![](https://static.isu.pub/fe/default-story-images/news.jpg?width=720&quality=85%2C50)
16 minute read
Sura 9. Nuru Iliwashwa Katika Usuisi
Juma chache baada ya kuzaliwa kwa Luther katika kibanda cha mchimba madini katika Saxe, Ulric Zwingli akazaliwa katika nyumba ndogo ya wachungaji katika milima mirefu ya Alpes. Alipokelewa pahali penye maubule makubwa, akili yake mwanzoni tu ikavutwa na utukufu wa Mungu. Kando ya babu wake mwanamke, alisikiliza hadizi chache za damani za Biblia alizokusanya kwa shida kutoka kwa hadizi na mafundisho ya kanisa yaliyotokea zamani.
Kwa umri wa miaka kumi na mitatu akaenda Berne, mahali palipokuwa shule lililokuwa la sifa sana katika Usuisi. Hapa, lakini, kukatokea hatari. Juhudi nyingi zikafanywa na watawa kwa kumvuta katika nyumba ya watawa. Kwa bahati baba yake akapata habari ya makusudi ya watawa. Aliona kwamba mafaa ya wakati ujao ya mwanawe yalikuwa ya kufa kwa ajili ya imani ya dini na akamwongoza kurudi nyumbani.
Agizo likasikiwa, lakini kijana hakuweza kurizika katika bonde lake la kuzaliwa, akaenda kufuata masomo yake huko Ba le. Ni hapo ambapo Zwingli alisikia mara ya kwanza injili ya neema ya Mungu isionunuliwa. Huko Wittembach, alipokuwa akijifunza (kiyunani) Kigiriki na Kiebrania, akaongozwa kwa Maandiko matakatifu, kwa hivyo nyali za nuru ya Mungu ikatolewa katika akili za wanafunzi aliokuwa akifundisha. Akatangaza kwamba kifo cha Kristo ni ukombozi wa kipekee wa mwenye zambi. Kwa Zwingli maneno haya ni nyali ya kwanza ya nuru unayotangulia mapambazuko.
Zwingli akaitwa upesi kutoka Bale kwa kuingia kwa kazi yake ya maisha. Kazi yake ya kwanza ilikuwa katika vilaya ya milima mirefu. Akatakaswa kama padri, “akajitoa wakfu na roho yake yote kwa kutafuta kweli ya Mungu.” Namna alizidi kutafuta Maandiko, zaidi tofauti ikaonekana kwake kati ya ukweli na mambo ya kupinga imani ya dini ya Roma. Akajitoa mwenyewe kwa Biblia kama Neno la Mungu, amri moja tu inayofaa na ya haki. Aliona kwamba Biblia inapaswa kuwa mfariji wake mwenyewe. Akatafuta usaada wowote kwa kupata ufahamu kamili wa maana yake, na akaomba usaada wa Roho Mtakatifu. “Nikaanza kumuomba Mungu kwa ajili ya nuru yake, “baadaye akaandika, “na Maandiko yakaanza kuwa rahisi zaidi kwangu.”
Mafundisho yaliyohubiriwa na Zwingli hayakupokewa kutoka kwa Luther. Yalikuwa mafundisho ya Kristo. “ikiwa Luther anahubiri Kristo,” akasema Mtengenezaji wa Usuisi, “anafanya ninavyofanya. ... Hakuna hata neno moja lililoandikwa nami kwa Luther wala lililoandikwa na Luther kwangu. Ni kwa sababu gani? ... Ili ipate kuonyeshwa namna gani
Roho wa Mungu anakuwa katika sauti moja kwake mwenyewe, hivi sisi wawili, bila mgongano, tunafundisha mafundisho ya Kristo kwa ulinganifu kama huo.”
Katika mwaka 1516 Zwingli akaalikwa kuhubiri katika nyumba ya watawa huko Einsiedeln. Hapa alipashwa kutumia kama Mtengenezaji mvuto ambao ungesikiwa mbali hata kuvuka milima mirefu (Alpes) alipozaliwa.
Katika vitu vya mvuto wa Einseideln ni sanamu ya Bikira, walisema kwamba ilikuwa na uwezo wakufanya. Juu ya mlango wa nyumba ya watawa kulikuwa na maandiko, “Ni hapa kunapatikana msamaha wa zambi zote.” Makundi mengi wakaja kwa mazabahu ya Bikira kutoka pande zote za Usuisi, na hata kutoka Ufaransa na Ujeremani. Zwingli akapata nafasi ya kutangaza uhuru kwa njia ya injili kwa watumwa hawa wa mambo ya ibada ya sanamu.
