Ndoto ya Mkombozi Kuwa na ulimwengu ambapo watoto wote wamepewa kipaumbele na wanahusishwa kikamilifu ili wawe watu wazima wenye kuzalisha/kuchangia katika jamii yao ya kidemokrasia na haki.
Dhamira ya Mkombozi Kuwawezesha watoto wa Tanzania wakue vema katika nyanja zote za kimaisha kwa kushirikiana na jamii na serikali ili kujenga jamii inayojali na yenye mshikamano ambayo inatoa kipaumbele kwa watoto.
Imeandikwa na: Joyce Kabue & Erin Dunne Imehaririwa na: Katie Bunten-Wren Imeandaliwa na: Erin Dunne Š 2012 Mkombozi
MATOKEO KATIKA NAMBA 377
367
Watoto waliudhuria elimu isiyo rasmi iliyoandaliwa na walimu wa Mkombozi mitaani
721
Watoto na vijana walihudumiwa mitaani kupitia programmu mbali mbali za mitaani
Watekelezaji wa masuala ya ulinzi wa mtoto na watu wenye wajibu kwenye jamii waliopokea mafunzo kuhusu ulinzi wa mtoto na haki za mtoto ili kuwawezesha kuboresha na kutekeleza mifumo imara ya ulinzi wa mtoto kama vile kamati za ulinzi wa mtoto katika kata tunazofanya kazi.
1,246
675
Watoto na vijana walipewa huduma ya moja kwa moja ya kisaikolojia kupitia mikutano yetu ya mmoja mmoja na msaada kwenye makundi
13,900 Watoto walijifunza kuhusu haki zao kupitia mafunzo ya haki za mtoto mashuleni
12,200 Wanajamii waliudhuria maonyesho ya usanii yaliyozingatia ulinzi wa mtoto, utetezi wa haki za watoto na kupunguza unyanyapaa kwa watoto walioko mitaani.
Watoto na vijana walisaidiwa kupitia huduma za moja kwa moja za Mkombozi
2,996
Mikutano ya ana kwa ana kati ya maafisa ustawi jamii wa Mkombozi na watoto walioko kwenye huduma zetu za moja kwa moja ilifanyika.
1,746
Watoto na vijana walipewa huduma ya afya.
BARUA YA UKARIBISHO
Katika mwaka 2012, mambo yafuatayo muhimu yalifanyika ili kufanikisha dhamira yetu: kutekelezwa kwa sensa ya 5 ya watoto 2012 ulikuwa ni mwaka wa mafanikio na wakuvutia kwa wanaojishughulisha mitaani, kufanikiwa kutoka katika hali ya Mkombozi, ni mwaka wa pili katika Mpango Mkakati wetu wa makazi ya watoto na kuwa makazi ya mpito, kuwa na mahu2011-2015. Tulimaliza mchakato wa kuhama kutoka kwenye siano mazuri, yaliyo rasmi na serikali ya mtaa na kupungua kwa makazi ya muda mrefu kwenda kwenye makazi ya kifamilia visa vya unyanyasaji wa mtoto katika jamii tunazofanya nazo ambayo ni ya muda mfupi na tumeanza kuona mafanikio ma- kazi. Mafanikio haya ya Mkombozi yametokana na ushirikano zuri. Kupitia idara yetu ya ushirikishaji jamii, tuliendelea kuzuia thabiti na wafadhili, mamlaka katika serikali za mtaa, wazazi, watoto kukimbilia mitaani kwa kufanya kazi na wadau wote ili wadau wengine, na watoto wenyewe. kuhakikisha watoto wanalindwa na kujaliwa. Mwaka 2012 Mkombozi ilikumbana na changamoto nyingi, ikiMkombozi tuliendelea kuona mafanikio makubwa katika kazi wemo ufinyu wa Bajeti na kuendelea kutegemea majengo ya zetu na kuamua kwamba ili kutoa taarifa kuhusu mafanikio kukodi kwa ajili ya ofisi zake. Kwa sasa tuna mipango imara hayo, tunahitaji kuelezea kwa ufasaha dhana ya mabadiliko ya kujenga majengo yetu wenyewe ikiwemo: