Tutaishije

Page 1

TUTAISHIJE? Mazingira mazuri kama yetu Kitu gani kinatufanya twaribu? Elimu tunayo ya kutosha Rasilimali zetu kuhifadhi Naam! Wakati umefika Wa sisi kuchukua hatua Kwa ajili ya ulimwengu wetu Na kuutnza utajiri wetu Ni wasaa wa kusema kweli Kuhusu mabadiliko ya tabia nchi Na kamwe kutorudi nyuma Vita hivi kuviendeleza Tutaishije dunia yetu ikigeuka? Tutaishije miti ikikatwa na mito kukauka? Tutaishije hewa yet ikichafuliwa? Tutaishije mimea na wanyama wakiathirika? Nina imani Kwa mazingira yenye ubora wa kudumu Kwa maendeleo yakuboresha maisha kikamilifu Na kwa ulimweng wenye ufanisi Jukumu ni letu sisi Kuchukua hatua sasa Kulinda ulimwengu tunaouenzi Kwa ajili yetu na vizazi vijavyo Lau sivyo, sijui tutaishije? Shairi limetungwa na Nelson Ochieng Opany (Al-Ustadh Weledi)


Turn static files into dynamic content formats.

Create a flipbook
Issuu converts static files into: digital portfolios, online yearbooks, online catalogs, digital photo albums and more. Sign up and create your flipbook.