“Musizani,” akasema, “kwamba Mungu yuko katika hekalu hii zaidi kuliko kwa upande mwingine wauumbaji. ... Je, kazi zisizofaa, safari za taabu, sadaka, masanamu, sala za Bikira ao za watakatifu zingeweza kuwapatia neema ya Mungu? ... Ni manufaa gani ya kofia ya kungaa, kichwa kilichonolewa vizuri, kanzu ndefu na yenye kuvutwa, ao viato vyenye mapambo ya zahabu?” “Kristo,” akasema, “aliyetolewa mara moja juu ya msalaba, ni toko na kafara, alifanya kipatanisho kwa ajili ya zambi za waaminifu hata milele.”
Kwa wengi lilikuwa uchungu wa kukatisha tamaa kuambiwa kwamba safari yao ya kuchokesha ilikuwa ya bure. Hawakuweza kufahamu rehema waliyotolewa bure katika Yesu Kristo. Njia ya mbinguni iliyowekwa na Roma iliwatoshelea. Ilikuwa ni rahisi sana kutumaini wokovu wao kwa wapadri na Papa kuliko kutafuta usafi wa moyo.
Lakini kundi lingine wakapokea kwa furaha habari za ukombozi kwa njia ya Kristo, na katika imani wakakubali damu ya Muokozi kuwa kipatanisho chao. Hawa wakarudi kwao kuonyesha wengine nuru ya damani waliyoipokea. Kwa hivi ukweli ukapelekwa mji kwa mji, na hesabu ya wasafiri kwa mahali patakatifu pa Bikira ikapunguka sana. Sadaka sasa zikapunguka, na kwa sababu hiyo mshahara wa Zwingli uliyokuwa ukitoka humo. Lakini jambo hilo lilimletea tu furaha namna alivyoona kwamba uwezo wa ibada ya sanamu ulikuwa ukivunjwa. Ukweli ukapata uwezo kwa mioyo ya watu.
Zwingli Akaitwa Zurich
Baada ya miaka mitatu Zwingli akaitwa kuhubiri katika kanisa kubwa la Zurich, mji mkubwa sana wa ushirika wa Suisi. Mvuto uliotumiwa hapa ulisikuwa mahali pengi. Wapadri waliomwita kwa kazi hiyo wakawa na uangalifu wa kumfahamisha hawakutaka mageuzi:
“
Utaweka juhudi yote kukusanya mapato kwa mfululizo bila kusahau kitu cho chote. ...
Utakuwa na juhudi ya kuongeza mapato kutoka kwa wagonjwa, kwa misa, na kwa kawaida kutoka kwa kila agizo la dini.” “Juu ya uongozi wa sakramenti, mahubiri, na ulinzi wa kundi, ... unaweza kutumia mtu mwingine, na zaidi sana katika mahubiri.”
Zwingli akasikiliza kwa ukimya kwa agizo hili, na akasema kwa kujibu, “Maisha ya Kristo yamefichwa mda mrefu kwa watu. Nitahubiri juu habari yote ya Injili ya Mtakatifu
Matayo. ... Ni kwa utukufu wa Mungu, kwa sifa ya mwana wake, kwa wokovu wa kweli wa roho, na kwa kujijenga katika imani ya kweli, ambapo nitajitoa wakfu kwa kazi yangu.”
Watu wakajikusanya kwa hesabu kubwa kwa kusikia mahubiri yake. Akaanza kazi yake kwa kufungua Injili na kueleza maisha, mafundisho, na mauti ya Kristo. “Ni kwa Kristo,” akasema, “ambapo natamani kuwaongoza ninyi kwa Kristo, chemchemi ya kweli ya wokovu.” Wenye maarifa ya utawala, wanafunzi, wafundi, na wakulima wakasikiliza maneno yake. Akakemea makosa bila hofu na maovu ya nyakati. Wengi wakarudi kutoka kwa kanisa kuu wakimusifu Mungu. “Mtu huyu,” wakasema, “ni mhubiri wa ukweli. Atakuwa Musa wetu, kutuongoza kutoka katika giza hii ya Misri.” Baada ya wakati upinzani ukaanza. Watawa wakamushambulia kwa zarau na matusi; wengine wakatumia ukali na matisho. Lakini Zwingli akachukua yote kwa uvumilivu.
