Minara ya Ulinzi Mahali salama, palipo juu kunaweza kusaidia katika ulinzi wa usiku na katika kuwaona ndovu wanapokaribia. Kutumia minara ya ulinzi na ulinzi wa usiku kunasaidia kuwawezesha wakulima kuchukua hatua kwa haraka na kuwa na mfumo wa utoaji maonyo mapema pale ndovu wanapokuwa karibu.
Njia ya 2: Kubwa au inayosimamiwa na jamii Kutumia jukwaa zito la chuma au la mbao.
Hii inafaa kwa maeneo yenye migogoro na njia kuu ambazo ndovu hupita mara kwa mara.
Ushirikiano bora wa jamii unahitajika ili kuweza kusimamia minara mikubwa.
Lengo kuu ni kumpa mlinzi eneo salama, lililo juu, na lenye kuonyesha sehemu kubwa ya eneo ili kulinda na kuona maeneo yanayozunguka, na kutuma ishara salama.
Njia ya 1: Ndogo, ya shambani Majukwaa madogo ya ulinzi yanaweza kutengenezwa juu ya mti au juu ya nyumba. Inaweza kuwa hatari kutokana na urefu hivyo itumiwe kwa umakini na uzoefu.
Vifaa muhimu vya ulinzi wa usiku Taa za kumulika au tochi Simu za mkononi Vizuizi vinavyotoa kelele Vifaa na mahitaji ya kulalia
1.
Inafaa Zaidi kutumika na vizuizi vinavyotoa kelele na vya taa.
Hii inafaa Zaidi kwa ulinzi binafsi wa shamba.
Kupitia Ulinzi shirikishi wakulima wanaweza kusaidia kupunguza uvamizi wa ndovu kwenye mazao na mashambani.
Kengele za kushtua kwa ajili ya kuonya Kutumia mtandao wa kengele za ng’ombe au makopo yaliyojazwa mawe pia kunaweza kufaa kuwashtua wakulima.
Kasha 1 1/2 x 1 1/2
Kama unajenga mnara mkubwa wa ulinzi, badili muundo kulingana na mahitaji yako maalum. Unaweza kuhitaji kibali maalum cha ramani.
Wavu mgumu (Geji kubwa) Sehemu 3 sawa
Sehemu ya kasha 1 1/2 X 1 1/2
Ngazi (kwenye bawaba)
Kufuli
1” x 1” Kasha la Geji kubwa
Bawaba
Seng’eng’e
Sehemu ya Kasha la 4” x 2”
Sehemu ya Kasha la 4” x 4”
Bawaba x2 Usawa wa ardhi
Mnara wa ulinzi wa jamii uliopo Sagalla (Mradi wa Elephants and Bees, Mei 2020)
vidokezo vya tahadhari:
Kuna vitu kadhaa vya hatari kubwa unapotumia minara ya ulinzi au majukwaa marefu. Tumia maelekezo ya usalama au protokali kwa ujenzi na matumizi ya minara. Hakikisha unaona vizuri na kuna mwangaza wa kutosha unapokuwa unatumia minara ya ulinzi usiku. Kuwa makini unapokuwa unapanda na kushuka jukwaa. Usipande mnara ukiwa umelewa pombe. Hakuna kukimbia wala kuruka kutoka kwenye mnara wa ulinzi.
Sifa na Katao la haki: Muundo huu wa Mnara wa Ulinzi wa Sagalla uliasiliwa na Mradi wa Ndovu na Nyuki, ulioundwa na Chris Campbell-Clause. Taarifa zaidi: elephantsandbees.com. Kwa fasihi na rasilimali zilizotumika, angalia Marejeleo. Utafiti zaidi na uchunguzi wa mifano hai unaweza ukahitajika kabla ya utekelezaji wa kila eneo. Usalama na tahadhari vinashauriwa kwa njia zote zilizowasilishwa kwenye kitabu hiki. * Save the Elephants haihusiki na gharama, uharibifu, au majeraha yanayotokana na njia hizi.
Sisitiza juu ya umakini wa hali ya juu kwa watoto na wazee.
2. Imetengenezwa Kenya (2021)
Imeandaliwa na Save the Elephants
www.savetheelephants.org
Michoro na Nicola Heath