IDDI AL-GHADIYR D.Kanju final.qxd
7/1/2011
4:31 PM
Page A
IDIL GHADIRI (‘Iydi ‘l-Ghadiyr)
Kimeandikwa na: Muhammad Ibrahim al-Muwahhid al-Qazwini
Kimetarjumiwa na: Abdul Karim Juma Nkusui
IDDI AL-GHADIYR D.Kanju final.qxd
7/1/2011
4:31 PM
Page B
ŠHaki ya kunakili imehifadhiwa na: AL-ITRAH FOUNDATION ISBN: 978 - 9987 - 512 - 34 - 8
Kimeandikwa na: Muhammad Ibrahim al-Muwahid al-Qazuwiniy Kimetarjumiwa na: Abdul Karim Juma Nkusui Kimepangwa katika Kompyuta na: Hajat Pili Rajab
Toleo la kwanza: Februari, 2011 Nakala: 1000 Kimetolewa na kuchapishwa na: Alitrah Foundation S.L.P. 19701 Dar es Salaam, Tanzania Simu: +255 22 2110640 Simu/Nukushi: +255 22 2127555 Barua Pepe: alitrah@raha.com Tovuti: www.alitrah.org Katika mtandao: www.alitrah.info
IDDI AL-GHADIYR D.Kanju final.qxd
7/1/2011
4:31 PM
Page C
YALIYOMO Aya ya Tabligh...................................................................................2 Kiapo cha utii cha chukuliwa kwa ajili ya Imam...........................10 Masheikh wawili watoa kiapo cha utii.............................................11 Wanawake watoa kiapo cha utii.......................................................13 Mshairi wa kwanza kati ya washairi wa Ghadir...............................13 Umuhimu wa tukio la Ghadir...........................................................14 Ushahidi wa hadith ya Ghadir.........................................................17 Rejea za tukio la Ghadir...................................................................20 Kukamilika kwa dini...................................................................... 29 Taji la Ukhalifa............................................................................... 31 Shahada ya tatu katika adhana.........................................................33 Mwenyezi Mungu na shahada ya tatu.............................................35 Mtume wa Mwenyezi Mungu na shahada ya tatu...........................36 Ahlul Bait na shahada ya tatu..........................................................38 Fatwa za Maulamaa.........................................................................40 Kisimamo pamoja na Sheikh As-Suduuq........................................42 Swali na Jawabu............................................................................. 45 Nembo ya Shia.................................................................................46 Kombora la Mbinguni.................................................................... 46 Iddi ya Al-Ghadir.............................................................................49 Imam Ali na Iddi ya Ghadir..............................................................51 Maimam wa Ahlul-Bait na Iddi ya Ghadir.......................................53 Shia na Iddi ya Ghadir......................................................................55 Iddi al-Ghadir huko mbinguni.........................................................58 Masjid al-Ghadir............................................................................ 60 Maelezo kuhusu ardhi ya Ghadir.....................................................62 Nafasi ya washairi katika Iddi ya Al-Ghadir....................................63
IDDI AL-GHADIYR D.Kanju final.qxd
7/1/2011
4:31 PM
Page D
NENO LA MCHAPISHAJI Kitabu kilichoko mikononi mwako ni tarjumi ya kitabu cha Kiarabu kiitwacho, ‘Iyd al-Ghadiyr kilichoandikwa na Muhammad Ibrahim al-Muwahhid al-Qazwini. Sisi tumekiita, Idil Ghadiri – Idi ya Ghadiri. Idi ya Ghadiri (Sikukuu ya Ghadir) imetokana na tukio kubwa la kihistoria. Tukio hili lilitokea katika jangwa la Ghadir Khumm katika njia ya msafara baina ya Makka na Madina wakati Mtukufu Mtume alipokuwa akirudi kutoka Makka ambako alikwenda kutekeleza ibada ya Hija. Hija hii ni maarufu sana na hujulikana kama Hijjatu ’l-Widaa’ (Hija ya Mwago). Ghadir ni tukio maarufu sana katika ulimwengu wa Kiislamu. Hakuna madhehebu ya Kiislamu hata moja ambayo haikutaja tukio hili, ingawa kuna tofauti kidogo ya mapokezi kati ya wasimulizi wake. Pamoja na hayo, ukweli unabakia palepale kwamba haitakamilika historia ya Uislamu bila ya kulitaja tukio hili. Qur’ani inatuthibitishia kwamba Uislamu ulikamilika baada ya tukio hili la Ghadir: “...Leo nimekukamilishieni dini yenu, na kuwatimizieni neema Yangu, na nimewapendeleeni Uislamu uwe dini yenu...” (5:3) Aya hii iliteremshwa kwa Mtume Muhammad (saw) pale Ghadir Khumm baada ya kumtangaza Imam Ali (as) kama Khalifa wake, kiongozi wa waumini wote na mrithi wake. Baada ya hapo Waislamu waliifanya siku hii kuwa Idi (Sikukuu) kama utakavyoona maelezo yake katika kitabu hiki.
IDDI AL-GHADIYR D.Kanju final.qxd
7/1/2011
4:31 PM
Page E
Tumekiona kitabu hiki ni chenye manufaa sana, hususan wakati huu wa maendeleo makubwa ya elimu katika nyanja zote, ambapo uwongo, ngano za kale na upotoshaji wa historia ni mambo ambayo hayana nafasi tena katika akili za watu. Kutokana na ukweli huu, Taasisi yetu ya Al-Itrah Foundation imeamua kukichapisha kitabu hiki kwa lugha ya Kiswahili, kwa madhumuni yake yaleyale ya kuwahudumia Waislamu, hususan wazungumzaji wa Kiswahili, ili kuongeza ujuzi wao katika masuala ya dini na ya kijamii. Tunamshukuru ndugu yetu, Ustadh Abdul Karim Juma Nkusui kwa kukubali jukumu hili la kukitarjumi kitabu hiki. Vilevile tunawashukuru wale wote walioshiriki kwa njia moja au nyingine hadi kufanikisha kuchapishwa kwake. Mchapishaji: Al-Itrah Foundation S. L. P. 19701 Dar-es-Salaam, Tanzania.
IDDI AL-GHADIYR D.Kanju final.qxd
7/1/2011
4:31 PM
Page F
DIBAJI Kwa jina la Mwenyezi Mungu Mwingi wa rehema Mwenye kurehemu. Shukurani zote ni za Mwenyezi Mungu, sala na salamu zimshukie bwana wetu na Nabii wetu Muhammad Mtume wa Mwenyezi Mungu, na ndugu yake, msaidizi wake, wasii wake, khalifa wake na kiongozi baada yake anayependeza mno kwake, Imam Amirul- Mu’minina Ali bin Abu Talib, na sala na salamu ziwashukie Ahlul-bait wa Mtume wa Mwenyezi Mungu wateule na viongozi wema waongofu, amana ya Mwenyezi Mungu na vipenzi vyake, na makhalifa wa Mtume Wake na mabwana wa mawalii wake, na hasa mwisho wa mawalii Imam wa kumi na mbili, Al-Mahdi anayesubiriwa kudhihiri, na laana ya Mwenyezi Mungu iwashukie maadui zao wote kuanzia sasa hadi siku ya Kiyama. Mtume wa Mwenyezi Mungu amesema: “Siku ya Ghadir Khum ni Iddi bora katika Iddi za umma wangu, nayo ni ambayo ameniamrisha Mwenyezi Mungu Mtukufu kumtawaza ndugu yangu Ali bin Abu Talib kuwa ni bendera ya umma wangu, wataongoka kwayo baada yangu, nayo ni siku ambayo Mwenyezi Mungu alikamilisha humo dini na kutimiza humo neema na kuwaridhia Uislaam kuwa ndio dini yao.”
IDDI AL-GHADIYR D.Kanju final.qxd
7/1/2011
4:31 PM
Page i
UTANGULIZI. IDDI AL-GHADIR NI NINI? Hili ni swali ambalo linakaririwa sana katika vinywa vya vijana ambao wana tatizo la upungufu wa itikadi, na wanakutana na mifumo batili na vikundi vilivyopotea ambavyo vinajaribu kupotosha na kutia shaka kwa kutoa tuhuma baina ya watu. Wanaulizana: Iddi Al–Ghadir ni nini? Imekuja kutoka wapi? Lini na vipi? Tulikuwa tumeeleza maudhui haya kwa ufafanuzi na uwazi zaidi katika kitabu chetu Al-Imam Aliyu Khalifatur-Rasuulillaahi, na kwa ajili ya kuwarahisishia ndugu zetu vijana, basi tumeyachapisha peke yake katika kitabu hiki pamoja na baadhi ya masahihisho na nyongeza kwa kutoa mchango wetu katika kueneza itikadi ya kiislamu na kuondoa shutuma zenye kupotosha‌.. Tunamuomba Mwenyezi Mungu atupe taufiki katika kuitumikia haki na watu wake, hakika yeye ni Mwenye kusikia dua na Mwenye kutoa msaada. Muhammad Ibrahim Al-Muwahid AL-Qazuwiniy 14/ 1/ 1401 A.H.
i
IDDI AL-GHADIYR D.Kanju final.qxd
7/1/2011
4:31 PM
ii
Page ii
IDDI AL-GHADIYR D.Kanju final.qxd
7/1/2011
4:31 PM
Page 1
IDDI AL-GHADIYR D.Kanju final.qxd
7/1/2011
4:31 PM
Page 2
Iddi al-Ghadiyr
AYA YA TABLIGHI Nayo ni kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu:
“Ewe Mtume fikisha yaliyoteremshwa kwako kutoka kwa Mola wako na kama hutofanya hivyo utakuwa hujafikisha ujumbe wake na Mwenyezi Mungu atakulinda kutokana na watu, hakika Mwenyezi Mungu hawaongozi watu makafiri.” (Surat al-Maidah: 67.) Watu wa historia na watu wa hadithi wanafasiri Aya hii kwamba: Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) alipanga kwenda Hijja mwaka wa mwisho katika uhai wake na ambayo baadae ilijulikana kama Hijjatul-Wida’a, habari ya safari yake ikaenea na watu wakaelekea Madina na wakajiunga na msafara wa Mtume hadi idadi ya waliotoka pamoja nae ikafikia laki moja na ishirini elfu.1 Mtume (s.a.w.w.) alipomaliza ibada ya Hijja aliondoka kurejea Madina. Alipowasili katika bonde la Juhfah katika ardhi ya Ghadir Khum, nayo ni sehemu ambayo kuna njiapanda za kwenda Madina, Iraki, Misri na Yemeni, na kuwasili kwake ilikuwa ni siku ya Alhamisi mwezi 18 Dhulhaji wakati wa dhuha. 1 Riwaya zimetofautiana katika idadi ya waliokuwa wameandamana na Nabii (s.a.w.w.) isipokuwa idadi hii ndio ambayo wameitaja baadhi ya wanahistoria kama vile Ibnu Sa’ad katika Tabaqaat Juz. 3 uk. 355. Na inasemekana walikuwa 124,000, na inasemekana ilikuwa ni pungufu ya hiyo, na inasemekana ilikuwa ni zaidi ya hiyo. 2
IDDI AL-GHADIYR D.Kanju final.qxd
7/1/2011
4:31 PM
Page 3
Iddi al-Ghadiyr Wakati msafara mkubwa unaendelea na safari yake, aliteremka Malaika Jibril kutoka kwa Mwenyezi Mungu kuja kwa Mtume (s.a.w.w.) akiwa na Aya Tukufu: “Ewe Mtume fikisha yaliyoteremshwa kwako kutoka kwa Mola wako na kama hutafanya hivyo basi utakuwa hujafikisha ujumbe wake na Mwenyezi Mungu atakulinda kutokana na watu, hakika Mwenyezi Mungu hawaongozi watu makafiri.� Na akamfikishia kwamba Mwenyezi Mungu anamwamuru amtawaze Ali ibn Abu Talib kuwa Imam kwa watu na Khalifa wake na wasii wake baada yake, na awafikishie yaliyoteremshwa humo kwake miongoni mwa uongozi na wajibu wa kila mtu kumtii. Nabii (s.a.w.w.) akasimama na akaamuru ambao bado wako nyuma wasubiriwe wafike kwake na waliotangulia warejee kwake, waislamu wote wakakusanyika kwake na wakati wa Swala ya Adhuhuri ukaingia, Mtume akasalisha watu. Hali ya hewa ilikuwa ni ya joto kali sana, hadi mtu kati yao alikuwa anaweka baadhi ya nguo zake juu ya kichwa chake na baadhi yake chini ya miguu yake kutokana na ukali wa joto, Mtume alitengenezewa kivuli kutokana na miti ya Samuraat na yakawekwa matandiko ya ngamia baadhi juu ya mengine hadi yakawa kama mimbari. Mtume (s.a.w.w.) akasimama juu ili kundi la watu wamuone na akapaza sauti yake na akawahutubia hotuba kali na ndefu, alianza kwa kumhimdi Mwenyezi Mungu na kumsifu na akatilia mkazo mazungumzo yake na maneno yake juu ya shakhisiya ya khalifa wake Imam Ali (a.s.) fadhila zake, sifa zake, msimamo wake na nafasi yake kubwa mbele ya Mwenyezi Mungu na Mtume Wake, na akawaamuru waislamu wamtii na kuwatii watu wa nyumba yake watukufu, na akahimiza kuwa wao ndio hoja za Mwenyezi Mungu na mawalii wake walio karibu, waaminifu wake katika dini yake na sheria yake, na kwamba kuwatii wao ni kumtii Mwenyezi Mungu na Mtume Wake, na kwamba wafuasi wake wataingia peponi na wapinzani wake wataingia motoni na mengine mengi yasiyokuwa hayo.
3
IDDI AL-GHADIYR D.Kanju final.qxd
7/1/2011
4:31 PM
Page 4
Iddi al-Ghadiyr Na kati ya aliyoyasema ilikuwa ni: “Enyi watu…. hakika mimi nahofia kuwa nitaitwa na nitaitika (wito), mimi ni mwenye kuulizwa na nyinyi ni wenye kuulizwa.2 Je, mtasemaje?” Sauti zikasikika huku na huko na wakasema: “Tunashuhudia kwamba wewe umeshafikisha, umetoa nasaha na umepigana jihadi, Mwenyezi Mungu akulipe kheri.” Akasema (s.a.w.w.): “Je, simnashuhudia kwamba hakuna Mungu isipokuwa Mwenyezi Mungu na kwamba Muhammad ni mja Wake na Mtume Wake, na kwamba pepo Yake ni ya kweli na moto Wake ni wa kweli, na kwamba mauti ni ya kweli na kwamba Kiyama kitakuja na wala hakuna shaka kwamba Mwenyezi Mungu atafufua walio makaburini.?” Wakasema: “Ndio, tunashuhudia hayo.” Akasema: “Ee Mwenyezi Mungu shuhudia.” Kisha akanadi: “Enyi watu: Hamsikii?” Wakasema: “Tunasikia, tunasikia.” Akasema (s.a.w.w.): “Hakika mimi nitawatangulia katika birika, na nyinyi mtanikuta kwenye birika, na kwamba upana wake ni kama upana uliopo baina ya Sana’a na Busra3 humo kuna vikombe vya fedha kama vile idadi ya nyota, basi tazameni namna gani mtanifuata katika vizito viwili.” Akanadi mwenye kunadi: “Ni nini vizito viwili ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu?” Akasema (s.a.w.w.): “Kizito kikubwa ni Kitabu cha Mwenyezi Mungu ncha yake moja iko kwa Mwenyezi Mungu, na ncha nyingine iko 2 Amesema Sayyid Sharafud-Dini katika sherehe ya kitabu chake cha AlMurajaat: Huenda kauli yake (s.a.w.w.): “Na nyinyi ni wenye kuulizwa” ni ishara ya aliyoyatoa Dailamiy na Ibnu Hajar katika Sawaiqu kwamba, Nabii katika tafsiri ya kauli ya Mwenyezi Mungu “Wasimamishe hakika wao ni nwenye kuulizwa,” yaani juu ya uongozi wa Ali. Na amesema Imam Al-Wahidiy: “Hakika wao ni mwenye kuulizwa juu ya uongozi wa Ali na Ahlul-baiti wake.” 3 Sanaa iko Yemen na Busra iko Syria. 4
IDDI AL-GHADIYR D.Kanju final.qxd
7/1/2011
4:31 PM
Page 5
Iddi al-Ghadiyr kwenye mikono yenu basi shikamaneni nacho na wala hamtapotea. Na kizito kingine ni kidogo, kizazi changu Ahlul-bait wangu, na kwamba Mwenyezi Mungu Mjuzi amenipa habari kwamba havitatengana hadi vitanifikia kwenye birika, na nimemuomba Mola Wangu hilo, basi msivitangulie mtaangamia na wala msivipuuze mtahiliki.” Na akasema (s.a.w.w.): “Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa rehema Mwenye kurehemu: Ewe Mtume fikisha yaliyoteremshwa kwako kutoka kwa Mola Wako na kama hutofikisha basi utakuwa hujafikisha ujumbe wake na Mwenyezi Mungu atakulinda kutokana na watu. Enyi watu! Sikuzembea katika kufikisha aliyoyateremsha kwangu na mimi ni mwenye kuwabainishia sababu ya kuteremka Aya hii. Hakika Jibril ameteremka kwangu mara tatu ameniamuru juu ya amani ya Mola Wangu nisimame mahala hapa na nimfahamishe kila mtu kwamba Ali ibn Abu Talib ni ndugu yangu wasii wangu, khalifa wangu na ni Imam baada yangu, na ambaye cheo chake kwangu ni kama vile cheo cha Harun kwa Musa isipokuwa hakuna Mtume baada yangu. Naye ni kiongozi wenu baada ya Mwenyezi Mungu Mtukufu na Mtume Wake, na Mwenyezi Mungu ameshateremsha juu ya hilo Aya katika kitabu chake: “Hapana si jingine Kiongozi wenu ni Mwenyezi Mungu na Mtume Wake na wale ambao wameamini ambao wanasimamisha Swala na wanatoa sadaka hali ya kuwa wamerukuu.” Na Ali amesimamisha Swala na ametoa sadaka hali ya kuwa amerukuu, anamtaka Mwenyezi Mungu katika kila hali…..”4 Kisha Mtume (s.a.w.w.) akashika mkono wa Imam Ali (a.s.) akaunyanyua hadi weupe wa kwapa zao ukaonekana, na akamfahamisha kwa watu wote. Akasema: “Enyi watu! Ni nani mwenye haki zaidi kwa waumini kuliko nafsi zao?” Wakasema: “Ni Mwenyezi Mungu na Mtume Wake.” Akanadi (s.a.w.w.): “Hakika Mwenyezi Mungu ni kiongozi wangu na, mimi ni 4 Biharul-An’war Juz 37 uk. 206.
5
IDDI AL-GHADIYR D.Kanju final.qxd
7/1/2011
4:31 PM
Page 6
Iddi al-Ghadiyr kiongozi wa waumini, na mimi ni mbora zaidi kwao kuliko nafsi zao, ambaye mimi ni kiongozi wake basi Ali ni Kiongozi wake.” Na alikariri mara tatu kisha akamuuomba Mwenyezi Mungu kwa kusema: “Ee Mwenyezi Mungu mpende atakayemtawalisha, na mfanye adui atakayemfanyia uadui, mpende atakayempenda, mchukie atakayemchukia, mnusuru atakayemnusuru, mdhalilishe atakayemdhalilisha, na izungushe haki pamoja naye popote atakapozunguka. Ee! kila aliyeko hapa amfikishie (habari hizi) asiyekuwepo. “Enyi watu! Hakika Mwenyezi Mungu amewawekea kiongozi na Imam, ni wajibu kutiiwa na Muhajirina, Answari na watakaowafuata wao kwa wema, kwa wajao na waliopo waajemi na waarabu, huru na mtumwa, mdogo na mkubwa, mweupe na mweusi na kwa kila anayemwamini Mwenyezi Mungu. Hukumu yake ni yenye kupita, kauli yake ni yenye kujuzu, amri yake ni yenye kutekelezwa. Amelaaniwa atakayemkhalifu na amehurumiwa atakayemfuata. Atakayemwamini, kumsikiliza na kumtii basi Mwenyezi Mungu ameshamsamehe. “Enyi watu! Hakika hiki ni kisimamo cha mwisho nasimama mahali hapa, sikilizeni na mtii na mfuate amri ya Mola Wenu kwani Mwenyezi Mungu ni kiongozi wenu na ni Mola Wenu, kisha baada yake ni Mtume wenu Muhammad kiongozi wenu ambaye amesimama anawahutubia, kisha baada yangu Ali ni kiongozi wenu na Imam wenu kwa amri ya Mwenyezi Mungu Mola Wenu, kisha uImam utakuwa katika kizazi changu, katika kizazi chake hadi siku mtakayokutana na Mwenyezi Mungu Mtukufu na Mtume Wake. Hakuna halali isipokuwa aliyoihalalisha Mwenyezi Mungu, wala hakuna haramu isipokuwa aliyoiharamisha Mwenyezi Mungu. Mwenyezi Mungu alinifahamisha halali na haramu na mimi nimemweleza (Ali) aliyonifundisha Mola Wangu kutoka katika Kitabu chake, halali yake na haramu yake.
