Moduli 1, Kilimo Hai (revised)

Page 1

Mkulima Mbunifu Moduli namba 1

KILIMO HAI Njia tofauti za kilimo Kwa kawaida viumbe hai vyote ni vya asili. Fikra na mtizamo juu ya kilimo hai inaonekana kama vile viumbe hai wana sehemu yao maalumu ambayo tangu miaka milioni nyingi iliyopita. Hii inajumuisha viumbe wadogo wadogo waliopo ardhini, kwenye mimea, wanyama pamoja na binadamu mwenyewe. Kwa hakika kilimo kinategemewa kwa asilimia kubwa uhalisia katika kuzalisha chakula. Ni muhimu basi kufanya utunzaji wa rasili mali zinazohitajika katika kilimo, na kuepuka teknolojia ambazo zinaweza kuwa hatarishi kwa afya za watu na mazingira. Mfumo wa kilimo hai umetelekezwa kwa kiasi kikubwa kutokana na mabadiliko katika sekta ya viwanda, ongezeko la watu na mahitaji makubwa ya chakula katika nchi zilizoendelea kwa karne nyingi na zinazoendelea hivi sasa. Ukianza na vigezo vya ongezeko la uzalishaji kwa kutegemea teknolojia ya viwanda kama vile uzalishaji wa Ammonium nitrate kama mbolea, na matumizi ya DDT kama dawa ya kuulia wadudu. Uwepo wa mimea ya chotara uliongeza uzalishaji zaidi. Wakati huo huo mbinu za uzalishaji wa mazao kwa njia za kiasili zilitoweka kote duniani na mabadiliko ya kilimo cha kisasa yakachukua mkondo wake wazi wazi, kabla ya kutokea madhara ya kilimo hicho. Madhara haya yanajumuisha uharibifu wa udongo, uchafuzi wa maji yaliyomo ardhini, mito, mabwawa, maziwa, kuangamiza wadudu marafiki, na aina nyinginezo za wanyama muhimu, kupunguza ufanisi wa wadudu, na viuatilifu kwenye mazao ya chakula. Kilimo hai kimejaribu kuangalia na kupata picha nzima ya mazingira siyo tu aina moja ya wadudu wanaweza kuuliwa, lakini kilimo hai kinajaribu kuweka sawa shughuli za kilimo kwa njia za asili za uzalishaji wa mazao ya chakula na mazao mengine kwa mzunguko wa kiasili. Shirika la kimataifa la harakati na mwendelezo wa kilimo hai IFOAM, limeweka mikakati na mbinu za asili katika kilimo hai kwa kuangalia maeneo muhimu manne: Afya, ikolojia, usawa, na uangalifu.

Rutuba ya udongo, mimea, binadamu

Mashamba ni sehemu ya ikolojia

Kilimo hai ni lazima kiwezeshe na kiongeze rutuba ya udongo, afya ya mimea, wanyama na binadamu. Udongo ni nguzo muhimu katika maisha ya viumbe wote kwa ujumla. Udongo ulioharibiwa hauwezi kuzalisha chakula kizuri pia malisho ya kutosha kwa ajili ya mifugo. Ili kuweza kupata chakula cha kutosha kwa ajili ya binadamu na malisho kwa wanyama, ni lazima kuboresha rutuba ya udongo. Afya ya binadamu na wanyama inaenda sambamba na umuhimu na ubora wa udongo.

Kilimo hai ni lazima kitegemee mzunguko na mfumo mzima wa ikolojia. Mambo hayo hayawezi kutenganishwa lazima yaende sambamba na si kinyume. Matumizi ya kilimo hai ni lazima yapokelewe katika hali zote na kukubalika katika nyanja za kilimo, kijadi, na kiutamaduni.

Usawa katika mahusiano yote

Uangalifu –Tahadhari

Wakulima wanaofanya kilimo hai wanahitaji kuona kuwa wanashirikishana katika maisha ya ulimwengu huu na viumbe hai wote, pamoja na hayo binadamu na wanyama wanatakiwa kupata nafasi yao ya kuwa na afya njema na furaha. Hii inajumuisha usawa katika ngazi zote na kwa pande zote kwa wakulima, wafanyakazi, walaji, wasindikaji, wasambazaji, na wafanyabiashara. Kilimo hai kinalenga kuhakikisha ubora wa maisha kwa kila mtu, na kuchangia ukombozi wa chakula na kupunguza umaskini. Uasili na mazingira ni lazima vitunzwe kwa ushirikiano na ikolojia.

