12 minute read
Sura 22. Unabii Unatimilika
Wakati ulipopita ambapo kuja kwa Bwana kulipotazamiwa kwanza wakati wa masika ya mwaka 1844 wale waliotazamia kuonekana kwake walikuwa katika mashaka na kutokuwa na hakika. Wengi wakaendelea kuchunguza katika Maandiko, kwa kupima tena ushuhuda wa imani yao. Maneno ya unabii, ya wazi na ya nguvu, yalionyesha kuja kwa Kristo kuwa karibu. Kugeuka kwa waovu na uamsho wa kiroho miongoni mwa Wakristo kulishuhudia kwamba ujumbe ulikuwa wa mbinguni.
Walihangaishwa na mambo ya unabii, ambayo walizania kama, kulingana na wakati wa kuja kwa mara ya pili, ilikuwa fundisho la kuwatia moyo kwa kungoja na uvumilivu katika imani,ili mambo yaliokuwa giza kwa akili yao sasa ifunuliwe. Miongoni mwa mambo haya ya unabii ilikuwa Habakuki 2:1-4. Hakuna mtu, hata, aliyefahamu kwamba kukawia kwa wazi wakati wa kungojea unakuwa katika unabii. Baada ya uchungu, andiko hili likaonekana kuwa la maana sana: “Maono haya ni kwa wakati ulioamuriwa, lakini kwa mwisho yatasema, wala hayatasema uwongo; hata yakikawia, uyangoje; kwa sababu yatakuja kweli, hayatachelewa. . . Mwenye haki ataishi kwa imani yake.”
Unabii wa Ezekieli pia ulikuwa faraja kwa waaminifu: “Bwana Mungu anasema hivi... Siku ni karibu, na kutimia kwa kila maono ... Nitasema, na neno nitakalolisema litatimizwa; wala halitakawishwa tena.” “Neno nitakalolisema litatimia.” Ezekieli 12:2325,28. Wale waliokuwa wakingoja wakafurahi. Yeye anayejua mwisho tangu mwanzo aliwapa tumaini. Kama mafungu kama haya ya Maandiko hayangekuwako, imani yao ingalianguka.
Mfano wa mabikira kumi wa Matayo 25 pia unaonyesha mambo ya maisha ya Waadventiste. Hapo paonyeshwa hali ya kanisa wakati wa siku za mwisho. Mambo yao ya maisha yamefananishwa na tendo la ndoa ya mashariki:
“Halafu ufalme wa mbinguni utafananishwa na mabikira kumi waliotwaa taa zao, wakatoka kwenda kukutana na bwana arusi. Watano wao walikuwa wapumbafu na watano wenye akili. Wale walio kuwa wapumbafu, walichukua taa zao, bila mafuta; lakini wenye akili walicukua mafuta ndani ya vyombo vyao pamoja na taa zao. Basi wakati bwana arusi alipokawia, wao wote wakasinzia na kulala usingizi. Lakini saa sita ya usiku kulikuwa kelele: Tazama, bwana arusi! tokeni kukutana naye.” Matayo 25:1-6.
Kuja kwa Kristo kama kulivyotangazwa na ujumbe wa malaika wa kwanza, kulifahamika kuwa mfano wa kuja kwa bwana arusi. Kuenea kwa matengenezo chini ya kutangaza kwa kuja kwa karibu kwa Kristo kukajibu kwa mfano wa mabikira. Katika mfano huu, wote walichukua taa zao, Biblia, “na wakaenda kukutana na bwana harusi.” Lakini wakati wapumbafu “hawakuchukua mafuta pamoja nao,” “wenye akili walichukua mafuta ndani ya vyombo vyao pamoja na taa zao.” Wa nyuma wakajifunza Maandiko ili kuchunguza ukweli na wakawa na akili ya kipekee, imani kwa Mungu ambayo haingeangushwa na kukata tamaa na kukawia. Wengine wakaendeshwa na musukumo, hofu yao ikaamshwa na ujumbe. Lakini imani yao ilijengwa juu ya imani ya ndugu zao, walitoshelewa na nuru yenye kuwayawaya ya maono, bila ufahamu kamili wa kweli wala kazi halisi ya neema ndani ya moyo. Hawa wakaendelea “kukutana” na Bwana katika matazamio ya zawadi ya mara moja lakini hawakutayarishwa kwa kukawia na uchungu. Imani yao ikaanguka.
