Abu Huraira

Page 1

Abu huraira check Lubumba.qxd

7/1/2011

10:45 AM

Page A

ABU HURAIRA

Kimeandikwa na: Sayyid Abdulhusain Sharafuddin al-Musawi

Kimetarjumiwa na: Ramadhani S.K. Shemahimbo


Abu huraira check Lubumba.qxd

7/1/2011

10:45 AM

B

Page B


Abu huraira check Lubumba.qxd

7/1/2011

10:45 AM

Page C

ŠHaki ya kunakili imehifadhiwa na: AL-ITRAH FOUNDATION ISBN: 978 - 9987 - 512 - 98 - 0

Kimeandikwa na: Sayyid Abdulhusain Sharafuddin al-Musawi Kimetarjumiwa na : Ramadhani S.K Shemahimbo Kimepangwa katika Kompyuta na: Hajat Pili Rajab Kimehaririwa na: Hemedi Lubumba (Abu Batul) Toleo la kwanza: April,2011 Nakala: 1000 Kimetolewa na kuchapishwa na: Alitrah Foundation S.L.P. 19701 Dar es Salaam, Tanzania Simu: +255 22 2110640 Simu/Nukushi: +255 22 2127555 Barua Pepe: alitrah@raha.com Tovuti: www.alitrah.org Katika mtandao: www.alitrah.info


Abu huraira check Lubumba.qxd

7/1/2011

10:45 AM

Page D

Yaliyomo Utangulizi …………………………….......................................................2 Abu Huraira ……………………………..................................................16 Jina Lake na Nasaba Yake ……………....................................................17 Maisha Yake Kifamilia, Kuwa Mwislamu na Usahaba Wake na Mtume…………………...........................................................................19 Wakati wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.).......................................................20 Katika Zama za Makhalifa Wawili wa Kwanza ………….......................25 Katika Zama za Uthman ……………………………………...................27 Katika Zama za Ali (a.s.) …………………………….............................31 Katika Zama za Mu’awiyah ………………………….............................34 Kuzishukuru Fadhila za Bani Umayyah ………………………..............32 Wingi wa Hadith Zake …………………………………..........................55 Allah amemuumba Adam kwa Sura Zake ……………………................55 Maelezo……....……………….................................................................59 Jahannam Haitajaa Mpaka Mwenyezi Mungu Aweke Mguu Wake Humo.........................................................................................................65 Mwenyezi Mungu Hushuka Hadi Kwenye Uwingu wa Chini Kila Usiku.........................................................................................................66 Suleiman Avunja Fat’wa ya Baba Yake Daudi ……….....……................67 Suleiman Anakwenda Kulala na Wanawake Mia Moja kwa Usiku Mmoja.......................................................................................................73


Abu huraira check Lubumba.qxd

7/1/2011

10:45 AM

Page E

Abu Huraira Musa Ampiga Kofi Malaika Wa Mauti …………………………............75 Jiwe Lakimbia na Nguo za Musa ………………………………….........77 Watu Wakimbilia kwa Mitume Wakitarajia Uombezi Wao ……….........80 Shaka Juu ya Mitume, Kumshutumu Lut, ...............................................85 Nzige wa Dhahabu Wamuangukia Ayub …………………......................91 Kumshutumu Musa kwa Kuchoma Kijiji cha Mchwa …………............92 Mtume Asahau Sehemu Mbili za Swala ………………………..............94 Mtume Muhammad Ajeruhi, Achapa Viboko,..........................................99 Shetani Aja Kuvuruga Swala ya Mtume ……………………................107 Mtume Aikosa Swala ya Al-Fajr (swala ya Asubuhi) …………............119 Ng’ombe na Mbwa Mwitu Waongea kwa Kiarabu Fasaha ……............126 Kumfanya Abu Bakr Kiongozi wa Hijja ……………………................128 Malaika Wazungumza na Umar ……………………………….............148 Mirathi ya Mtume ni kwa Ajili ya Sadaka ……….................................149 Abu Talib Akataa Kutamka Shahada ……….........................................156 Mtume Alionya Kabila Lake ………………….......................................158 Watu wa Abyssinia (Ethiopia) Wacheza Ndani ya Msikiti ……….........159 Ubatilishaji Kabla ya Wakati wa Kutumika ……………......................160 Kufanya Jambo Katika Kipinde Kisichoaminika ………………...........160 Umma Uligeuzwa Kuwa Panya ………………………….....................162 Wanaikataa Hadithi Yake Hivyo Anabadili Mawazo Yake ………........162 Hadith Mbili Zinazopingana …………………………………...............164 Watoto Waliozaliwa Punde Wazungumzia Kuhusu Ghaib ……….........165 Shetani Aiba kwa Ajili ya Watoto Wake Wenye Njaa …………............166 Mama Yake Awa Muislam kwa Du’a ya Mtume ………………...........168 Mtumishi wa Abu Huraira ……………………………..........................172 Hadithi ya Kubuni Juu ya Sadaka ……………………………...............174 E


Abu huraira check Lubumba.qxd

7/1/2011

10:45 AM

Page F

Abu Huraira Hekaya Nyingine Kuhusu Matokeo Mazuri ya Uaminifu …….............174 Hekaya ya Tatu Kuhusu Matokeo Mazuri ya Shukurani ……...............176 Hadithi Nyingine Kama Hiyo Iliyotangulia ………...............................178 Mwenyezi Mungu Anamsamehe Asiyeamini Kupindukia ……….........179 Mwenyezi Mungu Anamsamehe Mwenye Dhambi Milele ……............181 Musnad Yake ni Kama Mursal Yake ……………………………..........187 Kujifanya Kwake Amehudhuria Baadhi ya Matukio …………….........190 Waislam wa Mwanzoni Wazikataa Riwaya Zake ………………...........195 Malalamiko Yake Juu ya Wenye Kumshutumu …………………..........206 Kuziangalia Tabia na Sifa Zake …………………..................................217 Vichekesho Vyake ………………………………...................................221 Kifo Chake na Kizazi Chake …………………………..........................225 Hitimisho ………………………………................................................227

F


Abu huraira check Lubumba.qxd

7/1/2011

10:45 AM

Page G

NENO LA MCHAPISHAJI Kitabu kilichoko mikononi mwako ni tarjuma ya kitabu cha Kiingereza kiitwacho, Abu Huraira, kilichoandikwa na Sayyid Abdulhusain Sharafuddin al-Musawi. Kitabu hiki kinazungumzia maisha na wasifu wa sahaba machachari wa Mtukufu Mtume SAW na jinsi alivyoitumia nafasi hii pamoja na fursa alizozipata. Mwandishi wa kitabu hiki amefanya utafiti wa kina juu ya maisha ya sahaba huyu kwa sababu moja kubwa aliyoisema, ambayo ni umaarufu wake katika wingi wa hadithi alizosimulia kutoka kwa Mtukufu Mtume SAW mbali ya kweli kwamba aliishi naye kwa muda mfupi sana ukilinganisha na masahaba wengine. Hii ndio sababu kubwa iliyomfanya mwandishi huyu afanye utafiti juu ya sahaba huyu ili kujua undani wake. Ni muhimu kumjua mtu kama huyu kwani aliyosimulia kutoka kwa Mtukufu Mtume SAW ni mengi sana yakiwemo ya ukweli na kusingizia, na ya kuongoza na kupotosha. Tumekiona kitabu hiki ni chenye manufaa sana , hususan wakati huu wa maendeleo makubwa ya elimu katika nyanja zote, ambapo uwongo, ngano za kale na upotoshaji wa historia ni mambo ambayo hayana nafasi tena katika akili za watu. Kutokana na ukweli huo, Taasisi yetu ya Al-Itrah Foundation imeamua kukichapisha kitabu hiki kwa lugha ya Kiswahili kwa madhumuni yake yaleyale ya kuwahudumia Waislamu, hususan wazungumzaji wa Kiswahili. G


Abu huraira check Lubumba.qxd

7/1/2011

10:45 AM

Page H

Tunamshukuru ndugu yetu, Ramadhan S. K. Shemahimbo kwa kukubali jukumu hili la kukitarjumi kitabu hiki. Vilevile tunawashukuru wale wote walioshiriki kwa njia moja au nyingine hadi kufanikisha kuchapishwa kwa kitabu hiki. Ni matumaini yetu kwamba kitabu hiki kitakuwa ni changamoto kubwa kwa wasomaji wetu. Mchapishaji: Al-Itrah Foundation S. L. P. 19701, Dar-es-Salaam

H


Abu huraira check Lubumba.qxd

7/1/2011

10:45 AM

I

Page I


Abu huraira check Lubumba.qxd

7/1/2011

10:45 AM

Page 1


Abu huraira check Lubumba.qxd

7/1/2011

10:45 AM

Page 2

Abu Huraira Utangulizi Kwa Jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema Mwenye Kurehemu Huu ni uchunguzi na mapitio ya wasifu wa mmoja wa masahaba wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Amesimulia kutoka kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) Hadithi nyingi sana mpaka akavuka mipaka yote, na vitabu vya Hadith vya Sunni vimesimulia Hadith kutoka kwake mpaka zikavuka mipaka pia. Hatukuwa na njia yoyote mbele ya idadi hii kubwa ya Hadith zilizosimuliwa na bwana huyu (Abu Huraira) ila kutafuta juu ya vyanzo vyao kwa sababu zimeshughulisha maisha yetu ya kidini na kiakili moja kwa moja; vinginevyo tungeweza kuziachilia mbali na kuvitupilia mbali vyanzo vyake na kuangalia mambo mengine muhimu zaidi. Idadi hii kubwa ya riwaya zilizosimuliwa na bwana huyu zilienea kwenye matawi na mizizi ya dini zimewafanya mafaqihi wa Sunni kuzitegemea sana katika kushughulika na hukumu na Shari’ah ya Mwenyezi Mungu. Halikuwa jambo la ajabu kwao, kwani wao walifikiria kwamba masahaba wote walikuwa wakweli na waadilifu. Na kwa vile hapakuwa na ushahidi wa kulithibitisha hilo, hatukuwa na namna nyingine isipokuwa kufanya utafiti juu ya bwana huyu na riwaya zake ili kupata uhakika kuhusu kile kilichohusiana na matawi na mizizi ya sheria zilizowekwa na Mwenyezi Mungu. Hili limetufanya tuwajibike kuchunguza na kuangalia kwa makini wasifu wa mtu huyu (Abu Huraira) na Hadith zake. Nimekwenda mbali sana katika uchunguzi huu mpaka ukweli ukajitokeza katika kitabu hiki na jua la uhakika likaangaza, namshukuru Mwenyezi Mungu kwa hilo. Na kuhusu Abu Huraira mwenyewe, tutakufanya uone historia ya maisha yake na falsafa yake kama vile ilivyo hasa. Na kuhusu riwaya zake, tumezichunguza kwa uangalifu sana kuhusu wingi na ubora wake na haikuwezekana kwetu sisi, namuapa Mwenyezi Mungu, isipokuwa kuzikataa kama wenzake walivyozikataa wakati wa siku zake. Utayasoma 2


Abu huraira check Lubumba.qxd

7/1/2011

10:45 AM

Page 3

Abu Huraira hayo kwa kirefu mahali pake katika kitabu hiki, Insha’allah. Hivi iliwezekana kwa mtu mwenye busara kuikubali idadi hii kubwa ya riwaya zilizosimuliwa na mtu huyu, ambazo zilikuwa nyingi zaidi kuliko zote zilizosimuliwa na makhalifa wane, wake tisa wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na Bani Hashim wote, wanawake kwa wanaume? Je, anaweza mtu asiye na elimu, baadae akawa Mwislam na kwa hiyo kipindi cha muda wa usahaba wake na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alikuwa na uwezo wa kutambua kutoka kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) Hadith nyingi kiasi hicho, kiasi kwamba wale Waislam wa mwanzoni na jamaa zake Mkutufu Mtume (s.a.w.w.) hawakuweza kuzitambua? Busara kubwa na vigezo vya kisayansi haviwezi kukubali wingi wa maridhawa na maajabu yaliyosimuliwa na mtu huyu. Sunna katika falsafa yake, utaratibu na mielekeo yake ina tabia maalum ambayo watu wenye busara, watu wenye akili timamu na mabingwa wa lugha wanaielewa wazi. Wakati wanaposikia au kusoma jambo fulani la Sunna, wao wanaliona dhahiri kutokana na akili zao za kawaida na vigezo. Wanaviona vipengele vyake na dalili zake wazi wazi pia bila ya shaka wala kulitilia wasiwasi. Sunna ilikuwa ni ya juu zaidi kuliko kuwa na magugu yenye miiba, ambayo kwayo Abu Huraira amechoma zile akili nzuri na amejeruhi vile vigezo vya kisayansi kabla hajazigeuza au kuzibadili zile Shariah Tukufu na kumkosea Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na umma wake. Kwa kifupi, Sunna ilikuwa ni utaratibu wa Uislam na maisha, ambayo kutokana nayo, maisha lazima yawe ya mfano hasa katika maadili, imani, mahusiano ya kijamii, elimu na fasihi. Hivyo haikuwa ni busara kuwa kimya kuhusu uingiliaji huu wa kuhuzunisha katika dhati ya Uislam, ambayo imetoa mwito juu ya kuwa huru kutokana na imani za kipumbavu na imani za ushirikina ambazo akili imezikataa kwa uwazi kabisa. Hivyo 3


Abu huraira check Lubumba.qxd

7/1/2011

10:45 AM

Page 4

Abu Huraira ilikuwa ni muhimu kabisa kuvisafisha vitabu vya Hadith kwa kuondoa riwaya nyingi zilizosimuliwa na mtu huyu ambazo akili haizikubali. Nasema kwamba naweza nikaziona baadhi ya nyuso zikijikunja, na nyingine zikinywea na kujitanibu nami. Zinaweza kufanya hivyo, kwa sababu ya urithi, malezi na mazingira, kujihadhari kutokana na ukweli uliong’arishwa na utafiti, tofauti na walivyodhani kwamba masahaba wote walikuwa waadilifu na wakweli bila kuyajaribu matendo yao na simulizi zao kulingana na kigezo cha Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alichokiweka kwa umma wake. Kwa sababu usahaba kwa maoni yao ulikuwa ni utakatifu na yeyote aliyekimbilia huko hawezi kushutumiwa na lolote lile alilolifanya. Hili lilikuwa halikubaliki, na ni dhidi ya ushahidi na liko mbali kabisa na ukweli. Kwa kweli usahaba ulikuwa ni sifa kubwa sana lakini haukuwafanya masahaba wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kuwa maasum wasiotenda makosa. Miongoni mwa masahaba wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) walikuwepo watakatifu, wanyofu na wakweli, kadhalika na wasiojulikana. Pia walikuwepo wanafiki, waliofanya makosa na uhalifu. Qur’ani tukufu imetamka wazi: “….. na miongoni mwa watu wa Madina pia ni wakaidi katika unafiki; wewe huwatambui, Sisi tunawatambua hao.” (9:101). Hivyo tunaweza kuwategemea wale masahaba wakweli na kufanya utafiti ili kuwa na hakika kuhusu wale wasiofahamika, ambapo wale wenye hatia na wahalifu hawana thamani, wao wala riwaya zao. Haya ndio maoni yetu kuhusu yoyote yule anayesimulia Hadith ya Mtume. Qur’ani na Sunna ndio vilikuwa mwongozo wetu.1 Hatukuwasamehe 1 Lakini Sunni walikwenda mbali zaidi kwa kuweka uzingo mtakatifu kumzunguka yeyote anayeitwa sahaba mpaka wakawa wamekithiri. Walimwamini kila mmoja, mwema na muovu. Waliwafuata kibubusa watumwa walioachwa huru (ambao Mtukufu Mtume (s) aliwaacha huru alipoiteka Makka) na kila mmoja alimsikia au kumuona Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Walimkatalia yeyote aliyewapinga hao kupita mipaka yote. Rejea uk. 11-15 na uk. 23 katika kitabu chetu “Majibu ya Musa Jarallah.” (Answers of Musa Jarallah). 4


Abu huraira check Lubumba.qxd

7/1/2011

10:45 AM

Page 5

Abu Huraira kamwe waongo hata kama wao walikuwa wanaitwa masahaba kwa sababu ilikuwa ni kukosa uaminifu kwa Mwenyezi Mungu, Mtume Wake na kwa umma. Ilitosha kwetu sisi kutegemea juu ya fiqhi, unyofu na ukweli wa masahaba mashuhuri wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na Ahlul-Bayt wake, ambao yeye (s.a.w.w.) aliamuru kuwa na hadhi sawa na Qur’ani na kuwa mfano kwa ajili ya wenye hekima. Matokeo yake, tumekubaliana, hata kama tulikuwa na tofauti kwa namna fulani hapo mwanzoni, kwamba Sunni waliwaheshimu Abu Huraira, Samara bin Jundub, al-Mughira, Mu’awiyah, Amr ibn Al-Aas, Marwan bin Hakam na wanaofanana na hao, kwa sababu wao (Sunni) waliwatukuza Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na wale waliokuwa miongoni mwa masahaba wake. Wakati huo huo, tuliwalaumu kwa kumtukuza tu Mtukufu Mtume na Sunna yake kama mtu tu aliyekuwa tayari kupokea, ambaye alielewa maana ya utukufu na umashuhuri. Bila shaka, baada ya hilo, yule ambaye alimkanusha yeyote aliyehusisha kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) jambo lisiloaminika, alistahili kumheshimu Mtume na alistahili kuwa katika ile njia ambayo Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) aliipendelea juu ya umma wake. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alionya kwamba watakuwepo waongo wengi watakaozusha uongo wakati wa kusimulia Hadith zisizo sahihi na aliwaonya waongo hao kuja kuwepo katika Moto wa Jahannam. Hapa ninauchapisha uchunguzi huu katika kitabu (Abu Huraira) kwa ajili tu ya kuonyesha ukweli na kuitakasa Sunna na upachikwaji wake kwa Mtume maarufu aliyetakasika, ambaye kamwe hazungumzi kwa matamanio yake 53:3, kuwa muaminifu kwa ajili ya ukweli katika fikra njema na mnyofu katika kufikiri na kuwa mwadilifu kwa ajili ya haki kulingana na misingi ya kisayansi na kiakili, ambayo inakataa kumheshimu muongo anayezusha uongo mwingi na kuupachika kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na kuondolewa kwenye shutuma kwa sababu tu kwamba alikuwa mmoja wa masahaba wa Mtume. Tunakataa kuzikubali kijinga jinga riwaya zili5


Abu huraira check Lubumba.qxd

7/1/2011

10:45 AM

Page 6

Abu Huraira zosimuliwa na mtu huyu kuhusiana na Sunna ya Mtume, ambayo ilikuwa na stahiki kubwa ya kuheshimiwa kwa sababu ilikuwa ni ujumbe wa Mtukufu Mtume kwa ulimwengu wote hadi Siku ya Kiyama. Mtu yeyote asije kukunja uso wala kuhuzunika wakati tunapowasilisha kitabu kwa uchunguzi adilifu, kwani tunaheshimu fikra huru na hatutaki kuishusha chini ya nguvu kandamizi na kisha kuzungukwa na ukuta wa uwongo wa utukufu bandia “….. ndipo ukingo wa ukuta wenye mlango utapigwa kati yao, ndani yake kuna rehema na upande wake wa nje kuna adhabu.” (57:13) Hatutaki uso wowote kujikunja au mtu yoyote kuhuzunika, lakini kwa kweli tunataka kila mtu aliyeko chini ya wingu jeusi la Hadithi mbaya, zilizomfikia baada ya kupita zama baada ya zama, aweze kuwa huru kutokana na ushabiki au ushupavu na asome kitabu hiki kwa makini zaidi;

“Ambao husikiliza kauli (nyingi) kisha wakafuata zilizo nzuri zaidi. Hao ndio aliowaongoza Mwenyezi Mungu, na hao ndio wenye akili.” (39:18) Hatukusudii kwa kitabu hiki, namuapa Mwenyezi Mungu, kuuvunja umoja baina ya madhehebu mbalimbali za Waislam, ambao sasa utakuwa wenye kushughulika katika siku hizi za mwamko, bali kuuimarisha umoja na uhuru wa maoni na imani kuwekwa katika njia iliyo sahihi. Heshima ya kiakili ndio heshima bora zaidi ambayo watu wenye busara wote wanaitafuta hata kama ikiwagharimu fedha nyingi au maisha yao kwa sababu ni njia kuelekea kwenye utukufu na daraja kwa ajili ya umoja.

6


Abu huraira check Lubumba.qxd

7/1/2011

10:45 AM

Page 7

Abu Huraira Lakini endapo mmoja wa ndugu zetu muislam atageuzia mbali uso wake kwa dharau, namuomba kiasi tu ayasikilize maelezo haya rahisi na kisha atoe ushauri wake. Insha’allah atatukuta sisi tumedhamiria zaidi kuimarisha umoja baina ya Waislam licha ya miiba na ugumu vinavyochoma akili ya kuganda kwenye dhamiri. Hapa tutazungumza kuhusu mawazo mbalimbali tofauti; baadhi yao yalishughulika na akili na uwezo wake na upeo, baadhi yaligusa imani katika mielekeo na maana zake, baadhi yaligusa mienendo ya tabia, mengine yalikuwa pinzani yakikanusha kila mojawapo, mengine yalikuwa mbali na misingi ya kielimu yaliyofikiwa kutokana na asili ya kidini na mengi yao yalikuwa ni kuwasifu mno Bani Umayyah au kwa maoni ya jamii kwa siku hizo, na mengine yalikuwa ni dhana na wendawazimu. Lakini yote hayo yalikuwa mbali kabisa na haki. Moja ya maajabu ya Abu Huraira ni kwamba malaika wa mauti alikuwa akiwajia watu waziwazi, lakini alipokuja kwa Nabii Musa (a.s.) ili kuchukua roho yake, Musa alimpiga na kumng’oa jicho lake. Baada ya tukio hili, malaika wa mauti akawa anawaendea watu bila kuonekana! Ajabu nyingine moja ya Abu Huraira ilikuwa ni yale mashindano kati ya Musa na jiwe. Musa (a.s.) aliweka nguo zake juu ya jiwe ili aoge baharini mbali na watu. Jiwe hilo likakimbia pamoja na nguo za Musa (a.s.) na kumlazimisha alifukuze akiwa uchi kama alivyozaliwa mbele ya wana wa Israili ili kukanusha minong’ono inayosema kwamba Musa (a.s.) alikuwa ana henia. Kwamba Musa (a.s.) alilifukuza jiwe hilo huku akipiga makelele: “Ewe jiwe, nguo zangu. Ewe jiwe, nguo zangu.” Jiwe likasimama baada ya kukamilisha kazi yake. Kwamba Musa (a.s.) akaanza kulipiga jiwe hilo kwa fimbo yake vikali sana mpaka ikaweka alama juu ya jiwe hilo. Kulikuwa na alama sita au saba juu ya jiwe hilo. Jambo la kichekesho kabisa katika riwaya hii lilikuwa ni kule kusita kwa Abu Huraira kuhusu ile idadi ya makovu au alama juu ya jiwe hilo, kwa 7


Abu huraira check Lubumba.qxd

7/1/2011

10:45 AM

Page 8

Abu Huraira sababu ya uchamungu uliowekwa juu yake wa kutokusimulia Hadith isipokuwa pale anapokuwa na uhakika kana kwamba alikuwa na uhakika wa mwanga wa jua! Na; wale nzige wa dhahabu waliokuwa wakimuangukia Nabii Ayub wakati alipokuwa anaoga na kwamba alianza kuwakusanya katika nguo zake. Na; watoto wawili wachanga waliozaliwa punde wakiongea kwa busara na mantiki kuhusu ghaibu ambako hakukuwa na sababu ya kuvunja kanuni za asili. Na; ng’ombe na mbwa mwitu wanaoongea kiarabu fasaha na kuonyesha kwamba walikuwa na mantiki, hekima na elimu kuhusu ghaibu ambako hakuna sababu yoyote ya changamoto na miujiza. Abu Huraira aliisimulia Hadith hii kuonyesha ubora wa khalifa wa kwanza na wa pili. Na ushirikina mwingine wa ajabu: kwamba shetani alikuja kwenye makazi ya Abu Huraira usiku kwa siku tatu mfululizo kuja kuiba chakula kwa ajili ya wanawe wenye njaa. Na: kwamba taifa moja la Wana Israil lilipotea na baada ya kuwatafuta waliwakuta wamegeuka panya. Ushahidi ulikuwa ni kwamba pale walipopewa maziwa ya ngamia hawakuyanywa na walipopewa maziwa ya kondoo waliyanywa. Na: kwamba yeye (Abu Huraira) alikuwa pamoja na al-Ala’ wakiwa na jeshi la wapiganaji wapatao elfu nne. Walifika kwenye ghuba moja ambayo ilikuwa haijawahi kuvukwa hapo kabla yao na haitakuja kuvukwa baada yao. Al-Ala’ alikamata hatamu za farasi wake na akatembea juu ya maji! Jeshi hilo lilimfuata bila ya unyayo, kiatu au kwato kuloa maji! Na: riwaya yake kuhusu shanta yake, ambayo ilikuwa na tende chache kiasi, ambazo alilisha nazo jeshi zima wakati tende zikabakia kama 8


Abu huraira check Lubumba.qxd

7/1/2011

10:45 AM

Page 9

Abu Huraira zilivyokuwa. Alikuwa akiishi na shanta hii kwa kipindi chote cha Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), Abu Bakr, Umar na Uthman mpaka ilipoibiwa wakati wa mapinduzi dhidi ya Uthman. Na: riwaya yake kuhusu Nabii Daudi (a.s.), ambaye alimaliza kusoma Qur’ani Tukufu katika muda mfupi kabisa. Aliamuru farasi wake awekwe matandiko na kabla hajatandikwa matandiko hayo, yeye akawa amemaliza kuisoma Qur’ani yote. Je hiyo si kama mtu anayesema: Aliiweka dunia yote ndani ya yai? Katika baadhi ya riwaya zake, yeye ameshughulika na Mwenyezi Mungu Mutukufu. Ubunifu wake umetengeneza maumbile kadhaa kwa ajili ya Mwenyezi Mungu. Hayo yaepuke mbali na Yeye! Amesema kwamba Mungu alimuumba Adam kwa sura Yake Mwenyewe. Alikuwa na dhiraa sitini za urefu na dhiraa sabini za upana. Abu Huraira amepanua sana katika riwaya hii. Wakati fulani alisema: Kama mmoja wenu amegombana na mwenzie, aepuke kulenga usoni kwa sababu Mwenyezi Mungu amemuumba Adam kulingana na umbile Lake Mwenyewe. Wakati mwingine alisema: Adam ameumbwa kulingana na umbo la Mwingi wa Fadhila. Mtu huyu alipumbazwa na ubunifu wake wa kuchora picha kama hiyo kwa ajili ya Mwenyezi Mungu na Adam kwa maelezo na maelekezo mahiri, ambayo kama tutayahusisha na Uislam, tutaona mambo mengi ya ajabu yatakayotufanya tucheke na kulia kwa wakati mmoja huo huo. Alisimulia Hadith nyingine akisema kwamba Mwenyezi Mungu atautokea umma huu mnamo Siku ya Kiyama katika umbile tofauti na lile wanalolijua na atasema: Mimi Ndiye mungu wenu. Wao watasema: Mungu aepushilie mbali! Sisi hatutaondoka hapa mpaka atakapotujia Mungu wetu. Kama akija hapa sisi tutamtambua. Kisha Mungu atakuja kwa sura wanayoifahamu na atasema: Mimi ni Mungu wenu. Wao watasema: Wewe ni Mungu wetu. Kisha watamfuata.

9


Abu huraira check Lubumba.qxd

7/1/2011

10:45 AM

Page 10

Abu Huraira Yeye Abu Huraira aliisimulia hii katika hekaya ndefu yenye giza iliyojaa ubunifu, ikimuonyesha Mungu katika maumbile tofauti, akijigeuza sura, akija na kuondoka katika matendo ya uigizaji na mizaha, majadiliano na hila. Riwaya hii ilimdhihaki Mwenyezi Mungu kwa namna ambayo sio tu inayopingana na imani ya Kiislam na misingi ya kawaida tu ya uadilifu bali pia ile adabu bora kabisa kama tukikubali – Mungu aepushilie mbali – wazo la mfano mwema, naliwe mbali na Mwenyezi Mungu Mtukufu. Na Hadithi yake kwamba Jahannam haitajaa mpaka Mwenyezi Mungu atakapoweka mguu wake ndani yake! Katika moja ya maajabu yake kuonyesha kwamba Jahannam itajivunia kuwa na watu madhalimu na kiburi, wakati ambapo Pepo itakuwa nyonge kwa kuwa na watu masikini na waliokanganyikiwa. Na riwaya yake kwamba Mwenyezi Mungu huwa anashuka hadi kwenye uwingu wa chini kabisa kila usiku na kusema: “Nani atakayeniomba ili nimkidhie ombi lake?” Na nyingine nyingi kama hizo ambazo zilikuwa ndio chanzo cha kumpa mwili Mwenyezi Mungu kuanza katika zama za utata wa mawazo mengi, na kwa sababu yake kwamba namna nyingi za uasi na makosa kujitokeza.

*

*

*

*

*

Abu Huraira alisimulia Hadith nyingi kuhusu mitume (a.s.). Aliwaelezea kwa namna yoyote ile alivyotaka yeye. Katika moja ya Hadith hizo, alisimulia hofu za Siku ya Kiyama. Watu watakimbilia kwa Adam kisha kwa Nuh, kisha kwa Ibrahim kisha kwa Musa halafu kwa Isa (a.s.) katika ghasia zisizo na maana, kwani mitume hawa (kama alivyojifaragua Abu Huraira) wamezuiwa kufanya uombezi na Mwenyezi Mungu, ambaye alikasirika sana juu yao (hapo kabla) kwa kiwango ambacho Yeye hajakasirika kama hivyo kabla ya hapo, wala hatakuja kukasirika baada ya hapo, kwa sababu wao (hao Manabii) walikuwa wametenda makosa (yaliy10


Abu huraira check Lubumba.qxd

7/1/2011

10:45 AM

Page 11

Abu Huraira obuniwa na fikra za Abu Huraira). Abu Huraira hakupata njia yoyote ya kumpendelea Mtukufu Mtume Muhammad (s.a.w.w.) isipokuwa kuwashushia hadhi mitume wengine (amani iwe juu yao wote). Vilevile riwaya yake alipohusisha mashaka kwa Nabii Ibrahim (a.s.) wakati anaposema (akinukuu Qur’ani tukufu): “Na (kumbukeni) Ibrahim aliposema: Mola Wangu! Nionyeshe namna unavyofufua wafu…..” (2:260) ambamo Abu Huraira alimfanya Nabii Muhammad kuwa mwenye sababu ya kuwa na shaka kuliko Ibrahim na akamfanya Nabii Yusuf kuwa mbora zaidi kuliko Mtukufu Mtume Muhammad (s.a.w.w.) kwani yeye alikuwa na subira. Alimlaumu Nabii Lut pale anaposema:

“Akasema: Laiti ningekuwa na nguvu juu yenu, au nategemea kwenye nguzo yenye nguvu.” (11:80). Na Hadith yake ambayo ilionyesha kwamba Nabii Suleiman alivunja hukmu ya baba yake ambayo ilihusu mtoto ambaye akina mama wawili walidai kila mmoja wao kuwa ni wake, na Nabii Daudi akahukumu kwamba mtoto huyo alikuwa ni wa yule mwanamke mtu mzima. Suleiman akasema: “Nileteeni kisu ili nimkate mtoto huyu katika nusu mbili, kila mama mmoja achukue nusu moja.” Yule mama wa umri mdogo akalia: “Usifanye hivyo tafadhali.” Hivyo akaamua kwamba mtoto huyo ni wake. Ile tofauti kati ya manabii wawili kuhusu hukumu ya Mwenyezi Mungu ilikuwa haikutegemewa kwa mujibu wa Sharia ya Kiislam. Jambo la ajabu sana katika imani hii potovu ilikuwa kwamba Abu Huraira alisema kwamba yeye hajawahi kusikia juu ya sikkiin (kisu) katika maisha yake ambapo walikuwa wakikiita midya. Na riwaya yake kwamba Nabii Suleiman alisema: “Mimi nitakwenda kulala na wanawake mia moja usiku huu ambao kwamba kila mmoja 11


Abu huraira check Lubumba.qxd

7/1/2011

10:45 AM

Page 12

Abu Huraira atazaa mtoto wa kiume, ambaye atapigana kwa ajili ya Mwenyezi Mungu.” Malaika akamtaka aseme Insha’allah. Yeye hakusema hivyo. Hivyo hakuna yeyote kati ya wake zake hao aliyezaa mtoto wa kiume isipokuwa mmoja tu, ambaye alizaa nusu binadamu! Na Hadithi nyingine kuhusu mdudu chungu ambaye alimuuma Nabii Musa (a.s.). Musa akawaamuru wafuasi wake kuteketeza kijiji cha wadudu chungu hao. Kisha Mwenyezi Mungu akamtia msukumo: “Kwa sababu ya mdudu chungu aliyekuuma wewe, umeunguza taifa zima ambalo lilimtukuza Mwenyezi Mungu!” Na Hadith yake kuhusu Mtume Muhammad (s.a.w.w.) kwamba aliwadhuru, kuwakashifu, kuwalaani na kuwachapa viboko watu wasio na hatia kwa sababu tu ya hasira, kwa hiyo kuwadhuru kwake, kuwakashifu, kuwalaani na kuwachapa viboko kutakuwa ni ungamo kwa ajili ya dhambi zao. Kama hiyo ilihusishwa na Firauni, hiyo itakuwa ni aibu juu yake. Ni vipi kuhusu Mtume wetu maaasum! Baadhi ya watu walilaaniwa na Mtukufu Mtume na hawakustahili msamaha, je Abu Huraira atatulazimisha sisi kuwapenda na kuwaheshimu hao kama watu waadilifu? Ni vigezo vipi sahihi baada ya kigezo hiki cha kichekesho cha Abu Huraira? Katika Hadith nyingine yeye amesema kwamba shetani alikuja kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kuvuruga swala zake. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alimkaba shetani na akataka kumfunga kwenye nguzo kuwaruhusu watu wamtazame akiwa amefungwa, lakini alikumbuka usemi wa Nabii Suleiman (a.s.): “Akasema: Mola Wangu; nisamehe na unipe ufalme, asiupate yeyote baada yangu, bila shaka Wewe ndiye Mpaji.” (38:35), na kisha akamuacha huru. Na riwaya yake inayosema kwamba Mtume Muhammad (s.a.w.w.) alikuwa amelala na akaikosa swala ya al-Fajr.

12


Abu huraira check Lubumba.qxd

7/1/2011

10:45 AM

Page 13

Abu Huraira Na nyingine nyingi, ambazo zimefungua milango ya kusema kwamba mitume (a.s.) hawakuwa Maasum na waliweza kufanya makosa. Hii haikubaliki kwani inafuta ile maana halisi na asili ya utume.

* * * * * Kulikuwa na aina nyingine ya Hadith zake inayokuonyesha kupingana kwa uwazi kabisa. Zitazame Hadith mbili za Abu Salama, ambazo amezisikia kutoka kwa Abu Huraira kuhusu maambukizi. Alikataa katika ile Hadith ya kwanza na akaithibitisha katika ile ya pili. Abu Salama alimuuliza: “Je hukusema kwamba hakuna maambukizi?” Abu Huraira akaikataa Hadith yake ya kwanza na akaanza kubwabwaja kwa ki-Abyssinia. Angalia Hadith yake kuhusu Nabii Suleiman (a.s.) na wake zake. Wakati mwingine alisema kwamba wao walikuwa mia moja. Wakati mwingine tena akasema walikuwa tisini, sabini na sitini. Yote hayo yametajwa katika vitabu vya Hadith. Kama utaiona Hadith yake kuhusu kuhama, utaona wazi kwamba alikuwa ni mtumishi masikini mwenye njaa na mtembea pekupeku. Alimhudumia huyu na yule kwa ajili ya mlo. Yeye aliwezaje kuwa na mtumishi, ambaye alizungumzia kuhusu yeye huyo huko Sham1 (Damascus)? Yeye alisema (wakati wa utawala wa Muawiyah): “Nilipokuja kukutana na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) mtumishi wangu akanitoroka humo njiani. Wakati nilipokuwa na Mtukufu Mtume nikimtembelea, mtumishi wangu akaingia, na Mtume akaniambia: “Huyu ni mtumishi wako?” Mimi nikasema: “Ndio, nimemuacha huru kwa ajili ya Mwenyezi Mungu.” Angalia riwaya zake anazozungumzia kuhusu yeye mwenyewe wakati alipokuwa akiishi kwenye makazi ya Suffa.2 Utaona kwamba alikuwa 1 Hivi sasa ni Syria, Jordan, Palestina na Lebanoni 2 Makazi yaliyotengenezwa pembeni ya msikiti kwa ajili ya watu mafukara na masikini kuishi humo. 13


Abu huraira check Lubumba.qxd

7/1/2011

10:45 AM

Page 14

Abu Huraira mmoja wa wakazi mafukara walioishi humo. Aliishi ndani ya makazi hayo pamoja na kipindi cha uhai wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Yalikuwa ndio makazi yake mchana na usiku, kwani alikuwa hana ukoo wala nyumba hapo Madina. Alijivisha mwenyewe na kipande cha nguo ya sufi, ambacho chawa walikuwa wakitambaa humo. Alikifunga kipande hicho kwenye shingo kufikia kwenye miguu yake. Alikikusanya kwa mikono yake ili kuficha sehemu zake za siri zisionekane. Njaa ilimwangusha na kukosa fahamu baina ya mimbari na chumba cha msikiti huo. Hivyo ni wapi alikopata nyumba aliyojisingizia katika siku za mwisho za uhai wake? Ilikuwa ni sehemu ya riwaya aliyoisimulia huko Damascus kuhusu yeye mwenyewe na mama yake ambaye alikuja kuwa Mwislam kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), na Mtume kumuombea mama huyo na mwanawe, kama alivyosema yeye. Angalia malalamiko yake dhidi ya wale waliozikataa riwaya zake. Utayaona yakipingana na kutokuwa na thamani kiasi kwamba usikivu unayakataa kwa upuuzi wake na akili zinayakataa kwa kukosa kwake maana. Ushahidi wa Abu Huraira dhidi ya wale walioshutumu riwaya zake ulikuwa ni riwaya iliyosimuliwa na yeye mwenyewe akisema kwamba wakati mmoja alitandaza nguo yake mbele ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Mtukufu Mtume akaanza kutoa elimu kwa mikono yake na kuiweka kwenye nguo hiyo huku akisema kumwambia Abu Huraira: “Ikusanye na kuiunganisha kifuani kwako.� Abu Huraira aliikusanya kifuani kwake na akawa huru kutokana na kusahau; kwa hiyo yeye alikuwa ndiye sahaba bora kabisa katika kuihifadhi Sunna kichwani mwake na mwenye kuitambua sana. Ni ushahidi wa kidhihaka kiasi gani ambao uliwahudumia wapinzani wake kuliko kumhudumia yeye mwenyewe! Ulithibitisha kwamba kile walichokihusisha kwake kilikuwa ni sahihi kwamba yeye alisimulia Hadith kulingana na hasira zake bila ya kujua alichokuwa akikisema. Lakini hatuna wa kuhukumu kati yetu isipokuwa Allah.

14


Abu huraira check Lubumba.qxd

7/1/2011

10:45 AM

Page 15

Abu Huraira Ilikuwa inatosha kwetu sisi kwamba yeye alisimulia Hadith bila ya kuona na kusikia halafu akajifanya kwamba aliona na kusikia. Hapa ni mfano mmojawapo: Abu Huraira anasema kwamba siku moja aliingia nyumbani kwa Ruqayya, binti ya Mtukufu Mtume na mkewe Uthman. Yeye Ruqayya alikuwa ameshika chanuo mkononi mwake. Akasema: “Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alikuwa hapa na ameondoka muda mchache uliopita. Nilizichana nywele zake.” Ni uhakika kwamba Ruqayya alifariki katika mwaka wa tatu wa Hijiria baada ya vita vya Badr na Abu Huraira alikuja Madina na kuwa Mwislam katika mwaka wa saba Hijiria, baada ya vita vya Khaybar. Hivyo ni wapi angeweza kukutana na Ruqayya na chanuo lake?

*

*

*

*

*

Huu hapa ni mfano wa Hadith zake, ambazo zilikuwa mbali kabisa na misingi ya kielimu ya Uislam. Yeye amesema: “Mtume Muhammad (s.a.w.w.) alitutuma sisi kwenye kazi na akasema: “Kama mtamuona fulani na fulani (aliwataja kwa majina) wachomeni wote kwa moto.” Tulipokuwa tunataka kuondoka alisema: “Nilikuwa nimewaagiza kuwachoma moto watu wale wawili, lakini ni Mwenyezi Mungu peke Yake atakayewaadhibu watu kwa moto, hivyo kama mkiwaono basi wauweni.” Ulikuwa ni ubatilishaji wa jambo kabla ya wakati wake haujafikiwa. Lilikuwa haliwezekani kwa Mwenyezi Mungu na Mtume Wake. Alikuwa na Hadith nyingi zisizosadikika na za ubunifu. Tulitaja sita kati ya hizo mwishoni mwa Hadith zake arobaini mwishoni mwa kitabu hiki kuwa mfano wa hizo nyingine.

*

*

* 15

*

*


Abu huraira check Lubumba.qxd

7/1/2011

10:45 AM

Page 16

Abu Huraira Aliwasifu sana Bani Umayyah na wasaidizi wao kitumwa mno. Na alisifu maoni ya umma katika siku zile sana kupita kiasi. Tulizitaja baadhi ya Hadith zake kuhusiana na hili katika milango inayofuata. Unaweza ukazichunguza kwa uadilifu bila upendeleo kuona kwamba alikuwa mwenye njaa na alikuwa anataka kujaza tumbo lake kupitia uzushaji wa Hadith kwa ajili ya hili na lile. Alikuwa anataka kuridhisha udhanifu wake, udhanifu wa mtu ambaye alinyimwa furaha za maisha ya kawaida. Yeye, baada ya hapo, alikiri kwamba alikuwa mahali pa usalama katika umri ambao ulimdharaulisha na kumshindisha na njaa na kisha akatupwa kwenye zama ambazo zilikidhi njaa yake kiasi tu cha kuzusha Hadith. Baada ya hapo, je tunaweza kumuamini yeye na kumtegemea kama ushahidi? Je tuweke akili zetu na imani chini ya miguu yake bila ya kufikiri wala kutafakari? Kama hilo lilikuwa ni sahihi kulingana na akili na Shari’ah, basi ngoja Abu Huraira na wafuasi wake waende kwenye sehemu yao takatifu ambayo imesimamishwa na siasa na kuwekwa katikati ya Hadithi na urithi kadhaa. Na kama Hadithi na urithi vilikuwa ni chanzo cha utenganisho au chombo cha kutokukubaliana, ngoja viwe hivyo hadi jua litakapochomoza. – “…..Sitaki ila kutengeneza ninavyoweza na sipati kuwezeshwa haya ila kwa Mwenyezi Mungu, kwake ninategemea na kwake ninaelekea.” (11:88)

ABU HURAIRA Alisimulia kutoka kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) Hadithi za ziada – nyingi mno. Vitabu Sita vya Hadith vya Sunni na vitabu vyao vyingine vilivyobakia vimesimulia kutoka kwake Hadithi nyingi mno. Mbele ya idadi hii kubwa ya Hadith, hatukuwa na jinsi ila kuchunguza juu ya vyanzo vyake, kwa sababu zilihusu maisha yetu ya kidini na kiakili. Vinginevyo tungezigeuzia mgongo kuzipuuza hizo na msimuliaji wake na kushughulika na jambo jingine lenye umuhimu zaidi. 16


Abu huraira check Lubumba.qxd

7/1/2011

10:46 AM

Page 17

Abu Huraira Lakini Hadithi hizi nyingi zisizo na idadi zilienea kwenye matawi na mizizi ya dini ambazo ziliwafanya Sunni wote wa madhehebu manne na Asharia na wahadhiri wao kuziamini na kizitegemea wakati wanaposhughulika na Shari’ah (Fiqh). Hivyo hapakuwa na njia isipokuwa kutafiti juu ya msimuliaji mwenyewe na riwaya zake ili kuwa na hakika juu ya kanuni za Mwenyezi Mungu na Shari’ah Yake.

JINA LAKE NA NASABA YAKE * Abu Huraira alikuwa haeleweki wazi katika nasaba na familia. Watu walikuwa wanatofautiana sana kuhusu jina lake na lile la baba yake. Jina lake lilikuwa halifahamiki katika zama za kabla ya Uislam na zama za Uislam.3 Alikuwa akijulikana kwa jina lake la ukoo. Alikuwa anatokana na Douss. Ni kabila la Yemen lililoshuka kutokana na Douss bin Adnan bin Abdullah bin Zahran bin Ka’b bin al-Harith bin Ka’b bin Malik bin anNazhr bin al-Azd bin al-Ghouth. Ilisemekana4 kwamba jina la baba yake lilikuwa Umayr na alikuwa mtoto *Kwa jina la Allah, Mwingi wa rehma Mwenye kurehemu, na amani iwe juu ya waja Wake wateule. Abdul-Husein bin Sharafud-Din al-Musawi al-Aamily, anayetegemea radhi na msamaha wa Mwenyezi Mungu anasema: Huu ni ufafanuzi uliojumuisha rejea za kitabu hiki. Hatukuacha hata kidogo isipokuwa tumerejea kwenye chanzo chake. Tunategemea watafiti kukirejelea. Ninawasilisha kitabu hiki kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, na Mwenyezi Mungu akifanye kiwe chenye manufaa kwa wengine. 3 Hili lilitajwa hasa na Abu Umar bin Abdul-Birr katika wasifu wa Abu Huraira katika kitabu chake kiitwacho Al-Isti’ab. Kama ukisoma kuhusu wasifu wake katika vitabu vingine kama Al-Isaba, Usudul-Ghaba, Tabaqat ya Ibn Sa’ad na vingine utaona kwamba ukoo na nasaba hazikufahamika wazi. 4 Na Muhammad bin Hisham bin as-Sa’ib al-Kalbi aliyetajwa kwenye Tabaqat ya Ibn Sa’d katika wasifu wa Abu Huraira na kuthibitishwa na Abu Ahmed adDimyati kama ilivyo katika al-Isaba ya Ibn Hajar katika wasifu wa Abu Huraira. 17


Abu huraira check Lubumba.qxd

7/1/2011

10:46 AM

Page 18

Abu Huraira wa Aamir bin Abd Thi ash-Shara bin Tareef bin Ghiyath bin Abu Sa’b bin Hanayya bin Sa’d bin Tha’laba bin Sulaym bin Fahm bin Ghanam bin Douss. Mama yake alikuwa ni Umayma bint Sufayh bin al-Harith bin Shabi bin Abu Sa’b bin Hunayya bin Sa’d bin Tha’laba bin Sulaym bin Fahm bin Ghanam bin Douss.5 Alipewa jina la kiukoo la Abu Huraira kwa sababu ya paka mdogo aliyekuwa amempenda sana.6 Pengine ilikuwa ni kwa sababu ya mapenzi yake juu ya paka wake huyo kwamba alisimulia Hadith kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisema: “Mwanamke ataingia motoni kwa sababu ya paka. Alimfunga. Yeye hakumlisha wala hakumuacha ajilishe kwa wadudu wa ardhini.”7 Bibi Aisha, mke wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) aliikanusha Hadith hii kama utakavyosoma katika sehemu yake ya kitabu hiki, Insha’allah. 5 Kama ilivyokuwa imetajwa na Ibn Sa’d katika Tabaqat yake uk. 52, Sehemu ya 2 Juz. 4 6 Ibn Qutayba ad-Daynouri ametaja katika kitabu chake al-Ma’arif, uk. 93 kwamba Abu Huraira amesema: “Niliitwa Abu Huraira kwa sababu ya paka mdogo (kwa Kiarabu Hirra maana yake paka na huraira maana yake paka mdogo wa jikoni) niliyekuwa nikicheza naye.” Ibn Sa’d katika Tabaqat yake, katika wasifu wa Abu Huraira ameeleza kwamba Abu Huraira amesema: “Nilichunga kondoo na nilikuwa na paka mdogo. Usiku ulipoingia nilimuweka juu ya mti na asubuhi nilimshusha na kucheza naye, hivyo wakaniita Abu Huraira.” Yeyote aliyeandikua kuhusu wasifu wa Abu Huraira alilitaja hilo au jambo kama hilo. Alidumisha mapenzi kwa paka wake na kucheza naye katika siku za Uislam mpaka Mtukufu Mtume Muhammad (s.a.w.w.) akamuona akimuweka paka wake ndani ya mkono ya nguo yake. Hili lilitajwa na al-Fayrooz Abadi katika kitabu chake, Al-Qamuus al-Muhiit, makala juu ya hirra. 7 Imesimuliwa na Bukhari katika Sahih yake Jz. 2, uk. 149 na pia Ahmad bin Hanbal katika Musnad yake Jz. 2, uk. 261.

18


Abu huraira check Lubumba.qxd

7/1/2011

10:46 AM

Page 19

Abu Huraira MAISHA YAKE YA AWALI, KUWA MWISLAM NA USAHABA WAKE NA MTUKUFU MTUME (S.A.W.W.) Alizaliwa nchini Yemen na kukulia huko hadi alipopitisha umri wa miaka thelathini.8 Alikuwa mjinga sana kiasi kwamba alikuwa hana hata chembe ya umaizi, wala hata utambuzi japo kidogo. Alikuwa masikini aliyesahauliwa na zama, yatima aliyekumbwa na ufukara, akimtumikia huyu na yule, mwanaume au mwanamke kiasi cha kupata kujaza tumbo lake,9 miguu pekupeku, bila ya nguo, alipambana na fedheha hii, akifarijiwa na hali yake. Lakini pale Mwenyezi Mungu alipothibitisha kazi ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) hapo Madina baada ya vita vya Badr, Uhud na Ahzaab na kadhalika, hapakuwa na njia ya kuingia kwa masikini huyu aliyechanganyikiwa bali ile ya Uislam. Alihama kwenda kumtembelea Mtukufu Mtume Muhammad (s.a.w.w.) baada ya vita vya Khaybar katika mwaka wa saba wa Hijiria kwa mujibu wa wanahistoria wote. Na kuhusu usahaba na Mtume, huo ulikuwa ni miaka mitatu kama alivyotangaza mwenyewe katika moja ya riwaya zake zilizosimuliwa na alBukhari.10 8 Nilikuja kutoka Yemen wakati Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alipokuwa Khaybar. Wakati huo nilikuwa na umri wa zaidi ya miaka thelathini. 9 Abu Huraira alizungumza kuhusu yeye mwenyewe na akasema kama ilivyotajwa katika wasifu wake ndani ya Isaba, Hilyatul-Awliya, na vitabu vinginevyo: “Nilikuwa mtumishi wa Ibn Affan na binti ya Ghazwan. Niliongoza hamali lao wakati walipopanda na niliwahudumia waliposhuka kwa ajili ya chakula tu nipate kuishi.� 10 Ndani ya Sahih Bukhari yake, Jz. 2, uk.182. Pia imeelezwa katika wasifu wa Abu Huraira katika Issaba na Tabaqat. 19


Abu huraira check Lubumba.qxd

7/1/2011

10:46 AM

Page 20

Abu Huraira

WAKATI WA ZAMA ZA MTUKUFU MTUME (S.A.W.W.) Wakati Abu Huraira aliposilimu na kuwa Mwislam, alijiunga na mafukara wa Suffa ambao kama Abul-Fida alivyoeleza katika kitabu chake Taarikh al-Mukhtassar (Historia fupi), walikuwa ni masikini wasiokuwa na makazi wala ndugu. Walilala hapo msikitini na waliishi humo wakati wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Suffa ndio ilikuwa makazi yao, hivyo walijulikana kwa jina la Ahlus-Suffa. Wakati Mtume alipokuwa anapata chakula chake cha jioni, alikuwa anawakaribisha baadhi yao kula pamoja naye na aliwapeleka wengine kwenda kula na masahaba zake. Mmoja wa wakazi maarufu sana wa Suffa alikuwa ni Abu Huraira.11 Abu Nu’aim al-Isfahani amesema katika kitabu chake Hilyatul-Awliyah. Jz. 1, uk. 376 kwamba Abu Huraira alikuwa ndiye mkazi maarufu sana wa Suffa. Aliishi humo wakati wa uhai wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na hakutoka humo. Yeye alikuwa ndio mwanzilishi wa Suffa. Alizungumza kuhusu yeye mwenyewe kwamba alikuwa mmoja wa mafukara wakazi wa Suffa katika Hadith ndefu iliyosimuliwa na alBukhari.12 Abu Huraira amesema kama ilivyo katika Sahih Bukhari, Jz. 1, uk. 60: “Niliwaona sabini kati ya wakazi wa Suffa,13 hakuna hata mmoja kati yao 11 Rejea kwenye Sura ya (Siku za mwisho za uhai wa Mtume) katika kutaja majina ya masahaba wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) 12 Sahih Bukhari, Jz. 1, uk. 1 13 Hawa sabini kati ya wakazi wa Suffa waliuawa kishahidi mnamo siku ya kisima cha Ma’ouna kabla Abu Huraira hajawa Mwislam. Ilikuwa ni kama riwaya yake wakati aliposema: “Niliingia nyumbani kwa Ruqayya na alikuwa na chanuo mkononi mwake ….. ambapo alikuwa amekwisha kufariki kabla ya yeye kuja Madina. 20


Abu huraira check Lubumba.qxd

7/1/2011

10:46 AM

Page 21

Abu Huraira aliyekuwa na mavazi mwilini mwake. Walikuwa na ama msuli au kipande cha nguo kilichofungwa kwenye shingo zao, vingine vilifikia nusu ya miguu yao na vingine vilifikia visiginoni, ambavyo walivikusanya ili kuficha sehemu zao za siri zisionekane. Al-Bukhari amesimulia Hadith nyingine riwaya nyingine ndefu14 kwamba Abu Huraira alisema kwamba alijiweka kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kwa ajili ya kupata kula tu. Na nyingine iliyosimuliwa na Ibnul-Musayyab na Abu Slama kwamba Abu Huraira alisema kwamba: “Nilikaa na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kwa ajili ya kupata kula tu.”15 Katika riwaya nyingine, yeye alijizungumzia mwenyewe:16 “Nilikuwa mmoja wa wakazi wa Suffa. Wakati mmoja nilikuwa nimefunga. Nikaugua maradhi ya tumbo. Nikaenda kujisaidia haja na niliporudi nikakuta kwamba chakula kimekwisha kuliwa. Matajiri wa ki-Quraishi walikuwa wakileta chakula kwa wakazi wa Suffa. Nikasema: Niende kwa nani? Nikaambiwa niende kwa Umar ibn al-Khattab. Nikaenda kwake. Nilimkuta akishughulika na kumtukuza Mwenyezi Mungu baada ya swala. Nilisubiri hadi alipomaliza. Nikamwambia: Nisomee Qur’ani kidogo na unipatie chakula. Alisoma baadhi ya aya za Sura al-Imraan. Aliingia ndani na akaniacha mimi hapo mlangoni. Alichelewa. Nilidhania kwamba atabadili tu nguo zake kisha aniletee chakula. Hakukuwa na lolote katika hilo. Nilitoka kwenda kukutana na Mtukufu Mtume Muhammad (s.a.w.w.). Nilikwenda naye hadi tukafika nyumbani kwake. Alimwita mtumishi wake mweusi17 na akamwambia: “Hebu tuletee lile bakuli.” Alituletea bakuli 14 Sahih Bukhari, Jz. 1, uk. 24. Ilisimuliwa na wengine pia kama Abu Nu’aim katika kitabu chake Hilyatul-Awliyyah 15 Sahih al-Bukhari, Jz. 2, uk. 1 16 Hilyatul-Awliya’ ya Abu Nu’aim, Jz. 1, uk. 378 17 Tulikuwa hatujui kamwe wala kuwahi kusikia kwamba kulikuwa na mtumishi mweusi nyumbani kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). 21


Abu huraira check Lubumba.qxd

7/1/2011

10:46 AM

Page 22

Abu Huraira lililokuwa na chakula kidogo kilicholiwa na kubakishwa pembeni mwa bakuli hilo. Nilifikiria ni shayiri. Nilikula mpaka nikashiba kabisa.” Mara kwa mara alikuwa akijieleza yeye mwenyewe kwa kusema: “Naapa kwa jina la Allah, ambaye hakuna mungu isipokuwa Yeye, kwamba nililala chini kwenye sakafu na kuweka jiwe tumboni mwangu kwa sababu ya njaa. Wakati fulani nilikaa kwenye njia yao, mbayo kwayo hao (masahaba wa Mtume) walitoka nayo kutoka msikitini. Abu Bakr alipita karibu yangu. Nilimuuliza juu ya aya fulani ya Qur’ani ili tu anipatie chakula. Aliondoka zake bila kunipa chochote. Halafu Umar akapita karibu yangu na nikamuomba vivyo hivyo. Aliondoka zake bila kunipa chakula chochote. Kisha akapita Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) karibu yangu. Alitabasamu pale aliponiona mimi na akajua kilichokuwa akilini mwangu. Yeye akasema: “Abu Hirr.” Nikaitika, “Naam niko hapa.” Yeye akasema: “Nifuate.” Akatangulia nami nikamfuata. Aliingia ndani ya nyumba yake na akaniruhusu nami niingie humo. Tulikuta kikombe cha maziwa. Akauliza: “Maziwa haya yametoka wapi? Watu wa nyumbani humo wakasema: “Ni zawadi kutoka kwa mtu mmoja.” Yeye akasema: “Abu Hirr, nenda ukawakaribishe wakazi wa Suffa waje hapa.” Walikuwa ni wageni wa Uislam. Walikuwa hawana ndugu wa kuishi nao. Wakati Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alipokuwa amepata sadaka, alizituma sadaka zote kwao na pale alipopata zawadi aliigawana nao. Nikawa nimevurugikiwa. Nilidhania mimi nilikuwa na ubora zaidi ya wale watu wa Suffa kupata kinywaji kutokana na maziwa haya. Nilifikiria kwamba endapo wangefika, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) angeniamuru kuwapa maziwa hayo. Hivyo mimi nitapata nini kutokana na maziwa haya? Ilinilazimu kumtii Mtukufu Mtume. Nilikwenda na nikawakaribisha. Walikuja na wakaomba ruhusa. Wakaruhusiwa kuingia ndani na kukaa kwenye nafasi zao. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akasema: “Abu Hirr, chukua hicho kikombe cha maziwa na uwape wanywe.” Nilikichukua kikombe cha maziwa na nikaanza kuwapa mmoja baada ya mwingine na wote wakanywa wakatosheka hadi nikafikia kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). 22


Abu huraira check Lubumba.qxd

7/1/2011

10:46 AM

Page 23

Abu Huraira Akakichukua kikombe hicho, akatabasamu na kusema: “Abu Hirr, hakuna mwingine aliyebakia isipokuwa mimi na wewe.” Mimi nikasema: “Hilo ni sawa.” Yeye akasema: “Kaa chini na unywe.” Nilikaa chini na kikanywa. Alinitaka niendelee kunywa, nami nikanywa. Bado aliendelea kunitaka ninywe hadi nikasema: “Ninaapa kwa jina la Allah, ambaye amekutuma wewe kwa haki, kwamba siwezi kunywa zaidi ya hapo.” Yeye akasema: “Hebu nionjeshe.” Nilimpa kile kikombe. Alimtukuza na kumshukuru Mwenyezi Mungu, na akanywa yale yaliyobakia.’” 18 Pia ilisimuliwa katika Sahih Bukhari, Jz. 4, uk. 175 kwamba Abu Huraira alisema: “Nilizimia mara kwa mara katikati ya mimbari ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na chumba cha bibi Aisha. Wale waliokuja waliweka miguu yao kwenye shingo yangu wakifikiri kwamba nilikuwa na kichaa. Lakini sikuwa na kichaa. Ilikuwa ni kwa sababu ya njaa tu.” Thujjanahayn (mwenye mbawa mbili) Ja’far bin Abi Talib alikuwa mwenye hisani sana, mwenye huruma sana na mtoaji wa sadaka kwa masikini. Yeye mara kwa mara alimlisha Abu Huraira alipokuwa na njaa. Hivyo Abu Huraira alimuunga mkono na kumchukulia kama mbora wa watu baada ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kama ilivyotajwa ndani ya alIssaba (wasifu wa Ja’far). Al-Bukhari amesimulia19 kwamba Abu Huraira amesema: “Watu wanase18 Hadithi hii imesimuliwa ndani ya Sahih Bukhari katika sehemu nyingi za kitabu hicho, ambayo aliichukulia kuwa kama mmoja wa miujiza ya utume – kama ilikuwa ni kweli. Hatujui ni kwa nini haikusimuliwa na mwingine mbali na Abu Huraira, angalau na mmoja wa wale ambao walishirika na Abu Huraira katika kunywa maziwa hayo. Je, kulikuwa na umuhimu wowote wa changamoto hiyo na ukosa kifani wake? Hivi ilikuwa ni lazima kuvunja zile kanuni za asili? Miujiza haikujitokeza isipokuwa kulipokuwa na muhimu kwa ajili hiyo, ingawa tunakubali ukosa kifani wa Mwenyezi Mungu na manabii Wake. Ni dhahiri kwamba riwaya hii ilibuniwa na Abu Huraira ili kujipendekeza kwa watu wa kawaida hasa baada ya kufariki kwa masahaba mashuhuri na wale ambao Abu Huraira aliogopwa nao. 19 Sahih Bukhari, Jz. 2, uk.197. Imesimuliwa pia na Abu Nu’aim katika HilyatulAwliyyah’ Jz. 1, uk.117 23


Abu huraira check Lubumba.qxd

7/1/2011

10:46 AM

Page 24

Abu Huraira ma Abu Huraira amesimulia Hadith nyingi sana ambazo Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) anaweza kuwa hakuzisema. Nilikaa na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kiasi cha kukidhi njaa yangu tu. Sikula ama chakula kizuri wala kuvaa nguo mpya. Sikuhudumiwa na mtu yoyote. Niliminya tumbo langu kwenye ardhi kwa sababu ya njaa. Niliwaomba baadhi ya watu kunisomea aya za Qur’ani, ambazo nilikuwa tayari ninazijua, ili huenda wakanikaribisha kwa ajili ya chakula. Mbora zaidi kwa ajili ya masikini alikuwa ni Ja’far bin Abi Talib. Yeye alituchukua sisi kwenda kutupatia chakula chochote kilichopatikana ndani ya nyumba yake.20 Al-Baghawi ameitaja riwaya iliyosimuliwa na al-Maqbari21kwamba Abu Huraira amesema: Ja’far ibn Abu Talib aliwapenda sana masikini na alikaa nao. Aliwahudumia nao walimtumikia yeye. Alizungumza nao na wao walizungumza naye. Kwa hiyo Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alimwita baba wa masikini.22 At-Tirmidhi na Nassa’i wamesimulia kwamba Abu Huraira amesema: “Hakuna yeyote ambaye alivaa viatu, na akaendesha hamali na kutembea juu ya ardhi, aliyekuwa bora kuliko Ja’far bin Abu Talib baada ya Mtukufu Mtume Muhammad (s.a.w.w.).”23 20 Ibn Abd Rabbug al-Andalussi amesimulia katika kitabu chake al-Aqd al-Fariid, Jz. 1, kwamba Abu Huraira amesema: “Siku moja nilimfuata Ja’far bin Abi Talib na nilikuwa na njaa. Alipofika nyumbani kwake aligeuka na kuniona. Aliniomba niingie ndani. Mimi nikaingia. Alifikiri kwa muda kiasi lakini hakupata kitu chochote cha kula isipokuwa mfuko uliokuwa na kiasi cha siagi. Aliiteremsha kutoka juu ya rafu na akaufungua katikati yetu. Tulianza kulamba kilichokuwemo ndani yake wakati akiwa anaghani shairi fulani: Mwenyezi Mungu hajataka kutoka kwa mtu zaidi ya uwezo wake na mkono hautoi kwa ukarimu sana isipokuwa kile ulichonacho (mkono huo). 21 Rejea al-Issaba ya Ibn Hajar (wasifu wa Ja’far). 22 Imesimuliwa pia na Abu Nu’aim katika kitabu chake Hilyatul-Awliyyah, Jz. 1, uk.117 ikisimuliwa na Maqbari kutoka kwa Abu Huraira. 23 Imesimuliwa pia na Ibn Abdul-Birr katika kitabu chake al-Isti’ab.

24


Abu huraira check Lubumba.qxd

7/1/2011

10:46 AM

Page 25

Abu Huraira Suffa yalikuwa ndio makazi ya Abu Huraira, usiku na mchana. Hakuyaacha hayo na kwenda mahali pengine hadi Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alipoyaacha maisha haya ya kidunia yenye kusahaulika haraka na akajiunga na masahaba wakarimu. Kabla ya hapo Abu Huraira hakuweza kupata chochote cha kushibisha tumbo lake bila kukaa njiani kuwazuia wapita njia kulalamikia njaa yake. Hakuna jambo kubwa lililovutia nadhari yake. Hakutajwa ama katika vita au katika amani. Ndio! Imesimuliwa kwamba alikimbia kutoka kwenye jeshi katika vita vya Mu’ta.24 Alijifanya kuwa yeye ni mmoja kati ya wajumbe waliotumwa Makka na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) pamoja na Imam Ali kubeba ile Surat al-Bara’a na kwamba alikuwa anatangaza katika siku ya Hijja kubwa mpaka sauti yake ikawa na mikwaruzo. Alikuwa na Hadith mbili zinazopingana kuhusu hilo. Utakuja kuziona katika mlango wake maalum ndani ya kitabu hiki, Insha’allah. Alijisingizia kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alimfanya kuwa na shughuli maalum ya kuhifadhi Zaka ya Ramadhani, hayo utayaona katika Hadith ndefu.25

ZAMA ZA MAKHALIFA WAWILI WA MWANZO Tumezichunguza zama za Makhalifa wawili wa mwanzo, Abu Bakr na Umar bin al-Khattab, na tukadadisi ni nini kilichotokea katika siku zao lakini hatukupata kitu chochote cha maana cha kusema kuhusu Abu Huraira isipokuwa kwamba Umar alimtuma kwenda Bahrain mnamo mwaka wa ishirini na moja hijiria.26 Mnamo mwaka wa ishirini na tatu 24 Rejea al-Mustadrak, Jz. 3, uk. 42 utakuta kwamba Abu Huraira alishutumiwa juu ya hilo na hakujua aseme nini. 25 Sahih al-Bukhari, Jz. 2, uk. 29 26 Wakati pale Walii, al-Ala’ bin al-Hadhrami, ambaye aliteuliwa na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) Abu Bakr na Umar alipofariki. 25


Abu huraira check Lubumba.qxd

7/1/2011

10:46 AM

Page 26

Abu Huraira Khalifa Umar alimuengua na kumteua Uthman bin Abdul-Aass athThaqafi.27 Khalifa huyo sio tu alimuengua yeye Abu Huraira bali pia aliokoa kutoka kwake dirham elfu kumi kwa ajili ya hazina ya umma, akishutumu kwamba aliziiba ambapo zilikuwa ni mali wa Waislam. Lilikuwa ni suala maarufu sana. Ibn Abd Rabbih al-Maliki alisimulia ndani ya kitabu chake al-Aqd al-Fariid, katika kurasa zake mwanzoni za Juzuu ya kwanza, kwamba Khalifa Umar alimwitisha Abu Huraira na kumwambia: “Unajua vizuri kabisa kwamba nilikuwa nimekuteua kama Gavana wa Bahrain na ulikuwa pekupeku bila viatu, na sasa inanijia masikioni mwangu kwamba umenunua farasi kwa gharama ya dinari elfu moja na mia sita.” Abu Huraira akasema: “Tulikuwa na farasi ambao walizaana na zawadi zilikusanyika.” Khalifa akasema: “Nimefanyia mahesabu mapato yako na maisha yako na nikagundua kwamba ni zaidi ya kilicho chako na unapaswa kurudisha ziada hiyo.” Abu Huraira akasema: “Huwezi kufanya hivyo.” Umar akasema: “Ndio, ninaweza na nitakupiga mgongoni kwako.” Kisha Umar akasimama na kumchapa kwa fimbo yake 28 mpaka akamjeruhi na akamwambia: “Lipa hizo fedha na kuzirudisha mahali pake.” Abu Huraira akasema: “Nisamehe kwa ajili ya Mwenyezi Mungu.” Umar akasema: “Hilo litakuwa kama ilikuwa ni halali na kwamba umezirudisha kwa utiifu. Umetoka kwenye sehemu ya mbali Bahrain na kodi za watu ili kuziweka mifukoni mwako na sio kwa ajili ya Allah wala kwa ajili ya Waislam? Umayma amekuzaa wewe kwa ajili ya kuchunga punda tu.”29 Ibn Abd Rabbi amesimulia kwamba Abu Huraira amesema: “Wakati Umar aliponiuzulu mimi huko Bahrain, yeye aliniambia: “Ewe adui wa Mwenyezi Mungu na adui wa Qur’ani Yake, hivi umeiba mali ya 27 Ilisimuliwa katika Ta’rikh Ibn Athiir na wengineo wakati wa kuzungumzia kuhusu matukio ya mwaka wa 23AH. 28 Kichanga kikavu cha tende (kisichokuwa na tende) alichokuwa akitumia kukikamata mkononi mwake kama fimbo. 29 Ni methali. Umayma lilikukwa ni jina la mama yake. Maneno haya ya khalifa yalikuwa ni matusi mabaya sana. 26


Abu huraira check Lubumba.qxd

7/1/2011

10:46 AM

Page 27

Abu Huraira Waislam?” Abu Huraira akasema: “Mimi sio adui wa Mwenyezi Mungu wala wa Qur’ani Yake, bali mimi ni adui wa maadui zako. Mimi sikuiba mali ya Waislam.” Umar akasema: “Basi ni vipi ulivyopata dinari elfu kumi?” Yeye akasema: “Tulikuwa na kiasi cha farasi waliozaa, zawadi ambazo zilikusanyika na hisa zilizoongezeka.” “Umar alizichukua fedha hizo kutoka kwangu, lakini pale niliposwali sala ya al-Fajr, nilimuomba Mwenyezi Mungu anisamehe.’” Riwaya hii imesimuliwa na Ibn Abil Hadiid katika kitabu Sharh NahjulBalaghah, Jz. 3, uk. 104, chapa ya Misri, na imetajwa pia na Ibn Sa’d katika kitabu chake at-Tabaqat al-Kubra (wasifu wa Abu Huraira), Jz. 4, uk. 90, iliyosimuliwa na Muhammad bin Siiriin kwamba Abu Huraira amesema: “Umar aliniambia, ‘Ewe adui wa Mwenyezi Mungu na adui wa Qur’ani Yake, je umeiba mali ya Waislam ….. na kadhalika.” Ibn Hajar ameisimulia riwaya hii katika al-Issaba lakini aliirekebisha na kuipamba na kubadili ukweli kwa namna iliyotofautiana na wengine wote ili kutakasa umaarufu wa Abu Huraira. Lakini alisahau kwamba aliharibu jina la yule mtu, ambaye alimpiga Abu Huraira mgongoni na kuchukua fedha zake na kumuuzulu kwenye cheo chake.

ZAMA ZA KHALIFA UTHMAN Abu Huraira alikuwa mwaminifu sana kwa ajili ya familia ya Abul-Aass na Bani Umayyah wote wakati Uthman alipokuwa Khalifa. Aliungana na Marwan bin al-Hakam na wakajipendekeza kwa ukoo wa Abu Mu’iit, kwa hiyo yeye akawa mtu maarufu haswa baada ya kuzingirwa kwa nyumba ya Uthman wakati wa mapinduzi dhidi yake kwa sababu kwamba Abu Huraira alikuwa pamoja naye ndani ya nyumba hiyo. Hivyo akapata kuchanua baada ya kufifia, na umaarufu baada ya kutoeleweka. Alipata fursa wakati wa maasi, ya kupenyeza ndani ya nyumba ya Uthman na akawafanyia upendeleo familia ya Abul-Aass na Bani Umayyah wengine ambayo kwamba ikampa mvuto mkubwa juu yao na wasaidizi wao na ukaja kuiimarisha dola yao baadae. Hivyo wakalifuta lile vumbi la 27


Abu huraira check Lubumba.qxd

7/1/2011

10:46 AM

Page 28

Abu Huraira kutojulikana kwake na wakamsifia na kuweza kujulikana sana. Ingawa walijua kwamba hakupenyeza kwenye nyumba ili kuwa miongoni mwa waliozingirwa mpaka khalifa alipowaamuru wafuasi wake kuwa kimya na kuacha kupigana. Khalifa alifanya hivyo kwa ajili tu ya kuhifadhi damu yake na damu ya wafuasi wake. Abu Huraira alifahamu vyema kwamba wale waasi hawakumtaka yeyote isipokuwa Uthman na Marwan tu. Hilo lilimtia moyo wa kuwa miongoni mwa waliozingirwa. Alakulihali, bwana huyo aliitwaa fursa hiyo, mpango wake ulifanikiwa sana, na bidhaa (Hadith) zake zikauzika na kununuliwa sana. Kuanzia hapo Bani Umayyah na wafuasi wao walisikiliza riwaya zake kwa makini sana na wakajitahidi kiasi walivyoweza kuzitawanya na kuzieneza. Wakati huo huo alisimulia Hadith kulingana na matakwa yao. Kwa mfano, alisimulia kwamba Mtume Muhammad (s.a.w.w.) alisema: “Kila mtume alikuwa na rafiki mwandani, na wangu mimi ni Uthman.”30 Vile vile amesema: “Nimemsikia Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akisema kwamba: ‘Uthman ni mwenye haya sana, hivyo malaika wanaona haya mbele yake.”31 Pia alisema kwamba Mtukufu Mtume Muhammad (s.a.w.w.) amesema: “Kila Mtume anaye mkazi mwenzie huko peponi. Mkazi mwenzangu huko peponi ni Uthman.”32 30 Watu wote wenye akili timamu walikubaliana kwamba Hadith hii haikuwa ya kweli, bali marafiki wa Abu Huraira walimtoa kwenye uongo huu kwa kumlaumu Is’haq bin Najii’ al-Balti ambaye alikuwa mmoja wa wasimuliaji wa Hadith hii. Adh-Dhahabi ameitaja Hadith hii kwenye kitabu chake Mizan al-Itdal akithibitisha kwamba ilikuwa sio ya kweli. 31 Ibn Kathiir katika kitabu chake al-Bidaya wan-Nihaya, Jz. 7, uk. 203 32 Riwaya hiyo kwa kauli moja, ilikuwa ya uongo. Bali marafiki wa Abu Huraira waliigeuzia lawama hiyo kwa Uthman bin Khalid bin Umar bin Abdillah bin Waliid bin Uthman bin Affan ambaye alikuwa mmoja wa sanad ya wasimulizi wa riwaya hii. Adh-Dhahabi ameikataa riwaya hii kwenye kitabu chake al-Mizan alItdal. 28


Abu huraira check Lubumba.qxd

7/1/2011

10:46 AM

Page 29

Abu Huraira Abu Huraira vile vile amesimulia kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amesema: “Jibril alinijia na kuniambia: Mwenyezi Mungu anakuamuru kumuoza Uthman na Umm Kulthum (mwana wa kambo wa Mtume) kwa mahari sawa na ile ya Ruqaiyya (binti wa kambo mwingine wa Mtume.”33 Abu Huraira amesema: “Wakati mmoja niliingia nyumbani kwa Ruqayyah, binti ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na mke wa Uthman. Alikuwa na kitana mkononi mwake. Yeye akasema: “Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alikuwa hapa na ameondoka muda mfupi tu uliopita. Nilikuwa ninazichana nywele zake. Yeye akaniuliza: “Unafikiriaje juu ya Abu Abdillah (Uthman)?” Mimi nikasema: “Yeye ni mzuri tu.” Yeye akasema: “Mtukuze kwa sababu yeye ndiye anayefanana sana na mimi katika maadili miongoni mwa masahaba wangu.” Anaweza akaibadilisha Hadith kama alivyofanya kwa Hadith ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.): “Kutakuwa na maasi na kutoelewana baada yangu.” Wakasema: “Unatuamuru sisi tufanye nini basi?” Yeye (s.a.w.w.) akasema, huku akimuashiria kwa kidole Imam Ali: “Kuweni upande wa amir huyu na masahaba zake.” Lakini Abu Huraira alipendendelea kujipendekeza kwa familia ya Abul-Aas, Abu Mu’iit na Abu Sufyan, kwa hiyo akaigeuza

33 Ibn Munda ameisimulia Hadith hii na akasema kwamba ni dhaifu na imesimuliwa na Uthman bin Khalid al-Uthmani peke yake. Ibn Hajar al-Asqalani katika kitabu chake, al-Isaba, Jz. 4, (wasifu wa Umm Khulthum) akasema ni dhaifu na haikusimuliwa ila na Uthman bin Khalid al-Uthmani pekee.

