Mwongozo wa ufugaji wa kuku

Page 1

Sehemu ya 1

Muongozo wa ufugaji wa kuku

Nini maana ya kuku wa asili

Kuku wa asili ni jamii ya ndege wafugwao na takribani 99% ya kaya zilizopo vijijini katika nchi zinazoendelea ikiwa ni pamoja na Tanzania. Watu wengine huwaita kuku wa kienyeji.

Kuku hawa hufugwa kwa mtindo wa kuwafungia jioni na kuwafungulia asubuhi ili wajitafutie chakula chao wao wenyewe kama vile mabaki ya chakula, majani na wadudu. Kwa sababu hiyo, mfugaji

wa kuku wa asili hana gharama katika kuwatunza kuku hao lakini pia huambulia uzalishaji mdogo wa kuku hao na kusababisha mchango wa kuku hao katika pato la kaya kuwa mdogo. Katika mazingira ya sasa nchini Tanzania kuku wa asili hupendwa sana kuliwa ukilinganisha na kuku wa kisasa (asili yao mataifa ya Ulaya) kutokana na kutopewa madawa na vichocheo vya ukuaji kama ilivyo kwa kuku wa kigeni.


Mkulima Mbunifu

Ujenzi wa mabanda ya kuku

Mwangozo wa ufugaji wa kuku

Uwazi

hasa wakati wa usiku, inashauriwa kufunika sehemu zenye uwazi kwa kutumia magunia.

Banda la kuku ni lazima liwe na uwezo wa kupitisha hewa safi muda wote. Endapo banda limetengenezwa vizuri, ni lazima liwe na uwazi unaruhusu kupitisha hewa kutoka nyuma kwenda mbele. Banda ni lazima liwe na wavu kiasi cha mita 0.6, kwa upande wa nyuma na mita 1.0 kwa upende wa mbele wenye uwazi.

Mwanga

Ni lazima kuwe na mwanga wa kutosha katika banda la kuku. Mwanga ni lazima uwe wa kutosha kiasi cha mtu kuweza kusoma gazeti akiwa katikati ya banda la kuku. Unaweza kuweka bati la kupitisha mwanga katika paa la nyumba ya kuku ili kuongeza mwanga.

Hata hivyo katika sehemu zenye joto, uwazi ni lazima uwe mkubwa kiasi cha mita 2 kutoka juu. Lakini kama ni sehemu ambayo ni baridi sana

Ni vizuri kuwa na banda imara na la kisasa linalowapa kuku uhuru wa kutembea na mahala pa kulala

Banda la kisasa la kuku Wafugaji walio wengi ni mara chache sana huwajengea kuku banda la kisasa. Kuku ni lazima wapatiwe banda zuri na la kisasa linalowawezesha kuwa huru kuzunguka. Banda lenye msongamano husababisha kuku kuwa na huzuni na hata kuanza kudonoana. Banda zuri ni lazima liweze kuwakinga kuku dhidi ya hali mbaya ya hewa, wanyama wakali, pamoja na wezi. Banda ni lazima liwe na viota vya kutagia mayai.

mawe, na madebe ya mafuta.

Sakafu

Sakafu ya nyumba ya kuku inaweza kutengenezwa kwa sementi endapo mfugaji ana uwezo wa kufanya hivyo, lakini sakafu ya kawaida ya udongo ni nzuri zaidi.

Matandiko

Ni lazima Waya kuweka matandiko katika sakafu meshi ya banda la kuku. Sehemu ambapo kuku wakubwa wanaweza kutagia. Ni vizuri kutumia maranda, na si pumba zinazotokana na mbao. Kuku wanaweza kula pumba za mbao. Kwa kuku wanaokuwa na wanaohatamia, vipande vidogo na vilaini vya miti, na makapi kama vile pumba za mpunga, zinaweza kutumika.

Eneo

Unapochagua eneo la kujenga banda la kuku, hakikisha kuwa banda hilo halitizami upepo unapotokea, ni lazima liwe karibu na nyumbani, na lisiwe sehemu ambayo maji yanatuama. Vifaa vinavyohitajika Mfugaji ni lazima alenge kutumia vifaa rahisi, nafuu na vya kudumu. Kwa mfano; mafunjo (papyrus) mabanzi,

2

Banda la kisasa la kuku

Wafugaji walio wengi ni mara chache sana huwajengea kuku banda la kisasa. Kuku ni lazima wapatiwe banda zuri na la kisasa linalowawezesha kuwa huru kuzunguka. Banda lenye msongamano husababisha kuku kuwa na huzuni na hata kuanza kudonoana. Banda zuri ni Waya lazima liweze kuwakinga kuku dhidi ya hali mbaya ya hewa, wanyama wakali, pamoja na wezi. meshi Banda Waya ni lazima liwe na viota vya kutagia mayai. meshi

