Al Mahdi katika Sunna

Page 1

Al-Mahdi Katika Sunna (al-Mahdi fi ‘s-Sunnah)

Kimeandikwa na: Ayatullah al-Udhma Sayyid Sadiq al-Husaini al-Shirazi

Kimetarjumiwa na: Abdul Karim Juma Nkusui


Haki ya kunakili imehifadhiwa na: AL-ITRAH FOUNDATION ISBN: 978 - 9987 - 512 - 31 - 7 Kimeandikwa na:

Ayatullah Al-Udhma Swadiq Mahdiy al-Husein Shirazi Kimetajumiwa na: Abdul-Karim Juma Nkusui Kimehaririwa na: Dr. M. S. Kanju Email: mokanju2000@yahoo.com Kupangwa katika Kompyuta na: Hajat Pili Rajab. Toleo la kwanza:Februari.2009 Nakala:1000 Kimetolewa na kuchapishwa na: Alitrah Foundation S.L.P. 19701 Dar es Salaam, Tanzania Simu: +255 22 2110640 Simu/Nukushi: +255 22 2127555 Barua Pepe: alitrah@raha.com Tovuti: www.alitrah.org Katika mtandao: www.alitrah.info


YALIYOMO Imam Al-Mahdi.................................................................................5 Ulinganisho wa Qur’an......................................................................6 Maimam Kumi na wawili..................................................................9 Makhalifa kumi na Wawili..............................................................10 Kama idadi ya viongozi wa bani Israil............................................11 Dadisi na Fikiri................................................................................12 Ni nani kama sio Ahul Baiti (a.s).....................................................13 Bani Abbas.......................................................................................15 Kisa Kizuri.......................................................................................15 Ni nani Maimam kumi na Wawili....................................................15 Swali kwa mwanachuoni mwingine................................................17 Maangamio kwa mwenye kunichukia Mahdi..................................18 Isa ataswali nyuma yake..................................................................19 Hadithi ya kutaka kujua...................................................................20 Wa tisa wao ni Al-Qaim...................................................................21 Al-Mahdi atadhihiri na wala si vinginevyo.....................................22


Kuna Mahdi katika Umma wangu ............................................................23 Al-Mahdi katika kizazi cha Al-Husein......................................................24 Al-Mahdi ni katika Ahlul- Bait.................................................................26 Utajiri wa Jumla........................................................................................27 Tausi wa watu wa Peponi..........................................................................28 Al-Mahdi ni kabla ya Kiyama..................................................................30 Al-Mahdi ni mkarimu mno.......................................................................32 Al-Mahdi ni mwenye miujiza....................................................................33 Mimi Mahdi na Isa.....................................................................................34 Al-Mahdi atarekebisha Umma...................................................................35 Mwenyezi Mugu atawapenda na wao watampenda..................................36 Bay’a ya Mahdi katika al-Ka’aba..............................................................37 Atagawa hazina ya Al-Ka’aba...................................................................38 Al-mahdi ndio ghaibu................................................................................39 Wenye kuthibiti katika Uimamu wake......................................................41 Al-Mahdi katika sisi..................................................................................42 Ana nguvu zaidi kuliko mlima..................................................................43 Hao ndio kundi la Mwenyezi Mungu........................................................45 Kama sio Mahdi ardhi ingedidimia...........................................................49 Atatokea akiwa kijana...............................................................................50 Watetezi wa Mahdi....................................................................................51 Kwa ajili ya Mahdi Swala inakimiwa......................................................52 Bendera ya Mahdi......................................................................................53 Kila kitu kutamfurahia...............................................................................56 Alama za ajabu..........................................................................................59 Fitina mbaya kuliko fitina zote.................................................................60 D


Sauti ya mbinguni...........................................................................61 Dajaj................................................................................................63 Umma utakuwa mkubwa................................................................64 Uma Mchache.................................................................................65 Maisha ya Uadilifu..........................................................................67 Watapigania haki.............................................................................68 Hautabaki uharibifu.........................................................................69 Vita vyenye kuangamiza.................................................................70 Utawala wa Tano ni kwa al-Mahdi (a.s).........................................71 Maendeleo makubwa......................................................................72 Kusubiri Faraja................................................................................73 Anafadhila Tatu...............................................................................74 Kula Shayiri na kupigana jihadi......................................................75 Manasara watasilimu.......................................................................76 Kuhuisha Sunna na kuondoa Bidaa................................................77 Uelewano wa Jumla........................................................................78 Mimea kuzaa kwa wingi.................................................................79 Na Umri utakuwa mrefu................................................................ 80 Chini ya Bendera ya Ahlul Bait......................................................81

E


NENO LA MCHAPISHAJI Kitabu kilichoko mikononi mwako ni tarjumi ya kitabu cha Kiarabu kiitwacho, al-Mahdi fi ‘s-Sunnah kilichoandikwa na Ayatullah alUdhma Sayyid Sadiq al-Husaini al-Shirazi. Sisi tumekiita, Mahdi katika Sunnah. Kitabu hiki ni matokea ya utafiti wa kielimu pamoja na hoja zenye nguvu na utumiaji sahihi wa akili uliofanywa na mwanachuoni mwandishi wa kitabu hiki. Kwa Waislamu, imani ya kuja kwa Mahdi (Muhudi) karibu ya mwisho wa dunia ni imani ambayo ina asili katika dini.Waislamu wote bila kujali tofauti za madhehebu zao, wanakubaliana juu ya imani hii kwamba Mtukufu Mtume (saw) alisema kwamba: Hata iwe imebakia siku moja tu kwa dunia hii kufikia mwisho wake Allah Mwenye uwezo atairefusha siku hiyo ili kumwezesha Imam huyo kutawala na kuujaza ulimwengu huu uadilifu, amani na utulivu wakati ambapo ulikuwa umejaa ufisadi na dhuluma. Kitu cha kuvutia ni kwamba imani hii haiko kwa Waislamu tu bali hata katika dini nyingine wana imani kama hii kwamba atatokea mtu wakati wa mwisho ambaye ataondoa dhuluma na ufisadi na kuujaza ulimwengu huu uadilifu, amani na utulivu. Tumekiona kitabu hiki ni chenye manufaa sana, hususan wakati huu wa maendeleo makubwa ya elimu katika nyanja zote. Kutokana na ukweli huu, Taasisi yetu ya Al-Itrah Foundation imeamua F


kukichapisha kitabu hiki kwa lugha ya Kiswahili kwa madhumuni yake yaleyale ya kuwahudumia Waislamu, hususan wazungumzaji wa Kiswahili, ili kuongeza ujuzi wao katika masuala ya dini na ya kijamii. Tunamshukuru ndugu yetu, Ustadh Abdul Karim Nkusui kwa kukubali jukumu hili la kukitarjumi kitabu hiki. Vilevile tunawashukuru wale wote walioshiriki kwa njia moja au nyingine hadi kufanikisha kuchapishwa kwake. Mchapishaji: Al-Itrah Foundation S. L. P. 19701 Dar-es-Salaam, Tanzania.

G


DHULMA IMEKITHIRI, EWE IMAMU ZAMANI,15 SHAABAN 1425 A.H. Kwa jina lenye baraka, ninaanza kuandika, Nimtaje msifika, Imamu wetu hakika, Imam katoharika, kadhalika katukuka, Dhulma imekithiri, ewe Imamu zamani. Dhulma imekithiri, ewe Imamu zamani, Ufisadi na jeuri, mwingi mno duniani, Uovu na pia shari, tadhani tuko motoni, Dhulma imekithiri, ewe Imamu zamani. Uzao wako fanaka, sisi tumefarijika, Nusura tunaitaka, kwa haraka kutufika, Dhulma tumeichoka, ufisadi kadhalika, Dhulma imekithiri, ewe Imamu zamani. Ulipoghibu hakika, uovu ulitendeka, Kila kona ulifika, hadi kuvuka mipaka, Wanyonge wanateseka, masikini kadhalika, Dhulma imekithiri, ewe Imamu zamani. Hadithi nyingi hakika, Mtume ametamka, Wakati utajafika, watu dini kutoshika, Dunia wataitaka, dini hawatoitaka, Dhulma imekithiri, ewe Imamu zamani


Uovu utafurika, imani itatoweka, Aina zote kufika, dunia itachafuka, Kheri itageuka, kuwa shari bila shaka, Dhulma imekithiri, ewe Imamu zamani. Ndipo atadhihirika, Mahdi alotukuka, Kheri nyingi zitafika, na amani kadhalika, Dunia kutakasika, adha pia kuondoka, . Dhulma imekithiri, ewe Imamu zamani. Dhulma itaanguka, na uovu kufutika, Haki nafasi kushika, na watu kuneemeka, Kheri nyingi na baraka, kwa wingi zitakunjuka, Dhulma imekithiri, ewe Imamu zamani. Balaa zitaondoka, Mahdi atapofika, Dunia kubadilika, na kuijaza fanaka, Hakuna kulalamika, aidha kunung’unika, Dhulma imekithiri, ewe Imamu zamani. Mola uliotukuka, twaomba kwako fanaka, Utupe nyingi baraka, na neema kadhalika, Na adha kutuepuka, na peponi kutuweka, Dhulma imekithiri, ewe Imamu zamani. Tamati nimeshafika, beti zimekamilika, Rehema nyingi hakika, kwa Mtume kumfika, Ahalize kadhalika, ziwashukie baraka, Dhulma imekithiri, ewe Imamu zamani.


J



Al-Mahdi Katika Sunna

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa rehema Mwenye kurehemu. Amesema Mtume Mtukufu (s.a.w.w): “Lau kama isingebaki katika umri wa dunia isipokuwa siku moja, basi Mwenyezi Mungu angetuma mtu katika Ahalul-Bait wangu ili aijaze uadilifu kama itakavyokuwa imejazwa dhulma.”1 Shukrani zote ni za Mola wa walimwengu, rehema na amani zimfikie mbora wa viumbe vya Mwenyezi Mungu, mtukufu wa viumbe vyake, mwisho wa mitume wake, Bwana wetu, Mtume wetu, Muhammad bin Abdillah na Ahlul-Bait wake watoharifu. Ujumbe wote waliokuja nao Mitume wa Mwenyezi Mungu umekusanyika na umefanyiwa muhtasari katika ujumbe wa mwisho wa Mitume Muhammad (s.a.w.w) na ujumbe wa Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w), mafunzo yake na malengo yake yamekusanyika na kufanyiwa muhtasari katika kudhihiri kwa Imam Al-Mahdi anayesubiriwa (a.s), ujumbe ambao anaubeba katika bega lake kwa wanadamu, ujumbe huu umefupishwa katika Qur’anii Tukufu kwa ibara moja isemayo:- “Hakika sisi tumetuma Mitume wetu kwa ubainifu na tumeteremsha pamoja nao kitabu na mizani ili watu waishi kwa uadilifu.” Hivyo uadilifu ndiyo kitovu ambapo humo yanazunguka malengo ya Mitume katika maisha na bila ya hivyo hakutakuwa na thamani katika kheri, mafanikio na maendeleo katika ardhi, na maisha yatageuka kuwa ni kichaka wanachojificha humo wanyama wakali na humo wanahujumiwa watu wema.

1 Sunanu Abi Daudi. 2


Al-Mahdi Katika Sunna Jana mazungumzo kuhusu Imam Mahdi (a.s) yalikuwa ni mazumngumzo ya kwenye vikao na kumbi za kidini tu, ama leo na sisi tuko katika karne ya ishrini na moja mazungumzo kuhusu mrekebishaji anayesubiriwa yamekuwa ni mazungumzo ya wanadamu wote, dini zote, madhehebu zote, na nadharia za kifikra ulimwenguni leo zinazungumzia kuhusu umuhimu wa kutokea mrekebishaji ambaye ataleta uhuru, amani na utulivu katika ardhi. Na zinatufikia habari baina ya wakati mmoja na mwingine kwamba kuna mkutano huku na kongamano kule, na nadharia zinatolewa kuhusu maudhui haya muhimu wanajadili na kutoa maoni yao humo, nimeshuhudia kongamano katika mji mkuu wa Uingereza mwaka 1993 linajadili kuhusu mustakabala wa binadamu na ulimwengu, yakatolewa maudhui ya kudhihiri mrekebishaji ili kumuokoa binadamu kutokana na dhulma, uonevu na upotovu. Mmoja wa waliohudhuria kongamano Mnaswara akanidokeza kwamba yeye anaitakidi kwamba Isa (a.s) atadhihiri katika siku za mwisho wa Dunia na ataswali nyuma ya Imam wa waislamu jina lake ni Mahdi. Ikanijaa hali ya bashasha na furaha na mimi ninamsikiliza mtu huyu nikajua kuwa kadhia ya kumwitakidi Imam Mahdi imeanza kuvuka vizuizi na mipaka yote na kuwafikia wasiokuwa waislamu katika sehemu zote zinazoishi watu. Pamoja na uwazi na upana wote huu kuhusu imani juu ya Imam Mahdi kumebaki sehemu kubwa ya ujinga kwa wanaoamini Uislamu inayong’anga’nia kwa ukaidi katika kupinga jambo hili muhimu kati ya mambo muhimu ya dini. Na kitabu hiki ambacho kiko mikononi mwako - msomaji mtukufu kinaelezea sehemu tu kati ya yaliyotajwa na Sunna tukufu za Mtume kuhusu Imam Mahdi na ambazo zinakaribia elfu tatu. Mwandishi wa kitabu hiki kitukufu ni Faqihi, mwanachuoni mchamungu, ustadhi mahiri kati ya maustadhi wa fiqihi, usuli na elimu ya kiislam katika mji mtukufu wa Qum Tukufu, naye ni Ayatullah al-Udhuma Seyyid Sadiq As-Shiraziy ambaye ametunga vitabu vingine vingi katika fikra, 3


Al-Mahdi Katika Sunna aqaidi na thaqafah ya kiislamu. Tunamuomba Mwenyezi Mungu Mtukufu awaneemeshe waislamu kwa kumpa umri mrefu na awanufaishe waislamu kwa elimu yake, malipo na ujira wake ni kwa Mwenyezi Mungu. Msambazaji. Mchapishaji wa toleo la kiarabu.

4


Al-Mahdi Katika Sunna

UTANGULIZI IMAM AL-MAHDI Ni jina linalopatikana katika kila sehemu, katika vitabu vya dini vilivyotangulia, Zaburi, Injili, Taurati na katika Qur’ani kuna makumi mengi ya Aya zinazoelezea au zinazomuashiria (a.s), na katika maneno ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w) katika minasaba mbalimbali na katika Hadith mbalimbali Makka, Madina, katika Miraji na wakati wa kufariki, na katika maneno ya kizazi cha Mtume (s.a.w.w) Maimamu watukufu wote. Amirul-Muumina Ali (a.s) amemtaja mjukuu wake Mahdi, na Fatimah Zahra binti wa Mtume (s.a.w.w) amemtaja Mahdi, Imam Hasan (a.s) amemtaja mjukuu wa ndugu yake Al-Mahdi. Imam Husein (a.s) amemtaja mjukuu wake Al-Mahdi. As-Saajad Ali bin Husein, Al-Baqir Muhammad bin Ali, As-Sadiq Ja’far bin Muhammad, Al-Kadhim Musa bin Jafar, ArRidha Ali bin Musa, Al-Jawad Muhammad bin Ali, Al-Haadi Ali bin Muhammad na Al-Askari Hasan bin Ali wote wamemtaja mtoto wao AlMahdi. Na sahaba wa Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w) wamemtaja AlMahdi, Abubakr, Umar, Uthmani, Abdillah bin Umar, Abu Huraira, Sumratu bin Jundub, Salman, Abudhar, Ammar na wengineo wengi. Wake wa Mtume (s.a.w.w) wamemataja Al-Mahdi Aisha, Hafsa, Ummu Salamah na wengineo. Vilevile tabiina wamemtaja Al-Mahdi, Aunu bin Juhaifah, Abaayatu bin Raabiy, Qatadah na wengine wengi. Katika vitabu vya tafsiri vyote utakuta utajo wa Mahdi; Tafsiri Tabariy, Tafsiri Raaziy, Tafsiri Khaazin, Tafsiri Al-Alusiy, Tafsiri Ibni Kathir na Tafsiri Durul-Manthur na vingine vingi. Na katika Sihah utakuta jina la Mahdi; Al-Bukhary, Muslim, Ibnu Majaah, Abu Daudi, An-Nasaaiy, Ahmad na katika vitabu vyote vya Hadith utaku5


Al-Mahdi Katika Sunna ta utajo wa Mahdi. Katika Mustadrak As-Sahihain, Majmauz-Zawaid, Musnad Shafiy, Sunanu Daril-Qutny, Sunanul-Baihaqiy, Musnad Abu Hanifah, Kanzul-Umaal na vingine vingi. Na katika vitabu vya Ta’rikh utakuta jina la Mahdi; Tarikh Tabary, Tarikh Ibnu Al-Athir, Tarikh AlMasuud, Tarikh Suyuti, Tarikh Ibn Khaldun, na vingine vingi. Maulamaa wa madhehebu mbalimbali wamemuelezea Mahdi na wamemtaja katika mihadhara yao na khutuba zao, Maulamaa wa Kihanafi, Maulamaa wa Kishafi, Maulamaa wa Kihanbali, Maulamaa wa Kimaliki na wengineo kati ya maimamu wa madhehebu mengine, wafuasi wao, maulamaa, waandishi, washairi kila sehemu Mahdi ametajwa, kila kitabu kimemtaja Mahdi na kwa kila kinywa ametajwa Al-Mahdi….. Mbingu inasema Al-Mahdi …..na ardhi inasema ..…Al-Mahdi.

ULINGANISHO WA QUR’ANI. Tukilinganisha na kuhakiki Aya za Qur’ani Tukufu tunapata natija ifuatayo:Qur’ani imetaja Swala nayo ni kati ya faradhi muhimu za nguzo za Uislamu ambayo ikikubaliwa na mengine yanakubaliwa na ikikataliwa na mengine pia yatakataliwa, kama alivyosema Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w), imeitaja katika aya 78 tu. Qur’ani imetaja Zaka katika Aya 36, na imetaja Saumu katika aya 14, Hijja aya 12, lakini Imam Mahdi hisa yake katika Aya za Qur’ani ni nyingi sana kuliko hisa ya Swala, Zaka, Saumu na Hijja. Hakika fungu lake katika Qur’ani Tukufu linazidi Aya 100. Ndio, Aya 100 bali zinazidi, zimepokewa kuhusu Imam Mahdi (a.s) kwa aina mbalimbali katika tafsiri, sababu nuzul, taawil, dhahir, batwin n.k. Hii peke yake ni dalili kubwa juu ya Qur’ani kuipa kipaumbele kadhia ya Imam Al-Mahdi, kuhimiza kwake, kuitilia mkazo na kuikariri. Tumetunga kitabu maalum tumekiita (Al -Mahdi fiyl- Qur’ani)2 2 Kitabu hiki kimeshachapishwa. 6


Al-Mahdi Katika Sunna Ama katika Sunna, Hadith zilizopokewa kuhusu Imam Al -Mahdi (a.s) katika vitabu mbalimbali vya Tafsir, Hadith, Historia (Tarikh), Sihah, na vinginevyo vingi. Kama ningekusanya Hadith hizi zingezidi elfu tatu. Ndio, kwani ni nyingi kuliko elfu tatu, zote zinahusu Imam Al- Mahdi (a.s), na zingejaa mijaladi mingi. Ni nani huyu Al-Mahdi ambaye ana idadi hii kubwa ya utajo katika Qur’ani na Sunna? Hakika yeye ni tegemeo la mbinguni, yeye ndio lengo la sheria za Mwenyezi Mungu, yeye ndio anayetegemewa kutekeleza sheria ya dini katika dunia yote kwa mara ya kwanza katika historia ya mwanadamu. Kitabu hiki ni muhtasari wa baadhi ya yaliyopokewa kuhusu huyu Imam mtukufu ili kifungue - kwa msomaji - mwanya ambao kwawo atafahamu njia ya kumjua Imam Al-Mahdi (a.s) angalau kwa uchache. Swadiq Al - Husaini As-Shiraziy

7


Al-Mahdi Katika Sunna

MAELEZO Ni nani huyo Imam Mahdi? Ni ipi nafasi yake? Amezaliwa lini? Ataishi muda gani? Atadhihiri lini? Ametoka katika kizazi gani? Ni nani wazazi wake na ni nani babu zake? Kwa nini ameghibu? Nini faida ya kughibu kwake? Nani aliyetoa habari zake? Ni zipi alama kabla ya kudhihri kwake? Kudhihiri kwake kumeambatana na nini? Na nani wafuasi wake na idadi yao ni ngapi? Vipi atashika hatamu za uongozi wa dunia na ulimwengu huu? Ataamiliana vipi na waumini? Ataamiliana vipi na wanafiki na makafiri? Atadhihiri vipi na wapi? Ataishije na atahukumu namna gani? Na mengineyo kati ya maswali mengi, kitabu hiki kitayajibu kupitia Hadith tukufu ambazo zote zimekusanywa kutoka katika vitabu sita Sahih na kutoka katika vitabu vya Tafsiri, Hadith, Tarikh historia, ambavyo vimetungwa na wasiokuwa Shia katika madhehebu manne: Hanafi, Maliki, Shafi, na Hanbali. Lengo tangu awali lilikuwa kisitajwe chochote katika kitabu hiki kutoka katika kitabu cha Ahlu-Bait (a.s) ingawa wao ndio mahsusi kwenye mambo mfano wa hayo. Vilevile kwani wenye nyumba ndio wanaojua zaidi yaliyomo ndani ya nyumba. Hiyo ni ili kuziba njia kwa anayedhani au kwa usahihi zaidi anayedai kwamba yeye anadhani kwamba yanayoambatana na Al-Mahdi (a.s) ni kati ya mambo ambayo ni mahsusi kwa Shia, na kwamba wenye kuyanukuu na kuyapokea ni wao Shia tu.

8


Al-Mahdi Katika Sunna

NI HAYA TU. Hata hivyo hatukukusanya yote yaliyopokewa kuhusu Al-Mahdi (a.s) kutoka katika vitabu vya madhehebu mengine bali ni dondoo na muhtasari na kutaja mifano tu, kwani kukusanya yote kunahitaji kutunga mijaladi mingi na hayo tunawaachia wengine katika atakaowawezesha Mwenyezi Mungu baada yetu. Kwani kuna maulamaa wakubwa katika madhehebu mengine, mahafidhi wao, maimamu wao, na watunzi wao wamekwishatunga vitabu mahsusi kuhusu Imam Al-Mahdi (a.s). Wameandika vitabu maalumu katika baadhi ya hali zake, mambo yake na wamenukuu Hadith tukufu juu yake. Mfano wa hao ni: Allammah (wa Kishafi’i) Sheikh Jamaludiyn Yusuf bin Yahya bin Ali bin Abdur-Razaaq bin Ali Al-Muqadas as-Salimiy AdDimishqiy, ametunga kitabu maalum kuhusu Imam Al-Mahdi (a.s). Amekiita (Iqdu Durari fiy akhbaaril-Mahdi al-Muntadhir).

