Hifadhi na ulinzi wa chakula gharama:
Lengo: Kuanzisha mbinu za uhifadhi wa mazao zinazozuia ndovu, kulinda chakula chako kutokana na ndovu.
Mbona/Tatizo ni lipi? Mbali na kuvamia mazao, ndovu wanaweza kuharibu nyumba na mali wakitafuta chakula kilichohifadhiwa.
Uharibifu wa mali.
Hofu na wasiwasi.
Wakati mwingine ndovu hujifunza kukula chakula cha kawaida au chakula kinachopatikana kwa urahisi shambani au kilichohifadhiwa katika nyumba kwa kuwa huwa na virutubishi vingi.
Kupoteza mazao kutoka kwa mimea
Kupoteza chanzo cha chakula.
Jeraha kwa binadamu.
Miingiliano mingine mbaya au inayoweza kuwa hatari kati ya binadamu na ndovu.
Picha kuu za tatizo:
Uharibifu wa mali – Ndovu wanaweza kuharibu mali wakitafuta chakula kwa kuvunja nyumba ili kufikia vyanzo vya chakula.
1.
Ndovu wanaweza kukutana na wanadamu wanapotafuta chakula nyumbani au katika majengo yao.
Kukutana kusikotarajiwa na makabiliano ya moja kwa moja na ndovu yanaweza kuwa hatari sana au kusababisha kifo.
Utoshelevu wa chakula – Tishio kwa ghala za chakula na mapato kutokana na uuzaji wa chakula kwa kuwa ndovu wanaweza kula mavuno mengi. Hii inaweza kusababisha wasiwasi wa riziki na kaya kuwa katika hatari.
NJIA ZA KUSAIDIA KULINDA CHAKULA
Chakula huvamiwa lini?
VIDOKEZO VYA USAIDIZI NJIA SALAMA ZAIDI ZA KUHIFADHI CHAKULA
Hii kwa kawaida hutendeka wakati wa usiku ndovu wanapokuwa huru zaidi kutembea vijijini na mashambani.
Kuna aina tofauti za ghala za nafaka – tumia mbinu inayokufaa zaidi. Njia inayofaa zaidi ya kuzuia uvamizi wa ndovu ni kuhifadhi mazao katika ghala za saruji/matofali. Kwa bahati mbaya, aina hizi za ghala zinaweza kuwa za gharama ya juu na kuwa na kazi nyingi ya kujenga. Kila inapowezekana, wakulima wanapaswa kuhifadhi mazao yao katika vyombo visivyopitisha hewa ili ndovu wasinuse harufu yake.
Hakikisha kuwa nafaka yako imekauka vyema kabla ya kuhifadhi. Kibuyu kilichofungwa
Au katika msimu wa ukame wakati vyanzo vya chakula ni nandra zaidi kwa ndovu kupata.
Chombo cha ndoo
Chombo kikubwa cha plastiki
MIFANO YA GHALA ZA CHAKULA 1. Ghala za Mbao za zamani/zilizoezekwa Hizi kwa kawaida hujengwa kwa kutumia mbao.
Ndovu ni werevu sana na wana hisia za ajabu za kunusa. Wanaweza kunusa chakula kilichokomaa na kitamu na mavuno kutoka mbali.
Hata hivyo, ndovu wanaweza kuvunja au kuziharibu kwa urahisi na ni dhaifu zaidi na huwa katika hatari ya kuvamiwa na ndovu. Pia huwa katika hatari ya wadudu, ikiwa hewa inaweza kuingia. Matatizo ya baadhi ya ghala hizi za zamani yanaweza kushughulikiwa kwa kurekebisha muundo. Afrika Kusini
Chanzo: Taasisi ya Kimataifa ya Ndovu
https://elephantconservation.org/hec-in-nkala-game-management-area/
2.
Tumia mbinu zaidi ya moja kwa ulinzi/vizuizi vya kuzuia ndovu kusonga mbele. Kwa mfano – mazao ya kukinga, ua wa pilipili au kizuizi cha mawe meupe yenye ncha zenye makali. Tumia mbinu maalumu za ulinzi wa mipaka ili kulinda ghala za chakula au mazao yanayokua.
