AHLUBAYT NDANI YA TAF. ZA KISUNNI No 1 check Lubumba.qxd
7/1/2011
AHLUBAYT NDANI YA TAFSIRI ZA KISUNNI SEHEMU YA KWANZA KWA MUJIBU WA TABARI NA THA’LABI
Kimeandikwa na: Sheikh Nizar al - Hasan
Kimetarjumiwa na: Hemedi Lubumba (Abu Batul)
11:09 AM
Page A
AHLUBAYT NDANI YA TAF. ZA KISUNNI No 1 check Lubumba.qxd
B
7/1/2011
11:09 AM
Page B
AHLUBAYT NDANI YA TAF. ZA KISUNNI No 1 check Lubumba.qxd
7/1/2011
Š Haki ya kunakili imehifadhiwa na: AL-ITRAH FOUNDATION ISBN: 978 - 9987 - 512 - 93 - 5 Kimeandikwa na:
Sheikh Nizar al - Hasan Kimetarjumiwa na:
Hemedi Lubumba (Abu Batul)
Kupangwa katika Kompyuta na: Ukhti Pili Rajab. Toleo la kwanza: Januari, 2011 Nakala: 1000
Kimetolewa na kuchapishwa na: Alitrah Foundation S.L.P. 19701 Dar es Salaam, Tanzania Simu: +255 22 2110640 Simu/Nukushi: +255 22 2127555 Barua Pepe: alitrah@raha.com Tovuti: www.alitrah.org Katika mtandao: www.alitrah.info
11:09 AM
Page C
AHLUBAYT NDANI YA TAF. ZA KISUNNI No 1 check Lubumba.qxd
7/1/2011
11:09 AM
YALIYOMO Utangulizi....................................................................................................2 Ahlul Bayt (a.s) ndani ya Tafsir ya Tabari, inayoitwa Jamiul - Bayan Amtaawiil Ayil -Qur’an...............................................................................8 Ahlul Bayt (a.s) ndani ya Tafsiri ya At-Thaalabiy, inayoitwa Al-Kashfu Wal-Bayan Fii Tafsiril-Qur’ani.................................................................39
Page D
AHLUBAYT NDANI YA TAF. ZA KISUNNI No 1 check Lubumba.qxd
7/1/2011
11:09 AM
Ahlul Bayt Ndani ya Tafsiri za Kisunni
NENO LA MCHAPISHAJI Kitabu kilichoko mikononi mwako ni tarjuma ya kitabu cha Kiarabu kiitwacho, Ahlu ‘l-Bayti Fi Tafasiri Ahli ‘s-Sunnah kilichoandikwa na Sheikh Nazri Hasan. Sisi tumekiita, Ahlul Bayt Ndani ya Tafsiri za Kisunni. Hii ni sehemu ya kwanza inayochambua tafsiri za wanavyuoni wakubwa wa Kisunni – Tabari na Tha’labi. Ahlul Bayt, yaani Watu wa Nyumba ya Mtume Muhammad SAW ni viongozi ambao Mtume alituusia tuwafuate. Katika hotuba yake ndefu na maarufu aliyoitoa pale Ghadir Khumm katika msafara wake wa kurejea kutoka Hija yake ya mwisho, Mtukufu Mtume SAW alisema haya mbele ya masahaba na mahujaji zaidi ya laki moja: “...Nakuachieni vitu viwili vizito: Qur’ani na Ahlul Bayt wangu. Viwili hivyo havitaachana mpaka vinifikie katika [hodhi ya] Kawthar. Nawausia juu ya Ahlul Bayt wangu! Angalieni jinsi mtakavyojihusisha nao. Kama mkishikamana na viwili hivi hamtapotea kamwe...” (kwa maelezo zaidi soma kitabu cha al-Ghadir) Lakini bahati mbaya sana sio Waislamu wote wanaowafuata Ahlul Bayt AS pamoja na kwamba wanavyuoni wa madhehebu zote wameandika habari zao katika vitabu vyao na kuonesha kwamba hawa ni viongozi wa Umma huu wa Kiislamu. Mwandishi wa kitabu hiki anajaribu kuthibitisha hilo kwa kutoa rejea mbalimbali kutoka vitabu maarufu vya wanavyuoni wa Kisunni. Ni muhimu kukubaliana na kuziheshimu tofauti za kila mmoja na kutambua msimamo na mtazamo wa kila mmoja. Matatizo huja pale mtu anapolazimisha tabia, imani na mila zake zitawale wengine au kuzifisha itikadi na misimamo ya wengine. Ni muhimu kufikiria kila aina ya maoni katika kujaribu kuamua ukweli. Uislamu kimsingi uko dhidi ya kufuata kibubusa. E
Page E
AHLUBAYT NDANI YA TAF. ZA KISUNNI No 1 check Lubumba.qxd
7/1/2011
11:09 AM
Ahlul Bayt Ndani ya Tafsiri za Kisunni Wafuasi wa madhehebu nyingine wanaweza kuchambua uthibiti wa kitabu hiki ili kujenga maoni yao wenyewe kuhusu mtazamo mzuri wa mtu mwenyewe. Ni muhimu mtu kuelewa hoja za wale ambao hakubaliani nao. Inaweza ikasemwa kwamba wale ambao hawaelewi kabisa mtazamo wa maoni tofauti, hawaelewi kwa ukamilifu mtazamo wa kwao wenyewe. Tumekiona kitabu hiki ni chenye manufaa sana, hususan wakati huu wa maendeleo makubwa ya elimu katika nyanja zote, ambapo uwongo, ngano za kale na upotoshaji wa historia ni mambo ambayo hayana nafasi tena katika akili za watu. Kutokana na ukweli huo, Taasisi yetu ya Al-Itrah Foundation imeamua kuchapisha kitabu hiki kwa lugha ya Kiswahili kwa madhumuni yake yaleyale ya kuwahudumia Waislamu, hususan wazungumzaji wa Kiswahili. Tunamshukuru ndugu yetu, Hemedi Lubumba (Abu Batul) kwa kukubali jukumu hili la kukitarjumi kitabu hiki. Vilevile tunawashukuru wale wote walioshiriki kwa njia moja au nyingine hadi kufanikisha kuchapishwa kwake. Ni matumaini yetu kwamba kitabu hiki kitakuwa ni changamoto kubwa kwa wasomaji wetu. Mchapishaji: Al-Itrah Foundation
F
Page F
AHLUBAYT NDANI YA TAF. ZA KISUNNI No 1 check Lubumba.qxd
7/1/2011
11:09 AM
Ahlul Bayt Ndani ya Tafsiri za Kisunni
NENO LA JUMUIYA Hakika mirathi ya Ahlul-Bait ambayo imehifadhiwa na kambi yao na wafuasi wao dhidi ya upotovu inaonyesha ni kambi iliyokusanya aina mbalimbali za taaluma za kiislamu. Kambi hii imeweza kulea nafsi mbalimbali zilizo tayari kunywa kutoka kwenye chemchemu hiyo, na kuupa umma wa kiislamu wanavyuoni wakubwa wenye kufuata nyayo za ujumbe wa Ahlul-Bait. Wanavyuoni waliokusanya vidodosa na maswali mbalimbali ya madhehebu na mitazamo tofauti ya kifikira kuanzia ndani ya desturi ya kiisilamu hadi nje ya desturi hiyo, huku wao wakitoa majibu na utatuzi makini juu ya maswali hayo ndani ya karne zote. Jumuiya ya kimataifa ya Ahlul-Bait imefanya hima kutetea tukufu za ujumbe wa Uislamu na ukweli wake ambao umechafuliwa na makundi, madhehebu na wanaharakati mbalimbali wenye chuki na Uislamu. Jumuiya imefuata nyayo za Ahlul-Bait na za wafuasi wa kambi yao njema ambayo imefanya hima kujibu madai yenye kuendelea na daima ikajaribu kubaki ndani ya msitari wa mapambano kwa kiwango kinachohitajika ndani ya kila zama. Hakika uzoefu ambao umehifadhiwa ndani ya vitabu vya wanavyuoni wa kambi ya Ahlul-Bait katika dhamira hii ni wa aina ya pekee, kwa sababu una akiba ya kielimu inayotegemea akili na hoja, huku ukijiepusha na matamanio na upendeleo uliokatazwa. Unazungumza na wasomi na wanafikra wenye fani maalumu, mazungumzo ambayo yanakubalika kiakili na yanapokewa na maumbile yaliyo salama. G
Page G
AHLUBAYT NDANI YA TAF. ZA KISUNNI No 1 check Lubumba.qxd
7/1/2011
11:09 AM
Ahlul Bayt Ndani ya Tafsiri za Kisunni Jaribio hili la Jumuiya ya kimataifa ya Ahlul-Bait limekuja kuwapa watafuta ukweli hatua mpya ya uzoefu wa thamani kupitia mada na vitabu vinavyoandikwa na waandishi wa zama hizi ambao ni wafuasi wa madhehebu ya Ahlul-Baiti (a.s.) au miongoni mwa wale ambao Mwenyezi Mungu amewapa neema ya kujiunga na kambi hii tukufu. Achia mbali kwamba jumuia hii pia hujishughulisha na uchapishaji na uhakiki wa yale yenye faida toka katika vitabu vya ulamaa wa zamani wa kishia, ili vitabu hivi viwe maji matamu kwa nafsi zenye kuitafuta haki, ili ziweze kufikia kwenye haki ambayo inatolewa na Kambi ya Ahlul-Bayt ulimwengu mzima, ndani ya zama ambazo akili inaerevuka na nafsi na roho zinaboreka kwa kasi ya pekee. Tunatoa shukurani njema kwa Samahatu Sheikh Nazar Hasan kwa kuandika kwake kitabu hiki, na kwa ndugu zetu wote waliosaidia kukichapisha. Na sote tunategemea na kutaraji kuwa tutakuwa tumetoa kile tulichokiweza katika juhudi za kutekeleza baadhi ya wajibu tulionao mbele ya ujumbe wa Mtukufu Mola wetu Mlezi ambaye alimtuma Mtume Wake na uongofu na dini ya haki ili aipe ushindi dhidi ya dini zote. Na Mwenyezi Mungu anatosha kuwa shahidi.
Jumuiya ya kimataifa ya Ahlu-Bait Kitengo cha utamaduni
H
Page H
AHLUBAYT NDANI YA TAF. ZA KISUNNI No 1 check Lubumba.qxd
I
7/1/2011
11:09 AM
Page I
AHLUBAYT NDANI YA TAF. ZA KISUNNI No 1 check Lubumba.qxd
7/1/2011
11:09 AM
Page 1
AHLUBAYT NDANI YA TAF. ZA KISUNNI No 1 check Lubumba.qxd
7/1/2011
11:09 AM
Ahlul Bayt Ndani ya Tafsiri za Kisunni
UTANGULIZI Kila sifa njema ni ya Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wa viumbe wote. Rehema na amani zimwendee Mtume Muhammad, yeye na aali zake watoharifu. Na daima laana iwe juu ya wote walio maadui zao na wakanushaji wa fadhila zao. Qur’ani iliteremkia katika nyumba tohara na safi, ambazo imeidhinishwa zitukuzwe, katika nyumba za aali Muhammad watoharifu, ambazo Mwenyezi Mungu Mtukufu amezifanya makhsusi kwa ajili ya heshima na utukufu kuliko nyingine, na Mwenyezi Mungu akazighani (nyumba hizo) kupitia Aya za Qur’ani tukufu ambazo zitaendelea kubaki muda wa dahari yote zikisomwa usiku na mchana, na si nyumba za viumbe wengine. Kwa ajili hiyo tunawaona (a.s.) wao ndio watambuzi na wajuzi wa Kitabu cha Mwenyezi Mungu Mtukufu kuliko wengine wote, na kwa ajili hiyo tunamwona Amirul-Muuminina (a.s.) Ali bin Abu Talib (a.s.) akisema: “Lau nikitandikiwa mto kisha nikaketi juu yake nitahukumu baina ya wanataurati kwa Taurati yao na wanainjili kwa Injili yao, na baina ya wanazaburi kwa Zaburi yao na wanafurqan kwa Furqani yao. Wallahi hakuna Aya yoyote iliyoteremshwa bara au baharini, katika tambarare au jabali, mbinguni au ardhini, usiku au mchana, ila mimi namjua ni nani iliteremka kwa ajili yake, na iliteremka kuhusu nini.”1 Abu Naiim ameandika katika kitabu Hilyatul-Awliyai kutoka kwa Imam Ali (a.s.) kwamba alisema: “Wallahi hakuna Aya iliyoteremka ila najua iliteremka kwa ajili ya nani, na wapi iliteremka, na hakika Mola wangu Mlezi amenitunukia moyo wenye akili na ulimi wenye kudadisi.” Na pia Abu Naiim ameandika katika kitabu Hilyatul-Awliyai kutoka kwa Ibnu Masuud, amesema: “Hakika Qur’ani iliteremshwa kwa herufi saba, 1 Matwalibus-Suul, cha Ibnu Talha as-Shafiiyu Juz. 1, Uk. 125, chapa ya Taasisi ya Ummul-Qura. 2
Page 2
AHLUBAYT NDANI YA TAF. ZA KISUNNI No 1 check Lubumba.qxd
7/1/2011
11:09 AM
Ahlul Bayt Ndani ya Tafsiri za Kisunni hakuna herufi yoyote ila ina dhahiri na batini, na hakika Ali bin Abu Talib ndiye mwenye dhahiri na batini.” Na kuna kauli moja inanasibishwa na Amirul-Muuminina (a.s.): “Lau nikitaka kuwapigisha magoti ngamia arubaini kwa tafsiri ya Qur’ani ninaweza.” Kisha wao ndio wafasiri wa wahyi wa Mwenyezi Mungu Mtukufu, wenza wa Kitabu chake na Kitabu kitamkacho, haya ndio yathibitishwayo na Hadithi ya Vizito viwili: “Mimi ni mwenye kuacha kati yenu vizito viwili: Cha kwanza ni Kitabu cha Mwenyezi Mungu, humo mna uongofu na nuru…., na Ahlul-Baiti wangu, nawakumbusheni Mwenyezi Mungu kuhusu Ahlul-Baiti wangu, nawakumbusheni Mwenyezi Mungu kuhusu Ahlul-Baiti wangu.”2 Hivyo wao ndio wabainishaji, wafafanuzi na wafasiri wa misamiati ya Qur’ani Adhimu. Kwa sababu Kitabu cha Mwenyezi Mungu kina haja ya kupata mfasiri, mfafanuzi na mfasiri, hivyo ni aula kifani chake na mwenza wake ndiye mbainishaji, mfasiri, alimu na mjuzi wa Kitabu hicho na si mwingine. Kwa ibara nyingine tunaweza kusema: Hakika Ahlul-Baiti (a.s.) ndio waliokusudiwa, kuainishwa na kuashiriwa katika semi zake (s.w.t.). Bali ni katika nyumba zao ndimo kulimoteremka Kitabu, na wenye nyumba ndio wajuzi zaidi wa yale yaliyomo ndani ya nyumba yao. Kuanzia hapa tunawakuta Ahlul-Baiti (a.s.) siku zote wakiifasiri Qur’ani na Maneno ya Mwenyezi Mungu vizuri zaidi na kwa ukamlifu mno. Na watu wote wakirejea kwao bila kumtenga yoyote, na wala hatujaona tukio lililo kinyume na hali hiyo, hata Ibnu Abbas ambaye ni kinara na kiongozi wa wafasiri miongoni mwa sahaba yeye naye alikuwa ni mwanafunzi wa Ali (a.s.), yeye mwenyewe anasema: “Tafsiri ya Qur’ani niliyonayo ni kutoka kwa Ali bin Abu Talib (a.s.).” 2 Sahih Muslim, Juz. 4, Hadithi ya 1873. 3
Page 3
AHLUBAYT NDANI YA TAF. ZA KISUNNI No 1 check Lubumba.qxd
7/1/2011
11:09 AM
Ahlul Bayt Ndani ya Tafsiri za Kisunni Hapo hapo tunawaona ulamaa wa makundi mawili, Shia na Sunni wameifasiri Qur’ani Tukufu kupitia riwaya na nukuu, kama vile Tafsiri ya Ali bin Ibrahim al-Qummiy, Tafsirul-Ayyashiy na Furatil-Kufiy, KanzudDaqaiq ya Ibnu al-Mash’hadiy, al-Burhan ya Sayyid Hashim al-Bahraniy, Nurut-Thaqalayn ya Sheikh Abdu Ali al-Hawiziy, na wengineo miongoni mwa Maimamiya ambao wameifasiri Qur’ani kupitia Ahlul-Baiti (a.s.). Na miongoni mwa Masunni ni kama vile al-Haskaniy katika ShawahidutTanziil, Isfihaniy katika an-Nuru al-Mushtaalu na al-Wahidiy katika Asbabun-Nuzuul. Pia zipo tafsiri zilizozagaa huku na huko ambazo zinategemewa na Sunni katika utafiti na mchakato wa kielimu. Tafsiri hizi zimefasiri baadhi ya Aya tukufu kwamba walengwa halisi wa Aya hizo ni aali Muhammad (a.s.), hivyo tumejaribu kuzikusanya na kuziweka pamoja Aya hizi toka katika kabati za vitabu vya tafsiri muhimu zenye kutegemewa kwao. Miongoni mwazo ni: Jamiul-Bayan Fii Tafsiril-Qur’ani ya Abu Ja’far Muhammad bin Jarir bin Yazid bin Kathiir bin Ghalib at-Tabari, aliyefariki mwaka 310 A.H. Nasi hapa tumetegemea chapa ya Misri yenye juzuu 30. al-Kashfu wal-Bayan Antafsiril-Qur’ani ya Abu Is’haqa Ahmad ibnu Ibrahim at-Thaalabiy an-Nisaburiy al-Muqriu, aliyefariki mwaka 427 A.H. Maalimut-Tanziil ya Abu Muhammad Husain bin Masuud bin Muhammad, maarufu kwa jina la Farrau al-Baghawi as-Shafiy, aliyefariki mwaka 516 A.H. Nasi hapa tumetegemea chapa ya Beirut ambayo ina Juzuu 4. al-Kashaf Anihaqaiqit-Tanziil Wauyuunil-Aqawiil Fii Wujuhit-Taawiil ya Abu Qasim Mahmudu bin Umar bin Muhammad bin Umar alKhawarazimiy al-Hanafiy al-Muutazaliy az-Zamakhshariy, mwenye lakabu ya Jarullah, aliyefariki mwaka 538 A.H. Nasi hapa tumetegemea chapa ya Misri ya mwaka 1948 A.D.
4
Page 4
AHLUBAYT NDANI YA TAF. ZA KISUNNI No 1 check Lubumba.qxd
7/1/2011
11:09 AM
Ahlul Bayt Ndani ya Tafsiri za Kisunni Mafatihul-Ghaybi ya Abu Abdillah Muhammad bin Umar bin Husain bin Hasan bin Ali at-Tamimiy al-Bakriy at-Tarstaniy ar-Razi, mwenye lakabu ya Fakhrud-Din, maarufu kwa jina la Ibnul-Khatib as-Shafiy, aliyefariki mwaka 606 A.H. An’warut-Tanziil Waasrarut-Taawiil ya Kadhi Mkuu Nasrud-Din (AbulKhayri), Abdullah bin Umar bin Muhammad bin Ali al-Baydhawi asShafiy, aliyefariki mwaka 691 A.H. iliyo katika juzuu mbili, iliyochapishwa Misri mwaka 1968 A.D. al-Jamiu Liahkamil-Qur’ani ya Abu Abdillah Muhammad bin Ahmad bin Abubakri al-Ansariy al-Khazrajiy al-Undlusiy al-Qurtubiy, aliyefariki mwaka 761 A.H. iliyo katika juzuu ishirini, iliyochapishwa Misri mwaka 1950 A.D. Tafsirul-Qur’ani al-Adhiim ya Hafidh Imadud-Din (Abul-Fidai), Ismail bin Amru bin Kathiir bin Dhaw’u bin Kathiir bin Zar’i al-Baswriy adDamashqiy, Ibnu Kathiir, aliyefariki mwaka 774 A.H. iliyo katika juzuu tano, iliyochapishwa Beirut. ad-Duru al-Manthur Fii Tafsiri Bil-Maathur ya Hafidh Jalalud-Din (AbulFadhli), Abdurahman bin Abubakri bin Muhammad as-Suyuti, aliyefariki mwaka 911 A.H. iliyo katika juzuu nne, iliyochapishwa Misri. Ruhul-Bayan ya Allamah Sheikh Ismail Haqiyyu al-Barsiyyu, aliyefariki mwaka 1137 A.H. iliyo katika juzuu thelathini, nasi hapa tumetegemea chapa ya Uthmaniya ya mwaka 1330 A.H. Ruhul-Maaniy ya Allamah Abul-Fadhli Shihabud-Din, Sayyid Muhammad Al-Alusiy, aliyefariki mwaka 1270 A.H., iliyo katika juzuu thelathini, nasi hapa tumetegemea chapa ya Misri ambayo ilipigwa chapa na Al-Muniriyah mwaka 1345 A.H. Tafsirul-Qummiy, maarufu kwa jina la Mahasinut-Taawiili ya Allamah asSham Muhammad bin Jamalud-Din al-Qasimiy, aliyefariki mwaka 1322 A.H., iliyo katika juzuu kumi na saba, nasi hapa tumetegemea chapa ya 5
Page 5
AHLUBAYT NDANI YA TAF. ZA KISUNNI No 1 check Lubumba.qxd
7/1/2011
11:09 AM
Ahlul Bayt Ndani ya Tafsiri za Kisunni Beirut ya Ihyaut-Turathil-Arabiy ya mwaka 1415 AH. Tafsiri hizi zimepangwa kulingana na kipaumbele na umuhimu. Hivyo kutokana na wajibu wa kiitikadi na jukumu la kisheria, pia kutokana na kuwepo mapungufu ambayo ni lazima tuyazibe kwa kile kinachonasibiana na ukubwa wa mahitaji ya upungufu huo, na ili kuitikia wito wa Mwenyezi Mungu Ambaye mara kwa mara ametangaza katika Qur’ani wito wa kuwapenda aali Muhammad (a.s.) aliposema: “Sema: Kwa haya siombi malipo yoyote kwenu isipokuwa mapenzi kwa kizazi changu” (Sura Shura: 23), tumefanya kazi hii iliyobarikiwa ambayo inamimina maji kutoka katika bahari ya aali Muhammad (a.s.) iliyojaa na yenye kububujika. Na ni kutokana pia na umuhimu wa kazi hii katika kuthibitisha maarifa na nafasi ya Ahlul-Baiti (a.s.), ili uthibitisho huo uwe hoja yenye nguvu, na hapo utimie msemo “Nafuata kinywa chako.” Pia ni ili kuthibitisha kwamba wao ndio walioainishwa na kukusudiwa na Kitabu cha Mwenyezi Mungu Mtukufu. Kazi hii imeendelea toka siku ya kumi na nane ya mfunguo pili mwaka 1420 A.H. mpaka siku ya ishirini na tatu ya mfunguo tatu mwaka 1426 A.H., lakini kazi hii ilikumbwa na matatizo mengi ikiwa ni pamoja na hali kutotulia, kutopatikana rejea, na nyudhuru nyingine mfano wa hizo. Pamoja na hayo yote tulivumilia kwa kalamu ya mahaba na upendo wetu kwa wateule Ahlul-Baiti (a.s.) nyudhuru zote zilizotukabili, tukazama katika kina cha tafsiri na wafasiri ili tutoe humo johari na vito vya aali Muhammad (a.s.) baada ya kuwa vimefichwa na kufunikwa na vumbi la historia kwa sababu za siasa ya kidunia. Pia katika ziara yetu ya kitafsiri tumezitambua nafsi za wafasiri, hivyo tumegundua kwamba Ibnu Kathir ndiye mwenye maradhi makubwa ya nafsi na ndiye mwenye chuki kubwa dhidi ya Ahlul-Baiti (a.s.) na wafuasi wao wema. At-Thaalabiy ndiye mwadilifu na mwenye insafu kuliko 6
Page 6
AHLUBAYT NDANI YA TAF. ZA KISUNNI No 1 check Lubumba.qxd
7/1/2011
11:09 AM
Ahlul Bayt Ndani ya Tafsiri za Kisunni wengine. Utafiti huu tuliuwakilisha kwenye kongamano la mwaka la Sheikh Tusiy ambalo lilifanyika katika Jamhuri ya Kiislam ya Iran katika Jiji la Qum Takatifu, mwaka 1426 A.H. hatimaye ukapata tuzo katika kongamano hilo adhimu. Haya yote ni sehemu ya fadhila za Mola wangu na neema kutoka Kwake (s.w.t.), na ni sehemu ya msaada toka katika roho toharifu (a.s.), kwa sababu kazi hii ni kwa ajili yao na si kwa ajili ya mwingine. Mwisho tunainua mikono yote kutoa shukurani kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, tunamwomba maghufira dhidi ya utelezo na makosa yaliyotoka kwetu, kwa sababu umaasumu ni wa wenye nao. Pia tunamtaka msamaha msomaji mpendwa kutokana na makosa yasiyo ya kukusudiwa atakayoyakuta humu. Na kila sifa njema ni ya Mwenyezi Mungu Mola Mlezi wa viumbe wote. Nizar Hasan 2 Mfunguo Nne 1427 A.H. Qum Takatifu
