Ahlulbayt ndani ya tafsiri za kisunni (sehemu ya pili)

Page 1

Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 2 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

11:14 AM

AHLUL BAYT NDANI YA TAFSIR ZA KISUNNI SEHEMU YA PILI KWA MUJIBU WA BAGHAWI, RAAZI, ZAMAKHSHARI, BAYDHAWI NA QURTUBI Kimeandikwa na: Sheikh Nizar al - Hasan

Kimetarjumiwa na: Hemedi Lubumba (Abu Batul)

Page A


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 2 Check Lubumba.qxd

B

7/1/2011

11:14 AM

Page B


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 2 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

ŠHaki ya kunakili imehifadhiwa na: AL-ITRAH FOUNDATION ISBN: 978 - 9987 - 512 - 95 - 9 Kimeandikwa na: Sheikh Nizar al - Hasan Kimetarjumiwa na: Hemedi Lubumba (Abu Batul) Kimehaririwa na: Ust. A. Mohamed Kimepangwa katika Kompyuta na: Hajat Pili Rajab Toleo la kwanza:Januari,2011 Nakala: 1000 Kimetolewa na kuchapishwa na: Alitrah Foundation S.L.P. 19701 Dar es Salaam, Tanzania Simu: +255 22 2110640 Simu/Nukushi: +255 22 2127555 Barua Pepe: alitrah@raha.com Tovuti: www.alitrah.org Katika mtandao: www.alitrah.info

11:14 AM

Page C


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 2 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

11:14 AM

YALIYOMO Utangulizi..........................................................................................2 Ahlul Bayt (a.s) ndani ya Tafsir ya Al-Baghawi, inayoitwa Maalimut -Tanziil...............................................................................................8 Ahlul Bayt (a.s) ndani ya Tafsir ya Zamakhshari, inayoitwa AlKashafu Fii haqaiqit-Taawiil...........................................................28 Ahlul - Bayt (a.s.) ndani ya Tafsir ya Razi, inayoitwa At - tafsirul Alkabir au Mafatihul Ghaybi...............................................................41 Ahlul Bayt (a.s) ndani ya Tafsiri ya Al-Baydhawi, inayoitwa Anwarut Tanziil Waaasratut-Taawil................................................62 Ahlul Bayt (a.s) ndani ya Tafsiri ya al-Qurtubi, inayoitwa AlJamiuliahkamil - Qur’ani................................................................69

Page D


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 2 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

11:14 AM

Ahlul Bayt ndani ya Tafsiri za Kisunni No.2

NENO LA MCHAPISHAJI Kitabu kilichoko mikononi mwako ni tarjuma ya kitabu cha Kiarabu kiitwacho, Ahlu ‘l-Bayti Fi Tafasiri Ahli ‘s-Sunnah kilichoandikwa na Sheikh Nazri Hasan. Sisi tumekiita, Ahlul Bayt Ndani ya Tafsiri za Kisunni. Hii ni sehemu ya pili inayochambua tafsiri za wanavyuoni wakubwa wa Kisunni – Baghawi, Zamakhshari, Raazi, Baydhawi na Qurtubi. Ahlul Bayt, yaani Watu wa Nyumba ya Mtume Muhammad SAW ni viongozi ambao Mtume alituusia tuwafuate. Katika hotuba yake ndefu na maarufu aliyoitoa pale Ghadir Khumm katika msafara wake wa kurejea kutoka Hija yake ya mwisho, Mtukufu Mtume SAW alisema haya mbele ya masahaba na mahujaji zaidi ya laki moja: “...Nakuachieni vitu viwili vizito: Qur’ani na Ahlul Bayt wangu. Viwili hivyo havitaachana mpaka vinifikie katika [hodhi ya] Kawthar. Nawausia juu ya Ahlul Bayt wangu! Angalieni jinsi mtakavyojihusisha nao. Kama mkishikamana na viwili hivi hamtapotea kamwe...” (kwa maelezo zaidi soma kitabu cha al-Ghadir) Lakini bahati mbaya sana sio Waislamu wote wanaowafuata Ahlul Bayt AS pamoja na kwamba wanavyuoni wa madhehebu zote wameandika habari zao katika vitabu vyao na kuonesha kwamba hawa ni viongozi wa Umma huu wa Kiislamu. Mwandishi wa kitabu hiki anajaribu kuthibitisha hilo kwa kutoa rejea mbalimbali kutoka vitabu maarufu vya wanavyuoni wa Kisunni. Ni muhimu kukubaliana na kuziheshimu tofauti za kila mmoja na kutambua msimamo na mtazamo wa kila mmoja. Matatizo huja pale mtu anapolazimisha tabia, imani na mila zake zitawale wengine au kuzifisha itikadi E

Page E


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 2 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

11:14 AM

Ahlul Bayt ndani ya Tafsiri za Kisunni No.2 na misimamo ya wengine. Ni muhimu kufikiria kila aina ya maoni katika kujaribu kuamua ukweli. Uislamu kimsingi uko dhidi ya kufuata kibubusa. Wafuasi wa madhehebu nyingine wanaweza kuchambua uthibiti wa kitabu hiki ili kujenga maoni yao wenyewe kuhusu mtazamo mzuri wa mtu mwenyewe. Ni muhimu mtu kuelewa hoja za wale ambao hakubaliani nao. Inaweza ikasemwa kwamba wale ambao hawaelewi kabisa mtazamo wa maoni tofauti, hawaelewi kwa ukamilifu mtazamo wa kwao wenyewe. Tumekiona kitabu hiki ni chenye manufaa sana, hususan wakati huu wa maendeleo makubwa ya elimu katika nyanja zote, ambapo uwongo, ngano za kale na upotoshaji wa historia ni mambo ambayo hayana nafasi tena katika akili za watu. Kutokana na ukweli huo, Taasisi yetu ya Al-Itrah Foundation imeamua kuchapisha kitabu hiki kwa lugha ya Kiswahili kwa madhumuni yake yaleyale ya kuwahudumia Waislamu, hususan wazungumzaji wa Kiswahili. Tunamshukuru ndugu yetu, Hemedi Lubumba (Abu Batul) kwa kukubali jukumu hili la kukitarjumi kitabu hiki. Vilevile tunawashukuru wale wote walioshiriki kwa njia moja au nyingine hadi kufanikisha kuchapishwa kwake. Ni matumaini yetu kwamba kitabu hiki kitakuwa ni changamoto kubwa kwa wasomaji wetu. Mchapishaji: Al-Itrah Foundation

F

Page F


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 2 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

11:14 AM

NENO LA JUMUIYA Hakika mirathi ya Ahlul-Bait ambayo imehifadhiwa na kambi yao na wafuasi wao dhidi ya upotovu inaonyesha ni kambi iliyokusanya aina mbalimbali za taaluma za kiislamu. Kambi hii imeweza kulea nafsi mbalimbali zilizo tayari kunywa kutoka kwenye chemchemu hiyo, na kuupa umma wa kiislamu wanavyuoni wakubwa wenye kufuata nyayo za ujumbe wa Ahlul-Bait. Wanavyuoni waliokusanya vidodosa na maswali mbalimbali ya madhehebu na mitazamo tofauti ya kifikira kuanzia ndani ya desturi ya kiisilamu hadi nje ya desturi hiyo, huku wao wakitoa majibu na utatuzi makini juu ya maswali hayo ndani ya karne zote. Jumuiya ya kimataifa ya Ahlul-Bait imefanya hima kutetea tukufu za ujumbe wa Uislamu na ukweli wake ambao umechafuliwa na makundi, madhehebu na wanaharakati mbalimbali wenye chuki na Uislamu. Jumuiya imefuata nyayo za Ahlul-Bait na za wafuasi wa kambi yao njema ambayo imefanya hima kujibu madai yenye kuendelea na daima ikajaribu kubaki ndani ya msitari wa mapambano kwa kiwango kinachohitajika ndani ya kila zama. Hakika uzoefu ambao umehifadhiwa ndani ya vitabu vya wanavyuoni wa kambi ya Ahlul-Bait katika dhamira hii ni wa aina ya pekee, kwa sababu una akiba ya kielimu inayotegemea akili na hoja, huku ukijiepusha na matamanio na upendeleo uliokatazwa. Unazungumza na wasomi na wanafikra wenye fani maalumu, mazungumzo ambayo yanakubalika kiakili na yanapokewa na maumbile yaliyo salama. G

Page G


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 2 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

11:14 AM

Jaribio hili la Jumuiya ya kimataifa ya Ahlul-Bait limekuja kuwapa watafuta ukweli hatua mpya ya uzoefu wa thamani kupitia mada na vitabu vinavyoandikwa na waandishi wa zama hizi ambao ni wafuasi wa madhehebu ya Ahlul-Baiti (a.s.) au miongoni mwa wale ambao Mwenyezi Mungu amewapa neema ya kujiunga na kambi hii tukufu. Achia mbali kwamba jumuia hii pia hujishughulisha na uchapishaji na uhakiki wa yale yenye faida toka katika vitabu vya ulamaa wa zamani wa kishia, ili vitabu hivi viwe maji matamu kwa nafsi zenye kuitafuta haki, ili ziweze kufikia kwenye haki ambayo inatolewa na Kambi ya Ahlul-Bayt ulimwengu mzima, ndani ya zama ambazo akili inaerevuka na nafsi na roho zinaboreka kwa kasi ya pekee. Tunatoa shukurani njema kwa Samahatu Sheikh Nazar Hasan kwa kuandika kwake kitabu hiki, na kwa ndugu zetu wote waliosaidia kukichapisha. Na sote tunategemea na kutaraji kuwa tutakuwa tumetoa kile tulichokiweza katika juhudi za kutekeleza baadhi ya wajibu tulionao mbele ya ujumbe wa Mtukufu Mola wetu Mlezi ambaye alimtuma Mtume Wake na uongofu na dini ya haki ili aipe ushindi dhidi ya dini zote. Na Mwenyezi Mungu anatosha kuwa shahidi. Jumuiya ya kimataifa ya Ahlu-Bait Kitengo cha utamaduni

H

Page H


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 2 Check Lubumba.qxd

I

7/1/2011

11:14 AM

Page I


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 2 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

11:14 AM

Page 1


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 2 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

11:14 AM

Ahlul Bayt ndani ya Tafsiri za Kisunni No.2

UTANGULIZI Kila sifa njema ni ya Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wa viumbe wote. Rehema na amani zimwendee Mtume Muhammad, yeye na aali zake watoharifu. Na daima laana iwe juu ya wote walio maadui zao na wakanushaji wa fadhila zao. Qur’ani iliteremkia katika nyumba tohara na safi, ambazo imeidhinishwa zitukuzwe, katika nyumba za aali Muhammad watoharifu, ambazo Mwenyezi Mungu Mtukufu amezifanya makhsusi kwa ajili ya heshima na utukufu kuliko nyingine, na Mwenyezi Mungu akazighani (nyumba hizo) kupitia Aya za Qur’ani tukufu ambazo zitaendelea kubaki muda wa dahari yote zikisomwa usiku na mchana, na si nyumba za viumbe wengine. Kwa ajili hiyo tunawaona (a.s.) wao ndio watambuzi na wajuzi wa Kitabu cha Mwenyezi Mungu Mtukufu kuliko wengine wote, na kwa ajili hiyo tunamwona Amirul-Muuminina (a.s.) Ali bin Abu Talib (a.s.) akisema: “Lau nikitandikiwa mto kisha nikaketi juu yake nitahukumu baina ya wanataurati kwa Taurati yao na wanainjili kwa Injili yao, na baina ya wanazaburi kwa Zaburi yao na wanafurqan kwa Furqani yao. Wallahi hakuna Aya yoyote iliyoteremshwa bara au baharini, katika tambarare au jabali, mbinguni au ardhini, usiku au mchana, ila mimi namjua ni nani iliteremka kwa ajili yake, na iliteremka kuhusu nini.”1 Abu Naiim ameandika katika kitabu Hilyatul-Awliyai kutoka kwa Imam Ali (a.s.) kwamba alisema: “Wallahi hakuna Aya iliyoteremka ila najua iliteremka kwa ajili ya nani, na wapi iliteremka, na hakika Mola wangu Mlezi amenitunukia moyo wenye akili na ulimi wenye kudadisi.”

1 Matwalibus-Suul, cha Ibnu Talha as-Shafiiyu Juz. 1, Uk. 125, chapa ya Taasisi ya Ummul-Qura. 2

Page 2


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 2 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

11:14 AM

Ahlul Bayt ndani ya Tafsiri za Kisunni No.2 Na pia Abu Naiim ameandika katika kitabu Hilyatul-Awliyai kutoka kwa Ibnu Masuud, amesema: “Hakika Qur’ani iliteremshwa kwa herufi saba, hakuna herufi yoyote ila ina dhahiri na batini, na hakika Ali bin Abu Talib ndiye mwenye dhahiri na batini.” Na kuna kauli moja inanasibishwa na Amirul-Muuminina (a.s.): “Lau nikitaka kuwapigisha magoti ngamia arubaini kwa tafsiri ya Qur’ani ninaweza.” Kisha wao ndio wafasiri wa wahyi wa Mwenyezi Mungu Mtukufu, wenza wa Kitabu chake na Kitabu kitamkacho, haya ndio yathibitishwayo na Hadithi ya Vizito viwili: “Mimi ni mwenye kuacha kati yenu vizito viwili: Cha kwanza ni Kitabu cha Mwenyezi Mungu, humo mna uongofu na nuru…., na Ahlul-Baiti wangu, nawakumbusheni Mwenyezi Mungu kuhusu Ahlul-Baiti wangu, nawakumbusheni Mwenyezi Mungu kuhusu Ahlul-Baiti wangu.”2 Hivyo wao ndio wabainishaji, wafafanuzi na wafasiri wa misamiati ya Qur’ani Adhimu. Kwa sababu Kitabu cha Mwenyezi Mungu kina haja ya kupata mfasiri, mfafanuzi na mfasiri, hivyo ni aula kifani chake na mwenza wake ndiye mbainishaji, mfasiri, alimu na mjuzi wa Kitabu hicho na si mwingine. Kwa ibara nyingine tunaweza kusema: Hakika Ahlul-Baiti (a.s.) ndio waliokusudiwa, kuainishwa na kuashiriwa katika semi zake (s.w.t.). Bali ni katika nyumba zao ndimo kulimoteremka Kitabu, na wenye nyumba ndio wajuzi zaidi wa yale yaliyomo ndani ya nyumba yao. Kuanzia hapa tunawakuta Ahlul-Baiti (a.s.) siku zote wakiifasiri Qur’ani na Maneno ya Mwenyezi Mungu vizuri zaidi na kwa ukamlifu mno. Na watu wote wakirejea kwao bila kumtenga yoyote, na wala hatujaona tukio lililo kinyume na hali hiyo, hata Ibnu Abbas ambaye ni kinara na kiongozi 2 Sahih Muslim, Juz. 4, Hadithi ya 1873. 3

Page 3


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 2 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

11:14 AM

Ahlul Bayt ndani ya Tafsiri za Kisunni No.2 wa wafasiri miongoni mwa sahaba yeye naye alikuwa ni mwanafunzi wa Ali (a.s.), yeye mwenyewe anasema: “Tafsiri ya Qur’ani niliyonayo ni kutoka kwa Ali bin Abu Talib (a.s.).” Hapo hapo tunawaona ulamaa wa makundi mawili, Shia na Sunni wameifasiri Qur’ani Tukufu kupitia riwaya na nukuu, kama vile Tafsiri ya Ali bin Ibrahim al-Qummiy, Tafsirul-Ayyashiy na Furatil-Kufiy, KanzudDaqaiq ya Ibnu al-Mash’hadiy, al-Burhan ya Sayyid Hashim al-Bahraniy, Nurut-Thaqalayn ya Sheikh Abdu Ali al-Hawiziy, na wengineo miongoni mwa Maimamiya ambao wameifasiri Qur’ani kupitia Ahlul-Baiti (a.s.). Na miongoni mwa Masunni ni kama vile al-Haskaniy katika ShawahidutTanziil, Isfihaniy katika an-Nuru al-Mushtaalu na al-Wahidiy katika Asbabun-Nuzuul. Pia zipo tafsiri zilizozagaa huku na huko ambazo zinategemewa na Sunni katika utafiti na mchakato wa kielimu. Tafsiri hizi zimefasiri baadhi ya Aya tukufu kwamba walengwa halisi wa Aya hizo ni aali Muhammad (a.s.), hivyo tumejaribu kuzikusanya na kuziweka pamoja Aya hizi toka katika kabati za vitabu vya tafsiri muhimu zenye kutegemewa kwao. Miongoni mwazo ni: Jamiul-Bayan Fii Tafsiril-Qur’ani ya Abu Ja’far Muhammad bin Jarir bin Yazid bin Kathiir bin Ghalib at-Tabari, aliyefariki mwaka 310 A.H. Nasi hapa tumetegemea chapa ya Misri yenye juzuu 30. al-Kashfu wal-Bayan Antafsiril-Qur’ani ya Abu Is’haqa Ahmad ibnu Ibrahim at-Thaalabiy an-Nisaburiy al-Muqriu, aliyefariki mwaka 427 A.H. Maalimut-Tanziil ya Abu Muhammad Husain bin Masuud bin Muhammad, maarufu kwa jina la Farrau al-Baghawi as-Shafiy, aliyefariki mwaka 516 A.H. Nasi hapa tumetegemea chapa ya Beirut ambayo ina juzuu 4.

4

Page 4


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 2 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

11:14 AM

Ahlul Bayt ndani ya Tafsiri za Kisunni No.2 al-Kashaf Anihaqaiqit-Tanziil Wauyuunil-Aqawiil Fii Wujuhit-Taawiil ya Abu Qasim Mahmudu bin Umar bin Muhammad bin Umar alKhawarazimiy al-Hanafiy al-Muutazaliy az-Zamakhshariy, mwenye lakabu ya Jarullah, aliyefariki mwaka 538 A.H. Nasi hapa tumetegemea chapa ya Misri ya mwaka 1948 A.D. Mafatihul-Ghaybi ya Abu Abdillah Muhammad bin Umar bin Husain bin Hasan bin Ali at-Tamimiy al-Bakriy at-Tarstaniy ar-Razi, mwenye lakabu ya Fakhrud-Din, maarufu kwa jina la Ibnul-Khatib as-Shafiy, aliyefariki mwaka 606 A.H. An’warut-Tanziil Waasrarut-Taawiil ya Kadhi Mkuu Nasrud-Din (AbulKhayri), Abdullah bin Umar bin Muhammad bin Ali al-Baydhawi asShafiy, aliyefariki mwaka 691 A.H. iliyo katika juzuu mbili, iliyochapishwa Misri mwaka 1968 A.D. al-Jamiu Liahkamil-Qur’ani ya Abu Abdillah Muhammad bin Ahmad bin Abubakri al-Ansariy al-Khazrajiy al-Undlusiy al-Qurtubiy, aliyefariki mwaka 761 A.H. iliyo katika juzuu ishirini, iliyochapishwa Misri mwaka 1950 A.D. Tafsirul-Qur’ani al-Adhiim ya Hafidh Imadud-Din (Abul-Fidai), Ismail bin Amru bin Kathiir bin Dhaw’u bin Kathiir bin Zar’i al-Baswriy adDamashqiy, Ibnu Kathiir, aliyefariki mwaka 774 A.H. iliyo katika juzuu tano, iliyochapishwa Beirut. ad-Duru al-Manthur Fii Tafsiri Bil-Maathur ya Hafidh Jalalud-Din (AbulFadhli), Abdurahman bin Abubakri bin Muhammad as-Suyuti, aliyefariki mwaka 911 A.H. iliyo katika juzuu nne, iliyochapishwa Misri. Ruhul-Bayan ya Allamah Sheikh Ismail Haqiyyu al-Barsiyyu, aliyefariki mwaka 1137 A.H. iliyo katika juzuu thelathini, nasi hapa tumetegemea chapa ya Uthmaniya ya mwaka 1330 A.H.

5

Page 5


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 2 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

11:14 AM

Ahlul Bayt ndani ya Tafsiri za Kisunni No.2 Ruhul-Maaniy ya Allamah Abul-Fadhli Shihabud-Din, Sayyid Muhammad Al-Alusiy, aliyefariki mwaka 1270 A.H., iliyo katika juzuu thelathini, nasi hapa tumetegemea chapa ya Misri ambayo ilipigwa chapa na Al-Muniriyah mwaka 1345 A.H. Tafsirul-Qummiy, maarufu kwa jina la Mahasinut-Taawiili ya Allamah asSham Muhammad bin Jamalud-Din al-Qasimiy, aliyefariki mwaka 1322 A.H., iliyo katika juzuu kumi na saba, nasi hapa tumetegemea chapa ya Beirut ya Ihyaut-Turathil-Arabiy ya mwaka 1415 AH. Tafsiri hizi zimepangwa kulingana na kipaumbele na umuhimu. Hivyo kutokana na wajibu wa kiitikadi na jukumu la kisheria, pia kutokana na kuwepo mapungufu ambayo ni lazima tuyazibe kwa kile kinachonasibiana na ukubwa wa mahitaji ya upungufu huo, na ili kuitikia wito wa Mwenyezi Mungu Ambaye mara kwa mara ametangaza katika Qur’ani wito wa kuwapenda aali Muhammad (a.s.) aliposema: “Sema: Kwa haya siombi malipo yoyote kwenu isipokuwa mapenzi kwa kizazi changu” (Sura Shura: 23), tumefanya kazi hii iliyobarikiwa ambayo inamimina maji kutoka katika bahari ya aali Muhammad (a.s.) iliyojaa na yenye kububujika. Na ni kutokana pia na umuhimu wa kazi hii katika kuthibitisha maarifa na nafasi ya Ahlul-Baiti (a.s.), ili uthibitisho huo uwe hoja yenye nguvu, na hapo utimie msemo “Nafuata kinywa chako.” Pia ni ili kuthibitisha kwamba wao ndio walioainishwa na kukusudiwa na Kitabu cha Mwenyezi Mungu Mtukufu. Kazi hii imeendelea toka siku ya kumi na nane ya mfunguo pili mwaka 1420 A.H. mpaka siku ya ishirini na tatu ya mfunguo tatu mwaka 1426 A.H., lakini kazi hii ilikumbwa na matatizo mengi ikiwa ni pamoja na hali kutotulia, kutopatikana rejea, na nyudhuru nyingine mfano wa hizo.

6

Page 6


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 2 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

11:14 AM

Ahlul Bayt ndani ya Tafsiri za Kisunni No.2 Pamoja na hayo yote tulivumilia kwa kalamu ya mahaba na upendo wetu kwa wateule Ahlul-Baiti (a.s.) nyudhuru zote zilizotukabili, tukazama katika kina cha tafsiri na wafasiri ili tutoe humo johari na vito vya aali Muhammad (a.s.) baada ya kuwa vimefichwa na kufunikwa na vumbi la historia kwa sababu za siasa ya kidunia. Pia katika ziara yetu ya kitafsiri tumezitambua nafsi za wafasiri, hivyo tumegundua kwamba Ibnu Kathir ndiye mwenye maradhi makubwa ya nafsi na ndiye mwenye chuki kubwa dhidi ya Ahlul-Baiti (a.s.) na wafuasi wao wema. At-Thaalabiy ndiye mwadilifu na mwenye insafu kuliko wengine. Utafiti huu tuliuwakilisha kwenye kongamano la mwaka la Sheikh Tusiy ambalo lilifanyika katika Jamhuri ya Kiislam ya Iran katika Jiji la Qum Takatifu, mwaka 1426 A.H. hatimaye ukapata tuzo katika kongamano hilo adhimu. Haya yote ni sehemu ya fadhila za Mola wangu na neema kutoka Kwake (s.w.t.), na ni sehemu ya msaada toka katika roho toharifu (a.s.), kwa sababu kazi hii ni kwa ajili yao na si kwa ajili ya mwingine. Mwisho tunainua mikono yote kutoa shukurani kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, tunamwomba maghufira dhidi ya utelezo na makosa yaliyotoka kwetu, kwa sababu umaasumu ni wa wenye nao. Pia tunamtaka msamaha msomaji mpendwa kutokana na makosa yasiyo ya kukusudiwa atakayoyakuta humu. Na kila sifa njema ni ya Mwenyezi Mungu Mola Mlezi wa viumbe wote. Nizar Hasan 2 Mfunguo Nne 1427 A.H. Qum Takatifu

7

Page 7


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 2 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

11:14 AM

Ahlul Bayt ndani ya Tafsiri za Kisunni No.2 AHLUL-BAIT (A.S.) NDANI YA TAFSIRI YA AL-BAGHAWI, INAYOITWA: MAALIMUT-TANZIIL3

SURAT AL-BAQARAH Kauli ya Mwenyezi Mungu:

“Wale watoao mali zao usiku na mchana kwa siri na dhahiri, wana ujira wao kwa Mola wao Mlezi; wala haitakuwa hofu juu yao wala wao hawatahuzunika.” (Surat al-Baqarah: 274). Imepokewa kutoka kwa Mujahid, kutoka kwa Ibnu Abbas, amesema: “Aya hii iliteremka kwa ajili ya Ali bin Abu Talib; alikuwa na dirhamu nne hakuwa anamiliki nyingi zaidi ya hizo, akatoa sadaka dirhamu moja usiku na nyingine mchana, nyingine siri na nyingine dhahiri.”4

SURAT AALI IMRAN Kauli ya Mwenyezi Mungu:

“Na Malaika waliposema: Ewe Maryam! Hakika Mwenyezi Mungu amekuteua na akakutakasa na akakuteua juu ya wanawake wa ulimwenguni.” (Sura Aali Imran: 42). 3 Chapa ya Beirut ya Mwaka 2004 A.D. 4 Tafsirul-Baghawi Juz. 1, Uk. 197, Chapa ya Beirut ya Darul-Kutubi Al-Ilmiyah ya Mwaka 2004. Na ameipokea Ibnu Athiir katika wasifu wa Amirul-Muuminina Ali katika kitabu Usudul-Ghaba Juz. 4, Uk. 25. Na Tabarani katika kitabu alMuujam al-Kabir Juz. 3, Uk. 112 katika anwani: Yaliyopatikana kwa njia ya Ibnu Abbas. Na al-Wahidiy katika kitabu Asbabun-Nuzuul Uk. 64. 8

Page 8


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 2 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

11:14 AM

Ahlul Bayt ndani ya Tafsiri za Kisunni No.2 Ametupa habari Abu Bakri Said bin Abdullah Ahmad at-Tahiriy, amesema: “Ametupa habari babu yangu Abdurahman bin Abdus-Swamad al-Bazar kutoka kwa Qatadah kutoka kwa Anas kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) alisema: “Yakutosha katika wanawake wa ulimwenguni: Maryam binti Imran, Khadija binti Khuwaylid, Fatima binti Muhammad na Asia mke wa Firaun.”5 Kauli ya Mwenyezi Mungu:

“Na watakaokuhoji baada kukufikia elimu hii, waambie: Njooni tuwaite watoto wetu na watoto wenu, na wanawake zetu na wanawake wenu, na nafsi zetu na nafsi zenu, kisha tuombe kwa unyenyekevu tutake laana ya Mwenyezi Mungu iwashukie waongo.” (Sura Aali Imran: 61). Amesema: “…watoto wetu na watoto wenu, na wanawake zetu na wanawake wenu, na nafsi zetu na nafsi zenu..” imesemwa kwamba: Watoto wetu ni Hasan na Husein. Wanawake zetu ni Fatima na Nafsi zetu yaani ni yeye mwenyewe na Ali.6” Amesema: “Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) alipousomea ujumbe wa Najran Aya hizi na kuwaomba wafanye maombi ya laana walisema: Mpaka turejee na tutafakari jambo hili kisha kesho tutakuja tena. Wakajadiliana na kumwambia Aqib naye alikuwa ndiye wamfatae katika 5 Tafsirul-Baghawi Juz. 1, Uk. 232. 6 Hivyo ‘nafsi zetu na nafsi zenu’ inaonyesha kwamba uimamu umethibiti kwa Ali kwani Mwenyezi Mungu amemfanya ndio nafsi ya Mtume wa Mwenyezi

