al-Masa'ilu
'l-Islamiyyah
(Sheria za Kiislamu)
Kwa Mujibu wa Fatwa za Ayatullah al-Udhma Sayyid Sadiq Husaini Shirazi
Mtarjumi: Abdul Karim J. Nkusui
Kimechapishwa na: Ahlul Bayt Centre (ABC) S.L.P. - 7169, Arusha. Tanzania na Sayed Al-Shohada Charitable Committee S.L.P. - 15338, Kuwait
Haki ya kunakili imehifadhiwa na: Sayed Al-Shohadaa Charitable Committee
Kimetafsiriwa na:
Ustadh Abdul-Karim Nkusui Barua Pepe: abdulkarimjuma@yahoo.com
Toleo la kwanza: Augasti, 2008 Nakala: 3000
Kimechapishwa na: Ahlul Bayt Centre (ABC) S.L.P. - 7169, Arusha. Tanzania na Sayed Al-Shohada Charitable Committee S.L.P. - 15338, Kuwait Simu: +965 255 2560 Nukushi: +965 963 5403 DA’IYYAH - KUWAIT
YALIYOMO Hukumu za Taqlid. “ Kufuata”.........................................................2 Hukumu za Tohara............................................................................6 Hukumu za Maji..............................................................................11 Hukumu za kujisaidia......................................................................13 Istibra...............................................................................................16 Adabu za kujisaidia.........................................................................17 Najisi...............................................................................................18 Njia za kuthibitisha Najisi...............................................................25 Namna ya kunajisika vitu vilivyo Tohara........................................26 Mas’ala............................................................................................28 Vinavyotoharisha.............................................................................30 Kupungua theluthi mbili za juisi ya zabibu mbivu.........................34 Hukumu za vyombo.........................................................................39 Kuosha mikono miwili....................................................................40 Kupaka kichwa................................................................................41 Kupaka miguu mwili.......................................................................41 Udhu wa Irtimasi “kuzamisha”........................................................42 Masharti ya udhu.............................................................................43 Hukumu za udhu..............................................................................45
Al-Masailul Islamiyah Mambo ambayo yanapasa udhu.....................................................47 Vinavyobatilisha udhu.....................................................................48 Hukumu za udhu wa Jabirah (Bandeji)...........................................48 Josho za wajibu................................................................................49 Hukumu za Janaba...........................................................................50 Mambo ambayo ni haramu kwa mwenye Janaba...........................51 Mambo yaliyo makuruhu kwa mwenye Janaba..............................52 Mas’ala katika kuoga Janaba.........................................................53 Josho la mpangilio...........................................................................53 Josho la kuzama...............................................................................55 Hukumu za kuoga............................................................................55 Istihadha........................................................................................ . 58 Hukumu za Istihadha...................................................................... 59 Hedhi...............................................................................................65 Hukumu za Hedhi........................................................................... 68 Vigawanyo vya Hedhi.....................................................................72 Wenye Ada ya wakati na Idadi....................................................... 73 Nifasi.............................................................................................. 84 Kuoga josho la kugusa maiti...........................................................86 Hukumu za muhtadhari “anayekata roho”.......................................88 Hukumu baada ya mauti................................................................. 89 D
Al-Masailul Islamiyah Hukumu za kuosha maiti.................................................................91 Hukumu za kumkafini maiti............................................................93 Hukumu za tahaniti “kupaka�..........................................................95 Hukumu za swala ya maiti...............................................................95 Namna ya kuswali swala ya maiti...................................................97 Yaliyo Sunna katika swala ya maiti................................................98 Hukumu za kuzika...........................................................................99 Tayamamu.....................................................................................105 Hukumu za swala...........................................................................110 Swala za wajibu.............................................................................111 Swala za wajibu za kila siku......................................................... 111 Wakati wa Swala ya Adhuhuri na Alasiri..................................... 112 Wakati wa Swala ya Magharibi na Isha....................................... 113 Wakati wa swala ya Asubuhi.........................................................113 Hukumu za wakati wa swala ....................................................... 115 Swala za Sunna..............................................................................119 Swala ya Usiku..............................................................................120 Swala ya Ghufaila......................................................................... 121 Hukumu za Kibla...........................................................................121 Kusitiri mwili katika Swala...........................................................122
E
Masharti ya vazi la mwenye kuswali............................................123 Sharti la kwanza...........................................................................123 Sharti la pili..................................................................................124 Sharti la tatu..................................................................................125 Sharti la nne..................................................................................125 Sharti la tano.................................................................................126 Sharti la sita..................................................................................127 Sehemu ambazo hazilamu tohara ya mwaili wa mwenye kuswali.127 Yaliyosunna katika vazi la mwenye kuswali.................................129 Yaliyo makuruhu katika vazi la mwenye kuswali.........................129 Sehemu ya mwenye kuswalio.......................................................129 Shari la kwanza..............................................................................130 Sharti la pili...................................................................................130 Sharti la tatu...................................................................................131 Sharti la nne...................................................................................131 Sharti la tano..................................................................................131 Sharti la sita...................................................................................131 Sharti la saba..................................................................................131 Sharti la nene.................................................................................132 Sharti la tisa...................................................................................132 Hukumu za misikiti. .................................................................... 133 F
Sharti la tano Takbira ya kuhirimia swala.......................................................... 138 Sehemu Ambazo ni wajibu kukata Swala................................... 158 Shaka.............................................................................................157 Shaka zisizotiliwa maanani...........................................................160 Shaka ya kitu baada ya kupita sehemu yake.................................160 Shaka baada ya salamu..................................................................163 Mwingi wa shaka...........................................................................163 Shaka ya Imamu na Maamuma.....................................................163 Shaka zisizobatilisha swala........................................................... 167 Swala ya Ihtiyati............................................................................171 Sijida ya kusahau......................................................................... 172 Namna ya kuleta sijida ya kusahau.............................................. 174 Swala ya msafiri............................................................................176 Hukumu za makazi na kukaa siku kumi...................................... 183 Wajibu wa mtoto mkubwa kulipa swala zilizowapita wazazi wawili....................................................................................................188 Swala ya Jamaa..............................................................................190 Hukumu za Jamaa......................................................................... 192 Sunna za swala ya Jamaa...............................................................193 Swala ya majanga..........................................................................197 G
Swala ya majanga..........................................................................197 Swala ya Idd mbili “Al-fitri na Al-adhihaa”.................................200 Hukumu za Saumu.........................................................................202 Panyeto”Kuchezea utupu”.............................................................207 Kumzulia uongo Mwenyezi Mungu, Mtume (s.a.w.w) na Maimamu (a.s)................................................................................................207 Kufika vumbi zito kwenye koo.................................................... 209 Kuzamisha kichwa kwenye maji...................................................210 Kubaki na Janaba au hedhi au Nifasi mpaka Alfajiri...................211 Hukumu ya vitenguzi.....................................................................216 Mambo ambayo ni wajibu kupa kadhaa na kutoa kafara...............217 Kafara za Saumu...........................................................................217 Mambo ambayo ni wajibu kulipa kadha ya saumu bila kafara......220 Hukumu za Saumu ya kadhaa....................................................... 222 Hukumu za Saumu ya msafiri........................................................224 Njia za kuthibiti mwanzo wa mwezi............................................226 Saumu ambazo ni Haramu na makuruhu ....................................277 Hukumu za Khumsi.......................................................................230 Hukumu za Zaka............................................................................231 Hukumu za Hija.............................................................................235 Umra Tamatui................................................................................238 H
Umra ya Mufrad............................................................................245 Hukumu za ndoa........................................................................... 248 Hukumu za Talaka.........................................................................260 Hukumu za kuchinja mnyama na kumuwinda kwake.................. 265 Njia ya kisheria ya kuchinja..........................................................266 Masharti ya kuchinja ....................................................................267 Hukumu za kuwinda kwa silaha...................................................269 Hukumu za kula na kunywa..........................................................273 Mambo ya Sunna wakati wa kula.................................................274 Hukumu za miradhi.......................................................................277 Talaqin ya maiti.............................................................................283
I
Al-Masailul Islamiyah
UTANGULIZI Kwa jina la Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema mwenye kurehemu, rehema na amani zimwendee kipenzi chetu Mtume Muhammad (saww) na Aali zake wema, ama baad. Taasisi ya Sayed Shohadaa (as) kwa moyo mkunjufu na furaha kubwa inawaletea wasomaji wa lugha ya Kiswahili na hususan kuitajirisha maktaba ya Kiswahili kwa Muhtasari wa Sharia ya Kiislam kwa mujibu wa fat’wa za Ayatollah Al - Udhmaa As Sayed Swadiq Al-Hussein As Shirazi - Mwenyezi Mungu aidumishe kazi yake. Tarjama hii ilioko mikononi mwako ni matunda ya jitihada na juhudi kubwa za waalimu wa Madrasatul - Wahdah Singida ambao wametumia muda wao mwingi ili kufanikisha kazi hii nzuri; Kwa hawa na kwa kila aliyeshiriki kwa namna moja au nyingine katika kufanikisha kazi hii tunatoa shukrani zetu za dhati na tunawaombea kila la kheri kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu awalipe malipo mema. Imamu Swadiq Shirazi ametumia lugha rahisi na nyepesi jambo ambalo tunamatumaini kuwa litawasaidia wasomaji na kuwafanyia sahali katika kufuatilia na kujua hukumu za mas’ala ambayo aghlabu wanayahitajia katika maisha yao ya kila siku bila ya ugumu wowote. Tarjama hii imetoa kipaumbele katika mas’ala ambayo ni muhimu zaidi kwa waumini ili kuwarahisishia kujua Sharia ya dini yao hususan mas’ala ya Swala, saumu, ndoa, talaka, mirathi n.k. Ni matarajio yetu kuwa wasomaji wetu watakipokea kwa mikono miwili na J
Al-Masailul Islamiyah watanufaika kwa kupata utatuzi wa mas’ala mengi mbali mbali kwa njia nyepesi zaidi. Tarjama hii haikuzingatia utaratibu wa namba za mas’ala kama yalivyo katika kitabu cha asili bali mtiririko wa namba ni kulingana na mas’ala yaliyochaguliwa, hivyo ukitaka kufuatilia lazima urejee katika maudhui tajwa katika nakala ya asili ndio utajua namba ya mas’ala husika. Nia yetu katika tarjama hii ni kutoa mas’ala ambayo ni muhimu zaidi katika jamii pia hatukutaka kitabu kiwe ni kikubwa sana. Tunamuomba Mwenyezi Mungu atie wepesi na baraka katika kazi hii ili iwafikie waumini kwa haraka kwani Yeye ndio mwenye kuombwa msaada na taufiq Wasalaam S.S.Magwe Sayed Shohadaa Trust 4 Rabiul Akhir 1428AH - 22 April 2007
K
DIBAJI Kwa jina la Mwenyezi Mungu Mwingi wa rehema Mwenye kurehemu. Shukrani zote anastahiki Mwenyezi Mungu Mola wa viumbe, rehema na amani zimwendee kipenzi cha nyoyo zetu Mtume wetu Muhammad (s.a.w.w.) na kizazi chake chema, masahaba wake na wote waliomfuata kwa wema hadi Siku ya Kiyama. SAYYED SHUHADAA CHARITABLE COMMITTEE ni taasisi ya kidini inayojishughulisha na mambo ya waislamulimwenguni katika nyanja mbalimbali za maisha yao ya kila siku. Pamoja na kujali sana mambo ya waislamu pia inatoa kipaumbele katika suala la elimu kwa vijana wa kiislamu na kuwaendeleza ili kuwajenga katika maadili mema ya kumtumikia Mwenyezi Mungu na hatimaye wawe ni viongozi wazuri watakaohudumia jamii ya Kiislam na kuijenga kiroho, kimaadili na hatimaye kuwawezesha kufikia lengo lao la kuwepo hapa dunia kwa wepesi. Sambamba na hayo taasisi yetu pia inajishughulisha na mambo yafuatayo katika jamii:- Ujenzi wa Miskiti - Ujenzi wa Madrasa - Kuwaangalia wazee wasiojiweza - Kusaidia watoto yatima - Kuwasaidia maskini - Kutoa misaada ya kibinadamu wakati wa majanga - Kukusanya na kugawa nudhur, kafara, chinjo katika mwezi wa Dhul-Hajj na kutoa futari katika mwezi wa Ramadhani - Kuendesha Majlis za Muharram na minasaba mbalimbali ya kidini kama L
vile kuadhimisha Maulidi na Wafayaat ( vifo na mazazi ) - Kuchapisha vitabu mbalimbali vya kidini kama vile Misahafu, Juzuu Amma, vitabu vya fikra, dua n.k. - Na kuendesha na kusimamia semina mbalimbali za kidini. Tunamuomba Mwenyezi Mungu atupe wepesi na atufanyie sahali katika kufanikisha malengo yetu haya tuliyojiwekea, kwani Yeye ndiye wakuombwa msaada Wabillahi Tawfiq.
M
N
Al-Masailul Islamiyah
HUKUMU ZA TAQLID “KUFUATA” 1.Mas’ala: Niwajibu itikadi ya mwislamu katika Usul- Dini “misingi ya dini” iwe ni kutokana na dalili na hoja, na wala haijuzu humo kufanya taqlid, kwa maana ya kwamba mtu asikubali maneno ya yeyote bila ya dalili. Lakini katika hukumu za kidini na matawi yake ni wajibu ama awe ni mujitahid anayeweza kuchambua hukumu kutoka katika naswi “ Aya au Hadith” na ama awe ni mwenye kufanya taqlid kwa maana ya kwamba afanye amali kutokana na fat’wa za mujitahid ambaye ametimiza masharti na ama awe anafanya amali kwa njia ya kufanya ihtiyat “tahadhari” kwa namna ambayo atapata yakini kwamba ametekeleza wajibu. Kwa mfano kama jopo la mujitahid limetoa fat’wa kuharamisha jambo na jopo jingine limetoa fat’wa ya uhalali wa jambo hilo basi anachukua tahadhari ya kutolifanya jambo hilo au kama baadhi wametoa fat’wa ya wajibu wa kufanya amali na wengine wakatoa fat’wa ya kuwa kwake sunna basi anachukua tahadhari ya kufanya jambo hilo. Na ambaye sio mujitahidi wala hawezi kufanya ihtiyat “tahadhari” ni wajibu kwake kumfuata Mujitahid na kufanya amali kulingana na fat’wa zake. 2: Kufanya taqlid katika hukumu ni kufanya amali kwa mujibu wa fat’wa ya mmoja wa Mujitahidina. Ni wajibu Mujitahidi awe ni mwanaume, baleghe, mwenyeakili timamu, Shia Ithina Asharia, mtoto wa halali, awe hai, huru na mwadilifu. Mwadilifu ni mtu anayefanya yaliyo wajibu na kuacha yaliyoharamu kwa kiasi kwamba lau kama ukiulizia hali yake kwa jirani yake au kwa wanayeishi naye au watu wa mahali anapofanyia kazi basi wangekupa habari za wema wake, na kwa tahadhari mujitahid huyo awe ni mjuzi zaidi katika zama zake katika kufahamu hukumu na kuzichambua.kuliko mujtahid mwengine
2
Al-Masailul Islamiyah 3: Mujitahid na mjuzi zaidi anafahamika kwa moja kati ya njia tatu:i – Mtu mwenyewe kupata yakini ya hilo, kwa yeye mwenyewe kuwa ni kati ya wenye elimu na anaweza kumtambua mujitahid na mjuzi zaidi kwa ujuzi wake. ii - Wajuzi wawaili waadilifu kutoa taarifa juu ya hilo ambao wanaweza kumtambua Mujitahid na mjuzi zaidi kwa sharti wasipinge taarifa yao wajuzi wengine wawili. iii
Washuhudie hilo jopo la watu wenye elimu na ujuzi kati ya wanao weza kumtambua Mujitahid na mjuzi zaidi na wanaoaminiwa, na hukumu iliyo na nguvu zaidi ni kutosheleza taarifa ya mtu mmoja ikiwa ni mkweli.
4. Ikiwa ni vigumu kumtambua mjuzi zaidi inalazimu kwa tahadhari ya wajibu kumfuata anayedhaniwa kuwa yeye ni mjuzi zaidi, vivyo hivyo atamfuata ambaye anadhana dhaifu juu ya kuwa kwake mjuzi zaidi na anajua kutokuwepo kwa mjuzi zaidi mwingine asiyekuwa yeye kwa tahadhari ya sunna, ama kama kundi litalingana katika ujuzi basi atamfuata mmoja kati yao, lakini ikiwa mmoja wao ni mchamungu zaidi basi atamfuata yule mcamungu zaidi bila ya wengine kwa tahadhari ya sunna. 5. Inawezekana kupata fat’wa na rai ya mujitahidi kwa moja kati ya njia nne zifuatazo :Kusikia moja kwa moja kutoka kwa mujitahidi. Kusikia kutoka kwa waadilifu wawili wakinukuu fat’wa ya Mujitahidi. Kusikia kutoka kwa wanaoaminika na kutegemewa katika kunukuu kauli yake. Kupatikana fat’wa katika kitabu chake cha fat’wa, katika muundo unaoleta tumaini juu ya usahihi wa yaliyomo humo na usalama wake kutokana 3
Al-Masailul Islamiyah na makosa. 6. Maadamu mwenye kufanya taqlid hajapata yakini ya kubadilika fat’wa ya Mujitahidi na rai yake inajuzu kwake kufanya amali kulingana na yaliyomo ndani ya kitabu chake cha fat’wa lakini akidhania juu ya kuwepo mabadiliko katika fat’wa yake sio wajibu kuchunguza isipokuwa kama dhana inakubalika kiakili. 7. Mujitahid mjuzi zaidi akitoa fat’wa katika mas’ala haijuzu kwa anaye mfuta kumfuata mujitahidi mwingine katika mas’ala hayo kwa tahadhari ya wajibu, lakini kama hajatoa fat’wa bali amesema. “ Kwa tahadhari afanye kadha.” Kwa mfano akisema: “ kwa tahadhari alete tasbihi nne mara tatu” inalazimu kwa mwenye kuqalid kufanya kulingana na tahadhari hii au afanye kulingana na fat’wa ya mujitahid mwingine, ikiwa mujitahidi mwingine amesema inatosha kuileta mara moja basi anaweza kuileta mara moja, na hukumu ni hiyo hiyo ikiwa Marjii anayemfuata atasema. “Mas’ala haya ni mahala pa kutafakari au ni mahala pa mushkeli.” 8. Mujitahidi akitoa tahadhari baada ya kutoa fat’wa katika mas’ala mfano mtu akisema “Chombo kilichonajisika kinatoharika kwa maji ya kuru “birika” mara moja ingawa ni bora kukiosha mara tatu” haijuzu kwa anayemfuata mujtahid kumrejea mujitahidi mwingine katika mas’ala hayo na hii inaitwa tahadhari ya sunna. 9. Haijuzu kumfuata mujitahid aliyekufa kwa anayeanza taqlid, ama akifa mujitahid ambaye mtu anamfuata inajuzu kwake kubaki katika taqlid ya mujitahid aliyekufa katika mas’ala yote ambayo mwenye kuqalid hajayafanya wakati wa uhai wa mujitahid. 10. Mtu akifanya amali fulani kwa fat’wa ya mujitahid, kisha mwenye kufanya taqlid katika mas’ala hayo kwa fat’wa ya mujitahid aliye hai baada ya kufa marja wake wa kwanza haitajuzu kwake kubadili kutoka katika fat’wa ya mujitahid aliye hai kwenda kwenye fat’wa ya mar4
Al-Masailul Islamiyah jaa wake wa awali aliyekufa katika mas’ala hayo. Vivyo hivyo ikiwa mujitahid hakutoa fat’wa katika mas’ala hayo bali akatoa tahadhari na mwenye kuqalid akafanya kulingana na tahadhari hiyo kwa muda haijuzu kwake kurejea katika fat’wa ya mujitahid aliyekufa. 11. Inajuzu kubadili taqlid kutoka kwa mujitahid aliyekufa kwenda kwa mujitahid hai na wala haijuzu kubadili kutoka kwa mujitahid hai kwenda kwa mujitahid mwingine hai kwa tahadhari, isipokuwa ikiwa mujitahid wa pili ni mjuzi zaidi kuliko mujitahid wa kwanza au wa kwanza akipoteza sifa ya uadilifu. 12. Ni wajibu kwa mukalafu “aliye baleghe na mwenyeakiili tiomamu” kujifunza mas’ala ambayo aghlabu anayahitaji. 13. Yakitokea mas’ala ambayo mtu hajui hukumu yake ikiwa inawezekana kusubiri ni wajibu wake kusubiri hadi apate fat’wa ya marjaa anayemfuata na ikishindikana afanye kilicho wajibu kwake kwa kuchukua tahadhari kama kuna uwezekano. 14. Kama mtu akinukuu fat’wa ya mujitahid kwa yeyote fat’wa ikibadilika sio lazima kwake kumjulisha mabadiliko hayo, lakini akijua kuwa alikosea katika kunukuu fat’wa ni lazima kumjulisha yale aliyoyanukuu kwake kama kuna uwezekano. 15. Mukalafu akifanya amali kwa muda bila ya taqlid amali yake itasihi ikiwa itaafikiana na fat’wa ya mujitahid ambaye ilikuwa ni wajibu kwake kumfuata au ikiafikiana na fat’wa ya mujitahid ambaye imepasa kumfuata, ingawa kwa tahadhari iafikiane na mujitahid anayetaka kumfuata au akijua kwa njia nyingine kuwa amali zake zimeafikiana na hali halisi na kwamba ametimiza wajibu wake. 16. Taqlid inahusu hukumu zote, katika ibada, mikataba, wajibu, haramu, sunna, makuruhu na mubaha. 5
Al-Masailul Islamiyah
HUKUMU ZA TOHARA Maji halisi na mudhafu 17. Maji ama ni mutlaq ‘halisi’ na ama ni mudhafu. Mudhafu ni ambayo yamekamuliwa kutoka kwenye kitu, mfano maji ya komamanga, maji ya waridi au yaliyochanganywa na kitu mfano maji yaliyochanganywa na udongo n.k kiasi kwamba hayaitwi maji tu, na halisi ni yasiyokuwa hayo, nayo yamegawanyika sehemu tano:maji ya “kuru” birika maji machache maji yanayotiririka maji ya mvua maji ya kisima Maji ya birika 18. Kuru “birika” ni ambalo lina ujazo wa shibiri 3 upana, urefu na kina au ambalo jumla ya ujazo wake ni shibiri 27. 19. Maji ya birika hayanajisiki kwa kukutana tu na damu au mkojo au kitu chochote kilicho najisi au kilichonajisika mfano nguo iliyonajisika ila yakibadilika na kuchukua rangi ya najisi au harufu yake au ladha yake na hayanajisiki ikiwa hayajabadilika. 20. Maji ya birika hayanajisiki ikiwa yatabadilika bila ya kupatwa na najisi. 21. Kilicho najisi mfano damu kikikutana na maji yanayozidi kuru na baadhi ya rangi yake ikabadilika au harufu yake, ikiwa yaliyobakia ni 6
Al-Masailul Islamiyah machache kuliko kiwango cha kuru yote yatanajisika na ikiwa yaliyobakia ni kiwango cha kuru au zaidi ya kuru hayatanajisika yote bali kiasi kilichobadilika tu. 22. Ikiwa maji ya bomba yameungana na birika maji yaliyonajisika yatatoharika, lakini hayatohariki ikiwa yatadondokewa na matone tu, ila kikiwekwa kitu kwenye bomba ili maji yake yaungane kabla hayajawa matone na kuungana na maji yaliyonajisi, na kwa tahadhari ya sunna yachanganyike maji ya bomba na maji yaliyonajisika. 23. Kama akiosha kitu najisi kwenye bomba la maji yaliyoungana na birika, maji yanayodondoka kutoka kitu kilicho najisi yatakuwa tohara kama yataunganika na birika na hayajachukua rangi ya najisi au ladha yake au harufu yake na ikiwa humo hakuna viini vya najisi. 24. Kama kitaganda kiasi cha maji ya birika na yaliyobaki yakawa sio kiwango cha birika maji yaliyobaki yatanajisika kama yatakutana na najisi, vivyo hivyo yatanajisika kila yatakapo yeyuka kutoka katika barafu. 25. Maji ambayo yameshakuwa kuru ikitokea shaka kuwa yamepungua kiasi cha kuru au laa basi hukumu yake ni kuru yaani ni tohara na yanatoharisha na wala hayanajisiki kwa kukutana na najisi, na ambayo yalikuwa sio kuru ikitokea shaka kuwa yamekuwa kuru au laa basi hayatakuwa na hukumu ya kuru na kwa tahadhari ya lazima afanye utafiti katika maudhui haya kisha aratibu atoe hukumu iliyotajwa ikiwa hali halisi haitabainika. 26. Birika linathibitika kwa njia moja kati ya tatu:Mtu binafsi kupata yakini juu ya hilo Watu wawili waadilifu watoe habari au mtu mmoja mkweli Atoe habari ya hilo ambaye maji yako chini ya usimamizi wake kama vile mwangalizi wa bafu akisema: Maji yaliyopo katika tanki la bafu ni birika 7
Al-Masailul Islamiyah Maji machache 27. Maji machache ni maji ambayo hayatiririki ardhini na wala hayafikii kiasi cha birika. 28. Maji machache yakimwagwa kwenye kitu najisi au yakikutana na najisi yananajisika, lakini kama yatamwagiwa kutoka juu, juu ya kitu kilicho najisi au kwa mkupuo, kina najisika kiasi kilichokutana na najisi tu na kinachobakia kitakuwa tohara. 29. Maji machache yakimwagiwa kwenye kitu kilicho najisi ili kuondoa kiini cha najisi humo, kisha maji yakajitenga nacho maji yanayojitenga yatakuwa najisi na inalazimu kwa tahadhari ya sunna ajiepushe na maji ambayo yanamwagiwa juu ya kitu kilicho najisika baada ya kuondoka kiini cha najisi humo. 30. Maji yanayooshewa sehemu ya haja kubwa na ndogo yatakuwa tohara na wala hakitonajisika kitu kinacho kutana nayo kama masharti matano yatatimia pamoja na kuchukua tahadhari:Kama hayatachukua rangi ya najisi, harufu yake au ladha yake. Ikiwa hayatapatwa na najisi nyingine. Ikiwa hayatapatwa na chembechembe za kinyesi zinazoonekana. Ikiwa mkojo au kinyesi hakijatoka pamoja na damu. Ikiwa haja ndogo au kubwa haitavuka sehemu yake ya kawaida inayojulikana. Maji yanayotiririka 31. Maji yanayotiririka ni ambayo yanatoka ardhini na yanatiririka kama maji ya chemchem na mifereji. 32. Maji yanayotiririka hata kama ni machache ni kama kuru yakipatwa na najisi yatakuwa tohara maadam hayajabadilika rangi yake au harufu 8
Al-Masailul Islamiyah yake au ladha yake kwa sababu ya najisi. 33. Najisi ikikutana na maji yanayotiririka kitanajisika kiasi cha maji kilichobadilika kwa sababu ya najisi tu, na ambayo yameunganika na chemchem miongoni mwayo yatakuwa tohara hata kama ni machache kuliko kuru. Ama maji mengine ya mto ikiwa yatakuwa katika kiwango cha kuru au yakichanganyika na chemchem kwa njia ya maji ambayo hayajabadilika yatakuwa tohara vinginevyo yatakuwa najisi. 34. Chemchem inayobubujika masika na inaacha kububujika wakati wa kiangazi hukumu yake wakati inapotiririka ni hukumu ya maji yanayotiririka. 35. Maji ya chemchem ambayo hayatiririki lakini yanatoka kila yanapochotwa hukumu yake ni hukumu ya maji yanayotiririka, kwa maana kwamba hayanajisiki kwa kukutana tu na kiini cha najisi maadamu hayajabadilika rangi yake au ladha yake au harufu yake kwa sababu ya najisi. 36. Maji yaliyotuama karibu na mto unaoungana nayo hukumu yake ni hukumu ya maji yanayotiririka. 37. Maji ya hodhi za bafuni ikiwa yameungana na tanki basi ni kama maji yanayotiririka katika hukumu, hata kama ni machache kuliko kuru, kwa sharti tanki liwe na kiwango cha kuru. 38. Maji ya bomba ambayo yako katika bafu na majengo, ambayo yanamiminika katika bomba na karo ikiwa yanaungana na kuru - kama vile jokofu za maji ya kunywa- hukumu yake ni hukumu ya maji yanayotiririka. 39. Maji yanayotiririka juu ya ardhi lakini hayana chanzo toka ardhini yakiwa chini ya kiwango cha kuru na yakakutana na najisi yatanajisi9
Al-Masailul Islamiyah ka, ama ikiwa yanatiririka toka juu kwenda chini au kwa mkupuo na yakakutana na najisi chini maji yaliyo juu hayatanajisika. Maji ya mvua 40. Maji ya mvua yakinyeshea kitu kilicho najisi ambacho hakina kiini cha najisi, kitu kilichonyeshewa na mvua kitatoharika, matone ya mvua hayatoshelezi bali iwe kwa kiasi kwamba inaitwa mvua na inatiririka ardhini na kwa tahadhari ya sunna mvua iwe ni kwa kiasi inatiririka katika ardhi ngumu. 41. Hailazimu kukamua nguo, godoro n.k , sawa sawa likioshwa kwa maji ya mvua au mengineyo. 42. Mvua ikinyeshea kiini cha najisi na kikasambaa hadi sehemu nyingine matone yatakuwa tohara ikiwa hayaambatani na chembechembe za najisi, harufu yake, rangi yake, au ladha yake, mvua ikinyeshea damu na kusambaa ikiwa katika cheche kuna chembechembe za damu, harufu yake au ladha yake zitakuwa najisi. 43. Mvua ikinyeshea paa la nyumba au juu ya jengo na ikawa juu yake kuna kiini cha najisi maji yanayotiririka chini ni tohara hata kama yatakuwa yamepata kiini cha najisi maadam mvua inaendelea kunyesha. Ama baada ya kukatika akijua kuwa maji yanayotiririka kutoka kwenye paa yamepatwa na najisi basi yatakuwa najisi. 44. Ardhi iliyonajisi inatoharika kwa kunyeshewa na mvua , ikiwa mvua itanyeshea ardhi kisha maji yakapenya katika sehemu iliyo najisi chini ya paa sehemu hiyo itatoharika. 45. Udongo ulionajisi ambao kwa kunyeshewa na mvua unakuwa tope utakuwatohara. 46. Maji ya mvua yakikusanyika sehemu yakaosha kitu kilichonajisika 10
Al-Masailul Islamiyah wakati wa kunyesha mvua kitu hicho kinatoharika hata kama maji yaliyokusanyika ni chini ya kuru, hii ni kwa sharti yasichukue rangi ya najisi, harufu yake wala ladha yake. 47. Mvua ikinyeshea godoro tohara lililotandikwa juu ya ardhi iliyo najisi na maji yakatiririka juu ya ardhi, ardhi najisi inatoharika na godoro halitanajisika. Maji ya kisima 48. Maji ya kisima yanayotoka ndani ya ardhi ni tohara hata kama ni machache kuliko kuru maadam hayajabadilika rangi yake au harufu yake au ladha yake kutokana na najisi, lakini ni sunna yanapokutana na baadhi ya najisi yatolewe kiasi kilichotajwa katika vitabu vikubwa. 49. Najisi ikimwagiwa katika kisima ikabadili rangi yake au harufu yake kama mabadiliko hayo yataondoka basi maji yakisima yatatoharika ingawa kwa tahadhari ya sunna yachanganyike na maji mapya yanayotoka katika kisima. 50. Maji ya mvua au maji yoyote yakikusanyika katika shimo na yakawa ni machache kuliko kuru yananajisika kwa kukutana na najisi.
HUKUMU ZA MAJI 51. Maji mudhafu(ambayo maana yake imeelezwa katika mas’ala 17) hayatoharishi kitu najisi na wala haisihi kutawadhia wala kuoga josho. 52. Maji mudhafu vyovyote yatavyokuwa mengi (lakini si kwa wingi wa kisima cha mafuta) yananajisika kwa kukutana tu na najisi lakini kama maji mudhafu yakikingwa kutoka juu, kwenye ya kitu najisi, yatanajisika yaliyokutana na najisi tu, bila ya kunajisika yaliyo juu, mfano 11
Al-Masailul Islamiyah kama maji ya waridi yakimwagwa kutoka kwenye birika juu ya mkono ulio na najisi yananajisika yaliyofika kwenye mkono na ambayo hayajafika yatakuwa tohara, vivyo hivyo lau yakisukumwa kutoka chini kwenda juu kwa msukumo wa bomba na yakakutana na yaliyo juu yaliyonajisika sehemu ya chini haitonajisika. 53. Maji mudhafu yakichanganyika na maji ya kuru au maji yanayotiririka kiasi ambacho hayasemwi kuwa ni mudhafu yanatoharika. 54. Maji ambayo yalikuwa mutlaq na wala hayajulikani kama yamegeuka na kuwa mudhafu au laa yatahukumiwa kuwa ni mutlaq kwa maana kwamba yanatoharisha najisi na inafaa kutawadha na kuoga kwayo. Ama ambayo yalikuwa mudhafu mwanzo na wala haijulikani kabla ya hapo yalikuwa mutlaq au ni mudhafu hayatoharishi kilichonajisika, na kutawadha na kuoga kwayo ni batili lakini yakiwa kwa kiwango cha kuru au zaidi yakikutana na najisi hayahukumiwi kuwa ni najisi. 55. Maji ambayo hayajulikani kuwa ni mutlaq au mudhafu wala haijulikani je hapo kabla yalikuwa mutlaq au mudhafu, hayatoharishi kitu kilicho najisika, na kutawadha na kuoga kwayo ni batili, lakini yakiwa kwa kiwango cha kuru au zaidi yake na yakakutana na najisi hayahukumiwi kuwa yamenajisika. 56. Maji ambayo yamekutana na najisi mfano mkojo na damu yakabadilika rangi yake au harufu yake au ladha yake kwa sababu hiyo yatanajisika hata kama yanatiririka au yako katika kiwango cha kuru, lakini yakibadilika rangi yake au harufu yake au ladha yake kwa sababu ya ukaribu wake na najisi iliyo nje – kama ikiwa mzoga umetupwa karibu ya maji hayo ukabadili harufu ya maji – dhahiri ni kutonajisika kwake na wala si wajibu kufanya tahadhari ingawa ni bora kufanya hivyo. 57.Maji ambayo yamekutana na najisi mfano wa mkojo na damu rangi yake ikibadilika au harufu yake au ladha yake kwa sababu ya hiyo najisi 12
Al-Masailul Islamiyah yananajisika japo yawe yanatiririka au kufikia kiwango cha kuru, lakini endapo itabadilika rangi yake au harufu yake au ladha yake kwa ajili ya ukaribu wake na najisi iliyo nje yake, kama vile utupwe mzoga karibu na maji ukabadilisha harufu ya maji- kwa hukumu yenye nguvu -hayanajisiki wala si lazima kufanya ihtiyati- tahadhari- japokuwa ni bora. 58. Maji ambayo yameingia najisi mfano wa damu au mkojo ikabadilisha harufu yake au ladha yake au rangi yake,yatatoharika yakikutana na kuru au na maji yanayotiririka au yakinyeshewa na mvua moja kwa moja au upepo ukipeperusha maji ya mvua na kuyaingiza humo au maji ya mvua yametiririkia humo kutoka kwenye bomba la maji ya mvua, hayo yote yatatimia kwa sharti ya kutoweka mabadiliko wake. 59. Mabaki ya maji yaliyonywewa na mbwa, nguruwe au kafiri ni najisi na ni haramu kuyanywa, ama mabaki ya maji yaliyonywewa na mnyama ambaye ni halali kuliwa ni tohara na sio makuruhu kuyanywa. Ama mnyama aliye haramu kuliwa mabaki yake ni tohara ,lakini ni makuruhu kuyanywa isipokuwa mabaki ya paka sio makuruhu kuyanywa. 60. Endapo kitu kilichonajisika kitaoshwa ndani ya kuru au maji yanayotiririka maji yanayoatuka kutoka kwenye kitu kilichooshwa yatakuwa tohara.
HUKUMU ZA KWENDA HAJA 61. Ni wajibu- kwa mwanadamu- kustiri uchi wake - mbele ya kila aliyebaleghe, wakati wa kujisaidia na mbele ya mtu mwingene hata kama anayemuona ni mahram yake, kama vile dada yake, mama yake n.k. Ni wajibu kustiri uchi mbele ya kichaa, mtoto mwenye kutambua zuri na baya, lakini sio lazima kwa mke kusitiri uchi wake mbele ya mume wake au kinyume chake. 62. Si wajibu kusitiri utupu kwa kitu makhsusi bali hata akiusitiri kwa 13
Al-Masailul Islamiyah mkono wake inatosha. 63. Ni wajibu asielekee kibla wala kukipa mgongo wakati wa kujisaidia, yaani sehemu ya mbele ya mwili wake; tumbo lake, kifua chake na magoti yake yasielekee kibla au kinyume chake. 64. Endapo mwenye kujisaidia ameelekea kibla au amekipa mgongo haitotosha kwa kupindisha utupu wake mbali na upande wa kibla katika hali zote mbili. Na ikiwa hakuelekea kibla wala kukipa mgongo afanye ihtiyati ya wajibu kutoielekeza tupu yake upande wa kibla au kinyume chake. 65. Na kwa tahadhari ya sunna asielekee mwenye kujisaidia wala asielekeze mgongo kibla wakati wa kufanya istibraa (ambayo maelezo yake yatakuja katika mas’ala 73) na wakati wa kujitoharisha sehemu ya mkojo na ya haja kubwa pia. 66. Akilazimika kuelekea kibla au kukipa mgongo ili asionekane kwa asiyekuwa mahram yake hakuna ubaya kukielekea kibla au kukipa mgongo ,vivyo hivyo hakuna ubaya akilazimika kukielekea kibla au kukipa mgongo kwa ajili ya sababu nyingine. 67. Hailazimu kuchukua tahadhari ya kutomkalisha mtoto mchanga kwa namna ambayo atakuwa ameelekea kibla isipokuwa uharamu wa hilo uwe kwa upande mwingine, na kama mtoto mwenyewe akielekea kibla au akakipa mgongo hailazimu kumkataza kwa hilo. 68. Ni haramu kujisaidia katika sehemu tano:Vichochoro visivyopitika kama wenyewe hawaruhusu hilo, vivyo hivyo katika njia zinazopitika (zisizo fungwa) katika hali ya dharura kwa mpita njia. Miliki ambayo hairuhusiwi kujisaidia humo. Sehemu zilizowaqfu kwa watu mahsusi mfano katika madrasa za kidini 14
Al-Masailul Islamiyah n.k. Juu ya kaburi la muumini kama hilo litamdhalilisha .Sehemu za heshima ambazo haifai kujisaidia kutokana na heshima yake. 69. Sehemu ya haja kubwa haitohariki isipokuwa kwa maji katika hali tatu, baadhi ya hizo ni kwa tahadhari:Kama itagusa sehemu ya haja kubwa najisi kutoka sehemu nyingine. Kama itatoka pamoja na haja kubwa najisi nyingine kama vile damu. Kama haja kubwa itavuka sehemu ya haja kubwa zaidi ya inavyojulikana. Ama isiyokuwa katika hali zisizokuwa hizi inajuzu kutoharisha sehemu ya haja kubwa kwa maji au tambara au mawe n.k, kama utakavyokuja ufafanuzi wake ingawa kuosha kwa maji ni bora zaidi. 70. Sehemu ya haja ndogo haitohariki isipokuwa kwa maji na kama ikioshwa katika kuru au maji yanayotiririka mara moja baada ya kumalizika mkojo inatosha, lakini kwa maji machache inalazimu kuiosha mara mbili na ni bora kuiosha mara tatu. 71. Inajuzu kutoharisha sehemu ya haja kubwa kwa mawe, changarawe na mfano wake yakiwa makavu na tohara, na hakuna mushikeli ikiwa yana unyevuvyevu kidogo kiasi kwamba hauhamii kwenye sehemu ya haja kubwa, lakini ni wajibu afute kwa mawe yasiyopungua matatu na asafishe sehemu ya haja kubwa mara moja au mara mbili. 72. Kwa tahadhari yasunna mawe yawe matatu au matambara ya kufutia sehemu ya haja kubwa yawe matatu, jiwe kubwa lenye pembe tatu au tambara refu moja linatosha, na kama najisi haitatoka kwa vipande vitatu inamlazimu aongeze ambayo yatatosha kusafisha na kuondoa najisi yote, na hakuna mushikeli katika kubakia chembechembe ndogo sana zisizoonekana. 73 Haijuzu kufutia sehemu ya haja kubwa kwa vitu ambavyo ni wajibu kuviheshimu, mfano karatasi ambayo ina jina la Mwenyezi Mungu, manabii au mawasii (as) ,na kwa tahadhari ya sunna asifute kwa mifu15
Al-Masailul Islamiyah pa wala kwa vinyesi vya wanyama, kama ataondoa haja kubwa kwa vitu hivi ataasi na kupata dhambi, lakini dhahiri ni kwamba sehemu ya haja kubwa itatoharika. 74. Akipata shaka kuwa sehemu ya haja kubwa imetoharika au laa, ni wajibu atoharishe, ama ikiwa ni kawaida yake kutoharisha sehemu ya haja ndogo au kubwa haraka,basi ni kwa tahadhari ya sunna atoharishe. 75. Akishuku baada ya swala kwamba alitoharisha sehemu ya haja kubwa kabla ya swala au laa, swala yake aliyoswali itasihi, lakini inamlazimu kutoharisha kwa ajili ya swala zinazofuata, na kama atashuku ndani ya swala ni wajibu akate swala na kutoharisha, ama ikiwa ni ada yake kutoharisha sehemu ya haja mara tu baada ya haja basi itakuwa ni sunna kufanya tahadhari kwa kutoharisha, na wala hatakakata swala kwa ajili ya tahadhari hii ya sunna.
ISTIBRAA 76. Istibraa ni kitendo cha sunna wanachokifanya wanaume baada ya kumaliza haja ndogo ili kuwa na yakini ya kutobakia mkojo katika njia yake, na ina viwango, vilivyo bora zaidi ni kutoharisha sehemu ya haja kubwa kwanza kama atakwenda haja kubwa baada ya mkojo kukatika, kisha anakamua kwa kidole cha mkono wake wa kushoto kuanzia katika njia ya haja kubwa hadi kwenye shina la dhakari mara tatu kwa nguvu, kisha anaweka kidole gumba juu ya dhakari na kidole cha shahada chini yake kisha anakamua kwa nguvu hadi kwenye kichwa cha dhakari mara tatu. 77. Maji yanayotoka kwa mwanaume baada ya kumchezea mwanamke yanayoitwa madhii ni tohara, vivyo hivyo maji yanayotoka baada ya manii ambayo huitwa wadhii ni tohara, vilevile maji yatokayo aghlab baada ya mkojo ambayo huitwa wadii ni tohara kama hayajapatwa na 16
Al-Masailul Islamiyah mkojo. Na mtu akifanya istibrai baada ya mkojo kisha akatokwa na maji na akashuku kuwa ni mkojo au moja kati ya maji haya yaliyotajwa basi yatakuwa tohara. 78. Mtu akishuku je, amefanya istibrai baada ya haja ndogo au laa, na akatokwa na majimaji hajui ni najisi au ni tohara, hukumu yake ni najisi na udhu wake unabatilika, lakini kama ni kawaida yake kufanya istibrai baada ya kukojoa. Au akishuku kuwa amefanya istibrai kwa njia sahihi au laa, na yakatoka kwake maji maji hajui ni tohara au laa, yatakuwa tohara na udhu wake haubatiliki. 79. Ambaye hajafanya istibarai akiwa na yakini baada ya kupita muda baada ya kukojoa kwamba hakuna mkojo katika njia ya mkojo, kisha akaona maji maji na akashuku kuwa ni tohara au laa, yatakuwa tohara na udhu wake hautabatiliki. 80. Kwa kuacha istibrai maji maji yanayoshukiwa kuwa ni mkojo yatahukumiwa kuwa ni najisi na yanatengua tohara, hata kama kuacha kwake ni kwa dharura au kwa kughafilika. 81. Mwanamke hafanyi istibrai kutokana na mkojo, kama ataona maji maji na akakushuku kuwa ni tohara au laa, basi yatakuwa tohara na udhu wake au josho halitobatilika lake.
ADABU ZA KWENDA HAJA 82. Ni sunna wakati wa kujisaidia akae katika sehemu ambayo haonwi na mtu yeyote, na atangulize mguu wa kushoto wakati wa kuingia chooni, na atangulize mguu wa kulia wakati wa kutoka chooni.
83. Ni makuruhu kuelekea jua na mwezi wakati wa kujisaidia, lakini kara17
Al-Masailul Islamiyah ha hii hutoweka akifunika tupu yake kwa kitu, na vivyo hivyo ni makuruhu katika hali ya kujisaidia kuuelekea upepo, na ni makuruhu kujisaidia katika njia, vichochoro, mbele ya majumba, chini ya miti ya matunda, kula wakati wa kujisaidia, kukaa muda mrefu chooni na kujitoharisha mahali pa haja kubwa kwa mkono wa kulia na vile vile kuongea katika hali ya kujisaidia, na hakuna mushkeli kumtaja Mungu au kuongea kwa dharura. 84. Ni makuruhu kukojoa katika ardhi ngumu, katika mashimo ya wadudu na katika maji hususan ikiwa yametuama, vivyo hivyo ni makuruhu kukojoa kwa kusimama. Lakini si makuruhu kukojoa wima katika sehemu ambazo zimewekwa marumaru na changarawe zake. 85. Ni makuruhu kubana mkojo au haja kubwa, bali ni haramu ikiwa kubana huku kutadhuru mwili madhara makubwa. 86. Ni sunna mtu kujisaidia haja ndogo kabla ya swala kisha atawadhe, au kuoga na kuswali, vivyo hivyo ni sunna kujisaidia haja ndogo kabla ya kulala, kabla ya kujaamiiana na baada ya kutoka manii. NAJISI 87. Najisi ni kumi na moja:1. mkojo 4. mzoga 7. nguruwe 10. Pombe za kisasa 2. kinyesi 5. damu 8. kafiri 11. jasho la mnyama anayekula vinyesi 3. manii 6. mbwa 9. pombe za kienyeji 1 na 2 :Mkojo na kinyesi 88. Mkojo kuliwa kuliwa tohara.
na kinyesi cha binadamu na cha kila mnyama aliye haramu ni najisi, lakini mkojo na kinyesi cha mnyama aliye haramu ambaye damu yake haitoki kwa kasi wakati wa kuchinjwa ni Na vivyo hivyo mfano wa mbu, nzi -wanyama- wasio na 18
Al-Masailul Islamiyah nyama. Ama mkojo na kinyesi cha mnyama aliye halali kuliwa ni tohara. 89. Ni sunna kujiepusha na vinyesi vya ndege wasioliwa na hasa mkojo wa popo na kinyesi chake. 90. Mkojo na kinyesi cha mnyama anayekula vinyesi ni najisi, vivyo hivyo mkojo na kinyesi cha mnyama aliyeingiliwa na binadamu, vile vile mkojo wa mnyama aliyenyonya kwa nguruwe na kunawiri kutokana na maziwa yake. 3:Manii 91. Manii ya mwanadamu na ya mnyama anayetoka damu kwa kasi wakati wa kuchinjwa ni najisi. 92. Maji ya aina tatu madhii, wadhii na wadii ni tohara. 4:Mzoga 93. Mzoga wa mnyama mwenye damu itokayo kwa kasi ni najisi, sawa sawa amejifia mwenyewe au amechinjwa kwa njia isiyokuwa ya kisharia. Samaki ambapo hana damu itokayo kwa kasi mzoga wake ni tohara hata kama akifia kwenye maji. 94. Vitu visivyokuwa na uhai vinavyotokana na mnyama mfano sufi, nywele, manyoya, mifupa na meno, vyote ni tohara isipokuwa vinavyo tokana na mbwa na nguruwe. 95. Ikiwa sehemu ya mwili wa mwanadamu hai au mnyama hai mwenye kutoka damu kwa kasi wakati wa kuchinjwa itajitenga, basi nyama au kipande au kitu kingine chenye uhai ni najisi. 96. Magamba mepesi yanayojitokeza kwenye midomo au mahali pengine 19
Al-Masailul Islamiyah mwilini na ikiwa wakati wa kuanguka kwake umewadia, ni tohara japo akiyang’oa - mtu - kwa hiyari, lakini ni bora kujiepusha kwa ihtiyati ya sunna na magamba haya endapo yatang’olewa kabla ya wakati wa kuanguka kwake. 97. Yai litokalo tumboni mwa kuku aliyekufa, endapo gamba lake la juu litakuwa gumu ni tohara, lakini ni wajibu kulitoharisha kwa tahadhari. 98. Kitoto kichanga cha kondoo au mbuzi kikifa kabla hakijala nyasi, khamira (mazima aliyoyanyonya ambayo yako katika fuko la chakula) iliyomo tumboni mwake ni tohara, lakini ni lazima kuitoharisha kwa tahadhari. 99. Dawa ya mitishamba ya rojorojo, manukato, mafuta, rangi na sabuni zinazoagizwa toka nchi zisizokuwa za kiislamu, hukumu yake ni tohara maadamu tu mtu hajapata yakini ya unajisi wake. 100. Nyama, mafuta na ngozi zinazouzwa katika soko la waislamu ni tohara, vivyo hivyo vilivyo katika miliki ya waislamu, lakini ikifahamika kuwa mwislamu amevichukua kwa kafiri bila ya kuchunguza kuwa ni kutoka kwa mnyama aliyechinjwa kisheria au laa, basi ni najisi. 5. Damu. 102. Damu ya binadamu na kila mnyama atokaye damu kwa kasi wakati wa kuchinjwa ni najisi, na damu ya mnyama asiyetoka damu kwa kasi wakati wa kuchinjwa mfano samaki, mbu au ambaye anashukiwa, asiyejulikana kuwa anatoka damu kwa kasi wakati wa kuchinjwa au laa, kama vile nyoka ni tohara. 103. Mnyama ambaye ni halali kuliwa akichinjwa kisharia na ikatoka 20
Al-Masailul Islamiyah damu inayotakiwa kutoka, damu iliyobakia ndani ni tohara na inajuzu kula nyama yake bila ya kuiosha kutokana na damu, isipokuwa shingo yake inapasa kuiosha halafu iliwe, lakini ikiwa kiasi cha damu kutoka nje kitarejea hadi ndani ya nyama kutokana na kupumua, au kichwa cha mnyama kuwa juu wakati wa kuchinja, damu hiyo itakuwa najisi, ni wajibu kufanya tahadhari kufanya tahadhari kwa kujiepusha na damu iliyobakia ndani ya mnyama aliye haramu kuliwa kama atachinjwa kisheria. 104. Damu chache ambayo inaonekana katika yai la kuku ikiwa ganda lake jepesi la juu halijapasuka, ikiwezekana kuitoa damu hiyo bila ya kuchanganyika na yai basi yai litakuwa tohara. 105. Damu chache ionekanayo wakati wa kukamua maziwa wakati mwingine inanajisisha maziwa – kwa tahadhari 106. Damu inayotoka baina ya meno ikichanganyikana na majimaji ya kinywa na kwisha ni tohara, lakini kwa tahadhari ya sunna asiyameze. 107. Damu ambayo inaganda chini ya ngozi kwa sababu ya pigo kali, kama haitosemekana kuwa ni damu basi ni tohara, na ikisemekana kuwa ni damu basi ni najisi, na katika hali hii ngozi ikichanika au ukucha ukitoboka inalazimu kutoa damu iliyoganda kwa ajili ya udhu na josho, kama kutolewa hakutakuwa na tabu, na kama kutasababisha adha inalazimu kuosha pembezoni mwake kwa namna ambayo haitasababisha kunajisika, kisha aweke kitambaa au mfano wake kisha anapaka juu ya kitambaa na anatayamamu vile vile kwa tahadhari. 108. Kama hawezi kutambua kuwa hii damu iliyo chini ya ngozi imeganda au ni nyama imekuwa katika hali hiyo kutokana na kupigwa basi itakuwa tohara. 109. Bonge la damu likitumbukia
katika chakula wakati kimechemka, 21
Al-Masailul Islamiyah katika chakula wakati kimechemka chakula chote kitanajisika na chombo chake vile vile, na mchemko, joto au moto sio katika vitu vinavyotoharisha. 110. Maji ya njano yanayoonekana pembezoni mwa jeraha wakati wa kukifungua kinapo pona, kama hatajua kuchanganyika kwake na damu ni tohara, vivyo hivyo utando unaokuwa juu ya jeraha wakati kinapopona na hufanya tabaka jeusi juu yake, hilo tabaka jeusi ni tohara. kwa istihala ÂŤ kubadilika.Âť 6 na 7 - Mbwa na nguruwe 111. Mbwa na nguruwe wa nchi kavu ni najisi hata nywele zao, mifupa yao ma makucha yao na unyevunyevu wao. Lakini mbwa na nguruwe wa majini ni tohara. 112. Wanyama wote walio haramu kuliwa ila mbwa na nguruwe inakubalika kuchinjwa, kwa maana kuwa kama watachinjwa kisheria watakuwa tohara ingawa hawatakuwa halali kuliwa. 8- Kafiri 113. Kafiri ni najisi, naye ni ambaye anakanusha kuwepo kwa Mwenyezi Mungu na anayemshirikisha au anaepinga utume wa Muhammad (saww), vivyo hivyo kila anayekanusha wajibu katika wajibu wa dini, mfano swala na saumu ambayo waislamu wanaizingatia kuwa ni sehemu ya dini kwa sharti kuwa inalazimu kukanusha kwake huko kumkanusha Nabii (saww), na awe anajua kuwa hii ni katika wajibu wa dini, vinginevyo haitohukumiwa kuwa ni kafiri ingawa ni sunna kufanya tahadhari kujiepusha naye. Na anayepinga siku ya kiyama na madhambi makubwa, wajibu, nasibi, ghulati na khawariji wao wako katika hukumu ya kafiri.
22
Al-Masailul Islamiyah 114. Ahlul- kitab, kama vile manaswara, mayahudi na majusi kwa - tahadhari ya wajibu ni kujiepusha nao katika sehemu zisizokuwa za dharura na shida, hata kama hawajanajisika kwa kunywa pombe, kula mizoga na nyama ya nguruwe au kutumia kwao najisi zingine. 115. Mwili wote wa kafiri hata nywele, kucha na unyevunyevu vyote ni najisi. 116. Ikiwa mzazi wa mtoto asiyebaleghe, mama yake, babu yake, bibi yake, wote wakiwa ni makafiri basi mtoto pia atakuwa najisi, au ikiwa mmoja wa hawa ni mwislamu basi mtoto atakuwa tohara. 117. Asiyejulikana kuwa ni kafiri au mwislamu akiwa katika nchi ya kiislamu basi ni tohara, na hukumu zote za Uislamu zitatekelezwa kwake, inajuzu kuoa mwislamu na kuzikwa katika makaburi ya waislamu. 118. Yeyote katika waislamu akimtukana Nabii (saww), Fatma Zahra au mmoja wa maimamu kumi na mbili au akiwafanyia uadui basi atakuwa ni najisi. 9 -Pombe 119. Pombe na kila kileo cha asili ya majimaji ni najisi hata kama atakigandisha kwa njia yoyote ile, ama kikiwa hakina asili ya majimaji mfano bangi na hashishi ni tohara hata kama kikitumbukizwa kitu humo ili iwe maji maji. 120. Polishi inayotumika kwa kupaka na kung’arisha milango, viti, meza n.k. kama haijathibitika kuwa ni kileo basi ni tohara. 121. Zabibu mbivu au maji ya zabibu mbivu ikichemka yenyewe, ni haramu kuila au kuinywa ni, lakini ni tohara na wala haijuzu kuitumia (kuila na kuinywa) ila ikiwa siki, vivyo hivyo inaharamishwa kuitu23
Al-Masailul Islamiyah mia ikiwa itachemshwa kwa njia ya kupikwa, na haijuzu kuitumia ila baada ya kupungua theluthi mbili kwa kuichemsha kwa moto.
122. Tende, zabibu kavu na kishimishi na juisi zake, ni halali kama zitachemka zenyewe ingawa kwa tahadhari ya sunna hususani katika zabibu na kishimishi ni kujiepusha kutumia. 10 - Bia. 123. Bia nacho ni kinywaji kinachotengenezwa kwa shairi ni najisi, lakini maji yanayochukuliwa kutoka kwenye shairi kulingana na maelezo ya daktari kwa ajili ya tiba na ambayo yanaitwa “maji ya shairi� vivyo hivyo shairi inayopikwa katika mchuzi na shurbati ni tohara. 11 - Jasho la mnyama anayekula vinyesi 124. Kwa tahadhari ni wajibu kujiepusha na jasho la mnyama aliyezoea kula vinyesi vya watu, na jasho la kila mnyama anayekula vinyesi vya watu. Jasho la janaba lililotokana na haramu 125. Jasho la janaba iliyotokana na haramu sio najisi ingawa ni bora kuchukua tahadhari, ni sawasawa jasho limetoka wakati wa jimai au baada yake, kwa mwanaume au kwa mwanamke, kwa zinaa au kwa liwati, kwa kumwingilia mnyama au kwa kufanya punyeto. Na punyeto ni mtu binafsi kukusudia kujitoa manii. 126. Mtu akimwingilia mke wake katika wakati ambao ni haramu kwake kumwingilia, mfano akimwingilia wakati wa funga ya mwezi wa Ramdhani au katika hedhi, kwa tahadhari ya sunna ajiepushe na jasho lake. 24
Al-Masailul Islamiyah 127. Mwenye janaba linalotokana na haramu akitayamamu badala ya kuoga kutokana na udhuru, kisha akatoka jasho baada ya kutayamamu, inajuzu kwake kuswali pamoja na nalo, lakini udhuru wake ukiisha kisha akatoka jasho haifai kwake kuswali na jasho hilo na ni juu yake kujiepusha nalo kwa tahadhari ya sunna hadi aoge. 128. Akipata janaba kwa njia ya haramu kisha akamwingilia mke wake kwa njia ya halali, kisha akapata janaba kwa njia ya haramu, basi kwa tahadhari ya sunna - ajiepushe na jasho lake vile vile.
NJIA ZA KUTHIBITISHA NAJISI 129. Najisi inathibitika kwa moja ya njia tatu:Mtu binafsi kuwa na yakini kwa kunajisika kitu, akidhani kunajisika kitu, hailazimu kwake kujiepusha nacho, hakuna mushkeli kula katika migahawa na magenge ambayo watu wamezoea na wanakula humo ambao hawajali tohara na najisi ikiwa hajapata yakini kuwa chakula anachopewa ni najisi. Mmiliki au mtumiaji wa chombo anapotoa taarifa juu ya unajisi wa kitu, kama vile mke au mtumishi akisema chombo hiki au kitu hiki kilichopo mkononi na chini ya uangalizi wake ni najisi, basi inamlazimu kujiepusha nacho, na hii inaitwa habari ya mmiliki. Kutoa taarifa watu wawili kwa unajisi wa kitu, vivyo hivyo akitoa taarifa mtu mmoja mkweli kuhusu unajisi wa kitu inamlazimu kujiepusha nachokwa ilivyo na nguvu zaidi. 130. Ikiwa hajui unajisi wa kitu au utohara wake kwa kutokujua kwake mas’ala, mfano kutojua kuwa jasho la janaba ya haramu ni najisi au ni tohara, ni wajibu wake aulize ili ajue hukumu, lakini akipata shaka juu ya unajisi wa kitu au kutokuwa kwake najisi pamoja na kujua kwake mas’ala, mfano akishuku kuwa hii ni damu au sio damu? Au 25
Al-Masailul Islamiyah akiwa hajui kuwa hii ni damu ya kiroboto au damu ya binadamu, basi itakuwa tohara. 131. Kitu najisi ambacho anashaka kuwa kimekuwa tohara au laa kitabaki kuwa ni najisi, na kitu tohara ambacho anashuku kuwa kimenajisika au laa ni tohara, na kama anaweza kujua utohara wake au unajisi wake haitomlazimu kuchunguza. 132. Akijua kuwa moja kati ya vyombo viwili au nguo mbili imenajisika, na zote mbili alikuwa anazitumia na wala hajui ipi ndio imenajisika, ni wajibu ajiepushe nazo zote, lakini ikiwa hajajua kwa mfano, kuwa nguo yake ndio imenajisika au nguo ambayo haitumii kabisa na ambayo ni nguo ya mwingine, haitomlazimu kujiepusha na nguo yake.
NAMNA YA KUNAJISIKA VITU VILIVYO TOHARA 133. Kitu najisi kikikutana na kitu tohara na vyote viwili au kimoja wapo kina unyevunyevu kiasi kwamba unyevunyevu wa kimoja wapo unahamia kwa kingine, kitu tohara kinanajisika, ikiwa unyevunyevu ni mdogo sana kiasi kwamba hausambai kwa kingine hakitonajisika. 134. Kitu tohara kikikutana na kitu najisi na akashuku je vyote au kimoja wapo kilikuwa na unyevunyevu, kitu tohara hakitanajisika. 135. Kama kuna vitu viwili haijulikani kipi ni najisi na kipi ni tohara, kimoja wapo kikigusa kitu tohara chenye unyevunyevu, kitu tohara hakitanajisika, na kama kitu tohara kitagusa vyote viwili kitanajisika. 136. Ardhi, kitambaa na mfano wake kikiwa kimeloana inanajisika sehe26
Al-Masailul Islamiyah mu ambayo inagusana na najisi, na iliyobaki itakuwa tohara vivyo hivyo tikiti maji, tango n.k. 137. Mafuta, jamu na mfano wake ikiwa kwa namna ambayo kama itachukuliwa, kiasi nafasi iliyopo itajaa haraka basi itanajisika yote kwa kukutana tu na najisi, na ikiwa nafasi iliyopatikana kwa kupunguza haijai haraka basi hainajisiki kwa kupatwa na najisi, isipokuwa sehemu iliyokutana na najisi hadi nafasi hiyo ijae baadae, hivyo kinyesi cha panya kikidondokea katika hali hii ya pili itanajisika sehemu iliyogusana na kinyesi tu na iliyobaki itakuwa tohara. 138. Nzi au anayefanana naye katika wadudu akitua juu ya kitu najisi chenye unyevu nyevu, kisha akaruka na kutua juu ya kitu kingine tohara, chenye unyevunyevu kitu tohara kina najisika kama itajulikana kuwa nzi ana chembechembe za viini vya najisi,vivyo hivyo akipata yakini juu ya kugandamana najisi katika mguu wa mnyama kisha akapata shaka kuwa imeondoka au laa, ama ikiwa hakujua basi ni tohara. 139. Sehemu ya mwili ikinajisika na ikawa na jasho, kisha jasho najisi likatiririka kwenda sehemu nyingine, sehemu iliyofikiwa itanajisika, na ikiwa halitiririka hadi sehemu nyingine basi sehemu ya mwili iliyobaki itakuwa tohara. 140. Kamasi na makohozi yanayotoka puani na mdomoni yakiwa na damu sehemu iliyogusana na damu ni najisi na iliyobaki ni tohara, kikitoka kitu nje ya pua au kinywa sehemu ambayo anajua kuwa imegusana na sehemu iliyonajisika ni najisi, na sehemu ambayo anashuku katika kukutana na sehemu iliyonajisika itakuwa tohara. 141. Birika ambalo ndani yake kuna maji na chini yake kuna tundu ikiwekwa juu ya ardhi iliyonajisika, na maji yatokayo kwenye lile tundu yanajikusanya chini yake kiasi cha kuzingatiwa kuwa maji yaliyo 27
Al-Masailul Islamiyah ndani ya birika na yale ya chini ni mamoja yaliyo ndani ya birika pia yatakuwa yamenajisika. Na yakitiririka juu ya ardhi au yakipenya humo, endapo tobo la birika likiwa limeungana na ardhi iliyonajisi kiasi chakuwa inazuwia kububujika kwa majimaji ya ndani ya birika, yatahukumiwa kuwa yamenajisika pia, lakini ikiwa tundu haikuungana na ardhi iliyonajisika na wala hayahesabiki maji yaliyomo ndani ya birika na yaliyo nje ni mamoja au maji yaliyo katika birika yakitoka kwa nguvu na msukumo, yaliyo ndani ya birika hayatokuwa najisi. 142. Mtu akiingiza kitu mwilini na kikakutana na najisi, baada ya kukitoa kikiwa hakikuchafuka na najisi, kitakuwa tohara. Akiingiza bomba mahali pa kutokea haja kubwa au akidunga sindano au kisu na kitu mfano wa viwili hivyo mwilini na baada ya kukitoa hakikuchafuka na najisi hakitokuwa najsi, na vivyo hivyo mate au kamasi yakutanapo na damu mdomoni na puani, kisha yakitoka bila ya kuchafuka na damu yatakuwa tohara. 143. Kitu kilichonajisika kinanajisisha kama vile kiini cha najisi isipokuwa haitolazimu juu yake hukumu zake zote mfano kitu kikinajisika kwa mkojo, inalazimu kurudiarudia kukitoharisha kama maji ni machache na wala hailazimu kurudia rudia kwa kitu kilichokutana na kitu kilichonajisika kwa mkojo.
