mifumo ya kutoa maonyo ya simu za mkononi & taa za led Bekoni za Kushtua
Kutuma ujumbe na kupiga simu
Huu ni mfumo rahisi wa utumaji SMS kuwaonya watu kuhusu ndovu kukaribia mahali na kutaarifu Vikosi Kazi kwenye eneo.
Timu ya Nature Conservation Foundation wametengeneza programu kutumia simu za mkononi ili kuwasiliana na kijiji kizima kwa kutumia bekoni za ishara. Bekoni zinawekwa katika maeneo ya kimkakati, yaliyoinuka ili kupata uoni wa kutosha kwa wote wakazi na wageni kwenye eneo ambao watakuwa hawajui kuhusu uwepo wa ndovu. Inapojulikana kuwa ndovu wako umbali wa 1 km kutoka kwenye bekoni za kushtua, simu au ujumbe mfupi unaweza kutumwa ili kuwasha bekoni ambayo itatoa taa nyekundu zinazomulika.
Watu wanaoishi karibu wanahimizwa kujiunga na huduma hii. Hii ni mfumo mwepesi wa taarifa za kukusanya tunaotoa taarifa za mahali wanapoonekana ndovu kwa wale waliojiandikisha na huduma hii Watu wanaoishi katika upana wa kilomita mbili wa mahali ambapo ndovu wameonekana hivi karibuni, watapokea taarifa kwanza. Badala yake, jamii inaweza kusambaza taarifa kwa marafiki na familia, ambao nao watachukua hatua na tahadhari stahili. Utafiti uliofanywa na Ananda Kumar wa NCF’s kwenye eneo la Valparai huko Tamil Nadu katika milima ya Anamalai (nyumbani kwa idadi kubwa ya pili ya ndovu nchini India), kati ya 20022007 iligundua kuwa ndovu katika eneo hilo wana uwezekano mkubwa wa kupatikana ndani ya kilomita mbili (maili 1.2) ya eneo lao la siku iliyopita. Chanzo: Mongabay 2015, Kutumia Mbinu za Kimageuzi Kulinda Mazao Dhidi ya Ndovu.
vidokezo vya Tahadhari:
Taa zinafanya kazi kwa kupiga nambari kwenye simu ya mkononi.Kama mtu anaona ndovu, wanaweza kupiga simu na taa inawaka, kuwashtua watu kwamba kuna ndovu kwenye eneo.
Hatua za ziada
NCF pia ilitumia mabango ya saa 24-Ili kuwaonya watu kuhusu ndovu.
Vikundi vya Whatsapp vinaweza kuundwa kwa ajili ya utumaji wa ujumbe kwa umma na taarifa zinasambazwa kupitia apu. Vifaa vya redio pia vinaweza kutumika katika kutoa taarifa.
Kwa nini ni muhimu?
Hii inaweza kusaidia hasa katika kupunguza kukutana na ndovu kwa bahati mbaya, kukutana nao usiku, barabarani au mahali ambapo kuna uoni hafifu.
Kama ndovu wanashtushwa na kutokea ghafla kwa mtu mbele yao, wanaweza kughafirika na kushambulia. Kwa maonyo ya mapema ya mahali alipo ndovu, migogoro mingi itaepukwa. Kwa kutumia maarifa haya, watu wanaweza kutumia njia mbadala au kutumia onyo hilo kuwasaidia ndovu kubadili uelekeo.
Njia hii inahitaji ushirikishwaji na ushiriki wa jamii katika kupata jumbe, kutoa ripoti za eneo walipo ndovu, na kushirikishana taarifa.
Sifa na Katao la haki:
Kwa kila njia, kuna hatari ya ndovu kuzoea. Ni vyema kuchanganya njia mbalimbali.
Tumekusanyataarifa hizi kutoka vyanzo mbalimbali. Mawazo yaliyowasilishwa hapa yaliundwa na Ananda Kumar, wa Nature Conservation Foundation. Taarifa zaidi: www.ncf-india.org. Angalia Marejeleo. Save the Elephants inashauri kuwa na tahadhari katika njia na taarifa zote zilizokusanywa na kuwasilishwa kwenye kitabu hiki. Utafiti zaidi unaweza kuhitajikakabla ya utekelezaji wa eneo husika.
Inafaa kutumika na minara ya ulinzi. Njia hii imeonekana kufaa kwa ndovu wa Asia. Majaribio na uasili zaidi yanahitajika kwa Ndovu wa Kiafrika.
*Save the Elephants haihusiki na gharama, uharibifu na majeraha yanayotokana na njia hizi.
1. Imetengenezwa Kenya 2021
Imeandaliwa na Save the Elephants
www.savetheelephants.org
Michoro na Nicola Heath