![](https://static.isu.pub/fe/default-story-images/news.jpg?width=720&quality=85%2C50)
12 minute read
Sura 35. Uhuru wa Zamiri Unatishwa
Kanisa la Roma sasa linapendelewa sana na Waprotestanti kuliko miaka ya zamani. Katika inchi hizo ambamo Kanisa la Kikatoliki linapata mwendo wa kuunganisha kwa kupata mvuto, mawazo yanaanza kusimamiwa ya kwamba hakuna tofauti sana juu ya mambo ya lazima kama ilivyozaniwa na ya kwamba ukubali ule mdogo kwa upande wetu utatuongoza katika mapatano bora pamoja na Roma. Kulikuwa wakati Waprotestanti walifundisha watoto wao ya kwamba kutafuta umoja na Roma kungekuwa kutokuwa na uaminifu kwa Mungu. Lakini ni tofauti kubwa ya namna gani tunaona katika taarifa ya sasa!
Watetezi wa dini ya Rome (Papa) wanatangaza kwamba kanisa limeshitakiwa uwongo, ya kwamba si haki kuhukumu kanisa la leo kwa utawala wake wa mda wa karne nyingi za ujinga na giza. Wanarehemu ukali wake wakuogopesha kwa ushenzi wa nyakati zile.
Je, watu hawa hawakusahau madai ya kutoweza kukosa kulikowekwa na uwezo huu? Roma inadai ya kwamba “kanisa halikukosa kamwe; wala kukosa kwa wakati ujao, kufuatana na Maandiko, halitakosa daima.”
Kanisa la Roma halitaacha kamwe madai yake kwa kutoweza kukosa (infallibilité). Acha vizuizi (amri) vilivyoamriwa sasa na serikali za dunia vitoshwe na Roma irudishwe katika mamlaka yake ya kwanza, na hapo kwa upesi ingekuwa uamsho wa uonevu wake na mateso.
Ni kweli ya kwamba Wakristo wa kweli wanakuwako katika ushirika wa kanisa la Kikatoliki la Roma. Maelfu katika kanisa lile wanamtumikia Mungu kufuatana na nuru bora wanayokuwa nayo. Mungu anatazama na upendo wa huruma juu ya nafsi hizi, zilizolelewa katika imani ile ya kudanganya na isiyotosheleka. Ataleta mishale ya nuru kupenya giza, na wengi watakamata misimamo yao pamoja na watu wake.
Lakini Kanisa la Roma kama chama haliko tena katika umoja na habari njema ya Kristo sasa kuliko kwa wakati wa kwanza. Kanisa la Roma linatumia shauri lo lote kwa kupata utawala wa ulimwengu, kuanzisha tena mateso, na kuharibu mambo yote ambayo Waprotestanti wamefanya. Kanisa la Kikatoliki liko linapata nafasi kwa pande zote. Angalia kuongezeka kwa makanisa yake. Tazama uwingi wa vyuo vyao vikubwa (colleges) na seminaires, vinavyosimamiwa na Waprotestanti. Tazama usitawi wa utaratibu wa sala katika
Uingereza na maasi ya mara kwa mara kwa vyuo vya Wakatoliki.
Mapatano na Ukubali
Waprotestanti wamesaidia ama kupendelea mafundisho ya Kanisa la Papa; wamefanya mapatano na mkubaliano ambayo wakatoliki wenyewe wameshangaa kuyaona. Watu wanafunga macho yao kwa tabia ya kamili ya Kanisa la Roma. Watu wanahitaji kupinga maendeleo ya adui huyu wa hatari kwa uhuru wa watu na dini.
