Abbas alimwambia Ali kwamba asipoteze muda, lakini Ali alikataa kumsikiliza. Ali hakuwa na upungufu wa wanaomuunga mkono, lakini kwake yeye mazishi ya Mtukufu Mtume yalikuwa yenye umuhimu zaidi kwa wakati ule kuliko haja ya kushika mamlaka. Alikuwa akisita sana kushiriki katika harakati za kabla ya uchaguzi wa mrithi wa Mtume huku Mtume akiwa amelala maiti na hajashughulikiwa. Kusita kwa Ali kunyakua mamlaka kulimfanya Abbas amlaumu kwa kukawia kwake. Lakini kwa kweli ushauri huo na shutuma havikuwa na maana kwa sababu: a)
Mtukufu Mtume tayari alikuwa amemteua Ali kama mrithi wake kama baadhi ya Waislam wanavyoamini; na kama Waislam wangetaka kukubali kile ambacho Mtume amekisema, wasingesema alikuwa anaweweseka.
b)
Kama mambo ya Waislam yangeachwa mikononi mwao wenyewe na Mtume, uingiliaji wa Abbas ungewanyan'ganya Waislam haki yao ya kumchagua yeyote kama kiongozi.
MGOMBEA WA PILI WA URITHI WA MTUME Mgombea wa pili alikuwa ni Sa'd Ibn Ubaidah ambaye, mbali na kuumwa kwake, aliletwa mpaka Saqifa. Alipewa kura ya kuwa na imani na Ansari. Alianza hotuba yake kwa kumtukuza Allah, na kuwakumbusha watu jinsi gani Ansari walivyokuwa wema na wenye msaada kwa Uislam na kwa Mtume, pia kwamba waliitunza heshima ya Mtume kiasi kwamba alikuwa na imani juu yao mpaka ile siku ya kifo chake. Kisha akawaambia Maansari, "Ninyi lazima mlishughulikie hili jambo la urithi." Alishinda kura ya makubaliano ya kundi la Maansari, lakini baadhi ya watu walishangaa kwamba uamuzi utakuwa vipi endapo watapingwa na kundi la Muhajirina, kwa sababu walikuja kutoka Makka na Mtume, na walikuwa ndugu zake. Baadhi yao walijibu kwamba kiongozi mmoja angechaguliwa na Maansari, na mmoja na Muhajiriina, viongozi hao wawili wangefanya kazi pamoja. Sa'd alililalamikia hili akisema, halitawezekana.
58
ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO
MGOMBEA ALIYEFAULU Katika kusikia kwamba watu wamekusanyika huko Saqifah, Abubakr na Umar wakaenda huko. Waliungwa humo njiani na baadhi ya marafiki zao ambao ni: Usaid Ibn Hudhair, Uwaim Ibn Saideh, Asim Ibn Adi ambaye alitoka kabila la alAjlan katika Ansari, Mughira Ibn Shu'bah na Abdur-Rahman Ibn Aufi. (Wakati Abubakr na Umar waliposhika madaraka, watu hawa walipendelewa sana.). Abubakr alimpenda sana Usaid Ibn Hudhair zaidi kuliko Maansari wengine na Umar akimwita ndugu yake. Abubakr alionyesha mapenzi yake kwake baada ya kufa kwake. Pale Uwaim alipokufa, Umar alikaa juu ya kaburi lake na akasema, "Hakuna mtu yeyote duniani hapa anayeweza kusema ni mbora kuliko huyu mtu aliyelala katika kaburi hili." Abu Ubaidah aliteuliwa kama mkuu wa jeshi lililotumwa kupigana na Falme ya Warumi. Wakati Umar alipotaka kujichagulia mrithi, alijuta kwamba Abu Ubaidah hakuwa hai, kumtaja kama Khalifa wa Waislam anayefuata. Na kwa Mughira Ibn Shu'bah, Umar alitupilia mbali adhabu ya uzinifu kuhusu yeye na siku zote alikuwa miogoni mwa wakubwa wakati Umar alipokuwa Khalifa. Umar pia alimsaidia sana Abdur-Rahman Ibn Aufi, na akamchagua kama mtu maalum katika kuchagua Khalifa wa tatu. Watu hawa ndiyo wale waliouacha mwili wa Mtume na hawakushiriki katika mazishi yake, badala yake walikimbilia Saqifah kuchagua Khalifa wa kwanza, na wakapambana na Ansari katika kutawala Waislam. Baada ya kumtuliza Umar pale Saqifah, Abubakr alimshukuru Allah na akasema, "Uislam ulianzishwa na Muhajiriina, na ndiyo watu wa kwanza duniani kumwabudu Mwenyezi Mungu na kumuamini Mtume. Walikuwa marafiki na ndugu wa Mtume, kwa hiyo wana haki ya kumrithi. Hapana isipokuwa mtu dhalimu atakayebishana nao." Kisha Abubakr akawasifu Maansari, akisema, "Hakuna yeyote isipokuwa wale Muhajir wa mwanzoni walio karibu nasi kuliko ninyi. Wao watakuwa viongozi na ninyi mtakuwa mawaziri." Hubab Ibn Mundhar alisema, "Enyi Maansari, kuweni imara na muungane ili kwamba wengine watawatumikieni, na hakuna atakayethubutu kukupingeni. Vinginevyo watu hawa (Muhajirina) watafanya kwa mujibu wa mpango wa Abubakr ambao mmeusikia hivi punde, tujichagulie wenyewe mtawala wetu na tuwaache wao wachague mmoja kwa ajili yao." Umar akasema, "Wallah, watawala wawili hawawezi kutawala kwa wakati mmoja, mahali pamoja. Waarabu hawatakutiini ninyi (Maansari) kwa sababu Mtume alikuwa Muhajirina na kwa hili tunao ushahidi wa wazi. Ni wale tu ambao wameuacha waislamu watahoji kuhusu urithi kwenye urawala wa Muhammad."
59
ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO
Hubab Ibn Mundhir akasimama tena na akazungumza na ile hadhara akisema, "Enyi Maansari, msiwasikilize watu hawa, Umar na marafiki zake. Watakuporeni haki zenu na kukunyimeni uhuru wenu wa kuchagua. Kama hawakubaliani nanyi warudisheni nyumbani kwao, na muunde Serikali mnayotaka kuwa nayo. Wallah, mnastahili kuwa watawala kuliko mtu mwingine yeyote. Watu hawa (Muhajirin) ndiyo watu walewale ambao hawakumuamini Mtume kabla; na kama isingekuwa kwa ajili ya woga walionao juu ya panga zenu, wasingejisalimisha kamwe kwenye Uislam." Kisha akaendelea kuonyesha uungaji mkono wake kwa Maansari kama wangeuhitaji kama lile gogo la mti ambalo juu yake ngamia wanajikunia, au kama jiti kubwa ambalo chini yake watu wanapata hifadhi wakati wa mvua. Kisha akasema, "Tutafanya vita kama ni lazima, na kulazimisha matakwa yetu juu ya wale wanaotupinga." Umar akasema: "Mwenyezi Mungu na akuue wewe," akimuangusha chini, akimpiga mateke, na kushindilia udongo kinywani kwake. Abu Ubaidah ndipo akasema: "Enyi kundi la Ansari, mlikuwa wasaidizi wa kwanza wa Uislam, msiwe wasaliti wa kwanza." Kisha Bashir Ibn Sa'd wa kabila la Khazraj na wa kundi la Ansari akazungumza upande wa Kundi la Muhajirina katika kumpinga Sa'd Ibn Ubaidah. Viongozi hawa wawili wa kundi la Ansari walikuwa washindani kabla hawajaingia Uislam. Bashir Ibn Sa'd akasema: "Enyi watu wa kundi la Ansari, sisi Maansari tuliwapiga wapagani, na tukausaidia Uislam, siyo kwa ajili ya heshima ya kidunia bali kwa kumridhisha Allah tu. Tusiutafute ukubwa. Muhammad alitokana na Ma-Quraish, hawa Muhajirina, na mmoja wa ndugu zake anastahili kuwa mrithi wake zaidi kuliko sisi. Naapa kwa Allah, kwamba sitabishana naye (Ali). Ninatumaini hamtabishana vilevile." Abubakr kisha akasema: "Umar na Abu Ubaidah wapo kwa ajili yenu, thibitisheni yeyote kati yao kama kiongozi wenu." Lakini Umar na Abu Ubaidah wakajibu kwamba madhali Abubakr alikuwepo, hawangeweza kuukubali uteuzi huu. Abdur-Rahaman Ibn Aufi akasema: "Enyi Ansari, inakubalika kwamba ninyi ni wabora, lakini hakuna miongoni mwenu kama alivyo Abubakr, Umar au Ali." Mundhar Ibn Arqam akasema: "Hatuukatai ubora wa hao uliowataja, hususan mmoja ambaye hakuna mtu awezaye kumkataa." Alikuwa akimzungumzia Ali. Hapa, Maansari na baadhi ya watu wengine walikemea, "Hatumtaki yeyote ila Ali." Kwa mujibu wa Tabari na Ibn Athir, pale Maansari walipotambua kwamba Abubakr alikuwa karibu ashinde uchaguzi huo kwa msaada wa uungwaji mkono na Umar, wakasema kwamba Ali ndiye pekee waliyemtaka. Zubair Ibn Bakkar akasema kwamba baada ya Maansari kushindwa katika uchaguzi huo waliungana pamoja na kufanya mkarara (kuimba kwa kurudiarudia), 60
ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO
"Tunamtaka Ali tu." Imeandikwa kwamba baadae Umar alisema: "Palikuwa na kelele nyingi na ghasia mpaka nikaogopa pangetokea ugomvi, hivyo nikaushika mkono wa Abubakr kama Khalifa." Imeandikwa pia kwamba baadae Umar pia alisema, "Niliogopa kwamba kama watu wangetawanyika bila kuchagua mrithi, basi baadae wangechagua mtu ambaye tusingekubaliana naye hivyo kusababisha ugomvi, au kwamba wangemuunga mkono mtu huyo bila kuwa na hiari." Umar na Abu Ubaidah walitembea kuelekea kwa Abubakr, lakini Bashir Ibn Sa'd wa kabila la Khazraj, alikwenda haraka zaidi, akimpa Abubakr mkono wa kwanza, hivyo kumtambua yeye kama ndiye mrithi wa Mtume. Hubab Ibn Mundhar alimkemea Bashir akisema: "Oh Bashir Ibn Sa'd, ewe mwenye balaa, hata wazazi wako walikuchukia wewe. Umepuuza makualiano ya familia, hukuweza kuvumilia kumuona binamu yako (Sa'd) akiwa Mtawala." Bashir akasema, "Hapana, umekosea, sikutaka kutokubaliana na chaguo la watu. Mungu amewapa haki hiyo." Kabila la Aus liliona kwamba lile kabila la Khazraj lilikuwa madhubuti sana katika kumpendelea chifu wao mgombea, Sa'd. Kwa hiyo waliamua kumuunga mkono Abubakr, wakidhani kwamba kama Sa'd angechaguliwa, kabila la Aus lisingekuwa na sauti katika mambo ya baadae. Pale binamu yake Sa'd, Bashir, alimuunga mkono Abubakr waziwazi kwa kupuuza uamuzi wa watu wa kabila lake, ndipo kabila la Aus walitiwa moyo zaidi kumuunga mkono Abubakr na Usaid Ibn Hudhair, mmoja wa machifu wa kabila la Aus, haraka sana akaushika mkono wa Abubakr. Watu walipoona kwamba kabila la Khazraj lina wapinzani wengi sana, walisimama na kumuunga mkono Abubakr, na kwa mujibu wa Yaqoubi, walimpa mkono. Ilikuwa ni wakati huu ambapo Sa'd Ibn Ubaidah alikuwa karibu apondwe chini ya watu walipokuwa wanaruka zulia alilokuwa amekalia. Walinzi wa Sa'd walikuwa wanapiga ukelele "Ondokeni, mpeni Sa'd nafasi ya kupumulia." Ndiyo wakati huo Umar alipokemea, "Muueni Sa'd, Mungu na amuue huyo." Kisha akamfuata Sa'd akisema: "Nataka kukuponda chini ya miguu yangu." Kwa hili, Qais Ibn Sa'd alimwambia Umar, "Kama utadhuru japo unywele mmoja wa kichwa cha Sa'd, utakugharimu meno yako yote." Abubakr akakemea, "Umar, nyamaza. Katika nyakati hizi dhaifu tunahitaji utulivu juu ya yote." Umar akaondoka alipo Sa'd, lakini Sa'd akakemea nyuma yake, "Kama ningekuwa na uwezo wa kusimama, ningesababisha fujo hiyo katika Madina, kiasi kwamba wewe na rafiki zako mngejificha kwa woga. Kisha ningekurudisha kwa watu kama mtumishi wao, na siyo kama mtawala wao." Kisha akiwageukia watu wake, akasema: "Niondoeni mahali hapa." Wakafanya hivyo. Jauhari ameandika kwamba siku hiyo , Umar ambaye alikuwa amevaa rasmi kwa 61
ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO
tukio hili, alikimbia mbele ya Abubakr na akakemea, "Sikilizeni, watu wametoa mkono kwa Abubakr wa kiapo cha utii, ninyi pia mfanye vivyo hivyo." Kisha Abubakr akapelekwa Msikitini na watu, ili wengine waweze kumpa mkono. Kwa wakati huu Ali na Abbas walikuwa bado wanashughulika kuuosha mwili wa Mtume, waliposikia mwito "Allahu Akbar" kutoka Msikitini. Ali akauliza ni nini kinachotokea, Abbas akasema ni maajabu, lakini alilitarajia hilo.
ONYO: Bara' Ibn Azib alikwenda kwenye nyumba ya ukoo wa Bani Hashim akisema kwa sauti kubwa, "Oh Bani Hashim, watu wengi wamempa mkono wa kiapo Abubakr." Ukoo wa Bani Hashim wakaambiana wenyewe kwa wenyewe, "Kabla ya hapa Waislam hawajafanya namna hii bila kwanza kutuona sisi, ndugu wa karibu wa Muhammad." Abbas akajibu, "Kwa Mungu wa Ka'aba, yote yamekwisha." Kwa mujibu wa Bara' Ibn Azib, kama ilivyoandikwa na Yaqoubi, Abbas kisha akawaambia ukoo wa Bani Hashim: "Mmepoteza mamlaka yenu milele. Nilikushaurini kuchukua tahadhari, lakini mkapuuza onyo langu." Tabari ameandika kwamba kabila la Aslam lilikuja Madina, wakijazana kwenye vichochoro, wakimpa mkono wa kiapo cha utii Abubakr. Baadae Umar alizoea kusema, "Wallah, baada ya kuwaona kabila la Aslam wakimuunga mkono Abubakr, nilipata imani kwamba tumeshinda." Sheikh Mufid, katika kitabu chake al-Jamal, anasema kwamba ilikuwa ni bahati tu kwamba lile kabila la Aslam siku hiyo lilikuwa Madina, kama walivyokuja kununua mahitaji. Waliambiwa kwamba ni lazima wamuunge mkono mrithi wa Mtume kabla hawajauziwa mahitaji yao, wakafanya hivyo. Wafuasi wa Abubakr waliwachukua kuwapeleka Msikitini ambako Abubakr alikaa kwenye mimbar mpaka jioni, akipeana mkono na yeyote aliyetokea mbele yake. KIAPO CHA HADHARA Siku iliyofuatia matukio ya Saqifah, Abubakr alikaa kwenye ngazi za mimbari ndani ya Msikiti. Umar akasimama, akamshukuru Mungu, kisha akasema, "Maneno niliyosema jana hayakutoka kwenye Qur'ani wala hayakuwa maneno ya Mtume. Nilidhani kwamba Mtume atayashughulikia mambo yote yaliyowahusu watu, na kwamba atakuwa mtu wa mwisho kufa. Ameiacha Qur'ani kati yenu, na kama mtafuata maelekezo yake, itakuongozeni kama ilivyomuongoza Mtume. Sasa uongozi wenu uko mikononi mwa mtu bora miongoni mwenu, Sahaba wa Mtume, aliyekuwa naye pangoni. Simameni na mshike mkono wake." Bukhari anasema kwamba wengine walikubaliana na urithi wa Abubakr pale Saqifah, lakini onyesho 62
ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO
kubwa la hadhara la kiapo lilifanyika pale Msikitini. Imesemwa na Anas Ibn Malik kwamba, ilibidi Abubakr ashawishiwe na Umar, kwenda kukaa kwenye ngazi za mimbari ambapo watu walikwenda kumpa mkono. Baada ya kumshukuru Mungu, Abubakr alisema, "Enyi watu, utii wenu sasa uko kwenye dhamana yangu. Mimi siyo mbora zaidi miongoni mwenu, lakini kama niko sawa basi nifuateni. Kama ninakosea basi niongozeni. Kama ninamtii Mwenyezi Mungu na Mtume wake, basi nitiini. Kama simtii Mungu na Mtume wake, msinitii mimi. Sasa simameni kwa ajili ya Sala. Mwenyezi Mungu na akusameheni." BAADA YA KIAPO CHA UTII Siku ya Jumatatu, Mtume wa Mwenyezi Mungu - Rehema na amani ziwe juu yake na juu ya kizazi chake, alifariki dunia, badala ya kuhudhuria mazishi, watu walishiriki katika matukio matatu yaliyofikisha mchana wa siku iliyofuata, Jumanne. 1) 2) 3)
Maandamano. Onyesho la kwanza la kiapo cha utii huko Saqifah. Tangazo la mwisho la kiapo cha hadhara hapo Msikitini lililoishia na hotuba ya Umar na Abubakr kuongoza sala ya kundi zima.
Baada ya mlolongo wa mambo ya tukio la tatu yalipokwisha hiyo siku ya Jumanne, watu tena ndipo walipokwenda nyumbani kwa Mtume kutekeleza sala ya maiti. Mmoja mmoja, kundi kwa kundi.
MAZISHI YA MTUKUFU MTUME (S.A.W.W.) Masahaba wa Mtume walimwacha mikononi mwa ukoo wake. Toleo moja linaeleza kwamba Abbas, Ali, Fadhl na Saleh (mtumwa wa Mtume), walitayarisha mwili wake kwa ajili ya mazishi na wakamzika. Habari nyingine zinaeleza kwamba Ali, Fadhl, Qasam, watoto wawili wa Abbas na Shoqran (mtumwa wa Mtume), walihusika na mazishi ya Mtume. Baada ya tukio wakati hadhara ilipotoa kiapo cha utii, Jauhari katika kitabu chake 'Saqifah', anasema kwamba Abubakr aliwataka Umar, Abu Ubaidah na Mughirah kutoa maoni yao kuhusu tukio hili. Kwa pamoja walimshauri kupata ridhaa ya Abbas kwa kumgawia zawadi. Kisha baada ya Abbas kutoa radhi zake, Ali hataweza kufanya chochote kuwapinga. Watu wanne hawa wakamwendea Abbas usiku, na Abubakr, baada ya kumshukuru Mungu akasema, "Allah ametuma Wahyi wake kupitia kwa Muhammad kutuongoza sisi, na Muhammad alitimiza ujumbe wake mpaka Mungu akamchukua Kwake na akampa malipo yake. Muhammad aliwaachia watu kujichagulia njia yao wenyewe, na watu wamenichagua mimi kama 63
ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO
kiongozi wao. Sina woga. Mafanikio yangu yanakubaliwa na Mungu, ninamwamini Yeye, na nitarejea Kwake. Sasa habari zimekuja kwamba baadhi ya watu wamechukua fursa ya nafasi yako, na wananishutumu mimi mbali na kuungwa mkono na umma. Tumekuja kukuomba uungane nasi kama wengine walivyofanya, au kuutaka upinzani kusimamisha harakati zao. Na kwa malipo yako, sisi tutakuzawadia. Watu wanaijua nafasi yako, na ile ya rafiki yako, lakini wamekuwekeni pembeni. Enyi Bani Hashim tulieni, Mtume wa Mwenyezi Mungu alikuwa wetu kama vile alivyokuwa wenu" Umar akaongezea, "Kuja kwetu kwako hakuna maana kwamba tunakuhitaji.Tunakutaka tu ujiunge na wengine kwa usalama wako, vinginevyo utakutana na matokeo mabaya, hivyo lifikirie jambo hilo." Abbas naye, baada ya kumshukuru Mungu, akasema, " Allah alimchagua Muhammad kama Mtume wake, na msaidizi kwa marafiki zake, masahaba na wafuasi waaminifu. Allah aliwapendelea Waislam kwa kumtuma Mtume Muhammad. Sasa Allah amemchukua Kwake, na kuwaacha Waislam wamudu wenyewe mambo yao, kuchagua kiongozi sahihi kuwazuia wasipotee. Sasa, Abubakr, kama umeikalia nafasi hii kwa sababu ya uhusiano wako kwa Mtume, sisi tuko karibu sana naye kuliko wewe, na kama umechukua kiti hiki kwa idhini ya wafuasi wake, sisi pia ni wafuasi wake ambao kamwe hamkututaka ushauri. Kama umekichukua kama wajibu kwa niaba ya Waislam hatujaitoa kamwe haki hii kwako. Unajipinga mwenyewe kwa kusema watu wamekuchagua, na wakati huo huo kusema kwamba watu hawatoi ridhaa ya kurithi kwako. Kwa upande mmoja, unasema kwamba wewe ndiye mrithi wa Mtume. Kwa upande mwingine, unasema kwamba watu wamekuchagua. Kama hicho unachonipa, kile ambacho ni mali ya waumini, huna haki ya kukitumia; na kama ni chetu kwa haki tunakitaka kamili siyo kwa sehemu sehemu. Sisi ni tawi la mti wa Mtume, wewe ni wale tu wanaopata hifadhi katika majani yake. Hivyo nyamaza kimya." Abubakr na rafiki zake wakamwacha Abbas bila kufanikiwa malengo yao. HIFADHI KATIKA NYUMBA YA FATIMAH Umar anasema, "Baada ya kifo cha Mtume tuligundua kwamba baadhi ya watu wamekusanyika katika nyumba ya Fatimah ili kutupinga sisi." Hawa walikuwa ni Ali, Zubair, Abbas, Ammar Ibn Yasir, Utbah Ibn Abi Lahab, Salman Farsi, Abu Dhar, Miqdad Ibn Aswad, Bara' Ibn Azib, Ubai Ibn Ka'b, Sa'd Ibn Waqqas na Talha Ibn Ubaidullah. Wengine kutoka makundi ya Muhajir na Ansari walitajwa. Kwa vile Waislam walisita kutoa tofauti zao, waliandika tu kwamba baadhi ya watu walijikusanya pamoja kwenye nyumba ya Fatimah kwa upinzani. Kwa bahati mistari michache kuhusu upinzani huo imeandikwa katika kitabu cha historia cha Baladhuri. Baladhuri anasema kwamba Abubakr, baada ya kupingwa na Ali, alimuamuru Umar kumleta Ali mbele yake. Umar alikutana na Ali akajadili swala hilo naye. Ali akamwambia Umar, "Mnakamua ng'ombe wa urithi, nusu kwa ajili ya 64
ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO
Abubakr na nusu nyingine kwa ajili yako mwenyewe. Hivyo anakufanya wewe ndiye mrithi wake." Pia (Baladhuri) anasema kwamba Abubakr katika kitanda chake cha mauti aliitoa kauli hii. "Kuna mambo matatu tu ambayo nayajutia - natamani nisingepekua nyumba ya Fatima, ingawa walikuwa wanajiandaa kutupiga sisi………." Yaquubi anaandika katika juz.2,uk.115 wa kitabu chake kwamba Abubakr alisema, "Natamani nisingepekua nyumba ya Fatimah, na nisingetuma watu kwenda kumnyanyasa; hata kama nyumba yake ilikuwa ikitumika kama hifadhi ambayo ingesababisha vita." Wanahistoria wamewataja wafuatao kama wale waliokwenda kwenye nyumba ya Fatima kuwatawanya watu waliokuwa wamejihifadhi hapo: 1) 2) 3) 4) 5) 6) 7) 8) 9) 10)
Umar Ibn Al- Khatab Khalid Ibn Al-Walid Abdur Rahman Ibn Aufi Thabit Ibn Shammas Zaid Ibn Labid Muhammad Ibn Muslamah Salamah Ibn Salem Ibn Waqash Salamah Ibn Aslam Usaid Ibn Hudhair Zaid Ibn Thabit
Ali, Zubair na baadhi ya Muhajirina waliopinga urithi wa Abubakr, walikusanyika katika nyumba ya Fatimah, na baadhi ya silaha. Habari ilimfikia Abubakr kwamba upinzani umekusanyika kutoa mkono wa kiapo kwa Ali, hivyo akamtuma Umar na watu wengine kwenda kuwatawanya kwa nguvu au vinginevyo. Umar alichukua mienge ya moto unaowaka kwenda kwenye nyumba ya Fatima, na katika kuziona ndimi za moto, Fatima alimuuliza Umar kama alidhamiria kuichoma nyumba yake, Umar akasema, "Ndiyo, kama hamtawafuata Waislam wengine na kutoa kiapo kwa Abubakr." Iliandikwa katika kitabu cha 'al-Imamah wa al-Siyasah' kwamba Umar aliwaamrisha watu watoke nje ya nyumba hiyo, lakini walimpuuza. Umar akaagiza kuni na akawaambia wale walioko ndani ya nyumba, "Kama hamtoki nje, nitaichoma nyumba hii. Naapa kwa Allah Ambaye anayo roho yangu mikononi Mwake." Mtu mmoja akamwambia Umar kwamba Fatimah alikuwemo ndani ya nyumba hiyo naye akasema, "Halina umuhimu kwangu nani yumo ndani ya nyumba hii." Katika kitabu cha al-Ansabul Ashraf, juz.1, uk.586, imeandikwa kwamba Abubakr alimtaka Ali amuunge mkono, lakini Ali alikataa, kisha Umar akaelekea nyumbani kwa Ali na mwenge wa moto unaowaka. Mlangoni akamkuta Fatima ambaye alimwambia, "Unakusudia kuchoma mlango wa nyumba yangu?" Umar akasema, 65
ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO
"Ndiyo, kwa sababu hii inaimarisha imani iliyoletwa kwetu na baba yako." Jauhari katika kitabu chake anasema, "Umar na baadhi ya Waislam walikwenda nyumbani kwa Fatima kuichoma na pia kuwachoma wale waliokuwa katika upinzani." Ibn Shahna anasema, "Kuchoma nyumba na wakazi wake." Imeandikwa ndani ya Kanzul Ummal, juz.3,uk.140, kwamba Umar alimwambia Fatimah, "Najua kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu hakumpenda yeyote kuliko wewe, lakini hili halitanizuia kutekeleza uamuzi wangu, kama watu hawa watakaa ndani ya nyumba yako, nitauchoma mlango huu mbele yako." Wakati Abdullah Ibn Zubair alipokuwa anagombea madaraka, Bani Hashim walimtoroka kwenye njia ya mlimani. Abdullah alitoa amri ziletwe kuni awachome moto. Urwah, ndugu yake Abdullah, alitoa kisingizio cha kitendo cha kikatili cha ndugu yake akisema, "Ndugu yangu aliwatishia, kama walivyokuwa wametishiwa katika tukio lililopita walipokuwa hawatoi kiapo cha utii." Alimaanisha pale Bani Hashim walipokataa mamlaka ya Abubakr. Hafidh Ibrahim (mshairi wa ki-Misri) ametunga shairi lifuatalo kuhusu ngano hii: Umar yule mashuhuri alimwambia Ali mtukufu, Nitaichoma nyumba yako hatimaye, Kama hutautambua urithi wa Abubakr Kwenye kiti cha Mtume na ujumbe wake, Pamoja na Fatima kuwemo ndani, Umar ndiye mmoja pekee Aliyeweza kumwambia hivyo Ali, huyu shujaa wa Adnani. (Abubakr katika kitanda chake cha umauti aliubainisha uvamizi, kwenye nyumba ya Fatimah aliamuru ufanyike.) Yaqubi anasema: "Walikuja katika kundi na wakaishambulia nyumba ya Ali‌‌.. na yeye (Umar) akauvunja upanga wake (Ali) kisha (lile kundi) likaingia ndani ya nyumba." Tabari anasema, "Umar Ibn Khatab alikwenda nyumbani kwa Ali wakati Talha na Zubair na baadhi ya Muhajir walikuwemo ndani. Zubair alitoka nje na akamshambulia Umar, lakini aliteleza na upanga ukamtoka mkononi mwake. Wafuasi wa Umar wakamkamata na pia wakamkamata Ali wakati alipokuwa anasema, 'Mimi ni mtumishi wa Mwenyezi Mungu na ndugu yake Mtume.'" Walimleta kwa Abubakr na kumwambia ashike mkono wa Abubakr. Ali akasema, "Mimi ninastahili zaidi nafasi hii kuliko yeye. Mngepeana mkono wa kiapo na mimi. Hoja yenu na Ansari juu ya uhusiano wenu na Mtume, naweza kutumia hoja hiyo hiyo kwani niko karibu zaidi na Mtume kuliko nyinyi. Ansari walikubali maelezo yenu, nyie lazima pia mkubali yangu, ama sivyo ninyi ni wahalifu." Umar akasema, "Hatukuachii wewe mpaka ukubaliane nasi." Ali akajibu, "Kamueni 66
ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO
ng'ombe huyu na ugawane nusu kwa nusu na Abubakr. Mfanyie kazi yake leo, na kesho atakufanya wewe mrithi wake. Ninaapa kwa Allah kwamba sitakusikiliza wewe Umar, na sitaushika mkono wa Abubakr." Abubakr akamwambia Ali, "Sitakulazimisha kukubaliana na mimi." Abu Ubaidah akamwambia Ali, "Wewe ni kijana sasa hivi, Ewe Abul Hasan, hawa ndiyo watu wazima na wanajua jinsi ya kuuendesha urithi huu; wafuate sasa, na kama utabakia utawarithi, kwa sababu ya fursa zako na kwa sababu uko karibu sana na Mtume; na mtangulizi wa Uislam ambao kwao umepigania vita vitukufu (jihad)." Ali akajibu, "Enyi kundi la Muhajirina, muogopeni Mungu, msimnyang'anye Muhammad na kizazi chake mamlaka yao. Msihamishie kitovu cha Uislam kwenye nyumba yenu, kutoka kwenye sehemu yake halisi ya asili. Wallah, madhali kuna watu wajuzi katika Qur'ani, Sheria za Ki-Islam, na ngano za Mtume, miongoni mwetu familia ya Mtume, tunastahili zaidi kumrithi Mtume kuliko mtu mwingine yeyote. Wallah nyumba yetu inacho kile mnachokitaka. Msifuate matamanio yenu, vinginevyo mtazidi kupotea." Bashir Ibn Sa'd akasema, " Ee Ali, kama Maansari wangekusikia ulichosema hivi punde, hakuna hata mmoja ambaye angebishana na wewe, lakini yote yamekwisha, tumeushika mkono wa Abubakr." Bila ya kushikana mkono na Abubakr, Ali akarudi nyumbani. Ibn Abil Hadid amenakili kutoka kwa Jauhari kwamba pale Fatimah alipoona jinsi gani Ali na Zubair wanavyotendewa vibaya, alikuja mpaka mlangoni na akasema, " Abubakr, ni mapema kiasi gani umeighilibu familia ya Mtume wa Mwenyezi Mungu! Sitaongea tena na Umar kamwe pindi ningali niko hai." Simulizi nyingine anasema kwamba Fatimah huku akiwa analia, alitoka nje na kuwafukuza watu. Yaqubi anasema kwamba Fatimah alitoka nje na kusema, "Tokeni nyumbani kwangu, ama sivyo Wallah, nitafunua kichwa changu, na nitaomboleza kwa Allah na nywele zilizotulia." Hivyo watu walitawanyika kutoka nyumbani kwake hata wale waliokuwa wamejihifadhi pale. Nidhaam pia anasema, "Siku hii Umar alimpiga Fatimah tumboni na kumsababishia mimba yake kutoka, wakati akikemea na kuchoma nyumba (wakati wengine wameondoka na ni Ali na wanawe Hasan na Husein waliokuwa ndani)." Masud anasema kwamba baada ya kiapo siku ya Jumatatu na Jumanne, Ali alikwenda ja kwa Abubakr na kumwambia, "Umeharibu nafasi yetu, kwa vile hukutufikiria sisi." Abubakr akajibu, "Hiyo ni kweli, lakini nilihofia kungetokea uasi na ghasia." Yaqubi pia anasema kwamba baadhi ya watu walikwenda kwa Ali kumpa mkono wa kiapo, lakini Ali akawaambia waje siku inayofuata, na vichwa vilivyonyolewa, lakini ni watatu wao tu waliorudi. 67
ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO
Baada ya matukio hayo ya kiapo, Ali alikuwa akienda na Fatima, wakiwa wamepanda punda, nyumba hadi nyumba kuomba kura. Lakini watu walimwambia Fatima, "Ewe binti ya Mtume wa Mwenyezi Mungu, binamu yako angetutaka kumuunga mkono kwetu, tusingemchagua mtu mwingine yeyote ila yeye, lakini tayari tumekwisha kupeana mkono na Abubakr." Jibu la Ali lilikuwa ni hili, "Aibu hii, mlinitegemea mimi kuuacha mwili wa Mtume, na kujihusisha katika kugombea mamlaka?" Fatima alikuwa akisema kwamba Ali amefanya kile ambacho angepaswa kufanya, nao wamefanya mambo ambayo Allah angewauliza juu yake. Mu'awiyah katika barua yake kwa Ali, aliitaja simulizi hiyo hapo juu akisema, "Inaelekea kama ni jana tu pale ulipompakia mkeo kwenye yule punda, ambaye ungemuweka ndani ya nyumba yako, akiwa ameshika mikono ya wanao, Hasan na Husein,ukigonga milango ya nyumba za wale watu waliokuwepo kwenye Vita vya Badri, na kuwaambia wasimuunge mkono Abubakr, yule rafiki yake Mtume, ila wakuunge wewe mkono. Hata hivyo, ni watu wanne au watano tu waliokubali. Naapa kwa nafsi yangu mwenyewe, kwamba kama ungekuwa kwenye haki wangekuunga mkono wewe. Ulidai kile ambacho siyo chako. Ulisema mambo ambayo hayajasikika kabla. Naweza kuwa na kumbukumbu mbaya, lakini kamwe sitasahau maneno uliyomwambia Abu Sufyan, 'Ningekuwa na watu arobaini ningekwenda kuchukua haki yangu kutoka kwa watu hawa kwa nguvu.'" Katika vita vya Siffin, Amr Ibn Aas alimkumbusha Mu'awiyah kwamba Ali alisema, "Kama ningekuwa na watu arobaini ‌.." n.k. Amr Ibn Aas alikuwa na maana kwamba Ali aliyasema haya ile siku walipoivamia nyumba ya Fatimah. MWISHO WA MATUKIO PALE KWENYE KIAPO Usudu'l-Ghabah , juz.3,uk.222 kimeandika: "Wapinzani waliafikiana kumkubali Abubakr miezi sita baada ya onyesho la hadhara la kiapo kwake." Yaqubi juz.2,uk.105, "Ali alipeana mkono na Abubakr miezi sita baada ya onyesho la hadhara la kiapo." Istiab juz.2uk.244 na al-Tanbih al-Ashraf, uk.250, "Ali hakupeana mkono na Abubakr mpaka baada ya Fatima kufariki." Katika al-Imamah wa Siyasah imeandikwa kwamba Ali alitoa kiapo chake kwa Abubakr baada ya Fatima kufariki, ambapo ilikuwa siku 75 baada ya kifo cha Mtume. Kwa mujibu wa Zubair, Fatimah, baada ya mabishano aliyofanya na Abubakr kuhusu urithi wa Mtume, hakuongea tena naye kamwe. Dhuhari pia anasema kwamba Ali hakumpa mkono Abubakr mpaka miezi sita baada ya kiapo cha hadhara na Banu Hashim wakamfuatia. Katika Taysiir al-Wusuul, juz.2,uk.46, Dhuhari anasema, "Wallah, Ali 68
ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO
hakukubaliana na Abubakr mpaka ilipopita miezi sita na Bani Hashim wakamfuata. Wakati Ali alipoona kwamba watu wanamtelekeza, akajifungamanisha na Abubakr." Baladhuri katika Ansabul Ashraf, juz.1,uk.587, anasema, "Wakati Waarabu walipoukataa Uislam na wakabadilika kwenye uasi, Uthman alikwenda kwa Ali na kumshawishi amuunge mkono Abubakr, ili kuwapa moyo Waislam kuwapiga vita waasi chini ya Abubakr. Ali akapeana mkono wa kiapo na Abubakr, na mchafuko kati ya Waislam ukatulizwa. Kisha vikosi vya Waislam vikatayarishwa ili kuwapiga waasi." Baada ya kifo cha Fatimah, na kupoteza shauku kwa watu, Waislam wakagawanyika, cheo cha Abubakr kilikuwa imara, hivyo Ali akapatanishwa naye. Hata hivyo, Ali kamwe hakuyasahau matukio haya, hata pale aliposhika nafasi ya mrithi wa Mtume. Katika hotuba yake iitwayo Shaq-shaqiah, anasema, "Ilinibidi niwe mwenye subira kwa ajili ya maarifa ya kawaida, nilingojea kwa uvumilivu ingawa ilikuwa ni ngumu kama kuwa na mwiba kwenye macho yangu, na mfupa uliokwama kooni mwangu. Niliiona haki yangu ya urithi kwa Mtume ikichukuliwa kinyume toka kwangu, wakati siku za yule wa kwanza (Abubakr) zilipokwisha, na nuru ya maisha yake kuzimishwa; aliipitisha tunzo ya urithi wa Mtume mikononi mwa Ibn Khatab. Oh tofauti iliyoje kati ya kupanda ngamia, (kukabiliana na matatizo peke yako) na kukaa kwenye kiti kwa Hayan, akiishi maisha ya raha bila ya kujali katika kasri ya ndugu yake Jabir. Inashangaza kwamba Abubakr alikuwa akiwaomba watu wafute kiapo chao kwake kama mrithi wa Mtume, lakini kabla ya kifo chake, Abubakr kwa imara alimuweka Umar kuwa mrithi. Waporaji wawili wale waliugawa urithi kati yao wenyewe, kama kugawana matiti mawili ya ngamia yaliyojaa maziwa.
