uLINZI WA USIKU KWA KUTUMIA TAA NA MOTO Ndovu wanajulikana kwa kuvamia mashamba wakati wa usiku. Ili kupunguza ulinzi wa usiku, njia ya vizuizi vya taa na moto inaonekana kuwa inafaa zaidi kuwafukuza ndovu kutoka kwenye mashamba na maboma.
kidokezo
Kuwa na kisanduku cha kuwashtua ndovu kinaweza kuongeza ufanisi katika kuwazuia ndovu.
Kisanduku kinatakiwa kiwe na: Simu ya mkononi ili kutuma jumbe za SMS kwa jamii husika
Tochi/Taa yenye uwezo mkubwa
Ndovu wana akili na wanaweza kuingia kenye shamba bila kutoa sauti yoyote. Shirikiana na jirani yako kuwafukuza ndovu kabla hawajaingia kwenye shamba/eneo lako. Vizuizi vya taa na moto pamoja na kelele, vimekuwa vikitumika tangu zamani kufukuza ndovu. Watafiti wamegundua kuwa ndovu wanashtuliwa zaidi na taa za kumulika kuliko kubweka kwa mbwa. Angalia Kengele za Kushtua na Vizuizi vya kelele kwa maelezo zaidi
1.
Vuvuzela/mbiu ya mgambo, au kitu chochote kitakachoweza kutoa sauti kubwa pale kitakapotumika. Ni vyema kutotegemea taa na moto peke yake ili kulinda mazao yenu na nyumba zenu. Tumia pamoja na njia zingine za vizuizi na vikwazo shambani.
Mabomu ya Pilipili ambayo yameshaandaliwa kabisa kabla ya ulinzi wa usiku.
Kidokezo cha Tahadhari Mara zote tafakari kuhusu njia ya vizuizi unayotaka kutumia, ili usiwaweke watu wengine hatarini. Soma zaidi kuhusu: Kutumia Baruti Kuokoa Ndovu
Vizuizi vya Taa
Taa hizi huwekwa kwenye nguzo na uzio mmoja mmoja unaozunguka maeneo na mashamba, ili kuzuia ndovu kuingia. Angalia Kulinda Shule & Majengo kwa maelezo zaidi ya vizuizi vya majengo.
Zinafaa zaidi nyakati za usiku.
Mwanga mkali umefanikiwa sana katika kuwatisha ndovu kuondoka mashambani. Taa ambazo huwaka na kuzima kulingana na mwendo wa mnyama, zinaweza kusababisha tembo kukimbia mbali na chanzo cha mwangaza.
Taa za Mwanga Mkali na za Sola Taa za mwanga mkali/tochi ni zana imara na salama kwa ulinzi wa usiku.
Mfano Hai Kikundi cha Wahifadhi ‘Elephants Without Borders’ kimethibitisha kuwa taa za kumulika ni njia fanisi ya kuzuia ndovu nchini Botswana. Lengo lao lilikuwa kuchunguza kama uvamizi wa mashambani usiku unaweza kupungua kwa kuweka vizuizi vya taa. Kuna uwezekano wa ndovu kuzoea njia hizi. Inashauriwa kubadili mikakati mara kwa mara ili kuwaweka ndovu mbali na shamba lako.
Ndovu hawapendi taa za kumulika na hivyo hii ni njia nzuri sana na ya haraka ya kuwafukuza ndovu. Taa za sola zimulikazo pia zinaweza kutumika kutengeneza uzio wa mpaka kwenye mashamba na maboma.
2.
Vyanzo:
Taharuki kwenye disco: Vizuizi vya taa zimulikazo za sola hupunguza hasara zinazosababishwa na ndovu wa Kiafrika Loxodonta africana huko Wilaya ya Chobe, Botswana.
Botswana
faida
+
hasara
-
Ni rahisi taa kuibiwa. Taa za uzio zinahamishika, kwani taa zinawekwa juu ya nguzo moja moja.
Zinafaa usiku tu na si mchana.
Njia nzuri ya kuwazuia ndovu.
Ndovu wameonekana kuzoea taa baada ya muda fulani.
Taa za sola zinazomulika zinaweza kujichaji mchana ili zitumike usiku ambapo asilimia kubwa ya uvamizi hufanyika.
Baadhi ya ndovu wanaofukuzwa shambani wanaweza kurudi usiku huo huo.
Gharama za wastani. Matunzo ya wastani yanahitajika kuhakikisha nguzo hazivunjwi na ndovu.
KIDOKEZO POA
Taa za kumulika zimeonekana pia kuzuia wanyama pori wengine kama simba.
Mchanganyiko wa vizuizi vya sauti na taa vinaweza kuwa fanisi zaidi katika kuwazuia ndovu.
