Tabia njema kwa mujibu wa Ahlul Bayt (a.s)

Page 1

Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:19 PM

Page A

AKHLAQ AHLUL BAYT (A.S.) TABIA NJEMA KWA MUJIBU WA AHLUL BAYT (A.S)

Sehemu ya kwanza: Tabia njema na mbaya

MTUNZI: SAYYID MAHDI AS-SADR

MTARJUMI: SHEIKH MULAB. H. SALEH LULAT


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:19 PM

ŠHaki ya kunakili imehifadhiwa na: AL-ITRAH FOUNDATION ISBN: 9987 - 427 - 39 - 1 Kimeandikwa na: SAYYID MAHDI AS-SADR

Kimetajumiwa na: SHEIKH MULAB. H. SALEH LULAT

S. L. P. 19701, Dar-es-Salaam, Tanzania Email:info@alitrah.org Website:www.alitrah.org Kimehaririwa na: Dr. M. S. Kanju S. L. P. 19701, Dar-es-Salaam, Tanzania Email: mokanju2000@yahoo.com Website:www.alitrah.org Kimepangwa katika Kompyuta na: Ukhti Pili Rajab Toleo la kwanza: Juni 2007 Nakala: 1000 Kimetolewa na kuchapishwa na:

Al-Itrah Foundation P. O. Box 19701, Dar-es-Salaam, Tanzania Simu: +255 22 2110640 Fax: +255 22 2131036 Email: info@alitrah.org Website: www.alitrah.org www.alitrah.info

Page B


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:19 PM

Page C

YALIYOMO Tabia njema.......................................................................................2 Maana ya tabia njema........................................................................2 Ahlul Bayt (a.s) na kusifu Tabia njema.............................................3 Tabia mbaya.....................................................................................10 Tabia baina ya uongofu na upotofu.................................................11 Tiba ya Tabia mbaya.......................................................................13 Ukweli............................................................................................ 14 Matokeo ya ukweli..........................................................................16 Aina za ukweli.................................................................................17 Uongo..............................................................................................17 Maovu ya Uongo.............................................................................19 Sababu za Uongo.............................................................................20 Aina za Uongo.................................................................................21 Tabia ya Uongo................................................................................24 Uongo unaokubalika........................................................................25 Uvumilivu na kuzuia Hasira........................................................ ...25 Ghadhabu....................................................................................... 34 Sababu za ghadhabu........................................................................35 Madhara ya ghadhabu................................................................. ....36 Ghadhabu Nzuri na mbaya..............................................................36 Unyenyekevu...................................................................................39 Kutakabari.......................................................................................44 Mabaya ya kutakabari.....................................................................48 Sababu za kutakabari......................................................................49 Viwango vya kutakabari..................................................................50 Aina za kiburi..................................................................................50 Tiba ya kiburi................................................................................. 51


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:19 PM

Page D

Kutosheka........................................................................................52 Mema ya kukinai.............................................................................54 Tamaa............................................................................................. 56 Maovu ya Tamaa..............................................................................58 Tiba ya Tamaa..................................................................................59 Ukarimu...........................................................................................59 Mema ya ukarimu............................................................................61 Maeneo ya ukarimu.........................................................................62 Sababu za ukarimu...........................................................................64 Kufikiria wengine kuliko mwenyewe.............................................64 Ubakhili ..........................................................................................67 Maovu ya ubakhili...........................................................................69 Sura za ubakhili..............................................................................70 Tiba ya ubakhili...............................................................................70 Umiliki wa nafsi (Iffat)....................................................................77 Uhakika wa umiliki nafsi................................................................78 Kiwango cha kati kinachotakiwa.....................................................78 Mazuri ya umiliki nafsi....................................................................79 Mazuri ya uadilifu...........................................................................99 Dhulma..........................................................................................102 Aina za dhulma..............................................................................106 Matokeo mabaya ya dhulma.........................................................110 Tiba ya dhulma.............................................................................. 111 Ikhlas........................................................................................... 112 Fadhila za Ikhlasi...........................................................................114 Vizuizi dhidi ya Ikhlas...................................................................115 Vipi tutapata Ikhlas........................................................................116 Ria (kujionyesha)...........................................................................117 Aina za Ria....................................................................................120 Sababu za Ria.............................................................................. 121


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:19 PM

Page E

Baadhi ya ukweli wa mambo.........................................................121 Mabaya ya Ria ..............................................................................123 Tiba ya Ria.....................................................................................124 Tiba ya Ria kivitendo.....................................................................124 Kujisikia, Ghururi,(UJB)...............................................................125 Maovu ya kujiona..........................................................................127 Tiba ya Kujiona.............................................................................128 Yaqini............................................................................................ 129 Sifa za wenye Yaqini..................................................................... 131 Daraja za Imani............................................................................. 132 Aina za Imani.................................................................................133 Subira............................................................................................ 136 Aina za Subira...............................................................................139 Mazuri ya Subira...........................................................................145 Kushukuru.................................................................................... 147 Aina za Shukrani...........................................................................150 Fadhila ya kushukuru.....................................................................152 Vipi tutajipamba na (Tabia) ya kushukuru.....................................154 Kutawakali................................................................................... 155 Uhakika wa Tawakuli....................................................................159 Daraja za Tawakuli........................................................................160 Mema ya Tawakuli........................................................................160 Jinsi ya kufikia Tawakuli..............................................................162 Kumuogopa Mwenyezi Mungu.....................................................164 Hofu baina ya kuzidi na kupungua .............................................. 166


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:19 PM

Page F

Mazuri ya Hofu..............................................................................167 Jinsi ya kudiriki hofu.....................................................................169 Dokezo katika visa vya wachamungu............................................170 Kuwa na matumaini (matarajio) na Mwenyeezi Mungu..............171 Uhakika wa kutaraji.......................................................................179 Hekima ndani ya kutaraji na kuhofu.............................................180 Ghururi......................................................................................... 181 Aina za Ghururi.............................................................................182 Kughurika na dunia.......................................................................182 Kanuni ya milele............................................................................186 Maovu ya kughurika na dunia.......................................................189 Tiba ya ghururi..............................................................................190 Ghururi ya Elimu...........................................................................194 Taha inayokubalika na isiyokubalika.............................................199 Ghururi ya mali........................................................................... 199 Mali baina ya sifa na shutuma.......................................................200 Ghururi ya nasaba..........................................................................202 Husda............................................................................................ 204 Sababu za Husda............................................................................205 Maovu ya Husda............................................................................207 Tiba ya Husda............................................................................... 209 Kuteta........................................................................................... 209 Kujikinga na kusikiliza ya utesi.................................................. 212 Sababu za kuteta.......................................................................... 213 Hali inayojuzu kuteta.....................................................................215 Tiba ya kuteta................................................................................ 216 Kukashifu..................................................................................... 217 Umbea........................................................................................... 218 Sababu za umbea.......................................................................... 220 F


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:19 PM

Page G

Ubaya wa umbea........................................................................... 220 Jinsi ya kukabiliana na mmbea..................................................... 222 Lugha chafu, Kutusi na Qadhfu.....................................................222 Sababu za lugha chafu ..................................................................226 Maovu ya lugha chafu................................................................... 226 Kukejeli....................................................................................... 227 Maneno mazuri..............................................................................229 Maafa ya madhambi..................................................................... 234 Toba.............................................................................................. 242 Ukeli wa Toba................................................................................242 Fadhila za Toba..............................................................................243 Wajibu wa Toba na uharaka wake..................................................246 Kutubia upya................................................................................. 247 Utaratibu wa Toba......................................................................... 250 kukubali toba............................................................................... 250 Shauku za Toba............................................................................. 251 Kujihesabu na kujichunguza.........................................................252 Maana ya kujihesabu.................................................................... 252 Maana ya kujichunguza.................................................................252 Nidhamu ya kujihesabu.................................................................254 Kuchukua fursa ya Umri...............................................................256 Amali njema..................................................................................259 Kumtii na kumcha Mwenyeezi Mungu ...................................... 263 Hakika ya utiifu na uchamungu................................................... 268 Kuwa na msimamo imara............................................................. 272

G


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:19 PM

Page H

UTANGULIZI Sifa zote ni zake Mola wa walimwengu, na rehma na amani zimteremkie Mtume wetu Muhammad na Aali zake wema waliotoharika. Elimu ya tabia (akhlaq) ni elimu inayofundisha ubora wa tabia na ubaya wake na kutilia mkazo katika kujipamba na tabia njema na kujiepusha na tabia mbaya. Na elimu hii inachukua nafasi ya juu na daraja tukufu baina ya elimu kwa sababu ya utukufu wa maudhui yake na ukuu wa malengo yake. Elimu hii ndiyo nidhamu ya elimu zingine, njia ya ukamilifu, dalili ya fadhila na dhihirisho la uzuri wa elimu zote. Elimu zote zinategemea tabia njema, hupambika kwa uzuri wake na hupendeza kwa adabu zake. Ikikosekana tabia njema basi elimu inakuwa finyu bila faida na husababisha machukizo na kichefuchefu. Hakuna mshangao kwani ni tabia njema ndiyo inayokamilisha ndani ya mwanadamu maana ya utu na kumvika joho la uzuri, na ukamilifu, utukufu wa nafsi na karama. Pia kwa tabia mbaya mwanadamu huporomoka hadi daraja ya ushenzi na unyama. Athari ya tabia njema haikomei kwa watu binafsi bali inashika mataifa na kaumu. Tabia ndio kioo cha uhai wa taifa au kaumu na kigezo cha maendeleo au kubaki nyuma. Historia imejaa matukio na mafunzo yaonyeshayo kwamba kuharibika na kumomonyoka tabia ndiyo sababu iliyobomoa misingi ya tamaduni na kushindwa dola nyingi na falme.


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:19 PM

Page i

Kaumu yoyote ikikosa tabia njema, basi wawekeeni msiba na walilieni. Na yatutosheleza kuhusu utukufu wa tabia njema, ya kwamba Mtume (s) aliipa kipaumbele na akaijalia kuwa ndio lengo la kuja kwake kama alivyo sema: (nilitumwa ili nikamilishe tabia njema). Na hii ndiyo elimu ya tabia inayolenga kuadibisha dhamira ya watu, kunyoosha tabia zao na kuwapeleka kwenye mwenendo bora na wa mfano. Mifumo ya utafiti wa kimaadili na njia zake yahitilafiana kwa kutegemea watafiti wa zamani au wa sasa. Hitilafu hiyo ni kati ya anayechupa mipaka katika falsafa yake ya kimaadili ikaifanya kavu, ngumu kwa utekelezaji na yule anayehukumu kwa matamanio yake akaielezea kama vile mila zake hasa zilivyojengeka, mazingira finyu na hulka yake, jambo ambalo linaondolea mfumo huo ukamilifu na uasili. Haya yanafanya mifumo hiyo kutofaa kuwa katiba ya daima ya kimaadili kwa walimwengu. Kwa mtafiti mlinganishi kati ya mifumo hiyo, mfumo unaoonekana bora na kamili ni mfumo wa kiislamu, mfumo unaotegemea Qur’ani Tukufu na tabia njema za Mtume (s) na Ahlul Bait (s). Mfumo huu umepambwa kwa uwastani, usawa, usafi wa mafunzo, utukufu wa lengo, hekima ya kulingania na kufaa vizuri kwa kila zama na fikra. Mfumo huu ni wa pekee na mfano bora ambao unaweza kuwapandisha, watu na jamii, kuelekea kwenye ukamilifu wa kitabia na mfano wa kitabia bora kwa kutumia njia ya mvuto na mapenzi - inavutia akili na nyoyo - na kwa muda mfupi na njia nyepesi. Hii ni njia inayowakilisha utukufu wa adabu za ufunuo wa Mwenyezi Mungu (swt), ufasaha wa Ahlul Bayt (s), na hekima zao. Ahlul Bayt (s) i


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:19 PM

Page ii

wamefuata njia hii, wakachukua mafunzo yake na wakanywa maji ya kisima chake ili kuyabadilisha kwa watu kuwa hekima, adabu na masomo ya tabia ya pekee ambayo yanaangazia nafsi na kuitoharisha. Kwa ajili ya haya nimependa mfumo huu na kuandika kitabu hiki na kupangilia mada zake kwa nuru ya mfumo huo. Na ikiwa watu watafaidika na kuongoka na wengine wakashindwa, hilo halitii ila katika hekima na utukufu wa mafunzo yake, bali tatizo lipo katika hitilafu za maumbile ya watu na maelekeo yao ya kupokea mwongozo na kufaidika nao kama ilivyo kwa wagonjwa, dawa ile ile moja inaweza ikamtibu huyu na isimtibu yule. Linalosikitikisha sana na kuumiza roho, ni kwamba Waislamu baada ya kuwa viongozi wa mataifa mengine, wenye kushika bendera ya ubora na tabia njema, wamekwisha poteza nafasi yao kwa kukengeuka taratibu za kiislamu na tabia zake njema. Hili limewaweka katika hali duni na kubaki nyuma kitabia. Kwa hivyo basi ni wajibu kwa Waislamu ikiwa wanataka utukufu, karama na sifa njema, basi warejeshe yale ambayo waliyoyatupa katika urithi wao mkubwa wa tabia njema na wafaidike na rasilimali hiyo iliyohifadhiwa. Kwa kutekeleza hilo ndipo watarejesha imani ya watu na kuwa kama alivyotaka Mwenyezi Mungu: Umma bora ulioletwa kwa watu Na hilo ni tamanio ghali. Haiwezekani kupata hilo ila kwa jitihada za viongozi wenye ikhlasi wa umma wa kiislamu kuwahamasisha na kuwahimiza Waislamu kushikamana na tabia njema za kiislamu na pia kusambaza mafunzo yake yanayojenga na kuyaonyesha kwa watu kwa njia ya kuvutia ambayo itakayowafanya watu wapende kusoma na kufaidika nayo. Hili ndilo lililonisukuma kuandika kitabu hiki na kukipangilia kwa sifa zifuatazo: 1. - Kitabu hiki hakikuchukua elimu yote ya tabia, bali kimechota mafunii


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:19 PM

Page iii

zo muhimu na yenye athari kubwa kwa maisha ya mwanadamu. Nimejitahidi kadri ya uwezo wangu kuepuka lugha ya kitaalamu na maneno yake magumu na kutumia njia nyepesi na fupi kumpa nafasi msomaji afurahie na asichoke. 2. - Kuchagua hadithi kutoka katika vitabu vinavyotegemewa na rejea zinazoaminika kwa wanahadithi na wasimulia hadithi (marawi). 3. - Kutia umuhimu katika kutaja mema ya tabia njema na ubaya wa tabia mbaya na kuweka wazi athari za tabia hizo - njema na mbaya kwenye roho na kiwiliwili katika uhai wa mtu binafsi na jamii. La muhimu kutajwa hapa ni kwamba kipimo cha kitabia katika kukadiria fadhila za kitabia na kuweka mipaka ya ukweli wake ni: ukati na usawa uliyosalimika na israfu au upungufu.Tabia njema iliyoridhiwa ni ile iliyo ya kati baina ya kuchupa mipaka na kupungua, kama vile nukta inavyozunguka mzingo (duara). Iffat (kumiliki nafsi) ni fadhila baina ya tamaa na kudumaa (kutokuwa na harakati); utawa ukizidi, mtu anapooza na kutokuwa na harakati za kujishughulisha na mambo muhimu ya maisha na starehe zake halali. Na ikiwa utapungua, anakuwa na pupa na uroho, mwenye kuzama katika starehe na matamanio yake. Ushujaa ni fadhila baina ya ujasiri (kutojali kuangamia) na uoga: mtu akizidisha ushujaa anakuwa jasiri anayevamia mambo ambayo ni vyema kujiepusha nayo. Na ikiwa utapungua, basi mtu anakuwa muoga kiasi cha kuogopa kufanya ambayo ni vizuri kuyafanya. Ukarimu ni fadhila baina ya ubadhirifu na ubakhili: ukizidi ukarimu, mtu anafanya israfu na ubadhirifu na kufanya ukarimu kwa yule asiyestahiki kupewa. Ukipunguwa, mtu anakuwa mchoyo na bakhili kwa yale ambayo inatakiwa kutoa na kufanya ukarimu, nk‌ iii


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:19 PM

Page iv

Kwa sababu hiyo, imekuwa kupata tabia njema na kujipamba nazo na kusimama juu yake ni katika malengo makuu ambayo wenye akili za juu na nafsi tukufu wanashindania. Na bila shaka hawapati hilo ila wenye bahati kubwa. Na mimi nataraji kwamba Mwenyezi Mungu (s.w.t.) atanikubalia kazi yangu hii dhaifu na atanijaza thawabu kwa wema wake mkubwa na ukarimu mwingi. Na pia nataraji ataniwezesha na ndugu waumini kufaidika na kitabu hiki na kuongoka kwa nuru yake. Hakika Mwenyezi Mungu ndiye mpaji wa uongofu na tawfiqi (mafanikio).

Al-Kadhwimiyyah Sayyid Mahdi Sadr

iv


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:19 PM

Page v

NENO LA MCHAPISHAJI Kitabu kilichoko mikononi mwako, ni tarjuma ya kitabu cha Kiarabu, kwa jina la Akhlaq Ahlul Bayt (a.s.) (Elimu ya tabia kwa mujibu wa mafunzo ya Ahlul Bayt) (a.s) kilichandikwa na: SAYYID MAHDI AS SADR Tabia njema ni hali ya nafsi ambayo inasukuma kuwa na uhusiano mzurina watu, kushirikiana nao vyema kwa bashasha, kauli nzuri, mwenendo mzuri, uhusiano na upole. Ni ukweli usiopingika kwamba kuna mmomonyoka mkubwa sana wa maadili katika jamii yetu ya zama hii. Vijana wetu na hata watu wazima wanapupia sana katika kuiga tamaduni za nje hususan Magharabi, wakiwa na fikra kwamba kila kinachofanywa na watu wa magharibi ni maendeleo na kinafaa kuiga. Wakimuona Mzungu akitembea nusu uchi wao wanaona hayo ni maendeleo, na kesho utawaona nao wanatembea nusu uchi, ukiliza kulikoni wanakuambia haya ndio maisha na kwamba wewe umepitwa na wakati. Hili ni tatizo kubwa sana katika jamii yetu hii ya sasa. Lakini watu huiga mazuri na sio kuiga machafu. Mwandishi wa kitabu hiki anatuletea watu wa kuiga; watu wenye tabia nzuri, watu waliotakaswa na Mwenyezi Mungu (Qur'an33:33). Hawa ni watu wa nyumba ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) ambao walikuwa wachamungu, wakarimu, wapole na wenye tabia nzuri ya kuigwa. Hii yote ni katika juhudi za mwandishi huyu kutaka kurekebisha tabia na mwenendo katika jamii inayotuzunguka. Tumekiona kijitabu hiki ni chenye manufaa sana, na kitafaa sana katika kurekebisha tabia mbaya za watu, na badala ya kuiga machafu ya watu wa v


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:19 PM

Page vi

magharibu tuige mazuri ya watu kama hawa wachamungu. Tunamshukuru Ndugu yetu: SH. Mulaba h. Saleh Lulat kwa kukubali jukumu hili la kukifanyia tarjuma kitabu hiki. Vile vile tunawashukuru wale wote walioshiriki kwa njia moja au nyingine hadi kufanikisha kuchapishwa kwa kitabu hiki.

Mchapishaji: Al-Itrah Foundation P. O. Box 19701, Dar-es-Salaam, Tanzania Simu: +255 22 2110640 Fax: +255 22 2113107 Email: info@alitrah.org Website: www.alitrah.org

vi


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:19 PM

Page 1


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:19 PM

Page 2

Tabia njema kwa mujibu wa Ahlul Bayt (a.s)

TABIA NJEMA MAANA YA TABIA NJEMA

Tabia njema ni hali ya nafsi ambayo inasukuma kuwa na uhusiano mzuri na watu, kushirikiana nao vyema kwa bashasha, kauli nzuri, uhusiano kwa upole kama alivyofasiri Imamu Swadiq (s) pindi alipoulizwa kuhusu mipaka ya tabia njema na akafafanua kwamba tabia njema ni: “kuwa laini, na maneno yako yakawa mazuri, na ukakutana na nduguyo kwa uchangamfu mzuri�1 Katika matarajio ambayo kila mwenye akili safi anatamani kuyafikia na akajitahidi kuyahakikisha, ni yeye kuwa na shaksiya yenye mvuto, cheo cha juu na akapendwa na kutukuzwa na watu. Na hakika hilo ni tarajio ghali na lengo kubwa ambalo hawalifikii ila wenye fadhila na uwezo kama vile elimu, ukarimu, ushujaa na kama hayo katika mambo matukufu. Matukufu hayo hayawezi kuleta athari, kutukuzwa na utukufu wa daraja ila kwa kujipamba kwa uzuri wa tabia njema . Kwa sababu hiyo tabia njema ndiyo uti wa mgongo wa yote mema na msingi wa kupata sifa, utukufu na mahaba.

1. Al Kaafy

2


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:19 PM

Page 3

Tabia njema kwa mujibu wa Ahlul Bayt (a.s)

AHLUL BAIT(A.S) NA KUSIFU TABIA NJEMA Tazama jinsi Ahlul Bait (a.) wanavyotukuza tabia njema na kuhimiza kushikamana nayo kwa njia na mbinu mbalimbali zenye kuvutia: Mtume (s) anasema: 1. - “Wabora wenu ni wale wabora wenu kitabia, wanyenyekevu na makarimu ambao wanaozowea na wakazoeleka na watu na ambao nyumba zao huingiliwa”2 2. - “Mwenye tabia njema anaujira kama ule wa anayefunga na kusali.”3 3. - “Hamtaweza kuwapeleka watu kwa mali zenu, bali wapelekeni kwa tabia zenu”4 Muhammad al Baqir (a) amesema: 4.- “Hakika mkamilifu wa waumini kiimani ni yule mwenye tabia bora zaidi.”5 Ja’far as Swadiq (a) amesema: 5. - “Baada ya faradhi, Muumini hatangulizi kwa Mwenyezi Mungu (swt) amali aipendayo sana Mwenyezi Mungu (swt) kama vile kuwa mwingi wa tabia njema kwa watu”6 6. - “Hakika Mwenyezi Mungu (swt) anampa mja wake thawabu kwa kuzingatia tabia njema, kama vile anavyompa mujahid katika njia ya Mwenyezi Mungu (swt)”7 7.- “Hakika tabia njema inayeyusha madhambi kama vile jua linavyoyeyusha barafu”8 8. - “Wema na tabia njema vinajenga nyumba na kuongeza umri.”9 2. Al Kaafy 3. Al Kaafy 4. Al Kaafy 5. Al Kaafy 6. Al Kaafy 7. Al Kaafy 8. Al Kaafy 9. Al Kaafy

3


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:19 PM

Page 4

Tabia njema kwa mujibu wa Ahlul Bayt (a.s) 9. - “Ukitaka kuheshimiwa basi uwe laini, na ukitaka kudharauliwa basi uwe mgumu.”10 Na inatosha kwa tabia njema, utukufu na fadhila kwamba Mwenyezi Mungu (swt) hakutuma mitume na manabii kwa watu ila baada ya kuwapamba kwa hulka hii tukufu. Hulka hii ndiyo alama ya maadili yao mema na anuani ya shaksiya yao. Mtume (s) – bwana wa mitume - alikuwa mfano wa juu wa tabia njema. Aliweza kwa tabia yake ya mfano, kumiliki nyoyo na akili na kwa hilo akastahiki sifa ya Mwenyezi Mungu (swt) aliposema Mkweli wa kusema:

“Hakika wewe upo kwenye tabia bora kabisa.” (68:4) Akitoa taswira ya tabia ya Mtukufu Mtume, Imam Ali (a) anasema: “Alikuwa Mtume karimu kuliko watu wote, shupavu, mkweli, mtimiza wajibu, mpole na mtukufu kiuhusiano. Kila amuonaye basi humstahi sana na kumheshimu. Na anayeingiliana naye akamjua basi humpenda. Sijaona mfano wake kabla yake na baada yake”.11 Itutoshe kukumbuka yaliyompata kutoka kwa Maquraishi. Walimuandama na kumywesha kila aina ya shida na balaa mpaka wakamlazimisha kuhama jamaa zake na mji wake. Pindi Mwenyezi Mungu (swt) alipompa nusra na ushindi, walikuwa na hakika kwamba Mtume (s) atalipiza kisasi na kuwaadhibu. Lakini Mtume (s) aliwauliza: mwafikiria mimi nitawafanya je? Maquraishi wakamjibu: heri, wewe ni ndugu mwema na mtoto wa ndugu mwema. Basi Mtume (s) akawaambia mimi nasema kama alivyosema ndugu yangu Yusufu (a): Hakuna lawama kwenu leo, Mwenyezi Mungu (s.w.t.) akusameheni na hakika Yeye ni mwingi wa kurehemu 10. Tuhaful Uquul 11. Safinatul Bihaar 4


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:19 PM

Page 5

Tabia njema kwa mujibu wa Ahlul Bayt (a.s) (12:92). Nendeni, nyinyi ni waachwa huru. Imepokelewa kutoka kwa Anas kwamba alisema: Nilikuwa na Mtume (s) na alikuwa amejitanda burda yenye pindo nene. Akaja bedui mmoja akamvuta joho lake kwa nguvu kiasi kwamba lile pindo la burda likamuathiri mabegani kisha akasema: “Ewe Muhammad! nipakilie juu ya ngamia wangu wawili hawa uliyonacho katika mali ya Mwenyezi Mungu, hakika hunipakilii mali yako wala ya babako.” Akanyamaza Mtume (s) kisha akasema: “Mali, kweli ni mali ya Mwenyezi Mungu (swt) na mimi ni mtumwa wake”. Kisha akamwambia: “Huogopi kwamba utalipiziwa kisasi?” Yule bedui akajibu hapana. Mtume (s) akamwuliza: “kwa nini?” Akasema: “Kwa sababu wewe hulipi ubaya kwa ubaya.” Mtume akacheka na akaamrisha apakiliwe shairi kwenye ngamia mmoja na tende kwenye ngamia wa pili.12 Imam Ali (a) alisema: “Yahudi mmoja alikuwa akimdai Mtume dinari kadha. Akataka Mtume (s) amlipe lakini Mtume(s) akamwambia: “Ewe yahudi! Mimi sina cha kukulipa.” Yule yahudi akasema: “Mimi sitokuacha mpaka unilipe. Kwa hiyo nakaa pamoja nawe.” Akakaa na Mtume (s) mpaka akasali mahala hapo dhuhuri na alaasiri, magharibi na alfajiri. Wakawa masahaba wa Mtume wakimtishia na kumkamia. Mtume akawatazama kisha akasema: “Mtamfanya nini?!” Masahaba wakamjibu: “Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, yahudi anakufanya mahabusu wake!” Mtume akawaeleza: “Mola wangu hakunituma kudhulumu yeyote aliye na mkataba nasi (wafuasi wa dini zingine) au asiye.” Lilipopanda jua, yule yahudi akatamka: “Ash-hadu an laailaha illa llah wa ash-hadu anna Muhammadan ‘Abduhu wa Rasuluhu.” (kwamba nashuhudia ya kuwa hapana Mungu isipokuwa Allah na kwamba Muhammad ni mja wake na Mtume wake) na nusu ya mali yangu naitoa fisabilillah (itumike katika njia ya Mwenyezi Mungu) na naapa wallahi sikukufanyia hayo niliyoyafanya ila kutaka kuthibitisha sifa yako katika Taurati. Nilisoma sifa yako katika 12. Safinatul Bihaar 5


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:19 PM

Page 6

Tabia njema kwa mujibu wa Ahlul Bayt (a.s) Taurati kwamba: Muhammad mtoto wa Abdullah, mahali pa kuzaliwa Makkah na pa kuhamia Twayyibah. Si fidhuli wala mgumu wa moyo wala mwenye kupiga kelele (kupaza sauti) wala mwenye kujivika mambo machafu, wala mwenye lugha mbaya. Na mimi nashuhudia kuwa hakuna mungu isipokuwa Allah na kwamba wewe ni Mtume wa Mwenyezi Mungu. Basi mimi natoa mali yangu hii hapa, toa hukumu kuhusu mali hii kama vile Mwenyezi Mungu anavyoamrisha.” Na yahudi huyu alikuwa na mali nyingi.13 Na hivi ndivyo walivyokuwa maimamu wa Ahlul Bait (a) ambao wametoharishwa katika tabia zao njema na utukufu wa mwenendo wao. Wasimulizi wa hadithi (marawi) wametufikishia matendo ya ajabu na mafunzo ya milele kutoka maisha yao ya kuigwa na tabia zao za pekee. Katika hayo ni yale yaliyopokelewa kutoka kwa Imam Hasan al Askary (a) aliyesema: “Siku moja baba na mtoto walikuja kwa Imam Ali (a), akasimama na kuwapokea kwa heshima kisha akawakalisha mbele ya majlis yake na kisha mwenyewe akakaa mbele yao. Akaomba waletewe chakula. Baada ya kula, Qambar akaja na beseni, birika la maji na kitambaa. Imam Ali (a) akachukua birika na kumnawisha mkono baba na huku akikataa lakini Imam Ali (a) akamuapia kwamba lazima atamnawisha kama vilevile ambavyo angekubali kuoshwa na Qambar. Kisha akampa birika Muhammad bin Hanafiya ili amnawishe kijana mwenziwe na huku akisema: “Mwanangu kama kijana huyu angekuja bila ya baba yake ningemwagia maji ili aoshe mikono yake. Lakini Mwenyezi Mungu anakataa baba na mtoto kufanyiwa sawa ikiwa watakuwa mahala pamoja. Kwa hivyo baba kamwagia baba na mtoto amwagie mtoto mwenziwe. Muhammad bin Hanafiyyah akamwagia kijana mwenziwe. Kisha Imam al-Askary (a) akasema: “Atakayemfuata Imam Ali katika hilo basi yeye ni Shia kweli.”14 13. Al Bihaar, juz. 6 14. Safinatul Bihaar

6


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:19 PM

Page 7

Tabia njema kwa mujibu wa Ahlul Bayt (a.s) Na imepokelewa kwamba Imam Hasan (a) na Imam Husayn (a) walimwona mzee akitawadha kimakosa. Wakaanza kubishana, kila mmoja akimwambia mwenziwe hajui kutawadha. Wakamwendea yule mzee na kumtaka awe hakimu baina yao akiwatazama namna wanavyotawadha. Kila mmoja akatawadha kisha wakamuuliza nani kati yao katawadha vizuri? Mzee akajibu: nyote mnatawaza vizuri lakini ni huyu mzee mjinga ndiye asiyetawadha vizuri na sasa amejifunza kutoka kwenu na ametubia kwa baraka zenu na huruma yenu kwa umma wa babu yenu. Kijana (mtumishi) wa Imam Husayn (a) alifanya uhalifu ambao unastahiki adhabu. Akaamuru apigwe lakini akamwambia Imam Husayn (a): Ewe bwana wangu na ambao wanaoziwia hasira zao. Imam (a) akasema basi mwacheni. Akaongeza ewe bwana wangu na wenye kuwasamehe watu. Imam Husayn (a) akasema: nimekusamehe. Yule kijana akamalizia: Ewe bwana wangu na Mwenyezi Mungu huwapenda wafanyao wema. Imam Husayn (a) akasema upo huru kwa ajili ya kutaka radhi zake Mwenyezi Mungu na nakupa mara mbili ya kile nilichokuwa nakupa.15 As-Swauly anasimulia: “Yalitokea maneno baina ya Imam Husayn (a) na (ndugu yake) Muhammad bin al-Hanafiyyah. Muhammad bin alHanafiyyah akamwandikia Imam Husayn (a): ‘Ewe ndugu yangu, baba yangu na baba yako ni Ali, hunishindi wala sikushindi kwa hilo. Ama mama yako ni Fatima binti yake Mtume wa Mwenyezi Mungu. Hata kama ardhi ingekuwa dhahabu na ikawa milki ya mama yangu asingeweza kumfikia mama yako. Utakapo soma barua yangu hii basi njoo kwangu turidhiane. Hakika wewe unastahiki ubora zaidi kuliko mimi na amani ya Mwenyezi Mungu iwe juu yako na baraka zake.’ Imam Husayn (a) akafanya hivyo na haikuwahi kutokea chochote baina yao.”

15. Al Bihaar, juz. 10, uk. 145

7


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:19 PM

Page 8

Tabia njema kwa mujibu wa Ahlul Bayt (a.s) Kutoka kwa Muhammad bin Jaffar na wengine walisema: “Jamaa yake Imam Ali bin al Husayn (a) alimsimamia na kumtukana. Imam (a) akanyamaza na hakumjibu. Alipoondoka, Imam (a) akawaambia waliyokuwa wamekaa pamoja naye: “Mmesikia aliyoyasema mtu huyu? Basi mimi nataka tuende pamoja ili msikie jawabu langu kwake.” Wakamjibu: “Haya twende, tulikuwa tunataka umjibu.” Akachukua ndara zake na akaondoka na huku akisema: “Na wale ambao wanaozuwia ghadhabu na kuwasamehe watu na Mwenyezi Mungu awapenda wafanyao mema” (3:134). ‘Tuliposikia maneno hayo tukaelewa kwamba hatamwambia chochote. Alipowasili nyumbani kwa huyo bwana alimwita na kusema: ‘Mwambieni ni mimi hapa Ali bin Husayn (a).’ Akatoka huyo bwana kwa nia ya shari na huku akiwa na hakika kwamba huyo amekuja kulipiza kwa yale aliyoyafanya.” Imam Ali bin Husayn (a) akamwambia: “Ewe ndugu yangu! ulikuja na kunisimamia na ukasema na ukasema. Ikiwa uliyoyasema mimi ninayo, basi namuomba Mwenyezi Mungu (swt) anisamehe, na ikiwa sinayo basi namwomba Mwenyezi Mungu (swt) akusamehe.”16 Hakuna kitu chenye dalili zaidi kuhusu utukufu wa tabia njema na ukubwa wa athari yake katika kumuenzi mwanadamu na kumpa furaha kuliko hadithi ifuatayo: Imepokelewa kutoka kwa Ali bin Husayn (a) kwamba: “Watu watatu waliapa kwa Lat na Uzza ili wamuue Muhammad (s). Akaenda amiri wa waumini (Ali bin Abi Twalib) peke yake na akamuua mmoja kati ya watatu na akaja na wawili kwa Mtume (s). Mtume akaamrisha aletwe mmoja wao na kisha akamwambia: “Sema Lailahaillallah na kwamba mimi ni Mtume wa Mwenyezi Mungu”. Yule bwana akajibu: “Mimi kubeba jabali Qubeys ni bora kwangu kuliko kusema maneno hayo”. Mtume (s) akamwambia Imam Ali (a) ambwage chini na amkate kichwa. Kisha Mtume (s) akaamrisha aletwe yule wa tatu na akamwambia: 16. Al Bihaar, juz. 11, uk. 17 8


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:19 PM

Page 9

Tabia njema kwa mujibu wa Ahlul Bayt (a.s) “Sema Lailahaillallah na ushuhudie ya kwamba mimi ni Mtume wa Mwenyezi Mungu (swt).” Yule bwana akajibu: “ Niunganishe na wenzangu.” Mtume akamwamuru Ali (a.s.) ambwage chini na kumkata kichwa. Alipokuwa tayari kumkata kichwa, Jibril (a) akateremka kwa Mtume (s) na kumwambia: “Mola wako anakutumia salamu na anakwambia usimuue huyu kwa sababu yeye ni mwenye tabia nzuri, karimu kwa watu wake. Mtume (s) akamwamuru Ali (a) amuachie kwa sababu ni mtu mwenye tabia njema na mtoaji kwa watu. Yule mushrik akasema: “Hivi huyo ni mjumbe wa Mwenyezi Mungu anayekupa habari?” Mtume akajibu kwa ndiyo. Yule mushrik akasema: “Naapa wallahi sikuwahi kuziwia dirham kumpa ndugu yangu wala kukunja uso wangu katika vita, basi nashuhudia ya kwamba hakuna mola apasaye kuabudiwa ila Allah na hakika wewe ni Mjumbe wa Mwenyezi Mungu (swt). Akasema Mtume (s): “Huyu ni katika wale ambao tabia njema na ukarimu vimemvuta kwenye pepo ya neema.”17

17. Al Bihaar, juz. 2, uk. 210 9


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:19 PM

Page 10

Tabia njema kwa mujibu wa Ahlul Bayt (a.s)

TABIA MBAYA MAANA YA TABIA MBAYA Ni upotofu wa kinafsi ambao unamsababishia mtu mgandamizo, ugumu wa nafsi na kutawaliwa na ukali na hasira. Kwa hiyo tabia mbaya ni kinyume cha tabia njema. Tabia mbaya ina athari mbaya na matokeo hatari katika kumharibu mwenye hali hiyo na kuporomosha utukufu wake. Haya hupelekea mtu huyu kuchukiwa, kudharauliwa, kukosolewa na kulaumiwa. Na zinapozidi athari za tabia mbaya, basi huwa wakati huo ni sababu ya maovu na balaa za kimwili na kiroho.

QUR’ANI Na ikutoshe kuhusu uduni wa tabia hii na ubaya wa athari zake kwamba Mwenyezi Mungu (swt) amemwambia mbora wa mitume wake na mfano wa juu katika kila fadhila na ubora kwamba: “lau ungekuwa fidhuli mgumu wa moyo basi wangekukimbi (3:159). Kwa ajili ya hilo akili na mapokezi ya dini vimekataza na kutahadharisha kuhusu tabia mbaya.

HADITHI Hizi hapa baadhi ya riwaya: Mtume (s) alisema: - “Ni juu yenu kuwa na tabia njema, hakika tabia njema ipo (humpeleka 10


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:19 PM

Page 11

Tabia njema kwa mujibu wa Ahlul Bayt (a.s) mja) peponi bila muhali. Na jiepusheni na tabia mbaya, hakika ya tabia mbaya ipo (humpeleka mja) motoni hakuna muhali.”18 Na akasema tena: - “Amekataa Mwenyezi Mungu (swt) toba kwa mwenye tabia mbaya. Wakauliza watu: vipi ewe mjumbe wa Mwenyezi Mungu? Akajibu: Kwa sababu anapotubu dhambi moja huanguka ndani ya nyingine kubwa kuliko ya mwanzo.”19 Imam Ja’far Swadiq (a) alisema: - “ikiwa unataka uheshimiwe basi uwe laini na ukitaka kudharauliwa, basi uwe mkali”.20 Pia a kasema: -“Tabia mbaya huharibu vitendo kama vile siki inavyo haribu asali”. 21 Na pia akasema: “Ambaye itakuwa tabia yake mbaya ataadhibu nafsi yake mwenyewe.”22

TABIA BAINA YA UONGOFU NA UPOTOFU Kama vile mwili unavyoharibika kwa magonjwa na kuwa dhaifu na kukonda, hivyo hivyo tabia huathirika na magonjwa. Dalili za maradhi hayo hudhihiri katika hali ya udhaifu wa tabia na kuporomoka kinafsi. Kama vile mwili mgonjwa unavyotibiwa na siha yake ikarudi na kuwa tena na nguvu, hivyo hivyo tabia yenye ugonjwa hutibiwa na kurejesha nishati yake na kurekebishwa. Kurejesha usawa wa tabia kunategemea dalili za ugonjwa na hali ya mgonjwa. 18. Uyunu Akhbaru Ridhwa (Sheikh Sudduq) 19. Al Kaafy 20. Tuhaful Uquul 21. Al Kaafy 22. Al Kaafy

11


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:19 PM

Page 12

Tabia njema kwa mujibu wa Ahlul Bayt (a.s) Lau isingekua kwamba tabia hurekebishika na kuwa sawa, basi kazi, maelekezo na juhudi za mitume kurekebisha watu na kuwaongoza kwenye kheri zingeishia patupu bila mafanikio. Na binadamu wangekuwa kama wanyama na wenye thamani ndogo na hali mbaya kuliko mnyama; kwani mnyama huweza kupewa mazoezi na tabia yake ikabadilika. Farasi kaidi, kwa kupewa mafunzo, hubadilika na kuwa mpole, na pia wanyama wa porini hugeuka na kuwa wa kufuga. Itakuwaje mwanadamu ambaye ndiye mbora wa Viumbe, kwa vipawa na akili, asiweze kubadilika kwa mafunzo? Kwa ajili ya hiyo utaona kwamba mtu mpole mwenye tabia nzuri anaweza akabadilika akatoka ndani ya hali yake ya mfano na kuwa mkali, mwenye hasira, kwa moja ya sababu moja wapo zifuatazo: 1. - Udhaifu na unyonge utokanao na ugonjwa wa mtu na kuharibika siha yake au kwa sababu ya kuwa na dalili za uzee, mambo ambayo husababisha mvuto wa mishipa ya fahamu na kushindwa kuwa na subira na kuwastahamilia watu (kubeba shida, kuwa mtaratibu na mpole katika mahusiano na watu). 2. - Wasiwasi: huvuruga fikra za mtu mwenye akili na tabia njema na kumuondoa katika hali yake ya upole. 3. - Umaskini: huweza kusababisha hasira, ugomvi, na ukatili ikiwa ni namna ya kujitukuza dhidi ya unyonge wa umaskini, maumivu ya kukosa au huzuni kwa sababu ya kuondokewa na neema mtu aliyokuwa nayo. 4. - utajiri: mara nyingi humpelekea mwenye nao kwenye majivuno, majisi -fu, kiburi na kuchupa mipaka kama alivyosema mshairi: utajiri umefichuwa kwako tabia ambazo ni mbaya chini ya nguo ya umaskini zilikuwa zimejificha 12


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:19 PM

Page 13

Tabia njema kwa mujibu wa Ahlul Bayt (a.s) 5. - cheo: husababisha kufoka katika tabia na kujiona mbele ya watu, tabia ambayo hutokana na uduni wa nafsi na udhaifu wake au hulka mbaya. 6. - kujitenga na utawa: hii inaweza kusababisha hisia za kushindwa na unyonge, jambo linalomjalia aliyejitenga kuwa mwenye uzito wa moyo. (chuki, na hasira).

TIBA YA TABIA MBAYA Kwa kuwa tabia mbaya ni katika mambo mabaya na sifa duni kabisa, ni vyema kwa yule atakaye kuadabisha nafsi yake na kutoharisha tabia yake na hali hii chafu afuate nasaha zifuatazo: 1. - Akumbuke mabaya ya tabia mbaya na madhara yake makubwa na kwamba hupelekea kwenye ghadhabu ya Mwenyezi Mungu (swt), kudharauliwa na kukimbiwa na watu kama tulivyoeleza mwanzoni. 2. - Aweke mbele ya macho yake yale tuliyoyataja kuhusu fadhila za tabia njema na athari zake tukufu na yale yaliyopokelewa kutoka kwa Ahlul Bait (a) ya kusifu na kuhimiza tabia njema. 3. -

Kufanya mazoezi ya kudhibiti mishipa ya fahamu

4. -

Mazoezi kwa ajili ya kumiliki neva (mishipa ya fahamu) na kudhibiti mashambulizi ya tabia mbaya na mashtukizo yake. Na mazoezi hayo ni kwa kulipa muda kila analolifanya au kulisema, akifuata mwongozo wa Mtukufu Mtume (s) usemao: “jihadi iliyo bora ni ile ya mtu kujahidi nafsi yake iliyo baina ya pande zake mbili (mwili wake).� Kwa hiyo ambaye tabia zake zimeathirika na ugonjwa na kuharibika kwa sababu za kinafsi ni wajibu wake kufuata nasaha hizo hapo juu. Ama yule ambaye tabia yake itakuwa mbaya kwa sababu ya ugonjwa wa kimwili ni wajibu wake kutibu ugonjwa huo kwa njia za kitabibu na kurejesha afya yake na kupata vitu vya kuleta raha na utulivu, na pia kupoza neva. 13


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:19 PM

Page 14

Tabia njema kwa mujibu wa Ahlul Bayt (a.s)

1. UKWELI MAANA YAKE Ukweli ni kukubaliana kauli na hali halisi. Ukweli ni tabia njema na tukufu zaidi ya zote kwa sababu ya athari zake muhimu katika maisha binafsi na ya jamii. Ukweli ni pambo la mazungumzo. Ni alama ya msimamo na uadilifu na sababu ya mafanikio na kuokoka. Ni kwa sababu hiyo, ndani ya Qurani na Sunnah, sheria ya kiislamu imeisifu hulka hiyo na kuwahamasisha watu kujipamba nayo.

QUR’ANI Mwenyezi Mungu (swt) anasema:

“Na yule aliyekuja kwa ukweli na akausadiki hao ndiyo wamchao Mwenyezi Mungu. Watapewa wayatakayo kwa mola wao. Hiyo ndiyo jaza ya wafanyao mema.” (Az - Zumar, 39:33-34)

“Hii ni siku ambayo ukweli utawafaa wakweli. Malipo yao ni mabustani ambayo yapita mito chini yake, watakaa humo milele.” ( Al Maida, 5:119) 14


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:19 PM

Page 15

Tabia njema kwa mujibu wa Ahlul Bayt (a.s)

“Enyi mliyoamini! Mcheni Mwenyezi Mungu na muwe pamoja na wakweli.”(At Tawbah, 9:119) Na hivi ndivyo Ahlul Bait (a) walivyotukuza hulka hii na wakawalingania waumini kujipamba nayo kwa njia za hekima na kuvutia. Mtume (s) alisema: “Pambo la mazungumzo ni kusema ukweli. ”23 Amirul muuminina (a) alisema: “Muwe daima pamoja na ukweli kwani ukweli huokoa”.24 Imam Ja’far as Saadiq (a) alisema: “ Mtakapo taka kuwapima watu basi msighurike na sala zao wala saumu zao, bali wachunguzeni kwa kusema ukweli na kurejesha (timiza) amana, kwani mtu anaweza akazoea sana sala na saumu kiasi kwamba akiiacha anahisi ukiwa.”25 - “Ambaye ulimi wake utakuwa daima mkweli basi kazi yake itakuwa safi.”26 Kwa maana amali yake inakuwa safi na ya kuongezeka katika thawabu kwa baraka ya ukweli kwa sababu Mwenyezi Mungu (swt) anasema : “Hakika anakubali amali kutoka kwa wamchao Mwenyezi Mungu.” Na ukweli ni katika sifa bainifu ya uchamungu na sharti yake muhimu.

23.Al Imamat wa Tabswirah 24. Kamaalud Diin (Sudduq) 25. Al Kaafy 26. Al Kaafy

15


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:19 PM

Page 16

Tabia njema kwa mujibu wa Ahlul Bayt (a.s)

MATOKEO YA UKWELI Katika mambo yahitajikayo na ya muhimu kwa uhai wa jamii na ambayo ni msingi wake wa asili ni kuenea uelewano na kusaidiana baina ya watu wa jamii hiyo. Hayo ndiyo yawawezesha kubeba mzigo wa maisha na kufikia malengo yake na kuishi maisha bora na salama. Ulimi, bila shaka , ndiyo chombo cha uelewano na chanzo cha fikra. Na pia ulimi ndiyo mfasiri wa yale yapitayo ndani ya akili za watu. Kwa hiyo una dhima na nafasi kubwa na hatari katika uhai wa jamii na pia katika kuleta uelewano wa fikra na hisia za wanajamii hiyo. Maisha ya taabu au ya furaha hutegemea ulimi kuwa mwongo au kuwa mkweli. Watu huelewana na kuaminiana na kujenga mahaba na amani iwapo ulimi utakuwa na ukweli na ukatafsiri kwa uaminifu yaliyomo ndani ya nafsi. Ama ukiwa na hadaa, uongo na hiyana basi husababisha shari, watu kuepukana, kuchukiana na kubomoa jamii. Kwa hiyo ukweli ni dharura na haja ya msingi kwa kila jamii. Ukweli ni nidhamu ya kupatikana jamii iliyo na furaha, ni alama ya kwamba jamii hiyo ina tabia njema, ni dalili ya kwamba watu wake wanamsimamo sahihi na utukufu. Pia ndiyo sababu ya nguvu mtu kuwa na utajo mwema, sifa na thamani na watu kumwamini na kumtegemea. Ukweli, unaathari katika uhai wa watu. Pia unaathari katika kuokoa muda wenye thamani na kuleta utulivu wa kimwili na kiroho. Kwa mfano, ikiwa wanaouziana watakuwa wakweli, basi wataokoa muda kwa kujiepusha na majadiliano. Na waajiri (matajiri) ikiwa watashikilia ukweli, hili litahifadhi haki za watu na kuzaa uimara wa amani na raha.

16


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:19 PM

Page 17

Tabia njema kwa mujibu wa Ahlul Bayt (a.s) Ikiwa kila mtu atavaa joho la ukweli na akauzoea, basi wote tutachuma faida zake nyingi na mapato makubwa. Kinyume cha hapo, iwapo uongo utashamiri ndani ya jamii, misingi yake ya tabia njema huporomoka na kuenea udhia baina ya watu, kutoweka uelewano na kusaidiana. Jamii hiyo huwa hatarini kusambaratika na kuangamia. AINA ZA UKWELI Ukweli una sura na migawanyiko inayojitokeza katika maneno na vitendo. Hapa tunataja baadhi kwa umaarufu wake: 1. Ukweli katika usemi: hii ni kuelezea kitu kama kilivyo katika uhakika wake pasi na kuzua au kuficha. 2. Ukweli katika vitendo: ni kukubaliana kauli na vitendo kama vile kutekeleza kiapo, au ahadi. 3. Ukweli katika kuazimia: ni kuamua kufanya mambo ya kheri. Akiyatekeleza anakuwa mkweli wa azma vinginevyo ni muongo. 4. Ukweli katika nia: ni kusafisha nia yako na kila uchafu wa riya (kujionyesha) na kuwa na ikhlas (uaminifu) kwa kutaka ridhaa ya Mwenyezi Mungu pekee.

2. UONGO MAANA YAKE Ni kauli ya kuhalifu ukweli wa mambo. Ni katika aibu na uovu mbaya sana. Uongo ni chanzo cha maasi na shari na huzaa fedheha na kuporomoka. Kwa ajili hiyo, Sheria imeharamisha uongo, kuwakemea na kuwatishia wenye sifa hiyo katika Kitabu na sunnah.

17


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:19 PM

Page 18

Tabia njema kwa mujibu wa Ahlul Bayt (a.s)

QUR’ANI Mwenyezi Mungu anasema: “Mwenyezi Mungu hamwongozi ambaye ni mwenye israfu, muongo.”(Ghafir, 40:28)

“Adhabu kali ipo juu ya kila muovu, muongo. ”(Jaathiya, 45:7)

“Hakika wanazua uongo ambao hawaamini aya za Mwenyezi Mungu na hao ndiyo waongo.”(An Nahl, 16:105)

HADITHI Mtume wa Mwenyezi Mungu alisema katika hijja ya kuaga (hijjatul wada’): “Uongo umekithiri juu yangu na utazidi. Yeyote atakaeongopa juu yangu kwa kudhamiria basi atayarishe makazi yake motoni. Ikikujieni hadithi basi ipimeni na Kitabu cha Mwenyezi Mungu na Sunna Yangu. Ikikubaliana na Kitabu cha Mwenyezi Mungu basi ichukueni na ikikataana na Kitabu cha Mwenyezi Mungu na Sunna Yangu, itupilieni mbali.” 27 Amirul Muuminin Ali (a) alisema: “Kuzoea kusema uongo huzaa ufukara”.28 Imam Baqir (a) alisema: 27. Ihtijajut Tabrasi 28. Al Khiswal- Suduq 18


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:19 PM

Page 19

Tabia njema kwa mujibu wa Ahlul Bayt (a.s) “Hakika Mwenyezi Mungu (swt) amejalia kufuli kwa ajili ya shari. Na akajalia funguo za kufuli hizo kuwa ni pombe. Na uongo ni shari zaidi kuliko pombe.”29 Pia alisema (a.): “Alikuwa Ali b. Husayn akiwaambia watoto wake: ogopeni uongo, ukiwa mdogo au mkubwa katika hali ya umakini au ya mzaha. Ikiwa mtu ataongopa katika dogo, basi ataparamia kubwa. Je ! hamjui ya kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu (s) alisema haendelei mja kusema ukweli hadi pale Mwenyezi Mungu (swt) humwandika kuwa ni mkweli, na haendelei mja kuongopa hadi Mwenyezi Mungu (swt) humwandika muongo.”30 Tena alisema: “Hakika uongo ndiyo angamizo la imani.”31 Nabii Isa (a) alisema: “Ambaye huzidi uongo, basi nuru yake hutoweka”.32

MAOVU WA UONGO Uongo una madhara makubwa na maovu mengi. Ni kwa sababu hiyo Sheria imeharamisha na kuonya vikali kwa adhabu, yeyote atakayejihusisha na uongo. Baadhi ya maovu yanayosababishwa na uongo ni: 1. Kuwa na sifa mbaya, kuporomoka utukufu wa mtu, kutoweka uaminifu. Mtu muongo hasadikiwi hata kama atasema ukweli. Ushahidi wake haukubaliwi na wala ahadi zake hazipewi uzito wala kutegemewa. Na katika tabia ya mtu muongo ni kwamba husahau uongo wake na 29. Al Kaafy 30. Al Kaafy 31. Al Kaafy 32. Al Kaafy 19


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:19 PM

Page 20

Tabia njema kwa mujibu wa Ahlul Bayt (a.s) akazusha kinachopingana na uongo wake. Na huenda akazusha uongo juu ya uongo unaopingana ili kusaidia uongo aliyouzusha na mwishowe kuyafanya maneno yake kuwa ni machukizo, upuuzi na fedheha. 2. Kupungua kuaminiana baina ya watu na kuenea baina yao wasiwasi na kukataana. 3. Kupoteza muda mwingi na juhudi ili kupambanua la uhakika na la kughushi, ukweli na uongo. 4. Athari mbaya za kiroho na matokeo hatari ambayo yameelezwa mwanzoni.

SABABU ZA UONGO Zipo sababu zinazomsukuma mtu kuwa muongo. Ambazo zilizo muhimu ni: 1. Mazoea: mtu anaweza kuzoea kusema uongo kwa msukumo wa ujinga au kwa kuathiriwa na mazingira mabaya au kwa sababu ya udhaifu wa kinga ya kidini. Kwa hiyo, akakulia kwenye tabia hiyo mbaya na ikaenea mizizi yake katika nafsi yake. Kwa sababu hiyo, baadhi ya wanahekima (watu wenye hekima na busara) wamesema: “atakaeona utamu kunyonya uongo, ni vigumu kumwachisha�. 2. Tamaa: nayo ni katika sababu za nguvu sana zinazopelekea mtu kusema uongo na udanganyifu. Aongopa au kudanganya ili kufikia tamaa na ulafi wake. 3. Uadui na husda: wenye hulka hizo hawaachi kubuni na kuzua tuhuma na kupamba uzushi na uongo dhidi ya yule ambaye wanamchukia au wanamhusudu. Watu wema na wenye tabia nzuri ambao wanaojiepusha na batili, wamesumbuliwa na kuteswa kwa ajili ya tuhuma, uzushi na uvumi wa uchochezi. 20


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:19 PM

Page 21

Tabia njema kwa mujibu wa Ahlul Bayt (a.s)

AINA ZA UONGO Uongo una sura mbaya ambazo zinatofautiana kwa kiwango cha madhara na athari zake, kama vile: 1. Kiapo cha uongo. Ni katika sura chafu za uongo na yenye hatari na uovu sana kuliko aina zingine. Ni uovu ulio na ncha mbili: ni jeuri wazi dhidi ya Mola (swt) kwa kuapa kwa jina lake kiuongo na uzushi, pia ni uovu mbaya kwa kunyang’anya haki za watu na kuporomoka heshima. Kwa ajili ya hayo, maandiko matakatifu yamekemea uovu huo na kutahadharisha kama alivyosema Mtume (s): “Jiepusheni na yamini ya uongo, kwani hiyo yamini huziacha nyumba (miji, ardhi) bila watu (kama jangwa)”.33 Naye Imam Swadiq (a) alisema: "Yamini ni kama vile ardhi isiyo thabiti, inarithisha kizazi ufakiri.”

2. Ushahidi wa uongo. Ushahidi wa uongo, kama ilivyo yamini ya uongo, pia ni uovu hatari na dhulma mbaya inayobomoa. Matokeo yake ni watu kunyimwa haki zao, kuporwa mali zao na kuenea machafuko ndani ya jamii kwa waovu kusaidia maovu ya unyonyaji na utapeli. Maandiko yameonya dhidi ya uovu huo na kutahadharisha na adhabu iumizayo wenye uovu huo; Qurani imekataza uovu huo na kusema: 33. Al Kaafy 21


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:19 PM

Page 22

Tabia njema kwa mujibu wa Ahlul Bayt (a.s)

“Na jiepusheni na kauli ya uongo”.(Hajj, 22: 30) Mtume wa Mwenyezi Mungu (s) alisema: “Mtoa ushahidi wa uogo, pindi tu anamaliza kutoa ushahidi wake mbele ya hakimu, anakuwa amechagua makazi yake motoni, na hivyo hivyo anaeficha ushahidi.”34 Madhara ya yamini ya uongo na ushahidi wa uongo. Maovu haya yameharamishwa na kukemewa kwa matokeo yake mabaya na madhara yanayoangamiza duniani na akhera kama vile: 1. Uovu mkubwa dhidi ya nafsi yako. Bila shaka mzushi wa uovu huu anaifanyia uovu mkubwa nafsi yake kwa kuipambanisha na ghadhabu ya Mwenyezi Mungu na adhabu kama ilivyotajwa kabla. 2. Uovu mkubwa dhidi ya aliyesaidiwa. Ni uovu kwa yule aliyependelewa kwani hilo linamhimiza muovu huyo kuendelea kumeza haki za watu, kunyanganya mali zao na kuvunja heshima zao. 3. Uovu mkubwa dhidi ya aliyedhulumiwa. Kwa yamini na ushahidi wa uongo, mtu hudhalilishwa na kupoteza haki zake. Pia hisia na fikra zake hujeruhika na kuathirika vibaya. 4. Uovu mkubwa dhidi ya jamii. Maovu haya huharibu jamii yote kwa ujumla kwa kuenea vurugu, ufisadi na kuporomoka thamani ya dini na maadili mema. 5. Uovu dhidi ya Sheria ya Kiislamu. Bila shaka ni uovu mkubwa mtu kuchupa mipaka ya Mwenyezi Mungu (awj) na katiba takatifu, ambayo ni wajibu kila mwislamu aifuate na kuitekeleza. 34. Al Kaafy, Man laa Yahdhuruhul Faqih 22


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:19 PM

Page 23

Tabia njema kwa mujibu wa Ahlul Bayt (a.s) 3. Kuvunja ahadi Kutekeleza ahadi ni katika tabia njema ambazo hujipamba nazo watu watukufu wenye busara kama alivyowasifu Mwenyezi Mungu (swt) ndani ya Qurani:

“Na mtaje ndani ya Kitabu Ismail. Yeye alikuwa Rasuli Nabii” (Maryam, 19:54) Hii ni kwamba Nabii Ismail (a) alimuahidi mtu na akakaa kumsubiri hapo mahala bila kuondoka, mwaka mmoja, kwa ajili ya kuchunga ahadi. Ni jambo la kusikitisha kwamba leo hii tabia mbaya ya kuvunja ahadi imeenea baina ya Waislamu. Wanajifanya hawajui madhara yake mabaya katika kuporomosha kuaminiana baina yao, kuharibika mahusiano ya kijamii. Imam Ja’far Sadiq (a) alisema: “Ahadi ya muumini ni nadhiri isiyo na kafara. Atakayehalifu, basi ameanza kwa kumhalifu Mwenyezi Mungu, na hivyo kupambana na adhabu yake. Hiyo ndiyo maana ya kauli ya Mwenyezi Mungu isemayo: (Enyi mliyoamini! kwa nini mnasema msiyoyatenda? Ni kosa kubwa mbele ya Mwenyezi Mungu (swt) kusema msiyoyatenda! (As Swaff, 61:2-3)35 Na alisema pia (a.s.): "Hakika Mtume wa Mwenyezi Mungu (s) alimwahidi mtu penye jiwe kubwa na akamwambia: mimi nipo hapa nakusubiri hapa hadi urejee. Basi jua likawa kali sana hadi masahaba wakamwambia Mtume (s): ewe mjumbe wa Mwenyezi Mungu, lau ungesogea pale kivulini. Mtume akajibu: nilikwisha muahidi hapa. Na ikiwa hakuja itakuwa ni juu yake siku 35. Al Kaafy 23


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:19 PM

Page 24

Tabia njema kwa mujibu wa Ahlul Bayt (a.s) ya kiyama".36 4. Uongo wa masihara Kuna baadhi ya watu ambao wanaona ladha kuzusha uongo wa masihara ili kusema mambo ya ajabu kuhusu watu na kuwastihzai. Huu ni upuuzi hatari unaozaa chuki na madhambi. Imam Ja’far Swadiq (a) alisema: “Yeyote atakaetoa taarifa ya muumini akiwa analenga kumtia kasoro, au kubomoa utu wake ili asiwe na thamani mbele ya watu, basi Mwenyezi Mungu (swt) atamtoa chini ya wilaya (himaya, ulinzi) yake na kumweka chini ya wilaya ya Shetani, na Shetani hatamkubali”. 37

TIBA YA UONGO Uongo ni maradhi hatari ambayo kila mwenye akili lazima ajitahidi kujiepusha nao kwa kufuata nasaha zifwatazo: 1.- Atafakari maovu ya uongo kama ilivyoelezwa na ubaya wa athari zake kwa mwanadamu, kimwili na kiroho. 2.- Akumbuke fadhila za ukweli na faida zake tukufu kama zilivyoelezwa. 3. Afanye mazoezi ya kufuata ukweli na kujiepusha na uongo na ajenge ada ya kutekeleza zoezi hili la kinafsi hadi atakapopona tabia hii mbaya.

36. Ilal Sharai' 37. Al Kaafy 24


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:19 PM

Page 25

Tabia njema kwa mujibu wa Ahlul Bayt (a.s)

UONGO UNAOKUBALIKA Pamoja na kwamba uongo ni tabia mbaya na haramu kisheria, zipo hali, pia mazingira ambayo si ya kawaida yanayoruhusu uongo na Sheria ikajuzisha hilo, kama vile: Ikiwa kama kuna maslahi, au faida muhimu. Kwa mfano kumuokoa muumini na kumuepusha na kifo au kifungo au kuhifadhi utu na heshima yake au kuhifadhi mali yake. Uongo katika hali hii ni wajibu kisheria. - Ikiwa uongo ni wasila wa kufikia lengo linalotakiwa au shabaha ya kuleta islahi. Kwa mfano kupatanisha baina ya watu, kumridhisha mke na kumvuta, kuwahadaa maadui katika vita. Katika hali kama hizi, maandiko yamekubali mtu kutumia uongo kama alivyosema Imam Ja’far Sadiq (a): “Iko siku ambayo kila muongo utaulizwa kuhusu uongo wake kasoro katika hali tatu: mtu aliyefanya hadaa katika vita, vita hivyo vikamwondokea au mtu aliyepatanisha watu wawili, akutana na huyu tofauti na anavyokutana na huyu akikusudia kuwapatanisha au mtu aliyeahidi familia yake kitu na huku yeye hataki kuwatimizia.”

3. UVUMILIVU NA KUZUIA HASIRA MAANA YAKE Ni kuzuia nafsi kuathiriwa na vichochezi vya hasira. Na tabia hizi mbili ni katika hulka tukufu na dalili ya utukufu wa nafsi na tabia njema. Pia ni sababu ya mapenzi na upendo.

25


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:19 PM

Page 26

Tabia njema kwa mujibu wa Ahlul Bayt (a.s)

QUR’ANI Mwenyezi Mungu (swt) katika Kitabu Chake, amewasifu wavumilivu na wanaodhibiti hasira akasema:

…Na wajinga wakisema nao, basi wao hujibu: Amani! (Suratul Furqan, 25:63).

Mema na maovu hayawi sawa. Rudisha nyuma uovu kwa yaliyo mema zaidi. Hapo yule ambaye baina yako naye pana uadui atakuwa kama rafiki mkubwa. Lakini (jambo hili) hawatapewa ila wale wanaosubiri, wala hawatapewa ila wenye bahati kubwa. (Suratu Fuswilat, 41:34-35)

“…Na wanaojizuia na ghadhabu, na wenye kusamehe watu, na Mwenyezi Mungu huwapenda wafanyao wema. (Suratu Aali Imraan, 3:134) Na kwa mpangilio huo ndiyo yamekuja maelekezo ya Ahlul Bait (a).