69
ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO
MAONI YALIYOTOLEWA NA WATU MBALIMBALI KUHUSU HICHO KIAPO CHA UTII A. FADHIL IBN ABBAS Kwa mujibu wa Yaqubi, pale ukoo wa Bani Hashim walipozipata habari kuhusu kuchaguliwa kwa Abubakr kama mrithi wa Mtume, Fadhil Ibn Abbas aliliambia kabila la Quraish, "Kamwe hamtamrithi Mtume kwa udanganyifu, tunastahili sisi nafasi hiyo siyo ninyi, sisi ndiyo tulio na haki, hususan rafiki yetu Ali." Ndipo Utba Ibn Abi Lahab akasoma shairi lifuatalo: Mimi sikudhani kamwe watu watawaangusha Bani Hashim Wala kwamba watamwacha Abul Hassan peke yake, Alikuwa mtu wa kwanza kumfuata Muhammad, Na wa mwisho kuuacha mwili wake - kwa huzuni sana. Kumsaidia na kumliwaza Ali, Malaika walishuka, Kutoka mbinguni kuja kwenye kitanda cha umauti cha Mtume. Utba kisha akapokea ujumbe kutoka kwa Ali ukimtaka aache hayo, kwa sababu yalikuwa ni matakwa ya Ali kwamba Waislam wote wawe kwenye ushawishi mmoja. B. ABDULLAH IBN ABBAS Amesimulia mazungumzo haya na Umar: Umar: "Hivi unajua, Ibn Abbas, kwa nini watu hawakuuunga mkono ukoo wenu, ndugu wa Muhammad, kuwafanya warithi wake?" Abdullah: "Kama sijui, basi Kiongozi wa Waumini atanifahamisha." Umar: "Bani Hashim walitaka Mtume, na warithi wake wote wawe wanatoka kwenye ukoo wao, lakini sisi, Maquraish, kwa mafanikio kabisa tumechagua mrithi wake." Abdullah: "Naweza kuruhusiwa kusema kitu?" Umar: "Kama ikibidi, ewe Ibn Abbas." Abdullah: "Ingekuwa bora kwa Maquraish, kama wangeridhika na kile ambacho walichokipewa na Allah; basi kusingekuwa na wivu. Umesema kwamba hii haikuwa hivyo, kwamba Maquraish hawakutaka kile ambacho Mungu amewafadhilishia juu yao. Watu kama hawa wanazungumziwa ndani ya Qur'ani, 'Kwa sababu hawakuupenda wahyi wa Allah, amri zake, kazi zao hazikuwa chochote.'" 70
ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO
Umar:
"Sikutaka niamini kile nilichosikia kuhusu wewe, kwa sababu kingenifanya nipoteze heshima yangu juu yako milele."
Abdullah: "Kama kila kitu nilichokisema ni cha kweli, sitaogopa kuvunjiwa heshi ma, na kama nilichosema ni uongo, basi mtu kama mimi lazima ajisahihishe mwenyewe." Umar:
"Nimesikia kwamba umesema kwamba tumetwaa madaraka kwa kuwad hulumu watu ambao tunawaonea wivu?"
Abdullah: "Kila mtu anajua jinsi mlivyotumia dhulma, na vilevile juu ya wivu wenu, Shetani alimwonea wivu Adam na sisi ni watoto wa Adam ambaye alikuwa mkandamizwaji na wivu." C.
SALMAN FARSI
Jauhari amesimulia kwamba Salman, Zubair na Ansari walitaka kutoa mkono wa kiapo kwa Ali, na pale Abubakr alipokuwa Khalifa, Salman akasema, "Mumeipata dhahabu ndogo lakini mumeikosa dhahabu mama. Mumemchagua huyo mzee na mkasahau nyumba ya Mtume. Mngewaachia wamrithi Mtume, mungenufaika zaidi, na kusingekuwa na kutoelewana kati ya Waislam." D.
UMMA MISTAH
"Kutofautiana kati ya Ali na Abubakr kuliwakera Waislam." Umma Mistah binti ya Uthathah, alikwenda kwenye kaburi la Mtume na akasoma shairi lifuatalo: Tofauti kati ya Waislam zilianza, Mpendwa Mtume, mara tu baada ya ulipoondoka, Bila ya wewe, tulipoteza mwelekeo wetu tena, Kama maua na nyasi bila ya mvua. E.
ABU DHAR
Hakuwepo Madina wakati Mtukufu Mtume alipofariki, lakini aliposikia Abubakr amemrithi Mtume alisema, "Umepokea zawadi ndogo kwa ajili ya juhudi zako. Ungeunga mkono madai ya jamaa za Mtume kushika nafasi hiyo, ungelinufaika sana, na kusingekuwa na kutofautiana kati ya Waislam." F.
MIQDAD
Yaqubi amesimulia katika kitabu chake kutoka kwa msimuliaji ambaye amemuona mtu katika Msikiti wa Madina akiwa katika huzuni kubwa kana kwamba amenyang'anywa utajiri wake mkubwa. Mtu huyo alikuwa akisema, "Ni ajabu sana kwamba nafasi hiyo imeondolewa kwenye mikono ya watu wenye kustahiki." 71
ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO
G.
BIBI MMOJA KUTOKA BANI NAJJAR
Baada ya Abubakr kuchukua kiti cha Ukhalifa, alituma pesa kwa kila mwanamke wa Muhajirina na Ansari, Zaid Ibn Thabit alibeba fungu la bibi mmoja kutoka Bani Najjar kumpelekea, lakini alikataa kuzipokea akisema, "Abubakr anataka kuinunua dini yetu kwa kutoa rushwa." H.
ABU SUFIAN
Alikuwa ni Sakhr mwana wa Harb, mwana wa Umayya, mwana wa Abd Shams, mwana wa Abd Manafi. Alipigana na Mtume hadi ule wakati Mtume alipoiteka Makka na kupewa msamaha. Wakati wa kifo cha Mtume, hakuwapo Madina. Akiwa njiani kurudi hapo, Abu Sufian alipata habari juu ya kifo cha Mtume na za Abubakr kuwa mrithi. Aliuliza, "Walilichukulia vipi hili Abbas na Ali, wawili hawa waliodhulumiwa?" Alijulishwa kwamba walikuwa kimya majumbani kwao. Abu Sufian akaapa akisema, "Kama nitabakia nitawasaidia wao kujaza nafasi yao ya halali. Ninaona wingu la vumbi hewani linalohitaji damu kulisafisha." Alipoingia Madina alianza kusoma shairi hili lifuatalo: Oh Bani Hashim, msimpe mtu yeyote fursa Ya kuwa na wivu, hasa hawa Taim na Adi.5 Mamlaka ya ki-Islam yalianzishwa nanyi, Mwacheni Abul Hasan (Ali) aongoze, kama mnataka kuendelea. Kwa mujibu wa Tabari, Abu Sufian alisema, "Kuna vumbi katika hewa, Wallah, ni mvua ya damu tu inayoweza kulisafisha. Enyi wana wa Abd Manafi, kwa nini Abubakr aliruhusiwa kuwa ndiye mrithi wa Mtume? Wako wapi Ali na Abbas ambao walidhulumiwa?" Kisha alitaka kupeana mkono wa kiapo na Ali, lakini Ali alikataa. Abu Sufian ndipo tena akasoma shairi lifuatalo: Punda na siyo mtu muungwana, anaonyesha unyenyekevu, Kuna alama mbili tu za udhalili, Mambo ya hema chini ya nyundo nzito, na Ngamia wa mhamahamaji na mzigo wake. WITO WA ABU SUFIAN: "ENYI WANA WA ABD MANAFI." Hili lingeweza kubadili mwelekeo wa historia ya ki-Islam kama Ali angekuwa fidhuli, na angeshawishiwa na Abu Sufian kuasi dhidi ya Khalifa. Inashangaza kuona kwamba Abu Sufian, yule adui halisi wa Uislam, aliyepigana na Mtume mpaka alipoona ni vigumu kwake kuendelea kupigana, amejitolea msaada wake kwa Ali. Je, alikuwa na maana ya kusaidia kweli? Au kuchochea ugomvi? 5 Makabila ya Abubakr na Umar.
72
ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO
Cha kushangaza zaidi ni kukataa kwa Ali kukubali msaada toka kwa Abu Sufian na Abbas, wakuu wa makabila mawili yenye nguvu, wakati alikuwa akitafuta msaada kutoka sehemu yoyote inayowezekana. Baada ya kuyachunguza madhumuni ya Abu Sufian na Ali, hatukubakia na mashaka yoyote juu ya asili ya mipango yao. Mababu wa Mtume na Abu Sufian walikuwa mabinamu waliokuwa na migogoro ya ki-ukoo. Mapigano kati ya koo mbili hizi yaliishia na ukoo wa Mtume kushinda nafasi ya kuwa kama mkuu wa Kabila. Abu Sufian alikuwa ni mpinzani wa Mtume kwa nafasi ya utemi (uchifu), na msimamo wake juu ya Mtume kama kiongozi wa kidini ulikuwa ni ule wa kutojali. Kwa sababu hii, pale Mtume alipoiteka Makka, Abu Sufian alimwambia Abbas, "Mpwa wako ameanzisha ufalme mkubwa sana." Abbas akasema, "Huu ni utume siyo ufalme." Abu Sufian akaikubali kauli hii bila hoja. Ingawa Abu Sufian alishindwa na ndugu zake, hakutaka wageni kuwa na mamlaka, na kuliacha kabila lake mikono mitupu. Mtume alijaribu kuzuia mahusiano ya kiukoo kuingilia njia ya haki lakini hakufanikiwa sana. Tunaona, pale tunapoyaangalia matukio yaliyotokea kati ya koo wakati wa uhai wa Mtume, kwamba lile tukio la jinsi Abbas, ami yake Mtume, alivyomtetea Abu Sufian, ni mfano mzuri wa nguvu za fungamano la ukoo. Ibn Hisham aliandika kwamba ule usiku kabla ya kutekwa Makkah, kambi za Waislam ziliuzunguka mji huo. Abbas, ami yake Mtume, alipanda juu ya farasi wa Mtume, alikuwa akizurura akitaraji kuona baadhi ya maadui. Alitaka kuwajulisha juu ya shambulio linalokuja la Waislam, kumpa adui yoyote fursa ya kuomba msamaha. Alimkuta Abu Sufian aliyekuwa akiwapeleleza Waislam, Abbas akamwambia, "Shukuru Mungu nimekuona Abu Sufian, panda farasi, na nitakupeleka kwa Mtume, ili uweze kuomba hifadhi, au vinginevyo kesho kama utatekwa, unaweza ukakatwa kichwa." Abbas akapanda farasi huyo na Abu Sufian nyuma yake. Walipita makundi mengi ya Waislam ambao walikuwa wamewasha mioto mingi kuwatisha maadui, na ili kuangalia hatari yoyote inayowezekana kutokea. Waislam wale wakasema, "Tazama, ami yake Mtume juu ya farasi wake." Umar, kwa bahati, akamuona Abu Sufian na akakemea, "Yule adui wa Mwenyezi Mungu. Shukuru Mungu uko mikononi mwetu na huna ahadi ya mtu yoyote ya kukulinda wewe." Kisha Umar akakimbia kwa Mtume kuomba ruksa ya kumuua Abu Sufian. Lakini Abbas, juu ya farasi yule, alimpita Umar na kumkuta Mtume kwanza. Umar ndipo akafika na kusema, "Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, tunaye Abu Sufian pamoja nasi, akiwa hana dhamana yoyote ya usalama. Nipe ruksa nimkate kichwa." Lakini Abbas akasema, "Tulia ewe Umar, kama Abu Sufian angetoka kwenye kabila lako la Adi, usingesisitiza juu ya kumuua yeye. Lakini kwa vile anatoka Abd Manafi unasema maneno ya kikatili." Ngano hii inathibitisha kwamba mafungamano ya ukoo yalikuwa na nguvu wakati ule. Inaonyesha pia kwamba matilaba ya Abbas ilichomoza kutoka kwenye mapenzi ya kabila lake. Sababu ya dhihirisho la Abu Sufian dhidi ya Abubakr ilikuwa pia ni matokeo ya umuhimu wa ukabila. 73
ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO
Yale mamlaka ya juu kabisa ya ukoo wa Abd Manafi, ambao hawa Bani Hashim (familia ya Muhammad) na hawa Bani Umayya (familia ya Abu Sufiani) wametokana nao, ulikuwa unajulikana kwa kila mtu. Hivyo pale baba yake Abubakr alipoarifiwa kwamba mwanae amekuwa Khalifa, akasema, "Bani Hashim na Bani Umayyah wamekubaliana?" Alipojibiwa kwa kukubaliwa, akasema, "Kile Mungu anachokitaka, hakuna anayeweza kukizuia." Upole wa Abu Sufian kwa familia ya Muhammad, baada ya kifo chake, ulitokana na hisia za umoja wa kikabila. Kwani Abu Sufian alipigana na Mtume kila wakati alipopata fursa. Kusema kwake, "Kama nitabakia hai nitamsaidia Ali na Abbas kuikamata tena nafasi yao," hakukuwa na sababu ila upendo wa ki-kabila; kama ilivyo desturi ya Waarabu kusaidia ndugu wa karibu dhidi ya wageni wa mbali. Abu Sufiani, Abbas na Ali wana asili moja ya kikabila, Kabila la Qussai ambalo lilikuwa kubwa na maarufu sana. Hii ndiyo sababu Abu Sufiani alisema, "Yeyote aliye na Qussai kama mfuasi wake, kwa vyovyote atashinda." Abubakr na Umar walitoka kwenye makabila madogo ambayo hayakuweza kamwe kushindana na Qussai. (Qussai, asili ya kabila la Quraish lilikuwa ndiyo mzizi mkuu wa kabila la Abd Manafi, kabila la Bani Hashim na Abu Sufiani.) Ilikuwa ni desturi katika siku zile kwa kabila kupendelewa maslahi ya mmoja wa watu wake lenyewe. Ali, kwa kuungwa mkono na Abu Sufiani na Abbas, angeweza bila wasiwasi kumshinda Abubakr. Lakini Ali, yule shujaa, mwana wa Abi Talib, alikataa msaada wa kabila lake maarufu, kwa sababu desturi hii ilikuwa kinyume na mafundisho ya Ki-Islam. Kwa hiyo alishindwa na Abubakr. Kwa kweli, baada ya kifo cha Mtume, matukio yote yalishawishiwa na chuki ya makabila mengine kwa kabila lake au familia yake. Ansari walipendekeza kwamba Sa'd angekuwa ndiye mrithi wa Mtume kwa sababu tu ya upinzani kwa Muhajirina. Walijua kwamba baadhi ya Muhajiriina ni waumini wakubwa katika Uislam na kwa hiyo ni wenye kustahiki zaidi kutambuliwa. Lile kabila la Aus lilimuunga mkono Abu Bakr ili kumpinga Sa'd, mgombea wa kabila la Khazraj. Ile hotuba ya Umar pale Saqifah ilikuwa ni ushahidi wa kweli wa upendeleo wa ki-kabila. Uungaji mkono wa Abu Sufiani kwa Ali pia ulitokana na chuki ya ki-kabila. Ni Ali tu, ambaye alilelewa mapajani mwa Mtume tangu utoto wake, aliyetaka kushikilia Uislam, hivyo alitaka uungaji mkono wa wale Waislam ambao hawasukumwi na chuki za kikabila, na ambao hawakuwa na muungo wa kifamilia, watu kama Abu Dhar, Miqdad na Salman, ambao dhamira yao tu ni kuamini kwao imani ya Uislam. Hitimisho la simulizi hizo hapo juu, kuhusiana na Abu Sufiani kumuunga mkono Ali, lilikuwa kwamba, ingawa dhamiri ya Abu Sufiani haikuwa ya kidini, bali kwa sababu aliamini sana mamlaka ya kabila lake ambalo Ali ni mmojawapo - kwa sababu hii yeye peke yake alimuunga mkono Ali dhidi ya Abubakr. Abu Sufiani alikuwa mkweli kwa Ali katika upinzani kwa Abubakr kwa sababu ya chuki za kiukoo, lakini kama inavyotokea mara kwa mara mambo yasiyo sahihi yamesimuliwa, na Abu Sufiani na wote wale waliompinga Abubakr, walishutumiwa kwa 74
ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO
uasi na waliitwa wakorofi. Matukio yaliyopita kuhusu Abu Sufiani yanaifanya ngano ifuatayo kuwa rahisi kuiamini. Imesimuliwa kwamba Abu Sufiani alimuuliza Ali, "Kwa nini ulimkubalia Abubakr kumrithi Mtume? Kama ukitaka, nitaijaza mitaa yote ya Madina na askari wa farasi na wa miguu." Ngano inaendelea kama Ali anavyojibu, "Abu Sufiani, umekuwa kwa muda mrefu wa kutosha adui wa Uislam. Huwezi kusababisha madhara yoyote zaidi sasa. Lazima nikubali kwamba Abubakr anastahiki nafasi hiyo." Ngano hii haielekei kuwa sahihi kwa sababu msimuliaji hakuishi wakati wa tukio lenyewe. Pia baadhi ya ngano hizi za uongo zimesimuliwa na Awanah, aliyejulikana kuwa si wa kuaminika. Maelezo haya hayaendi sawa kwa sababu kama Ali angesema, "Nakubali Abubakr anastahiki nafasi hiyo," basi Abu Sufiani angemuuliza, "Kwa nini hupeani mkono wa kiapo naye?" Ambacho Ali kwa kweli alichokisema kilikuwa ni, "Kama ningekuwa na waumini arobaini wenye moyo wa sawasawa, ningepigana naye." Ali katika barua yake kwa Mu'awiyah anaandika, "Baba yako (Abu Sufiani) aliielewa haki yangu zaidi kuliko ufanyavyo wewe. Ungenijua mimi kama baba yako alivyonijua, ungekuwa na busara zaidi." Hiyo serikali ilikuwa inamuogopa Abu Sufiani, Umar alimwambia Abubakr, "Mpatie pesa kidogo ili kumnyamazisha." Abu Sufiani, akiwa hakuridhishwa na Ali, aliikubali posho hiyo. Tabari anasimulia kwamba Abu Sufiani hakuacha kutingisha mpaka mjukuu wake Yazid akateuliwa kama Kamanda wa Jeshi lililopelekwa Syria. I.
MU'AWIYAH
Mu'awiyah alimwandikia Muhammad, mtoto wa Abubakr, "Baba yako alijua, nasi tunajua kwamba Ali alistahiki kuwa mrithi wa Mtume. Tulimheshimu Ali sana sana. Pale Mtume wa Mwenyezi Mungu, rehma na amani juu yake, alipokamilisha ujumbe wake na roho yake ikaenda kwa Mungu, baba yako (Abubakr) na mkono wake wa kulia Umar, ndiyo watu wawili walioingilia haki ya Ali. Walipanga pamoja na wakamtaka Ali ashirikiane nao. Ali akakataa, nao wakala njama dhidi yake mpaka Ali akakubali. Hawakumruhusu kamwe Ali kushiriki katika siri yao mpaka Mungu alipozichukua roho zao. Sasa tuko kwenye njia ambayo baba yako aliitengeneza. Kama alikuwa kwenye njia ya sawa, tutamfuata yeye. Kama alikuwa kwenye njia potofu, mlaumu baba yako - siyo sisi kwa kumpinga na kutouachia Ukhalifa kwake. Amani iwe juu ya wale wanaotubu." J.
KHALID IBN SAID
Khalid, mwana wa Saeed, mwana wa Aas, alikuwa mmoja wa watu wa kwanza kuuingia Uislam. Ibn Qutaibah ndani ya Maarif, uk.128, anaandika, "Khalid alikuwa Mwislamu kabla ya Abubakr." Khalid alihama kwenda Ethiopia na pale Uislam ulipokua na kuwa na nguvu alirudi kutoka huko. Yeye na ndugu zake wawili, Amr 75
ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO
na Aban, wakawa, kwa amri ya Mtume, Wakusanya Kodi ambao walikusanya toka kabila la Madhaj. Kisha wakahamishiwa Sana'a huko Yemen. Wakati Mtume alipofariki, walirudi Madina, Abubakr akawauliza ni kwa nini wameviacha vituo vyao, nao wakajibu, "Tulichaguliwa na Mtume kwenye nafasi hii, na hatutamfanyia kazi mtu mwingine yeyote sasa kwa vile amekufa." Walitoa visingizio vingine, na hawakumpa Abubakr mkono wa kiapo, mpaka miezi miwili ikapita. Khalid aliwaambia Bani Hashim, "Ninyi ndiyo mti mtukufu, wenye matunda na nitawafuateni nyie." Alikwenda kwa Ali na Uthman siku moja na kuwaambia, "Nyie, kizazi cha Abd Manafi, hamkuichukulia nafasi yenu kwa makini mpaka wengine wamekupiteni." Alimchunuku Ali, na akamuomba ampe mkono wake, lakini ilikuwa imechelewa kwani Abubakr tayari alikwisha kuwa Khalifa. Hivyo Khalid alimkubali kama walivyofanya Bani Hashim.Abubakr hakujali tabia ya Khalid ya vurugu za upole, lakini Umar aliichukulia nongwa ya dhati. Baadae Abubakr alimteua Khalid kuwa mkuu wa kikosi cha jeshi lililopelekwa mpakani na Syria. Umar akabishana na Abubakr na kusisitiza kwamba amuondoe Khalid kwenye nafasi hiyo. Abubakr ndipo akamuondoa Khalid na kumteua Yazid mtoto wa Abu Sufiani kushika mahali pake. Khalid hakujali kama alikuwa askari ama kamanda, na alipigana kama askari katika mpaka wa Syria mpaka alipouawa shahidi katika mwaka wa 13 wa Hijiria, mausiku mawili kabla ya mwisho wa mwezi wa Mfungo nane. K.
SA'D IBN UBAIDAH
Sa'd Ibn Ubaidah alikuwa ndiyo mkuu wa kabila la Khazraj. Alikuwepo huko Aqabah (kama mmoja wa wakilishi waliokuja kutoka Madina kuelezea kuridhia kwao kumsaidia Mtume kama angetaka kuhama toka Makkah kwenda Madina). Sa'd alishiriki katika vita vyote Mtume alivyopigana,isipokuwa labda vile Vita vya Badr. Katika siku ya kutekwa Makka, alionyesha mwelekeo wa kivita akisema, "Hii ni siku ya kupigana, siku ambapo wanawake watachukuliwa mateka." Hivyo Mtume akaitoa bendera kwa mwanae Sa'd, aitwae Qais, na kupunguza hadhi ya Sa'd kuwa haji wa kawaida. Sa'd, akiwa ameshindwa katika juhudi zake za kumrithi Mtume, aliachwa kabisa wakati wa kutoa kiapo, lakini siku chache baada ya Abubakr kuwa Khalifa, Sa'd alitakiwa kumpa mkono, kama sehemu ya kabila lake ilivyofanya, lakini Sa'd alikataa na kusema, "Wallah, mradi ninayo mishale kwenye zaka langu ya kuweza kuwapigeni nyie, mkuki wa kuchovya kwenye damu yenu, na upanga, na nguvu katika mkono wangu, nitapigana nanyi kwa msaada wa wale wa kabila langu ambao bado wananitii. Sitapeana mkono wa kiapo na wewe, hata kama watu na majini watatangaza vita dhidi yangu katika kukusaidia wewe, mpaka ninakufa na kuipeleka kesi yangu kwenye mahakama ya mbinguni." Umar alimsisitiza Abubakr amlazimishe Sa'd kukubali, lakini Bashir Ibn Sa'd akasema alijua kwamba Sa'd ni mkaidi na hatakubali. Pia, alikuwa na sauti bado miongoni mwa watu wake na hangeweza kuuawa mpaka watu wengi wa kabila lake, na ndugu zake pia wawe wameuawa. Sa'd kwa hiyo hakuguswa kwa ushauri wa Bashir.
