Akaunti za
UCB
1
AKAUNTI YA PAMOJA
2
Ni akaunti maalum kwa ajili ya vikundi mbalimbali kuweza kujiwekea fedha (amana) na kuendesha shughuli mbalimbali ili kusimamia michango kwa urahisi zaidi na kukuza mtaji wa ki/vikundi na hatimaye kutimiza malengo na mipango waliyojiwekea. Walengwa wa Akaunti ya Pamoja: • Vikundi vya Kijamii na Ukoo. • VICOBA. • Asasi na taasisi mbalimbali. Jinsi ya Kufungua Akaunti Hii ya Pamoja: •
Jaza Fomu ya maombi kutoka Uchumi Benki
•
Ambatanisha mukhutasari wa kikao, kilichoridhia kufungua akaunti Benki ya Uchumi na uonyeshe waweka sahihi wa akaunti hiyo.
•
Picha 2 za pasipoti za waweka sahihi kama walivyoonyeshwa kwenye mukhutasari.
•
Waweka sahihi kama walivyoorodheshwa kwenye mukhutasari wa kikao waje na
kitambulisho halisi kimojawapo kati ya vifuatavyo: a) b) c) d) •
• • •
Kitambulisho cha kura Leseni ya udereva Kitambulisho cha utaifa Pasi ya kusafiria.
Barua ya utambulisho wa kikundi toka kwa mtendaji wa kata au kijiji, afisa maendeleo ya jamii au mwenyekiti wa serikali ya mtaa. Hati ya usajili. Katiba ya Kikundi Kianzio kisichopungua 50,000/=
Faida za Akaunti ya Pamoja • •
• • •
•
Hakuna gharama za uendeshaji Riba nzuri ya kuvutia kila mwisho wa mwaka kulingana na kiwango cha fedha zilizoko kwenye akaunti. Haina ukomo wa kuweka akiba. Unaweza kuweka akiba wakati wowote kupitia simu ya kiganjani, kwa wakala au benki. Endapo wanakikundi watahitaji kutoa shilingi 10,000,000/ au zaidi kikundi kitachajiwa gharama nafuu. Kupata mafunzo na ushauri bure kwa viongozi na wanachama kulingana na uhitaji wa kikundi.
NI AKAUNTI MAALUM KWA AJILI YA VIKUNDI MBALIMBALI KUWEZA KUJIWEKEA FEDHA
3
4
AKAUNTI YA WATOTO (ELIMU JUNIOR) Ni akaunti ambayo mzazi/mlezi anaweza kumwekea mtoto akiba ya maisha ya baadaye “Tengeneza kesho ya mwanao kwa kumfungulia akaunti ya Elimu Junior”. Akaunti hii hufunguliwa kwa jina la mtoto chini ya usimamizi wa mzazi au mlezi. Walengwa: Watoto chini ya umri wa miaka 18. Jinsi ya kufungua Akaunti ya Watoto - Elimu Junior: • • • •
Jaza fomu ya maombi kutoka Uchumi benki. Ambatanisha kivuli cha cheti cha kuzaliwa cha mototo au kivuli cha kiapo. Picha 1 paspoti ya mtoto. Picha 2 paspoti ya mzazi/mlezi
• •
Kianzio kisichopungua 20,000. Kitambulisho cha mzazi au mlezi kimojawapo kati ya hivi vifuatavyo: a) Kitambulisho cha kura, b) Leseni hai ya udereva, c) Kitambulisho cha utaifa , d) Pasi hai ya kusafiria
• •
Barua ya utambulisho ya mzazi/mlezi toka kwa mtendaji wa kijiji/kata. Uthibitisho wa mlezi kutoka mahakamani au wakili alie idhinishwa.