Wakati msingi wa kanisa la Roma linaimarishwa juu ya madanganyo, si la ushenzi na ujiinga. Huduma ya dini ya Kanisa la Roma kawaida ni ya kuvuta sana. Maonyesho yake mazuri sana mengi na kanuni kubwa za dini zinavuta watu na kunyamazisha sauti ya akili na zamiri. Jicho linavutwa kwa uzuri. Makanisa mazuri kabisa, maandamano makubwa ya ajabu, mazabahu ya zahabu, sanduku za kuwekea vitu vitakatifu za johari, mapicha mazuri, na muchoro bora vinavuta wenye kupenda uzuri. Muziki ni waajabu. Nukta za muziki nzuri za kutoka kwa sauti kubwa za kinanda zinachanganyika na nyimbo tamu sana za sauti nyingi kama inavyoongeza katika madari ya nyumba ya juu sana na sehemu ndefu ya nguzo ya majengo makubwa ya kanisa yake, yanavuta akili ya uchai na heshima.
Utukufu huu wa inje na ibada vinacheka tamaa za nafsi yenye kugonjwa ya zambi. Dini ya Kristo haihitaji mivuto ya namna hiyo. Nuru inayongaa kutoka kwa msalaba inaonekana safi na ya kupendeza na hakuna mapambo ya inje yanayoweza kuongeza damani yake ya kweli. Mawazo ya juu ya ufundi, malezi ya kupendeza tamaa, mara kwa mara yanatumiwa na Shetani kuongoza watu kusahau mahitaji ya nafsi na kuishi kwa ajili ya ulimwengu huu tu.
Fahari na sherehe ya kuabudu kwa Kikatoliki kunakuwa na uwezo wa kuvuta (kushawishi) kufanya mabaya, nzuri wakupoteza akili, na hiyo, wengi wamedanganyika. Wanajipatia uhakikisho juu ya Kanisa la Roma kuwa mlango wa mbinguni. Hakuna hata mmoja ila tu wale wanaoweka miguu yao kwa msingi wa kweli, ambao mioyo yao hufanywa upya kwa Roho ya Mungu, wanakuwa salama juu ya mvuto wake. Mfano wa utawa pasipo uwezo ni kitu kile wengi wanatamani.
Madai ya Kanisa kwa haki kwa ya kusamehe zambi yanaongoza wafuasi wa Roma kujisikia huru kwa zambi, na agizo la maungamo linaelekea vile vile kutoa ruhusa kwa uovu. Yeye anayepiga magoti mbele ya mtu aliyeanguka na anafungua katika maungamo mawazo ya siri ya moyo wake anapoteza cheo cha nafsi yake. Katika kufunua zambi za maisha yake kwa padri mwenye kufa wa kosa-cheo cha tabia yake ni chini, na anakuwa mchafu kwa hiyo. Mawazo yake juu ya Mungu ni ya kushusha cheo katika mfano wa mwanadamu aliyeanguka, kwa sababu kuhani anasimama kama mjumbe wa Mungu. Ungamo hili la haya la mtu kwa mtu ni chemchemi ya siri ambamo kumebubujika uwingi wa uovu unaochafua ulimwengu. Kwani kwa yeye anayependa anasa, ni kupendeza zaidi kuungama kwa mtu wa mauti kuliko kufungua roho kwa Mungu. Ni jambo la kupendeza zaidi kwa kiumbe mwanadamu kutubu kuliko kuacha zambi; ni rahisi kuhuzunisha wala kutesa mwili kwa nguo ya gunia kuliko kusulubisha tamaa za mwili.
Mfano Wa Kushangaza
Wakati walipozarau kwa siri kuja kwa mara ya kwanza kwa Kristo juu ya sheria ya Mungu, walikuwa wa kali kwa inje katika kushika amri zake, kuzilemeza kwa masharti yanayofanya utii kuwa mzito. Kama vile Wayuda walivyojidai kuheshimu sheria, vivyo hivyo watu wa kanisa la Roma wanajidai kwa heshima ya msalaba.