(Bashir, mtu wa kwanza kumpa mkono Abubakr alikuwa ni adui wa Sa'd.) Sa'd 76
ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO
hakuhudhuria kamwe ibada za jamaa zilizoendeshwa na watu wa utawala, na alihiji tofauti na makundi yaliyoongozwa na serikali. Kwa mtindo huu alizipitisha siku zake mpaka Abubakr alipofariki. Pale Umar alipomrithi Abubakr, alikutana na Sa'd na wakapeana kauli za maudhi. Sa'd akasema, "Abubakr alikuwa mhisani zaidi kuliko wewe, sipendi kuwa pamoja nawe." Umar akasema, "Kama mtu hapendi kuwa karibu na mtu mwingine, atakaa mbali." Ndipo Sa'd akaondoka Madina kwenda Damascus. Umar alituma mtu kwenda kuchukua mkataba na Sa'd au kumuua kama hatakubali. Mjumbe huyo alikutana na Sa'd kwenye shamba la miti ya matunda na akamtaka akubaliane na Umar. Sa'd akakataa na yule mtu akamtisha bila mafanikio. Kisha akamuua. Masudi amesimulia kwamba Sa'd hakutoa mkono wa kiapo, na alihamia Syria ambako aliuawa. Ibn Abd Rabbih amesimulia kwamba Sa'd aliuawa na mshambuliaji asiyejulikana, na kwamba majini walimuombolezea kama inavyoelezwa katika ubeti ufuatao: Tulimuua Sa'd, mkuu wa kabila la Khazraj, leo, Mapigo yetu mawili moyoni kwake hayakwenda kombo." Ndani ya Tabari, imeandikwa kwamba Sa'd alikuwa anakwenda haja pale mtu alipomshambulia na kumuua. Wakati mwili wake ulipogunduliwa baadae, ngozi yake ilikuwa imegeuka rangi ya kijani. Katika Usudu'l-ghabah, imeandikwa kwamba Sa'd hakumkubali Abubakr, wala Umar. Alihamia Syria ambako aliuawa. Kisha sauti ikaja toka shimoni na kuwajulisha watu juu ya mauwaji ya Sa'd. Mwili wake ulionekana karibu na nyumba yake huko Huuran ndani ya Damascus, na ulikuwa umegeuka rangi ya kijani. Abdulfattah ndani ya kitabu chake, al-Imam Ali Ibn Abi Talib, amesimulia kwamba watu wa kawaida wanasema kwamba Sa'd aliuawa na majini, lakini kwa kweli Khalid Ibn Walid na mmoja wa marafiki zake walimuua Sa'd, na kumtupa kwenye shimo. Ile sauti iliyosema kwamba Sa'd ameuawa ni ile ya rafiki yake Khalid, siyo ya majini. Baladhuri amesimulia kwamba Umar alimuamuru Khalid na Muhammad Ibn Muslima kumuua Sa'd na wakafanya hivyo. Mtu mmoja wa Kundi la Ansari alitunga ubeti ufuatao kuhusu kifo cha Sa'd: Sa'd aliuawa na majini wanasema, Ustadi ulioje; huo sio wa kawaida kabisa, njia……… Sa'd hakutenda dhambi ile iliyo ndogo kabisa katika nchi, Lakini vilevile hakuushika mkono wa Abubakr. Wanahistoria hawakupenda kuandika sababu ya kifo cha Sa'd. Baadhi yao wamelipuuza kabisa tukio hili, na wengine wamewashutumu majini. Kama wale 77
ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO
waliosema majini wamemuua Sa'd wangesema, "Majini waaminifu hawakupenda Sa'd ampinge Abubakr, hivyo wakamuua." Basi ngano hii ingewezekana kuaminika kirahisi. L.
UMAR
Tumetaja mishughuliko yake kwa upande wa Abubakr wakati wa kiapo. Umar alisema, "Wengine wanabashiri kifo changu, na wanamkisia mrithi wangu. Ngoja niwafafanulieni hili; kile kiapo na Abubakr lilikuwa ni kosa, lakini Mungu alituokoa na matokeo yake." TATHMINI YA SIMULIZI YA SEIF Tumeandika hapo kabla matukio ya kiapo cha utii kwa Seif na wengineo. Sasa tunafanya ulinganisho kati ya simulizi zao. Seif amesimulia kwamba: a)
Hakuna aliyekataa kula kiapo na Abubakr isipokuwa waasi au waliokaribia uasi; na kwamba kundi lote la Muhajiriin lilipeana mkono na Abubakr kwa hiari.
b)
Ali alitoka mbio nje ya nyumba yake katika nguo ya usiku kuokoa muda, baada ya kuwa amesikia kwamba watu wamepeana mkono wa kiapo na Abubakr, na kwamba alipeana mkono naye pia. Walimletea nguo zake baadae, na akazivaa.
c)
Qa'qa alisema, "Nilikuweko Msikitini kwa ajili ya sala ya mchana, wakati mtu mmoja alipoleta habari za kifo cha Mtume; na za kukusanyika kwa Kundi la Ansari pale Saqifah, kumfanya Sa'd kuwa mrithi wake kinyume na amri ya Mtume. Habari hii iliwafanya kundi la Muhajir kuwa na wasiwasi mkubwa."
d)
Hubab Ibn Mundhar alikuwa karibu amshambulie Abubakr kwa upanga wake, lakini Umar aliupiga upanga huo kutoka mkononi mwake. Kisha Maansari wakasongamana kumpa mkono Abubakr, wakiruka juu ya kichwa cha Sa'd, ambaye alikuwa mgonjwa na amekaa njiani mwao. Kosa hili la Maansari lilikuwa sawa na lile kosa lililotokea wakati wa ujahilia, lakini Abubakr alizuia matokeo yaleyale kwa nguvu zote.
e)
Sa'd alimwambia Abubakr, "Wewe na kabila langu, mmenilazimisha nikubaliane nawe." Walikuwa wamemwambia, "Tungekulazimisha kuuacha umma ungeweza kuwa na sababu. Lakini tumekufanya ujiunge na kila mtu mwingineo. Kama utakwenda kinyume na jamii, au kusababisha ufa, tutakukata kichwa chako."
f)
Hotuba mbili ndefu zilitolewa na Abubakr.
g) Khalid Said Amawi alivaa koti la hariri wakati wa amani, na Umar akamwamuru kulichana. Kwa sababu hii Khalid akamwambia Ali, "Ewe mjukuu wa Abd 78
ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO
Manafi, umelipoteza suala lako?" Ali akamwambia Khalid, "Unalichukulia hili kama mchezo?" Ndipo Umar akamwambia Khalid, "Mwenyezi Mungu akukwamishe mdomo wazi. Umesema kitu ambacho kitakamatwa na waongo (kutengeneza ngano za uzushi)." Tunapolinganisha namna Seif alivyosimulia matukio haya, na vile ambavyo wengine walivyosimulia, tunaona kwamba Seif ametengeneza kwa uhodari sana matukio ya kukidhi malengo yake, kwa mfano: A)
Anasema kwamba Ali na Sa'd walipeana mkono wa kiapo na Abubakr siku ile ile ya kwanza aliyomrithi Mtume. Bado wanahistoria wengine wametueleza juu ya kuakhirishwa kwa makubaliano ya Ali na Sa'd kwa Abubakr. Licha ya yale Seif anayosema, "Ali, kwa uwazi kabisa, aliidai nafasi hiyo, na Muhajirina na Bani Hashim, kwa makubaliano na Ali, walikataa kiapo na Abubakr. Watu wote hawa walitaka kupeana mkono wa kiapo na Ali, na alimradi kwa muda huo binti yake Mtume alikuwa hai, hawakumkubali Abubakr." Kama yale Seif anayosema ni kweli, na Ali alikwenda kwa Abubakr siku ile ya kwanza hasa, basi ni nani alikuwa anashughulika na maandalizi ya mazishi ya Mtume?
B) Sa'd hakukubaliana na Abubakr. Aliishi Damascus na majini wakamuua kwa mapigo mawili, kwa sababu hakuushika mkono wa Abubakr. C) Kwa kusema kwamba Maansari walitaka kuvunja mkataba wa Mtume, na kufanya kiapo na Sa'd, Seif anataka kusema kwamba Mtume alimchagua Abubakr. D) Seif alitaka kuthibitisha kuchaguliwa kwa Abubakr na Mtume, pale aliposema, "Usama alimtuma Umar kwa Khalifa Abubakr alipopata habari za kifo cha Mtume." Seif anaonyesha kwamba Abubakr alichaguliwa na Mtume. E) Seif alibuni maneno ya Qa'qa kama ifuatavyo: "Watu, mmoja baada ya mwingine kwa hiari zao walipeana mkono na Abubakr." Bado Qa'qa hakuishi kamwe. Amekuwepo tu katika ngano za Seif. F)
Kuthibitisha kwamba baadhi ya Maansari wanampinga Abubakr, anasema kwamba Hubab - mmoja kundi la Maansari, alishambulia kwa upanga wake. Kusema kweli alikuwa ni Zubair, binamu wa pili wa Mtume, aliyekuwa mmoja wa Muhajir - (Kundi la Ali) aliyeshambulia kwa upanga wake.
G)
Umar alitoa kauli kwamba ule uchaguzi wa Abubakr ulikuwa ni makosa. Seif pia aliuita upinzani wa Ansari ni makosa kumlinda Umar na kuthibitisha ile kauli aliyoitoa Umar, kwamba ilikuwa dhidi ya Maansari.
H)
Seif anasema kwamba hotuba mbili ndefu za uzinduzi zilitolewa na Abubakr baada ya kiapo cha hadhara. Muundo na maneno ya hotuba zile mbili zinaonyesha kwamba ni za kughushi; na ile hotuba ya kweli ya uzinduzi ya Abubakr ni tofauti kabisa. Ule muundo wa zile hotuba za kughushi siyo sawa 79
ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO
na ule wa hotuba za Makhalifa watatu mara baada ya Mtume. Pia hazikuandikwa vizuri kama kazi nyingine za Seif - inaelekea kwamba Seif hakuwa stadi katika kutunga hotuba za kidini. Tena, hotuba ndefu hazikuwa kawaida katika wakati wa Mtume na wa Abubakr. Hizi hotuba ndefu zilianza wakati wa Ukhalifa wa Umar, na zilifikia kilele wakati wa enzi ya Ali. Hotuba ya kwanza ya kiongozi yoyote kwa kawaida huwa ni fupi - ikionyesha ule mpango mpya. I)
Ule usemi uliotumiwa na Abubakr kwamba shetani alikuwa akikaa ndani yake, ulikuwa kiasi unachekesha na kushusha hadhi. Seif alitaka kueleza wazo la kwamba baada ya Mtume, watu hawakutaka tena kujihusisha na uchamungu na utakatifu. Maneno haya kutoka kwa Khalifa wa kwanza, Abubakr, yalifanana na dua yake baada ya jeshi la Usama liliposababisha Uislam kupata sifa mbaya.
J) Kitu cha kipekee kuhusu hotuba ya Abubakr inayodaiwa, kilikuwa kwamba, ilianzisha katika dini ya Kiislam mtazamo wa masikhara, kiasi kwamba watu wanaweza kuchukulia, kutoka kwenye hotuba ya kiongozi wa Waislam, kwamba Uislam haukuwa ni dini ya kweli, au baya zaidi kwamba hakukuwa na mungu.Sababu ya tafsiri hii potovu ya Uislam ya Seif, ni kwa sababu imeandikwa kwamba Seif alikuwa ni mkana mungu (asiyemuamini Mungu). K) Seif anasema kuhusu Khalid Ibn Sa'd Amawi kwamba Khalid alivaa nguo ya hariri, na Umar akaamuru kwamba ile nguo ichanwe. Kwa matokeo ya hili, hisia za Khalid kwa Abubakr na Umar zilikuwa ni za kisasi. Khalid akamwambia Ali, "Kabila lako (Abd Manafi) limeshindwa na kabila la Abubakr (Taim)." Ali akajibu, "Nafasi ya urithi wa Mtume, haihusiki chochote na umaarufu wa kikabila. Ni nafasi ya ki-ungu." Khalid akamwambia tena Ali, "Kabila lako linastahiki sana kwenye nafasi hii." Ndipo Umar akamwambia Khalid, "Mwenyezi Mungu akunyamazishe, umesema kitu ambacho kitawafanya waongo kuzua ngano." Hapa tena Seif anataka kusema kwamba ni Khalid tu aliyeamini kwamba umaarufu wa kikabila ulikuwa ndiyo dhamira ya watu kuwaunga mkono wagombea, vinginevyo, Muhajir na Ansari walikuwa hawana hatia kabisa kuchanganya siasa ya makundi na dini. Hivyo Ali na Umar wote walimdharau Khalid. Seif hapa tena anajaribu kuthibitisha kwamba hakukuwa na upinzani kwa Abubakr kuwa Khalifa. L) Seif anatuambia kwamba hakukuwa na hitilafu kati ya Ali na Umar, na kama hitilafu yoyote itaonekana baadae, watu watadhani chanzo chake ni Khalid. Kwa hiyo Umar akamwambia Khalid, "Baadae waongo watatunga ngano za kile ulichokisema." Hii ni nukta muhimu na yenye kufaa kuangaliwa. M) Kwa kumalizia, tusisahau kwamba Seif aliisimulia ngano hiyo hapo juu kutoka kwa Sakhr aliyekuwa mlinzi wa Mtume; lakini Mtume hakuwa na mlinzi mwenye jina hilo. 80
ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO
N)
Shambulizi la nguvu la Seif juu ya upinzani huo liko kwenye kusema kwake, "Hakuna yeyote aliyempinga Abubakr isipokuwa yule aliyekuwa muasi, au aliyekusudia kuuacha Uislam." Madai ya Seif yametoa sababu ya kuwafanya wasomaji waamini kwamba Waislam kwa pamoja walimkubali Abubakr kama Khalifa, mbali na wale waliougeuka Uislam. Hapa tutawatambulisha wale waliompinga Abubakr na kumuunga mkono Ali kwa moyo wote; hakuna yeyote anayeweza kumshuku yoyote kati yao kuhusika na shutuma za Seif za 'Uasi'. 1. 2. 3. 4. 5.
Zubair Ibn Al- Awam, binamu ya Mtume. Abbas, ami yake Mtume. Sa'd Ibn Waqqas, aliyeiteka Iraqi. Talha Ibn Ubaidullah. Miqdad Ibn Al- Aswad.
Wafuatao walikusanyika katika nyumba ya Fatima katika upinzani juu ya Abubakr. 6. 7. 8. 9. 10. 11. 12. 13. 14.
Abu Dhar Al- Ghifari. Salman Al- Farsi. Ammar Yassir. Bara Ibn Azib Al- Ansari. Ubbay Ibn Ka'b Al- Ansari. Fadhl Ibn Abbas, binamu ya Mtume. Abu Sufian Harb Al- Amawi. Khalid Ibn Said Al- Amawi. Aban Ibn Said Al- Amawi.
Kwa nyongeza ya hao kumi na wane hapo juu, hakuna katika Bani Hashim aliyepeana mkono wa kiapo na Abubakr mpaka binti ya Mtume alipofariki. Upinzani wao ulikuwa tu kwa sababu ya kumuunga mkono kwao Ali. Mbali na watu hawa, Sa'd Ibn Ubaidullah alimpinga Abubakr, kwa vile yeye mwenyewe alikuwa mgombea‌‌.Anaweza mtu yoyote kuamini kwamba yeyote kati ya hao hapo juu aligeuka kutoka kwenye imani ya Uislam? Au kwamba walikuwa waasi? Hawa walikuwa ndiyo wapinzani hapo Madina. Sasa tunawaelekea wale waliokuwa nje ya Madina. Baadhi yao waliuawa kwa sababu waliipinga hiyo serikali kama vile Malik Ibn Nuwayrah, ambaye Seif alimtaja kama muasi. Yale mapambano dhidi yao yaliitwa na Seif Vita Tukufu dhidi ya waasi.
81
ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO
HITIMISHO Seif ameichezea kwa ufundi sana historia ya Uislam katika ngano zake za uongo,kiasi kwamba wana historia, mutashirki, na hata ulimwengu wa Kiislam umewakubali wale mashujaa wa kubuni wa kitabu cha Seif kama masahaba wa kweli wa Mtume, na mashuhuri wa Kiislam. Tunaamini wakati umefika wa kuufichua, kwa utafiti na mjadala, ukweli kuhusu historia ya Uislam; na kumtambulisha Mtukufu Mtume wa Uislam na kizazi chake kitukufu, kwa walimwengu katika sifa zao bainifu, kuliko kuzihami ngano za Seif kwa jina la Uislam.
82
ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO
3. RIDDAH { UASI} MAANA YA KIARABU MAANA YA QUR'ANI KATIKA WAKATI WA MTUME KATIKA WAKATI WA ABUBAKR NA SEIF ULINGANISHO
83
ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO
RIDDAH (UASI) Wapinzani wa Abubakr, nje ya makao makuu waliitwa 'Waasi', na vita vilivyopiganwa dhidi yao vilifunikwa kwa udanganyifu kama Vitakatifu. UASI KATIKA UISLAM Uasi ni 'Irtidad' (kuritadi) kwa Kiarabu ikimaanisha 'geuka'. Qur'ani inasema, "Basi alipofika yule mwenye habari njema na akaiweka kanzu ya Yusufu usoni kwa Yaqub kuona kwake kulimrejea (Irtadda)." Neno 'Raddah' pia limetumika katika Qur'ani kumaanisha 'geuka kutoka kwenye dini' kama katika aya ifuatayo: "Enyi mlioamini, kama mtasikiliza kikundi cha wale waliopewa kitabu huko nyuma, watakurudisheni ( Yarudduukum) kwenye ukafiri mbali na imani yenu:" Tena katika aya hii: "Enyi mlioamini!Kama mtageuka (Yartadid) kutoka kwenye dini yenu, Mwenyezi Mungu ataleta watu wengine anaowapenda na wanaompenda Yeye. Ni wapole kwa waumini na n iwakali kwa makafiri. Tunasoma pia ndani ya Qur'ani: "Wanapigana na ninyi ili wakuondoeni (Yarudduukum) kutoka kwenye dini yenu, na kama mkiiacha imani yenu, na kisha mkafa, amali zenui zitakuwa bure."Lakini hili neno 'Irtaddah' limehusishwa mara kwa mara na uasi, kwamba si chochote ila uasi ndiyo unaokuja akilini pale linapotumika. WAASI WAKATI WA MTUME Baadhi ya Waislam waligeuka (waliritadi) kutoka kwenye Uislam wakati wa Muhammad kama wafuatao: Abdullah Ibn Abi Sarh. Abdullah alikuwa mmoja wa waandishi wa wahyi wa Qur'ani aliyekimbia kurudi Makkah toka Madina. Alikuwa akiwaambia Maquraishi, kwamba aliandika maneno tofauti na yale Muhammad aliyokuwa akimsomea. Kwa mfano, pale Muhammad aliposema, "Allah ni Mjuzi na Mwenye Hekima." Abdullah aliuliza kama anaweza kuandika "Allah ni Mwenye Nguvu zote na Hekima." Muhammad atasema, "Hiyo ni sawasawa kama inavyotumika." Ile siku alipoiteka Makka, Muhammad alisema, "Damu ya Abdullah haina thamani, na hata kama atatafuta kimbilio katika Ka'ba, ni lazima auawe." Uthman akamficha, na baadae akampeleka kwa Mtume akiomba msamaha, ambao alipatiwa. Muasi mwingine alikuwa ni Ubaidullah Ibn Jahesh, mume wa Umma Habiba, ambaye alihamia Ethiopia. Aliingizwa kwenye Ukristo, na akafa huko kama Mkristo. Abdullah Ibn Khatal alikuwa ni muasi mwingine aliyeuawa akiwa ameshika funiko 84
ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO
ya kuba Tukufu ya Ka'ba akitafuta kimbilio. UASI WAKATI WA ABUBAKR Habari zinazochoma moyo za kifo cha Mtume, zilienea kwa haraka kwenye rasi ya Arabia yote. Yale makabila ambayo, mpaka hapo, hayajaingia kwenye Uislam, yalishangilia, na yakaendeleza juhudi zao dhidi ya Uislam. Makabila ya kiislam pia yalishikwa na wasiwasi kwa sababu yalikwisha sikia kwamba baadhi ya masahaba wa Mtume, kwa sababu ya siasa ya makundi, walikuwa wakipigana wenyewe kwa wenyewe kwa ajili ya cheo cha ukhalifa. Kule kutoridhia kwa ndugu wa Mtume, Bani Hashim, na upinzani wa Sa'd, mkuu wa kabila la Khazraj, kwa Abubakr kama Khalifa, kulisababisha baadhi ya makabila ya Kiislam kukitilia shaka cheo cha Ukhalifa. Hawakukanusha imani yao, wala kukataa kusali au kupinga kulipa kodi, walikataa tu kulipa kodi inayostahili kwa serikali ya Abubakr. Wapinzani hawa waliitwa 'waasi' na walikuwa waondoshwe kwa vita vilivyobatizwa kama ni vya jihad. Baada ya kuwaangamiza wapinzani wao wa kiislam, serikali hiyo ikayapiga makabila ya kipagani na mitume wa uongo na washirika wao. Hatimae, vikosi vilitumwa nje ya Arabia. Vita vyote vile vilivyopiganwa wakati wa Abubakr, viliitwa Riddah, (vita dhidi ya waasi). Hivyo wale wapinzani wa Kiislam wa Abubakr nje ya Madina waliitwa 'Murtadiina' - Waasi. Dr, Hassan Ibrahim aliliunga mkono wazo hili katika kitabu chake: 'Historia ya Siasa za Kiislam'. Uk.251 : "Baada ya Mtume wa Mwenyezi Mungu kufariki na kifo chake kikathibitishwa, baadhi ya Waislam walisita juu ya ukweli wa Uislam, na wengine waliogopa kwamba Maquraish, au kwa kweli kabila lolote, linaweza kuingia madarakani na kuanzisha taifa la kidikteta. Walikuwa wakitambua kwamba ni Mtume wa Allah tu aliyekuwa mtakatifu (asiyefanya dhambi wala kosa), na mtu mwingine yeyote atakayemrithi yeye, hatakuwa na sifa hiyo, ambayo ilimuwezesha kuwaona watu wote, kama meno ya kitana, kuwa wako sawa. Kwa hiyo, walikuwa na mashaka kwamba kama mrithi wa Mtume atapendelea ukoo na kabila lake mwenyewe, na akayashusha makabila mengine, ingevuruga haki ya jamii ya Kiislam. Tunakisia hivi kwa sababu tunaona kwamba, baada ya Mtume, kila Mwarabu kiupendeleo aliunga mkono ukoo na kabila lake, na mwenendo wa kiarabu wa kizamani, ukarudi. Huko Madina, Maansari walikuwa na hofu kwamba Muhajiriin na Maquraishi wataingia madarakani. Makundi mawili haya yalikuwa yakitiliana shaka. Maansari walitaka serikali ya mseto. Muhajirina walitaka kiongozi atoke kwenye kabila lao, na msaidizi wake awe Ansari. Wale Aws na Khazraj, sehemu za Ansari, zilisalitiana zenyewe wakati wa uchaguzi wa Khalifa. Makka hakukuwa salama zaidi ya Madina kwani huo uchaguzi ulisababisha mgogoro wa kikabila huko vilevile. Bani Hashim hawakukubaliana na Abubakr kama Khalifa, Ali alikataa kumuunga mkono Abubakr na Abu Sufiani alijaribu kumshawishi Ali kuandaa mapinduzi ya serikali (coup d'etat). "Mwishowe Muhajirina, Maansari na Maquraish waliokuwa watangulizi katika 85
ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO
Uislam na wafuasi wa Uislam, na jamaa za Mtume, hawakuweza kuungana kuunda serikali kwa amani. Hili liliyafanya makabila mengine ya kiarabu kuishiwa na imani, na hatimae wakakata tamaa ya kuwa na sauti, au nafasi katika serikali hiyo. Kwa hiyo, wengi wao walimpinga Abubakr kama Khalifa na wakakataa kumlipa zaka iliyostahili. Baadhi ya wanazuoni wa kigeni wanalichukulia hili kama uasi, na kama ushahidi wa kuendelea kwa Uislam kwa upanga huko Arabia. Hilo siyo kweli hata hivyo, kwa sababu wale watu ambao Abubakr amewapiga kama waasi, walibakia waaminifu kwa Uislam." Walikuwa wa makundi mawili. 1)
Lile kundi lililoamini kwamba Zaka ilikuwa ni kodi ya Mtume, na baada ya kifo chake hakuna aliyestahili kuidai; hivyo walikataa kuilipa kwa Abubakr na kwa ajili hii akapigana nao. Umar alitoa maelezo kwa niaba ya watu hao akisema, "Mtume alikuwa akisema, 'Napigana na watu mpaka waamini Mungu Mmoja, na yeyote anayemuamini Mungu, damu yake na mali zake vitalindwa.'"
2)
Lile kundi ambalo hawakuamini hiyo dini. "Kwa kweli hawakuwa Waislam. Uongozi wa Kiislam katika wakati wa Abubakr ulijali tu juu ya kutekeleza hukumu za kifo, na haukuzingatia juu ya waasi wanaorejea kwenye Uislam."
Bado, kwa mujibu wa Uislam, kama ilivyoelezwa na Dr. Hassan Ibrahim, "Muasi yeyote lazima apate siku tatu za kujadili maoni yake na viongozi wa kidini. Hivyo 'wacha shutuma zithibitishwe kabla hajaangamia, na yule anaebakia salama anakuwa hivyo kwa uthibitisho.'" Kuliweka sawa jambo hili, tunarejea kwenye baadhi ya maoni ya viongozi wa Sunni. Imam Abu Hanifah anasema: "Muda mfupi kabisa unaoruhusiwa kwa mtu kurekebisha mawazo yake ni siku tatu. Kama Murtadi anaomba muda wa nyongeza, mpatie siku tatu za kujadili hoja zake." Imam Malik anasema: "Murtadi , awe mtumwa au muungwana, mwanamume au mwanamke, mpatie siku tatu tangu siku aliyothibitika kuwa ni Murtadi . Anaweza kupewa chakula na asiteswe." Imam Shafii anasema: "Murtadi, mwanamme au mwanamke, lazima aheshimiwe kwa sababu yeye alikuwa Mwislam wakati fulani. Wengine wanasema mpe nyongeza ya siku tatu." Imam Hanbal anasema: "Murtadi, mwanamme au mwanamke, kama siyo majinuni lazima aitwe kwenye Uislam kwa siku tatu." "Pamoja na maoni hayo hapo juu, siyo haki kusema kwamba Mwislam amekanusha imani yake kwa kukisia tu, labda kila Mwislam aseme kuwa ni muasi. Baadhi ya wanazuoni wa Kiislam wamesema kwamba kama mtu ni Mwislamu asilimia moja, siyo haki kumchukulia mtu huyo kama ni Murtadi mpaka iwe imethibitika kwamba kweli yuko hivyo."
86
ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO
Huu ndio mwisho wa maelezo ya Dr. Hassan Ibrahim ndani ya kitabu Historia ya Siasa za Kiislam. Ibn Kathir katika kitabu chake cha Albidaya Wannihaya, juz.6,uk.311, anasema: "Wapokezi wote, isipokuwa Ibn Majah, wameandika kwamba kwa mujibu wa Abu Hurairah, Umar alimkatalia Abubakr kupigana na watu, akisema kwamba Mtume alilinda roho na mali za yeyote aliyekiri Upweke wa Allah na Unabii wa Muhammad, labda walipopatikana na hatia. Abubakr akajibu, 'Wallah, nitawapiga wale ambao hawanilipi Zaka ile ambayo ilikuwa ikilipwa kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu. Na iwe ngamia au kamba ya kufungia ngamia. Wallah, nitampiga yeyote anayetofautisha kati ya kulipa Zaka na kusali. Nitawapiga mpaka wanipe ile zaka waliompa Mtume.' Umar akasema, 'Pale nilipoiona dhamira ya Abubakr ya kupigana, nikaelewa kwamba alikuwa na haki.'" Kwa mujibu wa Tabari (juz.2,uk.474), waasi walimwendea Abubakr kwa vikundi, wakikubali Swala, lakini wakipinga kulipa Zaka. Abubakr hakukubali maoni yao na aliwafukuza. Ibn Kathir ndani ya Albidaya Wannihayah (juz.6,uk.311), anasema kwamba makundi ya Waarabu yalikuwa yanakuja Madina waliokubali sala lakini wakakataa Zaka. Walikuwepo baadhi waliokuwa hawataki kutoa Zaka kwa Abubakr, baadhi yao walikuwa wakisoma ubeti huu: Pale Mtume alipokuwa miongoni mwetu, tulikuwa watiifu, Lakini kipindi cha Abubakr ni tukio la kipekee, Ambalo limetuvunja migongo yetu, tutaasi, Bado, anaweza akamfanya mwanae Khalifa hapo atakapokufa. Katika Tabari (juz.2,uk.48), Seif ameandika kutoka kwa Abu Makhnaf kwamba wapanda farasi wa kabila la Tay walitoa maneno juu ya wapanda farasi wa makabila ya Asad na Fazareh, wakati walipopishana. Lakini hapakuwa na mapambano kati yao. Watu wa Asad na Fazareh walipenda kusema, "Hatutakubaliana na AbulFasil" (lakabu ya Abubakr, ikiwa na maana ya baba wa mtoto wa ngamia). Wale wapanda farasi wa kabila la Tay hujibu, "Tuna uhakika mtakubaliana na Abul-FahlAkber." (yenye maana ya baba wa ngamia mkubwa, mtu mkubwa). Kutokana na ngano hiyo hapo juu inaeleweka kwamba ule uasi katika wakati wa Abubakr ulikuwa siyo wa kukana imani, bali ni katika kukwepa kulipa Zaka kwa Abubakr. Kwa vile makundi yaliyoshindwa ni ya Mabedui na Wahamaji, hayakuwa na nafasi ya kutawala, lakini wapinzani wao, watawala wa wakati huo, walikuwa na mamlaka mikononi mwao kwa muda mrefu, ikiwa ni pamoja na kile ambacho ndani yake historia ya wakati huu iliandikwa. Pia historia ya yale matukio ambayo imetufikia sisi yameandikwa kwa rejea zao. Ni juu yetu kuchunguza ukweli wa ngano zile zilizo andikwa juu ya watu walioshindwa.