Wakulima wa asili hutekeleza majukumu yao kama watumiaji makini wa ardhi. Ardhi kwa ajili ya kilimo na miundo mbinu mingine kama vile vyanzo vya maji, ni lazima zitunzwe katika hali nzuri, kwa ajili ya kizazi kijacho. Watu na wanyama ni lazima watunzwe na kuangaliwa kwa umakini ili kuhakikisha afya zao zinaendelea kuwa salama. Teknolojia ya kisasa, pamoja na njia za kiasili ni lazima zinchunguzwe na kuangaliwa kwa kufuata taratibu hizi za kiasili. Tahadhari za kuzuia ni lazima zizingatiwe kuzuia hatari zinazoweza kujitokeza na maamuzi ni lazima yazingatie thamani na mahitaji ya viumbe wote wanaoweza kuathiriwa.

Ili kuendeleza na kuboresha mazingira kwa kutumia miundo mbinu iliyopo, ni lazima kupunguza matumizi ya vitu visivyo vya asili kulingana na mazingira hayo, na ni lazima kuwepo matunzo ya malighafi zote za asili kama vile maji, udongo, na virutubisho vya asili vinavyotikana na mimea.


Mbinu za kilimo hai kwa ufupi Kilimo cha asili

Kulima kwa kufuata desturi

Mfumo wa kilimo cha asili unajumuisha muundo wa kilimo cha jadi ambao umekuwa ukitumika kwa karne nyingi sasa. Kwa kawaida hufanya matumizi mazuri ya miundo mbinu inayopatikana na njia za kienyeji, hali ya ikolojia na mahusiano thabiti. Ikiwa mbinu za kijadi zikifuatwa mbali na mabadiliko ya hali halisi, zinaweza kusababisha madhara, vinginevyo ni lazima zirekebishwe. Mfano mbinu ya kiasili ya kufyeka na kuchoma moto, hili si tatizo endapo ni sehemu ndogo tu ya ardhi ndiyo inayotumika kwa kilimo. Mbinu hiyo hiyo inaleta uharibifu wa misitu pamoja na ardhi, pale tu kunapokuwepo ongezeko la watu, hivyo kupunguza utunzaji wa ardhi.

Kulima kwa kufuata mila na desturi kuliongezeka kufuatia maendeleo ya kilimo katika karne iliyopita: Matumizi ya mashine katika kilimo, matumizi ya madawa, mbolea za viwandani, mbegu chotara na kilimo cha umwagiliaji. Mabadiliko katika teknolojia ni lazima yalenge kukuza uzalishaji duniani kote. Ongezeko la mabadiliko katika kilimo pia hujumuisha athari kama vile uchafuzi na uharibifu wa mazingira, uharibifu wa ardhi, au kuwa tegemezi kwa aina chache za mazao.

Kilimo hai

Kilimo mchanganyiko

Kilimo hai kinajumuisha kujifunga kimaadili na kufanya maamuzi ya kutotumia teknolojia ambazo zitasababisha madhara kwa binadamu pamoja na mazingira. Wakulima wanaofanya kilimo hai ni wachache sana duniani (lakini wanaongezeka).

Mtindo wa kilimo mchanganyiko unajumuisha faida za mbinu zote zinazotumika katika kilimo. Kinajaribu kupunguza na kuepuka madhara yanayotokana na kilimo cha kisasa kwa kujumuisha mbinu za kilimo hai, kwa kupunguza matumizi ya mbolea za viwandani na kemikali, na kuchagua kwa uangalifu viuatilifu. Katika nchi nyingi hii inaonekana kuwa njia sahihi ya kurekebisha madhara yanayotokana na kilimo cha kisasa.

Kwenye nchi ambazo kilimo hai kimefanikiwa, na soko la mazao ya kilimo hai limeendelezwa, wanaweza kufikia kiwango cha asilimia 5-10 katika soko la dunia ingawa inaweza kutofautiana kulingana na ukanda. Sehemu ambazo soko la mazao ya kilimo hai halijaanzishwa na kuendelezwa, msisitizo kwa mazao ya kilimo hai kwa kawaida ni mdogo. Kwa mfano nchini Kenya na Tanzania, kuna wakulima wachache sana ambao wamesajiliwa kwa ajili ya mazao ya kilimo hai na uuzaji nchi za nje.