Mungu, na kuungana kwa kuwa kitu kimoja ni muhali hivyo maana yake ni kwamba wanalingana katika mamlaka ila unabii. 9

Page 9


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 2 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

11:14 AM

Ahlul Bayt ndani ya Tafsiri za Kisunni No.2 rai: ‘Ewe mja wa Masihi unasemaje?’ Akasema: W’allahi enyi wakristo nimeshakujulisheni kwamba hakika Muhammad ni Nabii na Mtume, na wallahi katu hakuna watu walioombeana laana na Mtume kisha mkubwa wao akaendelea kuishi au mdogo wao kuzaliwa. Na kama mtafanya hivyo bila shaka tutaangamia, hivyo hakuna cha kufanya ila ni nyinyi kuendelea kubakia katika imani yenu kuhusu jamaa yenu (Isa), nendeni mkamuage mtu huyu na mrejee nchini kwenu.” Ndipo kesho wakaja kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) na Mtume akatoka akiwa amemkumbatia Husein na amemshika mkono Hasan huku Fatima akitembea nyuma yake na Ali akiwa nyuma ya Fatima. Akawaambia: “Mimi nitakapokuwa naomba nyinyi muwe mnaitikia.” Askofu wa Najran akasema: “Enyi wakristo! Mimi naziona nyuso hizi kama zitamuomba Mwenyezi Mungu auondoe mlima kutoka mahala pake, atauondoa, msiapizane naye mtaangamia, na hatabaki mkiristo yeyote hapa duniani mpaka siku ya Kiyama.” Wakasema: Ewe Abul-Qasim! Tumeona tusiapizane na wewe na tukuwache uendelee kuwa katika dini yako nasi tuendelee kubaki katika dini yetu. Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) akasema: “Mkikataa kufanya maapizano basi msilimu mtapata haki waliyonayo waislamu na mtawajibikiwa na yale yaliyo wajibu kwao.” Wakakataa, ndipo Mtume akawaambia: “Basi hakika nitawafukuzeni.” Wakasema: “Hatuna nguvu ya kupigana vita na waarabu, lakini sisi tunafanya suluhu na wewe usitushambulie kivita na wala usitufukuze na wala usitutoe katika dini yetu. Kwa sharti tukupe kila mwaka Hilla7 elfu mbili: Elfu moja katika mwezi wa Safar na elfu nyingine katika mwezi wa Rajab.” 10

Page 10


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 2 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

11:14 AM

Ahlul Bayt ndani ya Tafsiri za Kisunni No.2 Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) akafanya nao suluhu kwa sharti hilo na akasema: “Naapa kwa Yule Ambaye nafsi yangu imo mikononi mwake hakika adhabu imeshateremka juu ya watu wa Najran. Na lau wangefanya maapizano wangegeuzwa manyani na nguruwe na bonde lao lingewaka moto. Na Mwenyezi Mungu angeiteketeza Najran na watu wake hata ndege aliyopo juu ya mti. Wala mwaka usingepita wakristo wote wangekuwa wameteketea.”8

SURAT AL-MAIDA Kauli ya Mwenyezi Mungu: “Hakika Walii wenu hasa ni Mwenyezi Mungu na Mtume wake na wale walioamini ambao husimamisha Swala na hutoa Zaka wakiwa wamerukui.” (Sura al-Maida: 55). Ibnu Abbas na as-Sadiy wamesema kuhusu kauli yake (s.w.t.): “Hakika Walii wenu hasa ni Mwenyezi Mungu na Mtume wake na wale walioamini ambao husimamisha Swala na hutoa Zaka wakiwa wamerukui.” kwamba alimkusudia Ali bin Abu Talib, muombaji alipita kwake msikitini na hali akiwa amerukuu ndipo akampa pete yake.”9

7 Jina la pesa kama vile Dola, Shilingi, Paundi na mfano wa hizo. 8 Tafsirul-Baghawi Juz. 1, Uk. 240. Na ameipokea Hamwawi katika mlango wa kumi na nne katika kitabu Faraidus-Samtwayn Juz. 2, Uk. 23, Chapa ya Kwanza. Pia ameipokea Ibu al-Mughazaliy katika kitabu Manaqibu Amiril-Muuminina Uk. 263, Hadithi ya 310. Na al-Baghawi katika kitabu Misbahus-Sunnah Juz. 2, Uk. 201. Na pia ameipokea Ibnu Hajar katika kitabu as-Sawaiqul-Muhriqah Uk. 93. 9 Tafsirul-Baghawi Juz. 2, Uk. 38. Ameipokea al-Haythami katika mlango wa fadhila za Ali katika kitabu Majmauz-Zawaid Juz. 9, Uk. 134. Na al-Muttaqiy alHindiy katika Kanzul-Ummal Juz. 7, Uk. 305, Chapa ya Kwanza. Na Shablanji katika kitabu Nurul-Absar Uk. 69. 11

Page 11


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 2 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

11:14 AM

Ahlul Bayt ndani ya Tafsiri za Kisunni No.2 Na amesema Abu Ja’far Muhammad bin Ali al-Baqir (a.s): “Hakika Walii wenu hasa ni Mwenyezi Mungu na Mtume wake na wale walioamini…” iliteremka kwa ajili ya wale walioamini. Pakasemwa: Watu wanasema kwamba iliteremka kwa ajili ya Ali bin Abu Talib. Akasema: ‘Ali ni miongoni mwa wale walioamini.10”

SURAT AL-AN’FAL Kauli ya Mwenyezi Mungu: “Na walipokupangia njama wale waliokufuru ili wakufunge au wakuue au wakutoe, wakapanga njama na Mwenyezi Mungu akapanga njama na Mwenyezi Mungu ndiye mpangaji bora wa njama.” (Sura al-An’fal: 30). Ibnu Abbas amesema: “Jibril alimjia Mtume (s.a.w.w.) na kumpa habari na kumwamuru asilale katika kitanda chake alichokuwa akilala siku zote na Mwenyezi Mungu akampa idhini ya kutoka kuelekea Madina. Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) akamwamuru Ali bin Abu Talib alale kitandani kwake na kumwambia: “Jifunike shuka langu hili hakika hautofikwa na jambo likuchukizalo.” Kisha Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) akachukua fungu la udongo na Mwenyezi Mungu akawafumba macho yao na Mtume akawa anawanyunyuzia udongo juu ya vichwa vyao na hali akisoma: “Hakika sisi tumeiweka minyororo shingoni mwao nayo inafika videvuni, kwa hiyo vichwa vyao vikainuliwa.” Na akaenda zake pangoni huko Thauri akiwa na Abu Bakri na akamwacha Ali badala yake huko Makka akirudisha amana zilizokuwa kwake. Amana zilikuwa zikiwekwa kwake kutokana na ukweli wake na uaminifu wake. Mushrikuna walikesha wakimlinda Ali akiwa amelala katika kitanda cha Mtume wa Mwenyezi Mungu huku wakidhani kuwa ndiye Mtume (s.a.w.w.). Palipopambazuka walimzingira 10 Nurul-Absar Uk. 39. Na dhahiri kwamba iwapo kweli riwaya hii ni sahihi basi jibu la Imam hapa ni la mfumo wa Taqiyya ndio maana ametoa jibu la jumla. 12

Page 12


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 2 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

11:14 AM

Ahlul Bayt ndani ya Tafsiri za Kisunni No.2 na ghafla wakamkuta ni Ali, wakamuuliza rafiki yako yuko wapi? Akajibu sijui….”11

SURAT TAWBA Kauli ya Mwenyezi Mungu: “(Tangazo la) Kujitoa Mwenyezi Mungu na Mtume wake kwa wale mlioahidiana nao miongoni mwa mushrikina.” (Sura Tawba: 1). Amesema: Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) akasema: “Hakuna nusra nisipowanusuru.” Mwaka wa nane Hijriya akaandaa msafara kuelekea Makka, ulipoingia mwaka wa tisa Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) aliazimia kuhiji, kisha akasema: “Hakika mushrikina watahudhuria na kutufu uchi.” Ndipo akamtuma Abu Bakr awe kiongozi wa Hijja katika msimu huo, akampa pia Aya arobaini za mwanzo wa Surat Baraa akawasomee mahujaji wa msimu huo. Kisha baada yake akamtuma Ali aende na ngamia wake akawasomee mwanzo wa Sura Baraa na akamwamuru atangaze huko Makka, Mina na A’fara kwamba: Mwenyezi Mungu na Mtume wake (s.a.w.w.) wamejitoa katika dhima dhidi ya kila Mushriku na wala wasitufu na hali wakiwa uchi. Ndipo Abu Bakr akarejea na kusema: ‘Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu! Baba yangu na mama yangu ni fidia kwako, kuna lolote limeshuka kwa ajili yangu?’ Akasema (s.a.w.w.): ‘Hapana, lakini haipasi yeyote yule afikishe hili kwa niaba yangu ila mtu kutoka katika ndugu zangu.’12 Akaendelea mpaka akasema: “Ilipofika siku ya kuchinja Ali alisimama na kuwatangazia amri aliyotumwa na akawasomea Sura Baraa.” Zaid bin Thabit amesema: Tulimuuliza Ali ulitumwa kitu gani katika Hija 11 Tafsirul-Baghawi Juz. 2 Uk. 205. 12 An-Nasai ameiandika katika kitabu chake al-Khaswais Uk. 144, Chapa ya Beirut. Pia Ahmad bin Hanbal katika Musnad yake Juz. 3, Uk. 212, Chapa ya Kwanza. Ibnu Asakir katika Tarikh Damashq katika wasifu wa Amirul-Muuminin Ali Juz. 2 Uk. 376, Namba 878. 13

Page 13


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 2 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

11:14 AM

Ahlul Bayt ndani ya Tafsiri za Kisunni No.2 hiyo? Akasema: ‘Nilitumwa mambo manne: Mushriku haruhusiwi kuhiji wala kutufu na hali yu tupu. Yule ambaye kati yake na Mtume wa Mwenyezi Mungu kuna ahadi basi itaendelea mpaka mwisho wa muda wake, na yule ambaye ahadi yake haina muda basi muda wake ni miezi minne tokea sasa. Haingii peponi ila mwislamu. Na baada ya mwaka huu waislamu na mushrikina hawahiji tena pamoja.13 Baghawi amesema: Lau mtu akisema: Vipi Mtume wa Mwenyezi Mungu alimtuma Abu Bakr kisha akamuuzulu na kumtuma Ali? Tutajibu: Alimtuma Ali akatangaze Aya hizi, na sababu ni kwamba waarabu walikuwa wamezoea kwamba asiwakilishe katika kuweka mikataba yao na kujitoa katika mikataba hiyo ila yule aliye bwana wao au mtu kutoka katika ukoo wao.14 Kauli ya Mwenyezi Mungu: “Je, mnafanya kuwanywesha mahujaji na kuamirisha msikiti mtukufu ni sawa na yule aliyemwamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho na akapigana jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu? Hawawi sawa mbele ya Mwenyezi Mungu na Mwenyezi Mungu hawaongozi watu madhalimu.” (Sura Tawba: 19). Hasan, Shaabiy na Muhammad bin Kaab al-Qardhiy wamesema: “Iliteremka kwa ajili ya Ali bin Abu Talib, Abbas bin Abdul-Mutalib na Talha bin Shayba, kila mmoja alijigamba.” Talha akasema: ‘Mimi ndio mtunza Nyumba funguo zimo mikononi mwangu.’ Abbas akasema: ‘Mimi ndiye mgawa maji na msimamizi wake.’ Ali akasema: ‘Sijui mtasema nini. Bila shaka nimeswali miezi sita kabla ya mtu yeyote na mimi ndiye mwanajihadi.’ 13 Tafsirul-Baghawi Juz. 2, Uk. 225. 14 Tafsirul-Baghawi Juz. 2, Uk. 225. 14

Page 14


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 2 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

11:14 AM

Ahlul Bayt ndani ya Tafsiri za Kisunni No.2 Ndipo Mwenyezi Mungu akateremsha: “Je, mnafanya kuwanywesha mahujaji na kuamirisha msikiti mtukufu….”15

SURAT HUD Kauli ya Mwenyezi Mungu:

“Basi je, aliye na dalili wazi itokayo kwa Mola wake na anaifuata na shahidi atokaye kwake…..” (Sura Hud: 17). Palisemwa: Shahidi hapa ni Ali bin Abu Talib. Na Ali (a.s.) alisema: “Hakuna mtu yeyote miongoni mwa makuraishi ila kuna Aya moja ilishuka kwa ajili yake.” Ndipo mtu mmoja akamwambia: ‘’Ni ipi iliyoteremka kwa ajili yako?’’Ali akasema: “Na anaifuata na shahidi atokaye kwake..”16

15 Tafsirul-Baghawi Juz. 2, Uk. 232. Na pia ameiandika Ibnu al-Mughazali katika Manaqib Uk. 321, Hadithi ya 367 na 368. Na al-Wahidiy katika AsbabunNuzuul Uk. 182. Na Abul-Faraji al-Isfahani katika kitabu chake al-Aghaniy Juz. 4, Uk. 185. 16Tafsirul-Baghawi Juz. 2, Uk. 318. Na ameipokea al-Muttaqi al-Hindi katika Juz. 1, Uk. 251, Chapa ya Kwanza. Na Ibnu Asakir katika kitabu chake Tarikh Damashq katika wasifu wa Imam Ali Juz. 2, Uk. 420. Na Ibnu Abil-Hadid katika Sharhun-Nahji Juz. 2, Uk. 236. 15

Page 15


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 2 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

11:14 AM

Ahlul Bayt ndani ya Tafsiri za Kisunni No.2

SURAT AN-NAHLI Kauli ya Mwenyezi Mungu:

“Na tukampa wema katika dunia, na hakika yeye katika Akhera atakuwa katika watu wema.” (Sura an-Nahli: 122). Amesema Muqatil bin Hayyan: “Anamaanisha rehema anazoombewa katika umma huu, unaposema: Ewe Mwenyezi Mungu! Mrehemu Muhammad na Aali Muhammad kama ulivyomrehemu Ibrahim na Aali Ibrahim.”17

SURAT ISRAI Kauli ya Mwenyezi Mungu: “Siku tutakapowaita kila watu na Imam wao.....” (Surat Israi: 71). Imamu wao hapa imesemwa anamaanisha mama zao. Na hilo lina aina tatu za hekima, mojawapo ni sharafu ya Hasan na Husein (a.s.).18

17 Tafsirul-Baghawi Juz. 3, Uk. 74. 18 Tafsirul-Baghawi Juz. 3, Uk. 104. 16

Page 16


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 2 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

11:14 AM

Ahlul Bayt ndani ya Tafsiri za Kisunni No.2

SURAT HAJJ Kauli ya Mwenyezi Mungu: “Hawa mahasimu wawili waliohasimiana kwa ajili ya Mola wao...” (Surat Hajj: 19). Iliteremka kwa ajili ya wale waliojitokeza kupambana Siku ya Badri: Hamza, Ali, Ubayda bin al-Harith, Utba na Shayba watoto wa ar-Rabia na al-Walid bin Utba. Kutoka kwa Qays bin Ubada amesema kwamba Ali bin Abu Talib alisema: “Mimi ndiye wa awali ambaye atasimama mbele ya Rahman Siku ya Kiyama kwa ajili ya uhasimu.”19

SURAT SHUA’RAA Kauli ya Mwenyezi Mungu: “Na uwaonye jamaa zako walio karibu.” (Sura Shuaraa: 214). Kutoka kwa Abdullah bin Abbas kutoka kwa Ali bin Abu Talib, amesema: “Ilipoteremka Aya hii kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.): “Na uwaonye jamaa zako walio karibu.” Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) aliniita na kuniambia: ‘Ewe Ali! Hakika Mwenyezi Mungu ameniamuru niwaonye jamaa zangu walio karibu. Suala hilo likaniumiza kichwa na nikatambua kwamba nitakapowadhihirishia jambo hili nitakumbana na nisiyoyapenda toka kwao. Nikanyamaza mpaka aliponijia Jibril na kuniambia: Ewe Muhammad! 19 Tafsirul-Baghawi Juz. 3, Uk. 235. Na ameipokea Bukhari katika Sahih yake katika tafsiri ya Aya hii chini ya namba 4428 Juz. 17 katika ufafanuzi wa alKarmani Uk. 216, Chapa ya Beiruti. Na al-Khawarazimiy katika Manaqib Ali Juz. 107, Hadithi ya 12, Sura ya 16. 17

Page 17


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 2 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

11:14 AM

Ahlul Bayt ndani ya Tafsiri za Kisunni No.2 Hakika usipofanya unayoamrishwa Mola wako atakuadhibu. Ewe Ali! Tuandalie pishi la chakula na mguu wa mbuzi na utujazie birauli ya maziwa, kisha nikusanyie watoto wa Abdul-Mutalib ili niwaeleze na kuwafikishia yale niliyoamrishwa. Nikatekeleza aliyoniamrisha (s.a.w.w.). Kisha nikamwitia na wakati huo walikuwa wanaume arobaini, amezidi mtu mmoja au amepungua mmoja, humo walikuwemo ami zake: Abu Talib, Hamza, Abbas na Abu Lahabi. Walipokwishakusanyika kwake alinitaka niwaletee chakula nilichowatengenezea, nami nikawaletea. Nilipokiweka, Mtume wa Mwenyezi Mungu alichukua kipande kidogo cha nyama akakikata kwa meno yake kisha akakitupia pembezoni mwa sinia, akasema: “Chukueni kwa Jina la Mwenyezi Mungu.” Watu wakala mpaka wakatosheka. Naapa kwa Mwenyezi Mungu, chakula nilichowapa wote ni cha kuweza kula mtu mmoja. Kisha akasema wape watu kinywaji, nikaja na ile birauli wakanywa mpaka wakatosheka wote. Naapa kwa Mwenyezi Mungu kilikuwa ni kinywaji cha kutosheka mtu mmoja. Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) alipotaka kuwaeleza, Abu Lahabi alimtangulia kuongea, akasema: “Jamaa yenu amewaroga kwa karamu.” Ndipo kaumu wakatawanyika na wala Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) hakufanikiwa kuwaeleza, akasema (s.a.w.w.): “Kesho Ali. Hakika mtu huyu amenitangulia kusema yale uliyoyasikia, na hatimaye watu wametawanyika kabla sijawaeleza, hivyo tuandalie chakula mfano wa kile ulichoandaa kisha unikusanyie.” Nikatekeleza kisha nikawakusanya, kisha akanitaka nilete chakula nikawaletea naye akafanya kama alivyofanya jana, wakala na kunywa mpaka wakatosheka. Kisha Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) akaongea kwa kusema: “Enyi wana wa Abdul-Mutalib! Hakika mimi nimewaletea kheri ya dunia na akhera. Na hakika Mwenyezi Mungu ame18

Page 18


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 2 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

11:14 AM

Ahlul Bayt ndani ya Tafsiri za Kisunni No.2 niamuru niwalinganie kwayo, basi ni nani kati yenu atanisaidia katika jambo hili, awe ndugu yangu, wasii wangu na khalifa wangu?” Watu wote wakakaa kimya, nikasema na hali mimi nikiwa ndiye mdogo kiumri kuliko wote: Mimi ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, nakuwa waziri wako. Akaishika shingo yangu kisha akasema (s.a.w.w.): “Hakika huyu ni ndugu yangu, wasii wangu na khalifa wangu kwenu, hivyo msikilizeni na mumtii.” Kaumu wakanyanyuka na hali wakidhihaki na wakimwambia Abu Talib: “Bila shaka amekuamuru umsikilize Ali na kumtii.”20

SURAT AS-SAJDA Kauli ya Mwenyezi Mungu: “Je, aliye muumini ni sawa na aliye fasiki? Hawawi sawa.” (Surat As-Sajda: 18). Iliteremka ikimuhusu Ali bin Abu Talib na Walid bin Uqbah bin Abu Muit ndugu yake Uthman kwa upande wa mama. Kulikuwa na mzozo na maneno baina yao, Walid bin Uqbah akamwambia Ali: ‘Nyamaza wewe bado mtoto na mimi wallahi ni mfasaha kuliko wewe, mwenye meno makali kuliko wewe na shujaa kuliko wewe na hodari wa mapambano kuliko wewe.’ Ali akamjibu: ‘Nyamaza bila shaka wewe ni fasiki.’ Ndipo Mwenyezi Mungu akateremsha: “Je, aliye muumini ni sawa na aliye fasiki? Hawawi sawa.”21 20 Tafsirul-Baghawi Juz. 3, Uk. 343. Na ameiandika Ibn Asakir katika kitabu chake Tarikh Damashq katika wasifu wa Imam Ali Juz. 1, Uk. 99, Namba 137, Chapa ya Kwanza. Na Ahmad bin Hanbal katika Fadhailus-Sahaba Uk. 161, Hadithi ya 230, Chapa ya Kwanza. 21 Tafsirul-Baghawi Juz. 3, Uk. 433. Ameipokea Khatibu al-Baghdad katika kitabu chake Tarikhul-Baghdad Juz. 13, Uk. 321, Namba 7291. Muhibu Tabari katika ar-Riyadh an-Nadhrah Juz. 2, Uk. 206, Chapa ya Pili. Ibn Aatham al-Kufiy aliyefariki miaka ya 314 A.H. ameiandika katika kitabu chake al-Futuhu Juz. 2, Uk. 354, Chapa ya India. Na al-Hafidh al-Mazziy katika kitabu Tahdhibul-Kamal Juz. 8, Uk. 1475. Na al-Mas’ud katika Murujud-Dhahabi Juz. 2, Uk. 357, Chapa ya Misri. 19

Page 19


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 2 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

11:14 AM

Ahlul Bayt ndani ya Tafsiri za Kisunni No.2

SURAT AHZAB Kauli ya Mwenyezi Mungu: “Hakika si mengineyo, Mwenyezi Mungu anataka kuwaondolea uchafu, enyi watu wa nyumba ya Mtume, na kuwatakasa kabisa kabisa.” (Sura Ahzab: 33). Abu Said na jamaa wengine miongoni mwa tabiina akiwemo Mujahid, Qatadah na wengineo wamesema kwamba: Walengwa hapa ni Ali, Fatima, Hasan na Husein. Kutoka kwa Aisha Umul-Muuminina alisema kwamba: “Siku moja Mtume alitoka akawa amejifunika shuka lililodariziwa na manyoya meusi. Akaketi na ghafla akaja Fatima na akamfunika, akaja Ali akamfunika, akaja Hasan akamfunika, akaja Husein naye akamfunika, kisha akasema: “Hakika si mengineyo, Mwenyezi Mungu anataka kuwaondolea uchafu, enyi watu wa nyumba ya Mtume, na kuwatakasa kabisa kabisa.’” Kutoka kwa Ummu Salama mke wa Mtume (s.a.w.w.) amesema kwamba: “Hakika Aya hii iliteremka nyumbani kwangu: “Hakika si mengineyo, Mwenyezi Mungu anataka kuwaondolea uchafu enyi watu wa nyumba ya Mtume..” Mtume wa Mwenyezi Mungu akatuma ujumbe waje Fatima, Ali, Hasan na Husein, walipokuja akasema: ‘Hawa ndio Ahlul-Baiti wangu.’” Nikasema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu! Mimi sio miongoni mwa Ahlul-Baiti? Akanijibu: “Ndiyo, wewe sio inshaallah. “22 Kauli ya Mwenyezi Mungu:

“Hakika Mwenyezi Mungu na malaika wake wanamswalia (wanamtakia rehma) Nabii. Enyi ambao mmeamini! Mswalieni na mumsalimu kwa salamu.” (Sura Ahzab: 56). 22 Tafsirul-Baghawi Juz. 3 katika tafsiri ya Aya hii. Na pia ameipokea Baghawi katika kitabu Misbahus-Sunna Juz. 2, Uk. 200. Na pia Is’afur-Raghibina kwenye pambizo la Nurul-Absar Uk. 82. 20

Page 20


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 2 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

11:14 AM

Ahlul Bayt ndani ya Tafsiri za Kisunni No.2 Abdurahman bin Abi Layla amesema: Kaab bin Ajrah alikutana na mimi na kuniambia: Je nikupe zawadi niliyoisikia kutoka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.)? Nikasema ndio nizawadie. Akasema: Tulimuuliza Mtume wa Mwenyezi Mungu tukasema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu! Tutawaombeaje rehema enyi Ahlul-Baiti? Kwani Mwenyezi Mungu tayari ameshatufundisha namna ya kukusalimu.Akasema (s.a.w.w.): ?????? ???? ??? ????? ???? ?? ????? ??? ????? ??? ??????? ???? ?? ??????? ???? ???? ????. ?????? ???? ??? ????? ???? ?? ????? ??? ????? ??? ??????? ???? ?? ??????? ???? ???? ????. “Semeni: Ewe Mwenyezi Mungu! Mrehemu Muhammad na kizazi cha Muhammad kama ulivyomrehemu Ibrahim na kizazi cha Ibrahim, hakika wewe ni Muhimidiwa Msifiwa. Na mbariki Muhammad na aali Muhammad kama ulivyombariki Ibrahim na aali Ibrahim, hakika wewe ni Muhimidiwa Msifiwa.” Kutoka kwa Ibnu Mas’ud amesema: Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) alisema: “Mtu bora kwangu Siku ya Kiyama ni yule mwenye kunisalia sana.”23 Kauli ya Mwenyezi Mungu:

“Na wale ambao wanawaudhi waumini wanaume na waumini wanawake pasi na wao kufanya, hakika wamebeba dhulma kubwa na dhambi kumbwa.” (Sura Ahzab: 58).

