National Housing Corporation (NHC) Newsletter

Page 1

NYUMBA NEWSLETTER JARI DA LA S HI R I K A L A N Y U MB A L A TA I FA julAi - dEsemba 2014

>>

Rais Kikwete afungua nyumba za gharama nafuu

>>

Waziri Mkuu Pinda apongeza mpango wa NHC >>

Waziri Tibaijuka azindua Bodi mpya ya NHC

>> www.nhctz.com

TUNAJENGA TAIFA LETU

NHC yaimarisha utendaji, Uendeshaji na udhibiti 1

JULAI - DESEMBA 2014

/Nyumba Newsletter


Nyumba Newsletter/JULAI - DESEMBA 2014

2

www.nhctz.com


Karibu nhc

Yaliyomo

Page NYUMBA NEWSLETTER

3

Tahariri

2

Rais Kikwete afungua nyumba za gharama nafuu

3

Waziri Mkuu Pinda apongeza mpango wa NHC

4

Waziri Tibaijuka aizindua Bodi mpya ya NHC

5

Serikali yawahakikishia wawekezaji mazingira bora

7

nhc yaajiri wafanyakazi wapya 100

9

Jarida hili hutolewa na Shirika la Nyumba la Taifa mara mbili kwa mwaka Julai - Desemba 2014 ISSN NA. 0856-8510 BODI YA UHARIRI Mwenyekiti Nehemiah Kyando Mchechu Mhariri Mkuu Susan Omari

Wabunge watembelea Uturuki

10

Viongozi wa Shirika na Wizara wazuru Singapore

12

NHC yavutia wawekezaji nchini Dubai

12

Habari katika picha

17

NHC yafanikiwa katika utekelezaji mpango mkakati

17

Wastaafu utumishi NHC

20

Mhariri Habari Muungano K. Saguya Yahya Charahani Msanifu Kurasa Arnold Njuki Mchapishaji Iprint Ltd ANUANI S.L.P 2977, Dar es Salaam. Simu: +255 22 2105002, Baruapepe: dg@nhctz.com, Tovuti: www.nhctz.com. WATAYARISHAJI

Page

Limesanifiwa na Kutayarisha na: SHIRIKA LA NYUMBA LA TAIFA www.nhctz.com

Page

16

6 1

JULAI - DESEMBA 2014

/Nyumba Newsletter


TAHARIRI

Rais Dr. Jakaya Kikwete na aliyekuwa Mkuu wa mkoa wa Tanga Mh. Chiku Galawa pamoja na Kaimu Mkurugenzi wa shirika la Nyumba NHC Bw. Felix Maagi wakikata utepe kwa pamoja kama ishara ya uzinduzi wa mradi wa nyumba za gharama nafuu Mkinga Tanga.

TUNAUNGA MKONO AGIZO LA RAIS KIKWETE KWA HALMASHAURI

K

atika nyakati tofauti wakati akifungua nyumba za gharama nafuu zilizojengwa na NHC katika Halmashauri mbalimbali za Wilaya nchini, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk.Jakaya Mrisho Kikwete aliziagiza halmashauri zote nchini kutenga maeneo ya ardhi kwa ajili ya kulipatia Shirika la Nyumba la Taifa na taasisi zingine zinazojishughulisha na uendelezaji miliki, ili kuwezesha ujenzi wa nyumba za gharama nafuu. Rais Kikwete alitoa agizo hilo baada ya kufungua miradi ya nyumba za gharama nafuu zilizojengwa na NHC katika maeneo ya Mkinga- Tanga, Mkuzo-Ruvuma na Mnyakongo Kongwa. NHC inayo miradi ya aina hii katika Halmashauri kadhaa katika mikoa 19 hivi sasa. “jukumu la kila halmashauri sasa ni kuhakikisha inatenga ardhi ya kutosha na kulipatia shirika bila gharama yoyote kwa ajili ya kukamilisha azma yake hii njema ya kujenga nyumba za gharama nafuu�. Sisi Nyumba Newsletter, tunaunga mkono

Nyumba Newsletter/JULAI - DESEMBA 2014

na kupongeza kwa dhati agizo hilo la Rais Kikwete kwani limeangalia hali halisi na kuona umuhimu wa halmashauri kutenga maeneo kwa ajili ya kujenga nyumba za gharama nafuu. Kwa kufanya hivyo siyo tu kutasaidia wananchi wengi kupata makazi bora kwa gharama nafuu, bali kutaboresha pia mandhari ya miji yetu na kupunguza kasi ya makazi holela ambayo inakuwa siku hadi siku kutokana na idadi ya watu wanaohamia mijini kuongezeka kwa kasi. Aidha, ni Halmashauri hizi hizi zitakazonufaika na kupata kodi mbalimbali kutokana na uwekezaji utakaofanywa katika Halmashauri zao na waendelezaji Miliki. Kadhalika, kuwepo kwa nyumba katika Halmashauri hizo kutawawezesha watumishi wa Halmashauri hizo kupata nyumba na hivyo kupunguza hali ya watumishi kukimbia baadhi ya maeneo ya nchi kutokana na kukosa nyumba za kuishi.

watatekeleza agizo hilo la Mheshimiwa Rais kwa kuwa lina maslahi mapana kwa watanzania na Halmashauri husika. Utekelezaji wa agizo hilo kwa wakati utaondoa changamoto nyingi zinazozikabili Halmashauri zetu na kuziondolea Halmashauri jukumu la kujenga nyumba za watumishi wake kwa kuacha jukumu hilo kwa NHC yenye dhamana ya kuwezesha wananchi kupata nyumba. Kwa kuzingatia yote hayo, tunaona uwe ni utaratibu wa serikali za Miji na Wilaya kuanzia sasa wa kutenga ardhi kwa ajili ya waendelezaji wote wa miliki nchini ili kuboresha mandhari ya miji, kuondoa makazi holela na kupisha miradi mingine ya maendeleo. Tunaamini kuwa Halmashauri zitachukulia uamuzi huu kama fursa ya kuongeza siyo tu makazi bora kwa watu wake bali pia ajira na ustawi wa maisha kwa wakazi wake.

Pamoja na kuunga mkono na kupongeza uamuzi huo wa Rais, tunaamini kuwa watendaji wa Halmashauri hizo

2

www.nhctz.com


UZINDUZI GHARAMA NAFUU

RAIS KIKWETE AFUNGUA NYUMBA ZA GHARAMA NAFUU

• Afurahishwa na kasi ya ujenzi wa nyumba hizo katika halmashauri • Aziagiza Halmashauri kutenga maeneo ya ujenzi wa nyumba za gharama nafuu • NHC kujenga nyumba za gharama nafuu katika Halmashauri zote

Na Mwandishi Wetu,

R

AIS Jakaya Kikwete ameziagiza Halmashauri za Miji na Wilaya nchini kutenga maeneo kwa ajili ya kuwezesha NHC na waendelezaji wengine wa nyumba kujenga nyumba za gharama nafuu. Rais Kikwete aliyasema hayo alipofungua kwa nyakati tofauti miradi ya ujenzi ya nyumba za gharama nafuu iliyojengwa na NHC katika Halmashauri ya Wilaya ya Mkinga –Tanga, Mkuzo-Ruvuma na Mnyakongo – Kongwa. Katika hafla hiyo, Rais alilazimika kutoa agizo hilo baada ya kuelezwa kuwa NHC inalazimika kulipa fidia ya ardhi jambo linaloongeza gharama ya ujenzi wa nyumba zinazojengwa. Hivyo, Rais aliziagiza halmashauri zote nchini kutenga maeneo ya ardhi kwa ajili ya kulipatia Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) bila gharama yoyote ili liweze kutekeleza mradi wake wa ujenzi wa nyumba bora za gharama nafuu. “Nachukua nafasi hii kuwapongeza NHC kwa kujenga nyumba hizi za bei nafuu ambazo sisi serikali tunazihitaji sana ili kuwawezesha wananchi wetu kuishi kwenye makazi bora… wito wangu kwa kila halmashauri sasa ni kuhakikisha inatenga ardhi ya kutosha na kulipatia shirika bila gharama yoyote kwa ajili ya kukamilisha azma yake hii”, alisema. Akiwa Mkuzo Songea Rais Kikwete alirejea kauli yake aliyoitoa Kasera, Mkinga Tanga kwamba Halmashauri zizipatie taasisi zingine zinazojishughulisha na uendelezaji miliki kama NSSF, PPF, GEPF, PSPF na LAPF maeneo bila ya masharti ili ziweze kujenga

www.nhctz.com

Rais Jakaya Kikwete na Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Mh. Saidi Mwambungu (kulia), Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh. Profesa Anna Tibaijuka (kushoto) na Kaimu Mkurugenzi wa shirika la Nyumba NHC Bw. David Shambwe wakikata utepe kwa uzinduzi wa Mradi wa Nyumba za gharama nafuu, Mkuzo Songea Mjini

nyumba za gharama nafuu. Akijibu maombi mbalimbali ya Shirika, Rais alisema kuwa Serikali itafanyia kazi suala la kupunguza kodi ya VAT katika nyumba mpya kwa kuangalia uwezekano wa kuondolea kodi hiyo ili kuwarahisishia wananchi kuzinunua nyumba hizo. Awali, akitoa taarifa ya Shirika katika mradi wa Mnyakongo ulioko Kongwa, Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw. Nehemia Kyando Mchechu alisema kuwa lengo la kubuniwa kwa mradi wa nyumba za gharama nafuu ni kupunguza tatizo la uhaba wa nyumba hususan za watu wa kipato cha kati na chini linalowakabili wananchi katika maeneo mbalimbali nchini. Alisema kuwa mradi huu utasaidia juhudi za serikali za kuwaletea wananchi maisha bora kwa kuwezesha watumishi wa umma kuishi karibu na vituo vyao vya kazi na kuwaondolea gharama za usafiri. “Ni ukweli ulio wazi kwamba hapa nchini kuna mahitaji makubwa ya nyumba yanayokadiriwa kufikia zaidi ya nyumba 3

milioni tatu hivi sasa na yanaongezeka kwa idadi ya nyumba 200,000 kila mwaka wakati uzalishaji wa nyumba ni kiasi cha asilimia 10 ya mahitaji ya mwaka mzima,” alisema Bw. Mchechu alisema kuwa ujenzi wa mradi huu unahitaji ardhi ya kutosha ambapo alibainisha kuwa kwa sasa Shirika linakabiliwa na changamoto kadhaa ikiwemo halmashauri nyingi kutokuwa na mpango mahususi wa maendeleo ya ardhi na hivyo kusababisha NHC kulazimika kununua ardhi kwa fedha ya mikopo ya benki ili kulipa fidia. Alisema hatua hiyo inaongeza gharama ya nyumba hizo zinazoendelea kujengwa katika halmashauri mbalimbali. Alisema kuwa ujenzi wa nyumba za gharama nafuu utaongeza ajira katika Halmashauri. Mradi huo wa nyumba za gharama nafuu una nyumba zenye vyumba viwili na vyumba vitatu na imewekewa huduma muhimu za kijamii kama zahanati, shule ya chekechea na maduka ya bidhaa za aina mbalimbali.

JULAI - DESEMBA 2014

/Nyumba Newsletter


WAZIRI MKUU PINDA

WAZIRI MKUU AUPONGEZA MPANGO WA NHC WA KUTOA AJIRA Na Mwandishi Wetu,

W

AZIRI Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Mizengo Kayanza Peter Pinda amezitaka Halmashauri zote za Miji na Wilaya zilizoko nchini kuhakikisha zinaunga mkono juhudi za NHC za kuwapatia ajira vijana. Alizitaka Halmashauri hizo kuhakikisha kuwa vikundi vya vijana vya ujenzi wa nyumba nafuu (building brigades) vilivyoundwa visaidiwe kwa hali na mali kwa kuvifanya viwe sehemu ya miradi ya kila Halmashauri. Mh. Waziri Mkuu alitoa agizo hilo wakati akizungumza na wakufunzi wanafunzi kutoka VETA waliohitimu mafunzo yaliyotolewa na Wakala wa Serikali wa Utafiti wa Vifaa bora vya ujenzi (NHBRA) ya namna ya kutumia mashine za kufungamana kutengeneza matofali. Waziri Mkuu alifunga mafunzo hayo yaliyotolewa Jijini Dar es salaam kwa wakufunzi wataalam hao waliotoka katika kila Mkoa wa Tanzania Bara ambao sasa wanaendelea kutoa mafunzo kwa vikundi vya vijana vilivyoko katika Mikoa yao. Zaidi ya mashine 700 zimetolewa na NHC kwa ajili ya kuwezesha makundi ya vijana yaliyoundwa katika kila Halmashauri nchini kujiajiri kwa kutengeneza matofali kwa ajili ya ujenzi wa nyumba za gharama nafuu. Halmashauri hizo zimetakiwa kusaidia mpango huu wenye nia njema kwa kutoa maeneo kwa ajili ya vijana kuendeshea shughuli za mpango huo. Maeneo hayo yanapaswa kuwa na udongo unaofaa kutengenezea matofali na kuwa karibu na maeneo ya mjini ili kurahisisha masoko ya matofali watakayotengeneza. Waziri Mkuu alisema kuwa yeye binafsi alimshawishi Mkurugenzi Mkuu wa NHC, Bw. Nehemia Kyando Mchechu kuwa katika ujenzi wa nyumba za gharama nafuu nchini, ahakikishe kuwa anatafuta mbinu za kutumia teknolojia rafiki wa mazingira ili kuepuka janga la uharibifu wa mazingira unaosababishwa na matumizi makubwa ya

Waziri Mkuu Mizengo Pinda akikabidhi cheti kwa mmoja wa wahitimu wa mafunzo ya wataalam wa mashine za kutengeneza matofali kwa ajili ya ujenzi wa nyumba za gharama nafuu Mafunzo hayo yaliyoanza Januari 6 mwaka huu, yaliendeshwa na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) pamoja na Mamlaka ya Elimu ya Ufundi Stadi (VETA) kwa kushirikiana na Wakala wa Utafiti wa Vifaa Bora vya Ujenzi (NHBRA) iliyo chini ya Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi. Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa Nehemia Mchechu na kushoto kwa Waziri Mkuu ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Said Meck Sadick na kulia kwa Waziri Mkuu ni Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt Fenella Mukangara.

