KENGELE ZA KUSHTUA Kengele ya kushtua ni nini?
Hii inaweza kuwa njia nyepesi, isiyohitaji teknolojia kubwa ya kusaidia kwenye ulinzi wa shamba, kwa kuwashtua wakulima pale ambapo ndovu wanaingia shambani.
Pale waya unaposogezwa na ndovu, utatoa mlio wa kengele utakaosaidia kwenye jitihada za ulinzi wa usiku. Mlio wa kengele ni muhimu sana katika kuwashtua wakulima kuhusu uwepo wa ndovu, na inaweza kusaidia kuwafukuza ndovu kabla hawajaanza kula. Waya unapoguswa, utavuta kengele na kuisababisha ilie, hivyo kuwataarifu walio karibu na kusaidia katika ulinzi wa mazao.
Aina mbalimbali? Njia za kawaida na za kisasa zaidi Uzio wa waya za kushtua zinazoamsha ving’ora vya umeme. Vishtukizi vilivyozoeleka kama vile baruti, kengele au makopo yaliyojazwa mawe. Njia moja rahisi inayoweza ikatumiwa ni ya waya wa kujikwaa. Hii itaamsha kengele endapo itawekwa njiani wanapopita ndovu. Aina za kengele za kushtua zinazotumiwa mara kwa mara ni pamoja na mabomu na makopo yaliyojazwa mawe.
Kwa nini zinafaa? Kengele za kushtua zinafaa sana kwa utambuzi wa mapema wa ndovu na kuwaonya wengine. Wakati mwingine ndovu wanaweza kuwa wakimya sana, na si rahisi mara zote kuwaona wakiingia mashambani. Hii inaweza kusaidia kuepusha kukutana kwa bahati mbaya.
Tambua: hiki pia ni kizuizi kizuri cha sauti.
1.
Unaweza kuwa mbunifu zaidi na kutumia chochote ulichonacho ili kutengeneza kengele ya kupiga kelele.
Unaweza kuzitumia na kitu gani kingine? Kengele za kushtua zinakuwa na ufanisi mkubwa endapo zitatumiwa pamoja na njia za ulinzi wa usiku na vizuizi/mjumuisho wa vizuizi. Njia zingine za ulinzi wa usiku ni pamoja na; majukwaa ya mti, vibanda vya ulinzi, tochi, mifumo ya utambuzi wa mapema, taa kali, redio au simu za mkononi. Inasaidia kujua njia zinazotumiwa mara za kwa mara za ndovu kuingia na kutoka– ili kuelekeza jitihada za ulinzi hapo.
Aina ya 1: Kengele za Kushtua za Kawaida Njia ORODHA YA VIFAA
Makopo yaliyotumika tena
1.
Hakikisha unatengeneza vitundu vidogo vidogo pembeni ya makopo hii ni ili maji ya mvua yaweze kutoka na yasijikusanye kwenye kopo.
2.
3.
Ongeza mawe kadhaa kwenye kila kopo. Ukitikisa kopo linapaswa kupiga kelele!
4.
Unaweza kutumia kengele za mifugo kama zinapatikana.
Mabomba ya chuma chakavu pia yanaweza kukunjwa na kutumika kama kengele.
Mawe
5.
Seng’eng’e au waya
Vidokezo Weka kengele ya kushtua karibu na mahali pa kuingilia ndovu. Tumia njia za pilipili pamoja na waya wa kushtukiza.
2.
Weka msumari ndani ili kutengeneza mlio wa kengele.
7.
6.
Yatundike kwa kuzunguka upana wa shamba lako la mazao kwa kutumia seng’eng’e.
Kama kuna sehemu nyingi za kuingilia, weka kengele kwenye sehemu zote ili kuhakikisha ulinzi kamilifu wa mipaka.
Unaweza kutumia kifaa chochote kitoacho kelele ulichonacho.
Kama ndovu akijaribu kuingia ndani ya mpaka, watausukuma waya wenye kengele, na hii inaweza kumshtua mkulima.
