CHAGUZI ZA MAZAO & SHUGHULI ZA BUSTANI ZA JIKONI ENDAPO UNAISHI NA Ndovu Ndovu wanahitaji kiasi kikubwa sana cha chakula kuweza kuishi; hadi 450kg kwa siku. Panapokuwa na vipindi virefu vya ukame, chakula cha ndovu kinakuwa adimu na wanalazimika kutafuta chakula mashambani.
kidokezo
Inashauriwa kupanda mazao kwenye mashamba madogo, hasa kwenye maeneo waliopo ndovu, kwani ni gharama nafuu na fanisi Zaidi kulinda mazao machache dhidi ya ndovu kwa kutumia njia mbalimbali za kulinda mipaka.
Mashamba madogo huhitaji kiasi kidogo cha maji. Udongo huweza kushuka ubora endapo utakuwa unapanda mazao yale yale kila msimu (Kilimo cha zao moja). Ili kulima kwa mafanikio kwenye shamba la hekari 1-3, jaribu kutumia Mbinu za Kilimo-Hifadhi ili kulinda rutuba ya udongo na kuhifadhi maji.
Kama unaishi karibu na hifadhi ya taifa/mbuga za wanyama, panda mazao ambayo ndovu hawali ili kuhakikisha hawavutiwi na shamba lako. Haya yanaitwa mazao yasiyolika. Mazao hayo yanaweza kuwa mazao ya biashara na yanaweza kuwa chanzo mbadala cha kipato yatakaposindikwa. Ukiwa na kipato chako cha ziada unaweza kununua mazao ya chakula kama vile mahindi na maharagwe kutoka kwa wakulima ambao hawaishi karibu na maeneo walipo ndovu. Tumia mipaka ya ziada au njia za awali za kutoa maonyo kwenye shamba lako kulinda mazao yako yasivamiwe.
1.
kidokezo
Epuka kulima zao moja kwenye shamba moja kwa zaidi ya msimu mmoja wa kilimo. Lima kwa mzunguko mazao yasiyopendwa na ndovu kwa kila msimu na lima kwa kuchanganya ina mazao yanayozalisha nitrojeni kama vile maharagwe/na mazao jamii ya maharagwe ili kuipa afya ardhi.
Si
we ha zi k ma ya, uyal ta sio a mu .
Mazao Yasiyopendwa na ndovu Mazao yasiyopendwa na ndovu ni yale ambayo ndovu hawapendi kuyala. Ukipanda mazao haya yatapunguza ndovu kuvamia shamba lako. Ni njia salama ya kutengeneza kipato bila kuhitaji sana ulinzi wa mazao au wa mipaka dhidi ya ndovu.
Kidokezo muhimu Baadhi ya mazao yasiyopendwa na ndovu hayatawazuia kabisa ndovu kuingia shambani kwako. Ndovu bado wanaweza kukanyaga mazao hata kama hawayali.
Kulima mazao kama hayo kunapunguza changamoto ya kulinda mazao yako mara kwa mara. Unahitaji eneo dogo la kulimia ili kuweza kupanda mazao yasiyopendwa na ndovu. Hakikisha unakuwa na soko la kuuzia mazao yako kabla hujaanza kulima mazao yasiyopendwa na ndovu.
Mifano ya mazao yasiyopendwa na ndovu unayoweza kuvuna shambani kwako Gross, E. M., McRobb, R., & Gross, J. (2015).Kulima mazao mbadala kupunguza hasara kutokana na ndovu wa kiafrika.
Mchanganyiko wa njia za vizuizi shambani na ulinzi husaidia kutoa ulinzi zaidi dhidi ya ndovu kuingia shambani kwako.
Tangawizi Alizeti
Mazao mengi yasiyopendwa na ndovu yaliyoorodheshwa hapo juu huvumilia ukame, na huota vizuri panapokuwa na maji ya kutosha.
Vitunguu Swaumu
Biringanya Binzari
Bamia
2.
Pilipili Nyekundu
Pilipili Manga Ufuta
Viungo k.m. nanaa, rosmeri na mwarobaini
Mchaichai
Mpira
Matunda jamii ya ndimu kama vile malimao
Mazao kadhaa yasiyopendwa na ndovu yanaweza kupandwa kwa wima kwenye magunia ya unga, mikebe iliyopo nyumbani au kwenye bustani ndogo za jikoni. Njia hizi zinahitaji maeneo madogo ya kulimia, hivyo kuifanya iwe yenye bei nafuu na isiyohitaji maji mengi.