MAIMAM KUMI NA WAWILI. Amepokea Bukhari katika Sahih yake kutoka kwa Jabir bin Sumrah kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) amesema: “Kutakuwa na maamiri kumi na wawili” akasema kuna neno sikulisikia, baba yangu akasema: “Amesema kwamba wote ni katika makuraishi.” Muhammad bin Isa At-Tirmidhiy katika Sahih yake amepokea kutoka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w): “Watakuwepo baada yangu maamiri kumi na wawili,” kisha akasema kuna kitu sikukifahamu nikamuuliza anayefuatilia akasema: “Amesema wote ni katika makuraishi.” Muslim bin Hajaj Al-Qaithariy katika Sahih yake kutoka kwa Jabir bin Sumrah amesema: “Niliingia pamoja na baba yangu kwa Mtume nikamsikia anasema: ‘Hakika jambo hili halitamalizika hadi wapite kwao makhalifa kumi na wawili’ akasema: kisha akasema kuna neno sikulifahamu, nikamuuliza baba yangu. ‘Amesemaje?’ Akasema: ‘Amesema wote 9


Al-Mahdi Katika Sunna ni katika makuraishi.”’ Katika Sahih Muslim kutoka kwake amesema: “Amesema Mtume (s.a.w.w): ‘Jambo la watu halitaacha kuwa ni lenye kuendelea maadamu wataongozwa na watu kumi na wawili.’ Kisha Mtume akasema neno sikulielewa nikamuuliza baba yangu, Mtume wa Mwenyezi Mungu amesemaje? Akasema: ‘Wote ni katika makuraishi.”’

MAKHALIFA KUMI NA WAWILI. Sahih Muslim: Kutoka kwake vilevile amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu: “Uislamu hautaacha kuwa na nguvu hadi watimie makhalifa kumi na wawili.’ kisha akasema neno sikulisikia nikamuuliza baba yangu. ‘Amesemaje?’ Akasema: Amesema: ‘wote ni katika makuraishi.”’ Sahih Abu Daud As-Sajastaaniy: Kutoka kwake amesema kutoka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu amesema: “Dini hii haitaacha kuwa na nguvu hadi watimie makhalifa kumi na wawili,” watu wakasema Allahu Akbar na sauti zikawa nyingi kisha akasema neno sikulielewa nikamuuliza baba yangu: “Ewe baba amesemaje?” Akasema: ‘Amesema wote ni katika makuraishi.’” Musnad Ahmad bin Hanbal – Imam wa mahanbali - Kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) amesema: “Umma huu utakuwa na makhalifa kumi na wawili.” Al-Haakim An-Nisaaburiy katika Mustadrak as-Sahihain: Kutoka kwa Auni bin Juhaifah kutoka kwa baba yake amesema: “Nilikuwa pamoja na ami yangu kwa Mtume (s.a.w.w) akasema: ‘Halitaacha jambo la umma wangu kuwa jema hadi wapite makhalifa kumi na wawili’ kisha akasema neno na akapunguza sauti yake, nikamwambia ami yangu na alikuwa mbele yangu: ‘Amesemaje ewe ami yangu?’ Akasema: ‘wote ni katika makuraishi.”’ 10


Al-Mahdi Katika Sunna Taysirul-Wusuli Ilaa Jamiil-Usuli: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w): “Dini hii haitaacha kuwa na nguvu hadi watimie makhalifa kumi na wawili.” Ikasemwa kisha itakuwaje? Aksema: “Kisha itakuwa fitina na ikhitilafu.” Muntakhabu Kanzul-Umaal: “Umma huu utakuwa na viongozi kumi na wawili hatawadhuru atakayejaribu kuwadhalilisha, wote ni katika makuraishi.” Al-Haafidh Al-Qanduziy Al-Hanafiy katika Yanabi’ul-Mawaddah: Kutoka kwa Jabir bin Sumrah amesema: “Nilikuwa pamoja na baba yangu kwa Mtume (s.a.w.w) nikamsikia anasema: ‘Baada yangu kutakuwa na makhalifa kumi na wawili.’ Kisha akapunguza sauti yake nikamwambia baba yangu amesemaje baada ya kupunguza sauti yake? Akasema: ‘Alisema wote ni katika Bani Haashim.”’

KAMA IDADI YA VIONGOZI WA BANI ISRAILI. Musnad Ahmad – Imam wa Hanbali: Kutoka kwa Masuruq amesema: “Tulikuwa tumekaa kwa Abdillah bin Mas’ud naye anatusomea Qur’ani, mtu mmoja akamwambia: ‘Ewe Abu Abdur-Rahmani! Je mlimuuliza Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w) ni makhalifa wangapi watahukumu umma huu?’ Akasema Abdillah bin Mas’ud: ‘Hakuniuliza yeyote juu ya hili tangu nifike Irak kabla yako.’ kisha akasema: ‘Ndio tulimuuliza Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w) akasema: Ni kumi na wawili kama idadi ya viongozi wa Bani Israili.”’ Yanabi’ul-Mawaddah: Kutoka kwa Ibnu Mas’ud kutoka kwa Mtume amesema: “Makhalifa baada yangu ni kumi na wawili kama vile idadi ya viongozi wa Bani Israili.”

11


Al-Mahdi Katika Sunna Maelezo: Waislamu wote wameafikiana pamoja na kutofautiana madhehebu yao na vitabu vyao vya Tafsir, Hadith, Tarikh na hasa Sahih-Sita vimekubaliana kwamba:- Mtume wa Mwenyezi Mungu alitamka maneno haya. “Makhalifa baada yangu ni kumi na wawili na wote ni katika makurashi.” Hata kama matamshi yatatofautiana kwa tofauti ya mapenzi ya wapokezi, baadhi yao wamepokea kwa viongozi “Nuqabau” na baadhi wamenukuu kwa Maimam “Al-aimmah” na baadhi wameandika kwa Amiyan “Walahum ithnaaashara rajulan” na baadhi wameandika “Ithna a’shara amiran” na maana katika yote hayo ni moja na makusudio yanaafikiana na hili liko wazi na wala halifichikani.

DADISI NA FIKIRI. Jambo ambalo linapasa kufikiri ni: Hawa kumi na wawili ni akina nani? Jawabu linalokinahisha ambalo hakuna tena kujadili: Hakika wao ni ambao Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w) amewataja katika Hadith nyingine kwa majina yao nao ni:1. Ali bin Abu Talib (Al-Murtadha) 2. Hasan bin Ali (Al-Mujtabah) 3. Husein bin Ali (Ash-Shaahid) 4. Ali bin Husein (As-Sajjaad). 5. Muhammad bin Ali (Al-Baqir). 6. Ja’far bin Muhammad (As-Sadiq). 7. Musa bin Ja’far (Al-Kadhim). 8. Ali bin Musa (Ar-Ridhaa) 9. Muhammad bin Ali (Al-Jawad). 10. Ali bin Muhammad (Al-Hadiy) 11. Hasan bin Ali (Al-Askari) na 12. Al–Hujjatu Al-Mahdi. (al-Muntadhar) 12


Al-Mahdi Katika Sunna

NI NANI KAMA SIO AHLUL-BAITI (A.S)? Naongezea katika hayo, kwamba kwa wasiokuwa hawa hawapatikani makhalifa kumi na wawili (wengine) wanaokubaliwa na waislamu wote au hata na kundi moja la waislamu, sasa itakuwaje, na vipi wakubaliwe na waislamu kwa madhehebu zao zote? Jawabu: Ama Abu Bakr, Umar, Uthman, Ali hawa ni wane; wengine wanane wako wapi?

BANI UMAYYAH NA MAR’WAN. Ama Bani Umayyah na Bani Mar’wan inawezekana Mtume (s.a.w.w) akausia kwao? Je, inawezekana Mtume (s.a.w.w) kuwateua wao kuwa makhalifa? Hapana… hapana. Kwa sababu wao ni ambao wamefanya madhambi mabaya na makosa makubwa kwa Mtume na kwa waislamu. Na kurasa za historia yao ni nyeusi kila sehemu, huyu ni Muawiya na kauli yake alipotajwa Mtume (s.a.w.w) katika adhana: “Hapana wallah isipokuwa ni kuteketeza. Hapana wallah isipokuwa ni kuangamiza”.3 Hebu mtizame huyu Yazid bin Muawiya na kumuuwa kwake Husein mtoto wa binti wa Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w) na miongoni mwa wema na wabora wa Ahlul-Baiti, ndugu zake, wafuasi wake na kuteka kwake mabinti wa Ahlul-baiti kana kwamba ni wanawake wa kishirikina na makafiri, na hayo ni kwa kumpinga kwake Mwenyezi Mungu, Qur’ani, Wahyi, Utume na Siku ya Mwisho pale aliposema: “Bani Hashim wamechezea ufalme, hakuna habari iliyokuja wala wahyi ulioteremka.”4 3 Murujud-Dhahab Juz. 3, uk. 361. 4 Al-Bidayatuw-Wanihayah Juz. 8, uk. 192.

13


Al-Mahdi Katika Sunna Makusudio ya Hashim hapa ni Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w), na utume kuwa ni ufalme. Na huyu ni Al-Walid Al-Marwaniy anachana Qur’ani kwa mkuki na anaimba kaswida kwa kuieleza akikusudia Qur’ani: “Unamtisha kila mkaidi jeuri. Basi mimi ndio mkaidi jeuri. Utakapomwendea Mola Wako Siku ya Kiyama basi mwambie amenipasua Al-Walid.” 5 Na mengineyo mengi. Mtazame yeyote kati yao utamkuta ni kilele cha uovu, ukafiri, ufuska na dhulma. Je, Bani Umayyah na Mar’wan si ambao Mtume aliwaona kama vile nyani wanateremka juu ya mimbari yake likamuudhi hilo basi ikateremka kauli ya Mwenyezi Mungu:

“Hatukujaalia ndoto ambayo tumekuonyesha isipokuwa ni mtihani kwa watu.” (Surat Israi: 60). Je? Bani Umayyah na Mar’wan si ambao Qur’ani imewaeleza kwa kusema:

“Mti uliolaaniwa katika Qur’ani” (Surat Israi: 60). Al-Khatib Al-Baghidad amepokea katika Tarikh yake na Ibnu Abil-Hadid katika Sharh Nahajul-Balaagha kutoka kwa Umar bin Al-Khattab kwamba: “Mti mlaanifu ni Bani Umayayah. Je, kweli hawa ndio makhalifa wa Mtume (s.a.w.w)? 5 Muruuj-Dhahab, Jz. 3, uk. 216 14


Al-Mahdi Katika Sunna

BANI-ABBAS. Ama Bani Abbas, je, wao ndio wanaofaa kuwa makhalifa? Na wao ni nani? Je, ambao walikuwa wanapigana kwa ajili ya ufalme? Na baadhi wanawaua baadhi yao? Ndugu anamuuwa ndugu yake kwa ajili ya ufalme, au kuwauwa watoto wa Mtume (s.a.w.w), wajukuu zake na kizazi cha Mtume (s.a.w.w), maulamaa wa umma na wachamungu wake mfano:Musa bin Ja’far Al-Kaadhim, Ali bin Musa Ar-Ridhaa, Muhammad bin Ali Al-Jawad na Hasan bin Ali Al-Askariy.

Je wauaji wa hawa ndio makhalifa wa Mtume (s.a.w.w); na wao ndio ambao walikuwa wanakunywa pombe, wanacheza kamari, wanauwa watu wasio na hatia, historia yao imejaa uovu na mabaya,6 watakuwaje makhalifa wa Mtume? Vipi Mtume atasifu zama yao kuwa ni ya kheri? Hivyo ni nani hawa makhalifa wa Mtume (s.a.w.w)? Jawabu: Sio wengine isipokuwa ni Maimam kumi na mbili, kizazi cha Mtume (s.a.w.w) ambao aliwataja Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w) kwa Jabir bin Abdillah Al-Answariy7 Salman na wengineo.

KISA KIZURI. Hapa tunanukuu kisa kizuri kutoka India, inasemekana kwamba: Mmoja wa watu wa Rajuwaah India na alikuwa kati ya wasioamini Uimamu wa Maimamu kumi na wawili wa Ahlul-baiti (a.s) aliisikia Hadith ya Mtume (s.a.w.w) ambayo ni mutawatir “Makhalifa baada yangu ni kumi na mbili.” Akatafuta majina yao na asili zao ili asife kifo cha kikafiri bila ya kuwajua 6 Tarikh Baghdad Juz. 3, uk. 343. Sharh Nahajul-Balaghah Juz. 3, uk. 115.

7. Itakuja punde Hadith ya Jaabir, Salman na wengineo Insha’allah. 15


Al-Mahdi Katika Sunna makhalifa wa Mtume (s.a.w.w). Akatuma kwa maulamaa wa madhehebu manne Hanafi, Maliki, Shafi’i na Hanbali waitwe na akawaweka katika chumba kingine kisha akawa anawaita mmoja mmoja kwenye chumba chake maalum.

NI NANI MAIMAM KUMI NA WAWILI. Akamuuliza mmoja wao: Je, ni sahihi kwamba Mtume (s.a.w.w) amesema: “Makhalifa baada yangu ni kumi na mbili” ? Mwanachuoni: Ndio, hakika ni Hadith iliyopokelewa kwa tawatur kutoka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu. Akauliza: Ni nani hawa kumi na wawili? Mwanachuoni akawa anawataja: Abubakr, Umar, Uthman, Ali, Muawiya. Akasimama. Akauliza: “Hawa ni watano, kisha nani?” Mwanachuoni: “Kisha Abdul- Malik bin Mar’wan.” Akauliza: “Huyu ni wa sita kisha nani?” Mwanachuoni: “Kisha Umar bin Abdul-Azizi.” Akauliza: “Huyu ni wa saba, kisha nani?” Mwanachuoni: “Kisha Abul Abbas As- Safaah, kisha Al-Mansur kisha Harun Rashid kisha Al-Amin kisha Maamun hawa ni kumi na wawili.” Mkazi wa Rajaa: Niandikie majina yao katika karatasi ili niliweke. Mwanachuoni akaandika majina kumi na mbili katika karatasi kwa utarat16


Al-Mahdi Katika Sunna ibu ufuatao:- Abubakar, Umar, Uthman, Ali, Muawiya, Abdul – Malik bin Mar’wan, Umar bin Abdul-Azizi, Safaah, Al-Mansur, Harun, Al-Amin na Al-Maamun. Kisha akamshukuru na akamuaga na akamkirimu.

Swali kwa Mwanachuoni mwingine: Kisha akamwita Mwanachuoni mwingine peke yake kwenye chumba na akamuuliza swali lilelile: Je, ni Sahih kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w) amesema: “Makhalifa baada yangu ni kumi na wawili?” Mwanachuoni: Ndio imepokewa hivyo kwa tawatur kutoka kwa Mtume (s.a.w.w). Akasema: Naomba unitajie majina yao. Mwanachuoni akafanya haraka kutaja wanne wa mwanzo: Abubakr, Umar, Uthmani na Ali. Akauliza: Kisha nani? Mwanachuoni akanyamaza na kutafakari: Kisha Umar bin Abdul-Azizi. Akauliza: Kisha nani? Mwanachuoni: Al-Mansur. Akauliza: Kisha nani? Mwanachuoni: Kisha Haruna Rashid, kisha, Al-Amin, kisha AlMu’utasim, kisha Al-Mustai’yn kisha Al-Mutawakal. Hawa ni kumi na mbili.

17


Al-Mahdi Katika Sunna Akamuaaga Mwanachuoni wa pili ili amwite Alimu wa tatu na kumuelekezea swali lile lile, naye pia kama maulamaa wawili waliotangulia anakanganya na anataja baada ya Abubakr, Umar, Uthmani, Ali na nane katika Bani Abbasi, na anaacha kutaja Bani Umayyah na Bani Mar’wan kabisa hata Umar bin Abdul-Aziz, na anawaacha Al-Mu’utasim na AlAmin na kuwataja mahala pao Al-Maamun na Al-Haadiy. Vivyohivyo aliendelea kumwita mmoja mmoja na anamuuliza kuhusu majina ya maimam kumi na wawili na kila mmoja kati yao anataja majina ambayo hayajatajwa na mwingine kisha anamtaka aandike majina yao katika karatasi. Kisha akakusanya makaratasi akakuta kila moja linatofautiana na jingine, kisha akawaita maulamaa wote kwa pamoja na akawaambia: “Ni wa nini mkanganyiko huu katika kauli zenu, vipi hamjui maana ya Hadith iliyopokewa kwa tawatur kutoka kwa Mtume (s.a.w.w)? Kisha akawatangazia: Mimi nitawaacha na kushikamana na kizazi cha Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w) kwani maulamaa wao hawatofautiani katika majina ya maimam wao kumi na wawili wote tangu wakati wa Mtume (s.a.w.w) hadi leo wanajua majina ya Maimam wao.” Hivi ndivyo kilivyomalizika kikao bila ya mmoja kati ya hawa maulamaa kupata jibu la kumkinaisha huyo Mhindi.

MAANGAMIO KWA MWENYE KUMCHUKIA MAHDI. Katika Yaanabiul-Mawaddah ya Hafidh Al-Hanafiy amesema kutoka kwa Abu Tufail Amir bin Waathilah naye ni wa mwisho kufariki kati ya sahaba kwa itifaki, kutoka kwa Ali (a.s) amesema: “Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu: ‘Ewe Ali wewe ni wasii wangu, vita vyako ni vita vyangu, amani yako ni amani yangu, wewe ni Imam, baba wa maimam kumi na moja waliotoharika, wasiotenda dhambi na kati yao ni Al-Mahdi 18


Al-Mahdi Katika Sunna ambaye ataijaza ardhi uadilifu na usawa, basi maangamio kwa wenye kuwachukia.”’

ISA ATASWALI NYUMA YAKE. Yanabiul–Mawaddah: Kutoka kwa Abdillah ibn Abbas (r.a.) amesema: “Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w): ‘Hakika makhalifa wangu na mawasii wangu na hujjah ya Mwenyezi Mungu kwa viumbe baada yangu ni kumi na wawili, wa mwanzo wao ni ndugu yangu na wa mwisho wao ni mtoto wangu.’ Ikasemwa: ‘Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu ndugu yako ni nani?’ Akasema (s.a.w.w): ‘Ali bin Abu Twalib.’ Ikasemwa: ‘Na mtoto wako ni nani?’ Akasema (s.a.w.w): ‘Al-Mahdi ambaye ataijaza dunia uadilifu na usawa baada ya kujazwa dhulma na uonevu, naapa kwa ambaye amenituma kwa haki kuwa muonyaji kwamba, hata kama haitabaki katika umri wa dunia isipokuwa siku moja, basi Mwenyezi Mungu angeirefusha siku hiyo hadi atokee mtoto wangu AlMahdi, na atateremka Isa bin Maryam na ataswali nyuma yake, ardhi itaangaza kwa nuru yake na utawala wake utaenea toka Mashariki hadi Magharibi.”’

PAMOJA NA MTUME PEPONI Yanabiul–Mawaddah: Katika kadhia ya kuja myahudi kati ya Wayahudi wa Madina kwa Ali (a.s) na maswali yake kwake, Myahudi alisema: “Niambie umma huu baada ya Mtume wake utakuwa na Maimamu wangapi? Na niambie kuhusu makazi ya Muhammad yako wapi peponi? Na nieleze nani atakaa pamoja naye katika makazi yake?” Ali (a.s) akasema: “Umma huu baada ya Mtume wake utakuwa na Maimamu kumi na wawili, hawatowadhuru watakaowakhalifu.” Myahudi akasema: “Umesema kweli.” Ali akasema: “Muhammad ataishi katika pepo ya Adeni nayo iko katikati ya pepo, ni ya daraja la juu zaidi na iko karibu mno na Arshi ya 19


Al-Mahdi Katika Sunna Mwenyezi Mungu Mtukufu.” Myahudi akasema: “Umesema kweli.” Ali akasema: “Na ambaye ataishi pamoja naye katika pepo ni hawa kumi na wawili wa kwanza wao ni mimi na wa mwisho wetu ni Al-Qaim AlMahdi.” Akasema: “Umesema kweli.” Kifaayatul-Athar: Kutoka kwa Sa’id Al-Khudriy amesema: “Nimemsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu anasema: ‘Ahlul-Baiti ni tumaini kwa watu wa ardhini kama ambavyo nyota ni tumaini kwa watu wa mbinguni.’ Ikasememwa. ‘Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, Maimamu baada yako ni katika Ahlul-Baiti wako?’ Akasema: ‘Ndio, baada yangu kutakuwa na maimam kumi na wawili, tisa ni kutoka katika kizazi cha Husein, waaminifu, wasiotenda dhambi, na kati yetu ni Mahdi wa Umma huu. Eee! Hakika wao ni katika Ahlul-Bait wangu, kizazi changu, kutoka katika pande la nyama yangu na damu yangu, watu wana nini wananiudhi kwao, Mwenyezi Mungu asiwape shifaa yangu ”’

HADITH YA KUTAKA KUJUA Yanabi’ul-Mawaddah cha Al-Haafidh Al-Qanduziy Al-Hanafiy: Katika Hadith ya sahaba wa Mtume (s.a.w.w) kutaka kujua iliposhuka Aya hii:

“Leo nimewakamilishieni dini yenu na nimekutimizieni neema Zangu na nimewaridhia Uislamu kuwa dini yenu” (Surat Maidah: 3). Akasema (s.a.w.w): “Allahu Akbar kwa kukamilika dini, kutimizwa neema na Mola Wangu ni kuridhia ujumbe wangu na uongozi wa Ali baada yangu.” Wakasema: “Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu Aya hii ni mahsusi kwa Ali?” Akasema: “Bali ni kwake na kwa mawasii wangu siku ya Kiyama.” Wakasema: “Miongoni mwao ni kati yetu?” Akasema: “Ali ndugu yangu, mrithi wangu, wasii wangu na kiongozi wa kila muumini 20


Al-Mahdi Katika Sunna baada yangu, kisha mtoto wangu Hasan, kisha Husein, kisha tisa katika kizazi cha Husein, Qur’ani iko pamoja nao na wao wako pamoja na Qur’ani, hawatotengana nayo wala haitatengana nao hadi watakaponijia katika birika.” Akaendelea hadi aliposema: “Nakuulizeni kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, je mnajua kuwa Mwenyezi Mungu ameteremsha katika Suratul-Hajj: “Enyi mlioamini, rukuuni na sujuduni, mwabuduni Mola Wenu na fanyeni kheri,” hadi mwisho wa sura.8 (Surat Hajji: 7778). Salman akasema: “Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu ni nani hawa ambao wewe ni shahidi kwao na wao ni mashahidi kwa watu ambao Mwenyezi Mungu amewateua na wala hakujaalia kwao uzito katika dini mila ya Ibrahim”? Akasema: “Hilo ni mahsusi kwa watu kumi na tatu.” Salmani akasema: “Miongoni mwao ni kati yetu ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu”? Akasema: “Mimi, ndugu yangu Ali na kumi na moja katika kizazi changu.”

WA TISA WAO NI AL-QAIM Musnad Ahmad bin Hanbal: Imam wa Hanbali amesema: “Amesema Mtume (s.a.w.w) kwa Husein (a.s): ‘Huyu mwanangu ni Imam ndugu wa Imam baba wa Maimamu tisa, wa tisa wao ni Al-Qaim Al-Mahdi.”’