“Wakati bwana arusi alipokawia, wao wote wakasinzia na kulala usingizi.” Kwa kukawia kwa bwana arusi ni mfano wa kupitisha wakati, kukata tamaa, ni kukawia kwenye kuonekana kwa inje. Wale ambao imani yao iliimarishwa juu ya ujuzi wa kipekee wa Biblia walikuwa na mwamba chini ya miguu yao ambayo mawimbi ya uchungu hayakuweza kuharibu. “Wao wote wakasinzia na kulala usingizi,” kundi moja katika kuacha imani yao, lingine likangoja kwa uvumilivu hata mwangaza wazi zaidi ulipaswa kutolewa. Wale wa kijuujuu hawakuweza tena kuegemea kwa imani ya ndugu zao. Kila mmoja anapaswa kusimama ao kuanguka yeye mwenyewe.
Ukaidi wa Dini Unaonekana
Tangu wakati huu, ushupavu wa dini ukaanza kuonekana. Wengine wakaonyesha juhudi za ukaidi. Mawazo yao ya ukaidi yakakutana na kutokuwa na huruma kwa jamii kubwa ya Waadventiste, ndipo wakaleta laumu juu ya kazi ya ukweli.
Shetani alikuwa akipoteza watu wake, na kwa kuleta laumu kwa kazi ya Mungu, akatafuta kudanganya wengine waliokubali imani na kuwaendesha kwa nguvu kwa kupita kipimo. Ndipo wajumbe wake wakawa tayari wakivisia kupata kosa lo lote, kila kitu kisichokuwa kitendo cha kukubaliwa, na kulishikilia katika hali ya kupita kipimo ili kufanya Waadventiste wachukiwe. Kama angeweza kuleta watu wengi wa kutangaza imani ya kuja kwa mara ya pili, wakati uwezo wake ungeendelea kutawala mioyo yao, angepata faida Kubwa.
Shetani ni “mushitaki wa ndugu zetu.” Ufunuo 12:10. Roho yake inaongoza watu kutazama makosa ya watu wa Bwana na kuwashikilia akiwatangaza, lakini matendo yao mema yanapita bila kutajwa. Katika historia yote ya kanisa hakuna matengenezo yaliyofanywa bila kukutana na vizuizi vikubwa. Po pote ambapo Paulo alisimamisha kanisa wengine waliojidai kupokeo imani wakaingiza ujushi. Luther pia alivumilia kwa watu washupavu waliojidai kwamba Mungu alinena kwa njia yao, walioweka mawazo yao wenyewe juu ya Maandiko. Wengi walidanganywa kwa njia ya waalimu wapya na wakaungana na Shetani kwa kuondoa kwa nguvu mambo ambayo Mungu aliongoza Luther kujenga. Wesleys alikutana na werevu wa Shetani katika kusukuma katika ushupavu watu wasiyokuwa imara na wasiotakaswa.
William Miller hakuwa na huruma kwa ushupavu. “Ibilisi,” akasema Miller, “anakuwa na nguvu nyingi kwa mioyo ya wengine kwa siku ya leo.” “Mara nyingi, uso wa kungaa na upendo, shavu, lililolowana, maneno ya kukatwa na machozi, vimenipa ushahidi wa utawa wa moyo kuliko makelele yote katika ukristo.”