6
IDDI AL-GHADIYR D.Kanju final.qxd
7/1/2011
4:31 PM
Page 7
Iddi al-Ghadiyr “Enyi watu! Hakuna elimu isipokuwa Mwenyezi Mungu amenifundisha na kila elimu nimemfundisha Imam wa wachamungu na hakuna elimu isipokuwa nimemfundisha Ali naye ni Imam. Enyi watu! Msipotee wala msikimbie kutoka kwake wala msije mkatoka katika uongozi wake, yeye ndiye anayeongoza kwenye haki na anafanya kwa haki na kuiondoa batili na kuikataza, na wala haogopi kwa ajili ya Mwenyezi Mungu lawama ya mwenye kulaumu. Kisha yeye ndio wa kwanza kumwamini Mwenyezi Mungu na Mtume Wake na ambaye aliitoa muhanga nafsi yake kwa ajili ya Mtume, ambaye alikuwa pamoja na Mtume na wala hakuna yeyote anayemwabudu Mwenyezi Mungu pamoja na Mtume Wake katika wanaume isipokuwa yeye. “Enyi watu! Mheshimuni huyu, kwani Mwenyezi Mungu ameshamtukuza na mkubalini kwani Mwenyezi Mungu ameshamchagua. Enyi watu! Hakika yeye ni Imam kutoka kwa Mwenyezi Mungu na wala Mwenyezi Mungu hatokubali toba ya aliyepinga uongozi wake na wala hatomsamehe. Enyi watu! Mheshimuni Ali kwani yeye ni mbora wa watu baada yangu katika wanaume na wanawake maadamu riziki inateremka na maadamu kuna viumbe. Amelaaniwa amelaaniwa, amekasirikiwa amekasirikiwa atakayepinga kauli yangu hii na wala asiikubali. Kauli yangu ni kutoka kwa Jibril kutoka kwa Mwenyezi Mungu, basi naitazame nafsi kitu gani inakitanguliza kwa ajili ya kesho, na muogopeni Mwenyezi Mungu msije mkakhalifu basi mkateleza baada ya kuthibiti, hakika Mwenyezi Mungu ni mjuzi wa mnayoyafanya. “Enyi watu! Itafakarini Qur’ani na fahamuni Aya zake, angalieni Aya zilizo wazi kati yake na wala msifuate zenye utata (mutashabihaati), Wallahi hatowabainishia makemeo yake wala hatafafanua kwenu tafsiri yake isipokuwa ambaye mimi nimeshika mkono wake na nimempandisha kwangu na nimeunyanyua mkono wake.
7
IDDI AL-GHADIYR D.Kanju final.qxd
7/1/2011
4:31 PM
Page 8
Iddi al-Ghadiyr “Enyi watu! Huyu ni Ali ndugu yangu, wasii wangu mtambuzi wa elimu yangu, khalifa wangu katika umma wangu na katika tafsiri ya Kitabu cha Mwenyezi Mungu, mwenye kulingania Kwake mwenye kufanya kwa yanayomridhisha, mwenye kukataza maasi Yake, khalifa wa Mtume Wake na Amirul-Mu’minin na Imam mwenye kuongoza, mwenye kuwapiga vita wenye kutengua ahadi, waasi na wenye kuritadi katika amri ya Mwenyezi Mungu. “Enyi watu! Hakika Mwenyezi Mungu Mtukufu amekamilisha dini yenu kwa Uimam wake basi ambaye hatakuwa chini ya uongozi wake na uongozi wa atakayeshika nafasi yake katika kizazi chake hadi Siku ya Kiyama na akawa kampinga Mwenyezi Mungu Mtukufu basi hao amali zao zimebatilika na watakaa motoni milele, hawatapunguziwa adhabu na wala hawatahurumiwa. “Enyi watu! Huyu ni Ali aliyeninusuru zaidi kati yenu, mwenye haki zaidi kwangu kati yenu, aliye karibu yangu zaidi kati yenu, mtukufu wenu zaidi kwangu. Mimi na Mwenyezi Mungu tumemridhia na haikushuka Aya juu ya ridhaa ila kwake, na hakuwasemesha Mwenyezi Mungu wale walioamini isipokuwa ameanzia kwake, na haikushuka Aya ya kusifu katika Qur’ani isipokuwa kwake, wala Mwenyezi Mungu hakushuhudia pepo katika “Je, haikupita kwa mwanadamu dahari….” isipokuwa kwake, na wala haikuteremshwa kwa asiyekuwa yeye na wala hakumsifu kwayo asiyekuwa yeye. “Enyi watu! Yeye ni mwenye kunusuru dini, na mpiganaji wa Mtume wa Mwenyezi Mungu naye ni mchamungu, msafi, muongozaji mwenye kuongoka. Nabii wenu ni mbora wa Manabii na wasii wenu ni mbora wa mawasii, na watoto wake ni mawasii bora. Enyi watu! Kizazi cha kila Nabii kinatokana na mgongo wake na kizazi changu kinatoka katika mgongo wa Ali. Enyi watu! Hakika Ibilisi amemtoa Adam peponi kwa husuda, hivyo msimfuate amali zenu zisije zikabatilika na visigino vyenu vikateleza. Ee! Hakika hamchukii Ali isipoikuwa muovu na wala hampen8
IDDI AL-GHADIYR D.Kanju final.qxd
7/1/2011
4:31 PM
Page 9
Iddi al-Ghadiyr di Ali isipokuwa mchamungu na wala hamwamini isipokuwa Muumini mwenye ikhilasi. “Enyi watu! Mwaminini Mwenyezi Mungu, Mtume Wake na nuru iliyoteremshwa pamoja naye. Nuru itokayo kwa Mwenyezi Mungu iko kwangu kisha kwa Ali kisha katika kizazi chake hadi kwa Al-Qaimu Al-Mahdi. “Enyi watu! Baada yangu kutakuwa na maimam watakaolingania kwenye moto na siku ya Kiyama hawataokolewa. Hakika Mwenyezi Mungu na mimi tuko mbali nao, wao na wanaowanusuru na wafuasi wao watakuwa katika tabaka la chini la moto, na wataufanya uongozi kuwa ni ufalme wa kunyang’anyana. “Enyi watu! Nimewabainishieni na nimewafahamisheni na huyu Ali atawafahamisheni baada yangu. Ee! Hakika mimi - baada ya kumalizika hotuba yangu – nawataka mnipe mkono wa kiapo cha utii katika kumtii Ali na kumkubali kisha mtampa mkono wa kiapo cha utii baada yangu. “Enyi watu! Mimi nimempa utii Mwenyezi Mungu na Ali amenipa utii mimi, na mimi namchukulia utii kwenu kutokana na niaba ya Mwenyezi Mungu Mtukufu na atakayetengua utii hakika anatengua kwa ajili ya nafsi yake. “Enyi watu! Hakika fadhila za Ali ibn Abu Talib ziko kwa Mwenyezi Mungu na amekwisha ziteremsha katika Qur’ani na ni nyingi sana siwezi kuzitaja katika hotuba moja, basi atakayekuelezeni na kukufahamisheni mwaminini. Enyi watu! Atakayemtii Mwenyezi Mungu, Mtume, Ali na Maimam ambao nimewataja basi atakuwa amefaulu kufaulu kukubwa. Enyi watu! Wanaofanya haraka katika kumpa kiapo cha utii na kumfuata na kumsalimia kwa uongozi wa waumini, hao ndio wenye kufaulu katika pepo yenye neema.”
9
IDDI AL-GHADIYR D.Kanju final.qxd
7/1/2011
4:31 PM
Page 10
Iddi al-Ghadiyr Hotuba ya Nabii ikamalizika kwa kumteua Imam Ali ibn Abu Talib kuwa Amirul-Mu’minin kwa waumini na Khalifa wa Mtume wa Mola wa walimwengu.5
KIAPO CHA UTII CHACHUKULIWA KWA AJILI YA IMAM Kisha Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) akateremka na akawaamuru waislamu wote wampe kiapo cha utii Imam Ali ibn Abu Talib (a.s.) na wamsalimie kwa kumpongeza kwa kuwa kwake kiongozi wa waumini.6 Mtume (s.a.w.w.) akakaa katika hema lake maalumu na akamuamuru khalifa wake akae katika hema lingine kwa ajili ya kuwapokea wanaompongeza. Watu wakamiminika kwanza kwa Mtume (s.a.w.w.) kwa kumpongeza kwa Iddi hii tukufu na ukumbusho mtukufu nao wakawa wanasema: “Ndio tumesikia na tumetii amri ya Mwenyezi Mungu na Mtume Wake…...tumemwamini kwa nyoyo zetu.” Kisha wakaenda katika hema la Imam Ali Amirul-Mu’minin kumpa kiapo cha utii na kumpa 5 Biharul-An’war Juz. 37 uk. 204. Katika hotuba tumenukuu nukta za muhimu tu, na Tabarasiy ameipokea katika kitabu cha Ihtijaji, na Allamah Al-Majlisiy katika Biharul–An’war Juz. 37 uk. 204. Na katika Maulamaa wa Kisunni na masheikhe wao ameipokea: Al-Hafidh Ibnu Uqudah katika kitabu maalumu kama alivyoitaja mwanahistoria mashuhuri Ibnu Jarir alichokiita Kitabul-Wilaayat Fi Turiq Hadithi-Ghadir, na imechapishwa hotuba hii tukufu peke yake vilevile. 6 Imepokewa kwa Zayd bin Arqam kwamba Nabii (s.a.w.w.) alisema katika mwisho wa hotuba yake tukufu: “Enyi watu! Semeni tumekupa ahadi kutoka katika nafsi zetu na kiapo na kukupa mkono, tunakipeleka kwa watoto wetu na ahali zetu, na familia zetu na hatutaki katika hilo badili na wewe ni shahidi juu yetu, na inatosha kuwa Mwenyezi Mungu ni shahidi Ali kuwa ni Amirul-Mu’minina. Semeni tuliyowaambia na msalimieni.”
10
IDDI AL-GHADIYR D.Kanju final.qxd
7/1/2011
4:31 PM
Page 11
Iddi al-Ghadiyr mkono huku wakisema: “Amani iwe juu yako ewe Amirul-Mu’minin.”7 Nabii (s.a.w.w.) hakuondoka katika ardhi ya Ghadir isipokuwa baada ya waislamu wote kumpa kiapo cha utii Ali (a.s.). Zayd bin Arqam amesema: “Kiapo cha utii kiliendelea kwa muda wa siku tatu.”8 Ndio kiapo cha utii kiliendelea kwa muda wa siku tatu kwa sababu ya watu na idadi kubwa, haiwezekani kumpa kiapo cha utii kwa muda wa saa moja au siku moja.
MASHEIKH WAWILI WATOA KIAPO CHA UTII Aliondoka Abu Bakr na Umar kwenda kwa Mtume (s.a.w.w.) na wakamwambia: “Jambo hili ni kutoka kwako au ni kutoka kwa Mwenyezi Mungu?” Akasema Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.): “Je, jambo hili litakuwa limetoka kwa asiyekuwa Mwenyezi Mungu? Ndio ni jambo kutoka kwa Mwenyezi Mungu na Mtume Wake.” Wakasimama wakaenda kwa Ali (a.s.) na wakampa kiapo cha utii cha Uimam na ukhalifa, Umar akasema na huku anatoa mkono wa kiapo cha utii kwa Ali: “Hongera hongera kwako ewe mtoto wa Abu Talib.” Na katika habari nyingine: “Pongezi kwako, umekuwa ni kiongozi wangu na kiongozi wa kila muumini mwanaume na muumini mwanamke.”9 7 Kwa maelezo ya ziada rejea kitabu cha Al-Ghadir Juz. 1 uk. 270. 8 Al-Ghadir Juz. 1 uk. 270. 9 Kundi kubwa la maulamaa wa Kisunni na maimam wao wametaja tukio la masheikh wawili (Abubakr na Umar) kumpongeza Imam Ali kuwa ni AmirulMu’minin, kati ya hao ni: Ahmad bin Hambal katika Musnad, Juz. 4 uk. 241, Ibnu Jarir Tabari katika Tafsiir yake Juz. 3 uk. 428, Kaadhi Abubakr Al-Baqalaniy katika kitabu At-Tamhiydu Fi Usuulud-Diyn uk. 171, Haafidh Bin Swabagh Al–Malikiy katika Al-Fusulul-Muhimmah Juz. 2 uk. 169, Fakhrur-Raziy katika Tafsir yake Juz. 3 uk. 636 na Sheikh Al-Amin katika Al-Ghadir Juz. 1 uk. 270, humo ametaja masdari sitini za Hadithi ya kumpongeza. 11
IDDI AL-GHADIYR D.Kanju final.qxd
7/1/2011
4:31 PM
Page 12
Iddi al-Ghadiyr Mshangao mkubwa mno ni vipi Abu Bakr na Umar waliuliza swali hili kwa Nabii (s.a.w.w.)? Watu wote walitoa kiapo cha utii bila ya kuuliza swali na bila ya mushekili wowote, lakini vipi Masheikh wawili peke yao waliuliza swali hili? Je hapa ni mahala pa kuuliza swali hili? Je, hawakusikia kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu “Hatamki kwa matamanio isipokuwa ni wahyi unaofunuliwa.” (Suratun-Najm: 4). Je, haikuwafikia kauli ya Mwenyezi Mungu: “Alichokuleteeni Mtume kichukueni.” (Surat Hashir: 7). Je, hawakusoma kauli yake (s.w.t.): “Enyi mlioamini muitikieni Mwenyezi Mungu na Mtume Wake.” (Surat Anfaal: 24). Na jua fika kuwa Aya hizi zilikuwa zimeshateremka kabla ya tukio tukufu la Ghadir. Imam As-Sadiq (a.s.) amesema: “Mtume (s.a.w.w.) alipomaliza hotuba hii ya Al-Ghadir – ghafla alionekana kwa watu mtu mmoja mzuri mwenye kunukia vizuri akasema: “Wallahi sikumuona Muhammad kama alivyo hivi leo katu. Ni mkazo ulioje katika kusisitiza juu ya mtoto wa ami yake na anafunga kwake ahadi ambayo hataitengua isipokuwa aliyemkufuru Mwenyezi Mungu Mtukufu na Mtume Wake Mtukufu. Maangamio mabaya ni kwa atakayetengua ahadi yake.” Umar akageuka aliposikia maneno yake na akastaajabishwa na mandhari yake kisha akageuka kwa Nabii (s.a.w.w.) akasema: “Je hukusikia aliyoyasema huyu mtu? Amesema kadha wa kadha.” Mtume wa Mwenyezi Mungu akasema: “Ewe Umar unajua ni nani yule?” Akasema: “Hapana.” Nabii (s.a.w.w.) akasema: “Huyu ni Jibril, ole wako usije ukatengua hakika ukitengua basi Mwenyezi Mungu, Mtume Wake, malaika na waumini watakuwa mbali na wewe.”10
10 Biharul– An’war Juz. 37 uk. 219. Na Ihtijaji ya Tabarasiy. 12
IDDI AL-GHADIYR D.Kanju final.qxd
7/1/2011
4:31 PM
Page 13
Iddi al-Ghadiyr
WANAWAKE WATOA KIAPO CHA UTII Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) alikuwa anatilia mkazo katika kuimarisha misingi ya ukhalifa na kuthibitisha misingi ya Uimam kwa ukamilifu zaidi. Kwa ajili hiyo hakutosheka kwa kiapo cha wanaume tu, bali aliwaamuru wanawake na miongoni mwao ni wake zake kutoa kiapo cha utii kwa Imam Ali (a.s.), lakini kiapo cha utii cha wanawake kilikuwaje kwa Amirul-Mu’minin (a.s.)? Je, ni kwa kupeana mkono? Hali kupeana mkono mwanamke ajinabi na mwanamume ajinabi ni haramu, hivyo ilikuwaje? Jibu: Hakika Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) alichagua njia ya ishara kwa ajili ya wanawake kutoa kiapo cha utii, aliamuru kuletwe chombo chenye maji na akamwamuru Ali (a.s.) aingize mkono wake upande mmoja wa chombo na wanawake waje waingize mikono yao katika upande mwingine wa chombo na wamsalimie kwa kumpongeza kwa kuwa kwake Amirul-Mu’minin. Kwa njia hii nzuri na safi kilitimia kiapo cha utii kwa Amirul-Mu’minin kutoka kwa wanawake.
MSHAIRI WA KWANZA KATI YA WASHAIRI WA GHADIR Kisha akasimama Hassan bin Thabit mshairi wa Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) na akasema: “Niruhusu ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu nisome beti kuhusu Ali uzisikie.” Mtume (s.a.w.w.) akamwambia soma kwa baraka za Mwenyezi Mungu. Hassani akaanza kusoma: “Anawaita siku ya Ghadir-Khum Nabii wao, na alishamjia Jibrilu kwa amri ya Mola Wao, kwamba wewe ni ma’sum hivyo usiwe mwoga, wafikishie aliyoteremsha Mwenyezi Mungu Mola Wao kwako, na wala usiwao13
IDDI AL-GHADIYR D.Kanju final.qxd
7/1/2011
4:31 PM
Page 14
Iddi al-Ghadiyr gope maadui. Akasimama kwao hali mkono wake umenyanyua mkono wa Ali, hali anatangaza kwa sauti ya juu, akasema: ‘Ni nani kiongozi wenu na walii wenu?’ Wakasema na wala hawakudhihirisha kutokujua: ‘Mola wako ni walii wetu na wewe ni walii wetu, wala hutaona katu siku moja tunaasi.’ Akasema: ‘Simama ewe Ali kwani mimi nimekuridhia baada yangu uwe ni Imam mwenye kuongoza. Ambaye nilikuwa kiongozi wake basi huyu ni kiongozi wake, basi kuweni wenye kumnusuru na kumfuata kikweli kweli.’ Hapo aliomba: ‘Ewe Mwenyezi Mungu mpende atakayemtawalisha na mchukie atakayemfanyia Ali uadui, Ewe Mola mnusuru atakayemnusuru Imam wa uongofu kama vile mbalamwezi inavyoondosha giza.”’ Nabii akafurahishwa na beti hizi za kuonyesha mapenzi na utiifu, akadhihirisha tabasamu tukufu na akamshukuru Hasan kwa mashairi yake kwa kusema: “Hutaacha kuwa ni mwenye kuungwa mkono na Malaika maadamu utaendelea kutunusuru kwa ulimi wako.”11
UMUHIMU WA TUKIO LA GHADIR Msomaji mtukufu, tukio hili la kudumu lililo maarufu kwa jina la Tukio la Ghadir, ni miongoni mwa matukio maarufu ya kihistoria, na ni kati ya matukio makubwa katika maisha ya Nabii (s.a.w.w.) na wamelishuhudia sahaba laki na kumi elfu, ambao wao wenyewe walihudhuria, kati yao ni: Abu Bakr bin Abi Quhaafah. Umar bin Al-Khattab. Uthman bin Afaan. Abdur-Rahman bin Auf. Saad bin Abi Waqaas. Abu Huraira. 11 Al-Ghadir Juz. 1 uk. 34. Tadhkiratul-Khawas cha Sibtu Ibnu Jauzi uk. 20, As-Suyutwiy katika Risalatul-Izdihaar. Na Al-Kunjiy katika Kifaayatu-Twalib uk. 17. 14
IDDI AL-GHADIYR D.Kanju final.qxd
7/1/2011
4:31 PM
Page 15
Iddi al-Ghadiyr Abu Qudaamah Answaariy. Hudhaifah bin Al-Yaman. Abu Said Al-Khudriy. Zubair bin Al-Awaam. Twalha bin Ubaidullah. Abbas bin Abdul-Muttalib. Usamah bin Zaid. Ubayya bin Kaab. Al-Baraa bin Aazib. Anas bin Malik. Jabir bin Samrah. Hubah bin Jarir Al-Araniy. Hasan bin Thabit. Abu Ayubu Al-Answariy. Khalid bin Walid. Khuzaimah bin Thabit. Zayd bin Thabit. Sa’ad bin Ubaadah. Sahal bin Saad bin Sa’adiy. Qaisi bin Saad bin Ubaidillah. Al-Miqdad bin Amru Al-Kindiy. Abdillah bin Umar. Salman Al-Farsiy. Abu Dhar Al-Ghafaariy. Ammar bin Yaasir. Maimam wawili Hasan na Husein, mabwana wa vijana wa watu wa peponi na wengineo.12 Ama wanawake ambao walishuhudia na kuhudhuria tukio hilo ni wengi pia, mashuhuri kati yao ni: Fatmah Zahraa, binti wa Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.). 12 Rejea Al-Ghadir Juz. 1 uk. 41 utakuta majina kwa kirefu. 15
IDDI AL-GHADIYR D.Kanju final.qxd
7/1/2011
4:31 PM
Page 16
Iddi al-Ghadiyr Ummu Salamah, mke wa Mtume. Fatmah binti Hamza bin Abdul–Muttalib. Ummu Haaniy binti Abbas bin Abu Talib. Asmau binti Umais. Aisha binti Abu Bakr na wengineo katika wanawake. Na hukuti mwandishi au mtunzi ameandika au anaandika kuhusu maisha ya Nabii au maisha ya Imam Ali isipokuwa anataja kisa hiki kwa kifupi au kwa kirefu, ila kama mwandishi au mtunzi ni mwenye kuchukia haki au ni adui wa kizazi cha Muhammad au ni mamluki wa baadhi ya masultani waovu au mwenye kukanusha fadhila za Ahlul-bait (a.s.) au mfano wa hayo, hivyo basi hujifanya kasahau au kaghafilika kutaja tukio hili lenye kudumu. Ama tukio lenyewe hakuna nafasi ya kulikataa na kutilia shaka usahihi wake na kujadili sanadi yake, kwa sababu maulamaa wakubwa, mahafidh, muhadithina na wanahistoria wa zamani, wote wamethibitisha usahihi wake na ukweli wake na wamelitegemea hadi leo hii. Hakika tukio la Ghadir sio tukio lenye kupita na jepesi hadi liweze kusahaulika bali ni lazima litatajwa katika nyanja mbalimbali za kielimu, kama vile lugha, historia, tafsiri, hadithi, fasihi n.k. Mtu wa lugha kama ni mwadilifu lazima aashirie kwalo anapozungumzia maana ya neno: Ghadiyru Khum. Mwanahistoria naye kama ni mwadilifu vilevile lazima ataje tukio la Ghadir angalau kwa muhtasari katika historia ya Uislamu kwa kuwa ni tukio la kiislamu, na katika historia ya Nabii wa Uislamu (s.a.w.w.) kwa kuwa lilitokea katika Hijja yake ya mwisho (Hijatul-Widaa) na kabla ya kufariki kwa Nabii kwa siku sabini, na katika historia ya Imam Ali Amirul-Mu’minin (a.s.) kwa kuwa linahusiana naye na ndiye mhusika mkuu. Na mfasiri kama yuko huru kutokana na ushabiki (ta’asubu) lazima atataja tukio la Ghadir angalau kwa muhtasari wakati wa kufasiri Aya zili16
IDDI AL-GHADIYR D.Kanju final.qxd
7/1/2011
4:31 PM
Page 17
Iddi al-Ghadiyr zoshuka huko mfano Aya ya Tablighi, Aya ya Kukamilisha dini, Aya ya Kuteremka adhabu, na nyinginezo katika Aya nyingi zinazofungamana na ukhalifa wa Imam Ali Amirul–Mu’minina (a.s.) na Uimam wake kama vile Aya ya Kuonya. Na mwanahadithi lazima alitaje katika sehemu ya kutaja hadithi tukufu za Nabii kama vile kauli yake (s.a.w.w.) kwa Ali: “Wewe kwangu ni kama alivyokuwa Haruna kwa Musa isipokuwa hakuna Nabii baada yangu.” Na kauli yake (s.a.w.w.) akiashiria kwa Ali (a.s.): “Huyu ni ndugu yangu, wasii wangu, khalifa wangu na mrithi wangu baada yangu, msikilizeni na mtiini.” Na kauli yake (s.a.w.w.): “Ambaye mimi ni kiongozi wake basi Ali ni kiongozi wake.” Na nyinginezo katika mamia ya hadithi sahihi zilizopokewa kutoka kwa Nabii (s.a.w.w.) juu ya ukhalifa wa Imam Ali, vivyo hivyo katika nyanja zinginezo.