makazi ya mpito kuhusu kwanini tunafanya kazi tuifanyayo. Tulianza mchakato yanayoendana na malezi yetu. Mwaka 2013 tumeanzisha rasmi huu mwishoni mwa mwaka 2012 na kuja na dhana iliyo imara kampeni za kukusanya pesa kwa ajili ya kuendeleza ujenzi huu. ya mabadiliko na jedwali lenye mpango wa programu, vitu hivi Mradi wa ujenzi utasaidia kufanya shirika kuwa endelevu. Mwavinatia mkazo na kusisitiza umuhimu wa kazi zetu. Mpango huu ka 2012 ulikuwa mwaka mzuri na tunawashukuru wadau wote. haubadilishi kazi tunayoifanya bali utatuwezesha kuwa makini Tunawapongeza watoto wa Mkombozi kwa ustahimilivu, uwajina kazi zetu za msingi, kuwa na mwongozo katika majadiliano bikaji na uwezo wao wa asili wa kuweza kustawi uliotuwezesha na wafadhili wapya na kusaidia katika maandalizi ya mpango kufanya kazi zetu. Tunatarajia mafanikio zaidi katika mwaka mkakati mwingine. 2013. Kazi yetu husukumwa na mtazamo kwamba watoto wa Kitanzania watakuwa kwenye mazingira ambayo wanapendwa, wanajaliwa na kushirikishwa katika masuala yanayohusu maendeleo yao, hii ni ili kuwaondoa na kuwazuia watoto kwen- Fulgence Shirati da mitaani. Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini, Mkombozi
3
YALIYOMO KATIKA RIPOTI HII
- Mwaka 2012 Katika Namba - Nadharia ya Mabadiliko...5 - Kujengea Watoto Uwezo..7 - Kuwezesha Jamii........8 - Kushirikisha Familia......9 - Mafunzo na Uvumbuzi..10 - Mradi wa Ujenzi...11 - Taarifa ya Fedha...12 - Shukrani Maalum...13
4
NADHARIA YA MABADILIKO Watoto wa Tanzania wanaishi kwenye jamii ambazo wanakuwa salama, wanatunzwa, wanathaminiwa na kushirikishwa katika masuala yanayohusu maendeleo yao.
Serikali inaweka mifumo yenye kusitisha watoto waliodhalilishwa kuendelea kudhalilisha wengine.
Kila mtu anafahamu kile ambacho mtoto anahitaji kwa ajili ya kupata maslahi yao bora
Watoto wanaojihusisha mtaani wanasaidiwa kustawi (Mkombozi inakuwa na kumbukumbu zao na inawajibu kimaadili)
Kipaji/Uwezo asilia wa watoto haupotelei mtaani
Wote tunaelewa athari wanazopata watoto wanapokimbia majumbani
Kila mmoja anafanya kazi kwa ushirikiano‌.Watoto ni suala la kila mmoja Mfarakano na utengamano katika familia unakomeshwa
Mkombozi hufanya kazi kuhakikisha kwa kuzingatia vipande vyote vya duara. Mabadiliko yanaweza kufanyika ikiwa tutafanya kazi kwa pamoja kuwezesha ukuaji wa mtoto kwa ujumla katika maisha yake
TIMU YA MKOMBOZI
KUJENGEA WATOTO UWEZO Kila mtoto anayepitia Mkombozi, huwa tunaona mustakabali wake. Muda ambao watoto wanautumia Mkombozi, tunahakikisha kwamba tunawapa kila kitu kitakachowawezesha kuona na kujenga maisha mazuri. Kwa miaka sasa huduma zetu zimetanuka kujumuisha ushirikishaji familia na kuwajengea uwezo jamii ili kuweza kuwajibika zaidi. Hata hivyo kazi yetu muhimu zaidi inaendelea kuwa ni kuwajengea uwezo watoto wa mikoa ya Moshi na Arusha. Mkombozi imeendelea kufanya vizuri sana katika kutoa huduma za moja kwa moja kwa watoto. Katika hili la huduma za moja kwa moja, hakika tumezidi kwa kiwango kikubwa malengo yetu yote ya mwaka.
