Imam Ali (a.s) ndugu yake Mtume Muhammad (s.a.w.w) - Juzuu ya Kwanza

Page 1

Imam Ali binamu yake Mtume (s.a.w.w)Lubumba

Dr.Kanju.qxd

7/1/2011

4:34 PM

IMAM ALI (A.S.) NDUGU YAKE MTUME MUHAMMAD (S.A.W.)

Usahihishaji Upya wa Historia na Utafiti wa Kina wa Madhehebu ya Shia

JUZUU YA KWANZA

Kimeandikwa na: Sheikh Muhammad Jawad Chirri

Page A


Imam Ali binamu yake Mtume (s.a.w.w)Lubumba

Dr.Kanju.qxd

7/1/2011

ŠHaki ya kunakili imehifadhiwa na: AL-ITRAH FOUNDATION ISBN: 978 - 9987 - 512 - 56 - 0

Kimeandikwa na: Sheikh Muhammad Jawad Chirri

Kimetarjumiwa na: Salman Shou Kimepangwa katika Kompyuta na: Hajat Pili Rajab

Toleo la kwanza: Oktoba,2011 Nakala: 1000 Kimetolewa na kuchapishwa na: Alitrah Foundation S.L.P. 19701 Dar es Salaam, Tanzania Simu: +255 22 2110640 Simu/Nukushi: +255 22 2127555 Barua Pepe: alitrah@raha.com Tovuti: www.ibn-tv-com Katika mtandao: w.w.w.alitrah.info

4:34 PM

Page B


Imam Ali binamu yake Mtume (s.a.w.w)Lubumba

Dr.Kanju.qxd

7/1/2011

4:34 PM

Yaliyomo Utangulizi....................................................................................................2 SURA YA KWANZA Imam wakati wa kipindi cha Utume ...........................................................7 Nyumba ya mtukufu Mtume (s.a.w.w)........................................................7 . Kumbukumbu kuthibitisha ubora wao.......................................................11 SURA YA PILI Watu wa nyumba ya Muhammad..............................................................20 SURA YA TATU Watu muhimu na walazima.......................................................................29 Ukoo wa Al-Aus na Al-Khazraj................................................................32 Abu Talib ..................................................................................................32 Uislamu wa Abu Talib...............................................................................34 Sote tunawiwa naye...................................................................................39 SURA YA NNE Waislamu wa kwanza................................................................................48 SURA YA TANO Ndugu na Waziri........................................................................................54 Hadith zinazopingana................................................................................58

Page C


Imam Ali binamu yake Mtume (s.a.w.w)Lubumba

Dr.Kanju.qxd

7/1/2011

4:34 PM

Imam Ali (a.s.) Ndugu yake Mtume Muhammad (s.a.w.) Zawadi iliyotolewa....................................................................................61 Kwa nini zawadi kubwa hivyo kwa ajili ya Ujumbe................................63 Mtukufu Mtume (s.a.w.w) hakutaka kuwepo na visingizio......................65 Matokeo ya mkutano wa nyumba ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w).............66

SURA YA SITA Mkombozi............................................................................................... 68 Ukubwa wa kazi yenyewe.........................................................................72 Umuhimu wa kuwasilisha amana kwa wenyewe......................................73 Thamani isiyopungua................................................................................74

SURA YA SABA Nafasi ya Ali katika kujenga dola ya Kiislamu................................77 Ushindani wa hoja dhidi kukosa hoja..............................................79 Ubora kushindana na wingi............................................................80 Shujaa wa kipekee...........................................................................81

SURA YA NANE Vita vya Badr...................................................................................83

SURA YA TISA Vita vya Uhud..................................................................................86

SURA YA KUMI Vita vya Handaki.......................................................................................97

D

Page D


Imam Ali binamu yake Mtume (s.a.w.w)Lubumba

Dr.Kanju.qxd

7/1/2011

4:34 PM

Imam Ali (a.s.) Ndugu yake Mtume Muhammad (s.a.w.) SURA YA KUMI NA MOJA Vita vya Khaybar...........................................................................106 Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alizingira Khaybar............................109 SURA YA KUMI NA MBILI Udugu watangazwa........................................................................119 SURA YA KUMI NA TATU Nafasi ya Ali kutoka kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) ndani ya Qur’ani .........................................................................................127 SURA YA KUMI NA NNE Maula wa Waislamu.......................................................................134 SURA YA KUMI NA TANO Wasia wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w) usiotimizwa........................141

E

Page E


Imam Ali binamu yake Mtume (s.a.w.w)Lubumba

Dr.Kanju.qxd

7/1/2011

4:34 PM

NENO LA MCHAPISHAJI Kitabu kilichoko mikononi mwako ni tarjuma ya kitabu cha Kiingereza kiitwacho, The Brother of the Prophet. Sisi tumekiita, Imam Ali (as) Ndugu wa Mtume Muhammad (saw). Kitabu hiki kilitungwa na aliyekuwa muballighi mashuhuri wa dini ya Kiislamu ya Ushia nchini Marekani, Marehemu Sheikh Muhammad Jawad Chirri. Kitabu hiki ni wasifu wa mtu mkubwa ambaye alikuwa mwanamume wa kwanza kuamini Utume wa Muhammad (saw) na wa kwanza kusali nyuma yake. Imam Ali (as) hakuwa kiongozi wa Waislamu tu bali wa wanadamu wote. Maisha na mwenendo wa Imam Ali (as) umewavutia watu wote, marafiki na maadui, hali ambayo imemfanya kuwa kiongozi wa umma. Mtukufu Mtume (saw) alimtangaza mwanzoni kabisa mwa Ujumbe wake katika kile kikao mashuhuri kabisa cha “karamu ya jamaa”, aliposema: “Huyu ni ndugu yangu, wasii wangu, waziri wangu, khalifa wangu na mrithi wangu. Basi msikilizeni na mumtii.” Hili lilikuwa tangazo la mwanzo kabisa alilolitoa Mtukufu Mtume (saw) kwa ajili ya Imam Ali (as) na aliendelea kuwakumbusha Waislamu kuhusu uongozi wa Imam Ali baada yake katika matukio mengi yaliyofuata baadaye, kama vile katika tukio la Ghadir Khum pale aliposema: “Man kuntu mauwahu fahadha Aliyyun mawlahu – Yule ambaye mimi kwake ni kiongozi basi na huyu Ali ni kiogozi wake.” Na mwisho ni tukio la “Karatasi” pale Mtukufu Mtume (saw) alipokuwa ni mgonjwa na maradhi yamemzidi akaomba aletewe karatasi, kalamu na wino, mashuhuri kama “Hadithi ya karatasi.” F

Page F


Imam Ali binamu yake Mtume (s.a.w.w)Lubumba

Dr.Kanju.qxd

7/1/2011

4:34 PM

Tumekiona kitabu hiki ni chenye manufaa sana, hususan wakati huu wa maendeleo makubwa ya elimu katika nyanja zote, ambapo uwongo, ngano za kale na upotoshaji wa historia ni mambo ambayo hayana nafasi tena katika akili za watu. Kutokana na ukweli huo, Taasisi yetu ya Al-Itrah Foundation imeamua kukichapisha kitabu hiki kwa lugha ya Kiswahili kwa madhumuni yake yaleyale ya kuwahudumia Waislamu, hususan wazungumzaji wa Kiswahili. Tunamshukuru ndugu yetu, Maalim Dhikir U. Kiondo (ambaye sasa ni marehemu - Allah amrehemu) kwa kukubali jukumu hili la kukitarjumi kitabu hiki. Vilevile tunawashukuru wale wote walioshiriki kwa njia moja au nyingine hadi kufanikisha kuchapishwa kwake. Ni matumaini yetu kwamba kitabu hiki kitakuwa ni mwanga kwa wasomaji wetu na kuzidisha upeo wao wa elimu ya dini na ya kijamii. Mchapishaji: Al-Itrah Foundation S. L. P. 19701 Dar-es-Salaam. :

G

Page G


Imam Ali binamu yake Mtume (s.a.w.w)Lubumba

Dr.Kanju.qxd

7/1/2011

4:34 PM

BIBLIOGRAFIA UBAINIFU Tarehe zilizotajwa kwenye bibliografia hii zimetegemea Kalenda ya Kiislamu ambayo ilianza kwa tukio la Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kuondoka Makka na kwenda Madina. Tukio hilo la kuondoka huitwa ‘Hijiriya’ ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), ambalo lilitokea mwaka wa 622 Baada ya kuzaliwa Isa (a.s.). Endapo msomaji anataka kubadilisha tarehe kutoka tarehe za Kiislamu na kuwa kalenda ya Gregory – ya Nchi za Kimagharibi, lazima azingatie tofauti ya miaka 622 kabla ya Hijiriya. Zaidi ya hayo, mwaka wa mwandamo wa mwezi ambao Kalenda ya Kiislamu ndio msingi wake, unazo siku 354 tu. Hivyo mwaka huu ni pungufu kwa siku 11 kuliko mwaka wa jua. Kila miaka mia moja ya jua inakuwa miaka 103 ya miaka inayohesabiwa kwa kuandama kwa mwezi. Miaka elfu moja ya jua ni sawa na miaka 1030 inayohesabiwa kwa mwandamo wa mwezi.

QUR’ANI TUKUFU AMIINI (Sheikh Hussein Ahmad Al-Amiin) Al-Ghadiir (Tangazo lililosimuliwa la Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kuhusu Imam Ali hapo Ghadiir Khum), chapa ya pili ilifanywa na Al-Haidari Printing Tehran, 1372 Hijiriya. Al-Amiin ni mwandishi wa historia maarufu wa zama za leo. ASKARI (Sayyid Murtadha Al-Askari) Abdallah ibn Saba, chapa ya pili ilifanywa na Matabi-a Al-Kitab Al-Arabi mjini Cairo, 1381 A.H. Al-Askari ni mwandishi wa historia na theolojia wa zama za leo.

H

Page H


Imam Ali binamu yake Mtume (s.a.w.w)Lubumba

Dr.Kanju.qxd

7/1/2011

4:34 PM

ATHIIR (Ali Ibn Muhammad Al-Shaibani, ajulikanaye kama Ibn al-Athiir) Al-Kamil (kilicho kamilika), kitabu maarufu cha historia ya Uislamu, kilichochapishwa na Al-Azhari Printings 1301 Hijiriya. Pia kimepigwa chapa na Dar-Al-Kitab Al-Lubnani (The Lebanese House of Books), 1973 Baada ya kuzaliwa Isa. Nukuu zilizomo humu nyingi zinatoka kwenye chapa ya pili. Ibn Al-Athiir alikufa mwaka wa 750 Hijiriya. BALADHURI. (AL-Baladhuri). Ansabul-Ashraf (Nasaba za Masharifu). Kitabu maarufu cha historia ya Uislamu, kimechapishwa Jerusalem. Al-Baladhuri, ni mwandishi mashuhuri wa historia, alikufa mwaka wa 279 Hijiriya. BIRR (Yusuf Ibn Abdul-Birr) Al-Istii’ab Fi Maarifat al-Ass’hab (Elimu linganishi kuhusu Masahaba wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Kitabu maarufu cha historia ya Kiislamu, kimechapishwa na Al-Fajjala Printing, Cairo, mwaka wa 1970 AD. Ibn Abdul-Birr ni mwandishi wa historia maarufu, alikufa mwaka wa 463 Hijiriya. BUKHARI (Muhammad Ibn Isma’il, al-Bukhari). Sahih al-Bukhari (Sahih ya Al-Bukhari), mojawapo ya vitabu sita vilivyo Sahihi vyenye Hadith zilizoandikwa (Hadith ni tamko lililosimuliwa au tendo au uthibitisho wa kimya wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) Muhamamd s.a.w.w) Kitabu kilichapishwa na Muhammad Ali Subh huko Al-Azhar, Cairo, Al-Bukhari ni mchaguzi na mwandishi wa Hadith mashuhuri, alikufa mwaka wa 256 Hijiriya. DAWUD (Suleiman Ibn Al-Ash’ath Ibn Shaddad anayejulikana kama AbuDawood) Sunan Abu Dawood (Hadith za Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) zilizoandika). Mojawapo ya vitabu sita vya hadith zilizoandikwa, kilichochapishwa na Mustafa Al-Babi al-Halabi – Misri, mwaka 1952 AD. Abu Dawood ni I

Page I


Imam Ali binamu yake Mtume (s.a.w.w)Lubumba

Dr.Kanju.qxd

7/1/2011

4:34 PM

mkusanyaji na mwandishi wa Hadith mashuhuri alikufa mwaka 275 Hijiriya. FAIRUZABADI (Sayyid Murtadha Al-Fairuzabadi). Fadha-il Al-Khamsah Min As-Sihah Al-Sitta (Fadhila za watu watano, zilizoandikwa kwenye vitabu Sahihi Sita), chapa ya tatu ilifanywa na AlAlami Institute of Printing, Beiruti, mwaka 1973 AD, Al-Fairuzabadi ni mkusanyaji wa Hadith, mwanatheolojia na mwandishi wa Hadith wa zama za leo. HADIID (Izzud-Din, ajulikanaye kama Ibn Abil-Hadiid). Sharh Nahjul–Balaghah (Maelezo kuhusu Njia ya Ufasaha wa maneno yaliyokusanywa ya Imam Ali), kitabu kinachosomwa kwa wingi sana. Kimechapishwa na Dar Al-Kutub Al-Arabiyah Al-Kubrah (Nyumba Kubwa ya Vitabu vya Kiarabu), ya Mustafa Al-Babi, Cairo, Ibn AbilHadiid ni mwanatheolojia na mwandishi wa historia maarufu, alikufa mwaka 655 Hijiriya. HAIKAL (Dk. Muhammad Husein Haikal) Hayat Muhammad (Maisha ya Muhammad), Chapa ya tatu iliyofanywa na Dar Al-Kutub Al-Misriah (The Egyptian House of Books) Cairo, mwaka 1358 Hijiriya. Dr. Haikal ni mwandishi wa historia wa zama za leo. HAKIIM (Sayyid Muhammad Taqi Al-Hakim) Al-Madkhal Ila Darasat Al-Fiqh Al-Muqaran (Utangulizi kuelekea kwenye masomo ya Fiqhi linganishi) kilichapishwa na Dar Al-Andalus, Beirut. 1963 AD. Hakiim ni mwanatheolojia wa zama za leo. AL-HAKIM. (Muhammad Ibn Abdullah Al-Nissaburi, ajulikanaye kama Al-Hakim). J

Page J


Imam Ali binamu yake Mtume (s.a.w.w)Lubumba

Dr.Kanju.qxd

7/1/2011

4:34 PM

Al-Mustadrak Alas-Sahihain (Hadithi ambazo sahihi za Al-Bukhari na Muslaim imziacha). Hadith zilizomo kwenye kitabu hiki zinachukuliwa kuwa za kweli na wanachuoni Waislamu, isipokuwa zikataliwe na AlDhahabi, ambaye maoni yake yamechapwa pembezoni mwa kitabu cha AlMustadrak, kilichochapishwa na Al-Nasr Printing, Riyadh Saudia Arabia, mwaka 1335 Hijiriya. Al-Hakim ni mwanachuo, mwandishi wa Hadith na mkusanyaji wa Hadith maarufu, alikufa mwaka 405 Hijiriya. HALABI (Ali Ibn Burhanud-Diin Al-Halabi) Al-Siirah Al-Halabiyah (Wasifu wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) ulioandikwa na Al-Halabi), kilichochapishwa na Al-Maktaba Al-Kubra ya Mustafa Muhammad, Cairo, Al-Halabi ni mwandishi wa historia maarufu, alikufa mwaka 1044 Hijiriya. HANBAL (Ahmad Ibn Hanbal) Musnad Ahmad, kilichochapishwa na as-Sader Printing, Beiruti, mwaka 1969AD. Ibn Hanbal ni mmojawapo wa maimam wa matapo ya Kiislamu, alikufa mwaka 241 Hijiriya. HISHAMU (Abdul Malik Ibn Hisham) Al-Siirah Al-Nabawiyah (Wasifu wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), kilichochapishwa na Mustafa Al-Babi Al-Halabi, Misri, mwaka 1955 AD. Ibn Hisham ni mwandishi maarufu wa historia ya Kiislamu, alikufa mwaka 281 Hijiriya. HUSEIN (Dk. Taha Husein) Al-Fitnat Al-Kubra (Mgogoro wa Fitna Kubwa katika dini), Kilichapishwa na Dar Al-Maarif, Misri mwaka 1953 AD. Taha Husein ni mwanachuo na mwandishi wa historia wa zama hizi. JALALAIN (Jalalud-Din Muhammad Al-Halabi na Julalud-Din AsSuyuuti)

K

Page K


Imam Ali binamu yake Mtume (s.a.w.w)Lubumba

Dr.Kanju.qxd

7/1/2011

4:34 PM

Tafsiirul-Jalalain (Tafsiri za Jalal mbili kuhusu Qur’ani Tukufu) KHALID (Muhammad Khalid) Fi Rihab Ali (kwenye nyumba ya wageni ya Ali), Khalid ni mwandishi na mwanahistoria wa Misri wa zama za leo. MAJAH (Muhammad Ibn Majah) Sunnan Ibn Majah (Hadith zilizokusanywa na Ibn Majah). Mojawapo ya vitabu sita vilivyo sahih vya Hadith kilichochapishwa na Dar Ihya AlKutub Al-Arabiyah (Nyumba ya Uhuishaji wa Vitabu vya Kiarabu) ya Isa Al-Babi, Cairo, 1952 AD. Ibn Majah ni mkusanyaji na mwandishi wa Hadith maarufu, alikufa mwaka 275 Hijiriya. MAQSOUD (Abdul Fattah Abdul-Maqsoud) Al-Imam Ali Ibn Abi Talib (kitabu cha historia ya Imam Ali), kimechapishwa na Al-Irfan Printing, Beiruti, Abdul-Maqsoud ni mwandishi na mwanahistoria wa Misri wa zama za leo. MUGHNIYAH (Sheikh Muhammad Jawad Mughniyah). Hadhi Hiya Al-Wahhabiyah (Huu ndio Uwahabbi), Sheikh Mughniyah ni mwanatheolojia maarufu wa zama za leo. MUHSIN (Sayyed Muhsin Al-Amiin) Aayan Al-Shi’ah, kitabu chenye maelezo mengi kilichopangwa kwa alfabeti. Sayyid Muhsin ni mwanatheolojia na mwandishi wa historia maarufu wa zama za leo. MUSLIM (Ibn Al-Hajjaj Al-Qusheiri) Sahih Muslim (Ukweli na usahihi wa Muslim). Ni kimojawapo cha Vitabu sahihi sita vya Hadith kilichochapishwa na Muhammad Ali Subh Printing, Misri, mwaka 1349 Hijiriyya. Muslim ni mkusanyaji na mwandishi wa Hadith maarufu sana, alikufa mwaka 365 Hijiriya.

L

Page L


Imam Ali binamu yake Mtume (s.a.w.w)Lubumba

Dr.Kanju.qxd

7/1/2011

4:34 PM

MUTTAQI (Ali Ibn Hussamul-Diin Al-Hindi Al-Muttaqi) Kanzul-Ummal (Hazina ya waja wa Mwenyezi Mungu), mkusanyiko mkubwa wa hadith. Hadith zilizomo kwenye kitabu hiki zimewekwa katika mfululizo. MUTTAQI (Ali Ibn Hussamul-Diin Al-Hindi Al-Muttaqi) Muntakhab Kanzul-Ummal (hadith zilizoteuliwa kutoka kwenye KanzulUmmal) zilizochapishwa pembezoni mwa Musnad Ibn Hanbal, na asSader Printing, Beiruti. Al-Muttaqi ni mkusanyaji na mwandishi maarufu wa hadith ambaye aliishi mnamo Karne ya Kumi na Moja, Hijiriya. NISABUURI (Ali-Hasan Ibn Ahmad Al-Nisabuuri) Gharaibul - Qur’ani (fasili juu ya Qur’ani Tukufu) zimechapishwa pembezoni mwa Jami-ul-Bayan ya Al-Tabari (fasili zingine na Al-Tabari) na Al-Matba-ah Al-Meimaneyah, Misri, 1321 Hijiriya. Al-Nasabuuri ni mfasili wa Qur’ani tukufu, alikufa wakati wa karne ya nane Hijiriya. NISA’I (Ahmad Ibn Shu’aib Al-Nisa’i) Sunnan Al-Nisa’i (Hadith zilizokusanywa na Al-Nisai), kutoka kwenye Vitabu Sita Sahihi vya hadith vilivyopigwa chapa na Al-Matba-ah AlMeimaneyah, Misri, 1321 Hijiriya. Al-Nisa-i ni mteuzi na mkusanyaji wa hadith maarufu, alikufa 303 Hijiriya. RAYYAH (Mahmood Abu Rayyah) Adhwa-a Ala Al-Sunnah Al-Muhamadiyah (miale juu ya hadith za Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) zilizosimuliwa) chapa ya tatu imefanywa na Dar AlMaarif (Nyumba ya Maarifa), Misri, 1957 AD. Abu Rayyah ni mwandishi maarufu wa zama za leo. RAZZI (Fakhrud-Diin Muhammad Ar-Razzi) At-Tafsiir Al-Kabiir (Tafsiri pana za Qur’ani Tukufu) chapa ya pili imefanywa na Al-Matba-ah Al-Sarafiyah, mwaka 1304 Hijiriya. Ar-Razzi ni mwanatheolojia na mfasili wa Qur’ani Tukufu maarufu sana, alikufa M

Page M


Imam Ali binamu yake Mtume (s.a.w.w)Lubumba

Dr.Kanju.qxd

7/1/2011

4:34 PM

mwaka 606 Hijiriya. SAAD (Muhammad Ibn Saad Al-Zuhri, ajulikanaye kama Ibn Saad) Al-Tabaqat Al-Kubra (kitabu maarufu cha historia ya masahaba wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na wanafunzi wao), kilichapishwa na Dar asSader, Beiruti mwaka 1960 AD. Ibn Saad ni mtaalamu wa Historia ya Kiislamu maarufu, alizaliwa mwaka wa 168 Hijiriya. SHALTUTE (Sheikh Mahmood Shaltute) Tafsiir Al-Qur’ani (Tafsiri za Qur’ani Tukufu), kimechapishwa na Dar-AlQalam Printing, mwaka 1960 AD. Sheikh Shaltute ni Sheikh maarufu miongoni mwa masheikh wa Al-Azhar). SHARAFUD-DIIN (Sayyid Abdul Husein Sharafud-Diin). Al-Muraj’at (Majadiliano) kilichapishwa na Al-Irfan, Saida, Lebanon, mwaka 1936 AD. Sayyid Sharafud-Din ni mwanatheolojia na mwandishi wa historia maarufu wa zama za leo. SHABLANJI (Mumin Ibn Hussam Al-Shablanji) Nurul-Absar (Nuru ya Macho), chapa ya nane ilifanywa na Atif, mwaka 1973. AD, Misri. Al-Shablanji ni mkusanyaji maarufu wa Hadith, alizaliwa mwaka 1251 Hijiriya. TABARI (Muhammad Ibn Jariir Al-Tabari) History of Messengers and Kings (Historia ya Mitume na Wafalme). AlTabari ni mwandishi wa historia, mwanatheolojia na mfasili wa Qur’ani Tukufu maarufu, alikufa 310 Hijiriya. Nukuu zote katika Jz. 2, ambazo zilichukuliwa kutoka kwenye historia ya Tabari, zilichukuliwa kutoka Jz. 4, chapa ya 4, na Jz. 5, chapa ya 2, iliyochapishwa na Dar Al-Ma’arif ya Misri. TABARI (Muhammad Ibn Jariir Al-Tabari) Jami-ul-Bayan (Ubainifu Mkubwa), Tafsiri ya Qur’ani Tukufu, N

Page N


Imam Ali binamu yake Mtume (s.a.w.w)Lubumba

Dr.Kanju.qxd

7/1/2011

4:34 PM

kilichapishwa na Maimaneyah Printing, Misri, mwaka 1321 Hijiriya. TABARSI (Ahmad Ibn Ali Ibn Abi Talib At-Tabarsi) Al-Ihtijaji (mazungumzo) kilichapishwa na Al-Naaman Printing, Al-Najaf, Iraq, 1966 AD. At-Tabarsi ni mwanatheolojia maarufu aliyeishi katika karne ya sita Hijiriya. TIRMIDHI (Muhammad Ibn Isa At-Tirmidhi) Sunan At-Tirmidhi mojawapo ya vitabu Sita Sahih vya Hadith. Sehemu ya tano ilichapishwa na Al-Fajjalah Printing, Cairo, 1967AD. At-Tirmidh ni mteuzi na mwandishi wa hadith maarufu, alikufa 279 Hijiriya. WAQIDI (Muhammad Al-Waqidi) Al-Maghazi (uvamizi), kilichapishwa na Oxford Printing. Al-Waqid ni mtaalam wa historia Mwislamu maarufu, alikufa mwaka 207 Hijiriya. ZUHRAH (Sheikh Muhammad Abu Zuhrah) Al-Imam As-Sadiq, kilichapishwa na Dar Al-Fikr Ak-Arabi (Nyumba ya Fikra za Kiarabu zilizoandikwa) Misri. Sheikh Abu Zuhrah ni mwanatheolojia na mwandishi wa historia wa zama za leo.

O

Page O


Imam Ali binamu yake Mtume (s.a.w.w)Lubumba

Dr.Kanju.qxd

7/1/2011

4:34 PM

UTANGULIZI Imam Ali Foundation ilianzishwa kama chama cha kutoa msaada chenye lengo na madhumuni ya kueneza mafundisho ya Uislamu asilia kama ulivyo hubiriwa mwanzo na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na kama ulivyofafanuliwa na Ahlul-Bait watukufu, watu wa nyumba ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na uzao wake. Kitabu hiki ‘Ndugu wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.)’ ni mojawapo ya vitabu vizuri vilivyoandikwa na marehemu Muhammad Jawad Chirri. Alifafanua historia ya maisha ya Imam Ali (a.s) na akachanganua masuala mbali mbali muhimu ya maisha yake, ama wakati wa uhai wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) au baada ya kifo chake. Imam Ali (a.s) Foundation ilikiona kitabu hiki kuwa na mvuto na manufaa kwa wasomaji wa Kiingereza hususan ambapo inafahamika kwamba vitabu vichache sana vimeandikwa kuhusu Imam Ali (a.s) kwa lugha ya Kiingereza. Tumepata ari ya kukichapisha tena kitabu hiki kama faida ya Waislamu kwa ujumla na pia wasio Waislamu ambao wanataka kujifunza historia ya maisha ya mtu wa pili kwa umashuhuri kwenye Uislamu baada ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Toleo la kwanza la kitabu hiki lilikuwa na juzuu mbili zilizo tenganishwa. Ili kurahisisha zaidi namna ya kushika na kusoma, tulipendelea kukichapisha katika juzuu moja. Imam Ali (a.s) Foundation inakaribisha maoni yako kuhusu yale yaliyomo kwenye kitabu hiki. Kama unataka maelezo zaidi, tafadhali tuandikie. Imam Ali (a.s) Foundation. 18th Dhulhija, 1418/16th April, 1998. P

Page P


Imam Ali binamu yake Mtume (s.a.w.w)Lubumba

Dr.Kanju.qxd

7/1/2011

4:35 PM

KUHUSU MWANDISHI. Imam Muhammad Jawad Chirri ni mzalendo wa Lebanon na ni mhitimu (Graduate) wa taasisi ya kidini iliyo maarufu ya Najaf nchini Iraq. Yeye ni mwanatheolojia ya Kiislamu, mhadhiri mwandishi na mwanahistoria. Ni mwendeshaji wa kipindi cha redio cha kila wiki kiitwacho ‘Islam in Focus’ kinachotangazwa na WNIC. Katika vitabu vyake vilivyo chapishwa ni: Muslim Practice. Islamic Teaching Imam Husein, Leader of the Marteyrs. Inquiries About Islam (Maelfu ya maktaba za Marekani wamekitwaa kitabu hiki - Kitabu hiki pia kimetafsiriwa katika lugha ya Kiswahili na Taasisi ya Al-Itrah Foundation, kwa jina la “Maswali kuhusu Uislamu”). ‘Al-Khilafatu Fi Al-Dustous Al –Islam’ (The Calphate in the Islam constitution- Arabic). Amiir Al-Muminiin (The leader of Belivers –Arabic). Imam Chirri alialikwa na Detroit Muslim Community awe kiongozi wao wa kiroho. Alisaidia sana katika ujenzi wa Islamic Center of Detroit, mojawapo ya taasisi kubwa sana za Kiislamu - America ya kaskazini. Sasa hivi yeye ndiye Mkurugenzi wa Taasisi hii. Kazi ya Imam Chirri ilipanuliwa hadi Afrika ya Magharibi. Alipokuwa katika msafara wa kuhadhiri mnamo mwaka 1958, aliweza kuishawishi jamii ya Kilebanoni iliyoko Sierra Leone kujenga hospitali ya watoto kama zawadi kwa wazalendo wa nchi hiyo. Wakati alipotembelea Mashariki ya kati mwaka wa 1959, mwandishi huyu alilishughulikia tatizo la Kiislamu la siku nyingi na kufaulu kupata ufumbuzi wake. Kwa kipindi cha miaka elfu moja, Waislamu walikuwa wamegawanyika katika makundi mawili; Sunni na Shi’ah (wala hakuna hata upande moja baina ya hizo pande mbili uliotambua uthabiti wa Q

Page Q


Imam Ali binamu yake Mtume (s.a.w.w)Lubumba

Dr.Kanju.qxd

7/1/2011

4:35 PM

mafundisho ya kundi lingine licha ya makubaliano ya matapo yote mawili kuhusu mafundisho yote ya Qur’ani Tukufu na hadithi za Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) zilizosimuliwa kwa usahhihi. Mwandishi huyu alikutana na marehemu Sheikh mkuu wa Al-Azhar, Sheikh Mahood Shaltut mnamo tarehe 1, Julai, 1959. Alizungumza naye kuhusu suala hilo muhimu. Katika hitimisho la mazungumzo Sheikh Shaltut alikubali uthabiti wa Tapo la Kiislamu la Shia Jaafariya. Mwandishi huyu alimwomba Sheikh kutangaza usawa baina ya tapo la Shia Jaafariya na Sunni. Tangazo (fatwa) hilo lilirushwa hewani na kuchapishwa Julai 7, 1959. Tamko hili lilikuwa la kihistoria na la kwanza la namna yake tangu matapo hayo yalipotengana. Moyo wa udugu wa kweli wa Kiislamu unaweza kuwepo tu kwa uelewano wa pande zote miongoni mwa matapo mbali mbali ya Kiislamu. Ni kwa mtazamo huu kwamba Mwandishi anawasilisha kitabu hiki, ‘Ndugu yake Mtukufu Mtume (s.a.w.w.).’ Bila kuwa na haja ya kusema kwamba mabishano miongoni mwa matapo mbali mbali ya Kiislamu yanazunguka hasa zaidi kwenye historia ya Imam huyu mashuhuri. Ufahamu wa kweli na wa hakika wa nafasi yake katika Uislamu utawafanya Waislamu waelekee kwenye undugu wa kweli zaidi.

R

Page R


Imam Ali binamu yake Mtume (s.a.w.w)Lubumba

Dr.Kanju.qxd

7/1/2011

4:35 PM

Page 1


Imam Ali binamu yake Mtume (s.a.w.w)Lubumba

Dr.Kanju.qxd

7/1/2011

4:35 PM

Imam Ali (a.s.) Ndugu yake Mtume (s.a.w.w.)

UTANGULIZI. Wamarekani ambao wanatambua Uislamu na Waislamu kwa wastani ni wachache, na wale wanaojua wingi wa matapo ya Kiislamu na kwamba miongoni mwa Waislamu wapo Sunni na Shia ni wachache zaidi. Hata hivyo, matukio ya mapinduzi ya Iran yaliyotokea mwaka wa 1978-79, yaliweka habari za Waislamu kwa ujumla na hususan Waislamu wa madhehebu ya Shia kwenye kurasa za mwanzo za magazeti ya Magharibi na Mashariki. Hii ni kwa sababu Waislamu wa madhehebu ya Shia ni wengi zaidi miongoni wa Waislamu nchini Iran. Magazeti ya Marekani yalizungumzia habari kuhusu Shia kwa ufupi, na mara nyingi zilikuwa potofu. Hali hii iliimarisha zaidi msimamo wangu wa kuwepo haja ya kitabu cha Kiingereza kitakachoshughulikia tapo la Kiislamu la Shia chenye maelezo ya kina yaliyotegemezwa kwenye utafiti makini. Kwa vile hii ni madhehebu ya Imam Ali, mtoto wa Abu Talib, ingefaa kumchunguza huyu Imam mashuhuri na historia yake ya kisiasa na kidini. Kwani hii tu ndio njia pekee ambayo tunaweza kuelewa msingi wa madhehebu hii. Kutosheleza haja hii, niliandika kitabu na kukiita ‘Ndugu yake Mtukufu Mtume (s.a.w.w.).’ Hii ni lakabu aliyopewa Imam Ali ya kiupekee na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), ambaye alimfanya kuwa ndugu yake kutoka miongoni mwa Waislamu wote. Kamwe hakujichagulia mtu mwingine yeyote kama ‘ndugu yake.’ Lakabu hii ilikuwa ya thamani mno ndani ya moyo wa Imam; kwani kila alipojitambulisha hadharani alikuwa na desturi ya kutaja udugu wake kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) baada ya kutamka utumwa wake kwa Mwenyezi Mungu Muweza wa Yote. Na ilikuwa ni jambo la kupendeza kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kumuita Ali ‘Ndugu yangu.” 2

Page 2


Imam Ali binamu yake Mtume (s.a.w.w)Lubumba

Dr.Kanju.qxd

7/1/2011

4:35 PM

Imam Ali (a.s.) Ndugu yake Mtume Muhammad (s.a.w.) Waislamu wanakubaliana kwamba Imam Ali alikuwa na sifa bainifu ambazo hapana mtu mwingine alikuwa nazo miongoni mwa Waislamu. Yeye kutoka miongoni mwao ndiye tu mtu aliyelelewa na Mjumbe wa Mwenyezi Mungu tangu siku za utoto wake. Alilelewa naye kufuatana na kiwango cha maadili yake; halafu akamteua yeye kutoka miongoni mwa watu wote kuwa ‘ndugu yake.’ Wanachuoni wa Kiislamu, Sunni na Shia wanakubaliana kwamba Ali alikuwa na ujuzi mkubwa sana wa Kitabu cha Mwenyezi Mungu (Qur’ani) na mafundisho ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) miongoni mwa masahaba wote. Ali alikuwa hazina kubwa ya chanzo cha hekima na fasaha mno katika kuongea, mlinzi mkubwa zaidi wa Imani, imara zaidi katika kudumisha haki na mwenye kufanya juhudi kubwa katika njia ya Mwenyezi Mungu. Sifa hizi ni kigezo cha sifa bainifu za Kiislamu, kwani Qur’ani Tukufu imetangaza kwamba Mwenyezi Mungu hupendezwa na wale wanaojitahidi katika njia Yake kuliko wadumaavu; kwamba wale wajuao na wasiojua hawako sawa, na hutamka kwamba ubora zaidi miongoni mwa watu mbele ya Mwenyezi Mungu ni wale wamchao Mwenyezi Mungu zaidi. Hii huweka wazi kabisa kwamba Sunni na Shia si tu wanakubaliana kwenye kanuni zote za Kiislamu ambazo zimetajwa kwenye Qur’ani Tukufu au kwenye Hadith sahihi za Mtukufu Mtume (s.a.w.w) lakini pia wanakubaliana kuhusu nafasi ya Imam Ali kidini na kielimu katika Uislamu. Kwa hiyo Sunni na Shia wanapotofautiana hufanya hivyo kisiasa tu; kwani hutofautiana kwenye vipengele vya siasass na si nafasi ya Imam Ali kidini na kielimu katika Uislamu. Wakati wanakubaliana kwamba Ali alikuwa Khalifa mwadilifu ambaye alipata mamlaka kwa kuchaguliwa na watu, hawakubali kwa nyongeza ya hili iwapo alikuwa ni Khalifa kwa kuteuliwa na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Wale wasioamini kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alimteua Ali kama mrithi wake wanadhani kwamba nadharia ya uteuzi wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) wa Imam Ali ni nadharia ya utawala wa kurithiana kupi3

Page 3


Imam Ali binamu yake Mtume (s.a.w.w)Lubumba

Dr.Kanju.qxd

7/1/2011

4:35 PM

Imam Ali (a.s.) Ndugu yake Mtume Muhammad (s.a.w.) tia undugu wa damu. Wale wanaoamini kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alimteua Imam kama mrithi wake wanasema kwamba nadharia ya Imam Ali kuteuliwa na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) ni kinyume na nadharia ya utawala wa kurithiana. Waislamu pia hawakubaliani juu ya wajibu wake wa kisiasa/kidini katika historia ya Uislamu kama mwanasiasa mweledi. Ambapo wanakubaliana juu ya mshikamano wake kwenye kanuni ya haki kamili na uimara wake katika kutekeleza sheria za Kiislamu kwa moyo wote na kwa makini, na baadae wakawa hawakubaliani kwenye busara ya msimamo kama huo usiopindika. Kuna jambo lingine muhimu linalohusu nafasi yake ya kisiasa/kidini kwenye historia ya Kiislamu, yaani; nafasi yake katika kuanzisha dola ya Kiislamu. Kipengele hiki hakikutajwa wazi wazi wala hakikuwa suala la mjadala wenye uzito miongoni mwa wanahistoria na wanachuoni wa historia. Kwa vile Waislamu wanakubaliana kuhusu nafasi ya Imam kama mwanachuo mahiri wa dini, itakuwa ni kuzidisha kiasi mambo yasiyohitajika kujadili vipengele hivyo vya maisha ya Imam. Kwa hiyo, kitabu hiki hakipitii upya historia ya Imam kwa kinaganaga, wala hakizungumzii kuhusu ujuzi wake, ufasaha wake wa kujieleza au hekima yake. Wala hakizungumzii ucha-Mungu wake na msimamo wake kutopenda mambo ya dunia, wala hakizungumzii utendaji wake usio kawaida. Mazungumzo yake yamelenga juu ya nafasi ya Imam ya kisiasa/kidini katika Uislamu, uhusiano wake wa kiroho na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), na mchango wake katika kuasisi dola ya Kiislamu na kueneza Imani ya Uislamu.

4

Page 4


Imam Ali binamu yake Mtume (s.a.w.w)Lubumba

Dr.Kanju.qxd

7/1/2011

4:35 PM

Imam Ali (a.s.) Ndugu yake Mtume Muhammad (s.a.w.) Kitabu hiki kinamzungumzia yeye kama Khalifa na kama mwanasiasa mweledi. Pia kinazungumzia kile kilichosemwa kuhusu sera yake na uweledi wake kisiasa na sababu zilizosababisha mlundikano wa matatizo mengi ambayo yalimzuia kufika kwenye utawala wa amani na wa kudumu zaidi wakati wa siku za ukhalifa wake. Hatimaye, kitabu hiki kinazungumzia ukhalifa kama mfumo wa kidini na siasa, na aina ya ukhalifa ambao unaafikiana na jinsi ulivyo ujumbe wa Kiislamu. Kwa hiyo, kitabu hiki kina sehemu zifuatazo: Imam wakati wa zama za Utume. Imam wakati wa zama za Makhalifa watatu. Imam wakati wa utawala wake mwenyewe. Ukhalifa katika sharia ya Kiislamu, na hitimisho la mjadala. Nimejitahidi kugundua uhusiano baina ya matukio ya kihistoria ambayo yalihusisha maisha ya Imam na ambayo yalitokea wakati wa miaka hamsini na tatu tangu kuanza kwa utume hadi mwisho wa ukhalifa wa haki. Msomaji anaweza kuona kwamba matukio hayo yaliungana moja na lingine kwa mafungamano imara. Hivyo, yaliunda mlolongo wa sababu na athari, zilizofuatia miongoni mwa hizo ilikuwa ni matokeo ya mfano wake. Katika kusimulia matukio ya kipindi kile, sikutegemea tu vyanzo kutoka kwenye vitabu vinavyoheshimiwa vya historia, lakini nilijaribu kuongeza kwenye vyanzo hivyo, pale ilipowezekana, kile nilichopata kutoka kwenye vitabu vya Sahihi na vitabu vingine vya kutegemewa vya Hadith ambavyo vilikuwa na matukio hayo. Hii ni kwa sababu wasomi wengi wa Kiislamu hutegemea zaidi kwenye Hadith kuliko vitabu vya historia, hususan pale ambapo Hadith huandikwa kwenye vyanzo sahihi vinavyojulikana, na vitabu vingine vinavyotegemewa.

5

Page 5


Imam Ali binamu yake Mtume (s.a.w.w)Lubumba

Dr.Kanju.qxd

7/1/2011

4:35 PM

Imam Ali (a.s.) Ndugu yake Mtume Muhammad (s.a.w.) Sikujaribu kumzungumzia Imam kama mtu ambaye uhusiano wake maalum na Mola wake ulimtofautisha yeye na ukamwezesha kufanya miujiza na kuleta matukio yasiyo ya kawaida. Bali nilijaribu kumzungumza yeye kama mtu ambaye yupo chini ya kanuni za maumbile, muda na mahali, ambaye alijaribu kwa kadiri ya uwezo wake kuhifadhi kanuni takatifu na akaishi kwa kuzizingatia kanuni hizo na kwa ajili ya kanuni hizo. Ninayo matumanini kwamba kitabu hiki kitachangia kwenye uelewano mzuri na udugu madhubuti miongoni mwa Waislamu. Kwa hakika shaksia ya Imam na historia yake Binafsi ni vitu vinavyotia moyo, na kama Waislamu wapo tayari kupokea msukumo huo, utawaelekeza kwenye umoja na mshikamano. Kile ambacho kitaandikwa cha kweli kuhusu shaksia ya mtu ambaye aliteuliwa na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kuwa ndugu yake hakika kitakuwa na uwezo wa kuimarisha moyo wa udugu na upendo miongoni mwa Waislamu wote. Muhammad Jawad Chirri

6

Page 6


Imam Ali binamu yake Mtume (s.a.w.w)Lubumba

Dr.Kanju.qxd

7/1/2011

4:35 PM

Imam Ali (a.s.) Ndugu yake Mtume Muhammad (s.a.w.)

SURA YA KWANZA. IMAM WAKATI WA KIPINDI CHA UTUME. NYUMBA YA MTUKUFU MTUME (S.A.W.W.). Waislamu wote huwatukuza watu wa Nyumba ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) ambao huitwa Aali Muhammad au Ahlul Bait Muhammad. Msimamo huu ni utekelezaji wa makubaliano kufuatana na maelekezo ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) ambaye aliamuru Waislamu kuwaombea watu wa Nyumba yake wakati wowote wanaposwali na kumswalia yeye. Kwa kuwaamuru hivyo, kwa kweli aliwataka Waislamu kutenga sehemu kwa ajili yao karibu naye. Qur’ani Tukufu iliagiza kumswalia Muhammad na kumwombea rehema: “Hakika Mwenyezi Mungu na Malaika wake wanamtakia rehma na amani Nabii! Enyi mlioamini, mtakieni rehma na amani kwa wingi.1 Masahaba wengi walimuomba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) awafundishe wao jinsi ya kutekeleza amri hii. Wasimulizi wengi wenye kuheshimika sana (pamoja na Al-Bukhari na Muslim) waliandika kwenye vitabu vyao vijulikanavyo kama ‘Sahih’ kwamba Ka’ab Ibn Ujrah alieleza kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisema “Semeni: Mwenyezi Mungu mpe utukufu Muhammad na watu wa Nyumba ya Muhammad, kama Ulivyowapa utukufu watu wa Nyumba ya Ibrahim, Wewe ni Mwenye kusifiwa na Mtukufu. Mwenyezi Mungu, Mrehemu Muhammad na watu wa Nyumba ya Muhammad kama ulivyowarehemu watu wa Nyumba ya Ibrahim, kwa hakika Wewe ni Mwenye Kusifiwa na Mtukufu.”2 1 Qur’ani Tukufu (Sura 33:56). 2 Miongoni mwa Wahadith hawa ni: Al-Bukhari, ‘Sahih Al-Bukhari’ Sehemu ya 6, uk. 101 kwenye kitabu cha fasili ya Qur’ani Tukufu. Muslim, Sahih Muslim, sehemu ya 4, (Kwenye kumswalia Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) baada ya kutangazwa kwa Uislamu). uk. 136. Muhammad Ibn Majah, Sunan Ibn Majah, Juz. 1, hadith na. 904. Al-Tirmidhi, hadith na. 483, sehemu na. I, Hadith zingine zimeandikwa na Abu –Saeed, Abu Masood, Talhah na ibn Masood. Wote wanakubaliana na hadith hiyo juu ya Kaab Ibn Ujrah. 7

Page 7


Imam Ali binamu yake Mtume (s.a.w.w)Lubumba

Dr.Kanju.qxd

7/1/2011

4:35 PM

Imam Ali (a.s.) Ndugu yake Mtume Muhammad (s.a.w.) Alipokuwa anawaelekeza wafuasi wake kuhusu jambo fulani la kidini, Mjumbe wa Mwenyezi Mungu hakuwa akisema kwa matamanio yake ya kiBinadamu. Qur’ani inathibitisha kwamba alikuwa akisema tu yale yaliyofunuliwa kwake:

“Wala hatamki kwa matamanio. Hayakuwa haya ila ni ufunuo uliofunuliwa;” Sura ya 53, aya ya 3 -4.

JE! UTUKUFU HUU NI KWA SABABU YA UNDUGU? Inawezekana kuonekana kwamba kujumuisha watu wa Nyumba ya Muhammad katika kumswalia yeye wakati wa Swala ni kwa sababu ya uhusiano wao na undugu wa damu. Kama ni hivyo, haitakuwa ni kulingana na mtazamo wa mafundisho ya Kiislamu. Kuwapa wao hadhi ya kipekee namna hiyo kwa sababu ya uhusiano wao wa kindugu na Muhammad ni kutetea ubora wa kifamilia na inapingana na kanuni zifuatazo: Mbele ya Mwenyezi Mungu watu wote wapo sawa, kwani Qur’ani Tukufu ilitangaza:

“Hakika aliye mtukufu ziadi kati yenu kwa Mwenyezi Mungu ni huyo aliye mchaMwenyezi Mungu zaidi katika nyinyi.” Qur’ani tukufu, Sura ya 49:13. Mwenyezi Mungu hamuadhibu au kumpa thawabu mja wake kwa dhambi au matendo mema ya wazazi wake au ndugu zake wa karibu au wa mbali. 8

Page 8


Imam Ali binamu yake Mtume (s.a.w.w)Lubumba

Dr.Kanju.qxd

7/1/2011

4:35 PM

Imam Ali (a.s.) Ndugu yake Mtume Muhammad (s.a.w.) Kutoka kwenye Qur’ani Tukufu:

“Na iogopeni siku ambayo mzazi hatamfaa mwana, wala mwana hatamfaa mzazi lolote. Qur’ani, Sura 31:33. Mwenyezi Mungu hamuadhibu au kumpa thawabu mwanadamu kwa kilicho nje ya uwezo wake na bila hiyari yake. Kuwa na uhusiano au kutokuwa na uhusiano wa damu na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) si jambo la hiyari ya mtu Ibnasfi. Hakuna hata mmoja wetu aliyefanya uchaguzi kabla ya kuzaliwa kwetu kuwa na uhusiano au kutokuwa na uhusiano wa kindugu na familia maalum, utaifa au jamii. Kwa hivyo, ingekuwa vigumu sana kwa Waislamu kuamini kwamba wawajumuishe ndugu zake Muhammad katika swala kwa sababu tu wao ni ndugu zake. Ni kwa Sababu ya Ubora Wao Si kwa Sababu ya Kurithiana Kwao. Kuondoa mgongano huu ulio wazi, ni muhimu kujua kwamba neno ‘Aali Muhammad,’ ambalo linarudiwa mara kwa mara kwenye Swala za kila siku, halijumuishi ndugu zake wote. Ni idadi ndogo tu miongoni mwa ndugu zake ambao wamejumuishwa. Kama wote wengejumuishwa, ingekuwa ubaguzi wa kiukoo au kikabila kwa sababu wengi wao hawakufuata njia ya Muhammad, na kuwaweka juu ya wengine ni kutetea ubora wa kiukoo. Kuwa ndugu wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) hakumaanishi kukubaliwa na Mwenyezi Mungu. Wala hakuwapatii nafasi ndugu zake Peponi au kuwahakikishia kwamba hawataadhibiwa na Mwenyezi Mungu. Kwa mujibu wa mafundisho ya Kislamu, Mwenyezi Mungu ameumba Pepo kwa ajili ya yeyote atakayemtii Yeye, na mahali pa adhabu kwa ajili ya yeyote ambaye hatamtii Yeye, bila kujali uhusiano wa kifamilia, utaifa au jamii. Hata Qur’ani inayo sura ambayo inamsema vibaya Abu Lahab, ambaye alikuwa ami yake Mtukufu Mtume (s.a.w.w.).

9

Page 9


Imam Ali binamu yake Mtume (s.a.w.w)Lubumba

Dr.Kanju.qxd

7/1/2011

4:35 PM

Imam Ali (a.s.) Ndugu yake Mtume Muhammad (s.a.w.)

“Imeangamia mikono ya Abu Lahab na yeye pia ameangamia. Hayatamfaa mali yake wala alivyovichuma…”Qur’ani Tukufu, Sura 111:2-3. Ukweli ni kwamba neno Aali Muhammad maana yake ni ‘walioteuliwa’ tu miongoni mwa ndugu wa Muhammad. Hawa watu walioteuliwa hawakuteuliwa au kutukuzwa kwa sababu ya uhusiano wao wa kindugu na Muhammad, bali wameteuliwa kwa sababu ya uadilifu wao. Waliishi maisha halisi ya Kiislamu, walifuata maelekezo ya Qur’ani Tukufu na ya Mjumbe, na kamwe hawakuachana na vitu hivyo kwa maneno au vitendo. Mwenyezi Mungu anapotufahamisha sisi kwenye Kitabu Chake kwamba mbora zaidi miongoni mwa viumbe Vyake Binadamu ni wale waadilifu sana, na Mjumbe Wake anatuamuru sisi kuwatukuza watu wa nyumba yake wakati tunapomtukuza yeye, tunamaanisha kwamba wao ndio waadilifu zaidi baada ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Kama hawangekuwa hivyo, hawangestahiki utukufu kama huo wa pekee, na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) hangetuelekeza sisi kuwatukuza wao wakati wowote tunapolitukuza jina lake. Kufanya vinginevyo haingelingana na Qur’ani Tukufu. Hivyo, kwa kutuamuru sisi kuwaswalia wao wakati wowote tunapomswalia yeye, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kwa kweli alikuwa anatufahamisha sisi kuhusu ubora wao wa hali ya juu, kwamba wao ni watiifu sana kwa Mwenyezi Mungu na Mjumbe Wake.

10

Page 10


Imam Ali binamu yake Mtume (s.a.w.w)Lubumba

Dr.Kanju.qxd

7/1/2011

4:35 PM

Imam Ali (a.s.) Ndugu yake Mtume Muhammad (s.a.w.)