Katika matengenezo adui zake wakashitakiwa maovu ya ushupavu juu ya wale waliokuwa wakiomba sana kukataa ushupavu. Mwendo wa namna ileile ulikuwa ukifuatwa na wapinzani wa kazi ya kiadventiste. Hawakutoshelewa na kuzidisha makosa ya ushupavu, wakaeneza taarifa ambazo hazikuwa hata na uhusiano kidogo wa kweli. Amani yao ilikuwa ikisumbuliwa na kutangazwa kwa Kristo kuwa mlangoni. Waliogopa ingeweza kuwa kweli, huku wakatumaini kwamba haikuwako. Hii ilikuwa siri ya vita yao kwa kupinga Waadventiste.
Mahubiri ya ujumbe wa malaika wa kwanza yalielekea mara kukomesha ushupavu. Wale walioshirikiana kwa kazi hizi kubwa walikuwa katika umoja; mioyo yao ilijazwa na upendo wa mtu kwa mwenzake na kwa ajili ya Yesu, ambaye walimtazamia kumwona upesi. Imani moja, tumaini la baraka moja, wakahakikisha ngabo juu ya mashambulio ya Shetani.
Kosa Linasahihishwa
“Basi wakati bwana arusi alipokawia, wao wote wakasinzia na kulala usingizi. Lakini saa sita ya usiku kulikuwa kelele: Tazama bwana arusi anakuja! tokeni kukutana naye.”
Katika wakati wa jua kali wa mwaka 1844 ujumbe ukatangazwa katika maneno ya Maandiko kabisa.
Kile kilichoongoza kwa maendeleo haya kilikuwa ni uvumbuzi kwamba amri ya Artasasta kwa ajili ya kurudishwa kwa Yerusalema, ambayo ilisaidia kujua mwanzo wa hesabu ya siku 2300, ikafanyika katika masika ya mwaka wa 457 B.C., na si kwa mwanzo wa mwaka, kama ilivyoaminiwa. Hesabu kutoka masika ya mwaka 457, miaka 2300 ikamalizika wakati wa masika ya mwaka 1844. Mifano ya Agano la Kale pia ilielekeza kwa wakati wa masika kama wakati ambao “kutakaswa kwa mahali patakatifu” kulipaswa kufanyika.
Kuchinjwa kwa Kondoo wa Pasaka kulikuwa ni kivuli cha mauti ya Kristo, mfano ulitimilika, si kwa tukio tu, bali na kwa wakati. Kwa siku ya kumi na ine ya mwezi wa kwanza wa Wayuda, siku ile kabisa na mwezi ambapo kwa karne nyingi kondoo wa Pasaka alikuwa akichinjwa, Kristo akaanzisha karamu hiyo ambayo ilikuwa kwa kukumbuka mauti yake mwenyewe “Mwana-kondoo wa Mungu.” Kwa usiku uleule akakamatwa kwa kusulibiwa na kuuawa.
UNABII WA 2300 SIKU / MIAKA
Siku ya unabii = Mwaka mmoja
34 Kwa hesabu ya hizo siku mlizoipeleleza ile nchi, yaani, siku arobaini kila siku kuhesabiwa mwaka, mtayachukua maovu yenu, ndiyo miaka arobaini, nanyi mtakujua kufarikana kwangu. (Hesabu 14:34) 6 Tena utakapozitimiza hizo, utalala kwa ubavu wako wa kuume, nawe utauchukua uovu wa nyumba ya Yuda; siku arobaini, siku moja kwa mwaka mmoja, nimekuagizia. (Ezekieli 4:6)
457 k.k – 1844 - 2300 Siku/ Miaka. 14 Akamwambia, Hata nyakati za jioni na asubuhi elfu mbili na mia tatu; ndipo patakatifu patakapotakaswa. (Danieli 8:14) 24 Muda wa majuma sabini umeamriwa juu ya watu wako, na juu ya mji wako mtakatifu, ili kukomesha makosa, na kuishiliza dhambi, na kufanya upatanisho kwa ajili ya uovu, na kuleta haki ya milele, na kutia muhuri maono na unabii, na kumtia mafuta yeye aliye mtakatifu. 490 Siku / Miaka (Danieli 9:24)
25
457 k.k - Amri ya kujenga tena na kurejesha Yerusalemu (Amri ya Mfalme Artaxerxes).
