Child Labour and Child Work brief

Page 1


MUHTASARI

Kazi za Watoto na Utumikishwaji Watoto Tanzania

USHAHIDI KUTOKA UTAFITI WA WATU WENYE

UWEZO WA KUFANYA KAZI (2014–2021)

MUHTASARI

Kazi za Watoto na Utumikishwaji Watoto Tanzania

USHAHIDI KUTOKA UTAFITI WA WATU WENYE UWEZO WA KUFANYA KAZI (2014–2021)

© Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali Zanzibar na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto

Dodoma, Novemba 2024

Picha ya jalada: © UNICEF/Shehzad Noorani

Uhariri na mpangilio: Handmade Communications

Vifupi vya maneno

ILFS Integrated Labour Force Survey

(Utafiti wa Watu wenye Uwezo wa Kufanya Kazi)

ILO International Labour Organization (Shirika la Kazi Duniani)

NBS National Bureau of Statistics (Ofisi ya Taifa ya Takwimu)

OCGS Office of the Chief Government Statistician Zanzibar (Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali Zanzibar)

UNICEF United Nations Children’s Fund (Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto)

URT United Republic of Tanzania (Jamhuri ya Muungano wa Tanzania)

Muhtasari: Kazi za watoto na utumikishwaji watoto nchini Tanzania

MAENDELEO KATI YA MWAKA 2014 NA 2021

Kazi za watoto

Tanzania Bara: kutoka 34.9% hadi 25.8%

Zanzibar: kutoka 9.9% hadi 7.6%

Utumikishwaji watoto Ajira hatarishi

Tanzania Bara: kutoka 34.8% hadi 25.5%

Zanzibar: kutoka 9.5% hadi 7.5% Tanzania Bara: kutoka 34.3% hadi 24.8%

kutoka 9.1% hadi 7.4%

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MNAMO MWAKA 2021

Kazi za watoto

Utumikishwaji watoto Ajira hatarishi

Takriban watoto

milioni 5.1

UTUMIKISHWAJI WATOTO

zaidi ya milioni 5

watoto milioni 4.9

Saa za kazi kwa wiki 22.5 ya utumikishwaji wa watoto inatokea katika sekta ya kilimo 84.1%

Umri:

AJIRA HATARISHI

Miongoni mwa watoto walio katika ajira hatarishi, asilimia 82.8 wanafanya kazi hatarishi (zaidi kwenye kilimo); asilimia 75.5 wapo katika ajira zenye mazingira hatarishi (mfano, kubeba mizigo mizito, kufanya kazi katika maeneo yenye vumbi, moshi, gesi, au kufanya kazi usiku) na asilimia 19.5 hufanya kazi kwa saa nyingi

Chanzo: Uchambuzi wa Mwandishi kwa kutumia takwimu

Utangulizi

Taarifa hii fupi inawasilisha kwa muhtasari matokeo ya ripoti ya Child Work and Child Labour in the United Republic of Tanzania: Evidence from the Integrated Labour Force Survey (2014–2021), inayotokana na takwimu za hivi za karibuni za Utafiti wa Watu Wenye Uwezo wa Kufanya Kazi (ILFS) wa mwaka 2020/21.

Hii ni tathmini ya kwanza kuhusu Kazi za Watoto na Utumikishwaji Watoto

ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutoa matokeo yanayohusu nchi nzima, ikijumuisha Tanzania Bara na Zanzibar. Pia inaonesha mwenendo wa viashiria kwa kutumia taarifa kutoka Utafiti wa Watu Wenye Uwezo wa Kufanya Kazi wa mwaka 2014 ambazo zilitumika kwenye tathmini ya awali ya ajira ya watoto kwa Tanzania Bara (ILO and NBS, 2016) na Zanzibar (OCGS, 2016).