KUMBUKUMBU HUTHIBITISHA UBORA WAO. Waislamu wote wanakubaliana kwamba Ali, Binamu yake Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) ambaye Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) ‘alimteua kuwa ndugu’ na mkewe Fatimah (mama wa nuru), mtoto kipenzi cha Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, na watoto wao wawili, Al-Hasan na Al-Husein, wanatokana na watu walioteuliwa wa Nyumba ya Muhammad na kwamba wanajumuishwa katika Swala tunapomswalia yeye. Sifa za kiwango cha juu za ndugu wa Muhammad walioteuliwa ndio sababu kubwa kwa wao kupewa utukufu huu wa pekee. Imam Ali alisimama juu ya wenzake wote, baada ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Alikuwa mfuasi imara sana wa Mjumbe wa Mwenyezi Mungu. Hakusita kujitolea maisha yake kwa ajili ya kutangaza Uislamu. Wasomaji wa historia wanaweza kutambua kwa urahisi kwamba Imam Ali alikuwa mtetezi mkuu wa Uislamu na mfuasi imara wa hukumu zake. Msimamo wa Imam Ali kuhusu uwezo Binafsi na heshima ulikuwa wa pekee. Wakati wowote alipolazimika kuchagua baina ya kushikamana na maadili yake, na starehe za maisha ya dunia, bila kusita alichagua cha mwanzo – maadili yake. Historia inathibitisha kwamba alipendelea kupoteza uongozi wa Ulimwengu wa Waislamu kuliko kukubali sharti ambalo yeye hakuliamini. Alipewa uongozi huu kwa matarajio kwamba angeahidi kufuata Kitabu cha Mwenyezi Mungu, maelekezo ya Mjumbe, na suna za Makhalifa wawili wa mwanzo yakosekanapo maelekezo ya Qur’ani na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Alijibu: “Nitafuata Kitabu cha Mwenyezi Mungu na maelekezo ya Mjumbe Wake; na yakosekanapo mafundisho dhahiri ya vyanzo hivi viwili, nitajitahidi kadiri ya ujuzi na uwezo wangu.”3 3 Ibn Atheer, Al-Kamil (historia kamili) sehemu ya 3, uk. 35. 11

Page 11


Imam Ali binamu yake Mtume (s.a.w.w)Lubumba

Dr.Kanju.qxd

7/1/2011

4:35 PM

Imam Ali (a.s.) Ndugu yake Mtume Muhammad (s.a.w.) Ujuzi wake ulikuwa unashangaza kwa kina chake na ukubwa wake. Hotuba na mihadhara na maneno yake yaliyomo kwenye Nahjul Balaghah (njia ya Ufasaha) ni mambo yanayothibitisha uhakika wa taarifa ya usemi wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.): “Mimi ni Jiji la Elimu, na Ali ni Lango lake, kwa hiyo, yeyote anayetaka kuingia katika Jiji lazima apitie kwenye Lango.”4 Kumbukumbu ya watu wengine watatu wenye sifa Binafsi wa Nyumba ya Muhammad, Fatimah na watoto wake wawili Hasan na Husein, inaonesha kwamba walikuwa watumishi waaminifu sana wa Uislamu. Hadith (nyingi) sahihi zimezungumza kuhusu heshima na sifa zao kama washirika wa kudumu wa uadilifu na haki. Zayd Ibn Arqam alisema kwamba Mjumbe wa Mwenyezi Mungu alisema kumwambia Ali, Fatimah, Hasan na Husein: “Niko katika amani na yeyote yule ambaye yuko katika amani nanyi; na niko katika hali ya uadui na yeyote yule ambaye ni adui yenu.”5 Abu Huraira alisimulia kwamba, Mjumbe wa Mwenyezi Mungu alisema: “Yeyote anayempenda Al-Hasan na Al- Husein ananipenda mimi na yule anayewachukia wao ananichukia mimi.”6 Hubshi Ibn Janadah alisema kwamba alimsikia Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akisema: “Ali anatokana na mimi na mimi natokana na Ali na hapana mtu anayeniwakilisha mimi isipokuwa Ali.”7 Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) hakutaka kumtofautisha Ali kwa sababu tu alikuwa na uhusiano wa kindugu naye. Al-Abbas (ami yake) na watu 4 Al-Hakim, Al-Mustadrak, sehemu ya 3, uk. 26. 5 Ibn Majah, Sunan Ibn Majah, hadith Na. 145. 6 Ibid, Hadith Na. 143. 7 Ibid, Hadith Na. 119. 12

Page 12


Imam Ali binamu yake Mtume (s.a.w.w)Lubumba

Dr.Kanju.qxd

7/1/2011

4:35 PM

Imam Ali (a.s.) Ndugu yake Mtume Muhammad (s.a.w.) wengine na ukoo wa Hashim, pamoja na Ja’far (ndugu yake Ali) wote ni ndugu zake Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Wote hawa wangekuwa na sifa zinazostahiki kumwakilisha yeye. Lakini alisema; “Hapana yeyote anayeniwakilisha mimi isipokuwa Ali.” Wakati fulani Muawiyah alikuwa anamlaumu Ali mbele ya Saad Ibn Abu Waqass. Saad akamwambia: “Nilimsikia Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) anamwambia Ali: Wewe kwangu ni kama Haruna alivyokuwa kwa Musa. Lakini hapatakuwepo na Mtume mwingine baada yangu.”8 Hivyo, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alimpa Ali nafasi ya karibu baada ya ile yake, kwani nafasi ya Haruna ilikuwa inafuata baada ya ile ya Musa. Al-Bukhari ameandika kwenye Sahih yake kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisema: “Fatimah ni kiongozi wa wanawake wa Peponi.”9 Hakuna mtu anayeingia Peponi bali kwa wema wake, na yeyote anayeingia Peponi ni mtukufu mbele ya Mwenyezi Mungu. Kama Fatimah ni kiongozi wa wanawake wa Peponi, lazima atakuwa ni mwenye wema zaidi na mwanamke mtukufu zaidi mbele ya Mwenyezi Mungu. Al-Hakim ameandika kwenye Mustadrak yake kwamba Abu Dhar (sahaba mashuhuri wa Muhammad ambaye ukweli wake unajulikana kwa Waislamu) alisema kwamba; Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amesema: “Mfano wa watu wa Nyumba yangu ni kama ule wa Safina ya Nuhu. Yeyote aliyeingia humo alikuwa salama, na yule aliyeshindwa kuingia humo alikufa maji ….”10

8 Ibn Majah, hadithi Na. 121. 9 Al-Bukhari, Sahih Al-Bukhari, sehemu ya 5, (Sura ya utofautishaji wa ndugu zake Mtukufu Mtume (s.a.w.w.)) uk. 25. 10 Al-Hakim, Sahih Al-Mustadrak, sehemu ya 3, uk. 151.

13

Page 13


Imam Ali binamu yake Mtume (s.a.w.w)Lubumba

Dr.Kanju.qxd

7/1/2011

4:35 PM

Imam Ali (a.s.) Ndugu yake Mtume Muhammad (s.a.w.) Mtukufu Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) aliwaamuru Waislamu kuwafuata ndugu zake wateule. Kwa hiyo ndugu zake Muhammad wanafahamika kuwa kundi la ukweli, lililotofautishwa kwa sababu ya sifa njema na kazi kwa kuwa wanalo daraja miongoni mwa waja waadilifu sana wa Mwenyezi Mungu.

KWA NINI WAO WALIKUWA NI BORA KIASI HICHO? Kwa nini hawa watu wa Nyumba ya Muhammad waliwazidi watu wengine, walio Waarabu na wasio Waarabu kwa uadilifu? Mifano katika historia. Kuelewa sababu, tunapaswa tukumbuke kwamba yale yaliyotokea kwenye Nyumba ya Muhammad hayakuwa yasiyowahi kutokea katika historia ya Utume. Yapo matukio mengi ya aina hiyo. Mwenyezi Mungu Muweza wa Yote alimfanya Haruna kuwa msaidizi wa kaka yake Musa katika ujumbe wake wa kimbinguni. Hakumpa mtu yeyote heshima hii kutoka kwa Bani Israel. Hii ilikuwa ni kwa sababu ya kuwa na sifa stahiki za kiwango cha juu na jibu la ombi la Musa, kama ilivyotajwa kwenye Qur’ani Tukufu:

“(Musa) akasema: “Ewe Mola wangu Mlezi! Nikunjulie kifua changu, na unifanyie wepesi kazi yangu, na ulifungue fundo lililo katika ulimi wangu, wapate kufahamu maneno yangu. Na nipe waziri katika watu wangu, Haruna, ndugu yangu. Kwake yeye niongeze nguvu yangu. Na 14

Page 14


Imam Ali binamu yake Mtume (s.a.w.w)Lubumba

Dr.Kanju.qxd

7/1/2011

4:35 PM

Imam Ali (a.s.) Ndugu yake Mtume Muhammad (s.a.w.) umshirikishe katika kazi yangu…”Qur’ani Tukufu, 20:25-32. Nabii Ibrahim alimwomba Mola Wake Mlezi kuwafanya baadhi ya uzao wake kuwa ma-Imam wa watu. Mwenyezi Mungu alimkubalia ombi lake na Akaahidi kuwafanya Maimam kutoka kwenye uzao wake bila kuruhusu yeyote aliye muovu kupata cheo hicho cha juu. Kutoka katika Qur’ani Tukufu tunasoma:

“Na tulimtunukia Ibrahim Is’haqa na Ya’qub. Na tukajaalia katika dhuriya wake unabii na Kitabu na tukampa ujira wake katika dunia, naye hahika katika Akhera bila ya shaka ni katika watu wema.” Qur’ani Tukufu, 29:27. Pia Mwenyezi Mungu amechagua, pamoja na ndugu zake Ibrahim, ndugu zake Imran na akawapendelea zaidi ya wengine:

“Hakika Mwenyezi Mungu alimteua Adamu na Nuhu na kizazi cha Ibrahim na kizazi cha Imran juu ya walimwengu wote. Ni wazao wao kwa wao; na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusikia na Mwenye kujua.” Qur’ani Tukufu, 3:33-34

15

Page 15


Imam Ali binamu yake Mtume (s.a.w.w)Lubumba

Dr.Kanju.qxd

7/1/2011

4:35 PM

Imam Ali (a.s.) Ndugu yake Mtume Muhammad (s.a.w.) Zakaria aliomba kwa Muweza wa Yote apewe mtoto mwadilifu. Mwenyezi Mungu alijibu ombi lake, na Malaika wakampa habari njema:

“Pale pale Zakaria akamwomba Mola wake Mlezi, akasema: Mola wangu Mlezi! Nipe kutoka kwako uzao mwema. Wewe ndiye unayesikia maombi. Alipokuwa kasimama chumbani akiswali, Malaika akamnadia: Hakika Mwenyezi Mungu anakubashiria Yahya, atakayekuwa mwenye kusadikisha neno litokalo kwa Mwenyezi Mungu na ni bwana na mtawa na Nabii kwa watu wema.”Qur’ani Tukufu, 3:38-39 Kwa mujibu wa aya hizi Utume uliotangulia ule wa Muhammad ulichukua mkondo huo huo. Kutoka miongoni mwa uzao na ndugu zao hawa Mitume wapo watu waliochaguliwa ambao walifika kiwango cha juu sana cha uchaMungu na kwa hiyo walistahili kupewa mamlaka na Mwenyezi Mungu. Kwa nini Mwenyezi Mungu Aliwapa Manabii hao Watoto na Ndugu wenye sifa bora kama hao? Mwenyezi Mungu Muweza wa yote aliwaumba watu miongoni mwa ndugu na uzao wa Mitume hawa kwa kuitika na kujibu maombi yao au kama zawadi zao kwa jitihada zao katika kueneza ujumbe wa Mwenyezi Mungu. Kama Mitume wengine, Muhammad (s.a.w.w.) alipewa ndugu na kizazi wasio wa kawaida kama zawadi kwa jitihada zake katika kumtumikia Mwenyezi Mungu na majibu kwa maombi yake. Alituamuru sisi 16

Page 16


Imam Ali binamu yake Mtume (s.a.w.w)Lubumba

Dr.Kanju.qxd

7/1/2011

4:35 PM

Imam Ali (a.s.) Ndugu yake Mtume Muhammad (s.a.w.) tuseme: “Mwenyezi Mungu Mtukuze Muhammad na watu wa Nyumba yake,” na aliomba katika nyakati kadhaa kwa ajili ya utakaso wa watu hawa wa Nyumba yake. Al-Hakim anasimulia kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alimfunika Ali, Fatimah, Hasan na Husein kwa nguo na akaomba kwa kusema: “Ewe Mwenyezi Mungu, hawa ndio watu wa familia yangu. Ninakuomba Wewe umtukuze Muhammad na familia ya Muhammad.” Katika kujibu ombi lake maneno yafuatayo yaliteremshwa: “Mwenyezi Mungu anataka kuwaondoleeni uchafu nyinyi na kuwafanyeni watu wa familia ya Muhammad wasio na dosari.”11 Hivyo, ilikuwa kawaida kuwepo ndugu na uzao wa Muhammad wanamume na wanawake wenye sifa bora za kiwango cha juu zaidi cha uadilifu. Kinyume chake kama watu wa aina hii wasingekuwepo miongoni mwa ndugu zake Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), ingelikuwa ni jambo lisilo la kawaida kabisa. Mwenyezi Mungu aliwatukuza Ibrahim, Musa Zakaria na Mitume wengine, kwa kuwaumbia katika uzao na ndugu zao watu wenye sifa bora zaidi, na kuwapendelea zaidi ya watu wengine. Kwa nini basi asimtukuze Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) Wake wa mwisho na wa muhimu zaidi kwa kumuumbia miongoni mwa uzao wake na ndugu zake watu kadhaa wenye sifa bainifu kwa kiwango cha juu zaidi? Malipo ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) Qur’ani Tukufu inaweka wazi kwamba kuwapenda ndugu zake Muhammad (s.a.w.w.) ni wajibu wa Kiislamu. Mwenyezi Mungu alimwamuru Muhammad (s.a.w.w.) kuwaambia Waislamu kumzawadia yeye kwa 11 Al-hakim, Al-Mustadrak, sehemu ya 3, uk. 148. 17

Page 17


Imam Ali binamu yake Mtume (s.a.w.w)Lubumba

Dr.Kanju.qxd

7/1/2011

4:35 PM

Imam Ali (a.s.) Ndugu yake Mtume Muhammad (s.a.w.) kuwapenda ndugu zake wa karibu, kwa sababu ya kutimiza ujumbe wake wa kimbinguni,

“Hayo ndiyo aliyowabashiria Mwenyezi Mungu waja wake walioamini na wakatenda mema. Sema; Sikuombeni malipo yoyote kwenu ila mapenzi yenu kwa ndugu zangu wa karibu. Na anayefanya wema tutamzidishia wema. Hakika Mwenyezi Mungu ni Msamehevu Mwenye shukrani.”Qur’ani Tukufu 42:23 Mwenyezi Mungu anamwambia Muhammad kuwajulisha Waislamu wote kwamba malipo pekee anayoyataka kwa ajili ya kutimiza ujumbe wake wa kiMungu ni yale ya Waislamu kuwapenda ndugu zake. Hii ni kwa sababu tu kwamba watu hao (ndugu zake Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) ni watiifu mno kwa Mwenyezi Mungu na waja Wake wapendwa sana miongoni mwa Waislamu. Kwa kumuagiza Mtukufu Mtume Wake (s.a.w.w.) kufanya hivyo, kwa kweli aliwaamuru Waislamu kuwatukuza hao ndugu wateule wa Muhammad (s.a.w.w.), waweke matumaini yao kwa wateule hao, na kufuata njia wanayopita wao. Kwa kufuata amri hii ya mbinguni Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) aliwaambia wafuasi wake wote kuwapenda wateule hao. Alisema kwamba yeye hana uadui na yeyote asiye adui yao, na kwamba yeye yu vitani na yeyote anayewapiga vita wao. Aliwafikiria wao kuwa sawa na ile safina ya Nuh. Yeyote aliyepanda humo alisalimika, na yeyote aliyeshindwa kupanda humo aliangamia. 18

Page 18


Imam Ali binamu yake Mtume (s.a.w.w)Lubumba

Dr.Kanju.qxd

7/1/2011

4:35 PM

Imam Ali (a.s.) Ndugu yake Mtume Muhammad (s.a.w.) Nyumba ya Muhammad (s.a.w.w.) inaweza kuwa njia ya kuwaunganisha Waislamu. Muungano huu unaweza kutambulika pale ambapo Waislamu watachukua msimamo ambao Mwenyezi Mungu na Mtukufu Mtume Wake (s.a.w.w.) walioutaka wachukue kuhusu wateule hawa. Haingekuwa sahihi kwa Waislamu kumtenganisha Muhammad na watu wa Nyumba yake ambapo yeye mwenyewe alitaka kuunganishwa nao. Huu ni uthibitisho ulio wazi alipoelekeza kwamba wafuasi wake wanaunganishe jina lake na hao ndugu zake wateule wakati wowote walipomswalia, ama wakati wa Swala zao za kila siku au nje ya Swala zao.

* * * * *

19

Page 19


Imam Ali binamu yake Mtume (s.a.w.w)Lubumba

Dr.Kanju.qxd

7/1/2011

4:35 PM

Imam Ali (a.s.) Ndugu yake Mtume Muhammad (s.a.w.)

SURA YA PILI. WATU WA NYUMBA YA MUHAMMAD. Kwa kutegemea juu ya makubaliano ya kimya kimya miongoni mwa Waislamu, tuliwachukulia Imam Ali, mke wake Fatimah na watoto wao wawili Hasan na Husein kuwa ni watu wa Nyumba ya Muhammad (s.a.w.w.) iliyobarikiwa. Ushahidi wa kutegemewa zaidi katika jambo hili ni maneno ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) mwenyewe alipozungumza kuhusu Ahlul Bait Muhammad au ‘Itrah’ wake. Taarifa ya maneno ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kuhusu suala hili inaeweza kuainishwa katika namna mbili: Hadith zenye maelezo ambayo yanatofautisha Nyumba ya Muhammad (s.a.w.w.) na wengine ambao wangetenganishwa kwa maelezo hayo hayo. Hadith zenye kuwataja watu hawa wateule.

HADITHI ZENYE MAELEZO. Kutoka kwenye aina ya kwanza ni kama ifuatayo: Jabir Ibn Abdullah, sahaba maarufu alisimulia kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) wa Mwenyezi Mungu amesema: “Enyi watu, nimewaachieni vitu ambavyo kama mkivifuata, hamtapotea kamwe; Kitabu cha Allah na watu wa Nyumba yangu ambao ni Itrah wangu (ndugu wa karibu na kizazi changu.”12

Zayd Ibn Arqam, sahaba maarufu wa Muhammad, alisimulia kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisema: 12 Al-Tirmidhi; Sunan Al-Tirmidhi, sehemu ya 5, uk. 328 (hadith na. 3874). 20

Page 20


Imam Ali binamu yake Mtume (s.a.w.w)Lubumba

Dr.Kanju.qxd

7/1/2011

4:35 PM

Imam Ali (a.s.) Ndugu yake Mtume Muhammad (s.a.w.)

“Nimewaachieni vitu ambavyo kama mkivishikilia hamtapotea baada yangu. Kitabu cha Mwenyezi Mungu, kamba iliyonyooka kati ya Mbingu na Ardhi na watu wa Nyumba yangu ambao ni Itrah wangu. Hakika, (Kitabu cha Mwenyezi Mungu na watu wa Nyumba yangu) havitatengana mpaka viungane nami Siku ya Hukumu. Tahadharini jinsi mtakavyo jihusisha navyo baada yangu.”13 Zayd Ibn Thabit alisimulia kwamba Mtukufu Mtume Wake wa Mwenyezi Mungu amesema: “Ninawaachieni miongoni mwenu warithi wawili: Kitabu cha Mwenyezi Mungu; kamba iliyonyooka baina ya Mbingu na Ardhi, na watu wa Nyumba yangu (ambao ni Itrah). Hakika, vitu viwili hivyo (Kitabu na Itrah) havitaachana hadi Siku ya Hukumu.”14 Zayd Ibn Arqam alisimulia tena kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) wa Mwenyezi Mungu amesema mnamo siku ya Ghadir Khum: “Hivi karibuni mimi nitaitwa na Mwenyezi Mungu, na nitaitikia wito huo. Hakika, nimewaachieni vitu viwili vya thamani kubwa sana. Kimojawapo kati ya vitu hivi ni kikubwa zaidi kuliko kingine: Kitabu cha Mwenyezi Mungu, na ‘Itrah’ wangu watu wa Nyumba yangu. Tahadhari jinsi mtakavyo jihusisha navyo baada yangu. Havitaacha hadi Siku ya Hukumu.” Halafu akasema: 13 Al-Tirmidhi, Sunan al-Tirmidhi sehemu ya 5, uk. 329 (hadith Na. 3876). 14 Imam Ahmad alisimulia kwenye Musnad yake kutoka vyanzo viwili vya kutegewa, sehemu ya 5, uk. 181. 21

Page 21


Imam Ali binamu yake Mtume (s.a.w.w)Lubumba

Dr.Kanju.qxd

7/1/2011

4:35 PM

Imam Ali (a.s.) Ndugu yake Mtume Muhammad (s.a.w.) “Hakika Mwenyezi Mungu ni Mawla (kiongozi) wangu na mimi ni Mawla (kiongozi) wa kila muumini.” Halafu akanyanyua mkono wa Ali na akasema: “yeyote ambaye mimi ni Mawla wake na Ali ni Mawla wake. Mwenyezi Mungu, Mpende yule anayempenda yeye na mghadhibikie yule anayemfanyia yeye uadui.”15 Kwa hiyo, watu wa Nyumba ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) ni wale ambao wana sifa zifuatazo: Kuwa Itrah wa Muhammad. Itrah wa mtu ni ndugu zake wa karibu (kwa kuzaliwa) na dhuriya wake. Kwa ufafanuzi huu, wake zake Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na masahaba wake ambao si wa ukoo wa Hashim wametengwa. Uadilifu wa kiwango cha juu sana. Watu wa Nyumba ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) wameelezewa kwenye hadith hizi kama washirika wa kweli wa Qur’ani ambao kamwe hawataachana nayo. Hivyo wanamume na wanawake wasio wacha-Mungu hawastahiki kuwa kwenye Itrah, wawe ni Bani Hashimu au wasiwe Bani Hashimu. Kuwa na kiwango cha juu sana cha ujuzi wa Yale yaliyomo kwenye Qur’ani Tukufu na Mafundisho ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Wale ambao ujuzi wao wa dini ni mdogo huondolewa, hata kama ni ndugu wa karibu sana wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Wanalazimika kwa kukosa kwao ujuzi kuangukia kwenye kutokukubaliana na Qur’ani Tukufu, kwa makusudi au bila kukusudia. Watu wa Nyumba iliyobarikiwa kwa mujibu wa Hadith, wao wako salama dhidi ya kutokukubaliana na Kitabu cha Mwenyezi Mungu. Usalama wa aina hii hauwezi kuwepo bila ya ujuzi wa kina wa Qur’ani na mafundisho yote ya Kiislamu. Kukubaliana wenyewe wao kwa wao. Wanapokuwepo watu au makundi ya watu yanayopingana yenyewe kwa wenyewe, baadhi yao lazima 15 Al-Hakim, kwenye Sahih yake, Al-Mustadrak, sehemu ya 3, uk. 109. 22

Page 22


Imam Ali binamu yake Mtume (s.a.w.w)Lubumba

Dr.Kanju.qxd

7/1/2011

4:35 PM

Imam Ali (a.s.) Ndugu yake Mtume Muhammad (s.a.w.) watakuwa wamekosea na kutokubaliana na Qur’ani Tukufu. Kwa vile watu wote wa Nyumba wanakubaliana na Qur’ani Tukufu, lazima wao wenyewe kwa wenyewe wawe katika makubaliano kamili. Kuwa na Yakini katika ujuzi wote wa kidini. Kwa hili, wanachuo wa Kiislamu ambao tunawaita Mujtahidi, ambao wana uwezo wa kuendesha utafiti wa kidini na uundaji wa rai zao, wanaondolewa, hata kama ni wa ukoo wa Hashim (wanaohusiana na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Kuelewa hili zaidi, nukta chache lazima zitajwe: Tunapojaribu kujua hukumu za Kiislamu za matendo ya ibada na yasiyo ya ibada, ushahidi wetu mkubwa hutoka kwenye Qur’ani au kutoka kwenye Hadith za Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Wakati tunapokuta maelekezo bayana ya Qur’ani kuhusiana na suala fulani, ujuzi wetu hufikia kiwango cha yakini imma tuwe wanachuoni wa Kiislamu au maamuma. Kama hatupati maelekezo ya wazi ya Qur’ani, tunatafuta kutoka kwenye Hadith za Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Baadhi ya Hadith ziko wazi katika uelekezaji wake na zimesimuliwa na masahaba wengi sana. Tena, ujuzi wetu kupitia kwenye aina hii ya Hadith hupata yakini. Tatizo ni kwamba Hadith za aina hii si nyingi sana, na zilizo nyingi zimesimuliwa na sahaba mmoja au wawili au wachache sana. Kupitia kwenye Hadithi hizi, ujuzi wetu kuhusu hukumu ambazo tunajaribu kuzijua, kamwe hazifikii kiwango cha uhakika kwa sababu sahaba mwasilishaji hakuisimulia kwetu moja kwa moja, kwa sababu haishi katika wakati wetu, wala hakuandika Hadith hiyo kwenye kitabu. Mtu alipokea Hadith kutoka kwa sahaba. Na yeye akamsimulia mtu mwingine na kuendelea hivyo. Baadaye, Hadith hizo ziliandikwa kwenye kitabu baada ya kupita kwenye mikono ya watu wengi. Hivyo, ujuzi wetu kupitia Hadith za aina hii, ungekuwa hasa zaidi wa kubahatisha. Kuna sehemu zingine ambapo maelekezo ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) yamesimuliwa lakini hayapo bayana au katika njia mbili zinazopingana. Katika 23

Page 23


Imam Ali binamu yake Mtume (s.a.w.w)Lubumba

Dr.Kanju.qxd

7/1/2011

4:35 PM

Imam Ali (a.s.) Ndugu yake Mtume Muhammad (s.a.w.) hali kama hiyo, hitimisho linaweza kutolewa tu na wanachuo weledi au ‘mujitahidi.’ Hitimisho lililofikiwa na maoni yaliyoundwa na wanachuo kwenye hali yoyote katika hizo zilizotajwa hapo juu zaidi hasa ni la kukisia. Kwa kawaida hawafiki upeo wa uhakika wala hawakubaliani kwa yakini na Kitabu cha Mwenyezi Mungu. Uwezekano wa kutokukubaliana ni mkubwa sana, chukulia tu maoni ya upande mmoja katika kila suala. Kama tukifikiria maoni ya pande mbili zinazopingana za wanachuo wawili, tunakuwa na uhakika kwamba mmoja wapo hakubaliani na Qur’ani Tukufu kwa sababu maoni ya pande mbili yanapingana, na Qur’ani haiwezi kukubaliana na rai mbili zinazopingana. Kutokana na hili, inakuwa dhahiri kwamba Mujitahid ima wa ukoo wa Hashim au asiye wa ukoo wa Hashim, hawajumuishwi katika jamaa makhususi wa Nyumba ya Muhammad. Hii ni kwa sababu ujuzi wa Mujitahid hasa zaidi ni wa kukisia na katika hali nyingi haukubaliani na mafundisho halisi ya Qur’ani, ambapo ujuzi wa watu wa Nyumba unakubaliana kwa usalama kabisa na Kitabu cha Mwenyezi Mungu. Hii ni kwa sababu Hadith zilizotajwa kwenye kurasa za nyuma zinaonesha wazi kwamba ujuzi wa watu wa Nyumba ya Muhammad ni ujuzi wa uhakika na sio ujuzi wa kukisia; vinginevyo katika hali nyingi wangetengana na Qur’ani Tukufu. Katika hali hii tunapaswa kumfikiria mujitahid, kama vile Abdullah Ibn Abbas, (Binamu yake Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), aliyeko nje ya duru ya Nyumba, licha ya ujuzi wake mkubwa wa dini na kuwa ndugu wa karibu wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Masahaba wengine ambao hawakuwa ndugu wa karibu wa Muhammad wala hawakufikia kiwango cha Ibn Abbas katika ujuzi ni wazi kwamba wametengwa mbali. Vipi itawezekana kwa watu wa Nyumba ya Muhammad kupata Ujuzi wa Yakini katika Mafundisho yote ya Kiislamu? 24

Page 24


Imam Ali binamu yake Mtume (s.a.w.w)Lubumba

Dr.Kanju.qxd

7/1/2011

4:35 PM

Imam Ali (a.s.) Ndugu yake Mtume Muhammad (s.a.w.) Kuwa na ujuzi wa yakini wa mafundisho ya dini iliwezekana sana wakati wa uhai wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Ni mantiki kabisa kufikiria kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alimfundisha mwanafunzi wake, kama vile Ali, yote yale yaliyomo kwenye Qur’ani Tukufu na akamfahamisha sheria zote za Kiislamu ambazo zinaweza kufika idadi ya maelfu kadhaa. Ni sawa kufikiria kwamba mwanafunzi wa karibu kama huyo aliwafundisha baadhi ya wanafunzi wake yote yale aliyoyapokea kutoka kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Mawazo haya yanaungwa mkono na ukweli fulani: Ali alikuwa na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) tangu utoto wake hadi Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alipofariki. Alikuwa mwanafunzi wake mwaminifu na mshirika wake wa karibu. Alikuwa mwanafunzi wake mwenye akili na makini ambaye alihudhuria mafunzo yake ya hadharani na ya faraghani. Al-Hasan na Al-Husein (wajukuu wa Muhammad na watoto wa Ali) waliishi na baba yao kwa miaka mingi. Walikuwa washirika wake wa karibu sana, na Waislamu waliotakasika sana ambao walifanana na mwalimu wao na mwalimu wake. Hivyo unaweza kusema kwamba ujuzi wa yakini kuhusu Qur’ani Tukufu na maelekezo ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) ulikuwa unapatikana na kuwezekana kwa baadhi ya wanafunzi wa Muhammad.

HADITH MAKHUSUSI: Hadith mbali mbali za Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) ziliwataja watu wa Nyumba ya Muhammad. Muslim ameandika kwenye kitabu chake ‘Sahih’ kama ifuatavyo: “Aya ifuatayo ilipoteremshwa wakati wa mjadala baina ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na Wakristo kutoka Najran: ‘Watakao kuhoji katika haya baada ya kukufikia ilimu hii waambie: njooni tuwaite watoto wetu na watoto wenu, na wanawake wetu na wanawake wenu, na nafsi zetu na nafsi zenu, kisha tuombe kwa unyenyekevu na tuiweke laana 25

Page 25


Imam Ali binamu yake Mtume (s.a.w.w)Lubumba

Dr.Kanju.qxd

7/1/2011

4:35 PM

Imam Ali (a.s.) Ndugu yake Mtume Muhammad (s.a.w.) ya Mwenyezi Mungu iwashukie wenye kusema uwongo.’ (Qur’ani 3:61). Mtukufu Mtume wa Allah alimwita Ali, Fatimah, Hasan na Husein na akasema: Ee Mola wangu! Hawa ni watu wa familia yangu”16 At-Tirmidh, Ibn Manthur, Al-Hakim, Ibn Mardawaih na Al-Bayhaqi kwenye Sunan yake, wote hao waliandika masimulizi ya Ummu Salamah, mke wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), ambamo alisema: “Ndani ya nyumba yangu, iliteremka Aya ya Qur’ani (kutoka kwenye Sura ya 33): ‘…Hakika Mwenyezi anataka kukuondoleeni uchafu, enyi watu wa nyumba ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), na kukutakaseni sanasana.’ Ali, Fatimah, Al-Hasan na Al-Husein walikuwa nyumbani kwangu. Mjumbe wa Mwenyezi Mungu aliwafunika na nguo, kisha akasema: ‘Hawa ndio watu wa Nyumba yangu. Ee Mwenyezi Mungu waondolee uchafu na wafanye watoharifu na bila dosari.’” 17 Muslim kwenye Sahih yake aliandika kwamba, Aisha alisema: “Mtukufu Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) alitoka nje akiwa amejifunika shuka pana, lililotengenezwa kwa manyoya meusi. Fatimah, Hasan, Husein na Ali walikuja kwa kufuatana, halafu akawafunika kwa hilo shuka lake na akasema: “Hakika Mwenyezi Mungu anataka kuwaondoleeni uchafu wote kutoka kwenu, nyinyi watu wa Nyumba ya Muhammad na kuwatakaseni, msiwe na dosari.”18 Hadith mbili zifuatazo zimeandikwa kwenye Al-Durr Al-Manthur na AlSuyuti (kwenye Tafsiir yake ya Qur’ani): “Abu Al-Hamza (mmojawapo wa masahaba wa Mtukufu Mtume 16 Muslim, Sahih Muslim, sehemu ya 15 uk. 176. 17 Al-Tirmidhi, Sunan Al-Tirmidhi, sehemu ya 5, uk. 328 (hadith na.3875). 18 Muslim, Sahih Muslim, sehemu ya 15, uk. 194. 26

Page 26


Imam Ali binamu yake Mtume (s.a.w.w)Lubumba

Dr.Kanju.qxd

7/1/2011

4:35 PM

Imam Ali (a.s.) Ndugu yake Mtume Muhammad (s.a.w.) (s.a.w.w.) alisimulia kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) aliendelea kwa miezi minane mfululizo huko Madina, kuja mlangoni kwa Ali kila wakati wa Swala ya Alfajiri, akiweka mikono yake miwili kwenye pande mbili za mlango na kusema: Asalat, Asalat (Swala Swala) hakika Allah anataka tu kukuondoleeni uchafu wote kutoka kwenu, nyinyi watu wa Nyumba ya Muhammad, na kuwatakaseni msiwe na dosari”19 Ibn Abbas alisimulia: “Tumeshuhudia Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kwa kipindi cha miezi tisa alikuja kila siku mlangoni kwa Ali Ibn Abu Talib, wakati wa Swala ya Alfajiri na kusema: Assalaam Aleikum Wa-Rahmatullah Ahlul Bayt (a.s). Hakika Allah anataka kuwaondoleeni uchafu wote kutoka kwenu, watu wa Nyumba, na kuwatakaseni nyinyi msiwe na dosari.”20 Hadith hizi zinaonesha wazi kabisa kwamba kila mmojawapo wa watu hawa wanne ni mtu wa Nyumba ya Muhammad. Pia Hadith hizi zinawaondosha watu wengine wote waliokuwa hai wakati wa Muhammad, wa ukoo wa Hashim halikadhalika na wasio wa ukoo wa Hashim, miongoni mwa Waarabu na wasio Waarabu. Wateule waliozaliwa baada ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Tamko hili ambalo hata hivyo limewekewa mipaka, haliwaondoi watu wote wa ukoo wa Hashim ambao walizaliwa baada ya wakati wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Kundi la kwanza la Hadith tulizozitaja linaonesha kwamba watu wa Nyumba yake wataendelea baada ya kifo chake na kupitia nchi nyingi kwa 19 Al-Suyuuti, Al-Durr Al-Manthur sehemu ya 5, uk. 198 (ilisimuliwa na Sayyed Taqi Al-Hameem, Al-Ussul Al-Ammah kwa ajili ya Al-Fiqh Al-Muquram, uk. 155-156). 20 Ibid (yaani kama na. 28) 27

Page 27


Imam Ali binamu yake Mtume (s.a.w.w)Lubumba

Dr.Kanju.qxd

7/1/2011

4:35 PM

Imam Ali (a.s.) Ndugu yake Mtume Muhammad (s.a.w.) sababu watu wateule, kwa mujibu wa Hadith wataendelea kuwepo almuradi Qur’ani nayo inaendelea kuwepo. Kwa kuwaamuru Waislamu wafuate Kitabu cha Allah na watu wa Nyumba yake, na kwa kutangaza kwamba Ali, Fatimah, Hasan na Husein ni watu wa Nyumba yake, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kwa kweli alimweka Ali na wanawe wawili kwenye kiti cha uongozi wa umma. Hivyo, watoto wawili wanaume hawakuhitaji kuteuliwa na baba yao, na Husein hakuhitaji kuteuliwa na kaka yake Hasan.

* * * * * *

28

Page 28


Imam Ali binamu yake Mtume (s.a.w.w)Lubumba

Dr.Kanju.qxd

7/1/2011

4:35 PM

Imam Ali (a.s.) Ndugu yake Mtume Muhammad (s.a.w.)

SURA YA TATU WATU MUHIMU NA WA LAZIMA. Tunapopitia matukio muhimu kwa kukumbuka mambo ya zamani, yanayohusu historia ya taifa, tunaona kwamba matukio hayo na mabadiliko yao ya mwanzoni hayakutegemea juu ya wengi wa watu binafsi na makundi madogo ya watu ambao waliishi katika wakati huo makhususi. Kuwepo au kutokuwepo kwa mpiganaji huyu au mkulima yule au mfanya kazi au mfanya biashara au mwanasiasa hakukuathiri matukio hayo. Kila mtu binafsi, isipokuwa wachache sana, walikuwa si wa lazima au iliwezakana kumweka mwingine yeyote badala yake ambaye angeweza kufanya kazi kama hii. Kama mambo yalivyo, yapo makundi madogo na baadhi ya watu binafsi ambao hufanya kazi kubwa ambazo watu wengine hawawezi au hawataki kufanya. Makundi haya madogo na watu binafsi hawa wachache watakuwa na ulazima wa kuwepo, na kwa hiyo matukio makubwa yatahusishwa sana na makundi na watu hawa binafsi. Kuwepo kwa mtu yeyote anayeweza kufanya kazi ndogo (na hawa ndio wengi katika kila taifa) kuhusiana na tukio muhimu lazima liitwe tukio la kawaida na si la lazima. Tunasema kwamba kuwepo kwa watu kama hao au makundi madogo ni jambo la kawaida na si la lazima kuhusiana na tukio muhimu kwa sababu tukio hilo lingeweza kutokea kwa kuwepo au kutokuwepo kwa watu kama hao au kundi hilo, kwani kila mmoja wao anaweza kuondolewa na nafasi yake ikashikwa na mwingine. Tunapotazama kwa kukumbuka mambo ya zamani tangu mwanzo wa imani ya Uislamu na kunea kwake pole pole wakati wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), tunaona kwamba Uislamu ulihusishwa sana na kuwepo kwa idadi ndogo ya watu na kundi dogo la watu binafsi. 29

Page 29


Imam Ali binamu yake Mtume (s.a.w.w)Lubumba

Dr.Kanju.qxd

7/1/2011

4:35 PM

Imam Ali (a.s.) Ndugu yake Mtume Muhammad (s.a.w.) Hakuna haja ya kusema kuhusu uhusiano wa imani ya Uislamu na kuwepo kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), kwani yeye ndiye aliyepokea wahyi, akachukua ujumbe na akakutana na mambo ambayo hakuna mtu aliyewahi kukutana nayo. Ni yeye tu ndiye mtu ambaye sifa zake zilimfanya astahiki kupokea wahyi. Kwa kuwa imani ya Uislamu ilitegemea juu utu wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) katika kuanza kwake na kuendelea wakati wa kipindi cha Utume, tunaona kwamba kuendelea kwa Uislamu wakati wa kipindi hicho kulihusishwa sana na kwa ubayana pamoja na makundi madogo matatu ambayo yalilinda maisha ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na yakatoa mihanga mikubwa kwa ajili ya ulinzi wake.

UKOO WA HASHIM. Kundi dogo la kwanza miongoni mwa hayo makundi madogo lilikuwa ni ukoo wa Hashim. Ukoo huu ulitoa kile ambacho hakuna ukoo mwingine wa Makka uliofanya hivyo wakati wa miaka ambayo Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alitumia kati ya mwanzo wa Utume wake na mwanzo wa Hijrah yake. Kundi hili lilipata upendeleo wa heshima ya kumlinda Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) wakati wa miaka hiyo. Hakuna ukoo mwingine wa Makka ulioshiriki heshima hii. Koo zingine zilichagua kuwa na msimamo wa kiuadui kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), ujumbe wake na ukoo wake. Msimamo huo wa uadui ulimtishia Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na watu wa ukoo wake kwa hatari nyingi mfululizo. Hivyo, itakuwa ni haki kusema kwamba kuwepo kwa koo zingine za Makka kuhusiana na maendeleo ya ujumbe wakati wa kipindi hicho haikuwa tu dharura, bali pia ni nguvu hasi, kwani koo hizo hazikufanya lolote kama makundi katika kumsaidia Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kwa namna yoyote; kwa kweli walikwamisha maendeleo.

30

Page 30


Imam Ali binamu yake Mtume (s.a.w.w)Lubumba

Dr.Kanju.qxd

7/1/2011

4:35 PM

Imam Ali (a.s.) Ndugu yake Mtume Muhammad (s.a.w.) Baadhi ya wanamume na wanawake wenye uhusiano na hizi koo za Makka walimuamini Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na walitoa mihanga fulani kwa ajili yake na ujumbe wake, lakini walifanya hivyo kama watu binafsi. Makundi ambayo kwamba watu hao wanahusika nayo, yalichukua msimamo wa uadui kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), na yaliwatesa watu hao kwa sababu waliacha msimamo wao huo wa uadui. Lau kama koo za Umayya, Makhzum, Zuhra, Jumah na koo nyinginezo za Makka hazingekuwepo, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na Ujumbe wake angekuwa salama kutokana na hatari nyingi zilizokuwa zimemkabili. Imam Ali katika mojawapo ya ujumbe wake aliompelekea Muawiya alitamka yafuatayo: “Watu wetu (koo za Makka) walitaka kumuua Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) wetu na kuangamiza ukoo wetu. Walifanya njama na ukatili dhidi yetu. Walituzuia tusipate maji na walitufunika kwa nguo ya woga, walitulazimisha kuishi kwenye mlima wa mawe na waliwasha moto wa vita dhidi yetu, na Mwenyezi Mungu Muweza wa Yote aliamua kwa niaba yetu kuilinda dini Yake na kupigana kwa ajili ya heshima Yake. Muumini wetu alikuwa anatafuta thawabu za Mwenyezi Mungu, na mkanushaji wetu alikuwa anatetea hadhi yake. Waislamu wengine wa Kikureishi hawakuzongwa na yale yaliyokuwa yanatupata sisi, ama kwa muungano uliowalinda au kwa uhusiano na ukoo ambao ulikuwa tayari kuwalinda. Hivyo walikuwa salama dhidi ya mauaji. “Hapo ambapo vita ilipamba moto na masahaba hawakutaka kupigana, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) aliwaweka watu wa Nyumba yake mbele, akiwalinda masahaba wake kupitia kwao kutokana na joto la panga na mikuki.”21

21 Al-Sharif Al-Radhi Muhammad Ibn Al-Husein, Nahjul Balaghah Mkusanyiko wa maneno ya Imam Ali, sehemu ya 3, uk. 8-9. 31

Page 31


Imam Ali binamu yake Mtume (s.a.w.w)Lubumba

Dr.Kanju.qxd

7/1/2011

4:35 PM

Imam Ali (a.s.) Ndugu yake Mtume Muhammad (s.a.w.)

UKOO WA AL-AUS NA AL-KHAZRAJ. Makundi mengine mawili madogo ambamo muunganiko wa imani ya Uislamu ulikuwa umeunganishwa bayana katika hatua nyingine ya maendeleo ya harakati ya Kiislamu yalikuwa ni makabila mawili ya Al-Khazraj na Al-Aus. Makabila haya mawili yalibahatika kutoka miongoni mwa makabila ya Waarabu yaliyoko nje ya Makka kwa heshima yao ya kumlinda Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na ujumbe wake baada ya Hijra. Lau kama makabila mengine yangetaka kugawana heshima hii na makabila haya mawili, yangefanikiwa kuipata; bahati mbaya, makabila hayo yalichagua kuwa wapinzani wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) badala ya kumsaidia. Hivyo, kuendelea mbele kwa imani ya Uislamu kuliunganishwa na haya makundi matatu madogo. Kuwepo kwa makabila mengine na koo zingine ilikuwa si muhimu na kuliko ilivyo kawaida kuhusiana na imani ya Uislamu katika wakati huo. Kuwepo kwa koo na makabila hayo kulisababisha mwelekeo hasi na uliojaa hatari zilizotishia uhai wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na ujumbe wake.

ABU TALIB. Kama tunavyoona haya makundi madogo matatu yaliyounganishwa kwa uimara kwenye ujumbe wa Uislamu, historia ya imani hii inawasilisha kwetu watu wawili ambao kuwepo kwao ilikuwa lazima na muhimu wakati wa kipindi cha Utume. Mmojawapo wa watu hao wawili alikuwa Abu Talib, ami yake Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), mlezi wake wakati wa siku za utoto wake na mtetezi wake mkuu baada ya kuanza Utume wake. Ulinzi wa shujaa huyu kwa mpwa wake dhidi ya vitisho vya Makureishi (koo za Makka zisizo na uhusiano na ukoo wa Hashim) ulikuwa kipengele muhimu katika uendelezaji wa maisha ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na ujumbe wake. Koo za Makka 32

Page 32


Imam Ali binamu yake Mtume (s.a.w.w)Lubumba

Dr.Kanju.qxd

7/1/2011

4:35 PM

Imam Ali (a.s.) Ndugu yake Mtume Muhammad (s.a.w.) zilikuwa na chuki kubwa kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na zilikuwa na shauku ya kumuua. Kilichowazuia wasifanye hivyo ni kuwepo kwa Abu Talib, mkuu wa Makka, ambaye aliwaongoza Bani Hashim na akafanya kwa ajili yao na kwa ajili yake mwenyewe ngome isiyovunjika kumzunguka Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Wasomaji wa historia ya Kiislamu wanajua jinsi koo za Kikureishi walivyotoa makataa (sharti la mwisho) kwa Abu Talib la kumsitisha mpwa wake asiendelee kuwakashifu baba zao na kuwafedhehesha miungu wao na kudhihaki akili zao; vinginevyo, wangemkabili yeye na Muhammad kwenye uwanja wa vita hadi mojawapo ya makundi hayo mawili liangamie. Abu Talib hakuwa na shaka kwamba kukubali kwake changamoto ya Kikureishi kulimaanisha kifo chake na kuangamia kwa ukoo wake. Hata hivyo, hakumshinikiza mpwa wake kuacha kampeni yake. Alichofanya ni kumjulisha tu kuhusu makataa wa Makureishi, na halafu akamwambia kwa upole: “Niokoe mimi na wewe, mpwa wangu, na usinibebeshe mzigo nisioweza kuubeba.” Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alipokataa makataa yao ya mwisho alimtamkia ami yake kwamba kamwe hatabadilisha ujumbe wake kwa kupewa miliki ya ulimwengu wote, Abu Talib bila kukawia alibadilisha msimamo wake na aliamua kuendelea kuwa na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) hadi mwisho. Alimuita alipogeuza mgongo wake: “Njoo rudi, mpwa wangu.” Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) aliporudi, ami yake mkuu akamwambia: “Wewe mpwa wangu endelea. Sema unalotaka kusema, sitakusaliti wakati wowote ule.”22 Abu Talib alitimiza ahadi hii kubwa kwa heshima maalum. Mtu mmoja wa Makka alimtupia uchafu Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alipokuwa amerukuu, Abu Talib alikwenda huku akitikisa upanga wake akiwa ameshikilia 22 Ibn Hishamu, Wasifu wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), sehemu ya I, uk. 266. 33

Page 33


Imam Ali binamu yake Mtume (s.a.w.w)Lubumba

Dr.Kanju.qxd

7/1/2011

4:35 PM

Imam Ali (a.s.) Ndugu yake Mtume Muhammad (s.a.w.) mkono wa mpwa wake hadi alipofika kwenye Msikiti mtakatifu. Kundi la maadui lilikuwa limeketi hapo, na baadhi yao walipojaribu kusimama ili wamkabili Abu Talib, aliwaambia: “Kwa jina la Yule Ambaye Muhammad anamuamini, endapo yeyote kutoka miongoni mwenu atasimama kunikabili nitamkata kwa upanga wangu.” Halafu akawapaka uchafu kwenye nyuso na ndevu zao.23 Kabila la Kureishi liliunda muungano mkubwa dhidi ya Abu Talib na ukoo wake na wakaamua kutumia silaha ya njaa, kuzuia wasipate chakula badala ya kukabiliana ana kwa ana. Walitambua kwamba ukoo wa Hashim wangejibu mapigo endapo wangeshambuliwa; na kwamba hawangeangamizwa bila kuwatia hasara kubwa maadui zao. Hivyo, koo za Makka ziliweka vikwazo vya kiuchumi na kijamii dhidi ya ukoo wa Hashim. Hali ya vikwazo iliendelea kwa miaka mitatu ambapo watu wa ukoo wa Hashim walilazimika kuishi kwenye mlima wa mawe ulioitwa ‘Shi’ab Abu Talib.’ Ukoo wa Hashim wakati wa kipindi hicho wakati mwingine walilazimika kula majani ya miti kupunguza makali ya njaa. Wakati wa kipindi hicho, jambo kuu lililomshughulisha shujaa huyo mkongwe lilikuwa kulinda maisha ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) katika kipindi cha miaka hiyo, mara nyingi Abu Talib aliwaamuru watu wa familia yake hususan mwanawe Ali kulala kwenye kitanda cha Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), kwa lengo la kumlinda asiuawe.

UISLAMU WA ABU TALIB. Baadhi ya wanahistoria na waandishi wa Hadith wametoa taarifa kwamba Abu Talib alifariki dunia akiwa kafiri. Wengine walitoa taarifa kwamba Aya: “Haimpasi Nabii na walioamini kuwatakia msamaha washiriki23 Khalid Muhammad Khalid, Fiy Rihab Ali. 34

Page 34


Imam Ali binamu yake Mtume (s.a.w.w)Lubumba

Dr.Kanju.qxd

7/1/2011

4:35 PM

Imam Ali (a.s.) Ndugu yake Mtume Muhammad (s.a.w.) na, ijapokuwa ni jamaa zao, baada ya kwisha bainika kuwa hao ni watu wa motoni.” (Qur’ani; 9:113) iliteremshwa kuhusu Abu Talib, kwani Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alitaka kumwomba Mwenyezi Mungu kumsamehe na Mwenyezi Mungu alimkataza asifanye hivyo. Matamshi ya aina hiyo yalibuniwa kama sehemu ya kampeni za kashfa ambazo zilianzishwa na ukoo wa Umayya na washirika wao dhidi ya Imam Ali. Walijaribu kwa kubuni Hadith hizo ili kuthibitisha kwamba Abu Sufyani, baba yake Muawiya alikuwa bora zaidi ya Abu Talib baba yake Ali, wakidai kwamba Abu Sufyani alikuwa Mwislamu na Abu Talib alikufa akiwa kafiri. Waandishi wa Hadith na historia walizichukua Hadith hizi bila kuzingatia ushahidi wa udanganyifu wao. Hawakujaribu kuzipima Hadith hizi, lakini tarehe ya kuteremshwa kwa Aya hiyo hapo juu inasadikisha kwamba haikuteremshwa kwa sababu iliyomhusu Abu Talib. Aya hii ni sehemu ya sura ya Baraa (sura ya 9). Sura hii yote iliteremshwa Madina, isipokuwa Aya mbili za mwisho (129 na 130). Aya ambayo ni maudhui ya mjadala wetu ni ya 113. Sura ya Baraa iliteremshwa wakati wa mwaka wa 9 A.H. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alimuamuru Abu Bakr kutangaza sehemu ya kwanza ya sura hii wakati wa siku za kipindi cha Hija mwaka huo alipomtuma kama “Amir Al-Hajj” (kiongozi wa Hijja). Halafu Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alimpeleka Ali kuchua sehemu hiyo (ya Sura hiyo) kutoka kwake na kuitangaza (yeye badala ya Abu Bakr), kwa sababu Mwenyezi Mungu alimuamrisha kwamba Sura hiyo isitangazwe na mtu mwingine yeyote isipokuwa imma yeye Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) au mtu kutoka Nyumba yake. Sura inazungumzia matukio ambayo yalitokea wakati wa kampeni ya Taabuk ambayo ilifanyika mwezi wa Rajab wa mwaka wa tisa. Kwa kuwa Sura hii inayo Aya iliyotajwa hapo juu, Aya hii haingemaanisha Abu Talib kwa sababu alikufa Makka takriban miaka miwili kabla ya 35

Page 35


Imam Ali binamu yake Mtume (s.a.w.w)Lubumba

Dr.Kanju.qxd

7/1/2011

4:35 PM

Imam Ali (a.s.) Ndugu yake Mtume Muhammad (s.a.w.) Hijiriya. Kumwomba Mwenyezi Mungu kumsamehe makosa mtu ambaye alikwisha kufa kwa kawaida hufanyika wakati wa dua ya maziko. Maneno ya Aya yanaonesha hivyo kwani inassema: “Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na waumini hawaruhusiwi kumwomba Mwenyezi Mungu kuwasamehe makafir.� Hii inaonesha kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alikuwa na waumini wengine kwenye Swala ya jamaa alipoomba makafiri wasamehewe. Kusema kweli, Swala ya maziko ilikuwa haijaruhusiwa kabla ya Hijiriya. Swala ya kwanza iliyosalishwa na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kwa ajili ya maiti ilikuwa Swala yake kwa ajili ya Al-Bura Ibn Maarour wa Madina. Upo uwezekano mkubwa kwamba Aya husika iliteremshwa baada ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kuswalia maiti ya mmojawapo wa wanafiki waliokuwa wakijifanya Waislamu na kuficha ukafiri. Inawezekana kabisa kwamba Aya hii iliteremshwa wakati Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akiongoza Swala ya kuswalia maiti ya Abdullah Ibn Abu Saluul ambaye alikufa wakati wa mwaka wa tisa na ambaye alijulikana sana kwa unafiki wake, chuki yake kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na uadui wake kwa imani ya Uislamu. Kuhusu mtu huyu na wafuasi wake, Sura ya Al-Munafiquun (wanafiki) iliteremshwa kabla ya muda huo. Lau kama waandishi wa historia na wa Hadith (ambao kwa kutokuwa waangalifu waliandika Hadith ya kubuniwa kuhusu ukafiri wa Abu Talib) wangelifikiria kwa kina fulani na kwa mantiki, wasingeweza kufanya kosa hili la kutisha la kihistoria. Kusema kwamba Abu Talib alikuwa kafiri ni kusema kwamba alikuwa muumini wa ibada ya masanamu. Lakini imani hii haiwezi kuwa pamoja na imani yake katika ukweli wa Muhammad ambaye aliyakana masanamu na aliona kuheshimiwa na kuabudiwa kwao kama Mwenyezi Mungu ni uasi kwa Muumba.