87
ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO
Tabari katika kitabu chake (juz.6,uk.461), ameandika kutoka kwa Seif kwamba Waarabu waliikana imani yao baada ya Abubakr kuwa Khalifa. Uasi ulikuwa ndiyo mtindo wa kawaida wa wakati huo, lakini yalikuwepo makabila ambamo ni sehemu tu iliyokuwa ya kiuasi. Ni makabila ya ki-Quraish na Thaqif tu yaliyobakia kuwa waumini. Seif amempita Antara Ibn Shaddad na waandishi wengine wa uongo katika kubuni. Mashujaa wa ngano za Seif wanatembea kwenye maji bila kulowesha nyayo zao. Wanaongea na wanyama wa porini - malaika wanawasiliana nao - wanatoa chemchemi kutoka kwenye mawe huko jangwani. Zaidi ya hayo, Seif amesimulia ngano zake katika namna ya kuwapendeza watawala wa wakati huo, na kuuficha ukweli kwamba walikuwa wasiopendwa na watu. Ili kuonyesha ni katika mtindo gani Seif ameziandika ngano zake, tutazitoa baadhi yake kutoka kwenye kitabu chake, al-Futuuh Wal-Riddah zilizoandikwa katika kitabu cha Tabari.
88
ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO
4. MALIK IBN NUWAIRA KAMA ILIVYOANDIKWA NA SEIF NA WENGINEO MBALI NA SEIF ULINGANISHO
89
ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO
MALIK IBN NUWAIRA Bwana huyu alikuwa ni wa kabila la Yarbu na wa ukoo wa Tamim. Alikuwa akijulikana kama Abu Handhalah na lakabu yake ilikuwa Jafoul. Marzubani ameandika kwamba Malik Ibn Nuwaira alikuwa mshairi, msomi, na mpanda farasi mashuhuri katika kabila lake. Baada ya kuingia katika Uislam, Mtume alimteua kuwa mkusanya Zaka kwenye kundi la familia yake. Mtume alipofariki, Malik hakutoa makusanyo yake serikalini, bali aliyagawanya miongoni mwa familia yake akisema: Fedha mliyonipa nitairudisha, Matatizo ya kesho hayatuhusu sisi, Kama mtu, siku moja, atajaribu kuurudisha Uislam, Tutakuwa watiifu kwa Serikali hiyo. Tabari katika juz.2,uk.503, ameandika kile kisa kutoka kwa Abdul-Rahman Ibn Abubakr, kama ifuatavyo: "Wakati jeshi la Khalid lilipofika Butah, alituma kikundi cha askari wake, chini ya uongozi wa Zirar Ibn Azwar, kushambulia kabila la Malik usiku kucha. Abu Qatada, mmoja wa jeshi lile alisema baadae, 'Tulipolishtukizia kabila la Malik usiku kucha tuliwatishia. Walivaa mavazi yao ya kivita yenye deraya haraka haraka, na wakatangaza kwamba wao walikuwa ni Waislam. Kamanda wetu akawauliza ni kwa nini wana silaha, na wao wakamuuliza swali hilo hilo. Tuliwaambia waweke silaha zao chini, kama walikuwa ni Waislam, na wakafanya hivyo. Kisha tulisali sala zetu, na wao wakafanya vivyo hivyo.'" Ibn Abil-Hadid katika kitabu chake anasema, "Walipoacha silaha zao, wale askari wakawafunga pingu, na wakawapeleka kwa Khalid." Katika Kanzul Ummal, juz.3,uk.132, na ndani ya Yaqubi, juz.2,uk.110, ngano hiyo hapo juu imeandikwa kama ifuatavyo: "Malik Ibn Nuwaira pamoja na mkewe walikuja kwa Khalid. Khalid katika kumuona yule bibi alimpenda, na akamwambia mumewe, 'Hutarudi nyumbani kamwe, Wallah, nitakuua." Katika Kanzul Ummal, juz.3,uk.132, imeandikwa kwamba Khalid alimshutumu Malik kwa uasi, ambapo Malik alikataa na wote Abdullah Ibn Umar na Abu Qatada waliingilia kati kwa niaba yake. Lakini Khalid akamuamuru Zirar Ibn Azwar kumkata kichwa. Kisha Khalid akamchukua mke wake Umma Tamim na akalala naye. Katika Abdulfada uk.158 na ndani ya Alwafaiat, imeandikwa Abdullah Ibn Umar alizungumza bila mafanikio na Khalid kuhusu Malik, na Malik akaomba apelekwe kwa Abubakr kwa ajili ya uamuzi wake. Khalid akasema, "Mwenyezi Mungu 90
ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO
hatakusamehe kama mimi nitakusamehe," na akamuamuru Zirar kumkata kichwa. Malik alimuangalia mkewe akisema, "Wewe ndiyo sababu ya kuuawa kwangu." Khalid akasema, "Mungu amesababisha kifo chako kwa sababu ya uasi wako." Malik akasema, "Wallah mimi ni Mwislam na dini yangu ni Islam." Lakini Khalid akamuamuru Zirar kumkata kichwa chake. Imeandikwa ndani ya al-Isaba, juz.3,uk.337 kwamba Thabit Ibn Qasim ameandika ndani ya al-Dalail kwamba Khalid alimpenda mke wa Malik katika kumuona kwa mara ya kwanza, kwa vile alikuwa mzuri sana. Malik alimwambia mkewe, "Wewe umeniua." Imeandikwa pia katika al-Isaba kwamba Zubair Ibn Bakkar ameandika kutoka kwa Ibn Shahab kwamba Khalid aliamuru kichwa cha Malik kitumike kama nishati ya moto wa kupikia. Lakini kabla ya moto kuifikia ngozi ya kichwa cha Malik, chakula kikawa kimeiva, Malik alikuwa na nywele nyingi. Khalid, usiku uleule akamuoa mke wa Malik aliyeuawa. Abu Namir Sa'di ametunga shairi lifuatalo: Hivi wale wapanda farasi waliotushambulia wakati wa usiku, Wanajua kwamba kamwe hatutauona mwanga wa asubuhi? Khalid alikuwa amuondoe Malik kwa kweli, Kumchukua yule mwanamke aliyempenda hapo kabla, Khalid hakuwa na utashi wa kuepukana na matamanio yake, Na kuiambaa ile dhambi, hakuwa na uchamungu unaohitajika, Asubuhi ya usiku ule maskini yule mume akatoweka, Mke wake mikononi mwa Khalid. Imeandikwa katika al-Isaba kwamba Minhal aliuona ule mwili wa Malik usio na kichwa na akaufunika. Hiyo ilikuwa ni simulizi ya Malik. Na tuone sasa ni hatua gani zilichukuliwa na serikali kwa Jenerali wake. Yaqoubi ameandika kwamba Abu Qatada alilieleza tukio hili kwa Khalifa Abubakr na kusema, "Wallah sitakwenda popote chini ya uongozi wa Khalid. Amemuua Malik, japokuwa alikuwa Mwislam." Tabari ameandika kutoka kwa Ibn Abibakr kwamba Abu Qatada aliapa kwamba kamwe hatapigana chini ya Khalid. Yaqubi ameandika kwamba Umar Ibn AlKhatab alimwambia Abubakr, "Ewe mrithi wa Mtume wa Mwenyezi Mungu, Khalid aliangukia kwenye mapenzi na mke wa Malik, na siku hiyohiyo akamuua Malik ambaye alikuwa Mwislamu." Abubakr alimwandikia Khalid kutaka maelezo, na Khalid akaja kwa Abubakr akisema, "Ewe mrithi wa Mtume wa Mwenyezi Mungu, katika kumuua Malik nilifanya uamuzi wa sawasawa kabisa, lakini pia nilifanya kosa." 91
ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO
Mutammim Ibn Nuwaira, kaka yake Malik, alitunga idadi fulani ya mashairi akiomboleza mauaji ya ndugu yake. Alikwenda Madina na akajiunga kwenye Swala ya jamaa iliyoongozwa na Abubakr. Baada ya sala hiyo Mutammim aliegemea kwenye uta wake, na akimwambia Abubakr, alisoma: Ewe Ibn Azwar Uliutupa chini mwili wa mtu mwenye daraja, Wakati upepo mwanana wa asubuhi unapapasa mlango wetu. Ulimhadaa kwa kutumia jina la Mwenyezi Mungu, Lakini muumini Malik siku zote aliheshimu neno lake. Abulfada ameandika kwamba pale habari za Malik zilipomfikia Abubakr na Umar, Umar alimwambia Abubakr, "Khalid bila shaka amefanya zinaa; ufanye apigwe mawe." Abubakr akajibu, "Sitafanya hivyo." Umar kisha akasema kwamba Khalid ameuwa Mwislamu, na kwa hiyo ahukumiwe kifo. Abubakr akasema kwamba Khalid ametekeleza majukumu yake na aliyaelewa - pia amefanya kosa. Umar alimuomba Abubakr amfukuze Khalid. Lakini Abubakr akasema, "Kamwe sitaufutika upanga ambao Mungu ameutoa kwenye ala yake." Tabari ameandika kutoka kwa Ibn Abibakr kwamba Khalid alitoa kisingizio kwa Abubakr akisema kwamba Malik alimwambia, "Sidhanii kwamba sahiba wako (Mtume) alisema hili na lile." Khalid alijibu, "Hakuwa (Mtume) sahiba wako wewe?" na aliamuru akatwe kichwa chake na wanaume wote waliokuwa na Malik, wakatwe vichwa vyao pia. Habari ilipomfikia Umar, aliijadili na Abubakr akisema, "Yule adui wa Mungu ameua Mwislamu na, kama mnyama mara tu amemkera mke wake." Khalid alirudi nyumbani, kisha akaenda Msikitini akiwa amevaa joho lenye doa la kutu iliyotoka kwenye mavazi yake ya chuma ya kivita, na unyoya kwenye helmeti yake kama askari wa Kiislam. Alimpita Umar ambaye kwa ghadhabu alimvamia, akichomoa ule unyoya kwenye helmet yake huku akisema, "Kama mnafiki, umeua Mwislamu, na kama mnyama, ukamvamia mke wake, Wallah, nitakupiga mawe mpaka ufe. Hicho ndiyo unachostahili." Khalid alibaki kimya akidhani kwamba Khalifa Abubakr atasema kwamba ana hatia. Lakini pale Khalid alipotoa taarifa ya mafanikio ya safari yake na kukiri kosa lake, Abubakr alimsamehe. Akiwa njiani kurudi kutoka kumuona Khalifa, Khalid alimpita Umar tena na akamkemea: "Ewe mwana wa Umma Shamlah - sasa niambie kile ulichotaka kusema." Umar akaelewa kwamba Abubakr amemsamehe Khalid, na akaondoka pale Msikitini na akaenda nyumbani kimya kimya. Huu ndiyo mwisho wa kisa cha Khalid na Malik kwa mujibu wa rejea sahihi. Lakini 92
ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO
Seif ameielezea ngano hiyo katika matukio saba, kila moja likisifu jingine, na Tabari ameiandika na matukio ya mwaka wa 11 Hijiria kama ifuatavyo: NGANO YA MALIK KWA MUJIBU WA SEIF 1) Tabari wakati akiandika simulizi za Seif juu ya Bani Tamim na Sajah anasema, "Wakati Mtume wa Mungu alipofariki, wawakilishi wake katika Bani Tamim walihitilafiana kila mmoja juu ya ni nani wampe ile Zaka ambayo wameikusanya. Kwa kweli watu wa nchi ya Bani Tamim waligawanyika, wengine wakibakia waaminifu, na wakibishana na wale ambao hawakumtii Abubakr. Malik alikuwa mmoja wa upinzani na hakulipa Zaka aliyoikusanya kwa Abubakr. Sajah, ambaye alidai kuwa mtume, baada ya Mtume wa Mwenyezi Mungu, aliandika barua kwa Malik akiomba kukutana. Malik, Sajah na Waki walikutana na kufanya mkataba wa kutoshambuliana na kuwa na ulinzi wa pamoja. 2. Seif akiandika uasi wa watu wakazi wa Bahrain anasema, "Ala Ibn Hadhrami alitumwa kwenda kuwashughulikia waasi hukoYamama. Waligawanyika katika makundi mawili - waasi na waumini, wakibishana wenyewe kwa wenyewe. Wale waumini wakaungana na Ala Ibn Hadhrami. Malik na wenzie walikuwa huko Butah, na walikuwa na mabishano na Ala Ibn Hadhrami." 3. Seif pia, kuhusiana na matukio hayo hapo juu anasema, "Wakati Sajah aliporudi nyumbani, Malik alikuwa na mashaka na wasiwasi kidogo. Waki na Sama's walikubali kwamba walifanya makosa, hivyo walitubu kwa dhati, na wakatoa ile Zaka iliyocheleweshwa mara moja kwa Khalid. Hapakuwa na chochote kilichovurugika katika jimbo la Bani Handhala isipokuwa tabia ya Malik na wale aliokuwa nao huko Butah. Malik hakuwa imara - siku moja alikuwa sawasawa, na iliyofuatia akafanya mambo ya ajabu ajabu." 4. Seif tena anasimulia kwamba pale Khalid aliposafisha wilaya za Asad na Gatafan na waasi, aliondoka kwenda Butah alikoishi Malik. Maansari hawakuwa na uhakika kuhusu Malik, na hawakufuatana naye Khalid, wakisema kwamba walikuwa na amri ya Khalifa ya kubakia Buzakha. Khalid akasema ni juu yake kuwasiliana na Khalifa, kwani alikuwa ndiye kamanda wa jeshi. Alisema pia kwamba hatamlazimisha kamwe mtu yoyote kufuatana naye katika msafara wake wa kumshughulikia Malik. Kisha akaondoka zake. Maansari wakagundua kosa lao na wakiwa wanamfuata Khalid, hatimae wakamkuta. Khalid aliendelea mpaka akafika Butah, na kuona hakuna mtu pale. 5. Seif pia anasimulia kwamba Malik aliongea na watu wake kama ifuatavyo: "Enyi watu wa kabila la Bani Harbu, tuliwapinga viongozi na makamanda, lakini tulishindwa na kampeni yetu dhidi yao. Nawashauri msisimame kwenye njia yao. Nendeni kwenye miji yenu na majumbani kwenu. Watawala hawa 93
ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO
wameingia madarakani bila ridhaa ya watu." Baada ya hotuba hii watu wakatawanyika na Malik pia akaenda nyumbani. Hivyo pale Khalid alipowasili hapo Butah, hakukuta hata mtu mmoja hapo. Khalid ndipo akawatuma watu wake kama mubaligh wa kiislam, kuwakamata wale ambao hawakukubaliana na mawazo yao, na kumuua yeyote yule atakayepinga kutiwa mbaroni. Kwa kweli amri ya Abubakr ilitamka hivi: "Adhinini kila mtakapokwenda. Kama watu hawatajiunga na mwito wa sala, washambulieni ghafla, na wateketezeni kwa moto, au kwa njia nyingine yoyote. Kama watajiunga na mwito wa sala wapeni majaribio. Kama watakubali kulipa zaka yao, kubalini imani yao ya Kiislam, vinginevyo malipo yao ni kuangamia." Askari wa Khalid walikuja na Malik, binamu zake na baadhi ya watu wa kabila lake, kutoka kwenye msafara wao huo. Abu Qatada na baadhi ya askari wengine walitoa ushahidi kwamba Malik na watu wake walijiunga na mwito wa Swala, na walisali pamoja nao. Lakini kwa sababu ya tofauti katika ngano za askari hao kuhusu Malik, alifungwa kwa usiku mzima na watu wake. Lakini ulikuwa ni usiku wenye baridi kali sana, na Khalid akaamuru wafungwa wale wapashwe moto. Maneno yaliyotumiwa na Khalid katika kutoa amri hii, pia yana maana "kuua" katika lugha ya baadhi ya watu wa makabila 'idfau usara-akum' Hivyo wakamuua Malik na wenzake. Chakari (muuaji) wa Malik alikuwa Zirar Ibn Azwar. Mayowe ya kufa huko yalimtoa Khalid nje ya nyumba, ambapo alijua juu ya mauaji hayo. Akasema, "Kile Mungu alichoamuru, kimefanyika." Baada ya tukio hili Abu Qatada alibishana na Khalid, na akaenda Madina kutoa taarifa kwa Khalifa. Abubakr aliisikiza habari hiyo lakini akaonyesha kutoridhishwa na Abu Qatada. Umar akaingilia kati, hivyo Abubakr akamsamehe Abu Qatada, na akamrudisha kwenda kujiunga na Khalid kwenye medani ya vita. Khalid akamuoa Umma Minhal, mke wa Malik aliyeuawa, lakini hakuishi naye mpaka mwisho wa kipindi cha asubuhi cha mume wake wa kwanza. Umar akamwambia Abubakr "Kuna namna ya uasi katika upanga wa Khalid angalau kwenye suala la Malik." Abubakr hakujali kabisa kwani hajawakaripia watu wake kamwe kwa makosa yao. Hivyo alimuomba Umar aache kumkashfu Khalid na akasema, "Khalid anaweza kuwa hakuuelewa ujumbe wake." Abubakr ndipo akalipa fidia ya damu ya Malik, na akamwandikia Khalid kumwambia aje Madina. Khalid aliliarifu tukio hili kwa Abubakr aliyesamehe kosa la Khalid, lakini akamsuta kwa ndoa ile kwani ilikuwa kinyume na desturi ya Kiarabu. 6. Seif, mahali pengine, anasema kwamba baadhi ya askari walimshuhudia Malik akisali lakini wengine walilikataa hili na wakahalalisha kuuawa kwake. Kaka yake Malik alitunga mashairi ya maombolezo, na akadai fidia ya damu ya ndugu yake, na kurudishwa kwa wale wafungwa. Abubakr aliidhinisha kuachiwa kwa wale mateka. Umar alisisitiza kufukuzwa kwa Khalid kwa vile hakuweza kudhibiti upanga wake. Lakini Abubakr akasema kwamba hataurudisha upanga wa Mungu, ambao ulikuwa dhidi ya makafiri, kwenye ala yake. 94
ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO
7. Seif katika ngano yake ya mwisho, anasema kwamba Malik alikuwa na nywele nyingi. Pale vichwa vya wale waliouawa vilipotumika kama kuni za moto wa kupikia, moto ulifikia ngozi za vichwa vyote isipokuwa katika kichwa cha Malik, kwa sababu ya nywele zake nyingi. Mutammim alitunga shairi, na alielezea kupendezwa kwake na tumbo tupu la Malik kama mfano kwa askari wake wote. Umar ambaye alimuona Malik mbele ya Mtukufu Mtume pia alipendezewa na Malik. Hii ndiyo kumbukumbu ya mwisho ambayo imepatikana katika maandishi ya Seif kuhusu Malik. KIINI CHA NGANO ZA SEIF Kwa mujibu wa Seif, dondoo tatu za kwanza kati ya hizo saba hapo juu, zilitoka kwa Sa'ab, mtoto wa Atyya, ambaye naye alizisikia kutoka kwa baba yake, Atyya mtoto wa Balal. Hiyo dondoo ya tano na ya saba zilisimuliwa na Uthman, mtoto wa Suwaid, mtoto wa Math'abah. NI NANI HAWA SA'B, ATYYA NA UTHMAN? Hakuna dalili katika kitabu chochote cha historia ya Sa'b, Atyya au Uthman, hawa wasimulizi watatu wa asili; ambao Seif amewanukuu. Tunaweza kusema kwa hiyo kwamba hawa watatu ni miongoni mwa masahaba mia na hamsini wa Mtume waliobuniwa na Seif. Seif katika baadhi ya mambo kwenye ngano zake, amebadilisha watu wa kubuni, kama katika suala la Uthman, ambaye ameandika kutoka kwake. Hakuna dalili ya Uthman katika kitabu chochote isipokuwa kwenye kitabu cha Seif. Suwaid yule baba, na Math'ab (Shu'bah) babu yake Uthman walikuwa ni watu hasa waliokuwepo . Katika ngano ya mbwa pale Hawab, yule mwanamke halisi Umma Qirfa ni mama wa mtu wa bandia. Umma Zamal, na mwanaume halisi, Hurmuzah, ni baba wa Qumaziban, pia mtu wa bandia aliyebuniwa na Seif. KWA NINI NGANO ZA SEIF NI ZA UWONGO? Waandishi wa wasifu wametayarisha orodha ya wote na msimuliaji kila walioishi kutoka wakati wa Mtume, na mbele mpaka wakati wa utawala wa Bani Abbas, ambao wametawala baada ya utawala wa Amawiyah. Wale wapokezi ambao walimkuta Mtukufu Mtume ndiyo kundi la kwanza, wanaitwa Masahaba. Kundi la pili ni wale waliowakuta Masahaba, na walipokea ngano kutoka kwao, hawa wanaitwa Wafuasi (Tabi'in), na waliishi hadi mwaka wa 126. Kundi la mwisho la Tabiin wamekusanya mambo tu kutoka kwa wale tabi'in wa mwanzo, na waliishi hadi mwaka wa 132. Vilikuwepo vikundi kumi na nne kwa jumla, na cha mwisho kilikuwa wakati wa Mansoor, Khalifa wa pili wa Bani Abbas.
95
ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO
Waandishi wa wasifu wengine wameorodhesha wapokezi, waliokufa katika miaka kumi kama rika moja. Hivyo hasa, kundi la kwanza ni wale wapokezi waliokufa katika muongo wa kwanza, na kundi la pili ni wale waliokufa kwenye muongo wa pili, na kadhalika. Wale wapokezi waliitwa 'Wanazuoni' na wale waliowafikishia ngano hizo kwao waliitwa 'Sheikh'. Maisha ya kila Sheikh mmoja na Mwanazuoni yameandikwa kwa kina, walipoishi, na kama walikuwa Shia au Sunni, kama walikuwa wakereketwa kumpendelea Ali au dhidi ya Ali, kama walikuwa wapenzi au wapinga serikali. Hivyo vitabu vilivyotayarishwa viliwekwa katika orodha tofauti - vingine kwenye mpango wa alfabeti kama Tarikh Kabir, n.k. Vingine kulingana na wakati, kama Ibn Athir, n.k. Baadhi ya waandishi wa wasifu wameyapanga majina ya wapokezi kulingana na makazi yao, Makka, Madina, n.k. Elimu ya upokezi wa Hadithi ilikuwa ndiyo ya kuvutia sana na somo maarufu la wakati huo na waandishi mbalimbali wa wasifu wameyapanga majina ya wapokezi katika njia mbalimbali, na wametoa uangalifu wao wa hali ya juu katika kuandika hayo maelezo. Hata hivyo kuna vitabu vilivyoandikwa kusahihisha makosa ya waandishi wa wasifa, kama vile al-Mukhtalif, n.k., hivyo hakuna sababu yoyote ya mashaka juu ya utambulisho wa hao wapokezi. Kwa vile idadi ya wapokezi ilikuwa ndogo katika wakati wa Bani Umayya, na Seif aliandika vitabu vyake viwili kuwapendeza watawala wa wakati huo, Bani Umayya, ambapo hatuwezi kupata majina ya watu ambao Seif ameandika kutoka kwao, kwa msingi wa maelezo ya hapo juu, tunaweza kusema kwamba Seif amebuni hao wapokezi wake, na akanukuu kutoka kwa watu hawa bandia. MATIN YA NGANO ZA SEIF Katika masuala mengine, Seif ametumia majina ya baadhi ya wapokezi wa kweli katika ngano zake za uwongo, kama vile katika tukio la tano na la saba, tuliyokwishataja kabla. Uchunguzi makini na wa utaratibu, kulingana na kanuni za elimu ya ngano, unaonyesha kubatilika kwa dondoo hizo. ULINGANISHO Ulinganisho kati ya ngano ya Seif na masimulizi ya wapokezi wengine kuhusu Khalid unaonyesha kwamba Seif alilichezea hilo tukio kufuta shutuma za Khalid, za lile shambulio lake dhidi ya Malik, na ule uvamizi kwa mke wa Malik. Anayaandaa mandhari nyuma; kwanza kabisa kumshutumu Malik kwa kuwa na mashaka juu ya Uislam; pili yale mabishano ya waumini pamoja naye na tatu kurudi kwa Sajah, na kusita kwa Malik. Kisha kwa sababu rejea nyingine zimeeleza kwamba Malik alikuwa peke yake, Seif anadokeza kwamba Malik alikuwa na vikosi pamoja naye, lakini alivifuta siyo kwa sababu alitubia bali kwa sababu ya hofu yake. Seif kwa hiyo anatamka kwamba Malik alikuwa muasi. Katika ngano zingine Seif amedokeza uasi wa Malik, bila kutaja jina la Khalid ili 96
ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO
kuondoa mawazo ya kutoka kwenye amri ya Khalid ya kumuua Malik na uhwosiano wake na mke wa Malik. Seif ameubuni kule kupingana kwa wale askari na amri ya Abubakr, kumuangamiza Malik, mbele ya Khalid hivyo anamsafisha Abubakr vilevile na Khalid. Seif alitaka kuonyesha kwamba Khalid hakutaka kumuua Malik, alitoa amri tu ya kuwapasha moto wale wafungwa, lakini wale askari walidhani alimaanisha 'ua' kwa sababu ya kutoelewana kutokana na matatizo ya lahaja, bado yule aliyetoa amri, na wale machakari (wauaji) walikuwa na lahaja moja (Quraish na Bani Asad). Ukweli unabakia kwamba kuchukulia kwamba kutokuelewana kulisababisha mauaji, basi kwa nini vile vichwa vitumike kama kuni za moto wa kupikia.? Tabari ameandika ngano ya Malik kutoka kwa Seif na Ibn Athir, Ibn Kathir, Mirkhand wamenukuu yale 'mambo' yaliyoandikwa na Tabari. Kama nyaraka za wanahistoria wengine, kwa waandishi wengine, walioitaja ngano ya Malik kutoka kwenye rejea zingine mbali na Seif zitachunguzwa, basi hitilafu kati ya 'Matendo' ya Seif na ukweli hutokea. Zile rejea nyingine zinazoeleza kwamba Khalid alitoa amri ya dhahiri ya kumuua Malik ni kama ifuatavyo:
Futuuhul-Buldan
Cha Baladhuri
Uk.105
Tahdhib
Cha Ibn Asakir
Uk. 105, 112
Alkhamis
Cha Diyar Bakri, Juz.2
Uk. 333
an-Nihaya
Cha Ibn Athir, Juz.3
Uk. 257
as-Sawaiq al-Muhriqa Taj al-Aruus
Cha Ibn Hajar Al- Makki Cha Zabidi, Juz.8
(chapa ya Misri) Uk.21 Uk.75
Hiyo hapo juu ni moja ya vita zilizopiganwa kwa jina la Uasi (zilizopiganwa na Abubakr). Vita hii inaweza kuchukuliwa kama mfano.
97
ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO
5. NGANO YA ALA IBN HADHRAMI KUTOKA KWA SEIF NGAMIA WANAOTOROKA MUUJIZA WA CHEMCHEMI KUTOKA KWA WENGINE MBALI NA SEIF ULINGANISHO
98
ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO
NGANO YA ALA IBN HADHRAMI Ala Ibn Hazrami mwana wa Abdullah, mwana wa Ibad mwana wa Akbar mwana wa Rabi'a mwana wa Malik mwana wa Uwaif Hadhrami. Abdullah, baba yake, alikuwa mwenyeji wa Makkah na rafiki wa karibu sana wa Harb Ibn Umayya. Mtume alimteua kuwa Gavana wa Bahrain. Abubakr na Umar walimruhusu kushikilia nafasi yake mpaka alipokufa katika mwaka wa 14 au 21 Hijiria. (al-Istiab, chapa ya 3,uk.146-148 na al-Isaba, chapa ya 2,uk.491.) SEIF ANATUELEZA KUHUSU ALA IBN HADHRAMI Katika Tabari 2-522, 528 Seif ameandika kutoka kwa Minjab Ibn Rashid kwamba Abubakr alimwamuru Ala kuwapiga waasi wa Bahrain. Minjab alikuwa katika jeshi hilo. Anasema, "Tulifika katika bonde la Dahna, ambako Mungu aliamua kutuonyesha muujiza. Ala na sisi, tulikuwa wote tumeshuka kwenye vipando vyetu.Ghafla ngamia wetu wakashtuka na wakakimbia na mahitaji yetu yote, na wakatuacha bila kitu chochote katikati ya lile jangwa la mawe tupu. Pia kabla hatujapata muda wa kujenga mahema yetu. Tulihuzunika sana na kukanganyikiwa, na tukaachiana wosia zetu mmoja kwa mwingine. Mwito ukaja kutoka kwa Ala tumwendee - sisi wote. Hivyo tukajiunga naye. Aliuliza sababu ya kuvunjika moyo kwetu na tukajibu: 'Unategemea nini kwa kundi ambalo hakuna kitakachobakia kesho, isipokuwa sehemu yao katika historia.' Alituliwaza akisema, 'Waislam wanaweka imani yao kwa Allah, ukweli Allah hatawatelekeza wale ambao wako kwenye hali kama yetu.' Siku iliyofuata baada ya sala ya alfajir, Ala alipiga magoti nasi tukafanya vivyo hivyo na tukamuomba Mola atupe maji, Ala ndipo akaona viwimbi. Akamtuma mtu akaangalie kama yalikuwa ni maji, lakini ilikuwa ni mazigazi tu. Mazigazi hayo hayo yalichunguzwa baadae. Mara ya tatu mjumbe alirudi na habari kwamba kulikuwa na maji, hivyo vikosi vikanywa na vikaoga, kisha ghafla ngamia wetu walionekana, na walirudi kwa kupenda kwao wenyewe pamoja na mahitaji yetu salama vilevile kama wakati kabla hawajaondoka." Baada ya kuondoka mahali pale rafiki yangu Abu Huraira akaniuliza kama nitaweza kupajua pale mahali tena, ambapo yale maji yalipatikana. Nikajibu kwamba ninapajua pale mahali vizuri zaidi kuliko mtu mwingine yoyote. Aliniomba nimpeleke kwenye yale maji tena. Nikafanya hivyo; lakini palikuwa hapana maji, hapana kidimbwi, bado tukaona jagi limejaa maji. Abu Huraira akasema kwamba ni jagi lake ambalo aliliacha pale kwenye kidimbwi kwa makusudi kuona kama palikuwa na kidimbwi kweli pale ama ni muujiza ulitokea. Minjab aliapia kwamba hajawahi kuona maji pale kabla na Abu Huraira akamshukuru Mungu kwa muujiza huu. Kisha Seif anasema Ala alishinda vita hiyo (dhidi ya waasi) wakati wa usiku walipokuwa waasi wote wamelewa.
