NENO LA MSALABA - Toleo la Nane

Page 1

TOLEO LA NANE| DISEMBA 2022
NENO LA MSALABA
NA MCHUNGAJI RAPHAEL MARKO SALLU
ATAKAPOKUJA MWANA WA ADAMU ATAIKUTA IMANI DUNIANI?

NENO LA FARAJA KWA MSOMAJI

Neno la msalaba ni jarida ambalo Bwana ameniongoza kuliandika toka mwaka wa 1990. Tangu wakati huo limewafikia watu mbali mbali na wengi kushuhudia kwamba limewasaidia kuwajenga. Nami najua kwamba wewe ambaye unalisoma sasa si kwa bahati mbaya bali ni kwa mpango na kusudi la Mungu. Namuomba Bwana akufunulie akili zako upate kuyaelewa maandiko.Ili upate kitu cha kufaa kuwafundisha watu wengine.“Basi, sasa nawaweka katika mikono ya Mungu, na kwa Neno la neema yake ambalo laweza kuwajenga na kuwapa urithi pamoja nao wote waliotakaswa. ”Neema ya Bwana wetu Yesu Kristo na iwe pamoja nanyi nyote. Amina."

N E N O L A M S A L A B A
Mchungaji Raphael Marko Sallu
YALIYOMO ATAKAPOKUJA MWANA WA ADAMU ATAIKUTA IMANI DUNIANI? TOLEO LA NANE | DISEMBA 2022 ANWANI Mch. Raphael Marko Sallu Divine Grace Church - Kange, Tanga - Tanzania. raphaelsallu2@gmail.com +255 742 179 677 HAKI ZOTE ZIMEHIFADHIWA. Kudumu katika imani Usigeuzwe Usidanganyike Namna ya kuzijaribu Roho Kupima kwa Neno

A T A K A P O K U J A M W A N A

W A A D A M U A T A I K U T A I M A

“Nawaambia, atawapatia haki upesi; walakini, atakapokuja Mwana wa Adamu, je! Ataiona imani duniani?”

(Luka 18:8)

Nataka kusema maneno machache juu ya imani.Imani ninayoizungumzia ni imani ya wateule,ambayo mtume Paulo alisema hivi: “Paulo, mtumwa wa Mungu, na mtume wa Yesu Kristo; kwa ajili ya imani ya wateule wa Mungu, na ujuzi wa kweli ile iletayo utauwa;”

(Tito1:1)

Mtume Paulo alipomwandikia Tito barua,alijitambulisha kama mtumwa wa Mungu na mtume wa Yesu kwa ajili ya imani ya wateule wa Mungu.Hawa wateule wa Mungu ndiyo wale waiyoamini na kupewa uwezo wa kuwa watoto wa Mungu,hawa ndiyo waloitwa wateule wa Mungu. Na mimi ndiyo ninaosema nao hapa katika maandiko haya. Juu ya imani hii pia Petro alisema hivi: “Simoni Petro, mtumwa na mtume wa Yesu Kristo,

kwa wale waliopata imani moja na sisi, yenye thamani, katika hali ya Mungu wetu, na Mwokozi Yesu Kristo. (2 Petro 1:1) Mtume Petro aliwaandikia waliopata imani moja na wao,anasema imani hiyo ni yenye thamani katika hali ya Mungu wetu. Imani hii ndiyo ninayotaka kuilezea kwa kina katika somo hili,nami naamini siyo kwa bahati mbaya kwamba wewe unasoma,najua kwa hakika kwamba ni kwa mpango na kusudi la Mungu kwamba wewe usome,na ninaamini kwamba Bwana atakufunulia ili kwamba upate jambo la kukusaidia.Juu ya hii imani Yuda naye analo la kutuambia,alisema hivi:

“Wapenzi, nilipokuwa nikifanya bidii sana kuwaandikia habari ya wokovu ambao ni wetu sisi sote, naliona imenilazimu kuwaandikia, ili niwaonye kwamba mwishindanie imani waliyokabidhiwa watakatifu mara moja tu. “(Yuda 1:3)