…Basi ujue na kufahamu, ya kuwa tangu kuwekwa amri ya kutengeneza na kuujenga upya Yerusalemu hata zamani zake masihi aliye mkuu; kutakuwa na majuma saba; na katika majuma sitini na mawili utajengwa tena pamoja na njia kuu zake na handaki, naam, katika nyakati za taabu. (Danieli 9:25)
408 k.k - Yajenzi/ Kujenga upya wa Yerusalemu
Mwaka 27 - Ubatizo na Upako wa Yesu Kristo (Masihi). 27 Naye atafanya agano thabiti na watu wengi kwa muda wa juma moja; na kwa nusu ya juma hiyo ataikomesha sadaka na dhabihu; na mahali pake litasimama chukizo la uharibifu; na hivyo, hata ukomo, na ghadhabu iliyokusudiwa imemwagwa juu yake mwenye kuharibu (Danieli 9:26-27)
Mwaka 31 - Kusulibiwa na kifo cha Yesu Kristo. 26 Na baada ya yale majuma sitini na mawili, masihi atakatiliwa mbali, naye atakuwa hana kitu; na watu wa mkuu atakayekuja watauangamiza mji, na patakatifu; na mwisho wake utakuwa pamoja na gharika, na hata mwisho ule vita vitakuwapo; ukiwa umekwisha kukusudiwa. 27 Naye atafanya agano thabiti na watu wengi kwa muda wa juma moja; na kwa nusu ya juma hiyo ataikomesha sadaka na dhabihu; na mahali pake litasimama chukizo la uharibifu; na hivyo, hata ukomo, na ghadhabu iliyokusudiwa imemwagwa juu yake mwenye kuharibu (Danieli 9:26, 27)
Mwaka 34 - Stefano Anapigwa kwa Mawe. Mwisho wa Wayahudi. Injili kwa Ulimwengu. 14 Tena habari njema ya ufalme itahubiriwa katika ulimwengu wote, kuwa ushuhuda kwa mataifa yote; hapo ndipo ule mwisho utakapokuja (Mathayo 24: 14) 46 Paulo na Barnaba wakanena kwa ushujaa wakasema, Ilikuwa lazima neno la Mungu linenwe kwenu kwanza; lakini kwa kuwa mnalisukumia mbali, na kujiona nafsi zenu kuwa hamkustahili uzima wa milele, angalieni, twawageukia Mataifa (Matendo ya Mitume 13:46)
Mwaka 70 - Uharibifu wa Yerusalemu 1 Yesu akaenda zake, akatoka hekaluni; wanafunzi wake wakamwendea ili kumwonyesha majengo ya hekalu. 2 Naye akajibu akawaambia, Hamyaoni haya yote? Amin, nawaambieni, Halitasalia hapa jiwe juu ya jiwe ambalo halitabomoshwa. (Mathayo 24:1, 2) 15 Basi hapo mtakapoliona chukizo la uharibifu, lile lililonenwa na nabii Danielii, limesimama katika patakatifu (asomaye na afahamu)… 21
Kwa kuwa wakati huo kutakuwapo dhiki kubwa, ambayo haijatokea namna yake tangu mwanzo wa ulimwengu hata sasa, wala haitakuwapo kamwe (Mathayo 24: 15, 21)
Mwaka 1844 - Utakaso wa Hekalu Takatifu Zaidi na Mwanzo wa Hukumu Mbinguni.