Wakati Mungu anapojitayarisha kuvunja viungo vya pingu vya ujinga na ibada ya sanamu Shetani anatumika na uwezo mkubwa sana kwa kufunika watu katika giza na kufunga minyororo yao kwa nguvu zaidi. Roma ikaendelea kutia nguvu mpya kwa kufungua soko yake katika mahali pote pa Ukristo, ukitoa msamaha kwa mali. Kila zambi ilikuwa na bei yake, na watu walipewa chetibila malipo kwa ajili ya zambi kama hazina ya kanisa ililindwa yenyekujaa vizuri. ... Hivi mashauri mawili haya yakaendelea Roma kuruhusu zambi na kuifanya kuwa chemchemi ya mapato yake, Watengenezaji kulaumu zambi na kuonyesha Kristo kama kipatanisho na mkombozi.
Uchuuzi wa cheti cha Kuachiwa Zambi katika Usuisi
Katika Ujermani biashara ya kuachiwa (zambi) iliongozwa na mwovu sana Tetzel. Katika Usuisi biashara hii ilikuwa chini ya uongozi wa Samson, mtawa wa Italia. Samson alikuwa amekwisha kujipatia pesa nyingi kutoka Ujeremani na Usuisi kwa kujaza hazina ya Papa. Sasa akapitia Usuisi, kunyanganya wakulima masikini mapato yao machache na kulipisha zawadi nyingi kutoka kwa watajiri. Mtengenezaji kwa upesi akaanza kumpinga. Kufanikiwa kwa Zwingli kulikuwa namna hiyo kufunua kujidai kwa mtawa huyu hata akashurutisha kutoka kwenda sehemu zingine. Huko Zurich, Zwingli akahubiri kwa bidii juu ya wafanya biashara ya msamaha. Wakati Samson alipokaribia mahali pale akakutana na mjumbe aliyemtetea neno kutoka kwa baraza kwa kumwaambia aanze kazi, akatumia mwingilio wa hila, lakini, akarudishwa bila kuuzisha hata barua moja ya msamaha, kwa upesi akatoka Usuisi.
Tauni, au Kifo Kikubwa, kikapitia kwa Usuisi kwa nguvu sana katika mwaka 1519. Wengi wakaongozwa kuona namna ilikuwa bure na bila damani masamaha yaliokuwa wakinunua; wakatamani sana msingi wa kweli wa imani yao. Huko Zurich, Zwingli akagonjwa sana, na habari ikatangazwa sana kwamba alikufa. Kwa saa ile ya kujaribiwa akatazama kwa imani msalaba wa Kalvari, akatumaini kwamba kafara ya Kristo ilikuwa ya kutosha kwa ajili ya zambi. Aliporudi kutoka kwa milango ya mauti, ilikuwa kwa ajili ya kuhubiri injili kwa bidii kubwa sana kuliko mbele. Watu wao wenyewe walitoka kuangalia mgonjwa karibu ya kifo, wakafahamu vizuri kuliko mbele, damani ya injili.
Zwingli alifikia hali ya kuelewa wazi juu ya ukweli na kupata ujuzi ndani yake uwezo wake unaogeuza. “Kristo,” akasema, “... alitupatia ukombozi wa milele ... mateso yake ni ... kafara ya milele, na huleta kupona kwa milele; huridisha haki ya Mungu kwa milele kwa ajili ya wale wote wanaotegemea juu ya kafara yake kwa imani ya nguvu na ya imara. ... Panapokuwa imani katika Mungu, kunakuwa na juhudi inayoendesha na kusukuma watu kwa kazi njema.”
Hatua kwa hatua Matengenezo yakaendelea katika Zurich. Katika mushtuko adui zake wakaamka kwa kushindana kwa bidii. Mashambulio mingi yakafanywa juu ya Zwingli. Mwalimu wa wapinga imani ya dini anapashwa kunyamazishwa. Askofu wa Constance akatuma wajumbe watatu kwa Baraza la Zurich, kumshitaki Zwingli juu ya kuhatarisha amani na utaratibu wa jamii. Kama mamlaka ya kanisa ikiwekwa pembeni, akasema, machafuko kote ulimwenguni yatatokea.
Baraza likakataa kukamata mpango juu ya Zwingli, na Roma ikajitayarisha kwa shambulio jipya. Mtengenezaji akapaliza sauti: “Muache waje”; Ninawaogopa kama vile mangenge yanayo tokajuu yakimbiavyo mavimbi yanayo mgurumo kwa miguu yake.”