Waya meshi

Waya meshi Waya meshi

3


Mkulima Mbunifu

Vyakula vinavyohitajika kulishwa kuku

Vyakula vya kuleta nguvu mwilini

Vyakula vyenye asili ya wanga vitumikavyo mwilini mwa mnyama kuleta (kufua) nishati itumikayo kukidhi mahitaji ya mifumo ya mwili. Mfano wa vyakula katika kundi hili ni: nafaka (mahindi na pumba zake, mtama, mpunga, muhogo, viazi mviringo, vitamu na hata vikuu) (ii) Vyakula vyenye asili ya kuwa na mafuta kama ufuta karanga, alizeti na nazi. Nishati inayopatikana katika vyakula vyenye mafuta ni mara mbili zaidi ya vyakula vya wanga.

Mwangozo wa ufugaji wa kuku

ya kisamvu hiki yana protini kwa kiwango kinachowiana na cha majani ya mikunde. Kwa kuwa muhogo unalimwa kusini kote, kuna fursa kubwa ya kutumia majani yake katika lishe bora ya kuku vijijini. (ii) Vyanzo

vyenye asili ya wanyama: mfano rahisi mabaki kama vipande vidogo vya nyama, samaki, dagaa na damu kutoka machinjioni.

Vyakula vya kulinda mwili

Vifaranga wa kuku wa asili wanaokuwa vizuri bila mama zao kutokana na mfugaji kuwalisha vizuri, kuwachanja mdonde na kuwapa mchanganyiko wa vitamini toka madukani na kwa muda wa mchana kuwafungulia katika eneo lake.

Vyakula vya kujenga mwili

Vinapatikana kutoka makundi yafuatayo (i) Vyanzo vyenye asili ya mimea kama jamii ya mikunde kwa kutumia majani [kunde, fiwi, mbaazi, mpopote (Leucaena), mlonge (Moringa), na jamii asili ya mimea wanayoifahamu wafugaji katika mazingira ya vijiji vyao]. (ii) Jamii ya mikunde kwa kutumia mbegu zake km maharagwe, kunde, mbaazi, fiwi. Kitaalamu muhogo mtamu/baridi (Manihot esculenta) na jamii ya muhogo wa kisamvu tu, majani Mazingira yanayofaa kwa kuku wa asili kwakuwa yana majani mabichi yenye vitamini na protini na uwezekano wa wadudu kama mchwa chini ya majani yaliyo anguka na kukauka

4

Kundi hili linahusisha vyanzo vya vitamini na madini. (i) vyanzo vya vitamini katika mazingira ya vijiji ni: (i) aina ya vyakula kwa vitamini nne zifuatazo: A; D; E na K. (ii) aina ya vyakula vyenye vitamini za kundi la B (B1, B2, B6, B12). Wafugaji wanapaswa kufahamu uhusiano wa vitamini katika ufanisi wa kukamilisha mahitaji ya mifumo ya mwili: km mapungufu ya vitamini A yanapelekea kuku ashambuliwe na magonjwa kwa urahisi. Mfano hai ni upungufu mkali wa vyanzo vya vitamini hii vikiwa ni majani mabichi wakati wa kiangazi. Upungufu huu hupelekea kuku kutaga mayai yenye upungufu wa vitamini A. Hatima yake vifaranga wakianguliwa kutoka katika mayai hayo pia huwa na upungufu wa vitamini A. Athari ya upungufu huu ni udhaifu ambao unaambatana na vifo vingi vya vifaranga. Vyanzo vya kila aina ya vitamini vilivyopo katika mazingira ya vijiji ni: nafaka kwa kundi la vitamini B, na kundi la vitamini A,D,E na K linahusisha majani, mbegu, pia maua ya mimea asili iliyoko vijijini.

vya mayai kwenye kizazi cha kuku, madini yenye asili ya chokaa (katika mifumo ya kutengeneza mifupa mwilini na umuhimu wa kufua ganda la yai liwe imara). Vyanzo vya madini ya chokaa kwa ukanda wa pwani hutengeneza chokaa kwa kuchoma mawe wakitumia kuni. Chokaa hii ina jivu kutoka miti aina nyingi. Jivu na viini vilivyopo kwenye mawe ndiyo chokaa yenyewe ikiwa na kiwango kizuri cha madini ukilinganisha na ile itokayo viwandani.

