1 minute read
Ikoni na Picha.
“Kuabudu sanamu ... ilikuwa mojawapo ya upotovu wa Ukristo ambao uliingia kanisani kisiri na bila ya kutambuliwa au kuonekana. Upotovu huu haukujiendeleza, kama uzushi mwingine, mara moja, kwa kuwa ikiwa ungefanyika hivyo ungekumbwa na shutuma na kemeo: lakini, kwa kuanza kwake chini ya ufichaji mzuri, desturi moja baada ya nyingine ililetwa, kiasi kwamba kanisa lilikuwa limejaa sana ibada ya sanamu, sio tu bila upinzani wowote mwafaka, lakini bila uamuzi wowote wa malalamishi; na wakati baada ya muda mrefu kulipokuwa na jaribio la kuiondoa, maovu yalikuwa yamekithiri sana kutoweza kuondolewa .... Lazima ichukuliwe kuwa mwenendo wa ibada ya sanamu kwenye moyo wa mwanadamu, na dhamira yake ya kutumikia kiumbe zaidi ya Muumba ....
“Picha na sanamu zilianzishwa kwanza makanisani, sio za kuabudiwa, lakini ili zichukuwe mahali pa vitabu vya kutoa mafundisho kwa wale ambao hawawezi kusoma, au kusisimua ibada katika akili za wengine. Jinsi ilivyojibu kusudi kama hilo ni la kutiliwa shaka; lakini, hata ingawa ilikuwa hivyo hapo mwanzoni, ilikoma baada ya muda, na iligundulika kuwa picha na sanamu zilizoletwa ndani ya makanisa zilitia giza badala ya kuangazia akili za wasiojua zilidhoofisha badala ya kuinua ibada ya mwenye kuabudu. Ili kwamba, ijapokuwa wangekusudiwa kuelekeza akili za wanadamu kwa Mungu, waliishia katika kuwageuza kutoka kwake kwenda kwenye ibada ya vitu viliumbwa.”
Baraza Kuu la Saba, la Pili la Nicaea ambapo Ibada ya Picha ilianzishwa mnamo 787 KK, 1850
Joseph Mendham,