29


Abu huraira check Lubumba.qxd

7/1/2011

10:46 AM

Page 30

Abu Huraira Hadith hii kwa Uthman (badala ya Ali)34 na badala yake wakamzawadia kwa upendeleo wake huo. 34 Kwa sababu hii, al-Hakim ndani ya kitabu chake al-Mustadrak, Jz. 3, uk. 99 ameitaja Hadith hii chini ya mada ya ‘sifa za Uthman.’ Lakini ukweli ulikuwa kwamba isimuliwe katika sifa za Ali, kama ilivyokuwa Hadith ya Mtukufu Mtume: (Kutakuwa na mgawanyiko na kutoelewana miongoni mwa watu, hivyo huyu na wafuasi wake watakuwa upande wa haki. Alimnyooshea kidole Ali). Imesimuliwa na at-Tabarani katika kitabu chake KanzulUmmal, kutoka kwa Ka’b bin Ajra, Hadith namba 2635, Jz. 6. Na Hadith ya Mtukufu Mtume: (Kutakuwa na maasi baada yangu (baada ya kifo changu). Hivyo kuweni upande wa Ali ibn Abu Talib, kwa sababu yeye alikuwa wa kwanza kuniamini mimi (katika Uislam) na yeye atakuwa wa kwanza kupeana mikono na mimi katika Siku ya Kiyama. Yeye ndiye mkweli mkubwa na ndiye mpambanuzi wa umma huu). Ilikuwa imetajwa na Abu Ahmad Ibn Munda na wengine, kutoka kwa Abu Layla al-Ghifari. Imesimuliwa pia na Ibn AbdulBirr katika Isti’aab, ibn Hajar katika Isaba na wengine (katika wasifu wa Abu Layla). Na Hadithi ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kwa Ammar bin Yassir: “Ewe Ammar, kama ukimuona Ali akipita kwenye bonde na watu wote waliobakia wakipita kwenye bonde jingine, mfuate Ali na uwaache hao watu wengine kwa sababu hatakuongoza kwenye majaliwa mabaya wala hatakutoa kwenye njia ya mwongozo sahihi.” Imesimuliwa na alDaylamy katika kitabu chake Kanzul-Ummal, Jz. 6, uk. 155, Hadith namba 259 iliyosimuliwa na Ammar na Abu Ayyub. Na vile vile Hadith ya Mtukufu Mtume: “Oh, Abu Rafi’, litakuwepo baada ya kifo changu kundi la watu litakalopigana na Ali. Wajibu utakuwa ni kuwapiga.” Imetajwa na at-Tabarani katika Kanzul-Ummal, Jz. 6, Hadith namba 2589 kutoka kwa Muhammad bin Ubaydillah bin Abu Rafi’ kutoka kwa baba yake, kutoka kwa babu yake. Kuna Hadithi nyingi kama hizi lakini hatuwezi kuzitaja zote hapa. Inatutosha sisi Hadith ya Mtukufu Mtume: “Kuna mtu miongoni mwenu atapigana kwa ajili ya tafsiri ya Qur’ani kama mimi nilivyopigana kwa ajili ya kushuka kwake.” Watu walilitazamia hilo, miongoni mwao alikuwa ni Abu Bakr na Umar. Abu Bakr akasema: “Je ni mimi? Mtukufu Mtume akasema: Hapana. Umar akasema: Je ni mimi? Mtukufu Mtume akasema: Hapana. Bali ni yule anayerekebisha viatu.” Ilitajwa na al-Hakim katika al-Mustadrak yake Jz. 3, uk.122 akisema kwamba ilikuwa ni Hadith sahihi kwa mujibu wa al-Bukhari na Muslim. Imesimuliwa pia na Thalabi katika kitabu chake, Talkhiis na Ahmad katika Musnad, Jz. 3, uk. 33 kutoka kwa Abu Sa’id na Abu Nua’im katika kitabu chake Hilyatul-Awliyyah, Jz. 1, uk. 67 (katika wasifu wa Ali), na Abu Ya’ala katika Sunan yake, na Sa’id bin Mansuur katika Kanz, Jz. 6, uk. 155, Hadith namba 2585. Hadith inayozungumzia umuhimu wa kupigana na watu wenye hiana, wasaliti (Vita vya Ngamia) na maharamia (Vita vya Siffiin) na wakanaji waasi (Khawariji) zilithibitishwa na kila moja ikiihakikisha nyingine. Hadith za Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) zinazozungumzia maasi baada ya kifo chake zilikuwa zinajirudia na zilikuwa za kuashiria ubashiri wa Muhammad (s.a.w.w.). Zilikuwa za wazi katika kuhimiza kumfuata Imam Ali (a.s.). Ile Hadith iliyosimuliwa na al-Hakim kutoka kwa Abu Huraira ilikuwa ni mojawapo. Kilichothibitisha hivyo kilikuwa kwamba Mtume (s.a.w.w.) hakumuita yeyote kabisa kwa jina la ‘Amiir’ isipokuwa Ali. Na hapa ni Hadith ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kwa Anass: “Wa kwanza atakayeingia kupitia mlango huu, huyo ni Amiirul-Mu’miniin (Jemadari wa waumini) na bwana wa walezi …………...” Hii ilisimuliwa na al-Isfahani katika kitabu chake Hilyatul-Awliyyah, Jz.1, (wasifu wa Ali). Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) aliwaamuru masahaba zake kumwita Ali kwa jina la Amirul-Mu’miniin wakati wanapomsalimia yeye. Hili lilithibitishwa na riwaya nyingi zilizosimuliwa na kizazi cha Mtume (s.a.w.w.).

30


Abu huraira check Lubumba.qxd

7/1/2011

10:46 AM

Page 31

Abu Huraira WAKATI WA ZAMA ZA ALI (A.S.) Sauti ya Abu Huraira ilififia na kushuka chini wakati wa utawala wa Ali (a.s.). Alizingwa katika utusitusi wa kutotambulika tena na alikuwa akaribie kurudi kwenye hali yake ya awali. Alimgeuka Imam Ali na wala hakujaribu kumuunga mkono. Kwa kweli mwisho wa safari yake ulikuwa kwenye mikono ya maadui wa Imam Ali (a.s.). Wakati mmoja Mu’awiya alimtuma Abu Huraira na an-Nu’man bin Bashiir wakiwa Damascus, kwenda kwa Imam Ali (a.s.) kumuomba awapeleke wauaji wa Uthman kwa Mu’awiya ili apate kuwaadhibu kwa kumuua kwao Uthman. Kwa kufanya hivi, alichotaka Mu’awiya ni kwamba watakaporudi Damascus watamtoa yeye lawamani na kumtupia lawama zote Imam Ali, ingawa alijua kwamba Imam Ali hatawapeleka kwake hao wauaji wa Uthman. Hivyo alitaka kuwafanya Abu Huraira na an-Nu’man kuwa ushahidi mbele ya watu wa Damascus na kuwaonyesha kwamba yeye Mu’awiya alikuwa anayo sababu ya kupigana na Imam Ali (a.s.). Mu’awiya aliwaambia Abu Huraira na an-Nu’man: “Nendeni kwa Ali na mkamwambie atuletee wale wauji wa Uthman kwani yeye amewahifadhi. Kama akifanya hivyo, hakutakuwa na vita kati yetu na yeye. Kama akikataa, ninyi mtakuwa mashahidi dhidi yake. Halafu mtajitokeza mbele ya watu na kuwaelezea juu ya hilo.” Walikwenda kwa Imam Ali (a.s.). Abu Huraira akamwambia: “Oh, Abul-Hasan,35 Mwenyezi Mungu amekupa sifa na heshima katika Uislam, kwani wewe ni binamu yake Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Na binamu yako Mu’awiya ametutuma kwako akikuomba kitu cha kutuliza vita hivi na kumaliza uhasama kati yenu, ambacho ni kuwatuma wauaji wa binamu yake Uthman kwake ili akawauwe na Mwenyezi Mungu awasuluhisheni. Hivyo umma utakuwa salama kutokana na maasi na kutoelewana.” Kisha an-Nu’man naye akasema 35 Moja ya majina ya Imam Ali (a.s.). 31


Abu huraira check Lubumba.qxd

7/1/2011

10:46 AM

Page 32

Abu Huraira maneno kama hayo. Imam Ali (a.s.) akawaambia: “Hebu tusizungumze juu ya hilo. Oh, Nu’man, nieleze kuhusu wewe mwenyewe. Wewe ndiye mbora wa watu wako Ansari katika kuongoza?” Yeye akasema: “Hapana.” Imam Ali (a.s.) akasema: “Watu wako wote wamenifuata mimi isipokuwa wapotofu watatu au wane kati yao. Je, wewe ni mmojawapo kati ya wapotofu hao?” an-Nu’man akasema: “Kwa hakika nimekuja ili niwe pamoja na wewe na kubakia kwako, lakini Mu’awiya amenituma nije kukuambia hivyo. Nilitumaini kwamba hiyo itakuwa ni sababu ya kuja kukutana na wewe na nilitegemea kwamba Mwenyezi Mungu atawasuluhisheni. Kama wewe unaona vinginevyo mbali na hilo, basi mimi nitakuwa na wewe na sitaondoka na kukuacha..” Wanahistoria wamesema kwamba Imam Ali (a.s.) hakuzungumza hata neno moja na Abu Huraira. Yeye aliondoka kwenda Damascus na kumwambia Mu’awiya kuhusu yale yaliyotokea. Mu’awiya alimuamuru awaelezee watu kuhusu hilo. Yeye alifanya hivyo, na alifanya mambo mengi mengine yaliyomridhisha Mu’awiya. An-Nu’man alikaa na Imam Ali na kisha akatorokea Damascus na akawaambia watu wa huko kuhusu yaliyotokea …………mpaka mwisho wa kadhia hii.36

36 Kadhia hii imesimuliwa na Ibrahim bin Hilal ath-Thaqafi katika kitabu chake al-Gharat na Ibn Abil-Hadiid katika Nahjul-Balaghah, Jz. 1, uk. 213. Yule anayetaka kujua maelezo yake arejee humo, ili kuona nia za Mu’awiya na matendo ya kasoro za an-Nu’man katika kadhia hii. Imam Ali (a.s.) alimgeuzia mgongo Abu Huraira na hakuzungumza naye kwa sababu aliona kwamba Abu Huraira alikuwa mtu duni kwamba alijipendekeza kwa Mu’awiya na kuuza imani yake kwake kwa ajili ya maisha mafupi tu ya dunia. Imam Ali (a.s.) alijua ni nini lengo la Mu’awiya kwa kuwatuma watu hawa wawili, hivyo hakuwajibu kwa kukubali au kukataa. Kwa kweli aliyageuzia mgongo madai yao na akaongea na Nu’man kuhusu jambo jingine kabisa. Hili lilionyesha sera yake iliyofungamana kikamilifu. 32


Abu huraira check Lubumba.qxd

7/1/2011

10:46 AM

Page 33

Abu Huraira Wakati mambo yalipokuwa mabaya na vita vikaanza, hofu ilimwingia Abu Huraira moyoni na kufanya miguu yake itetemeke. Mwanzoni mwa maasi yale hakufikiria kwamba Imam Ali (a.s.) angeshinda vita hivyo, hivyo yeye alinywea mpaka chini na akaanza kuwatia unyonge wengine ili wasimsaidie Imam Ali kwa kuwaambia Hadith za uongo kwa siri. Moja ya Hadithi zake wakati huo ilikuwa kwamba alisema: “Nimemsikia Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akisema: ‘Kutakuwa na maasi; aliyekaa atakuwa ni bora kuliko aliyesimama na aliyesimama atakuwa ni bora kuliko anayetembea na anayetembea atakuwa ni bora kuliko anayekimbia. Yeyote atakayepata hifadhi naaikimbilie.”37 Abu Huraira alibakia kama alivyokuwa hadi ma-Khawariji walipoasi dhidi ya Imam Ali (a.s.) na Mu’awiya alipokuwa amepata nguvu zaidi. Aliikalia Misri na akamuua Gavana wake, ambaye aliteuliwa na Imam Ali (a.s.). Alianza kuharibu na kufanya mashambulizi dhidi ya dola ya Imam Ali (a.s.). Alimtuma Bissr bin Arta’a pamoja na jeshi la wapiganaji elfu tatu kwenda Hijazi na Yemen akiteketeza na kuharibu huko. Waliua, kuchoma na kuwakatakata watu kikatili kabisa. Walizikufuru sheria za Mwenyezi Mungu. Walivunja hadhi za wanawake na kuwateka vijana wadogo wa kiume na wasichana wa Waislam huko ili kushusha sura ya historia. Baada ya ukatili na maovu yote hayo, Bissr alilazimisha kwa nguvu heshima kwa Mu’awiya kutoka kwa watu wa Hijazi na Yemen.38 Kisha Abu Huraira akasambaza yaliyokuwa yamefichika moyoni mwake kwa Bissr 37 Imesimuliwa na Ahmad bin Hambali katika Musnad yake Jz. 2, uk. 282. Ilikuwa sio sahihi, kwa sababu Allah anasema: “Na endapo makundi mawili ya waumini yakigombana, suluhisheni baina yao; bali kama kundi mojawapo litadhulumu jingine. basi lipigeni lile lenye kudhulumu hadi lirejee kwenye amri ya Allah …..” 49:9 38 Rejea Nahj al-Hamiidi, Jz. 1, uk. 116-121 kwa ajili ya maelezo zaidi. Wanahistoria wote, ambao waliandika juu ya matukio ya mwaka wa 40 hijiria wamelitaja tukio hili lililofanywa na Mu’awiya. Ni maarufu kama vita vya Harra na at-Taff vya mwanawe Yaziid. 33


Abu huraira check Lubumba.qxd

7/1/2011

10:46 AM

Page 34

Abu Huraira bin Arta’a. Bissr akaona kwamba huyu ni mkweli kwa Mu’awiya na mwaminifu katika kuchukua utii kwa Mu’awiya kutoka kwa watu. Bissr akamteua Abu Huraira kuwa Gavana wa Madina wakati alipoondoka, baada ya kuwaamuru watu kumtii yeye. Aliongoza watu katika swala na akadhani amekuwa ndiye Gavana halisi wa Madina mpaka Jariya bin Qudama as-Sa’id alipokuja Madina pamoja na mashujaa wa koo bora wapatao elfu mbili waliotumwa na Imam Ali (a.s.). Abu Huraira alikuwa anawaongoza watu katika kuswali. Akakimbia. Jariya akasema:39 “Kama ningemkuta Abu Sannour,40 basi ningemuua. Wakati Jariya akiwa yupo huko Hijazi, alikuja kujua kwamba Imam Ali (a.s.) alikuwa ameuawa kishahidi. Alichukua utii kwa Imam Hasan ibn Ali ibn Abi Talib (a.s.) na akarudi mjini Kufah. Abu Huraira akarudi Madina akiongoza katika swala41 na akawa na nguvu sana mpaka Mu’awiya alipotawala.

WAKATI WA ZAMA ZA MU’AWIYA Abu Huraira aliishi katika siku bora za maisha yake wakati wa utawala wa Mu’awiya. Mu’awiya aliyatimiza matumaini mengi ya bwana huyu, hivyo alisimulia Hadith kwa namna Mu’awiya alivyotaka. Aliwasimulia watu riwaya za kushangaza kuhusu sifa za Mu’awiya na wengineo. 39 Imesimuliwa na Ibrahim bin Hilal ath-Thaqafi katika kitabu chake al-Gharat na Ibn Abil Hadiid katika Sharh Nahjul-Balaghah, Jz. 1, uk. 128. 40 Kwa Kiarabu neno Sannour maana yake ni paka. Jariya alimaanisha Abu Huraira. 41 Imesimuliwa na Ibnul-Athiir katika kitabu chake, Tariikh al-Kamil, Jz. 3, uk. 153.

34


Abu huraira check Lubumba.qxd

7/1/2011

10:46 AM

Page 35

Abu Huraira Hadithi za kubuni zilivuka mipaka katika dola ya Mu’awiya kulingana na mtandao wake wa habari ulivyotaka na sera zake zilihitaji kuwachukia Bani Hashim. Dola ya Mu’awiya ilikuwa na waongo wazushi wengi wakisimulia Hadith za Mtume kama vile Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alivyokuwa ameonya hapo kabla juu ya Hadith kama hizo. Waliendelea sana katika ubunifu wa Hadith kulingana na kile walichopewa msukumo kwacho na watawala. Wa kwanza wao alikuwa ni Abu Huraira. Aliwasimulia watu Hadith za kuchukiza sana akizungumzia kuhusu sifa za Mu’awiya. Moja ya Hadith hizo ilisimuliwa na Ibn Asakir kwa njia mbili, Ibn Adiy kwa njia mbili, Muhammad ibn Aa’ith katika njia ya tano, Muhammad bin Abd as-Samarqandi katika njia ya sita, Muhammad bin Mubarak as-Souri katika njia ya saba na al-Khatiib al-Baghdad katika njia ya nane kwamba Abu Huraira amesema: “Nilimsikia Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akisema: “Mwenyezi Mungu ameaminisha mwongozo Wake kwa watu watatu; mimi, Jibril na Mu’awiya!” Na nyingine iliyosimuliwa na al-Khatiib al-Baghdad kwamba Abu Huraira amesema: “Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alimpa Mu’awiya mshale na akamwambia: “Chukua mshale huu ukae nao mpaka utakapokutana nami huko Peponi!” Nyingine ilisimuliwa na Abul-Abbas al-Waliid bin Ahmad az-Zouzani katika kitabu chake, Shajaratul-Aql, katika njia mbili kwamba Abu Huraira alisema: “Nilimsikia Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akisema: “Kutakuwa na Kuba la lulu nyeupe lenye milango minne kwa ajili ya Abu Bakr. Upepo wa rehma unavuma kupitia humo. Nje yake kuna msamaha wa Mwenyezi Mungu na ndani mwake ni radhi za Mwenyezi Mungu. Anapokuwa na hamu na Mwenyezi Mungu, mlango hufunguka ili amuangalie Mwenyezi Mungu kupitia hapo.” Nyingine imesimuliwa na Ibn Habban kwamba Abu Huraira amesema: “Wakati Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alipotoka nje ya pango kuelekea Madina, Abu Bakr alishikilia kikuku cha farasi wake. Yeye akasema: “Oh, Abu Bakr, je nikupashe habari njema? Katika Siku ya Ufufuo, Mwenyezi Mungu atajitokeza kwa viumbe Wake kwa jumla na atatokeza kwako wewe kwa siri!”

35


Abu huraira check Lubumba.qxd

7/1/2011

10:46 AM

Page 36

Abu Huraira Na kile kilichoelezwa na Ibn Habban kwamba Abu Huraira alisema: “Wakati Jibril alipokuwa na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), Abu Bakr alipita karibu yao. Jibril akasema: Huyu ni Abu Bakr. Mtukufu Mtume akasema: Ewe Jibril, wewe unamfahamu yeye? Jibril akasema: Yeye ni maarufu zaidi huko peponi kuliko alivyo hapa duniani. Malaika wanamwita mtambuzi wa Quraishi. Yeye ni waziri wako katika uhai wako na ndiye Khalifa baada ya kifo chako.” Hadith nyingine imesimuliwa na Khatiib alBaghdadi kwamba Abu Huraira amesema: “Mtume Muhammad (a.s.w.w.) amesema: Malaika walisherehekea wakati wa kuzaliwa kwa Abu Bakr. Mwenyezi Mungu aliangalia kwenye Bustani ya Aden na akasema: Naapa kwa utukufu na ukuu wangu kwamba sitamwingiza yeyote ndani ya hii isipokuwa yule atakayempenda huyu mtoto aliyezaliwa hivi punde.” Na nyingine iliyotajwa na Ibn Adiy kwamba Abu Huraira amesema: “Nilimsikia Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akisema: wakati nilipopanda juu mbinguni (mi’raaj), katika kila mbingu niliyopita niliona kwamba imeandikwa; Muhammad ni Nabii wa Allah, Abu Bakr ni ……” 42 Abul-Faaj ibn al-Jawzi amesimulia Hadith kwamba Abu Huraira amesema: “Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) aliniambia kwamba wakati mmoja Pepo na Jahannam zilitambiana kwa fakhari. Jahannam ikasema kuiambia Pepo: Mimi ni bora kuliko wewe kwani ninao wale Mafirauni, madhalimu, wafalme na vizazi vyao. Mwenyezi Mungu aliipa msukumo Pepo kusema: Mimi ni bora kuliko wewe kwa sababu Mwenyezi Mungu alinipamba mimi kwa ajili ya Abu Bakr.” Na nyingine iliyotajwa na al-Khatiib kwamba Abu Huraira alikuwa amesema: “Siku moja Mtukufu Mtume (a.s.w.w.) alitoka nje akiwa amemuegemea Ali Ibn Abi Talib. Wao wakakutana na Abu Bakr na Umar. Mtukufu Mtume akamwambia Ali (a.s.): Je, wewe unawapenda hawa watu wawili? Ali akasema: Ndio, ninawapenda. Mtukufu Mtume akamwambia Ali: Wapende hawa ili uweze kuingia Peponi!” 42 Imesimuliwa pia na al-Khatiib katika kitabu chake Ta’rikh Baghdad, Jz. 5, uk.445. 36


Abu huraira check Lubumba.qxd

7/1/2011

10:46 AM

Page 37

Abu Huraira Hadith nyingine ni ile iliyosimuliwa na al-Khatiib al-Baghdad katika kitabu chake cha historia, Ta’rikh Baghdad na Ibn Shahin katika Sunan yake kwa njia mbili kwamba Abu Huraira amesema: “Nilimsikia Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akisema kwamba: “Kuna malaika themanini elfu katika mbingu ya chini wanaomuomba Mwenyezi Mungu kumsamehe yeyote anayempenda Abu Bakr na Umar, na uwingu wa pili malaika themanini elfu wanaomlaani kila anayemchukia Abu Bakr na Umar.” Nyingine ni iliyosimuliwa na al-Khatiib kwamba Abu Huraira amesema: “Nimemsikia Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akisema: Mwenyezi Mungu anao malaika elfu sabini huko mbinguni wakimlaani kila anayemkashifu Abu Bakr na Umar.” Hadithi zote hizi sio sahihi. Wote waliozisimulia Hadith hizi wametamka kwa pamoja kwamba zilikuwa ni batili. As-Suyuti amezipanga Hadith zote zilizobuniwa kulingana na nyororo zao za wasimuliaji na maelezo yao katika kitabu chake, al-La’ali alMassnuu’a. Lakini wao wakati wote walimtetea Abu Huraira kwa kuwalaumu wale wengine ambao wamesimulia kutoka kwa Abu Huraira kwa mujibu wa maoni yao kwamba kila Mwislam aliyemuona Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) au aliyesimulia kutoka kwake alikuwa sio aliyesalimika kutokana na makosa – maasum! Walifanya hivyo hivyo kwa kile udhanifu wa Abu Huraira ulichokibuni, kama Hadith yake: “Nilimsikia Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akisema: Huyu ni Jibril akiniambia kutoka kwa Mwenyezi Mungu kwamba yeyote anayempenda Abu Bakr na Umar ni mchamungu na yeyote anayewachukia ni mnafiki mlaghai.”43

43 Hadith hii imeonekana kwamba sio sahihi kwa makubaliano ya pamoja. AdhDhahabi ameisimulia Hadith hii katika kitabu chake, Mizanul-I’tdal (katika wasifu wa Ibrahim bin Malik al-Ansari) na amesema kwamba hiyo haikuwa sahihi. Kila mmoja alitumia ubatilifu kupingana na haki, yeye bila shaka angeshindwa. 37


Abu huraira check Lubumba.qxd

7/1/2011

10:46 AM

Page 38

Abu Huraira Abu Huraira amesema: Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amesema: Mwenyezi Mungu ameniumba mimi kwa nuru Yake, na amemuumba Abu Bakr kwa nuru yangu mimi na kisha akamuumba Umar kwa nuru ya Abu Bakr na akauumba umma wangu kwa nuru ya Umar. Umar ndio taa ya watu wa Peponi.” 44 Vile vile alisema: “Nilimsikia Mtukufu Mtume akisema: Abu Bakr na Umar ndio wabora wa Waislam wa mwanzo na wa mwisho.” 45 Na Hadith yake: “Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amesema: Masahaba wangu ni sawa na nyota. Yeyote atakayewafuata hao ataongozwa.”46 Na Hadithi yake: “Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amesema: Kulikuwa na Sura katika Biblia inayonielezea mimi na masahaba zangu; Abu Bakr, Umar, Uthman na Ali ….. kama punje ya mbegu inayochomoza chipukizi lake …..” 47 Na nyingine nyingi kiasi kwamba alifanya udhanifu wake kwenda hapa na pale katika kubuni. Vitabu vya Hadith vya al-Bukhari na Muslim48 vina Hadith nyingi mno za aina hiyo. 44 Hadith hii vile vile ilionekana si Sahihi kwa makubaliano ya pamoja. Dhahabi ameisimulia kwenye kitabu Mizanul-I’tdal (wasifu wa Ahmad Samarqandi). Rejea hicho ili kuona kwamba haikuwa sahihi na kwamba ilipingana na Qur’ani. Na walishindwa wale waliotaka kuficha ukweli wa wazi kwa batili isiyo na haya. 45 Huu ni kama ule ubatilishaji namna mbili zilizopita. Dhahabi ameisimulia katika Mizanul-I’tdal (wasifu wa Jairuun bin Waqid) na akasema sio sahihi, ni batili. 46 Adh-Dhahabi ameisimulia Hadith hii katika chake cha Mizanul-I’tdal (katika wasifu wa Kadhi Ja’far bin Abdul-Wahid 47 Imetajwa na adh-Dhahabi katika Mizanul-I’tdal yake (kwenye wasifu wa Muhammad bin Musa bin Atta ad-Damyatti) lakini wakati wote waliwalaumu watu wengine waliosimulia kutoka kwa Abu Huraira! Hadith hii ilijumuisha na aya ya Qur’ani; 48:29. 48 Muslim hapa ni jina la mmoja wa waliokusanya Hadith hizo katika kitabu chake, Sahih Muslim. 38


Abu huraira check Lubumba.qxd

7/1/2011

10:46 AM

Page 39

Abu Huraira

FADHILA ZA BANI UMAYYAH Utazigundua kirahisi zawadi za Bani Umayyah kwa mtu huyu kama ukifikiria juu ya hali zake mbili; moja kabla ya utawala wao ambapo alikuwa duni sana na mtwana, akiangalia chawa wanaotambaa kwenye nguo zake,49 na hali yake nyingine wakati wa utawala wao ambapo walimtoa kwenye tope la umasikini na kumvisha nguo za hariri.50 Walimfanya afunge nguo zake kwa hariri na walimvisha nguo za katani nyembamba.51 Walimjengea kasri huko al-Aqiiq.52 Walimzunguka kwa hisani zao na wakamfunika kwa zawadi zao. Walieneza utajo wake na kutangaza jina lake. Walimfanya kuwa Gavana wa Madina, ule mji wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.)53 na kumuoza yeye, wakati wa utawala wake, kwa Bissra binti 49 Haya yalichukuliwa kutoka kwenye Hadith ya Abu Huraira: Nilichukua nguo kutoka mgongoni kwangu na nikaitandaza kati yangu na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) huku nikiwa nikiwaangalia chawa waliokuwa wanatambaa juu yake ….. Ilisimuliwa na Abu Nu’aim katika Hilyatul-Awliyah, Jz. 1, uk.381 50 Ibn Sa’d ameisimulia katika kitabu chake Tabaqat (kwenye wasifu wa Abu Huraira) kutoka kwa Wahab bin Kaysan, Qatada na al-Mughiira kwamba Abu Huraira alikuwa akivaa nguo za hariri. 51 Al-Bukhari katika Sahih yake Jz. 4, uk. 175, amesimulia kwamba Muhammad bin Siriin amesema: Tulikuwa kwa Abu Huraira na alikuwa amevaa nguo za kitani nyembamba. 52 Alifariki ndani ya Kasri hili kama ilivyotajwa na Ibn Hajar katika al-Isaba, Ibn Qutayba katika al-Ma’arif na Ibn Sa’d katika Tabaqat. 53 Imetajwa na Imam Ahmad katika Musnad yake, Jz. 2, uk. 430, ikiwa imesimuliwa na Muhammad bin Ziyad, Ibn Qutayba katika al-Ma’arif yake kutoka kwa Abu Rafi’ na Imam Abu Ja’far al-Iskafi katika kitabu chake, Sharh an-Nahj al-Hamiid, Jz. 1, uk. 359, toleo la Misri.

39


Abu huraira check Lubumba.qxd

7/1/2011

10:46 AM

Page 40

Abu Huraira Ghazwan bin Jabir bin Wahab al-Maziniya, dada wa Utba bin Ghazwan54 na hakuweza kuota juu ya hilo au fikra zake zisingeweza kufikiri juu ya hilo, kwa sababu alijitahidi kumtumikia yeye (Bissra) akiwa miguu mitupu bila viatu, kwa ajili ya chakula tu. Mudharib bin Jiz’ amesema:55 “Nilikuwa natembea wakati wa usiku, na kulikuwa na mtu anatamka kwa mshangao: ‘Allahu Akbar’ mimi nikamfuata. Niligundua kwamba alikuwa ni Abu Huraira. Nikasema: ‘Hiki ni nini?’ Akasema: ‘Mimi ninamshukuru Mwenyezi Mungu. Nilikuwa nimeajiriwa na Bissra binti Ghazwan kwa ajili tu ya chakula changu. Niliongoza mahamali yao walipokuwa wamepanda na kuwahudumia waliposhuka, na sasa nimekuwa mume wake. Sasa mimi ninapanda, na ninaposhuka yeye ananihudumia. Kabla ya hapo, wakati alipofika kwenye uwanda au bonde, alishuka na kusema: ‘Sitaondoka mpaka unitengenezee uji.’ Sasa mimi ninapofika kwenye maeneo yale yale ninamwambia: ‘Sitaondoka mpaka unitengenezee uji.’”56 Mara kwa mara alikuwa akisema, wakati wa ugavana wake wa Madina: “Nilikulia kama yatima. Wakati nilipohamia nilikuwa masikini. Niliajiriwa 54 Yeye (Utba) alikuwa mshirika wa kabila la Abd Shams. Khalifa Umar (r.a) alimfanya yeye kuwa kiongozi wakati wa ushindi wa Waislam. Alianzisha mji wa Basra na akawa ndiye Gavana. Aliteka nchi nyingi na alikuwa mmoja wa masahaba maarufu wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na mmoja wa mashujaa. Alifariki wakati wa utawala wa Umar. Lakini Abu Huraira alimuoa dada yake baada ya muda mrefu tangu kifo chake. Ibn Hajar al-Asqalani katika kitabu chake, al-Isaba alimtaja Bissra na Hadith ya Abu Huraira pamoja naye. Alisema kwamba yeye, Bissra, alikuwa amemuajiri Abu Huraira wakati wa uhai wa Mtukufu Mtume, halafu akaja akaoana naye pale Marwan alipomkabidhi ugavana wa Madina katika kipindi cha Mu’awiya. 55 Imesimuliwa na Abul-Abbas as-Sarraj katika Ta’rikh na Ibn Hajar katika Isaba yake (wasifu wa Abu Huraira). 56 Imesimuliwa na Abu Khuzayma na Ibn Hajar katika kitabu chake al-Isaba.

40


Abu huraira check Lubumba.qxd

7/1/2011

10:46 AM

Page 41

Abu Huraira na Bissra binti Ghazwan kwa ajili ya chakula changu tu. Niliongoza mahamali yao walipopanda kusafiri na kuwahudumia wakati waliposhuka chini na sasa Mwenyezi Mungu amenioza mimi kwake. Shukurani kwa Mwenyezi Mungu, aliyeifanya dini kama msingi na akamfanya Abu Huraira kuwa imam.”57 Wakati mmoja yeye alisema: “Niliajiriwa na Bissra binti Ghazwan kwa ajili ya mlo wangu tu. Aliniamuru nipande wimawima na kutembea pekupeku. Baada ya hapo Mwenyezi Mungu akamfanya yeye kuwa mke wangu. Nilimuamuru yeye kupanda wima na kutembea pekupeku.”58 Siku moja aliwaongoza watu katika swala na pale alipomaliza akasema kwa sauti kubwa: “Shukrani ni zake Mwenyezi Mungu, aliyefanya dini kuwa msingi na akamfanya Abu Huraira kuwa imam baada ya kwamba alikuwa ni mtumishi kwa ajili ya Bissra binti Ghazwan kwa ajili ya mlo wake na hamali kwa ajili ya kupanda.”59 Siku moja alipanda kwenye mimbari ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na akasema: “Ashukuriwe Mwenyezi Mungu, ambaye amenifanya mimi niweze kula chakula kizuri, kuvaa nguo za hariri na kunioza mimi kwa Bissra binti Ghazwan baada ya mimi kuwa mtumishi wake kwa ajili ya malipo ya mlo wangu. Bissra alinifanya nibebe mizigo yake na kisha nikamfanya yeye anibebee mizigo yangu mimi.”60

57 Tabaqat cha Ibn Sa’d, sehemu ya pili, Jz. 4, uk. 53. 58 Rejea kwenye Tabaqat ya Ibn Sa’d, sehemu ya pili ya Juz. 4, uk. 53. 59 Rejea Hilyatul-Awliya’ ya Abu Nu’aim, Jz.1, uk. 379 60 Rejea Hilyatul-Awliya’ ya Abu Nu’aim, Jz.1, uk. 384. 41


Abu huraira check Lubumba.qxd

7/1/2011

10:46 AM

Page 42

Abu Huraira KUSHUKURU FADHILA ZA BANI UMAYYAH Bani Umayyah walimtumikisha Abu Huraira kama mtumwa kwa fadhila zao. Walijitwalia usikivu wake, uoni na moyo wake na kumfanya yeye kuwa muelekevu kwao. Hivyo alikuwa ndio njia ya mawasiliano ya sera zao. Alibadilika kulingana na uelekeo wao. Wakati mwingine alitunga Hadith zikionyesha sifa na ubora wao, na wakati mwingine akibuni Hadith kuonyesha ubora wa wale makhalifa wawili, Abu Bakr na Umar kulingana na matakwa ya Mu’awiya na kundi lake la kidhalimu. Kwani walikuwa na malengo ya kisiasa dhidi ya Imam Ali na kizazi cha Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) ambayo yasingeweza kufikiwa kama walivyofikiria – isipokuwa kwa kuwafadhilisha makhalifa wale wawili. Hivyo alijitokeza kubuni Hadith ambazo tumetaja baadhi yake hapo kabla. Kuna Hadith nyingi sana ambazo hatukuzitaja, kwa mfano, ile Hadith kuhusu kumfanya Abu Bakr kuwa Amiri wa Hijja katika mwaka wa tisa hijiria, mwaka ambao ilishuka Sura al-Bara’a kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), na ile Hadith inayosema kwamba malaika walizungumza na Umar. Sera za Bani Umayyah za kuwatweza Bani Hashim zilihitajia kuthibitishwa na kuenezwa kwa Hadith hizi mbili kwa kiasi Mu’awiya na wasaidizi wake walivyoweza. Walifanya kwa kila njia waliyoweza mpaka vitabu vyote vya Hadith Sahih vya Sunni vikazisimulia kama Hadith sahihi. Abu Huraira wakati mwingine alizikatakata Hadith kuhusu Imam Ali ili kubadili maana zake, kama riwaya yake: “Nilimsikia Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akisema: Jua halikuwahi kuzuiwa au kurudishwa kwa ajili ya mtu yeyote isipokuwa Nabii Yusha’ bin Nuun alipokuwa anatembea kuelekea Jerusalemu wakati wa usiku.”61 61 al-Khatiib katika Ta’rikh Baghdad, Jz. 7, uk. 35, na Jz. 9, uk. 99 42


Abu huraira check Lubumba.qxd

7/1/2011

10:46 AM

Page 43

Abu Huraira Na Hadith yake hii: “Wakati aya ya Qur’ani: “Na uwaonye jamaa zako wa karibu” 26:214 ilipoteremshwa, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisimama na akasema: Enyi maquraishi…..” Abu Huraira ameikata Hadith hiyo na hakuelezea maelezo yote ili kuibadili kulingana na sera za Bani Umayyah zilivyotaka. Hatuna jingine ila kusema tu kwamba, hakuna uwezo isipokuwa kwa Mwenyezi Mungu! Na Hadith yake; “Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amesema: Warithi wangu hawatarithi kile ambacho nitakuwa nimekiacha nyuma yangu.” Na nyingine: “Mtume Muhammad (s.a.w.w.) alimwambia ammi yake Abu Talib: ‘Sema: hapana mungu isipokuwa Allah …….’ mpaka Mwenyezi Mungu akashusha wahyi kwa Mtume: “Kwa hakika wewe huwezi kumuongoza umpendaye …..” 28:56, na Hadith nyingi tu za kuzusha. Walikuwa wakimtweza Imam Ali (a.s.) na familia ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Imam Abu Ja’far al-Iskafi vile vile amesema:62 “Mu’awiya alikuwa amewalazimisha masahaba wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na baadhi ya warithi wa masahaba hao kusimulia Hadith kuhusu Imam Ali za kumkashifu na kumkana yeye. Aliwapa hao mahongo kwa kazi hiyo. Hivyo walibuni Hadith zilizomridhisha yeye. Miongoni mwao alikuwa ni Abu Huraira, Amr ibn al-Aass na al-Mughiira bin Shu’ba. Miongoni mwa tabi’in alikuwa ni Urwa bin az-Zubeir …..” Abu Ja’far al-Iskafi huyu huyu pia anasema:63 “Wakati Abu Huraira alipokwenda Iraqi pamoja na Mu’awiya katika mwaka wa ‘Jama’a’, alikwenda kwenye msikiti wa al-Kufa. Alipoona kwamba watu wengi walikuwa wamekuja kumlaki, alipiga magoti na akapiga kichwa chake kwa mkono wake mara nyingi tu na kusema: “Enyi watu wa Iraqi, mnaweza mkasema kwamba ninabuni Hadith juu ya Mwenyezi Mungu na 62 Sharh Nahj al-Balaghah al-Hamiid, Jz. 1, uk. 358. 63 Sharh Nahj al-Balaghah al-Hamiid, Jz. 1, uk. 359. 43


Abu huraira check Lubumba.qxd

7/1/2011

10:46 AM

Page 44

Abu Huraira Mtume Wake (s.a.w.w.) ili niwe katika moto wa Jahannam. Wallahi ninaapa kwamba nilimsikia Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akisema kwamba: “Kila Nabii ana mahali patakatifu. Patakatifu pangu mimi ni Madina. Yeyote anayefanya uharibifu hapo Madina atalaaniwa na Mwenyezi Mungu, malaika na watu wote.” Ninaapa Wallahi kwamba Ali amefanya uharibifu hapo Madina!” Mu’awiya alipomsikia akisema hivyo, yeye alimthibitisha, na akamzawadia yeye na kumfanya Gavana wa Madina.” 64 Wakati mwingine alitunga Hadith zinazowalinda wanafiki wa ki-Bani Umayyah, ambao Mwenyezi Mungu na Mtume Wake walikuwa wamewalaani ili kuilinda dini na umma kutokana na unafiki na uharibifu wao. Lakini Abu Huraira alijipendekeza kwa Marwan na Mu’awiya na wasaidizi wao kwa kusema: “Nilimsikia Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akisema: “Ewe Allah, Muhammad ni binadamu tu. Huwa anakasirika kama wanadamu wengine wote. Kila mu’min ambaye nimemdhuru, kumtukana au kumpiga viboko, Wewe unaweza kuyafanya hayo kuwa ni sababu ya kumsamehe na kumsogeza karibu Yako katika Siku ya Kiyama.” Marwan na wanawe walijaribu wawezavyo kuieneza Hadith hii kwa njia nyingi mpaka vitabu vya Hadith vya Sunni (Sihah, Sunan na Masanid) vikaisimulia kama Hadith sahihi. Jukumu la Marwan na wanawe la kumwinua Abu Huraira kufikia kiwango cha hali ya juu na kumfadhilisha 64 Sufyan ath-Thawri ameisimulia kutoka kwa Abdur-Rahman bin Qassim kutoka kwa Umar bin Abdul-Ghaffar kwamba wakati Abu Huraira alipofika Kufa pamoja na Mu’awiya, alikaa kwenye lango la Kinda wakati wa usiku na watu wakakaa kumzunguka yeye. Siku moja kijana mmoja wa Kufa – anaweza akawa ni al-Asbagh bin Nabata – alifika na akamwambia: “Oh, Abu Huraira, ninakuuliza, Wallahi kama ulimsikia Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akimwambia Imam Ali ibn Abi Talib: “Ewe Allah, muunge mkono yule atakayemuunga mkono Ali na uwe adui kwa yule anayempinga huyu.” Abu Huraira akasema: “Ndio, nilisikia.” Yule kijana akasema: “Wallahi naapa, kwamba wewe umewaunga mkono maadui zake na kuwapinga wafuasi wake.” Kisha kijana huyo akaondoka. 44


Abu huraira check Lubumba.qxd

7/1/2011

10:46 AM

Page 45

Abu Huraira yeye kuliko wengine wote katika kuhifadhi, uangalifu na uchaji, lilikuwa limepata nguvu ya athari hadi leo hii. Walikuwa wamefanya mambo mengi ya kuwakinaisha watu waamini kwamba Abu Huraira alikuwa wa kutegemewa na mchamungu. Jambo mojawapo ni kwamba Marwan alijifanya kwamba alikuwa amemkalisha karani wake katika sehemu ya faragha ambayo asingeweza kuonwa na mtu yoyote yule na akamwita Abu Huraira aingie hapo. Alianza kumuuliza Abu Huraira kuhusu mambo mengi. Alimuuliza maswali mengi sana. Abu Huraira alijibu kwa Hadith za Mtukufu Mtume na yule karani, ambaye jina lake lilikuwa Zu’ayza’a alikuwa akiandika bila kumfanya yeyote amtambue. Aliandika Hadith nyingi sana. Marwan akangojea kwa takriban mwaka mzima na kisha akamwita Abu Huraira na akamuuliza maswali yaleyale. Yeye alijibu kwa majibu yale yale, hakuzidisha wala kupunguza neno. Marwan na karani wake wakaueneza uongo huu miongoni mwa watu wa Damascus na kufikia kila mahali mpaka hatimaye alHakim akauandika kwenye kitabu chake, al-Mustadrak al-Hakiim, Jz. 3, uk. 510. Na kwamba wakati Marwan alipotaka kuwaleta mashujaa na wapiganaji wake ili kuwazuia Bani Hashim wasimzike Imam Hasan (a.s.) karibu na kaburi la babu yake, Mtume Muhammad (s.a.w.w.), walikubaliana kabla na Abu Huraira kwamba aje ampinge sana Marwan na kumlaumu sana mbele ya watu, ili kuwahadaa na kuwafanya watambue kwamba Abu Huraira alikuwa mtu mkweli sana. Kwamba hakumuogopa mtu yoyote isipokuwa Mwenyezi Mungu na Mtume Wake na kwamba hakuna yoyote ambaye angeweza kusimama dhidi yake pindi atakapokuwa amekasirika kwa ajili ya Mwenyezi Mungu na Mtume Wake. Pale Abu Huraira alipofanya upinzani huu, Marwan alionyesha hasira zake. Pakawa na mabishano ya uongo na ghadhabu bandia kati yao. Abu Huraira akapinga kwa nguvu sana dhidi ya Marwan kuthibitisha kwamba yeye Abu Huraira alikuwa na nafasi maalum kwa Mtukufu Mtume 45


Abu huraira check Lubumba.qxd

7/1/2011

10:46 AM

Page 46

Abu Huraira (s.a.w.w.) ambayo hakuna sahaba yoyote au jamaa wa Mtume aliyekuwa nayo kwamba alikuwa na uwezo wa kupokea na kuhifadhi kutoka kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), ambao kwa huo aliwazidi hata waislam wa mwanzo kama Umar, Uthman, Ali, Talha, Zubeir na wengineo. Aliendelea zaidi katika kuelezea mwelekeo wake, ambao uliweka juu yake hadhi za hali ya juu za wale masahaba wa karibu na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Hivyo mabishano kati yao yakaisha na Marwan akakubali kunywea kwenye nafasi kubwa ya Abu Huraira katika Uislam na hadhi yake ya ujuzi katika Sunna. Yote hayo yalitendeka mbele ya watu. Mpango wao ukafanikiwa na Marwan aliweza kumtumia Abu Huraira kama nyenzo ya kupigana na Imam Hasan, Imam Husein, baba yao na watoto wao (a.s.). Ilikuwa ni propaganda iliyofanikiwa sana kwa ajili ya sera zao.

“Basi adhabu itawathibitikia wanaoandika kitabu kwa mikono yao, kisha wakasema: Hiki kimetoka kwa Mwenyezi Mungu, ili wakiuze kwa thamani ndogo, basi adhabu kali kwa yale waliyoyaandika kwa mikono yao na ole wao kwa yake wanayoyachuma.” 2:79

WINGI WA HADITH ZAKE Wale wote waliokusanya Hadith wamekubaliana kwa kauli moja kwamba Abu Huraira amesimulia Hadith nyingi zaidi kuliko mtu mwingine yeyote yule.65 Walizihesabu riwaya zake na kuzikuta kwamba zilikuwa jumla ya riwaya elfu tano na mia tatu na sabini na nne. Katika Sahih al-Bukhari peke 65 Rejea kwenye mstari wa mwisho wa ukurasa wa 240 wa Juz. 4 ya kitabu alIsaba cha Ibn Hajar ambao umejuisha na kitabu cha al-Isti’ab katika pambizo zake. 46


Abu huraira check Lubumba.qxd

7/1/2011

10:46 AM

Page 47

Abu Huraira yake alikuwa na Hadith mia nne na arobaini na sita.66 Tumegundua kwamba yale yote yaliyosimuliwa na makhalifa wanne, yakilinganishwa na Hadith za Abu Huraira yalikuwa pungufu zaidi kwa asilimia ishirini na saba. Abu Bakr amesimulia Hadith mia moja na arobaini na mbili.67 Umar alikuwa amesimulia Hadith mia tano na thelathini na saba.68 Yote ambayo Uthman alikuwa ameyasimulia yalikuwa ni Hadith mia moja na arobaini na sita.69 Na Hadith mia tano na themanini na sita zilisimuliwa kutoka kwa Ali.70 Hivyo jumla ni Hadith 1411, ambazo ukizilinganisha na Hadith za Abu Huraira utauona uwiano uko kama tulivyosema hasa. 66 Rejea kwenye kitabu cha al-Qastalani, Irshad al-Sari, Jz. 1, uk. 212, maelezo ya Hadith ya kwanza ya Abu Huraira iliyoandikwa na al-Bukhari katika Sahih yake, utakuta kwamba Abu Huraira amesimulia kutoka kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) Hadith 5,374 na kwamba katika hiyo Sahihi al-Bukhari alikuwa na Hadith 446. Ibn Hazim katika al-Milal wan-Nihal, Jz. 4, uk. 138 amesema kwamba Abu Huraira amesimulia Hadith 5374. 67 Ilisimuliwa na Suyuti katika Ta’rikh al-Khulafa’ (historia ya makhalifa), na anNawawi katika Tadh’hiib, Ibn Hazim katika al-Milal wan-Nihal, Jz. 4, uk. 137 na adh-Dhahabi katika kitabu chake, Mizanul-Itidal, ambaya amesema kwamba Hadithi za kweli za Abu Bakr zilikuwa chini ya Hadith ishirini. 68 as-Suyuti amesema katika kitabu chake Ta’rikh al-Khulafa’ kwamba Hadith za Umar zilikuwa mia tano na thelathini na tisa. Ibn Hazim amesimulia katika kitabu chake al-Milal wan-Nihal, Jz. 4, uk. 138 idadi hiyo hiyo na akasema kwamba Hadith za kweli za Umar zilikuwa takriban Hadith hamsini. 69 Jalalud-Din as-Suyuti katika kitabu chake Ta’rikh al-Khulafa’. 70 as-Suyuti; Ta’rikh al-Khulafa’ (kwenye wasifu wa Imam Ali). Ibn Hazim ndani ya kitabu chake al-Milal wan-Nihal, Jz. 4, uk.

47


Abu huraira check Lubumba.qxd

7/1/2011

10:46 AM

Page 48

Abu Huraira Hebu mtu yoyote mwenye busara afikirie juu ya Abu Huraira, kipindi chake kifupi cha kuwa Mwislam, kutofahamika vizuri kwake, kutokuwa na elimu kwake na yote yanayoweza kumfanya awe duni, halafu fikiria juu ya makhalifa wanne, haki yao ya utangulizi katika Uislam, mahudhurio yao wakati wa utungaji wa kanuni za Shariah, ujasiri wao kwa miaka hamsini na mbili; katika miaka ishirini na tatu kati ya hiyo wao walikuwa kwenye utumishi wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na ishirini na tisa yake walitawala umma na wakatawala nchi zingine. Waliziteka nchi za Kasra na Kaizari (Ceaser). Walijenga miji na nchi kadhaa, wakaeneza Uislam na wakatangaza hukumu za Shariah na Sunna. Sasa itawezekana vipi kwa Abu Huraira peke yake, kusimulia mara nyingi, kwa kiasi kama walivyosimulia juu ya Hadith za Mtukufu Mtume (s.a.w.w.)? Vile vile Abu Huraira hakuwa kama A’isha, ingawa naye amesimulia Hadith nyingi sana. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alikuwa amemuoa miaka kumi kabla Abu Huraira kuja kuwa Mwislam.71Yeye A’isha alikuwa katika nyumba ambayo ufunuo wa Mwenyezi Mungu ulikuwa ukishuka kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na mahali pa kuja na kuondoka pa Jibril na Mikaili (a.s.) kwa miaka kumi na nne. Yeye alifariki muda mfupi kabla ya kifo cha Abu Huraira.72 Ni tofauti kubwa kiasi gani iliyokuwepo kati ya usahaba huo wa watu wawili hawa na upeo wao! Upeo wake A’isha ulishindana na usikiaji wake na moyo wake ulizidi masikio yake. Alikuwa madhubuti sana. Hakuna 71 Ibn Abdil-Birr amesema katika kitabu chake, al-Isti’aab, kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alimuoa A’isha katika mwaka wa kumi wa utume – miaka mitatu kabla ya kuhajiri – hivyo ndoa ya A’isha ilikuwa ilikuwa kabla Abu Huraira kuwa Muislam katika mwaka wa saba wa hijiria. 72 A’isha alifariki katika mwaka wa hamsini na saba hijiria kabla ya kifo cha Abu Huraira katika muda mfupi baadae. Abu Huraira alimswalia A’isha swala ya maiti – kwa amri ya al-Waliid bin Utba bin Abu Sufyan, ambaye alikuwa amefanywa amiir wa Madina na ammi yake Mu’awiya. Alitaka kumuenzi Abu Huraira kwa vile A’isha alizikwa ndani ya Baqii’. 48


Abu huraira check Lubumba.qxd

7/1/2011

10:46 AM

Page 49

Abu Huraira lolote lililomtokea isipokuwa alilitungia shairi kulihusu. Urwa amesema kwamba hakuwahi kuona mtu yeyote mwenye elimu katika fiqhi, madawa au ushairi kuliko A’isha. Masruuq amesema kwamba amewaona baadhi ya masahaba maarufu wakimuuliza A’isha juu ya wajibati za kidini. Alilazimishwa kueneza riwaya zake kiasi kwamba aliwatuma wapiga mbiu wake kwenye nchi mbalimbali na aliongoza lile jeshi kubwa kwenda Basra. Na licha ya yote hayo, Hadith zake zilikuwa elfu mbili mia mbili na kumi.73 Hivyo Hadith zake zilikuwa chache kwa zaidi ya nusu ya zile za Abu Huraira. Kama ukijumlisha Hadith za A’isha na zile za Umm Salama (mke wa Mtukufu Mtume), ambaye alifariki baada ya kifo cha Abu Huraira kwa kupita muda mrefu, za wakeze wengine Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), za Imam Hasan, Imam Husein, Bibi Fatimah (binti ya Mtukufu Mtume) na zile za Makhalifa wanne unakuta kwamba zote kwa pamoja zilikuwa pungufu ya Hadith za Abu Huraira. Hili lilikuwa ni jambo la hatari sana! Hebu ngoja wale wenye busara walifikirie hili. Licha ya hayo, Abu Huraira alisingizia kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alimfahamisha yeye peke yake juu ya Hadith kadhaa ambazo hatazifichua kwa mtu yeyote yule. Aliziweka na kuzihifadhi ndani ya dhamira yake na kuzizika ndani ya kifua chake. Na kama unavyojua kwamba Abu Huraira alikuwa na kifua chenye ngome nzito kabisa na dhamiri ya ajabu! Hivyo yeye alisema: “Mimi nimehifadhi kutoka kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) vyombo viwili. Ninaeneza kile cha kwanza, lakini kama nitaeneza hicho kingine, koo hili linaweza kukatwa.”74 Yeye alisema: “Kama ningewaambia yale yote ninayoyajua, watu wangenirushia mabaki ya vyombo vya udongo na kusema: Abu Huraira ni mwendawazimu.” 73 Ibn Hazim katika kitabu chake, al-Milal wan-Nihal, Jz. 4, uk. 138 74 Sahih al-Bukhari, Jz. 1, uk. 24 49


Abu huraira check Lubumba.qxd

7/1/2011

10:46 AM

Page 50

Abu Huraira Alisema: “Kama ningewaambia yote niliyokuwa nayo kifuani mwangu, mngenitupia kinyesi.” Alisema: “Wanasema kwamba Abu Huraira amesimulia Hadith nyingi sana. Ninaapa Wallahi kwamba kama ningewaambia yote yale niliyoyasikia, basi mngenirushia kilima cha kinyesi na kamwe hamngezungumza nami tena.”75 Alisema: “Nimehifadhi kutoka kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) baadhi ya Hadith ambazo mimi sikuzisimulia juu yake kwenu. Kama ningekusimulieni juu yake hizo, basi mngenirushia mawe.”76 Yeye alisema: “Mimi nimehifadhi kutoka kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) mifuko mitano ya Hadith. Nimesimulia juu ya miwili kati yao, na kama ningesimulia juu ya wa tatu ninyi mngenirushia mawe.”77 Abu Huraira hakuwa mrithi mstahiki wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) wala khalifa baada yake kiasi cha kumpendelea kuliko wengine na kumwambia siri na elimu ambazo hakuweza kumwambia mwingine yeyote kati ya masahaba zake wa karibu au ndugu zake. Kulikuwa na maana gani ya kumweleza siri hizo wakati ambapo yeye alikuwa ni mtu dhaifu mwenye uchoyo ambao ulimzuia yeye kusema chochote kuhusu siri hizo isipokuwa kwamba angerushiwa mawe, kinyesi na takataka au kwamba koo lake lingekatwa? 75 Hadith tatu zilizopita zilisimuliwa na Ibn Sa’d katika kitabu chake Tabaqat, Jz. 4, uk. 57. 76 al-Hakim katika al-Mustadrak, Jz. 3, uk. 509, adh-Dhahabi katika Talkhiis. Ni hadhi kubwa kiasi gani aliyokuwa nayo Abu Huraira! Alisema: ….. mngenirushia mawe, mapande ya vyombo vya udongo, kilima cha kinyesi. Na aliposema kuhusu yeye mwenyewe ………. waliokuwa wanakuja waliweka nyayo zao juu ya shingo yangu ………. na alipozungumzia tumbo lake, chawa na mambo yake mengine. 77 Abu Nua’im katika Hilyatul-Awliya’ uk. 381 (wasifu wa Abu Huraira). 50


Abu huraira check Lubumba.qxd

7/1/2011

10:46 AM

Page 51

Abu Huraira Hivi isingekuwa bora kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kuelezea siri hizi kwa ajili ya wale makhalifa wa baada yake, ambao waliwaongoza watu kwa nia moja na ambao mataifa yaliwakubali na shingo za waarabu na wasiokuwa waarabu zilinywea na kutii? Wao walikuwa ni wabora kuliko Abu Huraira katika kufanya hivyo. Kama wao wangekuwa nazo siri hizo, wangezieneza kwenye nchi zote kama miali ya jua. Liepushiliwe mbali la Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kuweza kufanya jambo lisilo na faida. Hivi yeye angeweza kumwaminisha Abu Huraira siri zake ili zipotee vivi hivi bila faida yoyote? Na kwani Abu Huraira alikuwa ni nani kuweza kuteuliwa pekee kutokana na Waislam wote wa mwanzo? “Waliotangulia ndio waliotangulia, hao ndio watakaokaribishwa.” (56:10-11) Abu Huraira mara kwa mara alikuwa akisema: “Abu Huraira huwa haweki siri wala huwa haandiki.”78 Hadithi hii ilikuwa inakubalianaje na Hadith yake hii: “Nimehifadhi kutoka kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) vyombo viwili. Nimeeneza kimojawapo. Kama ningeeneza hicho kingine, koo hili lingekatwa,” na zile riwaya nyingine zenye maana hiyo hiyo kwamba alitunza siri? Hebu tuwaulize wale wanaofanya utafiti juu ya zile siri ambazo Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) aliziaminisha kwa Abu Huraira na kwamba Abu Huraira alifanya siri kujilinda yeye mwenyewe au kuweka hadhi yake. Je, siri hizo zilikuwa za namna ya siri ambazo Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) aliziaminisha kwa mlinzi wake Imam Ali (a.s.)? Je, zilihusu ukhalifa na makhalifa baada yake? Je, zilikuwa za namna nyingine? Kama zilikuwa za namna ile ya kwanza, kwa nini Abu Huraira azigeuke na kupingana nazo moja kwa moja? Maoni yake yangekuwa sawa na maoni ya Waislam wengine kwani yeye alikuwa ni mtu mmoja miongoni mwa wengine. Lakini kama siri hizo zilikuwa za namna nyingine, yeye asingeweza kujizuia kusimulia Hadithi 78 Ibn Sa’d katika Tabaqat, Jz. 2, uk. 119 51


Abu huraira check Lubumba.qxd

7/1/2011

10:46 AM

Page 52

Abu Huraira za kuchukiza na kufedhehesha! Je yeye hakusimulia kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alipitiwa na usingizi na akakosa swala ya al-Fajr? Na kwamba Shetani alimjia yeye Mtume na kuvuruga swala zake? Je, hakusimulia kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) wakati mmoja alisahau na akaswali swala ya rakaa mbili badala ya rakaa nne na wakati walipomuuliza watu: Je, ulisahau au umeiwekea swala hii masharti? Yeye alijibu: Sikusahau wala sikuweka shuruti. Hakusimulia kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alidhuru, kutukana, kulaani na kuwachapa viboko watu wasio na hatia kwa sababu tu alipandwa na hasira? Je, hakuhusisha kwa mitume (s.a.) mambo chungu nzima ambayo yalikuwa hayawezekani kwa wao kuyafanya kwa mujibu wa sheria au busara? Alisimulia kwamba Mtukufu Mtume Muhammad (s.a.w.w.) alisema: “Sisi ni wabora kuliko Ibrahim kuweza kuwa na shaka.” Alisimulia vilevile kwamba imani juu ya Allah ya Nabii Lut ilikuwa haina uhakika. Hakuwakashifu manabii Adam, Nuh, Ibrahim, Musa na Isa ambao ni lazima waheshimiwe na kuenziwa? Je, hakuhusisha kwa Nabii Musa kwamba alimpiga malaika wa mauti na kumng’oa jicho lake? Na kwamba wakati mmoja nabii Musa (a.s.) alikimbia akiwa uchi mbele ya Bani Israili, ambao walimuona sehemu zake za siri? Je, hakusimulia kwamba Nabii Suleiman, mwana wa Daudi alivunja amri ya baba yake? Na kwamba alikataa kusema Insha’allah, hivyo amali yake ikaanguka? Je, hakuhusisha kwa Mwenyezi Mungu mambo ambayo yasingeweza kukubaliwa na Sharia ama mantiki? Alisema kwamba Jahannam haitajaa mpaka Mwenyezi Mungu atakapoweka mguu wake ndani yake. Katika riwaya yake juu ya Siku ya Kiyama, yeye alisema kwamba Mwenyezi Mungu atawajia watu kwa sura tofauti na ile wanayoifahamu akiwaambia: 52


Abu huraira check Lubumba.qxd

7/1/2011

10:46 AM

Page 53

Abu Huraira “Mimi ni Mola wenu.” Wao watasema: “Mwenyezi Mungu aepushilie mbali!” Kisha anawajia kwa sura ile wanayoitambua! Wao watasema: “Wewe ni mungu wetu.” Abu Huraira amesema kwamba Adam aliumbwa kwa umbo la Mhisani Wake (Allah)! Na kwamba Mwenyezi Mungu amemuumba Adam kwa umbo kama Lake. Alikuwa na urefu wa dhiraa sitini na upana wa dhiraa saba. Utayaona mengi mengi ya maajabu yake kwenye mlango ufuatao ambayo yanasababisha kukatwa kwa koo, hivyo kwa nini amezisimulia kirahisi hivyo? Kwa kweli amesimulia riwaya hizo kana kwamba amewafanyia watu upendeleo fulani. Amesimulia itikadi za kidhana lakini hakuna mtu aliyemrushia jiwe, kinyesi au taka kwani ilikuwa wazi kwa yeyote aliyemfahamu. Tunateswa na watu madhalimu na tunakuwa hatuna wa kumkimbilia isipokuwa Mwenyezi Mungu Tungependa kuvuta usikivu wa wale watafiti wenye busara kwamba Abu Huraira amesema:79 “Hakuna aliyesimulia Hadith kutoka kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) zaidi kuliko nilivyosimulia mimi, isipokuwa Abdullah ibn Amr bin al-Aas kwa sababu yeye aliziandika na mimi sikuandika.” Alikiri kwamba Abdulla bin Amr alisimulia Hadith nyingi zaidi kuliko yeye alivyosimulia. Tulifanya utafiti juu ya riwaya za Abdullah na kugundua kwamba hazikuwa zaidi ya mia saba.80 Kwa hiyo zilikuwa chini ya moja ya saba ukizilinganisha na riwaya za Abu Huraira. Watafiti hao walichanganyikiwa sana jinsi ya kumtetea Abu Huraira katika kukinzana kwake. Lakini Ibn Hajar al-Qastalani na sheikh Zakariya al79 Riwaya iliyosimuliwa na Wahab bin Munabbih kutoka kwa ndugu yake Humam kutoka kwa Abu Huaraira na kutajwa katika Sahih al-Bukhari, Jz. 1, uk. 22 80 al-Qastalani katika kitabu Irshad as-Sari fii Sharh Sahih al-Bukhari, Jz.1, uk. 373 53


Abu huraira check Lubumba.qxd

7/1/2011

10:46 AM

Page 54

Abu Huraira Ansari wao walipata kisingizio wakati walipoielezea Hadith hii katika vitabu vyao81 kwamba Abdullah bin Amr bin al-Aas aliishi nchini Misri, na wale waliokwenda Misri walikuwa wachache sana kwa hiyo alisimulia chache tu ya Hadith zake, wakati ambapo Abu Huraira aliishi Madina ambapo palikuwa ndio mafikio ya Waislamu kutoka kila mahali, hivyo riwaya zake yeye zilikuwa nyingi mno. Simulizi ya Abu Huraira ilikuwa wazi sana kuvunja kisingizio hiki. Yeye alikubali kwamba hakuna aliyesimulia Hadith nyingi kutoka kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kuliko alizosimulia isipokuwa Abdullah bin Amr bin alAas. Mtu huyu, mwenyewe, alikiri kwamba riwaya za Abdullah zilikuwa ni nyingi kuliko za kwake yeye, hivyo hapakuwa na njia kwa kisingizio hiki cha wasimulizi hawa wawili. Nafasi kubwa na heshima aliyokuwa nayo Abdullah bin Amr huko Misri vilikuwa ni sababu nzuri za kumfanya yeye asimulie Hadith zake nyingi. Hakukuwa na mtu mwingine zaidi yake yeye huko Misri ambaye watu walimjua sana, isipokuwa baadhi ya masahaba wachache sana au wasafiri. Kwani alikuwa ndiye bingwa pekee katika Qur’ani, Shari’ah na Sunna ambaye watu walimkimbilia. Ni tofauti kubwa kiasi gani kati ya nafasi yake huko Misri na ile ya Abu Huraira hapo Madina! Kwani Abdullah alikuwa na cheo cha Faqihi mnyofu na sifa ya mtoto wa mshindi mkuu katika nyoyo za wamisri, ambapo Abu Huraira huko Madina alikuwa ni mmojawapo tu wa maelfu ya masahaba wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Wajumbe waliotembelea Madina walikwenda kwa wale masahaba mashuhuri na maarufu, ambao Abu Huraira alikuwa sio mmoja wao. Na vilevile alishutumiwa kwa kusimulia Hadith nyingi mno kupindukia kutoka kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Watu wa Madina mara nyingi walimlaumu kwa kusema: “Kwa nini muhajirun na Ansari hawakusimulia Hadith nyingi kama zake.” 81 al-Qastalani katika kitabu Irshad as-Sari na Zakariya katika Tuhfatul-Bari. Vilichapishwa kwa pamoja katika Juzuu kumi na mbili. Utakikuta kisingizio hiki katika Juzuu ya 1, uk. 373 54


Abu huraira check Lubumba.qxd

7/1/2011

10:46 AM

Page 55

Abu Huraira Nafasi yake hapo Madina isingeweza kumfanya asimulie Hadith nyingi hivyo. Ilikuwa haiaminiki kwamba riwaya zake ni nyingi kuliko riwaya za Abdullah, hasa baada ya kukiri kwake kwamba riwaya za Abdullah zilikuwa ni nyingi kuliko riwaya zake. Kwa nyongeza ni kwamba Abdullah bin Amr aliishi muda mrefu kiasi baada ya kifo cha Abu Huraira.82 Kwa kweli Abu Huraira alikiri juu ya hilo mwanzoni baada ya kifo cha Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) ambapo alikuwa hajazidi katika kusimulia Hadith. Alizidi kusimulia zaidi wakati wa utawala wa Mu’awiya ambapo hapakuwa na Abu Bakr, Umar Ali wala yeyote kati ya masahaba mashuhuri ambao Abu Huraira aliwaogopa.

