KITABU
Kwa Ajili ya Kuimarisha Maelewano kati ya Jamii na Huduma za Polisi wa Edmonton
KITABU kwa ajili ya kuimarisha amani
Nini Majukumu ya Polisi Katika Mji Wa Edmonton?
Kitabu hiki ni kwa ajili ya kusaidia kuelewa jukumu la polisi wa Edmonton, kutoa taarifa ya jinsi ya kupata huduma za polisi, na kueleza nini cha kutarajia kama utakutana na polisi. Pia kuelezea haki na wajibu wa jamii zote mbili na polisi.
Jukumu la Huduma ya Edmonton Polisi ni kutoa ulinzi wa maisha na mali, kudumisha amani ya umma na hali nzuri, na kuzuia, kuchunguza na kutatua uhalifu. Pindi polisi watashindwa kuzuia uhalifu, lengo lao ni kuchunguza na kuleta wahalifu katika mfumo wa sheria.
Uelewe vizuri ni jinsi gani Polisi inaweza kukusaidia, pia kusaidia kuimarisha amani na Huduma za Polisi ya Edmonton.
Watu wa Edmonton wana haki ya kujisikia salama katika nyumba zao na jamii zao. Polisi wanaelewa matatizo ya jamii tofauti na kufanya kazi ki-ukaribu sana na jumuiya hizo kuzuia uhalifu usitokee. Lengo lao ni kuboresha ubora wa maisha kwa wananchi wote katika mji wetu.
Tunatoa shukrani za dhati kwenye kitengo cha Uraia na Uhamiaji wa Canada kwa msaada wao wa kifedha, pamoja na Huduma za Polisi za Edmonton kwa ushirikiano wao, na kujitolea kuhudumia Jumuiya ya wakazi wa Edmonton na utofauti wa mira zao. Ushiriki wao husika imesababisha uzalishaji wa hiki kitabu
Maofisa wa polisi wana wajibu wa kufanya kazi zao kwa taaluma na kuonyesha kimaadili tabia katika kila kitu chao. Sheria ya Polisi ya Edmonton inasema kwamba wajumbe hawatakuwa na ubaguzi dhidi ya mtu yeyote kwa misingi ya rangi, taifa au kikabila asili, lugha, rangi, dini, jinsia, umri, kiakili au kimwili ulemavu, ngono, au nyingine yoyote ile.
Alliance Jeunesse-Famille de l’Alberta Society (AJFAS)
Kazi Ya EPS Inaongozwa na Uwazi wa Maadili: UMAHIRI - Kufanya mambo ya haki kwa sababu sahihi wakati wote. UWAJIBIKAJI - kuwajibika kwa maamuzi yetu wenyewe na vitendo. HESHIMU - Kumtendea wingine kama unavyotaka kutendewa. UBUNIFU - kutafuta ubora na ubunifu. UJASIRI - Kudumisha nguvu na changamoto kubwa. JAMII – Heshima na adabu za jamii mbali mbali kwamba ni wajibu wetu kulinda na kuhudumia jamii zetu.
Namba za Simu za Kuwasiliana Na hudumu za Polisi Edmonton Piga 9-1-1 kwa dharura tu. Kwa yasiyo ya dharura piga 780-423-4567 Nini ni dharura? Dharura ni pamoja na moto, uhalifu ukiwa unafanyika, au matibabu au tishio la kupoteza maisha ambayo linahitaji gari la wagonjwa (ambulensi). Nini siyo dharura? Yasiyo ya dharura ni pamoja na vitu kama wizi, kupoteza passport, udanganyifu na ajali ya gari ambayo hakuna majeruhi. Piga 780-423-4567 • Kama unahitaji mahudhurio ya ofisa wa polisi mahali ulipo • Kama unahitaji ushauri wa jinsi ya kuendelea na ripoti ya makosa ya jinai
Nini Cha Kufanya Polisi Wakaja Nyumbani Kwako? Nyumba yako ni mahali takatifu sana. Kwa kweli, mahakama ya Canada imeweza kutambua utakatifuwa nyumba ya mtu. Una haki ya siri katika nyumba yako na polisi wanaweza kuingia katika nyumba yako kutokana na hali fulani.
9-1-1 ni kwa DHARURA tu Ukipiga 9-1-1, opereta atajibu kwa kusema, ‘Dharura. Je, unahitaji Polisi, Moto au Ambulensi? Kama opereta wa 9-1-1 haelewi lugha unayozungumza , wao watakuuliza swali ili kujua ni lugha gani wewe unazungumza. Kama huwezi kuwasiliana kwa sababu yoyote, opereta mara moja atatuma maofisa wa polisi kwenye anwani hiyo uliyopigia simu.