23 Tafsirul-Baghawi Juz. 3, Uk. 467. 21

Page 21


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 2 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

11:14 AM

Ahlul Bayt ndani ya Tafsiri za Kisunni No.2 Muqatil amesema: “Iliteremka kwa ajili ya Ali bin Abu Talib, walikuwa wakimuudhi na kumkashifu.”24

SURAT AS-SHURA Kauli ya Mwenyezi Mungu:

“Sema: Kwa haya siwaombi malipo yoyote kwenu isipokuwa mapenzi katika ndugu. Na anayefanya wema tutamzidishia wema, kwa hakika Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa kusamehe, Mwingi wa shukurani.” (Sura as-Shura: 23). Abdul-Wahid Ahmad al-Malihiy amesema: “Kutoka kwa Bashari kutoka kwa Muhammad bin Ja’far, kutoka kwa Abdul-Malik bin Maysara, amesema: ‘Nilimsikia Taus akisimulia kutoka kwa Ibn Abbas kwamba aliulizwa kuhusu kauli yake (s.w.t.): “Sema: Kwa haya siwaombi malipo yoyote kwenu isipokuwa mapenzi katika ndugu...” Said bin Jubayri akasema: “Hao ni karaba ambao ni aali Muhammad.” Kadhalika wamepokea as-Shaabiy na Taus kutoka kwa Ibn Abbas kwamba alisema: “isipokuwa mapenzi katika ndugu” maana yake muwahifadhi karaba zangu, muwapende na kuuthamini udugu wangu. Na baadhi wamesema: Maana yake ni hakuna jingine ila kuwapenda karaba zangu na kizazi changu na mnithamini kupitia kwao, na hiyo ndio kauli ya Saidi bin Jubayri na Amr bin Shuaybu. Wametofautiana kuhusu karaba zake: Fatima 24 Tafsirul-Baghawi Juz. 3, Uk. 469 22

Page 22


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 2 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

11:14 AM

Ahlul Bayt ndani ya Tafsiri za Kisunni No.2 Zahrau, Ali na watoto wao wawili, na wao ndio walioteremshiwa: “Hakika si mengineyo, Mwenyezi Mungu anataka kuwaondolea uchafu enyi watu wa nyumba ya Mtume..”25

SURAT DUKHAN Kauli ya Mwenyezi Mungu: “Mbingu na ardhi hazikuwalilia, wala hawakupewa muda. “ (Sura Dukhan: 29). Atau amesema: “Kulia kwa mbingu ni ule wekundu wa kwenye ncha zake.” Na As-Sadiy amesema: “Alipouwawa Husein bin Ali (a.s.) mbingu ilimlilia na kilio chake ni wekundu wake.”26 Kauli ya Mwenyezi Mungu:

“Mwenyezi Mungu amekuahidini ngawira nyingi mtakazozichukua, kisha akakutimizeni haya, na akaizuia mikono ya watu isikufikieni, na ili iwe dalili kwa waumini na kukuongozeni njia iliyonyooka.” (Sura al-Fat’hu: 7). 25 Tafsirul-Baghawi Juz. 4, Uk. 111. Ibnu Hanbal ameipokea katika kitabu chake al-Fadhail Uk. 187, Hadithi ya 263. Ibnu Hajar amepokea shairi katika kitabu Sawaiqul-Muhriqah katika mlango wa kumi kutoka kwa Imamu wake, ash-Shafi’i likionyesha wajibu wa kuwapenda na kuwatii Aali Muhammad (a.s.): ?? ??? ????? ???? ???? ???? ??? ?? ???? ?? ?????? ????? ????? ?? ???? ????? ???? ?? ?? ????? ????? ?? ???? ?? Enyi watu wa nyumba ya Mtume wa Mwenyezi Mungu kuwapendeni ni faradhi toka kwa Mwenyezi Mungu iliyoteremshwa katika Qur’ani. Inatosha kwamba ni fahari kubwa kwenu kuwa yule asiyewasalia hana Swala. 26 Tafsirul-Baghawi Juz. 4 Uk. 136. Hili si jambo gumu, kwani wametaja katika tafsiri ya Aya hii kwamba: Muumini anapofariki mbingu na ardhi humlilia muda wa siku arobaini. Na bila shaka Imam Husein (a.s.) ni bwana wa waumini na kinara wao, na hili ni jamabo ambalo riwaya zote zinazozungumzia kufa kishahidi kwa Husein zimeafikiana juu yake. Kwa undani zaidi rejea kitabu KamiluzZiarati cha Ibnu Qawlayhi. 23

Page 23


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 2 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

11:14 AM

Ahlul Bayt ndani ya Tafsiri za Kisunni No.2 Kisa cha Khaybar amekipokea Sahlu bin Saad, Anas na Abu Huraira. Ndipo Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) akatoa habari akasema: “Hakika kesho nitamkabidhi bendera mtu ambaye anampenda Mwenyezi Mungu na Mtume Wake na Mwenyezi Mungu na Mtume Wake wanampenda. Mwenyezi Mungu ataleta ushindi mikononi mwake.” Akamwita Ali bin Abu Talib akamkabidhi bendera na kumwambia: ‘Nenda wala usigeuke nyuma.’” Akafika mji wa Khaybar na ndipo Marhabu aliyekuwa mlinzi wa ngome akatoka na hali amevaa deraya na juu ya kichwa chake kavaa jiwe alilolitoboa mfano wa yai. Ali akajitokeza kumkabili akampiga dharuba iliyopasua jiwe na deraya na kupasua kichwa chake mpaka upanga ukafika wenye magego yake. Na katika riwaya nyingine: “Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) akasema: “Hakika kesho nitamkabidhi bendera mtu ambaye anampenda Mwenyezi Mungu na Mtume Wake na Mwenyezi Mungu na Mtume Wake wanampenda.” Nikamfuata Ali na kumleta huku nikimwongoza kwani alikuwa amepatwa na maradhi ya macho. Mpaka tukafika kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) akamtemea mate na akapona na akamkabidhi bendera. Marhab akatoka na kusema: ?? ????? ????? ???? ????? ???? ??????? ???? ?????? ????? ??????? ???? ??? ??????? ?????? ??????? “Khaibar imeshajua kwamba hakika mimi ni Marhab mwenye silaha kali na komandoo mzoefu. Pindi moto wa vita unapowashwa, mara hufuma mshale na mara hupiga.”

24

Page 24


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 2 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

11:14 AM

Ahlul Bayt ndani ya Tafsiri za Kisunni No.2 Ali akajitokeza kumkabili naye akisema: ??? ???? ?????? ????? ????? ???? ?????? ????? ??????? ??????? ??????? ???? ??????? “Mimi ndiye ambaye mama yangu alinipa jina la Haidari (Simba) Kama simba pori mwenye kutisha Nitakuuweni kwa upanga wangu mauwaji ya kuteketeza. (kama kupima pishi)”27 Kauli ya Mwenyezi Mungu:

“Muhammad Mtume wa Mwenyezi Mungu na walio pamoja naye ni imara mbele ya makafiri na wenye kuhurumiana wao kwa wao, utawaona wakirukuu na kusujudu wakitafuta fadhila za Mwenyezi Mungu na radhi Yake. Alama zao ni katika nyuso zao kwa athari ya kusujudu, huo ndio mfano wao katika Taurati, na mfano wao katika Injili. Kama mmea uliotoa matawi yake, kisha yakautia nguvu, ukawa 27 Tafsirul-Baghawi Juz. 4, Uk. 177. 25

Page 25


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 2 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

11:14 AM

Ahlul Bayt ndani ya Tafsiri za Kisunni No.2 mnene ukasimama sawa sawa juu ya shina lake ukawafurahisha walioupanda, ili awakasirishe makafiri kwa ajili yao. Mwenyezi Mungu amewaahidi walioamini na kutenda mema katika wao msamaha na malipo makubwa.” (Surat al-Fat’ha: 29). Imepokewa kutoka kwa Mubaraka bin Fadhala kutoka kwa Hasan, amesema: “…Utawaona wakirukuu na kusujudu wakitafuta fadhila za Mwenyezi Mungu na radhi Yake.” Ni Ali bin Abu Talib. “Ukawa mnene ukasimama sawa sawa juu ya shina lake” Ni Ali bin Abu Talib, Uislamu uliimarika kwa upanga wake.28

SURAT MUJADILAH Kauli ya Mwenyezi Mungu:

“Enyi mlioamini! Mnaposema siri na Mtume, basi tangulizeni sadaka kabla ya kumsemesha hayo ni bora kwenu na ni safi sana, na ikiwa hamkupata basi Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa kusamehe, Mwenye kurehemu “ (Sura Mujadilah: 12). Mujahid amesema: “Walikatazwa kusema siri na Mtume (s.a.w.w.) mpaka watoe sadaka. Hakuna aliyeweza kusema naye siri ila Ali bin Abu Talib radhi za Mwenyezi Mungu zimwendee, alitoa sadaka ya dinari na akasema naye siri. Ndipo (baada ya sadaka hiyo) ikateremka ruhusa (iliyoondoa 28 Tafsirul-Baghawi Juz. 4, Uk. 186. al-Katib al-Baghdadiy amepokea katika kitabu chake Tarikh Baghdad Juz. 13, Uk. 153, Namba 7131. al-Haskaniy amepokea katika kitabu chake Shawahidut-Tanziil Juz. 2, Uk. 184, Namba 890, Chapa ya Kwanza. 26

Page 26


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 2 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

11:14 AM

Ahlul Bayt ndani ya Tafsiri za Kisunni No.2 sharti la sadaka.). Hivyo Ali alikuwa akisema: “Hakika katika Kitabu cha Mwenyezi Mungu kuna Aya ambayo hakuna yeyote aliyeifanyia kazi kabla yangu, wala hakuna yeyote atakayeifanyia kazi baada yangu, nayo ni Aya ya kusema siri na Mtume.”29 Kauli ya Mwenyezi Mungu:

“Na huwalisha chakula masikini na yatima na mfungwa hali ya kuwa wanakipenda. Tunakulisheni kwa ajili ya radhi za Mwenyezi Mungu tu, hatutaki kwenu malipo wala shukurani.” (Surat al-Insan: 8 - 9). Mujahid na Atau wamepokea kutoka kwa Ibnu Abbas kwamba: Iliteremka kwa ajili ya Ali. Yeye alifanya kazi kwa Myahudi kwa malipo ya shairi kidogo, akachukua theluthi ya shairi akatwanga na kuoka chakula kidogo, kilipoiva akatokea masikini na kuomba, ndipo wakampa chakula chote. Kisha wakaoka theluthi ya pili, kilipoiva alikuja yatima akaomba wakampa chote. Akaoka theluthi ya tatu iliyobaki na kilipoiva alikuja mfungwa toka kwa mushrikina, akaomba nao wakamlisha na kushinda siku hiyo bila kula.30

29 Tafsirul-Baghawi Juz. 4 katika tafsiri ya Aya hii. Na ameiandika an-Nasai katika kitabu Khaswaisu Amiril-Muuminina Uk. 176, Chapa ya Beirut. Na Humawi katika kitabu Faraidus-Samtwayn katika mlango wa 66 wa Samtwi ya Kwanza, Juz. 1, Uk. 358, Chapa ya Beirut. 30 Tafsirul-Baghawi Juz. 4, Uk. 397. Na al-Qunduziy katika Yanabiul-Mawaddah Juz. 1, Uk. 93 na Uk. 94. 27

Page 27


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 2 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

11:14 AM

Ahlul Bayt ndani ya Tafsiri za Kisunni No.2

AHLUL-BAIT (A.S.) NDANI YA TAFSIRI YA ZAMAKHSHARI, INAYOITWA AL-KASHAFU FII HAQAIQIT-TAAWIIL SURAT AALI IMRAN Kauli ya Mwenyezi Mungu: “…Kila mara Zakariya alipoingia Mihrab hukuta vyakula. Akasema: ‘Ewe Maryam, unatoa wapi hivi.’ Akasema: ‘Vinatoka kwa Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu humruzuku amtakaye bila hesabu.” (Aali Imran: 37). Zamakhshari ametaja katika tafsiri yake al-Kashafu anapoifasiri Aya hii tukufu kwamba: “Mtume alipatwa na njaa kipindi cha ukame ndipo Fatima akamfanyia kipaumbele baba yake kwa kumzawadia vipande viwili vya mkate na kipande cha nyama, naye (s.a.w.w.) akavirejesha kwa Fatima na kusema: ‘Chukua ewe binti yangu.’ Alipofunua bakuli akalikuta limejaa mikate na nyama, akapigwa na butwaa na akagundua kwamba vimeteremka kutoka kwa Mwenyezi Mungu. Mtume akamuuliza: ‘Umetoa wapi hivi?’ Akasema: ‘Ni kutoka kwa Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu humpa riziki amtakaye bila hesabu.” Mtume akasema: “Kila sifa njema ni ya Mwenyezi Mungu Ambaye amekufanya kifani wa seyida wa wana wa Israel (Mariam.)” Kisha Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) akawakusanya Ali bin Abu Talib, Hasan na Husein na watu wote wa nyumbani kwake wakala pamoja mpaka wakashiba na chakula kikabakia kama kilivyokuwa. Hivyo Fatima akawagawia majirani zake.31

31 Tafsirul-Kashafu Juz. 1, Uk. 321, Chapa ya Misri ya Mwaka 1948 A.D. Chapa ya Mustafa al-Babi al-Halbiy 28

Page 28


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 2 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

11:14 AM

Ahlul Bayt ndani ya Tafsiri za Kisunni No.2 Kauli ya Mwenyezi Mungu:

“Na watakaokuhoji baada kukufikia elimu hii, waambie: Njooni tuwaite watoto wetu na watoto wenu, na wanawake zetu na wanawake wenu, na nafsi zetu na nafsi zenu, kisha tuombe kwa unyenyekevu tutake laana ya Mwenyezi Mungu iwashukie waongo.” (Sura Aali Imran: 61). Zamakhshari amesema: “Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) alipowaita kwenye maapizano walisema: Mpaka turejee na tutafakari jambo hili. Walipoachana wakamwambia Aqib naye alikuwa ndiye wamfatae katika rai: ‘Ewe mja wa Masihi unasemaje?’ Akasema: ‘Wallahi enyi wakristo nimeshakujulisheni kwamba hakika Muhammad ni Nabii na Mtume, na bila shaka amewajieni na hoja yakinifu kuhusu mtu wenu (Yesu), wallahi katu hakuna watu walioombeana laana na Mtume kisha mkubwa wao akaendelea kuishi au mdogo wao kuzaliwa. Na kama mtafanya hivyo bila shaka tutaangamia, ila ni nyinyi kuendelea kubakia katika imani yenu na dini yenu, nendeni mkamuage mtu huyu na mrejee nchini kwenu.” Ndipo kesho wakaja kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) na Mtume akatoka akiwa amemkumbatia Husein na amemshika mkono Hasan huku Fatima akitembea nyuma yake na Ali akiwa nyuma ya Fatima. Akawaambia: “Mimi nitakapokuwa naomba nyinyi muwe mnaitikia.” 32 Jina la pesa kama vile Dola, Shilingi, Paundi na mfano wa hizo.

29

Page 29


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 2 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

11:14 AM

Ahlul Bayt ndani ya Tafsiri za Kisunni No.2 Askofu wa Najran akasema: “Enyi wakristo! Mimi naziona nyuso hizi kama zitamuomba Mwenyezi Mungu auondoe mlima kutoka mahala pake, atauondoa, msiapizane naye mtaangamia, na hatabaki mkiristo yeyote hapa duniani mpaka siku ya Kiyama.” Wakasema: “Ewe Abul-Qasim! Tumeona tusiapizane na wewe na tukuwache uendelee kuwa katika dini yako nasi tuendelee kubaki katika dini yetu.” Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) akasema: “Mkikataa kufanya maapizano basi msilimu mtapata haki waliyonayo waislamu na mtawajibikiwa na yale yaliyo wajibu kwao.” Wakakataa, ndipo Mtume akawaambia: “Basi hakika mimi nitawafukuzeni.” Wakasema: “Hatuna nguvu ya kupigana vita na waarabu, lakini sisi tunafanya suluhu na wewe usitushambulie kivita na wala usitufukuze na wala usitutoe katika dini yetu. Kwa sharti tukupe kila mwaka Hilla32 elfu mbili: Elfu moja katika mwezi wa Safar na elfu nyingine katika mwezi wa Rajab, na diraya thelathini za kawaida za chuma.” Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) akafanya nao suluhu kwa sharti hilo na akasema: “Naapa kwa Yule Ambaye nafsi yangu imo mikononi mwake, hakika adhabu imeshateremka juu ya watu wa Najran. Na lau wangefanya maapizano wangegeuzwa nyani na nguruwe na bonde lao lingewaka moto. Na Mwenyezi Mungu angeiteketeza Najran na watu wake hata ndege aliyopo juu ya mti. Wala mwaka usingepita wakristo wote wangekuwa wameteketea.”33Pia Zamakhshari amepokea kutoka kwa Aisha kwamba: “Siku moja Mtume alitoka akajifunika shuka lililodariziwa na manyoya meusi. Akaja Hasan akamfunika, kisha akaja Husein akamfunika, akaja Fatima na kisha Ali nao akawafunika, kisha akasema: “Hakika si mengineyo, Mwenyezi Mungu anataka kuwaondolea uchafu, enyi watu 33 Tafsirul-Kashafu Juz. 1, Uk. 326, Chapa ya Misri ya Mwaka 1948 A.D. 30

Page 30


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 2 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

11:14 AM

Ahlul Bayt ndani ya Tafsiri za Kisunni No.2 wa nyumba ya Mtume.� Zamakhshari akajiuliza kwa kusema: Ukiniambia: Hakuwaita kwenye maapizano ila ni kwa ajili ya kutaka kubaini ni nani muongo kati yake na hasimu wake, na kikawaida suala hili ni makhsusi kwake na kwa yule anayemkadhibisha, hivyo nini maana ya yeye kwenda na watoto na wanawake? Nitasema: Hiyo ni kuitia uzito hali yake ya kujiamini na kuwa na yakini na ukweli wa dai lake kiasi kwamba amepata ujasiri wa kuwatoa watu ambao ni vipenzi vyake na ni sehemu ya ini lake, hivyo huku akiwa na imani kwamba hasimu wake ni mwongo hakutosheka na kujitoa yeye mwenyewe tu, bali alitoka nao ili hasimu wake ahiliki pamoja na vipenzi vyake iwapo maapizano yatatimia. Amewahusisha watoto na wanawake kwa sababu wenyewe ndio vipenzi vya mtu na ndio mwambata wa moyo wa mtu, baadhi ya nyakati mtu hujitoa fidia kwa ajili yao na kupigana mpaka kuuwawa kwa ajili yao. Pia walikuwa wakienda nao kimoyo vitani ili wawazuiye kukimbia huku wakiwahami barabara kwa roho zao. Kisha ameanza kuwataja kabla ya nafsi ili abainishe umuhimu wa nafasi yao na ukaribu wao kiasi kwamba hupewa kipaumbele kabla ya nafsi na hivyo mtu hujitoa fidia kwa ajili yao. Na humo mna dalili yenye nguvu kuliko nyingine juu ya ubora wa Watu wa Kishamiya (a.s.), na mna hoja ya wazi juu ya kusihi kwa unabii wa Mtume (s.a.w.w.), kwa sababu hakuna yeyote miongoni mwa watu wa madhehebu yetu na walio nje ya madhehebu yetu aliyepokea kwamba walikubali wito huo (wa kufanya maapizano).34

34 Tafsirul-Kashafu Juz. 1, Uk. 326, Chapa ya Misri ya Mwaka 1948 A.D.

31

Page 31


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 2 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

11:14 AM

Ahlul Bayt ndani ya Tafsiri za Kisunni No.2

SURAT AL-AN’FAL Kauli ya Mwenyezi Mungu:

“Na iogopeni adhabu ambayo haitawapata peke yao wale waliodhulumu nafsi zao miongoni mwenu, na jueni kuwa Mwenyezi Mungu ni Mkali wa kuadhibu.” (Sura al-An’fal: 25). Zamakhshari amesema: “Imepokewa kwamba Zubair siku moja alikuwa akitembea na Mtume (s.a.w.w.) na ghafla Ali (a.s.) akatokeza na Zubairi akamfurahia. Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) akamwambia Zubair: “Unampendaje Ali?” Akajibu: “Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu! Baba yangu na mama yangu ni fidia kwako, hakika mimi nampenda kama nimpendavyo mwanangu au zaidi kuliko mwanangu.” Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) akamwambia: “Utakuwaje wewe utakapotembea usiku kwenda kupambana naye kivita?”35

SURAT TAWBA Kauli ya Mwenyezi Mungu:

“(Tangazo la) Kujitoa Mwenyezi Mungu na Mtume wake kwa wale mlioahidiana nao miongoni mwa mushrikina.” (Sura Tawba: 1). 35.Tafsirul-Kashafu Juz. 2 Uk. 11, Tafsiri ya Surat Anfal, Chapa ya Misri ya Mwaka 1948 A.D. 32

Page 32


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 2 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

11:14 AM

Ahlul Bayt ndani ya Tafsiri za Kisunni No.2 Iliteremka mwaka wa tisa wa hijiriya na ukombozi wa Makka ulikuwa mwaka wa nane. Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) alimtuma Abu Bakr awe kiongozi wa Hija ya msimu wa mwaka wa tisa. Alipokuwa njiani Jibril (a.s.) akateremka na kusema: “Ewe Muhammad! Hafikishi ujumbe wako ila mtu atokanaye na wewe.” Akamtuma Ali na Abu Bakr akarejea kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) na kusema: ‘’Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu! je kimeteremshwa chochote kutoka mbinguni?’’ Mtume (s.a.w.w.) akasema: ‘’Naam.’’36

SURAT YUSUF Kauli ya Mwenyezi Mungu: “Na akasema: Enyi wanangu, msiingie katika mlango mmoja bali ingieni katika milango mbalimbali.” (Sura Yusuf:67). Zamakhshari amesema: “Imepokewa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w.) kwamba alikuwa akiwakinga Hasan na Husein (a.s.) akisema:

?? ??? ?????? ??? ??? ?????? ?????? Nawakinga kupitia maneno timamu ya Mwenyezi Mungu dhidi ya kila jicho baya na dhidi ya kila shetani na jambo litishalo.”37

SURAT MARYAM Kauli ya Mwenyezi Mungu: “Hakika wale ambao wameamini na wakatenda mema Mwingi wa rehema atawajaalia mapenzi.” (Sura Maryam: 96). 36 Tafsirul-Kashafu Juz. 2, Uk. 26, Chapa ya Misri ya Mwaka 1948 A.D. 37 Tafsirul-Kashafu Juz. 2, Uk. 146, 33

Page 33


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 2 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

11:15 AM

Ahlul Bayt ndani ya Tafsiri za Kisunni No.2 Imepokewa kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) alimwambia Ali bin Abu Talib: “Ewe Ali sema: Ewe Mwenyezi Mungu! Nipe hifadhi Kwako na niwekee mapenzi katika nyoyo za waumini.” Ndipo Mwenyezi Mungu akateremsha Aya hii.38

SURAT ZUMARA Kauli ya Mwenyezi Mungu:

“Na anapotajwa Mwenyezi Mungu peke yake nyoyo za wale wasioamini Akhera huchukia, na wanapotajwa wale walio kinyume naye, mara wanafurahi.” (Sura Zumara: 45). Zamakhshari amepokea kwamba Rabiu bin Khaytham – Naye hakuwa msemaji - alipewa khabari za kuuawa Husein (a.s.) na akamkasirikia muuwaje wake. Watu wakasema kwamba hivi sasa ataongea, na hakuzidisha zaidi ya kusema: Bila shaka wameshatenda. Kisha akasoma Aya hii. Na imepokewa kwamba baada ya Aya hii alisema: Ameuawa yule ambaye Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) alikuwa akimkalisha juu ya mapaja yake na kuweka ulimi wake ndani ya kinywa chake.39

38 Tafsirul-Kashafu Juz. 2, Uk. 294, Chapa ya Misri ya Mwaka 1948 A.D. 39 Tafsirul-Kashafu Juz. 3 Uk. 34, Chapa ya Misri ya Mwaka 1948 A.D. 34

Page 34


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 2 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

11:15 AM

Ahlul Bayt ndani ya Tafsiri za Kisunni No.2

SURAT ASH-SHURA Kauli ya Mwenyezi Mungu: “Sema: Kwa haya siwaombi malipo yoyote kwenu isipokuwa mapenzi katika ndugu...” (Surat as-Shura: 23). Imepokewa kwamba: Ilipoteremka walimuuliza: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) ni akina nani hawa ndugu ambao ni wajibu juu yetu kuwapenda. Akasema: “Ni Ali, Fatima na watoto wake wawili.” Na hilo lathibitishwa na ile riwaya isemayo kwamba Ali bin Abu Talib alisema: “Nilimshitakia Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) husuda za watu dhidi yangu. Akasema: ‘Hivi huridhii kuwa mmoja kati ya wane. Wa kwanza kuingia Peponi ni Mimi, Wewe, Hasan, Husein. Wake zetu wakiwa kuliani kwetu na kushotoni kwetu. Na wajukuu zetu wakiwa nyuma ya wake zetu.” Mtume (s.a.w.w.) alisema: “Pepo imeharamishwa juu ya yule aliyewadhulumu Ahlul-Baiti wangu na akaniudhi kwa kuwaudhi kizazi changu. Yeyote atakayemtendea wema yeyote miongoni mwa kizazi cha AbdulMuttalib na ikawa hajalipwa kutokana na wema huo, basi mimi nitamlipa kesho atakapokutana nami Siku ya Kiyama.”40 Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) alisema: “Ehe! atakayekufa na hali awapenda aali Muhammad basi amekufa na hali ni shahidi. Ehe! atakayekufa na hali awapenda aali Muhammad basi amekufa na hali ameghufuriwa. Ehe! atakayekufa na hali awapenda aali Muhammad basi amekufa na hali ametubia. 40 Tafsirul-Kashafu Juz. 3, Uk. 81, Chapa ya Misri ya Mwaka 1948 A.D. 35

Page 35


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 2 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

11:15 AM

Ahlul Bayt ndani ya Tafsiri za Kisunni No.2 Ehe! atakayekufa na hali awapenda aali Muhammad basi amekufa na hali ni muumni aliyekamilika kiimani. Ehe! atakayekufa na hali awapenda aali Muhammad basi amekufa na hali malaika ameshambashiria Pepo, kisha Munkar na Nakir. Ehe! atakayekufa na hali awapenda aali Muhammad atasindikizwa Peponi kama biharusi asindikizwavyo kwenda nyumbani kwa mumewe. Ehe! atakayekufa na hali awapenda aali Muhammad Mwenyezi Mungu atawafungulia mlango malaika wa rehema wawe wenye kulizuru kaburi lake. Ehe! atakayekufa na hali awapenda aali Muhammad basi amefia ndani ya Sunna. Ehe! atakayekufa na hali awachukia aali Muhammad basi amekufa na hali ni kafiri. Ehe! atakayekufa na hali awachukia aali Muhammad hatoipata harufu ya Pepo.�41

SURAT MUJADILAH Kauli ya Mwenyezi Mungu:

“Enyi mlioamini! Mnaposema siri na Mtume, basi tangulizeni sadaka kabla ya kumsemesha hayo ni bora kwenu na ni safi sana, na ikiwa 41 Tafsirul-Kashafu Juz. 3, Uk. 82, Chapa ya Misri ya Mwaka 1948 A.D.

36

Page 36


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 2 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

11:15 AM

Ahlul Bayt ndani ya Tafsiri za Kisunni No.2 hamkupata basi Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa kusamehe, Mwenye kurehemu.” (Sura Mujadilah: 12). Ali bin Abu Talib (radhi za Mwenyezi Mungu zimwendee) alisema: “Hakika katika Kitabu cha Mwenyezi Mungu kuna Aya ambayo hakuna yeyote aliyeifanyia kazi kabla yangu, wala hakuna yeyote atakayeifanyia kazi baada yangu. Nilikuwa na dinari nikaichenji hivyo nikawa natoa dirhamu moja kila nisemapo siri naye.” Ibnu Umar alisema: “Ali alikuwa na mambo matatu, ambayo kuwa nalo moja kati ya hayo ni jambo nilipendalo mno kuliko kuwa na ngamia mwekundu: Kuozwa Fatima, kukabidhiwa bendera Siku ya Khaibar na Aya ya kuongea siri na Mtume.”42

SURAT TAGHABUN Kauli ya Mwenyezi Mungu:

“Bila shaka mali zenu na watoto wenu ni mtihani, na kwa Mwenyezi Mungu kuna malipo makubwa.” (Sura Taghabun: 15). Imepokewa kwamba: “Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) alikuwa akitoa hotuba na ghafla wakaja Hasan na Husein wakiwa wamevaa kanzu mbili nyekundu na hali wakidondoka na kuinuka, akateremka toka mimbarini akawafuata na kuwachukua na kuwaweka mapajani mwake juu ya mimbari, kisha akasema: ‘Mwenyezi Mungu amesema kweli. “Bila shaka mali zenu na watoto wenu ni mtihani,” nilipowaona hawa wawili sikuweza kuvumilia.’ Kisha akaendelea na Khutba yake.’”43 42 Tafsirul-Kashafu Juz. 3, Uk. 211, Chapa ya Misri ya Mwaka 1948 A.D. 43 Tafsirul-Kashafu Juz. 3, Uk. 236, Chapa ya Misri ya Mwaka 1948 A.D. 37

Page 37


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 2 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

11:15 AM

Ahlul Bayt ndani ya Tafsiri za Kisunni No.2

SURAT TAHRIM Kauli ya Mwenyezi Mungu:

“Na Mariam binti Imran aliyejilinda ubikira wake, na tukampulizia humo roho yetu na akayasadikisha maneno ya Mola wake Mlezi, na vitabu vyake na alikuwa miongoni mwa wanyenyekevu. “ (Sura Tahrim: 12). Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) amesema: “Kati ya wanaume wamekamilika wengi na wala hawajakamilika kati ya wanawake ila wanne: Asia binti Muzahim mke wa Firaun, Mariam binti Imran, Khadija binti Khuwaylid na Fatima binti Muhammad.”44

SURAT AL-HAQQAH Kauli ya Mwenyezi Mungu:

“Ili tuifanye ukumbusho kwenu, na sikio lisikialo lisikie.” (Sura alHaqqah: 12). Ilipoteremka Aya hii Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) alimwambia Ali (a.s.): ‘’Nilimwomba Mwenyezi Mungu alifanye hivyo sikio lako ewe 44 Tafsirul-Kashafu Juz. 3, Uk. 250, Chapa ya Misri ya Mwaka 1948 A.D.