• • • •

Ni wa kusaidia vijana mashine za kufyatua matofali Unalenga kutoa ajira zipatazo 7000 Zaidi ya mashine 700 zasambazwa katika Halmashauri Azitaka Halmashauri nchini kusaidia mpango huo

kuni mbichi ili kuchoma matofali. “Licha ya kuwa utengenezaji wa matofali ya kuchoma unatekeleza azma ya Serikali ya kutaka wananchi wake wawe na nyumba bora, kwa kweli roho huwa inaniuma hasa ukizingatia kiasi kikubwa cha miti inayokatwa kuyachoma hayo matofali hadi yawe imara, tena ikiwa mibichi,” alisema Mh. Pinda. Aliupongeza Wakala wa Serikali wa Utafiti wa Vifaa Bora vya Ujenzi (NHBRA) kwa kubuni mashine hizo ambazo alisema zinauzwa kwa bei ambayo Halmashauri zote zinaweza kuzimudu kuwanunulia vijana

wengine ili kupanua ajira. “Mkurugenzi Mkuu ameniambia kila mashine inauzwa shilingi 450,000/- na inaweza kutengeneza matofali 700 kwa siku moja, hayo matofali yanatumia mifuko saba tu ya saruji. Hili ni jambo linalowezekana!” alisisitiza. Hivyo, akawataka Wakurugenzi wa Miji na Wilaya kushiriki kikamilifu katika kuhakikisha kuwa mpango huu unakuwa endelevu ili vijana wanufaike na mpango huu. Alisema anataka Wakurugenzi hao wachangamkie haraka kuzinunua hizo mashine kwa sababu zinasaidia uhifadhi wa mazingira, zinachochea ufanisi wa teknolojia, zinapunguza gharama za ujenzi na zinasaidia kutoa ajira kwa vijana. Hata hivyo, Waziri Mkuu aliwasihi watakaoendesha miradi hiyo wasitoze bei kubwa kwa matofali watakayotengeneza ili wananchi wengi waweze kumudu bei na wabadili hadhi za makazi yao. Waziri Mkuu alimtaka Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw. Mchechu aweke mpango wa kuendeleza kampeni hiyo aliyoianzisha angalau kwa miaka mitano mfululizo ili mpango huo Continued page 10 >>

Nyumba Newsletter/JULAI - DESEMBA 2014

4

www.nhctz.com


BODI MPYA

WAZIRI TIBAIJUKA AIZINDUA BODI MPYA YA NHC • • • • •

Alipongeza Shirika kwa kazi nzuri Alitaka liongeze kasi ya kujenga nyumba za gharama nafuu Ataka vigezo vya kuuza nyumba hizo kwa wananchi stahili viwekwe Wenyewe wamshukuru, waahidi kufanya makubwa Serikali yaombwa kuondoa kodi ya VAT katika nyumba za gharama nafuu

Na Mwandishi Wetu,

W

AZIRI wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Kajumulo Tibaijuka, ameagiza Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) kuendelea na ujenzi wa nyumba za gharama nafuu ili kuendeleza falsafa iliyolianzisha Shirika hilo mwaka 1962 ya kuboresha makazi ya watu wa kipato cha chini na kati. “Ninachotaka kuwasisitizieni Bodi mpya na Menejimenti ya NHC, Shirika lisisahau lilipotoka liendelee na dhima ya kuanzishwa kwake mwaka 1962 kwa kuwajali pia wananchi kwa kujenga nyumba za gharama nafuu, suala la nyumba lilikuwa ni kampeni ya chama cha TANU,” alisema. Agizo hilo alilitoa Waziri Anna Tibaijuka Makao Makuu ya NHC, wakati alipokuwa akizindua Bodi mpya ya Wakurugenzi ya NHC yenye wajumbe saba hafla iliyohudhuriwa pia na Watendaji wa Shirika. Akizungumza katika hafla hiyo, Waziri Tibaijuka aliagiza Shirika kuendelea kutekeleza mabadiliko ya kuboresha huduma za Shirika ili kuongeza tija kubwa.“Nina imani kuwa mtaendelea na utaratibu huu mzuri wa kujenga nyumba za gharama nafuu ili kuwezesha Watanzania wengi zaidi kunufaika na mipango yenu mizuri mliyoianzisha,” alisema Tibaijuka. Waziri Tibaijuka alisema kuwa pamoja na kuwa hadi hivi sasa hakuna sera ya nyumba, aliiagiza Bodi na Menejimenti ya NHC kuhakikisha kuwa Shirika linajiendesha kwa kufuata misingi ya ushindani, lakini lisipoteze roho yake ya kujenga nyumba za gharama nafuu na kuwe na vigezo vitakavyowawezesha wenye sifa za kupata nyumba za gharama nafuu wanufaike na siyo wengine. Waziri Tibaijuka alilipongeza Shirika la Nyumba la Taifa na kubainisha kuwa hivi sasa Shirika hilo limeimarika licha ya kupitia katika changamoto nyingi sana huko nyuma na kwamba Shirika linaongozwa

www.nhctz.com

na Menejimenti yake huru, huku Serikali kupitia Wizara yake ikifanya jukumu lake la usimamizi. Akizungumzia mabadiliko ya Sheria, Waziri huyo alisema kuwa Serikali ilijitahidi kubadilisha sheria mbalimbali zilizokwamisha uwekezaji katika sekta ya nyumba. Alizitaja sheria hizo zilizofanyiwa marekebisho kuwa ni pamoja na sheria ya ardhi namba 4 ya mwaka 1999, sheria ya mikopo ya nyumba ya mwaka 2008 na sheria ya hati pacha katika majengo ya ghorofa ya mwaka 2008. Aidha, alisema kuwa mwaka 2010, Serikali iliagiza Shirika hili lifanyiwe mabadiliko makubwa na lisukwe upya kwa kulipatia uongozi mpya. Aliiambia Bodi kuwa Wizara yake imekuwa ikifanya mengi kuboresha sekta ya nyumba ikiwemo kuboresha sera na sheria mbalimbali kwa kuwa hatuwezi kuwa na nyumba bora bila ya kuwa na mazingira bora ya uwekezaji na sheria bora. Alisema kuwa Bodi ambayo ameizindua imelikuta Shirika na sekta ya uendelezaji miliki vikiwa katika hali nzuri, hivyo akaiagiza Bodi hiyo kuendeleza moto ule ule iliyokuwa nayo Bodi iliyomaliza muda wake. Alilitaka Shirika hilo kuweka uwiano mzuri kati ya nyumba za kupangisha na zile za kuuza ili kuweza kujilinda pindi kunapotokea kuporomoka kwa soko la nyumba. “Ninaomba kabisa Bodi yetu mpya tuangalie “sustainability” ya tunayoyafanya, washaurini hawa vijana wanunue nyumba zinazowazunguka humu mijini ili kuwa na vitega uchumi vilivyo katika mandhari nzuri, siyo mbananishe maghorofa kama ilivyo Kariakoo,”alisema. Naye, Mkurugenzi wa NHC Bw. Nehemia Kyando Mchechu, alisema kuwa Shirika la Nyumba la Taifa lina mali zenye thamani isiyopungua shilingi trilion 1.5 hivyo 5

changamoto kubwa iliyopo kwa sasa ni kuhakikisha wanatumia fursa zilizopo kuwapatia Watanzania makazi bora. Alisema kuwa Watanzania wana matumaini makubwa na Shirika hilo ambalo hivi sasa limedhamiria kufanya mabadiliko makubwa hasa yenye lengo la kujiimarisha kibiashara ikiwemo kujenga nyumba nyingi zaidi ili kukuza uchumi wa Taifa na wa mtu mmoja mmoja. Alisema pamoja na jitihada hizo, Shirika linakabiliwa na changamoto mbalimbali kama kulazimika kununua ardhi kwa gharama kubwa kwenye halmashauri za Wilaya hapa nchini. Pia alisema kuwa Shirika linalazimika kutengeneza miundombinu ya umeme, maji na barabara katika maeneo ya miradi na kuongeza gharama kubwa jukumu ambalo alisema linapaswa kufanywa na mamlaka zingine zinazohusika. Aliiomba Serikali kuondoa kodi kwenye mauzo ya nyumba mpya ambazo hazizidi shilingi milioni 100 hatua itakayosaidia watu wengi kuweza kununua nyumba kwa gharama ndogo. Wakizungumza katika hafla hiyo, Wakurugenzi hao wa Bodi waliipongeza Bodi iliyopita kwa kazi yao nzuri ya kuiongoza Menejimenti ya Shirika. Walimshukuru Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Waziri Tibaijuka kwa kuwapa jukumu zito la kulisimamia Shirika na wakaahidi kuendeleza mambo makubwa yaliyofanywa na Bodi iliyomaliza muda wake. Bodi hiyo inaundwa na Mwenyekiti Mheshimiwa Zakhia Hamdani Meghji, Bw. Diotrephes Mmari (aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi)ambaye ndiye Makamu Mwenyekiti wa Bodi hiyo, Bibi Subira Mchumo, Bw. Patrick Rutabanzibwa (aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi), Bw. Samson Kasalla (aliyekuwa Kamishna wa Jeshi la Polisi), Bibi Irene Isaka (Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Mifuko ya Jamii(SSRA), Bw. Bedason Shallanda kutoka Benki Kuu ya Tanzania na Bw.Charles Mafuru (Mkurugenzi wa Nyumba -Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi). JULAI - DESEMBA 2014

/Nyumba Newsletter


BODI MPYA KATIKA PICHA

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Kajumulo Tibaijuka akizungumza na watendaji wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) (hawapo pichani) kwenye uzinduzi rasmi wa Bodi mpya ya Shirika hilo uliofanyika kwenye Makao Makuu ya Shirika hilo jijini Dar es Salaam jana. (Picha zote kwa hisani ya kitengo cha Mawasiliano na Huduma kwa Jamii cha NHC)

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Anna Kajumulo Tibaijuka akimkabidhi mikoba Mwenyekiti mpya wa Bodi ya Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) , Mama Zakhia Hamdani Meghji.

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Anna Kajumulo Tibaijuka akimkabidhi mkoba Mjumbe mpya wa Bodi ya Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) , Diotrepes Mmari.

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Anna Kajumulo Tibaijuka katika picha ya pamoja na Mjumbe wa Bodi ya NHC, Irene Isaka.

Wajumbe wapya wa Bodi ya Shirika la Nyumba la Taifa wakiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Anna Kajumulo Tibaijuka.

Mjumbe mpya wa Bodi ya NHC, Charles Mafuru, ambaye pia ni Kaimu Mkurugenzi wa Nyumba wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi akiwaelekeza jambo watendaji wakuu wa Shirika la Nyumba (NHC) (hawapo pichani)


MAZINGIRA BORA

SERIKALI YAWAHAKIKISHIA WAWEKEZAJI MAZINGIRA BORA Nyumba la Taifa (NHC), limedhamiria kuyabadilisha maeneo ya jiji la Dar es Salaam na mikoa mingine nchini baada ya kuzindua ujenzi wa miji midogo inayojitegemea ndani ya miji ya sasa. Alisema kuwa miradi hiyo itakapokamilika itabadilisha mandhari ya maeneo mbalimbali nchini na kuyafanya kuwa ya kisasa.

• Ni wawekezaji wa ndani wa sekta ya miliki • Sheria na vivutio vingi katika sekta hiyo vyaboreshwa • NHC yadhamiria kubadilisha mandhari ya miji nchini.