UBORA WA HADITH ZAKE Hekima ya umaizi mzuri haikubali nyingi ya mtindo wa Hadith za Abu Huraira, na kigezo cha kisayansi na akili hakitoi ruhusa juu ya kuzikubali Hadith hizo. Hapa ni Hadith zake arobaini zikiwekwa mbele yako. Hebu tafakari juu ya hizo pamoja na ufafanuzi wetu kwa hekima na busara na kwa uadilifu bila upendeleo, na kisha unaweza kutoa maoni yako. 1. Allah alimuumba Adam kwa Sura Yake Mwenyewe: Masheikh wawili, al-Bukhari na Muslim83 wametaja riwaya iliyosimuliwa na Abdur-Razaq kutoka kwa Ma’mar kutoka kwa Humam bin Munabbih kwamba Abu Huraira alisema: “Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amesema: 82 Abu Huraira alifariki, kama ilivyoelezwa ndani ya al-Isaba ya Ibn Hajar, mnamo mwaka wa hamsini na saba au hamsini na nane hijiria na pia imesemekana kwamba ni mwaka wa hamsini na tisa. Abdullah yeye alifariki kwa mujibu wa chanzo hicho hicho, mnamo mwaka wa sitini na tano, au sitini na nane au wa sitini na tisa hijiria. Al-Qaysarani amesema katika kitabu chake Rijal-as-Sahihayn kwamba yeye alifariki mwaka wa tisini na mbili. Allah ndiye ajuaye zaidi. 83 Rejea Sahih al-Bukhari, Jz.4, uk. 57, Sahih Muslim, Jz. 2, uk. 481 na Musnad Ahmad, Jz.2, uk. 315. 55


Abu huraira check Lubumba.qxd

7/1/2011

10:46 AM

Page 56

Abu Huraira “Mwenyezi Mungu alimuumba Adam kama sura Yake Mwenyewe katika urefu wa dhiraa sitini.” Ahmad ameongeza84 katika njia nyingine kutoka kwa Sa’id bin al-Musayyab kwamba Abu Huraira alisema: “….. na upana wa dhiraa saba. Wakati Mwenyezi Mungu alipomaliza kumuumba, alimwambia: Nenda ukawasalimie wale Malaika waliokaa pale na usikie watakavyokusalimia. Itakuwa ni salam yako na ya kizazi chako. Adam alikwenda na akawaambia: As-salaam Alaykum (amani iwe juu yenu). Wao wakasema: As-Salaamu alayk wa rahmatullah. Wao waliongeza – wa rahmatullah – na rehma ya Allah. Kila mmoja aliyeingia Peponi alikuwa kama Adam katika dhiraa sitini urefu. Wanadamu wakaanza kukua kwa upungufu hadi siku hizi.” Hii isingeweza kamwe kuhusishwa na Nabii Muhammad (s.a.w.w.) au yeyote kati ya manabii wengine wala kwa walinzi wao. Huenda Abu Huraira alijifunza hilo kutoka kwa Wayahudi kupitia rafiki yake Ka’bul-Ahbar au mwingine yoyote. Muktadha wa Hadith hii ni sawasawa kabisa na kifungu cha ishirini na saba cha Maandiko ya Waebrania (wayahudi) – Agano la Kale. Haya hapa ni maandishi yenyewe kama yalivyo: “Mungu alimuumba mwanadamu kwa umbo Lake Mwenyewe. Kama umbo la Mungu alimuumba. Mwanaume na mwanamke aliwaumba.” Ametukuka Mwenyezi Mungu zaidi ya kuweza kumwelezea Yeye kwa kufikiria, kumwekea mipaka na kumfananisha. Mwenyezi Mungu atukuzwe na wamepotea wale waliomhusisha na hayo. Wanaweza wakaitafsiri Hadithi hiyo kwa kuhusisha kiwakilishi nomini hicho ‘umbo lake’ kwa Adam mwenyewe sio kwa Mwenyezi Mungu. Kisha maana ingekuwa kwamba Mwenyezi Mungu alimuumba Adam huko Peponi katika umbo lilelile aliloshuka nalo duniani. Kwamba Mwenyezi Mungu alimkamilisha kwa wakati mmoja na akamfanya mwenye dhiraa sitini urefu na dhiraa saba upana, umbo lilelile ambalo kizazi chake kililiona, na hakubadilika kutoka hatua moja kwenda nyingine. Adam hakuwa ni mbegu na kisha akawa bonge la damu halafu pande la nyama, na kisha mifupa iliy84 Irshad as-Sari, Jz. 7, uk. 90. 56


Abu huraira check Lubumba.qxd

7/1/2011

10:46 AM

Page 57

Abu Huraira ofunikwa na nyama, kisha kijusi, halafu kichanga kinachonyonya kisha mtoto aliyeachishwa ziwa na kisha kijana halafu hatimae mtu mzima mwenye urefu na upana wa kawaida. Hili ndilo ambalo wanaloweza kusema wale wanaomtukuza Mwenyezi Mungu na kukana kumhusisha na mwili katika kuitafsiri Hadith hii. Lakini ilisimuliwa na Abu Huraira kwa maneno haya: “Adam aliumbwa kwa kulingana na umbo la Mhisani (Allah).”85 Abu Huraira alikuwa na Hadith nyingine inayosema: “Nabii Musa (a.s.) alipiga jiwe kwa fimbo yake kwa ajili ya wana wa Israili na maji yakabubujika. Akawaambia: ‘Kunyweni maji enyi punda.’Ndipo Mwenyezi Mungu akamfunilia: ‘Unakusudia kuwafananisha binadamu niliowaumba kulingana na umbo Langu kuwa sawa na punda.” 86 Hili liliwatahayarisha wale wanaomtetea Abu Huraira na kuwafanya washindwe kwenye kiwakilishi nomino hiki wakitafuta tafsiri ya namna nyingine. Waliitafsiri Hadith ya Abu Huraira: “Mwenyezi Mungu alimuumba Adam kulingana na umbo Lake” na “Adam alikuwa ameumbwa kulingana na umbo la Mwingi wa rehema,” na katika Hadith yake kuhusu Nabii Musa (a.s.): “Nimewaumba kulingana na umbo Langu” kwamba Mwenyezi Mungu alimuumba Adam na kizazi chake kulingana na sifa za Mwenyezi Mungu. Mwenyezi Mungu yu hai, Mwenye kusikia, kuona, Muongeaji, Mtambuzi, Mwenye kupenda na kuchukia. Hivyo Yeye amezitoa sifa hizi kwa Adam na kizazi chake. 85 Al-Qastalani ameisimulia Hadith hii katika kitabu chake, Irshad as-Sari, Jz. 10, uk. 491 na akasema kwamba kiwakilishi nomino ‘yake’ katika Hadith ya Abu Huraira (Mwenyezi Mungu alimuumba Adam kulingana na umbo Lake …..) kiliashiria kwa Mwenyezi Mungu na sio kwa Adam. 86 Ibn Qutayba ameisimulia riwaya hii katika kitabu chake (Tafsiri ya Hadith mbalimbali) uk. 280, na akaifanya kama ushahidi kwamba kiwakilishi nomino ‘yake’ katika Hadith ya Abu Huraira: “Mwenyezi Mungu alimuumba Adam kulingana na umbo Lake” imeashiria kwa Mwenyezi Mungu na sio kwa Adam. 57


Abu huraira check Lubumba.qxd

7/1/2011

10:46 AM

Page 58

Abu Huraira Waliangukia kwenye kile walichokikimbia, kwa sababu sifa za Mwenyezi Mungu ziko mbali sana na ufananishwaji. Hili linakubalika kwa kauli moja miongoni mwa wale ambao wanaamini juu ya uvukaji mipaka wa Mwenyezi Mungu. Hususan pale tunaposema kwamba sifa Zake ni Yeye Mwenyewe na kwamba Yeye ndio Kweli kama ilivyowekwa katika kanuni zetu za fiqhi. Abu Huraira alikithiri katika Hadithi hii. Wakati mwingine aliisimulia kama ilivyo hapo juu na wakati mwingine alisema: “Kama mmoja wenu atagombana na mwenzie mwingine, basi naauepuke uso kwa sababu Mwenyezi Mungu alimuumba Adam kulingana na umbo Lake.”87 Wakati mwingine alisema: “Kama mmoja wenu atampiga mwenzie, basi aepuke kupiga uso na asiseme: “Mwenyezi Mungu auharibu uso wako na uso wa yoyote anayefanana na wewe, kwa sababu Mwenyezi Mungu alimuumba Adam kulingana na umbo Lake.”88 Ni dhahiri kwamba aliifunga njia mbele ya watetezi wake kurejea kwenye yoyote kati ya tafsiri mbili hizo. Kiwakilishi nomino ‘lake’ katika “….. kulingana na umbo lake” kisingeweza kurejea kwa Adam katika yoyote kati ya Hadith mbili hizo, bali ni lazima kirejee kwa Mwenyezi Mungu ili kusahihisha maana ya Hadith hizo. Mtu anaweza akahalalisha ukatazaji wa kupiga au kuharibu uso.89 Kumuumba Adam kiumbe hai, anayesikia, 87 Sahih Muslim, Jz. 2, uk. 397 88 Imesimuliwa na al-Bukhari katika al-Adab al-Mufrad na katika Musnad Ahmad, Jz. 2. uk. 434 89 Natamani Abu Huraira angehalalisha kukataza kupiba uso kwa ajili ya unyeti na uzuri wake na kwamba una viungo muhimu; masikio macho, pua, kinywa, midomo, meno, nyusi, uliojitokeza na mengineyo, kwa sababu ufahamu mwingi ni kwa hivyo. Kupiga uso kunaweza kuvidhuru viungo hivyo na kuviacha vimedorora au kubadili hali ya uso na hiyo itakuwa sura mbaya kwa sababu uso ni wa dhahiri na hauwezi kufunikwa. Lakini Abu Huraira alipendelea kupotosha ukweli hata kama wafuasi wake walijua au laa. Hatuna wa kumkimbilia isipokuwa Mwenyezi Mungu tu! 58


Abu huraira check Lubumba.qxd

7/1/2011

10:46 AM

Page 59

Abu Huraira anayeona, anayeongea, anayetambua mwenye kuhiari na kutohiari hakufanyi kuwa ni lazima kuuhifadhi uso kuliko viungo vingine. Kutafsiri Hadith zote mbili kwa mujibu wa yoyote kati ya tafsiri hizi kulikuwa batili. Kwa kweli Hadith hizi mbili zilikuwa hazina maana, isipokuwa zilimaanisha uso wa mwanadamu kwani ulifanana na uso wa Mwenyezi Mungu. Utukufu ni Wake Mwenyezi Mungu, Aliye juu, Mwenye enzi! Hivyo watafiti wa Sunni ambao waliamini juu ya kupinduka mipaka kwa Mwenyezi Mungu walichanganyikiwa kuhusu maana ya Hadith hizi na wakakimbilia kwa Mwenyezi Mungu, Aliye Mtambuzi zaidi.90 Maelezo: Kwanza: Kama Adam alikuwa na urefu wa dhiraa sitini, hivyo angekuwa, kwa mujibu wa mlingano wa viungo vyake, na upana wa dhiraa kumi na saba. Kama upana wake ulikuwa dhiraa saba, urefu wake lazima uwe dhiraa ishirini na nne na nusu, kwa sababu upana wa binadamu wa kawaida ni sawa na mbili ya saba ya urefu wake. Kwa nini Abu Huraira aseme kwamba Adam alikuwa na urefu wa dhiraa sitini na upana wa dhiraa saba? Je, Adam alikuwa na umbile lisilolingana na umbo lisilo na sura kamili? Kwa hakika hivyo sivyo! Mwenyezi Mungu amesema: 90 Imam an-Nawawi amesem: Baadhi ya mafaqihi walijiepusha kutokana na kutafsiri Hadith zote hizi na wakasema: Tunaamini kwamba zilikuwa za kweli na maana yake ya neno kwa neno haikukusudiwa. Zinaweza kuwa na maana inayofaa. Yeye alisema: Haya yalikuwa ni maoni ya watangulizi wa Sunni, ambayo yalikuwa ya tahadhari zaidi na salama zaidi ….. Rejea Sharh Sahih Muslim, ambayo imechapwa katika pambizo za Sharh Sahih al-Bukhari, Jz. 12, uk.18. AlQastalani amesimulia kitu kama hicho katika kitabu chake, al-Irshad as-Sari, Jz. 10, uk. 491, kisha akasema: ….. na hii ni salama zaidi. Hii inaonyesha kwamba wao waliamini kwamba Hadith hizi zilikuwa ni sahihi na za kweli. Mwenyezi Mungu aepushilie mbali! “….. na bila shaka nyumba iliyo mbovu zaidi ni nyumba ya buibui, laiti wangejua.” 29:41

59


Abu huraira check Lubumba.qxd

7/1/2011

10:46 AM

Page 60

Abu Huraira

“Hakika tumemuumba mwanadamu katika umbile lililo bora kabisa” (95:4) Pili: Maamkuzi ya Kiislam yalitungwa ulipofika Uislam. Nabii Muhammad (s.a.w.w.) amesema: “Wayahudi hawakukuoneeni wivu katika jambo lolote kwa kiasi kikubwa kama walivyokuoneeni wivu juu ya maamkizi yenu (salamu).”91 Kama salaam hizo hazikuhusu umma huu tu, Wayahudi wasingeuonea wivu. Ni vipi Abu Huraira amesema: “Wakati Mwenyezi Mungu alipokuwa amemuumba Adam, alimwambia: Nenda ukawasalimie wale Malaika na usikilize watakavyokusalimia, kwa sababu ni salamu zako wewe na kizazi chako.” Ni nini watakachokisema watafiti wenye busara kuhusu Hadith hii? Na watasema nini kuhusu Hadith yake kwamba watu walianza kupungua katika ukuaji katika kimo kuanzia hapo hadi leo hii? 2. Kumuona Mwenyezi Mungu Siku ya Kiyama katika maumbile (sura) mbalimbali: Wale masheikh wawili; Bukhari na Muslim, wametaja kwamba Abu Huraira alisema kwamba: “Watu fulani waliuliza: “Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, je tutaweza kumuona Mola Wetu Siku ya Kiyama?” Yeye akasema: “Je, mnaweza kukosa uwezo wa kuliona jua wakati hakuna mawingu?” Wao wakajibu: “Hapana, ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu.” Mtume (s.a.w.w.) akasema: “Je, mtashindwa kuuona mwezi kamili wakati pakiwa hakuna mawingu?” Wao wakasema: “Hapana, ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu.” Yeye Mtume (s.a.w.w.) akasema: “Basi mtamuona Mwenyezi Mungu kama hivyo katika Siku ya Kiyama. Mwenyezi Mungu atawakusanya watu na kusema: “Yeyote aliyeabudu kitu kingine basi naakifuate.” Kisha walioabudu jua watalifuata hilo jua, yey91 Rejea kitabu cha al-Qastalani, Irshad as-Sari, Jz. 10, uk. 492. 60


Abu huraira check Lubumba.qxd

7/1/2011

10:46 AM

Page 61

Abu Huraira ote aliyeabudu mwezi, huyo ataufuata mwezi na aliyewaabudu madhalimu naye atawafuata hao madhalimu. Umma huu utabakia na wanafiki wake. Mwenyezi Mungu atawajia na umbile tofauti na lile walilolijua na kusema: “Mimi ndimi Mola Wenu.” Wao watasema: “Mungu aepushilie mbali! hatutaondoka hapa mpaka Mola wetu atakapotujia. Kama atafika hapa sisi tutamtambua.” Kisha Mwenyezi Mungu atawajia katika sura na umbile wanalolijua na kusema: “Mimi ni Mola wenu.” Wao watasema: “Ndio, Wewe ndiwe Mola wetu.” Na watamfuata Yeye. Kisha ataumba daraja la Jahannam. Mimi ndiye wa kwanza kulivuka. Mitume wengine wataomba: “Ewe Mola Wetu, tuokoe, tuokoe!” Daraja hilo lina vigoe (ndoano) kama miba ya sa’dan.92 “Je, mmeiona Sa’dan?” Wakasema: “Ndio tumeiona.” Vigoe hivyo viko kama miba ya sa’dan, bali hakuna yeyote anayejua umashuhuri wake vigoe hivyo ukiacha Mwenyezi Mungu peke Yake. Vinawanyakua watu kulingana na matendo yao. Baadhi yao wataangamizwa, na baadhi wataangushwa kisha wataokolewa. Mwenyezi Mungu atakapomaliza kuhukumu miongoni mwa watu Wake na akataka kumwokoa yeyote amtakaye kati yao kutokana na Jahannam, yule aliyeshuhudia kwamba hapana mola isipokuwa Mwenyezi Mungu, atawaamuru malaika kuwatoa ndani ya Moto wa Jahannam. Watajulikana kwa alama zao za kusujudu (ndani ya swala). Mwenyezi Mungu utauharamisha moto wa Jahannam kuchoma zile alama zao za sajida za mwanadamu. Malaika watawatoa nje ya Jahannam na hali wameungua. Maji yanayoitwa maji ya uzima yatamwagwa juu yao nao watakua kama mbegu iliyoko kwenye ardhi yenye mbolea na rutuba. Kuna mtu atakayeuelekea Moto wa Jahannam na kusema: “Ewe Mola Wangu, upepo wa Moto umeniumiza na miale yake imenichoma. Ugeuzie uso wangu mbali na Jahannam.” Ataendelea kumuomba Mwenyezi Mungu mpaka Mwenyezi Mungu atasema: “Kama nikifanya hivyo, wewe utaniomba kitu kingine tena.” Yeye 92 Aina ya mbaruti unaopatikana huko Uarabuni. 61


Abu huraira check Lubumba.qxd

7/1/2011

10:46 AM

Page 62

Abu Huraira atasema: “Ninaapa kwa utukufu Wako kwamba mimi sitakuomba kitu kingine tena.” Mwenyezi Mungu ataugeuza uso wake mbali na Jahannam. Kisha atasema: “Ewe Mola Wangu, nielekeze kwenda Peponi.” Mwenyezi Mungu atasema: “Hukusema wewe kwamba hutaniomba kitu kingine tena? Ole wako, ewe mwanadamu! Wewe ni mlaghai kiasi gani!” Bado ataendelea kumuomba mpaka Mwenyezi Mungu atasema: “Kama nikifanya hivyo, wewe utaniomba kitu kingine tena.” Yeye atasema: “Ninaapa kwa utukufu Wako kwamba mimi sitakuomba kitu kingine tena.” Atamuahidi Mwenyezi Mungu kwa viapo vingi sana kwamba hatamuomba jambo jingine zaidi ya hilo. Mwenyezi Mungu atamsogeza karibu na lango la Peponi. Atapoona yale yaliyomo ndani ya pepo atakuwa mkimya kwa muda kiasi fulani halafu atasema: “Ewe Mola wangu, niruhusu niingie Peponi.” Mwenyezi Mungu atasema: “Je, hukuahidi kutokuniomba jambo jingine zaidi ya lile. Ole wako, ewe mwanadamu! Wewe ni msaliti kiasi gani!” Yeye atasema: “Ewe Mola wangu, usinifanye mimi kuwa mnyonge zaidi kati ya watu Wako.” Ataendelea kumuomba Mwenyezi Mungu, mpaka Mwenyezi Mungu atacheka!! Wakati Mwenyezi Mungu anapomcheka, Yeye atamruhusu kuingia Peponi. Anapokwisha kuingia Peponi, ataambiwa aombe kile anachokitaka. Ataomba. Kisha ataambiwa aombe tena, ataomba mpaka atajikuta haoni cha kuomba tena. Mwenyezi Mungu atasema: “Yote haya ni kwa ajili yako na mengine zaidi kama hayo.” Muslim ameisimulia Hadith hii kwa njia nyingine93 kwamba Abu Huraira amesema: “Mwenyezi Mungu atakuja kwa umma huu ambao una watu wachamungu na mafisadi katika Siku ya Ufufuo katika sura tofauti na ile waliyoiona kabla, atawaambia: “Mimi ni Mola Wenu.” Wao watasema: “Mungu aepushilie mbali!” Yeye atasema: “Je, kuna alama maalum kati yenu na Yeye ambayo kwayo ninyi mnamtambua Yeye?” Wao watasema: “Ndio, ipo alama.” Kisha Yeye ataufunua mguu. Yoyote aliyesujudu kwa imani thabiti na uaminifu (katika maisha yake ya duniani) kwa ajili ya Allah, Mwenyezi Mungu atamruhusu kusujudu, na yule aliyesujudu kwa unafiki na riya, Mwenyezi Mungu ataufanya mgongo wake kuwa tabaka 93 Sahih Muslim, Jz. 1, uk. 88. 62


Abu huraira check Lubumba.qxd

7/1/2011

10:46 AM

Page 63

Abu Huraira moja kiasi kwamba kila anapotaka kusujudu, anaangukia mgongo wake. Halafu watainua vichwa vyao na kuona kwamba Mwenyezi Mungu amebadilika na kuwa kwenye sura Yake ile ambayo waliiona wakati wa mwanzo. Yeye atasema: “Mimi ndimi Mola Wenu.” Wao watasema: “Ndio, hakika Wewe Ndiwe.” Mwenyezi Mungu ataweka daraja juu ya Jahannam ….. na kadhalika.” Ilikuwa ni Hadithi ndefu lakini Bukhari ameifupisha wakati alipofasiri Suratun-Nun ndani ya Sahih yake, Jz. 2, uk. 138. Maneno ya Hadithi hiyo ni kama yafuatayo: “Mimi (Abu Huraira) nimemsikia Mtume (s.a.w.w.) akisema: “Mola Wetu hufunua mguu Wake na kila mu’min, mwanamume na mwanamke, atasujudu mbele Yake, wakati yule aliyesujudu kwa unafiki na riya katika uhai wa duniani atataka kusujudu lakini atakuwa hawezi kwa sababu mgongo wake utakuwa kama tabaka moja.” Ni Hadith ya ovyo sana. Napenda kuwauliza wasomi na wenye elimu kama inakubalika kwao kwamba Mwenyezi Mungu anaweza kuwa na sura tofauti tofauti, ambazo watu wanazikataa baadhi yake na kuzitambua baadhi! Je, Mwenyezi Mungu anao mguu wa kuwa alama maalum inayowaelekeza watu kumtambua Yeye? Kwa nini iwe ni huo mguu na sio kiungo kinginecho? Inawezekana kumhusisha Mwenyezi Mungu na kucheka au kuja na kwenda katika kusogea huku na kule? Kwa hakika haiwezekani! Naapa kwa Yule ambaye amemtuma (Muhammad) kwa haki ….. “Nabii miongoni mwao anayewasomea aya Zake na kuwatakasa, na kuwafundisha Kitabu na Hekma, ingawa kabla ya hapo wao kwa hakika walikuwa katika upotovu wa wazi.” (3:164).

NENO KUHUSU KUMUONA ALLAH Masunni wanakubaliana kwa pamoja kwamba kumuona Mwenyezi Mungu kwa macho kunawezekana katika uhai wa duniani na wa kesho Akhera, na wanakubaliana kwamba kwa hakika itakuja kutokea katika maisha ya Akhera. Waumini watamuona Allah katika Siku ya Kiyama kwa macho yao, lakini makafiri hawatamuona kamwe.Wengi wao walifikiri kwamba kumuona Allah hakutatokea katika uhai wa duniani. Baadhi yao wanaweza 63


Abu huraira check Lubumba.qxd

7/1/2011

10:46 AM

Page 64

Abu Huraira wakasema itawezekana. Wale walioamini katika kubadilika mwili kwa Allah wamesema kwamba watamuona Mwenyezi Mungu katika Siku ya Kiyama kwa muunganiko wa mionzi kati ya macho yao na mwili Wake!!, kumuangalia kama vile wanavyoangaliana wao kwa wao. Watakuwa hawana mashaka juu ya hilo kama walivyokuwa hawana shaka juu ya jua na mwezi kamili wakati kulipokuwa hakuna mawingu angani, hiyo ni kwa mujibu wa Hadithi ya Abu Huraira. Wao, wale wanaoamini Mungu kuwa na mwili, wamezihalifu kanuni za kiakili na desturi na wakavunja makubaliano ya umma na wakaisaliti dini yao na mahitajio muhimu ya Uislamu. Hivyo hatuna neno nao. Na kuhusu wale wengine wa Ash’ari, ambao waliamini juu ya kuvuka mipaka kwa Mwenyezi Mungu, wao walisema kumuona Mwenyezi Mungu kulikuwa ni uwezo ambao Allah atawapa waumini kwa umahususi kuwafanya wamuone Yeye, sio kwa muunganisho wa mionzi kati ya muonaji na Yeye, wala kwa kumuelekea Yeye, wala kwa kumwekea mipaka, wala … wala … Haitakuwa kama uoanaji wa kawaida wa wanadamu. Utakuwa ni uonaji maalum unaoanguka kutoka kwa waumini juu ya Mwenyezi Mungu. Utakuwa hauna mipaka, wala mabadiliko, wala moja kati ya mielekeo sita. Hili haliwezekani na wala haliwezi kufikiriwa, isipokuwa labda Mwenyezi Mungu awape waumini katika maisha ya Akhera uoni mwingine ambao wenye mielekeo tofauti na hii ya uoni katika uhai wa dunia hii, kwa namna ambayo uoni wa macho utakuwa kama uoni wa kiroho (umaizi wa kiakili). Hili liko mbali sana na chanzo au sababu ya kutoelewana kati yetu. Pengine kutoelewana kati yetu ni kwa sababu ya matumizi ya maneno yenyewe.

64


Abu huraira check Lubumba.qxd

7/1/2011

10:46 AM

Page 65

Abu Huraira 3. Jahannam Haitajaa Mpaka Mwenyezi Mungu Aweke Mguu Wake Ndani Yake: Wale masheikh wawili; Bukhari na Muslim, wameitaja Hadith moja iliyosimuliwa na Abdul-Razak kutoka kwa Ma’mar, kutoka kwa Humam kwamba Abu Huraira alisema: “Pepo na Jahannam zilizozana kuhusu kila moja ilichokuwa nacho. Jahannam ikasema: “Nimependelewa kwa kuwa na wale watu wenye kiburi na madhalimu.” Pepo ikasema: “Vipi kuhusu mimi kwamba nimewaweka wale watu masikini na wanyonge.”Allah akaiambia Pepo: “Wewe ni huruma Yangu, ambayo ninampa yeyote nimtakaye.” Kisha Allah akaiambia Jahannam: “Wewe ni chombo changu cha mateso, ambacho ninamuadhibia nacho yeyote nimtakaye.” Kila kimoja lazima kijazwe. Lakini Jahannam haitajaa mpaka Mwenyezi Mungu atakapoweka mguu Wake ndani yake na kusema: “Inatosha, inatosha.” Kisha inajaa na baadhi ya sehemu zake kujiunga na zingine.’”94 Kwa kiasi chochote Abu Huraira alivyokuwa tajiri zaidi, alizidi kuwa mpumbavu zaidi.95 Yeye aliona kwamba Jahannam ni kubwa sana kiasi cha kutoweza kujazwa watu wasio watiifu na Mwenyezi Mungu akasema kwamba Yeye ataijaza:

“Akasema: Ni haki, na ndiyo haki niisemayo. Lazima nitaijaza Jahannam wewe na kwa wale wote wenye kukufuata miongoni mwao.” (38:84-85). Hivyo Abu Huraira akasimama mbele ya mambo hayo mawili, akiwa amechanganyikiwa akitafakari jinsi ya kusulihisha kati yao, hadi akapata ufumbuzi kuhusu tatizo hilo kwamba Mwenyezi Mungu ataweka mguu 94 Sahih Bukhari, Jz. 3, uk. 127, Sahih Muslim, Jz. 2, uk. 482, Musnad Ahmad, Jz. 2, uk. 314. 95 Methali. 65


Abu huraira check Lubumba.qxd

7/1/2011

10:46 AM

Page 66

Abu Huraira Wake ndani ya Jahannam, kwa sababu, kwa mujibu wa maoni ya Abu Huraira, mguu wa Mwenyezi Mungu lazima uwe mkubwa kuliko Jahannam kwa ukubwa au upana wowote Jahannam itakaokuwa nao. Na kwa vile Abu Huraira alikuwa mjanja na mwerevu sana hivyo hakuna cha ajabu katika kukusanya kati ya makinzano hayo mawili. Lakini kama angetafakari juu ya usemi wa Mwenyezi Mungu: “Akasema: Ni haki, na ndiyo haki niisemayo. Lazima nitaijaza Jahannam wewe na kwa wale wote wenye kukufuata miongoni mwao.” (38:84-85), ulimi wake ungefungika na angeondoka huku akiyumba na nguo yake chafu, kwa sababu aya hiyo imetamka kwamba Jahannam itajazwa na yeye na watu kama yeye, mashetani na wale waliowafuata miongoni mwa watu. Aidha, Hadith hii haiwezekani kwa mujibu wa mantiki na sharia. Je, Mwislam yeyote anayemtukuza Mwenyezi Mungu anaamini kwamba Mwenyezi Mungu anao mguu? Mtu yeyote mwenye akili timamu anaweza kuamini kwamba Mwenyezi Mungu ataweka mguu wake kwenye Moto wa Jahannam ili ijae? Nini neno la hekima juu ya hilo? Je mazungumzo haya yana umuhimu wowote? Ni kwa lugha gani Pepo na Jahannam zinazozana? Ni kwa kutumia hisia za aina gani wanazoweza kuwatambua wale ambao wanaingia ndani yao? Kuna neema gani ambazo wenye kiburi na madhalimu walizokuwa nazo ambazo Jahannam inajivunia wakati ambapo wanateseka? Na je, Pepo inafikiria kwamba wale walioingia ndani yake ni mafukara na masikini ilihali ni wale ambao Mwenyezi Mungu anawapendelea? Wao ni mitume, wakweli, mashahidi na watu waadilifu. Mimi sidhani kwamba Pepo na Jahannam ni wajinga kiasi hicho, wapumbavu na wapungufu wa akili hivyo. 4. Mwenyezi Mungu anashuka kila usiku kuja kwenye uwingu wa wa chini kabisa: Masheikh hao wawili wameitaja Hadith iliyosimuliwa na Ibn Shihab kutoka kwa Abu Abdullah al-Agharr na Abu Salama bin Abdur-Rahman kwamba Abu Huraira alisema: “Mola Wetu hushuka kuja uwingu wa chini kabisa 66


Abu huraira check Lubumba.qxd

7/1/2011

10:46 AM

Page 67

Abu Huraira kwenye theluthi ya mwisho ya kila usiku na kusema: “Mtu yeyote naaniombe nimpatie kile anachokitaka.”96 Yeye ametukuka na yuko mbali sana na kushuka na kupanda, kuja na kwenda, kusogea huku na huko na matukio mengineyo. Hadith hii na zile tatu za kabla zilikuwa ni chanzo cha mifano katika Uislam kwa vile ilitokea katika kipindi cha utata wa kiakili. Uasi wa kidini mwingi na mikengeuko ilijitokeza kutoka kwa Mahambali, hususan Ibn Taymiya, ambaye alipanda mimbari ya msikiti wa Bani Umayyah huko Damascus katika Ijumaa moja akihutubia. Alisema kupitia uasi wake wa kidini: “Mwenyezi Mungu anashuka hadi kwenye uwingu wa dunia kila usiku kama ninavyoshuka sasa hivi.” Akashuka kitato kimoja cha mimbari ili kuwaonyesha jinsi Mwenyezi Mungu anavyoshuka katika mwenendo halisi kutoka juu hadi chini. Faqihi mmoja wa ki-Maliki aliyeitwa Ibn Zahra alipingana naye na akayakanusha yale aliyokuwa ameyasema. Wale watu ndani ya msikiti walikimbilia kwa yule faqihi wa kimaliki wakampiga kwa mikono na viatu kwa nguvu sana mpaka kilemba chake kikadondoka chini. Wakambeba kumpeleka kwa yule kadhi wa kihanbali huko Damascus, ambaye aliitwa Izzuddiin bin Muslim. Yeye aliamuru awekwe gerezani na akamuadhibu baada ya hapo. … na kadhalika.97 5. Suleiman anaivunja hukmu ya baba yake Daudi: Wale masheikh wawili98 wameitaja Hadith iliyosimuliwa na Abu Huraira kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amesema: “Kulikuwepo na wanawake 96 Sahih Bukhari, Jz. 4, uk. 68 na Jz. 1, uk. 136. Sahih Muslim, Jz. 1, uk. 283, Musnad Ahmad Hambal, Jz. 2, uk. 258 97 Mvumbuzi Ibn Battouta alihudhuria tukio hili na akasimulia aliloliona kwenye katika kitabu chake, Rihla (Usafiri), Jz. 1, uk. 57. 98 Sahih Bukhari, Jz. 2, uk. 166. Sahih Muslim, Jz. 2, uk. 57. Musnad Ahmad Hanbali, Jz. 2, uk. 322.

67


Abu huraira check Lubumba.qxd

7/1/2011

10:46 AM

Page 68

Abu Huraira wawili na watoto wao wawili. Mbwa mwitu akaja na akamnyakua mmoja wa watoto hao. Wale wanawake wakazozana kila mmoja akijidai mtoto aliyeliwa na yule mbwa mwitu ni wa mwenzie. Walikwenda kwa Nabii Daudi ili wakaamuliwe naye kati yao. Alihukumu kwamba yule mtoto aliyebakia hai ni wa yule mwanamke mtu mzima. Wakaenda kwa Nabii Suleiman, mtoto wa Nabii Daudi, na wakamwelezea kile kisa. Yeye akasema: “Nileteeni kisu (sikkeen kwa kiarabu) ili nimkate huyu mtoto katika nusu mbili, nimpatie kila mmoja nusu moja.” Yule mwanamke kijana akalia na kusema: “Tafadhali usifanye hivyo, Mwenyezi Mungu atakuwa na huruma juu yako. Huyo ni wa mwanamke huyo hapo.” Nabii Suleiman alihukumu kwamba mtoto yule alikuwa wa yule mwanamke kijana’” Abu Huraira akasema: “Namuapa Mwenyezi Mungu kwamba nilikuwa sijasikia kuhusu sikkiin (kisu) kabla ya hapo. Tulikiita midya (kisu).” Tunayo maelezo kuhusu Hadith hii: Kwanza: Daudi (a.s.) alikuwa ni nabii, ambaye Mwenyezi Mungu alikuwa amemteua na kumtuma kuongoza watu wake na akamkabidhi kutawala juu ya ardhi kwa haki. Mwenyezi Mungu alisema: “Ewe Daudi! Hakika tumekujaalia kuwa khalifa ardhini, basi uwahukumu watu kwa haki….. (38:26) Mwenyezi Mungu amemsifu ndani ya Qur’ani Tukufu kwa kusema: “….. na umkumbuke mja wetu Daudi, mwenye nguvu, kwa hakika yeye alikuwa mwelekevu sana. Hakika sisi tuliitiisha milima pamoja naye, ikitukuza jioni na asubuhi. Na (pia) ndege waliokusanywa, wote walikuwa wanyenyekevu kwake. Na tukautia nguvu ufalme wake na tukampa hekima na akili ya kukata hukumu. (38;17:20). Na kwa hakika alikuwa mbele yetu mwenye cheo cha kukaribiana na mahala pazuri.” (38:40) “….. Na kwa hakika tumewafadhilisha baadhi ya manabii kuliko wengine, na Daudi tulimpa Zaburi.” (17:55). Mwenyezi Mungu alikuwa amempendelea Nabii Daudi (a.s.) kwa kumpa kitabu cha Zaburi. Alikuwa maasum, hususan katika hukmu na utawala kwa mujibu wa kile alichokisema Mwenyezi Mungu ndani ya Qur’ani: “….. na wasiohukumu kwa yale aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu, basi hao ndio madhalimu.” (5:45). 68


Abu huraira check Lubumba.qxd

7/1/2011

10:46 AM

Page 69

Abu Huraira Huyu mwana, Suleiman, alikuwa ndiye mrithi wa elimu ya baba yake, Daudi, hekima na utawala. Yeye pia alikuwa nabii maasum. Hivyo kwa nini avunje hukmu ya baba yake ambapo alijua kwamba baba yake ni nabii maasum? Ikiwa siku hizi, mufti mwenye sharti na sifa zote za kuhukumu, akahukumu baina ya watu wawili, basi itakuwa wajibu kwa mamufti wote kuheshimu uhalali wa fat’wa isipokuwa labda wakijua kwa uhakika kabisa kwamba ni ya makosa. Lakini miongoni mwa mitume, makosa yalikuwa hayawezekani kupatikana kwa sababu wote walikuwa ni maasum. Hivyo ilikuwa haiwezekani kwa Suleiman, ambaye alikuwa mtume, kuvunja fat’wa ya baba yake, ambaye Mwenyezi Mungu alikukwa amemfanya nabii na mtawala. Kuvunja kwake fat’wa ya baba yake kulimaanisha kukana utashi wa Mwenyezi Mungu na kukosa adabu na uchamungu mbele ya baba yake. Pili: Tofauti kati ya fat’wa za manabii wawili hawa zilikuwa zinaeleweka wazi, kwa mujibu wa Hadith hii. Ina maana kwamba mmoja wao alikuwa amekosea. Hili lilikuwa haliwezekani juu ya manabii hawa hasa kwa vile walikuwa wanahukumu kulingana na sheria ya Mwenyezi Mungu. Yeye Mwenyezi Mungu anasema: “….. na wasiohukumu kwa yale aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu, basi hao ndio waasi.” (5:47) Tatu: Hadith inaonyesha kwamba nabii Daudi alihukumu kwamba mtoto alikuwa ni wa yule mama mtu mzima bila ya ushahidi wowote kwa sababu tu alikuwa mkubwa zaidi. Hukumu kama hizi hazikuja ila kutoka kwa watu wajinga wasio na elimu, ambao hawakujua chochote kuhusu vigezo vya sheria na kanuni za mashitaka. Utukufu uwe kwake Mwenyezi Mungu na manabii Wake. Nne: Suleiman alihukumu kwamba mtoto alikuwa wa yule bi-mdogo kwa sababu tu alihofia juu ya mtoto yule kukatwa kwa kile kisu. Huu haukuwa ushahidi wa kutosha kwa nabii Suleiman kuweza kuhukumu kulingana nao huo, hususan baada ya huyo bi-mdogo kukiri kwamba mtoto alikuwa wa yule mwanamke mwingine, na pia baada ya hukumu ya baba yake. 69


Abu huraira check Lubumba.qxd

7/1/2011

10:46 AM

Page 70

Abu Huraira Tano: Nawashangaa, Wallahi, wale walioamuamini Abu Huraira pale aliposema: “Naapa kwa Mwenyezi Mungu kwamba mimi nilikuwa sijasikia juu ya sikkiin (kisu) kabla ya hapo. Tulikuwa hatukiiti kwa jina jingine isipokuwa la midya.” Jina la sikkiin lilikuwa maarufu sana miongoni mwa Waarabu, na sidhani kwamba kulikuwa na yeyote ambaye alikuwa haelewi maana yake. Kwa kweli, wengi wa watu wa kawaida walikuwa hawaijui hiyo midya. Hivi Abu Huraira hakusoma au kusikia Mwenyezi Mungu akisema ndani ya Surat Yusuf:99 “….. akampa kila mmoja wao kisu (sikkiin) …” (12:31). Yeye mwenyewe hakuwahi kusimulia kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisema: “Yeye, yule ambaye alifanywa hakimu kwa ajili ya watu, kana kwamba alichinjwa bila ya (sikkiin) kisu.” 100 Angalizo: Abu Huraira alidhani kwamba nabii Daudi na Suleiman “walipokata hukumu juu ya shamba” 21:78 walikuwa wanapingika katika hukumu zao hivyo ikawa rahisi kwake kubuni Hadith ile ya udhanifu ambamo hakujua kwamba wote walikuwa sahihi na kwamba hukumu na elimu zao vyote ni kutoka kwa Mwenyezi Mungu.

99 Surat Yusuf ilishushwa kwa Mtukufu Mtume, Muhammad (s.a.w.w.) huko Makka isipokuwa kwa aya nne ambazo zilishuka Madina, aya tatu za mwanzo pamoja na ya nne: “Kwa hakika katika Yusuf na ndugu zake yako mazingatio mengi kwa wenye kuuliza.” (12:7). Na Abu Huraira alisilimu miaka saba baada ya kushuka kwa sura hii, ambayo imekuwa ikisomwa na Waislam usiku na mchana, na aliwasikia wakiisoma ndani ya swala zao mara nyingi tu. 100 Imesimuliwa na Imam Ahmad Hanbal katika Musnad yake, Jz. 2, uk. 230 kwamba ilisimuliwa na Muhammad bin Ja’far kutoka kwa Shu’ba kutoka kwa alAla kutoka kwa Abu Huraira.

70


Abu huraira check Lubumba.qxd

7/1/2011

10:46 AM

Page 71

Abu Huraira Kesi yenyewe ilikuwa kwamba kondoo kadhaa waliingia kwenye shamba la mizabibu, ambalo vishada101 vya mizabibu yake vilikuwa vimechomoza, na wakala shamba hilo wakati wa usiku. Mtunza shamba la mizabibu na mchunga kondoo wakaenda kwa nabii Daudi (a.s.) ili aamue kati yao. Yeye aliona, kwa mujibu wa sheria aliyoshushiwa na Mwenyezi Mungu, kwamba alipaswa kuhukumu kwamba yule mtunza shamba la mizabibu alistahili achukue wale kondoo kwa sababu thamani ya kondoo wale ilikuwa sawa na thamani ya hasara iliyoingia kwenye shamba la mizabibu. Pale alipotaka kutamka hukumu yake, Mwenyezi Mungu aliibatilisha kwa kumshushia Suleiman, ambaye alikuwa ni mshirika na baba yake katika utume, kwamba hukumu katika kesi hii ilikuwa ni kuwatoa kondoo kwa mtunza mizabibu ili atumie kutokana na maziwa na sufi yake, na kulitoa shamba la mizabibu kwa mchunga kondoo ili alirekebishe kama lilivyokuwa mwanzo, kisha baada ya hapo kila mmoja wao atachukua kilicho mali yake. Mwenyezi Mungu alifanya kwa hukumu hii, matumizi kwa ajili ya mtunza shamba la mizabibu kutokana na kondoo kwa kufidia hasara iliyopatikana bila kumiliki kondoo hao na akamfanya mchunga kondoo kufanya kazi katika shamba la mizabibu ili kulirudisha katika hali yake ya awali. Wakati Mwenyezi Mungu alipomuelekeza Suleiman juu ya hilo, yeye alilitoa hilo kwa baba yake. Baba yake akamtaka kwa msisitizo kufanya kile Mwenyezi Mungu alichomshushia yeye juu yake. Huu ni mukhtasari wa yale yaliyotokea baina yao. Hapakuwa na ukinzano au kutokukubaliana kama sharia zingine zozote mbili za kiungu, ambazo mojawapo hubatilisha nyingine. 101 Kama ilivyosimuliwa kutoka kwa Imam Abu Ja’far al-Baqir na Imam Abu Abdillah as-Sadiq (a.s.)

71


Abu huraira check Lubumba.qxd

7/1/2011

10:46 AM

Page 72

Abu Huraira Haya hapa ni maneno ya Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka zaidi, ambayo yanalifafanua jambo hili:

“Na Daudi na Suleiman walipokata hukumu juu ya shamba, walipolisha humo mbuzi wa watu usiku, nasi kwa hukumu yao tulikuwa mashahidi. Hivyo tukamfahamisha Suleiman,102 na kila mmoja tukampa hekima na elimu, na tulifanya milima na ndege kuwa pamoja na Daudi imnyenyekee na imtakase Mwenyezi Mungu, na sisi tulikuwa ndio wenye kufanya.” (21:78-79) Yaangalie maneno ya Mwenyezi Mungu: “….. na kila mmoja tukampa hekima na elimu …..,” utakuta kwamba wote wawili walikuwa sahihi, kwa sababu ile elimu na hukumu ya kila mmoja wao vilitoka kwa Mwenyezi Mungu Azza wa Jallah. Lakini Abu Huraira ilidhania kuwa ni rahisi kuwalaumu manabii hao kwamba wanaweza kuhukumu kimakosa kama mamufti wengine wa kawaida. “Na (mayahudi) hawakupa heshima Mwenyezi Mungu kama anavyostahiki kuheshimiwa,” 6:91, pale walipojipa uhuru wao wenyewe wa kuhukumu kwa mujibu wa fikira zao wenyewe dhidi ya manabii, ambao walikuwa wasila baina ya Mwenyezi Mungu na waja Wake. Walidhani kwamba hao mitume wanaweza kuhukumu kinyume hata kati102 Yaani: Tulimuelekeza Suleiman hukumu hii na kwamba ilikuwa ibatilishe ile hukumu tuliyokuwa tumemuelekeza Daudi hapo kabla. 72


Abu huraira check Lubumba.qxd

7/1/2011

10:46 AM

Page 73

Abu Huraira ka kanuni na hukumu za kisheria, ambazo zilikuwa bila shaka yoyote, zimeteremshwa kwao kutoka kwa Mwenyezi Mungu; “….. na wasiohukumu kwa yale aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu, basi hao ndio makafiri.” (5:44) Kama utambuzi ungerejea akilini mwao, wangejua kwamba wale manabii hawakutoa uamuzi na hukumu kulingana na mawazo yao binafsi kwa sababu wangeyajua hayo kwa wahyi. Hili liliwezekana kwa mujitahidi wa umma kwa sababu lilikuwa ndio bora wanachoweza kukifanya. Lakini lilikuwa haliwezekani kwa mitume kwa sababu lilikuwa mara nyingi likielekezwa kwenye maoni ya mtu binafsi. Kama hao manabii wangehukumu kwa kulingana na mawazo yao, basi ingekuwa inawezekana kwa mujitahidi wengine kuwakosoa. Hapo basi ile heshima ya utume na manabii ingepotea. Hivi mujitahidi yeyote mwaminifu anaweza kuthubutu kumkosoa Nabii Muhammad (s.a.w.w.) na kukiuka hukumu yake? Kwa hakika hapana! Kwa kauli moja hiyo ni kufuru! Qur’ani Tukufu inatamka wazi kwamba Mtume Muhammad (s.a.w.w.) alikuwa akitenda kulingana na wahyi; “….. wala hazungumzi kwa matamanio yake, bali ni wahyi ambao unateremshwa kwake.” 53:3-4. Na hivyo ndivyo walivyofanya mitume na manabii wote (amani iwe juu yao). 6. Suleiman analala na wanawake mia moja katika usiku mmoja: Wale masheikh wawili, Bukhari na Muslim, wameitaja Hadith kwamba Abu Huraira amesema: “Nabii Muhammad (s.a.w.w.) amesema: Suleiman bin Daudi alisema: “Nitakwenda kulala na wanawake mia moja usiku wa leo. Kila mwanamke atazaa mtoto wa kiume ambaye atapigana katika njia ya Mwenyezi Mungu. Malaika akamwambia: Sema Insha’allah. Yeye hakusema hivyo na akaenda kulala nao. Hakuna aliyezaa isipokuwa mmoja tu, ambaye alizaa kiumbe nusu ya binadamu. Kama angesema Insha’allah, asingevunja kiapo chake na haja yake ingetimia.” Vilevile tunayo maelezo kuhusu Hadith hii: 73


Abu huraira check Lubumba.qxd

7/1/2011

10:46 AM

Page 74

Abu Huraira Kwanza: Nguvu ya kibinadamu haiwezi kumudu kulala na wanawake mia moja kwa usiku mmoja, kwa kiasi chochote cha nguvu mtu atakachokuwa nacho. Hili ni kinyume na kanuni za maumbile na haliwezi kutokea hata kidogo. Pili: Haikuwezekana kwa Nabii Suleiman (a.s.) kukiuka mapenzi ya Mwenyezi Mungu, hasa baada ya tahadhari iliyotolewa kwake na Malaika. Ni nini kilichomzuia kusema Insha’allah? Yeye hakuwa ni Mtume ambaye Mwenyezi Mungu amemtuma kuwaongoza watu katika njia ya Allah? Walikuwa ni wajinga walioupa mgongo utashi wa Mwenyezi Mungu na kupuuza kwamba mambo yote yapo mikononi Mwake Yeye! Mitume walikuwa mbali kabisa na ukosa dhamira wa wajinga. Walikuwa mbali kabisa na waliyofikiria wapungufu wa akili. Tatu: Abu Huraira alichanganyikiwa kuhusu idadi ya wake za Suleiman. Wakati fulani alisema walikuwa mia moja,103 na wakati mwingine alisema walikuwa tisini,104 wakati mwingine sabini,105 wakati mwingine sitini.106 Hadith zote hizi zimesimuliwa ndani ya vitabu vya Bukhari, Muslim na Ahmad Hanbali. Sijui watasema nini wale wanaomtetea mtu huyu! Je watasema kwamba Suleiman alifanya hivi mara nyingi na wake zake hao? Hivyo walikuwa mia moja mara ya kwanza na tisini mara ya pili na sabini au sitini katika mara zingine. Na kila mara Malaika alimtahadharisha lakini yeye hakusema Insha’allah. Sidhani kwamba watasema hivyo. Ingekuwa bora kwao kusema: Mpasuko ulikuwa mpana kwa mshona-viraka kuweza kuurekebisha.107 Muongo huwa hana kumbukumbu nzuri.108 103 Sahih Bukhari, Jz. 3, uk. 176. Musnad Ahmad, Jz. 2, uk. 229 na uk. 270. 104 Sahih Bukhari, Jz. 4, uk. 107 105 Sahih Bukhari, Jz. 2, uk.165 106 Sahih Muslim, Jz. 2, uk. 23. Katika mlango huohuo Muslim amesimulia Hadith iliyosimuliwa na Abu Huraira kutoka kwenye njia nyingine kwamba walikuwa sabini na nyingine iliyosimuliwa naye kwa njia ya tatu kwamba walikuwa tisini. 107 Methali 108 Methali 74


Abu huraira check Lubumba.qxd

7/1/2011

10:46 AM

Page 75

Abu Huraira 7. Musa ampiga kibao Malaika wa Mauti: Masheikh hao wawili; Bukhari na Muslim wametaja Hadith kwamba Abu Huraira amesema: “Mtume Muhammad (s.a.w.w.) amesema: Malaika wa mauti alikuja kwa nabii Musa na akamwambia: Itikia mwito wa Mola Wako! Musa akamchapa kibao malaika wa mauti kwenye jicho lake na akaling’oa. Malaika wa mauti akarudi kwa Allah swt. na akamwambia: Umenituma kwa mmoja wa waja Wako ambaye hakutaka kufa. Amening’oa jicho langu. Allah akamrekebishia jicho lake na akamwambia: Rudi kwa mja Wangu na umwambie: Kama unataka kuishi zaidi, uweke mkono wako juu ya mgongo wa dume la ng’ombe na uone ni kiasi gani cha nywele kitanasa kwenye mkono wako. Basi utaishi kwa kila unywele mwaka mmoja.”109 Ahmad bin Hambali ameisimulia Hadith hii katika Musnad yake, Jz. 2, uk. 315 kwamba Abu Huraira amesema: “Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amesema: Malaika wa Mauti alikuwa akiwatokea watu waziwazi. Alikuja kwa nabii Musa (a.s.). Nabii Musa akampiga usoni mpaka akamng’oa jicho lake …..” Ibn Jariir at-Tabari katika kitabu chake, Tariikh al-Umam walMuluuk (historia ya mataifa na wafalme) Juzuu ya kwanza amesimulia kwamba Abu Huraira amesema: “Malaika wa Mauti alikuwa akiwatokea watu waziwazi mpaka pale alipokuja kwa Nabii Musa. Nabii Musa alimpiga mpaka akamng’oa jicho lake …..” na mwisho wa riwaya akasema kwamba “Malaika wa mauti akaanza kuwajia watu kwa kificho baada ya kifo cha Musa (a.s.).”110 109 Sahih Muslim, Jz. 2, uk. 309, Sahih Bukhari, Jz. 2, uk. 163 na Jz. 1, uk. 158 110 Kama malaika wa mauti alikuwa akiwajia watu waziwazi hilo lingeenea sana miongoni mwa wote, kama miale ya jua la mchana. Kwa nini wasimulizi na wana historia wa mataifa mengine wakazikosa habari kama zilikuwa na ukweli wowote? Kwa nini ubunifu wa visa vya uongo na hekaya wasivinjari kwenye msisimko huu? Je, waliiacha heshima ya jambo hilo kwa ajili ya Abu Huraira?

75


Abu huraira check Lubumba.qxd

7/1/2011

10:46 AM

Page 76

Abu Huraira Unagundua wazi kwamba Hadithi hii ina mambo mengi, ambayo hayawezi kuhusishwa na Mwenyezi Mungu kamwe, Mitume Wake wala malaika Zake. Hivi inafaa kwa Mwenyezi Mungu kuchagua miongoni mwa watu Wake, mmoja ambaye anashambulia kama madhalimu hata kwa malaika wa Allah kwa sababu ya hasira na anayefanya kama wenye majivuno waasi au kuchukia kifo kwa kiasi cha wajinga wasiojua kitu? Hivi hilo liliwezekana kwa Musa (a.s.) ambaye Mwenyezi Mungu alimpendelea kwa kuongea naye na akamfanya mmoja wa manabii bora? Alichukiaje kifo wakati ambapo alitamani kukutana na Mwenyezi Mungu na kuwa karibu Naye? Ni kosa gani la malaika wa mauti, ambaye alikuwa si chochote bali mjumbe wa Mwenyezi Mungu kwake yeye, mpaka ampige na kumng’oa jicho lake? Hivi ilistahili kwa manabii wakubwa kuwakashifu na kuwapiga malaika, ambao walitumwa na Mwenyezi Mungu kuwajulisha juu ya kazi na amri za Mwenyezi Mungu? Mwenyezi Mungu na mitume na malaika Zake wawe mbali juu ya hilo! Kwa nini sisi tuliwakana wakaazi wa arRass, ma-Farao, Abu Jahl na wengine kama wao na kuwalaani mchana na usiku? Haikuwa ni kwa sababu waliikosea mitume wakati walipowajia na kazi na amri za Mwenyezi Mungu? Kwa vipi basi tunayahusisha yayohayo kwa mitume hao? Mungu aepushilie mbali! Hiyo ni kashfa kubwa kiasi gani! Inafahamika vyema zaidi kwamba uwezo wa wanadamu kwa pamoja, au kwa kweli, uwezo wa viumbe wote tangu mwanzo wa kuumbwa hadi Siku ya Kiyama hauwezi kusimama dhidi ya uwezo wa malaika wa mauti. Ilikuwaje rahisi kwa nabii Musa kumpiga yeye? Je, malaika huyo hakujitetea ingawa alikuwa na uwezo wa kumuua Musa, hususan kwa vile aliamriwa na Mwenyezi Mungu kufanya hivyo? Na ni lini malaika huyo alipokuwa na jicho la kung’olewa? Na usisahau kwamba malaika huyo alipoteza haki yake kwa ajili ya kichapo hicho na hilo jicho lililong’olewa. Hakuamrishwa na Mwenyezi Mungu kulipiza kisasi juu ya Musa (a.s.), ambaye kwenye Taurati yake Allah amesema: “Kwamba uhai ni kwa uhai, na jicho kwa jicho, na pua kwa pua, na sikio kwa sikio, na jino kwa jino, na (kwamba) kuna kisasi juu ya majeraha,” wala Allah 76


Abu huraira check Lubumba.qxd

7/1/2011

10:47 AM

Page 77

Abu Huraira hakumlaumu nabii Musa (a.s.) bali alimheshimu yeye kwa kumpa fursa ya kuchagua kati ya kufa au kuishi kwa miaka mingi mingine kwa kiasi cha nywele za dume la ng’ombe zitakazonasa kwenye kiganja chake cha mkono. Ninaapa kwa hadhi ya haki na heshima ya uadilifu na kwa kuwa kwao juu mbali na ubatili na uongo, kwamba mtu huyu amewatwisha watetezi wake kile wasichoweza kukibeba na amewachosha kwa Hadithi zake ambazo vichwa vyao havikuweza kuendana nazo, hasa ile Hadith yake: “Malaika wa mauti alikuwa akiwajia watu waziwazi kabla ya kifo cha nabii Musa (a.s.) lakini akawajia kwa kificho baada ya kifo chake Musa (a.s.)” Mwenyezi Mungu atuokoe kutokana na ulegevu wa akili na upuuzi wa uzungumzaji na utendaji. Hakuna uwezo isipokuwa kutoka kwa Mwenyezi Mungu, aliye juu na Mtukufu wa Enzi. 8. Jiwe lakimbia na nguo za Musa (a.s.): Masheikh hao wawili wamesimulia kwamba Abu Huraira amesema: “Mtume Muhammad (s.a.w.w.) amesema: “Wana wa Israili walikuwa wakioga uchi. Waliangaliana kwenye sehemu zao za siri. Musa (a.s.) alioga peke yake. Wao wakasema: ‘Wallahi hakuna kinachomzuia Musa kuoga nasi isipokuwa ni kwamba amekuwa na henia.’ Wakati mmoja Musa (a.s.) alikwenda kuoga. Aliweka nguo zake juu ya jiwe. Jiwe hilo lilikimbia pamoja na nguo za Musa. Nabii Musa (a.s.) alilifukuza jiwe hilo akipiga kelele: “Ewe jiwe, nguo zangu! Wee jiwe wee, nguo zangu!” Waisraili wakamuangalia Musa kwenye sehemu zake za siri na wakasema kwamba Musa alikuwa hana tatizo lolote, alikuwa sawasawa tu. Baada ya hapo jiwe hilo likasimama. Musa akachukua nguo zake na akaanza kulipiga jiwe hilo. Naapa kwa jina la Mwenyezi Mungu kwamba jiwe hilo lilipata kovu sita.’”111 111 Tumeieleza Hadith hii kwa mujibu wa Sahih Muslim, Jz. 2, uk.308. Bukhari ameisimulia katika Sahih yake Jz. 1, uk. 42 na Jz. 2, uk. 162. Ilisimuliwa na Ahmad Hanbal katika Musnad kwa njia nyingi kutoka kwa Abu Huraira katika Jz. 2, uk. 315. 77


Abu huraira check Lubumba.qxd

7/1/2011

10:47 AM

Page 78

Abu Huraira Al-Bukhari na Muslim wamesimulia katika Sahih zao kwamba Abu Huraira alisema kwamba ilikuwa ni kwa tukio hili ambalo Mwenyezi Mungu amelizungumzia katika maneno Yake:

“Enyi mlioamini, msiwe kama wale waliomtaabisha Musa, lakini Mwenyezi Mungu alimtakasa na yale waliyoyasema, naye alikuwa ni mwenye heshima mbele ya Mwenyezi Mungu.” (33:69) Unaweza kuona kutokuwezekana kulikokuwepo katika Hadith hii. Ilikuwa haiwezekani kumkashifu Nabii Musa (a.s.), ambaye alikuwa na heshima ya kuongea na Allah swt., kwa kufunua sehemu zake za siri mbele ya watu, kwa sababu hilo lingemdhalilisha na kushusha hadhi yake, hususan walipomuona akikimbia kulifukuza jiwe ambalo lilikuwa halioni wala kusikia, na huku akipiga ukelele: “Ewe jiwe, nguo zangu! Ewe jiwe, nguo zangu!” Kisha kusimama mbele ya jiwe hilo mbele ya watu akiwa uchi na kulipiga huku watu hao wakiangalia sehemu zake za siri kana kwamba alikuwa kichaa! Kama jambo hilo lingekuwa la kweli, Mwenyezi Mungu angelifanya. Hivyo kwa nini Musa awe na hasira na kuliadhibu jiwe hilo, ambalo lililazimika kufanya hivyo kwa sababu halina akili wala la kuhiari? Kulikuwa na faida gani katika kulipiga jiwe ambalo lilikuwa halina hisia? Kukimbia kwa jiwe hilo pamoja na nguo za Musa kusingempa yeye kisingizio chochote cha kujidhalilisha mwenyewe kwa kufunua sehemu zake za siri mbele ya watu. Angeweza kukaa mahali pake hapo mpaka mtu amletee nguo zake au kitu chochote cha kumsitiri kama mtu yeyote mwenye akili timamu ambavyo angefanya kama jambo kama hilo lingemtokea.

78


Abu huraira check Lubumba.qxd

7/1/2011

10:47 AM

Page 79

Abu Huraira Kukimbia huko kwa jiwe kulikuwa ni muujiza na jambo lisilo la kawaida. Lisingetokea isipokuwa kama kulikuwa na jambo la kusababisha changamoto au kuthibitisha jambo kubwa muhimu sana, kama kule kusogea kwa mti kwa ajili ya Mtume Muhammad (s.a.w.w.) huko Makka, wakati makafiri walipopendekeza kwa Mtume kuusogeza. Mwenyezi Mungu aliufanya mti huo kusogea kutoka mahali pake kwenda mahali pengine ili kuthibitisha utume wa Muhammad na kuhakikisha kazi ya ujumbe wake. Ilikuwa wazi kwamba suala la Musa kuoga ndani ya bahari halikuhitaji muujiza au changamoto, hususan pale ambapo ingesababisha kashfa kwa ajili ya Nabii huyo mbele ya watu kwa namna ambayo, yeyote ambaye angemuona au kusikia kuhusu hilo angemdhihaki na kumfanyia mzaha. Kwani kuthibitisha kwamba yeye hakuwa na henia hakukuwa na umuhimu sana kiasi kwamba kulihitaji kumdhalilisha Nabii huyo au kumshushia hadhi yake, wala haikuwa ni moja ya mambo muhimu yaliyohitaji muujiza. Ingeweza kujulikana vyema kwa wake zake, ambao wangeweza basi kueleza ukweli wa hali ya mambo. Hebu natuchukulie dhana ya kwamba alikuwa na henia, hilo lilikuwa na ubaya gani? Nabii Shu’aib alipata upofu na nabii Ayubu alikuwa mgonjwa kwa miaka arobaini. Manabii wote waliwahi kuugua na kufariki. Haikuwa ni dosari au udhaifu kwamba waliugua magonjwa hasa pale yalipokuwa hayakujulikana kwa watu kama henia. Haikuwezekana kwa wao kuwa na jambo linalosibu akili zao au ukarimu wao, au jambo lolote linaloweza kuwasababisha watu kukaa mbali nao au kuwafanyia mizaha na maskhara. Kwa kweli hiyo henia haikuwa ya namna hiyo. – Haikusimuliwa na mtu mwingine yeyote kwamba Musa alikuwa na henia isipokuwa Abu Huraira peke yake! Lakini lile tukio ambalo Mwenyezi Mungu amelizungumzia ndani ya Qur’ani kwa kusema kwamba: “Enyi mlioamini! msiwe kama wale waliomuudhi Musa, lakini Mwenyezi Mungu akamtakasa na yale waliyoyasema, …..” 33:69, lilikuwa, kama lilivyosimuliwa na Imam Ali na Ibn Abbas, kuhusu suala la kwamba wana wa Israili walimshutumu 79


Abu huraira check Lubumba.qxd

7/1/2011

10:47 AM

Page 80

Abu Huraira Musa kwa kumuua Harun. Lilisemekana pia kwamba lilikuwa ni kuhusu lile suala la Malaya, ambaye Qaarun alimshawishi kumshutumu Musa kuwa alikuwa na uhusiano mbaya na yeye lakini Mwenyezi Mungu akamtoa kwenye shutuma hizo ambapo yeye mwenyewe, malaya huyo alisema ukweli. Na ilisemekana kwamba walimsononesha kwa kumhusisha na uchawi, kusema uongo na wendawazimu walipoona ile miujiza yake. Nawashangaa Bukhari na Muslim kwamba waliongeza Hadith hizi kwenye sifa za Musa! Hivi kule kumpiga malaika na kumng’oa jicho kulikuwa ni sifa? Kule kukimbia mbele za watu uchi kulikuwa ni heshima? Ujinga huu ulikuwa na maana gani? Nabii Musa alikuwa mbali sana na hayo. Ilitosha kwa yeye kile ambacho Qur’ani imetamka kuhusu sifa zake na nafasi yake ya heshima na hadhi yake. 9. Watu wanakimbilia kwa Mitume wakitarajia shufaa (maombezi) zao: Masheikh hawa wawili wamesimulia riwaya ndefu ya Abu Huraira akisema kwamba: “Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amesema: Katika hiyo Siku ya Ufufuo Mwenyezi Mungu atawakusanya watu wote, wa mwanzo wao na wa mwisho wao katika sehemu moja. Muitaji ataweza kuwaona wote, na wao wote wataweza kumsikia yeye. Jua litashuka karibu zaidi. Watu watashindwa kuvumilia huzuni na hofu zao. Watasemezana wenyewe kwa wenyewe: “Hivi huoni hiyo huzuni uliyomo ndani yake? Hutafuti mtu wa kukuombea shufaa kwa Mwenyezi Mungu?” Watamwendea Adam (a.s.) na kumwambia: “Wewe ndiye baba wa wanadamu wote, Mwenyezi Mungu alikuumba kwa mikono yake na akakupulizia ndani yako baadhi ya neema Zake. Aliwaamuru malaika kusujudu mbele yako na wakasujudu. Tafadhali tuombee shufaa kwa Mola Wako. Wewe huoni hali tuliyomo?” Adam atasema: “Mola Wangu amekasirika sana leo kwa kiasi ambacho hajawahi kukasirika kabla, wala hatakasirika kama hivyo tena baadaye. Alinikataza kula kutoka kwenye mti ule nami nikawa sikumtii Yeye. Mimi, mimi, mimi mwenyewe! Nendeni kwa mwengine badala yangu. Nendeni kwa Nuh.” 80


Abu huraira check Lubumba.qxd

7/1/2011

10:47 AM

Page 81

Abu Huraira Wanakwenda kwa Nuh (a.s.) na kumwambia: “Ewe Nuh, wewe ulikuwa ndiye nabii wa kwanza kwa watu wa duniani. Mwenyezi Mungu alikuita wewe mja mwenye shukurani. Tafadhali tuombee shufaa kwa Mola Wako. Huoni hali tuliyokuwa nayo?” Nuh atasema: “Mola Wangu amekasirika sana leo kwa kiasi ambacho hajawahi kukasirika kabla, wala hatakasirika kama hivyo tena baada ya leo kwa sababu, wakati mmoja niliwalaani watu wangu. Nitabakia mwenyewe, mwenyewe, mimi mwenyewe! Nendeni kwa mwingine mbali ya mimi. Nendeni kwa Ibrahim.” Watakwenda kwa Ibrahim (a.s.) na kumwambia: “Ewe Ibrahim, wewe ni Nabii wa Mwenyezi Mungu na rafiki yake wa kweli miongoni mwa watu wote wa duniani, tafadhali tuombee shufaa kwa Mola Wako. Huoni hali tuliyonayo?” Yeye atasema: “Mola Wangu amekasirika sana leo kwa kiasi ambacho hajawahi kukasirika kabla, wala hatakasirika kama hivyo tena baada ya leo. Mimi nilisema uongo mara tatu. Nitabakia mimi mwenyewe, mwenyewe, mimi mwenyewe! Nendeni kwa mwingine badala yangu mimi. Nendeni kwa Musa.” Watakwenda kwa Nabii Musa (a.s.) na kumwambia: “Ewe Musa, wewe ni nabii wa Allah swt. Alikupendelea wewe kwa ujumbe wake na akaongea nawe peke yako miongoni mwa watu wote; tafadhali tuombee shufaa kwa Mola Wako. Hivi hutuoni ni hali gani tuliyonayo?” Musa atasema: “Mola Wangu amekasirika sana leo kwa kiasi ambacho hajawahi kukasirika kabla, wala hatakasirika kama hivyo tena baada ya leo. Mimi niliua mtu mmoja, ambaye sikuwa nimeamriwa kumuua. Mimi nitabaki mwenyewe, mwenyewe, mwenyewe. Nendeni kwa mtu mwingine badala yangu. Nendeni kwa Isa.” Watamwendea Isa (a.s.) na kumwambia: “Ewe Isa, wewe ni nabii wa Allah na neno Lake, ambalo alimfikishia Bikira Mariam na roho kutoka Kwake. Wewe uliongea na watu ukiwa bado kwenye susu la utoto wako; tafadhali tuombee shufaa kwa Mola Wako. Je, huioni hali tuliyonayo?” Isa (a.s.) atasema: “Mola Wangu amekasirika sana leo kwa kiasi ambacho hajawahi kukasirika kabla, wala hatakasirika kama hivyo tena baada ya leo. (Abu Huraira hakutaja kosa lake) Mimi nitabaki mwenyewe tu., mwenyewe, mwenyewe. Nendeni kwa Muhammad.” 81


Abu huraira check Lubumba.qxd

7/1/2011

10:47 AM

Page 82

Abu Huraira Watakwenda kwa Mtukufu Muhammad (s.a.w.w.) na kumwambia: “Ewe Muhammad, wewe ni Mtume wa Mwenyezi Mungu na ni wa mwisho kati ya mitume Wake. Mwenyezi Mungu alikusamehe makosa yako yote. Tafadhali tuombee shufaa kwa Mola Wako. Hutuoni tuko katika hali gani hii?” Ndipo mimi (Muhammad) nitakapokwenda kwenye mbingu na kusujudu mbele ya Mola Wangu. Allah atanipa fursa ya kumtukuza na kumshukuru Yeye kwa namna ambayo hakuna hata mmoja aliyewahi kupewa kabla yangu. Halafu itasemwa: “Ewe Muhammad, nyanyua kichwa chako na uombe chochote unachotaka, hicho wewe utapewa na uombezi (kushufaiya), uombezi wako utakubaliwa.” Mimi nitasema: “Ewe Mola Wangu, umma wangu! Ewe Mola wangu, umma wangu!” Hapo itanadiwa: “Ewe Muhammad, waingize watu miongoni mwa umma wako, wale ambao hawataadhibiwa, kwenye lango la kulia na watashirikiana milango mingine na watu wengine.”112 Abu Huraira katika riwaya hii, amethubutu kwa ufidhuli kabisa kuwakashifu na kuwadhalilisha manabii, ambao Mwenyezi Mungu amewateua kueneza ujumbe Wake miongoni mwa watu Wake, kwa namna ambayo kwamba shari’ah tukufu na Sunna vinaikataa kabisa. Sunna ilikuwa na namna au njia ya kuwatukuza mitume ambayo ilizifanya nyoyo kujaa staha takatifu na heshima na nyuso kunyenyekea kwao. Ilikuwa ni Sunna ya Mtukufu Mtume Muhammad (s.a.w.w.) na Qur’ani yake tukufu ambavyo vilieneza utukufu wa sifa za manabii hawa (a.s.) kote duniani, juu ya ardhi, ndani ya bahari na kuyagubika masikio ya zama zote kwa kuwasifia wao. Yote ambayo mataifa waliyajua kuhusu manabii hawa watukufu, ambayo yalifanya macho kunyenyekea mbele yao, na umaarufu ambao ulifanya tamaa za makuu kunywea na kushusha mbawa zao kidhalili mbele yao, yalikuwa ni kwa sifa za Qur’ani na Sunna ya Muhammad (s.a.w.w.). Bila ya ile Sunna iliyotakasika ya Nabii Muhammad (s.a.w.w.) na Qur’ani tukufu, hakuna yeyote katika vizazi vya baadae ambaye angejua chochote 112 Maelezo haya ni kwa mujibu wa Sahih Bukhari, Jz. 3, uk. 100. Ilisimuliwa na Muslim katika Sahih yake Jz. 1, uk. 97 na Ahmad Hanbali katika Musnad yake Jz. 2. 82


Abu huraira check Lubumba.qxd

7/1/2011

10:47 AM

Page 83

Abu Huraira kuhusu manabii hawa (a.s.) pale ambapo hapakuwa na ushahidi maalum au taarifa za kweli au riwaya yenye maana kamili kuhusu wao. Hivyo Nabii Muhammad alihifadhi historia ya mitume na mataifa na akakamilisha kwa Sunna na Qur’ani zile sifa tukufu na maadili bora na tabia njema. Alieneza zile sharia tukufu na mifumo ya hikma ambayo ilishushwa kwake kutoka kwa Mwenyezi Mungu, ambazo zingehakikisha furaha ya maisha ya kidunia na yale ya Akhera. Vyote, Qur’ani na Sunna vilikusanya sayansi, hekima, siasa, hadhi ya maisha ya dunia na ya akhera na kuihifadhi lugha ya Kiarabu mpaka Siku ya Kiyama. Riwaya hii ya Abu Huraira, pamoja na mbwabwajo na upuuzi wake, ilikuwa ya ajabu na ya tofauti kabisa na maneno ya Mtukufu Mtume Muhammad (s.a.w.w.) na inayopingana kabisa na Sunna. Lilikuwa ni jambo la mbali kabisa na Mtume wetu kuhusisha yale yaliyomo katika Hadith hii ya kipuuzi isiyo na muonjo wala maana. Adam alikuwa mbali kabisa na utovu wa utii kwa kufanya kosa ambalo lilimfanya Allah kumkasirikia sana hivyo. Allah alimkataza kuusogelea mti ili kumtukuza na kumuongoza yeye. Utukufu uwe juu ya Nuh. Yeye asingeweza kuwalaani watu wowote isipokuwa maadui wa Allah ili kujiweka karibu na Mola Wake. Ibrahim alikuwa mwaminifu sana kiasi cha kutoweza kusema uwongo! Kamwe hakufanya jambo lililomkasirisha Mwenyezi Mungu juu yake. Musa hakuua mtu yoyote, ambaye Mwenyezi Mungu angekasirika kwa ajili yake mtu huyo, bali alimuua mtu ambaye hakuwa na utukufu wala thamani. Allah, aliyetukuka zaidi asingewafanyia mitume Wake bali kwa huruma na upendo kama alivyosema: “Hakuna malipo ya ihsani ila kwa ihsani.” 55:60. Mitume walikuwa mashuhuri kuliko kufikiri juu ya Mola Wao kwamba aliwakasirikia sana kiasi kwamba hatakuja kukasirika tena kama hivyo sio kabla ya hapo wala baada ya hapo. Vilevile Nabii Muhammad asingeeleza lolote juu yao bali sifa na utukufu. Ni vipi watu watashauriana na kuwasiliana katika Siku ya Kiyama? Wao wapo kama Allah anavyosema:

83


Abu huraira check Lubumba.qxd

7/1/2011

10:47 AM

Page 84

Abu Huraira “….. kila mwanamke anyonyeshaye atamsahau amnyonyeshaye, na kila mwenye mimba ataizaa mimba yake, na utawaona watu kama wamelewa, kumbe hawakulewa, lakini ni adhabu ya Mwenyezi Mungu iliyo kali.” 22:2, na

“Siku ambayo mtu atamkimbia nduguye, na mama yake, na mkewe na watoto wake. Kila mtu miongoni mwao siku hiyo atakuwa na jambo litakalomtosha.” 80:34-37. Watawezaje, katika hali ngumu kama hiyo, kwenda kwa manabii, ambao wakati huo wako juu ya A’araf (sehemu kati ya Pepo na Jahannam)? Ni nini kitakachowazuia kwenda kwa Nabii Muhammad tangu safari ya mwanzo kabisa? Je, yeye sio mwenye hadhi tukufu, cheo cha juu kabisa na shufaa yake yenye kukubalika? Hakuna hata mmoja, hapo, anayempuuza yeye. Kwa nini Adam au Nuh au Ibrahim au Musa wasiwashauri kwenda kwa Muhammad moja kwa moja? Hawezi yeyote kati ya manabii hao kuwaliwaza wale watu masikini pale mwanzoni wanapowaomba shufaa au uombezi wao? Hivi manabii hao hawaijui nafasi tukufu ya Mtume Muhammad katika siku hiyo au wanapendelea kuongeza mateso na usumbufu wa waumini hao wanyonge wanaotafuta msaada? Tunaweza kumuuliza Abu Huraira kuhusu watu hao masikini: je wanatokana na umati wa Muhammad au kutoka kwenye umma mwingineo? Kama wanatoka kwenye umma wa Muhammad, nini kitakachowazuia kumwendea yeye tangu mwanzoni na kumuomba uombezi? Na kama wanatoka kwenye umma mwingine, kwa kweli hataweza kuzivunja juhudi zao na kuwakatisha tamaa kwa huruma zote hizo alizojaaliwa kupewa na Allah swt. na akamfanya yeye kuwa njia ya uombezi wa shufaa kati Yake na watu Wake. Kwa hakika hatawaangusha hao kwa vile yeye ndiye matu84


Abu huraira check Lubumba.qxd

7/1/2011

10:47 AM

Page 85

Abu Huraira maini ya wahitaji na amani kwa wenye hofu. Anawajibu wale wenye haja kwa fadhila zake na kuwatosheleza wenye kiu wanaomba kabla ya mwangwi wa sauti zao kurudi. 10. Mashaka ya Manabii, kumshutumu Lut, kumpendelea Yusuf kuliko Muhammad katika subira: Masheikh hao wawili wamesimulia kwamba Abu Huraira amesema: “Mtume Muhammad (s.a.w.w.) amesema: “Tunastahili mashaka kuliko Ibrahim pale aliposema (kama ilivyo katika Qur’ani): “Na Ibrahim aliposema: Mola wangu! Nionyeshe jinsi unavyofufua wafu, akamwambia: Je huamini? Akasema: Kwa nini, ninaamini, lakini ni ili moyo wangu utulie…..” 2:260. Mwenyezi Mungu awe na huruma juu ya Lut; amekimbilia kwenye msaada wenye nguvu. Kama ningekaa gerezani kwa muda mrefu kama Yusuf alivyokaa, ningemwitikia mlinganiaji.113 Hadith hii ilikuwa haiwezekani kwa sababu fulani fulani: Kwanza: Hadith hii ilishuhudilia kwamba Ibrahim alikuwa na mashaka lakini Mwenyezi Mungu akasema:

“Na hakika tulimpa Ibrahim mwongozo wake zamani na tulikuwa tukimjua.” 21:51 na

113 Rejea Sahih al-Bukhari Jz. 2, uk.158, Sahih Muslim, Jz. 1, uk.71 na Musnad Ahmad Jz. 2.

85


Abu huraira check Lubumba.qxd

7/1/2011

10:47 AM

Page 86

Abu Huraira

“Na hivyo tukamwonyesha Ibrahim ufalme wa mbinguni na ardhi, na ili awe miongoni mwa wenye yakini.” 6:75. Kuwa na yakini ndio kiwango cha hali ya juu cha elimu. Yule ambaye ana yakini juu ya jambo hawezi kuwa na shaka kuhusu hilo. Mantiki yenyewe inakataa kwamba manabii, wote kabisa, walikuwa na mashaka kuhusu mambo. Ilikuwa ni dhahiri kabisa. Na kwa kauli ya Mwenyezi Mungu: “Na Ibrahim aliposema: Mola wangu! Nionyeshe jinsi unavyofufua wafu, …..” 2:260 inaweza kuwa na maana kwamba Ibrahim alimuomba Mola wake kuhusu ni vipi anavyowapa uhai wafu na sio kule kuwapa uhai kwenyewe. Hili lisingewezekana isipokuwa kama kutoa uhai kwa wafu kulikuwa na uhakika kwake. Hii ni kusema; kutumia vipi katika swali kuna maana ya kuulizia kuhusu hali ya kitu kilichokuwepo na kinachojulikana kwa muulizaji na mwenye kuulizwa. Kwa mfano: Vipi hali ya Zayd? ina maana kwamba je, hajambo ama anaumwa? Na Zayd alianya vipi? ina maana je, alifanya vizuri au vibaya? Na kwa hiyo kusema kwake: “Mola wangu! Nionyeshe jinsi unavyofufua wafu,” hakukuwa chochote ila ni ombi la kuonyeshwa ni vipi kile ambacho alikuwa na hakika nacho – kutoa uhai kwa wafu – kingefanyika. Lakini kwa sababu kwamba mtu aliyekuwa haijui ile hadhi ya hali ya juu ya Ibrahim angeweza kufikiri kwamba ombi hili la Ibrahim limekuja kutokana na shaka juu ya uwezao wa Mwenyezi Mungu wa kuwahuisha wafu, Mwenyezi Mungu alitaka kuiondoa dhana hii, hivyo akamwambia: “Nini! na kwa hiyo wewe huamini? Yeye akasema: “Hapana, naamini” kwa maana ya kusema: “Mimi ninaamini juu ya uwezo wa kuhuisha wafu, 86


Abu huraira check Lubumba.qxd

7/1/2011

10:47 AM

Page 87

bali niliomba ili kutuliza moyo wangu wakati nitakapoona jinsi wafu watakavyokuwa hai tena baada ya viungo vyao kutengana ndani ya makaburi yao, ndani ya mapango, ndani ya matumbo ya wanyama wakali na katika maeneo ya kufariki kwao ndani ya majangwa au ndani ya bahari.” Kana kwamba alikuwa na shauku ya kuona jinsi hivyo itakavyotokea hivyo akasema “ili moyo wangu utulie,” ambayo ilikuwa na maana ya kupoza kiu yake kwa kuliona hilo likitendeka. Hii ndio ilikuwa maana ya aya hii. Yeyote atakayehusisha mashaka kwa Ibrahim juu ya uwezo wa Mwenyezi Mungu, kwa hakika huyo atakuwa amepotoka. Pili: Ilikuwa dhahiri kutokana na kauli yake: “Tunastahili zaidi kuliko Ibrahim katika mashaka,” kwamba Mtukufu Muhammad, pamoja na mitume wote, walikuwa katika mashaka na walistahili zaidi kuliko Ibrahim katika hilo. Tuchukulie kwamba yeye hakuwa na maana ya manabii wote, bali hasa alimaanisha yeye mwenyewe binafsi. Muktadha wa maneno hayo ulikuwa wazi kabisa kuonyesha Nabii Muhammad (s.a.w.w.) alikuwa anastahili zaidi kuwa na mashaka kuliko Nabii Ibrahim. Utukufu kwa Mwenyezi Mungu! Hii ilikuwa ni kashfa kubwa sana! Kigezo cha ijma, akili na desturi kilithibitisha ubatili wa Hadith hii. Hatujui, Wallahi naapa, kuwa ni kwa nini Mtume Muhammad (s.a.w.w.) alikuwa anastahili zaidi kuwa na mashaka kuliko Ibrahim, licha ya yale yote aliyomjaalia Mwenyezi Mungu yeye, ambayo hakuwajaalia mitume wengine wote wala malaika yeyote! Msaidizi na mlinzi wa Mtukufu Mtume Muhammad (s.a.w.w.), Imam Ali (a.s.), ambaye alikuwa ndio lango la jiji la elimu la Mtume na ambaye alikuwa kama alivyokuwa Harun kwa Musa isipokuwa kwamba hakuna mtume baada ya Muhammad amesema: “Kama pazia baina yangu na 87