Madini

Madini muhimu katika uzalishaji wa kuku ni: madini ya chuma katika mifumo ya kutengeneza chembechembe hai za damu, madini joto katika kuhimilisha mifumo ya kizazi kwa kulenga vifuko

5


Mkulima Mbunifu

Mwangozo wa ufugaji wa kuku

Matatizo ya ufugaji wa kuku a) Tatizo kubwa kuliko yote ni vifo vinavyotokana na magonjwa hususani Mdondo, upungufu wa vitamini na hususani vitamini A, ndui ya kuku na wadudu wa ndani (kama minyoo) na wa nje (kama utitiri, chawa na kupe). Yapo pia magonjwa yasiyojitokeza kwa kiwango kikubwa katika kuku wa asili kama vile Typhoid, Koksidia,

kuvimba kichwa na mafua n.k b) Upungufu wa lishe c) Ukosefu wa mabanda bora d) Wizi na wanyama walao kuku e) Elimu ndogo ya ufugaji bora kwa wafugaji.

Kuku waliokufa kwa Mdondo kutokana na kutopatiwa chanjo ya ya ugonjwa huo.

Ugonjwa wa mdondo/kideri Ugonjwa husababishwa na virusi, huathiri kuku wa rika zote wasiochanjwa na kusababisha vifo vya kutisha au hata kumaliza kundi lote la kuku. Hutokea zaidi wakati wa kiangazi na wafugaji huhusisha na uchanuaji wa maua ya miembe japo ugonjwa huanza miezi ya Aprili, Mei hadi Septemba japo waweza kutokea wakati wowote wa mwaka. Ugonjwa hauna tiba bali unakingwa kwa chanjo ijulikanayo kama I-2 inayovumilia joto kati ya 4-29ºс na kuku huchanjwa kwa tone moja tu jichoni kila baada ya miezi mitatu hadi minne (picha uchanjaji kwa kutumia I-2).

Upungufu wa Vitamini A huanzia kwa kuku wanaotaga mayai wakati wa kiangazi yakiwa na upungufu mkubwa wa Vitamini A na hivyo vifaranga wanaototolewa hukumbwa na ukosefu wa vitamini na kadri wakuavyo mahitaji huongezeka zaidi na kusababisha macho kuathirika. Dalili za awali za upungufu wa Vitamini A huonekana katika rangi ya kiini cha yai ambacho huwa kimepauka ukilinganisha na mayai yanayokuwa yametagwa masika ambapo vyanzo vya vitamini A na vitamini zingine huwa ni majani mabichi.

Mtaalam wa tiba ya mifugo toka SUA akielekeza namna ya kutumia chanjo ya I-2 kwa njia ya matone kwa wafugaji wa kuku wa asili Kilangala, Lindi vijijini

Upungufu wa vitamini A

Upungufu wa Vitamini A kwa kuku wa asili hujitokeza zaidi wakati wa kiangazi kwakuwa majani huwa yamekauka na nafaka zinazovunwa huwa hazitoshelezi mahitaji ya familia na kusababisha kuku kutopata chakula cha ziada mbali na kujitafutia wao wenyewe.

Dalili zingine ni vifaranga wadogo kufa ndani ya wiki mbili tangu watotolewe ama kuvimba macho na kutoa uchafu mithili ya kipande cha sabuni iliyolowekwa katika maji Wengine hufa kwa kushindwa kula kutokana na kutoona.

Udhibiti wa Kideri/Mdondo

• Ugonjwa hauna tiba lakini unazuilika kwa chanjo mf. I-2 na Lasota. • Chanjo ya I-2 inafaa kutumika katika mazingira ya vijijini kwakuwa inavumilia joto la kati ya 14-29ºC kwa siku 14. • Chanjo hutolewa kila baada ya miezi 3 au minne 4 kwa njia ya tone katika jicho moja tu la kuku. • Vifaranga wanaototolewa kabla ya muda wa chanjo hutakiwa kuchanjwa wafikapo umri wa siku 14 na kisha kuingizwa katika ratiba ya uchanjaji wa kundi la wakubwa. • Chanjo ya I-2 kama ilivyo chanjo zingine hutolewa kwa kuku waliowazima/wasiowagonjwa.

6

A B Viini vya mayai A) yaliyotagwa na kuku aliyepewa vitamin A wakati wa kiangazi; B) yaliyotagwa na kuku ambaye hakupewa vitamin A wakati wa kiangazi

Kuku akiwa na vifaranga wanaokuwa ambao wameathirika na upungufu wa vitamini A mwilini na kusababisha macho kuvimba (angalia duara).