Kuzaliwa upya kwa makazi ya mpito ya watoto Katika mwaka 2011 na 2012 kituo cha makazi ya watoto kilibadilishwa na kuwa makazi ya mpito kwa watoto. Makazi haya yameendelea kustawi katika mpangilio wetu mpya, ingawa ilibidi tubadilike ili kuendana na hali halisi na changamoto. Mwaka 2011 Mkombozi ilibadili mtazamo wake wa malezi, hii imeleta mafanikio na maendeleo makubwa katika mwaka 2012. Kuanzia mwaka 2011 badala ya kuwatunza watoto katika makazi yetu katika kipindi cha utoto wao, tuliamua kutoa kipaumbele katika kuwarudisha wototo wanaojishughulisha mtaani kwenye familia na jamii zao kupitia uunganishwaji na mlezi wa hiari/kambo. Kabla ya mabadiliko haya, watoto wengi walikaa na sisi kwa muda wa miaka 5-8, lakini kwa sasa makazi ya mpito yanaruhusu watoto kukaa kwa muda usiozidi mwaka 1, isipokuwa pale panapokuwa na sababu za msingi.
Ni muhimu kutambua mahitaji ya mtoto, na vile vile mazingira na mahitaji ya familia kwa ujumla. Maafisa ustawi jamii hufananisha taarifa kutoka kwa watoto na taarifa kutoka kwa wazazi, walimu na wazee kutoka katika jamii. Mara baada ya maafisa ustawi jamii kufanya tathmini ya jumla, makubaliano hufanyika na mtoto halafu mchakato wa kumuunganisha mtoto huanza mara moja. Mara nyingi watoto huunganishwa na familia zao katika kipindi cha miezi 6-8 baada ya kuja katika makazi ya mpito. Mara baada ya mtoto kuunganishwa na familia yake, maafisa ustawi wa jamii wetu huwasiliana mara kwa mara na familia na watoto. Vile vile hulipa ada za shule kuhakikisha watoto wanakuwa shuleni. Tangu kuanza kwa mchakato wetu mpya wa uunganishwaji, tumegundua kwamba ni watoto 8 kati ya 50 ambao huacha shule baada ya kurejeshwa kwenye familia. Tumeona kiwango cha mafanikio ya uunganishwaji kikiongezeka kutoka 45% kwenda 65%-70% mwaka mmoja baada ya kuunganishwa Mkombozi inaamini sehemu bora ya mtoto kuishi ni kwenye familia nyumbani. Dhumuni letu ni kutoa huduma zitakazowezesha familia kuchukua wajibu kwa watoto na vile vile tunadhani kuwaweka watoto kwenye vituo ni kuchukua wajibu kutoka kwa wazazi na jamiii kwa ujumla. Hivyo basi, Mkombozi huwaunganisha watoto kwenye familia zao au kwenye malezi ya hiari/kambo pale uunganishwaji na familia unapokuwa hauwezekani. Ili familia zichukue majukumu zaidi kwa watoto wao, Mkombozi hutoa huduma za kina kwa familia, kuwawezesha kiuchumi na kutoa mafunzo yenye kuleta ujuzi katika malezi.