7
Page 7
AHLUBAYT NDANI YA TAF. ZA KISUNNI No 1 check Lubumba.qxd
7/1/2011
11:09 AM
Ahlul Bayt Ndani ya Tafsiri za Kisunni
AHLUL-BAIT (A.S.) NDANI YA TAFSIRI YA TABARI, INAYOITWA JAMIUL-BAYAN ANITAAWIIL AYIL-QUR’ANI SURA AALI IMRAN Kauli ya Mwenyezi Mungu:
“Hakika Mwenyezi Mungu alimchagua Adam na Nuh na watoto wa Ibrahim na watoto wa Imran juu ya walimwengu wote.” (Sura Aali Imran; 3:33). Al-Muthana amenisimulia, amesema: “Abdullah bin Salih ametusimulia, amesema: Muawiya amenisimulia kutoka kwa Ali, kutoka kwa Ibnu Abbas kuhusu kauli yake (s.w.t.): “Hakika Mwenyezi Mungu alimchagua Adam na Nuh na watoto wa Ibrahim na watoto wa Imran juu ya walimwengu wote.” (Sura Aali Imran; 3:33), amesema: ‘Hao ni waumini toka aali Ibrahim, aali Imran, aali Yasini na aali Muhammad (s.a.w.w.).”3 Kauli ya Mwenyezi Mungu:
“Na Malaika waliposema: Ewe Maryam! Hakika Mwenyezi Mungu amekuteua na akakutakasa na akakuteua juu ya wanawake wa ulimwenguni.” (Sura Aali Imran; 3:42). 3 Tafsirut-Tabariy Juz. 3, Uk. 234. Inadhihiri toka katika baadhi ya tafsiri kama Tafsiri Al-Khazin, Durul-Manthuur na Shawahidut-Tanziil kwamba Aali Yasin ndio hao hao Aali Muhammad (s.a.w.w.). 8
Page 8
AHLUBAYT NDANI YA TAF. ZA KISUNNI No 1 check Lubumba.qxd
7/1/2011
11:09 AM
Ahlul Bayt Ndani ya Tafsiri za Kisunni Bushru ametusimulia, amesema: Ametusimulia Yazid, amesema: Said ametusimulia kutoka kwa Qatadah kuhusu kauli yake (s.w.t.): “Na Malaika waliposema: Ewe Maryam!” kwamba tumeambiwa kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) alikuwa akisema: “Yakutosha juu ya wanawake wa ulimwenguni: Maryam binti Imran, mke wa Firaun, Khadija binti Khuwaylid na Fatima binti Muhammad.”4 Nimesimuliwa kutoka kwa Ammar, amesema: Ametusimulia Ibnu Abi Ja’far kutoka kwa baba yake kuhusu kauli yake (s.w.t.): “Na Malaika waliposema...”, akasema: “Thabitu al-Bunaniy alikuwa akisimulia kutoka kwa Anas bin Malik kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) alisema: ‘Kati ya wanawake wa ulimwenguni wabora ni wanne: Maryam binti Imran, Asia binti Muzahim mke wa Firaun, Khadija binti Khuwaylid na Fatima binti Muhammad.”’ Amesema: Ametusimulia Adam al-Asqalani, amesema: Shaabah ametusimulia, amesema: Ametusimulia Amru bin Murrah, amesema: Nilimsikia Murrah al-Hamdani akisimulia kutoka kwa Abu Musa alAsh’ariy kwamba amesema: Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) alisema: “Kati ya wanaume wamekamilika wengi, na kati ya wanawake hajakamilika ila Maryam, Asia mke wa Firaun, Khadija binti Khuwaylid na Fatima binti Muhammad.” Amesema: Ametusimulia Abul-As’wad al-Misriy, amesema: Ametusimulia Ibnu Twiat kutoka kwa Umarat bin Ghazyat, kutoka kwa Muhammad bin Abdurahman bin Amru bin Uthman, kwamba alisimuliwa na Fatima binti Husein bin Ali kwamba: Fatima binti wa Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) alisema: “Siku moja Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) aliingia kwa Aisha nami nikiwa humo, akaninong’oneza nami nikalia, kisha akaninong’oneza tena nami nikacheka, Aisha akaniuliza kuhusu hali hiyo, nikamwambia: ‘Bila shaka umefanya haraka hivi kweli nikupe siri ya Mtume wa Mwenyezi Mungu?’ akaniacha. “ 4 Juz. 3, Uk. 263. 9
Page 9
AHLUBAYT NDANI YA TAF. ZA KISUNNI No 1 check Lubumba.qxd
7/1/2011
11:09 AM
Ahlul Bayt Ndani ya Tafsiri za Kisunni Alipofariki Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) Aisha alimuuliza, naye akamjibu: Ndio alininong’oneza akasema: “Jibril alikuwa akiipitia Qur’ani kila mwaka mara moja, na hakika mwaka huu kaipitia Qur’ani mara mbili, na hakika hakuna Nabii yeyote ila alipewa nusu ya umri wa Nabii aliyekuwa kabla yake, na hakika ndugu yangu Isa umri wake ulikuwa miaka mia moja na ishirini, nami hivi sasa nina miaka sitini, nami ni mwenye kufariki ndani ya mwaka huu, na hajapata mwanamke yeyote kati ya wanawake wa ulimwenguni kufikwa na msiba mfano wa ule utakaokufika, wala usiwe mwanamke usiye na subira” ndipo nikalia, kisha akasema (s.a.w.w.): “Hakika wewe ni mbora wa wanawake wa peponi.”5 Kauli ya Mwenyezi Mungu:
“Na watakaokuhoji baada kukufikia elimu hii, waambie: Njooni tuwaite watoto wetu na watoto wenu, na wanawake zetu na wanawake wenu, na nafsi zetu na nafsi zenu, kisha tuombe kwa unyenyekevu tutake laana ya Mwenyezi Mungu iwashukie waongo.” (Sura Aali Imran; 3:61). Ametusimulia Ibnu Hamid, amesema: Ametusimulia Jariri kutoka kwa Mughira, kutoka kwa Amir, amesema: “Akaamrishwa, yaani Mtume (s.a.w.w.) kuombeana laana na watu wa Najran kwa kauli yake (s.w.t.): “Na 5 Tafsirut-Tabari Juz. 3 Uk. 264. Vipi Fatima asiwe mbora wa wanawake wa peponi na hali yeye ndiye kiumbe mtukufu na mkweli kuliko wao. Mtume Muhammad (s.a.w.w.) alisema kuhusu haki yake kama ilivyo katika kitabu Bukhari Juz. 2 Uk. 185: “Fatima ni sehemu ya nyama yangu…”, na bila shaka ni kwamba Mtume ndiye mbora katika nyumba zote mbili (Dunia na Akhera) na Fatima ni kipande na sehemu ya baba yake, hivyo ni lazima Fatima awe mbora wa wanawake wa ulimwenguni katika nyumba zote mbili (Dunia na Akhera). 10
Page 10
AHLUBAYT NDANI YA TAF. ZA KISUNNI No 1 check Lubumba.qxd
7/1/2011
11:09 AM
Ahlul Bayt Ndani ya Tafsiri za Kisunni watakaokuhoji…”, hivyo (watu wa Najran) wakaahidiana wamwombee laana na wakamuahidi iwe ni siku ya kesho, ndipo wakaenda kwa Sayyid Askofu, naye alikuwa ndiye mwenye akili kuliko wao hivyo wakamfuata, wakaenda kwa mtu mwenye akili miongoni mwao, wakamweleza yale waliyokubaliana na Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.), akawaambia: “Mmefanya nini?” akawalaumu na kuwaambia: “Ikiwa kweli ni Mtume kisha akiwaombea mabaya katu Mwenyezi Mungu hatomghadhibisha kati yenu. Na ikiwa ni Mfalme akiwashinda katu hatowabakisheni.” Wakasema: Tutafanya nini nasi tayari tumeshamwahidi? Basi walipokwenda Mtume alikwenda na hali amemkumbatia Hasan na amemshika mkono Husein na Fatima akitembea nyuma yake, akawaita, wakasema: Tunajikinga kwa Mwenyezi Mungu. Kisha akawaita tena, wakasema: Mara zote tunajikinga kwa Mwenyezi Mungu. Mtume (s.a.w.w.) akasema: “Ingieni katika Uislamu mtapata haki waliyo nayo waislamu, na mtawajibikiwa na yale yaliyo wajibu kwa waislamu….”6 Ametusimulia Ibnu Hamid: Ametusimulia Isa bin Farqad kutoka kwa Abul-Jarud, kutoka kwa Zayd bin Ali kuhusu kauli yake (s.w.t.): “Njooni tuwaite watoto wetu na watoto wenu…” amesema: “Walikuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu, Ali, Fatima, Hasan na Husein.”7 Ametusimulia Muhammad bin Husein, amesema: Ametusimulia Ahmad bin al-Mufadhil, amesema: Kutoka kwa as-Sadiy kuhusu kauli yake (s.w.t.): “Na watakaokuhoji baada kukufikia elimu hii…”, Mtume (s.a.w.w.) aliwashika mkono Hasan, Husein na Fatima, akamwambia Ali tufuate, akatoka pamoja nao, siku hiyo hakuna nasara yeyote aliyejitokeza, Mtume akasema: “Lau wangejitokeza basi wangeteketea.”8 Yunus amenisimulia, amesema: Ibnu Wahbi ametupa habari, amesema: Ametusimulia Ibnu Zayd, amesema: Mtume wa Mwenyezi Mungu 6. Juz. 3 Uk. 299. al-Haskaniy ameiandika katika Shawahidut-Tanziil Juz. 1 Uk. 120, chapa ya Beirut. 7. Tafsirut-Tabari Juz. 3 Uk. 300. 8. Juz. 3 Uk. 300. 11
Page 11
AHLUBAYT NDANI YA TAF. ZA KISUNNI No 1 check Lubumba.qxd
7/1/2011
11:09 AM
Ahlul Bayt Ndani ya Tafsiri za Kisunni (s.a.w.w.) aliambiwa: “Lau ungewalaani kaumu ungekuja na nani uliposema: “…watoto wetu na watoto wenu…”? Akasema (s.a.w.w.): “Hasan na Husein.”9 Muhammad bin Sanan amenisimulia, amesema: Ametusimulia Abu Bakr al-Hanafiy, amesema: Ametusimulia al-Mundhir bin Thaalabah, amesema: Ametusimulia Ulbau bin Ahmar al-Yashkriy, amesema: Ilipoteremka Aya hii: “Waambie: Njooni tuwaite watoto wetu na watoto wenu…” Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) alituma waitwe Ali, Fatima, na watoto wao wawili Hasan na Husein, kisha akawaita wakristo ili waombeane laana. Kijana miongoni mwa Mayahudi akasema: “Ole wenu! Si waliwausieni jana ndugu zenu ambao waligeuzwa nyani na nguruwe kwamba msishiriki maapizo.” Wakaacha.10 Ametusimulia Hasan bin Yahya, amesema: Abdurazaq ametupa habari, amesema: Maamar ametupa habari kutoka kwa Qatadah kuhusu kauli Yake (s.w.t.): “Na watakaokuhoji baada kukufikia elimu hii…”, amesema: Mtume (s.a.w.w.) alipowakusudia watu wa Najran alimshika mkono Hasan na Husain, akamwambia Fatima tufuate, maadui wa Mwenyezi Mungu walipoona mwonekano huo wakarejea.11 Kauli ya Mwenyezi Mungu: “Na hakika Mwenyezi Mungu aliwatimizia miadi yake….” (Sura Aali Imran: 152). Ametusimulia Muhammad, amesema: Ametusimulia As’bat kutoka kwa as-Sadiy, amesema: Mtume wa Mwenyezi Mungu alipotokeza kwa mushrikina huko Uhud aliwaamuru askari wa mishale wakakaa juu ya mlima wakiwa wamezielekea ngamia za mushrikina, akasema: “Msitoke mlipo..” na akamfanya Abdullah bin Jubair kuwa kiongozi wao. Kisha akasimama Talha bin Uthman mshika bendera ya mushrikina akasema: 9. Tafsirut-Tabari Juz. 3 Uk. 301. 10. Tafsirut-Tabari Juz. 3 Uk. 301. 11. Tafsirut-Tabari Juz. 3, Uk. 301. Tunapata nukta zifuatazo kama faida kutoka katika Aya ya Maapizano: 12
Page 12
AHLUBAYT NDANI YA TAF. ZA KISUNNI No 1 check Lubumba.qxd
7/1/2011
11:09 AM
Ahlul Bayt Ndani ya Tafsiri za Kisunni “Enyi kundi la wafuasi wa Muhammad! Bila shaka nyinyi mnadai kwamba Mwenyezi Mungu atatuharakisha motoni kupitia panga zenu na atawaharakisheni peponi kupitia panga zetu, basi je yupo yeyote miongoni mwenu anayetaka Mwenyezi Mungu amuharakishe peponi kupitia upanga wangu au aniharakishe motoni kupitia upanga wake?” Akasimama Ali bin Abu Talib akasema: “Naapa kwa Yule Ambaye nafsi yangu imo mikononi Mwake, sitokuacha mpaka Mwenyezi Mungu akuharakishe motoni kupitia upanga wangu.” Ali akampiga dharuba lililokata miguu yake na hatimaye akaanguka chini, tupu yake ikafunuka, akasema: “Nakuomba kwa ajili ya Mwenyezi Mungu na udugu ewe binamu yangu.” Ndipo akamwacha, Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) akatoa Takbira na sahaba zake wakamwambia Ali: “Kitu gani kilikuzuia usimuuwe moja kwa moja.” Akasema: “Hakika binamu yangu aliniomba pindi utupu wake ulipofunuka, hivyo nikamwonea haya.”12
SURAT AL-MAIDA Kauli ya Mwenyezi Mungu:
“Hakika Walii wenu hasa ni Mwenyezi Mungu na Mtume wake na wale walioamini ambao husimamisha Swala na hutoa Zaka wakiwa wamerukui.” (Surat al-Maida: 55). Amesema: Ametusimulia Abdullah bin Salih, amesema: “Amenisimulia Muawiya bin Salih kutoka kwa Ali bin Talha, kutoka kwa Ibnu Abbas kuhusu kauli yake (s.w.t.): “Hakika Walii wenu hasa ni Mwenyezi Mungu na Mtume wake na wale walioamini…” inamkusudia Ali bin Abu Talib.”13 12. Tafsirut-Tabari Juz. 4, Uk. 125. 13.Tafsirut-Tabari Juz. 6, Uk. 288. Pia Al-Ayyashiy ameiandika katika tafsiri yake Juz. 1, Uk. 356, chapa ya Beirut. 13
Page 13
AHLUBAYT NDANI YA TAF. ZA KISUNNI No 1 check Lubumba.qxd
7/1/2011
11:09 AM
Ahlul Bayt Ndani ya Tafsiri za Kisunni Ametusimulia Muhammad bin Husein, amesema: Ametusimulia Ahmad bin al-Fadhlu, amesema: Ametusimulia Asbat kutoka kwa as-Sadiy, amesema: “Kisha akawajuza ni nani atakayewatawala, akasema: “Hakika Walii wenu hasa ni Mwenyezi Mungu na Mtume wake na wale walioamini ambao husimamisha Swala na hutoa Zaka wakiwa wamerukui.” Ali bin Abu Talib alipitiwa na ombaomba akiwa amerukui msikitini, ndipo akampa pete yake.” Ametusimulia Hinad bin as-Sariy, amesema: Ametusimulia Ubdat kutoka kwa Abdul-Malik, kutoka kwa Abu Ja’far, amesema: “Nilimuuliza kuhusu Aya hii: “Hakika Walii wenu hasa ni Mwenyezi Mungu na Mtume wake na wale walioamini…” Tukasema: Wale walioamini. Tukasema: Imetufikia kwamba iliteremka kwa ajili ya Ali bin Abu Talib. Akasema: “Ali ni miongoni mwa wale walioamini.” Ametusimulia Ismail bin Israil ar-Ramliy, amesema: Ametusimulia Aywabu bin Suwaydi, amesema: “Ametusimulia Utbah bin Abu Hakim kuhusu Aya hii: “Hakika Walii wenu hasa ni Mwenyezi Mungu na Mtume wake na wale walioamini…” akasema: Ali bin Abu Talib.” Amenisimulia al-Harith, amesema: Ametusimulia Abdul-Aziz, amesema: Ametusimulia Ghalib bin Ubaydullah, amesema: “Nimemsikia Mujahid akisema kuhusu kauli yake (s.w.t.): “Hakika Walii wenu hasa ni Mwenyezi Mungu na Mtume wake na wale walioamini…”, akasema: Iliteremka kwa ajili ya Ali bin Abu Talib, alitoa sadaka na hali akiwa katika rukuu.”14
14. Tafsirut-Tabari Juz. 6 Uk. 289. 14
Page 14
AHLUBAYT NDANI YA TAF. ZA KISUNNI No 1 check Lubumba.qxd
7/1/2011
11:09 AM
Ahlul Bayt Ndani ya Tafsiri za Kisunni
SURA AL-AN’AM Kauli ya Mwenyezi Mungu: “…Na toeni haki yake siku ya kuvunwa kwake…” (Sura al-An’am: 141). Ametusimulia Umar bin Ali, amesema: Ametusimulia Kathiir bin Hisham, amesema: Ametusimulia Ja’far bin Barqan kutoka kwa Yazid bin alAswam, amesema: “Ilikuwa mtende unapokatwa mtu huja na tawi lake na kuliweka pembezoni mwa msikiti, masikini huja na kulipiga kwa fimbo yake, zikipikutika tende huzila, ndipo siku moja Mtume wa Mwenyezi Mungu akaingia akiwa pamoja na Hasan na Husein (a.s.) mmoja wao akaokota na kula tende, Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) akamtemesha toka kinywani mwake. Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) na Ahlul-Baiti zake walikuwa hawali sadaka. Hivyo wakateremshiwa: “…Na toeni haki yake siku ya kuvunwa kwake…”15
SURA AARAF Kauli ya Mwenyezi Mungu: “Na tutaondoa chuki vifuani mwao……” (Sura Aaraf: 43). Ametusimulia Muhammad bin Abdul-Aala, amesema: Ametusimulia Muhammad bin Thawri kutoka kwa Maamar, kutoka kwa Qatadah, amesema: Ali bin Abu Talib alisema: “Hakika mimi16 nataraji bila shaka kuwa ndiye niliye miongoni mwa wale ambao Mwenyezi Mungu amesema kuwahusu: “Na tutaondoa chuki vifuani mwao……”
15. Tafsirut-Tabari Juz. 8, Uk. 57. 16. Tafsirut-Tabari Juz. 8, Uk. 183. al-Haskaniy ameandika katika kitabu Shawahidut-Tanziil Juz. 1, Uk. 220, kutoka kwa Abdullah bin Malil, kutoka kwa Ali (a.s.) kuhusu kauli yake (s.w.t.): "Na tutaondoa chuki vifuani mwao……" kwamba alisema (a.s.): "Iliteremka kwa ajili yetu." 15
Page 15
AHLUBAYT NDANI YA TAF. ZA KISUNNI No 1 check Lubumba.qxd
7/1/2011
11:09 AM
Ahlul Bayt Ndani ya Tafsiri za Kisunni
SURA AL-AN’FAL Kauli ya Mwenyezi Mungu: “Na walipokupangia njama wale waliokufuru ili wakufunge au wakuue au wakutoe…” (Sura al-An’fal: 30). Ametusimulia Hasan bin Yahya, amesema: Ametupa habari Abdurazaq, amesema: Baba yangu amenipa habari kutoka kwa Akrimah, amesema: “Pindi Mtume (s.a.w.w.) alipotoka kwenda pangoni alimwamuru Ali bin Abu Talib (a.s.) akalala kitandani kwake, wakakesha mushrikina wakimlinda, kila walipomwona amelala walidhani ndiye Mtume (s.a.w.w.) hivyo wakamwacha. Ilipofika asubuhi walimvamia na hali wakidhani ndiye Mtume (s.a.w.w.), ghafla wakajikuta wamemzingira Ali (a.s.).”17 Amenisimulia al-Muthana, amesema: Ametusimulia Abdurazaq kutoka kwa Maamar, amesema: Uthman al-Jazriy amenipa habari kwamba: Hakika Muqsim huria wa Ibnu Abbas alimpa habari kutoka kwa Ibnu Abbas kuhusu kauli yake (s.w.t.): “Na walipokupangia njama wale waliokufuru” kwamba alisema: “Makuraishi walishauriana usiku mmoja huko Makka, baadhi yao wakasema: Akiamka mfungeni kwa kizuizi. Wakimkusudia Mtume (s.a.w.w.). Na wengine wakasema: Muuweni huku wengine wakisema: Mfukuzeni. Ndipo Mwenyezi Mungu akamjuza Nabii wake mkakati huo. Ali bin Abu Talib akalala usiku huo juu ya kitanda cha Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na Mtume akatoka, walipofika asubuhi walimvamia na walipomuona kuwa ni Ali, Mwenyezi Mungu alizuia njama yao, wakasema: “Yupo wapi swahiba wako?” Akajibu: “Sijui.” Wakafuata nyayo zake na walipoufikia mlima na kupitia pangoni wakaona utando wa buibui mlangoni.” 17 Juz. 9, Uk. 228. al-Hafidh al-Haskaniy amesema katika kitabu chake Shawahidut-Tanziil Juz. 1, Uk. 96, kwamba: "Ali alipolala juu ya kitanda cha Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) Mwenyezi Mungu aliteremsha Qur'ani nayo ni kauli yake (s.w.t.): "Na miongoni mwa watu kuna ambaye huiuza nafsi yake kwa ajili ya kutaka radhi ya Mwenyezi Mungu na Mwenyezi Mungu ni Mwenye huruma juu ya waja." (Sura al-Baqarah: 207)." 16
Page 16
AHLUBAYT NDANI YA TAF. ZA KISUNNI No 1 check Lubumba.qxd
7/1/2011
11:09 AM
Ahlul Bayt Ndani ya Tafsiri za Kisunni Muhammad bin Husein, amesema: Ametusimulia Ahmad bin Mufdhil kutoka kwa as-Sadiy kuhusu kauli yake (s.w.t.): “Na walipokupangia njama wale waliokufuru ili wakufunge…”, amesema: “Ni pindi wazee wa kikuraishi walipokusanyika kushauriana kuhusu Mtume (s.a.w.w.). Ibilisi akaja kwa sura ya mtu mmoja miongoni mwa watu wa Najdi akaingia pamoja nao katika bunge. Baadhi yao wakasema: “Muhammad atakapolala kitandani kwake mshikeni na kumweka kizuizini katika nyumba, tumzuie kwa muda tuone itakuwaje.” Ibilisi akasema: “Hilo ulilosema ni baya mno, mtamweka kizuizini katika nyumba jamaa zake watakuja na kumtoa.” Wakasema mzee amesema kweli. Abu Jahli ambaye alipata ubora kwao kwa kutiiwa na Ibilisi akasema: “Bali tuliweke jukumu hili katika kila tumbo miongoni mwa matumbo ya kikuraishi, tumchague mtu mmoja toka kila tumbo na tumpe silaha na wote wamvamie Muhammad kwa pamoja, wampige pigo la mtu mmoja, hapo kizazi cha Abdul-Mutalib hawawezi kuwaua makuraishi hivyo hawatoambulia ila fidia tu.” Ibilisi akasema: “Umesema kweli, kijana huyu ndiye mwenye mawazo mazuri mno kati yenu.” Wakatekeleza hilo. Mwenyezi Mungu akampa habari hiyo Mtume Wake, akaenda pangoni na Ali bin Abu Talib akalala juu ya kitanda chake.”18 Kauli ya Mwenyezi Mungu: “Na jueni kwamba chochote mlichopata ghanima, basi khumsi yake ni ya Mwenyezi Mungu na Mtume na jamaa na mayatima na masikini na msafiri……” (Sura al-An’fal: 41). Amenisimulia Ibnu Wakiiu, amesema: Baba yangu amenisimulia kutoka kwa Sharik, kutoka kwa Khaswif, kutoka kwa Mujahid, amesema: “Aali Muhammadi haikuwa halali kwao sadaka ndipo akawawekea khumsi.”19 18. Tafsirut-Tabari Juz. 9, Uk. 229. 19.Tafsirut-Tabari Juz. 10, Uk. 5. Shawahidut-Tanziil Juz. 1, Uk. 218.