Na Mwandishi Wetu,

W

ADAU wa sekta ya uendelezaji miliki nchini wamehakikishiwa mazingira bora na salama kwa ajili ya uwekezaji katika sekta hiyo inayokuwa kwa kasi nchini katika siku za hivi karibuni. Hayo yamesemwa na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Profesa Anna Tibaijuka jijini Dar es Salaam, alipozungumza na wadau mbalimbali waliohudhuria kwenye jukwaa la wawekezaji wa ndani lililoandaliwa na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) ambalo pia lilishirikisha baadhi ya Wakuu wa Mikoa. Profesa Tibaijuka alisema kuwa mazingira bora ya uwekezaji katika sekta ya uendelezaji miliki yameshawekwa na Serikali kwa kuunda sheria rafiki za uwekezaji ambapo ongezeko la uwekezaji wa moja kwa moja kutoka nje ya nchi umekuwa na mageuzi ya kiuchumi yamefanywa na yamewezesha kuboreka kwa uchumi wa soko. Alisema programu mbalimbali za mabadiliko ya kisheria na kitaasisi yamefanywa na serikali ambayo yana lengo la kuboresha mazingira ya soko na uwekezaji binafsi katika sekta binafsi.

uwekezaji kwenye miradi ya Usa River na Safari Satellite City kule Arusha, na Salama Creek Satellite City-Dar es Salaam,” alisema Prof. Anna Tibaijuka. Mkurugenzi Mkuu wa NHC, Bw. Nehemia Kyando Mchechu, alisema kuwa fursa zilizopo katika sekta ya uendelezaji miliki ni za kuvutia na hazina ushindani mkubwa na ndiyo maana NHC imepanga kujenga nyumba nyingi zaidi kwa ajili ya biashara na makazi nchini kote. Katika kipindi cha miaka mitano iliyopita, sekta ya uendelezaji miliki imechukua nafasi ya tano kati ya vivutio kumi vikuu vya uwekezaji wa moja kwa moja kutoka nje ya nchi yaani Foreign Direct Investment (FDI). Bw. Mchechu alisema kuwa Shirika la

“Profesa Tibaijuka alisema kuwa mazingira bora ya uwekezaji katika sekta ya uendelezaji miliki yameshawekwa na Serikali kwa kuunda sheria rafiki za

Alisema pia kwamba maboresho ya kitaasisi kwa kutoa vipaumbele kwa miradi mbalimbali tayari yameshafanywa na Kituo cha Uwekezaji nchini (TIC) na taasisi nyingine za umma hali inayowarahisishia wawekezaji kuamua mahali sahihi pa kuwekeza.

uwekezaji ambapo ongezeko

“Ninachukua fursa hii kuwakaribisheni wawekezaji ambao mmeshiriki kwenye jukwaa hili, mchukue fursa hii kupata taarifa muhimu mnazozihitaji na hatimaye kuchukua fursa zilizopo tayari katika

yamewezesha kuboreka kwa

www.nhctz.com

la uwekezaji wa moja kwa moja kutoka nje ya nchi umekuwa na mageuzi ya kiuchumi yamefanywa na uchumi wa soko.

7

Bw.Mchechu alisema ujenzi wa miradi mitatu utaanza hivi karibuni ikiwemo ya miji midogo katika majiji ya Dar es Salaam na Arusha pamoja na kuendeleza nyumba zilizobomolewa ili kupisha uendelezaji mpya. Alisema katika jiji la Dar es Salaam, kutakuwa na mradi wa Salama Creek ulioko Kigamboni na Up Town Kawe ulioko ilipokuwa Tanganyika Packers ambayo italifanya jiji hilo kubadilika na kuwa la kisasa zaidi tofauti na linavyoonekana sasa. Bw. Mchechu alisema katika miradi hiyo, kutajengwa nyumba nyingi za kuishi, biashara na sehemu za huduma muhimu na kwamba itakapokamilika itabadili muonekano wa maeneo hayo. Alisema miradi mingine itakayotekelezwa ni ya Usa River na Safari City itakayojengwa Jijini Arusha na kwamba inalenga kulibadilisha jiji hilo ili kuwa la kisasa. Mkurugenzi Mkuu alisema kuwa mradi mwingine ambao utatekelezwa katika Jiji la Dar es Salaam, ni mradi wa ujenzi wa miji mdogo wa Luguruni. Mchechu alisema kuwa kila mradi utagharimu dola za Marekani milioni mbili (zaidi ya shilingi bilioni 3.4) na itakamilika kati ya kipindi cha miaka 7 mpaka 12. Alisema miradi mingine ambayo itatekelezwa ni pamoja na Bagamoyo, Dodoma, Mbeya, Mtwara, Lindi, Mwanza na maeneo mengine nchini. Mchechu alisema jukwaa hilo limetokana na mkutano mkubwa wa wawekezaji waliofanya hivi karibuni nchini Dubai ambalo liliwahusisha wawekezaji wa nje ili wawekeze katika sekta ya miliki nchini Tanzania.

JULAI - DESEMBA 2014

/Nyumba Newsletter


KAMATI POAC

RAIS KIKWETE AFUNGUA NYUMBA ZA GHARAMA NAFUU

Mchechu alisema kuwa lengo la kubuniwa kwa mradi wa nyumba za gharama nafuu ni kupunguza tatizo la uhaba wa nyumba hususan za watu wa kipato cha kati na chini linalowakabili wananchi katika maeneo mbalimbali nchini. Alisema kuwa mradi huu utasaidia juhudi za serikali za kuwaletea wananchi maisha bora kwa kuwezesha watumishi wa umma kuishi karibu na vituo vyao vya kazi na kuwaondolea gharama za usafiri. “Ni ukweli ulio wazi kwamba hapa nchini kuna mahitaji makubwa ya nyumba yanayokadiriwa kufikia zaidi ya nyumba milioni tatu hivi sasa na yanaongezeka kwa idadi ya nyumba 200,000 kila mwaka wakati uzalishaji wa nyumba ni kiasi cha asilimia 10 ya mahitaji ya mwaka mzima,” alisema

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Huduma kwa Jamii Cha Shirika la Nyumba la Taifa (National Housing) Susan Omari (kushoto) akitoa maelezo na kisha kukabidhi kwa Rais Dk. Jakaya Mrisho Kikwete mashine za kutengeneza matofali ya kufungamana ambazo zimekwishagawanywa kwenye wilaya zote za Mkoa wa Tanga ili kuwawezesha kuanzisha vikundi vya ujenzi vya vijana. Kulia ni aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Tanga Luteni Mstaafu Chiku Galawa. Mashine hizo zilitolewa wakati wa Uzinduzi wa nyumba za bei nafuu Wilayani Mkinga

• • •

Afurahishwa na kasi ya ujenzi wa nyumba hizo katika halmashauri Aziagiza Halmashauri kutenga maeneo ya ujenzi wa nyumba za gharama nafuu NHC kujenga nyumba za gharama nafuu katika Halmashauri zote

Na Mwandishi Wetu,

R

AIS Jakaya Kikwete ameziagiza Halmashauri za Miji na Wilaya nchini kutenga maeneo kwa ajili ya kuwezesha NHC na waendelezaji wengine wa nyumba kujenga nyumba za gharama nafuu. Rais Kikwete aliyasema hayo alipofungua kwa nyakati tofauti miradi ya ujenzi ya nyumba za gharama nafuu iliyojengwa na NHC katika Halmashauri ya Wilaya ya Mkinga –Tanga, Mkuzo-Ruvuma na Mnyakongo – Kongwa. Katika hafla hiyo, Rais alilazimika kutoa agizo hilo baada ya kuelezwa kuwa NHC inalazimika kulipa fidia ya ardhi jambo linaloongeza gharama ya ujenzi wa nyumba zinazojengwa. Hivyo, Rais aliziagiza halmashauri zote nchini kutenga maeneo ya ardhi kwa ajili ya kulipatia Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) bila gharama yoyote ili liweze kutekeleza mradi wake wa ujenzi wa nyumba bora za gharama nafuu. “Nachukua nafasi hii kuwapongeza NHC kwa kujenga nyumba hizi za bei nafuu ambazo sisi

Nyumba Newsletter/JULAI - DESEMBA 2014

serikali tunazihitaji sana ili kuwawezesha wananchi wetu kuishi kwenye makazi bora… wito wangu kwa kila halmashauri sasa ni kuhakikisha inatenga ardhi ya kutosha na kulipatia shirika bila gharama yoyote kwa ajili ya kukamilisha azma yake hii”, alisema. Akiwa Mkuzo Songea Rais Kikwete alirejea kauli yake aliyoitoa Kasera, Mkinga Tanga kwamba Halmashauri zizipatie taasisi zingine zinazojishughulisha na uendelezaji miliki kama NSSF, PPF, GEPF, PSPF na LAPF maeneo bila ya masharti ili ziweze kujenga nyumba za gharama nafuu. Akijibu maombi mbalimbali ya Shirika, Rais alisema kuwa Serikali itafanyia kazi suala la kupunguza kodi ya VAT katika nyumba mpya kwa kuangalia uwezekano wa kuondolea kodi hiyo ili kuwarahisishia wananchi kuzinunua nyumba hizo. Awali, akitoa taarifa ya Shirika katika mradi wa Mnyakongo ulioko Kongwa, Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw. Nehemia Kyando 8

Bw. Mchechu alisema kuwa ujenzi wa mradi huu unahitaji ardhi ya kutosha ambapo alibainisha kuwa kwa sasa Shirika linakabiliwa na changamoto kadhaa ikiwemo halmashauri nyingi kutokuwa na mpango mahususi wa maendeleo ya ardhi na hivyo kusababisha NHC kulazimika kununua ardhi kwa fedha ya mikopo ya benki ili kulipa fidia. Alisema hatua hiyo inaongeza gharama ya nyumba hizo zinazoendelea kujengwa katika halmashauri mbalimbali. Alisema kuwa ujenzi wa nyumba za gharama nafuu utaongeza ajira katika Halmashauri. Mradi huo wa nyumba za gharama nafuu una nyumba zenye vyumba viwili na vyumba vitatu na imewekewa huduma muhimu za kijamii kama zahanati, shule ya chekechea na maduka ya bidhaa za aina mbalimbali.

“Ni ukweli ulio wazi kwamba hapa nchini kuna mahitaji makubwa ya nyumba yanayokadiriwa kufikia zaidi ya nyumba milioni tatu hivi sasa na yanaongezeka kwa idadi ya nyumba 200,000 kila mwaka wakati uzalishaji wa nyumba ni kiasi cha asilimia 10 ya mahitaji ya mwaka mzima,” www.nhctz.com


WAAJIRIWA WAPYA

Na Mwandishi Wetu,

S

HIRIKA la Nyumba la Taifa (NHC) limeajiri wafanyakazi wapya 100 kutoka wa kada mbalimbali ikiwa ni jitihada za kuimarisha ikama na kuboresha huduma zake kwa umma.

NHC YAAJIRI WAFANYAKAZI WAPYA 100

Taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Uendelezaji Rasilimali watu imeeleza kuwa wafanyakazi hao walioajiriwa kuanzia Januari 2013 mpaka Oktoba 2014. Wfanyakazi hao ni wa taaluma za Usimamizi na Uendelezaji Miliki, Biashara, Utawala, Manunuzi, Sheria na Ugavi. Wafanyakazi hao ni pamoja na Mameneja Mkurugenzi wa Rasilimali Watu, James Rhombo akiwasilisha mada kwenye semina ya mafunzo kwa waajiriwa miradi ambao ni Bw. Etheldreder Koppa, wapya inayofanyika kwa siku mbili kwenye hoteli ya JB Belmonte iliyoko Golden Jubilee Tower, Jijini Dar es Bw. George Magembe, Bw. Samwel Metili, Salaam. Bw. Cliford Hungu na Bw. Subira Gudadi. • Ni wa kada mbalimbali za utumishi Maafisa Miliki walioajiriwa ni Mwasiti Jimmy, Amon Mazanda, Dastani Mgouya, Songoro Saidi, Lwitiko Ndigha, Emenick Sanga, Victor Lawrence Sheushi, Edward Haule, Amos Manyama, Costantine Yuda, Keneth Ntulo, Fadhili Anyegile, Augustino Sanga, Elizabeth Michael Maro, Wambura Jafari Chege. Maafisa Miliki wengine walioajiriwa ni Thomas Msambwa, Mukakaro Mukakaro, Humphrey Tarimo, Zenna Nyange, Goodluck Thomas, Ramadhani Sadicki na Philip Gawa.

•

Ni mkakakati wa kuimarisha ikama na ufanisi

na Seleki Apolinary, Mussa Efata, Gloria Otto Ringia, Lilian Reuben, Nimo William, Salim Mbwana Salum, Benson Shabani, Repson Yosia, Nancy Joseph na Baha j. Nkhangaa. Katika kada ya madereva wamo Nicholaus Lyimo, George Kyamba, Raphael Maliva, Anderson Fungo, Aquiline Mushi, Elias Polepole, Aidin Stafford, Mohamed Swanga na Abdulkher Abdallahtif.