MAS’ALA 144. Inaharamishwa kuitia najisi hati na maandishi ya Qur’an tukufu na ni wajibu kuondoa najisi kwayo haraka pindi inaponajisika, lakini likinajisika jalada lake ni wajibu kulitoharisha ikiwa kuacha kwake kunalazimu kuidharau, vivyo hivyo inaharamishwa kutia najisi (jalada lake) na ni wajibu kutoharisha haraka msikiti, sehemu takatifu, turba ya Imamu Hussein na hukumu ni hiyo hiyo katika turba ya Mtume 28
Al-Masailul Islamiyah Mtukufu na Maasumina wengine kwa tahadhari. 145. Ni haramu kuweka Qur’an juu ya najisi mfano damu, na mzoga hata kama ni mkavu kama itahesabiwa kuwa ni kudharau Qaur’an na ni wajibu kuiondoa katika vitu hivyo haraka. 146. Inaharamishwa kuiandika Qur’an kwa wino najisi hata kama ni herufi moja na kama akiandika ni wajibu kuifuta kwa kifuto au mfano wake. 147. Ni haramu kumpa kafiri Qur’an tukufu kama hiyo itasababisha kuidharau Qur’an na ni wajibu kuichukua Qur’an kutoka kwake. 148. Karatasi ya Qur’an tukufu au kitu kingine ambacho ni wajibu kukiheshimu kama vile karatasi ambayo imeandikwa jina la Mwenyezi Mungu, Nabii, Imamu au Fatma Zahra likiangukia chooni ni wajibu kulitoa na kulitoharisha hata kama hilo litalazimu kutoa gharama, na kama haiwezekani kuitoa basi kwa tahadhari ya wajibu aache kukitumia choo hicho hadi apate yakini ya kuyeyuka na kumalizika maandishi ya karatasi hiyo, vivyo hivyo turba ya Imamu Huseini ikiangukia chooni na ikashindikana kuitoa ni wajibu kuacha kujisaidia katika choo hicho hadi turba iyeyuke na kumalizika. 149. Ni haramu kula na kunywa najisi au kilichonajisika kama vile maji yaliyonajisika, vivyo hivyo inaharamishwa kumlisha mwingine hata kama ni mtoto lakini mtoto mwenyewe akila najisi si wajibu kumzuia ikiwa najisi hiyo haina madhara kwake. 150. Hakuna mushakeli kuuza au kuazima kitu kilichonajisika ambacho inawezekana kukitoharisha ikiwa muuzaji au mwazimishaji atatoa taarifa juu ya unajisi wake. 151. Mtu akiona mtu anakula najisi au anaswali na nguo najisi haimlazimu kumwambia. 29
Al-Masailul Islamiyah
152. Ikiwa sehemu ya godoro, mto au nyumba yake ni najisi na akaona mgusano wa nguo za wanaoingia katika nyumba hiyo au miili yao au kitu kingine na sehemu najisi nayo ikiwa na unyevunyevu ni lazima kwake kuwaeleza kwa tahadhari ya wajibu ikiwa wamekuwa wageni wake na wamekuja kwa wito wake. 153. Mwenye nyumba akijua wakati wa kula unajisi wa chakula ni wajibu wake kuwaeleza wageni wake, ama akijua hilo mmoja wa wageni sio lazima kwake kuwaeleza wengine.
VINAVYOTOHARISHA 154. Vinavyotoharisha vitu vilivyonajisika ni kumi na mbili:1. Maji 5. Kupungua theluthi mbili za juisi ya zabibu mbivu 2. Ardhi 6. Kuhama 8. Kuondoka kiini cha najisi 3. Jua 7. Uislamu 9. Kumtoharisha mnyama anayezoea kula kinyesi 4. Kubadilika 10. Kufuata 11. Kutoweka kwa mwislamu 12. Kutoka damu kiwango kinachojulikana kwa mnyama. MAJI 155. Maji yanatoharisha vitu kwa sharti nne:1- Yawe halisi 2- Yawe tohara 3- Yasiwe mudhafu wakati wa kutoharisha kitu kilicho najisika 4- Kusibaki baada ya kutoharisha kitu kilichonajisika kiini cha najisi 156. Utoharishaji wa vitu vilivyonajisika kwa maji machache unasharti zingine maelezo yake yatakuja baadae.
30
Al-Masailul Islamiyah 157. Ni wajibu katika kutoharisha chombo kilichonajisika kioshwe kwa maji machache mara tatu kwa tahadhari, na inatosha kukiosha mara moja katika kuru au maji yanayotiririka lakini chombo kilicho lambwa na mbwa au alichonywea humo ni wajibu kwanza kukisugua kwa mchanga tohara kisha kukitoharisha katika kuru au maji yanayotiririka mara mbili ama chombo kilicho dondokewa na ute wa mbwa au maji maji yake ni bora kukisugua kwa mchanga na kukiosha mara tatu. 158. Ikiwa mdomo wa chombo ambacho mbwa amelamba ni mfinyu na ikashindikana kusugua ndani ya chombo kwa udongo itamlazimu ikiwezekana kuzungusha tambara kwenye kijiti na kusugua ndani ya chombo kwa mchanga kwa njia hiyo hiyo ikishindikana anamwagia mchanga katika chombo na kutikisa kwa nguvu hadi mchanga ufike sehemu zote za ndani. 159. Chombo ambacho kimelambwa nguruwe au kunywa humo ni wajibu kukiosha kwa maji machache mara saba na inatosha kukiosha katika kuru au maji yanayotiririka mara moja na wala hailazimu kusugua kwa mchanga ingawa ni bora kusugua kwa mchanga. 160. Ikitakiwa kusafisha chombo kilichonajisika kwa pombe kwa maji machache inatosha mara tatu ingawa kwa tahadhari ni bora zaidi kukiosha mara saba kwa maji machache. 161. Mitungi na vyombo vya urembo vilivyotengenezwa kwa udongo ulionajisika au ambavyo maji najisi yamepenya ndani yake vikiwekwa kwenye kuru au maji yanayotiririka na maji yakaenea sehemu zote vitakuwa vimetoharika na ikitakiwa kutoharishwa ndani yake pia inalazimu vibakie katika kuru au maji yanayotiririka kwa muda ili maji yaenee sehemu zote za ndani. 162. Chombo kilicho najisi inawezekana kukitoharisha kwa maji 31
Al-Masailul Islamiyah machache kwa njia mbili:1. Kwa kujaza chombo maji kisha anayamwaga mara tatu. 2. Au kuweka kiasi cha maji kisha anayazungusha humo kiasi cha kufika sehemu zote zilizonajisika kisha anayamwaga na anarudia mara tatu. . 163. Kitu kikinajisika kwa mkojo wa mtoto mchanga ambaye hajaanza kula chakula na hajanyonya maziwa ya nguruwe au kafiri, kikimwagiwa maji mara moja kiasi kwamba maji yanafika sehemu zote zilizonajisika kinatoharika lakini ni sunna kufanya tahadhari kwa kumwgia maji mara mbili
2-Ardhi 164. Ardhi inatoharisha nyayo na viatu kwa sharti tatu :1. Ardhi iwe tohara 2. Iwe kavu 3. Kiini cha najisi kiondoke kama vile damu, mkojo au kilichonajisika kama vile udongo ulionajisika ambao umegandamana katika sehemu za nyayo au viatu kwa kutembea juu ya ardhi au kusugua juu yake kama ambavyo inamlazimu katika kutoharisha kwa ardhi, ardhi iwe ni udongo au jiwe, vile vile sehemu ya chini ya nyayo au kiatu haitohariki kwa kutembea juu ya godoro au jamvi, ama jiwe, changarawe, sementi iliyotengenezwa kwa changarawe hukumu yake ni hukumu ya ardhi inatoharisha. 165. Ni bora katika kutoharisha chini ya nyayo au viatu atembee juu ya ardhi hatua kumi na tano au zaidi hata kama najisi itaondoka kwa hatua chache kuliko hizo.
3 - Jua 166. Jua linatoharisha ardhi, majengo na mfano wake kama vile milango, 32
Al-Masailul Islamiyah madirisha ya majengo yakinajisika vivyo hivyo hutoharisha misumari iliyopigiliwa ukutani na hiyo ni kwa masharti matano baadhi yake ni kwa tahadhari:1. Kitu najisi kiwe na unyevuunyevu kiasi kikigusana na kitu unyevu nyevu wake unahamia kwake, kikiwa kikavu inalazimu kukiloanisha ili kikaushwe na jua. 2.Kiini cha najisi kiondoshwe kabla ya kupigwa jua. 3. Jua lisizuiliwe na kitu, kama jua litazuiliwa na pazia, mawingu n.k na likakausha (kitu hicho) hakitohariki, lakini kama mawingu au pazia ni jepesi sana kiasi halizuii jua hakuna mushkeli. 4. Jua peke yake likaushe kitu najisi, jua halitotoharisha kama litasaidiwa na upepo katika kukausha lakini hakuna mushikeli ikiwa upepo ni mdogo sana kiasi inasemwa kimekaushwa na jua. 5. Jua likaushe jengo ambalo najisi imepenya kwa mara moja yaani kwa mchomozo mmoja, ama jua likipiga juu ya ardhi na jengo lililonajisika na likikausha nje ya jengo na ardhi kisha likapiga mara ya pili na likakausha ndani yake itatoharika nje tu na ndani patabaki kuwa najisi.
4. Kubadilika 167. Kitu najisi kikibadilika kiasi kwamba kinaonekana katika sura ya kitu tohara kinakuwa tohara na hii inaitwa “kubadilika�ni sawa kubadilika ni kwa kiini cha najisi au kitu kilichonajisika mfano ubao ulionajisi kubadilika na kuwa majivu au mbwa kuzikwa katika ardhi ya chumvi na kugeuka chumvi lakini hakitohariki ikiwa uhakika wa kitu haujabadilika mfano ngano kuwa unga au kutengenezwa mkate au maziwa yaliyonajisi kutengenezwa jibini au mgando. 168. Pombe ikibadilika yenyewe na kuwa siki au kwa kubadilishwa mfano kuweka siki au chumvi humo inakuwa tohara. 169. Siki iliyotengenezwa kwa zabibu mbivu, kishimishi au tende najisi ni najisi kwa tahadhari ya wajib 33
Al-Masailul Islamiyah
5 - Kupungua theluthi mbili za juisi ya zabibu mbivu 170. Maji ya za bibu mbivu hayanajisiki ikiwa yatachemshwa kwa moto lakini ni haramu kuyanywa, na yakichemka na kupungua theluthi mbili na ikabaki theluthi moja ni halali kuinywa, lakini ikichemka yenyewe haiwi halali kuinywa isipokuwa ikigeuka siki. 171. Zikipungua theluthi mbili za juisi ya zabibu bila ya kuchemshwa kama iliyobaki itachemka yenyewe au kwa moto ni haramu kuinywa na ikitakiwa kuwa halali inalazimu kuchemshwa hadi ipungue theluthi mbili. 172. Punje ya zabibu ikitumbukia katika kitu kilichochemshwa kinachochemka kwa moto na punje ikichemka pamoja nacho sio wajibu kujiepusha nacho. 173. Ikitakiwa kutengenezwa jamu katika viungu na masufuria tofauti tofauti hakuna mushikeli katika kutumia mwiko katika chungu ambacho juisi yake imechemka katika viungu ambavyo havijachemka na vikichemka vyote asitumie mwiko kwa sababu ya uharamu -katika viungu ambavyo havijapungua theluthi mbili kwenye viungu ambavyo vimepungua thelutghi mbili pamoja na kutobadilika, vinginevyo hakuna mushkeli 6 - Kuhama 174. Inatoharika damu ya binadamu au mnyama anayetoka damu kwa kasi wakati wa kuchinjwa ikihama kwenda katika mwili wa mnyama asiyetoka damu kwa kasi na ikahesabika kuwa ni katika damu yake na hii inaitwa “kuhama�, ama damu ambayo anainyonya luba kwa mwanadamu ambapo haitwi damu ya luba bali damu ya binadamu 34
Al-Masailul Islamiyah inakuwa ni najisi. 175. Mtu akiua kunguni kwenye mwili wake na hajui kuwa damu iliyotoka ya kunguni au ni ambayo ameinyonya kutoka kwake basi ni tohara, vivyo hivyo akijua kuwa ni katika damu ya kunguni lakini imeshakuwa ni sehemu ya mwili wake, ama ikiwa muda wa kuinyonya na kumuuwa kwake ni mchache sana kiasi kwamba inasemwa kuwa hii damu ni damu ya binadamu au haijulikani kuwa ni damu ya kunguni au damu ya binadamu itakuwa najisi kwa tahadhari. 7 - Uislamu 176. Kafiri akitamka shahada yaani akisema “Ash hadu an laa ilaaha ila llah wa ash hadu anna Muhammadan rasulullah� anakuwa mwislam. Mwili wake, mate yake, makamasi yake na jasho lake vinatoharika baada ya kuslim. Lakini ikiwa kuna kiini cha najisi katika mwili wake wakati wa kusilimu kwake itamlazimu kuondoa najisi na kutoharisha sehemu yake bali kiini cha najisi kikiondoka kabla ya kusilimu kwake kwa tahadhari ya sunna atoharishe sehemu iliyonajisika. 177. Kafiri akitamka shahada mbili na wala haijulikani kuwa uislamu umeingia katika moyo wake au laa ni tohara lakini ikijulikani kuwa uislam haujaingia moyoni ni najisi lakini mnafiki ambaye hajasilimu kwa moyo lakini anatekeleza uislamu kivitendo ni tohara. 8. Kufuata 178. Kufuata: Ni kutoharika najisi kwa njia ya kutoharika kitu kilichonajisi kama vile kutoharika watoto kafiri wasiobaleghe kwa kusilimu mmoja wa wazazi wawili au babu na bibi. 179. Pombe ikiwa siki chombo chake kinatoharika kwa kufuata kwake hadi sehemu iliyofikia pombe vile vile kifuniko, kitambaa kina35
Al-Masailul Islamiyah chowekwa kwenye mdomo wa chombo kama kitalowana kwa unyevunyevu huo lakini sehemu ya nje ya chombo hicho ikilowana kwa pombe hiyo- kwa tahadhari ya sunna- ni kujiepusha nacho baada ya kugeuka siki. 180. Ubao au jiwe ambalo amelazwa juu yake maiti na nguo ambayo inafunika mwili wake na mkono unaomuosha vyote vinatoharika baada ya kukamalizika josha. 181. Anayetoharisha kitu mkono wake unatoharika baada ya kutoharika kitu hicho kilichonajisika. 182. Maji yanayobaki katika nguo au mfano wake baada ya kuitoharisha kwa maji machache na baada ya kutengana na maji ya kuoshewa ni tohara. 9. Kuondoka kiini cha najisi 183. Mwili wa mnyama unatoharika - na unajumuisha viungo vyote vya mwili wa mnyama hadi mdomo kwa upande wa ndege- kwa kuondoka najisi kwake ikitapakaa najisi mfano damu au kilichonajisika mfano maji, kisha kiini cha najisi au kilichonajisika kikaondoka unatoharika, vivyo hivyo inatoharika sehemu ya ndani ya mwanadamu kama vile tumbo, ndani ya pua na kinywa kwa kuondoa kiini cha najisi kwayo, damu ikitoka baina ya meno na ikamalizika katika maji maji ya kinywa haitomlazimu kutoharisha ndani ya kinywa vivyo hivyo meno ya bandia yakinajisika ingawa ni bora zaidi kuyatoharisha. 184. Vumbi au mchanga najisi ukiangukia kwenye nguo au godoro au mfano wake kisha akakung’uta au kutikisa kwa namna ambayo vumbi najisi inaondoka kwa (kufanya hivyo) itakuwa tohara. 10. Kumtoharisha mnyama anayekula vinyesi 36
Al-Masailul Islamiyah
185.Mkojo na kinyesi cha mnyama - aliyezoea kula vinyesi vya binadamu - ni najisi na ikitakiwa kumtoharisha ni lazima kumzuia mnyama huyo kwa muda kutokana na kula vinyesi kiasi ambapo hatoitwa mnyama anayekula vinyesi, na alishwe malisho tohara kwa muda huo. 186. Ngamia anazuiliwa siku arobaini, ng’ombe siku thelathini, kondoo na mbuzi siku kumi, bata siku saba au siku tano na kuku ni siku tatu, na mnyama atazuiwa kula najisi na alishwe chakula tohara katika muda huu na lau ikithibiti anuani ya(mnyama mla kinyesi) baada ya muda huu pia ni lazima azuiwiliwe kula najisi kwa muda mwingine ili asiitwe baada ya muda huo - mnyama anayekula kinyesi. 11. Kutoweka kwa mwislamu 187. Mwili wa mwislamu ukinajisika au nguo yake na kitu chake kingine kama vile vyombo, godoro n.k. ambavyo viko katika milki yake kisha akatoweka pamoja na vitu hivyo, vitu hivi vinahukumiwa kuwa ni tohara kama yatatimia masharti sita baadhi yake ni kwa tahadhari:1. Mwislamu atapaswa aitakidi unajisi wa kitu hicho ambacho kimetia najisi mwili wake au nguo yake n.k, ikiwa itagusa nguo yake au mwili wake maji ya zabibu iliyochemka naye haitakidi kuwa ni najisi kisha akatoweka basi kutoweka(kughibu) kwake hakutoharishi. 2. Mwislamu Ajue kufika najisi kwenye mwili wake au nguo yake au kinacho shabihiana na hivyo. 3. Mwislamu aonekane baada ya kutoweka kwake anatumia vitu hivyo katika amali ambazo zinatakiwa kuwa na tohara mfano kama anaswali kwa nguo hiyo iliyonajisika. 4. Mwislamu mwenyewe kutambua kuwa tohra inatakiwa katika amali 37
Al-Masailul Islamiyah hiyo ikiwa hatambui ulazima wa tohara kwa vazi la mweye kusali na akasali kwa nguo hiyo haiwezi kuzingatiwa kuwa nguo hiyo ni tohara kwa sabau ya kutoweka kwake. 5. Mwislamu huyo achukue jukumu la kutoharisha kitu hicho, akipata yakini kwamba hajakitoharisha kitu hicho hakitazingatiwa kuwa ni tohara, ama ikiwa hakuna tofauti baina ya tohara na najisi kwa mtazamo wa mwislamu huyo basi kukizingatia kuwa ni tohara wakati huo ni mahali pa mushikeli. 6. Mwislamu huyo awe baleghe - kwa tahadhari. 12. KUTOKA DAMU KWA KIWANGO KINACHOJULIKANA KWA MNYAMA 188. Mnyama aliyehalali kuliwa akichinjwa kwa njia ya kisharia na kutoka kwake damu kwa kiwango cha kawaida kinachojulikana, damu iliyobaki katika mwili wake itakuwa tohara.
MAS’ALA 189. Mtu binafsi kuwa na yakini kwamba kitu kilichokuwa najisi kimeshatoharika au wakitoa taarifa ya hilo watu wawiliwaadilifu inahukumiwa kuwa ni tohara, vivyo hivyo kama atatoa taarifa aliyetoharisha kitu kilichokuwa najisi kama atapata matumaini kwa kauli yake au ikiwa ndio mmiliki. 190. Mwakilishi wa mtu katika kutoharisha nguo yake kama atasema nguo hii imetoharika basi nguo hiyo itakuwa tohara. 191. Mwenye wasiwasi (mwingi) naye ni ambaye hapati yakini kwa utohara wakati wa kutoharisha kitu najisi inajuzu kwake kutosheka na dhana au afanye kama wanavyotoharisha watu wa kawaida kwa kitu najisi. 38
Al-Masailul Islamiyah
HUKUMU ZA VYOMBO 192. Chombo kilichotengenezwa kwa ngozi ya mbwa au nguruwe wa nchi kavu au mfu ni najisi na inaharamishwa kulia na kunywea humo, haifaikutawadhia wala kuogea na wala hakitumiki katika amali ambayo tohara ni sharti humo bali kwa tahadhari ya sunna asitumie ngozi ya mbwa au nguruwe au mfu hata kwa visivyokuwa vyombo. 193. Inaharamishwa kulia na kunywea katika vyombo vya dhahabu na fedha na kwa tahadhari ya sunna ni kuacha kuvitumia kabisa hata katika mapambo. 194. Chombo kilichopo katika milki ya asiyekuwa mwislamu ni tohara maadamu mtu hajapata yakini ya unajisi wake. 195. Hakuna mushikeli kutumia vyombo vilivyochovywa dhahabu na fedha.
UDHU 196. Yaliyo wajibu katika udhu ni: Nia, kuosha uso, kuosha mikono miwili, kupaka maji utosini na juu ya miguu miwili.
KUOSHA USO 197. Ni wajibu kuosha uso kwa mapana na marefu kuanzia kwenye maoteo ya nywele hadi mwisho wa kidevu, na upana ni sehemu iliyozungukwa na kidole gumba na kidole cha kati na kama hajaosha sehemu katika kiasi hicho udhu wake utabatilika na ili apate yakini ya kufika maji hadi kwenye kiasi hicho inamlazimu kuosha sehemu ya pembezoni mwake vile vile. 39
Al-Masailul Islamiyah
198. Kama uso wa mtu au kiganja chake ni kikubwa au kidogo kuliko maumbile ya watu wa kawaida inamlazimu atazame kiwango wanachoosha nyuso zao watu wa umbile la kawaida na mikono yao kisha aoshe, hukumu ni hiyo hiyo ikiwa nywele za utosi wa kichwa chake zimevuka mpaka wa kawaida na kuteremka hadi kwenye paji au ikiwa hana nywele kwenye utosi wa kichwa chake ni wajibu kuosha paji la uso kwa kiwango cha watu wenye maumbile ya kawaida. 199. Ni wajibu kuosha uso na mikono miwili kuanzia juu kwenda chini kama akiosha kuanzia chini kwenda juu udhu wake utabatilika. 200. Akiloanisha kiganja chake na akapaka kwacho uso wake na mikono yake na ikiwa kiwango cha maji maji ya kiganja ni kwa kiasi kwamba maji yanatiririka kidogo usoni na mikononi wakati wa kupaka kwake inatosha.
KUOSHA MIKONO MIWILI 201. Baada ya kuosha uso ni wajibu kuosha mkono wa kulia kisha mkono wa kushoto kuanzia kwenye kiwiko hadi kwenye ncha za vidole. 202. Ili kuwa na yakini kuwa ameosha kiwiko aoshe juu yake kidogo. 203. Anayeosha viganja vyake hadi kwenye vifundo viwili kabla ya kuosha uso ni wajibu wake aoshe mikono yake hadi kwenye ncha za vidole, na akiosha mikono yake hadi kwenye vifundo viwili na wala asioshe viganja viwili udhu wake unabatilika. 204. Muosho wa kwanza wa uso na mikono miwili ni wajibu na wa pili ni sunna, wa tatu na kuendelea ni haramu, ama ni muosho upi ni wa kwanza au wa pili au wa tatu hiyo inategemea nia ya mwenye kutawadha, kama atamwagia maji mara kumi kwa nia ya muosho wa 40
Al-Masailul Islamiyah kwanza hakuna mushikeli na zote zinazingatiwa kuwa ni muosho wa kwanza, na kama ataosha uso mara tatu kwa maana ya miosho mitatu basi muosho wa tatu utakuwa haramu.
KUPAKA KICHWA 205. Baada ya kuosha uso na mikono miwili ni wajibu kupaka utosi wa kichwa kwa unyevunyevu uliobaki kwenye kiganja, na kwa tahadhari ya wajibu apake kwa kiganja cha kulia kuanzia juu kwenda chini. 206. Robo ya utosi wa kichwa inayoelekeana na uso ndio sehemu ya kupaka, hivyo inatosha kupaka mahali na sehemu hiyo na kwa kiasi chochote ingawa ni wajibu kupaka kiwango cha upana wa kidole, na kwa tahadhari ya sunna urefu uwe kwa urefu wa kidole na upana uwe kwa upana wa vidole vitatu vilioungana. 207. Sio wajibu kupaka ngozi ya kichwa bali inasihi kupaka juu ya nywele za kichwa, lakini kama nywele za utosi wa kichwa chake ni ndefu sana kiasi kwamba kama akizichana zitafika usoni au zinaangukia sehemu ya pili kama za wanawake ni wajibu apake kwenye maoteo ya nywele.
KUPAKA MIGUU MIWILI 208. Baada ya kupaka kichwa ni wajibu kupaka juu ya miguu miwili kwa unyevunyevu ule ule wa udhu uliobakia katika viganja viwili kuanzia kwenye ncha za nywele hadi kwenye kongo mbili, na kwa tahadhari ya sunna ni kupaka hadi kwenye maungio ya mguu. 209. Kwa tahadhari ya sunna atangulize kupaka mguu wa kulia kabla ya mguu wa kushoto vivyo hivyo apake mguu wa kulia kwa mkono wa kulia na mguu wa kushoto kwa mkono wa kushoto.
41
Al-Masailul Islamiyah 210. Katika kupaka kichwa na sehemu ya juu ya miguu miwili ni wajibu kupitisha mikono juu ya sehemu hizi, kama ataweka kiganja chake juu ya kichwa chake na miguu yake, kisha akavuta kichwa na miguu badala ya kupitisha mikono yake udhu wake utabatilika. 211. Ni wajibu sehemu ya kupakwa iwe kavu, ikiwa itakuwa na unyevu nyevu kiasi ambacho unyevu nyevu wake unaathiri, unyevunyevu wa kiganja hiyo itakuwa kinyume na tahadhari ya wajibu, lakini hakuna mushkeli ikiwa unyevunyevu ni kidogo sana kiasi kuwa utapoonekana unyevu nyevu utasemwa kuwa ni unyevunyevu wa kiganja. 212. Kama unyevu nyevu wa kiganja utakauka na usibaki wa kupa kwayo, haijuzu kuchukua unyevunyevu kutoka nje bali ni wajibu kuchukua katika sehemu za udhu na kupaka kwa unyevunyevu huo. 213. Kupaka juu ya soksi na khuf ni batili, lakini hakuna mushkeli kupaka juu yake ikiwa ni kutokana na baridi kali au hofu kutokana na wezi na wanyama wakali na hakuweza kuvua soksi zake, na ikiwa juu ya soksi kuna najisi inamlazimu kuweka kitu tohara juu yake kisha apakae, na kwa tahadhari ya wajibu atayamamu vile vile. 214. Kama juu ya miguu kuna najisi na wala hawezi kutoharisha kwa ajili ya kupaka juu yake itamlazimu kutayamamu.
UDHU WA IRTIMASI “KUZAMISHA� 215. Udhu wa itrimasi: Ni mwenye kutawadha kuzamisha uso wake na mikono yake kwenye maji na kuutoa kwa nia ya udhu, na akiweka nia wakati wa kuzamisha uso wake na mikono yake katika maji na akabakia na nia yake hadi wakati wa kuitoa kwenye maji na akaendelea na nia yake hadi wakati wa kuutoa katika maji udhu wake unasihi, vivyo hivyo unasihi udhu wake kama atazamisha mkono wake wa 42
Al-Masailul Islamiyah kulia katika maji kwa nia ya udhu wa irtimasi na akaosha mkono wa kushoto kwa nia ya udhu usio wa irtimasi. 216. Katika udhu wa irtmasi vile vile ni wajibu kuosha uso na mikono kuanzia juu kwenda chini, anuie udhu wakati wa kuzamisha uso wake na mikono yake katika maji, ni wajibu aingize uso wake kuanzia kwenye paji la uso katika maji na mikono yake kuanzia kwenye kiwiko, na anuie udhu wakati wa kutoa sehemu hizi kwenye maji, ni wajibu atoe uso wake kuanzia upande wa paji na atoe mikono yake kuanzia kwenye kiwiko. 217. Hakuna mushikeli kutawadha baadhi ya viungo vyake kwa irtmasi na vingine kwa njia isiyokuwa ya irtimasi.
MASHARTI YA UDHU 218. Ili udhu usihi kuna masharti kumi na mbili:1. Maji ya udhu yawe tohara 2. Maji yawe halisi na sio mudhafu 3. Maji, chombo na sehemu anayotawadhia viwe mubaha “halali� 4. Chombo cha kutawadhia kisiwe cha dhahabu au fedha. 5. Viungo vya udhu viwe tohara wakati wa kuosha na kupaka 6. Wakati uwe unatosha kwa udhu na swala 7. Atawadhe kwa nia ya kujikurubisha, yaani kutekeleza amri ya Mwenyezi Mungu mtukufu kama atatawadha kwa ajili ya kupata ubaridi au kwa nia nyingine udhu wake unabatilika. 219. Sio lazima kutamka nia ya udhu au kuipitisha katika moyo bali inatosha kuwa mwangalifu wakati wa kutawadha kiasi kwamba lau akiulizwa swali ghafla nini anachofanya angesema natawadha. 8. Achunge utaratibu katika vitendo vya udhu yaani aanze kwa 43
Al-Masailul Islamiyah kuosha uso, mkono wa kulia, mkono wa kushoto, kupaka kichwa, kisha kupaka miguu miwili kama hatafuata utaratibu huu udhu wake utabatilika. 9. Afanye vitendo vya udhu kwa mfuatano. 220. Kama atatenganisha baadhi ya vitendo vya udhu kwa muda kiasi ambacho atakapotaka kuosha au kupaka kiungo kinachofuata viungo vilivyotangulia vitakuwa vimeshakauka udhu wake utabatilika. 221. Kama atafuatisha baina ya viungo vya udhu kimoja baada ya kingine bila ya kuchelewesha lakini unyevunyevu wa viungo vilivyotangulia ukakauka kwa sababu ya joto la mwili udhu wake utasihi. 10. Atawadhe mwenyewe yaani aoshe uso wake, mikono yake na apake sehemu za kupaka bila ya msaada wa yeyote na mtu akimtawadhisha au akimsaidia katika kufikisha maji kwenye uso wake au mikono yake au akapaka kichwa chake au miguu yake, udhu wake utabatilika. 222. Asiyeweza kutawadha mwenyewe ni wajibu amuweke mtu wa kumtawadhisha na kama akitaka ujira ampe akiweza, lakini mwenye kutawadhishwa anuie nia ya udhu na apake kwa mikono yake sehemu za kupaka, kama hawezi amuweke mtu atakayeshika mikono yake na kupaka kwayo sehemu za kupaka, na kama hilo haliwezekani ni wajibu mwakilishi wake achukue unyevunyevu kutoka katika kiganja cha mwenye kutawadhishwa na apake kwayo sehemu zake za kupaka. 11. Asiwe na kizuizi cha kutumia maji 12. Katika viungo vya udhu kusiwe na kizuizi cha kuzuia maji kufika kwenye ngozi
44
Al-Masailul Islamiyah
HUKUMU ZA UDHU 223. Ambaye anashuku sana katika vitendo vya udhu au sharti zake, mfano utohara wa maji au uhalali wake au kwa ghasb(bila ya ridhaa ya mwenyewe), ni wajibu asizingatie shaka yake. 224. Akishuku kuwa udhu wake umebatilika au laa, atahukumu kubaki kwa udhu wake, lakini kama hajafanya istibrai baada ya haja ndogo kisha akatawadha, na kisha akaona unyevunyevu baada ya udhu hajui ni mkojo au kitu kingine, udhu wake utabatilika. 225. Anayeshuku kuwa ametawadha au laa, ni wajibu atawadhe. 226. Anayejua kuwa ametawadha kisha akapatwa na kinachobatilisha udhu kama vile mkojo na wala hajui kipi kimetangulia, ikiwa ni kabla ya swala ni wajibu atawadhe, na ikiwa ni ndani ya swala anaivunja na kutawadha tena, na ikiwa ni baada ya swala , basi swala yake aliyoiswali itasihi, lakini atawadhe kwa swala zinazofuata. 227. Akishuku baada ya swala kuwa ametawadha kabla ya swala au laa, swala yake aliyoisali itasihi, lakini ni wajibu atawadhe kwa swala zinazofuata 228. Akishuku katikati ya swala kuwa ametawadha kabla ya kuingia kwenye swala au laa, swala yake inabatilika na ni wajibu atawadhe kisha aswali. 229. Akishuku baada ya swala kuwa udhu wake umebatilika kabla ya swala au baada ya yake, swala yake aliyoswali itasihi. 230. Mwenye ugonjwa wa salasi (kutoka mkojo) au mabutun “asiyeweza kuzuia haja kubwa� akitambua kuwa ugonjwa wake utampa fursa mwanzo wa wakati wa swala hadi mwisho kwa kiasi cha kutosha udhu na swala, ni wajibu aswali katika wakati huo, na kama fursa 45
Al-Masailul Islamiyah hiyo haitoshi isipokuwa kufanya vitendo vya swala ni wajibu kufanya vitendo vya wajibu tu na kuacha ya sunna kama vile kunuti, adhana na kukimu. 231. Kama maslusi au mabtun hapati fursa ya kiasi cha kutawadha na kuswali, bali mkojo au haja kubwa inadondoka wakati wa swala mara nyingi, kama sio vigumu kwake basi atawadhe kila mara, aweke chombo cha maji karibu naye na atawadhe kila unapotoka mkojo au haja kubwa na akamilishe swala, lakini kwa tahadhari ya sunna aswali swala ya pili kwa udhu mmoja hata kama udhu wake utabatilika katikati ya swala asijali. 232. Maslusi au mabtun ambaye hawezi kujizuia kama itamuwia vigumu kutawadha kila mara ni lazima kwake aswali kila swala kwa udhu mmoja. 233. Ni wajibu kwa ambaye ana maradhi ya kutokwa na upepo afanye kama anavyofanya maslus au mabtun, vivyo hivyo kwa asiyeweza kujizuia na usingizi. 234. Maslusi ambaye anadondokwa na mkojo mfululizo ni wajibu ajihifadhi mkojo usiruke hadi kwenye sehemu zingine za mwili wake kwa kuweka kifuko chenye pamba au vitu vingine, na kwa tahadhari ya wajibu atoharishe kifuko ambacho kina najisi, vivyo hivyo sehemu ya haja ndogo kabla ya kila swala ikiwa hakuna usumbufu, na vivyo hivyo inalazimu kwa mabatun. 235. Sio wajibu kwa maslusi au mabtun kulipa swala ambazo ameziswali katika maradhi yake baada ya kupona kama atakuwa ameziswali kama inavyotakiwa, lakini akipona ndani ya wakati wa swala ni bora airudie swala aliyoiswali katika wakati huo.
46
Al-Masailul Islamiyah
MAMBO AMBAYO YANAPASA UDHU 236. Udhu ni wajibu kwa mambo matano:1. Swala za wajibu isipokuwa swala ya maiti 2. Sijida au tashahud iliyosahauliwa 3. Tawafu ya wajibu katika ka’aba tukufu 4. Akiweka nadhiri, kiapo au kumwahidi Mwenyezi Mungu kuwa atatawadha 5. Akiweka nadhiri au akitaka kugusa, maandishi ya Qur’an kwa mwili wake. 237. Sio wajibu kutawadha kwa ajili ya sijida ya kusahau isipokuwa kutawadha katika sehemu hii ni jambo zuri. 238. Udhu ni wajibu ikiwa mtu atataka kutoharisha Qur’an iliyonajisika au akitaka kuitoa chooni, lakini kama kuchelewa kuitoa itakuwa ni kuidharau Qur’an afanye upesi kuitoa bila ya udhu. 239. Ni haramu kugusa maandishi ya Qur’an kwa mwili bila ya udhu, na kwa tahadhari ya wajibu asiguse kwa nywele zake isipokuwa zikiwa ndefu, lakini hakuna mushikeli kugusa tarjama ya Qur’an ya lugha yoyote. 240. Ni haramu kugusa jina la Mwenyezi Mungu kwa lugha yeyote bila ya udhu, na kwa tahadhari ya wajibu asiguse jina la Nabii mtukufu na Maimamu Masumini na Faatmah Zahra(a.s).
VINAVYOBATILISHA UDHU 241. Mambo yanayobatilisha udhu ni saba:1. Mkojo 47
Al-Masailul Islamiyah 2. Kinyesi 3. Upepo unaotoka katika sehemu ya haja kubwa 4. Usingizi unaoshinda usikivu na kuona kiasi kwamba sikio halisikii wala jicho halioni 5. Kila kinachoondoa akili kama vile ulevi, kichaa au kuzimia. 6. Istihadha utakuja ufafanuzi wake 7. Kila kinachowajibisha kuoga kama vile janaba na kugusa maiti kwa tahadhari.
HUKUMU ZA UDHU WA BANDEJI Bandeji ni ile ambayo inafungiwa jeraha au sehemu iliyoumia. 242. Ikiwa katika sehemu za udhu kuna jeraha, kidonda au mvunjiko na hakuna kitu juu yake, na maji hayamdhuru ni wajibu atawadhe kama kawaida. 243. Ikiwa sehemu kati ya sehemu za udhu kuna jeraha, kidonda au mvunjiko, na ikawa wazi na ikawa kumwagia maji juu yake kunadhuru, lakini hakumdhuru kupitisha mkono wenye unyevunyevu juu yake, basi kwa tahadhari ya wajibu ni kupitisha mkono wenye unyevunyevu juu yake, na kama hiyo pia inadhuru, au jeraha ni najisi haiwezekani kutoharisha, itamlazimu kuosha sehemu inayozunguka jeraha kuanzia juu hadi chini, na kwa tahadhari ya wajibu aweke kitambaa tohara juu ya jeraha na kupaka juu yake kwa mkono wenye unyevunyevu, na ikiwa haiwezekani kwake kutoharisha itamlazimu kuosha pembezoni mwa jeraha kisha atayamamu kwa tahadhari ya sunna. 244. Kama juu ya jeraha, kidonda au mvunjiko kuna bandeji, kama kuna uwezekano wa kufungua na kusafisha na maji hasidhuru, ni wajibu 48
Al-Masailul Islamiyah afungue na atawadhe kama kawaida, ni sawasawa bandeji iwe usoni, mkononi, utosini au juu ya mguu. 245. Kama bandeji itafunika uso wote au mkono wote au mikono yote, ni wajibu atawadhe udhu wa bandeji, na kwa tahadhari ya wajibu atayamamu. 246. Kama bandeji imefunika viungo vyote vya udhu basi kwa tahadhari ya wajibu atawadhe udhu wa bandeji na atayamamu vile vile. 247. Ikiwa katika viungo vya udhu hakuna jeraha, kidonda au mvunjiko, lakini maji yanamdhuru ni wajibu atayamamu, na kwa tahadhari atawadhe udhu wa bandeji. 248. Josho la bandeji ni kama udhu wa bendeji, lakini kwa tahadhari ya wajibu aoge josho wa bandeji kwa utaratibu, hata kama anaweza kuoga kwa kuzamia pamoja na masharti ambayo ni, tohara ya kiungo na kutodhurika kwa maji, kama hayatapatikana masharti ya kuoga kwa kuzamia basi aoge kwa utaratibu.
JOSHO ZA WAJIBU 249. Josho za wajibu ni saba:Kuoga josho la janaba Kuoga josho la hedhi Kuoga josho la nifasi Kuoga josho la istihadha Kuoga ikiwa umegusa maiti Kuosha maiti. Miogo ambayo inakuwa wajibu kwa sababu, kama vile nadhiri,ahadi n.k.
HUKUMU ZA JANABA 49
Al-Masailul Islamiyah
249. Janaba inapatikana kwa njia mbili:Kujamiana. Kutokwa na manii, sawasawa akiwa usingizini au akiwa macho, yawe yametoka machache au mengi, kwa kutamani au bila ya kutamani, kwa hiyari au bila hiyari. 250. Ikiwa mtu atatokwa na unyevunyevu na ikawa hajui kuwa ni manii au mkojo, ikiwa umetoka kutokana na matamanio, kwa nguvu na kulegea kwa mwili baada ya kutoka kwake, basi hukumu yake ni hukumu ya manii, na kama alama hizi tatu hazitokuwepo zote au baadhi, basi hayatakuwa na hukumu ya manii, lakini kwa mtu ambaye ni mgonjwa sio lazima unyevu nyevu huo utoke kwa nguvu, ukitoka kwa shahawa na mwili kulegea baada ya kutoka basi yatakuwa ni manii hata kama hayatatoka kwa nguvu. 251. Mtu akiingiza uume kwa kiasi cha kichwa au zaidi, ni sawasawa aliyeingiliwa awe Mwanamke au mwanamume “Allah atulinde na haya” iwe kwa mbele au nyuma, awe amebalehe au laa, manii ya toke au laa, basi wote wawili watapata janaba na ni wajibu waoge. 252. Ikiwa mtu atashuku kuwa ameingiza uume kwa kiasi cha kichwa au laa, sio wajibu wake aoge. 253. Akiingilia Mnyama – Mwnyezi Mungu atulinde na hayo - na akatokwa na manii kuoga kunatosheleza, na kama hajatokwa na manii na alikuwa na udhu kabla ya kumwingilia mnyama, pia inatosha kuoga peke yake, na kama alikuwa hana udhu basi ni kwa tahadhari ya wajibu aoge na kutawadha. 254. Kama manii yatatikisika katika sehemu yake na hayakutoka, kisha akashuku kuwa je, manii yametoka au laa, sio wajibu wake kuoga.
50
Al-Masailul Islamiyah 255. Mtu ambaye hawezi kuoga lakini anaweza kutayamamu, basi inajuzu kwake kumwingilia mke wake hata kama ni baada ya kuingia wakati wa swala. 256. Kama mtu ataona manii katika nguo zake na anajua kuwa yametoka kwake, kisha hajaoga, ni wajibu aoge, na ni wajibu alipe swala ambazo ana yakini kuwa ameziswali baada ya kutokwa na hayo manii na kabla ya kuoga. Lakini swala ambazo anadhani kuwa ameziswali baada ya kutokwa na manii sio lazima kuzilipa.
MAMBO AMBAYO NI HARAMU KWA MWENYE JANABA 257. Ni haramu kwa mwenye janaba mambo matano:Kugusa andiko la Qur’an tukufu au jina la Allah (swt) kwa mwili, na kwa tahadhari ya wajibu asiguse majina ya Manabii, Maimamu waliotoharika pia na Fatma Zahara (as). Kuingia katika Msikiti Mtukufu wa Makka na msikiti wa Nabii (saww), ni haramu hata kupita kwenye mlango na kutokea mlango mwingine. Kusimama na kubakia ndani ya Msikiti mwingine, na vile vile katika sehemu takatifu za Maimamu waliotoharika (as), lakini hakuna mushkeli kupita mlangoni na kutokea mlango mwingine, na pia inajuzu kuingia kwa ajili ya kuchukua kitu. Kuingia msikitini kwa kusudi la kuweka kitu, bali ni haramu kwa tahadhari ya wajibu kuweka kitu ndani hata bila ya kuingia ndani.
51
Al-Masailul Islamiyah Kusoma aya ya sajida katika moja ya sura “a’zaim” tukufu, nazo ni sura za Qur’ani ambazo zina sajida ya wajibu nazo ni:Suratus Sajdah nayo ni sura ya 32 Sura ya Fuswilat nayo ni sura ya 41 Sura ya Najim nayo ni sura ya 53 Sura ya Alaq nayo ni sura ya 96 258. Ni haramu kwa mwenye janaba kusoma aya ya Sajida, bali ni kwa tahadhari ya sunna asisome hata herufi moja katika sura hizi nne.
MAMBO YALIYO MAKURUHU KWA MWENYE JANABA 259. Ni makuruhu kwa mwenye janaba mambo tisa yafuatayo:Kunywa na kula, lakini akitawadha au akiosha mikono yake kabla ya kula na kunywa hapatakuwa na karaha Kusoma aya za Qur’ani zaidi ya aya saba zisizokuwa katika sura za sajida Kugusa kwa mwili pembezoni mwa Qur’ani; jalada lake na baina ya maandishi yake Kuweka Qur’an tukufu na kuibeba Kulala, lakini hakuna karaha akitawadha, au akitayamamu badala ya kuoga kama hana maji Kupaka hina n.k Kujipaka mafuta Kufanya jimai baada ya kujiotea usingizini.
52
Al-Masailul Islamiyah
MAS’ALA KATIKA KUOGA JOSHO LA JANABA 260.Kuoga josho la janaba ni sunna, na ni wajibu kwa ajili ya swala ya wajibu n.k. Lakini sio lazima kuoga janaba kwa ajili ya swala ya maiti, sajida ya kushukuru na sajida za Qur’an za wajibu, lakini ni bora kwa tahadhari ya sunna kuoga kwa ajili ya swala ya maiti. 261. Sio lazima wakati wa kuoga kunuwia wajibu au sunna, inatosha kunuwia kujikurubisha kwa Allah (swt) na kutekeleza amri yake. 262. Akiwa na yakini kuwa wakati wa swala umeingia na akanuwia kuoga josho la wajibu, kisha ikambainikia kuwa ameoga kabla ya wakati basi kuoga kwake kutasihi. 263. Josho la wajibu au sunna linagawanyika sehemu mbili:- Josho la mpangilio - Josho la kujizamisha.
JOSHO LA MPANGILIO 264. Katika josho la mpangilio ni wajibu kuanza kichwa na shingo kwanza, kisha upande wa kulia kisha upande wa kushoto kwa nia ya kuoga, na kama mwili wote uko ndani ya maji au chini ya bomba, atanuwia kuoga kwa kuanza na kichwa na shingo kisha upande wa kulia kisha upande wa kushoto. Kama atafanya kinyume na utaratibu huu kwa makusudi au kutokujua mas’ala, basi kwa tahadhari ya wajibu josho lake litabatilika. 265.Unapoosha upande wa kulia ni wajibu kuosha nusu ya kitovu na nusu ya sehemu ya siri na nusu nyingine unaiosha unapoosha upande wa kushoto, na kwa tahadhari ya sunna kuosha kitovu na sehemu ya siri 53
Al-Masailul Islamiyah yote wakati unapoosha pande zote mbili. 266. Ili kupata uhakika kuwa umeosha sehemu zote tatu yaani kichwa, shingo, upande wa kulia na upande wa kushoto, ni lazima kuzidisha kila sehemu unapoosha. Bali kwa tahadhari ya sunna kuosha upande wa kulia wote na upande wa kulia wa shingo na upande wa kushoto wote pamoja na upande wa kushoto wa shingo. 267. Mtu akijua baada ya kuoga kuwa hajaosha sehemu katika mwili na hajui ni wapi, basi lazima aoge kwa mara nyingine kwa tahadhari ya wajibu. 268. Kama mtu akijua baada ya kuoga kuwa hajaosha sehemu katika mwili, kama sehemu hiyo ipo upande wa kushoto inatosha aoshe upande wa kushoto tu, na ikiwa itakuwa upande wa kulia ni kwa tahadhari ya sunna baada ya kuiosha hiyo sehemu, aoshe upande wa kushoto kwa mara nyingine, na kama itakuwa kichwani au shingoni ni lazima aoshe hiyo sehemu, kisha upande wa kulia, kisha upande wa kushoto kwa mara nyingine. 269. Kama atashuku kabla ya kumaliza kuosha upande wa kushoto inatosheleza kuosha sehemu anayoishuku, lakini akishuku kuwa hajaosha sehemu katika upande wa kulia basi ni kwa tahadhari ya sunna kuosha sehemu aliyoishuku kisha aoshe upande wa kushoto kwa mara nyingine, na akishuku kuwa hajaosha sehemu ya kichwa na shingo, basi ni kwa tahadhari ya sunna baada ya kumaliza kuosha hiyo sehemu, aoshe upande wa kulia kisha upande wa kushoto.
JOSHO LA KUZAMA 270. Katika josho la kuzamia ni wajibu maji yaenee mwili mzima kwa mara moja, kama atazama katika maji kwa nia ya kuoga josho la kuzama ni wajibu anyanyue miguu yake juu ya ardhi. 54
Al-Masailul Islamiyah
271. Katika josho la kuzamia sio lazima wakati wa nia baadhi ya mwili uwe nje ya maji, bali anaweza kunuwia na mwili wote ukiwa ndani ya maji. 272. Kama akijua baada ya kuoga josho la kuzamia kuwa kuna baadhi ya sehemu za mwili hazijafikiwa na maji, sawasawa amejua hizo sehemu au laa, ni wajibu arudie kuoga. 273. Kama wakati hautomtosha kuoga josho la mpangilio, lakini unamtosha kuoga josho la kuzamia, ni lazima aoge kwa kuzama. 274. Mwenye kufunga saumu ya wajibu au akihirimia hija au umra, haijuzu kwake kuoga kwa kuzama katika hali ya saumu au ihramu. Lakini akioga kwa kusahau kuoga kwake utasihi.
HUKUMU ZA JOSHO 275. Katika kuoga josho la kuzamia ni lazima mwili wote uwe tohara, lakini katika joshoo la mpangilio sio lazima mwili wote uwe na tohara, na kama mwili wote utakuwa na najisi kisha akatoharisha kila sehemu kabla ya kuiosha inatosheleza. 276. Mtu akizini kama akitaka kuoga kwa maji ya moto, na mwili wake ukatoa jasho ,basi sio lazima aoge kwa maji ya baridi, japo ni bora aoge kwa maji ya baridi. 277. Katika kuoga janaba usipoosha hata unywele mmoja wa mwili josho lake litabatilika, lakini sio wajibu kuosha sehemu ambazo hazionekani mfano ndani ya sikio na pua. 278 Sehemu ambayo inashukiwa kuwa ni ya ndani au ya nje ya mwili ni lazima ioshwe kwa tahadhari. 55
Al-Masailul Islamiyah
279. Kama sikio lina shimo pana kwa kiasi kwamba kunaonekana ndani, ni wajibu kuiosha na kama haionekani ndani sio lazima ioshwe. 280. Ni wajibu kuondoa kila uchafu unaozuia maji kufika mwilini, na kama ataoga kabla ya kuhakikisha kuwa kuna kizuizi au laa, kisha akabaini kuwa kizuizi hakijatoka, josho lake litabatilika. 281. Kama atashuku wakati wa kuoga, shaka inayokubalika kwa wenye akili timamu, kuwa je kuna kizuizi kinachozuia maji kufika mwilini au laa, basi ni wajibu afanye uchunguzi ili kuhakikisha kuwa hamna kizuizi. 282. Katika kuoga ni lazima kuosha nywele ndogondogo ambazo zinahesabika kuwa ni sehemu ya mwili, na wala sio wajibu kuosha nywele ndefu zaidi, bali ikiwezekana maji kufika mwilini bila ya kulowana nywele josho litasihi. Lakini kama haitawezekana kufika maji mwilini mpaka uoshe nywele ni wajibu kuziosha nywele ili maji yafike mwilini. 283. Masharti yote ambayo yanafanya udhu usihi, mfano maji kuwa na tohara na kuwa ya halali, vilevile masharti haya yanazingatiwa katika kuoga, lakini sio lazima kuanza kuoga kuanzia juu mpaka chini, vilevile sio lazima katika josho la mpangilio kuosha upande unaofuata kwa haraka bila ya kuchelewesha,bali anaweza kuchelewesha baada ya kuosha kichwa na shingo kisha baadaye aoshe upande wa kulia na baada ya muda aoshe upande wa kushoto. 284. Anayeshindwa kuzuia mkojo au haja kubwa, kama maradhi yake yatampa ahueni kidogo kwa kiwango cha kuoga na kuswali tu, basi ni wajibu afanye haraka kuswali bila ya kuchelewesha, na vivyo hivyo hukumu ni hii kwa mwanamke mwenye damu ya istihadha.
56
Al-Masailul Islamiyah 285. Mtu akikusudia kutomlipa malipo mwenye bafu au akinuwia kutolipa taslimu josho lake litabatilika. 286. Kama mwenye bafu anaridhia malipo ya kuoga yacheleweshwe, lakini mwenye kuoga akanuwia kutolipa kabisa au atalipa lakini katika mali ya haramu, josho lake litakuwa na mushkeli. 287. Kama mtu akitaka kulipa malipo ya mwenye bafu katika mali ya haramu au ambayo haijatolewa khumsi, joshoo lake litabatilika isipokuwa mwenye bafu akiridhia kutochukua chochote. 288. Kama akishuku kuwa ameoga au laa ni wajibu aoge, lakini akishuku baada ya kuoga kuwa ameoga sawasawa au laa, sio lazima arudie kuoga. 289. Kama atatokwa na mkojo wakati anaoga, basi atakamilisha kuoga kisha atatawadha au ataacha na kuanza kuoga upya kwa nia ya wajibu ulio juu yake na kutawadha pia. 290. Kama akioga kwa ajili ya swala kwa kudhania kuwa wakati unamtosha kuoga na kuswali, kama wakati utatosha kuswali rakaa moja au zaidi ndani ya wakati swala yake inasihi. 291. Mwenye janaba akishuku kuwa ameoga au laa, swala zake alizoswali zitakuwa sahihi, lakini aoge kwa ajili ya swala zingine. 292. Mwenye kuwajibika kuoga josho nyingi, inajuzu aoge josho moja kwa nia ya josho zote, au aoge kila mmoja kwa nia yake. 293. Kama ataandika kwenye mwili wake aya ya Qur’an au jina la Allah ni wajibu kufuta kama itawezekana, na ikishindikana ni lazima atawadhe na kuoga josho la kuzamia, na kama atataka kutawadha na kuoga josho la mpangilio ni lazima maji yafike mwilini bila ya mkono wake kugusa sehemu iliyoandikwa katika mwili wake. 57
Al-Masailul Islamiyah
294. Aliyeoga josho la janaba hatawadhi kwa ajili ya swala, ama josho zingine za wajibu na sunna ni wajibu atawadhe kwa ajili ya swala, kwa sababu josho hizi hazitoshelezi udhu, isipokuwa josho la wa janaba tu.
ISTIHADHA 295. Damu ya istihadha ni moja ya damu ambazo zinatoka kwa mwanamke, na mwanamke ambaye anatokwa na damu hii anaitwa mustahadha. 296. Damu ya istihadha mara nyingi huwa ya njano, baridi, haichomi wala haitoki kwa nguvu, inawezekana ikawa nyeusi au nyekundu ya moto na nzito na inatoka kwa nguvu na kuchoma. 297. Istihadha inagawanyika sehemu tatu: Chache, wastani na nyingi. Chache: Ni ambayo hailoanishi pamba anayoiweka mwanamke katika uke. Wastani: Ni ambayo inaloanisha na kupenya ndani ya pamba lakini haitokezi nje ya kitambaa anachofungia pamba ili kuzuia damu isisambae mwilini mwake. Nyingi: Ni ambayo inapenya ndani ya pamba na kutokeza nje kwenye kitambaa anachofungia pamba.
HUKUMU ZA ISTIHADHA 58
Al-Masailul Islamiyah
298. Katika istihadha chache ni wajibu mwanamke atawadhe katika kila swala, abadilishe pamba na kutoharisha nje ya uke kama damu itakuwa imefika. 298. Katika istihadha ya wastani ni wajibu mwanamke aoge katika swala ya asubuhi josho la istihadha, kisha abadilishe pamba na kutoharisha nje ya uke kama damu itakuwa imefika, na kama hataoga katika swala ya asubuhi kwa makusudi au kwa kusahau ni wajibu kwake aoge katika swala ya Adhuhuri na Alasiri na kama hataoga kwa ajili ya Adhuhuri na Alasiri basi aoge kabla ya swala ya Magharibi na Isha, sawa sawa damu iwe imekatika au laa. 299. Katika istihadha nyingi ni wajibu aoge katika swala ya Asubuhi, Adhuhuri na Alasiri, Magharibi na Isha yaani josho tatu, kisha abadilishe pamba na kutoharisha nje ya uke. Na kama atatenganisha baina ya Magharibi na Isha ni wajibu aoge kwa ajili ya swala ya Isha. 300. Damu ya istihadha ikiendelea kutoka mpaka karibu na wakati wa swala, na kama mwanamke bado hajaoga na kutawadha, basi ni lazima kwake aoge na kutawadha wakati wa swala. 301. Mwenye istihadha ya wastani na nyingi ambaye ni wajibu kwake kutawadha na kuoga, kama atatanguliza kutawadha au kuoga inasihi. 302. Mwenye istihadha chache ikiwa ya wastani baada ya sala ya Asubuhi ni wajibu aoge kwa ajili ya sala ya Adhuhuri na Alasiri, na istihadha ya wastani ikiwa nyingi baada ya sala ya Adhuhuri na Alasiri ni wajibu aoge kwa ajili ya sala ya Magharibi na Isha. 303. Mwenye istadha chache au ya wastani ikiwa itakuwa nyingi baada ya swala ya Asubuhi ni wajibu aoge kwa ajili ya swala ya Adhuhuri na Alasiri, na aoge kwa mara nyingine kwa ajili ya swala ya Magharibi 59
Al-Masailul Islamiyah na Isha. 304. Mwenye istihadha ya wastani au nyingi akioga kwa ajili ya swala ya Asubuhi kabla ya kuingia wakati, josho lake litabatilika, lakini hakuna tatizo kama ataoga kwa ajili ya swala ya usiku karibu na adhana ya Alfajiri, na akaswali swala ya usiku, kisha wakati wa swala ya Asubuhi ukaingia na akafanya haraka kuswali. 305. Mwanamke mwenye istihadha ni wajibu atawadhe katika kila swala, iwe ya sunna au ya wajibu, na vile vile akitaka kurudia swala kwa tahadhari au akitaka kurudia swala aliyoiswali furada kuiswali jamaa, ni lazima afanye vitendo vyote anavyotakiwa kuvifanya mustadha. Lakini sio lazima afanye vitendo anavyotakiwa kuvifanya mustadha ikiwa anaswali rakaa ya Ihtiyati, sajda iliyosahauliwa, tashahudu iliyosahauliwa na sajda ya kusahau, kama atavifanya hivi baada ya swala bila kuchelewesha. 306. Ni lazima kwa mustahadha baada ya damu kukatika afanye vitendo vya mustadha katika swala ya kwanza atakayotaka kuswali, baada ya hapo sio lazima kuvifanya hivyo vitendo kwa ajili ya swala zingine. 307. Mustahadha kama hatambui yupo katika kundi gani ni lazima ajipime ili ajijue yupo kundi gani, ataingiza pamba ukeni na kusubiri kidogo kisha aitoe na baada ya kujua yuko kundi gani basi itakuwa ni istihadha yake. 308.Mwenye istihadha akianza kusali bila ya kujua yupo kundi gani, kama atakusudia kujikurubisha kwa Allah na akafanya vitendo vya mwenye istadha chache sala yake itasihi, na kama hatakusudia kujikurubisha kisha hajafanya wadhifa wake, akafanya wadhifa wa kundi lingine mfano yeye ni wastani akafanya wadhifa wa chache sala yake itabatilika.
60
Al-Masailul Islamiyah 309. Mwenye istihadha kama hawezi kujua yuko katika kundi gani, mfano hajui kuwa yeye yuko katika chache au wastani, basi ni lazima afanye wadhifa wa istihadha chache, na kama hajui kuwa yuko katika istihadha ya wastani au nyingi basi ni lazima afanye wadhifa wa istihadha ya wastani, lakini kama alikuwa anajua yuko katika kundi gani kati ya haya matatu, basi itabidi awe katika hilo kundi la zamani. 310. Damu ya istihadha ikibakia tumboni haibatilishi josho wala udhu, na ikitoka hata kama ni chache inabatilisha udhu na josho. 311. Mwanamke mwenye istihadha kama hataona damu inajuzu asali haraka na udhu alionao. 312. Mwenye istihadha akijua kuwa damu haijatoka tangu alipoanza kutawadha au kuoga, inajuzu kwake kuchelewesha sala mpaka wakati atakapokuwa tohara. 313. Mwenye istihadha akijua kuwa atatoharika kabisa kabla ya kumalizika wakati wa swala, au itakatika kwa muda wa kuweza kuswali basi ni kwa tahadhari ya wajibu asubiri mpaka huo wakati na kuswali atakapotoharika. 314. Kama itaonekana dhahiri kuwa damu imekatika na baada ya udhu na kuoga , na mustahadha akajua kuwa akichelewesha swala kwa muda wa kuweza kutawadha na kuoga atatoharika kabisa, ni wajibu acheleweshe swala na arudie kutawadha na kuoga baada ya kutoharika, kisha aswali, na kama wakati utakuwa mfinyu sio lazima arudie kutawadha na kuoga kwa mara nyingne, bali inajuzu aswali na udhu na josho lile ile. 315. Mwenye istihadha nyingi na ya wastani anapotoharika kabisa ni wajibu aoge, lakini kama akijua kuwa damu haijatoka kabla hajaoga sio lazima arudie kuoga. 61
Al-Masailul Islamiyah
316. Ni wajibu kwa mwenye istihadha chache baada ya udhu, na mwenye istihadha nyingi na ya wastani baada ya kutawadha na kuoga wasali bila ya kuchelewa, lakini hakuna tatizo kutoa adhana kukimu na kusoma dua kabla ya swala, pia inajuzu kufanya mambo ya sunna kama vile kunuti n.k. 317. Mwenye istihadha kama akichelewesha kusali baada ya kuoga, ni lazima arudie kuoga na kusali bila ya kuchelewa. 318. Kama damu ya istihadha itaendelea kutoka bila ya kusimama, ni lazima kwa tahadhari ya sunna kama hataogopa madhara kabla ya kuoga na baada ya kuoga achukue pamba na kuingiza ukeni ili kuzuia damu isitoke nje, lakini kama damu itakuwa haitiririki kila wakati ni lazima baada ya udhu na kuoga azuie damu, na kama atafanya uzembe kujihifadhi na akaacha damu inatoka ni lazima kwa tahadhari ya sunna arudie kuoga na kutawadha na arudie swala kama ameswali. 319. Kama damu haitakatika wakati wa kuoga, josho litasihi, lakini mwenye istihahadha ya wastani akiwa mwenye istihahadha nyingi wakati akioga, ni lazima aanze kuoga upya kwa tahadhari. 320. Kwa tahadhari ya sunna kwa mwenye istihahadha kuzuia damu isitoke mchana kutwa ambao atafunga saumu kwa kadiri atakavyoweza. 321. Mwenye istihahadha ambaye ni wajibu aoge, saumu yake itasihi kama ataoga jinsi inavyotakiwa, mfano akioga kwa ajili ya swala ya magharibi, kisha akaoga josho za mchana kwa ajili ya swala za wajibu za siku hiyo. Lakini kama hataoga kwa ajili ya swala ya magharibi na Isha na akaoga kwa ajili ya swala ya usiku kabla ya adhana ya alfajir,i na akaoga josho za mchana kwa ajili ya swala 62
Al-Masailul Islamiyah zake, saumu yake itasihi na kama atakuwa mustahadha baada ya swala ya alasiri na hajaoga saumu yake itasihi. 322. Mwenye istihadha chache ikiwa ya wastani au nyingi kabla ya swala, ni lazima afanye wadhifa wa istihadha ya wastani au nyingi, na kama istihadha ya wastani ikiwa nyingi lazima afanye wadhifa wa istihadha nyingi, na kama alikuwa ameoga kwa ajili ya istihadha ya wastani haitosadia, bali ni wajibu arudie kuoga kwa ajili ya istihadha nyingi. 323. Kama istahadha ya wastani itakuwa nyingi katikati ya swala basi ni kwa tahadhari ya wajibu avunje swala, kisha aoge na kutawadha na afanye vitendo vingine vya wajibu vya mwenye istihadha nyingi, kisha aswali, na kama wakati hautatosha kutawadha na kuoga, ni wajibu kwake atayamamu mara mbili, tayamamu moja ni badala ya kuoga na nyingine ni badala ya kutawadha, na kama wakati hautatosheleza kuoga na kutawadha basi ni wajibu kwake atayamamu badala yake, na kama ataoga itabidi atayamamu badala ya udhu, na kama atatawadha itabidi atayamamu badala ya kuoga, na kama wakati hautatosha kwa vyote viwili, haijuzu kukata swala, bali ataikamilisha kisha atalipa kwa tahadhari ya sunna. 324. Kama damu ikikatika katikati ya swala na mustadha hajui kuwa imekatika tumboni au laa, kama atajua baada ya swala kuwa imekatika ni wajibu kwake arudie kuoga, kutawadha na kuswali kwa mara nyingine. 325. Kama mwenye istihadha nyingi ikiwa ya wastani, ni wajibu afanye wadhifa wa istihadha nyingi katika swala ya kwanza, na wadhifa wa wastani kwa swala zinazofuatia. Mfano mwenye istihadha nyingi ikiwa ya wastani kabla ya adhuhuri, ni wajibu aoge kwa ajili ya swala ya adhuhuri na atatawadha kwa ajili ya swala ya magharibi na Isha, lakini kama hajaoga kwa ajili ya swala ya adhuhuri na ikawa 63
Al-Masailul Islamiyah wakati unamtosha kuswali swala ya alasiri tu, basi ni wajibu kwake aoge kwa ajili ya swala ya alasiri, na kama hataoga kwa ajili ya swala ya alasiri pia, ni wajibu aoge kwa ajili ya swala ya magharibi, na kama hataoga kwa ajili ya swala ya magharibi pia na wakati ukawa hautoshi, basi ni wajibu aoge kwa ajili ya swala ya Isha. 326. Kama damu ya istihadha nyingi itakatika kabla ya kila swala, kisha akaona damu, ni wajibu aoge katika kila swala kwa tahadhari ya wajibu. 327. Kama istihadha nyingi itakuwa istihadha chache ni wajibu kwake afanye wadhifa wa istihadha nyingi katika swala ya kwanza, kisha atafanya wadhifa wa istihadha chache katika swala zinazokuja, na vile vile istihadha ya wastani ikiwa istihadha chache, atafanya wadhifa wa istihadha ya wastani katika swala ya kwanza, kisha atafanya wadhifa wa istihadha chache katika swala zingine. 328. Kama mustahadha ataacha kufanya moja ya wadhifa wake wa wajibu, kama vile kuacha kubadilisha pamba basi swala yake inabatilika. 329. Mwenye istihadha chache kama anataka kufanya kitendo ambacho ni sharti awe na udhu, mfano anataka kugusa maandiko ya Qur’an, kama itakuwa ni baada ya swala basi ni wajibu kwake atawadhe. 330. Mustahadha kama ataoga josho za wajibu wake ataruhusiwa kuingia msikitini, kusimama ndani yake, kusoma sura zenye sajda za wajibu na kuonana kimwili na mume wake, hata kama hatafanya vitendo vingine ambavyo ni wajibu avifanye kwa ajili ya swala, mfano kubadilisha pamba na kitambaa. 331. Mwenye istihadha nyingi au ya wastani kama akitaka kusoma sura yenye sajida ya wajibu au kuingia msikitini kabla ya swala, basi ni 64
Al-Masailul Islamiyah kwa tahadhari ya wajibu aoge, na vile vile mume wake akimtaka waonane kimwili, lakini akitaka kugusa Qur’ani ni wajibu kwake atawadhe pia. 332. Swala ya majanga ni wajibu kwa mustahadha na ni wajibu kwake afanye vyote ambavyo ni wajibu katika swala za kila siku. 333. Kama mustahadha atawajibika kuswali swala ya majanga katika wakati wa swala za kila siku, ni wajibu kwake afanye kwa ajili ya swala ya majanga kila kinachokuwa wajibu kwake kwa ajili ya swala za kila siku, hata kama akitaka kuswali moja baada ya nyingine na wala haijuzu kuswali swala zote mbili kwa josho moja. 334. Mustahadha kama akitaka kulipa swala zilizompita ni wajibu afanye katika kila swala vyote ambavyo ni wajibu kwake kwa ajili ya swala za adaa (swala zinazoswaliwa kwa wakati). 335. Mustahadha akijua kuwa damu inayotoka kwake sio damu ya jeraha au jipu na wala sio damu ya hedhi au nifasi kisheria, ni wajibu afanye wadhifa wa mustahadha, bali hata akishuku kuwa ni damu ya istahadha au ni katika damu zingine, kama haitakuwa na alama za damu zingine, basi ni lazima kwake afanye wadhifa wa mustahadha kwa tahadhari ya wajibu.