99
ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO
Baada ya Ala kuwa na uhakika wa kuangamia kwa wale waasi alitoka na vikosi vyake kuelekea Darain; lakini kabla ya kuondoka alitoa hotuba kwa askari wake. Alisema kwamba Mungu ameonyesha muujiza katika nchi kuwatia moyo na yale maji (katika uvamizi wao unaofuatia kwa waasi). Kisha akaamuru mashambulizi akisema, "Tusonge mbele na tuivuke bahari, Mungu amewazingira maadui mahali pamoja kwa ajili yenu." Wale askari wakakemea, "Wallah, hatutakuwa na woga tena kamwe madhali tumeuona ule muujiza katika jangwa la Dahna." Ala akapanda (kipando) na pamoja na askari wake wakafika baharini. Waliingia baharini wengine juu ya vipando na wengine kwa miguu. Walikuwa wakisoma, "Ewe Mwingi wa Rehma, Mwenye upendo, Mvumilivu, Wa-milele, Uliye Hai, Mhuishaji, Unayejitosheleza, hapana Mungu ila Wewe. Oh, Mola wetu." Maji yalionekana kwao kuwa machache, kwa kina tu cha kiwiko cha mguu wa ngamia, ingawa umbali wa kisiwa kile ulikuwa ni safari ya siku moja kwa mashua kutoka ufukweni. Walikifikia kisiwa na vita vilivyopangwa vikatokea hapo (kati ya askari wa Ala na waasi) na maadui wakaangamizwa kabisa. Hakuna kati ya waasi aliyebakia kurudisha taarifa kwao. Mali na familia zao vilitekwa na kugawanywa. Askari wa kipando alipata elfu sita na wa miguu alipata elfu mbili. Afif Ibn Mundhar alitunga ubeti ufuatao juu ya tukio hilo: Mungu, Mwenye uwezo aliiweka bahari chini ya udhibiti wetu, Tukio la kushangaza mno kuliko jukumu lenyewe. Lililofanywa na Musa kwenye Bahari Nyekundu na Mto Nile. Ghadhabu ya Mungu ilimwangukia kila asiyeamini. Chemchem ilibubujika kutoka chini ya changarawe, Nasi tena, tukasikia mlio wa kengele za ngamia wetu. Mtawa mmoja alikuwa akisafiri pamoja na jeshi la Ala ambaye aliingia Uislam baada ya vikosi hivyo viliporudi Bahrain na ushindi na nchi kufagiwa waasi. Watu wakamuuliza mtawa yule kwa nini alisilimu. Alisema ameona dalili tukufu tatu, na aliogopa kubadilishwa kuwa mnyama kama hakuingia Uislam. Aliulizwa kuhusu dalili hizo tatu na alizitaja kama ifuatavyo: 1) Ile chemchem iliyotokea chini ya changarawe, 2) Kugeuka kwa bahari iliyochafuka. 3) Ile dua iliyosomwa na wale askari, kama ifuatavyo: "Ewe Mola, wewe ndiye Mwingi wa Rehema. Hapana Mungu ila Wewe, Uliyejiumba, hakuna kilichokuwepo kabla Yako, Wa milele, Mtambuzi, Hai usiyekufa kamwe, Muumba wa Yasiyoonekana na yale Yanayoonekana. Mmiliki wa kudumu. Unajua bila kujifunza." Mtawa yule akasema wale askari walikuwa kwenye haki hivyo malaika walikuwa upande wao. Hii ngano ya mtawa imerudiwa mara kwa mara baadae. Ala aliandika barua kwa Abubakr kumweleza kwamba baada ya kupata matatizo kiasi Mungu 100
ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO
aliwasaidia kwa kufanya chemchem kububujisha maji kutoka chini ya changarawe. Ala katika barua yake alimuomba Abubakr aviombee vikosi vya Waislam vinavyopigana katika njia ya Mwenyezi Mungu, na Abubakr akafanya hivyo, na kusema kwamba Mabedui wamezoea kusema, "Luqman, mwenye hekima, aliwazuia watu kuchimba kisima cha maji katika jangwa la Dahna, kwa sababu hakukuwa na kamba iliyokuwa ndefu ya kutosha kuyafikia maji ambayo yangekuwa mbali sana chini ya ardhi." Abubakr ndipo akasema kwamba kule kutokea kwa maji kulikuwa moja ya ishara kubwa sana za Allah na alikuwa haijawahi kusikiwa kabla na ummah mwingine, na akaongeza, "Oh Mola, usiiondoe neema ya Muhammad kutoka kwetu." Ibn Kathir katika kitabu chake (juz.6,uk.328-29), ameandika ngano hiyo hapo juu kutoka kwa Seif. Abulfaraj katika kitabu chake al-Aghani amenakili kutoka kwa Tabari ambaye naye ameandika kutoka kwa Seif. Wanazuoni wengine wameandika ngano hiyo kutoka kwa Seif. ASILI YA NGANO YA SEIF Seif amesimulia ngano ya Ala kutoka kwa Sa'b mtoto wa Atyya mtoto wa Balal, hii ni kwamba, ilipita kutoka kwa babu kwenda kwa baba na kwenda kwa mtoto. Tumeonyesha wakati tunajadili ngano ya Malik kwamba sanad-ya-kifamilia ya wapokezi hiyo hapo juu imebuniwa na Seif. NGANO YA ALA KUTOKA KWA WENGINE MBALI NA SEIF Baladhuri katika Futuuhul Buldan (uk.92-93) anasema kwamba wakati wa utawala wa Umar Ala alipelekwa Zara na Darain. Alifanya mkataba na watu wa Zara wa kuchukua theluthi moja ya dhahabu, fedha, na mali nyingine za mji huo kuongezea na nusu ya mali kutoka nje ya mji huo. Akhnas Ibn Amery, mwakilishi wa mji huo alimwambia Ala kwamba mkataba huo ulihusika tu na watu wa mji wa Zara na haukuhusika kwa jamaa zao walioishi mji wa jirani wa Darain. Ala alimchukua Karadhulnukri kama mwelekezaji wake, na wakavuka bahari juu ya ukanda wa ardhi kwenda Darain. Huko aliwashambulia wakazi, akawaua wapiganaji wao na kuziteka familia zao. VITA DHIDI YA WAASI {ULINGANISHAJI NA HITIMISHO} Seif anaandika kwamba: 1)
Chemchem ya ajabu ilitokea mahali ambapo hata Luqman, mwenye hekima, hakutegemea maji. 2) Wale ngamia walirudi kwa hiari zao wenyewe.
3) Wale askari walitembea juu ya bahari, kama juu ya ardhi, ni ajabu
101
ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO
zaidihata kuliko muujiza wa Musa. Kisha aliupa nguvu ukweli wa miujiza hii, kwa kuelezea juu ya mtawa anayesilimu kwa kuiona miujiza hiyo. Anatilia mkazo kwamba miujiza hii ilitokea kwa ajili ya barua ya Ala kwa Abubakr kumwomba baraka zake. Tabari, Hamawi, Ibn Athir, Ibn Kathir na baadhi ya waandishi wengine wanarudia ngano ya Seif katika vitabu vyao, na Waislam wameikubali kama historia ya kiislam. Hata hivyo, hapakuwa na muujiza, mji huo ulikuwa na njia ya kufikia bara kwa ukanda ambao kupitia humo askari hao ndimo walimotembea. Pia tukio hilo halikutokea wakati wa Abubakr, bali katika wakati wa utawala wa Umar. Seif ndiye peke yake anayehusika na ubunifu wa ngano hizi kwani yuko peke yake katika kuziwasilisha, kama vile tu alivyo peke yake anayesema kwamba hakuna katika maadui aliyebaki wa kupeleka habari nyumbani.
102
ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO
6. TUKIO LA MIBWEKO YA MBWA WA HAUW-AB KUTOKA KWA SEIF NA KWA WENGINE ULINGANISHO
103
ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO
HAUW-AB NCHI YA MIJIBWA Tabari katika juz.3,uk.490-407, ameandika kutoka kwa Seif kwamba Umma Zemal Salma, mfungwa wa kivita wa kike, alitolewa kwa Ayisha (mke wa Mtume) kama fungu lake la ngawira ya vita. Ayisha akamwacha huru, lakini akakaa ndani ya nyumba ya Ayisha. Siku moja Mtume alirudi nyumbani na kuwakuta wanawake wamekusanyika pamoja. Mtume aliwanyooshea kidole na akasema, "Mmoja wenu anawafanya mbwa wabweke katika nchi ya Hauwab." Baada ya Mtume kufariki, Umma Zemal Salma alilikusanya jeshi kulipiza kisasi juu ya Waislam waliowaua ndugu zake. Alipokuwa analikusanya jeshi lake kutoka Zafr na Hauwab, mbwa walimbwekea ngamia wake hapo Hauw-ab (kutimiza utabiri wa Mtume). Khalid (aliyekuwa Jenerali) alimtambua Umma Zemal Salma na akapigana dhidi yake. Askari wa Khalid wakakata miguu ya ngamia wake na wakamuua (Umm Salma). Hamawi ndani ya kitabu chake Mujamul Buldan, ameiandika ngano hiyo hapo juu kutoka kwa Seif. Ibn Hajar katika Isaba, juz.2,uk.325, ameiandika kwa kifupi bila kutaja rejea yake. CHANZO CHA NGANO YA SEIF Seif amesimulia ngano hiyo hapo juu kutoka kwa Sahl mtoto wa Yusuf na Abu Yaqub, ambao utambulisho wao haukuandikwa. Ibn Hajar na Ibn Abdul-Birr wamesema, "Siyo Sahl wala baba yake Yusuf wanaojulikana kwa mtu yoyote." Abu Yaqub ndani ya ngano za Seif ni "Said Ibn Ubaid" ambaye Dhahabi anasema, "Hajulikani." Baadhi ya waandishi wengine wanasema, "Yupo Said Ibn Ubaid mmoja lakini hajulikani kama Abu Yaqub." NI NANI ALIBWAKIWA NA MBWA HAPO HAUW-AB? Seif katika ngano ya Hauw-ab amechanganya matukio mawili pamoja. La kwanza, tukio la Ummu Qirfa, la pili, mbwa wa Hauwab. 1)
Ummu Qirfa: Kwa mujibu wa Ibn Sa'd na Ibn Hisham, msafara wa biashara wa Waislam ukiwa njiani kwenda Damascus uliporwa na kabila la Faraza Wadilqura. Mwislamu aliyekuwa mkuu wa msafara, Zaid, alijeruhiwa vibaya.
Yaqubi anasema kwamba Mtume alikuwa atume jeshi ugenini chini ya uongozi wa Zaid kwenda kuliadhibu kabila la Fazara. UmmuQirfa, mke wa chifu wa kabila hilo katika kujua makusudio ya Mtume alituma jeshi chini ya uongozi wa arobaini kati ya watoto wake mwenyewe kukutana na lile jeshi la Waislam karibu na Madina. Mapigano yaliyopangwa yakatokea hapo na wanaume wote wa kabila la Fazara wakauawa na wanawake wao wakachukuliwa mateka. Isipokuwa Ummu Qirfa na 104
ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO
binti mmoja aliyeitwa Jariah ukoo wote uliuawa. Hawa wawili walitekwa bila kuumizwa. Zaid aliamuru Ummu Qirfa auawe na akamchukua yule binti Jariah kwa Mtume ambaye alimtoa kwa ami yake mwenyewe, na mtoto wa kiume baadae alizaliwa na akaitwa Abdur-Rahman. Tukio hili lilitokea katika mwaka wa 6 wa Hijiria wakati wa uhai wa Mtume. 2)
Mbwa wa Hauwab: Hauwab ni mahali karibu na Basra. Kwa mujibu wa Ibn Abbas, Mtume aliwaambia wake zake: "Mmoja wenu atapanda ngamia mwenye manyoya mengi, mbwa watambwakia huko Hauwab, watu wengi watauawa mkono wako wa kulia, na kushoto kwako,6 kifo kitakutisha wewe, lakini utabakia salama."7 Kwa mujibu wa Ummu Salama (mmoja wa wake za Mtume), Mtukufu Mtume alitaja uasi wa mmoja wa wake zake, wale mama wa waumini (kama wanavyoitwa), Ayisha (mmoja wa wake za Mtume) akacheka. Mtume alitoa kauli juu yake akisema, "Inanielekeza kwamba mbwa wanakubwakia huko Hauwab ukiwa unafanya uasi kidhalimu dhidi ya Ali." Kisha Mtume akamwangalia Ali, akisema, "Kama jambo la Ayisha litakuja mikononi mwako, kuwa mvumilivu juu yake."
Kwa mujibu wa Tabari, juz.3,uk.475, na baadhi ya wanahistoria, ngano ni kama ifuatavyo: Urani, yule mtu aliyeuza ngamia wake kwa Ayisha alikuwa safarini akiwa amepanda ngamia wake. Mtu alimfuata, na akataka kununua ngamia wake. "Dirham elfu moja ndiyo bei yake," Alisema Urani, "Una wazimu?" Yule mtu akasema, "Nani anayelipa Dirham elf moja kwa ajili ya ngamia?" Urani akasema, "Ngamia huyu ana thamani ya Dirham elf moja kwa sababu ninaposhindana na mpandaji wangu ninampita, na hakuna anayeweza kunikuta mimi ninapompanda ngamia huyu." Yule mtu akasema, "Utafanya biashara vizuri nami kama utajua ni kwa ajili ya nani ninamtaka ngamia wako." Urani: Mwarabu: Urani: Mwarabu:
Ni kwa ajili ya nani unamtaka huyu ngamia? Kwa ajili ya mama yako. Nimemwacha mama yangu taabani nyumbani. Namtaka ngamia wako kwa ajili ya mama wa waumini, Ayisha. Urani: Basi mchukue kama zawadi kutoka kwangu. Mwarabu: Hapana, fuatana nami, nitakupa ngamia na pesa vilevile. Urani:
Nilikwenda na yule mtu, alinipa ngamia jike aliyekuwa wa
6 Ibn Kathir (juz.6,uk.212). 7 Salati katika Kasais (juz.2,uk.137) na Ibn Abd Bir katika al-Istiab.
105
ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO
Ayisha na Mtoto wake, na Dirham 400 au 600 vilevile. Kisha yule mtu akaniuliza kama nilizijua barabara pale, na nilimjibu kwa kumkubalia. Aliniomba niwaongoze, na nikawaambia jina la kila jangwa na mto tulioupita. Tulikuwa tukipita maji ya Hauwab pale mbwa walipobweka. Waliniuliza, "Jina la maji yale yanaitwaje?" Nikajibu, "Hauwab." Ndipo Ayeshah alipopiga ukelele na kumfanya ngamia wake akae chini na akasema, "Wallah, ni mimi ambaye mbwa wamenibwakia hapa Hauwab, nirudisheni." Watu wengine waliwakalisha ngamia wao chini kumzunguka Ayishah. Ayeshah kamwe hakusogea kutoka mahali pale mpaka siku iliyofuatia. Mpwa wake Ibn Zubair alikuja na akamwambia, "Ondoka haraka," kwa sababu Ali alikuwa anawafuata, na angewafikia mara tu. Urani ndipo akasema, "Waliondoka mahali pale na wakanilaani." Kwa mujibu wa Musnad Ibn Hanbal (juz.6,uk.97), Ibn Zubair alimwambia Ayishah, "Huu siyo wakati wa kutuangusha, pengine Mungu anakutaka wewe uingilie kati baina ya Waislam na kufanya amani miongoni mwao." Ndani ya Ibn Kathir (juz.7,uk.230), imeandikwa kwamba Masheikh wawili hawakuiandika ngano hii kwenye vitabu vyao ingawa inazo shuruti zote za kuifanya ikubalike kama ni sahihi kwao. Katika Tabari (juz.3,uk.485), imeandikwa kutoka kwa Zuhri kwamba wakati Ayishah alipowasikia mbwa wakibweka, aliuliza, "Mahali hapa panaitwaje?" Baada walipomwambia kuwa ni 'Hauwab' alijuta na kusema, "Wote ni wa Mwenyezi Mungu na Kwake yeye tutarejea." Kisha akaendelea akisema, " Ni mimi kwa kweli ambaye Mtume alinizungumzia kwa wake zake akisema angependa kujua ni nani atabwakiwa na mbwa hapo Hauwab." Ayisha alitaka kuondoka mahali pale, lakini Ibn Zubair alimshawishi kuendelea mbele. Mahali pengine Ibn Kathir (juz.7,uk.230), na Abulfaraj (uk.173), imeandikwa kwamba Ayishah alijuta, akisema, "Mimi ndiye yule mwanamke," lakini Ibn Zubair akamsaliti akisema kwamba mahali pale hapakuwa Hauw-ab. Katika Murujudh-Dhahab (juz.2,uk.248), imeandikwa kwamba Ibn Zubair na Talha waliapa kwa Allah kwamba mahali pale hapakuwa Hauwab, na wakaleta Waarabu hamsini kuapa vivyo hivyo na huo ulikuwa uongo wa kwanza kuapiwa katika Uislam. Katika Yaqoubi (juz.2,uk.157) na Kanzul-ummal (juz.6,uk.83-84), imeandikwa kwamba Ayisha alisema, "Niacheni nirudi. Haya ni maji yaleyale Mtume aliyozungumzia, akinionya juu ya mbwa wanaobweka." Walileta Waarabu hamsini ili 106
ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO
kuapa kwa Mwenyezi Mungu kwamba mahali pale hapakuwa Hauw-ab. Ndani ya al-Imama wa-Siasa (juz.1,uk.59-60), imeandikwa kwamba Ayisha alipowasikia mbwa wanabweka alimuuliza Muhammad Ibn Talha juu ya mahali pale na kadhalika. Muhammad alimwambia, "Ubarikiwe moyo wako. Sahau juu ya ngano hizi." Abdullah Ibn Zubair akashuhudia kwa uwongo, na wakaleta mashahidi wanaoongopa. Ule ulikuwa ushahidi wa kwanza wa uwongo katika Uislam. Wanahistoria wengine pia wameisimulia ngano hiyo hapo juu kutoka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu, kama vile Ibn Athir ndani ya al-Nihaya; Hamawi ndani ya Mujamul-Buldan, Zamakhshari katika al-Faiq; Ibn Taqtaqi katika al-Fakhri (uk.71) juzuu za Cairo; Zubaidi (juz.1,uk.195) chini ya neno Hauwab; Musnad Ahmad (juz.6,uk.52, 97); A'tham (uk.168-169); Sam'ani katika al-Ansab; Sira Halabiyyah (juz.3,uk.320-321); na Muntakhab Kanz (juz.5,uk.444-445). HITIMISHO Wanahistoria kwa makubaliano wameandika kwamba (mke wa Mtume) Ayisha alikuwa ndiye mtu pekee ambaye mbwa walimbwakia hapo Hauwab, kama ilivyotabiriwa na Mtume na wamelichukulia tukio hilo kama moja ya dalili za unabii wa Mtume Muhammad. Ni Seif pekee aliyelihusisha tukio la mbwa hao kwa Ummu Zemal Salma, mwanamke wa bandia kuwaridhisha wale ambao kwa sababu moja au nyingine, waliupenda uwongo wa Seif. Tabari kwa upande wake bahati nzuri, ameiandika ngano hiyo kutoka kwa wasimulizi wengine na Seif vilevile. Kwa hiyo, ile nia ya Seif ya kuzipindua ngano imefichuliwa. Kwa kuziandika ngano za Urani, yule mmiliki wa mwanzo wa ngamia aliyepandwa na mama wa waumini, na ngano ya Zuhri juu ya mbwa wale, Tabari ameudhihirisha uso halali wa Seif kwa wasomaji wake, mbali na nyakati zingine ambapo Tabari ameandika kutoka kwa Seif tu na akauficha ukweli. Mpaka hapa tumeandika baadhi ya ngano zilizosimuliwa na Seif katika wakati wa Abubakr, sasa zinafuata baadhi ya ngano zake katika wakati wa Umar.
107
ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO
7. KUUSAHIHISHA MTI WA FAMILIA WA ZIAD: KIINI CHA NGANO YA SEIF ZIAD NA ABU SUFYAN NGANO HIYO ILIVYOELEZWA NA WENGINE MBALI NA SEIF HITIMISHO
108
ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO
KUUSAHIHISHA MTI WA FAMILIA YA ZIAD Abu Mughaira Ziad alikuwa mtoto wa mtumwa wa kike aliyekuwa akiitwa Sumayya, wa mkulima wa Ki-Fursi, aliyemtoa kwa mganga mmoja aitwaye Harth Thaghafi, kwa malipo ya huduma yake ya tiba. Sumayya alizaa watoto wawili wa kiume Nafiia na Naafi, wakati bwana wake alipokuwa ni mganga Harth. Baadae Harth alipanga ndoa kati ya Sumayya na mtumwa wake wa Kirumi, Ubaid. Waliishi Taif. Abu Sufyan alikwenda Taif na akamuomba muuza baa mmoja afanye ukuwadi (ugawadi) kwa malaya kwa ajili yake. Yule muuza baa Abimaryam Selluli akamtambulisha Sumayya kwa Abu Sufyan na akawa mjamzito usiku uleule, na baadae akamzaa Ziad katika mwaka wa kwanza wa Hijiria, alipokuwa mke wa Ubaid. Wakati Mtume wa Allah alipoizingira Taif, mmoja wa watoto wa kiume wa Harth (yule mganga) ambae jina lake lilikuwa Nafiia alikimbilia kwa Mtume ambaye alimwacha huru na akimwita Abubakra. Harth akamwambia Naafi kwamba yeye alikuwa ndiye baba yake na hivyo akamzuia asikimbilie kwa Mtume kama kaka yake alivyofanya. Ndugu watatu hawa, Abubakra, Naafi na Ziad baadae waligeuka wakaitwa ' watumwa walioachwa huru na Mtume', Ibn Harth na Ibn Ubaid kama walivyofuatana. Mu'awiyah alimpendelea na kumpokea Ziad kuwa ndugu yake, na akamwita Ziad Ibn Abu Sufyan. Lakini baada ya Mu'awiyah na kuanguka kwa Ufalme wa Amawi, Ziad aliitwa, Ziad mtoto wa Baba Yake (ikimaanisha mwanaharamu) na wakati mwingine akiitwa Ziad mwana wa Sumayya kwa jina la mama yake.8 Wanahistoria wameandika ngano ya Mu'awiyah kutoa udugu wake kwa Ziad na kumlaumu Mu'awiyah kwa kitendo chake hiki. Seif, akidhamiria kumuondoa Mu'awiyah kwenye lawama na kuliondoa doa kutoka kwenye nguo ya Ziad, alibuni ngano ambayo Tabari ameiandika kwenye kitabu chake (juz.3.uk.259) miongoni mwa matukio ya mwaka wa 23 Hijiria, kama ifuatavyo: Mwarabu anayeitwa Ganzi alimlalamikia Umar kwamba Gavana wake Abu Musa aliipeleka kesi yake kwa katibu wake Ziad Ibn Abu Sufyan, na ngano inaendelea. Umar alimuuliza Ziad alivyoitumia zawadi yake ya kwanza aliyopewa. Ziad akasema kwamba alinunua uungwana wa mama yake na akamwacha huru. Kuhusu zawadi yake ya pili alisema kwamba alinunua uungwana wa mlezi wake Ubaid. Seif katika hiyo ngano ya kubuni hapo juu alinuia kuthibitisha kwamba Ziad aliitwa 'Ziad, mwana wa Abu Sufyan', hata wakati wa Khalifa Umar, na Khalifa hakukataa kumwita Ziad 'mwana wa Abu Sufyan', hivyo, alikuwa ni Mu'awiyah,
8 al-Kamil ya Ibn Athir - Matukio ya mwaka wa 44 Hijiria; al-Istiab juz.1,uk.548-555; al-Isabah , juz.1,uk.563.
109
ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO
mtoto wa Abu Sufyan, aliyempa Ziad udugu wake (kama ilivyoelezwa hapo juu, Mu'awiyah alishutumiwa na wanahistoria kwa kitendo hiki.) Zaidi ya hayo, Seif anajaribu katika ngano yake kumlinda Ziad vilevile, pale Ziad anapomtaja Ubaid kama mlezi wake. Cha zaidi, Seif anaielezea ngano hiyo kutoka wakati wa Khalifa Umar, ili kuifanya izidi kukubalika kwa Waislam. KIINI CHA NGANO YA SEIF Seif ameiandika ngano hiyo hapo juu kutoka kwa Muhammad, Talha na Muhallab. Seif ameandika ngano 216 ambazo zimeandikwa katika Tabari kutoka kwa Seif, ambaye naye ameiandika kutoka kwa Muhammad Ibn Abdullah Ibn Sawad Ibn Malik Ibn Nuwaira, ambaye hajulikani katika vitabu vyote vya historia isipokuwa ndani ya Ikmal ambacho mwandishi wake pia ameandika kutoka kwa Seif. Kuna Talha wawili. Mmoja ni Abu Sufyan, Talha Ibn Abdurahman ambaye hakuna dalili zake zinazoopatikana. Wa pili Talha Ibn A'lam aliyeishi Jian karibu na Ray (Tehran) na Seif hakumtaja bayana katika ngano yake. Seif ameandika ngano 67 kutoka kwa Muhallab Ibn Uqba al-Asadi, ambazo pia zinazopatikana kwa Tabari, lakini hakuna dalili yake inayoweza kupatikana katika kitabu cha wasifa chochote. ILIVYOELEZWA NA WENGINE MBALI NA SEIF Al-Daynawari katika kitabu chake, The long stories, uk.14 anasema: "Abu Musa alimwona Ziad Ibn Ubaid, mtumwa wa kabila la Thaqif, ni mtu mwenye tamaa ya maendeleo ajabu na mwerevu sana, na akamwajiri kama katibu wake. Ziad alikuwa na Mughaira kabla ya hapo." Ibn Abdulbarr katika kitabu chake, al- Istiab (juz.1,uk.548), anasema, "Kabla Mu'awiyah hajampa Ziad udugu wake alikuwa akiitwa Ziad Ibn Ubaid Thaqafi." Imeandikwa pia hapo, kwamba Ziad alinunua uungwana wa baba yake Ubaid na akamwacha huru ambalo lilikuwa tendo zuri sana. Katika al-Istiab, uk. 549 kutoka kwa Ibn Abdulbarr imeandikwa hivi: "Ziad alikuwa akijulikana kama Ziad Ibn Ubaid kabla ya kuungana na Mu'awiyah," kisha inaendelea, "Ziad alitoa hotuba mbele ya Khalifa Umar katika sherehe na hotuba yake ilimshangaza kila mtu." Mmoja wa wageni, Amr bin Al-Aas akasema, "Wallah, kama kijana huyu (mzungumzaji) angetoka kwenye kabila la Quraish, angeweza kuwa ndiye mtawala.� Abu Sufyan ndipo akasema, "Ninaijua asili yake." Ali akasema, "Ni nani baba yake?" Abu Sufyan akasema, "Ni mimi." Ali kisha akasema, "Acha Abu Sufyan (kuelezea uhusiano wako na mama yake Ziad)." Kisha Abu Sufyan akatunga ubeti ufuatao: Kama ningekuwa simuogopi mtu(Umar) ningesema, Wallah, Sakhr Ibn Harb angesaliti, Na wewe Ali, kwa hakika ungeamua, Wewe mwenyewe, ujuzi wa hotuba wa Ziad ni wa kutoka upande wa nani. Wanahistoria wafuatao wameandika hii ngano ya udugu wa Ziad na 110
ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO
Mu'awiya. Ibn Athir katika matukio ya mwaka wa 44 Hijiria. Ibn Abdulbarr ndani ya al-Istiab katika wasifu wa Ziad. Yaqoubi, juz.2, uk. 195. Masoud katika Muruuj al-Dhahabi, juz.2,uk.54. Suyuti katika matukio ya mwaka wa 41 Hijiria. Ibn Kathir, juz.8, uk.28. Abul Fada, uk.194. Tabari katika juz.4,uk.259, na katika matukio ya mwaka wa 44 Hijiria, pia katika matukio ya mwaka wa 160, uk.334-335. Sahih Muslim, juz.1,uk.57. Usudul Ghaba wal Isaba, kwenye wasifa wa Ziad. Ibn Asakir, juz.5,uk.409-421. Yaqubi, juz.4,uk. 160. Wanahistoria wengine wameirejea, lakini tumeamua hapa kuifanya fupi ngano hii. HITIMISHO Wanahistoria wote wameandika kwamba: a) Zaid alizaliwa kwenye kaya ya Ubaid na mke wake muasherati Sumayya aliyepewa mimba na Abu Sufyan usiku ule alipotambulishwa kwake na mtu anayeitwa Abimaryam Selluli. b) Abu Sufyan alimsaliti Ziad mbele ya Umar. c) Mu'awiyah alimpokea Ziad kama ndugu yake. d) Waislam walimshutumu Mu'awiyah ambaye alipuuza amri ya Mtume isemayo, ''mtoto ni wa kaya ambayo mke na mume wanaishi pamoja, hata kama mke huyo alipewa mimba hiyo na mgeni.' d) Baada ya kuanguka kwa utawala wa Amawi, Ziad wakati mwingine aliitwa 'Mtoto wa Baba Yake', na nyakati zingine 'Mwana wa Sumayya (mama yake)'. Seif alitaka kuondoa mzigo huo kutoka kwa Mu'awiyah, ambaye alimtunukia udugu wake Ziad, na akabuni ngano ambamo Ziad aliitwa, 'Mwana wa Abu Sufyan' katika wakati wa Umar, nyuma kabisa kabla ya Mu'awiyah, na kwa wakati huo Ubaid aliitwa mlezi wa Ziad, na bado tunajua kwamba Ziad katika moja ya hotuba zake alikiri kuwa mwana wa Ubaid kama ilivyoandikwa katika Yaqubi, juz.2,uk.195.