38

Page 38


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 2 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

11:15 AM

Ahlul Bayt ndani ya Tafsiri za Kisunni No.2 Ali.’’ Ali alisema: “Baada ya hapo sikuwahi kusahau chochote na wala sikupaswa kusahau.”45

SURAT AL-INSAN Kauli ya Mwenyezi Mungu:

“Na huwalisha chakula masikini na yatima na mfungwa hali ya kuwa wanakipenda. Tunakulisheni kwa ajili ya radhi za Mwenyezi Mungu tu, hatutaki kwenu malipo wala shukurani.” (Sura al-Insan: 8 - 9). Ibnu Abbas alisema: “Hasan na Husein walipatwa na maradhi, babu yao Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) alikwenda kuwaona akiwa pamoja na baadhi ya watu. Wakasema: “Ewe Abal-Hasan ni vizuri lau ukiweka nadhiri kwa ajili ya wanao.” Ndipo Ali, Fatima na mtumishi wao Fidha wakaweka nadhiri kwamba iwapo watapona watafunga siku tatu. Waliweka nadhiri na hali hawana kitu, ndipo Ali akaenda kwa Simon Myahudi wa Khaybar, akakopa toka kwake pishi tatu za ngano. Fatima akachukua pishi moja akatwanga na kuoka mikate mitano kulingana na idadi yao, wakaiweka mbele yao ili wafuturu, mara masikini akafika mlangoni kwao akagonga akisema: “Assalam Alaykum enyi watu wa nyumba ya Muhammad, mimi ni maskini katika watoto wa kiislamu nipeni chakula Mwenyezi Mungu atakupeni chakula cha Peponi.” Wakamfanyia kipaumbele na wao wakalala na hali hawajaonja ila maji tu na wakaamka wakiwa na Swaumu.

45 Tafsirul-Kashafu Juz. 3, Uk. 250, Chapa ya Misri ya Mwaka 1948 A.D. 39

Page 39


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 2 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

11:15 AM

Ahlul Bayt ndani ya Tafsiri za Kisunni No.2 Waliposhinda na Swaumu na kuweka chakula mbele yao mara akafika mlangoni kwao yatima naye wakamfanyia kipaumbele. Na mara mfungwa wa kivita akafika mlangoni kwao siku ya tatu, naye wakamfanyia hivyo hivyo. Asubuhi iliyofuata Ali aliwashika mkono Hasan na Husein na kwenda nao kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.). Alipowatizama na hali wao wawili wakitetemeka kama vifaranga alisema: “Hali niionayo kwenu yaniumiza mno.” Akasimama na kwenda nao, ndipo wakamkuta Fatima akiwa mihrabuni kwake na hali tumbo lake limeshikana na mgongo wake na macho yake yamezama. Hali hiyo ikamuuma sana, ndipo Jibril (a.s.) akateremka na kusema: “Ewe Muhammad pokea, Mwenyezi Mungu anakupa pongezi kwa kitendo cha watu wa nyumba yako.” Jibril (a.s.) akamsomea Sura hii.46

SURAT NASRI Kauli ya Mwenyezi Mungu:

“Basi mtakase Mola Wako kwa sifa njema na umuombe msamaha, hakika yeye ndiye apokeaye sana toba.” (Sura Nasri: 3). Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) alimwita Fatima (a.s.) na kumwambia: “Ewe binti yangu mpendwa! Nafsi yangu inajiomboleza.” Fatima akalia. Akamwambia: “Usilie, kwani hakika wewe ndiye wa kwanza kukutana nami miongoni mwa watu wangu.”47

46 Tafsirul-Kashafu Juz. 3, Uk. 297, Chapa ya Misri ya Mwaka 1948 A.D. 47 Tafsirul-Kashafu Juz. 3, Uk. 365. Nimemaliza mchakato juu ya tafsiri hii usiku wa Iddi ya mwaka 1425 A.H. katika Jiji la Qum Takatifu, saa tisa usiku.

40

Page 40


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 2 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

11:15 AM

Ahlul Bayt ndani ya Tafsiri za Kisunni No.2

AHLUL-BAIT (A.S.) NDANI YA TAFSIRI YA RAZI, INAYOITWA AT-TAFSIRU AL-KABIR AU MAFATIHUL-GHAYBI SURAT AL-FATIHA Kauli ya Mwenyezi Mungu:

“Kwa jina la Mwenyezi Mungu Mwingi wa rehema Mwenye kurehemu.” (Sura Al-Fatiha: 1). Kusoma Bismillahi kwa sauti: Mas’ala ya tisa katika hoja ya tano: Bayhaqiy amepokea katika kitabu Sunanul-Kubra kutoka kwa Abu Huraira kwamba: “Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) alikuwa akisoma Bismilahi Rahman Rahim kwa sauti katika Sala. Kisha Sheikh Bayhaqiy amepokea kwamba Umar bin Khattab, Ibnu Abbas, Ibnu Umar na Ibnu Zubair walikuwa wakiisoma kwa sauti.” Ama Ali bin Abu Talib yeye imethibiti kwa tawaturi kwamba alikuwa akisoma Bismillahi kwa sauti, na yule mwenye kumfuata Ali katika dini yake bila shaka huyo ndiye aliyeongoka. Na dalili juu ya hilo (kuwa bila shaka ameongoka) ni kauli ya Mtume (s.a.w.w.): “Ewe Mwenyezi Mungu! Iweke haki pamoja na Ali vyovyote awavyo.”48

48 At-Tafsiru al-Kabir cha Razi Juz. 1 Uk. 205, Chapa ya MaktabatutTawfiyqiyyah, Uhakiki wa Imad Zakiyyu al-Barudiy. Yapasa utambue ni hili tu ndilo nililofaidika nalo kutoka katika chapa hii iliyotajwa. 41

Page 41


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 2 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

11:15 AM

Ahlul Bayt ndani ya Tafsiri za Kisunni No.2

SURAT AL-BAQARAH Kauli ya Mwenyezi Mungu:

“Na akamfundisha Adam majina yote, kisha akaonyesha mbele ya Malaika, na akasema: Niambieni majina ya hawa ikiwa mnasema kweli.” (Sura Al-Baqarah: 31). Kutoka kwa as-Shaabiy amesema: “Nilikuwa kwa Hajjaj, mara akaletwa Yahya bin Yaamur mwanafiqhi wa huko Khurasan akiwa amefungwa pingu za chuma. Hajjaj akamwambia: “Wewe umedai kwamba Hasan na Husein ni kizazi cha Mtume wa Mwenyezi Mungu?” Akasema ndio. Hajjaj akasema: “Niletee dalili ya wazi toka katika Kitabu cha Mwenyezi Mungu la sivyo nitakukatakata kiungo kimoja baada ya kingine.” Akasema: “Ewe Hajjaj, nitakuletea ya wazi iliyo bayana toka katika Kitabu cha Mwenyezi Mungu.” As-Shaabiy anasema: Nikashangazwa na ujasiri wake kwa kusema: Ewe Hajjaj. Ndipo Hajjaj akamwambia: “Usiniletee Aya hii: ‘Tuwaite watoto zetu na watoto zenu.. “ Akamwambia: “Nitakuletea Aya iliyo wazi toka katika Kitabu cha Mwenyezi Mungu, nayo ni kauli yake: “Na Nuh tulimwongoza zamani na katika kizazi chake, Daud na Sulaiman na Ayub na Yusuf na Musa na Harun. Na hivyo ndivyo tuwalipavyo wafanya wema. Na Zakaria na Yahya na Isa na Ilyasa, wote walikuwa miongoni mwa watu wema.” (Sura An’aam:84 - 85). Nani aliyekuwa baba wa Isa na hali kaunganishwa na kizazi cha Nuh?” As-Shaabiy anasema: “Akainamisha kichwa muda kidogo kisha akainua kichwa na kusema: “Kana kwamba mimi sijawahi kuisoma Aya hii toka 42

Page 42


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 2 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

11:15 AM

Ahlul Bayt ndani ya Tafsiri za Kisunni No.2 katika Kitabu cha Mwenyezi Mungu. Mfungueni pingu yake na mpeni kiasi kadhaa cha mali.49 Bedui mmoja alimwendea Husein (a.s.) akamsalimu na kumwomba haja yake. Akasema: “Nilimsikia babu yako akisema: “Muombapo haja iombeni toka kwa mmoja kati ya watu hawa wanne: Ima mwarabu sharifu au bwana mkarimu, aliyehifadhi Qur’ani au mwenye uso wenye mvuto.” Ama kuhusu waarabu bila shaka wamepata sharafu kupitia babu yako. Ama ukarimu ninyi ndio chanzo chake na ndio tabia yenu. Ama Qur’ani ni ndani ya nyumba zenu ndimo ilimoshukia. Ama uso wenye mvuto ni kwamba mimi nilimsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) akisema: Mkitaka kunitazama mtazameni Hasan na Husein.” Husein (a.s.) akamwambia: “Ni ipi haja yako?” Akaiandika juu ya ardhi. Husein (a.s.) akamwambia: “Nilimsikia baba yangu Ali (a.s.) akisema: ‘Thamani ya kila mtu ni kwa kadiri ya mazuri ayatendayo.’ Na nilimsikia babu yangu akisema: ‘Wema ni kwa kadiri ya maarifa.’ Hivyo nakuuliza maswali matatu ukiweza kujibu vizuri jibu moja utapata theluthi ya haja yako kutoka kwangu, na ukijibu mawili utapata theluthi mbili na ukijibu matatu utapata haja yako yote toka kwangu. Na hapa nimebeba fuko la pesa toka Iraq. Akasema: “Uliza na wala hakuna ujanja na nguvu ila kutoka kwa Mwenyezi Mungu.” Akasema (a.s.): “Ni amali ipi iliyo bora?” Bedui akajibu: “Kumwamini Mwenyezi Mungu.” Akasema (a.s.): “Kipi kitakachomwokoa mja asihiliki?” Bedui akajibu: “Kumtumainia Mwenyezi Mungu.” Akasema (a.s.): “Kitu gani humpamba mtu?” Bedui akajibu: “Elimu yenye hekima.” Akasema (a.s.): “Akikosa hilo?” Bedui akajibu: “Awe na ukarimu.” 49 At-Tafsiru al-Kabir cha Razi Juz. 2, Uk. 194, Chapa ya Darul-Kutubi alIlmiyyah. 43

Page 43


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 2 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

11:15 AM

Ahlul Bayt ndani ya Tafsiri za Kisunni No.2 Akasema (a.s.): “Akikosa hilo?” Bedui akajibu: “Awe fukara mvumilivu.” Akasema (a.s.): “Akikosa hilo?” Bedui akajibu: “Basi asubiri kimondo kutoka mbinguni kimuunguze.” Husein akacheka na kumpa fuko la fedha.50 Kauli ya Mwenyezi Mungu:

“Na katika watu yuko auzaye nafsi yake kwa kutaka radhi ya Mwenyezi Mungu, na Mwenyezi Mungu ni Mpole kwa waja.” (Sura al-Baqarah: 207). Iliteremka kwa ajili ya Ali bin Abu Talib (a.s.) alilala juu ya kitanda cha Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) usiku aliotoka kwenda pangoni. Imepokewa kwamba alipolala juu ya kitanda chake Jibril (a.s.) alisimamam kichwani kwake na Mikail (a.s.) miguuni kwake na hali Jibril akinadi: “Pongezi pongezi! Nani mfano wako ewe Ali bin Abu Talib, Mwenyezi Mungu anajionea fahari kwako mbele ya Malaika.” Ndipo ikateremka Aya hii.51 Kauli ya Mwenyezi Mungu:

“Hao Mitume tumewatukuza baadhi yao zaidi kuliko wengine.” (Sura al-Baqarah: 253). Al-Bayhaqiy amepokea katika kitabu Fadhailus-Sahaba kwamba alitokeza Ali kwa mbali, ndipo Mtume akasema: “Huyu ni bwana wa Waarabu.” Aisha akasema: “Hivi wewe sio bwana wa Waarabu?” Mtume akasema: “Mimi ni bwana wa viumbe vyote na yeye ni bwana wa Waarabu.”52 50 At-Tafsiru al-Kabir cha Razi Juz. 2, Uk. 198, 51 At-Tafsiru al-Kabir cha Razi Juz. 5, Uk. 204. 52 At-Tafsiru al-Kabir cha Razi Juz. 6, Uk. 198. 44

Page 44


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 2 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

11:15 AM

Ahlul Bayt ndani ya Tafsiri za Kisunni No.2 Kauli ya Mwenyezi Mungu:

“Wale watoao mali zao usiku na mchana kwa siri na dhahiri, wana ujira wao kwa Mola wao Mlezi; wala haitakuwa hofu juu yao wala wao hawatahuzunika.” (Surat al-Baqarah: 274). Ibnu Abbas amesema: “Ali bin Abu Talib alikuwa na dirhamu nne hakuwa anamiliki nyingine zaidi ya hizo, akatoa sadaka dirhamu moja usiku na nyingine mchana, nyingine kwa siri na nyingine kwa dhahiri. Mtume (s.a.w.w.) akasema: “Kitu gani kilichokupelekea kufanya hivyo?” Akasema: Yaliyoniwajibisha kufanya hivyo ni yale aliyoniahidi Mola wangu Mlezi. Mtume akasema: “Umeshapata hilo.” Ndipo ikateremka Aya hii.53

SURAT AALI IMRAN Kauli ya Mwenyezi Mungu:

“Na Malaika waliposema: Ewe Mariam, hakika Mwenyezi Mungu amekuchagua na amekutakasa, na amekuchagua kuliko wanawake wa ulimwenguni.” (Sura Aali Imran: 42). Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) alisema: “Yakutosha katika wanawake wa ulimwenguni: Maryam, Asia mke wa Firaun, Khadija na 53 At-Tafsiru al-Kabir cha Razi Juz. 7, Uk. 83. 45

Page 45


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 2 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

11:15 AM

Ahlul Bayt ndani ya Tafsiri za Kisunni No.2 Fatima binti Muhammad.”54 Kauli ya Mwenyezi Mungu:

“Na watakaokuhoji baada kukufikia elimu hii, waambie: Njooni tuwaite watoto wetu na watoto wenu, na wanawake zetu na wanawake wenu, na nafsi zetu na nafsi zenu, kisha tuombe kwa unyenyekevu tutake laana ya Mwenyezi Mungu iwashukie waongo.” (Sura Aali Imran: 61). Imepokewa kwamba alipotoa dalili kwa wakristo wa Najran nao wakang’ang’ania ujinga wao aliwaambia: “Hakika Mwenyezi Mungu ameniamuru kwamba msipokubali hoja niapizane nanyi.” Wakasema: “Ewe Abal-Qasim! mpaka turejee na tutafakari jambo hili kisha kesho tutakuja tena.” Waliporejea wakamwambia Aqib naye alikuwa ndiye wamfuatae katika rai: “Ewe mja wa Masihi unasemaje?” Akasema: “Wallahi enyi wakristo, mmeshajua kwamba hakika Muhammad ni Nabii na Mtume, na wallahi katu hakuna watu walioombeana laana na Mtume kisha mkubwa wao akaendelea kuishi au mdogo wao kuzaliwa. Na kama mtafanya hivyo bila shaka tutaangamia.” Na Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) alikuwa katoka akiwa kajitanda kishamiya kilichodariziwa na manyoya meusi huku kamkumbatia Husein na amemshika mkono Hasan huku Fatima akitembea nyuma yake 54 At-Tafsiru al-Kabir cha Razi Juz. 8, Uk. 53. 46

Page 46


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 2 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

11:15 AM

Ahlul Bayt ndani ya Tafsiri za Kisunni No.2 na Ali akiwa nyuma ya Fatima. Akawaambia: “Mimi nitakapokuwa naomba nyinyi muwe mnaitikia.” Askofu wa Najran akasema: “Enyi wakristo! Mimi naziona nyuso hizi kama zitamuomba Mwenyezi Mungu auondoe mlima kutoka mahala pake, atauondoa, msiapizane naye mtaangamia, na hatabaki mkiristo yeyote hapa duniani mpaka Siku ya Kiyama.” Wakasema: “Ewe Abul-Qasim! Tumeona tusiapizane na wewe na tukuwache uendelee kuwa katika dini yako nasi tuendelee kubaki katika dini yetu.” Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) akasema: “Mkikataa kufanya maapizano basi msilimu mtapata haki waliyonayo waislamu na mtawajibikiwa na yale yaliyo wajibu kwao.” Wakakataa, ndipo Mtume akawaambia: “Basi hakika mimi nitawafukuzeni kwa kuwauwa.” Wakasema: “Hatuna nguvu ya kupigana vita na waarabu, lakini sisi tunafanya suluhu na wewe usitushambulie kivita na wala usitutoe katika dini yetu. Kwa sharti tukupe kila mwaka Hilla55 elfu mbili: Elfu moja katika mwezi wa Safar na elfu nyingine katika mwezi wa Rajab, diraya thelathini za chuma za kawaida.” Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) akafanya nao suluhu kwa sharti hilo.56 Fakhru Razi amesema: Aya hii inaonyesha kwamba Hasan na Husein (a.s.) walikuwa watoto wa Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.). Aliwaahidi kwamba atawaita watoto wake, ndipo akaja na Hasan na Husein hivyo ikawajibika kuwa watoto wake. Na linalotia nguvu kauli hii ni kauli ya 55 Jina la pesa kama vile Dola, Shilingi, Paundi na mfano wa hizo. 56 At-Tafsiru al-Kabir cha Razi Juz. 8, Uk. 80. Razi katika riwaya hii ameweka maelezo kwamba: “Tambua kwamba riwaya hii usahihi wake ni sawa na yenye itifaki baina ya wanatafsiri na wanahadithi.” 47

Page 47


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 2 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

11:15 AM

Ahlul Bayt ndani ya Tafsiri za Kisunni No.2 Mwenyezi Mungu iliyopo katika Surat An’aam: “Na Nuh tulimwongoza zamani na katika kizazi chake, Daud na Sulaiman na Ayub na Yusuf na Musa na Harun. Na hivyo ndivyo tuwalipavyo wafanya wema. Na Zakaria na Yahya na Isa na Ilyasa, wote walikuwa miongoni mwa watu wema.” (Sura An’aam:84 - 85). Na yajulikana kwamba Isa amenasibika kwa Ibrahim (a.s.) kupitia mama na si baba. Kauli ya Mwenyezi Mungu:

“Na shikamaneni na kamba ya Mwenyezi Mungu nyote na wala msifarakane. Na kumbukeni neema ya Mwenyezi Mungu iliyo juu yenu.” (Surat Aali Imran: 103). Imepokewa kutoka kwa Abu Said al-Khudriy kutoka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) kwamba alisema: “Hakika mimi nawaachieni vizito viwili kati yenu: Kitabu cha Mwenyezi Mungu kamba iliyonyooka toka mbinguni hadi ardhini. Na kizazi changu Ahlul-Baiti wangu.”57 Kauli ya Mwenyezi Mungu:

“Hakika wale waliokimbia miongoni mwenu siku yalipokutana makundi mawili, ni shetani ndiye aliyewatelezesha kwa sababu ya baadhi ya waliyoyachuma..” (Surat Aali Imran: 155). Razi amesema: “Muradi ni wale watu waliokimbia vitani Siku ya Uhudi. Muhammad bin Is’haqa ametaja kwamba theluthi ya watu walikimbia vitani na miongoni mwa waliokimbia vitani hapo ni Umar bin Khattab na 57 At-Tafsiru al-Kabir cha Razi Juz. 8 Uk. 162. 48

Page 48


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 2 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

11:15 AM

Ahlul Bayt ndani ya Tafsiri za Kisunni No.2 pia Uthman, yeye alikimbia pamoja na watu wawili miongoni mwa Maansari. Walikimbia mpaka wakafika eneo la mbali kabisa kisha wakarejea baada ya siku tatu. Mtume wa Mwenyezi Mungu akawaambia:”58 ????

SURAT NISAI Kauli ya Mwenyezi Mungu:

“Enyi watu! Mcheni Mola wenu Mlezi ambaye amewaumba kutokana na nafsi moja na akaumba kutokana na hiyo wa pili wake.” (Sura Nisai: 1). Mtume wa Mwenyezi Mungu alisema: “Fatima ni pande la nyama yangu. Huniudhi yale yanayomudhi yeye.”59

SURAT AL-MAIDA Kauli ya Mwenyezi Mungu:

“Hakika walii wenu hasa ni Mwenyezi Mungu na Mtume wake na wale walioamini ambao husimamisha Swala na hutoa Zaka wakiwa wamerukui.” (Sura Maida: 55). 58 At-Tafsiru al-Kabir cha Razi Juz. 9, Uk. 50. 59 At-Tafsiru al-Kabir cha Razi Juz. 9, Uk. 160. 49

Page 49


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 2 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

11:15 AM

Ahlul Bayt ndani ya Tafsiri za Kisunni No.2 Imepokewa kutoka kwa Abu Dharr kwamba alisema: “Hakika siku moja niliswali pamoja na Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) Swala ya Adhuhuri, muombaji akaomba msikitini na hakuna yeyote aliyempa, ndipo muombaji akainua mikono yake mbinguni na kusema: “Ewe Mwenyezi Mungu shuhudia kwamba bila shaka mimi nimeomba ndani ya msikiti wa Mtume wa Mwenyezi Mungu na sijapewa chochote na yeyote.” Kipindi hicho Ali alikuwa amerukuu ndipo akamwashiria kwenye chanda chake cha kulia kilichokuwa na pete. Muombaji alikwenda na kuchukua pete toka kwenye chanda chake na hali Mtume akitizama kwa macho yake. Mtume akasema: Ewe Mwenyezi Mungu! Ndugu yangu Musa alikuomba; akasema:

“Ee Mola wangu! Nipanulie kifua changu. Na unifanyie wepesi kazi yangu. Na ufungue fundo katika ulimi wangu. Wapate kufahamu kauli yangu. Na uniwekee waziri katika jamaa zangu. Ndugu yangu Harun. Nitie nguvu kupitia yeye. Na umshirikishe katika kazi yangu.” (Sura Twaha: 25 – 32), ukamteremshia Qur’ani yenye kutamka: Akasema: “Karibuni tutautia nguvu mkono wako kwa ndugu yako na tutakupeni ushindi..” (Sura al-Qasas: 35). Ewe Mwenyezi Mungu! Na mimi ni Muhammad Nabii Wako na chaguo Lako. Nipanulie kifua changu. Na unifanyie wepesi kazi yangu. Na uniwekee waziri katika jamaa zangu. Ndugu yangu Ali. Nitie nguvu kupitia yeye.”

50

Page 50


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 2 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

11:15 AM

Ahlul Bayt ndani ya Tafsiri za Kisunni No.2 Abu Dhari anasema: “Wallahi kabla Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) hajamaliza Jibril akateremka na kusema: Ewe Muhammad soma: “Hakika walii wenu hasa ni Mwenyezi Mungu na Mtume wake na wale walioamini ambao husimamisha Swala na hutoa Zaka wakiwa wamerukui.”60 Kauli ya Mwenyezi Mungu:

“Ewe Mtume! Fikisha uliyoteremshiwa kutoka kwa Mola wako; na kama hutafanya, basi utakuwa hukufikisha ujumbe Wake. Na Mwenyezi Mungu atakulinda na watu. Hakika Mwenyezi Mungu hawaongozi watu makafiri.” (Sura Maida: 67). Kutoka kwa Ibnu Abbas na Barau bin Azib wamesema: “Aya hii iliteremka kuonyesha fadhila za Ali bin Abu Talib (a.s.). ilipoteremka Aya hii Mtume alimshika mkono Ali na kusema: “Ambaye mimi nina mamlaka juu yake basi huyu ni mwenye mamlaka juu yake. Ewe Mwenyezi Mungu mpende yule atakayempenda na mfanyie uadui yule atakayemfanyia uadui.” Umar bin Khattab akamwendea na kumwambia: “Hongera ewe mwana wa Abu Talib, umekuwa mwenye mamlaka juu ya kila muumini wa kiume na wa kike.”61

60 At-Tafsiru al-Kabir cha Razi Juz. 12, Uk. 26. 61 At-Tafsir al-Kabir cha Razi Juz. 12, Uk. 48. 51

Page 51


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 2 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

11:15 AM

Ahlul Bayt ndani ya Tafsiri za Kisunni No.2

SURAT AL-AN’AAM Kauli ya Mwenyezi Mungu: “Na Nuh tulimwongoza zamani na katika kizazi chake, Daud na Sulaiman na Ayyub na Yusuf na Musa na Harun. Na hivyo ndivyo tuwalipavyo wafanya wema. Na Zakaria na Yahya na Isa na Ilyasa, wote walikuwa miongoni mwa watu wema.” (Sura An’aam:84 - 85). Aya hii inaonyesha kwamba Hasan na Husein (a.s.) ni katika kizazi cha Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.), kwa sababu Mwenyezi Mungu amemfanya Isa katika kizazi cha Ibrahim (a.s.) japokuwa hanasibiki kwa Ibrahim ila kupitia mama. Kadhalika Hasan na Husein (a.s.) ni katika kizazi cha Mtume wa Mwenyezi Mungu. Japokuwa wananasibika kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) kupitia mama lakini imewajibika wao kuwa miongoni mwa kizazi chake.62

SURAT TAWBA Kauli ya Mwenyezi Mungu:

“Je, mnafanya kuwanywesha mahujaji na kuamirisha msikiti mtukufu ni sawa na yule aliyemwamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho na akapigana jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu? Hawawi sawa mbele ya Mwenyezi Mungu na Mwenyezi Mungu hawaongozi watu madhalimu.” (Sura Tawba: 19). 62 At-Tafsir al-Kabir cha Razi Juz. 13, Uk. 66. 52

Page 52


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 2 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

11:15 AM

Ahlul Bayt ndani ya Tafsiri za Kisunni No.2 Talha bin Shayba, Abbas na Ali kila mmoja alijigamba. Talha akasema: ‘Mimi ndio mtunza Nyumba funguo zimo mikononi mwangu na hata nikitaka nalala humo.’ Abbas akasema: ‘Mimi ndiye mgawaji wa maji na msimamizi wake.’ Ali akasema: ‘Mimi ndiye mwanajihadi.’ Ndipo Mwenyezi Mungu akateremsha Aya hii.63

SURAT HUD Kauli ya Mwenyezi Mungu: “Basi je, aliye na dalili wazi itokayo kwa Mola wake na anaifuata na shahidi atokaye kwake…..” (Sura Hud: 17). Makusudio ya Shahidi hapa ni Ali bin Abu Talib (a.s.).64

SURAT AR-RAAD Kauli ya Mwenyezi Mungu: “Hakika wewe ni mwonyaji tu. Na kila kaumu ina wa kuwaongoza.” (Surat ar-Raad: 7). Mwonyaji ni Mtume (s.a.w.w.) na Mwongozaji ni Ali. Ibnu Abbas amesema: “Ilipoteremka aya hii, Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) aliweka mkono wake juu ya kifua chake na kusema: ‘Mimi ndiye mwonyaji.’ Kisha akaashiria mkono wake kwenye bega la Ali bin Abu Talib na kusema: ‘Ali wewe ndiye mwongozaji. Kupitia kwako wataongoka wenye kutaka kuongoka baada yangu.”65 63 At-Tafsir al-Kabir cha Razi Juz. 16, Uk. 11. 64 At-Tafsiru al-Kabir cha Razi Juz. 17, Uk. 201.