Wanaweka misalaba kwa makanisa yao, mazabahu yao, na mavazi yao. Po pote alama ya msalaba kwa inje inaheshimiwa na kutukuzwa. Lakini mafundisho ya Kristo yanazikwa chini ya desturi za uongo na malipizi makali. Roho aminifu zinalindwa katika woga wa hasira ya Mungu aliyechukizwa, wakati wakuu wa kanisa wengi wanaishi katika anasa na tamaa ya mwili.
Ni juhudi ya daima ya Shetani kusingizia tabia ya Mungu, asili ya zambi, na matokeo kwenye mti wa kuchoma wafia dini katika vita kuu. Madanganyo yake yanatoa watu ruhusa kwa zambi. Kwa wakati ule ule anaanzisha mawazo ya uwongo juu ya Mungu ili wamwangalie kwa hofo na chuki kuliko kwa upendo. Kwa njia ya mawazo yaliyopotoshwa juu ya tabia za Mungu, mataifa ya kishenzi waliongozwa kuamini kafara za kibinadamu kuwa za lazima kwakupata mapendo ya Mungu. Mambo makali ya kuogopesha yametendwa chini ya mifano mbalimbali ya ibada ya sanamu.
Umoja wa Upagani na Ukristo
Kanisa la Katoliki la Roma, kwa kuunganisha upagani na Ukristo, na, kama upagani, kusingizia tabia ya Mungu, lilitumia basi matendo makali. Vyombo vya mateso vilishurutisha watu kukubali mafundisho yake. Wakuu wa kanisa wakajifunza kuvumbua njia za kufanyiza mateso makubwa iwezekanavyo bila kuondoa maisha ya wale wasingekubali madai yake. Kwa mara nyingi yule aliyeteswa alipokea mauti kuwa kufunguliwa kuzuri.
Kwa wafuasi wa Roma kanisa lilikuwa na malezi ya shida, njaa, ya mateso ya mwili. Kwa kupata kibali cha Mungu, wenye kutubu walifundishwa kupasua vifungo ambavyo Mungu alivifanya kwa kubariki na kufurahisha maisha ya mwanadamu duniani. Uwanja wa kanisa unakuwa na mamilioni ya watu waliotoa maisha yao kwa masumbuko ya bure, kwa kukomesha, kama machukizo kwa Mungu, kila wazo na nia ya huruma kwa viumbe wenzao.
Mungu hakuweka kamwe mojawapo ya mizigo hii mzito juu watu wo wote. Kristo hakutoa mfano kwa wanaume na wanawake kujifungia wenyewe katika nyumba ya watawa (monasteres) ili kuweza kustahili kuingia mbinguni. Hakufundisha kamwe ya kwamba mapendo yanapashwa kukomeshwa.
Papa anadai kuwa mjumbe mkubwa wa Kristo. Lakini je, Kristo alijulikana daima kutupa watu kwa gereza kwa sababu hawakumtolea heshima kubwa kama Mfalme wa mbingu? Je, sauti yake ilisikiwa kuhukumu kwa mauti wale wasiomkubali?
Kanisa la Roma sasa linaonyesha uso mzuri kwa ulimwengu, kufunika kwa maneno ya kujitetea ukumbusho wake wa maovu ya kuchukiza. Limejivika lenyewe mavazi ya mfano wa Kikristo, lakini linakuwa lisilobadilika. Kanuni yo yote ya dini ya Roma katika vizazi vya wakati uliopita inakuwako leo. Mafundisho yaliyoshauriwa kwa miaka ya giza yangali yanashikwa. Dini ya Roma ambayo Waprotestanti wanaheshimu sasa ni ileile iliyotawala katika siku za Matengenezo (Reformation), wakati watu wa Mungu waliposimama kwa hatari ya maisha yao kufunua zambi lake.