7
KUWEZESHA JAMII
Kamati ya watoto katika makazi yetu ya mpito hukutana kila baada ya Ni wajibu wetu kwa pamoja kama jamii kuwalinda, kuwajali na kuwapa wiki mbili na inaushawishi wa moja kwa moja kwenye maamuzi yanayohusu ratiba ya kazi zao, ratiba ya chakula na hatua za kinidhamu. Katikipaumbele watoto. Kwa kuwa toka mwaka 2011 Mkombozi imebadili ka wilaya tatu tunazofanya nazo kazi, Mkombozi imekuwa ikifanya kazi mkakati katika utendaji, Mkombozi imezijumuisha programu zake za kushirikisha jamii na programmu zake za watoto katika kufanya kazi kwa ya kusaidia Mabaraza ya Watoto, wakati huo huo imekuwa ikiboresha mabaraza ambayo yamekuwa hayafanyi kazi au yamekuwa yakifanya pamoja ili kuja na matokeo makubwa na ufumbuzi wa kudumu. kazi duni. Kamati hizi zina mamlaka toka serikalini na hivyo basi wanawasiliana moja kwa moja na Mabaraza ya Wilaya ili sauti zao zisikike na Uhimizaji zaidi ulifanyika kuhusu umuhimu wa kushirikisha jamii katika kuwalinda na kuwajali watoto na vijana katika maeneo ya miradi yetu na wale wenye kufanya maamuzi serikalini. zaidi ya maeneo ya miradi. Hii iliongeza ushiriki wa jamii katika mipango Mkombozi kwa kushirikiana na AJISO, Polisi Jamii, Idara ya Maendeleo ya na utekelezaji wa masuala ya watoto. Jamii na Idara ya Ustawi wa Jamii walifanya mafunzo kuhusu ulinzi wa mtoto kwa lengo la kutambulisha na kuanzisha kamati za ulinzi wa mtoMkombozi ilipanua kazi zake za kushirikisha jamii kwa kujumuisha kazi zifuatazo: uundaji wa mfumo wa ulinzi wa mtoto ndani ya jamii, kuamsha to katika ngazi ya kata (CPCs). Kamati hizi huzingatia mausala ya haki ufahamu kwa kufanya kampeni dhidi ya unyanyasaji mtoto, msaada ka- za mtoto, unyanyasaji wa mtoto na kutambua mambo yanayowaathiri tika ushirikishaji mtoto, mpango wa kaka/dada mkubwa, kujengea uwezo watoto na vile vile kuangalia Sheria ya Ulinzi wa mtoto. Hii inatokana na walimu na mafunzo ya ujuzi katika malezi na vile vile utetezi katika ngazi hitajiko la kuamsha ufahamu kuhusu masuala ya ulinzi wa mtoto. Kamati hizi zimeshughulikia kesi nyingi za ulinzi wa mtoto zilizopelekwa ya taifa. kwao na watu kutoka katika jamii. Mkombozi inatambua kwamba visa Ushirikishwaji wa mtoto vingi vya unyanyasaji mtoto huwa havitolewi taarifa. Hivyo ni mafanikio Kama shirika lenye kumlenga mtoto, Mkombozi hutoa kikatika jamii kwa kamati kuweza kushughulikia kesi nyingi za udhalilpaumbele katika kuwapa watoto fursa za kushiriki katika ishaji wa mtoto. kufanya maamuzi ya masuala yanayohusu maisha yao na
Watoto walioko mitaani ni wako na wangu
8
familia zao. Ushirikishaji watoto hufanyika katika makazi yetu ya muda na katika jamii tunazofanya kazi. Kuwapa watoto ujuzi na fursa za kutumia sauti zao kujadili masuala yatakayoleta mabadiliko katika maisha yao na jamii zao, huwajengea watoto uwezo wa kujiamini katika kusimamia haki zao na haki za wengine.
Kamati zimekumbana na changamoto nyingi kama vile uhaba wa fedha na vitendea kazi. Mbeleni, Mkombozi inadhamiria kupeleka nyenzo zaidi kwa ajili ya jitihada hizi ili kuendelea kushirikisha jamii katika kuwapa kipaumbele na kuwalinda watoto.
KUSHIRIKISHA FAMILIA Sehemu bora kwa mtoto kukulia ni kwenye familia Mkombozi inaamini ya kwamba sehemu salama kwa mtoto kukulia ni kwenye familia. Hii nadharia/dhana imekuwa mtazamo katika kushirikisha familia ili kuhakikisha tunawalinda na kuwajali watoto wanaojishughulisha mitaani na wale ambao wako kwenye hatari ya kukimbilia mitaani. Kutokana na utafiti wa Mkombozi na wadau wengine, ni dhahiri kwamba watoto wengi hukimbilia mitaani kutokana na ukatili kwenye familia, kutojaliwa na umaskini mkubwa. Hivyo Mkombozi inaelewa kwamba familia lazima ziwezeshwe na kushirikishwa ili kufanikisha kwa ujumla uendelevu na ufumbuzi wa changamoto hizi. Ili kupata mafanikio katika kushirikisha familia, Mkombozi hutumia njia kama Ufanyaji Kazi wa Kina na Familia, mafunzo kuhusu malezi bora na mafunzo yenye kujengea uwezo kiuchumi ili kuwapa familia ujuzi na uwezo wa kutunza watoto wao. Kazi zetu na familia zinahakikisha uunganishwaji rahisi kati ya watoto na familia zao. Mkombozi inaamini kwamba tunawapeleka watoto nyumbani ambako watapendwa, watatunzwa na kulindwa.