111
ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO
8. NGANO YA MUGHAIRA IBN SHU'BA: KUTOKA KWA SEIF NA KWA WENGINE MBALI NA SEIF ULINGANISHO
112
ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO
NGANO YA MUGHAIRA IBN SHU'BA. Mughaira alikuwa wa Kundi la Muhajirina. Umar alimfanya Gavana wa Basra na akamfukuza baada ya kushutumiwa kwa zinaa. Alikuwa Gavana wa Kufa wakati alipofariki. Seif katika ngano inayofuata alijaribu kuonyesha kwamba lile dai la zinaa halikuwa na msingi. Tabari katika juz.3,uk.170-171, ameandika kutoka kwa Seif kwamba sababu ya Mughaira kushutumiwa kwa zinaa ilikuwa ni baadhi ya tofauti kati yake na Abubakra,9 mmoja wa mashahidi dhidi yake. Abubakra na Mughaira waliishi katika vyumba viwili vinavyotazamana. Siku moja upepo ulifungua dirisha la chumba cha Abubakra, alikuwa analifunga wakati alipomuona, kupitia dirisha la upande wa pili, Mughaira na mwanamke mgeni. Abubakra alikuwa na wageni na aliwaita waje kuona kinachofanyika kati ya Mughaira na mwanamke yule. Abubakra aliwaambia wageni wake kwamba alikuwa ni Ummu Jamil, mhudumu wa viongozi na watumishi wa serikali. Wageni wa Abubakra waliona kitu, lakini walingoja mpaka wakamuona yule mwanamke sawasawa kabla ya kukata shauri kuhusu hali hiyo. Seif sasa akizungumzia uendeshwaji wa kesi hiyo mahakamani, anasema kwamba Mughaira alimwomba Umar awadodose hawa mashahidi wanne ambao walikuwa watumwa, na akawaambia, "Mmeona nini kwangu, ama nilikuwa sina siri au mlichungulia kwenye nyumba yangu bila ruksa. Hata hivyo nilikuwa pamoja na mke wangu ambaye anafanana na Ummu-Jamil." Mashahidi wawili walieleza ngano hiyohiyo, wa tatu tofauti na wale wawili, na wa nne, Ziad akasema aliona mambo tofauti kabisa. Wale mashahidi watatu walichapwa kwa kutoa ushahidi wa uongo. Umar (Khalifa) akamwambia Mughaira, "Wallah, kama ungekuwa na hatia, ningekupiga mawe mpaka ufe." WANAHISTORIA WENGINE Ngano iliyoelezwa na wengine mbali na Seif kama ilivyoandikwa katika FutuuhulBuldan cha Baladhuri uk.423; Kitabul Ahkam cha Mawardi uk.280; Yaqubi juz.2,uk.124. Tabari na Ibn Athir miongoni mwa matukio ya mwaka wa 17 Hijiria ilikuwa kwamba Mughaira alikuwa na uhusiano na mwanamke aliyeitwa UmmuJamil, binti ya Afqam Ibn Mihjan Ibn Abi Amr Ibn Shu'ba. Alikuwa mke wa Hajaji Ibn Atik wa kabila la Thaqif. Sasa kisa chote kilichobakia kwa mujibu wa al-Aghani cha Abulfaraj, juz.14,uk.139-142: 9 Abubakra: jina lake ni Nafi mwana wa Masruh Habashi na inasemekana kwamba baba yake alikuwa akiitwa Harith Ibn Kelda Ibn Amr Ibn Alaj Ibn Abi Salma Ibn Abd al-Uzza Ibn Qais.
113
ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO
Mughaira Gavana wa Basra wa wakati wa Umar alizoea kumtembelea Raqta, mwanamke wa kabila la Thaqif, kwa siri katika nyumba yake. Mume wake alikuwa ni Hajaji Ibn Atik kutoka kabila la Thaqif. Siku moja Abubakra alikutana na Mughaira katika mtaa na akamuuliza anakokwenda. Mughaira akasema anakwenda kumuona mtu fulani. Abubakra akasema, "Gavana anakaa nyumbani na watu wanamtembelea yeye." Abubakra mara kwa mara alikuwa akimwambia Mughaira alipokuwa akimuona nje wakati wa mchana. Wanahistoria wamesema kwamba huyo mwanamke Mughaira aliyekuwa akimtembelea alikuwa jirani yake Abubakra. Siku moja, Abu bakra, ndugu zake wawili Naafi na Ziad na mtu mwingine anayeitwa Shibl Ibn Ma'bad, walikutana pamoja kuongea, mara upepo ukavuma na kufungua dirisha na wanaume hao wakamuona Mughaira katika chumba upande wa pili na mwanamke. Abubakra akawaomba wageni wake walithibitishe hili. Abubakra akangojea mpaka Mughaira alipotoka nyumbani kwa yule mwanamke na akamwambia, "Huwezi kuwa Gavana wetu tena, tumekuona na mwanamke."10 Mchana Abubakra alitaka kumzuia Mughaira kuongoza sala lakini watu waliingilia kati na kumwambia Abubakra amuandikie Umar (Khalifa) kuhusu Mughaira. Walimuandikia Umar ambaye aliamuru Mughaira na mashahidi waende Madina. Mughaira akajiandaa kwa kuondoka, na akampeleka mtumwa wa kike wa Kiarabu na mjakazi wake kama zawadi kwa Abu Musa (mwakilishi wa Umar). Hapo mahakamani Umar alimuuliza Abubakra kama alimuona Mughaira akifanya mapenzi na huyo mwanamke na Abubakra akatoa maelezo. Mughaira akasema, "Ulikuwa ukinipeleleza." Abubakra akasema, "Sikukikosa kile ambacho Mwenyezi Mungu atakuaibisha wewe." Umar alitaka maelezo zaidi, hivyo Abubakra akaelezea kile alichokiona. Pale shahidi wa pili alipoeleza kama yule wa kwanza, Umar akasema, "Mughaira nusu yako imekwenda." Shahidi wa tatu alifanya sawasawa na wale wengine wawili, kisha, Umar akasema, "Mughaira, robo tatu yako imekwenda." (Mughaira alivunjika moyo na akaomba msaada kwa kila mtu.) Mughaira alikutana na Muhajiriina na mama wa waumini (wake za Mtume) na akawaomba msaada, walimhurumia. Umar aliamuru wale mashahidi watatu watengwe, mpaka yule shahidi wa nne Ziad afike kutoka Basra. Viongozi wa Muhajirina na Masahaba wa Mtume walikusanyika Msikitini pale Ziad alipowasili. Mughira tayari alikuwa amekwisha andaa utetezi. Umar alipomuona Ziad anakuja, akasema, "Namuona mtu ambaye hatamuangusha jamaa wa kundi la Muhajirina, kama Mungu alivyoagiza." Alisema pia, "Namuona kijana ambaye hatoshuhudia chochote bali ukweli," kwa mujibu wa Muntakhab, juz.2,uk.413. Kwa mujibu wa Abulfida, juz.1,uk.171, Umar alimwambia Ziad, "Namuona mtu ambaye, nategemea, hatamfedhehesha sahaba yoyote wa Mtume wa Allah." 10 Kisa cha uzinifu wa Mughaira inasimuliwa na Ibn Jarir, Ibn Athir na Abul Fida katika Matukio ya mwaka wa 17 Hijiria.
114
ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO
Katika al-Aghani imeandikwa kwamba Uthman an-Nahdi alisema kwamba uso wa Umar ulibadilika rangi baada ya shahidi wa kwanza na uso wake ulionyesha majonzi baada ya shahidi wa pili, na uso wake ulikuwa jivu baada ya shahidi wa tatu, na Umar alipomuona Ziad anakuja akiwa amevaa nguo nyeupe alimpigia kelele, "Unajua nini, Ewe chozi la tai." Abu Uthman alipiga kelele kwa sauti kubwa sana akimuiga Umar kiasi kwamba msimuliaji alishituka sana. Mughaira akasema, "Ewe Ziad, mkumbuke Mungu na Siku ya Qiyamah. Mungu, Mtume Wake, Kitabu Chake na Mbora wa Waumini (Umar, Khalifa), wameiokoa nafsi yangu. Usiipoteze kwa kuelezea kile ambacho hukukiona." Ziad akasema, "Sikukiona walichokielezea, Ewe Mbora wa Waumini, lakini nimeona kituko cha kufedhehesha, na niliona kwamba Mughaira alikuwa hana pumzi baada ya kuhusiana na yule mwanamke." Ziad aliyakataa waliyoyaeleza wale mashahidi wengine watatu. Umar kisha akasema, "Allah Akbar. Simama Mughaira na uwachape viboko." Mughaira aliwachapa Abubakra na wale wengine wawili, viboko themanini kila mmoja. Hakim katika Mustadrak na Dhahabi, juz.3,uk.448, wanasema, "Umar akasema Allah Akbar, na akafurahia sana na akawachapa wale mashahidi watatu, lakini siyo Ziad." Imeandikwa katika Futuuhul-Buldan kwamba Shibl yule wa tatu alisema, "Shahidi mwaminifu anapata viboko licha ya hukumu ya Mwenyezi Mungu." Abubakra baada ya kuchapwa, alisema tena, "Nashuhudia kwamba Mughaira amefanya zinaa." Umar akaamuru aadhibiwe tena kwa kutoa ushahidi wa uongo. Ali akapinga akimwambia Umar, "Kama utamchapa huyo, nitampiga mawe rafiki yako (Mughaira) mpaka afe." Ali alikuwa na maana kwamba kama kauli ya pili ya Abu bakra itaruhusiwa, basi kauli hizo nne zitathibitisha kosa la Mughaira. Hivyo lazima apigwe mawe afe. Umar alimtaka Abubakra atubie. Abu bakr alimuuliza kama alitaka kumuondolea mzigo wa ushahidi wa uongo ili kumtakasa, kwa kauli yake inayofuatia, Umar alimjibu kwa kukubali. Abu bakra alisema kwamba hakutaka kutoa ushahidi mwingine zaidi. Wakati adhabu zilipokwisha, Mughaira aliwaambia wale mashahidi, "Ninamshukuru Mungu aliyewaaibisheni nyie." Umar akamwambia Mughaira, "Kimya!!, Mwenyezi Mungu apafanye pachafu hapo mahali walipokuona. Abubakra aliondoka mahali hapo huku akisema, "Wallah, sitaweza kusahau kituko hicho." Wale mashahidi wengine wawili walitubia hivyo ushahidi wao ulikubalika baadae. Abubakra alitakiwa kutoa ushahidi wake kwa ajili baadhi ya matukio mengine naye alisema, "Muombeni mtu mwingine. Abu Mughaira amevunja sifa yangu." Imeandikwa katika Al-Aghani na sherehe ya Nahj kwamba Ratqa, yule mwanamke katika suala la Mughaira kule Basra alikuwa akimtembelea Mughaira huko Kufa 115
ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO
pia. Umar safari moja alimuona Ratqa wakati wa hijja huko Makkah. Mughaira alikuwepo pia. Umar alimuuliza Mughaira kama alikuwa anamfahamu yule mwanamke. Mughaira akasema kwamba alikuwa ni Ummu Kulthum (mke wa Umar). Umar akamwambia Mughaira, "Ole wako, unanifanya mimi mjinga. Wallah, nina hakika Abubakra alikuwa na haki. Nina wasiwasi ninapokuona wewe, jiwe huniangukia kutoka mbinguni." Hassan Ibn Thabit alitunga beti zifuatazo: Kuzungumzia ukatili, ninayo imani thabiti, Kwamba ukatili halisi unatokana na kabila la Thaqif. Yule mtu mwenye jicho-moja aliyeuacha Uislam na akaanguka, Asubuhi moja ndani juu ya mwanamwali aliyefunikwa shali. Alidhani kwamba yuko kwenye upeo wa urijali, Akicheza na wasichana watumwa katika hali ya uchumba. Baladhuri katika Futuuhul-Buldan, uk.343 ameandika kwamba wakati Umar alipotaka kumfanya Mughaira kuwa Gavana wa Kufa, alimuuliza kama atarudia yale yaliyosemwa juu yake. Mughaira akasema, "Hapana." Hamawi katika juz.1,uk.642; Mustadrak, juz.3,uk.449; Wafaiat, juz.2,uk.455 na juz.5,uk.406; na Ibn Kathir, juz.7,uk.281, wameutaja ufuska wa Mughaira. ASILI YA NGANO YA SEIF Seif ameandika kutoka kwa Muhammad, Talha, Muhallah na Amr. Tumeelezea uongo wa hawa watatu wa kwanza katika ngano iliyopita. Seif amesimulia ngano sita kutoka kwa Amr Ibn Zian au Amr Ibn Rayyan mtu bandia wa kubuniwa na Seif kwa mujibu wa Mizanul-Itidal. HITIMISHO Seif alitaka kumuweka huru Mughaira kutokana na ile lawama ya ufuska kwa sababu aliteuliwa kuwa Gavana wa Khalifa. Ndipo akaigeuza kwa hila ile kadhia ya kweli ya ufuska iliyoandikwa na wanahistoria wengine wengi. Anasema Abubakra aliishi kwenye chumba mkabala na kile cha Mughaira na alimuona kupitia dirishani Ummu-Jamil chini ya Mughaira kisha akawataka wageni wake kulishuhudia hilo. Waliamua kumshutumu Mughaira lakini Mughaira na Umar wakawahoji mashahidi wale na kuthibitisha kwamba ushahidi wao ulihitilafiana. Seif pia anasema kwamba Umar alimwambia Mughaira, "Kama hatia yako ingethibitishwa, ningekupiga mawe mpaka ukafa." Wanahistoria mbali na Seif wameiandika ngano hii kinyume kama tulivyoandika. Kuigeuza ngano kumpendelea Mughaira aliye Gavana, Seif aliunda wapokezi na Tabari ameandika kutoka kwa Seif.
116
ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO
9. KIFUNGO CHA ABU MAHJAN KILIVYOSIMULIWA NA SEIF KUTOKA KWA WENGINE MBALI NA SEIF ULINGANISHO
117
ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO
KIFUNGO CHA ABU MAHJAN Abu Mahjan mtoto wa Habib Ibn Amr Ibn Umar, alikuwa katoka kabila la Thaqif. Alikuwa ni mshairi na mtu mwerevu sana. Aliingia Uislam wakati kabila lake lilipoukubali Uislam. Alikuwa mlevi na Umar alimpiga viboko mara saba au tisa kwa ajili ya ulevi. Kwa mujibu wa al-Aghani, juz.21,uk.142 watu wachache walipatikana walevi na walikamatwa. Umar aliwaambia, "Mmekunywa mvinyo na mnajua kwamba Allah na Mtume Wake wameukataza." Wakasema kwamba Mungu hajaukataza, na imeandikwa ndani ya Qur'ani kwamba waumini ambao ni wachamungu na wanaofanya amali njema hawawezi kuwa na hatia ya kula ama kunywa chochote. Umar aliwauliza wafuasi wake kuhusu maoni yao. Hawakuweza kufikia uamuzi wowote ule. Alimtuma mtu kwa Ali Ibn Abi Talib kutaka maoni yake. Ali alisema kwamba kulingana na watuhumiwa, tafsiri ya Qur'ani, basi si damu, mnyama mfu wala nguruwe imekatazwa. Umar alimuuliza Ali nini angewafanya hao? Ali akasema kwamba kama wanasema pombe haijakatazwa, ni lazima wauawe. Lakini kama watasema pombe imekatazwa na wameinywa, wapigwe viboko. Wale watuhumiwa walikubali kwamba pombe imekatazwa, hivyo walipigwa viboko. Pale Abu Mahjan alipopigwa alitunga beti zifuatazo: Katika dunia hii isiyo na uhakika mtu hawezi kupigana, Kulilia maziwa yaliyomwagika hakuwezi kuweka mambo sawa. Nimestahimili kwa uvumilivu kule kupotelewa na ndugu zangu, Lakini hata kwa siku moja sintastahimili kuipoteza pombe. Kwa kuipiga marufuku pombe, huyu bwana wa waumini ametufanya wanyonge. Tunakusanyika na kulia katika chumba ambamo zabibu inakamuliwa. Pale Abu Mahjan aliposema kwamba hata kwa siku moja hawezi kustahimili kuacha pombe, Umar akasema, "Umeifichua siri yako. Nitakuadhibu zaidi kwa sababu una shauku sana ya kunywa pombe." Ali akasema kwamba mtu asiadhibiwe kwa kitu ambacho hajakitenda, na akasoma kifungu kifuatacho cha Qur'ani: "Wanakiri (washairi) kwa kitu ambacho hawajakifanya." Umar akasoma sehemu ya Aya iliyobakia, "Ila wale walioamini na kufanya amali njema." Ali akamwambia Umar, "Unadhani ni waumini, ambapo Mtume wa Allah amesema kwamba pale mtu anapokunywa hawi muumini." Kulingana na al-Isaba, wakati mmoja Umar alifikiri Abu Mahjan alikuwa amelewa na akadai aruhusiwe kunusa pumzi zake. Abu Mahjan akasema, "Kufanya uchukunguzi kumekatazwa" na Umar akamuacha. Tabari katika juz.4,uk.152 miongoni mwa kadhia za mwaka wa 14 Hijiria anasema kwamba Umar aliwaadhibu baadhi ya wafuasi wake, mwanae na Abu Mahjan kwa sababu walikunywa pombe. Ibn Kathir katika juz.7,uk.48 anasema, "Abu Mahjan Thaqafi alipigwa viboko mara 118
ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO
saba kwa kulewa." Imeandikwa ndani ya Aqdulfarid kwamba miongoni mwa watu wa daraja la juu ambao wameadhibiwa kwa kulewa alikuwa ni Abu Mahjan, mlevi wa uhakika. Kwa mujibu wa al-Isaba na al-Aghani, Abu Mahjan alimpenda bibi mmoja aliyeitwa Shamus. Alijaribu bila mafanikio kuonana naye. Jirani wa bibi huyo alikuwa na mkandarasi ndani ya nyumba yake, Abu Mahjan alipata kazi kwa mkandarasi huyo ndipo akamuona bibi huyo kutoka juu ya ukuta. Kisha akatunga beti zifuatazo: Nilimuangalia Shamus ingawa Mungu amekataza, Kumuangalia mwanamke ambaye alipasa awe amefichwa. Kama mkulima anayekuja mjini kwa ajili ya likizo, Baada ya kuuza mazao yake, alikuwa mwenye furaha na bashasha. Mume wa Shamous alilalamika kwa Umar. Umar akampeleka Abu Mahjan uhamishoni huko Hazouzi,11 chini ya uangalizi wa Jahra al-Nasri na mtu mwingine. Umar aliwaambia walinzi hao wasimruhusu Abu Mahjan kubeba upanga wake. Abu Mahjan akauficha upanga wake katika mfuko wa unga, na hapo ufukweni kabla hajapanda chomboni alinunua kondoo na akafanya karamu kwa ajili ya walinzi wake. Kabla ya mlo, Abu Mahjan akajifanya kama anachukua unga atengeneze mkate. Aliutoa upanga wake kutoka kwenye mfuko ule, Jahra akauona na akakimbilia kwenye ngamia wake, akampanda na kwenda kwa Khalifa Umar kumuelezea kisa chake. Kulingana na al-Isaba na Istiab baada ya kuhamishwa Abu Mahjan alikwenda mpakani na Uajemi chini ya uangalizi wa Sa'd Ibn Waqqas. Ilikuwa ni Vita vya Qadisyya, Muhammad mtoto wa Sa'd alisema kwamba baba yake alimuweka Abu Mahjan minyororo kwa sababu alikuwa amelewa. Sa'd hakuwa mzima siku hiyo na Khalid Ibn Orfota aliliongoza jeshi, na Sa'd alikuwa amesimama juu ya kilima kuuangalia uwanja wa mapambano. Abu Mahjan ambaye alikuwa amefungwa pingu alitunga ubeti ufuatao: Ni huzuni iliyoje kufungwa katika minyororo. Na kuangalia watu wakitumia mikuki yao tena na tena. Kisha akamuomba Salmi, mke wa kamanda Sa'd, kumfungulia na kuahidi kama atapona, kurudi na kufungwa minyororo tena, na kama atakuwa ameuawa watakuwa wameondokana naye. Salmi akaiondoa minyororo mikononi na miguuni mwa Abu Mahjan. Kisha akarukia juu ya mgongo wa Balqa, farasi wa Sa'd akiwa na mkuki mkononi mwake. Aliwashambulia maadui. Askari walifikiria alikuwa ni malaika. Sa'd aliyaona mashambulizi ya mpanda farasi na akasema, "Ile miruko ni sawa na miruko ya farasi wangu (Balqa) na lile shambulizi la mkuki ni sawa na shambulizi la Abu Mahjan, ila kwamba Abu Mahjan amefungiwa.� 11 Hazouzi: Jina la mlima katika kisiwa ambamo watu walikuwa wakipelekwa uhamishoni wakati huo.
119
ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO
Adui aliposhindwa, Abu Mahjan alirudi. Wakaweka tena zile nyororo mikononi na miguuni mwake. Mkewe Sa'd akamuelezea Sa'd kile kisa cha Abu Mahjan. Kisha Sa'd akasema, "Wallah sitamuadhibu mtu yule kwa ulevi ambapo alileta ushindi kwa Waislam." Ndipo tena akaamuru Abu Mahjan aachiliwe huru. Abu Mahjan akasema, "Nilikuwa nikiipokea ile adhabu kama toba, sasa kwa sababu huniadhibu, sitakunywa tena." SIMULIZI YA SEIF Tabari katika juz.3,uk.43, anasema kwamba Sa'd aliwafunga wale watu waliokunywa mvinyo na kufanya matata. Sa'd aliwafedhehesha kwa kusema, "Kama tusingekuwa kwenye uwanja wa vita, ningewafundisheni somo ambalo wengine wangelijifunza kutokana nalo." Abu Mahjan alikuwa mmoja wao ambaye mikono na miguu yake ilikuwa imefungwa minyororo. Tabari katika juz.3,uk.55-57, anasema kwamba baada ya mke wa Sa'd kumfungulia Abu Mahjan na akapigana na maadui alirudi tena kule jela, na wakamfunga minyororo. Mkewe Sa'd alimuuliza Abu Mahjan ni kwa nini alikuwa kifungoni? Alisema, "Nilikuwa nikinywa mvinyo kabla ya kuingia Uislam. Sasa ninatunga beti za kuusifu mvinyo. Sa'd hapendi kwa hiyo ananifunga." Salmi alimwambia mumewe Sa'd kile Abu Mahjan alichokisema, hivyo Sa'd alimtoa jela, na akamwambia, " Sitakuadhibu kwa ajili tu ya kuzungumza kuhusu dhambi." Abu Mahjan akaapia kwamba hataongea mambo ambayo siyo mazuri. Abulfaraj katika al-Aghani, juz.2 ameiandika ngano hii iliyosimuliwa na Seif kutoka kwa Tabari. Ibn Hajar katika al-Isaba, juz.4,uk.175 anasema kwamba Fat'houn alimshutumu Abu Amr aliyeandika kwenye Istiab (kama ilivyotajwa kabla) kwamba Abu Mahjan mara nyingi alikuwa amelewa. Ilitosha kusema tu kwamba aliadhibiwa kwa ulevi. Ingekuwa vizuri kusema kile ambacho Seif amekiandika. Ibn Hajar kisha anaendelea kusema, "Seif ni dhaifu (asiyetegemewa) lakini tulichokiandika kina nguvu na kinajulikana sana." Ibn Fat'houn anakataa kwamba Sa'd alizembea kumuadhibu mlevi yoyote, na alibadili kile alichosema Sa'd, "Sitamuadhibu Abu Mahjan kwa ulevi," kuwa "Abu Mahjan hatakunywa tena kuweza kuadhibiwa." Masudi katika juz.2,uk.422-424 Muruuj al-Dhahabi, amenakili alichosimulia Seif bila ya kutaja jina la Seif. Lakini tunajua Masoudi ameandika kutoka kwa Tabari kwani alimtukuza sana Tabari mwanzoni mwa kitabu chake. ASILI YA NGANO YA SEIF Seif ameandika ngano hii kutoka kwa Muhammad, Talha, Ziad na Ibn Mihraq. Hawa wawili wa kwanza ni wale wale watu wa uongo tuliowataja katika ngano zilizopita. Seif amesimulia mara 53 ndani ya Tabari kutoka kwa Ziad ambaye hajulikani kwa waandishi wa wasifu kama alivyo Ibn Mihraq. 120
ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO
HITIMISHO Seif alitaka kumkosha Sa'd rafiki na Gavana wa Khalifa kutokana na kutotekeleza adhabu ya kidini juu ya mlevi. Kisha alibuni yale maongezi kati ya Abu Mahjan huyu mlevi na mke wa Sa'd aliyemfungulia kutoka kifungoni. Seif anasema kwamba mke wa Sa'd alimuuliza Abu Mahjan ni kwa nini Sa'd alimuweka kifungoni. Abu Mahjan alijibu kwamba ni kwa sababu aliongea upuuzi, na siyo kwa sababu alikunywa pombe. Lakini Muhammad, mtoto wa Sa'd, ameandika kwamba Abu Mahjan alimwambia mama yake, wakati alipomfungulia kwamba kama angeuawa katika ile vita wangekuwa wameondokana naye. Inavyoonekana, huyu mke wa kamanda Sa'd, aliijua rekodi ya nyuma ya Abu Mahjan, na bila shaka, na zile adhabu za mumewe zilizotolewa kwa Abu Mahjan kwa ulevi wake. Lakini Seif amesema kwamba Sa'd alimwachia Abu Mahjan akisema hatamuadhibu kwa kitu ambacho hakukifanya bali alikiongelea tu. Kisha Abu Mahjan anasema, "Sitaongea upuuzi tena." Ibn Fat'houn pia kwa kumpendelea Khalifa aliichagua ile ngano ya Abu Mahjan iliyosimuliwa na Seif. Masoudi yule mwanahistoria msomi anayeaminika akimfuata Tabari ameandika kile Seif alichosimulia. "Mwanadamu anaweza kufanya makosa." Hata hivyo, Seif na wale walioandika kutoka kwake hawawezi kuuficha ukweli.
121
ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO
10. SIKU ZA SEIF SIKU YA NG'OMBE ARMATH AQWAS IMAS JARATHIM: KUTOKA KWA SEIF KWA WENGINE MBALI NA SEIF ULINGANISHO
122
ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO
SIKU ZA SEIF Waarabu wanaiita siku ya tukio kama vile: Siku ya Jamal, Siku ya Siffin, Siku ya Hudaybia, kwa siku moja au zaidi ya moja kulingana na idadi ya siku ambazo tukio limechukua. Kwa hiyo, Siku ya Jamal, ina maana ile kadhia ya Vita vya Jamal. Seif amebuni baadhi ya matukio ambayo ameyaandika kama "Siku ya Kadha na Kadha", kama ile "Siku ya wale Ng'ombe", Siku ya Armath, Siku ya Jarathim. A - SIKU YA NG'OMBE Tabari katika juz.3,uk.12-14, ameandika kutoka kwa Seif kwamba Sa'd, alipokuwa akipigana na Waajemi, alifika sehemu inayoitwa Uzaibul Hijanat, karibu na Mto Furati (Euphrates). Alimtuma Asim Ibn Amr kwenda kununua kondoo au ng'ombe huko Maysan mji ulioko karibu na mto huo. Asim hakuona chochote kwa sababu watu hao waliwaficha ng'ombe wao. Lakini alikutana na mtu karibu na msitu na akamuuliza kuhusu kondoo au ng'ombe. Yule mtu aliapa kwamba hakujua pa kuwapata, ingawa alikuwa mchungaji wa kondoo. Mara ng'ombe mmoja akalia, "Wallah, anadanganya, tupo hapa." Hapo Asim akaingia kule msituni, akawaona ng'ombe na akawaleta kambini. Sa'd akaiandaa karamu na akaigawa miongoni mwa vikosi. Hajjaj baadae alizijua habari za kadhia hiyo na akaagizia apate mtu aliyekuwepo wakati ule na mahali pale. Nazir Ibn Abdshams na Zahir walimwambia Hajjaj kwamba walikuwepo wakati kadhia hiyo ilipotokea. Hajjaj mwanzoni hakuwaamini. Wakasema kwamba wao wasingeamini pia kama wasingeiona. Ndipo Hajjaj akashawishika kwamba walikuwa wanasema kweli na akawauliza watu walisema nini wakati huo? Wakasema kwamba watu waliichukulia kama ishara kutoka kwa Mungu, wakimaanisha radhi ya Mwenyezi Mungu na ushindi dhidi ya adui. Hajjaj basi akasema, "Namna hii ya tukio hutokea tu kwa watu waadilifu." Seif kwa hiyo anasema, "Hii ilikuwa ni Siku ya Ng'ombe". Mwana historia mwingine pekee mbali na Seif anayerejea kwenye tukio hili ni Baladhuri ambaye katika Futuuhul-Buldan, uk.314 anaeleza kwamba, lile jeshi la Sa'd lilipotaka mahitaji alituma kikosi kando ya mto kwenda kupora, mahitaji mengine yalikuja kutoka kwa Khalifa Umar aliyewatumia kondoo na ng'ombe kutoka Madina. VYANZO VYA NGANO YA SEIF Seif ameiandika ngano hii kutoka kwa Abdullah Ibn Muslim al-Okli na Karb Ibn Abi Karb al-Okli ambao majina yao hayamo kwenye vitabu vyovyote vya wasifu.