N I D U N I A N I ?
N A M C H U N G A J I R A P H A E L M A R K O S A L L U

Yuda anasema alipokuwa akifanya bidii sana kuwaandikia habari ya wokovu aliona inamlazimu kuandika habari za wokovu ili kuwaonya,kuwaonya nini? Kuwaonya kwamba inawapasa watu waliokoka waishindanie imani waliyokabidhiwa watakatifu. Hii imani ya thamani tumekabidhiwa sisi watakatifu tuliopo duniani. Kwa hiyo ndugu yangu msomaji,unatakiwa kabisa uishindaniye imani hii ambayo mwanzilishi wake ni Bwana Yesu.

“tukimtazama Yesu, mwenye kuanzisha na mwenye kutimiza imani yetu; ....”(Waebrania 12:2)

Unaona ndugu mwanzilishi wa imani hii ni Bwana wetu Yesu kwa hiyo inapasa kwanza kuishindania lakini pia kudumu katika imani hii maana Bwana atakaporudi atataka kuiona imani duninia kama tulivyosoma katika andiko letu la msingu Luka 18:8.

KUDUMU KATIKA IMANI

“mkidumu tu katika ile imani, hali mmewekwa juu ya msingi, mkawa imara; msipogeuzwa na kuliacha tumaini la Injili mliyosikia habari zake, iliyohubiriwa katika viumbe vyote vilivyo chini ya mbingu; ambayo mimi Paulo nalikuwa mhudumu wake. “(Wakolosai 1:23)

Kudumu katika imani,neno kudumu maana yake kuendelea Kwa hiyo tunaposema kudumu katika imani tunamaanisha kuendelea katika imani,haitoshi tu kuwa

umeamini,jambo la msingi ni kwamba uendelee katika imani hiyo.Mtume Paulo alipoliandikia kanisa la Wakolosai,katika mstari huo hapo juu,alisema “mkidumu tu katika ile imani.”

kwa kusema hivi inaonyesha wapo watu ambao hawataendelea na ile imani.Na kama mtu hataendelea na imani,atakuwa amepoteza nafasi yake.Kabla Paulo hajasema maneno haya mkidumu tu,alitangulia kusema hivi,hebu tuangalie haya maandiko.

“Na ninyi, mliokuwa hapo kwanza mmefarikishwa, tena adui katika nia zenu, kwa matendo yenu mabaya, amewapatanisha sasa; katika mwili wa nyama yake, kwa kufa kwake, ili awalete ninyi mbele zake, watakatifu, wasio na mawaa wala lawama; “(Wakolosai 1:21-22)

Unaona paulo anaelezea kwamba,hapo kwanza walikuwa wamefarikishwa tena walikuwa maadui katika nia zao,kwa sababu ya matendo mabaya,lakini anasema wamepatanishwa hawana uadui tena,na imetokea hivyo kwa kifo chake.

Na hiyo anasema ni ili awalete mbele zake watakatifu,wasio na mawaa wala lawama,ndipo akasema mkidumu tu katika ile imani,maana yaake nini? Kama mtu hatadumu katika imani,(1) anapoteza utakatifu,na (2)atalaumika. Ndiyo maana nasisitiza kuendelea na hii imani ya wokovu.

DISEMBA 2022 • NENO LA MSALABA

Ukiuangalia huo mstari wa ishirini na tatu kwa umakini,utaona kuna mambo yanayosababisha watu kutokudumu katika imani. Jambo la kwanza ni kutokuwekwa kwenye msingi.

Umeandikwa hivi: “mkidumu tu katika ile imani, hali mmewekwa juu ya msingi, mkawa imara; ....”(Wakolosai 1:23)

Unaona haya maneno.HALI MMEWEKWA JUU YA MSINGI,mtu asipowekwa juu ya msingi hawi imara,watu wengi hawajawekwa juu ya msingi na matokeo yake hawako imara,na wengine wamegeuzwa,kama tutakavyoona hapo mbele. Lakini tuangalie kwanini watu hawawekwi kwenye msingi? Na msingi ni nini? Kwanza tuangalie msingi ni nini.

