Mkulima Mbunifu Moduli namba 4
VIRUTUBISHO VYA MAZAO YA KILIMO HAI Ni namna gani virutubisho vya asili vya mimea hufanya kazi Mimea ya kijana ina uwezo wa kufanya fotosintesisi: Mwanga wa jua, hewa ya ukaa pamaoja na maji huzalisha chakula cha mimea aina ya wanga ambacho baadae husafirishwa sehemu mbalimbali za mimea na kuhifadhiwa katika namna ya wanga (carbohydrates). Chakula hicho hutumiwa na mimea pia mimea ina uwezo wa kutumia wanga na madini/virutubisho vya aina mbalimbali mfano nitrojeni,salfa na madini joto kutengeneza vyakula aina mbalimbali mfano protini,mafuta na vitamin.Hivyo mimea ni viwanda vya asili vinavyotengeneza vyakula vinavyoliwa na mimea yenyewe pamoja na wanyama. Binadamu na wanyama hutegemea kupata virutubisho kwa kula na kumeng’enya mimea au wanyama wengine wanaokula mimea tu (herbivorus). Binadamu na wanyama hupata madini kutokana na vyakula wanavyokula. Mimea inapata madini na virutubisho vingine kutoka kwenye udongo, hewa na maji. Hii hutegemea mzunguko mzima wa ikolojia, ambabayo viumbe wadogo waliomo ardhini wanakuwa wanajishughulisha kujilisha kwa kutumia viini asili na visivyo vya asili kutoka ardhini na kuvigeuza kuwa katika hali ya kemikali. Baadhi ya matokeo ya mchakato kuzalisha nitrate, ammonia na fosifeti, lakini pia mpangilio wote wa madini mengineyo huchukuliwa kupitia kwenye mizizi ya mimea na sehemu nyingine za mimea kama majani kisha kutumika kwenye mmea.
Utunzaji wa virutubisho vya asili: “Lisha udongo na si mimea” Elimu hii ya virutubisho asilia kwa mimea ni kutunza viumbe hai waliomo ardhini kwa sababu ni muhimu na wana jukumu katika kutengeneza virutubisho ambavyo mimea wakati wote hutegemea. Mkulima anayefanya kilimo hai anaamini kuwa hii inawezekana tu kwa kurutubisha na kuutunza udongo vizuri kwa kutumia mbolea zenye virutubisho vya asili, mkulima huyu huepuka kutumia mbolea na madawa ya kemikali kwa kuwa ni hatari kwa binadamu na viumbe hai wengine wote. Wakulima wanaozalisha kwa kutumia misingi ya kilimo hai ni lazima waimarishe na kuboresha udongo na ni lazima kusheheneza walichovuna. Kushindwa kutunza udongo na mazingira kwa ujumla inavyotakiwa haikubaliki katika kilimo hai na akitakuwa endelevu (sustainable) na udongo huchakaa haraka. Rutuba kwenye udongo inaweza kutengenezwa kwa kutumia mzunguko wa masalia ya mimea na wanyama, ambao huongeza woevu kwenye udongo. Masalia ya asili ni nguzo muhimu ya rutuba kwenye udongo. Inashikamanisha na kuimarisha virutubisho, kushamirisha shughuli za kibiolojia kwenye udongo, kuimarisha muundo wa udongo, kupunguza au kuweka uwiano wa tindikali (acid) kwenye udongo, kuruhusu maji kupenya kwenye udongo hivyo huzuia mmomonyoko wa udongo. Virutubisho vinavyotokana na viumbe hai ni muhimu sana kwa udongo uliochakaa, Mbolea za chumvi chumvi zilizo nyingi zina athari mbalimbali katika udongo ingawa hutoa mavuno mengi.