NA’ATHAL ANAMUULIZA MTUME (S.A.W.W.) Yanabi’ul-Mawaddah cha Al-Hafidh Al-Qanduziy Al-Hanafiy amesema: “Kutoka kwa Ibnu Abbas (r.a) amesema: ‘Alikuja Myahudi anayeitwa Na’athal akasema: Ewe Muhammad (s.a.w.w) nakuuliza juu ya mambo 8.Ukamilifu wake ni huu: Na fanyeni kheri ili mpate kufaulu na piganeni jihadi kwa ajili ya Mwenyezi Mungu ukweli wa kupigana jihadi yeye amewateua nyinyi na hakujaalia kwenu uzito katika dini, mila ya baba yenu Ibrahim, amewaita waislamu kabla na katika ulimwengu huu, ili Mtume awe shahidi kwenu na nyinyi muwe mashahidi kwa watu, basi simamisheni Swala, toeni Zaka, shikamaneni na kamba ya Mwenyezi Mungu yeye ni kiongozi wenu, ni kiongozi bora na mnusuru bora alioje (Al-Haji: 77 – 78). 21


Al-Mahdi Katika Sunna ambayo yananitatiza katika nafsi yangu, tangu siku nyingi kama utanijibu basi nitasilimu mbele yako.’ Akasema (s.a.w.w): ‘Uliza ewe Abu Ammaar.’ Akasema: ‘Ewe Muhammad ….. (hadi aliposema): Nieleze kuhusu wasii wako ni nani? Kwani hakuna Nabii isipokuwa ana wasii wake, hakika Mtume Musa bin Imran aliusia kwa Yusha’a bin Nun.’ Mtume (s.a.ww) akasema: ‘Hakika wasii wangu ni Ali bin Abi Talib, na baada yake ni wajukuu wangu wawili; Hasan na Husein, watafuatiwa na Maimamu tisa katika kizazi cha Husein.’ Akasema: ‘Ewe Muhammad nitajie majina yao.’ Akasema (s.a.w.w): ‘Baada ya Husein ni mtoto wake Ali, Ali akiondoka, ni mtoto wake Muhammad, Muhammad akiondoka ni mtoto wake Jafar, Ja’far akiondoka ni mtoto wake Musa, kisha baada yake ni mwanawe Ali, kisha baada ya Ali ni mwanawe Muhammad, akiondoka ni mtoto wake Ali, Ali akiondoka ni mtoto wake Al-Hasan, kisha Hasan akiondoka ni mtoto wake Al-Hujjah (a.s) Muhammad Al-Mahdi hawa ni kumi na wawili.”’

AL-MAHDI ATADHIHIRI NA WALA SI VINGINEVYO. Ametaja Muhammad bin Ali At-Tirmidhiy katika Sahih yake amesema: “Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w): ‘Haitamalizika dunia mpaka atawatawala Waarabu mwanaume kutoka katika Ahlul-baiti wangu jina lake ni kama jina langu.”’ Katika Sahih Tirmidhiy kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) amesema: “Atakuja mwanaume katika Ahlul-Baiti wangu jina lake ni kama jina langu.” Na kutoka kwa Abu Huraira amesema: “Kama usingebaki umri wa dunia isipokuwa siku moja tu basi Mwenyezi Mungu angeirefusha siku hiyo mpaka aje.”

22


Al-Mahdi Katika Sunna Na Ahmad amepokea katika Musnad yake kutoka kwa Mtume: “Hakitasimama Kiyama mpaka aje mwanaume katika Ahlul-Baiti wangu jina lake ni kama jina langu.”

KUNA MAHDI KATIKA UMMA WANGU Sahih Tirmidhiy: Kutoka kwa Abu Sa’id Al-Khudriy amesema: “Tulihofia hadath (kwisha Uislam) baada ya Mtume wetu basi tukamuuliza Mtume wa Mwenyezi Mungu akasema: ‘Hakika katika umma wangu kuna Mahdi atatokea na ataishi miaka mitano au saba au tisa.”’ Maelezo: Makusudio ya neno “hadath” ni kwisha Uislamu na kumalizika kabisa kama zilivyokwisha malizika dini zingine za Mitume wengi. Na kauli ya Mtume (s.a.w.w): “Hakika katika umma wangu kuna Mahdi” inamaanisha kuwa; Umma wangu haumaliziki wala hautasambaratika kwa sababu humo kuna Mahdi na huenda ni ishara ya ahadi ya Mwenyezi Mungu Mtukufu “Ili ushinde dini zote” (Surat Tauba: 33). Hivyo dini ya Ki-Islamu ikawa ni yenye kushinda dini zote, hivyo ni vipi itamalizika nafasi yake na hali ni hii. Sahih Abu Daud: Kutoka kwa Mtume amesema: “Kama usingebaki umri wa dunia isipokuwa siku moja, basi Mwenyezi Mungu angetuma mwanaume katika Ahlul-bait wangu ili aijaze dunia uadilifu kama itakavyokuwa imejazwa dhulma.” Sahih Abu Daud: Kutoka kwa Mtume (s.a.w.w): “Haitaondoka au haitamalizika dunia mpaka atawatawala Waarabu mwanaume katika Ahlul-bait wangu jina lake ni kama jina langu.” Akasema: “Na katika Hadith ya birika (hodhi): ‘Ataijaza dunia uadilifu na usawa kama itakavyokuwa imejazwa dhulma na uonevu.”’

23


Al-Mahdi Katika Sunna

MAHDI NI KATIKA KIZAZI CHA FATIMAH Sahih Abu Daud: Kutoka kwa Ummu Salamah amesema: Nimemsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w) anasema: ‘Al-Mahdi ni katika kizazi changu ni kutoka katika kizazi cha Fatimah.”’ Sahih Abu Daudi: Kutoka kwa Abu Sa’id Al-Khudriy amesema: “Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w): “Al-Mahdi anatokana na mimi, ataijaza dunia uadilifu na usawa kama itakavyokuwa imejazwa uonevu na dhulma, atatawala miaka saba.”’ Sahihul-Bukhariy: Kutoka kwa Nafi’i huria wa Abu Qitadah AlAnswariy: “Hakika Abu Huraira amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w): ‘Vipi nyinyi atakapoteremka Ibnu Maryam kwenu na Imam wenu ni katika nyinyi.”’

AL-MAHDI NI KATIKA KIZAZI CHA AL-HUSEIN. Sharh Nahjul-Balaghah ya Ibnu Abil-Hadid Al-Mu’utaziliy amesema: “Amepokea Qadhil-Qudhaat kutoka kwa Ismail bin Ubaadah kwa Sanad inayokwenda hadi kwa Ali (a.s), hakika yeye alimtaja Mahdi akasema: ‘Hakika yeye ni katika kizazi cha Husein.’ Na akataja umbo lake akasema: ‘Ni mwanaume mpana wa uso mzuri na mwenye pua ndefu na nzuri mwenye tumbo kubwa ana mapaja marefu mwenye meno meupe, katika shavu lake la kulia kuna alama nyeusi.”’ Sahih Ibnu Maajah: Kutoka kwa Alqamah kutoka ka Abdillah amesema: “Tulipokuwa tumekaa kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu walikuja vijana katika Bani Hashim, Mtume (s.a.w.w) alipowaona macho yake yakalengalenga machozi na rangi yake ikabadilika nikasema: Twaona kitu katika 24


Al-Mahdi Katika Sunna uso wako kinachotuchukiza? Akasema: ‘Hakika sisi Ahlul-bait, Mwenyezi Mungu ametuchagulia akhera badala ya dunia, na hakika Ahlul-Bait wangu baada yangu watapata balaa, kufukuzwa na kuteswa hadi itakapokuja kaumu kutoka Mashariki watakuwa na bendera nyeusi watataka kheri lakini hawatapewa basi watapigana na watanusurika watawapa wanachotaka, hawatakubali mpaka watampa bendera mwanaume katika Ahlul-bait wangu basi ataijaza dunia uadilifu kama itakavyojazwa dhulma, atakayefikia zama hizo basi awaendee hata kama ni kwa kutembea juu ya barafu.”’ Na katika Al-Burhan: “Hakika yeye ndio Mahdi.” Al-Bayaanu cha Kanji Ash-Shaafiy: Kutoka kwa Abu-Haruna Al-Abadiy amesema: “Nilimwendea Abu Sa’id Al-Khudriy nikamuuliza: Je ulihudhuria Badri? Akasema. ‘Ndio’, nikamwambia: Je, waweza kunieleza chochote ulichosikia kutoka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu kuhusu Ali na fadhila zake? Akasema: Sawa bali nitakuambia. Hakika Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w) aliugua, Fatimah aliingia kwake (a.s) kumjulia hali na mimi nimekaa kuliani kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w), alipoona aliyonayo Mtume (s.a.w.w) katika udhoofu akalia, Mtume wa Mwenyezi Mungu akamwambia: ‘Kitu gani kinakuliza ewe Fatimah….. (hadi aliposema): Ewe Fatimah hakika sisi Ahlul-Bait tumepewa mambo sita hakupewa yeyote katika waliotangulia wala hatapewa yeyote katika watakaokuja isipokuwa sisi Ahlul-Bait. Mtume wetu ni mbora wa Mitume naye ni baba yako, na wasii wetu ni mbora wa mawasii naye ni mume wako na shahidi wetu ni mbora wa mashahidi naye ni Hamza, ami wa baba yako, na kwetu kuna wajukuu wa umma huu nao ni watoto wako, na kwetu kuna Mahdi wa umma ambaye Isa ataswali nyuma yake.’ Kisha akapiga bega la Husein akasema: ‘Mahdi wa umma atatokana na huyu.”’ Maelezo: Katika Hadith hii “tumepewa mambo sita” na katika Hadith nyingine “mambo saba” kwa kuongeza Ja’far At-Tayaar, na huenda hapa imeondolewa kutokana na uandishi au mpokezi amekosea au amesahau au amepitiwa. Naongezea katika hayo kwamba: Hakika kuthibitisha kitu hakupingi kisichokuwa hicho kama wanavyosema maulamaa wa usuli. 25


Al-Mahdi Katika Sunna

AL-MAHDI NI KATIKA AHLUL-BAIT. Sahih Ibnu Maajah: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu: “Al-Mahdi ni katika Ahlul-Bait, Mwenyezi Mungu atamnyooshea (jambo) lake usiku.” Sahih Ibnu Maajah: Kutoka kwa Anas bin Malik amesema: “Nilimsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w) anasema: ‘Sisi kizazi cha AbdulMuttwalib ni mabwana wa watu wa peponi, mimi, Hamza., Ali, Ja’far, Hasan, Husein na Al-Mahdi.’” Musnad Ahmad bin Hanbal: Kutoka kwa Abu Sa’id Al-Khudriy: “Hakika Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w) amesema: ‘Dunia itajazwa dhulma na uonevu kisha atatoka mwanaume kutoka katika kizazi changu atatawala miaka saba au tisa basi ataijaza uadilifu na usawa.’”

AL-MAHDI KATIKA SIKU ZA MWISHONI Al-Mustadrak As-Sahihaini ya Hakim An-Nisaburi: Kutoka kwa Abu Sa’id Al-Khuduri (r.a) amesema. “Amesema Mtume (s.a.w.w): ‘Itateremka kwa umma wangu katika siku za mwishoni balaa kubwa kutoka kwa watawala wao ambapo haijapata kutokea balaa mbaya zaidi kuliko hiyo mpaka ardhi itakuwa finyu kwao na hadi dunia itajazwa dhulma na uonevu. Muumini hatapata pa kukimbilia kutokana na dhulma, basi Mwenyezi Mungu Mtukufu atatuma mwanaume katika kizazi changu ataijaza dunia uadilifu na usawa kama itakavyokuwa imejazwa dhulma na uonevu, wanaoishi mbinguni watamridhia na wanaoishi ardhini watamridhia, ardhi haitobakisha chochote katika kheri yake isipokuwa itakitoa wala mbingu haitabakisha chochote katika neema zake isipokuwa Mwenyezi Mungu ataitoa kwao yote, ataishi kwao miaka saba au nane au tisa, wafu watatamani kuwa hai kutokana na atakavyowaneemesha Mwenyezi 26


Al-Mahdi Katika Sunna Mungu watu wa ardhini kwa kheri yake.”’ Maelezo: “Watamridhia wanaoishi mbinguni na ardhini” Yaani: Atakuwa ni mwenye kupendwa kwa Mwenyezi Mungu na kwa watu, atapata ridhaa ya Mwenyezi Mungu na ridhaa ya watu. “Ardhi haitabakisha” Yaani: Mazao yatazidi na yataenea kila sehemu na wala mvua haitakatika kwao hivyo hawatapatwa na ukame wala njaa. “Watatamani” Yaani: Wafu watatamani lau wangekuwa hai wakaona wingi wa neema wa ajabu na wa kipekee.

UTAJIRI WA JUMLA Musnad Ahmad: Imam wa Hanbali amepokea kutoka kwa Sa’id AlKhuduri: Amesema Mtume (s.a.w.w): “Nawabashirieni Mahdi ataletwa kwa umma wangu kutokana na watu kuhitilafiana na matetemeko, basi ataijaza dunia uadilifu na usawa kama itakavyokuwa imejazwa dhulma na uonevu, watamridhia waishio mbinguni na duniani, atagawa mali (Swahahan).” Mwanaume mmoja akamuuliza: “Nini maana ya swahahan?” Akasema: “Kwa usawa baina ya watu.” Akasema: “Mwenyezi Mungu atazijaza nyoyo za umma wa Muhammad (s.a.w.w) utajiri na zitatosheka na uadilifu wake mpaka ataamuru mlinganiaji anadi kwa kusema: Nani ana haja ya mali? Hatasimama miongoni mwa watu isipokuwa mwanaume mmoja. Atamwambia: Mwendee Sadan, yaani mtunza hazina, mwambie Al-Mahlid anakuamuru unipe mali, atamwambia, jaza hadi atakapoiweka katika chumba na kujaa atajuta, na atasema: Je mimi ni mwenye tamaa zaidi katika umma wa Muhammad au nimeshindwa kuwa na utajiri wa moyo kama walionao? Akasema: Atairejesha basi hatokubaliwa na ataambiwa: Sisi hatuchukui chochote tulichokitoa.”

27


Al-Mahdi Katika Sunna

TAUSI WA WATU WA PEPONI. Kunuuzul–Haaqaiq cha Allammah Al-Munaadiy: Kutoka kwa Mtume (s.a.w.w): “Al-Mahid ni Tausi wa watu wa peponi.” Maelezo: Huenda kufananishwa na tausi ni katika upande wa uzuri na kutopatikana anayefanana naye, hivyo mfano wake katika pepo ni kama mfano wa tausi miongoni mwa ndege wa duniani. Al-Jamius-Swaghir cha Haafidh As-Suyutwiy As-Shaafiy: “Al-Mahdi ni mwanaume kutoka katika kizazi changu uso wake ni kama mbalamwezi.” Musnad Ahmad cha Imam wa mahanbali: Kutoka kwa Abu Sa’idi AlKhudriy amesema: “Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w): ‘Kiyama hakitosimama mpaka atawale mwanaume katika Ahlul-bait wangu, mtukufu wa umma wangu, ataijaza dunia uadilifu kama itakavyokuwa imejazwa dhulma kabla yake, ataishi miaka saba.”’ Al-Mustadrak as-Sahihaini: Kutoka kwa Abu Sa’id Al- Khuduri amesema: “Mtume wa Mwenyezi Mungu amesema: ‘Kiyama hakitosimama mpaka dunia ijae dhulma, uonevu na uadui, kisha atatoka katika Ahlul-bait wangu ambaye ataijaza uadilifu na usawa kama itakavyokuwa imejazwa dhulma na uadui.”’ Yanabul-Mawaddah: Kutoka kwa Qitadah amesema. “Nilimuuliza Sa’id bin Musayyib: Hivi Mahdi ni wa kweli? Akasema: ‘Ndio ni wa kweli, ni katika watoto wa Fatimah (a.s).’ Nikasema: Ni katika watoto wapi wa Fatimah? Akasema: ‘Kwa sasa imekutosha.”’

28


Al-Mahdi Katika Sunna

MWENYE KUKANUSHA NI KAFIRI. Al-Hafidh Al-Qanduziy Al-Hanafiy katika Yanabi’ul-Mawaddah: Kutoka kwa Jabir bin Abdillah Al-Answar (r.a.) amesema: “Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu: ‘Mwenye kukanusha kutokea Al-Mahdi basi ameshakufuru yale yaliyoteremshwa kwa Muhammad, na mwenye kukanusha kuteremka kwa Isa ameshakufuru na mwenye kukanusha kutokea kwa Dajjal pia ameshakufuru.”’ Maelezo: Ukafiri una daraja zifuatazo: Kwanza: Kumkanusha Mwenyezi Mungu kwa kumkataa. Pili: Kukanusha yale aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu Mtukufu. Tatu: Kukufuru neema za Mwenyezi Mungu, na kufuru iliyotajwa katika Hadith hii ni katika daraja la pili, kwa sababu Mwenyezi Mungu Mtukufu ndio ambaye amemteua Imam Al-Mahdi (kweli) hivyo kumkanusha kwake ni kumkanusha Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w) kwa sababu ni kumfanya Mtume kuwa muongo kwa kutoa kwake habari juu ya Al-Imam Al-Mahdi (a.s). Yanabi’ul-Mawaddah: Kutoka kwa Hudhaifah bin Al-Yamaan amesema: “Nimesikia Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w) akisema: ‘Ole wa umma huu kutokana na wafalme jeuri, vipi watauwa na kuwafukuza waislamu, isipokuwa mwenye kudhihirisha utii kwao, muumini mchamungu anawapendezesha kwa ulimi wake na anawakimbia kwa moyo wake, Mwenyezi Mungu atakapotaka kurejesha Uislamu uwe na nguvu, atamwangamiza kila mkaidi jeuri, naye ni Mwenye kuweza kwa ayatakayo, na kuutengeneza umma baada ya kuharibiwa. Ewe Hudhaifah lau kama usingebakia umri wa dunia isipokuwa siku moja, basi Mwenyezi Mungu angeirefusha siku hiyo mpaka atawale mwanaume katika kizazi 29


Al-Mahdi Katika Sunna changu na kuudhihirisha Uislamu, na wala Mwenyzi Mungu hakhalifu waadi wake naye ni Muweza wa kutimiza ahadi.”’

AL-MAHDI NI KABLA YA KIYAMA Nurul-Abswar cha Shabalanjiy As-Shaafiy: Kutoka kwa Maqaatil na wanaomfuata kati ya wafasiri katika tafsiri ya kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu “wainahu lailimu As-sa’ah”: Amesema kuwa ni Mahdi, atakuja siku za mwishoni na baada ya kutokea kwake itakuwa ndio alama ya Kiyama. Al-Bayaan ya Kanjiy Ash-Shafi’i: Amesema Sa’id bin Jubair katika tafsiri ya kauli ya Mwenyezi Mungu: “Ili ipate kuzishinda dini zote, ijapokuwa washirikina watachukia.” (Surat As-Swafat: 9). Ni Mahdi kutoka katika kizazi cha Fatimah (a.s). Katika Gharaibul-Qur’ani imepokewa katika habari “Mwenyezi Mungu amewaahidi wale walioamini miongoni mwenu na wakatenda mema, ya kwamba atawafanya makhalifa katika ardhi kama alivyowafanya makhalifa wa kabla yao…..” (Surat Nur: 55): “Lau usingebaki umri wa dunia isipokuwa siku moja tu Mwenyezi Mungu angeirefusha siku hiyo hadi atoke mwanaume katika umma wangu jina lake ni kama jina langu, lakabu yake ni kama lakabu yangu, ataijaza dunia uadilifu na usawa kama itakavyokuwa imejazwa dhulma na uonevu.”

AL-MAHDI NI KATIKA KIZAZI CHANGU. Al-Bayaanu ya Al-Kanjiy Shafi: Kutoka kwa Abu Salamah bin AbdurRahman bin Auf kutoka kwa baba yake amesema: “Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w): ‘Hakika Mwenyezi Mungu Mtukufu atatuma katika kizazi changu mwanaume mwenye mwanya na mzuri wa sura, ataijaza dunia na uadilifu, usawa na atagawa mali kwa wingi.”’ 30


Al-Mahdi Katika Sunna

KWA MAHDI MWENYEZI MUNGU ATAHITIMISHA Al-Bayaan ya Kanji: Kutoka kwa Ali bin Haushab alimsikia Mak’hul anasimulia kuhusu Ali bin Abu-Talib (a.s) akasema: “Nilisema ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu je, Mahdi ni katika asiyekuwa sisi?” Akasema Mtume (s.a.w.w): “Hapana, bali ni katika sisi ambako kwetu Mwenyezi Mungu atahitimisha dini kama alivyoanza kwetu, na kwetu watanusuriwa kutokana na fitna kama walivyonusuriwa kutokana na shirki, na kwetu Mwenyezi Mungu ataziunganisha nyoyo zao baada ya uadui na fitna na kuwa ni ndugu kama ambavyo wamekuwa ndugu baada ya uadui wa kishirikina.” Muntakhabu Kanzul-Umaal: “Lau kama usingebaki umri wa dunia isipokuwa siku moja basi Mwenyezi Mungu angeirefusha siku hiyo mpaka atawale mwanaume kutoka katika kizazi changu mlima Dailam na Costantinople.” Maelezo: “Jabalul-Dailam” kilikuwa ni kituo cha majusi na Mayahudi wakati wa Mtume (s.a.w.w) na “Costantinople” kilikuwa ni kituo cha Manaswara na maana ya “mpaka atawale mwanaume kutoka katika kizazi changu mlima Dailam na Costantinople.” ni kuwa dunia yote itakuwa chini ya utawala wake na pia vituo vya dini zingine, nacho ni kinaya cha kuunganika ulimwengu wote chini ya bendera ya kiislamu. Yanabi’ul-Mawaddah ya Haafidh Al-Qanduziy Al-Hanafiy: Kutoka kwa Abu Sa’idi: “Al-Mahdi ni katika sisi Ahlul-bait, mwenye kuinua kichwa asiye dhalili ataijaza ardhi na uadilifu kama itakavyokuwa imejazwa dhulma.” Al-Fusulul-Muhimah ya Allamaah Ibnu Swibagh, Abu Daudi na Tirmidhiy katika Sunan zao wote wamezirufaisha kwa Abdillah bin 31


Al-Mahdi Katika Sunna Mas’ud amesema: “Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu: “Lau kama usingebaki katika umri wa dunia isipokuwa siku moja basi Mwenyezi Mungu angeirefusha siku hiyo mpaka amtume humo mwanaume katika umma wangu kutoka katika Ahlul-bait wangu jina lake ni kama jina langu, aijaze dunia uadilifu kama itakavyokuwa imejazwa dhulma.’”