Hii imewezekana kutokana na ushirikiano na shirika la Juconi liliko Mexico. Shirika hili limekuwa likitoa mafunzo na msaada kwa maafisa ustawi jamii wetu katika kutekeleza program hizi. Mwaka 2012 tulipata mafanikio kwa asilimia 90% kutokana na mpango huu. Watoto wengi waliounganishwa na familia zao kupitia mpango wa Kufanya Kazi kwa Kina na Familia (TFI), wamebaki nyumbani na wanaendelea vizuri. Mfumo huu mpya wa kufanya kazi na watoto ni changamoto, wenye gharama, unachukua muda na rasimali. Vile vile unahitaji ufuatiliaji na subira hivyo matokeo yake huchukua muda. Mratibu wa Idara ya Watoto Moshi, Upendo Ramadhani, anasema kwamba, Mkombozi itaenedelea kuboresha jitihada hizi na kupanua wigo wake ili kusaidia familia zaidi zenye matatizo. Vile vile Maafisa Ustawi Jamii wa Mkombozi watapewa ujuzi na elimu kutoka shirika la Juconi-Mexico. Hii itaboresha ubora katika utendaji kazi huu na hivyo basi kuhakisha mafanikio zaidi katika miaka inayokuja.
Kufanya Kazi kwa Kina na Familia Katika kipindi chote cha mwaka 2012, Mkombozi iliendelea kufanya kazi na familia katika kuboresha kazi zake za kuzuia na kutatua. Kufanya kazi kwa kina na ubora na familia, ni njia ya ndani na ya umakini ya kutatua tatizo kwa familia yenye utengamano na isiyo tekeleza majukumu hatimaye kusababisha masuala mazito yanayopelekea ukatili.
11
MAFUNZO NA UVUMBUZI Sensa ya Mwaka 2012 Mkombozi hufanya kazi kuwawezesha: watoto walioko mtaani sasa hivi, zamani au walioko katika hatari ya kuwa watoto wanaojishughulisha mitaani kupitia kazi zetu mbalimbali ikiwemo: huduma zetu za moja kwa moja kwa mahitaji ya msingi, ushirikishaji jamii na kuamsha ufahamu kupitia utetezi. Katika kipindi cha mwaka 2012, timu yetu ya ufuatiliaji na tathmini ilifanya zoezi la sensa ya watoto wanaojishughulisha mitaani kwa lengo la kupata na kuchambua taarifa za watoto wanaojishughulisha mitaani katika manispaa za Moshi na Arusha. Sensa ya mwaka 2012 ilikuwa ni Sensa ya tano sasa kufanyika. Sensa itaendelea kufanyika kila baada ya miaka miwili. Sensa ya mwaka 2012 ilifanyika kwa masaa 10 katika kila mji huku kukiwa na timu ya wasaili/wahojaji wakifanya utafiti huo mitaani. Maswali yaliyokuwepo kwenye usaili huo yalikuwa yanahusu umri, jinsia, kujishughulisha mtaani, mahali wanapotokea, madawa ya kulevya na pombe, historia ya kielimu na shughuli za kila siku.
12
Lengo la ripoti ya sensa nikupata ufahamu wa makundi ya watu, mahitaji kwa watoto wanaojishughulisha mtaani katika Manispaa za Moshi na Arusha. Takwimu hizi hutumika katika kusaidia Mkombozi kwenye utetezi, kuchangisha fedha na vile vile kutoa taarifa kuhusu namna ya kuunda program zetu wakati tunapangilia kuhusu mustakabali wa baadae.
