WATOTO CHANZO CHA MABADILIKO
MAMBO YA KUJIFUNZA KUTOKANA NA MRADI WA MAJARIBIO WA KUKUZA UELEWA KUHUSU VVU NA UKIMWI KATIKA SHULE ZA MISINGI TANZANIA
Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi
Shirika la Maendeleo la Ubelgiji Tanzania
VIFUPISHO BTC Shirika la Maendeleo la Ubelgiji Tanzania (Belgian Technical Cooperation) KUEKUS Kamati ya Unasihi na Elimu ya Kuijkinga na UKIMW ya Shule TACAIDS Tume ya Kuthibiti Ukimwi Tanzania (Tanzania Commis sion for AIDS) TDHS Uchunguzi kuhusu Takwimu na Afya Tanzania (Tanza nia Demographic and Health Survey) THMIS Uchunguzi kuhusu Viashiria vya UKIMWI na Malaria Tanzania (Tanzania HIV and Malaria Indicator Survey) UKIMWI Upungufu wa Kinga Mwilini VVU Virusi Vya UKIMWI
Ripoti hii imeandaliwa/imehaririwa na Marleen (Mtaalamu wa VVU / UKIMWI, BTC), Hyacintha Musaroche (Mratibu wa Taifa wa Mradi, WEMU), Anna Patton (Afisa Mawasiliano, BTC) Picha zote na: BTC/Anna Patton, isipokuwa ilipoonyeshwa vinginevyo . Msanifu: Arnold Njuki Š WEMU/BTC Dar es Salaam, October 2012 Kano /Kanusho Maoni na mawazo yaliyomo humu ni ya waandishi wenyewe na si lazima yawakilishe Shirika la Maendeleo la Ubelgiji (BTC) au Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi (WEMU).
AU KIJANA? MTOTO, BALEHE
unawaelezea Umoja wa Mataifa ti ya tu wenye umri ka vijana kama wa . miaka 15 na 24 wale ana balehe au ni Kwa ujumla, vij 18. ya miaka 10 na wenye umri kati ri yote mwenye um Mtoto ni mtu ye 18. chini ya miaka
i wa enga wanafunz Mrad i huu uliwal nye , yaani wale we shule za msingi aka 7 na 13. umri kati ya mi
MAFUNZO YA LEO MAJUKUMU YA KESHO Kijitabu hiki kinawasilisha matokeo ya mradi wa Kukuza Uelewa kuhusu VVU na UKIMWI uliojaribiwa katika shule za msingi 28 Tanzania. Unasisitiza kuhusu mambo tuliyojifunza na kutoa mapendekezo kuhusu namna ya kuzipanua zaidi shughuli za mradi ili kuzifikia shule nyingi zaidi. Manufaa ya mradi huu yameshuhudiwa katika sehemu muhimu zilizolengwa na hii inadhihirisha kuwa, hata kwenye ngazi ya elimu ya msingi, watoto na vijana wadogo wanaweza kubadilisha sio tu tabia zao bali hata kusaidia mabadiliko ya mitazamo na matendo ya wanarika wenzao, familia na jamii kwa ujumla. Sifa muhimu zilizochangia kuleta matokeo haya ni pamoja na: •
Kufuata mifumo ya Kitanzania
•
Kujikita kwenye mazingira wezeshi
•
Mafunzo kamilifu kwa walengwa wote.
•
Matumizi ya sanaa na michezo
Mradi huu ambao ni wa aina yake katika Tanzania umefadhiliwa na Serikali ya Ubelgiji na kutekelezwa na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi (WEMU) ikisaidiwa na BTC – Shirika la Maendeleo la Ubelgiji. Kwa namna hii, uzoefu wa timu ya mradi, walimu, wanafunzi, kamati za shule maafisa wa serikali za mitaa unaweza kutoa mambo muhimu ya kujifunza kwa wadau wa elimu Tanzania na kwingineko. Inatarajiwa kuwa kijitabu hiki na ripoti* inayoambatana nacho vitahamasisha umuhimu wa kufikiria kuwekeza kwenye elimu ya VVU & UKIMWI katika shule za msingi na kuijumuisha elimu hiyo kwenye sera ya taifa. *Kijitabu hiki kinatokana na tathmini huru ya mradi wa majaribio iliyofanyika Julai 2012. Ripoti kamili inaweza kupatikana kwa kutuma maombi Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi.
1
Kuwekeza kwa watoto na vijana katika masuala ya VVU & UKIMWI na afya ya uzazi kuna manufaa makubwa katika mwitikio wa kitaifa dhidi ya janga hili. Hata hivyo, mara nyingi, vijana wa rika balehe wamewekwa kando katika jitihada za kitaifa dhidi ya VVU & UKIMWI, kwa sababu umri wao unaingizwa kwenye kundi la wenye miaka kati ya 15-49. Wanafunzi wengi wa shule za msingi wanaachwa waufikie umri wa balehe bila kujua ni nani wa kumwuliza, kwani mara nyingi, wazazi huona aibu na walimu wanadhani kuwa wanafunzi hawahitaji elimu ya uzazi. Kwa jinsi hii, wanafunzi wako hatarini kupotoshwa kiurahisi. Kwa ujumla, kuwatelekeza watoto kunamaanisha pia kuwa taasisi za kielimu zimeachwa zishughulikie suala hili bila msaada wa kutosha kutoka mashirika ya kitaifa na kimataifa. Katika muongo wa nne wa kuwepo UKIMWI, imedhihirika kwamba janga hili linaendelea kubadilika; mara nyingi limeonekana kuwa la kawaida hali likijikita zaidi katika makundi ya wahanga kama vile vijana na watoto waliobalehe / kuvunja ungo DR BENNETT FIMBO, MTAALAMU WA ELIMU NA MAENDELEO YA AFYA, NDIYE MWANDISHI WA TATHMINI YA MRADI HUU
TUMEJIFUNZA NINI? 1. Umuhimu wa kuwahusisha wadau wengi na ushirikiano
• • • •
Mazingira wezeshi yanahitajika ili kuwawezesha vijana Mafunzo kwa maofisa wa halmashauri na kamati za shule ni muhimu ili kuhakikisha umiliki na uendelevu wa mradi. Rasilimali vitu, kama vitabu, zinasaidia kuhakikisha masuala yana pewa nafasi na umakini unaostahili. Kazi kubwa bado inahitajika kuhakikisha kuwa huduma rafiki za afya zinafikiwa na vijana
2. Kuwa wazi kunaongeza ufahamu, ujasiri na mabadiliko ya tabia
• • •
Muunganiko wa shughuli za mradi umeonesha kuwa unaweza ku leta mabadiliko chanya ya tabia kwa wanafunzi Mafunzo ya kina na endelevu yanayohusisha wadau wote huleta uelewa halisi Watu ambao sio walengwa wakuu wa mradi wameripoti kuwa na ongezeko la ufahamu na mabadiliko ya tabia
3. Mbinu bunifu na shirikishi hufanya mafunzo kuwa na ufanisi zaidi
2
• •
Sanaa na michezo huwawezesha vijana kuzungumzia maswala ya afya ya uzazi na ujinsia kwa ujasiri zaidi Mbinu bunifu na shirikishi zina manufaa zaidi, yakiwa ni pamoja na kuboresha mahudhurio shuleni