Polisi anaweza kuingia kwenye nyumba yako wakati: • Mkiwakaribisha ndani au kuwaacha waingie ndani • Kuna hali ya dharura, kama vile wakati wewe umepiga 9-1-1 • Wana hati ya kisheria ambayo inaruhusu waokuingia, kama vile hati tafuta iliyotolewa na mwamuzi au hakimu
Kama opereta atatambua lugha unayoongea, atakuunganisha na Laini ya huduma ya lugha.
Ikiwa polisi watakuja mlangoni kwako, wajibu na kumbuka kuwa kipaumbele cha polisi ni kuhakikisha usalama wa watu.
Mkalimani ambaye anazungumza lugha yako atakusaidia kumwaambia opereta wa 9-1-1 dharura yako ni nini na wewe watakuletea huduma unayohitaji.
Wakati mwingine, ofisa wa polisi anaweza asielewe au kujua mila tofauti za utamaduni wako. Ni muhimu sana kumfahamisha Polisi ofisa matatizo yako. Kwa mfano, mwambie ofisa wa Polisi kama kuna mahali maalum kwa ajili ya maombi. Usiogope kuuliza maswali kama haukuelewa kitu. Pia, usiogope kuelezea jambo muhimu ambalo ofisa anaweza kuwa hakulielewa. Ofisa yupo kwa ajili kukusaidia wewe na jamii.
Itakuwaje Kama Siwezi Kuongea Au Kuelewa Kiingereza? Kwa wanachama wengi katika jamii, Kiingereza ni lugha ya pili. Kama huwezi kuzungumza Kiingereza, unatakiwa ujaribu kuwa na mtu katika familia au rafiki ambaye atakusaidia katika mambo yanayohusiana na polisi. Kama hili haiwezekani, Huduma za Polisi za Edmonton zina orodha ya Polisi wanaoongea lugha tofauti ambao wanaweza kukusaidia. Usije kusaini mkataba wowote au makaratasi yeyote ya kisheria mpaka ujue kikamilifu ni kitu gani unakubali.
Nifanye nini wakati Ofisa wa Polisi Akinisimamisha Mitaani? Unaweza kutambua maofisa wa polisi na sare zao. Mara nyingine, unaweza kukutana na maafisa ambao hawa javaa sare. Kama una mashaka juu ya utambulisho wa ofisa wa polisi, unaweza kuwaomba wakuonyeshe vitambulisho vyao rasmi, ikiwa ni pamoja na jina la Ofisa na namba ya beji. Ofisa anaweza kuuliza jina lako, anwani, nini unafanya au unakokwenda. Katika baadhi ya matukio, Ofisa anaweza kuuliza kuona nyingi, hutakiwi kuonyesha kitambulisho chako. Hata hivyo, ni vyema kuwa na heshima na kujibu maswali ya ofisa wa Polisi. Kama ukikataa kujibu maswali ya Ofisa au Ofisa anadhani wewe si-mkweli, Ofisa anaweza kuchukua hatua za kuchunguza kwa kina zaidi. Lengo la kila mtu ni kufikia azimio au kutatua uhalifu.
Maofisa wa Polisi wanaweza kukushika au kukuweka chini ya ulinzi kutokana na hali mbili: 1. Kama wakidhani au kuamini kwamba wewe ulitenda makosa 2. Kama wao kweli wamekuona wewe anayefanya kosa Kama ofisa wa polisi anakushika au kukukamata kwenye moja ya hali hizi mbili, lazima uwape jina lako, anwani, na kitambulisho chako. Maofisa wa polisi wameapishwa na wajibu wao ni kuzuia na kuchunguza uhalifu na kuweka amani. Kazi zao ni pamoja na kuhoji mashahidi kutokana na uhalifu uliotokea, na kuhoji watuhumiwa. Kama wahalifu wanaweza kutambuliwa kirahisi, au kotokana na mavazi yao, ingekuwa rahisi kufanya kazi ya Polisi, lakini ukweli ni kwamba maofisa wa polisi ni lazima wachunguze. Hii ina maana kuwa ofisa wa polisi anaweza kukuamba aongee na wewe kwa sababu ambazo zinaweza zisiwe na maana yeyote wakati huo. Je, usichukulie kama ni kosa ikiwa ofisa wa polisi atakuuliza maswali. Wanafanya kazi zao, kuzuia uhalifu na kusaidia kukulinda wewe na jamii salama.