Katika kundi la Maafisa Manunuzi waliajiriwa wamo Aman Sehaiya, Rukia Kidasi, Fransisca Francis Michael, Kaiza Straton, Paskalina Monko, Devina Msechu, Victor Christopher, Evarista Mallya, Castro Nzaye, Jimmy Mbogela, Anitha Aloyce, Ritha Mokimirya na Olga William.

Wafanyakazi wengine na vyeo vikiwa kwenye mabano ni Grayson Godfrey (Facility Manager), Rashid Omar Amani (Msaidizi Masjala), Iddi Khalifa Kitete (Msaidizi Masjala), Edna Lucas Chogo (Afisa Utumishi Mwandamizi) na Emmanuel Kabeya (Mwanasheria).

Wahasibu Wasaidizi walioajiriwa ni pamoja

Wengine ni Godlove Godwin (Afisa Utumishi), Gema Guerino Gamanywa (Afisa Utumishi), Telesphori Focus (Injinia wa Umeme), Nikundiwe Mmakasa (Mkaguzi wa Ndani Mwandamizi) Bulla Boma (Meneja Ofisi ya Mkurugenzi Mkuu) Tuntufye Mwambusi (Meneja Mauzo), Emmanuel Kyarwenda (Mhasibu Kodi), Sixtus Kilenga (Afisa Utawala Mwandamizi), John Laswai (Mwanasheria Mwandamizi) na Elias Mwashiuya (Meneja Huduma za Sheria.

Pichani baadhi ya Waajiriwa wapya kutoka kushoto Fatima Rajabu, wa tatu Clara Lumbanga, Felichism Mtenga na Lister Nyabilinyi wakisikiliza mada kutoka kwa Mkurugenzi wa Rasilimali Watu, James Rhombo wakati akiwasilisha mada kwenye semina ya mafunzo kwa waajiriwa wapya inayofanyika kwa siku mbili kwenye hoteli ya JB Belmonte iliyoko Golden Jubilee Tower, Jijini Dar es Salaam.

www.nhctz.com

Pia wamo Clara Matern Lumbanga (Afisa Mwandamizi Uendelezaji Biashara), Fatima Adadi Rajabu (Afisa Mwandamizi 9

Uendelezaji Biashara), Salvatory Venant Hinju (Afisa Mwandamizi Uendelezaji Biashara), Getrude E. Mallya (Afisa Utawala), Gloria E. Staki (Mapokezi), John Temu(Mhasibu Msaidizi), Rose Erasimus Uisso (Mhasibu Msaidizi), Rose Michael Mwandemani (Mhasibu Msaidizi), Khalid Maulid Mvungi(Mhasibu Msaidizi), Felichism S. Mtenga(Mhasibu Msaidizi),Hilda Anderson Temu(Mhasibu Msaidizi), Lister Joseph Nyabinyili (Mhasibu Msaidizi) na Mwita Bernard Megabe(Mhasibu Msaidizi). Wengine ni Domina Willbard Rwemanyila (Afisa Huduma kwa wateja)Dyana Hatuey Mwamba ((Afisa Huduma kwa wateja), Jackline Kilawe (Afisa Mapokezi), Edwin Martin Pesha (Dereva), Shija Samuel Shimbi(Dereva), John Gustav Masika (Dereva), Selemani A. Mashaka(Dereva), Sadiki Muhamed Mneka(Dereva), Simon Mhiliwa(Mhasibu Msaidizi) na Malima Mukama(Mhasibu Msaidizi). Menejimenti ya Shirika inawatakia wafanyakazi hao wapya kazi njema yenye kuliletea Shirika mafanikio zaidi hususan wakati huu ambapo Shirika linatekeleza mpango mkakati wake ambao unalenga kujenga nyumba 15,000 katika kipindi cha miaka mitano ijayo, idadi ambayo haijawahi kufikiwa na Shirika tangu kuundwa kwake Agosti 1, 1962.

JULAI - DESEMBA 2014

/Nyumba Newsletter


WASTAAFU << Continued page 4

WASTAAFU UTUMISHI NHC

uweze kuwa na matokeo chanya na maslahi mapana kwa jamii.

• Ni wa kada mbalimbali za utumishi • Walilitumikia Shirika kwa mafanikio makubwa

Na Mwandishi Wetu,

J

UMLA ya wafanyakazi arobaini wamestaafu rasmi utumishi wao kwa umma kwa mujibu wa sheria kwa nyakati tofauti kati ya Januari hadi Julai mwaka huu. Taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Uendelezaji Rasilimali watu imeeleza kuwa wafanyakazi hao waliostaafu katika kipindi hicho ni wa kada mbalimbali hususan za Uendelezaji Miliki, Utawala, Usimamizi Miliki na Ubunifu Majengo. Wafanyakazi hao na vyeo vyao walivyotumikia vikiwa kwenye mabano ni Joseph Mganga (Meneja Uendeshaji Miliki), Verynice J. Nassary (Accounts Technician), Simon Samo (Mhandisi), Jumanne Mtuli (Fundi Mchundo) Lusagana B. M. Lusagana (Meneja wa Miradi ya Ubia), Dekusura Kimaro (Karani wa Mahesabu) na Telly Swebe (Msaidizi Mwandamizi Utawala). Wengine ni Traiphon Ndunguru (Fundi Mwandamizi) , Khalfani Mhina Juma (Dereva), Lazaro Lwanyakasura (Fundi Mchundo), Omari Abbasi(Fundi Mwandamizi), Alexander Nicolaus (Msaidizi wa Ofisi) na Rajabu M. Ngubureni(Dereva). Pia katika orodha hiyo wamo Laurensia Justinian (Msaidizi Mahesabu) , Goodnes Meresi (Msaidizi wa Ofisi), Bakari Mnkande (Fundi Mchundo), Augustino Joseph (Mlinzi), Cecilia Sentala (Msaidizi masuala ya nyumba), Leonard C. Maganga (Mkusanya Madeni Mwandamizi). Wastaafu wengine ni Bakari Gumbo (Dereva), Michael Masudi (Mlinzi), Monica Mlay (Mhudumu Arusha), Modesta Gervas (Mhudumu

Nyumba Newsletter/JULAI - DESEMBA 2014

WAZIRI MKUU AUPONGEZA MPANGO WA NHC WA KUTOA AJIRA

Kinondoni), Anastazia Togoro (Mpiga chapa Shinyanga), Jane Nkwama (Mpiga chapa Arusha), Simon Shekigenda (Msaidizi masuala ya nyumba), Loyce Petro (Mkadiriaji Majengo Mwandamizi), Catherine Fumbuka (Mhasibu), Said Mnongane (Fundi Mchundo), Herman Kaseka (Afisa Nyumba Kilimanjaro), Marcus Mdugala, Sarah Mhanga (Mpiga chapa), Twahir Chamulume (Afisa Masjala), Allan Kabogo (Daktari wa Shirika), Damian Hugho (Mhasibu), Seleman Said (Afisa Stoo), Mathew Kabunga (Mwanasheria), Ally Nangwanda (Mhasibu Msaidizi), Alexander Nicholaus (Mhudumu), Omari Abbasi (Fundi) , Asubi Mwaigwisya (Fundi Mchundo) na Mathias Chilemba (Fundi Mchundo). Wengine ni Ng’aranga Magai (Meneja Mkoa –Kagera), Paul Mokimirya (Meneja Mkoa –Ruvuma), Suresh Dhrona – Meneja Ukaguzi wa Ndani, Mariam Kambi- (Meneja Mkoa Singida),Amina Salum(Mhudumu wa Ofisi- Ilala) na Yassin Simtitu(Mhandisi – Ruvuma). Katika hatua nyingine wafanyakazi watatu wa Shirika waliamua kuacha kazi wenyewe kwa hiyari yao na wengine kuachishwa kazi kwa sababu mbalimbali . Menejimenti ya Shirika inawatakia wafanyakazi hao wastaafu maisha mema na yenye mafanikio hasa baada ya kushiriki vilivyo kuliletea Shirika mafanikio makubwa hususan wakati huu ambapo Shirika limekuwa likitekeleza mpango mkakati wake ambao unalenga kujenga nyumba 15,000, idadi ambayo haijawahi kufikiwa na Shirika tangu kuundwa kwake Agosti 1, 1962.

10

Naye, Mkurugenzi Mkuu wa NHC, Bw. Nehemia Kyando Mchechu alisema kuwa chini ya sera ya NHC ya kusaidia miradi ya maendeleo inayofanywa na jamii (CSR), Shirika limekuwa linachangia pia sekta za afya na elimu na hivi sasa limelenga vijana hasa ili kutoa ajira katika sekta ya ujenzi. Aliwasihi Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wa Halmashauri watoe ushirikiano kwa Shirika ili mpango huo wa kutoa ajira kwa vijana uweze kufanikiwa. Aidha, alivitaka vikundi vya vijana vilivyoko katika Halmashauri hizo kuunda SACCOS zao ili kupanua shughuli zao za kiuchumi. Katika mpango huo, kila Halmashauri imepewa mashine nne, na kila mashine inahudumiwa na vijana 10 kwa hiyo itachangia ajira ya moja kwa moja kwa vijana zaidi ya 7000. Pamoja na msaada wa mashine, Shirika limetoa Shilingi laki tano (500,000/=) kwa kila Halmashauri kama kianzio cha vijana hao kununua vifaa muhimu vya kuwezesha kazi ya kufyatua matofali kuanza. Aidha, Shirika limegharamia utoaji wa mafunzo kwa vijana katika kila Halmashauri. Mpango huo umeligharimu Shirika zaidi ya shilingi milioni 700 hadi kukamilika. Akizungumza katika Mkutano wa Maafisa Vijana kutoka Mikoa yote ya Tanzania uliofanyika mjini Tabora Oktoba 16 mwaka huu, Mkuu wa Mawasiliano na Huduma kwa Jamii, Bibi Susan Omari aliwaomba wasaidie kufuatilia utekelezaji wa mpango huu. Maafisa Vijana hao walilishukuru Shirika kwa uamuzi huo wa kizalendo ambao umesaidia sana kutoa ajira kwa vijana na waliahidi kuunga mkono

Baadhi ya wahitimu wa mafunzo ya Ufundi wa utengenezaji Natofali kwakutumia teknolojia ya kisasa na kwa gharama nafuu wakimsikiliza Waziri Mkuu (hayupo pichana) wakati akiwahutubia kwenye hafla ya kufunga mafunzo yao na kuwakabidhi vyeti.

www.nhctz.com


Ziara Uturuki

Aliyekuwa Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Goodlucky Ole Medeye (katikati), akiwa na wabunge wa Tanzania wakitembelea nyumba zilizojengwa na Serikali nchini Singapore na kuuzwa wananchi

WABUNGE WATEMBELEA UTURUKI Na Mwandishi Wetu,

H

atua iliyopigwa na Serikali ya Uturuki katika kupanga upya na kuyaendeleza makazi yaliyokuwa na msongamano mkubwa wa watu, imeonekana kuwaduwaza wabunge wa Tanzania waliokuwapo kwenye ziara ya mafunzo katika miji ya Ankara na Istanbul iliyodhaminiwa na NHC. Katika ziara hiyo, Wabunge hao walielezwa kuwa Uturuki kupitia Mamlaka yake ya Usimamizi na Maendeleo ya Nyumba, iliyopo chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu (TOKI), iliwahamisha wakazi zaidi ya 6,500 waliokuwa wakiishi kwenye maeneo ya ujenzi holela na sasa eneo hilo katika Mji wa Ankara limepangwa na kuendelezwa upya na baada ya kukamilika litakuwa na uwezo wa kukaliwa na watu zaidi ya 18,000. Ujumbe wa wabunge hao, wengi wakiwa wajumbe wa Kamati ya Ardhi, Maliasili na Mazingira ulioongozwa na Mbunge wa Kuteuliwa, Zakia Meghji (CCM) (sasa Mwenyekiti wa Bodi wa Shirika la Nyumba la Taifa), huku kwa upande wa Serikali ukiongozwa na aliyekuwa Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Goodlucky Ole Medeye.

www.nhctz.com

Wengine katika ziara hiyo iliyoandaliwa na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) ni wawakilishi kutoka Kamati za Bunge za Bajeti na ile ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, pamoja na viongozi wakuu kutoka Halmashauri ya Wilaya za Arusha na Arumeru pamoja na Jiji la Arusha. Katika ziara hiyo ya siku sita, ilibainika kuwa tatizo linalokwaza uendelezaji wa makazi Tanzania ni gharama kubwa za ujenzi ambazo zinachangiwa na bei kubwa ya ardhi, riba ya mikopo ya benki na kodi ya ongezeko la thamani (VAT) baada ya nyumba kujengwa. Nchini Uturuki, TOKI hupewa ardhi na Serikali kwa gharama ndogo na nyumba zinazojengwa huuzwa pasipo kuongeza faida wala kutozwa kodi kutokana na Serikali kuwekeza fedha nyingi katika sekta hiyo, huku wale wanaouziwa wakilipa fedha hizo kwa miaka 20 bila kutozwa riba. Meneja wa Tawi la Uhusiano wa Kimataifa katika Idara ya Mipango miji ya TOKI, Sule Karabey alisema gharama za nyumba kwa ajili ya makazi yanayojengwa kwa ajili ya watu wenye kipato cha kati na cha chini,

11

huuzwa kwa fedha ambazo ni sawa na Shilingi 19.2 milioni za Tanzania. Kiasi hicho ni zaidi ya mara mbili ya gharama za nyumba za bei nafuu zinazojengwa na NHC na kuuzwa kwa wananchi. Mkurugenzi Mkuu wa NHC, Bw. Nehemia Mchechu mara kadhaa amekuwa akieleza kuwa gharama kubwa ya ardhi, kodi kwenye vifaa vya ujenzi na kwenye mauzo ya nyumba kuwa ni kikwazo kwa shirika hilo kujenga nyumba za gharama nafuu. Mchechu aliwaambia wabunge hao kuwa, kikwazo kingine ni kutokuwapo kwa huduma za jamii kama maji, umeme na barabara katika maeneo ambayo shirika lake linayaendeleza na kwamba wakati mwingine NHC hugharamia huduma hizo hivyo kusababisha gharama za nyumba kuongezeka. Mbunge wa Ubungo, John Mnyika (Chadema), alisema tatizo lililopo ni kukosekana kwa mawasiliano na uratibu miongoni mwa taasisi za Serikali na kwamba kama yangekuwapo hilo lisingekuwa tatizo.