17
Page 17
AHLUBAYT NDANI YA TAF. ZA KISUNNI No 1 check Lubumba.qxd
7/1/2011
11:09 AM
Ahlul Bayt Ndani ya Tafsiri za Kisunni Amenisimulia Ahmad bin Is’haqa, amesema: Ametusimulia Abu Ahmad, amesema: Katusimulia Sharik kutoka kwa Khaswif kutoka kwa Mujahid, amesema: “Mtume wa Mwenyezi Mungu na Ahlul-Bait wake hawakuwa wakila sadaka ndipo wakawekewa khumsi.” Amenisimulia Muhammad bin Ammara, amesema: Ametusimulia Ismail bin Aban, amesema: Ametusimulia Swabahu bin Yahya al-Mazniy kutoka kwa as-Sadiy, kutoka kwa Ibnu Daylamiy, amesema: Ali bin Husein (a.s.) alimwambia mzee mmoja wa Sham: “Hivi umewahi kusoma katika Surat al-Anfal: “Na jueni kwamba chochote mlichopata ghanima, basi khumsi yake ni ya Mwenyezi Mungu na Mtume na jamaa…” Mzee akasema: “Ndio, kwani nyinyi ndio hao?” Akasema (a.s.): “Ndio.” Amenisimulia al-Harith, amesema: Ametusimulia Abdul-Aziz, amesema: Ametusimulia Abdul-Ghaffar, amesema: Ametusimulia al-Man’hal bin Amru, amesema: Nilimuuliza Abdullah bin Muhammad bin Ali na Ali bin Husein kuhusu khumsi, wakasema: “Hiyo ni ya kwetu.” Nikamwambia Ali: “Hakika Mwenyezi Mungu anasema: “…na mayatima na masikini…” Akasema: “Mayatima wetu na maskini wetu.”20
SURA TAWBA Kauli ya Mwenyezi Mungu:
“(Tangazo la) Kujitoa Mwenyezi Mungu na Mtume wake kwa wale mlioahidiana nao miongoni mwa mushrikina.” (Sura Tawba: 1). Ametusimulia Ahmad bin Is’haqa, amesema: Ametusimulia Abu Ahmad, amesema: Ametusimulia Israil kutoka kwa Abu Is’haq, kutoka kwa Zayd bin Yushyau, amesema: “Iliteremka Sura Baraa Mtume wa Mwenyezi 20. Juz. 10, Uk. 8. 18
Page 18
AHLUBAYT NDANI YA TAF. ZA KISUNNI No 1 check Lubumba.qxd
7/1/2011
11:09 AM
Ahlul Bayt Ndani ya Tafsiri za Kisunni Mungu akamtuma nayo Abu Bakr kisha akamtuma Ali, akaichukua toka kwake. Abu Bakr aliporejea kwa Mtume akasema: ‘Je kuna chochote kilichoteremka kunihusu?’ Mtume (s.a.w.w.) akasema: ‘Hapana, lakini bila shaka nimeamrishwa niitangaze mimi mwenyewe au mtu kutoka katika Ahlul-Baiti wangu.”’21 Ametusimulia Ibrahim bin Said al-Jawhariy, amesema: Ametusimulia Husein bin Muhammad, amesema: Ametusimulia Sulayman bin Qarmi kutoka kwa Aamash, kutoka kwa Hakim, kutoka kwa Muqsim, kutoka kwa Ibnu Abbas, kwamba: “Hakika Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) alimtuma Abu Bakr na Sura Baraa, kisha akamtumia Ali aichukue toka kwake. Abu Bakr akasema: ‘Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu! kuna lolote limetokea kwangu?’ Akasema (s.a.w.w.): ‘Hapana, wala hafikishi kwa niaba yangu ila mimi mwenyewe au Ali.’ Alikuwa amemtuma Ali mambo manne: Haiingii peponi ila mwislamu, baada ya mwaka huu mushriku haruhusiwi kuhiji wala kutufu na hali mtupu. Na yule ambaye kati yake na Mtume wa Mwenyezi Mungu kuna ahadi basi itaendelea mpaka mwisho wa muda wake. Ametusimulia Ibnu Hamid, amesema: Ametusimulia Salmah, amesema: Ametusimulia Muhammad bin Is’haq kutoka kwa Hakim bin Ibad bin Hanif, kutoka kwa Abu Ja’far Muhammad bin Ali bin Husein bin Ali, amesema: “Ilipoteremka Sura Baraa kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) alimtuma Abu Bakr, akaambiwa: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu! ungemtumia mtu Abu Bakr. Akasema: ‘Hafikishi kwa niaba yangu ila mtu kutoka katika Ahlul-Baiti wangu.’ Kisha akamwita Ali bin Abu Talib na kumwambia: ‘Ondoka na kisa hiki toka mwanzo wa Baraa, watangazie watu siku ya kuchinja watakapokusanyika.’ Ali bin Abu Talib akatoka akiwa amepanda ngamia wa Mtume wa Mwenyezi Mungu al-Adhbau.”22 21. Juz. 10, Uk. 64. 22.Tafsirut-Tabari Juz. 10, Uk. 65. 19
Page 19
AHLUBAYT NDANI YA TAF. ZA KISUNNI No 1 check Lubumba.qxd
7/1/2011
11:09 AM
Ahlul Bayt Ndani ya Tafsiri za Kisunni Amenisimulia Muhammad bin Husein, amesema: Ametusimulia Ahmad bin al-Mufdhil, amesema: Katusimulia Asbat kutoka kwa as-Sadiy, amesema: “Aya hizi mpaka aya ya arubaini, Mtume wa Mwenyezi Mungu alimtuma nazo Abu Bakr na akamwamuru azitangaze kwa mahujaji. Alipotembea hadi kuufikia mti kwa Njia ya Dhilhalifa alimtumia Ali akaichukua toka kwake. Abu Bakr akarejea kwa Mtume na kusema: ‘Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu! baba yangu na mama yangu wawe fidia kwako, je kuna chochote kimeteremka kunihusu?’ Akasema (s.a.w.w.): ‘Hapana, lakini hafikishi kwa niaba yangu asiyekuwa mimi au asiyetokana na mimi.” Kauli ya Mwenyezi Mungu:
“Je, mnafanya kuwanywesha mahujaji na kuamirisha msikiti mtukufu ni sawa na yule aliyemwamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho na akapigana jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu? Hawawi sawa mbele ya Mwenyezi Mungu na Mwenyezi Mungu hawaongozi watu madhalimu.” (Sura Tawba: 19). Amenisimulia Yunus, amesema: Ibnu Wahbi ametupa habari, amesema: Nimepewa habari kutoka kwa Abu Swakhri, amesema: Nilimsikia Muhammad bin Kaab al-Qardhiyu akisema: “Talha bin Shayba toka kizazi cha Abdudar, Abbas bin Abdul-Mutalib na Ali bin Abu Talib kila mmoja alijigamba. Talha akasema: ‘Mimi ndio mtunza Nyumba, funguo zimo mikononi mwangu na hata nikitaka nalala humo.’ Abbas akasema: ‘Mimi ndiye mgawa maji na msimamizi wake na hata nikitaka nalala msikitini.’ 20
Page 20
AHLUBAYT NDANI YA TAF. ZA KISUNNI No 1 check Lubumba.qxd
7/1/2011
11:09 AM
Ahlul Bayt Ndani ya Tafsiri za Kisunni Ali akasema: ‘Sijui mtasema nini. Bila shaka nimeswali miezi sita kabla ya mtu yeyote na mimi ndiye mwanajihadi.’ Ndipo Mwenyezi Mungu akateremsha: “Je, mnafanya kuwanywesha mahujaji na kuamirisha msikiti mtukufu….””23 Muhammad bin Hasan amenisimulia, amesema: Ahmad bin al-Mufdhil ametusimulia, amesema: Amesema Asbat kutoka kwa as-Sadiy kuhusu “kuwanywesha mahujaji ….” kwamba: “Ali, Abbas na Shayba bin Uthman kila mmoja alijigaba. Abbas akasema: ‘Mimi ndiye mbora wenu, mimi huwanywesha mahujaji wa Nyumba ya Mwenyezi Mungu.’ Shayba akasema: ‘Mimi naamirisha misikiti ya Mwenyezi Mungu.’ Ali akasema: ‘Mimi nilihama pamoja na Mtume wa Mwenyezi Mungu na hupigana jihadi pamoja naye katika Njia ya Mwenyezi Mungu.’ ndipo Mwenyezi Mungu akateremsha: “….na yule aliyemwamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho na akapigana jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu?...”24
SURA HUD Kauli ya Mwenyezi Mungu: “Basi je, aliye na dalili wazi itokayo kwa Mola wake na anaifuata na shahidi atokaye kwake..” (Sura Hud: 17). Ametusimulia Muhammad bin Ammara al-Asadiy, amesema: Ametusimulia Zariq bin Marzuq, amesema: Ametusimulia Swabahu alFarai kutoka kwa Jabir, kutoka kwa Abdullah bin Yahya, amesema: Ali (a.s.) alisema: “Hakuna mtu yeyote miongoni mwa makuraishi ila Aya moja au mbili zilishuka kwa ajili yake.” Ndipo mtu mmoja akamwambia: ‘’Ni ipi iliyoteremka kwa ajili yako?’’ Ali akasema: “Hivi hausomi Aya iliyoteremka katika Sura Hud: “….. na anaifuata na shahidi atokaye kwake..”25 23. Tafsirut-Tabari Juz. 10, Uk. 96. 24. Shawahidut-Tanziil Juz. 1, Uk. 244. al-Manaqib cha Ibnu al-Mughazaliy, Hadithi ya 324. Ghayatul-Marami, Mlango wa 63. 25.Tafsirut-Tabari Juz. 12, Uk. 15. Rejea Tafsirul-Ayyashiy Juz. 2, Uk. 153. Na al-Burhan Juz. 2, Uk. 213. 21
Page 21
AHLUBAYT NDANI YA TAF. ZA KISUNNI No 1 check Lubumba.qxd
7/1/2011
11:09 AM
Ahlul Bayt Ndani ya Tafsiri za Kisunni
SURA AR-RAAD Kauli ya Mwenyezi Mungu:
“Hakika wewe ni mwonyaji tu. Na kila kaumu ina wa kuwaongoza.” (Sura ar-Raad: 7). Ametusimulia Ahmad bin Yahya as-Swufiy, amesema: Ametusimulia Hasan bin Husein al-Ansariy, amesema: Ametusimulia Maadh bin Muslim, amesema: Ametusimulia al-Harawi kutoka kwa Atau bin as-Saib, kutoka kwa Said bin Jubair kutoka kwa Ibnu Abbas, amesema: “Ilipoteremka: “Hakika wewe ni mwonyaji tu. Na kila kaumu ina wa kuwaongoza.” Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) aliweka mkono wake juu ya kifua chake na kusema: ‘Mimi ndiye mwonyaji na kila kaumu ina wa kuwaongoza.’ Akaashiria mkono wake kwenye bega la Ali bin Abu Talib na kusema: ‘Ali wewe ndiye mwongozaji. Kupitia kwako wataongoka wenye kutaka kuongoka baada yangu.”26
SURA AN-NAHLI Kauli ya Mwenyezi Mungu: “Na hatukutuma kabla yako ila wanaume tuliowapa wahyi. Basi waulizeni wenye ukumbusho ikiwa nyinyi hamjui.” (Sura an-Nahli: 43). Ametusimulia Ibnu Wakiu, amesema: Ametusimulia Ibnu Yaman kutoka kwa Israil kutoka kwa Jabir, kutoka kwa Muhammad bin Ali bin Husein bin Ali, Abu Ja’far, kuhusu kauli yake (s.w.t.): “Basi waulizeni wenye ukumbusho ikiwa nyinyi hamjui.” Amesema: “Sisi ndio wenye ukumbusho.”27 26. Juz. 13, Uk. 108. 27. Tafsirut-Tabari Juz. 14, Uk. 109. 22
Page 22
AHLUBAYT NDANI YA TAF. ZA KISUNNI No 1 check Lubumba.qxd
7/1/2011
11:09 AM
Ahlul Bayt Ndani ya Tafsiri za Kisunni
SURA ISRAI Kauli ya Mwenyezi Mungu: “Na mpe jamaa wa karibu haki yake na maskini na mwana njia, wala usifanye ubadhirifu.” (Sura Israi: 26). Amenisimulia Muhammad bin Ammara al-Asadiy, amesema: Ametusimulia Ismail bin Aban, amesema: Ametusimulia Swabahu bin Yahya al-Muzniy kutoka kwa as-Sadiy, kutoka kwa Abu Daylam, amesema: Ali bin Husein (a.s.) alimwambia mzee mmoja wa Sham: “Hivi umewahi kusoma Qur’ani?” akajibu ndio. Ali akasema: “Hivi hujasoma katika Sura Israi: “Na mpe jamaa wa karibu haki yake..”?” mzee akasema: ‘’Hivi nyinyi ndio jamaa wa karibu ambao Mwenyezi Mungu, Ambaye zimetukuka sifa Zake, ameamuru wapewe haki yao?!!” Ali akasema: “Ndio sisi.”28
SURA TWAHA Kauli ya Mwenyezi Mungu:
“Hakika mimi ni Mwingi wa maghufira kwa anayetubia na akaamini na akatenda mema tena akaongoka.” (Sura Twaha: 82). Wengine wamesema yale aliyotusimulia Ismail bin Musa al-Fazari, amesema: Umar bin Shakir ametupa habari, amesema: Nilimsikia Thabit alBunan akisema kuhusu kauli yake (s.w.t.) “Hakika mimi ni Mwingi wa maghufira kwa anayetubia na akaamini…” “Ni kuamini Uwalii wa AhlulBaiti wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.)”29
28. Juz. 15, Uk. 72. 29. Juz. 16, Uk. 195. 23
Page 23
AHLUBAYT NDANI YA TAF. ZA KISUNNI No 1 check Lubumba.qxd
7/1/2011
11:10 AM
Ahlul Bayt Ndani ya Tafsiri za Kisunni
SURA ANBIYAI Kauli ya Mwenyezi Mungu:
“Na hatukutuma kabla yako ila wanaume tuliowapa wahyi. Basi waulizeni wenye ukumbusho ikiwa nyinyi hamjui.” (Sura Anbiyai: 43). Amenisimulia Ahmad bin Muhammad Tusiy, amesema: Amenisimulia Abdurahman bin Salih, amesema: Amenisimulia Musa bin Uthman kutoka kwa Jabir al-Jaafiy, amesema: “Ilipoteremka: “Na hatukutuma kabla yako ila wanaume tuliowapa wahyi. Basi waulizeni wenye ukumbusho ikiwa nyinyi hamjui.” Ali bin Abu Talib alisema: ‘Sisi ndio wenye ukumbusho.’”
SURA HAJJ Kauli ya Mwenyezi Mungu:
“Hawa mahasimu wawili waliohasimiana kwa ajili ya Mola wao...” (Sura Hajj: 19). Amenisimulia Yaakub, amesema: Ametusimulia Haytham, amesema: Abu Hashim ametupa habari kutoka kwa Abu Mujliz, kutoka kwa Qaysu bin Ubada, amesema: “Nilimsikia Abudhari akiapa kiapo kwa ajili ya Aya hii: “Hawa mahasimu wawili waliohasimiana kwa ajili ya Mola wao...” kwamba iliteremka kwa ajili ya wale waliojitokeza kupambana Siku ya Badri: Hamza, Ali na Ubayda bin al-Harith. Na kwamba Ali alisema: “Mimi ndiye wa awali au wa kwanza atakayepiga magoti mbele ya Mwenyezi Mungu Siku ya Kiyama kwa ajili ya uhasama.”30 30. Juz. 17, Uk. 131. 24
Page 24
AHLUBAYT NDANI YA TAF. ZA KISUNNI No 1 check Lubumba.qxd
7/1/2011
11:10 AM
Ahlul Bayt Ndani ya Tafsiri za Kisunni
SURA SHUARAU Kauli ya Mwenyezi Mungu: “Na uwonye jamaa zako walio karibu.” (Sura Shuarau: 214). Amesema: Ametusimulia Salmah, amesema: Ametusimulia Muhammad bin Is’haqa kutoka kwa Abdul-Ghaffar bin al-Qasim, kutoka kwa alManhal bin Amru, kutoka kwa Abdullah bin al-Harith bin Nawfal bin alHarith bin Abdul-Mutalib, kutoka kwa Abdullah bin Abbas kutoka kwa Ali bin Abu Talib, amesema: “Ilipoteremka Aya hii kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.): “Na uwonye jamaa zako walio karibu,” Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) aliniita na kuniambia: ‘Ewe Ali! Hakika Mwenyezi Mungu ameniamuru niwaonye jamaa zangu walio karibu. Suala hilo likaniumiza kichwa na nikatambua kwamba nitakapowadhihirishia jambo hili nitakumbana na nisiyoyapenda toka kwao. Nikanyamaza mpaka aliponijia Jibril na kuniambia: Ewe Muhammad! Hakika usipofanya unayoamrishwa Mola wako atakuadhibu. Ewe Ali! Tuandalie pishi la chakula uweke mguu wa mbuzi na utujazie birauli ya maziwa, kisha nikusanyie watoto wa Abdul-Mutalib ili niwaeleze na kuwafikishia yale niliyoamrishwa.’ Nikatekeleza aliyoniamrisha (s.a.w.w.).’ Kisha nikamwitia na wakati huo walikuwa wanaume arobaini, amezidi mtu mmoja au amepungua mmoja, humo walikuwemo ami zake: Abu Talib, Hamza, Abbas na Abu Lahab. Walipokwishakusanyika kwake alinitaka niwaletee chakula nilichowatengenezea, nami nikawaletea. Nilipokiweka Mtume wa Mwenyezi Mungu alichukua kipande kidogo cha nyama akakikata kwa meno yake kisha akakitupia pembezoni mwa sinia, akasema: “Chukueni kwa Jina la Mwenyezi Mungu. “Kaumu wakala mpaka wakatosheka na wala sikuona ila sehemu ambazo mikono yao ilikuwa ikimega. Naapa kwa Mwenyezi Mungu Ambaye nafsi ya Ali imo mikononi mwake, chakula nilichowapa wote ni cha kuweza kula mtu mmoja. 25
Page 25
AHLUBAYT NDANI YA TAF. ZA KISUNNI No 1 check Lubumba.qxd
7/1/2011
11:10 AM
Ahlul Bayt Ndani ya Tafsiri za Kisunni “Kisha akasema wape watu kinywaji, nikaja na ile bilauri wakanywa mpaka wakatosheka wote. Naapa kwa Mwenyezi Mungu kilikuwa ni kinywaji cha kutosheka mtu mmoja. “Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) alipotaka kuwaeleza, Abu Lahab alimtangulia kuongea, akasema: “Jamaa yenu amewaroga kwa karamu.” Ndipo kaumu wakatawanyika na wala Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) hakufanikiwa kuwaeleza, akasema (s.a.w.w.): “Kesho Ali. Hakika mtu huyu amenitangulia kusema yale uliyoyasikia, kaumu wametawanyika kabla sijawaeleza, hivyo tuandalie chakula mfano wa kile ulichoandaa kisha unikusanyie. “Nikatekeleza kisha nikawakusanya, kisha akanitaka nilete chakula nikawaletea naye akafanya kama alivyofanya jana, wakala mpaka wakatosheka. Mtume akasema wape kinywaji nikawaletea bilauri wakanywa mpaka wote wakatosheka. Kisha Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) akaongea kwa kusema: “Enyi wana wa Abdul-Mutalib! Hakika mimi wallahi simjui kijana wa kiarabu aliyewaletea jamaa zake kitu bora kuliko hiki nilichowaletea. Hakika mimi nimewaletea kheri ya dunia na akhera. Na hakika Mwenyezi Mungu ameniamuru niwalinganie kwayo, basi ni nani kati yenu atanisaidia katika jambo hili, awe ndugu yangu na kadha wa kadha.” “Watu wote wakakaa kimya, nikasema na hali mimi nikiwa ndiye mdogo kiumri kuliko wote, mwenye tongotongo machoni (mtoto) kuliko wote, mwenye tumbo kubwa kuliko wote na mwenye muundi wenye majeraha madogo kuliko wote: “Mimi ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu nakuwa waziri wako.” Akaishika shingo yangu kisha akasema (s.a.w.w.): “Hakika huyu ni ndugu yangu na kadha wa kadha, msikilizeni na mumtii.” Kaumu wakaongea na hali wakicheka na wakimwambia Abu Talib: “Bila shaka amekuamuru umsikilize na kumtii mwanao.’”31
31. Tafsirut-Tabari Juz. 19, Uk. 121. 26
Page 26
AHLUBAYT NDANI YA TAF. ZA KISUNNI No 1 check Lubumba.qxd
7/1/2011
11:10 AM
Ahlul Bayt Ndani ya Tafsiri za Kisunni
SURA AS-SAJDA Kauli ya Mwenyezi Mungu:
“Je, aliye muumini ni sawa na aliye fasiki? Hawawi sawa.” (Sura AsSajda: 18). Ibnu Hamid ametusimulia, amesema: Ametusimulia Salmah bin al-Fadhli, amesema: Amenisimulia Ibnu Is’haq kutoka kwa baadhi ya maswahiba zake, kutoka kwa Atau bin Yasar, amesema: “Iliteremka Madina ikimhusu Ali bin Abu Talib na Walid bin Uqbah bin Abu Muit. Kulikuwa na maneno baina ya Walid na Ali, Walid bin Uqbah akasema: ‘Mimi ni mfasaha kuliko wewe, mwenye meno makali kuliko wewe na shujaa kuliko wewe.’ Ali akasema: ‘Nyamaza bila shaka wewe ni fasiki.’ Ndipo Mwenyezi Mungu akateremsha: “Je, aliye muumini ni sawa na aliye fasiki? Hawawi sawa.”32
SURA AHZAB Kauli ya Mwenyezi Mungu:
“Hakika si mengineyo Mwenyezi Mungu anataka kuwaondolea uchafu, enyi watu wa nyumba ya Mtume, na kuwatakasa kabisa kabisa.” (Sura Ahzab: 33). Amenisimulia Yunus, amesema: Ibnu Wahab ametupa habari, amesema: Amenisimulia Muhammad bin Al-Muthana, amesema: Ametusimulia Bakru bin Yahya bin Zaban al-Inziy kutoka kwa Abu Said al-Khidriy, ame32 Juz. 21, Uk. 107. 27
Page 27
AHLUBAYT NDANI YA TAF. ZA KISUNNI No 1 check Lubumba.qxd
7/1/2011
11:10 AM
Ahlul Bayt Ndani ya Tafsiri za Kisunni sema: Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) amesema: “Aya hii: “Hakika si mengineyo Mwenyezi Mungu anataka kuwaondolea uchafu, enyi watu wa nyumba ya Mtume, na kuwatakasa kabisa kabisa.” imeteremka kwa ajili ya watano: Kwa ajili yangu, Ali, Hasan, Husein na Fatima.”33 Ametusimulia Ibnu Wakiu, amesema: Ametusimulia Muhammad bin Bashir kutoka kwa Zakariya, kutoka kwa Mas’ab bin Shayba, kutoka kwa Swafiya binti Shayba, amesema: Aisha alisema: “Siku moja Mtume alitoka akajifunika shuka lililodariziwa na manyoya meusi. Akaja Hasan akamwingiza na kuwa pamoja naye katika shuka, kisha akasema: “Hakika si mengineyo Mwenyezi Mungu anataka kuwaondolea uchafu, enyi watu wa nyumba ya Mtume, na kuwatakasa kabisa kabisa.” Ametusimulia Ibnu Wakiu, amesema: Ametusimulia Muhammad bin Bakr kutoka kwa Hamad bin Salmah, kutoka kwa Ali bin Zayd, kutoka kwa Anas, amesema kwamba: “Hakika Mtume alikuwa akipitia nyumbani kwa Ali muda wa miezi sita kila alipotoka kwenda kusali, na alikuwa anasema: ‘Swala enyi Ahlul-Baiti. Hakika si mengineyo Mwenyezi Mungu anataka kuwaondolea uchafu, enyi watu wa nyumba ya Mtume, na kuwatakasa kabisa kabisa.”34 Amenisimulia Musa bin Abdurahman al-Masruqiy, amesema: Ametusimulia Yahya bin Ibrahim bin Suwayd an-Nakhaiy kutoka kwa Hilal – yaani Ibnu Maqlaswi-, kutoka kwa Zayd, kutoka kwa Shahru bin Hawshab, kutoka kwa Ummu Salama, amesema: “Mtume, Ali, Fatima, Hasan na Husein walikuwa kwangu, nikawaandalia henzirani wakala na kulala, akawafunika shuka kisha akasema: ‘Ewe Mwenyezi Mungu! hawa ni Ahlul-Baiti wangu, waondolee uchafu na watakase kabisa kabisa.”35 33 Juz. 22, Uk. 6. 34 Tafsirut-Tabari Juz. 19, Uk. 121. 35 Tafsirut-Tabari Juz. 22 Uk. 6. 28
Page 28
AHLUBAYT NDANI YA TAF. ZA KISUNNI No 1 check Lubumba.qxd
7/1/2011
11:10 AM
Ahlul Bayt Ndani ya Tafsiri za Kisunni Ametusimulia Wakiu, amesema: Ametusimulia Abu Naiim, amesema: Ametusimulia Yunus bin Abu Is’haqa, amesema: Abu Daud amenipa habari kutoka kwa Abul-Hamrau, amesema: “Niliishi Madina miezi sita bila kutoka zama za Mtume (s.a.w.w.), nilimwona Mtume kila ichomozapo alfajiri akienda kwenye mlango wa Ali na Fatima na kusema: “Hakika si mengineyo Mwenyezi Mungu anataka kuwaondolea uchafu.” Amenisimulia Abdul-Aala bin Waswil, amesema: Ametusimulia al-Fadhlu bin Dukyan, amesema: Ametusimulia Abdusalama bin Harbi kutoka kwa Kulthum al-Muharabiy, kutoka kwa Abu Ammar, amesema: “Mimi nilikuwa nimeketi kwa Wathila bin al-Asqau ndipo walipomtaja Ali na kumkashifu, walipoondoka akasema (Wathila): ‘Keti mpaka nikupe habari za huyu waliyemkashifu, mimi nilikuwa kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) pindi walipomjia Ali, Fatima, Hasan na Husein, akawafunika shuka lake kisha Mtume akasema: ‘Ewe Mwenyezi Mungu! hawa ni Ahlul-Baiti wangu. Ewe Mwenyezi Mungu! waondolee uchafu na watakase kabisa kabisa.”’ Amenisimulia Abdul-Karim bin Abu Umayri, amesema: Ametusimulia Walid bin Muslim, amesema: Ametusimulia Abu Amru, amesema: Amenisimulia Shaddad, amesema: Nilimsikia Wathilat bin al-Asqau akisimulia kwamba: “Nilimuulizia Ali nyumbani kwake, Fatima akanijibu kwamba ametoka lakini punde tu atakuja akiwa na Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.), punde Mtume wa Mwenyezi Mungu akafika na kuingia ndani nami nikaingia. Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) akaketi juu ya kitanda na kumkalisha Fatima kuliani kwake na Ali kushotoni kwake na Hasan na Husein mbele yake, akawafunika nguo yake na kusema: “Hakika si mengineyo Mwenyezi Mungu anataka kuwaondolea uchafu, enyi watu wa nyumba ya Mtume, na kuwatakasa kabisa kabisa.” Ewe Mwenyezi Mungu! Hawa ndio watu wa nyumba yangu, ewe Mwenyezi Mungu watu wa nyumba yangu ndio wenye haki zaidi (kuliko mtu baki).”36 Amenisimulia Abu Karib, amesema: Wakiu ametusimulia kutoka kwa 36 Tafsirut-Tabari Juz. 22 Uk. 7. 29
Page 29
AHLUBAYT NDANI YA TAF. ZA KISUNNI No 1 check Lubumba.qxd
7/1/2011
11:10 AM
Ahlul Bayt Ndani ya Tafsiri za Kisunni Abdul-Hamid bin Bahram, kutoka kwa Shahri bin Hawshab, kutoka kwa Fudhaylu bin Marzuq, kutoka kwa Atia kutoka kwa Abu Said al-Khudriy, kutoka kwa Ummu Salama, amesema: “Aya hii ilipoteremka: “Hakika si mengineyo Mwenyezi Mungu anataka kuwaondolea uchafu, enyi watu wa nyumba ya Mtume…” Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) alimwita Ali, Fatima, Hasan na Husein akawafunika kishamia cha Khaibari, akaseama: ‘Ewe Mwenyezi Mungu hawa ndio Ahlul-Baiti wangu. Ewe Mwenyezi Mungu waondolee uchafu na watakase kabisa kabisa.’ Ummu Salama akasema: ‘Mimi ni miongoni mwao?’ Akasema (s.a.w.w.): ‘We utaelekea katika kheri.” Ametusimulia Abu Karib, amesema: Ametusimulia Masw’ab bin alMiqdam, amesema: Ametusimulia Said bin Zarbiyu kutoka kwa Muhammad bin Sirini kutoka kwa Abu Huraira, kutoka kwa Ummu Salama, amesema: “Fatima alikwenda kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) akiwa amebeba chungu chake chenye uji akakiweka mbele yake, akasema (s.a.w.w.): ‘Yuko wapo mwana wa ami yangu na wanao?’ akasema: ‘Nyumbani.’ Akasema (s.a.w.w.) waite, Fatima akatoka na kwenda kwa Ali na kumwambia: ‘Itikia wito wa Mtume wewe na wanao.’ Ummu Salama anasimulia kwamba: Alipowaona wakija alinyoosha mkono wake hadi kwenye kishamia kilichokuwa juu ya kitanda akakivuta na kukitandika na akawakalisha juu yake, kisha akazishika pembe za kishamia kwa mkono wake wa kushoto akazikusanyia juu ya vichwa vyao na akanyoosha mkono wake wa kulia kwa Mola wake Mlezi na kusema: ‘Ewe Mwenyezi Mungu hawa ndio Ahlul-Baiti wangu, waondolee uchafu na watakase kabisa kabisa.”37 Ametusimulia Abu Karib, amesema: Ametusimulia Hasan bin Atiyah, amesema: Ametusimulia Fadhilu bin Marzuq kutoka kwa Atiyah kutoka kwa Abu Said kutoka kwa Ummu Salama mke wa Mtume (s.a.w.w.) kwamba: “Hakika Aya hii iliteremka nyumbani kwake: “Hakika si mengineyo Mwenyezi Mungu anataka kuwaondolea uchafu..”. Alisema: 37 Tafsirut-Tabari Juz. 22 Uk. 7. 30
Page 30
AHLUBAYT NDANI YA TAF. ZA KISUNNI No 1 check Lubumba.qxd
7/1/2011
11:10 AM
Ahlul Bayt Ndani ya Tafsiri za Kisunni “Nami nilikuwa nimeketi mlangoni, nikamwambia: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu! Mimi sio miongoni mwa Ahlul-Baiti? Akanijibu: ‘Hakika wewe utaelekea katika kheri, wewe ni miongoni mwa wakeze Mtume (s.a.w.w.).’” Ummu Salama alisema: “Ndani ya nyumba alikuwemo Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.), Ali, Fatima, Hasan na Husein radhi za Mwenyezi Mungu ziwaendee.” Ametusimulia Abu Karib, amesema: Ametusimulia Khalid bin Mukhallad, amesema: Ametusimulia Musa bin Yakub, amesema: Amenisimulia Hashim bin Utbah Ibnu Abu Waqqas, kutoka kwa Abdullah bin Wahab bin Zam’at, amesema: “Ummu Salama alinipa habari kwamba: Hakika Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) aliwakusanya Ali, Fatima, na Hasan na Husein kisha akawafunika nguo yake, kisha akaelekea kwa Mwenyezi Mungu na kusema: ‘Hawa ndio Ahlul-Baiti wangu.’ Ummu Salama akasema: ‘Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu! (Allah) Amenijumuisha pamoja nao?’ akasema (s.a.w.w.): ‘Hakika wewe ni miongoni mwa wake zangu.”’38 Amenisimulia Ahmad bin Muhammad at-Tusiy, amesema: Ametusimulia Abdurahman bin Salih, amesema: Ametusimulia Muhammad bin Sulayman al-Isbahani kutoka kwa Yahya bin Ubaydul-Makkiy, kutoka kwa Atau, kutoka kwa Umar bin Abu Samla, amesema: “Aya hii: “Hakika si mengineyo Mwenyezi Mungu anataka kuwaondolea uchafu, enyi watu wa nyumba ya Mtume…” iliteremka kwa Mtume (s.a.w.w.) hali akiwa nyumbani kwa Ummu Salama. Mtume akamwita Hasan, Husein na Fatima na kuwakalisha mbele yake, akamwita Ali akamkalisha nyuma yake, wakajifunika yeye na wao kishamia kisha akasema: ‘Ewe Mwenyezi Mungu hawa ndio Ahlul-Baiti wangu, waondolee uchafu na watakase kabisa kabisa.’” Amenisimulia Muhammad bin Ammara, amesema: Ametusimulia Ismail bin Aban, amesema: Ametusimulia Swabbah bin Yahya al-Mar’iyyu kutoka kwa as-Sadiy kutoka kwa Abu Daylam, amesema: Ali bin Husein (a.s.) 38 Tafsirut-Tabari Juz. 22, Uk. 8. 31
Page 31
AHLUBAYT NDANI YA TAF. ZA KISUNNI No 1 check Lubumba.qxd
7/1/2011
11:10 AM
Ahlul Bayt Ndani ya Tafsiri za Kisunni alimwambia mzee wa Sham: “Umewahi kusoma katika Sura Ahzab: “Hakika si mengineyo Mwenyezi Mungu anataka kuwaondolea uchafu, enyi watu wa nyumba ya Mtume, na kuwatakasa kabisa kabisa.’” Mzee akasema: “Hivi ni nyinyi hao? “ Ali bin Husein akasema: “Ndio ni sisi.” Ametusimulia Ibnu al-Muthana, amesema: Ametusimulia Abu Bakr al-Hanafiy, amesema: Ametusimulia Bakiri bin Mismar, amesema: Nilimsikia Amir bin Said akisema: Saad amesema: Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) alisema: “Wahyi ulipomteremkia alimchukua Ali, wanae na Fatima akawaingiza chini ya nguo yake kisha akasema: Mola wangu Mlezi hawa ndio ndugu zangu na Ahlul-Baiti wangu.”39 Ametusimulia Ibnu Hamid, amesema: Ametusimulia Abdullah bin Abdul-Quddus kutoka kwa Aamash, kutoka kwa Hakim bin Said, amesema: “Tulimtaja Ali bin Abu Talib radhi za Mwenyezi Mungu zimwendee mbele ya Ummu Salama, akasema: Kwa ajili yake iliteremka: “Hakika si mengineyo Mwenyezi Mungu anataka kuwaondolea uchafu, enyi watu wa nyumba ya Mtume, na kuwatakasa kabisa kabisa.” Ummu Salama akasema: Mtume (s.a.w.w.) alikuja nyumbani kwangu, akaniambia usimpe yeyote idhini ya kuingia. Akaja Fatima sikuweza kumzuia na baba yake, kisha akaja Hasan sikuweza kumzuia asiingie kwa babu yake na mama yake. Akaja Husain sikuweza kumzuia, akaja Ali sikuweza kumzuia, ndipo wakamzunguka Mtume (s.a.w.w.) wakiwa juu ya busati, Mtume wa Mwenyezi (s.a.w.w.) akawafunika kwa kishamia alichokuwa amejitanda, kisha akasema: ‘Ewe Mwenyezi Mungu hawa ndio Ahlul-Baiti wangu. Waondolee uchafu na watakase kabisa kabisa.’ Ndipo ikateremka Aya hii walipokusanyika juu ya busati. Nikasema ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu! Na mimi? Ummu Salama anasema: “Wallahi hakukubali bali alisema: Hakika wewe utaelekea katika kheri.”