Mifano Hai Eneo: Elephants & Bees Project, Sagalla, Kenya
Eneo: Zambia
Iligundulika kuwa ndovu waliepuka kula alizeti zilizopandwa kama chakula kwa ajili ya nyuki kwenye uzio wa nyuki.
Walifanya utafiti kwenye mashamba ya mahindi, vitunguu swaumu, tangawizi na mchaichai.
Ndovu wakati mwingine walikanyaga alizeti lakini vichwa vya alizeti viliweza kuvunwa na kukaushwa na mbegu zake kuuzwa/ kukamuliwa kuwa mafuta ya alizeti.
Alizeti huota haraka kwenye udongo wa Tsavo wenye madini ya chuma na miti yake inaweza kulishwa kwa mifugo au kutumika kama vifaa vya kutengenezea paa kwa ajili ya mizinga ya nyuki.
Mbegu/mafuta ya alizeti yana Vitamini C & E kwa wingi na yana bei nzuri kwenye masoko mengi ya ndani. Njia 2 za kusaidia kuishi kwa Amani na ndovu, Mradi wa Ndovu & Nyuki: https://elephantsandbees.com/2-methods-to-help-with-living-in-harmony-with-elephants/ Soma zaidi kuhusu: https://www.kenyanews.go.ke/farmers-opt-for-sunflowers-to-keep-jumbos-away/
hasara
-
Inabidi kuwepo na soko kwa ajili ya mazao mbadala. Kuhama kutoka kilimo cha zamani kwenda kilimo kipya inaweza kuchukua muda. Wakulima wanahitaji mafunzo ya namna nzuri ya kulima mazao mapya. Kuhamia kaika kulima mazao mpya kunahitaji ujuzi maalum na mpya ambao unaweza kuchukua muda ana pia gharama za majaribio.
3.
Matokeo ni kwamba mahindi, yakiachwa bila ulinzi yaliharibiwa kabisa na ndovu. Mchaichai ulikanyagwa na pia vitunguu na tangawizi vilikanyagwa kiasi. Ushahidi unaonyesha kuwa ndovu walionja michaichai na tangawizi lakini hawakuvila inamaanisha kuwa hawakuvutiwa na hayo mazao mawili. Waligundua kuwa tangawizi ilistawi vizuri, japo ilikanyagwa na ikaweza kuvunwa na kuuzwa, kwani huota chini ya udongo. Gross, E. M., McRobb, R., & Gross, J. (2015). Kulima mazao mbadala inapunguza athari inayosababishwa na ndovu.
Eneo: Sri Lanka Ndovu wa bara la Asia wa Sri Lanka hawali machungwa. Ili kupima ugunduzi huu, uchunguzi ulifanywa ukihusisha ndovu sita kutoka kwenye Bustani ya Taifa ya Sri Lanka. Dharmarathne, C., Fernando, C., Weerasinghe, C., & Corea, R. (2020). Mradi wa orange elephant ni mbinu mahsusi ya mjumuisho ya kupunguza migogoro baina ya wanadamu na ndovu nchini Sri Lanka. Communications Biology, 3(1).
Mradi wa Orange Elephant: Kwa kupanda uzio wa miti ya jamii ya ndimu pembeni ya mazao ya mpunga, familia za Sri Lanka vijijini ziliweza kutengeneza kizuizi cha ndovu kilichokuwa salama na endelevu. Ndovu hawana kawaida ya “kuvamia” miti yenye jamii ya ndimu na pia ni miti mirefu kiasi kwamba ndovu hawawezi kuikanyaga. (Vallery, A. 2015) Vallery, A. (2015, February 26). Shirika Hili la Kipekee Linatumia Machungwa Kuokoa Ndovu wa Asia.. One Green Planet.