KWA NINI UWEPO MRADI KAMA HUU? KUMBUSHO LA MUKTADHA VVU & UKIMWI KWA WATOTO NA VIJANA BALEHE Pamoja na kushuka kwa kiwango cha maambukizi katika Tanzania (kutoka 7% mwaka 2004 hadi 5.7% mwaka 2008), inakadiriwa kuwa watu milioni 2.2 wana VVU na UKIMWI. Katika maeneo ya mijini na katika miji midogo, kiwango cha maambukizi kipo juu zaidi (zaidi ya 9%) hali kukiwa na ongezeko la maambukizi mapya katika maeneo ya vijijini. Kuna ukosefu mkubwa wa takwimu kuhusu watoto na vijana wadogo. Kwa ujumla, takiwimu huzungumzia makundi yaliyopo kati ya miaka 15-49 au chini ya miaka 5 bila tarakimu kwa makundi ya kati. Hata hivyo, inakadiriwa idadi ya watoto wa Tanzania wenye VVU & UKIMWI inafikia 10%. Shirika la UNICEF linaonyesha kuwa idadi ya watoto wenye umri wa miaka 15 wenye VVU na UKIMWI ni 160,000 (2009). Hata watoto ambao hawajapata maambukizi, ni wahanga wa madhara ya ugonjwa huu. Takwimu za awali zilizokusanywa mwanzoni mwa mradi zilionyesha kuwa idadi kubwa ya wanafunzi (22.8%) wamewahi kuishi au walikuwa wakiishi na mtu mwenye VVU. Kitaifa, zaidi ya watoto milioni moja wamepoteza mzazi mmoja au wawili kwa sababu ya UKIMWI. Vyanzo: TACAIDS; THMIS; UNAIDS et al.; Chediel & Rajabu
VIJANA WANAFAHAMU NINI ? WAKO HATARINI KIASI GANI ? Pamoja na kuwepo kwa mkanganyiko, wanafunzi wa shule za msingi wana ufahamu wa mambo ya msingi kuhusu VVU & UKIMWI. Hata hivyo, hawautumii ufahamu huo moja kwa moja katika mazingira ya maisha halisi. Tafiti za awali zilizofanywa katika shule za mradi zimeonyesha kuwa wanafunzi wana ufahamu kuhusu VVU na UKIMWI, ingawa ufahamu huo unatofautiana :
3
Utandawazi ni changamoto kubwa kwa maendeleo ya wanafunzi wetu hususani wale wa darasa la III na IV, kwani wengi wao wameona mambo mengi na hata wameyajaribu… Unajua wanafunzi wanapenda kujaribu. Kwa hiyo, unapoongea nao wanafahamu tayari – baadhi yao wanafahamu kupitia vyombo vya habari. Kwa hiyo, mradi huu ni muhimu ili kuyaweka mambo katika mtazamo sahihi kuhakikisha watoto wetu wa shule za msingi na hata jamii zetu wanaweza kuzuia maambukizi ya virusi vya HIV na maambukizi mengine ya maradhi ya ngono AFISA ELIMU WA WILAYA, KARATU
79%
ya wanafunzi waliohojiwa walionekana kuwa na ufahamu kuhusu namna ya kuzuia maambukizi.
wanafunzi wa Dar es Salaam walionyesha kuwa na ufahamu zaidi ya wale wa wilaya za vijijini na kiwango cha imani potofu kuhusu VVU & UKIMWI kilikuwa kikubwa kwa wasichana kuliko wavulana. Wengi wa wanafunzi waliohojiwa (79%) walionekana kuwa na ufahamu kuhusu namna ya kuzuia maambukizi ingawa majibu waliyoyatoa kwa maswali mengine yalionyesha mkanganyiko. Kwa mfano, karibu theruthi moja ya wanafunzi walisema walimu wenye VVU hawatakiwi kufundisha kwa sababu wanaweza kuwaambukiza wengine. Theluthi ya Watanzania wako katika umri wa miaka 10 -24, kundi rika ambalo huanza kujihusisha na ngono. Katika moja ya utafiti (TDHS 2010), ilidhihirika kuwa 11% ya vijana wa kike na 8% ya vijana wa kiume walifanya ngono kwa mara ya kwanza kabla ya miaka kufikia umri wa miaka 15 ; 6% ya wasichana wa shule (msingi na sekondari) huacha shule kila mwaka kutokana na mimba (WEMU). Takwimu za mwanzo wa mradi zilionyesha kuwa 4% ya wanafunzi waliokusudiwa na mradi walikuwa wameshaanza kujihusisha na ngono. Katika Tanzania 80% ya maambukizi mapya hutokana na mahusiano ya kingono na vijana ndiyo walio katika hatari zaidi ya kuambukizwa. Ngono zisizo salama zimepungua kwa vijana – kwa mfano, idadi ya wasichana wenye umri kati ya 15-19 wanaofanya mapenzi na zaidi ya wenzi wawili imeshuka kutoka 5% hadi 2% kutoka 2004 – 2010 (TDHS 2004/2010). Hata hivyo, matumizi ya kondom bado ni madogo sana : katika tafiti nyingine idadi ya vijana wanaoripoti kutumia kondomu wakati wa tendo la kwanza la ngono ni chini ya theluthi moja (THMIS 2007-8).
NI ELIMU NA HUDUMA GANI ZINATOLEWA KWA VIJANA ? Sera za sasa za elimu zinajumuisha Afya ya Jinsia na Uzazi kwa Vijana (ASRH) ikiwa ni pamoja na ufahamu kuhusu VVU & UKIMWI. Hata hivyo, mamlaka husika hazina nyenzo na rasilimali fedha za kutosha kwa ajili ya masuala haya. Baadhi ya huduma za ushauri nasaha, kupima na matunzo kwa wenye UKIMWI zinatolewa lakini hazitoshelezi, na inawezekana watoto na vijana wa rika hawazifahamu au wanasita kuzitumia. Elimu ya VVU & UKIMWI imeingizwa kwenye mtaala wa elimu ya msingi kuanzia mwaka 2000. Kabla ya hapo, Wizara ya Elimu iliweka ilishaanzisha afua za kutekelezwa katika shule za msingi ambazo ni : Ufundishaji wa mada za VVU & UKIMWI darasani ; elimu rika ; huduma za unasihi ; na kuanzisha Kamati ya Unasihi na Elimu ya Kujikinga na UKIMWI ya Shule (KUEKUS) Hata hivyo, ubora wa elimu ya VVU na UKIMWI bado unatofautiana sana. Kwa kutumia masomo chukuzi ; ya Sayansi, Haiba na Michezo, na Uraia, Walimu
4
wa masomo haya wanatakiwa kufundisha mada za VVU na UKIMWI zilizoingizwa katika masomo hayo. Hata hivyo, mara nyingi mambo hayafanyiki hivyo kwa sababu ya kutokuwepo kwa mafunzo maalumu. Mara nyingi, walimu wanasita kuyakabili masuala nyeti ya afya ya uzazi na ujinsia. Utafiti wa awali wa mradi ulionyesha kukosekana kwa walimu, na baadhi yao walilalamika kuwa vifaa vya kufundishia havitoshelezi. Elimu rika ilionyesha kuwa na manufaa fulani lakini, mara nyingi, haifahamiki vizuri. Katika kila shule kuna walimu wanasihi wawili (wa kiume na wa kike) ambao wanaweza kuwaelekeza wanafunzi kwenye huduma za afya endapo zinahitajika. KUEKUS ina jukumu la kuhakikisha jamii inahusishwa na inasaidia katika utekelezaji wa elimu ya UKIMWI shuleni.
48%
ya wanafunzi walisema hawawezi kwenda kwenye huduma ya ushauri na upimaji wa VVU, kwa kuwa wanaogopa majibu mabaya
Takwimu za awali zilionyesha kuwa, katika shule husika, utoaji wa huduma za unasihi hazitoshelezi. Ni 63% tu ya wanafunzi waliohojiwa walikubali kuwa huduma kama hizo zilikuwepo. Katika baadhi ya maeneo, wajumbe wa KUEKUS waliteuliwa bila kupewa mafunzo wala majukumu ya kueleweka, jambo linalowafanya wasiwajibike. Mbali na hayo, idadi kubwa ya wanafunzi (48%) walisema kuwa wasingeweza kwenda kwenye huduma ya ushauri nasaha wa hiari na kupima, kwa sababu ya kuogopa matokeo mabaya. Hivi karibuni, baadhi ya shule za Tanzania zimekuwa zikiwatambulisha wanafunzi wenye UKIMWI kwa kuwavisha utepe mwekundu, kitu kinachoashiria kuwa miongoni mwa walimu na wazazi wana uelewa mdogo kuhusu namna ya kuwahudumia wenye UKIMWI kimwili na kisaikolojia.