HADITHI Amiri wa waumini Ali (a) alimsikia mtu akimtukana Qambar na ikawa Qambar ataka kumrudishia. Imam (a) akamwambia: 26


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:19 PM

Page 27

Tabia njema kwa mujibu wa Ahlul Bayt (a.s) “Taratibu ewe Qambar, mwache anayekutusi akiwa amefedheheka. Kwa kufanya hivyo utamridhisha Rahman na kumchukiza Shetani na utamuadhibu adui yako. Naapa kwa yule aliyeotesha mbegu na akaumba mwanadamu, muumini hakumridhisha Mola wake kwa jambo kama vile uvumilivu na hakumchukiza Shetani kwa jambo kama vile kunyamaza, na hakuna adhabu zaidi kwa mpumbavu kama vile kumnyamazia.” 38 Pia akasema (a): “Fidia ya kwanza anayoipata mwenye uvumilivu ni kwamba watu humnusuru na mjinga”.39 Imam Baqir (a) alisema: “Hakika Mwenyezi Mungu (awj) anampenda mwenye haya, mvumilivu.”40 Imam Ja’far Swadiq (a): “Panapotokea ugonvi baina ya watu wawili, basi huteremka malaika wawili na kumuambia yule mpumbavu: umesema na ukasema na wewe ndiye wastahiki uliyoyasema, basi utalipwa kwa yale uliyoyasema. Kisha wanamwambia yule mvumilivu: umesubiri na kuvumilia, basi Mwenyezi Mungu (swt) atakusamehe ikiwa utakamilisha hilo. Akasema: Yule mvumilivu ikiwa atamjibu, basi wale malaika wanaondoka.”41 Pia akasema (a): “Hakuna yeyote atakayezuia hasira yake ila Mwenyezi Mungu (a.w.j.) humzidishia utukufu duniani na akhera, na Mwenyezi Mungu (a.w.j.) amesema: (na wanaoziwia hasira, na wanaosamehe watu, basi Mwenyezi Mungu awapenda wafanyao wema). Kwa hiyo mahala pa hasira akamlipa hilo”.42 38. Majaalisu Shaykh Mufid 39. Al Kaafy 40. Al Kaafy 41. Al Kaafy 42. Al Kaafy 27


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:20 PM

Page 28

Tabia njema kwa mujibu wa Ahlul Bayt (a.s) Imam Musa al Kadhim alisema (a): “Uwe na subira kwa maadui wa neema, kwani hutaweza kumlipizia vizuri sana yule aliyemuasi Mwenyezi Mungu (swt) kwa kukufanyia ubaya, kama vile kumtii Mwenyezi Mungu (swt) kwa kumfanyia wema yeye”.43 Siku moja, aliwajia wanawe na kuwaambia: “Enyi wanangu! Mimi nakuusieni wasia, atakayeushika basi hatapotea. Akikujieni mtu na akakuambieni katika sikio la kulia chukizo, kisha akageuka kwenye sikio la kushoto na akatoa udhuru na kusema: sikusema chochote basi mkubalieni udhuru wake”.44 Na huenda wapumbavu wakafikiria ya kwamba uvumilivu ni katika dalili za udhaifu na sababu za unyonge. Lakini wenye akili huona tabia hiyo katika alama za uungwana na ubora wa tabia na sababu ya utukufu na ukarimu. Kila pindi mtu anapokuwa na uwezo mkubwa, basi tabia zake huwa njema na nafsi yake hutukuka na kujiepusha kukurubia wapumbavu katika ujinga wao na uzembe na huku akijikinga kwa uvumilivu na utukufu wa kufumbia macho na wema wa msamaha. Haya yanamfanya yeye kuwa mwenye sifa na utukufu. Mshairi kasema: Na mpumbavu kwa ujinga hunisemesha Lakini kwa aibu kumjibu najiepusha Azidisha upumbavu nami upole nazidisha Kama vile udi ukiungua harufu njema wazidisha. Inasemakana kwamba mtu mmoja alimtusi mmoja katika wenye hekima, lakini akajiziwia kumjibu. Alipoulizwa kuhusu msimamo wake huo, akajibu: “siwezi kuingia katika vita ambayo mshindi wake ni mwenye shari zaidi kuliko mshindwa”. 43. Al Kaafy 44. Kashful Ghumma (Arbaliy) 28


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:20 PM

Page 29

Tabia njema kwa mujibu wa Ahlul Bayt (a.s) Na katika yenye kupendeza yaliyotungwa na washairi katika kusifu uvumilivu ni yale aliyoyarawi (kusimulia hadithi) Imam Ridhwa (a) pindi alipoambiwa na Maamun amsomee mashairi mazuri aliyopokea kuhusu uvumilivu. Imam Ridhwa (a) akasema: Ikiwa yule chini yangu ujinga kanifanyia Nafsi yangu kurudishia ujinga naikatalia Na akiwa kwa kiwango cha akili yangu kafikia Kwa uvumilivu wangu nashika ili mfanowe kuepukia Na ikiwa kwa fadhila na akili sikumfikia Basi haki yake ya kutangulia na ubora navumilia Maamun akasema: maneno mazuri yaliyo je? Nani kayasema maneno haya? Imam (a) akajibu: baadhi ya vijana wetu. Bila shaka Mtume (s) na maimamu (a) waliyosafika wa nyumba yake walikuwa ni mfano wa juu katika uvumilivu, wazuri katika kusamehe, na wema wa kufumbia macho makosa ya watu. Kurasa za vitabu vya sirah na wasifu (mazuri ya mtu) vimejaa mienendo yao adhimu na kwa uchache tunataja yafuatayo: Imam Baqir (a) alisema: “Mwanamke wa kiyahudi aliyemtilia sumu mtukufu Mtume (s) katika (nyama ya) kondoo, aliletwa mbele yake na Mtume (a) akamuuliza: kipi kilikufanya kutenda hivyo? Akajibu, niliona ya kwamba akiwa ni nabii basi sumu haitamdhuru, ama akiwa ni mfalme basi watu watapata nafuu kwa kifo chake. Mtume (s) akamsamehe.� 45

45. Al Kaafy 29


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:20 PM

Page 30

Tabia njema kwa mujibu wa Ahlul Bayt (a.s) Pia Mtume (s) alisamehe watu wengi baada ya kuwa amekwisha pitisha wao kuuliwa. Katika hao ni Habbar ibn al Aswad ibn al Muttwalib ambaye alimtisha Zainab binti ya Mtume (s) na akatao mimba, tendo lilipelekea Mtume (s) kujuzisha auliwe. Lakini aliomba msamaha kwa Mtume (s) kwa tendo lake baya. Akasema: “Tulikuwa katika watu wa shirk, ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu (s) na Mwenyezi Mungu akatuongoza na kutuokoa na maangamio kwa kukutuma wewe. Basi samehe ujinga wa ngu na yote uliyoyajua kuhusu mimi. Hakika nakiri ubaya wa tendo langu, na kukubali dhambi yangu.” Mtume (s) akasema: “Nimekusamehe na Mwenyezi Mungu amekufanyia wema pindi alipokuongoza kwenye uislamu. Na uislamu unafuta ya kabla.” Na katika hao ni Abdullah b. Zuba’ry aliyekuwa akimkashifu Mtume (s) pale Makkah na kuzidisha katika hilo. Siku ya Fath Makkah alikimbia kisha akarejea kwa Mtume (s) na kuomba msamaha. Mtume (s) akamkubalia udhuru wake. Mwingine ni Wahshy aliyemuua Sayyidna Hamza (a). Aliposilimu, Mtume (s) alimuuliza: “Wewe ni Wahshy?” Akajibu: “Naam.” Mtume (s) akamtaka amueleze vipi alivyomuua ami yake. Alipomueleza, Mtume (s) alilia na kumwambia: “Uondoe uso wako nami nisikuone.”46 Na hivi ndivyo alivyokuwa Amiri wa waumini Imam Ali (a); mvumilivu sana kwa watu, na msamehevu zaidi kwa mkosaji. Aliwashika Abdullah b. Zubair, Marwan b. Hakam, na Said b. al‘Aas ambao walikuwa maadui zake wabaya sana na wenye kukusanya watu dhidi yake. Aliwasamehe na hakuwafuatishia ubaya. Na alimuachia Amr b. ‘Aas ambaye alikuwa ni mtu hatari sana kwake kuliko hata jeshi lenye maandalizi pindi alipojibwaga uchi ili kujiepusha na 46 Safinatul Bihar j.1

30


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:20 PM

Page 31

Tabia njema kwa mujibu wa Ahlul Bayt (a.s) dharba ya upanga wake Imam (a). Katika vita vya Siffin, jeshi la Muawiya lilimzuia maji ya mto Furati na huku wakimwambia: “Hupati hata tone hadi utakapoangamia kwa kiu.” Alipopigana nao na kuwaondosha hapo, aliwaruhusu maadui zake hao kunywa na kutumia maji hayo ya mto sawia na wanajeshi wake. Alimzuru Bibi Aisha baada ya vita vya Jamal na akamuaga kwa ukarimu sana na akamsindikiza kitambo cha maili kadha. Pia akampa mtu wa kumhudumia na kuwa naye.47 Imam Hasan b. Ali (a), alifuata mwenedo wa baba yake na babuye (s). Katika uvumilivu wake ni kama yale yaliyosimuliwa na al-Mubarrid na Ibn ‘Aisha kwamba mtu mmoja wa Sham alimuona Imam Hasan (a) amepanda pando lake na hapo akaanza kumshambulia kwa maneno ya laana. Imam Hasan (a) akawa amenyamaza hamrudishii. Alipomaliza, Imam Hasan (a) alimwendea na kumsalimia kisha akacheka na kumwambia: “Ewe mzee! Naona wewe ni mgeni, na huenda umefananisha. Lau ungetuomba tukuridhie basi tungekuridhia, na lau ungetuomba haja basi tungekupa, na lau ungetutaka mwongozo basi tungekuongoza, na ikiwa utatuomba tukubebee basi tutakubebea, na kama ukiwa mwenye njaa basi tutakushibisha, na kama ukiwa uchi basi tutakuvika, na ukiwa mwenye haja tutakujaza mapesa, na ukiwa umefukuzwa basi tutakuhifadhi, na kama utakuwa mhitaji basi tutakukidhia haja yako. Lau ungeelekeza pando lako kwetu na ukawa mgeni wetu hadi pale utakapoondoka ni bora kwako kwa sababu tunayo nafasi kubwa na jaha pia na mali nyingi.” Aliposikia maneno hayo ya Imam Hasan (a), alilia na kusema: “Nashuhudia ya kwamba wewe ni khalifa wa Mwenyezi Mungu katika ardhi, kweli Mwenyezi Mungu ajua wapi ajalia ujumbe wake. Wewe na baba yako mlikuwa ni wenye kuchukiza sana kwangu lakini hivi sasa wewe ndiye nikupendaye zaidi katika viumbe wa Mwenyezi Mungu.” Akaelekea kwa Imam Hasan (a) na akawa ni mgeni wake mpaka pale aliporejea na akawa mwenye 47. Abqariyatul Imam 31


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:20 PM

Page 32

Tabia njema kwa mujibu wa Ahlul Bayt (a.s) kuitakidi mahaba yao.48 Na hivyo ndivyo alivyokua Imam Husayn (a). Mtumishi wake alifanya makosa yanayostahili adhabu. Akaamrisha achapwe, lakini yule kijana akasema: “Ewe bwana wangu; na wale wanaoziwia hasira.” Imam akasema: “Hebu mwacheni.” Akaongeza yule kijana: “Ewe bwana wangu; na wanaowasamehe watu.” Imam akasema: “Nimekwisha kusamehe.” Akazidisha: “Mwenyezi Mungu huwapenda wafanyao mema.” Imam akasema: “Wewe nakuacha huru nikitaka radhi za Mwenyezi Mungu na ninakupa mara mbili kile nilichokuwa nakupa.” Nimesoma Sirah ya Ahlul Bait (a) nakuikuta ni njia pekee na mfano adhimu katika ulimwengu wa sirah na akhlaq (tabia njema). Kuhusu uvumilivu wa Imam Ali Zainul-Abidin (a), wasimulizi wa hadithi (marawi) wanasimulia kwamba alikuwa siku moja na wageni. Basi mtumishi wake akafanya haraka kuchoma nyama iliyokuwa ndani ya tanuri. Kisha akaileta haraka, lakini kibaniko kikamponyoka na kuangukia juu ya kichwa cha mtoto wa Imam Zainul-Abidin (a) aliyekuwa chini ya ngazi. Mtoto akafariki. Imam (a) akamwambia yule kijana aliyekuwa ametahayari: “Nakuacha huru kwani hukukusudia.” Akamtengeneza mwanaye na kumzika.49 Ama Imam Musa b. Ja’far (a) alipewa lakabu ya Kaadhwim (anayejiziwia na hasira) kwa wingi wa uvumilivu wake na kumeza hasira akitaraji radhi za Mwenyezi Mungu (swt). Imepokewa kwamba hapo Madina alikuwepo kijana katika watoto wa masahaba ambae alikuwa akimuudhi sana Abul Hasan Musa (a) na kumtukana amuonapo na kumtusi kwa sauti ya juu. 48. Al Bihar, Juz. 9, uk.95 49. Kashful Ghumma ( Al-Arbaliy ) 32


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:20 PM

Page 33

Tabia njema kwa mujibu wa Ahlul Bayt (a.s) Baadhi ya wafuasi wa Imam (a) wakamwambia: “Tuachie sisi tumuuwe fasiki huyu.” Imam (a) akawakataza sana na kuwazuia. Imam (a), akaulizia habari zake na kuambiwa ya kwamba analima katika maeneo ya mji wa Madina. Akamwendea shambani kwake na huku amempanda punda. Alipoingia shambani yule kijana akapiga kelele: “Hapana kukanyaga mimea yangu.” Imam (a) akaendelea kuikanyaga na punda wake hadi alipomfikia, akateremka na kukaa naye. Akamkabili kwa bashasha na kumchekesha kisha akamwuliza: “Ni kiasi gani umegharimia shamba lako hili?” Akajibu yule kijana: “Dinari mia moja.” Imam (a) akamwuliza: “Ni kiasi gani unatarajia kupata?” Kijana akajibu: “Mimi sijui ghaibu.” Imam (a) akasema: “Bali nimesema kiasi gani unatarajia?” Akajibu: “Natarajia kupata dinari mia mbili.” Hapo Imam (a) akatoa mfuko wenye dinari mia tatu na kumkabidhi akisema: “Hili shamba lako liko vile vile na Mwenyezi Mungu atakuruzuku unavyotarajia. Yule kijana akasimama na kumbusu Imam (a) kichwani na kumuomba amsamehe makosa yake. Abul Hasan (a) akatabasamu na kuondoka. Alipokwenda msikitini akamkuta yule kijana amekaa. Alipomuona akasema: “Hakika Mwenyezi Mungu (swt) ajua wapi anapoweka ujumbe wake.” Maswahiba (wa kijana yule) wakamrukia na kumuuliza: “Unajambo gani?! Kamwe ulikuwa husemi hivi!” Akawajibu: “Sasa mmesikia nililosema.” Na akawa anamuombea Abul Hasan (a). Wakamgombeza naye akawagombeza. Aliporejea Abul Hasan (a) nyumbani kwake, akawaambia waliokaa pale ambao walikuwa wamemtaka kumuua kijana yule: “Nilipi lililo bora baina ya haya mawili; mlilolitaka nyiye au nililolitaka miye? Hakika mimi nimerekebisha hali yake kwa thamani ambayo mmeijua na kuzuia shari yake.”50 Hakika al-Farazdaq alipatia pindi aliposema katika shairi lake la kumsifu Imam Ali Zainul-Abidin (a): Kwa walimwengu kuwapenda (Ahlul Bayt) ndiyo dini, na kuwabughudhi ni ukafiri Na ukuruba wao ndiyo njia ya kuokoka na mahala pa hifadhi 50. Al-Bihaar, juz. 11 33


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:20 PM

Page 34

Tabia njema kwa mujibu wa Ahlul Bayt (a.s) Ikiwa watahesabiwa wachaji Mungu basi wao ndiyo maimamu wao Na ikiwa itaulizwa nani wabora wa walimwengu, jibu ni: wao

4. GHADHABU MAANA YAKE Ghadhabu ni hali ya nafsi inayomchochea mtu kuhamaki (kufoka, kulipuka) kikauli na kivitendo. Ghadhabu ni ufunguo wa shari nyingi. Ni kichwa cha maovu na sababu ya migogoro na hatari. Yamepokewa mafundisho mengi ambayo yanatahadharisha na kulaani tabia mbaya hiyo:

HADITHI Amiri wa waumini Ali (a) alisema: “Jitahadhari na hasira, hakika hasira ni jeshi katika majeshi ya Iblis”.51 Na pia alisema: “Hasira ni aina ya wazimu, kwa sababu mwenye hasira hujutia. Na ikiwa hajutii, basi wazimu wake umejijenga vizuri”.52 Imam Baqir (a) alisema: “Mtu hupata hasira na haridhiki hadi pale atakapoingia motoni.”53 Imam Sadiq (a) alisema: “Ghadhabu ni ufunguo wa kila shari”.54 51. Nahjul Balagha 52. Nahjul Balagha 53. Al Kaafy, 54. Al Kaafy 34


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:20 PM

Page 35

Tabia njema kwa mujibu wa Ahlul Bayt (a.s) Hasira ni ufunguo wa maovu kwa yale matokeo yake ya uovu na hatari kama vile: kejeli, kuaibisha, matusi machafu, kupiga, kuua na mfano wake katika maovu.

Pia alisema (a): “Nilimsikia baba yangu akisema: siku moja, bedui alimjia Mtukufu Mtume (s) na kumuambia: mimi nakaa ubeduini, basi nifundishe mafunzo yanayokusanya kila kitu. Mtukufu Mtume (a) akamuambia: nakuamuru usiwe na hasira. Yule bedui akarejea ombi lake mara tatu mpaka akajirudi na kusema: sitomuuliza chochote baada ya hili. Hakuniamrisha chochote Mtume wa Mwenyezi Mungu ila kuwa ni kheri�.55

SABABU ZA GHADHABU Hasira haijitokezi kiholela au kwa mara moja, bali zipo sababu na vichochezi vinavyomfanya mtu awe na hisia kali, mwepesi wa kuathiriwa. Tukichunguza sababu, tunaweza kuzifupisha kama ifuatavyo: 1. Inaweza kuwa chanzo cha hasira ni afya mbaya kama vile afya kwa ujumla kuwa mbaya au mfumo wa neva (mtandao wa mishipa ya fahamu) kuwa dhaifu hali ambayo husababisha kulipuka haraka. 2. Inaweza ikawa chanzo ni nafsi. Kwa akili kuchoshwa au kupindukia katika ubinafsi, au kuwa na hisia za kudharauliwa na nuksani na mfano wa hayo katika hali za kinafsi ambazo haraka humchemsha mtu na kuchochea hasira yake. 3. Inaweza kuwa chanzo ni tabia. Mfano ni kama kuzoea ugomvi na kuhamaki haraka, jambo ambalo linapelekea tabia ya hasira kujijenga. 55. Al Kaafy 35


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:20 PM

Page 36

Tabia njema kwa mujibu wa Ahlul Bayt (a.s)

MADHARA YA GHADHABU Ghadhabu ina madhara makubwa na maafa yenye kuangamiza yanamdhuru mtu binafsi na jamii, kimwili na kinafsi, kimada na kitabia. Ni mara ngapi ghadhabu imejeruhi uhusiano mwema na kujaza nafsi na nia mbaya na kijicho na kukata kabisa mirija ya kupendana na kushikamana baina ya watu? Ni mara ngapi hasira imesweka watu ndani ya jela na kuwatia katika maangamio! Ni mara ngapi hasira imewasha moto wa vita na kumwaga damu na kuacha kafara ya maelfu wasio na hatia! Yote hayo ni tija ya hali ya hatari (mkorogano) kinafsi itokanayo na ghadhabu ambayo yaweza kusababisha mauti ya ghafla. Baada ya hapo mtu anageuka kuwa ni volkano yenye kuwaka inapasuka ikitoa hasira na shari, binadamu anakuwa mnyama au mnyama katika sura ya binadamu. Mwenyewe kwa ulimi wake anaropoka maneno machafu na matusi, kuchafua utu wa watu na mara kwa mkono wake anapiga na kutesa, hadi ya kufikia kuua. Ama ikiwa mwenye hasira hana uwezo na hasimu wake, basi majanga ya hasira yatamgeukia mwenyewe: mara atachana nguo yake na kujipiga kifuani na kichwani na mara atafanya vitendo vya wazimu kama vile kutukana wanyama na kupiga visivyohai.

GHADHABU NZURI NA MBAYA Ghadhabu ni silika muhimu. Ni silika hiyo imwezeshayo mwanadamu kuwa na hamasa, kukataa na kumsukuma kujitoa mhanga na kujitolea katika njia ya kukamilisha malengo matukufu kama vile kulinda itikadi, kulinda roho na mali, na utu. Kwa hiyo pindi mwanadamu anapojivua silika hii 36


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:20 PM

Page 37

Tabia njema kwa mujibu wa Ahlul Bayt (a.s) anakuwa ni shabaha la unyonge na utumwa kama inavyosemwa: “anaekasirishwa na asikasirike, basi yeye ni punda�. Kutokana na hayo tunaelewa kwamba hasira mbaya ni ile ambayo mtu huchupa mipaka na kutoka katika usawa wa mizani na kupingana na taratibu za akili na sheria. Ama hasira iliyokuwa ya kiwango cha kati ni katika sifa njema ambazo zamtukuza mtu na kukuza fikra zake. Mfano ni kama vile kukasirikia maovu na kukasirika katika njia ya Mwenyezi Mungu (swt).

NJIA ZA KUTIBU HASIRA Tumeelewa katika kurasa hizi upande mmoja katika sababu za ghadhabu na mabaya yake. Hapa tunatoa namna ya matibabu ya tabia hii hatari. Utaratibu huu wa tiba umeundwa na misingi ya hekima ya nafsi, na maelekezo ya kitabia. Katika misingi ifwatayo, huenda wagonjwa wa hasira watapata kitachowasaidia kupambana na ghadhabu na kuiponya: 1. Ikiwa chanzo cha hasira ni ugonjwa wa kiafya au udhoofu ( wagonjwa, wazee, wembamba wa umbile ) basi matibabu yao ni kwa njia za kiafya na kuongeza nguvu kiafya na kumpa mtu vitulizo vya nafsi na mwili kama vile kuwa na utaratibu mzuri wa chakula, kuwa na usafi, kufanya mazoezi muafaka, kuvuta hewa safi na kupumzisha misuli kwa kujinyoosha juu ya kitanda. Pamoja na hayo yote inabidi mtu kujiepusha na kuwa mbali na vile vinavyokerehesha nafsi na mwili kama vile kufikiria sana, kukesha kunakochosha, kusalimu amri mbele ya huzuni na mithili ya haya katika vichochezi. 2. Ikiwa sababu ni kuzidi ubinafsi, ubishi,ushindani, kustihzai, kutia aibu na mzaha unao chukiza, basi dawa katika hali kama hii ni kujiepusha sababu hizo na kuwa mbali kabisa na vichochezi hivyo.

37


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:20 PM

Page 38

Tabia njema kwa mujibu wa Ahlul Bayt (a.s) 3. - Kukumbuka mabaya ya ghadhabu na hatari zake na kwamba inamdhuru mwenye ghadhabu kuliko anaeghadhibikiwa. Hutokea jambo la upuuzi likazusha hasira na kuangamiza siha ya mtu na furaha ya maisha yake. Baadhi ya watafiti wa saikolojia wanasema: “achilia mbali jaribio lako la kuwaadhibu adui zako, kwani kwa kufanya hivyo unaiudhi zaidi nafsi yako kuliko unavyowaudhi. Pindi tunapowachukia maadui zetu basi tunawapa nafasi ya kutushinda. Hakika maadui zetu wanacheza kwa furaha ikiwa wanaelewa kwamba watusababishia usumbufu na adhabu. Hakika kuwachukia maadui zetu haiwaudhi wao bali sisi wenyewe na inajalia siku zetu na usiku kuwa jehanamu”. Na hapa ndipo inatakiwa kukumbuka fadhila za uvumilivu na athari zake tukufu na kwamba tabia hiyo humfanya mtu apendwe, asifiwe na kuvutia. Na msukumo bora kuhusu uvumilivu ni kauli ya Mwenyezi Mungu (swt):

“Mema na maovu hayalingani. Lipa uovu kwa lilio jema zaidi. Hapo yule ambaye baina yako naye pana uadui atakuwa kama rafiki wa karibu wa kukuonea uchungu. Lakini hawapewi wema huu ila wanao subiri, wala hawapewi ila wenye bahati kubwa.”(Fuswilat, 41: 34-35) 4. Nguvu ya hasira na visababishi vyake humpelekea mwenye hasira kupata adhabu ya Mwenyezi Mungu (swt) na huenda ikampambanisha na nguvu ya yule aliemghadhibisha. Imam Ja’far Sadiq (a) alisema: 38


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:20 PM

Page 39

Tabia njema kwa mujibu wa Ahlul Bayt (a.s) “Mwenyezi Mungu alimpa wahyi mmoja wa mitume wake kwamba: mwana wa Adam nikumbuke katika hasira yako, nitakukumbuka katika hasira yangu, sitakuangamiza katika wale niwaangamizao na uridhike nami pindi unaposhinda kwani ushindi wangu kwa ajili yako ni bora kuliko ushindi wako kwa ajili ya nafsi yako�.56 5. Vyema mwenye ghadhabu kuzuia moto wa ghadhabu na pia kufikiria sana kuhusu kauli yake na vitendo vyake pindi anapopagawa na hasira. Hilo litapunguza makali ya kuhamaki na kumrudisha katika hali nzuri na sawa. Na hawezi kupata hilo mtu ila kwa kuilazimisha nafsi na kumiliki neva ( mishipa ya fahamu). Amiri wa Waumini (a) alisema: "Ikiwa si mvumilivu basi jitie uvumilivu, kwani ni mara chache hutokea mtu anayejishabihisha na watu halafu asiwe pamoja nao". (Nahjul Balagha, hadithi ya 207) 6. - Ni katika tiba ya hasira: kujikinga na Shetani aliyelaniwa, kukaa chini mwenye hasira ikiwa amesimama, kulala ikiwa amekaa, kushika udhu na kunawa kwa maji baridi na kugusa mkono wa ndugu ikiwa amemkasirikia. Hakika hilo ni katika mambo yanayotuliza hasira.

5. UNYENYEKEVU MAANA Ni kuheshimu watu kulingana na uwezo wao na kutojikweza juu yao. Unyenyekevu ni tabia tukufu na silika yenye kuvutia, inavutia nyoyo, inachochea upendo na kuthamini. Na katika utukufu wa tabia hii, itutoshe kwamba Mwenyezi Mungu (swt) alimuamrisha mpenzi wake na bwana wa Mitume wake (s) kuwa mnyenyekevu.

56. Al Kaafy 39


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:20 PM

Page 40

Tabia njema kwa mujibu wa Ahlul Bayt (a.s)

QUR’ANI Mwenyezi Mungu (swt) anasema:

Na uteremshe ubawa wako (wa rehma) kwa wale waumini wanaokufwata. (Sura Shu’araa, 26:215)

HADITHI Ahlul Bait (a) wameitaja tabia hii tukufu kwa sauti na kuwatamanisha watu kwa maneno yao ya hekima na sirah yao iliyo mfano bora, na walikuwa wao ni vinara wa sifa njema na mwenge wa tabia bora. Mtume (s) alisema: “Hakika mpendwa wenu kwangu, na mkaribu wenu zaidi kikao kwangu siku ya Qiyama, ni yule mbora wenu kitabia, na mwingi wenu sana unyenyekevu. Na hakika, kati yenu aliye mbali nami sana siku ya Qiyama, ni wenye maneno mengi (kubwabwaja) ambao ndiyo wenye kiburi”.57 Amiri wa Waumini Imam Ali (a): “Ni ubora ulioje wa unyenyekevu kama ule wa matajiri kwa masikini?! Wafanya hivyo wakitafuta yalioko kwa Mwenyezi Mungu (swt). Na ubora wa hilo, ni kiburi cha mafakiri kwa matajiri wakitegemea kwa Mwenyezi Mungu (swt)”.58 Imam Ja’far Sadiq (a) alisema: “Mbinguni wapo malaika wawili wamekabidhiwa waja (wa Mwenyezi Mungu). Yeyote anaenyenyekea kwa ajili ya Mwenyezi Mungu (swt) basi 57. Kitaabu Qurbul Asnaad 58. Nahjul Balagha 40


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:20 PM

Page 41

Tabia njema kwa mujibu wa Ahlul Bayt (a.s) Malaika hao humyanyua, na yeyote anayetakabari basi Malaika hao humteremsha daraja�.59 Pia alisema: "Ni katika unyenyekevu kuridhia kukaa popote (bila kutaka penye hadhi, kwa maana ukaridhia sehemu fulani kwa kuwa ina hadhi na usikubali nyingine) katika kikao, pia kumsalimia unaekutana nae, na kuacha kubishana hata kama utakuwa ni mwenye haki, na kuchukia kusifiwa kwenye uchajimungu". 60 Ni muhimu kutaja hapa kwamba unyenyekevu unaosifiwa ni ule wa kiwango, usio na kuchupa mipaka wala kupunguwa. Unyenyekevu ukizidi ni sababu ya uduni na udhalili. Ama upungufu ni sababu ya kiburi na kujiona. Kwa hiyo mwenye akili ni vyema kuchagua njia ya kati isiyokuwa na udhalili na ubinafsi na hilo ni kwa kumpa kila mtu heshima na utukufu anaostahiki kulingana na cheo chake na vipawa vyake. Kwa sababu hiyo haifai kabisa kuwanyenyekea wabinafsi na wenye kujikweza juu ya watu. Unyenyekevu katika hali kama hii inaleta udhalili na kuwachochea madhalimu hawa kuedelea kufanya kiburi. Al Mutanabby (mshairi) anasema: Ikiwa utamtukuza mtu karimu basi umemmiliki Ama ukimtukuza muovu basi atakuasi Naye al-Ma’arry alisema: Ewe mtawala (wa popote pale) usidhulumu Wangapi kama wewe wamekuja na kuondoka! Nyenyekea pindi unapopewa utukufu Hilo ni miongoni mwa yanayozidisha utukufu 59. Al Kaafi 60. Al Kaafy 41


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:20 PM

Page 42

Tabia njema kwa mujibu wa Ahlul Bayt (a.s) Katika methali: unyenyekevu wa mtu katika utukufu wake ni kinga wakati wa kuporomoka dhidi ya furaha ya maadui. Hapa tunataja baadhi ya ubora wa Ahlul Bayt (a) na unyenyekevu wao wa mfano usio na kifani: Mtume (s) alikuwa ni mwingi wa unyenyekevu kuliko watu wote. Alikuwa akiingia nyumbani kwa watu, hukaa sehemu isiyo ya heshima na nyumbani kwake alikuwa akiwasaidia wakeze, akimkamua maziwa kondoo wake, akishona (kiraka) nguo yake, akishona kiatu chake, na kujifanyia kazi, kubeba mzigo wake sokoni, akikaa na mafukara na kula na masikini. Mtume (s) alipokuwa, akinongonezwa na mtu, haondoi kichwa chake mpaka yule mtu mwenyewe aamuwe kuondoa kichwa chake, anapompa mtu mkono hautoi mkono wake mpaka yule mtu aamue kutoa wa kwake, anapokutana na mtu yeye ndiye wa kwanza kutoa salaam, na wa kwanza kutoa mkono, kamwe hakunyoosha miguu yake mbele ya masahaba wake, anamuenzi anayeingia kwake na mara humtandikia nguo yake na kumpa mto alionao, akiwaita masahaba kwa majina ya uzazi (baba Fulani..) na kwa majina mazuri ili kuwatukuza, hamkatishi mtu kauli yake, na akigawa sawa mtazamo wa macho baina ya masahaba wake, na alikuwa mwingi wa kutabasamu kuliko yeyote na mwema wa nafsi.61 Abu Dharr al-Ghifaary alisema: Mtume (s) alikuwa akikaa pamoja na masahaba wake, na akitokeza mgeni basi hawezi kupambanua yupi ndiye Mtume mpaka aulize. Kwa sababu hiyo tukamuomba aweke mahala (maalumu) akija mgeni aweze kumfahamu. Tukamjengea benchi ya udongo, alipokuwa akikaa na sisi tukimzunguka. Imepokelewa kwamba Mtume (s) alikuwa safarini na akaamrisha aandaliwe kondoo. Mmoja katika masahaba akasema: “Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu mimi nitamchinja, mwingine akasema: mimi nitamchuna, 61. Safinatul Bihaar, juz. 1, uk. 415 42


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:20 PM

Page 43

Tabia njema kwa mujibu wa Ahlul Bayt (a.s) mwingine akasema: mimi nitampika, naye Mtume (s) akasema: nami nitakusanya kuni.’ Masahaba wakasema: ‘Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu (itakuwaje) sisi tunakutosheleza.’ Akawajibu: ‘Najua mnatosha, lakini nachukia kujitofautisha nanyi kwani Mwenyezi Mungu (swt) anachukia mja wake kujipambanua baina ya masahaba wake.’ Akasimama na kukusanya kuni.” 62 Imepokelewa kwamba Mtume (s) alikwenda kisimani kuoga. Hudhayfa bin alYamani akamshikia nguo kumsitiri hadi alipomaliza kuoga. Ilipofika zamu ya Hudhayfa kuoga, Mtume (s) akasimama kumsitiri. Hudhayfa akakataa katakata na kusema: “Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, tafadhali wewe usifanye hivyo.” Mtume (s) akakataa na kumsitiri mpaka akamaliza kuoga kisha akamwambia: “Kamwe hawakusuhubiana wawili ila yule aliye mwema zaidi kwa mwenzie ndiye apendwae zaidi na Mwenyezi Mungu.”63 Hivyo ndivyo pia alivyokua Imam Ali (s) katika utukufu wa tabia zake na unyenyekevu wake. Dhwaraar akimsifu alisema: “Alikuwa kama mmoja wetu, akitukurubisha pindi tunapomjia, akitujibu pindi tunapomuuliza, na kuitikia mwito wetu pindi tunapomuita, na kutupasha habari tunapomtaka. Pamoja na yote hayo ya kutukaribia tulikuwa tunamuogopa kwa haiba yake tunashindwa kumsemesha. Akitabasamu utadhani mfano wa lulu zilizopangwa vyema. Anawatukuza wana dini na kuwakaribisha maskini, mwenye nguvu hana tamaa ya kufanya dhulma, na wala dhaifu hakati tamaa na uadilifu wake”. Naye Imam Ja’far Sadiq (a) alisema: “Alitoka amiri wa waumini Ali (a) akiwa juu ya kipando. Masahaba wake wakamfuata nyuma, akageuka na kuwauliza: ‘Je! mna shida?’ Wakamjibu: ‘Hapana ewe Amiri wa waumini, lakini sisi tunapenda kutembea pamoja 62. Safinatul Bihaar, juz. 1, uk. 415 63. Safinatul Bihaar, juz. 1, uk. 416 43


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:20 PM

Page 44

Tabia njema kwa mujibu wa Ahlul Bayt (a.s) na wewe.’Akawaambia: ‘Ondokeni, kwani usuhuba wa mwenye kutembea kwa miguu na mwenye kipando ni ufisadi kwa mwenye kipando na madhila kwa mwenye kutembea.’”64 Kuhusu unyenyekevu wa Imam Husayn (a): Alipita na kuwakuta maskini wanakula (nyama ) wamekaa juu ya kisaa (nguo). Akawatolea salamu, nao wakamkaribisha kwenye chakula chao. Akakaa pamoja nao na kuwaambia: “Lau kama chakula hiki siyo cha sadaka ningekula pamoja nanyi.” Kisha akawaambia: “Simameni twende nyumbani kwangu.” Akawapa chakula, nguo na kuwapa pesa (dirhamu).65 Kuhusu Imam Ridhwaa (a): Msimulizi (rawi) anasema: “Nilikuwa pamoja na Imam Ridhwaa (a) katika safari yake ya Khurasan. Siku moja ikaandaliwa meza, na akawakusanya mawaly (watumwa walioachwa huru) kutoka Sudan na wengine, hapo nikamwambia: ‘Nafsi yangu iwe fidia yako, lau ungewatengea hawa meza yao.’ Akanijibu: ‘Kamwe usinene hivyo, hakika Mola (swt) ni mmoja, na mama ni mmoja na baba ni mmoja na ama malipo ni kwa matendo.’”66

6. KUTAKABARI MAANA YAKE Ni hali inampelekea mtu kujihisi bora (kujivuna), kujiona juu ya wengine, kikauli au kimatendo. Hulka hii ni katika maradhi hatari ya kitabia na mbaya zaidi kumwangamiza mwanadamu. Pia hupelekea mwenye tabia hii kuchukiwa, kudharauliwa na kukimbiwa na watu. 64. Mahasinul Barqy 65. Manaqib ibn Shahr Ashub 66. Al-Kaafy 44


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:20 PM

Page 45

Tabia njema kwa mujibu wa Ahlul Bayt (a.s) Kwa ajili ya hayo, Qur’an na Sunnah zimeshutumu tabia hii na kuikataza.

QUR’ANI Mwenyezi Mungu (swt) anasema:

“Wala usiwabeuwe watu, wala usitembee katika ardhi kwa maringo. Hakika Mwenyezi Mungu (swt) hampendi kila anaejivuna na kujifaharisha”. (Luqman, 31 :18)

“Wala usitembee katika ardhi kwa maringo. Hakika wewe huwezi kuipasua ardhi wala kufikia urefu wa milima. (Luqman, 31:18)

“Hapana shaka kuwa hakika Mwenyezi Mungu (swt) anayajua wanayoyaficha na wanayoyatangaza. Kwa hakika Yeye hawapendi wanaojivuna.”(An Nahl, 16 : 23)

45


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:20 PM

Page 46

Tabia njema kwa mujibu wa Ahlul Bayt (a.s) “Na siku ya Kiyama utawaona waliomsingizia uwongo Mwenyezi Mungu (swt) nyuso zao zimesawijika. Je! Si katika Jahannamu makazi ya wanaotakabari? (Az Zumar, 39:60)

HADITHI Mtume (s) alisema: “Hakika mpendwa wenu zaidi kwangu na mkaribu wenu zaidi kwangu kidaraja (makao) siku ya Kiyama ni mbora wenu kitabia na mwingi wenu wa kunyenyekea. Na wambali zaidi kwangu siku ya Kiyama ni wasemao sana na wao ndiyo wenye kutakabari.”67 Amiri wa waumini (a) Ali, katika moja ya hotuba zake alisema: “Zingatieni jinsi Mwenyezi Mungu (swt) alivyomfanya Ibilisi (l.a.) pindi alipobatilisha amali yake ya muda mrefu na juhudi yake kubwa kwa sababu ya kiburi cha muda mchache! Alikuwa amemwabudu Mwenyezi Mungu miaka elfu sita, haifahamiki ni katika miaka ya hapa duniani au ya akhera. Sasa nani baada ya Ibilisi atakayesalimika kwa kufanya uovu kama wa Ibilisi? Kamwe haiwezekani Mwenyezi Mungu (swt) kumwingiza peponi mwanadamu kwa jambo ambalo ndiyo sababu ya kufukuzwa malaika (alikuwa jini aliyefikia daraja ya malaika). Mwombeni Mwenyezi Mungu (swt) akuhifadhini na hatari za kiburi kama vile mnavyojihifadhi na mabalaa ya maisha. Kama ingelikuwa Mwenyezi Mungu (swt) ameruhusu kiburi kwa yeyote katika waja wake, basi angeliruhusu hilo kwa mitume lakini Mwenyezi Mungu (swt) amechukia kwao kiburi na kuridhia kwao unyenyekevu.”68 Imam Sadiq (a) alisema: Wako mbinguni malaika wawili wamepewa wajibu wa (kushughulikia) waja wa Mwenyezi Mungu. Kwa hiyo yeyote anayenyenyekea basi wao humnyanyua (daraja), na ikiwa atatakabari basi wao humteremsha (dara67. Al Bihaar, muj. 15, juz. 2, uk. 209 68. Nahjul Balaagha 46


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:20 PM

Page 47

Tabia njema kwa mujibu wa Ahlul Bayt (a.s) ja)”. 69 Pia alisema (a): “Hakuna mtu yeyote anayetakabari au kuwa jabari ila kwa udhalili alioupata ndani ya nafsi yake”.70 Imam Sadiq (a) kama alivyopokea kutoka kwa baba zake (a) alisema: “Siku moja Mtume (s) alipita penye mkusanyiko wa watu na kuwauliza: ni jambo lipi limewakusanya hapa? Wakamjibu: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, huyu hapa mwendawazimu kapandisha. Mtume akasema: huyo si mwendawazimu, lakini yeye kafikwa na mtihani. Kisha akasema: sasa mnataka niwafahamishe nani mwendawazimu kweli mwendawazimu? Tukajibu: Ndiyo ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu. Mtume akasema: Mwendawazimu ni yule ambaye anaetembea kwa maringo, ambaye shari yake haiaminiki wala kheri yake haitarajiwi; huyo ndiyo mwendawazimu ama huyu ni muathirika (kafikwa na mtihani)”.71 Pia alisimulia (a): “Baina ya Salman Farsy (r) na mtu mmoja yalizuka maneno na ugomvi. Yule mtu akasema: nani wewe Salman? Salman akajibu: ama mwanzo wangu na mwanzo wako ni nutfa (chembe hai) iliyoduni, na ama mwisho wako na mwisho wangu ni maiti inayooza. Na itakapokuwa siku ya Kiyama, na ikawekwa mizani, basi yule ambaye mizani yake itakuwa nzito huyo ndiye karimu, na yule ambaye mizani yake itakuwa hafifu huyo ndiye duni.”72 Pia kutoka kwake (a ) alisema: “Mtu tajiri mwenye mavazi safi alikuja kwa Mtume (s) na kukaa kwake. Punde akaja mtu maskini mwenye mavazi machafu na kukaa pembeni ya 69. Al Waafy, juz. 3, uk. 87 70. Al Waafy, juz. 3, uk. 150 71. Al Bihaar, muj. 15, juz. 3, uk. 125 72 Al Bihaar, muj. 15, juz. 3, uk.124 47


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:20 PM

Page 48

Tabia njema kwa mujibu wa Ahlul Bayt (a.s) yule tajiri. Yule tajiri akavuta nguo yake chini ya mapaja yake. Mtume (s) akamwuliza: je umehofu kwamba utapatwa na umaskini wake? Akajibu: hapana. Mtume (s) akamuambia: je umeogopa atapaka nguo zako uchafu? Akajibu: sivyo. Mtume (s) akasema: ni nini basi kilichokupelekea wewe kufanya ulilofanya? Akajibu: ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu mimi nina mwenza ambaye ananipambia kila uovu na kunifanyia kila jema kwangu kuwa baya. Sasa nimeamua kumpa ndugu yangu huyu nusu ya mali yangu. Mtume (s) akamuuliza yule maskini: je! umekubali? Akajibu: kamwe sikubali kwa sababu nahofu yasije yakaniingia yaliyomuingia (yule tajiri).�

MABAYA YA KUTAKABARI Ni wazi kwamba kiburi ni katika maradhi hatari ya kitabia ambayo yameenea baina ya jamii mbali mbali. Mabaya ya kiburi na athari zake mbaya kwenye maisha ya mtu. Anapotawaliwa mtu na kiburi, uzio wa majivuno na kujiona huzingira nafsi yake na hufanywa majinuni wa kupenda ubinafsi na kujionyesha. Hakuna kitakachomridhisha ila chenye sifa za kupamba na za uongo, jambo ambalo linamtia upofu hawezi kuona kasoro na aibu zake na wala hajali kuadibisha nafsi yake na kurekebisha kasoro zake. Matokeo yake ni kulaumiwa, kuchukiwa na kudharauliwa. Zaidi ya hayo ni kwamba mwenye kiburi ndiyo mwingi wa kukataa haki na usawa na yanayotakiwa na sheria na dini. Mabaya ya kiburi kwa jamii. Kiburi kinaeneza ndani ya jamii roho ya chuki na bughudha na kukata mawasiliano mema ya kijamii. Hakuna anayewafanyia uovu watu kama 48


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:20 PM

Page 49

Tabia njema kwa mujibu wa Ahlul Bayt (a.s) vile anavyofanya mwenye kiburi kwa kujikweza juu ya watu kwa majivuno yake na ubinafsi wake. Kiburi ni ugonjwa unaomkosesha mtu furaha na kumfanya achukiwe na kuishi katika upweke. Pia kwa wale wenye uhusiano naye huathirika kwa njia moja au nyingine.

SABABU ZA KUTAKABARI Tabia za mwanadamu - ziwe njema au mbaya - ni akisi za nafsi kwa mtu mwenyewe. Kama vile maji yabubujikayo kwenye chemchemi ni kielelezo cha asili ya maji hayo. Akisi hizo zinatoa nuru au kutia kiza, na matokeo yake huwa matamu au machungu kufuatana na nafsi kuwa nzuri au mbaya. Hakuna tabia yoyote iliyo mbaya ila chanzo chake ni kukengeuka nafsi au kuwa mbaya. Katika sababu za kutakabari; ni kupindukia mipaka katika kuikadiria nafsi yake, kutathmini vipawa vyake na fadhila zake na kuchupa mipaka katika kughurika na kujiona. Hatakabari yeyote ila anapoona yeye ana elimu nyingi au cheo kitukufu au mali nyingi au jaha iliyoenea na kama hayo katika visababishi vya ubinafsi na kutakabari. Na mwanzo wa kiburi unaweza ukawa ni uadui au hasadi au majivuno jambo linalopelekea wenye kasoro hizo kushindana na viongozi wema na watukufu na kudharau utukufu wao na kujikweza juu yao kwa aina mbalimbali za dharau kimatendo na kikauli kama inavyodhihiri katika mapambano ya wapinzani na wanaohasidiana katika mahafali na vilabu.

49


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:20 PM

Page 50

Tabia njema kwa mujibu wa Ahlul Bayt (a.s)

VIWANGO VYA KUTAKABARI Viwango vya kuathiriwa vinatofautiana; Daraja ya kwanza: Ni kiburi kimejificha ndani ya mtu mwenyewe, ikawa dalili zake na maovu yake hayakudhihiri. Tiba yake ni kwa unyenyekevu. Daraja ya pili: Hapa kiburi kimeota na dalili zake zimejitokeza kwa mtu kujikweza juu ya wengine na kuwatangulia katika mahafali na kujiona anapotembea, Daraja ya tatu: Ni pale kiburi kinapovuka mipaka na matatizo yake yakazidia hadi mwenyewe akashikwa na wazimu wa ukubwa, kupindukia mipaka katika kupenda jaha na kujionyesha. Hapo utamwona mwathirika akijitapa kwa mema yake na ubora wake na huku akiwaponda na kudharau wengine. Hii ni daraja mbaya zaidi ya kiburi.

AINA ZA KIBURI Kiburi kinagawanyika katika aina tatu: 1. Kiburi juu ya Mwenyezi Mungu (awj): Ni kule mtu kukataa kumwamini Mwenyezi Mungu (swt) na kukataa kumtii na kumwabudu. Na hiyo ni aina chafu zaidi kuliko zote ya ukafiri na mbaya kuliko yote ya kiburi. Hii ndiyo aina ya kiburi walichokuwa nacho akina Firauni, Namrud na mithili yao katika vinara wa ukafiri na majabari wa ukanamungu. 2. Kiburi juu ya Mitume: Ni kule mtu kukataa kuwasadiki na kunyenyekea. Hii aina imekurubia aina ya kwanza. 3. Kiburi juu ya watu: Ni kule mtu kuwadharau watu na kujikweza juu yao 50


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:20 PM

Page 51

Tabia njema kwa mujibu wa Ahlul Bayt (a.s) kikauli na kimatendo, na mfano wake ni kama vile kujivuna mbele ya maulamaa wachamungu na kususa kuwauliza masuala na kufaidika na elimu zao pamoja na miongozo yao, jambo ambalo linapelekea wenye kiburi kupata hasara na kuwa wajinga wa hakika za dini na hukumu za sheria tukufu.

TIBA YA KIBURI Kwa kuwa kiburi ni wazimu wa kitabia hatari wenye kuangamiza, ni vizuri kwa kila mwenye busara kuchukua tahadhari na kujitahidi - ikiwa dalili zake zimemsibu - kutibu nafsi yake na kuitoharisha na aibu zake. Hizi hapa baadhi ya nasaha ili kutibu ugonjwa huu hatari: 1. Kwanza, ajue mwenye kiburi ukweli kuhusu yeye na yale aliyonayo ya aina mbalimbali ya udhaifu na kutoweza: mwanzo wake ni kiini (chembe hai) kichafu, na mwisho wake ni mzoga uozao. Na baina ya hali mbili hizi yeye ni asiyejiweza, dhaifu, aumwa na njaa na kushikwa na kiu, mara hupatwa na maradhi, hufikiwa na ufakiri na madhara na uharibifu, pia humfika mauti na kutoweka. Mtu huyu hawezi kujiletea manufaa na kujikinga na mabaya. Ni haki ya mwenye kuwa na sifa hizi za unyonge kujiepusha na ubinafsi na kiburi kwa kujiongoza kwa aya tukufu ifuatayo:

“Hiyo ni nyumba ya akhera tumewatayarishia wale ambao hawataki kujitukuza ndani ya ardhi wala kufanya ufisadi. Na bila shaka mwisho mwema ni wa wale wachamungu.� (al Qasas, 28: 83) Mbora wa watu ni yule aliye mbora wao kitabia, mbora wao kunufaisha na mwingi wao kumcha Mwenyezi Mungu (swt) na kufanya wema. 51


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:20 PM

Page 52

Tabia njema kwa mujibu wa Ahlul Bayt (a.s) 2. Kisha akumbuke athari za unyenyekevu na mema yake, na ubaya wa kiburi na maovu yake na yale yaliyopokelewa kutokana na dalili za akili na kitabu kuhusu sifa ya unyenyekevu na kuhusu ubaya wa kiburi. Bazarjamhar anasema: “Tulikuta kwamba unyenyekevu pamoja na ujinga na ubakhili ni wa kusifiwa zaidi kwa wenye akili kuliko kiburi pamoja na adabu na utoaji; kwa hiyo wema ulioje mtukufu (unyenyekevu) uliozungukwa na maovu mawili (ujinga, ubakhili) na ni uovu uliyoje (kiburi) uliozungukwa na mema mawili (adabu, utoaji)!� 3. Aipe nafsi yake mazoezi ya unyenyekevu na kujipamba na tabia za wanyenyekevu ili kupunguza ukali wa kiburi ndani ya nafsi yake. Hii ni baadhi tu ya mifano: a. - Ikiwa katika mashindano ya kielimu imetokea mgongano na mjadala, ni vyema kwa mwenye busara kusalimu amri kwa mshindani wake ikiwa atampa hoja na kujiepusha na kujikweza na kubisha. b. Ajiepushe na kushindana na wenzake katika kugombea kuingia katika sherehe na kujitia mbele katika vikao. c. Aingiliane na mafakiri na masikini na kuanza kuwatolea salamu na kula nao pamoja meza moja na kuitikia mwito wao kwa kuwaiga Ahlul Bait (a).

7. KUTOSHEKA MAANA YAKE Ni kutosheka katika mali na kiasi anachohitajia mtu na kujitosheleza na kutotilia umuhimu katika kile kinachozidia hapo. Hii ni sifa tukufu ambayo ni tafsiri ya utukufu wa nafsi na ubora wa tabia.

52


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:20 PM

Page 53

Tabia njema kwa mujibu wa Ahlul Bayt (a.s)

HADITHI Hizi hapa ni baadhi ya fadhila za tabia hii kutoka katika maandiko: Imam Baqir (a) alisema: “Atakaetosheka na kile ambacho Mwenyezi Mungu (swt) amemruzuku basi yeye ni miongoni mwa matajiri kuliko wote”.73 Hakika mwenye kutosheka amekuwa miongoni mwa matajiri kuliko wote kwa sababu ukweli wa utajiri ni kutowahitajia watu. Na mwenye kuridhika, anaridhia na kutosheka na kile ambacho Mwenyezi Mungu (swt) amemruzuku; hahitaji wala kumwomba ila Mwenyezi Mungu (swt). Inasemekana kwamba pindi alipofariki Galeni (tabibu wa kigiriki wa karne ya pili) ilikutwa ndani ya mfuko wake kipande cha karatasi kimeandikwa: “Ulichokula bila israfu ni kwa ajili ya mwili wako, na ulichotoa sadaka ni kwa ajili ya roho yako, na ulichoacha ni kwa ajili ya wengine, na mfanya wema yuko hai hata kama amehamia akhera, na mfanya uovu ni maiti hata kama atabaki hai katika dunia hii, na kutosheka kunasitiri urafiki, na kupangilia kunazidisha kichache, na hakuna kwa mwanadamu kilicho na faida zaidi kuliko kumtegemea Mwenyezi Mungu (swt).”74 Mtu mmoja alimshitakia Abu Abdilah (a) kwamba anatafuta na anapata, lakini hatosheki na nafsi yake inamvuta kutaka zaidi na akasema: nifundishe jambo ambalo nitanufaika nalo. Abu Abdilah (a) akasema: “Ikiwa kinachokutosha kitakufanya usihitaji, basi kidogo ndani yake kitakufanya usihitaji; na ikiwa kwamba kinachokutosha hakikufanyi usihitaji, basi kila kilichomo ndani yake hakitokufanya usihitaji”.75 73.Al Waafy, juz. 3, uk. 79 74.Kashkul al bahai 75.Al Waafy, juz. 3, uk. 79 53


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:20 PM

Page 54

Tabia njema kwa mujibu wa Ahlul Bayt (a.s) Imam Baqir (a) alisema: “Ole wako macho yako kutamani yule aliye juu yako; inatosha aliyomwambia Mwenyezi Mungu Mtume wake (s) :

Wala yasikuvutie mali zao wala watoto wao,…(9:55) na pia akasema:

“Na usividokolee macho yako tulivyowastareheshea watu wengi miongoni mwao (makafiri na wenye kuabudu dunia) ikiwa ni mapambo ya maisha ya dunia… (20:131) Ikiwa chochote katika hayo kitakuingia nafsini mwako, basi ukumbuke maisha ya Mtume (s); kwani chakula chake kilikuwa shairi na halua yake tende na kuni zake makuti ya mtende ikiwa atayapata”.76

MEMA YA KUKINAI Kukinai kuna umuhimu mkubwa mno na athari kubwa katika maisha ya mwanadamu na kutimiza utulivu wa nafsi na mwili. Kukinai kunamkomboa mtu na utumwa wa kuabudu uyakinifu pia utumwa wa tamaa na uroho pamoja na matatizo yake yanayosumbua na udhalilishaji wake. Baada ya ukombozi, kukinai hupuliza ndani ya nafsi utukufu, ukarimu, enzi ya nafsi, kudhibiti nafsi na kujiepusha na mambo ya kidunia na kutaka wema kutoka kwa watu waovu. Mwenye kukinai na mahitaji ya msingi ndiye mwenye maisha ya furaha zaidi, ndiye mwenye akili iliyotulia, ndiye mwenye utulivu na amani kuliko yule mroho asiyetosheka ambaye anasumbuka kuridhisha tamaa 76. Al Waafy, juz. 3, uk. 78 54


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:20 PM

Page 55

Tabia njema kwa mujibu wa Ahlul Bayt (a.s) zake, na yule ambaye asiyeachana na wasiwasi, taabu na dhiki. Baada ya haya, kukinai humpa mtu mwamko wa kiroho, akili yenye kupenya na humsukuma kwenye kujiandaa kwa ajili ya akhera kwa kufanya matendo mema. Katika yaliyozungumzwa ya nadra kuhusu kukinai: Al-Khalil bin Ahmad al-Farahidy alikuwa akipata shida katika vibanda vya Basra wakati rafiki zake wagawana zawadi nono kwa elimu yake sehemu mbalimbali. Imeelezwa kwamba Sulayman bin Ali al Abasy, alimtumia mtu kutoka Ahwaz ili amuadabishe mwanae. Al-Khalil akamtolea mjumbe wa Sulayman mkate mkavu na akasema: kula, sina zaidi ya huu, na maadamu naupata huu, basi sina haja ya Sulayman. Mjumbe akasema: sasa nimfikishie ujumbe gani? Akasema: Muelezee Suleyman kwamba simuhitaji (pamoja na kutokuwa naye naishi katika maisha ya wasaa na utajiri) ila mimi si mwenye mali. Ufakiri ni katika nafsi na wala si katika mali, ufahamu hivyo, na hivyo hivyo utajiri ni katika nafsi na siyo kwa mali. Basi riziki ni kwa Qadari, kutokuwa na uwezo hakupunguzi na wala nguvu yoyote ile haiwezi kukuongezea riziki. Kutoka katika Kashkul Bahai, Bwana Uthman bin Affan alimtuma mtumwa wake na mfuko uliojaa dirham kwa Abu Dharr na kusema: Ikiwa atakubali basi wewe upo huru. Mtumwa akamletea Abu Dharr mfuko huo na akambembeleza aukubali, lakini akakataa. Yule mtumwa akamtafadhalisha na kumwambia kubali kwani ndani yake mna uhuru wangu. Abu Dharr akajibu ndiyo, lakini ndani yake mna utumwa wangu.77

77. Safinatul Bihar, juz. 1, uk. 483 55


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:20 PM

Page 56

Tabia njema kwa mujibu wa Ahlul Bayt (a.s) Diojanus al Kalby (Diogenes, karne ya 4 kabla ya Kristo), alikuwa katika vigogo wanahekima wa kiyunani. Alikuwa mwenye kujinyima na kuipa dunia nyongo, hataki kumiliki chochote na wala hana nyumba. Iskandari (Alexander the Great) alimwita siku moja katika kikao chake. Diojanus akamjibu mjumbe kwamba akamwambie Iskandari hivi: “Kile kilichokuzuia kuja kwetu ndicho kilichotuzuia kuja kwako; usultani wako na kutotuhitajia kumekuzuia, na mimi kutokuhitajia wewe kwa kukinai kwangu kumenizuia.” 78 Mansur, khalifa wa Bani Abbas, alimuandikia Imam Ja’far Sadiq (a):”Kwa nini huji kwetu kama vile wengine wanavyofanya?” Akajibu: “Hatuna chochote katika dunia hii ambacho tutakuogopea, na wala huna chochote katika akhera ambacho tutakutarajia, na wala haumo katika neema ili tukupongeze kwayo, na pia haumo katika balaa ili tukupe pole”. Mansur akamuandikia: “Suhubiana nasi ili utunasihi.” Imam (a) akamjibu: “Anayetafuta dunia hawezi kukunasihi, na yule atakaye akhera hawezi kusuhubiana nawe”. Ni maneno matamu yaliyoje ya Abul Firas al Hamdany kuhusu kukinai aliposema: Utajiri, ni ule utajiri wa nafsi yake mtu hata kama atakuwa mabega uchi miguu pekupeku Kila kile kilichopo juu ya ardhi hakitoshi. Ikiwa utakinai basi kila kitu kinatosha.

8. TAMAA MAANA YAKE: Ni kupindukia katika kupenda mali na kutaka iwe nyingi bila kutosheka na kiwango kilichowekwa. Ni katika sifa mbaya inayompelekea mtu kwenye aina mbalimbali ya maovu na madhambi. Na inamtosha mwenye uchu na 78. Kashkul al Bahai 56


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:20 PM

Page 57

Tabia njema kwa mujibu wa Ahlul Bayt (a.s) tamaa lawama, kwa kuwa kila anapozidisha tamaa basi huzidi huzuni na upumbavu.

HADITHI Mapokezi ya kukemea tabia hii mbovu: Imam Ali (a) alisema katika wasia wake kwa mwanae Hasan (a): “Elewa kwa yakini ya kwamba hutofikia matarajio yako, na wala hutokimbia ajali yako, na wewe upo katika njia ya wale wa kabla yako, basi punguza katika kutafuta na ufanye wastani katika kuchuma, hakika mara ngapi kutafuta kumepelekea kwenye vita, na si kila anaetafuta huruzukiwa na wala si kila mwenye kufanya wastani hunyimwa”.79 Imam Baqir (a) alisema: “Mfano wa mwenye tamaa ya dunia ni kama vile nondo wa hariri, kadiri anavyozidisha kusuka na kujizungushia nyuzi, ndivyo inakuwa muhali kwake kutoka hadi anapokufa kwa huzuni”.80 Kwa sababu hiyo mshairi amesema: Bakhili humaliza muda wake kwa kukusanya mali Na alivyoweka hazina hurithi na matukio na zama Kama vile nondo wa hariri, akijengacho humwangamiza Wakati wengine kwa akijengacho hunufaika Imam Sadiq (a) alisema: “Katika yaliyoteremka pamoja na wahyi kutoka mbingini: lau kama mwanadamu angekuwa na mabonde mawili yanabubujika dhahabu na fedha, basi angetaraji juu ya hayo la tatu. Ee mwanadamu! Hakika tumbo lako ni bahari katika mabahari, na bonde katika mabonde, halijazwi na chochote ila udongo”.81 Pia alisema (a): 79. Nahjul Balagha 80. Al Waafy, juz. 3, uk. 152 81. Al Waafy, juz. 3, uk. 154 57


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:20 PM

Page 58

Tabia njema kwa mujibu wa Ahlul Bayt (a.s) “Ufisadi unaofanywa na mbwa mwitu wawili wakali katika kundi la mbuzi ambao wameachwa bila mchungaji, mmoja akiwa mbele na mwingine nyuma yao, hauwezi kufikia ule unaofanywa na kupenda mali na utukufu katika dini ya mwislamu".(Mir'aatul-Uqul…) Hasan bin Ali (a) alisema: “Maangamio ya watu yamo katika mambo matatu: kiburi, uroho, na uhasidi. Ama kiburi ni maangamio ya dini na kwa hilo alilaaniwa Ibilisi; uroho ni adui wa nafsi, na kwa hilo aliondolewa Adam katika pepo; na hasadi ni mtangulizi (mwenye kufungua njia) wa shari na kwa hilo alimwua Qabil nduguye Habil.”82

MAOVU YA TAMAA Ni wazi kwamba pindi mtu anapotawaliwa na tamaa, humfanya mtumwa na kumsababishia matatizo na unyonge. Mwenye tamaa hawazi - wala kiu ya tamaa yake haikatiki - ila kuzidisha mali na kuyalimbikiza bila kuwa na kiwango maalum. Kila anapodiriki alichokitaka basi hutamani kingine, na hivyo ndivyo tamaa itampenya na kumfanya mtumwa hadi pale mauti yatakapomchukua na kuishia kuwa kafara ya mali na hasara. Mwenye tamaa ni mwenye juhudi sana kuliko watu wengine kutafuta mali na mchache wao kunufaika na kustarehe na mali hiyo; hudhikika kuichuma na kuilimbikiza na haraka ilioje anavyoiacha kwa mauti na kurithiwa na mtu ambaye huneemeka kwayo wakati yeye alihangaika na kujinyima ladha yake. Tamaa, baada ya haya na yale, mara nyingi humtupa mtu katika tope la tuhuma na yaliyoharamishwa na hivyo hivyo humzuia mtu kufanya matendo ya kheri kama vile kuunga kizazi (swilatu rahm), kuwasaidia wenye matatizo na maskini. 82. Kashful Ghumma 58


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:20 PM

Page 59

Tabia njema kwa mujibu wa Ahlul Bayt (a.s)

TIBA YA TAMAA Baada ya kufahamu maovu ya tamaa, kwa mukhtasari hizi zifuatazo ni njia na nasaha za kuitibu: 1. Mwenye tamaa akumbuke maovu ya tamaa na ubaya wake kidini na kidunia na kwamba kuhusu dunia, katika halali yake kuna hisabu na katika haramu yake mna adhabu na katika tuhuma kuna lawama. 2. Azingatie yaliyotajwa kabla kuhusu fadhila za kukinai na mema yake kwa kutafuta ndani ya sira ya mitume, mawasii na mawali kuhusu kuipa kwao nyongo dunia (zuhd) na kukinai kwao kwa kidogo. 3. Kuacha kutizama yule anayemzidi kiutajiri na kuneemeka na vivutio vya dunia, bali amtazame asiye navyo. 4. Kubana matumizi, hilo ni katika sababu muhimu katika kupunguza ukali wa tamaa; kwani israfu katika matumizi inahitaji mali nyingi. Imam Ja’far Sadiq (a) alisema: “Nampa dhamana yule atakayefanya uchache wa matumizi kwamba hatakuwa muhitaji”.83

9. UKARIMU MAANA YAKE Ukarimu ni kinyume cha ubakhili; ni kutoa mali au chakula au chochote kile chenye faida kisheria kwa moyo safi. Ni katika tabia tukufu kabisa na vipawa azizi na faida ya kubaki daima kuliko zingine. Na yatutosha ubora wake kwamba kila kilicho cha thamani na utukufu husifiwa kwa ukarimu na kunasibishwa nao. 83. Al Bihaar, muj. 15, juz. 2, uk. 199 59


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:20 PM

Page 60

Tabia njema kwa mujibu wa Ahlul Bayt (a.s)

QUR’ANI Mwenyezi Mungu (swt) anasema; “Hakika hii ni Qur’ani tukufu” (Waqia, 56:77), “Na akawajia mtume mtukufu”(Dukhan, 44:17), “Na mimea na cheo kitukufu”(Dukhan, 44:26) Kwa ajili ya hiyo Ahlul Bayt (a) wameisifu sana tabia hii na waliojipamba nayo kwa sifa adhimu.

HADITHI Imam Baqir (a) alisema: “Kijana mkarimu aliyeshikwa katika maasi ni bora kwa Mwenyezi Mungu (swt) kuliko mzee mwenye kuabudu, bakhili”.84 Imam Baqir (a) pia alisema: “Toa na uwe na yaqini na fidia kutoka kwa Mwenyezi Mungu (swt); hakika hafanyi ubakhili mja (mwanaume au mwanamke) kuhusu kutoa katika yale yanayomridhisha Mwenyezi Mungu (swt) ila hutoa marudufu katika yasiyomridhisha Mwenyezi Mungu”.85 Imam Ja’far Sadiq (a) alisema: “Alikuja mtu kwa bwana Mtume (s) na kusema: ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, ni nani aliye bora wa watu kiimani? Mtume akamjibu: yule aliye mwepesi zaidi wa kutoa”.86 Pia alisema (a) kwamba Mtume (s) alisema: “Mtu mkarimu yu karibu na Mwenyezi Mungu (swt), karibu na watu, karibu na pepo. Na bakhili yu mbali na Mwenyezi Mungu (swt), mbali na watu, karibu na moto”.87 84. Al Waafy, juz. 6, uk. 68 85. Al Waafy, juz. 6, uk. 68 86. Al Waafy, juz. 6, uk. 67 87. Al Bihaar, muj. 15, juz. 3 60


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:20 PM

Page 61

Tabia njema kwa mujibu wa Ahlul Bayt (a.s)

MEMA YA UKARIMU Jamii haipati fanaka wala kuonja utamu wa utulivu na amani na kuwepo fikra ya utulivu na maisha mazuri ila kwa watu wa jamii hiyo kujawa na roho ya kuoneana huruma na upole na kukubaliana kwao kihisia katika furaha na shida. Ni kwa hilo ndipo jamii inajitokeza kuwa kama jengo liliyoshikamana barabara, mmoja akiwa ameungana na mwenzie. Hali ya kuoneana huruma na kushikamana inan’gara kwa uzuri na utukufu. Na hapana shaka kwamba kule matajiri kuwaonea huruma na kuwa wakarimu kwa wenye shida na maskini ni hali yenye kuzidia utukufu na yenye athari daima. Na kwa kufikia msingi huu wa kibinadamu mtukufu (kuoneana huruma na kushikamana), wenye shida na maskini huhisi hisia za upendo na moyo safi kwa wale waliowajali na kuwatendea wema; jambo ambalo huifanya jamii kuneemeka na kuenea ndani yake uelewano, mshikamano na maisha mazuri. Ama kwa kughafilika na jambo hilo, basi jamii hukosa raha na kutawaliwa na husda, chuki, bughdha, na hila. Matokeo yake ni mlipuko wa mapinduzi wenye maangamizi; kupoteza nafsi, uharibifu wa mali na kupoteza heshima. Kwa ajili ya hilo, Sheria ya kiislamu imehimiza ukarimu, kutoa na kuwa na huruma kwa wenye shida na maskini na ikakemea tendo la jamii kuwaona wakitapatapa kwa shida na kuwaacha bila ya kuwajali na kuwasaidia. Uislamu unawatazama wale matajiri wenye uwezo, lakini wakajizuia kusaidia, kuwa ndio wa mbali kabisa na Uislamu. Mtume (s) alisema. 61


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:20 PM

Page 62

Tabia njema kwa mujibu wa Ahlul Bayt (a.s) “Yeyote yule atakayeamka asubuhi na wala asijali mambo ya Waislamu, basi yeye si muislamu”.88 Pia alisema (s): “Hakuniamini mimi yule anayelala ameshiba na jirani yake ananjaa; na wala Mwenyezi Mungu (swt) hatowatizama siku ya kiama watu wa kijiji ambao kati yao analala mtu na njaa”.89 Hakika Uislamu umewahimiza wafuasi wake kuwa na ukarimu ili wawe ni mfano wa juu katika kuoneana huruma na pia waneemeke kwa maisha mazuri na amani. Ukarimu ndiyo kiwango cha usalama wa jamii na dhamana ya furaha na maendeleo yake.

MAENEO YA UKARIMU Fadhila za ukarimu zinatofautiana kwa kuzingatia ni katika maeneo gani na uwanja gani umefanywa. Fadhila ya juu sana ni kwa ukarimu ambao umefanywa kwa sababu ya kutekeleza amri ya Mwenyezi Mungu (swt) na Sheria yake kama vile zakat, khums na mfano wake. Na hiki ndicho kipimo cha ukarimu na utoaji katika matumizi ya Sheria ya kiislamu, kama alivyosema Mtume (s): “Anayetekeleza yale ambayo Mwenyezi Mungu (swt) amemfaradhishia huyo ndiye mwingi wa kutoa kuliko wote”.90 Na uthibitisho bora wa wema na utoaji baada ya hapo ni familia ya mtu na watu wa nyumba yake. Pamoja na kwamba ni lazima kuwahudumia kisheria na kimila, wao ndiyo awla kufanyiwa wema na uzuri na kustahiki kutazamwa na kuonewa huruma kuliko yeyote. 88. Al Kaafy 89. Al Kaafy 90. Al Waafy, juz. 6, uk. 67 62


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:20 PM

Page 63

Tabia njema kwa mujibu wa Ahlul Bayt (a.s) Wako baadhi ya watu ambao wametoka katika mkondo huu wa kimaumbile halisi. Wao hutoa kwa wingi na ukarimu mapato yao kwa watu wa mbali na wageni kwa lengo la kupata umaarufu na kujigamba. Wakati huo huo huwafanyia ahli, na jamaa zao ubahili, wakaishi katika taabu na dhiki wakati hao ni watu wao wa karibu. Huo ni katika ubaya wa nafsi na kuwa na uelewa mbovu. Kwa sababu hiyo, Ahlul Bait (a) wameusia kuwa na huruma na ahli na kuwapa starehe kutegemeana na mahitaji ya maisha. Imam Ridha (a) alisema: “Inatakiwa mtu astareheshe familia yake ili wasije wakatamani kifo chake”.91 Naye Imam Musa (a) alisema: “Hakika familia ya mtu ni wafungwa wake, basi atakaeneemeshwa na Mwenyezi Mungu (swt), awafanyie wasaa wafungwa wake. Ikiwa hatofanya hivyo basi kuna hatari kwamba neema hiyo itaondoka ”.92 Baada ya hapo anayestahiki kufanyiwa wema ni ndugu wa damu kwa sababu ya uhusiano wa kizazi na kusaidiana katika shida na matatizo. Ni katika makosa makubwa, kuwanyima hisia hizo (za upendo) na kuwapa wa mbali na wageni. Kitendo hicho kinatazamwa kuwa ni dharau ya wazi na huchochea hasira yao na kujitenga. Hivi ndivyo inavyofaa kwa mtu karimu, kumtanguliza wa karibu zaidi aliye bora katika wanaostahiki uhusiano na kupewa; kama vile marafiki, majirani na wenye ubora na islahi.