Kanisa la Roma ni kama vile unabii ulivyotangaza kwamba lingekuwa, ni kukufuru kwa nyakati za mwisho. Tazama 2 Watesalonika 2 :3,4. Chini ya mfano wa kigeugeu linaficha sumu isiyobadilika ya nyoka. Je, uwezo huu, ambao ukumbusho wake kwa miaka elfu umeandikwa katika damu ya watakatifu, utakubaliwa kama sehemu ya kanisa la Kristo?
Badiliko katika Kanisa la Protestanti
Madai yamewekwa katika inchi za Kiprotestanti ya kwamba Dini ya Kikatoliki inakuwa tofauti kidogo kwa Dini ya Kiprotestanti kuliko nyakati za zamani. Hapo kumekuwa badiliko; lakini badiliko haliko katika kanisa la Roma. Kanisa la Katoliki linafanana sana na Kanisa la Kiprotestanti linalokuwa sasa kwa sababu Kanisa la Kiprotestanti kiliharibika tabia sana tangu siku za Watengenezaji (Reformateurs).
Makanisa ya Kiprotestanti, kutafuta mapendeleo ya ulimwen-gu, yanaamini kila kitu kibaya kuwa kizuri, na kama matokeo wataamini mwishoni kila kitu kizuri kuwa kibaya.
Wanakuwa sasa, kama ilivyokuwa, kujitetea kwa Roma kwa ajili ya mawazo yao isiyokuwa na mapendo kwake, kuomba musamaha kwa “ushupavu” wao. Wengi wanasihi sana ya kwamba giza ya kiakili na yakiroho iliyokuwa pote wakati wa Miaka ya Katikati ilisaidia Roma kueneza mambo ya uchawi na mateso, na ya kwamba akili kubwa zaidi ya nyakati za sasa na kuongezeka kwa wema katika mambo ya dini kunakataza mwamsho wa kutovumilia. Watu wanacheka sana wazo la kwamba mambo ya namna ile yanaweza kutokea kwa nyakati za nuru. Inapaswa kukumbukwa lakini ya kwamba kwa namna nuru inapotolewa zaidi, na zaidi giza ya wale wanaopotea na kuikataa itakuwa kubwa.
Siku ya giza kubwa ya walio elimishwa imesaidia kwa mafanikio ya kanisa la Roma (Papa). Siku ya nuru kubwa ya walioelimishwa nayo itasaidia vile vile. Katika miaka iliyopita wakati watu walipokuwa pasipo maarifa ya ukweli, maelfu walikamatwa kwa mtego, bila kuona wavu uliotandikwa kwa nyanyo zao. Katika kizazi hiki wengi hawatambui wavu na wanatembea ndani yake mara moja bila kufikiri. Wakati watu wanapotukuza mafundisho yao wenyewe juu ya Neno la Mungu, akili inaweza kutimiza maumivu makubwa kuliko ujinga. Kwa hivyo elimu ya uwongo ya wakati huu utahakikisha mafanikio ya kutayarisha njia kwa kukubali kanisa la Roma (Papa), kama kukataa kwa maarifa kulivyofanya katika Miaka ya Giza.
Kushika Siku ya Kwanza (Jumapili)
Kushika siku ya kwanza (jumapili) ni desturi ilioanzishwa na Roma, ambayo anadai kuwa alama ya mamlaka yake. Roho ya Kanisa la Roma (Papa) ya mapatano kwa desturi za kidunia, heshima kwa desturi za kibinadamu juu ya amri za Mungu inaenea sehemu zote za makanisa ya Waprotestanti na kuwaongoza kwa kazi ya namna moja ya kutukuza Siku ya kwanza (Jumapili) ambayo kanisa la Roma limeigeuza mbele yao.
Sheria za kifalme, baraza za kawaida na maagizo ya kanisa zilizokubaliwa na mamlaka ya kidunia zilikuwa ni hatua ambazo siku kuu za kishenzi zilifikia cheo cha heshima katika dunia la Wakristo. Mpango wa kwanza wa kulazimisha watu wote kushika Siku ya kwanza ya juma ilikuwa sheria iliyotolewa na Constantine. Ingawa ilikuwa kweli sheria ya kipagani, ilikazwa na mfalme akiisha kukubali dini ya Kikristo.