Kilimo hai kwa vitendo: Mtazamo Virutubisho hai

madini na mimea na baadhi yake zinaweza kutengenezwa kirahisi sana na wakulima wenyewe.

Mbole zisizo za asili hazitumiki katika kilimo hai. Virutubisho vya asili vinavyotokana na mimea hutumika kurutubisha udongo. Kuongeza rutuba kwenye udongo huchukuliwa kama nguzo muhimu. Mbolea za asili hutumika kuboresha au kushikilia rutuba ya udongo, hii inaweza kufanyika kwa kuongeza mbolea inayotokana na mifugo, mbolea vunde,na kuacha mabaki ya mazao shambani yatumike kama matandazo. Mbolea za asili huwa na virutubisho kama vile N, P, na K. Virutubisho hivi hupatikana kwa ajili ya mimea wakati viumbe hai wadogo walioko kwenye ardhi wanapovunja vunja mbolea hizo wakati wakila.

Udhibiti wa magugu

• Nitrojeni (N): Chanzo kizuri cha asili cha Nitrojeni kwa mimea kinatokana na mkojo wa wanyama na aina zote za samadi za wanyama, hasa zinazotokana na nguruwe na kuku. Mbolea zinazotokana na mimea na wanyama hutoa nitrojeni nzuri kwa mimea. Mimea jamii ya mikunde na mbolea vunde ni chanzo kizuri cha asili kuweza kuipatia mimea nitrojeni. Kuna vitu ambavyo vina nitrojeni kwa wingi kama vile chakula cha damu na chakula kinachotokana au chenye mchanganyiko wa manyoya.

Ufugaji wa asili

• Fosiforasi (P): Njia za asili za kupata fosiforasi ni kupitia mbolea ya miamba, mbolea ya kuku, na wanyama wengineo. • Potashiamu (K): Njia za asili za kupata potashiamu ni majivu, samadi ya mbuzi, kondoo, kuku na mifugo mingine.

Udhibuiti wa wadudu na magonjwa kwa njia za asili Kulima kwa mzunguko ni njia kuu ya kuweza kudhibiti wadudu na magonjwa. Mazao yanayostahili aina fulani ya wadudu na magonjwa ni lazima yapewe kipau mbele. Kilimo hai ni lazima kisaidie ustawi wa wadudu wenye faida pamoja na wadudu wanaosaidia kula visumbufu vya mazao, kwa kuwa husaidia kudhibiti wadudu kama vile vidukari. Kufanya udongo uwe na rutuba husaidia kufanya mimea kuwa na afya na kuiwezesha kukabiliana na wadudu na magonjwa. Kwa udhibiti wa moja kwa moja, unaweza kutumia dawa za asili zinazotokana na

Udhibiti wa magugu katika kilimo hai hutegemea mzungukoa wa mazao, kupanda mimea inayotambaa, na kutumia mbolea vunde sehemu ambayo kuna uhaba wa mimea inayotambaa, pamoja na kufunika ardhi kwa kutumia aina tofauti za matandazo (hii ni pamoja na kutumia plastiki). Kupalilia mapema, kuandaa ardhi mapema na kuacha mabaki ya mazao shambani, husaidia kupunguza wingi wa magugu. Kupalilia kwa mikono, au jembe, au kufyeka na kuacha magugu shambani kama matandazo ni muhimu kwa mazao mengi. Mifugo ni moja ya sehemu muhimu sana katika kilimo hai. Wanyama hutoa samadi ambayo hutumika kama mbolea. Mimea ya malisho inaweza kutumika katika mzunguko wa mazao. Nyasi na malisho ya jamii ya mikunde ni malisho bora kwa wanyama wanaocheua lakini pia husaidia kujenga udongo, kuupatia nitrojeni, na ni mazuri katika kufanya mzunguko wa mazao. Mifugo pia husaidia kula na kufanya mzunguko wa mabaki ya mazao. Inawezekana pia kuweka mbolea kwenye mimea bila kutumia mbolea ya mifugo. Lakini pia inaweza kupatikana kutokana na malighafi zinazoweza kutumika kutengeneza mboji, na hapa mimea jamii ya mikunde na mimea inayotambaa ni muhimu sana. Afya ya wanyama, inapewa kipaumbele kwa kuwa kuzuia magonjwa ni moja ya nguzo muhimu katika kilimo hai. Afya ya mifugo katika kilimo hai, huimarishwa kwa kuzingatia kuwa na mbegu bora, kuwa na malazi safi na makavu pamoja na nyumba bora, kuchunga pale inapowezekana, pamoja na ulishaji unaozingatia upatikanaji wa virutubisho vyote na kwa kiwango kinachojitosheleza. Inapendekezwa kuwapa chanjo na kuwapa dawa ya minyoo mara kwa mara. Endapo itatokea mlipuko wa magonjwa, inashauriwa kuwatibu kufuatana na ushauri wa mtaalamu wa mifugo.ushauri wa mtaalamu wa mifugo.