91. Al Waafy, juz. 6, uk. 61 92. Al Waafy, juz. 6, uk. 61 63


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:20 PM

Page 64

Tabia njema kwa mujibu wa Ahlul Bayt (a.s)

SABABU ZA UKARIMU Sababu za ukarimu zinatofautiana. Sababu ya juu kuliko zote na yenye mwisho wa kuhimidiwa ni ile inayokuwa katika njia ya Mwenyezi Mungu (swt) na kutarajia radhi Yake pekee na kupata malipo Yake. Msukumo unaweza ukatokana na kutamani sifa na kupata fahari. Pia inaweza ikawa sababu ni kupata faida fulani inayotarajiwa au woga kutokana na madhara yanayoogopwa. Mapenzi, yanachangia sana kwa kumsukuma mtu kutoa ili kumvuta mpenzi wake. Ni vyema kutaja kwamba, ukarimu haupendezi wala matunda yake kuwa matamu ila ikiwa mtoaji atajiepusha na masimango, ucheleweshwaji na pia kuukuza na kutajwa. Imam Sadiq (a) alisema: “Nimeona wema haufai ila kwa mambo matatu: kuuona mdogo, kuusitiri, na kuuharakisha. Ikiwa utauona mdogo, utaufanya mkubwa kwa yule anayeupokea; na ikiwa utausitiri, utakuwa umeukamilisha; na ikiwa utauharakisha, huleta raha. Ikiwa kinyume na hivyo utakuwa umeuharibu".93

10. KUFIKIRIA WENGINE KULIKO MWENYEWE MAANA YAKE: Ni daraja ya juu ya ukarimu, na hawajipambi na sifa hiyo adimu ila watu ambao wamejipamba na ukarimu, na wakafikia kilele chake, wakatoa bila 93. Al Bihaar, muj. 16, uk. 116 64


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:20 PM

Page 65

Tabia njema kwa mujibu wa Ahlul Bayt (a.s) uchoyo na huku wanahitajia, wakatoa na huku wamo katika taabu ya maisha.

QURANI Qurani imesifia ubora wao kwa kusema:

“ …Bali wanawapendelea kuliko nafsi zao, ingawa wao wenyewe ni wahitaji.” (al-Hashr, 59:9)

HADITHI Imam Ja’far aliulizwa: Ni sadaqa ipi iliyo bora? Akajibu: “Ni ile ya yule mwenye kichache, je hukusikia Mwenyezi Mungu (swt) alivyosema: “Na wanawapendelea kuliko nafsi zao, ingawa wao wenyewe ni wahitaji.”94 Na Mtume (s) alikuwa mfano wa juu kabisa katika kupendelea wengine. Jabir bin Abdulah (r) alisema: “Hakuombwa Mtume (s) kitu, kisha akasema hapana.” Imam Sadiq (a) alisema: “Mtume (s) alifika al Ji’rana, na akagawa mali. Wakawa watu wanamuomba na huku anawapa, mpaka wakamsukuma penye mti, ukachukua burda yake na kumkwaruza mgongo wake. Wakamwondoa pale na huku wanamuomba. Mtume (s) akasema: ‘Enyi watu nirudishieni burda yangu, wallahi lau kama ningekuwa na neema kwa idadi ya miti ya Tuhama ningekugawieni kisha msingenikuta muoga wala bakhili…’”95

94. Al Waafy, juz. 6, uk. 57 95. Safinatul Bihaar, juz. 1, uk. 607 65


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:20 PM

Page 66

Tabia njema kwa mujibu wa Ahlul Bayt (a.s) Alikuwa bwana Mtume (s) akipendelea wenye shida na maskini kuliko nafsi yake; akiwakirimu mali yake na chakula chake na kubaki na njaa, na wakati mwingine hufunga jiwe la njaa tumboni, ili kuwaliwaza. Imam Baqir (a) alisema: “Mtume hakushiba kwa kula mkate wa ngano siku tatu mfululizo toka Mwenyezi Mungu (swt) alipomtuma hadi alipomchukua”. 96 Na hivi ndivyo walivyokuwa Ahlul Bayt (s) wake katika ukarimu wao na kupendelea wengine: Imam Sadiq (a) alisema: “Ali (a) alimshabihi Mtume zaidi kuliko yeyote yule, alikuwa anakula mkate na mafuta na huku anawalisha watu mkate na nyama”.97 Ni kuhusu Imam Ali (a) na Ahlul Bayt ndiyo ayah hizi za Suratud-Dahr ziliteremka: “Na huwalisha chakula masikini na yatima na mfungwa hali ya kuwa wanakipenda. Tunakulisheni kwa ajili ya radhi ya Mwenyezi Mungu tu, hatutaki kwenu malipo wala shukurani.” (Suratud-Dahr, 76: 8-9). Wafuasi wa Ahlul Bayt (a) wamekubaliana ya kwamba ayah hii imeteremka inawahusu Ali, Fatimah, Hasan na Husayn.(a). Pia wanazuoni wakubwa (wasio mashia) wameipokea kama vile az-Zamakhshari alivyoitaja katika tafsiri yake ya al-Kashshaaf, alisema: “Imepokewa kutoka kwa Ibn Abbas ya kwamba Hasan na Husayn (a) waliuguwa na Mtume (s) akawazuru akiwa pamoja na watu, wakasema: ‘Ewe Abul-Hasan lau kama ungeweka nadhiri kwa ajili ya wanao.’ Imam Ali (a) akaweka nadhiri pamoja na Fatimah (a) na mtumishi wao Fiza, ya kwamba ikiwa watapona basi watafunga siku tatu. Walipopona, nyumbani hapakuwa na chochote. Imam Ali (a) akamkopa Sham’un yahudi wa Khaybar vibaba vitatu vya shairi. Bibi 96. Safinatul Bihaar, juz. 1, uk. 194 97. Al Bihaar, muj. 9, uk. 538 66


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:20 PM

Page 67

Tabia njema kwa mujibu wa Ahlul Bayt (a.s) Fatima akasaga kibaba kimoja na kutengeneza mikate mitano kwa idadi yao. Walipoiweka mbele yao ili wafuturu, akaja maskini anaomba kwa kusema: ‘Assalamu alaykum watu wa nyumba ya Muhammad, mimi ni maskini miongoni mwa maskini wa kiislamu, nipeni chakula Mwenyezi Mungu atakulisheni chakula cha peponi,’ wakajinyima na kumpa huyo maskini, wakalala na njaa wamefuturu maji peke yake. Wakafunga siku ya pili na ilipokuwa jioni akatokea yatima na kuomba, wakajinyima na kumpa yatima, na siku ya tatu akaja mfungwa na kuomba, nao wakafanya hivyohivyo. Walipoamka, Imam Ali (a) akawashika mkono Hasan na Husayn (a) na kwenda kwa Mtume (s). Mtume alipowaona wakitetemeka kama vifaranga kwa sababu ya njaa kali, akasema: “Haya ninayoyaona kwenu ni vibaya vilivyoje yanavyoniumiza!” Akasimama na kuondoka pamoja nao na akamwona Fatima (a) katika mihrab yake na huku tumbo lake limeshikana na mgongo, macho yake yametoka. Hali hiyo ikamuuma Mtume (s), hapo Jibril akateremka na kusema: “Ichukue (surah Dahr) ewe Muhammad, Mwenyezi Mungu amekusifu kuhusu watu wa nyumba yako (Ahlul Bayt).” Akamsomea sura hiyo. Vitabu vya sira vimejaa habari zao kuhusu kujinyima na kupendelea wengine. Nafasi ya kitabu hiki ni ndogo kuweza kuyanukuu.

11. UBAHILI MAANA YAKE: Kukataa kutoa katika yale ambayo ni vyema kufanya ukarimu. Kinyume cha ubahili ni ukarimu. Ubahili ni miongoni mwa tabia mbaya na sifa duni ambayo humsababishia mwenye tabia hiyo kudharauliwa, kuchukiwa na kuonekana duni. Uislamu 67


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:20 PM

Page 68

Tabia njema kwa mujibu wa Ahlul Bayt (a.s) umewatahadharisha Waislamu na tabia hiyo kwa tahadhari kubwa.

QUR’ANI Mwenyezi Mungu anasema:

“Lo! nyinyi ndio mnaitwa ili mtoe (mali) katika njia ya Mwenyezi Mungu, lakini wengine wenu wanafanya ubahili na afanyaye ubahili basi hakika anafanya ubahili kwa (kuidhuru) nafsi yake. Na Mwenyezi Mungu ni Mkwasi nanyi mafakiri, na kama mkirudi nyuma basi Mwenyezi Mungu ataleta watu wengine badala yenu, nao hawatakuwa mfano wenu.” (Surah Muhammad; 47:38)

“Ambao hufanya ubakhili na huwaamuru watu kufanya ubakhili na kuyaficha aliyowapa Mwenyeezi Mungu katika fadhila zake, na tumewaandalia makafiri adhabu yenye kudhalilisha.” (Surah Nisaa; 4:37)

“Wala wasidhani wale wanaofanya ubahili katika fadhila zake kuwa 68


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:20 PM

Page 69

Tabia njema kwa mujibu wa Ahlul Bayt (a.s) ni bora kwao, bali ni vibaya kwao, watafungwa kongwa za yale waliyofanyia ubahili siku ya Kiyama. Na urithi wa mbingu na ardhi ni wa Mwenyezi Mungu, Naye ni Mjuzi wa mnayoyafanya.” (Surah Aali Imraan; 3:180).

HADITHI Imam Ali (a) alisema: “Namstaajabia bahili, anauharakisha umaskini ambao aliukimbia, na utajiri alioutafuta unamponyoka, kwa hivyo duniani anaishi maisha ya ufukara na kesho akhera atahesabiwa hisabu ya matajiri”. Imam Ja’far Sadiq (a) kama alivyopokea kutoka kwa mababa zake alisema: “Imam Ali (a) alimsikia mtu akisema: bahili ni haini zaidi kuliko dhalimu. Hapo akasema: umenena uongo (hujapatia ukweli uovu wa mtu bahili), kwani dhalimu huenda akatubia, akaomba maghfira na kurejesha alichodhulumu kwa wenyewe, ama mtu bahili anapofanya ubahili hunyima zaka, sadaka, ndugu wa damu, ukarimu kwa mgeni na kutoa katika njia ya Mwenyezi Mungu (swt) na njia za kheri. Na haramu kwa mtu bahili kuingia peponi”. “Mtume alisema: mtu karimu yupo karibu na Mwenyezi Mungu (swt), karibu na watu, karibu na Pepo, ama bahili yupo mbali na Mwenyezi Mungu (swt), mbali na watu, karibu na Moto”.

MAOVU YA UBAKHILI Ubakhili ni hulka duni na tabia mbaya inayomsukuma mtu kwenye maovu mengi na hatari kubwa katika dunia na akhera. Ama hatari yake akhera: Hadithi za Ahlul Bayt (a) zimeelezea hatari 69


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:20 PM

Page 70

Tabia njema kwa mujibu wa Ahlul Bayt (a.s) hiyo na hususan kauli ya Imam Ali (a) aliposema: “Bahili hukataa kutoa zaka, sadaka, kuunga undugu, ukarimu kwa mgeni, kutoa katika njia ya Mwenyezi Mungu (swt), na milango ya kheri. Na ni haramu kwa bahili kuingia peponi�. Ama hatari yake duniani: Humfanya mtu achukiwe na adharauliwe na wakaribu yake sawia na wambali. Hutokea hata wa karibu yake na wapenzi kwake zaidi kutamani kifo chake ili wapate urithi. Juu ya yote hayo, bahili ni mwenye taabu zaidi na kukosa furaha kwa sababu huhangaika kukusanya mali na wala hapati raha kwayo. Punde mara amekufa na kuiacha mali kwa warithi wake. Kwa hiyo anaishi duniani maisha ya kifakiri na kesho akhera huhesabiwa hisabu ya matajiri.

SURA ZA UBAHILI Ubakhili una sura tofauti, na sura mbaya zaidi ni kufanya ubahili juu ya faradhi za kimali alizozifaradhisha Mwenyezi Mungu (swt) juu ya Waislamu kama nidhamu ya kiuchumi inayohuisha walio wanyonge. Pia tukitizama watu na hali zao, ubahili wa tajiri ni mbaya kuliko ule wa fakiri. Na pia ubahili juu ya familia, ndugu wa karibu, marafiki au wageni ni mbaya zaidi kuliko juu ya wengine. Na kujinyima na kujidhiki katika mambo ya dharura ya maisha kama vile chakula, nguo ilhali mtu ana hali nzuri ya maisha ni miongoni mwa sura mbaya zaidi za ubahili.

TIBA YA UBAHILI Kwa kuwa ubahili ni tabia duni na hulka yenye kuchukiza, ni muhimu kwa mwenye akili kupigana nayo na kutafuta tiba yake. Hizi hapa ni baadhi ya nasaha na maelekezo ili kuepuka tabia hiyo: 1. Kuzingatia mema ya ukarimu kama tulivyoelezea na pia maovu ya ubahili. Hilo bila shaka litapunguza ubahili. Na ikiwa hilo halikufaa, 70


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:20 PM

Page 71

Tabia njema kwa mujibu wa Ahlul Bayt (a.s) basi bahili adanganye nafsi yake kwa kuivutia kutoa kwa kutaka sifa na kufahamika. Atakapoona nafsi yake imetulia katika hali hiyo, basi aiadabishe kuwa na ikhlas na kutoa katika njia ya Mwenyezi Mungu (swt). 2. Ubahili una sababu na hivyo tiba yake inategemea sababu hizo, na ni kwa kuondoa sababu ndipo athari hutoweka. Sababu kubwa ya ubahili ni hofu ya ufakiri, na bila shaka hofu hii ni katika uvuvio wa Shetani. Qur’ani imetatua suala hilo kwa hekima ya juu sana na kukariri ya kwamba kufanya uchoyo hakumsaidii chochote bahili, bali humrejelea na kumfilisi. Mwenyezi Mungu (swt) anasema:

“Lo! nyinyi ndio mnaitwa ili mtoe (mali) katika njia ya Mwenyezi Mungu, lakini wengine wenu wanafanya ubahili na afanyaye ubahili basi hakika anafanya ubahili kwa (kuidhuru) nafsi yake. Na Mwenyezi Mungu ni Mkwasi nanyi mafakiri, na kama mkirudi nyuma basi Mwenyezi Mungu ataleta watu wengine badala yenu, nao hawatakuwa mfano wenu.” (Surah Muhammad; 47:38) Pia ikakariri ya kwamba kile anachokitoa mtu kwa ukarimu, kamwe hakipotei bure bali kinamrejelea mtoaji baadae kutoka kwa Yeye Mkarimu na Mtoaji riziki. Mwenyezi Mungu (swt) anasema:

71


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:20 PM

Page 72

Tabia njema kwa mujibu wa Ahlul Bayt (a.s)

“Sema: kwa hakika Mola wangu humkumnjulia riziki amtakaye katika waja wake, na humdhikisha amtakaye. Na chochote mtakachotoa, basi yeye atakilipa, Naye ni mbora wa wanaoruzuku.” (Surah Sabaa; 34:39) Hivyo ndivyo Qur’an ilivyohamasisha maradufu kuhusu ukarimu ikisisitiza ya kwamba mtoaji katika njia ya Mwenyezi Mungu (swt) ni kama anamkopesha Mwenyezi Mungu (swt) na kwamba Yeye Mwenyezi Mungu (swt) kwa ukarimu wake mpana atamlipa maradufu. Anasema (swt):

“Mfano wa wale wanaotoa mali zao katika njia ya Mwenyeezi Mungu, ni kama mfano wa punje moja itoayo mashuke saba, katika kila shuke punje mia. Na Mwenyeezi Mungu humzidishia amtakaye na Mwenyeezi Mungu ni Mwenye wasaa, Mwenye kujua.” (Suratul Baqarah; 2:261) Ama wale ambao ni watumwa wa ubahili, basi Qur’ani imewahofisha kwa tishio kubwa linalotikisa nafsi:

72


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:20 PM

Page 73

Tabia njema kwa mujibu wa Ahlul Bayt (a.s)

“Enyi mlioamini! hakika wengi katika makasisi na watawa wanakula mali ya watu kwa batili na kuwazuilia (watu) njia ya Mwenyezi Mungu. Na wale wakusanyao dhahabu na fedha wala hawazitoi katika njia ya Mwenyezi Mungu, basi wape habari ya adhabu iumizayo.” (Suratut-Tawbah; 9:34-35). Na katika sababu za ubahili ni wazazi kutilia maanani mustakbali wa watoto wao baada yao, kwa hiyo wanaibania mali ili iwe hazina kwa watoto wao na kuwalinda na ufukara. Na hii ni hulka ya kimaumbile yenye mizizi ndani ya mwanadamu ambayo haimzuru ikiwa itabaki katika mizani bila kupetuka mipaka. Qur’ani imetahadharisha wazazi na msukumo wa hulka hiyo ili wasije wakavutwa na mapenzi ya watoto wao na wakafanya ili kuwaridhisha yasiyokubaliwa na dini wala akili:

“Enyi mliamini! Mkimcha Mwenyezi Mungu atawapeni kipambanuzi na atawafutieni makosa yenu na kuwasameheni, na Mwenyeezi Mungu ni Mwenye fadhila kubwa.” (Suratul Anfaal:29) 73


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:20 PM

Page 74

Tabia njema kwa mujibu wa Ahlul Bayt (a.s) Ni makubwa yaliyoje haya aliyoyasema Imam Ali (a) katika barua yake: “Uliokuwa nayo mikononi mwako ya dunia yalikuwa na wenyewe kabla yako na yatakwenda kwa wengine baada yako. Bila shaka wewe ni mwenye kuwakusanyia watu wawili: mtu ambae atatumika katika yale ulioyachuma kwa kumtii Mwenyezi Mungu (swt), kwa hivyo akaneemeka kwa yale yaliyokusumbua, na mwingine ni yule atakayetumika kwa kumuasi Mwenyezi Mungu (swt) na hivyo kusumbuka kwa yale uliyomkusanyia. Na kwa hakika hakuna miongoni mwa hawa wawili yeyote anastahili wewe umpendelee juu ya nafsi yako, na umbebe juu ya mgongo wako. Nataraji rehema ya Mwenyezi Mungu (swt) kwa waliokwishaondoka, na riziki yake kwa waliobakia.”98 Kuhusu kauli yake Mweyezi Mungu (swt): “...Hivyo ndivyo Mwenyezi Mungu atakavyowaonyesha vitendo vyao kuwa majuto juu yao...” (Suratul Baqarah, 2:167). Imam Husayn (a) alisema: “Huyu ni mtu anaacha mali yake na asiitumiye katika njia ya Mwenyezi Mungu (swt) kwa sababu ya ubahili, kisha anakufa na kuimwachia yule atakayeitumia katika kumtii Mwenyezi Mungu (swt) au kumuasi. Ama ikiwa ataitumia (aliyeachiwa) kumtii Mwenyezi Mungu (swt), huyu mwenye mali ataiona katika mizani isiyoyake na hivyo kuiona ni hasara kwa kuwa mali ilikuwa ni yake. Ama ikiwa ataitumia (aliyeachiwa) katika maasi, ni yeye (mwenye mali) ndiye atakayekuwa amemuwezesha kwa mali hiyo mpaka akamuasi Mwenyezi Mungu (swt).”99 Wapo watu ambao wanaashiki mali kidhati na kupindukia katika kuipenda pasina kuichukuwa kuwa ni njia ya fanaka ya dini na dunia, bali waona raha tu kuilimbikiza. Kwa sababu hiyo wanaifanyia ubahili kweli kweli. Ashiki hii ya mali bila shaka huwadhiki wenyewe na kuwatokomeza katika maangamio. Mali siyo lengo, bali ni njia ya kufikia malengo ya maisha 98. Nahjul Balagha 99. Al Waafy, juz. 6, uk. 69 74


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:20 PM

Page 75

Tabia njema kwa mujibu wa Ahlul Bayt (a.s) haya au ya akhera. Malengo hayo yakikosekana, basi mali inakuwa ni duni isiyo na faida. Ni vipi mtu akusanye mali na kuilimbikiza?! Akifumba tu macho, mrithi anajichukulia na kuneemeka nayo. Mrithi anajipatia vya dezo wakati mrithiwa anaambulia taabu na kubeba mzigo. Qur’ani imekemea ashki hii ya mali na kuwaonya wenye tabia hiyo kwa indhari kali sana:

“Sivyo bali nyinyi hamuheshimu yatima. Wala nyinyi hamhimizi juu ya kulisha masikini. Na mnakula urithi kwa ulaji wapupa. Na mnapenda mali kwa pendo la kupita kiasi. Sivyo itakapovunjika ardhi vipande vipande. Na akaja Mola wako (amri ya Mola wako), na Malaika safu safu. Na siku hiyo italetwa jahannam, siku hiyo mwanadamu atakumbuka, lakini kutamfaa nini kukumbuka? Atasema: Laiti ningelitanguliza (wema) kwa ajili ya uhai wangu! Basi siku hiyo hataadhibu yeyote namna ya kuadhibu kwake. Wala hatafunga yeyote jinsi ya kufunga kwake.” (Suratul Fajr, 89:17-26) 75


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:20 PM

Page 76

Tabia njema kwa mujibu wa Ahlul Bayt (a.s) Pia akaonya katika

“Ole wake kila safihi, msengenyaji. Ambaye amekusanya mali na kuihesabu. Anadhani kuwa mali yake yatambakisha milele. Sivyo, Lazima atatupwa katika Hutama! Na nini kitakujulisha ni nini Hutama. Ni Moto wa Mwenyezi Mungu uliwashwa. Ambao unapanda nyoyoni. Hakika huo (Moto) utafungwa juu yao. Ndani ya nguzo ndefu ndefu.” (Suratul Humaza 104:1-9) Katika uwanja huu yanakwea kileleni maneno ya hekima ya Imam Ali (a) yasemayo: “Hakika dunia ni inayotoweka (fanaa), ni taabu (anaa), ni kupanda na kushuka (ghiyar), ni mazingatio (ibar). Kuhusu kutoweka, unatazama jinsi wakati unavyovuta upinde na kuachia mishale isiyokosea lengo na ambayo majeraha yake hayaponi. Unamdunga ugonjwa asiye na ugonjwa na mauti aliye hai. Kuhusu taabu, ni kwamba mtu anakusanya ambavyo hatakula, anajenga ambapo hatakaa, kisha anaondoka kurejea kwa Mola wake akiwa hana mali wala nyumba, Kuhusu kupanda na kushuka, bila shaka utamuona aliyeneemeka mara amekuwa mwenye kuhurumiwa, na mwenye kuhurumiwa mara ni mwenye kuneemeka, na hakuna baina yao ila ni neema iliyoondoka na balaa iliy76


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:20 PM

Page 77

Tabia njema kwa mujibu wa Ahlul Bayt (a.s) oteremka. Kuhusu mazingatio, ni kwamba mtu anafuatilia matarajio yake na huku inamnasa ajali yake, kwa hiyo hapati matarajio yake na wala habakishi alichokitarajia.” 100

12. UMILIKI WA NAFSI (IFFAT) MAANA Ni kujizuia na kujiepusha na yale yasiyohalali wala yasiyopendeza katika matamanio ya tumbo na kijinsia na kujikomboa na utumwa wa matamanio hayo yanayodhili. Ni miongoni mwa tabia bora inayoashiria upevu wa imani na utukufu wa nafsi na daraja ya juu ya utukufu.

HADITHI Mtume (s) alisema: “Wengi wa umma wangu wataingia motoni kwa sababu ya viwili: tumbo na utupu”101 Imam Baqir (a): “Hakuna ibada bora kwa Mwenyezi Mungu kama kumiliki tumbo na tupu”.102 Mtu mmoja alimuambia Imam Baqir (a): mimi ni dhaifu wa matendo, mchache wa sala na saumu, lakini nataraji kwamba nisile ila halali, wala kuoa ila halali. Imam akamuambia: “Kwani ni jihadi gani iliyo bora kuliko kumiliki tumbo na utupu?”103 100. Safinatul Bihaar, juz. 1, uk. 467 101. Al Bihaar, muj. 15, juz. 2, uk. 183 102. Al Waafy, juz. 3, uk. 65 103. Al Bihaar, muj. 15, juz. 2, uk. 184 77


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:20 PM

Page 78

Tabia njema kwa mujibu wa Ahlul Bayt (a.s)

UHAKIKA WA UMILIKI NAFSI Muradi wa umiliki nafsi si kuinyima nafsi inayoyatamani na kuyahitaji, yaliyo ya kisheria katika vyakula na jimai, bali lengo ni kubaki katika mizani na kiwango cha katikati, na hii ni kwa sababu kila ziada na kasoro ni yenye madhara kwa mwanadamu na sababu ya shida na kukosa fanaka. Ama ziada katika matamanio ya tumbo na jimai, humsukuma mtu katika maangamio makubwa na madhara hatari ambayo tutayazungumzia katika mlango wa (uroho). Ama kasoro, pia ina madhara, mtu hukosa kufaidi maisha na mazuri yake yanayokubalika kisheria na hivyo mwili kudhoofu na kukosa nishati kimwili na kiroho.

KIWANGO CHA KATI KINACHOTAKIWA Ni vigumu kuainisha kiwango cha kati kuhusu haja ya kimaumbile ya kula na kujimai. Sababu ni kwamba watu wanatofautiana kihaja na kiuwezo. Katika kula, kiwango kilicho sawa, ni mtu apate kile kiasi cha kumaliza haja yake ya chakula kwa kujilinda na uroho na kujaza tumbo. Na kiwango bora ni kile alichokiainisha Imam Ali (a) pindi akimuusia mwanae Imam Hasan (a) kwa kusema: “Ewe mwanagu mpenzi, je hutaki nikufundishe mambo manne yatakayokutosheleza na usihitajie tiba? Akamwambia: usikae kula chakula ila ikiwa unahisi njaa, usisimame kwa kumaliza kula ila ukiwa unahisi bado unakitamani, utafune vizuri, na utakapokwenda kulala, kwanza nenda haja. Ukifuata haya hutahitaji tiba”. Pia akasema (a): ndani ya Qur’ani kuna aya ambayo imekusanya tiba yote, nayo ni:

78


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:20 PM

Page 79

Tabia njema kwa mujibu wa Ahlul Bayt (a.s)

“Enyi wanadamu! (Waislamu) chukueni, pambo lenu kila mahala wakati wa ibada na kuleni (vizuri) na kunyweni (vizuri) wala msipite kiasi, hakika yeye hawapendi wapitao kiasi.” (Suratul A’raaf;7:31) Katika kujimai, kiwango sahihi, ni kuitikia mwito wa kimaumbile. Kukidhi haja sahihi (kuhisi anahitaji kufanya tendo lenyewe).

MAZURI YA UMILIKI NAFSI Hakuna shaka kwamba umiliki nafsi ni miongoni mwa tabia njema inayodhihirisha upevu wa imani na utukufu wa nafsi na kufungua njia ya maisha mazuri kwa jamii na mtu binafsi. Ni sifa njema ambayo humpamba mtu na kumweka mbali na madhila ya uroho na kumlinda na kujipendekeza kwa waovu ili kupata baraka zao na hivyo kumsukuma kutafuta njia za maisha na mahitaji yake kwa njia za kisheria.

13. UROHO, TAMAA, ULAFI (SHARAH) MAANA Kupindukia mipaka katika tamaa ya kula na ya kujamiiana. Kinyume chake ni umiliki nafsi. Ni katika hulka duni inayoashiria udhaifu wa nafsi, utumwa wa kitabia.

79


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:20 PM

Page 80

Tabia njema kwa mujibu wa Ahlul Bayt (a.s)

HADITHI Imam Sadiq (a) alisema: “Kila ugonjwa unatokana na kula zaidi kasoro homa, hutokeza kwa sababu zake”.104 Pia alisema (a): “Tumbo likishiba basi linachupa mipaka”.105 Pia alisema (a): “Hakika Mwenyezi Mungu (swt) anachukia kula sana”.106 Abul Hasan (a) alisema: “Lau kama watu wangekula kwa kiwango, basi miili yao ingekuwa na siha njema”.107 Imam Sadiq (a) kutoka kwa baba yake alisema: Amiri wa waumini alisema: “Anayetaka kubaki (yaani kuwa na umri mrefu) - na hakuna kubaki, basi vazi lake liwe nyepesi (yaani kuwa na mzigo mdogo wa madeni), ale mapema chakula, na apunguze kujamiiana na wanawake”.108 Na imam Ali (a) alikula tende za Daqal kisha akanywa maji na kupiga juu ya tumbo lake na kusema: yule ambaye tumbo lake litamuingiza motoni, Mwenyezi Mungu amuweke mbali. Kisha akasema methali: Hakika wewe pindi utakavyolipa tumbo lako mahitaji yake na sawia tupu yako (vitaambulia) kupata mwisho wa ubaya wote. 109

104. Al Waafy, juz. 11, uk. 67 105. Al Waafy, juz. 11, uk. 67 106. Rejea hapo juu 107. Al Bihaar, muj. 14, uk. 876 108. Rejea hapo juu, uk. 545 109. Safinatul Bihaar, muj. 1, uk. 27 80


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:20 PM

Page 81

Tabia njema kwa mujibu wa Ahlul Bayt (a.s)

MAOVU YA UROHO Uroho ni ufunguo wa matamanio, chanzo cha maangamio. Na yatosha ubaya kwa vile matamanio humfanya mtu kuwa mtumwa, na kumburuza katika maovu ya kiroho na kimwili. Na huenda sababu kuu ya umma kuzorota kimaendeleo, ni kutawaliwa na uroho na kuhadaiwa na mapambo ya dunia, vivutio vya anasa, mambo ambayo yanawapelekea udhaifu na kuporomoka. Uroho wa kula una madhara mengi: Matabibu wamethibitisha ya kwamba mengi ya maradhi, mistari na mikunjo inayoharibu sehemu laini za mwili kwa wanawake na wanaume, kulundikana kwa mafuta, macho yaliyozama, kukosa nguvu, na nafsi gonjwa, yote hayo yananasibishwa na ulafi na chakula chenye mafuta mengi. Pia imethibitika kwamba ulafi huchosha tumbo (fuko la chakula) na kusababisha aina ya matatizo ya kiafya kama vile mishipa ya damu kuwa migumu, angina (maradhi ya moyo yanayosababisha maumivu kifuani), shinikizo la damu (presha), kupoteza nguvu za fahamu, na kuishiwa uchangamfu na nishati.

TIBA YA UROHO Ulafi wa kula tiba yake ni: 1. Mroho ajikumbushe mazuri yaliyoelezwa kuhusu umilikinafsi na fadhila zake. 2. Atafakari mabaya ya uroho na maafa yake 3. Aiadabishe nafsi yake kuzingatia kiwango katika chakula na kujiepusha na ulafi mpaka hapo utakapotoweka. Hakika sheria za tiba ya kinga na ya kuponya ni kula kwa kiwango na kutofanya israfu kama ilivyoelezea kwa 81


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:20 PM

Page 82

Tabia njema kwa mujibu wa Ahlul Bayt (a.s) muhtasari aya ifwatayo: “Mle na mnywe na wala msifanye israfu” (Suratul A’raaf, 7:31) Ama uroho wa kujamiiana (utupu), tiba yake ni: 1. Mtu akumbuke madhara ya israfu ya kujamiana na maovu yake kimwili na kiroho. 2. Apigane na vichochezi (vinavyochochea tamaa ya kimaumbile) kama vile kutizama uzuri wa kike, kuchanganyika wanawake na wanaume, kuiacha fikra inaogelea katika njozi na ndoto za mchana na mengine kama hayo. 3. Ajiadabishe kudhibiti tamaa ya kimaumbile na kuizuiya kuchupa mipaka.

14. UAMINIFU NA HIANA MAANA Uaminifu: Mtu kutekeleza zile haki alizokabidhiwa (alizopewa kuhifadhi). Ni tabia njema na tukufu inayomfanya mtu kutegemewa na kuvutia na hivyo kupata mafanikio na kufuzu. Hiana: Kinyume cha uaminifu. Ni kukana haki na kuzichukua kwa jeuri. Ni miongoni mwa sifa duni inayopelekea mtu kupoteza utukufu na hivyo kufeli na kuharibikiwa.

QUR’ANI Mwenyezi Mungu (swt) amewasifu wenye tabia hii adhimu, na kuhimiza kujipamba kwayo na kujiepusha na hiana. Anasema:

82


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:20 PM

Page 83

Tabia njema kwa mujibu wa Ahlul Bayt (a.s)

“Na ambao kwa amana zao na ahadi zao ni wenye kuzitekeleza” (Suratul Mu’minun;23: 8)

“Enyi mlioamini msimfanyie khiyana Mwenyezi Mungu na Mtume na msikhini amana zenu na hali mnajua.” (Suratul Anfaal; 8 : 27)

“Hakika Mwenyeezi Mungu anawaamuruni kuwatekelezea amana zao wenyewe, na mtakapohukumu baina ya watu mhukumu kwa uadilifu. Hakika Mwenyeezi Mungu ni mwenye kusikia Mwenye kuona.” (Suratul Nisaa; 4 : 58)

HADITHI Mtume (s) alisema: “Kutekeleza amana huleta (huvuta) riziki na hiana huleta umaskini”110 “Hautaacha umma wangu kuwa kwenye kheri madama hawatafanyiana hiana, wakatekeleza amana, na wakatoa zaka. Pindi hawatafanya hayo, wataonjwa kwa ukame.” 111 “Siyo mfuasi wetu anayehalifu amana”112 110. Al Waafy, juz. 10, uk. 112 111. 112. Thawabul A'mal, Swadduq 83


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:20 PM

Page 84

Tabia njema kwa mujibu wa Ahlul Bayt (a.s) Imam Sadiq (a) alisema: “Msighurike na sala zao wala funga zao, hakika mtu huenda akashikamana na sala na saumu kiasi lau kama angeviacha angehisi upweke na kusononeka, kwa hivyo muwajaribu watu kwa kusema kweli na kutekeleza amana”113 “Mcheni Mwenyezi Mungu (swt), na tekelezeni amana zenu kwa waliokukabidhini, lau kama muuwaji wa Imam Ali (s) atanikabidhi amana basi nitairejesha kwake”.114

MEMA YA UAMINIFU NA MAOVU YA HIANA Uaminifu una dhima kubwa katika maisha ya kaumu na watu. Uaminifu ni nidhamu ya kazi zao na msingi wa mambo yao na anwani ya utukufu na msimamo wao, na njia ya maendeleo yao kimada na kiroho. Ni wazi kwamba anayejipamba kwa uaminifu hujenga kuthaminika na mvuto na kupata imani ya watu na hivyo kuwa mshirika wao katika mali zao na wanayoyachuma. Hilo linathibiti kwa kaumu zote, maisha yao hayapandi juu na kuchanua ila kwa kuwepo mazingira ya uaminifu. Ni kwa uaminifu ndiyo waarabu walimiliki usukani wa uchumi, viwanda na biashara na kuchuma faida kubwa lakini Waislamu ole wao! Walichagua hiyana na kuanguka. Walijifanya kupuuza uaminifu wakati ndiyo anuani ya misingi yao na alama ya utukufu wao.

113. Al Waafy, juz. 3, uk. 82 114. Al Waafy, juz. 10, uk. 112 84


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:20 PM

Page 85

Tabia njema kwa mujibu wa Ahlul Bayt (a.s) Kwa ajili hiyo hiana ni miongoni mwa sababu muhimu za kuanguka mtu katika nyanja za maisha kama vile vile ilivyo ni kiungo muhimu katika kudhoofisha kuaminiana baina ya watu na kueneza kuchukiana na kuogopana, hali ambayo husababisha jamii kukosa mwangalizi, na hivyo kuvunjika mahusiano, kuharibika maslahi na kupukutika nguvu zake.

AINA ZA HIANA Kuna aina tofauti za hiana, ubaya wake unahitilafiana kwa kuzingatia athari zake. Mbaya zaidi ni ile hiana ya kielimu ambayo wanaifanya waovu ambao wanaochezea ukweli wa elimu takatifu na kuuharibu kwa kupachika (ya uongo) na kubadilisha. Aina nyingine ni kutoa siri za Waislamu ambazo ni lazima kuzihifadhi. Kwani kuzifichua kutawasabibishia madhara na hatari. Nyingine ni hiana ya amana aliyokuwekesha mtu. Kuinyang’anya ni jinai juu ya hiana, wizi na uporaji. Hiana ina aina nyingi nyingine mbaya zinazodhuru watu, binafsi na jamii, kimwili na kiroho, kama vile udanganyifu, kughushi, kupunja kwenye mizani na mifano ya hayo.

85


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:20 PM

Page 86

Tabia njema kwa mujibu wa Ahlul Bayt (a.s)

15. UNDUGU WA KIROHO Zama za kijahilia zilikuwa ni uwanja wa maafa na misiba katika nyanja mbalimbali, kifikra na kimada. Katika maafa yake mabaya ni mmomonyoko wa maadili na vurugu, mambo yaliowapelekea watu kuishi kama wanyama kwa kuwa na sheria za msituni, kukataana, kuchinjana, kuangamiza na kunyang’anya, kulipiza kisasi na kutesa. Ulipodhihiri Uislamu na kuangazia walimwengu, uliweza kwa misingi yake ya milele na katiba yake ya pekee kuponya maafa hayo na kung’oa yale majanga. Mahala popote la ujahilia Uislamu ukasimamisha “umma bora uliyoletwa kwa ajili ya watu” kiitikadi na kisheria, pia kielimu na kikatiba. Imani ikachukua nafasi ya ukafiri, nidhamu mahala pa vurugu, elimu mahala pa ujinga, amani mahala pa vita na huruma mahala pa kuadhibu. Mafahimu (dhana) ya kijahilia yakaporomoka na nafasi yake ikachukuliwa na misingi mipya ya kiislamu. Mtukufu Mtume (s) akaanza kujenga umma ulio mfano bora ambao umezidi umma nyingine kinidhamu, kitabia na ukamilifu. Na kila mara Waislamu walipokwenda moja kwa moja chini ya bendera ya Qur’ani na uongozi wa Mtume Mtukufu (s) wamepanda ngazi za ukamilifu na kukwea ndani ya peo za utukufu. Kwa hilo wakafanikisha kusimika msingi wa undugu kwa namna ambao sheria na mifumo mingine haikuweza kufanya. Pingu za kiimani zikawa ni zenye nguvu zaidi kuliko zile za kinasaba. Pia uhusiano wa kiimani ukapanda juu ya uhusiano wa kindugu na kikabila, wakawa Waislamu ni umma mmoja, safu zimeshikana, jengo lao limesimama madhubuti na bendera yao inapepea, kamwe sumu na visababishi vya mifarakano havina penyo la kuwabomoa. 86


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:20 PM

Page 87

Tabia njema kwa mujibu wa Ahlul Bayt (a.s)

QUR’AN Mwenyezi Mungu anasema:

“Enyi watu! Hakika tumekuumbeni kutokana na mme na mke, kisha tukakujalieni kuwa jamii na makabila ili mfahamiane, hakika mbora wenu kwa Mwenyezi Mungu ni yule mchamungu”. (SurahHujurat, 49:13) Hivi ndivyo Qur’an takatifu ilivyoanza kupanda ndani ya nafsi za Waislamu mafahimu ya undugu wa kiroho kwa kulitilia hilo mkazo katika aya nyingi na kwa mbinu zenye hekima. Kwanza imeweka sheria ya undugu ili iwe ni kanuni kwa Waislamu. Mwenyezi Mungu anasema:

“Hakika waumini ni ndugu. Basi fanyeni suluhu baina ya ndugu zenu, na mcheni Mwenyezi Mungu (swt) ili mpate kurehemewa. (Suratul Hujurat, 49: 10) Kisha ikatilia mkazo undungu na kutahadharisha dhidi ya vyanzo vya mfarakano, kwa kukumbusha neema ya umoja na undugu (uliyoletwa na ) uislamu baada ya uadui wa muda mrefu na kuuana zama za ujahilia. Mwenyezi Mungu (swt) anasema:

“Na shikamaneni na kamba ya Mwenyeezi Mungu nyote wala msi87


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:20 PM

Page 88

Tabia njema kwa mujibu wa Ahlul Bayt (a.s) farakane. Na kumbukeni neema ya Mwenyezi Mungu iliyo juu yenu.” (Imran 3:103) Hivi ndivyo Uislamu ulivyofanya jihadi ya kutukuza undugu wa kiroho na ukaulinda na misukumo ya mfarakano na mgawanyiko kwa kuweka sheria na desturi za mahusiano ya kijamii katika mfumo wake wa milele. Hii ni baadhi ya mifano: 1. (Mfumo huo) ulinyanyua hisia za Waislamu na maono yao na kuwaepusha kutawaliwa na asabia na migogoro inayofarikisha na kuwaelekeza kuelekea kwenye lengo tukufu ambalo ni kumtii Mwenyezi Mungu (swt) na kumridhisha. Kwa maana kupenda na kuchukia, kutoa na kunyima, kunusuru na kudhili, yote hayo lazima yawe kwa ajili ya Mwenyezi Mungu (swt). Ni kwa hilo ndio kamba za undugu zinathibiti na migogoro inayofarikisha kutoweka na Waislamu kuwa kama jengo madhubuti kila mmoja ashikana na mwenzie.

HADITHI Hii ni baadhi ya athari za nyumba hii, amani iwe juu yao, katika jambo hili: Kutoka kwa Imam Baqir (a): Mtume (s) alisema: “Mapenzi ya muumini kwa muumini kwa ajili ya Mwenyezi Mungu ni katika matawi makuu ya imani. Kwa hiyo yeyote atakayependa, akachukia, akatoa, akanyima kwa ajili ya Mwenyezi Mungu ni katika wateule wa Mwenyezi Mungu.”115 Imam Swadiq (a) alisema: “Hakika wapendanao kwa ajili ya Mwenyezi Mungu watakuwa siku ya Kiyama juu ya mimbari za nuru, huku nuru ya nyuso zao na nuru ya miili yao na nuru ya mimbari zao imeeangazia kila kitu hadi wafahamike kwayo, na hapo itangazwe: hawa ndiyo wapendanao kwa ajili ya Mwenyezi Mungu.”116 115. Al Waafy, juz. 3, uk. 89 116. Rejea hapo juu 88


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:20 PM

Page 89

Tabia njema kwa mujibu wa Ahlul Bayt (a.s) Ali bin Husayn (a) alisema: “Mwenyezi Mungu (awj) atakapokusanya wa mwanzo na wa mwisho, atasimama mwenye kunadi aite kwa sauti ambayo watu watasikia, na kusema; wako wapi wapendanao kwa ajili Mwenyezi Mungu (swt)? Zitachomoza shingo baina ya watu na wataambiwa: Nendeni peponi pasi kuhesabiwa. Watakutana na malaika na kuwauliza: Wapi mwendako? Watajibu: Peponi pasi na hesabu. Watawauliza tena: Nyinyi ni watu aina gani? Watajibu: Sisi ni wapendanao kwa ajili ya Mwenyezi Mungu (swt). Watawauliza tena: Mlikukuwa mkifanya nini? Watajibu: Tulikua tukipenda na kuchukia kwa ajili ya Mwenyezi Mungu (swt). Hapo watasema: Ujira bora kwa wafanyao kazi.”117 Imam Sadiq (a) alisema: “Yeyote ambaye hatopenda kwa ajili ya dini na kuchukia kwa ajili ya dini, basi hana dini.” 118 Jabir al-Ja’fy kama alivyopokea kutoka kwa Imam Baqir (a) alisema: “Ukitaka kujua kama kwamba ndani mwako mna kheri basi utazame moyo wako. Ikiwa unapenda wenye kumti Mwenyezi Mungu (swt) na kuchukia wenye kumuasi Mwenyezi Mungu (swt), basi ndani mwako mna kheri na Mwenyezi Mungu (swt) anakupenda. Na ikiwa kinyume cha hivyo basi ndani mwako hamna kheri na Mwenyezi Mungu (swt) anakuchukia. Na hakika mtu huwa na yule ampendae.”119 2.Yaliwatamanisha sana Waislamu yale ambayo yanawaunganisha na kuwapa utukufu na fanaka kama vile kuusiana haki, kushirikiana katika mema, kuteteana kwa uadilifu na kusaidiana katika uwanja wa uchumi, kwani wao katika mtazamo wa dini ni familia moja. Inaifurahisha na kuihuzunisha kile kinachowafurahisha na kuwahuzunisha wanafamilia hiyo. Katiba yake ni: Aya 117. Al Bihaar, Muj 15,Juz. 1,.uk.283 118. Al Waafy, juz. 3, uk. 90 119. Kama hapo juu. 89


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:20 PM

Page 90

Tabia njema kwa mujibu wa Ahlul Bayt (a.s) “Muhammad ni Mtume wa Mwenyezi Mungu na wale walio pamoja naye ni wakali dhidi ya makafiri na wapole baina yao. (Suratul Fath; 48:29)” Wito wake ni kauli ya Mtume (s) isemayo: “Yeyote atakayeamka na asijali mambo ya Waislamu, basi huyo siyo mwislamu”.120 3. Uliwatahadharisha Waislamu na yale ambayo ni chanzo cha mfarakano na uadui, na pia ukawaonya na matendo machafu, kauli mbaya, kuteta na kusengenya, khiana na udanganyifu na mfano wa hayo katika yale yanayozusha fitina na chuki. Msingi wao katika hilo ni kauli ya Mtume (s) isemayo: “Muumini ni yule ambaye watu wamemuamini juu ya mali zao na damu zao. Na muisilamu ni yule ambae Waislamu wamesalimika na mkono wake na ulimi wake na muhajir (mwenye kuhama ) ni yule ambaye anahama maovu”.121 4. Ulito a fursa kukuza uhusiano wa kimapenzi baina ya Waislamu kama vile kutilia mkazo kutembeleana (kuzuru), kuhudhuria sherehe za dini, na kushuhudia mikusanyiko ya kiislamu kama vile sala ya jamaa, hija, nk.

16. ASABIYYA/TAASUBI MAANA YAKE Ni kule mtu kunusuru watu wake au kaumu yake au familia yake au nchi yake katika yale ambayo yanahalifu sheria na kuwa kinyume na haki na 120. Al Wafii, juz. 3, uk. 99 kut. al Kaafii. 121. Al Waafii, juz. 14, uk. 48 kut. al-Faqih 90


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:20 PM

Page 91

Tabia njema kwa mujibu wa Ahlul Bayt (a.s) uadilifu. Taasubi ni katika tabia yenye hatari na maangamizi zaidi katika kubaki nyuma Waislamu na kufarikisha umoja wao na kudhoofisha nguvu zao kiroho na kimada. Kwa ajili ya hayo Uislamu umepiga vita taasubi na kuwatahadharisha Waislamu na shari yake.

HADITHI Kutoka kwa Imam Husayn (a) alisema: Mtume wa Mwenyezi Mungu (s) alisema: “Yeyote yule ambaye ana punje ya hardali ya taasubi ndani ya nafsi yake basi Mwenyezi Mungu atamfufua siku ya Qiyama pamoja na waarabu wa jahiliyyah.”122 Imam Swadiq (a) alisema: “Atakayefanya taasubi basi Mwenyezi Mungu (swt) atamfunga na mkanda wa moto”. 123 Mtume (s) alisema: “Hakika Mwenyezi Mungu (swt) kwa Uislamu, amekwishaondosha ubora uliyokuwepo zama za ujahilia na kujifaharisha kwa jadi kulikoshamiri zama hizo. Bila shaka watu wote asili yao ni Adamu, na Adamu atokana na udongo. Kwa hiyo mbora kwa Mwenyezi Mungu (swt) ni yule mchamungu zaidi”.124 Imam al Baqir (a) alisema: “Kundi la masahaba wa Mtume (s) walikaa wakijinasibu na kujifaharisha 122. Al Waafii, juz. 14, uk. 48 kut. al-Faqih 123. Al Waafy, juz. 3, uk. 149 kut. al-Kaafy 124. Al Waafy, juz. 14, uk. 48, kut. al-Faqiih 91


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:20 PM

Page 92

Tabia njema kwa mujibu wa Ahlul Bayt (a.s) na kati yao akiwemo Salman. Umar akasema: Nasabu yako ni ipi ewe Salman na asili yako? Salman akamjibu: Mimi ni Salman mtoto wa mja wa Mwenyezi Mungu (Abdulah), nilikuwa nimepotea Mwenyezi Mungu (swt) akiniongoza kwa Muhammad (s), na nilikuwa maskini akanitajirisha kwa Muhammad (a), na nilikuwa mtumwa akaniachia huru kwa mapenzi ya Mwenyezi Mungu (swt). Hii ndiyo asili yangu na nasaba yangu ewe Umar. Kiisha akatoka Mtume (s) na Salman akampasha yale aliyoyasema Umar na vile alivyomjibu. Mtume (s) akasema: “Enyi kundi la maquraishi! Hakika nasabu ya mtu ni dini yake na utu wake ni tabia yake na asili yake ni akili yake. Mwenyezi Mungu (swt) anasema: ‘Enyi Watu hakika tumekuumbeni kutoka mme mmoja na mke na tukakujalieni kuwa jamii na makabila ili muweze kujuana. Hakika mbora wenu ni yule mchamungu wenu zaidi’. Mtume (s) akamuendea Salman na kumuanbia: ‘Hakuna katika hawa aliye na ubora juu yako ila kwa kumcha Mwenyezi Mungu. Kwa hivyo kwa yule utakayemshinda uchamungu basi wewe ni bora kuliko yeye”.125 Kutoka kwa Imam Swadiq (a) kama alivyopokea kutoka kwa baba yake kutoka kwa babu yake (a) alisema: “Ilitokezea siku moja baina ya Salman al-Farisy na mtu mmoja maneno ya ugomvi.Yule bwana akamuambia Salman: Kwani wewe nani ewe Salman? Salman akajibu: Ama mwanzo wangu na mwanzo wako ni nutfa (mbegu asili ya mwanadamu) chafu. Na ama mwisho wangu na mwisho wako ni kiwiliwili kinachooza. Itakapokuwa Siku ya Kiyama na mizani zikawekwa, yule atakayekuwa na mizani nzito ndiye bora na atakayekuwa na mizani hafifu ndiye duni”. 126 Katika kadhia ya Abu Lahab ambaye alikuwa katika waarabu halisi na ami yake Mtume (s), lakini Qur’ani ilitamka wazi uovu wake na adhabu yake kwa sababu ya kumkufuru Mtume (s) na kumpiga vita, kama katika aya hizi: “ Imeeangamia mikono miwili ya Abu Lahab na ameangamia, hait125. Al Bihaar muj. 15, juz. 2, uk. 95 126. Safinatul Bihaar, juz. 2.uk. 348 kut. Aamali Sudduuq 92


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:21 PM

Page 93

Tabia njema kwa mujibu wa Ahlul Bayt (a.s) omfaa mali yake na yale aliyochuma, atatokomezwa ndani ya moto wenye ndimi za moto” (Suratu Lahab, 111:1-3). Huu ni ushahidi wa kweli kuhusu usahihi wa Uislamu na kukataa kwake ushabiki wa asabiya na mahala pake ukaweka imani na uchamungu kuwa ndiyo vigezo vya ubora. Salman al Farisy alikuwa mbali kabisa na koo za kiarabu na Mtume Mtukufu (s) alimpa medali ya milele katika ubora na utukufu pindi aliposema: “Salman ni miongoni mwetu Ahlul Bait”. Na hakuipata nishani hii adhimu ila ni kwa sababu ya imani yake iliyopevu na ikhlas yake kubwa na kujizima katika Mwenyezi Mungu (swt) na Mtumewe.

UHAKIKA WA TAASUBI Bila shaka taasubi ambayo Uislamu umekataza ni ile ya kunusuriana kwenye batili na kusaidiana kwenye dhulma na kujifaharisha kwa tabia za kijahilia. Ama kushabikia haki na kuitetea na kunusuriana ili kutekeleza maslahi ya jumla ya Uislamu kama vile kutetea dini, kulinda dola kuu ya kiislamu, kuhifadhi heshima ya Waislamu na nafsi zao na mali zao ni taasubi nzuri inayopelekea kuunganisha malengo na juhudi na kufikia utukufu wa Waislamu. Imam Ali Zaynul-Abidin (a) alisema: “Taasubi inayompeleka mtu mwenyewe katika madhambi ni kule mtu kumwona mtu muovu wa kaumu yake kwamba ni bora kuliko wabora wa kaumu nyingine, na siyo taasubi mtu kupenda kaumu yake, bali taasubi ni kule kunusuru kaumu yake kwenye dhulma”.127

127. Al Waafy, juz. 3, uk. 149, kut. al-Kaafy 93


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:21 PM

Page 94

Tabia njema kwa mujibu wa Ahlul Bayt (a.s)

MAAFA YA TAASUBI Kwa kila yule anayesoma historia ya kiislamu na akafuatilia sababu za kuporomoka Waislamu, ataelewa ya kwamba magomvi ya kitaasubi ndiyo sururu yenye kubomoa na sababu ya awali iliyopelekea Waislamu kukataana na kuchanachana umoja wao na kugawa nguvu zao mambo ambayo yamepelekea Waislamu kuwa na hii hali tulio nayo hivi sasa. Udhalili na unyonge uliwavaa Waislamu pindi moto unaofarikisha ulipowaka baina yao na kamba za kupendana zikakatika na pingu za undugu zikadhoofika baina yao. Waislamu wakawa ni kigezo cha kukosa maendeleo, udhalili na kusambaratika baada ya kuwa wao ndiyo waliokuwa ni mfano wa ubora, kushikamana na utukufu utadhani hawakuwahi kusikia kauli ya Mwenyezi Mungu (swt) isemayo:

(Na shikamaneni na kamba ya Mwenyezi Mungu (swt) nyote kwa pamoja na wala msifarikiane, na kumbukeni neema ya Mwenyezi Mungu (swt) juu yenu pindi mlipokuwa ni maadui basi akaunganisha nyoyo zenu ‌‌.(3:103).

94


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:21 PM

Page 95

Tabia njema kwa mujibu wa Ahlul Bayt (a.s)

17. UADILIFU MAANA YA UADILIFU Uadilifu ni kinyume cha dhulma. Ni kinga ya nafsi inayomkataza mtu kudhulumu na kumsukuma kwenye uadililifu na kutekeleza haki na wajibu. Uadilifu ndiyo bwana wa fadhila na kigezo cha yote ya kujivunia. Bila shaka ni nguzo ya jamii iliyostaarabika na njia ya furaha na amani.

QUR’ANI Uislamu umetukuza uadilifu na kutilia mkazo jambo hilo katika Qur’ani na Sunnah. Mwenyezi Mungu (swt) anasema:

“Kwa hakika Mwenyezi Mungu anaamrisha uadilifu na hisani na kuwapa jamaa, na anakataza uchafu na uovu na uasi, na kuwaidhini, ili mpate kukumbuka.” (Suratun Nahl, 16:90)

“...Na msemapo, basi semeni kwa insafu ingawa ni jamaa, na tekelezeni ahadi ya Mwenyezi Mungu, hayo amekuusieni ili mpate kukumbuka”. (Surat ul An’am; 6:152)

95


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:21 PM

Page 96

Tabia njema kwa mujibu wa Ahlul Bayt (a.s)

HADITHI Imam Sadiq (a) alisema: “Uadilifu ni mtamu zaidi kuliko asali, ni mlaini zaidi kuliko siagi, na wenye harufu bora kuliko misk”.128 Imam Ali Zaynul-Abidin (a) aliambiwa na msimulizi: Nifahamishe sheria zote za dini. Akajibu: “Kauli ya kweli, hukumu ya uadilifu, na kutekeleza ahadi”.129

AINA ZA UADILIFU Zifuatazo ni baadhi ya aina muhimu za uadilifu: Uadilifu wa mwanadamu kwa Mwenyezi Mungu (swt): Hii ndiyo aina iliyobora ya uadilifu. Na ni vipi mwanadamu ataweza kutekeleza wajibu wa uadilifu kwa Muumba wake Mtukufu Mneemeshaji na ambaye neema zake hazina hesabu wala kikomo?! Na ikiwa uadilifu katika kulipa unakadiriwa kwa kipimo cha neema na utukufu wa mtoaji basi haiwezekani kabisa kutekeleza uadilifu kwake Yeye (Mwenyezi Mungu) ambaye ni lazima kuwepo, asiyehitaji kiumbe yeyote. Kwa udhaifu wake mwanadamu chochote atakachoweza ni kwa tawfiq yake Mwenyewe Mola (swt). Yote yahusuyo uadilifu wa Mwenyezi Mungu (swt) kwa kifupi ni: Kumwamini Yeye, kumpwekesha (tawhid), kuwa na ikhlas naye, kuwakubali mitume Wake na wawakilishi Wake kwa walimwengu, na kuitikia mahitaji ya hayo ambayo ni kujawa na mapenzi Yake, kumwabudu Yeye, kuishi kwa kumtii Yeye na kujiepusha na kumuasi. 128. Al Waafy, juz. 3, uk.89, kut. al-Kaafy) 129. Al Bihaar, muj. 16, uk. 125 96


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:21 PM

Page 97

Tabia njema kwa mujibu wa Ahlul Bayt (a.s) Uadilifu wa mwanadamu kwa jamii: Uadilifu huu ni kuchunga haki za wanajamii, kujizuia kuwaudhi na kuwafanyia ubaya, na mtu akawa ni mwenye kushirikiana nao kwa tabia njema na kuwapendea kheri, kuwa na huruma na wale wenye matatizo, mafakiri na wasiojiweza na mengine kama hayo katika yanayoleta uadilifu wa kijamii. Mwenyezi Mungu amefupisha swala la uadilifu kijumla katika aya ifuatayo:

“Kwa hakika Mwenyezi Mungu anaamrisha uadilifu na hisani na kuwapa jamaa, na anakataza uchafu na uovu na uasi, na kuwaidhini, ili mpate kukumbuka.” (Suratun-Nahl, 16:90) Imam Ali (a) kwa kifupi na balaghah alitoa taswira ya uadilifu kwa jamii kama ifuatavyo: “Ewe mwanangu ijalie nafsi yako kuwa ni mizani baina yako na wengine. Kwa hivyo uwapendee wengine yale unayojipendea nafsi yako, na usimtakie (ndugu yako) yale usiyojitakia wewe, basi usidhulumu kama vile ambavyo wewe hutaki kudhulumiwa na ufanye wema kama vile unavyotaka kufanyiwa wema na uchukie wewe (nafsi yako kufanya) yale unayochukia kwa wengine (kukufanyia), na uridhie kutoka kwa watu yale unayowaridhia kutoka kwako (ikiwa unawatakia watu jambo basi litake pia kwa nafsi yako), na usiseme usiyoyajua hata kama unayoyajua ni machache, na usiseme usiyopenda waseme juu yako”. Alimuusia mwanae mtukufu kuhusu yaliyopo baina yake na wengine ya kwamba awe muadilifu kama vile mizani, na akamwekea wazi aina za uadilifu na njia zake iwe wema au ubaya.

97


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:21 PM

Page 98

Tabia njema kwa mujibu wa Ahlul Bayt (a.s) Uadilifu wa waliyohai kwa jamaa waliyotangulia mbele ya haki. Hawa ni ndugu waliyoiacha dunia na starehe zake na kutangulia katika safari ambayo hawakupata ila vitambaa vya sanda na kijisehemu kidogo cha kaburi na huku wakawaachia jamaa zao mali na urithi. Kwa hiyo uadilifu ni kwamba hawa walio hai wawe na hisia za huruma na kulipa wema kwa ajili ya marehemu wao kama vile kutekeleza wasia wao, kulipa madeni yao, kuwapelekea thawabu ya amali njema, na kuwaombea msamaha, radhi na rehma kwa Mwenyezi Mungu (awj). Imam Sadiq (a) alisema: “Hakika maiti anafurahi kwa kumrehemu na kumtakia msamaha kama vile anavyofurahi aliyehai kwa zawadi anayopelekewa.” Na pia alisema: “Atakayefanya katika Waislamu amali njema kwa ajili ya marehemu , basi Mwenyezi Mungu (swt) atamzidishia ujira na Mwenyezi Mungu (swt) atamnufaisha maiti kwayo”.130 Uadilifu wa viongozi Kwa kuwa viongozi ndiyo wanaoendesha na kusimamia umma, ni wao ndiyo wapasao zaidi kujipamba kwa uadilifu na kutenda uadilifu. Uadilifu wao una nafasi na athari kubwa katika uhai wa watu. Ni kwa uadilifu wao ndiyo usalama hudumu na amani huenea na watu kuneemeka. Na kwa jeuri yao fadhila zote hizo huporomoka na matarajio kugonga mwamba. Matokeo ni watu kuishi katika wasiwasi, kutahayari, umaskini na shida.

130. Man la yahdhuruhul faqih 98


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:21 PM

Page 99

Tabia njema kwa mujibu wa Ahlul Bayt (a.s)

MAZURI YA UADILIFU Nafsi kimaumbile zimeumbwa zinapenda uadilifu na kuutaka na kuchukia dhuluma na kuikataa. Wanadamu, kwa kipindi chote alichoishi mwanadamu juu ya ardhi pamoja na tofauti zao za sheria na misingi, wametukuza uadilifu na kusifia fadhila zake na athari zake na pia wamejitolea muhanga katika njia ya kuusimamisha. Uadilifu ndiyo siri ya uhai wa kaumu mbalimbali na kigezo cha ubora wao na nguzo ya utukufu wao na hali nzuri. Pia ni dhamana ya usalama na fanaka. Madola makubwa hayakuanguka, staarabu mbalimbali hazikutoweka ila kwa kupotea uadilifu na kuudharau msingi wake muhimu. Ahlul Bayt (a) walikuwa ni mfano uliyo bora wa uadilifu. Maneno yao na vitendo vyao vilikuwa ni masomo ya milele yanayoangazia wanadamu utaratibu wa uadilifu, haki na wema. Hii ni baadhi ya mifano: Katika kipindi cha maradhi ya Mtume (s), Sawaadah bin Qays alimwambia: “ Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu pindi uliporejea kutoka Taif, mimi nilikupokea na wewe umempanda ngamia wako (aliechanwa sikio). Mkononi mwako ulikuwa na fimbo nyembamba. Ulipotaka kuondoka ulipandisha fimbo ikanipiga tumboni. Basi Mtume (s) akamwamuru alipizie kisasi. (Sawaadah) Akasema: Nionyeshe tumbo lako ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu (s). Mtume (s) alipomuonyesha, Sawaadah akasema: je unakubali niweke mdomo wangu juu ya tumbo lako? Alipomruhusu, Sawaadah akasema: Najikinga na mahali pa kisasi dhidi ya Mtume (s) na moto wa siku ya moto. Mtume (s) akasema: Ewe Sawaadah bin Qays je 99


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:21 PM

Page 100

Tabia njema kwa mujibu wa Ahlul Bayt (a.s) unalipiza kisasi au unasamehe? Akajibu: Bali nimesamehe ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu. Mtume akamuombea: Ewe Mwenyezi Mungu (swt) msamehe Sawaadah kama vile alivyomsamehe nabii wako Muhammad.”131 Abu Sa’id al-Khudhry alisema: “Bedui mmoja alikuja kwa Mtume (s) akimtaka amlipe deni yake. Akamsimamia mpaka akamwambia: nitakubana mpaka utoe changu. Masahaba wakamkaripia na kusema: Ole wako, hivi unajua unaseme na nani?!! Akajibu: Mimi naomba haki yangu. Mtume (s) akasema: Kwa nini hamkuwa pamoja na mwenye kuomba haki yake? Kisha Mtume (s) akatuma kwa Khawlah binti Qays ujumbe kwamba ikiwa ana tende basi amkopeshe Mtume (s) hadi pale atakapopata za kwake atarejesha. Bi Khawlah akamkopesha Mtume (swt) na yeye akamlipa huyo bedui na kumpa chakula. Akasema: Umetimiza, Mwenyezi Mungu (swt) akutimizie. Mtume akasema (s): “Hao (kwa maana wanaotimiza) ndiyo wabora wa watu. Hauwezi kutakasika umma ambao mnyonge wake hachukui haki yake pasi na kusukumwa”. Inasemekana ya kwamba huyo bedui alikuwa kafiri na baada ya kushuhudia tabia njema na bora za Mtume (s) alisema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu (s) sijawahi kuona mtu mwenye subira zaidi kuliko wewe.132 Na Amirul Muuminin Ali (a) alikuwa hivyo hivyo: Imam Ja’far Swadiq (a) alisema ya kwamba pindi Imam Ali (a) alipotawala alipanda mimbar na kumhimidi na kumsifu Mwenyezi Mungu (s) kisha akasema: “Mimi sitokunyimeni (sitochukua) hata dirham moja katika ngawira yenu ikiwa bado hapo Yathrib mazao yangu yanazaa (yanatoa tende). Muwe na yakini, ikiwa najinyima mnadhani ya kwamba nitakupeni?! Akasimama Aqil (ndugu yake halisi Imam Ali) na kumuambia: Hivi utatuweka kuwa sawa mimi na huyo mweusi wa Madina? Imam (a) 131. Safinatul Bihaar, juz.1, uk. 671 132. Fadhailul Khamsa mina Swihaahi Sitta, juz. 1, uk. 122 kut. Sahih ibnu Maaja. 100


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:21 PM

Page 101

Tabia njema kwa mujibu wa Ahlul Bayt (a.s) akamjibu: Kaa, hakuna hapa anayezungumza zaidi yako. Ubora wako juu yake hauwi ila kwa kutangulia au uchamungu.133 Katika kitabu cha Ibn Hajar kiitwacho Swawaiq, uk. 79, ameandika: Ibn Asaakir anaeleza kwamba Aqil alimwomba Imam Ali (a) kwa kusema: Mimi ni muhitaji na mimi ni faqiri basi nipe. Akamjibu: Subiri mpaka mgao wako utakapotoka pamoja na wengine Waislamu nitakupa pamoja nao. Lakini Aqil akazidi kumsisitizia ampe. Akamwambia mtu mmoja hapo: Mshike mkono na uende naye sokoni kwenye maduka na umwambie bomoa makufuli haya na chukua yaliyomo. Aqil akasema: Unataka kunishika mimi wizi? Imam Ali (a) akamjibu: Na wewe unataka kunifanya mwizi, kwa kuchukua mali ya Waislamu na nikupe wewe?! Aqil akasema: Nitamwendea Muawiyah. Akamjibu: Wewe na huyo. Akamwendea Muawiyah akamuomba naye akampa elfu mia moja (laki moja) kisha akamuambia panda mimbar na utaje lile alilokufanyia Ali (a) na lile ambalo nililokufanyia. Akapanda na baada ya kumhimidi Mwenyezi Mungu (swt) na kumsifu akasema (Aqil): Enyi watu nakufahamisheni ya kwamba nilimtaka Ali (a) juu ya dini yake, akahiari dini yake; na nilimtaka Muawiyah juu ya dini yake, akanichagua mimi dhidi ya dini yake.134 Kipindi watu walipokuwa wanamkimbia Imam Ali (a) na kwenda kwa Muawiyah wakifuata ya dunia aliyomiliki, baadhi ya masahaba wake walimuendea na kumuambia: Ewe Amiri wa waumini, toa hizi mali na uwafadhilishe hawa mabwana katika waarabu na maquraishi juu ya mawali (watumwa walioachwa huru) na wasio waarabu na (pia mpe) yeyote unayehofia kukukimbia na kwenda kwa Muawiyah. Akawajibu: "Hivi mnaniamrisha nitafute ushindi kwa dhulma? Hasha siwezi naapa wallahi ikiwa jua bado lachomoza na nyota yadhihiri mbinguni. Wallahi ingekuwa mali yao ni yangu mimi binafsi ningewagawiya sawa, sasa vipi wakati mali ni yao?�135 133. Al Bihar, muj. 9, uk.539 kut. al Kaafy 134. Fadhailul-Khamsa an Swihah sittah, juz. 3, uk. 15 135. Al Bihar, muj. 9, uk. 533 101


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:21 PM

Page 102

Tabia njema kwa mujibu wa Ahlul Bayt (a.s) Ibn Abbas anasema: Nilimuendea Amirul-Muuminina Ali (a) nikamkuta anatengeneza kiatu chake kisha akakiweka pamoja na mwenzie na akaniambia: Vikadirie thamani. Nikajibu kwamba havina thamani. Akaniambia: Pamoja na hilo. Nikamjibu kwamba ni kama sehemu ya dinari. Akasema: Wallahi viatu hivi kwangu navipenda zaidi kuliko ukhalifa wenu huu isipokuwa kwa sharti kwamba nisimamishe haki na kuondoa dhulma.”136 Pia ni yeye aliyesema: “Wallahi ikiwa nitalala juu ya miba ya sadani (mmea wenye miba) bila ya usingizi, na nikaburuzwa nimefungwa ndani ya pingu ni bora kwangu kuliko kukutana na Mwenyezi Mungu (swt) na Mtumewe (s) Siku ya Kiyama nikiwa nimedhulumu baadhi ya waja na kunyanganya kitu katika mali ya dunia inayotoweka. Na vipi nimdhulumu mtu kwa ajili ya nafsi ambayo haraka inaishia kwenye kutoweka na kubaki kwa muda mrefu ndani ya udongo”.137

18. DHULMA MAANA Kilugha: Ni kuweka kitu mahala ambapo siyo pake. Shirk ni dhulma kubwa kwa kuiweka mahala pa tawhidi. Kimatumizi: ni kupunguza (kunyima) haki, kumfanyia mwingine uadui kikauli au kimatendo kama vile kutukana, kuteta, kunyang’anya mali, kumpiga mtu au kuuwa na mengine kama hayo katika aina za dhulma kimada na kiroho. Dhulma ni katika hulka ambazo zenye mizizi katika nafsi nyingi na katika historia ndefu, walimwengu wamefikwa na aina mbali mbali za maafa na dhoruba ambazo zimefanya maisha kuwa giza na kuyabandika nembo ya majonzi ya kutisha. 136. Safinatul Bihaar, juz. 2, uk. 570 137. Safinatul Bihar, juz. 2, uk. 606, kut. An Nahjul Balagha 102


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:21 PM

Page 103

Tabia njema kwa mujibu wa Ahlul Bayt (a.s) Dhulma ni katika silika ya nafsi na ukimuona mwenye iffat (kumiliki nafsi) ni kwa sababu hadhulumu. Kwa ajili ya hilo dhulma imekuwa ndiyo jumla ya maovu na chanzo cha shari, kichochezi cha ufisadi na maangamizi. Ayah na hadithi zinazokemea na kuonya dhidi ya dhulma ni nyingi sana.

