FAO Rabies Brochure

Page 1

Kwa mnyama • Unapohisi au unapoona mbwa au mnyama mwenye dalili za Kichaa cha Mbwa, toa taarifa kwa mtaalam wa mifugo au serikali ya kijiji/mtaa iliyo karibu na eneo lako. • Mbwa au mnyama afungiwe kwa muda usiopungua siku kumi akipewa chakula na maji ili kuona kama atakufa ama la. Endao atakufa ndani ya muda huo, kuna uwezekano mkubwa kuwa alikuwa na kichaa cha mbwa. • Toa taarifa mapema kwa mtaalamu wa mifugo kwenye eneo lako unapoona mnyama mwenye dalili kwa ufuatiliaji na udhibiti zaidi. • Kumtambua mwenye mbwa au mnyama aliyekung’ata kutasaidia uchunguzi zaidi • kufahamu endapo ana ugonjwa ama alishapatiwa chanjo dhidi ya kichaa cha mbwa. JINSI YA KUZUIA KUENEA KWA UGONJWA WA KICHAA CHA MBWA •

Kuna njia mbalimbali za kudhibiti Kichaa cha Mbwa. Njia hizo husaidia jamii kujikinga au kuepu-ka kupata ugonjwa huo, pia kuwakinga wanyama kama mbwa, paka na wengine dhidi ya ugonjwa wa Kichaa cha Mbwa.

KUTOA KINGA TIBA DHIDI YA KICHAA CHA MBWA KWA MAKUNDI YAFUATAYO: • • •

Wafanyakazi wa maabara Watoa chanjo dhidi ya Kichaa cha Mbwa Wakusanyaji sampuli na mizoga ya wanyama

Kwa Wanyama • Mbwa na paka wapelekwe kuchanjwa dhidi ya Kichaa cha Mbwa kila mwaka au kulingana na ushauri wa mtaalamu wa mifugo. Chanjo ni njia pekee inayotumika kumkinga mbwa na wanyama wengine dhidi ya maambukizi ya virusi vya Kichaa cha Mbwa •

Zuia uzururaji wa mbwa na wanyama wengine wafugwao kwa kuwafungia katika mabanda, uzio au kuwafunga kamba kuanzia saa 12 alfajiri na kumfungulia saa 4 usiku.

Zingatia ufugaji bora wa mbwa kwa kuhakikisha kuwa anapatiwa haki zake za msingi (chakula cha kutosha, chanjo, tiba, kuogeshwa, nk).

Kuelimisha watoto wasicheze na mbwa wasiyemfahamu, pia kutoa taarifa kwa wazazi endapo watapata tukio la kukwaruzwa, kung’atwa au kulambwa sehemu yenye jeraha na mbwa anayehisiwa kuwa na Kichaa cha Mbwa. Epuka tabia hatarishi kama vile kumchokoza au kumpiga mbwa anayepita, anayekula au mwenye watoto.

Kichaa cha MBWA Chukua Hatua za Kujikinga

Kwa binadamu

FAHAMU KUHUSU

IMETOLEWA NA: Ofisi ya Waziri Mkuu Kwa kushirikiana na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Wizara ya Mifugo na Uvuvi pamoja na Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa


UTANGULIZI KICHAA CHA MBWA NI NINI? Kichaa cha Mbwa ni ugonjwa wa virusi unaoshambulia mfumo wa fahamu. KICHAA CHA MBWA HUWAPATA NANI? Kichaa cha mbwa huwapata wanyama walio kundi la mamalia. Hii ina maana Kichaa cha Mbwa kinaambukiza binadamu, wanyama wafugwao kama vile mbwa, paka, mbuzi, kondoo na ng’ombe, vilevile wanyama pori kama vile si, mbweha,mbwa mwitu wanakuwa na virusi ila mara nyingi hawaoneshi dalili za wazi.

• Mbwa na wanyama wengine wenye virusi vinavyosababisha Kichaa cha Mbwa huweza kuambukiza ugonjwa huu bila kuonesha dalili zozote. Hivyo, ni muhimu mtu yeyote aking’atwa na mbwa au mnyama mwingine atoe taarifa kwa Mtaalamu wa Afya katika Kituo cha kutolea huduma za Afya kilicho karibu,vilevile atoe taarifa kwa Mtaalamu wa mifugo ili hatua husika zichukuliwe. DALILI ZA KICHAA CHA WANYAMA NA BINADAMU

MBWA

KWA

KWA

Mara baada ya binadamu kung’atwa anaweza asioneshe dalili za ugonjwa huu, kwani huchukua muda kulingana na sehemu ya mwili iliyong’atwa. DALILI ZA KICHAA CHA MBWA KWA WANYAMA NI PAMOJA NA: • • • • •

• •

Kutokwa na mate mengi mdomoni Kung’ata vitu hovyo hovyo Kuzunguka hovyo Kuogopa maji Kubadili tabia; mbwa mkali kuwa mpole na mpole kuwa mkali(mbwa huonesha tabia zisizo za kawaida) Kupoteza fahamu Kupooza baadhi ya viungo na kufa

DALILI ZA KICHAA CHA MBWA KWA BINADAMU NI PAMOJA NA:

JE KICHAA CHA MBWA HUAMBUKIZWAJE? •

Kichaa cha mbwa huambukizwa kwa wanyama na binadamu kutokakana na kung’atwa na mnyama mwenye virusi vya Kichaa cha Mbwa. Binadamu pia anaweza kuambukizwa kwa kugusa au kuingiwa na mate ya mnyama aliyeathirika, kupitia jeraha/mchubuko, jicho, pua, mdomo.

• Homa • Kuumwa kichwa • Kuwasha sehemu ya jeraha • Maumivu ya mwili • Kuchanganyikiwa na kuvunja/kupiga vitu • Kuogopa mwanga • Kubweka kama mbwa • Kuogopa maji (pamoja na maji ya kunywa) • Kutokwa na mate mengi mfululizo • Kuweweseka na kushtuka mara kwa mara

• Kupooza, maisha.

kudhoofu

na

hatimaye

kupoteza

NAMNA YA KUHUDUMIA JERAHA LILILOTOKANA NA KUNG’ATWA NA MNYAMA Kwa binadamu. •

Mtu aliyeng’atwa na mnyama au kusababishiwa jeraha na mnyama apewe huduma ya kwanza kwa kuosha jeraha kwa maji mengi yanayotiririka na sabuni ya mche kwa walau dakika 15 na kidonda kisifungwe.

Mara tu baada ya kupata huduma ya kwanza akimbizwe Kituo cha kutolea - huduma za Afya ili kupatiwa chanjo kuzuia madhara dhidi ya Kichaa cha Mbwa.


Turn static files into dynamic content formats.

Create a flipbook
Issuu converts static files into: digital portfolios, online yearbooks, online catalogs, digital photo albums and more. Sign up and create your flipbook.