123
ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO
HITIMISHO Seif amebuni hii ngano ya ng'ombe na kuithibitisha kwa uchunguzi wa Hajjaj, na kubuni hilo jina kwa kuiita: Siku ya Ng'ombe. Seif hakutaka kuikosa fursa ya kubuni 'Siku' sawasawa na matukio ya kweli. B- SIKU ZA ARMATH, AQWAS NA IMAS Kulikuwa na mapigano yaliyoandaliwa huko Qadisyya kati ya Waislam na Waajemi kwa siku tatu. Seif aliita ile siku ya kwanza, Siku ya Armath, ya pili, Siku ya Aqwas, na ya tatu, Siku ya Imas. Amebuni mashujaa wa kabila lake mwenyewe la Tamim, kama vile ndugu wawili Qa'qa na Asim. Tabari ameziandika ngano za Seif na wanahistoria, Ibn Athir na Ibn Kathir wakanakili kutoka kwa Tabari. Hamawi pia amenukuu maandishi ya Tabari kuelezea maneno Armath, Aqwas na Emas. Ibn Abdun katika shairi lake, "Ibn Badroon" katika sherehe yake ya mashairi haya na Qalwashandi katika kitabu chake The days of Islam - siku za Uislam, ametumia ubunifu wa Seif wa siku hizo tatu hapo juu. Katika kitabu changu 'Masahaba mia moja na hamsini wa kubuni' (Masahaba wa Mtume), nimetoa maelezo zaidi juu ya siku hizo tatu chini ya majina ya Asim na Qa'qa. CHANZO CHA NGANO YA SEIF Seif ameziandika hizi Siku kutoka kwa Muhammad, Talha, Ziad na Ibn Mihraq wakisimulia kutoka kwa mtu wa Kabila la Tay na Ghosn akisimulia kutoka kwa mtu wa Kabila la Kanana. Tumesema hapo kabla kwamba Muhammad, Talha, Mihraq na Ziad walikuwa ni wapokezi bandia wa Seif. Seif ameandika ngano kumi na tatu kutoka kwa Ghosn ambaye kwamba hatuwezi kuona dalili zozote katika vitabu vya wasifu, na hatujui ni nani huyu mtu asiyetajwa jina wa kutoka Kabila la Kanana. C - SIKU YA JARATHIM Tabari ameandika ngano kumi na tano kutoka kwa Seif kuhusu kule kuvukwa kwa Mto Tigris na Sa'd. Hii ni ngano iliyoandikwa na Seif kwa ufupi: Baada ya Vita vya Qadisyya, jeshi la Waislam lilikusudia kuiteka Madain (makao makuu ya Uajemi). Sa'd, yule kamanda alitoa hotuba hapo kambini karibu na Mto Tigris (Dajla) na akawatahadharisha Waislam juu ya mashambulizi ya maadui kutoka kule mtoni. Aliwaambia kwamba yeye aliamua kuuvuka mto ule. Akauliza, "Nani yuko tayari kuongoza mashambulizi haya?" Asim Ibn Amr akasema kwamba yeye atakuwa wa mwanzo kushambulia. Asim pamoja na watu sitini wakaogelea mtoni, na wakapigana na adui na wakauteka ule upande mwingine wa mto. Kisha jeshi lote la Waislam likavuka ule mto. Mto ulikuwa umechafuka, lakini askari hao walikuwa wakiongea mmoja na mwingine kana kwamba wanatembea katika ardhi. Wakati wowote farasi akiwa amechoka, ile ardhi chini ya mto ilinyanyuka chini ya miguu yake, hivyo farasi huyo akasimama juu yake na kurudisha pumzi zake. Hakuna kitu cha ajabu zaidi kuliko hiki katika hii Siku ya Vita vya Madain. Hii 124
ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO
Siku ya Maji inayoitwa Siku ya Jarathim, ikimaanisha Siku ya Kilima Kidogo. Iliitwa Jarathim kwa sababu hakuna aliyechoka,na kwa sababu kilima kidogo kilinyanyuka chini ya miguu yake ili kwamba aweze kupata mapumziko. Seif alisimulia kutoka chanzo kingine kwamba askari mmoja alisema, "Tuliogelea katika mto huo na maji marefu sana yalifikia kwenye tumbo la farasi wakati wowote mpanda farasi aliposimama kwa ajili ya mapumziko. Mahali pengine Seif anasema kwamba wote walivuka mto huo ila mtu aliyeitwa Gharqdeh (ikimaanisha kuzama maji) aliyeanguka kutoka kwenye farasi wake. Mpokezi anasema kwamba inaelekea kwamba alimuona farasi wake akikung'uta maji kutoka kwenye manyoya ya shingoni mwake na mtu huyo akielea. Qa'qa alimvutia ukingoni na kumuokoa. Baada ya kuwa ameokolewa mama yake Qa'qa alimwambia Qa'qa, "Hakuna dada aliyezaa shujaa kama wewe." Abu Naim ametaja baadhi ya sehemu za historia hiyo hapo juu katika kitabu chake The Signs of the Apostleship (Ishara za Unabii), na akazihesabu kama ushahidi wa utume wa Mtume wa Uislam. CHANZO CHA NGANO YA SEIF Seif ameandika kutoka kwa Muhammad, Talha, Muhallab, Nazr Ibn Rufail na mtu asiyejulikana. Baadhi ya wapokezi hawa tuliwataja hapo kabla. Tabari ameandika ngano sitini na saba za Seif kutoka kwa Muhallab, Ibn Oghbeh Asadi, na ngano ishirini na nne za Seif kutoka kwa Ibn Rufail. Hakuna dalili za wapokezi hawa zinazoweza kuonekana katika vitabu vyovyote vya wasifu. Ngano za Seif kutoka kwa mtu asiye na jina ni dhahiri kwamba sizo za kweli. Vita ya Madain kwa mujibu wa wengine mbali na Seif. Hamawi katika juz.4,uk.33, Mu'jamul-Buldan anasema, "Wakulima wa Kiajemi walilisaidia jeshi la Waislam kwa kuwaonyesha sehemu za udhaifu wa Waajemi, kuwapa zawadi na mahitaji. Khalid Ibn Arfata aliwashambulia Waajemi bila mafanikio. Baadae Khalid Ibn Sabat aliiteka Madaen. Lile jeshi la Waislam lilielekezwa kwenye sehemu nyembamba za mto huo, hivyo wakavuka kutokea hapo." Katika Futuuhul-Buldan uk.323 anasema, "Jeshi la Waajemi liliwatupia mishale Waislam, lakini hakuna hata mmoja aliyeuawa ila askari mmoja kutoka Kabila la Tay aliyeitwa Salili Ibn Yazid Ibn Malik Sanbesya." HITIMISHO Seif alimfanya Asim kutoka kwenye kabila lake mwenyewe, ingawa ni wa bandia, kuwa ndiye shujaa wa ngano hii. Pia alisema, "Farasi yoyote aliyechoka, kilima kilitokea chini ya miguu yake." Lakini mtu alianguka kutoka kwenye farasi wake, na ile ardhi chini ya mto haikunyanyuka chini ya miguu yake, kwa sababu Qa'qa yule ndugu yake Asim alikuwa jirani kumuokoa. Askari wale waliuvuka mto kwa muujiza, kwa mujibu wa Seif. Lakini kwa mujibu wa wengine muongozaji aliwaonyesha 125
ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO
sehemu yenye kina kifupi cha maji, ukanda mwembamba au ukanda wa ardhi. Uharibifu mkubwa uliofanywa na Seif kwenye historia ya Uislam ni ubuniaji wake wa Masahaba (wa Mtume). Amewataja majina yao kwenye matukio ya uzushi na ya kweli, yaliyopotoshwa kwa njia moja au nyingine. Wanahistoria wamenakili majina ya Masahaba bandia wa Seif na ngano katika vitabu vyao, na Waislam wamelichukulia kwa uzito, na kuamini kwamba hawa watu wa kubuni walikuwa hasa ni masahaba wa Mtume. Ibn Abdulbirr katika kitabu chake al-Istiab, ameandika majina ya watu hawa na anasema, "Hawa ni masahaba wa Mtume baadhi yao wamekutana naye Mtume, wengine wamemuandikia au wametuma zaka zao kwake. Mtu yeyote ambaye jina lake limeandikwa katika tukio lolote linalomhusu Mtume limeorodheshwa. Hapa hata wale ambao majina yao na mashina ya koo zao hayakujulikana na hakuna hata mmoja aliyewajua ila kupitia kwa jamaa zao wa mbali." Seif amebuni watu wengi na amebadili majina au sifa za baadhi ya watu wanaojulikana vema, ili kupotosha mambo, mafundisho ya Mtume, na kuwadanganya watafiti na wanazuoni katika juhudi zao za kunakili matukio ya kweli. Baada ya miaka mingi ya kazi ngumu na kwa utafiti katika takriban vitabu vyote vya historia ambavyo vimenakili matukio katika siku za mwanzo za Uislam, nimeweza kuja na ngano za uongo na majina yaliyobuniwa na Seif, lenye uharibifu zaidi ya yote, likiwa ni ule ubuniaji wa Masahaba. Majina mia moja na hamsini ya Masahaba (wa Mtume) wa uongo waliobuniwa na Seif yameorodheshwa katika kile kitabu 'Hundred and Fifty Invented Sahabis' - Masahaba Mia na Hamsini wa Kubuni.
126
ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO
11. MASHAURIANO NA KIAPO CHA UTII KWA UTHMAN KAMA ILIVYOSIMULIWA NA SEIF NA WENGINE MBALI NA SEIF ULINGANISHO
127
ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO
MASHAURIANO NA KIAPO CHA UTII KWA UTHMAN Imeandikwa katika Tabari juz.3,uk.292 miongoni mwa kadhia za mwaka wa 23 Hijiria ikinakiliwa kutoka kwa Seif kwamba Umar alisema, "Nina hakika kwamba watu maarufu sana miongoni mwa Waislam hawa wawili (Ali na Uthman) - Mtume wa Mwenyezi Mungu alikuwa akiwasomea wao kile ambacho Jibril alimshushia kutoka kwa Allah." Katika kurasa za 266 na 305, kuhusu matukio ya mwaka wa 24 Hijiria imeandikwa hivi: "Katika siku ya tatu ya Muharram, Uthman alishinda kura za washauri wakati wa mchana. Wakati adhana yaSwala ya mchana ilipopigwa, Uthman alitoka nje ya chumba cha mikutano na kuongoza Swala." Tabari anaandika kutoka kwa Seif pia kwenye uk.305 kwamba pale wajumbe wa ushauri walipopiga kura kwa upande wa Uthman, alitoka nje ya ukumbi wa mikutano akionekana mwenye huzuni sana na akapanda kwenye mimbari ya Mtume, na akatoa hotuba. Baada ya kumshukuru Mungu na kumtakia rehma Mtume, alisema, "Enyi watu, mpo katika nyumba ambayo ina msingi dhaifu sana, ukiwapeni ukumbusho wa wakati wa uhai wenu. Kabla kifo hakijawakuteni, fanyeni amali njema, kwa sababu kifo kinakuja ghafla wakati wa mchana au usiku. Msiache shetani akawadanganyeni, msiyachukulie maisha kwa uhakika. Chukueni tahadhari kwa wale waliokufa kabla yenu. Msipoteze muda wenu bure. Jaribuni kadiri ya uwezo wenu. Hamtasahauliwa (mbele ya Allah). Wako wapi baba zenu na ndugu zenu waliolima ardhi hii kabla yenu, na wakaiacha? Lengo lenu liwe wokovu wenu. Allah ametoa mfano kwa maisha haya ya sasa na akasema, 'Wapigie mfano kuhusu maisha haya, yako kama mvua ambayo mimea ya kijani hustawi kama matokeo ya mvua.'" Kisha akasoma mpaka mwisho wa aya hii. Ndipo watu wakaja mbele na kumpa mkono kama wafuasi wake. NGANO YA MASHAURIANO KUTOKA KWA WENGINE MBALI NA SEIF (Umar Khalifa wa Pili, aliteua watu sita kukutana na kuchagua Khalifa wa Tatu miongoni mwao wao wenyewe.). Ibn Hisham katika kitabu chake As-syra juz.4,uk.334-337 amenakili kutoka kwa Abdulrahman Ibn Auf kwamba wakati wa Hijja huko Mina, mtu mmoja alimwambia Umar kwamba mtu mmoja alimwambia, "Kama Umar atakufa atamuidhinisha mtu fulani wa fulani kama Khalifa, pia uchaguzi wa Abubakr ulikuwa wa ghafla na kosa ingawa ulifanikiwa." Umar alimjibu kwa hasira, "Nitalishughulikia jambo hili usiku wa leo, na kuwaonya wale wanaotaka kupora huu urithi wa Mtume, Mungu Akipenda." Abdulrahman alimshauri Umar kuahirisha uamuzi wake mpaka warudi Madina kwa sababu walikuwepo watu wa aina zote katika Hija, lakini watu wakubwa na wanazuoni waliishi Madina. Umar alikubali na walipofika Madina katika Ijumaa ya kwanza, Umar alitoa hotuba na akasema, "Nilielewa kwamba mtu mmoja alisema kwamba kama Umar atakufa atamuidhinisha Fulani kama Khalifa. 128
ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO
Msiufanye ule usemi, 'uchaguzi wa Abubakr ulikuwa wa ghafla na kosa, lakini ulifanikiwa' ukawadanganyeni. Hata hivyo ndivyo ilivyokuwa, lakini Mungu alitulinda. Kumbukeni hakuna aliyekuwa maarufu kati yenu kama Abubakr. Mtu yeyote anayetoa mkono wa kiapo kwa mtu yeyote bila ya kushauriana na Waislam, anaonyesha kiapo chake hakina thamani, na watu wote hao ni lazima wauawe." Sehemu ya ngano hiyo hapo juu na maoni ya Umar yametajwa kabla pale tulipoelezea, "Watu walitafuta kimbilio kwenye nyumba ya Fatimah." Ibn AbilHadid, katika juz.2,uk.123 aliandika kutoka kwa Jahiz kwamba Ammar Ibn Yasir alisema kwamba baada ya Umar atamchagua Ali. Hii ilimfanya Umar awahutubie watu wa Madina akisema, "Watu wengine wanasema Talha Ibn Ubaidullah ndiye mgombea. Haileti tofauti yoyote kuwa mgombea ni nani, lakini jambo ni kwamba Mtume hakuwaamuru watu wake kuchagua Khalifa, na yule Khalifa wa kwanza pia, aliingia madarakani kwa uamuzi wa haraka na wenye pupa." Kwa neno moja uchaguzi wa Khalifa haukuwa ni desturi katika Uislam. Ni |Umar tu aliyeamua kuteua watu sita waliomchagua Khalifa wa tatu miongoni mwa wenyewe. Uamuzi wa Umar ulipangwa kabla ya kupigwa kwake upanga uliomuua, . Tutaona baadae kama Umar alikuwa na mtu mawazoni mwake kama mrithi wake au la. USHAURI NA UMAR Imeandikwa katika al-Ansabul Ashraf ya Baladhuri,uk.15-16 na Tabaqat ya Ibn Sa'd juz.3, uk.243, kwamba Umar alitoa hotuba siku ya Ijumaa, na baada ya kumshukuru Mungu na kumtakia rehma Mtume akasema, "Nimeota kijogoo kikinidonoa. Nadhani kifo changu kimekaribia. Watu wananiomba niteue mrithi. Mungu hataipuuza dini Yake, au Khalifa na madhumuni ya kumleta Kwake Mtume. Baada ya kufa kwangu, huyo Khalifa atachaguliwa na washauri sita. Mtume aliwafurahikia kabla hajafa. Ninajua watu wengine watanilaumu kwa kuchukua uamuzi huu. Watakuwa ni wale niliowashawishi kuukumbatia Uislam. Wale wanaopinga ni maadui wa Mwenyezi Mungu." Imeandikwa katika Iqdul-Faraid juz.3,uk.73, kwamba wakati Umar alipodungwa, watu walimtaka ateue mrithi. Yeye alisema, "Mtu bora kuliko mimi hakuchagua mtu na mwingine bora kuliko mimi hakuchagua mtu (alimaanisha Mtume na Abubakr). Abu Ubaidah asingekufa, ningemteua yeye kwani alikuwa ni mtu wa kuaminiwa kama Mtume alivyosema. Pia kama Salim yule huru wa Abu Hudhaifa angekuwa hai ningemteua kwa sababu alimpenda sana Mungu kiasi kwamba hakufikiri kamwe kutenda dhambi, hata bila ya hofu kutoka kwa Mungu." Umar aliombwa kumteua mwanae. Akasema kwamba inatosha kwamba Khatab mmoja anawajibika kwa Allah. Alitamani kama angekuwa huru mbele ya Allah, kuweka sawa mazuri na mabaya. Kisha akasema kwamba alitaka kuteua mtu wa kuwaongoza kwenye njia ya haki na akamnyooshea kidole Ali, lakini akasema kwamba bora asimchague, kwa sababu hakutaka kuchukua jukumu katika maisha haya, na yajayo. Baladhuri ameandika katika Ansabul Ashraf juz.5,uk.16, kwamba Amr Ibn 129
ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO
Maimoun alisema kwamba kwa kweli alimuona Umar akichomwa upanga na akamsikia akisema, "Nileteeni Ali, Uthman, Talha, Zubair, Abdulrahman Ibn Auf na Sa'd Ibn Waqqas." Akamwambia Ali, "Watu wanaweza kutambua kwamba wewe ni binamu ya Mtume na mkwe wake, na u mwenye elimu katika Uislam. Ukiwatawala watu hawa umuogope Mungu." Akamwambia Uthman, "Watu wanaweza kutambua kwamba wewe ni mkwewe Mtume, na u mtu mzima. Ukiwatawala watu hawa umuogope Mungu na usiwaache (ndugu zako) ukoo wa Mu'awiyyah kuwamudu watu." Kisha akamuita Suhaib, na akamwambia kwamba aongoze Swala kwa siku tatu na awaweke hawa watu (sita) wakiwa wamefungiwa ndani ya ukumbi wa mikutano kwa mashauriano. Kama kwa kauli moja watamchagua Khalifa, yeyote ambaye hakumuunga mkono akatwe kichwa chake. Walipoondoka (wale sita na Suhaib), Umar akasema, "Kama watamuacha yule kipara (alimaanisha Ali ambaye hakuwa na nywele za mbele ya kichwa chake) atawale, atawaongoza watu vizuri." Mwanae (Ibn Umar) akamwambia, "Basi mteue yeye." Akajibu kwamba hakutaka kuchukua hilo jukumu. Katika Riadhun-Nadhira juz.2,uk.72, baada ya usemi huo hapo juu wa Umar kuhusu Ali, imeandikwa kwamba Umar alisema, "Kama watu wangemuacha yule mwenye paji refu la uso refu (alimaanisha Ali) awaongoze kwenye njia ya haki, angefanya hivyo japo kwa upanga." Akaulizwa, "Kwa nini humteui yeye?" Akasema, "Yule aliyekuwa mbora kuliko mimi hakuteua (mrithi wake)." Baladhuri ameandika katika Ansabul Ashraf juz.5,uk.17, kwamba Waqedi amesema kwamba Umar alipokuwa akizungumzia mrithi, watu walimpendekeza Uthuman, Zubair, Talha, Sa'd au Abdulrahman. Alisema kwamba Uthaman angetoa nafasi za juu kwa jamaa zake. Zubair alikuwa muumin wakati wa amani, na asiyeamini anapokasirika. Talha alikuwa mkereketwa, Sa'd ni mzuri wa kuongoza jeshi lakini hangeweza kutawala hata kijiji, na Abdulrahman angeweza tu kumudu nyumba yake. Ibn Maimoun alisema kwamba Umar aliacha mrithi wake achaguliwe kutoka miongoni mwa watu sita, na akaomba kwamba mwanae Abdullah Ibn Umar awe na hao watu sita, lakini asichaguliwe. Baladhuri ameandika katika Absabul Ashraf kwamba Abi Mekhnaf alisema kwamba wakati Umar alipochomwa, alimuamuru Suhaib Ibn Abdullah Jod'an awaite viongozi kutoka Muhajirina na Ansar. Walipofika, Umar akasema, "Nimeyaacha mambo yenu mikononi mwa watu sita waliokuwa watangulizi katika Uislam, na Mtume alikuwa radhi nao wakati alipokufa. Watachagua mmoja kati yao kuwa kiongozi wenu (Khalifa)." Ndipo akawataja hawa watu sita. Alimuamuru Abi Talha Ziad Ibn Sahl Khazraji kuweka tayari askari hamsini kushinikiza suala la kumuunga mkono huyo Khalifa mpya. Aliamuru kwamba uchaguzi huo umalizike ndani ya siku tatu. Alimwambia Suhail aongoze Swala mpaka hapo Khalifa atakapokuwa amechaguliwa. Talha, mmoja wa wale wateuliwa sita hakuwepo Madina, Umar akasema kwamba wasimngojee baada ya siku tatu, na kwamba yoyote yule aliyechaguliwa, awe ndiye Khalifa, na mtu atakayempinga akatwe kichwa chake. Kisha Umar akamtuma mtu kwenda 130
ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO
kumjulisha Talha. Lakini Talha alipokuja Madina, Khalifa Umar alikuwa amekufa, na Uthuman alikuwa amechaguliwa kuwa kama Khalifa mpya. Talha alibakia nyumbani kwake katika kupinga. Uthuman alimwendea, Talha akasema, "Utauachia Ukhalifa nitakapokuwa sikubali." Uthuman alijibu kwa kukubali, ndipo Talha pia akashika mkono wa Uthu+-+man kama Khalifa. Imeandikwa katika Iqdul-Faraid uk.20 kwamba Talha alimwambia Umar kwamba alikuwa tayari kumpa mkono ndani ya Msikiti au hadharani . Abdullah Ibn Saad Abisarh alisema kwamba kabla ya Talha kutoa mkono wake wa kiapo, watu walikuwa na wasiwasi ikiwa kama asingekubali. Uthuman siku zote alimheshimu Talha mpaka alipozuiwa ndani ya nyumba yake kabla hajauawa. Ndipo Talha alipoonyesha upinzani mwingi kwa Uthaman kuliko mtu mwingine yeyote. Baladhuri ameandika katika Ansabul Ashraf uk.18 kwamba Umar alisema, "Wachache lazima wawatii wengi, na yeyote atakaepinga, mkate kichwa." Imeandikwa pia katika uk.19 kwamba Umar aliwaamuru wale wajumbe wa mashauriano kushauriana kwa siku tatu, na kama watu wawili watapiga kura kumpendelea mtu mmoja, na wawili wengine wakampigia mtu mwingine, basi kura zipigwe tena. Kama watu wanne watakuwa upande wa mtu mmoja, na mmoja tu akapinga, basi wanne hao watakuwa kwenye haki, kama watafungana watatu kwa watatu, watatu hao wakikubaliana na Abdulrahman watakuwa washindi kwa ajili ya kile Abdurahmani anacowachagulia Waislamu kitakuwa salama zaidi.. Baladhuri katika Ansabul Ashraf juz.5,uk.15, ameandika kwamba Umar alisema, "Watu wengine wanasema kwamba uchaguzi wa Abubakr ulikuwa ni kosa la ghafla, Mungu Alitulinda na madhara yake, na Umar hakuingia madarakani kwa kupigiwa kura, lakini nimeamua kwamba mrithi wangu achaguliwe kwa majadiliano. Kama wanne wako upande mmoja, na mmoja katika upande mwingine, chukueni upande wa wanne. Kama palikuwa na watatu dhidi ya watatu, kubalianeni na wale watatu ambao Abdulrahman atakuwa miongoni mwao. Kama Abdulrahman (atajishika mikono yake miwili) pamoja, mfuateni." Muttaqi pia ameandika katika Kanzul-Ummal juz.3,uk.160 kwamba Umar alisema, "Atakapojishika Abdulrahman mikono yake miwili pamoja basi mtamchukua yeye kama Khalifa." Muttaqi ameandika pia kutoka kwa Aslam kwamba Umar alisema, "Atakapomtaja Abdulrahman mmoja wao kama Khalifa itawabidi mumtii, na yeyote atakayejizuia na utii lazima akatwe kichwa." Ngano hizo hapo juu zinaeleza kwamba Umar aliyaacha mambo ya Waislam mikononi mwa Abdulrahman, na yale majadiliano ya wale watu sita aliowateua kumchagua Khalifa yalikuwa tu kama hatua za kiusalama za kuhakikisha mrithi wake anakalia kiti. Ali aliugundua mpango wa Umar kama ilivyoandikwa ndani ya Ansabul Ashraf, juz.5,uk.19, kwamba Ali alimsikia Umar akipendekeza uthibitisho wa Abdulrahman kwa uchaguzi wa Khalifa. Alisema kumwambia ami yake Abbas, "Wallah, tumeupoteza uchaguzi." Abbas akamuuliza, "Umejuaje?" Ali akasema, "Sa'd anampendelea Abdulrahman kwa sababu ni mabinamu. Abdulrahman ni mkwewe Uthuman, na ni rafiki yake. 131
ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO
Hawa watatu wako upande mmoja, hata kama Zubair na Talha wanipigie kura mimi, wao watashinda, na tutapoteza kwa sababu Abdulrahman yu miongoni mwao." Karibu mazungumzo hayo hayo yameandikwa katika Iqdul-Faraid, juz.13,uk.74. Baladhuri ameandika katika Ansabul Ashraf, juz.5,uk.20, kutoka kwa Abi Mikhnaf kwamba Ali alihofia kama Sa'd, Abdulrahman na Uthuman wangekubaliana pamoja. Kwa hiyo alimchukua Hasan na Husein kwenda nao kwa Sa'd na akamwambia, "Ewe Aba Is'haq, sikuja kukutaka unipigie kura badala ya Abdulrahman. Bali kama Abdulrahman atakuomba uchukue upande wa Uthuman tafadhali usikubali, kwa sababu mimi ni ndugu wa karibu mno kwako kuliko Uthuman." Ali akamtajia hili Sa'd na akamkumbusha uhwosiano wake, uhwosiano wa Hasan na Husein na uhwosiano wa Amina mama yake Mtume na Sa'd. Sa'd akamwambia Ali, "Umepewa ulichokiomba." Wakati Abdulrahman alipomtaka Sa'd ushauri, Sa'd alisema, "Ninakupigia kura wewe, lakini simpigii Uthaman, kwa sababu Ali anastahili nafasi hii zaidi kuliko Uthuman." Abu Talha (mlinzi mkuu) alikuja kwenye ukumbi wa mikutano kuwasisitiza wafikie uamuzi na akawaambia wale wajumbe wa mashauriano, "Mnaonyesha shauku ya majadiliano, lakini mnachelewesha mjadala wenyewe. Inaelekea kila mmoja wenu anatamani kuwa ndiye Khalifa." Abu Talha alipoiona ile hali alitokwa na machozi na akasema, "Niliwategemea wao wasiwe na tamaa ya nafasi hiyo, na nilihofia kuwa hakuna kati yao atakayelikubali jukumu hilo la kuwa Khalifa, na kwamba kila mmoja atajaribu kumtupia mwingine." Umar alimteua mwanae kama mjumbe wa mashauriano bila ya kuwa na kura, lakini mwanae hakujiunga na baraza hilo kama ilivyoandikwa katika Ansabul Ashraf, juz.5,uk.21. Abi Mikhnaf alisema kwamba Umar alizikwa siku ya Jumapili na Suhaib aliongoza Swala ya jeneza, na Abu Talha akaongoza ile Swala ya jamaa ya kila siku. Wale washauri hawakuanza kazi yao jioni ile, na asubuhi iliyofuatia walisimamia hazina kwa maombi ya Abu Talha, yule mlinzi mkuu. Abdulrahman aligundua kwamba wale washauri walikuwa wakinong'onezana kuwakatisha tamaa wagombea kisha akasema, "Sa'd na mimi tulifuta madai yetu kama wagombea mradi nimchague Khalifa, kwa sababu watu walikuwa wanangojea matokeo na walitaka kurudi kwenye miji ya nyumbani kwao. Wagombea wote walikubali isipokuwa Ali ambaye alisema, "Nitalifikiria hili." Abu Talha alikutana nao na Abdulrahman akamwambia alichopendekeza, na juu ya kutokukubali kwa Ali. Abu Talha alisema kumwambia Ali, "Muamini Abdulrahman na Waislam wengine vilevile. Yeye binafsi siyo mgombea kwa sababu halitaki hilo jukumu, kwa nini hukubaliani naye?" Basi Ali akamtaka Abdulrahman kuapa kwamba atakuwa muadilifu na ataupa kipaumbele ustawi wa Waislam mbele mbele kuliko mawazo ya matamanio yake binafsi, Abdulrahman akaahidi. Kisha Abdulrahman akamwambia Ali, "Usiwe na shaka."Hili lilitokea ama ndani ya nyumba ya hazina au katika nyumba ya Miswar Ibn Makhrama. Kwa maombi ya Abdulrahman wajumbe wote walitoa ahadi zao 132
ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO
kwamba yeyote atakayemchagua atakubaliwa. Abdulrahman akauchukua mkono wa Ali na akasema, "Apa kwa Mwenyezi Mungu kwamba nikikuchagua kama Khalifa, hutawapendelea Bani Abdulmuttalib, na utatenda kwa mujibu wa sunnah ya Mtume hasa." Ali akasema, "Nani anaweza kukubali kufanya hasa kama Mtume alivyofanya? Ninaweza kukubali tu kufanya kwa juhudi zangu zote." Ndipo Abdilrahman akauchukua mkono wa Uthuman na kumwambia, "Apa kwa Mwenyezi Mungu kwamba kama nitakuchagua kuwa Khalifa, hutawapendelea Bani Umayya na utamfuata Mtume, Abubakr na Umar." Uthuman akaapa kutenda kama hivyo, na akaahidi. Ali akamwambia Uthuman, "Umepata ulichokitaka." Kisha Abdulrahman akamwambia Ali namna hiyo hiyo. Ali akasema, "Ninaahidi kufuata sunnah ya Mtume na kufanya kile ninachodhani kwamba ni sahihi kwa mujibu wa Sheria za Kiislam." Wakati huo huo Uthuman aliendelea kusema, "Nina ahidi, kama Mitume walivyomuahidi Mwenyezi Mungu, kutenda kulingana na sunna ya Mtume, Abubakr na Umar." Ndipo Abdulrahman alipoushika mkono wa Uthuman na kumtangaza kuwa Khalifa. Wajumbe wote wa mashauriano walimpa mikono Uthuman, kuonyesha kumkubali kwao kama Khalifa, isipokuwa Ali aliyebaki amekaa baada ya wengine kuwa wamesimama kumthibitisha Uthuman, Abdulrahman akamwambia Ali, "Kubali ama sivyo nitakukata kichwa chako." Hakuna mjumbe aliyekuwa amebeba upanga isipokuwa Abdulrahman. Ilisemekana kwamba Ali alitoka kwenye ukumbi wa mikutano kwa hasira. Wajumbe wengine walimfuata akubali la sivyo wapigane naye. Ndipo Ali aliporudi na kupeana mkono wa kiapo na Uthuman. Baladhuri ameandika katika Ansabul Ashraf, Juz.5,uk.24 kutoka kwa Waqedi kwamba baada ya Uthuman kutoka nje ya ukumbi wa mikutano akiwa Khalifa, alikwenda kwenye mimbari. Alimshukuru Mola na kumtakia rehma Bwana Mtume, na akasema, "Enyi watu, kipando cha mwanzo ni kigumu. Tunao muda mwingi wa kutosha mbele yetu. Kama nitakuwa hai nitawaandalieni hotuba. Sikuwa mzungumzaji kabla, lakini Mungu atanifundisha jinsi ya kutoa hotuba." Imeandikwa katika Iqdul-Faraid, juz.2,uk.140, kwamba Uthaman alikuwa mmoja wa wale walioona vigumu kutoa hotuba. Imeandikwa pia katika albaian-watTabieen kwamba Uthuman alifanya makosa fulani fulani katika mimbari pale aliposema, "Enyi watu, Abubakr na Umar walikuwa wakitayarisha hotuba zao kabla." Abi Mekhnaf anasema kwamba Uthaman ndani ya mimbari alisema, "Sikuandaa hotuba na kamwe sijawahi kutoa moja .Kwa mapenzi ya Mungu, nitarudi hivi punde na kuongea nanyi." Imesimuliwa pia kwamba Uthaman alipanda kwenye mimbari na kusema, "Hatuna uzoefu wa kuhubiria watu, kama tuko hai Inshaallah, mtasikia hotuba nzuri. Niwaambie sasa kwamba kwa sheria ya Mungu, Ubaidullah mwana wa Umar amemuua Hurmuzan. Hurmuzan alikuwa Mwislamu lakini hakuwa na mrithi, mimi kiongozi na Khalifa nitamsamehe muuaji. Je, mnamsamehe?" Wote walijibu kwa kukubali, ila Ali aliyependekeza hukumu ya kifo kwa muua133
ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO
ji na akamnyooshea kidole Ubaidullah, akisema, "Oh wewe mnafiki, kama ningekupata ningekuua katika kulipiza kisasi kwa ajili ya kumuua Hurmuzan." Tabari katika kitabu chake juz.3,uk.292-302, ametengeneza ngano moja kutoka kwenye ngano zote hapo juu, na amefupisha baadhi ya sehemu zake kiasi kwamba matukio hayo hayakuelezewa sawasawa. Ameandika hii hotuba ya Uthaman kutoka kwa Seif peke yake. Tumeandika kidogo hapa kuhusu 'Ushauri' kuonyesha tofauti kati ya Seif na wengine katika kuyaandika matukio. Tutaelezea zaidi kuhusu mjadala wa wajumbe wa ushauri katika ukumbi wa mikutano baadaye. Seif hakupotosha kadhia hiyo hapo juu, lakini amebuni mamia ya ngano kuwalinda watawala wa wakati huo, na watu mashuhuri. Tabari ameonyesha upenzi maalum wa kuandika kutoka kwa Seif. Mtu yeyote kama atakaposoma matukio ya miaka ya 11-37 Hijiria kutoka kwenye kitabu cha Tabari, atagundua ni kiasi gani matukio hayo yamebuniwa na/au kugeuzwa.