USHAHIDI WA HADITHI YA GHADIR Ewe msomaji mtukufu! Hakika ushahidi wa hadithi ya Ghadir juu ya ukhalifa wa Imam Ali Amirul-Mu’minin (a.s.) na Uimam wake baada ya Mtume wa Mwenyezi Mungu moja kwa moja unategemea mambo mawili:Sanad Hoja Ama Sanad ya hadithi tumekwishaiashiria na kwamba iko katika daraja la juu kabisa la usahihi na nguvu, ni hadithi mutawatir, wameipokea sahaba wakubwa na watukufu wao kama tulivyotangulia kutaja. Amesema Al-Haafidh Ibnu Hajjar Al-Hanafiy katika Swawaiqul-Muhriqah uk. 25: “Hakika hiyo ni hadithi sahihi hakuna shaka humo, na wameshaitoa jamaa kama vile Tirmidhiy, An-Nasaaiy na Ahmad, na njia zake ni nyingi 17
IDDI AL-GHADIYR D.Kanju final.qxd
7/1/2011
4:31 PM
Page 18
Iddi al-Ghadiyr sana, kisha wameipokea sahaba kumi na sita. Na katika riwaya ya Ahmad ni kwamba wameisikia kutoka kwa Nabii (s.a.w.w.) sahaba thelathini na waliitumia kutoa ushahidi kwa Ali pindi alipopokonywa ukhalifa kama ilivyotangulia na itakuja baadae na sanadi zake nyingi ni sahihi na hasana, na wala hatazamwi aliyekosoa usahihi wake, wala aliyejibu kuwa Ali alikuwa Yemen, kwa kuwa imethibiti kurejea kwake toka huko na kuwahi Hijja pamoja na Nabii (s.a.w.w.). Na ama kauli ya baadhi yao kwamba ziada ya “Ewe Allah mpende atakayemtawalisha…….” hadi mwisho ni uzushi, kauli hiyo inapingwa kwani yamepokewa hayo kwa njia nyingi, kati ya hizo Adh-Dhahabiy amesema zilizo nyingi ni sahihi.” Nasema: Insha’allah tutataja maelezo ya baadhi ya maulamaa na hufaadh kuhusu usahihi wa sanad ya hadithi ya Ghadir, wakati wa kutaja uthibitisho na rejea za kihistoria. Ama hoja, pia iko katika daraja la juu kabisa, na hasa baada ya tanbihi ya viambatanisho vya mazingira na nukuu vinavyoizunguka hadithi. Neno Al-Maula alilolitumia katika kauli yake (s.a.w.w.): “Man kuntu maulaahu fa Aliyun maulaahu.” Maana yake ni mwenye haki zaidi na jambo na kulitawalia, kwa ajili hiyo Nabii (s.a.w.w.) alisema kwanza: “Je, mimi si nina haki zaidi kwa waumini kuliko nafsi zao?” Sahaba wake waliposema: “Ndio.” Nabii (s.a.w.w.) akasema: “Ambaye mimi ni kiongozi wake basi Ali ni kiongozi wake.” Maana yake ni kwamba haki ileile niliyonayo kwenu ndio ileile aliyonayo Ali (a.s.) kwenu, na kwa sababu hiyo imekuja kwa Fau atafri’i (tawi) na akasema: “Fa Aliyun maulaahu.” Yaani “Basi Ali ni kiongozi wake.” Hili ni la kwanza. Pili: Hakika kauli yake (s.a.w.w.): “Hakika mimi nakaribia kuitwa na kuitika (anaweza kunijia malaika wa mauti) na mimi ni mwenye kuulizwa na nyinyi pia ni wenye kuulizwa.” Ni dalili ya kuwa yeye amekaribia kufa na kwamba huu ni wakati wa kuusia na kuteua Imam baada yake ili yeye awe ni kigezo kwa waislamu baada yake. 18
IDDI AL-GHADIYR D.Kanju final.qxd
7/1/2011
4:31 PM
Page 19
Iddi al-Ghadiyr Tatu: Aliyoyafanya (s.a.w.w.) siku ya Ghadir Khum baada ya kuteremka Aya ya Tablighi, kwanza kushuka kwake katika ardhi kama hiyo katika jua kali, kuamuru kwake kurejea waliotangulia miongoni mwa waislamu na walio nyuma wawasili, kutoa hotuba kali, kunyanyua kwake mkono wa Ali (a.s.) kisha kuchukua kiapo cha utii kwa ajili yake kwa muda wa siku tatu, na kuteremka Aya ya kukamilika dini…… hayo yote sio kingine bali ni hoja iliyo wazi kwamba Nabii (s.a.w.w.) alikuwa katika kumteua khalifa baada yake. Nne: Hakika kauli ya Umar bin Al-Khattab kwa Imam Ali AmirulMu’minin (a.s.) wakati wa kutoa kiapo cha utii: “Hongera hongera ewe mtoto wa Abu Talib umekuwa kiongozi wangu na kiongozi wa kila muumini mwanaume na mwanamke.” Sio kingine ila ni ushahidi wa kwamba alifahamu ukhalifa wa Imam Ali kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w) na kwa ajili hiyo alikwenda kutoa kiapo cha utii na pongezi. Tano: Hakika kila aliyehudhuria siku ya Ghadir alifahamu kuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) alikusudia katika “Maula” Uimam na Ukhalifa, na kati yao ni Hasan bin Thabiti mshairi wa Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) ambapo aliiweka maana hii katika utungo wa shairi na akataka ruhusa kwa Nabii Mtukufu ili kusoma kaswida yake ambayo umekwishaisoma huko nyuma. Na maana hiihii ya Uimam na Ukhalifa ndio waliifahamu sahaba wengine na taabiina na wakaliweka tukio la Ghadir katika tenzi nzuri za mashairi kwa muda wote wa karne na vizazi.13 Maana hii hii aliifahamu Al-Haarith bin Nuuman Al-Fihriy kama utakavyosoma kisa chake katika sehemu itakayokuja. Ewe msomaji 13 Rejea kitabu cha Al-Ghadir cha Allammah Al-Amin, humo amewataja washairi wa Ghadir kuanzia karne ya kwanza hadi karne ya nne na kuelezea maisha yao na kaswida zao walizozitunga katika mnasaba huu. 19
IDDI AL-GHADIYR D.Kanju final.qxd
7/1/2011
4:31 PM
Page 20
Iddi al-Ghadiyr mtukufu! Huu ni muhtasari wa ushahidi wa hadithi ya Ghadir, na maulamaa wamefafanua hilo katika hadithi ambapo hakuna tena ziada juu yake na kama utataka ufafanuzi zaidi rejea kitabu Al-Muraja’at cha Sayyid Sharafud-Din.
REJEA ZA TUKIO LA GHADIR Ewe msomaji mtukufu! Ili uzidi kuwa na matumaini na yakini basi nakutajia majina ya baadhi ya rejea na vitabu ambavyo vimetaja tukio hili tukufu angalau kwa muhtasari ili uvirejee mwenyewe kama ukitaka ili usome tukio na wala usipatwe na shaka katika usahihi na ukweli wake. Kabla sijataja majina ya rejea lazima nitaje vidokezo: Kwanza: Baadhi ya vitabu na rejea hizi zimechapishwa mara nyingi na kwa ukubwa tofauti ambapo imesababisha ziada ya idadi ya kurasa zake au kupungua kwake kwa sababu ya ukubwa wa kitabu, kwa hiyo mimi nasisitiza juu ya ulazima wa kutafuta maudhui katika hali ya kutopatikana katika ukurasa uliotajwa katika kurasa zilizotangulia au zinazofuatia, na kutofanya haraka katika kutoa hukumu ya kutopatikana na kumtuhumu mtunzi kwa uwongo n.k. Bali kuwa na uhakika na yakini kuwa mimi sitaji ila rejea na vitabu maarufu na vinavyozingatiwa, na sina lengo lingine isipokuwa kubainisha ukweli na uhakika. Pili: Kumepokewa habari kwamba chuo kikuu cha Azhar huko Kairo kwa msaada wa moja kati ya nchi za kiarabu kimeunda kitengo cha siri kwa lengo la kuviangalia upya vitabu na rejea zote zinazotegemewa na Sunni, na kati ya hivyo ni Sahih Bukhari. Lengo la hayo ni kuondoa wanayotaka kuyaondoa na kupotosha ambayo wanataka kuyapotosha katika hadithi zilizopokewa kuhusu fadhila za Ahlul-baiti (a.s.) katika yale ambayo Shia wanaweza kuyatolea ushahidi juu ya ukweli wa madhehebu yao. Kitengo hiki ni cha siri kimefichwa na 20
IDDI AL-GHADIYR D.Kanju final.qxd
7/1/2011
4:31 PM
Page 21
Iddi al-Ghadiyr zimechapishwa baadhi ya rejea chapa mpya na humo baadhi ya hadithi zimeondolewa au zimepotoshwa katika baadhi ya maneno yake muhimu kama vile kupotosha neno “Khalifatiy” lenye maana ya khalifa wangu, na kulifanya “Khaliliy” lenye maana ya rafiki yangu. Nimeshasoma kitabu cha mmoja wa wapotoshaji anamshambulia humo Allammah Mtafiti Sayyid Abdul Husein Sharafud-Din (r.h) na anamtuhumu kwa uongo eti kwa sababu ametaja katika kitabu cha Al-Murajaat hadithi kutoka katika moja ya rejea maarufu, kisha mwandishi akarejea na humo hakukuta hadithi, basi akawa anatoa uongo na uzushi wa chuki dhidi ya Sayyid mtukufu. Jua kwamba kama tukijaalia ukweli wa mwandishi huyo basi sababu inarejea ima kwenye kuchapishwa kitabu hicho mara nyingi kama tulivyoashiria hapo nyuma, au kwa yale yanayofanywa na kitengo hicho miongoni mwa vitendo vya kuchezea hadithi. Nilikutana na maulamaa wawili na kila mmoja alikuwa amehifadhi Sahih Bukhari iliyochapishwa kabla ya miaka 100 huko Misri, akasema hakika katika chapa hii kuna hadithi ambazo hazipo katika chapa mpya. Alaa kulihali hakika kitengo hiki kinaleta hatari kubwa kwa Uislamu na athari zake. Je, haijatosha mustashirikina kuchezea historia yetu ya kiislamu na kupotosha ukweli wake hadi wakaja hawa ambao wanapotosha maneno kutoka katika asili yake na wanafanya hiyana hii kubwa katika athari za asili za kiislamu. Hakika hii inaonyesha ushabiki (ta’asubu) wa upofu walionao maumalaa waovu ambapo wanaona ni bora kupotosha hadithi au kuziondoa badala ya kukubali haki na kuifuata. Kwa ulimwengu wa kiislamu na kwa waislamu wote katika kila sehemu nasema: Hakika kitengo hiki kama kitaendelea na kazi yake ya uovu basi vitabu vyote na rejea za Kisuni zitakosa asili yake ya kihistoria na thamani yake ya kielimu na havitaweza kutegemewa kwa sababu ya kukosekana uaminifu kwavyo, hivyo wahini kuzuia jambo hilo 21
IDDI AL-GHADIYR D.Kanju final.qxd
7/1/2011
4:32 PM
Page 22
Iddi al-Ghadiyr kabla hamjapitwa na wakati. Hakika mimi sishangai chuo kikuu cha Azhar kukanusha habari hii baada ya kufichuka siri hii…. lakini tajirba ni dalili bora na chapa za zamani zimejaa katika maktaba. Msomaji mtukufu! Jua kuwa tuliyoyategemea katika kutaja tukio la Ghadir na mengineyo ni rejea zilizochapishwa zamani yaani kabla ya miaka ishirini na kuendelea. Tatu: Baadhi ya rejea hazijataja tukio la Ghadir kwa ukamilifu bali vimeashiria kwa muhtasari, zimetaja sehemu na kuacha sehemu zingine, kwa ajili hiyo nimejaribu kulisoma tukio hili tukufu kwa kuchukua kutoka katika kitabu hiki au kile. Isipokuwa rejea na athari za kihistoria zimeafikiana juu ya tukio nayo ni kwamba: Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) alisema wakati wa kuondoka kwake katika Hijjatul–Widaa katika ardhi ya Ghadir Khum na akanyanyua mkono wa Ali (a.s.) na akasema: “Ambaye mimi ni kiongozi wake basi Ali ni kiongozi wake, ewe Mwenyezi Mungu mpende atakayetawalisha…” hadi mwisho, kisha akachukua kiapo cha kumtii Imam toka kwa waislamu wote. Haya ndio makusudio na inatosha kuthibitisha ukhalifa wa Imam Ali AmirulMu’minin baada ya Mtume wa Mwenyezi Mungu moja kwa moja. Na yaha hapa ni baadhi ya majina ya vitabu vya rejea: Tafsir Asbabin-Nuzuul cha Waahidiy, anapotafsiri Aya ya Tablighi. Sahih Tirmidhiy Juz. 2 uk. 298, na amesema ni hadithi hasan sahihi. Sunnan Ibin Maajah Juz. 1 uk. 28 na 29. Sunnanul-Baghawiy Juz. 2 uk. 119. Mustadrakus-Sahihain cha Al–Haakim Juz. 3 uk. 109 na 533, ameipokea kwa njia nyingi. Al-Wilaayatu Fiy turqil-Hadithi Al-Ghadir cha mwanahisoria mashuhuri Muhammad bin Jarir At–Tabariy aliyefariki 310 A.H. Na ameipokea humo hadithi ya Al–Ghadir kwa njia zaidi ya 70. Na sababu iliyosababisha Tabariy kutunga kitabu hiki kama alivyotaja AlHamwainiy katika Mu’ujamul-Udabai, Juz.18 uk. 8 katika maelezo ya maisha ya Tabariy ni kwamba: Mmoja wa masheikh wa Baghdad alipinga 22
IDDI AL-GHADIYR D.Kanju final.qxd
7/1/2011
4:32 PM
Page 23
Iddi al-Ghadiyr tukio la Ghadir na akadai kwamaba Imam Ali alikuwa Yemen wakati wa Hijjatul–Wida’a, basi Tabariy aliposikia hilo akatunga kitabu hiki kumjibu na kuzungumzia usahihi wa hadithi zilizopokewa kuhusu Ghadir Khum. Ibnu Kathir katika Al-Bidayatu wan-Nihayah Juz. 5 uk. 208 amesema: “Na jambo hili la Al-Ghadir amelipa kipaumbele Abu Jafar Muhammad bin Jarir Tabariy mwenye Tafsir na Tarikh, basi alikusanya humo mijaladi miwili na akapokea humo njia zake na matamko yake.” Kitabu Man Rawa Hadithul-Ghadiyr Khum cha Abu Bakri Jaabiy aliyefariki 355 A.H. Amepokea humo hadithi ya Ghadir kwa njia 125 na ameitaja As-Sarawiy katika kitabu Al-Manaaqib Juz. 1, uk. 529. Ad-Dirayatu Fiy Hadithil-Wilayah cha Hafidh As-Sajastaniy chenye juzuu 17, humo amekusanya njia za hadithi ya Al-Ghadir kutoka kwa sahaba 120. Uddatul-Baswir Fiy Hajji Yaumul-Ghadir cha Karaajikiy.
