Utangulizi Kwa Ndovu

Page 1

Utangulizi kwa Ndovu

SPISHI ZA NDOVU

Jifunze mengi kuhusu ndovu hapa

Kuna spishi 3 tofauti za Ndovu:

MAMALIA WAKUBWA ZAIDI WA ARDHINI

Ndovu wa Savana wa Kiafrika

Ndovu ni nini?

Loxodonta africana Ndovu ni mamalia wakubwa zaidi wanaoishi duniani – ni wa familia ya Elephantidae.

Ndovu wa Savana wa Kiafrika wana uzito wa hadi kilogramu 7,000 na husimama mita 3.5 hadi 4 kwenye bega. Mita 1

Hutambulika haraka kwa mkonga wake mrefu (mdomo wa chini na pua iliyo refu), miguu yenye umbo la mhimili, na kichwa kikubwa, chenye masikio makubwa bapa.

Wana miguu minne, hula majani na hubadilika sana.

Ndovu ni wa rangi ya kijivu hadi kahawia, na nywele za mwili wake ni chache na zimekwaruzika.

Wana pembe refu zilizopindika.

Futi 3

Ndovu wa msituni wa Kiafrika Loxodonta cyclotis

Mita 1

Futi 3

Kuna spishi 3 tofauti za ndovu.

Ndovu wa msituni huishi katika misitu ya mvua, na walitambuliwa kama spishi tofauti mnamo 2021. Ni wadogo kiasi kuliko ndovu wa Savana na ni nadra kuwa wakubwa kuzidi kilogramu 5,000. Wana pembe nyembamba zaidi, zinazoelekea chini na masikio ya mviringo zaidi.

ndovu wa asia Elephas maximus

Hupatikana sanasana katika savana, nyika, na msituni lakini huishi katika makazi mbalimbali, ikijumuisha jangwani, vinamasi, milimani, uwanda wa juu maeneo ya joto jingi na joto kidogo, barani Afrika na Asia. Miaka mia moja tu iliopita, kulikuwa na milioni 10 za ndovu wa kiafrika walioishi katika bara la Afrika. Kufikia 2016, hata hivyo, idadi yake ilipungua hadi 450,000 tu.

1.

Mita 1

Futi 3

Ndovu wa Asia hujumuisha spishi tatu ndogo: ya Kihindi, au bara (E. maximus indicus), Sumatrani (E. maximus sumatranus), na ya Sri Lanka (E. maximus maximus). Huwa na uzito wa takribani kilogramu 4,000 na wana, urefu wa bega wa hadi mita 3.


Jinsi ya kutambua kila spishi Je, unajua kuwa hadi hivi karibuni, ndovu wa Msituni wa Kiafrika walichukuliwa kuwa spishi ndogo ya ndovu wa Kiafrika, lakini utafiti mpya uligundua kuwa ni spishi tofauti (IUCN 2021). Ndovu wa msituni wana pembe zisizopindika na masikio ya mviringo zaidi kuliko wa Savana. Ndovu wa Asia na wa Kiafrika hutofautishwa na umbo la masikio yao, mikonga na vichwa. Mikonga ya ndovu wa Kiafrika huenda ikapanulika zaidi, lakini ile ya ndovu wa Asia ni stadi na inaweza kubadilika. Njia bora ya kutambua tofauti kati ya ndovu wa Asia na wa Kiafrika ni umbo la masikio na kichwa. Ndovu wa Asia wana paji la uso lililochomoza zaidi na lililochongoka kuliko ndovu wa Kiafrika. Ndovu wa Kiafrika wana masikio makubwa zaidi, wanayotumia kueneza joto la mwili. Ndovu wa Kiume wa Kiafrika anawezafikia urefu wa mita 3.5 na uzito wa kati ya kilo 4,0007,500 .

Ngozi ni hadi milimita 32 kwa unene na kwingine takribani unene wa karatasi.

Ndovu wa Asia ni mdogo zaidi, akifikia mita 3, na uzito wa kilogramu 3,0006,000.

Kuna wakati idadi yake iliishi kwenye maeneo makubwa ya shamba. Kamwe sio hivi tena. Sasa wanaishi kwenye sehemu zilizogawanywa zaidio.

2016 kiwango cha ndovu wanaojulikana Ndovu wa Savannah wa Kiafrika

Chakula cha kila siku 4-7% ya uzito wa mwili. Hula spishi nyingi za mimea kama 173, ikijumuisha nyasi, majani, matunda na maganda na mizizi tofauti.