JAMBO LA KUKUMBUKA
Ingawa mazao jamii ya ndimu hayapendwi na ndovu wa Kiafrika, pia inaweza isiwe hailiki au haipendwi kabisa na ndovu. (Goss et al. 2016)
kilimo wima cha mifuko
Hii inahusisha kupanda wima mazao kwenye magunia yenye vitundu. Magunia yanawawezesha watu kulima mboga zenye virutubishi vingi, na zenye kustawi kwenye maeneo yenye ardhi na maji yasiyotosheleza. Mazao yenye kustawi sana yanavunwa kwenye eneo dogo la ardhi. Magunia kadhaa yanaweza kupandwa kwenye bustani ndogo ya jikoni karibu na nyumba hivyo ni rahisi kuyalinda dhidi ya ndovu.
Mboga za majani zikiota kwenye gunia wima, Elephants & Bees Research Centre, Sagalla, Kenya
Maji ya mvua kutoka kwenye paa la nyumba yako yanaweza kukusanywa na kunywesha kwa matone magunia haya na kuwezesha ulimaji mboga wa mwaka mzima.
Vifaa vinavyohitajika ili kuanza kilimo wima cha kwenye mifuko
Gunia (e.g. gunia la unga) au kiroba
Kopo (kopo tupu la rangi au kopo jingine la 4kg lililo imara)
Kitambaa kidogo
4.
Mbolea ya wanyama iliyotiwa dawa
Mkasi/kisu/kifaa chochote kidogo chenye makali kitakatengeneza matundu kwenye gunia
Mawe au changarawe
Udongo
Chepeo
Eneo dogo la kitalu ili kupanda miche
Jinsi ya kuandaa shamba la wima
1.
Weka gunia lako kwenye udongo na lijaze udongo wa kiasi cha 15-20cm ili kutengeneza msingi.
2.
Chagua eneo lenye jua la kutosha. Hakikisha hakuna usumbufu kutoka kwenye mifugo. Unaweza kuyaweka magunia kwa kukaribiana, ila ukaacha nafasi ya kutosha itakayoruhusu kukua kwa mimea kutoka pande zote.
Ondoa mfuniko kwenye kopo. Tumia kisu/au kifaa chenye makali, kisha kata upande wa chini wa kopo kwa umakini ili kutengeneza kopo lililo wazi.
3.
Weka kopo lililo wazi katikati, juu ya udongo kisha anza kujaza kopo mawe/changarawe mpaka juu ya kopo.
4.
8. 5.
5.
Liache kopo mahali lilipo na funika mdomo wa kopo na kitambaa ili kuzuia udongo usianguke kwenye mawe. Funga kitambaa au bana na mpira.
6.
Ongeza mchanganyiko wa mbolea na udongo nje ya kopo mpaka ufike kwenye ukingo wa juu wa kopo.
7.
Sambaza udongo kwa usawa kwa kutumia mikono na nyunyizia maji kidogo ili kuufanya uwe na unyevunyevu. Usimwage maji mengi sana kwani yatasababisha gunia liangukie upande.
Changanya mbolea na udongo kwa uwiano wa 1:1 ili kutengeneza mchanganyiko.
Ondoa kitambaa. Kikunje na Taratibu vuta kopo juu mpaka kitako cha kikopo kinafika usawa wa juu ya udongo. Kopo litaacha mabaki ya udongo nyuma yake. Usivute kopo zima kutoka kwenye udongo.
9.
10.
Jaza tena mawe kwenye kopo na rudia mchakato mpaka gunia lote lijae udongo.
kidokezo
Usijaze udongo mpaka juu kabisa ya gunia. Acha 5sm ya gunia likiwa halina udongo.
kidokezo
Mashimo yanatengenezwa kuruhusu mazao kukua kupitia mashimo hayo. Hakikisha mashimo yapo katika mstari ulionyooka kwenye gunia. Hii itazuia mazao kuzuia mazao ya chini kupata jua.
faida
Mawe yanasambaza maji kwa usawa, hivyo kuzuia maji yasituame chini ya gunia. Punde miche yako itakapokuwa tayari kwenye kitalu, ipande juu ya gunia na kwenye mashimo.
+
Shamba dogo ni rahisi kulilinda dhidi ya ndovu. Linatumia nafasi ndogo sana ya shamba. Unachohitaji ni gunia tu. Matunzo yake pia si ya hali ya juu. Inaokoa gharama. Ni nadra kwa magugu kuota ndani ya magunia, na kama yakiota, yanaweza kunyofolewa kwa mkono. Unaweza kutumia maji ya kufulia kukuzia mazao yako. Magunia yanaokoa maji. Hayahitaji maji mengi. Kiasi kikubwa cha mazao katika nafasi finyu.