Udhibiti wa upungufu wa Vitamini A Kuwa na bustani ya mchicha na majani kwa vijiji visivyo na shida ya maji. Kutumia vitamini mchanganyiko za madukani ambazo zina kiwango

7

kikubwa cha Vitamini A: Kuwapa kuku wanaotarajia kutaga wanywe kwa siku saba mfululizo na tena pamoja na vifaranga baada ya kutotoa.


Mkulima Mbunifu

Ndui ya kuku

Mwangozo wa ufugaji wa kuku

Wadudu wa kuku

duka la dawa za mifugo kwakuwa mchanganyiko wa maji na dawa hutofautiana kati ya dawa na dawa.

Minyoo ya kuku

Kuku aliyeathirika na ugonjwa wa ndui sehemu za kichwa

Huathiri kuku wa rika zote japo wadogo huathirika zaidi na hufa zaidi. Kuku huonesha vipele katika maeneo yasiyo na manyoya na kisha hutoa maji na kuacha vidonda ambavyo hatimaye hujenga kovu kwa baadhi ya kuku wanaopona. Ugonjwa hujitokeza zaidi wakati wa kiangazi na mwanzoni mwa msimu wa mvua. Pia ugonjwa huu husababishwa na aina ya virusi vijulikanvyo kama

fowl pox virus. Ugonjwa una chanjo inayochomwa kwa sindano maalum katika mabawa ya kuku. Hata hivyo kwa kuku walopewa kiwango kizuri cha vitamini A na zingine, matukio ya ndui huisha au kupungua sana. Hivyo ni vema kuwalisha kuku vyanzo mbalimbali vya vitamini A ili kuzuia ugonjwa wa ndui (tazama picha chini) na magonjwa mengine.

Udhibiti wa ndui ya kuku

A

1.

Chanja kuku athirika

kabla

hawaja-

2.

Kuku walioathirika: Tibu sehemu zilizoathirika kwa kuondoa mapele na kupaka dawa kama Iodini tincture (dawa ya joto)

Minyoo ipo ya aina nyingi kwa kuku lakini minyoo ya duara, mikubwa na mirefu iliyochongoka katika ncha zote mbili ijulikanayo kama Ascaridi galli ni hatari kiuchumi kwakuwa inanyonya chakula cha kuku kwa wingi na hatimaye kusababisha vifo vya kuku wadogo, wakati na hata wakubwa. Kutokana na hali hii kuku hupunguza uzalishaji kuanzia kutaga mayai na kushindwa kutotoa vizuri. Minyoo ina tiba ya dawa ya Piperazine citrate na yaweza kukingwa kwa kutoa dawa za minyoo kila baada ya miezi mitatu hasa wakati wa masika, mwanzoni mwa masika na mwishoni mwa masika.

A

Dawa ya minyoo

Ndege ni lazima wapatiwe dawa ya minyoo kuanzia wiki ya kwanza na kurudiwa tena baada ya wiki tatu, hii inaweza kwenda sambamba na chanjo, na kurudiwa katika kipindi hichohicho, hii itakuwa wamepata dawa ya minyoo mara 4 kabla ya kuwekwa kwenye banda kubwa wanapofikisha umri wa wiki 8. Hakikisha unatumia dawa sahihi kukabiliana na minyoo. Wakati unapowapa kuku dawa kupitia kwenye maji ya kunywa, hakikisha kuwa umechanganya kiwango kinachohitajika cha dawa, ambapo kuku hunywa kwa kipindi cha saa 4 (tunaweza kusema kiasi cha lita 6 kwa kuku mia moja, kuku wenye umri wa wiki 6 kwa siku). Ongeza maji baada ya kuku kumaliza maji yote yenye dawa.

B

Vimelea: Ndege wote wapuliziwe dawa na banda pia lipulizwe dawa inapotokea kuwepo na dalili ya vimelea. Unaweza kuwatumbukiza kuku kwenye dawa au kuwanyunyizia dawa ya unga. Epuka kuzamisha kichwa kwenye dawa, au kutumia njia hii wakati wa msimu wa mvua.

A) Minyoo ya kuku minyoo aina ya tegu; B) minyoo mviringo

Udhibiti wa minyoo ya kuku

Tumia dawa za minyoo kama vile Piperazine citrate, levamisole na promectine oral. Dawa hizi hupatikana katika maduka ya dawa za mifugo

Ni vema kuku wa asili kupewa dawa za minyoo mara moja kila baada ya miezi mitatu na wiki moja kabla ya chanjo ya I-2.