Kwa ujumla, timu yetu ya utafiti ilikusanya zaidi ya dodoso 1300 katika mji wa Moshi na Arusha. Mwanzoni mwa mwaka 2013, taarifa zilizokusanywa zitaingizwa katika mfumo wetu wa kuchambua data, na tunatarajia ripoti kamili kuzinduliwa katikati ya mwaka 2013. Taarifa za awali kuna wastani wa 865 watoto wanaojishughulisha mitaani katika miji yote miwili; 269 ni watoto wanaokuwa mtaani kwa muda mfupi tu na 106 ni wale wanakuwa mtaani muda wote katika mji wa Moshi. Kwa upande wa Arusha watoto 355 ni wale wa muda mfupi mtaani na 135 ni wale wa muda wote mtaani. Katika miji yote ya Arusha na Moshi, matokeo ya awali yanaonyesha ongezeko kubwa kwa watoto wanaojishughulisha mtaani. Kwa kuongezea, taarifa zinaonyesha kuongezeka kwa 39% kwa watoto wanaokuwa mtaani kwa muda mfupi mjini Arusha na kupanda kwa 14% kwa watoto wanaokuwa mtaani kwa muda mfupi mjini Moshi. Idadi inayokaribia robo tatu yaani 74% ya watoto walitoa taarifa kwamba kabla ya kuja mtaani walikuwa wanaishi kwenye manispaa ya Moshi na Arusha, wilaya mbili ambazo Mkombozi hufanya nazo kazi. Sensa inasisitiza hitajiko la kazi za Mkombozi kaskazini mwa Tanzania na inaonyesha maeneo ambayo jitihada zetu zinahitajika zaidi.
MPANGO WA BAADAYE... MRADI WA UJENZI Mkombozi imekuwa sana katika kipindi cha miaka 15 iliyopita, imefanya mambo muhimu katika kusaidia watoto wanaojishughulisha mitaani ili kubadili maisha yao na kusaidia jamii katika kuwalinda watoto. Hivyo basi shirika limetanuka na kuwa kubwa kieneo na kishughuli. Hii imepelekea shirika kutafakari namna ambavyo linaweza kuendelea vizuri na shughuli zake, ndoto yake na mahitaji yake ya majengo. Tathmini mbali mbali zilizofanyika Mkombozi zimesisitiza umuhimu wa Mkombozi kuwa na majengo yake ili kupunguza gharama zinazotokana na kukodi na ili tuweze kuwa endelevu katika programu zetu. Mkombozi ikiwa na majengo yake itaonyesha dhahiri kuwajibika kwake katika kuwapa kipaumbele watoto na kuwasaidia watoto wanaojishugulisha mitaani kustawi. Kufuatia maoni ya wadau wetu na malengo katika mpango mkakati wetu, Mkombozi inaamini kwamba kuwa na majengo yetu wenyewe itatuwezesha kushughulikia kwa ufanisi na uendelevu matatizo ya watoto wanaojishughulisha mtaani, watoto walioko katika mazingira magumu pamoja na jamii zao nchini Tanzania Kutokana na uchambuzi huo hapo juu na umuhimu wake, Mkombozi iliamua kuwa ni muhimu kuwa na eneo lake litakalokuwa na majengo kama sehemu muhimu ya mpango wake wa mbeleni. Na hii itakuwa msingi wa Mkombozi kupiga hatua nyingine ya maendeleo kama asasi. Ujenzi unaopendekezwa utakuwa na majengo yote ya Mkombozi ikiwemo: ofisi ya ulinzi wa mtoto, makazi ya muda ya watoto wote wakiume na wakike, madarasa yasiyo rasmi, maktaba, uwanja wa michezo, ukumbi wa mafunzo kwa jamii, sehemu ya matibabu, ofisi ya utawala , ofisi ya programmu na ofisi ya mikutano. Ujenzi huu utatoa makazi salama kwa watoto wa mitaani kuishi kabla ya kuunganishwa na familia zao. Vile vile kitakuwa ni kituo cha elimu kwa watoto wa Mkombozi na watoto kutoka jamii zinazozunguka. Ukumbi mkubwa utakuwepo kwa ajili ya haya yafuatayo: mafunzo kuhusu ulinzi wa mtoto kwa ajili ya kamati za ulinzi wa mtoto za baadae, mafunzo ya darasani kwa walimu, na mafunzo ya malezi bora kwa wazazi. Ukumbi utatoa nafasi kwa jamii kutafakari kuhusu ni kwa njia gani iliyo bora wanaweza kuwalinda watoto walio katika jamii zao. Vile vile kutoa nafasi kwa watoto kukutana kuzungumzia kuhusu haki za watoto kupitia mikutano ya kamati zao na michezo kama jioni ya msanii inayofanyika kila mwisho wa mwezi Ujenzi huu utafanyika katika ardhi yenye ukubwa wa ekari 1.5. Ardhi iliyonunuliwa na Mkombozi mwaka 2009 katika eneo la Maili Sita Moshi Mjini. Inakadiriwa mradi wa ujenzi utagharimu si chini ya dola 350,000 ambazo ni wastani wa fedha za Kitanzania Tsh 560,000,000. Tunanuia kuchangisha fedha hizi kupitia jitihada mbali mbali kama vile kuomba toka kwa wafahili, harambee, na kampeni mbali mbali ndani ya nchi. Mpaka sasa hivi, Mkombozi imeshakusanya wastani wa dola za kimarekani 81,000 kutoka mashirika ya Stars Foundation, Fred Foundation na michango kutoka ndani ya nchi. Kipaumbele kimekuwa katika kuhakikisha tunapata washirika na wafadhili zaidi ambao watasaidia katika mradi wa ujenzi. Tunatarajia kuanza ujenzi mwishoni mwa mwaka 2013.