Abul-Fuutuh
Al-
10. Al-Wilayatu Fiy Turuq Hadithil-Ghadir cha Haafidh Ibnu Uqudah aliyefariki 333 A.H. Amepokea humo hadithi ya Ghadir kwa njia 105. Amesema Ibnu Hajjar Al-Asqalaany katika Fatuhul-Bariy: “Ama hadithi “Ambaye mimi ni kiongozi wake basi Ali ni kiongozi wake.” Ameipokea Tirmidhiy na Annasaaiy na ina njia nyingi sana na ameshazikusanya Ibnu Uqudah katika kitabu maalumu na nyingi ya sanad zake ni sahihi na hassan.” 11. Tafsiru Fakhri Ar–Raaziy Juz. 3 uk. 636. 12. Tafsiru Ibnu Kathir Juz. 2 uk. 14. 13. Tafsiru Anisaburiy Juz. 6 uk. 194. 14. Tafsiru Durrul-Manthur ya Suyutiy Juz. 2 uk. 259. 15. Tafsiru Shaukaaniy Juz. 2 uk. 57. 16. Tafsiru Al-Manaar Juz. 6 uk. 464. 23
IDDI AL-GHADIYR D.Kanju final.qxd
7/1/2011
4:32 PM
Page 24
Iddi al-Ghadiyr 17. Tafsiru Ruhul-Maariy ya Al-Alusiy Juz. 2 uk. 350 na 249. Na amesema: “Imethibiti kwetu kwamba Mtume (s.a.w.w.) alisema katika haki ya Amirul-Mu’minin: (Mankuntu maulaahu fa Aliyun maulaah). “Ambaye mimi ni kiongozi wake basi Ali ni kiongozi wake.” 18. Tafsiru Tabariy Juz. 3 uk. 428. 19. Tafsiru Qurtubiy katika tafsiri ya Aya ya Tablighi. 20. Tafsiru Abu Said. 21. Tafsiru Siraajil–Muniyr cha Shiriyniy katika tafsiri ya Aya ya Tablighi. 22. Yanabiul-Mawaddah cha Qanduziy Al-Hanafiy uk. 40. 23. Al-Istiabu cha Ibnu Abdul-Barr Juz. 2 uk. 373. 24. Dhakhairul-Uqba cha Muhibu Tabariy Ashaafiy uk. 67. 25. Al-Fusulul-Muhimah cha Ibnu Swabagh Al-Maalikiy uk. 25. 26. Faidhul-Qadir cha Munawiy Ashaafiy uk. 218. 27. Usudul-Ghabah cha Ibnul-Athiir Juz 3 uk. 307 na Juz 5 uk. 205. 28. Al-Manaqib cha Al-Khawarizimiy Al-Hanafiy uk. 130 na 35. 29. Riyadhun-Nadhrah cha Muhibud-Din Tabariy Juz. 2 uk. 169. 30. Kifayatut-Talib uk. 15 cha Al-Haafidh Ashaafiy Al-Kanjiy aliyefariki 658 A.H. Na amesema: “Hii ni hadithi mashuhuri, hasan, wameipokea wakweli, na kuziweka pamoja sanadi hizi baadhi kwa baadhi yake ni hoja katika usahihi wa nukuu.” 31. Tarikhu –Khulafau cha Suyutiy uk. 114. 32. Tarikh Baghdad cha Khatibul–Baghdadiy Juz. 8 uk. 290 na Juz. 7 uk. 377 na Juz. 1 uk. 47. Al-Bidayatu Wan-Nihayah cha Ibnu Kathiir Juz. 5 uk. 208 na Juz. 7 uk. 348. Tarikh Ibnu Assakir. Tarikh Ibnu Khuldun katika utangulizi wa kitabu chake. Hulyatul-Awliyai cha Abu Naiym Juz. 4 uk. 23. Kanzul-Ummaal Juz. 6 uk. 398 na Juz. 2 uk. 154. Tahdhibut-Tahdhib cha Hafidh Ibnu Hajar Al-Asqalaaniy Juz. 7 uk. 337. 24
IDDI AL-GHADIYR D.Kanju final.qxd
7/1/2011
4:32 PM
Page 25
Iddi al-Ghadiyr Al-Iswabah cha Ibnu Hajar Al-Asqalaany Juz. 7, uk. 780 na Juz. 6, uk. 223 na Juz. 2, uk. 408. Musnad Ahmad bin Hanbal Juz. 4, uk. 372 na Juz. 1, uk. 118. Talkhiys cha Dhahabiy Juz. 3, uk. 533 na amasemea ni sahihi. Majmauz-Zawaid cha Haithamiy Juz. 9, uk. 107. Al-Muujamul–Kabiir cha Tabaraniy. Al-Khawas Al-Alawiyah cha Hafidh Anasaiy uk. 21, na 125. As-Swaiwaqul-Muhriqah cha Ibnu Hajar uk. 25 na 75 na amesema kuwa ni hadithi sahihi hakuna shaka humo. Al-Mawahibu Ad-Dhuniyah cha Qastalaaniy Juz. 7, uk. 13 na amesema: “Njia za hadithi hii ni nyingi sana na sanadi nyingi ni sahihi na hasan.” Mizanul–I’itidal Juz. 2, uk. 303. Matalibus–Suul cha Ibnu Talha Ashaafiy uk. 16 amenukuu kutoka kwa Tirmidhiy. Shamsul-Akhbar cha Al-Qarishiy uk. 38. Nuzulul-Abrar cha Badi Khishiy uk. 21 na amesema: “Hii ni hadithi sahihi mashuhuri na hakuacha kuzungumza katika usahihi wake isipkuwa mwenye ushabiki (ta’asubu), na mpinzani kauli yake haizingatiwi, kwani hadithi hii ina njia nyingi sana.” Al-Imamah Was-Siyasah cha Hafidh Ibnu Qutaibah Juz. 1. Muujamul–Udabai cha Yaqut Al-Hamawiy Juz. 18, uk. 84. Al-Milali Wanahli cha Shaharistaaniy. Tadhkiratul-Hufadh cha Haafidh Dhahabiy Juz. 3, uk. 231 na amesema: “Ama hadithi (man kuntu–maulaah) “Ambaye mimi ni kiongozi wake..” ina njia nzuri na nimeandika kitabu mahsusi juu ya hilo vilevile.” Naasema: Ameshaandika Hafidh Dhahabiy kitabu maalum kuhusu tukio la Ghadir tukufu na amekiita Tariyq Hadithil-Wilaayah. Nihayatul-Irbi Fiy Fununul-Adab cha Nawawiy. 56.Al-Khutat cha Maqriyzi. 57.Akhbar Duwal cha Qaramaniy Admishiqiy. 58.Siratul-Halabiyah cha Halabiy Ashafiy Juz. 3, uk. 302. 59.Musnad Abu Yaaliy Al- Muuswiliy. 60.Tadhkiratul-Khawasil-Ummah cha Sibit Ibnu Jauziy Al-Hanafiy uk.18. 25
IDDI AL-GHADIYR D.Kanju final.qxd
7/1/2011
4:32 PM
Page 26
Iddi al-Ghadiyr Amesema: “Wameafikiana maulamaa wa sira kwamba kisa cha Ghadir kilikuwa ni baada ya kurejea Nabii (s.a.w.w.) kutoka Hijjatul-Wida’a tarehe 18 Dhilhaji, aliwakusanya sahaba na walikuwa mia na ishirini elfu na akasema: “Ambaye mimi ni kiongozi wake basi Ali ni kiongozi wake.” Alisema Nabii (s.a.w.w.) ibara iliyo wazi bila ya kupinda wala kuashiria.” Mushikilul-Athar Juz. 2, uk. 308 cha Haafidh At-Tahawiy aliyefariki mwaka 279 A.H. Al-Manaaqib cha Ibnu Al-Maghaaziy Shaafiy aliyefariki 483 A.H. Amesema kutoka kwa Sheikh wake Abul-Qaasim baada ya kupokea kwake hadithi ya Al-Ghadiyr. “Hii ni hadithi sahihi kutoka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.w) na wameipokea takriban watu mia moja, kati ya hao ni watu kumi waliobashiriwa pepo, nayo ni hadithi iliyothibiti sijui ubovu wake, Ali amepwekeka na fadhila hii na wala hashirikiani naye yeyote.” Faraidus–Simtain cha Al-Juwayny Ashaafiy. At-Tamhiid Fiy Usulid-Diin cha Baqalaamiy. Al-Mirqaatu Fiy Sharhul-Mishkaati Juz. 5, uk. 568 cha Al-Harawiy AlQaaniy Al-Hanafiy aliyefariki 1014 A.H. bali baadhi ya Hufaadh wameihesabu kuwa ni mutawatir ambapo kuna riwaya ya Ahmad bin Hambal, kwamba wameisikia kutoka kwa Nabii sahaba thelathini na waliitumia kutoa ushahidi kwa Ali alipopokonywa ukhalifa wake. Sharhul-Mawahib cha Zarwaaniy Al-Maalikiy. Al-Bayan Wataarif cha Ibnu Hamza Ad-Dimishiqiy Al-Hanafiy. Zaynul-Fataa cha Aswimy na amesema: “Hadithi hii umma umeipokea na umeikubali, nayo inaafikiana na misingi.” Kisha akaipokea kwa njia nyingi. Sirul-Alamiyna uk. l9, cha Al-Ghazaliy aliyefariki 505 A.H. Amesema: “Hoja imeshinda kwa upande wake na jamhuri imeafikiana juu ya matini 26
IDDI AL-GHADIYR D.Kanju final.qxd
7/1/2011
4:32 PM
Page 27
Iddi al-Ghadiyr (matamko) ya hadithi kutoka katika hotuba yake (s.a.w.w.) katika siku ya Ghadir Khum, kwa muafaka wa wote, naye amesema: ‘Ambaye mimi ni kiongozi wake basi Ali ni kiongozi wake.”’ Al-Manaaqib cha Haafidh Abu Al-Faraj Ibnu Jauziy Al-Hanbaliy aliyefariki 598 A.H. Amesema: “Wameafikiana maulamaa wa sira kwamba tukio la Ghadir lilikuwa baada ya kurejea Nabii (s.a.w.w.) kutoka Hijjatul-Widaa 18 Dhilhaji na alikuwa pamoja na sahaba, mabedui na wanaoishi karibu na Makka na Madina, laki moja na ishirini elfu wamesikia kutoka kwake maneno haya, na washairi ni wengi katika kuelezea tukio hilo.” Is’afur-Raghibiina cha Swabana Ashaafiy kilichochapishwa, katika sharhu ya Nurul-Abswar uk.153. 72. Al-Muutaswar Minal-Mukhtasar cha Abu Al-Mahaasim Al-Hanafiy uk. 413. 73. Wasilatul-Maali Fiy Manaaqibil-Aal cha Sheikh Ahmad bin Bakathyr Al-Makkiy Ashafiy. 74. Asnal-Matwalib Fiy Manaaqib Ali bin Abutwalib uk. 3, cha Al-Jauziy Dimishiq Ashafiy aliyefariki 833 A.H humo amepokea hadithi ya Ghadir kwa njia themanini na akasema: “……. Ni mutawatir kutoka kwa Nabii (s.a.w.w.) wameipokea kundi kubwa kutoka kwa kundi kubwa na wala hazingatiwi aliyejaribu kuidhoofisha miongoni mwa asiyekuwa na ujuzi au elimu hii (yaani elimu ya hadithi).” Kisha aliyataja majina ya kundi la sahaba ambao wamepokea hadithi na katika yao ni Abu Bakr, Umar, Talha, Zubairi, Saad bin Abi Waqaasi, Abdur-Rahman bin Auf na wengineo. Kisha akasema: “Imethibiti vilevile kwamba kauli hii ilikuwa imetoka kwa Nabii (s.a.w.w.) siku ya Ghadir Khum.” 75. Asnaal-Matwalib cha Al-Bairtiy Ashafiy uk. 227. 76. Tashriful-Adhaana uk. 77 cha Haafidh Ali bin Muhammad bin As27
IDDI AL-GHADIYR D.Kanju final.qxd
7/1/2011
4:32 PM
Page 28
Iddi al-Ghadiyr Sadiq Al-Hadharamiy na akasema: “Ama hadithi “Ambaye mimi ni kiongozi wake basi Ali ni kiongozi wake.” ni mutawatir kutoka kwa Nabii (s.a.w.w.) kutoka katika riwaya ya zaidi ya watu sitini, na kama tutataja sanadi zote tutarefusha sana.” 77. Al-Uruwatul-Wuthuqah cha Sheikh Alau Diyn Asamnaniy aliyefariku 736 A.H. 78. Ansaabul-Ashiraf cha Baladhuriy. 79. As-Swalatul-Faakhirah Bil-Ahaadithil-Mutawatir chapa ya misri uk. 49 cha Mufti wa Sham Al-Haadi Al-Hanafiy. 80.Tafsiru-Thaalabiy. Msomaji mtukufu haya ni majina themanini ya vitabu na rejea zilizoandika tukio la Ghadir tukufu na vyote ni vya maulamaa wa Kisunni na maimam wao na mahafidhi wao. Na jua kwamba mimi hapa sikutaja vitabu vya rejea vya Shia hata kimoja ili msomaji asije akasema kuwa Shia pekee ndio waliotaja tukio la Ghadir. Hapana…. maulamaa wa Kisunni vilevile wametaja tukio hili la kihistoria. Kama ningetaka kutaja majina na rejea za Kishia ambazo zinazungumzia tukio tukufu la Ghadir, idadi ingekuwa kubwa mno, tukiongezea kwamba kuna rejea zingine za Kisunni hazikutajwa kabisa kwa ajili ya kufupisha kitabu, na anayetaka ziada ya ufafanuzi ni juu yake kurejea juzuu ya kwanza katika kitabu cha Al-Ghadir cha Sheikh Abdul-Husein Al-Amim. Msomaji mtukufu baada ya kutaja rejea hizi na vitabu vinavyozingatiwa, je kumebakia nafasi ya kupinga uongozi wa Imam Ali ibn Abu Talib na kwamba ni yeye tu ndio Khalifa wa Mtume wa Mwenyezi Mungu? Na je inajuzu kushikamana na asiyekuwa yeye katika ambao haikupokewa kwake nasi (aya au Hadithi) wala dalili? “Ni kitu gani baada ya haki isipokuwa ni upotovu.” “Hakika huu ni ukumbusho anayetaka afuate njia kuelekea kwa Mola Wake.”
28
IDDI AL-GHADIYR D.Kanju final.qxd
7/1/2011
4:32 PM
Page 29
Iddi al-Ghadiyr
KUKAMILIKA KWA DINI Tunarea tena kwenye mazungumzo kuhusu tukio la Ghadir tukufu tunasema: Kiapo cha utii kilipomalizika kwa Imam Ali Amirul-Mu’minin (a.s.) na kabla watu hawajatawanyika aliteremka Jibril kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) pamoja na Aya hii tukufu:
“Leo hii nimekukamilishieni dini yenu na nimekutimizieeni neema zangu na nimekuridhieni Uislamu kuwa dini yenu.” (Surat Al-Maidah: 3). Nabii (s.a.w.w.) akasema: “Allaahu Akbar kwa kukamilika dini, kutimia neema, na Mola Wangu ameridhia ujumbe wangu na uongozi wa Ali baada yangu.” Ewe msomaji mtukufu wameafikiana wafasiri na wanahadithi wa kishia kuwa Aya hii ya kukamilika dini imeteremka siku ya Ghadir. Na wamewaunga mkono juu ya hilo kundi kubwa katika maulamaa wa Kisunni, mahafidhi wao na wanahadithi wao kati yao ni:Al-Haafidh mwana historia Ibnu Jarir Tabary aliyefariki 310 A.H. katika Kitabul-Wilaayah kwa sanadi yake kutoka kwa Zayd bin Arqam. Al-Haafidh Ibnu Marduwaihi Al-Is’fahaaniy aliyefariki 410 A.H. kutoka kwa Abu Said Al-Khuduriy kama ilivyo katika Tafsir Ibnu Kathir Juz. 2 uk. 14.
29
IDDI AL-GHADIYR D.Kanju final.qxd
7/1/2011
4:32 PM
Page 30
Iddi al-Ghadiyr Al-Haafidh Jalaluddini As-Suyutwiy katika Tafsir yake Juz. 2, uk. 259 kutoka kwa Abu Said Al-Khudiry na Abu Huraira. Al-Haafidh Abu Bakr Al-Khatib Al-Baghdadi katika Tarikh Baghdad Juz.8 uk. 290 kutoka kwa Abu Huraira. Al-Haafidh Al-Haskaaniy katika Shaawahidut-Tanzil Al-Khatib Al-Khawarizimiy katika Al-Manaaqib uk. 80 na 94. Al-Juwainy Ashaafiy katika Faraid As-Samtwainy Juz.1. Al-Haafidh Ibnu Al-Maghaaziliy Ashaafiy katika Al-Manaqib, na wengineo. Ewe msomaji mtukufu hakika Aya hii tukufu ya kukamilika dini inatufanya tuzinduke na kutazama baadhi ya nukta na misingi muhimu. Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema: “Leo hii”: Tunaulizana ni siku gani hii, ambayo ina utukfu mkubwa kiasi hiki kwa Mwenyezi Mungu hadi akamilishe humo dini? Jawabu: Hakika ni siku ya Al-Ghadir tukufu, siku ya Ghadir yenye kudumu …siku ambayo alisherehekea Nabii (s.a.w.w.) kwa kumvika taji Ali ibn Abu Talib kwa taji la ukhalifa mtukufu na Uimam mkuu. “Leo hii nimewakamilishieni dini yenu” hii ina maana kuwa dini ilikuwa pungufu kabla ya siku hii, nayo ni siku ya Ghadir, siku ya kuteuliwa khalifa wa Mtume wa Mwenyezi Mungu na kwamba dini imekamilika kwa uongozi wa Ali na ukhalifa wake. Na maana ya hilo ni kwamba dini na imani bila ya Ali inazingatiwa kuwa ni pungufu, kama ambavyo dini na imani bila ya Mtume wa Mwenyezi Mungu inazingatiwa kuwa ni pungufu vilevile. “Na nimewatimizieni neema Yangu.” Na neema hii ni uongofu uliokamilika na uongozi uliokamilika ambao unapatikana kwa kumwamini Mwenyezi Mungu kuwa ndiye Mola na Muhammad kuwa ndiye Nabii na kwamba Ali ndiye Imam. Na kwa maana nyingine ni kwamba uongofu kamili unapatika kwa:- “La ilaaha ila llah, Muhammad Rasuulullah, 30
IDDI AL-GHADIYR D.Kanju final.qxd
7/1/2011
4:32 PM
Page 31
Iddi al-Ghadiyr Aliyun Waliyullah.” Na kana kwamba Mwenyezi Mungu anazingatia neema Zake zilizotangulia zilikuwa hazijakamilika kwa waja wake hadi “Siku” hiyo ambapo “Nimewatimizieni neema Zangu” kwa uongozi wa Ali ibn Abu Talib (a.s.). “Na nimewaridhia Uislamu kuwa dini yenu” ndio ….Uislamu ambao unaotokana na Tauhid, Unabii na Uimam ndio unaoridhiwa na Mwenyezi Mungu Mtukufu, uislamu uliochanganywa na mapenzi ya Ahlul-bait, na kuitakidi uongozi wao na uma’sum wao. Ama Uislamu ambao umeepukana na uongozi….umekosa kiungo cha itikadi ya Uimam wa Ahlul-baiti, na ambao umesimama katika kuwachukia Ahlul-baiti, huu unakataliwa mbele ya Mwenyezi Mungu na wala hauridhii (s.w.t.).
TAJI LA UKHALIFA. Umeshafahamu ewe msomaji kwamba Mtume wa Mwnyezi Mungu (s.a.w.w.) alimfanya Imam Ali ibn Abu Talib kuwa khalifa wake katika siku ya Ghadir …….., ilikuwa ni ada na bado inaendelea kwa wafalme na watawala kuwavika taji wale wanaotarajiwa kuwa watawala baada yao na makhalifa wao, kwa taji lililopambwa kwa dhahabu na kurembwa kwa johari na vito vya thamani, huwavisha siku ya kutawazwa kwao. Na kwa kuwa mawalii wa Mwenyezi Mungu hawadanganyiki kwa dhahabu, fedha na vinginevyo katika mapambo ya kimaada na wala hawajali mandhari haya yasiyo na thamani, pamoja na kwamba wana uwezo juu ya hayo na kutokushindwa kwao juu ya hilo....Mtume wa Mwenyezi Mungu – naye ndiye bwana wa mawalii wa Mwenyezi Mungu - alikuwa ni mwenye kuyapa mgongo mandhari haya na mwenye kupinga udanganyifu huu, nani mwenye kukubali maana ya kiroho, kwa sababu hii alimvika khalifa wake 31
IDDI AL-GHADIYR D.Kanju final.qxd
7/1/2011
4:32 PM
Page 32
Iddi al-Ghadiyr kwa taji ambalo ni ghali kuliko mataji ya wafalme wote na ambalo ni bora kuliko utajiri wa kilimwengu pamoja na urahisi wake….. Alimvika kwa mikono yake mitukufu taji la ukhalifa mtukufu na uimam mkuu, alimvika katika namna mahsusi kilemba chake kinachoitwa AsSahaabah14, ikiashiria utukufu, ubora, utakatifu na haiba….. katika mkusanyiko huo mkubwa, siku tukufu na sikukuu ya furaha. Katika sehemu hii anatusimulia Imam Ali (a.s.) juu ya kuvikwa taji hili tukufu la Nabii, anasema: “Alinivika kilemba Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) siku ya Ghadir Khum kwa kilemba maalumu, akaiteremsha ncha yake kwenye bega langu na akasema: ‘Hakika Mwenyezi Mungu amenipa nguvu siku ya Badir na Hunaiyn kwa malaika wenye kuvaa kilemba hiki.”’15 Na kutoka kwake (a.s.) kuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) alimvika kilemba kwa mikono yake, kikaanguka nyuma na kuteremkia mbele yake kisha Nabii akasema: “Geuka nyuma,” akageka kisha akamwambia: “Geuka mbele,” akageuka na akawageukia sahaba zake akasema: “Hivi ndivyo linavyokuwa taji la Malaika.” Ibnu Abbas anasema: “Mtume wa Mwenyezi Mungu alipomvika Ali (a.s) kilemba alisema: ‘Ewe Ali kilemba ni taji la Waarabu.”’16 Al-Halbiy anasema: “Mtume (s.a.w.w.) alikuwa na kilemba kinachoitwa As-Sahabah alimvika Ali ibn Abu Talib, na Ali alipokuwa akitokeza kwake basi anasema (s.a.w.w.): ‘Amekujieni Ali akiwa ndani ya As-Sahabah.’ Yaani kilemba chake ambacho alimpa.”17 14 Wanahistoria wanasema kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) alikipa jina mahsusi kila kitu kilichofungamana naye mfano: Kilemba chake alikiita As-Sahaabah, na fimbo yake aliita Mamshuq na ngamia wake alimwiita AlAdhabau, n.k. 15 Fusulul-Muhimah cha Ibnu As-Swibagha Al-Malikiy uk. 27. 16 Kitabul-Ghadir Juz.1 uk. 290. 17 Siratul-Halabiy Juz. 3 uk. 369. 32
IDDI AL-GHADIYR D.Kanju final.qxd
7/1/2011
4:32 PM
Page 33
Iddi al-Ghadiyr
SHAHADA YA TATU KATIKA ADHANA Baada ya tukio la Ghadir……….uliwadia wakati wa swala akasimama sahaba mtukufu Abu Dhar Al-Ghafaary au Bilal na akaadhini kwa ajili ya Swala. Na katika adhana baada ya kauli yake: “Ash’hadu anna Muhammadan Rasuulullah” akaongeza “Ash’hadu anna Aliyan Waliyullah.” Wanafiki na wapinzani wakafanya haraka kwenda kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) na wakalalamikia waliyoyasikia kutoka kwa Abu Dhar au Bilal, na wao wakawa wanasubiri kukemewa huyu mwadhini na kumkataza kutokana na ziada hii, isipokuwa Nabii (s.a.w.w.) akaelekeza lawama na makemeo kwao akasema: “Je hamkufahamu hotuba yangu hii juu ya uongozi wa Ali? Je hamkusikia kauli yangu kuhusu Abu Dhar kuwa: Haikufunika mbingu wala hajatembea ardhini mkweli wa kauli kuliko Abu Dhar?” Kisha akawaambia: “Hakika nyinyi mtageuka baada yangu kwa visigino vyenu.”18 Na katika mjadala huu umemuona Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) anaafiki ziada hii na anaikubali, na tambua kuwa ridhaa ya ma’sum ni hoja, na anaipitisha ili iwe ni sehemu katika adhana na itajwe kila linapotajwa jina la Mwenyezi Mungu na Mtume Wake na kila unapokuja utajo wa Laa ilaaha illa llahu na Muhammad Rasuulullah. Na kuna ihtimali kuwa Nabii mwenyewe ndiye aliyemwamuru Abu Dhar au Bilal kwa ziada hii katika adhana kwa kujua kwake kuwa wanafiki watakosoa hatua hii tukufu, na Mtume (s.a.w.w.) akajibu ukosoaji wao na kupitisha maneno ya Abu Dhari.
18 Kitabu Salaafah Fiy Amril-Khilaafah cha Sheikh Abdullaah Al-Maraaghiy. Naye ni kati ya maulamaa wa Kisunni katika karne ya saba hijiria, na amemtaja Sheikh Abdul-Adhim Ar-Rabiy katika kitabu As-Siyaasatul-Hussainiyah uk. 108 33
IDDI AL-GHADIYR D.Kanju final.qxd
7/1/2011
4:32 PM
Page 34
Iddi al-Ghadiyr Na unona jinsi Mtume wa Mwenyezi Mungu alivyotilia mkazo kuwapinga wale waliokosoa na akawaambia: “Je hamkufahamu hotuba yangu hii juu ya uongozi wa Ali?” Yaani nini maana ya hotuba hiyo ndefu ambayo niliitoa kwenu katika hali ya joto kali na jangwa lenye kuwaka? Na anazidi kuwapinga kwa ukali wake: “Je hamkusikia kauli yangu kuhusu Abu Dhar kuwa: Haikufunika mbingu wala hajatembea ardhini mkweli wa kauli kuliko Abu Dhar?” Yaani Abu Dhar hafanyi upuuzi bali yeye ni mkweli mwaminifu hasemi isipokuwa ukweli, basi ni kwa nini mkaja kunilalamikia juu yake? Kisha Mtume (s.a.w.w.) akafichua kuhusu uhakika wa wale wakosoaji na hatima yao kwa kauli yake: “Hakika nyinyi mtageuka baada yangu kwa visigino vyenu.” Yaani: hakika nyinyi mtapotoka baada yangu na kumwaasi khalifa wangu na mwisho wenu utakuwa mbaya, kana kwamba Mtume (s.a.w.w.) ameashiria kwa kauli yake kwenye kauli ya Mwenyezi Mungu.