AL-MAHDI NI MKARIMU MNO Al-Bayaan ya Al-Kanjiy Ash-Shafi’iy: Kutoka kwa Abu Sa’idi Al-Khuduri amesema. “Amesema Mtume (s.a.w.w): ‘Atakuja mtu baada ya kughibu kwa muda na kudhihiri fitina, anayeitwa Al-Mahdi ni mkarimu mno.”’ Yanabi’ul-Mawaddah: Kutoka kwa Ibnu Abbas amesema: “Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w): ‘Hakika ufunguzi wa dini hii ni wa Ali, akiuliwa dini itaharibika na hatoitengeneza isipokuwa Al-Mahdi.”’ Maelezo: Kauli yake (s.a.w.w): “Hakika ufunguzi wa dini hii ni wa Ali” ni ishara ya maneno aliyoyatoa Mtume (s.a.w.w) kuhusu Ali (a.s) katika mwanzo wa Uislamu ambapo alisema: “Haukusimama Uislamu isipokuwa kwa upanga wa Ali na mali ya Khadija.” Na pale aliposema (s.a.w.w): “Pigo la Ali siku ya Khandaq ni bora kuliko ibada ya thaqalayn (majini na wanadamu).” Na aliposema (s.a.w.w): “Mimi na Ali ndio baba wa umma huu.” Vilevile amesema (s.a.w.w) alipotoka Ali kupambana na Amru bin Abdi Wudd: “Imetoka imani yote kupambania na shirki yote.” Na aliposema (s.a.w.w) hali akimuomba Mwenyezi Mungu katika sehemu hiyohiyo: “Ewe Mola wangu ukitaka usiabudiwe basi hutoabudiwa.” Na mengineyo mengi. Yanabi’ul-Mawaddah: Kutoka kwa Ali (a.s) ameirufaisha: “Haitaondoka dunia mpaka atatawala katika umma wangu mwanaume katika kizazi cha Husein (a.s) ataijaza uadilifu kama itakavyokuwa imejazwa dhulma.” Yanabi’ul-Mawaddah: Kutoka kwa Hudhayfa bin Al-Yamani amesema: 32


Al-Mahdi Katika Sunna “Alituhutubia Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) akatukumbusha yatakayotokea hadi siku ya Kiyama kisha akasema: ‘Lau usingebaki katika umri wa dunia isipokuwa siku moja tu basi, Mwenyezi Mungu Mtukufu angeirefusha siku hiyo mpaka amtume mwanaume kutoka katika kizazi changu, jina lake ni kama jina langu.’ Salman akasimama na akasema: ‘Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu yeye ni kutoka kwa mtoto wako yupi?’ Akasema: ‘Ni kutoka kwa mjukuu wangu huyu.’ Na akamwashiria Husein (a.s) kwa mkono wake.” Yanabiul–Mawaddah: Kutoka kwa Faruwah Az-Zaniy, kutoka kwa Mtume (s.a.w.w): “Hakika dunia itajazwa dhulma na uadui kisha atatokea mwanaume katika Ahlul-bait wangu ataijaza uadilifu na usawa kama itakavyokuwa imejazwa dhulma na uadui.”

AL-MAHDI NI MWENYE MIUJIZA. Al-Burhaanu Fiy Alaamati Akhriz-Zaman cha Al-Mutaqiy Al-Hindiy AlHanafiy: Kutoka kwa Amirul-Mu’minina Ali bin Abi Talib amesema: “Mahdi atamwashiria ndege basi atatua mkononi mwake, atapanda mti katika sehemu ya ardhi basi utaota na kutoa majani.” Yanabi’ul-Mawaddah: Kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) hakika amesema kumwambia Ali bin Abi Talib: “Ewe Ali ogopa chuki ambazo ziko katika vifua vya ambao hawaidhihirishi isipokuwa baada ya mauti yangu, hao Mwenyezi Mungu anawalaani na wanawalaani wenye kulaani.” Kisha akalia (s.a.w.w.) na akasema: “Amenipa habari Jibril (a.s) kwamba wao watamdhulumu baada yangu, na hakika dhulma hiyo itabakia hadi atakapokuja mtawala wao, na hekima yao ikaenea na umma ukakusanyika katika mapenzi na nguvu yao, jambo litakuwa dogo na mwenye kumchukia atakuwa dhalili, wenye kusifu watakuwa ni wengi na hiyo ni itakapobadilika nchi, waja wakawa dhaifu na wakakata tamaa ya kupata faraja, wakati huo atadhihiri Al-Qaim Al-Mahdi kutoka katika kizazi changu, Mwenyezi 33


Al-Mahdi Katika Sunna Mungu atadhihirisha haki kwa panga zao na watu watawafuata kwa kuwapenda au kwa kuwaogopa.” Kisha akasema: “Enyi watu furahini kwa faraja, kwani ahadi ya Mwenyezi Mungu ni ya kweli hakhalifu, na hukumu Yake haipingwi, naye ni Mwenye kuhukumu, Mjuzi, na hakika nusura ya Mwenyezi Mungu iko karibu. Eee Mwenyezi Mungu hakika wao ni Ahlul-bait wangu wakinge kutokana na uchafu na watakase kabisa, Ee Mwenyezi Mungu waangalie, walinde, wanusuru wape nguvu na wala usiwadhalilishe, na nihifadhi kwao hakika wewe ni muweza wa ninayoyataka.”

MIMI, MAHDI NA ISA. Tarikh Dimishiq ya Ibnu Asaakar Ash-Shaafiy: Kutoka kwa Ibnu Abbas ni kwamba amesema: “Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu: ‘Vipi Umma utahiliki hali mimi niko katika mwanzo wake, Isa yuko katika mwisho wake na Mahdi yuko katikati yake.”’ Maelezo: Huenda maana ya Hadith hii ni kwamba Isa bin Maryam atashuka kutoka mbinguni baada ya kudhihiri Al-Mahdi hivyo akawa nyuma ya Mahdi, hivyo ikasihi kusemwa “Mtume yuko mwanzo, Mahdi yuko katikati na Isa yuko mwisho.” Sunanun-Nasaiy: Kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) hakika amesema: “Furahini furahini hakika umma wangu ni kama mvua haijulikani mwisho wake, ni bora au mwanzo wake, au kama bustani wamekula kwayo kundi mwaka mmoja, huenda mwisho wake kuna kundi litaneemeka zaidi na muda wake utakuwa ni mrefu zaidi na uzuri wake ni mzuri zaidi, vipi utahiliki umma hali mimi ni wa mwanzo wake, Mahdi yuko katikati na Isa yuko katika mwisho wake, lakini baina ya hayo kuna (shabkhu a’awaju) sio katika mimi wala mimi sio katika wao.” Maelezo: “Shabkhu” ni sauti ya maziwa wakati wa kukamua9 na huenda ni kinaya ya zogo na fujo ambayo wataifanya watu, wao wanajiona ni 9 Al-Qaamnusil-Muhytu maadatu: Shabkh. 34


Al-Mahdi Katika Sunna waislamu lakini wao hawamwamini Imam Al-Mahdi (a.s) kama tunavyoona leo, kwa sababu hiyo Mtume amewaita wapotovu kwa sababu wao wameacha njia ya Uislamu na mwendo wa Mtume (s.a.w.w). “Sio katika mimi” yaani sio waislamu, hata kama watadai ni waislamu. “Na Mimi sio katika wao” yaani Mimi sio Mtume wao, kwa sababu asiyekubali maneno yangu basi mimi sio Mtume wake bali Mtume wake ni yule anayemkubalia maneno yake.

AL-MAHDI ATAREKEBISHA UMMA. Yanabi’ul-Mawaddah: Kutoka kwa Abu Sa’idi Al-Khudriy amesema: “Aliingia Fatimah kwa baba yake katika maradhi yake akalia na akasema: ‘Ewe baba yangu naogopa upotovu baada yako.’ Akasema: ‘Ewe Fatimah hakika Mwenyezi Mungu amewaangalia watu wa ardhini basi akamteua baba yako akamtuma kuwa Mtume, kisha akaangalia mara ya pili akamteua kati yao mume wako akaniamuru nikuozeshe kwake basi nikakuozesha kwake na yeye ni mpole mno kati ya waislamu, mwingi wao wa elimu, wa mwanzo wao kusilimu.’ (hadi aliposema): ‘Na kwetu kuna wajukuu wa umma huu (Al-Hasan na Al-Husein) na wao ni watoto wako na kwetu kuna Al-Mahdi wa umma huu.”’ Basi Abu Haruna Al-Abadiy amesema: “Amesema Wahab bin Munabih: ‘Hakika Musa umma wake ulipopewa mtihani na ukamfanya ndama kuwa ni Mungu hilo likawa kubwa kwa Musa. Mwenyezi Mungu akasema: Ewe Musa waliokuwa kabla yako katika Manabii, watu wao walipewa mtihani na hakika umma wa Ahmad utapatwa na fitina kubwa baada yake hadi baadhi yao watawalaani baadhi, kisha Mwenyezi Mungu atatengeneza jambo lao kwa mwanaume kutoka katika kizazi cha Ahmad naye ni Mahdi.”

35


Al-Mahdi Katika Sunna Ibnu Abdi-Barr katika kitabu chake Al-Istiab Fiy Asimail-As’haab kutoka kwa Jabir As-Sudufiy kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) amesema: “Atatokea mwanaume katika Ahlul-Bait wangu ataijaza ardhi uadilifu.”

MWENYEZI MUNGU ATAWAPENDA NA WAO WATAMPENDA Yanabi’ul-Mawaddah: Kutoka kwa Ali (a.s) hakika amesema: “Mwenyezi Mungu ataleta kaumu anayoipenda na inayompenda na atatawala ambaye ni mgeni miongoni mwao, naye ni Al-Mahdi mwekundu wa uso na nywele za (rangi ya shaba), ataijaza ardhi uadilifu bila ya taabu, atatengana na mama yake na baba yake katika udogo wake na atakuwa na nguvu katika kulelewa kwake, atatawala dola ya waislamu kwa amani, zama zitakuwa nzuri kwake, maneno yake yatasikilizwa, wazee na vijana watamtii, ataijaza ardhi uadilifu kama itakavyokuwa imejazwa dhulma, na wakati huo utakamilika uimamu wake na ukhalifa wake na Mwenyezi Mungu atawafufua walio makaburini na hakitaonekana kitu isipokuwa makaburi yao tu, ardhi itatengenea, itakuwa nzuri na kumea, na kwake itatiririka mito yake, fitina na vita zitaisha, kheri na baraka zitakuwa nyingi.” Maelezo: “Atatengana katika udogo wake na mama yake na baba yake” kwa sababu Imam Al-Mahdi wakati wa kuzaliwa kwake ilikuwa ni kwa siri kama ilivyokuwa kuzaliwa kwa Musa bin Imran (a.s). Hiyo ni kwa sababu wafalme wa Bani Abbas walikuwa wanamfuatilia ili wamuuwe ili kumaliza kizazi cha Muhammad (s.a.w.w), lakini wao ni nuru katika nuru ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, basi ni vipi itazimwa nuru ya Mwenyezi Mungu. Kauli yake: “Mwenyezi Mungu atawafufua waliomo makaburini.” Ni kuashiria kauli yake (swt) kuhusu raja’ah. “Na siku tutafufua kundi katika kila umma.” (Surat Namli: 83). 36


Al-Mahdi Katika Sunna

BAYI’A YA MAHDI KATIKA AL-KA’ABA Al-Bayaan ya Kanjiy Ash-Shaafiy: Kutoka kwa Hudhayfah amesema: “Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu: ‘Lau usingebaki katika umri wa dunia isipokuwa siku moja basi, Mwenyezi Mungu angetuma humo mwanaume jina lake ni kama jina langu na tabia yake ni kama tabia yangu watu watambayi’i baina ya rukun na maqaamu. Mwenyezi Mungu kwake atairejesha dini na atampa ushindi, hivyo hatabaki katika uso wa ardhi isipokuwa anayesema Lailaha illa llahu,’ Salman akasimama akasema: ‘Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu ni katika mtoto wako yupi?’ Akasema: ‘Yeye ni kutoka kwa mtoto wangu huyu’ na mkono wake ukamgusa AlHusein (a.s).” Taaju Jaamiu’l–Usuuli ya Al-Jaaziry Ash-Shaafiy kutoka kwa Abu Sa’id kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) amesema: “Kati ya makhalifa wenu kuna khalifa atakayetoa mali na wala hatayakusanya na kuyahesabu.” Amesema katika Ghaayatul-Muamal Sharhi ya Taaj: “Huyu ndio AlMahdi (a.s) kwa dalili ya Hadith ifuatayo na hiyo ni kutokana na wingi wa ngawira na ufunguzi pamoja na ukarimu wa nafsi yake na kutoa kwake kheri kwa watu wake.” Kitabul–Mahdi: Kutoka kwa Abu Waail amesema: “Ali (a.s.) alimtazama Husein akasema: ‘Hakika mtoto wangu huyu ni Bwana kama alivyomwita Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w) na atatoka katika mgongo wake mwanaume anayeitwa kwa jina la Nabii wenu, atatoka wakati watu wako katika kughafilika, kuachwa haki na kudhihirisha dhulma, watafurahi kwa kutoka kwake naye ni mwanaume mwenye uso mweupe, mwenye pua ndefu, mwenye tumbo pana, mwenye mapaja marefu, katika shavu lake la kulia kuna alama nyeusi na mwenye mwanya, ataijaza ardhi uadilifu kama itakavyokuwa imejazwa dhulma na uonevu.”’ 37


Al-Mahdi Katika Sunna

ATAGAWA HAZINA YA AL-KA’ABA. Muntakhabu Kanzul–Umaal: Kutoka kwa Umar bin A-Khattab hakika yeye aliiaga Kaaba akasema: “Waallahi sijui ni ache hazina ya Baitul-mali na yaliyomo miongoni mwa silaha na mali au niigawe katika njia ya Mwenyezi Mungu?” Ali bin Abi Talib akamwambia: “Acha, kwani wewe sio mwenye kugawa kwani mgawaji wake ni katika sisi, kijana wa kikuraishi ataigawa katika njia ya Mwenyezi Mungu katika siku za mwishoni.” Maqatilu-Twalibiyn cha Abul Faraji Al-Isfahaaniy: Amesema Az-Zahiry kwamba: “Amenisimulia Ali bin Al-Husein kutoka kwa baba yake kutoka kwa Fatimah kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w) amemwambia: ‘Al-Mahdi ni katika kizazi chako.”’ Al-Burhaanu Fiy Alaamaat Mahdi Akhriz-Zaman cha Al-Mutaqiy AlHindiy Al-Hanafiy: Kutoka kwa Abu Huraira amesema: “Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w): ‘Lau usingebaki katika umri wa dunia isipokuwa usiku mmoja basi angetawala humo mwanaume kutoka katika Ahlul-Bait wangu.” Kutoka kwa Abu Huraira kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) amesema: “Kiyama hakitasimama mpaka atokee mwanaume katika Ahlul-bait wangu atawapiga vita hadi warejee kwenye haki.” Akasema: Nikasema: “Atawatawala kwa muda gani?” Akasema: “Miaka mitano na miwili (saba).” Maelezo: Kauli yake “Mitano na miwili” huenda anakusudia miaka mitano na miezi miwili, na huenda anakusudia miaka mitano na miaka miwili, yaani miaka saba, na kutenganisha baina yake katika kutaja, huenda ni kwa sababu muda wa kudhihiri Al-Mahdi (a.s) ni awamu mbili, moja ni miaka mitano na nyingine ni miaka miwili, na huenda si hivyo, Mwenyezi Mungu ndio anayejua zaidi.

38


Al-Mahdi Katika Sunna

AL-MAHDI NDIO GHAIBU Yanabi’ul-Mawaddah cha Al-Qanduziy Al-Hanafiy: Amesema Ja’far AsSadiq (a.s) katika kauli yake (s.w.t.) katika Surat Yunus: “Na wanasema: Kwa nini hakuteremshiwa Ishara kutoka kwa Mola Wake Mlezi? Sema: Mambo ya ghaibu ni ya Mwenyezi Mungu. Basi nyinyi ngojeni, na mimi ni pamoja nanyi katika wanaongojea.” (Surat Yunus: 20). Amesema: “Ghaibu katika Aya hii ni Al-Hujjatu Al-Qaaim Al-Mahdi.” Maelezo: Hakuna kizuizi juu ya hilo (lawezekana), kwani ghaibu husemwa kwa kilichoghibu katika dhahiri pamoja na kuwepo kwake, hivyo Mwenyezi Mungu Mtukufu ni ghaibu na Imam Al-Mahdi (a.s) ni ghaibu na mustabakali ni ghaibu n.k.

MAHDI ATAPIGANA KWA AJILI YA SUNNA Yanabi’ul-Mawaddah: Kutoka kwa Aisha kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) hakika yeye amesema: “Al-Mahdi ni mwanaume katika kizazi changu atapigana kwa ajili ya Sunna zangu kama ambavyo nilipigana kwa ajili ya wahyi.” Maelezo: Kauli yake (s.a.w.w): “Atapigana kwa ajili ya sunna zangu” ni ishara katika kupigana kwake na waislamu ambao wanapinga kuwepo kwake na wanapinga uimam wake, kwa sababu hiyo ni kupinga Sunna ya Mtume (s.a.w.w) iliyopokewa kuhusu yeye katika mamia ya hadith zilizoandikwa katika vitabu vyote vya tafsiri na vitabu vyote vya hadith na vitabu vya historia. Is’afur-Raghibiyna cha As-Swaban Al-Hanafiy: Kutoka kwa Mtume (s.a.w.w): “Al-Mahdi ni katika sisi, kwake itahitimishwa dini kama ambavyo ilifunguliwa kwetu.” 39


Al-Mahdi Katika Sunna Muntakhabu Kanzul-Umaal: Kutoka kwa Mtume (s.a.w.w): “Atatokea mwanaume katika Ahlul-Baiti wangu jina lake ni kama jina langu, tabia yake ni tabia yangu, ataijaza ardhi uadilifu na usawa kama itakavyokuwa imejazwa dhulma na uonevu.” Al-Burhaan Fi’alaamaati Mahdi Fi akhriz-Zamani cha Al-Mutaqiy AlHindi Al-Hanafiy: Kutoka kwa Ali bin Abi Talib hakika yeye alimwambia Mtume (s.a.w.w): “Je, Mahdi ni katika sisi au ni kwa asiyekuwa sisi ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu?” Akasema: “Bali ni katika sisi, Mwenyezi Mungu atahitimisha dini kwake kama ambavyo aliifungua kwetu, na kwetu watanusuriwa kutokana na fitina kama ambavyo waliokolewa kutokana na shiriki, na kwetu zitaunganishwa nyoyo zao baada ya uadui baina yao kama zilivyounganishwa nyoyo zao baada ya uadui wa shirki.” Maelezo: Imetangulia hadith inayofanana na hii, lakini hizo ni hadith mbili, na wala sio hadith moja iliyokaririwa. Tadhkiratul-Khawaas cha Sibtu Ibnul-Jauziy Al-Hanafiy: Kutoka kwa Ibnu Umar amesema: “Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w): ‘Atatokea katika siku za mwisho mwanaume katika kizazi changu jina lake ni kama jina langu, lakabu yake ni kama lakabu yangu ataijaza ardhi uadilifu kama itakavyokuwa imejazwa dhulma na huyo ni Al-Mahdi.”’ Al-Burhaan Fiy alaamaati Mahdi Akhirz-Zamani cha Al-Muntaqiy AlHindiy Al- Hanafiy: Kutoka kwa Ali amesema: “Jina la Mahdi ni Muhammad.” Al-Burhaan Fiy alaamaati Mahdi Akhirz-Zamani: Kutoka kwa Abu Said Al-Khudriy kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) amesema: “Jina la Mahdi ni kama jina langu.” Al-Jamius-Swaghir cha As-Suyutwiy Ash-Shaafiy: “Al-Mahdi anatokana na mimi, mweupe wa uso mwenye pua ndefu, ataijaza dunia uadilifu na 40


Al-Mahdi Katika Sunna usawa kama itakavyokuwa imejazwa dhulma na uonevu atatawala miaka saba.” Is’afur-Raghibiyna cha As-Swabaan Al-Hanafiy: “Vilevile imepokewa kuhusu ndevu zake kwamba: ‘Yeye ni kijana mwenye macho meusi, mwenye nyusi nyeusi na pua ndefu, mwenye ndevu nyingi, katika shavu lake la kulia kuna alama nyeusi na katika mkono wake wa kulia kuna alama nyeusi.”’

WENYE KUTHIBITI KATIKA UIMAMU WAKE Yanabil-Mawadah: Kutoka kwa Ibnu Abbas (r.a) amesema: “Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w): ‘Hakika Ali ni Imam wa umma wangu baada yangu, na kati ya watoto wake ni Al-Qaim Al-Mahdi anayengojewa ambaye atakapodhihiri ataijaza dunia uadilifu kama itakavyokuwa imejazwa dhulma na uonevu. Naapa kwa Yule ambaye amenituma kwa haki kuwa mbashiri na muonyaji, hakika wenye kuthibiti katika uimamu wake katika zama za ghaibu yake ni watukufu zaidi kuliko madini ya kibiriti.’ Jaabir bin Abdillah Al-Answar akasimama na akasema: ‘Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu mtoto wako Al- Mahdi ataghibu?’ Akasema: ‘Ndio, naapa kwa Mola Wangu atawachuja ambao wameamini na atawateketeza makafiri.10 Ewe Jaabir hakika jambo hili ni katika amri ya Mwenyezi Mungu na siri katika siri za Mwenyezi Mungu imefichwa kwa waja wa Mwenyezi Mungu, jihadhari na kushakia hilo kwani shaka katika jambo la Mwenyezi Mungu Mtukufu ni kufuru.”’ Maelezo: Kibiriti ni madini mepesi yenye rangi ya njano hayachemki kwa maji yanayochemshwa kwayo. Husemwa: Yakuti nyekundu au dhahabu nyekundu ni yenye thamani kuliko kibiriti chekundu. Hii yatumika kama mfano katika Kiarabu, kama vile msemo usemao: “Bora kuliko ngamia wekundu.”11 10 Suratul-Imran 141. 11 Aqrabul- Mawaridi, madatu: Kibrit 41


Al-Mahdi Katika Sunna Al-Mustadrak As-Sahihain cha Al-Hakim An-Nisaburiy: Amesema Ummu Salamah: “Nimemsikia Mtume (s.a.w.w) anamtaja Al-Mahdi akasema: ‘Ndio ni kweli, naye ni katika watoto wa Fatimah.”’

AL-MAHDI NI KATIKA SISI Yanabil-Mawadah: Kutoka kwa Abu Ayubu Al-Answar amesema: “Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w) kwa Fatimah (a.s): ‘Kati yetu kuna mbora wa Manabii naye ni baba yako, kati yetu kuna mbora wa mawasii naye ni mume wako, kati yetu kuna mbora wa mashahidi naye ni ami ya baba yako Hamza, na kati yetu kuna ambaye ana mabawa mawili anaruka kwayo peponi popote anapotaka, naye ni mtoto wa ami ya baba yako Jafar, na kati yetu kuna wajukuu wa umma huu mabwana wa vijana nao ni watoto wako, na kati yetu kuna Al-Mahdi naye ni katika kizazi chako.”’ Kanuzul-Haqaiq cha Allammah Al-Munawiy: Kutoka kwa Mtume (s.a.w.w): “Furahi ewe Fatimah Mahdi ni kutokana na wewe.” Muntakhabul Kanzul-Umaal: “Al- Mahdi ni mwanaume kati yetu kutoka katika kizazi cha Fatimah.”