15
Mapato kutoka kwa Wafadhili Comic Relief Foundation for Civil Society Anonymous UNICEF Railway Children IOM Investing in Children & their Societies Pestalozzi Children’s Foundation WISE DFID EveryChild SKI The Stars Foundation Firelight Foundation Jumla ya mapato
2012 TSH 446,792 125,000,000 340,345,250 9,520,004 98,934,720 156,041,248 179,244,813 108,500,000 304,266,134 119,535,021 77,500,000 22,692,890 1,541,133,288
2011 TSH 197,716,350 125,000,000 196,686,000 43,375,803 93,119,740 13,950,800 152,931,515 134,622,930 105,000,000 132,487,460 48,193,650 14,607,964 1,257,692,212
Matumizi Idara ya Watoto Idara ya Ushirikishaji Jamii Ufuatiliaji na Tathimini Uchangishaji fedha na mawasiliano Utumishi, Utawala na Fedha Uongozi/ Utawala Uchakavu
591,859,779 403,680,701 113,539,963 104,336,684 288,010,918 24,185,313 25,093,623
529,630,030 219,847,170 61,776,940 62,161,732 210,043,958 57,391,034 15,517,484
Jumla ya Matumizi 1,550,706,981 1,157,123,080
516
2012 MUHTASARI WA FEDHA
2012 wafadhili, washirika, wahisani na marafiki Mkombozi inawashukuru kwa upendo wenu katika ufadhili, ushirikiano na uhisani. Mlichowekeza kimetuwezesha kutanua wigo wa: huduma zetu, kutoa matumaini, na kubadilisha maisha. Ufadhili unatoa ujumbe ufuataa kwa watoto wa Mkombozi: Mna imani na wao, wanathamni na wanao uwezo. Shukrani za dhati kwa wafadhili wote waliotupa fedha: • • • • •
Comic Relief/ChildHope Foundation for Civil Society UNICEF Railway Children DFID
• • • • • •
WISE Foundation Investing in Children & their Societies EveryChild The Stars Foundation Firelight Foundation Pestalozzi Children’s Foundation
Shukrani za dhati kwa washirika, marafiki na wahisani hawa: 2way Development Volunteers, Arusha City Council, Bergen University, Bonite Bottlers, Children’s Radio Foundation, Consortium for Street Children, Cre8 East Africa, Don Bosco Brothers, Global Service Corps, Habari Node LTD, International School of Moshi (ISM), Kilimanjaro Film Institute, Kili Centre, Majengo Secondary School, Meat King, Northern Highland School Students, Opportunity Finance Institution-Arusha, Parenting in Africa Network, President Kikwete’s office, Proud2b Me Foundation, Radio 5 Arusha, Radio Sauti ya Injili, Railway Children Trekkers, Standard Chartered Bank, TTCL, Youth Challenge International, Arusha City Council, Moshi Municipal Council, Moshi District Council Kwa wafadhili wetu, washirika na wahisani mmoja mmoja; kwa utaalamu, ushauri na michango yenu tunasema asanteni asanteni Caucus for Children’s Rights (CCR), Amani Children Centre, Msamaria Centre, Legal and Human Rights Centre (LHRC), AJISO, KWIECO, Tanzania Child Rights Forum (TCRF), Children’s Dignity Forum (CDF), NOLA, Dogodogo Centre, SOS Children’s Village, Brigita & Sina,Erin Ross, Jobortunity, Kristian Johnson & Rob, Liza & Stephen