Mikanda ya Ufuatilizi ya GPS na Uzio wa Kijiografia

Page 1

Mikanda ya Ufuatilizi ya GPS na Uzio wa Kijiografia Mikanda ya ufuatiliaji ya GPS (mfumo wa mawasiliano wa kijiografia) ni mfumo sahihi wa urambazaji unaotegemea satelaiti na mfumo wa eneo ambao umewekwa kwenye ndovu ili kufuatilia mienendo yao katika muda halisi katika maeneo mbalimbali.

Save the Elephants (STE) inatumia vifaa vya ufuatilizi vya GPS ili kuelewa maisha ya ndovu, maamuzi na mahitaji yao. Mwanzilishi wa STE Dkt. Iain DouglasHamilton alikuwa mtu wa kwanza kufuatilia ndovu kwa kutumia mikanda ya redio (1969) na STE inaendelea kuwa mstari wa mbele katika teknolojia ya ufuatilizi. Mikanda huwa na vifaa vya teknolojia ya hali ya juu ya GPS ya Satelaiti au vifaa vya kufuatilia vya GSM ambavyo huruhusu wanasayansi na maafisa wanyama pori kufuatilia, kwa muda halisi, wakati na wapi wanyama hufanya harakati katika mazingira.

Kama spishi zinazohama hama, ndovu wengi barani Afrika hutumia muda wao mwingi nje ya maeneo yaliyohifadhiwa, hii inamaanisha kwamba wengi wao wanaweza kuvuka na kuingia kwenye vijiji na mashamba ya karibu. Kuongezeka kwa idadi ya watu kumechochea ujenzi wa makazi ya watu na barabara zinazozuia kabisa kupita au kukinga njia muhimu za uhamaji kwa wanyama pori.

Kuwafunga mikanda ndovu kunajaribu kupunguza migogoro na kuhakikisha usalama wa binadamu na ndovu.

Ndovu dume aitwaye Wide Satao akiwa amevishwa mkanda © Naiya Raja/Save the Elephants Soma zaidi kuhusu: Kufuatilia — Ufuatiliaji wa Muda Halisi (Machi 11, 2022) Save the Elephants.

1.

Tazama: Vita ya Nafasi | Mgogoro baina ya Binadamu/Ndovu Maasai Mara. (Mei 16, 2022).

Kenya inatumia mikanda ya GPS iliyounganishwa na satelaiti kuwalinda ndovu, watu (Septemba 9, 2016). Save the Elephants.


Pale ndovu waliofungwa mikanda wanapokaribia mashamba/maeneo ya jumuiya au wakiwa katika hatari yoyote, afisa wanyamapori wanaweza kuvijulisha vitengo vya kukabiliana na tatizo kwa haraka na doria ya ardhini ili kuelekea kwenye eneo na kujaribu kuwatisha ndovu kwa usalama ili waondoke, kwa kutumia njia mbalimbali za kuwazuia kama vile kelele na mabomu ya pilipili.

Hitaji la kuelewa mpangilio wa harakati za ndovu na mwingiliano na mashamba huturuhusu kuandaa mbinu madhubuti za kukabiliana na migogoro ili kupunguza viwango vya migogoro na kukuza uvumilivu kwa ndovu katika jamii za vijijini.

Dume aitwaye Manolo karibu na kijiji pembezoni mwa Ziwa Jipe © Save the Elephants

2.

Mifano Hai Ndani na pembezoni mwa Mbuga ya Wanyama ya Samburu huko Kaskazini mwa Kenya, ndovu mara nyingi hukutana na wafugaji na mifugo yao kwenye sehemu za maji kama vile mito. Samburu, Kenya

Ndovu waliovishwa mikanda kwenye eneo la Samburu wanafuatiliwa ili kuwazuia wasiingie katika migogoro na wanadamu, kwani mapigano mengine yanaweza kuwa hatarishi kwa ndovu na watu. Mikanda pia husaidia kuelewa ushoroba muhimu za ndovu na kuitahadharisha jamii kuwa makini zaidi kuhusu mahali salama pa kujenga nyumba zao na kuchunga mifugo yao.