QUR’ANI Mwenyezi Mungu (swt) anasema:

“Na nani dhalimu zaidi kuliko yule amzuliaye uongo Mwenyeezi Mungu au azikadhibishaye Aya zake? hakika madhalimu hawafaulu.” (Suratul An’am, 6:21)

“Na wale walioamini na kufanya vitendo vizuri basi atawalipa thawabu zao, na Mwenyezi Mungu hawapendi wenye kudhulumu.” (Suratu Aali Imraan, 3:57)

“... Hakika madhalimu watakuwa na adhabu yenye kuumiza. (Suratu Ibrahim, 14: 22)

103


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:21 PM

Page 104

Tabia njema kwa mujibu wa Ahlul Bayt (a.s)

“Na bila shaka tumekwisha viangamiza vizazi kabla yenu walipodhulumu, na Mitume wao waliwafikia kwa hoja wazi wazi, na hawakuwa wenye kuamini, hivyo ndivyo tunavyowalipa watu waovu.” (Suratu Yunus, 10: 13)

“Wala usidhani Mwenyezi Mungu ameghafilika na wanayoyafanya madhalimu. Hakika yeye anawaakhirisha mpaka siku ambayo macho (yao) yatakodoka.” (Suratu Ibrahim, 14:42)

“Na kama kila mtu aliyedhulumu angelikuwa na (yote) yaliyomo ardhini, bila shaka angeyatoa kujikomboa. Na watakapoiona adhabu wataficha majuto, na itahukumiwa baina yao kwa uadilifu nao hawatadhulumiwa.” (Suratu Yunus, 10:54)

HADITHI Imam Ali (a) alisema: “Wallahi lau ningepewa maeneo saba (mbingu) pamoja na yale yaliyo chini ya mizunguko yake ili nimuasi Mwenyezi Mungu (swt) kwa kumnyang’anya sisimizi punje ya shairi nisingefanya. Hakika dunia yenu kwangu haina thamani kama vile jani ndani ya mdomo wa nzige. Ali ana nini (la kufanya ) na neema ambazo ladha yake hutoweka na zisizo 104


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:21 PM

Page 105

Tabia njema kwa mujibu wa Ahlul Bayt (a.s) dumu?”138 Abu Baswir alisimulia: Watu wawili waliingia kwa Imam Ja’far Sadiq (a) kwa ajili ya udanganyifu baina yao. Pindi alipomaliza kuwasikiliza aliwaambia: “Hakika hakupata kheri mtu anayechuma dhulma. Hakika mdhulumiwa anachukuwa katika dini ya dhalimu zaidi kuliko kile ambacho dhalimu alichochukuwa katika mali ya mdhulumiwa”. Kisha akasema: “anayewafanyia watu shari basi na asikatae shari pindi atakapofanyiwa. Hakika mwanadamu huvuna kile alichokipanda na havuni mtu kitamu kutoka kwenye kichungu, na wala kutoka kwenye kitamu kichungu”. Wale watu wawili wakaelewana kabla ya kusimama.”139 Na alisema (a): “Atakayekula mali ya ndugu yake kwa dhulma, na hakumrejeshea, basi amekula kijinga cha moto Siku ya Kiyama”.140 Imam Sadiq (a) alisema: “Yeyote anayedhulumu, Mwenyezi Mungu (swt) humpa mtu uwezo juu yake ambae atakayemdhulumu au juu ya kizazi chake au juu ya kizazi cha kizazi chake.” Rawi (msimuluzi) akauliza: Ni vipi adhulumu mtu halafu kizazi chake kidhulumiwe? Akajibu: Mwenyezi Mungu (swt) anasema: (Suratun Nisaa, 4:9)141 Na sababu ya hadithi hiyo tukufu kuhusu kushikwa watoto kwa madhambi ya mababa zao ni kwa watoto ambao wameridhia dhuluma za wazazi wao au wakachukua urithi wao waliyoudhulumu. Katika kushikwa kwao 138. Nahjul Balagha 139. Al Waafy, juz. 3, uk. 162 kut. al Kaafy 140. Sawa na iliyo kabla 141. Al Waafy, juz. 3, uk.162 kut. Al Kaafy 105


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:21 PM

Page 106

Tabia njema kwa mujibu wa Ahlul Bayt (a.s) kuna kemeo la kihisia lenye kutisha linamfanya dhalimu arejee nyuma kufanya dhulma kwa kuhofia watoto wake watukufu. Pia ndani yake mna bishara kwa mdhulumiwa kwa kuwepo adhabu dhidi ya aliedhulumu pamoja na hilo kuwepo malipo ya dhulma yake kesho akhera. Kutoka kwa Imam Abu Abdilah (a) alisema kwamba Mtume alisema: “Yeyote anayeamka na hakudhamiria kufanya dhulma, basi Mwenyezi Mungu (swt) humsamehe aliyofanya (ya uasi yakiwa ni madhambi baina ya mja na Yeye Allah katika siku hiyo)”.142

AINA ZA DHULMA Zipo aina mbalimbali za dhulma. Hapa tunaashiria kwa haraka: 1. Dhulma ya mtu kwa nafsi yake. Hii ni kule mtu kudharau kuielekeza nafsi yake kumtii Mwenyezi Mungu (swt) na kuinyoosha kwa tabia njema na mwenendo unaoridhisha jambo ambalo linaisukumiza ndani ya mahangaiko ya upotofu. Matokeo ni kufeli na udhalili. “Na kwa nafsi na kwa yule aliyeitengeneza. Kisha akaifahamisha uovu wake na wema wake. Bila shaka amefaulu aliyeitakasa. Na bila shaka amepata khasara mwenye kuitweza.” (Suratu Shams, 91:7-10) 2. Dhulma ya mtu kwa familia yake. Hii ni kule mtu kutojali kuwalea malezi bora ya kiislamu na kughafilika kuwaelekeza mwelekeo wa kheri na wema na kuwaongoza kwa ukatili na nguvu, na kuwafanyia ubakhili katika mahitaji ya dharura na maisha mazuri, mambo ambayo yanapelekea mvurugiko wa maisha yao kimada na 142.Rejea ya hapo juu. 106


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:21 PM

Page 107

Tabia njema kwa mujibu wa Ahlul Bayt (a.s) kitabiya. 3. Dhulma ya mtu kwa jamaa zake. Hii ni kule kuwaweka kando na kuwadhili wakati wa shida na matatizo, na kuwanyima hisia za upendo na wema mambo ambayo yanapelekea kujitenga na kuvunja uhusiano. 4. Dhulma ya mtu kwa jamii. Hii ni kujikweza juu ya wengine na kutothamini haki zao na kudharau utukufu wao na kutojali mambo yao na maslahi yao. Na mfano wa hayo ni miongoni mwa yanayosababisha jamii kabaki nyuma na kudhoofika. Na katika dhulma chafu kijamii ni kudhulumu madhaifu ambao hawawezi kujitetea dhidi ya uadui wanaofanyiwa, lao ni kumshtakia na kumlilia Mwenyezi Mungu Mwadilifu na Rahimu katika majonzi yao na dhulma wanazofanyiwa. Kutoka kwa Imam Baqir (a) alisema: “Yalipomfika mauti baba yangu, alinikumbatia kifuani mwake na kusema: ‘Ewe mwanangu, nakuusia yale aliyoniusia baba yangu pindi yalipomjia mauti na akasema kwamba pia aliusiwa na baba yake (nayo ni): Ogopa dhulma ya mtu ambaye hana wa kumnusuru ila Mwenyezi Mungu (swt).”143 5.Dhulma ya watawala na wenye mamlaka. Hiyo ni kwa wao kuwa na jeuri, uonevu na kubana uhuru wa raia, kufanya duni utu wao na kunyang’anya mali zao na kuzitumia kwa maslahi yao wenyewe. 143. Al Waafy, juz. 3, uk. 162 kut. al Kaafy 107


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:21 PM

Page 108

Tabia njema kwa mujibu wa Ahlul Bayt (a.s) Dhulma hii ni mbaya kuliko zote na madhara yake ni makubwa sana katika jamii na hatima yake. Imam Sadiq (a) alisema: “Mwenyezi Mungu alimpa wahyi nabii katika manabii aliyekuwa katika mamlaka ya mtu jeuri kwamba: ‘Nenda kwa huyo jabari na umwambie: Mimi sikukupa wadhifa ili umwage damu na kunyang’anya mali, bali nimekupa madaraka ili uniondoshee sauti za wadhulumiwa, nami sitoiacha dhulma waliyotendewa hata kama ni makafiri”.144 Imam Sadiq (a) kama alivyopokea kutoka kwa baba zake kutoka kwa Mtume (s), alisema: “Moto utazungumza na watatu: Amiri, msomaji na tajiri. Utamwambia amiri: Ewe uliyepewa na Mwenyezi Mungu (swt) usultani na haukufanya uadilifu! Hapo utammeza kama vile ndege anavyomeza punje ya ufuta. Na utamwambiya msomaji: Ewe uliyejipamba kwa ajili ya watu na ukapambana na Mwenyezi Mungu (swt) kwa maasi, basi pia utammeza. Utamwambia tajiri: Ewe uliyepewa na Mwenyezi Mungu (swt) dunia kwa wingi na wasaa, maskini akakuomba kitu kidogo umkopeshe ukamyima kwa ubakhili, basi hapo utammeza”.145 Onyo kali hili siyo tu kwa watu jeuri bali inakusanya pia wale waliokuwa wenye nguvu katika kuwasaidia hao madhalimu na wakaridhia matendo yao na wakachangia katika jeuri yao. Wote ni sawa katika uovu na adhabu, kama vile ilivyopokelewa katika hadithi: Imam Swadiq (a) alisema: “Anayetenda dhulma, anayemsaidia, anayeridhia wote watatu ni washiriki”.146 Kwa sababu hiyo basi, kumnusuru madhlumu na kumhami na dhulma ya 144. Al Waafy, juz. 3, uk. 162 kut. Al Kaafy. 145 Al Bihaar, muj. 16, uk. 209, kut. Al Khiswaal li Sudduuq 146. Al Waafy, juz. 3, uk. 163, kut. al Kaafy 108


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:21 PM

Page 109

Tabia njema kwa mujibu wa Ahlul Bayt (a.s) madhalimu ni katika uchaji ulio bora na katika kitendo kikubwa zaidi cha kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu (swt). Imam Musa al Kadhim (a) anamwambia Ibnul Yaqtwiin: “Nipe dhamana ya jambo moja mimi nitakupa dhamana ya mambo matatu. Nipe dhamana kwamba hutokutana na yeyote katika wafuasi wetu katika nyumba ya ukhalifa isipokuwa wewe utamtekelezea haja yake, mimi nitakupa dhamana ya kwamba ukali wa upanga hautokusibu kamwe na wala hutokaa chini ya dari ya jela na kamwe ufakiri hautaingia ndani ya nyumba yako.”147 Na Abul Hasan (a) alisema: “Mwenyezi Mungu (swt), kwa mtawala, ana mawalii ambao kwao anawanusuru wapendwa wake”. Na katika hadithi nyingine akasema kwamba hao ndiyo waachwa huru wa Mwenyezi Mungu (swt) na Moto”.148 Imam Swadiq (a) alisema: “Kafara ya kazi ya mtawala ni kukidhi mahitaji ya ndugu (raia)”.149 “Kutoka kwa Muhammad bin Jamhur na wengine katika masahaba wetu alisema: “Najashi (sio yule mfalme wa uhabeshi) ambaye ni mmoja katika machifu, alikuwa gavana wa Ahwaz na Uajemi. Mmoja katika wenye kazi kwake akamwambia Imam Husayn (a): Mimi katika diwani ya Najashi nina kodi ya kulipa. Na kwa kuwa yeye ni mwenye utiifu kwako unaonaje ukamwandikia barua kwa ajili yangu? Imam Husayn akamwandikia: “Bismillahi rahmani rahim, mfurahishe nduguyo, bila shaka Mwenyezi Mungu (swt) atakufurahisha.” 147. Kashkuulul Bahaaiy (chapa ya Iran), uk. 124 148. Al Waafy, juz. 10, uk. 28, kut. al Faqih 149.Kama hapo juu. 109


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:21 PM

Page 110

Tabia njema kwa mujibu wa Ahlul Bayt (a.s) Najashy alipata ujumbe akiwa ndani ya kikao. Alipomaliza, akampa barua na kumwambia: Hii barua ya Abu Abdillah (a). Akaibusu na kuiweka juu ya macho yake na kusema: Nini haja yako? Akajibu: Katika diwani (rejesta) natakiwa kilipa kodi. Akamuuliza: Kiasi gani? Akajibu: Dirhamu elfu kumi. Najashy akamwita mwandishi wake na kumwamuru amfutie deni na kisha akatoa kiwango kama hicho na kumwamuru amwekee kwa ajili ya mwaka ujao. Kisha akamwambia: Je! Nimekufurahisha? Akajibu ndiyo. Akaamrisha aongezwe tena elfu kumi zingine na akamwambia: Je! nimekufurahisha? Akajibu: Ndiyo niwe muhanga wako. Akaamrisha apewe pando, kisha akapewa suriya na kijana wa kazi, na sanduku la nguo na kila mara akimuuliza, je! nimekufurahisha? Hata alipomaliza kila kitu akamwambia: Chukua zulia ya nyumba hii ambayo nilikuwa nakalia pindi uliponipoza ujumbe wa bwana wangu. Pia niletee haja zako zote. Akatoka bwana huyo na kwenda kwa Imam Husayn (a) na kumhadithia. Imam (a) akafurahi kwa alilofanya Najashy. Huyu bwana akamuuliza: Ewe mtoto wa Mtume (s) yamekufurahisha aliyonifanyia mimi? Akajibu: Hakika wallahi. Amemfurahisha Mwenyezi Mungu na mtumewe (s).150

MATOKEO MABAYA YA DHULMA Ni wazi kwamba kimaumbile mwanadamu hakubali dhulma na kwamba nafsi huru zinakataa na kuchukia dhulma na zinakuwa tayari kufa katika kupambana ili kuiondosha. Na bila shaka hakuna kitu ambacho ni chenye madhara zaidi kwa jamii na chenye kupelekea kuangamia kwake kama vile kutapakaa kwa dhulma na maafa yake. Kufumbia jicho dhulma huwapa nguvu mataghuti kuendelea kubobea katika upotofu na uovu, jambo ambalo linapelekea waathirika kufanya thawra na kulipizia kisasi. Matokeo yake ni kuenea vurugu na kusambaa ufisadi na uhai kugeuka kuwa ni uwanja wa mauwaji na maasi. Hayo ndiyo sababu ya kudidimia umma na kupoteza amani na maisha mazuri, utukufu na utawala wake. 150.Al Waafy, juz. 10, uk. 28, kut. al Kaafy 110


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:21 PM

Page 111

Tabia njema kwa mujibu wa Ahlul Bayt (a.s)

TIBA YA DHULMA Ni jambo gumu sana kutibu dhulma na kung’oa mizizi yake yenye kupenya hadi kina cha nafsi. Lakini inawezekana kupunguza fukuto lake na kulainisha ukali wake. Nayo ni kwa kuzingatia yafwatayo: 1. Kujikumbusha tuliyoyataja kuhusu faida za uadilifu na jumla ya athari zake nzuri katika uhai wa mwanadamu kama vile kueneza amani, kuelewana na maisha mazuri. 2. Kuzingatia yale tuliyoweka wazi kuhusu maovu ya dhulma na hasara zake kimada na kiroho. 3. Kujenga kizuizi cha dini, na hilo kwa kulea dhamiri na dhati na kuinawirisha kwa mafunzo ya imani na miongozo yake. 4. Kusoma na kuzingatia maisha ya mataghuti na yale yaliyowafika ya balaa za jeuri na matokeo yake mabaya. Katika kitabu Hayatul-Hayawaan kwenye kutaja (neno) alhajlaan (kwale wawili) imeandikwa kwamba: Baadhi ya viongozi wa makurdi walihudhuria kwenye meza ya baadhi ya maamiri na juu ya meza walikuweko kwale wawili waliochomwa. Yule mkurdi akawatazama kwale wale kisha akacheka. Amiri akamuuliza kisa na maana ya kicheko chake. Akajibu: Nilipokuwa bado kijana nilimvamia njiani tajiri mmoja na nilipotaka kumuua, alinisihi sana lakini bila mafanikio. Alipohakiki kwamba namuua hakuna hila, akawaelekea kwale wawili waliokuwa kwenye jabali na kuwaambia: Shuhudieni kaniua. Basi nilipowaona kwale hawa nilikumbuka upumbavu wake. Yule amiri pale pale akasema: “Mkateni kichwa, kwale wamekwisha shuhudia”.151 151. Kashkul bahai, tol. la Iran, uk. 21 111


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:21 PM

Page 112

Tabia njema kwa mujibu wa Ahlul Bayt (a.s) Katika kitabu Siraajul-Muluuk cha Abu Bakr at-Twartuusy imeandikwa kwamba siku moja Abdul Malik bin Marwan alikosa usingizi usiku, akamwitisha mliwazaji wake ili azungumze naye. Katika mazungumzo yao akamwambia: Ewe Amirul-Muuminina, hapo Mosul alikuwepo bundi na pia Basra alikuwepo bundi mwingine. Bundi wa Mosul akamchumbia mwanae binti wa bundi wa Basra. Bundi wa Basra akasema: Sitokubali mpaka unifanyie vijiji mia kuwa magofu. Hiyo ndiyo mahari yake. Bundi wa Mosul akasema: Sasa hivi siwezi hilo lakini ikiwa mtawala wetu ataendelea kuwa nasi na Mwenyezi Mungu (swt) akampa uhai mwaka mmoja basi hilo nitaliweza. Akaamka Abdul Malik na kusimamia kesi za dhulma na akawafanyia watu uadilifu katika kuwahukumu na akachunguza kazi za magavana.152

19. IKHLAS MAANA Ikhlas ni kinyume cha riya (kujionyesha). Ni kule kusafisha vitendo na madoa ya riya na kuvifanya kwa ajili ya Mwenyezi Mungu (swt) pekee. Ikhlas ndiyo nguzo ya mambo mema na mwili wa uchamungu, na johari ya ibada na kigezo cha usahihi wa amali na kukubalika kwa Mwenyezi Mungu (swt).

QUR’AN Sharia ya Kiislamu imetukuza sana ikhlasi na kutaja kwa wingi fadhila zake. Pia imewavutia watu kujipamba na ikhlasi na ikazibariki juhudi zao katika Aya mbalimbali na hadithi. 152. Safunatul Bihaar, juz. 1, uk. 110. 112


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:21 PM

Page 113

Tabia njema kwa mujibu wa Ahlul Bayt (a.s) Mwenyezi Mungu (swt) anasema:

“...Basi anayetumaini kukutana na Mola wake na afanye vitendo vizuri wala asimshirikishe yeyote katika ibada ya Mola wake.” (Suratul al Kahf; 18:110)

“Wala hawakuamrishwa ila kumwabudu Mwenyeezi Mungu kwa kumtakasia yeye dini, hali wameshikamana na haki, na wanasimamisha swala na kutoa zaka, na hiyo ndiyo dini madhubuti.” (al Bayyinah, 98:5)

“Kwa hakika sisi tumekuteremshia Kitabu kwa haki, basi muabudu Mwenyezi Mungu kwa kumtii kihalisi.” “ Sikilizeni! Utii halisi ni haki ya Mwenyeezi Mungu,....” (al Zumar, 39:2-3)

HADITHI Mtume(s) alisema: “Yeyote atakayefanya ikhlasi kwa ajili ya Mwenyezi Mungu (swt) siku arobaini basi Mwenyezi Mungu (swt) atazibubujisha chemchemi za hekima katika moyo wake na kwenye ulimi wake.”153 153. Al Bihaar, juz. 15, uk. 87 113


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:21 PM

Page 114

Tabia njema kwa mujibu wa Ahlul Bayt (a.s) Imam Jawad (a) alisema: “Bora ya ibada ni ikhlasi”.154 Imam Ridhwa (a) kama alivyopokea kutoka kwa baba zake alisema: Amiri wa waumini (a) alisema: “Dunia yote ni ujinga ila sehemu za elimu, na elimu yote ni ujinga ila ile iliyofanyiwa kazi, na kazi yote ni riya ila ile iliyo na ikhlasi, na ikhlasi ipo kwenye hatari mpaka pale mja atakapotizama kwa yapi atakayohitimishiwa”.155 Na Mtume (s) alisema: “Ewe Abu Dhar mtu hafahamu uelewa kamili mpaka awaone watu katika upande wa Mwenyezi Mungu (swt) kama vile ngamia, kisha arejee kwenye nafsi yake na awe yeye ni mwingi zaidi wa kuidharau nafsi yake”.

FADHILA ZA IKHLASI Vipimo vya amali vinatofautiana kwa tofauti ya malengo na sababu zilizochochea amali hizo. Kadri lengo linavyozidi kuwa tukufu na sababu kusafika na uchafu wa udanganyifu, unafiki, ndivyo matendo yanakuwa karibu na kubuli ya Mwenyezi Mungu (swt). Na bila shaka katika sharia ya kiislamu kichochezi cha vitendo ni niyyah. Kwa hivyo pindi niyyah inapolenga utakaso kwa ajili ya Mwenyezi Mungu (swt) na ikajiepusha na uchafu wa riya, basi hutukuka kwa sharafu ya radhi na kubuli ya Mwenyezi Mungu (swt). Na pindi nia inapojipaka tope la udanganyifu na riya, huambulia hasira na kukosa radhi za Mwenyezi Mungu (swt). 154. Al Bihaar, juz. 15, uk. 87 155. Al Bihaar, Juz.15, uk. 85 114


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:21 PM

Page 115

Tabia njema kwa mujibu wa Ahlul Bayt (a.s) Kwa sababu hiyo ikhlas imekuwa ni jiwe la msingi katika nyanja za akida na sheria. Na pia imekuwa ni sharti halisi ili vitendo kukubaliwa kwa kuwa ni kwa ikhlas ndiyo matendo yanatimia na kuelekea kwenye utiifu wa Mwenyezi Mungu (swt) na radhi zake. Na ni vyema vilivyoje katika fadhila za ikhlas kwamba inamkomboa mwanadamu na upotofu wa Shetani kama anavyosema: “Kwa utukufu wako, naapa mimi nitawapotosha wote isipokuwa waja wako wenye ikhlasi” (Surat Swad, 38:82-83).

VIZUIZI DHIDI YA IKHLASI Kwa kuwa ikhlasi ndiyo mwenge wenye kuangazia watu taratibu za uchajimungu wa kweli na utumwa hasa, basi Shetani amekuwa ni mwingi wa kuwanyatia watu ili kuwapotosha kwa aina mbalimbali za matamanio na matarajio yenye udanganyifu kama vile; kupenda umaarufu na jaha, kujipatia sifa na utukufu, kuzengea matamanio ya kimada ambayo yanadidimiza dhamiri na kuangamiza vitendo na kuviacha kama jangwa tupu lisilo na dhana (mafuhumi) ya uzuri, ukamilifu na utamu wa kutoa. Na inawezekana ushawishi wa Shetani kwa riya ukawa ni hafifu (usio rahisi kugunduwa) wenye makr (hila). Kwa hiyo mtu anaweza akafanya utiifu na ibada kwa msukumo wa ikhlas lakini ikiwa atachunguza na kuchekecha atakuta hizo amali zake zimechafuliwa na riya. Na hii ni katika mitelezo ya hatari na yenye kujificha sana na udanganyifu kweli. Pekee mawalii wasio na kifani ndiyo wanaoepuka hatari hii. Imehadithiwa kutoka kwa mmoja wa baadhi yao kwamba alisema: “ Kwa miaka 30 nilikuwa nasali msikitini jamaa katika safu ya kwanza. Lakini siku moja kwa udhuru nikachelewa na nikasali katika safu ya pili. Basi nikahisi aibu kwa watu kuniona katika safu ya pili. Kwa hivo nikafahamu ya kwamba kule watu kuniona katika safu ya kwanza kulikuwa kunanifu115


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:21 PM

Page 116

Tabia njema kwa mujibu wa Ahlul Bayt (a.s) rahisha na ilikuwa sababu ya kustarehe kwa moyo wangu�. Tunajikinga na usingizi wa kughafilika na udanganyifu wa riya na ghururi. Kwa sababu hiyo wachamungu (maurafaa) wanapupia kuficha ibada zao na uchaji wao kwa kuogopa hizo kasoro zilizojificha. Imenukuliwa kwamba mmoja katika wachamungu alifunga miaka arobaini na hakuna yeyote aliyeelewa, kwa wake wa karibu na wa mbali. Alikuwa akichukua chakula chake cha mchana na kukitoa sadaka njiani. Kwa hiyo watu wake wa nyumbani wanafahamu ya kwamba amekila sokoni na wale wa sokoni wanajua kwamba amekula nyumbani.

VIPI TUTAPATA IKHLASI Vichochezi na viharakishi vya ikhlasi ni vingi, tunaelezea kwa muhtasari katika nukta zifuatazo: 1. Kuchunguza fadhila za ikhlasi zilizotajwa na ukubwa wa athari zake katika ulimwengu wa akida na imani. 2. Katika vichochezi muhimu vya riya na malengo yake ni kule kutamani kuvuta sifa za watu na kupata ridhaa yao. Na ni kawaida kwamba haiwezekani kuwaridhisha watu, kwa kuwa wenyewe hawawezi kuridhisha nafsi zao wenyewe. Kwa hiyo wakutakwa ridha wa kweli ni Mwenyezi Mungu (swt) ambaye ndiye Mwenye uwezo wa mambo yote na Muweza juu ya kila kitu. Kwa hiyo inafaa kwa mwenye akili kuelekea kwake Mwenyezi Mungu (swt) na kumfanyia Yeye pekee ibada yake na uchaji. 3. Watu hawachelewi kugundua udanganyifu na riya na kuelewa hali halisi ya mtu. Kwa hiyo mwenye kujionesha hachelewi kupata aibu, jambo ambalo linamsababishia kuchukiwa na kudharauliwa.

116


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:21 PM

Page 117

Tabia njema kwa mujibu wa Ahlul Bayt (a.s) Nguo ya riya inaonyesha kile inachokisitiri ukijifunika nguo hiyo basi uko uchi Kwa hiyo ni lazima kwa mtu kujipamba kwa ukweli na ikhlasi na uzuri wa ndani (moyo) ili awe ni mfano bora wa uongofu na wema. Imepokelewa katika hadithi za zamani kwamba; mtu mmoja katika Bani Israil alisema: “Nitamwabudu Mwenyezi Mungu (swt) ibada ambayo nitakumbukwa kwayo”. Akakaa muda na huku akizidisha katika ibada lakini ikawa pindi apitapo mbele ya kundi la watu hunyooshewa kidole na kusemwa: “ Huyu muongo anajionyesha tuu.” Baadae akajirudi nafsi yake na kusema: “ Nimeitaabisha bure nafsi yangu na kupoteza umri wangu katika mambo yasiyo na maana. Sasa inafaa kumtumikia Mwenyezi Mungu (swt). Akafanya amali zake kwa ikhlasi kwa ajili ya Mwenyezi Mungu (swt). Basi ikawa kila apitapo mbele ya watu husema: Huyu mchamungu”.

20. RIYA (KUJIONYESHA) MAANA: Kutafuta jaha na ukuu ndani ya nafsi za watu kwa kuwaonyesha vitendo vya kheri. Ni katika mambo maovu sana tena ni uhalifu wa kutisha sana ambao kwa mwenye ria, matokeo yake ni hasara tupu na kuchukiwa. Kwa ajili hiyo aya na hadithi zimesimama kupiga vita hulka hiyo na kutahadharisha.

QUR’ANI Mwenyezi Mungu anasema kuhusu sifa za wanafiki:

117


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:21 PM

Page 118

Tabia njema kwa mujibu wa Ahlul Bayt (a.s)

“Hakika wanafiki wanataka kumdanganya Mwenyezi Mungu, naye atawaadhibu kwa sababu ya udanganyifu wao. Na wanaposimama kuswali, husimama kwa uvivu kujionyesha kwa watu, wala hawamtaji Mwenyezi Mungu ila kidogo tu.” (Suratun Nisaa, 4:142) Pia akasema:

“ ...Basi yeyote yule anayeterajia kukutana na Mola wake na afanye vitendo vizuri wala asimshirikishe yeyote katika ibada ya Mola wake.” (Suratul Kahf, 18:110) Ama yule anayetoa kwa kujionesha akaonya:

“Enyi mlioamini!Msiziharibu sadaka zenu kwa masimbulizi (masimango) na madhara, kama yule anayetoa mali yake kwa kuonyesha watu, wala hawamwamini Mwenyezi Mungu na siku ya mwisho. Basi 118


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:21 PM

Page 119

Tabia njema kwa mujibu wa Ahlul Bayt (a.s) mfano wake ni kama jiwe lenye mchanga juu yake, kisha likaifikia mvua kubwa na ikaliacha mtupu. Hawawezi kupata kitu katika walichokichuma, na Mwenyezi Mungu hawaongozi watu makafiri.” (Suratul Baqarah, 2:264)

HADITHI Imam Ja’far (a) amesema: Mtukufu Mtume (s) alisema: “Itakuja zama ambapo watu watakuwa kwa ndani ni waovu na kwa nje ni wazuri kwa ajili ya tamaa ya dunia na siyo yale yalio kwa Mwenyezi Mungu (swt). Dini yao itakuwa ni riya na wala haitawaingia hofu ya Mwenyezi Mungu (swt). Basi Mwenyezi Mungu (swt) atawabamiza na adhabu, kisha wamuombe kwa dua ya anayeangamia kwa kuzama, na asiwajibu”. 156 Pia alisema: “Kila ria ni shirk. Hakika yule anayefanya kwa ajili ya watu basi thawabu yake ipo kwa watu, na yule anayefanya kwa ajili ya Mwenyezi Mungu (swt) basi thawabu yake ipo kwa Mwenyezi Mungu (swt).”157 Pia alisema: “Hakuna mja yeyote ambaye anaficha matendo yake ya kheri isipokuwa Mwenyezi Mungu (swt) baada ya muda humdhihirishia kheri; na hakuna mja ambae anaficha matendo ya shari ila baada ya muda Mwenyezi Mungu (swt) humdhihirishia shari.”158 Imam Musa (a) kama alivyopokea kutoka kwa baba zake alisema: Mtume mtukufu (s) alisema: “Baadhi ya watu watapelekwa motoni na Mwenyezi Mungu (swt) 156. Al Waafy, juz. 3 uk. 147 157. Al Waafy, juz. 3 uk. 137 158. Al Waafy, juz.3 uk. 147 119


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:21 PM

Page 120

Tabia njema kwa mujibu wa Ahlul Bayt (a.s) atamwambia Malik: Uambie moto usiwaunguze miguu, walikuwa wakitembea wakienda misikitini, na wala usiwaunguze nyuso, walikuwa wakikamilisha udhu, na wala usiwaunguze mikono, walikuwa wakiinyanyua kwa ajili ya dua, na wala usiwaunguze ndimi kwani walikuwa wakisoma sana Qur’ani. Akasema: Hapo atawaambia Mlinzi wa Moto: Enyi waovu mlikuwa na hali gani? Watajibu: Tulikuwa tukifanya amali zetu kwa ajili ya asiyekuwa Mwenyezi Mungu (swt) kwa hivo tukaambiwa chukueni malipo yenu kwa wale mliokuwa mkifanya amali zenu kwa ajili yao.�159

AINA ZA RIA Migawanyiko ya ria ni kama ifuatavyo kwa muhtasari: 1. Ria ya itikadi: Nayo ni kudhihirisha imani na kuficha ukafiri. Huu ndiyo unafiki ambao ndiyo wenye madhara zaidi katika aina za ria na wenye hatari zaidi kwa Waislamu kwa sababu ya kujificha kwa vitimbi vyake. 2. Ria ya ibada pamoja na kuwa itikadi ni sahihi. Hii ni kwa kufanya ibada mbele ya watu, ili wakuone na huku akiwa peke yake anapuuza. Mfano ni kama vile kujionyesha kwa sala, funga, kurefusha rukuu na sijda, kutulia kwa kusoma na dhikr, kwenda misikitini, kusali jamaa, na mithili ya hayo katika aina za ria. Hapa ndipo mwenye kufanya ria anakuwa ni mwenye madhambi zaidi kuliko yule ambaye hafanyi ibada, kwa kumfanya Mwenyezi Mungu (swt) duni na kuwadanganya walimwengu. 3. Ria ya vitendo. Hii ni kama vile kujionyesha kwa vitendo vya unyenyekevu, kuweka ndevu ndefu, uso kuwa na athari ya sijda, kuvaa mavazi yasiyotamanika na mengine mfano wa hayo katika alama za 159. Al Bihaar, muj. 15, uk. 53 120


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:21 PM

Page 121

Tabia njema kwa mujibu wa Ahlul Bayt (a.s) utawa na kujinyima kwa kujifanya. 4.

Ria ya maneno. Hii ni kama vile kujidai mwenye hekima, kujionyesha kwa kazi ya kuamrisha mema na kukataza maovu, na kukumbusha malipo na adhabu, yote ikiwa ni kiunafiki na kiudanganyifu.

SABABU ZA RIA Zipo sababu zinazomchochea mtu kufanya ria ambazo tunazifupisha kama ifuatavyo: 1. Kupenda jaha. Hii ni katika sababu muhimu zaidi 2. Woga wa kulaumiwa. Hii ndiyo sababu ya ria ya ibada na matendo ya kheri ili kukwepa mapigo ya lawama na kuchunguzwa. 3. Tamaa. Ili kushibisha tamaa yake na kufikia malengo yake, mtu hudanganya kwa ria. 4. Kujificha. Watu waovu hujivika nguo ya wafanya wema ili kuficha maovu yao, na pia ili wasionekane. Hakuna shaka kwamba sababu hizo ni katika hila za Shetani na mitego yake hatari ambayo huwanasa watu kwayo. Atukinge Mwenyezi Mungu (swt) sote.

BAADHI YA UKWELI WA MAMBO Ili kukamilisha somo, ni lazima kuonyesha baadhi ya mambo na kuyaweka wazi: 1.- Wamehitilafiana wahakiki katika kauli zao kuhusu ubora wa kuficha uchamungu au kuudhihirisha. 121


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:21 PM

Page 122

Tabia njema kwa mujibu wa Ahlul Bayt (a.s) Kwa kifupi, hakika ukweli wa vitendo ni nia. Kwa hiyo mtu hapati ila kile alichonuwia. Ikiwa mtu kasafika na ria, basi ni sawa kwake kuweka wazi au kuficha matendo yake. Ama yule aliyechafuliwa na ria, pia ni sawa kuficha au kudhihirisha. Wakati mwingine huenda ikawa ni vyema kuficha. Hii ni kwa wale ambao hawawezi kujizuia na ria kwa kuwa katika hali ya dhahiri msukumo wa ria ni mkubwa. Wakati mwingine inakuwa ni vyema kuonyesha uchaji ikiwa mtu kaweza kujiepusha na ria na akakusudia lengo nzuri kama vile kuwavutia watu katika kheri na kuwasukuma kuiga mfano bora. 2. Yule atakayelenga ikhlasi katika uchaji wake, lakini pindi watu walipojua ukweli wake, akahisi raha moyoni mwake, basi hilo haliharibu katika ikhlasi yake kitu ikiwa chimbuko la furaha yake ni kuhisi kwake neema ya Mwenyezi Mungu (swt), Yeye kamdhihirishia mema yake na amemsitiria maovu yake kwa ukarimu wake. Imam Baqir (s) aliwahi kuulizwa kuhusu mtu anayefanya jambo la kheri, akaonekana, kisha akahisi furaha kwa hilo. Akajibu: “Hakuna ubaya ikiwa hakufanya hilo kwa ajili ya hayo; kwani hakuna yeyote ila anataka Mwenyezi Mungu (swt) adhihirishe ya kheri kuhusu yeye baina ya watu�.160 3. Kwa kuwa Shetani (l.a) ni mwenye juhudi kubwa katika kuwapotosha watu na kuwazuia na miradi ya kheri na uchaji kwa aina mbalimbali za vitimbi na upotoshi ni lazima mtu kuchukua tahadhari na kujikinga nae. Ni yeye ndiye huwashawishi watu kuacha ibada na uchaji. Akishindwa hilo, basi huwadanganya kwa ria na kuipendezesha kwao. Na akishindwa hili na lile basi huvuvia ndani ya nyoyo zao kwamba ni wenye ria katika amali zao ili awaghilibu kuacha vitendo vyao na kutovijali. 160. Al Waafy, juz. 3, uk. 148 122


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:21 PM

Page 123

Tabia njema kwa mujibu wa Ahlul Bayt (a.s) Ikiwa hali ndiyo hii, basi ni wajibu kumfukuza, na kutojali udanganyifu na wasiwasi wake kwa kuwa mtu mukhlis hayamdhuru mawazo kama hayo. Imam Sadiq (a) kutoka kwa baba yake (a); hakika Mtukufu Mtume alisema: “Shetani pindi atakapomjia mmoja wenu na yumo katika sala na akamwambia wewe unajionyesha, basi na airefushe sala yake kadri atakavyoona, madama wakati wa faradhi haukumponyoka. Hivyo hivyo afanye ikiwa anashughulikia jambo la akhera. Ama akiwa katika mambo ya dunia basi apumzike…”161

MABAYA YA RIA Ria ni katika tabia mbaya na kasoro zinazochukiza ambazo zinaashiria udhaifu wa nafsi na ugonjwa wa dhati na uelewa mfinyu na hii ni kwa kuwa ni njia ya hadaa na udanganyifu ambayo hutumiwa na vigeugeu na wapotofu kufikia malengo yao bila aibu ya kwamba jambo hilo ladhalilisha dini, na utukufu wa nafsi. Yamtosha mwenye kujionesha ubaya kwamba amefanya uovu mara mbili: kusimama dhidi ya Mwenyezi Mungu (swt) na kupuuza utukufu Wake kwa kuwapa kipaumbele viumbe kuliko Yeye katika kujikurubisha na kuwahadaa watu na kuwazuga kwa unafiki na ria. Na mfano wa mwenye ria katika upumbavu na utovu wa aibu ni kama vile mtu amekaa mbele ya mfalme mtukufu akiwa amedhihirisha ufuasi na ikhlasi kisha akamdanganya kwa kuwataka vijakazi wake au kuwavutia vijana wake. Bila shaka mtu huyu anastahili adhabu kali ya mfalme kwa sababu ya umalaya wake. Bila shaka mwenye ria ni mwenye uovu zaidi na dhambi kuliko huyo, kwa kuwa yeye anamdhalilisha Mwenyezi Mungu 161. Al Bihar, muj. 15, uk. 52 123


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:21 PM

Page 124

Tabia njema kwa mujibu wa Ahlul Bayt (a.s) (swt) na kuwadanganya waja Wake. Baada ya yote haya mwenye ria daima ni mwenye huzuni na matatizo. Anataka kuzivutia nyoyo za watu na kurandia ridhaa yao na ole wake kwani kuwaridhisha watu ni lengo lisilofikiwa. Kwa hiyo baada ya kuhangaika sana hujikuta kaambulia patupu mwenye hasara, kapoteza utukufu na dini. Na katika mambo thabiti ni kwamba uovu ndani ya nafsi hauchukui muda kujifichua na kumuacha mtu mwenye fedheha na hasara. Mshairi anasema: Tabia yeyote ile atakayokuwa nayo mtu, Itajulikana hata kama atafikiria watu hawatajua Hili Mtume (s) amelielezea pindi aliposema: “Anayeficha siri, Mwenyezi Mungu (swt) humvika joho la siri hiyo, ikiwa ni kheri basi huwa ni kheri, na ikiwa ni shari basi huwa ni shari�.162

TIBA YA RIA Baada ya kujua mabaya ya ria ni vyema tukaweka wazi nasaha muhimu za kiakhlaqi katika kutibu na kuifyeka. Na katika somo kuhusu ikhlasi tumegusia kidogo kuhusu mabaya ya ria na mema ya ikhlasi. Basi rejea.

TIBA YA RIA KIVITENDO. Tiba hiyo ni kwa kuzingatia nasaha zifuatazo: 1. Kumhukumu shetani na kuangamiza vitimbi vyake na hulka yake ya kujionesha kwa njia ya kimantiki inayokinaisha nafsi na kuridhisha dhamiri. 2. Kumzuia Shetani na kufukuza mara moja fikra zake kuhusu kujionyesha na kutegemea yale ambayo amejipamba nayo muumini ya kupenda ikhlasi na kuchukia ria. 162. Al waafy, juz. 3, uk. 147 124


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:21 PM

Page 125

Tabia njema kwa mujibu wa Ahlul Bayt (a.s) 3. Kujiepusha na fursa za ria na vidhihirisho vyake, na hili kwa kuficha ibada na utiifu na kuzisitiri wasijue watu hadi pale ambapo mtu atakapo jiamini nafsi yake na kujenga ikhlasi. Na katika yaliyozungumzwa kuhusu ria ambayo si ya kawaida ni kama haya: Bedui mmoja aliingia msikitini na akaona mtu anasali kwa unyenyekevu, basi hilo likamvutia na akasema: Ni vyema vilivyoje unavyosali? Yule bwana akasema: Pia nimefunga, na hakika sala ya mwenye kufunga ni bora sana kuliko ya yule asiyefunga. Basi yule bedui akamwambia: Tafadhali nichungie ngamia wangu huyu, hadi nitakapomaliza haja yangu. Alipotoka yule bedui ili kukidhi haja yake, huyu bwana akampanda ngamia na kutokomea. Yule bedui aliporejea akakuta hakuna mtu wala ngamia. Akamuulizia, bila mafanikio. Akatoka na huku akisema: Alisali na kunivutia, na akafunga na kunikusudia mimi, kumbe kusali na kufunga kote ni kwa ajili ya kupata ngamia?! Bedui mmoja alisali sala hafifu. Imam Ali (a) akamsimamia na fimbo na kumuambia: Rejea tena usali vyema. Alipomaliza kusali, Imam akamuuliza: Ipi bora, hii uliyosali vyema au ile ya mwanzo? Akajibu bali ile ya mwanzo! Imam akauliza: Kwa nini? Akajibu: Kwa sababu ile ya mwanzo ilikuwa kwa ajili ya Mwenyezi Mungu (swt), ama hii ya pili ni kwa ajili ya kuogopa mkwaju!

21.- KUJISIKIA, GHURURI (‘UJB) MAANA YAKE Ni mtu kuiona nafsi yake ni adhimu, tukufu kwa kuwa na sifa ya utukufu, kipawa kama vile elimu, mali, jaha na vitendo vyema. Kujiona kunatofautiana na kiburi. Kujiona ni mtu kuiona nafsi ni tukufu, ama kiburi zaidi ya hilo kunakujikweza juu ya wengine. 125


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:21 PM

Page 126

Tabia njema kwa mujibu wa Ahlul Bayt (a.s) Kujiona ni katika sifa mbaya na tabia zinazochukiza zinazoashiria uduni wa nafsi na ufinyu wa upeo na ufidhuli wa tabia. Sheria imelikataza hilo na kulitahadharisha.

QUR’ANI Mwenyezi Mungu (swt) anasema: “...Basi msijitakase nafsi zenu, Yeye anamjua sana anayetakasika.” (Najm, 53:32)

HADITHI Imam Baqir (a) alisema: “Matatu ni yenye kuvunja mgongo (yenye kuangamiza): Mtu ambaye anaona vitendo vyake ni vingi, kisha akasahau madhambi yake na kughurika na rai yake (kuona rai yake ni bora)”163 Kutoka kwa Imam Sadiq (a) kama alivyopokea kwa baba zake (a) alisema: “Yule ambaye kujiona kunamwingia ataangamia”.164 Pia alisema (a): “Iblis (l.a) aliwaambia majeshi yake: Ninapokuwa na uwezo juu ya mwanadamu katika matatu basi sijali anafanya nini, kwani hakubaliwi amali zake nayo ni pindi matendo yake yanakuwa mengi halafu akasahau madhambi yake na akaingiliwa na kujiona”.165 Pia alisema: “Mtu mmoja aalim (mjuzi mwenye elimu) alimjia mtu mmoja aabid (mwingi wa kuabudu) na kusema: Vipi sala yako? Akajibu: Mfano wa mtu kama mimi huulizwa kuhusu sala yake, wakati mimi namuabudu Mwenyezi Mungu (swt) toka enzi kadha wa kadha!? Yule aalim akauliza: Vipi kuhusu kulia kwako? Akajibu: Nalia mpaka majozi yangu yanabubujika. Yule 163. Rej. 35 164. Al Waafy, juz. 3, uk. 151 165. Al Bihar, muj. 15, juz. 3 126


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:21 PM

Page 127

Tabia njema kwa mujibu wa Ahlul Bayt (a.s) aalim akamuambia: Kucheka kwako na huku ukiwa ni mwenye kuogopa ni bora kuliko kulia kwako na huku wewe ni mwenye kujiona, hakika mwenye kujiona hakuna chochote kinachokubaliwa katika amali yake”.166 Pia alisema: Mtume wa Mwenyezi Mungu (s) alisema:“Isingekuwa kwamba dhambi ni bora kwa muumini kuliko kujiona, Mwenyezi Mungu (swt) asingejitoa baina ya mja wake muumini na dhambi abadan”.167 Pia kutoka kwa mmoja wa Maimamu wawili hawa alisema: “Watu wawili waliingia msikitini, mmoja ni mswalihina (mtaabid) na mwingine muovu (fasiqi). Lakini wakatoka msikitini na huku yule fasiki ni swiddiqi (mkweli wa daraja ya juu) na yule mtaabid ni muovu. Na hii ni kwa sababu yule mtaabid aliingia msikitini na huku ni mwenye kujiona kwa ibada yake, ikawa fikra yake yote katika hilo, na ama yule muovu fikra yake ikawa ni katika kujuta kuhusu uovu wake na akawa ni mwenye kumuomba Mwenyezi Mungu (swt) msamaha kwa kukumbuka madhambi yake.”168 Ni muhimu kukumbuka kwamba kujiona kuliko kubaya ni kule mtu kuona amali yake njema kuwa ni nyingi na kujionyesha kwayo. Ama kuwa na furaha ya kazi yako na huku ukinyenyekea kwa Mwenyezi Mungu (swt) na kumshukuru kukuwezesha kumtii, hilo halina ubaya bali ni jambo la kusifiwa.

MAOVU YA KUJIONA Kujiona kuna madhara na maovu: 1. Husababisha ubinafsi na kiburi, kwani yule anayejisikia humfanya awe na kiburi na kujikweza juu ya watu na kuwatenza nguvu. Hili husababisha watu kumchukia na kumuona duni. 166. Al Waafy, juz. 3, uk. 151 167. Al Bihar, muj. 15, juz.3 168. Al Waafy, juz. 3, uk. 151 127


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:21 PM

Page 128

Tabia njema kwa mujibu wa Ahlul Bayt (a.s) 2. Humfanya mtu asione mapungufu yake na maovu na hivyo basi kutoweza kuipamba nafsi yake na kupambana na mapungufu yake mambo ambayo yanamfanya kuogelea ndani ya dimbwi la ujahili na kubaki nyuma. 3. Hupelekea mtu kuona utiifu wake kuwa mwingi na kujionyesha kwawo, nakujisahaulisha madhambi na maovu. Katika hilo kuna madhara makubwa kwani linazuia mtu kutubia na kurejea kwa Mola Wake na hivyo kustahili adhabu na ghadhabu ya Mwenyezi Mungu (swt), na kukosa kubuli na ridhaa Yake.

TIBA YA KUJIONA Kwa kuwa kujiona na kutakabari (kuwa na kiburi) ni mapacha wenye asili moja ingawa kuna hitilafu katika mwelekeo - ‘ujb’ (kujiona), mtu kuiona nafsi yake ni tukufu bila na kuwepo kujikweza na kutakabari viko pamoja - kwa hiyo tiba yake ni moja na hili tumeliweka wazi katika mlango wa kutakabari. Ni vyema kwa mwenye kughurika na nafsi yake akadiriki kwamba vipawa mbalimbali na fadhila alizonazo, vitu ambavyo vinampelekea kujihisi bora, ni neema za Mwenyezi Mungu (swt) ambazo huzitoa kwa amtakaye katika waja wake. Kwa hivyo ni vyema mja akashukuru neema hizo na siyo kujisikia bora na kujiona. Pia neema, vipawa, fadhila vipo chini ya kudra na mabalaa ya maisha (hujafa hujaumbika). Kwa hivyo basi kwa nini mwanadamu ajisikie na kujiona?!! Katika ya ajabu yaliyonakiliwa kutoka kwa watu wema kuhusu kurekebisha hisia za kujiona: 128


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:21 PM

Page 129

Tabia njema kwa mujibu wa Ahlul Bayt (a.s) Mmoja wao alitoka usiku akienda kuzuru sehemu takatifu kwa ajili ya ibada na ziyara. Alipokuwa njiani, hali ya kujisikia ikamjia kwa kule yeye kutoka usiku uliyopindukia (karibu na alfajiri) na kuacha ladha ya kitanda na utamu wa usingizi kwa ajili ya ibada. Mara akatokeza muuza shaljam (aina ya mbegu zenye kutoa mafuta). Akamuendea na kumuuliza: Kiasi gani unapata faida kwa kuhangaika kwako usiku kama huu? Akamjibu: Napata dirhamu mbili au tatu. Basi akajirudi mwenyewe na kujizungumza: Nini kisa na maana ya kujiona wakati thamani ya kutoka kwangu usiku hakuzidi dirhamu mbili wala tatu?! Mwingine naye, siku za Lailatul-Qadr, alifanya amali nyingi (sala, dua na nyiradi mbalimbali) kiasi cha kuamsha hisia za kujiona. Ili kutibu hali hiyo akatumia hekima. Aliwauliza baadhi ya mutaabid: Ni kiasi gani unachotoza kwa kutekeleza amali za usiku huu nazo ni kadha wa kadha. Yule mtaabid akajibu: Nusu ya dinari. Basi huyu mchamungu akarejea kwenye nafsi yake na kujikaripia na kujitanabahisha: Nini kisa na maana ya kujisikia kwako wakati kiwango cha amali yako yote ni nusu ya dinari?!

22. YAQINI MAANA Ni kuitakidi misingi ya dini na yote ya muhimu katika dini kwa itikadi thabiti isiyotikiswa na shaka, inayokubaliana na ukweli wenyewe. Ikiwa haikubaliani na ukweli basi huo ni ujahili uliyokubuhu. Yaqini ndiyo ya kwanza katika fadhila za nafsi. Pia yaqini ndiyo bora ya vipawa vya Mwenyezi Mungu (swt) na alama ya mwamko na ukamilifu na njia ya mafanikio duniani na akhera. Kwa hiyo sheria imetilia sana umuhimu tabia hiyo na kuwatukuza wenye tabia hiyo kwa sifa nzuri kama zinavyoonyesha hadithi chache zifwatazo:

129


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:21 PM

Page 130

Tabia njema kwa mujibu wa Ahlul Bayt (a.s)

HADITHI Imam Sadiq (a) alisema: “Imani ni bora kuliko Uislamu, na yaqini ni bora kuliko imani na hakuna kitu kitukufu kama vile yaqini”.169 “Hakika amali ndogo ya kudumu ikiwa na yaqini, ni bora kwa Mwenyezi Mungu (swt) kuliko amali nyingi pasi na yaqini”.170 “Katika usahihi wa yaqini ya mtu mwislamu ni kwamba asiwaridhishe watu na kumuudhi Mwenyezi Mungu (swt), na pia asiwalaumu (watu) kwa yale ambayo Mwenyezi Mungu (swt) hakuwapa. Hakika riziki haipatikani kwa tamaa ya mwenye tamaa, na wala hairudishwi na chuki ya mwenye chuki. Lau angekimbia mmoja wenu riziki yake kama vile anavyokimbia mauti, basi ingemfikia tuu kama vile yatakavyomfika mauti.” “Mwenyezi Mungu (swt), kwa uadilifu Wake, amejalia furaha na raha katika yaqini na kuridhia na akajalia majonzi na huzuni katika shaka na kutoridhika”.171 “Alikuwa (Ali) Amiri wa waumini (a) akisema: Mja hatopata utamu wa imani hadi pale atakapojua kwamba lililomsibu halikua limkose na lile lililomkosa halikuwa limfike. Na hakika mwenye kudhuru na kunufaisha ni Mwenyezi Mungu Aliye juu”.172 “Mtume wa Mwenyezi Mungu (s) aliwasalisha watu sala ya asubuhi na akamuona kijana msikitini, kichwa chake kinayumba (kwa usingizi), rangi yake imekuwa njano, mwili wake umekonda na macho yake yametum169. Al Bihar, muj. 15, juz.2, uk. 57 170. Al Bihar, muj. 15, huz. 2, uk. 60 171. Al Waafy, juz. 3, uk. 54 172. Al Waafy, juz. 3, uk. 54 130


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:21 PM

Page 131

Tabia njema kwa mujibu wa Ahlul Bayt (a.s) bukia. Mtume akamuambia: Ewe fulani, umeamkamje? Akajibu: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, nimeamka ni mwenye yaqini. Mtume akashangaa na kumuambia: Hakika kila yaqini ina ukweli. Yaqini yako ina ukweli upi? Akajibu: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, ni yaqini yangu ndiyo imenihuzunisha, na kunikeshesha usiku na kuniweka na kiu mchana wa jua kali. Basi nimeinyima nafsi yangu dunia na vilivyomo, kiasi cha kwamba kama vile naiona Arshi ya Mola Wangu imesimamishwa kwa ajili ya hesabu na watu wote halaiki wamefufuliwa kwa ajili ya hilo nami nikiwemo. Nimekuwa kama vile naona watu wa peponi wananeemeka na kufahamiana na huku wakiegemea kwenye makochi, pia ni kama vile naona watu wa motoni nao humo wanaadhibiwa, wamesimamishwa kwa mstari. Hivi sasa ni kama vile nasikia sauti ya moto ikizunguuka katika masikio yangu. Mtume (s) akawaambia masahaba wake: Huyu ni mja ambaye Mwenyezi Mungu (swt) ameangazia moyo wake kwa imani. Kisha akamuambia (yule kijana): shikilia hayo uliyonayo. Yule kijana akamuambia Mtume (s): Niombee kwa Mwenyezi Mungu ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu nipate shahada nikiwa pamoja nawe. Basi Mtume (s) akamuombea na haikupita muda akatoka katika baadhi ya vita na Mtume (s) na akatunukiwa shahada baada ya watu tisa, yeye akiwa wa kumi.”173 Imam Ridha (a) aliulizwa kuhusu mtu anayesema kweli lakini anajifanyia israfu, anakunywa pombe na anafanya mengine madhambi makubwa na mwingine asiyefanya hayo lakini hana yaqini. Akajibu: “mwenye yaqini zaidi ni kama vile aliyelala kwenye njia sahihi. Akiamka anaendelea… ama yule mwenye yaqini hafifu ni kama vile aliyelala nje ya njia. Akiamka hajui njia iko wapi”.174

SIFA ZA WENYE YAQINI Pindi inapochanua nafsi kwa yaqini, na kuangaziwa na miale yake yenye nuru, basi wenye yaqini huakisi rangi za uzuri na ukamilifu wa kinafsi na 173. Al Waafy, juz. 3, uk.33 174. Safinatul Bihar, juz. 2, uk. 734 131


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:21 PM

Page 132

Tabia njema kwa mujibu wa Ahlul Bayt (a.s) kuwapandisha hadi kufikia upeo wa juu wa kiroho na kuwafanya wao ni wenye kumetameta kama vile nyota, wakijitenga wao na watu wengine kama vile kito chenye thamani hujitenga na changarawe. Katika sifa na vipawa vyao vyema vilivyo wazi ni kwamba utawakuta ni wenye kujitahidi kujipamba kwa tabia njema na vitendo vyema na kujiepusha na vile viovu na duni. Hawaghilibiwi na mapambo ya dunia na wala hayawapotoshi na juhudi zao za kuongeza uwezo wao wa kiroho kwa lengo la kufikia daraja za juu na furaha inayotarajiwa kesho akhera. Utawakuta ni watu ambao wamejisalimisha kabisa katika kumcha Mwenyezi Mungu (swt) kwa kutaka radhi zake na malipo mema, pia ni wenye kumtegemea Mwenyezi Mungu (swt) katika raha na shida, hawamtarajii wala kumwogopa yeyote yule ila Yeye, kwa kuwa na yaqini ya uzuri wa uendeshaji na hekima ya matendo ya Mwenyezi Mungu (swt). Kwa sababu hiyo, dua zao hujibiwa na karama zao hudhihiri, na kufadhiliwa utukufu na uangalizi kutoka kwa Mwenyezi Mungu (swt).

DARAJA ZA IMANI Ni vyema kwa kuwa nazungumzia suala la yaqini nikagusia kidogo baadhi ya maana za imani pamoja na daraja zake na pia aina zake ili kukamilisha somo na kuwapa mwanga zaidi waumini. Watu wanazidiana kwa kiwango kikubwa katika daraja za imani. Kati yao kuna yule ambae ni mbora wa juu katika uwanja wa imani, na mwingine duni anayezorota na yupo mwingine kati ya hao kama vile inavyotoa picha hadithi ifuatayo: Imam Sadiq (a) alisema: “Hakika imani ina daraja kumi kwa mithili ya ngazi, hupandwa daraja baada ya daraja. Na aliye kwenye daraja ya pili asimuambie aliye kwenye daraja ya kwanza wewe huko kokote hadi pale atakapomaliza daraja ya kumi. Kwa hivyo usimuachie aliye chini yako wakakuachia waliojuu yako. 132


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:21 PM

Page 133

Tabia njema kwa mujibu wa Ahlul Bayt (a.s) Na ukimuona aliye chini yako kwa daraja moja basi mpandishe kwako kwa upole na wala usimbebeshe lile asiloliweza ukamvunja, kwani yeyote anayemvunja muumini ni juu yake kumuunganisha (kumfidia hadi mambo yake kurejea sawa).”175

AINA ZA IMANI Imani imegawanyika katika aina tatu: ya kimaumbile (fitwry), iliyowekwa (mustawda’) na ya kuchuma (kasby). 1. Imani ya kimaumbile ni ile ambayo ni tuzo kutoka kwa Mwenyezi Mungu (swt), ameumbwa nayo mwanadamu, kama vile kwa mitume na mawasii (a). Hakika wao ni mfano wa juu kabisa kuhusu nguvu ya imani na ukamilifu wa yaqini. Wao hawasumbuliwi na shaka wala kuingiliwa na wasiwasi. 2. Imani iliyowekwa ni ile ambayo isiyokolea, haina mizizi, ipo juu ya ulimi, ambayo haraka inatikiswa na shaka na wasiwasi kama vile alivyosema Imam Sadiq (a): “Hakika mja huamka akiwa ni muumini na mchana ukampitia ni kafiri na pia akaamka ni kafiri na mchana ukampitia ni muumini na wako watu wanaovua imani kisha wakaivaa hao huitwa wenye kuvua”.176 Pia alisema: “Hakika Mwenyezi Mungu (swt) aliwaandaa mitume kimaumbile kwenye utume wao. Hawawezi abadan wakaritadi, pia akawaandaa mawasii kwenye uwasii wao, kamwe hawaritadi, pia (hivyo hivyo) baadhi ya waumini wamepewa kimaumbile imani, hawawezi kuritadi asilani. Na wapo ambao wamekopeshwa imani, ikiwa ataomba dua na kushikilia kwa mkazo, basi atakufa kwenye imani”.177 175. Al Waafy, juz. 3, uk. 30 176. Al Waafy, juz.3, uk. 50 177. Al Waafy, juz. 3, uk. 50 133


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:21 PM

Page 134

Tabia njema kwa mujibu wa Ahlul Bayt (a.s) Katika hadithi ifuatayo, Imam Sadiq (a) ameweka tofauti baina ya imani thabiti na ile iliyowekwa, alisema: “Hasara, majuto na maangamio yote ni kwa yule ambaye asiyefaidika na yale aliyoyaona na asijue ni jambo gani ambalo lipo juu yake, ni lenye kunufaisha au madhara. Mwenye kurawi (kusimulia hadithi) akauliza: kati ya hawa, ni kwa jambo gani atajulikana mwenye kuokoka? Akajibu: “yule ambaye matendo yanawafikiana na kauli, basi huyo mthibitishieni ushuhuda wa uokovu, na ama yule ambaye matendo yake ni tofauti na kauli yake, basi huyo ndiyo (mwenye imani) iliyowekwa.”178 3. Imani ya kuchuma ni imani hafifu ya kimaumbile ambayo mwenye kuwa nayo ameikuza na akaongeza kiwango chake hadi kukamilika na kupanda hadi daraja la juu. Nayo ina daraja na viwango. Haya ni baadhi ya wasia na nasaha kwa ajili ya kulinda ile imani ya maumbile na kuwezesha kupatikana ile ya kuchuma: 1. Kusuhubiana na waumini wema, na kujiepusha na watu waasi, waovu kwa kuwa mtu huathirika na sahiba yake na kuchukuwa katika tabia na hulka yake. Mtukufu Mtume (s) alisema: “Mtu hufuata mwenendo (dini) wa rafiki yake mpenzi, kwa hivyo na achunguze mtu gani wa kuwa rafiki yake”. 2. Kuacha kutizama vitabu vya upotofu na kusikiliza maneno ya wapotoshaji ambao wamepagawa na uovu wa kutia sumu fikra za watu na kuwaondoa katika itikadi na sheria za kiislamu na pia kuharibu mihimili ya imani na mafahimu yake (dhana, maana inayofahamika) katika nafsi zao. 3. Kufanya zoezi la kuchunguza na kutafakari kuhusu viumbe vya Mwenyezi Mungu (swt), kwa kuzingatia uzuri wa maumbile, ukamilifu wa nidhamu, na hekima ya uendeshaji inayostaajabisha. Mwenyezi Mungu anasema: 178. Kama hapo juu. 134


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:21 PM

Page 135

Tabia njema kwa mujibu wa Ahlul Bayt (a.s)

“ Na katika ardhi zimo dalili kwa wenye yakini. Na katika nafsi zenu, je hamuoni? (Ad Dhaariyaat, 51:20-21) 4. Katika mambo yanayosababisha imani na upatikanaji wake ni; jihadi ya nafsi na kuituliza katika kumtii Mwenyezi Mungu (swt) na kujiepusha kumuasi ili nafsi iimarike kwa mafahimu (dhana) ya imani na kung’ara kwa nuru yake. Nafsi ni kama vile maji safi ambayo hubaki ni yenye uangavu (kupitisha mwanga) na kumetameta maadamu hayakuchafuliwa na uchafu. Kama isingekuwa kutu ya madhambi na uchafu wa maovu ambavyo vinaharibu nyoyo na nafsi – na hivyo uzuri wake na nuru kuondoka - basi wengi wangepata nuru kwa imani na nafsi zao kung’ara kwa miale yake yenye nuru. Mwenyezi Mungu (swt) anasema:

“Na kwa nafsi na kwa yule aliyeitandaza. Kisha akaifahamisha uovu wake na wema wake. Bila shaka amefaulu aliyeitakasa. Na bila shaka amepata hasara mwenye kuitweza.” (Suratu Shams, 91: 7-10) Imam Sadiq (a) alisema: “Pindi mtu anapofanya dhambi, hutokeza ndani ya moyo wake doa jeusi; ikiwa atatubu, basi hufutika. Ama akizidi (madhambi) nalo huzidi hadi huenea moyo wote, basi hapo hawezi tena kufuzu”. 179

179. Al Waafy, juz. 3, uk. 167 135


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:21 PM

Page 136

Tabia njema kwa mujibu wa Ahlul Bayt (a.s)

23. SUBIRA MAANA Kuvumilia matatizo (shida, balaa, hasara…) pasi na kutapatapa (huzuni, kulalamika…) kwa maana nyingine ni; kuilazimisha nafsi kufuata yale yanayotakiwa na sheria na akili iwe ni amri au makatazo. Subira ni dalili ya busara na hekima, upana wa upeo, utukufu wa tabia, ushujaa uliokomaa na ustahamilivu. Pia ni chombo cha kupandisha uchamungu na kumridhisha Yeye (swt), sababu ya kufuzu na ngao inayolinda dhidi ya kicheko cha maadui na mahasidi.