Matokeo yanaweza kutumika kufuatilia maendeleo na juhudi za Serikali kuelekea kufikia Malengo ya Maendeleo Endelevu (Sustainable Development Goal ) hususan lengo la 8.7 linalohusu kukomesha utumikishwaji watoto katika namna zake zote na lengo la 16.2 linalohusiana kukomesha unyanyasaji, unyonyaji na biashara haramu ya watoto.

LENGO NAMBA 8.7 LA MALENGO YA MAENDELEO ENDELEVU

LENGO NAMBA 16.2 LA MALENGO YA MAENDELEO ENDELEVU

Kutokomeza utumikishwaji wa watoto wa aina zote

Kukomesha utumwa wa kisasa, biashara haramu na utumikishwaji watoto

Dhana muhimu

Kazi za watoto: Ushiriki wa watoto wenye umri wa miaka 5–17 katika shughuli yoyote ya kuzalisha bidhaa au kutoa huduma kwa matumizi ya wengine au kwa matumizi yao wenyewe kwa angalau saa moja kwa wiki.

Utumikishwaji watoto: Ushirikishwaji wa watoto katika kazi zilizopigwa marufuku na aina za kazi ambazo hazikubaliki kijamii na kimaadili kama inavyoelekezwa na sheria za nchi. Utumikishwaji watoto hujumuisha (1) aina mbaya zaidi za utumikishwaji watoto, ikiwemo ajira hatarishi za watoto, na (2) kufanyishwa kazi chini ya umri stahiki.

Utumikishwaji watoto katika ajira hatarishi: Ushiriki wa watoto katika eneo hatarishi la kazi au kazi hatarishi na katika hali hatarishi (mfano, kufanya kazi kwa muda mrefu, mazingira ya kutumia mashine hatarishi na vitu hatarishi na kubeba mizigo mizito).

Namna ya kupima kazi za watoto na utumikishwaji watoto

Ripoti hii imetumia takwimu kutoka tafiti mbili za utafiti wa Watu Wenye

Uwezo wa Kufanya Kazi (ILFS) zilizofanyika kati ya mwaka 2014 na 2020/21. Utafiti wa ILFS unajumuisha maswali yaliyoulizwa kwa watoto wenye umri wa miaka 5–17 kuhusu ushiriki kwenye shughuli za kiuchumi na zisizo za kiuchumi, mahudhurio ya shule, jumla ya saa ambazo watoto wamefanya kazi na vipengele vyenye maswali kuhusiana na afya na usalama katika mazingira ya kazi.

MBINU ZA UCHAMBUZI WA TAKWIMU

Uchambuzi unajumuisha maelezo ya viwango vya watoto wanaoshiriki kwenye kazi, wanaotumikishwa na na wanaotumikishwa katika ajira hatarishi, ikiwa ni pamoja na taarifa zingine kama wastani wa saa za kazi, sekta zinazohusishwa na ajira hizi, vichocheo vya utumikishwaji watoto, na kadhalika, ili kupata takwimu kuhusu watoto kufanya kazi na kutumikishwa katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Matokeo yote yametolewa kwa Tanzania Bara na Zanzibar.

TAKWIMU

Viwango vya kimataifa na mifumo ya kisera

MIFUMO

Viwango vya kimataifa kama vile vya Mkataba wa Shirika la Kazi Duniani

Namba 138 kuhusu Umri wa Chini na Mkataba Namba 182 kuhusu Aina Mbaya Zaidi za Utumikishwaji Watoto, pamoja na mifumo muhimu ya kitaifa kama vile Sheria ya Mtoto (2009, kama ilivyorekebishwa mwaka 2019) na Sheria ya Ajira na Mahusiano ya Kazi (2004, kama ilivyorekebishwa mwaka 2019) kwa Tanzania Bara na Sheria ya Watoto Namba 6 (2011) na Sheria ya Ajira Namba 11 (2005) ya Zanzibar zilitumika kama miongozo mikuu kwa ajili ya sera na programu kuhusu kazi za watoto na utumikishwaji watoto.