Mbolea zisizo za asili Mbolea za viwandani hutoa virutubisho moja kwa moja kwenye mimea kwa kiasi kikubwa, zikiwa zimeyeyushwa kwenye maji. Mmea unaweza kuzipata kwa haraka sana. Wakulima wa kilimo hai wana mashaka juu ya utaratibu huu: • Mbolea za chumvichumvi hazisaidii kuboresha uhai wa udongo, lakini zinapunguza endapo ziatatumika zenyewe bila kuwepo mbolea za asili kwa muda mrefu. Pia mbolea nyingi zisizo za asili huongeza tindikali (acid) kwenye udongo, na kujenga mazingira yasiyo rafiki kwa mimea na viumbe wengine. Matokeo yake udongo na mimea unaweza kuongeza utegemezi wa pembejeo za viwandani na kama azitatumika mfululizo, mavuno yanaweza kupungua kwa kiasi kikubwa. • Virutubisho vinavyoyeyuka kwenye maji, hasa nitrate zinakuwa rahisi sana kutirishwa na maji jambo ambalo pia linaweza kusababisha athari kwa mazingira kama vile kuchafua maji yaliyoko chini ya ardhi. • Kuwekea mimea mara mbili au tatu ya kiasi kikubwa cha aina fulani ya virutuibisho, inaweza kusababisha kutokuwa na uwiano kwenye mimea jambo linaloweza kusababisha ongezeko la magonjwa na wadudu waharibifu wa mimea.
Mbole za asili Kwenye kilimo hai, mbolea ni lazima ziwe za asili. Mbolea hizo ni lazima ziwe zinatokana na mimea na wanyama (Mbolea za mifugo, mbolea vunde, na mboji) ambazo zinakuwa na uwiano wa virutubisho tofauti na ilivyo kwa mbolea za viwandani, na zinakuwa na kiasi kilkubwa cha virutubisho vya asili. Kabla virutubisho vyake havijachukuliwa na mimea, mbolea za asili ni lazima zivunjwe vunjwe kwanza na viumbe hai waliko ardhini; na hivyo virutubisho vinaachiliwa taratibu kwa muda mrefu. Hii ina maana kuwa kuna wakati pia vinakuwa havipo, na kwa kiasi kinachohitajika na baadhi ya mimea. Mbolea za asili zinaweza kuoza haraka kupitia: • Maandalizi ya shamba, hii husaidia kuongeza hewa ya oksijeni (oxygen) kwenye udongo. • Kuongeza nitrojeni, hii husaidia kuongezeka kwa viumbe hai kwenye udongo na kufanya wawe achangamfu zaidi. • Unyevu, maji yanahitajika katika hatua zote za kibiolojia. Mbolea zilizo zoeleka kutumika katika kilimo hai zitaelezewa hapo mbeleni.
Mbolea ya mifugo Mbolea inayotokana na mifugo imekuwa chanzo muhimu cha virutubisho na ni mbolea asili kwa mamia na maelfu ya miaka mingi. Hii ni aina ya mbolea inayotumika zaidi. Kwenye kilimo hai inashauriwa kuwa mifugo ni kiungo muhimu kujumuishwa kwa ajili ya kuzalisha mbolea ili wakati wote kuwe na mzunguko wa virutubisho.
Virutubisho vinavyopatikana kwenye samadi Kiasi cha virutubisho kwenye samadi inayotokana na aina tofauti ya wanayama inatofautiana kwa kiasi kikubwa kulingana na utunzaji, aina ya mnyama, chakula anachopewa mnyama na mahali anapolala. Virutubisho hasa vya nitrojeni hupungua kulingana na muda. Nitrojeni hupotea kirahisi sana kupitia kwenye hewa na mvua. Ili kuepuka upotevu huo, funika rundo la mbolea na pia itumike wakati ambao ardhi ina unyevu unyevu, na uiweke kwa uangalifu. Kwa uwiano wa virutubisho vinavyotokana na mbolea ya mifugo, angalia jedwali la 1 kwenye ukurasa wa 4.
Athari za samadi
Utahitaji samadi kiasi gani kwa hekari moja? Utaratibu mzuri ni ng’ombe mmoja wa maziwa pamoja na ndama wake kuwa na uwezo wa kuzalisha mbolea inayotosheleza ekari moja iliyopandwa matete au aina nyingine za mazao kama vile mahindi, au viazi kwa mwaka. Hili ni kadirio la tani 15 za samadi kwa mwaka-kama utakusanya mbolea hiyo mfululizo. Zingatia: Ng’ombe wako na ndama wake wanahitaji ekari moja iliyopandwa majani ya malisho, na shamba hilo kuwekwa mbolea inayotokana nao wenyewe! Kuweka wazi zaidi: Mifugo hutoa mbolea ya kutosha kwa aili ya shamba la malisho yao wenyewe, lakini hakuna mbolea nyingi itakayobaki kwa ajili ya mazao mengine.
