![](https://assets.isu.pub/document-structure/230622092229-ed7357656061758bb4b0bc1289fe3033/v1/6d687118bda45c398b99cceb4aa18583.jpeg?width=720&quality=85%2C50)
1 minute read
Hekalu la Patakatifu
Ghafla giza lilitoweka msalabani. Na kwa sauti kama ya tarumbeta ambayo ilisikika kuvuma ulimwenguni kote, Yesu akapaza sauti, “Imekwisha.” “Ee Baba, mikononi mwako naiweka roho yangu.” Tena giza likaifunika nchi, na kukatukia tetemeko kuu la nchi. Kukawa na wasiwasi. Katika milima ya karibu miamba ilipasuka mapande na kuviringika mabondeni. Makaburi yalifunguliwa na wafu wakatupwa nje. Makuhani, askari, wanyongaji, na watu wote waliokuwapo hapo walianguka kifudifudi. Wakati sauti ya kilio “Imekwisha” iliposikika kutoka mdomoni mwa Kristo, ilikuwa ni wakati wa kutoa dhabihu ya jioni. Kondoo anayemwakilisha Kristo alikuwa ameletwa kuchinjwa. Lakini nchi ilitetemeka kwa sababu Bwana Mwenyewe alikaribia karibu. Kwa sauti ya mpasuko, pazia la hekalu likapasuliwa kwa mkono usioonekana vipande viwili toka juu hata chini; na kukifungua wazi kwa macho ya watu chumba cha patakatifu pa patakatifu palipokuwa pakijaa utukufu wa Mungu. Mahali patakatifu mno pa hekalu la dunia hapakuwa patakatifu tena. Kote kukawa na hofu kuu na kuchanganyikiwa.
Katika patakatifu pa duniani, siku ya upatanisho, wakati kuhani mkuu alipoingia katika patakatifu mno, huduma katika chumba cha kwanza cha patakatifu zilikoma. Hali kadhalika Kristo naye alipoingia katika patakatifu mno huko mbinguni ili kukamilisha kazi ya ukombozi, huduma katika chumba cha kwanza ilikoma. Halafu kazi katika chumba cha pili, yaani patakatifu mno; ilianza. Kristo alikuwa amemaliza sehemu moja ya kazi yake ya ukombozi, ndipo alianza sehemu ya pili ya kazi. Bado angali akiombea kwa Baba damu yake iwatakase wenye dhambi.
“Hekalu la Mungu lilifunguliwa huko mbinguni, ndipo sanduku la agano lake likaonekana katika hekalu lake”. Ufunuo 11:19. Sanduku la agano la Mungu jipya liko mbinguni katika patakatifu mno, chumba cha pili cha patakatifu. Katika huduma ya hema takatifu duniani, ambayo ilikuwa mfano wa kivuli cha ile ya mbinguni, chumba hiki kilifunguliwa tu wakati wa siku kuu ile ya upatanisho kwa ajili ya kutakasa patakatifu. Kwa hiyo upatanisho kwa ajili ya kutakasa patakatifu. Kwa hiyo tamko lile lisemalo kuwa hekalu la Mungu lilifunguliwa, na kwamba sanduku la ushuhuda likaonekana, lilikuwa utangulizi wa kuonyesha kuwa patakatifumno mbinguni palikuwatayarikufunguliwakatika chumbacha pili ili Kristo, Kuhani wetu Mkuu yuko tayari kuingia na kuanza kazi hiyo mwaka 1844.
Watu ambao wangefuatana naye katika huduma hiyo, waliona sanduku la agano lake.
Kadiri walivyojifunza juu ya hekalu waligundua kuwa
Kristo anabadili huduma na sasa anahudumu mbele ya agano la Mungu.
Sanduku lililokuwa katika hema takatifu hapa duniani lilikuwa na mbao mbili za mawe ambazo zilikuwa zimeandikwa juu yake sheria ya Mungu. Hekalu la Mungu lilipofunguliwa huko mbinguni, sanduku la agano lake lililonekana humo. Sheria hii ilionekana katika patakatifu pa patakatifu iliyonenwa na Mungu na kuandikwa na kidole cha chanda chake juu ya mbao mbili za mawe.