Mifumo ya kitaifa

TANZANIA BARA

• Sheria ya Mtoto (2009, iliyorekebishwa mwaka 2019): “Mtu hatamwajiri au kumfanyisha mtoto kazi ambazo zinaweza kuwa na madhara kwa afya, elimu, akili, mwili au kwa maendeleo ya kimaadili ya mtoto.”

• Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini (2004, iliyorekebishwa mwaka 2019)

ZANZIBAR

• Sheria ya Watoto Namba 6 (2011): “Hakuna mtu yeyote atakayemwajiri mtoto (yaani, mtu yeyote chini ya umri wa miaka 17) katika aina yoyote ya kazi isipokuwa kazi za nyumbani,” ambapo kazi hizo za nyumbani hazipaswi kuathiri uwezo wa mtoto kuhudhuria masomo na kuwa na muda wa kutosha wa kupumzika.

• Sheria ya Ajira Namba 11 (2005)

Matokeo muhimu

MUHTASARI

Mwaka 2021, karibu mtoto mmoja kati ya wanne wenye umri wa miaka 5–17 alihusishwa katika kazi na utumikishwaji watoto. Takriban watoto milioni

5.1 au asilimia 25.3 ya watoto wenye umri huo walishirikishwa kufanya kazi nchini Tanzania: asilimia 25.8 kwa Tanzania Bara na asilimia 7.6 kwa Zanzibar. Nchini Tanzania, asilimia 25.0 ya watoto wenye umri wa miaka 5–17 (zaidi ya watoto milioni 5) walihusishwa kwenye utumikishwaji watoto: asilimia 25.5 kwa Tanzania Bara na asilimia 7.5 kwa Zanzibar (angalia Kielelezo Namba 1). Karibu watoto wote wanaofanya kazi pia walihusishwa kwenye utumikishwaji watoto, na idadi kubwa wanatumikishwa katika ajira hatarishi kwa watoto. Hii ina maana kwamba watoto wengi wanaofanya kazi wanakabiliwa na madhara yanayoweza kuathiri ustawi wao na uwezo wao wa baadaye.

Kielelezo Namba 1: Kazi za watoto, utumikishwaji watoto na utumikishwaji watoto katika ajira hatarishi, miongoni mwa watoto wa umri wa miaka 5–17, Tanzania

URT Tanzania Bara Zanzibar

ya watoto

watoto katika ajira hatarishi

Chanzo: Uchambuzi wa Mwandishi kwa kutumia takwimu za Utafiti wa Watu wenye Uwezo wa Kufanya Kazi wa mwaka 2020/21

Asilimia
Kazi za watoto
Utumikishwaji
Utumikishwaji watoto

KAZI ZA WATOTO

Takriban watoto milioni 5.1 wanaofanya kazi Tanzania wanafanya kazi kwa wastani wa saa 20.0 kwa wiki (saa 20.0 kwa Tanzania Bara na saa 20.8 kwa Zanzibar). Watoto hao wanasema sababu kuu zinazopelekea wao kufanya kazi ni (1) ili kuweza kujifunza na kukuza ujuzi katika nyanja mbali mbali, kama sehemu ya makuzi yao, (2) kusaidia mradi/shughuli za familia, na (3) kuchangia pato la kaya (angalia Kielelezo Namba 2).

Uhusiano mkubwa kati ya kazi za watoto na utumikishwaji watoto Tanzania Bara na Zanzibar unaonesha kuwa karibu asilimia 98 ya watoto wanaofanya kazi wanafanya hivyo katika mazingira ya utumikishwaji (angalia Kielelezo Namba 3). Uhusiano huu unatokana zaidi na watoto kujihusisha na aina za kazi hatarishi (mfano, kilimo) au katika mazingira hatarishi (mfano, kubeba mizigo mizito na kuhusishwa na matumizi ya mashine hatarishi au vifaa hatarishi).