Ni faida gani zinazoweza kutarajiwa kutokana na kilimo hai? • Kilimo hai huongeza rutuba kwenye udongo kwa muda mrefu. Udongo hai una kiasi kikubwa cha vitubisho vinavyotokana na uozo wa malighafi za asili. Pia huongeza uwezo wa ardhi kuzalisha, kuhifadhi maji kwa muda mrefu na kukabiliana na ukame. • Kilimo hai hakihitaji kuwekeza gharama kubwa. Kilimo hai hutumia miundo mbinu inayopatikana kirahisi hivyo kumuepushia mkulima mdogo gharama za pembejeo za viwandani. • Utafiti wa hivi karibuni unaonesha kuwa kilimo hai kinaweza kuchukua nafasi ya aina nyingine za kilimo katika nchi zinazoendelea: Kilimo hai kinaongeza mavuno kwa mkulima baada ya muda mrefu, wakati amewekeza kidogo, na wakati huo huo kiasi kikubwa cha mazao kikizalishwa. Hii humfaidisha mkulima mdogo, ambaye mara nyingi yuko kwenye hatari ya kukumbwa na upungufu wa chakula, utapia mlo na madeni. • Kilimo hai hakimuweki mkulima pamoja na familia yake katika athari ya kupata magonjwa yanayotokana na matumizi ya kemikali na mbolea za viwandani. • Kilimo hai kinajumuisha tafiti za kisayansi na kilimo cha kijadi katika kilimo endelevu. • Hata kama kanuni za kilimo hai hazijazingatiwa ipasavyo, na hata kama hakuna soko la mazao ya kilimo hai yaliyozalishwa, mazao na bidhaa zake yanaweza kupatikana, na shamba pia kufaidika kwa kutumia mbinu za kilimo hai.

Soko la mazao ya kilimo hai Tanzania Ingawa taasisi nyingi zinasisitiza kilimo hai nchini Tanzania, kuna walaji wachache sana walio na uelewa wa bidhaa za kilimo hai. Soko la mazao ya kilimo hai lipo tu na kufahamika katika miji mikubwa kama vile Dar es Salaam na Arusha, na mashirika machache yaliyoidhinishwa katika kuuza nje mazao hayo. Hata hivyo, wakulima walio wengi wanaonyesha nia na shauku ya kuzalisha mazao kwa misingi ya kilimo hai kwa ajili ya soko la ndani na hata nje.

Uuzaji nje bidhaa za kilimo hai na usajili Kwa kawaida soko la nje la bidhaa za kilimo hai huhitaji usajili na nembo kwenye bidhaa. Kwa usajili, kampuni inayojitegemea ni lazima iwadhibiti wazalishaji (kwa kawaida mwaka mmoja) ili kudhibitisha kuwa bidhaa hiyo imezalishwa kwa kufuata misingi na vigezo vya kilimo hai. Vigezo vinaelezea kwa undani ni kwa namna gani bidhaa inaweza kuzalishwa, kuwekwa nembo na kuuzwa kama bidhaa ya kilimo hai. Mfano nchini Kenya, Shirika la viwango linatambua Shirika la viwango la uzalishaji wa kilimo hai, na pia shirika la viwango la bidhaa za kilimo hai kwa Afrika ya mashariki. Bidhaa za kilimo hai zilizothibitishwa kwa kawaida huuzwa bei ya juu kuliko bidhaa zilizozalishwa kwa njia nyinginezo. Usajili na kuweka nembo unahakikisha kuwa si kila mzalishaji anaweza kudai kuwa bidhaa yake imezalishwa kwa kufuata kilimo hai. Nembo husaidia kutoa uhakika kuwa ni kweli bidhaa husika imezalishwa kwa kuzingatia mfumo wa kilimohai. Kama umempata mnunuzi wa bidhaa za kilimo hai, ni lazima ufuate masharti na kanuni halisi za uzalishaji hai. Orodha ya mahitaji ni kubwa na inaweza kuwa tofauti na ile inayofuatwa katika kilimo cha jadi na kilimo cha kisasa. Unachohitajika ni kufahamu mahitaji halisi ya vigezo , mfano:-ni viini vipi vya kudhibiti wadudu na magonjwa vinavyoruhusiwa, Uzalishaji, uhifadhi na vifungashio vya bidhaa vinavyotakiwa. Udhibiti na usajili hugharamiwa na mkulima mwenyewe.