HEDHI 336. Damu ya hedhi ni damu ambayo inatoka kwenye mfuko wa uzazi wa mwanamke katika kila mwezi kwa siku maalumu. 337. Damu ya hedhi mara nyingi huwa ni ya moto, nzito nyeusi au nyekundu, inatoka kwa nguvu na inachoma. 338. Wanawake wa kikuraishi hukoma kutokwa na damu ya hedhi wanapofikisha umri wa miaka sitini, na wasio kuwa makuraishi hukoma kutokwa na damu ya hedhi wanapofikisha umri wa miaka 65
Al-Masailul Islamiyah hamsini, na kama wataona damu baada ya hapo haitakuwa damu ya hedhi hata kama ikiwa na alama za damu ya hedhi, bali itakuwa ni damu ya istihadha. 339. Damu ambayo anaiona binti kabla hajatimiza miaka tisa au anayoiona mwanamke baada ya kufikia umri wa kutotokwa na hedhi haitokuwa hedhi. 340. Mwanamke mwenye mimba kupata hedhi.
na mwenye kunyonyesha anaweza
341. Binti ambaye hajui kuwa ametimiza miaka tisa au laa, kama akiona damu ambayo haina sifa za hedhi haitokuwa hedhi, na kama itakuwa na sifa za hedhi basi itakuwa ni hedhi, inawezekana akawa ametimiza miaka tisa. 342. Mwanamke ambaye anashuku kuwa amekoma kutokwa na damu ya hedhi au laa, na wala hawezi kujua umri wake ni miaka mingapi? Kama ataona damu na wala hajui kuwa ni hedhi au laa, ni wajibu ajalie kuwa hajakoma kutokwa na damu ya hedhi. 343. Muda wa hedhi haupungui siku tatu wala hauzidi siku kumi, kama akiona damu kwa muda wa chini ya siku tatu hata kama ikiwa kidogo haitakuwa hedhi, na muda mchache unaotenganisha baina ya hedhi mbili ni siku kumi. 344. Ni wajibu siku tatu za hedhi ziwe kwa mfululizo, kama ataona damu kwa muda wa siku mbili kisha akatoharika siku moja, kisha akaona damu siku ya tatu, basi haitokuwa hedhi, ni juu yake kwa tahadhari ya sunna aache yaliyokatazwa katika hedhi na afanye vitendo vya istihadha, yaani aache kuonana kimwili, kuingia msikitini, kugusa maandiko ya Qur’ani, kugusa jina la Allah na kusoma sura zenye sajida za wajibu, na wakati huo huo afanye yaliyo wajibu kwa 66
Al-Masailul Islamiyah mustahadha, kutawadha, kuoga n.k, katika kila swala. 345. Sio lazima damu kutoka katika siku zote tatu, bali inatosha kuwepo damu ndani ya uke, lakini akitoharika katikati ya siku tatu kwa muda mfupi na muda huo uwe mfupi sana kwa kiasi kwamba itasemwa kuwa damu ilikuwa ndani ya uke katika muda wa siku tatu basi itakuwa hedhi. 346. Sio lazima aone damu katika usiku wa kwanza na usiku wa nne kwa muda wa siku tatu, lakini ni lazima isikatike usiku wa pili na usiku wa tatu, kama ataona damu kuanzia adhana ya Asubuhi ya siku ya kwanza na ikakatika wakati huo huo wa siku ya nne na haijakatika usiku wa pili, wa tatu na wa nne, itakuwa ni hedhi. 347. Kama ataona damu kwa muda wa siku tatu mfululizo kisha akatoharika, na kama ataona damu baada ya hapo na siku zote alizoona damu na alizotoharika kama hazizidi siku kumi, basi zote zitakuwa hedhi. 348. Kama ataona damu zaidi ya siku tatu na chini ya siku kumi na wala hajui kuwa ni damu ya jipu au jeraha au damu ya hedhi, basi ni wajibu aijalie kuwa ni hedhi, sawasawa atakuwa na yakini kuwa ni hedhi au anashaka katika hilo. 349. Kama ataona damu na hajui kuwa ni damu ya jeraha au hedhi kabla ya kupita siku tatu, basi kwa tahadhari ya wajibu afanye ibada zake na aache kila kinachokuwa wajibu kuachwa na mwenye hedhi mpaka itakapojulikana hali halisi. 350. Kama ataona damu kisha akashuku kuwa ni damu ya hedhi au ni damu ya istihadha, basi ni wajibu aijalie kuwa ni hedhi, kama itakuwa na alama za hedhi.
67
Al-Masailul Islamiyah 351. Kama ataona damu na akawa hajui kuwa ni damu ya hedhi au ni damu ya bikira, basi ni wajibu afanye uchunguzi kwa kuingiza pamba ndani ya uke na kusubiri kidogo kisha aitoe, kama damu haikuingia ndani ya pamba bali ikachovya pembeni basi itakuwa ni damu ya bikira, na kama damu itaingia ndani ya pamba yote basi itakuwa ni damu ya hedhi, na hii ni ikiwa damu ya bikira sio nyingi inayoweza kufanana na ya hedhi. 352. Kama ataona damu chini ya siku tatu na akatoharika, kisha akaona damu kwa muda wa siku tatu zingine, basi damu ya mara ya pili ni hedhi na ya kwanza sio hedhi hata kama itakuwa katika ada yake.
HUKUMU ZA HEDHI 353. Ni haramu kwa mwenye hedhi mambo yafuatayo:Ibada ambazo ni wajibu kutawadha au kuoga au kutayamamu, lakini ibada ambazo hazihitaji udhu au kuoga au kutayamamu mfano swala ya maiti, anaweza kuiswali akiwa katika hali ya hedhi. Mambo yote ambayo ni haramu kwa mwenye janaba. Jimai ni haramu kwa mwanaume na mwanamke, hata kwa kiasi cha kuingiza kichwa cha uume na kutotoka manii, bali ni kwa tahadhari ya wajibu asiingize kichwa hata kidogo na asimwingilie mwanamke mwenye hedhi kwa nyuma, lakini hakuna tatizo kumbusu. 354. Ni haramu kuonana kimwili kama hedhi itaendelea zaidi ya ada yake, lakini ni wajibu azijaalie siku hizo kuwa ni hedhi, kama ataona damu zaidi ya siku kumi ni wajibu ajalie ada za jamaa zake wa karibu kuwa ni hedhi yake, na itakuwa haramu kwa mume wake kumuingilia. 355.Siku za hedhi zinagawanyika sehemu tatu 68
Al-Masailul Islamiyah 1 – Siku za mwanzo 2 - Siku za katikati 3 - Siku za mwisho 356. Kama mume wake atamwingilia kwa mbele katika siku za mwanzo atatoa dinari moja kumpa fukara, na akimwingilia siku za katikati atatoa nusu dinari, na siku za mwisho atatoa robo dinari. Pia atatoa kafara kama atamwingilia kwa nyuma akiwa katika hedhi. 357. Ni kwa tahadhari ya sunna kwa mwanamume kutoa kafara kama akijua kuwa mke wake ana hedhi naye akamwingilia, lakini akimwingilia katika hali ya hedhi naye hajui hatawajibika kutoa chochote. 358. Sio wajibu kafara iwe ni dinari bali inaweza ikawa thamani yake. 369. Kama thamani ya kafara itatofautiana wakati alipomwingilia mke wake mwenye hedhi na wakati wa kumpa fukara, ni wajibu atoe thamani ya wakati anapompa fukara. 360. Kama mwanaume atamwingilia mke wake mwenye hedhi katika siku za mwanzo za hedhi na za katikati na za mwisho itabidi atoe kafara katika kila kundi kafara yake. 361. Mwanaume akimwingilia mke wake mwenye hedhi na akatoa kafara, kisha akarudia tena kumwingilia atatoa kafara kwa mara nyingine. 362. Mwanaume akimwingilia mke wake mwenye hedhi zaidi ya mara moja na hajatoa kafara wakati huo, basi ni kwa tahadhari ya sunna atoe kafara moja katika kila mara aliyomwingilia. 363. Kama mwanaume atajua katikati ya jimai kuwa mke wake ana hedhi, ni wajibu aache haraka na kama hataacha atalipa kafara kwa tahadhari 69
Al-Masailul Islamiyah ya sunna. 364. Mwanaume akizini na mwanamke mwenye hedhi au akimwingilia mwanamke ajinabia (asiyekuwa halali kwake) mwenye hedhi kwa kudhania kuwa ni mke wake, basi ni kwa tahadhari ya sunna atoe kafara. 365. Mtu ambaye hawezi kulipa kafara aombe msamaha kwa Allah (swt) hii ikiwa hana uwezo kuanzia mwanzo, lakini kama alikuwa anauwezo kisha akawa hana uwezo, basi kwa tahadhari ya sunna akipata uwezo alipe kafara. 366. Talaka ya mwanamke akiwa katika hedhi ni batili. 367. Mwanamke akisema mimi nina hedhi au nimetoharika kutokana na damu ya hedhi, kauli yake itakubalika ikiwa haijulikani kuwa ni muongo. 368. Kama mwanamke atatokwa na hedhi wakati wa kuswali swala yake itabatilika. 369. Kama mwanamke atashuku kuwa ametokwa na hedhi wakati wa swala au laa, swala yake inasihi, lakini akijua kuwa alitokwa na hedhi wakati wa swala basi swala yake itabatilika. 370. Baada ya mwanamke kutoharika kutokana na hedhi ni wajibu aoge kwa ajili ya swala na ibada zingine ambazo ni sharti kuwa na udhu, au kuoga, na kuoga josho la hedhi ni kama josho la janaba, lakini akitaka kuswali ni wajibu atawadhe kabla ya kuoga au baada ya kuoga. 371. Baada ya mwanamke kutoharika kutokana na damu ya hedhi akipewa talaka inasihi hata kama bado hajaoga, vilevile inajuzu kwa mume wake kumwingilia kabla ya kuoga, lakini kwa tahadhari ya sunna aoshe uke wake kabla ya jimai, na kwa tahadhari ya sunna ajiepushe na jimai kabla ya kuoga, ama mambo mengine ambayo yana70
Al-Masailul Islamiyah haramishwa wakati wa hedhi mfano, kubakia msikitini, kugusa maandiko ya Qur’an ambayo ni sharti awe na udhu haitakuwa ruhusa kwake mpaka aoge au atawadhe. 372.Kama maji hayatoshi kutawadha na kuoga, lakini yanatosha ama kuoga au kutawadha, basi ni wajibu aoge na atayamamu badala ya udhu kwa tahadhari ya wajibu, na kama hayatoshi kuoga, basi ni wajibu atawadhe halafu atayamamu badala ya kuoga, na kama hana maji kabisa ni wajibu atayamamu mara mbili, moja ni badala ya kuoga na nyingine ni badala ya udhu. 373. Mwanamke mwenye hedhi halipi swala za kila siku zilizopita wakati wa hedhi, lakini ni wajibu alipe saumu za wajibu zilizompita wakati wa hedhi. 374. Mwanamke akijua kuwa wakati wa swala umeingia na kama akichelewesha swala atatokwa na hedhi, basi ni wajibu kwake aswali haraka. 375. Kama atachelewesha swala mpaka wakati ukapita kwa kiwango cha swala kisha akapata hedhi, ni wajibu ailipe hiyo swala, mwanamke ambaye sio msafiri kama akichelewesha swala ya Adhuhuri kuanzia mwanzo wa wakati kisha akapata hedhi baada ya kupita muda wa kuweza kuswali rakaa nne, ni wajibu kwake ailipe, na kwa mwanamke msafiri akichelewa kwa kiwango cha rakaa mbili ni wajibu ailipe. 376.Kama mwanamke atatoharika mwisho wa wakati wa swala, na wakati ukatosha kuoga na kutawadha na maandalizi mengine kwa ajili ya swala na kuswali rakaa moja au zaidi ndani ya wakati, ni wajibu aswali na kama hataswali ni wajibu ailipe 377. Kama wakati hautoshi kuoga na kutawadha lakini ukatosha kutaya71
Al-Masailul Islamiyah mamu na kuswali, ni wajibu aswali hiyo swala, na vilevile kama wadhifa wake ni kutayamamu ni wajibu atayamamu na kuswali swala hiyo. 378. Mwanamke mwenye hedhi akishuku kuwa wakati unamtosha kuswali au laa, ni wajibu aswali swala hiyo. 379. Kama hajaswali kwa kudhania kuwa wakati haumtoshi kuswali rakaa moja na kufanya maandalizi mengine, kisha ikabainika kuwa wakati ulikuwa unatosha basi ni wajibu ailipe swala hiyo. 380. Ni sunna kwa mwanamke mwenye hedhi unapofika wakati wa swala ajisafishe, abadilishe pamba na kitambaa kisha atawadhe au atayamamu kama hataweza kutawadha, kisha akae katika sehemu ya kuswalia akielekea kibla na asome dhikiri, dua na kumswalia Mtume (saww) 381. Ni makuruhu kwa mwenye hedhi kusoma Qur’an tukufu, kuwa nayo, kuibeba na kugusa pembeni mwa maandiko, vilevile ni makuruhu kwake kupaka hina na n.k
VIGAWANYO VYA HEDHI 382. Wanawake wenye kutoka hedhi wamegawanyika katika sehemu sita; 1). Mwenye ada ya wakati na idadi: Yaani anaona damu ya hedhi katika miezi miwili mfululizo kwa wakati maalumu na kwa idadi maalumu mfululizo mwanzo wa mwezi mpaka siku ya saba. 2).Mwenye ada ya wakati:Yaani anaona damu ya hedhi katika miezi miwili mfululizo kwa wakati maalumu, lakini idadi inatofautiana katika mwezi wa kwanza na wa pili mfano; Anaona damu katika mwezi wa kwanza kuanzia mwanzo wa mwezi mpaka siku ya saba, na mwezi wa pili kuanzia mwanzo wa mwezi mpaka siku ya nane. 72
Al-Masailul Islamiyah
3). Mwenye ada ya idadi: Yaani idadi ya hedhi katika miezi miwili inalingana, lakini wakati wa kuona damu katika miezi miwili unatofautiana mfano: Anaona damu katika mwezi wa kwanza kuanzia siku ya tano mpaka siku ya kumi na mwezi wa pili kuanzia siku ya kumi na mbili mpaka siku ya kumi na saba. 4). Asiokuwa na ada maalumu sio ya wakati wala ya idadi: Hapo mwanzo alikuwa nayo lakini imeharibika, na wala haijatulia nakupata ada mpya. 5). Anayeanza: Naye ni ambaye anaona damu kwa mara ya kwanza. 6). Aliyesahau ada yake.
WENYE ADA YA WAKATI NA IDADI 383. Wenye ada ya wakati na idadi wanagawanyika sehemu tatu:Mwanamke ambaye anaona damu ya hedhi katika miezi miwili mfululizo kwa wakati maalumu na anatoharika kwa wakati maalumu mfano: Anaona damu katika miezi miwili mfululizo kuanzia mwanzo wa mwezi na anatoharika siku ya saba, ada yake inakuwa kuanzia mwanzo wa mwezi mpaka siku ya saba. Mwanamke ambaye hatohariki kutokana na damu lakini anaona damu katika miezi miwili mfululizo na kwa siku maalumu damu yenye sifa ya hedhi, lakini damu ambayo anaiona baada ya siku maalumu inakuwa na sifa za damu ya istihadha. Mfano anaona damu yenye sifa ya hedhi kuanzia mwanzo wa mwezi mpaka siku ya nane katika miezi yote miwili, kwa hiyo hii ni ada yake kuanzia mwanzo wa mwezi mpaka siku ya nane. Mwanamke ambaye anaona damu ya hedhi katika miezi miwili mfululizo kwa wakati maalumu na inaendelea kwa muda wa siku tatu au zaidi kisha 73
Al-Masailul Islamiyah anatoharika siku moja au zaidi, kisha anaona damu kwa mara nyingine, kama siku alizoona damu, na siku alizotoharika hazizidi siku kumi katika kila miezi miwili, basi siku zote hizo zitakuwa ni ada yake mfano: Akiona damu katika mwezi wa kwanza kuanzia mwanzo mpaka siku ya tatu, na katika mwezi wa pili akiona kuanzia mwanzo wa mwezi mpaka siku ya tatu, kisha akatoharika kwa muda wa siku tatu au zaidi au pungufu ya tatu, kisha akaona damu kwa mara nyingine kama siku alizoona damu, na siku alizotoharika hazizidi siku tisa, kwa hiyo ada ya huyu mwanamke ni siku tisa. 384. Mwanamke mwenye ada ya wakati na idadi kama akiona damu kabla ya ada au baada ya ada kwa siku mbili au tatu kwa kiasi kwamba itasemwa kuwa hedhi yake imetangulia au imechelewa, ni wajibu kwake afanye wadhifa wa hedhi (afanye anayo yafanya mwenye hedhi) hata kama damu haitakuwa na sifa za hedhi, na kama atajua baadae kuwa haikuwa ni damu ya hedhi mfano: Akitoharika kabla ya siku tatu basi ni wajibu kwake alipe ibada zilizompita. 385. Mwanamke mwenye ada ya idadi na wakati:kama akiona kabla ya ada yake na ikaendelea mpaka kwenye siku za ada yake na baada ya ada, kama siku zote alizoona damu hazizidi siku kumi basi zote zitakuwa ni hedhi. Na kama zitazidi siku kumi basi damu aliyoiona katika siku za ada yake zitakuwa ni hedhi, na damu ambayo aliona kabla na baada ya ada itakuwa ni damu ya istihadha, na ni wajibu alipe ibada zilizopita katika siku zilizotangulia ada au baada ya ada. Kama siku za ada na zilizotangulia ada hazizidi siku kumi basi zote zitakuwa ni hedhi. Na kama siku zitazidi siku kumi basi siku za ada peke yake zitakuwa ni hedhi na damu aliyoiona kabla ya ada itakuwa ni damu ya istihadha, na ni 74
Al-Masailul Islamiyah wajibu alipe ibada zilizompita. Kama ataona damu katika siku za ada na baada ya siku za ada kama siku zote hazitazidi siku kumi basi zote ni hedhi, na kama zitazidi siku kumi basi siku za ada peke yake zitakuwa ni hedhi na zilizobaki ni istihadha. 386. Mwenye ada ya wakati na idadi :Kama ataona damu katika baadhi ya siku za ada yake na akaona kabla ya ada, kama siku zote hazitazidi siku kumi, basi zitakuwa ni hedhi. Na kama zitazidi siku kumi, basi siku alizoona damu katika siku za ada yake zitakuwa ni hedhi, hata kama siku hizo zitakuwa chache au nyingi kuliko ada yake, na zilizobaki zitakuwa ni istihadha. Kama akiona katika baadhi ya siku za ada yake na baada ya ada na siku zote hazizidi kumi basi zote ni hedhi. Na kama siku alizoona damu zinazidi siku kumi ni wajibu ajalie siku zilizoingiliana na ada yake azifanye kuwa ni hedhi na zilizobaki ni istihadha. 387. Mwanamke mwenye ada ya wakati na idadi, kama akiona damu siku tatu au zaidi kisha akatoharika, kisha akaona damu kwa mara nyingine, na muda uliotenganisha baina ya damu mbili ni pungufu ya siku kumi, kisha siku alizoona damu na siku alizotoharika zinazidi siku kumi, mfano: aone damu kwa muda wa siku tano, kisha anaona damu kwa mara ya pili kwa muda wa siku tano zingine, kwa hali hii kutakuwa na sura zifuatazo:Damu aliyoiona kwa mara ya kwanza yote au baadhi ilingane na siku za ada yake na wala hailingani na damu atakayoiona baada ya kutoharika na siku za ada yake, basi hapa ni wajibu ajaalie kuwa ya kwanza ni hedhi na ya pili ni istihadha. 75
Al-Masailul Islamiyah
Damu ya kwanza isilingane na siku za ada yake, damu ya pili yote au baadhi ilingane na siku za ada yake, hapa ni wajibu aifanye damu ya pili kuwa ni hedhi na damu ya kwanza kuwa istihadha. Baadhi ya siku za kwanza na za pili kulingana na siku za ada yake, na damu ya kwanza iliyolingana na siku za ada isipungue siku tatu na damu yote iliyolingana na ada na siku alizotoharika zisizidi siku kumi, na kwa hali hii siku zote zitakuwa ni hedhi, na iliyotangulia ada na iliyochelewa itakuwa ni istihadha. Mfano kama ada imeanza siku ya tatu ya mwezi mpaka siku kumi na akaona damu katika moja ya miezi kuanzia mwanzo mpaka siku ya sita, kisha akatoharika kwa muda wa siku mbili, kisha akaona damu mpaka siku ya kumi na tano ya mwezi, basi atajaalia siku ya tatu mpaka ya kumi ni hedhi na kuanzia siku ya kwanza mpaka siku ya tatu, na kuanzia siku ya kumi mpaka siku ya kumi na tano ni istihadha. Baadhi ya damu ya kwanza na ya pili ikilingana na siku za ada lakini baadhi ya damu ya kwanza iliyolingana na ada iwe pungufu ya siku tatu, basi ni wajibu kwake katika hali hii ajiepushe na vilivyoharamu kwa mwenye hedhi katika siku za damu mbili na siku alizotoharika, na wakati huo huo atafanya vitendo vya mustadha na kufanya ibada kama ilivyo tajwa katika hukumu za mustadha. 388. Mwenye ada ya wakati na idadi, kama hataona damu katika wakati wa ada yake na akaiona wakati mwingine kwa kiwango cha ada yake, ni wajibu aifanye kuwa hedhi, sawa sawa iwe kabla ya ada au baada ya ada.
389. Mwenye ada ya wakati na idadi kama ataona damu wakati wa ada yake lakini idadi ikawa pungufu au zaidi ya ada ya hedhi, na damu aliyoiona kabla ya ada ikiwa na idadi ya ada, na kama kitenganishi baina ya damu ni siku kumi au zaidi, atajaalia damu mbili kuwa ni 76
Al-Masailul Islamiyah hedhi, na kama siku za damu mbili na siku alizotoharika hazizidi siku kumi basi zote zitakuwa ni hedhi. 390. Mwenye ada ya wakati na idadi kama akiona damu zaidi ya siku kumi, basi damu aliyoiona katika siku za ada itakuwa ni hedhi hata kama haina sifa za hedhi, na damu aliyoiona baada ya siku za ada ni istihadha hata kama ina sifa za hedhi, mfano: mwanamke ambaye ada yake ni kuanzia mwanzo wa mwezi mpaka siku ya saba, kama akiona damu kuanzia mwanzo wa mwezi mpaka siku ya kumi na mbili, atajaalia siku saba za mwanzo kuwa ni hedhi na siku tano za mwisho kuwa ni istihadha. 391. Wenye ada ya wakati wanagawanyika sehemu tatu:mwanamke ambaye anaona damu ya hedhi katika miezi miwili mfululizo kwa wakati maalumu kisha anatoharika baada yake siku kadhaa, lakini idadi ya siku katika kila mwezi inatofautiana. Mfano anaona damu katika miezi miwili mfululizo kuanzia mwanzo wa mwezi, na mwezi wa kwanza mpaka siku ya saba na mwezi wa pili mpaka siku ya nane, basi huyu ada yake ni kuanzia mwanzo wa mwezi. Mwanamke ambaye hatohariki kutokana na damu lakini damu ambayo anaiona katika miezi miwili mfululizo kwa wakati maalumu inakuwa na sifa ya hedhi, na damu anayoiona katika siku zingine inakuwa na sifa za istihadha na idadi ya siku anazoona damu yenye sifa za hedhi katika miezi miwili hailingani. Mfano damu anayoiona kuanzia mwanzo wa mwezi mpaka siku ya saba ya mwezi wa kwanza na mwezi wa pili kuanzia mwanzo wa mwezi, mpaka siku ya nane inakuwa na sifa za hedhi na inayobaki inakuwa na sifa za istihadha. Mwanamke ambaye anaona damu ya hedhi katika miezi miwili mfululizo kwa wakati maalumu kwa siku tatu au zaidi, kisha anatoharika kisha anaona damu kwa mara nyingine, lakini idadi ya siku alizoona damu mbili na alizotoharika hazizidi siku kumi, lakini katika mwezi wa pili inazidi 77
Al-Masailul Islamiyah siku hizi au zinapungua kuliko mwezi wa kwanza mfano: katika mwezi wa kwanza idadi ya siku ni nane na mwezi wa pili ni siku tisa, na huyu pia mwanzo wa mwezi utakuwa ni ada yake. 392.Mwenye ada ya wakati kama akiona damu, kabla ya ada au baada kwa siku mbili au tatu, ikiwa hedhi imetangulia au imechelewa ni wajibu kwake afanye wadhifa wa hedhi hata kama hiyo damu haina sifa za hedhi, na kama atatambua baadae kuwa haikuwa damu ya hedhi mfano: akitoharika kabla ya siku tatu, ni wajibu alipe ibada zilizompita, nani bora kwake aache yaliyo haramu kwa mwenye hedhi na kufanya yaliyo wajibu kwa mustahadha. 393. Mwenye ada ya wakati, kama akiona damu zaidi ya siku kumi na akawa hawezi kutambua siku za hedhi kwa njia ya alama basi itabidi ajalie ada ya jamaa zake wa karibu kuwa ni hedhi yake. Sawa sawa jamaa zake wawe wa upande wa baba au wa mama, wako hai au maiti kwa sharti ada zao wote ziwe sawa, lakini ada zao zikitofautiana mfano: baadhi yao ni siku tano na baadhi yao ni siku saba, basi inajuzu kwake kujaalia ada ya waliowengi kuwa ni ada yake. 394. Mwenye ada ya wakati ambaye anafanya ada ya jamaa zake wa karibu kuwa ni hedhi yake, basi ni wajibu afanye siku ambayo ilikuwa mwanzo wa ada yake katika kila mwezi kuwa ni mwanzo wa hedhi yake mfano: Mwanamke ambaye alikuwa anaona damu kila mwanzo wa mwezi na anatoharika siku ya saba au ya nane, na kama ataona damu katika moja ya miezi kwa muda wa siku kumi na mbili na ada ya jamaa zake ni siku saba ni wajibu afanye siku saba kuanzia mwanzo wa mwezi kuwa ni hedhi na inayobaki kuwa istihadha. 395. Mwanamke ambaye ni wajibu kwake aifanye ada ya jamaa zake wa karibu kuwa ni hedhi yake, kama hana jamaa au wakatofautiana ada zao ni wajibu kila mwezi kuanzia mwanzo wa mwezi mpaka siku ya saba afanye kuwa ni hedhi na inayobaki kuwa istihadha lakini kama 78
Al-Masailul Islamiyah alama za hedhi zitakuwa katika siku za katikati au za mwisho ni nyingi zaidi kuliko siku zingine, basi ni wajibu afanye mwanzo wa siku saba kuanzia katikati au kuanzia mwisho. 396. Wenye ada ya idadi wanagawanyika sehemu tatu:mwanamke ambaye idadi ya siku za hedhi yake katika miezi miwili mfululizo zinakuwa sawa, lakini wakati wa kuona damu katika miezi miwili unatofautiana, basi katika hali hii atajaalia siku zote alizoona damu kuwa ni hedhi mfano: Kama akiona damu katika mwezi wa kwanza kuanzia mwanzo mpaka siku ya tano, na katika mwezi wa pili kuanzia siku ya tano na katika mwezi wa pili kuanzia siku ya kumi na moja mpaka siku ya kumi na tano, ada yake itakuwa ni siku tano. Mwanamke ambaye hatohariki kutokana na damu, lakini yeye anaona damu katika miezi miwili mfululizo na katika siku maalumu damu yenye sifa za hedhi na katika siku zingine anaona damu yenye sifa za istihadha, na idadi ya siku amabzo ameona damu yenye sifa za hedhi katika miezi inalingana lakini wakati unatofautiana. Katika hali hii siku zenye sifa za hedhi zinakuwa ni ada yake mfano: Akiona damu kuanzia mwanzo wa mwezi mpaka siku tano na katika mwezi unaofuatia kuanzia siku tano na damu katika mida yote miwili inakuwa na sifa za hedhi na inayobaki inakuwa na sifa za istihadha basi ada yake itakuwa siku tano. Mwanamke anayeona damu katika miezi miwili mfululizo kwa muda wa siku tatu au zaidi kisha akatoharika kwa muda wa siku moja au zaidi, kisha akaona damu kwa mara nyingine lakini wakati wa kuona ukatofautiana katika miezi miwili, kama idadi ya damu mbili na siku alizotoharika hazijazidi siku kumi na idadi ya siku katika miezi miwili iko sawa, basi siku alizoona damu na siku alizotoharika zinakuwa ni ada yake mfano: kama akiona damu kuanzia mwanzo wa mwezi mpaka siku ya tatu kisha akatoharika kwa muda wa siku mbili kisha akaona damu kwa muda wa siku tatu zingine, na katika mwezi wa pili akiona damu kuanzia siku ya kumi na moja mpaka siku ya kumi na tatu, kisha akatoharika kwa muda wa siku 79
Al-Masailul Islamiyah mbili au zaidi au pungufu kisha akaona damu kwa mara nyingine na siku zote hazijazidi siku nane basi ada yake itakuwa siku nane. 397. Mwenye ada ya idadi kama akiona damu zaidi ya ada yake na ikazidi kumi itakuwa kama ifuatavyo:Kama damu yote itakuwa ina sifa moja ni wajibu ajalie idadi ya siku kuanzia wakati alipoona damu kuwa ada yake na inayobaki istihadha. Kama sifa za damu zitatofautiana baadhi ikawa na sifa za hedhi na nyingine za istihadha, kama damu yenye sifa za hedhi idadi yake italingana na ada yake ni wajibu ajalie siku hizo kuwa ni hedhi na zinazobaki kuwa istihadha. Kama siku ambazo damu itakuwa na sifa za hedhi zinazidi siku za ada yake atajalia idadi ya ada yake kuwa ni hedhi peke yake na inayobaki kuwa istihadha. Kama siku ambazo damu itakuwa na sifa za hedhi ni pungufu kuliko siku za ada yake, ni wajibu aongeze siku zingine katika siku za ada yake kuwa ni hedhi yake na zinazobaki ni istihadha. 398. Mwenye utata:Ni mwanamke ambaye anaona damu katika miezi kadhaa lakini hana ada thabiti sio ya idadi wala ya wakati, kama ataona damu zaidi ya siku kumi na damu yote ina sifa moja kama ada ya jamaa zake wa karibu ni siku saba, basi afanye siku saba kuwa ni hedhi na inayobaki kuwa ni istihadha, na kama ada yao ni chache mfano: Ni siku tano, ataifanya kuwa ni hedhi na kwa tahadhari ya sunna aache yaliyo haramu kwa wenye hedhi na kufanya wadhifa wa mustadha, katika tofauti baina ya siku saba na ada zao, na kama ada ya jamaa zake wa karibu ni zaidi ya siku saba, mfano ada yao ni siku tisa kwa hiyo yeye atafanya siku saba kuwa ni hedhi na siku mbili zilizobaki ataacha yaliyoharamu kwa wenye hedhi na kufanya wadhifa wa mustadha kwa tahadhari ya sunna. 80
Al-Masailul Islamiyah
399. Mwenye utata kama ataona damu zaidi ya siku kumi, na baadhi ya damu ina sifa ya hedhi na nyingine ina sifa ya istihadha, kama damu yenye sifa ya hedhi ni pungufu ya siku tatu au zaidi ya siku kumi ni wajibu afanye kama tulivyotaja katika mas’ala yaliyopita, lakini kama damu yenye sifa ya hedhi sio pungufu ya siku tatu wala zaidi ya siku kumi basi yote itakuwa ni hedhi. 400. Anayeanza: Ni mwanamke ambaye anaona damu kwa mara ya kwanza, kama ataona damu zaidi ya siku kumi yenye sifa moja, basi ni wajibu afanye ada ya jamaa zake wa karibu kuwa ni ada yake ambayo ni siku saba na zinazobaki kuwa ni istihadha. 401. Anayeanza kama ataona damu zaidi ya siku kumi baadhi yake ina sifa ya hedhi na nyingine ina sifa ya istihadha, kama damu yenye sifa ya hedhi ni zaidi ya siku tatu na haijazidi siku kumi basi yote itakuwa ni hedhi, lakini akiona damu kabla ya siku kumi kuisha damu yenye sifa ya hedhi pia, mfano: Akiona damu nyeusi kwa muda wa siku tano, na damu ya njano kwa muda wa siku tisa, kisha akaona damu nyeusi kwa muda wa siku tano zingine, basi ni wajibu afanye ada ya jamaa zake wa karibu kuwa ni hedhi yake na nyingine ni istihadha. 402. Anayeanza akiona damu zaidi ya siku kumi, na baadhi ya damu ina sifa ya hedhi na nyingine ina sifa ya istihadha kama siku ambazo zina sifa za hedhi ni chache kuliko siku tatu au zaidi ya siku kumi, basi atajalia ada ya jamaa zake wa karibu kuwa ni hedhi yake na inayobaki kuwa ni istihadha. 403. Aliyesahau: Ni mwanamke ambaye amesahau ada yake, kama ataona damu zaidi ya siku kumi, ni wajibu ajalie siku ambazo zina sifa ya hedhi kuwa ni hedhi, na ikiwa hataweza kupambanua kwa njia ya sifa na alama ni wajibu ajaalie siku saba za mwanzo kuwa ni hedhi na zinazobaki kuwa ni istihadha. 81
Al-Masailul Islamiyah
404. Anayeanza, mwenye utata, aliyesahau na mwenye ada ya idadi, kama wataona damu yenye sifa ya hedhi au wakawa na yakini kuwa damu itaendelea kwa muda wa siku tatu, ni wajibu kwao waache ibada, na ikibainika baadae kuwa haikuwa ni hedhi ni wajibu kwao walipe ibada zilizowapita, na kama hawajawa na yakini, na damu haikuwa na sifa ya hedhi, basi ni lazima kwa tahadhari ya wajibu wafanye wadhifa wa mustadha kwa muda wa siku tatu na waache yaliyoharamu kwa wenye hedhi, na kama hawatatoharika kabla ya siku tatu ni wajibu waifanye kuwa ni hedhi. 405. Mwenye ada: Sawa sawa awe ni wa idadi au wakati au idadi na wakati, kama wataona damu katika miezi miwili mfululizo inatofautiana na ada zao kwa idadi au wakati au idadi na wakati na ilikuwa ni ya aina moja katika miezi miwili katika idadi au wakati au katika idadi na wakati, atarejea ada yake aliyoiona katika miezi hii miwili Mfano: Kama alikuwa anaona damu kuanzia mwanzo wa mwezi mpaka siku ya saba, kisha anatoharika lakini yeye akaona katika miezi miwili mfululizo kuanzia siku ya kumi mpaka siku ya kumi na saba, kisha akatoharika basi ada yake itakuwa kuanzia siku ya saba mpaka siku ya kumi na saba. 406. Makusudio ya mwezi mmoja ni kuanzia kuonekana damu mpaka siku ya thelathini, na wala sio mwanzo wa mwezi, labda hedhi ianze mwanzo wa mwezi. 407. Mwanamke ambaye anaona damu katika mwezi mara moja, kama ataona damu mara mbili na damu zote mbili zina sifa ya hedhi, kama siku alizotoharika ni chache kuliko siku kumi ni wajibu azifanye damu mbili kuwa ni hedhi. 408. Kama akiona damu kwa muda wa siku tatu au zaidi, damu yenye sifa ya hedhi, kisha akaona damu kwa muda wa siku kumi au zaidi, damu yenye sifa ya istihadha, kisha akaona baada ya muda wa siku tatu, 82
Al-Masailul Islamiyah damu yenye sifa ya hedhi, basi ni wajibu ajalie damu ya kwanza na ya pili zilizokuwa na sifa ya damu ya hedhi kuwa ni hedhi. 409. Mwanamke akitoharika kutokana na hedhi kabla ya siku kumi, na akajua kuwa hakuna damu tumboni mwake, basi ni wajibu aoge kwa ajili ya ibada zake, na akipta dhana kwamba ataona damu kwa mara nyingine kabla ya siku kumi kwisha. Lakini kama atakuwa na yakini kuwa ataona damu kwa mara nyingine kabla ya siku kumi kwisha, basi asioge, bali damu ya kwanza na ya pili na siku ambazo zinakuwa baina ya damu mbili zote zitakuwa ni hedhi. 410. Kama mwanamke akitoharika kabla ya siku kumi kwisha, na akadhania kuwa bado kuna damu ndani ya tumbo, ni wajibu achukue pamba na kuingiza ndani ya uke na asubiri kidogo kisha aitoe pamba, kama pamba itakuwa ni safi basi ataoga na kufanya ibada, na kama pamba haitakuwa safi mfano: Ikawa na rangi ya njano, haitakuwa ni hedhi isipokuwa kama itakuwa katika siku za ada yake, bali hiyo itakuwa ni istihadha. Lakini kama pamba itakuwa na damu na haikuwa katika siku za ada yake au ada yake ni siku kumi, basi ni wajibu asubiri kama atatoharika kabla ya siku kumi ataoga, laa sivyo ataoga mwanzo wa siku ya kumi kama atatoharika mwanzo wa siku ya kumi, lakini kama damu yake itazidi siku kumi na ada yake ni pungufu ya siku kumi, kama akijua kuwa atatoharika kabla ya siku kumi au mwanzo wa siku kumi basi asioge, na kama akidhania kuwa damu itaendelea mpaka siku ya kumi basi kwa tahadhari aache ibada ikiwa damu ina sifa ya hedhi, japo ni bora kuacha yaliyoharamu kwa mwenye hedhi na kufanya wadhifa wa mustahadha, na kama atatoharika kabla ya siku ya kumi au mwanzo wa siku ya kumi basi yote itakuwa ni hedhi, na kama damu itazidi siku kumi basi ni wajibu afanye ada yake kuwa ni hedhi na inayobaki kuwa ni istihadha, na atalipa ibada zilizompita katika siku zilizozidi ada yake. 411. Kama atafanya baadhi ya siku kuwa ni hedhi kisha asifanye ibada, 83
Al-Masailul Islamiyah halafu akatambua baadae kuwa haikuwa ni hedhi ni wajibu kwake alipe swala na saumu zilizompita katika siku hizo, na kama atafanya ibada kwa kudhania kuwa hana hedhi kisha akagundua kuwa alikuwa na hedhi, basi ni wajibu kwake alipe saumu alizofunga katika siku hizo.
NIFASI 412. Damu inayoanza kutoka baada ya sehemu ya mtoto kutokeza nje kutoka tumboni na ikakatika kabla ya siku kumi au mwanzo ni mwa siku kumi ni damu ya nifasi au “uzazi�. 413. Damu anayoiona mwanamke kabla ya kutokeza sehemu ya mtoto nje kutoka tumboni sio damu ya nifasi. 414.Ili kuwa na uhakika wa damu ya nifasi sio lazima mtoto awe amekamilika kuumbwa, hata kama kikitoka kipande cha damu au mwanamke mwenyewe akijua kuwa kilichotoka kama kingebakia tumboni kingekuwa binadamu au wakunga wanne wakimwelezea kuwa kilichotoka kama kingebakia tumboni kingekuwa binadamu basi damu atakayoiona kwa muda wa siku kumi ni damu ya nifasi. 415. Damu ya nifasi haizidi siku kumi. 416. Kama akishuku kuwa kilichotoka kwake kama kingebakia tumboni kingekuwa ni binadamu au laa, basi ni kwa tahadhari ya wajibu afanye uchunguzi. Kama akibakia katika hali ya shaka basi damu inayotoka sio damu ya nifasi kisharia. 417. Ni haramu kwa mwenye nifasi kubakia msikitini, kugusa maandishi ya Qur’an tukufu kwa mwili na kila kilichokuwa haramu kwa mwenye hedhi, na mengineyo, kama ambavyo ni wajibu kwake 84
Al-Masailul Islamiyah vilevile ni sunna kwake na makuruhu kwake yote ambayo ni wajibu au sunna au makuruhu kwa wenye hedhi. 418. Haisihi kwa mwanamke kupewa talaka akiwa katika hali ya nifasi, isipokuwa kwa masharti yatakayotajwa katika hukumu za talaka, pia ni haramu kumwingilia kimwili, na kama mume wake atamwingilia katika hali hiyo basi ni kwa tahadhari ya sunna atoe kafara kama ilivyoelezwa katika hukumu za hedhi. 419. Ni wajibu kwa mwanamke aoge baada ya kutoharika kutokana na damu ya nifasi kisha afanye ibada, na kama ataona damu kwa mara ya pili, kama damu zote mbili na siku alizotoharika hazizidi siku kumi au zikawa kumi basi zote zitakuwa ni nifasi, na kama alikuwa amefunga katika siku alizotoharika ni wajibu alipe hiyo saumu. 420. Kama mwanamke akitoharika kutokana na damu ya nifasi na akadhania kuwa kuna damu tumboni mwake, ni wajibu aingize pamba ukeni na kusubiri kidogo, kama haijachovya chochote basi aoge kwa ajili ya ibada zake. 421. Kama damu ya nifasi itazidi siku kumi, kama atakuwa na ada katika hedhi basi atajalia kiwango cha ada yake kuwa nifasi na inayobaki kuwa istihadha, na kama hana ada katika hedhi, atajalia kuanzia siku ya kwanza mpaka ya kumi ni nifasi na siku zinazobaki kuwa istihadha. 422. Mwanamke ambaye ada ya hedhi yake ni chini ya siku kumi, kama ataona damu ya nifasi zaidi ya ada yake ya hedhi ni wajibu ajaalie kiwango cha ada yake kuwa nifasi, na baada ya hapo aache ibada kwa muda wa siku moja kwa tahadhari ya wajibu, na baada ya siku moja mpaka siku ya kumi ni sunna kwake kufanya wadhifa wa mustahadha, na kuacha kila kilichokuwa haramu kwa mwenye nifasi, na kiasi kitakachozidi kumi itakuwa istihadha, na ni wajibu ajaalie siku baada 85
Al-Masailul Islamiyah ya ada yake mpaka siku ya kumi kuwa istihadha, na atalipa ibada zilizompita katika siku hizo, mfano: mwanamke ambaye anakuwa na ada katika hedhi siku sita ,kama ataona damu katika nifasi zaidi ya siku sita ni wajibu ajalie siku sita kuwa ni nifasi na aache ibada katika siku ya saba kwa tahadhari ya wajibu, na katika siku ya nane, tisa na kumi ni sunna afanye wadhifa wa mustahadha mfano: Mwanamke ambaye ada yake katika kila mwezi ni kuanzia siku ya ishirini mpaka ishirini na saba, kama atajifungua siku ya kumi na damu ikaendelea kutoka kwa muda wa mwezi au zaidi ya mwezi bila ya kukatika, ni wajibu kwake ajalie siku ya kumi mpaka siku ya kumi na saba kuwa ni nifasi, na baada ya kupita siku kumi zilizotajwa na kama damu anayoiona ni katika siku za ada yake basi ni hedhi, sawa sawa iwe na sifa za hedhi au laa. 423. Mwanamke ambaye hana ada katika hedhi, kama ataona damu baada ya kujifungua kwa muda wa mwezi au zaidi, basi kumi la mwanzo ni nifasi na kumi la pili ni istihadha, na atakayoiona baada ya hapo kama ina sifa za hedhi basi ni hedhi la sivyo ni istihadha.
KUOGA JOSHO LA KUGUSA MAITI 424.Kama mtu atagusa mwili wa maiti uliopoa na haujaoshwa kwa mwili wake ni wajibu kwake aoge josho la kugusa maiti, ni sawa sawa awe amegusa usingizini au akiwa macho, kwa kutaka au laa, bali ni wajibu kuoga kama amegusa ukucha kwa ukucha au mfupa kwa mfupa, lakini sio wajibu kuoga kama atagusa mzoga wa mnyama. 425. Sio wajibu kuoga kama mtu atagusa maiti ya binadamu ikiwa haujapoa mwili wote, hata kama atagusa sehemu iliyopoa. 426. Kama mtu akigusa mwili wa maiti kwa unywele au akagusa unywele wa maiti kwa mwili au akagusa unywele wa maiti kwa unywele wake, kama nywele hazitakuwa ni ndefu sana kupita kiasi basi ni wajibu 86
Al-Masailul Islamiyah aoge. 427.Ni wajibu kuoga josho la kugusa maiti, kama akigusa maiti ya mtoto hata kama ikiwa ni kichanga cha miezi minne (umri wa kuwa tumboni), vilevile ataoga kwa tahadhari ya sunna, kama atagusa kichanga chini ya miezi minne inamaana kuwa, akizaliwa mtoto mwenye umri wa miezi minne akiwa maiti, kama mwili wake utakuwa wa baridi wakati wa kutoka basi ni wajibu kwa mama yake aoge josho la kugusa maiti kwa tahadhari ya wajibu, na kama umri wake utakuwa chini ya miezi minne sio wajibu kwa mama aoge. 428.Mtoto ambaye amezaliwa baada ya mama yake kuwa maiti, kama mwili wa mama yake utakuwa umepoa wakati wa kuzaliwa basi ni wajibu kwa mtoto aoge josho la kugusa maiti akibaleghe kwa tahadhari. 429.Kama mtu akigusa maiti ambayo tayari imeshaoshwa josho zote mitatu sio wajibu kwake kuoga josho la kugusa maiti. 430.Kama kichaa au mtoto akigusa maiti ni wajibu kwa kichaa aoge akipona na kwa mtoto akibaleghe. 431. Kama sehemu ya mwili wa mtu aliye hai ikikatika au maiti ambaye haijaoshwa na sehemu iliyokatika ina mfupa, na mtu akaigusa kabla ya kuoshwa ni wajibu kwa aliyegusa aoge josho la kugusa maiti, lakini kama sehemu iliyokatika haina mfupa sio wajibu aoge. 432. Ni kwa tahadhari ya wajibu kuoga josho la kugusa maiti, ukigusa mfupa usiokuwa na nyama na haujaoshwa, sawa sawa umekatika kutoka kwa maiti au kwa mtu hai, na vile vile ni lazima aoge akigusa jino lililong’ooka kutoka kwa maiti kama maiti bado haijaoshwa, lakini sio lazima aoge akigusa jino lililong’ooka kutoka kwa mtu hai, na halina nyama au likiwa na nyama kidogo sana. 433. Josho la kugusa maiti ni sawa na kuoga janaba katika namna, lakini 87
Al-Masailul Islamiyah mtu akioga josho la kugusa maiti akitaka kuswali ni wajibu kwake atawadhe pia. 434.Kama atagusa maiti nyingi au akagusa maiti moja mara nyingi basi inamtosheleza kuoga josho moja. 435. Hakuna tatizo kwa mwenye kugusa maiti ambayo haijaoshwa, kusimama msikitini, kufanya jimai au kusoma sura zenye sajda ya wajibu, lakini ni wajibu aoge na atawadhe kama akitaka kuswali n.k.
HUKUMU ZA MUHTADHARI “ANAYEKATA ROHO” 436. Mwislamu anayekuwa katika hali ya kutokwa na roho ni wajibu alazwe chali, nyayo za miguu yake zielekee kibla, sawa sawa awe ni mwanaume au mwanamke, mkubwa au mdogo kama haitowezekana kulazwa kwa mgongo, basi ni wajibu alazwe kwa mgongo kwa kadiri itakavyowezekana, na kama haitawezekana kulazwa kwa kifua kifudifudi ni wajibu akalishwe akielekezwa kibla na kama ikishindikana hivyo pia ni lazima alazwe kwa upande wa kulia au wa kushoto akielekezwa kibla. 437. Ni kwa tahadhari ya sunna kumwelekeza maiti kibla kama ilivyoelekezwa katika mas’ala iliyotangulia mpaka amalize kumuosha, lakini akimaliza kumuosha ni bora alazwe kwa kama anavyolazwa wakati anaposaliwa, mpaka atakapozikwa. 438. Kumuelekeza muhtadhari upande wa kibla ni wajibu kwa kila mwislamu na wala haihitaji idhini ya mwenyemamlaka na maiti, na kama baadhi (ya watu) watafanya haitakuwa wajibu kwa wengine. 439. Ni sunna kumsomea muhatadhari shahada mbili, majina ya maimamu kumi na mbili n.k. 88
Al-Masailul Islamiyah
440. Ni sunna kumsomea dua muhtadhari. 441.Ni sunna kumuweka muhtadhari kwenye sehemu ya kuswalia pindi anapozidiwa na uchungu wa kutokwa na roho. 442.Ni sunna kumsomea muhtadhari surat Yaasini, Swafaati, Ahzaabu, Ayatul – kursiyi na Aya ya 54 katika surati A’raafu na Aya tatu za suratul Baqara bali amsomee kila atachoweza katika Qur;an ili apate kustarehe. 443. Ni makuruhu kumuacha muhtadhari peke yake, vile vile ni makuruhu kumwekea kitu kizito juu ya tumbo, pia ni makuruhu kwa wenye janaba na wenye hedhi kuhudhuria sehemu aliyopo muhtadhari, kuongea, kulia sana, pia ni makuruhu wanawake kuachwa peke yao sehemu aliyopo muhtadhari.
HUKUMU BAADA YA MAUTI 444. Ni sunna baada ya kufa kufumbwa macho ya maiti, mdomo wake na kunyooshwa mikono yake na miguu yake, kisha afunikwe kwa shuka, na kama atafariki usiku ni sunna kuwashwa taa katika sehemu ambayo maiti ipo, pia waumini wapewe taarifa ili waje wasindikize jeneza na wafanye haraka kuzika, lakini ni wajibu wasubiri mpaka wapate yakini kuwa amefariki, vile vile ni wajibu kuchelewesha kuzika kama maiti ni mwanamke mweye mimba, na tumboni kwake kuna mtoto hai apasuliwe upande wa kushoto kisha mtoto atolewe na washone. 446.Ni wajibu wa kila mwislamu balaghe kuosha maiti ya mwiislamu, kuikafini, kuiswalia na kuizika hata kama maiti sio ya mwinathna Asharia, na kama baadhi watafanya mambo haya basi haitakuwa waji89
Al-Masailul Islamiyah bu kwa wengine. Kama mtu ataanza kumwandaa maiti sio lazima kwa watu wengine kufanya hivyo, lakini kama hatakamilisha basi itakuwa ni wajibu kwa wengine kukamilisha. 447. Kama mtu atakuwa na yakini kuwa fulani ana mwandaa maiti, sio wajibu kwake kufanya maandalizi, lakini akishuku au akidhani hivyo basi ni wajibu kwakwe afanye hivyo. 448. Kama atatambua kuwa maiti amekosewa kuoshwa, kukafiniwa, kuzikwa au kuswaliwa, ni wajibu arudie hayo kwa mara nyingine, lakini akishuku au akidhania kuwa mambo hayo sio sahihi, sio lazima kwake kufanya bali ajaalie kuwa ni sahihi. 449. Ni wajibu kuchukua idhini kwa walii wa maiti ili kumuosha kumkafini, kumswalia na kumzika. 450. Walii wa mwanamke ni mume wake na baada yake ni wanaume wanaomrithi maiti kwa utaratibu uliopo katika mirathi. 451. Kama mtu atasema mimi ni walii au walii wa maiti au walii wa maiti amenipa idhini ya kuosha maiti, kukafini na kuzika, kama watu wataamini maneno yake na hakuna mtu aliyedai hivyo, basi ataachiwa afanye hivyo. 452. Mtu kama atabainisha mtu wa kumuosha kabla hajafa, kumkafini, kumswalia na kumzika basi kwa tahadhari ya sunna achukue idhini ya walii wa maiti, na wala sio lazima kwa mtu aliyeidhinishwa na maiti kwa ajili ya maandalizi yake kukubaliwa wasia wake, lakini wasia ukikubaliwa ni wajibu afanye hivyo.
HUKUMU ZA KUOSHA MAITI 90
Al-Masailul Islamiyah 453. Ni wajibu kuosha maiti josho tatu:Kwa maji yaliyochanganywa na sidri “majani ya mkunazi” Kwa maji yaliyochanganywa na kafuri “karafuu maiti” Kwa maji halisi. 454. Ni wajibu sidri na kafuri zisiwe nyingi sana mpaka kufanya maji kuwa mudhafu vile vile ni wajibu zisiwe chache sana. 455. Kama sidri na kafuri haitoshi kwa kiwango kinachotakikana basi kwa tahadhari ya wajibu ichanganywe na maji kiasi. 456. Mtu aliyevaa ihramu kwa ajili ya hija au umra kisha akafariki kabla ya kukamilisha twawafu ya hija ni wajibu asioshwe na maji yaliyochanganywa na kafuri, badala yake ataoshwa na maji halisi 457. Kama itakosekana kafuri na sidri au moja wapo au zikawa za wizi, basi ni wajibu maiti aoshwe badala ya kila josho kwa maji halisi. 458.Ni wajibu anayeosha maiti awe ni muislamu wa madhehebu ya Shia Ithinasharia, awe amebaleghe, awe na akili timamu, awe anajua mas’ala ya kuosha pamoja na hukumu zake kama maiti hatakuwa ni shia ithina asharia basi sio lazima kwa anayeosha kuwa ni shia ithinasharia. 459. Ni wajibu kwa muoshaji akusudie kujikurubisha kwa Allah (swt) wakati wa kuosha, yaani aoshe maiti kwa kujikurubisha kwa Allah (swt) na kutekeleza amri yake (swt) 460. Ni wajibu maiti ya mtoto mwislamu ioshwe hata kama ni mtoto wa zinaa, ama kuoshwa kwa kafiri na watoto wake kukafiniwa na kuzikwa haijathibiti katika sharia, mtu ambaye alikuwa na kichaa kuanzia utotoni mpaka akabaleghe ni lazima aoshwe kama wazazi wake ni waislamu au mmoja wao, lakini kama wote sio waislamu haijuzu 91
Al-Masailul Islamiyah kuoshwa. 461.Ni wajibu kuosha kichanga chenye umri wa miezi minne au zaidi, lakini kama kina umri chini ya miezi minne basi ni lazima afungwe na kitambaa na azikwe bila ya kuoshwa. 462.Inajuzu kwa mwanaume kuosha maiti ya binti mwenye umri chini ya miaka mitatu, vilevile inajuzu kwa mwanamke kuosha maiti ya mtoto wa kiume ambaye umri wake haujavuka miaka mitatu. 463.Ni haramu kwa mwanaume kuosha maiti ya mwanamke, vilevile ni haramu kwa mwanamke kuosha maiti ya mwanaume, lakini inajuzu kwa mwanamke kuosha maiti ya mume wake, na mume pia kuosha maiti ya mke wake, japo kwa tahadhari ya sunna mwanamke asimuoshe mume wake na mwanaume asimuoshe mke wake. 464. Kama hatopatikana mwanaume wa kuosha maiti ya mwanaume basi inajuzu kwa mama yake, dada yake, shangazi yake, mama mdogo au mkubwa wamuoshe. 465. Ni bora mwili wa maiti usifunikwe wakati wa kuoshwa isipokuwa sehemu za siri ikiwa waoshaji na maiti ni jinsia moja. 466. Ni haramu kuangalia uchi wa maiti ila kwa mume na mke inajuzu kuangalia na kama muosha maiti ataangalia uchi wa maiti atapata dhambi, lakini haibatilishi josho la maiti. 467.Kama kuna sehemu najisi katika mwili wa maiti ni lazima itoharishwe kabla hajaoshwa, na kwa tahadhari ya sunna mwili wa maiti wote uwe na tohara kabla ya kuoshwa. 458.Namna yan kuosha maiti ni kama namna ya kuoga janaba kwa utaratibu, na kwa tahadhari ya wajibu maiti asioshwe josho la kuzama, ikiwa josho la utaratibu unawezekana. 92
Al-Masailul Islamiyah
469. Mtu akifa akiwa na janaba au hedhi sio lazima aoshwe josho la janaba au la hedhi, bali inatosha aoshwe josho la maiti tu. 470. Sio haramu kuchukua malipo kwa ajili ya kuosha maiti ikiwa ni kwa ajili ya kulingania, vinginevyo ni wajibu kutochukua, na kama atamuosha maiti kwa lengo la kuchukua malipo josho halitabatilika, lakini sio haramu kuchukua malipo kwa ajili ya baadhi ya vitu kama vile kuleta maji, sidri (majani ya mkunazi) au kafuri maiti. 471. Kama hakuna maji ya kuoshea maiti au kuna kizuizi cha kutumia maji basi inatosha kumtayamimisha maiti, tayamamu moja badala ya josho zote tatu, japo ni kwa tahadhari ya sunna kumtayamimisha tayamamu tatu, kila tayamamu badala ya josho moja. 472. Katika kumtayamimisha maiti ni wajibu kwa aliye hai kupiga ardhi kisha apake uso wa maiti na apake migongo ya viganja vya maiti.
HUKUMU ZA KUMKAFINI MAITI 473. Ni wajibu kumkafini maiti mwislamu kwa vipande vitatu vya nguo. 474. Kipande cha kwanza ni wajibu kianzie kwenye kitovu mpaka kwenye magoti, lakini ni bora zaidi kianzie kifuani mpaka kwenye nyayo, na cha pili ni wajibu kianzie mabegani mpaka kwenye miundi, na ni bora mpaka kwenye nyayo, na cha tatu ni wajibu kiwe kirefu zaidi kwa kiasi kwamba kinaweza kufunika mwili wote kwa urefu na upana. 475. Mali ya kununulia sanda ya maiti inachukuliwa kwenye theluthi ya mali yake. 476. Sanda ya mke ni juu ya mume wake hata kama mke ni tajiri, vile vile ni wajibu kwa mume kumtolea sanda mke wake aliyempa talaka rejea- kama yatakavyokuja maelezo yake katika hukumu za talaka 93
Al-Masailul Islamiyah ikiwa atafariki kabla ya kumalizika eda yake, na ikiwa mume sio baleghe au akiwa kichaa ni wajibu kwa walii wa mume kutoa sanda kutoka katika mali ya anayemsimamia. 477. Sanda ya maiti sio wajibu kwa jamaa zake wa karibu. 478. Haijuzu kumkafini maiti na ngozi ya mzoga na sanda ya wizi hata kama hakuna kitu kingine cha kumkafinia. 479. Haijuzu kumkafini maiti na sanda yenye najisi, hariri na kitambaa kilichochovya dhahabu, ila katika dharura. 480. Haijuzu kumkafini maiti na sufi au nywele za mnyama ambaye ni haramu kuliwa. 481. Kama sanda itanajisika na najisi ya maiti au na najisi nyingine, ni wajibu itoharishwe au ikatwe sehemu yenye najisi hata kama maiti atakuwa amewekwa kaburini, na kama haitawezekana kutoharishwa au kukatwa ni wajibu abadilishiwe sanda nyingine ikiwezekana. 482. Mtu akihirimia kwa ajili ya Hija au Umra kisha akafa ni wajibu akafiniwe kama wengine, wala hakutakuwa na tatizo kufunika uso na kichwa. 483. Ni sunna kwa mtu wakati wa uhai wake kuandaa sanda, sidri na kafuri (kwa ajili yake pindi atakapo kufa).
HUKUMU ZA TAHANITI “KUPAKA� 94
Al-Masailul Islamiyah 484. Ni wajibu kumpaka maiti kafuri maiti katika viungo vyake vya kusujudi baada ya kumuosha. 485. Ni kwa tahadhari ya wajibu kupaka kafuri kuanzia paji la uso, kiganja cha kulia na cha kushoto, goti la kulia na la kushoto, kidole gumba cha kulia na cha kushoto. 486. Ni bora kumpaka maiti kafuri kabla ya kumkafini. 487. Mtu akihirimia Hija au Umra, kisha akifa kabla ya kumaliza sa’ayi na kunyoa haijuzu kumpaka kafuri. 488.Mwanamke ambaye amefiwa na mume wake, kama akifa kabla ya kumaliza eda basi ni wajibu apakwe kafuri. 489.Kama kafuri haitapatikana ya kutosha basi sio lazima kupakwa.
HUKUMU ZA SWALA YA MAITI 490. Ni wajibu kumswalia maiti hata kama ni mtoto, kama wazazi wake ni waislamu au mmoja wao ni mwislamu na awe maiti huyo ametimiza umri wa miaka sita. 491. Ni wajibu kumswalia maiti, baada ya kuoshwa, kupakwa kafuri na kukafiniwa. 492. Sio lazima kwa anayetaka kuswali swala ya maiti awe na udhu au aoge au atayamamu, japo ni bora awe na udhu au aoge na atayamamu. 493. Ni wajibu kwa anayetaka kuswali swala ya maiti aelekee kibla, kama ilivyo wajibu kumlaza maiti kwa mgongo, kichwa chake kiwe upan95
Al-Masailul Islamiyah de wa kulia wa mwenye kuswali na miguu yake iwe upande wa kushoto wa mwenye kuswali. 494. Ni wajibu sehemu anayoswaliwa maiti isiwe ya kunyang’anya, pia ni wajibu sehemu ya mwenye kumswalia isiwe juu zaidi ya sehemu ya maiti. 495. Ni wajibu kwa mwenye kuswalia maiti asiwe mbali na maiti, lakini kama maiti anaswaliwa jamaa hakuna tatizo mtu kuwa mbali na maiti, kwa sharti safu za jamaa ziwe zimeungana. 496. Ni wajibu pasiwe na kizuizi baina ya maiti na mwenye kumswalia, lakini hakuna tatizo kama maiti itakuwa kwenye sanduku n.k. 497. Ni wajibu mwenye kuswali swala ya maiti asimame usawa wa maiti, lakini hakuna tatizo kwa mwenye kuswali jamaa kusimama pembeni mwa maiti. 498. Ni wajibu kusitiri sehemu za siri za maiti wakati wa kumswalia, na kama itashindikana kukafiniwa basi ni wajibu kusitiri sehemu za siri hata kama ni kwa ubao au jiwe n.k. 499. Ni wajibu kuswali swala ya maiti kwa kusimama na iwe ni kwa ajili ya kujikurubisha kwa Allah, na kubainisha katika nia maiti unayemswalia. 500. Mtu ambaye hawezi kuswali swala ya maiti kwa kusimama inajuzu kuswali akiwa amekaa. 501. Ni makuruhu kurudia rudia kuswali swala ya maiti mmoja, lakini hakuna karaha kurudiarudia kuswali swala ya maiti ya mwenye elimu au mcha Mungu.
96
Al-Masailul Islamiyah 502. Kama maiti itazikwa bila ya kuswaliwa kwa makusudi au kwa kusahau au kwa udhuru au ikijulikana baada ya kuzikwa kuwa swala ilikuwa ni batili, basi ni wajibu kuswali swala ya maiti, maiti akiwa kaburini maadamu kaburi halijafutika kabisa.
NAMNA YA KUSWALI SWALA YA MAITI 503. Swala ya maiti ina takbira tano. Takbira ya kwanza: Baada ya nia anasema “Ash hadu an laa ilaaha ila llahu wa anna Muhammadan rasulullah” Takbira ya pili anasema: Allahumma swali alaa Muhammad wa Aali Muhammad waswali alaa jami’il – ambiyaai wal mursaliina” Takbira ya tatu atasema: “ Allahumma ighfir lil muuminina wal muuminaat” Takbira ya nne atasema: “Allahumma ighfir lihaadhal mayit” kama ni mwanaume na akiwa mwanamke anasema “ Allahumma ighfir lihaadhihil mayitah” kisha analeta takibira ya tano na swala inamalizika. Katika takbira ya nne ikiwa maiti ni mtoto atasema: “ Allahumma ij’alhu liabawayhi walanaa salafan wafartwan waajran” na kama hali yake haijulikani kuwa ni mwanaume au ni mwanamke atasema: “ Allahumma ighfir liladhiyna tabuu watabi’u sabiylaka waqihim adhabal jahiym” na kama ni mnafiki atalaaniwa katika takbira ya nne. 504. Ni wajibu kusoma takbira na dua kwa kufuatiliza ili hali swala isiharibike. 505. Ni lazima kwa maamuma katika swala ya maiti naye asome takbira na dua haitoshelezi Imamu peke yake kusoma. 97
Al-Masailul Islamiyah 506. Sio sharti kuwa na tohara wakati wa kuswali swala ya maiti, bali inajuzu kwa mwenye kuswali, kuswali bila ya udhu na kuoga.