SIFA YA MRADI | KUENDANA NA MIFUMO YA KITANZANIA NINI Kwa kutumia miongozo, vitendea kazi, vifaa na wataalamu wa WEMU pamoja na kuongeza ubunifu wa ziada unapohitajika. KWA NINI Wafadhili wa kimataifa, ikiwemo Ubelgiji, wamejitolea kutekeleza Azimio la Paris linalosema kwamba misaada ya maendeleo ni lazima ijikite katika kuimarisha sera na utekelezaji wake. Kwa kutumia njia ya mfungamano (critical alignment), BTC ilifanya kazi na WEMU , kwani Mratibu wa Mradi alitoka ndani ya wizara, badala ya kutengeneza vifaa vipya au kuajiri mtaalamu elekezi kutoka nje, tulifanya kazi ya kuendeleza na kuimarisha vifaa ambavyo tayari vilikuwepo. Kwa mfano, kuimarisha zaidi miongozo ya sera, au kuzihuisha na kuzipa mafunzo KUEKUS zilizowekwa na WEMU. Uzoefu kutoka programu nyingine na nchi nyingine (kama vile kuhakikisha uwepo wa mazingira wezeshi, utumiaji wa sanaa na michezo, kusaidia waelimisha rika) viliongezewa kwenye hazina ya nyenzo na sera za WEMU.
5
HALI HALISI YA MRADI Wizara ya Elimu inatambua haja ya kuelekeza elimu ya VVU & UKIMWI kwa watoto wa umri mdogo kabisa kama ilivyobainishwa kwenye sera za sasa. Hata hivyo, mifumo na rasilimali kwa ajili ya utekelezaji wa sera hizo vinahitaji kuimarishwa ili viwe na ufanisi.
Mradi wa majaribio ulizilenga shule 28 katika wilaya saba za mikoa ya Dar es Salaam, Pwani, Arusha na Kilimanjaro
Mradi wa majaribio uliobuniwa na BTC-Shirika la Maendeleo la Ubelgiji kwa ushirikiano na WEMU ni matokeo ya moja kwa moja ya haja hiyo. Programu ya Kukuza Uelewa wa VVU na UKIMWI inayowalenga watoto na Vijana wa rika balehe katika shule za msingi ililenga kupunguza matatizo yanayohusiana na UKIMWI, afya ya uzazi na ujinsia, na kuwawezesha vijana kujilinda.
Marko Balenovic
6
TUNAANZIA UMRI MDOGO ? MFANO WA PROGRAMU KWA AJILI YA SHULE ZA MSINGI
Watoto wa umri wa elimu ya msingi lazima watazamwe kama kundi lengwa katika masuala yahusuyo uelewa kuhusu VVU & UKIMWI na afya ya uzazi na ujinsia kwa vijana balehe (ASRH). Kwanza kabisa, ni 36% ya wanafunzi wanaendelea na elimu ya sekondari (UNESCO, 2011); hivyo programu zozote zinazohusu elimu lazima zijikite katika ngazi ya elimu ya msingi ili ziwe na ufanisi. Kwa hakika, baadhi ya Watanzania wanahitimu elimu ya msingi wakiwa na umri mkubwa: katika shule zilizohusika na mradi, baadhi ya wanafunzi walikuwa na umri wa miaka 17. Pili, afya ya uzazi na ujinsia kwa vijana balehe haina maana ya kutoa elimu ya ngono au mada za watu wazima kabla ya wakati. Vifaa na mitaala ya WEMU vimeandaliwa mahususi kwa kila rika (kwa mfano, watoto wadogo kabisa hujifunza jinsi ya kuwa wasafi na wenye afya). Elimu rika inatolewa na watoto wa umri mkubwa zaidi (darasa la 5-7) tu.
ROMBO KARATU
BAGAMOYO DAR ES SALAAM
KINONDONI TANDALE
MKURANGA TEMEKE KIWALANI
ILALA
MBAGALA KUU
TAREHE : SEPTEMBA 2009 – DESEMBA 2012
SHULE 28, WILAYA 7 Dar es Salaam > Kinondoni, Ilala & Temeke pwani > Bagamoyo & Mkuranga Arusha > Karatu Kilimanjaro > Rombo
WASHIRIKANI: WIZARA YA AFYA NA USITAWI WA JAMII, OFISI YA WAZIRI MKUU – TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA, WIZARA YA FEDHA NA TACAIDS.
HUTEKELEZWA NA WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI; MAMLAKA YA SERIKALI ZA MITAA
BAJETI EURo 1,606,486
7
TULIFANYA NINI? Katika kila wilaya • Kutoa mafunzo kwa wafanyakazi wa Halmashauri ili kuwajengea uwezo na ari ya kusimamia shughuli zinazoendeshwa ndani ya shule. • Kutoa mafunzo kwa wafanyakazi wa Halmashauri ili wafanye kazi na vijana, na kujenga mfumo wa rufaa ili kuwasaidia vijana wapate huduma rafiki za afya. • Kufanya mapitio ya mihtasari ya masomo ya sayansi, Haiba na Michezo, na Uraia ili kuzibaini mada na mada ndogo za VVU & UKIMWI. • Kuandaa miongozo ya kufundishia na zana za ufuatiliaji na usimamizi. Katika kila shule • Kutoa mafunzo kwa walimu wote juu ya ufahamu kuhusu VVU & UKIMWI na stadi za maisha. • Kuhuisha na kutoa mafunzo kwa KUEKUS. • Kutoa mafunzo kwa walimu wanasihi kuhusu stadi za unasihi VVU na UKIMWI, stadi za maisha na uwezeshaji wa elimu rika. • Kutoa mafunzo kwa walimu, maafisa na wanafunzi kuhusu uelewa wa VVU & UKIMWI kupitia sanaa na michezo. • Kutoa mafunzo kwa wanafunzi ili wawe waelimishaji rika. • Kujenga na kuweka samani katika vyumba vilivyotengwa kwa ajili ya klabu za afya za shule.
MIONGOZO YA ELIMU YA VVU & UKIMWI KATIKA SHULE ZA MSINGI KAMA ILIVYOTOLEWA OKTOBA 2012 Mradi ulilenga kuisaidia Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi katika utekelezaji wa sera zilizopo. Hivyo tuliitumia miongozo ya Wizara na kuiongeza mingine kama ifuatavyo: • Mwongozo wa mafunzo kwa ajili ya Kamati za Unasihi na Elimu ya Kujikinga na UKIMWI za Shule (KUEKUS) • Mwongozo wa mafunzo kwa Walimu wanasihi kuhusu Uwezeshaji wa Elimu rika • Mwongozo wa utoaji wa elimu ya VVU /UKIMWI kwa madara ya 1,2,3,4,5,6 na 7 • Mwongozo wa Mafunzo kwa wawezeshaji wa wawezeshaji (ToT) • Mwongozo wa mafunzo kwa Walimu kuhusu matumizi ya sanaa na michezo katika kutoa elimu ya VVU naUKIMWI.
8
NANI TULIMFIKIA?