65 At-Tafsir al-Kabir cha Razi Juz. 19, Uk. 14. 53

Page 53


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 2 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

11:15 AM

Ahlul Bayt ndani ya Tafsiri za Kisunni No.2

SURAT TWAHA Kauli ya Mwenyezi Mungu: “Twaha.” (Sura Twaha: 1). Imesimuliwa kutoka kwa Jafar as-Sadiq (a.s.) kwamba Twa ni utakaso wa Ahlul-Bait. Na Ha ni uongofu wao.66

SURAT HAJJ Kauli ya Mwenyezi Mungu:

“Hawa mahasimu wawili waliohasimiana kwa ajili ya Mola wao...” (Surat Hajj: 19). Amenisimulia Qays bin Ubada kutoka kwa Abu Dharr kwamba alikuwa akiapa kuwa Aya hii iliteremka kwa ajili ya watu sita miongoni mwa Maquraishi waliojitokeza kupambana Siku ya Badri: Hamza, Ali na Ubayda bin al-Harith, Utbatu na Shayabatu watoto wa Rabiu na Walid bin Utbatu. Na kwamba Ali alisema: “Mimi ndiye wa awali ambaye atapiga magoti mbele ya Mwenyezi Mungu Siku ya Kiyama kwa ajili ya uhasimu.”67

66 At-Tafsir al-Kabir cha Razi Juz. 22, Uk. 2. 67 At-Tafsir al-Kabir cha Razi Juz. 23, Uk. 21. 54

Page 54


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 2 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

11:15 AM

Ahlul Bayt ndani ya Tafsiri za Kisunni No.2

SURAT AHZAB Kauli ya Mwenyezi Mungu:

“Hakika Mwenyezi Mungu na malaika wake wanamswalia (wanamtakia rehma) Nabii. Enyi ambao mmeamini! Mswalieni (Mtakieni rehma) na mumsalimu kwa salamu.” (Sura Ahzab: 56). Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) aliulizwa ni ipi namna ya kukusalia ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu? Mtume akasema: ‘’Semeni: ?????? ???? ??? ????? ???? ?? ????? ??? ????? ??? ??????? ???? ?? ???????. ????? ??? ????? ???? ?? ????? ??? ????? ??? ??????? ???? ?? ??????? ???? ???? ????. “ “Ewe Mwenyezi Mungu! Mrehemu Muhammad na aali Muhammad kama ulivyomrehemu Ibrahim na aali Ibrahim. Na mbariki Muhammad na aali Muhammad kama ulivyombariki Ibrahim na aali Ibrahim, hakika Wewe ni Muhimidiwa Msifiwa.’’

SURAT GHAFIR Kauli ya Mwenyezi Mungu:

“Na akasema mtu muumini aliyekuwa mmoja wa watu wa Firaun anayeficha imani yake; je, mtamuuwa mtu kwa sababu tu anasema Mola wangu Mlezi ni Mwenyezi Mungu?” (Sura Ghafir: 28). 55

Page 55


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 2 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

11:15 AM

Ahlul Bayt ndani ya Tafsiri za Kisunni No.2 Imepokewa kutoka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) kwamba alisema: “Wakweli ni watatu: Habibu Najjari muumini toka aali Yasin, Muumini toka aali Firaun ambaye alisema: “je, mtamuuwa mtu kwa sababu tu anasema Mola wangu Mlezi ni Mwenyezi Mungu?” na watatu ni Ali bin Abu Talib naye ndiye mbora wao.”68

SURAT AS-SHURA Kauli ya Mwenyezi Mungu: “Sema: Kwa haya siwaombi malipo yoyote kwenu isipokuwa mapenzi katika ndugu...” (Sura as-Shura: 23). Razi amesema: Mwandishi wa kitabu cha tafsiri al-Kashafu amenukuu kutoka kwa Mtume (s.a.w.w.) kwamba alisema: “Ehe! atakayekufa na hali awapenda aali Muhammad basi amekufa na hali ni shahidi. Ehe! atakayekufa na hali awapenda aali Muhammad basi amekufa na hali ameghufuriwa. Ehe! atakayekufa na hali awapenda aali Muhammad basi amekufa na hali ametubia. Ehe! atakayekufa na hali awapenda aali Muhammad basi amekufa na hali ni muumni aliyekamilika kiimani. Ehe! atakayekufa na hali awapenda aali Muhammad basi amekufa na hali malaika ameshambashiria Pepo, kisha Munkar na Nakir. Ehe! atakayekufa na hali awapenda aali Muhammad atasindikizwa Peponi kama biharusi asindikizwavyo kwenda nyumbani kwa mumewe. Ehe! atakayekufa na hali awapenda aali Muhammad Mwenyezi Mungu 68 At-Tafsiru al-Kabir cha Razi Juz. 27, Uk. 57. 56

Page 56


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 2 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

11:15 AM

Ahlul Bayt ndani ya Tafsiri za Kisunni No.2 atamfungulia milango miwili ya Pepo kaburini. Ehe! atakayekufa na hali awapenda aali Muhammad Mwenyezi Mungu atawafanya malaika wa rehema wawe wenye kulizuru kaburi lake. Ehe! atakayekufa na hali awapenda aali Muhammad basi amefia ndani ya Sunna. Ehe! atakayekufa na hali awachukia aali Muhammad basi amekufa na hali ni kafiri. Ehe! atakayekufa na hali awachukia aali Muhammad hatoipata harufu ya Pepo.”69 Haya ndiyo aliyoyapokea mwandishi wa al-Kashafu. Na mimi nasema: “Hakuna shaka kwamba Fatima, Ali, Hasan na Husein walikuwa na uhusiano wa nguvu mno na Mtume wa Mwenyezi Mungu. Na jambo hili ni yakini kwa nukuu mutawatiri hivyo ikawajibika wao wawe ndio aali zake. “Pia watu wametofautiana kuhusu Aali zake, wapo waliosema ni wale karaba zake na wengine wakasema ni umma wake. Tukisema karaba zake ndio Aali basi wao (Ali, Fatima, Hasan na Husein) ndio Aali. Na tukisema Aali ni umma wake uliokubali utume wake bado vilevile wao (Ali, Fatima, Hasan na Husein) ndio Aali zake. Hivyo inathibiti kwamba kwa kipimo chochote kile bado wao ni Aali zake.”70 Lakini je wasiokuwa wao nao wanaingia chini ya tamko Aali? Ni kwamba mwandishi wa Tafsirul-Kashafu amepokea kwamba ilipoiteremka Aya hii palisemwa: “Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu! Ni akina nani hawa karaba zako tuliowajibishwa kuwapenda?” Akajibu: “Ali, 69 At-Tafsiru al-Kabir cha Razi Juz. 27, Uk. 166, amenukuu kutoka katika tafsiri al-Kashafu. 70 At-Tafsiru al-Kabir cha Razi Juz. 27, Uk. 66. 57

Page 57


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 2 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

11:15 AM

Ahlul Bayt ndani ya Tafsiri za Kisunni No.2 Fatima na watoto wao wawili.” Hivyo imethibiti kwamba hawa ndio karaba wa Mtume (s.a.w.w.). na hili likithibiti inawajibika taadhima ya ziada iwe makhsusi kwao. Na hilo linathibitishwa na mambo mane: Kwanza: Kauli ya Mwenyezi Mungu: “Mapenzi katika ndugu.” Pili: Hamna shaka kwamba Mtume (s.a.w.w.) alikuwa akimpenda sana Fatima (a.s.), akasema: “Fatima ni pande la nyama yangu, huniudhi yale yanayomuudhi.” Na imethibiti kwa nukuu mutawatiri kutoka kwa Mtume Muhammad (s.a.w.w.) kwamba alikuwa akiwapenda Ali, Hasan na Husein. Likithibiti hilo inawajibika mfano wa hilo kwa umma wote (yaani umma wote uwapende) kwa mujibu wa kauli yake (s.a.w.w.): “Mfuateni ili mpate kuongoka.”71 Na kauli yake (s.w.t.): “Sema: Ikiwa nyinyi mnampenda Mwenyezi Mungu basi nifuateni Mwenyezi Mungu atawapenda”72 Na kauli yake (s.w.t.): “Bila shaka mnao mfano mwema kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu”73 Tatu: Hakika dua kwa ajili ya Aali ni hadhi adhimu, na kwa ajili hiyo ameifanya dua hii kuwa ni hitimisho la Tashahudi katika Swala. Nayo ni kusema: “Ewe Mwenyezi Mungu! Msalie Muhammad na Aali Muhammad na mrehemu Muhammad na Aali Muhammad.” Taadhima hii haijapatikana katika haki za mwingine asiyekuwa Aali. Hayo yote yanaonyesha kwamba kuwapenda Aali Muhammad ni wajibu. Imam Shafi amesema:

? ???? ??? ?????? ?????? ?????? 71 Sura Aaraf: 158. 72 Sura Aali Imran: 31. 73 Sura Ahzab: 21. 58

Page 58


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 2 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

11:15 AM

Ahlul Bayt ndani ya Tafsiri za Kisunni No.2 “Ewe uliye juu ya kipando! simama Mina eneo lenye changarawe. Mtangazie aliyopo maeneo ya bondeni na yale ya miinuko. Usiku watakapofurika mahujaji Mina. Kama yafurikavyo mawimbi ya mto Furati. Ikiwa kuwapenda Aali Muhammad ni urafidhi Basi vizito viwili vishuhudie kwamba mimi ni rafidhi.”74

SURAT AL-AHQAF Kauli ya Mwenyezi Mungu: “Na kubeba mimba na kumwachisha ziwa ni miezi thelathini” (Sura al-Ahqaf: 15). Amesema: Aya hii imeonyesha kwamba muda wa chini kabisa wa mimba kukaa tumboni ni miezi sita, kwa sababu jumla ya muda wote wa mimba na kunyonya ni miezi thelathini. Amesema (s.w.t.): “Na wazazi wawanyonyeshe watoto wao miaka miwiwli kamili;” hivyo katika miezi thelathini tukitoa miaka miwili kamili ambayo ni sawa na miezi ishirirni na nne, inabaki miezi sita ambayo ndio muda wa chini kabisa wa mimba kukaa tumboni. Imepokewa kutoka kwa Umar kwamba kuna mwanamke alipelekwa kwake na alikuwa amejifungua mimba ya miezi sita, ndipo (Umar) akaamuru apigwe mawe. Ali (a.s.) akasema: “Hastahiki kupopolewa mawe.” Na akataja kanuni ya ufumbuzi kama tulivyoeleza.75

74 At-Tafsir al-Kabir cha Razi Juz. 27, Uk. 66. 75 At-Tafsir al-Kabir cha Razi Juz. 28, Uk. 15. 59

Page 59


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 2 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

11:15 AM

Ahlul Bayt ndani ya Tafsiri za Kisunni No.2

SURAT AL-INSAN Kauli ya Mwenyezi Mungu:

“Na huwalisha chakula masikini na yatima na mfungwa hali ya kuwa wanakipenda. Tunakulisheni kwa ajili ya radhi za Mwenyezi Mungu tu, hatutaki kwenu malipo wala shukurani.” (Sura al-Insan: 8 - 9). Al-Wahidiy ametaja kutoka kwa jamaa zetu katika kitabu al-Basiti kwamba iliteremka kwa ajili ya Ali. Na mwandishi wa al-Kashafu toka kwa muutazila amekitaja kisa hiki kwa kupokea toka kwa Ibn Abbas kwamba alisema: Hasan na Husein (a.s.) walipatwa na maradhi, Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) alikwenda kuwaona akiwa pamoja na baadhi ya watu. Wakasema: “Ewe Abal-Hasan ni vizuri lau ukiweka nadhiri kwa ajili ya wanao.” Ndipo Ali, Fatima na mtumishi wao Fidha wakaweka nadhiri kwamba iwapo watapona watafunga siku tatu. Wakapona na hali wao hawana kitu, ndipo Ali akakopa toka kwa Simon Myahudi wa Khaybar, pishi tatu za ngano. Fatima akachukua pishi moja akatwanga na kuoka mikate mitano kulingana na idadi yao, wakaiweka mbele yao ili wafuturu, mara masikini akafika mlangoni kwao akagonga akisema: “Assalam Alaykum enyi watu wa nyumba ya Muhammad, mimi ni maskini katika watoto wa kiislamu nipeni chakula Mwenyezi Mungu atakupeni chakula cha Peponi.” Wakamfanyia kipaumbele na wao wakalala na hali hawajaonja ila maji tu na wakaamka wakiwa na Swaumu.

60

Page 60


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 2 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

11:15 AM

Ahlul Bayt ndani ya Tafsiri za Kisunni No.2 Waliposhinda na Swaumu na kuweka chakula mbele yao mara akafika mlangoni kwao yatima naye wakamfanyia kipaumbele. Na mara mfungwa wa kivita akafika mlangoni kwao siku ya tatu, naye wakamfanyia hivyo hivyo. Asubuhi iliyofuata Ali aliwashika mkono Hasan na Husein (a.s.) na kwenda nao kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.). Alipowatizama na hali wao wawili kutokana na njaa kali wakitetemeka kama vifaranga alisema: “Hali niionayo kwenu yaniumiza mno.” Akasimama na kwenda nao, ndipo wakamkuta Fatima akiwa mihrabuni kwake na hali tumbo lake limeshikana na mgongo wake na macho yake yamebadilika. Hali hiyo ikamuuma sana, ndipo Jibril (a.s.) akateremka na kusema: “Ewe Muhammad pokea, Mwenyezi Mungu anakupa pongezi kwa kitendo cha watu wa nyumba yako.” Jibril (a.s.) akamsomea Sura hii.76

SURAT AL-KAWTHAR Kauli ya Mwenyezi Mungu: “Hakika sisi tumekupa kheri nyingi.” (Sura al-Kawthar: 1). Amesema: Kheri nyingi (Kawthar) hapa ni watoto wake (s.a.w.w.). Wamesema: Kwa sababu Sura hii iliteremka ikiwa ni jibu kwa wale waliokuwa wakimkashifu Mtume (s.a.w.w.) kwa kutokuwa na watoto wa kiume. Hivyo maana yake ni kwamba Yeye (s.w.t.) atampa kizazi kitakachodumu muda wote. Hebu tazama ni watu wangapi wameuawa toka katika Ahlul-Baiti lakini bado ulimwengu umejaa wao, na hakuna Bani Umaiyya yeyote ambaye anatiliwa umuhimu na kuheshimiwa. Kisha tazama ni jinsi gani wao (Ahlul-Baiti) walivyotoa ulamaa wakubwa kama vile al-Baqir, as-Sadiq, al-Kadhim, ar-Radhi (a.s.) na Nafsuz-Zakiyya.77

76 At-Tafsir al-Kabir cha Razi Juz. 30, Uk. 244. 77 At-Tafsir al-Kabir cha Razi Juz. 32, Uk. 124. 61

Page 61


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 2 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

11:15 AM

Ahlul Bayt ndani ya Tafsiri za Kisunni No.2

AHLUL-BAIT (A.S.) NDANI YA TAFSIRI YA AL-BAYDHAWI, INAYOITWA AN’WARUT-TANZIIL WAASRARUT-TAAWIIL: SURAT AL-BAQARAH Kauli ya Mwenyezi Mungu: “Wale watoao mali zao usiku na mchana kwa siri na dhahiri, wana ujira wao kwa Mola wao Mlezi; wala haitakuwa hofu juu yao wala wao hawatahuzunika.” (Sura alBaqarah: 274). Imesemwa kwamba: “Aya hii iliteremka kwa ajili ya Amirul-Muuminina (a.s.), hakuwa anamiliki zaidi ya dirhamu nne, akatoa sadaka dirhamu moja usiku na nyingine mchana, nyingine siri na nyingine dhahiri.”78

SURAT AALI IMRAN Kauli ya Mwenyezi Mungu: “…Kila mara Zakariya alipoingia Mihrab hukuta vyakula. Akasema: Ewe Maryam unatoa wapi hivi. Akasema: Vinatoka kwa Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu humruzuku amtakaye bila hesabu.” (Sura Aali Imran: 37). Imepokewa kwamba Fatima alimzawadia Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) vipande viwili vya mkate na kipande cha nyama, naye akavirejesha kwa Fatima na kusema: “Chukua ewe binti yangu.” Alipofunua bakuli akalikuta limejaa mikate na nyama. Mtume akamwambia umetoa wapi hivi? Akasema: “Ni kutoka kwa Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu humpa riziki amtakaye bila hesabu.” Mtume akasema: “Kila sifa njema ni ya Mwenyezi Mungu Ambaye amek78 Tafsirul-Baydhawi iitwayo An’warut-Tanziil Waasrarut-Taawiil Juz. 1, Uk. 141, Chapa ya Pili ya Misri ya Mwaka 1968 A.D. 62

Page 62


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 2 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

11:15 AM

Ahlul Bayt ndani ya Tafsiri za Kisunni No.2 ufanya kifani wa bibi wa wana wa Israel (Mariam).” Kisha Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) akawakusanya Ali bin Abu Talib, Hasan na Husein na watu wote wa nyumbani kwake wakala pamoja mpaka wakashiba na chakula kikabakia kama kilivyokuwa. Hivyo Fatima akawagawia majirani zake.79 Kauli ya Mwenyezi Mungu:

“Na watakaokuhoji baada kukufikia elimu hii, waambie: Njooni tuwaite watoto wetu na watoto wenu, na wanawake zetu na wanawake wenu, na nafsi zetu na nafsi zenu, kisha tuombe kwa unyenyekevu tutake laana ya Mwenyezi Mungu iwashukie waongo.” (Sura Aali Imran: 61). Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) alipowaomba wafanye maapizano walisema mpaka tutafakari. Walipoachana wakamwambia Aqib naye alikuwa ndiye wamfuatae katika rai: “Unaonaje?” Akasema: “Wallahi enyi wakristo mmeshaujua utume wake na bila shaka amewajieni na hoja yakinifu kuhusu mtu wenu (Yesu), wallahi katu hakuna watu walioombeana laana na Mtume kisha mkubwa wao akaendelea kuishi au mdogo wao kuzaliwa. Na kama mtafanya hivyo bila shaka mtaangamia, hivyo ila ni nyinyi kuendelea kubakia katika imani yenu na dini yenu, nendeni mkamuage mtu huyu na mrejee nchini kwenu.” 79 Tafsirul-Baydhawi iitwayo An’warut-Tanziil Waasrarut-Taawiil Juz. 1, Uk. 158, Chapa ya Pili ya Misri ya Mwaka 1969 A.D.

63

Page 63


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 2 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

11:15 AM

Ahlul Bayt ndani ya Tafsiri za Kisunni No.2 Ndipo kesho yake wakaenda kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.), na Mtume akatoka akiwa amemkumbatia Husein na amemshika mkono Hasan huku Fatima akitembea nyuma yake na Ali akiwa nyuma ya Fatima. Akawaambia: “Mimi nitakapokuwa naomba nyinyi muwe mnaitikia.” Askofu wao akasema: “Enyi wakristo! Mimi naziona nyuso hizi kama zitamuomba Mwenyezi Mungu auondoe mlima kutoka mahala pake, atauondoa, msiapizane naye mtaangamia.” Wakamsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu na wakampa kodi ya Hilla80 elfu mbili na diraya thelathini za chuma. Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) akasema: “Naapa kwa Yule Ambaye nafsi yangu imo mikononi mwake, lau wangefanya maapizano wangegeuzwa nyani na nguruwe na bonde lao lingewaka moto. Na Mwenyezi Mungu angeiteketeza Najran na watu wake hata ndege aliyopo juu ya mti. Al-Baydhawi mwandishi wa tafsiri hii anasema katika maelezo yake: Nayo ni dalili ya unabii wake na ya ubora wa wale aliokwenda nao miongoni mwa Ahlul-Baiti wake.81

SURAT MAIDA Kauli ya Mwenyezi Mungu:

“Hakika walii wenu hasa ni Mwenyezi Mungu na Mtume Wake na wale walioamini ambao husimamisha Swala na hutoa Zaka wakiwa wamerukui.” (Sura Maida: 55). 80 Jina la pesa kama vile Dola, Shilingi, Paundi na mfano wa hizo. 81 Tafsirul-Baydhawi iitwayo An’warut-Tanziil Waasrarut-Taawiil Juz. 1, Uk. 164, Chapa ya Pili ya Misri ya Mwaka 1968 A.D. 64

Page 64


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 2 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

11:15 AM

Ahlul Bayt ndani ya Tafsiri za Kisunni No.2 Yenyewe iliteremka kwa ajili ya Ali (a.s.) pindi muombaji alipomwomba na hali amerukuu ndani ya Swala, akamvulia pete yake.82

SURAT TAWBA Kauli ya Mwenyezi Mungu:

“(Tangazo la) Kujitoa Mwenyezi Mungu na Mtume Wake kwa wale mlioahidiana nao miongoni mwa mushrikina.” (Sura Tawba: 1). Imepokewa kwamba ilipoteremka Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) alimtuma Ali (a.s.) akiwa amepanda al-Adhbau83 ili akawasomee mahujaji wa msimu huo. Kabla ya hapo alikuwa tayari keshamtuma Abu Bakr awe kiongozi wa Hija ya msimu huo. Pakasemwa: Kwa nini usingemtuma Abu Bakr akawasomee? Akasema: “Hafikishi kwa niaba yangu ila mtu atokanaye na mimi.”84

SURAT ISRAI Kauli ya Mwenyezi Mungu: “Siku tutakapowaita kila watu pamoja na viongozi wao.” (Sura Israi: 71). Pakasemwa: Viongozi wao: Yaani tutawaita kwa majina ya mama zao. Na hekima katika hilo ni kumtukuza Isa (a.s.) na kudhihirisha sharafu ya Hasan na Husein (a.s.).85 82 Tafsirul-Baydhawi iitwayo An’warut-Tanziil Waasrarut-Taawiil Juz. 1, Uk. 291, Chapa ya Pili ya Misri ya Mwaka 1968 A.D. 83 Jina la ngamia wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). 84 Tafsirul-Baydhawi iitwayo An’warut-Tanziil Waasrarut-Taawiil Juz. 1, Uk. 404, Chapa ya Pili ya Misri ya Mwaka 1968 A.D. 85 Tafsirul-Baydhawi iitwayo An’warut-Tanziil Waasrarut-Taawiil Juz. 1, Uk. 592, Chapa ya Pili ya Misri ya Mwaka 1968 A.D. 65

Page 65


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 2 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

11:15 AM

Ahlul Bayt ndani ya Tafsiri za Kisunni No.2

SURAT AHZAB Kauli ya Mwenyezi Mungu:

“Hakika si mengineyo, Mwenyezi Mungu anataka kuwaondolea uchafu, enyi watu wa nyumba ya Mtume, na kuwatakasa kabisa kabisa.” (Surat Ahzab: 33). Imepokewa kwamba siku moja Mtume (s.a.w.w.) alitoka na hali kajifunika shuka lililodariziwa na manyoya meusi. Akaketi na ghafla akaja Fatima akamfunika, kisha akaja Ali akamfunika, wakaja Hasan na Husein (a.s.) akawafunika, kisha akasema: “Hakika si mengineyo, Mwenyezi Mungu anataka kuwaondolea uchafu, enyi watu wa nyumba ya Mtume.”86 Kauli ya Mwenyezi Mungu:

“Na wale ambao wanawaudhi waumini wanaume na waumini wanawake pasi na wao kustahili, hakika wamebeba uzushi na dhambi kumbwa.” (Surat Ahzab: 58). Imesemwa: Iliteremka kwa ajili ya wanafiki pale walipokuwa wakimuudhi Ali (a.s.).87 86 Tafsirul-Baydhawi iitwayo An’warut-Tanziil Waasrarut-Taawiil Juz. 2, Uk. 245, Chapa ya Pili ya Misri ya Mwaka 1968 A.D. 87 Tafsirul-Baydhawi iitwayo An’warut-Tanziil Waasrarut-Taawiil Juz. 2, Uk. 252, Chapa ya Pili ya Misri ya Mwaka 1968 A.D. 66

Page 66


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 2 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

11:15 AM

Ahlul Bayt ndani ya Tafsiri za Kisunni No.2

SURAT AS-SHURA Kauli ya Mwenyezi Mungu:

“Sema: Kwa haya siwaombi malipo yoyote kwenu isipokuwa mapenzi katika ndugu...” (Sura as-Shura: 23). Imepokewa kwamba: Ilipoteremka palisemwa: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) ni akina nani hawa karaba zako ambao tumewajibishwa kuwapenda? Akasema: “Ali, Fatima na watoto wake wawili.”88

SURAT TAHRIM Kauli ya Mwenyezi Mungu:

“Na tukampulizia humo roho yetu na akayasadikisha maneno ya Mola Wake Mlezi, na vitabu vyake na alikuwa miongoni mwa wanyenyekevu.” (Sura Tahrim: 12). Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) amesema: “Kati ya wanaume wamekamilika wengi na wala hawajakamilika kati ya wanawake ila wanne: Asia binti Muzahim mke wa Firaun, Mariam binti Imran, Khadija binti Khuwaylid na Fatima binti Muhammad.”89 88 Tafsirul-Baydhawi iitwayo An’warut-Tanziil Waasrarut-Taawiil Juz. 2, Uk. 357, Chapa ya Pili ya Misri ya Mwaka 1968 A.D. 89 Tafsirul-Baydhawi iitwayo An’warut-Tanziil Waasrarut-Taawiil Juz. 2, Uk. 488, Chapa ya Pili ya Misri ya Mwaka 1968 A.D. 67

Page 67


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 2 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

11:15 AM

Ahlul Bayt ndani ya Tafsiri za Kisunni No.2

SURAT AL-INSAN Kauli ya Mwenyezi Mungu:

“Na huwalisha chakula masikini na yatima na mfungwa hali ya kuwa wanakipenda. Tunakulisheni kwa ajili ya radhi za Mwenyezi Mungu tu, hatutaki kwenu malipo wala shukurani.” (Surat al-Insan: 8 - 9). Kutoka kwa Ibnu Abbas amesema: “Hasan na Husein (a.s.) walipatwa na maradhi, Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) alikwenda kuwaona akiwa pamoja na baadhi ya watu. Wakasema: “Ewe Abal-Hasan ni vizuri lau ukiweka nadhiri kwa ajili ya wanao.” Ndipo Ali, Fatima na mtumishi wao Fidha wakaweka nadhiri kwamba iwapo watapona watafunga siku tatu. Wakapona na hali wao hawana kitu, ndipo Ali akakopa toka kwa Simon Myahudi wa Khaybar, pishi tatu za ngano. Fatima akachukua pishi moja akatwanga na kuoka mikate mitano, wakaiweka mbele yao ili wafuturu, mara masikini akafika mlangoni kwao wakamfanyia kipaumbele na wao wakalala na hali hawajaonja ila maji tu na wakaamka wakiwa na Swaum. Waliposhinda na Swaumu na kuweka chakula mbele yao mara akafika mlangoni kwao yatima naye wakamfanyia kipaumbele. Na mara mfungwa wa kivita akafika mlangoni kwao siku ya tatu, naye wakamfanyia hivyo hivyo. Ndipo Jibril (a.s.) akateremka na Sura hii na kusema: “Ewe Muhammad ipokee, Mwenyezi Mungu anakupa pongezi kwa kitendo cha watu wa nyumba yako.”90 90 Tafsirul-Baydhawi iitwayo An’warut-Tanziil Waasrarut-Taawiil Juz. 2, Uk. 526, Chapa ya Pili ya Misri ya Mwaka 1968 A.D. 68

Page 68


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 2 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

11:15 AM

Ahlul Bayt ndani ya Tafsiri za Kisunni No.2

AHLUL-BAIT (A.S.) NDANI YA TAFSIRI YA ALQURTUBI, INAYOITWA AL-JAMIU LIAHKAMIL-QUR’ANI SURAT AL-BAQARAH Kauli ya Mwenyezi Mungu:

“Na katika watu yuko auzaye nafsi yake kwa kutaka radhi ya Mwenyezi Mungu, na Mwenyezi Mungu ni Mpole kwa waja.” (Sura al-Baqarah: 207). Imesemwa kwamba Aya hii iliteremka kwa ajili ya Ali bin Abu Talib (a.s.) alipoachwa na Mtume (s.a.w.w.) alale kitandani kwake usiku aliotoka kwenda pangoni.91 Kauli ya Mwenyezi Mungu:

“Wale watoao mali zao usiku na mchana kwa siri na dhahiri, wana ujira wao kwa Mola wao Mlezi; wala haitakuwa hofu juu yao wala wao hawatahuzunika.” (Surat al-Baqarah: 274).