MAMBO YA SUNNA KATIKA SWALA YA MAITI:Mwenye kuswali awe na udhu, au aoge au atayamamu. Imamu asimame usawa wa maiti wakati wa kumswalia maiti, na kama mtu atamswalia furada pia asimame katikati ikiwa maiti ni mwanaume, ikiwa maiti ni mwanamke asimame usawa wa kifua cha maiti. Mwenye kuswali asiwe amevaa viatu. Anyanyue mikono kila anaposoma takbira. Mwenye kuswali asimame karibu sana na maiti, kwa kiasi upepo ukitikisa nguo yake inaweza kugusa jeneza. Ni sunna swala ya maiti kuswaliwa jamaa. Imamu wa jamaa asome takibira na dua kwa sauti na maamuma wasisome kwa sauti. Maamuma asimame nyuma ya Imamu hata kama ni mmoja. Amuombee maiti na waumini msamaha kwa Allah (swt) kwa wingi. 10.Aseme kabla ya swala “Aswalaatus swalaat, swalaat� mara tatu(badala ya kukimu). 11.Swala ya maiti iswaliwe katika sehemu ambayo watu wamezoea kuswalia maiti mara kwa mara. 12.Mwanamke mwenye hedhi akitaka kuswali swala ya maiti asimame 98
Al-Masailul Islamiyah nyuma peke yake. 507. Inasihi kuswali swala ya maiti msikitini, na ingawa ni makuruhu lakini sio makuruhu katika msikiti mtukufu wa Makka.
HUKUMU ZA KUZIKA 508.Ni wajibu maiti izikwe kwa kiasi kwamba harufu isienee, na wanyama wasiweze kutoa mwili ndani ya ardhi, na kama itahofiwa kuwa wanyama watafukua maiti basi ni lazima kaburi lijengewe. 509. Kama haiwezekani maiti kuzikwa, inajuzu kuwekwa kwenye jengo au sanduku badala ya kuzikwa. 510. Ni wajibu maiti alazwe kwa upande wa kulia ili sehemu ya mbele ielekee kibla 511. Kama mtu atafia kwenye meli ikawa mwili hautoharibika itabidi izikwe ardhini na kama mwili utaharibika itabidi afungiwe kitu kizito kisha izamishwe ndani ya maji 512. Mwanamke kafiri akifa na mtoto akafia tumboni au ikiwa bado hajawa na uhai, kama baba wa mtoto ni mwislamu basi ni wajibu mwanamke azikwe kwa kulazwa kwa upande wa kushoto ili mtoto aliye tumboni aelekee kibla. 513. Haijuzu mwislamu kuzikwa katika makaburi ya makafiri, na haijuzu kafiri kuzikwa katika makaburi ya waislamu. 514. Haijuzu kuzika mwislamu katika sehemu ambayo inasababisha udhalili mfano, katika sehemu ambayo uchafu unatupwa.
99
Al-Masailul Islamiyah 515. Haijuzu kuzika katika ardhi ya kunyang’anya au waqfu, mfano ardhi ya msikiti. 516. Haijuzu kuzika katika kaburi lingine, isipokuwa liwe ni la zamani sana na limekwisha. 517. Sehemu yoyote ya mwili ikitengana na mwili ni lazima izikwe pamoja na mwili, ni sunna katika uhai wa mtu anapokata kucha au kung’oka meno ayazike. 518. Kama mtu atafia ndani ya kisima na haiwezekani kutolewa, basi ni wajibu kisima kifukiwe na kuwa kaburi lake. 519. Kama mtoto atafia tumboni na kubakia kwake tumboni kukawa ni hatari kwa maisha ya mama yake ni wajibu atolewe haraka. 520. Mwenye mimba akifariki na mtoto tumboni yuko hai ni wajibu apasuliwe upande wa kushoto kisha mtoto atolewe na kisha ashonwe
MAMBO YALIYO SUNN KATIKA KUZIKA 521.Ni sunna kuchimba kaburi sawa na urefu wa mtu wa kawaida 522. Ni sunna kuchimba kaburi kwa mustatili, na kuwekwa alama juu yake ili kutofautisha na makaburi mengine, baada ya kumaliza kuzika ni sunna kumwagia maji juu ya kaburi na kuweka vidole kaburini kisha unasoma suratul Qadri mara saba na kumuombea msamaha maiti. 523. Ni sunna kubeba maiti ndani ya jeneza na kumwingiza kaburini taratibu na kusoma dua zilizopokelewa (kwenye kitabu) kabla ya kuzika na baada ya kuzika, na kufungua sanda, baada ya kuwekwa katika mwanandani shavu la maiti liwekwe juu ya ardhi na chini ya kichwa chake pawekwe udongo, na kuwekwa udongo au tofali nyuma ya mgongo wake ili asirudi nyuma, na kulala chali, na kabla ya kufuni100
Al-Masailul Islamiyah ka mwanandani mzikaji apige bega la kulia la maiti, na anaweka mkono wake wa kushoto juu ya bega la kushoto la maiti, na mdomo wake ukaribie sikio la maiti, na kumtikisa kwa nguvu, kisha asome talakini “talakini itakuja mwisho wakitabu Inshaallah.” 524.Ni sunna kuomboleza baada ya kuzika lakini kama muda umepita sana ni bora kuacha kuomboleza ili usifanye msiba kurudia upya, ni sunna kupeleka chakula kwenye nyumba ya msiba kwa muda wa siku tatu. 525. Ni sunna kwa mtu kufanya subira anapofiwa na jamaa zake wa karibu, hasa anapofiwa na mtoto wake, ni sunna kusema “Innaa lilaah wainnaa ilaihi raajiuuna” ni sunna kumsomea maiti Qu’ran tukufu na kumwomba Allah haja zako katika kaburi la baba yako na la mama yako, pia ni sunna kulijengea ili lisiharibike. 526 .Haijuzu kwa mtu kujirarua katika msiba, isipokuwa katika misiba ya maasumina inajuzu kila aina ya maombolezo. 527. Haijuzu kupasua mifuko katika misiba isipokuwa katika msiba wa baba na wa kaka, japokuwa ni bora kuacha pia. 528. Mwanamke kama atajirarua uso wake au akang’oa unywele wake basi ni wajibu wake aache mtumwa huru, au alishe mafakiri kumi au awape mavazi, na vile vile kwa mwanaume kama atachana mfuko au nguo zake katika msiba wa mke wake au mtoto wake. 529. Ni bora kufanya tahadhari kutolia kwa sauti, lakini misiba ya maasumini inajuzu kulia kwa sauti
SWALA YA WAHSHA 530. Ni sunna kuswali swala ya wahsha kwa ajili ya maiti baada ya kuzi101
Al-Masailul Islamiyah ka kwa usiku wake, ni rakaa mbili unasoma katika rakaa ya kwanza baada ya Al-hamdu ayatul kursiyi, mara moja, na katika rakaa ya pili unasoma baada ya Al-hamdu suratul- Qadir mara kumi, na baada ya swala unasoma Allahumma Swali alaa Muhammadi Waali Muhammad, wab’athi thawabahaa ilaa Qabri Fulani na ni bora utaje jina la maiti(mahala pa fulani). 531. Kama maiti atacheleweshwa kuzikwa au atapelekwa nchi nyingine, basi swala ya wahsha isicheleweshwe mpaka usiku atakaozikwa
Kufukua kaburi 532. Ni haramu kufukua kaburi la mwislamu hata kama liwe ni la mtoto au kichaa, lakini hakuna tatizo ikiwa mwili umekwisha kabisa na kuwa udongo. 533. Ni haramu kufukua makaburi ya manabii, maimamu, watoto wao mashahidi maulamaa, na watu wema hata kama imepita miaka mingi. 538. Sio haramu kufukua kaburi kwa mambo yafuatayo:Kama maiti atazikwa katika sehemu ya kunya’nganya na mwenyewe hajaridhia kuzikwa maiti hapo. Kama maiti atakafiniwa na sanda ya kunyang’anganya na mwenyewe hajaridhika. Kama maiti atazikwa bila kuoshwa au kukafiniwa au akioshwa kimakosa au hajaelekezwa kibla. Kama kuna haja ya kumuona maiti ili kuthibitisha haki. Kama atazikwa katika sehemu inayo sababisha kudhalilika, mfano katika 102
Al-Masailul Islamiyah makaburi ya makafiri au katika sehemu ya kutupia takataka. Kama kufukuliwa kaburi ni kwa ajili ya jambo la kisharia muhimu zaidi kuliko uharamu wa kufukua kaburi, mfano kutolewa mtoto hai aliye tumboni mwa mama yake aliyezikwa naye. Ikiogopewa kuwa wanyama watafukua na kuitoa maiti nje ya kaburi au itasombwa na maji au adui ataichukua. Kama maiti hajazikwa pamoja na sehemu ya mwili wake iliyojitenga naye na ikatakiwa kuzikwa pamoja naye, lakini kwa tahadhari ya wajibu sehemu hiyo iwekwe bila ya kuonekana mwili wa maiti
Josho za sunna 539. Josho la Ijumaa: Wakati wake ni kuanzia adhana ya alfajiri mpaka adhuhuri ya siku ya Ijumaa, na ni bora kuoga adhuhuri ikikaribia Josho la mwanzo wa usiku wa kwanza wa Ramadhani, na kila usiku wa witiri, mfano usiku wa tatu, wa tano, wa saba na wa tisa. Ni sunna kuoga kuanzia usiku wa ishirini na moja mpaka mwisho wa Ramadhani, sunna hii imetiwa mkazo zaidi katika usiku wa kwanza, usiku wa kumi na tano, usiku wa kumi na saba, usiku wa kumi na tisa, usiku wa ishirini na moja, usiku wa ishirini na tatu, usiku wa ishirini na tano, usiku wa ishirini na saba, usiku wa ishirini na tisa katika mwezi wa Ramdhani mtukufu. Josho la siku ya Iddul -fitri na Iddul - Adhuha, na wakati wake ni kuanzia adhana ya alfajiri mpaka magharibi, lakini ni bora kuoga kabla ya swala ya Idd. Josho la usiku wa kuamkia siku ya Idd ndogo na kubwa. 103
Al-Masailul Islamiyah
Josho la siku ya nane na ya tisa katika mwezi wa Dhul Hija, na ni bora kuoga siku ya tisa kabla ya Adhuhuri. Josho la siku ya kwanza, siku ya kumi na tano, siku ya ishirini na saba, na siku ya mwisho katika siku ya mwezi wa Rajab. Josho la siku ya Iddul - Ghadiri na ni bora kuoga kabla ya Adhuhuri Josho la siku ya nne na siku ya ishirini katika mwezi wa Dhul -Hija. Josho la siku ya Nairuzi, siku ya kumi na tano ya mwezi wa shambani na siku ya tisa na siku ya kumi na saba ya mwezi na Rabiul-awal na siku ya ishirini na tano ya mwezi wa Dhul Qa’ad. Kuosha mtoto anapozaliwa. Mwanamke kuoga baada ya kutumia manukato ambayo sio ya mume wake. Kuoga kwa mtu ambaye amekunywa pombe na akalala akiwa amelewa. Kuoga josho la kugusa maiti ambaye hajaoshwa. Josho la mtu ambaye hajaswali swala ya majanga kwa makusudi, hasa swala ya kupatwa kwa jua na mwezi. 540. Ni sunna kuoga kwa mtu ambaye ameenda kuona mtu aliyesulubiwa, lakini akimuona ghafla au ikiwa ameenda kutoa ushahidi sio lazima kuoga. 541. Ni sunna kuoga kabla ya kuingia Makka, Msikiti mtukufu wa Makka, Ka’aba, tukufu, na katika mji wa Madinatul Munawara, na katika msikiti wa Mtume (saww) na katika sehemu takatifu za maimamu na ni sunna kuoga kwa ajili ya Ihramu. 542. Ni sunna kuoga kwa ajili ya kuwazuru Maimamu watukufu (as) iwe 104
Al-Masailul Islamiyah kwa mbali au kwa karibu, na ni sunna kuoga kwa ajili ya kuomba haja zako kwa Allah (swt), vile vile ni sunna kuoga kwa ajili ya kutubu na kupata uchangamfu wa ibada. 543. Kama ikiwajibika kwa mtu kuoga josho nyingi za wajibu au baadhi yake ni wajibu inatosha kuoga josho moja kwa nia ya josho zote.
TAYAMAMU 544. Ni wajibu kutayamamu badala ya kutawadha na kuoga katika mambo saba:Kukosekana maji Kama hutaweza kufika yaliko maji Ikiwa maji yanamdhuru Akihofia kiu Maji aliyonayo kutotosha isipokuwa kutoharisha mwili na nguo Maji yakiwa sio halali Wakati wa swala ukiwa mfinyu.
Jambo la kwanza: 545.Mtu akiwa nyumbani ni wajibu atafute maji hadi akate tamaa, ndio atayamamu. 546. Kama mtu ataacha kutafuta maji mpaka wakati wa swala ukabakia mfinyu kisha akatayamamu, atakuwa ameasi lakini swala yake itakuwa sahihi. 547. Mtu kama ana maji yanayotosha kutawadha au kuoga, na akajua kuwa akiyamwaga hatapata maji, kama itakuwa ndani ya wakati wa swala, basi ni haramu kuyamwaga, pia ni bora asiyamwage kabla ya wakati wa swala
105
Al-Masailul Islamiyah 548. Mtu akijua kama hatapata maji kisha akabatilisha udhu wake baada ya kuingia wakati wa swala, au akamwaga maji baada ya kuingia wakati wa swala, atakuwa ameasi na kupata dhambi lakini swala yake itasihi akitayamamu.
Jambo la pili: 549. Kama hutaweza kufika katika sehemu ambayo ina maji kwa sababu ya uzee, basi ni wajibu utayamamu, pia ni wajibu utayamamu kama kutumia maji kuna kudhuru. 550. Kama italazimika kununua ndoo au kamba ya kuvutia maji au kukodisha basi ni wajibu anunue au akodishe. 551. Kama mtu hatapata maji mpaka akope hela za kununulia maji, basi ni wajibu akope ili anunue maji. 552. Kama kuchimba kisima hakumpatii taabu basi ni wajibu achimbe illi apate maji 553. Kama mtu atakupa maji bila masimango huna budi kuyachukua na kutawadhia, lakini kama kuna masimango ni lazima usiyachukue
Jambo la tatu: 554. Akihofia kwamba kutumia maji kutamdhuru au akihofia maradhi yake yatachukua muda mrefu au yatazidi au itakuwa vigumu kutibika kwa sababu ya kutumia maji, basi ni wajibu atayamamu, lakini kama maji yaliyochemshwa hayamdhuru ni wajibu atawadhe au aoge kwa kutumia maji ya moto. 555. Sio lazima apate yakini kuwa maji yatamdhuru, bali hata akidhania kuwa maji yatamdhuru na akawa na hofu basi ni wajibu atayamamu.
106
Al-Masailul Islamiyah 556. Mwenye ugonjwa wa macho kama maji yanamdhuru ni wajibu atayamamu. 557. Kama atatayamamu kwa sababu ya kuwa na yakini kuwa maji yatamdhuru, kisha akatambua kabla ya swala kuwa maji hayamdhuru, tayamamu yake itabatilika, na akijua hivyo baada ya swala ni bora arudie swala yake akiwa na udhu au aoge, na alipe ikiwa wakati umepita. 558. Mtu akijua kuwa maji hayamdhuru kama ataoga au kutawadha, kisha akajua baadae kuwa maji yanamdhuru basi josho lake na udhu wake utasihi.
Jambo la nne: 559. Kama akihofia kutumia maji katika kutawadhia au kuogea atakufa yeye au familia yake au rafiki yake au mtumishi, au kila aliye wajibu kwake kuokoa maisha yake kutokana na kiu kali, basi ni wajibu atayamamu badala ya kutawadha au kuoga. 560. Kama ana maji yaliyonajisika yanatosha kunywa yeye na familia yake na yaliyotohara kwa ajili ya udhu au kuoga, basi ni wajibu maji yaliyotohara yawe ni ya kunywa na atayamamu kwa ajili ya swala, na akitaka kumnywesha mnyama wake maji amnyweshe maji yaliyonajisika.
Jambo la tano: 561. Kama mwili au nguo ikinajisika na maji aliyonayo ni machache, mfano akitawadhia au kuogea hayatabaki, basi ni wajibu kwake atoharishe nguo au mwili wake kwa hayo maji kisha atayamamu kwa ajili ya swala.
107
Al-Masailul Islamiyah
Jambo la sita: 562. Kama ana maji au chombo ambacho ni haramu kutumia, mfano maji au chombo cha kunyang’anya basi ni wajibu atayamamu badala ya kuoga au kutawadha. 563. Kama wakati wa swala utakuwa mfinyu kama akitawadha au kuoga swala yote itakuwa nje ya wakati au baadhi, basi ni wajibu atayamamu.
Jambo la saba:
564. Kama atachelewesha swala kwa makusudi mpaka wakati ukawa hautoshi kutawadha au kuoga, atakuwa ameasi na kupata dhambi lakini swala yake itakuwa sahihi. 565. Kama akishuku kuwa je wakati utabakia kwa ajili ya swala kama atatawadha au kuoga, basi ni wajibu atawadhe au aoge.
Vitu ambavyo inasihi kutayamamu 566. Inasihi kutayamamu kwa udongo, mchanga na changarawe, yaani vipande vipande vya udongo au vya mawe. 567. Inasihi kutayamamu kwa kutumia ukuta wa udongo, na ni bora kuchukua tahadhari usitayamamu na ardhi au udongo mbichi na wakati huo huo kuna mkavu.
Namna ya kutayamamu badala ya udhu Nia. Kupiga kwa viganja viwili kwa pamoja juu ya kitu ambacho kinasihi kutayamamia
108
Al-Masailul Islamiyah Kupaka paji la uso lote kwa viganja viwili kwa kuanzia kwenye maoteo ya nywele mpaka juu ya pua. Kupaka juu ya kiganja cha kulia kwa tumbo la kiganja cha mkono wa kushoto kisha kupaka juu ya kiganja cha kushoto kwa tumbo la kiganja cha mkono wa kulia, kuanzia kwenye vifundo mpaka kwenye ncha za vidole.
Namna ya kutayamamu badala ya kuoga Katika tayamamu badala ya kuoga atanuia na kupiga ardhi kwa viganja vyake kisha anapaka paji la uso, kisha atapaka mgongo wa kiganja cha mkono wa kulia, kisha atapaka mgongo wa kiganja cha mkono wa kushoto, kisha atapiga udongo tena na kupaka viganja vya mikono yake kama ilivyotangulia.
Hukumu za kutayamamu 568. Ni wajibu kupaka paji la uso na mikono kwa kuanzia juu na kupeleka chini, na ni wajibu kutayamamu kwa kufuatilizia kiungo hadi kiungo kingine. 569. Ni wajibu wakati wa kutayamamu kubainisha nia kuwa unatayamamu badala ya udhu au kuoga, pia ni wajibu kubainisha kuwa unatayamamu badala ya josho gani, josho la janaba au josho la hedhi n.k. 570. Ni wajibu wakati wa kutayamamu paji la uso na viganja vya mkono viwe tohara. 571. Mtu ambaye hawezi kutayamamu mwenyewe ni wajibu atayayamamishwe. 572. Mtu ambaye ametayamamu kwa sababu ya udhuru, kisha udhuru huo 109
Al-Masailul Islamiyah ukaondoka basi tayamamu yake itabatilika. 573. Mambo ambayo yanatengua udhu yanatengua tayamamu pia. 574.Mtu ambaye hawezi kuoga, kama akiwajibika kuoga josho nyingi basi tayamamu moja inamtosheleza
HUKUMU ZA SWALA 575. Swala ni katika amali iliyo bora kabisa katika dini na iliyo na umuhimu mkubwa, bali swala ni nguzo ya dini, kama swala yako itakubaliwa basi amali zako zingine zitakubaliwa, na ikikataliwa na amali zako zingine hazitakubaliwa, mfano wa swala ni sawa na mtu anayeoga kila siku mara tano, ambaye uchafu hautabaki katika mwili wake. Vile vile mtu akiswali swala tano za faradhi atatakasika kutokana na madhambi na machafu. Na inapasa kwa mtu kuziswali swala zake mwanzo wa nyakati zake na mwenye kuzipuzia swala zake na kuzembea ni sawa na mtu asiyeswali, na atastahili adhabu akhera. Mtume (saww) amesema: “ Hayupo katika dini yangu mwenye kupuuzia swala yake”. Na Mtume (saww) amesema: “Hatapata maombezi yangu mwenye kupuuzia swala yake, na wala hataingia katika hodhi yangu”. Siku moja Mtume (saww) alikuwa msikitini, akaingia mtu mmoja na akawa akishughulika na kuswali, lakini bila ya kutimiza rukuu yake na sijda yake. Mtume (saww) akasema: “Huyu anadonoadonoa kama kunguru, lau akifa na hii ndio swala yake atakufa nje ya dini yangu”. Basi inamlazimu mtu adumishe swala zake sana asiziswali harakaharaka, 110
Al-Masailul Islamiyah na amnyenyekee Mola wake wakati wa swala, kwa hofu na heshima, na ajue kwamba kuna ambaye anaongea nae ,na ajue kwamba yuko mbele ya utukufu wa Mwenyezi Mungu na ufalme wake, awe dhalili na mnyonge, na lau mwenye kuswali akiyajua haya wakati wa swala, basi nafsi yake itayasahau mengine yote, na atajihisi kwamba yuko mbele ya Mwenyezi Mungu (swt) kama ilivyotokea kwa kiongozi wetu Amirul Muuminina Ali (as) walipoweza kumtoa mshale mguuni mwake bila ya yeye kuhisi wala kutambua. Hivi ndivyo yampasa mwenye kuswali atubie na kutaka istighifar kwa Mola wake na kuelekea kwa Mola wake na kuacha madhambi na maasi ambayo yanazuia kukubaliwa swala yake. Kama vile hasadi na kibri, kusengenya, kula haramu na ulevi, na kuacha kuzuia kutoa khumsi na zaka, bali kuacha maasi yote kwa ujumla. Pia yampasa aache vitendo vyenye kupunguza thawabu za swala. Asisimame katika swala huku akisinzia au akiswali huku akijizuia mkojo usimtoke au asiangalieangalie juu, na hali yuko katika swala. Anatakiwa afanye vitendo vyenye kumzidishia thawabu katika swala yake. Kama kuvaa pete ya akiki, kuvaa nguo safi, kujipaka manukato, kupiga mswaki na kuchana nywele.
SWALA ZA WAJIBU 576. Swala za wajibu ni: 1. Swala za kila siku 2. Swala za matukio (majanga) 3. Swala ya maiti 4. Swala ya tawafu ya wajibu ka’aba 5. Swala ya kuwalipia wazazi ambayo ni wajibu kwa mtoto mkubwa wa kiume 6. Swala inayokuwa wajibu kwa mtu kwa kuweka nadhiri au ahadi au kiapo au kuajiriwa(kuswali kwa niaba ya mtu).
SWALA ZA WAJIBU ZA KILA SIKU 111
Al-Masailul Islamiyah 577. Swala za wajibu za kila siku ni tano, swala ya Adhuhuri na Alasir, kila moja ina rakaa nne, na swala ya magharibi yenye rakaa tatu, na swala ya Isha yenye rakaa nne, na swala ya asubuhi yenye rakaa mbili. Ni wajibu kupunguza swala zenye rakaa nne katika safari kwa masharti ambayo ufafanuzi wake utaelezwa. Na maana ya kupunguza ni kuziswali swala zenye rakaa nne, rakaa mbili mbili.
WAKATI WA SWALA YA ADHUHURI NA ALASIRI 578.Swala ya Adhuhur na Alasir zina wakati mahsusi, na zina wakati wa kushirikiana, ama wakati ulio mahsusi kwa swala ya adhuhuri ni pale linapopinduka jua mpaka unapomalizika muda wa kiwango cha kuswali swala ya Adhuhur. Basi ikiwa mtu yeyote ataiswali swala ya Alasiri katika wakati huu kwa kusahau, swala yake itakuwa ni batili. Ama wakati mahsusi kwa swala ya Alasir ni ule uliobakia mpaka kuzama jua kwa kiwango cha kuweza kuswali rakaa nne za Alasiri, kama mtu hakuswali swala ya Adhuhuri mpaka wakati huu basi swala yake itakuwa ni kadhaa na ni juu yake kuiswali swala ya alasiri muda huu, kisha ailipe swala ya adhuhuri. Ama wakati wakushirikiana baina ya Adhuhuri na Alasiri ni muda ulio baina ya wakati mahsusi kwa swala ya adhuhuri, na muda mahsusi wa swala ya alasiri kiasi kwamba akiiswali swala ya alasiri katika muda huu wa kushirikiana kabla ya kuiswali swala ya adhuhuri kwa kusahau, swala yake itasihi na itahesabika kuwa ameswali alasiri, na ni wajibu wake kuiswali adhuhuri baada yake. 579. Mtu akishughulika na kuswali swala ya alasiri kabla ya kuiswali swala ya adhuhuri kwa kusahau, kisha akafahamu katikati kwamba 112
Al-Masailul Islamiyah amekosea ikiwa hili litakuwa katika wakati wa kushirikiana baina ya swala ya adhuhuri na alasiri ni wajibu kwake kubadili nia kwa kutia nia ya swala ya adhuhuri, yaani yeye atanuia hali yuko katika swala ya kwamba yote aliyofanya, na anayoyafanya sasa hivi na atakayoyafanya yatakuwa ni ya swala ya adhuhuri, na baada ya kukamilisha swala ya adhuhuri, ataswali swala ya alasiri, ama ikiwa haya yote aliyoyafanya ni katika wakati mahsusi kwa swala ya adhuhuri, basi yote aliyoyafanya yatakuwa ni batili, sawasawa amefahamu makosa yake katikati ya swala au baada ya swala.
WAKATI WA SWALA YA MAGHARIBI NA ISHA 590. Magharibi huingia pale unapoondoka wekundu wa mashariki, nao ni unaoonekana upande wa mashariki linapozama jua. 591. Kila swala ya magharibi na isha ina wakati wake mahsusi na zina wakati wa kushirikiana baina ya swala hizi mbili. Ama wakati mahsusi kwa swala ya magharibi ni mwanzo wa swala ya magharibi mpaka kumalizika muda kwa kiwango cha kuiswali swala ya magharibi, kiasi ambacho lau mtu msafiri akiswali swala ya isha katika muda huu kwa kusahau swala yake itabatilika. Ama wakati wa kushirikiana kati ya swala hizi mbili ni kati ya wakati mahsusi kwa swala ya magharib na wakati mahsusi wa swala ya isha kiasi kama mtu hakuiswali swala ya magharibi mpaka wakati huu itawajibika kuiswali swala ya isha kwanza kisha ataswali magharibi. Ama wakati wa kushirikiana kati ya swala hizi mbili ni baina ya wakati mahsusi kwa swala ya magharibi na wakati mahsusi kwa swala ya isha, kiasi ambacho lau mtu akiiswali swala ya isha katika wakati huu wa kushirikiana kabla ya kuswali magharibi kwa kusahau, kisha akafahamu kuwa amekosea, swala yake itasihi na itamlazimu kuiswali swala ya 113
Al-Masailul Islamiyah magharibi baada ya hapo. 592. Muda mahsusi na wa kushirikiana tuliouelezea katika mas’ala yaliyotangulia, unatofautiana kulingana na watu, kuhusu msafiri lau ukipita muda wa mwanzo wa adhuhuri kwa kiwango cha kuswali rakaa mbili, basi unaingia muda wa kushirikiana, ama kuhusu mtu ambaye si msafiri ni lazima kwake upite muda wa mwanzo wa adhuhuri kwa kiasi cha kuswali rakaa nne ndio ufike muda wa kushirikiana. 593. Ikiwa mtu atashughulika kwa swala ya isha kabla ya swala ya magharibi kwa kusahau na akafahamu katikati ya swala kuwa amekosea, ikiwa atakuwa ameiswali swala yote au baadhi yake katika muda wa kushirikiana na ikawa hakuingia katika rukuu ya rakaa ya nne, itamuwajibikia kubadilisha nia yake kwenda katika swala ya magharibi, na atazingatia aliyoyasoma na kuyafanya ni ya swala ya magharibi na hivyo itambidi akae ikiwa alikuwa amesimama pasi na kwenda kwenye rukuu ya rakaa ya nne na kukamilisha swala, kisha ataswali swala ya isha baada ya hapo. Na ikiwa atakuwa amekwenda kwenye rukuu ya rakaa ya nne ni wajibu kukamilisha swala kisha ataswali swala ya magharibi baada ya hapo. Ama akiiswali swala katika wakati mahsusi kwa swala ya magharibi, kama lau akiwa ni msafiri na akaswali Qaswir, swala yake itabatilika na atawajibika kuswali swala ya magharibi kisha swala ya isha kwa mpangilio. 594. Muda wa mwisho wa swala ya isha ni katikati ya usiku, hivyo ni lazima tuanze kuhesabu usiku pindi jua linapozama mpaka adhana ya alfajiri na sio kwa kuchomoza jua. Mwisho wa muda wa swala ya magharibi na isha kwa mtu mwenye dharura au aliyesahau au kwa aliyekuwa amelala au aliyechelewesha swala yake kwa ajili ya hedhi ni mpaka adhana ya alfajiri. 114
Al-Masailul Islamiyah
595. Lau akichelewesha swala ya isha mpaka katikati ya usiku bila udhuru, basi ni bora zaidi kuswali hata kabla ya swala ya alfajiri bila ya nia ya adaai wala kadhaa
WAKATI WA SWALA YA ASUBUHI 596. Baada ya kutokeza weupe upande wa mashariki unaoelekea juu, ambao unaitwa alfajiri ya mwanzo ya uongo, kisha weupe huu hupanuka zaidi, wakati huo huwa alfajiri ya pili, “alfajiri ya kweli� ama mwisho wa swala ya alfajiri ni kuchomoza kwa jua.
HUKUMU ZA WAKATI WA SWALA 597. Haijuzu kuanza kuswali mpaka uwe na uhakika wa kuingia muda wa swala au baada ya kupewa tarifa na watu wawili waadilifu ya kuingia wakati wa swala au kupata taarifa kwa mtu mmoja mwenye kuaminika. 598. Ikiwa mtu hawezi kupata uhakika wa kuingia wakati wa swala kwa kuwa yeye ni kipofu au kwa sababu ya mawingu au vumbi au kwa sababu yuko ndani ya jela, ni wajibu kwake kuchelewesha swala yake mpaka apate uhakika wa kuingia kwa wakati. 599. Ikiwa mtu atapewa taarifa na watu wawili waadilifu au akapata uhakika mwenyewe wa kuingia wakati wa swala, akaanza kushughulika na swala, kisha ikambainikia kwamba wakati wa swala bado haujaingia basi swala yake itabatilika na vivyo hivyo itabatilika akijua baada ya swala kwamba ameswali swala hiyo kabla ya kuingia wakati, lakini akitambua kuingia wakati akiwa ndani ya swala, au akatambua baada ya swala kwamba wakati wa swala umeingia na yeye yuko ndani ya swala, swala yake itasihi. 115
Al-Masailul Islamiyah 600. Ikiwa mtu atapata uhakika wa kuingia wakati wa swala na akaanza kuswali, kisha akashuku na hali yuko ndani ya swala kuwa je wakati umeingia au bado? Basi swala yake itakuwa na mushkeli, ama akiwa na yakini wakati wa kuswali na ana uhakika wa kuingia wakati wa swala itasihi, lakini akijua kuwa swala yote ameiswali nje ya wakati au akiwa hajui kuwa ameiswali ndani ya wakati au nje ya wakati swala yake itabatilika, bali hata akijua kwamba wakati umeingia akiwa anaswali ni wajibu arudie swala kwa tahadhari. 601 Mtu ambaye ana muda wa kuweza kuswali rakaa moja, ni wajibu kwake kuiswali swala kwa nia ya adaai, lakini haijuzu kwake kuichelewa swala kwa makusudi mpaka muda uwe mfinyu namna hii. 602.Mtu ambaye si msafiri ikiwa ana muda wa kuweza kuswali rakaa tano kabla ya kuzama jua ni wajibu kuswali swala ya adhuhuri na alasiri wakati huo, lakini ikiwa muda ni mchache zaidi ya huo, itamuwajibikia kuswali swala ya alasir peke yake, kisha ataiswali adhuhuri kadha na vivyo hivyo atakapobakiwa na muda wa kuswali rakaa nne kufikia nusu ya usiku, itampasa kuswali magharibi na isha katika muda huo, lakini muda ukiwa ni mchache zaidi ya huo, itambidi kuswali isha peke yake, kisha baada ya hapo ataswali swala ya magharibi kadhaa, ila mwenye dharura ameongezewa muda mpaka adhana ya alfajiri. 603.Msafiri aliyebakiwa na muda wa kuweza kuswali rakaa tatu kabla ya kuingia magharibi, ni wajibu kuiswali swala ya adhuhuri na alasiri katika muda huo. Na ikiwa muda ni mchache zaidi ya huo itamuwajibikia kuiswali alasiri peke yake kisha ataswali adhuhuri kadha, na ikiwa mtu amebakiwa na muda wa kuswali rakaa nne tu na kuingia nusu ya usiku ni wajibu kuswali magharibi na isha wakati huo ama akibakiwa na muda wa kuweza kuswali rakaa moja au zaidi ya rakaa moja ndio ifike katikati ya usiku itamuwajibikia kuswali magharibi haraka kwa nia ya adaai. 116
Al-Masailul Islamiyah Ni sunna kwa mtu kuswali swala mwanzo wa wakati, na riwaya nyingi zimepokelewa zikiusia jambo hili na kutilia mkazo sana na fadhila zina kuwa nyingi zaidi kila swala inaposwaliwa mwanzo wa wakati wake ila ikiwa kuchelewesha ni kwa ajili ya kutaka fadhila za kitu fulani, mfano kusubiria mpaka aweze kuswali swala ya jamaa. Kama mtu ana udhuru kiasi ambacho akitaka kuswali mwanzo wa wakati analazimika kutayamamu kwa ajili ya swala au kuiswali swala kwa nguo iliyo na najisi, ikiwa atajua kwamba udhuru wake utabakia mpaka mwisho wa wakati itajuzu kwake kuiswali swala mwanzo wa wakati, lakini akijua kuwa udhuru wake utaondoka itamuwajibikia kusubiri mpaka udhuru wake uondoke na kama udhuru wake haujaisha ataswali mwisho wa wakati, na wala haitomlazimu kusubiri kiasi cha kutokubakiwa na muda, ila kwa kiwango cha kuweza kufanya wajibu wa swala bila ya mustahabu. Bali inajuzu kuziswali swala katika muda wenye wasaa, ambapo anaweza kufanya mustahabu mfano kuadhini, kukimu, kusoma kunuti pamoja na kutayamamu. 604. Mtu ambaye hajui taratibu za swala, hukumu za shaka na kusahau na akashuku kuwa atatatizwa na moja wapo, ni wajibu kuchelewesha swala yake mpaka mwisho wa wakati, ili aweze kujifunza lakini akiwa na uhakika kwamba ataweza kukamilisha swala kwa njia sahihi inajuzu kuswali mwanzo wa wakati, na kama hakutokewa na mas’ala ambayo haelewi hukumu yake swala yake itasihi na akitokewa na mas’ala ambayo hajui hukumu yake inajuzu afanye kwa moja ya njia anazozijua na kukamilisha swala yake kisha ni wajibu kwake kuuliza hukumu ile baada ya swala na kuirudia swala kama aliiswali kinyume. 605. Ikiwa wakati wa swala ni mpana, na mwenye deni akamdai deni lake ni wajibu kwake kumlipa deni lake kwanza kama itawezekana kisha aendelee na swala, na vivyo hivyo ukimtokea wajibu mwingine wa haraka, mfano akiona najisi msikitini, ni wajibu kusafisha msikiti kwanza kisha ataswali na kama ataswali kwanza kisha aondoshe 117
Al-Masailul Islamiyah najisi atakuwa ametaasi, lakini swala yake itakuwa sahihi.
SWALA AMBAZO NI WAJIBU KUZISWALI KWA MPANGILIO 606. Ni wajibu kuiswali swala ya alasiri baada ya swala ya adhuhuri na swala ya isha baada aya swala ya magharibi, na kama ataswali alasiri kabla ya adhuhuri au isha kabla ya magharibi kwa makusudi basi swala yake itabatilika. 607. Akianza kuswali kwa nia ya swala ya adhuhuri na wakati huo akakumbuka kuwa ameswali adhuhuri haijuzu kwake kubadilisha nia kwenda kwenye swala ya alasir na vivyo hivyo hukumu ni hii katika swala ya magharibi na isha. 608. Akipata uhakika akiwa katika swala ya alasiri kwamba hajaswali adhuhuri, basi ni wajibu kwake kubadilisha nia kwenda kwenye swala ya adhuhuri na kama akikumbuka baada ya hapo kwamba ameswali adhuhuri kabla, itamlazimu kubadili nia yake kwenda kwenye swala ya alasiri na swala yake itasihi ikiwa hakufanya kitu katika swala iliyotangulia, kwa kusudio mahsusi kwa ajili ya adhuhuri. 609. Ikiwa atashuku akiwa katika swala ya alasiri kwamba ameswali swala ya adhuhuri, au laa, ni wajibu abadili nia yake kwenda kwenye swala ya adhuhuri kisha ataswali alasiri lakini ikiwa wakati ni mfinyu sana kiasi ambacho lau atatimiza swala na kutaka kuswali alasiri wakati wa magharibi utaingia, itamuwajibikia kukamilisha swala kwa nia ya alasiri na kwa sura hii ni juu yake ailipe adhuhuri 118
Al-Masailul Islamiyah nje ya wakati kwa tahadhari. 610. Akishuku katika swala ya isha kabla ya kwenda rukuu ya rakaa ya nne, kwamba ameswali magharibi kabla ya hapo au laa, ikiwa wakati ni mfinyu kiasi ambacho lau akikamilisha swala itaingia nusu ya usiku ni wajibu kukamilisha swala kwa nia ya isha, ama kama wakati unawasaa inamuwajibikia kubadili nia kwenda swala ya magharibi na kukamilisha rakaa tatu, kisha baada ya hapo ataswali swala ya isha. 611. Akishuku ndani ya swala ya isha baada ya kufika kwenye rukuu ya rakaa ya nne, kwamba ameswali magharibi kabla ya hapo au laa, itamuwajibikia kukamilisha swala yake kisha ataswali magharibi baada ya hapo. Kama atarudia swala aliyoiswali kabla kwa tahadhari, na katikati ya swala akakumbuka kwamba hakuswali swala ambayo ilikuwa ni wajibu kuiswali kabla ya hii swala, haijuzu kubadili nia yake kwenda kwenye swala iliyotangulia, mfano kama alikuwa anarudia swala ya alasiri kwa tahadhari na akakumbuka wakati huo kwamba hajaswali adhuhuri, haijuzu kubadili nia yake kwenda kwenye adhuhuri. 612. Haijuzu kubadili nia kutoka kadha kwenda kwenye adai, wala kutoka swala ya sunna kwenda kwenye swala ya wajibu. Ikiwa wakati wa swala za adai, ni mpana inajuzu kubadilisha nia kutoka swala za adai kwenda swala za kulipa ndani ya swala kama itawezekana kubadilisha kwa mfano, kama mtu anaswali adhuhuri inajuzu kwake kubadili nia yake kwenda swala ya asubuhi maadamu hajaingia katika rakaa ya tatu.
SWALA ZA SUNNA 119
Al-Masailul Islamiyah 613. Swala za sunna ni nyingi na pia huitwa swala za “nawafil” na zilizotiliwa mkazo katika sunna za kila siku “zilizowekwa kwa mpangilio” nazo ni za kila siku isipokuwa siku ya Ijumaa, ni rakaa 34 katika utaratibu ufuatao:-Sunna ya adhuhuri rakaa nane -Sunna ya alasiri rakaa nane -Suna ya magharibi rakaa nne -Suna ya isha rakaa mbili -Sunna ya swala ya usiku rakaa kumi na moja
SWALA YA USIKU 614. Wakati wa swala ya usiku unaanzia katikati ya usiku mpaka adhana ya alfajiri, na ni bora zaidi kuswali swala ya usiku karibu na adhana ya alfajiri. 615. Msafiri au mtu ambaye hawezi kuswali swala ya usiku baada ya katikati ya usiku inajuzu kwake kuswali mwanzo wa usiku. 616. Swala ya usiku ina rakaa kumi na moja, rakaa nane kati ya hizo ni sunna ya usiku, rakaa mbili ni shufaa, na rakaa moja ni witiri, na katika kila rakaa mbili kuna salam ila rakaa ya witiri yenyewe peke yake ina salam. 617. Ni sunna katika swala ya usiku kusoma sura ndefu katika rakaa ya kwanza na sura fupi katika rakaa ya pili na ni sunna katika sunna ya shufaa na witiri kusoma suratul – Falaq, Nnasi na Tauhidi au kusoma suratu Tauhid katika rakaa zote. 618. Ni sunna katika kunuti ya witiri kuwaombea waumina 40 aseme: “Ewe Mwenyezi Mungu msamehe fulani na fulani” uwataje kwa 120
Al-Masailul Islamiyah majina yao, na aseme mara 70 “Astaghafirullaha rabbii waatuubu ilaihi” na aseme mara saba “hadhaa maqamul – aaidhi bika mina nnaari” na aseme mara 300 “al’afuwa”.
SWALA YA GHUFAILA 619. Miongoni mwa swala za sunna ni swala ya Ghufaila ambayo huswaliwa baina ya Magharibi na Isha, nayo ina rakaa mbili na huswaliwa kama ifuatavyo: Utasoma katika rakaa ya kwanza baada ya Al hamdu “waddhannuun idhi dhahaba mughadhiban” iliyoko katika sura ya 88 aya 87 na katika rakaa ya pili baada ya Al hamdu “wa’indahu mafaatihul ghayib” mpaka mwisho wa aya iliyoko katika sura ya 6 aya ya 59 Na atasema katika kunuti “Allaahumma innii as,aluka bimafaatihil – ghayibi allatii laa yaalamuhaa illa anta an tuswalliya alaa Muhammad waali Muhammad” kisha unataja haja zako, kisha unasema “Allahumma anta waliyu ni’imatiy wal- qaadiru alayi twalabatii ta’alamu haajatiy faas’ aluka bihaq Muhammad waaalihi alaihi wa alaihimu ssalam lammaa qadhwaytahaa lii”
HUKUMU ZA KIBLA 620.Kibla ni ka’aba tukufu iliyoko katika Mji wa Makka hivyo ni wajibu kwa mwenye kuswali akiwa Makka kuilekea ka’aba yenyewe lakini mtu alioko mbali aelekee upande wa kibla, vivyo hivyo kwa jambo ambalo ni sharti kuelekea kibla kama vile kuchinja mnyama. 621. Mwenye kuswali swala zake za wajibu kwa kusimama ni wajibu kuelekea kibla kwa uso wake, kifua chake, tumbo lake na sehemu ya mbele ya miguu yake na kwa tahadhari ya sunna vidole vyake pia vieleke kibla. Anayeswali kwa kukaa akishindwa kukaa katika hali ya 121
Al-Masailul Islamiyah kawaida kuweka tumbo na miguu yake katika ardhi, ni wajibu aelekeze uso wake, kifua chake na tumbo lake kibla, na kwa tahadhari na miundi yake ielekee kibla. 622. Mtu ambaye hawezi kuswali kwa kukaa ni wajibu aswali kwa kulala kwa ubavu wa kulia kwa kuelekeza sehemu ya mbele ya mwili wake kibla, na kama hakuweza, basi aswali hali amelala kwa ubavu wa kushoto, na akishindwa alale kwa mgongo kwa kuelekeza matumbo ya miguu yake kibla. 623. Mwenye kutaka kuswali ni wajibu afanyejitihada ya kujua kwa yakini upande wa kibla, na inajuzu ategemee kauli ya watu wawili waadilifu au mtu mmoja mkweli. 624. Kama akishindwa kupata yakini kwamba kibla kiko upande upi, na hakupata mtu wa kuaminika wa kumwambia upande wa kibla, itamlazimu atumie dhana kwa kutazama mihrabu za miskiti ya waislam au makaburi yao au njia zingine zitakazomuwezesha kujua upande wa kibla. 625. Ambaye hakupata uhakika kibla kipo upande upi akitaka kufanya amali isiyo kuwa swala ambayo ni wajibu kuelekea kibla, mfano akitaka kuchinja mnyama itamlazimu awe na dhana ulipo upande wa kibla na akishindwa hilo atamchinja kumwelekeza upande wowote atakaoafiki katika hali ya dharura juu ya amali hiyo.
KUSITIRI MWILI KATIKA SWALA 626. Ni wajibu kwa mwanaume kusitiri mwili wake katika swala hata kama hakuna mtu yeyote anayemuona, na ni bora kusitiri kuanzia kitovuni mpaka magotini. 627. Na ni wajibu kwa mwanamke wakati wa swala kusitiri mwili wake wote hata kichwa na nywele, na kwa tahadhari ya sunna kusitiri chini 122
Al-Masailul Islamiyah ya unyayo wake pia, lakini si lazima kusitiri vile viungo vinavyooshwa katika udhu, yaani uso na viganja vya mikono mpaka kongo mbili, na vile vile migongo ya miguu mpaka kwenye kongo mbili lakini ili awe na yakini kwamba amesitiri yaliyowajibu kusitiriwa ni wajibu kusitiri sehemu za pembeni za uso na kusitiri kongo za viganja. 628. Kama mtu hakusitiri uchi wake katika swala kwa makusudi swala yake inabatilika. inajuzu kwa mwenye kuswali kusitiri uchi wake wakati wa swala kwa karatasi au majani ya miti na ikiwa ana kitu kingine ambacho anaweza kusitiri uchi wake kwa tahadhari ajisitiri kwa kitu hicho. Inajuzu kwa mwenye kuswali kusitiri uchi wake kwa udongo.
VAZI LA MWENYE KUSWALI 629. Kuna masharti sita kwa vazi la mwenye kuswali:Lazima liwe tohara Liwe la halali Lisiwe limetokana na mizoga Lisiwe limetokana na vitu vya wanyama ambao ni haramu kuliwa Lisiwe la hariri halisi au dhahabu, ikiwa mwenye kuswali ni mwanaume, ufafanuzi wake utakuja.
SHARTI LA KWANZA 630. Ni wajibu nguo ya mwenye kuswali iwe tohara na lau akiswali kwa nguo au mwili ulio na najisi kwa makusudi swala yake inabatilika. Mwenye kuswali na nguo au mwili ulio najisi naye hajui kwamba kuswali katika hali ile inabatilisha swala, swala yake itasihi. 123
Al-Masailul Islamiyah
631. Kama hajui unajisi wa kitu kwa kutokujua mas’ala, mfano kama hajui unajisi wa damu, kisha akaswali na nguo iliyo na najisi ya damu swala yake inasihi. 632. Kama hajui kwamba mwili wake au nguo yake ina najisi na akatambua hilo baada ya swala, swala yake itasihi. 633. Akiona damu katika mwili wake au vazi lake na akawa na uhakika kwamba ile si katika damu zilizonajisi, mfano akiwa na uhakika kwamba damu ile ni ya kunguni au ya mbu, na akafahamu baada ya swala kwamba damu ile ni katika damu zilizo najisi ambazo hazifai kuswali nazo, swala yake aliyoiswali itasihi. 634. Ambaye hana nguo nyingine isipokuwa hiyo yenye najisi, ni wajibu kuswali na nguo hiyo, hasa kama hataweza kuvua nguo yake kwa sababu ya baridi na mfano wa hilo swala yake itasihi. 635. Ambaye ana nguo mbili na akafahamu kwamba mojawapo ya nguo zake mbili ina najisi, lakini hafahamu ni ipi kati ya hizo iliyo na najisi, kama muda ni wasaa ni wajibu kuswali na nguo zake mbili, mfano akitaka kuswali adhuhuri na alasir ataswali nazo katika kila nguo moja, katika nguo hizo mbili lakini kama wakati hautoshi, itamuwajibikia kuswali na nguo mojawapo atakaeitaka lakini na kwa tahadhari alipe swala hiyo baada ya wakati katika nguo tohara.
SHARTI LA PILI 636. Ni wajibu nguo ya mwenye kuswali iwe ya halali, na mwenye kujua uharamu wa kuvaa nguo ya kunyang’anya lau akiswali na nguo ya wizi au nguo yenye uzi au vifungo au kitu kingine cha kunyang’anya swala yake inabatilika na hukumu hii pia ni kwa mtu ambaye hajui na mwenye kupuuzia. 124
Al-Masailul Islamiyah
637. Anayejua uharamu wa kuvaa nguo ya kunyang’anya, lakini hajui kubatilika kwa swala ya mwenye kuswali kwa nguo hiyo, kama ataswali kwa nguo hiyo ya kunyang’anya kwa makusudi swala yake itabatilika. 638. Kama hakujua au akisahau kwamba nguo yake ni ya wizi na akaswali na nguo hiyo, swala yake itasihi lakini kama mtu mwenyewe akinyang’anya nguo kisha akasahau kwamba nguo hii ni ya kunyang’anya basi kwa tahadhari arudie swala hiyo kwa nguo halali. 639. Kama mtu akiswali kwa nguo ya kunyang’anya kwa kulinda maisha yake au kwa ajili ya nguo hiyo isiweze kubwa swala yake itasihi. 640. Akinunua nguo na pesa ambayo haijatolewa khumsi au zaka, na akaswali na nguo hiyo, swala yake itakuwa na mushkeli
SHARTI LA TATU 641. Ni wajibu vazi la mwenye kusali lisiwe limechanganywa na vitu vinavyotokana na mizoga ya wanyama ambao hutoka damu kwa kasi wakati wa kuchinja kama vile mbuzi, na kwa tahadhari pia asiswali na vazi lililotengenezwa na vitu vya mizoga ya wanyama ambao damu zao hazitoki kwa kasi kama vile samaki na nyoka.
SHARTI LA NNE 642. Ni wajibu vazi la mwenye kuswali lisiwe limetokana na vitu vya wanyama ambao ni haramu kuliwa na swala itabatilika kutokana na vitu hivyo hata kama vazi hilo lina unywele mmoja. 643. Kama vazi lake lina kitu chochote kinachotokana na mate au makohozi au kitu kingine chenye unyevunyevu unaotokana na wanyama 125
Al-Masailul Islamiyah walio haramu kuliwa kama vile paka, kama vina unyevunyevu swala yake itabatilika na vikiwa ni vikavu na najisi yake imeshaondoka swala yake itasihi. 644. Akishuku kwamba vazi hili limetengenezwa kutokana na wanyama ambao ni halali kuliwa au walioharamu kuliwa, itajuzu kuswali na vazi hilo sawasawa limetengenezwa katika nchi za kiisalamu au zisizokuwa za kiisalmu. Akiswali na nguo ambayo hajui au akisahau kwamba imetokana na mnyama ambaye ni haramu kuliwa swala yake itasihi.
SHARTI LA TANO 645. Ni haramu kwa mwanaume kuvaa nguo yenye nyuzi zilizochovya dhahabu au vifungo vya dhahabu na itabatilisha swala, lakini hakuna mushkeli katika hilo kwa wanawake katika swala na nje ya swala. Ni haramu kwa mwanaume kujipamba kwa mapambo ya dhahabu mfano kuvaa mikufu ya dhahbu shingoni au kuvaa pete au saa ya dhahabu mkononi, na vitu vinayobatilisha swala, na ni wajibu kujiepusha na kuvaa fremu za miwani kama ni za dhahabu, lakini hakuna tatizo kujipamba mapambo ya dhahabu kwa wanawake katika swala na nje ya swala. 646. Ikiwa mwanaume atasahau kwamba pete yake au vazi lake ni la dhahabu, au akashuku na akaswali kwa pete au vazi hilo, swala yake inasihi, lakini katika hali ya kushuku ni wajibu kwake afanye utafiti na vivyo hivyo ni wajibu kufanya utafiti katika mas’ala mengine yaliyobakia mbali na haya tuliyoyaeleza.
126
Al-Masailul Islamiyah
SHARTI LA SITA 647. Ni wajibu vazi la mwenye kuswali lisiwe limetokana na hariri halisi hasa akiwa mwanaume na ni haramu pia kuvaa nje ya swala, ama kofia, mkanda na mfano wa hivyo ni kinyume na tahadhari. 648. Nguo ambayo haifahamiki kuwa ni ya hariri halisi au laa, haina mushkeli kuivaa wakati wa swala, hakuna tatizo katika leso iliyotengenezwa kwa hariri ikiwa ndani ya mfuko wa mwenye kuswali na haitabatilisha swala. Hakuna tatizo kwa wanawake kuvaa hariri ndani ya swala au nje ya swala. Hakuna kizuizi wakati wa dharura kuvaa nguo ya kunyang’anya au iliyotengenezwa kwa hariri au kuchanganywa na dhahabu au kutengenezwa kutokana na vitu vya mizoga na inajuzu kuswali navyo.
SEHEMU AMBAZO HAZILAZIMU TOHARA YA MWILI NA NGUO KWA MWENYE KUSWALI 649. Inasihi swala kwa kiwiliwili au nguo yenye najisi katika sehemu tatu:Ikiwa mwili au nguo ya mwenye kuswali itachafuka kwa damu iliyotoka kwenye jeraha au kidonda au jipu kutoka katika mwili wake. Mwili wake au nguo yake ikichafuka kwa damu iliyotoka kwa kiwango kidogo sana. Kama atalazimika kuswali kwa mwili au nguo iliyo na najisi. 650. Swala inasihi swala katika hali mbili ikiwa nguo za mwenye kuswali tu zina najisi. Ikiwa mavazi yake ni madogo mfano wa soksi au kofia vina najisi. Ikinajisika nguo ya mwanamke anaelea kwa mkojo wa mtoto mchanga. 127
Al-Masailul Islamiyah
651. Kama katika mwili wa mwenye kuswali au nguo yake kuna jereha au kidonda au jipu , itajuzu kwake kuswali kwa nguo hiyo mwilini madamu jeraha au kidonda au jipu halijapona ikiwa kutoharisha mwili au nguo au kubadilisha kwake kutakuwa na ugumu na pia ikiwa katika mwili au nguo kuna matapishi yaliyotoka kwa kuchanganyikana na damu au dawa iliyowekwa kwenye jeraha ikatia najisi. Mtu ambaye mwili wake umejeruhiwa akiona katika mwili wake au nguo yake damu na akawa hajui ni damu ya jeraha lake au ni damu nyingine inajuzu kwake kuswali katika hali hiyo. 652. Ikiwa kwenye mwili wa mtu kuna majeraha mengi na yakawa yamekaribiana kiasi cha kuhesabika kuwa ni jeraha moja hakuna mushikeli kuswali na damu yake maadamu hajapona lakini kama yametengana kiasi cha kuhesabika kila jeraha mahali pake basi kila jeraha likipona itamlazimu kutoharisha nguo au mwili kwa ajili ya swala kutokana na damu hiyo. 653. Ikiwa katika mwili au nguo ya mwenye kuswali kuna damu ya hedhi au istihadha au nifasi au damu ya mbwa au nguruwe au damu ya kafiri au mizoga swala yake itabatilika na pia kama kuna damu ya mnyama ambaye ni haramu kuliwa, lakini hakuna tatizo katika swala pamoja na damu zingine kama damu ya mtu au damu ya mnyama aliye halali kuliwa japo itaenea sehemu za mwili wake au nguo yake kwa sharti iwe damu yote hiyo ni chache sana.
YALIYO SUNNA KATIKA VAZI LA 128
Al-Masailul Islamiyah
MWENYE KUSWALI 654. Ni sunna katika vazi la mwenye kuswali mambo mengi miongoni mwa hayo ni kuvaa kilemba, kuvaa joho, kuvaa nguo nyeupe, kuvaa nguo iliyo safi zaidi, kujipaka manukato na kuvaa pete ya akiki.
YALIYO MAKURUHU KATIKA VAZI LA MWENYE KUSWALI 655. Yaliyo makuruhu katika vazi la mwenye kuswali ni mengi, miongoni mwa hayo ni kuvaa nguo nyeusi, ila kwa ajili ya kukumbuka misiba ya maasumina (as) sio makuruhu bali ni sunna, na kuvaa nguo chafu, yenye kubana, nguo za mwenye kunywa pombe, nguo za mtu ambaye hajiepushi najisi, nguo yenye picha, nguo isiyo na vifungo na kuvaa pete yenye picha.
SEHEMU YA MWENYE KUSWALI 656. Sehemu ya mwenye kuswali ina masharti tisa nayo ni:1. Iwe ya halali. 2. Iwe imetulizana isitikisike 3. Aweze kutimiza swala yake humo 4. Asiwe amekatazwa kubaki mle 5. Isiwe kusimama au kukaa sehemu ile ni haramu 6. Aweze kusimama, kurukuu na kusujudu humo 7. Asiwe mbele au amelingana na kaburi la maasum(as) 8. Sehemu hiyo isiwe na najisi yenye unyevunyevu 9. Paji lake la uso liwe limelingana na magoti yake na ncha za dole gumba vya miguu yake.
129
Al-Masailul Islamiyah
Sharti la kwanza 657.Ni wajibu sehemu ya mwenye kuswali iwe ya halali, mwenye kuswali katika sehemu iliyo nyang’anywa swala yake ni batili hata kama ataswali juu ya godoro au kitanda lakini hakuna mushkeli kuswali chini ya dari ya unyang’anyi na hema la unyang’anyi. 658. Mwenye kukaa katika sehemu ya msikiti kisha akaja mtu na akamnyanganya sehemu yake hiyo na akaswali, swala yake itakuwa na mushkeli. 659. Kama mtu akijua kuwa sehemu hii ni ya kunyang’anya na hajui kuwa kuswali katika sehemu hiyo kunabatilisha swala, kisha akaswali hapo basi swala yake itabatilika kama hakufahamu kwa kupuuzia. Mwenye kuwa na udhuru, na akaswali juu ya mnyama kama mnyama huyo tandiko lake alotandikiwa juu ya mgongo wake au ikiwa kiatu chake ni cha kunyang’anya swala yake ni batili, pia hukumu ni hii hii kwa mwenye kuswali swala za sunna juu ya mnyama huyo.
Sharti la pili 660. Ni wajibu sehemu ya mwenye kuswali iwe yenye kutulizana na kama atalazimika kuswali katika sehemu yenye kutikisika kwa sababu ya ufinyu wa wakati au sababu nyingine, mfano kuswali katika gari au treni au ndege, itamuwajibikia kutokusoma wakati wa mtikisiko na kutotulizana kwa mwili kama ataweza kufanya hivyo, hii ni kama hataharibu utaratibu wa swala la sivyo asome wakati wa mtikisiko, pia kama gari litageuka kutoka upande wa kibla kuelekea upande mwingine ni wajibu yeye ageukie kibla. Hapakatazwi kuswali katika gari au meli na vinginevyo vikiwa vimesimama.
130
Al-Masailul Islamiyah
Sharti la tatu 661. Ni wajibu kwa mwenye kuswali aweze kumaliza swala, haijuzu kuanza kuswali katika sehemu ambazo huna uhakika kwamba utaweza kutimiza swala hapo, kwa sababu ya mvua au msongamano au upepo mkali, lakini lau atashuku katika hilo au akawa na uhakika wa kutimiza swala, itajuzu kuanza kuswali, na ikikamilika swala itasihi.
Sharti la nne 662.Nisharti asiswali katika sehemu ambayo ni haramu kubakia humo kama vile kuswali chini ya dari inayokaribia kuanguka na kubomoka.
Sharti la tano 663. Ni sharti mtu asiswali juu ya kitu kilichokatazwa kusimama juu yake au kukaa kama vile mswala ulioandikwa jina la Mwenyezi Mungu.
Sharti la sita 664. Ni wajibu asiswali katika paa liloinama sana kiasi kwamba hawezi kusimama vizuri chini yake ama akilazimika kuswali katika sehemu hii ni lazima asimame, arukuu na asujudu kadri atakavyoweza.
Sharti la saba 665. Ni wajibu asilitangulie kaburi la Mtume na maimamu wakati wa kuswali vivyo hivyo asiswali kwa kulingana nalo kwa tahadhari ya wajibu.
131
Al-Masailul Islamiyah
Sharti la nane 666. Ni wajibu sehemu ya mwenye kuswali isiwe na najisi yenye unyevu nyevu unaohamia kwenye mwili wake au nguo yake na swala itabatilika ikiwa sehemu ya kusujudia ina najisi hata kama ni kavu na kwa tahadhari ya sunna sehemu ya mwenye kuswali isiwe najisi kabisa.
Sharti la tisa 667. Ni wajibu sehemu ya paji lake wakati wa kusujudu isiwe juu au chini zaidi kuliko. magoti yake na ncha za vidole gumba zaidi ya vidole vinne vilivyounganishwa. 668. Si lazima mwanamke kusimama mbali ya mwanaume katika swala isiyokuwa ya jamaa, wala mahali anaposujudia kuwa mbali kidogo na mahali aliposimama mwanaume, ingawa ni bora kufanya hivyo. 669. Ni makuruhu kwa mwanamke kusimama mbele ya mwanaume au kuwa sawasawa naye katika swala na kuanza kuswali pamoja lakini haiwalazimu kurudia swala kama wakifanya hivyo. Kama kuna kizuizi kati ya mwanaume na mwanamke kiasi ambacho mmoja hamuoni mwenzake au kati yao kuna umbali wa mita tano, au mmoja wao kasimama sehemu ya juu sana kiasi ambacho haitasadikishwa kutangulia kwa mwanamke au kuwa sawasawa, basi karaha huondoka. Ni haramu kwa mwanaume na mwanamke ambao sio mahramu kukaa chumba kimoja bila ya kuwa na mtu mwingine wa tatu na bila ya kuonekana na yeyote, na kwa tahadhari ni kwamba swala yao haitasihi katika sehemu hiyo, lakini kama mmoja ataswali na mwingine akaingia, swala yake haina mushkeli. 670. Kuswali sehemu ya kupigia muziki kama haihesabiki kuwa ni kusaidia kufanya katika maasi haina mushkeli.
132
Al-Masailul Islamiyah
SEHEMU ZILIZO SUNNA KUSWALI HUMO 671. Umepokewa msisitizo mkubwa katika sharia ya kiislamu kuhusu kuswali katika misikiti na msikiti uliobora zaidi ni msikiti wa Makka, kisha msikiti wa Mtume Madina kisha msikiti wa Al Kufa kisha msikiti wa Al Aqswaa kisha kila msikiti mkuu wa kila mji, kisha msikiti wa kila mtaa, kisha msikiti wa soko. 672. Ni bora kwa wanawake kuswali nyumbani lakini wakiweza kujilinda na wanaume ajinabiya basi itakuwa ni bora kuswali misikitini.
HUKUMU ZA MISIKITI 673. Ni haramu kutia najisi ardhi ya msikiti, dari yake, paa lake na sehemu za ndani za kuta, na ni wajibu kwa atakayefahamu unajisi wa moja ya sehemu hizo kuiondosha najisi haraka na kwa tahadhari ya wajibu ni kwamba imeharamishwa kutia najisi sehemu za nje za msikiti, na ikinajisika ni wajibu kwake kuiondosha haraka. 674. Kama hakuweza kusafisha msikiti au akihitajia msaada na hakupata haitamuwajibikia kusafisha, lakini ni wajibu kwake kwa tahadhari ya wajibu kumwambia mwenye uwezo wa kusafisha. 675. Sehemu ya msikiti ikinajisika na ikawa haiwezekani kutoharishwa kwake ila kwa kuchimba shimo, basi ni wajibu kuchimbwa na ikilazimu kuvunja sehemu kwa ajili ya kutoharisha inajuzu kuvunja sehemu hiyo. Ni haramu kutia najisi makaburi ya maimam, na lau mojawapo likinajisika ni wajibu kulitoharisha. Ni haramu kuingiza kiini cha najisi msikitini kama vile damu kama kutaudhalilisha msikiti bali kwa tahadhari ya sunna kutoingiza kiini cha najisi msikitini hata kama si kwa ajili ya kuudhalilisha msikiti lakini sio haramu kuingiza kitu kilicho najisika msikitini, ila kama itakuwa ni kwa ajili 133
Al-Masailul Islamiyah ya kuudhalilisha msikiti. 676. Haikatazwi kuweka mahema misikitini kwa ajili ya maatam na majilisi za maombolezo ya maimamu. Pia haikatazwi kutundika na kuipamba kwa vitambaa vyeusi na kuingiza vitu vya kupikia chai kama havitaleta madhara na havizui watu kuswali humo. 677. Haijuzu kuuza ardhi ya msikiti ikiwa msikiti umebomoka pia kuunganisha na njia kuu au kuunganisha na milki ya mtu mwingine. 678. Ni haramu kuuza madirisha ya msikiti na milango yake na vitu vingine na kama msikiti ukibomoka basi ni wajibu kwa kiongozi wa kisharia kuvitoa vitu na kuvitumia kuimarisha msikiti huo, na kama haiwezekani kuvitumia katika msikiti huo, ni wajibu kuvitoa katika misikiti mingine, na ikishindikana katika misikiti mingine, itajuzu kuviuza kwa ajili ya kuimarisha misikiti mingine. 679. Inachukiza kuwaruhusu wasio na akili na watoto kuingia msikitini, ila watoto kama kuingia kwao ni kwa ajili ya kujifunza swala na Qur’ani na mas’ala ya kisharia, malezi, mafunzo ya kiislam na mengineyo, pia inachukiza kwa mwenye kula vitunguu maji na saumu kama harufu ya mdomo wake itawaudhi watu.