B A) Kwa kuku mwekundu vipele vya ndui huwa vieusi B) kwa kuku mweupe vipele vya ndui huonekana vyeupe.

8

Kuku wanaweze kupewa dawa za minyoo wakati wowote endapo minyoo wataonekana kinyesi. Maelekezo ya kuchanganya dawa na maji yatatolewa kwa mtaalam katika

9

Kwa ujumla, ni lazima kuchukua hatua za makusudi kuwakinga kuku, hatua hizo ni kama vile kuwaweka vifaranga mbali na sehemu walipo kuku wakubwa, kuhakikisha kuwa nyumba ya kuku na vifaa vinavyotumika vipo katika hali ya usafi, kuzuia watu wanaokutembelea kuingia kwenye banda la kuku, kuhakikisha kuku wanaokufa wanafukiwa vizuri au kuchomwa moto, kuhakikisha kuwa wanyama wadogo wadogo kama vile panya hawaingii kwenye banda.


Mkulima Mbunifu

Mwangozo wa ufugaji wa kuku

Wadudu wa nje

Tiba ya magaga

Loweka miguu yenye magaga katika mafuta ya taa kila baada ya wiki mbili hadi magaga yapotee kabisa. Banda la kuku lililojengwa kwa malighafi zipatikanazo vijijini ambalo linazuia wadudu kama viroboto na utitiri kuzaliana. Kupe

Viroboto

Gumboro

Chawa

Utitiri pia huathiri miguu

wadudu kama vile Akheri powder™ au Sevin dust™ au zinginezo utakazoshauriwa na wataalamu. Kuua viroboto changanya kidogo na mafuta mgando ya kujipaka ili dawa ishike sehemu zenye viroboto wanaong’ang’ania.

Wadudu kama viroboto, chawa, kupe na utitiri husababisha vifo vya vifaranga, kunyonya damu na kusababisha usumbufu kwa kuku wanaohatamia.

Jinsi ya kudhibiti wadudu wa 3. Matumizi ya mafuta ya taa nje wa kuku 1.

2.

Tumia majivu au majani ya miti ifukuzayo wadudu (baadhi ya jamii) katika banda na viota vya kutagia kama kinga kwa kuku

4.

Tumia dawa za vumbi za kuua

10

kupaka katika viroboto kwenye kuku walioshambuliwa.

Ujenzi wa mabanda ya chaga za juu na kuta zinazopitisha hewa ya kutosha na kuzingatia usafi wa banda na vifaa vya kuku

Hivi ndivyo kuku aliye athiriwa na ugonjwa wa Gumboro anavyoonekana

Huu ni ugonjwa wa maambukizi ambao husababishwa na virusi na huwapata zaidi vifaranga wa kuku. Mara nyingi ugonjwa huu hutokea katika maeneo ambayo kuku wanafugwa kwa wingi. Ugonjwa wa Gumboro huambatana na dalili za kuku kuonyesha kama viungo kuvimba, kuuma, kushindwa kufanya kazi, na kupungua kwa basa kadri muda unavyoendelea. Ugonjwa huu unawapata kuku wadogo wenye umri kati ya wiki 3 hadi 6 ambao basa yao inafanya kazi. Mara chache ugonjwa huu unaweza kuwapata kuku hadi wenye umri wa wiki 18. Kwa mara ya kwanza ugonjwa ulitambuliwa katika

wilaya ya Delaware huko Marekani na ndiko ulikopewa jina hili la Gumboro. Baadaye kulingana na kuwa ugonjwa unashambulia kuku wenye basa inayofanya kazi ukaitwa pia IBD. Tanzania ugonjwa huu ulithibitishwa miaka ya 1980 japo hisia zilikuwepo hata kabla ya hapo. Mashambulizi ya ugonjwa huu hulenga mfumo wa kinga ya mwili (basa) wa kuku na ndiyo maana wadudu wengine wa magonjwa ambao mara nyingi hawana madhara huanza kuonyesha madhara.