39 Tafsirut-Tabari Juz. 22, Uk. 7. 32
Page 32
AHLUBAYT NDANI YA TAF. ZA KISUNNI No 1 check Lubumba.qxd
7/1/2011
11:10 AM
Ahlul Bayt Ndani ya Tafsiri za Kisunni Kauli ya Mwenyezi Mungu:
“Hakika Mwenyezi Mungu na malaika wake wanamswalia Nabii. Enyi ambao mmeamini! Mswalieni na mumsalimu kwa salamu.” (Sura Ahzab: 56). Ametusimulia Ibnu Hamid, amesema: Ametusimulia Harun kutoka kwa Anbasat kutoka kwa Uthman bin Mawhib kutoka kwa Musa bin Talha kutoka kwa baba yake, amesema: “Mtu mmoja alikwenda kwa Mtume (s.a.w.w.) na kumwambia: Nimemsikia Mwenyezi Mungu akisema: “Hakika Mwenyezi Mungu na malaika wake wanamswalia Nabii…” ni ipi namna ya kukusalia? Mtume akasema: ‘Sema: Ewe Mwenyezi Mungu! Mrehemu Muhammad na aali Muhammad kama ulivyomrehemu Ibrahim na aali Ibrahim, hakika wewe ni Muhimidiwa Msifiwa. Na mbariki Muhammad na aali Muhammad kama ulivyombariki Ibrahim na aali Ibrahim, hakika wewe ni Muhimidiwa Msifiwa.’”40 Ametusimulia Abu Karib, amesema: Ametusimulia Malik bin Ismail, amesema: Ametusimulia Abu Israil kutoka kwa Yunus bin Khabab, amesema: Bifaris alituhutubia akasema: “Hakika Mwenyezi Mungu na malaika wake wanamswalia Nabii…” amenipa habari yule aliyemsikia Ibnu Abbas akisema: ‘Hivi ndivyo ilivyoteremka. Tukamwambia: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu! Tumeshajua namna ya kukutolea salamu, ama sala tutakusaliaje? Akasema: Ewe Mwenyezi Mungu! Mrehemu Muhammad na aali Muhammad kama ulivyomrehemu Ibrahim na aali Ibrahim, hakika wewe ni Muhimidiwa Msifiwa. Na mbariki Muhammad na aali Muhammad kama ulivyombariki Ibrahim, hakika wewe ni Muhimidiwa Msifiwa.’41 40 Juz. 22, Uk. 43. 41 Tafsirut-Tabari Juz. 22, Uk. 44. 33
Page 33
AHLUBAYT NDANI YA TAF. ZA KISUNNI No 1 check Lubumba.qxd
7/1/2011
11:10 AM
Ahlul Bayt Ndani ya Tafsiri za Kisunni Ametusimulia Bushru, amesema: Ametusimulia Yazid, amesema: Ametusimulia Said kutoka kwa Qattadah kuhusu kauli yake (s..w.t.): “Hakika Mwenyezi Mungu na malaika wake wanamswalia Nabii…” amesema: “Ilipoteremka Aya hii walisema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu! Tumeshajua namna ya kukutolea salamu, ama sala tutakusaliaje? Akasema: ‘Semeni: Ewe Mwenyezi Mungu! Mrehemu Muhammad na aali Muhammad kama ulivyomrehemu Ibrahim na aali Ibrahim.”’ Ametusimulia Ibnu Hamid, amesema: Ametusimulia Jarir kutoka kwa Mughira kutoka kwa Ziyad kutoka kwa Ibrahim kuhusu kauli yake (s.w.t.): “Hakika Mwenyezi Mungu na malaika wake wanamswalia Nabii…” amesema: “Walisema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu! Tumeshajua namna ya kukutolea salamu, ama sala tutakusaliaje? Akasema: ‘Semeni: Ewe Mwenyezi Mungu! Mrehemu Muhammad mja wako na Mtume wako na Ahlul-Baiti wake, kama ulivyomrehemu Ibrahim hakika wewe ni Muhimidiwa Msifiwa.”’ Amenisimulia Ja’far bin Muhammad al-Kufiy, amesema: Ametusimulia Yaala bin al-Ajlahu kutoka kwa al-Hakam bin Utbah, kutoka kwa Abdullah bin Abu Layla, kutoka kwa Kaab bin Ajarah, amesema: “Ilipoteremka: “Hakika Mwenyezi Mungu na malaika wake wanamswalia Nabii…” nilimwendea na kumwambia: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu! Tumeshajua namna ya kukutolea salamu, ama sala tutakusaliaje? Akasema (s.a.w.w.): Sema: Ewe Mwenyezi Mungu! Mrehemu Muhammad na aali Muhammad, kama ulivyomrehemu Ibrahim na aali Ibrahim, hakika wewe ni Muhimidiwa Msifiwa. Na mbariki Muhammad na aali Muhammad, kama ulivyombariki Ibrahim na aali Ibrahim, hakika wewe ni Muhimidiwa Msifiwa.”
34
Page 34
AHLUBAYT NDANI YA TAF. ZA KISUNNI No 1 check Lubumba.qxd
7/1/2011
11:10 AM
Ahlul Bayt Ndani ya Tafsiri za Kisunni
SURA AS-SAFFAT Kauli ya Mwenyezi Mungu: “Amani kwa Ilyasin.” (Sura as-Saffat: 130). Amesema: Maana yake ni Salamu kwa aali Muhammad (s.a.w.w.).42
SURA AS-SHURA Kauli ya Mwenyezi Mungu:
“Sema: Kwa haya siwaombi malipo yoyote kwenu isipokuwa mapenzi katika ndugu...” (Sura as-Shura: 23). Ametusimulia Abu Karib, amesema: Abu Usama ametusimulia kutoka kwa Abdul-Malik bin Maysara kutoka kwa Taus kuhusu kauli yake (s.w.t.): “Sema: Kwa haya siwaombi malipo yoyote kwenu isipokuwa mapenzi katika ndugu...” amesema: “Ibnu Abbas aliulizwa kuhusu Aya hiyo, Ibnu Jubayri akasema: Hao ni karaba ambao ni aali Muhammad.”43 Amenisimulia Muhammad bin Ummara, amesema: Ametusimulia Ismail bin Aban, amesema: Kutoka kwa As-Sadiy kutoka kwa Abu Daylam amesema: Alipoletwa Ali bin Husein na hali ni mateka na kusimamishwa katika barabara kuu ya Damascus alisimama mzee mmoja kati ya watu wa Sham, akasema: ‘Kila sifa njema ni ya Mwenyezi Mungu ambaye amewauwa na kuwang’oeni na kung’oa mzizi wa fitina.’ Ali bin Husein radhi za Mwenyezi Mungu zimwendee akasema: ‘Umewahi kusoma Qur’ani?’ akajibu ndio. Akasema (a.s.): ‘Umewahi kusoma Aali Haa Miim?’ Akajibu nimewahi kusoma Qur’ani na sijawahi kusoma Aali Haa Miim. Akasema (a.s.): ‘Hujawahi kusoma: “Sema: Kwa haya siwaombi malipo yoyote 42 Tafsirut-Tabari Juz. 23, Uk. 96. 43 Juz. 25, Uk. 23. 35
Page 35
AHLUBAYT NDANI YA TAF. ZA KISUNNI No 1 check Lubumba.qxd
7/1/2011
11:10 AM
Ahlul Bayt Ndani ya Tafsiri za Kisunni kwenu isipokuwa mapenzi katika ndugu...”’ Mzee akasema: ‘Nyinyi ndio hao?’ Akasema (a.s.): ‘Naam ndio sisi.’
SURA MUJADILAH Kauli ya Mwenyezi Mungu:
“Enyi mlioamini! Mnaposema siri na Mtume, basi tangulizeni sadaka kabla ya kumsemesha, hayo ni bora kwenu na ni safi sana, na ikiwa hamkupata basi Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa kusamehe, Mwenye kurehemu “ (Sura Mujadilah: 12). Amenisimulia Muhammad bin Amru, amesema: Ametusimulia Abu Aswim, amesema: Ametusimulia Isa kutoka kwa Ibnu Abu Najihu kutoka kwa Mujahid kuhusu kauli yake (s.w.t.): “…basi tangulizeni sadaka kabla ya kumsemesha…” amesema: “Walikatazwa kusema siri na Mtume (s.a.w.w.) mpaka watoe sadaka. Hakuna aliyeweza kusema naye siri ila Ali bin Abu Talib radhi za Mwenyezi Mungu zimwendee, alitoa sadaka ya dinari. Ndipo (baada ya sadaka hiyo) ikateremka ruhusa (iliyoondoa sharti la sadaka.).”44 Ametusimulia Muhammad bin Ubaydu bin Muhammad al-Muhariby, amesema: Ametusimulia al-Mutalib bin Ziyad kutoka kwa Mujahid, amesema: Ali bin Abu Talib radhi za Mwenyezi Mungu zimwendee alisema: “Hakika katika Kitabu cha Mwenyezi Mungu kuna Aya ambayo hakuna yeyote aliyeifanyia kazi kabla yangu, wala hakuna yeyote atakayeifanyia kazi baada yangu, nayo ni: “Enyi mlioamini! Mnaposema siri na Mtume, basi tangulizeni sadaka kabla ya kumsemesha hayo ni bora kwenu na ni safi sana…..”” Amenisimulia Musa bin Abdurahman al-Masruqiy, amesema: 44 Juz. 28, Uk. 20. 36
Page 36
AHLUBAYT NDANI YA TAF. ZA KISUNNI No 1 check Lubumba.qxd
7/1/2011
11:10 AM
Ahlul Bayt Ndani ya Tafsiri za Kisunni Ametusimulia Abu Usama kutoka kwa Shablu bin Ubada kutoka kwa Mujahid kuhusu kauli yake (s.w.t.): “Enyi mlioamini! Mnaposema siri na Mtume …..” amesema: “Walikatazwa kusema siri na Mtume mpaka watoe sadaka. Hakuna aliyeweza kusema naye siri ila Ali bin Abu Talib radhi za Mwenyezi Mungu zimwendee. Alitoa sadaka ya dinari. Ndipo (baada ya sadaka hiyo) ikateremka ruhusa (iliyoondoa sharti la sadaka.). Abu Karib ametusimulia, amesema: Ametusimulia Ibnu Idirisa, amesema: Nilimsikia Laythu kutoka kwa Mujahid, amesema: Ali bin Abu Talib radhi za Mwenyezi Mungu zimwendee alisema: “Kuna Aya katika Kitabu cha Mwenyezi Mungu ambayo hakuna yeyote aliyeifanyia kazi kabla yangu, wala hakuna yeyote atakayeifanyia kazi baada yangu. Nilikuwa na dinari moja nikaichenji na kupata dirhamu kumi, nikawa kila niendapo kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) hutoa sadaka dirhamu moja.”
SURA TAGHABUN Kauli ya Mwenyezi Mungu:
“Bila shaka mali zenu na watoto wenu ni jaribio, na kwa Mwenyezi Mungu kuna malipo makubwa.” (Sura Taghabun: 15). Ametusimulia Abu Karib, amesema: Ametusimulia Uthman bin Najiyah kutoka kwa Husein bin Waqid, amesema: Abdullah bin Barida amesema: “Nilimwona Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) akitoa hotuba ghafla wakaja Hasan na Husein radhi za Mwenyezi Mungu ziwaendee wakiwa wamevaa kanzu mbili nyekundu na hali wakidondoka na kuamka, Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) akateremka toka mimbarini akawachukua na kuwanyanyua na kuwaweka mapajani mwake kisha akasema: ‘Mwenyezi Mungu na Mtume wake wamesema kweli. Bila shaka mali zenu na watoto wenu ni jaribio, nilipowaona hawa wawili sikuweza kuvumilia.’”45 45 Juz. 28, Uk. 126. 37
Page 37
AHLUBAYT NDANI YA TAF. ZA KISUNNI No 1 check Lubumba.qxd
7/1/2011
11:10 AM
Ahlul Bayt Ndani ya Tafsiri za Kisunni
SURA AL-HAQQAH Kauli ya Mwenyezi Mungu:
“Ili tuifanye ukumbusho kwenu, na sikio lisikialo lisikie.” (Sura alHaqqah: 12). Ametusimulia Ali bin Sahli, amesema: Ametusimulia Walid bin Muslim, amesema: Nimemsikia Makhula akisema: “Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) alisoma: “…na sikio lisikialo lisikie.” Kisha akamgeukia Ali na kusema: ‘Nilimwomba Mwenyezi Mungu sikio lako alifanye hivyo.’ Ali radhi za Mwenyezi Mungu zimwendee alisema: ‘Basi sikuwahi kusikia kitu chochote toka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu kisha nikakisahau.”’46 Amenisimulia Muhammad bin Khalqu, amesema: Amenisimulia Bushru bin Adam, amesema: Ametusimulia Abdullah Ibnu Zubair, amesema: Amenisimulia Abdullah bin Rustam, amesema: Nilimsikia Burayda akisema: “Nilimsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) akisema kumwambia Ali (a.s.): ‘Ewe Ali! Hakika Mwenyezi Mungu ameniamuru nikusogeze karibu, nisikutenge mbali na nikuelimishe nawe usikie vilivyo. Na Mwenyezi Mungu amehakikisha unasikia vilivyo.’ Ndipo ikateremka: “…na sikio lisikialo lisikie.”” Amenisimulia Muhammad bin Khalfu, amesema: Ametusimulia Ismail bin Ibrahim Abu Yahya at-Tamimiy kutoka kwa Burayda al-Aslamiy, amesema: “Nilimsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) akisema kumwambia Ali (a.s.): ‘Hakika Mwenyezi Mungu ameniamuru nikuelimishe, nikusogeze karibu, nisikunyanyapae na nisikutenge mbali.”’ 46 Tafsirut-Tabari Juz. 29 Uk. 55. 38
Page 38
AHLUBAYT NDANI YA TAF. ZA KISUNNI No 1 check Lubumba.qxd
7/1/2011
11:10 AM
Ahlul Bayt Ndani ya Tafsiri za Kisunni
SURAT AL-BAYYINA Kauli ya Mwenyezi Mungu:
“Hakika wale walioamini na kutenda mema, hao ndio wema wa viumbe.” (Sura al-Bayyina: 7). Ametusimulia Ibnu Hamid, amesema: Ametusimulia Isa bin Farqad kutoka kwa Abul-Jarud kutoka kwa Muhammad bin Ali kuhusu kauli yake (s.w.t.): “Hakika wale walioamini na kutenda mema, hao ndio wema wa viumbe.” amesema: Mtume akasema: “Ali ni wewe na wafuasi wako.”47
AHLUL-BAIT (A.S.) NDANI YA TAFSIRI YA AT-THAALABIY, INAYOITWA AL-KASHFU WAL-BAYAN FII TAFSIRIL-QUR’ANI
SURA AL-FATIHA Kauli ya Mwenyezi Mungu:
“Tuongoze njia iliyonyooka.” (Surat al-Fatiha: 6). Muhammad bin Abdullah al-Qayiniy ametupa habari, amesema: Ametusimulia Abu Hasan bin Uthman an-Naswibiy huko Baghdad, amesema: Ametusimulia Abul-Qasim, amesema: Ametusimulia Abu Hafsa Umar bin Ahmad bin Uthman, amesema: Baba yangu ametusimulia, amesema: Ametusimulia Hamid bin Sahli, amesema: Ametusimulia Abdullah 47 Juz. 30 Uk. 265. 39
Page 39
AHLUBAYT NDANI YA TAF. ZA KISUNNI No 1 check Lubumba.qxd
7/1/2011
11:10 AM
Ahlul Bayt Ndani ya Tafsiri za Kisunni bin Muhammad al-Ajliy, amesema: Ametusimulia Ibrahim bin Jabir kutoka kwa Muslim bin Hayyan kutoka kwa Burayda kuhusu kauli yake (s.w.t.): “Tuongoze njia iliyonyooka.” amesema: “Ni Njia ya Muhammad na aali zake amani iwe juu yao wote.”48
SURAT AL-BAQARAH Kauli ya Mwenyezi Mungu:
“Na katika watu yuko auzaye nafsi yake kwa kutaka radhi ya Mwenyezi Mungu, na Mwenyezi Mungu ni Mpole kwa waja.” (Sura al-Baqara: 207). At-Thaalabi amesema: Nimeona katika baadhi ya vitabu kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) alipotaka kuhama alimwacha badala yake Ali bin Abu Talib huko Makka ili alipe madeni yake na akabidhi amana zilizokuwa kwake. Na alimwamuru siku aliyotoka kwenda pangoni – Mushrikina wakiwa wameizingira nyumba yake - alale kitandani kwake na alimwambia: “Jitande joho langu la kijani na ulale juu ya kitanda changu hakika hutopatwa na lolote lichukizalo kutoka kwao inshaallah.” Ali alifanya hivyo. Ndipo Mwenyezi Mungu akawafunulia malaika (Jibril na Mikail): Hivi hamui kama Ali bin Abu Talib! nimeweka undugu kati yake na Muhammad naye amelala juu ya kitanda chake akijitoa fidia kwa niaba yake na kuupa uhai wake (Muhammad) kipaumbele kabla ya uhai wake binafsi. Teremkeni aridhini mkamlinde dhidi ya adui wake. `
Malaika Jibril akateremka na kukaa kichwani kwake na Mikail akakaa miguuni kwake na hali Jibril akinadi: “Pongezi pongezi! Ewe Ali! Mwenyezi Mungu anajionea fahari kwako mbele ya
48 Ameipokea Shahru Ashub katika kitabu al-Manaqib Juz. 2, Uk. 271. 40
Page 40
AHLUBAYT NDANI YA TAF. ZA KISUNNI No 1 check Lubumba.qxd
7/1/2011
11:10 AM
Ahlul Bayt Ndani ya Tafsiri za Kisunni Malaika.” Kwa ajili ya Ali Mwenyezi Mungu akateremsha kwa Mtume wake akiwa njiani kuelekea Madina: “Na katika watu yuko auzaye nafsi yake kwa kutaka radhi ya Mwenyezi Mungu, na Mwenyezi Mungu ni Mpole kwa waja.”49 Abu Muhammad Abdullah bin Muhammad Abdullah al-Qadhiy ametupa habari, amesema: Abu Husein Muhammad bin Uthman bin Hasan anNaswibiy ametusimulia huko Baghdad, amesema: Abu Bakr Muhammad bin Hasan bin Salih as-Subiiy ametusimulia huko Halbi, amesema: Ametusimulia Ahmad bin Muhammad bin Said, amesema: Ametusimulia Muhammad bin Mansur, amesema: Ametusimulia Ahmad bin Abu Abdurahman, amesema: Ametusimulia Hasan bin Muhammad Farqad, amesema: Ametusimulia al-Hakam bin Dhahir, amesema: Ametusimulia as-Sadiy kuhusu kauli yake (s.w.t.): “Na katika watu yuko auzaye nafsi yake kwa kutaka radhi ya Mwenyezi Mungu, na Mwenyezi Mungu ni Mpole kwa waja,” amesema: Ibnu Abbas alisema: “Iliteremka kwa ajili ya Ali bin Abu Talib (a.s.) pindi Mtume (s.a.w.w) alipowatoka Mushrikina na kwenda pangoni akiwa pamoja na Abu Bakr. Ali ndipo alipolala juu ya kitanda cha Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.).”50 Kauli ya Mwenyezi Mungu:
“Wale watoao mali zao usiku na mchana kwa siri na dhahiri, wana ujira wao kwa Mola wao Mlezi; wala haitakuwa hofu juu yao wala wao hawatahuzunika.” (Surat al-Baqara: 274). 49 Ameipokea al-Haskaniy katika kitabu Shawahidut-Tanziil Juz. 1, Uk. 123, Hadithi ya 133. Ameipokea al-Ghazali katika kitabu Ihyau Uluumid-Din Juz. 3, Uk. 238 katika kubainisha fadhila zake na utoaji kipaumbele wake. Ameipokea Ibnu Shahri Ashub katika kitabu chake Al-Manaqib Juz. 2, Uk. 65. 50 Rejea kitabu Sharhu Nahjul-Balagha cha Ibu Abil-Hadid Juz. 1, Uk. 789. 41
Page 41
AHLUBAYT NDANI YA TAF. ZA KISUNNI No 1 check Lubumba.qxd
7/1/2011
11:10 AM
Ahlul Bayt Ndani ya Tafsiri za Kisunni Amenipa habari Ibnu Fanjawihi, amesema: Ametusimulia Abu Ali bin Habish al-Maqriy, amesema: Ametusimulia Wahib kutoka kwa Ayub kutoka kwa Mujahid, kutoka kwa Ibnu Abbas, amesema: “Ali bin Abu Talib alikuwa na dirhamu nne hakuwa anamiliki nyingine zaidi ya hizo, akatoa sadaka dirhamu moja kwa siri na nyingine kwa dhahiri, nyingine usiku na nyingine mchana. Ndipo ikateremka Aya hii.”51
SURA AALI IMRAN Kauli ya Mwenyezi Mungu: “Hakika Mwenyezi Mungu alimchagua Adam na Nuh na watoto wa Ibrahim na watoto wa Imran juu ya walimwengu wote.” (Sura Aali Imran: 33). Abu Muhammad Abdullah bin Muhammad al-Qadhiy ametusimulia, amesema: Ametusimulia Abu Hasan Muhammad bin Uthman bin Hasan anNaswibiy, amesema: Ametusimulia Abu Bakr Muhammad bin Husein bin Salih as-Subiiy, amesema: Ametupa habari Ahmad bin Muhammad bin Said, amesema: Ametusimulia Ahmad bin Maytham bin Abu Naim, amesema: Ametusimulia Abu Junada as-Saluliy kutoka kwa Aamash kutoka kwa Abu Wail, amesema: Nimesoma katika Msahafu wa Abdullah bin Mas’ud: “Hakika Mwenyezi Mungu alimchagua Adam na Nuh na watoto wa Ibrahim na watoto wa Imran juu ya walimwengu wote.” Kauli ya Mwenyezi Mungu:
“Alipomzaa alisema: Mola wangu! Nimemzaa mwanamke, na 51 Ameipokea al-Wahidiy katika kitabu Asbabun-Nuzuul Uk. 64. Ibnu Asakir katika kitabu Taarikhud-Damashqi Juz. 2, Uk. 13, Hadithi ya 918. Na Tabari katika kitabu ar-Riyadh an-Nadhrah Juz. 2, Uk. 206. 42
Page 42
AHLUBAYT NDANI YA TAF. ZA KISUNNI No 1 check Lubumba.qxd
7/1/2011
11:10 AM
Ahlul Bayt Ndani ya Tafsiri za Kisunni Mwenyezi Mungu anajua sana aliyemzaa. Na mwanamume si kama mwanamke na nimemwita Maryam...” (Sura Aali Imran: 36). Abu Zar’at amepokea kutoka kwa Abu Huraira kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) alisema: “Yakutosha katika wanawake wa ulimwenguni: Maryam binti Imran, Asia mke wa Firaun, Khadija binti Khuwaylid na Fatima binti Muhammad.” Kauli ya Mwenyezi Mungu:
“…Kila mara Zakariya alipoingia Mihrab hukuta vyakula. Akasema: Ewe Maryam unatoa wapi hivi. Akasema: Vinatoka kwa Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu humruzuku amtakaye bila hesabu.” (Sura Aali Imran: 37). Kutoka kwa Jabir bin Abdullah amesema kwamba hakika Mtume (s.a.w.w.) alikaa siku kadhaa bila kula chakula mpaka hali hiyo ikawa nzito juu yake. Akaenda kwenye nyumba za wakeze lakini hakukuta chochote kwao ndipo akaenda kwa Fatima na kumwambia: “Ewe mwanangu mpendwa! Je una chochote ninachoweza kula kwani hakika mimi ni mwenye njaa?” Akamjibu: “Wallahi sina ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu kwa haki ya baba yangu na mama yangu.” Mtume alipotoka jirani wa Fatima alimletea Fatima vipande viwili vya mkate na finyango ya nyama. Fatima akawatuma Hasan na Husein waende kumwita Mtume (s.a.w.w.) naye akaenda. Fatima akamweleza na kumfunulia bakuli. Ghafla Fatuma akakuta bakuli limejaa mikate na nyama na akatambua kuwa ni baraka toka kwa Mwenyezi Mungu. Mtume (s.a.w.w.) akasema: Umetoa wapi hivi? Akajibu: “Ni kutoka kwa Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu humpa riziki amtakaye bila hesabu.” Mtume akamuhimidi Mwenyezi Mungu na kusema: “Kila sifa njema ni ya Mwenyezi Mungu Ambaye amekufanya kifani wa bibi 43
Page 43
AHLUBAYT NDANI YA TAF. ZA KISUNNI No 1 check Lubumba.qxd
7/1/2011
11:10 AM
Ahlul Bayt Ndani ya Tafsiri za Kisunni mtukufu wa wana wa Izrael (Mariam). Kwani hakika yeye alikuwa aruzukiwapo chochote na Mwenyezi Mungu husema: Hakika Mwenyezi Mungu humpa riziki amtakaye bila hesabu.” Kisha Mtume (s.a.w.w.) akampeleka ujumbe Ali aje. Akala Mtume na Ahlul-Baiti wake wote kwa pamoja mpaka wakashiba. Fatima alisema: “Bakuli lilibaki kama lilivyokuwa likiwa limejaa. Hivyo nikawagawia majirani zangu wote na Mwenyezi Mungu aliweka humo kheri nyingi na baraka.” Kauli ya Mwenyezi Mungu:
“Na watakaokuhoji baada kukufikia elimu hii, waambie: Njooni tuwaite watoto wetu na watoto wenu, na wanawake zetu na wanawake wenu, na nafsi zetu na nafsi zenu, kisha tuombe kwa unyenyekevu tutake laana ya Mwenyezi Mungu iwashukie waongo.” (Sura Aali Imran: 61). At-Thaalabi amesema: Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) alipousomea ujumbe wa Najran Aya hizi na kuwaomba wafanye maombi ya laana walisema: “Mpaka turejee na tutafakari jambo hili kisha kesho tutakuja tena.” Ndipo kesho wakaenda kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.), na Mtume akatoka akiwa amemkumbatia Husein na amemshika mkono Hasan huku Fatima akitembea nyuma yake na Ali akiwa nyuma ya Fatima. Akawaambia: “Mimi nitakapokuwa naomba nyinyi muwe mnaitikia.” Askofu wa Najran akasema: “Enyi wakristo! Mimi naziona nyuso hizi kama zitamuomba Mwenyezi Mungu auondoe mlima kutoka mahala pake, atauondoa, msiapizane naye mtaangamia, na hatabaki mkiristo yeyote hapa duniani mpaka siku ya Kiyama.” Wakasema: “Ewe Abul-Qasim! Tumeona tusiapizane na wewe na 44
Page 44
AHLUBAYT NDANI YA TAF. ZA KISUNNI No 1 check Lubumba.qxd
7/1/2011
11:10 AM
Ahlul Bayt Ndani ya Tafsiri za Kisunni tukuwache uendelee kuwa katika dini yako nasi tuendelee kubaki katika dini yetu. ” Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) akasema: “Mkikataa kufanya maapizano basi msilimu mtapata haki waliyonayo waislamu na mtawajibikiwa na yale yaliyo wajibu kwao.” Wakakataa, ndipo Mtume akawaambia: “Basi hakika mimi nitawafukuzeni kupitia waarabu.” Wakasema: “Hatuna nguvu ya kupigana vita na waarabu, lakini sisi tunafanya suluhu na wewe usitushambulie kivita na wala usitufukuze na wala usitutoe katika dini yetu. Kwa sharti tukupe kila mwaka Hilla52 elfu mbili: Elfu moja katika mwezi wa Safar na elfu nyingine katika mwezi wa Rajab.” Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) akafanya nao suluhu kwa sharti hilo na akasema: “Naapa kwa Yule Ambaye nafsi yangu imo mikononi mwake hakika adhabu imeshateremka juu ya watu wa Najran. Na lau wangefanya maapizano wangegeuzwa nyani na nguruwe na bonde lao lingewaka moto. Na Mwenyezi Mungu angeiteketeza Najran na watu wake hata ndege aliyopo juu ya mti. Wala mwaka usingepita wakristo wote wangekuwa wameteketea.”53 Kauli ya Mwenyezi Mungu:
“Kama mmepatwa jeraha, basi kuna kaumu wamekwishapata jeraha kama hilo, na siku za namna hii tutawaletea watu kwa zamu. Na ili apate kuwajua Mwenyezi Mungu ambao wameamini katika nyinyi na afanye miongoni mwenu mashahidi. Na Mwenyezi Mungu hawapendi madhalimu.” (Sura Aali Imran: 140). 52 Jina la pesa kama vile Dola, Shilingi, Paundi na mfano wa hizo. 53 Ameipokea Ahmad bin Hanbal katika kitabu al-Fadhail Uk. 27. al-Wahidiy katika kitabu Asbabun-Nuzuul Uk. 74. Na ameipokea pia Tabarani katika kitabu Dalailun-Nubuwa Juz. 1, Uk. 197, Sura ya 21. 45
Page 45
AHLUBAYT NDANI YA TAF. ZA KISUNNI No 1 check Lubumba.qxd
7/1/2011
11:10 AM
Ahlul Bayt Ndani ya Tafsiri za Kisunni Anas bin Malik amesema: Ali bin Abu Talib, Mwenyezi Mungu autukuze uso wake, alikuja siku hiyo kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) akiwa na majeraha zaidi ya sabini, yatokanayo na mikuki, pigo la mishale. Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) akawa anayapangusa nayo yanapona kwa idhini ya Mwenyezi Mungu kama vile hayakuwa ni majeraha.