KUADHINI NA KUKIMU 680. Ni sunna kwa mwanaume na mwanamke kuadhini na kukimu kabla ya swala za wajibu za kila siku, bali haifai kuacha kukimu lakini kabla ya kuanza kuswali swala za wajibu zisizokuwa za kila siku mfano swala za majanga ni sunna kusema mara tatu “As swalaatu aswalatu aswalat”(badala ya kukimu). 781. Adhana ina vipengele ishirini navyo ni:Allahu akbar x 4 134
Al-Masailul Islamiyah Ashahadu an llaa ilaaha illa llaah x 2 Ash hadu anna Muhammadan rasulullah x 2 Ash hadu anna Alliyyan waliyullah x 2 Hayya alaa swalaat x 2 Hayya alaal falah x 2 Hayya alaa khairil – amal x 2 Allah akbar x 2 Laa ilaaha illa llah x 2 683. Na iqama ina vipengele 19 yaani kwa kuondosha takbira mbili za mwanzo na tahalili moja ya mwisho na kuongezea qadi qaamatis swalaat mara mbili baada ya “Hayya alaa khairil – amali” 684. Haifai kutenganisha sana kati ya sentensi na vipengele vya adhana na kukimu na akitenganisha sana kuliko kawaida basi atapaswa arudie tena upya. 685. Akirudiarudia kwa kughani adhana na kukimu kiasi kwamba inakuwa kama wimbo katika vikao vya upuuzi na michezo inakuwa ni haramu. 686. Hakuna adhana katika swala za aina tano:Swala ya alasiri siku ya Ijumaa Swala ya alasiri siku ya arafa, nayo ni siku ya 9 ya mfungo 3 swala ya isha usiku wa Idul -Adhuhaa kwa aliyoko muzdalfa Swala ya alasiri na isha kwa mwenye istihadha Swala ya alasiri na isha kwa asiyeweza kuzui mkojo au haja kubwa, katika swala hizi huondoka adhana kama hakutenganisha kati ya swala hiyo na Swala iliyotangulia. 687. Pakiadhiniwa na kukimiwa kwa swala ya jamaa, hawataadhini wala kukimu wale watakaounga jamaa hawatolazimika kuadhini wala kukimu tena. 688. Hakuna kukimu kama mtu akikuta watu wanaswali jamaa au jamaa 135
Al-Masailul Islamiyah imemalizika na watu hawajaondoka katika safu, na akataka kuswali peke yake au kuswali swala ya jamaa nyingine kwa masharti matatu:Iwe pameadhiniwa na kukimiwa katika swala iliyotangulia Isiwe swala ya jamaa iliyotangulia ni batili kuungana jamaa mbili ya mwanzo na inayofuatia katika sehemu moja. 689. Ni sunna kwa anayechaguliwa kuadhini na kukim awe mwadilifu, anayefahamu nyakati za swala mwenye sauti ya juu na aadhini katika sehemu iliyonyanyuka.
MAMBO YALIYOWAJIBU KATIKA SWALA 690. Wajibati za swala ni kumi na moja:Nia Kisimamo Takbira ya kuhirimia swala Rukuu Sijida Kusoma Dhikir Tashahud Kutoa salam 10.Kufuata utaratibu 11.Kufuatanisha 691. Baadhi ya wajibati za swala ni nguzo kwa maana kama mwenye kuswali akiicha au akizidisha kwa makusudi au bila ya kukusudia swala yake inabatilika, na baadhi ya wajibati siyo nguzo, kwa maana kwamba swala inabatilika kwa kupunguza au kuzidisha kwa makusdui wala haibatiliki kwa kusahau. 692. Nguzo
za swala ni tano 136
Al-Masailul Islamiyah
Nia Takbira ya kuhirimia Kisimamo wakati wa takbira ya kuhirimia na kisimamo kilichoungana na rukuu (yaani kabla ya kurukuu) Rukuu Sijida mbili NIA 693. Ni wajibu kwa mwenye kuswali atie nia katika swala kwa kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu, na kutekeleza amri yake, wala hailazimu kupitisha moyoni au kuitamka kwa ulimi wake, bali yatosha kufahamu kwamba yeye anaswali rakaa nne za swala ya adhuhuri kwa ajili ya kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu. 694. Akinuia katika swala ya adhuhuri au alasiri kwamba anaswali rakaa nne lakini hakubainisha kwamba ni adhuhuri au alasiri basi swala yake itakuwa na mushikeli na ni wajibu kwa ambaye ana kadha ya adhuhuri na akataka kuswali adhuhuri kwa wakati au kadha katika wakati wa adhuhuri kubainisha kwamba anaswali kadha au adaa (kwa wakati). 695. Ni wajibu kwa mwenye kuswali kubakia na nia yake tangu mwanzo wa swala hadi mwisho na akighafilika wakati wa swala, kiasi lau akiulizwa unafanya nini? Ikawa hajui aseme nini, swala yake itabatilika.
137
Al-Masailul Islamiyah
TAKBIRA YA KUHIRIMIA 696. Takbira ya kuhirimia yaani kusema: “Allah akbar” ni wajibu katika kila mwanzo wa swala nayo ni nguzo katika swala na ni wajibu kufuatanisha kati ya neno “Allah” na neno “Akbar” pia ni wajibu kuyatamka kwa lugha ya kiarabu sahihi, na lau akitamka kwa kiarabu chenye makosa au kwa lugha isiyokuwa ya kiarabu, takbira yake haitasihi. 697. Ni wajibu kwa mwenye kuswali kutulizana wakati wa kuleta takbira ya kuhirimia, na kama akihirimia na hali anatikisika kwa makusudi, takbira yake inabatilika. 698. Ni wajibu kuhirimia, na kusoma Al hamdu, sura, dhikiri na dua kwa kiasi cha kusikia mwenyewe, kama ni kiziwi au asiyesikia vizuri au kwa sababu ya makelele mengi, ni wajibu kuhirimia kwa kiasi ambacho kama si kizuizi angesikia. 699. Bubu na mwenye matatizo ya ulimi yanayomfanya asiweze kutamka takbira kwa njia sahihi, ni wajibu kutamka kwa namna atakayoweza, na kama hakuweza kutamka chochote, itamlazimu kutamka kimoyo moyo, na aashirie katika kuhirimia kwa kutikisa ulimi wake kwa namna atakavyoweza. 700. Ni sunna kunyanyua mikono mpaka kwenye usawa wa masikio wakati wa kuhirimia na katika takbira zingine wakati wa swala.
KISIMAMO 701. Kisimamo wakati wa kuhirimia na kisimamo kabla ya kwenda kurukuu, visimamo hivi ni nguzo mbili, lakini kisimamo wakati wa kusoma Al hamdu na sura na kisimamo baada ya rukuu si nguzo laki138
Al-Masailul Islamiyah ni akiviacha kwa kusahau swala yake itasihi. 702. Ni wajibu kusimama kabla ya kuhirimia swala na baada ya kuhirimia kwa kiwango cha kuwa na uhakika kwamba amehirimia wakati wa kisimamo. 703. Akisahau kurukuu na akakaa baada ya Al hamdu na sura kisha akakumbuka kwamba hajarukuu ni wajibu kusimama na kisha arukuu, na akirukuu bila ya kusimama kwanza, swala yake inabatilika kwa sababu hajasimama kabla ya rukuu. 704. Ni wajibu asitikise mwili wake wakati wa kisimamo na asiegemee upande mmoja wala asiegemee kitu chochote, lakini hakuna tatizo lau akifanya mambo haya kwa dharura, kama ambavyo hakuna tatizo kama atatikisa miguu yake wakati wa kuinama kwenda kwenye rukuu. 705. Akishindwa kusimama wakati wa kuswali ni wajibu kukaa na akishindwa kukaa pia, ni wajibu kwake kulala lakini asisome chochote mpaka atulizane.
KUSOMA 706. Ni wajibu kusoma Al hamdu na sura kamili katika rakaa mbili za mwanzo katika swala za wajibu za kila siku. Kama wakati utakuwa ni mfinyu na akalazimika kutokusoma sura, mfano lau ataogopa kuibiwa au kudhuriwa na wanyama wakali au litamsibu jambo jingine kama atasoma sura, basi ni wajibu kwake asisome sura. 707. Akisoma sura kabla ya kusoma Al hamdu kwa makusudi swala yake itabatilika. Na akifanya hivyo kwa kusahau na akakumbuka wakati huo, itamlazimu kuacha sura kisha atasoma Al hamdu kisha atasoma sura kuanzia mwanzo.
139
Al-Masailul Islamiyah 708. Akisahau kusoma Al hamdu na sura au akasahau mojawapo kisha akakumbuka baada ya kufika kwenye rukuu swala yake itasihi. 709. Akikumbuka kabla ya kuinama kwenye rukuu kwamba hakusoma Al hamdu na sura ni wajibu kuzisoma, pia akikumbuka kwamba hakusoma sura peke yake, ni wajibu kuisoma, lakini akikumbuka katika hali ile kwamba hakusoma Al hamdu ni wajibu kuisoma Al hamdu kwanza kisha atairudia sura mara nyingine, na atafanya hivyo akijua baada ya kuinama na kabla ya kufika katika rukuu kuwa hakusoma Al hamdu na sura au mojawapo atarejea katika kisimamo na kusoma Al hamdu aliyoisahau. 710. Akikusudia katika swala ya wajibu kusoma mojawapo ya sura zenye sijda ya lazima swala yake itabatilika. 711. Ni wajibu kwa mwanaume kudhihirisha Al hamdu na sura katika swala ya asubuhi, magharibi na isha na ni wajibu kwa mwanaume na mwanamke kutokudhihirisha katika swala ya adhuhuri na alasiri. 712. Ni wajibu kwa mwanaume kudhihirisha kila neno la sura ya Al hamdu na sura atakayoisoma katika swala ya asubuhi, magharibi na isha hata herufi ya mwisho. 713. Inajuzu kwa mwanamke kutokudhihirisha au kudhuhirisha Al hamdu katika swala ya asubuhi, magharibi na isha lakini hatodhihirisha kama sauti yake itasikika na mtu ambaye si mahramu yake.
714. Mwanaume akikusudia kutokudhihirisha katika swala ambayo ni wajibu kudhihirisha swala yake itabatilika lakini lau akifanya hivyo kwa kusahau au kutokujua swala yake itasihi, na akifahamu kuwa amekosea wakati wakusoma Al hamdu na sura, haimlazimu kurudia aliyosoma kwa kukosea. 140
Al-Masailul Islamiyah 715. Akisoma kwa sauti ya juu sura ya Al hamdu na sura kinyume na sauti zilizozoeleka, kama akisoma kwa kupiga makelele ya juu, swala yake itabatilika. 716. Ni wajibu kujifunza swala ili asisome kwa makosa na ambaye hawezi kujifunza kutamka sawa sawa, ni wajibu kuswali kwa njia atakayoweza lakini ni vizuri kuswali jamaa. 717. Ni sunna katika swala zote kusoma suratul – Qadir katika rakaa ya kwanza na suratu tauhid katika rakaa ya pili. 718. Inachukiza kwa mtu kuacha kusoma suratu tauhid katika swala zake za kila siku. 719. Inachukiza kuisoma suratu tauhid yote kwa pumzi mmoja bila ya kusimama kwenye vituo. 720. Inachukiza kusoma katika rakaa ya pili sura aliyoisoma katika rakaa ya kwanza isipokuwa kama atasoma suratu tauhid.
RUKUU 721. Ni wajibu kuinama baada ya kusoma katika kila rakaa kwa kiwango cha kumuwezesha kushika magoti yaani kuweka viganja vya mikono yake magotini. 722. Hakuna tatizo akiinama kwa kiwango cha kushika magoti hata kama hakuweka viganja vyake juu ya magoti yake 723. Ni wajibu kuinama kuwe kwa nia ya kurukuu na akiinama kwa lengo lingine kama kuweka kitu au kukinyanyua haitojuzu kuhesabiwa kuwa ni rukuu. 730. Akirukuu kwa namna isiyoeleweka, kwa mfano lau akiinama kwa kuelemea upande wa kulia au wa kushoto, rukuu yake haitosihi hata 141
Al-Masailul Islamiyah kama mikono yake itafika kwenye magoti. 731. Ni bora kusema katika rukuu “Subhanallah” mara tatu au “Subhana rabbiyal – adhiim wabihamdih” mara moja lakini kama muda ni mfinyu au wakati wa dharura yatosha kusema “Subuhanallah” mara moja. 732. Ni wajibu dhikri ya rukuu iwe kwa kufuatana na kwa kiarabu sahihi na ni sunna kuikariri mara tatu au tano au zaidi. 733. Ni wajibu mwili wa mwenye kuswali kutulizana wakati wa kurukuu kiasi cha kuweza kuitamka dhikri ya wajibu na pia wakati wa kutamka dhikri ya sunna. 734. Akinyanyua kichwa chake makusudi kabla ya kukamilisha dhikiri ya wajibu swala yake inabatilika. 735. Akisahau kurukuu na akakumbuka kabla ya kufika katika sijda ni wajibu kusimama kisha alete rukuu na lau akisimama kwenye rukuu kwa kuinama swala yake itabatilika. 736. Akikumbuka kuwa hakurukuu na hilo ni baada ya kuwa ameshafika chini au baada ya kunyanyua kichawa chake kutoka kwenye sijda ya kwanza, itamlazimu asimame wima kisha arukuu, kisha alete sijda ya swala, kisha sijida ya sahau baada ya swala na kwa tahadhari arudie swala yake mara ya pili.
KUSUJUDU 737. Ni wajibu kwa mwenye kuswali kuleta sijida mbili baada ya rukuu, katika kila rakaa za wajibu na sunna, maana ya kusujudu ni kuweka paji la uso na matumbo ya viganja, magoti na vidole gumba vya 142
Al-Masailul Islamiyah miguu juu ya ardhi. 738. Sijda mbili ni nguzo, kama mwenye kuswali akiziacha katika swala ya wajibu kwa makusudi au kwa kusahau au akizidisha sijda mbili zingine, swala yake itabatilika. 739. Akipunguza au akizidisha moja ya sijida mbili kwa makusudi swala yake itabatilika 740. Kama hakuweka paji la uso wake ardhini kwa makusudi au kwa kusahau sijda hiyo haitahesabika hata kama ameweka sehemu zingine za kusujudia ardhini, lakini akiweka paji lake ardhini na hakuweka viungo vingine vya kusujudia sijda yake itasihi. 741. Ni wajibu kutulizana kwa mwili katika sijida kiasi cha kuleta dhikiri ya wajibu na pia katika dhikiri ya sunna. 742. Akikusudia kuleta dhikri ya sijda kabla ya kufikisha paji la uso wake ardhini na kutulizana mwili wake au akanyanyua kichwa chake kabla ya kutimiza dhikri ya sijda kwa makusudi swala yake itabatilika. 743. Akileta dhikri ya sijida kabla ya kufikisha paji lake ardhini na mwili wake kutulizana kwa kusahau na akafahamu makosa yake kabla ya kunyanyua kichwa katika sijda atarudia dhikri na swala yake itasihi. 745. Akitambua baada ya kunyanyua kichwa katika sijda kwamba ameleta dhikri kabla ya kutulizana mwili wake au amenyanyua kichwa kabla ya kutimiza dhikri ya sijida swala yake itasihi. 746. Akikusudia kunyanyua mojawapo ya viungo saba vya sijda wakati wa kuleta dhikri ya sijda, swala yake inabatilika lakini hakuna tatizo akinyanyua moja ya viungo vya sijda isipokuwa paji la uso katika hali isiyokuwa ya kuleta dhikri ya swala kisha akarejesha kiungo hicho ardhini mara nyingine.
143
Al-Masailul Islamiyah
VITU VINAVYOSIHI KUSUJUDIA JUU YAKE 747. Ni wajibu kusujudu juu ya ardhi na vinavyotokana na ardhi “isipokuwa vile vinavyoliwa au kuvaliwa� kama vile mbao na majani ya miti, wala haisihi kusujudu juu ya vitu vyenye kuliwa, kama vile matunda na vyenye kuvaliwa kama vile pamba na vitu vya madini kama vile dhahabu. 748. Haikatazwi kusujudu juu ya jani la zabibu likiwa kavu, kama sio kavu na liko katika muda wa kuweza kuliwa, haitajuzu kusujudu juu yake. 749. Inasihi kusujudu juu ya vitu vinavyoota katika ardhi na vyenye kuliwa na wanyama kama vile majani, pumba n.k 750. Kilicho bora zaidi kusujudia ni turba ya Imam Hussein (as) kisha udongo wa kawaida kisha jiwe kisha mimea. 751. Kama hana kitu chenye kusihi kusujudia juu yake au anacho lakini akawa hawezi kusujudu juu yake kwa sababu ya baridi kali au joto kali, basi kama ana nguo iliyotengenezwa kwa pamba au katani, ni wajibu kwake kusujudu juu ya nguo yake, na ikiwa nguo yake imetokana na vitu vingine ni wajibu kusujudu juu ya viganja vya mikono yake au kitu cha madini kama vile pete ya akiki lakini ni bora asisujudu juu ya viganja vyake kama kunauwezekano wa kusujudu juu ya kitu cha madini. Kusujudu katika ardhi ambayo haitulizani ni batili. 752. Hakuna tatizo katika swala yake kama akifahamu baada ya kusujudu kwamba amesujudu katika vitu ambavyo havisihi kusujudu juu yake. 753. Ni haramu kumsujudia asiyekuwa Mwenyezi Mungu na wanayofanya 144
Al-Masailul Islamiyah baadhi ya waumini kwa kuweka mapaji ya nyuso zao katika dharihi ya makaburi ya Maimamu watukufu hilo ni kwa ajili ya kumshukuru Mwenyezi Mungu na hakuna mushkeli humo, ama kubusu ukuta wa makaburi ya Maimamu jambo hilo linajuzu bali ni sunna na hilo sio sijida
SUNNA ZA SIJDA NA MAKURUHU ZAKE 753. Ni sunna katika sijida mambo yafuatayo:Mwenye kuswali aseme Allahu akbar akiwa amesimama kabla ya kwenda kusujudu, baada ya kunyanyua kichwa chake katika rukuu na kusimama wima, pia kwa mwenye kuswali kwa kukaa baada ya kukaa wima. Mwanaume kutanguliza mikono yake ardhini kwanza wakati wa kwenda kusujudu kisha magoti yake. Kuweka pua yake juu ya turba au kitu chenye kusihi kusujudia juu yake. Kuviunganisha vidole vya mikono yake na kuiweka mikono yake usawa wa ndwele za masikio yake kiasi kwamba ncha za vidole vyake vinakuwa vimeelekea kibla Kuomba katika sijida yake na kumwomba Mwenyezi Mungu kumkidhia haja zake na aombe kwa dua hii “ Yaa khairal – masiuliina wa yaa khairal – mu’utwiina, urzuqunii warzuqu iyaalii min fadhilika fainnaka dhul fadhilil adhiym” Kukalia paja la kushoto anapotoka katika sijda na kuweka mgongo wa mguu wa kulia juu ya tumbo la mguu wa kushoto. Alete takibira baada ya kukaa katika kila sijda na mwili wake utulizane. Aseme “Astaghafirullaha rabii waatubu ilaihi” Baada ya kukaa kutoka sijda ya kwanza na mwili wake utulizane. Arefushe sijida yake Aweke mikono yake juu ya mapaja anapokaa 145
Al-Masailul Islamiyah Alete takbira anapokwenda sijida ya pili katika hali ya kutulizana Amswalie Mtume na kizazi chake katika sijida yake Aweke mikono yake ardhini anapotaka kusimama Mwanaume asikutanishe viwiko vya mikono yake na tumbo lake na asiikutanishe na mbavu zake lakini mwanamke alaze viwiko vyake na tumbo lake ardhini na kuvibana viungo vya mwili wake. 754. Inachukiza kupuliza sehemu ya kusujudia kwa ajili ya kuondosha vumbi na lau ikitoka kutokana na kupuliza lafudhi ya herufi mbili mfano akisema fuu, kwa makusudi swala yake itabatilika.
SIJDA ZA QUR’AN ZILIZO WAJIBU 755. Sijda za wajibu zinapatikana kila moja katika sura nne nazo ni:surat Najmi: aya ya 62, Al Alaq aya ya 19, Fusswilat aya ya 37 na As Sajida aya ya 15 kila sura ina aya moja ya sijida ya wajibu na zinabainishwa katika misahafu mitukufu na ni wajibu kwa mtu atakapo isoma au kuisikia asujudu baada ya kukamilika kusomwa aya kwa haraka, na kama atasahau kusujudu wakati ule ule, basi asujudu akikumbuka. Inawajibika kusujudu kama ikisomwa aya kamili ama lau ikisomwa nusu haitolazimu kusujudu. 756.Akisikia aya ya sijda ikisomwa na mtoto ambaye hatofautishi jambo la kheri na la shari au akasikia kwa mtu ambaye hakukusudia kusoma Qur’ani, kwa tahadhari ya sunna asujudu, na pia akisikia aya ya sijda katika kanda za kaseti au redioni. Yatosha katika sijida ya Qur’an ya wajibu kuweka paji la uso ardhini kwa lengo la kusujudu hata kama hakusoma dhikri lakini ni sunna kusoma dhikri na ni bora kusema: “Laa ilaaha illa llahu haqan haqan, laa ilaha illa llahu imanan wataswidiyqan, laa illaha illallaahu ubudiyatan wariqan, sajadtu laka ya Rabi ta’abbudan wariqqan laa mustankifan 146
Al-Masailul Islamiyah walaa mustakbiran bal anaa abdun dhalilun dhaiifun khaaifun mustajiirun”
TASHAHUD 757. Ni wajibu kukaa katika kila rakaa ya pili ya swala za wajibu na katika rakaa ya tatu ya swala ya magharibi na rakaa ya nne ya swala ya adhuhuri, alasiri na isha na hilo ni baada ya kukaa kutoka sijida ya pili, na kusema hali umetulizana mwili wake “Ash hadu an laa ila ha illa llaahu wahadahu laa sharika lahu waash hadu anna Muhammadan abduhu warasuluhu Allahumma swali alaa Muhammadin waali Muhammadi” 758. Ni wajibu kuyasoma maneno ya tashahudi kwa kiarabu sahihi na kwa kufuatana kama inavyofahamika. 759. Akisahau tashahud na akasimama kisha akakumbuka kabla ya kurukuu kuwa hajaleta tashahud atakaa na kuleta tashahudi kisha atasimama na kusoma yaliyo wajibu katika rakaa hiyo na kukamilisha swala kisha ataleta sijda sahau baada ya swala kwa kusimama pasipo mahala pake na akikumbuka ndani ya rukuu au baada ya salamu atailipa tashahudi na kuleta sijia mbili za sahau kwa ajili ya tashahudi iliyo sahauliwa. 759. Ni sunna kwa mwanamke kubananisha mapaja yake wakati wa tashahudi.
KUTOA SALAM 760. Mwenye kuswali atasema baada ya tashahud katika rakaa ya mwisho ya swala na akiwa amekaa na kutulizana mwili wake “Assalaam alaika ayyuha nnabiyyu warahmatullah wabarakatuh assalam alainaa waalaa ibaadillah sswalihiyna assalaam alaikum warahmat147
Al-Masailul Islamiyah ullah wabarakatuh�. 761. Akisahau salam na akawa hakukumbuka ila baada ya kumalizika swala ni wajibu kwa tahadhari alete sijda mbili za sahau na ni vizuri zaidi kuirudia swala yake.
MPANGILIO 762. Akiacha mpangilio wa swala kwa makusudi mfano akasoma sura kabla ya Al hamdu au akasujudu kabla ya kurukuu swala yake itabatilika. 763. Akisahau nguzo miongoni mwa nguzo za swala kwa mfano akaleta sijida mbili kabla ya kuleta rukuu swala yake itabatilika. 764. Akisahau nguzo na akaleta kinachofuatia ambacho si nguzo, kwa mfano akisahau sijida mbili na akaleta tashahudi ni wajibu alete nguzo aliyoisahau kisha atarudia kusoma aliyoyasoma mwanzo kimakosa au kwa kusahau. 765. Akisahau ambayo si nguzo na akaleta nguzo inayofuata, kwa mfano lau akisahau Al hamdu na akashughulika na rukuu swala yake itasihi. 766. Akileta sijida ya kwanza kwa kuamini kuwa ni sijida ya pili itahesabika kuwa ni sijda ya kwanza au akileta sijida ya pili k0wa kuamini kuwa ni sijda ya kwanza itahesabika kuwa ni sijida ya pili na swala yake itasihi.
KUFUATANISHA 767. Ni wajibu kwa mwenye kuswali kuchunga mfuatano wa swala yaani alete vitendo vya swala kama vile kurukuu, kusujudu na tashahud kwa kufuatana na bila ya kutenganisha, pia achunge na afuatanishe katika dhikir ambazo anazisoma kama inavyofahamika, na lau atatenganisha kati 148
Al-Masailul Islamiyah ya mambo haya kiasi ambacho haitasemwa kwamba anaswali, swala yake itabatilika. 768. Akitenganisha kati ya herufi na manaeno ya swala kwa kushau lakini kutenganisha huko sio kwa kiasi cha kufuta utaratibu wa swala kama hakushughulika na nguzo inayofuata ni wajibu kurudia kisomo cha herufi na maneno yale kwa kufuatanisha na kwa njia yenye kufahamika na lau kama ameshughulika na nguzo iliyofuata swala yake itasihi. 769. Kurefusha rukuu na sijida na kusoma sura ndefu hakuvunji wala hakuharibu mfuatano wake.
KUNUTI 770. Ni sunna kusoma kunuti katika swala zote za wajibu na za sunna na hilo ni kabla ya kwenda rukuu ya rakaa ya pili bali ni vizuri kutokuacha kunuti katika swala za wajibu na ni sunna kusoma kunuti katika swala ya witiri japokuwa ni rakaa moja. 771. Katika kila rakaa ya swala ya ijumaa kuna kunuti na katika swala za majanga kuna kunuti tano, na katika swala ya Iddi rakaa ya kwanza ina kunuti tano na rakaa ya pili ina kunuti nne, na ni bora kutokuacha kunuti za swala ya Iddil- Fitri na Adhuhaa. 772. Ni Sunna kwa mwenye kuswali kudhihirisha kunuti yake lakini ni makuruhu kwa anayeswali jamaa kudhihirisha kunuti yake kama Imamu atasikia sauti yake.
KUMSWALIA MTUME (SAWW) 773. Ni sunna kumswalia Mtume na watu wa nyumbani kwake pindi 149
Al-Masailul Islamiyah usikiapo majina yake matukufu kama Muhammadi, Ahmadi au sifa yake kama Mustwafaa au lakabu yake kama Abul – Qasim na hata akisikia dhamiri inayomkusudia Mtume hata kama yupo kwenye swala. 774. Ni sunna kuandika “kumtamkia rehema Mtume” pindi unapoandika majina yake matukufu na pia kumtakia rehema Mtume na watu wa nyumbani kwake anapowataja. 775. Namna ya kumtakia rehema Mtume ni kusema: “Allahuma swali alaa Muhammadi wa Aali Muhammadi”
VINAVYO BATILISHA SWALA 776. Vitu vinavyobatilisha swala ni kumi na mbili:Kukosekana sharti miongoni mwa masharti ya swala. Kutenguka udhu au josho Kuweka mkono juu ya mwingine “juu ya tumbo” Kusema “amina” baada ya Al hamdu Kukipa kibla mgongo Kuzungumza Kukohoa Kulia kwa ajili ya mambo ya kidunia Kufutika sura ya swala Kula na kunywa Baadhi ya vifungu vya shaka Ziada au upungufu katika nguzo za swala na zinginezo kwa ujumla.
YA KWANZA 777. Cha kwanza katika vinavyobatilisha swala ni kukosekana katikati ya swala sharti miongoni mwa masharti yake, mfano atambue katikati ya swala kuwa sehemu anayoswalia ni ya unyang’anyi na 150
Al-Masailul Islamiyah hawezi kuhamia katika sehemu iliyohalali bila ya kufanya mambo mengi ya kufuta sura ya swala.
YA PILI 778. Cha pili katika vinavyobatilisha swala ni kupatwa katikati ya swala na moja ya vitenguzi vya udhu au josho, kwa kukusudia au kusahau au kwa dharura mfano kutokwa na mkojo. 779. Al- masluus– Anayetokwa na mkojo kila wakati, au al – mabtun – anayetokwa na haja kubwa mara kwa mara wakifanya kutokana na wadhifa wao ambao tumeutaja katika hukumu za udhu swala zao hazitabatilika. Na vile vile Mustahadha swala yake itasihi akitokwa na damu katika swala akizingatia hukumu za istahadha. 780. Mwenye kughafilika na akalala bila ya hiyari kama hatajua amelala ndani ya swala au baada ya swala, ni lazima arudie swala kwa tahadhari ya wajibu ndani ya muda, na ni sunna alipe nje ya wakati. 781. Akitambua kuwa amelala kwa kutaka kwake na akasahau kuwa amelala baada ya swala au katikati ya swala, swala yake itasihi. 782. Atakapoamka usingizini katika hali ya sijda na akashuku kuwa amelala katika sijda ya mwisho ya swala au katika Sijida ya kushukuru, “Baada ya swala” ni lazima arudie swala kwa tahadhari ya wajibu ndani ya wakati, na ni sunna airudie nje ya wakati
YA TATU 783. Cha tatu katika vinavyobatilisha swala ni “takfiri” nayo ni kuweka moja ya mikono miwili juu ya mwingine kama wafanyavyo wasiokuwa Shia.
151
Al-Masailul Islamiyah 784. Akiweka mkono juu ya mwingine ni lazima arudie swala na hata kama hatafanya mfano wa takfiri zao, lakini hakuna tatizo kama atafanya hivyo kwa kusahau, au kwa dharura au akifanya hivyo kwa kujikuna na mfano wake.
YA NNE 785. Cha nne katika vinavyobatilisha swala ni kusema “Amin” baada ya kusoma Al – hamdu ,na akisema hivyo kwa kusahau au taqiya swala yake haitobatilika.
YA TANO 786. Cha tano katika vinavyobatilisha swala ni kukipa kibla mgongo kwa kukusudia au kusahau au kwa kutokujua au akigeukia kulia au kushoto mwa kibla, bali hata kwa makusudi kwa kiasi kwamba haisemekani kuwa ameelekea kibla swala yake inabatilika hata kama hajageuka kulia au kushoto. 787. Akigeuza kichwa chake mwelekeo wa kibla kwa kukusudia au kwa kusahau kiasi kwamba anaweza kuona nyuma swala yake inabatilika, lakini akigeuza uso wake kidogo kwa kukusudia au kwa kusahau swala yake haibatiliki
YA SITA 788. Cha sita katika vinavyobatilisha swala ni kutamka neno lenye herufi mbili au zaidi hata kama halina maana lakini akifanya hivyo kwa kusahau swala yake haibatiliki. 789. Akitamka neno lenye herufi moja na lenye maana mfano “Qi” ambacho ni kitendo cha amri ambacho kinatokana na “waqaa, yaqii” kwa maana ya hifadhi, akifahamu maana ya kitendo hiki na akakusudia kutamka, swala yake inabatilika, kwa tahadhari ya wajibu arudie 152
Al-Masailul Islamiyah swala hata kama hakukusudia maana yake lakini alikuwa anatambua kuwa maana yake ni hiyo. 790. Hakuna tatizo katika kukohoa, kucheua na kupiga miayo kwenye swala, lakini kauli “akh” “ah” na zingine zenye herufi mbili zinabatilisha swala kama zikitamkwa kwa kukusudia. 791. Hakuna tatizo akitamka neno kwa kukusudia utajo mfano akisema: “Allahu Akbar” kwa sauti ya juu ya kumzindua mwenzake katika jambo fulani, na akitamka neno kwa kukusudia uzinduzi wa kufahamisha jambo fulani na bila kukusudia kuwa ni dhikri swala itabatilika. 792. Hakuna tatizo kusoma Qur’an katika swala isipokuwa sura za “Azaim” zenye sijida za lazima ambazo utajo wake umeshapita katika hukumu za janaba, na pia hakuna tatizo katika kutaja majina ya Mwenyezi Mungu katika swala, na pia hakuna tatizo kwenye dua, kwa tahadhari ya wajibu asiombe dua ila kwa kiarabu. 793. Hakuna tatizo katika kurudiarudia sehemu katika suratul - Hamdu au sura au mengineyo miongoni mwa dhikri za swala mara nyingi kwa tahadhari, pia hakuna tatizo akirudia rudia bila ya kukusudia au kutenganisha, lakini akirudia rudia kitu kwa sababu ya wasiwasi swala yake itaharibika kwa tahadhari
SALAMU KATIKA SWALA 794. Mwenye kuswali hatakiwi amsalimie yeyote lakini anaposalimiwa ni wajibu arudishe salamu kama alivyosalimiwa , yaani arudishe salamu kwa matamshi yale yale, mfano akiambiwa “Asalam Alaykum” mwenye kuswali arudishe salamu kwa kusema “ Asalamu Alaikum” lakini akisema “Alaikum Salam” kwa tahadhar aseme “Asalam Alaykum” 153
Al-Masailul Islamiyah 795. Ni wajibu kurudisha salamu haraka katika swala au nje ya swala, na akichelewa k`urudisha salamu kwa kukusudia au kwa kusahau kwa muda kiasi kwamba akirudisha salamu haitahesabika kuwa ni jawabu la ile salamu akiwa katika swala asirudishe salamu na akiwa nje ya swala si wajibu kurudisha salamu. 796. Si wajibu alete jawabu la salamu kwa nia ya dua kwa kunuia kwa kauli yake “Assalam alaikum� kuomba amani kutoka kwa Mwenyezi Mungu kwa yule aliyemsalimia lakini inajuzu alete kwa kusudio la kurudisha salamu. 797. Mwanamke akimsalimia mwanaume ajinabi katika swala au mwanaume akimsalimia mwanamke ajinabiya katika swala au ikiwa mwenye kusalimia ni mtoto wa kiume aliyepevuka, inajuzu kwa mwenye kuswali bali ni wajibu wake arudishe salamu. 798. Mwenye kuswali asiporudisha salamu atakuwa ameasi na amepata dhambi lakini swala yake inasihi. 799. Mtu akimsalimia mwenye kuswali kwa kukosea maneno kama itahesabika kuwa ni salamu au kama atakosea katika matamshi yake ni wajibu arudishe salamu na isipohesabika kuwa ni salamu si wajibu kurudisha, bali haijuzu kurudisha salamu ndani ya swala. 800. Si wajibu kuitikia salamu kwa anayesalimia kwa mzaha au kejeli pia haijuzu kumwitikia katika swala. 801. Mtu akisalimia kundi la watu ni wajibu kwa watu wale kuitikia salamu, pia inatosha akiitikia mmoja wao. 802. Mtu anaposalimia watu na akaitikia asiyekusudiwa kurudisha salamu haitaporomoka kwa waliokusudiwa bali ni wajibu wao kurudisha salamu. 154
Al-Masailul Islamiyah 803.Mtu anaposalimia watu na mwenye kuswali akaitilia shaka kuwa msalimiaji alimkusudia yeye au hakumkusudia, haijuzu kwa mwenye kuswali kurudisha salamu, na pia akitambua kuwa msalimiaji alimkusudia lakini wakajibu wengine inatosha, na akitambua kuwa msalimiaji alimkusudia yeye halafu hakujibu hata mmoja ni lazima yeye arudishe salamu. 804.Kuanza kusalimia ni sunna na imetiliwa mkazo kuwa mwenye kipando aanze kumsalimia asiye na kipando, aliyesimama kwa aliyekaa na mdogo amsalimie mkubwa ama kuitikia salamu ni wajibu. 805. Zikigongana salamu za watu wawili kwa tahadhari kila mmoja aitikie salamu ya mwingine. 806. Ni sunna kurudisha salamu kwa iliyobora zaidi nje ya swala, mfano mtu akisema “salam Alaykum” ajibu kwa kusema “salam alaikum warahmatu llaahi”
YA SABA 807. Cha saba katika vinavyobatilisha swala ni kucheka kwa sauti, kwa kukusudia au kwa dharura, ama akicheka kwa kusahau hakuna tatizo katika swala, isipokuwa asitoke katika sura ya swala, ama kutabasamu haibatilishi swala. 808. Ikibadilika hali yake kwa ajili ya kujizuia kudhihirisha sauti ya kicheko mfano, rangi yake kuwa nyekundu kwa tahadhari ya sunna arudie swala yake, lakini akitoka katika sura ya swala hapo atawajibika kurudia swala.
YA NANE 809. Cha nne katika vinavyobatilisha swala ni kukusudia kulia kwa sauti kwa ajili ya mambo ya kidunia, kwa tahadhari ya wajibu asilie kwa 155
Al-Masailul Islamiyah ajili mambo ya kidunia hata bila ya sauti lakini hakuna tatizo kulia kwa ajili ya kumnyenyekea Mwenyezi Mungu au kwa ajili ya mambo ya akhera kwa sauti ya juu au ya chini bali hili ni katika vitu vizuri na pia inajuzu kwa dhahiri kulia kwa misiba ya Mtume na watu wa nyumbani kwake “as.�
YA TISA 810. Cha tisa katika vinavyobatilisha swala ni kufanya kitendo kinachofuta sura ya swala kama kupiga makofi sana au kuruka sana n.k. kwa kukusudia au kusahau lakini hakuna tatizo kufanya kitu kisichofuta sura ya swala kama kuashiria kwa mkono. 811. Akinyamaza kwa muda mrefu kwenye swala kiasi kwamba haisemekani kuwa anaswali swala yake inabatilika. 812. Akileta kitendo katika swala au akinyamaza kwa muda, akitilia shaka kuwa imefutika sura ya swala au laa swala yake inasihi.
YA KUMI 813. Kumi katika vinavyobatilisha swala ni kula na kunywa, akila au kunywa katika swala kiasi kwamba haisemekani kuwa anaswali swala yake inabatilika kwa kukusudia au kwa kusahau. 814. Anayetaka kufunga ikiwa anajishughulisha na swala ya witiri kabla ya adhana ya alfajiri na akawa na kiu na akahofia kuingia Al fajiri kama atakamilisha swala ya witiri na atabanwa na kiu inaruhusiwa anywe maji katika swala kama maji yatakuwa mbele yake au karibu kwa hatua chache na ajihadhari na vinavyobatilisha swala kama vile kukipa kibla mgongo na mengineyo.
156
Al-Masailul Islamiyah 815. Akimeza mabaki ya chakula yaliyokuwepo katika meno au mdomoni haibatiliki swala. Ikibaki sukari na yanayofanana na sukari mdomoni kisha yakayeyuka katika swala kidogo kidogo na kuingia tumboni pia swala haibatiliki
YA KUMI NA MOJA 816. Cha kumi na moja katika vinavyobatilisha swala ni kutilia shaka katika swala za rakaa mbili, tatu au katika rakaa mbili za awali katika swala za rakaa mbili
YA KUMI NA MBILI 817. Cha kumi na mbili katika vinavyobatilisha swala ni kupunguza au kuongeza nguzo miongoni mwa nguzo za swala na pia kuongeza au kupunguza kwa kukusudia visivyokuwa nguzo lakini ziada ya takbiratul ihram kwa kusahau haibatilishi swala. 818. Akitilia mashaka baada ya kumaliza swala kuwa ameleta kinachobatilisha swala au laa swala yake inasihi.
YALIYO MAKURUHU KATIKA SWALA 819. Ni makuruhu kugeuza uso wake kulia na kushoto au kufumba macho au kugeuza macho kulia na kushoto au kuchezea ndevu au mikono au kuliza (kubinya au kuvunja) vidole au kutema mate au kuangalia hati ya Qur’an au kitabu au maandishi ya pete katika swala, vile vile kunyamaza katikati ya kusoma Al – hamdu au sura nyingine au kunyamza kwa ajili ya kusikiliza maneno ya mtu, bali ni makuruhu kuleta chochote kinachotoa unyenyekevu na umakini unaotakiwa katika swala.
157
Al-Masailul Islamiyah 820. Ni makuruhu kuswali wakati umebanwa na usingizi au mkojo au haja kubwa na pia kuvaa soksi zinazobana miguu katika swala.
SEHEMU AMBAZO NI WAJIBU KUKATA SWALA 821. Haijuzu kukata swala kwa hiyari, lakini hakuna kizuizi kukata swala kwa ajili ya kuhifadhi mali au kuondoa madhara ya kimali na kimwili. 822. Kama haiwezekani kwa mwenye kuswali kuhifadhi nafsi yake au kuhifadhi ambao anawajibika kuwahifadhi, au kuhifadhi mali ambayo ni wajibu kuihifadhi bila ya kukata swala, na pia ni makuruhu kukata swala kwa kuhifadhi mali isiyokuwa na muhimu. 823. Akijishughulisha na swala katika muda mpana kisha akadaiwa na anayemdai, ikiwezekana kulipa deni bila ya kukata swala alipe hali ya kuwa katika swala, na kama haitawezekana kulipa deni bila ya kukata swala, basi ni wajibu akate swala ili alipe deni, na kama hatakata swala, swala yake itasihi japo kuwa atakuwa ameasi, kwa kutokulipa deni. 824. Akifahamu katikati ya swala kunajisika msikiti, kama wakati wa swala ni mfinyu ni wajibu akamilishe swala, na kama wakati ni mpana ikiwezekana kutoharisha msikiti italazimu kuvunja swala, na ikiwezekana kutoharisha msikiti baada ya swala basi haitaruhusiwa kukata swala, na ikiwa kubakia najisi msikitini kunasabisha udhalili kwa msikiti katika sura hii ni wajibu kukata swala ili atoharishe msikiti, kisha aswali na pia ni wajibu kukata swala kama haitawezekana kutoharisha msikiti baada ya swala.
158
Al-Masailul Islamiyah 825. Mwenye kuwajibikiwa kukata swala kisha akaacha kukata na akakamilisha atakuwa ameasi japokuwa swala yake itasihi. 826. Akikumbuka kabla ya kuinama kwa kiasi cha rukuu kuwa amesahau adhana na iqama kama wakati utamruhusu ni sunna akate swala kwa ajili ya kuleta adhana na iqama.
SHAKA 827. Shaka za swala zimegawanyika katika mafungu 23 nane kati ya hizo zinabatilisha swala na sita ni wajibu zisizingatiwe na tisa hazibatilishi swala. 828. Shaka zinazobatilisha swala ni kama zifuatazo:Shaka ya idadi ya rakaa katika swala za rakaa mbili kama swala ya asubuhi au swala ya msafiri lakini akitilia shaka katika idadi ya rakaa katika swala za sunna zenye rakaa mbili na swala ya ihtiyati swala haibatiliki kwa sababu yake. Shaka katika idadi ya rakaa katika swala yenye rakaa 3 Akishuku katika swala ya rakaa nne kuwa ameswali rakaa moja au zaidi Akishuku katika swala ya rakaa nne kabla ya kukamilisha sijida ya pili kuwa ameswali rakaa mbili au zaidi. Shaka baina ya rakaa mbili au tano au rakaa mbili au zaidi ya tano. Shaka baina ya tatu na sita au tatu na zaidi ya sita . Shaka katika idadi ya rakaa kiasi kwamba hajui rakaa ngapi ameswali. Shaka baina ya rakaa nne na sita au baina ya rakaa nne na zaidi ya sita kabla ya kukamilisha sijida ya pili lakini kama akishuku baada ya sijida 159
Al-Masailul Islamiyah ya pili baina ya nne na sita au baina ya nne na zaidi ya sita kwa tahadhari ajengee kuwa ameswali rakaa nne kisha akamilishe swala, baada ya hapo alete sijida mbili za kusahau baada ya swala na pia arudie swala. 829. Mwenye kuswali akitokewa na moja ya shaka zinazobatilisha swala inaruhusiwa kukata swala au afikirie mpaka sura ya swala ifutike na akate tamaa ya kupata uhakika wa rakaa alizoziswali.
SHAKA ZISIZOTILIWA MAANANI 830. Shaka ambazo ni wajibu zisizingatiwe na wala zisitiliwe maanani ni kama zifuatazo:Shaka ya kitu baada ya kupita sehemu yake mfano apate shaka katika rukuu kuwa amesoma Al – hamdu au laa. Shaka baada ya salamu Shaka baada ya kupita muda wa swala Mwingi wa shaka Shaka ya Imam katika idadi ya rakaa wakikumbuka maamuma katika idadi ya rakaa, na vile vile shaka ya maamuma kama Imam akikumbuka idadi ya rakaa. Shaka katika swala za sunna.
1 – SHAKA YA KITU BAADA YA KUPITA SEHEMU YAKE 831. Akishuku katikati ya swala kuwa ameleta baadhi ya vitu vilivyokuwa ni wajibu au hakuvileta mfano – akitilia shaka kuwa amesoma Al – hamdu au laa, kama hajajishughulisha na yanayokuja 160
Al-Masailul Islamiyah baada ya Al hamdu au baada ya alichokuwa akikishuku basi asizingatie shaka yake. 832. Akitilia shaka katikati ya kusoma aya kuwa amesoma aya iliyopita au laa au akitilia shaka katika aya anayoisoma kuwa amesoma mwanzo wa aya au laa asizingatie shaka yake. 833. Akitilia shaka baada ya kurukuu na kusujudu kuwa ameleta baadhi ya mambo ya wajibu katika swala kama vile dhikri, utulivu wa mwili au laa, asizingatie shaka yake. 834. Akitilia shaka wakati anakwenda katika sijida kuwa ameleta rukuu au laa au alisimama wima baada ya rukuu au laa asizingatie shaka yake. 835. Akitilia shaka katika hali ya kunyanyuka kuwa ameleta sijida au tashahudi au laa, asizingatie shaka yake. 836. Mwenye kuswali kwa kukaa au kulala akitilia shaka katikati ya kusoma Al- hamdu au tasbihi nne kuwa ameleta tashahudi au sijida au laa ni wajibu asizingatie shaka yake. 837. Kama akishuka katika kuleta sijida au tashahudi kabla ya kusoma Al – hamdu au tasbihi, lazima alete alicho kitilia shaka. 838. Akishuku katika kutekeleza moja ya nguzo za swala kama atakuwa ameshapita hiyo sehemu aliyoishuku basi asizingatie shaka yake, kinyume na hapo kama alichotilia shaka atakumbuka baadae kuwa alishaleta nguzo ya swala, basi swala yake itabatilika kwa kuongeza nguzo ya ziada. 839. Akishuku katika kutekeleza kitu kisichokuwa ni nguzo kama atakuwa amepita hiyo sehemu asizingatie hiyo shaka la sivyo ataleta alichoki161
Al-Masailul Islamiyah tilia shaka, akikumbuka baada ya kuisoma kuwa alishaisoma kabla ya hapo swala yake inasihi, kwa kutozidisha nguzo, na ataleta sijida mbili za kusahau kwa tahadhari ya wajibu. 840. Akishuku katika kuleta moja ya nguzo za swala, kama amejishughulisha na ambacho kinafuata baada ya nguzo hiyo asizingatie shaka yake mfano akitilia shaka katikati ya tashahudu kuwa ameleta sijida mbili au laa, asizingatie shaka yake, ama akikumbuka kuwa hakuleta hiyo nguzo aliyoisahahu na kama atajishughulisha na nguzo nyingine swala yake itakuwa imebatilika mfano akikumbuka kabla ya kurukuu katika rakaa ifuatayo kuwa hajaleta sijida mbili katika rakaa iliyopita basi alete hizo sijida mbili, na kama atakumbuka katikati ya rukuu au baada ya rukuu swala yake inabatilika. 841. Akitilia shaka katika kutekeleza jambo ambalo si nguzo katika matendo ya swala, na akajishughulisha na kitendo kifuatacho baada ya hicho ni wajibu asizingatie shaka yake kwa mfano akitilia shaka katika kusoma sura kuwa amesoma Al – hamdu au laa, ni wajibu asizingatie shaka yake ama akikumbuka kuwa hakuleta kile kitendo kabisa kama hajajishughulisha na kitendo ambacho ni nguzo ni wajibu alete kitendo hicho alichokisahau, na kama atajishughulisha na nguzo swala yake inasihi, kwa hiyo akikumbuka akiwa katika kunuti kuwa hakusoma Al – hamduu ni wajibu asome Al – hamdu na akikumbuka katika hali ya rukuu swala yake inasihi. 842. Akishuku kuwa ametoa salamu ya swala au laa, au akishuku kuwa ameileta kwa usahihi au laa, kama shaka hizo mbili ni baada ya kujishughulisha na nyuradi zinazofuatia baada swala kama vile dua au kuanza swala nyingine, au baada ya kuleta kinachovunja swala na kutoka katika hali ya mwenye kuswali au akawa anajiona kuwa hali yake iko nje ya swala, basi asizingatie shaka yake ama shaka yake ikiwa kabla ya vitu hivi ni wajibu atoe salamu upya.
162
Al-Masailul Islamiyah
2 SHAKA BAADA YA SALAMU 843. Akishuku baada ya salamu kuwa swala yake imesihi au laa, mfano akitilia shaka kuwa amerukuu baada ya salamu, au akashuku baada ya salamu katika swala ya rakaa nne kuwa ameswali rakaa nne au tano asizingatie shaka yake, lakini ikiwa pande mbili hizi za shaka zinabatilisha swala mfano akishuku baada ya salamu katika swala ya rakaa nne kuwa ameswali rakaa mbili au tano swala yake inabatilika.
3. SHAKA BAADA YA KUPITA WAKATI 844. Akishuku baada ya kupita muda kuwa ameswali au laa, akidhani kuwa hakuswali kabisa, haimlazimu kuswali lakini akitilia shaka kabla ya wakati kwisha kuwa ameswali au laa au akidhani kuwa hakuswali kabisa ni wajibu aswali hata akidhani kuwa ameswali. 845. Akishuku baada ya kupita wakati kuwa ameswali kwa usahihi au laa asizingatie shaka yake. 846. Akitambua baada ya kupita wakati wa adhuhuri na alasiri kuwa ameswali rakaa nne tu, na hatambui kuwa ameziswali kwa nia gani ya adhuhuri au alasiri ni wajibu aswali rakaa nne zingine za kadha kwa nia ya yanayomuwajibikia. 847. Akitambua baada ya kupita wakati wa swala ya Magharibi na Isha kuwa ameswali moja wapo kati ya swala hizi na hajui ameswali rakaa tatu au nne ni wajibu alipe kadha ya Magharibi na Isha pamoja.
4- MWINGI WA SHAKA 848. Mtu akishuku mara tatu katika swala moja au akishuku katika swala tatu zinazofuatana kwa mfano asubuhi, adhuhuri na alasiri atahesabi163
Al-Masailul Islamiyah ka kuwa ni mwingi wa shaka kwa hiyo haimlazimu kuzingatia shaka yake kama wingi wa shaka zake unasababishwa na hasira, woga au fikra nyingi. 849. Mwingi wa shaka akishuku katika kutekeleza jambo ikiwa jambo hilo halibatilishi swala atajengea kuwa ametekeleza, mfano akishuku kuwa amerukuu au laa atajengea kuwa amerukuu, na kama ikiwa kutekeleza hilo jambo linabatilisha swala basi inabidi ajengee kuwa hajafanya, mfano akishuku kuwa ameleta rukuu moja au zaidi ya moja,anajengea kuwa hajaleta zaidi ya moja kwa sababu ziada ya rukuu inabatilisha swala. 850. Mwingi wa shaka akishuku katika sehemu moja tu katika swala, akishuku katika sehemu nyingine nje ya ile inatakiwa afanye kama afanyavyo mwingi wa shaka, mfano akiwa mwingi wa shaka katika sijida, kuwa amesujudu au laa, na akatilia shaka katika rukuu lazima afanye kama anavyofanya mwingi wa shaka yaani atarukuu kama alikuwa amesimama na hatazingatia shaka yake kama itakuwa baada ya kwenda sijida. 851. Mwingi wa shaka akishuku katika swala maalumu pasina zingine mfano akiwa anakithirisha shaka katika swala ya adhuhuri pasina zingine na akishuku kwenye swala zingine kama swala ya alasiri kwa mfano mwisho wa swala atafanya kama anavyofanya mwenye shaka ya kawaida. 852. Mwingi wa shaka akishuku katika swala katika sehemu maalumu pasina sehemu nyingine kama vile sehemu yenye makelele akiswali sehemu nyingine ikamtokea shaka ni wajibu afanye kama afanyavyo mwenye shaka ya kawaida. 853. Mwenye kushuku kwa sababu ni mwingi wa shaka ni wajibu afanye kama afanyavyo mwenye shaka ya kawaida na mwingi wa shaka 164
Al-Masailul Islamiyah asizingatie shaka yake maadamu hana uhakika wa kurudi katika hali ya watu wa kawaida 954. Mwenye kushuku katika nguzo miongoni mwa nguzo za swala kisha akawa hajazingatia shaka yake, kisha akakumbuka kuwa hakuileta ile nguzo kama hajajishughulisha na nguzo nyingine ni wajibu alete nguzo aliyoisahau, na ikiwa ameanza kujishughulisha na nguzo nyingine swala itakuwa imebatilika, mfano akishuku kuwa amerukuu au laa, akawa hajazingatia shaka yake, akikumbuka kabla ya sijida kuwa haja rukuu, ni wajibu alete rukuu aliyoisahau ama akikumbuka katika sijida ya pili swala yake inabatilika. 855. Mwingi wa shaka akishuku katika kuleta kisichokuwa nguzo na akawa hajazingatia shaka yake, akikumbuka kuwa hajaleta kabisa kile alichokuwa anakishuku, kama atakuwa hajapita hiyo sehemu lazima akilete na kama atakuwa amepita hiyo sehemu swala yake inasihi, mfano akishuku kuwa amesoma Al- hamdu au laa kisha akawa hajazingatia shaka yake akikumbuka katika kunuti kuwa hajasoma Al – hamdu ni wajibu asome Al – hamdu na akikumbuka katika rukuu swala yake inasihi.
5- SHAKA YA IMAMU NA MAAMUMA 856. Imamu akishuku katika swala ya jamaa katika idadi ya rakaa mfano akishuku kuwa ameswali rakaa tatu au nne, ikiwa maamuma wanauhakika kuwa ameswali rakaa nne na wakamfahamisha Imamu kuwa ameswali raka nne inamlazimu Imamu akamilishe swala, na haitamlazimu kuswali swala ya ihityati, vile vile Imamu akiwa na uhakika katika idadi maalumu za rakaa na maamuma akishuku katika idadi ya rakaa ni lazima kwa maamuma asizingatie shaka yake.
6- SHAKA KATIKA SWALA YA SUNNA 857. Akishuku katika swala za sunna, ikiwa upande wa wingi wa shaka 165
Al-Masailul Islamiyah unabatilisha swala atajengea katika uchache mfano ikimtokea shaka katika sunna ya asubuhi kuwa ameswali rakaa mbili au tatu itamlazimu ajengee kuwa ameswali rakaa mbili na ikiwa upande wa wingi wa shaka haubatilishi swala, mfano akishuku kuwa ameswali rakaa mbili au moja atafanya njia yoyote anayotaka yaani anaweza kujengea kuwa ameswali rakaa mbili na kukamilisha swala au kujengaea kuwa ameswali rakaa moja na kumalizia rakaa ya pili na swala inasihi. 858. Upungufu wa nguzo unabatilisha swala ya sunna lakini ziada yake haibatilishi swala, akisahau moja ya vitendo vya swala ya sunna na hakukumbuka ila baada ya kuingia katika nguzo, atakuwa na haki ya kuleta alichokisahau na kurudia ile nguzo mara nyingine mfano akikumbuka katika rukuu kuwa hakusoma Al- hamdu na akawa amesimama wima basi utambidi asome Al- hamdu na kurukuu mara ya pili. 859. Akishuku katika kuleta moja ya matendo ya swala ya sunna iwe ni katika nguzo au isiyokuwa nguzo itatakiwa alete alichokishuku, maadamu hajapita sehemu yake na asizingatie shaka yake kama atakuwa amepita hiyo sehemu. 860. Akidhani katika sunna ya rakaa mbili kuwa ameleta rakaa tatu au zaidi ya tatu asizingatie dhana yake na swala itasihi na kama atadhani kuwa ameleta rakaa mbili au chini ya mbili kwa tahadhari ya sunna atafanya kutokana na dhana yake mfano akidhani kuwa ameswali rakaa moja basi atakamilisha swala yake kwa kumalizia rakaa ya pili. 861. Akifanya katika swala ya sunna ambayo yanasababisha sijida ya kusahahu au akisahau sijida au tashahudu, haitamlazimu baada ya swala alete sijida sahau au kuleta kadha ya sijida iliyosahaulika au tashahudi iliyosahaulika, na ingawa kwa tahadhari alete alichokisahahu baada ya swala.
166
Al-Masailul Islamiyah 862. Akishuku kuwa ameswali swala ya sunna au laa kama swala hiyo haitakuwa ya muda maalum kama swala ya “Jafari Twayaar� atajengea kuwa hajaswali na vile vile atajengea kuwa hajaswali akitia shaka katika swala za sunna za kila siku ambazo zinakuwa na muda maalumu na ikiwa shaka yake ni kabla ya kupita muda na kama akitilia shaka baada ya muda kupita basi hatazingatia shaka yake.
7. SHAKA ZISIZOBATILISHA SWALA 863. Ni wajibu kwa mwenye kuswali kutafakari haraka akishuku katika idadi ya rakaa katika swala za rakaa nne na hiyo ni katika sura tisa, na kama fikra yake itampelekea kupata yakini au dhana katika moja ya pande mbili basi itabidi achukue ambayo inampelekea kupata yakini au dhana yake katika upande huo na kukamilisha swala, na kama mawazo yake na fikira zake hazitampa jawabu maalum basi atafanya kutokana na kanuni ambazo ufafanuzi wake utakuja baadae
SURA YA KWANZA 864. Akishuku baada ya kunyanyua kichwa katika sijida ya pili kuwa ameswali rakaa mbili au tatu katika sura hii ni wajibu ajengee kuwa ameswali rakaa tatu, atasimama na kuleta rakaa nyingine na kukamilisha swala kisha ataleta baada ya swala rakaa moja ya swala ya ihtiyati kwa kusimama na rakaa mbili kwa kukaa vilevile kama utakavyokuja ufafanuzi wake baadaye
SURA YA PILI 865. Akishuku kati ya rakaa mbili au nne baada ya kunyanyua kichwa katika sijida ya pili hapo ni wajibu ajengee kuwa ameswali rakaa nne na kukamilisha swala akiwa amekaa kisha ataleta rakaa mbili za swala ya ihtiyati baada ya swala kwa kusimama kwa tahadhari 167
Al-Masailul Islamiyah
SURA YA TATU 866. Akishuku kati ya rakaa mbili, tatu na nne baada ya sijida ya pili yaani hajui kuwa ameswali rakaa mbili, tatu au nne katika hali hii atajengea kuwa ameswali rakaa nne na atakamilisha swala hali ya kuwa amekaa kisha ataleta rakaa mbili za swala za ihtiyati kwa kusimama na rakaa mbili kwa kukaa pia.
SURA YA NNE 867. Akishuku kati ya rakaa nne na tano baada ya kunyanyua kichwa katika sijida ya pili, atajengea kuwa ameswali rakaa nne na kukamilisha swala hali ya kuwa amekaa na ataleta sijida mbili za kusahau baada ya swala. 868. Ikitokea moja ya shaka hizi nne baada ya kuleta dhikri katika sijida ya pili kabla ya kunyanyua kichwa katika sijida ya pili, basi atafanya kutokana na hukumu za shaka zilizotajwa na atarudia swala kwa tahadhari ya sunna na kama atarudia swala tu inatosha.
SURA YA TANO 869. Akishuku kati ya rakaa tatu na nne katika sehemu yeyote ya swala, lazima ajengee kuwa ameswali rakaa nne na akamilishe swala, kisha alete rakaa moja ya ihtiyati kwa kusimama au rakaa mbili kwa kukaa kwa tahadhari
SURA YA SITA 870. Akishuku kati ya rakaa nne na tano akiwa katika hali ya kusimama, lazima akae na atoe tashahudi na salamu na kukamilisha swala, kisha ataleta rakaa moja ya ihtiyati kwa kusimama au mbili kwa kukaa na kwa tahadhari ya wajibu alete sijida mbili za kusahau kwa ajili ya kisimamo cha ziada. 168
Al-Masailul Islamiyah
SURA YA SABA 871. Akishuku kati ya rakaa tatu au tano katika hali ya kusimama itamlazimu akae na atoe tashahudi na salamu na kukamilisha swala kisha alete rakaa mbili za ihtiyati kwa kusimama kwa tahadhari na kuleta sijida mbili za kusahau kwa ajili ya kisimamo cha ziada kwa tahadhari ya wajibu.
SURA YA NANE 872. Akishuku kati ya rakaa tatu, nne na tano katika hali ya kisimamo itamlazimu akae na atoe tashahudi na salamu na ataleta baada ya salamu sijida mbili za kusahau na kwa tahadhari ya wajibu alete sijida zingine za kusahau kwa ajili ya kisimamo cha ziada.
SURA YA TISA 873. Akishuku kati ya rakaa tano na sita katika hali ya kisimamo itamlazimu akae na alete tashahudi na salamu na ataleta baada ya salamu sijida mbili za kusahau na kwa tahadhari ya wajibu alete sijida zingine mbili za kusahau kwa ajili ya kisimamo cha ziada
MAS’ALA MENGINE 874. Mwenye kuswali ikimtokea shaka isiyobatilisha swala itamlazimu asikate swala kwa tahadhari, ama akianza swala nyingine baada ya kuvunja ya mwanzo basi swala yake ya pili itasihi. 875. Ikimtokea moja ya shaka zinazosababisha swala ya ihtiyati, akikamilisha swala yake na akianza swala nyingine bila ya kuleta 169
Al-Masailul Islamiyah swala ya ihtiyati na akawa ameanza swala mpya kabla ya kuleta kinachobatilisha swala, kama kugeuza uso pembeni mwa kibla, swala yake ya pili itabatilika pia kwa tahadhari, ama akijishughulisha na swala ya pili baada ya kuleta kinachobatilisha swala ya kwanza swala ya pili itasihi. 876. Inapomtokea mwenye kuswali moja ya shaka zisizobatilisha swala ni wajibu atulie na kufikiria kwa haraka kama ilivyotangulia, lakini akitambua kuwa hatasahau kitu kwa kuchelewa kidogo inajuzu kwake kufikiri kidogo baadae, mfano akishuku naye yuko katika sijida inajuzu kuahirisha kufikiria hadi baada ya sijida. 877. Dhana yake ikielemea moja kati ya pande mbili za shaka katika jambo moja, kisha dhana yake ikalingana katika pande zote mbili kwa mtazamo wake, ni wajibu afanye kulingana na hukumu za shaka na pande zote mbili zikilingana kwa mtizamo wake tangu mwanzo basi atajengea kutokana na kuelemea kwa moja ya dhana yake, na ni wajibu afanye kilichowajibu kwake, lakini dhana yake ikielemea moja ya pande mbili ni wajibu achukue upande ambao swala yake itasihi na kukamilisha swala. 878. Ambaye hajui kuwa dhana yake imeelemea upande mmoja au pande zote mbili, ni wajibu afanye kulingana na hukumu za shaka. 879. Akishuku katika tashahudi au baada ya kunyanyuka kuwa ameleta sijida mbili au laa, kisha ikamtokea hapo hapo shaka isiyobatilisha swala, ikitokea baada ya kukamilisha sijida mbili, mfano akishuku kuwa ameswali rakaa mbili au tatu atafanya kulingana na wadhifa tulioutaja na swala yake itasihi. 880. Akishuku katika hali ya kusimama kati ya rakaa tatu na nne au baina ya rakaa tatu, nne na tano, na akakumbuka kuwa hajaleta sijida mbili katika rakaa iliyopita swala yake inabatilika.
170
Al-Masailul Islamiyah 881. Ikiondoka shaka yake kisha ikamtokea shaka nyingine, mfano mwanzo alishuku kati ya rakaa mbili na tatu kisha akashuku mara ya pili baina ya tatu na nne, atafanya kulingana na shaka yake ya pili. 882. Akishuku baada ya swala kuwa ameshuku kati ya rakaa mbili au nne au kati ya tatu na nne ni wajibu afanye kwa shaka zote mbili. 883. Mwenye kuswali kwa kukaa akiweza kusimama katika kuleta swala ya ihtiyati ni wajibu ailete kwa kusimama.
SWALA YA IHTIYATI 884. Ambaye amewajibikiwa na swala ya ihtiyati ni wajibu anuie kwa haraka baada ya kumaliza swala, atahirimia na kusoma Al – hamdu tu atarukuu na kuleta sijida mbili na akiwa katika wale waliowajibikiwa na rakaa moja ya ihtiyati ataleta tashahudi baada ya sijida mbili na kutoa salamu, ama aliyewajibikiwa na rakaa mbili za ihtiyati atasimama baada ya sijida mbili na kuswali rakaa ya pili, kisha ataleta tashahud na kutoa salamu. 885. Katika swala ya ihtiyati hakuna sura wala kunut na lazima asidhihirishe sauti wakati wa kusoam Al- hamdu wala asidhihirishe nia yake na kwa tahadhari asidhihirishe hata bismillah pia. 886. Akitambua kabla ya swala ya ihtiyati kuwa swala yake ilikuwa sahihi haimlazimu kuleta swala ya ihtiyati na akitambua hivyo katikati ya swala ya ihtiyati haimlazimu kuikamilisha, bali inajuzu kuikatisha popote alipo. 887. Akishuku kati ya rakaa mbili, tatu na nne katika hali ya kuleta rakaa mbili za ihtiyati katika hali ya kusimama kabla ya kurukuu katika rakaa ya pili kwamba swala yake ilikuwa ni rakaa tatu lazima akae na kukamilisha swala ya ihtiyati rakaa moja.