Juhudi za waongozi wa kanisa ziendelesha kazi waliotamani kuharibu. Kweli ikaendelea kusambaa. Katika Ujeremani wafuasi wake, walipohuzunishwa kwa kutoweka kwa Luther, wakatiwa moyo tena walipoona maendeleo ya injili katika Usuisi. Namna Matengenezo yaliimarishwa katika Zurich, matunda yake yalionekana zaidi kabisa katika kuvunjwa kwa uovu na kuendeleshwa utaratibu.
Mabishano (Wafuasi wa kanisa la Roma)
Kwa kuona namna mateso ya kutangaza kazi ya Luther katika Ujeremani haikufanya kitu, Warumi wakakusudiakuwe mabishano na Zwingli. Walikuwa na hakika ya ushindi kwa kuchagua si makali tu pa vita bali waamuzi waliopashwa kuamua kati ya wabishanaji. Na kama wangeweza kupata Zwingli katika uwezo wao, wangefanya angalisho ili asikimbie. Shauri hili, basi, likafichwa kwa uangalifu. Mabishano yalipaswa kuwa huko Bade. Lakini Baraza la Zurich, kuzania makusudi ya watu wa Papa na walipoonywa juu ya vigingi vya moto vilivyowashwa katika makambi ya wakatoliki kwa ajili ya washahidi wa injili, wakamkataza mchungaji wao kujihatarisha maisha yake. Kwa kwenda Bade, mahali damu ya wafia dini kwa ajili ya ukweli ilikuwa imetiririka, ingeleta kifo kweli. Oecolampadius na Haller wakachaguliwa kuwa wajumbe wa Watengenezaji, wakati Dr. Eck mwenye sifa, akisaidiwa na jeshi la watu wenye elimu sana na wapadri, alikuwa ndiye shujaa wa Roma.
Waandishi wakachaguliwa wote kwa wakatoliki, na wengine wakakatazwa kuandika ao wasipotii wauwawe. Mwanafunzi mmoja, aliyeshiriki katika mabishano akaandika abari kila jioni juu ya mabishano yaliyofanyika mchana ule. Wanafunzi wawili wengine wakaagizwa kutoa kila siku barua za Oecolampadius, kwa Zwingli huko Zurich. Mtengenezaji akajibu, anapotoa shauri. Kwa kuepuka uangalifu wa mlinzi wa milango ya mji, wajumbe hawa walileta vikapo vya bata juu ya vichwa vyao na wakaruhusiwa kupita bila kizuizi.
Zwingli “alitumika zaidi,” akasema Myconius, “kwa mawazo yake, kukesha kwake usiku, na shauri alilopeleka Bade, kuliko angeweza kufanya kwa kubishana mwenyewe katikati ya adui zake.” Wakatoliki wakafika Bade na mavazi ya hariri ya fahari sana ya mapambo ya vitu vya damani. Wakasafiri na anasa sana, na kukaa kwa meza zilizojaa vyakula vitamu sana na divai nzuri sana. Kukawa tofauti kubwa sana kati yao na Watengenezajiambao chakula chao cha kiasi kikawakalisha kwa mda mfupi tu mezani. Mwenyeji wa Oecolampade, aliyempeleleza chumbani mwake, akamkuta akijifunza kila wakati ao akiomba, na akajulisha kwamba mpinga imani ya dini huyo alikuwa “mtawa sana.”
Katika mkutano, “Eckakapanda na majivuno katika mimbara iliyopambwa vizuri sana, lakini mnyenyekevu Oecompade, aliyevaa mavazi ya kiasi, akalazimishwa kuchukua kiti chake mbele ya mpinzani wake kwa kiti kilichochorwa vibaya sana.” Sauti ya nguvu ya Eck na majivuno mingi hakumtisha. Mtetezi wa imani alikuwa anatazamia mshahara mzuri. Wakati alipokosa mabishano bora, akatumia matukano na hata maapizo ama laana.
Oecolampade, mwenye adabu na mwenye kujihazari, akakataa kushiriki katika mabishano. Ingawa alikuwa mpole na adabu katika mwenendo, akajionyesha mwenyewe kuwa na uwezo na imara. Mtengenezaji akashikamana kwa nguvu katika Maandiko. “Desturi,” akasema, “haina uwezo katika Usuisi wetu, isipokuwa kwa sheria; sasa katika mambo ya imani, Biblia ndiyo sheria yetu.”
