Droni na njia za anga

Page 1

DRONI NA NJIA ZA ANGA Droni ni vifaa vya kuruka vinavyoweza kudhibitiwa kutokea ardhini kwa kutumia remoti kuwafukuza ndovu kutoka kwenye shamba kwenda kwenye usalama. Ni mbinu ya gharama kubwa, ya teknolojia ya hali ya juu inayoruhusu maafisa wanyamapori/watu walioruhusiwa kutoa muitikio wa haraka kupunguza migogoro ili kuwalinda wote binadamu na ndovu.

Droni za kuruka zinatoa mlio kama wa kundi la nyuki. Pale ndovu wanapokabiliana na droni inayoruka na kusogea yenye mlio kama wa kundi la nyuki, wataondoka kwenye eneo husika haraka mbali na muelekeo wa sauti. Kwa miaka mingi sasa wanasayansi wamekuwa wakijua kuwa droni zinazoruka karibu sana na wanyama, wakiwemo ndovu, zina uwezo mkubwa wa kuwasumbua na hata kuwaelekeza katika eneo fulani. Hahn na wenzie wamethibitisha hili kwenye mfano hai wao wa mwaka 2017, ukionyesha mafanikio ya 100% kwamba ndovu wanaweza wakafukuzwa kabisa kwenye maeneo yenye migogoro baina ya binadamu na ndovu kwa kutumia droni. Droni zinaweza pia kutumiwa kurekodi video na picha, inayoruhusu watafiti kuelewa harakati na tabia za ndovu, hivyo kusaidia kupunguza migongano.

https://www.pbs.org/newshour/show/drones-keep-elephants-away-people-tanzania

1.

Soma zaidi kuhusu: Utafiti umefanywa kuthibitisha kuwa droni zina mlio kama wa nyuki

Njia zingine za anga ni pamoja na kutumia helikopta kuwafukuza ndovu kwa usalama waondoke kwenye makazi na mashamba.


Mradi wa Ndovu wa Mara (Mara Elephant Project- MEP) nchini Kenya unatumia helikopta kwa ajili ya kazi hii na ni nyenzo muhimu sana kwenye mwongozo wa namna ya ya kukabiliana na migongano ya binadamu na ndovu.

Angalia Fahamu Tabia za Ndovu kwa taarifa zaidi

Soma zaidi kuhusu: Helikopta Pekee Mara. Mradi wa Ndovu wa Mara.

Lakini, baadhi ya ndovu inawezekana wakawa tayari wameshazoea sauti kubwa. Kwa mfano kwenye makundi ya ndovu jike, kiongozi pamoja na ndovu wengine wakubwa, wanaweza kuamua kutokuondoka ili kuwalinda watoto wao. Angalia namna ndovu wanavyofukuzwa kwa usalama kutoka kwenye mashamba: https://vimeo.com/435717204 , https://vimeo.com/465705025 , https://www.youtube.com/watch?v=D4-ZVdW1p3w&feature=youtu.be

Mfano Hai Mwaka 2016, MEP iliingia ubia na RESOLVE na Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori Tanzania ili kuanza programu ya mafunzo ya kupunguza migongano baina ya binadamu na ndovu kwa kutumia droni ndani ya mbuga za wanyama za Tarangire na Serengeti.

Soma zaidi kuhusu: https://maraelephantproject.org/mep-staff-trained-to-operate-drones-for-conservation/

Droni zilitumika jumla mara 51 kuyafukuza makundi ya ndovu, kwenye mashamba 38 na makazi 13 ndani ya mfumo wa ikolojia unaolindwa. Operesheni hii ilikuwa na mafanikio ya 100%. Waligundua kuwa kupeleka droni mbele na nyuma, nyuma ya ndovu kwa namna ya kuwachunga, ilikuwa ni njia salama zaidi ya kuwazuia ndovu kurudi kuelekea watu.

Timu 5 za wasimamizi wa wanyamapori waliongoza droni kwa kuitikia matukio ya ndovu kuvamia mashamba wakati wa kilele cha uvunaji wa mahindi.

2.

MEP iliandaa “Mwongozo wa Kurusha Droni” kwa ajili ya programu hii ambayo inapatikana ukiomba, ili kusaidia taasisi zingine kutumia droni na kupunguza migongano. Angalia Kuwalinda Ndovu wa Kenya Kutokea Angani


Changamoto 1. Uhalali na Vibali

Nchi zinazojulikana kutumia droni

Ni lazima utume maombi ili kupata vibali vya kisheria na leseni za kurusha droni ili kuimiliki nchini Kenya.

Afrika ya Mashariki, ya Kati na Kusini: Angola Burkina Faso Kenya Malawi Namibia Tanzania Zimbabwe

Una mfano hai wa kutushirikisha kuhusu matumizi ya droni yaliyofanikiwa nchini mwako?

