Ni mwongozo wa vitendo, mahususi kwa viongozi na wawezeshaji wenye nia ya kusaidia mashirika kufanyakazi na kukua kwa ustawi zaidi, mashirika yenye kujali watu na yenye kutumia mbinu bora zaidi katika kujenga jamii yenye misingi ya utu. Mwongozo huu umeandaliwa na kundi la mguu peku.
Mwongozo huu pamoja na tovuti yake umebeba dhana , mbinu, masimulizi na shughuli zilizofanyiwa utafiti na kujaribiwa. Lengo la mwongozo ni kuhamasisha na kuboresha mbinu za kuwezesha mashirika na harakati za kijamii katika kukabiliana na changamoto za kutenda, kujifunza, kukua na kupokea mabadiliko kwa lengo la kutimiza mahitaji ya jamii inayowazunguka. Ingawa mwongozo huu umewalenga viongozi na wawezeshaji wa mashirika (azaki za kiraia), ni matarajio yetu kuwa mwongozo huu utakuwa wa manufaa kwa mtu yeyote mwenye nia ya dhati ya kujenga mashirika yanayojali watu.