Je Ninalazimika kujibu maswali ya Polisi au Kujitambulisha Mwenyewe?
Nifanye Nini Polisi Akinisimamisha Wakati Naendesha Gari?
Kwa ujumla, haulazimiki kujitambulisha kwa askari polisi. Hata hivyo, kuna mambo ya kipekee, ambayo ni lazima ujitambulishe, mambo hayo ni kama yafuatayo: • Kama ni kuendesha gari • Kama umafanya kosa kama vile kosa la pombe, kosa la uzurulaji,kosa la kuendesha gari, au kosa la jinai.
Polisi wana mamlaka ya kusimamisha gari wakati wowote ili kuhakikisha kwamba dereva hajalewa pombe au madawa ya kulevya, gari haina matatizo, dereva ana leseni halali, na gari ina kibinafsi halali. Sababu kubwa polisi atasimamisha gari ni kuchunguza makosa ya usalama barabarani.
Katika mazingira haya, ni vyema kushirikiana na kujibu maswali ya ofisa wa Polisi.
Kosa la Uendeshaji: kuongeza kasi ya gari, kupita taa nyekundu au alama za kusimama Kushindwa kufanya, au keundesha karibu sana na gari jingine.
Ikiwa Polisi watadhani kwamba umefanya kosa au wanamashaka, watataka kujua wewe ni nani. Kuna sababu kadhaa kwa ajili ya kuwaambia polisi wewe ni nani: 1. Kama polisi wanatafuta mtu mwingine, unaweza kuepuka kizuizi au kukamatwa kwa kuonyesha kwamba wewe siyo mtu huyo; 2. Ikiwa polisi wanaamini kwamba umefanya kosa, na haujitambulishi kwao, wanaweza kukuweka chini ya ulinzi kwenye kituo cha Polisi mpaka wajue wewe ni nani; 3. Ikiwa Polisi wanafikiri umefanya kosa dogo, na ukajitambulisha mwenyewe wakaridhika, wanaweza kukupatia tiketi tu au watakupa taarifa ya tarehe unayotakiwa kufika mahakamani badala ya kukuweka chini ya ulinzi.
Yasiyo makosa ya Uendeshaji: Kushindwa kuvaa mikanda ya kiti, taa za breki mbovu, au kushindwa kutoa leseni ya dereva, usajili wa magari, au ushahidi wa kibinafsi wa gari.
Je Ofisa wa Polisi Anatakiwa Kunieleza Sababu Gani Niko Chini Ya Ulinzi? Ndiyo! Maofisa wa polisi lazima waambie watu sababu zinazowafanya wakamate watu au kuwekwa kizuizini. Hii ni matakwa ya kifungu 10 (a) ya Mkataba wa Canada wa Haki na Uhuru.
Makosa ya magari barabarani yako katika makundi mawili:
Sababu zingine zinazofanya usimamishwe wakati unaendesha ni pamoja na: • Kulewa pombe na kuendesha gari (dereva mlevi) na vituo vya uchunguzi. • Hatari au kutojali unaendesha gari • Uchunguzi wa uhalifu. Kwa mfano, wewe, wasafiri wako na / au gari yako inaweza kuwa ni sawa na maelezo ya mtu Ofisa wa Polisi anatafuta. • Usalama wasiwasi Mara nyingi, kusimamisha magari ni kipengele hatari zaidi kwenye kazi ya polisi. Maofisa wengi hujeruhiwa au huuawa wakati wakifanya kazi ya kusimamisha magari kuriko kazi nyingine yoyote. Maofisa lazima wajue matendo na tabia ya abiria wa gari, pamoja na kuangalia magari mengine. Kwa sababu hizi, maofisa wanafundishwa kusimamisha magari kwa kufuata utaratibu fulani. Unaweza kuwa na wasiwasi kwa nini wanakufatilia, lakini lengo lao sio kuwatisha nyinyi.