36

Page 36


Imam Ali binamu yake Mtume (s.a.w.w)Lubumba

Dr.Kanju.qxd

7/1/2011

4:35 PM

Imam Ali (a.s.) Ndugu yake Mtume Muhammad (s.a.w.) Kwa Abu Talib kuamini dini ya masanamu, alikuwa imma aamini kwamba Muhammad alikuwa anawapotosha watu kwa makusudi kuhusu Mwenyezi Mungu, au alikuwa anapagawa. Kama Abu Talib alikuwa kafiri, na licha ya hivyo akajitolea sana kwa ajili ya Muhammad, basi lazima alikuwa mwenye wazimu au mpumbavu isivyo kawaida. (Mwenyezi Mungu aepushilie mbali). Kama angeamini kwamba mpwa wake alikuwa mwendawazimu au mpotoshaji wa makusudi kuhusu Mwenyezi Mungu, Abu Talib angemzuia Muhammad na kuwa mpinzani wake imara badala ya kuwa mlinzi wake wa kutisha, kwani ujumbe wa Muhammad ulitegemewa kuleta uharibifu na kifo cha Abu Talib na ukoo wake. Abu Talib aliifungamanisha hatma yake na hatma ya mpwa wake. Hakujali lolote ambalo lingemtokea yeye na ukoo wake. Alishuhudia hatari zilizomzunguka yeye na ukoo wake na matatizo yaliyokuwa yamelundikana kumzunguka yeye kwa sababu ya ulinzi wake kwa mpwa wake. Licha ya yote yaliyotokea kwake na watu wa uko wake, historia haijaandika neno lolote kali kutoka kwa Abu Talib kuhusu mpwa wake. Kinyume chake, alijitoa mhanga yeye na watu wa ukoo wake kama wakombozi wa mpwa wake. Alimfanyia wema kuliko baba yeyote mwenye huruma na upendo alivyomfanyia mwanawe anayempenda sana. Alimwambia: “Mpwa wangu endela kutangaza ujumbe wako na sema lolote unalotaka kusema. Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sitakuacha kamwe kwenye hatari yoyote.� Abu Talib alikuwa mtu mwenye imani kubwa na itikadi madhubuti katika ukweli wa Muhammad. Aliishi na ujumbe huo kwa takriban miaka kumi na moja na matatizo ya Muhammad na yake yaliongezeka jinsi muda ulivyopita. Alikuwa mtu mwenye imani isiyo ya kawaida kuhusu ukweli wa Uislamu. Historia ilishuhudia sahaba mashuhuri wanakimbia pale hatari ilipozidi kuongezeka. lakini Abu Talib hakukimbia wala hakupoteza azma yake. Aliendelea kujitoa mhanga kwa ajili ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) katika kipindi cha uhai wake. 37

Page 37


Imam Ali binamu yake Mtume (s.a.w.w)Lubumba

Dr.Kanju.qxd

7/1/2011

4:35 PM

Imam Ali (a.s.) Ndugu yake Mtume Muhammad (s.a.w.) Hili lingetoa sifa thibitishi kwa yale aliyoandika At-Tabarsi kupitia sanad yake hadi kwa Imam Ja’far as-Sadiq (a.s.): “Wakati Imam Ali alipokuwa ameketi kwenye ‘Ruhbah’ huko Kufa akiwa amezungukwa na kundi la watu, mtu mmoja alisimama na akasema: “Ewe Amiri wa Waumini, wewe umo katika wadhifa huu mkubwa ambao Mwenyezi Mungu amekuweka wakati baba yako anateseka ndani ya Jahanamu.” Imam alijibu kwa kusema: “Nyamaza! Mwenyezi Mungu na aharibu mdomo wako! Kwa jina la Yule Aliyemtuma Muhammad akiwa na ukweli, kama baba yangu akiwaombea msamaha watenda dhambi wote katika uso wa ardhi, Mwenyezi Mungu angekubali uombezi wake.” 24 Alificha imani yake, na Mwenyezi Mungu amemlipa mara mbili. Abu Talib aliificha imani yake ili tu aweze kumpa ulinzi Muhammad. Lau angedhihirisha imani katika Uislamu, uhusiano wake na Makureishi ungekatika. Alitaka kuendeleza mazungumzo kati yake na Makureishi na kuhakikisha kwamba hayasitishwi kwani kinyume chake ni hali ambayo ingesababisha mapambano ya silaha kwenye vita vya kuamua mshindi na mshindwa ambavyo huenda vingesababisha maangamizi ya ukoo wake. Ngome ya ukoo wa Hashim iliyomzunguka Muhammad ingeanguka na makafiri wa Makka wangemkamata. Licha ya kuficha imani yake, Abu Talib zaidi ya mara moja, alidhihirisha waziwazi imani yake. Alipokuwa kitandani dakika chache kabla ya kukata roho, aliwaambia watu wa ukoo wa Hashim: “Ninawaamuruni muwe watu wema kwa Muhammad. Ni mtu pekee wa kuaminika miongoni mwa Kureishi, na mkweli wakati wote miongoni mwa Waarabu. Alileta ujumbe ambao umekubaliwa na moyo na kukataliwa na ulimi kwa kuogopa uadui. Kwa jina la Allah yeyote anayefuata njia ya Muhammad atakuwa kwenye 24 Al-Tabarsi, Al-Ihtijaj, sehemu ya I, uk. 341. 38

Page 38


Imam Ali binamu yake Mtume (s.a.w.w)Lubumba

Dr.Kanju.qxd

7/1/2011

4:35 PM

Imam Ali (a.s.) Ndugu yake Mtume Muhammad (s.a.w.) barabara iliyo sahihi na yeyote anayefuata mwongozo wake atafurahi katika maisha yake yajayo. Kama ningekuwa bado nina miaka ya uhai hapa duniani ningempa ulinzi dhidi ya hatari na ningemlinda dhidi ya maadui. “Na nyinyi, watu wa ukoo wa Hashim itikieni wito wa Muhammad na mwaminini. Mtafuzu na mtaongozwa vema. Msaidieni Muhammad; hakika yeye ni mwongozo kwenye njia iliyonyooka.�25

SOTE TUNAWIWA NAYE. Waislamu wote ni wenye kuwiwa kwa Abu Talib, kwani kuendelea kwa ujumbe wa Kiislamu ni matokeo ya mwenendo wa maisha ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) hadi Mwenyezi Mungu alipokamilisha ujumbe wake kwa mwanadamu. Ulinzi wa Abu Talib kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) ulikuwa kikwazo kikubwa kwa Kureishi. Wakati fulani nilitamka maneno haya kwenye semina ya Kiislamu na swali lifuatalo liliulizwa: Kama Mwenyezi Mungu Ndiye Ambaye alitaka ujumbe wa Uislamu uendelee na uenee, hakuwa na uwezo wa kuulinda na kuueneza bila ya Abu Talib na ulinzi wake kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.)? Katika jibu langu, nilisema ifuatavyo: Waisilamu wanaamini kwamba Mwenyezi Mungu alikuwa na uwezo wa kulinda maisha ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), na alikuwa na uwezo wa kuwafanya wana wa Adamu wote kuwa Waislamu na waumini katika Mwenyezi Mungu, Upweke wake na Siku ya Hukumu. Angewafanya wanadamu wote kuwa watiifu wa sharia za Akhera. Alikuwa na uwezo wa kufanya koo zote za Kureishi kumtii Muhammad. Pia Alikuwa na uwezo wa kwafanya watu wote kutii amri Zake bila hata kumuumba Muhammad. 25 Khalid Muhammad Khalid, Fiy Rihab Ali 39

Page 39


Imam Ali binamu yake Mtume (s.a.w.w)Lubumba

Dr.Kanju.qxd

7/1/2011

4:35 PM

Imam Ali (a.s.) Ndugu yake Mtume Muhammad (s.a.w.) Lakini, licha ya imani yetu kwa yote haya, tunatambua kwamba Mwenyezi Mungu hakufanya hivyo. Hakuwafanya watu wote kuwa waumini. Hakuingilia moja kwa moja kubadili fikra na itikadi zao. Alichofanya Yeye ni kuwapa uhuru wa kuchagua. Hii inamaanisha kwamba Mwenyezi Mungu hakutaka kuendesha matukio ya hapa duniani kimiujiza na kupitia uwezo wa kiMungu. Alichotaka kufanya Yeye ni kuendesha mambo ya duniani kufuatana na jinsi ya kimaumbile na uelekeo wake. Kwa hiyo, Mwenyezi Mungu aliteremsha Wahyi kwa mwanadamu aliyeitwa Muhammad na akaueneza Uislamu kupitia kwa mtu huyo. Mweza wa Yote hakuchagua kuwalazimisha Makureishi kuamini au kutokuamini. Makureishi walio wengi waliamua kumpinga Muhammad, na Abu Talib alichagua kuamini ujumbe wake na kumlinda yeye kwa vyote ilivyokuwanavyo; miongoni mwa watu na namna zilizokuwepo. Ulinzi huu wa Abu Talib kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) ulikuwa kipengele muhimu katika kuponya maisha ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na kuendesha ujumbe wake hadi Abu Talib alipoaga dunia. Kuhusisha ukafiri kwa mtu kama Abu Talib, ambaye alikuwa msaidizi kwa Waislamu wote kwa kulinda maisha ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kwa takriban miaka kumi na moja, ni moja wapo ya utovu wa shukrani mbaya sana. Ni zawadi juu ya fadhila kubwa kwa fedheha mbaya. Abu Talib alikuwa mtu wa kwanza miongoni mwa watu wawili mashuhuri ambao kwamba uendelezwaji wa imani ya Uislamu uliunganishwa kwao kwa uimara, na kuwepo kwao kuhusu uendelezaji wa imani ya Uislamu hakukuwa dharura.

IMAM ALI (A.S.). Mtu mwingine ambaye uendelezaji wa imani ya Uislamu katika kipindi cha siku za uhai wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) uliunganishwa kwa uimara ni mtoto wa Abu Talib, ambaye alichukua kazi ile ile baada ya kifo cha 40

Page 40


Imam Ali binamu yake Mtume (s.a.w.w)Lubumba

Dr.Kanju.qxd

7/1/2011

4:35 PM

Imam Ali (a.s.) Ndugu yake Mtume Muhammad (s.a.w.) baba yake, lakini katika kiwango kikubwa. Masahaba wengi sana walifanya jitihada kubwa kwa ajili ya Uisalmu na walimpatia Mtukufu Mtume wa Uislamu (s.a.w.w.) msaada unaostahili kupongezwa. Inatosha kuwataja Makhalifa watatu: Abu Bakr, Umar na Uthman sanjari na masahaba wengi wa Makka kama vile: Zubeir, Talha, Abdul Rahman Ibn Auf Abu Ubeida Ibn Jarrah, Saad Ibn Abu Waqass, Miqdad Ibn Aswad, Abdullah Ibn Mas’ud na Ammar Ibn Yasir. Ongezea kwa hawa, watu kutoka koo za Madina kama: Abu Dujana, na Qais Ibn Saad, baba yake Saad Ibn Ubadah, Saad Ibn Maadh na wengineo kutoka jamii nyingine kama vile: Abu Dharr, Salman Al-Farsi na masahaba wengine mamia zaidi ya hawa. Watu wote hawa walijitahidi katika njia ya Mwenyezi Mungu kwa kujitolea kutumia kiasi cha utajiri wao au maisha yao au vyote viwili. Kama tukiangalia upya kipindi cha Utume na majukumu ambayo masahaba hawa waadilifu walifanya, tunawaona kuwa ni watu wa lazima kama kundi. Hata hivyo, kila mmoja wao angeweza kubadilishwa na nafasi yake ikashikwa na sahaba mwingine na akatekeleza wajibu kama huo wa kwake. Ilikuwa inawezekana kumbadili Abu Bakr na nafasi yake ikachukuliwa na Umar na kutekeleza jukumu kama lile la kwake. Ilikuwa inawezekana kumbadili Abu Bakr, Umar na Uthman na nafasi hiyo ikachukuliwa na Ubeidullah Ibn Al-Jarrah, Talha na Zubeir. Ilikuwa inawezekana kumbadili Saad Ibn Ubadah na Saad Ibn Maadh au na mwanae Qais Ibn Saad Ibn Ubadah, au kumbadili Abu Dhar na Salman au Ammar Ibn Yasir au Miqdad Ibn Aswad. Majukumu ya masahaba hawa yalikuwa yanakaribiana au yanafanana. Kama Umar angekuwa sahaba wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) ndani ya pango mnamo usiku huo wa Hijiriya badala ya Abu Bakr, Uisilamu haungepotea kwa sababu ya mabadiliko hayo. Lakini jukumu la Ali katika kuponya maisha ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) ni kazi ambayo haingefanywa na mtu mwingine isipokuwa Ali. Ilikuwa rahisi kwa 41

Page 41


Imam Ali binamu yake Mtume (s.a.w.w)Lubumba

Dr.Kanju.qxd

7/1/2011

4:35 PM

Imam Ali (a.s.) Ndugu yake Mtume Muhammad (s.a.w.) Ali kutekeleza jukumu la sahaba mwingine yeyote wakati wa uhai wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), lakini haikuwa rahisi kwa sahaba mwingine yeyote kutekeleza jukumu la Ali. Ilikuwa rahisi kwa Ali kuwa sahaba wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) ndani ya pango la Thaur mnamo usiku wa Hijriah. Lakini haikuwa rahisi kwa Abu Bakr au sahaba mwingine yeyote kulala kwenye kitanda cha Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), kuokoa maisha ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kwa maisha yake, kujitoa kukabiliana na shambulio la Kureishi ambalo lilitegemewa kuja kutoka kwa mashujaa kumi wakisaidiwa na makafiri wote wa Makka. Ilikuwa haiwezekani kwa sahaba mwingine yeyote kutekeleza jukumu la Ali kwenye uwanja wa vita vya Badr ambako aliwaangamiza takriban asilimia 50 ya Makureishi. Hivyo, kwa juhudi zake binafsi alizidisha uzito wa kipimo, kwa kulipa upendeleo jeshi dogo la Kiislamu (kupata ushindi), ambapo imani ya Uislamu ilikuwa katika hatari. Ilikuwa haiwezekani kwa sahaba mwingine yeyote kutekeleza jukumu la Ali pale Uhud wakati masahaba walikimbia na kuondoka kwenye uwanja wa vita na kupanda juu ya mlima huku wakiwa hawataki kutazama nyuma kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), wakati Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alikuwa anawaita warudi pale alipokuwa. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alibaki peke yake kukabiliana na maelfu ya makafiri. Hakuna mtu yeyote aliyebaki naye isipokuwa Ali ili kukabiliana na vikosi vilivyokuwa na nia ya kumuua Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Ali alipambana na vikosi hivyo kimoja baada ya kingine na kuvilazimisha vilivyo vingi miongoni mwao kurudi nyuma hadi hapo ambapo masahaba wachache waliporudi na kumlinda Mtukufu Mtume wao (s.a.w.w.). Kama Ali naye angekimbia kama walivyokimbia masahaba wengine na wapagani wakapata fursa ya kufika alipokuwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) mkondo wa historia ungebadilika kama Muweza wa Yote hakuuhami Uislamu na Mtukufu Mtume wake (s.a.w.w.) kwa muujiza kabisa usio wa kawaida. 42

Page 42


Imam Ali binamu yake Mtume (s.a.w.w)Lubumba

Dr.Kanju.qxd

7/1/2011

4:35 PM

Imam Ali (a.s.) Ndugu yake Mtume Muhammad (s.a.w.) Haya ni matukio machache katika mengi yanayothibitisha wazi wazi kwamba jitihada za Ali zilikuwa kipengele imara sana katika kuleta ushindi wa imani ya Uislamu na kushindwa kwa maadui zake. Hii inathibitisha kwamba Ali alikuwa ngao ya kumlinda Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) dhidi ya hatari nyingi zilizozunguka maisha yake yenye thamani. Hii inamaanisha kwamba Ali alikuwa na sifa mbili muhimu na za kipekee: Mwendelezo wa Uislamu ambao ulitegemea uhai wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na ushindi wake wakati wa kipindi hicho uliunganishwa kwa uimara sana na kuwepo kwa Ali na jitihada zake. Muungano madhubuti baina ya kuzaliwa kwa serikali ya Kiislamu na kuwepo kwake. Ilikuwa haiwezikani kuasisiwa kwa dola ya Kiislamu kama maadui wa Uislamu wangepata ushindi na kuweza kuangamiza mamlaka hayo mapya. Kwa vile jitihada za Ali zilikuwa na athiri ya wazi katika kuzidisha uzito wa kipimo wa mamlaka mpya kwenye vita vya kuamua mshindi na mshindwa kati ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na maadui, ingekuwa ni haki kabisa kufikiria jitihada za Ali kuwa mojawapo ya vipengele muhimu sana katika kuzaliwa kwa Dola ya Kiislamu. Ni kiasi gani neno la Umar linaweza kuwa la haki pale alipomwambia mtu kwa kumshutumu Ali kuwa alikuwa na sifa ya kiburi: “Wallahi, nguzo ya Uislamu haingeasisiwa bila ya upanga wa Ali.�

UJASIRI WA PEKEE UKISAIDIWA NA UAMINIFU WA PEKEE. Ujasiri wa Ali usio wa kawaida na nguvu za kimwili tu zisingeweza kuwa ngao ya ulinzi wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) wala zisingefungamana na mwendelezo wa Uislamu na kuzaliwa kwa dola ya Kiislamu kwenye uwepo wake yeye. Kilichomfanya yeye aweze kuvuka mipaka ya uwezo wa kibinadamu ni uaminifu wake usio wa kawaida kuhusu kanuni za 43

Page 43


Imam Ali binamu yake Mtume (s.a.w.w)Lubumba

Dr.Kanju.qxd

7/1/2011

4:36 PM

Imam Ali (a.s.) Ndugu yake Mtume Muhammad (s.a.w.) Kimbinguni na utambuzi wake wa kina ambao kutokana nao aligundua ukweli usiojulikana, na kwawo ujasiri wake na nguvu zake za kimwili zilielekezwa katika kuutumikia ukweli huo. Historia ilishuhudia watu wengi wenye nguvu na ujasiri. Lakini ukosefu wa ujuzi wa ukweli au kutokuwepo na uaminifu kwenye ukweli kuliwafanya watu hao watumie yale waliyopewa miongoni mwa uwezo katika kusaidia uwongo na kupigana na ukweli; au kuliwafanya wajiabudu wenyewe wakitumia nguvu zao zote katika kupata utukufu wa udanganyifu au anasa zisizo na thamani. Tofauti na haya, Ali alikuwa mfano wa aina tofauti ya mtu ambaye ujuzi wake uliwafanya wao washuhudie moja kwa moja ukweli na kufurahia kujitoa mhanga, mambo ambayo watu wengine waliyaona hayavumiliki. Ali aliandamana na dunia hii kimwili ambapo roho yake iliunganishwa na dunia ya juu zaidi. Yeye na wale ambao walikuwa mfano kama yeye ndio ambao Mwenyezi Mungu aliwateuwa kuwa watawala hapa duniani!

Kuzaliwa kwake na utoto wake Mfungamano madhubuti kati ya juhudi za Ali na kuzaliwa kwa Dola ya Kiislamu haikuwa matokeo ya kubahatishwa. Bali ilikuwa matokeo ya mabadiliko ya kiroho yaliyoanza mapema katika maisha yake. Ali alikuwa anatayarishwa kwa ajili ya heshima ya kipekee tangu siku za utoto wake. Alikuwa na heshima ya pekee ya kuwa na mfungamano madhubuti kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) ambaye alimchukua na kumlea nyumbani kwake katika kipindi cha siku za utoto wake kama mmojawapo wa watu wa familia yake. Aliielekeza akili angavu ya utoto na maumbile angavu kuelekea kwenye ukweli. Alimkoleza Ali kutoka kwenye nguvu za imani yake, utambuzi, hikima na utakatifu. Akiwa mikononi mwa mwalimu huyo, Ali alikua kimaumbile na sifa zake zikastawi. Akawa kioo kinachoakisi nuru ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). 44

Page 44


Imam Ali binamu yake Mtume (s.a.w.w)Lubumba

Dr.Kanju.qxd

7/1/2011

4:36 PM

Imam Ali (a.s.) Ndugu yake Mtume Muhammad (s.a.w.) Mke wa Abu Talib, Fatimah Binti yake Asad (mwanamke ambaye Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alimchukulia kama mama yake wa pili), alimzaa Ali kwenye Kaaba. Hivyo, alikuwa binadamu wa kwanza kuzaliwa ndani ya Nyumba takatifu ya kale ya Mwenyezi Mungu. Ali alizaliwa miaka thelathini baada ya kuzaliwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), na miaka ishirini na tatu kabla ya hijiriya, mama yake alimpa jina la Haidari (simba) au Asad. Baba yake alimpa jina la Ali (juu). Majina haya mawili yalifaa kwani hatima yake alikuwa awe simba wa Mwenyezi Mungu na wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) Wake, kwani alikuwa ni mtu wa daraja ya juu sana baada ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) ambaye alimfanya kuwa ndugu katika undugu wa Kiislamu miongoni mwa Waislamu wote. Uwezo wa Abu Talib kama mtafutaji riziki ya familia yake ulishuka chini ya mahitaji ya familia yake hususan njaa ambayo iliwakumba watu wa Makka katika kipindi hicho. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alimshauri ami yake Al-Abbas kwamba wao wawili wajaribu kupunguza uzito wa mzigo wa familia ya Abu Talib kwa kuchukua baadhi ya watoto wake. Abu Talib alikubali ombi lao. Abbas alimchukua Jafar na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alimchukua Ali na aliishi naye hadi siku Utume wake ulipoanza.26 Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na Al-Abbas walikuwa na uwezo wa kipato, na walikuwa na uwezo wa kumpa Abu Talib mahitaji ya chakula wakati wa kipindi hicho kigumu na kuwaacha Ali na Jafar kwa wazazi wao. Lakini, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) aliamua kwamba yeye na ami yake wawachukue watoto hao wawili. Inaonesha kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alielewa na kutumia fursa ya ukame. Alimchukua Ali kwake na kujaribu kumpa Ali katika malezi yake chakula cha roho yake, pamoja na chakula cha mwili wake, akimtayarisha kwa kipindi kikubwa cha siku zake za usoni ambacho kilikuwa 26 Al-Hakim, Al-Mustadrak, sehemu ya 3, uk. 5-6 na kuendelea kwenye Wasifu wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), sehemu ya I, uk. 24 (mwandishi Ibn Hisham). 45

Page 45


Imam Ali binamu yake Mtume (s.a.w.w)Lubumba

Dr.Kanju.qxd

7/1/2011

4:36 PM

Imam Ali (a.s.) Ndugu yake Mtume Muhammad (s.a.w.) kinamngojea. Inaonesha kwamba alikuwa tayari kufanya hivyo hata kama Makureishi hawakuwa na ukame. Ali alikuwa sahaba wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) wa maana sana. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) mwenyewe alitujulisha kwamba uhusino wake na Ali haukuwa wa kawaida. Alimwambia: “Ali watu wanatoka kwenye nasaba mbali mbali, lakini wewe na mimi tunatoka kwenye nasaba moja.” Kama mambo yalivyo, kwa usemi huu, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) hakumaanisha kwamba Ali alikuwa ndugu yake kwa kuzaliwa na mwana wa ami yake wa kwanza, na kwamba babu yao alikuwa Abdul Muttalib, kwa sababu hiyo si taarifa muhimu. Mambo haya ni ya kawaida kwa watu. Aidha, Al-Abbas na Hamza walikuwa watoto wa Abdul Mutalib na Jafar na Aqeel walikuwa ndugu zake Ali. Uhusiano wao kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) ni kama ule wa Ali na yeye haswa. Alichomaanisha Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) ni kwamba nafsi ya Ali inafanana na nafsi ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na kwamba kwa uimara zaidi imeunganishwa kwake, kama vile ni nyongeza ya haiba yake. Hivyo, alitokana na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kama vile alivyosema yeye mwenyewe: “Na mimi natokana na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kama mmoja wa miti miwili ambayo chanzo chao ni kwenye mzizi mmoja, na kama vile sehemu ya chini ya mkono inavyochomoza kutoka sehemu ya juu ya mkono.”27 Inaelekea kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alimchukua Ali ambapo Ali alikuwa bado mtoto mdogo, kwani Ali mwenyewe alisema yafuatayo: “Na mnatambua nafasi yangu kutoka kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), undugu wa karibu wa kuzaliwa na nafasi maalum. Alikuwa akinikalisha kwenye paja lake nilipokuwa mtoto mdogo, akinilaza kitandani pake, nikiugusa 27Nahjul Balaghah, sehemu ya 3, uk. 73. 46

Page 46


Imam Ali binamu yake Mtume (s.a.w.w)Lubumba

Dr.Kanju.qxd

7/1/2011

4:36 PM

Imam Ali (a.s.) Ndugu yake Mtume Muhammad (s.a.w.) mwili wake mtakatifu na kunusa harufu nzuri ya manukato yake. Alikuwa na desturi ya kutafuna chakula na kukiweka mdomoni mwangu.”28 Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) aliishi kabla ya siku za Utume kama dunia ya peke yake. Aliishi kwenye jamii ambamo ujahiliya na kuabudu masanamu ni mambo yaliyoenea, kutakasa ushirikina na kuhalalisha tabia potofu za kimaadili. Bado yeye aliweza kutafakari yale ambayo akili za watu wa jamii yake hazikuweza kutambua. Usafi wa maumbile yake ulimwezesha kuona na kusikia ambayo watu hawakuweza kusikia na kuyaona. Aliishi katikati ya jamii yake kama kisiwa cha ujuzi, hikima na ustaarabu akiwa amezungukwa na bahari ya ushenzi na ujahiliya. Ali alikadiriwa awe sehemu ya dunia hiyo inayojitegemea na kuishi kwenye mazingira ya kisiwa hicho bila kuathiriwa na jamii iliyozunguka sehemu hiyo. Aliongezeka umri kama mwanga uliochukuliwa kutoka kwenye nuru ya Muhammad (s.a.w.w.). Tabia yake angavu na akili makini ni sifa ambazo zilimwezesha kufuata nyayo za Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na kuishi kwa kufuata kanuni na maadili yake. Imam alizungumza kuhusu makuzi yake chini ya maelekezo ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na mvuto wa mwambatano wake kwake katika kujenga tabia yake ya ubora wa juu: “Na yeye Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kamwe hakupata kuona neno la uwongo kwenye maneno yangu au uovu kwenye matendo yangu. Mwenyezi Mungu alimwambatanisha kwake (Muhammad) tangu wakati wa kulikiza kwake alipopewa malaika wa Mwenyezi Mungu mkubwa kuliko wote kumpitisha kwenye njia ya wema na kumfundisha yeye maadili ya hali ya juu sana ya dunia… Na nilikuwa ninamfuata kama mtoto amfuatavyo mama yake. Alikuwa na desturi ya kuisimamisha kwa ajili yangu kila siku bendera ya maadili yake na kuniamuru niifuate. Alikuwa na desturi ya kujitenga faragha kwenye pango la Hira kila mwaka na nilikuwa naye wakati ambapo hapana mtu mwingine ambaye angemuona. Na wakati wa kipindi cha siku za mwanzo wa Uislamu, palikuwepo na 28 Nahjul Balaghah, sehemu ya 2, uk. 15. 47

Page 47


Imam Ali binamu yake Mtume (s.a.w.w)Lubumba

Dr.Kanju.qxd

7/1/2011

4:36 PM

Imam Ali (a.s.) Ndugu yake Mtume Muhammad (s.a.w.) nyumba moja tu iliyokuwa inamhifadhi Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), Khadija, na mimi kama watatu wao, tulikuwa tunaona nuru ya Wahyi na kunusa harufu nzuri ya Utume.”29 Kwa wakati huo, Ali alifikia kwenye kunyanyuka kwake kiroho katika kiwango ambacho aliweza kusikia na kuona yale ambayo Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alikuwa anasikia na kuona wakati wa siku za mwanzo wa Utume wake. Yeye (Ali) alisema kwamba tukio fulani lilitokea wakati wa siku chache tangu kuanza Utume wake, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) aliniambia: “….Hakika unasikia ninachosikia na uonaona ninachoona, lakini wewe si Mtume. Wewe ni waziri na unafuata njia iliyo bora.” Kwa kuwa Ali alikwisha kwenda umbali mkubwa katika maendeleo yake ya kiroho kabla ya kuvuka umri wa miaka kumi, ilikuwa ni kawaida tu kwake kuongeza kwenye nafasi yake maalum sifa nyingine ya pekee ya kuwa muumini wa kwanza miongoni mwa waumini wa Utume wa Muhammad na kuwa mwepesi zaidi kuitika wito wake.

SURA YA NNE WAISLAMU WA MWANZO. Uwezo wa kiakili wa Ali (a.s.) na kuunganika kwa maisha yake na maisha ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) ulimwezesha yeye kufikiri kama mwanafalsafa akiwa na umri wa miaka kumi. Alikuwa na uwezo wa kutoa maamuzi yenye mantiki. Watu wa Makka walio wengi kwa muda wa miaka kumi na tatu walikataa kufumbua macho yao waione nuru ya Uislamu na walimzuia Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kuyafikia masikio yao. Hawakuweza kuzipatia akili zao uhuru kwa sababu walikuwa na msimamo wa: “Tumewakuta baba zetu barabarani, na sisi tunafuata nyayo zao.” 29 Nahjul Balaghah, sehemu ya 2, uk. 15. 48

Page 48


Imam Ali binamu yake Mtume (s.a.w.w)Lubumba

Dr.Kanju.qxd

7/1/2011

4:36 PM

Imam Ali (a.s.) Ndugu yake Mtume Muhammad (s.a.w.) Mwelekeo wa kufuata njia ya wahenga ulikuwa, na bado ni dhamira kuu dhidi ya mabadiliko ya dini. Muelekeo huu ulikuwepo na bado upo kama kizuizi kati ya wanafalsafa wa jamii ya kimagharibi na kukubalika kwa mafundisho ya Kiislamu. Lakini Ali (a.s.), katika mwaka wa kumi wa umri wake, alichukua mwelekeo ulio mantiki. Wakati Muhammad na Khadija walipokuwa wakisali, Ali aliingia chumbani kwao. Alisimama hadi Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alipomaliza kusali. “Mna msujudia nani?” Ali aliuliza. “Tuna msujudia Mwenyezi Mungu Yule Aliyenipatia Utume na kisha akaniamuru niwaite watu waje Kwake.” Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alijibu. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisoma Aya kutoka kwenye Qur’ani Tukufu, halafu akamlingania binamu yake akubali kuwa Mwislamu, Ali alivutiwa sana. Alimwomba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) muda ili awasiliane na baba yake. Alipitisha usiku ule katika hali ya msisimko mkubwa, na siku iliyofuatia, alikuja kutangaza Uislamu wake. Alikubali imani mpya bila kutaka ushauri kutoka kwa baba yake Abu Talib, akitoa hoja kwamba: “Mwenyezi Mungu aliniumba mimi bila kupata ushauri kutoka kwa Abu Talib. Kwa nini nitake ushauri wake ili nimuabudu Mwenyezi Mungu.”30 Ni usemi mfupi, lakini unatangaza fikra kubwa mno ya kujitegemea, uwezo wa kufanya maoni, na kina katika imani. Ni mantiki ambayo haiharibiwi na ukinzani. Ali alimpenda baba yake na aliamini kwamba mtoto anawajibu kumtii baba yake ipasavyo. Lakini alijua kwanba utii kwa baba si kitu kamili. Unayo mipaka yake. Ushauri unatakiwa hapo tu ambapo jambo halieleweki. Ukweli unapodhihiri, mashauriano hayana manufaa. Kwa Ali, ukweli wa Muhammad ulikuwa wazi kama mwanga wa mchana. Na ulikwisha kuwa wajibu wa Ali kuitikia wito wa Muhammad (s.a.w.w.) haraka sana. 30 Dkt. Muhammad Husein Haikal, Hayat Muhammad (maisha ya Muhammad). uk. 138. 49

Page 49


Imam Ali binamu yake Mtume (s.a.w.w)Lubumba

Dr.Kanju.qxd

7/1/2011

4:36 PM

Imam Ali (a.s.) Ndugu yake Mtume Muhammad (s.a.w.) Ujumbe ni mpya, na hajui msimamo wa baba yake utakuaje kuhusu imani mpya. Abu Talib anaweza akaamini kile ambacho mtoto wake mdogo ameamini. Kama hali itakuwa hiyo, ingemfurahisha baba kuona mwanawe anamtangulia kukubali ukweli. lakini Abu Talib anaweza akasita kukubali imani mpya na Ali hawezi kuchelewesha mwitiko wake kwa wito wa Mola wake Mlezi. Muumba wa Abu Talib na mwanawe anayo haki zaidi ya kutiiwa kuliko Abu Talib. Inajulikana sana kwamba Ali alikuwa Mwislamu wa kwanza. Ibn Hishamu aliandika kwamba Ali Ibn Abu Talib alikuwa mwanamume wa kwanza kumwamini Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na alisali naye akiwa na umri wa miaka kumi.31 Imeelezwa kwamba muda wa Swala ulipowadia, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alikuwa na desturi ya kwenda nje ya Makka, akifuatana na Ali kwa lengo la kuswali, halafu walirudi jioni. Imesimuliwa kwamba Anas Ibn Malik alisema: “Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alipewa Utume wake siku ya Jumatatu na Ali akamwamini Jumanne.”32 Muhammad Ibn Majah kwenye Sunan yake na Al-Hakim kwenye Mustadrak aliandika kwamba Ali alisema: “Mimi ni mja wa Mwenyezi Mungu na ndugu wa Mtukufu Mtume Wake (s.a.w.w.) na mimi ni muumini mkubwa kuliko wote kwenye Utume wake. Hakuna asemaye hivi baada yangu isipokuwa mwongo. Niliswali kwa miaka saba kabla ya watu wengine.” 33 Al-Hakim aliandika kwamba Salman Al-Farsi alisema kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisema: “Mtu wa kwanza miongoni mwenu kunywa 31 Ibn Hishamu, Al-Siirat, (Wasifu wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.)) sehemu ya I, uk. 245. 32 Al-Hakim, Al-Mustadrak, sehemu ya 3, uk. 112. 33 Ibn Majah, Sunan Ibn Majah, sehemu ya 1, uk. 44 (hadith ya 120). 50

Page 50


Imam Ali binamu yake Mtume (s.a.w.w)Lubumba

Dr.Kanju.qxd

7/1/2011

4:36 PM

Imam Ali (a.s.) Ndugu yake Mtume Muhammad (s.a.w.) kutoka kwenye Haudhi mnamo Siku ya Hukumu ni Mwislamu wako wa kwanza Ali mwana wa Abu Talib.” 34 Imam Ahmad Ibn Hanbal aliandika kwamba Maaqal Ibn Yasar alisema kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alimwambia mwanawe Fatimah: “Hungefurahi kwamba nimekuoza kwa Mwislamu wa kwanza katika taifa langu, yeye ni mjuzi na mwenye hikima sana.”35

Uislam wake ulikuwa na thamani gani? Wale wanaohoji kuhusu Ali kuwa Mwislamu wa kwanza si wengi. Lakini wapo wale wanaobisha kuhusu ubora wa kutangulia kwake kuingia kwenye Uislamu kukilinganishwa na kuingia kwenye imani mpya kwa masahaba wengine maarufu ambao Uislamu wao ulitanguliwa na Ali. wanahoji kwamba: Ali (a.s.) alikuwa bado katika mwaka wake wa kumi wa umri wake, hivyo isingetegemewa kutoka kwa mtoto kama huyo kufikiri kama mtu mzima na kutegemeza maoni yake kuchagua baina ya mambo yaliyomkabili. Yeye, kwa usahihi zaidi, anategemewa kuingia kwenye Uislamu si kwa sababu ya fikra safi lakini ni kwa sababu ya mwambatano wake na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), kwani yeye alilelewa na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kama mmojawapo wa familia yake. Kama Ali angekuwa mtoto wa kawaida hoja hii ingekubalika. Lakini Ali (a.s.) hakuwa mtoto wa kawaida wakati wa utoto wake. Ushahidi wote unaonesha kwamba alikuwa mmojawapo wa watu wenye kipaji ambao walikomaa katika miaka yao ya mwanzo na kuwazidi watu wazima wa kawaida katika kuelewa ukweli na maadili ya kiwango cha juu. Kama Ali (a.s.) angekuwa amepata msukumo kutokana na mwambatano wake kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), hangemuomba Mtukufu Mtume 34 Al-Hakim, Al-Mustadrak, sehemu ya 3, uk. 112. 35 Imam Ahmad, Al-Musnad, sehemu ya 3, uk. 136. 51

Page 51


Imam Ali binamu yake Mtume (s.a.w.w)Lubumba

Dr.Kanju.qxd

7/1/2011

4:36 PM

Imam Ali (a.s.) Ndugu yake Mtume Muhammad (s.a.w.) (s.a.w.w.) muda wa kutaka ushauri kutoka kwa baba yake. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alikuwa mlezi na mwalimu wake na Ali (a.s.) alikuwa tayari kufuata maelekezo yake ya maadili. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alikuwa na desturi ya kunyanyua bendera ya maadili yake kwa ajili yake kila siku na Ali (a.s.) alikuwa akifuatana naye kama mtoto anavyomfuata mama yake. Hakumwomba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) ampe muda wa kushauriana na baba au afikiri yeye mwenyewe iwapo kama angefuata mafundisho yake yoyote ya maadili mema. Lakini alipompatia dini mpya alimuomba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) ampe muda wa kupata ushauri kutoka kwa baba yake. Alitafakari sana mnamo usiku wa siku hiyo, na ukweli ulipodhihiri wazi kwake, aliamua kutokutaka ushauri kutoka kwa baba yake, na haraka sana alikubali wito wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Alikwenda kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) huku akitangaza Uislamu wake na alikuwa anatamka maneno yake ya hekima ambayo wala hapana mtoto wa kawaida ama mtu mzima wa kawaida angeweza kufikiria. Wito wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kwa Ali (a.s.) unatuambia kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) hakumfikiria Ali kama mtoto wa kawaida. Katika historia hatukuona kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alikwishampa wito mtoto yeyote mwingine isipokuwa Imam Ali (a.s.). Alikuwa na desturi ya kuwaita wanaume na wanawake tu, akitumaini watoto wao wangewafuata wazazi wao, kwa sababu watoto hawawezi kujiamulia mambo wao wenyewe au kupambanua uadilifu na dhambi. Alimpendelea Ali (a.s.) kwa kumlingania akubali imani mpya ambapo alikuwa na umri wa miaka kumi. Kwa kweli, alimpa Ali (a.s.) sifa mbili za pekee: Alikuwa mtoto pekee aliyemlingania kwenye imani na zaidi ya yote, alimlingania yeye kabla ya kumlingania mwanamume mtu mzima yeyote. Ningependa kusema kwamba kutia shaka juu ya umuhimu wa Ali (a.s.) kukubali imani kwa sababu ya umri wake mdogo haiwafikiani na imani 52

Page 52


Imam Ali binamu yake Mtume (s.a.w.w)Lubumba

Dr.Kanju.qxd

7/1/2011

4:36 PM

Imam Ali (a.s.) Ndugu yake Mtume Muhammad (s.a.w.) yetu kuhusu hikima ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na usahihi wa maoni yake. Tukio ambalo tutaliangalia katika Sura ifuatayo linaonesha kwamba maoni ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kuhusu Ali (a.s.) hayakubaliani na maoni ya wale wanaohoji kinyume chake. Al-Jahith na wanachuo wengine walijaribu kudhalilisha thamani ya Uislamu wa Ali (a.s.) kwa sababu ya udogo wa umri wake. Walipuuza ukweli kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alimchukua yeye kama waziri na ndugu ambapo Ali (a.s.) alikuwa hajavuka umri wa miaka kumi na tatu. Hali hii ilitokea kwenye mkutano wake na ndugu zake wa karibu nyumbani kwake mjini Makka. Si tu kwamba alimpa Ali sifa hizi, lakini pia aliwaambia watu waliohudhuria wamtii.

*

*

*

53

*

*

Page 53


Imam Ali binamu yake Mtume (s.a.w.w)Lubumba

Dr.Kanju.qxd

7/1/2011

4:36 PM

Imam Ali (a.s.) Ndugu yake Mtume Muhammad (s.a.w.)

SURA YA TANO. NDUGU NA WAZIRI. Katika kipindi cha miaka mitatu ya mwanzo wa Utume, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) hakuwalingania watu hadharani kuhusu imani mpya. Ujumbe ulibakia kuwa mazungumzo yasiyotangazwa kwani kutangazwa kwake kungesababisha mapambano na koo za watu wa Makka. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alijua kwamba makabila ya Makka na umma wa Waarabu hawangesita kutumia njia zozote za nguvu dhidi yake kama angedai wao wabadili dini yao. Hata hivyo, mapambano haya hayakukwepeka na yalitegemewa kuwa na hatari nyingi. Ujumbe haukutangazwa ili uwe siri. Ujumbe uliteremshwa ili uwabadilishe wanadamu na kubadilisha itikadi za watu na mwenendo wa maisha yao. Hili lisingetambuliwa isipokuwa kwa kuita kwa sauti pana, kuwaonya wazi wazi na kuwapa habari kuhusu ujumbe huo. Ili ujumbe wa dini mpya au itikadi mpya ufanikiwe, mtu mwenye ujumbe na wafuasi wake lazima wawe na uhuru wa kuongea na utekelezaji. Watu wa wastani hawana ujasiri wa kukubali itikadi mpya ambapo kukubali itikadi hiyo husababisha wao kupambana na jamii ambayo haitambui uhuru wa mtu binafsi. Jamii ya aina hii, kwa tabia yake hupenda kutumia nguvu, na si watu wengi ambao wapo tayari kuteseka kwa kupoteza nafsi zao, utajiri wao na uhai wao kwa sababu ya maadili. Ili kufanya uenezaji wa itikadi mpya kwenye jamii kama hii kuwezekana, uhuru wa kusema na kutekeleza lazima ulindwe na kuwekwa salama kwa ajili ya watu watakaoweza kuingia kwenye imani mpya. Vinginevyo, wangeogopa sana kubadili dini yao. Hii ina maana kwamba itikadi mpya itafanikiwa kwa kiwango kidogo tu, kama yatakuwepo mafanikio yoyote. Ni wale tu mashujaa wenye ujasiri usio wa kawaida wangeweza kujitokeza bila hofu, na watu wa aina hii sio wengi. 54

Page 54


Imam Ali binamu yake Mtume (s.a.w.w)Lubumba

Dr.Kanju.qxd

7/1/2011

4:36 PM

Imam Ali (a.s.) Ndugu yake Mtume Muhammad (s.a.w.) Kuhusu mtu wa ujumbe, uwezekano wa kufaulu kwake ni mdogo sana pale ambapo uhai wake na uhuru wa jamaa zake havikulindwa ingawa anaweza kuwa shujaa mkubwa. Kujitokeza kwake bila woga hakuleti ushindi kwenye jamii yenye vurugu. Kifo chake cha kuuwawa au cha kusababishwa na njia nyingine kabla ya kuanzisha dini yake kitasitisha ujumbe wake wote. Hivyo, haja ya kwanza kwa ajili ya kufanikiwa kwa dini mpya, katika jamii isiyo ya kidemokrasia, ni ngao ya kinga kuzunguka uhai wa mtu mwenye ujumbe na kulinda uhuru wa ndugu zake. Anahitaji wasaidizi madhubuti ambao watakuwa tayari kujitoa mhanga kwa ajili ya kumlinda kiongozi wao na ujumbe wake. Kama watu wa aina hiyo hawapatakani, ni muhimu pawepo na angalau msaidizi mmoja mwenye sifa zisizo za kawaida, ambaye anafanana na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kuhusu uaminifu, ujasiri na nguvu. Mtu wa aina hii angetegemewa kupatikana miongoni mwa ndugu zake mtu mwenye ujumbe kwani ndugu wanatumaniniwa kuwa na huruma zaidi kwake kuliko watu wengine. Qur’ani Tukufu inatuambia hivyo pale Musa alipopokea amri ya Mwenyezi Mungu: “Nenda kwa Firauni kwani hakika yeye amechupa mipaka,” akamuomba Mola wake Mlezi ampe msaidizi awe waziri wake kutoka kwenye watu wa familia yake!

“Musa akasema: Ewe Mola wangu Mlezi! Nikunjulie kifua changu. Na unifanyie wepesi kazi yangu. Na ulifungue fundo lililo katika ulimi wangu, wapate kufahamu maneno yangu. Na nipe waziri katika watu 55

Page 55


Imam Ali binamu yake Mtume (s.a.w.w)Lubumba

Dr.Kanju.qxd

7/1/2011

4:36 PM

Imam Ali (a.s.) Ndugu yake Mtume Muhammad (s.a.w.) wangu, Harun ndugu yangu. Kwake yeye niongeze nguvu zangu. Na umshirikishe katika kazi yangu.” Sura 20, Aya 25-32. Muhammad (s.a.w.w.) ni wa mwisho katika Mitume. Ujumbe wake ni hitimisho la ujumbe wote wa Mbinguni. Kwa hiyo, ujumbe wake, lazima ushinde na kudumu milele. Mwenyezi Mungu huendesha mambo ya dunia kwa kawaida kwa kufuata sharia ya asili na athari na kupitia uelekeo wa asili. Kwa hiyo, Hakumuamuru Mtukufu Mtume Wake Muhammad (s.a.w.w.) kukabiliana na jamii yote kwa wakati moja katika kuwalingania kwenye Uislamu, kwa sababu, hii ingesababisha kutofautiana kwa ujumbe badala ya kufanikiwa. Alimtaka aende pole pole katika mahubiri yake, Alimpa amri (baada ya miaka mitatu tangu mwanzo wa Utume wake) kuanza na ndugu zake wa karibu. Kutoka kwenye Qur’ani Tukufu:

“Na uwaonye jamaa zako walio karibu nawe. Na washushie bawa la upole wanaokufuata miongoni mwa waumini.”Qur'ani 26: 214-215. Wakati amri hii iliyopoteremka, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) aliwaita watu wa kizazi cha Abdul Mutalib (walikuwa wanamume arubaini) kwenye karamu ya chakula kidogo na maziwa. Walikula na kunywa hadi wakashiba. Halafu Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alizungumza akasema: “Enyi kizazi cha Abul-Muttalib, kwa jina la Mwenyezi Mungu simjui kijana yeyote miongoni mwa Waarabu ambaye ameleta kwa watu wake kitu kizuri kuliko kile ambacho mimi nimewaleteeni nyinyi, nimewaleteeni wema wa dunia hii na ile ya kesho Akhera, na Mwenyezi Mungu Ameniamuru niwaite nyinyi mkubaliane nacho. Ni nani miongini mwenu ambaye yu tayari kuwa waziri wangu katika ujumbe huu, na atakuwa ndugu yangu, wasii wangu na mrithi wangu?” 56

Page 56


Imam Ali binamu yake Mtume (s.a.w.w)Lubumba

Dr.Kanju.qxd

7/1/2011

4:36 PM

Imam Ali (a.s.) Ndugu yake Mtume Muhammad (s.a.w.) Hakuna ambaye aliyejitokeza isipokuwa Ali ambaye alikuwa mdogo kwa umri miongoni mwao. Alisimama na akasema: “Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), mimi nitakuwa waziri wako katika ujumbe huu.” Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alirudia tena wito wake lakini hapana yeyote aliyeitika isipokuwa Ali ambaye alirudia maneno yake. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) aliweka mkono wake kwenye shingo ya Ali na akasema: “Huyu ni ndugu yangu, wasii wangu na mrithi wangu kwenu. Msikilizeni na muwe watiifu kwake.” Wakacheka, wakimwambia Abu Talib: “Amekuamuru umsikilize mwanao na umtii yeye.”36 Hivyo, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) aliwaita ndugu zake wa karibu wakubali kuingia kwenye Uislamu lakini madhumuni yake yalikuwa kutafuta mtu miongoni mwao ambaye angemsaidia katika kueneza ujumbe. Kuukubali Uislamu ni muhimu sana lakini muhimu zaidi kumpata mtu miongoni mwa waliosilimu ambaye atakuwa tayari kwa lolote kuhakikisha ujumbe huo unafanikiwa. Na mamilioni mangapi ya Waislamu wa leo hawako tayari kuuhami Uisilamu hata angalau kwa kiwango kidogo sana!

36 Hadith hii imeandikwa na waandishi wafuatao: Ibn Al-Athiir, Al-Kamil, sehemu ya 2, uk. 22. Al-Tabari, History of Nations, Messengers and Kings, sehemu ya 2, uk. 217. Abu Al-Fida kwenye kitabu chake cha Tarikh, sehemu ya I, uk. 116. Imam Ahmad, Al-Musnad, sehemu ya I, uk. 111-119. Ibn Is’haq, Al-Baihgai kwenye Al-Dala’il (Al-Muttaqi Al-Hindi, Muntakhab Kanzul-Ummal kwenye pambizo ya Musnad Ahmad, sehemu ya 5, uk. 41-42, chapa ya Beiruti, mchapishaji Sades). 57

Page 57


Imam Ali binamu yake Mtume (s.a.w.w)Lubumba

Dr.Kanju.qxd

7/1/2011

4:36 PM

Imam Ali (a.s.) Ndugu yake Mtume Muhammad (s.a.w.)

HADITH ZINAZOPINGANA. Masheikh wawili: Al-Bukhari na Muslim hawakuandika tukio hili muhimu licha ya kwamba waandishi wengi wa historia na Hadith wamelitaja tukio hili. Muslim na wanahadith wengine walioandika taarifa ya tukio lililotokea baada ya tukio hili, waliandika taarifa kuhusu kutokeza kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) juu ya mlima Al-Safa na wito wake kwa watu wa koo za Kureishi za watu wa Makka na wito wake kwao kuamini katika imani mpya. Muslim na waandishi wengine waliandika taarifa ya kulitaja tukio hili lililochelewa na kulifunganisha na Aya ya kuwaonya ndugu wa karibu wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Muslim aliandika kwamba Abu Hurairah alihadithia ifuatavyo: Wakati Aya hii ilipoteremshwa “Na uwaonye ndugu zako wa karibu” Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) aliwaita Makureishi na walikwenda pamoja. Akawaambia kwa ujumla na hususan. Akasema: Enyi dhuriya wa Kaab Ibn Luay, jiokoeni msije mkaingia Jahanamu. Enyi watoto wa Murrah Ibn Kaab, jiokoeni msije mkawa watu wa Jahanamu. Enyi dhuriya wa Hashim, jiokoeni kutoka Jahanamu. Ewe Fatimah jiokoe usije ukatupwa Jahanamu. Kwani mimi sina uwezo wa kuwapeni ulinzi dhidi ya ghadhabu kutoka kwa Mwenyezi Mungu isipokuwa nyinyi mnao uhusiano wa kindugu na mimi ambao ningetaka kuuangalia kwa makini.”37 Inashangaza kuona kwamba Mwenyezi Mungu alimuamuru Mtukufu Mtume Wake (s.a.w.w.) kuwaonya ndugu zake wa karibu sana, ambao walikuwa dhuriya wa Abul Muttalib, lakini Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) aliwaita dhuriya wa Kaab Ibn Lu’ay na dhuriya wa Murrah Ibn Kaab ambao ni ndugu wa mbali sana. Haiingii akilini kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) anakataa kutii amri ya Mola Wake Mlezi. Na jambo la kushangaza zaidi ni kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alimuita Binti yake Fatimah hadharani, ili ajikomboe kutoka Jahannam 37 Muslim, Sahih Muslim, sehemu ya 3, uk. 79-80. 58

Page 58


Imam Ali binamu yake Mtume (s.a.w.w)Lubumba

Dr.Kanju.qxd

7/1/2011

4:36 PM

Imam Ali (a.s.) Ndugu yake Mtume Muhammad (s.a.w.) lakini Binti huyu alikuwa msichana Mwislamu aliyetakasika sana ambaye baba yake na mama yake walikuwa wazazi watakatifu zaidi ya wote. Fatimah, wakati wa kuteremshwa kwa Aya hiyo hapo juu, kwa mujibu wa waandishi wa historia, alikuwa na umri imma wa miaka miwili au miaka minane.38 Ni jambo lisilo na mantiki kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alimuambia mtoto mwenye umri wa miaka miwili au kwamba alimweka msichana Mwislamu mtakatifu (ambaye alikuwa hajabalehe mwenye umri usiozidi miaka minane) katika daraja moja na wapagani wa Banu Kaab na Banu Murrah. Na la kustaajabisha zaidi ni Hadith ya Aisha ambayo iliandikwa na Muslim kwenye Sahih yake kama ifuatavyo: “Aya ya kuwaonya ndugu ilipoteremshwa, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisema: “Ewe Fatimah binti Muhammad, Safiya, binti Abdul Mutalib, sina jinsi yoyote katika uwezo wangu kuweza kuwalinda nyinyi dhidi ya hasira ya Mwenyezi Mungu. Niombeni chochote mnachotaka kutoka katika utajiri wangu.”39 Hadith hii haikubaliani na ile ya nyuma, kwani hii inatoa habari kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) aliwaambia dhuriya wa Abbul Muttalib peke yao, ambapo Hadith nyingine ilitoa habari kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) aliwaambia hadharani, hasa zaidi si kwa wengine isipokuwa ukoo wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Na jambo la kustaajabisha katika Hadith hii ni kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alimuambia hadharani hususan binti yake mdogo Fatimah wakati akiwa juu ya mlima Safa wakati ambapo anaishi naye na alikuwa anamuona wakati wote. Pia inastaajabisha kwamba wito aliouelekeza kwa binti huyo na watu wengine ambao ni dhuriya wa Abdul Muttalib haukuwa na ujumbe wowote, kama vile kuwaita ili wamuabudu Mwenyezi Mungu au kuepuka ibada ya masanamu. 38 Al-Hakim kwenye Mustadrak yake sehemu ya 3, uk. 61, alitaarifu kwamba alizaliwa miaka 41 baada ya kuzaliwa kwa baba yake. 39 Muslim, kwenye Sahih yake, sehemu ya 3, uk. 79-80. 59

Page 59


Imam Ali binamu yake Mtume (s.a.w.w)Lubumba

Dr.Kanju.qxd

7/1/2011

4:36 PM

Imam Ali (a.s.) Ndugu yake Mtume Muhammad (s.a.w.) Aidha, Aisha alikuwa hajazaliwa wakati wa tukio hili. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alifariki dunia ambapo Aisha alikuwa na umri wa miaka 18 (kumi na nane) tu.40 Na tukio hili lililotokea miaka kumi kabla ya Hijiriya (miaka ishirini kabla ya mwisho wa uhai wake). Abu Huraira pia hakushuhudia tukio hili kwa kuona kwa macho yake kwa sababu alimuona Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kwa mara ya kwanza wakati akitokea Khaybar. (mwaka wa 7 A.H) 41 Na jambo la kustaajabisha kuliko yote ni kwamba Al-Zamkhshari alisimulia kwamba Aisha binti Abu Bakr na Hafsa binti Umar, walikuwa miongoni mwa watu ambao Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) aliwalingania baada ya kuteremshwa kwa Aya hii ya onyo (ambayo iliteremshwa kabla ya kuzaliwa kwa Aisha).42 Hii kwa wazi inaonesha kwamba waandishi au wasimuliaji wa Hadith hizi walichanganyikiwa sana. Hawakutilia maanani ukweli ya kwamba Aya inamuamuru Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kuwaonya ndugu zake wa karibu sana, ambao walikuwa dhuriya wa Abdul Muttalib, na kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) hatazamiwi kukataa kutii agizo la Mwenyezi Mungu. Kile ambacho Hadith hizi inakisimulia kinapingana na Aya yenyewe, na chochote kile ambacho hakikubaliani na Qur’ani Tukufu, lazima kipuuzwe. Tukio ambalo waandishi wa historia na Hadith wanasimulia kuhusu mkutano aliofanya na ndugu zake wa karibu sana ndio njia tu pekee ya kimantiki ambayo Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alitegemewa kufuata baada ya kuteremshwa kwa Aya hii.