Soma zaidi kuhusu: Taa za sola ili kuzuia wanyama zimependwa na wakulima.
Angalia Vizuizi vya Kelele kwa maeleo zaidi.
Minara ya Ulinzi
Mara nyingi uwepo wa kikundi cha wakulima ni moja ya njia bora sana za kukimbiza ndovu/kuwaweka mbali na mashamba. Doria ya kushirikiana ambapo wakulima wanapeana zamu za usiku ili kuona kama kuna ndovu wanakaribia, inaweza kufanyika. Huku wakiwa na tochi zenye mwanga mkali, ndovu wanaweza kuonekana wakiwa mbali na wanaweza kufukuzwa kabla hawajaingia kwenye eneo.
Inaruhusu ulinzi wa usiku kutokea umbali ulio salama, kwani doria ya miguu peke yake inaweza kuwa hatari nyakati za usiku. Ulinzi wa usiku juu ya minara ya ulinzi iliyojengwa kwenye mashamba na uwanja huweza kusaidia utambuzi wa mapema wa ndovu wakaribiao.
3.
Angalia vizuizi vya kelele kwa taarifa zaidi
Mavuvuzela yanaweza kupulizwa, mabati na ngoma yanaweza kupigwa ili kuwashtua walinzi, wakazi na majirani zako.
Vizuizi vya Moto Lengo lake ni kukimbiza ndovu mbali na mashamba na viwanja kwa kutumia aina mbali mbali za vizuizi vya moto.
Kuchoma mchanganyiko wa kinyesi cha zamani cha ndovu/ng’ombe pamoja na pilipili kunatengeneza wingu la moshi lenye harufu kali ambalo huwafukuza mbali ndovu.
Vifaa vinavyohitajika kwa ajili ya misokoto ya pilipili Njia za kitamaduni zinajumuisha kuwasha moto kwenye mashimo madogo juu ya ardhi katika ukingo wa kijiji, mbali na nyumba na mifugo. Kutathmini afua za shamba katika kupunguza migogoro baina ya binadamu na tembio katika wilaya ya Transmara, Kenya.
1) Misokoto ya Pilipili
Kipande 1 cha karatasi ngumu (0.75m × 0.5m); ya pakiti za maziwa, maboksi ya zamani
Majani makavu ya tumbaku 5 (ikiwa yanapatikana)
Pilipili kichaa kavu 15-20
Pilipili kavu, inapochomwa pamoja na vitu sahihi, hutoa moshi mkali sana unaowakera ndovu wakiuvuta. Majani makavu, nyasi na magugu
Kamba Angalia njia za Vizuizi za Pilipili kwa maelezo zaidi.
4.
Vyanzo:
Fimbo ndefu ya 1 m
Mkasi/kisu kukata karatasi ngumu Kuishi na Ndovu Assam- Kijitabu
1.
4.
Njia Kata karatasi ngumu na tandaza kwa usawa mchanganyiko wa majani makavu, nyasi na magugu.
Uchomeke kwa uimara msokoto kwenye tawi la mti lililo imara kwa kufunga kamba, ili msokoto uweze kushikiliwa mbali na wewe wakati unauwasha.
2.
5.
3.
Weka majani ya tumbaku na pilipili kavu juu yake.
Washa upande wa juu wa msokoto kwa moto na uache uanze kuwaka.
Kunja karatasi ngumu kutoka upande mmoja ili kufunga pamoja mahitaji, na kisha funga kwa kukaza na kamba.
kidokezo Inawezekana kusimika misokoto ya moshi kwenye ardhi, au ukaiweka sakafuni ili watu waweze kukaa katika umbali usalama mbali na ndovu na moshi.
kidokezo Angalia mwelekeo wa upepo.
Msokoto wa pilipili kwa wastani unaweza ukawaka kwa hadi dakika 15 hadi 20. Andaa mapema na hifadhi.
kidokezo za tahadhari
Usiwashe tochi za moshi au misokoto ya moshi wa pilipili ukiwa juu ya mnara wa ulinzi.
Usimkaribie ndovu kwa Zaidi ya mita 50
Mita 50
vyanzo:
5.
Mradi wa Assam Haathi: Kuishi na Ndovu Assam.
2) Mabomu ya pilipili
3) Madonge ya moto yazungukayo Donge la moto linalozunguka hutengenezwa na nguo za zamani, mnyororo na mafuta ya taa.
Angalia njia za Vizuizi ya Moto kwa maelezo zaidi.
Vifaa vinavyohitajika
Huu ni mchanganyiko wa pilipili na kelele ambao unalenga hisia za kunusa na kelele.