Ukisimamishwa na polisi wakati unaendesha gari • Punguza mwendo na usimame upande wa Upande wa kulia wa barabara. • Bakia ndani ya gari mpaka utakapo ruhusiwa na ofisa. • Fanya kile Ofisa anakwambia ufanye. • Weka mikono yako peupe (wazi) ili ofisa aione na usigeuke geuke ghafla. • Kuwa tayari kutoa nyaraka unazoombwa na Ofisa wa Polisi. Kama dereva wa gari, wewe ndio; kwa mujibu wa sheria, unatakiwa kuonyesha leseni, usajili na ushahidi wa kibinafsi wa gari. • Kama hati ziko kwenye pochi, au mfuko wa fedha, mwambie ofisa mapema kwamba utachukua vielelezo kutoka hapo. • Ukipewa tiketi ichukue kitulivu kuchukua tiketi sio kukubali kosa. Ukiwa ni dereva, ni wajibu wako pia kuhakikisha kuwa abilia wako wanafuata sheria. Sana sana wakiwa wanaonyesha mwenendo mbaya barabarani, kama vile kutupa vitu nje ya dirisha la gari, au kuninginia nje ya dirisha. Vile vile ni lazima uhakikishe kwamba abilia wako wamejifunga mkanda.
Haki Zangu Ni Zipi Ikiwa Nimewekwa Chini Ya Ulinzi? Mkataba wa Canada wa Haki na Uhuru Umetoa Sheria na Haki Zinazokulinda wewe ikiwa Umekamatwa au kuwekwa kizuizini na polisi. Haki hizi ni pamoja na: • Haki ya kufahamishwa ni kwa nini umekamatwa au kuwekwa chini ya ulinzi. • Haki ya kupata mwanasheria bila kuchelewa na ufahamishwe haki zako. Neno”Bila Kuchelewa” lina maana kwamba wakati kila kitu kimetulia na kila mtu yuko salama. • Haki ya simu kwa mwanasheria yoyote unayetaka. • Haki ya ushauri wa bure kutoka kwa wakili wa msaada wa kisheria. Kama umri wako ni chini ya miaka 18, una haki ya nyongeza ya kuwa na uwezo wa kuongea na mzazi au mtu mzima sahihi haraka iwezekanavyo. Polisi ni lazima wakueleze haki hizi.
Itakuwaje Nikikamatwa Na Sijui Kuongea Kiingereza? Kama wewe umakamatwa au umewekwa kizuizini na huwezi kuzungumza Kiingereza, polisi lazima kuchukua hatua ya kuwasiliana na wewe kwa lugha yako, kama kutumia mkalimani. Hii ni kwa sababu ya wao waweze kukufahamisha haki zako, na wakueleze hali ya kutolewa kwako kutoka kizuizini.
Ni Kipindi Gani Office wa Polisi Aneweza Kukupekua? Kwa ujumla, nguvu ya Ofisa wa polisi ya kukupekua inategemea na hali hasili ilivyo na imani ya Ofisa wa polisi. Kama umekamatwa, polisi wanaweza kukupekua kuona kama,kuna vitu ambavyo vinaweza kusaidia utoroke na ushahidi wa kosa ambalo umekamatwa nalo. Wao kwa kawaida “hupekua mwili,� polisi ofisa atakupekua mavazi yako yote, na mifuko yako yote. Hii haihusishi kuvua nguo labda kama umevaa kofia, jacketi au glove. Kulingana na hali, wanaweza kuwa na uwezo wa kupekua mazingira yako ya karibu, ikiwa ni pamoja na gari yako kama ulikuwa ndani ya gari umekamatwa na polisi. Kama umewekwa kizuizini kwa muda mfupi kwa sababu ya upelelezi, ofisa wa polisi wanaweza kukugonga kidogo kidogo na mikono yao kuanzia juu ya mwili wako mpaka chini, ili wahakikishe kwamba hauna silaha yeyote. Kama hujawekwa chini ya ulinzi au kizuizini, unaweza kukataa kupekuliwa. Vile vile unaweza kuwaruhusu polisi wakupekue kama kufanya hivyo kutawapunguzia tuhuma zao. Hata kama awali uliwakubalia wakupekue, unaweza kuwaomba waache kukupekua wakati wowote. Kama unafikili kwamba upekuaji ulikuwa sio sahihi, usimsumbue ofisa wa polisi. Badala yake fuata njia za kutoa malalamiko yako ambazo zimeorodheshwa katika kifitabu hiki au wasiliana na mwanasheria.