Utulivu, kutumia akili kwa Mtengenezaji, unyenyekevu na adabu ulioonyeshwa, ikavuta mafikara na watu wakachukia majivuno ya kiburi cha Eck.
Mabishano yakaendelea kwa mda wa siku kumi na mnane. Wakatoliki wakadai ushindi. Kwa namna wajumbe wengi walikuwa wa upande wa Roma, na baraza ikatangaza kwamba Watengenezaji walishindwa na pamoja na Zwingli, waondoshwe kanisani. Lakini mashindano yakatokea katika mvuto wa nguvu kwa ajili ya Waprotestanti. Baada ya mda mfupi tu, miji mikubwa ya Berne na Bâ le ikajitangaza kuwa kwa upande wa Matengenezo.
Sura 10. Maendeleo Katika Ujeremani
Kutoweka kwa ajabu kwa Luther kukaweka Ujeremani wote katika hofu kubwa. Habari ikatangazwa na wengi wakaamini kwamba aliuawa. Kukawa maombolezo makubwa, na wengi wakaapa kwa kitisho kulipiza kisasi cha kifo chake.
Ijapo waiishangilia mara ya kwanza kwa ajili ya kifo kilichozaniwa cha Luther, adui zake walijazwa na hofu kuwa sasa kwamba amekuwa mfungwa. “Njia moja tu inayotubakilia kwa kuokoa kesi letu,” akasema mmoja wao, “ni kuwasha mienge, na kumuwinda Luther katika ulimwengu wote na kumrudisha kwa taifa linalomwita.” Kusikia kwamba Luther alikuwa salama, ijapo alikuwa mfungwa, jambo hili likatuliza watu, huku wakisoma maandiko yake kwa bidii sana kuliko mbele. Hesabu ya wale walioongezeka wakajiunga kwa kisa cha mshujaa aliyetetea Neno la Mungu.
Mbegu ambayo Luther alipanda ikatoa matunda mahali pote. kutokuwapo kwake kukafanya kazi ambayo kuwako kwake hakungeweza kufanya. Na sasa mwongozi wao mkuu ameondolewa, watumikaji wengine wakafanya bidii ili kazi ya maana sana iliyoanzishwa isipingwe. Sasa Shetani akajaribu kudanganya na kuangamiza watu kwa kuwapokeza kazi iliyogeuzwa kwa hila pahali pa kazi ya kweli. Kwa namna kulikuwa
Wakristo wa uongo kwa karne la kwanza, ndipo kukatokea manabii wa uongo kwa karne ya kumi na sita.
Watu wachache wakajizania wenyewe kupokea mafumbulio ya kipekee kutoka Mbinguni na kuchaguliwa na Mungu kwa kutimiza kazi ya Matengenezo ambayo ilianzishwa kwa uzaifu na Luther. Kwa kweli, walibomoa kile Mtengenezaji alichofanya. Walikataa kanuni ya Matengenezo kwamba Neno la Mungu ni amri moja tu, ya kutosha ya imani na maisha. Kwa kiongozi kile kisichokosa wakaweka maagizo yao yasiyokuwa ya hakika, ya mawazo yao wenyewe na maono.
Wengine kwa urahisi wakaelekea kwa ushupavu na kujiunga pamoja nao. Mambo ya wenye bidii hawa yakaleta mwamsho mkubwa. Luther alikuwa ameamsha watu kuona haja ya Matengenezo, na sasa watu wengine waaminifu wa kweli wakaongozwa vibaya na madai ya “manabii” wapya. Waongozi wa kazi wakaendelea pale Wittenberg na wakalazimisha madai yao juu ya Melanchton: “Tumetumwa na Mungu kwa kufundisha watu. Tulikuwa na mazungumzo ya kawaida pamoja na Mungu; tunajua jambo litakalotokea; kwa neno moja, tunakuwa mitume na manabii, na tunatoa mwito kwa Mwalimu Luther.”
Watengenezaji wakafazaika. Akasema Melanchton; hapa panakuwa kweli roho za ajabu katika watu hawa; lakini roho gani? ... Kwa upande mwengine tujihazari kuzima Roho wa Mungu, na kwa upande mwengine, kwa kudanganywa na roho ya Shetani.”
Tunda la Mafundisho Mapya Limeonekana (limetambulika)
Watu wakaongozwa kuzarau Biblia ao kuikataa yote kabisa. Wanafunzi wakaacha mafundisho yao na kutoka kwa chuo kikubwa. Watu waliojizania kwamba ni wenye uwezo kwa kurudisha nafsi na kuongoza kazi ya Matengenezo wakafaulu tu kuileta katika uharibifu. Sasa Wakatoliki wakapata tumaini lao, nakulalamika kwa furaha. “Juhudi ya mwisho tena, na wote watakuwa wetu.”