171
Al-Masailul Islamiyah 888. Akishuku kuwa ameleta swala ya ihtiyati ambayo alitakiwa aswali au laa, ikiwa ni baada ya wakati hatazingatia shaka yake, na kama wakati bado upo na hakujishughulisha na kitu kingine na hajasimama sehemu aliyokuwa anaswalia, na hakuleta kinachobatilisha swala itamlazimu alete swala ya ihtiyat,i na kama ameleta kinachobatilisha au ametenganisha kati ya swala aliyoiswali na shaka hiyo muda mrefu hatazingatia shaka yake. 889. Akizidisha nguzo katika swala ya ihtiyati au akileta rakaa mbili badala ya rakaa moja, swala yake ya ihtiyati inabatilika na ni wajibu kurudia swala upya. 890. Hukumu ya dhana katika idadi ya rakaa ni hukumu ya yakini, ila dhana ikiwa ni ya kitu kinachosababisha kubatilisha swala katika hali hii, dhana haitakuwa na hukumu ya yakini, ama dhana katika vitendo vya swala ingawa haiko mbali na kuiunganisha na yakini, lakini pamoja na hivyo inalazimu kwa tahadhari ya sunna baada ya kuizingatia dhana akamilishe amali na arudie swala 891. Hakuna tofauti katika hukumu ya shaka, kusahau na kudhani katika swala za kila siku na swala zingine za wajibu, mfano akishuku katika swala za majanga kuwa ameleta rakaa moja au mbili, kwa kuwa swala ya majanga ina rakaa mbili hivyo shaka hiyo inabatilisha swala.
SIJIDA YA KUSAHAU 892. Ni wajibu kuleta sijida mbili za kusahau baada ya salamu kwa namna ambayo ufafanuzi wake utakuja na hii ni kwa mambo matano:(i) Akizungumza katikati ya swala kwa kujisahau (ii) Akitoa salamu sehemu isiyokuwa ya salamu, mfano akitoa salamu katika rakaa ya kwanza kwa kujisahau (iii) Akisahau moja ya sijida mbili (iv) Akisahau tashahudi 172
Al-Masailul Islamiyah (v) Akishuku baada ya sijida mbili katika swala ya rakaa nne kuwa ameswali rakaa nne au tano. 893. Akikaa kwa kujisahau katika mahali pa kusimama, mfano akikaa katika hali ya kusoma Al-hamdu na sura kwa kukosea, au akasimama katika mahali pa kukaa kama akisimama katika mahali pa tashahudi kwa kujisahahu, itamlazimu kwa tahadhari ya wajibu alete sijida mbili za kusahau, na kwa tahadhari ya wajibu alete sijida mbili za kusahau katika kila ziada au upungufu. Na hukumu za hali hizi zitatajwa katika mas’ala yajayo. 894. Mwenye kuswali akizungumza kwa kujisahau au akadhani kuwa swala yake imekamilika, ni wajibu alete sijida mbili za kusahau. 895. Si wajibu kusujudu sijida ya kusahu kwa kutamka herufi ambayo imesababishwa na kukohoa, kucheua na mengineyo, lakini akisema Ah, au Akh, kwa kusahau ni wajibu alete sijida mbili za kusahau. 896. Mwenye kurudia kusoma vizuri kwa kukosea mara ya kwanza, haitamlazimu alete sijida ya kusahau kwa kukosea. 897. Akizungumza muda mrefu katika swala kwa kujisahau yatahesabika maneno yake hayo kuwa ni neno moja inatosha alete sijida ya kusahau baada ya swala. 898. Mwenye kuleta tasbihi nne zaidi ya mara tatu kwa kujisahau haitamlazimu alete sijida ya kusahau. 899. Akileta salamu nje ya sehemu ya salamu, mfano alete salamu tatu zisizotajwa, inatosha alete sijida mbili za kusahau mara moja tu. 900. Asipoleta sijida mbili za kusahau baada ya salamu kwa kukusudia 173
Al-Masailul Islamiyah atakuwa ameasi na atawajibika alete kwa haraka, na kama hataleta ni lazima azilete wakati wowote atakapokumbuka na si lazima arudie swala. 901. Akishuku kuwa imewajibika kwake sijida mbili za kusahau au laa, haitamlazimu alete chochote. 902. Akitambua kuwa hakuleta moja ya sijida mbili za kusahau, itamlazimu alete sijida zingine mbili za kusahau.
NAMNA YA KULETA SIJIDA YA KUSAHAU 903. Namna ya kusujudu sijida ya kusahau: Baada ya salamu anuie nia ya sijida ya kusahau na kuweka paji la uso juu ya kinachosihi kusujudu juu yake na kusema “Bismillah wa billah wa swala llahu alaa Muhamadi wa aali Muhammad” au aseme “Bismillah wa billah allahuma swali alaa muhamadi wa aali Muhamadi”. Na ni bora aseme “Bismillah wabillah asalamu alayka ayuh nabiyu warahmatu llah wabakatuh” Kisha anakaa kisha anasujudu tena na kusoma moja ya dhikri hapo juu, atakaa na kuleta tashahudi na kutoa salamu moja.
KADHA YA SIJIDA AU TASHAHUDI ZILIZOSAHAULIKA 904. Ni sharti katika kadha ya sijida au tashahudi zilizosahaulika mambo yote yanayoshurutishwa katika swala kama vile, tohara ya mwili na mavazi na masharti mengineyo. 905. Akisahau sijida mara nyingi, mfano akisahau sijida katika rakaa ya kwanza na sijida katika rakaa ya pili ni wajibu azilipe baada ya swala 174
Al-Masailul Islamiyah ya pamoja na kuleta sijida mbili za kusahau kwa kila moja na hailazimu kuainisha, ama akisahau sijida katika rakaa ya kwanza na ya mwisho au akasahau tashahudi mbili, kwa tahadhari ya wajibu alete sijida ya mwisho aliyoisahau kwanza, kisha analeta tashahudi na salamu na baada ya hapo atalipa sijida ya kwanza, na vivyo hivyo itamlazimu alete tashahudi iliyosahaulika mwisho na kutoa salamu, kisha atalipa tashahudi ya kwanza, haya yote ni katika hali ya kutoleta kinachobatilisha swala kwa kukusudia au kusahau, ama akileta kinachobatilisha swala kwa kukusudia au kusahau ni lazima arudie swala. 906. Asipotambua kuwa amesahau tashahudi au sijida atawajibika kulipa zote mbili pamoja, na hakuna tatizo kutanguliza moja kati ya hizi mbili. 907. Akishuku kuwa amesahau tashahudi au sijida au laa, hatawajibika kulipa kadha. 908. Akishuku kuwa baada ya swala alileta sijida au tashahudi zilizosahaulika au laa, ikiwa wakati bado upo itabidi arudie kulipa, na kama wakati wa swala umeisha hatawajibika kuzilipa.
UPUNGUFU NA ZIADA KATIKA SEHEMU ZA SWALA NA MASHARTI YAKE 909. Akizidisha au kupunguza katika wajibati za swala kwa kukusudia swala yake inabatilika. 910. Akitambua katikati ya swala kuwa josho lake au udhu wake ulikuwa batili au alijishughulisha na swala bila ya udhu au josho, swala yake inabatilika, atairudia kwa udhu au josho, na akitambua baada ya swala ni wajibu airudie kwa udhu au josho ikiwa wakati bado upo, na kama 175
Al-Masailul Islamiyah wakati umekwisha ni lazima alipe kadha. 911. Akikumbuka kabla ya salamu kuwa amesahau rakaa katika mwisho wa swala ni wajibu alete hiyo rakaa kwa haraka. 912. Akikumbuka baada ya salamu kuwa amesahau rakaa au zaidi ya rakaa, akifanya kinachobatilisha swala kwa kusahau au kukusudia, mfano kukipa kibla mgongo, swala yake inabatilika, na kama hajafanya kinachobatilisha swala ni wajibu alete kwa haraka alichokisahau. 913. Akitambua kuwa ameswali kabla ya wakati au ameswali kwa kukipa mgongo kibla au kuelekea kulia au kushoto mwa kibla ni wajibu arudie swala ndani ya wakati na kuilipa kama wakati umeisha
SWALA YA MSAFIRI 914. Ni wajibu kwa msafiri kupunguza katika swala za rakaa nne yaani “Adhuhuri, Alasiri na Isha� na ataswali rakaa mbili badala ya rakaa nne na hiyo ni pindi yakipatikana masharti nane yafuatayo:1. Masafa ya safari yawe ni farsakha nane ( kilometa 45) 2. Akusudie tangu mwanzo wa safari kukata farsakha nane 3. Asibadili nia yake 4. Asipitie katika mji wake, na asikusudie kukaa siku kumi 5. Asisafiri kwa ajili ya mambo ya haramu. 6. Asiwe ni katika watu wanaohamahama ambao hawatulii sehemu moja. 7. Safari isiwe ndio kazi yake 8. Afike kwenye sehemu anayoruhusiwa kisheria kupunguza.
SHARTI LA KWANZA 176
Al-Masailul Islamiyah 915. Inatakiwa masafa anayosafiri yasipungue farsakha nane za kisheria na farsakha moja ni sawa na kilometa tano na nusu takribani. 916. Mwenye kufikisha jumla ya masafa yake kwenda na kurudi farsakha nane, akisafiri na kurudi siku hiyo hiyo, mfano akisafiri mchana akarudi usiku wake, kama hayajapungua masafa ya kwenda farsakha nne ni wajibu apunguze swala zake, lakini ikiwa kwenda ni farsakha tatu na kurudi ni farsakha tano, dhahiri atapunguza swala zake, ingawa ni kwa tahadhari ya sunna ni kukusanya baina ya kupunguza na kukamilisha. 917. Ikiwa safari yake kwenda na kurudi ni farsakha nane, na kama safari yake haichukui siku kumi, kama akisafiri leo na akarudi kesho au baada ya kesho au chini ya siku kumi ni wajibu apunguze swala zake na asifunge bali atalipa kadha kama yuko katika mwezi wa Ramadhani. 918. Ikiwa masafa hayajafika farsakha nane au msafiri hakujua kuwa safari yake inafika farsakha nane au haifiki hatapunguza swala zake. Ama akishuku safari yake imefikia farsakha nane au haikufika, ni wajibu wake afanye uchunguzi ili apate uhakika, na akipata habari kutoka kwa waadilifu wawili au mmoja au inajulikana baina ya watu kiasi cha kupata matumaini kuwa safari yake imefikisha farsakha nane basi atapunguza swala zake. 919. Mwenye kupata uhakika kuwa safari yake imefika farsakha nane kisha akapunguza swala zake, baada ya hapo akatambua kuwa safari yake haikufikia farsakha nane, itamuwajibikia arudie swala za rakaa nne ndani ya wakati au kadha kama wakati umepita. 920. Ikiwa safari ina njia mbili moja inafikisha farsakha nane na nyingine haifikishi farsakha nane, akisafiri kwa ile njia inayofikisha farsakha nane atapunguza swala, na kama atatumia njia ambayo haifikishi farsakha nane atakamilisha swala zake. 177
Al-Masailul Islamiyah
921. Ikiwa mji anaoishi una ukuta mwishoni mwa mji ni lazima aanze kuhesabu masafa ya kisheria hapo, yaani farsakha nane kuanzia kwenye ukuta wa mji, na kama hauna ukuta ni wajibu aanze kuhesabu masafa ya kisheria mwisho wa nyumba za mji.
SHARTI LA PILI 922. Ni sharti akusudie kukata masafara ya farsakha nane kuanzia mwanzo wa safari, na kama atasafiri masafa ambayo hayafiki farsakha nane kisha baada ya kufika hapo akakusudia kwenda sehemu nyingine kiasi kwamba akijumlisha masafa mawili yatafikisha farsakha nane, kwa kuwa hakukusudia tangu mwanzo wa safari kukata masafa haya ni wajibu akamilishe swala yake. 923. Asiyejua kuwa safari yake itafikisha masafa kiasi gani, mfano akisafiri kwa ajili ya kutafuta kitu kilichopotea na hajui atasafiri masafa kiasi gani mpaka akipate, ni wajibu akamilishe swala zake, na kama wakati wa kurudi atasafiri farsakha nane au zaidi ni wajibu apunguze swala zake. 924. Msafiri hapunguzi swala zake mpaka aazimie mwanzo wa safari kukata masafa ya farsakha nane. Mwenye kukusudia kukata masafa ya farsakha nane kama atapata rafiki, kama atakuwa na matumaini ya kumpata rafiki ni wajibu apunguze swala zake, na kama hana matumaini ya kumpata rafiki atakamilisha swala. 925. Mwenye kukusudia kukata masafa ya farsakha nane ni wajibu aanze kupunguza anapofikia kwenye sehemu asiyoona ukuta au kusikia sauti ya adhana, na kama atasafiri kidogo sana kiasi kwamba haisadiki kuwa ni msafiri ni wajibu wake akamilishe swala na kwa tahadhari ya sunna apunguze swala 178
Al-Masailul Islamiyah
926. Ikiwa katika safari yake anamfuata mtu mfano mtumishi akisafiri kwa kumfuata bwana wake, kama atatambua kuwa safari itafikisha farsakha za kisheria atapunguza swala, na kama hatambui kwa tahadhari amuulize bwana wake.
SHARTI LA TATU 927.Ni sharti msafiri asibadilishe azima yake ya kukata masafa ya kisheria njiani, akibadilisha lengo lake kabla ya kutimiza farsakha nne au akisitasita baina ya kuendelea na safari au kurudi atawajibika kukamilisha swala. 928. Akibadili nia yake baada ya kumaliza farsakha nne ikiwa aliazimia kukaa huko au kurudi baada ya siku kumi au akawa hana mwelekeo baina ya kurudi au kubakia ni wajibu akamilishe swala. 929. Akibadili nia yake baada ya kumaliza farsakha nne na akawa ameazimia kurudi siku ile ile ni wajibu kwake kupunguza hata kama akirudi kabla ya siku kumi. 930. Mtu akitoka kwenda sehemu maalum na akawa amekata sehemu fulani ya masafa, baada ya hapo akakusudia kwenda sehemu nyingine, kama jumla ya masafa ya sehemu anayoaanzia hivi sasa kwenda sehemu ya pili aliyoikusudia mwishoni ni farsakha nane atapunguza swala zake.
SHARTI LA NNE 931. Ni sharti msafiri asipitie kwenye mji wake kabla ya kufika farsakha nane na asikae sehemu siku kumi au zaidi, kama atataka kupitia kwenye mji wake kabla ya kukamilisha masafa ya kisheria au akitaka kukaa sehemu siku kumi atakamilisha swala zake. 179
Al-Masailul Islamiyah
932. Asiye jua kuwa atapitia kwenye mji wake, au laa au atakaa zaidi ya siku kumi au laa, ni wajibu akamilishe swala zake.
SHARTI LA TANO 933. Ni sharti asisafiri kwa ajili ya maasi au kitu cha haramu, kama atasafiri kwa ajili ya haramu kama vile kuiba, ni wajibu akamilishe swala yake na vile vile atakamilisha swala kama safari yenyewe ni ya haramu mfano kama inamdhuru au safari ya mke bila idhini ya mumewe, au safari ya mtoto aliyekatazwa na wazazi wake pamoja na kupatikana maudhi kwa kuwakhalifu kwao ikiwa safari ya hawa sio ya wajibu. Lakini safari ya hija ya wajibu ni wajibu wapunguze katika swala zao. 934. Ambaye safari yake sio ya haramu au hakusafiri kwa jambo la haramu anapunguza swala zake hata akifanya maasi katika safari hiyo, mfano kusengenya au kunywa pombe. 935.
Akisafiri kwa ajili ya kuacha wajibu ni wajibu akamilishe swala zake, aliyekuwa na deni na akawa na uwezo wa kulipa deni hilo kisha akasafiri ili asilipe deni ni wajibu akamilishe swala, lakini kama hakusafiri kwa ajili ya kuacha wajibu ni wajibu apunguze katika swala zake, hata kama itaafikiana na kuacha wajibu kwa sababu hiyo au italazimu hivyo.
936. Ikiwa safari yake si ya haramu lakini chombo alichosafiria ni cha unyang’anyi au ardhi aliyotembelea juu yake ilikuwa ya unyang’anyi atapunguza swala, na kwa tahadhari ya sunna akusanye baina ya kupunguza na kukamilisha. 937. Mwenye kusafiri pamoja na dhalimu na ikiwa si lazima asafiri nae, au amesafiri kwa ajili ya kumsaidia dhalimu ni wajibu akamilishe 180
Al-Masailul Islamiyah swala. Ama kama kuna ulazima wa kusafiri nae au safari yake na dhalimu ni kwa ajili ya kuwasaidia watakao dhulumiwa atapunguza swala. 938. Ambaye amesafiri si kwa ajili ya maasi akikusudia katikati ya safari kumalizia masafa yaliyobakia kwa ajili ya maasi ni wajibu akamilishe swala zake, lakini swala zake alizoziswali kwa kupunguza kabla ya hapo zitasihi.
SHARTI LA SITA 939. Ni shartia asiwe katika watu wa kuhamahama ambao wanahamahama na wasio kuwa na makazi maalumu wanatembea na nyumba zao wanapoona maji au majani wanapiga kambi hapo na yanapokwisha huhama na kwenda sehemu nyingine hawa ni wajibu kukamilisha swala zao. 940. Akisafiri mmoja wa watu hawa kwa ajili ya kutafauta malisho ya wanyama wao hata kama safari yake ikifikia masafa ya kisheria ni wajibu wake akamilishe swala hata kama hana mifugo yake. 941. Akisafiri miongoni mwa watu wanao hama hama kwa ajili ya hija, ziara au biashara na mengineyo atapunguza swala zake.
SHARTI LA SABA 942. Ni sharti safari isiwe ni kazi yake na kama shughuli yake ni utingo, dereva au baharia na wengineo atakamilisha swala kama safari yake si ya kwanza, lakini katika safari ya kwanza atapunguza swala zake hata kama safari yake itakuwa ndefu kiasi gani. 943. Ambaye safari ni kazi yake katika baadhi ya misimu ya mwaka, kama vile dereva ambaye huendesha gari lake kiangazi au masika ni 181
Al-Masailul Islamiyah wajibu akamilishe swala katika safari. 944. Ambaye shughuli yake ni safari akibaki kwenye mji wake siku kumi au zaidi ni wajibu apunguze swala zake katika safari yake ya kwanza ambaye atasafiri baada ya kukaa siku kumi. 945. Mtalii katika miji ambayo hajaifanya kuwa ni makazi yake ni wajibu akamilishe swala. 946. Ambaye safari si kazi yake na akawa anasafiri mara nyingi katika miji au vijiji kwa ajili ya kuchukua bidhaa ni wajibu apunguze swala zake.
SHARTI LA NANE 947. Ni sharti msafiri afike katika sehemu inayoruhusiwa kupunguza, yaani awe mbali na mji kiasi kwamba haoni ukuta wa mji au hasikii adhana. 948. Akisafiri na akifika sehemu anasikia adhana, lakini haoni ukuta wa mji au anaona ukuta, lakini hasikii adhana akitaka kuswali atakamilisha swala. 949. Msafiri anayerudi kwenye mji wake ni wajibu akamilishe swala zake pindi aonapo ukuta wa mji wake au asikiapo adhana, na msafiri anayetaka kukaa sehemu siku kumi akiona kuta za sehemu hiyo au akisikia adhana yake nilazima akamilishe swala. 950. Msafiri anayerudi kwenye mji wake ni wajibu akamilishe swala zake anapoona ukuta wa mji wake au kusikia adhana, na pia msafiri ambaye anataka kukaa kwenye sehemu siku kumi ataanza kukamilisha swala anapoona ukuta au kusikia adhana ya mahali anapoenda. 182
Al-Masailul Islamiyah
951. Akisafiri katika sehemu isiyokuwa na nyumba wala ukuta akifika kwenye sehemu ambayo kwa kawaida kama kungelikuwa na nyumba au ukuta zisingeonekana nilazima apunguze swala yake. 952. Ikiwa macho, masikio na sauti ya adhana si ya kawaida ni lazima apunguze swala katika sehemu ambayo macho ya kawaida hayaoni, au masikio ya kawaida hayasikii au sauti ya adhana ya kawaida haisikiki. 953. Mwenye kwenda kwenye mji wake ni lazima akamilishe swala aonapo ukuta wa mji au kusikia adhana.
HUKUMU ZA MAKAZI NA KUKAA SIKU KUMI 954. Mwenye kuchagua mji kwa ajili ya kuishi utahesabiwa kuwa ni mji wake hata kama hajazaliwa sehemu hiyo. 955. Akikusudia kuishi kwenye mji kwa muda maalum usiokuwa mji wake kisha akahama hapo, haitahesabiwa kuwa ni mji wake ila anapotaka kubaki muda mrefu kama mwaka au zaidi, kwa wanafunzi na wanachuo wanaosafiri kwa ajili ya kusoma huo mji unakuwa ni mji wao, kwa hiyo wanalazimika kukamilisha swala na kufunga, na vivyo hivyo hukumu ya Askari ambao wanapangiwa kukaa sehemu muda mrefu. 956. Mahali ambapo amekusudia kuishi miaka minne au mitano itahesabika kuwa ni mji wake, ikitokea safari kisha akarudi kwenye huo mji atawajibika kukamilisha swala. 183
Al-Masailul Islamiyah
957. Mwenye sehemu mbili mfano akikaa sehemu moja miezi sita na sehemu nyingine miezi sita, sehemu zote mbili zitahesabika kuwa ni miji yake, na vile vile hukumu hii itakuwa kwa mwenye kuchagua miji mingi kuwa makazi yake. 958. Akifika sehemu ambayo ilikuwa ni mji wake wakati uliopita lakini alihama, hakamilishi swala hata kama bado hajapata mji mwingine. 959. Msafiri ambaye hajakusudia kuishi siku kumi lakini amenuia endapo atapata rafiki sehemu nzuri atakaa siku kumi atapunguza swala zake. 960. Msafiri akikusudia kubaki sehemu siku kumi akibadilisha kusudio lake la kubaki siku kumi kabla ya kuswali swala ya rakaa nne au akawa hana mwelekeo kati ya kubaki au kuondoka ni wajibu apunguze swala zake, na kama ataondoka hiyo sehemu au alikosa mwelekeo baada ya kuswali swala ya rakaa nne, ni lazima akamilishe swala maadamu yuko huko. 961. Msafiri akijishughulisha na swala kwa nia ya kukupunguza na katikati ya swala akaazimia kukaa siku kumi ni lazima akamilishe swala. 962. Msafiri aliyekusudia kukaa sehemu siku kumi akikaa zaidi ya siku kumi ni lazima akamilishe swala zake na haimlazimu kunuia upya kukaa siku kumi zingine. 963. Msafiri aliyekusudia kukaa sehemu siku kumi ni wajibu wake kufunga saumu za wajibu na za sunna na kuswali swala ya ijumaa. 964. Msafiri ambaye amebaki sehemu siku thelathini kwa kukosa mwelekeo kuwa ataondoka lini, ni wajibu wake akamilishe swala baada ya siku thelathini hata kama atakaa kidogo.
184
Al-Masailul Islamiyah 965. Msafiri ambaye hana mwelekeo kwa muda wa siku thelathini ni lazima akamilishe swala zake baada ya siku thelathini, kama siku thelathini amekaa sehemu moja, ama ikiwa zimeisha kwa kukaa sehemu mbalimbali atapunguza swala zake hata baada ya siku thelathini.
MAS’ALA MENGINEYO 966. Inajuzu kwa msafiri akamilishe swala zake katika msikiti mtakatifu wa Makka, msikiti wa Mtume, msikiti wa Kufah na kwenye kaburi la Imamu Hussein (as) akiswali nje ya sehemu hizi au akiswali sehemu ambayo iko na umbali kidogo kiasi cha mita ishirini na tano kwa tahadhari ya sunna apunguze swala zake. 967. Anayetambua kuwa msafiri ni wajibu wake apunguze swala zake akikamilisha kwa kujisahau swala yake inabatilika. 968. Msafiri asiyejua kuwa ni wajibu kwake kupunguza swala akikamilisha swala yake inasihi. . 969. Akijisahau kuwa ni msafiri akakamilisha swala akitambua ndani ya wakati atarudia swala yake na akitambua baada ya wakati halazimiki kuswali kadha. 970. Ni sunna kwa msafiri baada ya kila swala aseme mara thelathini “Subhana llah, wal hamdulillah, walaa ilaha ila llahu wa llah akbar” imetiwa mkazo kuisema baada ya swala ya adhuhuri, alasiri na ishaa na ni bora alete dhikri hii baada ya swala hizi mara sitini.
SWALA YA KADHA 971. Ambaye hakuswali swala ya wajibu katika wakati wake ni wajibu 185
Al-Masailul Islamiyah ailipe hata kama alikuwa amelala wakati wote wa swala au wakati umepita kwa sababu alikuwa amelewa, au kazimia, lakini mwanamke halipi kadha za swala zilizompita katika hali ya hedhi na nifasi. 972. Akitambua baada ya wakati wa swala kuwa swala aliyoiswali ilikuwa ni batili ni wajibu aswali kadha. 973. Ambaye ana kadha za swala zilizompita ni lazima asizembee wala kupuuzia lakini sio wajibu kuzilipa kwa haraka. 974. Swala za kila siku zikimpita ambazo huwa na utaratibu kama adhuhuri, alasiri au magharibi na ishaa katika siku moja ni wajibu azilipe kwa utaratibu, ama nje na hapa ni kwa tahadhari ya sunna achunge utaratibu. 975. Akitaka kulipa swala nyingi zisizo za kila siku kama swala za matukio ambazo zimempita mara nyingi na akataka kulipa kadha za swala za kila siku, si lazima kulipa kadha kwa utaratibu. 976. Akipitwa na swala ya adhuhuri kisha siku nyingine akapitwa na swala ya alasiri au akapitwa na zote mbili na akawa hajui ni ipi iliyotangulia kumpita, inatosha alete swala mbili za rakaa nne nne kwa kunuia kuwa swala ya kwanza ni kadha ya siku ya kwanza na ya pili ni kadha ya siku ya pili. 977. Akitambua kuwa amepitwa na swala ya rakaa nne na hatambui kuwa ni adhuhuri au alasiri inatosha alete swala ya rakaa nne kwa nia ya swala iliyompita. 978 Akipitwa na swala tano na hajui ya kwanza kumpita ni ipi itabidi azingatie utaratibu ufuatao: Kwanza ataswali swala tisa kwa utaratibu, ataanza na swala ya asubuhi, adhuhuri, alasiri, magaharibi na ishaa kisha arudie upya swala ya asubuhi, adhuhuri, alasiri na magharibi na vile vile akipitwa na swala sita itabidi aswali swala kumi kwa utarati186
Al-Masailul Islamiyah bu huu huu na akipitwa na swala saba ataswali swala kumi na moja. 979. Mwenye kutambua kuwa amepitwa na swala ya asubuhi mara nyingi au swala ya adhuhuri mara nyingi na hajui kuwa imepita mara ngapi mara tatu au tano au sita, akilipa kadha kwa kiasi kidogo inatosha, na kama anajua idadi yake lakini akasahau itabidi alete kadha ambayo inampa uhakika, kama akiwa na uhakika kuwa swala ya asubuhi haijampita zaidi ya mara kumi basi kwa tahadhari ya sunna inabidi alete kadha ya swala ya asuhubi mara kumi. 980. Haijuzu kwa mtu mwingine kulipa kadha za swala zilizompita aliye hai hata kama ameshindwa kuzilipa. 981. Inajuzu kuswali swala za kadha na jamaa hata kama swala ya imamu ni adaa au kadha, hailazimu swala ya maamuma iafikiane na swala ya imamu, hakuna tatizo kama akilipa kadha ya swala ya asubuhi na imamu anaswali swala ya adhuhuri au alasiri. 982. Ni sunna kumhimiza mtoto na kumzoesha swala na ibada mbali mbali, bali ni sunna pia kumhimiza kulipa swala zilizompita na inajuzu kwa watoto kusimisha swala ya jamaa na imamu wao awe ni mtoto.
WAJIBU WA MTOTO MKUBWA KULIPA SWALA ZILIZOWAPITA WAZAZI WAWILI
187
Al-Masailul Islamiyah 983. Ni wajibu kwa mtoto mkubwa kulipa kadha ya swala na saumu zilizompita baba yake, bali na hata mama pia kama hazikumpita kwa kuasi na wakawa na uwezo wa kuzilipa, bali ni wajibu kulipa kadha za wazazi wawili baada ya kufa kwao au kuajiri mtu wa kulipa kadha zilizowapita, na zikiwapita swala na saumu bila ya udhuru wowote kwa tahadhari mtoto mkubwa awalipie. 984. Mtoto mkubwa akishuku kuwa wazazi wake walipitwa na swala au saumu sio wajibu wake kulipa kadha. 985. Kama mtoto mkubwa hafahamiki basi watoto wote watagawiwa yaliyowapita wazazi wao au achaguliwe mmoja wao. 986. Kama maiti ameusia kuwa aajiriwe mtu wa kulipa yaliyompita haitawajibika kwa mtoto mkubwa baada ya aliye ajiriwa kulipa kadha kwa njia sahihi. 987. Mtoto akitaka kulipa yaliyowapita wazazi wake ni lazima alipe kutokana na wadhifa wake, mfano kudhihirisha sauti katika swala ya asubuhi na magharibi na isha hata kama analipa kadha ya mama yake. 988. Ikiwa mtoto mkubwa hajabaleghe au alikuwa ni kichaa wakati wazazi wake wanakufa atalipa kadha baada ya kubaleghe, na kichaa atawalipia atakapopona, na akifa mtoto mkubwa kabla ya kubaleghe hatawajibika mtoto anayefuata. 989. Akifa mtoto mkubwa kabla ya kuwalipia wazazi wake si wajibu kwa mtoto anayefuata kulipa.
KUTOA UJIRA KWA AJILI YA SWALA ZA KADHA 188
Al-Masailul Islamiyah
990. Inajuzu kumwajiri mtu kwa ajili ya kulipa swala au ibada zingine na kama atajitolea mtu bila ya ajira itasihi. 901. Ni wajibu kwa mwenye kuiajiri nafsi yake katika kulipa swala za maiti awe ni mujitahidi au mwenye kujua hukumu za swala kwa uelewa na taqlidi sahihi. 902. Ni wajibu kwa muajiriwa amuainishe anayemuwalikilisha wakati wa nia na si lazima atambue jina lake, na inatosha anuie hivi: “Ninaswali kwa niaba ya yule nilioajiriwa kwa jili yake kwa kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu�. 903. Akiajiriwa mtu kwa ajili ya kulipa kadha ya maiti ikifahamika kuwa hajalipa kabisa au hajalipa kwa usahihi ni wajibu atoe ajira tena kwa mwingine ikiwa ni wajibu kwake kuajiri. 904. Akishuku kuwa muajiriwa amelipa au laa, akisema muajiriwa kuwa nimelipa na ni mkweli inatosha, na akishuku kuwa ametekeleza vilivyo au laa, si lazima aajiri upya mtu mwingine. 905. Haijuzu kumwajiri mtu mwenye udhuru kama vile mwenye wadhifa wa kutayamamu au mwenye kuswali kwa kukaa n.k 906. Inajuzu mwanamke kulipa kadha za mwanaume pia inajuzu kwa mwanaume kumlipia mwanamke na kila mmoja anafanya kulingana na wadhifa wake.
SWALA YA JAMAA 907. Ni sunna kuswali swala za kila siku kwa jamaa na imetiliwa mkazo kwenye swala ya asubuhi, magharibi na isha na hasa kwa aliyekaribu na msikiti na mwenye kusikia adhana. 189
Al-Masailul Islamiyah
908. Mtu mmoja akiswali nyuma ya Imamu malipo ya kila rakaa ni sawa na mwenye kuswali swala mia na hamsini, na kama watu wawili watamfuata malipo yao ni sawa na kuswali swala mia sita, na idadi inapoongezeka na malipo pia huongezeka mpaka kufikia kumi, wanapozidi kumi kama mbingu itakuwa ni katarasi na bahari kuwa wino na miti kuwa kalamu kisha waandishi wawe ni majini, watu na malaika hawataweza kuandika thawabu za rakaa moja. 909. Haijuzu kutohudhuria swala ya jamaa na haijuzu kuacha swala ya jamaa bila ya udhuru. 910. Ni sunna kwa mtu kungoja jamaa, na swala ya jamaa baada ya wakati wa mwanzo ni bora kuliko swala ya furada katika mwanzo wa wakati. 911. Hakuna tatizo Imamu au Maamuma akitaka kurudia swala aliyokwisha iswali kwa jamaa mara nyingine. 912. Ambaye hutokewa na wasiwasi katika swala ya furada na wasiwasi wake huisha anaposwali jamaa itamlazimu kwa tahadhari ya wajibu aswali jamaa. 913. Haijuzu kuswali swala za sunna kwa jamaa ila swala ya kuomba mvua au swala ya wajibu iliyokuwa sunna kwa sababu fulani, kama vile swala ya Iddil- ftiri, Iddil – Adhuha ambazo ni wajibu kwa kudhihiri Imamu (as) na ni sunna kwa kutokuwepo kwake, inajuzu kuziswali jamaa. 914. Asiyetambua kuwa Imamu wa jamaa anaswali swala za kila siku ambazo ni wajibu au swala ya sunna haijuzu kumfuata. 915. Safu za swala zikifika kwenye mlango wa msikiti swala inasihi kwa yule aliyeswali mbele ya mlango. 190
Al-Masailul Islamiyah
916. Ambaye amesimama kwenye sehemu ambayo hapati mawasiliano na safu ya mbele na kama hapati mawasiliano kwa imamu kwa kupitia maamuma wengine kulia na kushoto, haijuzu kwake kujiunga na imamu. 917. Hakuna tatizo kama sehemu ya maamuma iko juu zaidi kuliko sehemu ya imamu. 918. Akitenganisha mtoto mwenye kutambua zuri na baya katika safu moja, kama hawatambui kubatilika swala yake inajuzu kujiunga na jamaa. 919. Akitambua kuwa swala ya imamu ni batili, kama akitambua kuwa imamu hana udhu haijuzu kumfuata hata kama imamu hajajua hilo. 920. Akitambua maamuma baada ya swala kuwa imamu hakuwa muadilifu au alikuwa kafiri au swala yake ilikuwa batili kwa sababu miongoni mwa sababu mfano hakuwa na udhu swala inasihi. 921. Akinuia maamuma swala ya furada bila ya udhuru au pamoja na udhuru baada ya Al – hamdu na sura haimlazimu kusoma Al hamdu na sura lakini akinuia furada kabla ya kumaliza Al- hamdu na sura inabidi asome kiasi ambacho imamu amesoma, na kwa tahadhari arudie kuzisoma kwa nia ya kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu. 922. Akishuku maamuma kuwa amenuia swala ya furada au laa ni wajibu ajengee kuwa hajanuia nia ya furada na ataendelea na swala ya jamaa.
YALIYOLAZIMA KWA IMAMU WA JAMAA 191
Al-Masailul Islamiyah 923. Lazima imamu wa jamaa awe baleghe, mwenye akili na awe ni shia ithna asharia muadilifu, awe mtoto wa halali, awe anaswali swala kwa usahihi, ni lazima imamu awe ni Mwanaume kama atafuatwa na wanaume na hakuna tatizo kwa mtoto kufuatwa na watoto na pia mwanamke kufuatwa na wanawake. 924. Mwenye kuwa na uwezo wa kuswali kwa kusimama haijuzu kumfuata aliyekaa au aliyelala, ambaye anaswali kwa kukaa haijuzu kumfuata aliye lala, inajuzu kwa anayeswali kwa kulala amfuate aliyekaa na aliyekaa kwa aliyesimama. 925. Inajuzu kumfuata imamu ambaye nguo yake ina najisi au wadhifa wake ni kutayamamu au kwa udhu wa bandeji kama kuswali kwake na nguo yenye najisi au tayamamu au udhu wa bandeji ni kwa sababu ya udhuru. 926. Inajuzu kumfuata maslusi na mabtuni na pia inajuzu asiye kuwa mustahadha kumfuata mustahadha. 927. Kwa tahadhari ya sunna wasifuatwe wenye ukoma na balanga na yeyote.
HUKUMU ZA JAMAA 928. Ni wajibu kwa maamuma kumuainisha imamu katika nia, lakini hailazimu kumjua imamu kwa jina inatosha kusema ninamfuata imamu anayetuongoza. 929. Ni wajibu kwa maamuma alete vipengele vyote vya swala yeye mwenyewe ila kusoma Al- hamdu na sura hiyo ni kazi ya imamu. 930. Ni wajibu kwa maamuma asisome Al- hamdu na sura katika swala za asubuhi, magharibi na ishaa kama anasikia sauti ya imamu na hata kama hasikii sauti ya imamu vizuri na kama hasikii kabisa lazima 192
Al-Masailul Islamiyah asome kwa kutodhihirisha sauti. 931. Akirukuu kabla ya imamu kwa kujisahau na akajua kuwa nikirudi katika kisimamo sitamuwahi imamu katika kusoma, akisuburi mpaka imamu amkute kwenye rukuu swala yake inasihi. Na pia swala yake inasihi kama atanyanyua kichwa chake kutoka kwenye rukuu kwa lengo la kumfuata imamu kisha akarukuu na imamu mara ya pili. 932. Haijuzu kumfuata imamu akileta kunuti kwa kusahau katika sehemu isiyo ya kunuti au akileta tashahudi katika sehemu isiyo ya tashahudi kama ambavyo katika hali hii haijuzu kurukuu kabla ya imamu kurukuu bali atasubiri kisha atakamilisha yaliyo bakia pamoja naye ila akikusudia furada inajuzu kumkhalifu imamu.
SUNNA ZA SWALA YA JAMAA 933. Ni sunna kwa mamuma wa kiume asimame kulia mwa imamu na kama maamuma ni wa kike atasimama kulia mwa imamu kiasi kwamba sehemu yake ya kusujudia itakuwa sawa na magoti ya imamu au miguu ya imamu kama maamuma ni mwanaume na mwanamke au mwanaume na wanawake wengi ni sunna maamuma wa mwanaume asimame kulia mwa imamu na wanawake wasimame nyuma ya imamu na kama ni wanaume wengi na wanawake wengi ni sunna wanaume kuwa nyuma ya imamu na wanawake kuwa nyuma ya wanaume. 934. Ikiwa imamu na maamuma ni wanawake ni bora wasimame kwa usawa asitangulie imamu kwa maamuma. 935. Ni sunna kwa imamu kusimama katikati ya safu na wasimame wenye elimu na ucha Mungu nyuma yake katika safu ya kwanza 936. Ni sunna safu ziwe zimenyooka na bila ya kuwepo na mwanya wala 193
Al-Masailul Islamiyah kitenganishi chochote. 937. Ni sunna kwa waumini kusimama baada ya kauli ya imamu “Qad Qaamati swaalat� 938. Ni sunna kwa imamu kuchunga udhaifu wa maamuma asirefushe rukuu, kunuti na sijida ila akitambua kuwa wote wanapendezwa na hali hiyo. 939. Ni sunna akitambua imamu kuongezeka kwa maamuma mwingine arefushe rukuu mara mbili zaidi kisha asimame hata kama akitambua kuongezeka mwingine.
VILIVYO MAKURUHU KATIKA SWALA YA JAMAA 940. Ni makuruhu kwa maamuma kusimama peke yake katika safu moja ikiwa katika safu zingine kuna sehemu zilizo wazi. 941. Ni makuruhu kwa maamuma kuleta baadhi ya dhikri kwa sauti kiasi kwamba imamu anasikia. 942. Ni makuruhu kwa msafiri ambaye anapunguza swala zake kama adhuhuri, alasiri na ishaa afuatwe na asiye kuwa msafiri na pia ni makuruhu kwa asiye kuwa msafiri kumfuata msafiri.
SWALA YA IJUMAA 943. Swala ya ijumaa ni wajibu akiwepo Imamu (as) badala ya adhuhuri, 194
Al-Masailul Islamiyah lakini katika zama ya ghaiba ya Imamu inakuwa ni wajibu wa hiari, yaani mtu anakuwa na hiari katika siku ya Ijumaa kuswali adhuhuri au kuswali ijumaa lakini kwa tahadhari ya sunna akiswali ijumaa katika wakati huu wa ghaiba ya Imamu aswali na adhuhuri pia. 944. Swala ya Ijumaa ina rakaa mbili mfano wa swala ya asubuhi na imamu adhihirishe sauti yake katika kusoma Al- hamdu na sura na imetiliwa mkazo asome suratul- jum’a katika rakaa ya kwanza na suratul – munaafiquun katika rakaa ya pili, na ni sunna katika swala ya ijumaa kuleta kunuti mbili katika rakaa ya kwanza kabla ya rukuu na katika rukuu ya rakaa ya pili baada ya rukuu. Ni wajibu asirukuu baada ya kunuti ya rakaa ya pili na akirukuu baada ya kunuti swala inabatilika. 945. Shaka katika idadi ya rakaa kwenye swala ya ijumaa inabatilisha swala. 946. Ni sharti katika swala ya ijumaa yanayoshurutishwa katika swala za kila siku kwa kuongeza yafuatayo:1. Iswaliwe jamaa na si furada. 2. Iwe idadi ya wenye kuswali - imamu na maamuma - wawe saba waliobaleghe kwa uchache na kwa tahadhari ya wajibu katika hao asiwepo msafiri anayepunguza swala ikiwa imamu na mamuma ni watano swala inasihi. 3. Imamu ahutubie kabla ya swala khutuba mbili kwa ufafanuzi utakaokuja inshaallah. 4. Ikiwa kuna sehemu mbili za swala za ijumaa ni wajibu masafa baina ya ijumaa mbili hizo yawe ni kilometa tano na nusu 5. Kama maamuma watatawanyika katikati ya khutuba ya swala au 195
Al-Masailul Islamiyah kabla ya kuanza swala na idadi ikawa chini ya watu wanne swala ya ijumaa haitasihi ni wajibu waswali adhuhuri, na wakitawanyika katikati ya swala ni wajibu kwa imamu kukamilisha ijumaa kisha aswali adhuhuri. 947. Ni lazima vizingatiwe vitu vifuatavyo katika khutuba mbili:- Kumhimidi Mwenyezi Mungu – kumshukuru - Kumtakia rehma Mtume “Muhammad (saww) na kizazi chake kitukufu - Awalinganie watu katika kumcha Mwenyezi Mungu na kumuogopa - Asome sura kamili katika khutuba ya kwanza - Kuwatakia rehma maimamu na kuwataja kwa majina katika khutuba ya pili - Kuwaombea waumini maghfira 948. Ni lazima kumuhimidi Mwenyezi Mungu na kumtakia rehma Mtume Muhammadi (saww) na kizazi chake katika khutuba kwa lugha ya kiarabu lakini mawaidha na kuwalingania inajuzu kwa lugha ya waliohudhuria. 949. Ni lazima kwa imamu asome khutuba mbili mwenyewe, asisome mwingine kama ambavyo anatakiwa azisome akiwa amesimama kisha atenganishe khutuba ya pili kwa kukaa kikao kidogo na adhihirishe sauti ya khutuba kwa uchache wasikie watu wanne waliokamilisha masharti, na inapaswa waliohudhuria wote wasikie khutuba mbili. 950. Ni lazima kwa maamuma kwa ubora kusikiliza khutuba ya imamu, na wasizungumze mazungumzo yanayowafanya wasimsikilize imamu na wala wasiswali swala za sunna na wakae mkao wa swala, wasigeuke kulia na kushoto na wala wasigeuke geuke, na hakuna tatizo katika mambo haya baada ya khutuba na kabla ya swala.
196
Al-Masailul Islamiyah 951. Kama maamuma hawatasikiliza khutba mbili na wakawa wamegeuka kulia na kushoto watakuwa wamefanya kinyume na tahadhari lakini swala yao inasihi. 952. Si wajibu swala ya Ijumaa kwa asio baleghe, vichaa na wazee, wagonjwa, vipofu, wanawake, wasafiri na wanaokaa mbali na sehemu ya kuswalia kwa farsakha mbili wala kwa yule ambaye ni vigumu kuhudhuria katika swala wala katika wakati wa mvua, lakini mmoja wa hawa akihudhuria swala yake inasihi. 953. Inajuzu kwa aliyechelewa khutba mbili ahudhurie ijumaa na kuswali, na pia akimkuta imamu yuko kwenye rukuu ya rakaa ya pili itakuwa rakaa yake ya kwanza na akitoa salamu imamu atasimama kwa ajili ya rakaa ya pili na kukamilisha swala na ijumaa itakuwa imesihi.
SWALA YA MAJANGA 954. Ni wajibu kuswali swala ya majanga ambayo tutataja namna yake baadaye kwa sababu ya mambo yafuatayo:1. Kupatwa kwa Jua, hata kama itapatwa sehemu tu na hajaogopa yeyote 2. Kupatwa kwa Mwezi, hata kama itapatwa sehemu tu na hakuogopa yeyote 3. Tetemeko, hata kama hakuogopa yeyote 4. Radi, ngurumo, kimbunga, kuvuma kwa upepo mweusi na mwekundu n.k. ikiwa watu wengi wataogopa 955. Vikitokea vitu vingi ambavyo ni wajibu kuswali swala ya majanga ni wajibu aswali kwa kila tukio swala ya janga mfano: Ikitokea kupatwa kwa jua na likatokea tetemeko ni wajibu kuswali swala ya majanga mara mbili.
197
Al-Masailul Islamiyah 956. Mwenye kuwajibikiwa na swala nyingi za majanga, mfano likipatwa jua mara tatu na hakuswali kwa muda wake haitamlazimu wakati wa kadha kuainisha ni swala ipi anayoiswali bali inatosha kuswali idadi ya swala kulingana na idadi ya majanga yaliyompita. 957. Ni wajibu kuleta swala ya majanga tangu linapoanza kupatwa jua au mwezi na kwa tahadhari ya sunna asicheleweshe hadi weupe uanze kutokea. 958. Akiwajibikiwa na swala ya majanga katika wakati wa swala za kila siku, kama wakati utakuwa ni mpana atachagua yeyote ya kutanguliza, na kama wakati utakuwa ni mfinyu itabidi aswali swala ambayo muda wake ni mfinyu na kama wakati wa swala mbili hizi ni mfinyu atatanguliza swala ya kila siku. 959. Akitambua katikati ya swala ya kila siku kuwa wakati wa swala ya majanga ni mfinyu na wakati wa swala ya kila siku ni mpana atakatisha swala ya kila siku na kuswali swala ya majanga. 960. Ikitokea kupatwa kwa jua, mwezi, tetemeko na mwanamke yuko katika hedhi au nifasi hatawajibikiwa na swala ya majanga wala kadha yake lakini kwa tahadhari ya sunna aswali baada ya kutoharika.
NAMNA YA KUSWALI SWALA YA MAJANGA 961. Swala ya majanga ina rakaa mbili na kila raka kuna rukuu tano namna yake ni hii: “Alete takbira baada ya nia atasoma Al- hamdu na sura kamili na kurukuu kisha anasimama na kusoma Al- hamdu na sura kamili atafanya vivyo hivyo hadi mara tano na baada ya kusimama kutoka kwenye rukuu ya tano anaenda kwenye sijida mbili kisha anasimama kwa ajili ya rakaa ya pili, anafanya kama alivyofanya kati198
Al-Masailul Islamiyah ka rakaa ya kwanza na kuleta tashahudi na kutoa salamu. 962. Katika swala ya majanga inajuzu baada ya nia na kusoma Al- hamdu agawanye sura kwenye vifungu vitano atasoma aya au zaidi ya aya kisha anarukuu kisha ananyanyuka anasoma kifungu cha pili cha sura bila ya kusoma Al- hamdu kisha anarukuu vivyo hivyo mpaka rukuu ya tano mfano: asome baada ya Al-hamdu (bismillah rahmani rahim” kama anataka kusoma suratul – Ikhalas kisha anarukuuu kisha ananyanyuka anasoma Qul huwallahu ahad – kisha anarukuu kisha ananyanyuka anasoma Allahhu swamadu – anarukuu kisha anasoma lam yalid walam yuulad kisha anarukuu kisha ananyanyuka anasoma Walam yakun lahuu kufuwan ahad – anarukuu rukuu ya tano baada ya kunyanyuka hapo anaenda kwenye sijida mbili kisha ananyanyuka kwa ajili ya rakaa ya pili na anafanya kama alivyofanya kwenye rakaa ya kwanza. 963. Ni sunna kuleta takbira kabla ya kurukuu na baada yake ama baada ya rukuu ya tano na ya kumi ni sunna kusema “Samia llahu liman hamidah” 964. Ni sunna kuleta Qunuti kabla ya rukuu ya pili, ya nne, ya sita, ya nane na ya kumi na akileta Qunuti moja kabla ya rukuu ya kumi inatosha. 965. Kila rukuu katika rukuu za swala za majanga ni nguzo zinabatilisha swala kwa kuongezeka kwake au kupungua kwa kukusudia au kusahau. 966. Ni mustahabu kuleta swala ya majanga kwa jamaa na hapo haitawalazimu maamuma kusoma Al- hamdu na sura .
199
Al-Masailul Islamiyah
SWALA YA IDD MBILI “AL – FITRI NA AL – ADHIHAA” 967. Swala ya Idd mbili ni wajibu katika zama za kuwepo Imamu “as” na ni lazima iswaliwe jamaa na ni sunna katika zama za “ghaiba” kuswaliwa jamaa au furada. 968. Wakati wa swala ya Idd ni mwanzo wa kuchomoza jua mpaka jua linapopetuka. 969. Ni sunna kuswali swala ya Idd ya adhuhaa baada ya kunyanyuka jua kama ilivyo kwenye swala ya Iddil – fitri na atoe zaka kisha aswali Idd. 970. Swala ya Idd mbili ina rakaa mbili kwanza analeta takbira ya ihram kisha baada ya kusoma Al-hamdu na sura analeta takbira tano anakunuti baada ya kila takbira, analeta takbira nyingine na kurukuu kisha analeta sijida mbili, kisha anasimama kwa ajili ya rakaa ya pili baada ya Al hamdu na sura analeta takbira nne na anakunuti baada ya kila takbira kisha analeta takbira ya tano na kurukuu kisha analeta sijida mbili baada ya rukuu na analeta tashahudi na kutoa salamu. 971. Na inatosha kuleta dua yeyote katika kunuti za idd mbili lakini ni bora alete moja ya hizi dua mbili “Allahuma Ahlul kibriai wal adhama.waahalul juudi wal jabarut waahalul ‘af’wi wa rahma waahlu taqwaa walmaghifra as’aluka bihaqi hadhal yaumi alladhii ja’al tahu lili muslimiina I’ydan, wali Muhammadin swala llahu alayhi waalihi dhukhran wa sharafan wakaramatan wa mazidaan, an tuswaliya alaa muhammadin waali Muhammad, wa an tud khilanii fii kuli khayrin adkhalta fiihi Muhammad waala muhammad wa antukhirjanii min kuli suui akhrajta minhu muhammadan waala 200
Al-Masailul Islamiyah Muhammadi swalawatuka alayhi wa alayhimu allahumma inii as’aluka khayran maasaalaka minihu Ibaaduka swaalihuuna wa waa’udhubika mimaa istadha minhu ibaadukal mukhliswuna” 972. Ni sunna kuleta khutba mbili katika ghaiba ya Imamu baada ya swala na ni bora kutaja hukumu za fitri katika Iddil- fitri na hukumu za kuchinja katika iddil adhiha 973. Hakuna katika idd mbili hizi sura maalumu ya kusoma lakini ni bora asome katika rakaa ya kwanza suratu Shamsi (nayo ni sura ya 91) na katika rakaa ya pili suratul ghashiya (nayo ni sura ya 88) au asome katika rakaa ya kwanza suratul A’alaa (nayo ni sura ya 87) na katika rakaa ya pili suratul Shamsi. 974. Ni sunna kuswali swala ya Idd mbili uwanjani lakini Makka ni sunna kuswaliwa ndani ya msikiti mtukufu . 975. Ni sunna baada ya swala ya magharibi na isha, katika usiku wa idd ilfitri na baada ya swala ya asubuhi na vile vile hata baada ya swala ya Idd alete hizi takbira. “Allahu akbaru Allahu akbaru laa ilaaha ila llaha wa llahu akbaru walilahil hamdu,al-hamdu lilahi alaa maahadaanaa walahu shukri alaa maa aulaanaa” 976. Na takbira ya Iddul – adhuhaa atesema baada ya kauli ya “alaa ma hadaanaa” atasema “Allahu akbaru alaa maa razaqanaa min bahiimatil ana’am wal hamdulillah alaa maa ablaanaa” akiwa katika idd ya kuchinja ni mustahabu alete takbira baada ya sala kumi na tano ya kwanza ni swala ya adhuhuri katika siku ya Idd na ya mwisho ni swala ya asubuhi ya siku ya kumi na tatu katika mwezi wa dhul – hijja. 977. Akihudhuria maamuma na imamu yuko kwenye rukuu inajuzu kunuia 201
Al-Masailul Islamiyah kisha ataleta takbiratul -ihram na anaenda kwenye rukuu na inahesabika kuwa ni rakaa. 978. Akisahahu tashahudi au moja ya sijida mbilli katika swala ya Idd kwa tahadhari ya sunna alete kadha ya alichokisahau baada ya swala, na akifanya kinacholazimu sijida ya kusahau ni lazima alete sijida ya kusahau na akishuku katika Idadi ya rukuu na kunuti na akawa amejishughulisha na kinachofuatia basi asizingatie shaka yake.
HUKUMU ZA SAUMU 979. Saumu ni kujizuia na vitu vyote ambavyo vinafuturisha ( ambavyo vinamtoa mtu katika funga) kuanzia Adhana ya Alfajiri hadi Adhana ya magharibi kwa kutekeleza amri ya Mwenyezi Mungu, tutataja vinavyotengua saumu baadae
NIA
980. Si wajibu mfungaji kutamka kwa ulimi au kwa moyo mfano mtu kusema “ nafunga kesho� bali inatosha kujizuia na vinavyobatilisha saumu kuanzia adhana ya Alfajiri mpaka adhana ya magharibi kwa kutekeleza amri ya Mwenyezi Mungu lakini ili awe na yakini kwamba amefunga kwa muda wote inamlazimu kujizuia na vinavyobatilisha saumu kabla adhana ya Alfajiri kwa muda mchache na kufuturu baada ya adhana ya magharibi kwa muda mchache vile vile. 981. Inajuzu mfungaji kunuia kwa kila siku katika siku za mwezi wa Ramadhani kwa saumu ya siku inayofuata na ni bora kunuia katika usiku wa kwanza wa mwezi wa Ramadhani kwa nia ya kufunga mwezi mzima. 982. Muda wa nia ya funga ya mwezi wa Ramadhani ni mwanzo wa usiku mpaka adhana ya asubuhi. 202
Al-Masailul Islamiyah 983. Muda wa nia ya saumu ya sunna ni mwanzo wa usiku mpaka kuzama jua kwa kadri ya nia, ikiwa hajajishughulisha na kitu cha kutengua saumu mpaka wakati wote huo na akanuia saumu ya sunna basi saumu inasihi. 984. Mwenye kulala kabla ya adhana ya asubuhi bila ya kunuia saumu akiamka kabla ya adhana na akanuia funga inasihi funga yake, iwe funga yake ni ya wajibu au ya sunna na lau akiamka baada ya adhuhuri haitatosha kunuia funga ya wajibu. 985. Akitaka kuleta saumu ambayo siyo ya mwezi wa Ramadhani ni wajibu kwake kuiainisha saumu mfano anuie “ nafunga kadha au nadhiri” lakini katika mwezi wa Ramadhani sio lazima anuie “nafunga mwezi wa Ramadhani” bali akifunga kwa kutojua au kusahau kwamba yuko katika mwezi wa Ramadhani na akanuia vinginevyo anahesabiwa kuwa kafunga mwezi wa Ramadhani. Ikiwa anajua ni mwezi wa Ramadhani na akanuia saumu isiyokuwa ya mwezi wa Ramadhani kwa makusudi hata hesabiwa si katika mwezi wa Ramadhani wala saumu nyingine ambayo amenuia. 986. Akifunga mfano kwa nia ya mwanzo wa mwezi wa Ramadhani, kisha akatambua baadae kwamba ilikuwa siku ya pili au ya tatu ya mwezi wa Ramadhani inasihi funga yake. 987. Akinuia kufunga kabla adhana ya Asubuhi kisha akazimia na kuzinduka katikati ya mchana, kwa tahadhari ya wajibu atimize saumu ya siku hiyo na kuilipa kadha siku nyingine. 988. Akinuia kufunga kabla ya adhana ya asubuhi kisha akalala na asiamke ila baada ya magharibi, itasihi saumu yake. 989. Hakuna mushikeli mwenye kujiajiri kulipa kadha ya saumu ya maiti kufunga saumu yake ya sunna, lakini kwa yule ambaye alikuwa na 203
Al-Masailul Islamiyah kadha ya saumu iliyopita haijuzu kwake kuleta saumu ya sunna na lau akifunga saumu ya sunna kwa kusahau akikumbuka kabla ya adhuhuri inabatilika saumu yake ya sunna na inajuzu kubadili nia yake ya sunna kwa nia ya saumu ya kadha ambayo ni wajibu wake na lau akikumbuka baada ya adhuhuri itakuwa imebatilika saumu yake ya sunna na lau akikumbuka baada ya magharibi itakuwa imesihi saumu yake ya sunna 990. Kafiri akisilimu katika mwezi wa Ramadhani kabla ya Adhuhuri, haitosihi saumu yake hata kama hajala kitu chochote kwa muda wote huo na hata kama atakuwa amenuia kabla ya Adhuhuri. 991. Akifunga siku ya shaka kwamba ni mwisho wa Shaban au mwanzo wa mwezi.wa Ramadhani kwa nia ya saumu ya kadha au saumu ya sunna au vinginevyo kisha akajua wakati huo ni siku ya mwezi wa Ramdahani inamuwajibikia abadili nia yake ya mwanzo aliyokuwa nayo kwenda kwenye nia ya mwezi wa Ramadhani
VINAVYOTENGUA SAUMU 992. Vitenguzi vya saumu ni kumi:1. Kula 2. Kunywa 3. Jimai 4. Punyeto 5. Kumzulia Mwenyezi Mungu uongo au Mtume Muhammad ( saww) au Maimamu ( as) au Fatma Zahara (as) 6. Kufika vumbi zito kwenye koo 7. Kuzamisha kichwa chote kwenye maji 8. Kubaki na janaba au hedhi au nifasi mpaka adhana ya asubuhi 9. Kupiga bomba 10. Kujitapisha makusudi 204
1 na 2 Kula na kunywa 993. Akila mfungaji au akinywa kitu kwa makusudi basi saumu yake inabatilika ni sawa kile kilicholiwa au kilichonywewa ni kilichozoeleka kama vile mkate, maji na mfano wake au visivyozoeleka kama vile kula udongo na kunywa maji maji ya miti ni sawa kilicholiwa au kilichonywewa ni kidogo sana au ni kingi inabatilika saumu hata kwa kurudisha maji maji ya mswaki mdomoni baada ya kuutoa kwake na kumeza maji maji yake kwa haraka isipokuwa yakimalizika maji maji ya mswaki katika maji ya mdomoni kiasi kwamba haihesabiki kuwa amemeza maji maji ya kutoka nje. 994. Mfungaji akijua kuingia kwa Alfajiri na akawa anakula ni wajibu ateme kile alichokitia mdomoni kwa haraka na lau akikimeza kwa kusudi itabatilika saumu yake na inamuwajibikia kulipa kadha na kutoa kafara. Akila mfungaji au akinywa kitu kwa kusahau, haitobatilika saumu yake. 995. Ni vizuri zaidi mfungaji kujiepusha kutumia bomba kwa ajili ya tiba, sindano zenye kuongeza lishe mwilini au kuongeza nguvu, hakuna tatizo kutumia sindano zingine kwani hazibatilishi saumu kama sindano za ganzi na sindano za dawa. 996. Mfungaji akimeza mabaki ya chakula yaliyobaki kwenye meno yake kwa makusudi inabatilika saumu yake. 997. Mwenye kutaka kufunga si wajibu kwake kuondosha mabaki ya chakula yaliyobaki kwenye meno yake kabla ya adhana ya Alfajiri lakini akijua au akapata yakini kwamba mabaki yataingia kwenye koo lake wakati wa mchana ikiwa hakutoa mabaki hayo kwenye meno yake na kikaingia kitu katika mabaki ya chakula kwenye koo lake inabatilika saumu yake kwa tahadhari.
205
Al-Masailul Islamiyah 998. Kumeza mate hakubatilishi saumu hata yakijikusanya mdomoni kutokana na kuhisi athari ya uchachu na vinavyofanana na hivyo. 999. Mfungaji akipatwa na kiu kali kiasi kwamba anapatwa na matatizo au akiogopa kupata madhara kwa sababu ya kiu, inajuzu kwake kunywa maji kiasi cha kumwondoshea madhara lakini inabatilika saumu yake na ni wajibu kujiepusha na vitu vingine vinavyobatilisha saumu mchana wote ikiwa ni katika mwezi wa Ramadhani. 1000. Kumtafunia mtoto chakula au ndege na kuonja na mfano wake ambapo kwa kawaida hakifiki mpaka kwenye koo haibatilishi saumu hata kama ikifika kwenye koo ghafla lakini ikiwa alikuwa anajua mwanzo kwamba chakula kitafika mpaka kwenye koo itabatilika saumu yake na inamlazimu ailipe na ni wajibu atoe kafara pia.
JIMAI 1001. Jimai inabatilisha saumu hata kama hakuingiza ila kiasi cha kichwa cha dhakari na ikawa manii hayajatoka . Akiingiza kiasi kidogo cha kichwa cha dhakari na ikawa hayajatoka manii haibatiliki saumu yake. 1002. Akitia shaka je ameingiza kiasi cha kichwa cha dhakari au laa inasihi saumu yake. 1003. Akifanya jimai kwa kusahau kwamba amefunga au kulazimishwa ( kwa nguvu bila ya hiyari yake) saumu yake haibatiliki, lakini akikumbuka aliye sahau au akaacha kulazimishwa ni wajibu kuacha jimai na kama hataacha basi inabatilika saumu yake.
206
Al-Masailul Islamiyah
PUNYETO “ KUCHEZEA UTUPU� 1004. Mfungaji akifanya punyeto kwa kutumia njia ya kuchezea utupu wake kujitoa manii na akajitoa manii saumu yake inabatilika. 1005. Yakimtoka mtu manii bila ya hiyari yake haibatiliki saumu yake, lakini akifanya yale ambayo yanamfanya kutoka manii bila ya hiyari inabatilika saumu yake. 1006. Akijua mfungaji kwamba akilala mchana ataota, haitomlazimu kuacha kulala na akilala na akaota haitabatilika saumu yake. 1007. Akiamka mfungaji katika hali kujizuia kutoka manii.
ya kutoka manii haimlazimu
1008. Mfungaji aliyejiotea akijua kubakia manii katika njia ya mkojo na kwamba asipokojoa kabla ya kuoga yatamtoka manii baada ya kuoga, inalazimu kwa tahadhari ya sunna akojoe kabla ya kuoga 1009. Mfungaji akimchezea mtu kwa kusudi la kutoa manii inabatilika saumu yake kwa tahadhari hata kama hayatamtoka manii. 1010. Mfungaji akimchezea mtu sio kwa kusudio la kutoka manii, ikiwa anamatumaini kwamba manii hayatamtoka inasihi saumu yake, hata kama yatatoka bila kutarajia, lakini ikiwa hakuwa na matumaini ya kutotoka manii saumu yake itabatilika kama yatamtoka
207
Al-Masailul Islamiyah
KUMZULIA MWENYEZI MUNGU UONGO, MTUME (SAWW) NA MAIMAMU (AS). 1011. Akinasibisha mfungaji kwa makusudi uongo kwa Mwenyezi Mungu au Manabii au Maimamu watukufu (as) kwa kutamka au kuandika au kuashiria na mfano wake inabatilika saumu yake hata kama atatubu haraka au akisema nimesema uongo, na kwa tahadhari ya wajibu kama atamsingizia Fatma Zahara ( as) vilevile inabatilisha saumu. 1012. Akinukuu kitu kutoka kwa Mwenyezi Mungu au Nabii au Imamu maasum (as) kwa itikadi kwamba alichokinukuu ni sahihi kisha baadae akabaini kuwa sio sahihi, saumu yake haibatiliki. 1013. Ikiwa anajua kwamba kunasibisha uongo kwa Mwenyezi Mungu au Mtume wake ( saww) inabatilisha saumu na akakusudia kunasibisha kwa yale anayojua uongo wake, kisha akajua baadae kwamba yale aliyoyasema yalikuwa ya kweli, atalipa kadha ya siku hiyo kwa tahadhari ya wajibu. 1014. Akiulizwa mfungaji je, amesema Mtume ( saww) maudhui haya au hapana? Na ilikuwa inampasa aseme hapana lakini yeye akajibu kwa kusudi ndio badala ya hapana basi inabatilika saumu yake 1015. Akitoa habari kuhusu Mwenyezi Mungu au Mtume wake ( saww) za kweli, kisha akasema nimesema uongo au akanasibisha juu yao uongo usiku kisha akatilia mkazo katika mchana wa funga inabatilika saumu yake.