28 113
WALIMU WAKUU
ROMBO
WAlimu wanasihi WA SHULE
KARATU
182
WAFANYAKAZI WA WILAYA
476
BAGAMOYO
WAJUMBE WA KUEKUS
DAR ES SALAAM
700 840 879
MKURANGA
WAnaFUNZI WA SANAA NA MICHEZO
WAELIMISHAji RIKA
WALIMU
36,523
WANAFUNZI
WASIoKUSUDIWA MOJA KWA MOJA : WAZAZI, VIJANA NJE YA SHULE, WANAJAMII
9
MAMBO TULIYOJIFUNZA FUNDISHO LA 1 / UMUHIMU WA NJIA SHIRIKISHI INAYOHUSISHA WADAU WENGI • • • •
Mazingira wezeshi ya jumla yanahitajika katika kuwajengea uwezo vijana Mafunzo kwa Mamlaka za Serikali za Mitaa (LGAs) na kamati za shule yanasaidia kuhakikisha umiliki na uendelevu wa mradi Rasilimali vitu, vikiwemo vitabu husaidia kuhakikisha kuwa masuala yanapewa nafasi na umakini unaotakiwa Jitahada zaidi zinahitajika kuhakikisha kuwepo kwa huduma rafiki za afya kwa vijana
Ni katika muktadha upi vijana wanaweza kujifunza vyema zaidi kuhusu elimu ya ujinsia na afya ya uzazi ? Ni mambo gani wanahitaji ili wajisikie wamewezeshwa kujilinda ? Haya yalikuwa ni maswali ya msingi katika kuubuni mradi. Mradi ulilenga kujenga mazingira wezeshi ambayo yanafaa kwa kujifunza, kuelewa na kujisikia kuweza kubadili tabia. Mradi ulijumuisha shughuli mbalimbali za ziada, ndani na nje ya darasa ; lengo lilikuwa kuhakikisha uwepo wa rasilimali na miundombinu ya kutosha na kutafuta njia ya kupata ushiriki na msaada wa watu wazima walio karibu au wanaofanya kazi na watoto.
SIFA YA MRADI | KUJIKITA KATIKA KUJENGA MAZINGIRA WEZESHI Nini Kuhakikisha nyenzo na rasilimali bora zinapatikana. KWA nini Raisilimali watu na vitu zinaimarisha mafunzo. Hivyo, kuwepo kwa vitabu kwa kila mwanafunzi lilikuwa ni sharti muhimu. Jengo maalumu la klabu ya afya lilijengwa katika kila shule ili kuweka mazingira salama kwa ajili ya unasihi na pia kutumika kama muundombinu kwa ajili ya mikutano ya waelimishaji rika na makundi ya sanaa na michezo. Shule zilitakiwa kuandaa ratiba inayojulikana na ya kudumu kwa ajili ya shughuli zote. Mradi huu haukufanya kazi na walimu pekee bali pia ulitoa mafunzo kwa watu wazima wanaofanya kazi na vijana, wakiwemo maafisa afya wa wilaya. Kushirikiana zaidi KUEKUS kulisaidia katika kuhusisha jamii ili kupata msaada wao.
10
Chanzo cha kielelezo na Peter Leonard (2012)
Kifaa cha kutolea habari kilichoandaliwa na mradi.
11
Wajumbe wa KUEKUS walikuwa na nafasi kubwa katika kuhakiksha mradi unamilikiwa na kusaidiwa na wenyeji. Ingawa kamati hizi zilikuwa zimeundwa kabla, mradi uliongeza wajumbe hadi kufikia 17, ili kila kamati iwe na viongozi wawili wa dini (mwislam na mkristo) na wawili wenye UKIMWI (wa kiume na wa kike) pamoja na viongozi wa kijiji, wanafunzi na walimu. Wajumbe walipata mafunzo kuhusu mada za VVU & UKIMWI ; na majukumu yao yamewekwa wazi – kuiunganisha shule na jamii. Matokeo yake ni kwamba kamati hizi zilijihuisha zaidi na utoaji wa elimu, kusaidia kushughulikia dukuduku za baadhi ya wazazi na kuhakikisha kuwa watoto wanajisikia kuwa wanaweza kuwa wazi zaidi katika kuzizungumzia mada nyeti.
17
WANAKAMATI WA KUEKUS KATIKA KILA SHULE
Lengo mojawapo la mradi ilikuwa kuunda mfumo wa rufaa unaowaruhusu vijana kuwaona moja kwa moja wataalamu wa afya ambao pia wamepata mafunzo kuhusu namna ya kufanya kazi na vijana. Hata hivyo, hadi mwishoni mwa 2012, mfumo huu ulikuwa bado haufanyi kazi kama ilivyotarajiwa. Kwa mfano, hata baada ya mafunzo, maafisa wa afya hawakuwa wakizitembelea shule kama ilivyopangwa. Kuboresha mahusiano kati ya wizara husika (Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Wizara ya Afya na Usitawi wa Jamii, Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa) kunaweza kusaidia kuhakikisha upatikanaji wa huduma za afya. Masuala mengine yahusuyo mazingira wezeshi yalikuwa na mafanikio zaidi. Kulikuwa na ripoti za kuwepo kwa msaada wa karibu kwa waelimisha rika. Kulingana na maafisa na wakaguzi wa wilaya, hali haikuwa hivyo katika miradi ya nje ya shule. Njia ya kutumia « masomo ya darasani » iliyoanzishwa na wizara ilionekana kuwa na ufanisi endapo kukiwa na mazingira muafaka na wezezi. Kwa mfano, kuwepo kwa vitabu na nyenzo nyingine za kujifunzia ni kigezo muhimu katika mafunzo. Ilithibitishwa na watathmini wa mradi kuwa vitabu vilivyogawiwa kwa kila mwanafunzi wa darasa la 5-7 vilikuwa vikitumika sana. Kusisitiza
Kupitia vitabu vyake, programu hii imeboresha ufaulu wa wanafunzi wangu. Wanafunzi wangu wana uwezo wa kuelezea vizuri walichokisoma na uelewa wao uko juu sana MWALIMU MKUU, Bagamoyo
uwepo wa vitabu kunatoa ujumbe kwa wanafunzi na walimu kuhusu umuhimu wa somo husika na wakati mwingine imeonekana kukuza utamaduni wa kujisomea na uwezo wa kuelewa. Ujenzi wa vyumba kwa ajili ya vyama vya afya katika kila shule pia umekuwa na manufaa makubwa. Mmoja wa walimu wakuu wa Mkuranga alisema, “Wanajamii wanaiona programu hii ni makini kwa sababu ina ofisi”. Vyama vya afya ambavyo pia vinapokea wanachama kutoka nje ya shule vimewavutia sana wanajamii ambao sasa wanakuja kwa hiari kupata huduma. 12
Mwisho, mbinu chanya na ya wazi dhidi ya VVU & UKIMWI ambayo imechangiwa na shughuli nyingine zote za mradi imeboresha mitazamo kuhusu waathirika wa ugonjwa huu, katika baadhi ya maeneo. Mbali na kupungua kwa unyanyapaa dhidi ya wanaoishi na VVU na UKIMWI, shule ziko mstari wa mbele zaidi katika kuwasaidia wanafunzi. Kwa mfano, wanaweza kuwataka wazazi/walezi wa watoto waathirika kuwajulisha walimu hali yao ya afya ili waweze kuwasaidia kusimamia matumizi ya dawa, kuwapa kazi nyepesi na kuwapa chakula kwa wakati.