Samadi hujumuisha athari chache za afya na mazingira, hii ni kwa sababu samadi huwa na kiwango kikubwa cha vimelea vinavyosababisha magonjwa kwa wanyama na binadamu. Baadhi ya virutubisho vinavyoyeyuka vinaweza kusababisha uchafuzi wa hewa na maji, na inaweza pia kuwa na mbegu za magugu, vimelea, na madawa waliopewa mifugo. Samadi mbichi na mkojo, vinaweza kuchoma mimea pia kutokana na kiasi kikubwa cha amonia. Ili kulinda watu na mazingira kutokana na athari hiyo, mkulima anaweza: • Vundika/ozesha kinyesi cha mifugo na mkojo kabla ya kutumia. • Endapo utatumia samadi mbichi, weka angalau muda wa miezi miwili tangu ulipoweka mbolea mpaka kuvuna mazao kwa ajili ya matumizi ya binadamu. • Tumia samadi mbichi kwa kiwango cha kati na uisambaze kwa uangalifu.
Mbolea vunde inayotokana na mimea jamii ya mikunde, ni chanzo kikubwa cha nitrojeni Mbolea vunde ya mimea inayotambaa ni chanzo kikuu cha mbolea za asili na virutubisho, na inazuia mmomonyoko na kurutubisha ardhi. Mimea inayotumika kutengeneza mbolea vunde inaweza kupandwa baada ya msimu wa mazao, au ikapandwa mseto na zao la msimu. Inaweza kukatwa na kutumika kwa malisho. Yanaweza kukatwa au kuachwa shambani kama matandazo ambapo huoza na kutoa virutubisho kabla mazao mengine hayajapandwa. Aina nyingine za mimea huwa na mizizi mirefu kiasi kwamba huleta virutubisho juu ya ardhi na hustahimili ukame pamoja na upungufu wa virutubisho. Kwa maelezo zaidi tafadhali soma moduli ya MkM namba 6 “Mbolea vunde, mazao yanayotambaa, matandazo, palizi”
Kuwezesha kiasi kikubwa cha nitrojeni Mimea muhimu zaidi kwa ajili ya mbolea vunde ni mimea inayotambaa na jamii ya mikunde ambayo pamoja na bakteria ina uwezo wa kuchukua nitrojeni kutoka hewani na kutengeneza kirutubisho cha nitrate. Mimea hii inapo oza inaweza kutumika kama mbolea kwa ajili ya kukuzia mimea mingine. Kuongeza nitrojeni inaweza kuwa kati ya kilo 15-80 N kwa ekari moja! Mbolea vunde ndiyo njia pekee na yenye ufanisi kwa kulipatia shamba lako nitrojeni na kuchukua nafasi ya mbolea za viwandani.
Mbolea zinazotokana na miamba
Mbolea zinazotokana na miamba ni mbadala wa mboji, na zinatumika kwa kiasi kikubwa kwenye kilimo hai. Fosiforasi inayotokana na fisifeti inaondoa haraka tindikali (acid) kwenye udongo na inakuwa na faida kwa muda mrefu. Fosifate inayotokana na miamba kwa kawaida huwa na kalishamu pia na hupunguza tindikali (acid) kwenye udongo inapoyeyuka. Fosifeti huyeyuka kwenye ardhi taratibu na huwepo kwenye udongo kwa miaka mingi. Fosifeti ni lazima iongezwe kwenye mboji au samadi kama njia ya asili ya kupunguza tindikali (acid) na kuongeza njia za asili za uozeshaji kufanyika kwa kutumia aina maalumu ya fangasi ambao hufanya kuwepo na ongezeko la fosiforasi. Fosifeti inapochanganywa kwenye rundo la mboji kwa kiasi fulani unapoandaa rundo la mbolea, ni lazima ipatikane hapo baadae kwa ajili ya mimea. Si mimea yote huwa na hali inayofanana: Mimea jamii ya mikunde na ulezi hufanya vizuri zaidi na kuwa na muonekano wa moja kwa moja pale kunapokuwepo na ongezeko la fosifeti, wakati mahindi matokeo huonekana baada ya muda mrefu.
Viwango vya matumizi vinavyopendekezwa
• Kwa ujumla, tumia kilo 50-150 kwa ekari moja kwa mwaka • Kuboresha mbolea ya ekari moja, changanya kilo 100 za fosifeti kwenye tani 4 za mboji • Kwa kila shimo moja, changanya kijiko kimoja cha fosifeti ndani ya viganja 2-5 vya mboji na uchanganye vizuri na udongo wa juu. Kuwa makini usivute/pumulia unga wa fosifeti.udongo wa juu. Kuwa makini usivute/pumulia unga wa fosifeti.
