GOOD NEIGHBORS KIMATAIFA Jitahada nyingi zimefanyika kumkomboa mtoto wa kike lakini bado vikwazo ni vingi sana katika kufikia malengo yao. Hivyo, ni vyema kila mtu kushiriki katika kulinda utu wa mtoto wa kike kwa kupaza sauti kukataa ukatili majumbani na kutokomeza viashiria vyote vinavyopelekea ukiukwaji wa haki za mtoto wa kike. Mtoto wa kike anastahili kuwa huru na ana mchango mkubwa katika ustawi wa familia, jamii na taifa kwa ujumla.
KLABU ZA UTETEZI WA HAKI ZA MTOTO MASHULENI Shirika la Good Neighbors kwa kushirikiana na serikali pamoja na walimu lilifanikiwa kuunda klabu za utetezi wa haki za mtoto katika shule 18 zilizopo katika wilaya 3 ambazo ni Bagamoyo (9), Kinondoni (6) pamoja na Kigamboni (3). Lengo la kuundwa kwa klabu hizi ni kumwezesha mtoto kuwa na uelewa wa kutosha juu ya haki zake za msingi kama zilivyoainishwa kwenye sheria ya haki za mtoto ya mwaka 2009 na kuhakikisha kuwa, haki hizo zinalindwa na kuheshimiwa na kila mtu. Kazi kubwa ya klabu hizi ni kuelimisha jamii nzima wakiwemo watoto juu ya haki za mtoto kwa njia ya matamasha, vipeperushi, midahalo na semina mbalimbali. Shirika la Good Neighbors limekuwa likiwajengea uwezo klabu za utetezi kwa kuwapatia semina mahususi, mbinu mbalimbali za kufikisha ujumbe wa haki za mtoto pamoja na kuwawezesha katika kutoa elimu hiyo. Miongoni mwa mafanikio makubwa yaliyopatikana kutokana na kuwepo kwa klabu hizi mashuleni ni pamoja na kuongezeka kwa uelewa wa haki za watoto miongoni mwa wanafunzi mashuleni pamoja na jamii zilizo karibu na shule hizo. Pia, elimu hizo zinazotolewa na klabu kwa jamii zimepelekea kupungua kwa kiasi kikubwa kwa vitendo vya ukatili dhidi ya watoto. Shirika la Good Neighbors lina mpango wa kuendelea kuunda klabu hizi za utetezi kwenye shule mbalimbali ili kuhakikisha elimu hii inazifikia jamii nyingi zaidi kadiri iwezekanavyo.
GNI ni shirika la kimataifa lisilo la kiserikali la misaada ya kibinadamu na maendeleo ya jamii lenye kutambulika na baraza la kiuchumi na mambo ya kijamii la umoja wa kimataifa. GNI limepiga hatua kubwa katika malengo yake ya kusaidia watu dunia kote kupata maisha yenye ubora tangu kuanzishwa kwake 28/3/1991. Limeweza kufikia nchi 35 duniani kote GNI lilianzishwa 1991 jamuhuri ya watu wa korea na makao makuu yapo korea kusini. GNTZ lilianzishwa mwaka 2005 na likiwa na makao yake makuu Dar es salaam. Pia shirika toka kuanzishwa kwake Tanzania mwaka 2005 limeweza kutanuka na kufanya kazi katika mikoa ifuatayo Dar es salaam, Dodoma, Shinyanga, Pwani, Mwanza, Mbeya, Morogoro, na Kigoma.
MALENGO YETU GNTZ inajitahidi kubadilisha dunia kuwa yenye amani na usalama kwa kuhakikisha hakuna mtu yeyote atakaye pata shida ya njaa au kuathirika kwa ugonjwa wowote ule unaotibika.
KAZI ZETU □ Kutetea na kulinda haki za watoto □ Kuwajengea uwezo wananchi kiuchumi, kwa kuanzisha miradi mbalimbali kama vile ufugaji wa kuku, kilimo cha kahawa, ufungaji nyuki, kilimo cha mananasi, kilimo cha mihogo nk □ Kutoa misaada mbalimbali ya kielimu ikiwemo ujenzi wa shule, vifaa vya michezo, ugawaji wa daftari, unifomu, vitabu, nk. □ Kusaidia sekta ya afya katika kutoa elimu ya afya kwa kushirikiana na serikali pamoja na jamii, kutoa bima za afya kwa watoto, kujenga na kukarabati vituo vya afya na kutoa msaada wa vifaa mbalimbali kwa ajili ya matibabu.
VIPAO MBELE □ Tunafanya kazi mahali popote penye mahitaji bila kujali rangi, dini, itikadi na tofauti za jiografia. □ Tuna hamasisha kujitegemea na maendeleo bora ya mtu mmojammoja, familia na jumuiya kwa ujumla. □ Kulinda, na kutetea haki za watoto □ Tunaeneza ujumbe Duniani kote juu ya msisitizo wa heshima kwa wote, kuishi kwa umoja na maelewano.
MTOTO NI NANI? Mtoto ni mtu aliye na umri chini ya miaka kumi na nane.
HAKI ZA MTOTO
Plot 2407K, Block 2047B Tegeta Wazo, Dar es Salaam, Tanzania P.O Box 33104 DSM Tanzania Tel: +255 732991530 | Email: tanzania@goodneighbors.org
Haki ya Kutokutengwa Haki ya Jina na Utaifa Haki ya Kuishi na Wazazi au Walezi Haki ya Kupata Huduma Haki ya Kushiriki Michezo na Shughuli za Kiutamaduni Haki ya Huduma ya pekee kwa Mlemavu Haki kwa Mali za Wazazi Haki ya Kutoa Maoni