2.

Ndovu wa Msituni wa Kiafrika Maziwa ya Afrika Mashariki

Idadi ya sasa inayokadiriwa:

450,000+ Chanzo: Imetolewa kutoka kwa Kikundi cha Wataalamu wa Ndovu wa Afrika cha IUCN


mIKONGA YA NDOVU/Miiro Mkonga wa ndovu pi huitwa “mwiro”

Mwisho wa mkonga una michomozo iliyojipinda. Hii huruhusu ndovu kufanya kazi za ajabu, kama vile kuokota sarafu kutoka kwa sehemu bapa, au kupasua karanga, kupeperusha ganda na kuweka punje mdomoni.

Mkonga, au mwiro, wa ndovu ni mojawapo ya kiungo kimoja cha kipee zaidi na Badilifu uliobadilika kati ya mamalia. Muundo wa wanafamilia hii ni wa pekee, ambao hujumuisha Mastodoni wasioishi tena na mamothi. Mkonga umeungana na mdomo wa ju na pua; pua ziko kwenye ncha. Mkonga ni mkubwa na una nguvu, ukiwa na kilogramu 140 kwa ndovu mkubwa wa kiume na unaweza kuinua mzigo wa takribani kilogramu 250. Ni kama mkonga wa kawaida. Unaweza kusonga na una hisia, ambayo wakati mwingine humfanya kujitegemea kati ya wanyama wengine. Mkonga huu una takribani misuli 40,000.

Ndani ya mkonga kuna muungano changamani wa misuli mingi inayowezesha kusonga bila tatizo. Mkonga una hisia nyingi na unaweza kunusa hadi umbali wa kilomita 12.

3.

Ndovu wa Kiasia mara nyingi hukunja ncha ya mkonga wake kwenye kitu na kukichukua kwa njia iitwayo“kufumbata”. Ndovu wa Kiafrika hutumia njia ya “kufinya”, kuokota vitu jinsi binadamu angetumia kidole gumba na kidole cha shahada.

MATUMIZI YA MKONGA Ndovu hutumia mikonga yao kama mikono ya kawaida pia kwa njia zingine.

KUTUMIA KIFAA Ndovu hutumia mikonga yao kushika matawi na kujikuna kwenye sehemu ambayo mikonga na mkia hauwezi kufikia. Wakati mwingine hurusha matawi makubwa na vifaa kama onyesho la tishio.


SALAMU ZA NDOVU

Ndovu wanapokutana, mmoja hugusa uso wa mwingine, au kuunganisha mikonga.

KUPEPERUSHA VUMBI AU NYASI

“salamu hii ya mikonga” ni kama kusalimiana kwa mkono wa kawaida; ikionyesha hakikisho, mapenzi, salamu au kama njia ya kupima nguvu.

KUPUMUA

Ndovu pia hutumia mikonga yao kukusanya vumbi au nyasi ya kujinyunyizia kujilinda dhidi ya kuumwa na wadudu na jua.

Kupumua, kunywa, na kula ni kazi muhimu za mkonga. Hupumua sana kupitia mkonga kuliko mdomo.

KULA NA KUNYWA Ndovu hunywa kwa kunyonya kama lita 10 (galoni 2.6) za maji katika mkonga kisha kuyarusha mdomoni. Ndovu mkubwa anaweza kula pauni 200-400 (kilo 90-181) za chakula kwa siku. Hula kwa kung’oa nyasi, majani, na matunda wakitumia ncha ya mkonga na kutumia kuweka mdomoni.

4.

HATARI Ndovu wakishuku kuna hatari, huinua na kuzungusha mkonga kama kwamba wao ni “periskopu ya kunusa” wakinusa hewani ili kupata habari.


UTOAJI SAUTI Sauti hutoka kwenye sehemu maalumu katika kijisanduku cha sauti cha ndovu (zoloto). Huitwa “mfuko wa koromeo.”

Ndovu hutoa sauti zingine kwa kupiga mikonga yake kwenye sehemu ngumu ya ardhi, mti, au hata dhidi ya pembe zao.

Sauti za chini (kama mingurumo) sauti za juu (kama tarumbeta).

Tembo hutoa aina mbili za milio ya sauti kwa kubadilisha ukubwa wa puani huku hewa ikipita kwenye mkonga.