Eusebius, kama askofu aliyetafuta upendeleo wa watawala, na aliyekuwa rafiki wa kipekee wa Constantine, akaendesha matangazo ya kwamba Kristo alihamisha Sabato na kuiweka kwa siku ya kwanza (dimanche). Hakuna ushuhuda wa Maandiko uliotolewa kuwa uhakikisho. Eusebius yeye mwenyewe, bila kuwa na hakikisho akatangaza uwongo wake.
“
Vitu vyote,” anasema, “Kila kitu kilichokuwa kazi ya kufanya kwa Sabato, hivi tumevihamisha kwa siku ya Bwana”. 2
Kwa namna Kanisa la Roma lilipoimarishwa, kutukuzwa kwa Siku ya Kwanza kukaendelea. Kwa wakati mfupi siku ya saba iliendelea kushikwa kama Sabato, lakini baadaye badiliko likafanyika. Baadaye Papa akatoa maagizo ya kwamba padri wa wilaya alipaswa kukaripia wanaoharibu siku ya kwanza (dimanche) wasilete msiba mkubwa juu yao wenyewe na kwa jirani.
Amri za baraza zilizo hakikisha upungufu, wakubwa wa serkali wakaombwa sana kutoa amri ambayo ingeogopesha mioyo ya watu na kuwalazimisha kuacha kazi kwa siku ya kwanza (dimanche). Kwa mkutano wa wakubwa wa kanisa uliofanywa Roma, mipango yote ya mbele ikahakikishwa tena na kuingizwa katika sheria ya kanisa na kukazwa na wakubwa wa serikali1]
Lakini ukosefu wa mamlaka ya maandiko kwa ajili ya kushika siku ya kwanza (dimanche) ukaleta mashaka. Watu wakauliza haki ya waalimu wao kwa ajili ya kutia pembeni tangazo hili, “Siku ya saba ni Sabato kwa Bwana Mungu wako,” ili kuheshimu siku ya jua. Kwa kusaidia ukosefu wa ushuhuda wa Biblia, mashauri mengine yalikuwa ya lazima.
Musimamizi wa nguvu wa siku ya kwanza (dimanche), ambaye karibu mwisho wa karne ya kumi na mbili alizuru makanisa ya Uingereza, akapingwa na washuhuda waaminifu kwa ajili ya kweli; na kwa hivi nguvu yake ilikuwa ya bure hata akatoka kwa inchi wakati moja. Wakati aliporudi, akaleta mkunjo waonyesho ambayo alidai kutoka kwa Mungu mwenyewe, iliyokuwa na agizo la kulazimisha watu kushika siku ya kwanza (dimanche), pamoja na matisho ya ajabu kuogopesha wasiotii. Maandiko haya ya damani yalisemwa wala kutajwa kuwa ya kuanguka kutoka mbinguni na kupatikana pale Yerusalema juu ya mazabahu ya Simeona Mtakatifu, katika Golgotha. Lakini, kwa kweli yaliandikwa katika jumba kubwa la askofu kule Roma. Madanganyo na maandiko ya uwongo yalikuwa katika miaka yote yakihesabiwa ya kweli kwa watawala wa kanisa la Roma. (Tazama kwa Mwisho wa Kitabu (Nyongezo), hati kwa ukarasa 37.)
Lakini ijapo walifanya nguvu kwa kuanzisha utakatifu wa Siku ya kwanza (dimanche) wakuu wa kanisa la Roma wao wenyewe kwa wazi wakatubu kwamba sabato inatoka kwa mamlaka ya Mungu. Katika karne ya kumi na sita baraza la Papa ikatangaza: “Acha
Wakristo wote wakumbuke ya kwamba siku ya saba ilitakaswa na Mungu, na ilikubaliwa na kushikwa, si kwa Wayuda tu, lakini na kwa wengine wote wanaodai kuabudu Mungu; ingawa sisi Wakristo tumebadilisha Sabato yao kwa Siku ya Bwana.”4 Wale waliokuwa wakiharibu sheria ya Mungu walikuwa wanajua tabia ya kazi yao.