JULAI - DESEMBA 2014

/Nyumba Newsletter


Ziara Singapore

VIONGOZI WA SHIRIKA NA WIZARA

WAZURU SINGAPORE

Ujumbe wa NHC ukiangalia ramani ya Singapore inayoonyesha ujenzi wa miundombinu na makazi mbalimbali ya watu.

• • •

Watanzania watakiwa kufuata sheria za mipango miji Bodi ya NHC yatakiwa kuitisha mkutano wa wadau wa mipango miji Mipango miji Singapore imefanikiwa kutokana na raia wake na mamlaka zote kuzingatia sheria za mipango miji.

Na Mwandishi Wetu,

N

AIBU Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mh. George Simbachawene, amezitaka mamlaka zinazosimamia mipango miji nchini kuhakikisha kuwa sheria na taratibu zote za mipango miji zinafuatwa na kusimamiwa. Simbachawene alitoa kauli hiyo Jijini

Nyumba Newsletter/JULAI - DESEMBA 2014

Singapore alipokuwa akifanya majumuisho ya ziara ya siku nne nchini humo mwezi Julai,2014. Akiwa ameandamana na watendaji wa NHC na wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika, Naibu Waziri huyo alisema kuwa Tanzania ina sheria na taratibu zinazoongoza mipango miji kama ilivyo kwa Singapore, lakini kinachokosekana nchini mwetu ni usimamizi wa sheria na taratibu hizo. Akasema kuwa ili kuleta mwafaka katika usimamizi wa mipango miji nchini Tanzania, ni vema Bodi ya NHC na Menejimenti ya Shirika wakaangalia namna wanavyoweza kuwakutanisha wadau wa mipango miji ili kuona namna watakavyoweza kuibadili 12

miji ya Tanzania kwa kuwa na mpango kabambe wa kupanga miji hiyo. Mkutano huo wa wadau utaweza kujadili changamoto zilizopo katika usimamizi wa mipango miji ya Tanzania na kupata ufumbuzi wa changamoto hizo. Kwa mujibu wa Naibu Waziri huyo, katika nchi ya Singapore miji ikishapangwa kulingana na matumizi husika hakuna mtu au taasisi yoyote inayoweza kubadilisha kiholela mpango uliopitishwa tofauti na ilivyo kwa Tanzania. Hata hivyo, alisema changamoto kubwa iliyopo nchini ili kuyafikia hayo ni kutokana na kukosekana kwa uadilifu, nidhamu na utii wa sheria zinazoongoza mipango miji. www.nhctz.com


Naye, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni inayosimamia upangaji wa mji wa Singapore ya Surbana, Tay Hang Hock Luois, alitaja mambo mbalimbali yaliyosaidia upangaji wa mji huo kuanzia ilipopata uhuru wake mwaka 1963, kuwa ni utii wa sheria za mipango miji, usimamizi madhubuti wa serikali wa sheria na taratibu za mipango miji. Ziara hiyo ya mafunzo iliuwezesha ujumbe huo wa Tanzania kutembelea Mamlaka ya Mipango Miji ya Singapore na kampuni inayosambaza majisafi na salama katika mji wa Singapore ya Hyflux ambayo imeonyesha nia ya kupunguza tatizo la maji nchini Tanzania hasa maeneo zinakojengwa nyumba mpya na NHC.

Ujumbe wa NHC ukisikiliza maelezo kutoka kwa watendaji wakuu wa Halmashauri ya jiji la Holland Bukit Panjang Singapore wanaotumia mfumo wa Kampuni Surbana katika kufanikisha na kudhibiti matengenezo ya nyumba.

Ujumbe huo wa Tanzania ulipata pia fursa ya kutembelea Makao Makuu ya Shirika linalohusika na upangaji na uendelezaji miji (Surbana); Mamlaka ya Uendelezaji upya miji - Urban Redevelopment Authority (URA); Housing & Development Board (HDB na Mji mpya wa makazi eneo la Punggol. Shirika la Nyumba liliandaa ziara hiyo ya mafunzo ili kuweza kuwapatia watendaji hao uzoefu na kujifunza toka nchi zilizofanya vizuri duniani katika masuala ya Upangaji wa Miji, Viwango vya Majengo na Mikakati ya Uendelezaji wa Miji Mipya (Satellite Cities) kwa kushirikiana na Sekta binafsi. Ujumbe wa NHC ukisikiliza maelezo kutoka kwa watendaji wakuu wa Surbana ya Singapore.

Ujumbe wa NHC ukiwa katika picha ya pamoja (kutoka kushoto) ni Meneja Uendelezaji Biashara Willliam Genya, Meneja Biashara, Richard Ndeona, Meneja Huduma Miliki za Nyumba Grayson Godfrey, Meneja Fedha, Adolf Kasegenya, Mkurugenzi wa Uendelezaji Miliki, Hamad Abdallah, Jaffar Chege Wambura Ofisa Miliki Arusha, Meneja Mifumo ya Taarifa Suzanne Kyaruzi, Meneja Ofisi ya Mkurugenzi Mkuu Bulla Boma na Emson Kabwogi Afisa wa Ukaguzi wa Ndani NHC. Walikuwa katika ofisi za Mamlaka ya Uendelezaji Miji nchini Singapore.

www.nhctz.com

13

JULAI - DESEMBA 2014

/Nyumba Newsletter


WAWEKEZAJI

• •

Ni wa sekta ya nyumba Wawekezaji wengi waonyesha nia ya kuwekeza Tanzania

NHC yavutia wawekezaji

Na Mwandishi Wetu,

K

atika jitihada kubwa zinazofanywa na NHC katika kutengeneza fursa nyingi kwenye sekta ya uendelezaji wa makazi, Shirika limeweka historia kwenye medani ya kimataifa kwa kufanikiwa kwa mara ya kwanza kufanya kongamano la uwekezaji nchini Dubai. Katika kongamano hilo, Shirika lilifanikiwa kuonyesha fursa zilizopo kwenye sekta ya ujenzi wa nyumba nchini Tanzania, kwa makampuni makubwa ya ujenzi yaliyopo Mashariki ya Kati na kwingineko duniani ambayo yalihudhuria katika kongamano hilo. Tukio hili la kipekee na la kihistoria kwa Tanzania lilizinduliwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dk. Mohamed Gharib Bilal na lilihudhuriwa na makampuni makubwa ya ujenzi Dubai kama Damac, Nahkeel, Jumeirah na Emaar, ambayo yamehusika na ujenzi wa majengo makubwa na maarufu Dubai kama Burj Khalifa, Hoteli za Jumeira na Dubai Mall. Makampuni mengine yaliyohudhuria yalitoka ukanda wa Guba kama Qatar na Bahrain pamoja na nchi nyingine za Korea, Sweden na Romania na yameonyesha nia ya makampuni makubwa ya nchi hizo kuwekeza kwenye sekta ya makazi Tanzania. Akizungumzia kongamano hilo, Mkurugenzi Mkuu wa NHC, Bw. Nehemia Kyando Mchechu, alisema kuwa kongamano la Wawekezaji Wa Sekta ya Makazi Tanzania ni sehemu ya lengo kuu la NHC lenye dhamira ya kupanua ukuaji wa sekta ya nyumba nchini. Mchechu alisema kuwa kongamano hilo lilikuwa ni mkakati wa kuionyesha dunia kuwa Tanzania ni sehemu pekee yenye mazingira mazuri ya uwekezaji na urudishaji wa faida kwenye sekta ya makazi.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal (wa nne kutoka kulia) akijumuika na baadhi ya viongozi wakati alipohudhuria Mkutano wa GBF, uliofanyika kwenye Hoteli ya Atlantis jijini Dubai.

‘Tanzania inatoa fursa ya pekee linapokuja suala la uwekezaji kwenye sekta ya makazi barani Afrika na hii ni kutokana na uwazi pamoja na utulivu wa kisiasa na amani inayopatikana nchini, uchumi unaokua pamoja na ushirikiano mkubwa unaotolewa na serikali” ‘Tukio hili la kihistoria ni sehemu tu ya mpango kamili wa kuifahamisha dunia kuhusu fursa za uwekezaji kwenye sekta ya makazi zinazopatikana nchini” alisema

“Hatujawasahau dada na kaka zetu nyumbani Tanzania, wengi wao wana nafasi kubwa ya kuwekeza katika miradi ya uendelezaji wa sekta ya makazi nchini na tunataka kuhakikisha wanapata fursa hiyo pia”. Nyumba Newsletter/JULAI - DESEMBA 2014

14

Mchechu. Mchechu anaamini kuwa huu ni muda mwafaka kwa wawekezaji kuitazama Tanzania na Afrika kwa ujumla. Alibainisha kuwa hapo zamani ilikuwa ni vigumu kwa wawekezaji kuwekeza Afrika na Tanzania, lakini akasema kuwa kwa uchumi wa leo ni hatari nchi kuwazia kutowekeza Tanzania. Mchechu anasema kongamano hili linalenga kupata wawekezaji wenye uwezo wa kuanzia dola milioni 20 hadi dola nusu bilioni. ‘Tunajua uwezo wa uwekezaji unaotakiwa hauwezi kufikiwa kwa usiku mmoja na ndio maana miradi yetu mingi ni zaidi ya miaka 5 hadi 7, lakini tuna miradi ambayo inaanzia dola milioni kumi hadi www.nhctz.com


nchini Dubai

kuwa vibali vyote vya mradi vimepatikana na kinachotakiwa ni kuwekeza tu na kongamano hili lilikuwa muhimu kwa ajili

kukiwa kuna upungufu wa jumla ya nyumba milioni 3.8 na upungufu huo unakua kwa kiasi cha makazi 200,000 kwa mwaka, ambayo kwa hakika inatoa changamoto kubwa kwa Tanzania lakini ni fursa kubwa kwa wawekezaji’ alisema Makamu wa Rais. Naye, Balozi wa Tanzania kwenye nchi za Falme za Kiarabu, Mheshimiwa Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk akizungumza na wageni waalikwa alisisitiza namna sekta ya makazi ilivyoimarika nchini Tanzania. “Sekta ya makazi ndio sekta inayokua kwa kasi zaidi nchini Tanzania na tunakaribisha wawekezaji kutoka nchi za falme za Kiarabu” alisema Mbarouk. Kadhalika, Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mheshimiwa George B. Simbachawene, alisema kuwa msingi mkuu wa kukua kwa sekta ya makazi Tanzania umetokana na ushirikiano uliopo baina ya serikali na sekta binafsi ambao unaruhusu uwekezaji na ukuaji mzima wa sekta.