91 Tafsirul-Qurtubi Juz. 3, Uk. 21. Na pia imepokewa katika kitabu TadhkiratulKhuwas Uk. 35 na kitabu Shawahidut-Tanziil Juz. 1, Uk. 97 na kitabu FaraidusSamtwayni Juz. 1, Uk. 330. 69

Page 69


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 2 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

11:15 AM

Ahlul Bayt ndani ya Tafsiri za Kisunni No.2 Imepokewa kutoka kwa Ibnu Abbas kwamba alisema: “Aya hii iliteremka kwa ajili ya Ali bin Abu Talib (a.s.), alikuwa na dirhamu nne, akatoa sadaka dirhamu moja usiku na nyingine mchana, nyingine siri na nyingine dhahiri.”92

SURAT AALI IMRAN Kauli ya Mwenyezi Mungu:

“Na Malaika waliposema: Ewe Maryam! Hakika Mwenyezi Mungu amekuteua na akakutakasa na akakuteua juu ya wanawake wa ulimwenguni.” (Surat Aali Imran: 42). Imepokewa kwa njia sahihi kama ilivyopokewa kutoka kwa Abu Huraira kwamba (s.a.w.w.) alisema: ‘’Kati ya wanawake wa ulimwenguni wabora ni wanne: Maryam binti Imran, Asia binti Muzahim mke wa Firaun, Khadija binti Khuwaylid na Fatima binti Muhammad.”93 Na katika Hadithi ya Ibn Abbas ni kwamba Mtume alisema: ‘’Walio bora kati ya wanawake wa Peponi ni: Khadija binti Khuwaylid, Fatima binti Muhammad, Maryam binti Imran na Asia binti Muzahim.” Na katika njia nyingine kutoka kwake amesema walio bora kati ya wanawake wa Peponi ni: “Baada ya Mariam ni Fatima na Khadija.” Amepokea Musa bin Aqaba kutoka kwa Kuraybu kutoka kwa Ibn Abbas amesema: “Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) alisema: “Seyyida wa 92 Tafsirul-Qurtubi Juz. 3, Uk. 347. 93 Tafsirul-Qurtubi Juz. 4, Uk. 83. 70

Page 70


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 2 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

11:15 AM

Ahlul Bayt ndani ya Tafsiri za Kisunni No.2 wanawake wa peponi ni Mariam, Fatima, Khadija na Asia.” Kauli ya Mwenyezi Mungu:

“Na watakaokuhoji baada kukufikia elimu hii, waambie: Njooni tuwaite watoto wetu na watoto wenu, na wanawake zetu na wanawake wenu, na nafsi zetu na nafsi zenu, kisha tuombe kwa unyenyekevu tutake laana ya Mwenyezi Mungu iwashukie waongo.” (Surat Aali Imran: 61). Al-Qurtubi amesema: “Hakika Mtume (s.a.w.w.) alikwenda na Hasan na Husein na Fatima akitembea nyuma yake na Ali akiwa nyuma yao huku akisema: “Nitakapoomba muitikie.” Na anasema: Ulamaa wengi wamesema: “Hakika kuwaita Hasan na Husein wakati wa maapizano kwamba ni watoto: “tuwaite watoto wetu na watoto wenu” na kusema kuhusu Hasan: “Hakika mwanangu huyu ni bwana.” Uitaji huo ni makhsusi kwa ajili ya Hasan na Husein (a.s.), wao ndio waitwe watoto wa Mtume (s.a.w.w.) na si wengineo, hiyo ni kwa mujibu wa kauli yake: “Kila sababu na nasaba itakatika Siku ya Kiyama ila nasaba yangu na sababu yangu.” Kauli ya Mwenyezi Mungu: “Na bila shaka Mwenyezi Mungu alikusaidieni katika Badri hali nyinyi ni madhalili. Basi mcheni Mwenyezi Mungu ili mpate kushukuru.” (Surat Aali Imran: 123). Ibnu Is’haqa ametaja kutoka kwa Ammar binYasir kwamba alisema: “Mimi na Ali tulikuwa pamoja katikaVita vya Ashira huko Batnu Yanbui. 71

Page 71


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 2 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

11:15 AM

Ahlul Bayt ndani ya Tafsiri za Kisunni No.2 Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) alipofika hapo alikaa mwezi mmoja na hatimaye akafanya suluhu na Bani Mudliju na washirika wao kutoka Bani Dhamra kisha akawaaga. Ali bin Abu Talib (a.s.) aliniambia: “Upo tayari ewe Abul-Yaqdhan tuwaendee hawa jamaa? Kundi la Bani Mudliju linafanya kazi katika mto wao, twende tukachunguze jinsi gani wanavyofanya kazi.” Tukawaendea na tukaona ardhi ifaayo tukalala hapo. Wallahi hakuna aliyetuamsha ila Mtume wa Mwenyezi Mungu kwa nyayo zake. Tukaketi na hali tumetapakaa udongo na siku hiyo Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) alimwambia Ali: “Una habari gani ewe Abu Turab?” Naye akamweleza jambo letu. Mtume (s.a.w.w.) akasema: “Je, niwajulisheni watu wawili walio waovu mno kuliko watu wengine?” Tukasema, ndio ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu. Akasema: “Uhaymar wa kabila la Thamudi yule aliyemchinja ngamia. Na yule atakayekupiga dhoruba ewe Ali juu ya hiki.” Mtume wa Mwenyezi Mungu akaweka mkono wake juu ya kichwa cha Ali. “Mpaka hizi zilowane kwa damu yake.” Akaweka mkono wake juu ya ndevu zake.94

SURAT NISAI Kauli ya Mwenyezi Mungu:

94 Tafsirul-Qurtubi Juz. 4 Uk. 192 72

Page 72


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 2 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

11:15 AM

Ahlul Bayt ndani ya Tafsiri za Kisunni No.2 “Enyi mlioamini! Msikaribie Swala na hali mmelewa mpaka myajue mnayoyasema; wala mkiwa na janaba isipokuwa wapita njia mpaka muoge. Na muwapo wagonjwa au mkiwa safarini au akawa mmoja wenu ametoka chooni au mkagusana na wanawake, kisha msipate maji, basi tayamamuni na mchanga ulio twahara; mpake nyuso zenu na mikono yenu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa kusamehe Mwenye kughufiria.” (Surat Nisai: 43). Imepokewa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w.) kwamba haikuwa ni ruhusa kwa yeyote kupita ndani ya msikiti wala kukaa humo ila Ali bin Abu Talib (a.s.).95 Na ameipokea Atiyyat al-Awafiy kutoka kwa Abu Said al-Khudriy kwamba alisema: “Mtume wa Mwenyezi Mungu alisema: “Haipasi wala haifai kwa mwislamu kupatwa na janaba na akawa msikitini ila mimi na Ali.” Na linaloonyesha kwamba nyumba ya Ali ilikuwa msikitini ni ile riwaya aliyoipokea Shihab kutoka kwa Salim bin Abdullah, amesema: “Mtu mmoja alimuuliza baba yangu kuhusu Ali na Uthman ni yupi kati ya hawa wawili alikuwa bora? Abdullah bin Umar akamwambia: ‘Hii ni nyumba ya Mtume wa Mwenyezi Mungu.’ Huku akiashiria nyumba ya Ali (a.s.).”96 Umar bin Maymun amepokea kutoka kwa Ibnu Abbas kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) alisema: “Zibeni milango ila mlango wa Ali.” Akaacha mlango wake (Ali) tu msikitini.97 95 Tafsirul-Qurtubi Juz. 5, Uk. 207. Atau amepokea kutoka kwa Ibnu Abbas kwamba alisema: “Haikuwa Muta ila ni huruma ya Mwenyezi Mungu kwa waja wake na lau si Umar kukataza kuoa ndoa ya muda (Muta) asingelizini ila mwovu wa kupindukia.” Tazama Tafsirul-Qurtubi Juz. 5, Uk. 130. 96 Tafsirul-Qurtubi Juz. 5, Uk. 207. 97 Tafsirul-Qurtubi Juz. 5, Uk. 208. 73

Page 73


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 2 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

11:16 AM

Ahlul Bayt ndani ya Tafsiri za Kisunni No.2 Kauli ya Mwenyezi Mungu: “Enyi mlioamini! Mtiini Mwenyezi Mungu na mtiini Mtume na wenye mamlaka katika nyinyi.” (Sura Nisai: 59). Al-Qurtubi amesema: “Hakika muradi wa “Wenye mamlaka” ni Ali na Maimamu maasumina.”98

SURAT MAIDA Kauli ya Mwenyezi Mungu:

“Hakika walii wenu hasa ni Mwenyezi Mungu na Mtume wake na wale walioamini ambao husimamisha Swala na hutoa Zaka wakiwa wamerukui.” (Sura Maida: 55). Ibnu Abbas amepokea kwamba aya hii iliteremka kwa ajili ya Ali bin Abu Talib (a.s.), ni kwamba muombaji aliomba ndani ya msikiti wa Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) na hakuna yeyote aliyempa kitu. Muda huo Ali alikuwa amerukuu akiswali na hali kuliyani amevaa pete, ndipo akamwashiria muombaji mpaka akaichukua.99 Na imepokewa kwamba Ali (a.s.) alimpa muombaji kitu na hali akiwa katika Swala.100

98 Tafsirul-Qurtubi Juz. 5, Uk. 261. 99 Tafsirul-Qurtubi Juz. 6, Uk. 221. 100 Tafsirul-Qurtubi Juz. 6, Uk. 222. Kadhalika amepokea katika DhakhairulUqba Uk. 102; Shawahidut-Tanziil Juz. 1, Uk. 161. Na Manaqibul-Maghazali Uk. 311. Na Yanabiul-Mawaddah Uk. 218. 74

Page 74


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 2 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

11:16 AM

Ahlul Bayt ndani ya Tafsiri za Kisunni No.2

SURAT AL-AN’A’AM Kauli ya Mwenyezi Mungu:

“Na tukampa Is’haka na Yaakub, wote tukawaongoza, na Nuh tulimwongoza zamani na katika kizazi chake, Daud na Sulaiman na Ayub na Yusuf na Musa na Harun. Na hivyo ndivyo tuwalipavyo wafanya wema. Na Zakaria na Yahya na Isa na Ilyasa, wote walikuwa miongoni mwa watu wema.” (Sura An’aam: 84 - 85). Al-Qurtubi anasema: “Isa amejumuishwa katika kizazi cha Ibrahim na hali ni mtoto wa kupitia binti, hivyo watoto wa Fatima (a.s.) ni kizazi cha Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.).”101 Kauli ya Mwenyezi Mungu:

“Hakika Mwenyezi Mungu ndiye Mpasuaji wa mbegu na kokwa, hutoa mzima katika maiti, na mtoaji wa maiti katika mzima, huyo ndiye Mwenyezi Mungu, basi mnageuzwa wapi?” (Sura An’aam: 95). 101 Tafsirul-Qurtubi Juz. 7, Uk. 32. 75

Page 75


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 2 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

11:16 AM

Ahlul Bayt ndani ya Tafsiri za Kisunni No.2 Katika Sahih Muslim imepokewa kutoka kwa Ali (a.s.) kwamba alisema: “Naapa kwa yule ambaye huchipusha mbegu na kuumba nafsi, hakika yenyewe ni ahadi aliyoniahidi Mtume kwamba hanipendi ila muumini na wala hanichukii ila mnafiki.”102

SURAT AL-AA’RAF Kauli ya Mwenyezi Mungu:

“Sema: Ni nani aliyeharamisha mapambo ya Mwenyezi Mungu ambayo amewatolea waja wake na vitu vizuri vya riziki? Sema: Vitu hivyo ni kwa waumini katika maisha ya dunia na khasa Siku ya Kiyama. Hivyo ndivyo tunavyozibainisha Aya kwa watu wanaojua.” (Surat A’araf: 32). Imepokewa kutoka kwa Ali bin Husein bin Ali bin Abu Talib (a.s.) Sheikh wa Malik, kwamba alikuwa akivaa joho lililotengenezwa kwa hariri lenye thamani ya dinari khamsini, analivaa masika na inapofika kiangazi analitoa sadaka au analiuza na anatoa sadaka pato lake.103 102 Tafsirul-Qurtubi Juz. 7, Uk. 44. Na ameiandika al-Jazriy as-Shafi katika Asnal-Matwalib Uk. 55, na Ibnu Athir katika Usudul-Ghaba Juz. 6, Uk. 84 na Tahdhibut-Tahdhib Juz. 3, Uk. 479, na al-Iswabah Juz. 2, Uk. 35, na KanzulUmmal Juz. 6, Uk. 394, na ar-Riyadhun-Nadhrah Juz. 2, Uk. 224, na Nurul-Absar Uk. 72 na Hilyatul-Awliyai Juz. 6, Uk. 294. 103 Tafsirul-Qurtubi Juz. 7, Uk. 195. 76

Page 76


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 2 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

11:16 AM

Ahlul Bayt ndani ya Tafsiri za Kisunni No.2 Kauli ya Mwenyezi Mungu: “Na juu ya mahala palipoinuka patakuwa na watu watakaowafahamu wote kwa alama zao.” (Surat A’araf: 46). At-Thaalabi ametaja kwa njia yake kutoka kwa Ibnu Abbas kuhusu kauli yake (s.w.t.): “ Na juu ya mahala palipoinuka patakuwa na watu” kwamba ni sehemu ya juu iliyopo kwenye Sirat hapo atakuwepo Hamza, Ali bin Abu Talib na Jafar mwenye mbawa mbili (a.s.), wao watawatambua wale wenye mapenzi na wao kwa mng’aro wa nyuso zao na wale wenye chuki na wao kwa ufifiaji wa nyuso zao.104 Kauli ya Mwenyezi Mungu:

“Na Musa akamwambia ndugu yake Haruni: Shika nafasi yangu katika watu wangu na utengeneze wala usifuate njia ya waharibifu.” (A’araf: 142). Katika Sahih Muslim kutoka kwa Said bin Abi Waqqas amesema: Nilimsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) akimwambia Ali pindi alipomwachia nafasi yake alipoenda katika moja ya vita vyake: “Huridhii kwamba wewe una nafasi kwangu sawa na ile ya Harun kwa Musa ila ni kwamba hakuna Nabii baada yangu?”105 Kauli ya Mwenyezi Mungu: “Hakika wale wanaomcha Mungu zinapowagusa pepesi za Shetani mara hukumbuka tahamaki wamekwishaona njia.” (Sura A’araf: 201). 104 Tafsirul-Qurtubi Juz. 7, Uk. 212. 105 Tafsirul-Qurtubi Juz. 7 Uk. 277.

Ameiandika Sheikh Kamalud-Din Muhammad bin Talha as-Shafi katika kitabu chake Matalibus-Suul Fi Manaqibi Alir-Rasuul Juz. 1 Uk. 85, Chapa ya Muassasatu Ummil-Qura. 77

Page 77


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 2 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

11:16 AM

Ahlul Bayt ndani ya Tafsiri za Kisunni No.2 Iswamu bin al-Mutliq amesema: Niliingia Madina mara nikamwona Hasan bin Ali (a.s.), umbo na hulka yake vikanishangaza na ndipo husuda iliyokuwa imefichwa na kifua changu miongoni mwa chuki dhidi ya baba yake ikanijaa na ghafla nikasema: “Wewe ni mtoto wa mwana wa Abu Talib? “ Akasema ndio. Nikapindukia katika kumtusi na kumtusi baba yake. Akanitizama kwa jicho la upole na huruma kisha akasema: “Najikinga kwa Mwenyezi Mungu dhidi ya Shetani. Kwa jina la Mwenyezi Mungu Mwingi wa rehema Mwenye kurehemu: “Shikamana na kusamehe na amrisha mema na wapuuze majahili.” (Surat A’araf:199). Kisha akasema: “Jipunguzie uzito, najiombea na ninakuombea maghfira kwa Mwenyezi Mungu, lau ungetuomba msaada wa hali tungekusaidia. Lau ungetuomba msaada wa mali tungekupa. Lau ungetuomba tukuongoze tungekuongoza.” Akatambua majuto niliyokuwa nayo juu ya ukiukwaji uliyotokana na mimi. Akasema: “Hakuna lawama juu yenu leo, Mwenyezi Mungu atakusameheni, naye ni Mbora wa kurehemu. Je wewe ni mtu wa Shamu?” Nikasema ndio. Akasema: “Ni ada niijuayo toka kwa nyoka.106 Mwenyezi Mungu akupe uhai na kuinua heshima yako. Akupe afya njema na akusaidie. Eleza haja yako na matatizo yako kwetu utatukuta ni kinyume na dhana yako juu yetu, inshaallah.” Iswamu anasema: “Japo ardhi ni pana lakini niliona imenibana, nikatamani inimeze kisha nijifiche humo. Nikatoka hapo na hali hakuna mtu nimpendaye katika ardhi hii kuliko yeye na baba yake.”107

106 Waswahili husema: Mtoto wa nyoka ni nyoka. – Mtarjumi. 107 Tafsirul-Qurtubi Juz. 7 Uk. 397. 78

Page 78


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 2 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

11:16 AM

Ahlul Bayt ndani ya Tafsiri za Kisunni No.2

SURAT AL-AN’FAL Kauli ya Mwenyezi Mungu:

“Na walipokupangia njama wale waliokufuru ili wakufunge au wakuue au wakutoe na wakafanya hila na Mwenyezi Mungu akafanya hila na Mwenyezi Mungu ni Mbora wa wafanyao hila.” (Surat al-An’fal: 30). Hii ni kutoa habari za njama na hila walizokubaliana Mushrikina kumfanyia Mtume (s.a.w.w.) huko katika bunge lao, hivyo wakakubaliana wamuuwe na hivyo usiku wakamzingira na kumvizia kwenye mlango wa nyumba yake usiku kucha ili wamuuwe atakapotoka. Mtume (s.a.w.w.) akamwamuru Ali bin Abu Talib alale kitandani kwake na akamwomba Mwenyezi Mungu awafumbe macho wasione azimio lake. Mwenyezi Mungu akawafumba macho yao na walipofika asubuhi Ali alitoka na kuwaambia ndani ya nyumba hamna mtu yeyote.108 Kauli ya Mwenyezi Mungu: “Na jueni kwamba chochote mlichopata ghanima, basi khumsi yake ni ya Mwenyezi Mungu na Mtume na jamaa na mayatima na masikini na msafiri……” (Surat al-An’fal: 41). Al-Man’hal bin Amru amesema: Nilimuuliza Abdullah bin Muhammad bin Ali na Ali bin Husein kuhusu Khumsi, akasema: “Hiyo ni ya kwetu.” Nikamwambia Ali: Hakika Mwenyezi Mungu anasema: “…na mayatima na masikini na msafiri…” Akasema: “Mayatima wetu na maskini wetu.”109 108 Tafsirul-Qurtubi Juz. 7 Uk. 397. 109 Tafsirul-Qurtubi Juz. 8, Uk. 10. 79

Page 79


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 2 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

11:16 AM

Ahlul Bayt ndani ya Tafsiri za Kisunni No.2

SURAT TAWBA Kauli ya Mwenyezi Mungu:

“Je, mnafanya kuwanywesha mahujaji na kuamirisha msikiti mtukufu ni sawa na yule aliyemwamini Mwenyezi Mungu na siku ya mwisho na akapigana jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu? Hawawi sawa mbele ya Mwenyezi Mungu na Mwenyezi Mungu hawaongozi watu madhalimu.” (Sura Tawba: 19). Al-Qurtubi anasema: “Dhahiri ya Aya ni kubatilisha kauli ya aliyejigamba miongoni mwa Mushrikina kwa kunywesha mahujaji na kuamirisha msikiti kama alivyotaja as-Sadiy, amesema: Abbas alijigamba kwa kunywesha, na as-Shayba kwa kuamirisha na Ali kwa uislamu na jihadi. Mwenyezi Mungu akamuunga mkono Ali na kuwapinga hao wawili.110 Kauli ya Mwenyezi Mungu: “Bila shaka Mwenyezi Mungu amekusaidieni katika mapigano mengi na Siku ya Hunayn.” (Sura Tawba: 25). Waislamu walishindwa na kukimbia vitani na hakuna yeyote aliyemjali mwenzake. Mtume akabaki thabiti akiwa pamoja na ndugu zake Ali na Abbas. Siku hiyo ya Hunayni Ali (a.s.) aliuwa watu arobaini kwa mkono wake.111 110 Tafsirul-Qurtubi Juz. 8, Uk. 91. Asbabun-Nuzuul Uk. 164. Rabiul-Abrar cha Zamakhshari Uk. 484. Al-Fusuulul-Muhimmah Uk. 106. Manaqibul-Mughazaliy Uk. 321. Faraidus-Samtwayni Juz. 1, Uk. 203. 111 Tafsirul-Qurtubi Juz. 8, Uk. 97. 80

Page 80


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 2 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

11:16 AM

Ahlul Bayt ndani ya Tafsiri za Kisunni No.2 Kauli ya Mwenyezi Mungu: “Yeye ndiye aliyemtuma Mtume Wake kwa mwongozo na kwa dini ya haki ili ishinde dini zote, ingawa Mushrikina watachukia.” (Sura Tawba: 33). Yaani ni dini ya Uislamu izishinde dini zote. As-Sadiy amesema: “Hiyo ni pale atakapodhihiri Mahdi, hapo hatabaki yeyote ila ataingia katika Uislamu na kulipa kodi. Na zimeenea habari sahihi kwamba Mahdi ni kutoka kizazi cha Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.)112 Kauli ya Mwenyezi Mungu: “Na wale waliotangulia wakawa wa kwanza katika Muhajiri na Ansari...” (Sura Tawba: 100). Imepokewa kutoka kwa Zaid bin Arqam, Abu Dharr, Miqdad na wengineo kwamba: Wa kwanza kuupokea uislamu ni Ali (a.s.).113 Al-Hakim Abu Abdillah amesema: “Siijui tofauti ya wanahistoria juu ya kwamba Ali ndiye wa kwanza kuupokea uislamu.” Is’haqa bin Ibrahim Rahawayhi al-Handhaliy alikuwa mwandishi wa khabari, hivyo alikuwa akisema: Wa kwanza kusilimu katika wanawake ni Khadija na katika watoto ni Ali.114 Kauli ya Mwenyezi Mungu: “Bila shaka Mwenyezi Mungu amekwishapokea toba ya Mtume na Muhajiri na Ansari waliomfuata yeye katika saa ya dhiki….” (Sura Tawba: 117). Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) alitoka mwezi wa Rajab akakaa Tabuk mwezi wa Shabani na siku kadhaa katika mfungo wa Ramadhan. Akatuma kikosi chake na kufanya suluhu na jamaa kwa sharti la kodi. 112 Tafsirul-Qurtubi Juz. 8, Uk. 121. 113 Tafsirul-Qurtubi Juz. 8, Uk. 236. 114 Tafsirul-Qurtubi Juz. 8, Uk. 237. 81

Page 81


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 2 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

11:16 AM

Ahlul Bayt ndani ya Tafsiri za Kisunni No.2 Katika vita hivi alimwacha Ali Madina. Wanafiki wakasema: Amemwacha kwa sababu amemchukia. Akamfuata Mtume (s.a.w.w.) na kumwambia. Mtume akasema: “Huridhii kwamba una nafasi kwangu sawa na ile ya Harun kwa Musa.”115

SURAT HUD Kauli ya Mwenyezi Mungu:

“Basi je, aliye na dalili wazi itokayo kwa Mola Wake na anaifuata na shahidi atokaye kwake..” (Sura Hud: 17). Imepokewa kwamba Ibnu Abbas alisema: Shahidi ni Ali bin Abu Talib (a.s.).116 Imepokewa kutoka kwa Ali kwamba alisema: “Hakuna mtu yeyote miongoni mwa makuraishi ila Aya moja au mbili zilishuka kwa ajili yake.” Ndipo mtu mmoja akamwambia: ‘’Ni ipi iliyoteremka kwa ajili yako?’’Ali akasema: “….. Na anaifuata na shahidi atokaye kwake..”

SURAT AR-RAA’D Kauli ya Mwenyezi Mungu:

“Na katika ardhi mna vipande vilivyokaribiana. Na zipo bustani za mizabibu na mimea mingine na mitende ichipuayo kwenye shina na isiyochipua kwenye shina moja inayonyweshelezwa maji yaleyale.” (Surat ar-Raad: 4). 115 Tafsirul-Qurtubi Juz. 8, Uk. 280.