HIFADHI YA MAJI Unajua kuwa ndovu hutambua mitetemeko kupitia miguu yao?

Wakati mwingine hutoa sauti zinazosambazwa kwa masafa chini ya safu ya usikivu wa binadamu. Sauti hizi za masafa haya ya chini (hezi 5–24) zinaweza kuskika na ndovu wengine hadi kilomita 4 (maili 2.5) mbali.

Ndovu pia hutumia ‘mfuko wa koromeo kuhifadhi na kubeba maji.

Njia za pua Paa laini la kinywa

Tishu ya Aritenoidi

Ncha ya mkonga Umio Ncha ya mono Koo

Mawimbi ya sauti ya masafa ya chini hupitia ardhini na hewani, na majaribio yameonyesha kuwa ndovu wanaweza kutambua sauti za chini kabisa kama mawimbi ya tetemeko ardhini.

5.

Kiungo sauti Mfuko wa koromeo wenye maji

Kidakato

Katika siku zenye joto na nyakati ambapo hakuna maji karibu, ndovu hutumbukiza mikonga yao midomoni, kunyonya kiowevu na kujinyunyizia.


mSIKIO YA NDOVU Ndovu wa Kiafrika ana masikio makubwa kuliko wa kiasia. Njia moja ya kuwatofautisha ni kuwa masikio ya ndovu wa Kiafrika pia yana umbo la Bara la Afrika.

1. NDOVU HUTUMIA MASIKIO YAKE KUPUNGUZA JOTO Masikio ya ndovu yana eneo kubwa na yana maelfu ya mishipa ya damu nyembamba na iliyo karibu na ngozi. Ndovu hawana tezi nyingi za joto (hii ndiyo husaidia binadamu na wanyama wengine kutokana na kupata joto jingi).

Masikio makubwa huwasaidia kutohisi joto jingi. Huruhusu joto jingi la mwili kutoka kwenye mwili wa ndovu na kudhibiti halijoto ya mwili wao. Sehemu kubwa na wembamba wa masikio ya ndovu huwasaidia kusambaza joto na kudhibiti joto. Masikio makubwa ya ndovu pia hutumika kama pepeo kujipuliza wakati wa joto.

6.

2. MASIKIO YA NDOVU HUWASAIDIA KUSIKIA UMBALI MREFU Ndovu wana uwezo wa ajabu wa kusikia.

5

2.

li

m

ai

uweza kusikia masafa ya chini huwaruhusu kusikia sauti ya mbali kwa kuwa sauti za chini hufika mbali zaidi.

Masikio ya ndovu hutumiwa pamoja na nyayo za miguu yao na mikonga yao kusikia na kuhisi sauti kwa umbali mrefu. Wanaweza kuwasiliana kwa umbali wa maili 2.5 kutoka eneo walipo.

3. HUTUMIA MASIKIO YAO KUWASILIANA Kando na kusikia na kupunguza joto mwilini, ndovu pia hutumia masikio yao kuwasiliana. Watafiti wametambua kuwa ndovu pia hutumia lugha ya kimwili. Wanapojaribu kutisha ndovu wengine, binadamu au wanyama wengine, hutandaza masiko yao kwa kuyafungua. Kwa kufanya hivi, wanajaribu kuonyesha utawala na tishio. Ndovu pia hutumia masikio yao kuonyesha msisimuko na ucheshi.


nGOZI YA NDOVU

Ndovu hupenda sehemu ya matope. Hii huwasaidia kulinda ngozi dhidi ya wadudu na miale ya UV ya jua (urujuani).

Ngozi ya ndovu wa Kiafrika ndicho kiungo chake kikubwa zaidi na inaweza kuwa na uzito wa hadi kilogramu 900.

Unene wa ngozi ya ndovu hutofautiana mwili mzima.

Wana ngozi nene katika sehemu fulani kama mgongo na upande ambapo ni takribani sentimita 2–3.

Hata kama mamalia huyu mkubwa ana ngozi nene, anatomia ya ngozi yake humfanya kuwa na hisia ya mguzo. Ngozi ya ndovu huwa na hisia sana na neva kuu kuwa inaweza kutambua hata mdudu mdogo zaidi akiwa kwenye ngozi yake, na hata mabadiliko katika hali ya hewa.