SURA NISAI Kauli ya Mwenyezi Mungu:
“Enyi mlioamini! Msikaribie Swala na hali mmelewa mpaka myajue mnayoyasema; wala mkiwa na janaba isipokuwa mkiwa safarini mpaka muoge. Na muwapo wagonjwa au mko safarini au akawa mmoja wenu ametoka chooni au mkagusana na wanawake, kisha msipate maji, basi tayamamuni na mchanga ulio twahara; mpake nyuso zenu na mikono yenu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa kusamehe Mwenye kughufiria.” (Sura Nisai: 43). Ismaili bin Umaiyya amesema kutoka kwa Husein kutoka kwa Ummu Salama, amesema: Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) alisema: “Hakika kuingia ndani ya msikiti wangu ni haramu kwa kila mwanamke mwenye hedhi na kila mwanaume mwenye janaba ila kwa Muhammadi na Ahlul-Baiti wake: Ali, Fatima, Hasan na Husein (a.s.).”54 54 Tanbihi: at-Thaalabi katika kuifasiri kauli ya Mwenyezi Mungu: “Ambao mmestarehe nao katika wao, basi wapeni mahari yao yaliyo lazimu.” (Sura Nisai: 24) amesema: Ali bin Abu Talib alisema: ‘Lau si Umar kukataza kuoa ndoa ya muda (Muta) asingelizini ila mwovu wa kupindukia.”’ 46
Page 46
AHLUBAYT NDANI YA TAF. ZA KISUNNI No 1 check Lubumba.qxd
7/1/2011
11:10 AM
Ahlul Bayt Ndani ya Tafsiri za Kisunni
SURA MAIDA Kauli ya Mwenyezi Mungu:
“Hakika walii wenu hasa ni Mwenyezi Mungu na Mtume wake na wale walioamini ambao husimamisha Swala na hutoa Zaka wakiwa wamerukui.” (Sura Maida: 55). Ibnu Abbas amesema: as-Sadiy, Utba bin Hakim na Ghalib bin Abdullah wamesema: Kauli yake (s.w.t.): “Hakika walii wenu hasa ni Mwenyezi Mungu na Mtume wake na wale walioamini ambao husimamisha Swala na hutoa Zaka wakiwa wamerukui.” Alimkusudia Ali bin Abu Talib. Ombaomba alipita kwake na hali yeye karukui msikitini akampa pete yake. Kutoka kwa Ibayat bin ar-Rabiiyyu, amesema: Alipokuwa Abdullah Bin Abbas ameketi katika ukingo wa Kisima cha Zamzam ghafla alikuja mtu aliyekuwa kafunga kilemba. Ikawa kila Ibnu Abbas akisema: ‘Mtume wa Mwenyezi Mungu alisema’ naye husema: ‘Mtume wa Mwenyezi Mungu alisema’. Ndipo Ibnu Abbas akasema: Nakuomba kwa heshima ya Mwenyezi Mungu uniambie wewe ni nani? Akaondoa kilemba usoni na kusema: ”Enyi watu! Anayenitambua ameshanitambua. Mimi ni Jundub bin Junada niliyepigana vita vya Badri Abudhari al-Ghaffari. Nilimsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) kwa masikio yangu haya mawili la sivyo yapatwe na ukiziwi, akisema: “Ali ni kiongozi wa watu wema. Muuwaji wa makafiri. Atasaidiwa yule mwenye kumsaidia na atatelekezwa yule mwenye kumtelekeza.” “Hakika mimi siku moja niliswali pamoja na Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) Swala ya Adhuhuri, ombaomba akaomba msikitini na hakuna yeyote aliyempa, ndipo ombaomba akainua mikono yake mbinguni na kusema: “Ewe Mwenyezi Mungu shuhudia 47
Page 47
AHLUBAYT NDANI YA TAF. ZA KISUNNI No 1 check Lubumba.qxd
7/1/2011
11:10 AM
Ahlul Bayt Ndani ya Tafsiri za Kisunni kwamba bila shaka mimi nimeomba ndani ya msikiti wa Mtume wa Mwenyezi Mungu na sijapewa chochote na yeyote.” Kipindi hicho Ali alikuwa amerukuu ndipo akamwashiria kwenye chanda chake cha kulia kilichokuwa na pete. Ombaomba alikwenda na kuchukua pete toka kwenye chanda chake na hali Mtume akitizama kwa macho yake. “Mtume alipomaliza Swala yake aliinua kichwa chake mbinguni na kusema: ‘Ewe Mwenyezi Mungu! Ndugu yangu Musa alikuomba: Akasema: Ee Mola wangu! Nipanulie kifua changu. Na unifanyie wepesi kazi yangu. Na ufungue fundo katika ulimi wangu. Wapate kufahamu kauli yangu. Na uniwekee waziri katika jamaa zangu. Ndugu yangu Harun. Nitie nguvu kupitia yeye. Na umshirikishe katika kazi yangu.” (Sura Twaha: 25 – 32) ukamteremshia Qur’ani yenye kutamka: “Akasema: Karibuni tutautia nguvu mkono wako kwa ndugu yako na tutakupeni ushindi..” (Sura al-Qasas: 35). “Ewe Mwenyezi Mungu! Na mimi ni Muhammad Nabii wako na chaguo lako. Ewe Mwenyezi Mungu Nipanulie kifua changu. Na unifanyie wepesi kazi yangu. Na uniwekee waziri katika jamaa zangu. Ndugu yangu Ali. Nitie nguvu kupitia yeye.’” Abu Dharri anasema: “Wallahi kabla Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) hajamaliza Jibril akateremka kutoka kwa Mwenyezi Mungu na kusema: Ewe Muhammad soma. Akasema nisome nini? Akamwambia soma: “Hakika walii wenu hasa ni Mwenyezi Mungu na Mtume wake na wale walioamini ambao husimamisha Swala na hutoa Zaka wakiwa wamerukui.”55
Kauli ya Mwenyezi Mungu: 55 Ameipokea Humawi katika kitabu Faraidus-Samtwayn Juz. 1, Uk. 191, Chapa ya Beirut, Hadithi ya 162, Mlango wa 39. 48
Page 48
AHLUBAYT NDANI YA TAF. ZA KISUNNI No 1 check Lubumba.qxd
7/1/2011
11:10 AM
Ahlul Bayt Ndani ya Tafsiri za Kisunni
“Ewe Mtume! Fikisha uliyoteremshiwa kutoka kwa Mola wako; na kama hutafanya, basi hukufikisha ujumbe wake. Na Mwenyezi Mungu atakulinda na watu. Hakika Mwenyezi Mungu hawaongozi watu makafiri.” (Sura Maida: 67). Abu Ja’far Muhammad bin Ali amesema: “Maana yake ni: Fikisha uliyoteremshiwa kuhusu ubora wa Ali bin Abu Talib. Ilipoteremka Aya hii Mtume alimshika Ali mkono na kusema: Ambaye mimi nina mamlaka juu yake basi Ali ana mamlaka juu yake.” Kutoka kwa Adiy bin Thabit kutoka kwa al-Barrau, amesema: Tuliporudi pamoja na Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) tulifika sehemu iitwayo Ghadir Khum. Akanadi Swalatu Jamia, na akafagia chini ya miti miwili. Akauinua mkono wa Ali na kusema: “Mimi si nina mamlaka zaidi kwa waumini kuliko nafsi zao?” Wakajibu: “Ndio una mamlaka ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu?” Akasema: “Huyu ni mwenye mamlaka juu ya kila ambaye mimi nina mamlaka juu yake. Ewe Mwenyezi Mungu mpende yule atakayempenda na mfanyie uadui yule atakayemfanyia uadui.” Umari akamwendea na kumwambia: “Hongera ewe mwana wa Abu Talib, umekuwa mwenye mamlaka juu ya kila muumini wa kiume na wa kike.” Kutoka kwa al-Kalbiy, kutoka kwa Abu Salih, kutoka kwa Ibnu Abbas kuhusu kauli yake (s.w.t.): “Ewe Mtume! Fikisha uliyoteremshiwa kutoka kwa Mola wako..” amesema: Iliteremka kwa ajili ya Ali, Mtume aliamrishwa afikishe kwa ajili yake. Akauinua mkono wa Ali na kusema: “Ambaye mimi nina mamlaka juu yake basi huyu Ali ana mamlaka juu yake. Ewe Mwenyezi Mungu mpende ampendaye na mfanyie uadui amfanyiaye uadui.”56 56 Ameipokea Ibnu Asakir katika kitabu Taarikh Damashqi Juz. 2, Uk. 85, Chapa ya pili, Hadithi ya 588. 49
Page 49
AHLUBAYT NDANI YA TAF. ZA KISUNNI No 1 check Lubumba.qxd
7/1/2011
11:10 AM
Ahlul Bayt Ndani ya Tafsiri za Kisunni
SURA AL-AN’FAL Kauli ya Mwenyezi Mungu:
“Na jueni kwamba chochote mlichopata ghanima, basi khumsi yake ni ya Mwenyezi Mungu na Mtume na jamaa na mayatima na masikini na msafiri……” (Sura al-An’fal: 41). Az-Zahri amesema: “Fatima na Abbas walikuja kwa Abu Bakr kumwomba mirathi yao toka katika Shamba la Fadak na ghanima za vita vya Khaibar. Abu Bakr akawaambia: Nilimsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) akisema: ‘Sisi Manabii haturithiwi, tunayoyaacha ni sadaka.’” Man’hal bin Umar anasema: “Nilimuuliza Abdullah bin Muhammad bin Ali na Ali bin Husein kuhusu khumsi. Wakasema: ‘Ni ya kwetu.’ Nikamwambia Ali: Mwenyezi Mungu anasema: “…..na mayatima na masikini na msafiri……” Akasema: ‘Mayatima wetu, maskini wetu na wasafiri wetu.’”
SURA TAWBA Kauli ya Mwenyezi Mungu:
“(Tangazo la) Kujitoa Mwenyezi Mungu na Mtume wake kwa wale mlioahidiana nao miongoni mwa mushrikina.” (Sura Tawba: 1). Muhammad bin Is’haqa na Mujahid wamesema: Ulipoingia mwaka wa tisa Mtume wa Mwenyezi Mungu alikusudia kwenda Hija akasema: Bila shaka mushrikina watahudhuria ili wahiji na hali wakiwa uchi, sipendi kuhiji 50
Page 50
AHLUBAYT NDANI YA TAF. ZA KISUNNI No 1 check Lubumba.qxd
7/1/2011
11:10 AM
Ahlul Bayt Ndani ya Tafsiri za Kisunni mpaka watakapokuwa kinyume na hivyo. Ndipo Mtume wa Mwenyezi Mungu akamtuma Abu Bakr awe kiongozi awaongoze watu katika msimu wa Hija hiyo. Akampa aende na Aya arobaini toka mwanzo wa Sura Baraa ili akawasomee mahujaji wa msimu huo. Baada ya Abu Bakr kuondoka Mtume wa Mwenyezi Mungu alimwita Ali na kumwambia: “Nenda na kisa hiki kuanzia mwanzo wa Baraa kawatangazie watu watakapokusanyika.” Ali akotoka akiwa juu ya ngamia wa Mtume wa Mwenyezi Mungu mpaka alipomdiriki Abu Bakr huko Dhul-Halifa akaichukua Sura ile toka kwake. Abu Bakr akarejea kwa Mtume (s.a.w.w.) na kumwambia: ‘Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu! Baba yangu na mama yangu wawe fidia kwako, je kimeteremshwa chochote kunihusu?’ Mtume (s.a.w.w.) akasema: ‘Hapana, lakini hapaswi kufikisha kwa niaba yangu ila mimi mwenyewe.’ Au alisema: ‘Mtu atokanaye na mimi.’57 Kauli ya Mwenyezi Mungu:
“Na wale waliotangulia wakawa wa kwanza katika Muhajirina na Ansari...” (Sura Tawba: 1). Baadhi yao wamesema: Mwanamume wa kwanza kumwamini Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) ni Ali bin Abu Talib. Hiyo ni kauli ya Ibnu Abbas, Jabir, Zayd bin Arqam, Muhammad bin al-Munkadir, RabiarurRaayi na Abu Hazim al-Madaniy. Al-Kalbiy amesema: “Ali aliupokea Uislamu angali mtoto wa miaka tisa.” Mujahid na Ibnu Is’haqa wamesema: “Aliupokea Uislamu angali mtoto wa miaka kumi. ” 57 Al-Haskaniy amepokea kisa hiki kwa njia mbalimbali na kwa matamshi tofauti katika Hadithi ishirini kuanzia Hadithi ya 308 mpaka Hadithi ya 328 katika kitabu chake Shawahidut-Tanziil. 51
Page 51
AHLUBAYT NDANI YA TAF. ZA KISUNNI No 1 check Lubumba.qxd
7/1/2011
11:10 AM
Ahlul Bayt Ndani ya Tafsiri za Kisunni Na imepokewa kwamba Abu Talib alimwambia Ali: “Ewe mwanangu, ni imani gani hii uliyo nayo?” Akajibu: “Ewe baba yangu mpendwa, nimemwamini Mwenyezi Mungu na Mtume wake na nimesadikisha aliyoyaleta na nimeswali pamoja naye kwa ajili ya Mwenyezi Mungu. ” Akamwambia: “Hakika Muhammad halinganii ila kwenye kheri shikamana naye. ” Ubaydullah bin Musa amepokea kutoka kwa al-Alau bin Man’hal bin Umar, kutoka kwa Abbas bin Abdullah, amesema: “Nilimsikia Ali akisema: “Mimi ni mja wa Mwenyezi Mungu na ndugu wa mjumbe wake, na mimi ni Swidiqi mkubwa. Hatodai hayo baada yangu ila ni mwongo mzushi. Nimeswali miaka saba kabla ya watu. ” Kauli ya Mwenyezi Mungu:
“Enyi mlioamini! mcheni Mwenyezi Mungu na kuweni pamoja na wakweli.” (Sura Tawba: 119). Abdullah bin Muhammad bin Abdullah amenipa habari, amesema: Ametusimulia al-Kalbiy, kutoka kwa Abu Salih kutoka kwa Ibnu Abbas kuhusu Aya hii: “Enyi mlioamini! mcheni Mwenyezi Mungu na kuweni pamoja na wakweli.” Amesema: Ni kuwa pamoja na Ali bin Abu Talib na maswahaba wake.” Na Abdullah amenipa habari, amesema: Ametusimulia Muhammad bin Uthman, amesema: Ametusimulia Mufadhal bin Salih kutoka kwa Jabir kutoka kwa Abu Ja’far kuhusu kauli yake (s.w.t.): “Enyi mlioamini! mcheni Mwenyezi Mungu na kuweni pamoja na wakweli.” Amesema: “Ni kuwa pamoja na aali Muhammad.”58 58 Al-Haskaniy ameipokea katika kitabu chake Shawahidut-Tanziil, Hadithi ya 353. Na Sayyid Hashim al-Bahraniy katika kitabu Ghayatul-Marami Uk. 375, Mlango wa 77. 52
Page 52
AHLUBAYT NDANI YA TAF. ZA KISUNNI No 1 check Lubumba.qxd
7/1/2011
11:10 AM
Ahlul Bayt Ndani ya Tafsiri za Kisunni
SURA HUD Kauli ya Mwenyezi Mungu:
“Basi je, aliye na dalili wazi itokayo kwa Mola wake na anaifuata na shahidi atokaye kwake..” (Sura Hud: 17). Abdullah al-Qariu amenipa habari, amesema: Ametupa habari al-Qadhi Abul-Husain an-Naswibiy, amesema: Ametupa habari Hasan bin Hasan kutoka kwa Habban kutoka kwa al-Kalbiy, kutoka kwa Abu Salih, kutoka kwa Ibnu Abbas kuhusu kauli yake (s.w.t.): “Basi je, aliye na dalili wazi itokayo kwa Mola wake..” kuwa ni Mtume wa Mwenyezi Mungu. Na “..na anaifuata na shahidi atokaye kwake..” ni Ali peke yake.59 Abul Jarud ametupa habari kutoka kwa Habib bin Yasar kutoka kwa Zadhan, amesema: “Nilimsikia Ali akisema: “Naapa kwa Yule Ambaye ameotesha punje na kuumba nafsi, lau nikitandikiwa mto nikaketi juu yake nitawahukumu wanataurati kwa Taurati yao, wanainjili kwa Injili yao, wanazaburi kwa Zaburi yao na wanafurqan kwa Furqani yao. Naapa kwa Yule Ambaye ameotesha punje na kuumba nafsi, hakuna mtu yeyote miongoni mwa makuraishi aliyepitiwa na mtihani ila mimi najua matokeo yake kama utampeleka peponi au utamwingiza motoni.” Akasimama mtu mmoja na kumwambia: “Ni ipi Aya yako ewe Amirul-Muuminina iliyoteremka kuhusu madai yako? ” Akasema: “Basi je, aliye na dalili wazi itokayo kwa Mola wake na anaifuata na shahidi atokaye kwake..” Mtume wa Mwenyezi Mungu ana dalili ya wazi toka kwa Mola wake na mimi ni shahidi atokaye kwake. ”60 59 Ameipokea Ibnu Asakir katika kitabu Taarikh Damashqi Juz. 2, Uk. 420, Hadithi ya 928, kwenye wasifu wa Amirul-Muuminiina. 60 Ameiandika Humawi katika kitabu Faraidus-Samtwayn Juz. 1, Uk. 238, Mlango wa 63. 53
Page 53
AHLUBAYT NDANI YA TAF. ZA KISUNNI No 1 check Lubumba.qxd
7/1/2011
11:10 AM
Ahlul Bayt Ndani ya Tafsiri za Kisunni
SURA AR-RAAD Kauli ya Mwenyezi Mungu:
“Na katika ardhi mna vipande vilivyokaribiana. Na zipo bustani za mizabibu na mimea mingine na mitende ichipuayo kwenye shina na isiyochipua kwenye shina moja inayonyweshelezwa maji yaleyale. Na tunaifanya bora baadhi yake kuliko mingine katika kula. Hakika katika hayo kuna ishara kwa watu wanotia akilini.” (Sura ar-Raad: 4). Kutoka kwa Abdullah bin Muhammad bin Aqiil, kutoka kwa Jabir, amesema: “Nilimsikia Mtume wa Mewenyezi Mungu (s.a.w.w.) akimwambia Ali: “Watu wanatokana na miti tofauti. Na mimi na wewe tunatokana na mti mmoja.”61 Kauli ya Mwenyezi Mungu:
“Hakika wewe ni mwonyaji tu. Na kila kaumu ina wa kuwaongoza.” (Sura ar-Raad: 7).
61 Al-Haskaniy ameipokea katika kitabu chake Shawahidut-Tanziil, Hadithi ya 395. Na ameipokea Ibnu Asakir katika kitabu Taarikh Damashqi Juz. 1, Uk. 142, Hadithi ya 177, Chapa ya Pili. 54
Page 54
AHLUBAYT NDANI YA TAF. ZA KISUNNI No 1 check Lubumba.qxd
7/1/2011
11:10 AM
Ahlul Bayt Ndani ya Tafsiri za Kisunni Kutoka kwa Said bin Jubair, kutoka kwa Ibnu Abbas, amesema: “Ilipoteremka Aya hii Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) aliweka mkono wake juu ya kifua chake na kusema: ‘Mimi ndiye mwonyaji.’ Akaashiria mkono wake kwenye bega la Ali na kusema: ‘Ali wewe ndiye mwongozaji. Kupitia kwako wataongoka wenye kutaka kuongoka baada yangu.”62 Kutoka kwa Sufyan Ath-Thawriy, kutoka kwa Abu Is’haqa, kutoka kwa Zaid bin Yatbau, kutoka kwa Hudhayfa amesema kwamba: Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) alisema: “Mkimwacha Ali awatawale mtamkuta ni Kiongozi mwongozaji.” Kauli ya Mwenyezi Mungu:
“Wale ambao wameamini na wakafanya matendo mema, raha ni yao na marejeo mazuri.” (Sura ar-Raad: 29). Kutoka kwa Abu Ja’far amesema: Mtume wa Mwenyezi Mungu aliulizwa kuhusu kauli yake (s.w.t.): “…raha ni yao na marejeo mazuri.” akasema: “Tuba ni mti ambao shina lake limo ndani ya nyumba yangu na matawi yake yamewafikia watu wa Peponi.” Kisha akaulizwa tena mara nyingine akasema: “Ni mti wa peponi shina lake limo ndani ya nyumba ya Ali na matawi yake yamewafikia watu wa peponi.” Akaambiwa: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu! Mwanzo tulikuuliza ukasema: “Tuba ni mti shina lake limo ndani ya nyumba yangu na matawi yake yamewafikia watu wa Peponi.” Tukakuuliza tena ukasema: “Ni mti wa peponi shina lake limo ndani ya nyumba ya Ali na matawi yake yamewafikia watu wa peponi.” Vipi hili? 62 Ibu Hajar al-Asqalaniy ameiandika katika kitabu Lisanul-Mizan Juz. 2, Uk. 99.