Luther huko Wartburg, aliposikia mambo yaliyotendeka, akasema na masikitiko sana: “Nilifikiri wakati wowote kwamba Shetani angetumia mateso haya.” Akatambua tabia ya kweli ya wale waliojidai kuwa “manabii.” Upinzani wa Papa na mfalme haukumletea mashaka makubwa sana na shida kama sasa. Miongoni mwa waliojidai kuwa “rafiki” za Matengenezo, kukatokea adui zake wabaya kuliko kwa kuamsha vita na kuleta fujo.
Luther aliongozwa na Roho wa Mungu na kupelekwa mbali ya kujisikia binafsi. Huku kila mara alikuwa akitetemeka kwa matokeo ya kazi yake: “Kama ningelijua kwamba mafundisho yangu yaliumiza mtu mmoja, mtu mmoja tu, ingawa mnyenyekevu na mnyonge-lisipoweza kuwa, kwani linakuwa ni injili yenyewe ningekufa mara kumi kuliko mimi kuikana.”
Wittenberg yenyewe ilikuwa ikianguka chini ya mamlaka ya ushupavu wa dini isiyo ya akili na machafuko. Katika Ujeremani pote adui za Luther wakatwika mzigo huo juu yake. Katika uchungu wa roho akajiuliza, “Je, ni hapo basi kazi hii kubwa ya Matengenezo ilipaswa kumalizikia?” Tena, kama vile alikuwa akishindana na Mungu katika sala, amani ikaingia moyoni mwake. “Kazi si yangu, bali ni yako mwenyewe,” akasema. Lakini akakusudia kurudi Wittenberg.
Alikuwa chini ya laana ya ufalme; Adui zake walikuwa na uhuru wa kumuua, rafiki walikatazwa kumlinda. Lakini aliona kwamba kazi ya injili ilikuwa katika hatari, na katika jina la Bwana akatoka bila uwoga kupigana kwa ajili ya ukweli. Ndani ya barua kwa mchaguzi, Luther akasema: “Ninaenda Wittenberg chini ya ulinzi wa yule anayekuwa juu kuliko ule wa wafalme na wachaguzi. Sifikiri kuomba usaada wa fahari yako, wala kutaka ulinzi wako, ningependa kukulinda mimi mwenyewe. ... Hakuna upanga unaoweza kusaidia kazi hii. Mungu peke yake anapashwa kufanya kila kitu.” Katika barua ya pili, Luther akaongeza: “Niko tayari kukubali chuki ya fahari yako na hasira ya ulimwengu wote. Je, wakaaji wa Wittenberg si kondoo zangu? Na hainipasi, kama ni lazima, kujitoa kwa mauti kwa ajili yao?”
Uwezo wa Neno
Makelele haikukawia kuenea katika Wittenberg kwamba Luther alirudi na alitaka kuhubiri. Kanisa likajaa. Kwa hekima kubwa na upole akafundisha na kuonya: “Misa ni kitu kibaya; Mungu huchukia kitu hiki; kinapaswa kuharibiwa. ... Lakini mtu asiachishwe kwacho kwa nguvu. ... Neno ... la Mungu linapasa kutenda, na si sisi. ...Tunakuwa na haki kusema: hatuna na haki kutenda. Hebu tuhubiri; yanayobaki ni ya Mungu. Nikitumia nguvu nitapata nini? Mungu hushika moyo na moyo ukikamatwa, umekamatika kabisa. ...
“Nitahubiri, kuzungumza, na kuandika; lakini sitamshurutisha mtu, kwani imani ni tendo la mapenzi. ... Nilisimama kumpinga Papa, vyeti vya kuachiwa zambi, na wakatoliki, lakini bila mapigano wala fujo. Ninaweka Neno la Mungu mbele; nilihubiri na kuandika ni jambo hili tu nililolifanya. Na kwani wakati nilipokuwa nikilala, ... neno ambalo nililohubiri likaangusha mafundisho ya kanisa la Roma, ambaye hata mtawala ao mfalme hawakulifanyia mambo mengi mabaya. Na huku sikufanya lolote; neno pekee lilitenda vyote.” Neno la Mungu likavunja mvuto wa mwamusho wa ushupavu. Injili ilirudisha katika njia ya Kweli watu waliodanganywa.