2. Ghala ya matofali au saruhi au ‘Felumbus’ Ghala za nafaka za zamani zinaweza kuwa thabiti zaidi na kuwa katika hatari ya chini ya uvamizi kwa kutumia saruji badala ya matope, na kuongeza kifuniko kizito na mlango mdogo lakini ukidumisha umbo la zamani. Mlango wa ghala unaweza kufungwa, ikisaidia kuzuia wizi kutoka kwa watu pia. Felumbu/‘ghala ya nafaka iliyo salama kutokana na ndovu’- ni ghala ya chakula, yenye umbo la kikombe kikubwa kilichopinduliwa na imeundwa kwa matofali na saruji na inaweza kuhifadhi hadi tani moja ya nafaka ya mahindi. Kuna miundo tofauti inayotokana na huu. Zambia
Zimbabwe
Ghala isiyoweza kufikiwa na ndovu ni nini? Hiki ni chumba cha saruji kilichofunikwa chenye mwili uliowekelewa kwenye ardhi ya saruhi. Kina kifuniko kinachoweza kutolewa cha kutumia kujaza mazao na mlango mdogo kwenye sehemu ya chini, wa kufikia nafaka mara kwa mara.
Hii husaidia kuongeza ulinzi zaidi. Mawe meupe yenye makali yanaweza kutumika kuimarisha mijengo ya mbao. Angalia hati kuhusu Vizuio vya pilipili kwa jinsi ya kutumia pilipili kulinda ghala lako la nafaka.
Inajulikana kuwa ndovu hubomoa mijengo ya zamani na kuingia katika nyumba. Ghala hizi salama husaidia kupunguza uharibifu wa nyumba kwa kuwa ndovu huingia kijijini kutafuta chakula – kwa kuwa huifanya vigumu kwa ndovu kunusa chakula au kufikia nafaka.
Vyanzo:
Angalia Mpango wa Awely Red Caps, Awely Wildlife and People(2015) Eva Gross kwa maelezo ya ujenzi na muundo wa dhana - https://www.awely.org/en/information/
3.
Ni bora kwa kiwango cha familia moja au inayoshirikiwa na kikundi kidogo (Ushirikiano mwema unahitajika kati ya vikundi kwa kuwa nafaka zilizo ndani zimechanganywa). Chanzo: Ghala isiyofikiwa na ndovu liliyoanzishwa na kufanikiwa kujaribiwa na NGO iliyo Ufaransa French based NGO Awely – Wanyamapori na Watu na zaidi kutekelezwa na Uhifadhi Luangwa ya Kusini, Zambia.
Zambia
A. Matofali au saruji
+-
B. Ghala iliyokamilika ya saruji
Imeundwa kwa matofali na saruji ya kutengenezewa nchini. Faida: gharama ya chini – matofali yanaweza kutengenezewa kijijini. Mara mjengo wa matofali unapokauka, Tumia kipande cha mbao kupiga plasta upande wa nje kwa saruji ili kuimarisha mjengo zaidi.
Hasara: Kuni hutumika kuchoma matofali na isipofanyika inavyofaa, ghala inaweza kuwa na mipasuko. Inahitaji kujengwa vyema, au itakuwa katika hatari ya kupasuka.
vifaa
Hzi zinaweza kutumiwa kuhifadhi mifuko ya mahindi ya kilo 20 x 50, hadi kilo 1,000. Mifuko 3 ya saruji (kwa ujenzi, kifuniko na kupiga plasta).
Matofali 300 (ukubwa: L: 22.5 cm, W: 12 cm, H: 7 cm).
1 Toroli ya mawe.
1.
19 Toroli ya mchanga wa maji.
2. https://cslzambia.org https://cslzambia.org/human-wildlife-conflict-mitigation-community-engagement
Kuchimba msingi na kipenyo cha 145sm. Chimba mviringo wa kina cha 10sm.
3.
Weka mota moja ya saruji katika mviringo na uweke safu 3 za matofali. Itakapokauka, jaza katikati kwa kutumia mchanga, mawe, maji na uifinyilie. Mara msingi utakapokauka, wekelea kijikaratasi cha plastiki cha mita 2x2 juu ili kufunga na kuleta unyevu. Kisha wekelea matofali kwa mviringo ili kuunda ukuta wa mviringo. Tumia matofali 16 kwa kila safu. Acha matofali 1 kwa kila safu ili kuunda mlango mdogo mita10 –mita 10.
+ -
Faida: hakuna kuni zilizotumiwa na ghala ni thabiti. Hasara: ina gharama ya juu kwa kuwa kila nyezo lazima zinunuliwe.
vifaa
Vyanzo: FAO, https://www.fao.org/3/x0530e/X0530E05.htm Awely Red Caps Program, Awely Wildlife and People (2015) Eva Gross kwa maelezo ya ujenzi na muundo wa dhana; Conservation South Luangwa. Conservation Lower Zambezi Watch: Ghala za Chakula Zisizofikiwa na Ndovu kule South Luangwa, Zambia, 2021 - https://www.youtube.com/watch?v=MOncVdXF4BM; Zambia
4.