Mufano wa kushangaza wa mipango ya Roma ulitolewa katika mateso marefu ya mauaji juu ya Waldenses (Vaudois), wengine wao walikuwa washika Sabato. (Tazama Nyongezo.)
Historia ya makanisa ya Ethiopia na Abyssinia ni ya maana ya kipekee. Katikati ya huzuni ya Miaka ya Giza, Wakristo wa Afrika ya Kati walifichama kwa uso wa dunia na wakasahauliwa na ulimwengu na kwa karne nyingi wakafurahia uhuru katika imani yao. Mwishoni Roma ikajifunza juu ya maisha yao, na mfalme wa Abyssinia akadanganywa hata akakubali Papa kama mjumbe mkubwa wa Kristo. Amri ikatolewa kukataza kushikwa kwa Sabato chini ya malipizi makaii1] Lakini uonevu wa Papa (kanisa la Roma) kwa upesi ukawa nira ya kutia uchungu sana ambayo watu wa Abyssinia wakakusudia kuivunja. Wakuu wa Roma wakafukuziwa mbali kwa mamlaka yao na imani ya zamani ikarudishwa.
Wakati makanisa ya Afrika yalipokuwa yakishika Sabato katika utii kwa amri za Mungu, wakaepuka na kufanya kazi siku ya kwanza (dimanche) kwa kufuatana na desturi ya kanisa. Roma ikavunja Sabato ya Mungu kwa kujiinua mwenyewe, lakini makanisa ya Afrika, yakajificha karibu miaka elfu moja, hayakushirikiana kwa uasi huu. Walipoletwa chini ya Roma, wakalazimishwa kuweka pembeni kweli na kutukuza sabato ya uwongo. Lakini kwa upesi walipopata tena uhuru wao wakarudia kutii amri ya ine. (Tazama Nyongezo).
Mambo haya yanaonyesha wazi uadui wa Roma kwa ajili ya Sabato ya kweli na wasimamizi wake. Neno la Mungu linafundisha ya kwamba mambo haya yanapashwa kutendeka tena kwa namna kukaririwa kama vile Wakatoliki na Waprotestanti wanajiunga kwa kutukuza siku ya kwanza (dimanche).
Mnyama wa Pembe Mbili Mfano wa Mwana-Kondoo
Unabii wa Ufunuo 13 unatangaza ya kwamba mnyama wa pembe mbili mfano wa mwana-kondoo atafanya “dunia na wanaokaa ndani yake” kuabudu kanisa la Rome lililofananishwa na mnyama “alikuwa mfano wa chui. “Mnyama wa pembe mbili itasema vilevile “wale wanaokaa juu ya dunia, kufanyia sanamu yule mnyama”. Tena, naye anawafanya wote, “wadogo na wakubwa, na matajiri na maskini na wahuru na wafungwa,” wapokee chapa cha mnyama. Ufunuo 13:11-16. Amerika ni uwezo uliofananishwa na nyama yule wa pembe mbili mfano wa mwana-kondoo. Unabii huu utatimilika wakati
Mwungano wa mataifa ya Amerika watakapokaza kushika siku ya kwanza (dimanche), ambayo Roma inadai kama hakikisho kwa mamlaka yake.