Abu huraira check Lubumba.qxd

7/1/2011

10:47 AM

Page 88

Abu Huraira Mwenyezi Mungu lingeondolewa, isingeongezeka yakini yangu kuliko nilivyo na yakini juu ya Allah swt.114 Hiyo ilikuwa ni kusema kwamba imani yake juu ya Allah ilikuwa ya kiwango cha hali ya juu na isingeongezeka kwa sababu yeye, kwa kweli, alimjua Allah vizuri sana na alikuwa na yakini sana kuhusu Yeye na uwezo na mamlaka Yake. Hivyo ndivyo alivyokuwa Imam Ali, je ni vipi kuhusu bwana wa manabii na wa mwisho wa mitume wote (amani iwe juu yao wote)! Tatu: Katika kauli yake: “Mwenyezi Mungu awe na huruma juu ya Lut, alikimbilia kwenye msaada ulio na nguvu,” alimlaumu Lut na kumshutumu kwa kutokujiamini juu ya Mwenyezi Mungu ambapo, kwa kweli, Lut alitaka kuwachochea kabila lake na jamaa na ndugu zake na kushinda kwa usaidizi wake kwa ajili ya Mwenyezi Mungu kuwaamrisha watu kufanya mema na kuwakataza kufanya vitendo viovu. Mtukufu Mtume Muhammad (s.a.w.w.) asingeweza kumlaumu Lut au kukanusha kauli yake. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) asingeweza kumfikiria Lut jingine badala ya alilostahiki kama nabii mtukufu, bali alionya kwamba watakuwepo waongo wengi wenye kubuni Hadith! Nne: Katika maneno yake: “Kama ningekaa gerezani kwa muda mrefu kama vile alivyokaa Yusuf, mimi ningemwitika mlinganiaji,” yeye alimfadhilisha kwa uwazi kabisa, nabii Yusuf juu ya Mtume Muhammad. Hii ilipingana na ijma, vitabu vya Hadith na kile kilichothubutu kuwa muhimu miongoni mwa Waislam. Kama ukisema kwamba Nabii Muhammad alikuwa mnyonge kutamani busara, subira na hekima za Nabii Yusuf katika kuthibitisha ukosa hatia 114 Kauli hii ya Imam Ali ilikuwa maarufu. Al-Busiriy, yule mshairi, ameitaja kwenye shairi lake: Waziri wa binamu yake katika matendo mashuhuri. Angekuwa na furaha kama waziri angekuwa ndugu. Kuondolewa kwa pazia hakukuongeza kwenye yakini yake chochote. Ilikuwa ni jua bila ya kifunikacho. 88


Abu huraira check Lubumba.qxd

7/1/2011

10:47 AM

Page 89

Abu Huraira wake hadi ukweli ulipotokea na akaachiwa huru kutoka gerezani, sisi tutasema kwamba hilo lisingewezekana hivyo hata katika udhaifu, kwa sababu kama angejaribiwa kwa mtihani kama huo wa Nabii Yusuf, yeye angekuwa na busara na subira zaidi kuudhihirisha ukweli. Ni kutowezekana kiasi gani kulikokuwa kwa Mtume kumwitika mlinganiaji kwa kumlingania kutoka gerezani tu na kuipoteza ile hekima ambayo aliipendelea Yusuf alipomwambia mtumishi wa mfalme pale alipomwacha huru kutoka gerezani, kama anavyosema Mwenyezi Mungu: “….. Rudi kwa bwana wako na ukamuulize limekuwaje shauri la wanawake wale waliokata mikono yao, bila shaka Mola Wangu anazijua sana hila zao. (Mfalme) Akasema: Mlikuwa na kusudi gani mlipomtamani Yusuf kinyume cha matamanio yake? Wakasema: Hasha lillahi, sisi hatukujua ubaya wowote kwake. Mke wa mfalme akasema: Sasa haki imedhihirika, mimi ndiye niliyemtamani kinyume na nafsi yake, na bila shaka yeye ni miongoni mwa wakweli.” (Yuusuf; 50-51) Yeye hakutoka gerezani mpaka ukosa hatia wake ukang’ara kama jua lisilokuwa na mawingu. Hivyo Yusuf alikuwa na busara na subira kiasi kwamba hakujaribu kutoka gerezani haraka mapema mpaka alipopata alichokuwa akikitaka. Zaidi kuliko yote hayo, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alikuwa mwenye busara, subira, mpole, imara, mwenye dhamiri, hekima na maasum katika vitendo vyake vyote na maneno. Alikuwa ni yeye ambaye, kama wangeweka jua kwenye mkono wake wa kulia na mwezi kwenye mkono wa kushoto ili aitelekeze kazi na ujumbe wake kamwe asingefanya hivyo. Ingekuwa vyema na bora kwa Abu Huraira kusema: Kama Nabii Muhammad angekaa gerezani mara nyingi kwa kipindi kama alichokaa Yusuf, yeye kamwe asingemuomba mtu yeyote kumtoa gerezani humo kama Yusuf alivyofanya wakati ule, “Na (Yusuf) akamwambia yule aliyemdhania kuwa ataokoka katika wawili hawa: Unikumbuke mbeke ya bwana wako …..” 12:42. Hiyo ilikuwa ni kusema kwamba: 89


Abu huraira check Lubumba.qxd

7/1/2011

10:47 AM

Page 90

Abu Huraira kaelezee maadili na tabia zangu kwa mfalme na umweleze kuhusu kisa changu kwamba aweze kuwa na huruma juu yangu na kunitoa kwenye tatizo hili, “….. lakini shetani akamsahaulisha kumtaja kwa bwana wake, 12:42, yaani kwamba shetani alimfanya mtu yule kusahau kumtaja Yusuf mbele ya mfalme “hivyo Yusuf akakaa gerezani kwa miaka michache.” 12:42. Ule usahaulifu wa yule mtu na kukaa kwa Yusuf gerezani kwa kiasi cha miaka kulikuwa ni onyo kwake. Alikuwa asiombe bali huruma ya Mwenyezi Mungu. Hilo lilisemwa na Mtukufu Mtume Muhammad (s.a.w.w.) kama hivyo. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alifikwa na makubwa zaidi kuliko hayo matatizo ya Yusuf kuwa gerezani na mabaya zaidi kuliko yote yale ambayo familia ya Nabii Yaqub (a.s.) iliyapata. Kamwe hakuwahi kuwa mnyonge au kusalimu amri. Hakumuomba yeyote isipokuwa Mwenyezi Mungu. Yeye pamoja na kabila lake lote (la Bani Hashim) walifungiwa katika korongo kwa miaka. Walikuwa katika dhiki kubwa kabisa. Yeye, ukoo wake na waumini, wote walinyanyaswa sana kiasi kwamba hakuna nabii yeyote wa kabla yake aliyeteseka kiasi hicho kama yeye. Washirikina waliwaghasi yeye na ukoo wake kwa kiasi walivyoweza. Hapa ni baadhi ya kauli za Mwenyezi Mungu: “Na walipokufanyia hila wale waliokufuru ili wakufunge au wakuue au wakutoe …..” 8:30, na “Kama hamtamsaidia, basi Mwenyezi Mungu amekwisha msaidia (Mtume Wake) walipomfukuza wale waliokufuru, naye akiwa wa pili kati ya wawili walipokuwa katika pango, alipomwambia swahibu wake: Usihuzunike, hakika Mwenyezi Mungu yupo pamoja nasi, hivyo Mwenyezi Mungu akamteremshia utulivu juu yake, na akamsaidia kwa majeshi msiyoyaona …..” 9:40, na “Na bila shaka Mwenyezi Mungu alikusaidieni katika (vita vya) Badri hali ninyi mlikuwa wachache …..” 3:123, na “(Kumbukeni) mlipokuwa mkikimbia mbio wala hamkumtazama yeyote, na hali Mtume akiwaiteni nyuma yenu, Kisha akakupeni (Mwenyezi Mungu) dhiki juu ya dhiki ….. 3:153, na “Walipokujieni kutoka juu yenu na 90


Abu huraira check Lubumba.qxd

7/1/2011

10:47 AM

Page 91

Abu Huraira kutoka chini yenu, na macho yaliponywea na nyoyo zikapanda kooni, nanyi mkaanza kumdhania Mwenyezi Mungu dhana mbalimbali. Hapo waumini walijaribiwa na wakateremshwa kwa tetemeko kali.” 33:10-11, na “….. na siku ya Hunain, ambapo wingi wenu ulipokufurahisheni, lakini haukukufaeni chochote, na ardhi ikawa finyu juu yenu ingawa ilikuwa yenye wasaa, kisha mkakimbia mkirudi nyuma. Kisha Mwenyezi Mungu akateremsha utulivu wake juu ya Mtume wake na juu ya waumini, …..” 9:25-26, kwa nyongeza ya hali zake nyingine za ukarimu, ambamo alikutana na mazito mengi, lakini katika yote hayo yeye alikuwa imara kuliko milima. Alikabiliana na matatizo hayo kwa moyo mkuu na nafsi iliyotulia, hivyo yalitoweka mbele ya akili yake pana na tabia tulivu. Hakumuomba yeyote isipokuwa Mwenyezi Mungu kumtoa kwenye huzuni na wasiwasi. Aliendesha mambo yake kwa subira na kutegemea juu ya Allah. Hivyo vilikuwa wapi dhamira yake, subira, hekima na busara zinazofanana na zile za Yusuf, Yaqub, Is’haq, Ibrahim na waliobaki katika manabii (amani iwe juu yao wote)? 11. Nzige wa Dhahabu waanguka juu ya Ayyub (a.s.): Masheikh wawili wamesimulia kwa njia nyingi Hadith115 kwamba Abu Huraira amesema: “Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amesema: Wakati Ayyub (a.s.) alipokuwa anaoga ndani ya bahari akiwa uchi, nzige wa dhahabu walianguka juu yake. Alianza kuwakusanya kwenye nguo zake. Mola wake akamwambia: “Je, Mimi nisingeweza kukufanya usiwe na haja nao hawa?” Yeye akasema: “Ndio, kwa Utukufu Wako, lakini nilihitaji baraka Zako.” Hakuna yeyote aliyeiamini Hadithi hii isipokuwa wale wasio na umaizi wala akili. Kuumba nzige wa dhahabu kulikuwa ni muujiza na jambo lisilo la kawaida. Mwenyezi Mungu hakutaka kufanya hivyo isipokuwa pale ambapo palikuwa na lazima. Kwa mfano, kama kuthibitisha utume 115 Rejea Sahih Bukhari, Jz. 1, uk. 42 na Jz. 2, uk. 160 91


Abu huraira check Lubumba.qxd

7/1/2011

10:47 AM

Page 92

Abu Huraira kulitegemea juu ya muujiza, Mwenyezi Mungu angeufanya ili kuwa ushahidi kwa ajili ya utume na ujumbe wenyewe. Mwenyezi Mungu asingeumba nzige wa dhahabu bure bure tu kumuangukia Ayyub (a.s.) wakati alipokuwa akioga uchi peke yake. Kama walimuangukia juu yake na akaanza kuwakusanya kwenye nguo zake, hicho kingekuwa ni kitendo cha maana. Ingekuwa ni zawadi kutoka kwa Mwenyezi Mungu, ambayo amempendelea kwayo, na ni lazima ishukuriwe kwa kuikubali kwa heshima na sio kuigeuzia mgongo kidharau, kwa sababu kuikatalia mbali kungekuwa ni utovu wa shukurani, tabia ambayo mitume walikuwa mbali sana nayo. Kama manabii walilimbikiza mali, wangeitumia kwa ajili ya Mwenyezi Mungu ili kupata radhi Zake. Wangeitumia kwa kutekelezea mipango yao ya kimabadiliko. Mwenyezi Mungu alikuwa anatambua nia zao hivyo Yeye asingeweza kamwe kuwalaumu kwa kukusanya mali. 12. Kumlaumu Musa kwa kuchoma kijiji cha chunguchungu: Masheikh wawili hao, Bukhari na Muslim, wamesimulia kwamba Abu Huraira amesema: “Mtume Muhammad (s.a.w.w.) amesema: Mdudu chungu alimfinya mmoja wa manabii (Musa kama ilivyosimuliwa na Tirmidhi).116 Akaamuru kichomwe kijiji cha wadudu chungu na kikachomwa. Mwenyezi Mungu akamshushia: “Kwa nini umechoma moja ya taifa linalomtukuza Mwenyezi Mungu, ati kwa sababu tu kwamba mdudu chungu amekufinya?”117 Abu Huraira aliwapenda sana manabii. Alichanganyikiwa kuhusu kila suala la ajabu ajabu ambalo lilivimbisha macho na kuziba masikio. Manabii walikuwa na subira ndefu, mioyo mikuu na hadhi ya hali ya juu 116 Rejea Irshad as-Sari cha al-Qastalani, Jz. 6, uk. 288 117 Rejea Sahih Bukhari, Jz. 2, uk. 114; Sahih Muslim Jz. 2, uk.267; al-Adab cha Abu Dawud; an-Nasai cha Ibn Majah na Musnad Ahmad. 92


Abu huraira check Lubumba.qxd

7/1/2011

10:47 AM

Page 93

Abu Huraira kuliko alivyosimulia mpungufu wa akili huyu. Mlinzi wa Mtukufu Mtume Muhammad (s.a.w.w.), Imam Ali ibn Abi Talib (a.s.) alisema katika moja ya hotuba zake: “Naapa kwa jina na Allah, kama ningepewa zile dola saba na kila kilichokua chini ya mbingu zao ili kumuasi kwa kunyakua ganda moja la punje ya shayiri kinywani mwa mdudu chungu nisingeweza kufanya hivyo kamwe. Maisha haya ya dunia kwangu mimi ni duni sana kuliko jani lililoko kinywani mwa nzige anayelitafuna. Ali ana haja gani na furaha ya mpito na starehe yenye kuisha?” Ingawa Imam Ali (a.s.) hakuwa mtume, bali mlinzi mkweli, suala lake hili liliwakilisha umaasumu wa mitume dhidi ya yale ambayo wasio na elimu, wajinga waliyowahusisha nayo. Mwenyezi Mungu hajawahi kuchagua, kwa ajili ya ujumbe wake, mtu yeyote ambaye asingeweza kuwa mbali na shutuma hizo. Sifa zote ni za Allah na Aliyetukuka ni Yeye juu ya wanayoyasema wapumbavu! Wallahi sijui wale watetezi wa Hadith hii watasema nini kuhusu nabii huyu, ambaye aliteketeza wadudu chungu kwa moto, licha ya Mtume Muhammad (s.a.w.w.) kusema: “Hakuna anayeadhibu kwa Moto isipokuwa ni Mwenyezi Mungu peke Yake.”118 Walikubaliana kwa kauli moja kwamba kuchoma moto kumekatazwa kwa wanyama hai isipokuwa pale ambapo mwanadamu mmoja amemfanya mtu mwingine kufa kwa kumchoma moto, basi mlezi wa yule mtu aliyekufa anayo haki ya kumchoma yule mchomaji wa marehemu. Abu Dawud ameisimulia Hadith ya kweli kwamba Ibn Abbas amesema kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alikataza kuua mdudu chungu, nyuki , na kipwe. 118 Sharh Sahih Muslim, Jz. 11, uk. 6 cha an-Nawawi kilichochapishwa pembezoni mwa Sharh Sahih Bukhari 93


Abu huraira check Lubumba.qxd

7/1/2011

10:47 AM

Page 94

Abu Huraira 13. Mtume Asahau Rakaa Mbili za Swala: Masheikh hao wawili wamesimulia Hadith kwamba Abu Huraira amesema: “Mtume Muhammad (s.a.w.w.) aliswali swala moja ya mchana, nafikiri ilikuwa ni swala ya Asr,119 kwa rakaa mbili badala ya nne na akaimalizia hivyo. Kisha akasimama mbele ya kipande cha ubao kilichokuwa mbele ya msikiti na akaweka mkono wake juu yake.120 Miongoni mwa watu waliokuwemo msikitini humo alikuwa ni Abu Bakr na Umar, lakini waliogopa kumuuliza Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kuhusu hilo. Watu hao waliokuwa na haraka waliondoka msikitini hapo na wakajiuliza kama swala hiyo ilikuwa imepunguzwa. Mtu mmoja ambaye Mtume alimwita kwa jina la Dhul-Yadayn akamuuliza Mtukufu Mtume (s.a.w.w.): “Je, ulisahau au uliipunguza hii swala?” Mtukufu Mtume akasema: “Sikusahau wala swala haikupunguzwa.” Dhul-Yadayn akasema: “Ndio, wewe ulisahau.” Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akaswali rakaa nyingine mbili, akatoa salaam (mwisho wa swala), na akasema Allahu Akbar, na akasujudu kwa ajili ya sahau hiyo. Hadith hiyo ilikuwa sio ya kweli kwa sababu nyingi tu: Kwanza: Ilikuwa haiwezekani kwamba kusahau huku kulikuja kutoka kwa mtu ambaye aliiendea swala kwa moyo na nafsi. Ilikuja kutoka kwa yule ambaye hakuwa makini katika swala. Na mitume walikuwa mbali sana na usahaulifu na walikuwa watukufu sana kuweza kukashifiwa na walaghai. Hatujakuta kwamba usahaulifu kama huo ulitokea kwa mtume yeyote ule, hususan yule bwana wa mitume na wa mwisho wao (s.a.w.w.), amani iwe juu yao wote. 119 Ni kiasi gani Abu Huraira alivyokuwa na hekima na tahadhari! Huoni kwamba hakuamua kwa uhakika kwamba ilikuwa ni swala ya Alasiri na hakuthibitisha makisio yake! 120 Uchamungu wa Abu Huraira ulimfanya ataje hata kile kipande cha ubao na kwamba Mtume aliweka mkono wake juu yake, ambacho hakikuwa na uhusiano wowote na maudhui ya Hadith hiyo, lakini, ila tu alikuwa na tahadhari katika kutoa maelezo! 94


Abu huraira check Lubumba.qxd

7/1/2011

10:47 AM

Page 95

Abu Huraira Naapa kwa bwana wa Mitume (s.a.w.w.) kwamba kama usahaulifu kama huo ungepatikana kutoka kwangu, aibu na tahayari vingenizonga na wenye kuswali nyuma yangu wangenifanya kichekesho mimi na ibada yangu, hivyo ni vipi kuhusu hao mitume, ambao Mwenyezi Mungu amewateua kuwa mifano bora kwa walimwengu! Pili: Mtume Muhammad (s.a.w.w.) alisema: “Sikusahau na wala swala haijapunguzwa.” Sasa ingekuwaje kwa yeye, baada ya hayo, kutamka na kukubali kwamba alisahau? Hebu tuchukulie kwamba hakuwa maasum katika kusahau, lakini alikuwa maasum katika kutokuwa mkaidi na kukosa hikma katika Hadith zake kama zilikuwa zinapingana na ukweli. Hili lilikuwa na uhakika kwa waislam wote. Tatu: Abu Huraira alichanganyikiwa katika Hadith yake hii na riwaya zake zilikuwa tofauti. Wakati mwingine alisema: “Mtume Muhammad (s.a.w.w.) alituongoza katika moja ya swala mchana; ama ni swala ya Adhuhuri au Alasiri.” Alikuwa na mashaka kati ya swala hizo. Na katika wakati mwingine tena akasema: “Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alituongoza katika swala ya Alasiri,” kana kwamba alikuwa na hakika. Mara ya tatu yeye akasema: “Nilipokuwa ninaswali swala ya Adhuhuri pamoja na Mtukufu Mtume …..” Hadith hizi zimo ndani ya Sahih al-Bukhari na Sahih Muslim. Wale waliozielezea Sahih hizi walichanganyikiwa kwa kiasi kwamba waliingia katika kuathirika na wakajichukulia juu yao wenyewe kile wasichoweza kuhimili ili kutetea Hadith hizi kama walivyofanya walipokana maoni ya az-Zuhri pale alipothibitisha kwamba Dhul-Yadayn na Dhush-Shamalayn walikuwa ni mtu mmoja tu. Nne: Hadith imeonyesha kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) aliondoka kwenye sehemu yake ya kuswalia, akasimama na akaweka mkono wake kwenye kipande cha ubao mbele ya msikiti. Wale watu wenye haraka waliondoka pale msikitini na kusema: “Je, hii swala imepunguzwa?” DhulYadayn akamwambia Mtukufu Mtume (s.a.w.w.): “Je, ulisahau au umepunguza swala?” Mtukufu Mtume akasema: “Sikusahau na wala 95


Abu huraira check Lubumba.qxd

7/1/2011

10:47 AM

Page 96

Abu Huraira sikupunguza swala.” Yeye akamwambia Mtukufu Mtume: “Ndio, wewe ulisahau.” Kisha Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akawaambia masahaba zake: “Je huyu alikuwa sahihi?” Masahaba hao wakasema: “Ndio, alikuwa sahihi.” Nyingine iliyosimuliwa na Abu Huraira kwamba Mtume aliingia kwenye chumba cha msikiti na halafu akatoka nje halafu watu wakarejea. Yote hayo yalibatilisha swala hiyo, kwa sababu kwa mujibu wa Shari’ah ya kiislam, swala ni ibada yenye kuendelea mfululizo, ambayo haiwezi kukatishwa. Hivyo, ni vipi Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) angeweza kutegemea juu ya rakaa zake mbili za mwanzo na kuja kuzikamilisha kwa rakaa nyingine mbili ili kuzifanya ziwe nne, ile idadi sahihi ya rakaa za Adhuhuri au Alasiri? Tano: Dhul-Yadayn, ambaye alitajwa katika Hadith hii, alikuwa ndiye huyo huyo Dhush-Shamalayn,121 Ibn Abd Amr, mshirika wa kabila la Zuhra. Majina yote mawili yalihusika na mtu mmoja. Aliuawa kishahidi katika vita vya Badr. Hilo lilithibitishwa na kiongozi wa kabila la Zuhra, na mbora wa wale waliojua vizuri zaidi kuhusu washirika wao, Muhammad bin Muslim az-Zuhri, kama ilivyoelezwa na Ibn Abdul-Birr katika kitabu chake al-Isti’ab, Ibn Hajar katika kitabu chake al-Issaba, katika Sharh Sahih Bukhari na Sharh Sahih Muslim. Vile vile hilo lilithibitishwa na Sufyan ath-Thawri na Abu Haniifa pale walipoichukulia Hadith hiyo kuwa sio sahihi na wakatoa fat’wa za kuipinga.122 An-Nassa’i alitamka katika riwaya yake kwamba Dhul-Yadayn na Dhush-Shamalayn ibn Amr ni majina yaliyomhusu mtu mmoja huyohuyo. Yeye alisema:123 …..

121 Jina lake lilikuwa ni Umar au Amr kama ilivyotajwa ndani ya kitabu cha Ibn Hajar, al-Isaba. 122 Rejea kitabu cha an-Nawawi, Sharh Sahih Muslim, Jz. 4, uk. 235 iliyochapwa pembezoni mwa kitabu al-Irshad as-Sari cha al-Qastalani na Zakariyya alAnsari katika kitabu at-Tuhfa. 123 Rejea kitabu cha al-Qastalani, al-Irshad as-Sari Jz. 3,uk.267 96


Abu huraira check Lubumba.qxd

7/1/2011

10:47 AM

Page 97

Abu Huraira Dhush-Shamalayn ibn Amr alimwambia (Mtume): “Je, uliipunguza swala au wewe ulisahau?” Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akasema: “Ni nini alichokisema Dhul-Yadayn?” Kwa hiyo alithibitisha kwamba DhushShamalayn ndiye huyo huyo Dhul-Yadayn. Dhahiri zaidi kuliko hilo ni ile Hadith iliyosimuliwa na Ahmad bin Hanbal,124 kutoka kwa Abu Salama bin Abdur Rahma na Abu Bakr bin Abu Khaythama kwamba Abu Huraira alisema: “Mtukufu Mtume Muhammad (s.a.w.w.) aliswali swala ya Adhuhuri ama Alasiri kwa rakaa mbili na akaikamilisha kwa salam (tasliim) akisema Assalaam Alaykum. Dhush-Shamalayn bin Abd Amr, yule mshirika wa kabila la Zuhra akamwambia Mtume: “Je, ulipunguza swala au ulikuwa umesahau?” Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akasema: “Nini alichokisema Dhul-Yadayn?” Wao wakasema: “Yeye alikuwa sahihi.” Abu Musa alisimulia Hadith kutoka kwa Ja’far al-Mustaghfiri125 kutoka kwa Muhammad ibn Kathiir, kutoka kwa al-Awza’ii, kutoka kwa az-Zuhri, kutoka kwa Sa’iid bin al-Mussayab, Abu Salama na Ubaidullah bin Abdullah kwamba Abu Huraira alisema: “Mtume alimaliza swala baada ya rakaa mbili badala ya nne. Abd Amr126 bin Nadhla ambaye alitoka kwenye kabila la Khuza’a na mshirika wa kabila la Zuhra alisimama na akamwambia Mtukufu Mtume (s.a.w.w.): “Je, uliipunguza swala ama ulisahau?” ….. kujumlisha maneno ya Mtume, ‘Je Dhush-Shamalayn alikuwa yu mkweli?’ Riwaya zote hizi zilionyesha wazi kwamba Dhul-Yadayn aliyetajwa katika Hadith ya Abu Huraira alikuwa ni Dhush-Shamalayn ibn Abd Amr, yule mshirika wa kabila la Zuhra. Hakuna shaka kwamba Dhush-Shamalayn aliyetajwa hapo juu aliuawa katika vita vya Badr zaidi ya miaka mitano kabla Abu Huraira hajawa Mwislam. Muuaji wake alikuwa ni Usamah aj124 Ndani ya Musnad yake, Jz. 20, uk. 271 na uk. 284. 125 Al-Issaba ya Ibn Hajar, Jz. 20, uk. 271 na 284 126 Kama ilivyosimuliwa katika al-Issaba. Tazama alisema kwamba jina la Dhush-Shamalayn lilikuwa ni Abd Amr. 97


Abu huraira check Lubumba.qxd

7/1/2011

10:47 AM

Page 98

Abu Huraira Jasmi. Ibn Abd Birr pamoja na wanahistoria wote wamesema hivyo. Kwa hivyo, ingewezekana vipi kwa Abu Huraira kukutana naye katika swala moja nyuma ya Mtukufu Mtume Muhammad (s.a.w.w.)?! Baadhi ya wale ambao walimtetea Abu Huraira walithibitisha kwamba sahaba anaweza akasimulia kuhusu jambo ambalo hakulihudhuria, ama kwa kulisikia kuhusu hilo kutoka kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) au kutoka kwa sahaba mwingine. Aidha kifo cha Dhul-Yadayn miaka mitano kabla ya Abu Huraira kuwa Mwislam kusingemzuia yeye kusimulia Hadith hiyo. Utetezi huu kwa hakika ulikuwa sio sahihi. Abu Huraira alijifanya kwamba yeye alikuwa amehudhuria swala hiyo, na hilo limethibitishwa na wale wote waliosimulia Hadithi hii. Al-Bukhari ameisimulia Hadith hii ndani ya Sahih yake, Jz. 1, uk. 145 kutoka kwa Adam bin Shu’ba kutoka kwa Sa’d bin Ibrahim kwamba Abu Huraira alisema: “Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alituongoza sisi katika swala ya Dhuhri au Asri ….. na kadhalika.” Muslim ameisimulia katika Sahih yake, Jz. 1, uk. 215 kwamba Muhammad bin Siriin alisema: “Nilimsikia Abu Huraira akisema: Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alituongoza sisi katika moja ya swala za mchana, ama Dhuhri au Asri ….. na kadhalika.” Imam at-Tahawi alichanganyikiwa kuhusu Hadithi hii. Yeye alisema kwamba ilikuwa ni Hadith ya kweli, ingawa alikuwa na uhakika kwamba Dhul-Yadayn alikuwa ndiye Dhush-Shamalayn mwenyewe, yule mshirika wa kabila la Zuhra, ambaye aliuawa kishahidi katika vita vya Badr miaka mitano kabla Abu Huraira hajawa Mwislam, hivyo ilikuwa haiwezekani kwa wao kuwa pamoja katika swala moja. Kwa hiyo alilazimika kuitafsiri Hadithi ya Abu Huraira127 kama ifuatavyo: “Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alituongoza sisi katika swala (kimajazi) kwamba alikuwa na maana kwamba: aliwaongoza Waislam katika swala.” Jibu la utete wao wa kisingizio lilikuwa kwamba Abu Huraira alithibitisha 127 Rejea kitabu cha al-Qastalani, al-Irshad as-Sari, Jz. 3, uk. 266.

98


Abu huraira check Lubumba.qxd

7/1/2011

10:47 AM

Page 99

Abu Huraira kuhudhuria kwake kwa hakika kwa namna ambayo haingeweza kutafsiriwa hivi na vile, hapa na pale. Muslim amesimulia Hadith katika Sahih yake, Jz. 1, uk. 216 kwamba Abu Huraira alisema: “Nilipokuwa nikiswali swala ya Dhuhri pamoja na Mtume Muhammad (s.a.w.w.), yeye alimaliza swala hiyo baada ya rakaa mbili ….. na kadhalika.” Ni vipi kuhusu Hadithi hii? Ilikuwa inawezekana kweli kutafuta kisingizio cha kuitetea hii? Kwa kweli hapana sivyo! Lakini tulisumbuliwa na wale ambao kamwe hawatafakari! Hatuna makimbilio ila ni kwa Mwenyezi Mungu tu! 14. Mtume Muhammad aliwadhuru, aliwachapa, aliwatukana na kuwalaani watu wasio na hatia: Masheikh hawa wawili wamesimulia kwamba Abu Huraira alisema: “Mtume Muhammad (s.a.w.w.) amesema: ‘Ewe Allah, Muhammad si chochote bali ni mwanadamu. Huwa anachukia kama wanadamu wengine. Nilikuwa na ahadi nawe kwamba Wewe hutaivunja ahadi hiyo. Kila muumini nitakayemuudhi, kumchapa, kumtukana au kumlaani fanya iwe ni fidia kwa makosa yake na sababu ya kumfanya awe karibu na Wewe.”128 Haiyumkini kwa Nabii Muhammad na manabii wengine wote kumuudhi, kumchapa, kumtukana na kumlaani mtu yeyote ambaye hakustahili hilo wakiwa wametulia au wamekasirika. Kwa kweli wao manabii kamwe hawakukasirika vivi hivi ila kwa ajili ya Mwenyezi Mungu. Utukufu uwe juu ya Allah. Yeye ameepukana mbali na kutuma mitume ambao wangeweza kusukumwa na hasira na kuwachapa, kuwatukana, kuwalaani na kuwadhuru watu wasio na hatia. Mitume waliepukana mbali na kila maneno au vitendo vinavyoweza kupingana na umaasum wao au yale ambayo yasingemfaa ntu mwenye hekima na busara. Wachamungu na wapujufu, waumini na makafiri walijua vizuri kwamba 128 Imesimuliwa na Muslim ndani ya Sahih yake, Jz. 2, uk. 392, Sahih al-Bukhari Jz. 4, uk. 71 na Musnad Ahmad Jz. 2, uk. 243. 99


Abu huraira check Lubumba.qxd

7/1/2011

10:47 AM

Page 100

Abu Huraira kuuudhi, kuchapa, kutukana na kulaani mtu asiye hatia ilikuwa ni dhulma mbaya na uhalifu wa wazi, ambao waumini wameukana. Sasa ni vipi itawezekana kwa bwana wa mitume kufanya hivyo? Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amesema:129 “Kumtukana Mwislam ni kosa.” Abu Huraira amesema:130 “Ilisemwa kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.): “Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, uwalaani wanafiki.” Yeye (s.a.w.w.) akasema: “Mimi sikutumwa na Allah kuwa mwenye kulaani bali kuwa rehma kwa watu.” Hapo ni kwamba alikuwa pamoja na wanafiki, ni vipi atakuwa pamoja na waumini wasio na hatia? Yeye (s.a.w.w.) amesema:131 “Wenye kulaani hawatakuwa waombezi ama mashahidi mnamo Siku ya Kiyama.” Abdullah bin Amr amesema:132 “Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) hakuwa mkorofi au ayari, asiye muaminifu.” Yeye (s.a.w.w) alisema: “Wabora wenu ni wale wenye maadili mema.” Anas bin Malik amesema:133 “Mtukufu Mtume hakuwa mkorofi, mwenye kulaani au mtukanaji.” Abu Dharr134 alimwambia ndugu yake pale aliposikia kuhusu Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) “Panda kipando hadi kwenye bonde na ujaribu kusikia kutoka kwake.” Wakati ndugu yake aliporejea alimwambia: “Nimemuona akitoa amri kwa tabia tukufu za kiungwana kabisa.” Abdullah bin Amr amesema: “Niliandika kila kile nilichokisikia kutoka kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) ili kuweza kukihifadhi. Baadhi ya makuraishi wakanikataza kufanya hivyo na wakasema: “Unaandika kila kitu anachosema Mtukufu Mtume ambapo anaongea akiwa ametulia au akiwa na hasira? Mimi nilimwambia Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kuhusu hilo.

129 Imesimuliwa katika Sahih Bukhari Jz. 4, uk. 39 130 Rejea Sahih Muslim, Jz. 2, uk. 393. 131 Sahih Muslim, Jz. 2, uk. 393. 132 Sahih al-Bukhari Jz. 4, uk. 38. 133 Sahih al-Bukhari Jz. 4, uk. 39 134 Sahih al-Bukhari Jz. 4, uk. 38 100


Abu huraira check Lubumba.qxd

7/1/2011

10:47 AM

Page 101

Abu Huraira Alielekeza kidole chake mdomoni kwake na akasema: “Andika! Naapa kwa Yule ambaye nafsi yangu iko mikononi Mwake kwamba hakuna kinachotoka hapa (kinywani) isipokuwa ukweli.” Amr bin Shu’ayb amesema kwamba baba yake alisema kwamba babu yake alisema: “Je niandike kila ninachokisikia kutoka kwako.?” Yeye (s.a.w.w.) akasema: “Ndio, fanya hivyo.” Nikasema: “Ukiwa umetulia au umechukia?” Yeye akasema: “Ndio, kwa sababu mimi siongei kabisa isipokuwa ukweli tu.”135 Mtu mmoja alimuuliza Aisha (mke wa Mtukufu Mtume) kuhusu maadili ya Mtukufu Mtume Muhammad (s.a.w.w.). Yeye akamwambia: “Je, umesoma Qur’ani?” Yule mtu akajibu: “Ndiyo, nimesoma.” Aisha akasema: “Qur’ani ndio maadili yake.” Ni kauli safi ya namna gani hii ambayo kwamba alionyesha ufasaha wake na elimu juu ya maadili hasa ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Haishangazi! Yeye alimuona, akiwa pamoja na Qur’ani mbele ya macho yake (s.a.w.w.), akiigiza kwa vitendo mwongozo wake, akitafuta mwanga ndani ya elimu za Qur’ani hiyo, akifanya ibada kwa mujibu wa amri zake na makatazo, akifanywa kuwa na tabia njema kwa elimuadili ya Qur’ani, akiwajibika kwa ajili ya hekima ya Qur’ani, akifuatilia athari zake na kuzifuatilia Sura zake. Unaweza kuyaona maadili yake katika maneno haya ya Mwenyezi Mungu: “Na wale wanaowaudhi wanaume waumini na wanawake waumini pasipo wao kufanya kosa lolote, bila shaka wamebeba dhulma kubwa na dhambi zilizo dhahiri.” (33:58) “Na wale wanaojiepusha na madhambi makubwa na mambo mabaya na wanapokasirika wanasamehe.” (42:37). “….. na wenye kuzuia ghadhabu na wenye kuwasamehe watu, na Mwenyezi Mungu hupenda wafanyao wema.” (3:134) “….. na wajinga na wakisema nao, wao husema: Amani.” (25:63). “Shikamana na kusamehe na amrisha mema na wapuuze wajinga.” (7:199) “….. zuia mabaya kwa yaliyo mema zaidi, na mara yule ambaye baina yako na yeye pana uadui atakuwa kama rafiki mkub135 Rejea kitabu cha Ibn Abdul-Birr, Jami’ Bayan al-Ilm, uk. 36. 101


Abu huraira check Lubumba.qxd

7/1/2011

10:47 AM

Page 102

Abu Huraira wa.” (41:34) “….. na mtasema na watu kwa wema…..” (2:83): “….. na jiepusheni na usemi wa uongo.” (22:30). “….. wala msiruke mipaka. Hakika Mwenyezi Mungu hawapendi warukao mipaka.” (5:87) “Na tuna nini hata tusimtegemee Mwenyezi Mungu na hali ametuonyesha njia zetu? Na lazima tutayavumilia mnayotuudhi nayo, basi kwa Mwenyezi Mungu wategemee wenye kutegemea.” (14:12) “….. na bila shaka mtasikia udhia mwingi kutoka kwa wale waliopewa Kitabu kabla yenu na wale walioshiriki. Na ikiwa mtasubiri na mkamcha Mungu basi hakika hayo ni katika mambo ya kuazimia.” (3:186) “Na uinamishe bawa lako kwa yule anayekufuata katika wale walioamini.” (26:215) “Basi kwa sababu ya rehema za Mwenyezi Mungu umekuwa laini kwao na kama ungekuwa mkali na mshupavu wa moyo wangekukimbia. Basi wasamehe na uwaombee msamaha na ushauriane nao katika mambo, na unapoazimia basi mtegemee Mwenyezi Mungu …..” (3:159). Haya yalikuwa ndio maadili ya Mtukufu Mtume Muhammad (s.a.w.w.) na uhusiano wake na waumini na wengineo mbali na waumini. Yeye alisema: “Binadamu hasa ni yule ambaye anaweza kujidhibiti mwenyewe pale anapopandwa na hasira.”136 “Yule ambaye hana huruma atanyimwa ustawi.”137 “Kama huruma itaongezwa juu ya jambo, hilo litakuwa zuri sana, lakini inapokosekana kwenye jambo, basi huwa baya sana.”138 “Mwenyezi Mungu ni mpole, anapenda upole na anawalipa watu kwa upole wao kile ambacho halipi kwa ukatili au kwa jambo lingine lolote.139 “Mwislam halisi hasa ni yule ambaye watu wako salama kutokana na ulimi wake na mkono wake.”140 Inatutosha sisi ile kauli ya Mwenyezi Mungu akimwambia Mtume Muhammad (s.a.w.w.): “Na bila shaka una tabia 136 Sahih Muslim, Jz. 2, uk. 396. 137 Sahih Muslim, Jz. 2, uk. 390. 138 Sahih Muslim, Jz. 2, uk. 390. 139 Sahih Muslim, Jz. 2, uk. 390. 140 Sahih al-Bukhari Jz. 1, uk. 6 102


Abu huraira check Lubumba.qxd

7/1/2011

10:47 AM

Page 103

Abu Huraira njema, tukufu.” (68:4). Baada ya hayo, itawezekana vipi kwa Mtume Muhammad (s.a.w.w.) kulaani, kutukana, kuchapa na kudhuru watu wasio na hatia, eti kwa sababu tu alipandwa na hasira? Mwenyezi Mungu aliepushilie mbali hilo! “Hawakumuadhimisha Mwenyezi Mungu kama anavyostahiki kuadhimishwa. …..” (22:74) “….. lakini subira ni njema, na Mwenyezi Mungu ndiye aombwaye msaada juu ya haya mnayoyasema. (12:18). Kwa kweli Hadith hii ilibuniwa katika kipindi cha utawala wa Mu’awiyah. Abu Huraira alisifu sana Mu’awiyah na familia ya Abul-Aas na Bani Umayyah waliobakia kwa Hadith hii na kuziweka kando Hadith nyingine ambazo kwazo ilithibitishwa kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alikuwa amewalaani idadi kadhaa ya wanafiki na madhalimu wa ki-Bani Umayyah, ambao waliwazuia watu katika njia ya Allah na kujaribu kuifanya imepotoka, na kuwatambulisha hao kwa fedheha ya milele na kuwafanya watu wajue kwamba walikuwa mbali sana na Allah na Mtume wake. Hivyo Uislam na umma uweze kuwa salama kutokana na unafiki wao na uharibifu. Lilikuwa ni karipio kutoka kwa Mtume (s.a.w.w.) kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, Kitabu Chake, viongozi na Waislam wa kawaida. Wakati mmoja Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) aliwahi kuona katika ndoto kwamba familia ya al-Hakam bin Abul-Aass walikuwa wakirukaruka kwenye mimbari yake kama manyani na kuwazuia watu na kuwarudisha nyuma. Baada ya hapo hakuwahi kuonekana akitabasamu hadi alipofariki dunia.141 Mwenyezi Mungu alimshushia Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) aya ya Qur’ani, ambayo ilisomwa na Waislam usiku na mchana, ikizungumza kuhusu hilo: “….. Na hatukuifanya ndoto ile tuliyokuonyesha ila kwa kuwajaribu watu, na pia ule mti uliolaaniwa katika Qur’ani. Na tunawahadharisha laini haiwazidishii ila uasi mkubwa.” (17:60). Huo mti uliolaaniwa, ambao umetajwa ndani ya Qur’ani ulikuwa ni familia ya Umayyah. Mwenyezi Mungu alimfahamisha Mtume (s.a.w.w) kwamba wao watakuja kuchukua nafasi yake, kuwaua kizazi chake na kuuharibu 141 al-Mustadrak al-Hakiim, Jz. 4, uk. 480 103


Abu huraira check Lubumba.qxd

7/1/2011

10:47 AM

Page 104

Abu Huraira umma. Kwa sababu ya hilo, yeye hakuonekana akitabasamu hadi alipojiunga na Mwenyezi Aliye juu Zaidi – Allah swt. Ilikuwa ni moja ya ishara za utume wake na Uislam. Kulikuwa na Hadith nyingi za kweli na sahihi, hususan kutoka kwa Maimam Maasumina zinazozungumzia kadhia hii. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alitangaza habari ya wanafiki hawa kwamba: “Yule atakayeangamia ataangamia kwa ushahidi wa wazi, na yule atakayeishi ataishi kwa ushahidi wa wazi – na hakuna lililo wajibu kwa Nabii bali uwasilishaji wa dhahiri na wazi wa ujumbe wenyewe.” Wakati mmoja al-Hakam bin Abul-Aass aliomba ruhusa ya kukutana na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Mtume alimtambua yeye mwenyewe na sauti yake pia. Yeye (s.a.w.w.) akasema:142 “Mruhusuni aingie ndani! Laana iwe juu yake na juu ya kila mmoja katika kizazi chake isipokuwa walio waumini143 miongoni mwao na ni wachache kiasi gani watakavyokuwa! Wataheshimika katika maisha ya dunia na kisha duni kabisa katika Akhera. Wao wamejaa hila na udanganyifu. Wamepewa kila kitu katika maisha haya lakini hawatakuwa na fungu japo chembe la wema katika Akhera.” Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amesema:144 “Kama familia ya Abul-Aass watafikia wanaume thelathini, watagawana mali ya Waislam miongoni mwao, na kuwafanya watu kuwa watumwa wao na kuichafua dini ya 142 al-Mustadrak al-Hakiim, Jz. 4, uk. 481 143 Maskini muumini huyu hakuwa na nafasi, kwa mujibu wa Hadith ya Abu Huraira, ya kuwa karibu na Allah au kupata sehemu ya huruma, ambapo Mtume (s.a.w.w.) alimtoa katika laana hii, ambapo watetezi wa Abu Huraira walipendelea kwamba asingetolewa na walitegemea kama Mtume alikuwa amewalaani wao na baba zao kuwa toba kwa ajili ya dhambi zao na sababu ya kuwafanya wawe karibu na Allah swt. 144 Rejea Mustadrak al-Hakiim, Jz. 4, uk. 480

104


Abu huraira check Lubumba.qxd

7/1/2011

10:47 AM

Page 105

Abu Huraira Mwenyezi Mungu kulingana na maslahi yao.” Vile vile amesema (s.a.w.w.): “Kama Bani Umayyah watafikia wanaume arobaini watawafanya watu kuwa watumwa, na watachukua mali ya Waislam kama mali yao na kuibadilisha Qur’ani ili isimamie maslahi yao.”145 Kama kila mmoja alijaaliwa kupata kuzaliwa mtoto, walimpeleka kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) ili apate kumuombea. Wakati Marwan bin alHakam alipozaliwa, walimpeleka kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Mtume (s.a.w.w.) akasema: “Mtoeni nje huyu mjusi na mtoto wa mjusi, mlaaniwa na mtoto wa aliyelaaniwa.”146 Naye Aisha (mke wa Mtukufu Mtume) amesema: “Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alimlaani baba yake Marwan na hapo Marwan mwenyewe alikuwa hajazaliwa bado. Hivyo Marwan alijumuishwa katika laana ya Mwenyezi Mungu.”147 Ash-Shi’bi amesema kwamba Abdullah ibn Zubeir alisema: “Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alimlaani al-Hakam, baba yake Marwan, pamoja na wanawe.”148 Vitabu vya Hadith vimesimulia riwaya hizi zenye kujirudia rudia na nyingine mfano wa hizo. Vimethibitisha kwamba Bani Umayyah walikuwa wamelaaniwa na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Al-Hakiim ameitaja katika kitabu chake al-Mustadrak, katika mlango wa al-Fittan wal-Malahim (uhaini na ushupavu) riwaya za kutosha za namna hii, ambazo zilikuwa ni ujumbe mzuri kwa wenye busara kutafakari juu yake. Alihitimisha mlango huo kwa kusema: “Hebu watafiti juu ya haki wajue kwamba sikusimulia katika mlango huu, theluthi moja nzima ya yale yaliyosimuliwa kuhusu hili. Uhaini wa kwanza kabisa katika umma huu ulikuwa ni uchochezi wa 145 Mustadrak al-Hakiim, Jz. 4, uk. 479 146 Mustadrak al-Hakiim, Jz. 4, uk. 479 147 Mustadrak al-Hakiim, Jz. 4, uk. 481 148 Mustadrak al-Hakiim, Jz. 4, uk. 481 105


Abu huraira check Lubumba.qxd

7/1/2011

10:47 AM

Page 106

Abu Huraira Bani Umayyah. Sikuweza kukikamilisha kitabu hiki bila kuwataja wao.”149 Hili lilitosha kuthibitisha kile tulichokisema kwamba wao walibuni Hadith hii na nyingine kama hii ili kuziweka kando zile laana zilizotolewa na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) juu yao. Lakini kwa bahati mbaya umma uliwapendelea wale wanafiki waliolaaniwa dhidi ya kumpendelea Mtume wao bila ya wao kujitambua, pale walipoutetea ushirikina huu wa kuhifadhi umaarufu wa wale waliolaaniwa. Hawakujali kabisa kwamba wao walifanya makosa kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Umma haukuwa na sababu ya kulinda hadhi ya wale ambao Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alikuwa amewalaani na kuwahamisha kwa kuwafukuza kwa kutokana na udhalimu wao. Umma ulipoteza, kwa kufanya hivyo, yale manufaa au faida ambayo Mtume aliwatakia kwa kuwalaani na kuwafukuza wale wanafiki, ambao walibiringisha yale mawe katika usiku wa alAqaba ili kumpagawisha Mtume na kumtupa chini wakati alipokuwa akirejea kutoka kwenye vita vya Tabuuk. Ilikuwa ni kisa kirefu cha kweli, ambamo ilielezwa kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) aliwalaani katika wakati huo.150 Ilikuwa ni ajabu sana kwa Waislam kuwatetea watu wale, ambao walisababisha machungu mengi sana kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na waliojaribu kwa uwezo wao wote kulipiza kisasi! Walimdhuru yeye na waliid149 Mustadrak al-Hakiim, Jz. 4, uk. 481 – Ilikuwa ni wazi kutokana na hotuba yake kwamba alikuwa na hofu na watu wa kawaida (Ummah wa ki-Sunni) kuikataa Hadith hii aliyoitaja, lakini akawaomba radhi kwamba hakuweza kukamilisha kitabu chake bila ya kuwataja. Ndipo nikajua kile alichomaanisha yule mshairi mmoja aliposema: “Waislam hawakuwa ummah wa Muhammad, bali walikuwa ummah wa maadui zake.” 150 Rejea Musnad Ahmad Hanbal, Jz. 2. 106


Abu huraira check Lubumba.qxd

7/1/2011

10:47 AM

Page 107

Abu Huraira huru familia yake baada ya kifo chake.151 Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) aliwalaani na kuwaondoa kwenye neema ya Allah na kuwafanya waumini wawaepuke kwa sababu ya kile walichokitenda na ambacho wangeweza kufanya baadae, na wasiwafanya wao kuwa karibu na Mwenyezi Mungu kama hao waharibifu walivyosema. 15. Shetani aja kukatiza Swala za Mtukufu Mtume (s.a.w.w.): Masheikh hao wawili, Bukhari na Muslim, wamesimulia kwamba Abu Huraira alisema: “Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alitekeleza moja ya swala 151 Az-Zubayr ibn Bukar alitaja kisa kilichotokea Damascus baina ya Imam Hasan (a.s.) na wapinzani wake; Mu’awiyah, ndugu yake Utba, Ibn Aass, Ibn Uqba na ibn Shu’ba. Mabishano kati yao yalikuwa ni makali sana. Jambo ambalo kwamba Imam Hasan alikuwa amesema wakati huo lilikuwa: “Mnajua wazi kabisa kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alikuwa amemlaani Abu Sufyan (baba yake Mu’awiyah) kwa namna saba ambazo hamuwezi kuzikanusha.” Alizitaja namna zote, moja baada ya nyingine kisha akamwambia Amr bin Aass: “Wewe na watu wote hawa mnajua kwamba mlimdhihaki Mtukufu Mtume kwa beti sabini za mashairi na Mtume akasema: Ewe Allah! Wewe unajua kwamba mimi sisemi ushairi, na sitafanya hivyo. Oh, Allah, mlaani huyu kwa kila herufi ya shairi lake laana elfu moja, hivyo kuna laana zisizo na idadi kutoka kwa Mwenyezi Mungu juu yenu.” Rejea Sharh Nahjul-Balaghah ya al-Hamiidi, Jz. 2, uk. 104, at-Tabrasi katika kitabu chake, al-Ihtijaj, al-Majlisi katika Bihar yake, na wengine, Sunni na Shi’ah. Muslim amesimulia katika Sahih yake Jz. 2, uk. 392 kwamba ibn Abbas amesema: “Mtume alinituma nimuite Mu’awiyah aje kwake. Nilirudi na kumwambia Mtukufu Mtume: Mu’awiyah anakula. Mtume akasema: Nenda kamwite! Nilirudi nikasema: Anakula. Mtume akasema: Mwenyezi Mungu asilishibisha tumbo lake!” Ndani ya vitabu vyetu (vya ki-Shi’ah) kuhusu riwaya hii ilisimuliwa kwamba ibn Abbas alisema kwamba hapo Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alimlaani Mu’awiyah. Lililothibitisha hilo ni kwamba Muslim aliisimulia riwaya hii katika Sahih yake, lakini waliigeuza Hadith hiyo ili kulinda heshima ya wanafiki hao. 107


Abu huraira check Lubumba.qxd

7/1/2011

10:47 AM

Page 108

Abu Huraira zake na akasema: ‘Shetani alinijia na akajaribu kiasi alivyoweza ili kukatisha swala yangu. Allah alinisaidia mimi na kwamba niliweza kumkaba. Nilitaka kumfunga kwenye nguzo ili muweze kumuona wakati wa asubuhi, lakini nikakumbuka kauli ya Suleiman:

“Akasema: Mola Wangu! nisamehe na unipe ufalme, asiupate yeyote baada yangu, bila shaka Wewe ndiye Mpaji.” 38:35. 152 Manabii walikuwa mbali sana na hilo na walijitenga nalo kwa sababu lilipingana na umaasum wao na liliharibu hadhi na cheo chao cha hali ya juu. Mungu aepushilie mbali hilo! Hivi shetani angeweza kugombana na manabii au kuwasumbua au hata kulifikiria hilo? Mwenyezi Mungu alisema kumwambia Shetani:

“Hakika (kuhusu) waja Wangu, wewe hutakuwa na mamlaka juu yao, isipokuwa yule mwenye kukufuata katika wapotovu.” 15:42 Waislam wote walijua kwamba shetani alichanganyikiwa kwa kuzaliwa Mtukufu Mtume Muhammad (s.a.w.w.), kushangazwa kwa kuteuliwa kwake kuwa Mtume, akafadhaishwa na hijra, akawa mbumbumbu kwa kuinukia kwake pamoja na ujumbe, akayeyuka kama chumvi katika maji kwa muongozo wake, sheria na mifumo yake, aliruka kama mwonzi kutoka kwenye ibada yake, ambamo Mwenyezi Mungu alikuwa ameweka kanuni na siri ambazo ziliifanya (swala/ibada) kumzuia kutokana na kutenda maovu na matendo ya kuchukiza. 152 Rejea Sahih Bukhari, Jz. 1, uk. 143; Sahih Muslim, Jz. 1, uk. 204 na Musnad Ahmad, Jz. 2, uk.298 108


Abu huraira check Lubumba.qxd

7/1/2011

10:47 AM

Page 109

Abu Huraira Wakati Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) aliposimama kwa ajili ya swala, aliachana na kila kitu na kuugeuzia moyo wake kutoka kwenye kila jambo mbali na Mwenyezi Mungu. Alisimamisha swala yake kwa moyo mtulivu katika utumwa kwenye Upweke Wake, Mmoja na wa Pekee. Pale alipoanza swala yake kwa Allahu-Akbar, angeomba ulinzi wa Allah kutokana na Shetani kabla ya kusoma aya za Qur’ani kwa kutii kauli ya Mwenyezi Mungu:

“Na unapotaka kusoma Qur’ani, basi jikinge kwa Mwenyezi Mungu kutokana na Shetani afukuzwaye.” 16:98 Kwa kweli, pale alipoomba ulinzi wa Allah kutokana na Shetani, Mwenyezi Mungu humpatia ulinzi huo. Shetani alilijua vyema jambo hili hata kama hao wenye upungufu wa akili watalipuuza hilo! Abu Huraira alisimulia Hadith153 akisema kwamba kama shetani akisikia Adhana kutoka kwa Mwislam yeyote, angekimbia kwa woga na angetoa mashuzi kwa hofu. Hivyo angewezaje shetani kuthubutu kusogelea karibu na Mtume, ambaye alikuwa mtiifu kwa Allah, alisimama mbele Yake kwa swala ya uaminifu na kuomba hifadhi Yake? Ni vipi ambavyo shetani aliitafsiri swala ya Mtukufu Mtume? Kwa nini hakukimbia kwa woga na kutoa mashuzi kwake? Ni kiasi gani ambavyo hili lilikuwa haliwezekani! Mwenyezi Mungu amesema:

153 Rejea Sahih Bukhari, Jz. 1, uk. 78; na Sahih Muslim, Jz. 1, uk.153 109


Abu huraira check Lubumba.qxd

7/1/2011

10:47 AM

Page 110

Abu Huraira “Hakika yeye (shetani) hana mamlaka juu ya wale walioamini na wanaomtegemea Mola wao. Nguvu yake iko juu ya wale wanaomfanya kiongozi na wanaomshirikisha Mwenyezi Mungu. 16:99-100. Kama ukisema: “Unasemaje kuhusu aya hii ya Qur’ani:

“Na kama shetani akikushawishi kwa tash’wishi, basi jikinge kwa Mwenyezi Mungu, bila shaka Yeye ni Mwenye kusikia na Mwenye kujua.” 41:36. Sisi tunasema: “Mwenyezi Mungu, aliye Mtukufu alikuwa amemfundisha kipenzi Chake Muhammad maadili, ambayo kwayo Yeye alimfadhilisha kwenye ulimwengu wote kwamba kila Nabii, Malaika, shetani na wanadamu wameukiri upole wake na wamesalimu amri kwenye maadili yake. Hakukuwa na amri ndani ya Qur’ani isipokuwa yeye aliitii, na hakuna katazo lolote isipokuwa alikubaliana nalo, au kanuni isipokuwa aliizingatia akilini. Qur’ani ilikuwa mbele ya macho yake. Aliyaandama malengo yake na kuzifuata Sura zake. Hiyo aya hapo juu ilihusu upole wake na maadili yake, na vile vile aya zilizokuwa kabla ya hiyo katika Sura hiyo hiyo: “….. Zuia mabaya kwa yaliyo mema zaidi, na mara yule ambaye baina yako na yeye pana uadui atakuwa kama rafiki mkubwa. Na hakuna atakayepewa (jambo hili) ila wale wanaosubiri, wala hawatapewa ila wenye bahati kubwa.” 41:34-35 Haya yalikuwa ndio bora ya maadili ambayo Mwenyezi Mungu alikuwa amemfundisha mja na mtume Wake (s.a.w.w.). Yeye, kwa kweli, alikuwa hivyo tangu mwanzo wa ujumbe wake wakati aliposema, huku damu ikichirizika kwenye uso wake na ndevu zake: “Ewe Mola! waongoze watu wangu kwani hawaujui ukweli,” mpaka pale mpiga mbiu wake alipopiga mbiu mnamo siku ya Fat’hu – ushindi, wakati wa kutekwa Makka, na 110


Abu huraira check Lubumba.qxd

7/1/2011

10:47 AM

Page 111

Abu Huraira alikuwa katika siku zake za mwisho za uhai wake kwamba yeyote atakayeingia kwenye nyumba ya Abu Sufyan atakuwa yuko salama. Mwenyezi Mungu alikuwa amezisawazisha njia zote za kumfanya Mtume Wake kuyahimili maadili haya, ambayo yalifanya shingo kuinama kwa utukufu wa mwenendo wake na heshima ya tabia zake. Mwenyezi Mungu hakumfanya tu aweze kuhimili maadili haya, lakini pia alimuacha nayo kwa muda mrefu mpaka akafikia kiwangocha hadhi ya hali ya juu sana na kuwa na bahati na maadili haya. Hivyo Yeye amesema: “Na hakuna atakayepewa (jambo hili) ila wale wanaosubiri, wala hawatapewa ila wenye bahati kubwa.” 41:35. Kisha Mwenyezi Mungu akamuonya kutokana na uchochezi wa hasira, ambazo Mwenyezi Mungu aliwaumba binadamu pamoja nazo, na ghadhabu za moyo wakati mtu anapoudhishwa na adui yake. Allah aliita hali hiyo kuwa ni kichochezi au muingilio wa shetani, kiistiari, ili kumfanya Mtume kuiepuka na kuwa mbali nayo. Hivyo Allah akasema: “Na kama shetani akikushawishi kwa tash’wishi, basi jikinge kwa Mwenyezi Mungu, bila shaka Yeye ni Mwenye kusikia na Mwenye kujua.” 41:36. Ilikuwa na maana kwamba kama ushawishi wa hasira, ambao unaweza kuwa kama uchochezi wa kishetani, unaweza kukufanya wewe usitulie au kuwa na wasiwasi, basi wewe utafute hifadhi kwa Mwenyezi Mungu. Katika jambo hilo hilo kulikuwa na kauli ya Mwenyezi Mungu: “Shikamana na kusamehe na amrisha mema na wapuuze wajinga. Na kama wasiwasi wa shetani ukikusumbua, basi jikinge kwa Mwenyezi Mungu kwa sababu yeye ndiye Asikiaye, Ajuaye.” 7:199-200. Mwenyezi Mungu alitaka kumuweka mbali kipenzi chake kutokana na kukabiliana na wajinga, ambao waliona ushahidi lakini waliukana na wakazidi sana katika ukafiri wao, hivyo Yeye akamuamuru kuwaepuka na kuwapuuza hao. Na kwa uangalifu zaidi katika kumuelimisha na kumfadhilisha Mtukufu Mtume juu ya wanadamu wote. Mwenyezi Mungu alimuonya asiweke kinyongo chochote au chuki moyoni mwake wakati wajinga watakapomshambulia na ujinga wao na lugha chafu. Mwenyezi Mungu aliita hisia hii ya kawaida kama kishawishi au kichochezi cha shetani kiistiari, ili kumfanya Mtume Wake kuikwepa na 111


Abu huraira check Lubumba.qxd

7/1/2011

10:47 AM

Page 112

Abu Huraira kuiepuka, kwa sababu Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) hakuepuka kitu chochote zaidi ya kumuepuka kwake shetani na vitendo ambavyo vilikuwa kama vya shetani. Mwenyezi Mungu alitaka, kwa kutamka aya hii, kumwambia Mtume kuwa na subira mbele ya wajinga na sio kuwa na hasira nao. Sasa ilikuwa wapi maana hii kutoka kwenye kile alichokisema Abu Huraira kwamba Shetani alimshambulia Mtume na kuvuruga swala yake, ambayo ilikuwa haikubaliki kwa mujibu wa akili na mazingatio ya kidesturi? Kama ungesema: Vipi kuhusu aya hizi za Qur’ani: “Na hatukumtuma kabla yako Mtume wala Nabii ila anaposoma, shetai alitia fitina masomo yake. Lakini Mwenyezi Mungu huondoa anayoyatia shetani, kisha Mwenyezi Mungu huzimakinisha aya Zake, na Mwenyezi Mungu ni Mjuzi, Mwenye hekima. Ili alifanye lile analotia shetani kuwa ni fitna kwa wale wenye maradhi nyoyoni mwao na ambao nyoyo zao ni ngumu, na bila shaka madhalimu wamo katika uhalifu wa mbali. Na ili wajue wale waliopewa elimu kwamba hiyo ni haki iliyotoka kwa Mola wako …..” 22:52-54. Ilikuwa ikifahamika vema, kama umuhimu wa Uislam, kwamba Mtume Muhammad (s.a.w.w.) pamoja na manabii wengine wote wasingetumainia jambo lolote ambalo Mwenyezi Mungu hakubaliani nalo. Mitume wote walikuwa wameepukana mbali sana na jambo lolote ambalo halimridhishi Mwenyezi Mungu na ambalo lilikuwa haliwanufaishi watu. Mtume Muhammad alitumaini kwamba kila mtu, mahali popote duniani, kuamini na kuwa mtiifu kwa Mwenyezi Mungu. Shetani, kwa hila zake na vishawishi aliyavuruga matumaini haya na akawashawishi watu kama Abu Lahabi (ami yake Mtume) na Abu Jahal, ambao walishikiliwa na yeye, na kuwaelekeza mbali kabisa na kile alichowatumainia Mtume kupata mema ya dunia hii na ya Akhera. Lakini shetani aliwashawishi mpaka wakampiga vita Mtume ili kumuondoa kabisa. 112


Abu huraira check Lubumba.qxd

7/1/2011

10:47 AM

Page 113

Abu Huraira Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alitegemea kwa kila mtu ambaye alikuwa Mwislam kuwa mwaminifu kwa Mwenyezi Mungu, Qur’ani yake, Mtume wake na kwa watu wote kwa namna ambayo undani wake utakuwa kama udhahiri wake na uwazi wake wake kama usiri wake. Shetani aliwachombeza baadhi ya watu na kuwachanganya akili zao kwa kuyaharibu mategemeo haya matukufu, hivyo wakawa wanafiki. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alimtegemea kila mmoja katika umma wake kuiga utaratibu wake ulionyooka, na sio kukengeuka kutoka kwenye Sunna yake tukufu. Yote aliyotegemea ni kwamba umma wote ungekubaliana na mwongozo na kuendeshwa kwa mujibu wa amri na makatazo yake na kwamba hakuna wawili kati yao watakaogombana. Lakini shetani aliwanong’oneza uovu na kuwadanganya wao kuwa mbali na Sunna. Hivyo umma huo huo mmoja ukagawanyika katika matapo mengi chungu nzima. Shetani mdanganyifu aliyelaaniwa alijaribu kwa uwezo wake wote kuharibu yote Mtume aliyoyategemea kwa ajili ya watu na akawafanya wale ambao wameshawishika naye kugeukia mbali na Mtukufu Mtume na matumaini yake. Wale wote waliodanganyika na uwongo wa shetani walikuwa wengi mno. Yeye shetani aliandaa mitego na njama zake juu yao na akasimama tayari kuwaonyesha ukweli kwa vishawishi vyake, kuwa ni uongo na uongo kuwa ni kweli. Alitumia kila ujanja kuvuruga matumaini ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na kuwaelekeza watu mbali na yeye. Yote hayo yalimsumbua Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na kumfanya awe na wasiwasi na wakati wote kuwahofia watu kutokana na udanganyifu wa shetani. Aliogopa kwamba maasi na udanyanyifu vitaweza kuushinda ukweli. Kwa sababu ya hilo, Mwenyezi Mungu alimliwaza na kumtuliza kwa kumfunulia:

113


Abu huraira check Lubumba.qxd

7/1/2011

10:47 AM

Page 114

Abu Huraira

“Na hatukumtuma kabla yako Mtume wala Nabii ila anaposoma, shetani alitia fitina masomo yake. Lakini Mwenyezi Mungu huondoa anayoyatia shetani, kisha Mwenyezi Mungu huzimakinisha aya Zake, na Mwenyezi Mungu ni Mjuzi, Mwenye hekima.” 22:52. Ilimaanisha kwamba kila Nabii alipotumainia matakwa kwa ajili ya manufaa binafsi ama ya jumla, shetani angeyaharibu matamanio yake kwa kuwashawishi na kuwadanganya watu kuwaweka mbali na Mitume na ujumbe na kazi zao. Mitume wote walitumaini kwamba watu wote kila mahali juu ya ardhi wawe watiifu kwa Mwenyezi Mungu. Walitegemea kwamba waumini watakuwa na uaminifu halisi kwa Allah. Matamanio yao bora yalikuwa kwamba wazione kaumu zao zikikubaliana na miongozo yao na kusiwe na japo wawili wao wanaohitilafiana. Lakini shetani aliyapinga matamanio yao kwa kuwadanganya watu na kugeuza ukweli wa mambo. Hivyo kaumu ya Musa iligawanyika matapo sabini na moja, kaumu ya Isa ikagawanyika matapo sabini na mbili na kadhalika vivyo hivyo kwa kauma za Manabii wengine waliobaki. Oh, Muhammad, usiwe na wasiwasi sana kuhusu kushindwa kwa matumaini yako matukufu kwa mara nyingi na shetani kwa sababu matumaini ya Manabii waliotangulia yalikabiliana na majaaliwa kama hayo. Kwa hiyo wewe na wao mko sawa katika suala hili.

“Ndio desturi (Yetu) juu ya wale tuliowatuma kabla yako katika mitume wetu, wala hutapata mabadiliko katika desturi Yetu.” 17:77. 114


Abu huraira check Lubumba.qxd

7/1/2011

10:47 AM

Page 115

Abu Huraira Kwa vile Mtukufu Mtume Muhammad (s.a.w.w.) alihofia kwamba maasi ya shetani yanaweza yakashinda ukweli na haki, Mwenyezi Mungu akamhakikishia usalama pale aliposema: “Lakini Mwenyezi Mungu huondoa anayoyatia shetani, katika matumaini yako na matumaini ya mitume waliopita kabla yako. Lakini Mwenyezi Mungu alimuashiria kwamba ile haki, ambayo yeye na manabii waliopita waliileta kutoka kwa Mola wao itatawala. Mwenyezi Mungu amesema: “Kisha Allah anaimarisha mawasiliano yake” na “Mwenyezi Mungu ataidhihirisha haki kwamba ni haki kwa maneno yake japo waovu wachukie” 10:82 na “….. Basi lile povu litapita kama takataka, lakini vile vinavyowafaa watu vinakaa katika ardhi. Hivyo ndivyo Mwenyezi Mungu anavyopiga mifano.” 13:17 Mwenyezi Mungu alimtaka Mtume kuwa na uhakika kwamba manabii watashinda na shetani atashindwa. Amesema: “Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujua, Mwenye hekima.” Aliutambua uaminifu wa Mitume (a.s.) katika matamanio yao, kwa hiyo Yeye aliwasaidia kwa Roho Tukufu na akawaweka katika nafasi zao za kuheshimika na aliujua uadui wa Shetani kwa Mwenyezi Mungu na Mitume Wake. Kwa hakika Mwenyezi Mungu atamdhalilisha shetani kwa vitendo vyake viovu kutokana na hekima kwamba awatukuze wale wanaostahiki heshima, na kuwadhalilisha wale wanaostahili kuaibishwa kwani hekima ilikuwa ni kuweka mambo katika hali na nafasi zao stahilifu. Mwenyezi Mungu alitaka kuwatofautisha wale waovu na wema miongoni mwa watu Wake kwa hiyo aliwatahini kupitia shetani: “Yeye ataifanya ile minong’ono ya shetani kuwa ni mtihani kwa wale ambao nyoyoni mwao kuna maradhi” kwa sababu ya unafiki “na wale ambao nyoyo zao ni ngumu” ambazo hazikulainika kwa kumtaja Allah na yale aliyoyateremsha kwa sababu nyoyo zao zilitawaliwa na ukafiri ambao shetani aliwashawishi nao na akawaweka mbali na imani na muongozo, “na kwa hakika wale madhalimu” miongoni mwa wanafiki na makafiri “wamo kwenye upinzani mkubwa” kwa Mwenyezi Mungu na Mtume Wake. 115


Abu huraira check Lubumba.qxd

7/1/2011

10:47 AM

Page 116

Abu Huraira Macho yao hayakuiona haki, masikio yao yakawa viziwi na nyoyo zao zilikaliwa na shetani. Walitoa milio kila wakati palipokuwa na muovu mwenye kutoa milio (kama ya kunguru). “Na kwamba wale ambao wamepewa elimu waweze kujua” juu ya Upweke wa Allah, Hekima Yake na kutuma kwake Mitume “kwamba ni ukweli kutoka kwa Mola Wako hivyo waweze kuuamini” bila ya kutoa mazingatio yoyote kwa shetani au kwenye kutishia na kupoteza kwake. Pale Mwenyezi Mungu alipowajaribu watu ili kutofautisha kati ya waovu na wema, nyoyo za wale waovu (wenye mioyo migumu) zikawa ngumu zaidi na waumini wakawa na nguvu zaidi katika imani zao na uhakika. Mwenyezi Mungu akasema:

“Je, watu wanadhani wataachwa waseme tumeamini, nao wasijaribiwe? Na bila shaka tuliwajaribu wale walikuwa kabla yao, na kwa hakika Mwenyezi Mungu atawatambulisha wale waongo.” 29:2-3,

“Hakuwa Mwenyezi Mungu Mwenye kuwaacha waumini katika hali mliyonayo mpaka apambanue wabaya na wazuri.” 3:179

“Na ili Mwenyezi Mungu awatakase walioamini na awaangamize makafiri.” 3:141. Sio ajabu kwamba Mwenyezi Mungu atawajaribu watu kwa mateso na huzuni mbali mbali ili kupata sababu ya kuwapa thawabu au kuwaadhibu. Mwenyezi Mungu anasema: “….. Basi Mwenyezi Mungu ndiye hoja ikomeshayo, na kama angependa angewaongozeni nyote.” 6:149 na “….. ili aangamiaye aangamie kwa dalili dhahiri na asalimike wa kusalimika kwa dalili dhahiri…..” 8:42 116


Abu huraira check Lubumba.qxd

7/1/2011

10:47 AM

Page 117

Abu Huraira Ngoja turudi kwenye aya hiyo hiyo “Na hatukutuma kabla yako Mtume wala Nabii ila anapotamani, shetani alitia fitina matamanio yake.” Haikuwa na maana kwamba shetani alitia fitina yake katika moyo wa Mtume (Mungu aepushilie mbali!) bali ilimaanisha kwamba shetani alitia fitina yake katika yale matakwa ya Mtume kwa kuyaharibu ili kuwafanya wafuasi wake, yeye shetani, ambao wanatoa milio pamoja naye, wageuzie migongo kile Mtume alichotarajia ili kwamba hayo matumaini yake yasitimie. Hii hasa ndio ilikuwa maana ya aya hiyo, ambayo iligonga akili, ingawa hakuna hata mmoja kati ya wafasiri au mwingine yeyote kama ninavyojua – ambaye ameielezea. Ninashangaa ni vipi wameikosa hii ambapo ilikuwa ndio yenye kufaa zaidi kwa Qur’ani, kwa Mtume Muhammad (s.a.w.w.) na kwa manabii wengine wote (amani iwe juu yao). Haiwezi kufasiriwa kwa namna nyingine yoyote mbali na hiyo hata kidogo.154 Hebu turudi kwenye ile Hadith ya Abu Huraira: “Mtukufu Mtume alitekeleza moja ya swala zake na akasema: Shetani amenijia akijaribu kwa juhudi zake zote kuivuruga swala yangu. Mwenyezi Mungu akanisaidia kiasi nikaweza kumkaba. Nilitaka nimfunge kwenye nguzo ili muweze kumuona wakati wa asubuhi, lakini nikakumbuka kauli ya Suleimani: “Akasema: Mola Wangu! nisamehe na unipe ufalme, asiupate yeyote baada yangu…..” 38:35. Ningependa kuwauliza hawa masheikh wawili, ambao waliiheshimu na kuitetea Hadithi ya Abu Huraira; je huyo shetani alikuwa umbile la kimwili ambalo lingeweza kufungwa kwenye nguzo kama mfungwa aliyekamatwa ili aonwe na watu wakati wa asubuhi? Sidhani kwamba yeyote anaweza kusema hivyo. Kilichomhimiza Abu Huraira kusema hivyo kilikuwa ni kushindwa kwa akili yake kuielewa maana ya Qur’ani. Alidhani kwamba baadhi ya aya za 154 Niliielezea tafsiri hii katika gazeti la al-Irfan, toleo la 31, uk.113 na kurasa zinazofuatia. 117


Abu huraira check Lubumba.qxd

7/1/2011

10:47 AM

Page 118

Abu Huraira Qur’ani zilihisi mambo kama hayo pale aliposikia kauli ya Mwenyezi Mungu akizungumza kuhusu Suleiman (a.s.): “Basi tukamtishia upepo ukaenda polepole kwa amri yake kule anakotaka kufika. Na mashetani (pia tukamtiishia) kila ajengaye na azamiaye. Na wengine wafungwao minyororoni.” 38:36-38. Yeye alidhani walikuwa wamefungwa kwenye minyororo kama wanadamu. Hakuelewa kwamba walifungwa kwa mujibu wa ulimwengu wao wa kishetani kwa minyororo inayoendana na hali yao ya kishetani ili kuwazuia wao kutokana na kuangamiza ambapo hakuna hata mmoja wa wanadamu aliyeweza kuwaona. Abu Huraira amesema katika riwaya yake kwamba Mtume Muhammad (s.a.w.w.) alimuachia huru shetani huyo kwa sababu alikuwa amechukia kuwa na ufalme kama ule wa Suleimani (a.s.). Abu Huraira alisahau kwamba Mwenyezi Mungu alikuwa amempa Suleiman ufalme ambamo alitiisha kwa ajili yake upepo, ambao ulifanya safari ya mwezi mzima wakati wa asubuhi na safari ya mwezi mzima wakati wa jioni. Mwenyezi Mungu alitengeneza chemchemi ya shaba iliyoyeyushwa kumiminika kwa ajili ya Suleiman, na “miongoni mwa Majini walikuwepo wale ambao walifanya kazi mbele yake kwa amri ya Mola Wake; na yeyote aliyekiuka amri yetu kutoka miongoni mwao, tulimfanya aonje adhabu ya kuungua.” Majini walimjengea Suleiman ngome kadhaa, sanaa za uchongaji, mabakuli na vyungu vya kupikia. Mwenyezi Mungu alikuwa amempa Suleiman (a.s.) ambacho hakumpa Mtume Muhammad (s.a.w.w.). Hata kama Mtume Muhammad alimfunga shetani wa Abu Huraira, asingeweza kuwa sawa na Suleiman katika ufalme wake, kwani Suleiman alikuwa na kioja cha upepo, kumiminika kwa shaba iliyoyeyushwa na kufanya kazi kwa wale majini. Uthibitisho alioutoa Abu Huraira ulikuwa batili na Hadith yake ilikuwa ya uongo. Mtukufu Mtume asingeweza kamwe kuchanganyikiwa na akili au kubumbuaza hisia. Mtume (s.a.w.w.) alitegea mantiki katika hoja zake na katika kila jambo. Aliifanya mantiki kuwa ndio muamuzi kati ya haki na batili na alifanya uthamini wa ushahidi mbalimbali kuwa kwa mujibu wa Qur’ani tukufu, 118


Abu huraira check Lubumba.qxd

7/1/2011

10:47 AM

Page 119

Abu Huraira ambayo alituamuru kuifuata: “Je anayekwwenda kufudifudi kwa uso wake ni mwongofu zaidi au anayekwenda sawasawa katika njia iliyonyooka? 16. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) anaikosa swala ya Asubuhi (Fajr): Masheikh hawa wawili wamesimulia kwamba155 Abu Huraira alisema: “Tulisafiri wakati wa usiku pamoja na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na tukachelewesha sana wakati wa kulala. Hatukuamka mpaka jua likachomoza. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akasema: “Kila mmoja naaongoze kipando chake na tuondoke hapa. Ilikuwa ni mahali palipohudhuriwa na Shetani.” Tukafanya hivyo. Kisha akaomba maji ya kufanyia udhuu. Akafanya sijida mbili halafu akaiswali swala hiyo asubuhi kabisa.’” Mwongozo wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) ulikuwa mbali kabisa na Hadith kama hii. Mwenyezi Mungu amesema: Ewe Iliyejifunika nguo, simama usiku ila kidogo. Nusu yake au ipunguze kidogo. Au izidishe na uisome Qur’ani kwa vizuri.” Mpaka pale aliposema: “Kwa hakika Mola Wako anajua kwamba wewe husimama kumuabudu karibu na theluthi mbili za usiku, na wakati mwingine nusu yake…..” 73:20 Mwenyezi Mungu alizungumza na Mtume katika kauli nyingine: “Simamisha swala jua linapopinduka mpaka giza la usiku, na kusoma Qur’ani alfajiri. Hakika (kusoma) Qur’ani alfajiri kunashuhudiwa.156 Na katika usiku amka (kusoma Qur’ani) kwa kutahajudi kwayo, ni ibada zaidi kwako. 155 Hii imenukuliwa kutoka kwenye Sahih Muslim, Jz. 1, uk. 254 156 Mwenyezi Mungu aliifanya aya hii kuonyesha nyakati za swala. Dhuhr na Asri kuswaliwa katika muda wa kuanzia mchana hadi jua linapozama, lakini swala ya Dhuhr ilikuwa iwe kabla ya Al-Asr. Na swala za Magharibi na Isha kuswaliwa kuanzia wakati jua linapozama hadi giza la usiku wa manane lakini Magharibi itangulie kabla ya Isha. Mwenyezi Mungu pia akaitaja swala ya al-Fajr katika aya hiyo kutangaza kwamba swala hizo zilikuwa ni wajibu na kutamka nyakati za kuziswali. 119


Abu huraira check Lubumba.qxd

7/1/2011

10:47 AM

Page 120

Abu Huraira Huenda Mola wako akakuinua cheo kinachosifika.” 17:78-79. Mwenyezi Mungu alimtaka Mtume wakati wa usiku zaidi kuliko zile swala tano ambazo zilikuwa ni wajibu kwa Waislam wote, wakati ambapo ile swala ya usiku ilikuwa ni wajibu kwa Mtume peke yake. Mwenyezi Mungu amesema: “Na umtegemee Mwenye nguvu, Mwenye rehema. Ambaye anakuona unaposimama. Na mageuko yako miongoni mwa wale wanaosujudu.” 26:217-219. Ilikuwa na maana kwamba Mwenyezi Mungu alikuona wakati uliposimama kumuabudu Yeye wakati wa usiku pale ambapo hapakuwa na yeyote anayekuona wewe isipokuwa Yeye, na akaona mishuhuliko yako miongoni mwa waumini wakati ulipowaongoza katika kutekeleza swala. Vile vile Mwenyezi Mungu amesema akimwambia yeye Mtume (s.a.w.w.): “….. na mtukuze Mola wako kwa kumsifu kabla ya kuchomoza jua na kabla ya kuchwa. Na katika usiku mtukuze na baada ya kusujudu (katika swala).” 50:39-40. Yeye aliswali usiku mzima na alining’iniza kifua chake kwa kamba ili asipitiwe na usingizi.157 Aliendelea kusimama, kukaa, kusujudu mpaka miguu yake ikavimba.158 Kisha Jibril akamwambia (kutoka kwa Allah): “Jichunge hali yako mwenyewe. Inapaswa kuangaliwa na wewe.” Kisha akamfunulia: “Taha. Hatukukuteremshia Qur’ani ili upate mashaka. Bali iwe mawaidha kwa mwenye kunyenyekea.” 20:1-3. Aya ilikuwa na maana kwamba: Hatukuteremsha Qur’ani juu yako ili kukuchosha wewe kwa kufanya ibada, bali tuliiteremsha ili iwe ni ukumbusho kwa yule anayemuogopa Mwenyezi Mungu. Kwa hiyo jichunge mwenyewe na usijitwishe mwenyewe zaidi kwa yale usiyoweza kubeba. Bukhari aliweka milango ya kipekee ndani ya Sahih yake kwa ajili ya 157 Kama ilivyosimuliwa katika Majma’ul-Bayan, katika maelezo ya aya ya Taha. Ilisimuliwa na Qatada. 158 Rejea Sahih al-Bukhari, Jz. 1, uk.135; Rejea al-Kashshaf, wakati akitafsiri aya ya Taha. 120


Abu huraira check Lubumba.qxd

7/1/2011

10:47 AM

Page 121

swala ya usiku ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), sijida zake ndefu katika swala hiyo ya usiku na kusimama kwake mpaka miguu yake ikavimba na nyayo zake kupasuka. Hivyo ndivyo alivyojizoesha mwenyewe kufanya wakati wa usiku. Je ni vipi kuhusu zile swala tano za wajibu, ambazo zilikuwa mojawapo ya misingi, ambayo juu yake Uislam umesimamia? Je, yeye angelala na kupitwa na swala? Mungu aepushilie mbali! Na hilo lilikuwa mbali sana na kinyume na Mtume (s.a.w.w.) ambaye aliwasomea watu: “Zilindeni swala, na haswa swala tukufu ya usiku (wustwa) na simameni kwa ajili ya Mwenyezi Mungu kwa kunyenyekea.” 2:238 na aliwavuta watu: “Hakika wamefuzu wenye kuamini. Ambao ni wanyenyekevu katika swala zao.” 23:1-2, na amewaelezea waumini: “Na ambao swala zao wanazihifadhi. Hao ndio warithi. Ambao watairithi Pepo ya Firdausi, wao humo watakaa milele.” 23:9-11, na akawalingania watu: “….. basi simamisheni swala. Hakika swala kwa wenye kuamini ni faradhi iliyo na wakati maalum.” 4:103, na aliwafanya watu wote wasikie: “Hakika amekwisha kufaulu aliyejitakasa. Na akakumbuka jina la Mola wake na akaswali.” 87:1415. Qur’ani imejaa aya kama hizi ambazo Mtukufu Mtume (s.aw.w.) aliwafundisha watu hekima zake na hotuba nzuri. Ni mara ngapi ambapo Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) aliwachoma walegevu kwa: “Basi ole wao wanaoswali. Ambao wanapuuza swala zao. Ambao wao hujionyesha.” 107:4-6, na aliwafichua wanafiki wakati Mwenyezi Mungu alipomfunulia yeye kuhusu tabia zao: “….. wala hawafiki kwenye swala ila kwa uvivu, wala hawatoi ila huwa wamechukia.” 9:54, na alimshutumu mtu ambaye alilala na hakuswali swala ya usiku mpaka ikafika asubuhi kwa kusema: “Shetani alitengeneza maji kwenye sikio lake.”159 121


Abu huraira check Lubumba.qxd

7/1/2011

10:47 AM

Page 122

Abu Huraira Ilikuwa ni sitiari kiasi gani kuhusu wale ambao walijizoesha kulala bila ya kuswali ile swala ya usiku na ilikuwa ni balagha kiasi gani kutoka: “Mjumbe aliyeheshimika. Mwenye nguvu, mwenye nafasi ya hadhi kwa Mola wa Milki, mmoja wa kutiiwa, na mkweli kwenye amana.” Lilikuwa ni neno gumu kiasi gani, ambalo lingewafanya waumini kuhofia na kutolala kamwe bila ya kuswali swala ya usiku kama wangejifikiria vizuri juu ya nafsi zao wenyewe. Wale wachamungu na wapujufu, waumini na makafiri walijua na kushuhudia kwamba Mtume Muhammad (s.a.w.w.) alikuwa ndiye wa kwanza aliyetekeleza kanuni zake na alikuwa ndiye mfanya ibada bora aliyetimiza kanuni zake kwa uaminifu. Aliuelimisha umma wake kwa vitendo vyake zaidi kuliko kwa maneno yake. Asingemlaumu yule ambaye alilala bila kuswali swala ya usiku kwa ukali sana, kama yeye mwenyewe alilala mbele ya masahaba zake na akaikosa swala ya al-Fajr. Utukufu uwe kwa Mwenyezi Mungu! Hii ilikuwa ni kashfa kubwa kiasi gani! Abu Huraira mwenyewe alisimulia160 kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisema: “Shetani hufunga mafundo matatu kwenye ukosi wa kila mmoja wenu wakati anapolala. Endapo ataamka na kumtaja Allah, basi fundo moja hufunguka. Kama atafanya udhuu, lile fundo la pili litafunguka na iwapo ataswali na fundo la tatu litafunguka. Halafu atakuwa mchangamfu na mwenye mwelekeo mzuri, vinginevyo atakuwa mvivu na mwenye mwelekeo mbaya.” Riwaya hii ilikuwa na sitiari ya kibalagha kama ile iliyopita. Mtume 159 Rejea Sahih Bukhari, Jz. 1 uk. 136 160 Rejea Sahih Bukhari, Jz. 1, uk. 136. Ilikuwa ni ajabu ya Bukhari ya kiasi gani kwamba alisimulia riwaya hii katika kitabu chake, na vile vile ile riwaya inayozungumzia kuhusu kule kulala kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na kupitwa na swala ya al-Fajr! Pia rejea kwenye Musnad Ahmad, Jz.2, uk. 153.