QUR’ANI Ni utukufu ulioje kuhusu subira na wenye kusubiri, kiasi kwamba Mwenyezi Mungu (swt) amewasifu na kuwabariki sehemu zaidi ya sabini katika Qur’ani. Amewabashiria wenye subira radhi na upendo na kuwaahidi msaaada kama katika aya zifuatazo:

“Na Manabii wangapi (ambao) Wanachuoni wacha Mungu walipigana pamoja nao, na hawakulegea kwa yale yaliyowapata katika njia ya Mwenyeezi Mungu, wala hawakudhoofika wala hawakudhalilika, na Mwenyezi Mungu huwapenda wenye kusubiri.” (Sura Aali Imraan, 3:146) 136


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:21 PM

Page 137

Akhalaq Ahlul Bayt

“Na mtiini Mwenyeezi Mungu na Mtume wake wala msigombane, msije mkavunjika mioyo na kupoteza nguvu zenu, na vumilieni, bila shaka Mwenyezi Mungu yu pamoja na wenye kuvumilia.” (Sura Anfaal, 8:46) Pia Mwenyezi Mungu (swt) amewatunukia thawabu nyingi kama ilivyo katika sura:

“Sema: Enyi waja wangu mlioamini! mcheni Mola wenu, wale wafanyao wema katika dunia hii watapata wena, na ardhi ya Mwenyezi Mungu ina wasaa, bila shaka wanaofanya subira watapewa malipo yao pasipo hesabu.” (Zumar 39:10) Pia akawabubujia kila aina ya msaada na upole kama katika sura:

“Na kwa hakika tutawajaribuni kwa jambo la khofu na njaa na upungufu wa mali na nafsi na matunda, nawe wape habari ya furaha wenye 137


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:21 PM

Page 138

Tabia njema kwa mujibu wa Ahlul Bayt (a.s) kusubiri. Ambao ukiwafikia msiba, husema: Hakika sisi ni wa Mwenyezi Mungu na sisi tu ni wenye kurejea kwake. Hao juu yao ziko baraka na rehema kutoka kwa Mola wao, nao ndio wenye kuongoka.” (Suratul Baqara, 2:155-157)

HADITHI Ama Hadithi kutoka kwa Ahlul Bayt (a) ni nyingi: Imam Sadiq (a) alisema: “Subira kwa imani ni kama vile kichwa kwa mwili, kichwa kikiondoka basi na mwili huondoka na ndivyo ikiondoka subira, imani huondoka”.180 Imam Baqir (a) alisema: “Pepo imezungukwa na matatizo (masaibu, shida, mateso…) na subira. Yeyote atakayesubiri wakati wa matatizo hapa duniani basi ataingia peponi. Nayo Jahannamu imezungukwa na anasa na matamanio. Yeyote atakayeisabilia nafsi yake anasa na matamanio basi ataingia motoni”.181 Pia alisema: “Pindi mauti yalipomkurubia baba yangu, alinikumbatia kifuani mwake na kusema: Ewe mwanangu! Subiri kwenye haki hata kama itakuwa chungu, utapewa malipo yako pasi na hisabu”. 182 Imam Sadiq (a) alisema: “Yeyote miongoni mwa waumini atakayeonjwa kwa mtihani kisha akasubiri basi malipo yake ni sawa na ya mashahidi elfu moja”.183 Na huenda akauliza mtu: vipi mwenye kusubiri apewe malipo ya mashahidi elfu moja, wakati wao ndio mabingwa wa kusubiri kwenye jihadi na 180. Al Waafy, juz. 3, uk. 65 181. Kama hapo juu 182. Kama hapo juu 183. Al Waafy, juz. 3, uk. 66 138


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:21 PM

Page 139

Tabia njema kwa mujibu wa Ahlul Bayt (a.s) kujitoa muhanga? Muradi wake ni kwamba: mwenye kusubiri anastahiki malipo ya hao mashahidi pamoja na kuwa malipo yao kwa Mwenyezi Mungu (swt) ni maradufu. Imam Ali (a) alisema: “Yule ambaye subira haitamwokoa basi kutapatapa kutamwangamiza�.184

AINA ZA SUBIRA Subira inagawanyika katika aina mbalimbali kwa kutegemea hali na mahitaji. Zilizo muhimu ni: Subira kwenye matatizo na misiba (ya kupotelewa nafsi na mali). Hii ndio aina ya subira kubwa kuliko zote, pia ndio mafhumi iliyo tukufu zaidi yenye kuashiria utukufu wa nafsi, kujimiliki nafsi na uthabiti wa uamuzi. Mwanadamu ni shabaha ya matatizo na misiba mikubwa ambayo humfika kwa kumtenza nguvu na bila ya kutarajia na hujikuta hana uwezo wala nguvu kukabiliana nayo. Lililo kheri analolifanya mtahiniwa ni kutumia njia ya kusubiri. Hakika subira ndiyo kitulizo cha roho zilizoumia na faraja ya nafsi zenye mateso. Kama siyo subira basi mwanadamu angeangamia kwa ajili ya huzuni na maumivu. Kwa sababu hiyo aya na hadithi zimetilia mkazo mtu kujipamba kwa subira na kushikamana nayo. Mwenyezi Mungu (swt) anasema:

184.Nahjul Balagha 139


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:21 PM

Page 140

Tabia njema kwa mujibu wa Ahlul Bayt (a.s)

“Na kwa hakika tutawajaribuni kwa jambo la khofu na njaa na upungufu wa mali na nafsi na matunda, nawe wape habari ya furaha wenye kusubiri. Ambao ukiwafikia msiba, husema: Hakika sisi ni wa Mwenyezi Mungu na sisi tu ni wenye kurejea kwake. Hao juu yao ziko baraka na rehema kutoka kwa Mola wao, nao ndio wenye kuongoka.” (Suratul Baqarah, 2: 155-157) Imam Ali (a) alisema: “Ukiamua kusubiri qadari itachukua mkondo wake ukiwa ni mwenye kulipwa, na ukitapatapa, qadari (vivyo hivyo) itachukua mkondo wake ukiwa ni mwenye kutingwa”.185 Ni muhimu kutaja hapa kwamba subira inayokubalika iliyo njema na yenye kusifiwa ni ile ya mtu kusubiri katika matatizo ambayo hawezi kuyaondosha na kujinasua nayo, kama vile kumpoteza kipenzi, kunyanng’anywa mali au kuwindwa na adui… Ama kujisalimisha mbele ya matatizo na kusubiri wakati mtu ana uwezo wa kujikinga na kuyaondoa, hilo ni upumbavu usiyokubaliwa na uislamu. Mfano kusubiri kwenye ugonjwa wakati mtu anaweza kupata matibabu, kusubiri kwenye umaskini wakati unaweza kupata riziki yako, kusubiri wakati haki zako zinamezwa na huku unaweza kuzirejesha na kuzihifadhi. Ni wazi kwamba lile linalomzuia mtu na fadhila ya subira na kumvua ustahamilivu ni kule kutapatapa kulikopindukia, hali ambayo inapelekea nyoyo kuvunjika, kujipiga uso na kupindukia katika kulalamika na kunung’unika.

185. Kama hapo juu 140


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:21 PM

Page 141

Tabia njema kwa mujibu wa Ahlul Bayt (a.s) Ama maumivu ya nafsi na kuyatuliza kwa kulia au kulalamika kutokana na taabu na maumivu ya ugonjwa, haya ni katika dharura za hisia hai na tukufu kama alivyosema Mtume (s) pindi alipofariki mwanae Ibrahim: “Macho yanalia, moyo unahuzunika, lakini hatuneni yanayomuudhi Mola”. Zipo hadithi nzuri na zenye mvuto kuhusu visa vya wanaosubiri ambazo zinapelekea kustaajabu na kuenzi na kujifariji na watu hawa watukufu wasio na kifani. Imehadithiwa kwamba Kisra alimkasirikia Bozorgmehr basi akamfunga katika nyumba ya giza na kuamuru afungwe na minyororo ya chuma. Zikapita siku na yeye yupo katika hali hiyo. Wakatumwa watu kumuuliza hali yake, na (ajabu) wakamkuta mkunjufu wa nafsi, ametulia. Wakamuuliza: Vipi wewe tunakuona hali yako nzuri (utulivu wa nafsi) wakati upo katika shida na dhiki? Akajibu: Nilitengeneza tabia sita na kuzichanganya na kuzitumia. Hizo ndizo zimenifanya niwe kama mnavyoona. Wakamuambia tutajie huenda tukafaidika nazo wakati wa matatizo. Akasema: Hakika, ama tabia ya kwanza ni kumtegemea (kuweka matumaini kwa) Mwenyezi Mungu (a.w.j.), ama ya pili, ni kwamba kila kilichokadiriwa basi kipo; ama ya tatu, subira ndiyo njia pekee nzuri kwa mwenye matatizo: ama ya nne, ikiwa sikusubiri kwani nitafanya nini, siwezi kujisaidia kwa kutapatapa: ama la tano, inawezekana kukawepo mwingine mwenye matatizo zaidi yangu mimi: ama la sita, faraja inaweza ikatokea wakati wowote. Kisra, yalipomfikia maneno yale, akamuachia huru na kumtukuza.186 Kutoka kwa Imam Ridha (a) kama alivyopokea kutoka kwa babu zake (a) alisema: “Nabii Suleyman (a) siku moja aliwaambia masahaba wake: Hakika Mwenyezi Mungu (swt) amenijalia ufalme ambao hawezi kuupata yeyote baada yangu; kanifanyia upepo unanitii, pia watu, majini, ndege na wanyama wa porini. Kanifundisha lugha ya ndege na kunipa kila kitu, laki186. Safinatul Bihaar, juz. 2, uk. 7 141


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:21 PM

Page 142

Tabia njema kwa mujibu wa Ahlul Bayt (a.s) ni pamoja na yote hayo niliyopewa ya ufalme sijawahi kupata furaha mchana hadi usiku! Sasa nataka kesho niingie kasri yangu, nipande juu na nitazame milki zangu. Kwa hiyo msimruhusu yeyote kuja kwangu, yasije zuka mambo ambayo yatafanya siku yangu kuwa chungu. Ilipofika kesho, Nabii Suleyman (a) akashika fimbo yake na kupanda hadi sehemu ya juu kabisa ya kasri na kusimama na huku akiegemea fimbo yake akiangalia milki zake akifurahi kwa yale aliyopewa. Mara akamtokezea kijana mwenye wajihi mzuri na mavazi. Alipomwona Nabii Suleyman (a) akamuuliza: Nani kakuingiza ndani ya kasri hii, wakati nilikwishaamua leo niwe peke yangu?! Nani kakuingiza? Yule kijana akajibu: Mwenye kasri hii ndiye aliyeniingiza, na kwa idhini yake ndiyo nimeingia. Nabii Suleyman (a) akasema: Mwenye kasri anahaki zaidi juu yake kuliko mimi. Hebu wewe ni nani? Akajibu: Mimi ni Malakul-mawt (malaika wa kutoa roho). Akamuuliza: Kwani lipi limekuleta? Akajibu: Nimekuja ili nichukue roho yako. Nabii Suleyman (a) akamuambia: Tekeleza uliloamrishwa kufanya, hii ni siku yangu ya furaha na hataki Mwenyezi Mungu (swt) niwe na furaha isiyokuwa ya kukutana naye. Hapo Malakul-mawt akaichukuwa roho yake na huku ameegemea fimbo yake‌�187 Subira kwenye kumtii Mwenyezi Mungu na kushindana na maasi Ni wazi kwamba nafsi kimaumbile inakaidi na kuepuka nidhamu na taratibu zinazozuia uhuru wake na fursa yake ya kuingia katika viwanja vya matamanio, pamoja na kwamba zimewekwa kwa ajili ya kuitengeneza na kuipa fanaka. Kwa hivyo basi, nafsi inakataa kusalimu amri kwa hizo taratibu na nidhamu ila kwa kupambiwa na kupewa shauku au kwa indhari na vitisho. Kwa kuwa kusimama katika uchamungu na kujiepusha kumuasi ni mambo mazito kwa nafsi, basi kusubiri kwenye uchamungu na kushindana na 187. Safinatul Bihaar, juz.1, uk. 614 142


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:21 PM

Page 143

Tabia njema kwa mujibu wa Ahlul Bayt (a.s) maasi ni katika wajibu zenye umuhimu zaidi na bora ya matendo yakurubishayo. Zipo Aya tukufu na hadithi za Ahlul-Bayt (a) zinazotamanisha kusubiri kwenye uchamungu na pia kutahadharisha dhidi ya kumuasi Mwenyezi Mungu (swt) kwa kutumia njia zenye hikma na athari. Imam Sadiq (a) alisema: “Jisubirisheni kwenye kumtii Mwenyezi Mungu (swt), na mshindane katika kumuasi Yeye, kwani hakika dunia ni muda kama wa saa. Yale yaliyokwisha pita hayakufanyi ufurahi wala uhuzunike, ama yale yanayokuja hujui. Kwa hivyo basi jisubirishe kwenye huo muda wa saa moja, ni kama vile umekwisha furahi.”188 Pia alisema: “Itakapokuwa Siku ya Kiyama, kundi miongoni mwa watu litasimama na kuelekea mlango wa pepo na kugonga. Wataulizwa: Nyinyi ni akina nani? Watajibu: Sisi ndiyo wana subira. Wataulizwa: Kwenye nini mmesubiri? Watajibu: Tulikuwa tukisubiri kwenye kumtii Mwenyezi Mungu (swt) na kushindana dhidi ya maasi. Hapo atasema Mwenyezi Mungu (swt): Wamesema kweli, basi waingizeni peponi na hiyo ndiyo kauli ya Mwenyezi Mungu (swt) isemayo:

“Sema: Enyi waja wangu mlioamini! mcheni Mola wenu, wale wafanyao wema katika dunia hii watapata wema, na ardhi ya Mwenyezi Mungu ina wasaa, bila shaka wafanyao subira watapewa malipo yao pasipo hesabu.”(Sura Zumar, 39:10)189” 188. Al Waafy, juz. 3, uk. 63 189. Al Waafy, juz. 3, uk. 65 143


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:21 PM

Page 144

Tabia njema kwa mujibu wa Ahlul Bayt (a.s) Pia alisema: “Subira iko aina mbili: Subira wakati wa msiba, ni njema na nzuri, na bora kuliko hiyo ni subira kwenye yale ambayo ameyaharamisha Mwenyezi Mungu (swt) ili iwe kwako ni kinga”.190 Subira kwenye neema Hii ni kuidhibiti nafsi dhidi ya yanayochochea jeuri na kiburi. Subira hii ni katika alama za utukufu wa nafsi, busara na uono wa mbali. Subira kwenye matatizo na misiba haiwi bora kuliko subira kwenye starehe na vivutio vya maisha kama vile (jaha) umaarufu mkubwa, utajiri mwingi, utawala wenye nguvu na mfano wa hayo. Kukosa subira wakati wa misiba kunapelekea kwenye kutapatapa kunakoangamiza, kama vile kukosekana kwake wakati wa neema inavyozaa jeuzi na kiburi. Mwenyezi Mungu (swt) anasema:

“Sivyo, hakika mwanadamu anaasi sana. Kwa kujiona ametosha.” (Suratul Alaq, 96:6-7). Yote haya mawili ni mabaya yanachukiza. Muradi wa kusubiri kwenye neema ni: Kuchunga haki za neema hiyo na kuitumia katika fursa za kutenda wema kimada na kiroho; k.v. kuwachunga mafukara, kuwaokoa wakimbizi na kujali haja za waumini na kujikinga na mitelezo ya jeuri na ujabari. Subira ina aina nyingi zingine: Subira wakati wa vita: Ushujaa. Kinyume chake ni woga. Subira kujiepusha kuadhibu: Upole. Kinyume chake ni ghadhabu. Subira (kujiepusha) na anasa za maisha: Kuipa dunia nyongo (zuhd). 190. Kama hapo juu. 144


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:21 PM

Page 145

Tabia njema kwa mujibu wa Ahlul Bayt (a.s) Kinyume chake ni tamaa. Subira kwenye kuficha siri: Usiri. Kinyume shake ni kuropoka. Subira kwenye matamanio ya tumbo na utupu: Udhibiti-nafsi, stara. Kinyume chake ni ulafi, tamaa. Kwa haya, ni wazi kwamba subira ni nidhamu na muhimili thabiti wa tabia njema na pia ndiyo msingi wake uliyo imara.

MAZURI YA SUBIRA Kwa maelezo yaliyotangulia tunapata faida ya kwamba subira ni nguzo ya mambo mema, muhimili wa matendo mazuri na kichwa cha matukufu ya kujivunia. Subira ni kinga kwa mwenye majonzi na huzuni, inapunguza maumivu yake na kumlainishia matatizo yake na kumletea utulivu. Pia subira ni dhamana dhidi ya kutapatapa kunakoangamiza na pupa yenye kufedhehesha. Kama siyo subira, basi mwenye matitizo angevamiwa na magonjwa na shida na kuwa shabaha ya kicheko cha maadui na mahasidi. Juu ya yote subira ni tumaini la mwenye kutarajia yale aliyoyaandaa Mwenyezi Mungu (swt) kwa ajili ya wenye kusubiri, malipo makubwa na thawabu nyingi.

NI VIPI UTAKAVYOJENGA SUBIRA Hizi ni baadhi ya nasaha ambazo zinazoongoza jinsi ya kujenga subira na kujipamba kwayo: 1. Kutafakari kuhusu matendo mema ya subira na yale wanayoyachuma 145


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:21 PM

Page 146

Tabia njema kwa mujibu wa Ahlul Bayt (a.s) baadaye wenye kusubiri kama vile sifa nzuri, manufaa makubwa hapa duniani, na wingi wa malipo na thawabu kesho akhera. 2. Kutafakari kuhusu mabaya ya kutapatapa na ubaya wa athari zake katika maisha ya mwanadamu, na kwamba hilo halitasaidia kupoza kuungua nafsi yake na wala haitarejesha nyuma qadhaa na kubadilisha tukio. Bali matokeo yake ni adhabu, mateso na shida. Dale Canergie anasema: “Nimesoma katika miaka minane iliyopita kila kitabu, jarida na makala yanayohusu kutibu wasiwasi. Je unataka kujua nasaha iliyo ya busara na faida zaidi niliyopata katika kisomo changu kirefu? Nayo ni: “Ridhika na lile ambalo halina budi nyingine”. 3. Kuelewa uhakika wa maisha, kwamba maisha haya kimaumbile yamepigwa muhuri wa matatizo na shida. Haya maisha siyo nyumba ya raha na starehe, bali ni nyumba ya mtihani kwa muumini. Kama vile mwanafunzi anavyobanwa kwa mitihani ili kufichua kiwango cha elimu alichonacho, hivyo hivyo muumini anatahiniwa kuchunguza peo za imani yake na kiwango cha yakini. Mwenyezi Mungu (swt) anasema:

“ Je, watu wanadhani wataachwa waseme tumeamini, nao wasijaribiwe? Na bila shaka tuliwajaribu wale waliokuwa kabla yao, na kwa hakika Mwenyezi Mungu atawatambulisha wale waongo.” (Suratul Ankabut; 29: 2-3) 4. Kuzingatia na kujifariji na aina mbali mbali ya matatizo na misiba ambayo iliyowafika mabwana wakubwa na mawalii na wakastahamili 146


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:21 PM

Page 147

Tabia njema kwa mujibu wa Ahlul Bayt (a.s) na kusubiri kwa ajili ya Mwenyezi Mungu (swt). Hakika hilo ni katika vichochezi vya kustahamili na kusimama imara. 5. Kujiliwaza na kujifurahisha kwa yale yanayopunguza maumivu ya nafsi na kuzuia huzuni na hasira, kama vile kubadilisha hali ya hewa, kutembelea mazingira yenye kupendeza, na kujiburudisha na visa vizuri na hadithi zenye manufaa.

24. KUSHUKURU MAANA Kutambua neema uliyopata kutoka kwa mhisani, kisha ukamhimidi (ukamsifu) na ukaitumia neema hiyo kama anavyoridhia. Hii ni katika tabia za ukamilifu na alama za uzuri na utukufu. Ni sababu ya neema kuongezeka na kudumu. Shukrani ni wajibu kwa yule kiumbe anayeneemesha, sasa itakuwaje kwa mneemeshaji Muumbaji, ambae neema zake hazina kikomo wala hazihesabiki. Na shukrani haimsaidii chochote Mwenyezi Mungu (swt), kwa kuwa Yeye si muhitaji mutlaqan wa viumbe wake, bali shukrani hurejea kwa viumbe kwa kuwanufaisha, hii kwa kuwa shukrani ni kielelezo cha watu kuthamini neema Zake (swt) na kuzitumia katika uchaji na ridha Yake. Na katika hilo ndipo inapatikana furaha yao na fanaka ya maisha yao.

QUR’ANI Kwa sababu hiyo, Qur’ani na Sunnat vimetilia mkazo kujipamba na hulka hii ya kushukuru. Mwenyezi Mungu (swt) anasema:

147


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:21 PM

Page 148

Tabia njema kwa mujibu wa Ahlul Bayt (a.s)

“Basi nikumbukeni nami niwakumbuke, na mnishukuru wala msinikufuru.” (Suratul Baqarah, 2: 152)

“Na (kumbukeni) alipotangaza Mola wenu, kama mkishukuru bila shaka nitakuzidishieni, na kama mkikufuru, hakika adhabu yangu ni kali sana.” (Suratu Ibrahim, 14: 7)

“Walikuwa wakimfanyia alipendalo, kama ngome na masanamu na sinia kubwa kama hodhi, na masufuria makubwa sana yasiyoondolewa mahala pake. Fanyeni (vitendo vizuri) enyi watu wa Daudi kwa kushukuru, na ni wachache wanaoshukuru katika waja wangu.” (Suratus-Saba’a, 34: 13)

“Bila shaka ulikuwa ni Muujiza kwa (watu wa nchi ya) Sabaa katika makazi yao. Bustani mbili kulia na kushoto, kuleni katika riziki ya Mola wenu, na mumshukuru, mji mzuri, na Mola ni Mwingi wa kusamehe.” (Suratus-Saba’a, 34: 15) 148


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:21 PM

Page 149

Tabia njema kwa mujibu wa Ahlul Bayt (a.s)

HADITHI Kutoka kwa Abu Abdilah (a), Mtukufu Mtume (s) alisema: “Mwenye hali nzuri kichakula, anayeshukuru ana malipo kama ya mwenye kufunga ihtisaban (kwa kutaraji malipo yake Allah pekee), naye mwenye afya njema mwenye kushukuru, anamalipo kama ya yule aliye mgonjwa mwenye kusubiri, naye mwenye neema mwenye kushukuru, ana malipo kama ya yule muhitaji aliyetosheka”. 191 Imam Sadiq (a) alisema: “Anayetoa shukrani basi atapewa ziada, kwa kuwa Mwenyezi Mungu (swt) anasema: “Kama mkishukuru bila shaka nitakuzidishieni.”(Surat Ibrahim, 14:7) Pia alisema: “Kushukuru kila neema - hata kama itakuwa kubwa - ni kumhimidi Mwenyezi Mungu (awj) juu ya neema hiyo.” Pia akasema: “Hakumneemesha Mwenyezi Mungu (swt) mja kwa neema kisha akamhimidi kwa neema hiyo, isipokuwa kwamba kule kumhidi Mwenyezi Mungu (swt) kunakuwa ni bora kuliko neema hiyo na thamani zaidi.”192 Imam Baqir (a) alisema: “Sema mara tatu utakapomuona mwenye matatizo, pasi na yeye kukusikia: sifa zote ni zake Mwenyezi Mungu (swt) ambaye ameniepusha na haya aliyokujaribu kwayo wewe, kama angependa angefanya. Basi atakayesema hivyo, balaa hiyo haitomfika abadan.”193

191. Al Waafy, juz. 3, uk. 67 192. Al Waafy, juz. 3, uk.69 193. Al Bihaar, muj. 15, juz. 2, uk. 135 149


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:21 PM

Page 150

Tabia njema kwa mujibu wa Ahlul Bayt (a.s) Imam Sadiq (a) alisema: “Hakika mmoja kati yenu anakunywa funda la maji, na Mwenyezi Mungu (swt) akamwandikia pepo, kisha akasema: Hakika naachukuwe chombo na kukiweka kwenye mdomo wake na baada ya kusema bismillah na kunywa, akiweke kando na huku anahamu. Baada ya kumshukuru Mwenyezi Mungu (swt),aongeze tena kunywa, kisha akiweke kando. Tena amshukuru Mwenyezi Mungu (swt), na aongeze kunywa, kisha akiweke kando. Na tena amshukuru Mwenyezi Mungu (awj). Basi (kwa ajili ya hilo) Mwenyezi Mungu (awj) atamuandikia pepo.�194

AINA ZA SHUKRANI Zipo aina tatu za kushukuru: Shukrani ya moyo, shukrani ya ulimi, na shukrani ya viungo. Hii ni kwamba pindi nafsi ya mwanadamu inapojaa utambuzi na uelewa wa ukubwa wa neema za Mwenyezi Mungu (swt), na wingi wa neema juu yake, basi ulimi wake hujaa shukrani na himdi kwa Mpaji neema, Mtoaji. Na pindi nafsi na ulimi vinapolingana katika hisia za kubarikiwa na shukrani, basi viungo huathirika kwa msukumo wa nafsi na kuwa ni vyenye utiifu na kujisalimisha kwa Mwenyezi Mungu (swt) hii ikiwa ndiyo ishara ya kushukuru. Kwa ajili hiyo, aina za shukrani zimehitilafiana na njia zake kuwa nyingi: 1. Shukrani ya moyo: Kuwa na taswira ya neema na kuelewa kwamba neema hiyo yatokana na Mwenyezi Mungu (swt). 2. Shukrani ya ulimi: Kumhimidi Mpaji na kumsifu. 3. Shukrani ya viungo: Kuvitumia katika kumtii Mwenyezi Mungu (swt), na kujiweka mbali na maasi. Macho, kuyatumia katika nyanja za kuzinga194. Al Bihaar, muj. 15,jua.2, uk. 131 150


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:21 PM

Page 151

Tabia njema kwa mujibu wa Ahlul Bayt (a.s) tia na kutafakari na kuyazuia yasitazame yaliyoharamishwa. Ulimi, kuutumia katika kauli njema na kuuepusha na maneno machafu na maovu. Mkono, kuutumia katika haja zilizo halali na kuuzuia na kufanya maudhi na shari. Ni hivyo ndivyo inatakiwa kushukuru kila neema katika neema za Mwenyezi Mungu (swt) kwa matendo yanayolingana na neema hizo: Shukrani ya mali: Ni kuitoa katika njia ya kumtii Mwenyezi Mungu (swt) na kumridhisha. Shukrani ya elimu: Ni kuisambaza na kutangaza mafunzo (mafahimu) yake yenye kunufaisha. Shukrani ya jaha (utukufu, umaarufu, fahari, enzi, mamlaka…): Ni kuwanusuru walio dhaifu na wenye kukimbia dhulma, kwa kuwaokoa wasidhulumiwe. Na vyovyote atakavyopindukia mtu katika kushukuru, basi hawezi kuzishukuru neema kwa kiwango cha usawa kwa kuwa hata huko kushukuru kwenyewe ni udhihirisho wa neema ya Mwenyezi Mungu (swt) na kuwezeshwa (tawfiqi) naye. Kwa sababu hiyo mwanadamu hawezi kutimiza uhakika wa kushukuru, kama alivyosema Imam Sadiq (a): “Mwenyezi Mungu (swt) alimpa wahyi Musa (a) ya kwamba: Ewe Musa nishukuru ukweli wa kunishukuru. Musa (a) akasema: Ewe Mola (wangu) ni vipi mimi nitaweza kukushukuru ukweli wa kukushukuru wakati ambapo pia hiyo shukrani ninayokushukuru kwayo ni Wewe ndiye umenineemesha? Mwenyezi Mungu akasema: Ewe Musa, sasa umenishukuru kwa kuelewa kwamba hilo pia latoka kwangu”.195

195. Al Waafy, juz. 3, uk. 68 151


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:21 PM

Page 152

Tabia njema kwa mujibu wa Ahlul Bayt (a.s)

FADHILA YA KUSHUKURU Katika sifa za nafsi tukufu ni kukumbuka neema na fadhila, na kumshukuru mtoaji. Na kila ambapo neema hizo huwa ni adhimu, basi ndivyo zinavyostahili zaidi kukumbukwa (kuthaminiwa) na kustahiki shukrani nyingi. Kila tazamo litokalo jichoni, au neno litokalo kinywani, au kiungo kinachopelekwa na nguvu ya kutaka, au pumzi anazopumua mtu, vyote ni ruzuku adhimu za Mola na bila shaka hawazithamini ila waliyovikosa. Ikiwa ni wajibu kumshukuru makhluki (kiumbe) vipi kuhusu yule ambaye ndiye muumba Mtoaji neema, ambaye neema zake hazina hesabu wala kiwango? Zaidi ya hilo ni kwamba kushukuru kunamfanya mtu kuwa karibu na Mola wake na kupata radhi Yake. Pia ni sababu kwa mwenye kushukuru kuongezewa neema maradufu. Ama kukufuru neema ni katika alama za nafsi ovu na duni na pia ni ishara za kutokujua thamani na pia kiasi cha neema na dharura ya kuzishukuru. Hebu tazama jinsi Qur’ani Tukufu inavyoelezea kwamba kukufuru neema ni sababu ya kuhilikishwa kaumu na kutoweka kwa neema zao:

“Na Mwenyezi Mungu amepiga mfano wa mji uliokuwa na amani na utulivu, riziki yake ikaufikia kwa wingi kutoka kila mahala, lakini ukazikufuru neema za Mwenyezi Mungu kwa hiyo Mwenyezi Mungu akauonjesha vazi la njaa na khofu kwa sababu ya yale waliyokuwa 152


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:21 PM

Page 153

Tabia njema kwa mujibu wa Ahlul Bayt (a.s) wakiyafanya.” (Suratun-Nahl, 16: 112) Imam Ja’far (a) aliulizwa kuhusu aya isemayo:

“Lakini wakasema; Mola wetu! uweke mwendo mrefu kati ya safari zetu na wakajidhulumu nafsi zao. Ndipo tukawafanya hadithi na tukawararua vipande vipande kwa hakika katika hayo mna mazingatio kwa kila afanyaye subira sana, mwenye kushukuru.” (SuratusSabaa, 34:19) Naye akajibu kwamba hawa ni watu walikuwa na vijiji vimepakana, hawa wawaona wale, na pia mito inayopita, na mali nyingi dhahiri. Basi wakakufuru neema za Mwenyezi Mungu (swt) na wakabadili waliyokuwa nayo ya siha na amani. Mwenyezi Mungu (swt) akawabadilishia neema na Yeye habadilishi yaliyo kwa watu ila baada ya wao wabadili wenyewe. Kwa hivyo Mwenyezi Mungu (swt) akawateremshia mafuriko makubwa, akatawanya vijiji vyao na kubomoa nyumba zao na kutokomeza mali zao na mahala pa mabustani akawabadilishia mabustani mawili yenye matunda machungu, machachu na mitamariski (aina ya mti) pia na misidiri (aina ya mti) michache. Hayo ni malipo tuliyowalipa kwa kukufuru kwao, na hatumlipi (kwa adhabu) ila mwenye kuzidi kukufuru”.196 Pia imam Sadiq (a) alisema: “Hakika kaumu fulani nao ni (watu wa Tharthar) walimwagiwa neema ikafikia kiasi cha wao kuchukuwa ngano na kutengeneza mkate kisha wakawafutia watoto wao mavi na mwishowe likawa rundo la mikate kama mlima. Siku moja mwanaume mmoja akapita na huku mwanamke mmoja 196. Al Waafy, juz. 3, uk. 167 153


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:21 PM

Page 154

Tabia njema kwa mujibu wa Ahlul Bayt (a.s) anampangusa mwanae na mkate akamwambia: “Ole wenu! Mwogopeni Mwenyezi Mungu (swt), msibadili neema za Mwenyezi Mungu (swt) mlizonazo.” Yule mama akamjibu: “Kama vile unatutisha na njaa? Ama maadamu chemichemi zetu zimejaa maji hatuogopi njaa.” (Kwa kufr hiyo) Mwenyezi Mungu (awj) akachukizwa. Akazuia maji ya chemichemi na kuwanyima mvua na mimea. Kwa hiyo wakala na kumaliza walichokuwa nacho na mwishowe wakahitaji ule mlima wa mikate kiasi ya kwamba wakawa wanagawana kwa kupima”.197 Imam Ridha (a) kama alivyopokea kutoka kwa baba zake alisema kwamba Mtume Mtukufu (s) alisema: “Madhambi ambayo yanayoleta adhabu haraka sana ni kukufuru neema”.198

VIPI TUTAJIPAMBA NA (TABIA) YA KUSHUKURU Hizi ni baadhi ya nasaha ili mtu aweze kujipamba na ubora wa kushukuru: 1. Kutafakari jinsi Mwenyezi Mungu (awj) alivyowaneemesha waja wake kwa neema nyingi, uangalizi na upole. 2.- Kuacha kutazama wale walio na mali nyingi, waliyoneemeka kimaisha na anasa na kutazama mafukara na waliochini yako kimaisha kama alivyosema Imam Ali (a) Amiri wa waumini:“zidisha sana kutAzama yule ambae umemzidi riziki, hakika hilo ni katika milango ya kushukuru”.199 3. Mtu kukumbuka maradhi na matatizo ambayo Mwenyezi Mungu (swt) alimuokoa nayo kwa upole wake na baada ya ugonjwa akampa siha na nafasi ya matatizo akamfanyia wepesi na salama. 197. Al Bihaar 198. Al Bihaar 199. Nahjul Balagha 154


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:21 PM

Page 155

Tabia njema kwa mujibu wa Ahlul Bayt (a.s) 4. Kutafakari katika mazuri ya kushukuru na uzuri wa athari zake katika kuvuta upendo wa mneemeshaji na kuongeza neema zake. Pia ni vyema kuzingatia mabaya ya kukufuru neema na jinsi kunavyosababisha chuki (hasira) ya mneemeshaji na kutoweka kwa neema zake.

25. KUTAWAKALI MAANA Kutawakali ni kumtegemea Mwenyezi Mungu (swt) katika mambo yote na kuyakabidhi kwake pekee na kuachana na asiyekuwa Yeye. Na nguvu inayosababisha tawakuli ni nguvu ya roho na yaqini. Kwa hiyo kukosekana kwake kunatokana na udhaifu wa roho na yaqini au udhaifu wa roho na kuathirika kwake na yenye kutisha na kudanganya. Kutawakali ni moja katika dalili za imani na sifa za waumini. Ni moja katika fadhila zao tukufu ambayo ndiyo sababu ya utukufu wa nafsi zao, kiasi cha kuwaenzi wasitake msaada wa mahkuki (viumbe) na kumtegemea pekee Muumba ili kupata ya kuwanufaisha na kujiepusha na ya madhara. Aya na hadithi zimerudia mara nyingi kwa kutukuza (hulka hii) na kuvutia kwayo:

QUR’ANI Mwenyezi Mungu (swt) anasema:

“Na humpa riziki kwa mahala asipopatazamia, na anayemtegemea Mwenyezi Mungu basi yeye humtoshea, kwa hakika Mwenyezi Mungu anatimiza kusudi lake, hakika Mwenyezi Mungu amekwisha kiwekea kila kitu kipimo,” (Surat Talaq, 65: 3) 155


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:21 PM

Page 156

Tabia njema kwa mujibu wa Ahlul Bayt (a.s)

“... hakika Mwenyeezi Mungu anawapenda wenye kumtegemea.”(Aali Imran: 3:159)

“Sema: Halitatusibu ila alilotuandikia Mwenyezi Mungu, yeye ni Mola wetu, na Waumini wamtegemee Mwenyezi Mungu tu.” (Tawbah: 9 : 51)

“Akikusaidieni Mwenyezi Mungu, hapana yeyote mwenye kuwashinda na kama akiwaacheni ni nani atakayekusaidieni baada yake? Na kwa Mwenyezi Mungu peke yake wategemee wenye kuamini.” (Surat Aali Imraan, 3:160)

HADITHI Imam Ja’far Sadiq (a) alisema: “Hakika utajiri na utukufu vinatembea, vikipata sehemu ya tawakuli basi hujenga hapo”.200 “Mwenyezi Mungu alimpa wahyi Nabii Daud (a) kwamba: Hakuna katika waja wangu ambaye atakayeshikamana nami pekee (asitegemee viumbe) nikalitambua hilo katika nia yake, kisha mbingu na ardhi na vilivyomo 200. Al Waafy, juz. 3, uk. 56 156


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:21 PM

Page 157

Tabia njema kwa mujibu wa Ahlul Bayt (a.s) vikamfanyia vitimbi isipokuwa nitamfanyia njia baina yavyo. Na mja wangu hakushikamana na kiumbe katika viumbe vyangu, nikalitambua hilo katika nia yake, isipokuwa humzuilia sababu za mbinguni (msaada kutoka juu) na kuifanya ardhi chini yake haikaliki na sitojali katika bonde lipi ataangamia”. “Anayepewa matatu, hanyimwi matatu: Anayepewa dua, hupewa kubuli. Anayepewa shukrani, hupewa ziada. Anayepewa tawakuli (kutegemea), hupewa (msaada) inayotosheleza. Kisha akasema: Je umesoma kitabu cha Mwenyezi Mungu? Mwenyezi Mungu anasema (swt): “Na yeyote anayemtegemea Mwenyezi Mungu, basi anamtosha”.

“Na humpa riziki kwa mahala asipopapatazamia, na anayemtegemea Mwenyezi Mungu basi yeye humtoshea, kwa hakika Mwenyezi Mungu anatimiza kusudi lake, hakika Mwenyezi Mungu amekwisha kiwekea kila kitu kipimo.”(Surah Talaq, 65:3) Kisha akasema: “Ikiwa mtashukuru basi nitawazidishieni”

“Na (kumbukeni) alipotangaza Mola wenu, kama mkishukuru bila shaka nitakuzidishieni, na kama mkikufuru, hakika adhabu yangu ni kali sana.” (Surah Ibrahim, 14:7), na pia akasema: “niombeni nitakujibuni” 157


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:21 PM

Page 158

Tabia njema kwa mujibu wa Ahlul Bayt (a.s)

“Na Mola wenu husema: Niombeni nitakujibuni. Kwa hakika wale wajivunao kufanya ibada yangu, wataingia Jahannam wakifedheheka.” (Surah Ghaafir, 40:60). Imam Ali (a) katika wasia wake kwa Imam Hasan (a) alisema: “Iweke nafsi yako chini ya hifadhi ya Mola Wako katika mambo yote, hakika wewe utakuwa umeihifadhi ndani ya pango lisiloingilika (hifadhi madhubuti) na kujikinga kwa ngao tukufu”.201 Abu Abdilah (a) alisema kwamba Amiri wa waumini Ali (a) alisema:“Katika yale aliyomnasihi Luqman (a) mwanaye ni kwamba: Ewe mwanangu mpenzi! na apate mazingatio yule ambaye yaqini yake imepungua na nia yake dhaifu katika kutafuta riziki ya kwamba, Mwenyezi Mungu (swt ) alimuumba katika hali tatu na akadhamini mambo yake na kumpa riziki yake na ilhali hakuwa na chochote wala hila katika hali zote hizo, (kwa hivyo) Mwenyezi Mungu (t.w.t.) atamruzuku katika hali ya nne. Ama hali ya kwanza, ni pale alipokuwa katika tumbo la mama yake. Mwenyezi Mungu (twt) alimpa riziki yake akiwa mahala palipotulia ambapo joto wala baridi havimuudhi. Kisha Akamtoa ndani ya tumbo la mama yake na huku amemtayarishia riziki ambayo ni maziwa ya mama yake, riziki inayotosha na yenye uhai, yote haya akiwa hana nguvu wala uwezo. Kisha akaachishwa ziwa na kupewa riziki kwa jasho la wazazi wake kwa kuwepo huruma na mapenzi yake ndani ya nyoyo zao kiasi cha wao kujinyima kwa ajili yake. Sasa anapokuwa mkubwa na kupata akili na kuchuma mwenyewe, na mambo kumwendea magumu anakuwa na dhana na Mola wake na kukanusha kutoa haki katika mali yake na kujifanyia ubakhili na familia yote hayo kwa sababu ya kuogopea riziki yake na kuwa na dhana na yakini mbaya kuhusu atakayompa Mwenyezi Mungu (swt) karibuni au 201. Nahjul Balagha 158


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:21 PM

Page 159

Tabia njema kwa mujibu wa Ahlul Bayt (a.s) baadae (haraka au kuchelewa). Ni mja aliye mbaya kiasi gani huyu ewe mwanangu!”202

UHAKIKA WA TAWAKUL Maana ya tawakuli siyo kuweka pembeni sababu na njia zinazopelekea mambo mazuri kusimama na kuepuka mabaya. Pia siyo mtu kusimama mbele ya matukio na matatizo amefunga mikono yake bila ya kuwa na uamuzi wala azma yoyote. Ama hakika ya tawakuli ni kumtegemea Mwenyezi Mungu (a.w.j.) na kuweka imani yako Kwake. Ni kumtegemea Yeye pekee kinyume na viumbe vyote na sababu, kwa kuzingatia kwamba Yeye Mwenyezi Mungu (awj) ndiye chanzo cha kheri na Msababishaji wa kila sababu na Yeye pekee ndiye Mwendesha mambo ya waja wake na pekee Yeye ndiye Muweza wa kufanikisha malengo yao na matakwa yao. Hilo halipingi mwanadamu kuzifuata sababu za kimaumbile na njia zilizodhahiri ili kufikia malengo na maslahi yake kama vile kuchukua mahitaji wakati wa safari, kuchukua silaha ili kupambana na maadui, na kutafuta dawa dhidi ya maradhi, kujikinga na hatari na madhara, vyote hivi ni sababu za dharura kumlinda mwanadamu na kutekeleza makusudio yake. Na bila shaka Mwenyezi Mungu (s.w.t.) alikwishataka mambo yaende kwa kufuata sababu zake. Lakini inatakiwa kuweka matumaini kwake Mwenyezi Mungu (swt) na kumtegemea katika kutekeleza malengo na makusudio na sio sababu. Na dalili ya hilo ni kwamba bedui mmoja alipuuza kumfunga ngamia wake eti akimtegemea Mwenyezi Mungu (swt) amlinde, Mtukufu Mtume (s) akamuambia: “Mfunge halafu umtegemee Mwenyezi Mungu (swt)”.

202. Al Bahaar, muj. 15, juz. 2, uk. 155 159


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:21 PM

Page 160

Tabia njema kwa mujibu wa Ahlul Bayt (a.s)

DARAJA ZA TAWAKUL Watu wanatofautiana tofauti iliyo kubwa katika daraja za tawakuli kama vile wanavyotofautiana katika daraja za imani; daraja ya juu ni ya wale waliyotangulia wasio na kifani katika uwanja wa tawakuli, waliomtegemea Mwenyezi Mungu (swt) pekee, nao ni mitume na mawasii wao na mawalii ambao wamezungukia anga zao. Na katika mifano ya juu na yenye msisimko mkubwa ni kile kisa cha nabii Ibrahim (a) kwamba pindi alipotupwa ndani ya moto, Jibril (a) alimpokea hewani na kumuambia: Je unahaja yoyote? Akamjibu: Ama kwako sina, ananitosha Mwenyezi Mungu (swt) na ni mlinzi bora. Pia akamjia Mikail (a) na kumuambia: Ukitaka niuzime moto, hakika hazina za mvua na maji ziko mkononi mwangu. Nabii Ibrahim (a) akamuambia: Hapana sitaki. Naye malaika wa upepo akamjia na kumuambia: Lau ukitaka basi nitaurusha moto huu. Akamjibu: Hapana, sitaki. Jibril (a) akamuambia: Basi muombe Mwenyezi Mungu (swt). Akajibu: Sina haja ya kumuomba kwa kuwa ujuzi wake wa hali yangu wanitosha�.203 Baina ya watu yupo asiye kuwa na tawakul kwa sababu ya udhaifu wa hisia yake kiroho na uchache wa imani yake. Na baina ya peo hizi mbili wanasimama watu kwa daraja tofauti za tawakuli.

MEMA YA TAWAKULI Mwanadamu katika uhai huu ni mlengwa wa misiba, matatizo na balaa. Hawezi akaepuka fimbo na mkong’oto wa mitihani hiyo, mara anashinda na mara anabwagwa chini. Na ni mara nyingi humtupa chini, hujikuta 203. Safinatul Bihar, juz. 2, uk. 683 160


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:21 PM

Page 161

Tabia njema kwa mujibu wa Ahlul Bayt (a.s) amebwagwa hana nguvu wala uwezo, moyo umevunjika. Kutokana na hayo matatizo, hujikuta ndani ya wasiwasi unaochosha na fazaa ya kutisha, anahofia kushindwa, anaogopa ufukara na kutishwa na maradhi na kwa hiyo huteseka na aina mbalimbali ya vitisho vinavyotishia amani yake na utulivu wake. Ikiwa utamaduni wa sasa umeweza kupunguza makali ya maisha kwa marahisisho ya kiutamaduni na kwa kupatia nyenzo za kustarehekea, na amani lakini umeshindwa kuzivika nyoyo na utulivu na uthabiti na kuzifanya zihisi utulivi na amani kiroho jambo ambalo limepelekea wasiwasi kuendelea kuzitawala nafsi, jambo ambalo limepelekea kuzidi kwa maradhi ya kiroho (akili) na kusababisha wazimu na kujiua katika nchi zilizo juu kimaendeleo. Lakini sheria ya kiislamu imeweza kwa kanuni zake zilizo juu na mfumo wake wa kitabia uliobora kupunguza wasiwasi wa nafsi na hofu na kuzijaza nafsi kwa nishati kubwa za kiroho kama vile ukakamavu, uthabiti, yaqini, kujiamini, utulivu, kwa kumtegemea Mwenyezi Mungu (swt) ambaye ni Mbora wa kuendesha mambo, Mzuri wa kutenda na Mwingi wa neema. Na kuelewa kwamba uumbaji ni wake Mwenyezi Mungu (swt) pekee na amri na kwamba ni Muweza wa kila kitu. Na kwa haya bila shaka nafsi zinapata utulivu na kuifanya hofu kuwa ni amani na wasiwasi kuwa ni faraja na utulivu. Na baada ya hili, tawakuli ni katika sababu (sehemu) muhimu ya utukufu wa nafsi na ujuu wa ukarimu, utulivu wa dhamira na hayo kwa wenye tawakuli hujitenga na kutaka msaada kwa viumbe na kumkimbilia Muumba katika kujiepusha na madhara na kupata ya manufaa. Na huenda wanaostahili zaidi tawakuli kuliko watu wote ni mabwana wenye vyeo na majukumu makubwa kama vile wanamageuzi ili iweze kuwavika azma na msimamo katika kukabiliana na mateso ya watu na 161


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:21 PM

Page 162

Tabia njema kwa mujibu wa Ahlul Bayt (a.s) shida zao na kusonga mbele katika kutekeleza malengo yao ya kurekebisha na kwa kuruka kila pingamizi.

JINSI YA KUFIKIA TAWAKULI 1. Kurejea na kuzingatia aya na hadithi ambazo zinazungumzia ubora wake na athari yake nzuri katika kujenga utulivu na kuburudika. Katika maneno ya pekee mazuri yaliyotungwa kuhusu tawakuli ni kauli ya Imam Husayn (a) isemayo: “Ikitokea kwamba zama zimekuuma, basi usiwaegemee walimwengu Na kamwe usimuombe ila Mwenyezi Mungu, aliye juu Mgawa riziki. Na lau ungeishi na kuzunguuka toka mashariki hadi magharibi, basi usingekutana na yeyote ambaye anaweza kumfanya mtu awe na fanaka au maangamio.� Na katika yaliyonasibishwa na Imam Ali (a): Nimeridhia na yale aliyonigawia Mwenyezi Mungu. Na nimewakilisha jambo langu kwa Muumba Wangu. Kama vile Mwenyezi Mungu, katika yaliyopita, alivyotenda wema, Basi hivyo hivyo katika yaliyobaki atatenda wema. Baadhi ya watu watukufu wamesema: Matatizo yako uwe ni mwenye kuyapa nyongo Na mambo uyakabidhi mikononi mwa Qadhaa Huenda jambo likawa kwako ni lenye kuudhi Lakini katika hatima likawa ni lenye kuridhisha Mara hutokea sehemu ndogo ikapanuka (dhiki ikatoweka) Na mara hutokea sehemu kubwa ikawa ndogo (dhiki ikazidi) Mwenyezi Mungu amekuzoesha mazuri Chukulia kipimo yale yaliyokwisha pita.

162


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:21 PM

Page 163

Tabia njema kwa mujibu wa Ahlul Bayt (a.s) 2. Kuzidisha imani kuhusu Mwenyezi Mungu (awj) na kuwa na uthabiti kwamba anatenda wema, anapeleka mambo kwa hekima, ni mwingi wa upole na huruma na kwamba Yeye ndiye chanzo cha heri na msababishaji wa sababu na Muweza juu ya kila kitu. 3. Kutanabahi kuhusu uzuri wa kutenda kwake Mwenyezi Mungu (swt) na ukubwa wa msaada Wake kwa mwanadamu katika hatua zake mbalimbali na mambo yake kuanzia alipokuwa tumboni hadi mwisho wa umri wake na kwamba anayemtegemea basi Humtosha na anayemtaka Amuokoe basi humuokoa. 4. Kuzingatia mabadiliko ya hali za maisha na kubadilika siku baina ya watu; wangapi walikuwa mafakiri na baadaye kuwa matajiri, na wangapi matajiri wameishia kuwa mafakiri, na pia amiri (bwana, kiongozi, mwenye mamlaka) akaamka ni hohehahe asiye na uwezo, na hohehahe akaamka ni amiri mwenye mamlaka. Na hivyo ndivyo inavyotakiwa kutanabahi kuhusu ukubwa wa uwezo wake Mwenyezi Mungu (swt) katika riziki za waja wake na kuwaondolea balaa, na mithili ya hayo katika aina mbalimbali za mazingatio yanayoonyesha uwezo wa Mwenyezi Mungu (awj) na kwamba Yeye pekee ndiye anayestahiki kutegemewa, kuegemewa, na kutumainiwa kuliko yeyote yule. Na dalili ya mtu kuwa amepata tawakuli ni kule yeye kuridhia kadhaa yake Mwenyezi Mungu (swt) na kadari Yake iwe ni katika furaha au shida bila ya kuudhika, kutapatapa na kupinga. Na hiyo ni daraja ya juu hawaifikii ila watukufu waliokurubishwa.

163


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:21 PM

Page 164

Tabia njema kwa mujibu wa Ahlul Bayt (a.s)

26. KUMUOGOPA MWENYEZI MUNGU MAANA Ni nafsi kuuma kwa sababu ya kuogopa adhabu ya Mwenyezi Mungu (malipo ya kumuasi na kumhalifu). Hii ni katika sifa za mawalii na alama za wachamungu na sababu inayochochea msimamo sahihi na unyoofu. Pia ni ngao madhubuti dhidi ya mambo ya shari na maovu. Ni kwa ajili ya hayo ndiyo sheria ikalipa jambo hili umuhimu wa hali ya juu na kuwasifu wenye sifa hiyo kwa sifa tukufu .

QUR’ANI Mwenyezi Mungu anasema:

“... Kwa hakika wanaomuogopa Mwenyezi Mungu miongoni mwa waja wake ni wale tu wenye ujuzi, bila shaka Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu, Mwingi wa kusamehe”. (Suratu Fatir, 35:28)

“Hakika wale wanaomuogopa Mola wao kwa siri wao watapata msamaha na malipo makubwa.” (Suratul Mulk, 67: 12)

“Na ama yule aliyeogopa kusimama mbele ya Mola wake, na 164


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:21 PM

Page 165

Tabia njema kwa mujibu wa Ahlul Bayt (a.s) akaikataza nafsi matamanio (maovu). Basi kwa hakika pepo ndiyo makazi (yake)”. (Suratu an Nazia’at, 79: 40-41)

HADITHI Imam Sadiq (a) alisema: “Muogope Mwenyezi Mungu (swt) kana kwamba unamuona, na ikiwa kama humuoni basi yeye anakuona. Na ikiwa utaona kwamba Yeye hakuoni, basi umekufuru, na ikiwa wafahamu kwamba anakuona kisha ukamfanyia maasi, basi utakuwa umemfanya duni zaidi ya wanaokutizama”.204 Pia akasema: “Muumini yupo baina ya hofu mbili; (ya kwanza ni) dhambi ambayo iliokwisha pita, haelewi Mwenyezi Mungu (swt) kafanya nini (kuhusu dhambi hiyo), ( na ya pili ni) umri ambao umebaki haelewi ni kipi atakachokichuma katika yale yanayoangamiza. Kwa hiyo haamki ila ni mwenye hofu, na haimpi unyoofu ila hofu”.205 Pia akasema: “Hawezi kuwa muumini ni mwenye kuamini mpaka awe ni mwenye kuogopa na kutarajia, na hawezi kuwa hivyo (mwenye kuogopa na kutarajia) mpaka awe ni mwenye matendo kwa ajili ya anayoyaogopa na kuyatarajia”.206 Na katika makatazo ya Mtukufu Mtume (s): “Yeyote ambaye anayekabiliwa na ovu (zinaa…) au matamanio kisha akajiepusha kwa kuwa anamuogopa Mwenyezi Mungu (awj) basi Mwenyezi Mungu (awj) humharamishia moto na kumuepusha na fadhaa kubwa (ya siku ya kiama) na atamtekelezea yale aliyomuahidi katika kitabu chake 204. Al Wafy, juz. 3, uk. 57 205. Al Waafy, juz. 3, uk. 57 206. Kama hapo juu. 165


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:21 PM

Page 166

Tabia njema kwa mujibu wa Ahlul Bayt (a.s) katika kauli yake (awj):

“Na mwenye kuogopa kusimamishwa mbele ya Mola wake atapata Bustani mbili.” (Suratul ar Rahman; 55:46). Nao wanahekima wakasema: Maskini wee mwanadamu! Laiti angeliogopa moto (wa jahannamu) kama anavyoogopa ufakiri, basi angeliokoka na vyote hivyo, na lau angelitamani pepo kama vile anavyoitamani dunia, basi angelifuzu dunia na akhera, na lau angelimuogopa Mwenyezi Mungu (swt) katika siri kama vile anavyowaogopa viumbe wake katika dhahiri, angelipata fanaka hapa duniani na kesho akhera. Siku moja, mwanahekima aliingia kwa mfalme Mahdy (wa bani Abbas) na akamtaka ampe mawaidha. Akamuambia: Je sio kiti hiki ambamo walikaa baba yako na ami yako kabla yako? Akajibu: Ndiyo. Akamuuliza: Je walikuwa na matendo ambayo unataraji wataokoka kwayo? Akajibu: Ndiyo. Tena akamuuliza: Je walikuwa na matendo ambayo unawaogopea watahiliki kwayo? Akajibu ndiyo. Hapo mwanahekima akamuambia: “tenda yale uliyowatarajia na ujiepushe na yale uliyowahofia”.

HOFU BAINA YA KUZIDI NA KUPUNGUA Aya tukufu na hadithi zimetoa taswira ya umuhimu wa hofu na athari yake katika kumyoosha mwanadamu na kumuelekeza muelekeo wa kheri na fanaka na kumfanya anafaa kupata utukufu wa ridhaa ya Mwenyezi Mungu (swt) na neema Zake. Hofu, kama vile hulka zingine njema, haiwezi kusifiwa na kutukuzwa ila ikiwa imepambwa kwa kiwango cha kati, yaani sio kuzidi wala kupungua. Hofu ikizidi huifanya nafsi kuwa kame na kuangamiza ladha ya uzuri wa 166


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:21 PM

Page 167

Tabia njema kwa mujibu wa Ahlul Bayt (a.s) maisha na kumuacha mwenye hofu iliyopindukia ni mwenye kukata tamaa, mwenye kukimbia aliyetopea katika upotofu, anaikerehesha nafsi yake katika ibada na utii hadi mwisho kuitesa na kuiangamiza. Ama hofu ikipungua, hupelekea kupuuza na kushindwa kutekeleza wajibu na kuasi utii kwa Mwenyezi Mungu (swt) na kufuata maagizo Yake. Ama hofu na kutaraji vinapokuwa vimelingana, basi nafsi huwa na uhai, dhati inatukuka na nishati za kiroho hububujika kwa ajili ya kazi yenye mtazamo na manufaa. Kuhusu hilo imam Ja’far Sadiq (a) anasema: “Uwe na matarajio kwa Mwenyezi Mungu (swt) ambayo hayatakupelekea wewe kumuasi na uwe na woga naye ambao hautakukatisha tamaa na rehema Yake.”207

MAZURI YA HOFU Thamani ya tabia njema hupimwa kwa kiwango cha athari njema za kibinadamu, kheri na wema katika nafsi ya mtu, mambo ambayo ndiyo sababu ya fanaka na hali njema. Kwa kipimo hiki, hofu inachukua nafasi ya mbele kati ya tabia njema na kuwa na umuhimu wa juu katika ulimwengu wa itikadi na imani. Ni hofu hii ndiyo yenye kuchemsha nafsi na kuzihimiza kwenye kumtii Mwenyezi Mungu (awj) na kuzikataza kumuasi. Na kutoka hapo inazipandisha hadi daraja ya wachamungu wema. Na pindi hisia za hofu zinapokuwa na athari njema ndani ya nafsi, huitakasa nafsi na kuipandisha hadi kufikia daraja tukufu ya malaika, kama vile Imam Ali (a) alipokuwa akilinganisha baina ya malaika, mwanadamu na myama alivyosema: “Hakika Mwenyezi Mungu (awj) amewapa malaika akili pasi na shahwa (matamanio), na wanyama akawapa shahwa bila ya akili, na ama mwanadamu akampa vyote viwili. Kwa hivyo, yule ambaye akili yake itayashinda matamanio, atakuwa ni bora kuliko malai207. Al Bihar, muj. 15, juz. 2, uk. 188 167


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:22 PM

Page 168

Tabia njema kwa mujibu wa Ahlul Bayt (a.s) ka na yule ambaye matamanio yake yataishinda akili yake atakuwa ni duni kuliko wanyama”.208 Kwa ajili ya hilo tunakuta kwamba mwenye kumuogopa Mwenyezi Mungu (swt), huona rahisi taabu ya kumcha na uchungu wa hilo huuona mtamu, na huona uchafu utamu wa maasi na madhambi yote kwa sababu ya kuogopa hasira na adhabu Yake (swt). Kwa haya ndiyo mwanadamu hufuzu na kupata fanaka na maisha yake ya kimada na kiroho huchanua kama vile ulimwengu ulivyo na nidhamu na ilivyopangika vyema misingi yake ya mbinguni na ardhini kwa kumnyenyekea Mwenyezi Mungu (swt) na kuwenda kwa kufuata nidhamu na kanuni alizoziweka.

“Afanyaye mema mwanamume au mwanamke hali ya kuwa ni Muumini basi tutamhuisha maisha mema, na bila shaka tutawapa malipo yao kwa sababu ya matendo bora waliyokuwa wakitenda.” (Suratu Nahl, 16: 97) Na bila shaka haya maafa na balaa yanayokabili ulimwengu leo na huku kuenea kwa vurugu na madhambi ya jinai, kutawala wasiwasi, fadhaa na woga wa watu ni kwa sababu moja tu, nayo ni kutomjali Mwenyezi Mungu (swt) na kuipuuza (kuiweka kando) katiba yake na sheria zake.

“Na kama watu wa miji wangeamini na kumcha (Mwenyezi Mungu 208. Ilal sharai' 168


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:22 PM

Page 169

Tabia njema kwa mujibu wa Ahlul Bayt (a.s) lazima tungewafungulia baraka za mbingu na ardhi, lakini walikadhibisha, tukawaangamiza kwa sababu ya yale waliyokuwa wakiyachuma.” (Suratul A’raf; 7: 96)

JINSI YA KUDIRIKI HOFU Ni vyema kwa yule ambaye hisia za hofu zimepungua ndani ya nafsi yake kufuata nasaha zifuatazo: 1. Kusimika mizizi ya akida na kuimarisha imani ya Mwenyezi Mungu (swt), mafhumi (maana) ya kiyama, thawabu na adhabu, pepo na moto, kwa kuwa hofu ni katika matunda ya imani na athari zake kwenye nafsi.

“Hakika wenye kuamini ni wale tu ambao anapotajwa Mwenyezi Mungu nyoyo zao hujaa khofu, na wanaposomewa Aya Zake huwazidishia imani, na wakamtegemea Mola wao tu.” (Suratul Anfaal, 8:2) 2. Kusikiliza mawaidha fasaha na maneno ya hekima yenye faida ambayo yanapelekea mtu kuogopa. 3. Kujifunza hali za watu wenye kumuogopa Mwenyezi Mungu (swt), jinsi wanavyomuomba na kujikurubisha Kwake kwa kuogopa uwezo na adhabu Yake. Hebu tazama hii hali ya juu katika kunyenyekea na hofu, nayo ni katika minongono (munaajaat) ya Imam Ali Zainul-Abidin (a) na Mola wake: “Na kwa nini mie nisilie!! Na ilhali mimi sijui nini hatima yangu? Na naona nafsi yangu inazidi kunidanganya na masiku yangu yanaendelea 169


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:22 PM

Page 170

Tabia njema kwa mujibu wa Ahlul Bayt (a.s) kunihadaa na huku juu ya kichwa changu zinapiga mbawa za mauti, nina nini mimi nisilie? Naam nilie kwa ajili ya kutoka nafsi yangu, nilie kwa ajili ya kiza cha kaburi, nilie kwa ajili ya ufinyu wa kaburi langu, nilie kwa ajili ya kuulizwa na Munkar na Nakir, nilie kwa sababu ya kutoka kaburini nikiwa niko uchi, dhalili nikibeba mzigo wangu juu ya mgongo wangu, natazama mara kulia kwangu na mara kushoto, watu halaiki wamo katika jambo lisilo langu.

“Kila mtu miongoni mwao siku hiyo atakuwa na jambo litakalomtosha. Siku hiyo nyuso zitanawiri, zitacheka, zitachangamka. Na nyuso siku hiyo zitakuwa na mavumbi juu yao. Giza zito litazifunika.” (Surat Abasa, 80:37-41)

DOKEZO KATIKA VISA VYA WACHAMUNGU Kutoka kwa Imam Baqir (a) alisema: “Mwanamke mmoja mwasherati aliwatokea baadhi ya vijana wa kiisraeli na kuwavutia. Baadhi yao wakasema: mchamungu fulani lau angemuona huyu dada angevutika! Mwanadada huyu akayasikia maneno haya na kusema: Wallahi mimi sitakwenda nyumbani kwangu hadi nitakapomvuta. Akenda kwa mchamungu huyo usiku na kugonga mlango akinena: Unaweza kunihifadhi kwako? Yule mchamungu akakataa. Huyu mwanadada akasisitiza na kusema: Baadhi ya vijana wa kiisraeli wametaka kunibaka, kwa hivyo nifungulie ama sivyo watanikuta hapa na kunifanyia ushenzi. Aliposikia haya akafungua. Alipoingia tu akazibwaga chini nguo zake. Alipoona uzuri na umbo lake, nafsi yake ikavutika na akapeleka mkono wake kumshika. Lakini nafsi yake ikajirudi, na alikuwa na sufuria juu ya moto. Akenda akaweka mkono wake juu ya moto. Mwanadada akamwuliza: Unafanya nini? Akajibu: Ninauunguza 170


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:22 PM

Page 171

Tabia njema kwa mujibu wa Ahlul Bayt (a.s) kwa sababu ndiyo uliyofanya kazi. Akatoka (mwanadada huyu) mbio na kuwakuta baadhi ya waisraeli na kuwaambia: Haraka muwahini fulani ameweka mkono wake juu ya moto! Walipofika walikuta mkono umekwishaungua!”209 Kutoka kwa Imam Sadiq (a): “Katika waisraeli alikuwepo mchamungu ambaye siku moja alipata mgeni mwanamke mmoja wa kiisraeli. Akamtamani, lakini akawa kila anapomtamani anasogeza kidole katika vidole vyake kwenye moto hadi ilipofika asubuhi akamwambia: Haya nenda, ni mgeni mbaya kiasi gani ulikuwa kwangu!”

27. KUWA NA MATUMAINI (MATARAJIO) NA MWENYEZI MUNGU MAANA Ni kusubiri unachokitaka kwa kuwa kila sababu za kupatikana kwake zimekwishawekwa. Mfano ni kama vile mtu apande mbegu katika ardhi nzuri na kumwagilia na kuutazama mmea kisha akatarajia kupata mazao na manufaa. Ikiwa sababu hazitatangulizwa, basi matarajio hayo ni upumbavu na kujidanganya. Mfano mtu alime ardhi ya tope yenye chumvi na asijali kuitazama kisha asubiri mazao! Matumaini ni bawa la pili la hofu, mbawa mbili ambazo muumini huruka nazo katika anga za utiifu kwa Mwenyezi Mungu (swt), na kufuzu kwa utukufu wa ridha Yake na ukarimu wa neema Zake. Na hii ni kwa kuwa matumaini humsukuma mtu kwenye utii akiwa ni mwenye shauku na kuta209. Al Bihar, muj. 5 171


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:22 PM

Page 172

Tabia njema kwa mujibu wa Ahlul Bayt (a.s) ka kama vile hofu humsukuma kwenye kuogopa na kufadhaika. Pamoja na kwamba hofu na matumaini vinasaidiana kumfunda muumini na kumuelekeza mwelekeo wa kheri na wema, lakini matumaini ni yenye chimbuko lenye utamu zaidi na onjo bora zaidi kuliko hofu kwa sababu yanachimbuka kwenye kuwa na imani na Mwenyezi Mungu (swt) na kuwa na uhakika wa upana wa rehema ya Mwenyezi Mungu (swt), ukarimu wa msamaha Wake na wingi wa neema Zake.

QUR’ANI NA HADITHI Ni kawaida kwamba mtiifu kwa sababu ya kutaka na kutaraji ni bora kuliko mtiifu kwa sababu ya woga na hofu. Kwa ajili ya hilo bishara za matumaini ni nyingi na vichochezi vyake tele, na aya zake zenye kunawiri. Zifuatazo ni chache: 1. Kukataza kukata tamaa Mwenyezi Mungu (swt) anasema:

“Sema: Enyi waja wangu mliojidhulumu wenyewe! msikate tamaa katika rehema za Mwenyezi Mungu, bila shaka Mwenyezi Mungu husamehe dhambi zote, hakika yeye ni Mwingi wa kusamehe Mwenye kurehemu.” (Surat Zumar, 39:53)

172


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:22 PM

Page 173

Tabia njema kwa mujibu wa Ahlul Bayt (a.s) “Enyi wanangu! nendeni mkamtafute Yusuf na nduguye, wala msikate tamaa katika rehema ya Mwenyezi Mungu, Hakika hakati tamaa ya rehema ya Mwenyezi Mungu isipokuwa watu makafiri.” (Surat Yusuf, 12: 87) Mtume (s) alisema: “Mwenyezi Mungu (swt) atawafufua Siku ya Kiyama wenye kukata tamaa nyuso zao zimezidisha weusi juu ya weupe na kuambiwa; hawa ndio wakatao tamaa na rehma ya Mwenyezi Mungu (swt).”210 Amirul-Mu’minin (a) alimwambia mtu ambaye hofu imemfikisha kwenye kukata tamaa kwa sababu ya wingi wa madhambi yake: “Ewe wewe, kukata tamaa kwako na rehema ya Mwenyezi Mungu (swt) ni dhambi kubwa kuliko madhambi yako”.211 2. Upana wa rehma ya Mwenyezi Mungu (swt) na ukubwa wa msamaha Wake. Mwenyezi Mungu (swt) anasema:

“Kama wakikukadhibisha, basi waambie! Mola wenu ni Mwenye rehema nyingi na adhabu yake haizuiliwi kwa watu waovu.” (Suratul An’am, 6: 147)

210. Safinatul Bihar, juz. 2, uk. 451 211. Jamiu Sa'adaat, juz. 1, uk. 246 173


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:22 PM

Page 174

Tabia njema kwa mujibu wa Ahlul Bayt (a.s) “Na wanakuhimiza (ulete) mabaya kabla ya mema, hali zimekwisha pita adhabu za kupigiwa mfano kabla yao. Na hakika Mola wako ni Mwenye msamaha kwa watu juu ya dhulma yao, na hakika Mola wako ni Mkali wa kuadhibu.” (Suratul Ra’d, 13: 6)

“Hakika Mwenyezi Mungu hasamehe kushirikishwa naye, na husamehe yasiyokuwa hayo kwa amtakaye. Na mwenye kumshirikisha Mwenyezi Mungu, bila shaka amezusha dhambi kubwa. (Suratul Nisaa, 4: 48).