6.
Kopo linasaidia kutengeneza mlingoti wa mawe katikati ya gunia. Hapa ndipo utakuwa ukimwagilia maji.
kidokezo
11.
Baada ya gunia kujaa udongo na mawe, ukitumia kijiti/kifaa chenye ncha, tengeneza mashimo kwenye gunia kwa muundo wa zigizaga.
Kwa viroba vya neti, tengeneza vishimo vya saizi ya sarafu kote juu ya gunia kwa umbali wa 15sm kati ya shimo na shimo. Kwa viroba vingine, ukubwa wa mashimo unapaswa kuwa na upana wa 0.5sm.
Mwagilia kiwango cha wastani cha maji. Maji yakiwa mengi sana, yatamwagika nje ya mashimo na yataziba chini ya gunia. Unaweza kupanda hadi miche 50 kwenye gunia la ukubwa wa kawaida, na hadi miche 100 kwenye gunia kubwa. Kutengeneza bustani ya gunia | Shamba Chef
hasara
-
Uchavushaji hafifu: Ukiweka gunia lako kwenye eneo lililofungwa, lenye kivuli, itawafukuza wadudu wafanya uchavushaji, wakiwemo nyuki. Suluhu: panda mazao yenye kutoa maua nje ili kuvutia nyuki, hasa kama una uzio wa mzinga wa nyuki unaolinda shamba lako. Kwa kawaida mifuko ya saruji inaweza kutumiwa kwa msimu mmoja tu wa mavuno. Viroba va neti vinaweza kudumu kwa hadi miaka mitano, lakini vina gharama zaidi kuliko viroba vingine.
Aina ya Mazao kwa Kilimo cha Kwenye Viroba kidokezo
Hakikisha viroba vinalindwa vyeme dhidi ya ndovu. Tumia njia za ulinzi wa shamba & mipaka kwenye eneo lako.
Sukuma
Chelezi
Figiri
Letusi
Tangawizi
Mchaichai
Kotmiri/Gilgilani
Nyanya
Biringanya
Pilipili mbga
Uanzishaji wa kitalu kwa ajili ya miche Vitalu ni muhimu katika kusaidia mbegu kuwa kwa afya katika hatua za awali, kabla hazijapandwa kwenye shamba au kwenye bustani wima yako. Baadhi ya mbegu huchipua kwa taratibu na kama zikipandwa moja kwa moja shambani, zinaweza kufa kutokana na kuota kwa magugu.
Njia
1.
Chagua eneo lenye kivuli ndio uweke kitalu chako. Pia unaweza kutumia matairi ya gari ya zamani kama kitalu. Hivi vinaweza kuwekwa karibu na bustani wima yako kwa ajili ya wepesi katika umwagiliaji. Matairi ya zamani huhifadhi maji, hivyo kufanya kitalu chako kihifadhi maji vizuri zaidi.
7.
2.
Ondoa magugu na majani yote kwa mkono.
3.
Katua vizuri udongo ili pasibakie mapande. Usilime kwa ndani sana.
4.
Wiki 1 kabla ya kupanda mbegu, ongeza kiasi cha mboji kilichoandaliwa au mbolea ya wanyama iliyotiwa dawa/iliyooza.
6.
Kwa kutumia fimbo nyembamba, tengeneza mifereji midogo katika mistari kwenye kitalu.
Vitalu vingi havihitaji mbolea ili
mbegu. Mbolea kidokezo kuchepusha inaweza kuwekwa moja kwa moja kwenye shamba.
5. 8.
7.
Kwa mazao ya chini ya ardhi (k.m. viazi, vitunguu), panda mbegu kwa umbali wa 8sm kuelekea chini. Kwa mazao yanayoota juu ya ardhi (k.m Sukuma wiki), panda mbegu kwa umbali wa 2sm kuelekea chini kwenye mistari iliyoachana kwa usawa wa 15sm.
Loweka mbegu kwenye maji ya uvuguvugu kwa dakika 30 kabla ya kuzipanda. Hii itazisaidia mbegu kuchepua haraka.
Funika mbegu kwa udongo kiasi na kisha ongeza matandazo. Matandazo husaidia udongo kuhifadhi unyevunyevu. Mwagilia maji kwenye kitalu kwa kiasi cha wastani. Usimwagilie maji mengi sana.