“Kwa kadiri ya neema ya Mungu niliyopewa, mimi, kama mkuu wa wajenzi mwenye hekima, naliuweka msingi, na mtu mwingine anajenga juu yake. Lakini kila mtu na aangalie jinsi anavyojenga juu yake.

Maana msingi mwingine hakuna mtu awezaye kuuweka, isipokuwa ni ule uliokwisha kuwekwa, yaani, Yesu Kristo.” (1Wakorintho 3:10-11)

Kulingana na maandiko haya,msingi ni Yesu. Paulo anasema yeye ni mkuu wa wajenzi na kwamba amekwisha kuweka msingi. Sitaki leo kuelezea ukuu wa ujenzi wa Paulo,ila nataka tu kukuonyesha kwamba msingi aliouweka Paulo ni Bwana Yesu.

Sasa kwanini watu wengi hawajawekwa kwenye msingi? Ni wajenzi,wajenzi wengi badala ya kuwaweka watu kwa Yesu ambaye ndiye msingi,wanawaweka zaidi kwenye dini,au kwenye vitu badala ya kuwaweka kwenye msingi,kwa hiyo kama watu wengi hawawekwi kwenye msingi,ni kwa sababu ya wajenzi,kama mjenzi, atakazia juu ya dini zaidi ya neno la Mungu basi hao wanaojengwa watajengeka katika hilo analolijenga huyo mjenzi na wala si juu ya msingi,kama mjenzi atakazia juu ya mapokeo ya kusanyiko lake, na kuyafanya hayo mapokeo kuwa bila hayo mtu hajakamilika,basi huyo mjenzi atakuwa anawaweka watu wake nje ya msingi.

Hebu angalia hii: “Wakashuka watu waliotoka Uyahudi wakawafundisha wale ndugu ya kwamba, Msipotahiriwa kama desturi ya Musa hamwezi kuokoka".

Basi baada ya Paulo na Barnaba kushindana na watu hawa na kuhojiana nao sana, ndugu wakaamuru kwamba Paulo na Barnaba na wengine miongoni mwao wapande kwenda Yerusalemu kwa mitume na wazee kwa habari ya swali hilo.”(Matendo 15:1-2) Unaona wajenzi hawa watumishi waliyotoka Uyahudi,jinsi walivyofundisha mapokeo yao,na wakisema bila kuyafuata mapokeo hayo watu hawezi kusema wameokoka. Walitaka kuwatoa watu kwenye msingi Paulo akashindana nao,kwa sababu aliona wanapotosha.

DISEMBA 2022 • NENO LA MSALABA

Kwa hiyo watu wanatakiwa wawekwe kwenye msingi ili wawe imara. Na msingi ni Bwana Yesu.Jambo lingine,tunaloliona katika mstari wa ishirini na tatu,linalosababisha watu kutodumu katika imani,ni kugeuzwa. Hebu tuusome tena huu mstari:

“mkidumu tu katika ile imani, hali mmewekwa juu ya msingi, mkawa imara; msipogeuzwa na kuliacha tumaini la Injili mliyosikia habari zake, iliyohubiriwa katika viumbe vyote vilivyo chini ya mbingu; ambayo mimi Paulo nalikuwa mhudumu wake.” (Wakolosai 1:23)

Mtume Paulo,anaongelea swala la kugeuzwa na kuliacha tumaini la Injili,kwa kusema hivi Paulo inaonyesha watu wanaweza kugeuzwa na kuiacha imani,kwa maneno mengine ni kwamba watu hao waliogeuzwa wameshindwa kudumu katika imani na kuiacha. Nini kinasababisha hata mtu akaiacha imani? Ni mafundisho. Watu wasipokuwa makini Bwana atakapokuja hataiona imani duniani,kwa maneno mengine

hataikuta imani duninia watu watakuwa wameguzwa na kuliacha tumaini la Injili. Biblia inasema tusiamini kila mtu anayeleta mafundisho yake. Imaandikwa hivi: “Wapenzi, msiiamini kila roho, bali zijaribuni hizo roho, kwamba zimetokana na Mungu; kwa sababu manabii wa uongo wengi wametokea duniani.”(1 Yohana 41)