AL-MAHDI ATAVUNJA NGOME ZA UPOTOVU Al-Bayaan cha Al-Kanjiy Ash-Shaafiy: Kutoka kwa Al-Hilaliy kutoka kwa baba yake amesema: “Niliingia kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w) katika maradhi yake aliyofia, Fatimah alikuwa kichwani mwake akalia hadi akapaza sauti, Mtume (s.a.w.w) akamwangalia akasema ‘Kipenzi changu Fatimah kipi kinakuliza?’ Akasema. ‘Naogopa upotovu baada yako.’ Akasema: ‘Ewe kipenzi changu hujui kuwa Mwenyezi 42


Al-Mahdi Katika Sunna Mungu alitazama ardhi akamchagua baba yako hivyo akamtuma kwa ujumbe wake, kisha akatazama mara ya pili akamchagua mume wako na akanifunulia kuwa nikuoze kwake. Ewe Fatimah sisi ni Ahlul- bait, Mwenyezi Mungu ameshatupa vitu saba na hakupewa yeyote kabla yetu. Mimi ni mwisho wa Manabii, mbora wa Mitume na mbora wa wema mbele ya Mwenyezi Mungu na kiumbe kinachopendwa zaidi kwa Mwenyezi Mungu kati ya viumbe na mimi ndio baba yako. Na wasii wangu ni mbora wa mawasii na anayependwa zaidi kati yao kwa Mwenyezi Mungu naye ni mume wako. Kati yetu kuna ambaye ana mabawa mawili ya kijani ataruka nayo peponi pamoja na malaika popote anapotaka, naye ni mtoto wa ami ya baba yako na ndugu wa mume wako. Na kuna wajukuu wa umma huu, nao ni watoto wako Hasan na Husein, nao ni mabwana wa vijana wa peponi. Na baba yao naapa kwa Yule ambaye amenituma kwa haki yeye ni bora kuliko wao. Ewe Fatimah, naapa kwa ambaye amenituma kwa haki, hakika kati yao kuna Mahdi wa umma huu, dunia itakapochafuka, fitina ikadhihiri, pakakosekana pa kukimbilia, baadhi wakapigana na baadhi yao, mkubwa hatomhurumia mdogo wala mdogo hatomheshimu mkubwa, wakati huo Mwenyezi Mungu atamleta kwao ambaye atavunja ngome za upotovu na atafungua nyoyo zilizofungwa, atasimamisha dini siku za mwisho kama nilivyoisimamisha katika mwanzo wa zama, na ataijaza dunia uadilifu kama itakavyokuwa imejazwa dhulma na uonevu.”’

ANA NGUVU ZAIDI KULIKO MLIMA Al-Bayaan: Kutoka kwa Abdillah bin Umar amesema: “Mahdi atatoka katika kizazi cha Husein, atatokea upande wa Mashariki, lau kama milima itamkabili basi angeibomoa na kutengeneza njia za kupitia humo.” Maelezo: Hii ni kinaya kuhusu nguvu zake za kiungu ambazo zinamuunga mkono. 43


Al-Mahdi Katika Sunna Yanabiil-Mawaddah: Kutoka kwa Abu Is’haaq amesema: “Ali alisema na akamtazama mtoto wake: ‘Ambaye anaitakidi kuwa mtoto wangu huyu ni bwana, kama alivyomwita Mtume wa Mwenyezi Mungu, basi atatoka katika mgongo wake mwanaume atakayeitwa kwa jina la Mtume wenu, anafanana naye kwa umbo na wala hafanani naye kwa tabia.”’ Maelezo: Huenda makusudio ya hayo ni kwamba (Al-Mahdi) anafanana na babu yake Mtume (s.a.w.w) katika umbo na mwili na wala hafanani naye kwa sira na hukumu, hiyo ni kwa yale yaliyopokewa kwa tawatir katika Hadith, kwamba yeye atahukumu kwa hali halisi na kuacha dhahiri, hivyo atamuuwa kafiri hata kama atadhihirisha Uislamu kwa unafiki na uongo n.k, wakati ambapo Mtume (s.a.w.w) alikuwa anahukumu kwa dhahiri ambapo amesema (s.a.w.w) katika Hadith iliyopokewa kutoka kwake: “Hakika mimi nahukumu kwenu kwa Imani na ushahidi.” Yanabil-Mawadah: Kutoka kwa Da’abal bin Ali Al-Khaza’iy amesema: “Nilisoma kaswida kwa kiongozi wangu Al-Imam Ali Ridhaa (a.s) nilipofikia: ‘Kutokea kwa Imam hakunabudi ni lazima, atahukumu kwa jina la Mwenyezi Mungu na kwa baraka atampambanulia kwetu haki na batili, ataleta neema na kutekeleza adhabu.’ Ali Ridhaa akalia sana kisha akasema: ‘Ewe Da’abal ametamka Roho mtukufu kwa ulimi wako, unamjua huyu Imam?’ Nikasema: ‘Hapana isipokuwa mimi nimesikia kutokea kwa imam kutoka kwenu atajaza ardhi uadilifu na usawa.’ Akasema: ‘Hakika Imamu baada yangu ni mtoto wangu Muhammad, baada ya Muhammad ni mtoto wake Ali, baada ya Ali ni mtoto wake Hasan na baada ya Hasan ni mtoto wake Al-Hujjah Al-Qaim naye ndiye anayengojewa katika ghaibu yake, atakayetiiwa wakati wa kudhihiri kwake, ataijaza ardhi uadilifu na usawa kama itakavyokuwa imejazwa dhulma na uonevu. Ama ni lini atadhihiri, habari kuhusu wakati amenisimulia baba yangu kutoka kwa baba zake kutoka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu amesema: Mfano wake ni kama mfano wa Kiyama hakitowajia isipokuwa ghafla.”’

44


Al-Mahdi Katika Sunna

HAO NDIO KUNDI LA MWENYEZI MUNGU Yanabil-Mawadah: Kutoka kwa Jabir bin Abdillah Al-Answar katika Hadith ametaja humo kuingia kwa Jandal bin Junadah bin Jubayri kwa Mtume (s.a.w.w) na imani yake kwa Mwenyezi Mungu na Mtume wake Jandal alisema: “Hakika jana katika usingizi wangu nimemuona Musa bin Imran (a.s) anasema: ‘Ewe Jandal silimu katika mikono ya Muhammad (s.a.w.w), mwisho wa Manabii na shikamana na mawasii wake baada yake, nikasema: Nitaslimu, shukrani ni za Mwenyezi Mungu, nimeshasilimu na ameniongoa kwako.” Kisha akasema: “Nieleze ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu kuhusu mawasii wako baada yako ili nishikamane nao.” Akasema Mtume (s.a.w.w): “Mawasii wangu ni kumi na wawili.” Jandal akasema: “Hivi ndivyo tulivyowakuta katika Torati. Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu nitajie majina yao.” Akasema: “Wa mwanzo wao ni bwana wa mawasii, baba wa maimamu Ali, kisha Hasan na Husein, hivyo shikamana nao wala usikuhadae ujinga wa wajinga. Atakapozaliwa mtoto wangu Ali bin Husein Zainul-Abidiyn (a.s) basi Mwenyezi Mungu atapitisha hukumu yake kwako na chakula chako cha mwisho duniani ni maziwa utakayoyanywa.” Jandal akasema: “Tumekuta katika Torati katika vitabu vya manabii; Iliyaa, Shubar na Shabir, haya ni majina ya Ali, Hasan na Husein, ni nani baada ya Husein na majina yao ni yapi?” Akasema: “Atakapopita Husein basi Imam ni mtoto wake Ali lakabu yake ni Zainul-Abidiyn, baada yake ni mtoto wake Muhammad, lakabu yake ni Baaqir baada yake ni mtoto wake Ja’far anayeitwa As-Saadiq, baada yake ni mtoto wake Musa anayeitwa Kaadhim, baada yake ni mtoto wake Ali anayeitwa Ridhaa, baada yake ni mtoto wake Muhammad anayeitwa Taqiy na Zakiy, baada yake ni mtoto wake Ali anayeitwa Naqiy na Haadiy, baada yake ni mtoto wake Al- Hasan anayeitwa Al-Askariy, baada yake ni mtoto wake anayeitwa Al-Mahdiy, Al- Qaim na Al-Hujjah, ataghibu kisha atato45


Al-Mahdi Katika Sunna ka, atakapotokea ataijaza dunia uadilifu na usawa kama itakavyokuwa imejazwa dhulma na uonevu, ni uzuri ulioje kwa mwemye kusubiri katika ghaibu yake, uzuri ulioje kwa wachamungu kwa mapenzi yao, hao ndio wale aliowasifu Mwenyezi Mungu katika Kitabu Chake akasema: “Uongofu kwa wachamungu ambao wanaamini ghaibu.” (Surat AlBaqarah: 302). Kisha akasema:

“Hao ndio kundi la Mwenyezi Mungu. Ee hakika kundi la Mwenyezi Mungu ndilo lenye kufaulu. (Surat Mujadalah: 22).”

ATAWAFANYA BANI UMMAYYAH KUWA MAKAPI Ibnu Abil-Hadid Al-Mu’untaziliy katika Sharh ya Nahjul-Balaghah anasema. “Na miongoni mwayo yaani khutuba yake (a.s) ni: ‘Angalieni Ahlulbait wa Mtume wenu, wakikaa mahala basi kaeni, wakiwataka muwanusuru basi muwanusuru, kwani Mwenyezi Mungu atakuja kuondoa fitina, kwa mwanaume kutoka katika Ahlul-Bait, kwa haki ya baba yangu ni mtoto wa Imam bora, hatawapa isipokuwa upanga, vita tu, kwa muda wa miezi minne mpaka Makuraishi watasema kama huyu angekuwa ni katika kizazi cha Fatimah basi angetuhurumia, Mwenyezi Mungu atampiganisha na Bani Umayyah hadi awafanye kuwa makapi na pumba

46


Al-Mahdi Katika Sunna

“Wamelaaniwa popote watakapokuwa na watachukuliwa na kuuliwa, sunna ya Mwenyezi Mungu katika wale waliopita kabla yetu na wala hutapata mabadiliko katika sunna ya Mwenyezi Mungu.” (Surat Ahzab: 61 – 62.).” Yanabi’ul-Mawaddah: Ali (a.s) alihutubia baada ya kumalizika kwa vita vya Naharawan akataja njia za fitina maalum akasema: “Hilo ni jambo la Mwenyezi Mungu nalo litatokea katika wakati muafaka. Ee mtoto wa vijakazi bora! Hadi lini utasubiri? Furahi kwa nusura iliyo karibu kutoka kwa Mola Mwenye huruma, kwa haki ya baba yangu na mama yangu idadi ndogo majina yao hayafahamiki ardhini.” Yanabi’ul-Mawaddah: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w): ‘Al-Mahdi ni katika kizazi changu ataghibu, kisha atakapodhihiri ataijaza ardhi uadilifu na usawa kama itakavyokuwa imejazwa dhulma na uonevu.”’

GHAIBU MBILI Yanabi’ul-Mawaddah: Kutoka kwa Ali bin Abi Talib (a.s) amesema: “Hakika Al-Qaim kati yenu ataghibu mara mbili, ghaibu moja ni ndefu kuliko nyingine, hatothibiti katika Uimam wake isipokuwa mwenye nguvu, yakini na mwenye maarifa sahihi.” Maelezo: Ghaiba mbili: Mojawapo inaitwa Al-Ghaibatu As-Sughurah Ghaibu fupi nayo inaanzia pale alipofariki Al-Imam Al- Hasan Al-Askary (a.s) mzazi wa Al-Mahdi (a.s) mwaka 260 A.H. na inamalizikia pale alipo47


Al-Mahdi Katika Sunna fariki naibu wa nne mwaka 329 A.H. Na Ghaibu ndefu (Ghaibatul-Kubraa) inaanzia mwaka 329 A.H. na inaendelea hadi leo ambapo tunamuomba Mwenyezi Mungu aifanye ndio hatima na mwisho wake, na atuburudishe kwa kumuona hali ya kuwa ni mwenye kuturidhia na wala sio mwenye kutukasirikia. Ewe Mwenye huruma mno kuliko wenye huruma. Al-Burhaan Fiy Alaamaati Mahdi Akhriz-Zamani: Kutoka kwa Abu Abdillah Al-Husein bin Ali (a.s) amesema: “Hakika mwenye jambo hili, yaani Al-Mahdi ana ghaiba mbili mojawapo itakuwa ndefu mpaka baadhi yao watasema amekufa, na baadhi yao watasema ameondoka na wala hatojua sehemu yake isipokuwa (Maula), yaani mtu ambaye anamhudumia kati ya mawalii wa Mwenyezi Mungu.” Vinginevyo kufuzu kwa kukutana mara moja au mara nyingi katika sehemu mbalimbali ni katika yasiyokuwa na shaka humo, kwani wamebahatika kwa hili wengi miongoni mwa watu wema na wachamungu, na hii inakusanya baina ya pande mbili ambapo upande mmoja kuna wanaodai kumuona lakini hawakumtambua, na upande mwingine unaosema kuwa watafaulu kukutana naye wema wenye ikhilasi tu. Na wanaohesabiwa kuwa ni kati ya wale waliokutana naye (a.s) ni: Seyyid Bahrul-Uluum, Al-Muqadas Al-Ardabiliy, Sheikh Al-Answary, Al-Hajji Ali Al-Baghdad na wengineo ambao amewataja baadhi yao Al-Haji Mirzaa Husein An-Nuriy katika kitabu chake An-Najimut-Thaqib, na baadhi yao amewataja Sheikh Mahmud Al-Iraqiy katika kitabu chake Darus –Salaam, na Allammah Al-Majlisiy katika Biharul-An’war, na wengineo katika vitabu vingine. Mwenyezi Mungu atupe taufiki ya hilo kwa ukarimu wake.

48


Al-Mahdi Katika Sunna

ATAVUNJA MKUSANYIKO Yanabi’ul-Mawaddah: Kutoka kwa Ali bin Abi Talib amesema: “Katika sisi kuna Mahdi ambaye ataeneza katika dunia taa yenye nuru na atatembea humo kama mfano wa watu wema ili aondoe matatizo na kuwakomboa wanyonge, kuvunja mkusanyiko wa (nguvu ya) madhalimu, ataondoa mkusanyiko kwa kujificha kwa watu, hatoona mfuatiliaji nyayo zake hata kama atamfuatilia kwa kumuona.” Maelezo: Hadith hii ni ubainifu wa sira ya Imam Mahdi (a.s) katika siku za ghaiba yake nayo ni kwamba yeye atawaneemesha watu kwa baraka za kuwepo kwake, hata kama hawamuoni, au wanamuona lakini hawamtambui.

KAMA SIO MAHDI ARDHI INGEDIDIMIA. Yanabi’ul-Mawaddah cha Al-Qanduziy Al-Hanafiy: Kutoka kwa Ja’far as-Sadiq (a.s.) kutoka kwa baba yake kutoka kwa babu yake Ali bin AlHusein (a.s) amesema: “Sisi Maimamu wa waislamu ni Hujjah za Mwenyezi Mungu katika ulimwengu na viongozi wa waislamu, sisi ni tumaini la watu wa ardhini kama ambavyo nyota ni tumaini la watu wa mbinguni, kwa ajili yetu sisi “Amezishika mbingu zisianguke juu ya ardhi ila kwa idhini yake.”12 kwa ajili yetu sisi inateremshwa mvua, hutolewa rehema, na hutolewa baraka za ardhi, kama asingekuwepo juu ya ardhi mmoja miongoni mwetu basi ingedidimia pamoja na watu wake.” Kisha akasema: “Na haikubaki tangu Mwenyezi Mungu amuumbe Adamu (a.s) bila ya kuwepo Hujjah (khalifa) wa Mwenyezi Mungu humo, ama yuko dhahiri anajulikana au yuko katika ghaibu amefichikana, na wala ardhi haitabaki bila ya Hujjah (khalifa) mpaka Kiyama kisimame, kama si hivyo basi asingeabudiwa Mwenyezi Mungu.” 12 Suratul-Hajj: 60 49


Al-Mahdi Katika Sunna Suleiman, mpokezi wa Hadith akasema: “Nikamwambia Ja’far As-Sadiq (as): “Vipi watu watanufaika kwa Hujjah ambaye yuko ughaibuni amefichikana?” Akasema: ‘Vipi wananufaika kwa jua linapofunikwa na mawingu”’? Maelezo: Hapa kuna mfano mzuri ameutoa Al-Imam As-Sadiq (a.s), Jua faida zake zote zinazofanya uhai uwepo ziko hata kama litafunikwa na mawingu, bali watu watakosa joto lake tu, vilevile Al-Imam Al-Mahdi (a.s) faida yake ni kubwa nayo ni kuhifadhiwa ulimwengu kutokana na kuangamia watu wake, hali ya kuwa yeye amefichikana kwa watu, kilichokosekana kwa watu katika ghaiba yake ni baadhi ya faida tu.

ATATOKEZA AKIWA KIJANA. Yanabi’ul-Mawaddah: Kutoka kwa Al-Hasan bin Ali (a.s) hakika amesema: “Kama angedhihiri Mahdi basi watu wangemkataa kwa sababu atatokeza kwao akiwa kijana na wao wanadhani kuwa ni mzee kikongwe.” Yanabi’ul-Mawaddah: Kutoka kwa Muhammad bin Muslim amesema: “Nilimwambia Al-Baqir. ‘Nini taawili ya kauli yake (s.w.t.) katika SuratulAnfaal. “Nawapigeni mpaka pasiwepo na fitina na dini yote iwe ni kwa ajili ya Mwenyezi Mungu Mtukufu.” (Surat Anfaal: 39). Akasema: ‘Haijaja taawili ya Aya, itakapokuja taawili yake washirikina watapigwa vita hadi wampwekeshe Mwenyezi Mungu Mtukufu na wala kusiwepo na shirki na hiyo ni atakapodhihiri Al-Qaim wetu.”’ Yanabi’ul-Mawaddah: Kutoka kwa Rifah bin Musa amesema: “Nimemsikia Ja’far As-Sadiq (a.s) anasema katika kauli yake (s.w.t.): “Na kwake wamejisalimisha walio ardhini na mbinguni kwa hiyari na kwa lazima.” (Surat Ahzab: Al Imran: 83). Akasema: “Atakapodhihiri AlQaim Al-Mahdi hatabaki yeyote ardhini isipokuwa atatamka shahada. An Laa ilaaha illa llaahu wa anna Muhammadan Rasuulu llaahi.” 50


Al-Mahdi Katika Sunna Yanabi’ul-Mawaddah: Kutoka kwa Al- Baqir (a.s) amesema: “Hakika Uislamu utashinda dini zote wakati atakapo kuja Al-Mahdi.” Yanabi’ul-Mawaddah: Kutoka kwa Jafar-As-Sadiq (a.s) amesema: “Wakati atakapodhihiri Mahdi watafurahi waumini kwa nusura ya Mwenyezi Mungu.”13

WATETEZI WA MAHDI Sunanu Ibnu Maajah: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w): “Watatoka watu kutoka Mashariki basi watakuwa chini ya Mahdi; yaani katika utawala wake.” Maelezo: Yaani kundi la waumini litasimamisha Uislamu na kuimarisha misingi ya dini na kuamrisha mema, na kukataza maovu, na wataijaza nchi dini na imani, kama utangulizi wa kudhihiri Al-Imam Al-Mahdi (a.s). Hadith hii na mifano yake ambayo imepita, litakuja jawabu lake kwa kauli iliyoenea kwa baadhi ya watu wanaosema kwamba, kufuru na upotovu ni wajibu uenee ili umfanye Imam adhihiri haraka, nayo ni kauli ambayo haina dalili juu yake, kwani Hadith zinasema “Baada ya kujazwa dhulma na uonevu.” Na wala sio kufuru na upotovu, na dhulma na uonevu inahusu pia maasi ambayo wanafanyiana watu wenyewe au baadhi yao kwa baadhi, hivyo hakuna dhahiri yake katika kutekeleza kanuni ya kufuru ya nchi hadi iwe ni kikwazo cha kuamrisha mema na kukataza maovu ambazo ni wajibu mbili kubwa. Is’aafur-Raghibiyna cha As-Swaban Al-Hanafiy: “Imekuja katika riwaya kwamba wakati wa kudhihiri kwake atanadi juu ya kichwa chake malaika atasema: ‘Huyu ni Mahdi khalifa wa Mwenyezi Mungu basi mfuateni.’ Hadi akasema: ‘Na Mahdi atatoa sanduku katika pango la Antwakiyah na 13 Suratu Ruum: 4 51


Al-Mahdi Katika Sunna nakala ya Torat katika mlima Sham, ataitolea hoja kwa Wayahudi hivyo wengi watasilimu kwake.”’ Maswabihus-Sunnah cha Al-Baghaniy: Kutoka kwa Abu Said kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) katika kisa cha Mahdi amesema: “Mwanaume ataomba kwake, atasema: ‘Ewe Mahdi nipe, nipe’ akasema: ‘Basi atamuwekea katika nguo yake anayoweza kuyabeba.”’ Muntakhab Kanzul-Umaal: “Hakika katika umma wangu atatokea Mahdi ataishi miaka mitano au saba au tisa, atamjia mwanaume atasema: ‘Ewe Mahdi nipe nipe’, basi atamuwekea katika nguo yake anayoweza kuyabeba.” Yanabi’ul-Mawaddah: Kutoka kwa Amirul-Muuminina Ali (a.s) amesema: “Haitakuja nusura ya Mwenyezi Mungu mpaka ipuuzwe mno kwa watu kuliko mzoga, nayo ni kauli ya Mola Wangu Mtukufu katika Surat Yusuf: “Hadi Mitume watakapokata tamaa na wakadhani kuwa wao wameshadanganywa basi itawajia nusura yetu.” (Surat Yusuf: 11). Na hiyo ni wakati wa kudhihiri Al-Mahdi.” Muntakhabu Kanzul-Umaal: Kutoka kwa Mtume (s.a.w.w): “Anatokana na sisi ambaye Isa ataswali nyuma yake.”

KWA AJILI YA MAHDI SWALA INAKIMIWA Ghayatul-Maamuul: Amesema Mtume (s.a.w.w): “Mahdi atatokeza na wakati huo Isa bin Maryam ameshateremka, kana kwamba nywele zake zinadondoka maji, Mahdi atamwambia: ‘Tangulia uswalishe watu. Atasema: ‘Hakika swala hii imeshakimiwa, basi ataswali nyuma ya mtu atokanaye na kizazi changu naye ni Mahdi.”’ Yanabi’ul-Mawaddah: Kutoka kwa Hisham bin Muhammad amesema: 52


Al-Mahdi Katika Sunna “Al-Mahdi ni ambaye atamswalisha Isa bin Maryam.” Anuwarut-Tanzil: Katika tafsiri ya kauli yake (s.w.t.): “Na kwa hakika yeye ni alama ya Saa ya Kiyama.” (Surat Zukhruf: 61). katika Hadith imesemwa: “Atateremka Isa bin Maryam (a.s) kwa mara ya pili katika ardhi tukufu inayoitwa Afiyq na mkononi mwake ana silaha, kwayo atamuuwa Dajal kisha atakwenda katika Baitul-Muqadas huku watu wakiwa kwenye swala ya Asubuhi, Imam atarudi nyuma, hivyo Isa atamtanguliza na ataswali nyuma yake katika sheria ya Muhammad (s.a.w.w).” Amesema Ali bin Burhan Diyn Al-Halabiy Ash-Shafi’iy katika Siratu alHalabiyah: “Tunapokea kwamba itakuwa wakati wa swala ya Asubuhi na ataswali nyuma ya Mahdi baada ya kumwambia: ‘Tangulia ewe Ruhullah.’ Atasema: ‘Tangulia Swala imekimiwa kwa ajili yako.”’ Maelezo: Ardhul–Muqadasah: Yaani Sham na inayoizunguka. Imekuwa ni tukufu kwa sababu ni mahala walimozaliwa Mitume watukufu: Nuhu, Ibrahim, Musa, Isa na Manabii wengine (a.s). Dajal: Ni mtu atakayekuja Kwa watu kabla ya kudhihiri Mahdi (a.s) na ataeneza kwao maasi, madhambi na uovu na atakuwa ni katika viongozi wa uovu. “Ataswali nyuma yake kwa sheria ya Muhammad.” Yaani: Isa atafuata sheria ya Kiislamu katika namna ya kuswali na ataacha sheria yake na namna ya Swala ambayo ilikuwa ikitumika wakati wa unabii wake.