“Hakuwa Muhammad isipokuwa ni Mtume wameshapita kabla yake Mitume, je akifa au akiuliwa mtageuka nyuma kwa visigino vyenu, na atakaegeuka kwa visigino vyake hatomdhuru Mwenyezi Mungu chochote na Mwenyezi Mungu atawalipa wenye kushukuru.” (Surat AlImran: 144). Na maana ya maneno ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) ni kwamba Imam Ali ibn Abu Talib ni nguzo ya tatu katika dini baada ya Mwenyezi Mungu na Mtume Wake, na kwamba uimam ndio nguzo ya tatu ya kiislamu baada ya Tauhidi na Unabii. Ndugu yangu msomaji! Zaidi ya hadithi iliyotajwa kuna hadithi zingine zinaamrisha shahada ya tatu nayo ni kusema: “Ash’hadu anna Aliyan Waliyullah” baada ya shahada mbili. Na kwa 34
IDDI AL-GHADIYR D.Kanju final.qxd
7/1/2011
4:32 PM
Page 35
Iddi al-Ghadiyr kutazama umuhimu wa maudhui haya na wingi wa maswali juu ya hilo basi inafaa na ni dharura sana tuzungumze juu ya hili kwa ufafanuzi kisha turejee ili tuendelee na mazungumzo yanayohusiana na tukio tukufu la Ghadir.
MWENYEZI MUNGU NA SHAHADA YA TATU. Hakika wa kwanza aliyeamrisha kutajwa Imam Ali baada ya shahada mbili ni Mwenyezi Mungu Mtukufu. Imepokewa kutoka kwa Imam As-Sadiq (a.s.) kwamba amesema: “Alipoumba Mwenyezi Mungu mbingu na ardhi alimwamuru mwenye kunadi na akanadi: ‘Ash’hadu an laa ilaaha illa llahu’ mara tatu. ‘Ash’hadu anna Muhammadan Rasulullah’ mara tatu. Na Ash’hadu anna Aliyan Amirul-Mu’minin haqan’ mara tatu.”19 Tunaulizana: Kwa nini Mwenyezi Mungu ameamuru miito hii mitatu kwa pamoja? Na hiyo inaonyesha nini? Je, haionyeshi umuhimu wa mafungamano ya shahada hizi mbili na shahada ya tatu? Je, haionyeshi kwamba imani ni wajibu ikite juu ya shahada hizi tatu? – Jawabu ni ndio…. hivyo ndivyo. Tunarejea ili tutilie mkazo kwamba muumini katika mantiki ya Mwenyezi Mungu na Mtume Wake ni yule ambaye anaamini kwa kauli na kitendo Laa ilaaha ila llahu, Muhammadu Rasulullaah, Aliyun Amirul-Mu’minin Waliyullah. Kinyume cha hivi sio muumini bali ni mwislamu, hivyo inahifadhiwa kwa shahada mbili damu yake tu, mali yake na heshima yake. Aya zote za Qur’ani ambazo zinaanza kwa tamko “Enyi mlioamini” kwa hakika zinawahutubia walioamini shahada hizi tatu kwa pamoja. 19 Biharul-An’war Juz. 37 uk. 295. Na inayokaribiana na hiyo ni ile iliyomo katika Amaal cha As-Saduuq, majlis ya 88. Kwa nyongeza, rejea Surat al-Maida, aya ya 55, kwenye sababu ya kushuka kwa aya utakudhihirikia ukweli huu. 35
IDDI AL-GHADIYR D.Kanju final.qxd
7/1/2011
4:32 PM
Page 36
Iddi al-Ghadiyr Muhtasari wa mazungumzo ni kwamba Mwenyezi Mungu Mtukufu hakutosheka na shahada mbili bali aliamuru mlinganiaji wake aunganishe pamoja na hizo, shahada ya Amirul-Mu’minin kwa kutangaza uongozi wake, na hii ni dalili juu ya umuhimu wa kuleta shahada ya tatu kila unapokuja utajo wa Mwenyrezi Mungu na Mtume Wake.
MTUME WA MWENYEZI MUNGU NA SHAHADA YA TATU Ama kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.), hadithi zimepokewa kutoka kwake zikihusu Sunna ya kumtaja Imam Ali (a.s.) kila unapokuja utajo wa Mwenyezi Mungu na Mtume Wake. Katika yafuatayo tunataja mifano hiyo: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.): “Mwenye kusema: ‘Laa ilaaha ila llahu’ inafunguka kwake milango ya mbingu. Na mwenye kufuatiliza kusema Muhammad Rasulullah unakunjuka uso wa haki tukufu20 na anafurahika kwa hilo. Na mwenye kuifuatilizia kwa Aliyun Waliyu llaahi, Mwenyezi Mungu anamsamehe dhambi zake hata kama ni kama idadi ya matone ya mvua.” Hakika hadithi inaeleza waziwazi kujuzu kutaja jina la Imam Ali (a.s.) baada ya kumtaja Mwenyezi Mungu na Mtume Wake bila ya kutofautisha baina ya adhana na pinginepo bali ni kwa jumla na inahusu sehemu zote. 20 Haki hapa ni Mwenyezi Mungu Mtukufu na hakuna shaka kwamba kauli yake: “unakunjuka uso wa haki” ni katika upande wa majazi na sio wa uhakika, kwa sababu imeshathibiti katika nuru ya Qur’ani na akili kwamba Mwenyezi Mungu hana mwili wala hana viungo, na kauli yake “unakunjuka uso wa haki” ni kinaya ya ridhaa ya Mwenyezi Mungu kwa kauli hii. Nayo ni kumtaja Imam Ali baada ya kumtaja Mtume wa Mwenyezi Mungu kwa kauli hii. Na kuenea rehema yake Mwenyezi Mungu na maghufira yake kwa mwenye kusema hivyo. Na aina hii ya majazi ni nyingi katika Qur’ani tukufu na hadithi tukufu. 36
IDDI AL-GHADIYR D.Kanju final.qxd
7/1/2011
4:32 PM
Page 37
Iddi al-Ghadiyr Bali hadithi hii inaonyesha Sunna ya utajo huu, kutajwa kwake na ubora wake mbele ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, na kwa ajili hii amesema Mtume (s.a.w.w.): “Na mwenye kuifuatilizia kwa Aliyun Waliyu llaahi, Mwenyezi Mungu anamsamehe dhambi zake hata kama ni kama idadi ya matone ya mvua.”21 Je, baada ya haya; mosi tunahitaji dalili juu ya kujuzu? Pili dalili ya kuwa ni sunna? Je, yanafahamika maneno yaliyo dhahiri na wazi kuliko maneno ya hitimisho la Manabii? Na kama sentensi hii haikuwa ni yenye kuridhiwa kwa Mwenyezi Mungu, je Mwenyezi Mungu angesamehe madhambi ya mwenye kuisema, hata kama ni kama vile idadi ya matone ya mvua? Hakika Mwenyezi Mungu anawalingania waislamu kwa ulimi wa Mtume Wake wote waseme: Aliyun Waliyullahi kila wanaposema Laa ilaaha ila llahu Muhammadu Rasulullah katika adhana na kunginepo. Na kuna ihtimali kuwa yeye mwenyewe alimwamuru mwadhini kwa hatua hii tukufu na uwezekano huu hauko mbali kwa sababu sahaba mtukufu kama vile Abu Dhar au Bilal hawezi kufanya hivyo mwenyewe. Bali ni lazima kuna moja kati ya mawili: Ima itakuwa Nabii alimwamuru na au yeye alifahamu hivyo kutokana na hotuba ya Al-Ghadir na kisha Nabii akaipongeza na akaipitisha hatua yake na akaiafiki. Vyovyote iwavyo hata kama kusingekuwa na dalili juu ya kujuzu Sunna ya kutaja jina la Imam Ali (a.s.) katika adhana na penginepo isipokuwa ni kuwa hadithi ya Nabii iliyotangulia ingetosha kuwa ni dalili na hoja kwa ambaye moyo wake una maradhi. Ewe msomaji mtukufu, katika hadithi zilizotajwa katika maudhui haya ni ile ambayo imepokewa kwamba jamaa miongoni mwa waarabu, waajemi, waqibti na wahabeshi walihudhuria kwa Nabii (s.a.w.w.) na akawaambia: “Je mmekubali kushuhudia kwamba hakuna Mungu isipokuwa Mwenyezi Mungu peke Yake hana mshirika na kwamba Muhammad ni mja Wake na 21 Biharul-An’war Juz. 38 uk. 318. 37
IDDI AL-GHADIYR D.Kanju final.qxd
7/1/2011
4:32 PM
Page 38
Iddi al-Ghadiyr Mtume Wake, na kwamba Ali ibn Abu Talib ni Amirul-Mu’minin na kiongozi baada yangu?” Wakasema ndio. Mtume (s.a.w.w.) akakariri mara tatu na wao wakashuhudia hivyo.22 Kutokana na hadithi hii tunafahamu upeo wa kuuliza Nabii juu ya umuhimu wa shahada ya tatu na kwamba ndio yenye kukamilisha shahada mbili. Mtume (s.a.w.w.) hakutosheka kwa kukubali kwao mara moja bali alikariri mara tatu ili wafahamu vizuri kwamba imani inakita katika shahada hii ya tatu, na kwamba kujitenga nayo ni kama vile kujitenga na shahada zote, na hiyo inazingatiwa kuwa ni upotofu mkubwa. Amesema Mtume wa Mwnyezi Mungu (s.a.w.w.): “Naapa kwa aliyenituma kwa haki kuwa ni mwenye kubashiri, haikutulia Kursiyu, Arshi wala hazikuzunguka sayari na wala hazikusimama mbingu na ardhi hadi Mwenyezi Mungu alipoziandika Laa ilaaha ila llahu Muhammadu Rasulullah Aliyun AmirulMu’minin.”23
AHLUL-BAIT NA SHAHADA YA TATU Njoo pamoja na mimi ewe msomaji kwenye historia ya Ahlul-bait ambao Mwenyezi Mungu amewahifadhi kutokana na uchafu na akawatakasa kabisa …. ambapo utakuta kwamba wao walikuwa wanakariri maneno ya babu yao Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) na wote ni nuru moja. Huyu hapa Imam Jafar As-Sadiq mjukuu wa Mtume wa Mwenyezi Mungu na khalifa wake wa sita wa kisheria ameamuru kumtaja Imam Ali (a.s.) kila unapokuja utajo wa Mwenyezi Mungu na Mtume Wake. Imepokewa kutoka kwa Qasim bin Muawiya amesema: “Nilimwambia Abu Abdillah AsSadiq (a.s.) hawa24 wanapokea katika miraji yao kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) alipopelekwa miraji aliona katika arshi 22 Kitabu Al-Aamal cha As-Saduq uk. 230 majlis ya 60. 23 Biharul-An’war Juz. 27 uk. 8. 24 Anakusudia kwa “hawa” wapinzani wa Ahlul-bait (a.s.). 38
IDDI AL-GHADIYR D.Kanju final.qxd
7/1/2011
4:32 PM
Page 39
Iddi al-Ghadiyr (maandishi ya) Laa ilaaha ila llahu Muhammad Rasulullah, Abubakari AsSwiddiq. Imam akasema: ‘Subhanallaah! Wamebadilisha kila kitu na hili pia?’25 Nikasema ndio. Akasema (a.s.): ‘Hakika Mwenyezi Mungu Mtukufu alipoumba Arshi aliandika nguzo zake: Laa ilaaha ila llahu Muhammad Rasulullaah Aliyun Amirul–Mu’minina. Alipoumba Kursiyu akaandika: Laa ilaaha ila llahu Muhammad Rasulullaah Aliyun Amirul–Mu’minina. Alipoumba lawhu akaandika: Laa ilaaha ila llahu Muhammad Rasulullaah Aliyun Amirul–Mu’minina. Alipomuumba Israfiyl akaandika kwenye paji lake: Laa ilaaha ila llahu Muhammad Rasulullaah Aliyun Amirul–Mu’minina. Alipomuumba Jibril akaandika katika ubawa wake: Laa ilaaha ila llahu Muhammad Rasulullaah Aliyun Amirul–Mu’minina. Alipoumba milima akaandika juu ya vilele vyake: Laa ilaaha ila llahu Muhammad Rasulullaah Aliyun Amirul–Mu’minina. Alipoumba jua akaandika juu yake: Laa ilaaha ila llahu Muhammad Rasulullaah Aliyun Amirul–Mu’minina. Alipoumba mwezi akaandika juu yake: Laa ilaaha ila llahu Muhammad Rasulullaah Aliyun Amirul–Mu’minina.”’ Ewe msomaji! Tazama sentensi hii vizuri: “Kisha akasema (a.s.): ‘Atakaposema mmoja wenu: Laa ilaaha ila llahu Muhammad Rasulullaah basi aseme: Aliyun Amirul–Mu’minina Waliyu llahi.”’26 25 Sentensi hii katika maneno ya Imam As-Sadiq inatufunulia pazia la uzushi muovu ambao wameufanya wahalifu katika hadithi za Nabii kwa ajili ya kuwatengenezea watu wao sifa takatifu mkabala wa walizonazo Ahlul-bait katika shakhsiyah, uchamungu na utukufu waliopewa na Mwenyezi Mungu. Hivyo (a.s.) kwa mshangao akasema: “Subhanallaah wamebadilisha kila kitu hata hili pia?” Hapa unajua ukweli wa hadithi ya “watu kumi waliobashiriwa pepo” na mfano wake kuwa ni katika hadithi za uongo. 26 Biharul-An’ar Juz. 27 uk. 1. 39
IDDI AL-GHADIYR D.Kanju final.qxd
7/1/2011
4:32 PM
Page 40
Iddi al-Ghadiyr Ni utukufu ulioje wa hadithi hii. Hakika ni hadithi tukufu inatubashiria umuhimu wa kuiweka shahada ya tatu pamoja na shahada mbili katika sehemu zote. Tazama ewe msomaji jinsi Mwenyezi Mungu alivyotilia mkazo jina la Imam Ali (a.s.) kila ulipokuja utajo wake na utajo wa Mtume Wake (s.a.w.w.). Mkazo wote huu ni wa nini ? Ni wa nini msisitizo huu katika kuandika jina la Imam Ali (a.s) katika Kursiyu, Lawhu, paji la Israfyli, ubawa wa Jibrilu, ncha za mbingu, tabaka za ardhi, na vilele vya milima na kwenye jua na mwezi? Je, katika haya yote sio dalili ya kutakiwa kutaja jina la Imam Ali (a.s.) mbele ya Mwenyezi Mungu Mtukufu? Kisha wewe umeona kwamba Imam As-Sadiq (a.s.) anaamuru kwa kuelewa somo hili kutoka kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu na kusema: “Atakaposema mmoja wenu: Laa ilaaha ila llahu Muhammad Rasulullaah basi aseme: Aliyun 27 Amirul–Muuminina Waliyu llahi.”’ Na amri hii ni ya jumla inahusu adhana na penginepo. Amesema SheikhulIslaam Al-Majlisy baada ya kuashiria hadithi hii: “Inaonyesha juu ya Sunna ya hilo kwa ujumla, na adhana ni katika sehemu hizo, na imeshapita mifano ya hadithi hii katika mlango wa fadhila zake (a.s.).”28
FATWA ZA MAULAMAA Kwa kutegemea hadithi hizi tukufu na mifano ya hizo na nyinginezo katika dalili, maulamaa wa dini na mafaqihi wa sheria wametoa fatwa ya kujuzu kusema: “Ash’hadu anna Aliyan Amirul-Mu’minin Waliyu llah” katika adhana. Bali limetoa fatwa kundi kubwa kati yao juu ya Sunna ya hilo na kupendeza kwake, na wengine wametoa fatwa ya wajibu wake kwa anuani ya hukumu ya dharura (thanawiy) katika zama hizi. Baadhi ya 27 Biharul-An’ar Juz. 27 uk. 1. 28 Biharul-An’war Juz. 48 Kitabu Swalatu uk.111. 40
IDDI AL-GHADIYR D.Kanju final.qxd
7/1/2011
4:32 PM
Page 41
Iddi al-Ghadiyr maulamaa wameandika vitabu maalumu juu ya shahada hii na dalili ya kujuzu kwake, kuwa kwake Sunna na kupendeza kwake.29 Amesema Sheikh Muhammad Hasan mwandishi wa kitabu Al-Jawaahir kinachohusu fiqhi na ambacho kinazingatiwa kuwa ni katika vitabu vikubwa vya rejea vya kifiqhi na humo ndimo imo duru ya ijitihadi na istimbati, amesema katika risala ya Risalaatun-Najatil-Ibaadi anapozungumzia adhana: “Ni Sunna kumswalia Mtume na ahali zake – wakati wa kutajwa jina lake - na kukamilisha shahada mbili kwa Shahada ya Ali (a.s.) kuwa yeye ni walii wa Mwenyezi Mungu, na shahada ya kuwa yeye ni kiongozi wa waumini, hiyo ni katika adhana na penginepo.” Amesema Seyyid Al-Hakim: “Hakuna ubaya kuleta Shahada ya wilayah, kwa makusudio ya Sunna isiyo na mipaka, hiyo ni kutokana na habari iliyomo ndani ya Al-Ihtijaj: “Atakaposema mmoja wenu Laa ilaaha ila llahu Muhammad Rasulullah basi aseme: Aliyun Amirul-Mu’minin.” Bali hilo – katika zama hizi – linahesabiwa ni katika alama ya imani na nembo ya ushia, hivyo kwa upande huu inakuwa ni yenye kupendeza kisheria bali wakati mwingine inakuwa ni wajibu.”30 Kwa muhtasari ni kuwa ilivyo mashuhuri kwa mafaqihi na maulamaa ni kwamba Shahada ya tatu inapendeza na ni wajibu kuileta katika adhana kwa ajili ya kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu. Bali tumetaja baadhi ya maneno ya maulamaa (Mwenyezi Mungu awarehemu) kama 29 Katika walioandika katika maudhui haya ni Allamah As-Sayid Abdur-Razaq Al–Musawiy Al-Muqarram, ameandika kitabu maalumu kuhusu nembo hii tukufu amekiita Sirul-Imaan na ameshataja katika kitabu chake hiki majina yanayozidi sabini ya mafaqihi miongoni mwa mafaqihi wa sheria na maulamaa wa dini, na wote wanatoa fatwa ya kujuzu Shahada hii au kuwa kwake Sunna, au kuwa kwake wajibu. Mwenyezi Mungu amlipe mema As-Sayid Al-Muqarram kwa ajili ya haki na watu wake. 30 Mustamsaku–Wuthqa cha Ayatullah Al-Hakim. 41
IDDI AL-GHADIYR D.Kanju final.qxd
7/1/2011
4:32 PM
Page 42
Iddi al-Ghadiyr mifano katika yaliyotoka kwao miongoni mwa fatwa kuhusu maudhui haya. Baada ya yote haya yaliyotangulia tunasema: Hayo ni maneno ya Mwenyezi Mungu, na ni hizo hadithi za Mtume Wake, na zile ni hadhi za maimam watukufu, na hizi ni fatwa za maulamaa, je baada ya yote hayo kunabaki nafasi ya kutuhumu na kusema kuwa ni bidaa? Kwa faida zaidi tumeona ni bora tunukuu baadhi ya maneno ya mtunzi wa kitabu hiki katikka utangulizi wake katika kitabu cha Sirul-Imani cha Allaamah AlMuhaqiq Al-Kabir Seyyid Abdur-Razaq Al-Musawiy Al-Muqarram. Na ifuatayo ni nukuu hiyo.