Mafunzo ni muhimu kwa ajili ya uzalishaji uliosajiliwa Ni changamoto Kwa wakulima wadogo wadogo kuondokana na kilimo cha kisasa na kuingia katika kilimo hai. Baadhi ya mashirika yamekuwa yakiingia mikataba na wakulima kwa ajili ya kuzalisha kwa kuzingatia misingi ya kilimo hai, kisha kununua kwa ajili ya kuuza nje, na kwa kawaida huwapatia mafunzo. Kwa sababu ya gharama kubwa za kupata usajili, wakulima wadogo ni lazima wajiunge katika vikundi vya wazalishaji. Kisha gharama za usajili zikagawanywa kwao, hii itawapa unafuu mkubwa sana.

Soko la nyumbani la mazao ya kilimo hai: Saidia kulianzisha! Masoko machache ya ndani yasiyo rasmi, taasisi n.k, mara nyingine hayahitaji usajili, na badala yake yanaweza kutegemea gharama ndogo kutambulika. Kwenye miji mikubwa, kuna nafasi kubwa ya kupata soko la bidhaa za kilimo hai. Kuna mifano mingi ya mafanikio katika kuanzisha soko la bidhaa za kilimo hai. Kwa kutumia usajili na nembo, mlaji anaweza kushawishiwa na uhalisia wa bidhaa za kilimo hai. Kuna mashirika mengi ambayo kwa sasa yanajihusisha na kilimo hai, ikiwa ni pamoja na vikundi vya vijana. Kila siku vijana wamekuwa wakiweka mboga na bidhaa nyingine katika mashamba yao kwenye meza na kisha kuwaelewesha na kuwafundisha wanunuzi ni kwa jinsi gani hizo bidhaa zina ubora wa hali ya juu. Ni kwa nini wewe usiwafuate ukawa mfano wa kuigwa? Kama una uhakika na unachozalisha, basi wafahamishe walaji wa ndani kuhusu bidhaa zako, ubora wake na ni kwa nini wanunue kutoka kwako! Hii inaweza kufanyika kwa mdomo tu au kwa vipeperushi. Jivunie ulicho nacho.

Namna ya kuanza kilimo hai Kama una nia thabiti ya kuanzisha kilimo hai, Mkulima Mbunifu inashauri kufuata hatua hizi:

1.Angalia uwezekano wa kupata soko kwanza. Jiulize mwenyewe: • Ni wapi na kwa nani naweza kuuza mazao yangu ya kilimo hai?


• Naweza kuuza kwa bei gani?

2. Majaribio ya uzalishaji wa kilimo hai

• Ni kiasi gani ninaweza kuzalisha, kuwapatia wateja wangu?

Ukishakuwa na uhakika kuwa utauza mazao yako utakayozalisha kwa misingi ya kilimo hai, jaribu kwanza katika eneo dogo kwa kuzingatia kilimo hai. Zalisha kwa ajili ya soko, huku ukijizoeza uzalishaji wa kilimo hai. Baadhi ya mazao na magonjwa ni vigumu sana kudhibiti kwa misingi ya kilimo hai, na unakuwa na hatari ya kupoteza mavuno ya awali. Mbadala wake, unaweza kuangalia namna ya kutengeneza bidhaa nyingine kutokana na mazao hayo (kama kutengeneza jamu au kukausha kwa kutumia hewa)

• Ni nani washindani wangu? • Kuna mkulima yeyote, au kikundi cha wakulima ambacho kimefanikiwa katika kilimo hai, na je naweza kuungana nao, au naweza kujifunza kutoka kwao?