BENDERA YA MAHDI Yanabi’ul-Mawaddah cha Al-Qanduzy Al-Hanafiy: Kutoka kwa Naufu amesema: “Bendera ya Mahdi imeandikwa: Bayi’a ni kwa ajili ya Mwenyezi Mungu.” 53


Al-Mahdi Katika Sunna A-Burhan Fiy Alaamati Mahdi Akhriz-Zamaani: Kutoka kwa Ibnu Siriyni amesema: “Juu ya bendera ya Mahdi kumeandikwa bayi’a ni kwa ajili ya Mwenyezi Mungu.” Maelezo: Al-bayi’atu kwa maana ya Al-bay’u na imeitwa al-bayi’atu bayi’ah kwa sababu anayetoa bayi’ah anauza nafsi yake, hivyo yuko tayari kwa vita, amani, hukumu, kila amri na kila katazo na kila hukumu katika kila wakati. Na Bendera ya Mahdi imeandikwa Bayi’a ni kwa ajili ya Mwenyezi Mungu (Al- baiyi’atu lillaah) yaani Al-Mahdi ni mwakilishi wa Mwenyezi Mungu na kumbayi’i yeye ni kumbayi’i Mwenyezi Mungu, na huu ni mkazo wa Bayi’ah ambao unapatikana kwa waumini kwa ajili ya Mwenyezi Mungu Mtukufu katika Qur’ani Tukufu ambapo anasema: “Hakika Mwenyezi Mungu amenunua kwa waumini nafsi zao na mali zao na kwamba wao watapata pepo.”14 (Surat Tauba: 111). A-Burhan Fiy Alaamati Mahdi Akhriz-Zamaani cha Al-Muntaqiy AlHindiy Al-Hanafiy: Kutoka kwa Ibnu Umar: “Hakika Mtume (s.a.w.w) alishika mkono wa Ali akasema: ‘Atatoka katika mgongo wa huyu kijana ataijaza ardhi uadilifu na usawa, mtakapoona hayo basi mwandameni kijana wa Tamimiy kwani yeye atatokea upande wa Mashariki naye ni mshika bendera wa Mahdi.” Maelezo: “Kijana wa Tamimiy” ni mwanaume kutoka Bani Tamimiy atalingania kwenye haki na kwa Imam Mahdi, atatokea Mashariki ya kati na atakapokutana na Imam Al-Mahdi (a.s) atamkabidhi bendera yake, hivyo atakuwa ni mbeba bendera. Na katika baadhi ya Hadith: “Hakika mwanaume wa Tamimiy ni (Shu’aibu bin Swalehe) mjumbe wa Mtume wa Mwenyezi Mungu Shu’aibu kwa kaumu yake.” Kama itakavyokuja baadaye. 14 Suratul Tauba: 111. 54


Al-Mahdi Katika Sunna

Al-Burhan Fiy Alaamati Mahdi Akhriz-Zamaani: Kutoka kwa Ammar bin Yaasir amesema: “Sufiyan atakapofika Kufah na kuuwa wafuasi wa kizazi cha Muhammad atatokea Al-Mahdi na mshika bendera wake Shu’aibu bin Swalehe.” Maelezo: Sufiyan kama walivyosema na katika baadhi ya Hadith ni mwanaume atakayekusanya majeshi na kushambulia nchi na kuuwa watu kabla ya kudhihiri Imam Al-Mahdi (a.s), Imam atakapodhihiri atampiga vita na kumuuwa na atawateka wafuasi wake, baina yao kuna watakaomwamini Imam na kuna atakaowauwa.15 Na Shu’aibu bin Swaleh ni mjumbe aliyetumwa na Mtume Shu’aibu kwa kaumu yake ili awafanyie tablighi wakamchukua na kumuuwa na wakamtupa kwenye shimo. “Mtume Shu’aibu (a.s.) yeye – kama ilivyo katika Safinatul-Bihar ni Shu’aibu bin Mukiyl-bin Yashijab bin Madyan bin Ibrahim (a.s).16 Yanabi’ul-Mawaddah: “Abu Muhammad Hasan alipata mtoto akamwita Muhammad akamuonyesha kwa wafuasi wake siku ya tatu na kusema ‘Huyu ni Imam wenu baada yangu na khalifa wangu kwenu naye ndio AlQaim ambaye kwake zitanyooka shingo kwa kusubiri wakati dunia itakapojaa dhulma na uonevu atatokea na kuijaza uadilifu na usawa.”’

15 Safinatul-Bihar: Juz. 1, madatu sufun 16 Safinatul-Bihar Juz. 1, madatu Shiaib. 55


Al-Mahdi Katika Sunna

KILA KITU KITAMFURAHIA A-Burhan Fiy Alaamati Mahdi Akhriz-Zamaani: Kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) katika kisa cha Al-Mahdi na kumbayi’i kwake baina ya rukun na maqam, na kutokea kwake hali ya kuwa anaelekea Sham amesema: “Jibril atakuwa mbele yake na Mikaeli atakuwa nyuma yake, kwaye watafurahi watu wa mbinguni na wa ardhini, ndege, wanyama na samaki wa baharini.” Maelezo: “Baina ya rukun na maqam.” Yaani baina ya jiwe jeusi na Maqamu Ibrahim katika Ka’aba Tukufu, Mwenyezi Mungu ataizidishia utukufu, kwani yeye (a.s) atadhihiri huko mwanzo. “Nyuma yake.” Yaani kwa maana ya kwamba (a.s) atakuwa ameungwa mkono kwa amri ya Mwenyezi Mungu na Jibril na Mikael mmoja wao atakuwa mbele na mwingine nyuma yake. Watafurahi kwaye wote kwa sababu atatekeleza uadilifu halisi, na uadilifu kamili unaleta furaha kwa kila kitu.

ALAMA ZA KUJITOKEZA MAHDI Nurul-Abswar cha Shablanjiy Ashaafy: Kutoka kwa Abu Ja’far (a.s) amesema: “Watakapojifananisha wanaume na wanawake, wanawake kujifananisha na wanaume, wenye kuoa kufanya zinaa, watu kuacha Swala na kufuata matamanio, kuwa wepesi wa kumwaga damu na kuamiliana kwa riba, wakadhihirisha zinaa; kujenga majumba marefu, wakahalalisha uongo na kuchukua rushwa; wakafuata matamanio, wakauza dini kwa dunia, wakakata udugu, wakafanya ubakhili wa chakula, upole ukawa ni udhaifu na dhulma ikawa ni ufahari, watawala kuwa waovu na wasaidizi wakawa waovu, wanaoaminiwa wakafanya hiyana, wasomaji wakawa 56


Al-Mahdi Katika Sunna mafasiki, uonevu ukadhihiri, talaka zikawa nyingi, uovu ukaenea, ushahidi wa uongo ukakubalika, pombe zikanywewa, wanaume kulawitiana, na wanawake wakafanya msagano, mali za mafukara zikawa ni chumo, na sadaka ikawa ni deni, na waovu wakaogopwa kwa ndimi zao, Sufiyani atatokea kutoka Sham na Aliyaman atatokea Yemen na atadidimia katika sehemu iitwayo Baidai baina ya Makka na Madina. Na atamuuwa kijana katika kizazi cha Muhammad baina ya rukun na maqamu, na atanadi mwenye kunadi kutoka mbinguni: “Hakika haki iko naye pamoja na wafuasi wake” Akasema: “Atakapotokea (Al-Mahdiy) ataegemeza mgongo wake kwenye Al-Ka’aba na watakusanyika kwake watu mia tatu na kumi na tatu miongoni mwa wafuasi wake, atakachotamka mwanzo ni Aya hii “Mali aliyobakisha Mwenyezi Mungu kwenu ndiyo bora zaidi kwa ajili yenu ikiwa nyinyi ni wenye kuamini.” (Surat Hud: 86). Kisha atasema: “Mimi ndio salio la Mwenyezi Mungu, khalifa wake, na Hujjah yake kwenu.” Basi hatomsalimia yeyote isipokuwa atasema: As-salam alaika ya baqiyatullaah, basi hatobakia Myahudi wala Mnasara wala yeyote kati ya wanaoabudu asiyekuwa Mwenyezi Mungu, isipokuwa atamwamini na kumsadikisha, na mila itakuwa ni moja tu, mila ya Ki-Islam, na kila kilichopo ardhini katika yanayoabudia kinyume cha Mwenyezi Mungu moto utateremka kutoka mbinguni na kukiunguza.” Maelezo: Hadith hii na mfano wake inabeba alama nyingi za kudhihiri, nayo inahitaji kushereheshwa sherehe yenye kutosheleza, isipokuwa nafasi yetu ni finyu haituruhusu zaidi ya kuashiria katika baadhi ya nukta zake tu. “Wanaume kujifananisha na wanawake” ama kwa ukhabithi kwa kulawitiana au kujifananisha katika kazi, mwanamke anatoka kufanya kazi ngumu na majukumu mazito ambayo yanapingana na maumbile yake dhaifu, hisia zake laini. Au kujifananisha katika mavazi yake, na yote yanawezekana na mengineyo. Pia mambo hayo hayo “Na wanawake kujifananisha na wanaume” kwa kinyume chake. 57


Al-Mahdi Katika Sunna “Wepesi wa kumwaga damu” yaani kuuwa kutakuwa ni kitu chepesi kwa watu. “Wakahalalisha uongo” yaani watasema kuwa uongo ni halali na wala si haramu. “Na wasomaji” yaani wasomaji wa Qur’ani mafasiki, wanasoma kwa sauti nzuri tu na wala hawafaidiki kutokana na Qur’ani kwa kuifanyia kazi. “Dhulma itadhihiri” yaani dhulma itakuwa dhahiri shahiri, madhalimu hawataificha kwa kumuogopa yeyote wala kumwonea haya mtu yeyote. “Wanawake wakasagana” yaani hawataolewa, bali kila mmoja atatosheka kwa mwanamke mwenzie katika kukidhi matamanio yake ya kimwili, kitendo ambacho kinaitwa msagano katika Uislamu, nayo ni haramu kabisa na kuna adhabu mahsusi imetajwa katika vitabu vya Fiqhi, kwani inavunja familia, hudumaza kizazi na kisha kuumaliza umma. “Na mali kuwa ngawira” yaani mali ya mafakiri atakayeipata ataichukulia kuwa ni ngawira anaichukua mwenyewe anaila na kuikandamiza. “Na sadaka itakuwa kama deni” yeyote atakayetoa sadaka kwa kitu atachukulia ni kama deni lililotoka kwake hii ni kinaya ya kutoa sadaka hali ya kuwa anachukia. “Al-Yaman” Ni mtu atakayetokea kutoka Yemen atalingania haki na amani naye ni kati ya watakaohimiza amani kwa ajili ya Imam Al- Mahdi kama ilivyo katika Hadith ya Imam Al-Baaqir (a.s)17 “Kudidimia Baidai” Kudidimia kwa jeshi la Sufiyan ambalo litatoka Sham kwenda Makka kumpiga vita Mahdi (a.s), Hadith yake imeshapita katika 17 Safinatul-Bihar: Juz. 2 madatu yaman. 58


Al-Mahdi Katika Sunna baadhi ya Hadith. “Ambaye anamwabudu asiyekuwa Mwenyezi Mungu” yaani masanamu na mizimu n.k.

ALAMA ZA AJABU A-Burhan Fiy Alaamati Mahdi Akhriz-Zamaani cha Al-Mutaqiy AlHindiy Al- Hanafiy: Kutoka kwa Abdillah bin Abbas (r.a.) amesema: “Hatotoka Mahdi mpaka itokee alama kwenye jua.” Maelezo: Alama ambayo itatokea kwenye jua, yaani kama ilivyo katika baadhi ya Hadith ni kwamba kitaonwa kichwa kutoka katika jua kinanadi: “Ee ameshadhihiri walii wa Mwenyezi Mungu aliyeahidiwa hivyo toeni bayi’a kwake.” Na katika baadhi ya Hadith ni Jibril. A-Burhan Fiy Alaamati Mahdi Akhriz-Zamaani: Kutoka kwa Muhammad bin Ali amesema: “Mahdi wetu ana alama mbili hazijatokea tangu Mwenyezi Mungu aumbe mbingu na ardhi, mwezi, utapatwa usiku wa kwanza katika Ramadhani, jua litapatwa katika nusu ya mwezi na haijawahi kutokea tangu Mwenyezi Mungu aumbe mbingu na ardhi.” Maelezo: Kulingana na elimu ya anga ni muhali kupatwa mwezi mwanzo wa mwezi, na hiyo haijawahi kutokea katika historia ya mwezi, dunia na ulimwengu… Kama ambavyo ni mustahili katika elimu ya anga kutokea kupatwa kwa jua katikati ya mwezi, hivyo haijawahi kutokea katika historia ya jua, dunia na ulimwengu. Vile vile ni mustahili jua kutokea Magharibi kwa sababu italazimu kubadili mzunguko wa ardhi kulizunguka jua, na jambo hili ni kati ya mustahili wa awali, kwa sababau ni kukiuka taratibu nyingi za ulimwengu, nguvu ya mvutano n.k. Lakini Mwenyezi Mungu Muweza wa kila kitu atafanya mustahili huu uwezekane utakapowadia wakati wa kudhihiri walii Wake na mtekeleza sheria Zake Imam Al-Mahdi (a.s). 59


Al-Mahdi Katika Sunna

FITINA MBAYA KULIKO FITINA ZOTE A-Burhan Fiy Alaamati Mahdi Akhriz-Zamaani cha Al-Mutaqiy amesema: “Nilimwambia Muhammad bin Ali: Nimesikia kwamba atatokea kwenu mwanaume ambaye atatengeneza umma huu. Akasema: ‘Hakika sisi tunataraji ambayo watu wanayaona, na sisi pia tunataraji, lau isingebaki katika umri wa dunia isipokuwa siku moja, basi Mwenyzi Mungu angeirefusha siku hiyo mpaka yatimie ambayo umma unayatarajia kabla ya fitina mbaya kuliko fitina zote, mtu atashinda muumini na ataamka kafiri, atakayefikia hayo kati yenu basi amuogope Mwenyezi Mungu na awe ni kati ya mwenye kuilazimu nyumba yake.”’ Maelezo: “Wanaoilazimu nyumba yake” yaani kati ya wasioacha nyumba yake, na hii ni kinaya ya kutofuata watu katika nyendo zao za batili, na wala haina maana kwamba kuwaacha watu na mambo yao asiamrishe mema wala kukataza maovu, kwani haya ni mambo mawili makubwa ya wajibu ambayo kwayo faradhi zinatekelezwa, kama ilivyo katika Hadith, hayaachwi kwa mfano wa Hadith hii ambayo inaweza kusemwa kuwa ni ya ujumla. Na naitakidi kuwa maana ya Hadith hii ni ibara nyingine ya Hadith nyingine inayosema: “Kuwa katika watu na wala usiwe pamoja nao.” Ndio, hili ni jambo gumu, lakini naliwe maadamu liko kwa watu, na maadamu kutengamana pamoja nao ni kwa ajili ya kuwaamrisha mema na kuwakataza maovu. A-Burhan Fiy Alaamati Mahdi Akhriz-Zamaani: Kutoka kwa Abu Abdillah Al- Husein bin Ali (a.s.): “Mtakapoona alama kutoka mbinguni, moto mkubwa kutoka upande wa Mashariki utatokea kwa muda wa nusu siku, wakati huo ni faraja kwa aali Muhammad au faraja kwa watu nao ni wakati wa kuja Al-Mahdi (a.s).”

60


Al-Mahdi Katika Sunna Yanabiula- Mawadah: Katika kauli yake (s.w.t.): “Tukitaka tutateremsha kwao alama kutoka mbinguni.” (Surat Shu’arai: 4). Kutoka kwa Abu Baswir na Ibnul-Jaruud kutoka kwa Al-Baaqir (a.s.) amesema: “Atanadi mwenye kunadi kwa jina lake na jina la baba yake kutoka mbinguni.”

SAUTI YA MBINGUNI Yanabi’ul-Mawaddah cha Al-Qanduziy Al-Hanafiy: Katika kauli yake (s.w.t.) “Na sikiliza siku atakaponadi mwenye kunadi kutoka sehemu ya karibu siku watakayosikia sauti ya haki, hiyo ndio siku ya kutoka.” (Surat al-Qaf: 41 - 42). Kutoka kwa Imam Sadiq (a.s) amesema: “Atanadi mwenye kunadi jina la Al-Mahdi na jina la baba yake (a.s), na sauti katika Aya hii ni sauti kutoka mbinguni, na hiyo ndio siku ya kutoka Al-Mahdi.” A-Burhan Fiy Alaamati Mahdi Akhriz-Zamaani: “Atatokea Al-Mahdi na juu ya kichwa chake kuna malaika ananadi: huyu ni Mahdi (a.s) khalifa wa Mwenyezi Mungu, mfuateni.” Al-Bayanu cha Al-Kanjiy Ash-Shaafiy: Kutoka kwa Abdillah bin Umari amesema: “Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w): ‘Mahdi atatokea na juu ya kichwa chake kuna wingu, humo kuna mwenye kunadi, ananadi huyu ni Mahdi khalifa wa Mwenyezi Mungu, mfuateni.” Amesema katika Burhan, amesema katika Uqudu Durar: ‘Na wito huu utawafikia watu wote wa ardhini na kila watu watasikia kwa lugha yao.”’ Maelezo: Wito huu ulikuwa mzito katika masikio ambayo yalikuwa hayaamini ghaibu na uwezo wa Mwenyzi Mungu Mtukufu, lakini leo limekuwa ni jambo la kawaida na rahisi kueleweka, baada ya mwanadamu kuvumbua chombo ambacho kinawekwa katika kumbi kubwa katika nchi kubwa na katika kumbi za kawaida n.k. Anazungumza mtu kwa lugha ya kiarabu – kwa mfano - na chombo kinatarjumu maneno kwa lugha ya kiin61


Al-Mahdi Katika Sunna gereza, kifaransa, kifursi, kiurudu na nyinginezo na kuitawanya kwa kila mtu kulingana na lugha yake. Uislamu wote ni miujiza, kila elimu inapopanuka na teknolojia inapokua inadhihiri katika Uislamu miujiza na maajabu. Is’ aafur-Raghibiyna cha Al- As-Swabani Al-Hanafiy: Imekuja katika riwaya kwamba wakati wa kudhihiri kwake atanadi juu ya kichwa chake malaika: “Huyu ni Mahdi khalifa wa Mwenyezi Mungu, mfuateni.” A-Burhan Fiy Alaamati Mahdi Akhriz-Zamaani: Amepokea Abu Nuaiym kutoka kwa Ali amesema: ‘Hatatokea Mahdi mpaka iuliwe theluthi, ife theluthi na ibaki theluthi.” Maelezo: Hadith hii tukufu inaashiria mapigano ya makundi ambayo yanatokea leo na yalikuwa yanatokea zamani, na kuna ihtimali kutoka katika ulimwengu miongoni mwa vita vya dunia, na vita vya kienyeji ambapo watakufa baina ya muda na muda maelfu.

SUFIYANIY Yanabi’ul-Mawaddah: Kutoka kwa Al-Mahajjah kutoka kwa Ali (a.s) katika Aya hii “Na kama utaona watakapotishika basi hakuna kuponyoka” (Surat Sabai: 51). “Aya inakubali kutokea kwa Al-Mahdi, atatokea Sufiyani atatawala kwa kiasi cha muda wa mimba ya mwanamke miezi tisa jeshi lake litaelekea mji wa Madina, litakapofika Baidai Mwenyezi Mungu atalididimiza.” Maelezo: “Al-Baidai” yaani jangwa baina ya Madina na Makka litakuja tetemeko kubwa na mtingishiko, watakufa kwalo jeshi la Sufiyaniy linalotokea Shamu, na maelezo zaidi yatakuja katika hadith ifuatayo. A-Burhan Fiy Alaamati Mahdi Akhriz-Zamaani: Kutoka kwa AmirulMu’minina Ali bin Abi Talib (a.s.) amesema: “As-Sufiyan ni mwanaume 62


Al-Mahdi Katika Sunna mwenye mwili mkubwa, katika uso wake kuna athari za vipele, katika jicho lake kuna nukta nyeupe, atatokea upande wa mji wa Damascus na katika jumla ya watakaomfuata ni mbwa, atauwa na atapasua matumbo ya wanawake, atauwa watoto atawakusanya kwa jeuri na atawauwa hadi hatokataza mimea kung’olewa, ndipo atatokea mwanaume katika AhlulBaiti katika Haram (Makka) Sufiyan atapata habari, atatuma kwake askari katika askari wake, atawashinda, hivyo Sufiyani atamwendea pamoja na alionao hadi atakapofika Baidai atateketezwa hatonusurika isipokuwa mtoa habari juu yao.”

ALAMA TANO A-Burhan Fiy Alaamati Mahdi Akhriz-Zamaani: Kutoka kwa Abu Abdillah Husein bin Ali (a.s) amesema: “Mahdi ana alama tano: AsSufiyani, Al- Yamaniy, sauti kutoka mbinguni, kudidimia Baidai na kuuliwa nafsi isiyo na hatia.” Maelezo: Maana ya alama nne za mwanzo zimetangulia. Ama Nafsi isiyo na hatia, ni ambaye ametajwa katika baadhi ya hadith kuwa ni Seyyid AlHusein. Atatokea na atalingania haki na atauliwa kabla ya kudhihiri AlMahdi (a.s). A-Burhan Fiy Alaamati Mahdi Akhriz-Zamaani: Kutoka kwa Amr bin Al-Aas amesem: “Alama za kutokea Mahdi, litakapoteketezwa jeshi Baidai basi hiyo ndio alama ya kutokea Al- Mahdi.”

DAJAL Yanabi’ul–Mawaddah cha Al-Qanduziy Al-Hanafiy: Kutoka kwa Abu Amamah amesema: “Alituhutubia Mtume (s.a.w.w) na akamtaja Dajal, na akasema: ‘Uovu utateketeza Madina kama ambavyo mfua chuma anavyomaliza chuma na siku hiyo kutanadiwa nusra, nusra.’ Ummu Shariyki akasema: ‘Waarabu watakuwa wapi siku hiyo ewe Mtume wa Mwenyezi 63


Al-Mahdi Katika Sunna Mungu?’ Akasema: ‘Wao siku hiyo watakuwa wachache na wengi wao wako Baitul-Maqdis na Imam wao Al-Mahdi (a.s).”’ A-Burhan Fiy Alaamati Mahdi Akhriz-Zamaani: Kutoka kwa Abu Ja’far (a.s) amesema: “Mahdi atadhihiri siku ya Ashura nayo ni siku ambayo aliuliwa humo Husein bin Ali (a.s.) kana kwamba ni siku ya jumamosi siku ya kumi Muharram, atasimama baina ya rukun na maqaam Ibrahim, Jibril yuko kuliani kwake na Mikaeli yuko kushotoni kwake na wafuasi wake watamwendea toka kila pembe ya ardhi, itakunjwakunjwa kwao mpaka wampe kiapo cha utii, basi ataijaza ardhi kwao uadilifu kama itakavyokuwa imejazwa dhulma na uovu.” Maelezo: “Itakunjwakunjwa kwao” hivyo watahudhuria kutoka kila pande za ardhi, kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu punde tu watakuwa Makka mbele ya Imam Al-Mahdi (a.s). Hii sio ajabu kwani Qur’ani tukufu imetaja kwamba ardhi ilikunjwa kwa masafa ya maelfu ya maili kwa ajili ya Asif bin Barkhiya wasii wa Mtume wa Mwenyezi Mungu Suleiman bin Daud katika kisa cha kuhamisha kiti cha enzi cha Balqis kutoka Yemeni hadi Palestina kwa muda mchache kuliko punde moja ambapo alisema (s.w.t.):

“Akasema ambaye ana elimu miongoni mwa kitabu, mimi nitakuletea kabla hujafumba jicho lako, alipokiona kipo mbele yake….).(Surat Naml: 40).