KISIMAMO PAMOJA NA SHEIKH AS-SUDUUQ. Kila aliyesimama dhidi ya Shahada ya tatu katika adhana ameathirika kutokana na maneno ya Sheikh As-Suduq katika maudhui haya, ambapo ameinasibisha Shahada ya tatu katika adhana kwa Al-Mufawidhah, akawalaani na akajiweka mbali nao na akasema: “…..na Al-Mufawidhah, Mungu awalaani!! Wamezua habari na wameongeza katika adhana: “Muhammad wa Aali Muhammad Khairul-Bariyah” mara mbili. Na katika baadhi ya riwaya zao ni kuwa baada ya: “Ash’hadu anna Muhammadan Rasulullaahi” ni “Ash’hadu anna Aliyan Waliyullaah” mara mbili. Na kati yao kuna waliopokea badala ya hayo: “Ash’hadu anna Aliyan AmirulMu’minin haqan haqan” mara mbili ……” hadi mwisho wa maneno yake.31 Haya…… na katika kutafakari katika maneno ya Sheikhe As-Suduqu yanatubainikia yafuatayo:Kwanza: Kwa hakika kuna hadithi tukufu zilizopokewa kuhusu Shahada ya tatu katika adhana, lakini As-Suduqu amehukumu kuwa ni za uongo na 31 Man Laa Yahdhuruhu Al-Faqihi: Kitabu cha Swala, mlango wa Adhana. 42
IDDI AL-GHADIYR D.Kanju final.qxd
7/1/2011
4:32 PM
Page 43
Iddi al-Ghadiyr amekataa kutaja hadithi zake, wapokezi wake na sanadi zake. Na hii bila shaka sio njia ya istidilali wala sio mtindo wa utafiti na ijitihadi bali mtindo unaofuatwa na maulamaa na mafaqihi ni kutaja hadithi kwa sanadi zake na wapokezi wake kwanza, kisha kuzihukumu kwa usahihi au kwa ubovu, kuzikubali au kuzipinga, pamoja na kubainisha mtazamo wao wakati wa kubainisha sehemu za mushikeli na udhaifu katika sanadi au matini au hoja. Ama kuacha kuzitaja kabisa na kuziba njia kwa wanaokuja miongoni mwa maulamaa na muhadithina ili wasizione na kutoa maoni yao kwa mnasaba wa hadithi hizo, hii sio sahihi. Kwa sababu hii amesema mmoja wa maulamaa wetu naye ni Al-Faqihi Al-Kabir Sheikh Abdun-Nabiy Al-Iraqiy (Mwenyezi Mungu amrehemu)32 katika kuyaelezea maneno ya As–Suduq: “Hakusema yeyote katika Imamiyah kwamba katika sharti la habari kuwa hoja ni As-Suduq kuifanyia kazi au kutoipinga, hakuna mafugamano ya kukataa kwake au kukubali kwake na masuala ya habari ya wapokezi wachache kuwa hoja, hii ni katika mapito yao mengi. Kwani yeye - yaani As-Suduq – anazo fatwa za ajabu nyingi hakuziafiki yeyote kati ya maulamaa, kama vile masuala ya Nabii kusahau33 na akatupa hadithi ambazo zinasema haisihi Nabii (s.a.w.w.) kusahau, uwajibu wa Hijja kwa kila mwenye kuweza kila mwaka, kujuzu udhu na kuoga kwa maji mudhafu, utohara wa damu ikiwa ni kwa kiwango cha khumsi, utohara wa pombe, na kutonajisika maji machache kwa kukutana na najisi ….. kama zitakusanya fatwa zake za ajabu zitakuwa ni kitabu kikubwa kama ambavyo tumeashiria. Kwa ajili hiyo amesema Sheikh Al- Baharain katika Al-Hadaiq katika masuala ya maji mudhafu: ‘Hakika As-Suduq hakuwa ma’sum hadi kauli yake iwe ni hoja kwa asiye kuwa yeye au ilazimu kuifuata.”’ 32 Katika Risalutul-Hidayah anapozungumzia kuhusu shahada ya tatu ya uwalii kuwa ni sehemu ya adhana na iqama kama zilivyo sehemu zingine. uk. 39. 33 Maneno mazuri yalioje aliyoyasema mmoja wa Maulamaa: “Suduqu amesahau kwamba Nabii ni ma’sum hivyo hasahau.” 43
IDDI AL-GHADIYR D.Kanju final.qxd
7/1/2011
4:32 PM
Page 44
Iddi al-Ghadiyr Pili: Hakika Sheikh As-Suduq amezinasibisha kwa mufawidhah hadithi hizo ambazo zinathibitisha kuwa shahada ya tatu ni katika adhana. Tunaulizana: Al-Mufawidhah ni nani? Jawabu: Hakika Al-Mufawidhah kwa As-Suduq ni tofauti kabisa na Al-Mufawidhah waliotajwa katika vitabu, wewe ukirejea vitabu ambavyo vinawaeleza Al-Mufawidhah utaona vinasema: Al-Mufawidhah ni watu waliosema kwamba Mwenyezi Mungu amemuumba Muhammad na akamwachia kuumba dunia, hivyo yeye ni muumbaji wa vilivyo humo. Na inasemekana amemwachia hilo Ali. Na katika hadithi nyingine imekuja: “Mwenye kusema juu ya tafwidhi ameshamtoa Mwenyezi Mungu katika mamlaka yake.”34 Hii ndio maana ya Al-Mufawidhah iliyotajwa katika vitabu, lakini Sheikh As-Suduq anasema: “….. hakika Al-Ghulat na Al-Mufawidhah Mwenyezi Mungu awalaani!! wanapinga kusahau kwa Nabii (s.a.w.w.) na wanasema: Kama ingejuzu kusahau katika Swala ingejuzu kusahau katika tablighi, kwa sababu Swala ni faradhi kwake kama ambavyo talibighi ni faradhi kwake.”35 Inadhihirika katika maneno yake kwamba kila anayemwamini Nabii na ahali zake watoharifu itikadi kamili iliyokita na sahihi kabisa basi ni katika Ghulat na Mufawidhah, kwa sababu hiyo unamuona anawalaani Mufawidhah wanaoamini kutosahau kwa Nabii (s.a.w.w.). Na Shia wote tangu siku ya kwanza - wanaitakidi kutosahau kwa Nabii na wanampinga kila anayesema kuwa Nabii anasahau. Na katika maudhui haya anasema Sheikh wetu Al-Majlisiy wa kwanza, At-Taqih Al-Kabir Sheikh Muhammad Taqiy: “…….ambayo yanadhihiri kwake - kama itakavyokuja – yeye (yaani As-Suduq) anasema: Kila asiyesema kuwa Nabii anasahau basi yeye ni katika Al-Mufawidhah, kama ni hawa basi ni Shia wote isipokuwa As-Suduq na Sheikh wake, na kama sio hawa basi hatujui madhehebu yao hadi tuwanasibishie uzushi na laana.”36 34 Majmaul-Bahrain Juz. 223, madatu: Fawadha. 35 Man Laa Yahdhuruhu Al-Faqihi Juz. 1, uk. 359. 36 Raudhatul-Mutaqiyna Juz. 2 uk. 245. 44
IDDI AL-GHADIYR D.Kanju final.qxd
7/1/2011
4:32 PM
Page 45
Iddi al-Ghadiyr Tatu: Inadhihiri katika maneno ya Sheikh As-Suduqu kuhusu shahada ya tatu kwamba ilikuwepo katika adhana katika zama yake, yaani katika karne ya nne hijiria na Shia wakati huo walikuwa wako karibu na zama ya Ghaibu fupi (Ghaibatus-Sughura) na mawakala wanne waliowekwa na Imam Al-Hujjah Al-Mahdi (a.s.), hivyo kama shahada ya tatu ingekuwa ni bidaa katika adhana basi lingetoka katazo juu ya hilo kutoka kwa Imam AlMahdi (a.s.) kama ambavyo ilikuwa ni ada iliyozoeleka kutoka makatazo, ya kujiepusha na watu waovu, bidaa na batili, kama vile As-Shalmaghaniy na mfano wake. Bali inaonyesha kwamba jambo hili lilikuwa ni lenye kuafikiwa na Shia na hapakuwa na tofauti yeyote baina yao kuhusu shahada ya tatu katika adhana, hadi alipokuja Sheikh As-Suduq na akanyanyua bendera ya khilafu. Na sisi wakati tunamtazama sheikh As-Suduq kwa mtazamo wa heshima na utukufu hilo halituzuii sisi kujadili maoni yake ambayo ni mahsusi kwake kama ilivyo adabu ya maulamaa na mafaqihi wa zamani hadi wa leo.
SWALI NA JAWABU Muulizaji anaweza kuuliza na kusema: Tumekubali kupokewa habari na hadithi tukufu juu ya shahada ya tatu katika adhana lakini vipi tunaweza kuzitegemea na kusema kuwa ni sahihi? Jawabu: Sheikh At-Tuusiy ambaye ameitwa Sheikh madhehebu amezieleza habari hizo na hadithi hizo kuwa ni Shaadhu na maana ya Shaadhu hapa ni hadithi ambayo ameipokea mpokezi mkweli na ikawa inapingana na yaliyopokewa na jamhuri, na hili ni dalili kuwa hadithi hiyo ni sahihi lakini mafaqihi hawakuifanyia kazi. Hivyo Sheikh At-Tuusiy amethibitisha usahihi wa hadithi hizo tukufu. Zaidi ya hapo ni ile kanuni ya kuzifumbia macho (Tasaamuhu) hoja za Sunna, kanuni hii inakubalika baina ya maulamaa na mafiqihi wa zamani na wa leo.� Mwisho wa kunukuu.
45
IDDI AL-GHADIYR D.Kanju final.qxd
7/1/2011
4:32 PM
Page 46
Iddi al-Ghadiyr
NEMBO YA SHIA Haya maneno: Ash’hadu anna Aliyan Waliyullahi yameshakuwa ni nembo ya waislamu Mashia, wafuasi wa Ahul-bait (a.s.) wameshikamana nayo katika adhana na iqamah, na katika sehemu mbalimbali za kidini kwa kumtii Mwenyezi Mungu na Mtume Wake. Na kwa sababu hiyo wamepata upinzani na shutuma, lakini wao wamevumilia kwa ajili yake na wamekabiliana nazo na wamezidi kuwa na imani na mshikamano na nembo hii ya Mwenyezi Mungu, kwa sababu wao wanajua kuwa ni haki na hakuna baada ya haki isipokuwa upotovu, na ni juu ya kila mwislamu anayejilazimisha kushikamana na amri za Mwenyezi Mungu na Mtume Wake ashikamane na nembo hii na ailete katika adhana na penginepo. Tahadhari…tahadhari asije akaiacha, hivyo akawa katika wale aliowaambia Mtume (s.a.w.w.): “Hakika nyinyi ni wenye kugeuka nyuma baada yangu kwa visigino vyenu.” Ewe msomaji mtukufu! Tumezungumza sana kuhusu maudhui haya kwa kuangalia umuhimu wake mkubwa, na sasa tunarejea ili tuendelee na mazungumzo yetu yanayohusiana na tukio la Ghadir.
KOMBORA LA MBINGUNI Habari ya Ghadir ilisambaa katika kila pembe na yakawa ndio mazungumzo baina ya watu na waislamu wakawa wanamwita Imam Ali (a.s.) AmirulMu’minin baada ya tukio hilo. Ndipo mwanaume katika mabedui mwenye hasira, jina lake ni Nu’uman bin Harith Al-Fihriy ambaye alikuwa ni adui wa Ali (a.s.) na ni mwenye chuki na Ahlul-bait (a.s.) ikamfikia habari ya Ghadir na Nabii kumteua Ali kuwa khalifa baada yake, basi hilo halikumfurahisha na ndipo munkari wa kishetani ukampanda na akaonekana kwamba chuki inamchomachoma na shari inamsukuma kwenda kwa Nabii (s.a.w.w.) ili kupinga hatua hii tukufu. 46
IDDI AL-GHADIYR D.Kanju final.qxd
7/1/2011
4:32 PM
Page 47
Iddi al-Ghadiyr Jahili huyu hakujua kuwa hatua ya Mtume na maamuzi yake ni kutoka kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, na kana kwamba amesahau au ameghafilika kwamba Nabii (s.a.w.w.) hakubali rai ya yeyote mbele ya amri ya Mwenyezi Mungu. Nabii (s.a.w.w.) alikuwa anaswali katika hema na ndipo alipowasili huyu bedui mwasi na akasimamisha farasi wake mlangoni na akaingia kwa kiburi na chuki na akasimama mbele ya Nabii akisema: “Ewe Muhammad!” Nabii akanyanyua kichwa chake kwa huyu katili ambaye amemwita Mtume wa Mwenyezi Mungu kwa jina lake. Je, Mwenyezi Mungu hakuwakataza waislamu kumwita Nabii kwa jina lake binafsi. Je, Mwenyezi Mungu Mtukufu hakusema: “Msimwite Mtume kama baadhi wanavyowaita baadhi yao.” Na akasema: “Lakini ni Mtume wa Mwenyezi Mungu na hitimisho la Manabii.”? Nabii (s.a.w.w.) aliona kwamba ni mwanaume wa kibedui ambaye bado hajawa na adabu ya kiislamu na wala bado hajawa na utamaduni wa imani, kwa sababu hiyo Mtume (s.a.w.w.) alianza kusikiliza maneno ya huyu bedui: “Ewe Muhammad umetuamuru tushuhudie kwamba hakuna Mungu isipokuwa Mwenyezi Mungu, tukakubali. Umetuamuru kwamba tushuhudie kwamba wewe ni Mtume wa Mweneyzi Mungu tukakubali na katika nyoyo zetu kukiwa na kitu. Umetuamrisha tutoe Zaka, tufunge na tuhiji tukakubali. Hukuridhika kwa hayo hadi ukanyanyua mkono wa mtoto wa ami yako na ukamfadhilisha juu yetu, na ukasema: ‘Ambaye mimi ni kiongozi wake basi Ali ni Kiongozi wake.’ Je, hili ni jambo kutoka kwako au ni kutoka kwa Mwenyezi Mungu?” Eeh, ni uovu mbaya ulioje? Ewe mwenye ukosefu wa adabu na uchache wa haya! Je, huu ni utaratibu wa kumuuliza hitimisho la Manabii? Lakini Nabii (s.a.w.w.) alimgeukia na akaanza kumsikiliza kwa upole, tabia nzuri na mantiki ya hekima kwa kusema: “Ee! Naapa kwa ambaye hakuna Mungu isipokuwa Yeye, hakika hili ni kutoka kwa Mwenyezi Mungu.” Sasa itakuwaje? Je, kinachotakiwa si kutii na kusalimu amri? Je, si ni wajibu kuridhia na kufuata? Lakini bedui akaondoka akielekea kwenye 47
IDDI AL-GHADIYR D.Kanju final.qxd
7/1/2011
4:32 PM
Page 48
Iddi al-Ghadiyr farasi wake huku akisema: “Ewe Mwenyezi Mungu kama haya anayoyasema Muhammad ni kweli basi tuteremshie mvua ya mawe kutoka mbinguni au tuletee adhabu kali.” Hakukamilisha dua yake hadi Mwenyezi Mungu akamtupia jiwe dogo kutoka mbinguni, akamwangushia juu ya kichwa chake na likatokea nyuma, mwanaume mkaidi akaanguka juu ya ardhi hali ya kuwa ni maiti. Na hapo wahyi ukashuka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu kwa kusema:
“Muulizaji ameuliza juu ya adhabu itakayotokea. Juu ya makafiri hakuna awezaye kuizuia. Kutoka kwa Mwenyezi Mungu Mwenye utukufu wa daraja.” (Surat Al-Maa’riji: 1 - 3.) Nabii (s.a.w.w.) akawaambia sahaba zake: “Mmeona?” Wakasema ndio tumeona. Akasema: “Mmesikia?” Wakasema ndio tumesikia. Akasema: “Ni wema kwa mwenye kumtawalisha na maangamio ni kwa mwenye kumchukia, kana kwamba namwangalia Ali na wafuasi wake wamepanda katika ngamia za peponi, vijana wamevalishwa taji wamepakwa wanja hawana hofu wala huzuni, wameridhiwa na Mwenyezi Mungu, na hiyo ni kufaulu kukubwa.”37 Aya hii ilikuwa ni kombora katika uso wa wapinzani, kemeo kwa waasi, onyo kwa kila anayempiga vita Amirul-Mu’minin na kukataa tukio la Ghadir Khum, onyo kwake kwa ghadhabu ya Mwenyezi Mungu na Mtume Wake na mwisho mbaya, akhera yenye matatizo na adhabu iumizayo. Ewe msomaji mtukufu! Ama vitabu na rejea ambazo zinazotaja tukio na vinavyotaja kushuka Aya hizo juu ya hilo ni nyingi. Nakutajia baadhi yake 37 Biharul-An’war Juz. 37 uk. 167. 48
IDDI AL-GHADIYR D.Kanju final.qxd
7/1/2011
4:32 PM
Page 49
Iddi al-Ghadiyr ili ujue kwamba ukhalifa wa Imam Ali Amirul-Mu’minin ulithibiti mbinguni kabla ya ardhini na katika Qur’ani kabla ya hadithi, na kwamba Mwenyezi Mungu anamnusuru anayemnusuru Ali na anamdhalilisha anayemdhalilisha. Tafsirul-Qurtubiy, katika tafsiri ya Aya husika. Tafsiru Gharibul–Qur’ani ya Haafidhul–Harawiy katika tafsiri ya Aya husika. Tafsiru Abiy Su’ud Juz. 8, uk. 292. Tafsirus–Siraajul–Muniyr ya As-Shiriyniy Ashaafiy Juz. 2 uk. 364. Tafsirul-Manaaru, katika tafsiri ya Aya husika. Tafsiru Majmaul-Bayaan katika tafsiri ya Aya husika. Tafsirul-Mizaan ya Tabatabaiy katika tafsiri ya Aya husika. Tafsirus-Swafiy katika tafsiri ya Aya husika. Tadhkiratus-Sibtu Ibnu Jauziy Al-Hanafiy. 10.Faraidu As-Simtwain ya Sheikhul-Islam Al-Hamwainiy, mlango wa 13. 11. Al-Fusulul-Muhimah ya Ibnu As-Swibaagha Al-Maaliky uk. 26. 12. Faidhul-Qadiyr kwenye maelezo ya Jaamius-Swaghir Juz. 6, uk. 2318. 13. As-Siratul-Halabiyah Juz. 3, uk. 302 14. Maelezo ya Jaamius-Swaaghir ya Suyutwiy Juz. 2, uk. 378. 15. Nuurul-Abswar ya Shablanjiy As-Shaafiy uk. 78 Hizi ni rejea kumi na tano kati ya makumi ya rejea ambazo zimeandika kuhusu kushuka adhabu katika tukio hili, na hii inatosha kwa anayetaka kuongoka.
IDDI YA AL-GHADIR Huenda anuani hii mwanzoni itakuwa ni ngeni kwa baadhi na hatimaye wataulizana: Ni nini Iddi ya Al-Ghadir? Na nani anatambua Iddi ya AlGhadir kuwa ni Idd ya kiislamu? Lakini anuani hii inabadilika kwao kwa urahisi wakijua kwamba wa kwanza aliyeitambua siku ya Ghadir kuwa ni 49
IDDI AL-GHADIYR D.Kanju final.qxd
7/1/2011
4:32 PM
Page 50
Iddi al-Ghadiyr Iddi ya kiislamu ni Mtume wa Uislamu Muhammad (s.a.w.w.). Nabii (s.a.w.w.) alitangaza Iddi hii katika siku hiyo hiyo ya Ghadir baada ya kumteua Imam Ali ibn Abu Talib (a.s.) kuwa khalifa wake baada yake. Akasherehekea Iddi kwa kukaa katika hema lake na kuwapokea wapongezaji kwa kila furaha na moyo mkunjufu na kushirikiana nao katika furaha na shamrashamra, huku naye akiwaambia: “Nipongezeni nipongezeni kwani Mwenyezi Mungu Mtukufu amenijaalia kuwa ni mahsusi kwa Unabii na amejaalia Ahlul-baiti wangu kuwa ni mahsusi kwa Uimam.”38 Hatupati katika historia ya Nabii (s.a.w.w.) na maisha yake na furaha zake siku aliyosema humo nipongezeni.. nipongezeni…..isipokuwa siku ya Ghadir. Hata siku ya kuhama kwake Makka kwenda Madina na kunusurika kwake toka kwa washirikina hakusema nipongezeni. Na hata siku ya kuifungua Khaibar na kunusurika waislamu hakusema nipongezeni, lakini katika siku hiyo ya Ghadir alikuwa anakariri kauli yake: “Nipongezeni……nipongezeni…” Kwa nini? Kwa sababu yeye (s.a.w.w.) alikuwa anafahamu kwa kina utukufu wa siku hii na alikuwa anajua utukufu wa kumbukumbu hii na ubora wa Iddi hii. Kwa sababu hiyo Mtume (s.a.w.w.) alisema: “Siku ya Ghadir Khum ni bora zaidi kati ya Iddi za umma wangu nayo ni siku ambayo aliniamuru Mwenyezi Mungu Mtukufu kumteua ndugu yangu Ali ibn Abu Talib kuwa nembo (Bendera) ya umma wangu, wataongoka kwayo baada yangu, nayo ni siku ambayo alikamilisha humo dini, akatimiza humo neema na akawaridhia wao dini ya Uislamu.”39
38 Kitabu Sharaful-Mustafaa cha Haafidh Abiy Said Al-Khurukushiy Nisaaburiy.
An-
39 Rejea kitabu cha Al-Ghadir cha Al-Amini Juz. 1, uk. 283 na tumeshataja kwamba Aya ya kukamilisha dini imeshuka siku ya Ghadir. 50
IDDI AL-GHADIYR D.Kanju final.qxd
7/1/2011
4:32 PM
Page 51
Iddi al-Ghadiyr Na katika hadithi hii Nabii (s.a.w.w.) anaizingatia siku ya Ghadir kuwa: Kwanza ni Iddi ya kiislamu yenye kudumu miongoni mwa Iddi za kiislamu. Pili anaizingatia Iddi ya Ghadir Khum kuwa ni katika Iddi bora zaidi za kiislamu kuliko zingine.
IMAM ALI NA IDDI YA GHADIR. Baada ya Nabii Mtukufu (s.a.w.w.) akaja Imam Amirul-Mu’minin Ali (a.s.) na akaifanya siku ya Ghadir kuwa ni sikukuu ya kiislamu,40 alishahutubia (a.s.) ndani ya siku hiyo mwaka ambao Iddi ya Ghadir ilikuja pamoja na Ijumaa, na katika hotuba yake ni kauli yake (a.s.): “Hakika Mwenyezi Mungu Mtukufu amewakusanyia enyi waumini katika siku hii Iddi mbili kubwa tukufu, na wala haisimami mojawapo isipokuwa pamoja na mwenzake ili akamilishe kwenu neema zake nzuri, akuwekeni katika njia ya uongofu wake na kukuwekeni katika athari za wenye kuangaziwa kwa nuru ya uongofu wake … akajaalia Ijumaa kuwa ni mkusanyiko na akajaalia kuwa ni njia ya kutoharisha yaliyokuwa kabla yake na kusafisha ambayo kuchuma kumekutumbukizeni katika uovu, toka Ijumaa moja kwenda kweye mfano wake ….. Hivyo hakubali Tauhid isipokuwa kwa kumkubali Nabii wake (s.a.w.w.) kwa unabii wake na wala hakubali dini isipokuwa kwa uongozi wa uliyeamriwa uongozi wake, wala hazitapatikana sababu za utii wake isipokuwa kwa kushikamana na uma’sum wake na ma’sum wa Ahlul-bait na uongozi wake, hivyo akateremsha kwa Nabii Wake (s.a.w.w.) katika siku ya Dauhah41 ambayo yalibainisha matakwa Yake kwa vipenzi vyake na wateule wake, na akamwamuru kutangaza na kulipuuza kundi la watu wapotovu na wanafiki na akamhakikishia ulinzi Wake dhidi yao.” 40 Siku aliyopokea uongozi baada ya kuuliwa Uthman. 41 Nao ni mti mkubwa, siku ya Ghadir imeitwa hivyo kutokana na kuwepo miti mikubwa eneo hilo la ardhi ya Ghadir. 51
IDDI AL-GHADIYR D.Kanju final.qxd
7/1/2011
4:32 PM
Page 52
Iddi al-Ghadiyr Kisha Imam Ali (a.s.) akawaamuru kufanya sherehe ya Iddi katika siku hii akasema: “Sherehekeeni Iddi Mwenyezi Mungu awarehemu baada ya kumalizika mkusanyiko wenu kwa ajili ya kuwahudumia watoto wenu na kuwafanyia wema ndugu zenu na kumshukuru Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa yale aliyokupeni. Na kusanyikeni Mwenyezi Mungu atakusanya jambo lenu, na fanyianeni wema Mwenyezi Mungu atabariki huruma yenu, na peaneni zawadi katika neema za Mwenyezi Mungu kama alivyokuahidini thawabu kwayo kwa sikukuu nyingi za Iddi kabla na baada yake ila atatimiza mfano wake. Na kufanya wema humo kunaongeza mali na kuzidisha umri, na kuhurumiana humo kunaleta rehema na huruma ya Mwenyezi Mungu, na andaeni kwa ajili ya ndugu zenu na familia zenu miongoni mwa fadhila zake, jitahidini kwa ukarimu wenu kwa kile ambacho mnakiweza na dhihirisheni furaha baina yenu na bashasha katika kukutana kwenu.”42 Na amesema (a.s.) katika hotuba ya Iddi ya Al-Ghadir: Hakika hii ni siku tukufu humo kumetokea faraja na kunyanyuliwa daraja, na hoja zimesihi43 nayo ni siku ya uwazi na kutangaza cheo kilicho dhahiri, siku ya kukamilisha dini, siku ya ahadi iliyoahidiwa, siku ya mshuhudiaji na mwenye kushudiwa, siku ya kubainisha misingi kutokana na unafiki na upinzani, siku ya kubainisha ukweli wa imani, siku ya kufukuzwa shetani44 na siku ya burhani, hii ni siku ya upambanuzi ambayo mlikuwa mmeahidiwa, hii 42 Al-Ghadir Juz.1 uk. 284. Misbaahul-Mujtahidi cha Sheikh Tusiy uk. 524. 43 Nayo ni dalili na hoja kwa maana kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) ametilia mkazo katika siku ya Ghadir juu ya ukhalifa wa Imam AminulMuuminina (a.s.) na akahimiza zaidi kuliko wakati mwingine, hivyo hoja juu ya ukhalifa wake ikawa ni yenye nguvu zaidi. 44 Katika hadithi ni kwamba mashetani walipiga kelele kwa Ibilis kutokana na hotuba ya Nabii siku ya Ghadir kwa sababu haikuacha mwanya wa kupetuka juu uimam na uongozi, lakini Ibilisi akawapa habari ya njama ya Saqifah, ndipo wakatulia. Rejea Biharul-An’war Juz. 37 mlango unaouhusu habari za Ghadir. 52
IDDI AL-GHADIYR D.Kanju final.qxd
7/1/2011
4:32 PM
Page 53
Iddi al-Ghadiyr ni siku ya mkusanyiko mkubwa ambao nyinyi mnaupinga, hii ni siku ya uongofu na siku ya mtihani kwa waja, na siku ya hoja kwa mtetezi, hii ni siku ya kuanza kwa chuki katika nyoyo na njama za mambo, hii ni siku ya maelezo ya kisheria kwa watu mahsusi, hii ni siku ya Shaythu, hii ni siku ya Idrisi, hii ni siku ya Sham’un…….”45 Ewe msomaji mtukufu! Hakika kila sentensi katika sentensi za hadithi hii tukufu zina maana na zinaonyesha mambo na kadhia, tunaacha ufafauzi wake na tutauzungumzia mahala pengine.