Unaona mpendwa hii tahadhari,unaliona hili onyo alilolitoa mtume Yohana Anasema tusiamini kila roho,siyo kila roho inatoka kwa Mungu,nyingine zinatoka kwa shetani,na kazi yake kubwa ni kubomoa ,wakati roho zinazongozwa na Roho Mtakati ni kujenga,roho zinazoongozwa na shetani ni kubomoa,wakati roho zinazotokana na Mungu ni kuwaweka watu katika msingi,roho zinazotokana na shetani ni kuwageuza watu kuiacha imani. Kwa hiyo Yohana anashauri tusiamini kila roho bali tuzijaribu. Yohana anasema manabii wa uongo wengi wametokea,zingatia hili wengi,ndiyo wapo wengi tu,sikia na siyo manabii tu,hata na mitume wa uongo,na walimu wa uongo pia.

DISEMBA
• NENO LA MSALABA
2022
USIGEUZWE

USIDANGANYIKE

Neno la Msalaba

Katika nyakati hizi tulizonazo,nyakati hizi za siku za mwisho,watumishi wengi wa uongo wanafanya kazi na kudanganya wengi,neno la Mungu linatutaka sisi tulioamini tusidanganywe,hebu tusome mistari hii:

“Hata alipokuwa ameketi katika mlima wa Mizeituni, wanafunzi wake wakamwendea kwa faragha, wakisema, Tuambie, mambo hayo yatakuwa lini? Nayo ni nini dalili ya kuja kwako, na ya mwisho wa dunia? Yesu akajibu, akawaambia, Angalieni, mtu asiwadanganye.

Kwa sababu wengi watakuja kwa jina langu, wakisema, Mimi ni Kristo; nao watadanganya wengi.”(Mathayo 24:2-5).

Majibu ya Bwana Yesu,yanatupa kufikiri kwa kina,kwanza anasema angalieni mtu asiwadanganye,lakini pili anasema wengi watakuja kwa jina lake,wakisema yeye ni Kristo,nao watadanganya wengi.Jambo la kwanza anaonya,mtu asiwadanganye,alijua watu watadanganywa na kudanganyika,na ndicho kinachotokea wakati huu,watu wanadanganywa na wala hawajui kuwa wamedanganyika. Lakini mbili alisema wengi watakuja kwa jina lake,maana yake watasema wao ni wakristo,watasema wameokoka,halafu Bwana anasema watawadanganya wengi.

Na kwanini watafanikiwa kudanganya wengi? Ni kwa sababu watakuja kwa jina la Yesu,watu watawafikiria ni watumishi wa Yesu,kumbe siyo,na kwa sababu watu wanawafikiria ni watumishi wa Yesu,wataaminiwa,na kwa sababu hiyo kupata nafasi ya kuwadanganya wengi.

Ni mazungumzo kati ya Bwana Yesu na wanafunzi wake,katika mazungumzo haya,tunaona wanafunzi wakitaka kujua dalili za kuja kwa Bwana na mwisho wa dunia.

Mimi sipati shida sana na watu wasiomini wakidanganyika,kwa sababu wao ni waupande huohuo,wao hawageuzwi maana hawajawahi kugeuka,lakini mtu aliyeamini, ukakuta anamfuata nabii wa uongo anayepotosha,maanayake huyu mwamini anageuzwa kuiacha imani. Huyu mwamini ndiye aliyeambiwa, “angalienini mtu asiwadanganye” huyu mwamini ndiye aliyeambiwa,

D I S E M B A 2 0 2 2 • N E N O L A M S A L A B A

Neno la Msalaba

NAMNA YA KUZIJARIBU ROHO

Kuna namna mbili kubwa za kuzijaribu roho,(kuzipima) ninazozifahamu mimi. Namna ya kwanza ni kwa neno la Mungu. Namna ya pili ni kwa karama ya kupambanua roho. Katika karama tisa za roho,zinazoelezwa na Paulo,ipo karama ya kupambanua roho. Sasa katika somo hili mimi nataka kuelezea kuzijaribu kwa Neno la Mungu.