Kielelezo Namba 2: Sababu zinazotolewa na watoto ambazo zinapelekea kufanya kazi

Kujifunza ujuzi (kama sehemu ya malezi na makuzi)

Kusaidia mradi/ shughuli za familia

Kuchangia pato la kaya Hali ya kutaka kuwa sawa na wengine

Kuchangia pato la kaya mbali na wanapoishi

Chanzo: Uchambuzi wa Mwandishi kwa kutumia takwimu za Utafiti wa Watu wenye Uwezo wa Kufanya Kazi wa mwaka 2020/21

Kutokuwa na uwezo wa kugharamia elimu

Sababu nyingine

Kielelezo Namba 3: Uhusiano kati ya kazi za watoto na utumikishwaji watoto

Kazi za watoto (25.3%)

Watoto wanaotumikishwa (25.0%)

Watoto wanaofanya kazi lakini hawatumikishwi (0.4%)

Watoto wanatumikishwa katika ajira hatarishi (24.3%)

UTUMIKISHWAJI WATOTO

Watoto wasiofanya kazi na hawatumikishwi (74.6%)

Chanzo: Uchambuzi wa Mwandishi kwa kutumia takwimu za Utafiti wa Watu wenye

Uwezo wa Kufanya Kazi wa mwaka 2020/21

Watoto wapatao milioni 5 (asilimia 25.0) wanatumikishwa, ambapo watoto milioni 4.9 wanatumikishwa kwenye ajira hatarishi.

Nchini Tanzania, asilimia 25.0 ya watoto wenye umri wa miaka 5–17 wanahusishwa na utumikishwaji watoto, wakati asilimia 75.0 aidha hawafanyi kazi kabisa au wanafanya kazi zisizo na madhara (karibu watoto milioni 15.1). Watoto wanaotumikishwa wana uwezekano mkubwa wa kufanya kazi za kilimo zisizo za malipo (asilimia 84.1); kwa hakika utumikishaji watoto ni mkubwa zaidi maeneo ya vijijini (asilimia 29.6 dhidi ya asilimia 4.7 kwa Dar es Salaam na asilimia 13.8 maeneo mengine ya mijini). Kiwango cha utumikishwaji watoto kinaongezeka kadri watoto wanavyokuwa na umri mkubwa, kutoka asilimia 14.6 ya watoto wa umri wa miaka 5–11 hadi asilimia 46.4 ya watoto wa umri wa miaka 15–17. Utumikishwaji watoto ni mkubwa miongoni mwa wavulana kuliko wasichana (asilimia 27.1 dhidi ya asilimia 22.9) na wasichana wana uwezekano mkubwa kuliko wavulana kushiriki katika kazi za nyumbani zisizo za malipo (asilimia 86.7 dhidi ya asilimia 81.8). Watoto wanaohusishwa na utumikishwaji wanatumikishwa kwa wastani wa saa 22.5 kwa wiki.

UTUMIKISHWAJI WA WATOTO KATIKA AJIRA HATARISHI

Idadi kubwa ya watoto wanaohusishwa na utumikishwaji pia wanatumikishwa katika ajira hatarishi (asilimia 24.3 ya watoto wenye umri wa miaka 5–17 au watoto milioni 4.9). Asilimia 2.8 tu ya watoto wanaohusishwa na utumikishwaji hawashiriki katika ajira hatarishi au mazingira hatarishi (mfano, kufanya kazi chini ya umri stahiki). Ajira hatarishi (mfano, kilimo) pamoja na mazingira hatarishi (mfano, kufanya kazi usiku, kubeba mizigo mizito au kufanya kazi katika mazingira yenye vumbi, moshi, au gesi) ndio vitu vikuu vinavyochangia utumikishwaji hatarishi kwa watoto. Aidha vinaonesha uhusiano mkubwa

Tanzania Bara na Zanzibar, hali inayoashiria kuwa watoto wanakabiliwa na hatari nyingi kwa wakati mmoja (angalia Kielelezo Namba 4).