“Nikaona kimoja cha vichwa vyake, kama kimetiwa kidonda cha kufa; kidonda chake cha kufa kikapona; dunia yote ikastaajabia mnyama yule”. Ufunio 13:3. Kidonda cha kufa kinaonyesha kuanguka kwa kanisa la Roma (Papa) katika mwaka 1798. Baada ya hii, asema nabii, “kidonda chake cha kufa kikapona: na dunia yote ikastaajabia nyama yule”. Paulo akataja ya kwamba “mwana wa uharibifu” ataendelea na kazi yake ya madanganyo kwa mwisho kabisa wa wakati”. 2 Tesalonika 2:3-8. Na “watu wote wanaokaa juu ya dunia watamwabudu, wale, majina yao hayakuandikwa katika kitabu cha uzima”. Ufunuo 13:8. Katika Ulimwengu wa Zamani na mpya, kanisa la Papa litapokea heshima kwa heshima iliyotolewa kwa siku ya kwanza (dimanche).
Tangu katikati ya karne ya kumi na tisa, wanafunzi wa unabii wameonyesha ushuhuda huu kwa ulimwengu. Sasa tunaona maendeleo ya upesi kwa utimilifu wa unabii. Kwa waalimu wa Waprotestanti kunakuwa na madai ya namna moja ya mamlaka ya Mungu kwa ajili ya kushika siku ya kwanza (dimanche), na ukosefu wa namna moja wa ushuhuda wa maandiko, kama kwa waongozi wa kanisa la Roma (Papa). Tangazo ya kwamba hukumu za Mungu zinafikia watu kwa ajili ya kuvunja sabato ya siku ya kwanza (di-manche) litarudiliwa: tayari linaanza kulazimishwa.
Ni ajabu kwa werevu, Kanisa la Roma. Linaweza kusoma kitu gani kinapaswa kuwa ya kwamba makanisa ya Waprotestanti yanatoa heshima yake kwa Roma wanapokubali sabato ya uwongo na ya kwamba wanajitayarisha kuikaza kwa namna kanisa lenyewe lilifanya katika siku zilizopita. Kwa upesi gani litapata usaada wa Waprotestanti katika kazi hii si vigumu kuelewa.
Kanisa la Wakatoliki wa Roma linafanya muungano mkubwa chini ya mamlaka ya Papa, mamilioni ya washiriki wake katika kila inchi wanaagizwa utii kwa Papa, hata taifa lao liwe la namna gani wala serkali yao. Ijapo wanaweza kuapa kiapo kuahidi uaminifu kwa serikali, lakini kinyume cha hii kunakuwa kiapo wala naziri ya uaminifu kwa Roma.
Historia inashuhudia juu ya nguvu ya uerevu wa Roma kujiingiza mwenyewe katika mambo ya mataifa, kuweza kupata ustawi, kuendesha makusudi yake mwenyewe, hata kwa maangamizi ya watawala na watu.
Ni majivuno ya Roma kwamba hawezi kubadili kamwe. Waprotestanti hawajui wanalolifanya wanapokusudia kukubali usaada wa Roma kwa kazi ya kutukuza siku ya kwanza (dimanche). Kwa namna wanavyoelekea kwa kusudi lao, Roma inakusudia kuimarisha mamlaka yake, kujipatia tena uwezo wake uliopotea. Acha kanuni kwanza liimarishwe na kanisa liweze kutawala uwezo wa serikali; na desturi za dini ziweze kukazwa na sheria za dunia; kwa kifupi, ya kwamba mamlaka ya kanisa na ya serikali itatawala zamirina ushindi wa Roma umehakikishwa.
Jamii ya Waprotestanti itajifunza namna gani makusudi ya Roma inavyokuwa, ila tu wakati unapokwisha kupita kwa kuepuka mtego. Linasitawi kwa utulivu katika mamlaka.
Mafundisho yake yanatumia mvuto katika vyumba vya sheria, katika makanisa, na katika mioyo ya watu. Linaimarisha nguvu zake kuendesha maangamizo yake wakati mda utakapofika kwa kushangaza. Yote linayotumaini (kanisa) ni mahali pafaapo. Ye yote atakayeamini na kutii Neno la Mungu atapata laumu na mateso.