208
Al-Masailul Islamiyah
KUFIKA VUMBI ZITO KWENYE KOO 1016. Kufika vumbi zito kwenye koo kunabatilisha saumu, ni sawa likiwa ni vumbi la kilicho halali kuliwa, kama vile vumbi la unga wa ngano, au vumbi la kilichoharamu kuliwa, kama vile vumbi la udongo, na kwa tahadhari lisifike kabisa vumbi lisilokuwa zito kooni pia. 1017. Vumbi zito likitimka kwa sababu ya upepo na akawa hajazuia mfungaji vumbi kufika kooni kwa kutokuwa mwangalifu bila ya kughafilika na vumbi likafika kooni inabatilika saumu yake. 1018. Kwa tahadhari ya wajibu usimfikie mfungaji moshi mzito wa sigara na tumbaku na mfano wake kwenye koo pia, hakuna mushikeli katika moshi mdogo wa kawaida uliopo katika bafu. 1019. Ikiwa mfungaji hakujihifadhi likaingia vumbi zito au moshi mzito na mfano wake vikaingia kwenye koo ikiwa alikuwa na matumaini au yakini ya kutofika mpaka kwenye koo inasihi saumu yake, na ikiwa aliacha kujihifadhi kwa dhana ya kutoingia mpaka kwenye koo basi inamlazimu kwa tahadhari kuleta kadha ya saumu hiyo. 1020. Akisahau kwamba amefunga na akaacha kujihifadhi kutofika vumbi mpaka kwenye koo lake au kuingia vumbi na mfano wake vikaingia mpaka kwenye koo lake bila ya hiyari yake, haibatiliki saumu yake.
209
Al-Masailul Islamiyah
KUZAMISHA KICHWA KWENYE MAJI 1021. Mfungaji akizamisha kichwa chake kwenye maji (Yaani akaingiza kichwa chake chote kwenye maji ) kwa kusudi inabatilika saumu yake na hakuna kafara juu yake, hata kama mwili wake umebaki nje ya maji, lakini haitabatilika saumu yake lau akizamisha mwili wake wote kwenye maji na kikabaki kichwa chake nje ya maji. 1022. Akiingiza nusu ya kichwa chake kwenye maji mara moja na akaingiza nusu nyingine kwa mara nyingine haibatiliki saumu yake. 1023. Akishuku kwamba je ameingiza na amezamisha kichwa chake chote katika maji au laa inasihi saumu yake. 1024. Akizamisha kichwa chake katika maji lakini zikabakia nywele za kichwa chake nje ya maji inabatilika saumu yake. 1025. Kwa tahadhari ya wajibu asizamishe kichwa chake kwenye maji mudhafu. 1026. Akianguka mfungaji kwenye maji bila ya hiyari yake na akaingiza kichwa chake chote kwenye maji au akazamisha kichwa chake chote kwenye maji kwa kusahau kwamba amefunga haibatiliki saumu yake. 1027. Mfungaji akijiingiza mwenyewe kwenye maji na alikuwa na uhakika kwamba maji hayatofunika kichwa chake, yakifunika kichwa chake haitobatilika saumu yake, ama ikiwa hakuwa na uhakika na akajiingiza kwenye maji, na maji yakafunika kichwa chake inamlazimu alete kadha ya saumu hiyo kwa tahadhari ya wajibu. 1028. Akizamisha kichwa chake chote kwenye maji kwa nia ya kuoga na akawa amesahau kwamba amefunga inasihi kuoga kwake na funga 210
Al-Masailul Islamiyah yake. 1029 Akikusudia kuzamisha kichwa chake chote katika maji kwa ajili ya kuoga na anajua kwamba amefunga, ikiwa saumu yake ni saumu ya mwezi wa Ramadhani au ya wajibu maalumu inabatilika kuoga kwake na saumu yake, na ikiwa saumu yake ni ya sunna au ya wajibu usio kuwa maalumu kwa wakati, mfano saumu ya kafara inasihi kuoga kwake na inabatilika funga yake. 1030. Akizamisha kichwa chake chote katika maji kwa ajili ya kuokoa (mtu) aliye zama kwenye maji inamlazimu kuleta kadha ingawa kumuokoa yule mtu ni wajibu
KUBAKI NA JANABA AU HEDHI AU NIFASI MPAKA ALFAJIRI 1031. Mwenye janaba asipooga mpaka adhana ya alfajiri kwa kusudi au wadhifa wake ulikuwa ni kutayamamu na akawa hajatayamamu kwa kusudi mpaka ikafika alfajiri inabatilika saumu yake katika mwezi wa Ramadhani au kadha yake, ama zisizokuwa hizo katika funga za wajibu na sunna haibatiliki, na kwa tahadhari ya sunna kutoacha kuoga au kutayamamu kabla ya alfajiri, hasa katika wajibu maalum kama vile saumu ya nadhiri ya siku maalum. 1032. Asipooga au asipotayamamu mpaka adhana ya Alfajiri katika saumu ya wajibu ya wakati maalum kama vile saumu ya Ramadhani, lakini sio kwa kusudi, au kama akizuiwa na mtu kuoga au kutayamamu inasihi saumu yake. 1033. Mwenye janaba ambaye anataka kuleta saumu ya wajibu kama vile 211
Al-Masailul Islamiyah saumu ya mwezi wa Ramadhani, ikiwa hajaoga kwa kusudi mpaka wakati ukawa mfinyu ni wajibu atayamamu na afunge na saumu yake itasihi, ingawa ni bora kwake alipe kadha ya saumu hiyo pia. 1034. Mwenye janaba akisahau kuoga katika mwezi wa Ramadhani na akakumbuka baada ya kupita siku ni wajibu arudie saumu ya siku hiyo, na akikumbuka baada ya siku nyigine inamlazimu kulipa kadha ya siku ambazo anayakini kuwa alikuwa na janaba, mfano kama hakujua amebaki na janaba siku tatu au nne ni wajibu alipe saumu ya siku tatu kwa babu ndio kiasi alicho na yakini. 1035. Mwenye kukusudia kupata janaba katika siku za Ramadhani katika wakati usiotosheleza kuoga na kutayamamu inabatilika saumu yake, na ni wajibu kwake kulipa kadha na kafara ,lakini akisababisha kupata janaba katika wakati unaotosha kwa kutayamamu ni wajibu kwake atayamamu na afunge ,na ni bora alipe kadha ya siku hiyo. 1036. Mwenye kuwa na janaba katika usiku wa mwezi wa Ramadhani au akajua kwamba lau akilala hataamka mpaka alfajiri, ni wajibu kwake asilale, na akilala na asiamke mpaka alfajiri inabatilika saumu yake na ni wajibu kwake kadha na fakara. 1037. Akilala mwenye janaba usiku katika mwezi wa Ramadhani inajuzu kwake kulala mara ya pili kabla ya kuoga ikiwa ni kawaida yake kuamka kabla ya alfajiri, na ikiwa sio kawaida yake kuamka inajuzu kwake kulala kabla ya kuoga lau akitarajia kuamka mara ya pili kabla ya adhana ya Alfajiri, na kwa tahadhari asilale mpaka aoge. 1038. Mwenye kuwa na janaba usiku katika mwezi wa Ramadhani akitambua au ni kawaida yake kuamka kutoka usingizini kabla ya adhana ya Alfajiri ikiwa amenuia kuoga baada ya kuamka kwake na akalala na nia hiyo mpaka Alfajiri inasihi saumu yake. 212
Al-Masailul Islamiyah 1039. Mwenye janaba katika usiku wa mwenzi wa Ramadhani na ambaye anajua au anatarajia kwamba ataamka kabla ya adhana ya Alfajiri ikiwa hakutaka kuoga baada ya kuamka au akasitasita kwamba aoge au laa lau akilala na asiamke inabatilika saumu yake na ni juu yake kulipa kadha pamoja na kafara. 1040. Akijiotea mfungaji mchana sio wajibu kwake kufanya haraka kuoga japo ni bora kufanya hivyo. 1041. Akiamka mfungaji katika mwezi wa Ramadhani baada ya adhana ya Alfajiri akakuta amejiotea inasihi saumu yake hata kama akitambua kuwa amejiotea kabla ya adhana 1042. Mwenye kutaka kulipa kadha ya saumu ya mwezi wa Ramadhani akibakia na janaba mpaka adhana ya Alfajiri inabatilika saumu yake hata kama hakufanya hivyo kwa makusudi. 1043. Mwenye kutaka kulipa kadha ya saumu ya mwezi wa Ramadhani akiamka baada ya adhana ya Alfajiri na akakuta amejiotea na akatambua kwamba amejiotea kabla ya adhana ikiwa wakati wa kadha ni mfinyu, mfano ikiwa ni juu yake kulipa kadha ya siku tano na haikubakia hadi mwezi wa Ramadhani ila siku tano tu, inamlazimu afunge siku hiyo kwa tahadhari na afunge badala yake baada ya mwezi wa Ramadhani vilevile, na ikiwa wakati wa kadha sio mfunyu inabatilika saumu yake. 1044. Akibakia na janaba mpaka adhana ya Alfajiri katika saumu ya wajibu isiyokuwa saumu ya mwezi wa Ramadhani au kadha yake lakini sio kwa makusudi ikiwa saumu hiyo ni ya wajibu maalumu kwa wakati, mfano ikiwa aliweka nadhiri kufunga siku hiyo inasihi saumu yake na ikiwa siyo ya wajibu maalumu mfano saumu ya kafara basi kwa tahadhari ya sunna afunge badala ya siku hiyo siku nyingine 213
Al-Masailul Islamiyah 1045. Akitoharika mwanamke kutokana na hedhi au nifasi kabla ya adhana ya Alfajiri na akawa hajaoga kwa makusudi au ilikuwa wadhifa wake ni kutayamamu na akawa hajatayamam kwa makusudi inabatilika saumu yake katika mwezi wa Ramadhani bali na katika kadha na katika kila wajibu maalumu vile vile kwa tahadhari. 1046. Mwanamke ambaye anatoharika kutokana na hedhi au nifasi kabla ya adhana ya Alfajiri pia mwenye janaba ikiwa wakati hautoshi kwa kuoga, akitaka kufunga ni wajibu kwake kutayamamu na inasihi saumu yake kwa ilivyo na nguvu zaidi, ni sawa sawa ilikuwa ni saumu ya mwezi wa Ramadhani au ya wajibu maalumu au ya sunna. 1047. Akitoharika mwanamke kutokana na damu ya hedhi au nifasi kabla ya adhana ya Alfajiri na muda ukawa hautoshi sio kwa kuoga wala kutayamamu, au akajua baada ya adhana kwamba alishatoharika kabla ya adhana akitaka kufunga saumu ya wajibu maalumu kama vile saumu ya mwezi wa Ramadhani inasihi saumu yake, vivyo hivyo ikiwa saumu yake ni ya sunna au wajibu isiyo kuwa maalumu kama vile saumu ya kafara, inasihi saumu yake kwa kauli yenye nguvu zaidi. 1048. Akitoharika mwanamke kutokana na damu ya hedhi au nifasi baada ya adhana ya Alfajiri au akaona damu ya hedhi au nifasi katikati ya mchana inabatilika saumu yake hata kama imekaribia magharibi. 1049. Akisahau mwanamke kuoga josho la hedhi au nifasi na akakumbuka baada ya siku au zaidi inasihi saumu ya siku alizofunga 1050. Mwanamke mwenye istahadha akileta josho zilizotajwa katika hukumu za istihadha inasihi saumu yake. 1051. Mwenye kugusa maiti inajuzu kwake kufunga bila ya kuoga muogo wa kugusa maiti na akigusa maiti katika hali ya kufunga haibatiliki 214
Al-Masailul Islamiyah saumu yake.
KUPIGA BOMBA 1052. Kupiga bomba katika utupu wa nyuma kwa vitu vya maji maji inabatilisha saumu na hakuna kafara juu yake hata kama ni dharura au ilikuwa ni kwa ajili ya tiba, hakuna tatizo katika bomba isiyo ya maji maji japo ni bora kujiepusha nayo.
KUTAPIKA 1053. Akikusudia mfungaji kutapika hata kama akilazimika kwa ajili ya maradhi na mfano wake inabatilika saumu yake na hakuna kafara juu yake lakini akitapika kwa kusahau au bila hiyari yake inasihi saumu yake. 1054. Akiweza mfungaji kuzuia kutapika inalazimu ajizuie, ikiwa haitasababisha madhara au matatizo juu yake. 1055. Akiingia mbu au mfano wake katika koo lake lazima amtoe ikiwezekana na wala haibatiliki saumu yake, lakini akijua kumtoa kwake itamsababisha kutapika haimlazimu kumtoa na inasihi saumu yake. 1056. Akicheua na kikapanda kitu mpaka kwenye koo lake au mpaka kwenye kinywa chake ni wajibu akiteme nje na lau akimeza bila hiyari yake inasihi saumu yake lakini ikiwa hakijafika kwenye koo lake basi hakuna tatizo
HUKUMU YA VITENGUZI 215
Al-Masailul Islamiyah 1057. Akileta mfungaji moja ya vitenguzi kwa kusudi inabatilika saumu yake na hakuna tatizo kwayo ikiwa sio kwa makusudi, lakini akilala na janaba na ikawa hajaoga mpaka adhana ya Alfajiri inabatilika saumu yake. 1058. Mtu yeyote akiingiza kitu katika koo la mfungaji kwa lazima au akaingiza kichwa chake kwenye maji kwa kumteza nguvu haitabatilika saumu yake, lakini akilazimishwa kubatilisha saumu yake kama lau akiambiwa ikiwa huli chakula tutakudhuru kimali au kimwili akala kuepuka madhara inabatilika saumu yake. 1059. Inamlazimu mfungaji asiende sehemu ambayo anajua kwamba anaweza kulazimishwa kufungua na akifanya wakati huo kinachotengua saumu kwa kulazimishwa inabatilika saumu yake.
YALIYO MAKURUHU KWA MFUNGAJI 1060. Ni makuruhu kwa mfungaji kufanya mambo yafuatayo:1. Kuweka dawa kwenye macho 2. Kupaka wanja, kama ladha yake au harufu yake itafika hadi kwenye koo 3. Kufanya kila chenye kusababisha udhaifu kama vile kuumika au kujisaidia kwa wingi 4. Kuvuta ugoro “puani” ikiwa hajui kufika kwake hadi kooni, na kwa tahadhari ya wajibu ni kuacha hayo pamoja na kujua kuwa utafika hadi kooni 5 .Kunusa mimea yenye harufu (manukato) 6. Mwanamke kukaa ndani ya maji 7. Kuingiza vitu (vikavu) katika njia ya haja kubwa 8. Kuloanisha nguo ambayo iko mwilini 9. Kun’goa jino na kila ambacho kinasababisha kutoka damu mdomoni 10. Kupiga mswaki kwa mti mbichi 216
Al-Masailul Islamiyah 11 .Kutia maji mdomoni au kisichokuwa maji mdomoni bila ya sababu 12 .Kumbusu mke bila kusudi la kutoka manii 13 .Kitendo ambacho kinachosababisha kuamsha matamanio na ikiwa ni kwa kusudi la kutoka manii inabatilika saumu yake.
MAMBO AMBAYO NI WAJIBU KULIPA KADHA NA KUTOA KAFARA 1061. Mfungaji akikusudia kutapika au kuzama katika maji au kujipiga bomba kwa kitu cha maji maji mchana au akiwa na janaba usiku na akaamka kama tulivyoeleza katika Mas’ala yaliyotangulia, kisha akalala mara ya pili na akawa hajaamka mpaka adhana ya Alfajiri ni wajibu kwake kadha tu, na lau akileta kitenguzi kingine kwa makusudi ikiwa anajua kuwa jambo hili linabatilisha saumu yake ni wajibu kwake kadha na kafara, lakini kafara katika kukusudia kusema uongo juu ya Mwenyezi Mungu au Mtume na Ahlul- bait wake (as) ni katika upande wa tahadhari ya wajibu, na katika kukusudia kutapika au kuzama kwenye maji au kupiga bomba kwa kitu cha maji maji ni katika upande wa tahadhari ya sunna.
KAFARA ZA SAUMU 1062. Ambaye ni wajibu kutoa kafara ya saumu ya mwezi wa Ramadhani inamlazimu kumuacha mtumwa huru au afunge miezi miwili mfululizo au alishe maskini sitini au ampe kila mmoja miongoni mwao kibaba ( robo tatu ya kilo ) ya ngano au shairi au mfano wake, na ikiwa hataweza hivi vitu anakuwa na hiyari baina ya kufunga siku kumi na nane mfululizo au alishe mafukara kadri atakavyoweza, na ikiwa hakuweza kufunga wala kulisha ni wajibu kwake alete istighifari kwa Mwenyezi Mungu kwa kusema mara moja ( Astaghafiru llaahi) na kwa tahadhari ya wajibu atoe kafara atakapoweza na kupata uwezo wa kimali. 217
Al-Masailul Islamiyah
1063. Mfungaji akifanya jimai mara nyingi wakati wa mchana wa mwezi wa Ramadhani atatoa kwa kila mara kafara ikiwa amemwingilia kwa halali, ama ikiwa kumwingilia kwake ni haramu ni wajibu kwake kila mara atoe kafara zote tatu kwa pamoja. 1064. Akileta mfungaji kitenguzi kisichokuwa jimai kisha akamwingilia mke wake kwa tahadhari ya wajibu atoe kafara ya kila moja katika hayo. 1065. Akileta mfungaji kitendo cha halali ambacho kinabatilisha saumu kisichokuwa jimai, kama vile kunywa maji, kisha akaleta kitendo cha haramu kinachobatilisha saumu kisicho kuwa jimai pia, kama lau akila chakula cha haramu inamtosha kafara moja kwa yote. 1066. Akicheua mfungaji na kikapanda kitu mpaka mdomoni kwake, akikimeza makusudi inabatilika saumu yake na ni wajibu kwake kadha na kafara pamoja, na ikiwa kile kitu kinaharamishwa kuliwa kwake kama lau akicheua ikatoka damu mpaka mdomoni mwake kisha akameza damu kwa kusudi inabatilika saumu yake na ni wajibu juu yake kulipa kadha, na kwa tahadhari ya wajibu pia kutoa kafara ya kukusanya zote. 1067. Akiweka nadhiri ya kufunga siku maalumu akibatilisha saumu yake katika siku hiyo kwa makusudi ni wajibu wake amuache mtumwa huru au afunge miezi miwili mfululizo au alishe masikini sitini. 1068. Mfungaji akikusudia kubatilisha saumu yake kisha ukamtokea udhuru usiokuwa wa hiyari kama hedhi au nifasi au maradhi sio wajibu kwake kutoa kafara 1069. Akipata yakini kwamba ni mwanzo wa Ramadhani na akabatilisha saumu yake kwa kusudi kisha akabaini kwamba ilikuwa mwisho wa 218
Al-Masailul Islamiyah Shabani sio wajibu kwake kafara. 1070. Mfungaji akifanya jimai katika mwezi wa Ramadhani mke wake ambaye amefunga, ikiwa amemlazimisha katika kumwingilia ( yaani hakuwa radhi) ni wajibu kutoa kafara yake na kafara ya ( mke wake) pia, ama ikiwa alikuwa ameridhia kuingiliwa ni wajibu kwa kila mmoja atoe kafara yake. 1071. Mfungaji akikimwingilia mke wake ambaye amefunga katika mwezi wa Ramadhani hali akiwa amelala bila ya kuelewa ni wajibu kwake kafara moja na inasihi saumu ya mke na siyo wajibu kwake kulipa kadhaa wala kafara. 1072. Ambaye hafungi kwa ajili ya safari au maradhi haijuzu kwake kumlazimisha mke wake ambaye amefunga kufanya jimai, lakini akimlazimisha kumwigilia sio wajibu kutoa kafara. 1073. Ni wajibu kutozembea kutoa kafara lakini sio wajibu kufanya haraka. 1074. Ambaye analipa kadha ya saumu ya mwezi wa Ramadhani akikusudia kufanya kinachobatilisha saumu baada ya adhuhuri ni wajibu juu yake kulisha maskini kumi, kila maskini kibaba na akishindwa hivyo afunge siku tatu.
MAMBO AMBAYO NI WAJIBU KULIPA 219
Al-Masailul Islamiyah
KADHA YA SAUMU BILA KAFARA 1075. Ni wajibu kulipa kadha ya saumu bila kafara katika mambo yafuatayo:1. Akikusudia mfungaji kujitapisha au kuzama katika maji au kupiga bomba za sindano za maji maji mchana wa mwezi wa Ramadhani hakuna kafara ila katika upande wa tahadhari ya sunna. 2. Akiwa na janaba usiku wa mwezi wa Ramadhani na ikawa hakuzinduka katika usingizi wake mara ya pili mpaka adhana ya Alfajiri kwa namna ya mifano ambayo imepita katika mas’ala yaliyotangulia. 3. Ambaye hajafanya kinachotengua saumu lakini hakunuia saumu au amekusudia kutokufunga au anakusudia kufanya kinachobatilisha saumu - kwa tahadhari. 4. Kusahau kuoga janaba katika mwezi wa Ramadhani na akafunga pamoja na janaba siku moja au siku nyingi. 5. Mwenye kuleta kinachobatilisha saumu bila ya kuhakikisha kuwa ni asubuhi katika mwezi wa Ramadhani kisha akabaini kuingia kwa asubuhi ni wajibu kwake kulipa kadha ya siku hiyo, na vile vile mwenye kuleta kinacho batilisha saumu baada ya kuhakikisha kuwa ni asubuhi kwa kudhania kuingia asubuhi, bali hata mwenye kushuku kuingia kwa asubuhi baada ya kuhakiki na akaleta kinachobatilisha kisha akabaini kuingia kwa asubuhi ni wajibu kwake kulipa kadha 6. Mtu kupewa taarifa kutoingia asubuhi akaleta vinavyobatilisha kwa kauli ya mtoa habari kisha ikabainika kwake baada ya muda kwamba ilikuwa asubuhi. 7. Akipewa taarifa na mtu kuingia kwa asubuhi akawa hajaamini habari aliyopewa na mtoa habari au akachukulia kuwa mtoa habari ana mfa220
Al-Masailul Islamiyah nyia mzaha akaleta vinavyobatilisha kisha ikabainika kwake baada ya muda kwamba ilikuwa asubuhi. 8. Akifungua kipofu kwa kutegemea habari ya mtoa habari kisha akabaini kutoingia kwa magharibi. 9. Akiwa na yakini kuingia kwa magharibi katika anga safi kwa sababu ya giza akafungua kisha akabaini kwamba haikuwa imeingia magharibi, lakini akiwa na matumaini ya kuingia magharibi katika anga lilofunikwa kwa mawingu haimlazimu kulipa kadha pindi atakapofuturu kisha ikabainika kutoingia kwa magharibi. 10. Akiingiza maji katika mdomo wake kwa kuleta ubaridi au bila ya sababu yakaingia katika koo lake bila ya hiyari yake, na ama lau akisahu kwamba amefunga akameza maji au akasukutua kwa ajili ya udhu yakaingia maji katika koo lake bila hiyari yake hatolipa kadha. 1076. Akiingiza katika mdomo wake kitu kisichokuwa maji na kikaingia katika koo lake bila hiyari yake au akisukutua kwa maji yakaingia mpaka kwenye koo lake bila hiyari sio wajibu kwake kulipa kadha. 1077. Ni makuruhu kwa mfungaji kukithirisha kusukutua na akitaka kumeza mate yake baada ya kusukutua ni bora ateme mara tatu kisha ameze mate yake. 1078. Akipata shaka mfungaji je imeingia magharibi au laa , haijuzu kwake kufuturu, lakini akishuku je imekuwa alfajiri au laa, inajuzu kwake kufuturu baada ya kupata uhakika na kuchunguza
221
Al-Masailul Islamiyah
HUKUMU ZA SAUMU YA KADHA 1079. Kichaa akipona kichaa chake sio wajibu kwake kulipa kadha kwa yaliyompita katika saumu siku za kichaa chake. 1080. Akisilimu kafiri siyo wajibu kwake kulipa kadha ya saumu iliyompita katika siku za ukafiri wake, lakini lau akiritadi mwislam kisha akasilim baada ya kuritadi ni wajibu kwake kulipa kadha kwa yaliyompita katika saumu siku za kuritadi kwake. 1081. Ni wajibu kulipa kadha kwa yale yaliyompita katika saumu kwa sababu ya kulewa au kwa kutumia kwake kitu cha kulevya kwa ajili ya matibabu ya wajibu. 1082. Akifungua kwa siku nyingi kwa udhuru kisha akashuku wakati wa kuondoka udhuru ikiwa ni kutokana na uzembe ni wajibu kwake kwa tahadhari afunge siku nyingi zaidi kiasi cha kupata matumaini, mfano lau akisafiri kabla ya mwezi wa Ramadhani na wala hajui kwa uzembe, amerudi katika siku ya tano au ya sita katika mwezi wa Ramadhani, ni wajibu wake afunge siku sita kwa tahadhari, ama ikiwa hajui wakati wa kuondoka udhuru bila ya uzembe, inajuzu kwake alete kadha kwa uchache yaani siku tano, ingawa kwa tahadhari ya sunna alipe kadha ya nyingi zaidi yaani siku sita. 1083. Ikiwa ni wajibu alipe kadha ya Ramadhani nyingi na akawa hajaainisha katika nia kwamba anayoileta ni kadha ipi katika zile Ramadhani, inahesabika kuwa ni kadha ya Ramadhani ya kwanza. 1084. Inajuzu kwa mwenye kufunga kadha ya mwezi wa Ramadhani kufungua kabla ya adhuhuri ikiwa muda wa kadha sio mfinyu.
222
Al-Masailul Islamiyah 1085. Mtu akipitwa na saumu ya mwezi wa Ramadhani kwa ajili ya hedhi au nifasi au maradhi na akafa kabla ya kumalizika mwezi wa Ramadhani sio wajibu kulipiwa kadha kwa yaliyompita katika saumu ya mwezi huo. 1086 Akipitwa na saumu ya mwezi wa Ramadhani kwa ajili ya maradhi na yakaendelea maradhi yake mpaka Ramadhani nyingine haitomuwajibikia kulipa kadha kwa yale yaliyompita katika saumu ya mwezi huo, ni wajibu kwake ampe fakiri kwa kila siku kibaba cha chakula, yaani ngano au mkate wake au kibaba cha shairi au mkate wake, ama ikimpita saumu kwa ajili ya udhuru kama safari na ukaendelea udhuru wake mpaka Ramadhani nyingine inalazimu kwa tahadhari ya wajibu alipe saumu kwa siku ambazo zimempita na ampe fakiri kibaba kwa kila siku. 1087. Ugonjwa ukichukua miaka mingi ni wajibu kwake kulipa kadha ya Ramadhani ya mwisho tu baada ya kupona na atoe kibaba cha chakula kwa kila siku iliyopita katika miaka iliyopita, yaani ngano, shairi au mikate yake, tende au zabibu. 1088. Akichelewesha kadha ya saumu ya mwezi wa Ramadhani kwa miaka mingi ni wajibu kwake kulipa kadha na kutoa fidia moja kwa kila siku iliyompita. 1089. Akifungua katika mwezi wa Ramadhani kwa kusudi ni wajibu ailipe na afunge badala ya kila siku moja ( afunge) siku sitini au alishe mafakiri sitini au amuache mtumwa huru, na ikiwa hatolipa yaliyompita mpaka Ramadhani nyingine inamlazimu kutoa kibaba kingine badala ya kila siku ambayo hakufunga ukiongezea na kafara, na inamlazimu vile vile kulipa saumu zilizompita. 1090. Ni wajibu kwa mtoto mkubwa kulipa yale yaliyompita baba yake aliyefariki katika hali ya uhai wake katika saumu na swala kwa 223
Al-Masailul Islamiyah mujibu wa maelezo ambayo yamepita katika mas’ala yaliyotangulia, na vivyo hivyo amlipie mama yake baada ya kufariki kwake yale yaliyompita katika uhai wake katika saumu na swala , kwa tahadhari wajibu. 1091. Ikiwajibika kwa baba kulipa kadha ya saumu ambayo sio saumu ya mwezi wa Ramadhani, mfano saumu ya nadhiri, inamlazimu mtoto mkubwa kumlipia kwa tahadhari.
HUKUMU ZA SAUMU YA MSAFIRI 1092. Msafiri ambaye ni wajibu kwake kupunguza swala ni wajibu asifunge pia, na msafiri ambaye anakamilisha swala, mfano ambaye safari ni kazi yake au safari yake ni safari ya maasia, ni wajibu afunge. 1093. Hakuna mushikeli kusafiri katika mwezi wa Ramadhani lakini ni makuruhu kusafiri ikiwa ni kwa ajili ya kukimbia saumu. 1094. Ikiwajibika kwa mtu funga maalum isiyokuwa saumu ya mwezi wa Ramadhani kama vile saumu ya nadhiri maalum kwa wakati, basi ni lazima asisafiri katika siku hiyo maadamu halazimiki kusafiri -tahadhari ya wajibu - na akisafari ni lazima akusudie kukaa siku kumi na afunge kama inawezekana 1095. Akiweka nadhiri kufunga na akawa hajaainisha siku ambayo atafunga kwayo haijuzu kuileta akiwa safarini, lakini lau akiweka nadhiri kufunga siku maalumu katika safari basi lazima ailete katika safari, na vivyo hivyo akiweka nadhiri kufunga siku hiyo maalumu, ni sawa akiwa katika safari au hayuko safarini ni wajibu kufunga siku hiyo hata kama akiwa safirini.
224
Al-Masailul Islamiyah 1096. Inajuzu kwa msafiri kufunga sunna kwa siku tatu katika Mji wa Madinatul- munawara kwa kuomba haja. 1097. Kwa yule ambaye hajui kwamba safari inabatilisha saumu akifunga katika safari na katikati ya mchana akatambua hukumu, inabatilika saumu yake, na asipotambua mpaka magharibi inasihi saumu yake. 1098. Akisahau kwamba yeye ni msafiri au akasahau kwamba saumu ya msafiri ni batili na akafunga katika safari inabatilika saumu yake. 1099. Akisafiri mfungaji baada ya Adhuhuri ni wajibu akamilishe saumu yake, na akisafiri kabla ya Adhuhuri na akakusudia kukata masafa ya kisheria ( kama ilivyopita katika swala ya msafiri ) inalazimu kutengua saumu yake pindi anapofika katika mpaka wa kupunguzia ( yaani kutokuonekana kuta za mji na kutosikika adhana yake), na akibatilisha saumu yake kabla ya hapo ni wajibu kwake kafara kwa tahadhari ya wajibu. 1100. Akifika mfungaji kabla ya adhuhuri katika mji wake au sehemu ambayo anataka kukaa siku kumi hapo ikiwa hajaleta vinavyobatilisha saumu mpaka wakati huo ni wajibu afunge siku hiyo, na ikiwa ameleta vinavyobatilisha saumu sio wajibu kwake kufunga siku hiyo.
AMBAYE SIO WAJIBU KWAKE SAUMU 1101. Ikiwa hawezi kufunga saumu au saumu ina mletea matatizo kwa ajili ya uzee sio wajibu kwake kufunga, lakini inamlazimu kutoa kibaba cha chakula kwa maskini kwa kila siku kama yalivyotangulia maelezo yake. 1102. Yule ambaye hawawezi kufunga kwa ajili ya uzee akiweza na akapata upya uwezo wa kufunga baada ya mwezi wa Ramadhani inamlazimu alipe yale yaliyompita kwa tahadhari. 225
Al-Masailul Islamiyah 1103. Mwenye kiu ( ambaye anakuwa na kiu sana na hawezi kuvumilia kiu au inamletea matatizo sana) sio wajibu kwake saumu na inamlazimu kutoa badala ya kila siku kibaba cha chakula kwa fakiri, kwa mifano iliyopita maelezo yake na kwa tahadhari ya sunna asinywe maji kwa wingi ila kwa kiwango cha dharura na inamlazimu kulipa kadha kwa yaliyompita akiweza kufunga katika mwaka huo. 1104. Mwanamke anayenyonyesha mwenye maziwa machache, ni sawa awe ni mama wa mtoto au ameajiriwa au ananyonyesha bila malipo, ikiwa saumu inamdhuru au inamdhuru anaye nyonya sio wajibu kwake kufunga, na ni wajibu atoe kwa fakiri badala ya kila siku aliyofungua kibaba cha ngano au shairi au mikate yake, na ni wajibu alipe yaliyompita katika saumu akiweza kufunga katika mwaka huo, na akijitolea mwenye kunyonyesha mtoto bila ya malipo au akachukua ujira kwa baba wa mtoto au mama wa mtoto au mtu mwingine akitoa ujira wake sio wajibu kwa mama kumpa mnyonyeshaji mtoto, na kufunga. 1105. Mwanamke ambaye hawezi kufunga katika mwaka kwa sababu ya kubeba mimba au kunyonyesha wala hakuweza kulipa katika mwaka huo kwa sababu hiyo hiyo sio wajibu kwake kufunga wala kulipa kadha, ni wajibu kutoa kwa maskini kwa kila siku vibaba viwili vya chakula, kibaba baada ya mwezi wa Ramadhani na kibaba kingine mwisho wa mwaka, yaani kabla Ramadhani ya pili.
NJIA ZA KUTHIBITI MWANZO WA MWEZI 1106. Unathibiti mwanzo wa mwezi kwa mambo matano:1. Mtu mwenyewe kuuona mwezi mwandamo. 2. Kutoa habari ya kuonekana kwake watu ambao inapatikana yakini kutokana na maneno yao na vivyo hivyo kwa kila ambacho mtu 226
Al-Masailul Islamiyah anapata yakini kwa sababu yake. 3. Kupata habari kwa ( watu wawili) waadilifu kwamba wameona mwezi usiku, lakini wakihitalifiana katika wasifu wa mwezi hautothibiti mwanzo wa mwezi. 4. Kumalizika kwa mwezi uliotangulia wa shabani siku thelethini, hivyo unathibiti mwanzo wa mwezi wa Ramadhani na vivyo hivyo kwa miezi mingine. 5. Kiongozi wa kidini akitangaza kuonekana kwa mwezi. 1107. Akihukumu kiongozi wa sharia “Marja’a” kuthibiti mwanzo wa mwezi inalazimu kutekeleza hukumu yake hata kwa yule asiyemfuata, ikiwa hakuhukumu kiongozi mwingine kupinga. Lakini mwenye kujua kwamba kiongozi wa kisheria amekosea katika hukumu yake basi hawezi kufanya kwa mujibu wa hukumu ya kiongozi huyo. 1108. Hauthibiti mwanzo wa mwezi kwa utabiri wa wanasayansi na wanajimu, lakini mtu akipata yakini kwa sababu ya habari yao ni wajibu kufanya kwa mujibu wa habari yao. 1109. Ukithibiti mwezi mwandamo katika mji, haimaanishi kuthibiti kwa watu wa mji mwingie ila ikiwa miji miwili imekaribiana au ikijulikana kwamba anga lao ni moja.
SAUMU AMBAZO NI HARAMU NA MAKURUHU 1110. Inaharamishwa kufunga katika Iddil-fitiri na Idi Al- adhuha na vile vile inaharamishwa kufunga katika siku ya shaka kwamba ni mwisho wa shabani au ni mwanzo wa mwezi wa Ramadhani kama atafunga kwa nia ya mwanzo wa Ramadhani, na inaharamishwa kufun227
Al-Masailul Islamiyah ga katika siku za tashiriqi (mibano) kwa mwenye kuwa Minaa. 1111. Inaharamishwa kwa mwanamke kufunga sunna ikiwa hiyo ni katika kupoteza haki za mume wake na kwa tahadhari ya sunna asifunge sunna bila ya idhini yake hata kama hadhuru haki yake. 1112. Inaharamishwa kwa mtoto kufunga sunna ikiwa inaleta maudhi kwa wazazi wake au babu yake. 1113. Mwenye kujua kuwa saumu haimdhuru ni wajibu wake afunge hata kama akiambiwa na daktari kuwa saumu inamdhuru, na mwenye kuwa na yakini kwamba saumu inamdhuru au akadhani hivyo ni wajibu asifunge hata kama akiambiwa na daktari kwamba saumu haimdhuru na lau akifunga na hali ni hiyo saumu yake haitasihi
SAUMU YA SUNNA 1114. Ni sunna kufunga siku zote za mwaka ukiacha siku zilizotajwa ambazo ni haramu au makuruhu kufunga na imetiliwa mkazo kufunga baadhi ya siku ambazo ni: Siku ya Al hamisi katika mwanzo wa kila mwezi, Al hamisi ya mwisho na Jumatano ya kumi la kwanza la kila mwezi, na ikiwa hajafunga katika siku hizi ni mstahabu kwake alipe, ikiwa hatalipa kadha pia ni mstahabu atoe kwa fakiri badala ya kila siku - kibaba yaani gramu750 takribani - ya ngano au shairi au unga wake au mikate yake au 6/12 ya uzito wa fedha halisi – gramu moja na robo - na saumu ya siku ya kumi na tatu, kumi na nne na kumi na tano katika kila mwezi. Na saumu ya mwezi wa Rajab, Shabani na saumu ya siku ya Nairuzi na siku ya nne mpaka ya tisa katika mwezi wa shawwali na siku ya ishirini na tano na ishirini na tisa katika mwezi wa Dhil- qaad na siku ya kwanza mpaka ya tisa katika mwezi wa Dhil-hija ( siku ya Arafa) lakini ikiwa udhaifu unaosababishwa na saumu unamzuia kuleta dua siku ya Arafa ni 228
Al-Masailul Islamiyah makuruhu kufunga siku hiyo, na saumu ya Iddil-ghadiri ( 18 Dhilhija) na siku ya Mubahala ( 24 Dhil –hija) na siku ya kwanza, ya tatu na ya saba katika Muharam na siku ya kuzaliwa Mtume (saww) ( 17 Rabiul-Awwal) na saumu ya siku ya kumi na tano katika mwezi wa Jamaadul-ulaa na siku ya kupewa utume Mtume (saww ) 27 Rajab. 1115. Lau akijishughulisha kwa saumu ya mustahabu sio wajibu kwake kuitimiza mpaka magharibi, bali kama akialikwa na ndugu yake muumini kwenye chakula ni mustahabu kuitika wito wake na kufungua katikati ya mchana
SAUMU YA MAKURUHU 1116. Ni makuruhu kufunga siku ya Ashuraa na siku inayohisiwa kuwa ni Arafa au Iddul - Adhuha
WATU AMBAO NI SUNNA KUJIZUIA KULA 1117. Ni sunna kwa watu sita kujizuia kula katika mwezi wa Ramadhani hata kama hawafungi:1. Msafiri ambaye amekula safarini kisha akarudi kwenye nchi yake kabla ya Adhuhuri au akafika sehemu ambayo anataka kukaa hapo siku kumi. 2. Msafiri ambaye anafika katika nchi yake baada ya adhuhuri au sehemu ambayo anataka kukaa hapo kwa siku kumi. 3. Mgonjwa ambaye anapona kabla ya adhuhuri na akawa amekwisha kula kabla ya hapo. 4. Mgonjwa ambaye anapona baada ya adhuhuri, Mwanamke 229
Al-Masailul Islamiyah ambaye ametoharika katika damu ya hedhi au nifasi katikati ya mchana. 5. Kafiri ambaye anasilimu baada ya Adhuhuri. 1118. Ni sunna kwa mfungaji aswali magharibi na isha kabla ya kufuturu, lakini kama kuna mtu ambaye anamsubiri mezani au anashauku sana na chakula kiasi kwamba mawazo yake yote hayatakuwa kwenye swala ni bora afuturu kwanza, lakini afanye haraka kuswali kwa wakati wa fadhila kadri inavyowezekana.
HUKUMU ZA KHUMSI 1119. Khumsi ni wajibu katika vitu saba:1. Faida inayotokana na biashara 2. Madini 3. Kanzi 4. Mali ya halali iliyochanganyikana na mali ya haramu 5. Vito vya thamani vinavyotolewa baharini 6. Ngawira za vita 7. Ardhi anayoinunua kafiri dhimmiyi (aliye katika himaya ya dola ya kiislam) kwa mwislamu
Faida inayopatikana kutokana na biashara 1120. Ni wajibu kutoa khumsi katika ziada, baada ya kutoa matumizi ya mwaka mzima. 1121. Ni wajibu kutoa khumsi inapofikia kiwango maalum, itolewa moja ya tano 20%. 1122. Kiwango maalumu cha madini ya dhahabu ni gramu 68, fedha ni gramu 472 –kiwango hiki ni baada ya kutoa gharama zote. 230
Al-Masailul Islamiyah
1123. Ni wajibu khumsi igawanywe mafungu mawili:1. Fungu la maseyidi: Ni wajibu wapewe maseyidi maskini au maseyidi mayatima ambao ni mafukara au msafiri ambaye ni seyid. 2. Fungu la pili: ni la Imamu na katika zama hizi anapewa Mujitahidi ambaye ametimiza masharti au linatumika katika upande atakaotoa ruhusa litumike.
HUKUMU ZA ZAKA 1124. Zaka ni wajibu katika mambo tisa:1- Ngano 2 – Shairi 3 - Tende 4 - Zabibu 5- Dhahabu 6 - Fedha 7- Ngamia 8 -Ng’ombe 9 -Mbuzi na Kondoo
Masharti ya Zaka:1125. Zaka ni wajibu inapotimia kiwango maalum. Kiwango cha Ngano, Shairi, Tende na Zabibu ni kilo gram 847 na gram 207 baada ya kutoa gharama zote, na kiwango cha zaka yake ni 1/10 ikiwa imenyeshewa na mvua na kama imemwagiliwa zaka yake ni 1/20
Kiwango cha Dhahabu 1126. Dhahabu ina viwango viwili:1- Kiwango cha kwanza ni gram 72 na zaka yake ni 1/40. 2- Kiwango cha pili ni gramu 4/14 yaani zikiongezwa gram 4/14 katika gramu 72 ni wajibu kutoa 1/40 kutoka katika jumla ya gramu 4/86.
Kiwango cha Fedha 231
Al-Masailul Islamiyah
1127.Fedha ina viwango viwili:1. Mithiqal 105 ambayo ni sawa na gram 104 takribani na zaka yake ni 1/40. 2. Mithqal 21 ambayo ni sawa na gram 6/12 yaani inapoongezeka katika kiwango cha awali na zaka yake ni 1/40.
Zaka ya Ng’ombe, Ngamia, mbuzi na Kondoo 1128.Katika wanyama kuna masharti mawili:1- Wasifanye kazi kwa muda wa mwaka mzima. 2- Wawe wanakula majani mbugani wenyewe wasikatiwe majani na kulishwa.
Kiwango cha ngamia 1129. Kiwango cha kwanza ni ngamia watano zaka yake ni mbuzi mmoja. Kiwango cha pili ni ngamia kumi zaka yake ni mbuzi wawili. Kiwango cha tatu ni ngamia kumi na tano, zaka yake ni mbuzi watatu. Kiwango cha nne ni ngamia ishirini zaka yake ni mbuzi wanne. Kiwango cha tano ni ngamia ishirini na tano zaka yake ni mbuzi watano. Kiwango cha sita ni ngamia ishirini na sita na zaka yake ni ngamia ambaye ameingia mwaka wa pili. Kiwango cha saba ni ngamia thelathini na sita na zaka yake ni ngamia aliyeingia mwaka wa tatu. Kiwango cha tisa ni ngamia sitini na moja na zaka yake ni ngamia aliyeingia mwaka wa tano. Kiwango cha kumi ni ngamia sabini na sita na zaka yake ni ngamia wawili waloingia mwaka tatu. Kiwango cha kumi na moja ni ngamia tisini na moja zaka yake ni ngamia wawili walioingia mwaka wa nne. Kiwango cha kumi na mbili ni mia na ishirini na moja na kuendelea, hapo atahesabu arobaini arobaini na atatoa kwa kila ngamia arobani ngamia mmoja mwenye miaka mitatu au atahesabu hamsini hamsini na atatoa kwa kila ngamia hamsini ngamia mmoja mwenye miaka minne. 232
Al-Masailul Islamiyah
Kiwango cha Ng’ombe 1130. Kiwango cha kwanza ni ng’ombe thelathini na zaka yake ni ndama aliyeingia mwaka wa pili. Kiwango cha pili ni ng’ombe arobaini na zaka yake ni ndama aliyeingia mwaka wa tatu, idadi ikiwa zaidi ya viwango hivyo zitahesabiwa thelathini thelathini au arobaini arobaini na zaka yake ina tolewa kama tulivyotaja hapo juu.
Kiwango cha Mbuzi na Kondoo 1131.Kiwango cha kwanza ni mbuzi arobaini na zaka yake ni mbuzi mmoja. Kiwango cha pili ni mbuzi mia na ishirini na moja na zaka yake ni mbuzi wawili. Kiwango cha tatu ni mbuzi mia mbili na moja na zaka yake ni mbuzi watatu. Kiwango cha nne ni mbuzi mia tatu na moja na zaka yake ni mbuzi wanne.Kiwango cha tano ni mbuzi mia nne na kuendelea, hapa atahesabu mia mia na kila mia zaka yake ni mbuzi mmoja. Sio lazima kutoa zaka kutoka katika mbuzi wanaotolewa zaka bali inatosha kulipa kutoka kwenye mbuzi wake wengine au kutoa kiasi cha thamani kinacholingana na kima chake au kutoa kutoka katika aina nyingine. 1132. Wanaopewa zaka ni watu nane 1 – Fakiri 2 - Masikini naye ni ambaye hali yake ni mbaya zaidi kuliko fakiri 3- Anayekusanya zaka kwa amri ya Imamu au naibu wa Imamu 4-Wanaozoezwa nafsi zao nao ni:i) Makafiri ambao wakipewa zaka wanaelemea upande wa Uislamu au watawasaidia waislamu katika vita ii) Waislamu ambao nidhaifu wa imani 5- Kununulia watumwa na kuwaacha huru 233
Al-Masailul Islamiyah 6- Wenye madeni ambao wameshindwa kulipa 7- Katika njia ya Mwenyezi Mungu, katika mambo yenye manufaa kwa waislamu wote mfano, kujenga misikiti, shule, hospitali n.k 8- Msafiri ambaye ameishiwa na masurufu ya safari. 1133. Ni wajibu anayechukua zaka awe Shia Ithna Asharia, kama akitoa kitu kutoka katika zaka kwa yeyote kwa kuamini kuwa ni shia ni wajibu arudie kutoa zaka, isipokuwa kama atampa kutoka katika fungu la wanaozoezwa nyoyo zao.
Nia ya Zaka 1134. Ni wajibu kwa anayetoa zaka akusudie kujikurubisha kwa Allah (swt) pia ni wajibu kubainisha anachokitoa kuwa ni zaka ya mali au ni zaka ya Fitri. Lakini kama ikiwa ni wajibu wake kutoa zaka ya ngano au shairi hailazimu kuainisha kwamba anayotoa ni zaka ya ngano au shairi. 1135. Zaka ya fitri inakuwa wajibu kwa kila mtu ambaye ni baleghe, mwenye akili timamu, mwelewa na sio fakiri, kutoa yeye na (kumtolea) kila mmoja katika familia yake kilo tatu takriban kwa fakiri, za ngano, shairi, mtama n.k na kama akitoa thamani ya moja ya vitu hivi inatosha. 1136. Ambaye hamiliki chakula chake cha mwaka mzima na wala hana kazi ambayo inamuwezesha kupata chakula chake cha mwaka yeye na familia yake anahesabiwa kuwa ni fakiri na wala sio wajibu kwake zaka ya fitri. 1137. Ni wajibu kumtolea zaka ya fitri kila anayezingatiwa kuwa ni katika familia yake awe mdogo au mkubwa, mwislamu au kafiri, ni wajibu kumpa mahitaji yake au laa, awe anaishi katika mji wa mtoaji au laa. 234
Al-Masailul Islamiyah 1138. Ni wajibu kwa mwenyeji kumtolea zaka ya fitri mgeni anayekutembelea kabla ya magharibi kwa ridhaa yake.
Matumizi ya Zaka ya Fitiri 1139. Zaka ya fitiri inaweza kutumiwa katika moja ya mambo tuliyoyataja katika zaka ya mali.
Nia ya Zaka ya Fitiri 1140. Ni wajibu wakati wa kutoa zaka ya fitri kunuia nia ya kujikurubisha kwa Allah ( swt) na kutekeleza amri yake. 1141. Ikiwa mtu atatoa zaka ya fitri kabla ya mwezi wa Ramadhani haitasihi na kwa tahadhari asiitoe ndani ya mwezi wa Ramadhani, lakini kama akimkopesha fakiri mali kabla ya mwezi wa Ramadhani kisha ikamuwajibikia zaka ya fitri baadae inajuzu kuhesabia deni katika fitri.
HUKUMU ZA HIJA 1142. Hija ni wajibu kwa Muislamu mara moja katika maisha, ni wajibu wa haraka kwa mwenye uwezo. 1143. Hija ya kiislamu ni wajibu kwa masharti manne:1. Mtu awe amebaleghe, si wajibu kwa mtoto ambaye bado hajabaleghe lakini ni sunna kwa mtoto kuhiji akiruhusiwa na walii wake. 235
Al-Masailul Islamiyah
2. Awe mwenye akili, si wajibu kwa mwendawazimu. 3. Awe huru si wajibu kwa mtumwa, lakini ni sunna kwa mtumwa aende hija akiruhusiwa na walii wake. 4. Awe na uwezo na uwezo unamaanisha mambo yafuatayo:i) Awe na matumizi na nauli ya kutosha awe na uwezo wa kiafya ambao unamruhusu kuhiji. iii). Kusiwe na kizuizi njiani, muda uwe unatosha kufanya ibada ya hija. 1144. Ni sunna kwa asiyekuwa na uwezo wa kimali kuhiji. 1145. Ambaye hajatimiza masharti na akahiji katika hiyo hali, wajibu wa hija hautaondoka kwake bali ni wajibu ahiji atakapotimiza masharti. 1146. Hija ya kujitolea ni mtu kumuambia asiyemiliki kitu, mimi nitakupa matumizi yako na ya familia yako maadamu upo katika hija, wakati huo hija itakuwa wajibu kwake na kama atahiji katika hali hii itakuwa imemtosheleza kuhiji na sio wajibu tena kuhiji hata kama masharti yatatimia 1147. Aliyekuwa na uwezo katika miaka iliyopita kisha hakuhiji ni wajibu ahiji vyovyote itakavyowezekana hata kama amekosa uwezo. 1148. Si wajibu kwa mtu kuuza nyumba yake, kipando chake au vyombo vyake ili aende hija. 1149.Mwenye kuwa na mali ya kuhiji lakini hawezi kwenda hija kwa sababu ya uzee au maradhi basi ni wajibu kumpa mtu mwingine akahiji kwa niaba yake. 236
Al-Masailul Islamiyah
1150. Mtu akiweka nadhiri na akamuahidi Mwenyezi Mungu kwenda hija ni wajibu aende hija hata kama alishaenda hija kabla. 1151. Inajuzu katika hija ya sunna mtu anuie kwa niaba ya Mtume (saww) au Maimamu Maasumin (as) na wengineo waliokuwa hai au waliotangulia mbele ya haki na ataandikiwa thawabu za hija kama anavyoandikiwa aliyenuia hija kwa niaba yake. 1152. Mwanamke akitokwa na hedhi kabla ya ihramu, atahirimia katika hali hiyo na akitoharika kabla ya kusimama arafa atawajibika alete mambo ya umra, na kama hakutoharika mpaka muda wa kusimama arafa ni wajibu abadili na anuie, “Hija ya Ifradi� na atasimama arafa katika hiyo hali na kuleta matendo ya hija kisha analeta umra ya mufradi, vile vile mwanamke akitokwa na hedhi au akipatwa na nifasi baada ya Ihramu na kabla ya tawafu. 1153. Ikitokea tofauti baina ya shia na suni katika mwandamo wa mwezi kama haitawezekana kuleta mambo ya hija kutokana na mtizamo wa shia, basi itaruhusiwa kuleta kutokana na mtazamo wa suni na hija itasihi.
MIGAWANYO YA HIJA 1154. Hija imegawanyika sehemu tatu:1. Hija ya tamatui 2. Hija ya Qiraan 3. Hija ya ifraad 1155. Hija ya tamatui ni wajibu kwa aliye mbali na mji wa Makka kwa farsakha kumi na sita (16) au zaidi, hija ya Qiraan na hija ya Ifraadi 237
Al-Masailul Islamiyah ni wajibu kwa wanaoishi mji wa Makka na aliyembali na mji huo kwa chini ya farsakha 16. 1156. Ambaye wadhifa wake ni hija ya tamatui ni lazima alete umra kabla ya hija na ambaye wadhifa wake ni hija ya Qiraan au Ifraad ni lazima alete umra baada ya hija. Tofauti kati ya Qiraan na Ifraad ni kuwa mwenye kuhiji hija ya Qiraan anavaa ihram akiwa na mnyama wake, lakini mwenye kuhiji hija ya ifraad hawi pamoja na mnyama wake. 1157. Hija ya tamatui ina amali mbili:1. Umra tamatui 2. Na hija tamatui
UMRA TAMATUI 1158. Amali za umra tamatui ni tano nazo ni:1. Ihram 2 Kuzunguka ka’aba tukufu mara saba 3. Kuswali rakaa mbili za tawafu katika maqamu Ibarahim (as) au nyuma yake 4. Kukimbia “sa’ayi” baina ya safa na mar’wa mara saba. 5 Kupunguza nywele au ndevu au kukata kucha.
HIJA TAMATUI 1159. Hija tamatui ina amali kumi na tatu:1. Ihram 2. Kusimama arafa 3. Kusimama mash’ari - muzdalifa” 4. Kurusha mawe Aqaba - Mina 238
Al-Masailul Islamiyah 5.Kuchinja mnyama - Mina 6.Kunyoa au kupunguza nywele- Mina 7. Tawafu ya ziara 8. Rakaa mbili za swala ya tawafu ya ziara 9. Sa’ayi “kukimbia” kati ya safa na marwa 10. Tawafu nisaa 11. Rakaa mbili za tawafu nisaa 12.Kulala Mina usiku wa kumi na moja, kumi na mbili na wakati mwingine ni wajibu kulala usiku wa kumi na tatu pia. 13. Kurusha mawe katika sehemu tatu Mina siku ya kumi na moja, kumi na mbili na siku ya kumi na tatu kama akilala Mina.
AMALI ZA UMRA Ihram 1160. Ihram ni amali ya kwanza katika amali za umra tamatui, wakati wa ihram kwa ajili ya umra tamatui ni katika miezi ya hija (mfungo mosi, mfungo pili na mfungo tatu).
MIQAATI (VITUO) 1161. Sehemu ya kuvalia ihramu huitwa Miqati na miqati ni moja ya sehemu zifuatazo:1. Masjidi Shajara ni kituo cha watu wa Madina 2. Waadil aqiq ni kituo cha watu wapitao njia ya Iraki 3. Qurnul maanazil ni kituo cha watu wanaopita kutoka Twaif 4. Yalamlam ni kituo cha watu wanaopita kutoka Yemen 5. Al – Juhfa ni kituo cha watu wa Misri na Sham (Syiria na 239
Al-Masailul Islamiyah Jodan). 1162. Ni wajibu kwa kila mtu ahirimie katika kituo chake kama tulivyotaja na inasihi kwa mtu kuhirimia kabla ya kufika katika kituo kwa kuweka nadhiri.
VITU VILIVYO WAJIBU KATIKA IHRAM 1153.Vilivyowajibu katika ihram ni vitu vitatu:1. Nia: Anuie hivi (Nahirimia kwa ajili ya umra tamatui kwa kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu) ,na maana ya kuhirimia ni kujilazimisha kuacha vitu ambavyo tutavitaja baadae. 2. Tal- biya (wito): alete tal- bia nne kama ifuatavyo: “Labaika Allahumma labaika, labaika laa sharika laka labaika, innalhamda wa niamata laka wal - mulku, laa sharika laka�. 3. Kuvaa nguo mbili: Ni wajibu kwa wanaume, na si kwa wanawake, japokuwa ni kwa tahadhari ya sunna kwa mwanamke angalau mwanzo tu. 1164. Ni wajibu nguo hizo ziwe tohara na zisiwe za hariri wala ngozi ya mnyama ambaye ni haramu na zisiwe nyepesi kiasi kwamba mwili unaonekana.
YALIYO WAJIBU KUJIEPUSHA WAKATI WA IHRAM 1165. Ni wajibu kwa aliyevaa Ihram kujiepusha na vitu ishirini na nne:1. Kuwinda mnyama wa nchi kavu au kumsaidia anayewinda, kula windo au kuchinja ila ikiwa ni wanyama wakali wa porini 240
Al-Masailul Islamiyah ambao inaruhusiwa kujilinda nao kutokana na madhara. 2. Kuwakaribia wanawake kwa kuwaingilia au kubusu au kuwaangalia kwa matamanio. 3. Kuoa au kuozesha au kuwa shahidi. 4. Kujitoa manii kwa mkono (punyeto) au kitu chochote. 5. Kutumia manukato kama miski, zafarani au udi, kwa kula, kunusa, kujipaka mafuta n.k, pia ni haramu kuziba pua kutokana na harufu inayokarahisha. 6. Kuvaa nguo zilizoshonwa kwa wanaume, lakini inajuzu kuvaa kimkoba cha kuhifadhia fedha hata kama kitakuwa kimeshonwa. 7. Kupaka wanja. 8. Kujitazama katika kioo. 9 Kuvaa soksi kwa mwanaume au chochote kinachofunika mguu. 10. Kufanya ufuska yaani kusema uongo, matusi au kujifakharisha. 11. Kujadili – kuapa nayo ni kusema (laa wallaahi) – hapana wallah na kwa tahadhari ya wajibu ni kujiepusha na viapo kabisa. 12. Kuuwa wadudu kama viroboto, kunguni, chawa n.k. 13. kuvaa pete kwa kukusudia kuwa ni pambo. 14. Kutokuvaa mapambo kwa ujumla kama kujipaka hina au kuvaa bangili, hereni, isipokuwa kama anavivaa muda wote . 241
Al-Masailul Islamiyah
15. Kufunika kichwa chote au sehemu ya kichwa au sikio kwa wanaume bali ni haramu hata kujistiri kwa hina. 16. Mwanamke kusitiri uso wake kwa kitambaa kizito. 17. Kujipaka mafuta. 18 Kung’oa nywele kichwani au sehemu nyingine ya mwili hata kama ni unywele mmoja na hakuna tatizo kama nywele zitadondoka wakati wa udhu. 19. Kujitoa damu hata kama kwa kupiga mswaki. 20. Kung’oa jino hata kama damu haitatoka. 21. Kukata kucha. 22. Kujifunika mwavuli kwa wanaume wakati wa kutembea lakini hakuna tatizo kujifunika nyumbani. 23. Kukata mti au kun’goa mmea katika haram tukufu. 24. kubeba silaha kama bunduki au panga n.k.
KAFARA YA VITU VILIVYO HARAMISHWA KATIKA IHRAM. 1166. Vitu ishirini na nne vilivyoharamu katika ihram vimegawanyika katika sehemu tatu:1. Vilivyo haramu na ukivifanya kunawajibisha kafara tu. 2. Vilivyo haramu na ukivifanya hakuwajibishi kafara. 3. Vitu ambavyo kuvifanya kwake kunabatilisha hija na tunataja baadhi ya kafara kwa muhtasari 1167. Kafara ya vitu vilivyoharam katika ihram:242
Al-Masailul Islamiyah 1. Kafara ya kuwinda imeelezwa kwa kirefu katika ibada ya hija. 2. Kafara ya kufanya jimai ni kutoa ngamia au ng’ombe au kondoo kama ilivyoelezwa kwa ufafanuzi zaidi katika ibada ya hija. 3. Kafara ya kufunga ndoa kama mwanaume atamwingilia mwanamke ni ngamia kwa mwenye kufunga ndoa. 4. Kafara ya kufanya punyeto ni kama kafara ya kumwingilia mwanamke, na katika baadhi ya hali inabatilisha hija. 5. Kafara ya kutumia manukato ni kondoo. 6. Kafara ya kuvaa nguo iliyoshonwa ni kondoo. 7. Kafara ya kujipaka wanja ni kondoo. 8. Kafara ya kumtazama mwanamke ni kondoo. 9. Kafara ya kuvaa soksi ni kondoo. 10.Kafara ya ufuska ni kuomba msamaha. 11.Kafara ya kujadiliana ni ngamia au ng’ombe au kondoo. 12.Kafara ya kuua chawa ni kutoa sadaka ya kulisha maskini. 13. Kafara ya kujipamba ni kondoo kwa tahadhari. 14. Kafara ya kuvaa pete ni kondoo. 15. Kafara ya kufunika kichwa kwa wanaume ni kondoo. 16. Kafara ya mwanamke kufunika uso ni kondoo. 17. Kafara ya kujipaka mafuta ni kondoo. 18. Kafara ya kunyoa nywele ni kondoo au kufunga siku tatu au kulisha maskini sita. 19. Kafara ya kujitoa damu ni kondoo. 20. Kafara ya kung’oa jino ni kondoo. 21. Kafara ya kukata kucha ni kondoo wawili. 22. Kafara ya kujifunika mwavuli kwa wanaume ni kondoo. 23. Kafara ya kukata mti au kung’oa mmea wa haram ni ng’ombe au kondoo. 24. Kafara ya kuvaa silaha ni kondoo.
2. TAWAFU
243
Al-Masailul Islamiyah
1168. Mwenye kuhiji ataingia Makka baada ya kuhirimia umra na ataleta amali ya pili ya umra ambayo ni kuzunguka ka’aba tukufu. 1169. Namna ya kutufu: Kaaba iwe mkono wake wa kushoto na kuzunguka pembeni mwake mara saba na aanzie katika jiwe jeusi na amalizie hapo. 1170. Katika tawafu mambo yafuatayo ni sharti:1. Nia, atie nia kuwa anatufu 2. Tohara kutokana na hadathi kubwa kama vile janaba, hedhi, nifasi na hadathi ndogo yaani awe na udhu 3. Tohara ya nguo na mwili 4. Mwanaume awe ametahiriwa 5. Kustiri uchi na ni wajibu kwa mwenye kujistiri yale yote ambavyo ni wajibu kwa mwenye kujistiri katika swala 6. Tawafu: Iwe kati ya ka’aba tukufu na maqamu Ibrahimu 7. Jiwe la Ismaili liwe ndani ya tawafu 8. Mwili wote uwe nje ya ka’aba.
3. SWALA YA TAWAFU 1171. Amali ya tatu ni kuswali swala ya tawafu katika maqamu Ibarahim au nyuma yake. 1172. Swala ya tawafu ni kama swala ya asubuhi na unatia nia ya kuswali swala ya tawafu.
4. SA’I
244
Al-Masailul Islamiyah 1173. Amali ya nne katika amali za umra ni sa’i yaani kukimbia baina ya safa na mar’wa mara saba, na katika sehemu hii ni wajibu kwa mwenye kuhiji akate masafa kati ya safa na mar’wa mara saba kwa kuanzia safa na kumalizia mar’wa. 1174. Kutoka safa kwenda mar’wa inahesabika kuwa ni mzunguko mmoja, na kurudi kutoka mar’wa kwenda safa ni mzunguko mwingine. 1175. Nia ya kukimbia sa’i.
5 - KUNYOA AU KUPUNGUZA 1176. Baada ya kukamilisha Sa’i ni wajibu kuleta amali ya tano ambayo ni kupunguza nywele. 1177. Kupunguza: Inamaanisha kukata sehemu ya nywele za kichwa au kukata kucha. 1178. Baada ya kunyoa, vitu vilivyokuwa haramu kwa ajili ya ihramu vitakuwa halali ila viwili amabvyo uharamu wake ni kwa ajili ya utukufu wa haram navyo ni :1. kuwinda 2. kukata mti au kung’oa mmea wa haram.
UMRA YA MUFRAD 1179. Akitaka mtu kuleta umra peke yake atafanya amali mfano wa amali ya umra tamatui, lakini ataongeza tawafu nisai na swala ya tawafu nisai.
AMALI ZA HIJA TAMATUI 245
Al-Masailul Islamiyah 1180.
1. Kuhirimia Hija
Mambo ya hija ni kumi na tatu kama tulivyosema na amali ya kwanza ni kuvaa Ihramu, ni juu ya mwenye kuhiji baada ya kukamilisha mambo ya umra, ahirimie mara ya pili kwa ajili ya hija, na tofauti ni kuwa kuhirimia umra inakuwa katika moja ya vituo tulivyovitaja na kuhirimia hija inakuwa Makka na ni sunna iwe katika msikiti mtukufu. 1181. Wakati wa kuhirimia hija ni baada ya kumaliza umra tamatui mpaka wakati wa kusimama arafa.
2. KUSIMAMA ARAFA 1182. Amali ya pili katika amali za hija ni kusimama Arafa, yaani awe katika uwanja wa Arafa kuanzia adhuhri katika siku ya Arafa (siku ya tisa) mpaka kuzama kwa jua. 1183. Anuie katika kisimamo hiki.
3. KUSIMAMA KATIKA MASH’ARI “MUZDALIDA” 1184. Ni wajibu kwenda Mash’ari baada ya kutoka Arafa baada ya kuzama jua na awepo katika Mash’ari tangu mapambazuko ya Al-fajiri mpaka kuchomoza kwa jua katika siku ya Idd ambayo ni siku ya kumi. 1185. Inapokaribia kuchomoza kwa Al fajiri katika hiyo siku ni wajibu mwenye kuhiji anuie na kusimama katika mash’ari.
4 – 6 AMALI ZA MINA. 246
Al-Masailul Islamiyah
KUTUPA MAWE, KUCHINJA NA KUNYOA 1186. Ni wajibu kwenda Mina baada ya kuchomoza jua katika siku ya Idd na kufanya amali tatu:1. Kurusha mawe katika Aqaba (nayo ni jamaratul kubra) kwa mawe saba madogo kwa taratibu moja baada ya jingine 2. Kuchinja ngamia au ng’ombe au kondoo 3. Kunyoa kichwa chote au kupunguza, kama hija yake ni ya kwanza kwa tahadhari ya sunna anyoe kichwa chote.