Faida/Hasara Haiwazuii ndovu kuingia na si mara zote huwa ni kizuizi. Inafaa zaidi kwa kutoa onyo mapema. Inafaa zaidi itumike pamoja na minara ya ulinzi, vizuizi vya taa na kelele. Ndovu ni wanyama wenye akili sana na wanaweza kujifunza kutafuta namna ya kuweza kuingia.
Muundo na Wildlife Research and Conservation Society
KUTENGENEZA KENGELE YA KUSHTUA
Aina ya 2: Kengele za Kushtua za Mlangoni ORODHA YA VIFAA Bawaba za chuma Waya wa Umeme zenye vitundu viiwili
Kamba ya mshipi (kulingana na ukubwa wa shamba lako)
Mkasi
Kengele ya mlangoni (na mlio mkubwa)
Swichi
Misumari wa kawaida/ muundo wa U
Nyundo
vidokezo:
Unaweza kuhitaji kuilinda kengele kutokana na mvua kwa kuifunika na aina fulani ya paa au plastiki. Kama ndovu akitegua mfumo na kuvunja waya wa kushtua, itabidi irekebishwe haraka ili iendelee kufanya kazi. Hii inaweza kuwa ngumu na hata hatari nyakati za usiku au ndovu wanapokwepo maeneo ya karibu. Hizi zinaweza kusaidia endapo zitawekwa kwa usahihi. Hakikisha unazima kengele baada ya kuwa imeteguliwa la sivyo itaendelea kulia usku kucha na betri itakwisha. Baadhi ya kengele zinaweza kukuruhusu kuingiza sauti za ndovu akiwa amekwazika, ngurumo ya chui, mbwa kubweka au watu kupiga kelele.
Tazama video kwa taarifa zaidi ya jinsi ya kutengeneza kengele hii ya kushtukiza
Huu muundo umefadhiliwa na Asian Elephant Conservation Fund (USFWS) na unatekelezwa na Wildlife Research and Conservation Society. www.wrcsindia.org
vidokezo VYA Hadhari:
Mifumo ya awali ya utoaji maonyo inaweza kusaidia kung’amua uwepo wa ndovu, lakini ni njia za muda mfupi. Kuna hatari ya ndovu kuzoea mbinu. Ni vyema kutumia mbinu mbalimbali. Inaweza kuwashtua ndege na wanyama wengine. Kwa njia zote zitakazotumika, mara zote jali na upe usalama kipaumbele unapokutana na ndovu. Unapokuwa unalinda usiku, kuwa makini na tabia za ndovu na kaa umbali wa kutosha (Angalia Makala kuhusu utambuzi wa tabia za ndovu). Njia iliyotajwa hapo juu (Aina ya 2) imeonekana kuwa njia fanisi sana kwa ndovu wa Bara la Asia. Majaribio Zaidi na uasili unaweza ukahitajika kwa ndovu wa Kiafrika.
Ni muhimu kutumia bawaba. Unaweza ukahitaji kuitengenezeha kama ikibidi. Ubadilishaji wa muundo unaweza kuhitajika ili kufaa shamba lako zaidi. Tumia Mbinu anuai.
Sifa na Katao la haki: Tumekusanya taarifa kutoka vyanzo mbalimbali. Mawazo yaliyowasilishwa hapa yanatoka kwa Dr. Prachi Mehta, Wildlife Research and Conservation Society. Taarifa zaidi: www.wrcsindia.org. Angalia Marejeleo. Save the Elephants inashauri kuchukua tahadhari katika njia zote zilizoainishwa na kuwasilishwa kwenye kitabu hiki. Utafiti zaidi unaweza kuhitajika kabla ya utekelezwaji katika eneo husika. * Save the Elephants haihusiki na gharama, hasara au majeraha yoyote yatokanayo na njia hizi.
3. Imetengenezwa Kenya 2021
Imeandaliwa na Save the Elephants
www.savetheelephants.org
Michoro na Nicola Heath