FUNDISHO LA 2 | KUWA MAKINI KUNACHANGIA KUONGEZA MAARIFA, UJASIRI NA MABADILIKO YA TABIA • • •
Utafiti unaonyesha kuwa mradi ulisababisha mabadiliko chanya ya tabia miongoni mwa wanafunzi. Uelewa halisi hutokana na mafunzo ya kueleweka na endel evu ambayo yanawahusisha wadau wote. Walengwa wasiokusudiwa wameripoti pia kuongezeka kwa uelewa na mabadiliko ya tabia
Ni kwa namna gani tunaweza kuhakikisha uelewa thabiti wa HIV & UKIMWI na masuala yahusuyo gonjwa hili miongoni mwa wanafunzi na watu wazima? Wakati sera ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi yamekuwa ni kutoa mafunzo kwa idadi ndogo tu ya walimu katika kila shule, mradi ulisisitiza kuwepo kwa programu ya mafunzo inayowajumuisha walimu wote na maafisa afya na elimu katika kufanya kazi na vijana. Pia, mafunzo yalikuwa endelevu. Kwa mfano, walimu, walezi wa wanafunzi shuleni na wanasihi walihudhuria vipindi vya mafunzo kuhusu VVU na UKIMWI na Afya uzazi na ya ujinsia kwa Vijana katika mwaka wa pili na wa tatu wa mradi. Jambo la kufurahisha ni kuwa, pamoja mafunzo kuwa ya muda mrefu, hapakujitokeza tatizo la muda. Badala yake, mafunzo haya yaliongeza ari kwa wanafunzi na kuhakikisha uwepo wa wataalamu mbalimbali katika kila shule. Hali hii ilileta manufaa makubwa kwenye ubora wa ufundishaji na mafunzo kwa ujumla. Mwanzoni, nilikuwa na uelewa mdogo kuhusu ugonjwa huu na nilikuwa nafundisha bila ujasiri. Nilikuwa nikitumia uelewa wa jumla, nilioupata chuoni lakini baada ya mfululizo wa mafunzo haya, ninaweza kusema kuwa mimi ni mtaalamu wa VVU & UKIMWI … ndivyo ilivyo kwa wanafunzi… ninawaambieni kuwa wana ufahamu na ujasiri. Wanaweza kusimama mbele ya kadamnasi ya watu na kuzungumza kuhusu VVU na UKIMWI na mkashangaa MWALIMU, Bagamoyo
13
SIFA YA MRADI | / MBINU YA KUTOA MAFUNZO YA KINA NINI Kutoa mafunzo ya kina kwa kutumia njia shirikishi kwa walimu wote, wakiwemo walimu wakuu; wanasihi kadhaa, waratibu elimu kata, mafunzo kwa wafanyakazi wa halmashauri, wakaguzi wa shule na waelimishaji rika. KWA NINI Katika miongozo iliyopo ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, mafunzo ya Elimu ya UKIMWI yametolewa kwa walimu wachache tu na kuna wanasihi wawili tu kwa kila shule. Mradi huu ulitambua umuhimu wa walimu wote kuwa na uelewa na ujasiri wa kufundisha mada zinazohusu Afya ya Uzazi na ujinsia kwa Vijana; na kuwashirikisha pia walimu wakuu ili waunge mkono shughuli za mradi. Kozi za kunoa ubongo inahitajika kwa ajili ya uendelevu wa mradi na kulikabili tatizo la mabadiliko ya wafanyakazi. Utoaji wa mafunzo kwa maafisa wa wilaya wenye dhima ya kupanga na kusimamia sera za elimu ni muhimu katika kujenga mazingira wezeshi, kwa ajili ya kuzuia maambukizi na kutoa huduma kwa waathirika, na kuhakikisha wanatekeleza majukumu yao kwa umakini. Ingawa tulikuwa tunafundisha kuhusu VVU na UKIMWI kabla ya mradi, hatukuwa na ufanisi kwa sababu ya kutokulifahamu vizuri somo hili, na tulikuwa tukijisikia aibu kuwaambia wanafunzi masuala haya. MWALIMU, ROMBO
Walimu walipata ujasiri zaidi wa kuzungumzia VVU na UKIMWI na Afya ya uzazi na ujinsia na Uzazi kwa Vijana, na wameeleza kuwa sasa wanaweza kuyazungumzia masuala haya bila shida; jambo ambalo ni nadra kwa shule ambazo hazipo kwenye mradi. Kuwepo kwa ratiba maalamu kunasaidia kuleta umakini wa kutosha katika masuala ya kukuza uelewa. Mmoja wa maafisa kutoka wilayani anaeleza: “Programu hii inaonekana kuwa makini kwa sababu inaitaka shule kuweka ratiba inayoonyesha siku za mafunzo kwa wanafunzi”. Kwa mfano, siku moja katika juma inaweza kutumika kwa ajili ya waelimishaji rika na nyingine kwa ajili ya maonyesho ya vikundi vya sanaa na michezo. Umakini mkubwa unaowekwa kwenye elimu ya VVU & UKIMWI una manufaa katika masuala mbalimbali yanayoambatana na elimu hiyo. Kuzuia na kuukabili ugonjwa huu kunahitaji stadi za maisha ambazo pia zinashabihiana na masuala mengine ya maisha ya ujana: afya ya jinsia kwa ujumla, kubalehe / kuvunja ungo, kuwajibika, kusimamia haki, na kadhalika. Kutokana na elimu hii, tumejifunza kuheshimu via vyetu vya uzazi … tumefundishwa kwamba, katika umri huu tukiwa shuleni, tunatakiwa kutumia via vyetu vya uzazi kwa ajili ya kujisaidia tu na si vinginevyo … kwa sababu tukivitumia vinginevyo, tunaweza kupata mimba, virusi vya UKIMWI au magonjwa mengine ya ngono. MWELIMISHA RIKA, Bagamoyo
14
Majibu ya wanafunzi kwa maswali ya kujieleza yanaonyesha kuwa mbinu za kueleweka zilizoelezwa hapo juu zimekuwa na matokeo mazuri katika kukuza uelewa mahsusi miongoni mwa wanafunzi. Uelewa huo unajumuisha kujikinga na virusi vya UKIMWI na magonjwa mengine ya ngono kwa jumla na stadi za maisha. Haishangazi kuwa ufahamu huu unaendana na kuongezeka kwa ujasiri unaojidhirisha katika namna watoto na vijana wadogo wanavyozungumzia masuala kama hayo. Inaonekana kuwa ufahamu walionao wanafunzi umewawezesha zaidi kutambua mazingira hatarishi na kuwapa nguvu ya kutosha kuyaepuka. Kwa mfano, tathmini ya mwisho ya mradi ilionyesha kuwa katika wilaya ya Rombo, Afisa Elimu wa wilaya hajawahi kusikia msichana yeyote amepewa ujauzito, tangu kuanza kwa mradi katika shule nne pamoja na yeye binafsi kuulizia kuhusu suala hili. Pia katika mijadala ya vikundi, walimu wa Rombo walisema kwamba hawajamwona msichana yeyote akipata ujauzito tangu kuanza kwa mradi mwaka 2009. Kadhalika, walimu wakuu wa Karatu na Mkuranga waliripoti kupungua kwa mimba katika shule zao. Haya yanathibitishwa na majibu ya wanafunzi wenyewe kuhusu tabia zao.