Kwa ufupi, unapozalisha bidhaa kwa soko lolote, hatua ya kwanza wakati wote ni kutambua soko na wanunuzi. Ni lazima iwe wazi kuwa ni wapi pa kuuza na ni nani utamuuzia kabla ya kuanza kuzalisha!

Vigezo vingine unavyopaswa kuzingatia vinajumuisha: umbali kufika sokoni, bei sokoni, gharama za uzalishaji wa bidhaa yako, na muda bidhaa zako zinazoweza kukaa (Kipindi gani unaweza kuuza bidhaa zako kabla zianze kuharibika).

3. Panua uzalishaji wako kupitia kilimo hai Tekeleza hili pale tu unapoona kuwa inafaa na utauza bidhaa zako kwa faida. Hata hivyo hii ni sahihi na kawaida kabisa kwa bidhaa yoyote utakayozalisha!

Kilimo endelevu na kilimo hai: Taarifa zaidi

Taarifa zinazotolewa na Mkulima Mbunifu na TOF Kenya, zina manufaa sana kwa mkulima-maarifa haya yanaweza kutumiwa na mtu yeyote. Unaweza kuwasiliana na MkM +255 0717266007

www.mkulimambunifu.org

info@mkulimambunifu.org

+255 0785133005

Ujumbe mfupi

+255 0785496036 +255 0762333876

The Organic Farmers, www.organicfarmermagazine.org Infornet –biovision: Hizi ni taarifa kwa njia ya mtandao kuhusu kilimo hai na mbinu zake, na unakuwezesha kupata taarifa zote muhimu kuhusiana na kilimo hai kwa nchi za Afrika ya Mashariki: Uzalishaji wa mazao, ufugaji, ardhi, na utunzaji wa maji, pia malaria.

Namna unavyoweza kutumia infonet-biovision: 1. Andika anuani hii: www.infonet-biovision.org hakikisha kuwa hujakosea, kisha bofya “enter” 2. Infonet ikishatokea kwenye komputa yako, chagua somo unalotaka. Endapo una tatizo na aina Fulani ya zao kwa mfano Kakara (passion) bofya sehemu ya “Mazao/ matunda/mboga”. Orodha ya matunda na picha zake itatokea. Bofya kwenye picha au maneno, kwa zao la kakara utahitajika kusogea chini kidogo ili kulitafuta. 3. Utakapo bofya kwenye zao hilo, utapata taarifa kadha wa kadha kuhusiana na kakara (passion). Kwa juu utapata taarifa kwa ujumla pamoja na mahitaji ya zao hilo. Ukisogea chini utapata orodha ndefu ya wadudu na magonjwa, pamoja na picha kubwa kukuwezesha kutambua, ikiwa ni pamoja na mapendekezo ya namna ya kukabiliana nayo. 4. Endapo unahitaji kutambua na kufahamu ugonjwa ambao haufahamu, chukua sehemu yam mea iliyoathiriwa uwe nayo wakati wa kufungua. Unaweza kuandika taarifa mbalimbali ambazo zinaweza kukusaidia. Unaweza kutafuta msaada wa kuchapisha sehemu ya taarifa hizo utakazohitaji. Infonet-biovision inapatikana kwenye CD. Unaweza kuagiza kutoka Mkulima Mbunifu kupitia 0717266007 au info@mkulimambunifu.org Moduli hii imechapishwa na Mkulima Mbunifu kwa ushirikiano na The Organic Farmer (info@organickenya.org, P.O. Box 14352-00800 Nairobi, Kenya, +254 20 440398), Biovision Africa Trust, www.biovision.ch

Imeandaliwa na Theres SZekely na kutafsiriwa na Ayubu Nnko Mkulima Mbunifu: S.L.P. 14402 Makongoro Street Arusha Rununu: 0717 266 007, 0785 133 005 www.mkulimambunifu.org Barua pepe: info@mkulimambunifu.org


Turn static files into dynamic content formats.

Create a flipbook
Issuu converts static files into: digital portfolios, online yearbooks, online catalogs, digital photo albums and more. Sign up and create your flipbook.