Tazama zaidi kuhusu Kuwalinda Ndovu wa Afrika na Save the Elephants

Ndovu wakipita karibu na kijiji huko Samburu © Jane Wynyard/Save the Elephants


Sehemu za Mkanda

Ndovu dume aitwaye Mangelete alifungwa mkanda kwenye Hifadhi ya Taifa ya Tsavo Magharibi (2022) na kisha akahamishwa. Tsavo, Kenya

VHF Transmita Betri Accelerometer

Moduli za kipima kasi zinaweza kutoa data za haraka kuhusu shughuli za ndovu, k.m, pale ndovu anapotoka nduki/kukimbia ghafla, anapotembea polepole, na pale anapokuwa hasogei kabisa na labda anaweza kuwa amekufa au kujeruhiwa.

Mara kwa mara alikuwa akivunja uzio na kuvamia mazao kwenye kijiji cha karibu na jamii haikufurahia. Kwa sasa hivi yupo chini ya uchunguzi wa maafisa wanyama pori walioidhinishwa. Kumhamisha ndovu dume © Sheldrick Wildlife Trust

Soma habari kamili kuhusu: Kumhamisha Ndovu Dume Msumbufu Kupitia Mkanda Wake.

Tim, ndovu dume maarufu anayependa sana nyanya kutoka Amboseli alijikuta akipenda ladha ya vyakula vya kulimwa na hivyo alikuwa mlengwa mzuri wa kuvishwa mkanda. Data zake za kufuatiliwa zilitoa uelewa kuhusu tabia yake ya uvamizi wa mazao ya Amboseli, Kenya na kuwezesha washirika wa uhifadhi kuboresha mikakati ya doria ya maafisa wanyama pori ili wanakijiji waweze kuishi kwa amani zaidi na ndovu.

Amboseli, Kenya

Maafisa wanyamapori walimfuatilia Tim kwa kutumia EarthRanger na waliweza kumfukuza yeye na ndovu mwingine mbali na mashamba, na hivyo kuzuia uvamizi mwingi wa mazao.

Mkanda unajumuisha transmita ya VHF, na betri, kitu kizito na mkanda.

Satelaiti ya GPS au kifaa cha kufuatilia GSM Ukanda mzito wa viwanda Mzingo wa kola 3-4m Uzani wa counterweight

Mkanda huzunguka shingo ya ndovu huku kifaa cha kufuatilia kikikaa juu, ambapo ishara zinaweza kuwa na nguvu zaidi, huku uzito ukiwa unaning’inia kati ya ncha mbili za ukanda chini ya kidevu cha ndovu, ili kuufanya mkanda ukae kwa uwiano. Ganda la nje la sehemu ya juu limetengenezwa kwa gundi nzito ambayo hutoa ulinzi mkali ili kuzuia vifaa vyote vilivyomo ndani kuvunjika. Miundo ya mikanda imebadilika baada ya uzoefu wa miaka mingi kwenye tasnia na kila chapa ya mkanda ina faida na hasara tofauti. Mkanda wa satelaiti unaweza kudumu kwa miaka mitatu hadi minne ambapo baada ya hapo inahitaji kubadilishwa au kuondolewa. Muda wa kudumu wa mkanda hutegemea na mipangilio utakayohitaji kwenye mkanda (k.m, maeneo mangapi kwa siku na mara ngapi unapakua data).

Mikanda haiathiri mtindo wa maisha wa ndovu. Aina ya mikanda iliyozoeleka kutumika Afrika ni pamoja na; African Wildlife Tracking, Savannah Tracking na Vectronics.

Namna mikanda ya GPS inavyofanya kazi Mifumo ya GPS inatoa taarifa kuhusu eneo/mahali alipo ndovu angalau kila baada ya saa moja (muda unaweza kubadilishwa).

Kuvisha mkanda wa ufuatilizi Tsavo, Kenya © Naiya Raja/ Save the Elephants

Frank Pope wa Save The Elephants akiwaeleza wanawake wa Kimaasai jinsi simu ya mkononi inavyotumika kuona mahali alipo ndovu aliyevikwa mkanda wa kufuatilia. © Paul Obuna/WildlifeDirect

Kahumbu, P. (2021, October 29). Siku tuliyomvika mkanda Tim, ndovu maarufu. The Guardian.