Baadhi ya wajumbe waliofika kwenye kongamano la uwekezaji Dubai ambalo lilihudhuriwa na kampuni kubwa za ujenzi Dubai kama Damac, Nahkeel, Jumeirah na Emaar, ambazo zimehusika na ujenzi wa majengo makubwa na maarufu Dubai kama Burj Khalifa, Hoteli za Jumeira na Dubai Mall. Tukio hili la kipekee na kihistoria kwa Tanzania lilizinduliwa na Makamu wa Rais, Dk. MohammedGharib Bilal .

dola milioni mia, kwahiyo kiasi chochote ambacho mwekezaji atakuwa nacho kati ya kiwango hicho tuna fursa za kuwekeza naye’ anasema Mchechu. Kati ya miradi ya NHC iliyoonyeshwa kwa wawekezaji ni pamoja na miradi mitatu ambayo itaendelezwa kwa kipindi cha miaka 5 hadi 10. Hii inajumuisha miradi miwili ya kuendeleza Arusha inayoitwa Safari City na USA River ambayo kwa pamoja itakuwa na jumla ya nyumba 8000, pamoja na mradi wa kuendeleza makazi Dar es Salaam utakaofahamika kama Salama Creek Satellite City ambao utakuwa na jumla ya nyumba 9,500. Miradi hii yote iko tayari kwa maana ya www.nhctz.com

ya kupata uwekezaji unaotakiwa. Akizungumza katika kongamano hilo, Makamu wa Rais, Mheshimiwa Dk Mohamed Gharib Bilal alielezea kuwa serikali ya Tanzania imefanya kazi kubwa ya kutengeneza fursa katika sekta ya makazi ikiwemo kuzifanyia mabadiliko sheria mbalimbali zinazohusu sekta hiyo. Sheria hizo ni pamoja na sheria ya hati pacha, sheria ya mikopo ya nyumba na uanzishwaji wa kampuni ya kuwezesha mikopo ya nyumba (TMRC) ambazo kwa hakika zimechangia mabadiliko makubwa kwenye sekta ya makazi. ‘Tanzania kwa sasa inashuhudia mafanikio makubwa kwenye sekta ya makazi, huku

15

Bw. Mchechu alisema kuwa wawekezaji wa ndani ya Tanzania hawataachwa nyuma na akabainisha kuwa nao watashirikishwa katika kuekeza katika miradi ya ujenzi. “Hatujawasahau dada na kaka zetu nyumbani Tanzania, wengi wao wana nafasi kubwa ya kuwekeza katika miradi ya uendelezaji wa sekta ya makazi nchini na tunataka kuhakikisha wanapata fursa hiyo pia”. Kongamano hili lilifanyika kwa ushirikiano kati ya Balozi Mdogo wa Tanzania Dubai, Mheshimiwa Omary Mjenga pamoja na Balozi Maalumu wa Mambo ya Kiuchumi, Bwana Cleophas Ruhumbika, ambao walishughulikia taratibu za kongamano pamoja na kualika makampuni ya uwekezaji ya Dubai. “Tuna furaha kubwa kufanya kazi bega kwa bega na Shirika la Nyumba la Taifa kwenye tukio hili la kihistoria’ anasema Mjenga. ‘ Sehemu kubwa ya kazi yetu hapa Dubai ni kuwezesha fursa kwa Tanzania ambayo inaendana na wajibu wetu hapa. Pia tuna furaha kubwa kuwa tukio limekuwa la mafanikio makubwa na nina hakika kuwa fursa zaidi za wawekezaji kuja Tanzania zitazidi kufunguka’ anamalizia Mjenga.

JULAI - DESEMBA 2014

/Nyumba Newsletter


HABARI KATIKA Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Anna Kajumulo Tibaijuka katika picha ya pamoja na Wajumbe mpya ya Bodi ya NHC na wakurugenzi wa NHC

Baadhi ya maafisa wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) waliohudhuria mafunzo kazini kuhusiana na masuala ya kisheria ‘Dispute adjudication (Module 3)’ chini ya mkataba wa Shirikisho la Ushauri wa kitaalamu wa kihandisi (FIDIC). Mafunzo hayo yaliratibiwa na Chama cha Wahandisi Washauri Tanzania (ACET).

Mkurugenzi wa shirika la nyumba la taifa Nehemia Mchechu akiwa na mkuu wa wilaya ya Mbeya Norman Sigalla katika maandamano ya Jubilee ya miaka 50 ya shule ya sekondari Mbeya Day. Shirika la Nyumba la Taifa lilichangia kiasi cha shilingi milioni 20.

Nyumba Newsletter/JULAI - DESEMBA 2014

16

www.nhctz.com


PICHA Mkurugenzi wa Fedha wa NHC Felix Maagi akikabidhi hati ya umiliki wa nyumba za makazi za Medeli, Dodoma kwa Mkurugenzi wa Utawala na Raslimali watu wa BOT Bw Leonard Kisarika. BOT imenunua nyumba katika mradi huo kwa ajili ya wafanyakazi wake.

Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Bi.Zakhia Meghji akizungumza kwa ufupi mbele ya wageni waalikwa mbalimbali wakiwemo baadhi ya Wakuu wa Mikoa na Wadau mbalimbali kwenye jukwaa la Uwekezaji wa sekta ya nyumba.

Wabunge na watendaji wa Shirika la Nyumba la Taifa wakiwasili katika eneo la Kunduchi Range (Tanganyika Packers) kilichokabidhiwa kwa Shirika la Nyumba na Jeshi la Wananchi wa Tanzania JWTZ) na baadaye kuelekea mradi wa Kawe City

www.nhctz.com

17

JULAI - DESEMBA 2014

/Nyumba Newsletter


SAFARI CITY - ARUSHA

Nyumba Newsletter/JULAI - DESEMBA 2014

18

www.nhctz.com


UPTOWN - KAWE

www.nhctz.com

19

JULAI - DESEMBA 2014

/Nyumba Newsletter


YAIMARISHA UTENDAJI

NHC YAFANIKIWA KATIKA UTEKELEZAJI MPANGO MKAKATI •

Yaimarisha udhibiti wa rasilimali zake

Sera za kuongeza ufanisi zaanzishwa

Taswira ya Shirika yaboreshwa kwa kuwajali wateja

Mwandishi Wetu,

Moja ya vigezo muhimu kwa taasisi yoyote yenye nia ya kusonga mbele kwa kasi ya kuridhisha ni kuwa na utawala bora kwa maana ya utendaji, uendeshaji na uthibiti wa rasilimali zake unaozingatia viwango vya ubora wa hali ya juu katika kutekeleza majukumu yake ya siku hadi siku. Si ajabu ndio maana hata Shirika la ubora wa viwango la kimataifa au the International Standards Organisation (ISO) limeingiza viwango vya utendaji kazi au utoaji huduma kwa taasisi zisizo na majukumu ya moja kwa moja ya uzalishaji kama ilivyo kwa NHC au taasisi kama Shirika la Posta, Kampuni za uchukuzi nk. Ni kwa msingi huo Shirika la Nyumba la Taifa limeweza kuanzisha utaratibu wa kudhibiti matumizi ili yasizidi makadirio ya bajeti. Mambo kadhaa yaliyoainishwa katika mpango mkakati wa miaka mitano yamepata mafanikio kadhaa na sasa Shirika la Nyumba linaaminika sana katika utoaji wa huduma zake. Kadhalika, Shirika lilikuwa miongoni mwa mashirika ya umma yaliyofuata taratibu za manunuzi kwa kupata alama asilimia 86 kwa mwaka 2012/2013 zikilinganishwa na asilimia 37 za mwaka 2009/2010. Vilevile, Shirika limeanzisha mifumo ya mawasiliano ya teknolojia ambayo imeongeza ufanisi katika uendeshaji wa shughuli zake. Mifumo hii ni pamoja na Mansoft, Document Management System, Asset Management System, Geographical Information System na Fleet Management System. Sera zatayarishwa kuongeza ufanisi Shirika limeanzisha sera mbalimbali ambazo zinaliongoza katika utendaji wa shughuli zake na zinalenga kuongeza ufanisi katika utekelezaji wa majukumu yake. Baadhi ya sera zilizoanzishwa ni pamoja na Sera ya Nyumba Newsletter/JULAI - DESEMBA 2014

Mfumo wa upimaji utendaji kazi waanzishwa ili kuongeza ufanisi

Mafunzo, Sera ya Fedha, Sera ya Uwekezaji, Sera ya Ukaguzi, Sera ya Mawasiliano ya Teknolojia, Sera ya Manunuzi, Sera ya Usimamizi wa Nyumba, Sera ya Huduma kwa Jamii, Sera ya Mawasiliano na vyombo vya habari na Sera ya Afya. Mfumo wa udhibiti na tahadhari ya majanga na matukio hasi waanzishwa Shirika liliweza kuanzisha mfumo wa kutambua mapema tahadhari ya majanga na matukio hasi na hivyo kuepukana na gharama kubwa zinazotokana na majanga hayo. Lafanikiwa katika kutumia rasilimali watu kikamilifu Kuongeza ufanisi katika kutumia rasilimali watu ni moja ya mikakati mipya ya NHC katika kuhakikisha linatimiza majukumu yake kwa ufanisi mkubwa na hivyo kukidhi mahitaji ya wateja na matarajio ya serikali juu ya huduma bora katika sekta ya nyumba hapa nchini. Ili kuweza kutumia vema rasilimali watu iliyo nayo, Shirika liliboresha muundo wake ili uendane na mpango mkakati pamoja na majukumu yake yanayoendelea kupanuka. Vilevile, Shirika linawapatia wafanyakazi wa ngazi za chini mafunzo ya kuwaongezea ujuzi na kuwapangia majukumu mengine yenye tija kwa Shirika. Pamoja na mafanikio haya, Shirika limeweza kuajiri wataalamu wa fani mbalimbali kwa ajili ya kuongeza tija katika utendaji. Ajira hizi mpya, zimeweza kupandisha uwiano kati ya wafanyakazi wenye taaluma na wasiokuwa na taaluma kutoka asilimia 22 kwa 78 mnamo mwaka 2010 na kufikia asilimia 51 kwa 49 hivi sasa. Lengo ni kuwa na uwiano wa wafanyakazi wenye taaluma asilimia 70 dhidi ya wale wasiokuwa na taaluma asilimia 30 ifikapo Juni, 2015.

20

Ili kuboresha utendaji wa kazi, Shirika limeanzisha mfumo wa kupima utendaji wa wafanyakazi wake (balance score card) na kuwatambua wafanyakazi bora kila mwaka kwa ajili ya kuwabakiza (retention) na kuwandaa kuchukua nafasi za walio juu yao (succession plan). Mikataba mbalimbali yaboreshwa kuleta tija Kuanzia mwaka 2010 Shirika liliweza kupitia mikataba kati yake na wadau. Kati ya mikataba 186 ya ubia iliyokuwepo, Shirika lilifuta mikataba 59 ambayo haikuwa na tija kwa NHC na Taifa. Vilevile, Shirika lilirekebisha mikataba mingine 311. Shirika linaendelea na marekebisho ya mikataba ya upangaji kwa ajili ya kuiboresha ili ilete tija kwa Shirika na wapangaji. Marekebisho ya sheria namba 2 ya mwaka 1990 Shirika kwa kushirikiana na Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, linaendelea na mchakato wa kurekebisha Sheria Na. 2 ya mwaka 1990 iliyoliunda upya. Lengo la marekebisho haya ni kuliwezesha kupanua wigo wa shughuli zake za kuwa mwendelezaji mkuu; kuliwezesha kuendesha shughuli zake katika mazingira shindani; kuoanisha sheria ya Shirika na sheria zingine na kuliwezesha kujitafutia mitaji kwenye soko la fedha. Lafanikiwa kupunguza mashauri mahakamani Tangu mwaka 2010 Shirika limeweza kupunguza kesi zilizokuwa mahakamani kwa zaidi ya asilimia 50. Aidha, Shirika lilishinda kesi 185 kati ya kesi 190 ambazo ni sawa na asilimia 97. Vilevile, Shirika limeweza kubuni mikakati ya kuzuia kuibuka kwa kesi mpya. Kwa sasa Shirika lina kesi 121 zilizopo mahakamani katika masuala mbalimbali na nyingi zina muelekeo wa kumalizika hivi karibuni. www.nhctz.com


Kuboresha Taswira ya Shirika Shirika limekuwa likitekeleza mkakati wa kubadili mtazamo hasi juu ya shirika kwa kuanzisha utaratibu wa kuuelimisha umma kuhusu shughuli zake kupitia vipindi vya televisini na redio vya Maisha ni Nyumba. Pamoja na juhudi nyingine za kuboresha utendaji wa Shirika, vipindi hivi vimesaidia kuondoa mtazamo hasi wa jamii na wadau wake na hivyo kupunguza malalamiko dhidi ya Shirika. Mtazamo chanya wa Shirika umeongezeka kutoka asilimia 40 mwaka 2010 na kufikia asilimia 76 mnamo Desemba, 2013. Kuboresha mwonekano wa Shirika (rebranding) Shirika limekamilisha mchakato wa kubadilisha mwonekano wake ili kupanua fursa za biashara, kuondoa mtazamo hasi wa wateja wake na kukuza soka la nyumba za Shirika, ili kwenda sambamba na malengo yake ya sasa. Kuboresha sera ya uwajibikaji kwa jamii Kupitia sera yake ya huduma kwa jamii, Shirika limedhamiria kuchangia katika kupunguza tatizo la ajira kwa vijana. Kwa kushirikiana na Chuo Cha Mafunzo ya Ufundi (VETA) cha Dar es Salaam; Wakala wa Utafiti wa Vifaa bora vya Ujenzi na Majengo (NHBRA); na Halmashauri za Wilaya, Shirika linaendelea na mpango wa mafunzo kwa vijana yanayoambatana na kuwapatia vijana mashine za kutengeneza matofali yanayofungamana (soil-cement stabilized interlocking bricks) na mtaji. Chini ya mpango huu, Shirika limetoa mashine nne kwa kila Halmashauri nchini kwa ajili ya kuwajengea vijana uwezo wa kujiajiri wenyewe kupitia miradi ya kutengeneza matofali. Katika utaratibu huu zaidi ya mashine 700 zimetolewa katika Halmashauri mbalimbali nchini na gharama ya mradi huu inakadiriwa kufikia zaidi ya shilingi milioni 700. Mpango huu utakapokamilika utaweza kuwapatia ajira ya moja kwa moja vijana 7000 kwa awamu ya kwanza. Lengo ni kuendelea na mpango huu mpaka uweze kufikisha ajira za vijana 200,000 kwa nchi nzima.