Itakuwaje Kama Nina Malalamiko Kuhusu Polisi? Wananchi wanatarajia kuwa maofisa wetu wa polisi watakuwa wamejiweka katika kiwango cha juu cha ubora. Wasiwasi wa raia na malalamiko yao yakiletwa mbele, ni lazima yachunguzwa kwa njia ya haki na kwa wakati muafaka. Tawi la wataalam viwango la EPS lina jukumu la kuchunguza malalamiko dhidi ya polisi kwa njia ya haki, ya uhakika na bila ya upendeleo. Unaweza kulalamika kuhusu sera au huduma zinazotolewa na Polisi ya Edmonton, au juu ya mwenendo wa ofisa wa polisi wa EPS. Malalamiko yeyote ni lazima yawe ki-maandishi na ni lazima ya sainiwe. Unaweza kuandika malalamiko yako kwenye barua au unaweza kutumia fomu ya kiwango, ambayo unaweza kuipata kutoka kituo cha polisi ya EPS yoyote au kutoka kwenye tume ya Polisi ya Edmonton. Ni lazima kufanya malalamiko ndani ya mwaka mmoja baada ya tokeo hilo lilitokea. Malalamiko ni lazima barua itumwe, faksi au uipeleke kwa mtu yeyote wa EPS kituo cha polisi, Ofisa wa EPS, au kwa utume wa Polisi Ofisi. Unaweza pia kupigia simu Polisi Ya Huduma ya Edmonton, mtaalamu Waviwango tawi kwa nambari ya simu 780-421-2676
Ili Kufikia Tume Ya Polisi Ya Edmonton: Katika maeneo ya Edmonton eneo: Simu: (780) 414-7510 Fax: (780) 414-7511 Au andika kwa: Tume ya Polisi Edmonton (Edmonton Police Commission) Suite 171, 10235-101 Street Edmonton, Alberta T5J 3E9 Tume ya Polisi ya Edmonton inatoa mwangaza wa huduma za Polisi wa Edmonton. Ni kazi yao kuhakikisha kwamba huduma ya polisi hutoa ufanisi, ufanisi na uwajibikaji wa polisi kwa watu wote wa Edmonton. Utaalamu na ufanyaji kazi ya upolisi kwa dhati ndio sifa ambazo EPS na Tume ya Polisi ya Edmonton wanachangia. Tume huhakikisha kwamba malalamiko yote yanashughulikiwa kwa ufamisi wa pande zote mbili.
Nawezaje Kuwa Ofisa Wa Polisi? Huduma za Polisi zinayo juhudi ya dhati kutafuta watu ambao watawakilisha jamii mbalimbali za mji wetu kuwa maofisa wa polisi. Hapa Edmonton utamaduni na mila mbali mbali umeongezeka na ni lengo la huduma za polisi Edmonton kuongeza huduma za polisi wakizingatia jamii inayohudumiwa. Ili ufikiriwe kujiunga katika kazi ya upolisi, ni lazima uwe na angalau sifa chache kama zilivyoorodheshwa na sheria za huduma za polisi.
Hasa lazima: • Uwe raia wa Canada au uwe mkazi wa kudumu wa canada; • Uwe na uwezo wa kufanya kazi hiyo kiakili na kimwili,Ukuzingatia usala wako na usalama wa watu wengineKatika jamii; • Uwe umemaliza dalasa la 12 au sawa yake (GED). Ikiwa ulisomea nje ya Canada, cheti cha Tathmini ya Kimataifa Kinahitajika. • Uwe na tabia nzuri na mwenendo mzuri, Kwamba uwe ni mtu ambaye watu wengine watafuata mfano wako wa kuwa mwaminifu na muadilifu; • Uwe na leseni halali ya udereva ya Alberta na usiwe na makosa zaidi ya sita yatakayokukusanyia pointi mbaya; • Uwe na vyeti halali vya huduma ya kwanza/CPR Daraja C. Wakati wa kuulizwa maswali ya kibinafsi; • Uweze kupita wakikuchunguza kuhusu usalama pamoja na mambo yako yaliyopita pamoja na mikopo na hundi ya kumbukumbu.
Kwa habari zaidi: nenda katika tovuti ya Huduma ya Polisi kwa www.edmontonpolice.ca au kupiga 780-421-2233
SWAHILI VERSION
Huduma za Polisi wa Edmonton kukubali kwa shukrani za Alliance Jeunesse-Famille de L’Alberta Society kwa ajili ya kujenga dhana ambayo imesababisha uzalishaji wa kijitabu hiki.
AJFAS’ main mission is to prevent crime amongst Francophone immigrant youths and families, as well as to help them find a sense of belonging in the Albertan society and workplace.
Translated by The Family Centre