* * * * *

40 Ibn Saad, Al-Tabaqat, sehemu ya 8, uk. 61. 41 Al-Tabaqat, sehemu ya 4, uk. 327. 42 Ali Ibn Burhanud-Din Al-Halabi, Al-Siirat Al-Halabiyah, (Wasifu wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.)) Sehemu ya I, uk. 321. 60

Page 60


Imam Ali binamu yake Mtume (s.a.w.w)Lubumba

Dr.Kanju.qxd

7/1/2011

4:36 PM

Imam Ali (a.s.) Ndugu yake Mtume Muhammad (s.a.w.)

ZAWADI ILIYOTOLEWA. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alikuwa karibu sana kupambana na waabudu masanamu. Kwa hiyo, alihitaji waziri ambaye alikuwa na ujasiri, uaminifu, uimara na umadhubuti kama wa kwake. Wanaume arobaini kutoka dhuriya wa Abdul-Muttalib wangekuwa rasilimali muhimu kwa Uislamu kama wangekubali kusilimu. Lakini kama walikuwa watu wa kawaida, hawangeweza kukabiliana na umma wa Makka na Waarabu wa Makka. Hivi karibuni Mwenyezi Mungu atamuamuru Mtukufu Mtume Wake (s.a.w.w.) kupanua wito wake kwa Waarabu wote, halafu kwa mataifa mengine pia, na watakataa kuitikia wito huo kwa vurugu kwa miaka mingi iliyofuata. Watu arobaini wa kawaida wangeogopeshwa na uadui wa Makka na Bara Arabu; lakini mtu mmoja mwenye ujasiri ataweza kukabiliana na chochote ambacho Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) angepambana nacho. Kwa hili, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) aliwazungumzia kuhusu lengo hili muhimu baada ya utangulizi mfupi sana akisema: “Ni nani miongoni mwenu yu tayari kuwa waziri wangu katika kazi hii? (yeyote ambaye atakuwa tayari kufanya hivyo), atakuwa ndugu yangu, wasii wangu na mrithi wangu.� Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) angewezaje kutoa ahadi kama hiyo? Tuchukulie kwamba wote au wengi wao walikubali kusilimu na kuwa Waislamu hapo hapo kwenye mkutano na wakamuahidi msaada wao. Angefanya nini? Ingeweza kufikiriwa kwamba watu wote hao wangekuwa ndugu zake, lakini ni vigumu sana kutambua kwamba wote wangekuwa mawasii wake. Na kama hilo linaweza kudhaniwa, haingewezekana kwamba kila mmoja wao angekuwa mrithi wake. - Kwa uchambuzi kido61

Page 61


Imam Ali binamu yake Mtume (s.a.w.w)Lubumba

Dr.Kanju.qxd

7/1/2011

4:36 PM

Imam Ali (a.s.) Ndugu yake Mtume Muhammad (s.a.w.) go tu mtu anaweza kulitambua jibu lake. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alikuwa anatambua vema kwamba walio wengi miongoni mwa watu hao hawangekuwa na ujasiri wa kuahidi kwake msaada halisi kwa Uislamu kwani msaada wa aina hiyo ungewapambanisha na jamii na kuwaingiza kwenye vita ambavyo vingekwisha kwa kupata hasara ya uhai wao. Msaidizi wa kweli wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) lazima awe mtu ambaye si wa kawaida, na watu waliohudhuria walikuwa watu wa wastani tu. Lilitokea kwenye mkutano linathibitisha wazi ukweli ambao Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alitegemea kuuona. Hakuna kati yao aliyekuwa tayari kujitokeza wala kuwa na moyo wa kudiriki kuahidi kwake msaada isipokuwa mtu mmoja tu, na miaka iliyofuata ilithibitisha kwamba mtu huyo ndiye aliyefaa kwa kazi hiyo. Kwa nini pawepo na zawadi hizi maalum? Ni wazi kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alitaka kufuata nyayo za Musa (a.s.). Musa (a.s.) alimuomba Mola wake ampe waziri kutoka miongoni mwa familia yake, na hapa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) aliwakusanya ndugu zake wa karibu akitafuta kutoka miongoni mwao waziri. Waziri wa Musa (a.s.) alikuwa ndugu yake Harun. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) hakuwa na kaka wa kuzaliwa naye kwa sababu alikuwa ni mtoto wa pekee kwa wazazi wake, Abdullah na Amina. Kufuata mwendo wa Musa (a.s.) alitaka kumfanya waziri wake awe ndugu yake pia. Mwendo huo huo hutumika katika nafasi ya mrithi. Harun alikuwa mrithi wa Musa (a.s.) miongoni mwa watu wake wakati Musa (a.s.) alipokwenda mlimani kusikiliza maneno ya Mola Wake na akawa katika faragha kwa siku arobaini. Kabla ya kwenda mlimani, alimwambia Harun, kwa mujibu wa Qur’ani Tukufu:

62

Page 62


Imam Ali binamu yake Mtume (s.a.w.w)Lubumba

Dr.Kanju.qxd

7/1/2011

4:36 PM

Imam Ali (a.s.) Ndugu yake Mtume Muhammad (s.a.w.) “Utakuwa mrithi wangu miongoni mwa watu wangu na tenda wema na usifuate mwenendo wa waovu.” Qur'ani; Sura 7:142 Alichosema Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kwa Ali, miaka mingi baada ya tukio hili, huunga mkono hali hii na kuthibitisha usahihi wake. Alipomwacha Madina wakati wa safari yake ya kwenda Tabuk, alimwambia: “Ali, je, haitakuridhisha wewe kuwa kwangu kama Harun kwa Musa (a.s.) isipokuwa kwamba hakutakuwa na Mtume mwingine baada yangu?”43 Kumpa Ali vyeo vyote vya Harun isipokuwa utume humaanisha kwamba Ali alikuwa kama Harun katika vyeo vingine vilivyobakia: uwaziri, udugu na urithi. Tamko la Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kwenye mkutano uliotajwa hapo juu na tamko hili yanaafikiana na yanashabaha kwenye lengo moja.

KWA NINI ZAWADI KUBWA HIVYO KWA AJILI YA UJUMBE? Inaweza kusemwa: Kwa nini Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) ampe Ali zawadi kubwa hivyo kwa ajili ya Ujumbe wake? Je, cheo cha msaidizi (au waziri) wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) si zawadi kubwa? Jibu ni kwamba uwaziri wa Ali si zawadi kutoka kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) bali ni kama kusema ni zawadi kutoka kwa Ali. Wilaya hii au usaidizi huu ni kujitoa muhanga kukubwa upande wa waziri. Ili kuliweka hili wazi, nigependa kusema kwamba kuna aina mbili za ujumbe: Idara ya kuendesha mambo ya dola iliyopo. Mtu wa idara kama hiyo ni mshauri kwa kiongozi wa dola kwa mamlaka ya kutoka kwa mkubwa wake 43 Muslim katika Sahih yake, sehemu ya 15, uk. 175. Al-Bukhari aliiandika katika Sahih yake sehemu ya 5. 63

Page 63


Imam Ali binamu yake Mtume (s.a.w.w)Lubumba

Dr.Kanju.qxd

7/1/2011

4:36 PM

Imam Ali (a.s.) Ndugu yake Mtume Muhammad (s.a.w.) au kutoka kwenye mkutano (wa Bunge) au kutoka kwa watu. Idara ya kuasisi na kusimamisha dola. Hapa waziri atakuwa msaidizi wa mkubwa wake katika kufanikisha kusimamisha dola ambayo haikuwepo au katika kueneza imani mpya ambayo bado haijafahamika kwa watu. Kazi ya waziri wa aina hii ni kubeba yeye na mkubwa wake, wajibu mkubwa sana wa kuanzisha imani na dola na kukabiliana pamoja naye hatari zote. Atakuwa ngao yake ya kumlinda wakati wote, akiwa tayari kujitoa muhanga kwa ajili ya usalama wa mkubwa wake. Idara ya aina ya kwanza ni zawadi kutoka kwa kiongozi wa serikali kwenda kwa waziri wake na kupewa heshima kubwa kwa kumnyanyua na kumpa cheo kikubwa. Idara ya aina ya pili si zawadi kutoka kwa mkubwa bali ni zawadi kutoka kwa waziri. Ni muhanga mkubwa ambao waziri anaoutoa wakati wote kwa ajili ya kumlinda mkubwa wake na kuwezesha ujumbe wake ufaulu. Waziri wa aina hii na mkubwa wake hukutana na hatari nyingi na matatizo ambayo hayawezi kuwapata watu wengi. Waziri ambaye Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alikuwa anamtafuta kutoka miongoni mwa ukoo wake alitoka kwenye aina ya pili wala sio kutoka aina ya kwanza. Hapakuwepo na dola iliyoanzishwa, wala hapakuwepo na jumuiya ya Waislamu. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) hakuwa (na hata baada ya Dola ya Kiislamu kuanzishwa) anahitaji mshauri wa kumshauri yeye jinsi ya kueneza ujumbe au kuasisi dola. Alikuwa anahitaji mtu mwenye uaminifu na ushujaa usio wa kawaida akiwa mtiifu kikamilifu kwa Mwenyezi Mungu na Mtukufu Mtume Wake (s.a.w.w.). Mtu ambaye anastahiki kuwa ndugu yake Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na mrithi wake baada ya kuondoka kwake hapa duniani lazima awe na nafsi ambayo ni takatifu kiasi cha kutosha kuweza kuwa kama nyongeza ya nafsi ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) mwenyewe. Lazima afanane naye kwa 64

Page 64


Imam Ali binamu yake Mtume (s.a.w.w)Lubumba

Dr.Kanju.qxd

7/1/2011

4:36 PM

Imam Ali (a.s.) Ndugu yake Mtume Muhammad (s.a.w.) kiwango cha juu katika ujuzi, hikma na awe mpingaji wa masilahi binafsi. Kwa maneno mengine, lazima awe nakala halisi ya Mtume huyu mkuu. Ndio, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) hakuwa anahitaji mtu ambaye angemshauri kuhusu njia ya busara ambayo angepaswa kuchukua. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alikuwa mwenye akili mno na busara sana. Alikuwa tu na haja ya waziri ambaye angemsaidia kwa tendo lake kubwa, muhanga na kazi za kiushujaa. Waziri huyo angekuwa mpokeaji wa ujuzi wake na kuweza kumwakilisha Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) itokeapo haja ya kufanya hivyo na kukalia kiti chake baada yake.

MTUKUFU MTUME (S.A.W.W.) HAKUTAKA KUWEPO NA VISINGIZIO Mtu asiwe na shaka hata kwa dakika moja kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) pengine alikuwa hatambui ni nani angekuwa waziri wake kabla ya kuzungumza na watu wa ukoo wake. Yeye alijua kwamba hapakuwepo na yeyote miongoni mwa kundi hilo ambaye alikuwa na sifa za waziri anayehitajika isipokuwa Ali. Hata hivyo, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) hangemchagua Ali kuchukua kazi hiyo kubwa na kuacha nafasi ya visingizio miongoni mwa ndugu wengine. Hangeruhusu vizazi vijavyo viseme kwamba kama angemuomba mtu mwingine badala ya Ali angewapata watu wengi wenye sifa zinazofaa. Hangeturuhusu tuanze kushangaa iwapo kama Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alikuwa na upendeleo kwa Ali na akamuona kuwa na sifa bora bila ya sababu iliyo dhahiri. Palikuwepo umuhimu wa kuwapa watu wengine wa ukoo wake fursa ya kuonesha msimamo wao na kwa hiyo kudhihirisha ustahiki wa Ali.

65

Page 65


Imam Ali binamu yake Mtume (s.a.w.w)Lubumba

Dr.Kanju.qxd

7/1/2011

4:36 PM

Imam Ali (a.s.) Ndugu yake Mtume Muhammad (s.a.w.)

MATOKEO YA MKUTANO WA NYUMBA YA MTUKUFU MTUME (S.A.W.W.). Mkutano ambao Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) aliitisha na kuwakusanya dhuriya wa Abdul-Muttalib ulizaa mapatano ya kipekee ambayo historia haijapata kushuhudia tukio kama hilo wala haijashuhudia tukio lililo sawa na hilo kwa ubora na malengo ya juu. Ni mapatano kati ya Mtume wa mwisho wa Mwenyezi Mungu, Mfikishaji wa Ujumbe wa Mbinguni, na waziri wake Ali Ibn Abu Talib ambaye wakati wa makubaliano hayo umri wake haukuwa zaidi ya miaka kumi na tatu (13). Kiini cha makubaliano kilikuwa na mambo mawili: Kiapo juu cha Ali kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kuwa atakuwa waziri wake katika kutekeleza ujumbe wake huu mkubwa. Ahadi juu ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), iliyotolewa katika muundo wa tangazo ambamo aliwaambia watu wa ukoo wake wakati mkono wake ukiwa juu ya kichwa cha Ali: “Huyu ni ndugu yangu, wasii wangu, na mrithi wangu kwenu. Msikilizeni yeye na mtiini yeye.� Inafaa kuangalia kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alitimiza ahadi yake mara moja hapo hapo kwenye mkutano. Hakungoja Ali atimize ahadi yake. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) aliweka ahadi yake katika muundo wa malipo ya mara moja kwa waziri wake. Alitangaza wakati akiwa bado mkutanoni kwamba Ali alikuwa ndugu yake na akamfanya kuwa wasii wake na mrithi wake. Hakungoja Ali atimize ahadi yake kwa sababu alijua kwamba neno la Ali lilibeba maana yake kamili na kwamba neno lake na tendo lake ni vitu vilivyoungana na kamwe havingepingana vyenyewe kwa vyenyewe. Ali alijiweka chini ya mamlaka ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) tangu hapo alipotamka ahadi yake. Miaka kadhaa ilipita kabla ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) hajataka msaada wa haraka wa Ali. Baba yake Ali alikuwa bado hai na mwenye nguvu, akilinda maisha ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), na 66

Page 66


Imam Ali binamu yake Mtume (s.a.w.w)Lubumba

Dr.Kanju.qxd

7/1/2011

4:36 PM

Imam Ali (a.s.) Ndugu yake Mtume Muhammad (s.a.w.) waumini walikuwa bado hawajaruhusiwa na Mwenyezi Mungu kupigana na maadui zao. Pia hatari dhidi ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) ilikuwa haijafikia upeo wa kutisha. Wakati wa hatari ulitokeza miaka kumi baada ya mkutano na baada ya kifo cha Abu Talib. Watemi wa Makka wakiwa kwenye ‘nadwa’ (chama chao) walishauriana na kuamua kuyakatisha maisha ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alimuita waziri wake kuanza kutekeleza ahadi yake. Hivyo usiku wa ukombozi ulifika na Ali alikuwa mkombozi wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na mdhamini wake. Ali alitamka neno lake ambapo alitambua ukubwa wa kazi ambayo kwayo aliahidi kumsaidia Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Alikuwa anatambua kabisa kwamba kwa sababu ya ukubwa wake kazi hiyo ilionekana kama haingewezekana. Kazi ililenga kubadilisha itikadi za jamii na mwenendo wake wa maisha. Ililenga katika kuifanya jamii ifuate kanuni za ki-Mungu ambazo hazikubaliani na desturi zao. Ali alitambua kwamba kazi hii ingepata pingamizi kutoka pande zote za jamii. Ali alitambua kwamba kufaulu kwa kazi hii hakungepatikana hadi hapo ambapo ingeshinda makundi yote ya uadui na kwamba umuhimu wa kuanzisha dola ya Kiislamu iliyotegemewa kwenye msingi wa kanuni mpya zilizoteremshwa ulikuwepo. Dola ya aina hii ingelinda kanuni hizo na uhuru wa wafuasi wao. Kazi kama hii haiwezi kutekelezwa hata na taifa lote, bila kujali ushindi wake dhidi ya makundi ya upinzani. Kazi hii ndio ambayo Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alidhamiria kupata na ni kazi ambayo Ali aliahidi kusaidia kwa msaada wake na kwa kukabiliana na yote yale ambayo yangempata Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) katika kuifanikisha kwake. Kwa kuwa mkutano ulikubali matokeo haya, ilitegemewa kwamba Ali atatimiza ahadi yake kubwa kama ilivyotegemewa, kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) angetangaza siku zijazo kwa Waislsamu wote kile alichotangaza 67

Page 67


Imam Ali binamu yake Mtume (s.a.w.w)Lubumba

Dr.Kanju.qxd

7/1/2011

4:36 PM

Imam Ali (a.s.) Ndugu yake Mtume Muhammad (s.a.w.) kwa ndugu zake wa karibu kuhusu Ali. Tutaona kwenye kurasa zifuatazo kwamba Ali alitimiza alichoahidi kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) baada ya kuanzishwa kwa dola ya Kiislamu alitangaza kwa Waislamu kile alichotangaza kwa watu arubaini dhuriya wa Abdul Muttalib.

* * * * * *

SURA YA SITA MKOMBOZI Ongezeko la haraka la idadi ya Waislamu Madina liliwatia moyo watu wa Madina na likawapa msukumo wa kumuita Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) aende jijini kwao, kwa kutoa ahadi ya kumlinda yeye kwa uwezo wote. Kwa ahadi hii Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alikubali mwaliko wao. Makafiri wa Makka walitambua nini kilichofanyika. Walishauriana kwa siri na walihitimisha kwamba kifo cha Muhammad ilikuwa ndio tu njia ya kuzuia kuenea kwa Uislamu. Kutoka katika kila ukoo wa Makka, mtu mwenye nguvu na jasiri aliteuliwa kumshambulia Muhammad wakati wa usiku muafaka. Hivyo koo zote za Makka zingeshiriki katika mauaji yake. Muweza wa Yote alimfichulia siri hiyo Mtukufu Mtume Wake (s.a.w.w.) na akamuamuru aondoke Makka usiku huo wa mauaji. Kuondoka kwake akiwa chini ya uchunguzi wao kulitazamiwa kumpambanisha ana kwa ana na hatari. Kama nyumba zingine za Makka, nyumba ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) ilikuwa haikuhifadhiwa na kutoonekana kwa macho. Mtu aliyeko nje angeweza kuona mazingira ya ndani. Kwa hiyo, kitanda cha Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kilitakiwa kiwe na mtu; vinginevyo maadui wangegundua kwamba ameondoka na wangeweka vizuizi barabarani na kumtafuta 68

Page 68


Imam Ali binamu yake Mtume (s.a.w.w)Lubumba

Dr.Kanju.qxd

7/1/2011

4:36 PM

Imam Ali (a.s.) Ndugu yake Mtume Muhammad (s.a.w.) hadi wampate. Lakini yeyote ambaye amelala kwenye kitanda cha Muhammad usiku huo lazima awe tayari kufa kwani kwa hakika shambulio lilikuwa linakuja. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alimpa taarifa Ali kuhusu njama hiyo na alimuomba alale kwenye kitanda chake. Kama ilivyotegemewa, Ali wala hakusita kukubali wito huo wa hatari, wala kufikiria hatima ya maisha yake mwenyewe. Alifikiria kitu kimoja tu cha muhimu: Hatima ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). “Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu,” aliuliza “je utakuwa salama?” Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alipojibu kwa kukubali Ali alipomoka chini ardhini na kusujudu, akamshukuru Mwenyezi Mungu kwa kumhakikishia usalama Mtukufu Mtume Wake (s.a.w.w.). Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alimteua Ali kwa ajili ya kazi nyingine. Alimwagiza kutoa kwa watu wa Makka katika siku zifuatazo amana zao ambazo alizokuwa nazo Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alikuwa mhifadhi wa amana za watu wa Makka, marafiki na maadui wote kwa pamoja. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alikuwa mtu Mwaminifu kwa watu wa Makka. Si mwingine ambaye angewasilisha amana hizo kwa niaba ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) isipokuwa mdhamani na mwakilishi wake, Ali. Waandishi wa Hadith wamesimulia kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alimteua Ali kwa ajili ya kazi nyingine ya tatu katika usiku huo. Al-Hakam amesimulia kwamba Ali alisema kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alikwenda naye kwenye Kaaba (mnamo usiku huo wa Hijiriya) kujaribu kuharibu lile sanamu kubwa kuliko yote la Makureishi. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisimama juu ya mabega ya Ali ili aweze kufika kwenye paa la Kaaba lakini aligundua kuwa Ali hangehimili uzito wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Alishuka chini na akamwambia Ali apande juu na asimame kwenye mabega yake na alifanya hivyo. na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akasimama. Ali alihisi hata kama angetaka kufika mbinguni angeweza. Ali alikwenda hadi kwenye paa la Kaaba. Alilitikisa hilo sanamu kubwa zaidi 69

Page 69


Imam Ali binamu yake Mtume (s.a.w.w)Lubumba

Dr.Kanju.qxd

7/1/2011

4:36 PM

Imam Ali (a.s.) Ndugu yake Mtume Muhammad (s.a.w.) kuliko yote ambalo lilitengenezwa kwa shaba na kufungwa kwenye paa. Alipolishika sanamu hilo Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alimwambia alitupe chini. Ali alifanya hivyo na sanamu hilo likavunjika.44 Ilionekana kama vile kazi hii ilitekelezwa kabla ya wale walanjama hawajaizunguka nyumba yake Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), na kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na Ali walirudi nyumbani kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) baada ya kukamilisha kazi hii; halafu Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) aliondoka wakati maadui walikuwa wanaizunguka nyumba yake. Ali alibaki hapo ili atekeleze kazi zingine kubwa mbili: Kulala kwenye kitanda cha Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na kuwasilisha amana za watu wa Makka. Ibn Al-Athiir kwenye nakala yake ya historia (Al-Kamil) alitaarifu kwamba Malaika Jibril alimwendea Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na akamwambia asilale kwenye kitanda chake usiku huo na kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alimuamuru Ali alale kwenye kitanda chake. Na pia alimteua Ali kuwasilisha kile kilichokuwa katika mikono yake kama amana kwa wenyewe watu wa Makka na akamjulisha kwamba maadui hawatamdhuru. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alichota ukafi wa udongo na akautupa kwenye vichwa vya maadui ambao walikuwa wanaizunguka nyumba yake na aliondoka hapo bila kuonekana huku akisoma Sura ya 36 (Yasin). Walipoona kuwa kitanda cha Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kilikuwa kimelaliwa na mtu, maadui waliamini kwamba Muhammad ndiye aliyelala kwenye kitanda chake. Walisubiri hadi asubuhi na Ali alipoamka, walimtambua. “Muhammad yuko wapi?” Walimuliza. “Sijui.” Ali alijibu, “Mlimuambia aondoke na akaondoka.” Wakampiga Ali, wakampeleka Msikitini, wakamzuia kwa saa moja, halafu wakamwachia huru.45 44 Al-Hakim, Al-Mustadrak, sehemu ya 3, uk. 5 45Ibn Al-Athiir, Al-Kamil, sehemu ya 2, uk. 72 70

Page 70


Imam Ali binamu yake Mtume (s.a.w.w)Lubumba

Dr.Kanju.qxd

7/1/2011

4:36 PM

Imam Ali (a.s.) Ndugu yake Mtume Muhammad (s.a.w.) Pia imesimuliwa kwamba wakati weupe wa alfajiri ulipokaribia, walikwenda nyumbani kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na walishangaa kuona kwamba aliyelala kitandani alikuwa Ali, sio Muhammad. Ali alisimama na wakamuliza; “Yuko wapi Muhammad?” Aliwaambia hajui alikokwenda. Vurugu zilianza, na Ali aliukandamiza mkono wa kiongozi wao, na kusababisha upanga wake huo uanguke. Ali alifanikiwa kuushika upanga na aliweza kuwatoa nje. Wakuu wa Makka walitambua kwamba njama zao zilivunjika. Watu wa Makka wakiwa katika makundi walikwenda kila upande kumtafuta Muhammad. Kundi moja ambalo liliongozwa na mtaalam wa kufuatilia alama, walielekea upande haswa aliolekea Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) hadi walipokaribia Pango la Thaur. Abu Bakr aliyekuwa anajificha na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) humo pangoni, aliogopa sana na alitoka jasho aliposikia kishindo cha miguu yao. Walipokaribia mlango wa Pango, Abu Bakr alinong’ona kwenye sikio la Mtukufu Mtume (s.a.w.w.): “Endapo mmoja wao akitazama chini ya miguu yake atatuona.” Kwa utulivu Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alijibu: “Usiogope, Allah yuko pamoja na sisi.” Muweza wa Yote alimlinda Mtume wake (s.a.w.w.) asidhuriwe na maadui zake, na Hijira ya kihistoria ambayo kwayo imani ya Uislamu na Waislamu walihamishwa kutoka kwenye unyonge kwenda kwenye hali ya heshima na nguvu, ikaanza.

* * * * *

71

Page 71


Imam Ali binamu yake Mtume (s.a.w.w)Lubumba

Dr.Kanju.qxd

7/1/2011

4:36 PM

Imam Ali (a.s.) Ndugu yake Mtume Muhammad (s.a.w.)

UKUBWA WA KAZI YENYEWE. Sasa hebu tujaribu kutathmini muhanga wa Ali na ukubwa wa kazi yake. Wakati Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alipokubali mwaliko wa Waislamu wa Madina, Waislamu wa Makka walikwishafikia idadi ya 150. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) aliwaruhusu au kwa usahihi zaidi aliwasihi Waislamu hawa wahamie Madina. Alifanya hivyo licha ya yeye kutambua kuhusu hatari mpya ambayo ilijitokeza baada ya makubaliano yake na watu wa Madina. Alijua kwamba watu wa Makka hawangemruhusu aondoke jijini kwao akiwa salama. Angeweza kuwaweka Waislamu kadhaa mashuhuri karibu naye kwa madhumuni ya kumpa kinga dhidi ya hatari iliyokuwa karibu sana kutokea. Angeweza pia kumteua mmoja yeyote miongoni mwao kulala kwenye kitanda chake wakati huo. Lakini Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) hakufanya hivyo; badala yake, aliwasihi waondoke Makka kabla yake na akampa Ali kazi hiyo ngumu. Alimchagua Ali kwa sababu alitambua kwamba mtu atakayelala kwenye kitanda chake usiku huo lazima awe na sifa hizi zifuatazo: Mapenzi yake kwa Mwenyezi Mungu, Mtume Wake (s.a.w.w.) na dini yake lazima yawe makubwa zaidi kuliko yale ya kujipenda yeye binafsi. Lazima awe na moyo wa ujasiri ambao ungemwezesha kukabiliana na kifo katika njia ya Mwenyezi Mungu kwa kuridhika mwenyewe. Lazima awe na moyo usiokata tamaa ambao utamfanya asiwe na hofu ya kuwa mpweke, wakati atakapokuwa anakabiliana na vurugu ya hasira za jumuiya ya Makka kwa sababu ya kukwamisha njama dhidi ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Zaidi ya haya, alitakiwa awe na subira kwa kiasi cha kutosha kuweza kuficha taarifa zote kuhusu Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), bila kujali kiasi cha mateso ambayo angeyapata.

72

Page 72


Imam Ali binamu yake Mtume (s.a.w.w)Lubumba

Dr.Kanju.qxd

7/1/2011

4:36 PM

Imam Ali (a.s.) Ndugu yake Mtume Muhammad (s.a.w.) Ilikuwa vigumu sana, kama sio kutowezekana, kumpata mtu mwingine isipokuwa Ali ambaye alikuwa tayari kutekeleza wajibu huo na alifanya kwa utulivu sana na bila woga. Hapa tunaweza kuelewa maana ya kazi na msaada ambao Ali alimuahidi Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) miaka kumi kabla ya tukio hili.

UMUHIMU WA KUWASILISHA AMANA KWA WENYEWE Inafaa kutambua kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alimteua Ali kurudisha amana (zilizokuwa kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kwa watu wa Makka. Hii inadhihirisha wazi kwa vitendo kile alichomuahidi Ali kuhusu ukabidhi wasii. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) angeweza kumteua mtu mwingine yeyote mbali ya Ali kuwashilisha amana hizo. Palikuwepo na wasi wasi mkubwa kuhusu kunusurika kwa Ali, kwa sababu ya hatari iliyozingira kazi yake. Waislamu wengine hawakuwa hatarini, hivyo Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) angetegemewa kumteuwa Abu Bakr au sahaba mwingine kwa ajili ya kukabidhi amana kuliko Ali. Lakini alimteuwa Ali licha ya hatari iliyomzingira.

UBASHIRI WA AJABU Kumchagua Ali kukabidhi amana kunathibitisha kwamba Ali alikuwa ndiye mtu pekee wa kumwakilisha Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Kule kumfanya Ali kuwa naibu wake, kwenyewe kulikuwa ni ubashiri wa kipekee. Mwenyezi Mungu alimfunulia Muhammad kwamba Ali angepita hali hiyo ya hatari kwa salama na kwamba angeweza kukabidhi amana hizo. Kama Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) hangekuwa na uhakika kwamba Ali angenusurika kwenye kilele cha mgogoro huo, angempa kazi hiyo mtu mwingine badala ya Ali. Kazi ya kukabidhi amana ilikuwa na umuhimu 73

Page 73


Imam Ali binamu yake Mtume (s.a.w.w)Lubumba

Dr.Kanju.qxd

7/1/2011

4:36 PM

Imam Ali (a.s.) Ndugu yake Mtume Muhammad (s.a.w.) wake ambao ulimlazimisha Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kuchagua njia ya uhakika kabisa ya kuziwakilisha. Hivyo, ilikuwa ni kazi ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kumchagua mtu wa kutekeleza kazi hiyo ambaye alitumainiwa kunusurika, kuliko mtu ambaye alitegemewa kufa.

THAMANI ISIYOPUNGUA. Msomaji anaweza kudhani kwamba Ali alikuwa na uhakika wa kunusurika na uhakika wake aliupata kutoka kwenye taarifa ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na kutokana na yeye kuteuliwa naye (Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kukabidhi amana, kwani hali hii inaonesha kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alikuwa na uhakika wa nusura ya Ali. Kama hali ingekuwa hii, tukio hili lingepoteza umuhimu wake, kwani mtu aliyelala kwenye kitanda cha Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) hangedhuriwa bila kujali ukubwa wa hatari iliyozingira tukio hilo. Ukweli ni kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alimteua Ali kuwasilisha amana baada ya kukubali kazi ya ukombozi bila kusita au kuwa na kuhangaika na kile ambacho kingemtokea wakati wa usiku huo. Kwa Ali, yote yalikuwa sawa, auawe au asiuawe, almuradi Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) awe salama. Ali ni mtu ambaye alikuwa anaomba kifo cha kishahidi kama lengo la mwisho wake. Ali aliamini kwamba kufa kishahidi ni faida kubwa na ushindi wa hali ya juu sana. Tunatambua ukweli wa jambo hili tunaposoma yale yaliyoandikwa kwenye Nahjul-Balaghah ambamo Ali anasema kuhusu kuteremshwa kwa Aya ifuatayo: “Watu wanadhani wataachwa hivi hivi tu, wanasema: tumeamini, bila kuwapa mtihani?� Imam anatuambia kwamba Aya hii ilipoteremshwa alikumbusha Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kuhusu maneno yake aliyoyasema wakati ambapo Imam alihuzunishwa kwa sababu alikuwa hajapata kifo cha kishahidi ambacho 74

Page 74


Imam Ali binamu yake Mtume (s.a.w.w)Lubumba

Dr.Kanju.qxd

7/1/2011

4:36 PM

Imam Ali (a.s.) Ndugu yake Mtume Muhammad (s.a.w.) Waislamu wengine wengi walipata kwenye vita vya Uhud. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alimwambia Ali katika wakati huo: “Furahia, kifo cha kishahidi kinakujia.” Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alithibitisha tamko lake la siku za nyuma akasema: “Hivyo ndivyo itakavyokuwa. Uvumilivu wako utakuwaje siku hiyo?” Imam alijibu hoja: “Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), hapa haitakuwa mahali pa uvumilivu. Itakuwa sehemu ya furaha mno na shukrani.”46 Muweza wa yote alimjulisha Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alipokuwa anahama kwenda Madina kwamba angerudi Makka: “Kwa hakika yule aliyekuamuru kuwasilisha ujumbe wa Qur’ani Tukufu atakurudisha…” Wahyi huu ulikuwa ahadi kutoka kwa Mwenyezi Mungu kwa Mtume Wake (s.a.w.w.) kumfanya yeye anusurike kwenye matatizo yote hadi hapo atakapomrudisha Makka bila kujali vita vyovyote ambavyo atashiriki. Hivyo Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alishiriki vita vingi sana ambapo alikuwa na uhakika na usalama wake. Utambuzi huu haukupunguza thamani ya jitihada yake, kwani alikuwa ameazimia kufanya hivyo hata kama hakuahidiwa ulinzi wa Ki-Mungu. Pia hii ni kweli kuhusu Ali. Imani yake kuhusu kunusurika kwake mpaka atakapowasilisha dhamana kwa wenyewe haipunguzi ukubwa wa kujitoa kwake mhanga, kwa sababu alikuwa tayari kujitoa mhanga na kumuokoa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) iwe amejulishwa kunusurika kwake au kifo chake cha kishahidi. Historia ya Ali baada ya Hijra inathibitisha hitimisho hili. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) hakumjulisha Ali kwamba angenusurika kwenye vita vya Uhud, lakini kutokuwa na taarifa hiyo hakukumzuia Ali kuwa karibu na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), akampa ulinzi yeye mwenyewe na kupambana na vikosi kimoja baada ya kingine na kuvilazimisha kurudi nyuma baada ya masahaba wote kukimbia.

46 Nahjul-Balaghah, sehemu ya 2, uk. 5. 75

Page 75


Imam Ali binamu yake Mtume (s.a.w.w)Lubumba

Dr.Kanju.qxd

7/1/2011

4:36 PM

Imam Ali (a.s.) Ndugu yake Mtume Muhammad (s.a.w.) Muweza wa Yote alimlinda Mtume Wake (s.a.w.w.) dhidi ya njama za Makureishi na akamwezesha kufika Madina salama ambapo alipata nguvu na msaada. Lakini Makureishi hawakutegemewa kuchukua msimamo wa amani au kulala ambapo Muhammad alikuwa bado yu hai. Kwao Makureishi kuwepo kwa Muhammad ilikuwa hatari kubwa sana iliyotishia dini yao na ushawishi wao. Walitegemea uwezo wake ungeongezeka kufuatana na muda unavyopita na kwamba angerudi akiwa na jeshi ambalo Makureishi hawangeweza kukabiliana nalo. Kwa hakika kunusurika kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kuliwafanya Makureishi wawe na ari na azima zaidi ya kumuua na kupambana naye kwa nguvu zaidi. Walitegemea kuanzisha vita vya kudumu muda mrefu dhidi yake na wafuasi wake. Walikuwa tayari kutumia kila walichokuwa nacho katika uwezo wao na ushawishi wao kupigana naye, na kuyaamsha makabila ya wapagani na ya wasiokuwa wapagani waanzishe mapigano dhidi yake. Walitaka kufanikiwa katika kukamilisha kwa njia ya mapambano kile walichoshindwa kukamilisha kwa njia ya majaribio ya kumuua. Ukombozi wa Ali kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) mnamo usiku wa Hijra ulikuwa ni kukamilisha ahadi aliyotoa kwenye mkutano wa Nyumbani kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) ambapo alimuahidi Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kuwa waziri wake. Matukio yaliyofuata baada ya tukio la Hijra yalimtaka Ali amsaidie Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kwa kiwango kikubwa zaidi na bora zaidi, mwaka hadi mwaka hadi hapo ambapo ushindi wa ujumbe wa Mbinguni ulipopatikana. Dini ya Uislamu haingeweza kuendelea na kuenea isipokuwa pale wafuasi wa Uislamu walipokuwa wamekombolewa kutoka kwenye woga na kuwawezesha kufurahia uhuru wa kidini. Hali hii haingepatikana isipokuwa dola yenye uwezo iliyotegemezwa kwenye kanuni za imani hiyo mpya iwe imeasisiwa. Dola kama hiyo haingeasisiwa isipokuwa pale ambapo nguvu za uovu zilizokuwa zinatishia dini ziwe zimeshindwa.

76

Page 76


Imam Ali binamu yake Mtume (s.a.w.w)Lubumba

Dr.Kanju.qxd

7/1/2011

4:36 PM

Imam Ali (a.s.) Ndugu yake Mtume Muhammad (s.a.w.) Tutaona kwenye kurasa zifuatazo kwamba Ali alikuwa ni yule waziri wa kipekee ambaye alikuwa na uwezo wa kutosha kumsaidia Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) aweze kufanikisha malengo haya. Hivyo, Ali alipata sifa hizo mbili za kuwa Mkombozi wa Mwisho wa Mitume na heshima ya kuwa kabidhi wasii wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) (kwa vitendo) ambaye alimkaimu katika kukabidhi watu wa Makka amana zao walizompa awatunzie. Sifa zote mbili zilikuwa za kipekee. Kazi zake mbili zilipotimizwa kwa mafanikio, Ali aliondoka kwenda Madina. Alipofika Quba, alimkuta Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) anamngojea ili aingie naye jijini, ambalo lilikusudiwa kuwa makao makuu ya Uislamu.

* * * * *

SURA YA SABA. NAFASI YA ALI KATIKA KUJENGA DOLA YA KIISLAMU. Kujiamulia mambo ni haki isiyohamishika ya kila umma, na kwa hiyo, kila umma unayo haki ya kuanzisha dola na kuasisi serikali ya kitaifa. Dola kama hiyo inayo haki ya kuwaunganisha watu wake wote chini ya bendera moja, isipokuwa kama serikali halali kwa sehemu za taifa moja zilikwishaanzishwa. Haki hizo ni za kawaida na hakuna nguvu yenye haki ya kuzuia taifa au watu wa nchi wasizitekeleze.

77

Page 77


Imam Ali binamu yake Mtume (s.a.w.w)Lubumba

Dr.Kanju.qxd

7/1/2011

4:36 PM

Imam Ali (a.s.) Ndugu yake Mtume Muhammad (s.a.w.) Umma wa Kiarabu katika wakati wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) haukuwa na tofauti (na mataifa mengine). Una haki ya kusimamisha dola na kuasisi serikali. Hii sio haki tu bali vile vile ni jukumu la taifa la Kiarabu. Lakini bado, kwa sababu ya mazingira yasiyo ya kawaida, Warabu katika Hijaz, Najd na Tuhama, walikuwa wakiishi bila serikali ya aina yoyote. Hapakuwepo na mamlaka ya kudhibiti uhalifu katika taifa na kuwawezesha watu kuishi kwa amani na usalama wa mali zao, maisha yao, na heshima yao. Makabila ya Kiarabu yalikuwa ni maadui wa kulipizana. Hakuna heshima, damu, au mali ya kabila fulani ilikuwa inaheshimiwa na kabila lingine. Vurugu kwao ilikuwa ni jambo la kawaida na hapakuwepo na umuhimu wa mabadiliko; na kama mtu yeyote alifikiria kuleta mabadiliko, hakuwa na njia za kuyafanikisha. Waarabu waliobakia wa Yemen, Syria na Iraq, walitawaliwa na mamlaka za kigeni ambazo hazikuwa na haki ya kuwatawala. Ilikuwa wajibu wa serikali yoyote mpya kujaribu kuwakomboa kutoka kwenye utawala wa wageni na kuwaunganisha na Waarabu wengine, bila kujali kanuni zozote za kidini. Lakini hapakuwepo na mtu wa kutekeleza jukumu hili au kuzitekeleza haki hizi. Mwenyezi Mungu Muweza wa Yote alitaka kuwaokoa Waarabu na mataifa mengine na kuwakomboa kutoka kwenye vurugu za kijamii, kisiasa na kidini. Alimtuma Muhammad kuwaongoza wanadamu kwenye njia iliyonyooka na Alitaka taifa la Kiarabu kuwa sehemu ya kuanzia. Labda Waarabu walikuwa watu wanaohitaji mno mwongozo wa aina hiyo, na kama wangeongozwa na kiongozi wa ki-Mungu, wangekuwa na sifa nzuri ya kubeba ujunbe Wake na kuupeleka kwenye mataifa mengine. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alijaribu kuwasilisha ujumbe wake na kuanzisha dola. Nguvu za vurugu kutoka kwa wapagani na wasio mapa78

Page 78


Imam Ali binamu yake Mtume (s.a.w.w)Lubumba

Dr.Kanju.qxd

7/1/2011

4:36 PM

Imam Ali (a.s.) Ndugu yake Mtume Muhammad (s.a.w.) gani zilijaribu kwa uwezo wao wote kumzuilia asitimize kazi yake, wakaanzisha vita ya muda mrefu dhidi yake. Ilikuwa haiwezikani kwake yeye kutekeleza kazi yake bila kukubali changamoto kutoka kwao na kukutana nao kwenye uwanja wa vita na kuwashinda kabisa. Ilikuwa ni haki na pia wajibu wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kuzishinda nguvu za maadui ili kwamba aweze kusimamisha dola mpya kutoka kwenye aina mpya na ya mfano bora. Dola ya Kiislamu ambayo alikuwa anajaribu kuisimamisha haikuwa nguvu ya kudhibiti ambayo ilitawala watu kinyume na matakwa yao na kujiweka yenyewe juu yao. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alitaka kuasisi dola na serikali ambayo kwayo mtawala na watawaliwa wapo sawa na ni ndugu wa kila mmoja. Mtu au watu wenye nguvu katika dola hii hawataheshimiwa kwa ajili ya nguvu zao, wala mnyonge hatanyimwa haki yake kwa sababu ya unyonge wake. Serikali ambayo Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alitaka kuanzisha ilikuwa imepangiwa kumwelekeza mwanadamu kwa Muumba wa Ulimwengu na kuyafanya mataifa halikadhalika na watu binafsi watambue kwamba Yeye Ndiye Mtawala wao wa kweli. Hivyo, wangetii Amri Zake na wangepata furaha ya kidunia na kiroho iliyokwisha pangwa katika kumtii Yeye. Serikali iliyopangwa ingepanuka kama matokeo yake yenyewe ya kufuata kanuni zilizowekwa ambazo zingewanyanyua watu na kuwafanya waishi kiroho juu ya kiwango chao wenyewe cha ubinadamu.

USHINDANI WA HOJA DHIDI KUKOSA HOJA. Makundi ya vurugu na uovu ya watu wa Makka na jumuiya nyingine za Waarabu zenye kuendeleza uovu na hali ya kutokuwepo serikali si tu kwamba zilimnyima Muhammad haki ya kusimamisha dola na serikali, bali pia yalijaribu kimzuia yeye na wafuasi wake kutekeleza ibada zao za kidini. Walimnyima yeye na wafuasi wake haki ya kuishi maadamu tu 79

Page 79


Imam Ali binamu yake Mtume (s.a.w.w)Lubumba

Dr.Kanju.qxd

7/1/2011

4:36 PM

Imam Ali (a.s.) Ndugu yake Mtume Muhammad (s.a.w.) waliamini katika Mwenyezi Mungu mmoja. Makundi haya ya vurugu yalimfukuza Muhammad na wafuasi wake kutoka kwenye nyumba zao na kuacha mali zao. Walitaka kumwaga damu yake na ile ya wafuasi wake. Lau kama makundi haya yasingefanya kitu chochote bali kumzuia Muhammad kusimamisha dola, angekuwa na haki ya kupigana na kuwashinda kwani kuendelea kuwepo mamlaka yao ilimaanisha kuendelea kuwepo dhulma kwa wanyonge na kukosekana kwa usalama kwa jamii, zaidi ya yote, Muweza wa Yote hangeabudiwa na Upweke Wake haungekubaliwa. Makundi maovu yalikuwa vikwazo vya mkabala ambavyo uondoaji wake ni haja ya muhimu kwa ajili ya kusimamisha dola iliyopangwa. Ilkuwa vigumu kuifanya dola hiyo iwepo bila ya kuangamiza mkabala wake. Hivyo dola ya Kimbinguni imekadiriwa kuzaliwa katika uwanja wa mapambano wakati muasisi wa dola na wafuasi wake watakapoikubali changamoto ya kundi la waovu.

UBORA KUSHINDANA NA WINGI. Mwanzoni mwa Hijra, Waislamu walikuwa wachache sana kwa idadi kulinganishwa na makundi ya Waarabu yaliyokuwa wapinzani wao. Waislamu walizidiwa sana kwa idadi na hawakuwa na silaha za kutosha. Kwa ajili ya Imani ya Uislamu kuweza kushinda na kusimamisha dola, ilitakiwa iwe na mbinu mbili zifuatazo: Uingiliaji kati wa Mwenyezi Mungu ambamo kwamba yale makundi yanayoendeleza uovu yangeangamizwa kimuujiza. Mwenyezi Mungu anaweza kufanya hivyo na hakuna chochote kinachozidi uwezo Wake. Wakati wowote anapotaka kufanya jambo lolote huliambia tu “Kuwa na likawa.� Hata hivyo, ni dhahiri kwamba haingetokea hivyo. Mweza wa 80

Page 80


Imam Ali binamu yake Mtume (s.a.w.w)Lubumba

Dr.Kanju.qxd

7/1/2011

4:36 PM

Imam Ali (a.s.) Ndugu yake Mtume Muhammad (s.a.w.) Yote huendesha matukio ya dunia kupitia jinsi mambo yaendavyo kiasili. Huwajaribu waumini, na hawafaulu mtihani mpkaka wajaribu kuyatekeleza yale anayowaamuru kufanya, kutoa katika njia Yake kile wanacho miliki katika mali na uwezo wao. Njia nyingine ambayo kwamba ingewezekana idadi ndogo ya Waisalamu kupata ushindi, ilikuwa ni kuwa na sifa ya ubora ambayo ingewezesha kupata ushindi dhidi ya maadui wenye sifa ya wingi ambao ni duni. Na hivi ndivyo ilivyotokea.

SHUJAA WA KIPEKEE. Hapa tunamuona Ali Ibn Abu Talib (a.s.) karibu ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Alithibitisha kuwa shujaa wa kipekee na mkubwa mno; wanadamu kamwe hawajashuhudia mtu wa kuwa sawa naye katika historia ya ‘Jihad.’ Msomaji anaweza kukumbuka kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) aliwakusanya ndugu zake wa karibu baada ya kuanza kwa utume wake, akitafuta kutoka miongoni mwao naibu ambaye angemsaidia katika kazi yake ngumu. Hakuna mtu miongoni mwa ukoo wake wa Bani Hashim aliyejitokeza na kuitika wito wake isipokuwa Ali. Alisema, “Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, mimi nitakuwa naibu wako.” Baada ya kusikia hayo Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) aliwaambia Bani Hashim: “Huyu (Ali) ni ndugu yangu, wasii na mrithi wangu.” Tukio hili lilitokea miaka kumi kabla ya Hijiriya, wakati huo Ali alikuwa na umri wa miaka kumi na mitatu. Wakati wa kipindi cha miaka kumi ya tukio hili, ujanadume wa Ali ulipata nguvu isiyolinganishika. Hili lilidhihirika wazi kabisa mnamo usiku wa Hijra alipolala kwenye kitanda cha Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), na kutoa mfano wa hali ya juu katika historia ya ukombozi wa Kiislamu. Ujanadume huu ulikusudiwa kugeuzwa kuwa ushujaa wa kipekee pale wakati Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na wafuasi wake walipokubali changamoto ya maadui zao na wakaendelea kutetea 81

Page 81


Imam Ali binamu yake Mtume (s.a.w.w)Lubumba

Dr.Kanju.qxd

7/1/2011

4:36 PM

Imam Ali (a.s.) Ndugu yake Mtume Muhammad (s.a.w.) uhuru wao mtakatifu, huku wakijaribu kusababisha kuzaliwa kwa dola ya Kiislamu ambayo ilipangiwa kubeba mwenge wa mwongozo kwa ajili ya wanadamu. Hakuna mtu isipokuwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alitegemea neno ‘Waziiruk’ (waziri wako) ambalo Ali alilitamka kwenye mkutano wa kihistoria kuwa na maana yake kamili na kububujikwa na ushujaa mkubwa sana. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alikuwa ni mtu peke yake tu ambaye alitegemea kutoka kwa Ali kumbukumbu yake yote ya siku zijazo. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alikuwa msanifu na mwasisi wa Dola ya Kiislamu. Waziri wake Ali (a.s.) alikuwa mwondoshaji wa makundi ya upinzani ambayo yalikuwa kizuizi cha kuanzishwa kwa Dola hiyo, kwani yeye alikuwa shujaa na mbeba bendera ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kwenye vita vya uamuzi.47 Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alimfanya Ali kuwa amiri jeshi mkuu wa kila kikosi cha jeshi alichokuwemo. Kamwe hajamuweka chini ya ukamanda wa yeyote isipokuwa wake. Wakati wowote alipobeba bendera ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alirudi na ushindi na historia ya kuvutia. Uongozi wake ulikuwa wa mtindo wa pekee; Yeye hakuwa amiri jeshi ambaye alilindwa na wapiganaji wake. Yeye kwa usahihi zaidi, alikuwa kiongozi aliyesimama mstari wa mbele akiwaongoza wapiganaji wake kwa uhalisi. Katika matukio zaidi ya moja, wapiganaji wake walichukuwa hifadhi kwake, na alikuwa mlinzi wao kwenye vita zaidi ya moja. Mara kwa mara masahaba walio wengi walikimbia na kumuacha Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) peke yake, na Ali alisimama naye, na kumlinda huku akiendeleza mapigano dhidi ya maadui na kufidia nguvu ya ulinzi ya masahaba waliokimbia ambayo Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) aliikosa, kwa kutumia ustadi wake wa kishujaa. 47 Ibn Saad kwenye Al-Tabaqar, sehemu ya 3, uk. 25. Al-Hakim pia aliandika taarifa hii kwenye Al-Mustadrak yake, sehemu ya 3, uk. 111. 82

Page 82


Imam Ali binamu yake Mtume (s.a.w.w)Lubumba

Dr.Kanju.qxd

7/1/2011

4:36 PM

Imam Ali (a.s.) Ndugu yake Mtume Muhammad (s.a.w.) Ali alipigana vita kumi na nane (18) akiwa na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Zaidi ya hayo aliongoza vikosi vingi sana. Inatosha kusema kwamba kwa ufupi michango yake muhimu inweza kujisawiri kwenye vita vya kuamua mshindi na mshindwa: Badr, Uhud, Muuta na Khaybar. Hivi vita vinne vilikuwa kweli vya hatima ya Uislamu na Waislamu. Kuendelea kuwepo kwa Uislamu siku za baadaye ilitegemea matokeo ya vita hivi.