122


Abu huraira check Lubumba.qxd

7/1/2011

10:47 AM

Page 123

Abu Huraira (s.a.w.w.) alitaka kuuonya umma wake kutokana na Shetani na kuwachochea kumtii Mwenyezi Mungu. Kama Abu Huraira alikuwa mkweli katika riwaya hii, lazima atakuwa muongo pale aliposimulia ile riwaya ya kulala kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na kupitwa na swala ya al-Fajr. Abu Huraira alisimulia kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisema: “Hakuna swala ambayo ni ngumu sana kwa wanafiki kuliko ile ya al-Fajr na Isha. Kama wangejua swala mbili hizi zina nini ndani yake, watakuja kuziswali hata kwa kutambaa. Nilikuwa karibu nimuamuru Muadhini kufanya Iqamah ya swala na kisha kumuagiza mtu kuongoza watu katika swala na ningechukua mwenge kuwatishia nao watu ambao hawajaja kuswali bado.” Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) aliwahimiza watu kuswali, alitilia umakini zaidi kwa swala ya al-Fajr na aliwatishia wale ambao hawakuja kuswali swala hiyo kwa kuwachoma kwa moto. Baada ya yote hayo, je ilikuwa inaaminika na kukubalika kwamba yeye mwenyewe alilala na hakuswali swala hiyo? Kwa hakika ni hapana! Mwenyezi Mungu anaweza kuwa na huruma kwa Abdallah bin Rawaha, yule sahaba aliyeuawa kishahidi, pale aliposema:161 “Miongoni mwetu alikuwepo Mtukufu Mtume. Akisoma Kitabu Kitukufu wakati alfajiri ilipoanza kutoa mionzi yake. Alitufanya sisi tuone mwongozo baada ya upovu wetu, Hivyo nyoyo zetu zikamuamini yeye kwamba kila alichokisema kingetokea. Aliutumia usiku wake mbali na kitanda chake, 161 Rejea Sahih Bukhari, Jz. 1, uk. 138. 123


Abu huraira check Lubumba.qxd

7/1/2011

10:47 AM

Page 124

Abu Huraira wakati wengine walikuwa kwenye usingizi mzito.” Hebu turudi kwenye riwaya yenyewe ili tuelezee kile kilichobakia kuikanusha. Kwanza: Wao (mafaqihi na waandishi wa vitabu vya Hadith) wamesema kwamba moyo wa Mtume (hisia) hazikulala hata pale macho yake yaliposinzia. Sahih zao zimelitamka hilo wazi wazi.162 Hii ilikuwa ni moja ya ishara za utume na Uislam, kwa hiyo haikustahili kwa yeye kulala na kuikosa swala ya al-Fajr, kwa sababu endapo macho yake yalisinzia, moyo wake ungekuwa makini kwenye wajibati zake. Wakati mmoja aliswali swala ya usiku na akaenda kulala kabla ya kuswali swala ya witri. Mmoja wa wake zake akamwambia: “Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, unalala kabla hujaswali swala ya witri?” Yeye akasema: “Macho yangu yanalala lakini moyo wangu haulali.”163 Alikuwa na maana kwamba alikuwa na uhakika kwamba hatapitwa na swala ya witri kwa sababu alikuwa anaipenda sana na moyo wake ulikuwa makini juu yake japokuwa macho yake yalikuwa yanalala. Kama alikuwa hivyo kwa swala ya witri, vipi yeye kuhusu wakati alipolala kabla ya swala ya al-Fajr? Pili: Abu Huraira alitamka, kama ilivyosimuliwa na Sahih Muslim, Jz. 1, uk. 254 kwamba kadhia hii ilitokea kwa Mtukufu Mtume wakati wa kurejea kwake kutoka kwenye vita vya Khaybar. Ni vipi Abu Huraira amejidai kwamba alikuwa na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) wakati huo? Abu Huraira

162 Rejea Sahih Bukhari, Jz. 1, uk. 179 163 Rejea Sahih Bukhari, Jz. 2, uk. 124


Abu huraira check Lubumba.qxd

7/1/2011

10:47 AM

Page 125

Abu Huraira alisilimu na kuwa Mwislam baada ya vita hivi kama wanahistoria walivyoeleza kwa makubaliano ya kauli moja.164 Tatu: Abu Huraira amesema katika riwaya moja: Mtukukfu Mtume (s.a.w.w.) amesema: “Hebu kila mmoja wenu amuongoze mnyama (kipando) wake. Mahali hapa pamehudhuriwa na shetani.” Na sisi tukafanya hivyo. Ilikuwa inajulikana vizuri kabisa kwamba Shetani kamwe hakumkaribia Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na watu wote walijua vema vilevile kwamba Abu Huraira alikuwa ni masikini sana na hakuwa hata na chochote cha kushibisha tumbo lake lenye njaa kwacho, hivyo ni kutoka wapi alikopata mnyama wa kipando wa kumuongoza njia kama alivyosema: Na sisi tukafanya hivyo!? Nne: Abu Huraira amesema: “….. halafu Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akaomba maji ya kuchukulia udhuu. Alisujudu mara mbili na kisha akaswali swala ya Subhi” Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) ameswali swala ya asubuhi kufidia au kwa kadhaa ya al-Fajr ambayo aliikosa (kwa mujibu wa Abu Huraira), lakini haku164 Abu Huraira alisema katika siku za mwisho za uhai wake: “Mimi na wachache kutoka katika kabila langu tulikuja Madina kukiri Uislam wetu wakati Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alikuwa ameondoka kwenda Khaybar na kumteua Siba’ bin Arafat al-Ghifari kama mwandamizi wake hapo Madina. Tuliswali swala ya alFajr pamoja naye. Alitugawia chakula na pesa. Tuliondoka hadi tukamkuta Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) pale alipoishinda Khaybar. Mtume alizungumza na Waislam kushirikiana nasi katika mafungu yao.” Riwaya hii haikusimuliwa na mtu mwingine yeyote isipokuwa Abu Huraira lakini ummah (Sunni) waliitegea hiyo, kama walivyofanya wakati wote kwa Hadith za Abu Huraira, na wamethibitisha kuwepo Khaybar kwa Abu Huraira pamoja na Mtume (s.a.w.w.) bila ya ushahidi wowote wa kweli. kwa mujibu wa mmoja wa Maimam wetu Ma’sum, Abu Huraira alikuja Madina na akawa Muislam baada ya kurudi kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kutoka Khaybar. 125


Abu huraira check Lubumba.qxd

7/1/2011

10:47 AM

Page 126

Abu Huraira jua zile sijida mbili Mtukufu Mtume alizifanya kwa sababu gani na zilikuwa ni nini! An-Nawawi ameziruka hizo wakati alipoielezea Hadith hii. Tano: Ilikuwa ni kawaida kwa majeshi na viongozi kuwa na walinzi wa kuwalinda wakati walipotaka kulala, hususan kama alikuwepo mfalme au mtu maarufu miongoni mwao. Na kuhusu Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), yeye alikuwa na maadui wengi. Walikuwepo wanafiki wengi ndani ya jeshi lake, ambao walikuwa wakisubiria kujilipizia wenyewe juu ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Yeye Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) asingejitofautisha mwenyewe kutokana na viongozi ili kujilinda yeye mwenyewe na jeshi lake. Alikuwa hawezi kulala, pamoja na masahaba wake katika jangwa lile lililozingirwa na maadui zake miongoni mwa washirikina na wayahudi wakaidi, isipokuwa pakiwa na walinzi wa kuwalinda. Je asingetoa mazingatio kwa suala hili muhimu, ambapo alikuwa ndiye bwana wa watu wenye busara kabla ya kuwa bwana wa Mitume? Hivyo je, wale walinzi walikuwa wamelala pia kama walivyolala waadhini? Kwa hakika hapana! lakini ilikuwa ni waongo, wale ambao Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alikuwa ameonya dhidi yao! Sita: Katika usiku ule, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alikuwa pamoja na jeshi la wapiganaji elfu moja na mia sita; Miongoni mwao wakiwemo mashujaa bora mia mbili. Haingewezekana kwamba wote walikuwa wamelala na kwamba hakuna aliyekuwa macho hata mmoja. Hebu tuchukulie kwamba hawakuamka wao wenyewe, je hawakuamshwa na milio na sauti za kwato za farasi mia mbili zinazopiga juu ardhini wanaotaka majani yao wakati wa asubuhi? Ni unyongevu kiasi gani waliokuwa nao wote, watu na farasi! Inaweza kuwa ni moja ya miujiza ya Abu Huraira!

17. Ng’ombe na mbwa wa mwitu waongea kwa kiarabu fasaha: Masheikh hao wawili wamesimulia kwamba Abu Huraira amesema: “Mtukufu Mtume Muhammad (s.a.w.w.) aliswali swala ya al-Fajr, akaja 126


Abu huraira check Lubumba.qxd

7/1/2011

10:47 AM

Page 127

Abu Huraira mbele ya watu akasema: “Wakati mmoja alikuwepo mtu anamuongoza ng’ombe wake. Alimswaga na kumpiga. Yule ng’ombe akasema: Sisi hatukuumbwa ili tupigwe bali kwa ajili ya kulima kwa plau!” Watu wakasema: “Alhamdulillah! ng’ombe anazungumza!” Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akasema: “Sisi tunaliamini hilo; mimi, Abu Bakr na Umar, ingawa hao wote hawapo hapa. Vilevile alikuwapo mtu anayechunga kondoo wake. Mbwamwitu akaja akamchukua mmoja wao. Yule mtu akamfuata yule mbwamwitu na akamuokoa yule kondoo. Yule mbwamwitu akamwambia yule mtu: “Umemuokoa kutoka kwangu mimi!, ni nani atakayemuokoa kama atakuja simba siku moja na kumchukua, wakati ambapo hapatakuwa na mchunga mwingine juu yake isipokuwa mimi?” Watu wakasema: “Alhamdulillah, mbwamwitu naye anaongea?” Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akasema: “Sisi tunaliamini hilo; mimi, Abu Bakr na Umar, ingawa hao wote hawapo hapa.165 Abu Huraira alikuwa anapenda sana vituko na mambo ya ajabu. Alikuwa na vicheko sana wakati alipokuwa akizungumza mambo yasiyo ya kawaida, kama kule kukimbia kwa jiwe pamoja na nguo za Musa (a.s.), au pale Musa alipompiga kofi malaika wa mauti na kumng’oa jicho lake, kudondoka kwa nzige wa dhahabu juu ya nabii Ayub na mfano wa yasiyowezekana yake kama hayo. Na hapa ameelezea juu ya ng’ombe na mbwa mwitu anayeongea, ambao waliongea kwa kiarabu fasaha kuonyesha kwamba walikuwa na akili, ujuzi na hekima. Alizungumzia juu ya jambo ambalo kwa hakika halikuwahi kutokea na wala halitakuja kutokea kamwe hata kidogo. Kanuni za kawaida ambazo Mwenyezi Mungu ameziweka kwa kila kile alichokiumba zilifanya hili kuwa haliwezekani isipokuwa kama kungekuwa na ulazima wa muujiza wa kuwa ishara ya kuthibitisha utume wa mmojawapo wa mitume Yake ama jambo linalohusiana na Mwenyezi Mungu. Suala la yule mtu ambaye alimuongoza ng’ombe wake kwenye shamba na kumswaga, hilo 165 Rejea Sahih Bukhari, Jz. 2, uk. 171 na 190; Sahih Muslim, Jz. 2, uk. 316 na kurasa zinazofuatia, na Musnad Ahmad, Jz. 2, uk. 246 127


Abu huraira check Lubumba.qxd

7/1/2011

10:47 AM

Page 128

Abu Huraira halikuhitaji changamoto yoyote au muujiza ambao kwamba Allah angevunja kanuni za maumbile kwa ajili yake. Vivyo hivyo ndio ilikuwa kwa mchunga kondoo, pale mbwamwitu alipovamia kondoo wake. Hadith hii ilikuwa sio ya kweli kabisa, kwani Allah asingefanya miujiza bure bure tu. Abu Bakr na Umar hawakuwa wenye kuhitaji sifa kama hiyo. Kwa kweli kama wangemsikia akiisimulia hiyo, wangeweza kumuadhibu yeye. Lakini alimtaja Abu Bakr na Umar ili kutimiza mwelekeo wake wa vioja, na wakati huo huo kutembea kwenye kivuli chao kwani alijua hakuna atakayekataa yale aliyoyasema, vinginevyo angeshutumiwa kwa kuwakashifu makhalifa hao wawili; Abu Bakr na Umar. 18. Kumfanya Abu Bakr kiongozi (Amiir) wa Hijja: Masheikh hawa wawili wamesimulia kwamba Hamiid bin Abdur-Rahman bin Awf amesema kwamba Abu Huraira alimwambia kwamba Abu Bakr alimtuma yeye Abu Huraira wakati wa hijja ambayo Mtume (s.a.w.w.) alimfanya Abu Bakr kuwa Amiir mwaka mmoja kabla ya Hijja ya Muago (Hijja ya mwisho kabla ya kufariki Mtume), pamoja na baadhi ya watu katika Siku ya Kafara (kuchinja) kuwajulisha watu kwamba washirikina hawataruhusiwa kuja kuhiji na kwamba hakuna mtu yoyote atakayetufu alKa’ba akiwa uchi baada ya mwaka huo.166 Bukhari amesimulia Hadith nyingine kutoka kwa Hamiid kwamba Abu Huraira amesema: “Abu Bakr alinituma miongoni mwa kundi la wapiga mbiu kwenda Mina katika Siku ya Kuchinja kwenda kuwatangazia watu kwamba hakuna mushrikina watakaoruhusiwa kuja kuhiji na hakuna mtu atakayetufu al-Ka’ba akiwa uchi baada ya mwaka huo. Halafu Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akamtuma Ali (a.s.) nyuma yetu kwenda kuwasomea Surat al-Bara’a. Ali alitangaza pamoja nasi kwa watu hapo Mina katika Siku ya Kuchinja (kutoa kafara).167 166 Rejea Sahih al-Bukhari, Jz. 1, uk. 192 na Sahih Muslim, Jz. 1, uk.517 167 Sahih al-Bukhari, Jz. 3, uk. 90

128


Abu huraira check Lubumba.qxd

7/1/2011

10:47 AM

Page 129

Abu Huraira Haishangazi iwapo kama sera ya Bani Umayyah ndio iliyolazimisha juu ya Abu Huraira na Hamiid, Hadith hii ya uwongo, na vilevile haitoshangaza iwapo kama wote wawili walijitolea kwa hiari kufanya hivyo. Kwa kweli Abu Huraira alikwenda Damascus, makao makuu ya Bani Umayyah, akifanya biashara ya kuuza bidhaa zake (Hadith), ambazo zilipata soko na kununuliwa vizuri sana huko. Propaganda dhidi ya Imam Ali na kizazi cha Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) ilikuwa ndio biashara bora yenye mapato ya faida kwa wale wajuvi, walaghai huko. Hamiid alitengenezwa kwa mikono ya Mu’awiyah kubeba Hadith kama hizi. Alijifanya kama mchamungu na mwenye kujizuia. Alipendelea sana kusikia kutoka kwa maadui wa Imam Ali (a.s.).168 Yeye alikuwa kama wale maadui wakali wa ki-Bani Umayyah wa Imam Ali (a.s.). Huyu hakuwa ni jambo la kushangaza kwa sababu yeye alikuwa ni mtoto wao. Mama yake alikuwa Ummu Kulthuum bint Aqaba bin Abu Mu’it Thakwan bin Umayyah bin Abd Shams. Alikuwa ni dada yake Waliid bin Aqaba. Bibi yake alikuwa ndiye mama wa Uthman bin Affan. Jina lake lilikuwa ni Arwa bint Kurayz bin Rabii’a bin Habiib bin Abd Shams. Baba yake, Abdur-Rahman alikuwa mpinzani dhidi ya Imam Ali (a.s.). Hivyo haishangazi kwamba Abu Huraira na Hamiid walikubaliana kueneza uzushi huu, ambao mamluki wao waliuhamishia kila mahali haraka haraka kuliko kasi ya upepo. Ni nini kilichoibatilisha riwaya hii kwamba Abu Huraira (kabla hajaneemeka na starehe za Bani Umayyah) amesema: “Nilikuwa miongoni mwa ujumbe ambao Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) aliutuma pamoja na Imam Ali (a.s.) kwenda kutangaza Surat al-Bara’a.” Mwanawe, al-Muharrir alimuuliza: “Mlijulisha juu ya nini?” Yeye akasema: “Hakuna atakayeingia Peponi isipokuwa waumini, hakuna mushrikina watakaokuja kuhiji baada ya mwaka huu, hakuna mtu atakayezunguka (kutufu) al-Ka’aba akiwa uchi 168 Alisimulia kutoka kwa Mu’awiyah, an-Nu’man bin Bashiir, al-Mughiira bin Shu’ba, Abdullah bin Zubeir, Marwan na wengine kama hao. Riwaya zake zilisimuliwa na Bukhari na Muslim. 129


Abu huraira check Lubumba.qxd

7/1/2011

10:47 AM

Page 130

Abu Huraira na yeyote ambaye ana mkataba na Mtukufu Mtume utakuwa na thamani kwa muda wa miezi minne.169 nililia kwa hilo mpaka sauti yangu ikakauka na kuwa na mikwaruzo.” Hii ilikuwa ndio riwaya yake sahihi iliyosimuliwa katika vitabu vya wanahistoria na vya wale walioikusanya Hadith hiyo. Hakumtaja Abu Bakr. Alisema kwamba wale mahujaji, ambao Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) aliwatuma kwenda Makka walikuwa chini ya uongozi wa Imam Ali (a.s.) Uamiir huo huo ambao Abu Huraira aliupachika kwa Abu Bakr. Kama Abu Huraira alitumwa na Mtukufu Mtume pamoja na Imam Ali, nini itakuwa maana ya usemi wake: “Abu Bakr alinituma mimi pamoja na wapiga mbiu wengine katika Siku ya Kuchinja ya hijja ile,” na usemi wake mwingine: “Halafu Mtume akamtuma Ali kutufuata nyuma yetu na

169 Mafaqih wameikanusha Hadith hii (utakuwa na thamani kwa muda wa miezi minne) kwa sababu kile kilichojumuika katika hotuba ya Imam Ali (a.s.) katika siku hiyo (mushrikina yeyote ambaye ana mkataba na Mtukufu Mtume utadumu hadi mwisho wa muda wake, kwa kiasi chochote muda wake utakavyokuwa, na ambaye ana mkataba usio na mpaka wa kukoma, huo utakuwa na thamani kwa muda wa miezi minne). Ilikuwa dhahiri kwamba Abu Huraira hakuhudhuria kwenye msimu huo wa hijja kuweza kujua ni nini walichokitangaza. Ilikuwa ni kawaida kwake, kwa sababu mara nyingi alijifanya kusingizia kuhudhuria yale matukio aliyoyazungumzia, lakini kwa kweli hakuyahudhuria, kwa hiyo aliyasimulia kiuongo uongo.

130


Abu huraira check Lubumba.qxd

7/1/2011

10:47 AM

Page 131

Abu Huraira kutangaza pamoja nasi?” Haikuwa chochote ila kupingana kwao.170

“Wanataka kuizima nuru ya Mwenyezi Mungu kwa vinywa vyao, lakini Mwenyezi Mungu amekataa isipokuwa kuitimiza nuru yak, ijapokuwa makafiri wanachukia.” 9:32. Inshallah nitanyoosha ukweli wa Hadith hii mbele yenu katika baadhi ya vipengele: Kwanza: Ni kuweka sawa ule uhalisia wa kazi yenyewe “kutumwa pamoja na Surat al-Bara’a” kwa mukhtasari: Wakati Surat al-Bara’a ilipoteremka kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alimtuma Abu Bakr kwenda kuisoma katika siku ya hijja kubwa mbele ya wote waliohudhuria na kutangaza mpango wa Allah swt. na Mtume Wake kutoka kwenye makubaliano baina ya Waislam na washirikina, hakuna mshirikina atakayeruhusiwa kufika kwenye al-Ka’ba, hakuna hata mtu mmoja atakayeingia Peponi ila waumini tu na hakuna mtu atakayeruhusiwa kuizunguka Kaaba akiwa uchi. Wakati Abu Bakr alipokwenda na sura ya Bara’a, kabla ya kufika mbali, Mwenyezi Mungu akamfunulia Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kwamba hakuna yeyote atakayetekeleza jukumu hilo la mbinguni isipokuwa ni yeye mwenyewe Mtume au mtu atokanaye na familia yake. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alimuita Imam Ali (a.s.) na akamuamuru kumfuata Abu Bakr na kuichukua al-Bara’a kutoka kwake, halafu yeye aende Makka ili kutekeleza jukumu hilo yeye mwenyewe. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alimpa mamlaka kamili Imam Ali ya kuwa kiongozi (Amiir) wa hijja kati170 Kupingana kati ya riwaya mbili hizo kulikuwa dhahiri kuhusu mtumaji wa Abu Huraira na wapiga mbiu wengine, mahali pa kutuma; Madina au Makkah na tarehe ya kutuma; iwapo kama ni ile Siku ya Kuchinja yenyewe au kabla yake. 131


Abu huraira check Lubumba.qxd

7/1/2011

10:47 AM

Page 132

Abu Huraira ka mwaka ule171 na kumuachia Abu Bakr uhuru wa kuamua ama kurudi Madina au kuendelea pamoja na mahujaji. Imam Ali alimpanda ngamia jike wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) aliyeitwa al-Adhba’ na akatoka kumfuata Abu Bakr. Abu Bakr akamuulia Imam Ali: “Kwa nini umekuja, ewe Abul-Hasan? Imam Ali akasema: “Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) ameniamuru mimi kuzichukua aya za al-Bara’a kutoka kwako na niende kubatilisha mkataba wa makubaliano na washirikina.172 Uko huru kurudi Madina au kufuatana na mimi.” Yeye akasema: “Nitarejea kwake.” Ali akaenda Makka pamoja na mahujaji wa Madina. Abu Bakr akaelekea kurudi Madina. Alimwambia Mtukufu Mtume (s.a.w.w.): “Uliniamini mimi na jambo ambalo nilishikwa na shauku nalo, lakini pale nilipokwenda kuli171 Rejea kwenye kitabu cha at-Tabarsi, Majma’ul-Bayan, Jz. 3, uk. 3. 172 Kama ukisema: kwa nini Mtukufu Mtume alimuamuru Abu Bakr kwenda na al-Bara’a kubatilisha makubaliano ya washirikina katika siku ya Hijja na kisha akamuuzulu kabla ya wakati wa Hijja kufika? Je, hiyo haikuwa ni namna ya kufuta jambo kabla ya kufika kwa wakati wa kulitekeleza, ambalo lilikuwa haliwezekani kwa Mwenyezi Mungu na Mtume Wake? Kwa hakika hapana! Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alimtuma Abu Bakr na kisha akamuamuru kurudi na akamtuma Ali badala yake, kuongezea kwa Ali (a.s.) ubora ambao usingekuwa kama angemtuma Ali tangu mwanzo. Jambo kama hilo lilitokea kwa Ibrahim. Mwenyezi Mungu alimuamuru kumchinja mwanawe. Pale alipojaribu kufanya hivyo, Mwenyezi Mungu alimfunulia: “Kwa hakika umeonyesha ukweli wa ile ndoto; hakika hivyo ndivyo tunavyowalipa watendao mema,” na alimfidia mwanawe kwa kafara na hakumwachia amchinje mwanawe kwa vile Ibrahim hakuamriwa hasa na Mwenyezi Mungu kumchinja mwanawe bali kujaribu kufanya hivyo ili kuonyesha watu ubora wa Ibrahim na mwanawe na hapakuwa na ubatilishaji wowote katika jambo hili. Ilikuwa vivyo hivyo wakati Mtukufu Mtume alipomtuma Abu Bakr kwenda kuiteka Khaybar halafu akamtuma Umar, lakini wote walirudi bila ushindi, walishindwa. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akasema: “Kesho nitakabidhi bendera kwa mtu ambaye anampenda Allah na Mtume Wake na wao wanampenda yeye. Anashinda kwa msaada wa Mwenyezi Mungu.” Aliikabidhi bendera hiyo kwa Ali (a.s.) na Ali akaiteka Khaybar. Ubora wa Ali ulionekana vizuri zaidi kuliko kama angetumwa tangu mwanzo. Yalikuwepo mambo mengi kama haya. 132


Abu huraira check Lubumba.qxd

7/1/2011

10:48 AM

Page 133

Abu Huraira tenda uliagiza mimi nirudi. Je, Mwenyezi Mungu ameteremsha jambo lolote kuhusu mimi?” Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akasema: “Hapana, lakini Jibril (a.s.) ameniambia kutoka kwa Allah kwamba hakuna yeyote angeweza kutekeleza jukumu hili la ki-Ungu ukiacha mimi mwenyewe au mtu kutoka kwenye familia yangu. Ali anatokana na mimi na hivyo yeye atalifanya badala yangu.” Riwaya zenye maana hii zilisimuliwa kwa wingi na Maimam maasumin.173 Pili: Baadhi ya yale ambayo yameelezwa na ummas (wa Masunni) yamethibitisha yale tuliyoyaeleza hapo juu. Hapa ni riwaya ya Abu Bakr kama ushahidi wa wazi. Yeye amesema: “Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alinituma na Surat al-Bara’a kwenda Makka kutangaza kwamba hakuna mshirikina atakayeruhusiwa kuja hijja baada ya mwaka huu, hakuna hata mtu atakayezunguka al-Ka’ba akiwa uchi, hakuna atakayeingia Peponi isipokuwa waumini, yeyote aliyekuwa mapatano na Mtukufu Mtume, yatakuwa na hai mpaka wakati wa tarehe yake na kwamba Mwenyezi Mungu na Mtume Wake wameachana na washirikina. Nilikuwa nimeondoka kwa muda wa siku tatu kisha Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akamwambia Ali: “Mfuate Abu Bakr na mwambie arejee kwangu. Ichukue Bara’a kutoka kwake na uende ukaitangaze.” Niliporudi kwa Mtukufu Mtume huko Madina, nililia na kumwambia: “Je kumetokea jambo lolote kuhusu mimi?” Yeye akasema: “Hakuna ila jema tu lililotokea kuhusu wewe. Lakini niliamriwa kwamba hakuna mtu ambaye angetekeleza majukumu yangu ya kimungu isipokuwa mimi mwenyewe au mtu wa familia yangu.” Hii ndio ilikuwa riwaya ya Abu Bakr.174 Je unadhani kwamba kulia kwake na mhemko kuliendana vema na kule kumfanya Amiir wa hijja au kwa kule kuenguliwa kutokana na hilo? Hivyo ndivyo ilivyokuwa riwaya ya Imam Ali175 pale aliposema: “Wakati aya kumi za Bara’a zilipokuwa zimeshuka kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), alimwita Abu Bakr na kumtuma kwenda kuwasomea watu wa Makka. 173 Rejea kwenye Tafsiir ya Ali bin Ibrahim pale alipokuwa akitafsiri Surat Tawba (Bara’a) na Sheikh al-Mufiid katika Irshad yake. 174 Rejea kwenye Musnad Ahmad, Jz. 1, uk. 2 175 Musnad Ahmad, Jz. 1, uk. 151 133


Abu huraira check Lubumba.qxd

7/1/2011

10:48 AM

Page 134

Abu Huraira Halafu akaagiza niitwe mimi na akasema: “Mfuate Abu Bakr. Popote utakapomkuta, chukua kitabu kutoka kwake na uende ukakisome kwa watu wa Makka. Mimi nilimkuta na nikakichukua kitabu hicho kutoka kwake. Yeye alirudi kwa Mtukufu Mtume na akamwambia: “Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, kuna jambo lolote lililofunuliwa kuhusu mimi?” Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akasema: “Hapana, lakini Jibril amenijia na kuniambia kwamba hakuna mtu yoyote atakayewajulisha juu ya ufunuo huo isipokuwa mimi mwenyewe au mtu atokanaye na mimi.” Imam Ali (a.s.) amesema katika riwaya nyingine:176 “Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alimtuma Abu Bakr na Bara’a kwa watu wa Makka halafu akanituma mimi kumfuata yeye na akaniambia: “Chukua kitabu kutoka kwa Abu Bakr na uende Makka.” Nilimkuta na nikachukua hicho kitabu kutoka kwake. Yeye akarudi kwa huzuni kwenda Madina. Alimuuliza Mtukufu Mtume: “Je kuna lolote lililoshuka kuhusu mimi?” Mtume (s.a.w.w.) akasema: “Hapana, lakini nimeamrishwa kwamba nitajulisha mimi kuhusu hilo au mtu kutoka kwenye familia yangu.” Hadith nyingine iliyosimuliwa na Ibn Abbas, ambaye alilalamika kuhusu maadui wa Imam Ali na akaanza kuzungumza kwa kirefu kuhusu sifa na ubora wa Imam Ali (a.s.) na hali ya kumfadhilisha yeye juu ya umma wote baada ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Yeye alisema:177 “….. kisha Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akamtuma Abu Bakr na Surat-Tawba (Bara’a) na baadae akamtuma Ali kumfuata na kuichukua kutoka kwake. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akasema: “Hakuna mtu yeyote atakayekwenda nayo isipokuwa mtu ambaye anatokana na mimi, nami natokana na yeye.” Wapinzani wa Ali walikubali kushindwa na Ibn Abbas. Kama Abu Bakr alikuwa ndiye Amiir wa hijja mwaka ule wasingekubali kushindwa na Ibn Abbas. Walikuta ushahidi wake ni wenye msimamo, kwa hiyo walijiweka 176 Imesimuliwa na an-Nissa’i katika kitabu chake al-Khasa’is al-Alawiyah, uk. 20, Imam Ahmad bin Hambal na wengineo 177 Rejea kitabu cha al-Hakiim, Mustadrakul-Hakiim, Jz.3, uk. 32, Thalabi katika al-Talkhiis al-Mustadrak, an-Nassai katika al-Khassais al-Alawiyah uk. 6 na Musnad Ahmad, Jz. 1, uk. 331 134


Abu huraira check Lubumba.qxd

7/1/2011

10:48 AM

Page 135

Abu Huraira chini yake (kwa kuridhia). Ibn Abbas wakati mmoja alisema: “Nilikuwa ninatembea na Umar sehemu fulani ndani ya Madina wakati aliponiambia: “Ewe Ibn Abbas, mimi nadhani swahiba wako (Imam Ali) amekosewa.” Nilidhani kwamba nisingeliachia hilo lipite vivi hivi. Mimi nikamwambia: “Ewe Amirul-muuminin, mrudishieni haki yake.” Aliondoa mkono wake kutoka kwenye mkono wangu na akaondoka huku akinung’unika kwa muda kidogo halafu akanyamaza. Mimi nikamfuata. Yeye akasema: “Ewe Ibn Abbas, nadhani walimnyima (ukhalifa) kwa sababu walimuona kuwa bado ni mdogo sana.” Mimi nikasema: “Ninaapa kwamba Mwenyezi Mungu na Mtume Wake hawakumuona yeye kuwa ni mdogo sana wakati walipomuamuru yeye kuchukua Surat al-Bara’a kutoka kwa swahiba wako.” Hapo yeye akaondoka kwa haraka haraka.”178 178 Ilisimuliwa na az-Zubair bin Bukaar bin Abdullah bin Mus’ab bin Thabit bin Abdullah bin az-Zubair bin al-Awwam katika kitabu chake, al-Muwaffaqiyyat, ambacho alikiandika kwa ajili ya al-Muwaffaq bi-llah, mwana wa Mutawakkil, khalifa wa Bani Abbas. Ilikuwa ni siri ya Mwenyezi Mungu ambayo ilikuwa haiwezi kufichika, na Nuru Yake ambayo kamwe haiwezi kuzimwa kwamba azZubair bin Bukaar mwenyewe aliisimulia Hadith kama hiyo katika kitabu chake. Ibn Bukaar alikuwa anafahamika kwa uadui wake na Imam Ali (a.s.) na Bani Hashim. Yeye ambaye alitakiwa na mmoja wa Bani Hashim kuapia katikati ya kaburu tukufu na mimbari ya Mtukufu Mtume na akaapia kwa uongo, kwa hiyo Mwenyezi Mungu akamuadhibu kwa ukoma. Aliwatukana ma-Alawiyah (kizazi cha Imam Ali) na babu yao, Imam Ali (a.s.). Wao wakaazimia kumuua. Yeye akakimbilia kwa ammi yake Mus’ab bin Abdullah bin Mus’ab na akamsihi amuombe al-Mu’tassim, khalifa wa Bani Abbas kumlinda lakini ammi yake hakumjibu kwa sababu yeye ammi yake hakuwa kama yeye katika uadui wake kwa Alawiyah (hii ilisimuliwa na Ibn Athiir katika kitabu chake, Tariikh al-Kamil - wasifu wa al-Mu’tassim). Baba yake, Bukaar alikuwa ni adui mkubwa wa Imam ar-Ridhaa (a.s.). Imam ar-Ridhaa alimuomba Allah dhidi yake. Alianguka kutoka kwenye kasri yake na akavunja shingo yake. Babu yake, Abdullah bin Mus’ab alitoa fat’wa kwa Harun ar-Rashid, khalifa wa Bani Abbas, kumuua Yahya bin Abdullah bin al-Hasan. Alimwambia ar-Rashid: “Oh, Amirul-muminina, muuwe huyo na mimi nitakuwa mwenye kuwajibika kwa ajili yake.” Ar-Rashid akasema: “Yeye ana mkataba na mimi wa kumlinda yeye.” Akasema: “Hastahili mkataba huo.” Aliivuta ile hati ya mkataba kwa nguvu kutoka kwa Yahya na akaichana kwa mikono yake. Ulikuwa ni uhasama waliourithi, mmoja baada ya mwingine, kutoka kwa babu yao Abdullah bin Zubair hadi ukamfikia az-Zubair bin Bukaar, ambao kwawo alipata upendeleo wa karibu na Mutawakkil kwa kumchagua kumfundisha mwanawe al-Muwaffiq. al-Mutawakkil aliamuru apewe dirham elfu kumi, makabati kumi ya nguo na nyumbu kumi wa kubeba mizigo yake kwenye Samarra. Alimuelimisha mwanawe Muwaffaq na akamwandikia kitabu chake alMuwaffaqiyyat, ambacho kilikuwa ni kitabu kizuri ajabu ambacho tumenukuu sana ndani yake katika kitabu hiki na vitabu vinginevyo. 135


Abu huraira check Lubumba.qxd

7/1/2011

10:48 AM

Page 136

Abu Huraira Aling’ara kiasi gani wakati alipomzidi khalifa kwa hoja hii fasaha. Hakumpa khalifa njia yoyote ya kujibu, hivyo aligeuka na kuondoka haraka. Kama swahiba wake alikuwa ndiye Amiir katika msimu ule wa hijja, kama alivyodai Abu Huraira, yeye asingeondoka haraka isipokuwa ni kwamba aliujua ukweli, kwa sababu yeye alikuwa pamoja na Abu Bakr wakati alipoondoka kuelekea Makka pamoja na Sura ya Bara’a na pale aliporudi bila kukamilisha kazi hiyo. Hivyo yeye alijua kila kitu kuhusu kadhia ile kuliko mtu mwingine yeyote. Wakati mmoja Hasan al-Basri aliulizwa kuhusu Imam Ali (a.s.). Yeye akasema: “Niseme nini kuhusu yeye, ambaye alikuwa na sifa nne; kukabidhiwa al-Bara’a, pili ile Hadith ya Mtukufu Mtume kuhusu yeye katika vita vya Tabuuk, tatu Hadithi ya Mtume kuwaambia Waislam: “Nimewaachieni vizito viwili; Kitabu cha Mwenyezi Mungu Qur’ani na watu wa nyumba yangu ahlul-Bayt,” na ya nne kwamba yeye wakati wote alikuwa ni kiongozi na hajaongozwa na mtu yeyote kamwe, wakati ambapo wale wengine (Abu Bakr, Umar ….. n.k) waliongozwa na viongozi (katika jeshi).179 Ilikuwa inafahamika wazi kwamba al-Hasan al-Basr alikuwa muaminifu kwa Abu Bakr na alijitolea mwenyewe kueneza sifa na ubora wake. Kama Abu Bakr alikuwa ndiye Amir wa hijja katika mwaka ule wa Surat alBara’a, yeye al-Basr asingelificha hilo na asingeshuhudilia kwa Ali kwamba kamwe hakuongozwa na mtu yeyote, na asingeeleza kwamba Abu Bakr aliongozwa na wengine. Kama ukiichunguza hotuba yake utajua kwamba alitambua kule kukabidhiwa al-Bara’a na akajua kwamba ni ubora unaomhusu Ali na hakukuwa na mwingine zaidi yake aliyestahiki vyema kwa sifa hiyo. Wakati masahaba walipokuwa wakimtukuza Imam Ali (a.s.) hapo Madina wakati wa utawala wa Abu Bakr na Umar, walikuwa wakiitaja sifa hii kama moja ya ubora wake na hakuna aliyebishana nao kuhusu hilo. 179 Rejea Sharh an-Nahj al-Hamiid, Jz. 1, uk. 369. 136


Abu huraira check Lubumba.qxd

7/1/2011

10:48 AM

Page 137

Abu Huraira Sa’d bin Abi Waqqas amesema:180 “Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alimtuma Abu Bakr na Sura ya Bara’a. Alipokuwa amekwisha kupita sehemu ya njia, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akamtuma Ali kumfuatia na akaichukue kwenda nayo Makka. Abu Bakr akakosa utulivu na raha. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akasema: “Hakuna mtu yeyote wa kutekeleza wajibat zangu za ki-mbinguni ukiacha mimi mwenyewe au mtu kutoka kwenye familia yangu.” Anass bin Malik alisema:181 “Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alimtuma Abu Bakr na sura ya Bara’a, kisha baadae akamwita na kumwambia: “Hakuna mtu wa kuiwasilisha hii isipokuwa mtu wa familia yangu.” Yeye (s.a.w.w.) akamwita Ali (a.s.) na akaikabidhi kwake. Jamii bin Umayr al-Laythi alimuuliza Abdullah bin Umar kuhusu Imam Ali (a.s.). Ibn Umar akamkaripia na kusema: “Hii ni nyumba ya Mtume (s.a.w.w.) ndani ya msikiti na hii ni nyumba ya Ali (a.s.). Wakati mmoja Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alimtuma Abu Bakr na Umar182 pamoja na Surat al-Bara’a kwenda Makka. Walipokuwa wako njiani kuelekea Makka, mpanda kipando akaja. Waliuliza alikuwa ni nani. Yeye akasema: “Mimi ni Ali. Ewe Abu Bakr, nipatie mimi hicho kitabu ambacho unacho.” Abu Bakr akasema: “Kuna tatizo lolote kuhusu mimi?” Ali akasema: “Sidhani ila wema tu.” Ali akachukua kitabu hicho na akaelekea Makka. Abu Bakr na 180 Rejea kitabu cha an-Nassai, al-Khassa’is al-Alawiyah, uk. 20 na Musnad Ahmad Hanbal. 181 al-Khassa’is al-Alawiyah, uk. 20 na Musnad Ahmad Hanbal, Jz.3, uk.216 182 Umar alikuwa rafiki ya Abu Bakr wakati huo. Alikuwa miongoni mwa masahaba mia tatu ambao waliondoka na Abu Bakr. Lakini Umar alikuwa mwenzi wa karibu sana wa Abu Bakr, kwa hiyo yeye alirejea Madina pamoja naye. Masahaba hao, baada ya kurejea Abu Bakr, walijiunga na Ali, ambaye aliwaongoza kama Amiir wao kwenda Makkah. Wote walishuhudia kwamba Abu Bakr alirejea Madina kwa unyonge. 137


Abu huraira check Lubumba.qxd

7/1/2011

10:48 AM

Page 138

Abu Huraira Umar wakarejea Madina na wakamuuliza Mtukufu Mtume (s.a.w.w.): “Kuna nini kilichotokea kuhusu sisi?” Mtume (s.a.w.w.) akasema: “Hakuna kilichotokea kuhusu ninyi isipokuwa wema tu, bali ilishuka kwangu kwamba hakuna yeyote atakayetekeleza wajibu wangu wa kimbinguni isipokuwa mimi mwenyewe au mtu atokanaye na familia yangu.” Vitabu vya Hadith vimeeleza wazi kwamba Abu Bakr alirejea Madina akiwa mnyonge na alikuwa na hofu kwamba kuna kilichofunuliwa kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kuhusu yeye. Hili halikustahili kwamba alikuwa ndiye Amir wa msimu ule wa hijja. Lakini zile propaganda dhidi ya Imam Ali (A.s.) zilikuwa na nguvu sana kiasi kwamba zilileta athari wakati wa kuanza kwa Uislam. Tatu: Kufutwa kwa mkataba na washirikina kulileta matokeo makubwa kwa Waislam. Vile vile kulimletea Imam Ali utukufu na umaarufu karibu na waarabu wote, wakati Mwenyezi Mungu na Mtume Wake walipofanya kazi hii, hususan baada ya kurudishwa kwa Abu Bakr. Sifa nyingine nyingi zilithibitisha kwamba Imam Ali (a.s.) alikuwa ndiye mbora wa umma na wa karibu sana na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akiwa hai au amekufa. Wakati Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alipoufuta mkataba wa washirikina, akawazuia kuja kuhiji na kuja Makka, na akatangaza kwamba Pepo imezuiwa juu yao, dini ilikamilika na hali ya Waislam ikawa bora na yenye nguvu kuliko hapo kabla kamwe. Waislam walipata heshima na utukufu. Ghadhabu za washirikina zilinyamazishwa na shingo zao zikasalimu amri kwa Waislam. Hivyo dini ikawa yote ni kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, utukufu uwe juu Yake. Mwenyezi Mungu alipenda yote hayo yatimizwe na mja Wake na mlinzi wa Mtume Wake, Ali ibn Abu Talib (a.s.) ili kumtukuza yeye, kuonyesha ubora wake, na kukuza umashuhuri wake, ili kutangaza umuhimu wake, kusafisha njia ya kumdhaminisha na cheo cha ukhalifa baada ya Mtukufu 138


Abu huraira check Lubumba.qxd

7/1/2011

10:48 AM

Page 139

Abu Huraira Mtume (s.a.w.w.) na kutangaza kiutendaji rasmi katika mwaka unaofuatia kwamba yeye atakuwa ndiye Khalifa baada ya Mtume (s.a.w.w.)183 Umashuhuri wa Ali (a.s.) ulienea miongoni mwa waarabu kama mwanga wa asubuhi, kwani kufutwa kwa mkataba wowote, kwa mujibu wa kanuni zao, kulikuwa kufanywe na chifu (kiongozi mkuu), ambaye alifikia makubaliano ya mkataba huo, na hakuna yeyote mbali na yeye anayeweza kufanya hivyo isipokuwa yule ambaye angemuwakilisha yeye au atakayekuwa mrithi wake, ambaye lazima awe jasiri na mwenye nguvu, ambaye hajapatwa na makosa na hakuwa na mashaka katika maamuzi yake au alipovunja au kuzithibitisha hukumu (fat’wa). Ni kipi kitakachokuongoza kwenye chote kile kilichokuwa ni maneno ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kwa Imam Ali pale alipomtuma kuichukua alBara’a kutoka kwa Abu Bakr: “Ama niende nayo mimi au uende wewe.” Imam Ali akasema: “Kama ni lazima iwe, basi mimi nitakwenda.” Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akasema: “Anza kwenda. Allah atauimarisha ulimi wako na kuuongoza moyo wako.”184 Ilikuwa ni dhahiri kabisa kwamba kazi hiyo, ambayo isingeweza kufanywa na yeyote isipokuwa na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) au mtu kama yeye (kwa cheo) ilikuwa ni kazi muhimu sana ambayo Ali alipata ushindi kwa kuikamilisha. Aliushinda wakati, hakuna yeyote ambaye angeweza kumtangulia yeye na hakuna yeyote atakayesimama naye au kukitarajia cheo chake. Yoyote yule ambaye amechunguza vizuri kule kurudishwa kwa Abu Bakr kutoka kwenye kazi hiyo, atakuwa ameuona ukweli dhahiri. Ilikuwa ni kusema kwamba, Mtukufu Mtume aliithibitisha sababu pale aliposema: “Jibril amenijia na kuniambia: “Hakuna mtu yeyote wa kutekeleza kazi 183 Kubatilishwa kwa mkataba wa washirikina kulikuwa katika mwaka wa tisa hijiria na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alimtangaza Imam Ali kuwa Khalifa baada yake katika mwaka wa kumi hijiria, wakati alipokuwa akirejea kutoka kwenye hijja yake ya mwisho. 184 Rejea Musnad Ahmad, Jz. 1, uk. 150 139


Abu huraira check Lubumba.qxd

7/1/2011

10:48 AM

Page 140

Abu Huraira yako tukufu ya ki-mbinguni isipokuwa wewe mwenyewe au mtu kutoka kwenye familia yako.” Katika matini ya kiarabu alisema “LAN” ambayo ina maana kwamba “kamwe haiwi.” Maana ya Hadith hii ni “Hakuna mtu yeyote kabisa wa kufanya lolote – katika kazi ya ki-mbingu – badala yako isipokuwa mtu kutoka kwenye familia yako.” Kama utasema kwamba Hadith hii itakuwa inahusiana na kazi hii tu hasa na sio kwa kazi nyingine kwa jumla; sisi tunasema kwamba hii haikuwa Hadithi pekee yenye maana hii tu basi. Zilikuwepo nyingi mfano wa hii. Katika siku ya Arafa ya hijja ya muago (ya mwisho ya Mtukufu Mtume), Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), kutokea juu ya mgongo wa ngamia jike wake, alijaribu kuvuta nadhari ya mahujaji ili kuwajulisha juu ya kimbilio lao ili kukamilisha kazi ya ujumbe wake. Yeye aliwaita kwa sauti kubwa. Wote walimgeukia kwa macho na masikio yao na nyoyo zao pia. Akasema: “Ali anatokana na mimi, na mimi natokana na Ali. Hakuna mtu hata mmoja atakayebeba kazi zangu isipokuwa mimi mwenyewe na Ali.”185 Ni kukabidhi gani huko, ambako kulikuwa kwepesi kwa ulimi lakini kuzito kwa kipimo. Kulimpa Ali (a.s.) mamlaka kutekeleza kazi za Mtukufu Mtume mwenyewe na kumfanya yeye kukabidhiwa siri za Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kama Haruun alivyokuwa kwa Musa (a.s.), bali tu kwamba yeye Ali hakuwa nabii ila waziri na mlezi, ambaye aliendesha mambo kama mtume wake na akahukumu baina ya watu badala yake. Hicho kilikuwa ni kilele ambacho Mwenyezi Mungu na Mtume Wake hawakumruhusu yeyote isipokuwa Ali kukipanda: “….. basi rudisha macho yako nyuma, je unaona kosa? Tena rudisha macho mara kwa mara, mtazamo wako utarudia hali ya kuhangaika na kuchoka.” 185 Rejea Sunan Ibn Maja, Jz. 1, uk. 92. Ilisimuliwa na at-Tirmidhi na an-Nassai. Ilikuwa ni Hadith ya 2531 katika uk. 153, Jz. 6 ya Kanzul-Ummal. Ilisimuliwa katika Musnad Ahmad Jz. 4, uk. 164. 140


Abu huraira check Lubumba.qxd

7/1/2011

10:48 AM

Page 141

Abu Huraira Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alimnyanyua Imam Ali (a.s.) kwenye kiwango cha juu zaidi kuliko kiwango cha umma. Alichanganya nyama yake na nyama ya Ali, damu yake mwenyewe na damu ya Ali na kusikia, kuona kwake, moyo na nafsi yake pamoja na vyake yeye mwenyewe pale aliposema: “Ali anatokana na mimi, na mimi natokana na Ali.” Hili halikutosha juu yake hadi aliposema: “Hakuna mtu yoyote wa kubeba kazi zangu isipokuwa mimi mwenyewe au Ali.” Aliweka kila kitu katika Hadith hii na akawafanya watu waelewe kile alichokusudia kusema. Haikuwa ni ajabu kwa hilo, kwani Mwenyezi Mungu amesema: “Na kwa hakika tuliwachagua kwa ujuzi kuliko walimwengu. Na tukawapa katika mambo (yetu) ambayo ndani yake mna neema zilizo dhahiri.” 44:32-33. Hebu wenye busara wauchunguze mkataba huu vizuri ili kujua kwamba haukuwa na tofauti katika umuhimu na zile Hadith za siku ya Ghadiir Khum. Kule kubeba kazi za Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), ambako kulihusika na Mtume mwenyewe na Ali tu na kulizuiwa kwa mtu mwingine yoyote kuzifanya, kwenyewe tu kulikuwa ni utekelezaji wa sheria usiokuwa na makosa kama kule kutokuwa na makosa kwa Qur’ani tukufu. Hivyo ilikuwa ni sababu ya dhahiri kwamba umma ulipaswa kutii kama walivyotii amri za Qur’ani tukufu. Hili lilithibishwa na Hadith ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.): “Ali yuko pamoja na Qur’ani, na Qur’ani iko pamoja na Ali. Kamwe havitengani.”186 Na Hadith yake: “Rehema ziwe juu ya Ali! Ewe Allah, igeuzie haki kwa Ali popote atakapogeukia.”187 Na Hadithi nyingi kama hizo, ambazo zimetangaza umaasum wa Imam Ali (a.s.). “Mola wetu! Tumeyaamini uliyoyateremsha, na tumemfuata mtume, basi tuandike pamoja na wenye kushuhudia.” 3:53. Nne: Maadui wa Ali (a.s.), ambao walimkosea na wakajaribu kumharibia 186 Imesimuliwa na al-Hakiim katika al-Mustadrak, Jz. 3, uk. 124 187 al-Mustadrakul-Hakiim, Jz. 3, uk. 124 141


Abu huraira check Lubumba.qxd

7/1/2011

10:48 AM

Page 142

Abu Huraira jina lake, na pia Abu Huraira, aliyewasifu maadui wa Ali, wote wameibadilisha Hadith hii na kuugeuzia ubora wake mbali na yeye. Maadui zake miongoni mwa washirikina na wapinzani wake, ambao walivunja utiifu kwenye utawala wake na wakapigana naye katika vita vya Ngamia, wale ambao waliasi dhidi ya utawala wake pale walipopigana naye katika vita vya Sifiin na Makhaariji, ambao waliritadi kwenye njia ya sawa ya Uislam, wote kwa pamoja walijaribu kufanya hivyo. Maadui zake, hususan wale wenye nguvu za utawala kama vile Mu’awiyah na wafuasi wake waliwatumia mamluki wao kuzigeuza sifa na ubora wa Imam Ali kwa kiasi walivyoweza, au mamluki hao walijipendekeza kwa Bani Umayyah kwa kufanya hivyo. Ali hakuwa na hatia na wao hawataweza kusamehewa kamwe, kwani Mwenyezi Mungu alimtukuza Ali kwa sifa hizi kubwa kwa sababu alifikia nafasi ya juu sana karibu na Mwenyezi Mungu kwa imani na jihadi yake. Hawakuweza kustahimilia ule utukufu na heshima ya Ali na zile sifa alizokuwa nazo, uaminifu wake kwa Mwenyezi Mungu, kwa Mtume na kwa umma, shaksia yake, maadili yake, udugu wake na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), mke wake na kizazi chake, kwa hiyo walijitahidi kwa uwezo wao wote kumharibia jina lake na kugeuza maadili yake yote. Nge wa husuda alitambaa kwenye nyoyo za wanafiki. Watoto wa yule mla-maini188 walishika nafasi ya juu kabisa ya chuki kwa Ali (a.s.). Hawakuiacha fursa yoyote ya kupigana naye, kumdhalilisha na kuwachochea watu dhidi yake. Waliendeleza hila zao, wakavunja utiifu wao kwake, wakamnyima utawala wake wa haki na wakakiua kizazi chake. Waligeuza migongo yao kwa kile alichowaamuru Mtukufu Mtume, kuwapenda na kuwatii. Walichokitenda dhidi yake kiliijaza nafasi na kuifunika dunia. Yote hayo hayakuwaridhisha wao mpaka wakatangaza laana juu yake, kama yale matamshi ya (Iqama) kukimu swala. 188 Alikuwa ni Hind, mke wa Abu Sufyan na mama yake Mu’awiyah. Alipasua kifua cha Hamza, ammi yake Mtume, alipokuwa ameuawa katika vita vya Uhud na akala ini lake. 142


Abu huraira check Lubumba.qxd

7/1/2011

10:48 AM

Page 143

Abu Huraira Je, hawakuipotosha Sunna tukufu pale walipochana kila kitu kilichohusika na kumfadhilisha Imam Ali (a.s.)? Waliamua bila ushahidi wowote kwamba zile Hadith sahihi zilikuwa ni za uwongo. Walizitafsiri zile zilizokuwa wazi kwa kulingana na matakwa yao. Waliwashutumu wasimuliaji kuwa ni wenye kuleta upinzani. Waliigeuza sehemu kubwa ya Sunna na kubadili zile maana halali za Hadith kama vile Abu Huraira alivyoeleza katika Hadith hii pale aliposema: “Abu Bakr alinituma mimi ….. kisha akamtuma Ali nyuma yetu kwenda kutangaza pamoja nasi …..” kana kwamba Ali katika msimu ule wa hijja alikuwa kama mmojawapo tu wa watangazaji waliotumwa na Abu Bakr kutangaza pamoja na Abu Huraira. Halikuwa ni jambo la kushangaza kwa Abu Huraira kwa ushupavu wake katika kubuni Hadith na kuzielekeza zikiwa zimepambwa kwa mapambo ambayo wengi waliyapenda na ile sera ya kawaida ikakubalika na zikaenezwa kwa propaganda ya uongo. Je hakuhamisha ubora kutoka kwa Ali kwenda kwa Abu Bakr kwa kuipendeza serikali na kuwafanya watu wampende kwa kuzua kilichowafurahisha wao? Ni kitendo gani alichofanya! Aliinyamazisha midomo kuongea maneno ya haki kwa kuhofia umma usije kupanga njama dhidi yao na serikali kulipiza kisasi. Na ni nini tena baada ya hapo? Abu Huraira alitaka kwa Hadith hii kufagilia mbali kile cheo cha heshima ambacho Mwenyezi Mungu na Mtume Wake walikichagua kwa ajili ya Ali (a.s.) katika msimu ule wa hijja. Alielekea kusema: 1. Kazi ambayo Ali (a.s.) aliyokwenda kufanya, ilikuwa ni kwa amri ya Abu Bakr, ambaye alikuwa ndiye Amiir wa hijja kama Abu Huraira alivyojidai kusema. Kwamba Imam Ali (a.s.) hakukidhi kutekeleza kazi hiyo, hivyo Abu Bakr akamtuma Abu Huraira pamoja na baadhi wenye nguvu na wagumu kama yeye Abu Huraira kuchukua uangalifu zaidi kuhusu kazi hiyo.

143


Abu huraira check Lubumba.qxd

7/1/2011

10:48 AM

Page 144

Abu Huraira 2. Ali (a.s.) hakuwa na kitu zaidi ya waliyokuwa nayo Abu Huraira na kundi lake ambao walitumwa na Abu Bakr katika kazi hiyo, kwa sababu wao walifanya vile vile kama alivyofanya yeye Ali (a.s.). Ilikuwa inatosha kuikanusha Hadith hii kwamba Mwenyezi Mungu alimuona Abu Bakr hakufaa kwa ajili ya kazi ile. Alimfunulia Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kumrudisha na kuchagua mmoja wa watu wawili pekee wenye uwezo wa kufanya kazi hii; ama Mtume mwenyewe au mlinzi wake Ali. Abu Huraira, kabla hajaajiriwa kuwahudumia Bani Umayyah katika propaganda yao, alisimulia juu ya tukio hili bila ya kueleza kwamba Abu Bakr alikuwa ndiye Amiir au hata kumtaja kabisa. Alijifanya kwamba yeye na wale wapiga mbiu wengine walikuwa pamoja na Ali. Rejea kwenye Hadith hii iliyotajwa hapo juu. Hatuziamini Hadith zake zote, wala kwamba alitangaza katika Siku ya kutoa Kafara, au kwamba alihudhuria kamwe kwenye msimu huo wa hijja. Namuapa Mwenyezi Mungu kwamba hatuamini katika chochote alichosimulia. Tano: Ile propaganda ya kisiasa, wakati wa utawala wa Bani Umayyah, ilitenda jinai kubwa dhidi Hadith za Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) mbali na yale yaliyozushwa na kubuniwa na mamluki wao kwa kuwapendeza hao watawala na jinsi walivyojaribu kwa nguvu zote kuifanya ile Hadith ya Hamiid iliyosimuliwa kutoka kwa Abu Huraira kuifanya iwe ya kweli. Kubuni Hadith ilikuwa ni hila nzuri sana ya wenye kujipendekeza ili waishi kwayo. Wale wenye kusifu walikuwa na ustadi wa kupamba na kutangaza biashara zao (Hadith) ambazo hakuna aliyezihisi kwa wakati ule isipokuwa wale watambuzi nao walikuwa ni wachache kiasi gani! Nyuma ya wale wenye kusifu walikuwepo mamluki wa wale ambao walikusanya na kuandika Sunna na Hadith, wadanganyifu wenye weledi, wanafiki 144


Abu huraira check Lubumba.qxd

7/1/2011

10:48 AM

Page 145

Abu Huraira ambao walijifanya kuwa wachamungu na wenye kujinyima kama Hamiid bin Abdur-Rahman, Muhammad bin Ka’b al-Qardhi na wengine kama hao, machifu wa makabila katika miji na masheikh wa koo katika jangwa, ambao wakati wowote waliposikia chochote kutoka kwa wale wenye kujipendekeza, walikieneza miongoni mwa umma na mikusanyiko ya zile nchi zilizotekwa hivi punde, walioelezwa kutoka juu ya mimbari, wakazitegemea kama kisingizio na wakazichukulia kama sharia. Wale waumini wenye kuaminika hawakuwa na cha kufanya bali kunyamaza kimya mbele ya wale mamluki wanaojipendekeza, ambao walilindwa na watawala. Endapo wale masikini waliulizwa kuhusu kile wale waongo walichozusha miongoni mwa Hadith, hususan zile zilizozungumzia kuhusu ubora wa Abu Bakr na Umar, wangewaogopa watu ambao waliwafuata watawala kibubusa, kama wangesema kweli. Wao wangewaogopa wale wadanganyifu na wale wanaodanganywa pia. Hivyo ukweli mwingi ulipotea na uasi mwingi uliwekwa kama misingi ya sharia. Uasi huu, wa Hamiid na Abu Huraira ulikuwa ndio bahati kubwa kwa wenye nguvu dhidi ya familia ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Walibuni Hadith nyingi nyingine zenye maana hiyo hiyo na wakahusisha mojawapo kwa Imam Ali (a.s.) mwenyewe, ya pili kwa ammi yake Abdullah Ibn Abbas, ya tatu kwa sahaba wake Jabir bin Abdullah al-Ansari na ya nne kwa mjukuu wake, mrithi wa elimu yake, Imam Muhammad al-Baqir (a.s.). Ilikuwa ni njama ambayo maadui wa Ali waliitumia na waliiendeleza katika kuwadhalilisha Bani Hashim bila kuwaacha watu na umma kwa jumla kujua ukweli. Watu waliokuja baada yao walizikusanya Hadith hizo kama zilivyokuwa na wakaziandika vya kupendeza sana. Walichukulia kile walichokikusanya kama Hadith za kweli bila kuzingatia hata kidogo. Mdhaifu wa sanadi ya wapokezi wa ile Hadith, ambayo ilihusishwa kwa Imam Ali ulikuwa ni Abu Zar’a Wahab bin Rashid. Alikuwa na chuki sana juu ya Imam Ali. Aliutwaa uhasama huo kwa Bani Hashim kutoka kwa mwalimu wake, Abu Yaziid Yunus bin Yaziid bin an-Najjad al-Ibli, huria 145


Abu huraira check Lubumba.qxd

7/1/2011

10:48 AM

Page 146

Abu Huraira wa Mu’awiyah.189 Mdhaifu wa sanadi ya wapokezi wa ile Hadith, ambayo ilihusishwa kwa Ibn Abbas alikuwa ni Abul Qassim Muqsim bin Majza’a. Yeye alitangaza uadui wake kwa Imam Ali (a.s.). Al-Hakiim alifikiria kwamba mtu huyu alikuwa ni mmoja wa watu wasimulizi wa Hadith wa Bukhari na alisimulia riwaya zake za kubuni zilizohusishwa kwa ibn Abbas katika alMustadrak yake.190 Muqsim hakuwa mwaminifu kama al-Bukhari alivyoeleza katika kitabu chake. Adh-Dhahabi katika kitabu chake al-MizanulI’tidal amenukuu kutoka kwa al-Bukhari na Ibn Hazim kwamba bwana huyu hakuwa mkweli. Ibn Sa’d amesema katika Tabaqat 191 yake kwamba alikuwa amekithiri katika usimuliaji wa Hadith na alikuwa sio mkweli wa kuaminika. Kwa sababu hakuwa mkweli, Bukhari na Muslim hawakusimulia Hadith zake isipokuwa moja tu iliyosimuliwa na Bukhari kwamba Abdul Kariim bin Malik alisema kwamba alikukwa amemsikia Muqsim akisema: “Ibn Abbas amesema: ‘Wale ambao hawakwenda kupigana katika vita vya Badr na wale ambao walipigana hawawezi kamwe kuchukuliwa kuwa wako sawa.’” al-Bukhari hakusimulia lolote katika Sahih yake isipokuwa riwaya hii tu ya Muqsim, akithibitisha kwamba alikuwa sio mkweli. Alisimulia Hadith hii kwa vile ilikuwa haina fat’wa yoyote ya kisheria mbali na kwamba 189 Abu Nasr al-Kalabathi, Abu Bakr al-Isbahani na Abul Fadhl ash-Shaybani, ambaye alikuwa akijulikana kama Ibnul Qaysarani alisimulia katika vitabu vyake kwamba Yunus bin Yaziid alikuwa ni mtumwa aliyeachwa huru na Mu’awiyah. Rejea kwenye kitabu cha Ibnul Qaysarani uk. 485. Yunus huyu huyu alisimulia kwamba Abu Talib hakuwa mu’min wakati alipofariki. Rejea Sahih Muslim, Jz. 1, uk. 30. 190 al-Mustadrakul-Hakiim, Jz. 3, uk. 51 191 Tabaqat, Jz. 5, uk. 346 146


Abu huraira check Lubumba.qxd

7/1/2011

10:48 AM

Page 147

Abu Huraira haikusemwa na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) Mdhaifu wa ile Hadith, ambayo ilihusishwa kwa Jabir ulikuwa ni Abu Salih is’haq bin Najiid al-Malti. Yeye alikuwa mwenye kuchukiza, muovu, mwingi wa uongo. Alikuwa jasiri sana katika kuzua Hadith kama ilivyoelezwa na wote walioandika kuhusu watu wa Hadith. Mdhaifu wa ile Hadith iliyohusishwa kwa Imam Muhammad al-Baqir (a.s.) alikuwa ni Muhammad ibn Ish’aq ambaye alisimulia Hadith hiyo katika kitabu chake cha wasifu, ambayo aliijaza uasi wa kidini na maajabu ambayo hayawezi kuaminika. Kwa njia yoyote ile, ilikuwa ni rahisi kuzikanusha Hadith hizi za kuzushwa kwani zilikuwa duni kama wasimulizi wake. Maelezo yake yalikuwa dhaifu na yenye kupingana na ukweli wa wale ambao zilikuwa zimehusishwa kwao. Kwa kweli zilikuwa zinapingana na riwaya zilizosimuliwa na Abu Bakr, Ali, ibn Abbas, ibn Umar, Saad na Anass ambazo tulizisimulia katika hoja ya pili ya mlango huu. Haikulingana na tabia ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) ambaye hakuwahi kamwe kumteua mtu yeyote kumsimamia Ali katika wakati wa uhai wake, bali Ali wakati wote alikuwa ndiye jemadari na mshika bendera katika vita vyote vya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Ilikuwa ni tofauti kwa wengine kama vile Abu Bakr, Umar na wengineo ambao walikuwa chini ya uongozi (ukamanda) wa kijana wa miaka kumi na nane, Usamah bin Ziyad wakati Mtukufu Mtume alipokuwa anaondoka kwenda kwenye ulimwengu bora. Katika vita vya Dhat asSalassil, wao Abu Bakr na Umar walikuwa chini ya ukamanda wa Amr bin Aass.192 Na kuhusu Ali, yeye hakusimamiwa na kamanda yoyote katika uhai wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Mtukufu Mtume hakumtuma yeye na jeshi la 192 Rejea kwenye al-Mustadrakul-Hakiim, Jz. 3, uk. 43 na Talkhiis ya athThaalabi. 147


Abu huraira check Lubumba.qxd

7/1/2011

10:48 AM

Page 148

Abu Huraira Usamah wala na jeshi la Amr bin Aass au jeshi lolote lile la Abu Bakr na Umar wakati alipowatuma Khaybar. Wakati wao waliporejea, yeye (s.a.w.w.) alimpeleka Ali na wote hao walikuwa chini ya ukamanda wa Ali (a.s.) mpaka pale alipoiteka Khaybar. Wakati Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alipomtuma Khaliid bin al-Walid kwenda Yemen pamoja na jeshi, na akamtuma Ali pamoja na jeshi jingine, aliwaambia wote kwamba, endapo watakutana, basi Ali atakuwa ndie kamanda wa majeshi yote mawili, na kama watatengana tena, hapo kila mmoja atakuwa kamanda wa jeshi lake.193 19. Malaika wazungumza na Umar: Al-Bukhari amesimulia194 kwamba Abu Huraira alisema: “Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amesema: “Baadhi ya watu kati ya Bani Israili, ambao waliishi kabla yenu, walizungumzishwa na Malaika ingawa wao hawakuwa mitume. Kama kuna mtu yoyote katika umma wangu ambaye ni kama wao, basi atakuwa ni Umar.”195 Bukhari alisimulia Hadith nyingine196 kutoka kwa Abu Huraira kwamba alisema: “Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisema: “Walikuwepo watu miongoni mwa umma ambao waliishi kabla yenu, ambao walisemeshwa na Malaika. Kama umma wangu unaye mtu kama hao, basi atakuwa ni Umar.” Ilikuwa ni Hadith ya kuzushwa ambayo Abu Huraira alikuwa ameibuni pamoja na maneno ya kuipamba miaka mingi baada ya kifo cha Umar. Ilijitokeza kama vile tu ile sera ya watu wa tabaka la juu walivyotaka, na umma kwa wakati ule ulijikongoja pamoja nayo kwa furaha. Ile sera ya 193 Rejea Musnad Ahmad Hanbal, Jz. 5, uk. 356 194 Ndani ya Sahih al-Bukhari yake, Jz. 2, uk.194 195 Rejea kitabu cha al-Qastalani, Irshaad as-Sari, Jz. 7, uk. 349 196 Sahih al-Bukhari, Jz. 2, uk. 171. 148


Abu huraira check Lubumba.qxd

7/1/2011

10:48 AM

Page 149

Abu Huraira kihasama ya Bani Umayyah dhidi ya Imam Ali (a.s.) na Bani Hashim ilihitajia kumkweza Abu Bakr na Umar hadi kwenye nafasi ya mitume na watawa maasum. Umma ulikuwa na hamasa sana kwa ushindi uliopatikana katika vipindi vya utawala vya makhalifa wawili hao, Abu Bakr na Umar, hivyo Abu Huraira aliwafurahisha wote; mtawala na watu wanaotawaliwa kwa Hadith hii na zinazofanana nayo, kwa hiyo alipata nafasi ya upendeleo wa karibu na watawala na miongoni mwa umma. Kama Abu Huraira angezisimulia Hadith hizi katika wakati wa uhai wa Umar, fimbo ya khalifa ingepata sehemu yake ya kuchapa kutoka mgongoni kwake, lakini nafasi ilikuwa huru kwa yeye kuzungumza chochote alichokitaka. Ilikuwa inafahamika vyema kwa wale watambuzi na wenye hekima kwamba wale ambao Malaika waliongea nao walikuwa ama ni mitume au mawasii wa mitume, ambao wote walikuwa ni maasum. Malaika hao walizungumza na mitume ana kwa ana lakini kuhusu mawasii wao, Mwenyezi Mungu aliwazindua na ukweli huo kana kwamba Malaika waliongea nao, lakini kwa kweli hapakuwa na mzungumzaji pale. Hakuna shaka kwamba Umar alipata hadhi ya juu sana katika Uislam na alifanya vyema kwa ajili ya umma, lakini yeye hakuwa mtume wala hakuwa wasii maasum, hivyo Malaika wasingezungumza naye. Zaidi ya hayo ni kwamba utendaji wa Umar wakati wa uhai wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na baada ya kufariki kwake haukustahiki yeye kusemeshwa na Malaika hata kidogo. 20. Urithi wa Mtume ni kwa ajili ya sadaka: Masheikh hao wawili wamesimulia kwamba197 Abu Huraira alisema kwamba: “Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amesema: “Warithi wangu hawapaswi kugawana hata dinari yangu moja miongoni mwao. Kile nilichokiacha mimi, baada ya kutoa matumizi ya wake zangu na watumishi wangu, 197 Rejea Sahih al-Bukhari, Jz. 2, uk. 125, na Sahih Muslim, Jz. 2, uk. 74 149


Abu huraira check Lubumba.qxd

7/1/2011

10:48 AM

Page 150

Abu Huraira chote ni kwa ajili ya sadaka.” Hadith hii ilisimuliwa na Abu Bakr peke yake tu. Aliitumia kama kisingizio cha kumzuia Fatima az-Zahra, binti ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), kupata urithi wake baada ya kifo cha baba yake. Masheikh hawa wawili na wengineo wamesimulia kwamba Aisha (mke wa Mtukufu Mtume) amesema:198 “Fatima binti ya Mtukufu Mtume alituma kwa Abu Bakr akimuomba mirathi ya baba yake. Abu Bakr akasema: “Mtume amesema: Sisi hatuachi urathi. Kile tunachokiacha sisi kinatakiwa kiwe kwa ajili ya sadaka.’”199 Abu Bakr alikataa kumpatia chochote katika urithi wa baba yake. Fatima alimkasirikia sana Abu Bakr. Alimsusa yeye na hakuzungumza naye hadi alipofariki dunia. Yeye Fatima aliishi kwa miezi sita baada ya kufariki baba yake. Wakati alipofariki, mume wake alimzika wakati wa usiku (kama alivyotaka katika wasia wake) na Abu Bakr hakumsalia swala ya jeneza Bibi Fatima (a.s.). Ndio, yeye alikasirika sana. Alivaa hijabu yake na akatoka nyumbani kwake pamoja na wanawake wenzie. Mwendo wake ulikuwa sawa sawa tu kama ule wa baba yake, hadi alipofika kwa Abu Bakr, ambaye alikuwa miongoni mwa mkusanyiko wa Muhajiriina, Ansari na wengineo. Waliweka pazia baina yake na wao. Alipiga kite na akawafanya wote waliohudhuria kulia machozi. Hadhara hiyo ilitingishika. Alisubiri kidogo hadi kupiga kwikwi kwao na hisia zikatulia. Alianza hotuba yake kwa kumtukuza na kumshukuru Mwenyezi Mungu. Aliendelea na hotuba yake ambayo ilifanya macho ya watu yashindwe kuona na nyoyo zikasalimu amri. Angeweza kuwarudisha kwenye njia ya haki lakini siasa zilifunika kila kitu wakati huo!

