Nyua za Mizinga ya nyuki

Page 1

Nyua za Mizinga ya nyuki Ndovu huonyesha hisia mbaya kwa nyuki.

Ua wa mizinga ni mifululizo ya mizinga ya nyuki iliyounganishwa na waya na kujengwa ikizunguka nje ya shamba ili kusaidia kulinda mazao kutokana na uvamizi wa ndovu. Nyuki hutoa asali na huduma za uchavushaji kwa mkulima.

Miundo Tofauti ya Mizinga

Ndovu wakijaribu kuingia katika eneo la ua, hujaribu kupitia kwenye waya hii inayounganisha mizinga.

MMIZINGA YA MWIGO AU BANDIA

Hii itavuta waya. Na kufanya mizinga kuyumba, na kuwafanya nyuki kutoka.

Mizinga “ya mwigo” au bandia husaidia kupunguza gharama za ua na kusaidia kupeana umbali kati ya vikundi vya nyuki.

Mzinga wa Langstroth Mizinga bandia ni kama kivuli cha mizinga na inaweza kusaidia kuwadanganya ndovu wanaokaribia ua.

Ua wa mizinga hutengenezwa kwa sehemu 5 kuu: 1.Nguzo 2.Vivuli 3.Mizinga ya nyuki 4.Mizinga bandia ya nyuki 5.Waya

ORODHA YA VIFAA:

Hutumika bora ikijumuishwa na vizuio vingine.

www.elephantsandbees.com

(hulinda hekari 1 au mita 300 za mstari wa ua)

Mzinga wa baa la juu wa Kenya

Vifaa vya Kuchimba

Kifaa cha kupima

Mzinga wa zamani wa magogo

1.

Nguzo 60

Koleo

Vivuli 15

Kilo 25 za waya iliyopakwa madini/isiyopata kutu

Mizinga 15 bandia

Kilo 25 za waya ya kuunganisha

Mizinga 15 ya nyuki


UTARATIBU WA KUJENGA Kupima

Angalia Mwongozo wa Ujenzi wa ua wa mizinga (4th Ed.) wa ndovu na nyuki kwa maelezo zaidi kuhusu ua na ujenzi www.elephantsandbees.com

KUCHIMBA NGUZO

Mita 2.5-3

Kila nguzo inapaswa kuwa na urefu wa mita 2.5-3. Mashimo ya nguzo yanapaswa kuchimbwa angalau sentimita 60 kwenda chini.

1

2

Kwanza tambua eneo la shamba lako ambalo ungependa kulinda.

Jenga ua wako wa mizinga kwenye mzunguko wa eneo hili la kupanda.

3

Pima mita 7 hadi mwanzo wa jozi inayofuata ya nguzo, ili kuunda mpango wa mita 3-7-3-7.

3m

7m

7m

3m

20m

Kivuli cha mizinga yako ya nyuki

30 cm

Iliyoezekwa

2.

Tabaka za mbao

Weka kwenye mchanga na ufinyilie vizuri iwezekanavyo ili kuhakikisha kuwa nguzo ni thabiti.

60cm/ Futi 2

Nguzo za kutundika mizinga ya nyuki na mizinga bandia zinapaswa kuwa umbali wa mita 3.

Kutundika mizinga ya nyuki

Kunapaswa kuwa na mzinga mmoja wa nyuki na mzinga mmoja bandia kwa kila mita 20 za ua wa mzinga wanyuki.

Mizinga ya nyuki inapaswa kutundikwa mita 1.2-1.5 kwenda juu ili kurahisisha uvunaji wa asali.

Vivuli hukinga mizinga kutokana na joto jingi inayoweza kuzifanya nyuki kutoroka. Vivuli vinapaswa kutundikwa sentimita 30 juu ya mzinga kwa mzunguko mwema wa hewa. Vinaweza kuundwa kutoka na tabaka za mbao zilizogundishwa au kuezekwa kutoka kwa miti iliyofumwa na nyasi iliyokauka. Shikiza waya ya kuunganisha kwenye kila kona ya kivuli na uipinde kwenye nguzo. Hii itaifanya kuwa rahisi kubadilisha kivuli ikiwa itahitajika.

1.2-1.5m

Na iweze kuonekana iwezekanavyo kwa ndovu anayekaribia.


Kuunganisha ua wa mizinga HATUA YA 1: SEHEMU ZA KUUNGANISHIA

1

2

Kata waya yenye madini au isiyopata kutu katika sentimita 30. Hizi zitatumiwa kutundika mizinga ya nyuki). (Utahitaji 4 kwa kila mzinga wa nyuki).

3

Ingiza vipande hivi katika sehemu ya kushikiza kwenye kona ya mizinga.

Zungusha upinde kwenye sehemu ya mwisho ya kila kipande.