* * * *

SURA YA NANE VITA VYA BADR. Vita vya Badr vilikuwa vya muhimu sana miongoni mwa Vita vya Kiislamu vya mustakabali wake. Kwa mara ya kwanza wafuasi wa imani mpya walipewa mtihani mzito. Kama ushindi ungekuwa upande wa jeshi la makafiri ambapo majeshi ya Kiislamu yalikuwa bado yapo katika rika la mwanzo wao wa kukua, imani ya Uislamu ingeishia hapo. Hapana mtu mwingine aliyekuwa anatambua umuhimu wa matokeo ya Vita hivyo kama Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Tunaweza kusoma kina cha wasi wasi wake kwenye maombi ya dua yake kabla ya vita kuanza aliposimama akimuomba Mola Wake Mlezi: “Ewe Allah! Hawa ni Qureishi, wamekuja na majisifu yao yote na majigambo yao yote, wakijaribu kumfedhehesha Mtume Wako. Ewe Mola Wangu, ninakuomba Wewe kesho uwadhalilishe. Ewe Mola Wangu kama kundi hili la Waislamu likiangamia leo, Wewe hutaabudiwa!� 48

48 Ibn Hishamu, Wasifu wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), Sehemu ya 2, uk. 621. 83

Page 83


Imam Ali binamu yake Mtume (s.a.w.w)Lubumba

Dr.Kanju.qxd

7/1/2011

4:36 PM

Imam Ali (a.s.) Ndugu yake Mtume Muhammad (s.a.w.) Kwenye vita hivi ambapo jeshi la makafiri lilikuwa na wapiganaji 950 na Waislamu hawakuzidi 314 (pamoja na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), ulinzi wa Kiislamu ulikuwa mchanganyiko wa vipengele vitatu vinavyofanana na safu tatu za ulinzi: Haiba ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), uongozi wake na uimara wake usio na mfano. Kwa Waisilamu alikuwa kimbilio la mwisho hapo Badr na kila vita alivyoshiriki. Bani Hashim (Ukoo wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) wakiongozwa na Ali Ibn Abu Talib ambaye aliingia kwenye Vita hivi kwa kiasi fulani akiwa hajulikani, hatimaye alitoka humo akiwa na umaarufu wa kivita usio linganishika. Ustadi wake wa kupigana kijeshi ukawa mada mashuhuri katika mazungumzo ya misafara ya Waarabu katika Rasi yote ya Bara Arabu. Mamia ya masahaba wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) ambao nyoyo zao zilijaa imani na utayari wa kujitolea muhanga. Wengi wao waliona kifo cha kishahidi kuwa mafanikio makubwa, yanayoweza kulinganishwa na uhai na ushindi. Masahaba hawa wazuri walikuwa jeshi la Uislamu, safu yake ya kwanza ya ulinzi na ukuta mnene, ambao nyuma yake Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alikuwa na tabia ya kusimama. Walikuwa walinzi na washambuliaji. Ama kwa ukoo wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), wao walikuwa ndio wa kwanza aliokuwa akiwaita kutoa mhanga mzito, kabla ya mwingine yeyote yule. Walikuwa na desturi ya kusimama kwenye safu ya kwanza ya ulinzi, wakifungua njia kwa ajili ya jeshi kwa kupita kwao katikati ya safu za maadui. Mashambulizi ya jumla yalipoanza na kila sahaba aliyekuwepo kushiriki, ukoo wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) ulikuwa ndio uliokuwa wenye kuwaangamiza zaidi maadui, walifanya hivyo huko Badr na kwenye vita vilivyofuata.

84

Page 84


Imam Ali binamu yake Mtume (s.a.w.w)Lubumba

Dr.Kanju.qxd

7/1/2011

4:36 PM

Imam Ali (a.s.) Ndugu yake Mtume Muhammad (s.a.w.) Vita vilianza wakati Utbah Ibn Rabiah, mwanae Al-Walid, na kaka yake Sheibah (wote kutoka uko wa Umayya) waliposimama mbele ya jeshi lao la makafiri na wakamwambia Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) awatolee kwao wapiganaji wanaolingana nao (kwa hadhi) kwa mapigano rasmi ya watu wawili wawili. Mamia ya masahaba walikuwepo karibu naye, na wengi wao walikuwa na matumaini ya kuitwa na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), lakini Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) aliamua kuanza na familia yake mwenyewe. Mzigo ulikuwa mzito na mzigo mzito unaweza tu kubebwa na watu ambao mzigo huo ulikuwa wa kwao. Aliwaita Ali, Hamza na Ubaidah Ibn AlHarith (wote kutoka kwenye ukoo wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.)) kukabiliana na mashujaa hao watatu. Ali aliamuua Al-Waliid na Hamza alimuua Utbah, halafu wote wawili walimsaidia Ubaidah dhidi ya mshindani wake Sheibah. Sheibah alikufa hapo hapo na Ubaidah alikuwa shahidi wa kwanza katika vita hivi. Alikufa baada ya kupoteza mguu wake. Mashambulizi ya jumla yalipoanza mamia ya masahaba walishiriki kwenye mapambano. Walijitoa muhanga na kumridhisha Mola Wao Mlezi. Lakini watu wa Nyumba ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) walijibainisha wenyewe. Jitihada za Ali zilikuwa za kipekee katika vita hivi. Hanthala Ibn Abu Sufyani alipokabiliana naye, Ali aliyeyusha macho yake kwa pigo moja la upanga wake. Alimwangamiza Al-Aus Ibn Saeed, na kumchoma kwa mkuki wake, huku akisema: “Hamtabishana na sisi kuhusu Mwenyezi Mungu baada ya leo.” Vita vilipopamba moto, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alichota changarawe zilizojaa kiganja chake. Alitupa changarawe hizo kwenye nyuso za wapagani, huku akisema: “Nyuso zenu na zisawijike. Ewe Mwenyezi Mungu ziogofye nyoyo zao na udhoofishe miguu yao.” Makafiri walikimbia bila kumtazama mtu yeyote. Waislamu waliendelea kuwaua na kuchukua mateka. Makafiri sabini (70) walikufa, na Waislamu walichukua mateka sabini kutoka miongoni mwao. Historia ilihifadhi majina hamsini (50) tu miongoni mwa makafiri sabini 85

Page 85


Imam Ali binamu yake Mtume (s.a.w.w)Lubumba

Dr.Kanju.qxd

7/1/2011

4:36 PM

Imam Ali (a.s.) Ndugu yake Mtume Muhammad (s.a.w.) waliouawa. Wapagani ishirini49 au ishirini na mbili50 waliuawa na Ali. Vita hivi viliweka msingi wa Dola ya Kiislamu na vilitengeneza miongoni mwa Waislamu jeshi la kutambulika kwa wakazi wa Rasi ya bara Arabu. Hata hivyo, hatupaswi kupuuza ukweli kwamba iliwachukua masahaba mia tatu na kumi na mbili (312) kufanikisha asilimia 60 ya matokeo ya vita ambapo Ali peke yake alifanikisha asilimia 40. Haitakuwa kutia chumvi kusema kwamba juhudi zake zilikuwa kipengele cha muhimu sana katika kuyaleta mapigano kwenye ushindi wake wa mwisho. Lau kama tukiondoa asilimia arubaini yake matokeo ya vita labda yangebadilika. Kwa upande mwingine kama tukimtoa sahaba mwingine yeyote kwenye vita, matokeo ya vita hayangebadilika.

* * * * * *

SURA YA TISA. VITA VYA UHUD Makureishi walitoka kwenye vita vya Badr kwa matokeo ya kushangaza ambayo hawakuyategemea. Walikuwa wanajiamini kwamba wangewaangamiza Waislamu kwa urahisi. Kwani, Makureishi walikuwa wengi sana na jeshi la akiba kubwa na lojistiki zaidi. Pamoja na hivyo, ghafla walijikuta wamepoteza mashujaa wao sabini (70) na viongozi, pamoja na mateka sabini kwenye vita vya siku moja! Na juu ya yote, kipigo kikubwa walichokipata, kilitoka mikononi mwa kundi ambalo walikuwa na desturi ya kulidhalilisha. 49 Ibn Hisham, Wasifu wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) uk. 708-713. 50 Al-Waqidi, Al-Maghazi (chapa ya Oxford), sehemu ya I, uk. 152. 86

Page 86


Imam Ali binamu yake Mtume (s.a.w.w)Lubumba

Dr.Kanju.qxd

7/1/2011

4:36 PM

Imam Ali (a.s.) Ndugu yake Mtume Muhammad (s.a.w.) Makureishi hawakutaka kukubali kushindwa pale mwishoni. Walishindwa katika mapambano lakini waliamini kwamba kamwe hawatashindwa kwenye vita. Walichohitaji cha muhimu ni kuunda jeshi ambalo Waislamu hawangeweza kupigana nalo. Chuki kubwa iliyokuwa kwenye nyoyo za Makureishi na shauku yao ya kufuta aibu ya kushindwa kwenye vita vya Badr na hamasa yao ya kulipa kisasi cha viongozi wao waliouawa iliongeza kwenye ukubwa wao wa nguvu za kisilaha, nguvu kubwa mno ya kisaikolojia. Makureishi waliandaa jeshi la wapiganaji elfu tatu (3000) kwa ajili ya vita vya kulipiza kisasi kulinganisha na wapiganaji mia tisa na khamsini (950) walioshiriki kwenye vita vya Badr. Jeshi hili lilifadhiliwa kifedha, na mpangilio wa usafirishaji watu na vifaa (lojistiki) wake vyote vilipatikana kutokana na pato la msafara wa biashara ambalo lilitengwa kwa ajili ya vita vya kulipiza kisasi. Hivyo, jamii ya Makureishi, mwaka mmoja baada ya vita vya Badr, walitembea kuelekea Madina kwa lengo la kuwaangamiza Waislamu, dini yao, na Mtume wao Mtukufu (s.a.w.w.). Jeshi la Makka liliwasili sehemu iitwayo Uhud ambapo ipo umbali wa maili tano kutoka Madina. Hapo, vita vilivyotazamiwa vilitokea. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) aliendelea kupanga majeshi yake, akiyaweka kwenye sehemu za kimkakati. Aliwaweka mabingwa wa shabaha hamsini (50) kwenye mteremko wa Mlima wa Uhud, akawaelekeza walinde upande wa nyuma wa Waislamu dhidi ya kikosi cha farasi cha makafiri (kilichoongozwa na Khalid Ibn Al-Walid). Aliwaamuru wasiondoke kwenye nafasi yao kwa vyovyote vile itakavyokuwa.

VIPENGELE VYA ULINZI WA KIISLAMU. Katika vita vya pili vya mustakabali wa Waislamu, ulinzi wa Kislamu ulikuwa na vipengele hivyo hivyo vitatu muhimu ambavyo vilitimiza wajibu wao katika Vita vya Badr:

87

Page 87


Imam Ali binamu yake Mtume (s.a.w.w)Lubumba

Dr.Kanju.qxd

7/1/2011

4:36 PM

Imam Ali (a.s.) Ndugu yake Mtume Muhammad (s.a.w.) Uongozi bora wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na uimara wake. Watu wa Nyumba ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na ushujaa wao. Jeshi la Kiislamu lenye masahaba mia saba (700), nyoyo za wengi wao zilijaa imani na hali kuwa tayari kwa kujitoa muhanga. Mwanzo wa vita vya Uhud vilifuata mbinu za mwanzo wa Vita vya Badr. Talhah Ibn Abu Talhah (kutoka ukoo wa Banu Abdur dar), mbeba bendera ya makafiri, aliwapa Waislamu changamoto, akasema: “Wapo wapiganaji wa mapigano rasmi ya watu wawili?” Aliyeitika wito wake ni yule yule aliyeitika kwenye Vita vya Badr. Ali alimwendea na walipambana ana kwa ana, Ali alimshughulikia haraka sana kwa pigo la upanga wake ambalo lilipasua kichwa chake. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alifurahi. Akatamka kwa sauti kubwa; “Mwenyezi Mungu Mkubwa” (Allah Akbar), na Wislamu waliitikia vivyo hivyo, kwani shujaa mkubwa zaidi ya wote kwenye jeshi la makafiri aliuawa. Abu Saad Ibn Abu Talhah (kaka yake Talha) alibeba bendera na akawapa Waislamu changamoto akasema: “Masahaba wa Muhammad, mnadai kwamba anayekufa katika kundi lenu anakwenda Peponi na anayekufa katika kundi letu anakwenda Jahannamu. Kwa jina la Al-Lat, mnadaganya. Kama mngekuwa mnajiamini hivyo baadhi yenu wangekwishapambana na mimi. Hebu mmoja wenu naaje apigane na mimi.” (Dr. M. Haykal, The Life of Muhammad, uk. 289). Ali alijitokeza na Abu Saad hakuwa na bahati zaidi ya kaka yake Talha. Watu wa Abdul–Dar waliendelea kubadilishana wabeba bendera kwa watu wao, na Waislamu waliendelea kuwaangamiza. Ali alimuua Artat Ibn Sharhabil, Shureih Ibn Qaridh na mtumwa wao, Sawab.

88

Page 88


Imam Ali binamu yake Mtume (s.a.w.w)Lubumba

Dr.Kanju.qxd

7/1/2011

4:36 PM

Imam Ali (a.s.) Ndugu yake Mtume Muhammad (s.a.w.) Waandishi wa historia wameandika kwamba Hamza alimuua Uthman Ibn Abu Talha, Assim Ibn Thabit aliwapiga mishale yake Musafi na Al-Harith, watoto wawili wa Talhah, Al-Zubeir alimuua kaka yao Kilab, na Talhah Ibn Ubeidullah alimuua kaka yao mwingine Al-Jallas.

ALI NA WABEBA BENDERA. Hata hivyo Ibn Al-Athiir aliandika kwamba Ali peke yake aliwaua wabeba bendera wote kwenye vita vya Uhud na akasema kwamba Abu Rafi alilisimulia hilo.51 Na At-Tabari pia alifanya hivyo. Kifo cha wabeba bendera kiliongeza ari ya Waislamu na wakatetemesha nyoyo za makafiri. Kufuatia kifo cha wabeba bendera, Waislamu walifanya shambulizi kubwa lililoongozwa na Ali, Hamza, Abu Dujana, na wengine. Shambulizi la Waisilamu liliwaogofya makafiri, lakini Waislamu katika harakati hizi walimpoteza shujaa mkubwa sana Hamza simba wa Mwenyezi Mungu, na mjomba wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Wahshi mtu wa kutoka Habeshi alimchoma mkuki alipokuwa anapigana. Hata hivyo, makafiri walilazimishwa kukimbia na kuondoka kwenye kambi zao. Waislamu waliingia kwenye kambi za makafiri na wakaendelea kukusanya chochote walichokiona, silaha na rasilimali bila kupata upinzani kutoka kwa makafiri.

KUSHINDWA BAADA YA USHINDI. Tukio hili lililainisha midomo ya walenga shabaha khamsini ambao Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) aliwaweka kwenye mteremko wa Mlima Uhud kulinda sehemu ya nyuma ya Waislamu dhidi ya vikosi vya uasi vya makafiri. Walenga shabaha hawakuzingatia neno la kiongozi wao Abdullah Ibn Jubeir, ambaye aliwakumbusha wao kuhusu maelekezo ya Mtukufu 51 Ibn al-Athiir, al-Kamil, sehemu ya 3, uk. 107 89

Page 89


Imam Ali binamu yake Mtume (s.a.w.w)Lubumba

Dr.Kanju.qxd

7/1/2011

4:36 PM

Imam Ali (a.s.) Ndugu yake Mtume Muhammad (s.a.w.) Mtume (s.a.w.w.) ambayo aliyafanya kuwa ya lazima kwao kutokuondoka hapo. Si zaidi ya kumi waliozingatia maneno yake. Khalid Ibn Al-Waliid na wapanda farasi wake walipoona idadi ndogo ya mabingwa wa shabaha, walianza mashambulizi ya jumla na kuwaua. Makafiri waliokuwa wanakimbia waliowaona wapanda farasi wao wanapigana na kushambulia. Walirudi kwenye vita ambapo Waislamu walijishughulisha na kukusanya ngawira. Waislamu walishtuka na kuchanganyikiwa. Walianza kupigana lakini hawakutambua walikuwa wanapigana na nani. Waislamu wengi waliuawa na Waislamu wenyewe, halafu wakakimbia bila kugeuka nyuma, ambapo Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alikuwa anawaita warudi kwenye uwanja wa vita. Qur’ani Tukufu inatutaarifu kuhusu hali ya Waislamu katika saa hii ya kuhofia:

“Na Mwenyezi Mungu alikutimilizieni miadi yake, vile mlivyokuwa mnawauwa kwa idhini yake, mpaka mlipolegea na mkazozana juu ya amri, na mkaasi baada ya Yeye kukuonesheni mliyoyapenda. Wapo miongoni mwenu wanaotaka dunia, na wapo miongoni mwenu wanaotaka Akhera. Kisha akakutengeni nao (maadui) ili akujaribuni. Naye sasa amekwisha kusameheni. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye fadhila juu ya Waumini.” Qur’ani Sura ya 3:151-152.

90

Page 90


Imam Ali binamu yake Mtume (s.a.w.w)Lubumba

Dr.Kanju.qxd

7/1/2011

4:36 PM

Imam Ali (a.s.) Ndugu yake Mtume Muhammad (s.a.w.)

NANI ALIYEBAKI NA MTUKUFU MTUME (S.A.W.W.)? Masahaba walikimbia na kujihusisha na usalama wao tu! Historia imetaja watu pekee saba wa Makka (Ali, Abdul -Rahman Ibn Auf, Saad Ibn Abu Waqass, Talha Ibn Ubeidah, Al-Zubeir Ibn Al-Awam, Abu Ubeidah Ibn AlJarrah. Na watu saba wa Madina wa aina ya pekee (Al-Hubab Ibn AlMunthir, Abu Dujannah, Sahl Ibn Huneif, Assim Ibn Thabit, Saad Ibn Mu’ath, As-ad Ibn Hudheir au Saad Ibn Abadah na Muhammad Ibn Muslim). Watu hawa, kwa mujibu wa baadhi ya waandishi wa historia walibaki na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) ambapo masahaba wengine walikimbia.52 Kufuatana na yale tunayosoma kwenye Al-Mustadrak iliyoandikwa na AlHakim, tunaelewa kwamba Ali Ibn Abu Talib (a.s.) alikuwa ndiye tu aliyebaki na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kwa kipindi cha vita. Masahaba wengine waliotajwa kwamba walibaki na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), kwa uhakika walikuwa ndio wa kwanza kurudi kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) baada ya kumwacha. Al-Hakim ameleza kwamba Ibn Abbas alisema: “Ali anazo sifa bainifu nne ambazo ni zake pekee. Alikuwa mwanamume wa kwanza kusali na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Alikuwa wa kwanza mbeba bendera ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) aliyebaki na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kwenye vita mnamo siku ya Al-Mihras (vita vya Uhud, ambapo yamekusanyika maji yaitwayo Al-Mihras), na ni yeye ambaye aliikosha maiti ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na kuiweka kaburini.53 Al-Hakim pia amesimulia kwamba Saad Ibn Abu Waqass alisema: “Watu 52 Al-Waqid, Al-Maghazi, (imesimuliwa na Ibn Abil-Hadiid kwenye fasili yake ya Nahjul Balagha, Juz. 3, uk. 388.

53 Al-Hakim, kwenye Al-Mustadrak yeke sehemu ya 3, uk. 111. 91

Page 91


Imam Ali binamu yake Mtume (s.a.w.w)Lubumba

Dr.Kanju.qxd

7/1/2011

4:36 PM

Imam Ali (a.s.) Ndugu yake Mtume Muhammad (s.a.w.) walipokimbia na kumwacha Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) mnamo siku ya Uhud, nilikwenda pembeni na nikajisemea mwenyewe kwamba nitajilinda mwenyewe… halafu Al-Miqdad alimwambia yeye: “Saad, huyu ni Mtukufu Mtume (s.a.w.w.).”54 Al-Hakim pia ameelezea kwamba Az-Zubeir alisema kuhusu Vita vya Uhud, “Na walifichua sehemu yetu ya nyuma kwa wapanda farasi, na tukashambuliwa kutokea nyuma, na mtu alipiga ukelele Muhammad ameuawa. Tukarudi nyuma na maadui wakatukimbiza.”55 Pia alisimulia kwamba Abu Bakr alisema: “Watu walipomwacha Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) mnamo siku ya Uhud nilikuwa mtu wa kwanza kurudi kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) … halafu akataja kwenye Hadith kwamba Abu Ubeidah Ibn Al-Jarrah akamfuata yeye.” (Al –Hakim, Al-Mustadrak sehemu ya 3, uk. 78).

MTUKUFU MTUME (S.A.W.W.) ALISHIRIKI. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alibaki kwenye uwanja wa vita akiwa na dhamiri kamili na uimara baada ya makafiri kwenda karibu naye. Yeye mwenyewe alipigana kwa nguvu, Saad Ibn Abu Waqass alisimulia kwamba alishuhudia mtu ambaye uso wake ulifunikwa, na hakumjua ni nani. Makafiri walikwenda karibu naye na Saad alifikiri kwamba wangemzidi nguvu yeye. Lakini mtu huyo alichukua changarawe zilizojaa kwenye kiganja chake na akazitupa kwenye nyuso zao na wakarudi nyuma… hatimaye Saad aligundua kwamba mtu huyo alikuwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.).56 Alitumia upinde wake na akatupa mishale yake yote hadi ikawa upinde hautumiki tena. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alipoachwa bila ulinzi baada ya jeshi lake kuru54 Al-Hakim aliandika kwenye Al-Mustadrak, sehemu ya 3, uk. 26-28. 55 Al-Hakim, Al-Mustadrak, sehemu ya 3, uk. 27-28. 56 Taarifa hii pia imeandikwa na Ibn Hisham kwenye Wasifu wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), sehemu ya 2, uk. 78. 92

Page 92


Imam Ali binamu yake Mtume (s.a.w.w)Lubumba

Dr.Kanju.qxd

7/1/2011

4:36 PM

Imam Ali (a.s.) Ndugu yake Mtume Muhammad (s.a.w.) di nyuma, Ubay Ibn Khalaf alijaribu kumshambulia yeye. Baadhi ya masahaba walimzuia Ubay asimkaribie Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), lakini Mtume aliwazuia wasifanye hivyo. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akapambana na Ubay na kumpiga upanga ambapo pigo hilo lilionekana kana kwamba halijamuathiri. Lakini Ubay alisema: “Kwa jina la Mwenyezi Mungu, kama akinitemea mate ataniua.” Ubay alikufa mahali paitwapo ‘Saraf’ alipokuwa anarudi Makka.

JITIHADA ZA ALI. At-Tabari alisimulia kwamba Abu Rafi alisema: “Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alishuhudia kundi la makafiri linamwendea yeye. Akamwambia Ali: “Washambulie hao.” Ali aliwashambulia na aliwalazimisha kurudi nyuma na akamuua Amr Ibn Abdullah Al-Junnahi. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akaliona kundi lingine linamwendea na alimwambia Ali kuwashambulia na alifanya hivyo. Aliwatawanya na akamuua Sheibah Ibn Malik, mmojawapo wa watoto wa Amir Ibn Luay. Akishangazwa na kujitoa muhanga kwa Ali, Malaika Jibril alisema: “Ewe Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), ni mkombozi aliyoje huyu Ali!” Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alijibu: “Anatokana na mimi, na mimi ninatokana naye.” Jibrail akasema: “Na mimi ninatoka kwenu nyinyi wote wawili.”57 Walisikia wakati huo sauti inasema: “Hapana kijana (aliyejaa ujanadume) isipokuwa Ali, na hapana upanga unaolinganishwa na Dhulfiqar (upanga wa Ali).” Kikosi kilifika kutoka kwa Kinanah ambamo watoto wanne miongoni mwa watoto wa Sufyani Ibn Uweif walikuwemo: Khalid, Abu Al-Shaatha, Abu Hamza na Ghurab. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akamwambia Ali: “Kishughulikie kikosi hiki.” Ali akakishambulia kikosi hicho, ambacho 57 Sayyed Muslim, Al-Amiin kwenye Aayan Al-Shiah, sehemu ya 2, uk. 195. AlFairuzabadi aliandika taarifa hii kwenye kitabu chake: Fada-il Ak-Knamsah, sehemu ya 2, uk. 317 (akisimulia kutoka kwa Al-Tabari). Na Ibn Al-Athiir kwenye Historia Al-Kamil, sehemu ya 2, uk. 107, taarifa sawa na hii. 93

Page 93


Imam Ali binamu yake Mtume (s.a.w.w)Lubumba

Dr.Kanju.qxd

7/1/2011

4:36 PM

Imam Ali (a.s.) Ndugu yake Mtume Muhammad (s.a.w.) kilikuwa na takriban wapiganaji wapanda farasi hamsini (50). Alipigana nao akiwa hana kipando hadi akawatawanya. Walikusanyika tena na Ali akawashambulia tena. Hali hii ilirudiwa mara kadhaa hadi akawaua watoto wanaume wa Sufyani na akaongeza wengine sita zaidi….”58 Ibn Hisham amesimulia kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alianguka kwenye moja ya mashimo yaliyochimbwa na kufunikwa na Abu Amir ambaye alitegemea Waislamu wangeangukia humo. Goti la Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) lilijeruhiwa. Ali alishika mkono wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na akamvuta na kumtoa kwenye shimo na Talha Ibn Ubeidullah alimsaidia hadi Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akasimama.59 Muslim kwenye Sahih yake ameandika kwamba Sahl Ibn Saad alisema ifuatavyo: “Uso wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) ulipata jeraha, na jino lake moja lilivunjika, na deraya ya kulinda kichwa ilipasuka. Fatimah Binti yake Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alikuwa anaosha damu na Ali alikuwa anamwaga maji ya Al-Mihras, aliyokuja nayo, kwenye jeraha. Alipoona kwamba maji yalizidisha kutoka kwa damu, Fatimah alichoma mkeka, akaweka kiasi ya jivu kwenye jeraha na damu ilikoma kutoka.”60

58 Ibn Abu Al-Hadeed kwenye Sharh Nahjul-Balagha, Juz. 1, uk 372. 59 Ibn Hishamu, Wasifu wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) sehemu ya 2, uk. 80. 60 Muslim, kwenye Sahih yake, sehemu ya 12, uk. 148.

94

Page 94


Imam Ali binamu yake Mtume (s.a.w.w)Lubumba

Dr.Kanju.qxd

7/1/2011

4:36 PM

Imam Ali (a.s.) Ndugu yake Mtume Muhammad (s.a.w.)

HITIMISHO Haitakuwa vigumu kwa msomaji kuweza kufafanua yafuatayo: Vita vya Uhud vilikuwa ni vita ambavyo mustakabali wa Uislamu ulitegemea humo. Kifo cha wabeba bendera ya jeshi la makafiri mwanzoni mwa vita kilikuwa na athari yake muhimu katika kuinua hamasa ya Waislamu na kuvunja moyo wa makafiri ambao walikuwa wengi mara nne zaidi ya Waislamu. Wabeba bendera mbele ya macho ya wapiganaji katika siku zile walikuwa ndio viongozi wa jeshi. Kifo chao kilikuwa na athari kubwa kwa hamasa ya jeshi. Historia imeandika kwamba Abu Sufyani aliwaambia Banu Abdul Dar: “Enyi Banu Abdul-Dar, tunatambua kwamba mnayo haki zaidi kuliko ukoo wowote wa Makka kubeba bendera (kwa sababu mila ya watu wa Makka imewapa ukoo wa AbdulDar haki ya kubeba bendera vitani). Tulishindwa katika Vita vya Badr kwa sababu ya bendera. Ishikeni bendera yenu kwa uhakika na muilinde au mtupatie sisi.” Usemi huu uliwakasirisha ukoo wa Abdul-Dar. Kwa kuwa walikataa kuachia haki yao ya kubeba bendera, Abu Sufyani alisema: “Ngoja bendera nyingine zaidi iongezwe kwenye hiyo.” Wakasema; “Ndio, lakini bendera ya nyongeza pia itabebwa na mtu kutoka Banu Abdul-Dar, na hakuna makubaliano mengine kinyume na haya.” Makafiri wa Makka walishuhudia bendera yao ikianguka mara kumi mwanzoni mwa vita, na nyoyo zao zilivunjika pamoja na bendera mara kumi. Kwa mshangao wao, waliona kwamba walikuwa wanakabiliana na uwezo mkubwa sana. Ali ndiye aliwaangamiza wabeba bendera, au wengi wao. Hii ilikuwa ni ishara ya kushindwa kwa jeshi la Makka katika awamu ya kwanza. 95

Page 95


Imam Ali binamu yake Mtume (s.a.w.w)Lubumba

Dr.Kanju.qxd

7/1/2011

4:36 PM

Imam Ali (a.s.) Ndugu yake Mtume Muhammad (s.a.w.) Waislamu waliposhindwa kwenye awamu ya pili, hakuna mtu aliyebaki na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) isipokuwa Ali na masahaba wengine kumi na tatu wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Hawa kumi na tatu walikuwa wa kwanza kurudi baada ya kukimbia kwao. Ni dhahiri kwamba ulinzi wa Ali katika saa hiyo ya uamuzi ulikuwa na thamani zaidi kuliko ulinzi wa masahaba kumi na tatu ukiwekwa pamoja. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alikuwa shabaha ya mashambulizi ya makafiri. Wakati ambapo kikosi kilicholenga kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), Ali (a.s.) alikishambulia na kukilazimisha kurudi nyuma. Hivyo, hatutakosea kama tukisema kwamba Ali katika vita vya uamuzi alikuwa na sifa ya kipekee ya kuwa mlinzi mkuu wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na Ujumbe wake, dhidi ya makundi ambayo hapana mwingine ambaye angepambana nayo na kufuzu isipokuwa Ali (a.s.). Vita vya Badr viliweka msingi wa Dola ya Kiislamu, lakini Vita vya Uhud vilikaribia kuharibu msingi huu kama hapangekuwepo idadi ndogo ya mashujaa wakiongozwa na Ali. Makafiri waliona kwamba vita vya Uhud vilikwisha wao wakiwa washindi. Makafiri walilishinda jeshi la Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na Waislamu walipoteza masahaba sabini, miongoni mwao shujaa mkubwa kabisa Hamza ami yake Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), Simba wa Mwenyezi Mungu. Lakini ushindi wa makafiri haukuwa na uwezo wa kuamua. Lengo lao lilikuwa kumpata Muhammad na Muhammad (s.a.w.w.) alikuwa bado yu hai. Alikuwa mtu wa hatari kubwa sana kwao. Kwa hiyo ilikuwa muhimu kwao kupigana vita vingine vyenye uwezo wa kuamua ambapo wangefanikiwa lengo ambalo walishindwa kufanikisha kwenye Vita vya Uhud. Vita vya Uhud vilitokea wakati wa mwaka wa tatu baada ya Hijira. Miaka miwili baadaye, vita vya tatu vya uamuzi ambapo makafiri walikusanya jeshi lao kubwa kupindukia, vilitokea.

96

Page 96


Imam Ali binamu yake Mtume (s.a.w.w)Lubumba

Dr.Kanju.qxd

7/1/2011

4:36 PM

Imam Ali (a.s.) Ndugu yake Mtume Muhammad (s.a.w.)

SURA YA KUMI. VITA VYA HANDAKI Jamii ya Qureishi ilikuwa na ndoto moja muhimu. Kumwangamiza Muhammad na dini yake. Makabila ya kipagani yaliyoko nje ya Makka nayo yalikuwa na ndoto hiyo hiyo. Kama watu wa Makka, makabila haya yalimuoma Muhammad kuwa hatari inayotishia dini yao. Imani hii iliwapambanisha makabila haya na Waislamu kwenye vita nyingine ambapo Waislamu walikuwa washindi. Makabila haya, kwa hiyo, yalikuwa kama jamii ya Makka kwani na yenyewe yalijaa hasira na chuki kuhusu Muhammad na dini yake.

MAKABILA YASIYO WAPAGANI. Palikuwepo na migongano baina ya Waislamu na baadhi ya watu wa kitabu ambao walikuwa jirani na Madina iliyosababishwa na kukiuka kwao makubaliano waliyoyafanya na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Makabila hayo ni kama Banu Natheer na mengineyo, yalihamishwa na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Ujumbe kutoka kwa watu hawa ulikwenda Makka na jamii zingine za Kiarabu wakati wa mwaka wa tano baada ya hijira, yakawa yanatangaza vita dhidi ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na kujaribu kuandaa majeshi ya Waarabu kwa ajili ya vita vilivyopendekezwa. Hawakuhitaji juhudi nyingi katika kuwashawishi watu wa Makka wakubali vita dhidi ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Mwitiko wao kwenye wito huu ulikuwa wa haraka na bila kusita, waliandaa wapiganaji elfu nne, (4,000). Jeshi hili lilisaidiwa na wapiganaji wengine elfu sita (6000) kutoka makabila ya Ghatafan, Saleem na mengine. Hivyo, wapiganaji elfu kumi waliondoka kuelekea Madina.

97

Page 97


Imam Ali binamu yake Mtume (s.a.w.w)Lubumba

Dr.Kanju.qxd

7/1/2011

4:36 PM

Imam Ali (a.s.) Ndugu yake Mtume Muhammad (s.a.w.) Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akapata habari ya uvamizi uliokuwa unaelekea kutokeza siku chache kabla ya jeshi hilo kufika Madina. Akawataka ushauri masahaba wake, na Salman Al-Farsi (Mwajemi) alimshauri Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kuchimba handaki kuzunguka mji wa Madina kuzuia wavamizi wasiweze kuingia mjini hapo. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) aliwaamuru Waislamu (ambao walikuwa takriban elfu tatu) kutekeleza mpango huo. Handaki lilichimbwa mnamo muda wa siku sita. Walipoona handaki, wavamizi walishangaa na walitambua kwamba haingekuwa rahisi wao kuingia Madina. Hivyo waliona ni muhimu kuzunguka Madina badala ya kuivamia moja kwa moja. Banu Quraidha, jamii kutoka wafuasi wa kitabu, iliungana na jeshi la makafiri baada ya kuwasili. Jamii hii ilikuwa na makubalino ya amani na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Kitendo chao cha kihaini kilikuwa mshangao wa kuogofya kwa Waislamu. Kwa kukiuka makubaliano, jamii hii iliwapa jeshi la makafiri vikosi vingine zaidi na silaha. Ikawa ni wajibu wa Waislamu kuongeza safu nyingine zaidi kwenye safu zao za ulinzi.

WAISLAMU KATIKA HOFU KUBWA. Walikuwepo wanafiki wengi miongoni mwa Waislamu ambao walisambaza uvumi wa kuogopesha ambao ulizidisha hofu ya Waislamu. Qur’ani Tukufu inatuambia kuhusu hali ya wasi wasi mkubwa wa kisaikolojia ambayo Waislamu waliishi nayo kipindi hicho. “Tazama! Walipokujieni kutoka juu yenu, na kutoka chini yenu, na macho yalipokodoka, na nyoyo zikapanda kooni, nanyi mkamdhania Mwenyezi Mungu dhana mbali mbali. Hapo ndipo Waumini walipojaribiwa, na wakatikiswa mtikiso mkali. Na waliposema wanafiki na wale wenye maradhi katika nyoyo zao; Mwenyezi Mungu na Mtume Wake hawakutuahidi ila udanganyi98

Page 98


Imam Ali binamu yake Mtume (s.a.w.w)Lubumba

Dr.Kanju.qxd

7/1/2011

4:36 PM

Imam Ali (a.s.) Ndugu yake Mtume Muhammad (s.a.w.) fu tu. Na kundi moja miongoni mwao lililosema: Enyi watu wa Yathrib! Hapana kukaa nyinyi! Rudini. Na jingine miongoni mwao likaomba ruhusa kwa Mtume kwa kusema: “Hakika nyumba zetu ni tupu. Wala hazikuwa tupu; hawakutaka ila kukimbia tu.� (alAhzab; 33:10-13) Kinyume chake, jeshi la makafiri lilikuwa linapata hamasa ya hali ya juu sana. Kwao ushindi lilikuwa jambo la uhakika. Madina ilizingirwa na wao, na wakazi wake hawakuwa na ujasiri wa kutoka humo. Kujiamini kwao na hamasa yao ni hali ambazo zilipata msukumo zaidi na kuongezeka pale ambapo Bani Quraidha walipoungana nao. Tukio hili liliwafanya wabadili mkakati yaani badala ya kuzingira Madina waliamua kuvamia moja kwa moja.

KUBAHATISHA KWA AMR. Amr Ibn Abdwuud akifuatana na Dhirar Ibn Al-Khattab, Akramah Ibn Abu Jahl, na wengine walitafuta na kuona sehemu nyembamba ya handaki. Farasi wao waliruka kuvuka handaki na kuingia Madina kupitia kwenye sehemu hiyo nyembamba. Lau tukio hili la kijasiri lingefanikiwa wapiganaji wengi wa makafiri walitegemewa kuwafuata na kufanya iwezekane kwa jeshi lote kupita kwa kutumia sehemu ile nyembamba ya handaki, kwani wangeunganisha pande mbili za shimo kwa kujaza udongo ile sehemu nyembamba ya handaki. Waislamu walikwua katika hali ya mshtuko na kutishika kabla ya wapiganaji hawa makafiri kuvuka na kuwa upande wao. Hatari mpya iliyosababishwa na kuvuka kwa makafiri hao, ilifanya hamasa ya Waislamu kushuka zaidi kuliko ilivyokuwa kabla.

99

Page 99


Imam Ali binamu yake Mtume (s.a.w.w)Lubumba

Dr.Kanju.qxd

7/1/2011

4:36 PM

Imam Ali (a.s.) Ndugu yake Mtume Muhammad (s.a.w.)

WATU WENYE IMANI THABITI. Licha ya kwamba nyoyo za Waislamu walio wengi zilijaa hofu, baadhi yao hawakutikiswa na hatari hii mpya. Kwa usahihi zaidi tukio hili liliimarisha imani zao kwa Mwenyezi Mungu, Mtukufu Mtume Wake (s.a.w.w.) na ushindi ulioahidiwa na kuwa madhubuti zaidi. Watu hawa walikuwa tayari kujitoa muhanga na mmojawao hakika aliazimia kujaribu kuizuia hatari hiyo, halafu kuiondosha. Qur’ani Tukufu inatuambia kuhusu hamasa ya waumini hawa.

“Na Waumini walipoyaona makundi, walisema: “Haya ndiyo aliyotuahidi Mwenyezi Mungu na Mtume Wake. na Mwenyezi Mungu na Mtume Wake wamesema kweli. Na hayo hayakuwazidisha ila imani na utiifu. Miongoni mwa waumini wapo watu waliotimiza waliyoahidiwa na Mwenyezi Mungu. Baadhi yao wamekwisha kufa, na baadhi wanangojea, wala hawakubadilisha (ahadi) hata kidogo.”Qur’ani Tukufu, 33:22-23. Qur’ani Tukufu haituelezi kuhusu idadi ya waumini hao ambao imani yao iliongezeka baada ya hatari kuzidi kuwa kubwa. Waumini hawa inawezekana labda walikuwa ishirini au wachache tu. Hata hivyo, wakati mwingine imani hubakia kama hali ya fikira tu bila kubadilika na kuwa vitendo. Baadhi ya imani ni hai (kiutendaji), hububujika nguvu na kumpeleka muumini akabiliane na hatari na hunyanyuka kwenye upeo wake na juu. Idadi ya hawa waumini mashuhuri inabakia bila kujulikana. 100

Page 100


Imam Ali binamu yake Mtume (s.a.w.w)Lubumba

Dr.Kanju.qxd

7/1/2011

4:36 PM

Imam Ali (a.s.) Ndugu yake Mtume Muhammad (s.a.w.)

MWITIKIO WA ALI. Hata hivyo, historia imetujilisha kuhusu mmojawao kwa sababu ya mafanikio yake makubwa kwenye vita hivi, kuweza kuizuia na kuiondosha hatari hiyo ambayo ilitikisa msingi wenyewe wa Dola ya Kiislamu. Mtu huyo si mwingine isipokuwa Ali Ibn Abu Talib. Amr Ibn Wudd, ambaye alivuka handaki alikuwa mtu maarufu miongoni mwa Waarabu. Alishiriki katika vita hivi, kwa majivuno akitengenezea mahali pake pajulikane kwa watu. Kule kuvuka kwake tu kutoka upande mmoja na kwenda upande mwingine wa handaki, akiwa na idadi ndogo ya wapiganaji, inaonesha kwamba mtu huyu alikuwa jasiri sana. Alikuwa ni yeye peke yake miongoni mwa wapiganaji elfu kumi (10,000) ambaye alijaribu kuwavamia Waislamu moja kwa moja na kuwapa changamoto kamili wakati ambapo alikuwa nao upande mmoja. Kuvuka kwa Amr na wenzake, kulidhihirisha kwa Waislamu hatari mpya na ya kutisha na mshangao wa kuogofya ambao hawakuutegemea kamwe. Ilibakia kidogo mlango ufunguliwe uwe wazi kabisa, na mamia na maelfu ya watu wangetegemewa kufuata. Mshangao huo hata hivyo haukumuogopesha Ali (a.s.). Historia inatuambia jinsi akili ya Ali ilivyotulia na kuwa akini tayari kwa mapigano ya haraka, kwani kwa wepesi sana aliizuia hatari, halafu akaiondosha. Aliongoza idadi ndogo ya waumini, haraka sana alikwenda mahali hapo ambapo safu ya ulinzi ya Kiislamu ilivunjwa kwa kuvuka kwa Amr. Yeye na wenzake walisimama pale, na kuzuia maadui wengine wasimfuate Amr.61 Alipoizuia hatari mpya, iliweza kuondoshwa kabisa. Akiwa amepanda farasi wake, Amr alizunguka hapa na pale katika eneo la 61. Ibn Hisham, Wasifu wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), sehemu ya 2, uk. 224. 101

Page 101


Imam Ali binamu yake Mtume (s.a.w.w)Lubumba

Dr.Kanju.qxd

7/1/2011

4:37 PM

Imam Ali (a.s.) Ndugu yake Mtume Muhammad (s.a.w.) Sal’a, akitazamana ana kwa ana na Waislamu na kuwapa changamoto: “Yuko mpiganaji wa pambano la wawili.?” Alirudia wito huu lakini hapakuwepo na jibu kutoka kwa masahaba. Hali hii ilimlazimisha Ali kuondoka kwenye nafasi yake ambapo alikuwa anawazuia wapiganaji makafiri wasimfuate Amr kwa kuvuka handaki. Kwa kujibu changamoto ya Amr, Ali aliondoka mahali hapo kwa muda na iendelee kulindwa na wapiganaji wachache waliokuwa pamoja naye. Ali alimsogelea Amr na akamwambia wapigane kwenye pambano la watu wawili. Amr akajibu kwa majigambo: “Kwa nini, ewe mtoto wa kaka yangu (Amr alikuwa rafiki yake Abu Talib, baba yake Ali)? Kwa jila la Mwenyezi Mungu, nisingependa nikuue.” Ali akajibu: “lakini, kwa jila la Mwenyezi Mungu ningependa nikuue.” Pambano fupi lakini kali sana baina ya mashujaa wawili hawa likatokea. Ali alimuua Amr upesi mara moja tu na wapiganaji waliofuatana naye wakakimbia., wakijaribu kuvuka handaki kwa mara nyingine kutoka upande wa Waislamu kwenda upande wa makafiri. Ali alitamka kwa sauti kubwa: Allahu Akbar, (Mwenyezi Mungu Mkubwa) na Waislamu nao walifanya hivyo. Kifo cha Amr kilikuwa mwisho wa hatari mpya. Wale waliokuwa naye walikimbia, wakijaribu kujiokoa; lakini walio wengi waliuawa kabla hawajavuka na kwenda upande mwingine. Ali alitoa mchango mkubwa sana katika kuuhami Uislamu katika vita hivi wakati ambapo hatari dhidi ya Imani mpya ilikuwa imefikia kilele chake. Kwenye vita hivi Waislamu walikabiliwa na hatari kubwa zaidi ambayo haijapata kutokea. Vipengele vya ulinzi wa Kiislamu vilikuwa ni vile vile vitatu ambavyo vilitumiwa wakati wa vita vya Badr na Uhud: Uimara wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na uongozi wake bora; ushujaa wa Ali na dhamira nzito ya jeshi la Kiislamu. Kipengele cha nne kiliongezwa kwenye vita hivi: Dhima ya Salman Al102

Page 102


Imam Ali binamu yake Mtume (s.a.w.w)Lubumba

Dr.Kanju.qxd

7/1/2011

4:37 PM

Imam Ali (a.s.) Ndugu yake Mtume Muhammad (s.a.w.) Farsi (Muajemi) ambaye alimshauri Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) lichimbwe handaki kuzunguka Madina. Dhima ya jeshi la Kiislamu wakati wa Vita vya Uhud ilikuwa ndogo kuliko dhima ya wakati wa Vita vya Badr. Na ilikuwa na muhimu mdogo kwenye Vita vya Handaki kuliko kama ilivyokuwa kwenye vita vya Uhud, kwani Waislamu wakati wa Vita vya Handaki hawakuthubutu hata kumkabili adui. Walichofanya ni kuchimba handaki tu kuzunguka Jiji kabla ya kuwasili jeshi la makafiri halafu wakasimama nyuma ya handaki hadi mwisho wa vita. Dhima za vipengele viwili vya kwanza vya ulinzi vilifanana na vile vya Vita vya Badr na Uhud na labda kubwa zaidi, Uimara wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), uongozi wake, mikakati ya vita na kasi yake ya kuchimba handaki vilikuwa ni muhimu zaidi katika kuwapitisha salama Waislamu kwenye kilele cha hatari. Dhima ya Ali kwenye vita hivi ilikuwa kubwa sana katika historia ya ulinzi wa Kiislamu.

UKUBWA WA MCHANGO WA ALI. Haingekuwa na mantiki kusema kwamba Waislamu kwa pamoja walikuwa hawawezi kumuua Amr, ambaye yeye mwenyewe asingeweza kushinda dhidi ya maelfu ya Waislamu. Lakini hali haikuwa hivyo. Amr alitaka pambano la watu wawili. Pambano la aina hii haliwezi kushirikisha zaidi ya watu wawili. Ilifikiriwa kuwa ni kitendo cha aibu watu wawili au zaidi kupambana na mtu mmoja. Amr aliwapa changamoto Waislamu wote wamtoe mmoja wao kupigana naye. Hakuna hata mmoja aliyekuwa tayari kumkabili isipokuwa Ali. Wala haingekuwa na mantiki kusema kwamba Amr alikuwa ndio uwezo wote wa majeshi ya makafiri, na kwamba kifo chake kilikuwa ndio 103

Page 103


Imam Ali binamu yake Mtume (s.a.w.w)Lubumba

Dr.Kanju.qxd

7/1/2011

4:37 PM

Imam Ali (a.s.) Ndugu yake Mtume Muhammad (s.a.w.) kushindwa kwa majeshi yote ya washirika. Lakini ingekuwa na mantiki kuthibitisha mambo mawili muhimu: Hatua ya Ali kuziba sehemu ya kupita na kuwazuia wengine wasimfuate Amr ilisitisha hatari na kuizuia. Kama sehemu ya kupita ingebaki wazi, idadi kubwa ya wapiganaji wa kipagani wangemfuata Amr na kuvuka kwao kungesababisha kuanzishwa daraja kati ya pande mbili za handaki. Daraja kama hilo lingewezesha jeshi lote la adui kuvuka. Saa moja ya uzembe ingesababisha kushindwa vibaya sana kwa jeshi la Kiislamu. Hili halikutokea kwa sababu Ali alikuwa mwepesi kujibu kwake ile hatari mpya, akili makini, tulivu na kujizatiti na kuwa tayari kushughulikia kilele cha hatari iliyo kubwa sana.. Kifo cha Amr kilithibitishia jeshi la makafiri kwamba walikuwa hawawezi kuvuka handaki tena, na kwamba lile ambalo Amr hakufanikisha halingefanikishwa na wengine. Kwa hali hii jeshi la makafiri lililazimika kuchukua chaguo mojawapo ya mawili, kuondoka kwenye uwanja wa vita au kuendelea kuizingira Madina hadi Waislamu wajisalimishe au walazimike kuvuka handaki na kupigana na makafiri. Kuendelea kuzingira Madina ni jambo ambalo lilikwisha kuwa nje ya uwezo wa jeshi la makafiri. Lilikuwa halina chakula cha kutosha kulisha wapiganaji makafiri elfu kumi (10,000) pamoja na farasi na ngamia wao ambako kungewawezesha kuendeleza mzingiro kwa kipindi cha miezi au majuma kadhaa. Zaidi ya haya, kimbunga cha upepo mkali kilitokea na kuendelea kusababisha uharibifu mkubwa kwa jeshi la makafiri na kufanya maisha yao kuwa ya dhiki. Kimbunga kilitanguliwa na mabishano baina ya wapagani na washirika wao wa Kiyahudi ambayo yalisababisha ushirikiano wao katika vita hivyo kuwa mgumu sana. Hivyo palikuwepo na chaguo moja tu kwa jeshi la makafiri kuchukua baada ya kushindwa kwa jaribio la Amr na kifo chake: Kuondoka kwenye uwanja wa vita, na ndivyo walivyofanya. Lazima tusisahau jambo muhimu! Kifo cha Amr na wengi wa wapiganaji aliofuatana nao ni tukio 104

Page 104


Imam Ali binamu yake Mtume (s.a.w.w)Lubumba

Dr.Kanju.qxd

7/1/2011

4:37 PM

Imam Ali (a.s.) Ndugu yake Mtume Muhammad (s.a.w.) ambalo liliwapa hamasa Waislamu. Matumanini yao ya kuendelea kuishi na kupata ushindi yalihuishwa. Yote haya yalikuwa matokeo ya jitihada za Ali, na kwa hili tunaweza kuelewa maana ya tangazo la Mtukufu Mtume (s.a.w.w.): “Pambano la Ali, dhidi ya Amr Ibn Abd Wudd kwenye Vita vya Handaki linazidi uzito wa matendo mema ya taifa langu lote hadi Siku ya Hukumu.”62 Jeshi hilo la washirika likaondoka na Waislamu wakavuka mgogoro huo wa hatari kwa usalama. Kujiamini kwao kuhusu siku za usoni kwa sababu ya kushindwa kwa jeshi la washirika baada ya maandalizi makubwa sana, kulirudi tena. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisema baada ya makafiri kuondoka kwenye uwanja wa vita: “Baada ya leo, sisi tutawavamia na sio wao kutuvamia sisi.”63

******

62 Al-Mustadrak, sehemu ya 3, uk. 32. 63 Ibn Hisham kwenye kitabu cha Wasifu wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), sehemu ya 2, uk. 254. 105

Page 105


Imam Ali binamu yake Mtume (s.a.w.w)Lubumba

Dr.Kanju.qxd

7/1/2011

4:37 PM

Imam Ali (a.s.) Ndugu yake Mtume Muhammad (s.a.w.)

SURA YA KUMI NA MOJA. VITA VYA KHAYBAR. Mengi ya makabila ya Waarabu wasio wapagani wa wakazi wa Hijaz walikataa kukubali Dini ya Uislamu. Dini yenyewe iliwazuia Waislamu wasiilazimishe kwenye makabila, kwa sababu walitokana kwenye watu wa kitabu. Kuchipukia kwa Dola ya Kiislamu mwanzoni mwa Hijiriya, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alitiliana saini hati ya makubaliano ambayo kwayo alidhibiti uhusiano baina ya makabila haya (ya pembezoni na ndani ya Madina) na Waislamu kwa kuwapa haki sawa na zile za Waislamu. Kwenye hati hiyo; Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) aliandika yafuatayo: “Yeyote atakayeungana na waliosaini maandiko haya, atastahiki kusaidiwa na sisi na hatadhulumiwa kwa vyovyote vile, wala Waislamu hawatashirikiana dhidi yao. Wana wa Auf ni Jamii ya waumini. Watu wa Kitabu wanaruhusiwa kufuata dini yao kama wanavyoruhusiwa Waislamu kufuata dini yao, na ndivyo ilivyo kwa washirika wao isipokuwa mtu anaye dhulumu au anayetenda dhambi. Kwani kufanya hivyo anajiumiza mwenyewe. Watu wa kitabu kutoka Banu Al-Harith na Banu Al-Shateebah wanayo haki sawa na watu wa Banu Auf. “Watu wa kitabu watatumia mali ya hazina yao na Waislamu watatumia kutoka kwenye hazina yao. Watasaidiana wao kwa wao dhidi ya yeyote anayeanzisha vita dhidi ya watu waliosaini hati hii. Waliotia saini hati hii wanastahiki ushauri wa maelewano, uaminifu na msaada na si kupigana….”64 64 Ibn Hishamu, Wasifu wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) sehemu ya 1, uk. 503. 106

Page 106


Imam Ali binamu yake Mtume (s.a.w.w)Lubumba

Dr.Kanju.qxd

7/1/2011

4:37 PM

Imam Ali (a.s.) Ndugu yake Mtume Muhammad (s.a.w.) Hati hii ni kweli kwamba ni ya kwanza ya aina yake katika historia ya uhuru wa kidini na kiini cha tangazo la haki za binadamu ambalo wanadamu wamehangaikia kulipata kwa karne nyingi. Sidhani kwamba kundi lolote dogo la kidini liliwahi kupata usalama wa aina hiyo au haki chini ya serikali yoyote kabla ya karne za hivi karibuni. Kundi hilo dogo la kidini lilitegemewa kuukubali msimamo huu wa ukarimu kuhusu imani yake. Wangelazimika kuchukua msimamo wa aina hii kuelekea kwenye dini ambayo inaheshimu ujumbe ambao wanauamini na kuuona kuwa wa kimbinguni usiopungua thamani yake. Kwani dini ya Uislamu inakubali ujumbe wa Isa, Musa (a.s.) na kuukamilisha. Kundi hili dogo la kidini lilitabiria majirani zao makafiri, juu ya Mtume mtarajiwa ambaye ametajwa kwenye kitabu chao. Walikuwa na desturi ya kuwatishia majirani zao makafiri na ukaribu wa ujio wake na kuahidi wao kuwa ni wafuasi wake. Huyu Mtume mtarajiwa alipokuja na Mwenyezi Mungu akawaonesha wao ndani yake kile walichokitarajia, wakachukua msimamo wa chuki kuhusu yeye na wakamlipa uvumilivu wake kwa kuvunja makubaliano yote waliyotiliana saini naye. Kundi hili dogo la kidini kwa dhahiri lilikuwa linatarajia huyu Mtume mpya kuchangia naye msimamno wa chuki kuhusu Isa na wafuasi wake. Walipoona Qur’ani Tukufu inazungumzia utakatifu wa Isa, ukweli wake na utakatifu wa mama yake, wakageuka wakawa dhidi ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Labda hawakupenda kitu kingine kwenye Uislamu. Dini hii hukataza riba, na inasimama dhidi ya unyonyaji na ukiritimba wa soko. Hali hii iliwaogopesha, kwa sababu ilikuwa tabia yao kutoza riba kubwa kwenye mikopo yao waliyokopesha jirani zao. Utawala huria ambao ulienea kwenye Rasi ya Bara Arabu ulikuwa ni ardhi yenye rutuba kwao. Waliweza kwenda hapa na pale miongoni mwa makabila, wakipanda na kukuza hisia za chuki miongoni mwao. Kuanzisha serikali yenye nguvu na sheria kamili na 107

Page 107


Imam Ali binamu yake Mtume (s.a.w.w)Lubumba

Dr.Kanju.qxd

7/1/2011

4:37 PM

Imam Ali (a.s.) Ndugu yake Mtume Muhammad (s.a.w.) utaratibu itawakoseha faida walizokuwa wakizifaidi. Kundi hilo dogo la kidini lilichagua kushirikiana na makafiri ili kuweza kuliweka taifa la Kiarabu katika hali ya ujinga, umasikini na dhuluma, ambako watu walikosa usalama wa maisha, heshima na mali zao. Kama walivyo makafiri, kundi hilo dogo halikutaka kuona taifa la Kiarabu linatekeleza haki yake ya kuanzisha serikali ya kuziunganisha jamii za Kiarabu na kuwaelekeza, pamoja na mataifa mengine, kwa Muumba wa Ulimwengu. Kundi hili dogo la kidini lilionesha kwenye Dola mpya ya Waislamu tishio linalofanana na lile la makabila ya makafiri. Msomaji anaweza kukumbuka kwamba ujumbe kutoka kwenye kundi hilo dogo la kidini uliweza kuandaa kwa ajli ya Vita vya Handaki wapiganaji elfu kumi kutoka Makka na jamii zingine kwa kutumia propaganda yao ya kivita, kwa lengo la Vita vya Handaki. Unaweza kukumbuka pia kwamba Banu Quraidhah (kutoka kwenye kundi hili dogo) walikiuka makubaliano yao na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Waliungana na maadui zake waliposhuhudia jeshi la makafiri likipata mafanikio kwenye mapambano, hivyo kuufanya mgogoro kuwa mkubwa zaidi ambao hajapata kukabilana nao. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) aliwaadhibu Banu Quraidhah adhabu kali sana baada ya jeshi la washirika kuondoka eneo la Madina. Aliwafanya walipe gharama kubwa kutoka kwenye damu zao na mali zao kwa makosa yao ya wazi kabisa. Hata hivyo, wengi wao miongoni mwa kundi hili dogo walikuwa ni wakazi wa Khaybar na ngome zake nyingi sana ambazo zilikuwa takriban maili thamanini kutoka Madina. Jumuiya hii ilionesha hatari kwa usalama wa Dola ya Kiislamu, na muda ulifika wa kuwadhalilisha hawa watu wa Khaybar baada ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kufanya suluhu ya kuacha vita na makafiri wa Makka hapo Al-Hudaibiyah.