Pearson, KCMC Doctors, Mark Norbury, Rosalind Yarde-Jumbe, Ryan Butt, Shaun Giddens, Mr & Mrs Mwaibasa,Mayor- Moshi Rural, Regional Commissioner Kilimanjaro, Regional Commissioner Arusha, Regional Police Commandant Arusha, Regional Police Commandant Kilimanjaro, Wakuu wa kata zetu 13 ambazo ni: Sokoni 1, Unga Limited, Kaloleni Arusha, Ngarenaro, Kaloleni Moshi, Majengo, Njoro, Pasua, Boma Mbuzi, Rau, Uru Mashariki, Uru Kusini and Kibosho Magharibi. Kamati za ulinzi wa mtoto Moshi Vijijini, Moshi Mjini na katika Manispaa ya Arusha. Pia tunapenda kuishukuru Bodi ya Wadhamini ya Mkombozi kwa kutupa mwongozo wenye mikakati, Timu ya Uongozi wa Mkombozi kwa uongozi wao makini, Wafanyakazi wote kwa kujituma na kujitoa katika kufanikisha mipango ya mwaka 2012.
ASANTE!
HARD LIFE BOYS Klabu ya “Hard Life” ilizaliwa kutokana na vijana wawili wa Kitanzania wanaopenda ubunifu. Vijana hawa walikutana na kuishi Mkombozi kwa miaka mingi. Mwishoni mwa mwaka 2011 walianza kuishi maisha ya kujitegemea kama watu wazima. Kile kilichoanza kama banda la kuku kilibadilika na kuwa sehemu ya sanaa hatimaye shughuli ya kuingiza kipato ambayo iliwafikia makumi ya watoto kwenye jamii. Wanapoulizwa kuhusu uzoefu wao, Morgan, kiongozi wa kundi husema kwa sasa umekuwa mzuri sana. Wanaishukuru Mkombozi kwa kuwatoa mitaani, kuwatambua, na kukuza ujuzi wao wa sanaa kiasi cha kwamba wanategemea kipato chao cha usanii. Vile vile kikundi hiki hutoa mafunzo kwa watoto na vijana wengine. Kikundi kimekuwa na kinashirikisha watoto na vijana wengi zaidi wanaojihusisha mitaani. Huwapa mafunzo ya sanaa ambayo huwawezesha kuwa wenye kujitegemea. Morgan anaelezea kwamba kikundi kinatarajia kuanzisha shule ya sanaa ambayo itawafunza vijana namna ya kutumia katika kujiendeleza.
MAFANIKIO KWA MWAKA
2012 TIMU YA KURUKA KAMBA YA MKOMBOZI Timu ya kuruka kamba ya Mkombozi, ambayo huwakilisha Tanzania katika Afrika Mashariki ilishiriki katika mashindano ya kuruka kamba yanayojulikana kama Freestyle yaliyoandaliwa na One World; shindano moja la kuruka kamba la “one rope USA” lilifanyika Mombosa, Kenya. Luka Alex kijana wa Mkombozi alipata medali na kutambuliwa kama kijana aliyekuwa na nidhamu wakati wa mashindano hayo. Ndugu Simon Nyembe, mwalimu wa michezo wa Mkombozi, anasema watoto hawa wameendelea kujithamini, na kujiamini ambako huwafanya wajitume, washindane na wawe wastahimilivu.
Mkombozi S.L.P 9601 Moshi Tanzania Moshi Simu: +255 27 2754793 Arusha Simu: +255 272544319 info@mkombozi.org www.mkombozi.org Facebook: MkomboziTanzania Twitter: @MkomboziTZ Mkombozi ni asasi ya Kitanzania iliyosajiliwa chini ya wadhamini (Namba ADP/12097). Marafiki wa Mkombozi wamesajiliwa kama asasi nchini Uingereza (Namba 1101318). Mkombozi imesajiliwa kama asasi Marekani katika kundi la mashariki ya 501(c) ambayo hayalipi kodi.