9.
Mbegu zitaanza kuchipua baada ya siku 5-7. Zikiwa zinaanza kuchipua, ondoa matandazo na weka kivuli kilicho juu ya kitalu.
Kidokezo
Tumia paa lililoezekwa (kwa manyasi na makuti makavu) ili kuhakikisha jua linafika.
10.
Kwa umakini, ondoa miche yoyote yenye udhaifu na upande kwenye kitalu kingine ili uitunze ikiwa tofauti. Hakikisha udongo una unyevunyevu lakini haujalowana sana. Maji mengi sana au machache sana yataua miche. Unapokuwa unahamisha miche kutoka kwenye kitalu kwenda kwenye shamba/gunia, beba mche kwa makini huku ukiwa na mizizi yake, kisha taratibu upande kwenye udongo mpya.
Kidokezo muhimu
Vitalu vinahitaji matunzo, usimamizi na ujuzi wa kutosha. Sio mbegu zote zinahitaji kupandwa kwenye kitalu. Hii ni pamoja na nafaka, karoti, gilgilani, n.k. 1. Kuanzisha kitalu 2. Jinsi ya kung’oa miche
8.
Bustani za Jikoni
Umwagiliziaji wa Matone
Hii inafaa kwani inapunguza tatizo la maji kutuama linalohusishwa na aina nyingine za matumizi ya maji.
Bustani ya jikoni ya Kituo cha Biashara cha Wanawake (WEC) cha kambi ya utafiti ya Elephants and Bees, Sagalla, Kenya
Vifaa vya umwagiliaji wa matone hufungwa kwa kawaida, kukiwa na mabomba ya kupitisha matone yanayoachana kwa 2m.
Bustani za jikoni huwa zipo karibu na nyumba na huwawezesha wakulima kupanda mazao mengi ya aina mbalimbali kwenye eneo dogo.
Endapo hakutakuwa na matangi, vifaa vya umwagiliziaji vinaweza kufungwa kwa kutumia ndoo.
Bustani ya jikoni inayofaa familia moja huwa ya ukubwa wa 12m kwa 10m na hufunikwa kwa neti nyeusi ili kuruhusu mwangaza wa jua wa kutosha, na pia kuzuia wadudu.
Kwa kawaida bomba/mpira huunganishwa chini ya ndoo/tangi ili kudhibiti mmiminiko wa maji.
Mfumo mwepesi wa umwagiliziaji wa matone unaweza kufungwa kwenye bustani ya jikoni. Pia unaweza kujumuisha kilimo wima cha kwenye viroba kuhakikisha unapata mazao mengi kwenye nafasi ndogo. https://elephantsandbees.com/permaculture-garden/
Sifa na Katao la haki:
Tumekusanya taarifa kutoka vyanzo mbalimbali ambavyo vinapatikana kote kwenye Makala. Kitabu hiki hakijamaliza yote. Jifunze na chunguza Zaidi kuhusiana na shuguli za shambani, angalia Marejeleo. Baadhi ya maneno asilia yanayotumiwa mara kwa mara yametumiwa hapa ili kurahisisha uelewa. Tafiti Zaidi zinaweza kuhitajika kabla ya utekelezaji wa eneo husika. *Save the Elephants inashauri tahadhari kwa kila taarifa zilizokusanywa na kuwasilishwa kwenye kitabu hiki.
Maji ya mvua yanaweza kukusanywa kwenye ndoo.
kidokezo
Mara zote hakikisha unatumia njia za kulinda/kuzuia shamba kuhakikisha ndovu hawaingii kwenye bustani yako. Tumia njia mjumuisho ili kuongeza ufanisi wa vizuizi. Panda mimea inayofukuza wanyama kama vile mwarobaini na maua ya marigold ili kuwafukuza wadudu.
Hasara
-
Msaada wa kitaalamu unahitajika ili kufunga mfumo wa umwagiliziaji wa matone. Gharama ya kununua mfumo ni kubwa. Wakulima ni lazima wawe na ujuzi na maarifa haya namna gani mfumo unafanya kazi. Kama haujafungwa vizuri, maji yatapotea na udongo unaweza kutota maji.
9. Imetengenezwa Kenya 2022
Imeandaliwa na Save the Elephants
www.savetheelephants.org
Michoro na Nicola Heath