MAIMAM WA AHLUL-BAIT NA IDDI YA GHADIR Na baada ya Imam Ali Amirul-Mu’minin alikuja Imam Hasan na Husein na maimam watukufu katika kizazi chake (a.s.) wakaitukuza siku ya Ghadir46 na wakaizingatia kuwa ni Iddi yao. Katika kila mwaka wanakusanyika humo na wanapongezana kwa furaha na kila bashasha na wanajikurubisha kwayo kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, kwa kufunga, kusali na kuomba dua Kwake na wanafanya mema na ihsani sana, na wanalisha chakula kwa wingi kwa ajili ya kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa yale aliyowaneemesha katika siku hiyo miongoni mwa Aya juu ya AmirulMu’minin, na walikuwa wanaunga udugu wao humo na wanawapa familia zao hidaya na wanawatembelea ndugu zao na wanawaamuru wafuasi wao kufanya hivyo.47 Na hivi sasa ewe msomaji mtukufu tunakuletea hadithi tatu: Kutoka kwa Abu Hasan Al-Laithiy kutoka kwa Imam As-Sadiq (a.s.) aliwaambia wale waliohudhuria miongoni mwa wafuasi wake: “Je, mnajua 45 Biharul-An’war Juz. 37, uk. 164. 46 Nayo ni siku ya 18 katika Dhulhaji. 47 Hizi ni dondoo kutoka katika Al-Muraja’at uk. 197. 53
IDDI AL-GHADIYR D.Kanju final.qxd
7/1/2011
4:32 PM
Page 54
Iddi al-Ghadiyr siku ambayo Mwenyezi Mungu aliupa nguvu Uislamu na akadhihirisha kwayo mnara wa dini na akaifanya kuwa ni Iddi yetu na wafuasi wetu na Shia wetu?” Wakasema: “Mwenyezi Mungu, Mtume Wake na mtoto wa Mtume Wake wanajua, je ni siku ya Iddi Al-Fitri ewe bwana wetu?” Akasema (a.s.): “Hapana.” Wakasema ni Iddi Al-Udhha? Akasema (a.s.): “Hapana, hizi ni siku mbili tukufu, na siku ya kinara cha dini ni bora kuliko hizo, nayo ni siku ya kumi na nane Dhulhaji, na Mtume wa Mwenyezi Mungu aliporejea katika Hijja ya Al-Widaa alipowasili katika bonde la Khum….” Hadi mwisho wa hadithi. Kutoka kwa Furat bin Ahnaf alimwambia Imam As-Sadiq: “Mwenyezi Mungu anijalie niwe fidia kwa ajili yako, je, waislamu wana Iddi bora kuliko Iddi Al-Fitri na Iddi Al-Udhha, Ijumaa na Arafa?” Akasema (a.s.): “Ndiyo, bora zaidi na tukufu zaidi kwa Mwenyezi Mungu kwa cheo, nayo ndiyo siku aliyoikamilisha Mwenyezi Mungu humo dini na akateremsha kwa Nabii wake Muhammad (s.a.w.w.): ‘Leo hii nimekukamilishieni dini yenu na nimewatimizeini neema zangu na nimemwadihieni uislamu kuwa ndiyo dini yenu.’” Nikamwambia ni siku gani? Akasema: “Hakika Manabii wa Bani Israili walikuwa anapotaka mmoja kati yao kuacha wasia na uongozi baada yake basi anapofanya hivyo wanaijalia siku hiyo kuwa ni Iddi, na hakika ni siku ambayo Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) alimtawaza humo Ali kwa watu kuwa kiongozi, na yakateremshwa humo yaliyoteremshwa, dini ikakamilika humo, na humo zikatimia neema kwa waumini.” Nikasema: Inatupasa tufanye nini katika siku hiyo? Akasema: “Ni siku ya ibada, kumshukuru Mwenyezi Mungu na kumhimidi, kufurahi kwa yale aliyowapa Mwenyezi Mungu miongoni mwa uongozi wetu, hakika mimi napenda kwenu mfunge siku hiyo.”48
48 Al-Ghadir Juz.1 uk. 285. 54
IDDI AL-GHADIYR D.Kanju final.qxd
7/1/2011
4:32 PM
Page 55
Iddi al-Ghadiyr Kutoka kwa Abdur-Rahmani bin Salim kutoka kwa baba yake amesema: “Nilimuuliza Abu Abdillah As-Sadiq (a.s.): Je, waislamu wana Iddi zaidi ya siku ya Ijumaa, Iddi Al-Fitri na Iddi Al-Udhha? Akasema: ‘Ndio, iliyo bora na tukufu zaidi.’ Nikasema: Ni Iddi ipi hiyo Mwenyezi Mungu anijaalie niwe fidia kwako? Akasema (a.s.): ‘Siku ambayo Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) alimtawaza humo Amirul-Mu’minin na akasema: Ambaye mimi ni kiongozi wake basi Ali ni kiongozi wake.’ Nikasema: Ni siku gani? Akasema (a.s.): ‘Siku utaifanyia nini? Hakika imeshapita lakini ni siku ya kumi na nane ya Dhul-Hija.’ Nikasema: Inatupasa tufanye nini siku hiyo?’ Akasema: ‘Mtajeni Mwenyezi Mungu humo kwa kufanya ibada, kumswalia Mtume wa Mwenyezi Mungu na ahali zake, kwani Mtume wa Mwenyezi Mungu alimuusia AmirulMu’minin kuifanya siku hiyo kuwa ni Iddi, hivyo ndivyo Manabii walivyokuwa wanafanya, walikuwa wanawausia mawasii wao na wanaifanya siku hiyo kuwa ni Iddi yao.”’49
SHIA NA IDDI YA GHADIR Kutokana na hadithi hizi tukufu ambazo zinahimiza watu kuifanya siku ya Ghadir kuwa ni Iddi ya kiislamu na zinawaelekeza watu kwenye ibada na wema, ndio maana unaona waislamu wa madhehebu ya Shia50 katika nchi zote tangu zama za Maimam watukufu hadi leo hii wanaichukulia siku ya Ghadir kuwa ni Iddi yao ya kila mwaka, wanajikurubisha kwa Mwenyezi Mungu kwa kufanya kumbukumbu ya mnasaba huu mtukufu kwa kusali, kusoma Qura’ni na dua zilizopokelewa kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kukamilisha dini na kutimiza neema kwa uongozi wa AmirulMu’minin (a.s.), wanatembeleana na hali ya kuwa na furaha na bashasha na wanajikurubisha kwa Mwenyezi Mungu kwa kufanya mema na kuwafurahisha jamaa na majirani, mmojawapo anapokutana na mwenzake katika siku hii anampa mkono na kusema: Shukurani ni kwa Mwenyezi Mungu 49 Al-Kaafiy cha Sheikh Al-Kulainy Juz. uk. 402. 50 Wao ni wafuasi wa Imam Ali mbao wanamfuata kwa sababu yeye ni haki na haki iko pamoja naye kama alivyosema Nabii (s.a.w.w.). 55
IDDI AL-GHADIYR D.Kanju final.qxd
7/1/2011
4:32 PM
Page 56
Iddi al-Ghadiyr Mtukufuu ambaye ametujaalia kushikamana katika uongozi wa AmirulMu’minina na Maimam watoharifu. Na linakusanyika kundi kubwa la Shia katika Iddi hii tukufu huko Najaf Tukufu ambapo kuna kaburi la Imam Amirul-Mu’minin (a.s.) na idadi ya wanaokusanyika katika kaburi lake kwa ajili ya ziara ni nusu milioni51 na wanakuja kutoka katika kila sehemu ili kutia mkazo katika nafsi zao, kina cha mapenzi na umadhubuti wa itikadi kwa Imam wao wa haki AmirulMu’minina (a.s.), na kusajili katika nafsi zao utukufu wa kuhudhuria katika kaburi lake tukufu. Hawasogei wala hawaondoki mpaka walizunguke kaburi tukufu na kumzuru Imam wao, kumsalimia na kumpongeza kana kwamba yuko mbele yao.52 Na wanasoma katika kumzuru kwake hotuba iliyopokewa na baadhi ya Maimam watukufu ambayo inajumuisha ushuhuda wa kutangulia kwa Amirul-Muminina katika Uislamu, misimamo yake mitukufu, kutangulia kwake kutukufu, jihadi yake kubwa, kutaabika kwake katika kuweka misingi ya dini, na kumhudumia kwake bwana wa Manabii na Mitume……… na kwa yale aliyonayo (a.s.) kati ya fadhila na sifa ambazo kwazo Nabii amemteua kuwa Khalifa siku ya Ghadir.53 Naam….. hii ni 51 Idadi hiyo ni kwa mujibu wa ripoti za hapo awali, lakini kwa hivi sasa ni zaidi ya hapo - Mhariri. 52 Kwa sababu Imam ni Imam akiwa hai au maiti, na kwa sababu Imam yu hai anaruzukiwa mbele ya Mwenyezi Mungu kwa mujibu wa kauli yake (s.w.t.): “Wala msidhani wale waliouliwa katika njia ya Mwenyezi Mungu kuwa ni wafu bali wako hai…” Na kwa mujibu wa kauli yake (s.w.t.): “Wala msiseme kwa ambao wanauliwa katika njia ya Mwenyezi Mungu kuwa ni wafu bali wako hai…” 53 Kama si ufinyu wa nafasi basi ewe msomaji ningekutajia mifano ya maneno ya ziyara hiyo ili uone humo utamu, ladha ya imani , utakaso wa moyo na vuguvugu la shauku. Ziyara hiyo imetajwa katika vitabu vya dua na ziyara hivyo rejea huko. 56
IDDI AL-GHADIYR D.Kanju final.qxd
7/1/2011
4:32 PM
Page 57
Iddi al-Ghadiyr desturi ya waislamu wa madhehebu ya Shia kila mwaka, na makhatibu wao wameendelea katika kila zama na kila mji katika kudumisha kuadhimisha, kutilia mkazo na kuzungumzia tukio la Ghadir kwa muhtasri na kwa kirefu.54 Na inadhihirika kwa mtafiti kwamba Shia sio peke yao ndio wameifanya siku ya Ghadir kuwa ni Idd ingawa wao ndio walioizingatia zaidi kuliko watu wengine, bali hata wasiokuwa wao katika waislamu walikuwa wanazingatia kuwa ni Iddi pia…. Ametaja mtafiti mkubwa Allamah Sheikh Al-Amin (r.a) katika kitabu cha Ghadir Juz. 1, uk. 267 kwamba AlAbaiyruniy ameihesabu siku ya Ghadir kuwa ni katika sikukuu walizozifanya waislamu55 na kwamba Ibnu Talha Ashaafiy ameandika katika kitabu Mataalibus-Suul uk. 53 anapozungumzia Iddi ya Ghadir kwamba: “Siku ya Ghadir Khum ameitaja (yaani Amirul-Mu’minin) katika hotuba yake. Na siku hiyo ikawa ni Iddi na sikukuu kwa sababu ni wakati aliotamka humo Nabii wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) cheo hiki kitukufu na akamtukuza humo kuliko watu wote.” Mfuasi huyo wa Shafiy ameongeza katika ukurasa wa 56 hivi: “Na kila maana inayowezekana kuthibitishwa miogoni mwa zile zinazoonyeshwa na tamko la Maula la Mtume (s.a.w.w.) basi alilijaalia kwa Ali, nacho ni cheo kikubwa, nafasi ya juu, daraja la juu, na sehemu tukufu aliyompa bila ya mwinginewe. Kwa sababu hii siku hiyo imekuwa ni siku ya Iddi na sikukuu ya furaha kwa wafuasi wake.” Amesema Sheikh wetu mtukufu Al-Amin: “Neno hili limetupa faida kwamba waislamu wote wanashirikiana katika kusherehekea siku hiyo, ni sawa dhamiri iliyopo kwenye “wafuasi wake” iwe inarejea kwa Nabii (s.a.w.w.) au wasii. Ama kwa wa kwanza iko wazi na ama kwa wa pili ni kuwa: Waislamu wanamfuata Amirul-Muminina ni sawa katika hilo kuna 54 Hizi ni dondoo kutoka katika Al-Muraja’at uk. 198. 55 Kitabu Al-Athaarul-Baaqiyatu Fil-Quruunil-Khaaliya uk. 334. 57
IDDI AL-GHADIYR D.Kanju final.qxd
7/1/2011
4:32 PM
Page 58
Iddi al-Ghadiyr wanaomfuata kwa kuzingatia kuwa ni khalifa wa Mtume bila fasili (utenganisho) au anayemuona kuwa ni khalifa wa nne katika makhalifa ……Na vitabu vya historia vinatueleza juu ya hili kwa kuafikiana na kukubaliana umma wote wa kiislamu Mashariki na Magharibi, na kwamba Wamisri, Wairaki na Wamoroko wanaizingatia kwa utukufu wake tangu karne za mwanzo, na kwao imekuwa ni siku iliyoshudiwa kwa Swala, dua, hotuba na kusoma mashairi kama ilivyoelezwa kwa ufafanuzi katika kamusi.
IDDI AL-GHADIR HUKO MBINGUNI Ewe msomaji wetu! Mazungumzo yetu yalikuwa hadi sasa juu ya Iddi ya Ghadir na sherehe zake ardhini. Ama hivi sasa imewadia duru ya swali hili: Kitu gani kinafanyika mbinguni siku ya Iddi ya Ghadir? Swali hili halijibu yeyote isipokuwa Imam ma’sum anaekubalika kwa Mwenyezi Mungu ambapo elimu yake ni katika elimu ya babu yake Al-Mustafa (s.a.w.w.) Nabii mwenye mawasilano ya mbiguni, ambaye anajua na hali yeye yuko ardhini yanayofanyika mbinguni kwa idhini ya Mwenyezi Mungu. Hivyo njoo pamoja na mimi hadi kwa Imam wa nane wa Ahlul-bait (a.s.) Imam Ali Ar-Ridhaa (a.s.) ili atueleze yanayofanyika mbinguni siku ya Iddi ya Al-Ghadir kila mwaka. Amesema (a.s.): “Hakika siku ya Ghadir katika mbingu ni mashuhuri zaidi kuliko ardhini.56 Mwenyezi Mungu ana kasri katika Firdaus yenye tofali za fedha na tofali za dhahabu, humo kuna kuba elfu mia moja nyekundu na elfu mia moja za yakuti za kijani, udongo wake ni miski na ambari, humo kuna mito minne, mto wa pombe, mto wa maji, mto wa maziwa na mto wa asali, pembezoni mwake kuna miti ya matunda ya aina zote, kuna ndege 56 Huenda sababu ni kwamba walio mbinguni wote ni waumini na kwa ajili hiyo wanasherehekea wote katika siku ya ukhalifa wa Imam Ali Amirul-Muminina. Ama watu wa ardhini humu kuna waumini na wasiokuwa waumini, na wala hawasherehekei Iddi ya Ghadir isipokuwa waumini tu. 58
IDDI AL-GHADIYR D.Kanju final.qxd
7/1/2011
4:32 PM
Page 59
Iddi al-Ghadiyr miili yao ni ya lulu na mabawa yao ni ya yakuti, wanaimba kwa kila aina ya sauti. Inapofika siku ya Ghadir wanakuja kwenye kasri hiyo walio mbinguni, wanamtukuza Mwenyezi Mungu, kumsabihi na kufanya tahalili, ndege hao huruka na kutua juu ya maji hayo wanajigaragaza katika miski na ambari hiyo. Malaika wanapokusanyika basi wanarukaruka na kuwanyunyizia marashi hayo juu yao. Na wao katika siku hiyo wanapeana zawadi ya manukato ya Fatmah, na unapowadia mwisho wa siku hunadiwa: Ondokeni nendeni kwenye sehemu zenu kwani mmeshanusurika kutokana na hatari na kuteleza hadi mwakani kwa utukufu wa siku hii ya leo kwa kumkirimu Muhammad na Ali….. hivyo wao wanapeana zawadi hadi siku ya Kiyama.”57 Ewe msomaji mtukufu! Hakika katika jumla ya ada zinazoendelea kwa watu katika sikukuu ni watu kupeana zawadi baadhi yao kwa baadhi, kwa sababu zawadi ni nembo ya upendo na alama ya urafiki. Na kwa kawaida zawadi hutofautiana kwa kutofautiana mtoa zawadi na mpewa zawadi, kuna zawadi rahisi na kuna zawadi za ghali…… Na umeshasoma katika hadithi ya Imam Ridhaa (a.s.) kwamba zawadi ya walio mbinguni katika siku ya Iddi ya Ghadir ni manukato ya Fatmah (a.s.).
Basi ni yapi manukato ya Fatmah? Jawabu: Amepokea As-Sufuriy Ashaafiy kutoka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) kwamba amesema: “Naapa kwa aliyenituma kwa utukufu na akanifanya mahsusi kwa ujumbe, hakika Mwenyezi Mungu alimuoza Fatmah kwa Ali …… kisha aliamrisha mti wa Tuba upukutishe kwao lulu mbichi pamoja na duru nyeupe, zabarjadi ya kijani pamoja na yakuti nyekundu.”58 57 Biharul-An’war Juz. 270 uk.165, vile vile ameipokea Sheikh Tusiy katika Amaal. 58Nazahatul-Majaalis Juz. 233. Na yanayofanana na hayo yamo katika kitabu Hilyatul-Awliyaai cha Abu Na’im Juz. 59, na katika Riyaadhun-Nadharah cha Muhibu Tabariy Juz. 2 uk. 184. 59
IDDI AL-GHADIYR D.Kanju final.qxd
7/1/2011
4:32 PM
Page 60
Iddi al-Ghadiyr Vile vile kutoka kwa Anas bin Malik amesema: “Nabii alipokuwa msikitini alimwambia Ali: Huyu ni Jibril amenipa habari kwamba Mwenyezi Mungu amekuozesha Fatmah na wameshuhudia katika kukuozesha kwake malaika arobaini elfu, na ameufunulia (ameupa wahyi) mti wa Tuba uwapukutishie duri, yakuti, hulu na hulali, basi ukawapukutishia na hurlaini wakaanza kuziokota kwa sahani za duri, huli na hulali, hivyo wao wanapeana zawadi kwazo hadi siku ya Kiyama.”