Na hii ni kwa sababu kila mtu anatakiwa atumie neno kupima kwamba roho hii inatokana na Mungu? Hiki kinachofanyika kinatokana na Mungu? Kupima kwa karama nitaelezea kwenye somo lingine la karama. Na hii kupima kwa kupambanua kwa karama ya kupambanua si kila mtu anaweza kupima,ila ni kwa mwenye karama hiyo.

KUPIMA KWA NENO

Ili kupima kwa neno,kwanza mpimaji ni lazima awe na ufahamu wa Neno la Mungu. Pili awe na ufahamu wa kutafsiri maandiko Mungu ametupa neno la Mungu ili kutuongoza,na kwa neno hili la Mungu ndilo lililotuambia tusiamini kila roho bali

tuzijaribu,pia mahali pengine neno linasema hivi: “Msimzimishe Roho; msitweze unabii; jaribuni mambo yote; lishikeni lililo jema; “(1Wathesalonike 5:19-21)

Hapa neno linasema,msimzimishe ,yaani msizuie utendaji wa Roho Mtakatifu ndani ya mtu,pia msitweze unabii,maana yake msizarau unabii,kwanini unajua,kwasababu,huduma ya unabii imetolewa na Mungu kwa kusudi la Mungu la kuujenga mwili wa Kristo,kama zilivyo huduma nyingine,kwa hiyo wapo manabii ambao wanaongozwa na Roho Mtakatifu,na wapo pia wanaoongozwa na shetani,na pia wapo wanaongozwa na roho zao wenyewe.

Kwa sababu hiyo ndiyo nmaana neno linasema,jaribuni mambo yote lishikeni lilo jema. Sasa namna ya kujaribu,au kwa maneno mengine kupima,ni kwa neno la Mungu

Labda mtu mmoja anajiuliza napimaje kupitia neno? Kama nilivyosema kule juu ni muhimu mpimaji alielewe neno,ili nabii anapotoa ujumbe aupime huo ujumbe kama unakubaliana na neno la Mungu,au anapofanya ishara hizo ishara zinakubaliana na neno?

D I S E M B A 2 0 2 2 • N E N O L A M S A L A B A

Neno la Msalaba

Mtakatifu ndiye anayetoa karama na kumuongoza nabii katika utendaji,kama nabii huyo ni wa kweli. Na kama nabii ni wa uongo ataongozazwa na roho ya shetani,sasa ili kujua kama mtu huyu anaongozwa na Roho wa Kristo,kuna tabia ya Roho wa Kristo itajionyesha kwa huyo nabii,hebu tusome maandiko haya:

“Lakini yeye atakapokuja, huyo Roho wa kweli, atawaongoza awatie kwenye kweli yote; kwa maana hatanena kwa shauri lake mwenyewe, lakini yote atakayoyasikia atayanena, na mambo yajayo atawapasha habari yake.

Yeye atanitukuza mimi, kwa kuwa atatwaa katika yaliyo yangu na kuwapasha habari.”(Yohana 16:13- 14).

Unaona,maneno haya aliyasema Bwana Yesu wakati akiwa hapa ulimwenguni,na aliongea juu ya Roho Mtakatifu,na kwamba huyo Roho hatanena kwa shauri lake. Ninalotaka hasa tuliangalie ni mstari wa kumi na nne,ambao unasema,yeye atanitukuza mimi.

Hiyo ni tabia ya Roho,kwamba katika utendaji wake kusudi kubwa ni kumtukuza Yesu. Sasa ukimuona nabii anajitukuza ujue hiyo siyo Roho wa Mungu. Yaani anataka ajulikane yeye zaidi ya Yesu,ujue huyo siye. Utakuta mtumishi anatumia nguvu kubwa ili ajulikane kwamba amefanya jambo fulani,ujue hiyo ni Roho nyingine.