108

Page 108


Imam Ali binamu yake Mtume (s.a.w.w)Lubumba

Dr.Kanju.qxd

7/1/2011

4:37 PM

Imam Ali (a.s.) Ndugu yake Mtume Muhammad (s.a.w.)

MTUKUFU MTUME (S.A.W.W.) ALIZINGIRA KHAYBAR. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) aliporudi kutoka Al-Hudaibiyah, alikaa Madina kwa siku kumi na tano tu. Akigeuza fikra zake kwenye kundi hilo dogo, aliondoka kwenda Khaybar, akiwa na wapiganaji wa kujitolea elfu moja na mia sita (1600), ambao walikuwepo Al-Hudaibiyah. Baada ya kusafiri kwa muda wa siku tatu, yeye na jeshi lake walipiga kambi karibu na ngome za Khaybar wakati wa usiku. Asubuhi ya siku iliyofuata watu wa Khaybar wakiondoka kwenda mashambani kwao, walishangaa kuona jeshi la Waislamu, walirudi nyuma na kusema kwa mshangao: “Muhammad na jeshi!� Inafaa kuzingatia kwamba vita hivi havikuwa vya kidini. Havikuwa na lengo la kuwalazimisha watu wa Khaybar kukubali Imani ya Kiislamu. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kamwe hakuwalazimisha wafuasi wowote wa kitabu kubadili dini yao. Tumekwishasema kwamba hati iliyoandikwa na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) wakati wa mwaka wa kwanza wa Hijiriya, iliwapatia watu wa kundi dogo la kidini ndani na pembezoni ya Madina, uhuru wao wa kidini, pamoja na haki za kiraia kama wangezingatia yaliyomo kwenye mkataba. Kwa bahati mbaya, hawakuzingatia makubaliano ya hati hiyo. Kwa usahihi zaidi walikuwa tishio kwa usalama wa Dola na uhuru wa Waislamu. Hivyo, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alikuwa na wajibu wa kuwadhibiti. Msomaji anaweza kukumbuka kwamba elementi za ulinzi wa Kiislamu kwenye vita tatu zilizopita zilikuwa tatu: Uongozi bora wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na uimara wake na hekima na tabia, ambavyo utakatifu wake uliamuru utiifu wa kila aliyejitolea. Ushujaa wa watu wa Nyumba ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na Mamia ya waumini waaminifu ambao idadi yao iliendelea kuongezeka. 109

Page 109


Imam Ali binamu yake Mtume (s.a.w.w)Lubumba

Dr.Kanju.qxd

7/1/2011

4:37 PM

Imam Ali (a.s.) Ndugu yake Mtume Muhammad (s.a.w.) Unaweza ukakumbuka kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alimpoteza mtu wa ukoo wake Ubeidah Ibn Al-Harith kwenye Vita vya Badr halafu akampoteza ami yake Hamza kwenye vita vya Uhud. Imeelezwa kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), kwenye Vita vya Handaki alimuomba Mwenyezi Mungu ili amuhifadhi Ali kwa ajili yake baada ya kumchukua Ubeidah huko Badr na Hamza huko Uhud. Ali alishiriki vita tatu za nyuma na alikuwa shujaa kwenye vita vyote hivyo. Alikuwa wa kwanza na wa mbele kabisa miongoni mwa wapiganaji kwenye mapambano ya ulinzi na mashambulizi. Matendo yake katika vita vyote vitatu yalikuwa vipengele muhimu katika kuelekeza matokeo ya vita, kuifikisha vita kwenye mwisho mzuri na kuzima moto wake. Hata hivyo, Ali hakuweza kuwa wa kwanza katika kuongoza Vita vya Khaybar. Kwa sababu ya kiafya hakuwepo mwanzoni mwa vita na kutokuwepo kwake kulisababisha upungufu wa dhahiri. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alizingira Khaybar na hali hiyo iliendelea kwa kipindi cha wiki kadhaa bila kuleta matokeo yoyote. Mapigano madogo baina ya pande mbili yalikuwa yanatokea kila siku. Waislamu hawakufanya vizuri katika mapigano hayo. Matumizi ya Waislamu yalianza kupungua haraka. Kwa sababu hii, Waislamu walijaribu kupika nyama ya punda kwenye Vita vya Khaybar, lakini Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) aliwazuia wasile nyama hiyo. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alimpa bendera Abu Bakr. Akaongoza jeshi kuelekea kwenye ngome ya Na’im. Watu wa Khaybar walijitokeza na kuanza kupigana na Waislamu, na Waislamu walishindwa kufanya vema, kwa hiyo walilazimishwa kurudi nyuma. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) siku iliyofuata alimpa bendera Umar na yeye hakuwa na bahati kama Abu Bakr.

110

Page 110


Imam Ali binamu yake Mtume (s.a.w.w)Lubumba

Dr.Kanju.qxd

7/1/2011

4:37 PM

Imam Ali (a.s.) Ndugu yake Mtume Muhammad (s.a.w.)

MTU WA LAZIMA. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alijikuta anakabiliwa na tatizo zito sana. Kuzingira tayari kuliendelea zaidi kuliko ilivyotakiwa kuwa. Chakula kikapungua na kuwa kichache. Hadi hapo jeshi la Kiislamu lilishindwa kudhibiti ngome yoyote. Je, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) aendelee kuzingira Khaybar bila ya matokeo mazuri, au asiendelee kuzingira ngome na arudi Madina? Tukio la aina hii lingeashiria kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) ameshindwa vibaya sana katika vita hivyo. Kama msomaji hataweza kutathmini ukubwa wa jitihada za Ali kwenye vita vya siku za nyuma. Vita vya Khaybar vinathibitisha dhahiri kwamba kuwepo kwa Ali ilikuwa lazima katika kufikisha vita hivi vya kuamua mshindi na mshindwa kwenye mwisho wenye faida kwao.

UFUMBUZI NI ALI. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisikitishwa kuona kwamba mashambulizi yake ya jumla katika muda wa siku mbili mfululizo hayakufuzu, kwa hiyo kuleta ufumbuzi wenye matokeo ya haraka kuhusu tatizo hili, ni uongozi wa Ali ndio tu ufumbuzi uliofaa. Masheikh wawili, Al-Bukhari na Muslim wanatuambia kwenye vitabu vyao vya Sahih yale yaliyotokea. Wamesimulia kwamba, Sahl Ibn Saad, (sahaba mashuhuri) alisema: “Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisema hapo Khaybar: ‘Nitampa bendera hii mtu ambaye kupitia kwake Mwenyezi Mungu ataleta ushindi. Yeye anampenda Mwenyezi Mungu na Mtume Wake, na Mwenyezi Mungu na Mtume Wake wanampenda yeye.’” Masahaba walipitisha usiku wakiulizana wao kwa wao: “Ni nani mtu huyu ambaye Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alimaanisha?” Asubuhi walimwendea Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na kila mmoja wao alikuwa na matumaini kwamba yeye ndiye atakuwa mtu wa bendera. “Yuko wapi Ali Ibn Abu Talib?” Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) aliuliza. “Anaugua maradhi ya kuvimba macho.” Wakasema. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akamuagiza Ali aje. Ali alipoletwa kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) aliyatibu macho ya Ali kwa 111

Page 111


Imam Ali binamu yake Mtume (s.a.w.w)Lubumba

Dr.Kanju.qxd

7/1/2011

4:37 PM

Imam Ali (a.s.) Ndugu yake Mtume Muhammad (s.a.w.) mate yake yaliyoneemeshwa na akamuombea dua. Macho ya Ali yakapona haraka sana kama vile hayakuwa na uvimbe wowote. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akampa Ali bendera na Ali akauliza. “Ewe Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) nipigane nao hadi wawe Waislamu kama sisi?” Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akasema: “Endelea hadi ufike kwenye makazi yao. Waite waje kwenye Uislamu na wajulishe kuhusu wajibu wao kwa Mwenyezi Mungu na Uislamu. Kwa jina la Mwenyezi Mungu, kama atamuongoza mtu mmoja kupitia kwako na kufuata njia iliyo sahihi, itakuwa bora kwako kuliko kumiliki utajiri wenye thamani kubwa.”65

UONGOZI WA KIPEKEE. Ali alikwenda, akiwa amebeba bendera na kinyume na ilivyo kawaida, kwa uhalisi yeye ndiye aliyeongoza jeshi. Salamah Ibn Al-Akwa alisema: “Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Ali alitoka na bendera akikimbia na kuhema. Tulikwenda tukimfuata nyuma hadi alisimika bendera kwenye lundo la mawe karibu na ngome. Mtu mmoja kutoka ndani ya ngome alikwenda kwa Ali na kumuuliza: “Wewe nani?” na akajibu; “Mimi ni Ali Ibn Abi Talib.” Mtu huyo akasema: “Kwa yale yaliyoteremshwa kwa Musa (a.s.) umekwisha shinda.” (jina la Ali maana yake ni ‘juu’). Kama Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alivyotabiri, Muweza wa Yote alimpa Ali ushindi. Alimshinda adui kabla hajarudi kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.).”66 Pia Salamah alisema: “Marhab (shujaa maarufu wa watu wa Khaybar) alitokea kwa majivuno na kutoa changamoto. Ali alimpiga pigo moja kwa upanga wake na kugawa kichwa chake vipande viwili, na ushindi ulifanikishwa.”67 Abu Rafi, sahaba wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisema: “Tulikwenda na 65 Sahih Al-Bukhari, sehemu ya 5, uk. 171 na Muslim kwenye Sahih yake, sehemu ya 15, uk. 178-179. 66 Ibn Hisham, Wasifu wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) sehemu ya 2, uk. 335. 67 Al-Hakim, Al-Mustadrak, sehemu ya 3 uk. 28-29. 112

Page 112


Imam Ali binamu yake Mtume (s.a.w.w)Lubumba

Dr.Kanju.qxd

7/1/2011

4:37 PM

Imam Ali (a.s.) Ndugu yake Mtume Muhammad (s.a.w.) Ali Ibn Abu Talib (a.s.) ambapo Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alimpeleka na bendera yake. Alipokaribia ngome, wakazi wa ngome hiyo walitoka nje na alipigana nao. Mtu mmoja kutoka miongoni mwa maadui akampiga Ali pigo moja na Ali akapoteza ngao yake. Ali alichukua mlango kwenye ngome na akajikinga nao hadi mwisho wa pambano. Mimi na watu saba tulijaribu kuusogeza mlango huo, lakini tulishindwa.�68 Maadui waliokuwa wanarudi nyuma walikimbilia ndani ya ngome baada ya pambano kali ambalo halikudumu muda mrefu baada ya kifo cha Marhab. Walijaribu kujitetea kwa kuingia kwenye ngome na kufunga mlango wake baada ya kushindwa mapigano ya ana kwa ana. Lakini mkakati huo haukuwasaidia. Ali alifungua mlango na kuingia ndani ya ngome na wapiganaji wake wakamfuata. Alifunguaje lango hilo kubwa? Ni yeye au yeyote miongoni mwa wapiganaji wake aliingia ndani kwa kupanda ukuta na kufungua lango hilo kutokea kwa ndani? Waandishi wa historia wala wasimulizi wa Hadith hawakuandika kwamba Waislamu waliingia ndani ya ngome kwa kupanda ukuta. Hivi Ali kwa kutumia uwezo usio wa kawaida, ndivyo alivyoutengua mlango kama baadhi ya Hadith zilivyojulisha? Kwa hili uwezekano upo, huenda ikawa kweli. Kwani muujiza mwingine ulifanywa na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) mnamo siku ambapo macho ya Ali yaliponywa na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kwa kutemea mate yake ya baraka. Kutanguka kwa mlango kunaelekea kulikuwa ni muujiza wa nyongeza uliotokea siku hiyo. Lakini mlango ambao Abu Rafi alitujulisha sisi kwamba Ali aliutumia kama ngao ndio huo huo mlango wa ngome. Ali alipoingia kwenye ngome, alimaliza uwezo wa kujitetea wa watu wa ngome hiyo. Hawangeweza kushinda pambano la pili baada ya kushindwa la kwanza. Ngome ilichukuliwa na Waislamu kabla ya safu ya nyuma ya jeshi kuungana na safu ya mbele. Ngome zingine zilifuatia ngome ya 68 Hishamu, Wasifu wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) sehemu ya 2, uk. 335. 113

Page 113


Imam Ali binamu yake Mtume (s.a.w.w)Lubumba

Dr.Kanju.qxd

7/1/2011

4:37 PM

Imam Ali (a.s.) Ndugu yake Mtume Muhammad (s.a.w.) Naim. Ziliangukia mikononi mwa Waislamu moja baada ya nyingine hadi eneo lote la Khaybar likasalimu amri kwenye Dola ya Waislam.

HITIMISHO. Msomaji anaweza kufikia hitimisho lifuatalo kwa urahisi sana: Vita vya Khaybar vilikuwa moja wapo ya vita muhimu vya mustakabali wa Waislamu. Vilitanguliwa na vita viwili ambamo Waislamu hawakufanya vizuri. Waislamu walishindwa kwenye vita vya Uhud na wakakimbia isipokuwa wachache wao. Hii ilifuatiwa na vita vya Handaki ambapo Waislamu walikuwa wanajitetea badala ya kushambulia. Walishtuka na kuogopa isipokuwa wale ambao Muweza wa Yote aliwaimarisha. Nyoyo zilifika hadi kwenye makoo yao. Vita viliisha na Waislamu hawakudiriki kukabiliana na maadui zao au kuvuka kutoka upande wao na kwenda upande wa adui. Walibaki nyuma ya Handaki lao. Waislamu walizidi maadui zao kwa idadi kwenye Vita vya Khaybar. Kama wangeshindwa kuwadhibiti maadui zao, kutokufaulu kwao ingekuwa ishara ya kuonesha udhaifu wao na kuyashawishi makabila mengi yenye chuki kuwashambulia Waislamu na watu wa Khaybar wangekuwa ndio kiini cha majeshi ya uvamizi siku za usoni. Zaidi ya hayo Waislamu wenyewe, kwa sababu ya kushindwa kwao katika Khaybar, wangepoteza hali yao ya kujiamini na wangeona kwamba ushindi wao dhidi ya maadui wao wengi ni uwezekano ulioko mbali sana. Kwa upande mwingine, kama Waislamu wanapata ushindi dhidi ya watu wa Khaybar, matokeo yangekuwa kinyume chake. Ushindi ungeongeza hamasa yao na kumwondosha adui hatari na kuyafanya makabila mengine ya Waarabu kuwaheshimu Waislamu na kusita kuwashambulia wao. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) hakufurahiwa na msururu wa matukio ya vita. Jeshi lake liliendelea kuzingira ngome kwa muda mrefu. Akiba ya chakula ilipungua. Kama kuzingira kukiendelea na Waislamu hawawezi kushinda dhidi ya maadui, Waislamu wangelazimika kurudi nyuma na kuondoa 114

Page 114


Imam Ali binamu yake Mtume (s.a.w.w)Lubumba

Dr.Kanju.qxd

7/1/2011

4:37 PM

Imam Ali (a.s.) Ndugu yake Mtume Muhammad (s.a.w.) mzingiro huo. Huu ungekuwa ni msiba mkubwa wa kushindwa kwa Waislamu. Kwa hiyo, kwa kufuata agizo la Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), waliendesha mashambulizi ya jumla mawili kwa muda wa siku mbili mfululizo chini ya uongozi wa Abu Bakr halafu Umar. Kwa kuwa Waislamu walishindwa kuteka ngome yoyote wakati wa mashambulizi mawili hayo, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alitambua kwamba Waislamu walikuwa wanakabiliwa na mtafaruku usio wa kawaida. Alitaka upatikane ufumbuzi wenye matokeo ya haraka kutatua tatizo hilo. Kufuatana na mtazamo wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), aliamua kufanya muujiza ili amwezeshe Ali kutimiza kazi yake, kwa sababu uongozi wa Ali ulikuwa ndio tu ufumbuzi wa tatizo hilo. Ali alikuwa anaugua maradhi ya uvimbe wa macho, na hangeweza kutimiza kazi hiyo ngumu mpaka macho yake yatibiwe. Lau kama angekuwepo mtu mwingine mwenye uwezo wa kutimiza kazi hiyo, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) asingempa mamlaka hayo Ali. Ali alisamehewa kwenye kazi ya Jihad kwa sababu ya hali yake isiyo ya kawaida, lakini hali ilikuwa mbaya sana na hapakuwepo na mwingine zaidi ya Ali ambaye angeweza kukabili hatari hiyo na kuibuka mshindi.

MIUJIZA MIWILI. Kupona kwa macho ya Ali kwa kutumia mate ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) ilikuwa moja ya miujiza miwili. Muujiza wa pili ni utabiri wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.): Aliwajulisha Waislamu kwamba mtu ambaye angeongoza jeshi siku ya tatu angeweza kwa msaada wa Mwenyezi Mungu kuteka ngome zote. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kama mwanadamu hangeweza kubashiri kwamba Mwenyezi Mungu angefungua milango ya ngome kwa kufanikisha ushindi wa Ali. Uwezekano wa Ali kuuawa ulikuwepo au kuumizwa vibaya, na hiyo ingemzuia yeye (Ali) kuendelea na kampeni yake. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) hakutamka maneno yake kwa kujiamini yeye mwenyewe. Alitamka maneno hayo kwa kutegemea tu 115

Page 115


Imam Ali binamu yake Mtume (s.a.w.w)Lubumba

Dr.Kanju.qxd

7/1/2011

4:37 PM

Imam Ali (a.s.) Ndugu yake Mtume Muhammad (s.a.w.) Wahyi wa Mwenyezi Mungu. Ni Mwenyezi Mungu peke Yake ndiye aliyekuwa na uwezo wa kutambua nini kingetokea kwa Ali na kwamba angerudi baada ya Mwenyezi Mungu kufungua milango ya ngome kupitia kwenye mikono yake. Jeshi lote lilishindwa na halikuweza kuteka ngome pale ambapo Ali hakuwepo. Ni kuwepo kwa Ali peke yake ndio ilikuwa njia ya kupata ushindi. Hii itathibitisha kwa dhahiri kwamba Ali ndiye aliyetoa mchango mkubwa zaidi baada ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kuasisi Dola ya Waislamu, kwani, yeye Ali alikuwa mtekelezaji wa mbinu ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na muangamizaji wa maadui zake. Kwa ukweli wa tamko hili, Umar, Khalifa wa pili, alithibitisha alipomwambia mtu aliyemshutumu Ali kuwa mwenye kiburi; “Mtu kama Ali anayo haki ya kuwa na majivuno. Kwa jina la Mwenyezi Mungu, nguzo ya Uislamu haingesimamishwa bila ya upanga wa Ali. Na yeye ndiye hakimu wa daraja la juu sana wa umma huu, Mwislamu wake wa mwanzo kabisa na anayeheshimiwa sana.” (Sharh Nahjul-Balaghah ya Ibn Abil Hadiid, Jz.3, uk. 179)

WIZARA YA ASILI. Muweza wa Yote alimuimarisha Mtukufu Mtume Wake (s.a.w.w.) kupitia kwa binamu yake Ali ambaye alimuahidi miaka kumi kabla ya Hijira kuwa Naibu wake kwenye kazi yake kubwa. Lau kama Ali hangeahidi kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kwenye mkutano wa ukoo kuwa “waziri” wake, hangefanya tofauti na vile alivyofanya. Mwambatano wa Ali kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) ulikuwa wa asili, ambao haukuhitaji ahadi au makubaliano.

116

Page 116


Imam Ali binamu yake Mtume (s.a.w.w)Lubumba

Dr.Kanju.qxd

7/1/2011

4:37 PM

Imam Ali (a.s.) Ndugu yake Mtume Muhammad (s.a.w.) Hakutoa ahadi kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kwa ajili ya uwaziri wake na msaada kamili ili apate daraja muhimu ambazo Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alimuahidi. Ali alitoa ahadi yake kwa sababu aliamini kwamba msaada wake kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) ulikuwa ni kazi ambayo yeye aliumbiwa kuitekeleza. Mapenzi juu ya Mwenyezi Mungu na Mtukufu Mtume Wake (s.a.w.w.) yalijaa moyoni mwake, na kwa hiyo aliweka dhamana ya uhai wake kwa kuwafurahisha wao.

CHAGUO LA MWENYEZI MUNGU. Wakati Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alipompatia Ali daraja za undugu, wasii na mrithi, alitamka hayo kwa amri ya Mwenyezi Mungu, na Mwenyezi Mungu humchagua kwa ajili ya daraja hizi yule tu ambaye anazo sifa zinazoendana nazo. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), kwa upande mwingine hakumpa Ali daraja hizi kwa sababu ya ahadi ya msaada wake, lakini ni kwa sababu Ali alikuwa mwenye kustahiki. Lau kama kazi ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) haingekuwa inahitaji jitihada na kutoa muhanga kwa Ali, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) hangechagua ndugu au wasii au Khalifa mwingine asiye kuwa yeye, kwani Ali alikuwa mfano wake mkubwa sana kwa maadili, kutenda haki na utambuzi. Ali alikuwa Mwislamu wa kwanza na alikuwa mtiifu sana kwa Mwenyezi Mungu na Mtukufu Mtume Wake (s.a.w.w.), na kwa hiyo alikuwa kipenzi cha Mwenyezi Mungu na Mtukufu Mtume Wake (s.a.w.w.). Hakuna haja ya ushahidi unaong’ara zaidi ya tangazo la Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) huko Khaybar. “Nitampa bendera mtu ambaye kupitia kwake Mwenyezi Mungu ataleta ushindi. Anampenda Mwenyezi Mungu na Mtume Wake, na Mwenyezi Mungu na Mtume Wake wanampenda yeye.” 117

Page 117


Imam Ali binamu yake Mtume (s.a.w.w)Lubumba

Dr.Kanju.qxd

7/1/2011

4:37 PM

Imam Ali (a.s.) Ndugu yake Mtume Muhammad (s.a.w.) AT-Tirmidhi kwenye Sunan yake (mojawapo ya Sahih-Sita)69na Al-Hakim kwenye Al-Mustadrak yake,70 wamesimulia kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alipewa nyama ya ndege iliyopikwa. Aliomba na katika maombi yake alisema: “Ewe Mwenyezi Mungu, niletee kipenzi chako kutoka miongoni mwa viumbe vyako ale ndege huyu pamoja na mimi.� Ali peke yake alikuja na akala pamoja naye. Kwa sababu Ali ndiye tu alikuwa na sifa ya kuwa ndugu, wasii na mrithi wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alimpa daraja tatu hizi kabla ya mwanzo wa kazi yake kubwa mno ya kujitoa muhanga. Hii inathibitisha kwamba alikuwa chaguo la Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kwa vyeo vilivyotajwa hapo juu, bila kujali haja ya ujumbe kwa kujitoa kwake muhanga. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alipompa Ali vyeo hivi, mashahidi wa tukio hilo hawakuzidi watu thelathini au arubaini. Wote walikuwa watu wa ukoo wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Ilikuwa tu ni jambo la muda muafaka kwake yeye kutangaza kwa Waislamu wote kile alichotangaza kwa watu wa ukoo wake. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) aliamua kufanya hivyo pole pole. Alianza kwa kutangaza udugu wake kwa Ali mwanzoni mwa Hijira.

* * * * *

69 Al-Tirmidhi, kwenye Sunan yake, sehemu ya 5, uk. 300 (hadith Na. 3805) 70 Al-Hakim, Al-Mustadrak, sehemu ya 3, uk. 130-131. 118

Page 118


Imam Ali binamu yake Mtume (s.a.w.w)Lubumba

Dr.Kanju.qxd

7/1/2011

4:37 PM

Imam Ali (a.s.) Ndugu yake Mtume Muhammad (s.a.w.)

SURA YA KUMI NA MBILI. UDUGU WATANGAZWA. Kiini cha Dola ya Kiislamu kilianza mwanzoni mwa Hijira. Kuasisiwa kwa dola hii ilikuwa sampuli kifani ya kipekee katika historia ya mwanadamu. Kabla ya Uislamu hatujui dola yoyote iliyoanzishwa katika misingi ya udugu uliotokana na imani ua Upweke wa Mwenyezi Mungu na Haki Yake ya ulimwengu wote ambayo inakataza ubaguzi wa kiukoo, kitaifa na kijamii. Kusema kweli ni vigumu kuona katika historia mfano dhahiri isipokuwa ule wa Dola ya Kiislamu ya siku za mwanzo wa Uislamu ambamo serikali ilianzishwa kama matokeo ya hiyari ya watu kushirikiana mawazo ya kiroho na ya kidunia. Hata hivyo, udugu huu wa jumla unaweza kubakia kama ni wazo la dhahania tu kama hakuna mfano wake halisi uliotekelezwa. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alitaka kuwapa Waislamu mfano halisi kupitia udugu mdogo mdogo, uhusianao maalum baina ya Waislamu wawili, ambao kwawo kila mmoja wao anakuwa ndugu wa mwenzake katika (imani ya) Mwenyezi Mungu na anamtendea mwenzake kama anavyomtendea ndugu yake wa kuzaliwa naye. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alitoa tangazo la undugu wa watu binafsi mnamo mwaka wa kwanza wa hijiriya, lakini udugu mmoja ulikwishaanzishwa miaka kumi kabla ya Hijira. Huu ni udugu ambao aliuasisi baina yake na Ali kwenye mkutano uliofanyika nyumbani kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) hapo Makka. Imeandikwa kwenye Al-Siirat Al-Halabiyah kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) aliweka undugu baina ya Abu Bakr na Umar, baina ya Atban Ibn Malik na Umar; baina ya Abu Bakr na Kharijah Ibn Zayd; Baina ya Abu Ruwaim Al-Khath’am na Bilal; baina ya Usaid Ibn Hudheir na Zayd Ibn Haritha, baina ya Abu Ubeidah na Saad Ibn Maath; baina ya AbdullRahman Ibn Auf na Saad Ibn Al-Rabi. 119

Page 119


Imam Ali binamu yake Mtume (s.a.w.w)Lubumba

Dr.Kanju.qxd

7/1/2011

4:37 PM

Imam Ali (a.s.) Ndugu yake Mtume Muhammad (s.a.w.) Halafu akanyanyua mkono wa Ali Ibn Abi Talib, akasema: “Huyu ni ndugu yangu.” Hivyo Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na Ali wakawa ndugu.71 Ibn Hisham kwenye kitabu chake cha Sira (wasifu wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.)) alisimulia yafuatayo: “Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), baada ya Hijira aliwaambia Waislamu: ‘Kuweni ndugu katika Mungu. Kila wawili wenu lazima wawe ndugu.’ Halafu akaunyanyua mkono wa Ali Ibn Abi Talib na akasema: ‘Huyu ni ndugu yangu.’ Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), kiongozi wa Mitume, Imam wa watenda haki; yule ambaye halinganishwi na mja yeyote katika waja wa Mwenyezi Mungu, yeye na Ali Ibn Abi Talib wakawa ndugu. Hamza, Simba wa Mwenyezi Mungu na Mtume Wake na Zayid Ibn Harith wakawa ndugu na Abu Bakr na Kharijah Ibn Zuhair wakawa ndugu. Umar Ibn Khattab na Atban Ibn Malik wakawa ndugu …”72 Aina hii ya undugu unaweza kukidhi angalau moja ya madhumuni mawili yafuatayo: Undugu huu huwa mbadala wa uhusiano wa damu kwa ule wa kiroho. Wakati watu wawili wanapokuwa wanatoka kwenye koo mbili, makabila mawili au jamii mbili tofauti, undugu wao katika kanuni na imani huchukua nafasi ya undugu wa kuzaliwa. Hii hufanya ndugu wawili katika dini kuwa tayari kushirikiana katika kutangaza dini yao. Ndugu wote wawili hupata kinga dhidi ya uadui kama kutokuelewana kunatokea kati ya mmoja wa ndugu wawili na jamaa wa ndugu mwingine. Undugu huu wa kati ya watu wawili kutoka makabila mawili au koo mbili hufanya kila mmoja kuwa rafiki wa jamaa wa ukoo au kabila la mwingine, na kila mmoja wa ndugu wawili humpenda mwenzake, na kila mmojawao anao ndugu ambao kwamba hutendeana mapenzi. Ndugu hawa wa kuzali71 Ali Ibn Burhanudeen Al-Halabi, Wasifu wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), sehemu ya 2, uk. 97. 72 Ibn Hisham, sehemu ya 1, uk. 505. 120

Page 120


Imam Ali binamu yake Mtume (s.a.w.w)Lubumba

Dr.Kanju.qxd

7/1/2011

4:37 PM

Imam Ali (a.s.) Ndugu yake Mtume Muhammad (s.a.w.) wa kupitia kwenye udugu huu huwa na mfungamano usio wa moja kwa moja kwa undugu wa kiroho wa ndugu yao wa kuzaliwa. Hivyo, undugu wa kidini huwa ni upanuzi wa undugu wa kuzaliwa, na undugu wa kuzaliwa huwa upanuzi wa udugu wa kidini. Inapokuwa ni kwa chaguo la Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), undugu wa aina hii ni ushahidi wa mfanano wa pamoja wa kiroho baina ya ndugu wawili. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alitambua vema kuhusu masahaba wake zaidi kuliko walivyojijua wenyewe. Masahaba wawili wanaweza kuwa hawajui kuhusu mfanano wao wa kiroho kama anavyojua yeye. Hivyo, pale ambapo huwafanya wawili kuwa ndugu, udugu wao unatakiwa kuongeza ushirikiano wao na kuendeleza kukua katika uwiano kwenye uaminifu wao kwenye dini yao.

UMUHIMU WA UNDUGU. Tukiangalia undugu baina ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na Ali kabla na baada ya Hijira, tunaona kwamba undugu wao haukidhi haja ya lengo la kwanza, yaani: Kutengenezwa kwa uhusiano wa karibu baina ya watu wawili kutoka kwenye koo, makabila au jamii mbili tofauti. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na Ali hawakutoka kwenye miji miwili tofauti au makabila mawili tofauti au koo mbili tofauti. Wao walikuwa mabinamu wa kwanza. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) hakumtaka undugu yeyote kabla au baada ya Hijira isipokuwa Ali. Kutokana na hili, tunaweza kuhitimisha kwamba lengo la undugu baina ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na Ali lilikuwa ni kutangaza mfanano wao wawili hao wa kiroho. Undugu baina ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na Ali ni ukweli unaojulikana sana katika historia ya Uislamu. Ulisimuliwa kupitia wasimulizi wengi. Undugu huu ulikuwa wa maana na muhimu sana kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.).

121

Page 121


Imam Ali binamu yake Mtume (s.a.w.w)Lubumba

Dr.Kanju.qxd

7/1/2011

4:37 PM

Imam Ali (a.s.) Ndugu yake Mtume Muhammad (s.a.w.) Al-Hakim kwenye Al-Mustadrak yake alisimulia kwa njia mbili kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alimwambia Ali: “Wewe ni ndugu yangu hapa duniani na Akhera.”73 Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alitoka nje ambapo uso wake ulikuwa unang’aa. Abdul Rahman Ibn Auf alimuuliza: “Kuna habari gani nzuri?” Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akasema; “Habari njema zimekuja kwangu kutoka kwa Mola wangu Mlezi kuhusu ndugu yangu na binamu yangu na binti yangu. Kwamba Mwenyezi Mungu anamuoza Ali kwa Fatimahh!”74 Halafu alimwambia Ali: “Wewe ni ndugu yangu, sahaba wangu na mshirika wangu huko Peponi.” 75 Wakati mwingine Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alimwambia Ali: “Wewe ni ndugu yangu na waziri wangu, unalipa deni langu na kutimiza ahadi yangu …” 76 Fatimah alipopelekwa kwenye nyumba ya mume wake Ali, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alimwambia Ummu Aiman: “Niitie ndugu yangu.” Akasema (kwa utani): “Ni ndugu yako halafu unamuoza binti yako?” Akajibu: “Ndio, Ummu Aiman.” Alimuitia Ali, na akaja …”77 Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alipokuwa taabani kitandani mwake, alisema: “Niiteni ndugu yangu.” Wakamuita Ali na alikwenda kwake. Akasema: “Njoo karibu na mimi,” na Ali alifanya hivyo. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) 73 Al-Hakim, kwenye Al-Mustadrak yake sehemu ya 3, uk. 14. Sharaful Deen Al-Murajaat, uk. 130. 74 Ibn Hajaf, As-Sawa’iq Al-Muhriqah, uk. 403 (iliyosimuliwa na Sharaful Deen Al-Murajaat, uk. 130. 75 Al-Muttaaqi Al-Hind, Kanzul-Ummal, hadith Na. 6105. 76 Al-Tabarani, kwenye Maj’mau yake kubwa ya hadithi (iliyosimuliwa na Ali Multaqi Al-Hindi kwenye Kanzul-Ummal, na kuchapishwa pembezoni mwa Musnad Imam Ahmad, sehemu ya 5, uk. 32. 77 Al-Hakim kwenye Al-Mustadrak yake, sehemu ya 3, uk. 159. 122

Page 122


Imam Ali binamu yake Mtume (s.a.w.w)Lubumba

Dr.Kanju.qxd

7/1/2011

4:37 PM

Imam Ali (a.s.) Ndugu yake Mtume Muhammad (s.a.w.) aliegemea kwa Ali na aliendelea kumwambia maneno hadi hapo roho yake takatifu ilipotoka kwenye mwili wake.78 Hadith hizi ni chache tu miongoni mwa nyingi nyinginezo zinazozungumzia undugu wa Ali na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Zinaonesha wazi kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alimchagua yeye kama ndugu kwa sababu alikuwa ndiye mwenye kumfuatia baada yake katika kutakasika na tabia njema. La sivyo Ali asingekuwa chaguo lililotegemewa, kwani alikuwa na umri wa miaka thelathini pungufu kwa umri wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Ni dhahiri alimteuwa yeye kwa sababu alikuwa ni yeye tu aliyekuwa anastahili heshima hii ya kipekee.

MKWE WA MTUKUFU MTUME (S.A.W.W.). Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alimpa Ali heshima ya pekee kwa kumchagua kuwa mkwe wake. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alimuoza Ali binti yake, Fatimah Az-Zahra (Mama mwenye nuru), ambaye kwa niaba yake, baba yake alisadikisha kwamba Fatimah ni kiongozi wa mabibi wa Peponi, au kiongozi wa wanawake waumini.79 Pia alisema: “Fatimah ni kipande cha mwili wangu, yeyote anayemuudhi yeye, atakuwa ameniudhi mimi.”80 Aisha, mke wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), pia alisema kuhusu Fatimah: “Kamwe sijapata kuona mwenye kufanana zaidi na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) katika namna ya kuzungumza kama Fatimah, binti wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Wakati wowote Fatimah alipokuja kwa baba yake, Mtume alikuwa na tabia ya kumkaribisha yeye, alikuwa akisimama kwa 78 Ibn Saad, Al-Tabaqat, sehemu ya 2, uk. 263. 79 Al-Bukhari alisimulia kupitia sanad yske mpaka kwa Aisha katika Sahih yake

kwenye sehemu ya Mwanzo wa Uumbaji, Sura ya Uthibitisho wa Utume, sehemu ya 5, uk. 25. 80 Al-Bukhari kwenye Sahih yake, sura ya “Uadilifu wa Fatimah.” 123

Page 123


Imam Ali binamu yake Mtume (s.a.w.w)Lubumba

Dr.Kanju.qxd

7/1/2011

4:37 PM

Imam Ali (a.s.) Ndugu yake Mtume Muhammad (s.a.w.) ajili yake, akimshika mkono wake na kumkalisha mahali alipokuwa ameketi yeye (Mtukufu Mtume (s.a.w.w.).”81 Pia Aisha alisema kuhusu Fatimah: “Kamwe sijapata kushuhudia mtu mkweli kuzidi Fatimah baada ya baba yake.” 82 Masahaba maarufu walimposa Fatimah lakini Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) aliwakatalia, akisema: “Ninangojea maelezo kuhusu ndoa yake.” (Alikuwa na maana kwamba alikuwa anangoja agizo kutoka kwa Mwenyezi Mungu). Ali alipomposa Fatimah, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alimkaribisha Ali, na Ali akamuoa binti wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) mnamo mwaka wa kwanza baada ya Hijira. Fatimah alipelekwa nyumbani kwa mume wake mwaka uliofuata baada ya Hijira. Alipelekwa nyumbani kwa mume wake mwaka uliofuata baada ya Vita vya Badr. Ndoa hii ilikusudiwa kuwa ya pekee katika umuhimu wake. Kati ya matunda yatokanayo humo ni vito viwili vya taifa hili. Al-Hasan na Al-Husein, ambao kuhusu wao Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisema: “Malaika alikuja kutoka Mbinguni kuniletea mimi habari njema: Kwamba Fatimah ni kiongozi wa wanawake wa Peponi, na kwamba Al-Hasan na Al-Husein ni viongozi wa vijana wa Peponi.83 Kwa kuzaliwa kwao, iliundwa familia tukufu sana. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) aliwaagiza Waislamu waisalie familia hii wakati wowote wanapo mswalia yeye. hii ni familia ambayo watu wake Waislamu wanahimizwa kuwafuata. 81 Al-Hakim, kwenye Al-Mustadrak yake, sehemu ya 3, uk. 154. 82 Al-Hakim Al-Mustadrak, sehemu ya 3, uk. 160. 83 Al-Tirmidhi kwenye Sunan yake (miongoni mwa Sahih Sita). sehemu ya 2, uk. 306. 124

Page 124


Imam Ali binamu yake Mtume (s.a.w.w)Lubumba

Dr.Kanju.qxd

7/1/2011

4:37 PM

Imam Ali (a.s.) Ndugu yake Mtume Muhammad (s.a.w.)

FAMILIA ILIYOTUKUZWA NA MWENYEZI MUNGU. Katika yote ambayo Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisema kuhusu Ali na watu wa familia yake, alisema kwa mamlaka ya Mwenyezi Mungu na alitegemea agizo la Mwenyezi Mungu na Wahyi Wake. Muweza wa Yote aliteremsha aya kumi na nane (18) kwa mfuatano kuhusu kujitoa muhanga kwa familia hii, mapenzi ya familia hii kwa Mwenyezi Mungu, na nafasi ya watu wake huko Peponi. Kwenye kitabu chake AlWalid Al-Basiit, Imam Razi kwenye fasili yake pana kuhusu Qur’ani Tukufu; Az-Zamakh-Shari kwenye Kashaf yake na Nizamud-Din AlNisaburi kwenye fasili yake ‘Gara’ibul Qur’ani.’84 na As-Shablanji, kwenye kitabu chake Noorul Absar,85 aliandika kwamba Ibn Abbas alisema kwamba: “Al-Hasan na Al-Husein waliugua, Ali na Fatimah waliweka nadhiri ya kufunga saumu ya siku tatu ya kumshukuru Mwenyezi Mungu endapo watoto wao wawili wangepona. Watoto wao wawili nao pia waliweka nadhiri kama walivyofanya wazazi wao na mtumishi wao Fidhah naye alifanya hivyo. Watoto hao wawili wakapona na familia ilifanya saumu ya siku tatu mfululizo. Kulikuwa hakuna chakula kwa ajili ya familia hiyo katika kipindi cha siku tatu hizo isipokuwa kiasi kidogo cha mkate wa shayiri. Wakati wa futari ulipowadia (jioni) mtu masikini alikwenda mlangoni kwao, akitafuta chakula. Familia ilimpa chakula chote kilichokuwepo. Jioni iliyofuata, yatima alikwenda kwao akaomba chakula na familia ilifanya kama ilivyofanya jioni ya kwanza. Mnamo siku ya tatu jioni mateka alikwenda kwao 84 Nizamudeen Al-Nisaburi, kwenye ‘Gharai’bul- Qur’ani yake maandishi yaliyochapwa kwenye pembe ya Fasili ya Al-Tabari, kwenye Qur’ani, sehemu ya 29, uk. 112-113. 85 Sayed Al-Shablanji, Nuurul Absar, uk. 112-114. 125

Page 125


Imam Ali binamu yake Mtume (s.a.w.w)Lubumba

Dr.Kanju.qxd

7/1/2011

4:37 PM

Imam Ali (a.s.) Ndugu yake Mtume Muhammad (s.a.w.) akaomba chakula. Famili alifanya kama iliyofanya katika siku mbili za nyuma. Kuhusu tukio hili, Muweza wa yote aliteremsha Sura ya 76; adDahr ambamo tunaona Aya zifuatazo:

“Hakika watu wema watakunywa katika kikombe kilichochanganyika na kafuri. Ni chemchem watakaoinywa waja wa Mwenyezi Mungu, wakayamiminisha kwa wingi. Wanatimiza ahadi na wanaiogopa siku ambayo shari yake inaenea sana, ….. Na huwalisha chakula juu ya kukipenda kwake, masikini na yatima na wafungwa. Hakika sisi tunakulisheni kwa wajihi wa Mwenyezi Mungu, Hatutaki kwenu malipo wala shukrani. Hakika sisi tunaiogopa kwa Mola wetu Mlezi hiyo siku yenye shida na taabu. Basi Mwenyezi Mungu atawalinda na shari ya siku hiyo, na atawakutanisha na raha na furaha. Na atawajazi Bustani za Peponi na maguo ya hariri kwa vile walivyo subiri”Qur’ani, ad-Dahr; 76:5-12

126

Page 126


Imam Ali binamu yake Mtume (s.a.w.w)Lubumba

Dr.Kanju.qxd

7/1/2011

4:37 PM

Imam Ali (a.s.) Ndugu yake Mtume Muhammad (s.a.w.)

SURA YA KUMI NA TATU NAFASI YA ALI KUTOKA KWA MTUKUFU MTUME (S.A.W.W.) NDANI YA QUR’ANI. Wakati wa mwaka wa tisa baada ya Hijira, ujumbe wa Wakristo kutoka Najran, Yemen, walikwenda Madina kuulizia kuhusu Uislamu na wajadiliane na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kuhusu dini. Yalifanyika mazungumzo baina ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na ujumbe huo ambapo Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alielezea hali bayana ya Uislamu kwenye mafundisho ya Masihi. Ujumbe wa Wakristo ulichagua kuendelea kubakia kwenye msimamo wao hasi. Wahyi uliteremshwa kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) ukimuamuru awaite wajumbe hao kwenye maombi yatakayofanywa na pande zote mbili, wamwombe Mwenyezi Mungu Mweza wa yote kushusha adhabu Yake kwa wale ambao watasema uwongo baina ya hizo pande mbili. Kutoka kwenye Qur’ani Tukufu tunasoma:

“Watakao kuhoji katika haya baada ya kukufikilia ilimu hii waambe: Njooni tuwaite watoto wetu na watoto wenu, na wanawake wetu na wanawake zenu na sisi wenyewe ni nyinyi wenyewe, kisha tuombe kwa unyenyekevu tutake laana ya Mwenyezi Mungu iwashukie waongo.” Surat al-Imran; 3 Aya ya 61

127

Page 127


Imam Ali binamu yake Mtume (s.a.w.w)Lubumba

Dr.Kanju.qxd

7/1/2011

4:37 PM

Imam Ali (a.s.) Ndugu yake Mtume Muhammad (s.a.w.) Inafaa kuangalia kwamba hakuna Hadith hata moja inayosema kwamba watu wa familia hii waliwatamkia kwa sauti wale watu waliowapa chakula: “Hakika sisi tunakulisheni kwa wajihi wa Mwenyezi Mungu. Hatutaki kwenu malipo wala shukrani:” Maneno haya yalikuwa ndani ya nyoyo zao, si kwenye ndimi zao, lakini Mwenyezi Mungu alisema wazi kwenye Kitabu chake yale waliyoyafanya siri kwenye nyoyo zao.

USHAHIDI WA KIPEKEE Qur’ani Tukufu haina ushahidi wowote wa aina hii kuhusu familia nyingine yoyote ya Waislamu. Hii ni kwa sababu hakuna familia nyingine iliyotoa kile ambacho familia hii ilijitolea muhanga. Hatujui familia nyingine ambayo ilikuwa karibu sana hivyo kwamba watu wake wote waliwapa wengine kwa ajili ya kumpenda Mwenyezi Mungu chakula chao muhimu kwa muda wa siku tatu mfululizo. Hata hivyo, familia hii ilitegemewa kuzizidi familia nyingine zote katika kujitoa muhanga. Kwani Ali alikuwa ndugu yake Mtukufu Mtume (s.a.w.w.): Mke wake alikuwa binti ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.); na watoto wao wawili, kwa ushahidi wa Aya ya ‘Mubahalah’ wanaitwa watoto wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Watu wa familia hii walikuwa ndio ambao Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alikwenda nao wakati Mwenyezi Mungu Muweza wa Yote alipoamuru kuwaita ujumbe wa Wakristo wa Najran wakutane kwenye Mubahila (maombi ya pande mbili zinazopingana, wamwombe Mwenyezi Mungu kuwaadhibu wale watakaoonekana kusema uwongo). Kuwawasilisha wao mnamo siku hiyo ulikuwa ni ushahidi unaong’ara kwamba wao walikuwa na daraja la juu zaidi miongoni mwa Waislamu kuhusu kukubalika kimaadili, na hususan kumuwasilisha Ali ilionesha kwamba uhusiano baina ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na Ali ulivuka mpaka wa udugu na kufikia kiwango cha umoja. 128

Page 128


Imam Ali binamu yake Mtume (s.a.w.w)Lubumba

Dr.Kanju.qxd

7/1/2011

4:37 PM

Imam Ali (a.s.) Ndugu yake Mtume Muhammad (s.a.w.) Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) katika kutekeleza amri iliyoteremshwa, aliuita ujumbe wa Kikristo kwa maombi. An-Nisaburi kwenye tafsir yake ya Qur’ani Tukufu, iitwayo ‘Ghara’ibul-Qur’ani na Aja’ibul-Furqan” aliandika yafuatayo: “Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) aliuambia ujumbe wa Kiskristo: Mwenyezi Mungu ameniamuru kuwaiteni nyinyi tuombe pamoja ili waongo waadhibiwe.” Wakasema “Ewe Abu Al-Qasim (kuniya ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.)), tutafikiria kuhusu jambo hili, halafu tutakuja kwako.” Walifanya mkutano ulioongozwa na mshauri wao, Al-Aquib. Walipomwomba awape ushauri, alisema: “Kwa jina la Mwenyezi Mungu, mlikwishatambua kwamba Muhammad ni Mjumbe wa Mwenyezi Mungu. Aliwaambieni ukweli ulio sahihi kuhusu mtu wenu, Masihi. Kwa jina la Mwenyezi Mungu, wakati wowote watu wanapompa changamoto Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na kuomba pamoja naye ili waongo waadhibiwe, watu wazima wao hawataishi muda mrefu na watoto wao hawatakua. Yatakuwa ni maangamizi yenu kama mkikubali changamoto lake. Kama mkisisitiza kuendelea na dini yenu, fanyeni mkataba wa amani baina yenu na mtu huyu na mrudi nchini kwenu. “Ujumbe wa Kikristo uliporudi kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), waliomuona anakwenda kuelekea sehemu ya kufanyia maombi, akiwa amevaa joho lililotengenezwa kwa manyoya meusi, akiwa amembeba AlHusein mkononi mwake, na kumwongoza Al-Hasan kwa mkono wake, akiwa amefuatana na Fatimah aliyekuwa nyuma yake na Ali akiwa nyuma ya Fatimah. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) aliwaambia watu wanne wa familia yake: “Ninapoomba, nyinyi semeni ‘Amina.’” Walipomuona Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na familia yake, kasisi wa ujumbe aliliambia kundi lake: “Enyi Wakristo, ninaona nyuso ambazo maombi yao yatajibiwa hata kama ni kuondosha mlima. Msikubali changamoto yao. Endapo mtakubali, mtaangamia na Wakristo hawataishi kwenye uso wa ardhi hii.”