1810 Siku / Miaka - Kazi ya Yesu Kristo kama Kuhani wetu Mkuu katika Hekalu la Mbinguni. 14 Basi, iwapo tunaye kuhani mkuu aliyeingia katika mbingu, Yesu, Mwana wa Mungu, na tuyashike sana maungamo yetu. 15 Kwa kuwa hamna kuhani mkuu asiyeweza kuchukuana nasi katika mambo yetu ya udhaifu; bali yeye alijaribiwa sawasawa na sisi katika mambo yote, bila kufanya dhambi. 16 Basi na tukikaribie kiti cha neema kwa ujasiri, ili tupewe rehema, na kupata neema ya kutusaidia wakati wa mahitaji (Waebrania 4:14-16).
Vivyo hivyo mifano ya kuelekea kwa kuja kwa mara ya pili inapaswa kutimizwa kwa wakati ulioonyeshwa katika kazi ya mfano. Kutakaswa kwa mahali patakatifu, ao Siku ya Upatanisho, kulitukia kwa siku ya kumi ya mwezi wa saba wa Wayuda wakati kuhani mkuu, alipokwisha kufanya upatanisho kwa ajili ya Israeli yote, na kwa hivyo akaondoa zambi zao kutoka kwa mahali patakatifu, akaja na kubariki watu. Kwa hiyo iliaminiwa kwamba Kristo angeonekana kuja kutakasa dunia kwa kuharibu zambi na wenye zambi, na kubariki watu wake wanaomungojea kwa kuwapa kutokufa. Siku ya kumi ya mwezi wa saba, Siku kuu ya Upatanisho, wakati wa kutakaswa kwa mahali patakatifu, ambao katika mwaka 1844 ulianguka kwa tarehe ya makumi mbili na mbili ya Oktoba, ilizaniwa kama ni wakati wa kuja kwa Bwana. Siku 2300 zingemalizika wakati wa masika, na mwisho ikaonekana kuwa wazi bila ubishi.
“Kilio cha Usiku wa Manane”
Maneno yakawa na hakikisho la nguvu, na “kilio cha usiku wa manane” kikasikiwa kwa maelfu ya waaminifu. Kama mawimbi, tukio hili likazambaa kwa nguvu toka mji kwa mji, kijiji kwa kijiji. Ushupavu ukatoweka kama baridi kali ya alfajiri kabla ya jua kutokea. Kazi ilikuwa ya namna moja na ile ya nyakati za kurudi kwa Bwana ambako miongoni mwa Israeli wa zamani walifuata ujumbe wa karipio kutoka kwa watumishi wake. Hapo kulikuwa furaha nyingi sana, lakini Zaidi uchunguzi mwingi wa moyo, ungamo la zambi, na kuacha dunia. Hapo kulikuwa kujitoa wakfu kwa Mungu.
Kwa miendo yote ya dini tangu siku za mitume, hakuna mojawapo yaliojiepusha zaidi kwa upungufu wa kibinadamu na werevu wa Shetani kuliko ile iliokuwa kwa wakati wa masika ya mwaka 1844. Kwa mwito, “Tazama bwana arusi anakuja,” wale waliokuwa wakingojea “wakaamka, wakatengeneza taa zao”; wakajifunza Neno la Mungu kwa usikizi mkuu ambao haukuwako mbele. Hawakukuwa wenye vipawa zaidi, bali wenye kuwa wenye unyenyekevu zaidi na wenye bidii, waliokuwa wa kwanza kutii mwito. Wakulima wakaacha mavuno yao katika mashamba, wafundi wa mashine wakaacha vyombo vyao na kwa furaha wakaenda kutoa maonyo. Makanisa kwa kawaida yakafunga milango yao juu ya ujumbe huu, na kundi kubwa la wale walioukubali wakajitenga kwao.
Wasiosadiki waliokusanyika kwa mikutano ya Waadventiste wakaona uwezo wa kusadikisha ukihuzuria ujumbe, “Tazama, bwana arusi anakuja!” Imani ikaleta majibu kwa maombi. Kama manyunyu ya mvua juu ya inchi yenye kiu, Roho ya neema akashuka juu ya watafutao kwa bidii. Wale waliotazamia upesi kusimama uso kwa uso pamoja na Mkombozi wao wakaona furaha kubwa. Roho Mtakatifu akalainisha moyo.