MASJID AL-GHADIR Tukio la Ghadir lilichukua nafasi muhimu katika historia ya kiislamu na maisha ya Mtume (s.a.w.w.) hivyo sehemu ambayo lilitokea tukio hili imekuwa ni msikiti maarufu. Waislamu huenda na kusali humo na kukumbuka siku hiyo tukufu na sehemu takatifu aliyosimama humo Mtume (s.a.w.w.) kwa kumtangaza khalifa baada yake. Imepokewa kutoka kwa Imam Jafar As-Sadiq (a.s.) kwamba amesema: “Ni Sunna kusali katika msikiti wa Ghadir kwa sababu Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) alimtawaza humo Amirul-Mu’minin, nayo ni sehemu ambayo Mwenyezi Mungu aliidhihirisha humo haki.”59 Na kutoka kwa Hasan Al-Jamaal amesema: “Nilimchukua Abu Abdillah As-Sadiq (a.s.) kutoka Madina hadi Makka, tulipowasili katika msikiti wa Ghadir alitazama kushoto mwa msikiti akasema: ‘Hiyo ni sehemu ya nyayo za Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) ambapo alisema: Ambaye mimi ni kiongozi wake basi Ali ni kiongozi wake.”’ Hadi mwisho wa hadithi.60
59 Biharul-An’war Juz. 37 uk.173. 60 Biharul-An’war Juz. 37 uk.172 na 221.
60
IDDI AL-GHADIYR D.Kanju final.qxd
7/1/2011
4:32 PM
Page 61
Iddi al-Ghadiyr Abdur-Rahmani bin Al-Hajaji alimuuliza Imam Musa bin Ja’far (a.s.) kuhusu kusali katika msikiti wa Ghadir Khum akasema (a.s.): “Sali humo kwani humo kuna fadhila na baba yangu alikuwa anaamuru juu ya hilo.”61 Amesema Sheikh mwandishi wa Al-Jawaahiri: “Vilevile ni mustahabu kwa anaerejea kupitia njia ya Madina kusali katika msikiti wa Ghadir na kuomba humo dua kwa wingi, nayo ni sehemu ambayo Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) alimteua Ali Amirul-Mu’minin.”62 Na wanatahistoria wametaja sehemu ya msikiti huu kuwa ni baina ya Ghadir na chemchemu63 lakini kwa masikitiko makubwa ni kwamba hakuna athari ya msikiti huu leo kwani jengo lake limebomoka na hakuna athari yeyote, umekuwa ni habari tu baada ya kuwepo kwake, jengo lake halikujengwa upya hadi leo, pamoja na kwamba: Ni nyumba katika nyumba ambazo Mwenyezi Mungu ameruhusu kutajwa humo jina lake na ni msikiti katika misikiti ya Mwenyezi Mungu ambayo ameamrisha kuimarishwa. Kama ambavyo umezingatiwa kuwa ni katika athari za kiislamu ambazo ni wajibu kuzihifadhi ili kudumisha historia ya kiislamu, watu wake na athari zake. Hakika hiyo ni kuhuisha kumbukumbu tukufu, kwani unalirejesha tukio hilo la kihistoria tukufu katika fikra, tukio ambalo linazingatiwa kuwa ni alama ya imani. Na huenda hii ndio sababu ya kupuuzwa kwake na kutojengwa upya jengo lake. Na hata njia inayoelekea huko na ambayo ilikuwa ni njia ya mahujaji baina ya Madina na Makka kwa karne nyingi imebadilishwa kwa kuwekwa njia nyingine, na hatimaye imesahaulika na 61 Wasailus-Shiah kitabu kinachohusu Swala, mlango unaohusu misikiti. 62 Inklopedia ya Jawahirul-Kalaam Juz. 20 uk. 75. 63 Muujamul-Buldan Juz. 2 uk. 389. 61
IDDI AL-GHADIYR D.Kanju final.qxd
7/1/2011
4:32 PM
Page 62
Iddi al-Ghadiyr athari zake zimetoweka….. Hakuna ujanja wala nguvu ila kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu.
MAELEZO KUHUSU ARDHI YA GHADIR Jarida la Turaathunaa64 lilisambaza makala mazuri kuhusu ardhi ya Ghadir Khum na mahala pake kijiografia na kihistoria ya Ustadh Dr. Sheikh Abdul–Haadiy Al-Fadhiliy ambaye alisafiri mara mbili kwenda katika sehemu hiyo tukufu. Hapa tunadondoa yafuatayo kutoka katika jarida hilo: Hakika Ghadir Khum ni sehemu ya bonde la Juhfah na iko katika mwanzo wa bonde na mwisho wa bonde la Al-Kharaar, nayo iko umbali wa kilometa nane kutoka katika kituo cha Juhfah, upande wa kushoto wa njia kwa wanaokuja kutoka Madina kwenda Makka, Kusini Mashariki mwa Rabigh kwa kilometa 26 takriban. Na bonde la Ghadir ni bonde kubwa sana, ardhi yake ni tambarare kwa sababu hiyo inaweza kuingia humo idadi kubwa ya watu tofauti na ardhi ya Al-Khazinah ambayo ina miinuko na vilima, ambapo hawawezi kukusanyika watu humo kwa upande mmoja. Hapa unafahamika uchaguzi mzuri wa Mtume (s.a.w.w.) ambapo alichagua ardhi hii pana kwa ajili ya kutoa hotuba na kuchukua kiapo cha utii toka kwa watu. Na sehemu hii kwa sasa inajulikana kwa jina la Ghurubah na watu wanaishi humo kutoka mji wa Hirbu, na mwandishi alikutana na baadhi yao huko.
64 Linalotolewa na taasisi ya Ahlul–baiti (a.s.), Qum – Iran toleo No. 25.
62
IDDI AL-GHADIYR D.Kanju final.qxd
7/1/2011
4:32 PM
Page 63
Iddi al-Ghadiyr Na humo kuna chemchem ya maji kaskazini magharibi katika sehemu hiyo, na inaonyesha ilikuwepo tangu zama za Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) na bado inaendelea kuwepo hadi leo. Kama ambavyo kuna dimbwi ambalo chemchem iliyotajwa inamwaga maji yake humo. Na kuna idadi kubwa ya miti ya Samuru, nao ni mti wenye miba na ni mti mkubwa, na kwa ajili hiyo umeashiriwa kwa jina la Dauhah, kama ilivyo katika hadithi na mashairi. Na Dauhah ni mti mkubwa uliotawanyika na wenye matawi mengi.
NAFASI YA WASHAIRI KATIKA IDDI YA AL-GHADIR. Washairi tangu karne ya kwanza hijiriya hadi karne hii wanashiriki katika sherehe hii ya kidini ya kila mwaka yenye kudumu, na wana nafasi muhimu ya kueleza kina cha mapenzi yao na ufuasi wao kwa Imam mtukufu, kupitia kaswida zilizotungwa, na beti za mashairi ambazo zinazungumzia Iddi ya Ghadir na aliyevikwa taji katika Iddi ya Ghadir, naye si mwingine bali ni Amirul-Mu’minin Ali (a.s.).65 Hata wasiokuwa waislamu kuanzia Manasara na wengineo wameshiriki kutunga kaswida na kueleza kuhusu ukweli wa mapenzi kwa shujaa wa binadamu na Uislamu Ali Amirul-Mu’minin (a.s.). Nakudondolea kidogo tu ewe msomaji kati ya mamia ya kaswida ambazo zimetungwa katika mnasaba wa Ghadir. Beti hizi ni kutoka katika kaswida ya Ustadh Paulo Salamah, mshairi wa Kinasara maarufu anasema: 65 Rejea inklopedia ya Al-Ghadir ya Sheikh Al-Amin ili uone kaswida zilizotungwa katika mnasaba huu wa kidini wenye kudumu. 63
IDDI AL-GHADIYR D.Kanju final.qxd
7/1/2011
4:32 PM
Page 64
Iddi al-Ghadiyr “Usiseme Shia wanampenda Ali, hakika kila mwadilifu ana wafuasi, yeye ni fahari ya kihistoria na wala sio fahari ya watu wanaemtambua na kumfanya kuwa kiongozi. Utajo wake linapotanda giza la usiku unaangaza kama mapambazuko ya asubuhi. Ewe Ali wa zama, haya ni maneno yangu, nimesikiliza humo wahyi wa Imam waziwazi. Ewe Amiri wa ubainifu, hii ni ahadi yangu, namshukuru Mungu kwamba nimeumbwa na mtimiza ahadi. Ewe Amiri wa Uislamu yanitosha kuwa fahari, kwamba mimi kwako ni mfuasi mdogo. Ilidhihiri haki kwa Nasara mpaka akahesabika kwa wingi wa mapenzi yake kuwa ni mfuasi wa Ali. Mimi ni kati ya wanaopenda ushujaa na wahyi, uadilifu na tabia nzuri, hata kama Ali hakuwa Nabii, lakini tabia yake ilikuwa ya Kinabii. Ewe mbingu shuhudia na ardhi pia kubali na nyenyekea hakika mimi nimemtaja Ali.” Na anapohamia katika kumbukumbu ya Iddi ya Al-Ghadir yenye kudumu anasema: “Alirejea kutoka Hijjatul-Wida’a tukufu, na kundi la mahujaji kama vile mawimbi ya bahari. Waliwasili wenye kurejea kwenye bonde la Khum kana kwamba msafara upo katika tanuri. Waliwasili humo hali ya kuwa wamechoka, hali wanaswaga ngamia wao ili watembee haraka. Ndipo Nabii alipoona jambo zito nalo kwake ni mtihani mgumu. Alikuja Jibril hali akisema: ‘Ewe Nabii wa Mwenyezi Mungu fikisha maneno ya Mola muokozi, eleza wewe uko katika ulinzi kutokana na watu, tangaza habari za mbinguni kwa watu, tangaza ujumbe wa Mwenyezi Mungu wahyi wenye kudumu na hoja ya milele.’” Mlinganiaji akawaita watu ili waje wasikilize. Watu wakarejea kwa kuitika wito, wakamzunguka kama duara la mwezi ukiangazia ardhi kwa miale yake yenye nuru. Wote wanasubiri tangazo na hakuna shaka katika jambo, kwani kauli ni muhimu mno. Nabii hakuwaita kwa jambo jepesi na ardhi ya bonde inawaka kwa joto. Nabii akapanda mimbari ya Haudaji, akiyavutia masikio kusikiliza maneno muhimu: ‘Enyi watu hakika Mwenyezi Mungu ni kiongozi wenu na ni kiongozi wangu, mwenye kuninusuru na mwokozi wangu, kisha mimi ni kiongozi wenu hadi mwisho wa dahari. Ewe Mola Wangu ambaye mimi ni kiongozi wake kweli, basi hatopinga 64
IDDI AL-GHADIYR D.Kanju final.qxd
7/1/2011
4:32 PM
Page 65
Iddi al-Ghadiyr kuwa Ali ni kiongozi wake. Ewe Mola Wangu wapende wanaompenda mtoto wa ami yangu, na mnusuru khalifa wangu mwenye kuninusuru, kuwa adui kwa mwenye kumfanyia uadui na mdhalilishe kila mpinzani na mdhalilishe muovu.’ Alisema hayo hali akishika mkono wa Ali, na kunyanyua mkono wa Haidar shujaa. Zikaonekana nywele za kwapa wakati wa kushikana mikono katika sehemu mashuhuri, kana kwamba Nabii ananyanyua bendera ya utukufu wa Iddi ya kiongozi mwenye kunusuriwa na kiongozi wa zama. ‘Fadhila za Ali ziko wazi kwa wenye kuona kweli anafaa kuwa msaidizi. Haidar mume wa Fatmah na baba wa wajukuu wawili na shujaa wa siku ya kukata shingo (vita), mtoto wa Mtume wa kulea na mtoto wa mlezi wake aliyejitolea katika kumpunguzia ufakiri, faqihi mkubwa na mwenye kupatia rai katika viumbe vya Mwenyezi Mungu na kwa mwenye kutaka msaada wa uongofu. Nitakutana nanyi katika birika, ambapo Ali atawatangulia mapema, nitawauliza waumini vipi mlihifadhi Qur’ani katika jambo la msaidizi wangu. Msipotee, shikamaneni na Kitabu cha Mwenyezi Mungu na kizazi changu na Amiri.’ Alitamka Nabii kwa Ali maneno yaliyo wazi kama mchana bila ya sitara, majazi, kufunika wala mkanganyo ambao fahamu inaweza kufasiri, wapongezaji wengi wakamwendea, kaumu ikadhihirisha alama ya heshima, wakamjia sahaba wawili mapema wakasema haraka kwa kueleza: ‘Pongezi umekuwa kiongozi wa waumini kwa baraka unafaa kuwa Imam.’ Wakampongeza wake wa Nabii hali ya kuwa wanasoma kaswida wakiongoza kundi kubwa: ‘Iddi yako ni Iddi ewe Ali, hata kama atanyamaza hasidi au mwenye kuzuia mbaramwezi.’ Mwenyezi Mungu akateremsha Aya baada ya hapo, siku ya kukamilika dini yake tukufu, siku ya furaha ilikuwa ni siku ya joto kali, na machweo matukufu yalikuwa ni ya siku ya Ghadir”66 66 Diwani ya ‘Iydil-Ghadir cha mshairi Paulo Salamah uk.106. 65
IDDI AL-GHADIYR D.Kanju final.qxd
7/1/2011
4:32 PM
Page 66
Iddi al-Ghadiyr
ORODHA YA VITABU VILIVYO CHAPISHWA NA AL-ITRAH FOUNDATION: 1. 2. 3. 4. 5. 6. 7. 8. 9. 10. 11. 12. 13. 14. 15. 16. 17. 18. 19. 20. 21. 22. 23. 24. 25. 26. 27. 28.
Qur'an Al-Kariim - Tafsir Al-Kashif Juzuu ya kwanza mpaka Thalathini Uharamisho wa Riba Uharamisho wa uwongo Juzuu ya Kwanza Uharamisho wa uwongo Juzuu ya Pili Hekaya za Bahlul Muhanga wa Imamu Husein (A.S.) Mikingamo iliyomzunguka Imamu Ali (A.S.) Hijab vazi Bora Ukweli wa Shia Ithnaashari Madhambi Makuu Mbingu imenikirimu Abdallah Ibn Saba Khadijatul Kubra Utumwa Umakini katika Swala Misingi ya Maarifa Kanuni za Ndoa na maadili ya Familia Bilal wa Afrika Abudharr Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu Salman Farsi Ammar Yasir Qur'an na Hadithi Elimu ya Nafsi Yajue Madhehebu ya Shia Ukusanyaji na Uhifadhi wa Qur'an Tukufu Al-Wahda Ponyo kutoka katika Qur'an. 66
IDDI AL-GHADIYR D.Kanju final.qxd
7/1/2011
4:32 PM
Page 67
Iddi al-Ghadiyr 29. 30. 31. 32. 33. 34. 35. 36. 37. 38. 39 40. 41. 42. 43. 44. 45. 46. 47. 48. 49. 50. 51. 52. 53. 54. 55. 56. 57. 58. 59. 60.
Uislamu mfumo kamili wa maisha ya kijamii Mashukio ya Akhera Al Amali Dua Indal Ahlul Bayt Udhuu kwa mujibu wa Kitabu na Sunna. Haki za wanawake katika Uislamu Mwenyeezi Mungu na sifa zake Amateka Na Aba'Khalifa Nafasi za Ahlul Bayt (a.s) Adhana. Upendo katika Ukristo na Uislamu Nyuma yaho naje kuyoboka Amavu n’amavuko by’ubushiya Kupaka juu ya khofu Kukusanya swala mbili Bismillah ni sehemu ya Qur’ani na husomwa kwa Jahara Kuwaongoza vijana wa kizazi kipya Kusujudu juu ya udongo Kusheherekea Maulidi Ya Mtume (s) Tarawehe Malumbano baina ya Sunni na Shia Kupunguza Swala safarini Kufungua safarini Umaasumu wa Manabii Qur’an inatoa changamoto as-Salaatu Khayrun Mina -'n Nawm Uadilifu wa Masahaba Dua e Kumayl Sauti Ya Uadilifu wa Binadamu Umaasumu wa Mitume - Faida Zake Na Lengo Lake Umaasumu wa Mitume - Majibu Ya Aya Zenye Utata Umaasumu wa Mitume - Umaasumu wa Mitume Muhammad (s) 67
IDDI AL-GHADIYR D.Kanju final.qxd
7/1/2011
4:32 PM
Page 68
Iddi al-Ghadiyr 61. 62. 63. 64. 65. 66. 67. 68. 69. 70. 71. 72. 73. 74. 75. 76. 77. 78. 79. 80. 81. 82. 83. 84. 85. 86. 87. 88. 89. 90. 91. 92.
Nahju’l-Balaghah - Juzuu ya Kwanza Nahju’l-Balaghah - Juzuu ya Pili Kuzuru Makaburi Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Kwanza Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Pili Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Tatu Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Nne Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Tano Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Sita Tujifunze Misingi Ya Dini Sala ni Nguzo ya Dini Mikesha Ya Peshawar Malezi Ya Mtoto Katika Uislamu Ubora wa Imam 'Ali Juu ya Maswahaba Na Ushia ndio njia iliyonyooka Hukumu za Kifikihi zinazowahusu Wanawake Liqaa-u-llaah Muhammad (s) Mtume wa Allah Amani na Jihadi Katika Uislamu Uislamu Ulienea Vipi? Uadilifu, Amani na Mtume Muhammad (s) Mitala na Ndoa za Mtume Muhammad (s) Urejeo (al-Raja’a ) Mazingira Utokezo (al - Badau) Sadaka yenye kuendelea Msahafu wa Imam Ali Uislamu na dhana Mtoto mwema Adabu za Sokoni Johari za hekima kwa vijana Maalimul Madrasatain Sehemu ya Kwanza Maalimul Madrasatain Sehemu ya Pili 68
IDDI AL-GHADIYR D.Kanju final.qxd
7/1/2011
4:32 PM
Page 69
Iddi al-Ghadiyr 93. 94. 95. 96. 97. 98. 99. 100. 101. 102 103. 104. 105. 106. 107. 108. 109. 110. 111. 112. 113. 114. 115. 116. 117. 118. 119. 120. 121. 122. 123. 124. 125.
Maalimul Madrasatain Sehemu ya Tatu Tawasali Imam Mahdi katika Usunni na Ushia Maana ya laana na kutukana katika Qur’ani Tukufu Hukumu ya kujenga juu ya makaburi Swala ya maiti na kumlilia maiti Shiya na Hadithi (kinyarwanda) Mariamu, Yesu na Ukristo kwa mtazamo wa Kiislamu Hadithi ya Thaqalain Fatima al-Zahra Tabaruku Sunan an-Nabii Historia na sera ya viongozi wema (Sehemu ya Kwanza) Historia na sera ya viongozi wema (Sehemu ya Pili) Mahdi katika sunna Kusalia Nabii (s.a.w) Ujumbe -Sehemu ya Kwanza Ujumbe - Sehemu ya Pili Ujumbe - Sehemu ya Tatu Ujumbe - Sehemu ya Nne Ngano ya kwamba Qur’ani imebadilishwa Iduwa ya Kumayili Maarifa ya Kiislamu. Ukweli uliopotea sehemu ya Kwanza Ukweli uliopotea sehemu ya Pili Ukweli uliopotea sehemu ya Tatu Ukweli uliopotea sehmu ya Nne Ukweli uliopotea sehmu ya Tano Johari zenye hekima kwa vijana Safari ya kuifuata Nuru Idil Ghadiri Myahudi wa Kimataifa Kuanzia ndoa hadi kuwa Wazazi 69
IDDI AL-GHADIYR D.Kanju final.qxd
7/1/2011
4:32 PM
Page 70
Iddi al-Ghadiyr 126. 127. 128. 129. 130. 131. 132. 133. 134. 135. 136. 137. 138. 139. 140.
141. 142. 143. 144. 145. 146. 147. 148. 149. 150. 151. 152. 153. 154.
Visa vya kweli sehemu ya Kwanza Visa vya kweli sehemu ya Pili Muhadhara wa Maulamaa Mwanadamu na Mustakabali wake Imam Ali binamu ya Mtume Sehemu ya Kwanza Imam Ali binamu ya Mtume Sehemu ya Pili Khairul Bariyyah Uislamu na mafunzo ya kimalezi Vijana ni Hazina ya Uislamu. Yafaayo kijamii Kusoma sura zenye Sijda ya wajibu Taqiyya Vikao vya furaha Shia asema haya Sunni asema haya Wewe wasemaje? Uislamu na Mazingatio Sehemu ya Kwanza Uislamu na Mazingatio Sehemu ya Pili Azadari-Kuhuzunika na Kuomboleza Sunna katika Kitabu Fiqhi al-Sunnah Mtazamo Mpya - Wanawake katika Uislamu Kuonekana kwa Allah Tabia njema kwa Mujibu wa Ahlul-Bayt (Sehemu ya Kwanza) Tabia njema kwa Mujibu wa Ahlul-Bayt (Sehemu ya Pili) Ndugu na Jirani Ushia ndani ya Usunni Maswali na Majibu Elimu ya Ghaibu ya Maimamu Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No.1 Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No.2 Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No.3
70
IDDI AL-GHADIYR D.Kanju final.qxd
7/1/2011
4:32 PM
Page 71
Iddi al-Ghadiyr
BACK COVER Idi ya Ghadiri (Sikukuu ya Ghadir) imetokana na tukio kubwa la kihistoria. Tukio hili lilitokea katika jangwa la Ghadir Khumm katika njia ya msafara baina ya Makka na Madina wakati Mtukufu Mtume alipokuwa akirudi kutoka Makka ambako alikwenda kutekeleza ibada ya Hija. Hija hii ni maarufu sana na hujulikana kama Hijjatu ’l-Widaa’ (Hija ya Mwago). Ghadir ni tukio maarufu sana katika ulimwengu wa Kiislamu. Hakuna madhehebu ya Kiislamu hata moja ambayo haikutaja tukio hili, ingawa kuna tofauti kidogo ya mapokezi kati ya wasimulizi wake. Pamoja na hayo, ukweli unabakia palepale kwamba haitakamilika historia ya Uislamu bila ya kulitaja tukio hili. Qur’ani inatuthibitishia kwamba Uislamu ulikamilika baada ya tukio hili la Ghadir: “...Leo nimekukamilishieni dini yenu, na kuwatimizieni neema Yangu, na nimewapendeleeni Uislamu uwe dini yenu...” (5:3) Aya hii iliteremshwa kwa Mtume Muhammad (saw) pale Ghadir Khumm baada ya kumtangaza Imam Ali (as) kama Khalifa wake, kiongozi wa waumini wote na mrithi wake. Baada ya hapo Waislamu waliifanya siku hii kuwa Idi (Sikukuu) kama utakavyoona maelezo yake katika kitabu hiki. Kimetolewa na kuchapishwa na: Alitrah Foundation S.L.P. 19701 Dar es Salaam, Tanzania Simu: +255 22 2110640 Simu/Nukushi: +255 22 2127555 Barua Pepe: alitrah@raha.com Tovuti: www.alitrah.org Katika mtandao: www.alitrah.info
71
IDDI AL-GHADIYR D.Kanju final.qxd
7/1/2011
4:32 PM
Iddi al-Ghadiyr
72
Page 72