198 Rejea Sahih al-Bukhari, Jz. 3, uk. 37, Sahih Muslim, Jz. 2, uk. 72 na Musnad Ahmad Hanbal, Jz. 1, uk. 6 199 Hadith hii ilikanushwa na Bibi Fatima (a.s.) na Maimam ma’sumin wote (a.s.) 150


Abu huraira check Lubumba.qxd

7/1/2011

10:48 AM

Page 151

Abu Huraira Yule ambaye alisikia hotuba yake aliyoitoa siku ile,200 ataweza kujua kwamba walikuwepo kati yake yeye na watu,201 Abu Bakr na Umar. 200 Rejea kitabu cha at-Tabari, al-Ihtijaj na Bihar al-Anwar. Baadhi ya wanahistoria wa Sunni wameielezea hotuba hii katika vitabu vyao kama vile Abu Bakr Ahmad bin Abdul Aziz aj-Jawhari katika kitabu chake, Kitab as-Saqifa na Fadak. Rejea Nahjul-al-Hamiid, Jz. 4, uk. 87, uk. 93, na uk.94. 201 Alimwambia Abu Bakr, wakati alipokataa kumpa mirathi ya baba yake: “Oh, Abu Bakr, kama wewe ukifariki ni nani atakayekurithi?” Abu Bakr akasema: “Wanangu wa kiume na familia yangu.” Bibi Fatima akasema: “Basi ni kwa nini wewe umerithi mirathi ya Mtume badala ya kizazi chake na familia yake?” Yeye akasema: “La sikufanya hivyo, ewe binti ya Mtume.” Bi. Fatima akasema: “Ndio, kwa hakika umefanya hivyo. Umeichukua Fadak (eneo kubwa lililopandwa mimea), ambayo ilikuwa mali binafsi ya Mkutufu Mtume (s.a.w.w.) mwenyewe na ukatunyima sisi kile ambacho Allah amekifunua (wahyi) toka mbinguni kuwa ni chetu.” Rejea kitabu cha Abu Bakr bin Abdul Aziz, Kitab as-Saqifa na Fadak, Jz. 4, uk. 87. Ilisimuliwa pia katika ukurasa wa 82, kwamba wakati Fatima alipomuomba Abu Bakr urithi wake, yeye alimwambia: “Nilimsikia Mtukufu Mtume akisema: “Mtume hawarithishi.” Lakini mimi ninamsaidia yeyote yule ambaye Mtukufu Mtume alikuwa akimsaidia na ninatumia kwa yeyote ambaye Mtume alikuwa akitumia juu yake.” Bibi Fatima akasema: “Oh, Abu Bakr, binti zako wewe warithi mali yako lakini binti ya Mtume asimrithi baba yake?” Yeye akasema: “Hivyo ndivyo ilivyo.” Ahmad pia ameisimulia Hadith kama hiyo ndani ya Musnad yake Jz. 1, uk. 10, Jawhari ameisimulia katika Kitab as-Saqifa na Fadak, Jz. 4, uk. 81, riwaya iliyosimuliwa na Umm Hani bint Abu Talib kwamba Fatima alimwambia Abu Bakr: “Kama wewe ukifariki, ni nani atakayekurithi?” Yeye alijibu: “Kizazi na familia yangu.” Fatima akasema: “Basi kwa nini wewe unamrithi Mtume badala yetu sisi?” Yeye akasema: “Oh, ewe binti ya Mtume wa Mwenyezi Mungu, baba yako wewe hakuacha kitu chochote.” Akasema: “Ndio aliacha. Lilikuwa ni lile fungu ambalo Mwenyezi Mungu alitutengea sisi (kwa mujibu wa Qur’ani) na likawa mali yetu, ambayo sasa imo mikononi mwako.” Abu Bakr akamwambia: “Mimi nilimsikia Mtukufu Mtume akisema: “Kama Fadak ni njia ya riziki aliyotupa sisi Mwenyezi Mungu na nitakapofariki itakuwa ni kwa ajili ya Waislamu.” Kulikuwa na hotuba nyingine ya Bibi Fatima kuhusu ukhalifa iliyosimuliwa na Jawhari katika Kitab as-Saqifa na Fadak, Jz. 4, uk.87 kwamba Fatima bint al-Husein alisema: “Wakati Fatima, binti ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alipokuwa mgonjwa sana, wanawake wa Muhajiriina na Ansari walikusanyika kumzunguka yeye na wakamuuliza: “Una hali gani, ewe binti ya Mtume?” Yeye akasema: “Nimeyajutia maisha yenu maovu na kuwachukia wanaume wenu …….” Ilisimuliwa pia na Imam Abul-Fadhl Ahmed bin Abu Tahir ndani ya kitabu chake, Balaghat an-Nissa’ uk. 23, al-Majlisi ndani ya Biharul-Anwar na at-Tabarsi ndani ya al-Ihtijaj yake.

151


Abu huraira check Lubumba.qxd

7/1/2011

10:48 AM

Page 152

Abu Huraira Alithibitisha haki zake kwa ushahidi wa wazi uliotolewa kwa mujibu wa Qur’ani tukufu ambao haukuweza kukatalika. Yeye, Bibi Fatima alisema: “Je, mligeuzia migongo yenu kwa makusudi kwenye Kitabu cha Allah, ambaye amesema: “Na Suleiman alikuwa mrithi wa Daudi. (27:16) na akasema wakati alipokuwa akizungumza kuhusu Zakaria: “….. basi nipe mrithi kutoka kwako. Atakayenirithi na awarithi ukoo wa Yaakub na umfanye, ewe Mola Wangu, awe mwenye kuridhisha.” (19:5-6) “….. na ndugu wa nasaba wana haki zaidi wao kwa wao katika Kitabu cha Mwenyezi Mungu …..” (8:75) “Mwenyezi Mungu anawausia kuhusu watoto wenu, mwanaume apate sawa na fungu la wanawake wawili …..” (4:11) Na akasema tena: “Mmelazimishwa mmoja wenu anapofikiwa na mauti, kama akiacha mali, kuwausia wazazi wawili na jamaa kwa uadilifu, ni wajibu kwa wamchao Mungu.” (2:180). Kisha akasema: “Je, Mwenyezi Mungu alikufanyeni ninyi kuwa mahususi kwa aya ya Qur’ani na akamuondoa baba yangu? Wewe unao utambuzi zaidi wa Qur’ani kuliko baba yangu na binamu yangu Ali? Au unasema kwamba: wale wa dini mbili tofauti hawapaswi kurithiana wao kwa wao?” Alihojiana nao kwa kutoa ushahidi kutoka kwenye Qur’ani tukufu, ambao ulithibitisha wazi kwamba mitume waliwarithisha watoto na vizazi vyao kupitia zile aya kuhusu Daudi na Zakaria. Alikuwa haswa ana ufahamu zaidi wa msingi wa Qur’ani, kuliko wale ambao walikuja wakiwa wamechelewa baadae kabisa, baada ya kushuka kwa Qur’ani na wakageuza ile maana ya mirathi kutoka kwenye rasilimali kwenda kwenye ubashiri na busara bila ya ushahidi wowote ule. Walicheza tu na ile maana halisi ya maneno! Kama hiyo ilikuwa ni kweli, Abu Bakr na wale wote

152


Abu huraira check Lubumba.qxd

7/1/2011

10:48 AM

Page 153

Abu Huraira waliokuwa wamehudhuria pale wangekosa kukubaliana naye kuhusu hilo.202 Kulikuwepo na baadhi ya ushahidi unaothibitisha kurithi rasilimali kwa mitume kama ilivyosimuliwa na Allamal-Huda katika kitabu chake, ash-Shafi.203 202 Hawakupingana naye kuhusu urithi wa Mtume (iwapo ilikuwa ama elimu na hekima mbali na rasilimali) au kitu kingine chochote. Walimnyang’anya tu mirathi yake, ambapo Abu Bakr alisema: “Oh, ewe binti ya Mtume, Mwenyezi Mungu hakuumba yoyote mpendwa kwangu kuliko baba yako, Mtume Muhammad (s.a.w.w.). Nilitamani mbingu ingeanguka juu ya ardhi wakati baba yako alipofariki. Naapa Wallahi, kwamba kama Aisha (binti ya Abu Bakr) angekuwa mwenye haja ni bora kwangu kuliko wewe kuwa mwenye shida. Hivi mimi ninawapa (watu) weupe na wekundu haki zao halafu nikunyime wewe haki yako, ambapo wewe ni binti ya Mtume? Mali hii haikuwa mali binafsi ya Mtume bali ilikuwa ni ya Waislam. Aliitumia kwa ajili ya Allah. Alipofariki mimi nikawa ndiye mwenye wajibu kwayo.” Yeye Bi. Fatima akasema: “Sitazungumza na wewe baada ya sasa.” Abu Bakr akasema: “Lakini mimi sitakutelekeza.” Yeye akasema: “Nitaomba kwa Allah dhidi yako.” Akasema: “Mimi nitakuombea Mungu.” Kabla hajafariki, Fatima aliagiza kwamba Abu Bakr asije akaswalia jeneza lake. Rejea Kitab as-Saqifa na Fadak, Jz. 4, uk. 80, utakuta kwamba yeye hakupingana naye kuhusu maana ya mirathi wakati alipotaja zile aya mbili za Daudi na Zakariah, lakini alisingizia kwamba mali ile haikuwa mali binafsi ya Mtume. Fatima hakuridhika kwani yeye alikuwa ndiye mtambuzi bora wa mambo ya baba yake. Bali hakuna nguvu ila kwa Allah, Mwenye Enzi, Mtukufu. 203 Allamal-Huda alifikiria kwamba Zakaria alihofia juu ya binamu zake kurithi mali yake, kwa vile alikuwa hana mtoto wa kiume, na walikuwa waovu na mafisadi. Ilikuwa haiwezekani kwamba wanaweza wakawa manabii au wachamungu wenye hekima kwamba alihofia wangerithi hadhi yake ya elimu, hekima na utume, bali alikuwa akihofia watarithi mali yake na kuitumia katika uharibifu na uovu wao, kwa hiyo alimuomba Mola wake kumpatia kijana ambaye atakuwa mwenye kufaa kurithi mali yake kuliko binamu zake hao waovu. Allamal-Huda pia alifikiria kwamba wakati Zakariah alipomuomba Mola wake kumfanya mrithi wake anayeridhisha hilo lilimaanisha kurithi mali yake. Kama Zakariah alimaanisha urithi wa utume, ingekuwa haileti maana kumuomba Mwenyezi Mungu kumfanya mwanawe awe mwenye kuridhisha sawa kabisa kama kusema: “Ewe Allah, tuletee mtume na umfanye awe mwaminifu na sio muongo. 153


Abu huraira check Lubumba.qxd

7/1/2011

10:48 AM

Page 154

Abu Huraira Kisha alihojiana nao akithibitisha haki yake ya kurithi kwa kuwaonyesha aya nyingine za Qur’ani kuhusu mirathi. Kama yeye alikuwa ni tofauti na watu wengine kuhusu jambo hili, basi baba yake, (s.a.w.w.) na mume wake (a.s.) wangemueleza yeye kwa uwazi kabisa na wasingemuacha alazimike kujitokeza kama mjinga asiyejua kitu katika kudai kile ambacho hakustahiki na kujiaibisha mwenyewe na hadhi yake kwa kubishana bila ushahidi wowote kiasi kwamba ingeishia kwenye uadui. Ilikuwa haiwezekani kwa Mtukufu Mtume na wasii wake kufanya hivyo. Mtukufu Mtume Muhammad (s.a.w.w.) alimpenda sana binti yake Fatima az-Zahra’ na alimjali sana zaidi kuliko aina ya baba wengine na watoto wao. Alimkumbatia wema wake mkunjufu na alikuwa tayari kabisa kujitolea muhanga mwenyewe binafsi hasa kwa ajili yake.204 Alifurahia sana kuwa naye karibu. Alikuwa na uangalifu mwingi katika kumlea na kumkuza kwa maadili na hadhi ya hali ya juu kabisa. Alifanya juhudi zote ziwezekanazo kumuelimisha yeye. Alimlisha na kumjaza elimu ya Mwenyezi Mungu na Shari’ah hadi akafikia kileleni mwa kila wema na kila utukufu wa tabia. Hata hivyo, angeweza kulifanya ni siri lile lililohusu wajibu wake wa kisheria? Mungu aepushilie mbali hilo! Angewezaje kufanya hivyo na kumuacha apambane na yote yale yaliyomkuta baada ya kifo chake kwa sababu ya mirathi hiyo? Kwa hakika hilo ni hapana! Alikuwa mbali sana nalo hilo. Je, mume wake, yule mwenza na ndugu yake Mtume (s.a.w.w.) aliipuuza Hadith hii licha ya elimu yake kubwa na hikma na kwamba yeye alikuwa ndiye Mwislam wa kwanza, binamu yake Mtume na mkwe wake, licha ya hadhi yake, cheo cha juu, uwasii na ile heshima maalum aliyokuwa nayo Mtukufu Mtume juu yake? Kwa nini iwe Mtume aliifanya ni siri na asiifichue kwa Imam Ali (a.s.), ambaye alikuwa na sifa zote hizo na tabia 204. Wakati mmoja Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) zzzlimtaja yeye na akasema: "Baba yake anajitoa muhanga mwenyewe kwa ajili yake." Alilirudia hilo mara tatu katika Hadith iliyosimuliwa na Ahmad bin Hanbal na Ibn Hajar katika kitabu chake, as-Sawa'iq al-Muhriqah, uk. 109. 154


Abu huraira check Lubumba.qxd

7/1/2011

10:48 AM

Page 155

Abu Huraira tukufu ambazo hakuna mwingine yeyote awaye aliyekuwa nazo? Vipi kuhusu hao Bani Hashim wote, ambao hawakuwahi kamwe kuisikia Hadith hii, mpaka wakaja kushangazwa kwa kuisikia baada ya kufariki kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.)? Kwa nini hata wake za Mtume hawakujua chochote kuhusu Hadith hii ambapo walimwendea Uthman na kumtuma akawaombee kuhusu mafungu yao kutoka kwenye mirathi ya Mtume (s.a.w.w.)?205 Iliwezekana vipi kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kumwambia mtu ambaye alikuwa hahusiki kwa chochote kile katika mirathi yake, kuhusu mirathi hiyo na asiwaambie warithi wake halisi? Tabia ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) haikuwa hivyo. Yeye alizitangaza amri za Allah kwa ukweli na uaminifu kabisa. Haikuwahi kusemekana kamwe kwamba yeye alizificha kanuni za kisheria sirini. Aliwatendea kabila lake na jamaa zake kwa upole na taadhima kabisa. Kulikuwa bado kuna neno alilolisema Fatima (a.s.) ambalo lilivuta mioyo ya watu na kupandisha hasira zao kwa hali ya juu kabisa. Ilikuwa ni kule kusema kwake kuwa: “au unataka kusema kwamba wale wa dini mbili tofauti hawapaswi kurithiana wao kwa wao?� Hilo lilikuwa ni kusema kwamba: wakati uliponizuia urithi wa baba yangu juu yangu, ulitaka kusema kwamba mimi sikuwa kwenye dini ya baba yangu (sio Mwislam) na kama ungelithibitisha hilo, ungekuwa na kisingizio cha kisheria cha kunizuia mimi kumrithi baba yangu. Sisi hatuombi ila hukumu ya Mwenyezi Mungu! Hata hivyo, Fatima (a.s.) alishindwa kupata urithi wake kwa sababu ya Hadith hii, ambayo ni khalifa peke yake aliyeisimulia. Haikusimuliwa na mtu mwingine yoyote mbali na yeye. Inaweza ikasemwa kwamba ilisimuliwa na Malik bin Auss bin al-Hadthan.206 205 Rejea Kitab as-Saqifa na Fadak cha Abu Bakr aj-Jawhari na pia kwenye Sharh an-Nahj al-Hamiid, Jz. 4, uk. 83. 206 Rejea kwenye an-Nahj al-Hamiid, Jz. 4, uk. 91 155


Abu huraira check Lubumba.qxd

7/1/2011

10:48 AM

Page 156

Abu Huraira Ilisemekana kwamba Ali na al-Abbas 207 walikwenda kwa Umar wakati wa ukhalifa wake ili kuhukumu baina yao. Uthman, Abdur-Rahman, azZubair na Sa’d208 walikuwa pamoja na khalifa. Khalifa akawaambia: “Hivi mnajua kwamba Mtukufu Mtume alisema: ‘sisi mitume haturithiwi. Kile tunachokiacha baada yetu kinatakiwa kiwe ni sadaka.’” Wale waliohudhuria pale walilazimika kumwamini yeye. Halikuwezekana kwao isipokuwa kukubali riwaya za makhalifa hao wawili, hasusan kwa wakati ule. Na kuhusu Abu Huraira, yeye alikuwa si chochote cha kutajwa siku hizo. Hakuna yoyote aliyemsikiliza wala kumjali. Zaidi ya hayo, alishutumiwa kwa lafudhi yake mbaya. Hakuthubutu, akiwa na watu wale mashuhuri, kusimulia Hadith yoyote. Kwa kweli, hakujiona yeye mwenyewe kustahili kujiunga na wale ambao khalifa aliwaamini na kuwasikiliza, kwa hiyo hakusema neno lolote kuhusu jambo hili kwa wakati mpaka hawa masahaba wakubwa walipokufa, na nchi kama Sham, Misri, Afrika, Iraq, Persia, India na nchi nyinginezo zilipotekwa na watu wake wakawa Waislamu. Waislamu waliingia kwenye zama mpya. Kisha Bani Umayyah walimsifia Abu Huraira na kulinyanyua jina na utajo wake. Walimvua vazi lake la uvunguvungu wa kutofahamika na wakamfanya achanue baada ya kufifia kwake. Ikawa sasa ni rahisi kwake kusema chochote alichotaka. Hivyo akaanza kuueleza umma juu ya nini kilichowafanya wao wampende na kushikamana naye. Hivyo aliwafurahisha watawala na umma kwa Hadith hii ambayo ilimuongezea hadhi khalifa wao mpendwa miongoni mwa umma. 21. Abu Talib akataa kutamka Shahada: Abu Huraira amesema: “Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alimwambia ami yake Abu Talib: “Sema kwamba hakuna mungu isipokuwa Allah na mimi 207 Ami yao Mtukufu Mtume na Ali (a.s.) 208 Rejea Sahih al-Bukhari, Jz. 2, uk. 124 156


Abu huraira check Lubumba.qxd

7/1/2011

10:48 AM

Page 157

Abu Huraira nitakuja kulishuhudia hilo kwa ajili yako katika Siku ya Kiyama.” Ami yake akasema: “Ningelisema hilo ili kukuliwaza wewe lakini nilihofia kwamba Maquraishi wangenilaumu na kusema kwamba alilifanya hilo kwa sababu ya kukosa uvumilivu.” Hivyo Allah akamshushia Mtume Wake aya hii: “Kwa hakika wewe huwezi kumuongoza umpendaye, lakini Mwenyezi Mungu humuongoza amtakaye, …..” (28:56) Abu Huraira amesema mahali pengine: “Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alimwambia ami yake wakati alipokuwa anafariki: “Sema kwamba hakuna mungu isipokuwa Allah nami nitalishuhudia kwa ajili yako Siku ya Kiyama.” Ami yake alikataa kusema hivyo. Kwa hiyo Allah akamteremshia Mtume Wake (s.a.w.w.): “Kwa hakika wewe huwezi kumuongoza umpendaye, lakini Mwenyezi Mungu humuongoza amtakaye, …..”209 Abu Talib, Mwenyezi Mungu awe na huruma juu yake, alifarika katika mwaka wa kumi wa utume wa Mtukufu Mtume Muhammad (s.a.w.w.), yaani miaka mitatu kabla ya hijra. Ilisemekana pia kwamba alifariki katika mwaka wa tisa au wa nane. Hivyo alifariki miaka kumi kabla Abu Huraira hajafika Hijaz. Basi ni vipi Abu Huraira awakute Mtukufu Mtume na ami yake wakati wakiwa wanazungumza kuhusu hicho alichokisimulia kana kwamba aliwaona kwa macho yake na kuwasikia kwa masikio yake? Bali alikuwa mmoja wa wale ambao imani na akili zao hazikuwaongozea ndimi zao! Hadith hii ilikuwa ni moja kati ya zile nyingi ambazo zilibuniwa na mamluki kuwapendeza maadui wa Ali (a.s.) na kizazi chake. Dola ya Bani Umayyah ilijaribu kila kilichowezekana kuieneza. Kulikuwa na vitabu vingi vilivyoandikwa na wanachuoni kukanusha riwaya hii na kuthibitisha imani ya Abu Talib kwa ushahidi wa dhahiri. Yeyote yule anayetaka kujua ukweli wa uaminifu wa Abu Talib na uchamungu wake, yeye ambaye ni SS209 Rejea Sahih Muslim, Jz. 1, uk. 31 157


Abu huraira check Lubumba.qxd

7/1/2011

10:48 AM

Page 158

Abu Huraira ami yake Mtume, ambaye aliwajibika juu ya Mtukufu Mtume tangu utoto wake (s.a.w.w.), akamlea na kumkuza, akamhifadhi na kumlinda yeye, basi arejee kwenye vitabu hivyo.210 Abu Talib alisema katika moja ya mashairi yake: “Ewe Allah, kuwa Wewe ni shahid, Nimeamini katika ujumbe wa Muhammad.211 22. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alionya kabila lake: Masheikh wawili hawa212 wamesimulia kwamba Abu Huraira alisema: “Wakati Mwenyezi Mungu alipomshushia Mtukufu Mtume: “Na uwaonye jamaa zako wa karibu.” (26:214) alisimama na akasema: “Enyi watu wa Quraishi, mimi sibadiliki kwa ajili yenu karibu na Mwenyezi Mungu (katika Siku ya Kiyama). Enyi wana wa Abd al-Manafi, sibadiliki kwa ajili yenu mbele ya Mwenyezi Mungu. Oh, Abbas, sibadiliki kwa ajili yako mbele ya Mwenyezi Mungu. Oh, Safiyya, sibadiliki kwa ajili yako mbele ya Mwenyezi Mungu. Oh, Fatima binti Muhammad, omba chochote katika mali yangu bali sitabadilika kwa ajili yako mbele ya Mwenyezi Mungu.”213 210 Rejea ‘al-Hujja ala ath-Thahib ila Takfiir Abu Talib’ cha Imam Shamsud-Diin Abu Ali Fakhar bin Sharif Ma’d al-Musawi na ‘Sheikh al-Abtah’ cha Sayyid Muhammad Ali Sharafud-Diin al-Musawi. 211 Abu Talib alikuwa na ushairi mwingi unaoonyesha imani yake. 212 Rejea Sahih al-Bukhari, Jz. 2, uk. 86, Sahih Muslim na Musnad Ahmad. 213 Quraishi lilikuwa ni kabila kubwa lililokuwa likiisha mjini Makka. Abd Manaf alikuwa ni mmoja wa babu zake Mtukufu Mtume. Abbas alikuwa ami yake. Safiyya alikuwa ni shangazi yake na Fatima alikuwa ni binti yake Muhammad (s.a.w.w.)

158


Abu huraira check Lubumba.qxd

7/1/2011

10:48 AM

Page 159

Abu Huraira Aya hii ya Qur’ani ilishushwa kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) mwanzoni kabisa mwa Uislam na kabla haujaenea mjini Makka, ambapo Abu Huraira alikuwa bado yuko Yemen. Alikuja Hijaz miaka ishirini baada ya kushuka kwa aya hii. Ameikata Hadith hiyo na kuigeuza kama kawaida kulingana na sera za Bani Umayyah na masharti ya propaganda yao dhidi ya Imam Ali na Bani Hashim. Wakati aya hii iliposhuka kwa Mtume (s.a.w.w.) yeye aliwakusanya jamaa zake, miongoni mwao wakiwemo ami zake, Abu Talib, Hamza, al-Abbas (Mwenyezi Mungu awe radhi nao) na Abu Lahabi (laana juu yake) na akawataka wamuamini Mwenyezi Mungu. Yeye aliwaambia: “Ni yupi kati yenu atakayenisaidia kutekeleza kazi yangu hii na awe ndugu yangu, waziri wangu, mlinzi, mrithi na mwandamizi (khalifa) wangu?” Ali, ambaye alikuwa ndio mdogo kabisa kati yao wakati huo alisema: “Mimi nitakuwa waziri wako katika kutekeleza kazi yako hiyo.” Mtukufu Mtume aliishika shingo ya Ali na akasema: “Huyu ni ndugu yangu, waziri, mlinzi, mrithi na khalifa wangu kwenu. Msikilizeni na mumtii.”214 23. Wahabeshi wacheza ndani ya msikiti: al-Bukhari amesimulia kwamba Abu Huraira amesema: “Wakati Wahabeshi walipokuwa wakicheza na singe zao mbele ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) ndani ya msikiti, Umar aliingia na akaanza kuwarushia changarawe. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akamwambia Umar: “waache waendelee kufanya hivyo.”215 Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alikuwa mbali sana na mchezo na juu zaidi kuliko utovu wa adabu na purukushani. Yeye alijua vizuri sana, zaidi kuliko mtu yoyote yule, juu ya yale matendo yaliyokatazwa. Asingeweza kamwe kuwaruhusu watu wasiojua kucheza ndani ya Msikiti mbele yake. Alikuwa na shughuli wakati wote na majukumu ya ki-Mungu. Hakuwa na 214 Rejea kwenye al-Muraj’at ya Sharafud-Diin al-Musawi. 215 Ndani ya Sahih al-Bukhari Jz. 2, uk. 120 159


Abu huraira check Lubumba.qxd

7/1/2011

10:48 AM

Page 160

Abu Huraira muda wa kutumia kwa mchezo au upuuzi. Alikuwa mbali zaidi na kuruhusu msikiti wake mtukufu kuwa wa mchezo na upuuzi. “ ….. ni neno kubwa litokalo katika vinywa vyao, hawasemi ila uongo tu.” (18:5) 24. Kubatilisha kabla ya wakati wa utekelezaji: al-Bukhari amesimulia kwamba Abu Huraira alisema: “Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alitutuma sisi katika msafara na akatuambia: “Kama mkiwaona (hao watu wawili), wachomeni kwa moto!” Kisha wakati tunakaribia kuondoka akatuambia: “Niliwaamrisheni kuwachoma (watu wale wawili) kwa moto, lakini hakuna wa kutesa kwa moto isipokuwa Mwenyezi Mungu. Hivyo kama mkiwapata hao basi wauweni wote.” Hadith hii haikuwa sahihi kwa sababu ilionyesha kubatilishwa kwa amri kabla ya kuitekeleza. Ilikuwa haiwezekani kwa Mwenyezi Mungu na Mtume wake kufanya hivyo. Wakati Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) aliposema – wachomeni kwa moto – ilifunuliwa kwake na Mwenyezi Mungu: “Wala hazungumzi kwa matamanio yake, bali ni wahyi ulioteremshwa.” (53:3-4), hivyo pale Mtume alipoibatilisha (kwa mujibu wa wahyi wa Mwenyezi Mungu) kabla ya kuitekeleza hilo lingeonyesha kutokujua kwa Mwenyezi Mungu! Allah aepushilie mbali hilo! Utukufu ni wa Kwake, Aliye juu Mwenye Enzi.” 25. Kufanya jambo katika kipindi kisichoaminika: al-Bukhari ameeleza kwamba Abu Huraira amesema: “Mtukufu Mtume (s.a..w.w.) amesema: “Qur’ani tukufu ilirahisishwa kwa nabii Daudi. Aliamuru watu wake kutandika mnyama wake wa kipando na alimaliza kusoma Qur’ani kabla hawajamaliza kumtandika mnyama huyo.”216 Ilikuwa haiwezekani kwa njia mbili; Kwanza: Qur’ani iliteremshwa kwa Mtume Muhammad (s.a.w.w.) na 216 Sahih al-Bukhari Jz. 3, uk. 101 na Jz. 2, uk. 164 160


Abu huraira check Lubumba.qxd

7/1/2011

10:48 AM

Page 161

Abu Huraira haikushushwa kabla ya hapo. Ni vipi aliisoma nabii Daudi? Watetezi wa Abu Huraira walihalalisha hilo kwa kusema yeye kwa kusema Qur’ani alimaanisha Zaburi na Taurati kwa sababu vitabu hivyo vilikuwa ni muujiza kama ilivyokuwa Qur’ani. Waliitafsiri riwaya ya Abu Huraira kama walivyotaka na sio kama mwenyewe alivyomaanisha. Na Mwenyezi Mungu ndiye Mtambuzi zaidi! Pili: Huo muda wa kumtandika mnyama huyo wa kipando ulikuwa mfupi sana kwa Daudi kuweza kusoma hiyo Qur’ani, iwapo alimaanisha Qur’ani ya Muhammad au hiyo Zaburi na Taurati. Ni dhahiri kwamba akili haikubali mambo haya yasiyowezekana. Hivyo ilikuwa ni upuuzi kile al-Qastalani alichokisimulia kuhusiana na hili wakati aliposema: “Hadith hii imethibitisha kwamba Mwenyezi Mungu alifupisha wakati kwa ye yote aliyemtaka kati ya watu wake kama alivyofupisha umbali kwa ajili yao. An-Nawawi amesema: “Baadhi ya watu waliisoma Qur’ani yote mara nne wakati wa usiku na mara nne wakati wa mchana. Nilikuwa nimemuona Abut-Tahir huko Jerusalem katika mwaka wa mia nane na sitini na saba hijiria na nilikuwa nimesikia wakati huo kwamba alikuwa akiisoma Qur’ani yote zaidi ya mara kumi ndani ya usiku na wakati wa mchana. Sheikhul-Islam al-Burhan bin Abu Shariif aliniambia kwamba Abut-Tahir alikuwa ameisoma Qur’ani mara kumi na tano ndani ya mchana na usiku. Hili ni jambo ambalo hatuwezi kulielewa isipokuwa kwa kulirudisha kwenye upaji na uwezo wa ki-Mungu.” Kamwe halitawezekana isipokuwa pale tutakapoweza kuiweka dunia ndani ya yai. Watu wenye akili na busara wanajua vema kwamba kuminya muda na umbali ni jambo lisilo na kweli ni njozi. Hebu chukulia kwamba hilo lingekuwa kweli. Lilikuwa na faida gani basi? Lingeweza kusababisha matatizo mengi tu.

161


Abu huraira check Lubumba.qxd

7/1/2011

10:48 AM

Page 162

Abu Huraira Kama angezungumzia kuhusu kuibana hotuba, hiyo ingeweza kuwa ya kufaa zaidi ingawaje ingekuwa ni ndoto. Hadith hii haingeweza kuchukuliwa kama muujiza kwa ajili ya Nabii Daudi (a.s.) kwa sababu miujiza ilikuwa ni mambo ya ajabu lakini alichokizungumzia Abu Huraira katika Hadith hii kilikuwa kilichokosa mantiki zaidi kabisa. 26. Umma uligeuzwa kabisa na kuwa mapanya: Masheikh wawili hawa walisimulia kwamba Abu Huraira alisema: “Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amesema: “Umma wa wana wa Israili ulikuwa umepotea na hawakujua ni nini walichokuwa wamekifanya. Nafikiri waligeuzwa na kuwa panya, kwa sababu wakati panya walipopewa maziwa ya ngamia hawakuyanywa na walipopewa maziwa ya kondoo waliyanywa.” Ulikuwa ni upuuzi kiasi gani ambao hata watu wapumbavu wangeweza kuubeza, labda kama wangekuwa wendawazimu. Lakini masheikh hawa wawili walimwamini punguani huyu na wakasimulia vichekesho vyake kama ushahidi. Kama yale aliyoyasema hayakuaibisha Uislam, tungeweka kamba yake kwenye shingo yake na tukamuacha ale majani kwa uhuru kabisa pamoja na wengine kama yeye. lakini tulilazimika kuitetea ile Sunna isiyo na makosa kwa uwezekano wowote ambao tungeweza, kwa sababu itikadi hizi za kidhana zilikuwa ndio mapungufu mabaya kabisa yaliyouumiza Uislamu. 27. Wanaikataa Hadith yake, hivyo anabadili mawazo: Muslim amesimulia kwamba Abdul-Malik bin Abu Bakr amesema kwamba Abu Bakr alisema: “Nilimsikia Abu Huraira akisimulia katika riwaya zake:217 “Yeyote ambaye alikuwa hana tohara wakati ilipoingia al-Fajr, 217 Alimbeza yeye wakati alipomchukulia yeye kama mhadithiaji, ambaye alipokea pesa kwa ajili ya kusimulia hekaya. 162


Abu huraira check Lubumba.qxd

7/1/2011

10:48 AM

Page 163

Abu Huraira alikuwa asifunge.” Nilimuelezea Abdul-Rahman juu ya hilo naye akamuuliza baba yake. Baba yake alilikanusha hilo. Abdul-Rahman na mimi tukaenda kwa Aisha na Umm Salama (wake za Mtume). Abdul-Rahman akawauliza na akaniambia mimi kwamba: “Wote wawili wamesema kwamba Mtukufu Mtume alikuwa hana tohara asubuhi moja bila ya kuota na kunajisika218 na alifunga. Halafu tukaenda kwa Marwan ambaye alikuwa Gavana wa Madina aliyewekwa na Mu’awiyah. Abdul-Rahman alimwambia Marwan hilo. Marwan akasema: “Nakuombeni muende kwa Abu Huraira akakanushe riwaya yake.”219 Tulikwenda kwa Abu Huraira. Abdul-Rahman akamweleza hilo. Yeye akasema: “Wao (wake za Mtume) wamesema hivyo?” akasema: “Ndio, walisema hivyo.” Abu Huraira akasema: “Wao walijua zaidi kuliko mimi. Niliisikia hiyo kutoka kwa alFadhl na wala sikuisikia kutoka kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.).” Alibadili mawazo yake na kuihusisha Hadith hiyo na al-Fadhl.220 Ilikuwa ni hakika kwamba al-Fadhl alifariki wakati wa utawala wa Abu Bakr221 na suala hili lilijitokeza wakati wa utawala wa Mu’awiyah. Hivyo ilikuwa ni rahisi kwa Abu Huraira kusema kwamba alikuwa ameisikia kutoka kwa al-Fadhl na sio kutoka kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Kama al-Fadhl angekuwa yuko hai, Abu Huraira asingethubutu kusema hivyo. 218 Mtukufu Mtume alikuwa mkamilifu kabisa, aliyeheshimiwa na kutukuzwa kuliko walivyofikiri wao. Alikuwa mbali sana na ukosa tohara na ndoto za kunajisika nazo hususan wakati wa siku za kufunga. Mitume wote hawakuwa na ndoto kama hizo. Walitukuka na walikuwa maasum. 219 Marwan alitaka kuweka heshima ya Abu Huraira kabla habari hizo hazijaenea na kumsababishia kashfa. 220 Rejea kwenye Sahih Muslim, Jz. 1, uk. 412 221 Hili lilikuwa ni sahihi ingawa ilisemekana kwamba alifariki wakati wa utawala wa Umar. Vyovyote iwavyo, yeye alifariki kabla ya suala hili kutokea. Rejea kwenye wasifu wa al-Fadhl ndani ya Isti’ab, Issaba, Usudul-Ghaba, Tabaqat Ibn Sa’d na vitabu vinginevyo. 163


Abu huraira check Lubumba.qxd

7/1/2011

10:48 AM

Page 164

Abu Huraira 28. Hadith mbili zinazopingana: Al-Bukhari amehadithia riwaya222 iliyosimuliwa na Abu Salama kwamba Abu Huraira alisema: “Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amesema: ‘Hakuna maambukizi, hakuna Safar223 na hakuna Hama.224” Mmoja wa mabedui alimuuliza Mtume (s.a.w.w.): ‘Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, ngamia wetu wanatembea juu ya mchanga kama swala, lakini wanakuwaje, wakati wanapochanganyika na ngamia wenye upele na wao wanakuwa na upele?’ Mtukufu Mtume akauliza: ‘Basi ni nani aliyemuambukiza huyo wa kwanza?’” Moja kwa moja baada ya Hadith hii, al-Bukhari alisimulia Hadith nyingine kutoka kwa Abu Salama kwamba yeye alimsikia Abu Huraira akisema: “Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amesema: “Hakuna mgonjwa anayepaswa kuchanganyika na wenye afya njema.” Abu Salama akamwambia Abu Huraira: “Wewe hukusimulia kwamba hakuna maambukizi.” Yeye aliikana Hadithi yake ya kwanza225 na akaanza kunung’unika kwa kiAbyssinia.’”226 222 Rejea kwenye Sahih al-Bukhari, Jz. 4, uk. 15; na Sahih Muslim, Jz. 2, uk. 258 223 Pengine alikataa kile waarabu walichofikiria kwamba katika mwezi huu wa Safar mabalaa mengi hutokea, hususan katika Jumatano yake ya mwisho. 224 Ndege, ambaye Waarabu wa kabla ya Uislamu walisingizia kwamba nafsi au mifupa ya wafu iligeuka kuwa ndege huyo. Uislamu ulikanusha ushirikina huu. Inaweza kusemekana pia kwamba Hama alikuwa ni bundi, ambaye waliona dalili ya bahati mbaya ndani yake, na wakati Uislamu ulipokuja ulilikanusha hilo. 225 Hofu ilikuja kuwa kubwa kwa mshonaji kufanya marekebisho (methali). Ni vipi watetezi wa Abu Huraira watakavyozitafsiri Hadith hizi mbili ili kuepuka mgongano uliopo baina yao? 226 Alinung’unika kwa ki-Abyssinia kwani Kiarabu chake kilishindwa baada ya kuwa amechanganyikiwa asijue la kusema. 164


Abu huraira check Lubumba.qxd

7/1/2011

10:48 AM

Page 165

Abu Huraira Hii wakati wote imekuwa ndio hali ya wale wanaotembea katika njia mbili!

“Hili ni tangazo liwafikie watu (wote) liwaonye, na wapate kujua yeye ni Mwenyezi Mungu Mmoja tu, na ili wenye akili wakumbuke.” (14:52) 29. Watoto wawili waliozaliwa na kuongea kuhusu Ghaib: Masheikh hao wawili wameandika227 Hadith kutoka kwa Abu Huraira kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amesema: “Kulikuwa na Myahudi mmoja aliyeitwa kwa jina la Jurayj. Wakati alipokuwa anaswali, mama yake alikuja na kumwita. Alijiambia mwenyewe: “Sasa nimjibu yeye au niendelee na swala yangu?” Mama yake akasema: “Oh, Allah, usimfanye afariki mpaka atakapokutana na wale makahaba.” Siku moja wakati Jurayj alipokuwa ndani ya makao yake ya utawa, kahaba mmoja alikuja kumshawishi. Yeye alikataa kumkubalia. Kahaba huyo akaenda kwa mchunga kondoo na akafanya mapenzi naye. Alizaa mtoto wa kiume na akasingizia kwamba alikuwa ni mtoto wa Jurayj. Watu wakamjia Jurayj, wakabomoa nyumba yake ya utawa, wakamuangusha na kumdhalilisha. Yeye akachukua wudhuu,228 akaswali kisha akaja kwa yule mtoto aliyezaliwa. Alimuuliza yule mtoto: “Baba yako ni nani?” Yule mtoto mchanga akajibu akasema: “Baba yangu ni yule mchunga kondoo.” Watu wakamwambia Jurayj: “Tutakujengea nyumba yako ya utawa kwa dha227 Rejea Sahih al-Bukhari, Jz. 2, uk. 49; Jz. 1, uk. 143 na Sahih Muslim, Jz. 2, uk. 377. 228 Hivi Abu Huraira hakujua kwamba wudhuu haukuwa umepitishwa kama sheria kabla ya Uislamu? 165


Abu huraira check Lubumba.qxd

7/1/2011

10:48 AM

Page 166

Abu Huraira habu.” Yeye akasema: “Si kwa chochote isipokuwa udongo wa ufinyanzi.” Wakati mwanamke wa kiyahudi alipokuwa anamnyonyesha mwanawe, mtu mmoja akiwa kwenye kipando chake alipita karibu naye. Mama huyo akasema: “Oh Allah, mfanye mwanangu awe kama yeye.” Yule mtoto aliacha titi la mama yake na akasogea karibu na yule mtu na akasema: “Oh Allah, usinifanye niwe kama yeye.” Kisha akarudi kuendelea kunyonya ziwa la mama yake. (Abu Huraira akasema: kana kwamba nilikuwa namuona Mtukufu Mtume akinyonya kidole chake!). Halafu yule mama akapita karibu na mwanamke mfungwa. Akasema: “Oh Allah, usimfanye mwanangu kuwa kama mwanamke huyu mfungwa.” Yule mtoto akaacha ziwa la mama yake na akasema: “Oh Allah, nifanye niwe kama yeye (mwanamke) huyu.” Mama yule akamuuliza mwanawe: “Kwa nini umefanya hivyo?” Mtoto akasema: “Yule mtu mwenye kipando alikuwa ni mmoja wa madhalimu, lakini kuhusu yule mfungwa wa kike, watu walisema: “Zainabu ameiba,” lakini yeye hakuiba.” Jurayj hakuwa mtume wala hata mmojawapo wa hao watoto wawili. Hapakuwa na sababu yoyote ya kutokea kwa miujiza hapo. Walichokifanya watoto hao wawili kilikuwa kinyume na maumbile “….. ndilo umbile Mwenyezi Mungu alilowaumbia watu. Hakuna mabadiliko katika maumbile ya viumbe wa Mwenyezi Mungu, hiyo ndiyo dini iliyo ya haki lakini watu wengi hawajui.” (30:30) 30. Shetani aiba kwa ajili ya wanawe wenye njaa: Al-Bukhari amehadithia kwamba Abu Huraira alisema: “Mtume Muhammad (s.a.w.w.) aliniaminisha na uwekaji wa zaka za Ramadhani. Mtu mmoja alikuja (nyumbani kwangu) na akaanza kukusanya baadhi ya chakula (cha zaka). nilimkamata na nikasema: “Wallahi nitakupeleka kwa Mtukufu Mtume.” Yeye akasema: “Mimi nina shida sana na nina watoto.” Mimi nikamwacha huru. Asubuhi yake Mtume akaniambia: “Mtu wako uliyemkamata alifanya nini jana usiku?” Nikasema: “Alinilalamikia kwamba alikuwa na shida sana na kwamba alikuwa na watoto wenye njaa. 166


Abu huraira check Lubumba.qxd

7/1/2011

10:48 AM

Page 167

Abu Huraira Nilimuonea huruma nikamuacha huru.” Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akasema: “Yeye alikuambia uongo. Atakuja tena.” Nilimuangalia kwa tahadhari. Alikuja tena na akaanza kukusanya chakula. Nilimkamata na nikasema kwamba nitampeleka kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Yeye akasema: “Mimi nina shida na ninao watoto. Niachie niende na sitarudi tena.” Asubuhi yake Mtume akaniambia: “Mateka wako alifanya nini jana usiku?” Nikasema: “Alinilalamikia kwamba alikuwa na shida na alikuwa na watoto. Nikamhurumia na nikamuacha huru.” Yeye, Mtume (s.a.w.w.) akasema: “Huyo alikuambia maneno ya uongo. Atarudi tena huyo.” Nilimchunga katika usiku wa tatu yake. Yeye akaja tena na akaanza kukusanya chakula. Mimi nikamkamata na nikamwambia kwamba nitampeleka kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Yeye akasema: “Ngoja nikufundishe maneno fulani ambayo Mwenyezi Mungu atakunufaisha kwayo. Wakati unapokwenda kulala, soma Qur’ani ayat al-Kursi. Utalindwa na Malaika na Shetani hatakusogelea mpaka asubuhi.” Nikamwacha huru. Asubuhi yake Mtume akaniuliza: “Mateka wako amefanya nini usiku wa jana?” Mimi nikamweleza yale yote yaliyotokea usiku.Yeye akasema: “Hivi unajua uliongea na nani kwa mikesha yote mitatu iliyopita?” Mimi nikasema: “Hapana, simjui ni nani.” Yeye akasema: “Huyo alikuwa ni Shetani.” Huu ulikuwa ni ushirikina ambao hakuna ambaye angeuamini isipokuwa yule ambaye akili yake ilikuwa likizo au ana ugonjwa wa akili. Abu Huraira alitumbukia kwenye shimo refu na Hadithi hii. Pale alipomuonea huruma yule mwizi ina maana kwamba alimuamini. Katika kumwamini mwizi, Abu Huraira aliikataa ile Hadith ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) vile alipomwambia yeye: “Huyo amesema uongo” mara tatu. Abu Huraira alianguka mpaka chini kwenye upande ule mwingine pale alipoapa kwa jina la Allah kwamba angempeleka mwizi huyo kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) lakini akavunja kiapo chake na akawa na huruma juu ya mwizi huyo na akamwacha huru kwa mara ya kwanza, ya pili na ya tatu. Hivi kuvunja kiapo kwa mujibu wa mawazo ya Abu Huraira kulikuwa kunaruhusiwa? 167


Abu huraira check Lubumba.qxd

7/1/2011

10:48 AM

Page 168

Abu Huraira Kulikuwa na mweleka wa tatu ambao haungeweza kusameheka. Abu Huraira alikuwa haruhusiwi kutoa kitu kutoka kwenye zaka bali aliaminishwa kuichunga tu kama alivyosema mwanzoni mwa riwaya yenyewe.229 Hivyo ni vipi alimruhusu mwizi huyo kutwaa kutoka kwenye zaka? Je, ilikuwa inaruhusiwa kwa mdhamini kuvunja hazina yake mara tatu mfululizo? Baada ya uvunjaji huu, je anaweza kuelezewa kuwa ni mwenye kuaminika? Ni riwaya za ajabu kiasi gani ambazo Abu Huraira ametusimulia kuhusu Shetani! Wakati mmoja alisema kwamba alikuja kuiba chakula kwa ajili ya watoto wake. Katika wakati mwingine amesema kwamba angekimbia na mashuzi yake iwapo angesikia Adhana. Katika mara ya tatu alisema kwamba Shetani alikuwa amefungwa kwenye nguzo ndani ya msikiti ili aonwe na watu wote, na riwaya nyingine nyingi, ambazo watu wenye akili timamu na busara zao wangeweza kudharau kuzisikiliza. Tunamuomba Mwenyezi Mungu atuepushe na unyongevu wa akili! 31. Mama yake Awa Mwislam kwa dua ya Mtume (s.a.w.w.): Muslim amesimulia230 kwamba Abu Huraira alisema: “Nilikuwa nikimlingania mama yangu ili awe Mwislam wakati alipokuwa mshirikina. Siku moja nilipokuwa ninamlingania juu ya hilo, yeye akamkashifu Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Mimi nilikwenda kwa Mtukufu Mtume na nilikuwa ninalia. Nilimwambia: “Mama yangu amekukashifu wewe. Tafadhali muombee kwa Mwenyezi Mungu.” Yeye akasema: “Ewe Allah, tafadhali muongoze mama yake Abu Huraira.” Nikatoka nje nikiwa mwenye furaha tele. Nilipofika nyumbani nilikuta mlango umefungwa. Mama yangu akasikia shindo za miguu yangu. Yeye akasema: “Bakia hapo hapo ulipo, ewe Abu Huraira.” Nilisikia sauti ya mmiminiko wa maji. Alioga na 229 Rejea al-Irshad as-Sari ya Qastalani, Jz. 5, uk. 231 230 Katika Sahih yake, Jz. 2, uk. 357; Musnad Ahmad Hanbal, Jz. 2, uk. 319; Ibn Sa’d katika Tabaqat, Jz. 4, uk. 54 na Ibn Hajar katika kitabu chake, al-Issaba. 168


Abu huraira check Lubumba.qxd

7/1/2011

10:48 AM

Page 169

Abu Huraira akavaa nguo zake na ushungi wa hijab na kisha akafungua mlango. Akasema: “Nashuhudia kwamba hakuna mungu isipokuwa Mwenyezi Mungu na kwamba Muhammad ni mja na Mtume Wake.” Nilirudi kwa Mtume (s.a.w.w.) na nilikuwa ninalia kwa sababu ya furaha. Nilimwambia Mtukufu Mtume (s.a.w.w.): “Furahia! Mwenyezi Mungu amejibu dua yako. Amemuongoza mama yangu.” Mtume (s.a.w.w.) alimtukuza Mwenyezi Mungu. Mimi nikamwambia: “Ewe Mjumbe wa Allah niombee kwa Mwenyezi Mungu anifanye nipendeke mimi na mama yangu kwa waumini na sisi tuwapende pia.” Yeye Mtume (s.a.w.w.) akasema: “Oh, Allah mpendezeshe mja wako huyu na mama yake kwa waumini na uwapendezeshe waumini kwao hawa.” Hivyo kila muumini, ambaye alinisikia au kuniona mimi alinipenda.” Tunayo maelezo kiasi kuhusu Hadith hii: Kwanza: Hadith hii haikuwa imesimuliwa kutoka kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na mtu mwingine isipokuwa Abu Huraira peke yake. Hivyo ni ya kuchukuliwa kama nyinginezo zinazofanana nayo. Pili: Kama mama yake alikuwa ni mshirikina, alisisitiza ushirikina na ukafiri, akakataa kuwa Mwislam na akamkashifu Mtukufu Mtume kila alipolinganiwa kuwa Mwislam, hivyo ni kwa nini alihama kutoka Yemen, mahali alipozaliwa na nchi yake, kuja Madina, nchi ya Uislam na makao makuu ya Mtukufu Mtume na wasaidizi wake? Kwa nini asikae, kama alivyokuwa mwanzo, ndani ya nchi yake na masanamu yake kama watu wengine wa Yemen kwa wakati ule? Ni vipi watetezi wa Abu Huraira watakavyojibu swali hili? Hivi wanajua lolote kuhusu kuhama kwake, kuwa kwake Mwislam na mambo mengine kuhusu yeye yaliyotajwa na mtu mwingine mbali na Abu Huraira? Kama wanalo lolote kuhusu yeye, hebu nawatuelekeze kwenye hilo. Mimi, Wallahi sikuona yeyote kati ya masahaba aliyemtaja yeye isipokuwa khalifa Umar wakati alipomuondosha kutoka kwenye falme ya Bahrain. Yeye alimwambia: “Umayma alikuchukua wewe kwa sababu ya kuchunga punda tu.” Hili halikuonyesha lolote zaidi ya kujua jina lake mama huyo. Wanahistoria wamemtaja kwa 169


Abu huraira check Lubumba.qxd

7/1/2011

10:48 AM

Page 170

Abu Huraira mujibu wa kile Abu Huraira alichokisema kuhusu yeye na hakuna mwingine tena. Tatu: Abu Huraira alikuwa mmoja wa wakazi masikini kabisa wa Suffa. Aliomba watu kwenye mitaa kumpatia cha kutafuna ili kumuweka hai. Umemsikia yeye alipozungumza kuhusu yeye mwenyewe wakati wa utawala wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kwamba mara kwa mara alikuwa akizimia kati ya mimbari ya Mtume na chumba cha Aisha na wageni waliokuja pale waliweka miguu yao juu ya shingo yake wakidhania kwamba alikuwa mwendawazimu lakini hakuwa na wendawazimu chochote. Ilikuwa ni kwa sababu ya njaa. Umemsikia kukiri kwake kuhusu yeye mwenyewe na wakazi wengine wote wa Suffa. Walikuwa hawana ndugu wala nyumba. Walikuwa wakilala ndani ya msikiti huo. Hiyo baraza (Suffa) ya msikiti huo ilikuwa ndio nyumbani mwao wakati wa mchana na usiku. Abu Huraira alikuwa ndiye maarufu sana kati ya wale walioishi hapo Suffa. Kwa kweli yeye alikuwa ndiye muanzishaji wa Suffa. Hivyo nyumba hiyo aliipata kutoka wapi, ambayo ameizungumzia juu yake ndani ya Hadith hii? Nne: Kama kile alichokisema Abu Huraira ndani ya riwaya hii kilikuwa ni cha kweli, ingekuwa ni moja ya dalili za utume na Uislamu ambamo Mwenyezi Mungu alijibu dua ya Mtukufu Mtume mara moja na kumuongoza mama yake Abu Huraira na akamgeuza yeye kutoka kwenye kuwa mwingi wa kufuru na kupotoka na kuwa mtiifu mwaminifu.231 Dalili na miujiza ya utume huo ilikuwa maarufu sana na ilienea. Masahaba wote waliisimulia. Kwa nini waligeuzia migongo yao mbali na dalili hii kiasi kwamba hakuna aliyeisimulia isipokuwa Abu Huraira? Tano: Kama ilikuwa kweli kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alimuomba Mwenyezi Mungu kwa ajili ya Abu Huraira na mama yake kuwapen231 Abu Huraira alisema kwamba mama yake alioga na kuvaa nguo zake na hijab, kisha akafungua mlango. 170


Abu huraira check Lubumba.qxd

7/1/2011

10:48 AM

Page 171

Abu Huraira dezesha kwa waumini na kuwapendezesha waumini kwao wao, familia ya Mtume, ambao walikuwa ndio mabwana wa waumini na viongozi wa umma na dini, na wao wangempenda yeye. Kama ilikuwa hivyo basi kwa nini wale Maimam kumi na mbili na mafaqihi wa wafuasi wao walimshusha hadhi na hawakuwa na habari kabisa na riwaya zake? Hawakutoa mazingatio yoyote kwenye riwaya zake. Imam Ali (a.s.) alisema:232 “Muongo kabisa wa watu, au alisema: muongo kabisa wa watu walio hai ni Abu Huraira ad-Doussi.” Kama Abu Huraira alikuwa akipendwa na waumini na wao walipendwa na yeye, basi Umar wakati alipokuwa akimwondosha kutoka falme ya Bahrain asingesema kumwambia: “Ewe adui wa Allah na adui wa Qur’ani Yake, wewe uliiba mali ya Waislamu ….. na kadhalika.” Ni vipi adui wa Mwenyezi Mungu apendwe na waumini na wao wapendeze kwake? Wakati mmoja Umar alimpiga kwenye kifua chake233 ambapo alianguka chini. Wakati mwingine alimpiga kwa fimbo yake mpaka akamjeruhi mgongo wake na akachukua kutoka kwake dinari elfu kumi alizokuwa ameziiba kutoka kwenye hazina ya Waislamu. Alimpiga yeye kwa mara ya tatu wakati alipomwambia:234 “Umesimulia Hadith nyingi za Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na nadhani umebuni na kusema uongo mwingi.” Siku moja Umar alimwambia kwa hasira: “Inakubidi uache kusimulia Hadith laa sivyo nitakufukuza na kukuhamishia kwenye nchi ya Yemen au nchi ya manyani.”235 Kulikuwa na matukio mengi mengine ambayo yalitokea kati ya Abu Huraira na Abdullah ibn Abbas na kati yake yeye na Aisha na wengine 232 Kulikuwa na riwaya nyingi sana zilizosimuliwa na Maimam Ma’sumin zenye maana hiyo hiyo. Rejea kwenye Sharh an-Nahjul-Balaghah ya Abu Ja’far alAskafi, Jz. 1, uk. 360 233 Rejea Sahih Muslim, Jz. 1, uk. 334 234 Rejea kwenye Sharh an-Nahj al-Hamiid, Jz. 1, uk. 360 235 Rejea kitabu Kanzul-Ummal cha ibn Assakir, Jz. 5, uk.239 171


Abu huraira check Lubumba.qxd

7/1/2011

10:48 AM

Page 172

Abu Huraira ambayo hayakuonyesha dalili zozote za upendo. Ndio, kulikuwa na mapenzi baina yake na familia ya Abul Aass, Abu Mu’iit na Abu Sufyan. Hadith zake zilimpendezesha kwao kwani walipata lile lengo lao walilokuwa wakilitafuta kwa muda mrefu ndani ya Hadith hizo la kueneza propaganda zao za uongo. Walichopendelea kwake ni zile fadhila na zawadi zao. Walimstawisha baada ya kififia kwake na wakamfanya maarufu baada ya utusitusi wa kutojulikana kwake. Marwan bin alHakam mara kwa mara alimteua kama naibu wake kila alipoondoka Madina.236 Alimuoza kwa Bisra binti Ghazwan ambaye alikuwa hawezi hata kumuangalia mpaka hapo Bani Umayyah walipofanya hilo la kumuoza. Alipougua kabla ya kufariki kwake, Marwan alimtembelea mara kwa mara, akimzawadia na kumuombea apone na apate afya njema. Wakati Abu Huraira alipofariki, Marwan alikuwa mstari wa mbele katika mazishi yake. Mtoto wa Uthman alibeba jeneza lake mpaka walipofika Baqii. al-Waliid bin Utbah bin Abu Sufyan aliongoza swala ya maiti na akatuma mjumbe kwa ami yake, Mu’awiyah akimuelezea juu ya kifo cha Abu Huraira. Mu’awiyah aliamuru kulipwa kwa warithi wa Abu Huraira dinari elfu kumi na kuwatunza kwa wema. Uliona matunzo na fadhila za Bani Umayyah kwa Abu Huraira na utii wake wa kutumikia. Je, wao walikuwa ndio waumini ambao Mwenyezi Mungu aliwapendezesha kwake na kumpendezesha yeye kwao kwa mujibu ya istilahi yake? 32. Mtumishi wa Abu Huraira: Al-Bukhari amesimulia kwamba Abu Huraira alikuwa amesema: “Wakati nilipokuja kutoka Yemen kuja kukutana na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) hapa Madina, nilijisemea humo njiani: Ni usiku mrefu wenye matatizo kiasi gani huu! Lakini nilikuwa nimeokolewa kutoka kwenye nchi ya ukafiri. Mtumishi wangu alitoroka humo njiani mwangu kuja Madina. 236 Rejea kwenye Tabaqat ya Ibn Sa’d; al-Ma’arif ya ibn Qutayba na Musnad Ahmad 172


Abu huraira check Lubumba.qxd

7/1/2011

10:48 AM

Page 173

Abu Huraira Nilifika kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na nikamtolea heshima zangu kwake. Wakati nilipokuwa na Mtume, mtumishi wangu akatokea. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akaniambia: “Oh, Abu Huraira, huyu ni mtumishi wako.” Mimi nikasema: “Nilimuacha huru kwa ajili ya Mwenyezi Mungu.” Abu Huraira alichanganya akili za watu na kushangaza hisia! Alisema kwamba alikua kama yatima na pale alipohama alikuwa masikini sana. Aliajiriwa na fulani bin fulani kwa ajili ya chakula tu. Aliongoza vipando vyao walipokuwa wamepanda na aliwatumikia pale waliposhuka. Baada ya hapo alifanya kuwa alikuwa na mtumishi wakati alipohama na kisha akamwacha huru kwa ajili ya Allah! Ni wazi kwamba alihadithia riwaya hii katika siku zake za mwisho za uhai wake alipokuwa anafurahia starehe za fadhila za Bani Umayyah. Hivyo alisahau vile alivyokuwa wakati wa kuhama kwake, baada na kabla yake pale alipokuwa anakufa njaa, mikono mitupu, mwenye kuhuzunisha na mwenye kusononeka. Matumbo yake yaliunguruma na utumbo wake ulikoroma. Alitupwa barabarani akitegemea juu ya ini lake kwa sababu ya njaa, akiwaomba wapita njia kupata kitafunwa ili kumfanya apate kuishi. Yeye mwenyewe amewahi kusema: “Naapa kwa Allah, ambaye hapana mungu isipokuwa Yeye, nilikuwa nikitegemea maini yangu kwa sababu ya njaa. Niliweka jiwe juu ya tumbo langu ….. na kadhalika.” Alisema katika riwaya nyingine: “Nilikuwa nikizimia mara kwa mara kati ya mimbari ya Mtume na nyumba ya Aisha. Waliokuwa wakija waliweka miguu yao juu ya shingo yangu wakidhani mimi ni mwendawazimu. Lakini nilikuwa sina wazimu chochote, bali ilikuwa ni njaa tu.” Nyingi nyingine ya Hadith zake, ambazo zilionyesha kwamba alikuwa hajali aibu na kwamba kudharauliwa kulikuwa hakumuumi yeye. Chote alichokuwa akikitaka tu kilikuwa ni kushibisha tumbo lake tupu. Hivyo ni kutoka wapi huko alikopata mtumishi ambapo alikuwa katika hali hii ya umasikini kama hii? Kama tukimuuliza Abu Huraira kwamba ni vipi Mtume alivyomfahamu mtumishi wake wakati tu alipoingia ndani, tutamtahayarisha bwana mkubwa huyo kwani Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) hakumjua mtumishi huyo 173


Abu huraira check Lubumba.qxd

7/1/2011

10:48 AM

Page 174

Abu Huraira kabla! Pengine Abu Huraira alikuwa na ukuu na utukufu ambao ulimfanya awe na uwezo wa kumfunulia Mtukufu Mtume kuhusu yeye na mtumishi wake! 33. Hadith ya kudhaniwa kuhusu sadaka: Muslim amesimulia kwamba Abu Huraira alisema: “Mtume Muhammad (s.a.w.w.) amesema: “Wakati mtu mmoja alipokuwa jangwani, alisikia sauti katika moja ya mawingu ikisema: “Nenda ukanyweshe lile shamba la yule bwana (ikamwita kwa jina).” Wingu hilo likasogea na likaenda kunyesha kwenye shamba la bwana yule. Kulikuwa na mtu ndani ya shamba hilo akitiririsha maji na chepe lake. Akamuuliza yeye kuhusu jina lake. Akajibu kwa jina lilelile alilolisikia kwenye lile wingu. Yule mkulima akamuuliza yule mtu: “Kwa nini unaulizia juu ya jina langu?” Akasema: “Nilisikia sauti katika lile wingu. Ililiamuru wingu hilo kunyesha juu ya shamba lako na ikataja jina lako. Je, unaweza kuniambia unafanya nini na shamba lako hili?” Yeye akasema: “Mimi ninangoja mpaka miti yangu itoe matunda, halafu ninatoa thuluthi yake kama sadaka.”237 Hili lilikuwa haliwezekani kutokea kwani lilikuwa kinyume na kanuni za maumbile. Abu Huraira aliibuni kama hekaya akidhamiria kurejelea kwenye matokeo mazuri ya sadaka. Aliihusisha kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kama alivyozoea kufanya na Hadith zake za kubuni. Hivyo hatuna wa kukimbilia ila kwa Mwenyezi Mungu. 34. Hekaya nyingine kuhusu matokeo mazuri ya uaminifu: Al-Bukhari amesimulia kwamba Abu Huraira alisema: “Mtume Muhammad (s.a.w.w.) amesema: “Myahudi mmoja alimuomba mtu mmoja juu ya watu wake kumkopesha dinari elfu moja. Alimtaka alete mashahidi wake kuja kulishuhudia hilo. Yeye akasema: “Mwenyezi Mungu anatosha 237 Rejea Sahih Muslim, Jz. 2, uk. 533 174


Abu huraira check Lubumba.qxd

7/1/2011

10:48 AM

Page 175

Abu Huraira kuwa shahidi.” Akamuomba alete mdhamini wake. Yeye akasema: “Allah ni mdhamini tosha.” Alimpa fedha hizo ziwe zimelipwa katika tarehe maalum. Mkopaji huyo alisafiri kwa bahari. Baada ya kumaliza kazi yake alijaribu kutafuta meli ili arudi na ili aweze kulipa fedha hiyo kwa mwenyewe lakini hakupata meli yoyote. Alichukua kipande cha kigogo na akakichimba shimo. Aliweka dirham elfu moja hizo pamoja na barua ndani ya kipande hicho cha kigogo. Akakiziba na akaja nacho hadi baharini. Yeye akasema: “Ewe Mwenyezi Mungu, Wewe unajua kwamba nimekopa dirham elfu moja kutoka kwa bwana yule. Alinitaka nimletee mdhamini. Mimi nilisema kwamba Mwenyezi Mungu alikuwa ni mdhamini tosha na yeye akanikubalia. Alinitaka shahidi mimi nikasema Mwenyezi Mungu alikuwa shahidi tosha naye akakubali. Nimejaribu kiasi cha uwezo wangu kupata meli ili niende nikamlipe fedha zake lakini sikuweza kupata meli yoyote. Sasa Wewe ndio mhazini wangu.” Akazitupa fedha hizo baharini na akaondoka. Mkopeshaji alikwenda baharini akitegemea kwamba kunaweza kutokeza meli itakayoleta fedha zake. Aliona kipande cha kigogo ndani ya maji. Akakichukua kwenda nacho nyumbani kama kuni. Alipokichanja aliona zile fedha na barua.”238 Hadith hii iko mbali sana kutokana na mazingatio yoyote yale. Sio Shari’ah au akili ambayo ingeruhusu kutupa fedha dirham elfu moja baharini. Haitaweza kufikiriwa kwamba ni maarifa kama fedha hizo zisingemfikia mwenyewe. Watu wenye hekima walichukulia utendaji huu kama upumbavu au wendawazimu na huyo mfanyaji ni lazima awe chini ya katazo. Kama jambo hili lilitokea kwa wayahudi ama taifa lolote lile, Mtume Muhammad (s.a.w.w.) asingeweza kulielezea hilo bila maelezo yoyote kwa ajili ya kutowahimiza waumini wa umma wake kutolifanya kama hilo. Hata hivyo, ilikuwa ni muhali kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kusema kama hivyo lakini Abu Huraira alilisema hilo kama zile riwaya za kubuni na akaihusisha kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kiasi cha kuuza bidhaa zake (Hadith) vizuri. 238 Sahih al-Bukhari, Jz. 2, uk. 26 175


Abu huraira check Lubumba.qxd

7/1/2011

10:48 AM

Page 176

Abu Huraira 35. Hekaya ya tatu kuhusu matokeo mazuri ya shukurani: Al-Bukhari amesimulia riwaya kutoka kwa Abu Huraira kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisema: “Kulikuwa na wayahudi watatu. Mmoja alikuwa mkoma, mwingine alikuwa na upara na yule wa tatu alikuwa ni kipofu. Mwenyezi Mungu alitaka kuwajaribu. Alituma Malaika kwao. Malaika alimwendea yule mwenye ukoma na akamuuliza: “Ni nini unachokipenda zaidi?” Yeye akasema: “Rangi safi na ngozi nzuri. Watu hawanipendi.” Malaika akampigapiga kiupendo (pat) na akawa amepona. Alipewa rangi nzuri na ngozi ya kupendeza. Malaika akamuuliza: “Ni utajiri gani unaoupenda?” Yeye akasema: “Ngamia.” Akapewa ngamia jike mwenye mimba, ambaye alikuwa karibu na kuzaa. Malaika akasema: “Mwenyezi Mungu ataibariki kwa ajili yako.” Akaenda kwa yule mwenye upara na akamuuliza: “Ni nini unachokipenda zaidi?” Yeye akajibu: “Nywele nzuri. Watu wananichukia.” Malaika akampigapiga kimapenzi na akawa amepewa nywele nzuri. Malaika akamuuliza: “Ni utajiri upi unaoupendelea?” Yeye akasema: “Ng’ombe.” Akampa ng’ombe mwenye mimba na akasema: “Mwenyezi Mungu atambariki kwa ajili yako.” Akaja kwa yule kipofu na akamuuliza: “Ni nini unachokipendelea zaidi?” Yeye akasema: “Kupata uoni wangu tena.” Malaika akampigapiga kwa upendo na Mwenyezi Mungu akamjaalia kuona. Malaika akamuuliza: “Ni utajiri gani unaopendelea zaidi?” Yeye akajibu: “Kondoo.” Akampatia kondoo jike. Yule ngamia jike, ng’ombe na kondoo jike wakazaliana. Yule mtu wa kwanza akawa na bonde la ngamia. Yule wa pili akawa na bonde la ng’ombe wengi na yule wa tatu akawa na bonde la kondoo. Malaika yule akamjia yule mtu mwenye ukoma katika umbile kama la yule mwenye ukoma kabla hajapona na akamwambia: “Mimi ni masikini, nimepoteza kila kitu changu safarini mwangu na sina mtu wa kunisaidia isipokuwa Mwenyezi Mungu na wewe. Nakuomba, kwa Yeye ambaye 176


Abu huraira check Lubumba.qxd

7/1/2011

10:48 AM

Page 177

Abu Huraira alikupa rangi nzuri, ngozi safi na utajiri, unipatie ngamia wa kupanda kwenye safari yangu.” Yule mtu akasema kwamba alikuwa na mahitaji mengi sana na akakataa kumpatia huyo ngamia. Malaika akasema: “Nadhani mimi ninakufahamu wewe. Hivi wewe hukuwa mkoma na masikini na kwamba watu walikuwa wakikuchukia wewe? Halafu Mwenyezi Mungu akakujaalia neema zote hizi.?” Yule mtu akasema: “Nimerithi yote haya kutoka kwa mababu zangu.” Yule Malaika akasema: “Kama umesema uongo, basi Mwenyezi Mungu akurudishe kwenye hali uliyokuwa nayo hapo kabla.” Akaja kwa yule aliyekuwa na upara katika umbile kama alilokuwa nalo wakati alipokuwa na upara na masikini na akamuomba kama vilevile alivyomuomba yule mwenye ukoma. Yeye naye akatoa majibu yale yale. Malaika yule akasema: “Kama umesema uongo, Mwenyezi Mungu akurudishe kama ulivyokuwa mwanzo kabla ya hapa.” Kisha akaja kwa yule kipofu katika hali kama aliyokuwa nayo wakati alipokuwa kipofu na masikini na akamwambia: “Mimi ni masikini na mpitanjia. Sina kitu chochote, na hakuna mtu wa kunisaidia isipokuwa Mwenyezi Mungu na wewe. Ninakuomba, kwa Yeye, ambaye alikurudishia uoni wako, unipe kondoo jike ili anifae katika safari yangu.” Yule bwana akasema: “Mimi nilikuwa kipofu na Mwenyezi Mungu akanirudishia kuona kwangu. Nilikuwa masikini na Mungu akanifanya kuwa tajiri. Unaweza kuchukua chochote kile unachotaka. Wallahi, mimi sitakuzuia kuchukua chochote kwa ajili ya Allah.” Yule Malaika akasema: “Mimi nimekujaribuni nyote. Mwenyezi Mungu amekuwa radhi na wewe lakini hakuridhika na wale marafiki zako wawili.” Riwaya hii ni moja ya nguo za Abu Huraira ambayo aliidarizi na kuinakishi. Ilionekana kama mchezo wa kuigiza kizahania wa kisasa, ambao wachezaji wake wanaucheza katika kumbi zao siku hizi. Alitaka kuonyesha tu, kwa riwaya hii, yale matokeo ya kuwa na shukurani na kutokuwa na shukurani. 177