HATUA YA 2: KUTUNDIKA MIZINGA KWENYE NGUZO

4

5

6

Hakikisha pindo ziko imara kwa kuzungusha polepole mara 2-3. Ili kutundika mzinga, ingiza kipande kipya cha waya yenye madini kwenye kila upindo na kwa msumari kwenye nguzo. Mzinga unapaswa kuning’inia karibu mita 1 kutoka kwa ardhi.

Zungusha upindo kidogo katika waya karibu nusu kati ya mzinga na nguzo. Hii itatumiwa kutundika kivuli juu ya mzinga wa nyuki kwa kutumia waya nyembamba ya kuunganisha.

HATUA YA 3: KUTUNDIKA MIZINGA BANDIA KWENYE NGUZO

7

8 Ning’iniza kivuli kwa kuunganisha pindo hizi kwenye mashimo katika kivuli kwa kutumia waya ya kuungnaisha.

3.

Dhana sawa ya mizinga bandia. Unganisha mzinga bandia kwenye nguzo kwa kutumia waya iliyopakwa madini na uzungushe upindo kidogo karibu nusu.


VODOKEZO VYA UDHIBITI

Hatua ya 4: KUUNGANISHA WAYA KUU YA UA INAYOUNGANISHA MIZINGA YOTE YA NYUKI PAMOJA

9

Hakikisha kuwa waya inapitia upande wa nje wa nguzo.

10

Usipinde waya ili itakapokazwa sana iachane badala ya kuvuta nguzo na mizinga ya nyuki chini.

Ikiwa mzinga wa nyuki uko chini sana kwenye ardhi (chini ya mita 1.2), unaweza kuwa katika hatari ya wawindaji kama wanyama walao asali.

Ikiwa unaweza, weka maji safi karibu ili nyuki wanywe wakati wa jua nyingi.

Nguzo dhaifu au zisizo thabiti zinaweza kuanguka wakati wa mvua nyingi mizinga inapojaa asali. Waya inayofaa na inayotunzwa ni muhimu sana kwa ua kufanya kazi vyema!

Ni muhimu kuhakikisha kuwa mizinga yako ni safi iwezekanavyo. Nyuki hawatataka kuingia kwenye mzinga ikiwa kuna wadudu.

Nguvu nyingi sana kutoka kwa ndovu itaifanya waya kuachana badala ya, kuvuta mzinga chini.

Usikate mimea ya kiasili itoayo maua au miti ambapo nyuki hupata chakula.

Kutumia girisi kwenye waya hufukuza wadudu.

Wahimize nyuki kwa kupanda mimea na mazao yenye maua.

Sehemu nyeti za mwili kama masikio na mkonga wa ndovu hasa huwa katika hatari ya kuumwa nanyuki.

Vidokezo vya tahadhari:

Hakikisha kuwa umejenga ua umbali ulio salama kutoka kwa nyumba zilizo karibu, mifugo na barabara. Tumia nguo za kujikinga na uwe mwangalifu kila wakati unaposhughulikia nyuki. Kazi yoyote kwenye mizinga yenye nyuki inapaswa kufanywa usiku kukiwa na baridi. Nyuki wa asali wa kiafrika ni wakali sana na kuumwa na nyuki kunaweza kuwa hatari ikiwa una mzio.

Baadhi ya spishi za miti zinaweza kukatwana kupandwa tena. Mizizi yake inaweza kukua tena na kuunda ua ‘hai’ wa miti wa kutundika mizinga yako mizinga inaweza kutumiwa kusaidia kulinda miti.

Kupanda alizeti ni wazo nzuri kwa kuwa nyuki huzipenda, na ndovu hawazipendi! Tembeleya https://beesfordevelopment.org kwa rasilimali za kufuga nyuki

Kupaka nta safi ya nyuki kwenye ufito na kupaka propoli karibu na mlango kunaweza kuvutia nyuki wanaopita na kuwafanya kuingia mzingani. Mizinga inapaswa kuwa na nyuki ili kufaa kama mbinu ya kizuio.

Sifa na Katao la Haki: Wazo hili lilianzishwa na Dk. Lucy King, Elephants and Bees Project, Save the Elephants. Maelezo zaidi: elephantsandbees.com. Kwa makala na rasilimali zilizotumika, angalia Marejeleo. Huenda utafiti zaidi ukahitajika kabla ya kila utekelezaji maalumu wa eneo. Nashauriwa kuwepo kwa usalama na uangalifu kwa kila mbinu zilizopeanwa katika kijisanduku hiki cha vifaa. *Save the Elephants haitawajibika kwa gharama, uharibifu, au majeraha yanayotokana na matumizi ya mbinu hizi

4. Imetengenezwa Kenya (2021)

Imeandaliwa na Save the Elephants

www.savetheelephants.org

Michoro na Nicola Heath


Turn static files into dynamic content formats.

Create a flipbook
Issuu converts static files into: digital portfolios, online yearbooks, online catalogs, digital photo albums and more. Sign up and create your flipbook.