Siku hizi mtu akiniambia njoo nikupe pesa au lifti, ninamjibu “Subiri kidogo nikavae nguo”, halafu sirudi tena mwanafunzi, Rombo
“MMEJIFUNZA NINI KUTOKANA NA MRADI HUU?” (Idadi ya Sampuli = 776) Majibu ya papo kwa papo
Jumla % (N=776)
Me % (N=370)
Ke% (N=388)
Jinsi ya kujilinda
34.9
38.9
32.2
Kuepuka vishawishi
33.8
33.8
34.3
Kuacha unyanyapaa
24.6
26.2
23.2
Uelewa wa magonjwa ya zinaa
15.7
15.9
15.7
Kuepuka tabia hatarishi
15.2
14.6
21.4
UKIMWI
14.8
12.2
17.8
Epuka mashugar mammy /dadi
13.8
14.6
12.9
Kuacha ngono
8.9
7.6
10.3
Ujasiri na kujiamini
8.4
9.5
7.7
Kuepuka utoro & makundi hatarishi
5.9
8.1
3.9
Kuepuka mimba & ndoa za utotoni
5.5
5.1
6.2
Kuepuka kutembea usiku
4.8
3.2
6.4
Kuepuka pombe & madawa ya kulevya
3.6
3.8
3.6
Stadi za maisha
3.2
4.1
2.6
Afya ya Uzazi
2.7
3.8
1.5 15
Katika kipindi cha nyuma, wanafunzi wengi walikuwa wamezoea kwenda kwenye ngoma za utamaduni za usiku…………tatizo ni kwamba walipokwenda kule walikutana na watu wengine toka kijijini ambao waliwashawishi na kuwaingiza katika kufanya ngono…….wakati mwingine, mabinti wadogo wanabakwa na watu wazima hasa wakiwa wamelewa. Lakini baada ya elimu hi,i tunashukuru kwamba wengi wameelimika na hawaendi tena MWELIMISHA RIKA, mkuranga
“JE, UELEWA ULIOUPATA UMEBADILISHA TABIA YAKO?” (Idadi ya sampuli=776) Mabadiliko ya tabia
Idadi
Asilimia
752
96.91
13
1.68
Hakuna jibu
3
0.39
Sijui
8
1.03
776
100
Ndiyo Hapana
Jumla
“NI TABIA GANI ULIYOBADILISHA?” (Namba ya sampuli =776) Aina ya mabadiliko
Waliotaja %
Wasiotaja %
Kuacha ngono
46.5
53.5
Kuchelewa kuanza ngono
58.9
41.1
Kufanya ngono na mpenzi mmoja
1.9
98.1
Kutumia kinga
0.8
99.2
Kuepuka ngoma za usiku
7.7
92.3
Baada ya mafunzo, nilitambua kwamba UKIMWI ni kama ugonjwa mwingine wowote …….kwahiyo, nilianza kuwaelimisha wengine, hasa nilipowakuta wamekaa katika vijiwe bila kazi ambako mara nyingi wanauliza maswali.”
Ufahamu na ujasiri ulioonyeshwa na walimu pamoja na wanafunzi uko dhahiri pia katika jamii nje ya shule.Kwa mfano, watu waishio na virusi waliohojiwa walisema wako na ujasiri kuhusu hali zao; unyanyapaa na kutengwa sio tatizo kubwa. Kama anavyoeleza mwanamke mmoja wa Mkuranga, mjumbe wa KUEKUS “Baada ya kujihusisha katika kamati hii, tulipata mafunzo juu ya VVU na UKIMWI. Nilishawishika kwamba watu wengine wanapaswa kufahamu kuhusu hali yangu, kwamba nimeathirika na VVU. Awali, nilikuwa naogopa kufanya hivyo, lakini baada ya mafunzo, nimejua kwamba huu ni ugonjwa kama ugonjwa mwingine wowote.”
KIJANA WA KIKE AISHIYE NA VVU mkuranga
Wajumbe wa KUEKUS ambao ni viongozi wa dini pia waliona tofauti, kama mmoja wao kutoka Karatu alivyoeleza: “Ilikuwa ngumu kuzungumzia VVU na UKIMWI hadharani, hasa kwetu sisi waislamu. Lakini baada ya kuhudhuria mafunzo, kwa uhakika tumepata nguvu ya kuongea na watu wetu.”
16
FUNDISHO LA 3 | UBUNIFU, MBINU SHIRIKISHI ZA UFUNDISHAJI KUNA FANYA UJUZI KUWA WA KUFAA ZAIDI • Shughuli za Sanaa na michezo zinawawezesha vijana wadogo kugundua na kujihusisha na mada za afya ya uzazi kwa kujiamini zaidi • Ubunifu na mbinu shirikishi unaweza kuchangia kukuza/kuimari sha mahudhurio Kuwafundisha vijana wadogo kuhusu maswala ya afya ya uzazi na ujinsia kupitia maonesho ya kisanaa imeonesha kuwa njia ya kufaa kurudisha heshima ya wasomaji na kuboresha utambuzi wa haki zao ( Bosmans et al., 2012). Mradi uliongeza njia shirikishi kupitia sanaa na michezo kwenye hazina ya programu za elimu UKIMWI ya Wizarani. Hii ilijumuisha kuwaongoza wanafunzi kufanya utafiti kuhusu matatizo yao ya afya ya uzazi na ujinsia, kuyachambua na kupendekeza njia za utatuzi. Kwa kutumia maigizo, michezo au muziki, wanafunzi wanaweza kujielezea kwa uhuru katika mada nyeti, hata katika hadhara. Kupitia maonesho wanayoyaandaa, vijana huishirikisha pia hadhirawakiwauliza kupendekeza masuluhisho kwa walichokiona. Hii inamaanisha kuwa ujumbe wao huwafikia pia wazazi, majirani na vijana nje ya shule.
Kwa sababu wanafunzi wanapenda maigizo watakuja mara zote shule na hawatapenda kukosa vipindi – kwa sababu pia watakosa maigizo. MWELIMISHAJI RIKA, Temeke
Kwa mbinu hizi za ufundishaji, wanafunzi wanajifunza kwa haraka; wanajihusisha na majadiliano kuhusu VVU & UKIMWI kwa sababu wanasawiri kinachotokea hasa katika jamii.
SIFA YA MRADI | KWA KUTUMIA SANAA NA MICHEZO NINI Kutumia sanaa na michezo kufikisha ujumbe wa afya ya uzazi kwa vijana balehe. KWA NINI Miiko ya kiutamaduni inayoendelea kuwepo inaleta ugumu wa kujadili kwa uwazi mada nyeti kama kufanya ngono , lakini kwa kutumia maigizo au nyimbo walimu na wanafunzi wanaweza kujieleza. Mbinu shirikishi za kujifunza zinawawezesha vijana wadogo kuchukua nafasi za kuongoza – na wanafunzi wadogo wanalifurahia somo. Kama ilivyo miongozo ya sanaa na michezo, elimu rika (kwa darasa la 5-7 pekee) pia inawapa wanafunzi nafasi ya msingi katika mchakato wa mafunzo. Waelimishaji rika wa kike na wa kiume katika kila mkondo wanachaguliwa na wanadarasa na kupewa mafunzo na walimu wanasihi. Halafu, waelimishaji rika hao wanaandaa vipindi wanavyowezesha mara kwa mara kwa wenzao kwa
17
Mradi huu umekuwa na manufaa ya aina mbili. Kwanza, umewapa uwezo wa kupambana na VVU & UKIMWI bila woga. Pili, umewapa uwezo wa kujibu / kujieleza vizuri na kwa usahihi katika masomo mengine ya taaluma MWALIMU MKUU, Bagamoyo
kutumia nyenzo wanazopewa na mwongozo wa wanasihi. Ujasiri waliouonyesha tangu kuanza kwa mradi (Mmoja wa wahojiwa wa Karatu alisema “Sasa tunaweza kuzungumza na mtu yeyote kwa uwazi kuhusu ugonjwa hili”) unaambatana na utayari wa kutaka kuwashirikisha wengine walichojifunza ndani na nje ya shule. Mmoja wa walimu wakuu Rombo alisema: “Waelishaji rika wetu wamekuwa na uwezo wa kuwaelimisha wengine”. Pia utumiaji wa mbinu hizi unaonekana kuwa umechangia kuongeza mahudhurio, kwani wanafunzi wana ari zaidi ya kuhudhuria madarasa hayo na hivyo hawawezi kukosa shule. Maafisa elimu wa wilaya na walimu wakuu wameripoti kuwa kiwango cha utoro kimeshuka katika shule zilizohusika na mradi katika wilaya saba. Kupungua kwa idadi ya wanafunzi wanaoacha shule kutokana na mimba za utotoni kumeboresha mahudhurio; na hii inaweza kuwa ni sababu ya kuongezeka kwa ufaulu. Kama ilivyoripotiwa na Afisa Elimu wa Wilaya ya Rombo na Mkaguzi wa Shule wa Wilaya ya Kinondoni, kiwango cha ufaulu kimeongezeka katika shule lengwa, tangu kuanza kwa mradi. Maoni kama hayo yalitolewa pia na walimu wakuu wa Shule ya Msingi Kwangao (Shule yenye ufaulu wa juu zaidi Wilayani Rombo) na Shule ya Msingi ya Hekima (moja ya shule zenye ufaulu wa juu zaidi wilayani Kinondoni) na walimu wengine mbali mbali.