UMMA UTAKUWA MKUBWA Al-Mutadrak As-Sahihain cha Al-Haakim An-Nisaburiy: Kutoka kwa Abu Said Al-Khudriy (r.a) hakika Mtume wa Mwenyezi Mungu amesema: “Atatokea katika mwisho wa umma wangu Al-Mahdi, Mwenyezi Mungu 64


Al-Mahdi Katika Sunna atamnyeshelezea mvua, ardhi itatoa mimea yake na atagawa mali sana, wanyama watazaliwa kwa wingi na umma utakuwa mkubwa.” Maelezo: “Mwenyezi Mungu atamnyeshelezea mvua” yaani mvua itanyesha kwa wingi hivyo itakuwa ni sababu ya mazao na kheri kuwa nyingi. “Atagawa mali sana” yaani kwa wingi, hatatoa kwa yeyote nusu wala robo. “Umma utakuwa mkubwa” yaani umma wa kiislamu utakuwa mkubwa mno. Al-Mustadrak As-Sahihain cha Al-Haakim An-Nisaburiy: Kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) amsema: “Katika umma wangu kutakuwa na Mahdi kama atatawala kwa muda mchache basi ni miaka saba vinginevyo ni tisa, umma wangu utaneemeka humo kwa neema ambapo haujawahi kuneemeka kabla yake, ardhi itatoa baraka zake zote na wala haitabakisha kitu na mali siku hiyo itakuwa kama vile mchanga (nyingi), mtu atasimama na kusema chukua.”

UMMA MCHACHE Yanabi’ul-Mawaddah: Kutoka Abu Khalidi Al-Kaabil kutoka kwa AlImam Ja’far As-Sadiq (a.s) katika kauli yake (s.w.t.): “Shindaneni kwa kheri popote mtakapokuwa Mwenyezi Mungu atawakusanyeni nyote.” (Surat Al-Baqarah: 148). Amesema: “Yaani wafuasi wa AlMahdi wako mia tatu na kumi na tatu na wao wallahi ni umma mchache, watakusanyika katika muda wa saa moja kama vile mawingu ya kipupwe yaliyotawanyika.” Maelezo: Kufananishwa na mawingu ya kipupwe ni kwa sababu mawingu wakati wa kipupwe yanakusanyika haraka, na wafuasi wa Al-Imam Mahdi (a.s) watakusanyika kutoka pande zote za ardhi kwa haraka mno kwa Imam (a.s).

65


Al-Mahdi Katika Sunna Yanabi’ul–Mawaddah: Katika kauli Yake (s.w.t.): “Na hata kama tutawacheleweshea adhabu hadi muda uliohesabiwa umma mchache” (Surat Hadid: 8). Akasema: “Hakika umma mchache ni wafuasi wa AlMahdi katika akhiri zamani, ni watu mia tatu na kumi na tatu kama vile idadi ya Ahlul-Badri, watakusanyika katika muda wa saa moja kama yanavyokusanyika mawingu ya kipupwe.” Tarikh Ibni Asakir Ash-Shaafiy: “Atakapodhihiri Al-Mahdi wa Aali Muhammadi Mwenyezi Mungu atamkusanyia watu wa Mashariki na watu wa Magharibi hivyo watakusanyika kama yanavyokusanyika mawingu ya kipupwe, ama waambata ni katika watu wa Kufah na ama watu wema mbadala watatoka Shaam.” Maelezo: “Atamkusanyia watu wa Mashariki na watu wa Magharibi” yaani ulimwengu utakuwa chini ya amri yake kwa haraka ya ajabu kwa sababu yeye (a.s) atakuja wakati dhulma na huku uonevu umefunika ulimwengu wote, na watu wote wanamsubiri mtu anayeita wito wa ukombozi na nusura, hivyo atakapodhihiri Imam Al-Mahidi (a.s) na kuita wito wa haki, watu wote watamwamini. Na tumeshaeleza maudhui haya kwa ufafanuzi zaidi katika kitabu chetu kuhusu Al-Imam (a.s) kwa jina la AlMahdi Al-Muntadhir Khatamul-Musiyai. “Waambata” huenda makusudio yake ni wasaidizi na wafuasi wa daraja la kwanza, ambao ni watu wa karibu mno na Imam hadi wakaitwa waambata. “Watu wema mbadala” ni kinaya ya wema, wachamungu ambao kila anapoghibu au kufa mmoja wao, Mwenyezi Mungu anambadilisha kwa mtu mwingine kati yao. “Shaam” katika historia na elimu ya Hadith sio Shaam ya sasa, bali makusudio yake ni sehemu ya Syria, Lebanon, Palestina, Jordan na sehemu ya Uturuki kulingana na mgawanyo wa nchi za hivi sasa. Na huenda hawa wema mbadala au sehemu kati yao ni kutoka Jabalu A’amil ambayo 66


Al-Mahdi Katika Sunna imekuwa tangu zama ya mwanzo ya Uislamu ni yenye kutetea haki na imani hadi leo, na imetoa maelfu na maelfu ya maulamaa wachamungu, hadi maulamaa wameandika vitabu mahsusi kuhusu Jabalu A’amil, na kati ya vitabu hivyo ni Amalul-Aamili Fiy Ulamaai Jabali Aamili cha mwanchuoni mkubwa al-Muhadith Sheikh Muhammad Al-HurrulAamiliy, Mwenyezi Mungu amrehemu.

MAISHA YA UADILIFU Yanabi’ul-Mawaddah: Katika kauli yake (s.w.t.): “Jueni kwamba Mwenyezi Mungu ataihuisha ardhi baada ya kufa kwake” (Surat alHadid: 17). Kutoka kwa Salaam bin Mustaniyr kutoka kwa Baqir (a.s) amesema: “Mwenyezi Mungu ataihuisha kwa Al-Mahdi, atafanya uadilifu kwayo hivyo ataihuisha ardhi kwa uadilifu baada ya kufa kwake kutokana na dhulma.” Yanabi’ul-Mawaddah: Katika kauli yake (s.a.w.w): “Na hakuna katika Ahlul-kitab isipokuwa watamwamini kabla ya kufa kwake, Siku ya Kiyama atakuwa shahidi juu yao” (Suratun-Nisai: 159). Amesema: “Hakika Isa atateremka duniani kabla ya Siku ya Kiyama hivyo hatabaki yeyote katika mila ya Kiyahudi wala nyingineyo isipokuwa watu watamwamini kabla ya kufa kwao, na Isa ataswali nyuma ya Imam AlMahdi (a.s).” Tadhikratul-Khawas cha Sibtwi Ibnu Jauziy Al-Hanafy: Amesema Asadiy: “Mahdi na Isa bin Mariyam watakutana utakapowadia wakati wa Swala, Mahdi atamwambia Isa: ‘Tangulia.’ Isa atasema: ‘Wewe ndio unafaa zaidi.’ Hivyo Isa ataswali nyuma yake hali ya kuwa maamuma.”

67


Al-Mahdi Katika Sunna

WATAPIGANIA HAKI Sahih Muslim: Amesema Jabir bin Abdillah: “Nilimsikia Mtume (s.a.w.w) anasema: ‘Halitaacha kundi katika umma wangu kuwa ni lenye kupigania haki waziwazi hadi siku ya Kiyama.’ Akasema: ‘Atateremka Isa bin Maryam, Amiri wao atasema: ‘Njoo tuswalishe’, atasema: ‘Hapana, hakika baadhi yenu kwa baadhi ni maamiri kwa ukarimu wa Mwenyezi Mungu kwa umma huu.”’ Maelezo: Hadith hii inaonyesha kuendelea kulingania kwa ajili ya Mwenyezi Mungu na haki katika dunia hadi wakati wa kudhihiri Al-Mahdi (a.s). Na hili ni jawabu kwa wenye kudumaa, ambao wanasema: “Ni wajibu dunia ijae ukafiri, upotovu hadi atakapodhihiri Imam Al-Mahdi. Hivyo tusifanye chochote ili adhihiri haraka” nayo ni makosa katika pande nyingi, tumetaja baadhi yake huko mwanzo. Is’aafur-Raghibiyna cha As-Swabani Al-Hanafiy: “Imekuja katika riwaya kwamba wakati wa kudhihiri atanadi juu ya kichwa chake malaika: ‘Huyu ni Mahdi khalifa wa Mwenyezi Mungu mfuateni.’ Basi watu watamtii na kumpenda sana, naye atatawala ardhi kuanzia Mashariki hadi Magharibi na kwamba watakaompa kiapo cha utii kwanza baina ya rukun na maqam ni kama vile idadi ya Ahul-Badr kisha watakuja wachamungu wa Shaam, wema wa Misri, watukufu wa Mashariki na mfano wao, na Mwenyezi Mungu atatuma kwake jeshi kutoka Khurasan kwa bendera nyeusi kisha ataelekea Shaam, na katika riwaya nyingine ataelekea Kufah na kuna uwezekano wa kukusanya yote, hakika Mwenyezi Mungu Mtukufu atamuongezea malaika elfu tatu na kwamba Ahlul-Kahfi ni kati ya wasaidizi wake. As-Suyutwiy amesema: ‘Na wakati huo inatafsiriwa kucheleweshwa kwao katika muda huu ni kukirimiwa kwao kwa utukufu wa kuingia kwao katika umma huu kwa kumfuata kwao khalifa wa haki. Na kwamba katika mwanzo wa jeshi lake kuna mwanaume kutoka katika Tamimiy mwenye ndevu chache anayeitwa Shu’aib bin Swalehe, na kwamba Jibril atakuwa mbele ya jeshi lake na Mikaeli atakuwa nyuma yake, na kwamba Sufiyan 68


Al-Mahdi Katika Sunna atatuma kwake jeshi kutoka Shaam na litateketezwa Baidai, hatonusurika kati yao isipokuwa mtoa habari, hivyo Sufiyani ataelekea kwake pamoja na alionao na nusra itakuwa pamoja na Mahdi (a.s.) na atamuuwa Sufiyani.’”

HAUTABAKI UHARIBIFU Is’aafur-Raghibiyna: “Na katika baadhi ya athari ni kwamba atatokea katika miaka ya witiri (hadi aliposema) na kwamba utawala wake utafika Mashariki na Magharibi na itadhihiri kwake hazina na wala hautabakia katika ardhi uharibifu isipokuwa ataurekebisha.” Muntakhabu Kanzul–Umaal: Kutoka kwa Ali amesema: “Ee ni huruma ilioje kwa ardhi! Hakika Mwenyezi Mungu humo ana hazina sio katika dhahabu wala fedha, lakini humo kuna wanaume wamemjua Mwenyezi Mungu ukweli wa kumjua nao ni wafuasi wa Al-Mahdi akhiriz-zamani.”

AL-MAHDI NI NGOME IMARA Yanabi’ul-Mawaddah: Kutoka katika kitabu Al-Mahajjah: “Haikuwa kauli ya Luti kwa kaumu yake “Lau kama ningekuwa na nguvu kwenu au nijifiche kwenye ngome imara.” (Surat Huud: 80), ila kwa kutamani nguvu ya Al-Qaim Al-Mahdi na nguvu ya wafuasi wake, nao ni ngome madhubuti kwani mwanaume kati yao ni sawa na nguvu za watu arobaini, na kwamba moyo wa mmoja wao una nguvu kuliko uimara wa kipande cha chuma kama wangepitia kwenye milima ya chuma basi ingesambaratika, hawatoziweka panga zao hadi Mwenyezi Mungu aridhike.”

MKALI KULIKO SIMBA Yanabi’ul-Mawaddah cha Al-Qanduziy: Kutoka kwa Abu Ja’far Al-Baqir (a.s) amesema: “Hakika Mwenyezi Mungu Mtukufu atatia hofu katika nyoyo za wanaotupenda atakaposimama Qaim wetu na kudhihiri Mahdi wetu mtu atakuwa mkali kuliko simba na mwepesi kuliko mkuki.” 69


Al-Mahdi Katika Sunna Is’aafur-Raghibiyna cha As-Swabani Al-Hanafiy: “Katika baadhi ya athari ni kwamba yeye atatokea katika miaka ya witiri moja au tatu au tano au saba au tisa na kwamba baada ya kupewa kiapo cha utii Makka ataondoka kuelekea Kufah kisha Sham, atatawanya askari wake kwenda kwenye miji na kwamba mwaka mmoja katika miaka yake utakuwa ni sawa na miaka kumi.” Maelezo: Yaani ni sawa na miaka kumi katika maendeleo, kiuchumi na kisiasa kwenda katika neema, amani, kuenea kwa raha na utulivu katika ulimwengu wote. Yanabi’ul-Mawaddah: Katika kauli yake (s.w.t.): “Enyi mlioamini subirini na vumilieni.” (Surat Al-Imran: 200). Akasema: “Subirini katika kutekeleza faradhi na vumilieni adha za adui yenu na shikamaneni na Imam wenu Al-Mahdi anayesubiriwa.”

VITA VYENYE KUANGAMIZA As-Salimy amesema katika Uqudud-Durar kutoka kwa Abu Abdillah Husein bin Ali (a.s) amesema: “Mtakapoona moto upande wa Mashariki siku tatu au saba basi mtapata faraja ya Aali Muhammad Insha’allah.” Akasema: “Kisha atanadi mwenye kunadi kutoka mbinguni kwa jina la Mahdi basi watasikia kuanzia Mashariki hadi Magharibi hadi hatabaki anayesinzia isipokuwa atazinduka wala aliyelala isipokuwa ataamka wala aliyekaa isipokuwa atasimama kwa miguu yake kutokana na fadhaa, Mwenyezi Mungu amhurumie yule ambaye atasikia sauti hiyo na kuitikia, kwani hiyo ni sauti ya Jibril Malaika mwaminifu.” Maelezo: Haya ndio ambayo yametangulia katika baadhi ya Hadith kwamba alama itatokea katika jua, hiyo haikuwa wazi, na hii “kutoka mbinguni” iko wazi na iliyo wazi inafafanua ambayo haiko wazi. Nazo ni katika alama alizoziweka Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa umuhimu wa kudhihiri 70


Al-Mahdi Katika Sunna Al-Qaim Al-Mahdi (a.s), na huenda makusudio ya moto ni vita vya nyukilia au vinginevyo.

UTAWALA WA TANO NI WA AL- MAHDI (A.S) As-Swawiqul-Muhriqah: cha Ibnu Hajar Ash-Shaafiy: Kutoka kwa AbulQasim At-Twabaraniy kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) kwamba amesema: “Baada yangu kutakuwa na makhalifa kisha baada ya makhalifa kutakuwa na maamir, kisha baada ya maamir kutakuwa na wafalme na baada ya wafalme kutakuwa na madikteta kisha atatokea mwanaume katika AhlulBait wangu ataijaza ardhi uadilifu na usawa kama ambavyo itakuwa imejazwa dhulma.” Maelezo: Utawala wa aina nne utatangulia kudhihiri kwa Al-Imam AlMahdi (a.s): Makhalifa: Watadai kuwa ni makhalifa wa Mtume (s.a.w.w). Maamir: Hawadai ukhalifa bali wanadai kuwa ni watawala kwa ajili ya kutengeneza, kukomboa na kuhifadhi mali. Madikteta: Hawadai chochote bali ni udhalimu na udikteta na baada ya tajirba hii yote chungu, na baada ya mambo kufikia ukingoni atadhihiri Imam Al-Mahdi kwa dola ya haki, kheri na amani.

MAANA YA DAJAL Uqudu Durar cha As-Salimiy Ash-Shafi’iy: Kutoka kwa Abu Abbas Ahmad bin Yahya bin Taghlab amesema: “Hakika Dajal ameitwa Dajal kwa udanganyifu wake, inasemwa dajaltu As-saifa, unapoichovya kwa rangi ya mng’aro ya udanganyifu. Maelezo: Dajal ni kila uongo au udanganyifu ambao haupo kabisa. Dajala upanga, ni kuupaka rangi inayohadaa watu, kuwa ni halisi au chuma kizuri kiasi inang’ara kama vile kioo, Hivyo Dajal ni uwongo mtupu, hauna mashiko.

71


Al-Mahdi Katika Sunna

MAENDELEO MAKUBWA Al-Fusulul-Muhimah cha Ibnu As-Swibagh Al-Malik: Kutoka kwa Abu Ja’far (a.s) kutoka kwake amesema: “Atakapodhihiri Al-Qaim atakwenda Kufah, atapanua misikiti yake na atavunja sehemu zote zinazotokeza katika barabara, atafukia vyoo na mifereji inayoelekea katika vichochoro, hataona bidaa isipokuwa ataiondoa wala hatoona Sunna isipokuwa ataihuisha, atafungua Costantinople, China na milima ya dailam.” Maelezo: Dola atakayoiasisi Imam Al-Mahdi (a.s) ni dola yenye maendeleo makubwa, maendeleo kwa maana yake pana, upeo wake na aina zake, ataiasisi Imam Al-Mahdi (a.s). “Atapanua misikiti yake” kwa sababu watu wote watakuwa chini ya bendera ya imani. “Atavunja sehemu zilizojitokeza” ili zisibane wapitaji na vyombo vya usafiri na mji utakuwa mzuri ajabu. “Atavunja vyoo na mifereji” ili kutekeleza usafi mpana wa kiislaam. “Costantinople” markazi kubwa ya Manaswara. “China” markazi ya budhaa, ulahidi na ushirikina. “Milima ya daiylam” ni markazi ya Wayahudi na wengineo katika wakati huo. Hakika yeye ataunganisha ulimwengu chini ya bendera ya maendeleo makubwa katika nyanja zote, kifikra, kielimu, kisiasa, kitabia n.k.

72


Al-Mahdi Katika Sunna

KUSUBIRI FARAJA Yanabi’ul-Mawaddah cha al-Hanafihy: Kwa sanadi yake kutoka kwa Amirul-Mu’minina (a.s) amesema: “Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w): ‘Ibada bora ni kusubiri faraja.’ Al-Hafidhi Al-Qanduziy mtunzi wa kitabu hiki amesema: “Yaani kusubiri kudhihiri Al-Mahdi.” Maelezo: Kusubiri faraja na marekebisho kwa kudhihiri Imam Al-Mahdi (a.s) kunafanya kazi mbili kwa pamoja: Ya kiroho na kikazi. Ama kiroho ni kwa mapenzi na mawadda ambayo ni wajibu kwa watu kwa Imam kwa kauli yake (s.w.t.): “Isipokuwa kuwapenda jamaa zangu wa karibu.” (Surat Shura: 23). n.k. Ama kikazi ni kwa kufanya kazi kwa ajili ya Uislam na kujiandaa kuwa askari wa kiislamu atakapodhihiri Imam ili mtu awe ni miongoni mwa watakaoridhiwa na Imam (a.s.)

AL-MAHDI YUKO KATIKA VITABU VYOTE Uqudu Durar cha As-Salimiy Ash-Shaafiy: Kutoka kwa Amru Al-Maqariy katika Sunan yake, na Al-Hafidh Nuiym bin Hamad kutoka katika vitabu vya wachungaji ameeleza kwamba: “Hakika mimi namkuta Mahdi ameandikwa katika vitabu vya Manabii, utawala wake sio wa dhulma wala wa mabavu.” Maelezo: Yaani utajo wa Mahdi uko katika vitabu vya Mitume vilivyoteremshwa kwao kutoka kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, yaani vitabu vyote vya Mitume.

UTULIVU NA UNYENYEKEVU Uqudu Durar: Kutoka kwa Al-Harithi bin Al-Mughiyrah An-Nadhariy amesema: “Nilimuuliza Abu Abdillah bin Ali (a.s) kwa kitu gani atafahamika Al-Mahdi?” Akasema: “Kwa utulivu na unyenyekevu.” 73


Al-Mahdi Katika Sunna Uqudu Durar: Kutoka kwa Al-Hafidh Abu Muhammad Al-Husein katika kitabu Al-Maswabiyhu kutoka kwa Ka’abul-Akhbaar amesema: “AlMahdi atamnyenyekea Mwenyezi Mungu kama vile unyenyekevu wa tai kwa mabawa yake.” Maelezo: Ni utulivu wa moyo na utulivu wa ndani, na utulivu wa dhahiri ambao unahusu viungo, na Imam Mahdi ana moyo uliojaa utulivu na viungo vyenye kufunikwa na unyenyekevu na utulivu, hivyo yeye ni mnyenyekevu kwa Mwenyezi Mungu kama ambavyo inajulikana, na hayo yote ni kufuatana na imani kubwa ….. ikhilasi ya jumla katika kila dogo na kubwa.

ANA FADHILA TATU Uqudu Durar: Kwa sanad yake kutoka kwa Twausi amesema: “Alama ya Mahdi ni kwamba atakuwa mkali kwa watumishi, mkarimu wa mali na mwenye huruma kwa maskini.” Maelezo: Moyo unajaa huruma kwa wanaostahiki kuhurumiwa nao ni maskini na mkono utakuwa na ukarimu wakutoa mali kwa imani na yakini kwa amri ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, na mkali kwa watumishi, nao ni watumishi wa Imam ili mmoja wao asitumie cheo chake kwa kudhulmu au kuiba au kumuabisha yeyote kwa ubaya. Hakika yeye ni mwenye fadhila tatu.

ATAWATAJIRISHA MAFAKIRI Uqudu Durar: Kutoka kwa Nuaiym bin Hamad katika kitabu cha Al-Fitan, kutoka kwa Abu Rumiyah amesema: “Al-Mahdi atawaonjesha maskini siagi.” Maelezo: Miito yote katika ulimwengu wa kimaada kuhusu usawa inakusudia kuwafanya matajiri kuwa fukara na kupora utajiri kutoka kwao 74


Al-Mahdi Katika Sunna kwa jina la mafakiri, bila ya kumfilisi tajiri, hivyo Imam atafanya usawa kwa kutajirisha. Na watu leo wanafanya usawa baina ya watu kwa kuwafanya wawe fukara, tazama tofauti baina ya mfumo wa mwanadamu na mfumo wa mbinguni.

KULA SHAYIRI NA KUPIGANA JIHADI Uqudu Durar: Kwa sanadi yake kutoka kwa Husein bin Ali (a.s) kwamba amesema: “Atakapotokea Mahdi hakutakuwa baina yake na waarabu na makuraishi isipokuwa upanga, hivyo hawataki Mahdi adhihiri haraka, vazi lake halitakuwa isipokuwa ni gum) la kivita tu, hatokula isipokuwa shayiri, na wala hakutakuwa na kitu kingine isipokuwa ni mauti chini ya kivuli cha upanga tu.” Maelezo: “Ila upanga” kwa sababu sehemu katika Waarabu watamkataa na watampinga, kwa kiburi na ujeuri watampiga vita, hivyo atawauwa na (a.s), ni kama babu zake watoharifu, anakula mkate wa shayiri na wala hajali kufa hali upanga wake unapigana katika njia ya Mwenyezi Mungu, hiyo ni kwa kutekeleza Qur’ani kama inavyotakikana, na kuilinda Qur’ani kwa upanga.