“Sema: Enyi waja wangu mliojidhulumu wenyewe! msikate tamaa katika rehema za Mwenyezi Mungu, bila shaka Mwenyezi Mungu husamehe dhambi zote, hakika Yeye ni Mwingi wa kusamehe Mwenye kurehemu.” (Suratu Zumar, 39: 53) Imepokelewa hadithi kutoka kwa Mtume (s): “Kama isingekuwa kwamba nyinyi mnafanya madhambi na kumuomba Mwenyezi Mungu (swt) maghfira, basi Mwenyezi Mungu (swt) angeleta (angeumba) watu wanaofanya madhambi na kumuomba maghfira kisha akawasamehe. Hakika muumini ni yule anayefanya madhambi na haraka akatubia,(hakika muumini ni mwenye kupewa mtihani na mwenye kutubia sana), je hamkusikia kauli ya Mwenyezi Mungu isemayo: ‘Mwenyezi Mungu anawapenda watubiaao sana.’” (Al-Baqarah; 2:222). 212 212. Al Waafy, juz. 3, uk. 51 174


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:22 PM

Page 175

Tabia njema kwa mujibu wa Ahlul Bayt (a.s) Imam Sadiq (a) alisema: “Itakapokuwa Siku ya Kiyama, Mwenyezi Mungu ataitandaza rehema Yake hadi Ibilisi atatamani rehema hiyo.” 213 Sulayman bin Khalid anasema: “ Nilimsomea Abu Abdilah (a) aya hii:

“Ila yule aliyetubia na kuamini na kufanya vitendo vizuri, basi hao ndio Mwenyezi Mungu atawabadilishia maovu yao kuwa mema, na Mwenyezi Mungu ni mwingi wa kusamehe, Mwenye kurehemu” (Al Furan, 25:70). Akajibu : Aya hii ni kuhusu nyinyi. Siku ya Kiyama ataletwa muumini mwenye madhambi na kusimamishwa mbele ya Mwenyezi Mungu (awj), na Yeye ndiye atakayemfanyia hisabu yake. Atamsimamisha kwenye madhambi yake moja baada ya nyingine na kumuambia: Ulifanya kadha, siku kadha, saa kadha. Atasema: Nakiri ewe Mola wangu. Ataendelea kumsimamisha hadi madhambi yake yote, na yeye akikiri kwa kila dhambi. Mwenyezi Mungu atamuambia niliyasitiri duniani na leo ninayasamehe, kwa hiyo mbadilishieni mja wangu hayo kuwa mema. Sahifa yake itanyanyuliwa ili watu waione. Watasema: Subhanallah! Huyu bwana hakuwa na dhambi hata moja?! Hii ndiyo kauli ya Mwenyezi Mungu ( basi hao ndio Mwenyezi Mungu atawabadilishia maovu yao kuwa mema, (Suratul Furqan: 25: 70). 214 3. Dhana njema kuhusu Mwenyezi Mungu, Karimu. Hii ni msukumo wa nguvu zaidi wa matumaini. 213. Al Bihar, muj. 3, uk. 274 214. Kama hapo juu. 175


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:22 PM

Page 176

Tabia njema kwa mujibu wa Ahlul Bayt (a.s) Imam Ridhwa (a) amesema: “Uwe na dhana njema kwa Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu anasema: ‘Mimi niko kwenye dhana ya mja wangu kuhusu Mimi; ikiwa ni kheri basi (mimi kwake) ni kheri, na ikiwa ni shari basi (mimi kwake) ni shari.’”215 Imam Sadiq (a) alisema: “Mja wa mwisho atakayepelekwa motoni atageuka (kumgeukia Mwenyezi Mungu). Mwenyezi Mungu atasema: Haraka mrudisheni. Atakapoletwa Mwenyezi Mungu atamuambia: Mja wangu, dhana yako kwangu ilikuwa ipi? Atajibu: Ewe Mola Wangu, dhana yangu Kwako ilikuwa kwamba unisamehe madhambi yangu na uniingize kwenye pepo Yako. Mwenyezi Mungu atasema: Enyi malaika Wangu, naapa kwa nguvu Zangu na utukufu Wangu na neema Zangu na mitihani Yangu na ujuu wa nafasi Yangu, huyu mja Wangu hakunidhania vyema hata saa moja katika uhai wake. Na laiti angenidhania kwa wema saa moja katika uhai wake, basi nisingemhofisha na moto. Mkubalieni uongo wake na mumuingize peponi. Kisha Abu Abdullah(a) akasema: Mja hakumdhania wema Mwenyezi Mungu isipokuwa Mwenyezi Mungu huwa kwenye dhana yake kuhusu Yeye, na hamdhanii ubaya ila Mwenyezi Mungu huwa kwenye dhana yake kuhusu Yeye. Na hilo ndio kauli Yake (awj): “Na hiyo dhana yenu mliyomdhania Mola wenu imekuangamizeni, na mmekuwa miongoni mwa wenye hasara.” (Surat Fuswilat; 41:23).216 4. Uombezi wa Mtume (s) na Maimamu waliyotoharika (a) kwa wafuasi wao na wapenzi wao. Imam Ridhwa (a) kutoka kwa baba zake kutoka kwa Amirul-Mu’minin (a) alisema: Mtume wa Mwenyezi Mungu (s) alisema: “Itakapokuwa Siku ya Kiyama tutapewa mamlaka ya kutawalia hesabu za wafuasi (mashia) wetu; yule ambaye dhulma yake itakuwa baina yake na Mwenyezi Mungu (awj), tutatoa hukmu na atatujibu, ama yule ambaye dhulma yake ni baina yake na watu, tutaomba tupewe zawadi (waliyodhulumiwa wasamehe kwa ombi letu) na tutapewa, na yule atakayekuwa na dhulma baina yake na 215. Al Waafy, juz. 3, uk. 59 216. Al Bihar, muj. 3, uk. 274 176


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:22 PM

Page 177

Tabia njema kwa mujibu wa Ahlul Bayt (a.s) sisi, sisi ni wenye kustahiki zaidi kusamehe”.217 Ath-Tha’laby, ametoa katika tafsiri yake al Kabir, kwa isnadi kwa Jarir bin Abdullah al-Bajaly, kwamba alisema: Mtume wa Mwenyezi Mungu (s) alisema: “hakika mwenye kufa akiwa kwenye mapenzi ya Ahlul Bayt (a), amekufa shahidi, hakika anayekufa kwenye mapenzi ya Ahlul Bayt (a), amekufa amesamehewa, hakika anayekufa akiwa na mapenzi ya Ahlul Bayt (a), amekufa mwenye kutubia, hakika anayekufa akiwa na mapenzi ya Ahlul Bayt (a), amekufa muumini mwenye kukamilika imani, hakika anayekufa akiwa na mapenzi ya Ahlul Bayt (a) malaika wa mauti humpa bishara ya pepo, kisha Munkar na Nakir, hakika anayekufa akiwa na mapenzi ya Ahlul Bayt (a) hupambwa na huigizwa peponi kama anavyopelekwa biharusi kwa mumewe, hakika anayekufa akiwa na mapenzi ya Ahlul Bayt (a) hufunguliwa katika kaburi yake milango miwili hadi peponi, hakika anayekufa akiwa na mapenzi ya Ahlul Bayt (a) Mwenyezi Mungu hujalia kaburi lake kuwa ni mahala pa ziara kwa malaika wa rahma, hakika anayekufa akiwa na mapenzi ya Ahlul Bayt (a), amekufa kwenye Sunna na jamaa, hakika anayekufa akiwa na bughdha ya Ahlul Bayt (a), atakuja Siku ya Kiyama ameandikwa baina ya macho yake: aliyekata tamaa na rehema ya Mwenyezi Mungu…” Hii hadithi, al Allamah Zamakhshary, kwenye tafsiri ya aya 33:33, katika tafsiri yake ya Kashshaaf, ameiweka katika hadithi mursal iliyokubalika na wote. Wameirawi waandishi katika vitabu vya manaqib na fadhail (vinavyoelezea daraja na sifa za watu) mara ikiwa ni mursal na mara nyingine musnad.218 Ibn Hajar katika kitabu chake ‘Swaa’iq’ uk. wa 103, anaripoti hadithi ifuatayo: “Siku moja Mtume (s) aliwatokea masahaba wake na huku wajihi wake 217. Al Bihar, muj. 3, uk. 301 218. Al Fusul Muhimmah - cha Sayyid Abdul Husayn Sharafuddin 177


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:22 PM

Page 178

Tabia njema kwa mujibu wa Ahlul Bayt (a.s) umeng’ara kama kamari. Abdurahman b. Awf akamuuliza kuhusu hilo, akamjibu (s): Hii ni kwa sababu ya bishara ambayo imenijia kutoka kwa Mola wangu kuhusu ndugu yangu na mtoto wa ami yangu na pia binti yangu, ya kwamba Mwenyezi Mungu amemuoza Fatima (a) kwa Ali (a) na akamuamuru Ridhwan – malaika anayechunga pepo – akautikisa mti Tuubaa na hapo ukabeba karatasi kwa idadi ya wapenzi wa Ahlul Bayt (a) wangu na akaumba chini yake malaika wa nuru, akampa kila malaika karatasi. Ifikapo Siku ya Kiyama malaika wataita baina ya halaiki ya watu na yeyote awapendaye Ahlul Bayt (a) atakabidhiwa karatasi hiyo ambayo ndani yake kuna kuachwa huru na moto na hatoachwa hata mmoja. Kwa hivyo ndugu yangu (Ali) na binti yangu (Fatima) wamekuwa ndiyo fidia ya kuachwa huru wanaume na wanawake wa umma wangu na Moto.”219 Ibn Hajar katika kitabu chake hichohicho ukurasa wa 96 anaripoti: “Mwenyezi Mungu alipoteremsha aya hizi: “Hakika wale walioamini na kutenda mema, hao ndio wema wa viumbe. Malipo yao kwa Mola wao ni Mabustani ya milele yanayopita mito chini yake, watakaa humo milele Mwenyezi Mungu amewaridhia nao wamemridhia (malipo) hayo ni kwa yule anayemuogopa Mola wake.” (Suratul Bayyinah; 98:7-8), “Mtume (s) alimuambia Ali (a): Hao ni wewe na Shia wako. Utakuja wewe na Shia wako Siku ya Kiyama mmeridhia na huku mmeridhiwa, na maadui zako watakuja ni wenye ghadhabu wamevunjika”.220 5. Matatizo na maradhi ni kafara ya madhambi ya muumini. Imam Sadiq (a) amesema: “Ewe Mufaddhal! Jihadhari na madhambi, na uwatahadharishe Mashia wetu. Wallahi naapa nyinyi mnalengwa (na madhambi) zaidi kuliko wengine. Hakika mmoja wenu anaadhiriwa na 219. Al Fusul Muhimmah, uk. 44 220. Rejea ya hapo juu, uk. 39 178


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:22 PM

Page 179

Tabia njema kwa mujibu wa Ahlul Bayt (a.s) utawala, anapatwa na ugonjwa, rizki yake inabanwa, anateswa wakati wa mauti hadi waliohudhuria wanasema, jamani kateseka na mauti!; yote haya kwa sababu ya madhambi yake.” Aliponiona nimeathirika na maneno hayo akaniuliza: “Ewe Mufaddhal unajua ni kwa nini haya (lazima yamfike)? Nikajibu: Sijui! niwe fidia yako.’ Akaniambia: “Wallahi yote hayo ni kwa sababu hamtaadhibiwa kwayo kesho Akhera. Kwa hiyo mmetanguliziwa hapa duniani”.221 Kutoka kwa Abi Abdillah (a): Mtume (s) alisema: “Mwenyezi Mungu alisema: “Kwa nguvu Zangu na utukufu Wangu sitamtoa mja duniani na mimi nataka kumrehemu mpaka nitakapo mtakasa na madhambi yake imma kwa magonjwa ndani ya mwili wake, imma dhiki katika riziki yake, na imma hofu katika dunia yake. Na ikiwa patasalia salio (la madhambi), basi nitamfanyia ugumu wakati wa mauti…”222 Kutoka kwa Abu Ja’far (a): Mtume (s) alisema: “Huzuni na balaa humvaa muumini hadi pale humuacha hana dhambi hata moja.” 223 Imam Sadiq (a) alisema: “Hakika muumini hutishwa ndani ya usingizi wake akasamehewa madhambi yake, na hakika hupewa mtihani ndani ya mwili wake akasamehewa madhambi yake”.224

UHAKIKA WA KUTARAJI Katika ambayo yanafaa kutajwa, ni kwamba kutarajia – kama tulivyotangulia kueleza - hakuna faida wala matunda ila baada ya kukamilika baadhi ya sababu zinazopelekea kufana kwake, na kukamilika malengo yake. Vinginevyo huwa ni kujipumbaza na kujidanganya. 221. Al Bihar, muj. 3, uk. 35 222. Al Waafy, juz.3, uk. 172 223. Rejea ya hapo juu. 224. Rejea ya hapo juu. 179


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:22 PM

Page 180

Tabia njema kwa mujibu wa Ahlul Bayt (a.s) Ni upumbavu kabisa mtu ambaye ametupilia mbali njia za uchajimungu na akazivaa njia za upotofu bila ya kujali, kisha akaitamanisha nafsi yake kuwa na matarajio. Hiyo ndiyo ghururi batili na hila inayopotosha. Hebu natuwatazame mabwana watukufu, wateule baina ya walimwengu kama vile mitume, mawasii na mawalii, jinsi walivyotopea ndani ya uchamungu na kukita ndani ya ibada na ilhali ya kuwa wao ni wakaribu zaidi na ukarimu wa Mwenyezi Mungu na kutarajia zaidi rehema yake. Kwa hivyo basi, kutaraji kuna thamani tu pale ambapo kutapatikana njia za uchamungu na kufanya amali njema kama alivyosema Imam Sadiq (a): “Hawezi kuwa muumini mwenye kuamini mpaka pale atakapokuwa ni mwenye kuogopa na kutaraji. Na hawezi kuwa ni mwenye kuogopa na kutaraji hadi pale atakapoyafanyia kazi yale anayoyaogopa na kuyataraji”.225 Pia aliambiwa (a): Kundi katika wafuasi (wapenzi) wako wametopea katika maasi na kusema eti wanataraji. Akasema: “Wamesema uongo na wala sio wafuasi (wapenzi) wetu. Hao ni watu wamedanganywa na matamanio yao ya uongo. Anayetaraji jambo, basi hulishughulikia, na anayehofu kitu, hukikimbia”.226

HEKIMA NDANI YA KUTARAJI NA KUHOFU Watu wanahitilafiana hitilafu kubwa katika tabia na mwenendo. Kwa hivyo basi katika kuwaongoza na kuwaelekeza inatakiwa kuzingatia lipi linalowafaa kuwarekebisha katika kutaraji na kuhofu. 225. Al Waafy, juz. 3, uk. 58 226. Al Waafy, juz. 3, uk. 57 180


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:22 PM

Page 181

Tabia njema kwa mujibu wa Ahlul Bayt (a.s) Kati yao kuna wale ambao warekebishwa na matumaini, nao ni: 1. Waasi ambao wanajutia kupindukia mipaka katika madhambi, wakajaribu kutubia lakini wakakata tamaa na msamaha wa Mwenyezi Mungu kwa sababu ya ukubwa na uwingi wa madhambi yao. Katika hali kama hii, tiba ni kutibu kwanza kukata kwao tamaa kwa kujenga matumaini katika ukubwa wa upole wa Mwenyezi Mungu na upana wa rehema Yake na msamaha Wake. 2. Pia yule ambaye anayejidhiki nafsi yake kwa ibada na kuidhuru hutibiwa kwa mutumaini. Ama ambao hurekebishwa na hofu: Kati yao ni wale waasi makaidi ambao wametopea katika maasi na wanaojidanganya kwa matumaini. Tiba yao ni kwa kuwahofisha na kukemea kukali, kwa kuwakamia na mateso makali na adhabu idhalilishayo. Ni matamu maneno haya ya mshairi aliposema: Unatarajia uokovu na ilhali hukufuata nyayo zake, Hakika safina haielei pasipo kuwa na maji.

28. GHURURI MAANA YAKE Ni kule mwanadamu kujidanganya kwa udanganyifu wa kishetani na rai ya makosa. Mfano: Mtu anayetoa mali aliyonyang’anya katika njia za kheri na wema akiamini ni wema kwake na akitaraji ujira na thawabu. Kwa sababu hiyo akawa ameghururika na amedanganywa. Ni hivi ndivyo wengi wanajidanganya kwa ghururi na matendo yao yakawa na sura nyingine, wanaamini kwamba yako sahihi na kufuzu, lakini lau wangechanganua kidogo wangeona ile sura halisi kwamba matendo 181


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:22 PM

Page 182

Tabia njema kwa mujibu wa Ahlul Bayt (a.s) yao ni batili na ghururi. Ni kwa sababu hiyo ndiyo maana ghururi ni mshirika hatari wa Shetani, na silaha yake yenye kupenya zaidi, na mbinu yake yenye kutisha zaidi. Ghururi ina sura na rangi mbalimbali kwa kuzingatia mielekeo tofauti ya wenye ghururi na sababu za ghururi zao. Kati yao kuna wenye kughurika na dunia na mapambo yake yanayodanganya, wengine wanaghurika na elimu, uongozi, mali, ibada na mfano wa hayo.

AINA ZA GHURURI Hapa tutazipambanua aina muhimu za ghururi na kutoa nasaha namna ya kutibu kila aina ya hizo za ghururi.

A. KUGHURIKA NA DUNIA Wengi wanaosifika na ghururi hii ni wale wenye imani dhaifu, wenye kudanganywa na starehe za dunia na vivutio vyake, kwa hiyo wanajisahaulisha ukweli kwamba dunia ni yenye kutoweka na kwamba baadaye unafuatia uhai wa milele. Ili kujitetea na msimamo wao huu, wenye kughurika na dunia hutumia hoja mbili batili (zenye ulinganifu batili) zifuatazo: Mosi: Hakika dunia ni sawa na fedha taslimu wakati akhera ni sawa na fedha unayodai (deni). Pili: Ni kwamba starehe za dunia ni uhakika ama zile za akhera – kama wanavyodai - hazina uhakika. Na bila shaka lililo yakini ni bora kuliko lililo na shaka. Kwa hoja hizi, bila shaka watu hawa wamekosea na kupotea upotevu uliowazi. Kuhusu hoja ya kwanza, taslimu ni bora kuliko mkopo ikiwa biashara hizo zinalingana katika mizani ya maslahi. Ama ikiwa ya mkopo 182


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:22 PM

Page 183

Tabia njema kwa mujibu wa Ahlul Bayt (a.s) ina maslahi zaidi, basi ni bora. Mfano ni kama yule anayewekeza pesa ili anufaike marudufu baadae, au anayejikataza matamanio na vitamu vilivyopo akilenga kuwa na siha njema katika maisha marefu ya baadae. Baina ya starehe za dunia na zile za Akhera kuna tofauti kubwa sana. Starehe za dunia ni zenye kutoweka zenye uchungu wa shida na majonzi, wakati zile za akhera ni za milele na furaha. Kuhusu hoja ya pili pia wamekosea kwa kuwa na shaka na maisha ya kesho Akhera kwa sababu mitume na mawasii wao, na pia maulamaa wametuthibitishia hilo. Kadhalika wengi katika kaumu zilizotangulia. Wote walikuwa na yakini na Akhera, yakini isiyo na shaka. Ikiwa hali ndiyo hii, shaka ya wenye ghururi ni wazimu mbali na dini na akili. Je, huoni jinsi mgonjwa anavyoamini kwamba dawa aliyopewa na matabibu inatibu? Na haikatai ila mtoto asiye na ujuzi au aliyeghafilika. Baada ya kujua hayo, tazama jinsi Qur’ani na Sunnah zinavyotoa picha ya ukweli wa dunia na ghururi zake. Dunia ni kama vile mwanga wa umeme wa radi au sarabi (mazigazi).

QUR’ANI Mwenyezi Mungu (swt) anasema:

183


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:22 PM

Page 184

Tabia njema kwa mujibu wa Ahlul Bayt (a.s) “Jueni ya kwamba maisha ya dunia ni mchezo na upuuzi na pambo na kujifaharisha baina yetu, na tamaa ya kuzidiana katika mali na watoto (Mfano wake ni) kama mvua ambayo mazao yake huwafurahisha wakulima, kisha yanakauka ukayaona yenye rangi ya manjanao, kisha yanakuwa yenye kuvunjika vunjika, na katika Akhera ni adhabu kali na (pia) msamaha wa Mwenyezi Mungu na radhi ( yake) na maisha ya dunia siyo ila ni starehe idanganyayo tu.” (Suratul Hadid, 57: 20)

“Hakika mfano wa maisha ya dunia ni kama maji tuliyoyateremsha kutoka mawinginu, kisha mimea ya ardhini wanayokula watu na wanyama ikachanganyika pamoja, hata ardhi ilipokamilisha uzuri wake na ikapambika na wenyeji wake wakadhani kuwa wana nguvu juu yake, amri yetu ikaifikia usiku au mchana na tukaifanya imefyekwa, kama kwamba jana haikuwepo. Hivyo ndivyo tunavyozieleza Aya kwa watu wanaofikiri.” (Suratu Yunus, 10: 24)

“Ama yule aliyeasi. Na akapenda zaidi maisha ya dunia. Basi kwa hakika Jahannam ndiyo makao. Na ama yule aliyeogopa kusimama 184


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:22 PM

Page 185

Tabia njema kwa mujibu wa Ahlul Bayt (a.s) mbele ya Mola wake, na akaikataza nafsi matamanio (maovu). Basi kwa hakika Pepo ndiyo makazi (yake).” (Suratu Naziat, 79: 37-41)

HADITHI Imam Sadiq (a) alisema: “Mbwa mwitu wawili, mmoja mbele ya zizi la kondoo - wasio na mchungaji - na mgine nyuma, hawana madhara sawa na yale ya kupenda dunia na utukufu katika dini ya mwislamu”.227 Pia alisema (a): “Atakayekuwa asubuhi na jioni dunia ndiyo inamhangaisha zaidi, basi Mwenyezi Mungu (swt) ataweka umaskini baina ya macho yake na kuparaganya jambo lake na hatopata ndani ya dunia ila gawo lake. Na yule ambaye asubuhi na jioni, akhera ndiyo inamhangaisha, Mwenyezi Mungu (swt) atajalia utajiri katika moyo wake na kumkusanyia jambo lake” 228 Imam Baqir (a) alisema: “Mfano wa anayepupia dunia ni kama ule wa mdudu wa hariri. Kila anapozidisha kujizung’ushia nyuzi ndivyo inakuwa kwake muhali kuponyoka hadi yatakapomfika mauti”229 Imam Ali (a) alisema: “Hakika dunia ni yenye kutoweka, taabu, kupanda na kushuka, na mazingatio. Katika kutoweka kwake ni kule unakoona zama ni zenye kuvuta upinde wake, mishale imekaa vizuri kwenye upinde, kamwe haikosei na majeraha yake hayaponi, inamdunga aliye na siha, maradhi na yule aliye hai, na mauti. “Na katika taabu yake ni kule mtu kukusanya yale ambayo hatayala, na 227. Al Waafy, juz 3, uk. 152 228. Al Waafy, juz. 3, uk. 154 229. rejea 97 185


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:22 PM

Page 186

Tabia njema kwa mujibu wa Ahlul Bayt (a.s) kujenga ambapo hatakaa, kisha anaondoka na kurejea kwa Mwenyezi Mungu na huku hana mali aliyochukua wala jengo alilohamisha. “Na katika kupanda na kushuka ni kule wewe unamuona aliyeneemeka mara (ameporomoka) ni mwenye kuonewa huruma, na yule mwenye kuonewa huruma mara (amepanda) na kuneemeka. Baina yao hakuna ila neema iliyotoweka na shida iliyoteremka. “Na katika mazingatio ni kule mtu anasimamia matarajio yake na mara ajali yake inamnyakua, kwa hiyo hakuna matarajio yaliyofikiwa wala mwenye kutaraji aliyeachwa.”230 Imam Musa al Kadhim (a) alisema: “Ewe Hisham hakika wenye akili ni wale waliofanya juhudi (kuipa nyongo dunia) na wakataraji katika Akhera kwa sababu wao walielewa ya kwamba dunia ni yenye kutafuta na kutafutwa na pia Akhera ni yenye kutafuta na kutafutwa. Basi yule anayetafuta Akhera, dunia itamtafuta hadi atakapopata kamili rizki yake na yule anayetafuta dunia, akhera itamtafuta na yatamfika mauti na kumharibia dunia yake na Akhera yake.” 231

KANUNI YA MILELE Watu wote kwa pamoja wanawafikiana katika kulalamika dhidi ya dunia kwa kule kufikwa na mateso yake. Furaha ya dunia ina uchungu wa huzuni na raha yake imezongwa na shida. Kamwe dunia haiwi safi kwa yeyote wala kuneemeka kwayo. Kuna ambao wanaashiki ya dunia, wanaipenda hasa na kuicharukia, jambo ambalo limewafanya kuwa katika hali duni kwa kupambana na kupigana. 230. Safinatula Bihar, juz. 1, uk. 467 231. Tuhaful-Uqul 186


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:22 PM

Page 187

Tabia njema kwa mujibu wa Ahlul Bayt (a.s) Wengine wapo wenye kufanya zuhd (kuipa dunia mgongo), wakajitenga kwa kukimbia starehe na raha - ndani ya nyumba za watawa, jambo lilowafanya kuwa makundi yaliyoparaganyika wanaishi kando na maisha. Ulipodhihiri Uislamu na watu wakiwa na mielekeo hiyo miwili, uliweza – kwa hikma yake ya juu na uwezo wake wa kuongoa uliyoshamiri - kuweka nidhamu ya daima inayooanisha dini na dunia na kuweka pamoja mahitaji ya maisha na shauku za roho kwa mfumo ambao unakwenda sambamba na fikira ya mwanadamu na kumhakikishia maisha ya furaha na fanaka. Kwa hivyo utaona mara inawatahadharisha wanaohusudu maisha ya dunia kuhusu udanganyifu wake na ghururi zake ili kuwakomboa na utumwa wake kama vile hadithi zilizotajwa zilivyotoa picha. Kwa upande mwingine, inawavuta wale wenye kujidhiki, wanaokimbia mazuri ya maisha na taratibu kuwapeleka kufaidi mazuri na vivutio vya maisha haya ili wasijikate na harakati za maisha na hivyo kuwa ni shabaha ya umaskini na unyonge. Imam Sadiq (a) alisema: “Si miongoni mwetu yule atakayeacha dunia yake kwa ajili ya akhera yake, na vilevile akhera yake kwa ajili ya dunia yake.” Na pia: “Itumikie dunia yako kana kwamba utaishi milele, na uitumikie akhera yako kana kwamba utakufa kesho.” Na kwa nidhamu hii ya pekee ulichanua utamaduni wa Kiislamu na Waislamu wakazama chini kabisa katika njia za ukamilifu na ngazi za maendeleo ya kimwili na kiroho. Na kwa mwangaza wa kanuni hii tunagundua hakika zifuatazo: 1. Kustarehe kwa yanayoburudisha na mazuri ya halali ni matendo mema hakuna ubaya kwa sharti tu yasiingilie ya haramu na ubadhirifu kama alivyosema Mwenyezi Mungu (swt). 187


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:22 PM

Page 188

Tabia njema kwa mujibu wa Ahlul Bayt (a.s)

Sema: Ni nani aliyeharamisha mapambo ya Mwenyezi Mungu ambayo amewatolea waja wake na vitu vizuri vya riziki? Sema: Vitu hivyo ni kwa waumini katika maisha ya dunia (na) khasa siku ya Kiyama. Hivyo ndivyo tunavyozibainisha Aya kwa watu wanaojua.” (Suratul A’raaf, 7:32). Na Amirulmu’minin (a) alisema: “Jueni enyi waja wa Mwenyezi Mungu (swt) ya kwamba wachamungu waliondoka na wakiwa (wamefaidi) dunia inayotoweka na kutaraji (thawabu) za akhera inayobaki. Wakashirikiana na watu wa dunia katika dunia yao na wala wao hawakushirikiana nao katika akhera yao. Wakaishi pazuri na kufaidi chakula kizuri, wakajipatia hapa duniani yale waliyoyapata matajiri waliyoneemeka, na wakachukua waliyoyachukua masultani wajeuri, kisha wakaiacha na huku wakiwa na masurufu ya kutosha na biashara yenye faida.”232 2. Kuwa na milki nyingi, kuwa na vitu vya thamani na vinavyotamaniwa ni pia matendo mazuri na ya kusifiwa kwa sharti tu yasichanganyike na haramu au yakamwondoa mtu kwenye dhikri ya Mwenyezi Mungu (swt) na kumcha. Ama ikiwa pamoja na milki kubwa, malengo yako ni kutotegemea watu na kumridhisha Mwenyezi Mungu (swt), kwa kuwafanyia wema ndugu, kuwasaidia wenye shida, kuanzisha miradi ya kheri kama vile misikiti, shule, hospitali, basi hayo ni katika uchajimungu bora na kujikurubisha 232. Nahjul Balagha 188


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:22 PM

Page 189

Tabia njema kwa mujibu wa Ahlul Bayt (a.s) kwa juu zaidi. Imam Sadiq (a) alisema: “Hukuna kheri ndani ya yule asiyekusanya mali kwa njia ya halali ili ajisitiri na kulipa deni lake na pia kuwafanyia wema jamaa zake”.233 Mtu mmoja alimuambia Abu Abdillah (a): “Wallahi sisi tunaisaka dunia na tunataka tuipewe.” Akasema: “Unataka kufanya nini na dunia?” Akamjibu: “Naitaka ili nikidhi mahitaji yangu na ya familia yangu, nisaidie jamaa, nitoe sadaka, nihiji na kufanya umra.” Hapo Abu Abdillah (a) akamuambia: “Hiyo siyo kuisaka dunia bali hiyo ni kuisaka akhera”.234 3. Kupenda kubaki ndani ya dunia, kamwe siyo jambo baya, bali inategemea makusudio na malengo. Atakayeipenda kwa ajili ya malengo makubwa, matukufu kama vile kuzidisha uchamungu na kuongeza matendo mema basi hilo ni jambo linalopendeza. Na ama yule atakayeipenda dunia kwa ajili ya malengo duni kama vile kufanya madhambi na kuabudu matamanio, bila shaka hilo ni ovu lisilotakiwa kama alivyosema Imam Ali Zaynulabidin (a): “Nakuomba (Ewe Mola) unizidishie umri ikiwa umri wangu ni katika kunyenyekea kwa kukutii. Ikiwa umri wangu ni malisho ya Shetani, basi nichukue kwako.” Kwa kufanya mukhtasari wa yaliyoelezwa hapo juu, ni kwamba kupenda dunia kusikotakiwa ni kule kupenda kunakomhadaa mtu na kumtokomezea mbali na uchamungu na kujiandaa na maisha ya akhera.

MAOVU YA KUGHURIKA NA DUNIA 1. Kuweka pazia inayozuia baina ya akili na uhakika wa mwanadamu. Kwa hivyo habaini mapungufu na maovu yake yatokanayo na kupupia 233. Al Waafy, juz. 10, uk. 9 234. Rejea ya hapo juu. 189


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:22 PM

Page 190

Tabia njema kwa mujibu wa Ahlul Bayt (a.s) na kucharukia maisha. 2. Kuhangaika na kuteseka. Ghururi huwasukuma walioathirika nayo kuwa na maisha ya taabu na kupambana nayo bila kutosheka au kuzingatia kwamba lazima maisha yatatoweka, jambo linalowafanya wataabike kama vile inavyosema hadithi inayohusu mdudu wa hariri; kadri anavyojizungushia nyuzi ndivyo inakuwa muhali kwake kuponyoka hadi anapokufa kwa kuhangaika. 3. Baada ya hili na lile, ghururi ni miongoni mwa vikengeushi na vipumbazishi dhidi ya kujitayarisha na kujiweka sawa kwa ajili ya akhera na kutenda matendo mema ambayo ndiyo sababu ya maisha mema akhera na neema zake milele. Mwenyezi Mungu anasema:

“Ama yule aliyeasi. Na akapenda zaidi maisha ya dunia. Basi kwa hakika Jahannam ndiyo makao. Na ama yule aliyeogopa kusimama mbele ya Mola wake, na akaikataza nafsi matamanio (maovu). Basi kwa hakika Pepo ndiyo makazi (yake).� (Suratu Naziat, 79: 37-41)

TIBA YA GHURURI 1. Kurejea na kuzingatia aya na hadithi zilizopokelewa kuhusu ubaya wa kughurika na dunia na hatari zake za kutisha. 2. Mitume wote, mawasii na wenye hekima wamekubaliana kuhusu kutoweka kwa dunia na kubaki milele akhera. Kwa mwenye akili ni lazima apendelee kinachodumu milele juu ya kile kinachotoweka na kuji190


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:22 PM

Page 191

Tabia njema kwa mujibu wa Ahlul Bayt (a.s) tayarisha kwa ajili ya furaha ya milele na neema zinazodumu.

“Lakini nyinyi mnapenda zaidi maisha ya dunia. Hali akhera ni bora na yenye kudumu. Hakika haya yamo katika vitabu vya kwanza. Vitabu vya Ibrahim na Musa.” (Suratul A’ala, 87: 16-19). 3. Kufaidika na mawaidha mazuri na hekima zenye kuongoa na visa vyenye mazingatio kuhusu majuto yaliyowafika masultani na wafalme majabari kwa kughurika na dunia na kupoteza maisha yao katika starehe na ufasiki. Miongoni mwa mawaidha yenye mvuto sana na nguvu ya kuathiri zaidi nafsi ni maneno ya Imam Ali (a) kwa mwanae Imam Hasan (a) alipomuusia: “Uhuishe moyo kwa mawaidha, na ufishe kwa zuhdi, na upe nguvu kwa yakini, na utie nuru kwa hekima, na udhalilishe kwa kukumbuka mauti, na ufanye ukiri kutoweka, na uuonyeshe majanga ya dunia na uupe tahadhari na mashambulizi ya maisha na kubadilika vibaya usiku na mchana (hujafa hujaumbika) na uweke mbele yake habari za waliyotangulia na uukumbushe yaliyowafika waliokuwako kabla yako waliotangulia na kisha tembea katika majumba yao na athari zao na utazame katika waliyoyafanya, wameondoka wapi, na wapi wamekwenda na kukaa. Utakuta wamewaacha wapenzi na kwenda kukaa nyumba ya ugeni na kana kwamba pia punde utakuwa miongoni mwao; basi tengeneza mahala pako na usiuze akhera yako kwa dunia yako.235 Na miongoni mwa hekima za juu ni ifwatayo: Wanahekima wamemshabihisha mwanadamu ambaye ametopea ndani ya dunia na kughurika nayo na kughafilika kabisa na yaliyo nyuma yake na 235 Nahjul Balagha 191


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:22 PM

Page 192

Tabia njema kwa mujibu wa Ahlul Bayt (a.s) mtu ambaye ananing’inia ndani ya kisima ameshikiliwa na kamba kiunoni. Chini yake lipo joka limepanua kinywa linasubiri kummeza na juu wapo panya wawili, mmoja mweusi na mwingine mweupe ambao wanaitafuna kamba ile taratibu bila kupumzika. Sasa pamoja na kuona joka na kamba inavyolika, huyu mtu ameshugulika na asali kidogo ambayo imepakwa kwenye ukuta wa kisima na kuchanganyika na udongo na kukusanyika juu yake zamburi (aina ya mdudu kama nyigu) wengi. Anashughulika na kuramba asali na kuwafukuza wadudu, akili yake yote imeshughulishwa na wala hatanabahi juu kuna nini na chini kunamsubiri nini! Tafsiri: kisima ni dunia, kamba ni umri, joka ni mauti, panya wawili ni usiku na mchana wanaopunguza umri, asali iliyochanganyika na udongo ni starehe za dunia zilizochanganyika na matatizo na maovu, zamburi ni wanadamu. Katika mazingatio bora kabisa kuhusu kuondoka kwa maisha hata kama yatadumu kiasi gani ni kwamba Nabii Nuhu (a) aliishi miaka 2500 kisha malaika wa mauti alimjia na yuko juani na kumuambia: “Amani iwe juu yako.” Naye akajibu na kumuuliza: “Nini haja yako ewe Malaika wa mauti?” Akamjibu: “Nimekuja ili nichukue roho yako.” Akamuambia (a): “Niache niondoke juani na kwenda chini ya kivuli.” Akamkubalia, kisha Nabii Nuhu (a) akasema: “Ewe Malaika wa mauti, muda wote nilioishi duniani ni mithili ya huku kutoka juani na kwenda kivulini!!” Basi akatekeleza aliloamrishwa, akachukua roho yake. Katika mazingatio kuhusu wafalme waovu, ni yale alioyasema Mansur (al Abassy) pindi alipofikwa na mauti: “Tumeuza akhera kwa usingizi mmoja”. Naye Harun Rashid (al abassy) pindi anapochagua kafani zake wakati umauti unamfika alikuwa akikariri maneno haya:

192


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:22 PM

Page 193

Tabia njema kwa mujibu wa Ahlul Bayt (a.s)

“Mali yangu haikunifaa. Ukubwa wangu umenipotea.” (Suratul Haqqa; 69: 28-29) Abdulmalik bin Marwan katika maradhi yake aliulizwa: “Unajiona je ewe baba Marwan?” Akajibu: “Najiona kama vile alivyosema Mwenyezi Mungu:

“Na (Siku ya Kiyama tutakwambieni) bila shaka mmetuijia mmoja mmoja kama tulivyo kuumbeni mara ya kwanza, na mmeyaacha nyuma tuliyokupeni, na hatuwaoni waombezi wenu pamoja nanyi ambao mlidai kuwa ni washirika (wa Mwenyezi Mungu) kwenu bila ya shaka yamekatika (mahusiano yaliyokuwa) baina yenu, na yamekupoteeni mliyokuwa mkidai.” (Suratul An’am, 6: 94) Zaytun al Hakim (mwenye hekima, tabibu) alimuona mtu kwenye ufukwe wa bahari mwenye huzuni na majonzi, anasikitikia dunia. Akamuambia, ewe kijana, kwa nini huzuni hii kwa ajili ya dunia? Lau kama ungekuwa unautajiri mwingi na umepanda bahari, kisha meli ikapata ajali ukawa unazama, je lengo lako halitakuwa tu kuokoka hata kama kila ulichokimiliki kitakupotea? Akajibu: Ndiyo. Kisha akamuuliza: Lau kama ungekuwa mfalme juu ya dunia na wakakuzunguka ambao wanataka kukuuwa, je muradi wako hautakuwa ni kusalimika kutoka mikononi mwao, hata kama kitaondoka kila unacho kimiliki? Akajibu: Naam. Basi, akamuambia wewe 193


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:22 PM

Page 194

Tabia njema kwa mujibu wa Ahlul Bayt (a.s) ndiyo huyo tajiri na huyo mfalme. Akafarijika mwanaume huyo kwa maneno haya ya hekima. Mmoja katika maurafaa (wajuzi waliojikurubisha na Mwenyezi Mungu) alimuambia mtu mmoja tajiri: Iko je namna yako ya kutafuta dunia? Akajibu: Natafuta sana. Akamuuliza: Je umediriki unachokitafuta? Akajibu: Hapana. Basi akamuambia, hii (dunia) ambayo umepoteza umri wako ukiitafuta na hukupata muradi wako, sasa vipi hiyo (akhera) ambayo hukuitafuta?! Hakuna shaka kwamba haya mawaidha hayawezi kumnufaisha ila yule ambaye ana moyo ulio salama na akili inayozingatia. Ama wale ambao maisha yamewafanya watumwa na kupiga muhuri juu ya nafsi zao, mawaidha mazuri hayawasaidii kama alivyosema mmoja wa maurafaa: “Moyo ukishanyweshwa mapenzi ya dunia mawaidha hata yakiwa mengi hayanufaishi kama vile mwili ukiwa umekolea ugonjwa, wingi wa dawa hausaidii�.

B. GHURURI YA ELIMU Katika aina za ghururi na udanganyifu wake ni kughurika na elimu na upana wa maarifa jambo linalosababisha, kwa baadhi ya watu watukufu, kiburi na kujisifu na pia kushindana vibaya kwa ajili ya jaha na kurukia matamanio na mfano wake miongoni mwa tabia mbovu ambazo haziwafai hata wajinga achilia mbali maulamaa. Na hutokea wengine baadhi wakapindukia mipaka katika kujiona na ghururi wakapandwa na wazimu wa ukubwa na kujikweza juu ya watu kwa kiburi na kudharau. Wenye kughurika na elimu wameshindwa kuelewa kwamba elimu siyo lengo lenyewe bali ni wasila (njia) ili kumfunda mtu na kumfikisha kwenye ukamilifu na furaha, dunia na akhera. Ikiwa elimu haitahakiki 194


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:22 PM

Page 195

Tabia njema kwa mujibu wa Ahlul Bayt (a.s) malengo hayo matukufu, itakuwa ni juhudi iliyopotea na mateso yanayotaabisha, na ghururi inayodanganya.

“Mfano wa wale waliopewa Taurati kisha hawakuichukua, ni kama mfano wa punda anayebeba vitabu vikubwa vikubwa, mfano mbaya mno wa watu waliozikadhibisha Aya za Mwenyezi Mungu, na Mwenyezi Mungu hawaongozi watu madhalimu.” (Suratul Jum’ah, 62:5) Amepatia vyema mshairi aliposema: Lau kama wanaelimu wangeilinda basi ingewalinda na laiti wangeitukuza katika nafsi zao ingetukuka lakini wameidhili ikadhalilika, na kwa tamaa wamefunika nuru yake mpaka ikawa ni giza Elimu ni kama mvua inayonyesha kwa wingi juu ya ardhi nzuri na kuibadilisha kuwa mabustani yaliyoshamiri, na kusheheni neema na uzuri. Ama ikiteremka juu ya ardhi iliyo na chumvi, haitoi manufaa yoyote. Hivi ndivyo elimu huwarejeshea waliowatukufu (watu wema) uzuri na utukufu (mng’aro) na ama yule aliye muovu humzidishia ukhabithi na uovu. Ni vipi mjuzi aghurike na elimu yake wakati yeye siyo pekee katika uwanja huu, ulimwengu (watu) umeshuhudia, toka enzi na hivi sasa maulamaa waliyobobea na kutukuka katika uwanja wa elimu, na wakapasua katika peo zake na wakawa ni wenye athari za kielimu zinazobaki daima.

195


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:22 PM

Page 196

Tabia njema kwa mujibu wa Ahlul Bayt (a.s) Kamwe haifai elimu kuwa sababu ya majivuno wala ghururi kwa kuwa wajibu wa mtu mjuzi ni mzito na kuhesabiwa kwake ni zaidi kuliko mtu mjinga na hoja juu yake ni zaidi. Ikiwa hatachunga nuru ya elimu na kufanya kazi kulingana na mahitaji ya elimu, basi elimu inageuka kuwa ni maangamio juu yake na yeye kubadilika kuwa mfano mbaya kwa watu. Tazama jinsi Ahlul Bayt (a) wanavyotoa picha ya maovu ya maulamaa na hatari zao: Mtume (s) alisema: “Kaumu miongoni mwa watu wa peponi wataona kaumu miongoni mwa watu wa motoni na watasema: Ni kipi kilichokuingizeni motoni wakati sisi tumeingia peponi kwa fadhila za maadabisho na mafunzo yenu? Watajibu: tulikuwa tukiamuru mema na wala hatuyafanyi.” 236 Imam Jafar (a) kutoka kwa baba yake alisema: Mtume (s) alisema: “Aina mbili za watu katika umati wangu wakiongoka, basi umati wote umeongoka, na wakiharibika basi umati wote umeharibika. Akaulizwa: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu (swt) ni nani hawa? Akajibu: Mafaqihi (wajuzi wa sheria za Mwenyezi Mungu) na maamiri (wenye mamlaka)”237 Imam Sadiq (a) alisema: “Atasamehewa mtu mjinga dhambi sabini kabla ya kusamehewa mjuzi dhambi moja.” 238 Kwa hiyo inawapasa ulamaa na watu watukufu kuwa ni kigezo chema kwa watu na mfano wa tabia bora, na wajiepushe kadri ya uwezo wao matelezo ya ghururi na silika zake chafu na wawe makini kudiriki maana ya aya ifuatayo:

236. Al Waafy fi Waswiyyatihi 237. Al Bihar, muj, 1, uk. 83 238. Al Waafy, mujalad wa akili na elimu, uk. 52 196


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:22 PM

Page 197

Tabia njema kwa mujibu wa Ahlul Bayt (a.s)

“Hivyo nyumba ya akhera tutawafanyia wale wasiotaka kujitukuza katika ardhi wala (kufanya) ufisadi, na mwisho (mwema) ni kwa wacha Mungu.” (Suratul Qasas, 28: 83)

C. GHURURI YA JAHA (MAMLAKA, UONGOZI, CHEO CHA JUU…) Jaha, (mamlaka..) inatazamiwa kuwa miongoni mwa sababu ya nguvu ya ghururi na yenye kuchochea zaidi. Utawaona wenye mamlaka (madaraka), wanatakabari juu ya watu kwa ghururi na majivuno na kudhalilisha heshima zao kwa kujivuna na kiburi. Katika zama zote, watu wameishi matatizo haya na kuonja kwa majonzi uchungu wa ghururi ya wenye mamlaka. Hawa walioghurika na utawala wameghafilika ya kwamba kupindukia mipaka katika ghururi na ubinafsi ni jambo halitakiwi na uislamu, nao umeonya kwa indhari mbali mbali na vitisho katika maisha hapa duniani na kesho akhera. Pia tabia hiyo inafanya watu wawachukie, wawaghadhibikie na kuwalaani na hivyo basi kupoteza tendo adhimu na ghali katika maisha nalo ni mapenzi ya watu na huruma yao, wakati ambapo ilikuwa wao kwa nafasi zao wangeweza kuwavuta watu na kuongeza rasilimali yao ya kupendwa na watu na kupata upendo wa umma. Wafanyie wema watu utazimiliki nyoyo zao Daima wema humfaya mtu mtumwa Kiungo muhimu zaidi katika kupunguza makali ya ghururi na kuminya misukumo yake mikali ni kutafakari na kuzingatia yale yanayowafika 197


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:22 PM

Page 198

Tabia njema kwa mujibu wa Ahlul Bayt (a.s) wenye ghururi kuhusiana na kubadilika hali na zama, na nguvu ya qadari. Mwenye mamlaka ni kama aliepanda simba mkali hajui ukomo wa ghadhabu yake na ukali wake. Historia imesheheni aina mbalimbali za mawaidha na mazingatio kuhusu hilo. Miongoni mwayo ni yale aliyoeleza Abdullah bin Abdu Rahman kwamba, siku moja niliingia kwa mama yangu siku ya Idul Adhha, mwaka wa 190 H., nikamuona kwake bibi kizee mwenye nguo mbovumbovu zimechanika, lakini mwenye ufasaha! Nikamuuliza mama: Ni nani huyu bibi? Akanijibu: Huyo ni shangazi yako Abaya mama yake Ja’far bin Yahya al Barmaky (alikuwa ni mtu wa pili kwa cheo baada ya khalifa zama za utawala wa ki-Abbasi). Basi nikamsalimia na kumkaribisha kwa ucheshi na kusema: Ha! Hivi maisha yamekugeukia namna hii ninavyoona? Akanijibu: Ndiyo ewe mwanangu, tulikuwa ndani ya madeni ambayo maisha yameyarejesha. Nilipomtaka anielezee habari zake, alinieleza: “Kwa mukhtasari, kuna wakati Idul Adhha ilinipitia nikiwa na wafanyakazi (wa kike) mia nne, ni ilhali nikiona kwamba mwanangu kanitupa, leo nimekujia naomba ngozi mbili za kondoo, moja kwa ajili ya tandiko na nyingine ya kujifunika!” Hali hiyo ilinifanya nisikie huruma sana na nikampa dirham kadha, fadhila ambayo ilimfanya atake kufa kwa furaha.239 Siku moja, mmoja katika watoa mawaidha aliingia kwa Harun Rashid, naye akamtaka ampe mawaidha. Hapo akamwambia: “Unaonaje ikiwa utanyimwa maji wakati una kiu unayahitaji, utayanunua kwa kitu gani?” Harun Rashid akajibu: “Kwa nusu ya ufalme wangu.” Tena akamuuliza: “Unaonaje ikiwa yatazuiwa pindi yanatoka, utayanunua na nini?” Akajibu: “Kwa nusu iliyobaki.” Hapo akamuambia Harun: “Usikudanganye ufalme ambao thamani yake nywesho la maji.” Inafaa kwa mwenye akili kudiriki ya kwamba yote anayojivunia, iwe ni mali, elimu, au jaha na uwezo ni neema na hisani za Mtoaji neema Mkuu 239. Safinatul Bihaar, muj. 2, uk. 609 198


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:22 PM

Page 199

Tabia njema kwa mujibu wa Ahlul Bayt (a.s) alizomtunukia. Kwa hiyo zinastahili kusifiwa na kushukuriwa na wala siyo kujivuna na kujiona.

JAHA INAYOKUBALIKA NA ISIYOKUBALIKA Kutafuta jaha siyo moja kwa moja jambo baya, bali inatofautiana kutegemea tofauti ya malengo. Atakayeitafuta kwa ajili ya lengo linalokubalika kisheria na kwa lengo tukufu, kama vile kumnusuru aliyedhulumiwa, kumsaidia dhaifu, kuiepushia nafsi yako na wengine dhulma‌ jaha aina hiyo inakubaliwa na ya kusifiwa. Ama atakayeitafuta kwa malengo ya kuwa na mamlaka na kuwa juu ya watu, na kuwahukumu hiyo ni jaha duni na isiyotakiwa. Katika baadhi ya sura za jaha, malengo yanaweza yakawa yanachanganya. (Mifano ya sura hizo ni kama vile) kuutaka uimamu wa jamaa, kushughulika na kuwaelekeza watu na kuwaongoza na kuwa juu katika kuongoza vitivo vya kiroho muhimu. Katika hali kama hiyo malengo hubainika kwa kutazama je hao wenye nafasi za juu wana ikhlas njema, utukufu wa lengo na kuwapendea watu kheri au wana sifa ya ubinafsi, na kuzibania fursa. Hii ni miongoni mwa ghururi, Mwenyezi Mungu (swt) atuepushe.

D. GHURURI YA MALI Hivyo hivyo, mali huchochea nguvu zilizolala za ghururi na kuakisi kwa wenye tatizo hilo sura mbaya za ghilba, utapeli na kudanganya. Ghururi hii huwachanganya matajiri wenye kupenda jaha, na kwa hivyo huwasukuma kutoa kwa wingi na ukarimu mali zilizochanganyika na haramu. Kwa kufanya hilo hujiona wanafanya mema wakati wameghurika na kujidanganya.

199


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:22 PM

Page 200

Tabia njema kwa mujibu wa Ahlul Bayt (a.s) Baadhi yao huenda wakaonyesha dhahiri huruma kwa watu masikini, lakini kisiri wakawa mabakhili. Yote hayo kwa ajili ya kupata umaarufu na sifa. Wengine wapo ambao wanashindwa kutimiza haki za Mwenyezi Mungu (swt) za faradhi kwa sababu ya ubakhili na akatosheka na kutekeleza ibada ambazo hazidai gharama wala kutoa, k.v. Sala, Saumu, wakidai kuondolewa dhima kwa hilo. Hii ni ghururi kwa sababu ni wajibu kutekeleza faradhi za Mwenyezi Mungu (swt) iwe za kiroho au za kimada. Kila faradhi ina umuhimu wake katika ulimwengu wa akida na sheria. Kwa ajili ya hiyo, mali ni katika vichochezi hatari kabisa vya ghururi na vishawishi vyake. Imam Sadiq (a) alisema: “Ibilisi anasema: Miongoni mwa yaliyonisumbua kwa mwanadamu, moja katika haya matatu kutoka kwake hayatanisumbua; kuchukua mali isiyohalali au kuizuia penye haki yake au kuiweka pasipo mahala pake” Imam Ali (a) alisema: “ Mtume (s) alisema: “Hakika dinari na dirham ziliangamiza waliyokuwepo kabla yenu. Na nyinyi pia zitawaangamizeni.”

MALI BAINA YA SIFA NA SHUTUMA Mali ina mazuri yake na mabaya, madhara na manufaa. Mali humpa mtu furaha au maangamio kutegemea jinsi alivyoipata na malengo ya kuitumia. Katika mema yake, mali ni zana madhubuti inayomuwezesha mtu kutekeleza njia za maisha na kupata mahitaji ya uhai. Pia ni sababu yenye nguvu kwa wenye mali kuwa na izzah (utukufu) na kutohitajia watu waovu. Pia ni nyenzo ya kupata mambo ya kuhimidiwa na utukufu, kama asemavyo Sharifu Radhwi (Mwenyezi Mungu amurehemu): 200


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:22 PM

Page 201

Tabia njema kwa mujibu wa Ahlul Bayt (a.s) Kamwe hakudanganywa aliyenunua utukufu kwa mali Hakika mali huwekwa kwa ajili ya haja za marijali Na mwanamume ni yule anayelenga mali kuwa thamani ya utukufu Vile vile mali ni katika njia za kujiandaa (kwa kukusanya mahitaji) kwa ajili ya Akhera na kupata furaha ya milele humo. Katika mabaya ya mali: humsukuma mtu kuogelea katika mambo yasiyoaminika na kufanya ya haramu na maovu kama vile kuchuma kwa njia za haramu au kukataa kutoa haki za kisheria alizofaradhishiwa na Mwenyezi Mungu (swt) au kutumia mali katika njia za upotevu na machafu, mambo ambayo maangamizo yake yamewekwa wazi katika maandiko hapo kabla. Zaidi ya hayo, mali ni miongoni mwa vipumbazishi na vikengeushi vya nguvu sana kuhusu dhikri ya Mwenyezi Mungu (awj) na kujiandaa na maisha ya kesho Akhera.

“Enyi mlioamini! yasikusahaulisheni mali yenu wala watoto wenu kumkumbuka Mwenyezi Mungu, na wafanyao hayo, basi hao ndio wenye hasara.� (Suratul al-Munafiqun, 63: 9). Mali haishutumiwi kiujumla, bali inategemea njia na malengo yake. Ikiwa njia na malengo ni sahihi na tukufu, mali hiyo inakuwa sababu ya sifa na kutukuzwa. Ama kinyume chake inakuwa ni sababu ya lawama na shutuma. Kwa kuwa nafsi ni zenye kupenda mali, kwa kuikusanya na kuiweka, ni vyema kwa muumini mwenye mtazamo na muamko asije akajidanganya 201


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:22 PM

Page 202

Tabia njema kwa mujibu wa Ahlul Bayt (a.s) kwa mng’aro wake na akaghurika na vivutio vyake. Ni vizuri akawaidhika na jinsi wenye kughurika na mali wanavyokosa malipo akhera na kuambulia tu walichoweza kukitumia katika mali zao. Ama kwa vyote vya ziada wao wamefilisika. Ni wakusanyaji waaminifu wa mali, kwa bidii na taabu kisha wanaiacha ikiwa ni tonge nono na tamu kwa ajili ya warithi. Kwao ni mzigo na kwa watoto ni furaha na urithi hawakuutolea jasho.

E. GHURURI YA NASABA Wako ambao wanaoghurika na utukufu wa nasaba zao na kunasibiana na Ahlul Bayt (a). Kwa hivyo wanadhania ya kwamba wataokoka kwa ukuruba wao na watukufu hawa hata kama watapotoka na mwenendo wao na wakafuata njia za upotofu. Hii ni ghururi danganyifu kwa sababu Mwenyezi Mungu (swt) humtukuza mtiifu hata kama atakuwa ni mtumwa mhabeshi na humdhalilisha muasi hata kama ni bwana Mquraishi. Ahlul Bayt (a) hawakupata matendo hayo matukufu ya milele na kupata utukufu na karama kwa Mwenyezi Mungu (awj) ila kwa jitihada yao katika kumtii Mwenyezi Mungu na kuzama ndani ya ridhaa yake. Watoto kughurika na utukufu wa wazazi wao na ukoo wao na huku wao hawafuati mwenendo wao ni katika ndoto za mchana na hadaa za ghururi. Je umewahi kuona mtu leo mjinga kesho akaamka ni mjuzi basi tu kwa ubora wa wazazi wake? Au mtu muoga akawa shujaa basi tu kwa ushujaa wa mababu zake? Au mtu duni akawa karimu, mwenye moyo mkunjufu basi tu kwa ukarimu wa mababu zake? Sivyo hata kidogo, Mwenyezi Mungu (swt) hawezi kumuweka sawa mtu mtiifu na muasi, au mwenye 202


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:22 PM

Page 203

Tabia njema kwa mujibu wa Ahlul Bayt (a.s) jitihada na yule aliyetulia. Tazama jinsi Qur’ani inavyoelezea unyeyekevu wa Nabii Nuhu (a) kwa Mola Wake katika kumuombea mwanae mpenzi aepukane na gharika la tufani. Lakini hilo halikumsaidia chochote kwa ukafiri wa mwanawe na upotofu wake: “Na Nuhu akamuomba Mola wake, akasema: Ewe Mola wangu! hakika mwanangu ni katika watu wa nyumbani kwangu, na hakika ahadi Yako ni haki, na Wewe ni bora wa mahakimu”. ( Surat Hud, 11: 45-46) Natumsikilize bwana wa mitume (s) jinsi anavyowapa watu wa familia yake darasa la milele katika kumcha Mwenyezi Mungu (swt) na kumuogopa na kuacha kabisa kughurika na utukufu wa nasaba na ukoo kama ilivyopokelewa kutoka kwa Imam Ja’far Sadiq (a) kwamba alisema: “Mtume alisimama juu ya mlima Swafaa na kusema: “Enyi Bani Hashim, enyi Bani Abdul Mutwalib, mimi ni mtume wa Mwenyezi Mungu kwenu, na mimi ni mwenye huruma kwenu, na amali yangu ni yangu na kila mmoja wenu amali yake ni yake. Kamwe msiseme Muhammad ni miongoni mwetu kwa hivyo tutaingia anapoingia. Kwa hiyo wafuasi wangu; wawe miongoni mwenu au wasio nyinyi Bani Abdul Muttwalib, ni wale wachamungu tu. Hakika ni kwamba sitowajua Siku ya Kiyama mkija mmebeba dunia juu ya migongo yenu na watu wengine wamebeba akhera. Hakika nimekwishakupeni udhuru kwa yale yaliyopo baina yangu na nyinyi na baina yangu na Mwenyezi Mungu kuhusu nyinyi”.240 Ni vyema kwa mwenye akili akajiepusha na fitna ya kughurika na ubora wa nasaba na ajitahidi katika kuiadibisha nafsi yake na kuitakasa na kuielekeza kwenye kheri na mema kwa kufuata kauli ya mshairi isemayo: Mwanaume hasa ni yule asemaye mimi ndiye huyu hapa na wala mwanaume si yule asemaye alikuwa baba yangu… 240. Al-Waafy, juz. 3, uk. 60 203


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:22 PM

Page 204

Tabia njema kwa mujibu wa Ahlul Bayt (a.s)

29. HUSUDA MAANA Ni mtu hasidi kutamani neema aliyokuwanayo mtu (anayehusudiwa) imuondokee na aipate yeye. Ikiwa hatotamani imuondokee bali akatamani kuwa na mithili yake, hilo si jambo baya. Hiyo ndiyo ‘ghibtwah’ (kutamani kuwa na hali kama ya fulani) Husda ni katika hulka duni kabisa na sifa mbaya. Ni upotovu mbaya sana wa ki-akhlaki kiathari na kishari. Hasidi haachi kuwa ni mwenye huzuni na taabu, mwenye kuchukia ‘qadha’(amri, uamuzi) ya Mwenyezi Mungu (swt) kwa waja wake na neema Zake juu yao. Kwa hivyo daima ni mwenye kuungua moyo wake dhidi ya anayemhusudu, akijitahidi katika hila yake lakini asifaulu na natija moto wa husda yake humrejea na kumuangamiza mwenyewe.

QUR’ANI Tazama jinsi Mwenyezi Mungu (swt) alivyoonyesha ubaya wa husda na hasidi kwamba baada ya kumtaka mja Wake amwombe kinga dhidi ya viumbe alimwamrisha aombe kujikinga na shari ya hasidi, kama asemavyo: “Na shari ya hasidi anapohusudu.” (Suratul Falaq, 113:5)

HADITHI Kwa ajili hiyo zimepokelewa hadithi nyingi zikilaumu na kutahadharisha kuhusu husda. Mtume (s) alisema: 204


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:22 PM

Page 205

Tabia njema kwa mujibu wa Ahlul Bayt (a.s) “Husda inakula (inaangamiza) matendo mazuri kama vile moto unavyochoma kuni.”241 Amiri wa waumini, Imam Ali (a) alisema: “Sijaona dhalimu aliyeshabihiana sana na aliyedhulumiwa kama hasidi, (daima mwenye kuhangaika, moyo wenye kutangatanga na huzuni isiyokatika”. Imam Hasan alisema: “Kuangamia kwa watu kumo katika mambo matatu: kiburi, tamaa, na husda. Ama kiburi, ndiyo maangamizi ya dini na kwa hilo alilaaniwa Ibilisi. Ama tamaa, ni adui wa nafsi, na kwa ajili ya hilo Adam (a) aliondolewa peponi. Na husda ndiyo mpasua njia wa maovu na kwa hilo Qabil alimuua Habil”. Na siku moja Mtume (s) aliwaambia masahaba wake: “Hakika umekwisha kunyemeleeni ugonjwa wa mataifa yaliyokutangulieni, nao ni husda; haunyoi nywele bali hunyoa (unafyeka) dini na anasalimika na huo ugonjwa yule tuu anayezuia mkono wake na kuuhifadhi ulimi wake na akawa si mwenye kumteta ndugu yake muumini”.242

SABABU ZA HUSDA Husda ina sababu ambazo kwa ufupi ni hizi zifuatazo: 1. Ubaya wa nafsi Kuna watu wana hulka ya ubaya na uovu. Utawaona wanahuzunika kwa furaha na heri ya wenziwao na kufurahi pindi watu wanapofikwa na mabaya na matatizo. Na pia huwahusudu kwa neema alizowatunuku Mwenyezi Mungu (swt) hata kama baina yao hakuna uadui wala uhasama. 241. Al Bihaar, muj. 15, juz. 3 242. Al Bihaar, muj. 15, juz. 3, uk. 131 205


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:22 PM

Page 206

Tabia njema kwa mujibu wa Ahlul Bayt (a.s) 2. Uadui. Hii ni sababu ya nguvu zaidi inayoleta husda na yenye ukali zaidi katika kumdhuru hasidi na kumuondolea neema. 3. Ushindani. Ushindani uliopo kwa wenye maslahi na wenye malengo yaliyoshirikiana; kama vile husda ya wenye kazi zilizolingana, kuhusudiana watoto ili kupata fadhila kwa wazazi wao, kuhusudiana marafiki wa viongozi na maamiri katika kujikurubisha kwao. Hivyo ndivyo utakuta kwamba sababu za husda zinazidi katika makundi ambayo yana malengo ya aina moja. Huwezi ukakuta kuhusudiana baina ya wenye mielekeo na malengo tofauti, mfanyabiashara humhusudu mwenzie mfanyabiashara na sio mhandisi wala mkulima. 4. Umimi (ubinafsi) Pia watu wanaweza wakagubikwa na husda kwa sababu ya msukumo wa ubinafsi na kujitanguliza, kutaka kuwa juu ya wengine na kupenda kujionyesha na kuwa si wa kawaida. 5. Kudharau Husda inaweza ikawa chanzo chake ni dharau ya hasidi dhidi ya mhusudiwa, na kwa hivyo akaona neema za mhusudiwa ni nyingi na hivyo akamhusudu. Hutokea sababu zote zikakusanyika katika mtu mmoja na kugeuka kuwa ni volkano inayolipuka kwa husda na uovu na kusimama dhidi ya anayemhusudu msimamo uliyojaa ghadhabu na uduni, hawezi kujizuia hilo na hivyo kumfanya kuwa mshari, muovu na hatari. 206


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:22 PM

Page 207

Tabia njema kwa mujibu wa Ahlul Bayt (a.s)

MAOVU YA HUSDA Katika maradhi ya kitabia, husda inajipambanua kwa kuwa ni yenye madhara zaidi kuliko yote. Pia husda ina matokeo mabaya zaidi kuliko tabia zingine katika dini ya hasidi na dunia yake. 1. Madhara ya husda hapa duniani Miongoni mwa madhara yake yanayomsibu hasidi haraka hapa duniani ni maisha kumchafukia na kumfanya aishi na huzuni wasiwasi na taabu kwa ajili ya kuchukizwa na neema ambazo Mwenyezi Mungu (swt) amewatunukia waja Wake, neema ambazo ni nyingi na kubwa, jambo ambalo humfanya azidi kutaabika na kumsababishia maradhi ya mwili na nafsi yanayoangamiza. Pia husda humsibu ndani ya akiba ya maisha yenye thamani zaidi; utukufu wake na heshima yake. Matokeo yake ni hasidi kuvaa sifa mbaya na kudharauliwa, na kuchukiwa na kukataliwa na watu na maumbile. Pia humsibu katika tabia zake, utamwona hakereki na kumteta anayemhusudu kwa aina mbalimbali za tuhuma na uongo haramu na haachi juhudi yoyote katika kuzusha fitna zinazofarakanisha baina yake yeye na wapenzi wake na ndugu wa damu, yote hayo ili kumuudhi na kumdhalilisha. Na wengi kati ya watu ambao wanahusudiwa na ikawasibu shari na hatari ya husda ni ulamaa waliyong’ara kwa elimu na ubora kwa kule mahasidi kupambana nao kwa ajili ya utukufu wa daraja na uwezo. Kwa hiyo wanahangaika chini juu kuwadharaulisha na kuwatia ila na kuwashambulia kwa kila uovu. 207


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:22 PM

Page 208

Tabia njema kwa mujibu wa Ahlul Bayt (a.s) Bila shaka hii ndiyo siri ya dhulma dhidi ya watu hawa bora na kunyimwa nafasi ya kutukuzwa na utukufu. Hutokea mishale ya husda ikakosea shabaha na hivyo ikamrejelea mwenyewe hasidi kwa huzuni na uchungu ndani ya nafsi na kumuacha anayehusudiwa na utukufu na sifa kama asemavyo Abu Tamaam: Atakapo Mwenyezi Mungu kutandaza fadhila iliyojificha basi huipa ulimi wa hasidi Kama sio moto kuunguza vilivyo uzunguuka basi yasingejulikana manukato ya harufu nzuri ya udi. Kama isingekuwa kuogopea madhara ya baadae, ya hasidi yangezidi kuwa ni kheri kwa mhusudiwa. Na mwingine anasema: Ikabili husda ya mtu hasidi kwa subira, hakika subira yako itamuangamiza Hakika moto unajitafuna, ikiwa haukupata kitu cha kuchoma. 2. Madhara ya husda akhera Bila shaka umefahamu hasidi anavyotumia njia mbalimbali za kumwaga sumu na kuharibu kwa kumteta mhusudiwa na kuvunja utu wake. Uovu huu bila shaka unavuta adhabu ya Mwenyezi Mungu (swt) juu ya hasidi na kutafuna mema yake kama vile moto unavyochoma kuni. Pia kuwaka moto katika nafsi yake na kughadhibika juu ya aliyoyataka Mwenyezi Mungu (swt) ya kuwatunuku waja wake neema ni sababu ya kupata adhabu na madhila.