18
HITIMISHO HATA WATOTO WA UMRI WA SHULE YA MSINGI WANAWEZA KUWA CHANZO CHA MABADILIKO Tathmini ya mwisho ya mradi ya mwaka 2012 inathibitisha kuwa matokeo yaliyoshuhudiwa katika baadhi ya shule yanaonyesha hali ilivyo katika takribani shule zote zilizohusika. Katika kila wilaya, shule zilizohusishwa katika mradi zilionyesha mabadiliko chanya yanayozitofautisha na shule nyingine.
Wazazi wengi wamekuwa na utayari zaidi kupimwa. MWALIMU, MKURANGA
Mafunzo ya kina yaliyotolewa katika mazingira wezeshi, yameonyesha mafanikio katika kuongeza ufahamu na ujasiri katika kuchangia mabadiliko ya tabia na katika kuwahusisha vijana na wale wanaofanya kazi nao ili kukabiliana na VVU & UKIMWI, kwa uwazi na ujasiri zaidi. Pia programu hii imeonyesha kuchangia katika kuboresha mahudhurio na ufaulu. Chanzo cha mabadiliko haya ni wanafunzi waliohamasika. Kuongezeka kwa ujasiri wa wanafunzi katika kuvikabili VVU na UKIMWI kumeshuhudiwa mara kwa mara na walimu na wafanyakazi wa serikali. Wakati wa kazi za darasani na nje ya darasa, vijana wanazungumza kwa uwazi na wanaweza kujieleza. Namna ambavyo wanafunzi walizungumza kuhusu hali ya maisha, katika tathmini yetu, ni ishara ya ukomavu na ujasiri walioujenga na unaowasaidia kuepuka tabia na mazingira hatarishi. Uwezeshaji wa aina hii unadhihirika hasa kwa wasichana wanaoonekana kumudu vyema majukumu yao kama waelimishaji rika. Mbali na wanafunzi kuonyesha uwezo wa kubadili tabia zao, wamedhihirisha kuwa wanao pia uwezo wa kuwaeleza na kuwashawishi wengine kufanya kama wao. Wajumbe wa KUEKUS walieleza kuwa wanafunzi kutoka shule zilizohusika na mradi, hasa wale waliopata mafunzo ya uelimishaji rika, huwashirkisha ndugu zao na hata wazazi wao walichojifunza. Pia wazazi na majirani hujifunza kupitia maonyesho shuleni na tafiti ambazo wanafunzi wanahamasishwa kuzifanya katika jamii zao. Matokeo yake ni mabadiliko ya tabia kwa watu wazima, kwa mfano, katika kutumia vyumba vya vyama vya afya na kuamua kupima VVU. Kujadili mada za Afya ya uzazi na ujinsia kwa Vijana na VVU na UKIMWI bado kuna ugumu, katika umri mdogo. Walimu wameripoti kuwa baadhi ya wazazi wamekuwa wakilalamika kuwa watoto wao wanafundishwa mambo yasiyoendana na umri wao. Hata hivyo, malalamiko yao yanaonesha uelewa finyu na siyo kuikataa elimu kama hiyo. Mmoja wa walimu wakuu kutoka Bagamoyo alisema: “Tuliwaeleza (wazazi) kuhusu programu hii na umuhimu wake. Mwishoni walielewa na hata wanafunzi wanatueleza kuwa, sasa wazazi wao, wanaweza kuuzungumzia ugonjwa huu kwa uwazi�
Pia wazazi wameelimika kuhusu shughuli za usiku na wamegundua kuwa si nzuri kwa watoto wao MWALIMUw, mkuranga
19
Ujumbe umetolewa na mradi. Chanzo cha kielelezo na Peter Leonard (2012)
NI JUKUMU LETU WAZAZI KUZUNGUMZA NA WATOTO WETU JUU YA AFYA YA UZAZI NA UKIMWI
20
KUTOKA KWENYE MAJARIBIO KUELEKEA KWENYE SERA: HATUA ZINAZOFUATA Mradi huu umethibitisha uwezo wa vijana kubadilisha desturi hasi na kuleta mabadiliko ya tabia. Mwanzoni, sikuwa nimeshawishika kuhusu mbinu hii, bali sasa nimeona ufanisi wake. Lakini kama mradi hautaendelea, manufaa haya yatapotea baada ya muda. Kila kizazi kipya kinastahili kupata kile ambacho mradi umetoa kuhusu afya ya jinsia na uzazi kwa vijana na ninashauri kuwa waandaaji wa sera wa Tanzania watafute namna ya kuuendeleza mradi huu. DR. BENNET FIMBO, BINGWA WA ELIMU NA UKUZAJI WA AFYA. MWANDISHI WA TATHMINI YA MWISHO YA MRADI
Waandaaji wa sera, wakiwemo viongozi wa juu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi na wale wa Tume ya Taifa ya kudhibiti UKIMWI Tanzania ambayo inaratibu mwitikio wa kitaifa dhidi ya VVU na UKIMWI, wapo tayari kusaidia ili mradi uendelee. Pia wengi wa waliohusika katika mradi wameonyesha utayari wa kusaidia maendeleo na upanuzi wa mradi. Kwa mfano, walimu wa Temeke wametumia njia zao wenyewe kutoa mafunzo yasiyo rasmi kwa walimu wa shule za karibu ambazo hazikuhusishwa katika mradi. Pia wafanyakazi wa wilaya wanasema wanatumaini mradi utaendelea. Hata hivyo, shughuli za mradi haziwezi kupanuliwa wala kuendelezwa kwa muda mrefu bila uwepo wa rasilimali endelevu. Wakati mradi ukikaribia mwisho, timu ya mradi inajitahidi kuhakikisha mambo mazuri ya mradi yanaendelezwa na mradi wenyewe unapanuliwa kuzifikia shule zaidi ya zile 28 za mradi wa majaribio. Moja ya mafanikio ya mradi hadi sasa ni kukubaliwa na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kwa nyenzo na miongozo iliyoandaliwa na mradi (kwa mfano, Mwongozo wa Mafunzo kwa Walimu katika Matumizi ya Sanaa na Michezo katika kutoa elimu ya VVU na UKIMWI)
Nitajaribu kuzihamasisha Mamlaka za Serikali za Mitaa kutenga rasilimali kutoka bajeti ya Halimashauri ili mradi uendelee hata baada ya udhamini wa BTC kwisha AFISA ELIMU WA WILAYA, KARATU
21
Tume ya Taifa ya Ukimwi haiwezi kukamilika bila kuwahusisha watoto wa umri wa shule ya msingi. Katika umri huu, wana uwezekano mkubwa wa kujenga uelewa na maarifa yanayohitajika kuzuia sababu hatarishi na kuwashawishi wengine kuiga: wao ndiyo sababu ya mabadiliko na watu wa kuigwa. Nilipoangalia maonyesho yao mazuri, nilifurahishwa sana kwani wanonyesha uwezo na ujasiri katika kile wanachokifanya. Kuupanua mradi huu hadi ngazi ya kitaifa kutahitaji uwekezaji mkubwa lakini naamini itakuwa ni matumizi mazuri ya fedha, na ninaunga mkono uwekezaji huo MORRIS LEKULE, TACAIDS mjumbe wa kamati ya ushauri ya mradi
22
1. KUTUMIA VIZURI KASI NA ARI YA SASA •
Kuwahusisha wadau wa mradi katika majadiliano kuhusu hatua zitakazofuata na kuendelea kufanya kazi na washirika (ikiwemo Tume ya Kuthibiti Ukimwi Tanzania -TACAIDS) na taasisi husika za Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi (Vikundi vya Kiufundi Vinavyohusisha wadau mbalimbali) ili kuandaa mpango kazi wa kueleweka.