WAYAHUDI WATASILIMU Uqudu Durar: Kwa sanadi yake kutoka kwa Suleiman bin Isa amesema: “Ilinifikia kuwa katika mkono wa Mahdi itadhihiri Tabutis-Sakinah (sanduku) katika Ziwa la Tibriyah litabebwa na kuwekwa mbele yake katika Baitul– Maqdis, Wayahudi watakapoliona watasilimu.” Uqudu Durar: Amesema: “Na katika baadhi ya riwaya hakika ameitwa AlMahdi kwa sababu yeye ataongoza kwenda ilipo Torati hivyo ataitoa katika milima ya Shaam na kwayo atawalingania Wayahudi, kwa ajili hiyo litasilimu kundi kubwa. Amesema: Al-Madainiy ametaja katika Sunan yake: ‘Hakika ameitwa Al-Mahdi kwa sababu yeye ataongoza kwenda 75


Al-Mahdi Katika Sunna katika milima ya Sham ili atoe humo vitabu vya Torati kwayo atawajadili Wayahudi, na hivyo litasilimu kwake kundi la Wayahudi.”’ Is’aafur–Raghibiyna cha As-Swaban Al-Hanafiy amesema: “Hakika AlMahdi atatoa tabutis-sakiynah katika Pango la Antwakiyah na vitabu vya Torati kutoka katika Mlima Shaam kwayo atawajadili Wayahudi, hivyo wengi kati yao watasilimu.”

MANASARA WATASILIMU Yananbiul–Mawadah cha Al-Qanduziy Al-Hanafiy kutoka kwa Abu Huraira amesema: “Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w): ‘Wallahi itateremka kwa Mariyam hukumu ya uadilifu hivyo watavunja msalaba, watauwa nguruwe, wataondoa kodi, watamwacha mpiga gitaa, hivyo hawatamwendea na itaondoka chuki, husuda na uadui.” Maelezo: Huenda ilivyo Sahih ni kuteremka kwa Ibnu Maryam, yaani Isa (a.s), kwa sababu Hadith tukufu inaelezea kuondoka sheria inayodaiwa kuwa inatoka kwa Isa bin Maryam (a.s), ndio maana amesema: Hukumu ya uadilifu. Kwa sababu uadilifu unapasa kunasibishwa kwa Isa na katika mila ya Isa, na maadamu Isa bin Maryam atamfuata Imam Al-Mahdi na atajisalimisha pamoja naye kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, hivyo ni lazima na wao wawe hivyo pia. “Watavunja msalaba” kwa sababu utabainika kwa Manaswara uwongo wa msalaba na kwamba Isa hakuwa amesulubiwa. “Na watauwa nguruwe” kwa sababu ni haramu katika Uislamu na Manaswara wakati huo watasilimu, hivyo nguruwe hatoliwa baada ya siku hiyo.

76


Al-Mahdi Katika Sunna “Na itaondolewa kodi” kwa sababu hatobaki Myahudi wala Mnaswara katika dini yao bali watasilimu, na atakayepinga naye anajua haki atauliwa. “Na wataacha gita” yaani wapiga gitaa na waimbaji wataacha kuimba nyimbo katika makanisa, na wala hatoenda yeyote kwa mpiga gitaa. “Husuda, chuki na uadui utaondoka” kwa sababu ardhi yote wakati huo itakuwa ni kitu kimoja, ndugu wenye kupenda sana kama ilivyosema Qur’ani Tukufu: “Ili ishinde dini zote” (Surat Tauba: 33).

KUHUISHA SUNNA NA KUONDOA BIDAA Uqudu Durar cha As-salimy Ash-Shaafiy: Kwa sanadi yake kutoka kwa Ali bin Abi Talib (a.s) katika Hadith amemtaja humo Al-Mahdi na atakayoyafanya hadi aliposema: “Hakutokuwa na bidaa isipokuwa ataiondoa na wala hakutokuwa na Sunna isipokuwa ataihuisha.” Uqudu Durar: Kutoka kwa Abdillah bin Atwa’a amesema: “Nilimsikia Abu Ja’far Muhammad bin Ali Al-Baaqir (a.s) kutoka kwake, nilimwambia atakapotoka Al-Mahdi sera gani atafuata? Akasema: ‘Atavunja yaliokuwepo kabla yake kama alivyofanya Mtume (s.a.w.w) na Uislamu utaanza upya.”’ Maelezo: Yaani atavunja ambayo yameingizwa katika Uislamu miongoni mwa uchafu, uzushi, batili, kuhalalisha haramu na kuharamisha halali, kati ya ambayo madhehebu mbalimbali na matamanio yameyaingiza na wala sio kwamba atavunja yote yaliyokuwepo kabla yake, kwani Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w) vilevile hakuvunja yote yaliyokuwepo kabla yake bali alivunja, upotovu na batili. Mtume ni muasisi wa Uislamu na Imam Al-Mahdi ni mujadid (mwenye kurejesha upya) Uislamu.

77


Al-Mahdi Katika Sunna

UELEWANO WA JUMLA Uqudur Durar cha As-Salimiy Ash-Shaafiy: Kwa sanadi yake kutoka kwa Ali bin Abi Talib (a.s) katika Hadith amesema: “Mahdi atatuma kwa magavana wake katika miji yote kufanya uadilifu baina ya watu, kondoo watachunga pamoja na mbwa mwitu katika sehemu moja, watoto watacheza pamoja na nyoka na nge na wala hawatawadhuru kwa chochote, shari itaondoka na kubakia kheri, mtu atapanda kibaba na atavuna vibaba mia saba kama alivyosema Mwenyezi Mungu Mtukufu, zinaa, kunywa pombe na riba vyote vitaondoka, watu wataelekea kwenye ibada, sheria, dini, twawafu, kuswali jamaa na umri utakuwa mrefu, miti itazaa na baraka zitaongezeka, waovu watahiliki na watabaki wema na wala hatobaki mwenye kuwachukia Ahlul-Bait.” Maelezo: Hakuna ubaya kusimama na kutaamali kwa haraka katika sentensi hizi ili tuseme baadhi ya maneno na kufafanua kidogo.

URAFIKI WA WANYAMA “Kondoo atachunga pamoja na mbwa mwitu.” Kondoo kwa tabia yake anaogopa mbwa mwitu, hivyo hachungi pamoja naye bali anakimbia kutoka alipo, na mbwa mwitu kwa desturi yake ni mshambuliaji anashambulia kondoo na kumuuwa, hivyo huyu hachungi pamoja na yule wala yule hachungi pamoja huyu, sasa itakuwaje katika zama za Al-Imam Al-Mahdi (a.s) hawa watachunga pamoja? Jawabu: Kuna mawili: Ama ushambuliaji wa mbwa mwitu sio utashi wa asili bali ni utashi wa muda tu, kutokana na njaa au njaa huwa inamchukua kwa muda mrefu hadi inakuwa ni pupa na kugeuka kuwa utashi, na kwa mkabala wa woga wa kondoo kwa mbwa mwitu nao sio utashi wa asili bali ni kwa kujua kwake awali ushambuliaji wa mbwa mwitu kwake au kujua kwake hali ya mkabala ambayo ni hali ya ushambuliaji wa mbwa mwitu 78


Al-Mahdi Katika Sunna kwa kutazama kwake n.k. Na katika zama ya Imam Al-Mahdi (a.s) mbingu na ardhi zitafungua baraka zake, hivyo mbwa mwitu hatokuwa na njaa wala hali ya kutaka kushambulia, na kwa upande mwingine hakutakuwa na woga kwa kondoo. Na ima huo utakuwa ni muujiza kutoka kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu kama vile miujiza ya Mitume na mawalii. Na huenda ni kwa ukarimu wa Imam na ukarimu wa watu katika utawala wake na wakati wake, kwa sababu hiyo utaathiri kwa miale yenye kupenya hadi kwa wanyama wapole na wanyama wakali, kama ambavyo imegundua hayo elimu ya kisasa katika uvumbuzi wa kielimu wa karibuni. Na kwa hiyo tunaweza kufungua fumbo la kielimu kwa sentensi ifuatayo: “Na watoto watacheza na nyoka na nge.”

MIMEA KUZAA KWA WINGI “Atapanda kibaba na atavuna vibaba mia saba kama alivyosema Mwenyezi Mungu” hii ni kuashiria kauli yake (s.w.t.): “Kama mfano wa punje moja inatoa mashuke saba na katika kila shuke kuna punje mia saba.” (Surat Al-Baqarah: 261). Na sababu katika hilo iko wazi, mvua ikinyesha kwa wingi na ardhi ikatoa baraka zake mapato ya kilo moja yatakuwa ni sawa na kilo mia saba. Namna gani? Jawabu: Hadi sasa haijawahi kutokea popote, wala katika wakati wowote kwamba kila punje inatoa punje mia saba na wala punje mia hazijawahi kutokea katika shuke moja. Itatokea lini na Qur’ani Tukufu imeshatoa habari hiyo? Je, Qur’ani inasema kitu ambacho hakiwi? Je, Qur’ani inazungumzia kitu ambacho hakina ukweli?

79


Al-Mahdi Katika Sunna Hapana……. kisha hapana. Hivyo itakuwa lini? Hakika ni katika utawala wa Imam Al- Mahdi na wala si vinginevyo.

NA UMRI UTAKUWA MREFU “Na umri utakuwa mrefu” kwa nini? Kwa sababu umri mfupi unatokea aghalabu kwa sababu ya kupetuka katika manhaji Sahihi, uchovu, mbinyo wa kinafsi n.k. Na tiba ya kisasa inakiri kwamba viungo vya mwili wa mwanadamu vinaweza kufanya kazi zake bila ya kupumzika kwa maelfu ya miaka kama hakutakuwa na pingamizi inayosababisha kusimama. Na katika zama ya Imam Al-Mahdi (a.s) kheri zitaenea, imani itatapakaa, watu wataneemeka kwa utulivu na kwa manhaji Sahihi zilizosalimika… Hivyo kwa nini umri uwe mfupi?

AMANA ZITATEKELEZWA Mazingira ya kiimani yatawafanya watu wawe na imani, na imepokewa katika Hadith tukufu: “Watu wanafuata dini ya wafalme wao.” Kiongozi kwa mfano ni Imam Al-Mahdi (a.s) ambaye ndiye chemchem ya imani na chimbuko la uchamungu, msingi wa wema na kheri, ni rahisi kuwafanya watu kuwa wema kwa wepesi. Hivyo hakutakuwa na hiyana katika amana, watu watapata amana na vilevile watazifikisha.

WAOVU HAWATAKUWEPO “Na waovu watahiliki.” Waovu wako aina mbili: Kuna ambao nasaha haiwafai, mazingira ya kheri wala wahyi hauwezi kuwarekebisha. Aina hii Al-Imam atawauwa kwani ni viini vya uonevu, uovu na uharibifu.

80


Al-Mahdi Katika Sunna Na kuna aina ambayo mazingira mazuri na hali ya imani inairekebisha, hivyo itabadilika katika zama za Imam Al-Mahdi na kuwa nzuri. Hivyo kwa kuwepo haya na yale hakutabaki shari wala waovu.

CHINI YA BENDERA YA AHLUL-BAIT (A.S) “Wala hatobaki anayewachukia Ahlul-Baiti” Maadui wa Ahlul-bait wako aina mbili:Kwanza: Asiyejua haki yao na fadhila zao, na hawa katika zama za Imam watakuwa wameshawajua, hivyo watawaamini, watawaenzi na kuwapenda na kuwafuata. Pili: Mkaidi ambaye amesema juu yake Al-Imam Amirul-Mu’minina (a.s) katika maneno yake: “Na hakika sisi tuna maadui hata kama tungewaonjesha asali iliyo safi basi wasingezidisha kwetu isipokuwa chuki.” Na aina hii ataipiga vita Imam Al-Mahdi na kuiuwa, ili atoharishe ardhi kutokana na uovu wao na audui wao. Hivyo hatabaki mwenye kuwachukia Ahlulbait. Na utafiti wa maudhui haya ni mrefu, kuna dalili na mifano mingi isipokuwa sisi tunafupisha kwa muhtasari kwa yale ambayo yanafaa muhtasari huu.

MWISHO Hadith hizi tukufu kuhusu Imam Al-Mahdi (a.s) anayesubiriwa sio kingine isipokuwa ni mifano tu ya rundo kubwa kati ya Hadith zilizopokelewa na kauli zilizopokewa kutoka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w) na kutoka kwa Ahlul-bait (a.s) ambao Mtume (s.a.w.w) ametuamuru kuchukua kutoka kwao na kuwafuata na kutoka kwa sahaba wake ambao wamepokea na wamenukuu maneno yake na wakayasimulia kwa waliokuja baada yao miongoni mwa tabiina, na wao kwa waliowafuata... rundo hili ambalo linafikia bila ya kutia chumvi, maelfu ya Hadith na wala sio mamia tu. 81


Al-Mahdi Katika Sunna Tumechagua Hadith hizi katika hazina kubwa na uchaguzi wetu ulihusu yaliyopokewa katika vitabu sita vilivyo Sahih (Al-Bukhari, Muslim, Tirimidhiy Ahmad, An-Nasaiy na Abu Daudi) … Kisha wanaofuata kati ya Maimam wa Hadith na mahafidhi miongoni mwa wafuasi wa madhehebu manne (Hanafi, Malik, Shafi na Hanbali). Sikupokea katika kitabu hiki Hadith hata moja kutoka katika vitabu vya Shia, na hiyo ili iwe na nguvu katika hoja na dalili. Aidha nimefupisha kwa muhtasari huu ili kila mtu aweze kunufaika kwayo katika kila sehemu, nyumbani, shuleni na ofisini, njiani, ndani ya treni, gari na ndege, katika bustani, baharini na katika matembezi. Na katika kila sehemu ….. atatoa kitabu hiki mfukoni mwake na atakisoma, au atasoma baadhi yake kisha atakiweka ili akirejee mara nyingine katika sehemu nyingine na kukamilisha sehemu iliyobakia au atakirudia kukisoma. Yote hayo ni ili watu wachukue kwa Imam wao Al-Mahdi fikra inayowafungulia njia ya kumwamini na kuwa na mapenzi na mawadda naye na kuomba taufiki kwa Mwenyezi Mungu ili amnusuru na kumtumikia. Anayetaka kujua zaidi basi arejee rejea kubwa ambazo tumetaja baadhi ya majina yake ambapo mimi nimenukuu, mfano: Vitabu sita vilivyo Sahih, na Yanabi’ul-Mawaddah, Al-Bayan Fiy Alaamati Mahdi Fiy AkhrizZamani, Al-Anqariyul-Hasan Fiy Ahawali Swahib Zaman, Al-Mahdi, Muntakhabul-Athar Fiy Al-Imamith-Thaniy Ashara, Kanzul–Umaal, Nurul-Abswar, Shawahidut-Tanziyl n.k. “Ee Mwenyezi Mungu hakika sisi tunataka kutoka kwako dola tukufu, kwayo uupe nguvu Uislam na watu wake, na udhalilishe kwayo unafiki na watu wake, na utujaalie humo miongoni mwa walinganiaji kwenye utii wako, na waongozaji katika njia yako, na uturuzuku kwayo Utukufu wa dunia na Akhera.”

82


Al-Mahdi Katika Sunna BIBLIOGRAFIA MUHIMU ZA KITABU:Qur’ani Tukufu Sahih Bukhari – Muhammad bin Ismail Sahih Tirimidhiy – Muhammad bin Isa. Sahih Muslim – Muslim bin Hajaj Al-Qaathary Sunanul-Mustafaa – Abu Daudi As-Sajastaniy Sunanu–Ibnu Majah Al-Qaithiri Sunanu An-Nasaiy Musnad Ahmad bin Hanbal Tarikh Dimshiq – Ibnu Asakir Kanzul-Umaal – Al-Mutaqiy Al-Hindiy Tadhikratul–Khawaas – Sibtwi Ibnu Jauziy Al-Hanafiy. Maswabiyhu Sunah – Al-Baghawiy Aqrabul-Mawarid – As-Shartuniy. Al-Qamusil-Muhtwi – Al-Fairus Abadiy. Al-Istia’b – Ibnu Abdi Barr Siyratul-Halabiyah – Ali bin Ibrahim Uqudu Durar – Jamalu Diyn as-Salimiy Al-Mustadraku as-Sahihain – Al-Hakim An-Nisaburiy Taisyrul–Waswili Ilaa Jaami’il-Usuuli – Al-Jazariy As-Shafiy Yanabi’ul-Mawaddah – Hafidh Al-Qanduziy. Al-Fusulul-Muhimah – Ibnu As–Swibagh (Al-Malik). Al-Jamius-Swaghir – As-Suyutwiy. Nurul-Abswar – As-Shabalnjiy Sharhu Nahjul-Balaghah – Ibnu Abil Hadid Is’a fur-Raghibiyna - Muhammad As-Swaban (Al-Hanafi). Al-Mun’jid – Ma’alufu Al-Yasu’iy. Majmaul-Baharain - Sheikh Twariyh. Mukhtari Swihaah - Al-Fuyumiy. Lisanul-Arab - Ibnu Mandhur. Al-Bayan - Al-Kanjiy As-Shafi Maqaatilut-Twalibiyiyna - Abu Faraj Al-Isfahani. 83


Al-Mahdi Katika Sunna Al-Burhan Fiy Alaamat Mahdi Akhri Zaman – Al-Mutaqiy Al-Hindiy – Ash-Shaafiy. Kunuzul–Haqaiq - Allamaah Al-Munawiy. Na vinginevyo ambavyo vimetajwa katika mahala pake.

84


Al-Mahdi Katika Sunna

ORODHA YA VITABU VILIVYO CHAPISHWA NA AL - ITRAH FOUNDATION: 1. 2. 3. 4. 5. 6. 7. 8. 9. 10. 11. 12. 13. 14. 15. 16. 17. 18. 19. 20. 21. 22. 23.

Qur'an Al-Kariim - Tafsir Al-Kashif Juzuu ya kwanza mpaka Ishirini na mbili Uharamisho wa Riba Uharamisho wa uwongo - Juzuu ya kwanza Uharamisho wa uwongo - Juzuu ya pili Hekaya za Bahlul Muhanga wa Imamu Husein (A.S.) Mikingamo iliyomzunguka Imamu Ali (A.S.) Hijab vazi Bora Ukweli wa Shia Ithnaashari Madhambi Makuu Mbingu imenikirimu Abdallah Ibn Saba Khadijatul Kubra Utumwa Umakini katika Swala Misingi ya Maarifa Kanuni za Ndoa na maadili ya Familia Bilal wa Afrika Abudharr Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu Salman Farsi Ammar Yasir Qur'an na Hadithi 85


Al-Mahdi Katika Sunna 24. 25. 26. 27. 28. 29. 30. 31. 32. 33. 34. 35. 36. 37. 38. 39 40. 41. 42. 43. 44. 45. 46. 47. 48. 49. 50. 51. 52. 53. 54.

Elimu ya Nafsi Yajue Madhehebu ya Shia Ukusanyaji na Uhifadhi wa Qur'an Tukufu Al-Wahda Ponyo kutoka katika Qur'an. Uislamu mfumo kamili wa maisha ya kijamii Mashukio ya Akhera Al Amali Dua Indal Ahlul Bayt Udhuu kwa mujibu wa Kitabu na Sunna. Haki za wanawake katika Uislamu Mwenyezi Mungu na sifa zake Amateka Na Aba'Khalifa - Kinyarwanda Nafasi za Ahlul Bayt (a.s) Adhana. Upendo katika Ukristo na Uislamu Nyuma yaho naje kuyoboka - Kinyarwanda Amavu n’amavuko by’ubushiya - Kinyarwanda Kupaka juu ya khofu Kukusanya swala mbili Bismillah ni sehemu ya Qur’ani na husomwa kwa Jahara Kuwaongoza vijana wa kizazi kipya Kusujudu juu ya udongo Kusheherekea Maulidi Ya Mtume (s) Tarawehe Malumbano baina ya Sunni na Shia Kupunguza Swala Safarini Kufungua safarini Umaasumu wa Manabii Qur’ani inatoa changamoto as-Salaatu Khayrun Mina'n-Nawm 86


Al-Mahdi Katika Sunna 55. 56. 57. 58. 59. 60. 61. 62. 63. 64. 65. 66. 67. 68. 69. 70. 71. 72. 73. 74. 75. 76. 77. 78. 79.

Uadilifu wa Masahaba Dua e Kumayl Sauti Ya Uadilifu wa Binadamu Umaasumu wa Mitume - Faida Zake Na Lengo Lake Umaasumu wa Mitume - Majibu Ya Aya Zenye Utata Umaasumu wa Mitume - Umaasumu wa Mitume Muhammad (s) Nahju’l-Balaghah - Juzuu ya Kwanza Nahju’l-Balaghah - Juzuu ya Pili Kuzuru Makaburi Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Kwanza Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Pili Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Tatu Tujifunze Misingi Ya Dini Sala ni Nguzo ya Dini Mikesha Ya Peshawar Malezi Ya Mtoto Katika Uislamu Ubora wa Imam 'Ali Juu ya Maswahaba Na Ushia ndio njia iliy onyooka Shia asema haya, Sunni asema haya, Wewe wasemaje? Liqaa-u-llaah Muhammad (s) Mtume wa Allah Amani na Jihadi Katika Uislamu Uislamu Ulienea Vipi? Uadilifu, Amani na Mtume Muhammad (s) Mitala na Ndoa za Mtume Muhammad (s) Amali za Ramadhani

82.

Ujumbe Sehemu ya Kwanza

83.

Ujumbe sehemu ya Tatu

84.

Swala ya Maiti na Kumlilia Maiti 87


Al-Mahdi Katika Sunna 85.

Amali za Ramadhani

86.

Ujumbe sehemu ya Pili

87.

Ujumbe sehemu ya nne

88.

Ujumbe sehemu ya Tatu

89.

Al-Mahdi katika Sunna

90.

Tabarruku

91.

Ukweli wa Shia

92.

Mariam, Yesu na Ukristo kwa Mtazamo wa Kiislamu

93.

Amali za Ramadhani

94. 95.

Hadithi Thaqalain Sunna Za Nabii Muhammad (s)

88


Al-Mahdi Katika Sunna

BACK COVER Kwa Waislamu, imani ya kuja kwa Mahdi (Muhudi) karibu ya mwisho wa dunia ni imani ambayo ina asili katika dini.Waislamu wote bila kujali tofauti za madhehebu zao, wanakubaliana juu ya imani hii kwamba Mtukufu Mtume (saw) alisema kwamba: Hata iwe imebakia siku moja tu kwa dunia hii kufikia mwisho wake Allah Mwenye uwezo atairefusha siku hiyo ili kumwezesha Imam huyo kutawala na kuujaza ulimwengu huu uadilifu, amani na utulivu wakati ambapo ulikuwa umejaa ufisadi na dhuluma. Kitu cha kuvutia ni kwamba imani hii haiko kwa Waislamu tu bali hata katika dini nyingine wana imani kama hii kwamba atatokea mtu wakati wa mwisho ambaye ataondoa dhuluma na ufisadi na kuujaza ulimwengu huu uadilifu, amani na utulivu. “Hakika ulimwengu unalingojea suluhisho litakaloukusanya chini ya bendera moja na tamko moja.” (Bertrand Russell) “Hakika haiko mbali siku ambayo ulimwengu wote utatawaliwa na amani na usafi na watu kuwa katika hali ya kupendana na undugu.” (Albert Einstein) Kimetolewa na kuchapishwa na: Al-Itrah Foundation P.O. Box 19701, Dar es Salaam, Tanzania Simu: +255 22 2110640 Fax: +255 22 2127555 Email: info@alitrah.org 89


Turn static files into dynamic content formats.

Create a flipbook
Issuu converts static files into: digital portfolios, online yearbooks, online catalogs, digital photo albums and more. Sign up and create your flipbook.