Abu huraira check Lubumba.qxd

7/1/2011

10:48 AM

Page 178

Abu Huraira 36. Riwaya nyingine ya kubuni kuhusu dhulma: Masheikh hao wawili wamesimulia riwaya kutoka kwa Abu Huraira kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amesema: “Mwanamke mmoja aliingizwa Jahannam kwa sababu ya paka. Alimfungia ndani paka huyo, na hakumpatia chakula wala kumuacha aede kujitafutia mwenyewe wadudu wa kula.” Riwaya hii ilikataliwa na Aisha, mke wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Yeye alimwambia Abu Huraira: “Muumini ana heshima kubwa mbele ya Mwenyezi Mungu kuliko kuteswa kwa moto kwa ajili ya paka. Unaposimulia Hadithi za Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) fikiria vizuri jinsi utakavyosimulia.”239 37. Hadithi ya tano ya kubuni: Al-Bukhari ameitaja Hadith iliyosimuliwa na Abu Huraira kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amesema: “Kahaba mmoja alimuona mbwa akitweta kisimani. Alikuwa karibu ya kufariki kwa kiu. Kahaba huyo akavua kiatu chake kimoja, akakifunga na kitambaa chake cha ushungi na akamchotea yule mbwa maji kutoka kisimani humo. Mwenyezi Mungu akamsamehe dhambi zake kwa kufanya hivyo.” 38. Hadithi nyingine kama hiyo iliyopita: Al-Bukhari alisimulia Hadith kutoka kwa Abu Huraira kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amesema: “Wakati mtu mmoja alipokuwa anatembea njiani, alijisikia kiu sana. Aliona kisima na akashuka kwenda kunywa maji. Wakati alipokuwa anatoka, alimuona mbwa akihema kana kwamba amekula ardhi kwa sababu ya kiu. Yule mtu akashuka, akajaza kiatu chake maji, akakikamata kiatu chake kwa midomo yake na akamfanya mbwa huyo kunywa maji. Alimshukuru Mwenyezi Mungu na Mwenyezi Mungu 239 Rejea al-Irshad as-Sari, Jz. 7, uk. 84. 178


Abu huraira check Lubumba.qxd

7/1/2011

10:48 AM

Page 179

Abu Huraira akamsamehe madhambi yake kwa ajili ya hilo.”240 Hadithi hii na ile iliyotangulia zilitoka kwenye ubunifu wa Abu Huraira kuonyesha matokeo mazuri ya huruma na upole. 39. Allah anamsamehe kafiri aliyekithiri: Muslim amesimulia kwamba Ma’mar alisema: “Az-Zuhri aliniambia: “Nikuhadithie juu ya riwaya mbili za kustaajabisha?241 Hamiid bin AbdurRahman aliniambia kwamba Abu Huraira alisema: “Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amesema: “Mtu mmoja alikithiri katika kutenda madhambi. Alipokuwa karibu ya kufariki, aliwaamuru wanawe: “Kama nikifariki, mnapaswa kunichoma, kuniponda na kunitawanya baharini katika siku yenye upepo mkali. Kama Mungu wangu akinikamata mimi242, Yeye atanitesa kwa kiwango ambacho hajamtesa kwacho mtu mwingine yeyote kama mimi.” Wanawe walifanya kile alichowaagiza kufanya. Allah akaiambia ardhi: “Toa kile ulichokibeba!” Mtu huyo alirudishwa kama alivyokuwa kabla ya kifo chake. Mwenyezi Mungu akamuuliza: “Kwa nini ulifanya hivyo?” Yeye akasema: “Nilikuwa nikikuhofia Wewe, Mungu Wangu.” Kisha Mwenyezi Mungu akamsamehe madhambi yake. Hamiid aliniambia vilevile kwamba Abu Huraira alisema: “Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amesema: “Mwanamke mmoja aliingizwa katika Moto wa Jahannam kwa sababu ya paka. Alimfunga paka huyo na hakumlisha wala kumuacha ajilishe mwenyewe kwa kula wadudu.”243 240 al-Irshad as-Sari, Jz. 2, uk. 150 241 Az-Zuhri alikuwa na haki ya kushangazwa na Hadith mbili hizi. Wote wenye hekima wangeshangazwa nazo hizo! 242 Angalia kwamba alikuwa haamini kwamba Mwenyezi Mungu alikuwa na uwezo wa kumfufua yeye baada ya kutekeleza wasia wake huo. Hivyo alikufuru juu ya hilo. 243 Rejea Sahih Muslim, Jz. 2, uk. 444 179


Abu huraira check Lubumba.qxd

7/1/2011

10:48 AM

Page 180

Abu Huraira Kama mwanamke huyo aliyemfunga paka huyo alikuwa ni muumini, kama Aisha alivyosema, angekuwa ni mwenye kuheshimika zaidi mbele ya Mwenyezi Mungu kuliko kuteswa kwenye Moto wa Jahannam kwa sababu ya paka. Kama alikuwa ni kafiri, angekuwa ndani ya Jahannam kwa ajili ya ukafiri wake. Na kuhusu mfanya madhambi aliyekithiri, yeye hakustahili msamaha. Yeye hakuvuka mipaka tu katika kufanya madhambi maishani mwake, bali pia aling’ang’ania katika ukafiri wake hata wakati akiwa yu karibu na kufariki kwamba alikuwa amekata tamaa juu ya huruma za Mwenyezi Mungu. Alidhani Mwenyezi Mungu hatakuwa na uwezo wa kumfufua yeye kama wangemchoma na kutawanya majivu yake. Hivyo alikuwa ni kafiri. Na kafiri kamwe hatastahili msamaha hata kidogo. Mtindo wa Hadith hii ulikuwa kama mtindo ule wa Hadithi za kubuniwa. Hadith ilielekea kuonyesha kwamba mwanadamu hapaswi kukata tamaa dhidi ya rehma za Mwenyezi Mungu hata kama akiwa amekithiri katika kutenda madhambi na asidhani kwamba anaweza kuwa salama kutokana na mateso Yake hata kama angekuwa muumini. Mambo haya mawili hayakuhitaji kuonyeshwa kwa ngano hizi za Abu Huraira. Yalithibitishwa wazi na Qur’ani tukufu: “ ….. na wala msikate tamaa katika rehema ya Mwenyezi Mungu. Hakika hakati tamaa ya rehema za Mwenyezi Mungu isipokuwa watu makafiri. (12:87); “Je, wamesalimika kuadhibiwa na Mwenyezi Mungu? Hawaaminishi adhabu ya Mwenyezi Mungu ila watu (ambao watakuwa) wenye hasara.” (7:99). Qur’ani tukufu na Sunna zilikuwa juu sana ya Hadith hii na mtindo wake. Tuseme kwamba ule wasia wa yule mtenda dhambi aliyekithiri ulikuwa wa kweli na ulikuwa ndio sababu ya madhambi yake kusamehewa na Mwenyezi Mungu, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) asingeisimulia hiyo bila ya maelezo yoyote! Angewatia moyo watenda madhambi waliokithiri wa umma wake kuendeleza madhambi yao. Hili kwa kweli lilikuwa haliwezekani kwa Mtume kulifanya. 180


Abu huraira check Lubumba.qxd

7/1/2011

10:48 AM

Page 181

Abu Huraira 40. Allah anamsamehe mwenye dhambi milele: Abu Huraira alisema kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amesema: “Mtu mmoja alitenda dhambi na akamuomba Mwenyezi Mungu amsamehe. Mwenyezi Mungu akasema: “Mja wangu ametenda dhambi na kisha akatambua kwamba anaye Mungu, ambaye anasamehe dhambi na kuadhibu kwa ajili ya dhambi.” Akatenda dhambi tena na akamuomba Mwenyezi Mungu amsamehe. Mwenyezi Mungu akasema: “Mja wangu ametenda dhambi na kisha akatambua kwamba anaye Mungu, ambaye anasamehe dhambi na kuadhibu kwa ajili ya dhambi.” Na kisha akafanya dhambi tena na kumuomba Mwenyezi Mungu amsamehe. Mwenyezi Mungu akasema: “Mja wangu ametenda dhambi na kisha akatambua kwamba anaye Mungu, ambaye anasamehe dhambi na kuadhibu kwa ajili ya dhambi. Fanya lolote ulitakalo, Mimi nimekwisha kukusamehe”244 Hii ilikuwa ni kama zile Hadith zilizotangulia kwa maana na mtindo. Ilikuwa imesukwa kwa mikono ya Abu Huraira kwa nyuzi za ubunifu wake kuwa kama hekaya za mabibi vikongwe na wahadithiaji. Alielekea kusema kwamba msamaha wa Allah ulikuwa hauna mipaka. Jambo hili lilikuwa limethibitishwa wazi na Qur’ani tukufu, Sunna, akili na ijma ya umma, kwa kweli pamoja na ijma ya mataifa na dini zote. Ilikuwa ni moja ya mambo muhimu ya Uislamu na dini nyinginezo. Halikuhitajia hekaya za Abu Huraira kulithibitisha hilo. Mwenyezi Mungu alikuwa hana huruma kwa mtu yoyote kama akitenda yale ambayo Yeye Mwenyezi Mungu aliyakataza. Amesema: “Na kama angelizua juu yetu baadhi ya maneno, lazima tungemshika kwa mkono wa kulia. Kisha kwa hakika tungelimkata mshipa mkubwa wa moyo, na hapana mmoja wenu ambaye angeweza kutuzuia naye.” (69:44-47). Baada ya hayo, ni vipi Mwenyezi Mungu angeweza kumpa heshima huyu mtu mwenye dhambi, ambaye alivunja toba yake mara nyin244 Rejea Sahih Muslim, Jz. 2, uk. 445 181


Abu huraira check Lubumba.qxd

7/1/2011

10:48 AM

Page 182

Abu Huraira gi na kisha amwambie: Fanya lolote unalolitaka. Mimi nimekwisha kukusamehe? Ni kwa lipi ambalo muumini huyu dhaifu alistahili heshima ya Allah ambayo hakuna hata mmoja kati ya mitume, manabii au wakweli (sidiqiin) aliyeipata? Ni hekaya ngapi kama hizo ambazo Abu Huraira amewaambia hao madhalimu ili kurahisiha uhalifu na dhambi zao. Yeye amesema: “Malaika wa mauti alikuja kwa mtu aliyekaribia kufariki. Hakukuta lolote (tendo) jema lake yeye. Aliufungua moyo wake lakini hakukuta chochote ndani yake. Akafungua mataya yake na akakuta kwamba ulimi wake ulikuwa umenasa kwenye taya lake pamoja na usemi wa – hapana mungu isipokuwa Allah. Mwenyezi Mungu akamsamehe kwa ajili ya hilo tu.”245 Moja ya upuuzi wa Abu Huraira ulikuwa ni kusema kwake: “Iqama kwa ajili ya swala ilitamkwa na wenye kuswali wakasimama katika safu kwa ajili ya kuswali. Wakati Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) aliposimama katika kisomo chake kuongoza swala hiyo, akakumbuka kwamba alikuwa hana tohara.”246 Utukufu uwe juu ya Mtume! Yeye alikuwa tohara nyakati zake zote. Alikuwa wakati wote ana wudhuu wake. Mitume wote walikuwa Maasum na mbali kabisa na huyu punguani alichoropoka. Kama hicho alichokisema kingehusishwa kwa waumini wakweli na waaminifu, mbali na kwa manabii, kingeweza kuwadhalilisha, hivyo ni vipi kuhusu Mitume (a.s.)? Alisimulia riwaya akizungumzia kuhusu kukataza kumpendelea Mtume Muhammad juu ya nabii Musa.247 Katika nyingine alisema: “Yeyote atakayesema kwamba Mtume Muhammad (s.a.w.w.) ni bora kuliko nabii 245 Rejea kitabu cha historia, Tariikh Baghdad cha Khatiib al-Baghdadi, Jz. 9, uk. 125 246 Rejea Sahih al-Bukhari, Jz.1, uk. 41 247 Sahih al-Bukhari, Jz. 2, uk. 40 182


Abu huraira check Lubumba.qxd

7/1/2011

10:48 AM

Page 183

Abu Huraira Yunus bin Metti (Jonah) huyo atakuwa amesema uongo.”248 Umma ulikubaliana kwa pamoja kwamba Mtukufu Mtume Muhammad (s.a.w.w.) alifadhilishwa juu ya mitume wote wengine. Hilo lilithibitishwa kwa ushahidi mwingi wa wazi na kuchukuliwa kama moja ya mambo ya lazima katika Uislamu. Alisimulia kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amesema: “Hakuna hata mmoja atakayeingia Peponi kwa ajili ya matendo yake.” Wakasema: “Wala hata wewe, Mjumbe wa Allah?” Yeye akasema: “Wala mimi pia.”249 Riwaya hii ilikuwa ni ya kutupiliwa mbali kwa sababu ilipingana na Qur’ani. Mwenyezi Mungu amesema: “Hakika haya ni malipo yenu, na juhudi zenu zimekubaliwa.” (76:22) Alisimulia kwamba250 Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amesema: “Hakuna Mtume yeyote aliyetumwa na Mwenyezi Mungu isipokuwa kwamba alichunga kondoo.” Riwaya hii bila shaka yoyote ilikuwa batili. Na Hadith yake251 kwamba Nabii Ibrahim (a.s.) alitahiriwa kwa tezo252 wakati alipokuwa na umri wa miaka themanini. Vile vile alisimulia Hadith253 kwamba Nabii Isa - Yesu (a.s.) alimuona mtu mmoja akiiba. Yeye akamwambia : “Je, umeiba kitu.” Yule mwizi akasema: “Hapana, sikuiba. Naapa kwa Yeye Mungu mmoja.” Nabii Isa akamwamini na hakuamini macho yake. Abu Huraira alisimulia kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amesema: 248 Sahih al-Bukhari, Jz. 2, uk. 82 249 Sahih al-Bukhari, Jz. 4, uk. 6 250 Sahih al-Bukhari, Jz. 2, uk. 22 251 Sahih al-Bukhari, Jz. 4, uk. 65 252 Anaweza kurithi tezo hii kutoka kwa babu yake Nuh, ambaye aliitumia kwa kutengenezea Safina yake! 253 Sahih al-Bukhari, Jz. 2, uk. 168 183


Abu huraira check Lubumba.qxd

7/1/2011

10:48 AM

Page 184

Abu Huraira “Wakati Mwenyezi Mungu alipomuumba Adam, alimpambaja pambaja kwenye mgongo wake. Wanadamu wote Allah atakaowaumba mpaka Siku ya Kiyama watatoka kwenye mgongo wa Adam kama chembechembe. Kisha Mwenyezi Mungu akaweka kati ya macho ya kila mmoja wao nuru inayong’ara. Mwenyezi Mungu akawaonyesha kwa Adam. Akauliza: “Hawa ni kina nani Mola Wangu?” Allah akasema: “Hawa ni kizazi chako.” Adam akamuona mmoja ambaye alipenda ile nuru baina ya macho yake. Akamuuliza Mwenyezi Mungu yule alikuwa ni nani. Mwenyezi Mungu akasema: “Huyo ni mwanao Daudi.” Adam akauliza: “Umri wake umeukadiria kuwa wa urefu gani?” Mwenyezi Mungu akasema: “Miaka sitini.” Adam akasema: “Chukua miaka arobaini kutoka kwenye umri wangu na uiongeze kwenye umri wake uwe wa miaka mia moja.” Mwenyezi Mungu akasema: “Hiyo itaandikwa, na kufungwa kabisa na haitabadilishwa kamwe.” Wakati Malaika wa mauti alipokuja kwa Nabii Adam (a.s.) kuchukua roho yake, Adam akasema: “Bado kuna miaka arobaini ya umri wangu.” Malaika akasema: “Wewe hukuitoa hiyo kwa mwanao Daudi?” Adam akakana, hivyo na kizazi chake pia kikakana vile vile.”254 Ilikuwa ni kama ile riwaya yake kuhusu Adam na Musa (a.s.) pale walipobishana, kana kwamba walikuwa ni muumini wa falsafa ya jaala na kadara. Alionyesha kwamba Adam alimshinda Musa kwa nyudhuru nyingi sana ambazo hazikuwastahili Mitume, ambao lazima watukuzwe. Ni upendo kiasi gani aliokuwa nao juu ya matukio ya ajabu na yasiyokuwa ya kawaida. Kwa nyongeza juu ya yale uliyosoma katika kurasa zilizopita, hapa kuna Hadith mbili za kumalizia mlango huu: Ya kwanza: Yeye alisema kwamba wakati mmoja alikuwa pamoja na alAla’ bin al-Hadhrami walipokuwa wametumwa kwenda Bahrain pamoja na jeshi la watu elfu nne. Walitoka mpaka walipofika ghuba fulani katika bahari, ambayo hakuna mtu aliyewahi kuiingi ndani yake kabla yao na 254 Rejea Mustadrak al-Hakiim, Jz. 2, uk. 325; na Talkhiis al-Mustadrak ya athThalabi. 184


Abu huraira check Lubumba.qxd

7/1/2011

10:48 AM

Page 185

Abu Huraira wala hakuna atakayeingia baada yao. Al-Ala’ alikamata kwenye hatamu za farasi wake na akatembea juu ya maji hayo. Jeshi likamfuata yeye. Naapa kwa jina la Mwenyezi Mungu kwamba hakuna mguu wetu wala kwato ya vipando vyetu ambayo ililowa maji.”255 - Kama hii ilikuwa ni kweli, ingesimuliwa na kila mmoja aliyekuwa kwenye jeshi hilo, ambao walikuwa ni watu elfu nne. Kwa nini ilisimuliwa na Abu Huraira peke yake tu? Ya pili: Yeye alisema: “Mimi nilikumbwa na balaa tatu wakati nilipoingia kwenye Uislamu ambayo sijawahi kukumbwa na kama hiyo hapo kabla; kifo cha Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) ambaye nilikuwa sahaba wake, mauaji ya Uthman na shanta (havesack).” Wakauliza: “Shanta ilikuwa ni kitu gani?” Nikasema: “Tulikuwa na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) katika safari. Yeye aliniuliza mimi: “Je, kuna chochote kwako?” Nikasema: “Tende kiasi kwenye shanta.” Alinituma niilete. Aliishika na kuomba. Akaniambia niwakaribishe watu kumi kati ya waliokuwepo. Nikafanya hivyo. Walikula hata wakashiba. Halafu nikawakaribisha kumi wengine na kuendelea vivyo hivyo mpaka jeshi lote likala katika tende hizo. Shanta hilo lilikuwa bado lina tende. Mtume (s.a.w.w.) akaniambia: “Kama unataka kuchukua kiasi kutoka kwenye shanta hilo ingiza mkono wako ndani yake na usilipindue.” Nimekuwa nikila kutoka kwenye shanta hili muda wote katika muda wa uhai wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), Abu Bakr, Umar na Uthman. Wakati Uthman alipouliwa, shanta hilo likaibiwa. Je niwaeleze ni kiasi gani nilichokuwa nimekula kutoka kwenye shanta hilo? Nimekula kutoka kwenye shanta hilo zaidi ya wasaq256 mia mbili.” Hakuna shaka kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alilisha idadi kubwa ya 255 Ilisimuliwa na Abu Bakr bin Muhammad al-Waliid al-Fihri at-Taroushi, ambaye alijulikana kama ibn Randa. Ad-Dimyari ameinukuu hii kutoka kwake katika kitabu chake, Hayat al-Haywan (maisha ya wanyama). Ilisimuliwa pia katika al-Istii’ab na Issaba. 256 Wasaq ni kipimo cha ujazo kilichotumiwa na waarabu kwa wakati ule. Wasaq mia mbili zilikuwa ni takriban sawa na kilo thelathini na tano. 185


Abu huraira check Lubumba.qxd

7/1/2011

10:48 AM

Page 186

Abu Huraira watu kwa chakula kichache katika nyingi ya siku zake zilizobarikiwa. Hiyo ilikuwa ni moja ya dalili za utume wake na ujumbe wake. Lakini Hadith hii ilibuniwa hasa na Abu Huraira ili kugusa hisia za makundi ya Bani Umayyah na kundi la wafuasi wao ambao walikuwa bado watiifu kwa shati la Uthman na vidole vya mke wake wakilia na kupiga mayowe. Alifanya hivyo ili kuchochea fadhila zao na kuomba misaada na sadaka zao. Ilikuwa ni moja ya njia zake za kushangaza katika kuwafurahisha na kuwapendezesha Bani Umayyah na kuomba fadhila zao. Kilichothibitisha kwamba ilikuwa imebuniwa na Abu Huraira kilikuwa kwamba alibadilika badilika katika Hadith hii kama kinyonga. Aliisimulia Hadith hii katika njia nyingi mbalimbali, kama ilivyojulikana wazi kwa watafiti, ambao walichunguza vitabu vya Sunna na Hadith.257 Abu Huraira alikuwa na gunia zima lililokuwa na hili shanta na vitu vingine. Lilikuwa ni mfuko wake wa elimu. Alichota kutoka humo chochote, wakati wowote na vyovyote alivyotaka. Angeweza mara kwa mara kuulizwa: “Ulilisikia hili kutoka kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.)?” Yeye alijibu: “Hapana, linatoka kwenye gunia la Abu Huraira.” 258 Kitabu hiki hakitaweza kubeba maajabu yote ya Abu Huraira. Tulichokitaja kati ya hayo kilikuwa kinatosha kuwa kama ushahidi wa kuthibitisha kile tulichokikusudia. Shukrani zote anastahiki Mwenyezi Mungu.

257 Hadith hii ilisimuliwa na Ahmad bin Hanbal kwa njia mbili na Abu Bakr alBayhaqi naya kwa njia mbili. Ilisimuliwa pia na wengineo kwa njia tofauti zenye ukinzano mwingi. Rejea kwa Ibn Kathiir, ambaye alizitaja nyingi ya tofauti hizo katika kitabu chake, al-Bidaya wan-Nihaya, Jz. 6, uk. 116. 258 Sahih al-Bukhari, Jz. 3, uk. 189 186


Abu huraira check Lubumba.qxd

7/1/2011

10:48 AM

Page 187

Abu Huraira

MUSNAD YAKE NI KAMA MURSAL259 YAKE Abu Huraira alikuwa akihusisha kwa Mtukufu Mtume kile alichokisikia juu ya Hadith za Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kutoka kwa mtu yoyote kana kwamba yeye mwenyewe alikuwa amezisikia kutoka kwa Mtukufu Mtume moja kwa moja, bila ya kutafuta ushahidi wowote wa uhakika. Kama ulikuwa una mashaka juu ya hilo, tafadhali hebu angalia usemi wake: “Mtukufu Mtume Muhammad (s.a.w.w.) alimwambia ami yake Abu Talib: “Sema hapana mungu isipokuwa Allah. Nitalishuhudia hilo kwa ajili yako katika Siku ya Kiyama.” Ami yake akasema: “Ninahofia kwamba Maquraishi wanaweza kunilaumu kwa hilo.”260 Ilikuwa ni hakika kwa wote kwamba Abu Talib alikuwa amefariki miaka kumi kabla ya Abu Huraira kuja Hijaz. Hivyo ni vipi aliweza kuwasikia (Mtume na ami yake) wakiongea pamoja pale aliposimulia Hadith hii katika namna ambayo ni kana kwamba aliwaona kwa macho yake na kuwasikia kwa masikio yake? Alisema: “Wakati Mwenyezi Mungu alipomshushia Mtume (s.a.w.w.): “Na uwaonye watu wako wa karibu.”, alisimama na kusema: “Enyi watu wa Quraishi, sitabadilisha kwa ajili yenu mbele ya Mwenyezi Mungu mnamo Siku ya Kiyama.”261 259 Musnad: Riwaya ambayo imesimuliwa na sanad ya kweli inayofahamika vizuri ya wasimulizi. Mursal: Riwaya ambayo imesimuliwa na wasimulizi wasiojulikana au bila ya kutaja wasimuliaji wenyewe. 260 Ilisimuliwa na Muslim katika Sahih yake, Jz. 1, uk. 31. 261 Ilisimuliwa na Bukhari katika Sahih al-Bukhari, Jz. 2, uk. 86, katika Sahih Muslim na Musnad Ahmad. Tuliitaja katika mlango uliopita na kuitolea maelezo juu yake. 187


Abu huraira check Lubumba.qxd

7/1/2011

10:48 AM

Page 188

Abu Huraira Mafaqihi wote na wanachuoni wamekubaliana kwa pamoja kwamba hii aya ya Qur’ani iliteremshwa kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) mwanzoni mwa ujumbe wa Uislam na kabla ya kuutangaza mjini Makka, ambapo Abu Huraira alikuwa bado anaabudu masanamu huko Yemen. Alikuja Hijaz miaka ishirini na tano baada ya kushuka kwa aya hii. Ameisimulia Hadith hii kana kwamba alikuwa mmojawapo wa waliohudhuria kumuona Mtume (s.a.w.w.) kwa macho yake akisimama na kumsikia kwa masikio yake wakati akiwaonya watu wa kabila lake. Amesema: “Mtume (s.a.w.w.) aliomba ndani ya swala yake akisema: “Oh Allah, muokoe Salama bin Hisham, muokoe al-Waliid, muokoe Ayyash bin Abu Rabii’a. O Allah, waokoe wale waumini wanaoonewa (ambao walizuiwa na washirikina ili wasihame pamoja na wale wengine kutoka Makka kwenda Madina).262 Hili lilitokea miaka saba kabla Abu Huraira hajaja Hijaz na kuwa Mwislam. Aliisimulia kana kwamba alikuwa na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) wakati alipokuwa anaswali. Amesema: “Abu Jahl amesema: “Je, Muhammad anamsujudia Mungu wake miongoni mwenu?” Ikasemwa: “Ndio.”263 Kama Abu Jahl kweli alikuwa amesema hivyo, itakuwa ni miaka ishirini kabla Abu Huraira hajafika kutoka Yemen na akawa Mwislam. Alisimulia kana kwamba alisikia na kuona yaliyotokea. Alikuwa wapi kutoka kwenye mapambano ya ar-Rajii’ na kiongozi wake Aassim bin Thabit al-Ansari, ambaye aliuawa katika pambano hilo, kuweza kulielezea kana kwamba aliona kila kitu?”264 Mapambano haya yalitokea katika mwaka wa nne hijiria, miaka mitatu kabla Abu Huraira 262 Rejea Sahih al-Bukhari, Jz. 2, uk. 105 263 Sahih Muslim, Jz. 2, uk. 117 264 Sahih al-Bukhari, Jz. 2, uk. 117 188


Abu huraira check Lubumba.qxd

7/1/2011

10:48 AM

Page 189

Abu Huraira hajafika Hijazi na kuwa Mwislam. Mtu yeyote ambaye alichunguza mwenendo wa Abu Huraira katika kusimulia Hadith, angaweza kujua kwamba alikuwa kama vile tu tulivyosema. Hadith hizi chache zilikuwa zinatosha kuthibitisha hilo. Ahmad Amiin aliligundua hilo na akasema kuhusu Abu Huraira: “Ilielekea kwamba hakusimulia kile alichokuwa amekisikia kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) tu, bali alisimulia hata aliyokuwa ameelezwa na watu wengine.265 Abu Huraira mwenyewe alikiri kwamba wakati aliposimulia kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisema: “Yeyote ambaye alikuwa hana tohara (mwenye janaba) wakati wa alfajiri kuchomoza, alikuwa hapaswi kufunga.” Aisha na Umm Salama waliikanusha riwaya hiyo. Alimshutumu alFadhl bin al-Abbas, ambaye alikuwa amekwisha kufariki wakati huo,266 kuwa ndiye aliyelisema hilo. Alisema kwamba alikuwa ameisikia kutoka kwa al-Fadhl na kwamba hakuisikia kutoka kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Hata hivyo alikiri, iwapo ilikuwa kweli au uongo, kwamba aliihusisha kwa Mtukufu Mtume yale aliyokuwa ameyasikia kutoka kwa watu wengine. Kama utasema: Kwani kuna nini endapo kama ataihusisha na Mtukufu Mtume ile aliyoisikia kutoka kwa mtu mwingine? Sisi tunasema: Hilo si neno, lakini Hadith hiyo isichukuliwe kama ni Hadith sahihi labda kama sanadi yote ya wasimuliaji itajulikana na kuthibitishwa kwamba wote ni waaminika. Hiyo ina maana ya kusema kwamba uaminifu wa msimuliaji lazima uthibitishwe kama sharti la Hadith hiyo kuwa ya kweli. Hadithi hiyo lazima isichukuliwe kuwa ya kweli kama msimuliaji alikuwa hajulikani. Kwa neno moja, nyingi ya Hadith za Abu Huraira zilikuwa kwa namna 265 Fajrul-Islam (Kuchomoza kwa Uislam), uk. 262. 266 Rejea Sahih al-Bukhari, Jz. 1, uk. 225. 189


Abu huraira check Lubumba.qxd

7/1/2011

10:49 AM

Page 190

Abu Huraira ambayo haikuweza kutegemewa. Zilichanganyika na Hadith zake za kweli ambapo ilitufanya sisi kuziepuka zote kwa mujibu wa kanuni ya mashaka na tahadhari.

KUJIFANYA KWAKE AMEHUDHURIA BAADHI YA MATUKIO Bwana huyu ametulazimisha kumtilia mashaka. Alijifanya kwamba alikuwa amehudhuria baadhi ya matukio ambayo hakuwahi kamwe kufanya hivyo. Alisema: “Wakati mmoja niliingia ndani ya nyumba ya Ruqayya, binti yake Mtume na mkewe Uthman. Alikuwa ameshika kitana mkononi mwake. Akasema: “Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) ameondoka hapa kitambo kidogo kilichopita. Nilimchana nywele zake. Yeye akaniambia: “Unamuonaje Abu Abdillah (Uthman)?” Nikasema: “Yeye ni mzuri tu.” Akaniambia: “Mfanyie hisani! Yeye ndiye anayefanana sana na mimi katika maadili.” Ilisimuliwa na al-Hakiim,267 ambaye alisema: Hadith hii ina sanadi ya kweli ya wasimulizi lakini maneno yake sio ya kweli, kwa sababu Ruqayya alikuwa amefariki katika mwaka wa tatu hijiria wakati wa vita vya Badr, ambapo Abu Huraira alikuja na akawa Mwislamu baada ya vita vya Khaybar.” Adh-Dhahabi ameisimulia Hadith hii katika kitabu chake, Talkhiiss alMustadrak na akasema: “Ilikuwa ni kweli kwa upande wa wasimuliaji wake, lakini maneno yake yalikataliwa kwani Ruqayya alifariki wakati wa vita vya Badr ambapo Abu Huraira alikuwa Mwislam wakati wa vita vya Khaybar.”

267 Rejea al-Mustadrak al-Hakiim, Jz. 4, uk. 48 190


Abu huraira check Lubumba.qxd

7/1/2011

10:49 AM

Page 191

Abu Huraira Abu Huraira amesema: “Mtume (s.a.w.w.) alituongoza katika swala ya Dhuhri au al’Asri na aliimalizia swala hiyo kwa rakaa mbili (badala ya nne). Dhul-Yadayn akamuuliza: “Je, umeipunguza swala hii au umesahau?” – Dhul-Yadayn aliuawa kwenye vita vya Badr miaka kadhaa kabla Abu Huraira kuwa Mwislamu. Ni mara ngapi yeye amejigamba: “Tuliiteka Khaybar lakini hatukupata dhahabu au fedha. Tulipata kondoo, ng’ombe, ngamia, bidhaa na nyumba.”268 Alisema hivyo ingawa hakushiriki kamwe katika vita hivyo. Alikuja kuwa Mwislamu baada ya Waislamu walipokuwa wamekwishaiteka Khaybar na vita vilikuwa vimekwisha tayari. Hivyo, wale walioielezea Hadith hii, walichanganyikiwa walipofikia kule kusema kwake – tuliiteka Khaybar. Waliihalalisha kwa kusema kwamba Abu Huraira aliisimulia kiistiari. Alizungumzia Waislamu wenzake.269 Alisema: “Tulipigana pamoja na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) huko Khaybar. Mtume alimwambia mtu mmoja, ambaye alijifanya kuwa ni Mwislamu kwamba yeye atakuwa Motoni. Wakati mapigano yalipoanza, yule mtu alipigana kijasiri sana mpaka akawa na majeraha mengi sana. Baadhi ya watu walikuwa karibu watilie mashaka maneno ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Mtu huyo aliugulia maumivu ya majeraha yake. Alichomoa baadhi ya mishale kutoka kwenye zaka lake na akajiuwa kwa kuitumia hiyo.”270 Tunayo maelezo namna mbili kuhusu Hadith hii: Ya kwanza: Alijifanya kwamba alishiriki katika vita hivyo pamoja na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), na imethibitishwa kwamba yeye hakuwepo 268 Rejea Sahih al-Bukhari, Jz. 3, uk. 37. 269 Rejea al-Irshad as-Sari, Jz. 8, uk. 154 na Tuhfatul Bari ambavyo vilichapishwa pamoja kama kitabu kimoja. Hayo ameyasema as-Sindi katika maelezo yake juu ya Hadith hiyo katika pambizo ya Sahih al-Bukhari. 270 Sahih al-Bukhari, Jz. 3, uk.34 na Jz. 2, uk. 120. 191


Abu huraira check Lubumba.qxd

7/1/2011

10:49 AM

Page 192

Abu Huraira pale. Wale ambao walitoa maoni juu ya Hadith hii, walikuja kuchanganyikiwa na wakahalalisha kwamba Abu Huraira alisema kiistiari kwa sababu alikuja kutoka Yemen baada ya vita vya Khaybar kama vile alivyosema al-Qastalani.271 Ya pili: Huyo mtu ambaye alijiuwa mwenyewe, alikuwa ni yule mnafiki Qazman bin al-Harith, mshirika wa kabila la Zafar. Yeye alipigana kwa ajili ya kutaka umaarufu. Suala lake ambalo Abu Huraira amelitaja, lilikuwa ni maarufu sana.272 Aliuawa katika vita vya Uhud miaka mingi kabla Abu Huraira kuja Hijaz na kuwa Mwislam. Abu Huraira alikuwa hana uhakika kuhusu yeye, kwa hiyo alivuruga kila kitu. Abu Huraira amesema: “Nimewaona wakazi sabini wa makao ya Suffa kwamba hakuna hata mmoja kati yao aliyekuwa na nguo mwilini mwake.”273 Hao sabini wote waliuawa kishahidi katika mapambano ya kisima cha Ma’una. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alihuzunika sana kwa ajili yao. Aliomba dhidi ya wauwaji wao kwa muda wa mwezi mzima. Mapambano haya yalitokea katika mwaka wa nne hijiria, miaka kadhaa kabla ya Abu Huraira kufika toka Yemen. Sasa ni vipi kwamba yeye aliwaona hao? Al-Qastalani amesema kwamba hao sabini, ambao Abu Huraira aliwaona walikuwa ni wengine mbali na wale waliouawa. Mwenyezi Mungu ndiye Mtambuzi zaidi!

271 Katika kitabu chake, al-Irshad as-Sari, Jz. 6, uk. 322. 272 Ilisimuliwa na al-Waqiidi, ibn Iss-haq, ibn Hajar katika Issaba yake na wengineo. Huyu Qazman alipigana kijasiri katika vita vya Uhud dhidi ya washirikina mpaka Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akaambiwa: “Hakuna hata mmoja wetu aliyefanya kama alivyofanya yeye.” Mtukufu Mtume akasema: “Hata hivyo, yeye atakuwa ndani ya Jahannam.” Alijeruhiwa vibaya sana. Alisimika upanga wake ardhini, akakandamiza kifua chake juu yake na kujiuwa mwenyewe. Rejea Sahih al-Bukhari, Jz. 2, uk. 101. 273 Sahih al-Bukhari, Jz. 2, uk. 60. 192


Abu huraira check Lubumba.qxd

7/1/2011

10:49 AM

Page 193

Abu Huraira Baada ya kukagua na kuchunguza kuhusu Abu Huraira, tuliona kwamba, mara kwa mara alisimulia Hadith za Mtume, ambazo hakuzisikia kutoka kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na mara nyingi alieleza kuhusu matukio ambayo hakuwahi kuyahudhuria au alijifanya kwamba alikuwa amehudhuria. Angependezewa na jambo alilolisikia kutoka wa Ka’bul-Ahbar274 au mtu mwingine na alilisimulia kana kwamba alilisikia kutoka kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kama alivyofanya kwenye Hadith hii: “Mwenyezi Mungu alimuumba Adam kulingana na sura yake Mwenyewe katika dhiraa sitini urefu na dhiraa sabini upana.” Yote hayo yaliwafanya waumini kuepukana na riwaya zake. Ninashangaa kwa nini wale waliokusanya Hadith walijaza vitabu vyao na Hadith zilizosimuliwa na mtu huyu bila ya kuzingatia maajabu yake na vioja vyake au bila ya kuona utungaji na ubunifu wake! Kama umechunguza Sahih hizi mbili za Bukhari na Muslim, ungestaajabu juu ya ushamba wa masheikh hawa wawili. Hapa ni mfano wa kuthibitisha ukweli huu: Muslim amesimulia katika Sahih yake (mlango wa sifa za Abu Sufyan) riwaya kutoka kwa Akrima bin Ammar al-Ijli al-Yamami kwamba Waislamu hawakumuangalia Abu Sufyan na hawakukaa pamoja naye. Alimwambia Mtukufu Mtume (s.a.w.w.): “Oh, Mjumbe wa Allah nakuomba kwa ajili ya kunipatia mambo matatu.” Mtukufu Mtume akasema: “Ndio, nitafanya hivyo.” Yeye akasema: “Ninaye mbora na mzuri zaidi miongoni mwa Waarabu, binti yangu Ummu Habiiba. Nitamuoza yeye kwako.” Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akasema: “Ndio.” Yeye akasema:

274 Myahudi ambaye baadae alikuja kuwa Muislamu 193


Abu huraira check Lubumba.qxd

7/1/2011

10:49 AM

Page 194

Abu Huraira “Mwanangu Mu’awiyah, mfanye awe karani wako.” Mtukufu Mtume akasema: “Ndio.” Yeye akasema: “ na uniamuru nipigane na makafiri kama nilivyokuwa nikipigana na Waislamu.” Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akasema: “Ndio.”275 Ilisimuliwa na Muslim peke yake pale alipozungumzia kuhusu sifa za Abu Sufyan! Ilichukuliwa kwa kauli ya pamoja kwamba ni batili. Abu Sufyan alisilimu kwa nguvu baada ya kutekwa Makka. Kabla ya hapo yeye alikuwa ni adui mkubwa wa Mwenyezi Mungu na Mtume Wake (s.a.w.w.). Na kuhusu binti yake Ummu Habiiba, ambaye jina lake lilikuwa ni Ramla, yeye alikuwa Mwislam kabla ya hijra. Alikuwa ni mmojawapo wa Waislam waaminifu. Alikuwa miongoni mwa wale ambao walihamia Abyssinia akimtoroka baba yake na watu wao. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alimuoa wakati baba yake akiwa amekithiri katika ukafiri wake na amekithiri katika kupigana vita dhidi ya Mtume (s.a.w.w.). Wakati Abu Sufyan aliposikia kwamba Mtume amemuoa binti yake, alisema: “Yule mkaidi hataweza kushindwa.” Alikuja Madina akitafuta kuongeza muda wa makubaliano na Mtukufu Mtume ya kusitisha vita. Alikwenda nyumbani kwa binti yake. Alipotaka kuketi chini, Ummu Habiiba, binti yake, akakunja tandiko lake. Abu Sufyan akasema: “Unanizuia mimi kuketi 275 Sahih Muslim, Jz. 2, uk. 361. Ilikuwa sio Hadith ya kweli iliyobuniwa na Akrima al-Yamami kama ilivyokuwa imethibitishwa na ibn Hazim. Adh-Dhahabi amesema katika kitabu chake Mizan al-I’tidal kwamba Akrima al-Yamami alibuni Hadith iliyokataliwa iliyosimuliwa ndani ya Sahih Muslim kuhusu yale mambo matatu ambayo Abu Sufyan alimuomba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) ampatie. Riwaya nyingine ya uongo iliyosimuliwa na Akrima kwamba Mtume (s.a.w.w.) alisema: “Abu Bakr ndiye mbora wa watu.” Ilisimuliwa na ibn Adiy katika kitabu chake, al-Kamiil, ambacho kilikuwa ni kitabu bora kati ya vitabu katika kubain-

isha wale waliobuni Hadith. Hayo yalisemwa na adh-Dhahabi katika Mizan yake

194


Abu huraira check Lubumba.qxd

7/1/2011

10:49 AM

Page 195

Abu Huraira kwenye tandiko lako?” Yeye akamjibu: “Ndio, ninakuzuia. Hili ni tandiko la Mtume na wewe ni kafiri uliye najisi.” Wengi wa wanahistoria wameyataja maneno haya wakati walipozungumza juu ya Ummu Habiiba.276 Shukrani ziwe kwa Mwenyezi Mungu kwa ajili ya muongozo Wake. Ashukuriwe Mwenyezi Mungu ambaye ametufanya sisi tuweze kubainisha haki. Rehma na amani ya Mwenyezi Mungu iwe juu ya Muhammad, Mtume na kiongozi wetu.

WAISLAM WA MWANZONI KABISA WANAZIKATAA RIWAYA ZAKE Watu walikataa na kukanusha kukithiri kwa Abu Huraira katika kusimulia Hadith wakati wa uhai wake. Alipindukia mipaka yote na alikuwa na mtindo wa kipekee ambao uliwafanya watu wamtilie mashaka na kuzishuku riwaya zake. Waliikataa idadi na ubora wa Hadith zake na wakamshutumu waziwazi. Yeye mwenyewe amesema: “Watu wanasema Abu Huraira anasimulia Hadith nyingi. Mwenyezi Mungu ndiye hakimu kesho Akhera. Wanasema kwamba kwa nini Muhajiriin na Ansari hawasimulii kama anavyosimulia yeye …..” Alikiri kwamba vyote, wingi na ubora wa Hadith zake unastahili kukataliwa, kwa hiyo yeye aliwatishia watu kwa uchungu sana wakati aliposema: “Mwenyezi Mungu ndiye hakimu kesho Akhera.” Alionyesha mwishoni mwa Hadith hii kwamba labda akilazimika kwa mujibu wa wajibu wake wa kisheria, yeye hatasimulia chochote kamwe kwa vile walikuwa wanamshuku. Akasema: “Isipokuwa kwamba aya hizi mbili: “Hakika wale wanaoficha tuliyoyateremsha katika dalili zilizo wazi na muongozo, baada ya sisi kuzibainisha kwa watu Kitabuni, hao hulaaniwa na Mwenyezi Mungu na hulaaniwa na wenye kulaani. Ila wale waliotubu 276 Sharh ya an-Nawawi iliyochapwa pambizoni mwa Irshad as-Sari na TuhfatulBari, Jz. 11, uk. 360 195


Abu huraira check Lubumba.qxd

7/1/2011

10:49 AM

Page 196

Abu Huraira na kusahihisha na kuweka wazi, basi hao nitawakubalia, na Mimi ni Mwelekevu sana, Mwenye kurehemu.” (2:159-160), zilikuwamo ndani ya Qur’ani, vinginevyo mimi nisingewaambieni kitu chochote kamwe.”277 Ilikuwa wazi kuthibitisha kile tulichokisema sisi. Nyingine iliyo wazi zaidi ni ile iliyosimuliwa na Abu Raziin278 kwamba yeye alisema: “Abu Huraira alitujia sisi, akapiga kifuani kwake kwa mkono wake na akasema: “Ninyi mnasema kwamba Abu Huraira anahusisha uongo kwa Mtume ili kwamba muwe mmeongoka na kwamba mimi nitapotoka.” Wakati alipokuja Iraqi pamoja na Mu’awiyah na akauona ule mkusanyiko mkubwa, wa watu waliokuja kumlaki, yeye alipiga magoti na akaanza kupiga upara wake ili kuvuta nadhira zao. Walipokusanyika kumzunguka yeye, akasema: “Enyi watu wa Iraqi, mnajifanya kwamba mimi ninahusisha uongo kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) ili nijichome mwenyewe katika Jahannam? ….. na akaanza kumkashifu Imam Ali ili kuwapendeza Bani Umayyah.279 Kilichotosheleza jambo hili ni kwamba wale ambao walizikataa Hadith zake na kumshutumu walikuwa ni wale miongoni mwa masahaba mashuhuri. Ahmad Amiin amesema280 kuhusu Abu Huraira: “Masahaba mara nyingi walimshutumu kwa kule kukithiri kwake katika kusimulia Hadith na wakamshuku (kuwa ni mwongo) kulingana na alichokisimulia Muslim katika Sahih yake.” Kisha akataja Hadith mbili kutoka kwenye Sahih Muslim zinazoonyesha kumshutumu na kumtilia shaka yeye. Mustafa Sadiq ar-Rafi’i amesema kuhusu hili: “Aliyezidi sana katika kusimulia Hadith miongoni mwa masahaba alikuwa ni Abu Huraira. 277 Imesimuliwa na al-Bukhari na Muslim katika Sahih zao. Tutalizungumzia hili pamoja na maelezo katika Mlango unaofuata, Insha’allah. 278 Sahih Muslim, Jz. 2, uk. 217. 279 Rejea an-Nahj al-Hamiid cha Abu Ja’far al-Iskafi, Jz. 1, uk. 359. 280 Katika kitabu chake, Farjul Islam, uk. 262. 196


Abu huraira check Lubumba.qxd

7/1/2011

10:49 AM

Page 197

Abu Huraira Usahaba wake na Mtume ulikuwa wa miaka mitatu tu, kwa hiyo Umar, Uthman, Ali na Aisha walizikataa Hadith zake na kumtilia shaka yeye. Alikuwa ni msimuliaji wa kwanza katika historia ya Uislamu kutiliwa mashaka (kushutumiwa kwa kubuni). Aisha alikuwa ndiye wa mstari wa mbele kabisa kati ya wale waliozikanusha Hadith zake.281” An-Nazzam amesema: “Umar, Uthman, Ali na Aisha walimuona Abu Huraira kama ni muongo.”282 Ibn Qutayba amesema: “An-Nazzam alimshutumu Abu Huraira kwa kulaumiwa kwake kwa uongo na Umar, Uthman, Ali na Aisha kwamba Abu Huraira amesuhubiana na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kwa miaka mitatu tu, lakini alisimulia kutoka kwake Hadith nyingi mno, ambazo zilikuwa zaidi ya zile zilizosimuliwa na yoyote kati ya masahaba wa kwanza na waliotangulia, ambao walimshuku yeye na kukataa ukithirishaji wake.283 Wao wamesema: “Imekuwaje wewe peke yako kuyasikia yote hayo? Ni nani aliyeyasikia pamoja na wewe?” Aisha alikuwa ndiye aliyezidi kabisa katika kuzikataa Hadith zake kwani yeye alibakia hai kwa muda mrefu, ambamo Abu Huraira alisimulia Hadith zake. Umar pia alizidi sana kuwa dhidi ya wasimulizi waliokithiri, au wale walioeleza juu ya fat’wa za kisheria bila ya ushahidi ….. mpaka mwisho wa Hadith yake, ambayo ilithibitisha kile alichokisema an-Nazzam. Alifanya hivyo kwa nguvu zote bila ya kumjali yeye kwa ajili ya haki, wakati wote alizungumza kwa uadilifu na uwazi kabisa! Na kwa kile ibn Qutayba alichosingizia kwamba: “Masahaba walinywea wakati Abu Huraira alipowaeleza kuhusu cheo chake maalum karibu na Mtukufu Mtume,” kilikuwa ni ujinga na bure tu. Masahaba mashuhuri walimjua vizuri na hawakuhitaji mtu yoyote kuwatambulisha kwake. Kama wangekuwa na chembe ya heshima kwake yeye, wasingemshutumu 281 Rejea kwenye kitabu chake, al-Adab al-Arab, Jz. 1, uk. 282. 282 Rejea Ta’wiil Mukhtalif al-Hadith cha ibn Qutayba, uk. 27. 283 Ibn Qutayba alitaka kumkana an-Nazzam, lakini bila kujijua aliithibitisha riwaya yake na kuongezea kwenye orodha yake ya wakataaji wale masahaba wote wa mwanzo 197


Abu huraira check Lubumba.qxd

7/1/2011

10:49 AM

Page 198

Abu Huraira kamwe na kumuona kama muongo. Uliiona simulizi284 yake kwamba alikuwa akianguka chini hali ya kuzimia (wakati wa uhai wa Mtume) baina ya mimbari na chumba cha Aisha. Wageni wakija walikuwa wakiweka miguu yao kwenye shingo yake wakidhania kwamba alikuwa ni kichaa. Hivi hilo lilistahili heshima na hadhi? Kwa kifupi, ilithubutu kwamba masahaba wote wakweli walimtilia shaka na kuzikataa Hadith zake. Lakini walipokwenda dunia njema ya akhera, na wale waliokuja baada yao wakaamua kwamba masahaba wote kwa jumla walikuwa waadilifu na wema na wakakataza kuwashutumu. Walilifanya hilo kama ni hukmu ya kisheria (fat’wa) na hivyo wakazifungia akili zao, wakang’oa macho yao, wakaweka vifuniko kwenye nyoyo zao na wakaziba masikio yao. Watu wakawa: “Ni viziwi, mabubu na vipovu na hivyo hawatarejea.” (2:18) Utukufu ni juu ya Maimam Maasum ambapo waliwaweka masahaba, kila mmojawao, mahali pao wanapostahili, ambamo wao wenyewe tayari walikwisha kuwemo humo.285 Hivyo mawazo yao kuhusu Abu Huraira hayakuwa tofauti na alichokiwaza Ali, Umar, Uthman na Aisha. Mashia, tangu enzi za Ali mpaka siku hizi wameshikilia kwenye njia ya Maimam wao. .284 Mwanzoni kabisa mwa kitabu hiki. 285 Ahmad Amiin alisema katika kitabu chake, Fajrul Islam uk. 259: “Ilielikea kwamba masahaba wenyewe walishutumiana wao kwa wao na kumpendelea mmoja juu ya mwingine wakati wa zama zao. Kama mtu alisimulia Hadith angeulizwa juu ya ushahidi wake. Wakati mmoja Abu Huraira alisimulila Hadith, ambapo ibn Abbas aliikanusha, na akasimulia Hadith nyingine ambayo Aisha aliikanusha. Fatima binti Qays alisimulia Hadith kutoka kwa mume wake ambayo Umar aliikanusha na akasema: “Je, tunaacha Kitabu cha Mola Wetu na Sunna ya Mtume wetu kwa ajili ya riwaya ya mwanamke? Hatujui kama ni ya kweli au uongo, yeye hukumbuka na kusahau! Aisha pia aliikanusha na akamwambia Fatima huyo: “Wewe humuogopi Mwenyezi Mungu!” Yalikuwapo masuala mengi kama hayo. 198


Abu huraira check Lubumba.qxd

7/1/2011

10:49 AM

Page 199

Abu Huraira Mu’tazila wote wanaweza wakawa na maoni hayohayo. Imam Abu Ja’far al-Iskafi amesema: “Abu Huraira alikuwa ameambukizwa katika akili yake kwa mujibu wa masheikh wetu. Hadithi zake zilikanushwa na wao. Wakati mmoja Umar alimpiga na kusema: “Umekithiri katika Hadith zako. Unaweza kuwa muongo unayehusisha uongo kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.).” Sufyan ath-Thawri amesimulia kutoka kwa Mansuur kwamba Ibrahim at-Taymi alisema: “Hawakutegemea juu ya Hadith za Abu Huraira, isipokuwa zile ambazo zilikuwa ni kuhusu Pepo na Jahannam.” Abuu Usama alisimulia kwamba al-A’mash alisema: “Ibrahim alikuwa mkweli katika kusimulia Hadith. Nilikuwa nikimuonyesha kila nilichokisikia katika Hadith. Siku moja nilimletea Hadith fulani zilizosimuliwa na Abu Salih kutoka kwa Abu Huraira. Yeye aliniambia: “Niache mbali na Abu Huraira! Walizitupilia mbali nyingi ya Hadith zake.” Imesimuliwa kwamba Imam Ali (a.s.) alisema: “Mtu muongo asiyeaminika kabisa (au alisema wa walio hai), ambaye anahusisha uongo kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) ni Abu Huraira ad-Doussi.” Abu Yusuf alisimulia kwamba alikuwa amemwambia Abu Haniifa: “Baadhi ya Hadith zinazotufikia sisi zinapingana na analojia – mwenendo wetu. Tufanye nini nazo hizo?” Yeye akasema: “Kama zimesimuliwa na watu wakweli basi tutazitegemea na kuacha maoni yetu pembeni.” Mimi nikasema: “Unasemaje juu ya Abu Bakr na Umar?” Akasema: “Wao hao walikuwa wakweli.” Nikasema: “Je Ali na Uthman?” Akasema: “Na wao walikuwa hivyo.” Aliponiona ninawataja hao masahaba, yeye akasema: “Masahaba wote walikuwa wema na waadilifu isipokuwa baadhi ya wachache.” Aliwataja baadhi, na kati ya hao walikuwemo Abu Huraira na Anas bin Malik. Imam Abu Hanifa na wafuasi wake waliziweka pembeni Hadith za Abu Huraira kama zingepingana na mwenendo wao, kama walivyofanya kwa Hadith yake kuhusu yule ‘missrat’.286 Abu Huraira alisimulia kwamba 286 Ni ng’ombe, kondoo jike au ngamia jike ambaye hakukamuliwa kwa siku kadhaa ili kufanya maziwa yabakie kwenye kiwele chake kwa ajili ya kumdanganya mnunuzi kwamba alikuwa anatoa maziwa mengi. 199


Abu huraira check Lubumba.qxd

7/1/2011

10:49 AM

Page 200

Abu Huraira Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisema: “Msiyafungie maziwa kwenye viwele vya kondoo au ngamia wenu. Yoyote yule atakayemnunua atakuwa na uchaguzi baada ya kuwakamua, ama kuwaweka kama amekubali au kuwarudisha kwa wafugaji wenyewe pamoja na kipimo maalum (takriban kilo 3) cha tende.” Wao hawakuizingatia Hadith hii na wakasema: “Abu Huraira alikuwa sio faqih na Hadith yake ilipingana na mwenendo wetu moja kwa moja. Kumkamua mnyama kulionekana kama ni kukiuka haki za mwingine, ambapo lazima zifidiwe kwa thamani kama hiyo, lakini kipimo hicho cha tende hakiwi ni kimojawapo.287 Tulijua kwamba Abu Haniifa na wafuasi wake walidhani kwamba swala inaweza kubatilika kwa aina yoyote ya mazungumzo, ambayo yalikuwa sio sehemu ya swala ama kwa kusahau au kwa kufikiria kwamba labda swala imekwisha. Fiqhi ya kihanafiya ilikuwa wazi kuhusu jambo hili. Kadhalika hilo ndio lilikuwa wazo la Sufyan ath-Thawri. Hivyo riwaya hiyo ya Abu Huraira ilikuwa haina thamani miongoni mwao, wakati aliposema kwamba wakati mmoja Mtukufu Mtume alisahau na kumaliza swala baada ya rakaa mbili badala ya nne kisha akaacha kisomo chake na akaingia chumbani kwake. Aliporudi, aliulizwa: “Je, ulipunguza swala au ulisahau?” Yeye akasema: “Swala haikupunguzwa na mimi sikuwa nimesahau.” Wakasema: “Ndio ulisahau.” Na baada ya mabishano baina yake na wao, yeye aliwaamini na akaimalizia swala kwa rakaa mbili nyingine. Kisha akaleta sajida ya kusahau. Kwa mujibu wa Hadith hii, Malilk, Shafi’i, Ahmad na al-Awza’ei walitoa fat’wa kwamba kuongea (maneno ambayo sio sehemu ya swala) kwa mtu, ambaye amesahau kwamba alikuwa anaswali au alifikiri kwamba alikuwa amemaliza swala yake, hayatabatilisha swala yake. Lakini Abu Hanifa, ambaye hakuzingatia kabisa riwaya za Abu Huraira, yeye alisema kwamba kuongea wakati wa swala kungeifanya iwe batili.288 287 Rejea Fajrul-Islam cha Ahmad Amiin, uk. 263. 288 Rejea Sharh Sahih Muslim ya an-Nawawi, Jz. 4, uk. 234 200


Abu huraira check Lubumba.qxd

7/1/2011

10:49 AM

Page 201

Abu Huraira Natumalizie mlango huu kwa baadhi ya matukio yaliyotokea kati Ya Abu Huraira na baadhi ya masahaba ili kukuonyesha wewe walimchukulia kwa namna gani. Abu Huraira alisema: “Wakati riwaya yangu ilipotajwa kwa Umar, yeye aliniita mimi na kusema: “Wewe ulikuwa pamoja nasi siku ile pale tulipokuwa ndani ya nyumba ya yule bwana?” Nikasema: “Ndio, nilikuwepo, wakati Mtukufu Mtume aliposema: “Yeyote atakayehusisha Hadith ya uongo kwangu mimi, mahali pake kwa yakini patakuwa ndani ya moto wa Jahannam.”289 Hii inathibitisha kwamba hakusimulia kamwe Hadith mbele ya Umar, wala hakuwa mmoja wa wale ambao Umar aliwaona na kuwasikia wakisimulia Hadith. Kwa kweli Umar aliisikia Hadith hii kutoka kwa watu na akamshutumu kwa kusema uwongo. Alimuita na akamtahadharisha na moto wa Jahannam endapo atadanganya. Siku moja Umar alimkemea kwa kusema:290 “Ama uache kusimulia Hadith au nitakuhamishia kwenye ardhi ya Douss291 au ardhi ya manyani. Siku moja Umar alimkasirikia sana kwa kupindukia mipaka kwake katika kusimulia Hadith. Alimpiga kwa fimbo yake na kumkaripia kwa kusema: “Umekithiri na riwaya zako na mimi nadhani umehusisha Hadith za uongo kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.).” Umar alimfukuza kutoka kwenye falme ya Bahrain baada ya kuwa amempiga mpaka akamjeruhi. Alirejesha kutoka kwake dinari elfu kumi kwenye hazina ya umma. Alimkaripia kwa maneno makali. Wakati wa enzi ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) Umar aliwahi kumpiga mpaka akaangukia 289 Ilisimuliwa na Musaddad katika Musnad yake, na ibn Hajar katika Issaba yake. 290 Rejea kwenye Kanzul-Ummal ya Ibn Asakir, Jz. 5, uk. 239. 291 Mahali pa kuzaliwa pa Abu Huraira. 201


Abu huraira check Lubumba.qxd

7/1/2011

10:49 AM

Page 202

Abu Huraira mgongo wake hadi ardhini.292 Wakati Imam Ali alipokuwa amezisikia riwaya za Abu Huraira, yeye alisema: “Aliye muongo kabisa miongoni mwa watu (au alisema) wa walio hai kuhusu Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) ni Abu Huraira ad-Doussi.” Abu Huraira mara kwa mara alisema: “Mwandani wangu aliniambia.” “Nilimuona mwandani wangu.” “Mwandani wangu, Mtukufu Mtume aliniambia.” Ali (a.s.) akalisikia hilo. Alimwambia Abu Huraira: “Ni lini Mtukufu Mtume amekuwa mwandani wako, ewe Abu Huraira?” Imam Ali (a.s.) aliyakanusha maneno ya Abu Huraira kwa sababu alikuwa hamuamini.293 Ni dhahiri Ali alikuwa sahihi kwani (yeye yupo na Qur’ani na Qur’ani iko pamoja naye. Viwili hivyo havitatengana mpaka vifike kwenye haudhi ya Mtukufu Mtume katika Siku ya Kiyama).294 Aisha alimwita Abu Huraira baada ya kuwa amesikia Hadith zake. Alimwambia: “Ni Hadith gani hizo, ambazo tunazisikia kwamba umezisimulia kuwa ni za Mtukufu Mtume? Hivi wewe umesikia mengine mbali na tuliyoyasikia sisi, au umeona zaidi kuliko tuliyoona sisi?” Yeye akasema: “Mama, kioo na wanja (kuhl) vilikushughulisha sana mbali na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.)”295 Abu Huraira alisimulia riwaya akisema kwamba mwanamke, mbwa na punda296 wanabatilisha swala. Aisha aliikanusha hiyo na kusema: “Nilimuona Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akiswali wakati nikipita kati yake 292 Sahih Muslim, Jz. 1, uk. 34. 293 Ibn Qutayba amesema hayo katika kitabu chake, Ta’wiil Mukhtalif al-Hadith, uk. 52. 294 Imesimuliwa na al-Hakiim katika Mustadrak yake, at-Tabari katika Awsat yake na ibn Asakir katika Kanzul-Ummal yake, Jz. 6, uk. 153. 295 Rejea al-Mustadrak ya al-Hakiim, Jz. 3, uk. 509 na adh-Dhahabi katika Talkhiis al-Mustadrak. Bila shaka Aisha alikataa kisingizio chake .296 Kama wangekuwa mbele ya mtu wakati anaposwali (kwa mujibu wa Abu Huraira). 202


Abu huraira check Lubumba.qxd

7/1/2011

10:49 AM

Page 203

Abu Huraira na kibla.” Alisimulia Hadith kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alikataza kutembea na kiatu kimoja. Wakati Aisha alipolisikia hilo, alitembea na kiatu kimoja na akasema kwamba yeye angepingana na Abu Huraira. Alisimulia kwamba: “Yeyote ambaye alikuwa hana tohara (mwenye janaba) ilipochomoza al-Fajr, alikuwa asifunge.” Wakati Aisha na Hafsa waliposikia waliikanusha hiyo, yeye akaifuta Hadith yake hiyo na akaomba msamaha kwamba hakuwa ameisikia kutoka kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) bali alikuwa ameisikia kwa al-Fadhl bin Abbas, ambaye alikuwa amefariki kwa wakati huo.297 Wakati mmoja watu wawili walikuja kwa Aisha na wakasema: “Abu Huraira amesimulia kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amesema: “Ndege mbaya (kisirani) hakuna ila kwa wanawake na vipando.” Aisha alitaharuki sana na akasema: “Naapa kwa Yule ambaye aliiteremsha Qur’ani kwa Abul-Qasim Muhammad kwamba huyo ambaye ameieleza Hadith hii alikuwa ni muongo.”298 Siku moja alikaa kando ya chumba cha Aisha akisimulia Hadith kuhusu Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Yeye Aisha alikuwa akishughulika na kumtukuza Mwenyezi Mungu. Wakati alipomaliza, alisema: “Ni ajabu iliyoje! Abu Huraira anakaa pembeni ya chumba changu akihusisha Hadith kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na kunifanya mimi nisikie hayo. Nilikuwa nikishughulika na kumtukuza Mwenyezi Mungu. Kama ningempata ningekanusha Hadith zake.”299 297 Riwaya hizi tatu (kuhusu mwanamke, mbwa na punda; kutembea na kiatu kimoja na hii) zilisimuliwa katika Ta’wiil Mukhtalif al-Hadith ya ibn Qutayba. 298 Ta’wiil Mukhtalif al-Hadith, uk. 126. 299 Rejea kwenye Sahih Muslim, Jz. 2, uk. 358 na 538. 203


Abu huraira check Lubumba.qxd

7/1/2011

10:49 AM

Page 204

Abu Huraira Alisimulia kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisema: “Wakati wowote mmoja wenu anapoamka kutoka usingizini, naaoshe mikono yake. Hajui mikono yake ilikuwa wapi wakati wa usiku mzima.” Aisha aliikataa hiyo300 na akasema: “Tunafanya vipi na hiyi ‘mihrass’301?” Alisimulia kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisema: “Yoyote anayebeba jeneza analazimika kuchukua wudhuu.” Ibn Abbas aliikanusha na akasema: “Kubeba vipande vikavu vya mbao hakuhitajii wudhuu.”302 Abdullah bin Umar alisimulia Hadith akisema: “Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) aliamuru kuuawa kwa mbwa isipokuwa wale mbwa wanaowinda na mbwa wa ng’ombe.” Wakamwambia ibn Umar kwamba Abu Huraira amewaongeza mbwa wa mashambani. Hakulijali hilo na akasema: “Abu Huraira analo shamba.” Alimshutumu kwa kuongeza mbwa wa mashambani kwenye Hadith ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) ili kuendelea kumweka mbwa wake na shamba.303 Abu Huraira alisimulia Hadith kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amesema: “Yeyote anayeweka mbwa mbali na mbwa-muwindaji, mbwa wa ng’ombe au mbwa wa shamba, Mwenyezi Mungu atachukua karati moja kutoka kwenye ustahili wake.” Wakati walipoitaja Hadith ya Abu Huraira mbele ya ibn Umar, yeye akasema: “Mwenyezi Mungu amhurumie Abu Huraira. Alikuwa ana shamba.” Alimshutumu kwa kuongeza kwake hilo kwenye Hadith hiyo kwa ajili ya manufaa yake. Salim bin Abdullah bin 300 Rejea Fajrul Islam ya Ahmad Amiin, uk. 259. Aisha aliikanusha Hadith hii kwa sababu hakumuamini yeye lakini kisingizio chake kuhusu hiyo ‘mihrass’ kilikuwa hakina mantiki. 301 ‘Mihrass’ ni jiwe moja kubwa lililokuwa na shimo lililojazwa maji kwa ajili ya kuoga. Lilikuwa ni zito sana. 302 Ilisimuliwa na Ahmad Amiin katika kitabu chake Fajrul Islam, uk. 259. 303 Rejea Sahih Muslim, Jz. 1, uk. 625. 204


Abu huraira check Lubumba.qxd

7/1/2011

10:49 AM

Page 205

Abu Huraira Umar pia alimshutumu kwa hilo, katika Hadith iliyosimuliwa na Muslim.304 Ibn Umar hakuiamini riwaya ya Abu Huraira juu ya nungunungu na bado aliendelea kuitilia mashaka kuhusu Hadith hiyo. Ibn Umar alimsikia Abu Huraira akisimulia: “Yeyote aliyefuatilia mazishi, huyo atapata karati moja ya tendo jema,” yeye hakumuamini, na akasema kwamba Abu Huraira alikuwa amekithiri kwa Hadith zake. Alimtuma mtu mmoja kwa Aisha akamuuliza kuhusu riwaya hiyo. Pale Aisha alipoithibitisha riwaya hiyo ndipo yeye akaiamini.305 Wakati Aamir bin Shurayh bin Hani aliposikia Abu Huraira akisimulia: “Yeyote anayependa kukutana na Mwenyezi Mungu swt. Mwenyezi Mungu anapenda kukutana naye na yoyote anayechukia kukutana na Mwenyezi Mungu, na Mwenyezi Mungu naye huchukia kukutana naye,” yeye hakumuamini mpaka alipomuuliza Aisha. Aisha aliisimulia na kumtolea maelezo juu yake.306 Kama tungetaja mambo yote, ambayo masahaba walikanusha riwaya za Abu Huraira na kuzithibitisha kwamba ni za uongo, tungekuwa tunapoteza wakati wetu bure, lakini hayo yangetosha kuthibitisha yale tuliyotaka kuyasema. Ilitosha kwamba Umar, Uthman, Ali na Aisha walizikataa na kuzikanusha Hadith zake. Iliamuliwa na sharia ya Kiislamu kupenda kushutumu (sahaba) kuliko kuhalalisha kile alichoshutumiwa nacho panapokuwa na upinzani. Lakini katika suala hili hapakuwa na upinzani hata kidogo kwa sababu hisia peke yake hazikupinga ukanushaji wa wale watu mashuhuri. 304 Sahih Muslim, Jz. 1, uk. 626. 305 Sahih Muslim, Jz. 1, uk. 349; al-Hakiim katika Mustadrak, Jz. 3, uk. 510 amesimulia kitu kama hicho. 306 Sahih Muslim, Jz. 2, uk. 422 205


Abu huraira check Lubumba.qxd

7/1/2011

10:49 AM

Page 206

Abu Huraira Na kuhusu kuwachukulia masahaba wote kama waaminifu na wema, hapakuwa na ushahidi wa kulithibitisha hilo. Hao masahaba wenyewe hawakujua lolote kuhusu jambo hilo. Kama tukichukulia hivyo, itatumika kwa wale wasiojulikana na sio kwa yule ambaye Umar, Uthman, Ali na Aisha walimuona kama muongo na kuwa na mapungufu mengi ambayo yalithibitishwa kwa ushahidi mwingi tu. Sisi, Mashia tuna fikra ya wastani kuhusu masahaba, ambayo tunaieleza kwa kina katika kitabu chetu “Answers of Musa Jarallah.” Yoyote anayetaka kujua kuhusu hilo naarejee kwenye kitabu hicho.