134
ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO
12. QUMMAZBAN MWANA WA HURMUZAN KWA MUJIBU WA SEIF: KUTOKA KWA SEIF TOKA KWA WENGINE MBALI NA SEIF ULINGANISHO
135
ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO
QUMMAZBAN MWANA WA HURMUZAN KWA MUJIBU WA SEIF Abi Mansur alimsikia Qummazban akisema, "Waajemi wanaoishi Madina walikuwa wakitembeleana - safari moja baba yangu alikutana na Firuz akiwa ameshika jambia lenye ubapa kila upande. Baba yangu akamuuliza Firuz, 'Kwa nini unalitaka jambia hili?' Firuz akasema, 'Nitakata.' Baada ya Umar kujeruhiwa, mtu mmoja akasema kwamba alimuona Hurmuzan akimpa Firuz jambia lile. Ubaidullah (mtoto wa Umar) ndipo akaenda kumuua Hurmazan (baba yangu). Wakati Uthuman alipokuwa Khalifa, aliniambia nilipize kisasi juu ya Ubaidullah na nimuuwe. Kila mtu alitaka Ubaidullah auawe isipokuwa wachache walioniomba nimsamehe. Nikawauliza kama nilikuwa na haki ya kumuua (Ubaidullah), wakakubali. Kisha nikawauliza, 'Mnaweza kunizuia kumuua muuaji wa baba yangu?' Walijibu kuwa hawawezi na wakamuapia Ubaidullah. Hata hivyo nilimsamehe Ubaidullah, yote kumridhisha Mungu na watu wale. Ndipo watu wale wakaninyanyua na kunipeleka nyumbani kwangu wakiwa wamenibeba juu ya mabega yao." (Mwisho wa ngano ya Qummazban). Seif katika ngano ya pili ameandika kwamba Abdulrahman Ibn Abubakr alisema, "Usiku wa jana nilimuona Abu Lulu (Firouz) akiongea na Jufaina na Hurmuzan. Waliponiona wakatawanyika haraka haraka. Walidondosha jambia lenye bapa mbili. Lilikuwa ndiyo silaha iliyotumika kumkatia Umar. Ni watu wachache tu walioruhusiwa kubakia pale ndani ya Msikiti baada ya kukatwa kule. Mmoja wao mtu wa kutoka kabila la Tamimi, alimfukuza Abu Lulu, akamkamata, akamuua, na akaleta lile jambia pamoja na yeye (Abu Lulu). Lilikuwa ni lile jambia lililoelezwa. Ubaidullah mtoto wa Umar alisubiri mpaka baba yake alipokufa, ndipo akamuua Hurmuzan na Jufaina ambaye alikuwa ni mwalimu wa Kikristo. Suhaib (Gavana wa muda), Gavana wa Madina alimtuma Amr Ibn Al-Aas kumtia mbaroni Ubaidullah. Amr Ibn Aas alijaribu mara nyingi mpaka akilipata lile jambia na kumtia mbaroni Ubaidullah." NGANO KAMA ILIVYOELEZWA NA WENGINE MBALI NA SEIF Tabari ameandika kutoka kwa Miswar Ibn Makhrama kwamba baada ya Ubaidullah (mtoto wa Umar) kumuua Hurmuzan, Jufaina na binti ya Abu Lulu, alisema, "Wallah, nitawauwa wale ambao wanahusika na kifo cha baba yangu." Sa'd aliuchukua ule upanga kutoka kwa Ubaidullah na kumfunga ndani ya nyumba yake mpaka Uthuman alipotoka ndani ya nyumba yake na kuwaambia baadhi ya Ansari na Muhajir kuhusu maoni yao juu ya Ubaidullah kama muuaji wa watu wasio na hatia. Ali akasema kwamba ni lazima auwawe. Baadhi ya Muhajir wakasema, "Umar ameuawa jana, na mwanae auawe leo?" Amr Ibn Aas akamwambia Uthuman, "Una bahati kwamba damu ilimwagwa kabla hujawa 136
ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO
Khalifa." Tumetaja hapo kabla kwamba Baladhuri katika ile ngano ya mashauriano alisema kwamba Khalifa Uthuman katika kutokea kwake kwa mara ya kwanza hadharani alisema, "Kwa sheria ya Allah, Ubaidullah amemuua Hurmuzan. Ninamsamehe Ubaidullah kwa niaba ya Waislam wote kwa sababu, Hurmuzan hana mrithi." Kisha Uthuman akaomba idhini ya Waislam. Wote walikubali isipokuwa Ali ambaye alisema, "Huyu mnafiki lazima auawe, kwa sababu ameua Waislam wasio na hatia." Kisha akamnyooshea kidole Ubaidullah na kusema, "Nitakuua kulipiza kisasi cha Hurmuzan." Uthuman akasema, "Nitalipa fidia ya damu ya kuuawa Hurmuzan." Ziad Ibn Labid Bayazi akatunga ubeti ufuatao kuhusu mauaji ya Hurmuzan: Ubaidullah, ilikuwa ni uovu kwako kumuua Hurmuzan, Mwislamu asiye na hatia, bila sababu ya maana. Uthuman alikulinda, na akaokoa damu yako, Lakini hakuna atakayekulinda kutokana na kisasi cha Mungu. Ubaidullah alilalamika kwa Uthuman naye akamuamuru Ziad aache. Ndipo Ziad akatunga ubeti ufuatao dhidi ya Uthuman: Aba Amr wakati Ubaidullah alipochomoa upanga wake, Alikuwa anataka kutenda kosa, Wallah. Kumsamehe mhalifu na kutenda dhambi, Hivi mashujaa wawili wanafikia mwisho kwa wakati mmoja. Huna haki ya kumsamehe muuaji, Na kama ukifanya hivyo, nina hakika unakosea.
HITIMISHO Seif anasema kwamba Hurmuzan alikuwa na mtoto wa kiume, Qummazban. Pia anaandika ngano kutoka kwa mtoto huyo. Wanahistoria wengine wanasema kwamba kwa sababu Hurmuzan hakuwa na mrithi, Khalifa Uthuman alimsamehe Ubaidullah kwa niaba ya Waislam mbali na kufidia kwake damu ya Hurmuzan. Seif pia anasema mtu kutoka kabila la Tamimi alimuua Abu Lulu kuthibitisha heshima kwa ajili ya mmoja wa jamaa yake wa kikabila asiyejulikana.
137
ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO
13. MIJI ILIYOBUNIWA NA SEIF. ULINGANISHO
138
ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO
MIJI ILIYOBUNIWA NA SEIF Seif amebuni baadhi ya miji kama vile Dolouth, Tawus, Alejrana Wa Na'manaleraq, Alqordouda, Nhar-att, Thanyya Thanyyatul Rakab, Qodais, Wayakhord, Alwalaja na Alhawafi, ambayo inatajwa na Hamawi ndani ya Mujamul-Buldan, na Tabari na wengineo. Yaqut Hamawi alikuwa muangalifu sana kuandika ngano adimu na za kipekee katika kitabu chake Mujamul-Buldan. Ameandika nyingi ya ngano za Seif katika kitabu chake anapoelezea mambo ya ajabu kuhusu mahali au mji. Inavyoonekana Hamawi alikuwa na muswada wa kitabu cha Seif kama inavyoweza kuonekana wakati anaporejea kwa Jubar, Ja'rana, Shairja na Sahid katika kitabu chake cha jogorafia, Mujamul-Buldan. Muswada huo uliandikwa kwa mkono na Abibakr Muhammad Ibn Ahmad Ibn Abdulbagi Albaghdadi Hafidh (kafa 489 Hijiria)12. Alikuwa akiitwa Ibn Khaziba na ameandika baadhi ya maoni katika pambizo vilevile, na amesimulia kutoka kwa Abibakr Alkhatie. Katika pambizo hizo kulikuwa na maoni yaliyotolewa na Abibakr Ibn Seif. Alikuwa ama ni Abibakr Ahmad Ibn Bakr Ibn Seif Jessaini, ambaye wasifa wake umeandikwa na Hamawi na Sam'ani, chini ya jina Jessaini, au Abubakr Ahmad Ibn Abdullah Ibn Seif Ibn Said Sajestani ambaye kutoka kwake Ibn Asakir ameandika ngano zote za Seif, na Ibn Nadim ameandika jina lake katika kitabu chake, Alfihrist, uk.119 kwa jina la Ubaidullah Sajestani. Hamawi ameandika baadhi ya ngano za Seif katika kitabu chake kwa namna ileile kama Tabari, lakini kuna tofauti moja kati yao. Tabari ameandika matukio kwa namna ambayo matukio machache yanafanya ngano kamili. Pia anatoa kama kawaida, vyanzo vyake vya habari. Lakini Hamawi wakati mwingine ameandika sehemu ya tukio, kwa sababu alipenda ule mtindo wa ushairi au nathari ambayo limeandikiwa. Wala halitaji jina la Seif katika (matukio) mengi yao. Tunaweza kuona baadhi ya ngano za Seif kwa Hamawi ambazo hazikuandikwa ndani ya Tabari na kinyume chake. Kila mmoja wa wanahistoria hawa wawili amechagua zile tungo za Seif zinazokidhi malengo yake mwenyewe. Hamawi ameandika vipande kutoka kwa Seif chini ya majina ya miji kama ifuatavyo: 1. DOLUTH Mtu kutoka kabila la Abdulqais anayeitwa Suhara anasema, "Katika Vita vya Hurmazan, vilivyotokea pale Ahwas, mji ulio kati ya Doluuth na Dujail, nilimkuta Harim Ibn Hayan na nikachukua kichanga cha tende toka kwake…………… n.k."
12 Tarikhul Kamil juz.10,uk.178; Shazarat-u-Dhahab, Matukio ya mwaka wa 489 Hijiria; Lisanul Mizan juz.6,uk.57, 479; na Tadhkiratul Hafidh al-Dhahabi, uk.1224.
139
ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO
Tabari ameandika katika juz.1,uk.2537, mwaka wa 13 Hijiria ngano hiyo hapo juu mpaka "kichanga cha tende". Ambapo Hamawi anaendelea katika kuandika kwake zaidi ya Tabari. Kwa hiyo Hamawi anaweza kuwa hakuandika kutoka kwa Tabari na lazima awe alipata ujuzi zaidi wa muswada wa Seif. 2. TAWUS Hamawi anasema kwamba ni mahali katika jimbo la Fars (ndani ya Iran). Seif alisema kwamba Ala Ibn Hazrami alituma kikosi kwa njia ya baharini kwenda Tawus bila ridhaa ya Umar. Hamawi ameiandika ngano hii ambayo pia imeandikwa na Tabari kutoka kwa Seif katika juz.1,uk.2545-2551, mwaka wa 17 Hijiria, lakini Hamawi ameandika pia shairi lililotungwa na Khalid Ibn Munzir ambalo Tabari ameliacha. 4. JI'RANA NA NA'MAN Ni sehemu mbili katika Iraq kwa mujibu wa Seif, kama ilivyoandikwa na Hamawi. Hamawi amelitaja jina la Seif katika sehemu kumi au zaidi. Lakini kuna miji mingi ambayo ameandika juu yake katika kitabu chake bila ya kutaja jina la Seif. Msomaji wa habari za baadae anaweza kudhani kwamba Hamawi ameeleza maoni yake mwenyewe, mfano ni Qorduda. 4. QORDUDA Wakati Tulaiha, yule mtume wa uongo alipofika Sumeira, alipokea ujumbe kutoka kwa Thamama Ibn Oas Ibn Lam Altai usemao, "Nina watu kama mia tano, kama unataka msaada wowote. Tupo hapa Qorduda na Ansur kwenye michanga." Hamawi amechukua ngano hiyo hapo juu kutoka kwa Tabari 13. Ibn Hajar pia ametumia taarifa zilizochukuliwa kutoka kwa Tabari alipokuwa akiandika wasifa wa Thamama. Hakuna dalili ya Qorduda na Thamama popote pale isipokuwa kwenye ngano za Seif. 5. MTO UTT Khalid Ibn Al-Walid alimtuma mmoja wa majenerali wake anayeitwa Utt Ibn Abi-Oh, aliyekuwa anatoka kwenye kabila la Bani Sa'd, kwenda Duwraqestan. Jenerali huyo aliweka kambi kando ya mto na baadae mto huo uliitwa Mto Utt kwa jina la jenerali huyo. Msomaji tena anaweza kufikiri kwamba Hamawi ameandika hilo kwa maamuzi yake mwenyewe, hata hivyo ameiazima ngano hiyo kutoka kwa Tabari. Ibn Hajar pia ameandika ngano hiyohiyo ambayo inaelezea neno Utt (kutoka kwa Tabari).14 13 Tabari juz.1,uk.1892; Ertedad Ghetpan, mwaka wa 11 Hijiria. 14 Tabari juz.1,uk.2052; habari kufuatia Hayrih.
140
ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO
6. IRMATH AGHWATH NA AMAS Majina haya yaliyoelezwa na Hamawi yameazimwa kutoka kwa Tabari kama tulivyoelezea hapo kabla kwenye vita vya Qadisyya. 7. ALTHENI, THANYA TALKERAB, AL QODAIS, AL MAQR, WAYAKHURD WALAJA NA ALHAWAFI Ni baadhi ya majina Hamawi aliyoazima kutoka kwa Tabari, juz.1,uk.2026, 2648, 2230-33, 43, 65, 88, 94, 2326-38, 2037-38 na 2618-25 na pia 2169 kimpangilio bila ya kutaja jina la mbuniaji wao Seif. Hamawi ameandika juu ya sehemu nyingine na miji katika kitabu chake Mujamul-Buldan. Amezipata kutoka kwenye kitabu cha Seif, na tunashindwa kuzipata kwenye vitabu vingine vyovyote vya jogorafia au historia, kwa majina: 1. Safat Jaziratul-Arab, cha Abi Muhammad Alhassan Ibn Ahmad Ibn Yaqub IbnYusuf Ibn Daud, anayejulikana kama Ibn Haik (kafa 334 A.H - 945/6 A.D.). 2. Futuuhul-Buldan, cha Baladhuri. 3. Mukhtasarul-Buldan, cha Abibakr Ahmad Ibn Muhammad Hamdani anayejulikana kama Ibn Faqih aliyeishi katika karne ya 3 Hijiria. 4. Atharul-baqua anil Quruunil khaliah, cha Aburaihan Muhammad Ibn Ahmad alBirouni Kharazmi (kafa 440 A.H.) 5. Mujam Mastu'jim, cha Abi Ubaid Abdullah Ibn Abul-Aziz Ibn Mas'ab Albakri Alwazir (kafa 478 A.H.) 6. Taqwimul-Buldan, cha Ismail Sahib Hama (kafa 432 A.H.) Wanajogorafia wawili wa wakati mmoja hawakumwamini Hamawi na hawakuzitaja sehemu hizo katika vitabu vyao. 1. Lesyrenj, kitabu chake ni: Cities of East Khalifate (Miji ya Ukhalifa wa Mashariki) 2. Umar Reza Kehala, kitabu chake ni: Geography of Arabian Peninsula (Jogorafia ya Peninsula ya Arabia).
141
ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO
14. SEIF NA TAREHE ZA KADHIA HIZO ULINGANISHO
142
ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO
SEIF NA TAREHE ZA KADHIA HIZO Seif hakubuni ngano tu, bali pia amezibadili tarehe za kadhia za kweli. 1. Tabari juz.2,uk.553-56 kuhusu Vita vya Ubolla,15 ameandika kutoka kwa Seif kwamba Abubakr alimtuma Khalid kwenda Iraq. Wapagani walikuwa wamepiga kambi kati ya ugavi wa maji na jeshi la Khaud. Allah akatuma mawingu ya mvua kuwasaidia Waislam. Waislam walipigana na kushinda Vita hivyo vya Ubolla. Khalid alipeleka moja ya tano ya ngawira (kama kodi) na Tembo mmoja Madina. Wanawake wa hali ya chini wa Madina wakauliza, "Huyu Tembo ni kiumbe cha Allah au ametengenezwa na binadamu?" Kisha Tabari anasema, "Vita vya Ubolla vina tofauti kubwa sana kama ilivyoandikwa na wanahistoria wa kuaminika, vilitokea wakati wa Umar, katika mwaka wa 14 Hijiria na kamanda alikuwa ni Utba Ibn Ghazwan na siye Khalid." Seif ameweka tarehe isiyo sahihi ya kisa hicho na vilevile akawawasilisha kinyume kamanda na Khalifa. 2. Tabari katika juz.2,uk.89 ameandika kwamba Umar alimtuma Utba Ibn Ghazwan kwenda Basra katika mwaka wa 14 Hijiria na Seif ameandika mwaka wa 16 Hijiria. Ibn Kathir ameiandika tofauti hii katika juz.7,uk.47-48 ya kitabu chake. 3. Ile kadhia ya Yarmuuk, imeandikwa katika juz.7,uk.61 na Ibn Kathir kwamba kadhia ya Yarmuuk ilitukia katika mwaka wa 15 Hijiria kwa mujibu wa Laith Ibn Sa'd , Ibn Lahba'a, Abima'shar, Walid Inb Muslim, Yazid Ibn Ubaida, Khalifa Ibn Khayat, Ibn Kalbi, Muhammad Ibn Aiz, Ibn Asakir na msomi wetu Dhahabi, lakini Seif na Tabari wanasema kwamba ilitokea mwaka wa 13 Hijiria. Ibn Kathir tena ameitaja kadhia hii katika marejeo yake ya kwenye mwaka wa 13 Hijiria. Ibn Asakir juz.1,uk.159 anasema, "Seif amesema kwamba kadhia hii ilitokea katika mwaka wa 13 Hijiria kabla ya kutekwa Damascus lakini hakuna hata mmoja aliyekubaliana naye." 4. Kadhia ya Fihl. Imeandikwa katika juz.7,uk.25,ya Ibn Kathir, "Ile kadhia ya Fihl ilitokea kabla ya kutekwa Damascus kwa mujibu wa wanahistoria wengi. Lakini Abujafar Ibn Jazir (Tabari), akimfuata Seif, anasema kwamba ilitokea baada ya kutekwa Damascus." Baladhuri ameandika katika Futuuhul-Buldan,uk.137, "Inasemekana kwamba ile kadhia ya Fihl wa Jordan ilitokea siku mbili kabla ya mwezi wa Dhilqada haujaisha, hii ni kusema, miezi mitano baada ya Umar kuwa Khalifa." 15 Ubolla ni jina la mji karibu na ule Mto Tigris na Basra. Basra ilikuja kuwa mji katika wakati wa Umar ambapo Ubolla, mji wa zamani kabisa, ulikuwa makao makuu ya jeshi kwa amri ya Kasra, kutoka Mujamul-Buldan.
143
ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO
5. Kuondoka kwa Hercules kutoka Syria . Tabari ameandika kwenye kitabu chake juz.3,uk.99 "Hercules aliondoka Syria kwenda Constantinople katika mwaka wa 15 Hijiria kwa mujibu wa Ibn Is'haq. Lakini kulingana na Seif lilikuwa ni mwaka wa 16 Hijiria." Ibn Kathir ameitaja tofauti hii katika kitabu chake juz.7,uk.53. Baladhuri amekubaliana na Abu Is'haq katika Futuuhul-Buldan uk.162 6. Kutekwa kwa Orshelim: Tabari juz.3,uk.103 ameandika kutoka kwa Seif, "Mkataba kati ya Umar na Wapalestina ulikuwa katika mwaka wa 15 Hijiria." Ibn Kathir juz.7,uk.57ameandika kwamba kutekwa kwa Palestina kulikuwa katika mwaka wa 16 Hijiria kwa mujibu wa wanahistoria wote isipokuwa Seif. Baladhuri katika uk.165-166, anasema kwamba hii ilitokea katika mwaka wa 16-17 Hijiria. 7. Kutekwa kwa Algire: Tabari ameandika katika juz.3,uk.155: "Katika mwaka wa 17 Hijiria, Algire ilitekwa kwa mujibu wa Seif." Lakini Ibn Is'haq anasema ilikuwa katika mwaka wa 19 Hijiria. Ibn Kathir katika juz.7,uk.76 na Hamawi katika Mujamul-Buldan wameitaja tofauti hii. Baladhuri katika uk.204-205 amekubaliana na tarehe za Ibn Is'haq za mwaka wa 19 Hijiria. 8. Tauni ya Amawas: Tabari ameandika katika juz.3,uk.161-163, "Ibn Is'haq anasema kwamba ilikuwa kwenye mwaka wa 18 na Seif anasema kwamba ilikuwa katika mwaka wa 17 Hijiria." Ibn Kathir ameandika zile simulizi kuhusu Tauni hii katika kitabu chake, juz.7,uk.77-79 na amelitaja kosa la Seif na katika uk.78 amasema, "Muhammad Ibn Is'haq na Abuma'shar na baadhi ya wengineo wanasema kwamba ilitokea katika mwaka wa 18." Baladhuri ameandika katika Futuuhul-Buldan uk.165 kwamba ile Tauni ya Amawas ilikuwa katika mwaka wa 18 Hijiria. 9. Ile kadhia ya baina ya Waajemi na Waislam: Tabari ameandika kwamba kwa mujibu wa Seif, ilitokea katika mwaka wa 15, lakini alikuwa katika mwaka wa 16 kulingana na Ibn Is'haq na Waqedi. Ibn Kathir ameitaja tofauti hii katika juz.7uk.60 wa kitabu chake. 10. Vita vya Korasani: Tabari katika juz.3,uk.244 na Ibn Kathir katika juz.7,uk.126 wameandika kutoka kwa Seif kwamba ilitokea katika mwaka wa 18 Hijiria, lakini wengine wanasema ilitokea katika mwaka wa 22 Hijiria. 11. Vita vya Tabaristan: Waqedi, Abuma'shar na Madaini wameandika kwamba Sa'd Ibn Aas alipigana huko Tabaristan katika mwaka wa 30 Hijiria. Lakini Seif anasema kwamba Suwaid Ibn Muqarran aliifanya mikataba ya Tabaristan katika wakati wa Umar (nyuma kabisa kabla ya mwaka wa 30 Hijiria).
144
ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO
HITIMISHO Kwa miaka mingi, nimefanya utafiti makini katika historia ya Uislam, visa na Sunnah za Mtume Muhammad (s.a.w.w.). Mwaka 1949 nilizikuta ngano za Kiislam zenye kutia mashaka katika Vitabu vya Historia vya Kiislam. Nilishangazwa kwamba katika mifano mingi, ukweli umepuuzwa na/au kuachwa. Badala yake uongo na watu bandia vimejitokeza katika vitabu vya historia, na hususan katika miaka ya mwanzoni ya Uislam, yaani, zama za Makhalifa wanne wa mwanzo na utawala wa Bani Umayya (hasa Mu'awiyya). Nimefuatilia uongo huu na hawa watu wa bandia katika vingi ya vitabu vinavyopatikana, khususan vile maarufu, ambavyo vimekuwa kwa kawaida ndiyo vyanzo (rejea) vikuu vya habari kwa wanahistoria wengine na (hata) wanahistoria wa Magharibi waliobobea hasa kwenye Historia ya Kiislam. Baada ya uchunguzi makini, nilitosheka, bila ya kiwingu chochote cha mashaka, kwamba baadhi yake zimeghushiwa kwa malengo maalum. Chanzo cha uongo na hawa watu bandia (wa kubuni) ni Seif Ibn Umar al-Tamimi, mwandishi wa alFutuuh al-Kabir Wal-Riddah na al-Jamal wal Masiir Ayeshah wa Ali. Seif anatofautiana na waandishi wa kweli siyo tu katika maandishi bali hata katika Sanadi kwa kutumia simulizi za watu ambao hawapo. Seif alizibuni ngano hizi na watu wasiokuwepo ili kuwaridhisha wale waliotaka kuufunika ukweli na kuwasilisha matukio ya historia kinyume kabisa na yalivyokuwa. Baadhi ya wanahistoria waliziona ngano za Seif zikikubaliana na hisia zao, kwa sababu tu Seif amebuni katika ngano zake watu wenye fadhila ajabu, mashujaa na watu wenye uzuri wa kipekee na busara kutoka kwenye watawala wa wakati huo, magavana na makamanda wa majeshi. Amebuni pia mambo ya ajabu, kinyume kabisa na kanuni za desturi asili ili kuzifanya zionekane kama ni miujiza, kama mchanga kugeuka kuwa maji, bahari kugeuka kuwa mchanga na ng'ombe kuongea na watu kuonyesha mahali walipojificha kwa jeshi la Waislam, n.k. Zaidi ya hayo, hao watawala, magavana, makamanda na watu mashuhuri katika miaka ya mwanzo ya Uislam, walijihusisha binafsi katika mambo ambayo yalikuwa hayafai. Ngano za Seif zilizifunika dosari zile kwa visingizio dhahiri, na hivyo amezuia shutuma dhidi yao. Kwa mfano tunayaona yafuatayo katika maandishi ya Seif: 1. Seif ameandika kwamba Ali Ibn Abi Talib, alitoa kiapo cha utii kwa Abubakr siku ileile watu wengine walipotoa viapo vyao!! Ambapo, ukweli ni kwamba Ali alikataa kutoa ridhaa yake na kiapo mpaka na baada ya mke wake (binti ya Mtume, Fatima) alipofariki. 145
ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO
2. Seif ameandika kwamba Sa'd Ibn Ubadah, bila kupenda alitoa kiapo chake!! Ambapo ukweli ni kwamba alikataa kutoa kiapo chake cha utii, na kwa matokeo ya hili, aliuawa kule kwenye sehemu yake ya uhamishoni, Howran. 3. Seif ameandika kwamba wale watu wote kutoka makabila mbalimbali, walioamriwa kuuawa, na wake zao walichukuliwa kama wafungwa wa kivita walikuwa Murtadi (waliokubali Uislam na baadae wakaukana!!). Ambapo, ukweli ni kwamba walikataa kutoa kiapo cha utii kwa Abubakr. 4. Seif ameandika Hadith ya Mtume, alipokuwa anajulisha juu ya mwanamke anayepanda ngamia na kukaribia Hauwab kuwa ni Ummu Zumal !! Tunajua sasa kwamba alikuwa ni Ayishah, Ummul-Mu'minin (binti yake Abubakr na mke wa Mtume). 5. Seif ameandika kwamba Mughaira Ibn Sho'abih (yule Gavana wa wakati wa Umar) alikuwa ndani ya nyumba yake, alipoonekana akijamiiana na mwanamke, wale waliomuona hawakuweza kumuona huyo mwanamke na angeweza kuwa ni mke wake !! Tumegundua, kwamba maandishi ya wengine yanapingana na hili kabisa. Mughaira Ibn Sho'abih alikuwa katika nyumba ya Ummu Jamil na alikuwa akijamiiana na mwanamke huyu, pale alipoonekana. 6. Seif ameandika kwamba Abu Mahjan Thaqafi alifungwa wakati wa Umar, kutokana na shairi alilolisoma lenye kupendelea pombe !! Ukweli ni kwamba alikuwa hasa amelewa wakati wote. Pengine baadhi ya wanahistoria wa Magharibi wamekipata pia walichokuwa wanakitafuta katika ngano za kubuni za Seif, hicho ni, mauaji mengi na tabia za kikatili zinazofanywa na majeshi na askari wa Uislam. Tumeona katika ngano za Seif kwamba Khalid Ibn Walid alishughulika kwa siku tatu usiku na mchana kukata vichwa wale wafungwa wa kivita; kwa nyongeza, tumeona kwamba Khalid aliwakata vichwa hata watu wasiokuwa na hatia, yote haya kwa sababu Khalid aliapia kwamba 'atafanya mto kutokana na damu yao' !! Upuuzi usio shaka. Wanahistoria wa Magharibi wamesoma katika ngano za Seif kwamba ile idadi ya watu waliouwawa katika nyingi ya vita katika siku za mwanzoni za Uislam ilikuwa imevuka zaidi ya laki moja, kudhihirisha tabia za unyama na ukatili wao wa kuwaangamiza wanadamu kama Hekalu na Mongole. Wameona katika maandishi ya Seif kwamba Waislam wengi nje ya mzunguuko wa Makka na Madina walikuwa Murtadi baada ya Mtume Muhammad (SAW), na walikuwa wasilimishwe tena kwa nguvu na kwa upanga, kuashiria kwamba Uislam uliendelea na kupanuka kwa mabavu !! Na hatimae, hao wanahistoria wa Magharibi wamejua kupitia maandishi ya Seif kwamba Myahudi anayeitwa Abdullah Ibn Saba, alikuwa na athari sana kwa wafuasi wa mara baada ya Mtume, kugeuza mawazo yao kutoka kwenye 146
ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO
mafundisho makuu ya Uislamu kusababisha uasi, uliowafanya kumuuwa Khalifa. Yote haya yametokea kama matokeo ya jitihada za Myahudi wa ajabu !! n.k. Pengine, wanahistoria wa Magharibi walizipenda sana ngano za Seif kiasi kwamba waliegemeza kazi ya uchanganuzi wao juu ya maandishi ya Seif na hawakuhangaika kuchimbua kwenye maandishi ya wengine na hawakutaja juu ya vitabu vyenye kutegemewa zaidi. Baada ya utafiti makinifu katika maandishi ya Seif ndani ya al-Futuuh Wal-Riddah na al-Jmal wa Masiir Ayeshah wa Ali, tunafikia kwenye ukweli huu hasa, kwamba maandishi ya Seif yameathiri kwa kiasi kikubwa sana waandishi wengine wengi, pamoja na waandishi mashuhuri kama vile Tabari, Ibn Athir, Ibn Kathir na Ibn Khaldun. Zaidi ya hayo, tunapolinganisha maandishi ya Seif na yale ya maandishi mengine, tunafikia kwenye uamuzi huu kwamba baadhi ya wanazuoni wengi wa Hadithi walikuwa na haki kabisa kusema kwamba: "Seif alikuwa mdanganyifu na mwandishi muongo." Kiasi Seif alivyokuwa zindiq (zandiki, mnafiki), ambao baadhi ya wanazuoni wa Hadithi na wasomi wamemshutumu, kinavyohusika, tutalijadili jambo hili katika kile kitabu - 'One hundred and Fifty Sahabis Mukhtalagh' (Masahaba 150 wasiowahi kuwepo). Katika kitabu cha tatu, tutajaribu kukijadili na kukichambua kitabu cha Seif, al-Jamal‌Seif alikiandika kitabu hicho kwa nia ya kuelezea kile chanzo cha maasi katika wakati wa Khalifa Uthuman, kuwalinda watawala wa Bani Umayya kama vile Mu'awiyya na Abdullah Ibn Abi Sarh, na tutaelezea sababu ambazo Waislam katika nchi mbalimbali walikuwa wamechukia na kukirihishwa na watawala wa Bani Umayyah, n.k. Tutajaribu kuzichambua Ngano hizi, vyanzo na wapokezi wake katika kitabu hicho cha tatu .
147
ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO
148
ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO
149