11

Kuenea kwa ugonjwa huu hutokea kwa kuku kugusana, kinyesi chenye


Mkulima Mbunifu

sana. Endapo itatolewa kwa usahihi, kinga ya mwili inaweza kuongezeka. Hakuna tiba kamili inayotolewa kwa ajili ya basa ya kuku, na matumizi ya aina tofauti tofauti za dawa zinaweza kuchochea zaidi ongezeko la vifo. Hatua muhimu kama vile kuongeza uwepo wa hewa ya kutosha na kunywesha maji kwa wingi inaweza kuwa na faida zaidi.

virusi vya ugonjwa huu, mwangalizi wa kuku, njia ya hewa, vifaa vya kulishia, na mara nyingine wadudu na ndege wa porini. Ni ugonjwa unaosambaa kwa haraka sana kutoka kuku mmoja kwenda kwa mwingine. Kuku ambao hustahimili maambukizi ya awali wanaweza kupona kwa haraka katika kipindi cha wiki mbili. Chanjo ya ugonjwa huu inapatikana lakini ni lazima itumiwe kwa umakini

Mahepe (Mareks) A

B

A) Muonekano wa jicho la kuku ambaye hajaathiriwa B) Jicho la kuku mwenye ugonjwa wa Mahepe

Ugonjwa wa mareki ni ugonjwa wa kuku unaotokana na maambukizi yanayosababishwa na virusi. Ugonjwa huu una dalili tofauti tofauti zilizo wazi. Moja wapo ni pamoja na miguu au mabawa kupooza, macho kuvimba, kuwa na uvimbe kwenye moyo, mirija ya uzazi, korodani, misuli na mapafu. Pia kuwa na vivimbe kwenye vitundu vya manyoya.

kutokea mpaka kufikia asilimia 100. Vifo vinavyotokana na maambukizi huendelea taratibu au kwa kasi kwa wiki chache. Kuku walioathirika huwa wanakuwa wepesi kushambuliwa na magonjwa mengine yanayosababishwa na wadudu nyemelezi pamoja na bakteria. Kwa kawaida njia ya maambukizi hupitia njia ya hewa, na kwa kiasi kikubwa ugonjwa huenezwa kutoka ndege mmoja kwenda mwingine.

Hali ya afya ya ndege kuzorota huwa ni asilimi 10-50, na vifo vinaweza

12

Mwangozo wa ufugaji wa kuku

Dalili za ugonjwa huu ni

• Kupooza kwa miguu, mabawa na shingo

rangi ya kijivu

• Kupoteza uzito

• Sehemu ya ngozi nyoya lilipoota huvimba na kuwa rafu

• Kutokuona vizuri

• Sehemu ya ndani ya jicho kuwa na

Mharo mwekundu (coccidiosis) Huu ni ugonjwa wa ndege unaosababishwa na vimelea wadogo sana wanaoujulikana kama coccidian, ugonjwa huu huambatana na kuku kuharisha pamoja na kusaababisha vifo. Kuku walioathiwa na ugonjwa huu huonyesha dalili zifuatazo. Kati ya majuma manne hadi kumi hivi, baada ya kuambukizwa kuku huharisha damu, Kuku ambao wameshikwa na ugonjwa huu, huonekana wemedhoofika sana na huwa kama wamevaa koti, na shingo yao huinama chini.

Kinyesi cha kuku wenye ugonjwa wa mharo mwekundu (Coccidiosis)

Mfugaji inampasa ahakikishe kuwa haruhusu unyevunyevu kwenye takataka zinazowekwa ndani ya chumba kwa kulalia kuku, hasa kwenye nyumba ya kulelea vifaranga sehemu ambazo humwagwa sana maji ovyo kuzunguka vyombo vya maji.

Kuku hao hawashughuliki kutafuta chakula wala maji, na husinzia mara kwa mara kwenye pembe za nyumba. Vifo hutokea vingi kila siku. Kuku wakubwa ambao hawakufa hukuwa taratibu sana. Utagaji wa mayai hucheleweshwa au hupungua. Wakati mwingine kinyesi cha kuku hao huwa na rangi ya kahawia baadaye kuwa na damu. Ugongwa huu hupona haraka kama matibabu yataanza mapema. Mfugaji amwone haraka bwana mifugo aliye karibu naye, ili amshauri dawa ambazo zinatumika, kwa sehemu mbalimbali. Uzingatiaji wa masharti ya dawa ni jambo muhimu sana. Kuushinda ugonjwa huu kunategemea usafi wa mfugaji.

Sehemu hizi ni lazima zitupiwe macho mara kwa mara. Ikiwezekana vyombo vya maji na chakula viwekwe kwenye chakula au maji.

13

Vifaranga wasisongamane sana kwenye chumba kidogo. Chakula cha vifaranga kitiwe dawa ya kuzuia ugojwa huu, na hii ndio njia iliyo bora zaidi na yenye uhakika katika kuzuia ugonjwa huu. Dawa huleta matokeo mazuri sana iwapo itaambatana na usafi.