116 Tafsirul-Qurtubi Juz. 9, Uk. 16. 82

Page 82


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 2 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

11:16 AM

Ahlul Bayt ndani ya Tafsiri za Kisunni No.2 Imepokewa kutoka kwa Jabir bin Abdullah kwamba alisema: Nilimsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) akimwambia Ali (a.s.): “Watu wanatokana na miti tofauti. Na mimi na wewe tunatokana na mti mmoja.” Kisha Mtume (s.a.w.w.) akasoma: “Na katika ardhi mna vipande vilivyokaribiana. Na zipo bustani za mizabibu na mimea mingine na mitende ichipuayo kwenye shina na isiyochipua kwenye shina moja inayonyweshelezwa maji yaleyale.”117

SURAT NAHLI Kauli ya Mwenyezi Mungu:

“Anayemkataa Mwenyezi Mungu baada ya imani yake (ataadhibiwa) isipokuwa yule aliyelazimishwa hali moyo wake unatulia kwa imani.” (Sura Nahli: 106). Imepokewa kutoka kwa Anas bin Malik kwamba alisema: Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) alisema: “Pepo ina shauku na watu watatu: Ali, Ammar na Salman.”118

SURAT ISRAI Kauli ya Mwenyezi Mungu:

“Kama mkifanya wema mtajifanyia wema nafsi zenu, na kama mkifanya ubaya, basi mtajifanyia wenyewe...” (Surat Israi: 7). 117 Tafsirul-Qurtubi Juz. 9, Uk. 283. 118 Tafsirul-Qurtubi Juz. 10, Uk. 181. 83

Page 83


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 2 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

11:16 AM

Ahlul Bayt ndani ya Tafsiri za Kisunni No.2 Kutoka kwa Ibnu Abbas amesema: Mwenyezi Mungu alimfunulia Muhammad (s.a.w.w.) kwamba: “Hakika mimi nilimuua Yahya bin Zakariya mara elfu sabini. Na hakika mimi nitamuua mtoto wa binti yako maradufu ya elfu sabini.”119 Na kutoka kwa Qarrat bin Khalid amesema: Mbingu haikumlilia yeyote ila Yahya bin Zakaria na Husein bin Ali. Na wekundu wake ndio kilio chake. Kauli ya Mwenyezi Mungu: “Siku tutakapowaita kila watu pamoja na viongozi wao.” (Surat Israi: 71). Muhammad bin Kaab amesema: Viongozi wao: Yaani mama zao. Ili kudhihirisha sharafu ya Hasan na Husein (a.s.).120

SURAT KAHFI Kauli ya Mwenyezi Mungu:

“Na ama yule kijana, basi wazazi wake walikuwa waumini, na tukahofia kwamba asije akawapelekea katika uasi na ukafiri.” (Sura Kahfi: 80). Abu Umar bin Abdul-Barri katika kitabu at-Tamhid kutoka kwa Ali (a.s.) kwamba Ali alisema: “Mtume (s.a.w.w.) alipofariki na kufunikwa na nguo kuna sauti ilitoka upande mmoja wa nyumba, wakawa wanasikia sauti lakini hawamwoni msemaji: ‘Assalam Alaykum Warahmatullah Wabarakatuhu. Assalamu Alaykum Ahlal-Bayt.”’121 119 Tafsirul-Qurtubi Juz. 10, Uk. 217. 120 Tafsirul-Qurtubi Juz. 10, Uk. 297. 121 Tafsirul-Qurtubi Juz. 11, Uk. 44. 84

Page 84


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 2 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

11:16 AM

Ahlul Bayt ndani ya Tafsiri za Kisunni No.2

SURAT MARYAM Kauli ya Mwenyezi Mungu:

“Hakika wale ambao wameamini na wakatenda mema Mwingi wa rehema atawajaalia mapenzi.” (Sura Maryam: 96). Imesemekana kwamba iliteremka kwa ajili ya Ali (a.s.). Al-Barau bin Azib amesema: Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) alimwambia Ali bin Abu Talib: “Ewe Ali sema: Ewe Mwenyezi Mungu! Nipe hifadhi Kwako na niwekee mapenzi katika nyoyo za waumini.”122

SURAT ANBIYAI Kauli ya Mwenyezi Mungu: “Na hatukutuma kabla yako ila wanaume tuliowapa wahyi. Basi waulizeni wenye ukumbusho ikiwa nyinyi hamjui.” (Surat Anbiyai: 43). Jabir al-Jaafiy, amesema: “Ilipoteremka Aya hii Ali bin Abu Talib alisema: ‘Sisi ndio wenye ukumbusho.’”123

SURAT FURQAN Kauli ya Mwenyezi Mungu: “Naye ndiye aliyemuumba mwanadamu kutokana na maji na akamjaalia kuwa na nasaba na ukwe. Na Mola wako ni Mwenye uwezo.” (Sura Furqan: 54). 122 Tafsirul-Qurtubi Juz. 11, Uk. 161. 123 Tafsirul-Qurtubi Juz. 11, Uk. 272. 85

Page 85


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 2 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

11:16 AM

Ahlul Bayt ndani ya Tafsiri za Kisunni No.2 Amepokea Muhammad bin Is’haqa kutoka kwa Yazid bin Abdullah bin Qusayti kutoka kwa Muhammad bin Usama bin Zaid kutoka kwa baba yake kwamba alisema: “Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) alisema: “Ewe Ali! Wewe ni mkwe wangu na baba wa wanangu. Na wewe ni kutokana na mimi na mimi ni kutokana na wewe.”124

SURAT NAMLU Kauli ya Mwenyezi Mungu:

“Na Suleiman alimrithi Daud. Na akasema: Enyi watu! Tumefunzwa usemi wa ndege. Na tumepewa kila kitu. Hakika hii ni fadhila iliyo dhahiri.” (Sura Namlu: 16). Hasan bin Ali bin Abu Talib (a.s.) amesema: “Kipozamataza aliapo huwa anasema: Ewe Mungu wangu! Walaani wenye kuwabughudhi Aali Muhammad.”125

SURAT AS-SAJDA Kauli ya Mwenyezi Mungu:

“Je, aliye muumini ni sawa na aliye fasiki? Hawawi sawa.” (Surat AsSajda: 18). 124 Tafsirul-Qurtubi Juz. 13, Uk. 60. 125 Tafsirul-Qurtubi Juz. 13, Uk. 166. 86

Page 86


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 2 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

11:16 AM

Ibnu Abbas na Atau bin Yasar wamesema: “Iliteremka ikimuhusu Ali bin Abu Talib na Walid bin Uqbah bin Abu Muit. Walizozana na ndipo Walid bin Uqbah akasema: ‘Mimi ni mfasaha kuliko wewe, mwenye meno makali kuliko wewe na shujaa kuliko wewe.’Ali (a.s.) akasema: ‘Nyamaza bila shaka wewe ni fasiki.’ Ndipo ikateremka Aya hii.126 Az-Zajjaj na anNuhhas wametaja kwamba iliteremka kwa ajili ya Ali na Uqba bin Abi Muit.

SURAT AHZAB Kauli ya Mwenyezi Mungu:

“Hakika si mengineyo, Mwenyezi Mungu anataka kuwaondolea uchafu, enyi watu wa nyumba ya Mtume, na kuwatakasa kabisa kabisa.” (Surat Ahzab: 33). Al-Kalbiy amesema: Nao ni Ali, Fatima, Hasan na Husein tu. Katika kuthibitisha hili kuna Hadithi kutoka kwa Mtume (s.a.w.w.). ummu Salama amesema: Aya hii iliteremkia nyumbani kwangu. Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) alimwita Ali, Fatima, Hasan na Husein akawafunika kishamia cha Khaybar, akasema: ‘’Hawa ndio Ahlul-Bait wangu.” Akasoma Aya. Kisha akasema: ‘’Ewe Mwenyezi Mungu waondolee uchafu na watakase kabisa kabisa.’’ Ummu Salama akasema: ‘Mimi ni pamoja nao ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu?’ Akasema (s.a.w.w.): ‘Wewe bakia ulipo na wewe upo katika kheri.”’ Hadithi hii ameiandika Tirmidhi na wengineo.127 126 Tafsirul-Qurtubi Juz. 14, Uk. 105. Shawahidut-Tanziil ya al-Haskaniy Juz. 1, Uk. 445. Manaqibul-Maghazaliy Uk. 324. Asbabun-Nuzuul Uk. 236. 127 Tafsirul-Qurtubi Juz. 14, Uk. 182. 87

Page 87


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 2 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

11:16 AM

Ahlul Bayt ndani ya Tafsiri za Kisunni No.2 Al-Qurtubi amesema: “Jambo hili limeenea katika habari kwamba ilipoteremka Aya hii Mtume (s.a.w.w.) alimwita Ali, Fatima, Hasan na Husein, akachukua kishamiya na kuwafunika, kisha akainua mkono wake mbinguni na kusema: ‘’Ewe Mwenyezi Mungu hawa ndio Ahlul-Bait wangu. Ewe Mwenyezi Mungu waondolee uchafu na watakase kabisa kabisa.”128 Kauli ya Mwenyezi Mungu:

“Hakika Mwenyezi Mungu na malaika wake wanamswalia Nabii. Enyi ambao mmeamini! Mswalieni na mumsalimu kwa salamu.” (Surat Ahzab: 56). Malik amepokea kutoka kwa Ibnu Mas’ud al-Ansariy alisema: “Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) alikuja na kutukuta tumeketi katika baraza la Saad bin Ubada. Bushru bin Saad akamwambia: Mwenyezi Mungu ametuamuru tukuswalie ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, basi ni vipi tutakavyokusalia? “ Mtume akakaa kimya mpaka tukatamani kwamba asingemuuliza. Kisha akasema Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.): “Semeni: ?????? ???? ??? ????? ???? ?? ????? ??? ????? ??? ??????? ???? ?? ???????. ? ???? ??? ????? ???? ?? ????? ??? ????? ??? ??????? ???? ?? ??????? ???? ???? ????. 128 Tafsirul-Qurtubi Juz. 14, Uk. 84. Pia imepokewa katika Tafsirul Kabir ya Razi Juz. 22, Uk. 137. Ruhul-Maaniy Juz. 16 Uk. 284. ManaqibulKhawarazmiy Uk. 23. Manaqibul-Maghazaliy Uk. 301. Tafsirul-Qummiy Juz. 2, Uk. 67. 88

Page 88


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 2 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

11:16 AM

Ahlul Bayt ndani ya Tafsiri za Kisunni No.2 “Ewe Mwenyezi Mungu! Mrehemu Muhammad na aali Muhammad kama ulivyomrehemu Ibrahim na aali Ibrahim. Na mbariki Muhammad na aali Muhammad kama ulivyombariki Ibrahim na aali Ibrahim juu ya walimwengu, hakika wewe ni Muhimidiwa Msifiwa. Na salamu ni kama mlivyojifunza.’’129 Amesema Abu Umar: “Shuuba na Thawru wamepokea kutoka kwa alHakam bin Abdurahman bin Abi Layla, kutoka kwa Kaabiy bin Ajrah, amesema: Ilipoteremka: “Enyi ambao mmeamini! Mswalieni na mumsalimu kwa salamu;” mtu mmoja alikuja kwa Mtume (s.a.w.w.) na kumwambia: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu! Tumeshajua namna ya kukutolea salamu, ni ipi namna ya kukuswalia? Mtume akasema: ‘’Sema: ?????? ???? ??? ????? ???? ?? ????? ??? ????? ??? ??????? ???? ?? ???????. ? ???? ??? ????? ???? ?? ????? ??? ????? ??? ??????? ???? ?? ??????? ???? ???? ????. “Ewe Mwenyezi Mungu! Mrehemu Muhammad na aali Muhammad kama ulivyomrehemu Ibrahim na aali Ibrahim. Na mbariki Muhammad na aali Muhammad kama ulivyombariki Ibrahim na aali Ibrahim, hakika wewe ni Muhimidiwa Msifiwa.’” Al-Qurtubi amesema: “Tumepokea katika kitabu as-Shifa cha Kadhi Iyadhi kwa njia ya upokezi ulioungana kutoka kwa Ali bin Abu Talib (a.s.), alisema: “Alizihesabu mikononi mwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.). na akasema (s.a.w.w.): Naye alizihesabu mikononi mwa Jibril na kusema hivyo ndivyo zilivyoshuka kutoka kwa Mola Mwenye nguvu:

129 Tafsirul-Qurtubi Juz. 14, Uk. 233. 89

Page 89


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 2 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

11:16 AM

Ahlul Bayt ndani ya Tafsiri za Kisunni No.2

?????? ???? ??? ????? ???? ?? ????? ??? ????? ??? ??????? ???? ?? ??????? ???? ???? ????. Ewe Mwenyezi Mungu! Msalie Muhammad na aali Muhammad kama ulivyomsalia Ibrahim na aali Ibrahim. Hakika wewe ni Muhimidiwa Msifiwa. ?????? ???? ??? ????? ???? ?? ????? ??? ????? ??? ??????? ???? ?? ??????? ???? ???? ????. Ewe Mwenyezi Mungu! Mbariki Muhammad na aali Muhammad kama ulivyombariki Ibrahim na aali Ibrahim. Hakika wewe ni Muhimidiwa Msifiwa.

Ewe Mwenyezi Mungu! Mrehemu Muhammad na aali Muhammad kama ulivyomrehemu Ibrahim na aali Ibrahim. Hakika wewe ni Muhimidiwa Msifiwa. ?????? ?????? ??? ????? ???? ?? ????? ??? ????? ??? ??????? ???? ?? ??????? ???? ???? ????. Ewe Mwenyezi Mungu! Muhurumie Muhammad na aali Muhammad kama ulivyomuhurumia Ibrahim na aali Ibrahim. Hakika wewe ni Muhimidiwa Msifiwa.�130

130 Tafsirul-Qurtubi Juz. 14, Uk. 234.

90

Page 90


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 2 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

11:16 AM

Ahlul Bayt ndani ya Tafsiri za Kisunni No.2 Kauli ya Mwenyezi Mungu:

“Na wale ambao wanawaudhi waumini wanaume na waumini wanawake pasi na wao kufanya, hakika wamebeba dhulma kubwa na dhambi kubwa.” (Surat Ahzab: 58). Imesemwa kwamba: Iliteremka kwa ajili ya Ali. Hakika wanafiki walikuwa wakimuudhi na kumzushia uongo.131

SURAT AS-SSAFFAT Kauli ya Mwenyezi Mungu: “Amani kwa Ilyasin.” (Surat as-Saffat: 130). As-Suhayliy amesema: “Baadhi ya wanatheiolojia wanapotoa maana za Qur’ani wamesema kwamba Aali Yasin ni Aali Muhammad (a.s.). “132

131 Tafsirul-Qurtubi Juz. 14, Uk. 240. 132 Tafsirul-Qurtubi Juz. 15, Uk. 120 91

Page 91


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 2 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

11:16 AM

Ahlul Bayt ndani ya Tafsiri za Kisunni No.2

SURAT SWAD Kauli ya Mwenyezi Mungu:

“Na tukautia nguvu ufalme wake na tukampa hikima na kukata hukumu.” (Sura Swad: 20). Imepokewa kwamba Ali bin Abu Talib alisema: “Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) aliponipeleka Yaman kundi moja la watu lilichimba shimo ambalo ni mtego wa simba, na hatimaye simba akanasa humo. Watu wakamuonea huruma simba ndipo watu wanne wakaingia humo kwa mtindo wa kubebana (kwa lengo la kumnasua). Simba akawajeruhi na kuwauwa. Watu wakashikiana silaha na kukaribia kuuwana. Ndipo nikawafuata na kuwaambia: Mnataka kuwauwa watu mia mbili kwa ajili ya watu wanne?! Njooni niwatoleeni hukumu, mkiiridhia ndio itakayokuwa hukumu kati yenu, na kama mkiikataa basi shitaka lenu nitalipeleka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu kwani yeye ndiye mwenye haki zaidi ya kutoa hukumu. Basi wa kwanza toka juu akamtengea robo ya fidia, wa pili theluthi ya fidia, wa tatu nusu ya fidia na wa nne fidia nzima. Na akawajibisha fidia hizo zitolewa na wale waliochimba mtego wa simba, wayape makabila manne. Baadhi wakaridhia na wengine wakakasirika, kisha wakaenda kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) na kumsimulia kisa. Akasema (s.a.w.w.): “Mimi nitatoa hukumu baina yenu.” Ndipo mmoja wao akase-

92

Page 92


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 2 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

11:16 AM

Ahlul Bayt ndani ya Tafsiri za Kisunni No.2 ma: “Hakika Ali tayari ameshatoa hukumu baina yetu.” Akamsimulia jinsi Ali alivyotoa hukumu. Mtume akasema: “Hukumu ni kama alivyoitoa Ali.”133 Huku ndiko kukata hukumu na elimu ya hukumu ambayo imegusiwa na moja ya tafsiri za Hadithi ya Mtume: “Jaji wenu Mkuu ni Ali.”134 Kauli ya Mwenyezi Mungu:

“Warudisheni kwangu, na akaanza kuwapangusa miguu na shingo.” (Sura Swad: 33). At-Tahawi ameandika katika kitabu Mushkilul-Hadithi kutoka kwa Asmau binti Umays kwamba Mtume (s.a.w.w.) alikuwa akipewa wahyi na hali kichwa chake kikiwa juu ya mapaja ya Ali, akawa hajaswali mpaka jua likazama. Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) akasema: “Umeshaswali ewe Ali?” Akasema bado. Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) akasema: “Ewe Mwenyezi Mungu! Hakika yeye alikuwa katika kukutii wewe na kumtii Mtume Wako, naomba ulirudishe jua kwa ajili yake.” Asmau anasema: “Nililiona limezama mara ghafla nikaliona baada ya kuzama limechomoza juu ya mlima na ardhi. Na hiyo ilikuwa huko Khaybari.135 “ 133 Tafsirul-Qurtubi Juz. 15, Uk. 163. 134 Tafsirul-Qurtubi Juz. 15, Uk. 164. 135 Tafsirul-Qurtubi Juz. 15 Uk. 197. Ameandika al-Hafidh Shafi’i katika kitabu Kifayatul-Matalib Uk. 381. Na katika at-Thaqib Fil-Manaqib cha Ibnu Hamza Uk. 253. Na Aamali cha Sheikh Mufid, Baraza la 11, Uk. 65. Na Tarikhu Damashqi cha Ibnu Asakir kwenye wasifu wa Imam Ali Juz. 2, Uk. 284. Na YanabiulMawaddah Uk. 137. Na Tadhkiratul-Khuwas Uk. 49 na al-Bihar Uk. 171. Pia jua lilirudi kwa mara nyingine kwa ajili ya Ali huko Babylon Iraq, pale alipotaka kuuvuka mto wa Bebilon. Hilo limeandikwa na Ibnu Shahri Ashub katika kitabu alManaqib Juz. 2, Uk. 318. Sharhun-Nahji Juz. 1, Dalailus-Sidqi Juz. 2, Uk. 300. Tafsiru Nurut-Thaqalayn Juz. 5, Uk. 225. al-Bihar Juz. 41, Uk. 171. 93

Page 93


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 2 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

11:16 AM

Ahlul Bayt ndani ya Tafsiri za Kisunni No.2

SURAT AS-SHURA Kauli ya Mwenyezi Mungu: “Sema: Kwa haya siwaombi malipo yoyote kwenu isipokuwa mapenzi katika ndugu...” (Surat as-Shura: 23). Katika Bukhari kutoka kwa Taus kutoka kwa Ibnu Abbas kwamba aliulizwa kuhusu kauli yake (s.w.t.): “….. Isipokuwa mapenzi katika ndugu,” Said bin Jubayri akasema: Karaba ni Aali Muhammad.136 Na katika riwaya ya Said bin Jubair kutoka kwa Ibnu Abbas amesema: Mwenyezi Mungu alipoteremsha: “Sema: Kwa haya siwaombi malipo yoyote kwenu isipokuwa mapenzi katika ndugu...” walisema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu! Ni akina nani hawa karaba zako ambao tunapaswa kuwapenda? Akasema: “Ni Ali, Fatima na watoto wao wawili.” Na pia lathibitishwa na riwaya ya Ali bin Abu Talib ambayo alisema: “Nilimshitakia Mtume (s.a.w.w.) kuhusu husuda za watu dhidi yangu. Akasema: ‘Hivi huridhii kuwa mmoja kati ya wanne. Wa kwanza kuingia Peponi ni: Mimi, Wewe, Hasan, Husein na kizazi chetu.”’137 Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) alisema: “Pepo imeharamisha juu ya yule aliyewadhulumu Ahlul-Bayt wangu na akaniudhi kwa kuwaudhi kizazi changu.” Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) alisema: “Atakayekufa na hali awapenda aali Muhammad basi amekufa na hali ni shahidi.”138 Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) alisema: “Atakayekufa na hali awapenda aali Muhammad Mwenyezi Mungu atawafanya malaika wa 136 Tafsirul-Qurtubi Juz. 16, Uk. 21. 137 Tafsirul-Qurtubi Juz. 16, Uk. 22. 138 Tafsirul-Qurtubi Juz. 16, Uk. 23. 94

Page 94


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 2 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

11:16 AM

Ahlul Bayt ndani ya Tafsiri za Kisunni No.2 rehema wawe wenye kulizuru kaburi lake. Atakayekufa na hali awachukia aali Muhammad atakuja Siku ya Kiyama na hali imeandikwa baina ya macho yake mawili: Amekata tamaa na rehema za Mwenyezi Mungu. Atakayekufa na hali awachukia aali Muhammad hatoipata harufu ya Pepo. Atakayekufa na hali awachukia aali zangu hana fungu lolote katika shafaa yangu.�139 Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) alisema: “Atakayekufa na hali awapenda aali Muhammad basi amekufa na hali ni shahidi. Ehe! atakayekufa na hali awapenda aali Muhammad basi amekufa na hali ni muumini aliyekamilika kiimani. Ehe! atakayekufa na hali awapenda aali Muhammad basi amekufa na hali malaika ameshambashiria Pepo, kisha Munkar na Nakir. Ehe! atakayekufa na hali awapenda aali Muhammad Mwenyezi Mungu atamfungulia milango miwili kaburini ya kuelekea Peponi. Ehe! atakayekufa na hali awapenda aali Muhammad Mwenyezi Mungu atawafanya malaika wa rehema wawe wenye kulizuru kaburi lake. Ehe! atakayekufa na hali awapenda aali Muhammad basi amefia ndani ya Sunna. Ehe! atakayekufa na hali awachukia aali Muhammad atakuja Siku ya Kiyama na hali imeandikwa baina ya macho yake mawili: Amekata tamaa na rehema za Mwenyezi Mungu. Ehe! atakayekufa na hali awachukia aali Muhammad basi amekufa na hali ni kafiri. 139 Tafsirul-Qurtubi Juz. 16, Uk. 23. 95

Page 95


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 2 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

11:16 AM

Ahlul Bayt ndani ya Tafsiri za Kisunni No.2 Ehe! atakayekufa na hali awachukia aali Muhammad hatoipata harufu ya Pepo.”140 Ibnu Abbas amesema: Ni mapenzi kwa Aali Muhammad (s.a.w.w.).141

SURAT ZUKHRUF Kauli ya Mwenyezi Mungu: “Na akalifanya neno hili liwe lenye kubaki katika kizazi chake ili warejee.” (Sura Zukhruf:28). As-Sadiy amesema: “Hao ni Aali Muhammad (s.a.w.w.).142”

SURAT AD-DUKHAN Kauli ya Mwenyezi Mungu: “Mbingu na ardhi hazikuwalilia; wala hawakupewa muda.” (Surat ad-Dukhan: 29). As-Sadiy amesema: Alipouawa Husein bin Ali (a.s.) mbingu ilimlilia na kilio chake ni wekundu wake.143 Jarir amesimulia kutoka kwa Yazid bin Abi Ziyad kwamba alisema: “Alipouawa Husein bin Ali bin Abu Talib (a.s.) mbingu ilipatwa na wekundu muda wa miezi minne. Na wekundu wake ndio kulia kwake.” 140 Tafsirul-Qurtubi Juz. 16, Uk. 24. 141 Tafsirul-Qurtubi Juz. 16, Uk. 24. 142 Tafsirul-Qurtubi Juz. 16, Uk. 77. 143 Tafsirul-Qurtubi Juz. 16. Ameipokea al-Bayhaqiy katika Dalailun-Nubuwa Juz. 6, Uk. 472. Ameiandika pia Suyuti katika kitabu al-Khasaisul-Kubra Juz. 2, Uk. 127. Dhahabi katika kitabu Tarikhul-Islami Juz. 2, Uk. 348. TadhkiratulKhuwas Uk. 284. Tarikhul-Khulafai Uk. 80. 96

Page 96


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 2 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

11:16 AM

Ahlul Bayt ndani ya Tafsiri za Kisunni No.2 Muhammad bin Sirin amesema: “Tulipewa habari kwamba wekundu uliyopo kwenye mawingu haukuwapo awali mpaka pale Husein bin Ali (a.s.) alipouwawa.” Sulayman al-Qadhi amesema: “Tulinyeshewa na mvua ya damu siku Husein alipouawa.” Kutoka kwa Qurrat bin Khalid amesema: “Mbingu haikumlilia yeyote ila Yahya bin Zakaria na Husein bin Ali. Na wekundu wake ndio kulia kwake.”

SURAT MUJADILAH Kauli ya Mwenyezi Mungu:

“Enyi mlioamini! Mnaposema siri na Mtume, basi tangulizeni sadaka kabla ya kumsemesha hayo ni bora kwenu na ni safi sana, na ikiwa hamkupata basi Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa kusamehe, Mwenye kurehemu.” (Sura Mujadilah: 12). Imepokewa kutoka kwa Mujahid kwamba: “Hakika wa awali aliyetoa sadaka katika amri hiyo ni Ali bin Abu Talib (a.s.) alitoa na akaongea siri na Mtume (s.a.w.w.).” Al-Qashayrii na wengineo wametaja kutoka kwa Ali bin Abu Talib (a.s.) kwamba alisema: “Hakika katika Kitabu cha Mwenyezi Mungu kuna Aya ambayo hakuna yeyote aliyeifanyia kazi kabla yangu, wala hakuna yeyote atakayeifanyia kazi baada yangu, nayo ni: “Enyi mlioamini! Mnaposema 97

Page 97


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 2 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

11:16 AM

Ahlul Bayt ndani ya Tafsiri za Kisunni No.2 siri na Mtume, basi tangulizeni sadaka kabla ya kumsemesha hayo ni bora kwenu na ni safi sana…..” nilikuwa nina dinari nikaichenji, hivyo ikawa kila nisemapo siri na Mtukufu Mtume natoa sadaka dirhamu moja mpaka zikaisha.” Ibnu Umar alisema: “Ali alikuwa na mambo matatu, ambayo kuwa nalo moja kati ya hayo ni jambo nilipendalo mno kuliko kuwa na ngamia mwekundu: Kuozwa Fatima, kukabidhiwa bendera Siku ya Khaibar na Aya ya kuongea siri na Mtume.”144

SURAT MUMTAHINA Kauli ya Mwenyezi Mungu:

“Enyi mlioamini! Msiwafanye adui zangu na adui zenu kuwa marafiki.” (Sura Mumtahina: 1). Al-Qushayri na Thaalabi wametaja kwamba: Hatibu bin Abu Balta’ah alikuwa ni mtu wa Yaman na alikuwa na mshirika na mmoja kati ya watu wa Bani Asad huko Makka. Akaja Madina kutoka Makka Sara kijakazi wa Abi Amru bin Swayfiy bin Hashim bin Abdu Manafi, na hali Mtume wa Mwenyezi Mungu akijiandaa kuikomboa Makka. (Sara) Alipokuwa anatoka kurudi Makka Hatib alimfuata na kumwambia: “Nakupa dinari kumi na kishamia kwa sharti kwamba unifikishie barua hii kwa wakazi wa Makka: Hakika Mtume wa Mwenyezi Mungu anawakusudieni hivyo chukueni tahadhari.”