7 – 11 – AMALI ZA MAKKA. 1187. Baada ya kukamilisha amali za Mina mwenye kuhiji anaweza kwenda Makka siku hiyo hiyo ya Idd na kufanya amali tano:1.Tawafu ya ziara mara saba 2. Rakaa mbili za tawafu ya ziara kwenye maqamu Ibrahimu au nyuma yake 3. Sa’i “kukimbia” baina ya safa na mar’wa 4. Tawafu nisai, nayo ni kama tawafu ya hija 5. Rakaa mbili za tawafu nisai.
12. – KULALA MINA 1188. Ni wajibu kwa mwenye kuhiji kulala Mina siku ya kumi na moja, kumi na mbili na ya kumi na tatu pia, na kiwango cha wajibu kulala mina ni nusu ya usiku kuanzia mwanzo wake au mwisho wake, na inajuzu kujishughulisha na ibada Makka badala ya kulala mina. 1189. Kama mwenye kuhiji hakulala ni wajibu atoe kafara kwa kila siku kondoo na atahesabika ameasi akiacha kulala mina japokuwa hija yake ni sahihi. 247
Al-Masailul Islamiyah
13. KUTUPA MAWE 1190. Ni wajibu kwa mwenye kuhiji kutupa mawe sehemu tatu katika mchana wa siku alizolala mina, yaani siku ya kumi na moja, kumi na mbili na siku ya kumi na tatu kama akilala mina, atatupa mawe saba katika nguzo ya kwanza, mawe saba nguzo ya katikati mawe saba na jamratul aqaba mawe saba, na kwa kufanya hivi atakuwa amekamilisha amali za hija.
HUKUMU ZA NDOA 1191. Ni wajibu katika ndoa ya daima na ndoa ya muda kusoma swigha “tamko” la ndoa na wala haitoshi kuchukuana kwa kuelewana, ama wanaooana wasome wenyewe au waweke wakili atakayesoma kwa niaba yao. 1192. Na wakili sio sharti awe mwanaume bali inajuzu awe mwanamke kwa kumuwakilisha mwanaume au mwanamke. 1193. Haijuzu kwa mwanamke na mwanaume kuangaliana kama mume na mke mpaka wapate yakini kuwa wakala wao tayari ameshafunga ndoa, na dhana haitoshi. 1194.Inajuzu kwa mtu mmoja kusoma swigha ya ndoa kwa pande zote mbili au kusoma swigha kwa niaba ya mwanamke kwa kujiozesha mwenyewe, iwe katika ndoa ya daima au ya muda, lakini ni bora kufanya tahadhari kwa kuwakilishwa na watu wawili.
Namna ya kufunga ndoa ya daima 1195. Ikiwa wenye kuoana watasoma swigha wenyewe basi mwanamke atasema baada ya kubainishwa kiwango cha mahari “zawajtuka nafsiy alaa swadaqil maalum” Nimekuozesha nafsi yangu kwa mahari 248
Al-Masailul Islamiyah maalumu), kisha mwanaume aseme haraka “Qabitu nikaaha” (Nimekubali kuoa). Kama waoaji watawakilishwa katika kufunga ndoa, kama jina la mwanamke ni Fatma na jina la mwanaume ni Ahmad basi wakili wa mwanamke atasema: Zawwajtuka muwakilatiy Fatwimah muwakilaka Ahmad alaswadaaqil maalum “Nimemuozesha wakala wangu Fatma wakala wako Ahmad kwa mahari maalum”, kisha wakili wa mwanaume atasema haraka Qabiltu nikaha limuwakiliy Ahmad “Nimekubali nihaha kwa niaba ya wakala wangu Ahmadi kwa mahari maalumu”.
Namna ya kufunga ndoa ya muda. 1196.Kama wanaooana watafunga ndoa wenyewe, basi mwanamke atasema baada ya makubaliano ya mahari na muda: Zawajtuka nafsiy fiyl mudatil maalumati wa alaa swadaqil maalum “Nimekuozesha nafsi yangu kwa muda maalum na kwa mahari maalumu”, kisha mwanaume atasema haraka: Qabiltu “nimekubali”, na ndoa inasihi, na kama wataweka wakala basi wakala wa mwanamke atasema: Zawajtu muwakilatiy muwakilaka fiy mudatil maalumati wa alaa swadaqil maalum“Nimemuozesha wakala wangu, wakala wako kwa muda maalumu na kwa mahari maalum”, kisha wakala wa mwanaume atasema haraka: Qabiltu nikaha limuwakiliy “Nimekubali ndoa kwa niaba ya wakala wangu”, ndoa inasihi. 1197. Masharti ya ndoa:Ndoa ifungwe kwa lugha ya kiarabu kwa kutamkwa kwa usahihi na kama wanaooana hawajui kiarabu, basi waweke mtu wa kufunga ndoa kwa niaba yao anayefahamu kiarabu vizuri, na kama haitawezekana kabisa, basi ifungwe kwa lugha yeyote, lakini ni wajibu waseme maneno yanayo maanisha: “Nimekuozesha na nimekubali” katika lugha yao. Ni wajibu ndoa ifungwe kwa kusoma swigha kwa pande mbili, kwamba mwanamke akusudie kwa kusema: “Nimekuozesha nafsi 249
Al-Masailul Islamiyah yangu kwamba nimekuwa mke wako, na mwanaume akusudie kwa kusema: Nimekubali nikahi� nimeridhia hayo. Wanaofunga au wanaofungisha ndoa wawe wamebaleghe. Kama wakala atafungisha ndoa ni lazima ataje majina ya wanaooana. Wanaooana wawe wameridhia kuoana, kama mwanamke akilazimishwa kukubali katika dhahiri, lakini ikajulikana kuwa ameridhia moyoni ndoa inasihi. 1198. Kama atakosea kutamka hata herufi moja ndoa itabatilika kwa tahadhari kwamba itabadilisha maana yake. 1199. Kama mtu atamuozesha mwanamke kwa mawanaume bila ya ridhaa yao, kisha wakaridhia baadae kwa kutamka, ndoa inasihi. 1200. Binti aliyebaleghe ambaye anaelewa masilahi yake kama akitaka kuolewa, naye ni bikira ni bora achukue idhini kwa baba yake au kwa babu yake kwa upande wa baba na wala sio lazima kuchukua idhini kwa mama yake au kwa kaka yake. 1201. Kama baba na babu hawapo na binti sio bikira basi sio lazima kupata idhini kwa baba au kwa babu wa upande wa baba tu.
Kasoro ambazo inajuzu kuvunja ndoa kwa ajili yake 1203. Kama mwanaume atajua baada ya ndoa kuwa mke ana moja kati ya kasoro hizi inajuzu kuvunja ndoa:Wazimu Ukoma Mbalanga 250
Al-Masailul Islamiyah Upofu Kiwete Njia ya mkojo na ya hedhi kuwa ni moja au sehemu ya haja kubwa na njia ya hedhi kuwa moja Kuota mfupa au nyama ndani ya uke na unazuia jimai Kama mwanamke atajua kuwa mume wake amekatika uume au hana nguvu za kiume au amehasiwa basi inajuzu kuvunja ndoa. 1204. Mume akivunja ndoa kwa moja ya kasoro tulizozitaja basi ni wajibu watengane bila ya talaka. 1205.Mwanamke akivunja ndoa kwa sababu mume wake hana nguvu za kiume, basi ni wajibu kwa mume kumpa nusu ya mahari, lakini kama mwanaume au mwanamke akivunja ndoa kwa moja ya aibu tulizozitaja, kama hawajaonana kimwili sio wajibu kwa mwanaume kumpa mwanamke chochote, na kama atamwingilia basi ni wajibu ampe mahari yote.
Wanawake ambao ni haramu kuwaoa 1206. Ni haramu kuoa wanawake ambao ni mahramu mfano, mama, binti, dada, mama mkwe, shangazi, mama mkubwa au mdogo, bibi, mjukuu, binti wa dada yako mke wa baba, na mke wa mtoto wako. 1207. Ukioa mwanamke kisha ukamwingilia basi, binti wa mke wako, binti wa binti wa mke wako na binti wa mtoto wa kiume wa mke wako wanakuwa ni mahramu wako na ni haramu kuwaoa. 1208. Haijuzu kuoa binti ambaye ni mchumba wa mtu mwingine maadam bado anamafungamano naye. 1209. Wafuatao ni maharimu wa mwanaume: Shangazi wa baba yake, mama mkubwa au mama mdogo wa baba yake, shangazi wa babu yake, shangazi wa mama yake, mama mkubwa au mama mdogo wa mama yake, shangazi wa bibi yake, mama mkubwa au mdogo wa 251
Al-Masailul Islamiyah bibi yake. 1210. Wafuatao ni maharimu wa mwanamke: Mkwe, babu ambaye ni mzazi wa wa baba mkwe, mtoto wa mume wake na mtoto wa mtoto wa mume wake, wawe wamezaliwa au bado. 1211. Haijuzu kuoa binti wa dada wa mke na binti wa kaka yake bila ya idhini ya mke, lakini akioa bila ya idhini ya mke wake na baadaye akatoa idhini basi ndoa itasihi. 1212. Mtu akizini na shangazi na mama mkubwa au mdogo kabla ya kumuoa binti wa shangazi au mama, basi haijuzu tena kumuoa huyo binti. 1213. Mtu akimuoa binti wa shangazi au wa mama mkubwa au mdogo na kabla ya kumwingilia akazini na shangazi au na mama mkubwa au mdogo ni bora achukue tahadhari ajitenge nae. 1214.Mtu akizini na mwanamke ni bora achukue tahadhari asimuoe binti wa huyo mwanamke aliyezini naye, kama mtu akioa mwanamke kisha akamwingilia na baada ya hapo akazini na mama mkubwa, basi mke wake hatakuwa haramu, japo ni bora atengane naye bila ya talaka. 1215.Haijuzu mwanamke wa kiislamu kuolewa na kafiri, mkristo, myahudi au asiyekuwa hao. Haijuzu kwa mwislamu kuoa mwanamke kafiri, lakini inajuzu kuoa mwanamke wa kikristo au wa kiyahudi ndoa ya daima au ya muda. 1216.Kama atazini na mwanamke ambaye yuko kwenye eda ya talaka rejea basi mwanamke huyo atakuwa haramu kwake, na akizini na mwanamke ambaye yuko katika eda ya ndoa ya muda au katika eda ya kufiwa basi inajuzu baada ya hapo kumuoa. 252
Al-Masailul Islamiyah
1217. Mtu akizini na mwanamke ambaye hana mume wala hayupo katika eda inajuzu kumuoa, lakini ni bora achukue tahadhari ya kusubiri mpaka huyo mwanamke aone damu ya hedhi kisha amuoe. 1218. Ni haramu kuoa mwanamke akiwa katika eda. 1219. Mtu akijua kuwa mwanamke huyu ana mume pamoja na hivyo yeye akamuoa, basi ni wajibu watengane na asimuoe tena. 1220. Mtu akizini na mwanamke mwenye mume basi huyo mwanamke hatakuwa haramu kwa mume wake hata kama hatatubu, japo ni bora kwa mume wake ampe talaka lakini ni wajibu ampe mahari yake yote. 1221. Mtu akimlawiti kijana basi mama wa huyo kijana, dada yake na binti yake wanakuwa ni haramu kwa mwenye kulawiti 1222.Mtu akimlawiti mtu baada ya kumuoa mama yake au dada yake au binti yake basi mke wake hatakuwa haramu kwake. 1223. Mtu aliyehirimia hija kisha akaoa hali ya kuwa amehirimia ndoa inabatilika, kama alikuwa anajua kuwa ndoa katika hali ya Ihramu ni haramu pamoja na hivyo akaoa basi mwanamke huyo atakuwa haramu kwake milele. 1224. Ni haramu kuoa ukiwa katika hali ya Ihramu. 1225.Mwanaume kama hatafanya tawafu nisai katika hija basi mke wake atakuwa haramu kwake, na vile vile mwanamke kama hatafanya tawafu nisai mume wake atakuwa haramu kwake, lakini wakifanya hiyo tawafu uharamu utaondoka.
253
Al-Masailul Islamiyah 1226. Mwanamke akipewa talaka tatu anakuwa haramu kwa mume wake, lakini akiolewa na mume mwingine kisha akaachika au huyo mume wake akifa, basi inajuzu aolewe na mume wake wa kwanza.
Hukumu za ndoa ya daima 1227. Mwanamke aliyeolewa ndoa ya daima haruhusiwi kutoka ila kwa idhini ya mume wake, ni wajibu asimkatalie mume wake anapotaka kustarehe naye, na asimnyime unyumba bila ya sababu ya kisheria, na akimtii mume wake katika hilo, basi ni wajibu kwa mume wake kumpatia chakula, mavazi na sehemu ya kukaa (nyumba), na kama mwanaume hatamtimizia hayo itakuwa ni deni awe na uwezo au laa. 1228. Kama mwanamke akimnyima unyumba, basi hastahiki mavazi na nyumba, lakini mahari atapewa. 1229. Haijuzu kwa mwanaume kumlazimisha mke wake kufanya kazi za nyumbani. 1230. Mwanamke ambaye anamtii mume wake lakini hatoi matumizi, basi inajuzu kwake katika hali hii achukue matumizi katika mali ya mume wake bila ya idhini yake ikiwa anajiweza, lakini kama hajiwezi basi sio wajibu kumtii mume wake wakati wa kutafuta riziki. 1231. Sio wajibu kwa mwanaume kulala kwa mke wake usiku katika kila siku siku nne. 1232. Haijuzu kwa mwanaume kuacha kumwingilia mke wake zaidi ya miezi minne. Ikiwa ni mmoja kwa shahiri 1233. Kama mahari haijabainishwa wakati wa kufunga ndoa, ndoa itasihi, na mwanaume kama atamwingilia basi ni wajibu ampe mahari. 1234. Kama wakati wa kufunga ndoa hawatabainisha muda wa kulipa 254
Al-Masailul Islamiyah mahari ya mke, basi inajuzu kwa mke kumnyima unyumba mume wake mpaka apewe mahari, sawa sawa mwanaume awe na uwezo au laa, lakini mke akiridhia kumpa unyumba kabla ya kupewa mahari basi haijuzu kwake tena kumnyima unyumba baada ya hapo bila ya udhuru wa kisheria.
Ndoa ya mut’a “Muda� 1235. Ni kwa tahadhari ya wajibu usiache kuonana kimwili na mke wa muda zaidi ya miezi minne. 1236. Mke wa ndoa ya muda hana haki ya kupewa matumizi hata kama amebeba mimba ya mume wake. 1237. Mke wa muda hana haki ya kumtaka mume wake kulala kwake kama ambavyo hamrithi mume wake na mume pia hamrithi mke. 1238. Mke wa ndoa ya muda kama hajui kuwa hastahiki kupata matumizi na hastahiki kumtaka mume wake kulala kwake ndoa itasihi, na haimlazimu mume wake chochote kwa sababu ya kutokujua kwake. 1239. Inajuzu kwa mke wa muda kutoka bila ya ruhusa ya mume wake, lakini kama kutoka kwake kutasababisha haki za mume wake kupotea itakuwa ni haramu kutoka bila ruhusa. 1240. Mke wa ndoa ya muda kama atazawadiwa na mume wake muda uliobakia, basi ni wajibu apewe mahari yote waliyoafikiana na hii ni kama amemwingilia, na kama hajamwingilia atampa nusu ya mahari. 1241. Inajuzu kwa mwanaume kufunga ndoa ya daima na mke wake wa ndoa ya muda kabla ya muda wa ndoa ya muda kwisha, pia anaweza kumuoa kwa mara ya pili ndoa ya muda, akiwa katika eda ya ndoa ya muda ya kwanza. 255
Al-Masailul Islamiyah
Hukumu za kuangalia 1242. Ni haramu kwa mwanaume kuangalia mwili wa mwanamke ajinabiya, pia ni haramu kuangalia mwili wa binti ambaye umri wake haujatimia miaka tisa, lakini anatambua baya na zuri, ni haramu kuangalia hata nywele zake na kwa mwanamke pia ni haramu kuangalia mwili wa mwanaume ajinabii. 1243. Hakuna tatizo kwa mwanaume kuangalia uso na viganja vya mwanamke wa kikristo na wa kiyahudi. 1244. Ni wajibu kwa mwanamke kusitiri mwili wake pamoja na nywele zake kwa mwanaume ajinabii, na kwa tahadhari asitiri mwili wake kwa mtoto wa kiume ambaye hajabalehge lakini anaelewa kizuri na kibaya. 1245. Ni haramu kuangalia uchi wa mwingine, hata uchi wa mtoto anayetambua zuri na baya, lakini mume na mke inajuzu kwao kuangaliana mwili mzima. 1246. Ni wajibu kwa mwanaume asiangalie mwili wa mwanaume kwa matamanio, na mwanamke asiangalie mwili wa mwanamke kwa matamanio. 1247. Katika hali ya dharura inajuzu kwa nesi kumchoma sindano mwanamke mwenzake au mwanaume ambaye sio mume wake, au kusafisha uchi wa mwanamke mwenzake au uchi wa mwanume ambaye sio mume wake, na kama akitaka kugusa uchi wa mwanaume ni wajibu avae glovsi katika viganja vyake halafu aguse au apige sindano au asafishe. 1248. Katika hali ya dharura inajuzu kwa mwanaume kumtibu mwanamke ajinabiya kwa kumwangalia mwili wake au kumgusa, lakini kama 256
Al-Masailul Islamiyah anaweza kumtibu bila ya kumwangalia au kumgusa ni lazima asimwangalie au asimguse. 1249.Yeyote akilazimika kumtibu mwingine kuangalia uchi wake na hakuna njia nyingine ila kuangalia uchi basi hakuna tatizo katika hilo.
Mas’ala katika ndoa 1250. Anayeogopa kufanya haramu kwa sababu hajaoa basi ni wajibu aoe. 1251. Mume akiweka sharti katika ndoa kuwa mke awe bikra, kisha ikabainika kuwa hana bikra basi inajuzu kwake kuvunja ndoa. 1252. Ni haramu kwa mwanamke na mwanaume kukaa faragha katika sehemu ambayo hakuna uwezekano wa mtu mwingine kuingia, sawa sawa wawe katika ibada, katika maongezi mengine au wamelala au wako macho, lakini ikiwa kuna uwezekano wa kuingia mtu mwingine hakuna tatizo. 1253. Kama mwanaume atabainisha mahari wakati wa ndoa, lakini katika nia yake hatompa hiyo mahari, ndoa itasihi lakini ni wajibu atoe hiyo mahari. 1254. Mwislamu ambaye anakanusha kuwepo Allah au Nabii au siku ya mwisho au hukumu katika hukumu za wajibu kama vile swala na saumu, na anajua kuwa ni katika wajibu wa dini basi atakuwa ni murtadi. 1255. Mwanamke akiritadi kabla ya kuingiliwa na mume wake basi ndoa yake itabatilika, na kama ataritadi baada ya kuingiliwa naye amekoma kutokwa na damu ya hedhi pia ndoa itabatilika, lakini kama hajakoma kutokwa damu ya hedhi ni wajibu akae eda, na kama atasilimu kabla ya muda wa eda kwisha ndoa yake haitabatilika, na 257
Al-Masailul Islamiyah akibakia katika kuritadi kwake mpaka muda wa eda ukaisha basi ndoa inabatilika. 1256. Mwanaume aliyezaliwa katika uislamu akirtadi mke wake anakuwa haramu kwake, na ni wajibu kwa mwanamke akae eda ya kufiwa ambayo ni miezi mnne na siku kumi. 1257. Mwanaume ambaye hajazaliwa katika uislamu kisha akasilimu, halafu akaritadi kabla hajamwingilia mke wake basi ndoa inabatilika, na kama ataritadi baada ya kumwingilia mke wake, kama mke wake atakuwa katika umri wa kupata damu ya hedhi basi ni wajibu wake akae eda ya kufiwa, na kama mume wake atasilimu kabla ya muda wa eda haujaisha basi ndoa haibatiliki, la sivyo inabatilika 1258. Mwanamke akiolewa akiwa na binti wa mume mwingine, basi mume wake wa pili anaweza kumuozesha huyo binti kwa kijana wake wa mke wake mwingine, vile vile akimuozesha kijana wake binti basi yeye anaweza kumuoa mama wa binti huyo. 1259. Kama mwanamke akizini kisha akapata mimba haijuzu kuitoa hiyo mimba. 1260. Kama mwanaume atazini na mwanamke asiyeolewa wala hana eda, kama atamuoa baada ya hapo kisha akazaliwa mtoto na hawajui kuwa ni wa halali au ni wa haramu atakuwa ni mtoto wa halali. 1261. Kama mtu akioa mwanamke na hajui kuwa yuko katika eda au laa, na mwanamke naye hajui, kisha akazaliwa mtoto atakuwa ni wa halali kisheria, lakini kama mwanamke anajua kuwa yuko katika eda basi mtoto atakuwa ni wa huyo mwanaume kisheria, lakini ndoa itakuwa ni batili. 1262.Mwanamke akisema nimekoma kutokwa na damu ya hedhi au akisema mimi sina mume, kauli yake itakubaliwa, lakini kama atakuwa anatuhumiwa kwa uongo itabidi ufanyike uchunguzi. 258
Al-Masailul Islamiyah
1263. Mwanaume akioa kisha akaambiwa huyo mwanamke ana mume na akasema mimi sina mume na kama haijathibiti kisheria kuwa alikuwa na mume basi ni wajibu kauli ya mwanamke ikubaliwe. 1264. Haijuzu kwa baba kumtenganisha binti yake na mama yake kabla hajatimiza miaka saba, na kwa mtoto wa kiume kabla hajatimiza miaka miwili. 1265. Binti akibaleghe tu ni sunna kufanya haraka kumuozesha kwani Imamu Swadiq (as) amesema: “Katika maisha mazuri ya mtu asitoke hedhi binti yake nyumbani kwake�. 1266. Kama mwanamke ataelewana na mume wake asipewe mahari ili mume wake asioe mwanamke mwingine basi ni wajibu kwa mwanamke asiombe mahari, na ni wajibu kwa mwanaume asioe mwanamke mwingine. 1267.Mtoto wa zinaa akioa na akapata mtoto atakuwa ni mtoto wa halali. 128. Mwanaume akimwingilia mke wake katika mwezi wa Ramadhani au katika hedhi atakuwa ameasi na kupata dhambi, lakini mtoto atakayezaliwa kutokana na hicho kitendo atakuwa ni wa halali. 1269.Mwanamke akipata yakini kuwa mume wake amefariki safarini na baada ya eda ya kufiwa akaolewa, kisha akarudi mume wake wa kwanza kutoka safarini, ni wajibu watengane na mume wa pili na atakuwa halali kwa mume wake wa kwanza, lakini kama mume wa pili alisha mwingilia ni wajibu kwa mwanamke baada ya kutengana akae eda, na mume wa pili ampe mahari yote, lakini sio wajibu kwa mume wa pili kumpa matumizi akiwa katika eda.
259
Al-Masailul Islamiyah
HUKUMU ZA TALAKA 1270. Ni sharti kwa mwanaume anayetoa talaka kwa mke wake, awe amebaleghe, awe na akili timamu, awe na hiyari, na kama atalazimishwa kutoa talaka, basi talaka itakuwa batili, ni sharti pia kukusudia talaka kama atasema swigha ya talaka kwa mzaha haitasihi. 1271. Ni sharti wakati wa kutoa talaka mke awe ametoharika kutokana na damu ya hedhi na damu ya nifasi na mume wake asiwe amemwingilia katika hiyo tohara 1272. Talaka ya mke inasihi akiwa katika hali ya hedhi na nifasi katika mambo matatu yafuatayo:Kama mume hajamwingilia baada ya ndoa. Akijua kuwa ana mimba na kama hajajua kuwa ana mimba akamtaliki katika hali ya kuwa na hedhi kisha baadae ikabainika kuwa alikuwa na mimba, basi ni bora arudie talaka kwa mara nyingine Kama mume akiwa mbali na mke akawa hajui kuwa ametoharika kutokana na damu ya hedhi na nifasi au laa. 1273. Kama atampa mke wake talaka kwa kudhania hana hedhi, kisha ikabainika baadaye kuwa alikuwa na hedhi wakati wa kupewa talaka basi talaka itakuwa batili, na kama atatoa talaka kwa kudhania kuwa ana hedhi lakini ikabainika baadae kuwa alikuwa tohara basi talaka inasihi, anayejua kuwa ana hedhi au nifasi kisha akasafiri na akataka kumpa talaka akiwa safarini ni wajibu asubiri atoharike kutokana na hedhi au nifasi katika muda wake wa kawaida kisha atamtaliki akitaka. 1274. Mwanaume akitaka kumpa talaka mke wake asiyepata hedhi kwa ajili ya maradhi ni wajibu asimwingilie kwa muda wa miezi mitatu 260
Al-Masailul Islamiyah tangu alipomwingilia kisha ampe talaka. 1275. Talaka ni lazima iwe kwa lugha ya kiarabu na isikilizwe na wanaume wawili waadifilifu, kama mume mwenyewe akitaka kusoma swigha ya talaka na jina la mke ni Fatma ni wajibu aseme “Zaujatiy Faatwimat twaaliq”, na kama ataweka wakala ni lazima wakala aseme “Zaujatu Muwakily twaaliq” 1276. Mwanamke wa ndoa ya muda hana talaka bali kutoka kwa mume wake ni kumalizika kwa muda wa ndoa au azawadiwe muda uliobaki, kwa mume kusema “wahabtukil- mudah”, na wala sio lazima ishuhudiwe na mashahidi wawili na wala sio sharti asiwe na hedhi.
Eda ya Talaka 1277. Binti ambaye hajatimia miaka tisa na mwanamke ambaye amekoma kutokwa damu ya hedhi hawana eda, na mume wake kama atamwingilia kisha akampa talaka basi inajuzu kuolewa baada ya kupewa talaka bila ya kukaa eda. Lakini haijuzu kumwingilia binti mdogo. 1278. Mwanamke ambaye anapata hedhi akipewa talaka ni wajibu akae eda yaani akipata hedhi mara tatu eda inaisha, lakini akipewa talaka kabla hajaingiliwa basi hakai eda anaweza kuolewa tu baada ya kupewa talaka. 1279. Mwanamke ambaye haoni damu yake ya hedhi na ana umri wakupata hedhi akipewa talaka na mume wake ni wajibu akae eda kwa muda wa miezi mitatu. 1280. Mwenye mimba akipewa talaka eda yake inaisha akijifungua tu au kwa mimba kuharibika mfano kama akipewa talaka kisha akajifungua baada ya saa eda inaisha. 261
Al-Masailul Islamiyah
Eda ya ndoa ya muda 1281.Mwanamke ambaye aliolewa ndoa ya muda, muda ukiisha eda yake ni kuona hedhi mbili na mwanamke ambaye hapati hedhi ni kwa tahadhari ya wajibu asiolewe kwa muda wa siku arobaini na tano.
Eda ya mwanamke ambaye amefiwa na mume 1282. Eda ya mwanamke ambaye amefiwa na mume ni miezi minne na siku kumi. 1283. Ni haramu kwa mwenye eda kuvaa nguo zenye mapambo, kupaka wanja na kila aina ya mapambo.
Talaka ya bain na talaka rejea 1284. Talaka ya baain ikishatolewa haijuzu kwa mwanaume kumrejea mke wake bila ya ndoa mpya. 1286. Talaka ya baain imegawanyika sehemu tano:Talaka ya binti ambaye hajatimia miaka tisa Talaka ya mwanamke ambaye amekoma kutokwa damu ya hedhi Talaka ya mke ambaye hajaingiliwa baada ya ndoa Talaka ya kujivua na mubaraati Talaka ya mke aliyepewa talaka tatu. 1287. Talaka rejea ni talaka ambayo inajuzu kwa mwanaume kumrejea mke wake akiwa katika eda bila ya kufunga ndoa upya. 262
Al-Masailul Islamiyah
Hukumu za talaka rejea 1288. Mwanaume anaweza kumrejea mke wake kwa njia mbili:Atamke kauli inayomaanisha kuwa amemrejea Afanye kitendo kinachoonyesha kuwa amemrejea. 1289. Mwanaume akimpa talaka mke wake talaka tatu na alikuwa anamrejea katika talaka ya kwanza na ya pili au alimwacha mara mbili kisha akamuoa upya baada ya kila talaka anakuwa haramu kwake mpaka aolewe na mwanaume mwingine, kama akipewa talaka na mume wa pili inakuwa halali kumuoa baada ya hapo kwa masharti yafuatayo:Mume wa pili amuoe ndoa ya daima. Mume wa pili amwingilie kimwili na ni bora atokwe na manii. Mume wa pili amtaliki au afe. Eda ya talaka ya mume wa pili au eda ya kufiwa ya mume wa pili imalizike.
Talaka ya kujivua 1290. Talaka ya kujivua ni mwanamke kumpa mume wake mali ili apewe talaka. 1291. Mume mwenyewe akitaka kusoma swigha ya talaka basi atasema “Zaujatiy Fatwimah khaala’atuha a’laa maa badhalat”
Talaka ya mubaraati 1292. Talaka ya mubaaraati ni mume na mke kuchukiana wote, basi mke atampa mume wake mali ili apewe talaka. 263
Al-Masailul Islamiyah 1293. Kama mume mwenyewe atampa talaka basi atasema “Baaraatu zaujatiy Fatwimah a’ala mahariha fahiya twaliqu” 1294. Ni wajibu mali anayoichukua mume katika talaka ya mubaaraati isizidi mahari, lakini hakuna tatizo kama itazidi katika kujivua.
Mas’ala katika eda na talaka 1295. Mwanaume akizini na mwanamke ajinabiya kwa dhana kuwa ni mke wake ni wajibu kwa mwanamke akae eda. 1296. Mwanaume akizini na mwanamke na anajua kuwa sio mke wake sio wajibu kwa mwanamke kukaa eda, iwe amejua kuwa mwanaume sio mume wake au amedhania kuwa ni mume wake. 1297. Mwanaume akimhadaa mke wa mtu apewe talaka ili yeye amuoe na mwanamke akafanya hivyo na mume wake akampa talaka, basi talaka na ndoa zitasihi, lakini mume aliyemuoa na mwanamke watapata dhambi kubwa sana. 1298. Mwanamke ambaye mume wake amepotea na anataka kuolewa na mume mwingine ni wajibu arejee kwa mujitahidi mwadilifu au wakala wake na kufanya kulingana na maoni yake.
Hukumu za kujivua na mubaaraati 1299.Talaka ya mubaaraati ni kama talaka ya kujivua katika hukumu zote ila katika mambo matatu:Chuki katika mubaarati inakuwa katika pande zote mbili lakini katika kujivua chuki inakuwa kwa mwanamke tu. Ni lazima mali anayoichukua mwanaume katika mubaraati isizidi 264
Al-Masailul Islamiyah mahari lakini katika talaka ya kujivua inaweza ikazidi mahari. Mwanaume akitoa talaka ya mubaaraati kwa lafdhi ya mubaaraati basi ni kwa tahadhari ya sunna baada ya “Baar’atuki” aseme haraka “Faanti twaaliqu” kinyume na talaka ya kujivua.
HUKUMU ZA KUCHINJA MNYAMA NA KUMUWINDA KWAKE 1300. Akichinjwa mnyama ambaye ni halali kuliwa katika njia ambayo tutaitaja baadae, nyama yake itakuwa halali na mwili wake ni tohara awe wa porini au wa nyumbani. 1302. Mnyama aliyeingiliwa na mtu au mnyama aliyezoea kula vinyesi vya watu asipotoharishwa kisheria nyama yake haitakuwa halali baada ya kuchinjwa. 1303. Akiwinda wanyama wa porini ambao nyama zao ni halali kama vile swala, au mnyama ambaye nyama yake ni halali ambaye alikuwa wa nyumbani kisha akawa wa porini kama ng’ombe, ngamia wa nyumbani akikimbia atakuwa ni tohara na halali, lakini wanyama wa nyumbani kama mbuzi, kuku wa nyumbani na wanyama halali wa porini wanao fugwa nyumbani hawawi tohara wala halali kwa kuwindwa. 1304. Wanyama wa porini ambao ni halali kuliwa wanakuwa tohara au halali kwa kuwindwa wanapokuwa na uwezo wa kukimbia au kuruka, hivyo kifaranga cha ndege hakiwi halali kama hakiwezi kuruka au mtoto wa swala hawi halali kama hawezi kukimbia. 1305. Mnyama ambaye ni halali kuliwa na asiyekuwa na damu inayotoka kwa kasi kama samaki, akijifia atakuwa tohara lakini haijuzu kuliwa . 265
Al-Masailul Islamiyah 1306. Mnyama ambaye ni haramu kuliwa kama nyoka hawawi halali kwa kuchinjwa lakini mzoga wake ni tohara. 1307. Mnyama akizaa mtoto amekufa au akitolewa tumboni amekufa ni haramu kula nyama yake.
NJIA YA KISHERIA YA KUCHINJA 1308. Njia ya kisheria ya kuhalalisha mnyama ni kukata mishipa minne chini ya shingo na haitoshi kukata kidogo bali ni wajibu kuikata kwa ukamilifu. 1309. Akikata baadhi ya mishipa minne kisha akasubiri hadi akafa kisha akamalizia mishipa mingine hata kama hajasubiri kwa muda mpaka kufa kwa mnyama huyo akawa hajakata mishipa kwa mfuatano kama ilivyozoeleka, kama atakata mishipa iliyobaki kabla ya kufa kwa mnyama atakuwa ni halali, lakini kwa tahadhari ya sunna ni kujiepusha na huyo mnyama. 1310. Mbwa mwitu akikata shingo ya mbuzi kiasi kwamba mishipa minne haijabaki ambayo ni wajibu kuikata wakati wa kuchinja, huyo mnyama atakuwa haramu, lakini kama akikata baadhi ya shingo au sehemu nyingine na mishipa minne ikawa imebakia nyama yake inakuwa tohara na halali kama atachinjwa kisheria.
MASHARTI YA KUCHINJA 1311. Kuchinja kisheria kuna masharti matano:Mchinjaji awe ni muislamu, mwanaume au mwanamke asiye dhihirisha uadui kwa watu wa nyumba ya Mtume na kama atakuwa ni mtoto wakiislamu anayejua zuri na baya inajuzu kuchinja. 266
Al-Masailul Islamiyah Achinjwe mnyama kwa kisu kikali, kama hakitapatikana na mnyama akataka kufa bila kuchinjwa inajuzu atumie kitu chochote kikali kama chupa, jiwe n.k. Amuelekeze kibla wakati wa kuchinja yaani (uso wa mnyama, mikono, miguu na tumbo vielekezwe kibla na kama hakumuelekeza kibla kwa kukusudia nyama itakuwa haramu, lakini akisahau au akiwa hajui au akiwa hajui upande wa kibla au hakuweza kumwelekeza mnyama kibla hapatakuwa na tatizo akimchinja katika hali hizi. Akitaka kuchinja au kuweka kisu shingoni ataje jina la Mwenyezi Mungu kwa nia ya kuchinja na inatosha kusema “Bismaillah” na akitaja jina la Mwenyezi Mungu sio kwa nia ya kuchinja, mnyama hatatoharika na nyama yake itakuwa haramu, na vile vile kama hakutaja jina la Mwenyezi Mungu kwa kutojua lakini hakuna tatizo kwa aliyesahau. Ajitikise mnyama angalau mtikisiko mdogo baada ya kuchinjwa, mfano kupepesa jicho, kutikisa mkia au miguu yake.
NJIA YA KISHERIA YA KUCHINJA NGAMIA 1312. Akitaka kumhalalisha ngamia ili awe tohara na halali ni wajibu kwa kuongezea kuzingatia masharti yaliyo tangulia katika kuchinja ataingiza kisu au kinachofanana na kisu katika “luba” nayo ni sehemu ya juu iliyoingia ndani ambayo imekutana na shingo na hii inaitwa “nahri”, kudunga inalazimu kumuelekeza kibla yaani uso wake uelekee kibla. 1313. Ni bora wakati wa kumdunga ngamia awe amesimama na hakuna tatizo kama atakuwa amelala kwa ubavu ila aelekee kibla. 14. Kama atachinjwa ngamia badala ya nahri au ikatumika nahri kwa 267
Al-Masailul Islamiyah mbuzi au ng’ombe badala ya kuchinjwa nyama zitakuwa ni haramu na mwili utakuwa ni najisi, lakini akikata mishipa ya ngamia kisha akatumia njia ya nahri kwa njia tuliyoitaja nyama yake itakuwa halali na mwili wake utakuwa tohara ,na pia mbuzi au ng’ombe ikitumika njia ya nahri na kabla ya kufa ikakatwa mishipa minne nyama zitakuwa ni halali na miili yao itakuwa ni tohara. 1315. Mnyama akiwa mkaili na ikashindikana kuchinjwa kwa njia iliyotajwa kisheria au akiangukia kisimani kiasi kwamba anataka kufa huko na haikuwezekana kumchinja kisheria, inajuzu kumjeruhi katika sehemu yeyote ya mwili ili afe kwa sababu ya jeraha ,na atakuwa halali na haimlazimu kumuelekeza kibla lakini lazima azingatie masharti mengine tuliyoyataja katika kuchinja.
MAMBO YA SUNNA WAKATI WA KUCHINJA 1316. Ni sunna katika kuchinja mambo yafuatayo:1. Ni sunna katika kumchinja mbuzi amfunge mikono yake miwili na mguu mmoja ama ng’ombe, ni sunna kumfunga mikono miwili na miguu pia na anauacha mkia, ama ngamia ni sunna kumfunga mikono na kwa ndege ni sunna amuache baada ya kumchinja ili afurukute. 2. Mwenye kuchinja aelekee kibla. 3. Ampe mnyama maji kabla ya kumchinja. 4. Asimtese mnyama, anoe kisu chake vizuri na afanye haraka kumchinja na asimuonyeshe kisu kabla ya kuanza kumchinja.
YALIYO MAKURUHU WAKATI WA KUCHINJA 1317. Ni makuruhu katika kuchinja mambo yafuatayo:1. Kukata mishipa kuanzia kisogoni 2. Kutenganisha kichwa cha mnyama na mwili kabla ya kutoka kwa roho, lakini akifanya hivyo kwa kughafilika, au kwa sababu kisu ni 268
Al-Masailul Islamiyah kikali mno na bila yakutarajia hivyo haitakuwa makuruhu 3. Kumchuna mnyama kabla ya kutokwa na roho 4. Kukata nyama yake kabla ya kutokwa na roho 5. Kumchinja mnyama na mwingine anamwangalia 6. Kumchinja mnyama usiku au mchana kabla jua halijapetuka katika siku ya ijumaa, hakuna tatizo wakati wa dharura na haja 7.Mfugaji kumchinja mnyama aliyemlea mwenyewe.
HUKUMU ZA KUWINDA KWA SILAHA 1318. Akiwinda mnyama wa porini aliye halali kuliwa kwa silaha, nyama yake inakuwa halali na mwili wake unakuwa tohara kwa masharti matano:Silaha ya kuwindia iwe ni yenye kukata kama vile kisu, panga au kitu kikali kama mshale ambao makali yake yanakata mwili wa mnyama, mtu akiwinda kwa kutumia mtego au fimbo au jiwe na mengineyo na mnyama huyo akafa kwa ajili hiyo, hatatoharika na nyama yake itakuwa ni haramu. Na kuwinda kwa silaha za moto kama vile bunduki kama risasi yake ina makali ya kuweza kuchana mwili wa mnyama basi huyo mnyama atakuwa tohara na nyama yake pia ni halali, na kama silaha haina makali kiasi kwamba inaingia kwenye mwili wa mnyama kwa nguvu na kumuua, kwa dhahari ni halali lakini akimuunguza kwa joto lake na akafa kwa sababu hiyo utohara wake na uhalali wake ni mahali pa mushikeli. Ni wajibu muwindaji awe muislamu au mtoto wa muislamu mwenye kutofautisha kati ya zuri na baya, na pindi anapowinda kafiri au mwenye uadui na watu wa nyumba ya Mtume (saww) mnyama huyo 269
Al-Masailul Islamiyah hatakuwa halali. Atumie silaha ya kuwindia na kama atarusha risasi sehemu pasina kukusudia kupiga mnyama kisha akapiga mnyama bila ya kutegemea mnyama hatakuwa halali na pia hatokuwa tohara. Ataje jina la Mwenyezi Mungu wakati wa kutumia silaha na asipotaja jina la Mwenyezi Mungu kwa kukusudia mnyama huyo hatakuwa halali, lakini akisahau hakuna tatizo. Akute mnyama ameshakufa au amkute akiwa hai na wakati wa kuchinja ukawa mfinyu, kama muda ulikuwa unamruhusu kuchinja halafu akaacha kumchinja mpaka akafa nyama yake itakuwa ni haramu. 1319. Wakishirikiana watu wawili katika kuwinda mmoja muislamu na mwingine ni kafiri na mmoja akataja jina la Mwenyezi Mungu na mwingine hakutaja kwa makusudi huyo mnyama hatakuwa halali. 1320. Akiwinda kwa silaha au mbwa wa wizi windo litakuwa ni halali kwake, lakini atakuwa ameasi na ni wajibu wake atoe ujira kwa mwenye silaha au mbwa. 1321 Akiwinda kwa upanga au mfano wake akawa amemkata mnyama vipande viwili na kwa kuzingatia masharti, na mnyama akakatika vipande viwili na kikabaki kichwa na shingo kwa kujitenga na mwili, akikuta amekufa atakuwa halali vipande vyote na vile vile akimkuta hai lakini hakupata wakati mpana wa kumchinja, ama wakati wa kuchinja ukiwa mpana na ikawezekana kumchinja, basi kipande kilichojitenga na kichwa kitakuwa haramu, na upande wenye kichwa utakuwa halali kama atamchinja kisheria, la sivyo huo upande pia uatakuwa haramu.
270
Al-Masailul Islamiyah 1322. Akiwinda mnyama na akamchinja na wakakuta tumboni mwa mnyama kuna mtoto mfu, kama amekamilika kimaumbile na akawa ameota manyoya au sufi na ikawa kifo cha mtoto kimesababishwa na kuchinjwa kwa mnyama huyo, mtoto atakuwa tohara na halali.
KUWINDA KWA KUTUMIA MBWA 1323. Mbwa akiwinda mnyama wa porini ambaye nyama yake ni halali utohara na uhalali wa huyo mnyama utatimia kwa masharti sita:1. Mbwa awe amefundishwa kiasi kwamba akitumwa anaenda na akiambiwa simama anasimama na ikawa ni kawaida yake kiasi kuwa hawezi kula kabla ya kufika mwenyewe na hakuna tatizo akimla mnyama bila kutarajia 2. Atumwe na mwenyewe kushika mnyama na kama mbwa akiondoka kushika mnyama bila ya kuamrishwa na mwenyewe huyo mnyama atakuwa haramu. 3. Na anayemtuma mbwa awe ni muislamu au mtoto wa muislamu mwenye kutofautisha kati ya kheri na shari, na kama anayemwamrisha ni kafiri au ana chuki na watu wa nyumba ya Mtume (saww) windo la huyo mbwa litakuwa haramu. 5. Ataje jina la Mwenyezi Mungu pindi anapomwamuru mbwa na kama ataacha kutaja jina la Mwenyezi Mungu kwa kukusudia hilo windo litakuwa haramu na kama atakuwa amesahau haitakuwa na mushikeli. 6. Mnyama afe kwa sababu ya kujeruhiwa na meno ya mbwa kama atamnyonga mnyama au akifa kwa kukimbia au kuogopa hatakuwa halali 7. Mwenye kumtuma mbwa amkute amekufa au akimkuta hai wakati wa 271
Al-Masailul Islamiyah kuchinja ukawa ni mfinyu, kama wakati ukiwa unatosha kumchinja mfano, amkute akiwa anapepesa macho yake au kutikisa mkia au miguu kama hatomchinja mpaka akafa hata kuwa halali.
KUVUA SAMAKI 1324. Akivua samaki mwenye magamba kwenye maji na akafia nchi kavu atakuwa ni tohara na nyama yake ni halali na akifia kwenye maji atakuwa ni tohara lakini nyama yake ni haramu, ama samaki ambaye hana magamba yeye ni haramu hata kama akitolewa kwenye maji akiwa hai na akafia nchi kavu. 1325. Sio sharti mvuvi wa samaki awe muislamu na pia si wajibu kutaja jina la Mwenyezi Mungu wala kuelekea kibla na kumchinja kwa kisu, hivyo inajuzu kula samaki aliyevuliwa na kafiri lakini ni wajibu muislamu azingatie kuvua kwake na ajue kuwa samaki amevuliwa akiwa hai na amefia nchi kavu. 1326. Samaki aliyekufa ambaye hajulikani kuwa amevuliwa akiwa hai au amekufa, kama samaki atakuwa kwa muislamu atakuwa halali na kama atakuwa kwa kafiri atakuwa haramu hata kama akisema amemvua akiwa hai, ila mtu akipata matumaini kwa maneno yake. 1327. Hailazimu kujiepusha kula samaki aliye hai.
KUWINDA SENENE/NZIGE 1328. Akimshika senene/nzige hai kwa mkono wake au kwa njia nyingine atakuwa ni halali baada ya kufa kwake na si lazima aliyeshika senene awe muislamu, na pia si lazima kutaja jina la Mwenyezi 272
Al-Masailul Islamiyah Mungu wakati wa kuwashika, na ukiwapata senene kwa kafiri na haijulikani kuwa amewachukua wakiwa hai au wakiwa wamekufa hawatakuwa halali kuliwa hata kama akisema amewachukua wakiwa hai, ila kama atapata matumaini kutokana na maneno yake.
HUKUMU ZA KULA NA KUNYW A 1329. Ni halali kula nyama ya kuku, njiwa, ndege wenye mwiba nyuma ya mguu na ni haramu kula popo, tausi na kila ndege ambaye ana makucha kama vile kipanga, mwewe na ambaye kupiga mabawa wakati wa kuruka ni mara chache kuliko kutulizana, na kila ndege asiye na mwiba nyuma ya mguu wake ila ikiwa kupiga mabawa ni kwingi kuliko kutulizana basi atakuwa halali. 1330. Kama kipande cha nyama kikijitenga na mwili wa mnyama mfano: Mkia au kipande cha nyama ambacho kinakatwa kwa mbuzi aliye hai, kipande hicho ni najisi na ni haramu. 1331. Ni haramu vitu vifuatavyo kwa mnyama aliyechinjwa kisheria:1. Kinyesi 2. Damu 3. Uume 4.Uke 5. Mfuko wa kuhifadhi mtoto tezi na kokwa mbili 8. Kitu mfano wa punje katikati ya ubongo 9. Kandama 10. Mshipa wa uti wa mgongo 11. Makamasi nyongo kibofu 12. Mboni ya jicho mishipa iliyo baina ya kwato. 1332. Ni haramu kula chochote kinachomzuru mtu kwa madhara makubwa. 273
Al-Masailul Islamiyah 1333. Ni makuruhu kula nyama ya punda na farasi na kama mtu akiwaingilia wanyama hawa nyama zao zitakuwa ni haramu, na ni wajibu kuwatoa nje ya mji na kuwauza sehemu nyingine. 1334. Na mtu akimwingilia mnyama mwenye kuliwa kama ng’ombe na mbuzi, basi mkojo na kinyesi chake kitakuwa najisi na maziwa yatakuwa haramu kunywewa, na ni wajibu kumuuwa mnyama huyo kwa haraka na mwenye kumwingilia alipe thamani yake kwa mwenye ng’ombe. 1335. Ni haramu kukaa sehemu inayonywewa pombe au kileo chochote, na pia ni haramu kula chochote katika meza inayonywewa pombe juu yake. 1336. Ni wajibu kwa kila muislamu kumlisha na kumnywesha muislamu mwenzake anayekaribia kufa kwa njaa au kwa kiu na kumuokoa kutokana na mauti na kuhiliki, na vivyo hivyo kwa kila nafsi yenye kuheshimika.
MAMBO YA SUNNA WAKATI WA KULA 1337. Ni sunna katika kula mambo yafuatayo:1. Kuosha mikono miwili kabla ya kula 2. Kuosha mikono miwili baada ya kula 3. Mwenye nyumba aanze kula kabla ya yeyote na amalize baada ya kumaliza wote. 4. Kutaja jina la Mwenyezi Mungu unapoanza kula lakini kama kwenye meza kuna vyakula vingi basi atataja jina la Mwenyezi Mungu katika kila aina ya chakula. 5. Kula kwa mkono wa kulia 6. Ale kwa vidole vitatu au zaidi na asile kwa vidole viwili. 7. Ale kinachomuelekea katika chakula kama wanaokula ni wengi 274
Al-Masailul Islamiyah 8. Ale tonge dogo 9. Ale kwa muda mrefu na wala asifanye haraka katika kula 10.Atafune chakula vizuri 11.Alambe vidole vyake baada ya kula 12.Amshukuru Mwenyezi Mungu baada ya kula 13.Achokonoe meno yake baada ya kula lakini asichokonoe kwa kijiti cha mkomamanga, muwa wala kwa mti wa mtende. 14. Aokote mabaki ya chakula yaliyodondoka kwenye meza na kuyala na kama atakuwa anakula porini au jangwani ni sunna kuwaachia ndege na wanyama 15. Ale chakula mwanzo wa mchana na mwanzo wa usiku na asile katikati ya mchana na katikati ya usiku 16. Aanze kula kwa chumvi na kumalizia kwa chumvi 17. Aoshe matunda kabla ya kuanza kula 18. Alale chali baada ya chakula na kuweka mguu wake wa kulia juu ya mguu wa kushoto.
YALIYO MAKURUHU WAKATI WA KULA 1338. Yaliyomakuruhu wakati wa kula ni:1. Kula wakati umeshiba 2. Kula sana 3. Kuangalia uso wa mwenzako wakati wa kula. 4. Kula chakula cha moto 5. Kupuliza unachokula au unachokunywa 6. Kukata mkate kwa kisu 7. Kuweka mkate chini ya chombo 8. Kula nyama na kutobakisha kitu kwenye mfupa 9. Kumenya matunda ambayo yanawezekana kuliwa bila kumenywa 10. kutupa tunda kabla ya kulila kwa ukamilifu.
275
Al-Masailul Islamiyah
MAMBO YA SUNNA WAKATI WA KUNYWA MAJI 1339. Yafuatayo ni sunna wakati wa kunywa:1. Anywe maji kwa kunyonya 2. Anywe maji mchana kwa kusimama na usiku kwa kukaa 3. Amtaje Mwenyezi Mungu kabla ya kunywa na baada ya kunywa amshukuru Mwenyezi Mungu 4. Anywe maji kwa funda tatu 5. Awe na kiu ya maji na asinywe bila ya kuwa na kiu. 6. Amkumbuke Imamu Hussein “as” na watu wa nyumba ya Mtume na awalaani waliomuuwa Imamu Husein.
YALIYO MAKURUHU WAKATI WA KUNYWA MAJI 1340.Ni makuruhu wakati wa kunywa mambo yafuatayo:1. Kunywa maji sana 2. Kunywa maji baada ya kula chakula chenye mafuta 3. Kunywa maji usiku kwa kusimama 4. Kunywa maji kwa mkono wa kushoto 5. Kunywa maji katika sehemu iliyovunjika au iliyo na mapengo katika kikombe.
HUKUMU ZA MIRATHI 1341. Ambao wanarithi kwa nasaba ni tabaka tatu:Kwanza: Wazazi wa marehemu na watoto wake, kama hakuna watoto basi watoto wa watoto wao na kuteremka chini, na anarithi kwao kila aliyeku276
Al-Masailul Islamiyah wa karibu zaidi kwa marehemu na maadamu anapatikana mmoja katika tabaka hili hatarithi yeyote kutoka katika tabaka la pili. Pili: Babu, bibi na ndugu wa marehemu na kama hawapo basi watoto wao wanarithi na kila aliye karibu zaidi na marehemu na maadamu anapatikana yeyote katika tabaka hili harithi yeyote kutoka katika tabaka la tatu. Tatu: Ami, shangazi, mjomba na mama wadogo wa marehemu na watoto wao na maadamu anapatikana yeyote kati ya ami, shangazi, mjomba na mama wadogo hatorithi yeyote kati ya watoto wao, lakini kama marehemu ataacha Ami wa upande wa baba tu na mtoto wa Ami wa upande wa baba na mama, mtoto wa ami wa upande wa baba na mama atarithi bila ya Ami wa upande wa baba tu. 1342. Kama marehemu hana ami, shangazi,mjomba na mama wadogo wala watoto wao wala watoto wa watoto wao watarithi ami wa baba yake na mama yake, shangazi zao na wajomba zao kama hawapo watoto wao na kama hawapo basi wanarithi ami, shangazi, wajomba na mama wadogo wa babu na bibi yao na kama hawapo basi watarithi watoto wao. 1343.Mume na mke kila mtu anamrithi mwenzake kwa utaratibu utakao kuja pamoja na kila tabaka katika matabaka matatu yaliyotajwa.
MIRATHI YA TABAKA LA KWANZA 1344. Marehemu akiacha mtu mmoja katika tabaka la kwanza kama vile baba au mama au mtoto wa kiume au mtoto wa kike anarithi mali yote na kama ataacha watoto wa kiume wengi au watoto wakike wengi mali itagawanywa sawa baina yao, na kama ataacha mtoto mmoja wa kiume na mtoto mmoja wa kike mali itagawanywa sehemu tatu, mtoto wa kiume atapewa sehemu mbili na mtoto wa kike atapewa sehemu mmoja, na kama ataacha watoto wa kiume wengi na watoto wa kike wengi basi mali itagawanywa kwa namna 277
Al-Masailul Islamiyah ambayo mtoto wa kiume atarithi mara dufu ya mtoto wa kike. 1345. Kama marehemu ataacha wazazi wawili mali itagawanywa sehemu tatu mzazi wa kiume atapewa sehemu mbili na mzazi wa kike atapewa sehemu moja, na kama marehemu ataacha pamoja na ndugu wawili wa kiume au dada wawili au kaka na dada wawili na wote wakawa ni wa upande wa baba tu au wa upande wa mama wao hawatarithi kwa marehemu maadamu marehemu ana baba na mama isipokuwa mama wa marehemu kwa sabau yao atarithi moja ya sita “1/6” na mali iliyobaki atapewa baba wa marehemu. 1346. Marehemu akiacha wazazi wawili na binti mmoja kama marehemu hana kaka wawili wala dada wawili au dada wanne au kaka mmoja na dada wawili wa upande wa baba mali itagawanywa sehemu tano, baba na mama kila mmoja atarithi sehemu moja na binti atarithi sehemu tatu na kama marehemu ana kaka wawili au dada wanne au kaka na dada wawili wa upande wa baba mali itagawanywa sehemu sita baba na mama kila moja atapata sehemu moja na binti atapewa sehemu tatu, sehemu iliyobaki “1/6” itagawanywa sehemu nne baba atapewa sehemu moja na binti atapewa sehemu zilizobakia kwa mfano kama itagawanywa mali ya marehemu sehemu 24 binti atapewa sehemu 15, baba atapewa sehemu 5 na mama atapewa sehemu 4. 1347. Marehemu akiacha wazazi wawili na mtoto wa kiume mali itagawanywa sehemu sita wazazi wawili kila mmoja atapewa sehemu moja na sehemu nne atapewa mtoto wa kiume, na akiacha pamoja nao watoto wengi wa kiume au watoto wengi wa kike mali itagawanywa sawa baina yao, ama wakiwa ni watoto wa kiume na watoto wa kike mali itagawanywa kwa namna ambayo mtoto wa kiume atachukua mara dufu ya mtoto wa kike. 1350. Marehemu akiacha baba na mtoto mmoja wa kiume au mama na mtoto mmoja wa kike mali itagawanywa sehemu sita sehemu moja anapewa baba au mama na sehemu zilizobaki anapewa mtoto wa kiume. 278
Al-Masailul Islamiyah 1351. Marehemu akiacha baba na mtoto wa kiume na binti au mama na watoto wa kiume na binti mali itagawanywa sehemu sita, sehemu moja anapewa baba au mama na sehemu zilizobakia zitagawanywa kwa namna ambayo mtoto wa kiume atapata mara dufu ya binti. 1352. Marehemu akiacha baba na binti mmoja au mama na binti mmoja mali itagawanywa sehemu nne sehemu moja atapewa baba au mama na baki atapewa binti. 1353. Marehemu akiacha baba tu na watoto wa kike wengi au mama tu na watoto wengi wa kike mali itagawanywa sehemu tano, sehemu moja atapewa baba au mama na sehemu zilizobakia zitagawanywa kwa watoto wa kike kwa usawa. 1354. Kama marehemu hajaacha mtoto wa kiume wala binti watarithi watoto wa watoto wake wa kiume hisa ya watoto wa kiume hata kama wao watakuwa ni wanawake, na watoto wa kike watarithi hisa ya watoto wake wa kike hata kama watakuwa ni wanaume mfano, kama marehemu ataacha mjukuu wa kiume wa binti yake na mjukuu wa kike wa mtoto wake wa kiume mali itagawanywa sehemu tatu, sehemu moja atapewa mtoto wa kiume wa binti yake na sehemu mbili atapewa mtoto wa kike wa mtoto wake wa kiume.
MIRATHI YA TABAKA LA PILI 1355. Tabaka la pili linalorithi kwa nasaba ni babu, bibi, ndugu wa kiume na wa kike wa marehemu na kama hajaacha ndugu wakiume na wakike basi watoto wao ndio watarithi. 1356. Marehemu akiacha ndugu wa kiume tu au ndugu wa kike tu basi mali yote ni yake, na wakiwepo ndugu wa kiume wengi na ndugu wa kike wengi wa wazazi wawili mali itagawanywa baina yao kwa usawa, na ikiwa ndugu wa kiume wengi na ndugu wa kike wengi 279
Al-Masailul Islamiyah ndugu wa kiume watarithi mara dufu ya ndugu wa kike, mfano kama ataacha ndugu wa kiume wawili na ndugu mmoja wa kike mali itagawanywa sehemu tano kila ndugu wa kiume atapewa sehemu mbili na ndugu wa kike atapewa sehemu moja. 1357. Kama marehemu ataacha ndugu wa kiume na ndugu wa kike wa wazazi wawili, ndugu wa kiume na ndugu wa kike wa upande wa baba tu hawatarithi, kama ataacha ndugu wa kiume au ndugu wa kike wa upande wa baba tu atarithi mali yote, na akiacha ndugu wa kiume kama ndugu wakiwa wengi wa upande wa baba tu mali itagawanywa baina yao kwa usawa, na kama ataacha ndugu mmoja wa kiume na ndugu wakike wengi mwanaume atarithi mara dufu ya mwanamke. 1358. Marehemu akiacha ndugu wa kiume mmoja au ndugu wa kike mmoja tu wa upande wa mama, atarithi mali yote na akiacha ndugu wa kiume wengi au ndugu wa kike wengi wa upande wa mama tu mali itagawanywa baina yao kwa usawa. Marehemu akiacha ndugu wa kiume na ndugu wa kike wa wazazi wawili au ndugu wa kiume na ndugu wa kike wa upande wa baba tu na ndugu wa kiume au wa kike wa upande wa mama tu, ndugu wa upande wa baba tu hawatarithi na mali itagawanywa sehemu sita, sehemu moja atapewa ndugu wa kiume na ndugu wa kike wa upande wa mama tu, na sehemu zilizobaki ni za ndugu wa kiume, na ndugu wa kike wa wazazi wawili na wanaume watarithi mara dufu ya wanawake. 1359. Marehemu akiacha ndugu wa kiume na ndugu wa kike wa wazazi wawili, ndugu wakiume na ndugu wakike wa upande wa baba tu na ndugu wa kiume na ndugu wakike wa upande wa mama tu ndugu wa kiume na ndugu wa kike wa upande wa baba hawatarithi na mali itagawanywa sehemu tatu, sehemu itagawanywa baina ya ndugu wa kiume na ndugu wa kike wa mama kwa usawa na iliyobakia watapewa ndugu wa wazazi wawili na mwanaume atapata mara dufu ya mwanamke. 280
Al-Masailul Islamiyah 1360. Marehemu akiacha kaka na dada wa upande wa baba tu na kaka au dada wa upande wa mama tu mali itagawanywa sehemu sita, sehemu moja ni ya kaka au dada wa upande wa mama, na iliyobaki itagawanywa baina ya kaka na dada wa upande wa baba tu na mwanaume atapata mara dufu ya anayopata mwanamke. 1361. Marehemu akiacha kaka na dada na mke, mke atarithi kwa namna ambayo utakuja ufafanuzi wake, na kaka na dada watarithi kwa namna iliyotangulia kutajwa katika mas’ala yaliyotangulia, vivyo hivyo akifa mke na akaacha kaka, dada na mume wake, mume atarithi nusu ya mali na kaka na dada watarithi kwa namna iliyotajwa katika mas’ala yaliyotangulia, lakini kurithi kwa mke au mume haipunguzi hisa ya kaka na dada wa wazazi wawili au wa upande wa baba tu. 1362. Marehemu akiacha babu au bibi ni sawa awe wa upande wa baba au wa upande wa mama tu, atarithi mali yote, babu akiwepo mzazi wa babu hatarithi.
MIRATHI YA TABAKA LA TATU 1363. Tabaka la tatu ni Ami wa marehemu, wajomba, mama wadogo na watoto wao kama hatakuwepo yeyote katika tabaka lililotangulia. 1364. Marehemu akiacha Ami, shangazi ni sawa awe ni wa upande wa wazazi wawili au wa upande wa baba tu anarithi mali yote, na akiacha Ami wengi au shangazi wengi mali itagawanywa baina yao kwa usawa. 1365. Marehemu akiacha mjomba au mama mdogo anarithi mali yote na akiacha mjomba na mama mdogo na wote ni wa upande wa wazazi wawili au wa upande wa baba tu mali itagawanywa baina yao kwa usawa na kwa tahadhari waelewane katika kugawana. 281
Al-Masailul Islamiyah
MIRATHI YA MUME NA MKE 1366. Mke akifariki na akawa hajaacha watoto mume anarithi nusu ya mali yake na inayobaki wanapewa watu wengine wa upande wa mke na ikiwa ana watoto kwa huyo mume au kwa mume mwingine mume anarithi robo ya mali yake na iliyobaki wanarithi wengine. 1367. Mume akifariki na akawa hajaacha watoto, mke anarithi robo ya mali na iliyobaki wanarithi wengine na kama ana watoto kwa huyo mume au kwa mume mwingine mke atarithi moja ya nane (1/8). 1368. Mke harithi ardhi na wala harithi nyumba, jengo na miti, lakini anarithi thamani yake. 1369. Mke akitaka kurithi ardhi au kutumia vitu ambavyo havirithi ni wajibu atake idhini kwa warithi wengine na vivyo hivyo warithi wengine kwa tahadhari ya wajibu wasitumie vitu ambavyo mke anarithi thamani yake kabla hawajampa hisa yake isipokuwa kama atatoa idhini vinginevyo muamala utakuwa batili. 1370. Kama marehemu ana mke zaidi ya mmoja na hana watoto robo ya mali yake itagawanywa kwa wake zake kwa usawa na kama ana watoto (1/8) moja ya nane ya mali yake itagawanywa kwa wake kwa usawa. 1371. Kama ataoa mke katika hali ya maradhi kisha akafa kwa maradhi hayo mke wake atamrithi hata kama hakumwingilia. 1372. Mke akiachwa talaka rejea kisha akafa katika eda mume wake atamrithi, vivyo hivyo kama mume atafariki ndani ya eda yake mke atarithi, lakini kama mmoja akifa baada ya kumalizika eda ya talaka 282
Al-Masailul Islamiyah rejea au katika eda ya talaka bain hatamrithi. 1374. Mwislamu anarithi kwa kafiri lakini kafiri harithi kwa mwislamu hata kama atakuwa ni mtoto wa marehemu au baba yake. 1375. Mtu akimuuwa yeyote kwa makusudi au kwa dhulma hatamrithi.
TALAQIN YA MAIT
283
Al-Masailul Islamiyah
284
Al-Masailul Islamiyah
285
BACK COVER Historia fupi ya Ayatullah al-Udhmaa Sayyid Sadiq Shirazi (dama dhilluhu). Amezaliwa katika mwezi wa Dhilhijjah mwaka 1360 Hijria mwafaka na mwaka 1948 Miladia katika mji mtukufu wa Karbala, Iraq. Amesoma kwa marjaa taklidi na maulamaa wakubwa katika vyuo vikuu vya kidini (hawza) hadi akafikia daraja la juu kabisa la kutoa fatwa na ijtihadi na kuwa mujtahidi. Amelelewa katika nyumba kongwe ya ukoo wenye elimu kubwa na uliobobea katika fikihi, ijtihadi, jihadi na kujitolea. Ayatullah Shirazi amekua na kupambika umri wake kwa moyo wa ikhlasi, ucha Mungu, amali na fikra njema zinazokwenda sambamba na mafundisho ya Qur’ani Tukufu na Ahlul Bait (a.s.). Ametunga vitabu vingi katika viwango mbalimbali ya ufahamu, miongoni mwao vikiwepo: Sharh al-‘Urwatu ‘l-Wuthqaa, Ijtiha wa Taqlid, Bayanu ‘l-Usul, Qa’idah La Dharar Walaa Dhiraar, n.k. Vivyo hivyo, ameandika vitabu vya masomo kwa ajili ya wanafunzi wa Hawza, k.v. Rawdhah Fiy Sharh al-Lum’ah, Sharh al-Sharaa’i’, Sharh atTabsirah, Sharh Suyuti, Sharh Samadiyyah, Mu’jazi Fiy Mantiq, n.k. Zaidi ya miaka ishirini sasa, Ayatullah Sayyid Sadiq Shirazi amekuwa akitoa darsa za khariji za Usuli Fikihi ambazo ni darsa za juu kabisa katika Hawza. Wanafunzi na hata maulamaa waliofikia daraja la ijtihadi ni miongoni wa wenye kuhudhuria darsa zake na kunufaika kwazo.