Namba 4: Muingiliano kati ya vipengele vya utumikishwaji watoto katika ajira hatarishi

Chanzo: Uchambuzi wa Mwandishi kwa kutumia takwimu za Utafiti wa Watu wenye Uwezo wa Kufanya Kazi wa mwaka 2020/21

Angalizo: Kwa madhumuni ya uwasilishaji, ukubwa wa miduara hauendani na kiwango cha asilimia.

Watoto wasiotumikishwa ajira hatarishi: 75.2%
Mazingira hatarishi
hatarishi
wa ziada
Bara Zanzibar
Watoto wasiotumikishwa ajira hatarishi: 92.6%
Mazingira hatarishi
Sekta hatarishi
Kielelezo

MWENENDO WA VIASHIRIA

Kati ya mwaka 2014 na 2021, kulikuwa na kushuka kwa viwango vya kazi za watoto, utumikishwaji watoto na utumiishwaji katika ajira hatarishi kwa watoto kwa kati ya asilimia 9 mpaka 10 kwa Tanzania Bara na kati ya asilimia 1 mpaka 3 kwa Zanzibar (angalia Kielelezo Namba 5). Kiwango cha watoto wanaoshiriki katika kazi za watoto kilipungua kutoka asilimia 34.9 hadi 25.8 kwa Tanzania Bara na kutoka asilimia 9.9 hadi 7.6 kwa Zanzibar. Kwa upande wa utumikishwaji watoto, kiwango cha mabadiliko kinafanana, kwa tofauti ya asilimia 9.3 Tanzania Bara (kutoka asilimia 34.8) na asilimia 2.0 kwa Zanzibar (kutoka asilimia 9.5).

Kati ya mwaka 2014 na 2020/21, kiwango cha utumikishwaji watoto kilipungua kwa asilimia 9.1 kwa Tanzania Bara na kwa asilimia 2.3 kwa Zanzibar.

Kielelezo Namba. 5: Mwenendo wa viashiria vya kazi ya watoto na utumikishwaji watoto wenye umri wa miaka 5–17, Tanzania

Chanzo: Uchambuzi wa Mwandishi kwa kutumia takwimu za Utafiti wa Watu wenye Uwezo wa Kufanya Kazi wa mwaka 2014 na 2020/21 Angalizo: Tofauti dhahiri za kitakwimu kati ya mwaka 2014 na 2020/21 zinaoneshwa kama ifuatavyo: ***p

ELIMU, KAZI ZA WATOTO NA UTUMIKISHWAJI WATOTO

Mahudhurio shuleni yanatofautiana kulingana na umri, yakiongezeka kutoka

asilimia 56.1 ya watoto wenye umri wa miaka 5 hadi asilimia 92.1 ya watoto wenye umri wa miaka 10. Viwango vya mahudhurio shuleni vinapungua baada ya umri wa miaka 10 hadi asilimia 49.6 kwa watoto wenye umri wa miaka 17. Kiwango cha watoto wanaofanya kazi kinaongezeka kadri umri unavyoongezeka, kuanzia asilimia 4.3 ya watoto wenye umri wa miaka 5 hadi asilimia 51.4 ya watoto wenye umri wa miaka 17. Pale kiwango cha mahudhurio kinapoanza kupungua (miaka 10–11) ongezeko kubwa la kiwango cha watoto wanaofanya kazi linaonekana (angalia Kielelezo Namba 6).

Asilimia 25.3 ya watoto wenye umri wa miaka 5–17, wanafanya kazi na asilimia 79.3 wanahudhuria shule. Idadi kubwa ya watoto (asilimia 64.0) wanaohudhuria shule hawafanyi kazi, asilimia 10.0 wanafanya kazi na hawako shuleni wakati asilimia 15.3 ya watoto wanafanya kazi na pia kuhudhuria shule. Watoto wanaochanganya kazi na shule wanaweza bado kuwa katika hatari ya elimu yao kuathiriwa na kazi: watoto wanaofanya kazi walieleza kuhusu hatari ya kuumia na afya duni (asilimia 26.2), athari kwenye madaraja ya ufaulu shuleni (asilimia 8.5) na unyanyasaji (kimwili, kihisia na kingono – chini ya asilimia 2).