Mnyororo imara wa chuma
Jifunze jinsi mabomu ya pilipi yanavyotengenezwa na kutumiwa Tanzania Soma zaidi kuhusu: https://www.nature.org/en-us/about-us/where-wework/africa/stories-in-africa/using-fireworks-to-save-elephants/
hasara
-
Upepo na hali ya hewa ni mambo muhimu katika kung’amua jinsi moto unavyoweza kuwa fanisi katika kuwafukuza ndovu. Kiasi kikubwa cha pilipili kinahitajika ili njia hizi zifanikiwe.
Nguo ya zamani/ tambala
1.
Funga tambala liwe kama mpira kisha ning’iniza kwenye mnyororo na iweke tayari.
Ina ufanisi wa muda mfupi, kwani vifaa vyake huungua kwa muda mfupi.
Mara zote kumbuka
2.
Hakikisha kuwa moshi haupepei kuelekea kwa watu na mifugo kwani moshi huu ukivutwa husababisha maumivu/hukera. Epuka kutumia vizuizi vya moto kama uelekeo wa upepo hauko vizuri. Hii inaweza ikasababisha ndovu wakimbie kwenye uelekeo wa nyumba na watu. Ni fanisi zaidi pale misokoto ya pilipili inapoandaliwa mapema.
6.
Mafuta ya taa/ petroli
Weka kiasi cha mafuta ya taa kwenye chombo, nayo pia yaweke tayari.
3. Punde ndovu watakapoonekana, chovya donge la nguo kwenye mafuta ya taa na kwa umakini liwashe moto.
4.
Kumbuka haya unapotumia moto
Lizungushe hewani kwa mduara mkubwa. Wakati mnyororo unazunguka hewani, unakuwa unatoa sauti ya mvumo na kuwaka sana.
Tazama namna madonge ya moto yazungukayo yanavyofanya kazi: https://www.youtube.com/watch?v=CKeVmhbvZUY
Moto unaweza kuwa hatari kama hautasimamia vizuri.
Usiache moto bila usimamizi.
Moto mkubwa ni hatari na ni wa kuepuka. Hii inaweza kusababisha hatari ya kusambaa na kuingia mwituni.
Washa moto mbali na nyumba/maboma.
Mara zote kuwa makini sana unapokuwa unashugulika na moto.
kidokezo za tahadhari
Hakikisha unazima kabisa moto baada ya ndovu kuondoka.
Hakikisha hakuna watu unapokuwa unazungusha donge la moto hewani. Mara zote ni salama zaidi kuwapa watu taarifa mapema kuwa utatumia moto kuzuia ndovu wanaokaribia.
Mehta, P. (2012). Jinsi ya Kulinda Mazao yako dhidi ya Ndovu. Mwongozo Muhimu kwa Wakulima na Idara ya Misitu. Imefadhiliwa na Asian Elephant Conservation Fund, USFWS.
Kidokezo vya Tahadhari:
Tochi za moto kazi yake ni moja tu, kufukuza ndovu. Usiwadhuru ndovu kwa tochi za moto.
Unaweza kutupa pilipili kwenye mashimo ya moto, kwenye ukingo wa shamba lako, kama hujaandaa madonge mapema. Tumia tochi za moto pale inapobidi tu, kwani hizi zinaweza kuwa hatari kwa wote wanadamu na ndovu. Tumia vizuizi na uzio fanisi kwa ulinzi wa shamba ili kuepuka matumizi ya moto ya mara kwa mara. Angalia Kulinda Shule & Majengo kwa maelezo zaidi ya vizuizi vya majengo.
7.
Imetengenezwa Kenya 2022
Imeandaliwa na Save the Elephants
Usimkimbize ndovu na tochi za moto.
Usiwarushie miti inayowaka, mikuki au chochote kinachoweza kutoboa ngozi ya ndovu na kuwajeruhi. Hii inaweza kuwafanya wawe wagomvi na wasiotabirika.
Sifa na Katao la haki:
Tumekusanya rasilimali kutoka vyanzo mbalimbali. Baadhi ya mawazo yalizowasilishwa hapa yanatoka Elephants Without Borders, Wildlife Research & Conservation Society na The Assam Haathi Project. Baadhi ya maneno halisi yaliyotumika yamerahisishwa kwa ajili ya wepesi wa uelewa. Angalia Marejeleo kwa fasihi na maelezo zaidi kuhusiana na Ulinzi wa Usiku na Vizuizi vya Moto. Save the Elephants inashauri kuwa na tahadhari katika njia zote na taarifa zote zilizokusanywa na silishwa kwenye kijitabu hiki. Utafiti Zaidi unaweza kuhitajika kabla ya utekelezaji wa eneo husika. * Save the Elephants haihusikia na ghrama, hasara au majeraha yoyote yatakayotokana na matumizi ya njia hizi.
www.savetheelephants.org
Michoro na Nicola Heath