Mifuko 7 ya saruji (3 ya matofali na 3 ya ujenzi, kifuniko na kupiga plasta)
Kipande cha mbao (cha kupiga plasta kwenye mjengo wa matofali).
Toroli 1 ya mawe
Toroli 30 za mchanga wa mtoni
Vidokezo Mijengo iliyojengwa vibaya inaweza kupasuka – ikiwaruhusu wadudu kama mchwa au wadudu walao nafaka kuingia. Hakikisha kuwa hakuna miatuko au mashimo katika ghala lako kwa kuwa wadudu wataweza kuvamia ghala lako. Makazi yanapaswa kujengwa na kutuzwa ipasavyo, kwa kutumia maagizo ya ujenzi. (Angalia kijitabu cha Awely kwa maelezo zaidi)
3. Mapipa ya ukuta thabiti Kwa kawaida hutumika katika hali ya hewa kavu (ya kitamaduni katika eneo la Sahel la Afrika). Kwa kawaida hutengenezwa kwa mbao, matope au udongo.
Mfano = pipa la ‘Pusa’ Ilianzishwa na Indian Agricultural Research Institute(I.A.R.I.). Silo hizi zinaweza kutengenezwa kwa matofali ya ardhi/yaliyokaushwa kwa jua. Ni za umbo la mstatili na lina uwezo wa tani 1 hadi 3.
Tengeneza kifuniko kinachoweza kuwekwa na kuondolewa wakati wa msimu huo mwingine. Funga kifuniko vizuri. Mapipa haya makubwa zaidi ya kuhifadhi yanaweza kufaa zaidi kwa uhifadhi wa nafaka za kijiji.
Mlango – Unda mlango mdogo kwenye sehemu ya chini ili kufikia nafaka yako. Unaweza kujumuisha kufuli katika muundo wako ili kusaidia kuzuia wizi. Hakikisha ni pana vya kutosha ili kutoshea sepeto ya kuchota nafaka zako. Ni muhimu kufunga kwa kifuniko na kufunga mlango ipasavyo ili kusiwe na wadudu wanaoweza kuingia. Paa hupendekezwa ili kusaidia kulinda chumba kutokana na vipengele vya muda mrefu. Uchunguzi na utunzaji wa mara kwa mara unahitajika. Nafasi ya kuingia
Osha na ukaushe ghala lako baada ya kila mavuno.
Fremu ya mbao
Mahindi uhitaji kukaushwa kabisa ili kuhifadhi. Gharama ya mwanzo ya juu ya uwekezaji kwa sababu ya vifaa vinavyohitajika, lakini utunzaji wa kiwango cha chini inapojengwa.
vyanzo:
Angalia Awely Red Caps Program, Awely Wildlife and People (2015) Eva Gross kwa maelezo ya ujenzi na mtindo wa wazo. Conservation South Luangwa https://www.youtube.com/watch?v=MOncVdXF4BM
5.
Ukuta nje Ukuta wa ndani Karatasi ya plastiki
Karatasi ya plastiki huzuia unyevu kuingia kwenye ghala. Hakikisha kifuniko hakiwezi kuingiza maji ya mvua. Nafasi ya kutoka
https://www.fao.org/3/t1838e/T1838E14.HTM#Alternative%20storage%20 technology%20at%20farm/village%20level
4. Tangi la maji la kufanya mihogo kukomaa
5. Chaguo zingine za hifadhi Mbinu za zamani za kuhifadhi za shambani/kijijini
NJIA ZA KUHIFADHI ZA MUDA MFUPI
Eneo – Afrika ya Kati – Katika baadhi ya maeneo, Mihogo ndicho chakula kikuu na familia nyingi huitegemea kila siku.
Nafaka zinahitaji kukaushwa vizuri kabla ya kuhifadhiwa
Ulaji wa mihogo unaweza kuwa hatari kwa kuwa mumea huu huwa sumu na huhitaji kuwekwa katika maji kwa siku 2-5 ili kuondoa sumu.
Hifadhi ya juu
Mpango- ujenzi wa tangi ndogo la kuifanya mihogo kukomaa kijijini ambapo watu wanaweza kuhifadhi mifuko yao ya mihogo yao kwa njia salama. Hii huondoa hitaji la kwenda mtoni mara kwa mara.
faida
+
hasara
-
Huppeana mahali salama pa kuifanya mihogo kukomaa.