3.

Transmita kwenye mkanda zinatuma ishara kupitia satelaiti, ambayo huruma taarifa kwenye Kanzidata kuu, au kwenye programu kwenye simu, kwa mfano WildTracks na EarthRanger. Kama mkanda ukipata hitilafu, antena ya kutoa mwelekeo hutumika kutambua mawimbi yanayotolewa na Transmita za VHF (Masafaa ya Hali ya Juu) ndani ya mkanda. Mlio wa “beep-beep-beep” hutolewa kwenye redio kadri ndovu wanapokaribia kipokezi.


Ishara wakati mwingine huharibiwa na vizuizi kwenye mazingira, kama vile vilima/ milima, makorongo, mimea mnene, n.k.

Apu ya EarthRanger/WildTracks EarthRanger ni programu iliyotengenezwa na Vulcan Inc (ukiwa na mchango kutoka Save the Elephant) inayotumiwa katika maeneo kadhaa yaliyohifadhiwa duniani kote ambayo inaonyesha mienendo yote ya wanyama ili kusaidia kukabiliana na changamoto kama vile migogoro kati ya binadamu na wanyama pori. Katuni ya Mienendo ya Ndovu kwenye EarthRanger, MEP.

WildTracks ni programu ya kufuatilia iliyotengenezwa na Save the Elephants pamoja na Vulcan Inc ambayo ina manufaa makubwa pale harakati za wanyama zinapoonyeshwa ili kuangazia kasi wanayotembelea na mahali wanaposafiri mchana na usiku. Kama ndovu wakikaribia makazi ya watu, apu hizi zinaweza kutuma arifa kwa maafisa wanyamapori, hivyo kuwawezesha kuchukua hatua kabla ya tukio kutokea.

Kwa kutumia programu hizi, ndovu waliovishwa mikanda wanaweza kufuatiliwa mtandaoni kutoka popote duniani.

Soma zaidi kuhusu: Mkanda wa Kwanza wa GPS wa Kuwafuatilia Ndovu , Ufuatilizi wa Ndovu wa Save the Elephants kwa GPS , Kufuatilia ndovu kupitia teknolojia ya simu ya mkononi.

Mikanda ina transmita za redio zilizo na masafa tofauti, ili kila ndovu aweze kupatikana kwa kutumia masafa ya kipekee. Kufuatilia harakati za ndovu kupitia maombi ya WildTracks © Save the Elephants

Jukwaa la Ufuatiliaji wa EarthRanger © Mara Elephant Project

Soma zaidi kuhusu: STE Tracking App & The conservation apps revolutionizing how rangers work.

Uzio wa Kijiografia wa Kielekroniki Uzio wa Kijiografia wa Kielekroniki, ni kifaa kinachotumia GPS au Utambuzi wa masafa ya redio (RFID) ili kuunda mipaka pepe ya kijiografia kwenye kifaa. Mipaka hii inaitwa Geo-fences. Hakuna vizuizi halisi vya ardhini, hivyo watu na ndovu hawawezi kuviona kwa macho yao.

Dkt. Lucy King akitumia antena kumtafuta ndovu aliyevishwa mkanda © Madi Chan.

4.

Ufuatilizi wa VHF kumtafuta ndovu aliyevishwa mkanda huko Ziwa Jipe. Elephants & Bees.

Uzio wa kijiografia unaweza “kuwekwa alama” karibu na uzio wa hifadhi, vijiji vya eneo husika, mashamba nk. Uzio wa kijiografia, Sagalla, Kenya, uliotengenezwa kwa kutumia Apu ya WildTracks © Save the Elephants


Kama ndovu atatoka nje ya eneo analojulikana kuwepo na ama avunje uzio “uliowekwa alama” au kuingia katika kijiji cha eneo hilo na kuvamia mazao, mkanda utatuma ujumbe mfupi wa SMS, barua pepe au ujumbe wa WhatsApp kwa maafisa wanyamapori walioidhinishwa kuwataarifu kuhusu tatizo la muda huo na mahali alipo ndovu, kuwezesha kuchukuliwa kwa hatua ya haraka. Ingawa mikanda ya GPS na GSM inatumika sana, uzio wa kijiografia bado unatumika zaidi nchini Kenya na baadhi ya nchi za Afrika. Lakini, inaweza kuwa nyenzo nzuri kwa spishi zingine pia. Mipaka halisi ina gharama sana kwa maana ya muda na pesa na pia husababisha mgawanyiko wa makazi ya wanyama jambo ambalo linaweza kuibua migogoro na kuzuia uhamaji wa spishi zilizoathiriwa. Soma zaidi kuhusu Mipaka ya kijiografia, Save the Elephants.

