Siku ya dunia ya Ndege Wanaohama 2011

Page 1

Siku ya dunia ya Ndege wanaohama 2011 Mabadiliko ya matumizi ya ardhi kwa mtazamo wa ndege 14 – 15 Mei

Ungana nasi kusherehekea Siku ya Ndege Wanaohamahama 2011! Ndege wanaohamahama hupaa maelfu ya kilomita kila mwaka, wana mtazamo wa kipekee wa dunia. Kwa bahati mbaya, mtazamo huo usiokuwa na ushindani huwawezesha kutambua mabadiliko makubwa ambayo sasa ni tishio kwa mazingira ya sayari yetu. Kila mwaka maeneo yanayotegemewa na ndege wanaohamahama katika safari zao yanaharibiwa. Kulingana na jinsi mazingira hayo yanavyoharibiwa, hakuna uhakika kwamba makao yanayohitajika na ndege hao katika njia yao ya kuhama, yatakuwepo wakati mwingine watakaporejea. Mengi ya mabadiliko hayo mengi yanasababishwa na matumizi mabaya ya ardhi na binadamu, na yana pigo la moja kwa moja kwa idadi ya ndege wa kuhamahama, ambao wanaathiriwa sana na mabadiliko yoyote yanayovuruga maeneo wanayotumia katika mzunguko wao wa kuhama. Vipengee vingi vya matumizi ya ardhi na binadamu vinaharibu makao ya ndege hao kabisa. Kwa mfano, ukuaji wa miji na mbinu mbovu ya kilimo inaweza kutatiza na unaweza kuharibu kanda nzima inayotumiwa kama njia ya kuhama ya ndege hao kila mwaka. Tofauti na hayo, matumizi ya ardhi na mafuta mbadala huondoa au huharibu chemichemi ya maji muhimu na makao ya aina nyingi za ndege wa kuhamahama. Ingawa maisha ya binadamu yanategemea mabadiliko haya ya maeneo asili, matumizi mema ya ardhi ni muhimu ili kupunguza athari ya uharibifu wa raslimali kama vile maji, mchanga, madini, mimea na wanyama -wakiwemo ndege wa kuhamahama. Kauli mbiu ya mwaka huu ya kuadhimisha Siku ya ndege wa kuhamahama Duniani ni ‘Mabadiliko ya matumizi ya ardhi kwa mtazamo wa ndege’. Tunataka kuhamasisha umma kuhusu mabadiliko makubwa yanayosababishwa na matumizi ya ardhi na binadamu kwa ndege wa kuhamahama na mazingira wanayotegemea. Ungana na wengine kote duniani na ushiriki katika maadhimisho ya siku ya ndege wa kuhamahama duniani kuanzia tarehe 14-15 Mei 2011 kwa kupanga matukio ya kuwatizama ndege, mipango ya kuelimisha, hotuba, maonyesho ya sanaa na matukio mengine: kwa njia zozote utakazotumia, mchango wako utasaidia kufanikisha kampeni hii. Tafadhali tuarifu na wengine kote duniani kuhusu mipango yako ya WMBD kwa kuisajili katika tovuti yetu ya WMBD: www.worldmigratorybirdday.org. Siku ya kusherehekea ndege wanaohamahama duniani ni ya kimataifa, kampeni ya hamasisho la kila mwaka la kuimarisha uhifadhi wa ndege wa kuhamahama na mazingira yao kote duniani. Imeandaliwa na shirika la AfricanEurasian Migratory Waterbird Agreement (AEWA) na Convention on Migratory Species (CMS): Mikataba miwili ya kimataifa kuhusu wanyama pori inayoratibiwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la mradi wa uhifadhi wa Mazingira, (UNEP). Kwa maelezo zaidi: www.worldmigratorybirdday.org Mabango ya WMBD 2011 yatapatikana afisini ya kamati la UNEP/AEWA kutoka mwezi wa Machi 2011. Kwa budi ya kutafsiri bango kwa lugha yako ya mama –tafadhali angiza toleo. Kwa kuangiza toleo la bango (WMBD) na kwa maelezo zaidi: Bibi Dunia Sforzin Kamati la UNEP/AEWA Telefoni: +49 (0)228 815 2454 Kipepesi +49 (0)228 815 2450 Barua pepe: contact@worldmigratorybirdday.org


Turn static files into dynamic content formats.

Create a flipbook
Issuu converts static files into: digital portfolios, online yearbooks, online catalogs, digital photo albums and more. Sign up and create your flipbook.