Wale waliokubali ujumbe wakafikia wakati ambao walitumainia kukutana na Bwana wao. Wakaomba sana mtu kwa mwenzake. Wakakutana mara kwa mara katika mahali pa uficho kushirikiana pamoja na Mungu, na sauti ya maombezi ikapanda mbinguni kutoka mashambani na vichakani. Hakikisho la kibali cha Mwokozi yalikuwa ya lazima zaidi kwao kuliko chakula cha kila siku, na kama wingu lilitia giza katika akili zao, hawakutulia hata walipoona ushuhuda wa neema ya rehema.
Kukatishwa Tamaa Tena
Lakini tena, wakati wa kutazamia ukapita, na Mwokozi wao hakutokea. Sasa wakaona kama Maria alivyofanya wakati alipokuja kwa kaburi la Mwokozi na kukuta linapokuwa wazi, akapaza sauti na kulia: “Wameondoa Bwana wangu, wala sijui pahali walipomuweka.” Yoane 20:13.
Hofu kwamba habari ingeweza kuwa kweli ikatumiwa kama kizuio juu ya ulimwengu usiosadiki. Lakini walipoona hakuna alama za hasira ya Mungu, wakafunika tena hofu yao na kuendelea na laumu lao na cheko. Kundi kubwa lililojidai kuamini wakaacha imani yao. Wenye kuzihaki wakavuta wazaifu na wenye kuogopea vyeo na hawa wote wakajiunga katika kutangaza kwamba ulimwengu unaweza kudumu kwa namna ileile kwa maelfu ya miaka.
Waaminifu waliojitoakwa kweli walikuwa wameacha vyote kwa ajili ya Kristo, na kama walivyoamini, wakatoa onyo lao la mwisho kwa ulimwengu. Kwa hamu kubwa sana walikuwa wameomba , “Kuja Bwana Yesu.” Lakini sasa kwa kuchukua tena mzigo wa matata ya maisha na kudumu kwa matusi ya ulimwengu wenye kuzihaki lilikuwa jaribu la kutisha sana.
Wakati Yesu alipopanda juu ya punda na kuingia Jerusalem kama mshindi wanafunzi wake waliamini kwamba alitaka kuketi juu ya kiti cha ufalme cha Dawidi na kukomboa Israeli kwa magandamizi. Kwa matumaini ya juu, wengi wakatandika mavazi yao ya inje kama zulia (tapis) katika njia yake wala kutapanya mbele yake matawi yenye majani mengi ya ngazi. Wanafunzi walikuwa wakitimiza kusudi la Mungu,lakini wakaangamizwa kwa uchungu mkali. Lakini siku chache zikapita kabla hawajashuhudia kifo cha maumivu makubwa cha Mwokozi na kumlaza ndani ya kaburi. Matumaini yao yakafa pamoja na Yesu. Hata wakati Bwana alipofufuka toka kaburini ndipo wakaweza kufahamu kwamba mambo yote yalitabiriwa kwa unabii.
Ujumbe Ulitolewa kwa Wakati Uliofaa
Kwa namna ileile Miller na washiriki wake wakatimiza unabii na wakatoa ujumbe ambao Maongozi ya Mungu yalitabiri ulipashwa kutolewa kwa ulimwengu. Hawangeweza kuutoa wangefahamu kabisa mambo ya unabii yanayoelekea uchungu wao, na kutoa ujumbe mwengine kuhubiriwa kwa mataifa yote kabla ya kuja kwa Bwana. Habari za malaika wa kwanza na wa pili zilitolewa kwa wakati unaofaa na zilitimiza kazi ambayo Mungu aliyokusudia waitende.
Dunia ilikuwa ikitazamia kwamba kama Kristo hangetokea, Kiadventiste kingeachwa . Lakini wakati watu wengi walipoacha imani yao kulikuwa wengine waliosimama imara.