208


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:22 PM

Page 209

Tabia njema kwa mujibu wa Ahlul Bayt (a.s)

TIBA YA HUSDA Hizi ni baadhi ya nasaha kwa ajili ya kutibu husda. 1. Mtu kuacha kutazama yule aliyemzidi kwa jaha, mafanikio na fanaka bali na amtupie jicho yule aliye chini yake ili kung’amua msaada wa Mwenyezi Mungu (swt) kwake na neema Zake juu yake. 2. Kujikumbusha maovu ya husda na maagamizi yake kidini na kidunia na aina mbalimbali za mabaya na mabalaa yanayowasibu mahasidi. 3. Kuwa macho na njia ya Mwenyezi Mungu (swt) na kuwa na imani kuhusu hekima yake ya kuongoza waja Wake na kujisalimisha na hukumu Yake Husda kuwa yenye kulaumiwa na kwamba ni lazima kujiweka kando na aibu zake mbaya yatosha kuwa ni sababu ya kuikataa tabia hiyo na kujiepusha nayo. Ni vyema kwa wazazi kujiepusha kupendelea watoto wao kuhusu msaada na kuwafanyia wema kwani hilo huzaa ndani ya nafsi zao sumu za husda na mizizi yake mibaya.

30. KUTETA MAANA Ni kumtaja muumini kwa yale asiyoyapenda iwe ni katika maumbile yake au tabia au yanayohusiana naye. Kuteta siyo kwa ulimu tuu, bali inakusanya yote ambayo yanatoa hisia ya 209


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:22 PM

Page 210

Tabia njema kwa mujibu wa Ahlul Bayt (a.s) kumporomosha (kumtweza) mwingine kwa kauli, matendo, kuandika au kumueleza wazi. Mtume (s) alielezea maana yake kwa kusema: “Je! mnajua nini kuteta? Wakajibu: Mwenyezi Mungu na Mtumewe wanajua. Akawaambia: Kumtaja ndugu yako kwa yale anayochukia. Akaambiwa: Je! unaonaje ikiwa ndugu yangu anayo ninayoyasema? Akajibu: Ikiwa anayo unayoyasema umemteta (hiyo ndiyo kuteta) na ikiwa hana basi umemkashifu (kumsema kwa ubaya asionao, buhtani)”.

QUR’ANI Kuteta ni katika tabia duni sana na sifa mbaya. Pia ni miongoni mwa maovu hatari sana na yatutosha maovu yake kwamba Mwenyezi Mungu (swt) hulishabihisha la mtetaji na anayekula nyama ya ndugu yake maiti akasema:

“Enyi mlioamini! jiepusheni sana na dhana kwani dhana ni dhambi wakati mwingine, wala msipeleleze, wala baadhi yenu wasiwatete wengine, Je, mmoja wenu anapenda kula nyama ya nduguye aliyekufa? Mnalichukia hilo na mcheni Mwenyezi Mungu, bila shaka Mwenyezi Mungu ni Mwenye kupokea toba Mwenye kurehemu.” (Suratul Hujuraat, 49: 12) Pia Mwenyezi Mungu (swt) akasema kwa kukataza uovu huu:

210


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:22 PM

Page 211

Tabia njema kwa mujibu wa Ahlul Bayt (a.s)

“Mwenyezi Mungu hapendi kelele za maneno mabaya, ila kwa mwenye kudhulumiwa. Na hakika Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa kusikia, Mjuzi.” (Suratun Nisaa, 4: 148)

HADITHI Kwa sababu hiyo zimepokelewa hadithi nyingi zinazokataza na kuonya kuhusu kuteta: Mtume (s) alisema: “Kuteta kunaharibu haraka zaidi dini ya mtu kuliko vile donda ndugu linavyoozesha ndani ya tumbo lake.”243 Imam Sadiq (a) alisema: “Atakayesimulia kuhusu muumini habari akilenga kwa hilo kumfedhehesha na kubomoa utu wake ili awe duni mbele ya macho ya watu, basi Mwenyezi Mungu (swt) atamuondoa chini ya Himaya (ulinzi, ubwana, uongozi) Yake na kumuweka chini ya Himaya ya Shetani”244 Imam Sadiq (a) alisema: “Usitete, ukatetwa, na usimchimbie ndugu yako shimo ukaanguka ndani yake, hakika wewe jinsi utakavyowalipa (wafanyia) wenzio, ndivyo utakavyolipwa (fanyiwa)”.245 243. Al Bihaar, muj. 15, uk. 177 244. Al Bihaar, muj. 15, uk. 187 245. Al Bihaar, muj. 15, uk. 185 211


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:22 PM

Page 212

Tabia njema kwa mujibu wa Ahlul Bayt (a.s) Pia alisema: Mtume (s) alisema: “Yeyote atakayetangaza ovu atakuwa kama yule aliyelianzisha. Na atakayemtia aibu muumini kwa lolote, basi hatokufa mpaka alifanye”. 246

KUJIKINGA NA KUSIKILIZA YA UTESI Kwa mwenye akili ni vyema akajiepusha na kufuatana na watetaji na kuwasikiliza. Hakika mwenye kumsikiliza mtetaji ni pacha wake na mshirika katika ovu hilo. Na hasameheki na hilo ila kwa kukataa kitendo hicho cha kuteta kwa ulimi wake au kubadilisha mazungumzo au kukimbia kikao chenye kuteta. Ikiwa hataweza yote hayo basi ni juu yake kuchukia kwa moyo wake ili asalimike na dhambi ya kushirikiana katika kuteta. Baadhi ya wanahekima wamesema: “Ukimuona anayeteta watu, basi jitahidi kadri uwezavyo asikujuwe. Hakika wenye bahati mbaya zaidi naye ni wale wanaofahamiana naye”. Na kama ilivyo lazima kujikinga kusikiliza ya kuteta, hivyo pia ni muhimu kulinda kutokuwepo kwa muumini na kutetea utukufu wake pindi anapotajwa kwa yenye kumdhili. Imam Sadiq (a) alisema: Mtume (s) alisema: “Atakayelinda heshima ya ndugu yake muisilamu, basi pepo imekuwa lazima juu yake vyovyote vile”. Muhimu kutaja kwamba uharamu wa kuteta ni hasa kwa yule anayeitakidi haki na wala si kwa watu wapotofu. 246. Al Bihaar, muj. 15, uk. 188 212


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:22 PM

Page 213

Tabia njema kwa mujibu wa Ahlul Bayt (a.s)

SABABU ZA KUTETA Zipo sababu zinazopelekea kuteta. Sababu kuu ni hizi zifuatazo: 1. Uadui au husuda, hizi ni sababu za nguvu zaidi zinazochochea husuda na kuvunja heshima ya mhusudiwa ili kukata kiu ya kisasi na chuki. 2. Masihara, utani, hii inapelekea kumteta, kumvunjia heshima na kumuiga mtu ili kuchekesha 3. Kujisifu na kujigamba: Hii ni kwa kutaja maovu ya mwingine kwa kujidai na kujigamba kuepukana nayo 4. Kuwa sambamba na wenza: mara nyingi mtu anajikuta anateta ili kwenda sambamba na marafiki wenye kujifurahisha kwa kuteta na kuogopa kutengwa ikiwa hatashirikiana nao katika hilo.

MAOVU YA KUTETA Katika malengo muhimu kabisa ambayo uislamu ulifanikiwa kuyafikia na ukayapa kipaumbele ni umoja wa Waislamu, kushirikiana pamoja na undugu baina yao ili wawe ni mfano wa juu kabisa kinguvu, utukufu na sifa. Uislamu ukatukuza lengo hili tukufu na kuwa desturi ya daima kwa Waislamu kwa sheria na taratibu ulioziweka. Kwa hivyo uislamu ukawahimiza Waislamu kufanya yale yanayozidisha upendo na mahaba na kutia nguvu uhusiano wa kijamii na kuwezesha kufikia undugu na ushirikiano, nayo ni kama vile tabia njema, kuwa mkweli, kurejesha amana, kujali mambo ya Waislamu, kuchunga maslahi yao ya jumla. Pia ukawakataza kufanya yote yale ambayo yanachana utulivu wa nyoyo na kusababisha chuki na kinyongo vinavyozaa kukataana na kutojaliana. Nayo ni kama vile uongo, kudanganya, khiyana, kudhihaki nk...

213


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:22 PM

Page 214

Tabia njema kwa mujibu wa Ahlul Bayt (a.s) Kwa kuwa (tabia ya) kuteta ni kisababishi hatari na sururu inayoangamiza katika kubomoa jengo la jamii na kuharibu mahusiano yake thabiti, sharia ya kiislamu imeiharamisha na kuihesabu katika madhambi makubwa. Miongoni mwa madhara ya kuteta ni kwamba kunapanda sumu za bughdha na mfarakano katika safu za waumini na hivyo kuchana ubora wa mahaba, kukata pingu za urafiki na kuvunja mausiano ya kindugu. Hii ni kwa kuwa kuteta kunaweza kukamfikia anayetetwa na kuchochea hasira yake dhidi ya mtetaji na kumfanya alipe kisasi na kumrejeshea shutuma ya kumdhalilisha, na ni mara nyingi tu kuteta kumezua fitina hatari na maafa yenye kujaa huzuni. Haya ni mbali na mabaya na maovu yake ya kiroho ambayo maandiko (Qur’ani na Sunna) yameyaweka wazi pindi yaliposema waziwazi kwamba Siku ya Kiyama, kuteta kunafilisi mema ya mtetaji na kupewa mtetwa. Ikiwa hana mema basi hugawiwa madhambi ya mtetwa kama alivyosema Mtume (s): “Siku ya Kiyama ataletwa mmoja wenu na atasimamishwa mbele ya Mwenyezi Mungu (awj) na kupewa kitabu chake. Hapo hataona mema yake na atasema: Ewe Mola Wangu hiki si kitabu changu, mimi sioni ndani yake utiifu wangu. Hapo atamuambia: Hakika Mola wako hapotei wala hasahau, amali yako imepotea kwa kuwateta watu. Kisha ataletwa mwingine na kupewa kitabu chake. Ataona ndani yake utiifu (Amali njema) mwingi na kusema: Ewe Mola wangu hiki si kitabu changu, mimi sikufanya mema haya, na atamuambia: Fulani alikuteta na hivyo umelipwa mema yake”.247

247. Jamiu Saadaat, juz. 2, uk. 301 214


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:22 PM

Page 215

Tabia njema kwa mujibu wa Ahlul Bayt (a.s)

HALI INAYOJUZU KUTETA Kuteta haramu ni kule kukusudia kumteremsha muumini hadhi yake na kumdhalilisha. Ikiwa hilo halikukusudiwa bali kukawepo lengo la maana, basi inajuzu kuteta na hakuna uharamu. Ulamaa wametaja inajuzu kuteta katika hali zifuatazo: 1. Mashtaka ya mtu mdhulumiwa ili kupata haki yake kwa hakimu. Katika hali kama hii inajuzu kumshtakia mtu mwingine huo uovu na dhulma. 2. Nasaha kwa mwenye kutaka ushauri katika jambo fulani kama vile ndoa na amana. Inajuzu katika hali hii mshauri kutaja aibu alizoulizwa. Inajuzu pia kumtahadharisha muumini na usuhuba wa mtu fasiki au mtu mpotevu kwa kutaja maovu yao ya ufasiki na upotoshi, ili kumlinda na shari zao na upotovu wao. Inajuzu pia kumuumbua shahidi ikiwa mtu ataulizwa. 3. kumfichua aliyedai nasaba ya uongo. 4. Kuumbua, kulaumu maneno maovu au madai batili kisheria 5. Kutoa ushahidi dhidi ya wenye kufanya maovu na mambo ya haramu 6. Dharura ya kutambulisha, hii ni kutaja majina ya kupanga ambayo si mazuri lakini ni lazima kuwatambulisha wenyewe kama vile yule kilema, yule mwenye macho mekundu nk. 7. Kukataza maovu: Hii ni kutaja maovu ya mtu kwa yule anayeweza kumrekebisha na kumkataza kuyafanya. 215


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:22 PM

Page 216

Tabia njema kwa mujibu wa Ahlul Bayt (a.s) 8. Kumteta anayejidhihirisha kwa ufasiki kama vile kunywa pombe, kucheza kamari, lakini kwa sharti ya kutozidisha juu ya yale anayojidhihirisha nayo kwa sababu hakuna kuteta kwa mtu fasiki. Katika hali zote zilizotajwa hapo juu, mtu hana budi kulenga lengo tukufu na salama na kujiepusha vichochezi duni kama vile uadui, hasadi na mfano wake.

TIBA YA KUTETA Tiba hii ni kwa kufuata nasaha zifuatazo: 1. Kutafakari tuliyobainisha kuhusu maovu ya kuteta na hatari zake kubwa duniani na akhera 2. Kutilia maanani utakaso wa nafsi na kuipamba kwa tabia njema na kuikinga na aibu za watu na maovu yao. Aliulizwa Muhammad bin Hanafiyyah: Nani aliyekuadibisha? Akajibu: “Mola wangu aliniadibisha katika nafsi yangu. Kwa hivyo yale niliyoyaona kuwa ni mazuri kwa watu wenye busara na mtazamo niliwafuata kwayo na kuyafanyia kazi, na yale niliyoyaona kuwa ni mabaya kwa wajinga nilijiepusha nayo na kuyaacha. Hayo yalinifikisha kwenye hazina za elimu.� 3. Kubadili kuteta kwa maongezi yanayoburudisha, visa vinavyovutia na hadithi ngeni zenye maana. 4. Kuipa nafsi mazoezi kuulinda ulimi na kuuzuia na vitangulizi vya kuteta.

216


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:22 PM

Page 217

Tabia njema kwa mujibu wa Ahlul Bayt (a.s)

KAFARA YA KUTETA Utaratibu wake ni huu: Baada ya mtu kujutia kufanya uovu kama huu na kutubia ni juu yake kujenga mapenzi kwa mtetwa na kumuomba msamaha (ili kuondolewa mzigo) ikiwa atasamehe, vinginevyo kumfanyia mapenzi na kumtaka msamaha ndiyo malipo ya uovu wa kuteta. Hii ni ikiwa mtetwa yu hai na kwamba kuomba udhuru hakutachochea hasira na chuki. Ama ikiwa itahofiwa hilo au akawa ni maiti au hayupo, katika hali hii, la lazima ni kumuombea istighfar (msamaha). Hiyo ndiyo kafara ya kumteta. Kutoka kwa Abu Abdillah (a): “Mtume aliulizwa nini kafara ya kuteta? Akajibu: Muombee istighfaar kwa Mwenyezi Mungu (swt) yule uliyemteta kila mara unapomkumbuka”.248 Kauli yake Mtume (s): “Kila mara unapomkumbuka” maana yake kila unapomtaja kwa kumteta.

31. KUKASHIFU MAANA Ni kumtuhumu muumini na kumsingizia ya uongo ambayo hakuyafanya. Hii ina uovu na dhambi zaidi kuliko kuteta.

QUR’ANI NA HADITHI Mwenyezi Mungu (swt) anasema:

248. Al Bihaar, muj. 15, uk. 184 217


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:22 PM

Page 218

Tabia njema kwa mujibu wa Ahlul Bayt (a.s) “Na mwenye kuchuma kosa au dhambi, kisha akamsingizia nayo asiye na kosa, basi kwa hakika amebeba uongo na dhambi iliyo wazi.” (Suratu Nisaa, 4: 112) Na Mtume (s) alisema: “Atakayemkashifu muumini wa kike au wa kiume au akamsema ambayo hana, basi Mwenyezi Mungu (awj) atamsimamisha Siku ya Kiyama juu ya kilima cha moto mpaka atakapokuwa huru na yale aliyoyasema kuhusu huyo muumini”249

UMBEA MAANA Ni kupeleka maneno, mazungumzo - ambayo watu wanachukia kuenea kwake - kutoka kwa mtu hadi mwingine ili kumuudhi, kumuumiza na kumvunja anayezungumzwa. Umbea ni katika maovu machafu sana ya kiakhlaki na yenye hatari zaidi katika maisha ya mtu binafsi na jamii. Mbea ni mtu muovu kuliko wote na khabithi kwa kusifika kwake kwa kuteta, unafiki, khiana, kusaliti, na ufisadi baina ya watu na kufarikisha baina ya wapendanao. Ni kwa sababu hiyo ndiyo aya na hadithi zimekemea na kuonya kuhusu tabia hiyo:

QUR’ANI Mwenyezi Mungu (swt) anasema:

249. Safinatul Bihaar, Muj.1, uk. 110 218


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:22 PM

Page 219

Tabia njema kwa mujibu wa Ahlul Bayt (a.s) “Wala usimtii kila mwapaji sana, aliye dhalili. Msengenyaji aendaye akitia fitina. Azuiaye kheri, arukaye mipaka, mwenye hatia. Mwenye roho ngumu, (na) juu ya hayo, mwana wa haramu.” (Suratul Qalam, 68: 10-13) Na maana ya ‘zaniim’ ni mwanaharamu, jambo ambalo linaashiria ya kwamba umbea ni katika tabia za wanaharamu na huluka ya watoto wa kuokotwa. Pia akasema: “Adhabu kali ipo juu ya kila mbea msengenyaji (Suratu Humaza, 104:1) ‘humaza’ ni mbea, na ‘lumaza’ ni mtetaji. Kutoka kwa Abu Abdilah (a) alisema: alisema Mtume (s): “Hamtaki niwaambiye muovu wenu zaidi? Wakajibu: Bila shaka Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu. Akasema: Watembeaji kwa umbea, wafarikishaji baina ya wapendanao, maadui wa wasio na kasoro”250 Imam Baqir (a) alisema:“Pepo ni haramu kwa watiaji aibu, watembeaji kwa umbea”. Imam Sadiq (a) alimwambia Mansur: “Usikubali maneno ya mtu ambaye Mwenyezi Mungu (swt) amemharamishia pepo na akafanya nafasi yake kuwa ni moto anapokuambia kuhusu jamaa zako (wa damu) na watu wa nyumba yako.” Hakika mbea ni shahidi wa uongo, mshirika wa Iblis katika kuwaghilbu watu. Mwenyezi Mungu (swt) anasema:

250. Al Waafy, juz. 3, uk. 164 219


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:22 PM

Page 220

Tabia njema kwa mujibu wa Ahlul Bayt (a.s) “Enyi mlioamini! kama fasiki akikujieni na habari yoyote, basi pelelezeni, msije mkawadhuru watu kwa ujahili na mkawa wenye kujuta juu ya yale mliyoyatenda.� (Suratul Hujuraat, 49: 6)

SABABU ZA UMBEA 1. Kumuaibisha anayeongelewa na kumvunjia hadhi 2. Kuonyesha mapenzi na ukuruba kwa anayepelekewa umbea.

UBAYA WA UMBEA Umbea umekusanya aina mbili za uovu hatari: kuteta na umbea. Kila umbea ni kuteta na siyo kila kuteta ni umbea. Maovu ya umbea ni kama yale ya kuteta bali yenyewe ni mabaya zaidi kwa uovu wa kusambaza yaliyo ya siri na aibu za mtu na kumvunjia hadhi. Na hutokea yakachochea umwagaji damu, kupora mali, kuvunja heshima ya vilivyo vitakatifu na kupoteza utukufu.

JINSI YA KUKABILIANA NA MMBEA Kwa kuwa mmbea ni miongoni mwa wafisadi hatari sana na mwingi wa ubaya na shari kwa watu ni lazima kujihadhari naye, na kujikinga na vitimbi na ufisadi wake na hili ni kwa kufuata nasaha zifuatazo: 1. Kumkadhibisha mmbea kwa ufasiki wake na kutoaminika, kama alivyosema Mwenyezi Mungu: (Suratul Hujuraat:6) 2. Asimfikirie ndugu yake muumini vibaya, kwa mtu kuletewa umbea kwa kauli yake Mwenyezi Mungu (Suratul Hujuraat: 12) 3. Umbea usimfanye akaanza kupeleleza na kutaka kuhakiki aliyoyasema mmbea kwa kauli ya Mwenyezi Mungu: (Suratul Hujuraat:12) 220


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:22 PM

Page 221

Tabia njema kwa mujibu wa Ahlul Bayt (a.s) 4. Asipeleke umbea wa mmbea (kwa kusimulia umbea alioletewa), kwani atageuka kuwa mmbea na mtetaji. Imepokelewa kwamba mtu mmoja alimjia Imam Ali (a) kwa haraka (akiwa na habari). Akamuambia: Tutachunguza uliyoyasema, ikiwa ni kweli basi tutakuchukia na ikiwa ni uongo basi tutakuadhibu. Na ikiwa unataka tukufumbie macho, basi tutakufumbia macho. Yule mtu akasema: Nifumbie macho ewe Amiri wa waumini!”251 Kutoka kwa Muhammad bin Fudhwayl: Nilimuambia Imam Musa (a): Niwe muhanga wako! napata habari kuhusu mmoja katika ndugu zangu ambayo nachukia. Namuuliza kuhusu hilo, anakana, wakati walionipa taarifa ni watu wanaominika. Akanijibu: Ewe Muhammad, kadhibisha macho yako na masikio yako kuhusu ndugu yako. Ikiwa watashuhudia watu waapaji hamsini, na yeye akakueleza jambo, basi msikilize na uwakadhibishe na kamwe usieneze lolote kuhusu yeye la kumvunjia hadhi na utu wake. Ukifanya hivyo (kuwasikiliza waapaji) utakuwa miongoni mwa wale ambao Mwenyezi Mungu anasema:

“Kwa hakika wale wanaopenda uenee uchafu kwa walioamini, watapata adhabu yenye kuumiza katika dunia na Akhera, na Mwenyezi Mungu anajua na nyingi hamjui.” (Suratun Nur, 24: 19)252

251. Safinatul Bihaar, muj. 2, uk. 613. 252. Al Bihaar, muj. 15, uk. 188 221


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:22 PM

Page 222

Tabia njema kwa mujibu wa Ahlul Bayt (a.s)

KUSINGIZIA MAANA Hii ni sura mbaya sana ya umbea na yenye madhara zaidi na uovu. Hapa lengo hasa ni kumuangamiza yule anayesingiziwa kwa kumsingizia kwa watu wanaoogopwa wenye mamlaka na nguvu. Waathirika wengi wa uovu huu ni watu wakubwa wenye enzi na utukufu, wenye kuhusudiwa kwa sababu ya sifa na ubora wao. Hili linawasukuma mahasidi wao kujaribu kuwadhalilisha na kuwaumiza, jambo ambalo wanashindwa kwa njia hiyo. Kushibisha husda yao na ukhabithi wao wanakimbilia mbinu hii ya kusingizia bila kutanabahi kwamba vitimbi hivyo huenda vikaishia kapuni, vikashindwa na kuwageukia kuwa ni fedheha na adhabu na yule msingiziwaji kuibuka na utukufu na heshima zaidi. Kwa ajili ya hilo msingiziaji amekuwa ni mtu muovu zaidi na hatari zaidi kwa khiana na shari kama ilivyopokelewa kutoka kwa Imam Sadiq (a) kutoka kwa baba zake kutoka kwa Mtume (s) alisema: “Muovu wa watu ni muthlith (mwenye kuangamiza watatu). Ikaulizwa: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu ni nani muthlith? Akajibu: Ni yule anayemsingizia ndugu yake kwa mtawala, matokeo yake anaangamia yeye, ndugu yake na mtawala�.253

33. LUGHA CHAFU, KUTUSI NA QADHFU MAANA Fuhsh (lugha chafu): Kunena, kuelezea mambo ambayo inachukiza kuyaweka wazi, kama vile maneno ya kujamiana kimwili na viungo vyake. 253. Al Bihaar, muj. 15, uk. 191 222


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:22 PM

Page 223

Tabia njema kwa mujibu wa Ahlul Bayt (a.s) Haya yanazungumzwa na wajinga, ama wenye utukufu huyaelezea kwa kinaya na alama kama vile ‘kugusa, kushika’. Hivyo ndivyo wanafasihi wanavyotumia maana ya kinaya kwa maneno na mafhumi ambayo wanajiepusha kuyaweka wazi kwa sababu za kiadabu kama vile mama watoto, familia kumaanisha mke, kukidhi haja kwa maana ya haja ndogo au kubwa. Kuashiria ukoma na upara, kwa shavu hii ni kwa sababu kuwekwa wazi maneno kama haya ni jambo lisilo kubalika na wenye akili na wajuzi. Ama kutusi ni kama vile kusema: ‘Ewe mbwa, nguruwe, punda, msaliti na mfano wake yanayoleta maana ya kudharau na kudhalilisha. Ama kadhfu ni kama vile kusema ewe mtoto wa zinaa, ewe mume wa mwanamke mzinifu, ewe dada wa mzinifu. Haya mambo matatu ni katika maovu mabaya sana ya ulimi na maafa hatari ambayo sheria na akili vimeyakataa na kwa hivyo maandiko matakatifu yametoa onyo kali.

QUR’ANI NA HADITHI Kuhusu lugha chafu (fuhsh), Mtume (s) alisema: “Mwenyezi Mungu (swt) ameharamisha pepo kwa kila mtoaji lugha chafu, mchache wa haya, asiyejali anayoyasema wala anayoambiwa. Ikiwa utamchunguza (kuhusu familia) utakuta ni mwana wa dhambi (haramu) au nusu mwana wa shetani. Akaulizwa: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu (swt), na katika watu kuna nusu mwana wa shetani?! Mtume (s) akajibu: Hukusoma kauli ya Mwenyezi Mungu (swt):

223


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:22 PM

Page 224

Tabia njema kwa mujibu wa Ahlul Bayt (a.s)

“Na wavute uwezao miongoni mwao kwa sauti yako, na uwakusanyie wapandao farasi wako, na waendao kwa miguu, na shirikiana nao katika mali na watoto na uwaahidi, Lakini shetani hawaahidi ila udanganyifu.” (Suratul Israai, 17: 64).254 Na maana ya ushirika wa Shetani kwa watu katika mali ni kule kuwasukuma wachume mali kwa njia za haramu na kuitumia katika njia za upotofu na madhambi. Ama ushirika wake katika watoto ni kushirikiana na wazazi wa kiume wakati wa jimai ikiwa hawataji jina la Mwenyezi Mungu (swt) wataki wa tendo. Na mtoto wa dhambi maana yake ni mwana wa zinaa. Kutoka kwa Abu Abdilah (a), Mtume (s) alisema: “Miongoni mwa waovu wa waja wa Mwenyezi Mungu (swt) ni yule ambaye wanachukia watu kukaa naye kwa sababu ya lugha chafu” 255 Imam Sadiq (a) alisema: “Yeyote ambaye watu wanaogopa ulimi wake yuko motoni” 256 Pia Imam (a) aliliambia kundi la Mashia akasema: “Enyi Mashia kuweni ni pambo kwetu na msiwe ni aibu (doa) juu yetu. (Kwa hivyo basi) waambieni watu maneno mazuri, na lindeni ndimi zenu, mzizuie kuingilia mambo ya watu na kunena maneno machafu”257

Kuhusu kutukana. 254. Al Waafy, juz. 3, uk. 160 255. Al Waafy, juz. 3, uk. 160 256. Al Bihaar, muj. 15, juz. 2, uk. 192 257. Al Bihaar, muj. 15, juz. 2, uk. 192 224


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:22 PM

Page 225

Tabia njema kwa mujibu wa Ahlul Bayt (a.s) Kutoka kwa Abu Ja’far (a), Mtume (s) alisema:“Kumtusi muumini ni fusuq (kupotea njia, uasi..), na kumuuwa ni kufuru, na kula nyama yake ni maasi, na kama ilivyo lazima kuheshimu damu yake ndivyo ilivyo lazima kuheshimu mali yake”.258 Imam Musa (a) alisema kuhusu watu wawili wanaotukanana: “Anayeanza ndiye dhalimu zaidi na mzigo wake na wa mwenzie yote juu yake ila iwe mdhulumiwa kachupa mipaka”. Ama Kadhfa Imam Baqir (a) alisema: “Hakuna mtu yeyote ambaye anampachika muumini aibu isipokuwa atakufa kifo kibaya, na kustahili kutorejea kwenye kheri”. Imam Sadiq (a) alikuwa na rafiki ambaye alikuwa hamuachi pindi endapo mahala. Siku moja walitembea pamoja baina ya watengeneza viatu wakiwa na kijana mtumishi wa kisindi akiwafuata nyuma. Yule sahiba wa imam akageuka mara tatu akimtafuta kijana wake asimuone. Alipogeuka mara ya nne (na kumuona) akamuambia: Ewe mtoto wa mwanamke kibarua (malaya)! Ulikuwa wapi? Msimulizi wa hadithi anasema: Imam Sadiq (a) akapandisha mkono wake na kujipiga kwenye paji la uso kisha akasema: Subhana Allah! vipi unamkadhifu mama yake! Ulikuwa muda wote ukinionyesha kwamba una uchamungu, lakini sivyo. Akajitetea: Niwe fidia yako hakika mama yake ni msindi mushrik. Imam (a) akamjibu: Hivi hujui ya kwamba kila kabila lina nikah! Uwe mbali nami. Msimulizi wa hadithi anasema: Sikumuona tena akitembea naye hadi yalipowafarikisha mauti. 259

258. Al Waafy, juz. 3, uk. 160 259. Al Waafy, juz. 3, uk. 161 225


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:22 PM

Page 226

Tabia njema kwa mujibu wa Ahlul Bayt (a.s)

SABABU ZA LUGHA CHAFU Ni wazi kwamba, hayo maneno machafu, kwa kiasi kikubwa, chanzo hasa ni uadui, husda, ghadhabu au tabia mbaya. Na mara nyingi chanzo chake ni malezi mabaya, adabu mbaya na kuzowea matusi na kutojali mabaya yake.

MAOVU YA LUGHA CHAFU Bila shaka lugha chafu, iwe ni maneno machafu (fuhsh), matusi (sabb), kuchafua (qadhf), ina madhara hatari na maovu yasiyokadirika. Baadhi yake ni haya: Humvua mtu sifa za utu wenye adabu na tabia njema na kuuharibu kwa uduni na unyama. Huleta uadui na chuki, na hivyo kuharibu mahusiano ya kijamii na kusababisha wanajamii kukataana na kuchukiana. Wenye tabia hiyo hukumbana na adhabu ya Mwenyezi Mungu kama vile ilivyoelezwa hapo kabla. Kwa kuzingatia hayo, imetiliwa mkazo sana kudhibiti na kuhifadhi ulimi na cheche zenye sumu za lugha chafu. Amiri wa waumini (a) alisema: “Ulimi ni mnyama mkali, ukiuachia unaua�

226


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:22 PM

Page 227

Tabia njema kwa mujibu wa Ahlul Bayt (a.s)

34. KUKEJELI MAANA Ni kuelezea, kudhihirisha maneno ya watu au vitendo vyao au sifa zao kwa kuwadharau na kuwachekelea kwa njia ya matendo au kauli. Sheria imeharamisha hilo kwa kuwa linaleta uadui na kusimika chuki na kuharibu mahusiano mazuri baina ya Waislamu. Ni vipi mtu atathubutu kumkejeli muumini?! Ni vipi kumvunjia hadhi na kumtia aibu wakati watu wote, isipokuwa maasumu (mitume na mawasii wao) hawakosi aibu na mapungufu na kwamba hujafa hujaumbika, iko siku anaweza akajikuta kejeli zinamlenga na dharau? Kwa sababu hizo maadiko matakatifu yameonya na kutahadharisha kuhusu tabia mbaya hiyo.

QUR’AN NA HADITHI

“Enyi mlioamini! wanaume wasiwadharau wanaume wenzao huenda wakawa bora kuliko wao, wala wanawake wasiwadharau wanawake wenzao, huenda wakawa bora kuliko wao. Wala msitukanane kwa 227


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:22 PM

Page 228

Tabia njema kwa mujibu wa Ahlul Bayt (a.s) kabila wala msiitane kwa majina mabaya (ya kejeli), jina baya baada ya imani ni uovu, na asiyetubu, basi hao ndio madhalimu.” (Suratul Hujurat, 49:11)

“Kwa hakika wale waliokosa walikuwa wakiwacheka Waumini.” Na walipopita karibu yao walikonyezana. Na waliporudi kwa watu wao walirudi wakishangilia.” (Suratul Mutwaffifin, 83:29-32) Imam Sadiq (a) alisema: “Atakayehadithia maneno kuhusu muumini akilenga kumuaibisha na kuporomosha utu wake ili awe duni katika macho ya watu, Mwenyezi Mungu (swt) humtoa chini ya wilaya (himaya, mapenzi…) Yake na kumueka chini ya himaya ya Shetani naye Shetani hatamkubali”.260 Pia alisema: Mtume wa Mwenyezi Mungu alisema (s): “Msifuatilie mianguko (mapungufu, aibu, makosa,…) ya waumini. Hakika anayefuatilia mianguko ya waumini, basi Mwenyezi Mungu (swt) atafuatilia mianguko yake. Na anayefuatiliwa na Mwenyezi Mungu (swt), basi lazima atamfedhehi hata kama ni ndani ya nyumba yake”.261 Ni vyema kwa mwenye akili kujiepusha na kudhihaki ili kujiepusha na madhambi yake na kujikinga na maafa yake na awathamini watu kwa kiwango cha imani zao na uzuri wao na uzuri wa undani (nafsi, fikra, nia, malengo… ) wao na hivyo kufumbia macho mapungufu na aibu zao kama ilivyopokelewa: 260. Al Waafy, juz. 3, uk. 163 261. Al Waafy, juz. 3, uk. 84 228


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:22 PM

Page 229

Tabia njema kwa mujibu wa Ahlul Bayt (a.s) “Mwenyezi Mungu (swt) amewaficha mawalii wake baina ya waja wake, basi usimuone duni yeyote mja katika waja wa Mwenyezi Mungu (swt), huenda akawa yeye ndiye walii Wake nawe hutambui”.

35. MANENO MAZURI Yeyote atakayefanya uchunguzi wa matukio ya matatizo ya kijamii na migogoro inayovuruga usafi wa jamii atafahamu ya kwamba chanzo chake aghlabu ni ulimi na kutupiana matusi na lugha chafu yanayopelekea kuchanika kwa mahusiano ya kijamii na kuwasha moto wa chuki, kisasi, uadui wa kurithi, husuda…baina ya wanajamii. Ni kwa ajili ya hilo ndiyo ikawa kuudhibiti ulimi na maovu hayo na kuuzoesha maneno mazuri na mazungumzo matukufu ni dharura muhimu ambayo maslahi ya mtu na jamii yanahitajia. Maneno mazuri, uzuri wa lugha ni katika alama za utukufu na ukamilifu. Pia ni sababu ya kutukuzwa na chachu ya kushinda na kufaulu. Sheria imetilia mkazo kujipamba na adabu za kuzungumza na kauli njema kwa aya nyingi na hadithi na kutilia mkazo bila kukatika ili kueneza amani ya kijamii na kuyapa nguvu mahusiano ya jamii.

QUR’ANI Mwenyezi Mungu (swt) anasema:

“Na waambie waja wangu waseme yaliyo bora, maana shetani huchochea ugomvi kati yao. Hakika shetani kwa mwanadamu ni adui 229


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:22 PM

Page 230

Tabia njema kwa mujibu wa Ahlul Bayt (a.s) dhahiri.” (Suratul Israa’, 17:53)

“... na mseme na watu kwa wema. .” (Suratul Baqara, 2:83).

“Mambo mazuri na mabaya hayawi sawa. Zuia (ubaya) kwa yaliyo mema zaidi, na mara yule ambaye baina yako na yeye pana uadui atakuwa kama rafiki mkubwa.” (Suratul Fuswilat, 41: 34)

“Na ushike mwendo wa katikati, na uteremshe sauti yako, bila Shaka sauti ya punda ni mbaya kuliko sauti zote.” (Suratul Luqman, 31: 19)

“Enyi mliyoamini! muogopeni Mwenyezi Mungu na semeni maneno ya sawa. Atakutengenezeeni vizuri vitendo vyenu na atakusameheni madhambi yenu, na anayemtii Mwenyezi Mungu na Mtume Wake bila shaka amefaulu kufaulu kukubwa.” (Suratul Ahzaab, 33: 70-71)

230


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:22 PM

Page 231

Tabia njema kwa mujibu wa Ahlul Bayt (a.s)

HADITHI Mtu mmoja alimuambia Abul Hasan (a): Niusie. Akamjibu. “Hifadhi ulimi wako utakuwa azizi (mwenye utukufu, nguvu…) na usiwawezeshe watu kukuendesha ukawa mtumwa”.262 Mtu mmoja alimjia Mtume (s) na kumuambia: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu niusiye. Akamuambia: “Hifadhi ulimi wako!” Tena akamuomba (mara ya pili): Niusiye ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu. Akamjibu: “Hifadhi ulimi wako!” (kwa mara ya tatu) akamuomba, ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, niusiye. Na Mtume akamjibu: “Hifadhi ulimi wako!” Ole wako kwani ni kipi kitakacho wabwaga watu juu ya pua zao motoni kama siyo mavuno ya ndimi zao”.263 Imam Sadiq (a) alimuambia Ubbaad bin Kathir al Baswry as-Sufy: “Ole wako ewe Ubbaad! Usighurike ya kwamba umehifadhi tumbo lako na utupu wako, hakika Mwenyezi Mungu (swt) anasema ndani ya kitabu chake: “Enyi mliyoamini! muogopeni Mwenyezi Mungu na semeni maneno ya sawa. Atakutengenezeeni vizuri vitendo vyenu na atakusameheni madhambi yenu, na anayemtii Mwenyezi Mungu na Mtume wake bila shaka amefaulu kufaulu kukubwa.” (Suratul Ahzab, 33:70-71) Hakika Mwenyezi Mungu (swt) hatakukubalia chochote mpaka useme kauli njema na adilifu”264 Imam Ali Zaynul-Abidin (a) alisema: “Kauli njema inaongeza mali na kuzidisha riziki na kuakhirisha ajali na kupendwa na familia na huingiza peponi” 262. Al Waafy, juz. 3, uk. 85 263. Al Waafy, juz. 3, uk. 85 264. Al Waafy, juz. 3, uk. 85 231


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:22 PM

Page 232

Tabia njema kwa mujibu wa Ahlul Bayt (a.s) Hizi beti zanasibishwa kwa Imam Sadiq (a): Uzoweshe ulimi wako kauli ya kheri utafaidika (utapata heshima) Hakika ulimi huzowea yale uliyouzoesha. Kutoka kwa Imam Musa (a): Mtume (s) alisema: “Mwenyezi Mungu amrehemu mja ambaye asema kheri akavuna au akanyamaza kuhusu ovu akasalimika�. Kutokana na maandiko hayo tunagundua wazi kwamba kuna dharura ya kushikamana na adabu za kuongea na kuuhifadhi ulimi na matusi na kuuzowesha lugha nzuri na kauli njema. Kauli iliyopimwa na tukufu ina utamu na athari ndani ya nyoyo za watu, marafiki pia maadui. Katika marafiki huzidisha upendo na kudumisha mapenzi na hivyo basi huzuia ushawishi wa Shetani katika kuharibu mahusiano ya urafiki na upendo. Ama katika maadui, hulainisha hisia zao na hupunguza madhara na vitimbi vyao. Kwa ajili hiyo tunakuta watu watukufu hufanya mazoezi ya kudhibiti ndimi zao na kuzihifadhi zisiteleze na kuporomoka ndani ya madhambi. Imesimuliwa kwamba wafalme wanne walikaa na kuzungumza: Mfalme wa Fursi akasema: Kamwe sijajuta juu ya ambalo sikulisema mara moja, lakini mara nyingi nimejuta juu ya lile nililolisema. Naye Kaizari wa Rumi akasema: Naweza zaidi kurudisha lile ambalo sikulisema kuliko lile ambalo nililolisema. Mfalme wa China akasema: Maadamu sijasema neno basi nimelimiliki, ama ninapokuwa nimelisema, basi limenimiliki. Mfalme wa India akasema: Ajabu ni kutoka kwa yule anayesema neno, ikiwa litasimamishwa linadhuru, na ikiwa halitasimamishwa halitofaa. 232


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:22 PM

Page 233

Tabia njema kwa mujibu wa Ahlul Bayt (a.s) Hakuna jambo linaloashiria zaidi upumbavu wa mtu kama kubwabwaja, kusema sana (kuingilia ya watu) na kuwa na ulimi mchafu. Imam Ali (a) alimkuta mtu anasema sana (yasio na maana), akasimama na kumuambia: “Ewe wewe bila shaka unawandikisha malaika wako wawili (wanaonakili matendo yako) barua kuiwakilisha kwa Mwenyezi Mungu (swt). Kwa hivyo zungumza yanayokuhusu na acha kabisa yasiyokuhusu.” Pia alisema (a): “Yule ambaye maneno yake yanazidi, basi makosa yake huzidi, na yule ambaye makosa yake huzidi basi aibu yake hupungua, na yule ambaye aibu yake hupungua, basi uchamungu wake hupungua, na yule ambaye uchamungu wake hupungua, basi moyo wake hufa, na yule ambaye moyo wake unakufa, basi huingia motoni”. Kutoka kwa Sulayman bin Mahraan, alisema: Niliingia kwa Imam Sadiq (a) akiwa na kundi la Mashia na kumsikia akisema: “Enyi Mashia kuweni kwetu ni pambo na wala msiwe juu yetu ni aibu. Waambieni watu yaliyo mazuri na mhifadhini ndimi zenu na mziepushe na kuingilia ya watu na kauli mbaya”.265 Maandiko yamesisitiza sana kunyamaza na kuumiliki ulimi ili kujilinda na maafa yake hatari na hivyo kusalimika. Imam Sadiq (a) alisema: “Kunyamaza ni hazina iliyojaa, pia ni pambo la mtu mpole na sitara ya mtu mjinga”. 266 Imam Baqir (a) alisema: “Abu Dhar alikuwa akisema: Ewe mwenye kutaka elimu, hakika ulimi huu 265. Al Bihaar, muj. 15, juz. 2 uk. 192 266. Al Waafy, juz. 3, uk. 85 233


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:22 PM

Page 234

Tabia njema kwa mujibu wa Ahlul Bayt (a.s) ni ufunguo wa kheri na ufunguo wa shari, linda ulimi kama vile unavyolinda dhahabu yako na pesa yako� 267 Imehadithiwa ya kwamba Qis bin Saidah na Aktham bin Swayfy walikutana na mmoja wao akamuambia mwenziwe: Mangapi uliyoyapata ya aibu katika mwanadamu? Akajibiwa: Mengi, hayahesabiki, (lakini) nilikuta kuna jambo ikiwa atalitumia mwanadamu basi litasitiri aibu zote ambalo ni kuhifadhi ulimi.

MAAFA YA MADHAMBI Baina ya maradhi ya kimwili yanayomsumbua mwanadamu na madhambi anayoyachuma kuna ushabihiano mkubwa kuhusu chanzo na matokeo (ya maradhi hayo) juu yake. Kama vile maradhi mengi aghlabu chanzo chake ni kwenda kinyume na taratibu za siha ambazo zimewekwa na matabibu, hivyo hivyo madhambi yanatokana na kuhalifu kanuni za Mwenyezi Mungu (na nidhamu yake) ambazo aliziweka kwa ajili ya islahi ya wanadamu na kuwapa maisha ya furaha. Pia kama vile kila ugonjwa unavyohusika na madhara maalum na athari mbaya kwa mgonjwa hivyo hivyo ndivyo yalivyo madhambi. Kila aina ya dhambi ina matokeo mabaya na madhara makubwa na athari hatari ambazo zinamsababishia mwanadamu aina ya mabalaa na mateso. Ingawa maradhi na madhambi vimeshirikiana katika ubaya na adha, lakini madhambi ni yenye shida zaidi na athari mbaya zaidi kuliko maradhi. Ni rahisi kutibu mwili lakini ni vigumu kutibu nafsi. Ni kwa sababu hiyo ndiyo maana dhambi zikawa ni sumu inayoangamiza, 267. Al Waafy, juz. 3, uk. 85 234


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:22 PM

Page 235

Tabia njema kwa mujibu wa Ahlul Bayt (a.s) na vimea hatari vinavyochochea ndani ya mwanadamu uharibifu na kumsukumiza kwenye hatari na maangamio.

QUR’ANI Hebu tazama jinsi Qur’ani inavyotoa picha ya kutisha kuhusu maafa ya madhambi na hatari zake katika aya zifuatazo: Mwenyezi Mungu anasema:

“Na tunapotaka kuuangamiza mji tunawaamrisha mafisadi wake, lakini wanaendelea na maasi humo, hapo kauli ina hakiki juu yake, na tunauangamiza maangamizo makubwa.” (Israa’, 17:16)

“Je hawaoni umma ngapi tulizoziangamiza kabla yao? Tuliwamakinisha katika nchi tusivyokumakinisheni (nyinyi) na tukawapelekea mvua iendeleayo, na tukaifanya mito ipite chini yao. Na tukawaangamiza kwa sababu ya dhambi zao, na tukaumba baada yao umma nyingine.” (Al An’aam, 6:6)

235


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:22 PM

Page 236

Tabia njema kwa mujibu wa Ahlul Bayt (a.s) “Na kama watu wa miji wangeamini na kumcha (Mwenyezi Mungu) lazima tungeliwafungulia baraka za mbingu na ardhi, lakini walikadhibisha, tukawaangamiza kwa sababu ya yale waliyokuwa wakiyachuma.” (Al A’raaf, 7:96)

“Hayo ni kwa sababu Mwenyezi Mungu habadilishi kabisa neema aliyowaneemesha watu mpaka wabadilishe yalimo ndani ya nafsi zao, na kwamba Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusikia, Mjuzi.” (Al Anafaal, 8:53)

“Na msiba uliokupateni ni kwa sababu ya matendo ya mikono yenu, na (pia) anasamehe mengi.” (As-Shura, 42:30)

“Uharibifu umedhihiri barani na baharini kwa sababu ya yale iliyoyafanya mikono ya watu, ili awaonjeshe (adhabu ya) sehemu ya waliyoyafanya huenda wakarudi.” (Ar Rum, 30:41). Hivi ndivyo zimepokelewa hadithi kutoka kwa Ahlul Bayt (a) wakitahadharisha maafa ya madhambi na wakaweka wazi kwamba yale yanayoikumba jamii na mtu binafsi ya matatizo na mitihani kama vile kuenea dhuluma, maradhi, kupungukiwa riziki yote sababu ni madhambi na maovu.

236


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:22 PM

Page 237

Tabia njema kwa mujibu wa Ahlul Bayt (a.s)

HADITHI Hizi ni baadhi ya hadithi: Imam Sadiq (a) kama alivyopokea kutoka kwa baba zake alisema: Mtume wa Mwenyezi Mungu (s) alisema: “Nashangazwa na mtu ambaye anajiepusha na chakula akiogopa maradhi, vipi huyu hajiepushi madhambi akiogopa moto (wa jahannam)!!” Imam Ridhaa (a) alisema: Mtume wa Mwenyezi Mungu alisema: “Mwenyezi Mungu (swt) anasema: Ewe mwanadamu hunifanyii usawa! Nakufanyia mapenzi kwa neema, wewe unanichukia kwa maasi, kheri yangu kwako ni yenye kushuka, na shari yako kwangu ni yenye kupanda, na haachi malaika mtukufu kila mchana na usiku kuniletea amali yako chafu. Ewe mwanadamu! Lau ungesikia wasifu wako kutoka kwa mtu mwingine na wewe hujui nani msifiwa, bila shaka haraka ungemchukia”.268 Imam Sadiq (a) alisema: “Pindi mtu anapofanya dhambi basi hujitokeza ndani ya roho yake doa nyeusi. Ikiwa atatubu hilo doa hufutika, ama akizidisha (madhambi, basi doa hilo) huongezeka hadi kuenea roho yote, hapo kamwe hawezi kufaulu tena.” Pia akasema (a): “Alikuwa baba yangu (a) akisema: Hakika Mwenyezi Mungu (swt) amepitisha qadhaa (hukumu) isiyobadilika kwamba hawezi kumneemesha mja kwa neema kisha akaimuondolea, mpaka afanye dhambi anayostahili kwayo adhabu”. Naye imam Baqir (a) alisema: “Hakika mja anamuomba Mwenyezi Mungu (awj) haja, na kwa shani yake anakuwa tayari kumkidhia baada ya muda si mrefu au baadae. Lakini mja 268. Al Bihaar, muj. 15, juz. 3, uk. 156 237


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:22 PM

Page 238

Tabia njema kwa mujibu wa Ahlul Bayt (a.s) anafanya dhambi na hivyo Mwenyezi Mungu (swt) anawaambia malaika: Msimkidhie haja yake, msimpe kwani amempata ghadhabu yangu na kustahili kunyimwa nami”. Pia akasema (a): “Tulikuta katika kitabu cha Mtume (s): Pindi itakapodhihiri baada yangu zinaa basi vifo vya ghafla vitaongezeka, na vipimo na mizani vitakapo punguzwa, Mwenyezi Mungu (swt) atawashika kwa ukame na upungufu, na watakapozuia zaka, basi ardhi itazuia baraka zake za mimea, matunda na madini yote, na watakapokengeuka katika hukumu, basi watasaidiana kwenye dhuluma na uadui, na pindi watakapovunja ahadi, basi Mwenyezi Mungu (swt) atampa uwezo adui yao juu yao, na pindi watakapokata kizazi, basi Mwenyezi Mungu (swt) ataiweka mali katika mikono ya waovu, na watakapoacha kuamrisha mema na kukataza maovu, na wakaacha kuwafuata wabora katika watu wa nyumba yangu (Ahlul Bayt) Mwenyezi Mungu (swt) utawatawalisha juu yao waovu wao, na hivyo wabora wao wataomba na wala hawatajibiwa.”269 Mtume (s) alisema: “Mwenyezi Mungu (swt) anapoughadhibikia umma, kisha usiteremshiwe adhabu, basi bei zao hupanda, umri huwa mfupi, biashara hukosa faida, mazao huwa machache, mito hukosa maji ya kutosha, mvua huwa nadra, na waovu wao huwa na madaraka juu yao.” 270 Imam Sadiq (a), alisema (kama ilivyosimuliwa na bwana Mufaddhal): “Ewe Mufaddhal, jihadhari na madhambi na uwatahadharishe mashia wetu kwa sababu Wallahi athari yake ni ya haraka sana kwenu kuliko yeyote. Hakika mmoja wenu yanamfika madhila kutoka kwa mtawala na hilo kwa sababu ya madhambi yake, na mara humfika maradhi na sababu ni madhambi yake, na mara riziki hufungwa na hilo si kwa lingine ila madhambi yake. Na pia hufanyiwa ugumu wakati wa mauti na hilo ila kwa 269. Al Waafy, juz. 3, uk. 173 270. Al Waafy, juz. 3, uk. 173 238


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:22 PM

Page 239

Tabia njema kwa mujibu wa Ahlul Bayt (a.s) madhambi mpaka waliohudhuria wakasema: Eh! hakika mauti yamemdhiki! Alipoona yaliyoniingia akasema: “Unajua kwa sababu gani hilo ewe Mufaddhal? Nikajibu: Sijui, niwe fidia yako. Akaniambia: “Wallahi, hilo ni kwa sababu kesho akhera hamtaadhibiwa kwa hayo, kwa hiyo adhabu yenu imetangulizwa duniani”.271 Imam Ali (a): alisema: “Jilindeni na madhambi. Hakuna balaa wala kupungukiwa riziki ila kwa sababu ya madhambi, hata mkwaruzo, kuteleza (ukaanguka ukaumia) au msiba (balaa yeyote ile)” Mwenyezi Mungu (swt) anasema: Na yanayokufikeni ya misiba ni kutokana na yale yaliyochumwa na mikono yenu, naye anasamehe mengi. “Na msiba uliokupateni ni kwa sababu ya matendo ya mikono yenu, na (pia) anasamehe mengi.” (Suratul Shuura, 42:30) Wakati mwingine Shetani huwaghilibu baadhi ya watu wasiokuwa na ujuzi kwamba ikiwa kweli kama madhambi yanaangamiza basi wangeangamia waliokita ndani ya uasi, wasiojali kufanya madhambi. Lakini pamoja na uasi, maisha yao ni mazuri zaidi na furaha. Hii ni kwa sababu ukweli kwao umejificha ya kwamba Mwenyezi Mungu (swt) hashindwi kuwashika (ni muweza juu ya kila kitu) wala hahofu kupoteza (milki ni yake), bali ni kwamba anawapa muda waasi na kuahirisha adhabu yao kwa kuzingatia maslahi yao, huenda wakarejea kwenye utii wa Mwenyezi Mungu (swt) na uongofu. Pia inaweza ikawa sababu ni huruma juu ya wasio na hatia na wanyonge (ambao hawahusiki na madhambi) ambao watadhurika ikiwa wenye madhambi watachukuliwa hatua haraka. Au pia Mwenyezi Mungu (swt) anawavuta hao watu waovu, hatua baada ya hatua, ili wazidishe maovu na hivyo awabamize na adhabu kali 271. Al Bihaar

239


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:22 PM

Page 240

Tabia njema kwa mujibu wa Ahlul Bayt (a.s) isiyochelea, kama inavyosema Qur’ani na pia riwaya nyingi. Mwenyezi Mungu (swt) anasema:

“Wala wasidhani wale waliokufuru kwamba muda tunaowapa ni bora kwao, hakika tunawapa muda ili wazidi maovu, na wana adhabu yenye kudhalilisha.” (Aali Imraan, 3:178) Pia anasema:

“Na kama Mwenyezi Mungu angeliwaadhibu watu kwa sababu ya yale waliyoyachuma, asingeliacha juu ya ardhi hata mnyama mmoja. Lakini Yeye anawaahirisha mpaka muda maalumu, basi itakapowafikia ajali yao, hapo bila shaka Mwenyezi Mungu anawajua vyema waja wake.” (Fatir, 35:45) Imam Sadiq (a) alisema: “Pindi Mwenyezi Mungu (swt) anapomtakia mja kheri, akafanya dhambi, humfuatishia nakma na kumkumbusha kuomba istighfar, na anapomtakia mja shari, akafanya dhambi, humfuatishia neema (akatanua kwayo) ili kumsahaulisha istighfar, na hiyo ndiyo kauli ya Mwenyezi Mungu (swt):

240


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:22 PM

Page 241

Tabia njema kwa mujibu wa Ahlul Bayt (a.s) “Basi niache na anayeikadhibisha hadithi hii, karibuni tutawavuta kidogo kidogo kwa mahala wasipopajua.” (Qalam, 68: 44) hii kwa kuwapa neema pindi wanapoasi”.272 Imam Musa (a) alisema: “Mwenyezi Mungu (swt) alijalia katika kila mchana na usiku mnadi anayenadi: taratibu, taratibu, waja wa Mwenyezi Mungu (swt) na kufanya maasi, lau kama isingekuwa wanyama walio malishoni, wachanga wanaonyonya na wazee wenye kurukuu, basi adhabu ingeteremshwa juu yenu na kutikiswa kwayo sawa sawa.”273 Huenda ikagonga ndani ya akili ya kwamba mitume na mawasii ni maasumu (hawatendi dhambi), sasa ni vipi wanapatawa na aina mbalimbali ya mitihani na shida? Kujibu mushkeli huo ni vyema kufahamu ya kwamba madhambi yanahitilafiana kwa kuzingatia tofauti za watu na kiwango cha imani yao, upeo wa utiifu wao na utumwa kwa Mwenyezi Mungu (swt). Kuhusu jambo jema la furaha, huenda watu wawili wakawa na maoni tofauti. Mmoja anaweza akalichukulia kwamba ni jambo zuri ama mwingine akaona kwamba ni dhambi na jambo baya kwa kumkengeusha na dhikri ya Mwenyezi Mungu (swt) na ibada. Kwa kuwa mitume ndiyo mfano bora katika kumuamini Mwenyezi Mungu (swt) na kuzama katika utiifu wake na kupagawa kumwabudu, wao kuacha lililo awla (bora) linatazamwa kuwa ni dhambi na kasoro, kama inavyosemwa: “mema ya watu wema ni maovu kwa waliyokurubia kwa Mwenyezi Mungu”. 272. Al Waafy, juz. 3, uk. 173 273. Al Waafy, juz, 3, uk. 168 241


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:23 PM

Page 242

Tabia njema kwa mujibu wa Ahlul Bayt (a.s) Sababu ya mitihani na matatizo siyo tu madhambi, pia inaweza kuwa ni njia ya kuidhihirisha subira ya mtahiniwa na uthabiti wake kwenye kumtii Mwenyezi Mungu (pia qadari na matakwa Yake). Pia inaweza ikawa ni njia ya kupata maradufu ujira kwa mtahiniwa na thawabu nyingi kwa kusubiria juu ya mateso na kumkabidhi mambo yake Mwenyezi Mungu (swt).

36. TOBA Umekwishaelewa katika somo lililotangulia maafa ya madhambi na madhara yake kiroho na kimwili na kushabihiana kwake na maradhi ya kimwili katika uharibifu na athari mbaya juu ya mwanadamu. Kama ipasavyo kufanya haraka kutibu mwili na vijidudu vya maradhi kabla ya kuzidiwa mwili na kudhoofika na hivyo kushindwa kupambana, ndivyo pia ni muhimu kupupia kuitakasa nafsi na kuitoharisha na uchafu wa madhambi na maovu kabla maafa yake hayajawa hatari na hivyo kuwa vigumu kukabiliana nayo. Kama yanavyotibiwa maradhi ya kisiha kwa kunywa dawa zenye karaha na kujiepusha na chakula (diet) kitamu, hivyo hivyo ndivyo yanavyotibiwa madhambi kwa kuonja shida ya toba na kutubia na kujing’oa kutoka ndani ya matamanio yanayogandamiza na kuangamiza.

UKWELI WA TOBA Toba ya kweli haikamili ila baada ya kupita daraja tatu: Hatua ya kwanza: Daraja ya mwamko wa dhamira. Hii ni mtenda dhambi kuwa na simanzi na majuto kwa kumuasi Mwenyezi Mungu (swt) na kujitwika adhabu yake. Pindi nafsi ya mtenda dhambi inapojaa aina hii ya hisia ndipo inapopiga hatua ya pili. 242


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:23 PM

Page 243

Tabia njema kwa mujibu wa Ahlul Bayt (a.s) Hatua ya pili: :Hii ni hatua ya kurejea na kutubia kwa Mwenyezi Mungu (swt), na kuwa na azma ya kweli kwenye kumtii Mwenyezi Mungu (swt) na kujiepusha na kumuasi. Pindi anapokuwa na hali hiyo ndipo anapoingia hutua ya tatu. Hatua ya tatu: Hatua ya kusafisha nafsi na taka la madhambi na kufuta (athari ya) madhambi kwa matendo mema ambayo yanayotunisha mtaji wa mema na kubomoa maovu. Kwa hayo ndipo toba ya kweli inapatikana. Hivyo basi toba siyo mchezo wa upuuzi au maneno yanayonenwa na ulimi, bali ni kurejea na kutubia kwa Mwenyezi Mungu (swt) kikweli na kujiepusha na kumuasi kwa azma na uamuzi hasa. Kwa hiyo mwenye kuomba toba kwa ulimi tuu na akawa hajali maasi ni muongo, kama alivyosema Imam Ridhwa (a) : “Mwenye kutubia dhambi kisha akaifanya basi huyo ni kama mwenye kumfanyia stihzai Mola wake”.

FADHILA ZA TOBA Toba ina fadhila nyingi sana na matendo matukufu. Qur’ani imeelezea hayo na pia hadithi za Ahlul Bayt (a). Ni fadhila kubwa iliyoje kwamba toba ni pozo la madhambi na safina ya uokovu na kizibo cha usalama kuepuka adhabu ya Mwenyezi Mungu (swt). Kwa upendo na urahimu wake Mwenyezi Mungu (swt) hawezi kuwaachia wakosefu wakitangatanga katika giza la madhambi na jangwa la uasi, pasi na kuwafunika na upole Wake na msamaha Wake mkubwa. Ndiyo maana Mwenyezi Mungu (swt) amewavutia sana kutubia na akawaandalia toba. Anasema (swt):

243


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:23 PM

Page 244

Tabia njema kwa mujibu wa Ahlul Bayt (a.s)

“Na wanapokufikia wale wanaoamini Aya zetu, basi waambie: Amani iwe juu yenu, Mola wenu amejilazimisha rehema, kwamba atakayefanya miongoni mwenu uovu kwa ujinga, kisha akatubu baada yake na akafanya wema basi Yeye ndiye Mwingi wa kusamehe, Mwenye kurehemu.” (Suratul An’am, 6: 54)

“Sema: Enyi waja wangu mliojidhulumu wenyewe! msikate tamaa katika rehema za Mwenyezi Mungu, bila shaka Mwenyezi Mungu husamehe dhambi zote, hakika yeye ni Mwingi wa kusamehe Mwenye kurehemu. (Suratul Zumar, 39:53)

“Nikawaambia: Ombeni msamaha kwa Mola wenu, hakaka Yeye ni Mwingi wa kusamehe. Atakuleteeni mawingu yanyeshayo mvua nyingi. Na atakupeni mali na watoto na atakupeni mabustani, na atakufanyieni mito.” (Suratul Nuh, 71:10 – 12)

244


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:23 PM

Page 245

Tabia njema kwa mujibu wa Ahlul Bayt (a.s) “Hakika Mwenyezi Mungu huwapenda wanaotubu na wanaojitakasa.” (Suratul Baqarah, 2:222) Imam Sadiq (a): “Pindi mja anapotubia toba ya kweli, Mwenyezi Mungu (swt) humpenda na kumsitiri duniani na akhera. Rawi (msimulizi wa hadithi) akauliza: Ni vipi Mwenyezi Mungu (swt) atakavyo msitiri? Akajibu: Atawasahaulisha malaika wake yale waliyomuandikia ya madhambi na pia atavipa wahyi viungo vyake vimfichie siri ya madhambi yake na pia sehemu ya ardhi isifichue aliyoyafanya juu yake ya madhambi na hivyo kurejea kwa Mola wake na hana shahidi wa kushuhudia madhambi yake”. 274 Kutoka kwake pia :“Mja muumini anapofanya dhambi, Mwenyezi Mungu (swt) humpa muda wa masaa saba. Ikiwa atatubia haandikiwi (dhambi). Ama yakipita masaa na hakuomba maghfira, basi anaandikiwa ovu moja. Na hakika muumini anaikumbuka dhambi yake baada ya miaka ishirini mpaka amuombe Mola wake maghfira, basi humsamehe. Ama kafiri huisahau hapo hapo.” 275 Pia alisema: “Hakuna muumini ambaye anafanya katika usiku na mchana madhambi makubwa arobaini kisha akasema na huku ni mwenye kujutia: ‘Namuomba Mwenyezi Mungu (swt) msamaha ambaye hakuna mungu ila Yeye Aliye hai Asiye mhitaji, Muumba wa mbingu na ardhi, Mwenye enzi na utukufu, na ninamuomba amsalie Mtume na aali zake na akubali toba yangu’ ila Mwenyezi Mungu (swt) humsamehe, na hakuna heri katika mtu ambaye anafanya kwa siku, zaidi ya madhambi makubwa arobaini .” Imepokewa kutoka kwa imam Ali Ridhwa (a) kutoka kwa baba zake alisema: Mtume (s) alisema:“Anayetubia dhambi ni kama asiye na dhambi”. 274. Al Waafy, juz. 3, uk. 183 275. 245


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:23 PM

Page 246

Tabia njema kwa mujibu wa Ahlul Bayt (a.s) Pia alisema: “Hakuna chochote apendacho sana Mwenyezi Mungu (swt) kama muumini mwenye kutubia”. Kutoka kwa Abu Abdillah (a) au Abu Ja’far (a), alisema: “Nabii Adam (a) alisema: Ewe Mola umempa Shetani uwezo juu yangu na ukamwezesha kutembea ndani mwangu kama vile damu, basi nijalie nami chochote. Akamjibu: Ewe Adam, nimekujalia kwamba yeyote katika kizazi chako atakayeazimia ovu, hataandikiwa chochote, na ikiwa atafanya ovu, basi ataandikiwa ovu moja. Ama atakayeazimia wema, ataandikiwa wema, na akiufanya basi ataandikiwa mema kumi. Adam akaomba: Ewe Mola nizidishie. Akamjibu: Nimekujalia kwamba yeyote katika kizazi chako atakayefanya ovu kisha akaniomba maghfira, basi nitamsamehe. (Adam) akaomba tena: Ewe Mola nizidishie. Akamjibu: Nimewajalia toba hata katika dakika za mwisho nafsi inapotoka. Akasema: Ewe Mola yanitosha”.

UWAJIBU WA TOBA NA UHARAKA WAKE Hakuna shaka kuhusu uwajibu wa toba, kwa akili na maandiko kuthibitisha hilo. Ama akili, ni dharura mtu kujilinda na kujikinga na mambo yanayosababisha madhara na hatari zinazopelekea mtu kuteseka na kuangamia. Kwa sababu hiyo ni lazima kujikinga kwa toba na hivyo kuepuka maafa ya madhambi na athari zake mbaya katika maisha haya na ya baadae. Ama maandiko, Qur’ani na sunnah vimefaradhisha toba na kuihimiza kwa aina za vivutio na wepesi. Kutoka kwa Abu Abdullah (a), alisema: “Alisema Mtume wa Mwenyezi Mungu (s): Yeyote atakayetubu mwaka mmoja kabla ya kufa kwake, Mwenyezi Mungu atakubali toba yake. Kisha akasema: Hakika mwaka ni muda mrefu, atakayetubia mwezi mmoja kabla 246


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:23 PM

Page 247

Tabia njema kwa mujibu wa Ahlul Bayt (a.s) ya kufa kwake, Mwenyezi Mungu atakubali toba yake. Kisha akasema: Hakika mwezi ni muda mrefu, atakayetubia Ijumaa moja kabla ya kifo chake, Mwenyezi Mungu atakubali toba yake. Kisha akasema: Hakika Ijumaa ni muda mrefu, atakayetubia siku moja kabla ya kifo chake, Mwenyezi atakubali toba yake. Kisha akasema: Hakika siku moja ni muda mrefu, atakayetubia kabla hajashuhudia kifo, Mwenyezi Mungu (swt) atakubali toba yake.” Imam Ja’far Sadiq (a) kutoka kwa baba yake alisema: “Mtume wa Mwenyezi Mungu (s) alisema: “Hakika Mwenyezi Mungu (swt) ana ziada ya riziki ambayo humpa amtakaye katika viumbe wake, na Mwenyezi Mungu (swt) kila inapochomoza alfajiri humyooshea mikono yake muasi (katika kipindi cha) usiku, je atatubia ili amsamehe, na pindi linapozama jua, humyooshea mikono yake mfanya dhambi (katika kipindi cha) mchana, je atatubia amsamehe.”

KUTUBIA UPYA Miongoni mwa watu kuna wale ambao wanaongoka baada ya kupotea na kusimama sawa baada ya kwenda upande. Kwa njia ya toba na kujuta, kwa kuitikia mwito wa imani na dhamiri huru, wanafanikiwa kusahihisha madhambi yao. Kwa upande mwingine, ni mara nyingi tu mwanadamu hughuriwa na starehe za dunia na kumfanya mtumwa wa vivutio vyake na hivyo kujikuta anatenda maasi upya kwa kupelekwa na mkondo wake mkali. Kwa hali hiyo huishi katika pambano kali baina ya akili na matamanio, mara inashinda na mara inashindwa. Na hili ndilo linalowazuia wengi kutubia upya, kwa kuchelea kwamba watarejea kuanguka na hivyo kuendelea kuogelea katika maasi.