•
Kuongeza matumizi na uzalishaji wa nyenzo na miongozo inayotumiwa na kuandaliwa na mradi.
•
Kushirikishana uzoefu wa mradi miongoni mwa wadau ndani na nje ya Tanzania.
2. UPANUZI WA MRADI KUZIFIKIA SHULE NYINGI ZAIDI KWA KUINGIZA MAMBO MAZURI KATIKA SERA YA TAIFA •
Kuwepo kwa majadiliano ya wazi na waundaji wa sera na mamlaka husika (k.m. Taasisi ya Elimu Tanzania) kuhusu kuyaingiza mambo mazuri ya mradi kwenye sera na miongozo ya taifa. Mahali pa kuanzia panatakiwa kuwa Mpango unaokuja wa Maendeleo ya Elimu ya Msingi na Mkakati wa Taifa wa Sekta mbalimbali wa Kuzuia VVU.
3. KUTAFUTA VYANZO NA NJIA MPYA ZA UFADHILI •
Kutokana na maelewano baina ya wafadhili, Ubelgiji inatoa misaada yake kwa sekta mbili tu (usimamizi wa maliasili na maboresho ya serikali za mitaa). Kwisha kwa mradi wa sasa ndio utakuwa mwisho wa misaada ya Ubelgiji kwenye sekta ya Elimu, na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi itatakiwa kutafuta misaada mahali pengine kwa ajili ya upanuzi wa mradi. Tanzania imeendelea kutegemea ufadhili wa nje katika shughuli za VVU & UKIMWI. 97% ya gharama zote hutoka kwa wafadhili. Kutokana na kupungua kwa misaada ya VVU & UKIMWI kimataifa, kutakuwa na changamoto kubwa. Wizara italazimika kufanya yafuatayo:
•
Kutafuta wafadhili wengine na / au washirika binafsi.
•
Kubuni mbinu mpya za kupunguza gharama bila kupunguza manufaa ya mradi. Kwa mfano, inawezekana kuwatumia walimu waliopata mafunzo katika shule zilizohusika na mradi kutoa mafunzo kwa wengine katika wilaya zao na kuangalia pia uwezekano wa walimu hao kutoa elimu ya VVU kwenye vyuo vya walimu.
4. KUSIMAMIA UTEKELEZAJI NA KUHAKIKISHA MRADI UNAENDELEA KWA MUDA MREFU •
Kuhakikisha kuwa dhamana ya elimu ya ukimwi kupitia shule za msingi inapewa kwa taasisi yenye uwezo wa kusimamia utekelezaji kwa ufanisi. Kwa sasa, TACAIDS (Tume ya kudhibiti UKIMWI ya Taifa) na Wizara ya Elimu ndio wanaosimamia.
•
Kutegemea na kutumia shughuli zitakazofuata katika kuendelea kuboresha mpango huu.
•
Kuendelea kushirikishana na kubadilishana uzoefu na wadau nje ya Tanzania.
•
Kuendelea kusimamia malengo kuhusu VVU na UKIMWI katika mipango ya maendeleo ya taifa ya muda mrefu na wa kati.
23
MAELEZO Mafunzo yaliyoelezwa katika kijitabu hiki yanatokana na tathmini huru iliyofanywa kwa kutumia dodoso, hojaji na mijadala ya vikundi mwezi Julai 2012. Wafanya tathmini, walizitembelea shule mbili katika kila wilaya 2saba zilizohusika na mradi na kuwahoji jumla ya wanafunzi 776 (darasa la 5-7 wa umri kati ya miaka 11-17). Katika shule hizo 14, mwenyekiti wa KUEKUS, viongozi wa dini ambao ni wajumbe wa KUEKUS, walimu na waelimishaji rika walihojiwa pia. Walimu wakuu 26, kutoka shule 28 walihojiwa. Ingawa shule zisizohusika na mradi hazikulengwa na tathmini hii, maofisa wa wilaya walithibitisha kuwepo kwa “tofauti kubwa sana” kati ya shule zilizohusika na zile ambazo hazikuhusika kwenye mradi katika wilaya zao. Katika ngazi ya serikali za mitaa, Maafisa wote wa Elimu Wilaya, Wakaguzi wa Shule, Waratibu wa Elimu Kata, Waratibu wa VVU na UKIMWI wa Halmashauri na Watu Husika katika Wilaya walihojiwa. Kwenye ngazi ya taifa, taasisi zifuatazo zilihusishwa: Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, BTC, Tume ya UKIMWI ya Taifa, na Wizara ya Afya na Usitawi wa Jamii kupitia Mpango wa Taifa wa Kudhibiti UKIMWI na Kitengo cha Elimu ya Uzazi. Ripoti kamili ya tathmini (Dr Bennet Fimbo, “Mafunzo na Mambo Mazuri Kutoka kwenye Programu ya Elimu ya VVU & UKIMWI”, Augusti 2012) inapatikana kwa kutuma maombi Wizara ya Elimu.
VYANZO VINGINE
• • • • • • • • • •
24
R.W Chediel and A.S Rajabu, Project Baseline report: ‘HIV-AIDS Awareness Creation Programme: A Programme Targeting Youths and Adolescents in Primary Schools’. April 2011 (Data gathered 2010-11). Bosmans M., F. Gonzalez, E. Brems & M. Temmerman (2012), ‘Dignity and the right of internally displaced adolescents in Colombia to sexual and reproductive health’ in Disasters. October 2012; 36(4):617-34. MoEVT, Basic Education Statistics in Tanzania (BEST) 2011-2. TACAIDS, ‘National Multisectoral HIV Prevention Strategy 2009-2012’. November 2009. TACAIDS, ‘National HIV and AIDS Response Report 2010 for Tanzania Mainland’. August 2011. ‘Tanzania Demographic and Health Survey 2010’ (TDHS), National Bureau of Statistics and ICF Macro. 2011. ‘Tanzania HIV/AIDS and Malaria Indicator Survey 2007-08’ (THMIS).TACAIDS, ZAC, NBS, OCGS, and Macro International Inc. 2008. UNESCO, ‘Global Education Digest 2011: Comparing Education Statistics Across the World’. 2011. UNA IDS, UNE SCO, UN ICEF, UN FPA and WHO, ‘Children and AIDS: Fifth Stocktaking Report 2010’. November 2010.
Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi
Ministry of Education and Vocational Training Kivukoni Front, P.O Box 9121, Dar es Salaam (+255) 022 2122 373 psmoevt@moe.go.tz www.moe.go.tz
BTC (Shirika la Maendeleo la Ubelgiji) ni wakala wa Utekelezaji wa mipango ya Maendeleo ya serikali ya Ubelgiji. Ubelgiji inafadhili miradi zaidi ya 300 katika nchi 20 katika Afrika, Asia, na nchi za Amerika ya kusini.
BTC Tanzania, PO BOX 23209, Dar es Salaam (+255) 022 266 8050 representation.tan@btcctb.org www.btcctb.orG