Namba

na kazi za watoto, Tanzania

Utumikishwaji watoto kunaweza kuingilia masomo ya watoto kwa kuwanyima fursa ya kuhudhuria shule, kuwafanya waache shule mapema au kuwalazimisha kuchanganya masomo na kazi nzito na za muda mrefu. – ILO

ya watoto Umri wa watoto katika miaka

Watoto wanaofanya kazi Watoto wanaohudhuria shule

Chanzo:

Uwezo wa Kufanya Kazi wa mwaka 2020/21
Kielelezo
6: Mahudhurio shuleni
Asilimia

VICHOCHEO VYA UTUMIKISHWAJI WATOTO

Uchambuzi wa kina ulionesha tabia za mtu binafsi na za kaya zinazoweza kuchochea utumikishwaji. Hata kama uchambuzi huu haukuonesha kisababishi, ikiwa na maana kuwa sio tabia ambayo imepelekea utumikishwaji watoto, ilionekana kwamba watoto wanaohudhuria shule, watoto wenye vyeti vya kuzaliwa, wasichana, watoto wenye umri wa miaka 5–11 na watoto wanaoishi katika kaya zenye hali nzuri ya uchumi walikuwa na uwezekano mdogo kuhusika kwenye utumikishwaji watoto. Watoto wenye umri mkubwa, wavulana, watoto wahamiaji, watoto wa vijijini na watoto wanaoishi katika kaya masikini zaidi walionekana mara kwa mara kwenye utumikishwaji.

Vichocheo vya utumikishwaji watoto

Uwezekano mdogo wa kutumikishwa watoto

• Kuhudhuria shule

• Kuwa na cheti cha kuzaliwa

• Kuwa msichana

• Kuwa mtoto mdogo (miaka 5–11)

• Kuishi katika kaya yenye hali nzuri ya uchumi

Uwezekano mkubwa wa kutumikishwa watoto

• Kuwa mtoto mkubwa (miaka 15–17 na miaka 12–14)

• Kuwa mvulana

• Kuishi vijijini

• Kuishi katika kaya maskini

Mapendekezo muhimu

Wakati uchambuzi ulilenga kutoa makisio ya hivi karibuni ya hali ya kazi za watoto na utumikishwaji watoto, wadau muhimu waliohusika katika mchakato wa tathmini hii pia walitoa mapendekezo muhimu ya kisera:

• Kupunguza vizuizi vya kifedha: Umaskini ngazi ya kaya unachukuliwa kuwa moja ya sababu kuu za utumikishwaji watoto. Kupunguza vizuizi vya kifedha ngazi ya kaya inapaswa kuwa sehemu muhimu kwa ajili ya mkakati jumuishi wa kisera.

• Kuongeza ufahamu miongoni mwa viongozi wa jamii, walezi na watoto: Wadau kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na wenye Ulemavu); Ofisi ya Rais (Kazi, Uchumi na Uwekezaji) – Zanzibar; Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum; Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto – Zanzibar; Mashirika ya kimataifa na mashirika ya kiraia wote walielezea umuhimu wa kuongeza ufahamu miongoni mwa viongozi wa jamii, walezi na watoto. Kampeni za uhamasishaji zinapaswa kujumuisha wahusika kadhaa katika jamii, kama vile watoto, walezi na viongozi wa jamii.

• Kuchukua hatua jumuishi: Hatua jumuishi katika kutokomeza utumikishwaji watoto zinahitajika ambapo mipango ya kupunguza umaskini inaunganishwa na kampeni kuhusu ufahamu wa utumikishwaji watoto na taarifa nyingine.