Huhitaji ufikiaji wa pampu ya maji inayofanya kazi.
Huboresha maisha ya jamii kwa kupunguza juhudi/muda unaohitajika kwenda mtoni, kwa kubeba mifuko mizito ya mihogo.
Wakulima ambao ni wazee wanaweza kuchukua muda kukubali dhana mpya na kupendelea kuendelea kutumia mbinu za zamani za kuhifadhi mihogo ili kujiepusha na sumu.
vidokezo:
Ushirikiano mwema wa jamii unahitajika.
vyanzo: 6.
Utafiti zaidi unahitajika.
Unaweza kutumia mbinu ya mawe meupe/pilipi ili kuimarisha mbinu hii ya kuhifadhi chakula dhidi ya ndovu wadadisi.
https://encosh.org/en/initiatives/water-tank-for-cassava-maturation/ (Mpango wa NGO wa Antoine Ede)
Kuning’iniza mazao ili yakauke kunaweza kuyafanya kutofikiwa na wadudu kwa muda mfupi.
Kuhifadi ardhini/sakafu Mazao mengi huhitaji kukaushwa kabla ya kuhifadhiwa ili kuyazuia kuoza.
Majukwaa ya Mbao Wazi
Njia za kawaida za kuhifadhi.
Magunia
NJIA ZA UHIFADHI ZA MUDA MREFU Kibuyu, kitoma, Vyungu vya udongo
Silo za chuma na matangi Pa kuingizia
chupa
Vikapu vya kuhifadhia Pipa la plastiki (hori) vilivyotengenezwa kwa vifaa vya mimea au silo
Hifadhi
Pa kutolea
Teknolojia mbadala ya hifadhi katika ngazi ya shambani/kijiji Hifadhi ya chini ya ardhi Jiwe
Matope
Sehemu ya ardhi
Sehemu iliyotengenezwa kwa saruji
NJIA ZINGINE ZA KUSAIDIA KULINDA CHAKULA KUTUMIA MBINU ZA PAMOJA
Hutumika katika maeneo makavu, ambapo tabaka la maji halihatarishi vilivyo ndani. Matatizo machache ya wanyama wagugunaji na wadudu, halijoto kwa kawaida haibadiliki. Hakuna haja ya ukaguzi wa kila wakati. Hasara hujumuisha kazi nyingi ya ujenzi, ugumu wa kuondoa ghala za nafaka na pia maji yanaweza kuingia.
Sakafu ya shimo inaweza kuimarishwa kwa mawe, mchanga au saruji; na kuta zinaweza kuimarishwa kwa kinyesi cha ng’ombe, waya inayotumiwa kujenga nyumba ya kuku ikiwa imepigwa plasta kwa saruji. Safu mbili za saruji, kila safu ikiwa na unene wa takribani sentimita 5, huku waya ya kujenga nyumba ya kuku ikiwa ndani kati ya safu hizi mbili inaweza kuongeza uthabiti. Inapendekezwa kuweka nafaka katika mifuko ya plastiki na kuiweka katika shimo. Kuchimba fuo ndogo zikizunguka shimo kunaweza kusaidia kuyafanya maji yasiingie katika nafaka zilizohifadhiwa. https://www.fao.org/3/t1838e/T1838E13.htm
7.
Tumia mbinu za pamoja kwa ulinzi wa ziada na ustahimilivu. Mfano: ongeza kipande cha waya au pilipili ili kulinda ghala yako ya nafaka.
KILIMO CHA MAZAO MBADALA
USIHIFADHI CHAKULA NYUMBANI MWAKO AU MAHALI UNAKOLALA
Angalia Chaguzi Za Mazao & Shugulu Za Bustani Za Jikoni.
Kulima na kuuza mazao mbadala ambayo ndovu hawapendi kula, kama mazao yenye mafuta muhimu, ambayo pia hayatavutia ndovu yanapohifadhiwa. Ndovu wa Kiafrika wameonekana kujiepusha na pilipili, alizeti, nyasi ya limau, tangawizi na kitunguu saumu na ndovu wa Kiasia huonekana kujiepusha na mrehani, citronela, chamomile, giligilani, nyasi ya limau, nanaa, na bizari.