Mkulima Mbunifu

Mwangozo wa ufugaji wa kuku

Maswali yanayo ulizwa mara kwa mara na wafugaji sehemu nyingi vijijini na majibu ya wataalam Swali: Endapo nitachanja kuku wangu dhidi ya mdondo lakini jirani zangu hawakuchanja kuku wao, je kuku wangu hawataathirika ugonjwa unapotokea kwa majirani?

kuvimba macho linatokea wakati wa kiangazi na mwanzoni mwa mvua kutokana na ukosefu vitamini na hususani vitamini A ambazo hupatikana katika majani mabichi.

Jibu: Kinga itokanayo na chanjo hufikia kiwango cha juu kabisa siku ya 14 na endapo ugonjwa utafika kwa jirani yako wakati kuku wako wamekwisha chanjwa kwa chanjo sahihi basi ni dhahiri kwamba hawataathirika kwa ugonjwa huo.

Wakati wa kiangazi kuku hushindwa kula majani makavu na hivyo kupata upungufu wa vitamini hizo. Ugonjwa huo wa upofu wa macho/kuvimba macho hujulikana kama Avitaminosis A (ukosefu wa vitamini A mwilini)

hula mayai au wao wenyewe kudonoana? Jibu: Kuku hula mayai kutokana na upungufu wa protini miilini mwao na upungufu huo husababisha tabia ya wao kudonoana kwa lengo la kupata protini tabia ambayo hujenga mazingira ya kupata bacteria na virusi na kusababisha hata vifo. Mayai kuliwa hupunguza uzalishaji wa kuku. Ili kuepuka matatizo kama haya chakula cha kuku kinapaswa kuwa na asilimia 19 ya protini katika mchanganyiko wake. Vinginevyo, kuku wanapaswa kupunguzwa midomo kama ilivyo kwenye picha ifuatayo.

Swali: Ni kwanini kuku hunyonyoka manyoya wakati wa kiangazi?

Jibu: Kuku hunyonyoka manyoya kutokana na upungufu mkubwa wa protini kutokana na majani yenye protini kukauka, wadudu kuwa wachache wakati huo na upungufu wa vitamini A ambayo ni muhimu katika kuimarisha ngozi inayoshikilia manyoya. Swali: Kwanini wakati mwingine kuku

Swali: Je ni ugonjwa gani unaoambatana na kutokwa kwa vipele/vidonda sehemu zisizo na manyoya kwa kuku?

Swali: Wakati mwingine tunapo-chanja kuku kwa kutumia I-2 kuku wetu huanza kufa kwa wingi. Je hii inatokana na nini?

Jibu: Ugonjwa huo hujulikana kama ndui ya kuku (Fowl pox) na huathiri kuku wa rika zote. Ijapokuwa wale wadogo huathirika zaidi na hata kufa kuliko wakubwa.

Jibu: Chanjo yoyote inapaswa kuchanjwa kwa kuku wasio wagonjwa na ambao hawapo kwenye mwatamio wa vimelea vya ugonjwa (muda ambao kuku anapata vimelea hadi dalili zinapojitokeza). Chanjo ina vimelea vya ugonjwa vilivyopunguzwa nguvu ya kusababisha ugonjwa. Endapo vitachanjwa kwa kuku wenye vimelea tayari, basi vitaongezea makali ya vimelea katika mwatamio na kuharakisha kujitokeza kwa ugonjwa na hatimaye kwa magonjwa yasiyo na tiba kuku atakufa. Hivyo chanjo ni lazima itolewe kwa kuku wazima na kabla ya mwatamio. Vinginevyo kuku ni lazima watakufa

Ugonjwa hujitokeza zaidi baada ya ukame mrefu na mwanzoni mwa msimu wa mvua katika mazingira ya mabanda ya sakafu za chini na machafu na yanayovuja maji. Hata hivyo ugonjwa huu haujitokezi kwa kuku waliopewa mchanganyiko wa vitamini na hususani vitamini A wakati wa kiangazi. Vinginevyo ugonjwa hukingwa kwa chanjo ya kuchoma kwenye mabawa ambao huhitaji utaalam. Swali: Mara baada ya kuku kuanza kunya kinyesi chenye minyoo, hudhoofika na ghafla unaweza kumkuta kuku kafa bandani. Je tufanyeje ili kuepuka hasara kama hiyo?

Swali: Hata kama tukiwachanja kuku wetu zidi ya Mdondo, bado kuna vifo vya kutisha kwa vifaranga na kuku wakati wakiwa na dalili za kuvimba macho hasa wakati wa kiangazi. Je, huu ni ugonjwa gani? Je hausababishwi na matone ya chanjo? Jibu: Tatizo la vifo vingi vya vifaranga na vifaranga wakubwa baada ya

wenye minyoo mfugaji anaweza kuwa na utaratibu wa kuwapatia kuku wake dawa za minyoo mara moja kila baada ya miezi mitatu.