Mbolea ya ziada Mzunguko wa mazao, kuweka samadi, mbolea vunde, mimea inayotambaa na mboji hutoa kiasi kikubwa sana cha madini. Mbolea ya ziada inaweza kuwa na faida au umuhimu katika mazingira maalumu,lakini kwa udongo hafifu, na kwa udongo ambao umetumika kwa miaka mingi, inahitajika mikakati thabiti ya kuufufua udongo, hasa kwa kutumia mbolea vunde na mimea inayotambaa ambayo kwa kawaida huongeza virutubisho vya asili kwenye udongo.
Ulishaji wa folia Folia hutoa virutubisho vya kijani kwa majani ya mmea na shina lake. Folia zinazouzwa zinatokana na samaki walioyeyushwa au magugu maji, wakati chai (mbolea maji) inatokana na mimea, samadi, au mboji na inaweza kutengenezwa na mkulima mwenyewe.
Mboji Mboji ni chanzo kizuri sana cha virutubisho vya asili, hasa kwa shamba dogo. Ni chanzo kinachopendekezwa kwa ajili ya fosiforasi inapochanganywa na fosifeti. Mboji ina kiasi kidogo sana cha nitrojeni ulinganisha na mbolea za viwandani. Lakini ni muhimu sana kwa kuwa huongeza kiasi cha virutubisho vya asili na kuboresha rutuba katika udongo. Kwenye samadi iliyoiva vizuri, virutubisho vinakuwa imara na uyeyukaji wake hupungua. Magugu pamoja na magonjwa pia hupungua. Ni vigumu kuzalisha na kutumia mboji nyingi shambani. Mara nyingi upatikanaji wa mboji ni mdogo.
Majivu Majivu ni moja ya chanzo muhimu cha kalishamu na potashiamu. Yanaweza kuchanganywa kwenye mboji. Majivu hasaidia kuongeza pH kwenye udongo (kupunguza asidi). Hata hivyo yakitumika kwa kiwango kikubwa na mara kwa mara, yanaweza kuharibu mpangilio mzima wa udongo.
Zaidi kuhusu Nitrojeni (N) Upungufu wa nitrojeni kwenye mimea husababisha njano ya kufanana kwa majani yaliyokomaa, kuelekea upande wa juu wa mmea. Kwenye mimea michanga, upungufu wa nitrojeni husababisha mimea kupauka, kuwa na kijani ambacho hakijakolea na shina kuwa dhaifu.
Folia inaweza kutoa baadhi ya virutubisho pale vinapohitajika kwa haraka. Kwa kawaida hutoa virutubisho vya haraka vya nitrojeni. Mbolea ya folia zimeonekana kuwa na uwezo mkubwa wa kusisimua mizizi na shughuli za kibiolojia katika eneo la mimea.
Madini mbadala Madini mbadala ambayo ni muhimu ni kama vile kalishamu, magnesiamu, shaba, chuma, na mengineyo yanaweza kufanyika mara baada ya udongo kupimwa. Wakulima wanaofanya kilimo hai wanashauriwa udongo wao kupimwa mara kwa mara ili kubaini aina ya madini inayokosekana.
Linganisha aina mpya ya bidhaa mara zote Upatikanaji wa bidhaa mbadala kwa kiasi kikubwa kama vile Tindikali (acid) ya humic, enziamu, vichocheo, vichocheo vya shughuli za kibiolojia, vinapatikana katika maduka ya pembejeo. Lakini ufanisi wake hauko dhahiri. Wakulima wa kilimo hai wanashauriwa kizijaribu-lakini wakato wote wawe makini kufuatilia aina mpya ya pembejeo na mwangalizo! Hii inamaanisha kuwa usitumie pembejeo mpya kwenye zaidi ya nusu ya shamba lako kwanza, na mwisho ulinganishe mavuno kutoka sehemu uliyotumia njia za kawaida na sehemu ulipotumia aina hizo za pembejeo.
Sasa unaweza kuona ni kwa nini mimea jamii ya mikunde ni muhimu sana: Inabadilisha nitrojeni inayopata kutoka hewani kuingia katika mzunguko wa kutengeneza nitrate.