Faida za akaunti ya Elimu Junior. • • • • • • •
Hakuna gharama za uendeshaji za kilamwezi. Kiwango kizuri cha riba kila mwaka kulingana na kiwango cha pesa kwenye akaunti yako. Unaweza kuweka akiba kila mara kupitia simu yako ya kiganjani,wakala au benki. Humjengea mototo utamaduni wa kujiwekea akiba. Kuweka akiba kwa mahitaji muhimu ya mtoto kama ada ya shule na fedha za matumizi. Unaweza kutoa fedha kila baada ya miezi 3 pasipo gharama ya kutolea. Utapata taarifa za benki yako kila mara pasipo gharama zozote.
TENGENEZA KESHO YA MWANAO KWA KUMFUNGULIA AKAUNTI YA ELIMU JUNIOR
5
6
AKAUNTI YA HUNDI (UCHUMI CURRENT ACCOUNT) Akaunti hii hurahisisha ulipaji wa malipo mbalimbali na kwa haraka zaidi kwa kutumia hundi ili kutimiza malengo yako ya biashara. Walengwa •
Watu binafsi
•
Vikundi vya kijamii
•
Asasi na taasisi mbalimbali za kidini na zisizo za kidini.
•
Makampuni.
Mahitaji ya kufungua Akaunti hii - Kampuni •
Hati ya Usajili kutoka BRELA
•
Leseni ya biashara
•
Hati ya utambulisho wa mlipa kodi (TIN)
•
Idhini ya bodi ya kampuni kufungua akaunti Uchumi Benki.
•
Memorandum and Article of Association (MEMART)
•
Jaza fomu ya maombi kutoka Uchumi Benki
•
Picha 2 za paspoti za waweka sahihi
•
Kianzio shilingi 50,000/= (akaunti ya mtu binafsi) na shilingi 100,000/= kwa akaunti ya kampuni au taasisi.
•
Kitambulisho kimojawapo kati ya hivi: a) Kitambulisho cha kura b) Leseni hai ya udereva c) Kitambulisho cha utaifa d) Pasi hai ya kusafiria
Faida: • Utaweza kumiliki akaunti ya fedha za kigeni (US Dolla,Euro) • Unapata kitabu cha hundi na kadi ya ATM kwa mtu binafsi. • Gharama nafuu za uendeshaji • Hakuna makato ya dirishani kila unavyotoa/ kulipa kwa hundi. • Taarifa za kibenki kila mara bila gharama zozote. • Huduma za kibenki kupitia simu ya mkononi. • Wepesi wa kuhamisha fedha kwenye akaunti zingine ndani na nje ya benki • Urahisi wa huduma za mikopo. • Muda mfupi wa kuhudumiwa. UTAWEZA KUMILIKI AKAUNTI YA FEDHA ZA KIGENI (US DOLLA, EURO)
7
AKAUNTI YA VIJANA 8
Akaunti hii ni maalumu kwa vijana wenye umri kuanzia miaka 18-35, ni akaunti mahususi kwa kuwekeza akiba na kukuza mtaji. Akaunti hii inaweza kufunguliwa na kijana au kikundi cha vijana. Walengwa: •
Kijana mwenye umri wa miaka 18-35
•
Vikundi vya vijana/wajasiriamali katika umri huo
Mahitaji: •
Jaza fomu ya maombi kutoka Uchumi Benki
•
Picha 2 za paspoti saizi
•
Kianzio kisichopungua shilingi 50,000/=
•
Kitambulisho halisi kati ya hivi: a) Kitambulisho cha kura,
b) Leseni hai ya udereva, c) Kitambulisho cha utaifa, d) Pasi hai ya kusafiria •
Barua ya utambulisho toka kwa afisa mtendaji wa kata/kijiji.
Faida za akaunti ya Vijana: •
Kiwango kizuri cha riba kila mwaka kulingana na kiwango cha fedha ulizonazo kwenye akaunti.
•
Hakuna gharama za uendeshaji.
•
Hakuna makato yoyote unapohitaji kutoa fedha
•
Hakuna ukomo wa kuweka akiba.
•
Kila mara unaweza kuweka akiba kupitia simu ya kiganjani, wakala au benki.