55
Page 55
AHLUBAYT NDANI YA TAF. ZA KISUNNI No 1 check Lubumba.qxd
7/1/2011
11:10 AM
Ahlul Bayt Ndani ya Tafsiri za Kisunni Akajibu: “Hakika nyumba yangu na nyumba ya Ali kesho ni moja sehemu moja.”63 Kauli ya Mwenyezi Mungu:
“Na wale ambao wamekufuru wanasema wewe hukutumwa. Sema: Mwenyezi Mungu anatosha kuwa shahidi baina yangu na nyinyi na yule mwenye elimu ya Kitabu.” (Sura ar-Raad: 43). Abdullah bin Atau amesema: “Nilikuwa nimeketi na Abu Ja’far msikitini ndipo nikamwona Ibnu Abdullah bin Salam pembeni. Nikamwambia Abu Ja’far: “Wanadai eti ambaye ana elimu ya Kitabu ni Abdullah bin Salam. Akasema: “Hakika huyo (mwenye elimu ya Kitabu) ni Ali bin Abu Talib.”64 Kutoka kwa Abu Umar Zadhan, kutoka kwa Hudhayfa kuhusu kauli yake (s.w.t.): “…na yule mwenye elimu ya Kitabu.” Alisema: “Huyo ni Ali bin Abu Talib.”65
SURA MARYAM Kauli ya Mwenyezi Mungu:
“Hakika wale ambao wameamini na wakatenda mema Mwingi wa rehema atawajaalia mapenzi.” (Sura Maryam: 96). 63 Ibnu al-Batriq ameiandika katika kitabu Khasaisul-Wahyi al-Mubin Uk. 209, Chapa ya Pili, Mlango wa Tatu. Na pia kaiandika Tabarasiy katika Tafsiri yake Majmaul-Bayan anapoifasiri Aya hii. Na kaiandika al-Irbaliy katika kitabu Kashful Ghummah Juz. 1, Uk. 323. 64 Ameiandika Ibnu al-Mghzaliy katika kitabu chake al-Manaqib, Hadithi ya 258 Uk. 313. 65 Ameiandika Abu Naiim al-Asfahaniy katika kitabu an-Nuru al-Mushtaalu Fii Maa unzila Minal-Qur’an Fii Ali, Uk. 152, Sura ya kumi na tisa. 56
Page 56
AHLUBAYT NDANI YA TAF. ZA KISUNNI No 1 check Lubumba.qxd
7/1/2011
11:10 AM
Ahlul Bayt Ndani ya Tafsiri za Kisunni Kutoka kwa al-Barau bin Azib amesema: “Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) alimwambia Ali bin Abu Talib: “Ewe Ali, sema: Ewe Mwenyezi Mungu! Nipe hifadhi Kwako na niwekee mapenzi katika nyoyo za waumini.” Ndipo Mwenyezi Mungu akateremsha: “Hakika wale ambao wameamini na wakatenda mema Mwingi wa rehema atawajaalia mapenzi.”66
SURA TWAHA Kauli ya Mwenyezi Mungu: “Twaha.” (Sura Twaha: 1). Amesema Ja’far bin Muhammad as-Sadiq (a.s.): “Twaha: Ni utakaso wa Ahlul-Baiti wa Muhammad.” Kisha akasoma: “Hakika si mengineyo Mwenyezi Mungu anataka kuwaondolea uchafu, enyi watu wa nyumba ya Mtume, na kuwatakasa kabisa kabisa.” (Sura Ahzab: 33).
SURA NURU Kauli ya Mwenyezi Mungu:
“Katika nyumba ambazo Mwenyezi Mungu ameruhusu ziinuliwe na kutajwa humo jina lake, wanamtakasa humo asubuhi na jioni.” (Sura Nuru: 36). Akasimama mtu mmoja na kumuuliza: “Ni nyumba zipi hizi ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu?” Akasema: “Nyumba za Manabii.” Abu Bakr akasimama na kusema: “Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu! Nyumba hii ni miongoni mwazo, nyumba ya Ali na Fatima?” Akajibu: “Ndio ni miongoni mwazo bali ndio iliyo bora kuliko nyingine.” 66 Ameiandika Humawi katika Juz. 1, Uk. 8, Mlango wa 14. 57
Page 57
AHLUBAYT NDANI YA TAF. ZA KISUNNI No 1 check Lubumba.qxd
7/1/2011
11:10 AM
Ahlul Bayt Ndani ya Tafsiri za Kisunni
SURA FURQAN Kauli ya Mwenyezi Mungu:
“Naye ndiye aliyemuumba mwanadamu kutokana na maji na akamjaalia kuwa na nasaba na ukwe. Na Mola wako ni Mwenye uwezo.” (Sura Furqan: 54). Amesema: Iliteremka ikimuhusu Mtume (s.a.w.w.) na Ali bin Abu Talib. Mtume alimuozesha Ali kwa Fatima, naye ni mtoto wa ami yake na mume wa binti yake, hivyo wao wawili wakawa na nasaba na ukwe.
SURA SHUA’RAU Kauli ya Mwenyezi Mungu:
“Na uwonye jamaa zako walio karibu.” (Shua’rau: 214). Kutoka kwa Abu Is’haqa amesema: Ilipoteremka Aya hii: “Na uwonye jamaa zako walio karibu.” Mtume wa Mwenyezi Mungu aliwakusanya watoto wa Abdul-Muttalib kipindi hicho wakiwa ni wanaume arobaini. Mtu mmoja kati yao alikuwa akila mbuzi mzima. Akamwamuru Ali aandae mguu wa mbuzi akautengeneza chakula kisha Mtume akasema: “Karibuni kwa jina la Mwenyezi Mungu. ” Watu wakakaribia na wakala mpaka wakatosheka. Kisha baada ya hapo akaomba maziwa akanywa funda moja kisha akawaambia: “Kunyweni kwa jina la Mwenyezi Mungu.” Wakanywa mpaka wakatosheka. Ndipo Abu Lahabi akawatangulia kwa kusema: “Huu ndio uchawi aliowaroga mtu huyu.” Mtume akanyamaza hakusema chochote siku hiyo. 58
Page 58
AHLUBAYT NDANI YA TAF. ZA KISUNNI No 1 check Lubumba.qxd
7/1/2011
11:10 AM
Ahlul Bayt Ndani ya Tafsiri za Kisunni Kisha siku iliyofuata waliwaita na kuwaandalia chakula na kinywaji mfano wa kile. Kisha Mtume wa Mwenyezi Mungu akawaonya, akasema: “Enyi wana wa Abdul-Muttalib! Hakika mimi ni mwonyaji kwenu kutoka kwa Mwenyezi Mungu. Na ni mbashiri wa yale ambayo hakuna yeyote aliyewaletea. Hakika mimi nimewaletea kheri ya dunia na akhera. Silimuni na mnitii mtaongoka. Na ni nani ataniunga mkono na kunisaidia awe mrithi wangu, wasii wangu na khalifa wangu kwa watu wangu na anilipie deni langu.” Kaumu wakakaa kimya. Akarudia wito huo mara tatu. Mara zote hizo kaumu walikaa kimya na Ali akisema: “Mimi.” Mtume wa Mwenyezi Mungu akasema: “Wewe.” Kaumu wakanyanyuka na hali wakimwambia Abu Talib: “Bila shaka amekuamuru umsikilize na kumtii mwanao.”
SURA NAMLU Kauli ya Mwenyezi Mungu:
“Na Suleiman alimrithi Daud. Na akasema: Enyi watu! Tumefunzwa usemi wa ndege. Na tumepewa kila kitu. Hakika hii ni fadhila iliyo dhahiri.” (Sura Namlu: 16). Ja’far bin Muhammad as-Saddiq amepokea kutoka kwa baba yake kutoka kwa babu yake, kutoka kwa Hasan bin Ali, amesema: “Kipozamataza – aina ya ndege – aliapo huwa anasema: Ewe Mungu wangu! Walaani wenye kuwabughudhi aali Muhammad.” Kauli ya Mwenyezi Mungu: “Watakaokuja na wema watapata bora kuliko hayo. Nao watasalimika na.” (Sura Namlu: 89). Kutoka kwa Abu Daud as-Sabuiy, kutoka kwa Abdullah banal-Jadliy, ame59
Page 59
AHLUBAYT NDANI YA TAF. ZA KISUNNI No 1 check Lubumba.qxd
7/1/2011
11:10 AM
Ahlul Bayt Ndani ya Tafsiri za Kisunni sema: Niliingia kwa Ali bin Abu Talib akaniambia: “Ewe Abdullah nikueleze wema ambao atakayeuleta Mwenyezi Mungu atamwingiza peponi?” Nikamwambia ndio. Akasema: Wema huo ni kutupenda sisi na uovu ni kutubughudhi sisi.”
SURA AHZAB Kauli ya Mwenyezi Mungu:
“Hakika si mengineyo Mwenyezi Mungu anataka kuwaondolea uchafu, enyi watu wa nyumba ya Mtume, na kuwatakasa kabisa kabisa.” (Sura Ahzab: 33). Amesema: Bakru bin Yahya bin Rayyan al-Askari ametusimulia, amesema: Ametusimulia Aamash kutoka kwa Atia, kutoka kwa Abu Said al-Khudri, amesema: Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) alisema: “Aya hii: “Hakika si mengineyo Mwenyezi Mungu anataka kuwaondolea uchafu, enyi watu wa nyumba ya Mtume, na kuwatakasa kabisa kabisa.” imeteremka kwa ajili ya watano: Kwa ajili yangu, Ali, Hasan, Husein na Fatima.”67 Ametusimulia aliyemsikia Ummu Salama akisema kwamba: “Mtume (s.a.w.w.) alikuwa nyumbani kwake ndipo akaja Fatima akiwa na chungu chenye uji na kuingia nacho kwa Mtume. Mtume akamwambia mwite mumeo na wanao. Alikuja Ali, Hasan na Husein wakaingia kwa Mtume na wakaketi wakinywa uji huo na hali Mtume akiwa juu ya kitanda chake cha mbao kilichotandikwa kishamia cha Khaibari. 67 Ameipokea al-Haythami katika Majmauz-Zawaid, Mlango wa Fadhila za Ahlul-Baiti, Juz. 9, Uk. 167. Na al-Wahid katika kitabu chake Asbabun-Nuzuul Uk. 267. 60
Page 60
AHLUBAYT NDANI YA TAF. ZA KISUNNI No 1 check Lubumba.qxd
7/1/2011
11:10 AM
Ahlul Bayt Ndani ya Tafsiri za Kisunni Nikiwa chumba kingine naswali ghafla Mwenyezi Mungu aliteremsha Aya hii: “Hakika si mengineyo Mwenyezi Mungu anataka kuwaondolea uchafu, enyi watu wa nyumba ya Mtume, na kuwatakasa kabisa kabisa.” Nikaingiza kichwa chumbani kwa Mtume na kumwambia: Je na mimi ni pamoja nanyi ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu? Akasema: “Hakika wewe upo katika kheri. Bila shaka wewe upo katika kheri.”68 Kutoka kwa Awamu bin Hawshab, amesema: “Amenisimulia mtoto wa ami yangu toka kizazi cha Harith bin Taymullah anayeitwa Mujmiu, amesema: Niliingia na mama yangu kwa Aisha, mama yangu akamuuliza kwa kusema: “Umeona ulikuwa sawa kutoka na kwenda kupigana Vita vya Jamali?” Akasema: Hakika ilikuwa na makadara kutoka kwa Mwenyezi Mungu. Kisha akamuuliza kuhusu Ali. Aisha akasema: “Umeniuliza kuhusu mtu aliyekuwa akipendwa sana na Mtume wa Mwenyezi Mungu kuliko watu wote. Mume aliyekuwa akipendwa sana na Mtume wa Mwenyezi Mungu kuliko watu wote. Nilimuona Ali, Fatima, Hasan na Husein wamefunikwa nguo na Mtume wa Mwenyezi Mungu kisha akasema: ‘Hawa ndio Ahlul-Baiti wangu na ndugu zangu wa karibu, hivyo waondolee uchafu na uwatakase kabisa.’ Nikasema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu! Je mimi ni miongoni mwa ndugu zako? Akasema: ‘Wewe ni mtu baki hakika wewe utaelekea kwenye kheri.’ 69 Kutoka kwa Abdullah bin Ja’far at-Twayyar, kutoka kwa baba yake, amesema: “Mtume alipoitazama rehema ikishuka toka mbinguni (mvua) alisema: ‘Ni nani atakayeniitia?’ alisema mara mbili. Zainab akasema: “Mimi ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu.” 68 Ameipokea Ahmad bin Hanbal katika kitabu al-Fadhail Uk. 79, Hadithi ya 11, Chapa ya Kwanza. Na katika kitabu al-Musnad Uk. 292. 69 Ameiandika Ibn Asakir katika Tarikh Damashqi Juz. 2, Uk. 163, Chapa 2, Hadithi 650. 61
Page 61
AHLUBAYT NDANI YA TAF. ZA KISUNNI No 1 check Lubumba.qxd
7/1/2011
11:10 AM
Ahlul Bayt Ndani ya Tafsiri za Kisunni Akasema: Niitie Ali, Fatima, Hasan na Husein. Akamweka Hasan kuliani kwake, Husein kushotoni kwake na Ali na Fatima usoni kwake. Kisha akawafunika kishamia cha Khaibar na kusema: “Ewe Mwenyezi Mungu kila Nabii ana ndugu na hawa ndio ndugu zangu.” Ndipo Mwenyezi Mungu akateremsha: “Hakika si mengineyo Mwenyezi Mungu anataka kuwaondolea uchafu, enyi watu wa nyumba ya Mtume, na kuwatakasa kabisa kabisa.” Zainab akasema: ‘Ewe Mtume wa Mwenyezi niingie pamoja nanyi?’ Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) akasema: “Baki hapo hapo, bila shaka inshaallah utaelekea katika kheri.”70 Kutoka kwa Awzaiy, kutoka kwa Shaddad Abu Ammar, amesema: “Niliingia kwa Wathila bin al-Asqau nikamkuta ameketi na baadhi ya watu. Ndipo walipomtaja Ali na kumkashifu nami nikamkashifu. Walipoondoka (Wathila) akaniambia: ‘Hivi kweli umemkashifu mtu huyu?!!!’ Nikamwambia nimeona watu wanamkashifu nami nikashirikiana nao kumkashifu. Akaniambia je nikueleze yale niliyosikia kutoka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.)? Nikasema ndio nieleze. Akasema: “Nilikwenda kwa Fatima nikimuulizia Ali. Fatima akanijibu kwamba ameelekea kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.), nikaketi na punde Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) akaja na kuingia akiwa pamoja na Ali, Hasan na Husein akiwa amemshika kila mmoja wao (Hasan na Husein) mkono. Akawaita Ali na Fatima na kuwakalisha mbele yake. Na akamkalisha Hasan na Husein kila mmoja pajani kwake. Kisha akawafunika nguo yake na kusoma Aya hii: “Hakika si mengineyo Mwenyezi Mungu anataka kuwaondolea uchafu, enyi watu wa nyumba ya Mtume, na kuwatakasa kabisa kabisa.” Kisha akasema: Ewe Mwenyezi Mungu! Hawa ndio watu wa nyumba yangu. Na watu wa nyumba yangu ndio wenye haki zaidi (kuliko mtu baki).”71 70 Ameipokea Ibnu al-Mughaziliy katika kitabu al-Manaqib Uk. 305. Na alHaythamiy katika Majmauz-Zawaid Juz. 9, Uk. 167. 71 Ameiandika Ibnu Hanbal katika kitabu chake al-Musnad Juz. 4, Uk. 107. Na katika kitabu chake al-Fadhail Uk. 66, Hadithi ya 102, Chapa ya Kwanza. 62
Page 62
AHLUBAYT NDANI YA TAF. ZA KISUNNI No 1 check Lubumba.qxd
7/1/2011
11:10 AM
Ahlul Bayt Ndani ya Tafsiri za Kisunni Kutoka kwa Zayd bin Arqam, amesema: “Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) alisema: “Nawaapizeni kwa Mwenyezi Mungu kuhusu Ahlul-Baiti wangu. Nawaapizeni kwa Mwenyezi Mungu kuhusu Ahlul-Baiti wangu.” Kutoka kwa Nafiu Abu Daud, kutoka kwa Abul-Hamrau, amesema: Niliishi Madina miezi tisa kama vile ni siku moja (yaani sikutoka nje ya Madina muda wa miezi tisa). Mtume wa Mwenyezi Mungu alikuwa anakuja kila siku asubuhi na kusimama kwenye mlango wa Ali na Fatima na kusema: “Swala. Hakika si mengineyo Mwenyezi Mungu anataka kuwaondolea uchafu, enyi watu wa nyumba ya Mtume, na kuwatakasa kabisa kabisa.”72 Kauli ya Mwenyezi Mungu:
“Hakika Mwenyezi Mungu na malaika wake wanamswalia Nabii. Enyi ambao mmeamini! Mswalieni na mumsalimu kwa salamu.” (Sura Ahzab: 56). Ametupa habari Abdurahman bin Abu Layala, amesema: Amenisimulia Kaab bin Ajara, amesema: Ilipoteremka: “Hakika Mwenyezi Mungu na malaika wake wanamswalia Nabii. Enyi ambao mmeamini! Mswalieni na mumsalimu kwa salamu.” Nilisema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu! Tumeshajua namna ya kukutolea salamu ni ipi namana ya kukusalia? Mtume akasema: ‘’Semeni: Ewe Mwenyezi Mungu! Mrehemu Muhammad na aali Muhammad kama ulivyomrehemu Ibrahim na aali Ibrahim, hakika wewe ni Muhimidiwa Msifiwa. Na mbariki Muhammad na aali Muhammad kama ulivyombariki Ibrahim na aali Ibrahim, hakika 72 Ameipokea Dhahabi katika kitabu chake Mizanul-Iitidal Juz. 2, Uk. 381.
63
Page 63
AHLUBAYT NDANI YA TAF. ZA KISUNNI No 1 check Lubumba.qxd
7/1/2011
11:11 AM
Ahlul Bayt Ndani ya Tafsiri za Kisunni wewe ni Muhimidiwa Msifiwa. ‘’ Kutoka kwa Ibnu Mas’ud al-Ansariy alisema: “Mtume alikuja na kutukuta tumeketi katika baraza la Saad bin Ubada. Bushru bin Saad akamwambia: Mwenyezi Mungu ametuamuru tukuswalie ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, basi ni vipi tutakavyokusalia?” Mtume akakaa kimya mpaka tukatamani kwamba asingemuuliza. Kisha akasema (s.a.w.w.):
Semeni: “Ewe Mwenyezi Mungu! Mrehemu Muhammad na aali Muhammad kama ulivyomrehemu Ibrahim na aali Ibrahim. Na mbariki Muhammad na aali Muhammad kama ulivyombariki Ibrahim na aali Ibrahim katika walimwengu, hakika wewe ni Muhimidiwa Msifiwa.” Na salamu ni kama mlivyojifunza. Kauli ya Mwenyezi Mungu:
“Hakika wale ambao wanamuudhi Mwenyezi Mungu na Mtume wake, Mwenyezi Mungu amewalaani duniani na Akhera, na amewaandalia adhabu ya kufedhehesha. Na wale ambao wanawaudhi waumini wanaume na waumini wanawake pasi na wao kufanya, hakika wamebeba dhulma kubwa na dhambi kumbwa.” (Sura Ahzab: 57 58). Muqatil amesema: “Iliteremka kwa ajili ya Ali. Hiyo ni pale baadhi ya wanafiki walipokuwa wakimuudhi na kumtukana.”73 73 Ameipokea al-Wahidiy katika kitabu chake Asbabun-Nuzuul Uk. 273. 64
Page 64
AHLUBAYT NDANI YA TAF. ZA KISUNNI No 1 check Lubumba.qxd
7/1/2011
11:11 AM
Ahlul Bayt Ndani ya Tafsiri za Kisunni
SURA YASIN Kauli ya Mwenyezi Mungu:
“Ikasemwa: Ingia peponi! Akasema: Laiti watu wangu wangejua, jinsi Mola wangu alivyonighufuria na akanifanya katika waheshimiwa.” (Sura Yasin: 26 - 27). Kutoka kwa Abdurahman bin Abu Layla, kutoka kwa baba yake, amesema: “Mtume wa Mwenyezi Mungu alisema: “Vinara wa umma ni watatu hawajamkufuru Mwenyezi Mungu hata kidogo: Ali bin Abu Talib, rafiki wa Yasin na muumini wa aali Firaun. Wao ndio wasadikishaji wakubwa: Habib an-Najar muumini wa aali Yasin, Hazbil muumini wa aali Firaun na Ali bin Abu Talib naye ndiye mbora wao.”74
SURA AS-SSAFFAT Kauli ya Mwenyezi Mungu: “Amani kwa Ilyasin.” (Sura as-Saffat: 130). Atakayesoma Aali Yasin kwa kukokoteza basi amekusudia Aali Muhammad.75 74 Ameipokea Ibnu Asakir katika kitabu Taarikh Damashqi Juz. 2 Uk. 282, Hadithi ya 813. 75 Kuna riwaya nyingi zimepokewa zikisema kwamba Aali Yasin katika Aya hii ndio hao hao Aali Muhammad (a.s.). al-Haskaniy amepokea Hadithi saba zikiwa na maana hii, kuanzia Hadithi ya 791 mpaka ya 797. Na al-Irbaliy naye kazitaja katika kitabu chake Kashful-Ghumma Juz. 1, Uk. 324 katika anwani inayozungumzia Aya zilizoteremka kumuhusu Ali. Unaweza kurejea huko. 65
Page 65
AHLUBAYT NDANI YA TAF. ZA KISUNNI No 1 check Lubumba.qxd
7/1/2011
11:11 AM
Ahlul Bayt Ndani ya Tafsiri za Kisunni
SURA GHAFIR Kauli ya Mwenyezi Mungu:
“Wale wanaobeba Arshi, na wanaoizunguka, wanamsabihi kwa kumuhimidi Mola wao, na wanamuamini na wanawaombea msamaha walioamini. Mola wetu! Umekienea kila kitu kwa rehema na ujuzi. Basi wasamehe ambao wametubu na wakaifuata Njia Yako, na waepushe na adhabu ya Jahannamu.” (Sura Ghafir: 7). Amepokea Said bin Jubair kutoka kwa Abul-Hamrau mtumishi wa Mtume (s.a.w.w.), amesema: “Nilimsikia Mtume (s.a.w.w.) akisema: “Siku nilipopelekwa mbinguni niliona nguzo ya Arshi imenakishiwa kwa: Hapana Mungu apasaye kuabudiwa kwa haki ila Mwenyezi Mungu mmoja. Na hakika Muhammad ni Mtume wa Mwenyezi Mungu. Nimempa nguvu kupitia Ali na nimemsaidia.”76 Amepokea Said bin Jubair kutoka kwa Abul-Hamrau mtumishi wa Mtume (s.a.w.w.), amesema: Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) alisema: “Hasan na Husein ni hereni za Arshi na si zile za kutungikwa (za kuvaa na kuvuliwa bali ni za asili zisizoachana na Arshi).”
76 Al-Muttaqi al-Hindiy ameipokea ndani ya kitabu chake Kanzul-Ummal Juz. 6, Uk. 158. 66
Page 66
AHLUBAYT NDANI YA TAF. ZA KISUNNI No 1 check Lubumba.qxd
7/1/2011
11:11 AM
Ahlul Bayt Ndani ya Tafsiri za Kisunni
SURA AS-SHURA Kauli ya Mwenyezi Mungu:
“Sema: Kwa haya siwaombi malipo yoyote kwenu isipokuwa mapenzi katika ndugu...” (Sura as-Shura: 23). Kutoka kwa Said bin Jubair, kutoka kwa Ibnu Abbas amesema: Ilipoteremka: “Sema: Kwa haya siwaombi malipo yoyote kwenu isipokuwa mapenzi katika ndugu...” walimuuliza: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) ni akina nani hawa ndugu ambao ni imewajibishwa juu yetu kuwapenda. Akasema: “Ali, Fatima na watoto wake wawili.”77 Kutoka kwa Amru bin Musa, kutoka kwa Zayd bin Ali bin Husein kutoka kwa baba yake, kutoka kwa babu yake Ali bin Abu Talib, amesema: “Nilimshitakia Mtume kuhusu husuda za watu dhidi yangu. Akasema: ‘Hivi huridhii kuwa mmoja kati ya wanne. Wa kwanza kuingia Peponi. Ni Mimi, Wewe, Hasan, Husein na wake zetu wakiwa kuliani kwetu na kushotoni kwetu. Na wajukuu zetu wakiwa nyuma ya wake zetu. Na wafuasi wetu wakiwa nyuma yetu.”’ Kutoka kwa Shahru Hawshab, kutoka kwa Ummu Salama, kutoka kwa Mtume (s.a.w.w.) kwamba alimwambia Fatima: “Niitie mume wako na wanao.” Wakaja na ndipo akawafunika kishamia cha kutoka Fadak, akainua mikono yake juu yao na kusema: “Ewe Mwenyezi Mungu! Hawa ndio aali Muhammad, ziweke rehema 77 Ameiandika al-Mughzali katika kitabu chake al-Manaqib Juz. 352, Uk. 307. Na al-Fayruz Abad katika kitabu chake Fadhailul-Khamsa Juz. 1, Uk. 250. 67
Page 67
AHLUBAYT NDANI YA TAF. ZA KISUNNI No 1 check Lubumba.qxd
7/1/2011
11:11 AM
Ahlul Bayt Ndani ya Tafsiri za Kisunni zako na baraka zako juu ya Muhammad na aali Muhammad. Hakika wewe ni Muhimidiwa Msifiwa.” Nikainua kishamia ili niingie, ghafla akakivuta na kusema: “Hakika wewe u katika kheri.” Abu Hazim amepokea kutoka kwa Abu Huraira, amesema: Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) alimtazama Ali, Fatima, Hasan na Husein, kisha akasema: “Mimi ni mwenye kumpiga vita yule mwenye kuwapigeni vita. Na ni mwenye kuishi naye kwa amani yule mwenye kuishi nanyi kwa amani.” Kutoka kwa as-Sadiy, kutoka kwa Abu Daylam, amesema: “Alipoletwa Ali bin Husein na hali ni mateka na kusimamishwa katika barabara kuu ya Damascus alisimama mzee mmoja kati ya watu wa Sham, akasema: “Kila sifa njema ni ya Mwenyezi Mungu ambaye amewauwa na kuwang’oeni na kung’oa mzizi wa fitina.” Ali bin Husein akasema: ‘Umewahi kusoma Qur’ani?’ akajibu: “Ndio.” Akasema (a.s.): ‘Umewahi kusoma Aali Haa Miim?’Akajibu: “Nimewahi kusoma Qur’ani na sijawahi kusoma Aali Haa Miim.” Akasema (a.s.): ‘Umewahi kusoma: “Sema: Kwa haya siwaombi malipo yoyote kwenu isipokuwa mapenzi katika ndugu...”’ Mzee akasema: ‘Nyinyi ndio hao?’ Akasema (a.s.): ‘Naam ndio sisi.’” Ametusimulia Ali bin Musa Ridha (a.s.), amesema: “Amenisimulia baba yangu Musa bin Ja’far (a.s.), amesema: Ametusimulia baba yangu Ja’far bin Muhammad as-Sadiq (a.s.), amesema: “Pete ya baba yangu Muhammad bin Ali (a.s.) ilikuwa imenakishiwa kwa nakshi ya: Dhana yangu nzuri ni kwa Mwenyezi Mungu, kwa Nabii mwaminiwa, kwa wasii mwenye ihisani na kwa Husein na Hasan.” Muhammad bin Abdurahman az-Zaafaraniy, amesema: “Aliniapia Ahmad bin Ibrahim al-Jarjaniy, amesema: Mansur al-Faqihu, amesema: “Ikiwa kwa kuwapenda kwangu watano faradhi zangu hutukuka; na kuwachukuia kwangu wenye kuwafanyia uadui ni urafidhi, basi mimi ni rafidhi.”