Aina zote za nitrojeni zinazoweza kutumiwa na mimea, na ambazo zinapatikana ardhini, au kutokana na mbolea chumvichumvi zina tabia ya kubadilika na kupotea. Zinaweza kuyeyushwa na kupotea kw njia ya maji na hewa. Hii ndiyo sababu mboji na samadi hazitakiwa kuachwa kupigwa na jua au mvua, na hazitakiwi kuwekwa juu ya udongo. Ni lazima zitumike haraka kwa kuwa kiasi chake cha nitrojeni hupungua haraka.
Kilimo hai na nitrojeni Utunzaji wa nitrojeni pengine huenda ikawa ni changamoto kubwa zaidi katika kilimo hai. Mzunguko wa nitrojeni hutokana na vyanzo viwili tu. Kutokana na mimea jamii ya mikunde na kutokana na mbolea ya mifugo ambayo kwa kawaida ni mboji. Mzunguko wa mboji walau husaidia kuimarisha sehemu ya nitrojeni ambayo inapatikana kwenye mimea ya aina zote na mbolea inayotokana na mifugo. Nitrojeni inayopatikana kwa njia hii ni imara zaidi na haizami na kupotea ardhini haraka lakini pia haiko tayari kwa matumizi ya mimea. Matokeo yake mazao ya kilimo hai yanaweza kukua taratibu sana, na mara nyingine kuwa na majani kidogo yenye kijani cha kutosha.
Fosiforasi (P) Fosiforasi ni muhimu kwa mimea na wanyama pia kwa kuwa inachukua nafasi ya nguvu katika ukuaji na uzalishaji, maua na matunda. Ni vigumu sana kugundua upungufu. Mimea inakuwa mifupi na hukua taratibu sana. Shina pamoja na sehemu za chini za mmea zinaweza kuwa na rangi ya zambarau.
Kwenye udongo wenye afya na wenye mbolea ya asili ya kutosha, aina ya fangasi maalumu ambao hujishikiza kwenye mizizi, husaidia mmea kupata fosiforasi kutoka kwenye udongo. Fosiforasi haipotei kirahisi kama ilivyo nitrojeni.
Potashiamu (K)
baadae nafasi katika mishipa ya jani huwa na rangi ya njano (intervenal chlorosis), wakati mishipa ikibakia kuwa ya kijani. Jani linaweza kuanza kujikunja. Udongo wa Afrika kwa kawaida hauna kiasi kikubwa cha potashiamu, kwa kuwa huondolewa kirahisi na mvua.
Upungufu wa potashiamu huanza kwa majani kuwa na rangi ya kahawia, kukauka nchani, hasa kwa majani yaliyokomaa, na
Jedwali 1: Viwango vya virutubisho kwenye mbolea za asili Nitrojeni
• Mimea jamii ya mikunde ambayo hutumika kama mbolea vunde au matandazo hutoa kati ya kilo 20-80 za N/kwa hekari ambayo inaweza kutumika kwa mazao yatakayofuata.
Fosiforasi (P₂O₅)
• Majivu 3-7%
• Chakula cha mifupa 12-25%
• Mbolea 12kg/t
• Mbolea ya kuku 10-25kg/t
• Chakula cha damu/Manyoya hutoa 12-15% N. Hizi hutumika moja kwa moja kwenye mazao.
• Mbolea ya nguruwe 3-6kg/t
• Mkojo wa aina yoyote huwa na urea (mpaka kiasi cha 1% N). Siyo wazo la kijinga kukojoa juu ya rundo la mboji.
• Mbolea ya ng’ombe 2-3 kg/t
• Mbuzi/kondoo 2.5-4 kg/t • Mboji *4kg/t
• Mbolea ya kuku 8-20kg N/t • Mbolea ya nguruwe 3-5Kg N/t • Mbolea ya mbuzi/kondoo 2-4Kg N/t • Mbolea ya ng’ombe 2-3 Kg N/t • Mboji * 1kg N/t • Mbolea maji inayotokana na mimea hutoa nitrojeni kirahisi na inaweza kutumika kwenye majani au folia.
Potashiamu (K₂O)
• Fosifeti 20-33%
ya
mbuzi/kondoo
• Mbolea ya ng’ombe 5-12kg/t • Mbolea ya kuku 5-12kg/t • Mboji *6kg/t • Mbolea ya nguruwe 3-7 kg/t • Mkojo: 1-3 kg/t
* Viini kwenye mbolea inayotokana na mbogamboga. Kama mbolea imetengenezwa kutokana na mbolea ya mifugo, mbolea ya miamba, na majivu, mbolea hiyo itakuwa na kiwango kikubwa cha virutubisho. Virutubisho kwenye samadi na mboji vinakuwepo kwa kiwango kikubwa kulingana na namna kilivyowekwa, kuhifadhiwa na ubora wa malisho.