144 Tafsirul-Qurtubi Juz. 17, Uk. 302. 98

Page 98


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 2 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

11:16 AM

Ahlul Bayt ndani ya Tafsiri za Kisunni No.2 Sara akatoka na ndipo Jibril akateremka na kumpa habari hiyo Mtume (s.a.w.w.), naye akamtuma Ali na Ammar bin Yasir, akawaambia: “Nendeni mpaka Rawdhatukhakhi,145 hapo pana mwanamke mwenye barua iliyotoka kwa Hatibu kwenda kwa Mushrikina. Mnyang’anyeni na mumwache aende zake na iwapo hatowapeni basi ikateni shingo yake.” Wakamkuta eneo hilo, wakamwambia: Ipo wapi barua? Akaapa kwamba hana barua. Wakapekua mizigo yake na hawakukuta barua, ndipo walipokusudia kurejea. Ali akasema: “Wallahi hatujasema uongo wala hatujadanganywa.” Akauandaa upanga wake na kumwambia: “Toa barua la sivyo wallahi nitakuvua na kuikata shingo yako.” Alipoona msisitizo ndipo akaitoa barua toka kwenye nywele zake.146

SURAT TAGHABUN Kauli ya Mwenyezi Mungu:

“Bila shaka mali zenu na watoto wenu ni mtihani, na kwa Mwenyezi Mungu kuna malipo makubwa.” (Sura Taghabun: 15). Tirmidhi na wengineo wamepokea kutoka kwa Abdullah bin Burayda kutoka kwa baba yake, amesema: “Nilimuona Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) akitoa hotuba na ghafla wakaja Hasan na Husein wakiwa wamevaa kanzu mbili nyekundu na hali wakidondoka na kuamka, akateremka toka mimbarini akawafuata na kuwachukua, kisha akasema: ‘Mwenyezi Mungu amesema kweli. Bila shaka mali zenu na watoto wenu 145 Jina la eneo lililopo baina ya Makka na Madina kwa umbali wa maili kumi na mbili kutokea Madina. 146 Tafsirul-Qurtubi Juz. 18, Uk. 51. 99

Page 99


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 2 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

11:16 AM

Ahlul Bayt ndani ya Tafsiri za Kisunni No.2 ni jaribio, nilipowaona hawa wawili wakitembea huku wakidondoka sikuweza kuvumilia mpaka nimekatisha mazungumzo yangu na kuwanyanyua.”147

SURAT TAHRIM Kauli ya Mwenyezi Mungu: “…..Basi Mwenyezi Mungu ni mlinzi wake, na Jibril na waumini wema na Malaika….” (Sura Tahrim: 4). Akrima na Said bin Jubayri wamesema: Waumini wema ni Ali bin Abu Talib.148 Asmau binti Umays alisema: “Nilimsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) akisema: “Na waumini wema” ni Ali bin Abu Talib.”149

SURAT AL-HAQQAH Kauli ya Mwenyezi Mungu:

“Ili tuifanye ukumbusho kwenu, na sikio lisikialo lisikie.” (Surat alHaqqah: 12). Makhul amepokea kwamba: Ilipoteremka Aya hii Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) alisema: ‘’Nilimwomba Mwenyezi Mungu alifanye hivyo sikio la Ali.’’150 Thaalabi ametaja kwa kusema: Ilipoteremka: “na 147 Tafsirul-Qurtubi Juz. 18 Uk. 143. 148 Tafsirul-Qurtubi Juz. 18 Uk. 189. 149 Tafsirul-Qurtubi Juz. 18 Uk. 192. 150 Tafsirul-Qurtubi Juz. 18 Uk. 264. 100

Page 100


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 2 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

11:16 AM

Ahlul Bayt ndani ya Tafsiri za Kisunni No.2 sikio lisikialo lisikie.” Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) alisema: ‘’Nilimwomba Mola wangu Mlezi alifanye hivyo sikio lako ewe Ali.’’ Kutoka kwa Abu Barzatu al-Aslamiy amesema: “Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) alimwambia Ali: “Hakika Mwenyezi Mungu Mtukufu ameniamuru nikusogeze karibu nisikutenge mbali, na nikuelimishe nawe usikie vilivyo. Na Mwenyezi Mungu amehakikisha unasikia vilivyo.”151

SURAT AL-MAARIJI Kauli ya Mwenyezi Mungu:

“Muulizaji aliuliza juu ya adhabu itakayotokea. Juu ya makafiri, hapana awezaye kuizuia.” (Surat al-Maariji: 1 - 2). Ibnu Abbas na Mujahid wamesema: “Muulizaji hapa ni al-Harith bin Nu’man al-Fihri. Hiyo ni pale alipofikiwa na habari za kauli ya Mtume kuhusu Ali (a.s.): “Ambaye mimi nina mamlaka juu yake basi Ali ana mamlaka juu yake.” Alimpanda ngamia wake na kuja mpaka alipofika Abtahu aliteremka kisha akasema: “Ewe Muhammad! Umetuamrisha kuhusu Allah tushahidilie kwamba hapana Mungu wa haki ila Allah na kwamba wewe ni Mtume wa Allah, tumekubali hilo kutoka kwako. Tuswali Swala tano tumekubali hilo kutoka kwako. Tutoe Zaka tumekubali hilo kutoka kwako. Kisha haujatosheka kwa haya yote mpaka umemfanya binamu yako bora juu yetu! Je jambo hili ni kutoka kwako binafsi au ni kutoka kwa Mwenyezi Mungu?”

151 Tafsirul-Qurtubi Juz. 18 Uk. 264. 101

Page 101


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 2 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

11:16 AM

Ahlul Bayt ndani ya Tafsiri za Kisunni No.2 Mtume akasema: “Naapa kwa yule ambaye hapana Mungu ila Yeye, hakika hili ni kutoka kwa Mwenyezi Mungu.” Al-Harith akageuka na kuelekea kwenye mnyama wake huku akisema: “Ewe Mwenyezi Mungu! Ikiwa ayasemayo ni haki basi tuteremshie mvua ya mawe kutoka mbinguni au tuletee adhabu iumizayo.” Wallahi kabla hajamfikia ngamia wake Mwenyezi Mungu akamwangushia jiwe utosini na likatokea nyumani kwake likamuuwa papo hapo. Ndipo ikateremka: “Muulizaji aliuliza juu ya adhabu itakayotokea.”152

SURAT AL-MUDATHIR Kauli ya Mwenyezi Mungu:

“Kila nafsi itafungika kwa chumo ililochuma Isipokuwa watu wa kheri.” (Sura al-Mudathir: 38 - 39). Abu Ja’far al-Baqir (a.s.) amesema: “Sisi na wafuasi wetu ndio watu wa kheri. Na kila mwenye kutuchukia ndiye aliye rehani wa matendo yake.”153

SURAT AL-INSAN Kauli ya Mwenyezi Mungu:

“Na huwalisha chakula masikini na yatima na mfungwa hali ya kuwa wanakipenda. Tunakulisheni kwa ajili ya radhi za Mwenyezi Mungu tu, hatutaki kwenu malipo wala shukurani.” (Sura al-Insan: 8 - 9). 152 Tafsirul-Qurtubi Juz. 18 Uk. 278. 153 Tafsirul-Qurtubi Juz. 19 Uk. 85. 102

Page 102


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 2 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

11:16 AM

Ahlul Bayt ndani ya Tafsiri za Kisunni No.2 Kutoka kwa Mujahid kutoka kwa Ibnu Abbas amesema: “Hasan na Husein walipatwa na maradhi, babu yao Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) alikwenda kuwaona, waarabu kwa jumla na masahaba wa Mtume wa Mwenyezi Mungu nao pia walikwenda kuwaona. Ali akasema: “Ikiwa wanangu watapona nitafunga siku tatu kumshukuru Mwenyezi Mungu.” Mtumishi wao Nubiyatu akasema: “Ikiwa mabwana zangu wawili watapona nitafunga siku tatu kumshukuru Mwenyezi Mungu.” Fatuma naye akasema mfano wa hayo na pia Hasan na Husen wakasema nasi tutawajibikiwa mfano wa hilo. Vijana wawili wakapata afya njema na hali nyumbani kwa aali Muhammad hawana kitu si kichache wala kingi. Ali akaenda kwa Myahudi, Simon bin Hariya mtu wa Khaybar, akakopa toka kwake pishi tatu za shairi. Akaja nazo mpaka akaziweka ndani, ndipo Fatima akachukua pishi moja akatwanga na kuoka mikate. Ali alipomaliza kuswali pamoja na Mtume alikuja nyumbani na kikawekwa chakula mbele yake, funga yao ya siku ya kwanza ilipopita mara masikini akafika mlangoni kwao akagonga akisema: “Assalam Alaykum enyi watu wa nyumba ya Muhammad, mimi ni maskini katika watoto wa umma wa Muhammad, nami ni mwenye njaa, nipeni chakula Mwenyezi Mungu atakupeni chakula cha Peponi.” Ali akamsika, akasoma shairi: ????? ???? ?????? ???????? ?? ???? ???? ?????? ??????? ??? ?????? ??????? ???????? ?? ???? ??????? ?? ????? ???? ??? ???? ???????? ???? ????? ????? ????? ???? ????? ??????? ????? ?????? ???????? ??????? ??????? ????? ??????? ?????? ???? ??? ???????? ???????? ????? ????? ???? ?? ????? ??? ?????? Fatima mwenye ubora na yakini, ewe binti wa mbora kuliko watu wote. 103

Page 103


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 2 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

11:16 AM

Ahlul Bayt ndani ya Tafsiri za Kisunni No.2 Hivi humwoni mkata masikini amesimama mlangoni akitoa sauti ya uchungu. Akimshitakia Mwenyezi Mungu na akinyenyekea. Analalamika kwetu kwamba ni mwenye njaa na mwenye huzuni. Kila mtu ni rehani wa yale aliyoyachuma na mwenye kutenda kheri atabainika. Ahadi yetu ni Pepo ya juu aliyoiharamisha Mwenyezi Mungu kwa bakhili.Na bakhili ana kisimamo dhalili, Moto utamvuta gerezani.154 Fatima naye akasoma shairi: ?????? ???? ???? ???? ????? ?? ??? ?? ???? ??? ???????? ??????? ?? ????? ?? ??????? ????????? ??? ?????? ??????? ???? ??? ?????? ?? ???????? ?? ????? ???????? ????????? ??????? ?????? ?? ?????? Amri yako kwangu ewe binamu yangu ni yenye kutekelezwa, sina haja na uduni wala udhalili. Naharakisha kumpa mkate, namlisha wala sisubiri muda. Nataraji nitakapowashibisha wenye njaa nitaungana na wabora na jamaa. Na nitaingia Peponi na hali nikiwa na uombezi. Wakampa chakula na wakashinda mchana kutwa na usiku kucha bila kuonja chochote ila maji. Ilipofika siku ya pili Fatima akachukua pishi akatwanga na kuoka mikate. Ali alipomaliza kuswali pamoja na Mtume (s.a.w.w.) alikuja nyumbani na kikawekwa chakula mbele yao, mara akafika mlangoni kwao yatima akagonga akisema: “Assalam Alaykum enyi watu wa nyumba ya Muhammad, yatima toka katika watoto wa muhajirana ambaye baba yangu amekufa kishahidi siku ya Aqabah, nipeni chakula Mwenyezi Mungu 154 Tafsirul-Qurtubi Juz. 19, Uk. 129. 104

Page 104


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 2 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

11:16 AM

Ahlul Bayt ndani ya Tafsiri za Kisunni No.2 atakupeni chakula cha Peponi.� Ali akamsikia, akasoma shairi: ????? ???? ??????? ??????? ??? ????? ??? ????????? ??? ??? ????? ??? ??????? ??? ????? ?????? ??? ???? ????? ??????? ?? ???? ?? ????? ?????? ??? ??????? ???? ???? ?????? ???????? ????? ?? ?????? ??? ??????? ?????? ??????? ???????? Fatima binti wa Sayyid karimu, binti wa Nabii asiye mwanaharamu. Mwenyezi Mungu amemleta yatima, atakayewahurumia watu leo naye atahurumiwa. Ataingia Peponi na hali amesalimika, bila shaka Pepo imeharamishwa juu ya muovu. Hatovuka Siratu iliyonyooka bali ataangukia motoni mpaka Jahim. Kinywaji chake humo ni usaha na maji ya moto.155 Fatima naye akasoma shairi akisema:

?????? ????? ???????? ?????? ??????? ?? ?????? ???? ?? ?????? ??? ????? ??? ????? ?????? ????????? ?

Namlisha leo wala sijali, namtanguliza Mwenyezi Mungu kabla ya familia yangu. Wameshinda na njaa na wao ni wanangu, mdogo wao atauawa katika vita. Huko Karbala atauawa kwa njama, ole wake na adhabu yule mwenye kumuuwa. 155 Tafsirul-Qurtubi Juz. 19, Uk. 130. 105

Page 105


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 2 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

11:16 AM

Ahlul Bayt ndani ya Tafsiri za Kisunni No.2 Moto utamvuta mpaka chini na hali mikononi mwake kafungwa pingu na minyororo.156 Wakampa chakula na wakashinda siku mbili mchana kutwa na usiku kucha bila kuonja chochote ila maji. Ilipofika siku ya tatu Fatima akachukua pishi lililobaki akatwanga na kuoka mikate. Ali alipomaliza kuswali pamoja na Mtume (s.a.w.w.) alikuja nyumbani na kikawekwa chakula mbele yao, mara mateka wa kivita akafika mlangoni kwao akagonga akisema: “Assalam Alaykum enyi watu wa nyumba ya Muhammad, mnatuteka na kutufunga na wala hamtupi chakula! Nipeni chakula mimi ni mateka wa Muhammad.� Ali akamsika, akasoma shairi: ????? ?? ???? ?????? ????? ???? ????? ????? ?????? ????? ???? ??? ???? ?? ???? ???? ???? ???? ??? ????? ?????? ??????? ?????? ?? ????? ?????? ??? ?????? ?????? ???????? ?? ???? ??????? ??? ??????? Ewe binti wa Mtume Ahmad, binti wa Mtume bwana mtiiwa. Mwenyezi Mungu amempa jina la Muhammad, bila shaka Mwenyezi Mungu amempamba kwa huruma. Huyu hapa mfungwa wa Mtume mwongozaji, amezuiliwa kwa kufungwa pingu yake na kizuizi. Mbele ya Aliye juu Mmoja mwenye kupwekeshwa, wanayoyalima wakulima watayavuna. Fatima naye akasoma shairi akisema: ?? ???? ??? ??? ???? ???? ?? ????? ????? ?? ???????? ?????? ?????? ???? ????? ?? ???? ?? ?????? ???? ?????? ????? ?? ?????? ?????? ???????? ??????? ??? ??? ???? ?? ???? ???? ????? ???? ???? 156 Tafsirul-Qurtubi Juz. 19, Uk. 130. 106

Page 106


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 2 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

11:16 AM

Ahlul Bayt ndani ya Tafsiri za Kisunni No.2 Kati ya kile kilicholetwa hakijabaki ila pishi moja, bila shaka kitanga changu kimeondoka pamoja na mkono157 wangu. Wallahi wanangu wana njaa, ewe Mola usiuache (mkono) upotee. Baba yao ni mwenye kutenda kheri, hutenda wema kwa kuanza. Na juu ya kichwa changu sina hijabu ila hijabu iliyofumwa kwa kamba. Wakampa chakula na wakashinda siku tatu mchana kutwa na usiku kucha bila kuonja chochote ila maji. Ilipofika siku ya nne wakiwa tayari wameshatimiza nadhiri yao, Ali alimshika Hasan mkono wa kulia na Husein mkono wa kushoto na kwenda nao kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) na hali wao wawili wakitetemeka kama vifaranga kutokana na ukali wa njaa. Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) alipowatizama alisema: “Ewe Abal-Hasan! Hali niionayo yaniumiza mno, twendeni kwa binti yangu Fatima.” Wakaenda kwake wakamkuta akiwa mihrabuni kwake na hali tumbo lake limeshikana na mgongo wake na macho yake yamebadilika kutokana na ukali wa njaa. Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) alipomtazama na kutambua njaa aliyonayo kupitia uso wake, alilia na kusema:158 “Ee Mwenyezi Mungu nakuomba msaada, Ahlul-Baiti wa Muhammad wanakufa kwa njaa.”159 Jibril (a.s.) akateremka na kusema: “Assalam Alayka. Mola wako Mlezi anakusalimu. Ewe Muhammad pokea, Mwenyezi Mungu anakupa pongezi kwa kitendo cha watu wa nyumba yako.” Mtume akasema: “Nichukue nini ewe Jibril?” 157 Mkono na Kitanga hapa ni kinaya ya Pishi la Kwanza na la Pili. Hivyo anaomba pishi hizo zisiende na kupotea bure bali ziambatane na malipo mema. – Mtarjumi. 158 Tafsirul-Qurtubi Juz. 19, Uk. 132. 159 Tafsirul-Qurtubi Juz. 19, Uk. 132.

107

Page 107


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 2 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

11:16 AM

Ahlul Bayt ndani ya Tafsiri za Kisunni No.2 Jibril (a.s.) akamsomea:

“Na huwalisha chakula masikini na yatima na mfungwa hali ya kuwa wanakipenda. Tunakulisheni kwa ajili ya radhi za Mwenyezi Mungu tu, hatutaki kwenu malipo wala shukurani.” (Sura al-Insan: 8 - 9).160 Kauli ya Mwenyezi Mungu:

“Humo wataegemea viti vya enzi humo hawataona jua wala baridi.” (Surat Insan: 13). Ibnu Abbas amesema: “Pindi watu wa Peponi watakapokuwa peponi ghafla wataona mwanga kama mwanga wa jua na Pepo imeangazwa kwa mwanga huo. Watasema: Mola wetu Mtukufu amesema: “Hawataona jua wala baridi.” hii ni nuru ya nini? Ridhwan atawaambia: “Hili si Jua wala si Mwezi, lakini huyu ni Fatima na Ali wamecheka, na kutokana na nuru ya kicheko chao Pepo imeangaziwa.” Na kwa ajili ya hao wawili Mwenyezi Mungu aliteremsha Sura:

“Hakika ulimfikia mtu wakati fulani wa zama ambapo hakuwa kitu kinachotajwa.” (Sura Insan: 1)”

160 Tafsirul-Qurtubi Juz. 19, Uk. 132. 108

Page 108


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 2 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

11:16 AM

Ahlul Bayt ndani ya Tafsiri za Kisunni No.2 Ibnu Abbas akasoma shairi:

Mimi ni mfuasi wa kijana ambaye kwa ajili yake iliteremshwa Sura Hal Ataa. Huyo ni Ali Al-Murtadha ambaye ni binamu wa al-Mustafa.�161

161 Tafsirul-Qurtubi Juz. 19,Uk. 136.

109

Page 109


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 2 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

11:16 AM

Ahlul Bayt ndani ya Tafsiri za Kisunni No.2

ORODHA YA VITABU VILIVYO CHAPISHWA NA AL-ITRAH FOUNDATION 1. 2. 3. 4. 5. 6. 7. 8. 9. 10. 11. 12. 13. 14. 15. 16. 17. 18. 19. 20. 21. 22. 23. 24. 25.

Qur'an Al-Kariim - Tafsir Al-Kashif Juzuu ya kwanza mpaka Thalathini Uharamisho wa Riba Uharamisho wa uwongo Juzuu ya Kwanza Uharamisho wa uwongo Juzuu ya Pili Hekaya za Bahlul Muhanga wa Imamu Husein (A.S.) Mikingamo iliyomzunguka Imamu Ali (A.S.) Hijab vazi Bora Ukweli wa Shia Ithnaashari Madhambi Makuu Mbingu imenikirimu Abdallah Ibn Saba Khadijatul Kubra Utumwa Umakini katika Swala Misingi ya Maarifa Kanuni za Ndoa na maadili ya Familia Bilal wa Afrika Abudharr Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu Salman Farsi Ammar Yasir Qur'an na Hadithi Elimu ya Nafsi Yajue Madhehebu ya Shia 110

Page 110


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 2 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

Ahlul Bayt ndani ya Tafsiri za Kisunni No.2 26. 27. 28. 29. 30. 31. 32. 33. 34. 35. 36. 37. 38. 39 40. 41. 42. 43. 44. 45. 46. 47. 48. 49. 50. 51. 52. 53. 54. 55. 56.

Ukusanyaji na Uhifadhi wa Qur'an Tukufu Al-Wahda Ponyo kutoka katika Qur'an. Uislamu mfumo kamili wa maisha ya kijamii Mashukio ya Akhera Al Amali Dua Indal Ahlul Bayt Udhuu kwa mujibu wa Kitabu na Sunna. Haki za wanawake katika Uislamu Mwenyeezi Mungu na sifa zake Amateka Na Aba'Khalifa Nafasi za Ahlul Bayt (a.s) Adhana. Upendo katika Ukristo na Uislamu Nyuma yaho naje kuyoboka Amavu n’amavuko by’ubushiya Kupaka juu ya khofu Kukusanya swala mbili Bismillah ni sehemu ya Qur’ani na husomwa kwa Jahara Kuwaongoza vijana wa kizazi kipya Kusujudu juu ya udongo Kusheherekea Maulidi Ya Mtume (s) Tarawehe Malumbano baina ya Sunni na Shia Kupunguza Swala safarini Kufungua safarini Umaasumu wa Manabii Qur’an inatoa changamoto as-Salaatu Khayrun Mina -'n Nawm Uadilifu wa Masahaba Dua e Kumayl 111

11:16 AM

Page 111


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 2 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

Ahlul Bayt ndani ya Tafsiri za Kisunni No.2 57. 58. 59. 60. 61. 62. 63. 64. 65. 66. 67. 68. 69. 70. 71. 72. 73. 74. 75. 76. 77. 78. 79. 80. 81. 82. 83. 84. 85.

Sauti Ya Uadilifu wa Binadamu Umaasumu wa Mitume - Faida Zake Na Lengo Lake Umaasumu wa Mitume - Majibu Ya Aya Zenye Utata Umaasumu wa Mitume - Umaasumu wa Mitume Muhammad (s) Nahju’l-Balaghah - Juzuu ya Kwanza Nahju’l-Balaghah - Juzuu ya Pili Kuzuru Makaburi Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Kwanza Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Pili Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Tatu Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Nne Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Tano Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Sita Tujifunze Misingi Ya Dini Sala ni Nguzo ya Dini Mikesha Ya Peshawar Malezi Ya Mtoto Katika Uislamu Ubora wa Imam 'Ali Juu ya Maswahaba Na Ushia ndio njia iliyonyooka Hukumu za Kifikihi zinazowahusu Wanawake Liqaa-u-llaah Muhammad (s) Mtume wa Allah Amani na Jihadi Katika Uislamu Uislamu Ulienea Vipi? Uadilifu, Amani na Mtume Muhammad (s) Mitala na Ndoa za Mtume Muhammad (s) Urejeo (al-Raja’a ) Mazingira Utokezo (al - Badau) Sadaka yenye kuendelea 112

11:16 AM

Page 112


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 2 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

Ahlul Bayt ndani ya Tafsiri za Kisunni No.2 86. 87. 88. 89. 90. 91. 92. 93. 94. 95.

Msahafu wa Imam Ali Uislamu na dhana Mtoto mwema Adabu za Sokoni Johari za hekima kwa vijana Maalimul Madrasatain Sehemu ya Kwanza Maalimul Madrasatain Sehemu ya Pili Maalimul Madrasatain Sehemu ya Tatu Tawasali Imam Mahdi katika Usunni na Ushia

96.

Maana ya laana na kutukana katika Qur’ani Tukufu

97.

Hukumu ya kujenga juu ya makaburi

98.

Swala ya maiti na kumlilia maiti

99.

Shiya na Hadithi (kinyarwanda)

100.

Mariamu, Yesu na Ukristo kwa mtazamo wa Kiislamu

101.

Hadithi ya Thaqalain

102

Fatima al-Zahra

103.

Tabaruku

104.

Sunan an-Nabii

105.

Historia na sera ya viongozi wema (Sehemu ya Kwanza)

106.

Historia na sera ya viongozi wema (Sehemu ya Pili)

107.

Mahdi katika sunna

108.

Kusalia Nabii (s.a.w)

109.

Ujumbe -Sehemu ya Kwanza

110.

Ujumbe - Sehemu ya Pili

111.

Ujumbe - Sehemu ya Tatu

112.

Ujumbe - Sehemu ya Nne 113

11:16 AM

Page 113


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 2 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

Ahlul Bayt ndani ya Tafsiri za Kisunni No.2 113.

Ngano ya kwamba Qur’ani imebadilishwa

114.

Iduwa ya Kumayili

115.

Maarifa ya Kiislamu.

116.

Ukweli uliopotea sehemu ya Kwanza

117.

Ukweli uliopotea sehemu ya Pili

118.

Ukweli uliopotea sehemu ya Tatu

119.

Ukweli uliopotea sehmu ya Nne

120.

Ukweli uliopotea sehmu ya Tano

121.

Johari zenye hekima kwa vijana

122.

Safari ya kuifuata Nuru

123.

Idil Ghadiri

124.

Myahudi wa Kimataifa

125.

Kuanzia ndoa hadi kuwa Wazazi

126.

Visa vya kweli sehemu ya Kwanza

127.

Visa vya kweli sehemu ya Pili

128.

Muhadhara wa Maulamaa

129.

Mwanadamu na Mustakabali wake

130.

Imam Ali binamu ya Mtume Sehemu ya Kwanza

131.

Imam Ali binamu ya Mtume Sehemu ya Pili

132.

Khairul Bariyyah

133.

Uislamu na mafunzo ya kimalezi

134.

Vijana ni Hazina ya Uislamu.

135.

Yafaayo kijamii

136.

Kusoma sura zenye Sijda ya wajibu

137.

Taqiyya

138.

Vikao vya furaha 114

11:16 AM

Page 114


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 2 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

11:17 AM

Ahlul Bayt ndani ya Tafsiri za Kisunni No.2 139.

Shia asema haya Sunni asema haya Wewe wasemaje?

140.

Uislamu na Mazingatio Sehemu ya Kwanza

141.

Uislamu na Mazingatio Sehemu ya Pili

142.

Azadari-Kuhuzunika na Kuomboleza

143.

Sunna katika Kitabu Fiqhi al-Sunnah

144.

Mtazamo Mpya - Wanawake katika Uislamu

145.

Kuonekana kwa Allah

146.

Tabia njema kwa Mujibu wa Ahlul-Bayt (Sehemu ya Kwanza)

147.

Tabia njema kwa Mujibu wa Ahlul-Bayt (Sehemu ya Pili)

148.

Ndugu na Jirani

149.

Ushia ndani ya Usunni

150.

Maswali na Majibu

151.

Mafunzo ya hukmu za ibada

152

Ahlul Bayt ndani ya tafsiri za Kisusunni No 2

153.

Ahlul Bayt ndani ya tafsiri za Kisusunni No 3

155.

Abu Huraira

156.

Kati ya Alama kuu za dini Swala ya Jamaa. na Adabu za Msikiti na Taratibu zake.

157.

Uadilifu katika Uislamu

115

Page 115


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 2 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

11:17 AM

Ahlul Bayt ndani ya Tafsiri za Kisunni No.2

BACK COVER Ahlul Bayt, yaani Watu wa Nyumba ya Mtume Muhammad SAW ni viongozi ambao Mtume alituusia tuwafuate. Katika hotuba yake ndefu na maarufu aliyoitoa pale Ghadir Khumm katika msafara wake wa kurejea kutoka Hija yake ya mwisho, Mtukufu Mtume SAW alisema haya mbele ya masahaba na mahujaji zaidi ya laki moja: “...Nakuachieni vitu viwili vizito: Qur’ani na Ahlul Bayt wangu. Viwili hivyo havitaachana mpaka vinifikie katika [hodhi ya] Kawthar. Nawausia juu ya Ahlul Bayt wangu! Angalieni jinsi mtakavyojihusisha nao. Kama mkishikamana na viwili hivi hamtapotea kamwe...” (kwa maelezo zaidi soma kitabu cha al-Ghadir) Lakini bahati mbaya sana sio Waislamu wote wanaowafuata Ahlul Bayt AS pamoja na kwamba wanavyuoni wa madhehebu zote wameandika habari zao katika vitabu vyao na kuonesha kwamba hawa ni viongozi wa Umma huu wa Kiislamu. Mwandishi wa kitabu hiki anajaribu kuthibitisha hilo kwa kutoa rejea mbalimbali kutoka vitabu maarufu vya wanavyuoni wa Kisunni. Kimetolewa na kuchapishwa na: Alitrah Foundation S.L.P. 19701 Dar es Salaam, Tanzania Simu: +255 22 2110640 Simu/Nukushi: +255 22 2127555 Barua Pepe: alitrah@raha.com Tovuti: www.alitrah.org Katika mtandao: www.alitrah.info

116

Page 116


Turn static files into dynamic content formats.

Create a flipbook
Issuu converts static files into: digital portfolios, online yearbooks, online catalogs, digital photo albums and more. Sign up and create your flipbook.