247


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:23 PM

Page 248

Tabia njema kwa mujibu wa Ahlul Bayt (a.s) Ni muhimu hawa watu wakaelewa ya kwamba mwanadamu ni shabaha ya upotofu na udanganyifu wa Shetani na hakuna yeyote anayeweza kusalimika na hila zake zaidi ya mitume na mawasii (juu yao amani). Kwa hivyo basi linalofaa zaidi kwao ni kwamba pindi Shetani anapowaangusha chini kwa udanganyifu wake, wanatakiwa wafanye upya ahadi ya kutubu na kujutia kwa nia ya kweli na uamuzi thabiti, ikiwa watapotea na kwenda upande, hilo lisiwakatishe tamaa kufanya upya toba, na pia kuelewa na kudiriki maana ya maneno ya Mwenyezi Mungu:

“Sema: Enyi waja wangu mliojidhulumu wenyewe! msikate tamaa katika rehema za Mwenyezi Mungu, bila shaka Mwenyezi Mungu husamehe dhambi zote, hakika yeye ni Mwingi wa kusamehe Mwenye kurehemu.” (Az Zumar, 39:53) Hivyo hivyo hadithi za Ahlul Bayt (a) zimehimiza sana kufanya upya toba na kuendelea kujutia ili kuwaokoa waathirika wa madhambi wasizame kabisa na kusombwa nayo. Muhammad bin Muslim (a) anasimulia: Imam Baqir (a) alisema: “Ewe Muhammad bin Musilim, dhambi za muumini, ikiwa anatubia zinasamehewa, kwa hivyo naashughulike jinsi ya kuanza upya baada ya toba na maghfira, ama Wallahi, toba ni kwa ajili ya wenye imani. Nikamuuliza: Je vipi ikiwa atarejea katika madhambi baada ya toba na maghfira, kisha akarudi katika toba? Akajibu: Ewe Muhammad bin Muslim hivi kweli Mwenyezi Mungu (swt) ataacha kumsamehe mja wake wakati anajutia na kuomba msamaha!! Tena nikauliza: Je ikiwa atarudia na kufanya hivyo mara nyingi, anafanya dhambi kisha anatubia? Akasema: pindi muumini atakaporejea kwa kuomba maghfira na toba, basi Mwenyezi Mungu (swt) atampokea kwa msamaha na maghfira, na hakika 248


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:23 PM

Page 249

Tabia njema kwa mujibu wa Ahlul Bayt (a.s) Mwenyezi Mungu (swt) ni ghafuru na rahimu, anakubali toba na kusamehe maovu, kwa hivyo tahadhari na kuwakatisha tamaa waumini na rehema ya Mwenyezi Mungu (swt)”. Abu Basir anasimulia: “Nilimuuliza Abu Abdilah (a) kuhusu:

“Enyi mlioamini! tubuni kwa Mwenyezi Mungu toba iliyo ya kweli, huenda Mola wenu akakufutieni maovu yenu na kukuingizeni katika Pepo zipitazo mito chini yake, siku ambayo Mwenyezi Mungu hatamfedhehesha Mtume na wale walioamini pamoja naye, nuru yao itakwenda mbele yao na pande zao za kulia (na kushoto) na huku wanasema: Mola wetu! tutimizie nuru yetu na tusamehe, hakika Wewe ni Mwenye uwezo juu ya kila kitu.” (Suratu Tahrim, 66:8). Yeye akajibu: Hiyo ni dhambi ambayo hatairejea abadan. Nikasema: Nani kati yetu anayeweza kuacha kabisa na asirejee dhambi! Akanijibu: Ewe Abu Muhammad, hakika Mwenyezi Mungu (swt) anapenda kati ya waja wake wale ambao wafanyao sana madhambi na kutubia sana.” Hakuna ajabu kwa Mwenyezi Mungu (swt) ampende mwingi wa madhambi na mwingi wa toba. Kurejelea kufanya madhambi na kutotubia ni dalili wazi ya kwamba dhamiri imekufa na imani kuangamia na kutojali kumtii Mwenyezi Mungu (swt). Hilo bila shaka linapelekea ghadhabu na adhabu ya Mwenyezi Mungu (swt). 249


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:23 PM

Page 250

Tabia njema kwa mujibu wa Ahlul Bayt (a.s)

UTARATIBU WA TOBA Ni lazima mwenye kutubia kufahamu njia (taratibu) za toba na jinsi gani atakavyojiepusha na athari ya madhambi na mzigo wake hatari ili aweze kulipa (kufuta) kila ovu kwa uchaji na toba inayostahiki. Madhambi yana sura na pande mbalimbali: Madhambi ambayo ni baina ya mja na muumba wake mtukufu, nayo ni sehemu mbili: kuacha ya wajibu na kufanya ya haramu. Ya kuacha wajibu, ni kama vile kuacha kusali, kufunga, kuhiji, kutoa zakat, nk…Njia ya kutubia madhambi haya ni kujitahidi kutekeleza wajibu, kwa kila juhudi iwezekanayo. Ama ya haramu, ni kama vile zinaa, kunywa pombe, kamari, nk… Njia ya kutubia ni kujutia kwa kuyafanya na kuwa na azma ya kweli ya kuyaacha. Ama yapo madhambi ambayo ni baina ya mtu na watu, na hayo ndiyo yenye matokeo na dhima kubwa na magumu zaidi kusafisha, kama vile kunyang’anya mali za watu, kuuwa nafsi isiyo na hatia, kumuaibisha muumini kwa kumtukana, kumpiga, kumsengenya au kumkashifu. Toba ya madhambi haya, ni kwa kumridhisha kwanza uliye mtendea uovu, na kurejesha ulivyodhulumu kwa wenyewe kadri iwezekanavyo. Ikiwa atashindwa mtu kufanya hivyo itabidi aombe maghfira na kuzidisha rasilimali yake ya mema na kumlilia Mwenyezi Mungu (swt) awafanye aliyowakosea wawe radhi naye siku ya kiama.

KUKUBALI TOBA Hakuna shaka kwamba toba ya kweli liliyokamilisha masharti ni yenye kukubalika kwa dalili ya Qur’an. Mwenyezi Mungu (swt) anasema: “Naye ndiye anayepokea toba za waja wake, na husamehe makosa, na 250


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:23 PM

Page 251

Tabia njema kwa mujibu wa Ahlul Bayt (a.s) anayajua mnayoyatenda.”(S. Shuraa, 42:25)

“Mwenye kusamehe madhambi na Mwenye kupokea toba, mkali wa kuadhibu, Mwenye ukarimu, hakuna aabudiwaye ila yeye tu, marejeo ni kwake.”(S. Ghaafir, 40:3) Tulikwisha elezea katika fadhila za toba kiasi fulani cha aya na hadithi kuhusu toba, na pia kufuzu wenye kutubia, kwa sababu ya utukufu wa radhi za Mwenyezi Mungu (swt), ukarimu wa msamaha wake na uwingi wa neema zake. Na ushahidi wenye nguvu juu ya hilo ni hadithi ya Mtume (s) pindi aliposema: “Kama isingekuwa nyinyi mnafanya madhambi kisha mkamuomba Mwenyezi Mungu (swt) maghfira, basi angeumba viumbe ili wafanye madhambi kisha wamuombe msamaha, na awasamehe. Hakika muumini ni mwingi wa madhambi na mwingi wa toba (muftan tawwaab). Je hukusikia kauli ya Mwenyezi Mungu “Hakika Mwenyezi Mungu huwapenda wanaotubu na wanaojitakasa?” (Suratul Baqarah, 2:222)

SHAUKU ZA TOBA Huu ni mukhtasari wa nasaha kuhusu toba na yatosha kumpa mtu shauku ya kukimbilia toba: Mwenye madhambi akumbuke yaliyoelezwa ndani ya aya tukufu na hadithi kuhusu maafa ya dhambi na madhara yake kimwili na kiroho katika uhai huu na kesho akhera na pia kuhusu onyo la Muumba la adhabu.

251


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:23 PM

Page 252

Tabia njema kwa mujibu wa Ahlul Bayt (a.s) Aweke mbele ya macho yake fadhila za toba na mema mazuri walioyafanya wenye kutubia na yale aliyowazawadia Mwenyezi Mungu (swt), wingi wa msamaha, wingi wa malipo na msaada wa juu na upole.

37. KUJIHESABU NA KUJICHUNGUZA MAANA KUJIHESABU Ni mtu kujihesabu kila siku kwa yale aliyoyafanya iwe ni ya uchaji na wema au ya madhambi na maovu. Ikiwa ya uchaji yatazidia ya maasi, na mema kuzidia ya uovu, basi mtu amshukuru Mwenyezi Mungu (swt) kwa hayo aliyomuwezesha na kumtukuza kwayo, kumtii na kupata radhi zake. Na ikiwa yatazidia maasi, ni juu yake kuiadibisha nafsi yake kwa kujutia na kukemea upotofu wake na kuacha kwake kumtii Mwenyezi Mungu (swt).

MAANA YA KUJICHUNGA Ni kuidhibiti nafsi na kuihifadhi isichupe mipaka kwa kuacha ya wajibu na kuvamia ya haramu. Ni awla kwa mwenye akili, anayetafuta nuru ya imani na yaqini, kuizoesha nafsi yake kujihesabu na kujichunga (kwani nafsi ni yenye kuamuru maovu). Ikiachiwa (kutoijali), basi inapotoka na kusombwa ndani ya maasi na matamanio na kumuangamiza mwenyewe. Ama pindi inapodhibitiwa kwa kuelekezwa na kuadibishwa, nafsi huchomoza kwa mema na kuchanua kwa matukufu na kumuinua mwenyewe kwenye furaha na fanaka.

252


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:23 PM

Page 253

Tabia njema kwa mujibu wa Ahlul Bayt (a.s) “Na kwa nafsi na kwa yule aliyeitengeneza. Kisha akaifahamisha uovu wake na wema wake. Bila shaka amefaulu aliyeitakasa. Na bila shaka amepata hasara mwenye kuitweza.” (Suratu Shams, 91: 7-10). Pamoja na hayo ni kwamba kujihesabu na kujichunga kuna umuhimu mkubwa sana katika kujiandaa kuikabili hesabu Siku ya Kiyama na vishindo vyake vinavyotisha na hivyo kuhisi umuhimu wa kujitayarishia matendo ya wema na kheri ambayo ndiyo sababu ya kuokoka na fanaka ya marejeo yake. Kwa sababu hizo, maandiko yametilia mkazo na kuhamasisha jambo hili kwa njia mbalimbali:

HADITHI Imam Sadiq (a) alisema: “Ikiwa mmoja wenu anataka kumuomba Mola Wake kitu na ampe, basi naakate matumaini na watu wote na asiwe na matumaini ila na Mwenyezi Mungu (swt). Pindi Mwenyezi Mungu (swt) atakapojua hilo, kuhusu mja wake, hataomba kitu ila atampa. Kwa hivyo zihesabuni nafsi zenu kabla hamjahesabiwa. Kiyama ina vituo (visimamo) hamsini. Kila kituo kina kusimama miaka elfu moja, kisha akasoma:

“Malaika na roho hupanda kwake katika siku ambayo muda wake ni miaka elfu hamsini.” (Suratul Ma’arij, 70:4). Imam Musa (a) alisema: “Sio miongoni mwetu yule asiyejihesabu kila siku. Ikiwa amefanya wema humuomba Mwenyezi Mungu (swt) amzidishie na ikiwa ametenda uovu, 253


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:23 PM

Page 254

Tabia njema kwa mujibu wa Ahlul Bayt (a.s) humuomba Mwenyezi Mungu (swt) msamaha na kutubia”. Imam Husayn (a): Mtu mmoja alimjia Mtume na kumtaka amuusie, Mtume baada ya kumtaka kufuata wasia wake, kwa kukariri mara tatu, alisema (s): “Mimi nakuusia pindi utakapoamua jambo basi tafakari mwisho wake, ikiwa ni mzuri, lifanye na ikiwa ni mbaya, liache”. Imam Sadiq (a) akimnasihi mtu mmoja alisema: “Hakika wewe umejaliwa kuwa ni tabibu wa nafsi yako, na umebainishiwa ugonjwa, umefahamishwa dalili ya siha na kuonyeshwa dawa. Sasa tazama vipi kipimo chako juu ya nafsi yako.” Imam Musa (a) alisema: “Imam Ali (a) alisema: Hakika Mtume (s) alituma jeshi (kwa ajili ya jihad) na pindi liliporejea akasema: Karibuni watu ambao mmetekeleza jihadi ndogo na imebakia juu yao jihadi kuu. Ikaulizwa: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu (s) ni ipi tena hiyo jihadi kuu? Akajibu: Jihadi dhidi ya nafsi iliyo ndani yako.”

NIDHAMU YA KUJIHESABU Wanamaadili (wanaoshughulika na elimu ya akhlaq) wameelezea utaratibu wa kujihesabu kwa upana, ama mimi nitaufupisha katika mambo mawili muhimu: La kwanza kabisa ambalo ni awla kuihesabu nafsi ni utekelezaji wa faradhi, mambo ambayo Mwenyezi Mungu (swt) ametuwekea ni kuwa ni wajibu, kama vile Sala, Saumu, kuhiji, Zaka na mfano wa hayo. Mja akiyatekeleza hayo kwa sura inayotakikana, ni kwamba amemshukuru Mwenyezi Mungu (swt) na kuipa nafsi yake matumaini katika yale ambayo Mwenyezi Mungu (swt) amewaahidi wanaomtii ikiwa ni thawabu nyingi na malipo makubwa.

254


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:23 PM

Page 255

Tabia njema kwa mujibu wa Ahlul Bayt (a.s) Na ikiwa atayapuuza na kushindwa kuyatekeleza, basi aiogopeshe nafsi yake kwa yale ambayo Mwenyezi Mungu (swt) amewakamia wale ambao ni waovu na wakaidi kwa adhabu kali, na hivyo ajitahidi katika kuyatekeleza na kuyasahihisha. kuihesabu nafsi katika kufanya madhambi na machafu kwa kuikemea kwa nguvu na kuijutisha kwa iliyoyafanya ya maovu kisha kujitahidi kurekebisha hayo kwa kujutia na toba ya kweli. Mtume (s) alitoa mfano wa juu kabisa kuhusu kuhesabu nafsi na kujitahadhari na madhambi madogodogo na yasiyotiliwa manani kama alivyosimulia Imam Ja’far Sadiq kwamba: “Mtume aliwasili katika ardhi isiyo na mimea akawambia masahaba wake: tuleteeni kuni. Wakajibu: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, sisi tupo hapa katika ardhi isiyo na mimea, kwa hiyo hakuna kuni hapa. Akawaamrisha: Kila mmoja naaje na chochote kile atakachoweza. Wakaja wakazimwaga mbele yake na hapo akasema: Hivi ndivyo dhambi zinavyojikusanya. Kisha akasema: Jitahadharini na madhambi yanayodharauliwa (kwa udogo wake), hakika kila kitu kina mwenye kukiuliza, na muulizaji wa madhambi hayo ameandika:

“Kwa hakika sisi tunawahuisha wafu, na tunayaandika waliyoyatanguliza na nyayo zao, na kila kitu tumekihifadhi katika daftari lenye kubainisha.” (Surat Yasin, 36:12). Miongoni mwa mawalii kuna walii alikuwa akihesabu nafsi yake kwa namna inayostaajabisha. Mfano ni huu uliyonukuliwa kuhusu Tawba bin Swammah ambaye alikuwa wakati mwingi – usiku na mchana - anahesabu 255


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:23 PM

Page 256

Tabia njema kwa mujibu wa Ahlul Bayt (a.s) nafsi yake. Siku moja akahesabu yaliyopita katika umri wake, akakuta ana umri wa miaka sitini. Akahesabu siku zake zilikuwa ni siku elfu ishirini na moja na mia tano. Akasema: Eee ole wangu! Nitakutana na Malik (malaika wa moto) nikiwa na dhambi elfu ishirini na moja! Kisha akapigwa na mshutuko na nafsi yake kutoka. Ni beti nzuri ilioje hii: Ikiwa mtu ataipa nafsi yake kila tamanio Na akawa hakuikataza basi itang’ang’ania kila batili

38. KUCHUKUA FURSA YA UMRI Lau kama mwanadamu angepima baina ya starehe zote za uhai huu na mapambo yake na umri wake angekuta ya kwamba umri ni ghali zaidi na wenye thamani zaidi, na kwamba hakuna chochote katika vile vya thamani katika uhai huu kinacholingana na umri wake. Sababu ni kuwa unaweza kupata vitu au kupata tena ulivyovipoteza, ama umri ni muda maalum ambao mwanadamu hawezi kamwe kuzidisha muda wake na kurefusha kiwango chake kilichokadiriwa.

“Na kila umati una muda, basi utakapowafikia muda wao hawatakawia hata saa moja wala hawatatangulia.” (Suratul A’raf, 7: 34) Pia ni muhali kurejesha yaliyokwisha pita katika umri hata kama mtu atatoa vyote katika milki ya uhai huu.

256


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:23 PM

Page 257

Tabia njema kwa mujibu wa Ahlul Bayt (a.s) Kwa kuwa mwanadamu ni mwingi wa kughafilika kuhusu thamani na utukufu wa umri, basi huupoteza kwa israfu bila kuzingatia umri uliyokwishakatika wala kuchukuwa fursa yake aliyopata. Kwa sababu hiyo, Ahlul Bayt (a) wametoa maelekezo kuweka wazi nafasi muhimu ya umri na dharura ya kuutumia katika yanayompa mwanadamu furaha na starehe katika uhai wake wa dunia na akhera. Katika wasia wake kwa Abu Dharr (r), bwana wa Mitume (s) alisema: “Ewe Abu Dharr, kwenye umri wako uwe ni mchoyo zaidi kuliko dirham zako na dinari” Imam Ali (a) alisema: “Hakika dunia ni siku tatu: siku iliyopita (imepita)na yake na wala haitorudi, siku ambayo umo hivi sasa, ni haki juu yako kupata faida yake, na siku hujui wewe ni miongoni mwa wenye siku hiyo, na huenda utaondoka ndani yake. Ama siku iliyopita (ni sawa) na mkufunzi mwenye hekima, ama siku ambayo umo ndani yake (ni sawa na ) rafiki anayeaga, na ama siku ya kesho, ni kwamba mikononi mwako huna ila matumaini.” Pia alisema: “Hakuna siku inayompitia mwanadamu isipokuwa inamuambia: mimi ni siku mpya, na mimi nishahidi juu yako, kwa hivyo sema na utende yaliyomema, mimi nitakushuhudia kwa hilo siku ya kiyama, nami kamwe hutaniona baada ya hapa.” Imesimuliwa kwamba mtu mmoja alikuja kwa Imam Ali Zainul-Abidin (a) akimlilia hali yake, hapo akasema: “Maskini mwanadamu, katika kila siku anamisiba mitatu na wala hazingatii mmojawapo! Na lau angezingatia basi ingekuwa kwake rahisi misiba na mambo ya dunia. Ama msiba wa kwanza: siku ambayo inapunguka katika umri wake. Akasema: akipata upungufu katika mali yake huhuzunika, wakati zama ndizo zenye kurithi mali hiyo na wala umri humrejeshei chochote. Ama wa pili: anataka kupata riziki yake yote, na huku ikiwa halali 257


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:23 PM

Page 258

Tabia njema kwa mujibu wa Ahlul Bayt (a.s) huhesabiwa na ikiwa haramu huadhibiwa. Ama wa tatu ni mkubwa zaidi. Akaulizwa: ni upi? Akajibu: hakuna siku ipitayo ila kakurubia akhera kwa hatua na huku hajui hatua peponi ama motoni. Na akasema: Siku ambayo mwanadamu ana umri mkubwa ni siku anayozaliwa.” Wanahekima walisema, hajasema yeyote maneno haya ya hekima kabla yake. Imam Sadiq (a) alisema: “Subirini kwenye kumtii Allah na subirini kwenye kutomuasi. Hakika dunia si chochote ila saa moja. Hayatakupatia furaha wala huzuni yaliyopita, ama yajayo huyajui, kwa hivyo subiri kwenye hiyo saa uliyomo, ni kama vile umekwisha fikia fanaka”. Imam Baqir (a) alisema: "Watu wasikupotoshe na nafsi yako, kwani amri itakusibu wewe siyo wao na usipitishe mchana wako kwa haya na yale (ya upuuzi) kwani pamoja nawe yuko anayehifadhi amali yako (malaika). Fanya wema, kwa sababu sijaona jambo bora zaidi ili kufuta dhambi na kwa haraka zaidi kama kufanya jambo jema" Imam Jaa’far Sadiq (a) alisema ya kwamba Mtume (s) alisema: “Fanya haraka kutumia (mambo) manne kabla ya manne, ujana wako kabla ya uzee, afya yako kabla ya ugonjwa, utajiri wako kabla ya ufakiri, na uhai wako kabla ya mauti.” Imam Baqir (a) alisema ya kwamba Mtume (s) alisema: “Siku ya Kiyama, hautopita mguu wa mja mbele ya Allah (swt) mpaka aulizwe kuhusu mambo manne: umri wako katika nini umeumalizia, kiwiliwili chako katika nini umekichakaza, mali yako wapi umeipata na wapi uliiweka, na pia kuhusu mapenzi yetu Ahlul Bayt”. Wamesema baadhi ya wanahekima: Hakika mwanadamu ni msafiri, na vituo vyake ni sita. Na amekwisha maliza vitatu, vinabaki vitatu; alivyokwisha safiri ni: 258


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:23 PM

Page 259

Tabia njema kwa mujibu wa Ahlul Bayt (a.s) 1. Ulimwengu kabla ya kutunga mimba yake, 2. Tumbo la mama yake, 3. Kutoka tumbo la mama yake na kuingia uwanja wa dunia Ama vituo ambavyo hajasafiri ni: 1. Kaburi, 2. Uwanja wa mahshar (kufufuliwa), 3. Pepo na moto Sisi hivi sasa tumo katika kituo cha tatu, na muda wa kusafiri ni umri wetu. Masiku yetu ni farsakh (1farsakh = 5.5km), na masaa yetu ni maili na pumzi zetu ni hatua. Miongoni mwetu yuko ambaye kabakiza mafarsakh, na mwingine maili na mwingine hatua. Ni maneno mazuri yaliyoje ya mshairi, Mapigo ya moyo wa mwanadamu yanamuambia Hakika uhai ni dakika na sekunde

AMALI NJEMA Umeelewa katika mazungumzo yaliyotangulia thamani ya muda na utukufu wa umri na kwamba ndiyo hazina kubwa na ghali ya uhai. Kwa kuwa muda ndivyo ulivyo, ni wajibu kwa mwenye akili kuutumia ipasavyo ikiwa ni katika mambo mema na malengo makubwa, mambo ambayo ndiyo sababu ya fanaka na furaha kimwili na kiroho, duniani na akhera, kama alivyosema Bwana wa mitume (s): “Haifai kwa mwenye akili kutilia maanani ila mambo matatu: kutengeneza maisha bora, kujiandaa (kwa kuchuma mema) kwa ajili ya uhai wa kesho, au starehe kwa yasiyo haramu�. Haya ndiyo malengo ya juu na shabaha tukufu ambayo kwa kweli inafaa kupitisha umri wako katika kuyafikia. 259


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:23 PM

Page 260

Tabia njema kwa mujibu wa Ahlul Bayt (a.s) Na kwa kuwa mwanadamu anasukumwa kimaumbile kutafuta maisha na kupata starehe za kimada, kwa mbinde zote, amekuwa ni mwenye kasoro katika kufanya matendo mema na kujiandaa kwa ajili ya maisha ya kesho akhera. Kwa sababu hiyo ndiyo maana aya na hadithi zimetilia sana mkazo kuhusu maisha ya akhera na kujiandaa kwayo kwa matendo mema. Mwenyezi Mungu (swt) anasema:

“Afanyaye mema mwanamume au mwanamke hali yakuwa ni Muumini basi tutamhuisha maisha mema, na bila shaka tutawapa malipo yao kwa sababu ya matendo bora waliyokuwa wakitenda.” (Suratu Nahl, 16:97)

“Afanyaye ubaya hatalipwa ila sawa na hayo, na afanyaye wema, akiwa mwanamume au mwanamke naye ni Muumini, basi hao wataingia Peponi, wataruzukiwa humo bila ya hesabu.” (Suratu Ghafir, 40:40),

“Mwenye kutenda wema basi ni kwa ajili ya nafsi yake, na mwenye 260


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:23 PM

Page 261

Tabia njema kwa mujibu wa Ahlul Bayt (a.s) kufanya uovu ni juu yake, kisha mtarudishwa kwa Mola wenu.” (Suratu Jathiyah, 45:15)

“Basi anayefanya wema sawa na chembe atauona.” “Na anayefanya uovu sawa na chembe atauona.” (Suratu Zilzaalah, 99:7-8) Mtume (s) alisema: “Ewe Abu Dharr, hakika wewe umo katika mpito wa usiku na mchana, katika mustakbali unaopunguzwa, na vitendo vinavyohifadhiwa na mauti ambayo yatakuja ghafla. Anayepanda kheri karibuni atavuna kheri, na anayepanda shari karibuni atavuna majuto, na kila mkulima huvuna mfano wa kile akipandacho.” Qays bin ‘Aswim alisema: nilifuatana na ujumbe miongoni mwa Bani Tamim kwa bwana Mtume (s), na nikaomba: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu (s) tupe mawaidha ambayo tutanufaika nayo. Mtume (s) akasema: “Ewe Qays pamoja na utukufu kuna udhalili, pamoja na uhai kuna mauti, pamoja na dunia kuna akhera na hakika kila kitu kina mhasibu, na juu ya kila kitu mwangalizi, na hakika kila jema lina thawabu, na kila ovu lina adhabu, na kila ajali (mauti) ina muda uliyowekwa. Ewe Qays, hakuna budi lazima uwe na rafiki utakayezikwa naye na huku yuko hai, na atazikwa nawe na huku wewe ni maiti, ikiwa atakuwa ni mtukufu basi atakutukuza na akiwa muovu atakusaliti, kisha hatofufuliwa ila na wewe, nawe hutofufuliwa ila pamoja naye, na hautaulizwa ila kuhusu yeye, kwa hiyo usimfanye ila kuwa mwema, akiwa mwema utafarijika naye, na ikiwa atakuwa muovu hutochukizwa ila naye, huyo ni amali yako.

261


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:23 PM

Page 262

Tabia njema kwa mujibu wa Ahlul Bayt (a.s) Imam Ali (a) alisema: “Mja pindi anapokuwa katika siku ya mwisho katika siku za dunia na siku ya kwanza katika siku za akhera, hufanyiwa mfano wa mali yake, watoto wake, na amali yake. Hapo huigeukia mali yake na kusema: Wallahi nilikuwa mroho na mchoyo juu yako, sasa kwako nina nini? Mali itamjibu: Chukuwa kwangu kafani yako. Atawageukia watoto wake na kuwaambia: Wallahi nilikuwa nawapenda na nilikuwa nawalinda, sasa nina nini kwenu? Watoto watamjibu: Tutakufikisha hadi kaburini kwako na kukusitiri ndani yake. Kisha atageikia amali yake na kusema: Wallahi kwako nilikuwa mchache wa kutenda na ulikuwa juu yangu mzito, leo kwako nina nini? Amali yake itamjibu: Ama mimi ni sahiba wako katika kaburi yako na siku ya kufufuliwa kwako mpaka nitakapoletwa mimi na wewe mbele ya Mola Wako”. Ikiwa alikuwa mja mwema wa Mwenyezi Mungu (swt), atamjia mtu mwenye harufu nzuri sana mwenye mandhari nzuri sana na mavazi maridadi na atamuambia: Uwe na bishara njema ya starehe, furaha na pepo ya neema, na unapokuja ni mahala bora. Atamuuliza: Kwani wewe nani? Atamjibu: Mimi ni amali yako njema, acha dunia nenda peponi…” Imam Sadiq (a) alisema: “Pindi anapowekwa maiti ndani ya kaburi yake hufanyiwa mfano wa mtu na humwambia: Eee wewe, tulikuwa watatu; ilikuwepo riziki yako nayo imekatika kwa kufika ajali yako, walikuwepo ahli zako nao wamekuacha na kuondoka, na nilikuwepo mimi amali yako na nimebaki nawe pamoja na kwamba nilikuwa sina thamani kwako”. Pia alisema (a): Mtume (s) alisema: “Yule atakayefanya wema katika umri wake uliyobakia, basi hatochukuliwa kwa yale yaliyopita katika madhambi yake, na atakayefanya uovu katika umri wake uliyobakia, basi atachukuliwa kwa ya mwanzo na ya mwisho”.

262


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:23 PM

Page 263

Tabia njema kwa mujibu wa Ahlul Bayt (a.s) Vyema kanena mshairi huyu aliposema: Walimwengu, shauku yao ni uhai na wala sioni Ya kwamba uhai mrefu wazidisha ila alinacha Na utakapohitajia hazina Kamwe hutopata hazina kama matendo mema

KUMTII NA KUMCHA MWENYEZI MUNGU Mwanadamu, miongoni mwa viumbe vingine ni kiumbe bora kwa mengi matukufu aliyokirimiwa na Mola wake tofauti na viumbe vingine. Mwenyezi Mungu (swt) anasema:

“Na hakika tumewatukuza wanadamu na tumewabeba nchi kavu na baharini, na tumewaruzuku katika vitu vizuri na tumewatukuza kuliko wengi wa wale tuliowaumba, kwa utukufu mkubwa.� (Suratul Israa; 17:70). Katika dalili zilizo wazi za mwanadamu kutukuzwa na kupewa kipaumbele ni kule kuteuliwa kuwa khalifa ndani ya ardhi na kuteuliwa miongoni mwao mitume na manabii ambao walitumwa na sheria na taratibu zakunadhimu maisha yao na hivyo kupata fanaka duniani na akhera. Lakini kwa bahati mbaya wanadamu wengi wametawaliwa na anasa na matamanio ya nafsi zao na hivyo kuzidiwa na nguvu za uasi dhidi ya taratibu za Mwenyezi Mungu (swt) na sheria Zake. Matokeo yake ni kutangatanga katika jangwa la uasi na kuporomoka kati263


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:23 PM

Page 264

Tabia njema kwa mujibu wa Ahlul Bayt (a.s) ka njia za upotofu na huko kuteseka kwa mapigo ya kutahayari, wasiwasi na kukosa furaha. Na laiti kama wangeitikia mwito wa kumtii Mwenyezi Mungu (swt) na kwenda kwa mwongozo wa taratibu na nidhamu Yake, basi wangepata fanaka na wangepata kufuzu kukubwa.

“Na kama watu wa miji wangeamini na kumcha (Mwenyezi Mungu ) lazima tungeliwafungulia baraka za mbingu na ardhi, lakini walikadhibisha tukawaangamiza kwa sababu ya yale waliyokuwa wakiyachuma.� (Suratul Aaraaf, 7:96) Je umeona jinsi ulimwengu ulivyo na nidhamu, sehemu zake zimepangika na nidhamu imetulia kwa mamilioni ya vizazi na miaka?! Hii kwa kumtii na kumyenyekea Mwenyezi Mungu (swt) na kwenda kwa mahitaji ya sharia zake na kanuni! Je umeona jinsi ulivyochanua uhai wa viumbe hai na kusimama imara kwa kufuata matakwa yake Mwenyezi Mungu (swt) na hikma ya nidhamu, upangaji na uendeshaji wake?! Je umeona jinsi watu wanavyotekeleza ushauri na maelekezo ya wagunduzi wa vifaa vya kazi (mashine za kazi) ili kuhakikisha usalama na utumiaji bora?! Je umeona jinsi watu wanavyofuata nasaha na maelekezo ya matabibu na kustahamili matatizo ya matibabu na ugumu wa kuchunga utaratibu wa chakula (diet) almuradi aweze kupona?! Sasa ni kwa nini mwanadamu asimtii muumba wake mtukufu, na mwendeshaji wake mwenye hekima, ambaye anajua yake ya ndani na siri, yanay264


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:23 PM

Page 265

Tabia njema kwa mujibu wa Ahlul Bayt (a.s) ofaa na yanayomdhuru?! Ni muhali kwa mwanadamu kapata anayoyatamani kwa dhati yakiwa ni fanaka, amani, utulivu na starehe ila kwa kumtii Mola Wake na kufuata sheria na kanuni zake. Tazama jinsi Mwenyezi Mungu (swt) anavyowahamasisha waja wake kwenye utiifu na kumcha na kuwatahadharisha athari mbaya za uasi, na Yeye ni Asiyemuhitaji wa chochote. Anasema:

“Wamelaaniwa popote waonekanapo wakamatwe na wauawe kabisa.” (Suratul Ahzab, 33:61)

“Kipofu hana lawama, wala kilema hana lawama, wala mgonjwa hana lawama (wasipokwenda vitani). Na anayemtii Mwenyezi Mungu na Mtume Wake atamuingiza katika mabustani yapitayo mito chini yake, na atakayegeuka atamuadhibu adhabu iumizayo.” (Suratul Fath, 48:17) Ama kuhusu taqwa, kheri ya dunia na akhera imeshikilia hapo. Hizi ni baadhi ya aya: 1. Mahaba ya Mwenyezi Mungu (swt). Anasema (swt):

265


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:23 PM

Page 266

Tabia njema kwa mujibu wa Ahlul Bayt (a.s)

“Isipokuwa wale mlioahidiana nao miongoni mwa washirikina kisha hawakumsaidia yeyote dhidi yenu, basi watimizieni ahadi yao mpaka muda wao, hakika Mwenyezi anawapenda wanaomuogopa.” (Suratut Tawbah, 9:4) 2. Kuokoka na matatizo na kuweka sababu ya riziki. Anasema (swt):

“Kwa neema ya Mola Wako wewe si mwendawazimu. Na kwa hakika una malipo yasiyokatika.” (Suratut Qalam, 68: 2-3) 3. Ushindi na msaada. Anasema (swt):

“Kwa hakika Mwenyezi Mungu yu pamoja na wale wanaomcha, na wale wenye kufanya wema.” (Suratun Nahl, 16:128) 4. Kutengeka matendo na kukubaliwa.

“Enyi mlioamini! muogopeni Mwenyezi Mungu na semeni maneno ya 266


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:23 PM

Page 267

Tabia njema kwa mujibu wa Ahlul Bayt (a.s) sawa. Atakutengenezeeni vizuri vitendo vyenu na atakusameheni madhambi yenu, na anayemtii Mwenyezi Mungu na Mtume Wake bila shaka amefaulu kufaulu kukubwa.” (Suratul Ahzab, 33:70-71) 5. Bishara njema wakati wa mauti.

“(Hao ndio) ambao wameamini na wakawa wanamcha Mwenyezi Mungu. Wao wana bishara njema katika maisha ya dunia na katika Akhera. Hakuna mabadiliko katika maneno ya Mwenyezi Mungu. Huko ndiko kufuzu kukubwa.’ (Suratu Yunus, 10:63-64) 6. Kuokoka na moto.

“Kisha tutawaokoa wale wamchao (Mungu) na tutawaacha wale madhalimu humo wamepiga magoti.” (Suratu Maryam,19:72) 7. Kubaki peponi milele.

“Na harakieni kuomba msamaha kwa Mola Wenu na Pepo ambayo upana wake ni mbingu na nchi iliyoandaliwa kwa wenye kumcha Mwenyeezi Mungu.” (Suratu Aali Imraan, 3:133) 267


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:23 PM

Page 268

Tabia njema kwa mujibu wa Ahlul Bayt (a.s) Inadhihiri wazi katika yaliyotajwa hapo juu ya kwamba taqwa ndiyo hazina kuu inayokusanya matarajio na matumaini mbalimbali ya kimada na kiroho, kidunia na kiakhera.

HAKIKA YA UTIIFU NA UCHAMUNGU Utiifu: Ni kunyenyekea kwa Mwenyezi Mungu (awj) na kutekeleza amri Zake na makatazo Yake. Taqwa: Asili yake kujikinga, kwa maana ni kuihifadhi nafsi na yale yanayoidhuru kesho akhera, na kuidhibiti kufanya yanayoinufaisha huko akhera. Hivi ndivyo hadithi mutawatir za Ahlul Bayt (a) zilivyosisitiza na kuvutia kwenye kumtii Mwenyezi Mungu (awj) na kumcha na pia kutahadharisha kumuasi na kumhalifu. Imam Hasan (a) alisema katika mawaidha yake mashuhuri kwa Junada: “Tumika kwa ajili ya dunia yako kama vile utaishi milele na tumika kwa ajili ya akhera yako kama vile utakufa kesho. Ikiwa unataka utukufu bila ya ndugu, na haiba bila ya utawala, basi toka kwenye udhalili wa kumwasi Mwenyezi Mungu (awj) na ingia katika utukufu wa kumtii Mwenyezi Mungu (awj)”. Imam Sadiq (a): “Muwe na subira kwenye kumtii Mwenyezi Mungu (awj), na mjisubirishe kutomuasi Mwenyezi Mungu (awj), hakika dunia ni saa moja, yaliyotangulia hayatakupa furaha wala huzuni, na ambayo hayajafika huyajui, kwa hivyo subiri kwenye hiyo saa ambayo umo ndani yake, ni kama utakuwa umefurahi”.

268


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:23 PM

Page 269

Tabia njema kwa mujibu wa Ahlul Bayt (a.s) Pia akasema: “Itakapokuwa Siku ya Kiyama litasimama kundi la watu na kuelekea lango la pepo na kubisha hodi. Wataulizwa: Nani nyinyi? Watajibu: Sisi ndiyo watu wa subira. Wataulizwa: Kwenye nini mmesubiri? Watajibu: Tulikuwa tukisubiri kwenye kumtii Mwenyezi Mungu (awj) na kusubiri kwenye kutomuasi Mwenyezi Mungu (awj). Mwenyezi Mungu (awj) atasema: Wamenena kweli, waingizeni peponi, na hiyo ndiyo kauli ya Mwenyezi Mungu (awj) isemayo: “... bila shaka wanaofanya subira watapewa malipo yao pasi na hesabu.”(Suratu Zumar, 39:10) Imam Baqir (a) alisema: “Ukitaka kujua kwamba ndani yako mna kheri, basi tazama moyo wako; ikiwa unapenda watu wachamungu na kuchukia watu waovu, (hiyo ni dalili ya kwamba) ndani yako mna kheri, na Mwenyezi Mungu (awj) anakupenda. Na ama ikiwa unachukia watu wachamungu na kupenda watu waovu, basi ndani yako hamna kheri na Mwenyezi Mungu (awj) anakubughudhi. Mtu yu pamoja na yule ampendaye”. Pia alisema (a): “Kamwe hajamjua Mwenyezi Mungu (swt) yule anayemuasi”, kisha akasema beti hizi: Unamuasi Mwenyezi Mungu na huku unadhihirisha mapenzi yake! Hili naapa kwa uhai wako ni jambo la kustaajabisha! Kama penzi lako lingekuwa la dhati, basi ungemtii Hakika mwenye kupenda ni mtiifu kwa yule ampendaye. Hasan bin Musa al-Washaa al-Baghdady alisema: Nilikuwa Khurasan pamoja na Imam Ali bin Musa ar Ridhwa (a) katika majlisi yake. Zaid bin Musa (ndugu yake) alikuwepo, na huku akijifaharisha juu ya watu waliokuwepo akisema sisi, sisi…Abul Hasan (a) (Imam Ridhwa) alipomsikia alimgeukia na kumuambia: Ewe Zayd! Hivi yamekudanganya maneno ya wauza mboga wa Kufa ya kwamba Fatima (a) alihifadhi tupu 269


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:23 PM

Page 270

Tabia njema kwa mujibu wa Ahlul Bayt (a.s) yake kwa hivyo Mwenyezi Mungu (swt) akaharamisha kizazi chake kuingia motoni! Basi hilo siyo ila kwa Hasani (a) na Husayn (a) na kizazi cha tumbo lake makhsusi. Ama vipi itakuwa Musa bin Ja’far (a) anamtii Mwenyezi Mungu (swt), anafunga mchana na kusimama usiku na wewe unamuasi kisha mje nyote ni sawa siku ya kiyama? Hivi wewe ni azizi zaidi kuliko yeye kwa Mwenyezi Mungu (swt)! Ali bin Husayn (a) alikuwa akisema: “Kwa mtenda mema miongoni mwetu ana ujira mara mbili, na kwa muovu miongoni mwetu, ana adhabu mara mbili”. Kisha (Imam) akanigeukia (Hasan bin al-Washaa) na akasema: Ewe Hasan, ni vipi mnavyosoma hii aya ya Suratul Huud, (11:46) inayomhusu mwanaye Nabi Nuh (a) na kukanwa na Mwenyezi Mungu. Nikasema: Wako watu wanaosoma (amila ghaira swalihin, kwa maana hakutenda mema) na wengine (amalun ghairu swalihin, kwa maana mwanaharamu) na hivyo akamkana kutoka kwa baba yake. Imam akasema: “Sivyo, huyo mtoto alikuwa mwanaye halisi, lakini alipomuasi Mwenyezi Mungu (swt), akamkana kutoka kwa baba yake. Hivyo ndivyo ilivyo na kwetu, yule aliye miongoni mwetu kisha asimtii Mwenyezi Mungu (swt), basi yeye si miongoni mwetu, na wewe ikiwa utamtii Mwenyezi Mungu (swt), basi utakuwa ni miongoni mwetu Ahlul Bayt (s)”. Imam Baqir (a) alisema: Mtume alisimama kwenye Saffaa na kusema: “Enyi Bani Hashim, enyi Bani Abdul Muttwalib, mimi ni mtume wa Mwenyezi Mungu (swt) kwenu, na mimi ni mwenye huruma juu yenu, nami nina amali yangu, nanyi kila mtu ana amali yake. Kwa hiyo msijesema Muhammad ni miongoni mwetu kwa hiyo tutaingia anapoingia. Hasha Wallahi! mawalii (rafiki, mpenzi, msaidizi…) wangu ni wale tu wachamungu na siyo miongoni mwenu wala wengine. Ole wenu nisije wafahamu Siku ya Kiyama mnakuja mmebeba dunia juu ya migongo yenu na huku wanakuja watu wamebeba akhera, mtanabahi kwani nimekwisha toa udhuru kwenu kwa yale yaliyo baina yangu na nyinyi, pia baina yangu 270


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:23 PM

Page 271

Tabia njema kwa mujibu wa Ahlul Bayt (a.s) na Mwenyezi Mungu (swt) kuhusu nyinyi”. Imam Baqir (a) kama ilivyopokewa na Jabir, alisema: “Ewe Jabir, hivi unafikiri ya kwamba inatosha kwa wenye kusema kwamba wao ni mashia kudai mahaba yetu sisi Ahlul Bayt (a)?! Wallahi, mashia wetu ni wale wamchao Mwenyezi Mungu (swt) na kumtii - mpaka akasema: Muogopeni Mwenyezi Mungu (swt) na fanyeni matendo yenu kwa kutaraji yaliyoko kwa Mwenyezi Mungu (swt). Hakuna baina ya Mwenyezi Mungu (swt) na yeyote kati yenu undugu, mja apendwaye zaidi kwa Mwenyezi Mungu (swt) na mtukufu zaidi ni yule mchamungu zaidi miongoni mwenu, na mtendaji zaidi kwa kumtii. Ewe Jabir, Wallahi hakurubiwi Mwenyezi Mungu (swt) ila kwa utiifu. Mimi sina uwezo wa kumuweka mtu kando na moto na wala hakuna yeyote mwenye hoja juu ya Mwenyezi Mungu (swt). Kwa yule yeyote atakayekuwa ni mtiifi kwa Mwenyezi Mungu (swt), basi ni wallii (mfuasi, mpenzi, mtetezi, sahiba…) wetu na atakayekuwa ni muasi kwa Mwenyezi Mungu (swt), basi yeye ni adui yetu, kwa hivyo yeyote yule hapati wilaya (mapenzi, ulinzi, ubwana,…) yetu ila kwa matendo na kumuogopa Mwenyezi Mungu (swt) ”. Mufaddhal bin Umar alisimulia: Nilikuwa pamoja na Imam Sadiq (a) na tukakumbuka matendo. Mimi nikasema: Ni dhaifu iliyoje amali yangu? Imam akasema: “Acha kusema hivyo! Muombe Mwenyezi Mungu (swt) msamaha. Kisha akasema: Hakika amali ndogo pamoja na uchamungu ni bora kuliko nyingi isiyo na uchamungu. Nikauliza ni vipi itakuwa nyingi bila ya uchamungu? Akajibu: Naam, mfano mtu analisha (maskini), mpole kwa jirani zake, mkarimu kwa wageni, lakini ukifunguka mbele yake mlango wa haramu huingia mara moja, hii ndiyo amali bila ya uchamungu. Ama mwingine yeye hana kitu, lakini unapofunguka mlango wa haramu kamwe haingii ndani yake”.

271


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:23 PM

Page 272

Tabia njema kwa mujibu wa Ahlul Bayt (a.s) Mshairi anasema: Kamwe jambazi njiani siyo shujaa Bali shujaa ni yule mchamungu Mche Mwenyezi Mungu kwa sababu Hufaulu mwenye moyo uliyo pamoja na uchamungu

39. KUWA NA MSIMAMO IMARA (KATIKA KUTEKELEZA KANUNI) Nidhamu na kanuni zina umuhimu wa juu kabisa na athari kubwa katika uhai wa mataifa na watu. Hayo ndiyo chanzo cha maendeleo na mwelekeo katika ummah na kigezo cha kuendelea au kurudi nyuma. Kwa hiyo pindi ambapo kanuni na nidhamu za ummah zinapokwenda juu hiyo ni dalili ya ustaarabu na maendeleo. Na pindi zinapoporomoka hiyo ni dalili ya ujinga na kubaki nyuma. Na kanuni zilizo bora na zenye utukufu zaidi ni zile zinazoratibu uhai wa mwanadamu - mmoja au jamii - na kuhifadhi uhuru wake na utukufu wake na kumhakikishia amani yake na raha na kumuwekea njia za kufikia furaha na amani dunia na akhera. Ni wazi kwamba kanuni hata kama zitakuwa nzuri na tukufu, kamwe hazitaweza kuhakiki matarajio ya ummah na kuupa kheri inayotarajiwa, ila ikiwa ummah utakumbatia kanuni hizo na kupigania kuzilinda na kuzitekeleza katika nyanja mbalimbali za uhai. Ni kwa sababu hiyo ndiyo ikawa msimamo kwenye msingi wa haki ni katika wajibu wa ummah ulio mtakatifu, kwani ni huo msimamo ndio huuwezesha kufikia malengo yake.

272


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:23 PM

Page 273

Tabia njema kwa mujibu wa Ahlul Bayt (a.s) Ubinadamu katika historia yake ndefu, haujawahi kupata kanuni kamili na bora kama zile za uislamu. Ni kanuni zilizochukua mambo yote na matukufu yaliyozifanya kuwa za milele na kuziweka juu ya kila sheria. Hizo ndizo kanuni pekee ambazo zinavaana vyema na maumbile ya mwanadamu, na kuweka uwiano baina ya misingi ya kiroho na kimada na kuwahakikishia wafuasi wake furaha duniani na akhera. Kwa kuelezea kuhusu utukufu wake natuangalie jinsi kanuni za kiislamu zilivyoweza - kwa muda mchache usiozidi robo karne – kuhakiki ushindi wa imani na miujiza ya mageuzi na kuongoa, jambo ambalo sheria zingine hazikuweza kufanya. Ziliweza kuubadilisha ummah wa kiarabu uliozama katika ujahiliyyah na kuwa ummah bora uliosimamishwa kwa ajili ya watu kiutamaduni, kifahari, kielimu, na kitabia. Waislamu wa mwanzo hawakuhodhi utukufu na kuwa bila na kifani kiutamaduni na kielimu ila kwa sababu ya kuwa na msimamo kwenye kanuni zao za milele na kujitolea kuzihami kwa hali na mali. Ama msiba uliowasibu Waislamu leo, na kupigwa mikwaju ya maafa isiyokoma, sababu ni kukengeuka na kuitupa misingi yao. Tazama jinsi Qur’ani tukufu inavyowasifu Waislamu wenye msimamo kwenye kanuni zao tukufu na wenye kushikamana na misingi mitakatifu ya imani: Hakika wale wanaosema: Mola Wetu ni Mwenyezi Mungu, kisha wakawa na msimamo thabiti (kwenye haki), basi malaika huwateremkia (wakiwaambia): Msihofu wala msihuzunike, na furahieni Pepo mliyokuwa mkiahidiwa.

273


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:23 PM

Page 274

Tabia njema kwa mujibu wa Ahlul Bayt (a.s)

“Sisi ni Walinzi wenu katika maisha ya dunia na katika Akhera, na humo mtapata mtakavyoviomba. Ni takrima itokayo kwa Mwingi wa kusamehe, Mwenye kurehemu.” (Surat Fuswilat, 41:31-32). Mtume Mtukufu (s) na Ahlul Bayt wake walikuwa ni mfano wa juu katika kuwa na msimamo wa kuhami dini na kujitoa muhanga na kila kilicho ghali. Mtume (s) alikuwa kila pindi ambapo giza la kimbunga cha matatizo linapotanda na nguvu za ukafiri na udhalimu zinaposhikamana dhidi yake, basi huzidi uthabiti na kuendelea kutangaza ujumbe wake. Na mfano usio na mithili ni kauli yake (s): “Lau kama wangeweka jua ndani ya mkono wangu wa kulia na mwezi katika mkono wangu wa kushoto, kamwe nisingeacha jambo hili hadi pale atakapolidhihirisha Mwenyezi Mungu (swt) au nikaangamia nikilipigania”. Kwa uthabiti huu kama jabali, nguvu zote za shirk zilinywea na kujisalimisha mbele ya Mtume (s). Imam Ali (a), kama vile alivyokuwa Mtume (s), pindi alipopewa ukhalifa kwa sharti afuate kitabu cha Mwenyezi Mungu, Sunna ya Mtume (s) na mwenendo wa makhalifa wawili (Abubakr na Umar), alikataa na kushikilia msimamo wake na rai sahihi kwa kusema: “Bali nitafuata kitabu cha Mwenyezi Mungu (swt), Sunna ya Mtume (s) na ijtihadi ya rai yangu”. Pia baadhi katika watu wa karibu yake walimshauri awavute wale ambao kwa sababu ya tamaa – wamekataa uadilifu wake ( imam Ali ) na kukimbilia takrima ya Muawiya, kwa kuwapa mali na kuwafadhilisha mabwana katika waarabu na maquraishi juu ya wasio waarabu na kila ambaye inahofiwa kumkimbilia Muawiya. Hapo, akithibitisha msimamo wake 274


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:23 PM

Page 275

Tabia njema kwa mujibu wa Ahlul Bayt (a.s) usiotetereka na kushikamana kwake na katiba ya Uislamu na kwamba yuko mbali na njia mbaya za unyonyaji kwa kuwajibu: “Ni vipi mnaniamrisha nitafute ushindi kwa udhalimu?! Kamwe Wallahi sitofanya hilo maadamu jua linachomoza na nyota kung’ara mbinguni. Wallahi, hata kama mali yao ingekuwa ni yangu, basi ningeigawa kwa usawa baina yao, sasa nifanyeje wakati mali ni yao (na sio yangu)?” Mfano mwema kama huo waliuiga wateule miongoni mwa wafuasi wa Imam. Pamoja na kukabiliwa na kila aina ya mateso, vitisho na adhabu, walikuwa ni mfano wa pekee katika swala la kuwa na msimamo na kuthibiti kwenye haki na kuitetea. Vitabu vya sira vimepambwa na matendo yao ya fahari na kumbukumbu njema, mambo ambayo yameweza kubakisha milele athari zao kwa kila zama na kizazi. Hii ni baadhi ya mifano: Hajjaj bin Yusuf Thaqafi alisema siku moja: Nataka kumnasa mmoja katika masahaba wa Abu Turab (Imam Ali) nijikurubishe kwa Mwenyezi Mungu (swt) kwa damu yake. Akaambiwa: Hatujui yeyote aliyekuwa na usuhuba naye kwa muda mrefu kama Qambar mtumishi wake. Akatuma akatafutwe, na alipoletwa akamuambia: Wewe ndiye Qambar? Akajibu: Naam. Akamuambia: Abu Hamdaan? Akajibu: Naam. Akamuambia: Ali alikuwa bwana wako? Akajibu: Mwenyezi Mungu (swt) ndiye bwana wangu na Ali ni bwana wa neema yangu (aliyenineemesha). Akamuambia: Ikane dini yake. Akamjibu: Nikiikana dini yake utanionesha dini bora isiyo hiyo? Akamwambia: Nitakuuwa, kwa hiyo chagua kifo kizuri kwako. Akamjibu: Hilo nimekuachia, chagua. Akasema: Kwa nini? Akamjibu: Kwa sababu wewe hivyo utakavyoniuwa, nami nitakuuwa mfano wake, na bwana wangu Amiri wa waumini alinitabiria ya kwamba kifo changu kitakuwa kuchinjwa kwa dhulma pasi na haki. Hajjaj akatoa amri na Qambar akachinjwa. Imesimuliwa ya kwamba siku moja Muawiya alimtumia Abu Aswad adDually zawadi na vitamutamu akilenga kumvutia kwake na kumtaka aachane na kumpenda Imam Ali (a). Punde akaingia binti yake mdogo na 275


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:23 PM

Page 276

Tabia njema kwa mujibu wa Ahlul Bayt (a.s) kumega tonge ya vitamutamu na kuiweka mdomoni. Abu Aswad akamuambia: Ewe binti yangu tema kwani hiyo ni sumu. Vitamu hivi katutumia Muawiya ili kutughilibu tuachane na mapenzi ya Imam Ali na Ahlul Bayt (a). Binti huyo mdogo akasema: Mwenyezi Mungu auharibu uso wake, anatughilibu kuachana na bwana aliyetoharika kwa kutupa vitamu vilivyowekwa zafarani! Ole wake kwa mtumaji na mlaji. Basi akajitapisha na kusema: Hivi wewe mtoto wa Hindi ni kwa vitamu vilivyowekwa zafarani Wataraji tukuuzie yetu matukufu na dini!? Mwenyezi Mungu atulinde, vipi litakuwa hili, Na ihali ya kuwa bwana wetu ni Amiri wa waumini (Imam Ali)? Rashid al-Hajary alikuwa ni miongoni mwa masahaba wa karibu wa Imam Ali (a). Aliletwa mbele ya Ziyad (l.a.) na kumuambia: Mpenzi wako alikuambia kwamba tutakufanya nini? Akajibu: Mtanikata mkono wangu na mguu wangu na kisha mtanisulubu. Ziyad akasema: Wallahi nitakadhibisha maneno yake. Muachieni! Alipotaka kutoka akasema: Mrudisheni, hatuoni chochote kinachokufaa zaidi kama alichosema sahiba wako (Imam Ali), kwani hutaacha uovu wako ukibaki hai. Mkateni mikono yake na miguu yake na huku akizungumza. Akasema: Msulubuni kwa kumyonga. Natusikilize maneno ya masahaba wa Imam Ali (a) ya kubaki milele ambayo yanadhihirisha mapenzi yao ya dhati kwa Imam na kuthibiti kwao kwenye kumfuata na kujitolea kwa hali na mali katika njia yake: Amr bin al Humuq anamuambia Imam Ali (a) anasema: “Wallahi ewe Amiri wa waumini, mimi sijakupenda wala kukupa kiapo cha utii kwa sababu za kiundugu (hakuna undugu baina yetu) wala kwa kutamani mali, wala kutaka utawala utakaonitukuza, lakini nimekupenda kwa sababu ya mambo matano: Wewe ni mtoto wa ami yake Mtume, na wa kwanza uliyemuamini, na pia ni mume wa bibi wa wanawake wa ummah Fatima binti Muhammad, pia 276


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:23 PM

Page 277

Tabia njema kwa mujibu wa Ahlul Bayt (a.s) ni wasii wake, pia ni baba wa kizazi kilichobakia kwetu kutoka kwa Mtume (s), pia ni wewe uliyowatangulia watu katika Uislamu, na miongoni mwa muhajirina hakuna mwenye jihadi kama yako. Laiti kama ningekalifishwa kuchukua milima mirefu na kuchota mabahari yaliyojaa ili niweze kumpa nguvu akupendaye na kumdhili adui yako, kamwe nisingeona kwamba nimetimiza kila wajibu ulio juu yangu kuhusu haki yako. Imam Ali (a) akasema: “Ewe Mwenyezi Mungu (swt) unawirishe moyo wake kwa uchamungu na umuongoze njia iliyonyooka. Laiti ndani ya jeshi langu pangekuweko mia kama wewe.” Hujr akasema: Wallahi ingekuwa hivyo basi jeshi lako lingekuwa zuri na wachache miongoni mwao wangekudanganya. Imesimuliwa ya kwamba Imam Ali (a) alimwambia Hujr bin ‘Aady atTwaaiy: Vipi hali yako ikiwa utaitwa kunikana, na huenda ukasema nini? Akajibu: Wallahi ewe Amiri wa waumini lau nikatwe kwa panga kipande kipande, na ukokwe moto kisha nitupwe ndani yake basi nitakubali hayo kuliko kukukana. Imam akamwambia: “Ewe Hujr umewafikishwa na kila kheri, Mwenyezi Mungu (swt) akujaze kheri kutoka kwa Ahlul Bayt wa nabii wako.” Hisham al-Mirqaal akiwa anaongoza upande wa kushoto (wa jeshi) la Imam Ali hapo Siffin alisema: Wallahi sitaki yote yaliyokuwepo juu ya ardhi na iliyoyabeba, na yote yaliyo chini ya mbingu na iliyoyafunika yawe yangu ikiwa nitampenda adui yako na kuwa adui wa mpenzi wako. Imam Ali (a) akamuombea akasema: “Ewe Mola mtunukie kufa shahidi katika njia yako na kuwa pamoja na Nabii wako.” Imesimuliwa ya kwamba alikuja mtu mmoja mweusi na kuingia kwa Imam Ali na kumuambia, mimi nimeiba, nitakase. Imam akasema: huenda uliiba kwa sababu ya kutokuweko kiziwizi! Akamjibu: sivyo ewe Amiri wa waumini, nimeiba nikiwa na kiziwizi, nitakase. Imam akasema: Huenda umei277


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:23 PM

Page 278

Tabia njema kwa mujibu wa Ahlul Bayt (a.s) ba kisichofikia kiwango! Akamjibu: Ewe Amiri wa waumini, sivyo, nimeiba kilicho fikia kiwango. Alipokiri mara tatu, Imam Ali akakata mkono wake. Huyo mtu akaondoka na huku akisema njiani: Amenikata Amiri wa waumini, Imamu wa wachamungu, kiongozi wa mabwana watukufu mashuhuri, Amiri mkuu wa dini na bwana wa mawasii. Akaendelea kumsifu hata Hasan (a) na Husayn (a) wakamsikia. Walipowasili kwa baba yao wakamueleza: Tumekutana njiani na mtu mweusi anakusifu. Imam Ali (a) akatuma arudishwe na alipoletwa akamuambia: Mimi nimekukata mkono kisha unanisifu?! Akajibu: Ewe Amiri wa waumini, hakika wewe umenitakasa, na hakika mapenzi yako yamechanganyika na nyama yangu na mifupa yangu, lau kama ungenikata vipande vipande kamwe yako mapenzi yasingetoweka moyoni mwangu. Imam (a) akamuombea na akarejesha mahala pake kilichokatwa na akapona na kuwa kama zamani. Imam Husayn (a) na watu wa nyumba yake waliotoharika na masahaba wake watukufu walifikia kilele cha juu kabisa katika kuthibiti kwenye haki na kushikamana nayo katika hali ya mateso na misiba isiyostahamilika. Siku ya Ashura, Imam Husayn (a) alisimama na huku amezingirwa na wanajeshi 30,000, wakidhamiria kumdhalilisha na kumuuwa, na kunguruma mbele yao kwa sauti inayogonga (mwangwi) na kutangaza bayana kukataa kwake na utukufu wake kwa kutamka maneno ambayo yatabaki milele, yenye kugonga katika kila zama na ambayo yataendelea kuwa ni katiba hai wanayoitukuza waliohuru na wasiokubali udhalili, nayo ni: "Ala! mwanaharamu mtoto wa mwanaharamu (Ubaydullah bin Ziyad) kashikilia baina ya mawili; ima mapambano au udhalili. Na kamwe haiwezekani sisi kuchagua udhalili. Kwa sababu Mwenyezi Mungu (swt) na Mtume wake wanalitukataza na pia waumini. Haiwezekani watu walionyonya wema na tohara, ushujaa, hamasa na utukufu kuchagua kumtii muovu na kuacha mapambano ya watu watukufu." . Imam Husayn (a) anasisitiza msimamo wake kwenye haki kwa kukhitari (kupendelea) kifo na muhanga kuliko maisha ya utumwa na udhalili, anasema: 278


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:23 PM

Page 279

Tabia njema kwa mujibu wa Ahlul Bayt (a.s) “Wallahi sitokupeni mkono wangu mithili ya mtu dhalili, wala sitokutambueni mithili ya wanavyofanya watumwa”. “Mimi sioni mauti ila kwamba ni raha, na kuishi na madhalimu ila kwamba ni karaha (madhila…)”. Na hivi ndivyo masahaba wa Imam Husayn (a) walivyofuata mwenendo na mfano wake katika kuthibiti kwenye haki na kutoa muhanga nafsi zilizo tukufu. Imam Husayn (a) aliwahutubia hotuba iliyojaa mapenzi, sifa, na huruma kwa kusema: “Ama baada, hakika mimi sijui masahaba wenye kutimiza ahadi yao wala bora kama nyinyi. Pia sijui Ahlul bayt (watu wa nyumba) walio wema wala bora zaidi ya Ahlul bayt wangu. Mwenyezi Mungu (swt) akujazeni kutoka kwangu kheri. Naona umesalia muda mchache kukabiliana na hawa watu, basi jueni kuwa nimekuruhusuni, ondokeni nyote nikiwa nimewavua wajibu wenu kwangu, huu ni usiku umekutandeni kwa hivyo uchukueni kama ngamia (pando la kuondokea) kisha kila mmoja miongoni mwenu na ashike mkono wa mmoja katika watu wa nyumba yangu na kisha tawanyikeni katika watu wenu na miji yenu, hadi pale Mwenyezi Mungu (swt) atakapoleta faraja. Hakika watu hawa wanayemtaka ni mimi. Wakinipata basi hawatakuwa na haja ya kumtafuta yeyote.” Muslim bin Awsajah akasimama na akasema: “Vipi sisi tutaondoka na kukuacha peke yako!!! Ni udhuru gani tutatoa mbele ya Mwenyezi Mungu (swt) ikiwa tutashindwa kutekeleza haki yako? Ama Wallahi sitokuacha mpaka nitakapo choma ndani ya vifua vyao na mkuki wangu na kuwapiga kwa upanga wangu (maadamu mkono wangu waweza kushika silaha) na lau ikiwa sina silaha ya kupigana nao, nitawapiga kwa mawe. Wallahi hatutokuacha mpaka Mwenyezi Mungu (swt) ajue ya kwamba sisi tumehifadhi mahala pa siri ya Mtume katika wewe. Wallahi lau ningejua ya kwamba nitauliwa, kisha nikahuishwa, kisha nikauliwa, kisha nikachomwa, kisha nikatawanywa (na upepo) halafu nikafanyiwa namna hivyo mara 70, kamwe nisingekuacha hadi pale nitakapoyakuta mauti kwa ajili 279


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:23 PM

Page 280

Tabia njema kwa mujibu wa Ahlul Bayt (a.s) yako. Na vipi nisifanye hivyo wakati ni kuuliwa mara moja na baadaye ni utukufu mkubwa usio na ukomo�. Zuhayr al-Qayn akasimama naye akasema: Napenda laiti ningeuliwa kisha nikafufuliwa kisha nikauliwa kisha nikafanyiwa hivyo mara elfu moja, ili Mwenyezi Mungu akuepushe kwa hilo kuuliwa wewe na hawa vijana wa nyumba yako. Na wengine miongoni mwa masahaba wakazungumza maneno yanayoshabihiana wakasema: Wallahi sisi hatutakuacha, bali nafsi zetu tutazitoa muhanga kwa ajili yako, tutakukinga kwa shingo zetu, nyuso zetu na mikono yetu, tutakapouliwa sisi tutakuwa tumetimiza haki zenu juu yetu. Hivyo ndivyo masahaba wa Imam Husayn (a) kwa maneno yenye kusisimua walivyodhihirisha uthibiti wao na kujitoa muhanga katika kumfuata na kumnusuru. Ni kiasi gani Waislamu wa leo ni wahitaji kupata mwongozo wa jihadi ya hawa watu watukufu wasio na kifani na kufuata nyayo zao katika kushikamana na dini na kuthibiti kwenye misingi yake na kujitolea muhanga katika kunusuru haki ili waweze kurudisha utukufu wao uliopotea na heshima iliyopokonywa na hivyo basi kuziokoa nafsi zao na udhalili wa kushindwa na hasara moja baada ya nyingine.

280


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:23 PM

Page 281

Tabia njema kwa mujibu wa Ahlul Bayt (a.s)

ORODHA YA VITABU VILIVYO CHAPISHWA NA AL-ITRAH FOUNDATION: 1. 2. 3. 4. 5. 6. 7. 8. 9. 10. 11. 12. 13. 14. 15. 16. 17. 18. 19. 20. 21. 22. 23. 24. 25. 26. 27. 28. 29. 30.

Qur'an Al-Kariim - Tafsir Al-Kashif Juzuu ya kwanza mpaka kumi na sita Uharamisho wa Riba Uharamisho wa uwongo Juzuu ya kwanza Uharamisho wa uwongo Juzuu ya pili Hekaya za Bahlul Muhanga wa Imamu Husein (A.S.) Mikingamo iliyomzunguka Imamu Ali (A.S.) Hijab vazi Bora Ukweli wa Shia Ithnaashari Madhambi Makuu Mbingu imenikirimu Abdallah Ibn Saba Khadijatul Kubra Utumwa Umakini katika Swala Misingi ya Maarifa Kanuni za Ndoa na maadili ya Familia Bilal wa Afrika Abudharr Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu Salman Farsi Ammar Yasir Qur'an na Hadithi Elimu ya Nafsi Yajue Madhehebu ya Shia Ukusanyaji na Uhifadhi wa Qur'an Tukufu Al-Wahda Ponyo kutoka katika Qur'an. Uislamu mfumo kamili wa maisha ya kijamii Mashukio ya Akhera 281


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:23 PM

Page 282

Tabia njema kwa mujibu wa Ahlul Bayt (a.s) 31. 32. 33. 34. 35. 36. 37. 38. 39 40. 41.

Al Amali Dua Indal Ahlul Bayt Udhuu kwa mujibu wa Kitabu na Sunna. Haki za wanawake katika Uislamu Mwenyeezi Mungu na sifa zake Amateka Nafasi za Ahlul Bayt (a.s) Adhana. Upendo katika Ukristo na Uislamu Nyuma yaho naje kuyoboka Amavu n’amavuko by’ubushiya

282


Akhlaq Ahlul bayt

FINAL MZEE RAMADHANIl.qxd

7/15/2011

12:23 PM

Page 283

Tabia njema kwa mujibu wa Ahlul Bayt (a.s)

BACK COVER AKHLAQ AHLUL BAYT Ni ukweli usiopingika kwamba kuna mmomonyoka mkubwa sana wa maadili katika jamii yetu ya zama hii. Vijana wetu na hata watu wazima wanapupia sana katika kuiga tamaduni za nje hususan Magharabi, wakiwa na fikra kwamba kila kinachofanywa na watu wa magharibi ni maendeleo na kinafaa kuiga. Wakimuona Mzungu akitembea nusu uchi wao wanaona hayo ni maendeleo, na kesho utawaona nao wanatembea nusu uchi, ukiliza kulikoni wanakuambia haya ndio maisha na kwamba wewe umepitwa na wakati. Hili ni tatizo kubwa sana katika jamii yetu hii ya sasa. Lakini watu huiga mazuri na sio kuiga machafu. Mwandishi wa kitabu hiki anatuletea watu wa kuiga; watu wenye tabia nzuri, watu waliotakaswa na Mwenyezi Mungu (Qur'an33:33). Hawa ni watu wa nyumba ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) ambao walikuwa wachamungu, wakarimu, wapole na wenye tabia nzuri ya kuigwa. Hii yote ni katika juhudi za mwandishi huyu kutaka kurekebisha tabia na mwenendo katika jamii inayotuzunguka.

Kimetolewa na kuchapishwa na: Al-Itrah Foundation P. O. Box 19701, Dar-es-Salaam, Tanzania Simu: +255 22 2110640 Fax: +255 22 2113107 Email: info@alitrah.org Website: www.alitrah.org

283


Turn static files into dynamic content formats.

Create a flipbook
Issuu converts static files into: digital portfolios, online yearbooks, online catalogs, digital photo albums and more. Sign up and create your flipbook.