WANYAMA WAHARIBIFU Kuwa mwangalifu wa udhibiti wa wanyama waharibifu unapohifadhi chakula. Mbinu/dhana hizi za kuhifadhi chakula zinaweza kusaidia kuokoa chakula kinachoweza kuharibiwa na wadudu (inaweza kuwa ya msaada dhidi ya wanayma waharibifu). Kutumia mbinu thabiti/salama ya uhifadhi wa nafaka ni muhimu, kwa kuwa ndovu sio tishio la pekee kwa mavuno ya mazao.
8.
Ukiweza, jaribu kutohifadhi chakula nyumbani mwako/katika mahali uapolala. Wakulima pia wanahimizwa kuhifadhi mazao yao nje ya nyumbani ili kupunguza uwezekano wa majeraha na/au uharibifu wa nyumba endapo ndovu watavamia. Gross et al. (2020) – “Hupendekeza hitaji la kupunguza kuvutia kwa vijiji vinavyohifadhi chakula katika sehemu salama zilizofungwa, mbali na sehemu za kulala na kuhimiza uanzishaji wa ghala zilizo salama kutokana na tembo, zinazofaa kwa mazingira maalum ya eneo linalolengwa.”
KUKAUSHA NA KUHIFADHI CHAKULA/MAVUNO Hakikisha kuwa umekausha chakula chako kabisa k.m mahindi kabla ya kuhifadhi. Maji yoyote katika nafaka yako yatafanya chakula kuoza au kukuza bakteria. Vyumba vya uhifadhi havipaswi kupitisha unyevu na vinapaswa kuwa na hewa ya kutosha.
ULINZI MKALI WA USIKU Ulinzi wa siku unapaswa kuratibiwa na kupangwa vyema. “Uzoeaji wa ndovu kwa usumbufu wa binadamu ni suala la hatari, linaloweza kuongezeka, hasa wakati mbinu za ulinzi zinaendelezwa kwa njia isiyoratibiwa na isiyofaa.” (Gross et al. 2019)
Changamoto zingine za uhifadhi wa chakula na hasara ya nafaka: Angalia Minara ya Ulinzi kwa maelezo zaidi.
VIDOKEZO + VYA UZINGATIAJI
Pangeni zamu na majirani wako ya kulinda dhidi ya ndovu mazao yanapokomaa au wakati tu yamevunwa na yanakauka.
Wadudu waharibifu na wanyama wengine wadogo (wadudu/ndege/wanyama wagugunaji)
Vijiumbe
Mbinu za kuhifadhi chakula zisizofikiwa na ndovu zinaweza kusaidia kupunguza uharibifu wa ndovu, lakini huenda zisizuie ndovu bado kujaribu kufikia vyanzo vya chakula. Hakikisha umejenga mjengo vyema na kwa ubora = ili kuongeza ulinzi wa nafaka. Kwa mbinu zote, kuna hatari ya ndovu kuzoea. Ni bora kuchanganya na kubadilisha mikakati. Ndovu ni werevu sana na wanaweza kubadilisha tabia yao baada ya muda. Zingatia ubadilishanaji au kuchanganya mbinu. Kuwa mwangalifu kila wakati na uupe kipaumbele usalama wako unapokumbana na ndovu. Unapolinda usiku, kuwa mwangalifu wa tabia ya ndovu na ukae umbali salama. Katao la haki –Tumia ghala ya nafaka Inayofaa kwako-https://postharvest.nri.org/lossreduction/choosing-the-right-grain-store/metal-silosand-tanks Zingatia tofauti katika Uhifadhi wa Majira makavu dhidi ya majira ya unyevu.
Hali ya hewa/Halijoto/ Unyevu
Wizi
Chaguo za hifadhi za kibinafsi dhidi ya zile za jamii
Sifa na Katao la haki:
Tumekusanya maelezo yaliyo hapo juu kutoka kwa vyanzo vingi. Mawazo yaliyopeanwa hapa ni ya Conservation Lower Zambezi, Conservation South Luangwa, Awely CAPS Programme and the International Elephant Foundation. Angalia Marejeleo kwa maelezo zaidi. Save the Elephants inashauri kuwepo kwa uangalifu kwa mbinu zote zilizokusanywa na kutolewa katika kijisanduku hiki cha vifaa. Utafiti zaidi huenda ukahitajika kabla ya kila utekelezaji maalumu wa eneo. Save the Elephants haitawajibikia gharama, au uharibifu wowote unaotokana na matumizi ya mbinu hizi.
9. Imetengenezwa Kenya 2022
Imeandaliwa na Save the Elephants
www.savetheelephants.org
Michoro na Nicola Heath