68
Page 68
AHLUBAYT NDANI YA TAF. ZA KISUNNI No 1 check Lubumba.qxd
7/1/2011
11:11 AM
Ahlul Bayt Ndani ya Tafsiri za Kisunni Kutoka kwa Anas bin Malik amesema: “Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) amesema: “Sisi ni kizazi cha Abdul-Muttalib mabwana wa watu wa Peponi: Mimi, Hamza, Ja’far, Ali, Hasan, Husein na Mahdi.” Ali bin Musa Ridha (a.s.) amesema: “Amenisimulia Baba yangu Musa bin Ja’far (a.s.), amesema: Amenisimulia Baba yangu Ja’far bin Muhammad (a.s.), amesema: Amenisimulia baba yangu Muhammad bin Ali (a.s.), amesema: Amenisimulia baba yangu Ali bin Husein (a.s.), amesema: Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) alisema: “Pepo imeharamisha juu ya yule aliyewadhulumu Ahlul-Baiti wangu na akaniudhi kwa kuwaudhi kizazi changu. Yeyote atakayemtendea wema yeyote miongoni mwa kizazi cha Abdul-Muttalib na ikawa hajalipwa kutokana na wema huo, basi mimi nitamlipa kesho atakapokutana nami Siku ya Kiyama.” Ametusimulia Yaala bin Ubaydu kutoka kwa Ismail bin Abu Khalid, kutoka kwa Qaysu bin Abu Hazim, kutoka kwa Jarir bin Abdullah al-Bajliy, amesema: Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) alisema: “Ehe! atakayekufa na hali awapenda aali Muhammad basi amekufa na hali ni shahidi. Ehe! atakayekufa na hali awapenda aali Muhammad basi amekufa na hali ameghufuriwa. Ehe! atakayekufa na hali awapenda aali Muhammad basi amekufa na hali ametubia. Ehe! atakayekufa na hali awapenda aali Muhammad basi amekufa na hali ni muumini aliyekamilika kiimani. Ehe! atakayekufa na hali awapenda aali Muhammad basi amekufa na hali malaika wa mauti ameshambashiria Pepo, kisha Munkar na Nakir. Ehe! atakayekufa na hali awapenda aali Muhammad Mwenyezi Mungu atawafanya malaika wa rehema wawe wenye kulizuru kaburi lake. Ehe! atakayekufa na hali awapenda aali Muhammad Mwenyezi Mungu atamfungulia milango miwili ya Pepo kaburini. Ehe! atakayekufa na hali awapenda aali Muhammad atasindikizwa Peponi kama biharusi asindikizwavyo kwenda nyumbani kwa mumewe. Ehe! atakayekufa na hali awapenda aali Muhammad basi amefia ndani ya Sunna na Jamaa.
69
Page 69
AHLUBAYT NDANI YA TAF. ZA KISUNNI No 1 check Lubumba.qxd
7/1/2011
11:11 AM
Ahlul Bayt Ndani ya Tafsiri za Kisunni Ehe! atakayekufa na hali awachukia aali Muhammad atakuja Siku ya Kiyama na hali imeandikwa baina ya macho yake mawili: Amekata tamaa na rehema za Mwenyezi Mungu. Ehe! atakayekufa na hali awachukia aali Muhammad basi amekufa na hali ni kafiri. Ehe! atakayekufa na hali awachukia aali Muhammad hatoipata harufu ya Pepo.” Kauli ya Mwenyezi Mungu:
“Na anayefanya wema tutamzidishia wema. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa maghufira Mwingi wa shukrani.” (Sura as-Shura: 23). Kutoka kwa as-Sadiy, kutoka kwa Abu Malik, kutoka kwa Ibnu Abbas kuhusu kauli yake (s.w.t.): “Na anayefanya wema tutamzidishia wema.” amesema: “(Wema hapo) Ni kuwapenda aali Muhammad.”78
SURA AZ-ZUKHRUF Kauli ya Mwenyezi Mungu:
“Na waulize Mitume wetu tuliowatuma kabla yako: Je, tulifanya miungu mingine iabudiwe badala ya Mwingi wa rehema.” (Sura azZukhruf: 23). Kutoka kwa Abdullah bin Mas’ud, amesema: Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) amesema: “Malaika aliniijia na kuniambia: ‘Ewe 78 Ameipokea al-Mughazaliy katika kitabu chake al-Manaqib, Hadithi ya 360 Uk. 316. Na al-Haskaniy katika kitabu chake Shawahidut-Tanziil, Hadithi ya 846. 70
Page 70
AHLUBAYT NDANI YA TAF. ZA KISUNNI No 1 check Lubumba.qxd
7/1/2011
11:11 AM
Ahlul Bayt Ndani ya Tafsiri za Kisunni Muhammad! Waulize tuliowatuma kabla yako miongoni mwa Mitume, tuliwatuma walinganie nini.’ Nikasema uliwatuma walinganie nini? Akasema: ‘Walinganie uwalii wako na uwalii wa Ali bin Abu Talib.”’79
SURA AD-DUKHAN Kauli ya Mwenyezi Mungu:
“Mbingu na ardhi hazikuwalilia; wala hawakupewa muda.” (Sura adDukhan: 29). As-Sadiy amesema: “Alipouwawa Husein bin Ali (a.s.) mbingu ilimlilia na kilio chake ni wekundu wake.” Ametupa habari Abu Bakr al-Jawzaqiy kutoka kwa Hisham, kutoka kwa Muhammad bin Sirin, amesema: “Tulipewa habari kwamba wekundu uliyopo kwenye mawingu haukuwapo awali mpaka pale Husein (a.s.) alipouwawa.” Ametusimulia Hammad bin Salma, amesema: “Ametupa habari Sulaymu al-Qadhi amesema: “Tulinyeshewa na mvua ya damu pindi Husein alipouwawa.”
SURA AL-AHQAF Kauli ya Mwenyezi Mungu: “…Basi leo mtapewa adhabu ya fedheha….” (Sura al-Ahqaf: 20). Na Kauli ya Mwenyezi Mungu: “….Bali imewapotea, na huo ndio uwongo wao na waliyokuwa wakiyatunga.” (Sura al-Ahqaf: 28). Kutoka kwa Thawbani huria wa Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) amesema: Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) alikuwa anaposafiri mtu 79 Ameipokea Ibnu Asakir katika kitabu chake Taarikh Damashqi Juz. 2, Uk. 98, Hadithi ya 602, Chapa ya Pili. 71
Page 71
AHLUBAYT NDANI YA TAF. ZA KISUNNI No 1 check Lubumba.qxd
7/1/2011
11:11 AM
Ahlul Bayt Ndani ya Tafsiri za Kisunni wa mwisho kumuaga ni mtu toka katika ndugu zake. Na wa kwanza atakayeingia kwake kumsalimu baada ya kurejea ni Fatima. Aliporudi toka kwenye moja ya vita alisimama mlangoni kwa Fatima na ghafla akamwona Hasan na Husein wamevaa pingu mbili za fedha. Akarudi na hakuingia kwake. Fatima alivyoona hivyo akadhani kwamba hakuingia kutokana na aliyoyaona. Akatoka ndani na kuwavua watoto pingu. Watoto wakalia, ndipo akaikata na kuigawa vipande viwili kati yao. Wakaenda kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu na hali wakilia, Mtume wa Mwenyezi Mungu akaichukua pingu ile toka kwao na kusema: “Ewe Thawbani nenda na hii kwa watoto wa fulani (familia moja ya huko Madina) na umnunulie Fatima mkufu na bangili za meno ya ndovu.” Na akasema: “Hakika hawa ni Ahlul-Baiti wangu, sipendi wale vizuri vyao katika maisha ya dunia.”
SURA AL-FAT’HU Kauli ya Mwenyezi Mungu:
“Mwenyezi Mungu amekuahidini ngawira nyingi mtakazozichukua, kisha akakutimizeni haya, na akaizuia mikono ya watu isikufikieni, na ili iwe dalili kwa waumini na kukuongozeni njia iliyonyooka.” (Sura al-Fat’hu: 20). Kutoka kwa Ibnu Jarir, amesema: “Ametusimulia Ibnu Bashari, amesema: Ametusimulia Muhammad bin Ja’far, amesema: Wametusimulia baadhi yao, wamesema: Tulitoka pamoja na Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) kwenda Khaibar usiku. Amir bin al-Ukui alikuwa pamoja nasi, ndipo mtu mmoja akamwambia, ewe Amir bin al-Kui mbona hautusikilizishi mashairi yako. Amir alikuwa ni malenga hodari basi akawa anawaghania watu huku akisoma mashairi.” Msimuliaji anasema: “Tukawazingira mpaka tukapatwa na njaa kali kisha 72
Page 72
AHLUBAYT NDANI YA TAF. ZA KISUNNI No 1 check Lubumba.qxd
7/1/2011
11:11 AM
Ahlul Bayt Ndani ya Tafsiri za Kisunni Mwenyezi Mungu akatupa ushindi. Hiyo ni kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) alimkabidhi bendera Umar na wakaondoka pamoja naye wale waliofanikiwa kwenda naye hadi wakafika Khaibar, kisha Umar na jamaa zake wakakimbia. Wakarejea kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) huku jamaa zake wakimshutumu kwa uoga naye akiwashutumu wao kwa uoga. Kipindi hicho Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) alikuwa anasumbuliwa na maumivu ya kichwa hivyo hakuweza kutoka kwenda kuwaeleza chochote watu. Abu Bakr akachukua bendera ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) naye alikwenda akapambana mapamabano makali sana. Kisha akarejea na ndipo akaichukua Umar tena na kupambana mapambano makali kuliko alivyopamabana katika mapambano ya kwanza. Kisha akarejea. Ndipo Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) akapewa habari hizo, akasema: “Hakika kesho nitamkabidhi bendera mtu ambaye anampenda Mwenyezi Mungu na Mtume wake na Mwenyezi Mungu na Mtume wake wanampenda. Ataichukua kwa nguvu.” Na hapo hakuwepo Ali. Ilipofika kesho Abu Baki, Umar na makuraishi kwa ujumla walitamani jambo hilo kila mmoja akitaraji awe ndiye mtu huyo. Mtume wa Mwenyezi Mungu akamtuma Salma bin al-Kui amwite Ali. Akamwita, na Ali alikuja akiwa juu ya ngamia wake mpaka akasogea karibu mno na Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) hali akiwa anaumwa macho. Salma anasema: “Nilikuja naye nami nikimwongoza mpaka kwa Mtume (s.a.w.w.). Akasema Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.): “Vipi hali yako?” Akajibu: “Nimepatwa na maradhi ya macho.” Akamwambia: “Sogea karibu yangu.” Akasogea na ndipo akamtemea mate machoni basi kuanzia muda huo hakuugua macho mpaka anaingia kaburini. Kisha akamkabidhi bendera, akaondoka na bendera huku akiwa amevaa joho la rangi ya urujuani nyekundu. Akafika mji wa Khaibar na ndipo Marhab aliyekuwa mlinzi wa ngome akatoka na hali amevaa dirizi (deraya) ya rangi ya njano na juu ya kichwa chake kavaa jiwe alilolitoboa mfano wa 73
Page 73
AHLUBAYT NDANI YA TAF. ZA KISUNNI No 1 check Lubumba.qxd
7/1/2011
11:11 AM
Ahlul Bayt Ndani ya Tafsiri za Kisunni yai huku akisema:
“Khaibar imeshajua kwamba hakika mimi ni Marha; mwenye silaha kali na komandoo mzoefu. Pindi moto wa vita unapowashwa, mara hufuma mshale na mara hupiga. Himaya yangu huwa haikaribiwi.” Ali akajitokeza kumkabili naye akisema:
Mimi ndiye ambaye mama yangu alinipa jina la Haidari (Simba) Kama simba pori, shujaa mkali. Nitakuuweni kwa upanga wangu mauwaji ya kuteketeza. Wakapigana mapigo mawili na ndipo Ali akamuwahi na kumpiga pigo moja lililopasua jiwe na dirizi na kukipasua kichwa vipande viwili mpaka upanga ukafika kwenye megego. Na hatimaye aliuteka mji na ushindi ukapatikana mikono mwake. Abu Rafiu huria wa Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) anasema: “Tulitoka pamoja na Ali pindi Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) alipomtuma akiwa amemkabidhi bendera yake. Alipoikaribia ngome walitoka wanangome na akapambana nao. Ndipo mtu mmoja miongoni mwa mayahudi akampiga na hatimaye ngao yake ikadondoka. Ali akang’oa mlango wa ngome na kuugeuza ngao yake, basi uliendelea kuwa mikononi mwake kama ngao na hali yeye akipigana mpaka Mwenyezi Mungu alipompa ushindi. Baada ya kumaliza aliutupa chini, hakika (lau ungekuwepo) ungeniona nikiwa mmoja katika kundi la watu saba tukijitahidi kuugeuza mlango huo lakini hatuwezi.” Kauli ya Mwenyezi Mungu: “Muhammad Mtume wa Mwenyezi Mungu na walio pamoja naye ni imara mbele ya makafiri na wenye kuhurumiana wao kwa wao….” (Sura al-Fat’ha: 29). 74
Page 74
AHLUBAYT NDANI YA TAF. ZA KISUNNI No 1 check Lubumba.qxd
7/1/2011
11:11 AM
Ahlul Bayt Ndani ya Tafsiri za Kisunni Ahmad bin Yazid ad-Daybajiy amesema: Ametusimulia al-Madaniy kutoka kwa Zayd, kutoka kwa Ibnu Umar, amesema: Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) alimwambia Ali: “Ewe Ali! Wewe ni mtu wa Peponi na wafuasi wako ni watu wa Peponi.”
SURA RAHMAN Kauli ya Mwenyezi Mungu:
“Amezikutanisha bahari mbili. Baina yao kuna kizuizi haziingiliani.” (Sura Rahman: 19 - 20). Ametusimulia Abu Hudhuyfa kutoka kwa baba yake, kutoka kwa Sufyan at-Thawri amesema kuhusu “Amezikutanisha bahari mbili. Baina yao kuna kizuizi haziingiliani.” Kwamba ni Fatima na Ali. Na akasema kuhusu kauli yake (s.w.t.): “Katika hizo mbili hutoka lulu na marijani.” (Sura Rahman: 22): kwamba ni Hasan na Husein. Na “Baina yao kuna kizuizi haziingiliani.” Ni Muhammad. Kauli ya Mwenyezi Mungu:
“Karibu tutawakusudieni, enyi vizito viwili.” (Sura Rahman: 31). Mtume (s.a.w.w.) alisema: “Bila shaka mimi ni mwenye kuwaachia vizito viwili kati yenu: Kitabu cha Mwenyezi Mungu na kizazi changu.” Akavijaalia kuwa ni vizito viwili kwa sababa ya utukufu ulivyonao na thamani iliyonavyo.
75
Page 75
AHLUBAYT NDANI YA TAF. ZA KISUNNI No 1 check Lubumba.qxd
7/1/2011
11:11 AM
Ahlul Bayt Ndani ya Tafsiri za Kisunni
SURA MUJADILAH Kauli ya Mwenyezi Mungu:
“Enyi mlioamini! Mnaposema siri na Mtume, basi tangulizeni sadaka kabla ya kumsemeza hayo ni bora kwenu na ni safi sana, na ikiwa hamkupata basi Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa kusamehe, Mwenye kurehemu.” (Sura Mujadilah: 12). Mujahid amesema: “Walikatazwa kusema siri na Mtume (s.a.w.w.) mpaka watoe sadaka. Hakuna aliyeweza kusema naye siri ila Ali bin Abu Talib radhi za Mwenyezi Mungu zimwendee, alitoa sadaka ya dinari. Ndipo (baada ya sadaka hiyo) ikateremka ruhusa (iliyoondoa sharti la sadaka.).” Ali bin Abu Talib radhi za Mwenyezi Mungu zimwendee alisema: “Hakika katika Kitabu cha Mwenyezi Mungu kuna Aya ambayo hakuna yeyote aliyeifanyia kazi kabla yangu, wala hakuna yeyote atakayeifanyia kazi baada yangu, nayo ni: “Enyi mlioamini! Mnaposema siri na Mtume, basi tangulizeni sadaka kabla ya kumsemeza hayo ni bora kwenu na ni safi sana…..” ilifaradhishwa kisha hukumu yake ikafutwa.” Ibnu Umar alisema: “Ali alikuwa na mambo matatu ambayo kuwa nalo moja kati ya hayo ni jambo nilipendalo mno kuliko kuwa na ngamia mwekundu: Kuozwa Fatima, kukabidhiwa bendera Siku ya Khaibar na Aya ya kuongea siri na Mtume.”
76
Page 76
AHLUBAYT NDANI YA TAF. ZA KISUNNI No 1 check Lubumba.qxd
7/1/2011
11:11 AM
Ahlul Bayt Ndani ya Tafsiri za Kisunni
SURA TAGHABUN Kauli ya Mwenyezi Mungu:
“Bila shaka mali zenu na watoto wenu ni jaribio, na kwa Mwenyezi Mungu kuna malipo makubwa.” (Sura Taghabun: 15). Kutoka kwa Husein bin Waqid Kadhi wa Muruwu, amesema: Abdullah bin Barida amenisimulia kutoka kwa baba yake, amesema: “Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) alikuwa akitoa hotuba na ghafla wakaja Hasan na Husein wakiwa wamevaa kanzu mbili nyekundu na hali wakidondoka na kuamka, Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) akateremka toka mimbarini akawafuata na kuwachukua na kuwaweka mapajani mwake juu ya mimbari, kisha akasema: ‘Mwenyezi Mungu amesema kweli. Bila shaka mali zenu na watoto wenu ni jaribio, nilipowaona hawa wawili sikuweza kuvumilia.”
SURA TAHRIM Kauli ya Mwenyezi Mungu: “…..Basi Mwenyezi Mungu ni mlinzi wake, na Jibril na waumini wema na Malaika….” (Sura Tahrim: 4).
Kutoka kwa Muhammad bin Ja’far bin Muhammad bin Ali bin Husein bin Ali bin Abu Talib (a.s.) amesema: “Amenisimulia mtu mmoja mwaminifu akiivusha toka kwa Ali bin Abu Talib (a.s.), amesema: Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) alisema kuhusu kauli yake (s.w.t.): “…na waumini wema…”: ‘Ni Ali bin Abu Talib.’”80 80 Ameiandika Ibnu Hajar al-Haythamiy katika kitabu as-Swawaiqul-Muhriqah Uk. 144. 77
Page 77
AHLUBAYT NDANI YA TAF. ZA KISUNNI No 1 check Lubumba.qxd
7/1/2011
11:11 AM
Ahlul Bayt Ndani ya Tafsiri za Kisunni Kutoka kwa Musa bin Ja’far, kutoka kwa baba yake, kutoka kwa babu zake (a.s.), kutoka kwa Asmau binti Umaysi amesema: “Nilimsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) akisema: ‘Na waumini wema ni Ali bin Abu Talib.’”81 Kauli ya Mwenyezi Mungu:
“Na Mariam binti Imran aliyejilinda tupu yake….” (Sura Tahrim: 12). Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) amesema: “Kati ya wanaume wamekamilika wengi na wala hawajakamilika kati ya wanawake ila wanne: Asia binti Muzahim mke wa Firaun, Mariam binti Imran, Khadija binti Khuwaylid na Fatima binti Muhammad.”
SURA AL-HAQQAH Kauli ya Mwenyezi Mungu:
“Ili tuifanye ukumbusho kwenu, na sikio lisikialo lisikie.” (Sura alHaqqah: 12). Kutoka kwa Abu Hamza at-Thumali amesema: “Amenisimulia Abdullah bin Hasan, amesema: Ilipoteremka Aya hii: “Ili tuifanye ukumbusho kwenu, na sikio lisikialo lisikie.” Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) alisema: ‘’Nilimwomba Mwenyezi Mungu sikio lako alifanye hivyo ewe Ali.’’ Ali akasema: “Baada ya hapo sikuwahi kusahau chochote na wala sikupasa kusahau.”82 81 Ameipokea al-Humawi katika kitabu chake Faraidus-Samtwayni Juz. 1 Uk. 363, Chapa ya Kwanza, Mlango wa 67, Hadithi ya 290. 82 Al-Haskaniy ameiandika katika kitabu chake Shawahidut-Tanziil. 78
Page 78
AHLUBAYT NDANI YA TAF. ZA KISUNNI No 1 check Lubumba.qxd
7/1/2011
11:11 AM
Ahlul Bayt Ndani ya Tafsiri za Kisunni Kutoka kwa Burayda al-Aslamiy amesema: Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) alimwambia Ali: “Hakika Mwenyezi Mungu Mtukufu ameniamuru nikusogeze karibu nisikutenge mbali, na nikuelimishe nawe usikie vilivyo. Na Mwenyezi Mungu amehakikisha unasikia vilivyo.”
SURA AL-MAARIJI Kauli ya Mwenyezi Mungu:
“Muulizaji aliuliza juu ya adhabu itakayotokea. Juu ya makafiri, hapana awezaye kuizuia.” (Sura al-Maariji: 1 - 2). Sufyan bin Uyayna aliulizwa kuhusu kauli yake (s.w.t.): “Muulizaji aliuliza” iliteremka kumhusu nani? Akasema: “Umeniuliza suala ambalo hakuna aliyeniuliza kabla yako. Baba yangu alinisimulia kutoka kwa Ja’far bin Muhammad kutoka kwa baba zake, alisema: Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) alipofika Ghadir Khum aliwaita watu wakakusanyika. Akaunyanyua mkono wa Ali na kusema: “Ambaye mimi nina mamlaka juu yake basi huyu Ali ni mwenye mamlaka juu yake.” Habari hizo zikazagaa na kuenea miji mbalimbali, ndipo zikamfikia alHarith bin Nuuman al-Fihriy. Akaja kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) akiwa amepanda ngamia wake. Alipofika Abtahu aliteremka na kumfunga ngamia wake kisha akamfuata Mtume katikati ya kundi la masahaba zake. Akasema: “Ewe Muhammad! Umetuamrisha tushahidilie kwamba hapana Mungu wa haki ila Allah na kwamba wewe ni Mtume wa Allah, tumekubali hilo kutoka kwako. Umetuamuru tuswali Swala tano tumekubali hilo kutoka kwako. Umetuamrisha tutoe Zaka tumekubali. Umetuamrisha kuhiji tumekubali. Umetuamrisha tufunge mwezi mzima tumekubali. Kisha haujatosheka kwa haya yote mpaka umenyanyua mikono ya binamu yako na kumfanya bora juu yetu ukasema: ‘Ambaye mimi nina mamlaka juu yake basi huyu Ali ni mwenye mamlaka juu yake.’ Je jambo hili ni kutoka kwako binafsi au ni kutoka kwa Mwenyezi 79
Page 79
AHLUBAYT NDANI YA TAF. ZA KISUNNI No 1 check Lubumba.qxd
7/1/2011
11:11 AM
Ahlul Bayt Ndani ya Tafsiri za Kisunni Mungu?” Mtume akasema: “Naapa kwa yule ambaye hapana Mungu ila Yeye, hakika hili ni kutoka kwa Mwenyezi Mungu. Al-Harith akageuka na kuelekea kwenye mnyama wake huku akisema: “Ewe Mwenyezi Mungu! Ikiwa ayasemayo ni haki basi tuteremshie mvua ya mawe kutoka mbinguni na utuletee adhabu iumizayo.” Kabla hajamfikia mnyama wake Mwenyezi Mungu akamwangushia jiwe utosini na likatokea nyumani kwake akadondoka hapo hapo na kuuwawa. Mwenyezi Mungu akateremsha: “Muulizaji aliuliza juu ya adhabu itakayotokea. Juu ya makafiri, hapana awezaye kuizuia.”83
SURA AL-MUDTHIR Kauli ya Mwenyezi Mungu:
“Kila nafsi itafungika kwa ilizozichuma. Isipokuwa watu wa kheri.” (Sura al-Mudathir: 38 - 39). Kutoka kwa Abu Hamza at-Thumali kutoka kwa Abu Ja’far al-Baqir (a.s.) amesema: “Sisi na wafuasi wetu ndio watu wa kheri.”84
83 Ameipokea Ibnu Batrik katika sura ya pili ya kitabu chake Khaswaisul-Wahyi al-Mubin Uk. 31, Chapa ya Kwanza. 84 Al-Haskaniy ameiandika katika kitabu chake Shawahidut-Tanziil Juz. 2, Uk. 388, Hadithi ya 1038.
80
Page 80
AHLUBAYT NDANI YA TAF. ZA KISUNNI No 1 check Lubumba.qxd
7/1/2011
11:11 AM
Ahlul Bayt Ndani ya Tafsiri za Kisunni
SURA AL-INSAN Kauli ya Mwenyezi Mungu:
“Wanatimiza nadhiri na wanaiogopa siku ambayo shari yake itaenea. Na huwalisha chakula masikini na yatima na mfungwa hali ya kuwa wanakipenda. Tunakulisheni kwa ajili ya radhi za Mwenyezi Mungu tu, hatutaki kwenu malipo wala shukurani. Hakika sisi tunaogopa kutoka kwa Mola wetu siku yenye shida na taabu. Basi Mwenyezi Mungu atawalinda katika shari ya siku hiyo na kuwakutanisha na neema na furaha. Na atawapa mabustani na hariri kwa sababu walisubiri. Humo wataegemea viti vya enzi humo hawataona jua wala baridi.” (Sura al-Insan: 7 - 13). Alitusimulia huko Basara Abul-Hasan Muhammad bin Ahmad bin Suhayli bin Ali bin Mahran al-Bahiliy, alisema: Alitusimulia Abu Mas’ud Abdurahman bin Fahri bin Hilal, alisema: Alitusimulia al-Qasim bin Yahya kutoka kwa Abu Ali al-Anbariy, kutoka kwa Muhammad bin as-Saib, kutoka kwa Abu Salih, kutoka kwa Ibnu Abbas. 81
Page 81
AHLUBAYT NDANI YA TAF. ZA KISUNNI No 1 check Lubumba.qxd
7/1/2011
11:11 AM
Ahlul Bayt Ndani ya Tafsiri za Kisunni Abul-Hasan bin Mahran amesema: Na alinisimulia Muhammad Zakariya al-Basriyu, alisema: Amenisimulia Said bin Waqid al-Mazniy, alisema: Alitusimulia al-Qasim bin Bahram kutoka kwa Laythu, kutoka kwa Mujahid kutoka kwa Ibnu Abbas kuhusu kauli yake (s.w.t.): “Wanatimiza nadhiri na wanaiogopa siku ambayo shari yake itaenea.” Alisema: Hasan na Husein walipatwa na maradhi, babu yao Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) alikwenda kuwaona akiwa pamoja na Abu Bakr na Umar na waarabu kwa jumla walikwenda kuwaona. Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) akasema: “Ewe Abal-Hasan ni vizuri lau ukiweka nadhiri kwa ajili ya wanao. Na kila nadhiri isiyotimia haina wajibu wowote.” Ali akasema: “Ikiwa wanangu watapona ugonjwa walionao nitafunga siku tatu kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu.” Vijana wawili hao wakapata afya njema na hali nyumbani kwa aali Muhammad hawana kitu si kichache wala kingi. Ali akaenda kwa Simon bin Jaba mtu wa Khaibari, naye alikuwa ni Myahudi, akakopa toka kwake pishi tatu za ngano. Na katika Hadithi ya al-Mazniy ni kwamba: “Ali alikwenda kuomba kuchambua pamba kwa jirani yake myahudi aliyekuwa akiitwa Simon Jaba. Alimwambia: “Je unaweza kunipa pamba akuchambulie binti Muhammad kwa malipo ya pishi tatu za ngano?” Akasema: Ndio. Akampa naye akaja na pamba na ngano. Akamweleza hayo Fatima naye akakubali na kutii. Wamesema: “Fatima akachukua pishi moja akatwanga na kuoka mikate mitano, kila mmoja mkate mmoja. Ali alipomaliza kuswali pamoja na Mtume swala ya Maghrib alikuja nyumbani na kikawekwa chakula mbele yake, mara masikini akafika mlangoni kwao akagonga akisema: “Assalam Alaykum enyi watu wa nyumba ya Muhammad, mimi ni maskini katika watoto wa kiislamu nipeni chakula Mwenyezi Mungu atakupeni chakula cha Peponi.”