129

Page 129


Imam Ali binamu yake Mtume (s.a.w.w)Lubumba

Dr.Kanju.qxd

7/1/2011

4:37 PM

Imam Ali (a.s.) Ndugu yake Mtume Muhammad (s.a.w.) Ujumbe ukazingatia onyo hilo la kasisi wao na wakamwambia Mtukufu Mtume (s.a.w.w.): “Ewe Abu Al-Qasim, tumeamua kutofanya maombi ya ‘Mubahila’ na wewe.”86 At-Tabari kwenye tafsir yake ya Qur’ani Tukufu aliandika Hadithi nyingi kupitia kwa wasimulizi wengi mbali mbali kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alifuatana na Ali, Fatimah, Al-Hasan na Al-Husein kwenye tukio la Mubahila.87 Muslim kwenye Sahih yake aliandika kwamba Saad Ibn Abu Waqass alisimulia kwamba baada ya Wahyi wa Aya ifuatayo: “Watakao kuhoji katika haya baada ya kukufikilia ilimu hii waambie; “Njooni tuwaite watoto wetu na watoto wenu, na wanawake zetu na wanawake zenu na sisi wenyewe na nyinyi wenyewe, kisha tuombe kwa unyenyekevu tutake laana ya Mwenyezi Mungu iwashukie waongo.” Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) aliwaita Ali, Fatimah Hasan na Husein, halafu akasema: Mwenyezi Mungu hawa ndio watu wa familia yangu.”88

KWA NINI ALI ALIJUMUISHWA? Muweza wa Yote alimuamuru Mtukufu Mtume Wake (s.a.w.w.) awaambie wajumbe wa Najran: “Njooni! tuwaite watoto wetu na watoto wenu, na wanawake zetu na wanawake zenu na nafsi zetu na nafsi zenu….” Katika kuitekeleza amri hii, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alikwenda nao, AlHasan na Al-Husein, kwa sababu walikuwa watoto wa binti yake Fatimah na kwa hiyo, wao ni watoto wake Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Alikwenda 86 Utaona kwenye fasili Al-Nisabri kwenye Qur’ani iliyochapwa pembeni mwa Fasili ya Al-Tabari, sehemu ya 2, uk. 192-193. 87 Al-Tabari kwenye Fasili yake kuhusu Qur’ani, sehemu ya 2, uk. 192. 88 Muslim, kwenye Sahih yake, sehemu ya 15, uk. 176. 130

Page 130


Imam Ali binamu yake Mtume (s.a.w.w)Lubumba

Dr.Kanju.qxd

7/1/2011

4:37 PM

Imam Ali (a.s.) Ndugu yake Mtume Muhammad (s.a.w.) na Fatimah kwa sababu anawawakilisha wanawake kutoka kwa watu wa Nyumba yake. Lakini kwa nini alimjumuisha Ali ambaye wala hakuwa anatoka kwa watoto ama kutoka kwa wanawake? Ali hana nafasi katika Aya hii isipokuwa amejumuishwa kwenye neno ‘nafsi.’ Kuwa pamoja naye Ali inaonesha kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alimfikiria Ali kama upanuzi wa utu wake yeye binafsi. Kwa kumfikiria Ali hivyo, alimnyanyua juu ya Waislamu wote. Mara nyingi Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisema: “Ali anatokana na mimi, na mimi ninatoka Ali.” Hubshi Ibn Janadah alisimulia kwamba alisikia Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), anasema: “Ali anatokana na mimi, na mimi ninatokana na yeye, na hapana anayeniwakilisha isipokuwa Ali.”89 Mazungumzo baina ya Imam Ali Ar-Ridha na Al-Ma’mun (Khalifa mashuhuri wa Banu Abbas) yalikuwa kama ifuatavyo: Al-Ma’mun: “Ni uthibitisho gani uliopo kuhusu ukhalifa wa babu yako (Ali)?” Imam Al-Ridha: “Uthibitisho ni neno la Mwenyezi Mungu ‘na sisi na nyinyi’ hapa Imam alikuwa na maana kwamba kwa kumjumuisha Imam Ali kwenye tukio la ‘Mubahila’ Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alimfanya yeye ongezeko la yeye mwenyewe; na yeyote aliye ongezeko la utu wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) atakuwa Imam wa Waislamu.” Al-Ma’mun: “Hii ingekuwa kweli kama hapangekuwa ‘na wanawake zetu na wanawake zenu.’” Al-Ma’mun alimaanisha kwamba inawezekana kwamba miongoni mwa Waislamu walikuwemo wanamume wengine ambao walikuwa kama Ali 89 Ibn Majah kwenye Sahih yake (hadith Na. 143). 131

Page 131


Imam Ali binamu yake Mtume (s.a.w.w)Lubumba

Dr.Kanju.qxd

7/1/2011

4:37 PM

Imam Ali (a.s.) Ndugu yake Mtume Muhammad (s.a.w.) ambao wangekuwa ni ongezeko la utu wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), lakini hakutaka kuwapekela wote. Aliamua kumpeleka mmoja wao, Ali, kama mwakilishi wa wengine walio sawa naye. Ushahidi wa usemi huu ni ‘wanawake zetu,’ kwa kuwa neno hili linajumuisha wanawake wote ambao wana uhusiano wa kindugu na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kwa kuzaliwa au kwa ndoa. lakini Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alimpeleka Fatimah ambaye ana uhusiano naye wa undugu wa kuzaliwa kama mwakilishi wa wanawake ambao wana uhusiano naye. Imam Al-Ridha: “Hoja hii ingekuwa ya kweli kama pasingekuwepo na maneno ‘Na watoto wetu na watoto wenu’”! Alikuwa na maana kwamba Fatimah alipelekwa kama mwanamke ambaye hakuwepo wa kumlinganisha naye na si mwakilishi wa wanawake anaolingana nao katika familia ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Kama wanawake wengine wangelikuwa wanalingana na Fatimah, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) angewapeleka wao na Fatimah. Kwani aliwapeleka Al-Hasan na Al-Husein pamoja, kwa sababu hawa walikuwa wanalingana wao kwa wao na hakumpeleka mmojawao kama mwakilishi wa watoto wake. Kwa hiyo, kumwasilisha Ali kwenye tukio hili ni uthibitisho kwamba Ali ni yeye peke yake tu ambaye Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alimfikiria kwa ongezeko la utu wake.” Imesimuliwa kwamba Amr Ibn Al-Aas alimuuliza Mtukufu Mtume (s.a.w.w.): “Ni nani kipenzi chako zaidi miongoni mwa watu?” Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisema: “Abu Bakr” halafu akamuuliza: Nani anayefuata? Na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.); akasema ‘Umar’ Ibn Al-Aas akasema; “Halafu Ali nafasi yake ni ipi?” kisha Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) aligeuka na akawatazama watu waliokuwa wamemzunguka, akasema: “Mtu huyu anauliza kuhusu nafsi.”90

90 Al-Muttaqi Al-Hindi, Kanzul-Ummal, Sehemu ya 15, (uadilifu wa Ali), uk. 125 (hadith Na. 361).

132

Page 132


Imam Ali binamu yake Mtume (s.a.w.w)Lubumba

Dr.Kanju.qxd

7/1/2011

4:37 PM

Imam Ali (a.s.) Ndugu yake Mtume Muhammad (s.a.w.) Nimetaja kwenye sura ya nyuma kwamba tangazo la Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) baada ya Hijira halikuwa na lengo la kutimiza ahadi aliyompa Ali kabla ya Hijira, kwani alitimiza ahadi yake kwa Ali kwa kumfanya Ali kuwa ndugu wa kiroho mnamo siku hiyo ya mkutano uliofanyika nyumbani kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Aidha, hakumuahidi Ali kwa tangazo hilo kufanyika katika siku za usoni. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alitangaza jambo hilo kwa Waislamu kwa hiari yake kwa sababu Ali alistahiki sifa hiyo ya pekee na kwa sababu kutangazwa kwake kungewatayarisha Waislsamu kisaikolojia kwa uongozi wa Ali siku zijazo. Alitaka kulionesha taifa, Mnara wa uongozi ambao umma utahitajia baada ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Wakati Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alipotangaza kwa Waislamu kuhusu sifa ya pekee aliyompa Ali kwa kumfanya kuwa ndugu wa kiroho, alitarajiwa pia kutangaza hadharani sifa zingine mbili za juu sana ambazo alikwishampa; kuwa wasii wake na mrithi wake, kwani kilichokuwa kinahitajiwa zaidi na umma kuliko chochote ni uongozi bora ambako taifa lingekimbilia baada ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Uongozi kama huo ndio ambao ungelinda mwendelezo wa ujumbe wa Kiislamu katika usahihi wake. Pia ungeweza kuulinda umma dhidi ya upotofu kutoka kwenye nji ya haki katika muda wake mrefu wa baadae. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alichagua kutangaza uongozi huu wakati wa mwaka wa kumi baada ya Hijira pale alipokuwa anarudi kutoka kwenye hija yake ya mwisho. Alitangaza kwa maelfu ya mahujaji kwamba Ali alikuwa na haki ya kuendesha mambo ya Waislamu kama vile Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alivyokuwa anafanya. Hili lilimaanisha kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alitangaza kwamba Ali atakuwa ndiye mrithi wake. Pia tangazo hilo lilikuwa na maana ya Ali kuwa wasii wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), kwani yeyote ambaye Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alimteuwa kuendesha mambo ya Waislamu, pia angekuwa wasii wake.

133

Page 133


Imam Ali binamu yake Mtume (s.a.w.w)Lubumba

Dr.Kanju.qxd

7/1/2011

4:37 PM

Imam Ali (a.s.) Ndugu yake Mtume Muhammad (s.a.w.)

SURA YA KUMI NA NNE MAULA WA WAISLAMU. Mwaka wa kumi baada ya Hijira ulijaa matukiuo muhimu. Matukio mawili miongoni mwa matukio hayo yalikuwa maarufu na yalielekeza kwenye imani ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) katika kukaribia kwake kifo chake na kwamba alikuwa anakaribia kuitwa na Mwenyezi Mungu na kwamba angeitika wito huo. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alitangaza kwa wakazi wa Rasi ya Bara Arabu kwamba angekwenda Hija. Aliwashawishi wafuatane naye wakati wa siku za safari yake ili wapate fursa ya kujifunza kutoka kwake namna ya utekelezaji wake; na akiwa na shauku kuhusu hali ya Waislamu siku za usoni, alitaka kupendekeza kwao kile ambacho Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) hupendekeza wafuasi wake wafanye katika siku za baadaye, kwani alidhani kwamba hawangemuona mnano mwaka uliofuata. Makumi ya maelfu ya mahujaji walifanya haraka kuungana na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Aliendelea kuwaongoza wakiwa wamevaa ‘Ihram’. Wakizunguuka Kaaba, wakisali wakitembea kati ya Safa na Marwa; na kukaa kwa muda huko Arafa na wakati wa kutoa sadaka ya kuchinja. Wafuasi wake walimfuata na walifanya vile alivyowaamuru wafanye. Walipokuwa Arafa aliwahutubia, na Ujumbe wake ulipendeza sana. Aliwatangazia wafuasi wake mwanzoni mwa hotuba yake kuhusu ukaribu wa kifo chake aliposema baada ya kumwomba Muweza wa Yote: “Enyi watu, sikilizeni maneno yangu, kwani sijui kama nitakutana na nyinyi baada ya mwaka huu mahali hapa wakati wowote….”

134

Page 134


Imam Ali binamu yake Mtume (s.a.w.w)Lubumba

Dr.Kanju.qxd

7/1/2011

4:37 PM

Imam Ali (a.s.) Ndugu yake Mtume Muhammad (s.a.w.) Halafu aliwaambia kuhusu utakatifu wa damu ya mwanadamu na rasilimali ya Waislamu, akasema: “Enyi watu, kwa hakika maisha yenu na mali zenu ni vitu vitakatifu kwenu kama siku yenu hii ya leo na mwezi wenu huu mpaka mtakapokutana na Mola wenu. Na mtakutana na Mola wenu na Atawaulizeni kuhusu matendo yenu, na mimi nimefikisha Ujumbe kwenu.”91 Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) aliendelea kuwahimiza watu kulipa madeni yao (kurudisha amana kwa wenyewe) na kutangaza kwamba kila aina yoyote ya riba imeharamishwa. Uislamu umeharamisha kulipa kiasi cha mauaji yaliyofanyika kwenye kipindi cha kabla ya Uislamu. Pia alisisitiza haki za wanawake na akasisitiza undugu wa Kiislamu. Jukumu kubwa la Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) lilikuwa hali ya umma wake katika siku za usoni. Kwani alikuwa anatambua vema kuhusu mgogoro ambao umma utaupata, haikutarajiwa kuuacha umma bila ya mnara wa uongozi ambamo humo ndimo watu wangevuka salama kwenye migogoro ya siku za usoni. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), kwa hiyo, aliwatangazia Waislamu kile alichofikiria kuwa usalama dhidi ya upotofu kutoka njia iliyonyooka, kama watachagua kuwa na usalama huo. At-Tirmidhi kwenye Sahih yake alisimulia kupitia sanad yake mpaka kwa Jabir Ibn Abdullah Al-Ansari, kwamba alisema: “Nilimuona Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kwenye Hija yake mnamo siku ya Arafa alipokuwa amepanda ngamia wake wa kike (Al-Qusswa), anahutubia, na nilimsikia anasema: ‘Enyi watu, nimewaachieni miongoni mwenu kile ambacho kama mkishikamana nacho kamwe hamtapotoka: Kitabu cha Mwenyezi Mungu na watu wa Nyumba yangu.”92 91 Ibn Hishamu, Wasifu wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), sehemu ya 2, uk. 6. 92 Al-Tirmidhi, kwenye Sahih yake, sehemu ya 5, uk. 328, Al-Tirmidhi pia alisema kwamba Abu Dharr, Abu Saeed (Al-Khudri) Zayd Ibn Arqam, na Hudhaifa Ibn Usaid walitaarifu yanayolingana na haya. 135

Page 135


Imam Ali binamu yake Mtume (s.a.w.w)Lubumba

Dr.Kanju.qxd

7/1/2011

4:37 PM

Imam Ali (a.s.) Ndugu yake Mtume Muhammad (s.a.w.) Kwa maneno haya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alitangazia umma wake kwamba aliliachia kile ambacho kingekuwa salama dhidi ya kupotoka na kuacha njia iliyonyooka kama umma ungeshikamana na kile alichokiacha. Usalama huo unafanyizwa na vitu viwili vilivyo linganifu: Mojawapo ya vitu hivyo ni Wahyi wa Mwenyezi Mungu ambao umeandikwa kwenye Qur’ani Tukufu, na cha pili ni watu wa Nyumba ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) ambao wanao utambuzi wa ufasili wa Qur’ani Tukufu na mafundisho ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Inafaa kuangalia kwamba umma wa Waislamu hawajui maneno haya ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) yaliyosimuliwa, bado maneno haya yalisimuliwa na takriban masahaba ishirini. Kile wanachokijua umma wa Waislamu ni kile ambacho Ibn Hisham aliandika kwenye Wasifu wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisema kwenye hotuba yake huko Arafa: “Nimewaachieni miongini mwenu ambacho kama mkijiimarisha nacho, hamtapotoka kamwe; Kitabu cha Mwenyezi Mungu, agizo lilolo dhahiri, na mafundisho ya Mtume Wake (s.a.w.w.) (yaani Sunna).” Aidha, Waislamu hawa wanadhani kwamba kuna ukinzani baina ya Hadith ya kwanza na ya pili. Ni muhimu ieleweke kwamba wasimulizi wa yale aliyoandika Ibn Hisham hawajulikani, majina yao hayakuandikwa kwenye Hadith, kwa hiyo, isifikiriwe kama ni sahihi. Lazima pia ifahamike kwamba Al-Bukhari na Muslim hawakuandika neno ‘Sunnat Nabiyah’ (mafundisho ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.)) kwenye taarifa zao juu ya hutuba ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) mnamo siku ya Arafa. Masheikh wawili wametaja tu Kitabu cha Mwenyezi Mungu.93 Aidha, Kitabu cha Mwenyezi Mungu kinajulikana sana kwa Waislamu, na kiliandikwa wakati wa uhai wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). “Sunnat (Mafundisho ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), kwa upande mwingine, 93 Al-Bukhari, Sahih Bukhari, sehemu ya 8, (kitabu cha Hija), uk. 184 aliandika hadith bila kutaja ‘Sunnah’ Mafunzo ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.)). 136

Page 136


Imam Ali binamu yake Mtume (s.a.w.w)Lubumba

Dr.Kanju.qxd

7/1/2011

4:37 PM

Imam Ali (a.s.) Ndugu yake Mtume Muhammad (s.a.w.) haikuandikwa wakati wa uhai wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), na yale yaliyoandikwa kuhusu Hadith miongo mingi baada yake bado sio eneo kamili la makubaliano miongoni mwa Waislamu. Kuna Hadith nyingi zenye kukinzana kwenye vitabu tunavyoviita Sahih. Mathalan, imeandikwa kwenye baadhi ya Sahih kwamba Abdur-Rahman Ibn Abu Umeirah alisimulia kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alimwombea Muawiyah, akasema: “Mwenyezi Mungu mwongoze vema na mwezeshe awaongoze watu kwenye njia iliyonyooka.” Pia imesimuliwa kwenye Sahih moja kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alimwambia Ammar Ibn Yasir: “Ammar uwe na furaha, kundi la wachokozi litakuua.” Bado kundi lililomuua Ammar lilikuwa kundi la Muawiya. Ambapo Muawiya ni kiongozi wa wachokozi kwa hiyo hangeongozwa wala watu hawangeongozwa naye kuelekea njia iliyonyooka. Hadith inayomsifu mtu kama Muawiya haiwezi kuwa usalama dhidi ya upotofu. Kwa usahihi zaidi inaweza kuwa sababu ya mchafuko. Mtu ambaye alipigana vita na Imam Ali, Imam wa haki na ndugu yake Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), vita ambavyo vilisababisha vifo vya makumi ya maelfu ya Waislamu, hawezi kuwa kiongozi wa kuelekeza kwenye njia iliyonyooka. Ili kile alichosema Ibn Hisham kikubaliwe kimantiki, tunatakiwa kuelewa tamko la Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kutoka kwenye neno ‘Sunnah,’ maelezo ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na matendo yake ambayo yanaeleweka kuwa yametoka kwake. Haya yanaleta usalama dhidi ya upotofu kama tukiyafuata. Lakini kile kinachojulikana katika matamshi na matendo yake ni kidigo sana, kwa sababu Hadith zilizo nyingi hazikuandikwa na waandishi wengi katika kila kiungo cha sanad yake ya simulizi; badala yake zilikuwa na mwandishi mmoja au waandishi wawili au waandihsi wachache. Nyingi ya Hadith hizi zinapingana zenyewe. Kwa hiyo, hatuwezi kupata uhakika kupitia kwenye Hadith hizo kuhusu yale aliyoy137

Page 137


Imam Ali binamu yake Mtume (s.a.w.w)Lubumba

Dr.Kanju.qxd

7/1/2011

4:37 PM

Imam Ali (a.s.) Ndugu yake Mtume Muhammad (s.a.w.) asema au aliyoyatenda Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Ipo njia moja tu yenye mantiki ambayo tukiitumia, tunaweza kuwa na uhakika wa Sunnah za Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) mwenyewe angeweza kutujulisha vyanzo vya kuaminika ambavyo vinatujulisha kwa usahihi alichosema na alichofanya. Hadith ya kwanza ambayo ilisimuliwa na zaidi ya masahaba ishirini, inatujulisha sisi kile chanzo cha kuaminika yaani; watu wa Nyumba ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) ambao walikuwa wanajua tafsiri ya Kitabu cha Mwenyezi Mungu na maelekezo ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kwa ukamilifu. Kwa njia hii, Hadith za At-Tirmidhi na Ibn Hisham zingekuwa zinakubaliana zenyewe na kujielezea zenyewe kwa zenyewe. Ali alikuwa na ujuzi wa Qur’ani na maneno na matendo ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na tafsir zake. Waislamu wangeepuka upotofu kama wangezingatia tafsir yake na kumsaidia kuwasilisha ujuzi wake kwenye umma. Hata hivyo, tukio lingine maarufu ambalo lilitokea wakati wa mwaka wa mwisho wa uhai wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) limefanya jambo hili kuwa wazi sana. Tukio lilikuwa lenye kujieleza kikamilifu kuhusu elementi za usalama dhidi ya upotofu. Tukio hilo maarufu lilikuwa tangazo la Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) la Ghadiir Khum. Alipokuwa anarudi kutoka Hija yake ya mwisho kwenda Madina, alisimama mahali hapo kuwaambia maelfu ya mahujaji ambao alikuwa nao kwamba, Ali Ibn Abu Talib ni ‘mawla’ (Mlezi) wa kila muumini. Al-Hakim kupitia kwa wasimulizi wake mpaka kwa Abu Tufail alisimulia kwamba Zayd Ibn Arqam alisema: “Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alipokuwa anarudi kutoka kwenye Hija ya Mwisho, alisimama Ghadiir Khum. Aliwaamuru Mahujaji kufagia uchafu uliokuwa chini ya miti mahali hapo. 138

Page 138


Imam Ali binamu yake Mtume (s.a.w.w)Lubumba

Dr.Kanju.qxd

7/1/2011

4:37 PM

Imam Ali (a.s.) Ndugu yake Mtume Muhammad (s.a.w.) Halafu akasema: ‘Mimi nitaitwa na Mwenyezi Mungu hivi karibuni na nitaitika wito huo. Ninawaachieni miongoni mwenu vitu viwili vya thamani, mojawapo ya vitu hivyo viwili ni kikubwa kuliko kingine: Kitabu cha Mwenyezi Mungu na Itrah wangu (watu wa Nyumba yangu). Tahadharini na jinsi mtakavyovitendea vitu hivi kwani havitatengana mpaka viungane na mimi Siku ya Hukumu.’ Halafu akasema: ‘Kwa hakika Mwenyezi Mungu ni Mawla wangu (Mlezi) na mimi ni Mawla wa kila muumini. Yeyote yule ambaye mimi ni Mawla wake, huyu Ali ni Mawla wake. Mwenyezi Mungu, mpende yeyote anayempenda Ali na mchukie yeyote anayemchukia Ali.”94 Kutokana na tukio hili tunaelewa kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alitaka kuwatangazia Waislamu katika kituo hicho, mambo matatu muhimu ambayo yanahusiana yenyewe kwa yenyewe: Alikuwa anategemea kuondoka hapa duniani baada ya muda si mrefu. Kwa hiyo, alizungumza nao kama vile alikwishaitwa na Mola Wake. Kwa kuwa alikaribia kukutana na Mola Wake, aliona ni jambo la lazima kuwa na namna ya uongozi kwa ajili ya wafuasi wake ambao ungeangaza njia iliyonyooka kwa ajili yao baada ya kutokuwepo yeye. Kwa hiyo aliwatangazia kwamba alikuwa anawaachia Kitabu cha Mwenyezi Mungu na ‘Itrah’ wake (watu wa Nyumba yake); na kwamba kama wanakifuata Kitabu cha Mwenyezi Mungu na Itrah watakuwa wamepata dhamana ya mwendelezo wa kuwa kwenye njia iliyonyooka katika wakati wao wa karibu na wa mbali wa siku zijazo. Watu wa Nyumba ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) walikuwa waongoze umma kwa sababu tu kulikuwa hakuna watu wa kuwalinganisha nao katika ujuzi wao wa tafsir ya Kitabu na maelekezo ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na kuvifuata kwao vyote viwili. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alitaka kuutangazia umma wote kwamba mtu ambaye alikuwa na sifa zote za 94Al-Hakim, Al-Mustadrak, sehemu ya 3, uk. 109. 139

Page 139


Imam Ali binamu yake Mtume (s.a.w.w)Lubumba

Dr.Kanju.qxd

7/1/2011

4:37 PM

Imam Ali (a.s.) Ndugu yake Mtume Muhammad (s.a.w.) uongozi huo kutoka miongoni mwa ndugu zake wa karibu alikuwa ni Ali Ibn Abu Talib. Kwa hiyo, alimweka kwenye nafasi yake na akamfanya kuwa mbadala wake mwenyewe. Mwenyezi Mungu ni Mlezi wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) ni Mlezi wa walioamini. Anayo haki ya kuendesha mambo ya walioamini zaidi kuliko walioamini kuendesha mambo yao wenyewe, na Ali ndiye ambaye anayo haki iliyo sawa na ile ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) katika kuwaongoza Waislamu na kuendesha mambo yao. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alikuwa anatambua vema kwamba watu hutofautiana katika kuhifadhi kwenye kumbu kumbu yale wanayo yasikia na kuelewa yale wanayohifadhi kwenye kumbu kumbu. Kwa hiyo alikuwa anategemewa kuandika kwenye hati maalum yale aliyoyatangaza kwa mdomo hapo Ghadiir Khum, bila kuacha mwanya wa kisingizio kwa yeyote kubisha siku za usoni kuhusu yale yaliyokuwemo kwenye tangazo. Lakini hakufanya hivyo. Historia haitujulishi kuhusu kuwepo kwa hati yoyote iliyoandikwa kwa imla ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na kulakiriwa kwa lakiri yake iliyobarikiwa, akitangaza kwamba alimteua Ali au mtu mwingine yeyote kwa uongozi wa umma baada yake. Kwa sababu gani hati ya aina hiyo isiwepo? Tutapata jibu kwenye kurasa zifuatazo.

* * * * * * *

140

Page 140


Imam Ali binamu yake Mtume (s.a.w.w)Lubumba

Dr.Kanju.qxd

7/1/2011

4:37 PM

Imam Ali (a.s.) Ndugu yake Mtume Muhammad (s.a.w.)

SURA YA KUMI NA TANO WASIA WA MTUKUFU MTUME (S.A.W.W.) USIOTIMIZWA. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) hakuacha wasia ulioandikwa, ingawa Qur’ani Tukufu inamuamuru kila Mwislamu kutengeneza wasia:

“Imeelezwa pale ambapo kifo kinapo mkaribia yeyote miongoni mwenu, kama ataacha vitu vyovyote vyenye thamani, kwamba atengeneze wasia kwa wazazi wake au ndugu zake wa karibu kwa njia iliyohalali. Huu ni wajibu wa kila mwenye kupenda haki; endapo mtu yeyote anabadilisha wasia baada ya kusikia, hatia itakuwa kwa wale wanaobadilisha. Kwani Mwenyezi Mungu husikia na hutambua vitu vyote.”Surat al-Baqarah; 2:180-181. Licha ya kwamba Aya inazungumzia kuhusu umuhimu wa kutengeneza wasia, bila kubainisha mbinu iliyotumika, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) aliwaamuru Waislamu, kutengeneza wasia wao kwa maandishi. Muslim kwenye Sahih yake aliandika yafuatayo:

141

Page 141


Imam Ali binamu yake Mtume (s.a.w.w)Lubumba

Dr.Kanju.qxd

7/1/2011

4:37 PM

Imam Ali (a.s.) Ndugu yake Mtume Muhammad (s.a.w.) Abu Salim alisimulia kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisema: “Mtu mwenye kitu ambacho angekitengenezea wasia, hana haki ya kukaa siku tatu bila ya kuwa na wasia wake wa maandishi.” Abdullah Ibn Umar alisimulia kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisema: “Mtu ambaye anacho kitu cha kukitengenezea tamko la wasia, hana haki ya kukaa siku mbili bila kuwa na wasia wake wa maandishi.” Muslim alisimulia pia kwamba Abdullah Ibn Umar alisema: “Kwa kuwa nilisikia haya kutoka kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), kamwe sikukaa hata siku moja bila ya wasia wangu wa maandishi.”95 Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alikuwa na haki ya kuchelewesha wasia wake kwa siku, miezi, miaka kadhaa, kwa sababu yeye alikuwa kwenye miadi ya pekee ya Mola Wake. Upo uwezekano mkubwa kwamba alipata taarifa kutoka Mbinguni kwamba hangeaga dunia hadi dini ya Uislamu imekamilika. Hata hivyo, wakati wa mwaka wa kumalizia Hija yake ya mwisho, Aya ifuatayo iliteremshwa: “…Leo nimekukamilishieni Dini yenu, na nimekutimizieni neema yangu na nimechagua Uislamu kuwa dini yenu…”96 Kwa Wahyi huu Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alihisi ukaribu wa kifo chake, na kwamba ulikuwa wakati wa kutengeneza wasia wake. Hivyo, alipokuwa njiani akirudi kwenda Madina kutoka kwenye Hija yake alisimama huko Ghadiir Khum ili atoe tangazo muhimu ambamo alisema: “Mimi ni mwanadamu mwenye hali ya kuweza kufa. Mjumbe wa 95 Hadith hizi tatu zimeandikwa na Muslim kwenye Sahih yake, Sehemu ya 11 (kitabu cha wasia), uk. 74-75. Hadith ya pili pia imeandikwa na Al-Bukhari, kwenye Sahih yake, sehemu ya 4, uk. 3. 96Qur’ani Tukufu, al-Maidah; 5:3. 142

Page 142


Imam Ali binamu yake Mtume (s.a.w.w)Lubumba

Dr.Kanju.qxd

7/1/2011

4:37 PM

Imam Ali (a.s.) Ndugu yake Mtume Muhammad (s.a.w.) Mola Wangu anakaribia kuja kwangu na nitaitika (Wito Wake kwa kuondoka hapa duniani).” Halafu akatangaza kwamba Ali, kama alivyo Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), anayo haki zaidi juu ya walioamini kuliko walioamini wenyewe, na kwamba Ali ni Mlezi wa kila muumini (tazama Sehemu ya 14). Wasia wa Maandishi ni Lazima kwa Mambo Yenye Umuhimu. Ingawa wasia wa mdomo unafaa, wasia wa maandishi ni wa lazima, hususan kwenye jambo muhimu kama kumteua mrithi wa kuongoza umma. Tamko la mdomo linaweza kusahauliwa, kuongezwa, kupunguzwa au kuwa si sahihi. Lakini wasia wa maandishi na kupigwa muhuri na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) si rahisi kubadilishwa. Kwa hiyo, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alitarajiwa kutengeneza wasia kama huo, lakini hakufanya hivyo. Inasemekana kwamba aliwaambia Waislamu kwa mdomo kufuata Kitabu cha Mwenyezi Mungu na mafundisho yake, na kwamba huu ulikuwa wasia wa kutosha. Mimi sikubali kwa sababu ifuatayo: Wasia uliotayarishwa na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) unatarajiwa kuwapatia Waislamu maelekezo mapya kuhusu shughuli za umma siku za usoni baada ya kifo chake. Kukubali mafundisho ya Qur’ani Tukufu na ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) si ya aina hii, kwa sababu umuhimu wake unaonekana wazi kwa Waislamu, na kwa sababu utiifu kwa Mwenyezi Mungu na Mtukufu Mtume Wake (s.a.w.w.) umerudiwa tena na tena kuandikwa kwenye Qur’ani Tukufu.

“Enyi mlioamini! Mtiini Mwenyezi Mungu, na mtiini Mtume ….”Qur’ani, an-Nisaa; 4:59 143

Page 143


Imam Ali binamu yake Mtume (s.a.w.w)Lubumba

Dr.Kanju.qxd

7/1/2011

4:37 PM

Imam Ali (a.s.) Ndugu yake Mtume Muhammad (s.a.w.)

“Na anachokupeni Mtume kichukueni, na anachokukatazeni jiepusheni nacho…” Qur’ani 59:7 Tamko la Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) lisiloandikwa haliwezi kuwa na athari kama neno la Mwenyezi Mungu ambalo limeandikwa kwa kurudiwa kwenye Kitabu Chake. Kwa hiyo, tamko lenye kujidhihirisha lenyewe haliwezi kuwa wasia uliotarajiwa na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) anatarajia kufuata amri ya Mwenyezi Mungu kuliko mtu yeyote katika umma kama ambavyo imetamkwa kwenye Kitabu Chake na kufanya yale ambayo yeye mwenyewe aliwaagiza wafuasi wake kufanya. Kama Ibn Umar au Mwislamu mwingine yeyote anatakiwa kuandika wasia kwa sababu anao utajiri kidogo wenye kiasi cha kutayarishiwa wasia na familia ndogo ya kutunza, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alikuwa na ujumbe wa mwisho wa Mbinguni wa kuhifadhi na umma wote kuulinda na kuutelekeza. Migogoro Iliyotarajiwa Ilihitaji Wasia wa Maandishi Imani ya Uislamu ilikuwa bado kama mmea mchanga ambao mizizi yake ilikuwa bado haijapenya kwenye kina cha jamii ya Waarabu, na hatari dhidi ya imani zilikuwa nyingi sana. Sote tunajua kwamba vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyotokea baada ya kifo cha Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) ni kwa sababu ya kuritadi wakazi wengi wa Arabuni. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alikuwa anatambua vema kuhusu hatari hizo. Al-Hakim kwenye Sahih yake Al-Mustadrak alian dika kwamba Abu Muwaihibah, sahaba wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisema: “Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) ameniambia: ‘Mimi nimeagizwa na Mwenyezi Mungu kuwaombea watu wa Al-Baqii (uwanja wa makaburi uliopo Madina) ili 144

Page 144


Imam Ali binamu yake Mtume (s.a.w.w)Lubumba

Dr.Kanju.qxd

7/1/2011

4:37 PM

Imam Ali (a.s.) Ndugu yake Mtume Muhammad (s.a.w.) wasamehewe madhambi. Njoo twende’ Nilikwenda na yeye. Aliposimama katikati ya makaburi alisema: ‘Amani iwe kwenu, enyi watu wa makaburini. Hongera kwenu kwa yale ambayo mko nayo. Hamjui Mwenyezi Mungu amewaepusheni na mambo gani. Majaribu ya kupima imani yanakuja kama kipande cha usiku wa giza, moja linafuata lingine….”87

ABU BAKR ALIANDIKA WASIA Hatuwezi kufikiria kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alikuwa hajihusishi na mambo ya umma ya siku za usoni kuliko sahaba wake Abu Bakr ambaye hakuondoka hapa duniani kabla ya kumteuwa mrithi (Umar). Alifanya hivyo licha ya ukweli kwamba umma wakati wa kifo chake ulikuwa umevuka hatari ya vita vya wenyewe kwa wenyewe na ulifikia muafaka wa amani ya ndani ya umma. Alifanya vile kwa sababu alijua kwamba kuwaacha Waislamu bila kumteua kiongozi ingekuwa uzembe wa maslahi yao na kuhatarisha usalama wao wa siku zijazo.

MAZUNGUMZO BAINA YA UMAR NA MWANAYE. Inafaa kuangalia hekima ya Abdullah Ibn Umar katika mazungumzo yake na baba yake kwani wakati huo baba alikuwa katika dakika zake za mwisho: Abdullah: “Ungeteua mrithi wako. Umar: “Nimteue nani?” Abdulah: “Jaribu uwezavyo. Wewe sio Mola wao. Chukulia kama unamuita mwangalizi wa shamba lako kwa muda. Je, hungependa awe na mrithi katika kipindi ambacho hatakuwepo hadi atakaporudi huko tena?” 97 Al-Hakim, kwenye Al-Mustadrak yake, sehemu ya 3, uk. 5-6. Ibn Hisham pia alisimulia hadith hii kwenye nakala yake ya Wasifu wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), sehemu ya 2, uk. 642. Ibn Saad pia alisimulia kwenye Al-Tabaqat, yake sehemu ya 2, uk. 204. 145

Page 145


Imam Ali binamu yake Mtume (s.a.w.w)Lubumba

Dr.Kanju.qxd

7/1/2011

4:37 PM

Imam Ali (a.s.) Ndugu yake Mtume Muhammad (s.a.w.) Umar: “Ndio.” Abdullah: Chukulia kama unamuita mchungaji wa kondoo wako. Je, hungependa apate mrithi hadi atakaporudi kwenye kondoo?”98 Ingawa Umar alikataa kumteuwa mrithi, alitekeleza jambo la kulingana na hilo. Aliteuwa masahaba wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) sita. Aliwapa haki ya kuteuwa Khalifa kutoka miongoni mwao. Aliwaamuru kufuata walio wengi endapo patakuwepo wengi. Aliwaagiza wafuate kundi la AbdulRahman Ibn Awf pale ambapo watu sita waligawanyika sawa kwa sawa. Hivyo, hakuuacha umma wa Waislamu bila maelekezo. Alibaini mbinu ambayo kwayo Khalifa angechaguliwa. Kwa Kawaida Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) Aliacha Warithi Wakati Alipokuwa Hayupo. Na kitu cha kushangaza zaidi katika jambo hili ni kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alikuwa na kawaida ya kumteua mrithi wakati wowote alipoondoka Madina kwa muda wa siku chache au wiki chache. Alipoondoka kwenda Badr, alimteua Abu Lubabah. Alipoondoka kwenda Doumat Al-Jendal, alimteua Ibn Arfatah. Alipoondoka kwenda Banu Quraidhah, alimteuwa Ibn Umm Maktuum. Pia alimteua huyu huyu alipokwenda Thii Qirad. Alipoondoka kwenda Banu Mustalaq, alimteua Abu Dharr. Alipoondoka kwenda Khaybar alimteuwa Numailah. Alipoondoka kwenda Makka, alimteuwa Abu Raham. Alipoondoka kwenda Tabuk alimteuwa Ali. Alipoondoka kwenda Hija ya mwisho alimteua Abu Dujanah.99 98 Ibn Saad, Al-Tabaqat, sehemu ya 3, uk. 343. Muslim kwenye Sahih yake pia alisimulia hadith inayofanana na hii, sehemu ya 12, uk. 206. 99 Ibn Hisham, Wasifu wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). 146

Page 146


Imam Ali binamu yake Mtume (s.a.w.w)Lubumba

Dr.Kanju.qxd

7/1/2011

4:37 PM

Imam Ali (a.s.) Ndugu yake Mtume Muhammad (s.a.w.) Hivyo, kwa mfululizo alikuwa anawateua warithi wake wakati wowote alipopanga kuondoka Madina. Hata hivyo alipoagana na umma wake kwa heri ya daima milele hakuacha hati yoyote ya urithi!!!

MTUKUFU MTUME (S.A.W.W.) ALIZUIWA KUANDIKA WASIA. Kutokuwepo kwa wasia wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) wa maandishi kwa kweli inashangaza. Lazima palikuwepo na sababu isiyo ya kawaida iliyomzuia Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) asiandike wasia! Hata hivyo, tunapoangalia upya taarifa zilizoandikwa za matukio ya siku za mwisho za Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), tunaona kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alitaka kuandika wasia, lakini hakuweza kufanya hivyo. Al-Bukhari aliandika kwenye Sahih yake kwamba Ibn Abbas amesimulia: “Maradhi ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) yalipokuwa ya hatari, alisema: “Nileteeni bamba, ambamo nitaandikia maelekezo kwa ajili yenu ambayo mkiyazingatia hamtakengeuka baada yangu.” Umar akasema: “Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amezidiwa na maradhi yake (hajui hata analosema). Tunacho Kitabu cha Mwenyezi Mungu. Kinatutosha Kitabu cha Mwenyezi Mungu.” Watu waliokuwepo hapo walihojiana wao kwa wao kwa nguvu. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akasema: “Ondokeni hapa, msifanye mabishano mbele yangu.” Ibn Abbas alitoka nje, akisema: “Msiba, msiba wote huu ndio uliomzuia Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kuandika hati yake.”100 Muslim kwenye Sahih yake aliandika kwamba Sa’iid Ibn Jubeir alisimulia kwamba Ibn Abbas alisema: “Siku ya Alhamisi, ni siku iliyoje siku ya Alhamisi.’ Halafu akalia hadi akalowesha ardhi kwa machozi yake. Nikasema: Ewe Ibn Abbas, ni siku gani ya Alhamisi? Akasema: ‘Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alikuwa mgonjwa 100 Sahih Al-Bukhari, sehemu ya 1, uk. 39. 147

Page 147


Imam Ali binamu yake Mtume (s.a.w.w)Lubumba

Dr.Kanju.qxd

7/1/2011

4:37 PM

Imam Ali (a.s.) Ndugu yake Mtume Muhammad (s.a.w.) mahututi na akasema: ‘Nileteeni bamba la kuandikia maelekezo yenu, ili msije kengeuka baada yangu.’ Wakabishana, na mabishano hayakutakiwa kufanyika mbele ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Na wakasema: ‘Nini kimetokea? Ametoa njozi? Muulizeni yeye.’ Akasema: ‘Ondokeni hapa, hali niliyonayo ni nzuri zaidi (kuliko mnavyofikiria). Nina waachieni mfanye mambo matatu: Waswageni makafiri watoke katika Rasi ya Arabuni, wapeni wajumbe (wa makabila mbali mbali ambao watatembelea Madina) vitu vingi kama nilivyokuwa nikiwapa.’ Sa’iid akasema: Yeye Ibn Abbas alinyamaza kimya kuhusu jambo la tatu, au alilitamka lakini nimesahau.”101 Ubeidullah Ibn Abdullah Ibn Utbah alisema kwamba Ibn Abas alisimulia: “Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alipokaribia kufa Umar Ibn Al-Khattab alikuwa miongoni mwa watu waliokuwepo hapo karibu na kitanda chake. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisema: ‘Nileteeni bamba la kuandikia maelekezo yenu, ili msije kukengeuka baada yangu.’ Umar akasema; ‘Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amelemewa na maradhi, mnacho Kitabu cha Qur’ani Tukufu. Kitabu cha Mwenyezi Mungu kinatutosha’ Wale waliokuwepo hapo hawakukubaliana na walibishana. Baadhi yao walisema; ‘Mleteeni Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kile anachokitaka. Humo ataandika maelekezo ambayo baada yake hamtapotoka.’ Baadhi yao walisema alivyosema Umar. Walipopiga kelele sana na kubishana mbele yake, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akasema: ‘Tokeni hapa.’ Ibn Abbas alikuwa akisema: ‘Msiba, Msiba wote huu ulikuwa kwa sababu ya mabishano yao na mzozo ambayo yalimzuia Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kuandika maelekezo hayo kwa ajili yao.”102 101 Muslim kwenye Sahih yake sehemu ya 11, (Mwishoni mwa kitabu cha Wasia) uk. 89, Ibn Saad pia aliandika kwenye Al-Tabaqat, sehemu ya 2, uk. 242. Pia Imam Ahmad aliandika kwenye Musnad yake sehemu ya 1, uk. 222. 102 Muslim kwenye Sahih yake, Sehemu ya 11, uk. 95. Hadith inayofanana na hii imeandikwa na Ibn Saad kwenye Al-Tabaqat yake, sehemu ya 2, uk. 244. Imam Ahmad pia aliandika hadith hii kwenye Musnad yake sehemu ya 1, uk. 336. 148

Page 148


Imam Ali binamu yake Mtume (s.a.w.w)Lubumba

Dr.Kanju.qxd

7/1/2011

4:37 PM

Imam Ali (a.s.) Ndugu yake Mtume Muhammad (s.a.w.) Ibn Saad kwenye At-Tabaqat yake aliandika kwamba Jabir Ibn Abdullah Al-Ansari alisimulia: “Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alipokuwa anaugua maradhi ambayo ndio aliyofia, aliagiza apelekewe bamba ili aliandikie taifa lake maelekezo (ambayo baadaye) yangewapa kinga ya kutokengeuka wala kupotoka. Hapo ndani palitokea ubishi na kelele kubwa. Umar Ibn Al-Khattab aliongea na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alikataa alichosema (Umar).”103 Pia imeandikwa kwenye At-Tabaqat, kwamba Umar Ibn Al-Khattab alisimulia: “Tulikuwa na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), na palikuwepo na pazia kati yetu na wanawake. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akasema: ‘Nileteeni viriba vya maji saba vilivyojaa maji (kwa lengo la kumwagia mwili wake ili kupoza homa yake), na nileteeni bamba la kuandikia na kidau cha wino. Humo nitaandika maelezo kwa ajili yenu ambayo baadaye yatawapeni kinga msikengeuke.’ Wanawake wakasema: ‘Mleteeni Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) yale anayaoyataka’” Umar akasema: “Nikawaambia wanawake hao: Nyamazeni. Nyinyi ni masahaba wake wa kike. Kama anaugua mnalia; akipona, mnaikumbatia shingo yake.” Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akasema: ‘Wao ni bora zaidi yenu.’”104

103 Ibn Saad ameandika hadith hii kwenye Al-Tabaqat yake, sehemu ya 2, uk. 242. Hadith ya namna hii imeandikwa na Jabir kwenye sehemu ile ile ya 2, uk. 244. Kwenye taarifa hii Jabir alisema: Walizungumza kwa kelele kubwa sana, mbele ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) hadi akaikataza.” 104 Ibn Saad, Al-Tabaqat, sehemu ya 2, uk. 143-244

149

Page 149


Imam Ali binamu yake Mtume (s.a.w.w)Lubumba

Dr.Kanju.qxd

7/1/2011

4:37 PM

Imam Ali (a.s.) Ndugu yake Mtume Muhammad (s.a.w.) Pia imeandikwa kwenye At-Tabaqat kwamba Zainab mke wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), aliwaambia: “Kwani hamsikii Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) anachosema, kujaribu kuandika maelekezo kwa ajili yenu?” Wakabishana, na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akasema: ‘Ondokeni hapa!’”105

TUKIO HILI LISILO LA KAWAIDA LAZUA MASWALI MENGI. Kwa nini Umar alimpinga Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na akaongoza upinzani wa kumzuia asiandike wasia wake? Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alitaka kujaribu kuandika nini? Kwa nini Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) hakuandika wasia wake baada ya kuchukizwa na upinzani wa Umar? Inawezekanaje maelekezo yake kuwa usalama wa umma dhidi ya kukengeuka? Baadhi ya wanavyuoni wanasema kwamba Umar alipinga wasia wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kwa sababu ya huruma. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alikuwa anakufa na alikuwa amechoka sana. Kuandika maelekezo wakati kama huo kungeongeza uchovu wake. Umar hakutaka Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) ajiongezee shida wakati huo. Ni dhahiri kwamba maelezo haya ni yenye makosa. Ni lini iliruhusiwa Mwislamu kumzuia Mwislamu mwenzake, wa kawaida au mashuhuri, kuandika wasia wake ambapo anakaribia kukata roho? Kuandika wasia ni mojawapo ya wajibu wa kidini ambao kila Mwislamu anatakiwa kutimiza kabla hajafa. 105 Ibn Saad, Al-Tabaqat, sehemu ya 2, uk. 244. 150

Page 150


Imam Ali binamu yake Mtume (s.a.w.w)Lubumba

Dr.Kanju.qxd

7/1/2011

4:37 PM

Imam Ali (a.s.) Ndugu yake Mtume Muhammad (s.a.w.) Umekwisha soma kwamba Abbullah Ibn Umar alisimulia kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisema: “Mtu ambaye anacho kitu cha kuandikia wasia, hana haki ya kukaa siku mbili isipokuwa wasia wake uandikwe.� Wajibu wa kila Mwislamu, hususan aliye maarufu kama Umar, anatakiwa kumsaidia ndugu yake Mwislamu katika kutimiza wajibu wake wa kidini badala ya kumzuia asifanikishe. Umar na wengine wote waliokuwepo wakati huo walikuwa na wajibu wa aina mbili kuhusu jaribio la kuandikwa wasia wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alikuwa Mwislamu, ni Mtume wa Waislamu na muasisi wa dini hiyo. Ilikuwa wajibu wa Umar kumpa msaada wake wote kutimiza wajibu wake. Pia ilikuwa wajibu wa Umar kumsadia kuandika wasia wake kwa sababu Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisema kwamba wasia wake unaleta usalama kwenye umma dhidi ya kukengeuka. Kila mara Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alikuwa mkweli. Wakati wasia wake ulikuwa wenye usalama kama hivyo, ingekuwa ni jukumu la haraka na muhinu sana kwa Umar, kama Mwislamu mashuhuri na mwaminifu kwa umma, kukaribisha yale aliyotaka Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Kwa nafasi yake kubwa katika Uislamu, Umar anatarajiwa kuwa mtu mwenye furaha sana kuweza kupata maelekezo kama hayo yenye usalama ambao ulikuwa muhimu kwa kuwepo kwa Waislamu. Kitu gani kingekuwa muhimu zaidi kwa umma, pale ambapo Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alikuwa anakaribia kuuacha na Wahyi wa Mwenyezi Mungu ulikuwa unakaribia kukoma, kuliko kupata maelekezo ambayo yangemulika njia ya umma na kupata usalama wake wa siku za usoni? Aidha, wajibu wa masahaba wote waliokuwepo kwenye tukio hilo ulikuwa ni kutii amri ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Aliwaagiza wampe bamba ili aandike wasia wake. Agizo la Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) lilikuwa lazima litekelezwe kwa utii wa kiwango cha juu.

151

Page 151


Imam Ali binamu yake Mtume (s.a.w.w)Lubumba

Dr.Kanju.qxd

7/1/2011

4:37 PM

Imam Ali (a.s.) Ndugu yake Mtume Muhammad (s.a.w.) Ni makosa kusema kwamba Umar alimpinga Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kwa sababu ya huruma na kwamba hakutaka ajiongezee uchovu kwa kuandika maelezo. Kwa kweli upinzani wa Umar ulimsababishia Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) maumivu makubwa zaidi. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alikuwa kwenye siku zake za mwisho hapa duniani. Wakati Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alipokuwa kwenye siku za uhai wake akiwa imara na mwenye kushughulika, alikuwa na desturi ya kuwaamuru Waislamu na wao walikuwa na tabia ya kukimbilia kutimiza matakwa yake hata kama ilimaanisha kutumia utajiri wao na damu zao. Sasa akiwa kwenye siku zake za mwisho hapa duniani, aliwaomba wampe kitu rahisi kuliko vyote (bamba la kuandikia tu, na kidau cha wino), na agizo lake lilikataliwa. Bila shaka, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alihuzinishwa sana kwa msimamo wao. Hakuna ambacho kingeonesha hasira yake zaidi ya kuwambia: “Ondokeni hapa,” na jibu lake kwa Umar: “Wao (wanawake) ni bora zaidi yenu.” Lau kama wangempa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kile alichokitaka, wangempunguzia maumivu yake. Hakuna chochote katika wakati huo ambacho kingemfurahisha zaidi Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kuliko kutimiza wajibu wake wa kidini kwa kuunusuru umma wake dhidi ya kupotoka. Abu Bakr aliandika wasia wake ambamo alimteua Umar kuwa mrithi wake. Alifanya hivyo wakati yupo mahututi kitandani pake akizimia ambapo alikuwa anasema imla ya wasia wake kwa Uthman. Umar hakumlaumu Uthman kwa kumsaidia Khalifa katika kuandika wasia wake. Na ingekuwa ni ubaya ulioje kumzuia Abu Bakr wakati kama huo kuandika wasia wake …. Umar mwenyewe alipigwa kisu na kuumizwa vibaya. Hakujizuia kuandika wasia kwa Waislamu na kuwaeleza alichotaka, bila kujali maumivu makali, kutokwa na damu nyingi na kuzirai mara kwa mara. Wakati yupo 152

Page 152


Imam Ali binamu yake Mtume (s.a.w.w)Lubumba

Dr.Kanju.qxd

7/1/2011

4:37 PM

Imam Ali (a.s.) Ndugu yake Mtume Muhammad (s.a.w.) kwenye hali hiyo ya kusikitisha, aliwaamuru masahaba sita wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kuteua Khalifa kutoka miongoni mwao, kufuata wingi wa kura, kama ukiwepo, na kumuunga mkono Abdul Rahman Ibn Auf pale ambapo masahaba sita wamegawika sawa kwa sawa. Waislamu walitii agizo lake na kutekeleza wasia wake kwa ukamilifu, licha ya kwamba wasia wake haukuleta usalama kwa umma kama kinga dhidi ya upotofu. Badala yake wasia huo uliwaongoza kumchagua Khalifa mwenye moyo wa ukarimu na mdhaifu katika kutoa maamuzi, udhaifu ambao ulisababisha mauaji yake, na mauaji yake yalileta misiba isiyoweza kukisiwa. Ni vigumu sana kuamini kwamba Umar alipinga pendekezo la wasia wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kwa sababu ya kuhofia afya yake. Upo uwezekano wa kutoa maelezo mengine: inawezekana kwamba Umar alijua nini kingeandikwa kwenye wasia uliopendekezwa, kama haingekuwa kwa maslahi ya umma. Hivyo, tunaweza kupata jibu tutakapokuwa tunajaribu kujibu swali la pili.

JE! MTUKUFU MTUME (S.A.W.W.) ALITAKA KUANDIKA NINI? Haileti mantiki kufikiria kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alikuwa anajaribu, katika kipindi hicho kigumu, kuandika kitabu chenye mafundisho yake na sheria za Kiislamu kwa kinaganaga. Wala hakuwa anajaribu kuwaandikia Waislamu mukhtasari wa mafundisho ya Kiislamu. Kwani Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alikuwa anatambua vema kwamba muda wake wa kuwa hapa duniani ulikuwa mfupi sana. Aidha, kama Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) angeliandika mukhtasari wa mafundisho ya Kiislamu wakati huo, hangeweza kuwanusuru Waislamu dhidi ya kukengeuka. Mukhtasari wa mafundisho ya Kiislamu yamo kwenye Kitabu cha Mwenyezi Mungu, na pamoja na hayo, Waislamu bado 153

Page 153


Imam Ali binamu yake Mtume (s.a.w.w)Lubumba

Dr.Kanju.qxd

7/1/2011

4:37 PM

Imam Ali (a.s.) Ndugu yake Mtume Muhammad (s.a.w.) hawakubaliani, wanabishana kuhusu maelezo ya mukhtasari hizo za jumla. Na kwa sababu hii, wengi wao walipotea. Mtukufu Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) aliishi miaka 23 baada kuanza kwa Utume wake. Kamwe hakuwa anaandika mafundisho yake wala mukhtasari wa mafundisho ya Kiislamu wala hakumuagiza Mwislamu yeyote kufanya hivyo. Bado alikuwa kwenye kilele cha afya ya kufundisha na kufikisha ujumbe wa Wahyi. Kwa hekima fulani, aliamua kutokufanya hivyo, haiingii akilini kwamba wakati huo mgumu na mfupi aanze kufanya kile ambacho hakufanya wakati wa kipindi cha miaka 23 ya Utume wake. Wala Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) hakuwa anajaribu kuwaamuru Waislamu kufuata Kitabu cha Mwenyezi Mungu na mafundisho yake mwenyewe. Qur’ani Tukufu, kama ambavyo nimesema, huwaamuru Waislamu kumtii Mwenyezi Mungu na Mtume Wake. Bado, hilo si nusura ya umma dhidi ya kukengeuka. Watu bado wapo katika kutokuelewana kuhusu tafsiri ya Qur’ani Tukufu na usahihi wa mamia ya Hadithi. Tena ingewezekanaje mafundisho ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kuunusuru umma dhidi ya uovu ambapo hayakuandikwa na yeye, na kufuatana na maoni ya Waislamu wengi sana, hakuteua mtu yoyote kuwataarifu Waislamu kuhusu ukamilifu wa mafundisho yake. Madhumuni ya jaribio la maelekezo ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) haingekuwa vitu viwili ambavyo Saeed Ibn Jubier alikumbuka kutoka kwa Ibn Abbas, yaani: Kuwaswaga makafiri waende nje ya Rasi ya Arabuni na kuwapa wajumbe wa kiasi kilicho sawa kama alivyokuwa anafanya yeye. Vitu vyote viwili havingenusuru umma dhidi ya upotofu. Madhumuni ya jaribio la maelekezo ingewezekana kuwa kile kitu ambacho Ibn Abbas alinyamaza kimya bila kujibu au kilichosahauliwa na Sa’iid.