Virutubisho vya mazao ya kilimo ni suluhisho? Haiwezi kukataliwa kuwa hali ya kilimo nchini Tanzania na katika nchi nyinginezo za Afrika inaonekana kuwa tete. Ukilinganisha na nchi nyingi zinazoendelea kwenye bara hili, kiwango cha uzalisha wa chakula katika kaya kinapungua na ni miongoni mwa mabara ya chini zaidi duniani. Kuna sababu nyingi ambazo zimeibuliwa kulingana na hili. Mapungufu ya serikali na uwekezaji katika kuendeleza kilimo ni sababu moja wapo. Jambo lingine ni ongezeko kubwa la watu katika miongo michache iliyopita, jambo linalosababisha ukosefu wa ardhi, hivyo kusababisha uharibu wa misitu na ardhi. Kwenye hali ya hewa ya tropiki ambapo uozaji wa mimea na mbolea za asili hufanyika kwa haraka sana, kupanda mazao mara kwa mara kunaweza kuwa na matokeo yasiyomazuri. Udongo ndio unaoathirika zaidi kwa kuwa virutubisho huzama ardhini kirahisi, na kiwango cha mmomonyoko kinaweza kuwa juu sana. Kunaweza pia kuwepo uhaba wa maji kwa kuwa ardhi inapoteza uwezo wake wa kuhifadhi maji. Pamoja na mabadiliko ya tabia nchi yanayoendelea, hii ni muhimu. Ruzuku ya mbolea za viwandani ilisaidia kuboresha uzalishaji wa mazao kwa kiasi fulani, lakini siyo ubora wa udongo. Nchi nyingi za kiafrika zilipo acha kutoa ruzuku ya mbolea, wakulima walio wengi tayari walikuwa kwenye ardhi ambayo ilishaharibika. Siku hizi wakulima wadogo wanaweza kununua aina yoyote ya mbolea za viwandani kwa shida sana,
hii inatokana na kuwa madini ya udongo yanapanda bei kila kukicha. Mbegu zisizo kuwa na ubora na mavuno kidogo ni tatizo zaidi. Lakini umuhimu wa mazao yaliyoboreshwa hauwezi kuonekana kwenye sehemu ambayo virutubisho vimepungua kwenye udongo! Pamoja na utunzaji hafifu wa maji, hii ni sababu kubwa kuwa na ongezeko la mavuno hafifu kila mara katika nchi za Afrika. Mkulima anaweza kufanya nini katika hali hii ambayo haitii matumaini? Hatuwezi kukuahidi kuwa kilimo hai ndicho suluhisho la kila kitu. Lakini ni sehemu muhimuu sana ya kupata utatuzi. Kuboresha uzalisha wa ardhi, huanza nakujenga rutuba kwenye ardhi na kwa uangalifu mkubwa kuitunza. Watu wengi hudhania kuwa kuchanganya mbinu za kilimo hai na za kisasa, ni njia yenye matumaini zaidi. Madhara yanayotokana na mbinu za kisasa ni lazima yaepukwe, na kutumia kwa ujanja pembejeo zote za kisasa, wakati huo mbinu za kuongeza uzalishaji kutoka pande zote zikichangia. Ni lazima pia ufahamu kuwa kuongeza mbolea za asili kwenye udongo huchukua miaka mingi. Lakini baada ya muda mrefu, inakuwepo na hakuna chaguo lingine, kama uharibifu wa ardhi utasimamishwa. Ni vyema kuanza sasa!
Moduli hii imechapishwa na Mkulima Mbunifu kwa ushirikiano na The Organic Farmer (info@organickenya.org, P.O. Box 14352-00800 Nairobi, Kenya, +254 20 440398), Biovision Africa Trust, www.biovision.ch
Imeandaliwa na Theres SZekely na kutafsiriwa na Ayubu Nnko Mkulima Mbunifu: S.L.P. 14402 Makongoro Street Arusha Rununu: 0717 266 007, 0785 133 005 www.mkulimambunifu.org Barua pepe: info@mkulimambunifu.org