MALALAMIKO YAKE DHIDI YA WANAOMSHUTUMU Abu Huraira alilalamika dhidi ya wale ambao walimshutumu yeye kwa kupindukia kwake katika kusimulia Hadith kwa kusema: “Wanasema kwamba Abu Huraira anasimulia Hadith nyingi mno! Mwenyezi Mungu ndiye hakimu wetu katika Siku ya Kiyama! Wanasema kwa nini Muhajirina na Ansari hawasimulii (Hadith za Mtume) kwa wingi kama yeye anavyofanya. Ndugu zangu Muhajirina walikuwa wameshikwa na mishughuliko ya sokoni na ndugu zangu Ansari walikuwa wakishughulika katika mabustani yao (ya mitende), ambapo mimi nilikuwa masikini niliyejiweka karibu na Mtume kwa ajili ya kula. Hivyo nilikuwa mhudhuriaji wakati wao walikuwa hawapo na mimi nilifahamu ambapo wao walisahau.” Wakati mmoja Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisema: “Kama mmoja wenu atasambaza nguo yake mpaka nitakapomaliza hotuba yangu, kisha akaikusanya kifuani mwake, yeye hatasahau kamwe kitu chochote katika maneno yangu. Mimi nilikusanya nguo yangu, ambayo nilikuwa sina nyingine zaidi ya hiyo (mwilini) mpaka Mtukufu Mtume alipomaliza hotuba yake, kisha nikaikusanya kifuani mwangu. Naapa kwa Yule ambaye amemtuma 206


Abu huraira check Lubumba.qxd

7/1/2011

10:49 AM

Page 207

Abu Huraira Mtume wake kwa haki kwamba kamwe sikusahau chochote kati ya maneno yake hadi leo. Wallahi isipokuwa tu kwamba kuna aya mbili ndani ya Qur’ani:

“Hakika wale wanaoficha tuliyoyateremsha katika dalili zilizo wazi na muongozo, baada ya sisi kuzibainisha kwa watu Kitabuni, hao hulaaniwa na Mwenyezi Mungu na hulaaniwa na wenye kulaani. Ila wale waliotubu na kusahihisha na kuweka wazi, basi hao nitawakubalia, na Mimi ni Mwelekevu sana, Mwenye kurehemu.” (2:159-160), zilikuwamo ndani ya Qur’ani, vinginevyo mimi nisingewaambieni kitu chochote kamwe.” Kwa vyovyote Abu Huraira alivyokuwa tajiri zaidi, alizidi kuwa mjinga.307 Yeye alitaka kuwaridhisha washutumu wake, ambao walimshutumu kwa idadi yake kubwa na ubora wa Hadith zake, hivyo alisimulia Hadith hii ili kujitetea mwenyewe na kulalamika dhidi yao, lakini ni utetezi wa kipuuzi kiasi gani alioufanya! Kwa kweli yeye, bila kutambua, aliwapa wapinzani wake ushahidi dhidi yake mwenyewe, ambao ulithibitisha kwamba kile walichomhusisha nacho kilikuwa ni cha kweli. Naapa kwa heshima ya ukweli na ya wasema kweli kwamba sijaona miongoni mwa yote yale ambayo wabunifu wamekifanya, Hadith baridi zaidi au iliyo mbali zaidi na ukweli kuliko hii. Nisingetaja wala kuzungumzia kuhusu 307 Methali. 207


Abu huraira check Lubumba.qxd

7/1/2011

10:49 AM

Page 208

Abu Huraira Hadith hii isipokuwa kwa vile masheikh hawa wawili na wengine kama wao wameitaja kwenye Sahih zao kwa furaha kabisa na kiibada kabisa kwenye mawazo yao kuhusu masahaba. Kwa hilo walipinga ule ushahidi wa kiakili na kidesturi na wamepinga mawazo na fikra za Waislam wa awali mashuhuri kabisa. Tunayo maelezo kiasi kuhusu ubatili wa riwaya hii: Kwanza: Abu Huraira alisingizia kwamba Muhajirina walikuwa mbali na Mtume (s.a.w.w.) kwa sababu walikuwa wakishughulika kufanya biashara masokoni na Ansari walikuwa wakifanya kazi katika mabustani yao. Aliwasukuma Waislamu wote wa mwanzoni wa Muhajirina na Ansari kwa fimbo moja. Kulikuwa na thamani yoyote kwa ajili ya kusema kwake Muhajirina wote walikuwa mashughuli na biashara masokoni baada ya maneno ya Mwenyezi Mungu: “Watu ambao haiwashughulishi biashara wala kuuza katika kumkumbuka Mwenyezi Mungu …..” (24:37). Kile kilichopingana na Qur’ani kilistahili chochote mbali na kutupiliwa mbali? Na Abu Huraira alikuwa ni nani kuwa mhudhuriaji wakati masahaba wa karibu kabisa na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) walikuwa mbali naye? Na ni nini alichokihifadhi ambapo wao wamekisahau? Alilisema hilo kwa mwezi mzima bila ya aibu au woga kwani aliyasema hayo kwenye kipindi cha wakati wa Mu’awiyah, ambapo kulikuwa hakuna Umar, Uthman, Ali, Talha, az-Zubair, Salman, Ammar, al-Miqdadi, Abu Dharr au wengine kama hao. “….. ni neno kubwa litokalo katika vinywa vyao, hawasemi ila uongo tu.” (18:5). Neno lake lilikuwa mbali na ukweli kiasi gani! Watu wote walikuwa wanaijua nafasi ya Ali kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), udugu wa karibu na heshima maalum. Alimuweka mapajani mwake wakati alipokuwa mtoto mdogo, alimkumbatia kifuani mwake, nyama yake safi halisi iligusana na nyama yake Ali, alivuta harufu ya manukato yake, Mtume alitafuna na kumuwekea mdomoni kwake. Hakuwahi kamwe kumpata na uongo wowote katika maneno yake wala kosa katika vitendo vyake. Mwenyezi Mungu alimuunganisha kwa Mtume (s.a.w.w.) mkuu wa malaika Zake wote tangu alipoacha kunyonya ili amuongoze katika uungwana na maadili ya hali ya 208


Abu huraira check Lubumba.qxd

7/1/2011

10:49 AM

Page 209

Abu Huraira juu ya ulimwengu huu. Ali alimfuata Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kama mtoto wa ngamia anayenyonya anavyomfuata mama yake. Mtume alipandisha bendera ya maadili kwa ajili ya Ali (a.s.) kila siku. Alimuamuru Ali kumuigiza yeye. Ali alikuwa na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) pamoja na Khadijatul-Kubra, mkewe Mtume kwenye pango la Hirra’ wakiiona nuru ya Jibril na ujumbe wake na kuvuta harufu ya manukato ya utume. Baada ya hapo alikuja kuwa lango la mji wa elimu ya Mtume, hakimu bora wa umma, hifadhi ya siri za Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na mlinzi wake, mrithi wa utawala wake, muondoaji wa huzuni zake, adhimu zaidi kati ya masahaba zake na aliyekuwa na elimu ya Kitabu. Baada ya yote hayo, hivi Ali alisahau katika Sunna kile ambacho Abu Huraira alikihifadhi, au aliweka siri kile Abu Huraira alichokitangaza? “….. utukufu ni Wako, huu ni uongo mkubwa.” (24:16) Kwa kweli ni wachache tu kati ya Muhajirin waliokuwa wakishughulika katika masoko. Kwa nini wale ambao hawakuwa na shughuli yoyote na biashara au uuzaji kama vile Abu Dharr, al-Miqdad, Ammar, na wale sabini wenzake Abu Huraira katika makazi ya suffa, ambao walikuwa hawana nguo za kufunika miili yao isipokuwa kipande cha nguo kilichofungwa kwenye shingo zao ….. kama yeye mwenyewe alivyowaelezea, wote hao wasisimulie Hadith nyingi sana kama yeye? Kwa kweli jumla ya Hadith zao zote zilikuwa ni chache kuliko zake. Vivyo hivyo kwa Ansari. Sio kwamba wote walikuwa na mabustani na rasilimali kama Abu Huraira alivyosingizia. Mmoja wa hao, ambaye hakuwa na milki yoyote alikuwa ni Salman Farsi, ambaye Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kuhusu yeye alisema: “Salman ni mmoja wetu, sisi watu wa familia ya Mtume.” Yeye vilevile alisema: “Kama dini ingekuwa kwenye kilimia (thurea), Salman angeweza kuipata.” Aisha alisema: “Salman alikuwa na mkutano na Mtume (s.a.w.w.) kila usiku ambao alikaa naye zaidi kuliko tulivyokaa sisi.” Ali (a.s.) alisema: “Salman al-Farsi alikuwa ni kama yule bwana wa hekima Luqman. Yeye alikuwa amezifahamu elimu za zama za mwanzoni na zijazo. Yeye ni bahari ya elimu ambayo 209


Abu huraira check Lubumba.qxd

7/1/2011

10:49 AM

Page 210

Abu Huraira haitafifia kamwe.” Ka’bul Ahbar alisema: “Salman amejazwa na elimu na hekima.” Hii ilikuwa ni mbali na sifa nyingine zilizotajwa kuhusu yeye. Watu walijua vema kwamba Abuu Ayyub al-Ansari aliishi kwa riziki ambayo hakuna chochote kilichomtoa kwenye elimu na ibada. Kadhalika kwa akina Abu Sa’iid al-Khudri, Abu Fudhala al-Ansari na mafaqihi wengine mashuhuri wa ki-Ansari. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) hakutumia muda wake katika vurugu na ghasia. Alipanga nyakati zake, mchana na usiku kulingana na kazi iliyotakikana kwa wakati huo. Ni dhahiri kwamba aliweka wakati maalum kwa ajili ya kuhutubia na kufundisha Waislamu kuhusu dini yao na maisha, ambako kusingepingana kamwe na nyakati zao za kazi au shughuli masokoni. Muhajirina na Ansari walishikamana na hadhara hizi za heshima na Mtukufu Mtume na walikuwa makini zaidi katika kujua na kujifunza kuliko hawa mapunguani walivyoropoka. Pili: Kama kile Abu Huraira alichosingizia kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alikuwa amewaambia masahaba zake: “Kama yoyote kati yenu atatandaza nguo yake mpaka nitakapomaliza hotuba yangu na kisha akaikusanya kifuani mwake, huyo kamwe hatakuja kusahau chochote kati ya maneno yangu hata kidogo” kilikuwa ni kweli, masahaba wote wangeshindana katika kufanya hivyo. Wangepata wema mkubwa bila ya kujitahidi na kupata elimu ya milele bila ya kutumia pesa. Sasa ni kipi kilichowazuia kujishindia hilo na ni nini kilichowakwamisha katika kutandaza nguo zao kwa ajili ya hilo? Ni vipi wangeipoteza fursa kubwa kama hiyo? Hivi walikuwa ni wapuuzi kiasi hicho kuweza kukataa kile ambacho Mtume (s.a.w.w.) aliwakaribisha kwacho? Kwa kweli ni hapana! Wao walikuwa ni masahaba zake waaminifu, ambao walijitahidi katika kumtii yeye katika kila alichokisema. Tatu: Kama yale aliyoyasema Abu Huraira yalikuwa ni kweli, masahaba wangejutia sana kile walichokipoteza cha wema mkubwa na elimu nyingi

210


Abu huraira check Lubumba.qxd

7/1/2011

10:49 AM

Page 211

Abu Huraira kupita kiasi. Masikitiko yao makubwa kuhusu kile walichokikosa kwa kutotandaza nguo zao mbele ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), ambacho kilikuwa hakina gharama wala kuchokesha, yangeenea miongoni mwa watu na kusimuliwa katika vitabu na kwamba wangelaumiana wenyewe kwa wenyewe kuhusu uchaguzi wao mbaya katika kuacha jambo muhimu kama hilo. Angalau kwa kiasi fulani wangemuonea wivu Abu Huraira, ambaye alikuwa na nguo moja tu ambapo wao walivaa nguo mbili au tatu, yeye akajipatia wema huo peke yake. Hapakuwa na chochote cha namna hiyo hata kidogo. Abu Huraira alikuwa ameichomoa Hadith hiyo kutoka kwenye mkoba wake mwenyewe. Nne: Kama yale aliyoyasema Abu Huraira yalikuwa ni kweli, yangesimuliwa na masahaba wengine ambao Mtume (s.a.w.w.) aliwakaribisha kwa ajili ya jambo hilo, kwa kweli kama ilikuwa hivyo, masahaba hao wangeichukulia kama ni dalili mojawapo ya utume na kama ushahidi wa dini yenyewe. Ingekuwa maarufu kama jua la mchana. Ilielekea kwamba jua la Abu Huraira liliwaka usiku wa manane wakati watu walipokuwa wamelala, kwa hiyo hakuna mwingine zaidi ya yeye aliyesimulia hilo! Tano: Kulikuwa na tofauti nyingi katika riwaya zake kuhusu kadhia hii. Wakati mmoja alisema kama ilivyosimuliwa na al-A’raj:308 “Siku moja Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisema kuwaambia masahaba zake: “Kama yeyote kati yenu atatandaza nguo yake mpaka nitakaapomaliza hotuba yangu na kisha akaikusanya kifuani mwake, kamwe huyo hatasahau cho308 Rejea Sahih al-Bukhari, Jz. 2, uk. 34; na Sahih Muslim, Jz. 2, uk. 375. AlBukri amesimulia katika Sahih yake Jz. 2, uk. 1 riwaya kutoka kwa Sa’id bin alMusayyab kutoka kwa Abu Salama kwamba Abu Huraira alisema: “Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisema katika moja ya Hadith zake: “Hakuna mmoja kati yenu atakayetandaza nguo yake mpaka nimalize hotuba yangu kisha aikusanye kifuani mwake isipokuwa atayatambua yote nitakayoyasema.” Nilitandaza nguo yangu niliyokuwa nimevaa mpaka akamaliza hotuba yake. Kisha nikaikusanya kifuani mwangu. Sikusahau kamwe kitu chochote kati ya hotuba yake ile.” 211


Abu huraira check Lubumba.qxd

7/1/2011

10:49 AM

Page 212

Abu Huraira chote kati ya hotuba yangu.” Mimi nilitandaza nguo yangu, ambayo nilikuwa sina nyingine mwilini zaidi ya hiyo, mpaka Mtume akamaliza hotuba yake. Nikaikusanya kifuani mwangu. Naapa kwa Yule ambaye alimtuma Mtume kwa haki kwamba kamwe sikusahau chochote kati ya hotuba ile ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Wakati mwingine yeye alisema, kama ilivyosimuliwa na al-Maqbari:309 “Nikasema: ‘Ewe Mjumbe wa Allah, mimi wakati mwingine husahau yale ninayoyasikia kutoka kwako.’ Yeye akasema: ‘Tandaza nguo yako!’ Alichota kwa mikono yake elimu na akaiweka kwenye nguo yangu kisha akasema: ‘Ikusanye kifuani mwako.” Nikafanya hivyo. Sikusahau chochote baada ya hapo hata kidogo.’” Unaona kwamba Hadithi hiyo kwa mujibu wa riwaya ya kwanza iliyosimuliwa na al-A’raj ilikuwa ni baina ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na masahaba zake, na kwamba alikuwa ni Mtume aliyewaambia watandaze nguo zao akiwahofia wao kutokana na kusahau, ambapo kulingana na riwaya ya pili iliyosimuliwa na al-Maqbari ilikuwa ni kati ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na Abu Huraira tu basi, na kwamba Abu Huraira alimuomba Mtume huku akilalamikia kusahau kwake. Riwaya ya kwanza iliyosimuliwa na al-A’raj ilikuwa ikionyesha kwamba (bila kusahau) ilihusu ile hotuba ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) katika ule muda maalum tu kwani alisema (yale maneno ya Mtume), ambapo katika riwaya ya pili iliyosimuliwa na al-Maqbari, yeye aliifanya ya jumlajumla. Hiyo ilikuwa ni kusema kwamba yeye asingesahau chochote hata kidogo. Alisema: “Sikuwahi kamwe kusahau chochote baada ya hapo hata kidogo.” Wale ambao waliielezea Hadith hii walichanganyikiwa na hawakujua jinsi ya kuihalalisha hiyo mpaka ibn Hajar akaamua katika kitabu chake 309 Rejea kwenye Sahih al-Bukhari, Jz. 1, uk. 24 212


Abu huraira check Lubumba.qxd

7/1/2011

10:49 AM

Page 213

Abu Huraira kwamba suala hili lilitokea mara mbili;310 mara moja ile bila kusahau ilihusu yale maongezi maalum ya Mtume (s.a.w.w.), na ile bila kusahau nyingine ilihusu wote, ima Hadith zile zilizotangulia au zijazo za Mtukufu Mtume (s.a.w.w.).311 Muslim ameisimulia katika njia ya tatu kutoka kwa Yunus, kutoka kwa ibnul-Musayyab kwamba Abu Huraira alisema: “….. Mimi sikusahau kamwe, baada ya siku ile, chochote kile ambacho Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alichoniambia.” Riwaya hii ni ya jumla zaidi kuliko ile ya alA’raj na ya kufaa zaidi kwa hilo kuliko ile riwaya ya Maqbari. Ibn Sa’d katika Tabaqat yake amesimulia Hadith kutoka kwa Amr bin Mardas bin Abdur-Rahman al-Jundi kwamba Abu Huraira alisema: “Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) aliniambia nitandaze nguo yangu. Mimi nikafanya hivyo. Yeye alinizungumza kutwa nzima. Kisha nikaikusanya nguo yangu kifuani mwangu. Sikusahau kitu chochote kati ya yale aliyoniambia.” Kule kusema kwake kutwa nzima hakukutajwa katika riwaya zile nyingine zote isipokuwa katika hii moja iliyosimuliwa na al-Jundi. Abu Ya’la ameisimulia kutoka kwa Abu Salama katika njia tofauti kabisa na njia zote za Hadith hii. Alisimulia kwamba Abu Huraira alikuwa amekwenda kumtembelea Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) wakati alipokuwa mgonjwa. Alimsalimia Mtume, wakati yeye Mtume akiwa ameegemea kwenye kifua cha Ali (a.s.) na mkono wa Ali ukiwa juu ya kifua cha Mtume (s.a.w.w.) akimkumbatia na miguu ya Mtume ikiwa imenyooshwa. Mtume (s.a.w.w.) akamwambia: “Oh, Abu Huraira, sogea karibu yangu.” Yeye akasogea. Kisha Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akamwambia: “Nisogelee.” Akasogea. Kisha akamwambia: “Nisogelee.” Alisogea mpaka 310 Rejea kwenye Irshad as-Sari ya Qastalani, Jz. 1, uk. 380 311 Kama suala hili lilitokea mara moja badala ya mara mbili, ingeenea kama mwanga. Sasa kwa nini masahaba wasiichukulie kwa makini kiasi kwamba hakuna hata mmoja wao aliyeisimulia isipokuwa Abu Huraira? 213


Abu huraira check Lubumba.qxd

7/1/2011

10:49 AM

Page 214

Abu Huraira vidole vyake vikagusana na vidole vya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Mtume akamwambia akae chini. Yeye akakaa. Mtume akamwambia: “Nisogezee ncha ya nguo yako.” Abu Huraira akatandaza nguo yake na akaisogezea kwa Mtume. Mtume (s.a.w.w.) akamwambia: “Oh Abu Huraira, napendekeza kwako baadhi ya vitendo kwamba wewe si wa kuondoka madhali ungali hai, unapaswa kuoga kila asubuhi ya siku ya Ijumaa, usiongee ovyo, usifanye mchezo usio na maana, kufunga siku tatu kila mwezi kwa sababu ni sawa na kufunga kwa umri mzima, na swala ya al-Fajr, usiiache hiyo hata kama utaswali usiku mzima kwa sababu imejaa mema tele.” Mtume alisema hivyo mara tatu. Kisha akamwambia akusanye nguo yake kwake mwenyewe. Yeye aliikusanya nguo yake hiyo kifuani mwake.312 Abu Ya’la amesimulia kutoka kwa al-Waliid bin Jamii’ kwamba Abu Huraira alisema: “Nililalamika kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) juu ya udhaifu wa kuhifadhi kwangu. Yeye akaniambia: “Fungua nguo yako.” Mimi nikaifungua. Kisha akasema: “Ikusanye kifuani mwako.” Nikafanya hivyo. Baada ya hapo sikusahau Hadith yoyote kamwe.” Abu Ya’la amesimulia kutoka kwa Yunus bin Ubayd kutoka kwa al-Hasan al-Basri kwamba Abu Huraira alisema: “Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisema: “Nani atachukua neno moja au mawili au matatu, kisha ayafunge kwenye nguo yake ajifunze na kisha ayafundishe kwa wengine?” Mimi nikatandaza nguo yangu mbele yake wakati alipokuwa anaongea, kisha nikaikusanya. Nataraji kwamba sikusahau neno hata moja kati ya yale aliyokuwa ameyasema. Ahmad alisimulia Hadith, kiasi fulani kama ile iliyosimuliwa na alMubarak bin Fudhala kutoka kwa Abu Huraira. Abu Nu’aim amesimulia kutoka kwa Abdullah bin Abu Yahya kutoka kwa Sa’id bin Abu Hind kutoka kwa Abu Huraira kwamba Mtukufu Mtume 312 Rejea kitabu cha ibn Hajar, al-Issaba, (wasifu wa Abu Huraira). 214


Abu huraira check Lubumba.qxd

7/1/2011

10:49 AM

Page 215

Abu Huraira (s.a.w.w.) alimwambia: Oh Abu Huraira, huniulizi kuhusu neema, ambazo wenzako wananiuliza kuzihusu hizo!” Mimi nikasema: “Nakuomba unifundishe kile ambacho Mwenyezi Mungu amekufundisha wewe.” Nilivua nguo yangu na nikaitandaza kati yangu na yeye. Chawa walikuwa wanatambaa juu ya nguo hiyo. Yeye alinizungumzia mpaka nikaielewa hotuba yake. Aliniambia: “Ikusanye kwako.” Baada ya hapo sikusahau hata herufi kutoka katika yale aliyokuwa ameniambia.” Yeyote aliyeichunguza Hadith hii katika njia zake tofauti za usimuliaji angeweza kuiona iko tofauti katika maneno ya maana zake. Maneno yake au maana zilikuwa tofauti na zilipingana, kwani kwa hakika Hadith yenyewe ilikuwa ovyo ovyo tu. Shukurani ziwe kwa Mwenyezi Mungu kwa ajili ya hilo. Sita: Yeye alisema: “Nilitandaza nguo yangu, ambayo nilikuwa sina nyingine zaidi ya hiyo mwilini mwangu.” Hii ilionyesha kwamba sehemu zake za siri zingeweza kutokeza. Al-Qastalani na Zakariyya al-Ansari waliitafsiri Hadith yake ili kutafuta udhuru kwa ajili yake. Wao walisema kwamba yeye alitandaza sehemu ya nguo yake ili sehemu zake za siri zisionekane. Saba: Simulizi hii ilionekana kama hekaya za uongo. Utukufu uwe kwa Mwenyezi Mungu! Asingeweza kuacha upayukaji huu uchanganyike na miujiza ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Hakuna hata mmoja kati ya watu wa hekima na busara ambaye angeamini ujinga huu. Miujiza ya Mtume (s.a.w.w.) iliwapumbaza watu wenye akili sana na iliwashinda madhalimu kwa utaratibu mzuri na njia ya wastani ya miujiza hiyo. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) aligongagonga kwenye kifua cha Ali na akasema, wakati alipomtuma kwenda Yemen kama hakimu: “O Allah, muongozee moyo wake na muelekezee ulimi wake.” Ali (a.s.) akasema: “Naapa Wallahi kwamba kwa hakika sikuwahi kusita kamwe katika hukumu niliyotoa baina ya watu wawili wowote wale baada ya hapo.” 215


Abu huraira check Lubumba.qxd

7/1/2011

10:49 AM

Page 216

Abu Huraira Wakati ile aya ya Qur’ani tukufu: “Ili tuifanye ni ukumbusho kwenu, na sikio lisikialo lipate kusikia.” (69:12) iliposhuka kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), yeye alisema kumwambia Ali (a.s.): “Nilimuomba Mwenyezi Mungu alifanye kuwa ni sikio lako.”313 Ali (a.s.) alisema: “Sikuwahi kusahau chochote kile baada ya hilo, ingawaje nilikuwa sijasahau kabla ya hapo.” Mtukufu Mtume (s.a.w.w.)314 amesema katika siku ya (vita vya) Khaybar wakati alipokabidhi bendera kwa Ali: “Eh, Mwenyezi Mungu, mlinde na umuokoe kutokana na joto na baridi.” Ali amesema: “Baada ya hayo sikuteseka kwa joto wala baridi.” Yeye alivaa nguo nyepesi wakati wa baridi ya kipupwe na nguo nzito wakati wa kiangazi kuthibitisha hilo na kuvuta nadhari ya mara kwa mara kwenye miujiza ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Wakati Jabir alipolalamika kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kwamba baba yake alikuwa anadaiwa, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alikwenda pamoja naye hadi kwenye uga wake wa kupuria nafaka. Alitembea kuzunguka ule mrundikano wa matunda na akamuomba Mwenyezi Mungu neema zake. Akakaa karibu nao. Wale wakopeshaji wakaja na wakachukua madeni yao kutoka kwenye mrundikano huo. Kile kilichobakia katika rundo hilo kilimtosheleza Jabir na familia yake! Wakati Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alipotaka kumfanyia mtu hisani, alimuomba Mwenyezi Mungu kwa ajili yake na alipotaka kumdhuru mtu (ambaye amestahili hilo) alimuomba Mwenyezi Mungu dhidi yake kama alivyofanya kwa Mu’awiyah. Alisema: “Ewe Mwenyezi Mungu, usilijaalie kushiba tumbo lake!” Na vivyo hivyo alifanya kwa al-Hakam bin Abul-Aass. Lakini hakuna mtu aliyethubutu kusema kwamba Mtume alifanya kitu chochote katika hayo ambayo Abu 313 Imesimuliwa na az-Zamakhshari katika kitabu chake, Kashshaf; na athTha’labi katika Tafsiir yake na ar-Razi na wengineo. 314 Ilisimuliwa na Ahmad bin Hanbal katika Musnad yake, ibn Abu Shayba na ibn Jariij. Rejea kwenye Muntakhab Kanzul Ummal, Jz. 5, uk. 44. 216


Abu huraira check Lubumba.qxd

7/1/2011

10:49 AM

Page 217

Abu Huraira Huraira aliyoeleza. Kwa sababu hekima yake, ambayo ilimulika na kuangaza njia kwa ajili ya macho yaliyopotoka na akasafisha njia hiyo kwa alama za muongozo ilikuwa mbali sana juu ya hilo.

KUZITUPIA MACHO SIFA ZAKE Tulizifuatilia Hadith zake zinazozungumzia juu ya sifa za Abu Huraira na tumegundua kwamba chanzo pekee cha Hadithi hizo, katika kila hali, kilikuwa ni Abu Huraira mwenyewe. Ibn Abdul Birr amesema katika kitabu chake, al-Issti’ab: “Abu Huraira alisilimu na kuwa Mwislam katika mwaka wa vita vya Khaybar. Alishiriki katika vita hivyo pamoja na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Kisha akaambatana na Mtume (s.a.w.w.) akitafuta elimu. Aliridhika kwa kutokuwa na kingine chochote isipokuwa chakula chake. Mkono wake ulikuwa mkononi mwa Mtume (s.a.w.w.). Alikwenda pamoja naye popote pale alipokwenda. Alikuwa wa mbele kabisa miongoni mwa masahaba katika kuhifadhi Hadith za Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Alihudhuria na Mtukufu Mtume yale ambayo Muhajirina na Ansari hawakuyahudhuria kwa sababu hao Muhajirina walikuwa wakishughulika na biashara na Ansari walishughulika katika kufanya kazi kwenye mabustani yao. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alishuhudia kwamba Abu Huraira aliweka umakini sana kwenye elimu na Hadith. Wakati mmoja alimwambia Mtume (s.a.w.w.): “Ninasikia mengi kutoka kwako na ninahofia kwamba huenda nikasahau baadhi yake.” Mtukufu Mtume akamwambia atandaze nguo yake. Yeye akafanya hivyo. Mtume akamwaga kwa wingi (!) kwenye nguo yake na akamwambia aikusanye kwenye kifua chake. Abu Huraira amesema: “Niliikusanya kwangu. Kamwe sikusahau kitu chochote baada ya hapo hata kidogo.” Sifa hizi zilinakiliwa kutoka kwenye riwaya za Abu Huraira mwenyewe, ambamo aliongea kuhusu yeye mwenyewe. Hatukupata chanzo kingine 217


Abu huraira check Lubumba.qxd

7/1/2011

10:49 AM

Page 218

Abu Huraira cha sifa hizi mbali na Abu Huraira mwenyewe. Kadhalika hivyo ndivyo ilivyokuwa kwa sifa nyingine zilizomwaga juu yake bila kustahili. Kuwa kwake Mwislamu katika mwaka wa Khaybar kulikuwa ni kweli kwa sababu hilo lilisimuliwa na wengine zaidi ya yeye mwenyewe, lakini kwamba aliwahi kushiriki katika vita hivyo pamoja na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) hilo halikusimuliwa na mwingine yoyote isipokuwa yeye mwenyewe. Na kuhusu aliyoyasema kwamba aliambatana sana na Mtukufu Mtume kwa ajili ya elimu na kusoma sio kwa chochote zaidi ya kushibisha tumbo lake, kwamba mkono wake ulikuwa mkononi mwa Mtume (s.a.w.w.) na kwamba alikwenda naye popote alipokwenda Mtume (s.a.w.w.), mambo yote haya yalisingiziwa na yeye mwenyewe pale aliposema: “Nilifika Madina wakati Mtume akiwa yuko Khaybar. Nilikuwa na umri wa zaidi ya miaka sitini wakati huo. Nilijiambatanisha naye hadi alipofariki. Nilikwenda naye kwenye nyumba za wake zake.315 Nilimtumikia, nimepigana pamoja naye na nilikwenda Hijja316 pamoja naye. Mimi nilikuwa ndiye mtambuzi zaidi wa Hadith zake. Wallahi baadhi ya masahaba ambao walikuwa na Mtukufu Mtume kwa muda mrefu kabla yangu waliniuliza mimi kuhusu Hadith zake kwani walijua nilivyokaa karibu naye. Miongoni mwao alikuwemo Umar, Uthman, Ali, Talha, az-Zubayr …..” Wenye akili wataweza kushangaa kuthubutu kwa mtu huyu kusimulia Hadith kama hizo, ambazo zilikuwa sio sahihi wala sio za kweli. Lakini wakati walipojua ukweli kwamba hakusimulia Hadith hizi na nyingine kama hizo wakati 315 Je, maadili ya hali ya juu ya Mtume huyu mashuhuri yaliruhusu hivyo, na kwa hiyo akachanganyika na wake zake kirahisi hivyo kama alivyosema fidhuli huyu? 316 Kwa Kiarabu, kitenzi saidizi alichotumia kilikuwa na maana ya mfululizo, ambacho kilimaanisha kwamba alikuwa akienda hija na Mtume (s.a.w.w.) kila mwaka. Ulikuwa ni uongo wa dhahiri kwa sababu baada ya hijra Mtume hakufanya hija isipokuwa mara moja tu, ambayo ilikuwa ni ile hija ya muago. 218


Abu huraira check Lubumba.qxd

7/1/2011

10:49 AM

Page 219

Abu Huraira wa masahaba wakubwa bali alithubutu kuzisimulia wakati baada ya wengi wa masahaba hao kuwa wamekwisha kufariki na nchi za Sham, Iraq, Afrika na Uajemi zilikuwa zimetekwa na huko masahaba wakawa wamesambaa hapa na pale, na kwamba wale Waislamu wapya wa zile nchi zilizotekwa walikuwa hawajui chochote kuhusu nini kilichotokea wakati wa uhai wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), walimpuuza. Basi yeye pamoja na waongo wengine walijikuta wakiwa katika dunia nyingine ambayo ilikuwa haijui chochote kuhusu zama za mwanzo za Uislamu. Walikuta kwamba dunia yao mpya iliwaamini na waliwasikiliza kwa heshima kuu kwani walikuwa ni kumbukumbu ya masahaba wa Mtume, ambao waliaminishwa na Sunna na kwamba walipaswa kuitangaza. Zaidi ya hayo, dola ya Bani Umayyah ilifanya kila ililoweza vizuri kabisa kuwaunga mkono na kuwasaidia. Hivyo walikuwa na fursa kubwa sana ya kusema kila walichotaka cha maajabu na viroja, ambavyo vilikuwa havikubiliki kisharia na kiakili. Walisimulia Hadith za kipumbavu na za ovyo kwa ajili ya manufaa yao na kutumikia sera ya madikteta madhalimu, ambao waliitumia dini ya Mwenyezi Mungu kama njia ya kutekelezea malengo yao binafsi na waliwafanya watu kama watumwa wao. Waligawana mali ya Waislamu miongoni mwao wenyewe kana kwamba ilikuwa ni urithi wao. Waongo wale walijitolea kwa waonevu wasio na haki ambao, kwa kufidia hilo, waliwazawadia kwa njia zote za starehe na walijaribu wawezavyo kuwasaidia hususan katika zama za Mu’awiyah. Wale waongo walikuwa ndio wasaidizi wao wakuu, wasemaji na wapelelezi wa dola ya Umayyah: “Basi adhabu itawathibitikia wale wanaoandika kitabu kwa mikono yao, kisha wakasema: Hiki kimetoka kwa Mwenyezi Mungu …..” (2:79). Nashangaa Wallahi kwa al-Bukhari, Muslim, Ahmad na wengineo, ambao walikuwa na busara na utaalamu mkubwa, kuongozwa kijinga kabisa na kile ambacho Abu Huraira na waongo wenzie walikiropoka. Je wanaweza wakajua ni lini Ali, Umar, Uthman, Talha, az-Zubayr na hao wengine kwamba ni lini walimuuliza Abu Huraira? Je, walimuuliza katika hali 219


Abu huraira check Lubumba.qxd

7/1/2011

10:49 AM

Page 220

Abu Huraira wakiwa macho kabisa au katika usingizi au katika ulimwengu wa zahania? Je, walimuuliza kuhusu Hadith zipi? Ni nani aliyehadithia hivyo isipokuwa Abu Huraira mwenyewe? Ni yupi miongoni mwa wanahistoria au waandishi wa vitabu vya Hadith au vya wasifu ambaye amesema kwamba hawa masahaba wakubwa wamesimulia hata riwaya moja tu317 kutoka kwa Abu Huraira? Ni lini wao walizijali riwaya zake? Sisi hatukuona kwamba yeye aliwahi kusimulia Hadith yoyote mbele yao. Wala hakuthubutu kufanya hivyo. Mara nyingi wao walimuacha na kuzikanusha riwaya zake kama ilivyoelezwa katika kurasa zilizotangulia. Sasa hebu turudi nyuma kwenye kile Abdul Birr alichokisema kuhusu Abu Huraira. Kusema kwake kwamba “Abu Huraira alikuwa ndiye mbora kati ya masahaba katika kuhifadhi Hadith za Mtukufu Mtume” kilinakiliwa kutoka kwenye riwaya ya Abu Huraira, ambamo alisema: “Mimi nilikuwa mtambuzi zaidi wa Hadith zake.” Kusema kwake kwamba “alihudhuria mikutano ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), ambayo Muhajirina na Ansari hawakuhudhuria” kulikaririwa kutoka kwenye riwaya ya Abu Huraira ambamo alikuwa amezungumzia kuhusu kutandaza nguo yake mbele ya Mtukufu Mtume kama tulivyotangulia kusema kabla, pamoja na maelezo yetu. Kusema kwake kwamba “Mtume alishuhudia kwamba yeye alizingatia kwa makini sana kwenye elimu na Hadith” kulinukuliwa toka kwa Abu Huraira akisema: “Nilisema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, ni yupi 317 Al-Hakiim, katika wasifu wa Abu Huraira, aliwahesabu wale ambao walisimulia Hadith kutoka kwa Abu Huraira. Walikuwa ni masahaba ishirini na nane, Ali, Umar, Utuman, Talha na az-Zubayr walikuwa hawamo miongoni mwao. Hao wengine waliosimulia kutoka kwake, walisimulia mambo kuhusu Pepo na Jahannam au maadili na elimu. Hakuna hata mmoja kati yao aliyesimulia angalau hata riwaya moja kuhusu hukmu za kisheria na wajibat. 220


Abu huraira check Lubumba.qxd

7/1/2011

10:49 AM

Page 221

Abu Huraira mwenye furaha sana katika kupata uombezi wako? Yeye akasema: “Nilidhani kwamba hakuna atakayeniuliza juu ya jambo hili la thamani zaidi yako wewe nilipokuona ukitoa usikivu sana kwenye Hadith.318 Miongoni mwa sifa zake, ambazo wale walioandika juu ya wasifu wake wamezizungumizia kwa kirefu, ilikuwa ni lile shanta lake, ambalo kutoka humo alikuwa amekula zaidi ya wasaq319 mia mbili za tende, ile ya mtumwa wake aliyetoroka, ambaye alikuwa amemuacha huru kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, kuweka kwake vyombo viwili vya elimu ambavyo alieneza kimoja na kingine akakifanya siri, ile dua ya Mtukufu Mtume juu ya mama yake, kutembea kwake juu ya maji mpaka akaivuka ghuba bila ya kulowa, na nyingi ya riwaya zake za kuchekesha na za huzuni kwa wakati huohuo! Mwenyezi Mungu awe pamoja nasi katika kushuhudia yote hayo!

SHERE ZAKE ZA KUCHEKESHA Imam Ahmad bin Hanbal amesimulia320 Hadith kuhusu Abu Huraira kutoka kwa Muhammad bin Ziyad akisema: “Marwan, ambaye alikuwa Walii wa Madina wakati wa utawala wa Mu’awiyah, wakati mwingine alimteua Abu Huraira kuwa naibu wake wakati alipoondoka Madina. Abu Huraira aliipiga ardhi kwa miguu yake akisema: “Pisha njia! Pisha njia! Amiir amekuja.” Aliashiria kwake yeye mwenyewe. 318 Ilisimuliwa na al-Bukhari katika Sahih yake na Ibn Hajar katika al-Issaba ambapo Abu Huraira amesema: “Nilifuatana na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kwa miaka mitatu. Hakuna aliyekuwa bora zaidi yangu katika kuzielewa Hadith.” 319 Wasaq ilikuwa ni kipimo cha ujazo miongoni mwa Waarabu. Wasaq mia mbili zilikuwa ni takriban kilo elfu thelathi na tano. 320 Musnad Ahmad, Jz. 2, uk. 43.

221


Abu huraira check Lubumba.qxd

7/1/2011

10:49 AM

Page 222

Abu Huraira Ibn Qutayba ad-Daynuuri amesimulia katika kitabu chake, al-Ma’arif, uk. 94 kwamba Abu Rafi’i alisema: “Marwan wakati mwingine alimteua Abu Huraira kuwa Amiir wa Madina (wakati yeye mwenyewe aliposafiri). Alipanda kwenye punda mwenye matandiko mgongoni mwake na ufumwele wa mtende juu ya kichwa chake. Alipokutana na mtu yoyote, yeye alisema: “Safisha njia! Amiir amekuja.” Aliweza kupita wakati mwingine watoto wanacheza wakati wa usiku. Ghafla aliruka hadi kati miongoni mwao na kudunda dunda ardhi kwa miguu yake …..”321 Abu Na’iim amesimulia katika Hilyatul Awliya, Jz. 1, uk. 382 kwamba Tha’laba bin Abu Malik al-Qardhi alisema: “Siku moja Abu Huraira, ambaye alikuwa kwa wakati huo ndiye Amiir aliyeteuliwa na Marwan, alipita katikati ya soko akiwa amebeba mzigo wa kuni. Alisema: “Safisha njia kwa ajili ya Amiir, Oh ibn Abu Malik!” Mimi nikasema: “Hivi vinatosha.” Yeye akasema: “Safisha njia kwa ajili ya Amiir pamoja na mzigo juu yake.” Abu Na’iim vilevile amesimulia Hadith kutoka kwa Ahmad bin Hanbal kutoka kwa Uthman ash-Shahhan kwamba Farqad as-Sabkhi alisema: “Abu Huraira alikwenda kuzunguka Ka’ba akisema: “Ole kwa tumbo langu! Kama nikilishibisha litakinahi, na kama nikiliacha na njaa litaniaibisha.” Ilisimuliwa na Rabii-ul Abrar kwamba Abu Huraira alisema: “Oh Allah, nijaalie meno yenye kusaga, tumbo lenye kumeng’enya na njia ya nyuma yenye kutawanya.” Vile vile imesimuliwa na Rabii-ul Abrar kwamba Abu Huraira alipenda sana ‘madhiira’ (aina ya supu iliyopikwa pamoja na mtindi). Aliila pamoja na Mu’awiyah lakini wakati wa swala ulipowadia, yeye aliswali swala hiyo nyuma ya Imam Ali (a.s.). Alipoulizwa kuhusu hilo, yeye akasema: 321 Ilisimuliwa na ibn Sa’d katika Tabaqat Jz. 4, uk. 60. 222


Abu huraira check Lubumba.qxd

7/1/2011

10:49 AM

Page 223

Abu Huraira “Madhiira ya Mu’awiyah ilikuwa inanenepesha sana lakini swala nyuma ya Ali ilikuwa ni bora zaidi.” Hivyo alipachikwa jina la sheikh alMadhiira.322 Abu Uthman an-Nahdi alisema kwamba wakati mmoja Abu Huraira alikuwa katika safari pamoja na watu wengine. Walisimama kwa ajili ya mapumziko. Walipoandaa chakula, walimtuma mmojawao kwenda kumkaribisha Abu Huraira mahali alipokuwa anaswali. Yeye akasema kwamba alikuwa amefunga. Walipokuwa wanakaribia kumaliza kula yeye akaja akajiunga na kuanza kula. Walimuangalia yule mwenzao waliyekuwa wamemtuma kumwita Abu Huraira. Akasema: “Kwa nini mnaniangalia? Naapa kwamba yeye alisema kuwa amefunga.” Abu Huraira akasema: “Amesema kweli. Nilimsikia Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akisema: “Kufunga mwezi wa Ramadhani na kisha siku tatu za kila mwezi, hiyo ni sawa na kufunga kwa umri mzima.” Nilifunga zile siku tatu za mwanzo wa mwezi. Nimefunga kwa ajili ya kurudia funga na nimefungulia kwa mujibu wa uwepesishaji wa Allah.”323 Al-Bukhari amesimulia kwamba324 Muhammad bin Siriin alisema: “Tulikuwa pamoja na Abu Huraira (ndani ya nyumba fulani). Alikuwa 322 Kwa mujibu wa riwaya hii ilielekea kwamba yeye alihudhuria vita vya Siffin (baina ya Ali na Mu’awiyah) na kwamba alizifurahisha pande zote mbili ili asije akajizuia mwenyewe kurudi kwenye upande ulioshinda. Nimeona karibu na Siffiin, kati ya Iraq na Syria, sehemu takatifu inayoitwa Abu Huraira. Zaidi ya mtu mmoja waliniambia kwamba Abu Huraira katika baadhi ya siku za vita vya Siffiin, aliswali swala zake pamoja na jeshi la Imam Ali na alikula chakula na jeshi la Mu’awiyah. Lakini vita vilipoanza, yeye alikimbilia mlimani. Wakati alipoulizwa kuhusu hilo, yeye alisema: “Ali ni mtambuzi zaidi, na chakula cha Mu’awiyah kinanenepesha, na kule mlimani ni salama zaidi.” 323 Rejea kitabu cha Abu Na’iim, Hilyatul-Awliya’ Jz. 1, uk. 385. 324 Sahih al-Bukhari, Jz. 4, uk. 157, ilisimuliwa pia na Abu Na’iim katika Hilyatul-Awliya’ Jz. 1. uk. 379. 223


Abu huraira check Lubumba.qxd

7/1/2011

10:49 AM

Page 224

Abu Huraira amevalia nguo mbili za kitani zilizotariziwa. Alipenga pua zake kwa nguo hizo na akasema: “Umashuhuri gani! Abu Huraira anasafisha pua zake kwa kitani. Nakumbuka pale nilipoanguka chini kwa kuzimia kati ya mimbari ya Mtume na chumba cha Aisha. Wageni waliokuja waliweka miguu yao kwenye shingo yangu wakidhania mimi ni mwendawazimu. Lakini haikuwa ni uwendawazimu. Ilikuwa ni kwa sababu ya njaa.” Ibnul-Athiir amesema katika kitabu chake, al-Bidayah wan-Nihayah kwamba Abu Huraira alicheza mchezo wa sida (cider), ambao ulikuwa ni mchezo wa Kiajemi unaochezwa na watoto. Ibn Mandhuur katika kitabu chake Lissan al-Arab, ameongeza kwenye hilo kama katika riwaya ya Yahya bin Kathiir: “Hiyo sida (cider) ni Shetani mdogo. Anamaanisha kwamba ni jambo la kishetani.”325 Ad-Dimyeri amesema katika kitabu chake, Hayat al-Haywan (maisha ya wanyama) kuhusu sataranji (chesi): “As-Sa’luuki amesimulia kwamba Amir wa waumini Umar bin Khattab, Abul-Bissr na Abu Huraira waliruhusu kucheza sataranji. Ilikuwa ni maarufu katika vitabu vya Fiqh kwamba Abu Huraira alicheza mchezo wa saratanji. Al-Aajuri amesimulia kwamba Abu Huraira alisema: “Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amesema: “Kama ukipita karibu na wale wanaocheza Azlam, saratanji na dadu – yote michezo ya kamari – hao usiwasalimie.”326

325 Rejea kwenye al-Lissan al-Arab, Jz. 6, uk. 30. 326 ad-Dimyeri aliwashuku wasimulizi wa riwaya hii na akakanusha alichokisema Sawli kwamba Imam Zainul-Abidiin aliruhusu mchezo wa saratanji. Ilikuwa ni hakika kwamba Maimam ma’sum wote walikataza kucheza saratanji. Kadhalika alifanya hivyo Malik bin Anass, Ahmad Hanbal na Abu Haniifa. 224


Abu huraira check Lubumba.qxd

7/1/2011

10:49 AM

Page 225

Abu Huraira

KIFO CHAKE NA KIZAZI CHAKE Alifariki dunia kwenye kasri yake huko al-Aqiiq.327 Alibebwa kupelekwa Madina na watoto wa Uthman bin Affan mpaka walipofika makaburi ya alBaqii’ kama namna ya shukurani badala ya fikra zake nzuri kuhusu baba yao.328 al-Waliid bin Utbah bin Abu Sufyan, ambaye alikuwa ndiye Amiir wa Madina wakati huo, aliswalia jeneza sala ya maiti badala ya Marwan ambaye alikuwa amefukuzwa.329 Al-Waliid alijitokeza kuswalia jeneza hilo, licha ya kwamba ibn Umar, Abu Sa’id al-Khudri na masahaba wengine walikuwepo hapo, kumuenzi Abu Huraira kwa malipo ya huduma zake kubwa alizotoa kwa ajili ya Bani Umayyah. Al-Waliid alimtumia ami yake Mu’awiyah barua akimuelezea juu ya kifo cha Abu Huraira. Mu’awiyah alimwandikia mpwa wake: “Tafuta warithi wake na uwalipe dinari elfu kumi. Wafanyie hisani na wafanye wastarehe karibu na wewe kwa sababu Abu Huraira alimuunga mkono Uthman na alikuwa pamoja naye ndani ya nyumba yake wakati alipouliwa.” Alifariki mnamo mwaka wa hamsini na saba ama (ilisemekana) hamsini na nane au hamsini na tisa hijiria. Yeye alikuwa na umri wa miaka sabini na nane. Na kuhusu kizazi chake, kama tulivyojua, alikuwa na kijana aliyeitwa alMuharrir na binti. Al-Maharrir alikuwa na kijana aliyeitwa Na’iim, ambaye alisimulia kwamba babu yake Abu Huraira alikuwa ana uzi ambao ulikuwa na mafundo elfu mbili. Alikuwa halali mpaka alipokuwa amemtukuza 327 Ilisimuliwa na Ibn Hajar ndani ya al-Issaba, ibn Abdul Birr katika alIsstii’ab, ibnul-Hakiim katika al-Mustadrak na wanahistoria wengine. 328 Rejea kwenye kitabu cha ibn Sa’d, Tabaqat, Jz. 4, uk. 63 329 Rejea al-Isstii’ab, Issaba, Tabaqat na al-Mustadrak (kwenye wasifu wa Abu Huraira) 225


Abu huraira check Lubumba.qxd

7/1/2011

10:49 AM

Page 226

Abu Huraira Mwenyezi Mungu kwa uzi wake wenye mafundo elfu mbili.330 Na’iim pia alisimulia kutoka kwa babu yake kwamba mtu mmoja alimuuliza Mtukufu Mtume (s.a.w.w.): “Unanishauri nifanye biashara nacho?” Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alimwambia: “Shughulika na nguo! Kwa sababu mfanyabiashara wa nguo anawapendea watu kuwa wakati wote katika hali nzuri na utajiri.” Ibn Sa’d amemtaja al-Maharrir katika Tabaqat yake na amesema kwamba alisimulila Hadith chache na kwamba alifariki wakati wa utawala wa Umar bin Abdul-Aziz.

330 Rejea Hilyatul Awliya’ Jz. 1, uk. 380 na 383. 226


Abu huraira check Lubumba.qxd

7/1/2011

10:49 AM

Page 227

Abu Huraira

HITIMISHO Natuhitimishe kitabu chetu kwa maneno mawili ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) aliyokuwa ameyasema kwa hekima kubwa kama ushahidi wa kuthibitisha ule mkengeuko wa wale wapotokaji ili kuwaonya watu kutokana nao. Neno la kwanza: lilimhusu Abu Huraira, ar-Rahhal bin Anwa na al-Furat bin Hayyan. Wakati mmoja walipokuwa wanatoka nje ya mkutano wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), yeye alisema kuwahusu wao: “Kiu ya mmoja wenu katika Jahannam ni kubwa zaidi kuliko ya mwingine. Ana akili ya kihaini.”331 Abu Huraira na al-Furat mara kwa mara walikuwa wakisema hilo kwamba hawakuwa wakijihisi kuwa salama mpaka ar-Rahhal alipofanya usaliti na akauawa pamoja na yule muongo Musaylama. Kana kwamba wao (Abu Huraira na al-Furat) walijaribu kuyatafsiri maneno ya Mtukufu Mtume kumhusu mmoja wao tu kwa vile ar-Rahhal aliasi baada ya kifo cha Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Wamevuruga ule ukweli wa Hadith hiyo ya Mtume ambapo yeye aliifanya ya jumla kwao. Ilikuwa ni kama yale maneno ya Mwenyezi Mungu: “Je mmoja wenu anapenda kuwa na bustani ya mitende na mizabibu …..” (2:266), “….. mmoja wao anapenda apewe umri wa miaka elfu moja …..” (2:96), “Na anapoambiwa mmojawao yale aliyompigia mfano Mwenyezi Mungu …..” (43:17), “Na mmoja wao anapopewa habari ya (kuzaliwa mtoto) wa kike, uso wake huwa mweusi, naye amejaa chuki.” (16:58). Na mifano mingine mingi ndani ya Qur’ani, Sunna na mazungumzo ya 331 Rejea al-Issaba na al-Issti’ab (wasifu wa Furat). Vile vile ilisimuliwa na wanahistoria wengine. 227


Abu huraira check Lubumba.qxd

7/1/2011

10:49 AM

Page 228

Abu Huraira Waarabu. Waarabu walisema katika kuwasifia: “Mkono wa mmoja wao unanyesha dhahabu. Moyo wa mmoja wao umefurika huruma,” na walisema katika kuwabeza: “Uso wa mmoja wao ni alama ya ufidhuli. Na moyo wa mmoja wao ni mgumu kuliko mawe.” Kwa hiyo maneno ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) hayakumhusu mtu mmoja wao mahususi bali yaliwahusu wote watatu. Huu ulikuwa ndio ukweli wa Hadith hiyo. Kama Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) angetaka kumuashiria mmoja hasa kati ya watatu hao, basi angeonyesha wazi kwa kumtaja jina lake au mwelekeo unaopambanua na asingesema Hadith iliyovurugika, ambalo lilikuwa haliwezekani kwa Mtukufu Mtume, kwa sababu wale wasiokuwa na hatia wangekosewa. Hivyo kama alijulikana kwamba mmoja wao alikuwa mhaini na kwamba atakuwa katika moto wa Jahannam bila ya kujua hasa alikuwa ni yupi, basi watatu hao wote wangeshiriki katika hukmu hiyo. Baada ya hayo haikuwa ni kuwaamini au kutegemea riwaya zao au ushahidi wao, na ilifaa kutowakabidhi lolote kati ya mambo ya Waislamu. Wangekuwa wamekataliwa kwenye haki za raia, na umma ulipaswa kuwaepuka katika lolote lile lililohusu ukweli na uadilifu kwa mujibu wa kanuni za Kiislamu kuhusiana na mashaka. Huo ulikuwa ni ushahidi tosha wa kuwakataa wote watatu. Ni dhahiri kabisa kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) angemuelezea wazi kabisa huyo msaliti, ambaye atakuwa ndani ya Jahannam, na asingewaacha wale wasio na hatia kuteswa na ubashiri wake alimuradi walikuwa wanaishi pamoja na mawazo mabaya ya watu kuhusu wao. Kwa hakika asingefanya hivyo, isipokuwa ni kwamba wote watatu hao walikuwa ni sawasawa. Kama utasema: Inawezekana Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alimlenga arRahhal kwa kusema jambo fulani au aliashiria kwake yeye na kwamba hilo likawa halikujulikana kwetu.

228


Abu huraira check Lubumba.qxd

7/1/2011

10:49 AM

Page 229

Abu Huraira Sisi tunasema: Kama kungekuwa na jambo kama hilo, lisingeweza kutojulikana kwa Abu Huraira na al-Furat, ambao hawakupata jambo lolote la kuwafanya wajihisi kuwa salama isipokuwa pale ar-Rahhal aliporitadi ndipo wakasujudu kumshukuru Allah. Baada ya hilo walikuwa mara kwa mara wakisema kwamba walikuwa hawajihisi salama mpaka pale arRahhal alipofanya hivyo.332 Kama utasema: Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) aliyasema hayo kwa ujumla kabla ar-Rahhal hajaasi na kujiunga na Musaylama Muongo na akawa ameuliwa pamoja naye. Hivyo baada ya ar-Rahhal kufanya hivyo, ilikuja kuwa wazi kwamba ni yeye mwenyewe, ambaye alimaanishwa na Mtume kwa Hadith hii bila ya hao wengine wawili. Sisi tunasema: Ilieleweka kutoka kwenye maneno ya Mtukufu Mtume: “….. mmoja wenu …..” kwamba yaliwahusu wote bila kubagua kama tulivyoeleza hapo kabla na tukanukuu mifano kama hiyo kutoka kwenye Qur’ani tukufu. Yalikuwa hayahusiani chochote na kuasi kwa ar-Rahhal kwani alikuwa mbaya hata kabla ya hapo. Kadhalika na hao marafiki zake wawili. Pili: Ilikuwa haiwezekani kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kuficha ukweli wakati ulipokuwa unatakiwa au kuuchelewesha mpaka muda wake upite. Wakati katika suala hili ulihusika kwenye muda ule ule wa kutamkwa neno hili na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Ikiwa mmoja wapo yoyote kati ya hawa watatu alistahiki heshima au kustahiwa kokote, Mtume angemtangaza yule msaliti kati yao kwa jina. Kwa kweli tangu waingie kwenye Uislamu walikuwa wakitiliwa mashaka kwenye riwaya zao, ushahidi na kila kitu kingine. Kama ilikuwa sio lazima kuwakataa wote watatu, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) angeonyesha jina la mmoja wao kabla hajafariki. Asingeliacha suala la kuasi kwa ar-Rahhal kufafanua Hadith yake! 332 Kusujudu kwao na kusema kama maneno hayo kulisimuliwa katika alIsstii’ab, al-Issaba na katika vitabu vingine vya historia. 229


Abu huraira check Lubumba.qxd

7/1/2011

10:49 AM

Page 230

Abu Huraira Tatu: al-Furat bin Hayyan alikuwa ni mpelelezi kwa ajili ya washirikina na jicho la Abu Sufyan la kumchunguzia Mtume na Waislam. Wakati Waislamu walipotaka kumuua kwa mujibu wa maagizo ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) yeye alitangaza kuwa ni Mwislamu ili kuokoa maisha yake. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akasema:333 “Kuna baadhi yenu, mimi ninawazawadia kubakia ni Waislamu. Mmoja wao ni al-Furat bin Hayyan.” Hivyo na yeye pia alikuwa ni mbaya kama ar-Rahhal. Kwa hivyo tutawezaje kuamua kwamba yeye Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) katika Hadith yake alimrejelea ar-Rahhal na sio al-Furat, ambaye alikuwa Mwislamu kwa ajili ya kuokoa maisha yake tu, au Abu Huraira, ambaye alijikatia tiketi yake ya kwenda Jahannam kabla ya marafiki zake hao wawili kwa mujibu wa Hadith ya Mtume: “Yeyote atakayehusisha Hadith ya kubuni na mimi, huyo atakalia nafasi yake katika Jahannam.” Neno la pili: Hili lilimhusu Abu Huraira, Samara bin Jundub al-Fazari na Abu Mahthuura al-Jumahi, ambao Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) siku moja aliwaonya kwa kusema: “Wa mwisho wenu kufariki atakuwa ndani ya Jahannam.”334 Ilikuwa ni mbinu ya hekima ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kuwaondoa washirikina katika kushiriki katika mambo ya Waislamu. Kwa vile Mtume alijua ukweli uliofichika wa wale watu watatu, hivyo alitaka kudukiza ndani ya akili za umma wake yale mashaka juu yao ili kuwaepuka ili wasije wamwaminisha mmoja wao na shughuli ambayo ilikuwa ifanywe na muumini mwaminifu. Yeye alisema kwamba mmoja wao, ambaye alikuwa 333 Rejea al-Isstii’ab na al-Issaba. al-Hakiim katika al-Mustadrak, Jz. 4, uk. 366 amesimulia kwamba al-Furat alikuwa ni mpelelezi na mshirika wa Abu Sufyan. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) aliamuru kuuawa kwake. Alipita karibu na baadhi ya Ansari na akasema: “Mimi ni Muislamu.” Wakamwambia Mtume kwamba yeye amesema kuwa ni Muislamu. Mtume akasema: “Kuna baadhi yenu tunawapeleka kwenye imani yao ya kujisingizia. Mmoja wao ni al-Furat bin Hayyan.” 334 Rejea al-Issaba na al-Istii’ab (wasifu wa Samara bin Jundub). 230


Abu huraira check Lubumba.qxd

7/1/2011

10:49 AM

Page 231

Abu Huraira afariki wa mwisho kabisa atakuwa katika Jahannam bila kumuanisha mmoja maalum kati ya watatu hao. Siku zikapita, usiku na mchana na Hadith hiyo ikabakia kama ilivyo bila ufafanuzi au nyongeza mpaka Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alipoungana na Mpendwa wake Aliyetukuka huko katika dunia njema na bora. Hivyo umma ulipaswa kuwaacha wote katika nafasi yoyote inayowahusu waumini na kuwanyima zile haki kwa mujibu wa kanuni ya kidesturi na kiakili kuhusu mashaka. Kama watu watatu hawa hawakuwa wote sawa katika suala hili, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kwa hakika angembainisha mmoja wao. Kama wewe utasema: kunaweza kukawa na ubainishaji kuhusu mmoja wao lakini ulikuwa haukufahamika kwetu sisi kwa sababu ya kipindi kirefu. Sisi tunasema: Kama kweli ilikuwa hivyo, wasingekuwa wote watatu wanahofia kutokana na onyo hilo.335 Hakukuwa na tofauti yoyote katika suala hili ikiwa hakukuwa na ufafanuzi wowote au kuwa limejulikana. Watu wote watatu walichangia hukmu hiyohiyo ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), kwa hiyo ilikuwa itumike kwa yoyote kati yao. Kama ukisema kwamba: Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alilisema hilo kwa ujumla kabla ya yule wa kwanza na wapili hawajafariki. Baada ya vifo vyao ilikuja kuwa wazi kwamba yeye yule ambaye alibakia baada yao, alikuwa ndiye aliyekusudiwa kuwa ndani ya Jahannam. Hivyo hapakuwa na tatizo lolote. Sisi kwanza tunasema: ulijua vyema kama sisi tulivyosema kabla kwamba ilikuwa haiwezekani kwa mitume kuficha ukweli pale unapohitajika au kuuchelewesha mpaka muda wake ukapita. Ulijua vile vile kwamba wakati wake ulihusika na muda ule ule wa kutamkwa kwa onyo hili. Kama mmoja 335 Kama ilivyokuwa wazi kwa wale waliokagua mambo yao hao kuhusiana na hili ndani ya vitabu vya wanahistoria. 231


Abu huraira check Lubumba.qxd

7/1/2011

10:49 AM

Page 232

Abu Huraira wa watu watatu hawa alikuwa mkweli na wa kustahika, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) angelionyesha hilo kwa kuainisha mmoja wao ili kutowakosea wale wasio na hatia. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alikuwa mbali sana na hali ya kumzuia mtu haki yake, au kumhuzunisha mtu ambaye alikuwa hana hatia na hakustahili kuaibishwa, na akamuacha akiwa ameaibika mpaka alipokufa bila ya kujua kutokuwa na hatia kwake isipokuwa kama alikufa, kwa mujibu wa udhaniaji batili huu, kabla ya hao wenzake wawili. Pili: Sisi, Wallahi, tulijaribu kwa uwezo wetu wote katika kutafiti na kuchunguza ili kujua ni nani alikuwa wa mwisho wao katika kufariki lakini hatukuweza kwa sababu riwaya kuhusu tarehe za vifo vyao zilitatiza na zinapingana.336 Tatu: Tabia tukufu na maadili bora ya hali ya juu ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), ambaye (alisononeka wakati waumini walipatwa na huzuni, mwenye huruma sana kwa ajili yao na alikuwa mpole juu yao),337 asingewakabili wale ambao alikuwa akiwaheshimu, kwa maneno makali kama hayo: “wa mwisho wenu kufariki atakuwa ndani ya Jahannam.” Ilikuwa haiwezekani kwa yeye, ambaye alikuwa na uadilifu wa hali ya juu, kumshitusha mtu, ambaye hakustahili kushitushwa kwa maneno kama haya “kiu kali kabisa kwa mmoja wenu ndani ya Jahannam.” Kama mmoja wa watu wale watatu alikuwa mwema, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) asingemuingiza katika mshituko huu mkali na ufidhili wa kikatili, lakini wahyi 336 Mmoja wa wanahistoria alisema kwamba Samara alikuwa amefariki mnamo mwaka wa hamsini na saba hijiria na Abu Huraira alifariki mwaka wa hamsini na tisa. Hii ilipingana na nyingine inayosema kwamba Abu Huraira alifariki mwaka wa hamsini saba hijiria na kadhalika kwa riwaya za wanahistoria waliobaki. Lakini inayoelekea zaidi kati ya riwaya ilionyesha kwamba wote watatu walifarika katika mwaka wa hamsini na tisa hijiria bila kuanisha miezi au tarehe za vifo vyao. 337 Kama Mwenyezi Mungu alivyomueleza ndani ya Qur’ani Tukufu.

232


Abu huraira check Lubumba.qxd

7/1/2011

10:49 AM

Page 233

Abu Huraira ulimlazimu yeye kufanya hivyo kwa ajili ya Mwenyezi Mungu na kwa umma kwa sababu “Wala hasemi kwa matamanio ya nafsi yake, hayakuwa bali ni wahyi uliofunuliwa.� (53:3-4). Ilikuwa inatosha kwa Abu Huraira kuwemo kwenye aibu yake hiyo, ambayo Hadith za Mtume zimemuingiza humo. Hebu fanya uamuzi wewe mwenyewe wakati unapoona madhambi yalilyofanywa na Samara; kukithiri kwake kunakotisha katika kumwaga damu za Waislamu,338 kuuza pombe waziwazi hadharani,339 kumkosea al-Ansari, kutokumtii Mtukufu Mtume wakati alipomwita ili kusuluhisha baina yake na mtu mwingine katika suala lililotokea kati yao kuhusu mtende wa Samara, ambao ulikuwa ndani ya nyumba ya mtu huyo. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alimuahidi kwamba atakuja kupata mmoja huko Peponi badala ya ule lakini alikataa katika namna ambayo ilionyesha kwamba yeye hakuwa muumini.340 Wakati mmoja alijeruhi kichwa cha ngamia jike wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kwa usodai na dharau, licha ya matendo yake mabaya mengi. Na kuhusu Abu Mahthuura, yeye alikuwa mmoja wa watumwa walioachwa huru na mmoja wa wale ambao Mtukufu Mtume aliwazawadia na kuwavutia kwenye Uislamu ili kuweza kuwa salama kutokana na njama zao dhidi ya Waislamu. Alikuja kuwa Mwislamu baada ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alipoiteka Makka na baada ya kuwa amerudi kutoka kwenye vita vya Hunayn kwa ushindi kabisa dhidi ya kabila kubwa la Hawazin. Kwa wakati ule hapakuwa na mtu ambaye alikuwa akichukiwa sana na Abu Mahthuura zaidi ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na maamrisho yake. Alikuwa mara kwa mara akimkejeli mpigambiu wa Mtume (s.a.w.w.) ambaye alikuwa akiadhini, na akamuigiza kwa sauti kubwa katika namna ya dhihaka. Lakini zile pesa za fedha (masilva) ambazo Mtume alikuwa 338 Rejea Sharh an-Nahj al-Hamiid, Jz. 1, uk. 363 ili kuona maelezo zaidi juu ya hilo. Rejea Tariikh Tabari, matukio ya mwaka wa hamsini hijiria na mlango wa nane wa kitabu chetu al-Fusuul al-Muhimma. 339 Rejea Musnad Ahmad, Jz. 1, uk. 25 340 Rejea Sharh Nahjul-Balaghah ya Ibn Abil-Hadiid, Jz. 1, uk. 363. 233


Abu huraira check Lubumba.qxd

7/1/2011

10:49 AM

Page 234

Abu Huraira akimpatia, pamoja na ngawira za Hunayn, ambazo Mtume alizawadia watumwa walioachwa huru wa maadui zake, ambao walipigana dhidi yake na maadili yake mema yaliyomkumbatia yeyote aliyetangaza shahada mbili, pamoja na ukali wake kwa wale ambao hawakutoa shahada hizo, yote hayo yaliwafanya Waarabu kuwa Waislamu makundi kwa makundi. Na kwa hiyo Abu Mahthuura na wengine kama yeye walilazimika kusilimu bila hiari. Yeye hakuhamia Madina mpaka alipofariki mjini Makka. Mwenyezi Mungu alizijua vyema nia alizokuwa amezificha bwana huyu! Neno moja limebakia ambalo lililsemwa na Ibn Abdul-Birr kuhusu onyo hili linalowahusu watu watatu hawa. Amesema katika kitabu chake alIssti’ab kuhusu Samara bin Jundub: “Alifia Basra katika enzi za utawala wa Mu’awiyah mnamo mwaka wa hamsini na nane hijiria. Aliangukia kwenye chungu kilichojaa maji moto, ambacho alikuwa akae juu yake kama matibabu kwa sababu alikuwa anaugua kutokana na pepopunda mbaya na akafariki. Hilo liliweka mpaka wa maneno ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) pale alipomwambia yeye, Abu Huraira na wa tatu pamoja nao: “Wa mwisho kufariki kati yenu atakuwa katika moto wa Jahannam.” Ilikuwa ni tafsiri ya ajabu, ambayo matini ya maneno hayo haikuwa na maana hiyo. Hakuna hata mtu mmoja aliyeielewa kwa namna hii hata hao watu watatu wenyewe, ambao walilengwa na Hadith hii, hawakutilia shaka maana yake, kwa hiyo kila mmoja wao alitamani, kama ilivyokuwa imeelezwa na wanahistoria, kwamba angefariki kabla ya wenzake hao wawili. Haikuwa na uhakika kwamba Samara alifariki baada ya hao wawili. Ibn Abdul-Birr amesema kwamba yeye alifariki mwaka wa hamsini na nane hijiria, ambapo Abu Huraira kwa mujibu wa riwaya za al-Waqidi, ibn Numayr, ibn Ubayd, Ibnul-Athiir na wengineo, yeye alifariki mwaka wa hamsini na tisa hijiria ambao na Abu Mahthuura pia alifariki. Ilisemekana pia kwamba Abu Mahthuura alifariki mwaka wa sabini na tisa. Ibnul-Kalbi amesema kwamba Abu Mahthuura alifariki baada ya Samara. Hivyo uhalalishaji wa Ibn Abdul-Birr kuhusu Hadith hii ulikuwa si chochote bali upuuzi mtupu. 234


Abu huraira check Lubumba.qxd

7/1/2011

10:49 AM

Page 235

Abu Huraira Hili lilikuwa ndio la mwisho katika yale tuliyotaka kuyasema ili kuiweka wazi Sunna tukufu kutokana na dosari hizi za kufedhehesha zilizohusishwa kwenye kiini cha Uislamu na moyo wake mkuu. Shukrani kwa Mwenyezi Mungu, ambaye ametufanya sisi tufanikiwe kuifanya kazi hii ndogo, ambayo tunamuomba Mwenyezi Mungu iwe yenye manufaa kwa ajili ya waumini na kuifanya pia iwe kumbukumbu katika Siku ya Kiyama. Rehema na amani ya Mwenyezi Mungu iwe juu ya Bwana na Mwisho wa Mitume, Muhammad (s.a.w.w.) na kizazi chake na masahaba zake wema. Kitabu hiki kilikamilishwa katika mji wa Suur. Lebanoni, mnamo siku ya Alhamisi, mwezi ishirini na tatu Ramadhani,1362A.H. sawa na tarehe ishirini na tatu ya Septemba, 1943, na mwandishi ambaye anatarajia rehema za Mwenyezi Mungu, Abdul Husein bin sharif Yusuf bin sharif Jawad bin sharif Isma’iil bin Muhammad bin Muhammad bin Sharafud-Diin, ambaye jina lake hasa lilikuwa ni Ibrahim bin Zainul-Abidiin bin Ali Nuurud-Din bin Nuurud-Diin Ali bin Izziddiin al-Hussayn bin Muhammad bin al-Husayn bin Ali bin Muhammad bin Tajuddiin, ambaye alikuwa maarufu kama Abul Hasan bin Muhammad, ambaye jina lake la ukoo lilikuwa Shamsuddiin bin Abdullah, ambaye jina lake la ukoo lilikuwa Jalaluddiin bin Ahmad bin Hamza bin Sa’dullah bin Hamza bin AbusSa’adat Muhammad bin Abu Muhammad Abdullah, mkuu wa machifu wa Talibiti katika Baghdad,341 bin Abul Harith Muhammad bin Abul Hasan Ali, ambaye alikuwa maarufu kama ibnul-Daylamiyya, bin Abu Tahir Abdullah bin Abul Hasan Muhammad al-Muhaddith bin Abut-Tayyib Tahir bin al-Husein al-Qat’ei bin Musa Abu Sibha bin Ibrahim al-Murtadha bin Imam al-Kadhiim bin Imam as-Sadiq bin Imam al-Baqir bin Imam ZainulAbidiin bin Imam Abu Abdillah al-Husein, Bwana wa mashahidi, mjukuu wa Mtukufu Mtume na mwana wa Amirul-Mu’minin, bwana wa mawasii, Ali bin Abi Talib. Rehma na amani ya Mwenyezi Mungu iwe juu ya Mtukufu Mtume na kizazi chake (a.s.). 341 Waliokuwa na uhusiano na kizazi cha Abi Talib. 235


Abu huraira check Lubumba.qxd

7/1/2011

10:49 AM

Page 236

Abu Huraira

ORODHA YA VITABU VILIVYO CHAPISHWA NA AL-ITRAH FOUNDATION 1. 2. 3. 4. 5. 6. 7. 8. 9. 10. 11. 12. 13. 14. 15. 16. 17. 18. 19. 20. 21. 22. 23. 24. 25.

Qur'an Al-Kariim - Tafsir Al-Kashif Juzuu ya kwanza mpaka Thalathini Uharamisho wa Riba Uharamisho wa uwongo Juzuu ya Kwanza Uharamisho wa uwongo Juzuu ya Pili Hekaya za Bahlul Muhanga wa Imamu Husein (A.S.) Mikingamo iliyomzunguka Imamu Ali (A.S.) Hijab vazi Bora Ukweli wa Shia Ithnaashari Madhambi Makuu Mbingu imenikirimu Abdallah Ibn Saba Khadijatul Kubra Utumwa Umakini katika Swala Misingi ya Maarifa Kanuni za Ndoa na maadili ya Familia Bilal wa Afrika Abudharr Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu Salman Farsi Ammar Yasir Qur'an na Hadithi Elimu ya Nafsi Yajue Madhehebu ya Shia 236


Abu huraira check Lubumba.qxd

7/1/2011

10:49 AM

Page 237

Abu Huraira 26. 27. 28. 29. 30. 31. 32. 33. 34. 35. 36. 37. 38. 39 40. 41. 42. 43. 44. 45. 46. 47. 48. 49. 50. 51. 52. 53. 54. 55. 56.

Ukusanyaji na Uhifadhi wa Qur'an Tukufu Al-Wahda Ponyo kutoka katika Qur'an. Uislamu mfumo kamili wa maisha ya kijamii Mashukio ya Akhera Al Amali Dua Indal Ahlul Bayt Udhuu kwa mujibu wa Kitabu na Sunna. Haki za wanawake katika Uislamu Mwenyeezi Mungu na sifa zake Amateka Na Aba'Khalifa Nafasi za Ahlul Bayt (a.s) Adhana. Upendo katika Ukristo na Uislamu Nyuma yaho naje kuyoboka Amavu n’amavuko by’ubushiya Kupaka juu ya khofu Kukusanya swala mbili Bismillah ni sehemu ya Qur’ani na husomwa kwa Jahara Kuwaongoza vijana wa kizazi kipya Kusujudu juu ya udongo Kusheherekea Maulidi Ya Mtume (s) Tarawehe Malumbano baina ya Sunni na Shia Kupunguza Swala safarini Kufungua safarini Umaasumu wa Manabii Qur’an inatoa changamoto as-Salaatu Khayrun Mina -'n Nawm Uadilifu wa Masahaba Dua e Kumayl 237


Abu huraira check Lubumba.qxd

7/1/2011

10:49 AM

Page 238

Abu Huraira 57. 58. 59. 60. 61. 62. 63. 64. 65. 66. 67. 68. 69. 70. 71. 72. 73. 74. 75. 76. 77. 78. 79. 80. 81. 82. 83. 84. 85.

Sauti Ya Uadilifu wa Binadamu Umaasumu wa Mitume - Faida Zake Na Lengo Lake Umaasumu wa Mitume - Majibu Ya Aya Zenye Utata Umaasumu wa Mitume - Umaasumu wa Mitume Muhammad (s) Nahju’l-Balaghah - Juzuu ya Kwanza Nahju’l-Balaghah - Juzuu ya Pili Kuzuru Makaburi Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Kwanza Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Pili Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Tatu Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Nne Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Tano Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Sita Tujifunze Misingi Ya Dini Sala ni Nguzo ya Dini Mikesha Ya Peshawar Malezi Ya Mtoto Katika Uislamu Ubora wa Imam 'Ali Juu ya Maswahaba Na Ushia ndio njia iliyonyooka Hukumu za Kifikihi zinazowahusu Wanawake Liqaa-u-llaah Muhammad (s) Mtume wa Allah Amani na Jihadi Katika Uislamu Uislamu Ulienea Vipi? Uadilifu, Amani na Mtume Muhammad (s) Mitala na Ndoa za Mtume Muhammad (s) Urejeo (al-Raja’a ) Mazingira Utokezo (al - Badau) Sadaka yenye kuendelea 238


Abu huraira check Lubumba.qxd

7/1/2011

10:49 AM

Page 239

Abu Huraira 86. 87. 88. 89. 90. 91. 92. 93. 94. 95.

Msahafu wa Imam Ali Uislamu na dhana Mtoto mwema Adabu za Sokoni Johari za hekima kwa vijana Maalimul Madrasatain Sehemu ya Kwanza Maalimul Madrasatain Sehemu ya Pili Maalimul Madrasatain Sehemu ya Tatu Tawasali Imam Mahdi katika Usunni na Ushia

96.

Maana ya laana na kutukana katika Qur’ani Tukufu

97.

Hukumu ya kujenga juu ya makaburi

98.

Swala ya maiti na kumlilia maiti

99.

Shiya na Hadithi (kinyarwanda)

100.

Mariamu, Yesu na Ukristo kwa mtazamo wa Kiislamu

101.

Hadithi ya Thaqalain

102

Fatima al-Zahra

103.

Tabaruku

104.

Sunan an-Nabii

105.

Historia na sera ya viongozi wema (Sehemu ya Kwanza)

106.

Historia na sera ya viongozi wema (Sehemu ya Pili)

107.

Mahdi katika sunna

108.

Kusalia Nabii (s.a.w)

109.

Ujumbe -Sehemu ya Kwanza

110.

Ujumbe - Sehemu ya Pili

111.

Ujumbe - Sehemu ya Tatu

112.

Ujumbe - Sehemu ya Nne 239


Abu huraira check Lubumba.qxd

7/1/2011

10:49 AM

Page 240

Abu Huraira 113.

Ngano ya kwamba Qur’ani imebadilishwa

114.

Iduwa ya Kumayili

115.

Maarifa ya Kiislamu.

116.

Ukweli uliopotea sehemu ya Kwanza

117.

Ukweli uliopotea sehemu ya Pili

118.

Ukweli uliopotea sehemu ya Tatu

119.

Ukweli uliopotea sehmu ya Nne

120.

Ukweli uliopotea sehmu ya Tano

121.

Johari zenye hekima kwa vijana

122.

Safari ya kuifuata Nuru

123.

Idil Ghadiri

124.

Myahudi wa Kimataifa

125.

Kuanzia ndoa hadi kuwa Wazazi

126.

Visa vya kweli sehemu ya Kwanza

127.

Visa vya kweli sehemu ya Pili

128.

Muhadhara wa Maulamaa

129.

Mwanadamu na Mustakabali wake

130.

Imam Ali binamu ya Mtume Sehemu ya Kwanza

131.

Imam Ali binamu ya Mtume Sehemu ya Pili

132.

Khairul Bariyyah

133.

Uislamu na mafunzo ya kimalezi

134.

Vijana ni Hazina ya Uislamu.

135.

Yafaayo kijamii

136.

Kusoma sura zenye Sijda ya wajibu

137.

Taqiyya

138.

Vikao vya furaha 240


Abu huraira check Lubumba.qxd

7/1/2011

10:49 AM

Page 241

Abu Huraira 139.

Shia asema haya Sunni asema haya Wewe wasemaje?

140.

Uislamu na Mazingatio Sehemu ya Kwanza

141.

Uislamu na Mazingatio Sehemu ya Pili

142.

Azadari-Kuhuzunika na Kuomboleza

143.

Sunna katika Kitabu Fiqhi al-Sunnah

144.

Mtazamo Mpya - Wanawake katika Uislamu

145.

Kuonekana kwa Allah

146.

Tabia njema kwa Mujibu wa Ahlul-Bayt (Sehemu ya Kwanza)

147.

Tabia njema kwa Mujibu wa Ahlul-Bayt (Sehemu ya Pili)

148.

Ndugu na Jirani

149.

Ushia ndani ya Usunni

150.

Maswali na Majibu

151.

Mafunzo ya hukmu za ibada

152.

Ahlul Bayt ndani ya tafsiri za Kisusunni No1

153

Ahlul Bayt ndani ya tafsiri za Kisusunni No 2

154.

Ahlul Bayt ndani ya tafsiri za Kisusunni No 3

155.

Abu Huraira

241


Abu huraira check Lubumba.qxd

7/1/2011

10:49 AM

Page 242

Abu Huraira

BACK COVER Huu ni uchunguzi na mapitio ya wasifu wa mmoja wa masahaba wa Mtukufu Mtume SAW.. Abu Huraira amesimulia kutoka kwa Mtukufu Mtume SAW hadithi nyingi sana mpaka akavuka mipaka yote, na vitabu vya hadithi vya Sunni vimesimulia hadithi kutoka kwake mpaka vikavuka mipaka pia. Hatukuwa na njia yoyote mbele ya idadi hii kubwa ya hadithi zilizosimuliwa na Abu Huraira ila kutafuta juu ya vyanzo vyao, kwa sababu zimeshughulisha maisha yetu ya kidini na kiakili moja kwa moja; vinginevyo tungeweza kuziachilia mbali na kuvitupilia mbali vyanzo vyake na kuangalia mambo mengine muhimu zaidi. Idadi hii kubwa ya riwaya zilizosimuliwa na bwana huyu zilienea kwenye matawi na mizizi ya dini na kuwapelekea mafakihi wa Sunni kuzitegemea sana katika kushughulika na hukumu na sharia za Mwenyezi Mungu. Ungana na mwandishi wa kitabu hiki ili upate kumjua sahaba huyu machachari wa Mtukufu Mtume s.a.w na jinsi alivyoitumia nafasi hii pamoja na fursa alizozipata. Kimetolewa na kuchapishwa na: Alitrah Foundation S.L.P. 19701 Dar es Salaam, Tanzania Simu: +255 22 2110640 Simu/Nukushi: +255 22 2127555 Barua Pepe: alitrah@raha.com Tovuti: www.alitrah.org Katika mtandao: www.alitrah.info

242


Abu huraira check Lubumba.qxd

7/1/2011

10:50 AM

Page 243

Abu Huraira

243


Turn static files into dynamic content formats.

Create a flipbook
Issuu converts static files into: digital portfolios, online yearbooks, online catalogs, digital photo albums and more. Sign up and create your flipbook.