www.nhctz.com

TANZIA Na Mwandishi Wetu,

MKURUGENZI Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) anasikitika kutangaza vifo vya wafanyakazi wake watano, vilivyotokea kwa nyakati tofauti. Akizungumzia vifo hivyo Mkurugenzi Mkuu, Bw.Nehemiah Mchechu aliwapa pole wafanyakazi wote kwa kuondokewa na wafanyakazi Fatuma Kibiki aliyefariki mwishoni mwa mwaka jana na Rashid Jakulagiza aliyefariki usiku wa kuamkia Alhamisi ya Januari 10 mwaka huu, nyumbani kwake Gongolamboto. Kifo kingine ni cha mfanyakazi Omari Issa Malibiche aliyekuwa dereva aliyefariki dunia nyumbani kwake usiku wa kuamkia Februari 14, mwaka jana. Alizikwa kwao Lindi. Mfanyakazi mwingine wa NHC aliyeiaga Dunia ni Adam Mwinyekule aliyekuwa akifanyia kazi bohari ya Mkoa wa Upanga aliyefariki Machi 17 mwaka jana na kuzikwa kwao Mbeya. Mwaka huu Machi 25, Jeremiah Mchome aliyekuwa Mhasibu Idara ya Fedha Kinondoni alifariki dunia na mazishi yake yakafanyika huko Same, Kilimanjaro. Mfanyakazi mwingine Luangano Kikoti alifariki dunia asubuhi ya Jumamosi ya Aprili 5 mwaka huu katika hospitali ya Tumaini, Dar es Salaam. Shirika pia lilimpoteza Batholomeo Brashi aliyekuwa AfisaNyumba Msaidizi Mkoa wa Iringa aliyefariki mchana wa Oktoba 9 katika Hospitali ya Taifa Muhimbili na ambaye alizikwa kwao Mpanda. Mwingine ni Melesiana Casturi aliyekuwa mhudumu wa ofisi Bukoba aliyefariki tarehe 21 Septemba, 2014 na Joseph Lyapula aliyekuwa Boharia Mkoani Mwanza ambaye alifariki tarehe 1 Novemba, 2014 katika Hospitali ya Mwananchi Jijini Mwanza. Alizikwa nyumbani kwao Heka Manyoni Singida Novemba 4 mwaka huu. “Mungu amewapenda zaidi na imempendeza yeye kuwachukua wenzetu kutangulia katika safari ambayo sote tutapita na kila mtu kwa wakati wake aujuao Mola Maulana,�alisema Mchechu. Amewashukuru wale wote ambao waliweza kwenda kutoa pole na kuwaona ndugu na familia ya Marehemu katika kipindi kigumu cha maombolezo na kwamba uwepo wao ulikuwa ni uwakilishi wa Shirika na Wafanyakazi wote. Amewapa pole wafanyakazi wote, marafiki wa karibu wa Marehemu, ndugu na jamaa wote, Mungu azilaze roho za Marehemu mahala pema Peponi. Amina!

21

JULAI - DESEMBA 2014

/Nyumba Newsletter


MCHANGO WA NYUMBA

Nhc Yadhamiria Kuongeza Mchango Wa

Nyumba Katika Pato La Taifa Na Mwandishi Wetu,

P

ato la ndani la Taifa lolote duniani hutokana na mchango wa sekta mbalimbali za uzalishaji na huduma. Katika sekta hizi aghalabu sekta ya nyumba imejitokeza kuwa na mchango mkubwa katika kila nchi kutokana na ukweli kuwa imejichukulia umuhimu wa pekee katika maisha ya kila siku ya binadamu duniani kote. Ukweli huu upo dhahiri kwa kuwa huwezi kukuta mji wowote mkubwa au mdogo duniani kote usio na nyumba za makazi, majengo ya biashara kama hoteli, kumbi za mikutano, shule na vyuo. Majengo mengine yanatumika kwa uzalishaji kama viwanda na sehemu za kutolea huduma mbalimbali. Ni ukweli usiopingika kuwa sekta ya nyumba inayazunguka maisha ya kila siku ya binadamu. Sekta hii kwa kiasi kikubwa ndio inayomtambulisha binadamu na maendeleo yake au ustaarabu wake kwani kama mji au Jiji limepangwa vema na kujengeka kikamilifu basi taswira inayojengwa kwa watu wa Jiji lile na nchi lililopo huwa ni chanya kwamba nchi hiyo imeendelea na watu wake wana uchumi mzuri. Hii ndio sababu iliyolifanya Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) kuandaa mpango mkakati wa miaka mitano 2010/112014/15 wa kuleta mapinduzi katika sekta ya nyumba hapa nchini. Mkakati huo umelenga kuhakikisha kuwa sekta hii inatoa mchango mkubwa katika kukuza pato la Taifa na uchumi wa nchi kwa ujumla. Taarifa za kitaalamu juu ya mchango wa sekta ya nyumba kwa pato na uchumi wa Taifa hapa nchini zinaonyesha kuwa sekta hiyo inatoa mchango wa asilimia 1.0 tu huku sekta hiyo hiyo katika nchi zilizoendelea huchangia kati ya asilimia 50 mpaka 70 ya pato la Taifa kwa mwaka. Katika kuhakikisha sekta ya nyumba inachangia kwa kiasi kikubwa pato la Taifa mpango mkakati wa NHC unalenga

Nyumba Newsletter/JULAI - DESEMBA 2014

Mchoro wa namna litakavyokuwa jengo la Eco Residence litakaloanza kujengwa katika kitalu namba 67 kwenye makutano ya mitaa ya Ngano na Wakulima, Dar es Salaam litakapokamilika litakuwa na ghorofa 16, sehemu za makazi 118 na kuwa makazi ya watu zaidi ya 840 wakati kabla lilikuwa makazi ya familia moja

kuhakikisha kuwa sekta hii inakuza pato na uchumi wa Taifa hadi kufikia asilimia 11. Kwa sasa Tanzania inakabiliwa na changamoto ya uhaba mkubwa wa nyumba bora ambao unakadiriwa kuwa zaidi ya nyumba 3,000,000 huku pengo hilo likikua kwa takriban nyumba 200,000 kwa mwaka. Upungufu wa nyumba ni mkubwa zaidi sehemu za mijini ambako asilimia 37.5 ya Watanzania ndiko wanakoishi. Shirika la Nyumba la Taifa likiwa chombo cha Serikali, linatarajiwa kukabiliana na changomoto hii.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, kutokana na kuongezeka kwa mahitaji ya nyumba nchini na mchango wa nyumba katika kukuza ustawi wa wananchi, Serikali ililiagiza Shirika kujielekekeza zaidi kwenye ujenzi wa nyumba badala ya usimamizi wa miliki

22

zake pekee. Kwa kupitia ujenzi wa nyumba na hasa zile za gharama nafuu, Shirika linatakiwa kuwawezesha wananchi kumiliki nyumba kupitia fursa ya Sheria za Hati Pacha na Mikopo ya Nyumba za mwaka 2008. Ili kufanikiwa katika kukidhi matarajio ya serikali kwa upande mmoja na yale ya wananchi kwa upande wa pili, serikali iliagiza NHC kutumia miliki zake kwa ajili ya maendeleo na kuweza kujiendesha kibiashara. Shirika la Nyumba la Taifa limekuwa katika safari ndefu ya kuleta mageuzi katika sekta ya miliki nchini tangu Serikali ilipoamua kufanya mageuzi katika utendaji kazi na uendeshaji kazi wake. Katika safari hii, Shirika limepewa jukumu la kutatua uhaba wa nyumba pamoja na kukuza mchango wa

www.nhctz.com


MALENGA WETU

sekta hii ambayo mchango wake kwenye pato la Taifa bado upo chini, ukilinganisha na uwezo wa sekta nzima ya ujenzi wa nyumba nchini. Kutokana na umuhimu wa sekta ya nyumba katika kuchangia maendeleo ya jamii na ukuaji wa uchumi, Shirika lilitayarisha mpango mkakati wa miaka mitano ambao umekuwa dira ya kuleta msukumo mpya wa sekta ya nyumba nchini.

HEBU TUFUNGE MIKANDA 1. Naanza kuwasalimu, wafanyakazi wa nyumba

8. Tulikotoka zamani tulikuwa na aibu

Nyote ninawaheshimu, awaongoze muumba ,

Viongozi na jirani hata wale maswaibu

Tuyashike ya muhimu, ili tusije kuyumba

Tulisema hadharani, rushwa imetuaribu

Kutokana na kufanikiwa kwa kiasi kikubwa kutekelezwa kwa mpango mkakati wa 2010/11-2014/15 thamani ya mali za shirika ambazo kwa asilimia kubwa ni nyumba na majengo mbalimbali inaonyesha kukua hadi kumiliki majengo 2,389 yenye sehemu ya nyumba 17,111 yenye thamani ya shilingi trilioni 2.911

Shirika sasa lapaa hebu tufunge mikanda

Shirika sasa lapaa hebu tufunge mikanda

Juhudi zilizofanywa za mabadiliko ya sekta ya nyumba zilianza Machi 2010, ambapo Serikali iliteua uongozi mpya wa Shirika kwa maana ya Bodi ya Wakurugenzi na Menejimenti kwa nia ya kuimarisha utendaji na ufanisi wa Shirika ili liweze kuwa na mchango mkubwa katika kutatua tatizo la uhaba wa nyumba nchini. Jukumu la kwanza la uongozi huu, lilikuwa ni kutayarisha mpango mkakati wa ambao umeainisha mwelekeo mpya na malengo mapya ya Shirika. Kwa kiasi kikubwa uongozi wa NHC ulioteuliwa mwaka 2010 unahusika na kuongezeka kwa kasi ya ujenzi wa nyumba za Shirika ambazo ama zinauzwa au kupangishwa. Ni uongozi huu ambao umeleta chachu ya kuona kuwa sekta ya nyumba kupitia NHC inachangia kwa kiwango cha juu zaidi katika ukuaji wa pato la ndani kwa kujiwekea lengo la kuchangia asilimia 11 ya pato la Taifa kwa kushirikisha wadau wa sekta hii zikiwemo benki. Hivi sasa nyumba za gharama nafuu zimejengwa katika mikoa takriban 19 huku nyumba za vitega uchumi na za makazi kwa ajili ya watu wa kipato cha kati na juu zikiwa zimeshamiri kujengwa na kuuzwa katika maeneo mbalimbali nchini.

www.nhctz.com

2.

Leo nasema ukweli, siyo kama najigamba

Mambo yameshamiri, uwanjani tunatamba

Tuwe sote stamili, mafanikio kuchimba

Shirika sasa lapaa, hebu tufunge mikanda

3.

Mikakati tulopanga, neema yajitokeza

Rushwa haitasikika, mabaya kutokomea

Hakuna wa kutupinga , kwa pamoja tumeweza

Shirika sasa lapaa hebu tukaze mikanda

Tumetengeza mizinga, tuachane na kucheza

Shirika sasa lapaa, hebu tufunge mikanda

10. Ewe kipenzi cha watu, juhudizo endeleza

4.

Tulipokuwa Singida, malengo tumeyaweka

Tukamilishe kwa muda, tusije tukabweteka

Kila mjumbe shuhuda, malengo kukamilika

Shirika sasa lapaa, hebu tufunge mikanda

5.

Kwa pamoja tunaweza, kujenga nyumba kwa wingi

9. Tumshukuru Rabuki, Mchechu katuletea Kaja nusuru Shirika, leo tunaendelea

Angalia kila mtu, kipatoche kuongezeka Tupamoja kila kitu, Jahazi kuliongoza Shirika sasa lapaa, hebu tufunge mikanda 11. Viongozi waridhika, ubingwa tumeshapewa

Tusije tukapotoka, kwa sifa tunazopewa

Tuweze kutekeleza, hiyo sera ya msingi

Buti tumeshalikaza, kujenga nyumba kwa wingi

Jahazi likitoboka tutakuja laumiwa

Shirika sasa lapaa hebu tufunge mikanda

6.

