Moduli 2, Kilimo Mseto Na Mzunguko (revised)

Page 1

Mkulima Mbunifu Moduli namba 2

KILIMO MSETO NA MZUNGUKO Kilimo huanza kwa kupanda mazao kwa mzunguko

Mbinu za asili za kilimo zinaweza kusaidia kuboresha kilimo na kuleta ufanisi kwa wakulima wadogo wadogo. Kulima kwa mzunguko ni mbinu namba moja, na situ katika kilimo hai. Ni muhimu sana katika kulinda mazao, na kuwezesha kuwa na rutuba endelevu katika udongo, na chakula cha uhakika - na mtindo huu unapatikana bila gharama yoyote kwa kila mmoja.

Kulima kwa mzunguko: Muhumu kwa mazao yenye afya Kilimo cha mzunguko siku zote kimekuwa kama moyo kwa matokeo mazuri ya kilimo. Kama aina moja ya zao likipandwa katika eneo moja kwa misimu tofauti mfululizo, unaweza kuona kuwa linafanya vibaya kila wakati. Hii inafahamika na wakulima wote ulimwenguni kote kwa karne nyingi, wakulima wamekuwa wakitumia mfumo huu wa kulima kwa mzunguko ili kuepuka madhara hayo. Ni kwa siku za hivi karibuni tu mtindo huu umetelekezwa na baadhi ya wakulima katika sehemu chache duniani. Mbolea na madawa ya viwandani yanaweza lakini ni kwa kitambo tu, huleta madhara mabaya yanayozuia kuendeleza mazao. Baada ya muda mrefu kiasi zaidi cha mbolea na madawa huhitajika kwa lazima, ambapo husababisha kuongezeka gharama, athari za kemikali, na kufanya wadudu na magonjwa kujenga usugu wa madawa.

Faida zaidi: Udongo bora na uhakika wa chakula • Mzunguko wa mazao huboresha muundo wa udongo kutokana na mizizi tofauti, na mazao tofauti. Mizizi inayoenda chini sana husaidia kulainisha udongo, kuwezesha ardhi kunyonya maji na kuongeza unyevu kwenye udongo. Rutuba ya udongo hubaki ilivyo au kuongezeka kutokana na aina ya mazao yanayopandwa kwa mzunguko, na mengine kuwa na uwezo wa kuongeza nitrojeni kwenye udongo mfano jamii ya mikunde ambayo pia ipo kwenye mzunguko. • Katika mzunguko mzuri, zao moja hufuata lingine katika hali ambayo udongo hufunikwa ili kuzuia mmomonyoko wa udongo. • Kilimo cha mzunguko huongeza uhakika wa chakula: Endapo aina nyingi za mazao zitapandwa na zao moja likaanguka, kutakuwa na madhara kidogo sana kuliko vile ambavyo aina chache za mazao zingepandwa.

Kwa nini misimu yote kilimo cha mzunguko kinahitajika Kuna sababu mbili kubwa ni kwa nini mzunguko wa mazao ni muhimu:

Mzunguko wa mazao unaopendekezwa (fuata mtiririko). Anza na zao tofauti katika sehemu tofauti shambani mwako.

Jumuisha majani ya malisho

Kanuni tofauti kwa mazao tofauti! Ni muda gani unatakiwa kusubiri kabla ya kupanda aina flani ya zao katika eneo moja? Hii inategemeana na aina ya wadudu na magonjwa yanayofungamana na zao hilo. Baadhi ya magonjwa na wadudu wanaweza kuishi kwenye udongo kwa miaka mingi. Wengine hawawezi kuishi kwa muda mrefu. Kwenye jedwali la 1 “Jamii ya mimea na mimea inayopandwa mara kwa mara kwa misimu tofauti” katika ukurasa unaofuata, unaweza kuona ni kwa namna gani unavyoweza kupanda mazao yanayopandwa mara kwa mara katika eneo moja, na ni matatizo gani unaweza kukumbana nayo endapo utapanda mara kwa mara. Mboga mboga zinaathiriwa zaidi na magonjwa kuliko nafaka, hivyo zinatakiwa mzunguko kwa umakini sana. Kuwa mzoefu wa aina ya mimea

1. Aina nyingi za magonjwa na wadudu, na hata magugu, hutokana na aina flani ya mimea na yanaweza kuongezeka pale tu kunapokuwa na aina ya zao ambalo hutegeana. Huweza kuishi wakati wa kiangazi na hata baridi kwa kuishi kwenye masalia shambani. Wanafurahia sana endapo msimu ujao utapanda tena aina ya zao ambalo ni chakula chao. Wataanza mara moja kuzaliana zaidi.

Aina ya mimiea inayotokana na jamii ya mimea inayofanana, kwa kawaida huathiriwa na aina inayofanana ya wadudu na magonjwa. Hii ni kwa sababu viazi mviringo, nyanya, pilipili hoho, na bamia, vyote vinatoka katika familia moja ya jamii ya mimea, hivyo unaweza kupanda moja wapo katika sehemu yako ya shamba unayofanya mzunguko wa mazao katika mwaka.

2. Wakati wa ukuaji, kila zao linahitaji aina flani ya virutubisho kutoka kwenye udongo. Kama ukipanda aina moja ya zao katika sehemu moja msimu kwa msimu, hii itasababisha kudhoofisha udongo, ukuwaji hafifu, na kupata mimea dhaifu ambayo pia ni rahisi kushambuliwa na wadudu na magonjwa.

Ni vizuri kufanya mzunguko wa mazao ya majani, matunda, mazao ya mizizi, jamii ya mikunde, na nafaka kama vile ambavyo jamii nyingi za kiafrika tayari wanafanya. Wazo hili huzingatia utofauti wa virutubisho vinavyohitajika. Lakini kwa afya ya mimea hii haitoshi, kama unavyoweza kuona kwenye mfano wa nyanya (zao linaloliwa tunda) na viazi (zao la mizizi) yote ni matunguja (nightshade) na hayatakiwi kufuatana.


Turn static files into dynamic content formats.

Create a flipbook
Issuu converts static files into: digital portfolios, online yearbooks, online catalogs, digital photo albums and more. Sign up and create your flipbook.
Moduli 2, Kilimo Mseto Na Mzunguko (revised) by Mkulima Mbunifu - Issuu