•
Unaweza kutoa fedha kila baada ya miezi 3 bila gharama yoyote.
•
Taarifa za kibenki pasipo gharama zozote. 9
NI MAALUMU KWA VIJANA WENYE UMRI KUANZIA MIAKA 18-35
10
AKAUNTI YA WOSIA Akaunti ya Wosia kutoka Uchumi Benki ni akaunti ya akiba iliyobuniwa kwa lengo la kusaidia wanafamilia wakati mteja wake yupo hai au amefariki kulingana na maelekezo ya awali aliyoyatoa benki. Walengwa: •
Watu binafsi.
•
Taasisi za kidini.
Faida za Akaunti ya Wosia; •
Faida kubwa kila mwaka kulingana na kiwango cha fedha ulichonacho kwenye akaunti ya Wosia UCB.
•
Hakuna makato pindi unapotoa fedha Benki.
•
Unaweza kuweka akiba kila mara kupitia simu ya kiganjani, wakala au benki.
•
Umilikishwaji pindi mmiliki wa akaunti ya Wosia amefariki.
•
Viwango vizuri vya kufungulia.
•
Taarifa za kibenki kila mara pasipo gharama yoyote.
11
ILIBUNIWA KWA LENGO LA KUSAIDIA WANAFAMILIA WAKATI MTEJA WAKE YUPO HAI
12
AKAUNTI YA AKIBA HABA NA HABA Akaunti zetu za akiba zinakupa nafasi ya kufurahia maisha kwa kuweka akiba kidogo kidogo (haba na haba) na kufanya fedha yako ikuzalishie.Ukiwa na akaunti ya haba na haba UCB unawezakufanya miamala kadri uwezavyo kupitia simu ya kiganjani, wakala, benki na kwenye ATM mashine zote za Umoja Switch nchi nzima. Mahitaji ya kufungua akaunti ya Haba na Haba: • Jaza fomu ya maombi ya Uchumi Benki • Kianzio kisichopungua 20,000 • Picha 2 za paspoti • Barua ya utambulisho toka kwa afisa mtendaji wa kijiji au kata
•
Kitambusho halisi kati ya hivi: a) Kitambulisho cha kura b) Leseni hai ya udereva c) Kitambulisho cha utaifa d) Pasi hai ya kusafiria
Faida ya Haba na Haba • Kiwango kizuri cha riba. • Unaweza kuweka akiba kila mara kupitia simu yako ya kiganjani, wakala au Benki. • Gharama nafuu za uendeshaji • Huduma za kibenki kupitia ATM kwa saa 24. • Unaweza kufungua akaunti ya fedha za kigeni (US Dollar,Euro) • Unaweza kufungua akaunti ya pamoja (Saving Joint account). • Kuhamisha fedha.
13
ILIBUNIWA KWA LENGO LA KUSAIDIA WANAFAMILIA WAKATI MTEJA WAKE YUPO HAI
14
TAJIRIKA FIXED ACCOUNT (AKAUNTI YA MUDA MAALUMU) Tajirika Fixed Account ni akaunti inayozalisha riba kulingana na kiwango cha riba na muda ambao fedha hizo hukaa benki. Walengwa: • Watu binafsi • Taasi za kidini na asasi mbalimbali • Kampuni • Vikundi
Faida: • Viwango vizuri vya riba. • Hutumika kama dhamana ya mkopo. • Haina gharama zozote za uendeshaji. • Haina makato yoyote.
15
AKAUNTI INAYOZALISHA RIBA KULINGANA NA KIWANGO CHA RIBA NA MUDA AMBAO FEDHA HIZO HUKAA BENKI
AKAUNTI YA HAZINA Akaunti hii inampa mstaafu uhuru wa kuweka na kutoa fedha zake bila gharama yoyote lakini pia atapata faida kulingana na fedha zilizopo katika akaunti yake.