Kushindwa kupata leseni inaweza kupelekea kutozwa faini au hata kufungwa.

2. Ndovu Kuzoea

Angalia zaidi kuhusu droni

FAIDA

+

Ina nafuu katika matunzo yake kuliko helikopta. Ni salama kuirusha na kuidhibiti.

Droni zina uwezo wa kuwa njia fanisi ya kuzuia ndovu, hata hivyo kuna utafiti mdogo kuhusu hali ya uzoeaji na ufanisi wa muda mrefu wa mbinu hii. Tafiti zinaonyesha kuwa njia nyingine za kuzuia ndovu, kama vile Vizuizi vya Kelele na Kengele za Kushtua, baada ya muda fulani hupungua ufanisi, wakati zingine kama vile uzio wa mizinga ya nyuki, huendelea kuwa fanisi.

Barabara haihitajiki ili droni kutua. Inaweza ikadhibitiwa kwa rimoti ardhini, kwa umbali ulio salama na ndovu. Inafaa katika kuwafukuza ndovu nje ya mashamba & majengo. Kama ikitumiwa vizuri, inaweza ikawa ya muda mrefu. Teknolojia ya droni na betri zake zinaimarika siku hadi siku.

3.

Angalia Uzio wa Mizinga ya Nyuki kwa taarifa zaidi


3. Usumbufu Baadhi ya tafiti zimegundua kuwa droni zinaweza kuwasumbua wanyamapori. Spishi mbalimbali za ndege, reptilia, na mamalia zimerekodiwa kubadili tabia kutokana na droni.

4. Mafunzo

5. Maadili

Droni zote zinahitaji wataalamu waliofunzwa ili kufanya kazi kwa ufanisi.

Droni zinaweza kuingilia faragha ya watu, kwani droni nyingi zina uwezo wa kupiga picha na kurekodi video.

Rebolo-Ifrán, N., Graña Grilli, M., & Lambertucci, S. A. (2019). Droni kama Tishio kwa Wanyama Pori: YouTube Yaisaidia Sayansi katika Kutoa Uthibitisho Kuhusu Madhara Yake. Uhifadhi wa Mazingira, 46(3), 205–210. https://doi.org/10.1017/s0376892919000080

Vidokezo

6. Gharama Droni ni vifaa vya gharama kubwa. Kadri ambavyo aina ya droni inavyokuwa na teknolojia ya hali ya juu, ndivyo ambavyo gharama ya kununua na kuitunza inavyokuwa kubwa. Kuwafunza watu kurusha droni pia huongezea gharama. Baadhi ya droni si fanisi sana nyakati za usiku kwani zinaweza kupata shida kuruka usiku.

http://moef.gov.in/wp-content/uploads/2017/08/HEC-management-guideline-Final1.pdf

Muda wa wastani ambao droni isiyokuwa ya gharama sana inaweza kuruka ni dakika 20-25. Betri zinahitaji kuchajiwa baada ya hapo. Imetengenezwa Kenya 2022

Kukiuka sheria hizi kunaweza kusababisha utozwaji wa faini kubwa na ikiwezekana kifungo. Endesha droni kwa umakini ili kuepuka kuanguka au kukwama kwenye miti. Mara zote hakikisha unaendesha droni katika umbali salama na wanyamapori na watu, ili kuepuka majeraha.

Kuna hatari kubwa ya kuanguka au kuruka karibu sana na ndovu.

4.

Usitumie vibaya droni, hasa ndani ya umbali fulani na uwanja wa ndege/eneo lenye ulinzi/mipaka ya nchi, ambapo huwa kuna vizuizi vya hali ya juu zaidi.

Imeandaliwa na Save the Elephants

Sifa na Katao la haki: Tumekusanya taarifa hizi kutoka vyanzo mbalimbali vilivyopatikana kwenye makala nzima. Vyanzo vikuu ni pamoja na: Connor Bennet na Mara Elephant Project (Mradi wa Ndovu wa Mara). Mwongozo huu sio kamilifu. Kujifunza zaidi kuhusu na kuchunguza kuhusu Droni na Njia za Anga, angalia Marejeleo. Baadhi ya maneno halisi kwa kawaida ndio hutumiwa yamerahishsiwa kwa uelewa mwepesi. Save the Elephants inashauri tahadhari kwa taarifa zote zilizokusanywa na kuwasilishwa kwenye kitabu hiki. Utafiti zaidi unaweza kuhitajika kabla ya utekelezaji wa mbinu husika. *Save the Elephants haihusiki na gharama, uharibifu au majeraha yoyote yatokanayo na matumizi ya njia hizi.

www.savetheelephants.org

Michoro na Nicola Heath


Turn static files into dynamic content formats.

Create a flipbook
Issuu converts static files into: digital portfolios, online yearbooks, online catalogs, digital photo albums and more. Sign up and create your flipbook.