Miaka nyingi baadaye ushupavu wa dini ukainuka pamoja na matokeo ya ajabu. Akasema Luther: “Kwao Maandiko matakatifu yalikuwa lakini barua yenye kufa, na wote wakaanza kupaaza sauti, ‘Roho! Roho! ‘ Lakini kwa uhakika sitafuata mahali ambapo roho yao inawaongoza.”
Thomas Munzer, alikuwa na bidii zaidi miongoni mwa washupavu hawa, alikuwa mtu wa uwezo mkubwa, lakini hakujifunza dini ya kweli. “Alipokuwa na mapenzi ya kutengeneza dunia, na akasahau, kama wenye bidii wote wanavyofanya, kwamba ilikuwa kwake mwenyewe ambaye Matengenezo ilipashwa kuanzia.” Hakutaka kuwa wa pili, hata kwa Luther. Yeye mwenyewe akajidai kwamba alipokea agizo la Mungu kuingiza Matengenezo ya kweli: “Ye yote anayekuwa na roho hii, anakuwa na imani ya kweli, ijapo hakuweza kuona Maandiko katika maisha yake.”
Waalimu hawa wa bidii wakajifanya wenye kutawaliwa na maono, kuona kuwa kila mawazo na mvuto kama sauti ya Mungu. Wengine hata wakachoma Biblia zao. Mafundisho ya Munzer yakakubaliwa na maelfu. Kwa upesi akatangaza kwamba kutii watawala, ilikuwa kutaka kumtumikia Mungu na Beliali. Mafundisho ya uasi ya Munzer yakaongoza watu kuvunja mamlaka yote. Sherehe za kutisha za upinzani zikafuata, na mashamba ya Ujeremani yakajaa na damu.
Maumivu Makuu ya Roho Sasa Yakalemea Juu ya Luther
Wana wa wafalme wa upande wa Papa wakatangaza kwamba uasi ulikuwa tunda ya mafundisho ya Luther. Mzigo huu hakupashwa lakini kuleta huzuni kubwa kwa Mtengenezaji kwamba kisa cha kweli kilipaswa kuaibishwa kwa kuhesabiwa pamoja na ushupavu wa dini wa chini zaidi. Kwa upande mwengine, waongozi katika uasi walimchukia Luther. Hakukana madai yao kwa maongozi ya Mungu tu, bali akawatangaza kuwa waasi juu ya mamlaka ya serkali. Katika uhusiano wakamshitaki yeye kuwa mdai wa msingi.
Roma ilitumainia kushuhudia muanguko wa Matengenezo. Na wakamlaumu Luther hata kwa ajili ya makosa ambayo alijaribu kwa bidii sana kusahihisha. Kundi la ushupavu, likadai kwa uongo kwamba lilitendewa yasiyo haki, wakapata huruma ya hesabu kubwa ya watu na kuzaniwa kuwa kama wafia dini. Kwa hiyo wale waliokuwa katika kupingana na Matengenezo wakahurumiwa na kusafishwa. Hii ilikuwa kazi ya roho ya namna moja ya uasi wa kwanza uliopatikana mbinguni.
Shetani hutafuta kila mara kudanganya watu na kuwaongoza kuita zambi kuwa haki na haki kuwa zambi. Utakatifu wa uongo, utakaso wa kuiga, ungali ukionyesha roho ya namna moja kama katika siku za Luther, kugeuza mafikara kutoka kwa Maandiko na kuongoza watu kufuata mawazo na maono kuliko sheria za Mungu. Kwa uhodari Luther akatetea injili kwa mashambulio. Pamoja na Neno la Mungu akapigana juu ya mamlaka ya manyanganyi ya Papa, wakati aliposimama imara kama mwamba kupinga ushupavu uliojaribu kujiunga na Matengenezo.
Pande zote za upinzanihuweka pembeni Maandiko matakatifu, kwa faida ya hekima ya kibinadamu kutukuzwa kawa chemchemi ama asili ya ukweli. Kufuata akili za kibinadamu kwa kusudi lakuabudu kama Mungu na kufanya hii kanuni kwa ajili ya dini. Kiroma kinadai kuwa na uongozi wa Mungu ulioshuka kwa mustari usiovunjika toka kwa mitume na kutoa nafasi kwa ujinga na uchafu vifichwe chini ya agizo la “mitume”. Maongozi yaliyodaiwa na Munzer yalitoka kwa mapinduzi ya mawazo. Ukristo wa kweli hukubali Neno la Mungu kama jaribio la maongozi yote.