154

Page 154


Imam Ali binamu yake Mtume (s.a.w.w)Lubumba

Dr.Kanju.qxd

7/1/2011

4:37 PM

Imam Ali (a.s.) Ndugu yake Mtume Muhammad (s.a.w.) Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) Alitaka Kumtaja Mrithi Wake. Ni mantiki kufikiria kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alitaka kuteua kiongozi ambaye alimfikiria kuwa mwenye ujuzi sana katika mafundisho ya Kiislamu, mwaminifu sana kwa Mwenyezi Mungu na dini Yake, na yule ambaye angekuwa upanuzi wa utu wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Kiongozi huyo angekuwa na mamlaka ya juu sana katika umma, na kupitia kwa uongozi wake umma ungefuata njia iliyonyooka. Kwa dhahiri, kiongozi aliyekusudiwa hakuwa Umar au Abu Bakr. Kama angekuwa mmojawao, Umar angekuwa na furaha sana kuona maelekezo ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) yameandikwa. Kwani tunamuona Umar baada ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kutawafu akijaribu kuhalalisha uongozi wa Abu Bakr kwa sababu yeye alikuwa sahaba wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kwenye pango wakati wa Hijira au kwa yeye kuwa kiongozi wa Swala ya jamaa wakati wa maradhi ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Kama Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) angemteua Abu Bakr kwa pendekezo la maelekezo yake, Umar asingehitaji uthibitisho kama huo. Wala hangehitaji kubishana na wazalendo wa Madina kuhusu sifa za Abu Bakr. Maneno ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) ya siku ya Ghadiir Khum, alipomtangaza Ali kuwa Mawla (Mlezi) wa Waislamu, yalikuwa bado mapya katika kumbukumbu ya Umar. Wakati Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) aliposema akiwa mahututi kitandani, kuhusu maelekezo ya maandishi ambayo kwayo baada yake Waislamu hawatakengeuka, haraka sana Umar alikumbuka tangazo la Ghadiir Khum na matamko mengine mengi. Maneno yote yanakaribia kuwa sawa na yale yaliyomo kwenye matamko kuhusu ‘Itrah’ wake kwa ujumla na hususan Ali. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisema, na Zayd Ibn Arqam alisimulia: “Nimewaachieni vitu ambavyo kama mkishikamana navyo kamwe hamtapotoka baada yangu. Kitabu cha Mwenyezi Mungu, kamba iliyotandawaa baina ya Mbingu na ardhi na Itrah wangu. Vyote viwili, Kitabu na Itrah havitaachana hadi vitakaponifikia 155

Page 155


Imam Ali binamu yake Mtume (s.a.w.w)Lubumba

Dr.Kanju.qxd

7/1/2011

4:37 PM

Imam Ali (a.s.) Ndugu yake Mtume Muhammad (s.a.w.) kwenye haudhi mnamo Siku ya Hukumu. Tahadharini kuhusu jinsi mtakavyovitendea baada yangu.”106 Imam Ali (a.s.) alisimulia kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alitangaza mnamo siku ya Ghadiir Khum: “Yeyote ambaye Mwenyezi Mungu na Mtukufu Mtume wake (s.a.w.w.) ni ‘Mawla’ wake, Ali huyu ni ‘Mawla’ wake. Nimewaachieni vitu ambavyo kama mkishikamana navyo, kamwe hamtakengeuka. Kitabu cha Mwenyezi Mungu, ni kamba yake iliyoshikiliwa kwa mkono Wake na mikono yenu, na watu wa Nyumba yangu.”107 Zaydi Ibn Thabit alisimulia kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisema: “Ninawaachieni miongoni mwenu makhalifa wawili, Kitabu cha Mwenyezi Mungu na Itrah wangu. Tahadharini na jinsi mnavyovitendea baada yangu. (viwili hivyo) Havitaachana hadi viungane nami mnamo Siku ya Hukumu.”108 At-Tirmaidhi kwenye Sahih yake kupitia kwa wasimulizi wake, kwa Jabir Ibn Abdullah Al-Ansari, kwamba alisema: “Nimemuona Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kwenye Hija yake mnamo Siku ya Arafa alipokuwa amepanda ngamia wake jike (AlQuswira), akihutubia, na nilimsikia anasema: ‘Enyi watu, nimnewaachieni miongoni mwenu vitu ambavyo kama mkishikamana navyo, kamwe hamtapotea: Kitabu cha Mwenyezi Mungu na watu wa Nyumba yangu.”109 Matamko haya na mengine mengi yanayofanana na haya yalikuwa bado 106Al-Tirmidhi, sehemu ya 5, uk. 328. 107 Iliyoandikwa na Ibn Rahawaih, Ibn Jareer, Ibn Abu Assim, na Al-Mahamili kwenye Amali yake (Kanzul Ummal, sehemu ya 15, hadith Na. 356) 108 Imam Ahmad kwenye Musnad yake, sehemu ya 5, uk. 181. 109 Al-Tirmidhi, kwenye Sunan yake ya 5, uk. 328. Al Tirmidhi alisema pia kwamba Abu Dharr, Abu Sa’id Al-Khudri, Zayd Ibn Arqam, na Hudhaifa Ibn Usaid walisimulia hadith inayofanana na hii. 156

Page 156


Imam Ali binamu yake Mtume (s.a.w.w)Lubumba

Dr.Kanju.qxd

7/1/2011

4:37 PM

Imam Ali (a.s.) Ndugu yake Mtume Muhammad (s.a.w.) yanarindima kwenye masikio yake. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) aliposema kuhusu maelekezo ambayo baada yake hawatapotea, Umar kwa kutumia akili zake, haraka sana alielewa nia yake: Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) anajaribu kuandika jina la Ali kwenye maelekezo yake. Haraka sana akaanza upinzani wake. Kwa Nini Umar Alipinga Wasia huo? Umar Wakati wa utawala wake alitoa jibu kwenye mazunguzmo yaliyosimuliwa baina yake na Ibn Abbas: Umar: “Ulimwacha kwa jinsi gani binamu yako?” Ibn Abbas: Nilimwacha akicheza na vijana wa umri wake. (akidhani kwamba Umar alimaanisha Abdullah Ibn Ja’far). Umar: “Sikuwa na maana hiyo. Nilimaanisha mtu wako mkubwa (Ali), mtu wa Nyumba ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.).” Ibn Abbas: “Nilimwacha akiwa anachota maji kwa ndoo kutoka kwenye kisima kwa ajili ya kumwagilia michikichi … huku akiwa anasoma Qur’ani Tukufu.” Umar: “Dhabihu ya ngamia itakuwa ni kafara yako kama utanificha mimi. Hivi bado anashikilia moyoni mwake kitu kuhusu ukhalifa?” Ibn Abbas: “Ndio” Umar: “Je anadai kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alimteua yeye? Ibn Abbas: “Ndio, na ninaongeza kwa hilo kwamba nilimuuliza baba yangu kuhusu madai ya Ali kuhusu kuteuliwa na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akasema Ali alisema kweli.” Umar: Kulikuwa na maneno mazito kutoka kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) (kuhusu Ali) ambayo hayana uthibitisho ulio wazi wala kuondoa 157

Page 157


Imam Ali binamu yake Mtume (s.a.w.w)Lubumba

Dr.Kanju.qxd

7/1/2011

4:37 PM

Imam Ali (a.s.) Ndugu yake Mtume Muhammad (s.a.w.) kisingizio. Kwa kipindi fulani alikuwa anapima nguvu zake kuona kama angeweza kumteua yeye. Wakati anaugua maradhi alitaka kumteua yeye na nilimzuia asifanye hivyo kwa sababu inayohusu usalama wa Uislamu siku za usoni. Kwa jina la Mola wa Ka’aba, Kureishi hawataungana na kumfuata yeye, na kama angekuwa Khalifa, Waarabu nchini kote wangeasi dhidi yake.”110 Umar alikuwa na wasiwasi juu ya nusura ya Uislamu katika siku za usoni. Uaminifu wake hauna maswali, lakini kwanini uongozi wa Ali ungekuwa usio na manufaa kwa Uislamu kama Waarabu wangeasi dhidi yake? Waarabu walimgomea Abu Bakr. Maelfu kwa maelfu waliritadi wakati wa utawala wake. Hata hivyo bado Umar hakufikiria kwamba alikosea kuunga mkono uongozi wa Abu Bakr. Tena, yeye alijuaje kwamba Waarabu wangeasi dhidi ya Ali? Hivi hapakuwepo na uwelekeo kwamba Ali angekuwa ndiye mwenye kukubalika zaidi kwao kwa sababu ya uhusiano wake wa karibu sana na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na umarufu wake kama shujaa, uadilifu wake na utambuzi wake wa Uislamu? Sasa, ni vipi alitegemea Waarabu wote wangemuasi Ali? Watu wa Madina walikuwa Waarabu, na wao walikuwa ndio kundi kubwa la nguvu ya Uislamu wakati huo, na wao walikuwa na moyo mzuri kabisa kwa Ali. Kwa kweli, walibakia kidogo tu wangehamia kwake hata baada ya uchaguzi wa Abu Bakr. Hata wakati ambapo Ali alichaguliwa kwa kuchelewa, watu wa Madina walimuunga mkono kwa ukamilifu. Waarabu wengine waliokuwa kwenye majigambo ya Kiislamu isipokuwa Syria, kwa hiari walimpa ahadi ya kumtumikia. Ni kweli kwamba sehemu ya watu wa Basra, Iraq, walimuasi 110 Ibn Abu Al-Hadiid, kwenye fasili ya Nahjul Balagha, Juz. 3, uk. 278. Na Ahmad Ibn Talin kwenye kitabu chake cha Historia Tari’kh Baghdad (SharafudDeen, Al-Murajaat). 158

Page 158


Imam Ali binamu yake Mtume (s.a.w.w)Lubumba

Dr.Kanju.qxd

7/1/2011

4:37 PM

Imam Ali (a.s.) Ndugu yake Mtume Muhammad (s.a.w.) na kwamba watu wa Syria walikataa kutoa kiapo cha utii kumtumikia. Lakini hali hii ilijitokeza hapo tu ambapo viongozi kutoka Kureishi walipowachochea. Mamilioni ya watu katika dola ya Waislamu walikubali uongozi wake (Ali) wakati ambapo Waislamu wengi walikwishasahau sifa zake za daraja lake la juu. Kama Ali angepewa uongozi mara tu baada ya kifo cha Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), na kwa kupitia kwenye wasia wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) wa maandishi, Waarabu, bila shaka wangekubali zaidi uongozi wake. Umar alisema kwamba Kureishi kamwe hawataungana kumsaidia Ali. Hii inaweza kuwa kweli. Hata hivyo. Tusisahau kwamba Kureishi waliungana katika kumpinga Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na wakapigana naye kwa miaka ishirini na moja. Je, Utume wa Muhammad ungesitishwa kwa sababu ya upinzani wa Kureishi?� Akiwa anajua kipindi cha giza cha miaka ya nyuma ya Kureishi Umar asingeuchukulia upinzani huo kwenye muelekeo wa kuwa ni alama ya kutoaminika. Kwa usahihi zaidi angeufikiria kama ushahidi wa ukamilifu wa muelekeo huo. Tena, nani waliokuwa viongozi wenye nguvu wa Kureishi wakati alipokuwa anatawafu Mtukufu Mtume (s.a.w.w.)? Abu Sufyani na viongozi wengine wa kabla ya Uislamu tayari walikwishashindwa na kupoteza ushawishi wao. Viongozi wenye mvuto wakati huo walikuwa Ali, AlAbbas, Abu Bakr, Umar, Abu Ubediah, Uthman, Abdur-Rahman Ibn Awf, Talha, Az-Zubeir na masahaba waadilifu kutoka Makka. Viongozi hawa walitarajiwa kutii maelekezo ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na kuwanasihi watu wengine wa Makka wafanye hivyo. Zaidi ya hayo, historia inashuhudia kwamba Abu Sufyani pamoja na kinyongo chake dhidi ya Ali (ambaye aliwauwa watoto wake wawili, Hanthalah, Al-Waleed na ndugu zake wa karibu watatu katika kuhami Uislamu), alikuwa tayari kumsaidia Ali na si Abu Bakr. 159

Page 159


Imam Ali binamu yake Mtume (s.a.w.w)Lubumba

Dr.Kanju.qxd

7/1/2011

4:38 PM

Imam Ali (a.s.) Ndugu yake Mtume Muhammad (s.a.w.)

Kama Kureishi walikuwa na hiari au hawana ya kumsidia Ali, Umar angelikumbuka kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alikuwa na ujuzi mkubwa zaidi kuhusu watu wa Makka na Waarabu wengine kuliko yeye (Umar). Ni Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), na sio Umar aliyekwishapigana nao, na alikuwa na utambuzi wa mambo yao na masahaba wote kuliko walivyokuwa wanajitambua wenyewe. Umar pia angekumbuka kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alikuwa anahangaika zaidi kuhusu hatima ya Uislamu mnamo siku za usoni kuliko yeye. Kwa mihangaiko yake yote kuhusu hatima ya Uislamu na utambuzi wake wa saikolojia ya Waarabu, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alitaka kuliandika jina la Ali kwenye wasia wake. Uongozi wa Ali ulikuwa ndio jibu la hakika kwa matatizo ya Waislamu.

ALIWEZAJE KULETA USHINDANI NA MTUKUFU MTUME (S.A.W.W.)? Kama mambo yalivyo, tunakabiliwa na swali kubwa: Idhaniwe kwamba Umar alikuwa na uhakika wa ukamilifu wa maoni yake. Kwa nini alijiruhusu kumpinga Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), pamoja na yale yanayojulikana kuhusu yeye kuwa muongofu na mtiifu kwa Mwenyezi Mungu na Mtukufu Mtume Wake (s.a.w.w.)? Katika kujibu swali hili, lazima tujue kwamba masahaba walikuwa wakipingana na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) mara kwa mara kwa mambo ya kidunia. Walijipa fursa kufanya hivyo kwa sababu waliamini kwamba Uislamu uliwapa wao haki ya kukataa kukubaliana naye katika mamnbo hayo. Waliamini kimakosa pia kwamba uongozi wa Waislamu ulikuwa miongoni mwa mambo yao ya kidunia. Umar mwenyewe aliwahi kumpinga Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) zaidi ya mara moja.

160

Page 160


Imam Ali binamu yake Mtume (s.a.w.w)Lubumba

Dr.Kanju.qxd

7/1/2011

4:38 PM

Imam Ali (a.s.) Ndugu yake Mtume Muhammad (s.a.w.) Kupingana na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) Mnamo Siku Ya AlHudaybiyyah. Ni ukweli unaojulikana sana kwamba Umar alipingana na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kuhusu masharti ya makubaliano baina ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na makafiri kuhusu kusimamisha vita kwa muda kati ya Waislamu na makafiri wa Makka mnamo siku ya Hudaybiyyah. Ilikuwa mojawapo ya masharti yaliyosemwa kwamba Mwislamu yeyote kutoka Makka ambaye alikwenda kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) bila ruhusa ya watu wa Makka ni lazima arudishwe Makka. Lakini endapo Mwislamu kwa hiyari yake alichagua kuwaacha Waislamu na kuungana na kambi ya watu wa Makka, watu wa Makka hawatawajibika kumrudisha kwa Waislamu. Sharti hili Umar na masahaba wengine wengi waliona kama vile lina uonevu kwa Waislamu. Hata hivyo, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alitambua vema zaidi yao. Mtu anayeacha kambi ya Uislamu na kuungana na kambi ya upagani hatawanufaisha Waislamu kama akirudishwa kwao kwa nguvu, na Uislamu haumhitaji mtu kama huyo. Ibn Hisham amesimulia kwenye kitabu chake cha Wasifu wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kama ifuatavyo: “Wakati makubaliano yalipofikiwa na kukawa hakuna kilichobakia isipokuwa kuandika mkataba, Umar aliruka …. halafu akamwendea Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na akasema: “Ewe Mtukufu Mtume, hivi wewe sio Mtume wa Mwenyezi Mungu?” Mtukufu Mtume (s.a.w.w.): “Ndio, ndivyo nilivyo.” Umar: “Hivi sisi si Waislamu?” Mtukufu Mtume (s.a.w.w.): “Ndio, nyinyi ni Waislamu.” Umar: “Hivi (watu wa Makka) si makafiri?” Mtukufu Mtume (s.a.w.w.): “Ndio wao ni makafiri.” Umar: “Kwa nini tukubali fedheha hii kwenye dini yetu?” Mtukufu Mtume (s.a.w.w.): “Mimi ni mja wa Mwenyezi Mungu na Mtume Wake. Sitaacha kumtii Mwenyezi Mungu, na Yeye hatoniacha 161

Page 161


Imam Ali binamu yake Mtume (s.a.w.w)Lubumba

Dr.Kanju.qxd

7/1/2011

4:38 PM

Imam Ali (a.s.) Ndugu yake Mtume Muhammad (s.a.w.) mimi.”111 Umar alikuwa akisema baada ya hapo: “Bado ninatoa sadaka, ninafunga saumu, ninaswali na kuwaachia huru watumwa kama fidia ya makosa yangu niliyoyafanya. Kutokubaliana na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) Kuhusu Suala la Usama. Palikuwepo na wakati mwingine ambapo masahaba mashuhuri walitofautiana na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Muda mfupi kabla ya kifo chake, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alimteua Usama Ibn Zayd Ibn Harith kuwa kamanda wa jeshi la Waislamu ambalo aliamuru liondoke kwenda Jordan na Palestina. Abu Bakr, Umar, Abu Ubaidah na masahaba wengine mashuhuri, isipokuwa Ali, walikuwepo kwenye jeshi hilo. Masahaba wengi walishutumu uteuzi wake wakifikiri kwamba alikuwa na umri mdogo mno kuwaongoza wao. Jambo hili lilipofikishwa kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), alikwenda Msikitini ambapo alikuwa mgonjwa. Alipanda kwenye mimbari na akasema katika hotuba yake: “Enyi watu, tekelezeni msafara wa jeshi la Usama. Endapo mnalaumu uteuzi wake, mlilaumu uteuzi wa baba yake kabla yake. Anazo sifa za kuwa kiongozi na baba yake alikuwa anazo sifa hizo.”102 Hawakutaka kwenda hadi Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alitoka tena, ambapo alikuwa mahututi na akiwa ameshika kichwa chake. Akasema: “Enyi watu, tekelezeni msafara wa jeshi la Usama. Tekelezeni msafara wa jeshi la Usama.” 111 Ibn Hishamu, Wasifu wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), sehemu ya 2, uk. 216217. Hadith kama hii imeandikwa na Muslim katika Sahih Muslim. 102 Ibn Saad, Al-Tabaqat, sehemu ya 2, uk. 249. 162

Page 162


Imam Ali binamu yake Mtume (s.a.w.w)Lubumba

Dr.Kanju.qxd

7/1/2011

4:38 PM

Imam Ali (a.s.) Ndugu yake Mtume Muhammad (s.a.w.) Lakini masahaba hawakuondoka. Usama na watu wengine walipiga kambi karibu na Madina, wakangojea ni nini Mwenyezi Mungu atakachofanya kwa hatima ya Mtume Wake.113 Baada ya kutawafu Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), wengi miongoni mwa masahaba wake walijaribu kumfukuza Usama, ingawa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) ndiye alimteua na kwa mkono wake uliobarikiwa alimkabidhi bendera. Umar alikwenda na kusema kwa niaba ya masahaba wa Madina, akimwambia Abu Bakr amfukuze Usama na kumteua mtu mwingine badala yake. Abu Bakr aliruka na kuvuta kichwa cha Umar na huku akisema: “Mama yako na awe mfiwa kwa kifo chako na nikupoteze wewe, mwana Al-Khattab. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alimteua yeye na wewe unaniambia nimfukuze!”114 Masahaba kutoka Kureishi walidhani kwamba kama Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) angemtaja Ali kwenye wasia wake, uongozi ungebakia kwenye Nyumba yake na haungefikiwa na wengine katika Makureishi. Kama Ali angepata urithi, Al-Hasan na Al-Husein watoto wa Ali na viongozi wa vijana wa Peponi kwa ushahidi wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) mwenyewe, wangekuwa warithi wake. Hapangekuwepo na fursa ya uongozi kwa masahaba wa Makka au wasio wa Makka, bila kujali daraja zao za juu, kuufikia uongozi wa Waislamu. Masahaba walikuwa binadamu kama watu wengine. Walikuwa na malengo yao na wapenda umaarufu, na hawakutaka kuona mlango wa uongozi umebamizwa kabisa mbele yao. Walitaka mlango ubaki wazi. Hivyo ingekuwa rahisi kwao kuufikia uongozi. Koo nyingine za Makka zingewa113Ibid, uk. 249. 114 Al-Halabi kwenye “Wasifu wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.)” sehemu ya 3, uk. 336, na Addahlani kwenye “Wasifu wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.),” na Ibn Jariir kitabu chake cha Historia ambamo aliandika tukio la mwaka wa 12 Hijiriya (AlMurajaat, mwandishi Sayeed Sharaful-deen, uk. 225). 163

Page 163


Imam Ali binamu yake Mtume (s.a.w.w)Lubumba

Dr.Kanju.qxd

7/1/2011

4:38 PM

Imam Ali (a.s.) Ndugu yake Mtume Muhammad (s.a.w.) saidia wao kuliko Ali. Koo hizo za Makka zilikuwa tayari kumkubali sahaba yeyote asiyekuwa Bani Hashim badala ya Ali. Walikuwa na kinyongo kibaya dhidi yake, na walikuwa wakimuonea wivu kwa sifa yake nzuri ya jitihada zake kwa ajili ya Uislamu, ujuzi wake wa dini, uhusiano wake na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na ushujaa wake. Kama mrithi wa kwanza wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) angekuwa sahaba ambaye si ‘Bani Hashim’ (Mtu wa ukoo wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.)), koo nyingine za Makka zingepata uongozi kwa sababu zote ziko sawa. Hakuna hata ukoo mmoja ambao ni dhalili au bora kuliko mwingine. Taym (Ukoo wa Abu Bakr) si bora zaidi kuliko Uday (ukoo wa Umar), na ukoo wa Uday si bora zaidi kuliko ukoo wa Umayad, au ukoo wa Zuhrah au ukoo mwingine wowote wa Makka. Ibn Al-Athiir aliandika mazunguzo baina ya Umar na Ibn Abbas ambayo yanaonesha kwamba Umar na Makureishi wote walikuwa na fikira hii. Umar: “Ibn Abbas, unatambua kitu kilichowafanya watu wako (Makureishi) wasiwape nyinyi (Bani Hashim) uongozi baada ya Muhammad?” Ibn Abbas: “Kama sijui, Amiri wa Waumini (Umar) anaweza kuniambia.” Umar: “Hawakupenda kuwaruhusu nyinyi mhodhi yote mawili Utume na Ukhalifa, kwa tahadhari msije mkawatawala watu wenu. Makureishi (jamii ya Makka) iliamua hivyo. Ilifanya jambo jema na ilifuzu.” Ibn Abbas: “Kama Amiri wa Waumini ataniruhusu kusema na kuzuia hasira yake, nitasema.” Umar: “Sema.” Ibn Abbas: “Umesema Makureishi walijichagulia na wakafanya jambo la sawa na wakafuzu. Kama Makureishi wangechagua kufanya jambo ambalo Mwenyezi Mungu amewachagulia, haki ingekuwa upande wao bila kukataliwa au kuonewa wivu. Kuhusu usemi kwamba hawakutaka kutu164

Page 164


Imam Ali binamu yake Mtume (s.a.w.w)Lubumba

Dr.Kanju.qxd

7/1/2011

4:38 PM

Imam Ali (a.s.) Ndugu yake Mtume Muhammad (s.a.w.) ruhusu kuwa na Utume na Ukhalifa, kwa hakika, Mwenyezi Mungu amesema kuhusu baadhi ya watu wenye msimamo kama huo na kutamka: “Hiyo ni kwa sababu hawakutaka yale ambayo yamefunuliwa na Mwenyezi Mungu, kwa hiyo alitangua matendo yao mema.’” Umar: “Ewe Ibn Abbas, kwa jina la Mwenyezi Mungu, niliwahi kusikia mambo kuhusu wewe ambayo sikutaka kuyaamini, nisije nikakupotezea heshima yako.” Ibn Abass: “Ewe Amiri wa Waumini, ni mambo gani hayo uliyoyasikia kuhusu mimi? kama ni kweli yasiwe sababu yako wewe kunivunjia heshima; kama ni udanganyifu, mtu kama mimi lazima awe na uwezo wa kujitetea na kujisafisha kutokana na uzushi.” Umar: Nasikia unasema kwamba ‘waliuchepua ukhalifa kutoka kwetu kwa sababu ya wivu, uchokozi na dhuluma.” Ibn Abbas: “Ewe Amiri wa Waumini kuhusu dhuluma, imedhihirika kwa wasiojua na wenye hekima; kuhusu wivu, Adam alifanyiwa wivu na sisi ni watoto wake wanaoonewa wivu.” Umar: “Iko mbali sana. Enyi wana wa Hashim kwa jina la Mwenyezi Mungu, nyoyo zenu zinakataa kuhifadhi chochote isipokuwa wivu wa kudumu.” Ibn Abbas: “Ewe Amiri wa Waumini, usifanye haraka. Usizielezee kwa njia hii nyoyo za watu ambao Mwenyezi Mungu amezijaalia kutokuwa na doa na amewatakasa kutokana na wivu na imani mbovu. Moyo wa Mtume wa Mwenyezi Mungu unatokana na nyoyo za wana wa Hashim.” Umar: “Ibn Abbas! toka hapa kwangu, kaa mbali nami.” Ibn Abbas: Nitaondoka.” (ibn Abbas anasema): Nilipokuwa najaribu kusimama, Umar alihisi kuaibika na akasema: Ibn Abbas, usiondoke hapo ulipo. Kwa jina la Mwenyezi Mungu, ninaichunga haki yenu na kupenda 165

Page 165


Imam Ali binamu yake Mtume (s.a.w.w)Lubumba

Dr.Kanju.qxd

7/1/2011

4:38 PM

Imam Ali (a.s.) Ndugu yake Mtume Muhammad (s.a.w.) kile kinachowafurahisha nyinyi.” Ibn Abbas: “Ee, Amiri wa Waumini, mimi ninastahili haki inayotoka kwako na kwa kila Mwislamu. Yeyote anayechunga haki hiyo hujinufaisha mwenyewe, na yeyote asiyeiangalia hupata hasara.”115 Umar na masahaba wengine walifikiri kwamba kwa kuwa koo za Makka hazimuungi mkono Ali kwa sababu ya wivu na kinyongo, ingekuwa busara zaidi kuwa na kiongozi mwingine na si yeye, licha ya yeye kuteuliwa na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Makureishi ni jamii ambayo ilipiga vita Uislamu na Utume kwa kipindi cha miaka ishirini na moja, halafu wakaukubali Uislamu kwa shingo upande baada ya kushindwa kuwa mwamuzi wa hatima na kudumu kwa umma wa Waislamu. Kuungwa mkono na jamii ya Makka kilikuwa ndio kipengele chenye uamuzi kwa mgombea yeyote wa uongozi wa Kiislamu. Hili ni jambo la kushangaza. Lakini ilikuwa ndio mantiki ya matukio.

KWA NINI MTUKUFU MTUME (S.A.W.W.) HAKUSISITIZA KUANDIKA MAELEKEZO YAKE? Sasa tumefika kwenye swali la tatu: “Kwa nini Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) hakuandika maelekezo yake ijapokuwa Umar alipinga? Jibu linadhihirika wazi; Madhumuni ya nia ya maelekezo ni kunusuru umma usije ukakengeuka. Kipengele hiki kinaweza kikatambulika tu kama mwandishi wa maelekezo alikuwa na fahamu, tahadhari, anajua alichokuwa anasema. Lakini mbinu ya upinzani tayari ilikuwa inaonesha mashaka kuhusu ufahamu wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na ukamilifu wa akili yake wakati huo. Wakasema: “Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amelemewa na maradhi yake’ au ‘Nini kimemtokea au je ameota njozi? Muulizeni!” 115 Ibn Al-Atheer, Al-Kamil, sehemu ya 3, uk. 31. 166

Page 166


Imam Ali binamu yake Mtume (s.a.w.w)Lubumba

Dr.Kanju.qxd

7/1/2011

4:38 PM

Imam Ali (a.s.) Ndugu yake Mtume Muhammad (s.a.w.)

Maneno yote haya yalimuonesha Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kama vile hana fahamu na hajui anachokisema au angalau yanapanda fikira ya mashaka kwenye akili za wengine kuhusu fahamu za Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na ukamilifu wa kufikiri kwake. Masahaba wengine kwenye mkutano huo walikubaliana na upinzani wa Umar. Ambapo ukamilifu wa maneno ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) unatiliwa shaka, maelezo yanafanywa kuwa hayana athari. Kama mashaka ya namna ile yamedhihirishwa wakati alipokuwa bado yu hai, ingekuwa rahisi zaidi kuyadhihirisha baada ya kifo chake. Kwa kulingana na hali hii, maelekezo yaliyokusudiwa yalipoteza umuhimu wake na hayangekidhi haja ya lengo lake. Sa’iid Ibn Jubier alisema kwamba Ibn Abbas alisimulia: “Maradhi ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) yalipoongezeka, alisema: ‘Nipeni kidau cha wino na bamba. Nitaandika maelekezo yenu ambayo baada yangu yatawapa kinga kamwe hamtakengeuka.’ Baadhi ya wale waliokuwa naye wakasema: ‘Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) anaota njozi.’ Halafu Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) aliulizwa kama bado anataka kuandika maelekezo. Akasema: “Baada ya nini?” (kwa manufaa gani baada ya hayo ambayo yamesemwa).116 Na hatimaye tumefika kwenye swali la nne na la mwisho kuhusu somo hili.

116 Ibn Saad, Al-Tabaqat sehemu ya 2, uk. 242 167

Page 167


Imam Ali binamu yake Mtume (s.a.w.w)Lubumba

Dr.Kanju.qxd

7/1/2011

4:38 PM

Imam Ali (a.s.) Ndugu yake Mtume Muhammad (s.a.w.)

INGEWEZEKANAJE MAELEKEZO YA MTUKUFU MTUME (S.A.W.W.) KUWA NI NUSURA YA UMMA DHIDI YA KUKENGEUKA? Hakuna mtu mwenye haki ya kudai kwamba anajua kile alichokijua Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kuhusu mbinu ambayo angelitumia katika kunusuru umma wake dhidi ya upotofu. Hata hivyo, yanayoonekana kwa wazi ni kama ifuatavyo: Nusura Dhidi ya Mgawanyiko Wa Madhehebu. Endapo Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) angemtaja mtu bayana kwenye nyaraka wakati fahamu zake na ukamilifu wake wa kufikiri haujatiliwa mashaka, angeuepusha umma kutokana na mgawanyiko mkubwa. Kama angemtaja Ali au Abu Bakr au yeyote mwingine kwenye maagizo, Waislamu wangejisalimisha kwenye uongozi wake na mgawanyiko wa Waislamu katika madhehebu ya Sunni na Shia haungetokea. Mgawanyiko huu uliotokea kama matokeo ya mabishano kuhusu nani alikuwa mrithi wa halali wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Ni Abu Bakr au Ali? Kwani Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) angelazimika kumtaja yeyote kati ya hawa watu wawili au mwingine, mgawanyiko kama huo haungetokea. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alitoa matamshi mengi kuhusu Ali lakini hati iliyoandikwa inayoathari kubwa zaidi. Matamshi ya mdomo kama tulivyosema, yanaweza kukatiliwa, kuongezwa, kupunguzwa au kusahauliwa. Maelezo yaliyoandikwa si rahisi kuyabadilisha kwa namna yoyote. Abu Bakr alimtaja Umar kwa maandishi. Na wafuasi wote wa Abu Bakr walifuata maelekezo yake. Maelekezo ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) yangekuwa na athari zaidi na yangeaminiwa zaidi kuliko ya Abu Bakr. Kumtaja mrithi kwa maelekezo ya namna hiyo, ingezuia kutokeza kwa ‘Khawariji’ (mafundisho ya waliojitenga), kundi ambalo linamkana Ali na 168

Page 168


Imam Ali binamu yake Mtume (s.a.w.w)Lubumba

Dr.Kanju.qxd

7/1/2011

4:38 PM

Imam Ali (a.s.) Ndugu yake Mtume Muhammad (s.a.w.) Uthman na linawaita Waislamu kuunda dola ya Waislamu bila ya serikali. Vita vya Sifini ambavyo vilisababisha kutokeza mafundisho haya, havingetokea. Vita vya wenyewe kwa wenyewe baina ya Imam Ali na Muawiya na kabla ya hapo, vita vya Basrah, Iraq, baina ya Imam Ali upande mmoja na upande mwingine Aisha, Talha na Az-Zubeir, vilikuwa ni matokeo ya kuuawa kwa Uthman, Khalifa wa tatu. Kama Ali angekuwa ametajwa kuwa Khalifa, kwenye maagizo yaliyoandikwa, Uthman angeuawa kabla ya kuwa Khalifa, kwa sababu Ali alidumu kuliko yeye. Kama Ali angekuwa Khalifa kufuatana na maagizo yaliyoandikwa kutoka kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), Muawiya hangekuwa Khalifa, wala mwanae mhalifu Yazid hangeweza kuwauwa watoto wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) huko Karbala. Wala vita baina ya mtoto wa Az-Zubeir na Umayad na misiba mingine mingi na vita havingetokea. Matukio yote haya yalikuwa matokeo ya kutokuwepo maelekezo ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) yaliyoandikwa. Kama maelekezo ya namna hiyo yangekuwepo historia ya Uislamu ingebadilika, na tungekuwa tunasoma historia ya Uislamu iliyo tofauti na hii tunayosoma leo. Ningependa kutamka haraka haraka kwamba simfikirii Khalifa wa pili (Umar) kwa upinzani wake wa kuzuia kuandikwa maelekezo yaliyopendekezwa kwamba anahusika na mgawanyiko wa Waislamu na mengine yote yaliyofuata. Umar alikuwa binadamu ambaye hangeweza kutabiri hatima ya umma wa Waislamu. Yote yale ambayo Umar alikuwa anayafikiria ni kwamba uongozi wa Waislamu baada ya kifo cha Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) ni mojawapo ya mambo ya kidunia ambayo masahaba wa Makka walikuwa na haki ya kuamua kufuatana na masilahi yao yalivyohitajia. Hakutaka Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) aandike neno la mwisho kuhusu jambo hili ili mlango uwe wazi kwa masahaba. Kama Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) angeandika maagizo 169

Page 169


Imam Ali binamu yake Mtume (s.a.w.w)Lubumba

Dr.Kanju.qxd

7/1/2011

4:38 PM

Imam Ali (a.s.) Ndugu yake Mtume Muhammad (s.a.w.) yake, neno lake huwa la mwisho. Qur’ani Tukufu inatamka:

“Haiwi kwa Muumini mwanaume wala muumini mwanamke kuwa na hiari katika jambo, Mwenyezi Mungu na Mtume Wake wanapokata shauri katika jambo lao. Na mwenye kumuasi Mwenyezi Mungu na Mtume Wake basi hakika amepotea upotofu ulio wazi.” Qur’an Tukufu, Surat al-Ahzab; 33:36. (Inafaa kuzingatiwa kwamba uamuzi wa Dini ukitamkwa kwa mdomo, unakuwa ni wa mwisho kama ule wa kuandika. Vinginevyo, maamuzi na matamshi yote ya Mtukufu Mtume yasingekuwa yanatufunga, kwa sababu hayakuandikwa wakati wa uhai wake). Mtu pekee ambaye alikuwa na uwezo wa kuona mustakabali wa baadae, na sio kwa kupitia uwezo wake binafsi bali kupitia Wahyi alikuwa ni Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) mwenyewe. Yeye alikuwa ameuona, kwa mwanga wa Mwenyezi Mungu, mustakabali wa umma wake na kwamba kama utabakia bila ya maagizo ya maandishi, basi mitihani ya kujaribu imani itaukumba juu yake kama vipande vya usiku wa giza (na hili ndio ambalo sahaba wake, Abu Muwaihibah alilolisimulia). Hivyo, yeye alitaka kuuondolea umma mitihani hiyo ambayo ingevuruga na kuharibu umoja. Na kwa ajili ya hili yeye alisema: “Nileteeni kidau cha wino na bamba ili niandike humo maagizo ambayo baada yake hamtapotea kamwe.” Nusura Dhidi Ya Mgawanyiko wa ki-Fiqhi: Maagizo ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) yaliyoandikwa ambamo anamtaja mrithi wake hayangekuwa tu salama ya taifa dhidi ya mgawanyiko wa 170

Page 170


Imam Ali binamu yake Mtume (s.a.w.w)Lubumba

Dr.Kanju.qxd

7/1/2011

4:38 PM

Imam Ali (a.s.) Ndugu yake Mtume Muhammad (s.a.w.) madhehebu lakini pia dhidi ya ongezeko la matapo ya Sharia (Fiqhi) ya Kiislamu. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alitangaza kwamba Qur’ani na Itrah wake ( watu wa Nyumba yake) ni nusura dhidi ya kukengeuka na kwamba Qur’ani Tukufu na ‘Itrah’ havitaachana hadi Siku ya Hukumu. Kama Ali (kiongozi wa watu wa Nyumba ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.)) angekuwa ndiye Mwislamu mwenye mamlaka ya juu sana baada ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), angekuwa ndio salama hiyo. Alikuwa mtambuzi thabiti wa juu sana wa Qur’ani Tukufu na mafundisho ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Makhalifa wawili wa kwanza (Abu Bakr na Umar), pamoja na ujuzi wao wote mkubwa katika Uislamu, walikuwa na desturi ya kukimbilia kwake walipokutana na yale wasiyoyajua. Mara nyingi Umar alikuwa akisema: “Kama ushauri wa Ali usingekuwa unapatikana, Umar angeangamia kidini.” Na alisema: “Mwenyezi Mungu na aniweke mbali na tatizo gumu ambalo Abu Hasan (Ali) atakuwa hayupo.” Ibn Saad alisimulia kwamba Ali alisema: “Kwa jina la Mwenyezi Mungu, haipo Aya ambayo siijui imeteremshwa kuhusu nini na wapi na kuhusu nani. Mola Wangu amenijaalia akili yenye ufahamu na ulimi fasaha na wenye kudadisi.”117 Ali aliulizwa kwa nini yeye, miongoni mwa masahaba wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), alikuwa ndiye msimuliaji mkubwa sana wa maneno yake Mtukufu Mtume (s.a.w.w.)? Ali akajibu: “Alikuwa akinitaarifu mimi wakati nilipomuuliza na alianzisha mafundisho yake nilipokuwa kimya.”118 Sa’iid Ibn Al-Musavab alisema: “Hapana mtu mwingine isipokuwa Ali aliyekuwa akisema: “Niulizeni kabla sijaondoka.”119 117 Muttaqi Hind kwenye Kanzul Ummal, Sehemu ya 15, uk. 113. 118 Ibid, uk. 113 119 Ibid, uk. 113. 171

Page 171


Imam Ali binamu yake Mtume (s.a.w.w)Lubumba

Dr.Kanju.qxd

7/1/2011

4:38 PM

Imam Ali (a.s.) Ndugu yake Mtume Muhammad (s.a.w.) Ali ndiye mtu yule ambaye Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisema: “Mimi ni Jiji la Elimu na Ali ni Lango lake. Yeyote anayetaka kuingia kwenye Jiji lazima aingie kupitia kwenye lango.”120 Ummu Salama (Mke wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.)) alisimulia kwamba alimsikia Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) anasema: “Ali yuko pamoja na Qur’ani, na Qur’ani iko pamoja na Ali. Hawataachana hadi Siku ya Hukumu.”121 Kama Ali angekuwa mrithi wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) mara baada ya kifo chake kupitia kwenye maagizo ya maandishi, maelekezo hayo ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) yangelikwisha julikana na Waislamu wangekubaliana nayo katika matawi mbali mbali ya Sharia ya Kiislamu. Hivyo, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alitaka kumtumia Ali kama nguvu ya kuunganishia Waislamu wote katika vizazi vyote, na hali hii ingeweza kuwazuia wasikengeuke.

120 Al-Hakim, Al-Mustadrak, sehemu ya 3, uk. 124 121 Al-Hakim, Al-Mustadrak, sehemu ya 3, uk. 127. 172

Page 172


Imam Ali binamu yake Mtume (s.a.w.w)Lubumba

Dr.Kanju.qxd

7/1/2011

4:38 PM

Imam Ali (a.s.) Ndugu yake Mtume Muhammad (s.a.w.)

ORODHA YA VITABU VILIVYO CHAPISHWA NA AL-ITRAH FOUNDATION 1. 2. 3. 4. 5. 6. 7. 8. 9. 10. 11. 12. 13. 14. 15. 16. 17. 18. 19. 20. 21. 22. 23. 24. 25. 26.

Qur'an Al-Kariim - Tafsir Al-Kashif Juzuu ya kwanza mpaka Thalathini Uharamisho wa Riba Uharamisho wa uwongo Juzuu ya Kwanza Uharamisho wa uwongo Juzuu ya Pili Hekaya za Bahlul Muhanga wa Imamu Husein (A.S.) Mikingamo iliyomzunguka Imamu Ali (A.S.) Hijab vazi Bora Ukweli wa Shia Ithnaashari Madhambi Makuu Mbingu imenikirimu Abdallah Ibn Saba Khadijatul Kubra Utumwa Umakini katika Swala Misingi ya Maarifa Kanuni za Ndoa na maadili ya Familia Bilal wa Afrika Abudharr Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu Salman Farsi Ammar Yasir Qur'an na Hadithi Elimu ya Nafsi Yajue Madhehebu ya Shia Ukusanyaji na Uhifadhi wa Qur'an Tukufu 173

Page 173


Imam Ali binamu yake Mtume (s.a.w.w)Lubumba

Dr.Kanju.qxd

7/1/2011

4:38 PM

Imam Ali (a.s.) Ndugu yake Mtume Muhammad (s.a.w.) 27. 28. 29. 30. 31. 32. 33. 34. 35. 36. 37. 38. 39 40. 41. 42. 43. 44. 45. 46. 47. 48. 49. 50. 51. 52. 53. 54. 55. 56. 57.

Al-Wahda Ponyo kutoka katika Qur'an. Uislamu mfumo kamili wa maisha ya kijamii Mashukio ya Akhera Al Amali Dua Indal Ahlul Bayt Udhuu kwa mujibu wa Kitabu na Sunna. Haki za wanawake katika Uislamu Mwenyeezi Mungu na sifa zake Amateka Na Aba'Khalifa Nafasi za Ahlul Bayt (a.s) Adhana. Upendo katika Ukristo na Uislamu Nyuma yaho naje kuyoboka Amavu n’amavuko by’ubushiya Kupaka juu ya khofu Kukusanya swala mbili Bismillah ni sehemu ya Qur’ani na husomwa kwa Jahara Kuwaongoza vijana wa kizazi kipya Kusujudu juu ya udongo Kusheherekea Maulidi Ya Mtume (s) Tarawehe Malumbano baina ya Sunni na Shia Kupunguza Swala safarini Kufungua safarini Umaasumu wa Manabii Qur’an inatoa changamoto as-Salaatu Khayrun Mina -'n Nawm Uadilifu wa Masahaba Dua e Kumayl Sauti Ya Uadilifu wa Binadamu 174

Page 174


Imam Ali binamu yake Mtume (s.a.w.w)Lubumba

Dr.Kanju.qxd

7/1/2011

4:38 PM

Imam Ali (a.s.) Ndugu yake Mtume Muhammad (s.a.w.) 58. 59. 60. 61. 62. 63. 64. 65. 66. 67. 68. 69. 70. 71. 72. 73. 74. 75. 76. 77. 78. 79. 80. 81. 82. 83. 84. 85. 86.

Umaasumu wa Mitume - Faida Zake Na Lengo Lake Umaasumu wa Mitume - Majibu Ya Aya Zenye Utata Umaasumu wa Mitume - Umaasumu wa Mitume Muhammad (s) Nahju’l-Balaghah - Juzuu ya Kwanza Nahju’l-Balaghah - Juzuu ya Pili Kuzuru Makaburi Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Kwanza Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Pili Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Tatu Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Nne Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Tano Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Sita Tujifunze Misingi Ya Dini Sala ni Nguzo ya Dini Mikesha Ya Peshawar Malezi Ya Mtoto Katika Uislamu Ubora wa Imam 'Ali Juu ya Maswahaba Na Ushia ndio njia iliyonyooka Hukumu za Kifikihi zinazowahusu Wanawake Liqaa-u-llaah Muhammad (s) Mtume wa Allah Amani na Jihadi Katika Uislamu Uislamu Ulienea Vipi? Uadilifu, Amani na Mtume Muhammad (s) Mitala na Ndoa za Mtume Muhammad (s) Urejeo (al-Raja’a ) Mazingira Utokezo (al - Badau) Sadaka yenye kuendelea Msahafu wa Imam Ali 175

Page 175


Imam Ali binamu yake Mtume (s.a.w.w)Lubumba

Dr.Kanju.qxd

7/1/2011

4:38 PM

Imam Ali (a.s.) Ndugu yake Mtume Muhammad (s.a.w.) 87. 88. 89. 90. 91. 92. 93. 94. 95.

Uislamu na dhana Mtoto mwema Adabu za Sokoni Johari za hekima kwa vijana Maalimul Madrasatain Sehemu ya Kwanza Maalimul Madrasatain Sehemu ya Pili Maalimul Madrasatain Sehemu ya Tatu Tawasali Imam Mahdi katika Usunni na Ushia

96.

Maana ya laana na kutukana katika Qur’ani Tukufu

97.

Hukumu ya kujenga juu ya makaburi

98.

Swala ya maiti na kumlilia maiti

99.

Shiya na Hadithi (kinyarwanda)

100.

Mariamu, Yesu na Ukristo kwa mtazamo wa Kiislamu

101.

Hadithi ya Thaqalain

102

Fatima al-Zahra

103.

Tabaruku

104.

Sunan an-Nabii

105.

Historia na sera ya viongozi wema (Sehemu ya Kwanza)

106.

Historia na sera ya viongozi wema (Sehemu ya Pili)

107.

Mahdi katika sunna

108.

Kusalia Nabii (s.a.w)

109.

Ujumbe -Sehemu ya Kwanza

110.

Ujumbe - Sehemu ya Pili

111.

Ujumbe - Sehemu ya Tatu

112.

Ujumbe - Sehemu ya Nne

113.

Ngano ya kwamba Qur’ani imebadilishwa 176

Page 176


Imam Ali binamu yake Mtume (s.a.w.w)Lubumba

Dr.Kanju.qxd

7/1/2011

4:38 PM

Imam Ali (a.s.) Ndugu yake Mtume Muhammad (s.a.w.) 114.

Iduwa ya Kumayili.

115.

Maarifa ya Kiislamu.

116.

Ukweli uliopotea sehemu ya Kwanza

117.

Ukweli uliopotea sehemu ya Pili

118.

Ukweli uliopotea sehemu ya Tatu

119.

Ukweli uliopotea sehmu ya Nne

120.

Ukweli uliopotea sehmu ya Tano

121.

Johari zenye hekima kwa vijana

122.

Safari ya kuifuata Nuru

123.

Idil Ghadiri

124.

Myahudi wa Kimataifa

125.

Kuanzia ndoa hadi kuwa Wazazi

126.

Visa vya kweli sehemu ya Kwanza

127.

Visa vya kweli sehemu ya Pili

128.

Muhadhara wa Maulamaa

129.

Mwanadamu na Mustakabali wake

130.

Imam Ali binamu ya Mtume Sehemu ya Kwanza

131.

Imam Ali binamu ya Mtume Sehemu ya Pili

132.

Khairul Bariyyah

133.

Uislamu na mafunzo ya kimalezi

134.

Vijana ni Hazina ya Uislamu.

135.

Yafaayo kijamii

136.

Kusoma sura zenye Sijda ya wajibu

137.

Taqiyya

138.

Vikao vya furaha

139.

Shia asema haya Sunni asema haya Wewe wasemaje? 177

Page 177


Imam Ali binamu yake Mtume (s.a.w.w)Lubumba

Dr.Kanju.qxd

7/1/2011

4:38 PM

Imam Ali (a.s.) Ndugu yake Mtume Muhammad (s.a.w.) 140.

Uislamu na Mazingatio Sehemu ya Kwanza

141.

Uislamu na Mazingatio Sehemu ya Pili

142.

Azadari-Kuhuzunika na Kuomboleza

143.

Sunna katika Kitabu Fiqhi al-Sunnah

144.

Mtazamo Mpya - Wanawake katika Uislamu

145.

Kuonekana kwa Allah

146.

Tabia njema kwa Mujibu wa Ahlul-Bayt (Sehemu ya Kwanza)

147.

Tabia njema kwa Mujibu wa Ahlul-Bayt (Sehemu ya Pili)

148.

Ndugu na Jirani

149.

Ushia ndani ya Usunni

150.

Maswali na Majibu

151.

Mafunzo ya hukmu za ibada

152.

Ahlul Bayt ndani ya tafsiri za Kisusunni No 1

153

Ahlul Bayt ndani ya tafsiri za Kisusunni No 2

154.

Ahlul Bayt ndani ya tafsiri za Kisusunni No 3

155.

Abu Huraira

156.

Kati ya Alama kuu za dini Swala ya Jamaa.

157.

Mazingatio kutoka katika Qur’an sehemu ya Kwanza

158.

Mazingatio kutoka kaitka Qur’an sehemu ya Pili

159.

Mazingatio kutoka katika Uislamu sehemu ya kwanza

160.

Mazingatio kutoka katika Uislamu sehemu ya Pili

161.

Hukumu zinazomuhusu mkuu wa kazi na Mfanyakazi

162.

Falsafa ya mageuzi ya Imam Husein (a.s)

163.

Huduma ya Afya katika Uislamu

164.

Hukumu za Mgonjwa 178

Page 178


Imam Ali binamu yake Mtume (s.a.w.w)Lubumba

Dr.Kanju.qxd

7/1/2011

4:38 PM

Imam Ali (a.s.) Ndugu yake Mtume Muhammad (s.a.w.) 165.

Falsafa ya Mageuzi ya Imam Husein

166.

Uislamu Safi

167.

Majlis ya Imam Husein

168.

Mshumaa

169.

Tiba ya Maradhi ya Kimaadili

170.

Uislam wa Shia

171.

Amali za Makka

172.

Amali za Madina

173.

Uislamu na mfumo wa Jamii ya dini nyingi

174.

Sira ya Imam Ali kuhusu Waasi

175.

Ukweli uliofichika katika neno la Allah

176.

Elimu ya Tiba za Kiislam Matibabu ya Maimamu

177.

Falsafa ya Dini

179

Page 179


Imam Ali binamu yake Mtume (s.a.w.w)Lubumba

Dr.Kanju.qxd

7/1/2011

4:38 PM

Imam Ali (a.s.) Ndugu yake Mtume Muhammad (s.a.w.)

BACK COVER Imam Ali (as) hakuwa kiongozi wa Waislamu tu bali wa wanadamu wote. Maisha na mwenendo wa Imam Ali (as) umewavutia watu wote, marafiki na maadui, hali ambayo imemfanya kuwa kiongozi wa umma. Mtukufu Mtume (saw) alimtangaza mwanzoni kabisa mwa Ujumbe wake katika kile kikao mashuhuri kabisa cha “karamu ya jamaa”, aliposema: “Huyu ni ndugu yangu, wasii wangu, waziri wangu, khalifa wangu na mrithi wangu. Basi msikilizeni na mumtii.” Hili lilikuwa tangazo la mwanzo kabisa alilolitoa Mtukufu Mtume (saw) kwa ajili ya Imam Ali (as) na aliendelea kuwakumbusha Waislamu kuhusu uongozi wa Imam Ali baada yake katika matukio mengi yaliyofuata baadaye, kama vile katika tukio la Ghadir Khum pale aliposema: “Man kuntu mauwahu fahadha Aliyyun mawlahu – Yule ambaye mimi kwake ni kiongozi basi na huyu Ali ni kiogozi wake.” Na mwisho ni tukio la “Karatasi” pale Mtukufu Mtume (saw) alipokuwa ni mgonjwa na maradhi yamemzidi akaomba aletewe karatasi, kalamu na wino, mashuhuri kama “hadithi ya karatasi.” Kimetolewa na kuchapishwa na: Alitrah Foundation S.L.P. 19701 Dar es Salaam, Tanzania Simu: +255 22 2110640 Simu/Nukushi: +255 22 2127555 Barua Pepe: alitrah@raha.com Tovuti: www.ibn-tv-com Katika mtandao: w.w.w.alitrah.info

180

Page 180


Imam Ali binamu yake Mtume (s.a.w.w)Lubumba

Dr.Kanju.qxd

7/1/2011

4:38 PM

Imam Ali (a.s.) Ndugu yake Mtume Muhammad (s.a.w.)

181

Page 181


Imam Ali binamu yake Mtume (s.a.w.w)Lubumba

Dr.Kanju.qxd

7/1/2011

4:38 PM

Imam Ali (a.s.) Ndugu yake Mtume Muhammad (s.a.w.)

182

Page 182


Imam Ali binamu yake Mtume (s.a.w.w)Lubumba

Dr.Kanju.qxd

7/1/2011

4:38 PM

Imam Ali (a.s.) Ndugu yake Mtume Muhammad (s.a.w.)

183

Page 183


Turn static files into dynamic content formats.

Create a flipbook
Issuu converts static files into: digital portfolios, online yearbooks, online catalogs, digital photo albums and more. Sign up and create your flipbook.