Sehemu nyembamba za ngozi ni nyuma ya masikio, karibu na macho na ndani ya mkonga wake. Kwenye sehemu hizi, ngozi yake ni nyembamba kama karatasi. Ngozi ya ndovu ina mikunjo sana. Utafiti wa ngozi ya ndovu umeonyesha kuwa wana mfumo tatanishi wa nyufa ndogo kwenye ngozi yao. Wakati wa kuoga, nyufa na mikunjo hii hujaa maji na matope. Husaidia kuwalinda dhidi ya joto la jua, na huwaruhusu kuendelea kutohisi joto.

Mguu wa NDOVU Mguu wa ndovu umeundwa kwa njia ambayo ndovu kwa kweli hutembea kwenye ncha za vidole zake. Wayo wa mguu wa ndovu umeundwa kwa tishu ngumu za uunganishaji zenye mafuta ambazo huwa kama sponji ya kuzuia mshtuko na huruhusu ndovu kusoga kimya. ‘Mto huu nyumbufu wa sponji” husababisha kelele nyingi (ikijumuisha vishindo vya miti na na matawi) kutosikika.

Ndio maana ndovu wanaweza kuwa kimya kabisa

7.


NDOVU WA KIASIA Nyuma

Kwa sababu ya wanavyotembea, ndovu pia huitwa ‘dijitigredi’ na wako katika kikundi cha wanyama kinachojumuisha farasi, ng’ombe, kondoo, ngamia na vifaru.

NDOVU WA KIAFRIKA Mbele

Kucha 4 za vidole

Kucha 5 za vidole

Ndovu wengi wa kiasia huwa na kucha 5 za vidole kwenye miguu ya mbele na kucha 4 za vidole kwenye miguu ya nyuma.

Mguu wa nyuma

Mbele

Nyuma

Kucha 4 za vidole

Kucha 3 za vidole

Ndovu wengi wana kucha 4 za vidole kwenye miguu ya mbelea na kucha 3 za vidole kwenye miguu ya nyuma. Hii hutofautiana kati ya ndovu.

Alama ya mguu pia inaweza kukupa maelezo muhimu kuhusu ndovu.

Mguu wa mbele

Mguu wa mbele wa ndovu ni wa mviringo, huku mguu wa nyuma ukiwa na umbo la yai.

Alama za miguu ya ndovu zinaweza kusaidia kutambua umri wa ndovu, au hata urefu wa ndovu.

Ndovu wana uwezo wa kuwa na hisia za kipekee za kuhisi kwa sababu ya seli ziitwazo “chembe za pacinia.”

Miguu ya ndovu ina matumizi mengi.

Huwa na hisia kali za mtetemeko.

Huunda mashimo ambayo hukusanya maji.

Ndovu pia wanaweza kuwa na seli hizi katika nyayo za miguu zao, nyingi zikiwa mbele na nyuma (miguu na eneo la kisigino). Kuwa na “chembe za pacinia” kwenye miguu yao huwaruhusu kuhisi mingurumo ya chini ya ndovu wengine na hata kusoga kwa ardhi.

Vidokezo vya Tahadhari

Ndovu ni wanyama wa pori na wanaweza kuwa hatari sana. Tahadhari kila wakati na uupe kipaumbele usalama wako unapokumbana na ndovu. Jifunze zaidi kuhusu ndovu ili kuelewa jinsi ya kuwatambua, na jinsi ya kutambua tabia ya ndovu.

Husaidia kuchimba mizizi kutoka kwa ardhi. Husaidia kutembea kwenye ardhi ngumu.

Sifa na Katao la Haki: Tumekusanya habari kutoka kwa vyanzo vingi. Vyanzo vikuu vinajumuisha: Elephant Voices, Save the Elephants, www.encyclopedia.com. Mwongozo huu sio wa kina. Kwa maelezo zaidi na kusoma mengi zaidi, angalia References. Save the Elephants hutoa ushauri wa tahadhari kwa njia zote na habari inayokusanywa na kupeanawa katika kijisanduku hiki cha vifaa. * Save the Elephants haigharamii gharama yoyote, uharibifu au majeraha yanayotokana na matumizi ya maelezo haya .

8. Imetengenezwa Kenya 2021

Imeandaliwa na Save the Elephants

www.savetheelephants.org

Michoro na Nicola Heath


Turn static files into dynamic content formats.

Create a flipbook
Issuu converts static files into: digital portfolios, online yearbooks, online catalogs, digital photo albums and more. Sign up and create your flipbook.