Kwa kurudi kwake Wartburg, Luther akatimiza kutafsiri Agano Jipya, na injili ikatolewa upesi kwa watu wa Ujeremani katika lugha yao wenyewe. Ufasiri huu ukapokewa kwa furaha kubwa kwa wote waliopenda ukweli.
Wapadri wakashtushwa kwa kufikiri kwamba watu wote wangeweza sasa kuzungumza pamoja nao Neno la Mungu na kwamba ujinga wao wenyewe ungehatarishwa. Roma ikaalika mamlaka yake yote kuzuia mwenezo wa Maandiko. Lakini kwa namna ilivyozidi kukataza Biblia, ndivyo hamu ya watu ikazidi kujua ni nini iliyofundishwa kwa kweli. Wote walioweza kusoma wakaichukua kwao na hawakuweza kutoshelewa hata walipokwisha kujifunza sehemu kubwa kwa moyo. Mara moja Luther akaanza utafsiri wa Agano la Kale.
Maandiko ya Luther yakapokewa kwa furaha sawasawa katika miji na katika vijiji.
“Yale Luther na rafiki zake waliyoandika, wengine wakayatawanya. Watawa, waliposadikishwa juu ya uharamu wa kanuni za utawa, lakini wajinga sana kwa kutangaza neno la Mungu ... wakauzisha vitabu vya Luther na rafiki zake. Ujeremani kwa upesi ukajaa na wauzishaji wa vitabu wajasiri.”
Kujifunza Biblia Mahali Pote
Usiku waalimu wa vyuo vya vijiji wakasoma kwa sauti kubwa kwa makundi madogo yaliyokusanyika kando ya moto. Kwa juhudi yote roho zingine zikahakikishwa kwa ukweli.
“Kuingia kwa maneno yako kunaleta nuru; kunamupa mujinga ufahamu.” Zaburi 119:130.
Wakatoliki walioachia mapadri na watawa kujifunza Maandiko sasa wakawaalika kwa kuonyesha uwongo wa mafundisho mapya. Lakini, wajinga kwa Maandiko, mapadri na watawa wakashindwa kabisa. “Kwa huzuni,” akasema mwandishi mmoja mkatoliki, “Luther alishawishi wafuasi wake kwamba haikufaa kuamini maneno mengine isipokuwa Maandiko matakatifu.” Makundi yakakusanyika kusikia mambo ya kweli yaliyotetewa na watu wa elimu ndogo. Ujinga wa hawa watu wakuu ukafunuliwa kwa kuonyesha uongo wa mabishano yao kwa msaada wa mafundisho rahisi ya Neno la Mungu. Watumikaji, waaskari, wanawake, na hata watoto, wakajua Biblia kuliko mapadri na waalimu wenye elimu.
Vijana wengi wakajitoa kwa kujifunza, kuchunguza Maandiko na kujizoeza wenyewe na kazi bora ya watu wa zamani. Walipokuwa na akili yenye juhudi na mioyo hodari, vijana hawa wakapata haraka maarifa ambayo kwa wakati mrefu hakuna mtu aliweza kushindana nao. Watu wakapata katika mafundisho mapya mambo ambayo yalileta matakwa ya roho zao, na wakageuka kutoka kwa wale waliowalea kwa wakati mrefu na maganda ya bure ya ibada za sanamu na maagizo ya wanadamu.
Wakati mateso yalipoamshwa juu ya waalimu wa ukweli, wakafuata agizo hili la Kristo:
“Na wakati wanapo watesa ninyi katika mji huu, kimbilieni kwa mji mwengine.” Matayo 10:23. Wakimbizi wakapata mahali mlango karibu ulifunguka kwao, na waliweza kuhubiri Kristo, wakati mwengine ndani ya kanisa ao katika nyumba ya faragha ao mahali pa wazi. Kweli ikatawanyika kwa uwezo mkubwa usio wa kuzuia.
Ni kwa bure watawala wa kanisa na wa serkali walitumia kifungo, mateso, moto, na upanga. Maelfu ya waaminifu wakatia muhuri kwa imani yao kwa kutumia damu yao, na huku mateso ilitumiwa tu kupanua ukweli. Ushupavu ambao Shetani alijaribu kuunganisha hayo, matokeo yalikuwa wazi kinyume kati ya kazi ya Shetani na kazi ya Mungu.