• Kuzingatia sekta ya viwanda kama sekta ya mfano wa kuigwa: Baadhi ya wadau walizungumzia jukumu la sekta ya viwanda na jinsi vyeti

na ukaguzi vinaweza kusaidia kuongeza viwango vya ubora wa ajira na kuondoa hali ya utumikishwaji watoto katika sekta ambazo hali hii bado inajionyesha.

Aidha, kulikuwa na mapendekezo matatu kuhusu upatikanaji wa takwimu na kuboresha namna ya kupima hali ya watoto kufanya kazi na kutumikishwa kwa siku zijazo:

• Aina mbaya zaidi za utumikishwaji watoto: Uchambuzi wa takwimu za aina mbaya zaidi za utumikishwaji watoto haukuweza kujumuishwa kwenye ripoti hii kutokana na unyeti wa maswali na ugumu wa kuwafikia walengwa. Inashauriwa kuhakikisha kujumuisha taarifa za aina mbaya za utumikishwaji watoto kupitia uchambuzi wa ziada kama vile utafiti wa kina (qualitative research ) au utafiti maalum.

• Kazi za nyumbani hatarishi: Kwenye ripoti hii, haikuwezekana kujumuisha takwimu juu ya hali hatarishi ya kazi za nyumbani zisizo za malipo. Inapendekezwa kuwa katika tafiti zijazo, maswali kuhusu hali hatarishi yaulizwe kwa kila aina ya shughuli, ikijumuisha kazi zisizo za malipo.

• Kazi za kilimo: Idadi kubwa ya watoto wanaohusishwa kwenye utumikishwaji hufanya kazi zinazohusiana na kilimo cha mazao. Utafiti wa Watu Wenye Uwezo wa Kufanya Kazi (ILFS) una taarifa chache kuhusu aina za mazao ambayo watoto hulima. Taarifa zaidi juu ya aina ya mazao inaweza kusaidia kutathmini utofauti wa kazi zinazohusiana na kilimo.

Nyaraka muhimu Marejeo

Kwa taarifa zaidi, tafadhali rejea ripoti kuu: National Bureau of Statistics, Office of the Chief Government Statistician Zanzibar and United Nations Children’s Fund (2024). Child Work and Child Labour in the United Republic of Tanzania: Evidence from the Integrated Labour Force Survey (2014–2021). Dodoma: NBS, OCGS and UNICEF.

International Labour Organization and National Bureau of Statistics (2016). Tanzania National Child Labour Survey 2014: Analytical report. Geneva: ILO. Available at: <https://webapps.ilo.org/wcmsp5/groups/public/---africa/---roabidjan/---ilo-dar_es_salaam/documents/publication/wcms_502726.pdf>.

National Bureau of Statistics (2022). Integrated Labour Force Survey 2020/21: Analytical report. Dodoma, Tanzania: NBS. Available at: <https://www.nbs.go.tz/ index.php/en/census-surveys/labour-statistics/791-2020-21-integrated-labourforce-survey-ilfs-analytical-report>.

National Bureau of Statistics et al. (2008). Child Work and Child Labour in Tanzania: The Integrated Labour Force Survey, 2006. URT. Available at: <https://www.nbs.go.tz/nbs/takwimu/labour/2006_Child_Labour_Report.pdf>.

Office of the Chief Government Statistician Zanzibar (2016). Zanzibar Child Labour Survey 2014: General report.

UNICEF Tanzania

S.L. Posta 4076

Dar es Salaam

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Simu: +255 22 219 6600

Barua pepe: daressalaam@unicef.org

https://www.unicef.org/tanzania/

@UNICEFTanzania

@UNICEFTanzania

@uniceftz

http://www.youtube.com/user/UNICEFtanzania

Turn static files into dynamic content formats.

Create a flipbook
Issuu converts static files into: digital portfolios, online yearbooks, online catalogs, digital photo albums and more. Sign up and create your flipbook.