Roho Mtakatifu atamtukuza Yesu,atataka Bwana Yesu atukuzwe,na yeye hata asitajwe. Hebu ona watumishi hawa: “Basi alipokuwa akiwashika Petro na Yohana, watu wote wakawakusanyikia mbio katika tao lile lililoitwa tao la Sulemani, wakishangaa sana.

Hata Petro alipoyaona haya akawajibu wale watu, Enyi Waisraeli, mbona mnastaajabia haya, au mbona mnatukazia macho sisi, kana kwamba tumemfanya huyu aende kwa nguvu zetu sisi, au kwa utauwa wetu sisi?”(Matendo 3:11-12)

HIli lilikuwa ni tukio lililofanywa na kina mtume Petro la kumponya mtu kiwete muombaji,na baada kuponywa kwa kiwete huyo watu wangi walistajabu wakakusanyika kwa kina Petro,na Petro alipoona akawauliza wale watu,mbona mnatukazia macho sisi,kwa maneno mengine mbona mnatutazama sisi?

D I S E M B A 2 0 2 2 • N E N O L A M S A L A B A

Kana kwamba tumemfanya mtu huyu aende kwa nguvu zetu sisi,au kwa utauwa wetu sisi? Petro alimtukuza Yesu,na hii ni kwa sababu Roho Mtakatifu alisema Bwana atakapokuja atamtukuza Yesu. Ukisoma mstari wa kumi na sita maneno yanasema hivi:

“Na kwa imani katika jina lake, jina lake limemtia nguvu mtu huyu mnayemwona na kumjua; na imani ile iliyo kwake yeye imempatia huyu uzima huu mkamilifu mbele yenu ninyi nyote.”(Matendo 3:16)

Baada ya Petro kuwambia wale watu kwamba wasikaziwe macho wao,ndipo wakawaeleza namna yule kiwete alivyoponywa,kwamba ni kwa imani katika jina lake,yaani jina la Yesu,na imani iliyo kwake kiwete ilimpa uzima mkamilifu. Sikia ndugu yangu mambo yote yanatokea kwa sababu ya jina la Yesu,si kwa sababu ya kitu chochote kile. Kuna mambo yananishangaza siku za leo,kwamba watu wanaamini katika vitu badala ya kuaminishwa katika jina la Yesu. Nimewaona watu wanaaminishwa juu ya maji zaidi ya jina la Yesu,ukiona hivyo ujue kuna shida.Biblia inasema, “Wala hakuna wokovu katika mwingine awaye yote, kwa maana hapana jina jingine chini ya mbingu walilopewa wanadamu litupasalo sisi kuokolewa kwalo.”(Matendo 4:12)

Hapana wokovu,hakuna uponyaji,katika mwingine awaye yote,wala kingine,kwa maana hapana jina jingine nchini ya mbingu tukilopewa litupasalo sisi kuokolewa ikiwa ni pamoja na

kuponywa,isipokuwa jina la Yesu. Jina la Yesu linatosha. Mungu na akusaidie usigeuzwe wewe mtu uliyezaliwa mara ya pili,kuviamini vitu badala ya Yesu. Vitu vitaisha Yesu ni wa milele,na yupo kila mahali.

Kwa hiyo ukiona nabii hamtukuzi Yesu anajitukuza yeye ujue huyo siye.Roho Mtakatifu ndani yetu atamtukuza Yesu,na hiyo itaonekana wazi kwa nabii wa kweli. Mungu akubariki Neema ya Bwana Wetu Yesu Kristo na iwe pamoja nanyi. Amina.

D I S E M B A 2 0 2 2 • N E N O L A M S A L A B A Neno la Msalaba

NENO LA MSALABA

T O L E O L A N A N E
Na Mchungaji Raphael Marko Sallu

Turn static files into dynamic content formats.

Create a flipbook
Issuu converts static files into: digital portfolios, online yearbooks, online catalogs, digital photo albums and more. Sign up and create your flipbook.