Mifano Hai

Taarifa za Jumla

Dume la ndovu aitwaye Kimani alikuwa ndovu wa kwanza kufungwa mkanda na kujaribiwa chini ya Geofencing (Ol Pajeta) kutokana na Kenya ujuzi wake wa kuvunja uzio na kuvamia mazao.

Mikanda inatakiwa kuwekwa juu ya ndovu na watu walioidhinishwa ipasavyo tu na data nyeti zinaweza kufikiwa na wao pekee, kwa kuwa data hii inaweza kutumiwa vibaya kwa nia mbaya. Mfano wa arifa ya SMS pale ndovu aliyevishwa mkanda (Genghis Khan) alipovuka uzio wa kijiografia © Save the Elephants

Maarifa na mafunzo ya hali ya juu yanahitajika ili kutumia teknolojia hii. Uharibikaji wa mkanda unaweza kutokea na mikanda huchakaa kila baada ya miaka michache, hivyo inahitaji kubadilishwa. Wakati mwingine jamii hufikiri kumvisha ndovu mkanda humaanisha umiliki na uwajibikaji kwa uharibifu anaosababisha. Mchakato wa kuvisha mkanda unahitaji nguvu ya watu na ni gharama kumvika ndovu mkanda na ndio maana sio ndovu wote wana mikanda.

“ndovu hawa ni wenu na wangu wote wawili kulinda”

STE iliweka SIM kadi ya simu ya mkononi kwenye mkanda wa Kimani, kisha ikaweka “mpaka pepe wa kijiografia” ambao ulizunguka mipaka ya hifadhi.

Kimani alipokaribia uzio pepe, mkanda wake ulituma ujumbe mfupi kwa maafisa wanyamapori. Kegol ni mmoja wa ndovu wakubwa katika Mradi wa Mara Elephant (MEP) ambaye alivishwa mkanda na kufuatiliwa kwa kushirikiana na STE (2015). Anajulikana kwa kutoka kwenye usalama wa Hifadhi ya Mara Kaskazini kwa hiyo uzio wa kijiografia huwekwa karibu na vijiji na mashamba yaliyo hatarini. Kama Kegol akivuka kwenda eneo lisilo salama ili kuvamia mashamba, kwa mfano, MEP ingepokea arifa kuwafahamisha kuwa kuna hatari ya mgogoro baina ya binadamu na ndovu.

Sifa na Katao la haki:

Kuweka mkanda kunahusisha kumlaza ndovu jambo ambalo linaweza kuwa hatari kwa ndovu.

Tumekusanya taarifa hizi hapo juu kutoka kwa vyanzo mbalimbali vilivyofanyiwa marejeleo kote kwenye kijtiabu. Vyanzo vikuu ni Save the Elephants na Mara Elephant Project. Kujifunza zaidi kuhusu Mikanda ya Ufuatilizi ya GPS na Uzio wa Kijiografia, angalia Marejeleo. Baadhi ya maneno halisi yamerahisishwa kwa uelewa mwepesi. Save the Elephants inashauri tahadhari kwa taarifa zote zilizokusanywa na kuwasilishwa kwenye kitabu hiki. Utafiti zaidi unaweza kuhitajika kabla ya utekelezaji wa mbinu husika. *Save the Elephants haihusiki na gharama, uharibifu au majeraha yoyote yatokanayo na matumizi ya njia hizi.

5.

Imetengenezwa Kenya 2022

Imeandaliwa na Save the Elephants

www.savetheelephants.org

Michoro na Nicola Heath


Turn static files into dynamic content formats.

Create a flipbook
Issuu converts static files into: digital portfolios, online yearbooks, online catalogs, digital photo albums and more. Sign up and create your flipbook.