Matunda ya kazi ya adventiste, roho ya uchunguzi wa moyo, ya kukana dunia na kutengeneza maisha, ikashuhudia kwamba ilikuwa kazi ya Mungu. Hawakusubutu kukana kwamba Roho Mtakatifu alishuhudia kwa mahubiri ya kuja kwa Yesu mara ya pili. Hawakuweza kuvumbua kosa katika nyakati maalum za unabii. Adui zao hawakufaulu kuangusha maelezo yao ya unabii. Hawakuweza kukubali kukana msimamo uliofikiwa kwa njia na juhudi, kujifunza Maandiko kwa maombi, katika akili zilizoangaziwa na Roho wa Mungu na mioyo ya kuchomwa kwa uwezo wake wenye uzima, ambao ulisimama imara na kupinga watu wa elimu na usemaji.
Waadventiste waliamini kwamba Mungu aliwaongoza kutoa onyo la hukumu. Wakatangaza, “limechunguza mioyo ya wote waliolisikia, ... ili wale watakaochunguza mioyo yao wenyewe, waweze kujua upande gani ... wangepatikana, kama Bwana angefika sasa wangepaza sauti, `Huyu ndiye Mungu wetu, Tumemungoja, naye atatuokoa;’ ao wangeita miamba na milima kuanguka juu yao kuwaficha mbele ya uso wake yeye anayeketi juu ya kiti cha enzi!
Mawazo ya wale walioendelea kuamini kwamba Mungu aliongoza yanaelezwa katika maneno ya William Miller: “Tumaini langu katika kuja kwa Kristo ni la nguvu kwa daima, nimefanya tu, baada ya miaka ya uangalifu, kila nilichoona wajibu wangu kufanya.”
“Maelfu mengi, kwa mfano wote wa kibinadamu, walifanywa kwa kujifunza Maandiko katika mahubiri ya wakati; na kwa njia ile, katika imani na kumwangiwa kwa damu ya Kristo, wamepatanishwa kwa Mungu.”
Imani Inaimarishwa
Roho ya Mungu ilikuwa ingali inakaa kwa wale ambao hawakukataa nuru kwa wepesi waliopokea na kulaumu ujumbe wa kurudi kwa Yesu “Basi, msitupe mbali matumaini yenu, kwa maana yana zawadi kubwa. Kwa sababu munahitaji uvumilivu, ili mukikwisha kufanya mapenzi ya Mungu, mupate ile ahadi. Kwa kuwa bado kidogo sana, Yeye anayekuja atakuja, wala hatakawia. Lakini mwenye haki ataishi kwa imani: Naye kama akirudi nyuma, roho yangu haina furaha naye. Lakini sisi si watu wa kurudi nyuma kwa kupotea, lakini sisi ni pamoja nao walio na imani ya kuokoa roho zetu.” Waebrania 10:35-39.
Onyo la upole hili linaambiwa kwa kanisa katika siku za mwisho. Linaonyeshwa kwa wazi kwamba Bwana angetokea kwa kukawia. Watu hapa walioambiwa walifanya mapenzi ya Mungu katika kufuata uongozi wa Roho yake na Neno lake; lakini hawakuweza kufahamu kusudi lake katika maisha yao. Walijaribiwa kwa mashaka kwamba Mungu alikuwa akiwaongoza kwa kweli. Kwa wakati huu maneno yalikuwa ya kufaa: “Sasa mwenye haki ataishi kwa imani.” Wakainama kwa matumaini ya kukata tamaa, wangaliweza kusimama tu kwa imani katika Mungu na kwa Neno lake. Kwa kukana imani yao na kukana uwezo wa Roho Mtakatifu ambaye alitumikia katika ujumbe ingekuwa kurudi nyuma kwa uharibifu. Maendeleo yao tu ya salama ilikuwa nuru waliokwisha kupokea kwa Mungu, kuendelea kuchunguza Maandiko, na kungoja kwa uvumilivu na kukesha kwa kupokea nuru zaidi.