Jibu: Minyoo ina tiba na dawa zinapatikana katika maduka ya dawa za mifugo. Mbali na kutibu kuku

14

Mtaalam wa mifugo akielekeza kwa vitendo ukataji wa midomo kwa kuku wenye tabia ya kula mayai (kijiji cha KiwalalaNarunyu, Lindi)

Swali: Ni kwanini kuku hutaga mayai mengi na kutotoa machache tu?

wa kuku wakati wa usiku na kukabili wanyama na ndege walao kuku?

Jibu: Sababu yaweza kuwa ni kuku kutokaa kwenye mayai kwa muda mrefu kutokana na kukosa chakula, kuku aatamiaye kufungiwa nje kwa zaidi ya masaa mawili, minyoo, wadudu na upungufu wa vitamini katika mayai.

Jibu: Fuga mbwa angalau wawili, mmoja afungwe karibu na banda usiku na mmoja abaki huru. Kwa upande wa ndege kama mwewe ni vema kuwafungilia kuku mida ya saa nne hadi tano asubuhi wengi wao wakiwa wamekwisha winda na kuchoka. Mbwa watasaidia pia kuwafukuza wanyama walao kuku.

Swali: Je naweza vipi kukabili wizi

15


Mkulima Mbunifu

Hifadhi mayai kwa muda mrefu

Mayai ni bidhaa hafifu na inayoharibika kwa haraka. Hivyo, ni lazima ishikwe kwa uangalifu na kutunzwa vizuri baada ya kutagwa ili yasivunjike au kuharibika.

• Utunzaji sahihi wa mayai huyafanya yaepukane na madhara yanayoweza kutokana na viumbe wadogo wadogo kama vile bakteria, wanyama walao mayai, upotevu wa unyevu, au joto wakati wa uhifadhi na kusafirisha kwenda sokoni, jambo linaloweza kuyafanya yavunjike. Mayai kama ilivyo kwa viumbe hai wengine yanahitaji kupumua.

• Wafugaji wenye uzoefu wamekuwa na uwezo wa kuhifadhi mayai kwa kipindi cha miezi 6-7 kwa kutumia jokofu. Kamwe usihifadhi mayai unayokusudia kutumia kwa ajili ya kuhatamiwa kwenye jokofu.

• Trei za kuhifadhia mayai ziwekwe kwenye sehemu yenye hewa inayozunguka, hasa hewa ya oxijeni. Weka trei katika hali ya usafi, zisiwe na harufu ili kuepuka kufishwa au kusababisha hali yoyote inayoweza kusababisha uharibifu.

• Wafugaji wadogo hutumia kuku au ndege mwingine ambaye hupewa mayai na kuyahatamia mayai hadi kuanguliwa. Kuku wa kienyeji ni wazuri sana wanapotumiwa kwa ajili ya uzalishaji wa vifaranga. Hata hivyo, kwa uzalishaji mzuri ni lazima mfugaji ahakikishe kuwa kuku anapewa mayai yenye uwezekano mkubwa wa kuanguliwa.

• Mayai yanaweza kuharibika kwa haraka kutokana na joto kali. Mayai ni lazima pia yakingwe dhidi ya joto kali pamoja na unyevu. Ni lazima kuhakikisha kuwa mayai yanahifadhiwa sehemu yenye ubaridi, ambayo siyo kavu sana, vinginevyo yatapoteza unyevu kwa haraka endapo yatawekwa sehemu kavu.

Muongozo huu umechapishwa na Mkulima Mbunifu kwa ufadhili wa Biovision Foundation www.biovision.ch na Biovision Africa Trust www.biovisionafricatrust.org Imeandaliwa kwa ushirikiano wa watafiti: Dr Albano Oscar Mbyuzi (VIC Mtwara), Dr Erick V.G.Komba (FVM, SUA), Mr. Rutashobya R.C.T (LRC Naliendele) na kuhaririwa na Ayubu Nnko, John Cheburet. Mpangilio: James Wathuge Mkulima Mbunifu: S.L.P. 14402 Makongoro Street Arusha Rununu: 0717 266 007, 0785 133 005 www.mkulimambunifu.org Barua pepe: info@mkulimambunifu.org

16


Turn static files into dynamic content formats.

Create a flipbook
Issuu converts static files into: digital portfolios, online yearbooks, online catalogs, digital photo albums and more. Sign up and create your flipbook.