Kwa spidi tumeanza Mindu, Ubungo Kibada

Katavi na kule Mwanza, Mchikichini Singida

12 . Tamati nimeshafika, kalamu naweka chini

Za kuuza na kutunza, hiyo ndiyo yetu mada

Shirika sasa lapaa, hebu tufunge mikanda

Shirika sasa lapaa, hebu fungeni mikanda

Niwaache wahusika, waingia mitamboni

Maneno haya kushika tukiwepo vituoni

7. Natoa msisitizo, bidii iwe kazini

Shirika sasa lapaa, hebu tufungeni mikanda

Ili uje pata tuzo, kaskedi kusaini

Ukileta matatizoutaja tozwa faini

Shirika sasa lapaa, hebu tufunge mikanda

(Doctor) MOHAMMED MNEKA BOX 2977, DAR ES SALAAM.

23

JULAI - DESEMBA 2014

/Nyumba Newsletter


BARAZA LA WAFANYAKAZI

KATIBU MKUU ARDHI AFUNGUA BARAZA KUU LA WAFANYAKAZI limeweka msingi mkubwa wa kukumbukwa katika Taifa letu na vizazi vijavyo kama tunavyomkumbuka Baba wa Taifa wa kueneza ujenzi wa nyumba za gharama nafuu katika miji mingi baada ya Uhuru wa Taifa letu. “ Ili kuzifanya nyumba hizo zinazojengwa kuwa nafuu, narudia kusisitiza agizo alilolitoa Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Jakaya Mrisho Kikwete kuwa Halmashauri za Miji na Wilaya zilipatie Shirika la Nyumba na waendelezaji wengine wa Miliki maeneo ya kujenga nyumba hizo bila kuhitaji fidia kubwa,” alisema.

Picha ya pamoja ya Wajumbe wa kikao cha Baraza Kuu la Wafanyakazi wa Shirika la Nyumba la Taifa kilichofanyika hoteli ya Tanga Beach Resort, Tanga

• • •

Asisitiza uadilifu katika utendaji kazi ili kuleta tija Ataka kasi ya ujenzi wa nyumba za gharama nafuu iendelezwe Wafanyakazi waazimia kuongeza tija katika utendaji

Na Mwandishi Wetu,

Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Alfayo Japan Kidata amefungua kikao cha Baraza Kuu la Wafanyakazi wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), akisisitiza uadilifu mkubwa miongoni mwa wafanyakazi ili kuliwezesha Shirika kutoa huduma za makazi zilizo bora kwa wananchi. Akizungumza wakati wa ufunguzi wa kikao hicho kilichofanyika kwenye Hoteli ya Tanga Beach Resort, jijini Tanga, Bw. Kidata alisema kuwa uadilifu ndiyo utakaowawezesha wafanyakazi wa Shirika kutenda kazi zao kwa ufanisi mkubwa. Alisema kuwa wafanyakazi hao wakitenda kazi zao kwa juhudi na maarifa huku wakitambua umuhimu mkubwa wa sekta ya nyumba waliyopewa dhamana ya kuisimamia, kutalifanya Shirika hilo kuweza Nyumba Newsletter/JULAI - DESEMBA 2014

kutekeleza malengo yake ya kuwajengea Watanzania nyumba bora. Alisema utendaji kazi wenye uwazi, uadilifu na weledi wa hali ya juu ndiyo utakaowaongezea heshima kubwa wafanyakazi hao na kujenga taswira nzuri ya Shirika katika jamii ya watanzania. Akizungumzia kasi ya ujenzi wa nyumba za gharama nafuu katika miji mbalimbali ya Halmashauri za Miji na Wilaya nchini, Katibu Mkuu huyo alilipongeza Shirika kwa kurejesha utaratibu huo wa kizalendo aliouanzisha Baba wa Taifa.

Alisema pamoja na juhudi na ubunifu mbalimbali uliofanywa na NHC uliosaidia kuongeza kasi ya ujenzi wa nyumba za kada zote, Serikali inaamini kuwa kasi ikiongezeka zaidi katika ujenzi wa nyumba, licha ya kuwa Shirika litakuwa limetekeleza ilani ya uchaguzi ya chama tawala na litakuwa limeisaidia pia Serikali katika juhudi zake za kuondoa umaskini nchini. Likiwasilisha maazimio ya Mkutano huo wa Baraza Kuu, yaliyowasilishwa na Meneja wa Mkoa wa Tabora Bw. Erasto Chilambo, wajumbe wa Baraza hilo wamemshukuru Katibu Mkuu kwa kuwa mstari wa mbele katika kufanikisha uandaaji wa Mpango Mkakati wa Shirika wa miaka kumi unaoanzia 2015. Aidha, Baraza linamshukuru kwa kufanikisha upatikanaji wa hati miliki ya eneo la Kawe, Tanganyika Packers.

“ Nafahamu kuwa hivi sasa mmeshaifikia mikoa 19 na mnayo matumaini makubwa ya kufikia mikoa yote kufikia Desemba mwaka huu. Utaratibu huu unaolenga kuwawezesha wananchi wa kipato cha kati na chini kumiliki nyumba, umepongezwa sana na Serikali Kuu na viongozi mbalimbali wakiwemo Waheshimiwa Wabunge.

Kadhalika, Baraza hilo limeazimia kila mkoa uhakikishe unaongeza mapato yake ili kupata uwezo wa kujiendesha kibiashara. Ili kufanikisha hilo, jitihada zitafanyika kwa kila mkoa kuwezeshwa kupata walau mradi mmoja wa jengo la biashara ambalo litaongeza mapato ya mkoa husika.

Hivyo, mnayo dhima na jukumu kubwa la kuusimamia mpango huu ili ndoto hiyo ya kuwawezesha watu wengi kumiliki nyumba iweze kutimizwa,”alisema.

Aidha, alisema kwa kuwa ujenzi wa nyumba za gharama nafuu ni kioo cha Shirika la Nyumba mbele ya Jamii, jitihada zote zichukuliwe kuhakikisha kwamba miradi yote inajengwa na kusimamiwa

Alisema kwa kufanya hivyo Shirika litakuwa 24

www.nhctz.com


MILIKI NYUMBA

kwa kuzingatia ubora, muda na gharama iliyokusudiwa. Baraza hilo liliazimia pia kuwa makusanyo ya kodi ni uti wa mgongo wa uendeshaji wa majukumu mbalimbali ya Shirika, hivyo mikoa yote inawajibika kukusanya mapato yote kwa wakati. Azimio jingine ni kuhakikisha kuwa mikoa yote iwezeshwe kufanya matengenezo yote ya lazima kwa majengo ya Shirika ili kuboresha huduma kwa wapangaji. Azimio jingine la Baraza lililotolewa ni kuongeza jitihada za kuuza na nyumba na kukusanya mapato ya mauzo ya nyumba hizo zifanyike siyo tu na kitengo cha mauzo bali liwe jukumu nambari moja kwa kila mfanyakazi na hasa katika kipindi hiki ambapo Shirika limepanua wigo wa ujenzi wa nyumba za makazi na biashara nchi nzima. Naye, Mkukurugenzi Mkuu wa NHC, Bw. Nehemia Kyando Mchechu, alisema licha ya Shirika kupata mafanikio kadhaa,, zipo changamoto zinazoikabili sekta ya nyumba ikiwemo gharama kubwa ya vifaa vya ujenzi na upatikanaji wa mikopo ya nyumba ya muda mrefu yenye riba nafuu. Bw. Mchechu alisema kuwa, ikiwa Serikali itapunguza kodi gharama ya nyumba inaweza kupungua, jambo ambalo linaweza kuwasaidia wananchi wa kawaida kuzinunua. “Tunaiomba Serikali kuangalia upya kodi zilizoongezeka, kwa sababu zimechangia kupanda kwa gharama za nyumba,�alisema Mchechu.

Hatua rahisi za kumiliki

nyumba yako leo 1 2 3 4 5

Chukua fomu ya kununua Nyumba kutoka ofisi yoyote ya mkoa popote nchini au kwenye tovuti ya shirika. Rudisha fomu iliyojazwa ikiwa na uthibitisho wa kulipiwa na malipo ya 10% (ikiwa na VAT) ya thamani ya Nyumba husika. Maombi yako yatapitiwa kwa umakini ili kuhakikisha kunakuwa na usawa katika uchaguaji wa watu wanaostahili kulingana na Vigezo na masharti ya NHC na taratibu za Jamhuri ya Tanzania. Kama umefanikiwa, utatumiwa barua za kuthibitishiwa kukubaliwa maombi yako. Barua zitatolewa kwa wote waliokidhi Vigezo vilivyowekwa. Utatakiwa kulipa 90% iliyobaki kulingana na thamani ya nyumba husika ndani ya siku 90 tangu umepewa.

6 7 8 9

Endapo ukishindwa kulipa ndani ya siku 90, NHC itatoa nyumba kwa Waombaji waliopo kwenye orodha ya wanao subiri. Orodha ya wanaosubiri itakuwa na majina ya waombaji waliolipia malipo ya mwanzo lakini wakakosa nafasi kwa kuwa nyumba zote zilishapata watu. Kama ukishindwa kulipia kiasi kilichobakia, au ukakosa nafasi ukiwa kwenye orodha ya wanaosubiri, kiasi cha 10% kilicholipwa kinaweza kutumiwa kulipia kwenye miradi mingine ya NHC na waliopo kwenye orodha ya wanaosubiri au kurudishiwa pesa zao. Mauzo ya nyumba za mradi husika yatatangazwa yamefungwa pindi Waombaji waliofanikiwa kupata nyumba wamemaliza kufanya malipo yao yote.

10 NHC itafanya utaratibu wa kutafuta hati za nyumba na kisha kuwapatia

wanunuzi walioweza kulipia pesa zote taslimu au kupitia taratibu za mkopo. Miliki nyumba yako sasa. Kumiliki nyumba

Alisema, mkakati uliopo ni kuhakikisha kuwa, miradi iliyoanzishwa inakwisha katika kipindi kilichopangwa ili iweze kusaidia wananchi.

Utaratibu huu unaolenga kuwawezesha wananchi wa kipato cha kati na chini kumiliki nyumba, umepongezwa sana na Serikali Kuu na viongozi mbalimbali wakiwemo Waheshimiwa Wabunge

www.nhctz.com

25

JULAI - DESEMBA 2014

/Nyumba Newsletter


SHIRIKA LA NYUMBA LA TAIFA Makao Makuu S.L.P 2977 SIMU: +255 22 2105002 NUKUSHI: +255 22 2105000 BARUA PEPE: dg@nhctz.com TOVUTI: www.nhctz.com TUNAJENGA TAIFA LETU

1.

MKOA WA UPANGA S.L.P 9634, Dar es Salaam SIMU: 022 2128314 022 2128305 / 022 2128306

2 .

MKOA WA KINONDONI S.L.P 23200, Dar es Salaam SIMU: 022 2667150

3 .

MKOA WA ILALA S.L.P 25110 Dar es Salaam SIMU: 022 2863126

4.

MKOA WA TEMEKE S.L.P 45674 Dar es Salaam SIMU: 022 2866829 022 2863121

5.

MKOA WA MWANZA /GEITA /SIMIYU S.L.P 1683, Mwanza SIMU: 028 2503047 028 2503048

8.

MKOA WA MBEYA/NJOMBE S.L.P 541, Mbeya SIMU: 025 2502482 025 2500699

15.

MKOA WA DODOMA S.L.P 391, Dodoma SIMU: 026 2323151

9.

MKOA WA ARUSHA S.L.P 883, Arusha SIMU: 027 2755052 027 2502995

16.

MKOA WA SHINYANGA S.L.P 478, Shinyanga SIMU: 028 2762045

10.

MKOA WA KILIMANJARO S.L.P 1458, Moshi SIMU: 027 2755052 027 2754080

17.

MKOA WA KAGERA S.L.P 369, Bukoba SIMU: 028 2220035/36

18.

MKOA WA SINGIDA S.L.P 254, Singida SIMU: 026 2502332

19.

MKOA WA KIGOMA S.L.P 271, Kigoma SIMU: 028 2802844

20.

MKOA WA LINDI S.L.P 206, Lindi SIMU: 023 2202054

11.

MKOA WA TANGA S.L.P 5041, Tanga SIMU: 027 2644479 027 2644480

12.

MKOA WA MOROGORO S.L.P 892 Morogoro SIMU: 023 2603268 023 2604535

6. MKOA WA MTWARA S.L.P 67, Mtwara SIMU: 023 23333

13.

MKOA WA IRINGA S.L.P 206, Iringa SIMU: 026 2702603

7. MKOA WA TABORA S.L.P 166, Tabora SIMU: 026 2604530 026 2604752

14.

MKOA WA MARA S.L.P 257 Musoma SIMU: 028 2622032

Nyumba Newsletter/JULAI - DESEMBA 2014

26

21. MKOA WA RUVUMA S.L.P 65, Songea Ruvuma 22. MKOA WA KATAVI S.L. P 375 MPANDA,KATAVI.

www.nhctz.com


Turn static files into dynamic content formats.

Create a flipbook
Issuu converts static files into: digital portfolios, online yearbooks, online catalogs, digital photo albums and more. Sign up and create your flipbook.