82
Page 82
AHLUBAYT NDANI YA TAF. ZA KISUNNI No 1 check Lubumba.qxd
7/1/2011
11:11 AM
Ahlul Bayt Ndani ya Tafsiri za Kisunni Ali akamsika, akasoma shairi:
“Fatima mwenye ubora na yakini, ewe binti wa mbora kuliko watu wote. Hivi humwoni mkata masikini amesimama mlangoni, akitoa sauti ya uchungu. Akimshitakia Mwenyezi Mungu na akinyenyekea. Analalamika kwetu kwamba ni mwenye njaa na mwenye huzuni. Kila mtu ni rehani wa chumo lake na mwenye kutenda kheri atabainika. Ahadi yake ni Pepo ya juu, aliyoiharamisha Mwenyezi Mungu kwa bakhili. Na bakhili ana kisimamo dhalili, Mola Mlezi atamtupa gerezani (motoni). Kinywaji chake humo ni maji ya moto na usaha.� Naye Fatima akasoma shairi: ?????? ???? ???? ???? ????? ?? ??? ?? ???? ??? ???????? ??????? ?? ?????? ???? ?????? ????????? ??? ?????? ??????? ???? ??? ?????? ?? ???????? ?? ????? ???????? ????????? ??????? ??????? ??? ?????? Amri yako kwangu ewe binamu yangu ni yenye kutekelezwa. Sina haja na uduni wala udhalili. Umenyonyeshwa katika kheri maziwa ya ngamia, 83
Page 83
AHLUBAYT NDANI YA TAF. ZA KISUNNI No 1 check Lubumba.qxd
7/1/2011
11:11 AM
Ahlul Bayt Ndani ya Tafsiri za Kisunni namlisha wala sisubiri muda. Nataraji nitakapowashibisha wenye njaa, nitaungana na wabora na jamaa. Na nitaingia Peponi na hali nikiwa na uombezi. Wakampa chakula na wakashinda mchana kutwa na usiku kucha bila kuonja chochote ila maji. Ilipofika siku ya pili Fatima akachukua pishi akatwanga na kuoka mikate. Ali alipomaliza kuswali pamoja na Mtume (s.a.w.w.) alikuja nyumbani na kikawekwa chakula mbele yao, mara akafika mlangoni kwao yatima toka katika watoto wa muhajirana ambaye baba yake alikufa kishahidi siku ya Aqabah, akagonga akisema: “Nipeni chakula Mwenyezi Mungu atakupeni chakula cha Peponi.” Ali akamsikia, akasoma shairi: ????? ???? ??????? ??????? ??? ????? ??? ????????? ??? ??? ????? ??? ??????? ??? ????? ?????? ???? ???? ?????? ?? ????? ??????? ?? ????? ?????? ??? ??????? ????? ?? ?????? ??? ??????? ?????? ??????? ???????? Fatima binti wa Sayyid karimu. Binti wa Nabii asiye muovu. Mwenyezi Mungu amemleta yatima. Atakayewahurumia watu naye atahurumiwa. Ahadi yake ni katika Pepo yenye neema. Bila shaka Pepo imeharamishwa juu ya muovu. (Usipompa) Mikono yako itakuwa katika moto wenye kuunguza, kinywaji chake ni usaha na maji ya moto.”
84
Page 84
AHLUBAYT NDANI YA TAF. ZA KISUNNI No 1 check Lubumba.qxd
7/1/2011
11:11 AM
Ahlul Bayt Ndani ya Tafsiri za Kisunni Fatima naye akasoma shairi akisema: ???? ?????? ??? ????? ????? ????? ??? ????? ?????? ?????? ????? ?????? ???????? ????? ?? ??????? ?????? ????? ???????? ?????? ??????? ?? ?????? ???? ?? ?????? ??? ????? ??? ????? ?????? ????????? ?????? ????? ?? ???????? Hakika mimi nampa wala sijali, namtanguliza Mwenyezi Mungu kabla ya familia yangu. Wameshinda na njaa na wao ni wanangu, mdogo wao atauwawa katika vita. Huko Karbala atauwawa kwa njama, ole wake na adhabu yule mwenye kumuuwa. Moto utamvuta mpaka chini, na hali mikononi mwake kafungwa pingu na minyororo. Kizuizi juu ya kizuizi. Wakampa chakula na wakashinda siku ya pili mchana kutwa na usiku kucha bila kuonja chochote ila maji. Ilipofika siku ya tatu Fatima akachukua pishi lililobaki akatwanga na kuoka mikate. Ali alipomaliza kuswali pamoja na Mtume (s.a.w.w.) alikuja nyumbani na kikawekwa chakula mbele yao, mara mfungwa wa kivita akafika mlangoni kwao akagonga akisema: “Assalam Alaykum enyi watu wa nyumba ya Muhammad, mnatuteka na kutufunga na wala hamtupi chakula! Nipeni chakula mimi ni mateka wa Muhammad.� Ali akamsikia, akasoma shairi:
????? ?? ???? ?????? ????? ???? ????? ????? ?????? ??? ????? ?????? ??????? ?????? ?? ????? ?????? 85
Page 85
AHLUBAYT NDANI YA TAF. ZA KISUNNI No 1 check Lubumba.qxd
7/1/2011
11:11 AM
Ahlul Bayt Ndani ya Tafsiri za Kisunni Ewe binti wa Mtume Ahmad. Binti wa Mtume bwana mtiiwa. Huyu hapa mfungwa wa Mtume mwongozaji. Amefungwa pingu yake na kizuizi. Anatulalamikia njaa imembana. Atakayelisha chakula leo atakikuta kesho. Mbele ya Aliye juu Mmoja mwenye kupwekeshwa. Wanayoyalima wakulima watayavuna. Mlishe bila masimango yachafuayo. Ili ulipwe yale yasiyokwisha. Fatima naye akasoma shairi akisema:
Kati ya kile kilicholetwa hakijabaki ila pishi moja Bila shaka kitanga changu kimeondoka pamoja na mkono85 wangu. Wallahi wanangu wana njaa, ewe Mola usiuache (mkono) upotee. Hutenda wema kwa kuanza, yule ambaye ni mpana karimu mwenye uwezo. Na juu ya kichwa changu sina hijabu, ila hijabu iliyofumwa kwa kamba. Wakampa chakula na wakashinda siku ya tatu mchana kutwa na usiku kucha bila kuonja chochote ila maji. Ilipofika siku ya nne wakiwa tayari wameshatimiza nadhiri yao, Ali alimshika Hasan mkono wa kulia na Husein mkono wa kushoto na kwenda nao kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) na hali wao wawili wakitetemeka kama vifaranga kutokana na ukali wa njaa. Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) alipowatizama alisema: “Ewe Abal-Hasan! 85 Mkono na Kitanga hapa ni kinaya ya Pishi la Kwanza na la Pili. Hivyo anaomba pishi hizo zisiende na kupotea bure bali ziambatane na malipo mema. – Mtarjumi. 86
Page 86
AHLUBAYT NDANI YA TAF. ZA KISUNNI No 1 check Lubumba.qxd
7/1/2011
11:11 AM
Ahlul Bayt Ndani ya Tafsiri za Kisunni Hali niionayo yaniumiza mno twendeni kwa binti yangu Fatima.” Wakaenda kwake wakamkuta akiwa mihrabuni kwake na hali tumbo lake limeshikana na mgongo wake na macho yake yamebadilika kutokana na ukali wa njaa. Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) alipomtazama na kutambua njaa aliyonayo kupitia uso wake, alisema: “Ee Mwenyezi Mungu nakuomba msaada, Ahlul-Baiti wa Muhammad wanakufa kwa njaa.” Jibril (a.s.) akateremka na kusema: “Ewe Muhammad pokea, Mwenyezi Mungu anakupa pongezi kwa kitendo cha watu wa nyumba yako.” Mtume akasema: “Nichukue nini ewe Jibril?” Jibril (a.s.) akamsomea:
87
Page 87
AHLUBAYT NDANI YA TAF. ZA KISUNNI No 1 check Lubumba.qxd
7/1/2011
11:11 AM
Ahlul Bayt Ndani ya Tafsiri za Kisunni “Hakika ulimfikia mtu wakati fulani wa zama ambapo hakuwa kitu kinachotajwa. Kwa hakika tulimuumba mtu kutokana na mbegu ya uhai iliyochanganyika, tunamjaribu, hivyo tukamfanya ni mwenye kusikia mwenye kuona. Hakika sisi tumemuongoza njia awe mwenye kushukuru au awe mwenye kukufuru. Hakika sisi tumewaandalia makafiri minyororo na pingu na moto uwakao. Hakika watawa watakunywa katika kikombe kilichochanganyika na kafuri. Chemchemu watakayoinywa waja wa Mwenyezi Mungu, wataitiririsha mtiririko. Wanatimiza nadhiri na wanaiogopa siku ambayo shari yake itaenea. Na huwalisha chakula masikini na yatima na mfungwa hali ya kuwa wanakipenda. Tunakulisheni kwa ajili ya radhi za Mwenyezi Mungu tu, hatutaki kwenu malipo wala shukurani. Hakika sisi tunaogopa kutoka kwa Mola wetu siku yenye shida na taabu. Basi Mwenyezi Mungu atawalinda katika shari ya siku hiyo na kuwakutanisha na neema na furaha. Na atawapa mabustani na hariri kwa sababu walisubiri. Humo wataegemea viti vya enzi humo hawataona jua wala baridi.” (Sura al-Insan: 1-13) – mpaka mwisho wa Sura.86 Qatadah bin Mahran al-Bahiliy amesema katika Hadithi hii kwamba: “Mtume akaharakisha mpaka akaingia kwa Fatima (a.s.). alipoiona hali yao waliyonayo aliwakumbatia na kuanza kulia, kisha akawaambia: “Naona nyinyi mna siku tatu na mimi ni mwenye kughafilika nanyi.” Ndipo Jibril (a.s.) akateremka na Aya hizi: Hakika watawa watakunywa katika kikombe kilichochanganyika na kafuri. Chemchemu watakayoinywa waja wa Mwenyezi Mungu, wataitiririsha mtiririko. Akasema: “Hiyo ni chemchemu iliyopo katika nyumba ya Mtume (s.a.w.w.) inatiririka kwa kusambaa kwenye nyumba za Manabii na waumini. 86 Al-Haskani ameipokea kwa mhtasari kwa matamshi mbalimbali katika Hadithi ishirini, kuanzia Hadithi ya 1042 mpaka Hadithi ya 1061, katika kitabu chake Shawahidut-Tanziil. Sheikh as-Swaduq amepokea Hadithi 11 katika al-Majlis na Hadithi 44 katika Amalis-Swaduq Uk. 212. Ibnu al-Batriq ameipokea kwa njia yake kutoka kwa at-Thaalabi katika sura ya 12 ya kitabu chake Khaswaisul-Wahyi al-Mubin Uk. 100. Na katika kitabu chake kingine Al-Awasit katika sura ya 36 Hadithi ya 570 amepokea kutoka kwenye kitabu al-Umdat Uk. 180. Na ameipokea al-Khawarazimiy kwa njia yake kutoka kwa at-Thaalabi katika sura ya 17 ya kitabu Manaqibu Amiril-Muuminina Uk. 188, Chapa ya Al-Gharri. 88
Page 88
AHLUBAYT NDANI YA TAF. ZA KISUNNI No 1 check Lubumba.qxd
7/1/2011
11:11 AM
Ahlul Bayt Ndani ya Tafsiri za Kisunni Wanatimiza nadhiri: Yaani Ali, Hasan, Husein na mtumishi wao Fidha. Wanaiogopa siku ambayo shari yake itaenea. Na huwalisha chakula masikini na yatima na mfungwa hali ya kuwa wanakipenda. Na hali wana haja nacho lakini wanmpa kipaumbele mwingine. Masikini: Ni miongoni mwa masikini wa kiislamu. Yatima: Ni miongoni mwa mayatima wa kiislamu. Mfungwa wa kivita: Ni miongoni mwa mateka toka kwa Mushrikina. Na wanapowapa chakula husema: Tunakulisheni kwa ajili ya radhi za Mwenyezi Mungu tu, hatutaki kwenu malipo wala shukurani. Hakika sisi tunaogopa kutoka kwa Mola wetu siku yenye shida na taabu. Wallahi hawakulisema hili kwa ndimi zao bali kwa dhamira zao ndani ya nyoyo zao. Ndipo Mwenyezi Mungu akafichua dhamira zao kwamba wanasema: “Hatutaki malipo wala shukurani kutoka kwenu msije baadae kutusimbulia. Lakini sisi tumekupeni kwa ajili ya Mwenyezi Mungu kwa ajili ya kutaka thawabu zake.” Mwenyezi Mungu akasema: Basi Mwenyezi Mungu atawalinda katika shari ya siku hiyo na kuwakutanisha na neema:- Katika sura zao. Na furaha:- Katika nyoyo zao. Na atawapa mabustani:- Watakayoishi humo. Na hariri kwa sababu walisubiri:- Watakayovaa na kutandika. Humo wataegemea viti vya enzi humo hawataona jua wala baridi.” Ibnu Abbas amesema: “Pindi watu wa Peponi watakapokuwa peponi ghafla wataona mwanga kama mwanga wa jua na Pepo imeangazwa kwa mwanga huo. Watu wa Peponi watasema: Ewe Ridhwan, Mola wetu Mtukufu amesema: “Hawataona jua wala baridi.” Ridhwan atawaambia: “Hili si Jua wala si Mwezi, lakini huyu ni Fatima na Ali wamecheka, kicheko ambacho kimeiangazia Pepo kutokana na nuru ya kicheko chao.” Na kwa ajili ya hao wawili Mwenyezi Mungu aliteremsha: “Hakika ulimfikia mtu wakati fulani wa zama ambapo hakuwa kitu kinachotajwa.” Mpaka “Na juhudi yenu imethaminiwa.”87 87 Kuanzia Aya ya Kwanza mpaka ya Ishirini na Mbili. – Mtarjumi. 89
Page 89
AHLUBAYT NDANI YA TAF. ZA KISUNNI No 1 check Lubumba.qxd
7/1/2011
11:11 AM
Ahlul Bayt Ndani ya Tafsiri za Kisunni At-Thaalabiy anasema: Nina shairi kuhusu hilo:
Mimi ni mwenye kumtawalisha, kijana ambaye kwa ajili yake, aliteremshiwa Sura Hal Ata.
SURA AL-BALAD Kauli ya Mwenyezi Mungu: “Je, anadhani kuwa hapana yeyote anayemuona?” (Sura al-Balad: 7). Kutoka kwa Ibnu Abbas amesema: Mtume wa Mwenyezi Mungu alisema: “Nyayo ya mtu haitonyanyuka Siku ya Kiyama mpaka aulizwe kuhusu mambo mane: Umri wake aliutumia katika nini. Mali yake aliichumaje na aliitumiaje. Kazi yake, alifanya nini katika kazi yake. Na kuhusu mapenzi yetu watu wa nyumba ya Mtume.”
SURA AD-DHUHA Kauli ya Mwenyezi Mungu: “Na Mola wako hivi karibuni atakupa na utaridhika.” (Sura ad-Dhuha: 5). Ja’far bin Muhammad amesema: Mtume wa Mwenyezi Mungu aliingia kwa Fatima akiwa amejifunika kishamia kilichotokana na pamba (kizito) na hali akitwanga kwa mkono wake na akimnyonyesha mwanae. Macho ya Mtume wa Mwenyezi Mungu yakadondosha machozi baada tu yakumtazama. Akasema (s.a.w.w.): “Ewe mwanangu mpemdwa! Yaanze machungu ya dunia uje kupata utamu wa Akhera. Bila shaka Mwenyezi Mungu ameniteremshia: “Na Mola wako hivi karibuni atakupa na utaridhika.”88 88 Nimemaliza kuitafiti Tafsiri hii siku ya ishirini na nne ya Mfungo Tatu, siku ya Mubahala, Mwaka 1425 huko katika Jiji la Qum Takatifu. 90
Page 90
AHLUBAYT NDANI YA TAF. ZA KISUNNI No 1 check Lubumba.qxd
7/1/2011
11:11 AM
Ahlul Bayt Ndani ya Tafsiri za Kisunni
ORODHA YA VITABU VILIVYO CHAPISHWA NA AL-ITRAH FOUNDATION 1. 2. 3. 4. 5. 6. 7. 8. 9. 10. 11. 12. 13. 14. 15. 16. 17. 18. 19. 20. 21. 22. 23. 24. 25. 26.
Qur'an Al-Kariim - Tafsir Al-Kashif Juzuu ya kwanza mpaka Thalathini Uharamisho wa Riba Uharamisho wa uwongo Juzuu ya Kwanza Uharamisho wa uwongo Juzuu ya Pili Hekaya za Bahlul Muhanga wa Imamu Husein (A.S.) Mikingamo iliyomzunguka Imamu Ali (A.S.) Hijab vazi Bora Ukweli wa Shia Ithnaashari Madhambi Makuu Mbingu imenikirimu Abdallah Ibn Saba Khadijatul Kubra Utumwa Umakini katika Swala Misingi ya Maarifa Kanuni za Ndoa na maadili ya Familia Bilal wa Afrika Abudharr Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu Salman Farsi Ammar Yasir Qur'an na Hadithi Elimu ya Nafsi Yajue Madhehebu ya Shia Ukusanyaji na Uhifadhi wa Qur'an Tukufu 91
Page 91
AHLUBAYT NDANI YA TAF. ZA KISUNNI No 1 check Lubumba.qxd
7/1/2011
11:11 AM
Ahlul Bayt Ndani ya Tafsiri za Kisunni 27. 28. 29. 30. 31. 32. 33. 34. 35. 36. 37. 38. 39 40. 41. 42. 43. 44. 45. 46. 47. 48. 49. 50. 51. 52. 53. 54. 55. 56. 57.
Al-Wahda Ponyo kutoka katika Qur'an. Uislamu mfumo kamili wa maisha ya kijamii Mashukio ya Akhera Al Amali Dua Indal Ahlul Bayt Udhuu kwa mujibu wa Kitabu na Sunna. Haki za wanawake katika Uislamu Mwenyeezi Mungu na sifa zake Amateka Na Aba'Khalifa Nafasi za Ahlul Bayt (a.s) Adhana. Upendo katika Ukristo na Uislamu Nyuma yaho naje kuyoboka Amavu n’amavuko by’ubushiya Kupaka juu ya khofu Kukusanya swala mbili Bismillah ni sehemu ya Qur’ani na husomwa kwa Jahara Kuwaongoza vijana wa kizazi kipya Kusujudu juu ya udongo Kusheherekea Maulidi Ya Mtume (s) Tarawehe Malumbano baina ya Sunni na Shia Kupunguza Swala safarini Kufungua safarini Umaasumu wa Manabii Qur’an inatoa changamoto as-Salaatu Khayrun Mina -'n Nawm Uadilifu wa Masahaba Dua e Kumayl Sauti Ya Uadilifu wa Binadamu 92
Page 92
AHLUBAYT NDANI YA TAF. ZA KISUNNI No 1 check Lubumba.qxd
7/1/2011
11:11 AM
Ahlul Bayt Ndani ya Tafsiri za Kisunni 58. 59. 60. 61. 62. 63. 64. 65. 66. 67. 68. 69. 70. 71. 72. 73. 74. 75. 76. 77. 78. 79. 80. 81. 82. 83. 84. 85. 86.
Umaasumu wa Mitume - Faida Zake Na Lengo Lake Umaasumu wa Mitume - Majibu Ya Aya Zenye Utata Umaasumu wa Mitume - Umaasumu wa Mitume Muhammad (s) Nahju’l-Balaghah - Juzuu ya Kwanza Nahju’l-Balaghah - Juzuu ya Pili Kuzuru Makaburi Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Kwanza Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Pili Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Tatu Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Nne Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Tano Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Sita Tujifunze Misingi Ya Dini Sala ni Nguzo ya Dini Mikesha Ya Peshawar Malezi Ya Mtoto Katika Uislamu Ubora wa Imam 'Ali Juu ya Maswahaba Na Ushia ndio njia iliyonyooka Hukumu za Kifikihi zinazowahusu Wanawake Liqaa-u-llaah Muhammad (s) Mtume wa Allah Amani na Jihadi Katika Uislamu Uislamu Ulienea Vipi? Uadilifu, Amani na Mtume Muhammad (s) Mitala na Ndoa za Mtume Muhammad (s) Urejeo (al-Raja’a ) Mazingira Utokezo (al - Badau) Sadaka yenye kuendelea Msahafu wa Imam Ali 93
Page 93
AHLUBAYT NDANI YA TAF. ZA KISUNNI No 1 check Lubumba.qxd
7/1/2011
11:11 AM
Ahlul Bayt Ndani ya Tafsiri za Kisunni 87. 88. 89. 90. 91. 92. 93. 94. 95.
Uislamu na dhana Mtoto mwema Adabu za Sokoni Johari za hekima kwa vijana Maalimul Madrasatain Sehemu ya Kwanza Maalimul Madrasatain Sehemu ya Pili Maalimul Madrasatain Sehemu ya Tatu Tawasali Imam Mahdi katika Usunni na Ushia
96.
Maana ya laana na kutukana katika Qur’ani Tukufu
97.
Hukumu ya kujenga juu ya makaburi
98.
Swala ya maiti na kumlilia maiti
99.
Shiya na Hadithi (kinyarwanda)
100.
Mariamu, Yesu na Ukristo kwa mtazamo wa Kiislamu
101.
Hadithi ya Thaqalain
102
Fatima al-Zahra
103.
Tabaruku
104.
Sunan an-Nabii
105.
Historia na sera ya viongozi wema (Sehemu ya Kwanza)
106.
Historia na sera ya viongozi wema (Sehemu ya Pili)
107.
Mahdi katika sunna
108.
Kusalia Nabii (s.a.w)
109.
Ujumbe -Sehemu ya Kwanza
110.
Ujumbe - Sehemu ya Pili
111.
Ujumbe - Sehemu ya Tatu
112.
Ujumbe - Sehemu ya Nne
113.
Ngano ya kwamba Qur’ani imebadilishwa 94
Page 94
AHLUBAYT NDANI YA TAF. ZA KISUNNI No 1 check Lubumba.qxd
7/1/2011
Ahlul Bayt Ndani ya Tafsiri za Kisunni 114.
Iduwa ya Kumayili
115.
Maarifa ya Kiislamu.
116.
Ukweli uliopotea sehemu ya Kwanza
117.
Ukweli uliopotea sehemu ya Pili
118.
Ukweli uliopotea sehemu ya Tatu
119.
Ukweli uliopotea sehmu ya Nne
120.
Ukweli uliopotea sehmu ya Tano
121.
Johari zenye hekima kwa vijana
122.
Safari ya kuifuata Nuru
123.
Idil Ghadiri
124.
Myahudi wa Kimataifa
125.
Kuanzia ndoa hadi kuwa Wazazi
126.
Visa vya kweli sehemu ya Kwanza
127.
Visa vya kweli sehemu ya Pili
128.
Muhadhara wa Maulamaa
129.
Mwanadamu na Mustakabali wake
130.
Imam Ali binamu ya Mtume Sehemu ya Kwanza
131.
Imam Ali binamu ya Mtume Sehemu ya Pili
132.
Khairul Bariyyah
133.
Uislamu na mafunzo ya kimalezi
134.
Vijana ni Hazina ya Uislamu.
135.
Yafaayo kijamii
136.
Kusoma sura zenye Sijda ya wajibu
137.
Taqiyya
138.
Vikao vya furaha
139.
Shia asema haya Sunni asema haya Wewe wasemaje? 95
11:11 AM
Page 95
AHLUBAYT NDANI YA TAF. ZA KISUNNI No 1 check Lubumba.qxd
7/1/2011
11:11 AM
Ahlul Bayt Ndani ya Tafsiri za Kisunni 140.
Uislamu na Mazingatio Sehemu ya Kwanza
141.
Uislamu na Mazingatio Sehemu ya Pili
142.
Azadari-Kuhuzunika na Kuomboleza
143.
Sunna katika Kitabu Fiqhi al-Sunnah
144.
Mtazamo Mpya - Wanawake katika Uislamu
145.
Kuonekana kwa Allah
146.
Tabia njema kwa Mujibu wa Ahlul-Bayt (Sehemu ya Kwanza)
147.
Tabia njema kwa Mujibu wa Ahlul-Bayt (Sehemu ya Pili)
148.
Ndugu na Jirani
149.
Ushia ndani ya Usunni
150.
Maswali na Majibu
151.
Mafunzo ya hukmu za ibada
152.
Ahlul Bayt ndani ya tafsiri za Kisusunni No 1
153
Ahlul Bayt ndani ya tafsiri za Kisusunni No 2
154.
Ahlul Bayt ndani ya tafsiri za Kisusunni No 3
155.
Abu Huraira
156.
Kati ya Alama kuu za dini Swala ya Jamaa. na Adabu za Msikiti na Taratibu zake.
157.
Uadilifu katika Uislamu
96
Page 96
AHLUBAYT NDANI YA TAF. ZA KISUNNI No 1 check Lubumba.qxd
7/1/2011
11:11 AM
Ahlul Bayt Ndani ya Tafsiri za Kisunni
BACK COVER Ahlul Bayt, yaani Watu wa Nyumba ya Mtume Muhammad SAW ni viongozi ambao Mtume alituusia tuwafuate. Katika hotuba yake ndefu na maarufu aliyoitoa pale Ghadir Khumm katika msafara wake wa kurejea kutoka Hija yake ya mwisho, Mtukufu Mtume SAW alisema haya mbele ya masahaba na mahujaji zaidi ya laki moja: “...Nakuachieni vitu viwili vizito: Qur’ani na Ahlul Bayt wangu. Viwili hivyo havitaachana mpaka vinifikie katika [hodhi ya] Kawthar. Nawausia juu ya Ahlul Bayt wangu! Angalieni jinsi mtakavyojihusisha nao. Kama mkishikamana na viwili hivi hamtapotea kamwe...” (kwa maelezo zaidi soma kitabu cha al-Ghadir) Lakini bahati mbaya sana sio Waislamu wote wanaowafuata Ahlul Bayt AS pamoja na kwamba wanavyuoni wa madhehebu zote wameandika habari zao katika vitabu vyao na kuonesha kwamba hawa ni viongozi wa Umma huu wa Kiislamu. Mwandishi wa kitabu hiki anajaribu kuthibitisha hilo kwa kutoa rejea mbalimbali kutoka vitabu maarufu vya wanavyuoni wa Kisunni. Kimetolewa na kuchapishwa na: Alitrah Foundation S.L.P. 19701 Dar es Salaam, Tanzania Simu: +255 22 2110640 Simu/Nukushi: +255 22 2127555 Barua Pepe: alitrah@raha.com Tovuti: www.alitrah.org Katika mtandao: www.alitrah.info
97
Page 97