16
Mahitaji ya kufungua akaunti ya Hazina: • Jaza fomu ya maombi kutoka Uchumi Benki • Kianzio kisichopungua shilingi 50,000/= • Picha 2 za paspoti • Barua ya utambulisho toka kwa afisa mtendaji wa kijiji au kata • Kitambulisho halisi kati ya hivi vifuatazo: i. Kitambulisho cha kura ii. Leseni hai ya udereva iii. Kitambulisho cha utaifa iv. Pasi hai ya kusafiria Faida ya akaunti ya Hazina • Haina makato yoyote ya mwezi • Kiwango nafuu cha kufungua akaunti • Faida kubwa kulingana na salio kwenye akaunti yako • Kuweka pesa bila ukomo kwa kadiri uwezavyo • Haina kima cha chini • Wastaafu watakuwa na fursa ya kupata mikopo yenye riba nafuu na yenye mchakato rahisi ili kuweza kujikimu na kuboresha maisha yao katika kipindi cha ustaafu wao. • Kutoa fedha bure ndani ya Benki.
AKAUNTI YA MKULIMA Ni akaunti iliyotengenezwa mahsusi kwa ajili wakulima na wafugaji wadogo. Mteja anaweza kuweka fedha kidogokidogo kadri anavyopata na kupata faida. Mahitaji ya kufungua Akaunti ya Hazina: • Jaza fomu ya maombi kutoka Uchumi Benki • Kianzio kisichopungua 5,000 tu • Picha 2 za paspoti • Barua ya utambulisho toka kwa afisa mtendaji wa kijiji au kata • Kitambulisho halisi kati ya hivi vifuatavyo: i. Kitambulisho cha kura. ii. Leseni hai ya udereva. iii. Kitambulisho cha utaifa. iv. Pasi hai ya kusafiria. Faida za Akaunti ya Wakulima; • Mmiliki wa akaunti hii anaweza kupata huduma za kibenki kwa saa 24/7 kupitia wakala, simu au ATM • Hakuna gharama zozote za uendeshaji • Hakuna makato ya mwezi • Mchakato rahisi wa kufungua akaunti hii • Kiwango nafuu cha kufungulia akaunti • Kuweka pesa bila ukomo,kadri uwezavyo • Kupata mkopo kwa masharti nafuu. • Kupata ushauri wa kifedha. • Hakuna makato unapotoa fedha dirishani.
17
NOTES
18
OUR BRANCH (NETWORKS) MOSHI LUTHERAN Centre Building, Market Street (Opposite the Central Bus Terminal) P.O. Box 7811, Moshi, Tanzania. (+255) 748 465 131 customerservice@uchumibank.co.tz MOSHI LUTHERAN Centre Building, Market Street (Opposite the Central Bus Terminal) P.O. Box 7811, Moshi, Tanzania. (+255) 748 465 131 customerservice@uchumibank.co.tz MOSHI LUTHERAN Centre Building, Market Street (Opposite the Central Bus Terminal) P.O. Box 7811, Moshi, Tanzania. (+255) 748 465 131 customerservice@uchumibank.co.tz MOSHI LUTHERAN Centre Building, Market Street (Opposite the Central Bus Terminal) P.O. Box 7811, Moshi, Tanzania. (+255) 748 465 131 customerservice@uchumibank.co.tz MOSHI LUTHERAN CENTRE Building, Market Street (Opposite the Central Bus Terminal) P.O. Box 7811, Moshi, Tanzania. (+255) 748 465 131 customerservice@uchumibank.co.tz MOSHI LUTHERAN CENTRE Building, Market Street (Opposite the Central Bus Terminal) P.O. Box 7811, Moshi, Tanzania. (+255) 748 465 131 customerservice@uchumibank.co.tz
Moshi Lutheran Centre Building, Market Street (Opposite the Central Bus Terminal) P.O. Box 7811, Moshi, Tanzania. (+255) 748 465 131 customerservice@uchumibank.co.tz