Tabia ya Kufahamu ya Ndovu Ni muhimu kuelewa na kuwaheshimu ndovu. Kufahamu tabia ya ndovu kunaweza kusaidia kujiepusha na uwezekano wa maingiliano hatari.
2. ENEO LA TAHADHARI
– ndovu wanawezakuwa waangalifu
Wanafahamu uwepo wako. Wanaweza kutulia na kuchunguza maeneo yao. Wanaweza kuinua mikonga yao kunusa au kuacha kula.
Kupotea kwa makazi ya ndovu kwa sababu ya upanuzi wa makazi ya watu na kilimo kunalazimisha maingiliano zaidi kati ya ndovu na binadamu.
Ni muhimu utulie.
4 MAENEO YA NAFASI YA KIBINAFSI
Kuchunguza tabia ya ndovu Sifa: ‘Kuelewa Ndovu’ na The Elephant Specialist Advisory Group, 2017 , na Miongozo ya Usalama wa Ndovu kutoka kwa Elephant Human Relations Aid.
ENEO HATARI
Kuna maeneo manne ya usalama wa kibinafsi wa ndovu.
ENEO LA ONYO
Kuwa mwangalifu wa unachopaswa kufanya unapojipata katika lolote la maeneo haya.
ENEO LA TAHADHARI
Ndani ya maeneo haya yote unapaswa kukaa kimya na kutulia.
ENEO LA STAREHE
Kunusa au kukuangalia
3. ENEO LA ONYO
Hapa, ndovu hahisi kutishiwa.
1.
– Ndovu wanaweza kuonyesha ishara za onyo
Tazama ishara za kutisha kutoka kwa ndovu kama kutikisa kichwa, kusimama akiwa ameinua kichwa, au kuonyesha kukasirika. Unapaswa kusogea polepole mbali na eneo la kibinafsi la ndovu.
Kutikisa kichwa
- Huenda ndovu ametulia
Katika eneo hili, ndovu hutulia na huenda wakaendelea na shughuli zao. Ni kama hata haupo.
Kugusa uso au sikio
Hapa, ndovu anaweza kuwa amekasirishwa na kuwepo kwako.
Kupiga hatua mbele, kuinua pembe, kubembeza mkonga mbele.
1. ENEO LA STAREHE
Kusikiliza
Kikundi cha ulinzi
MATUKIO UNAPOWEZA KUKUTANA NA ndovu
4. ENEO LA HATARI
Ndovu wanaweza kushambulia au kukimbia Eneo hili huchochea jibu la ndovu la vita au kukimbia.
Vita Ndovu anaweza kuelekea upande wako.
Ndovu wakikaribia shamba lako, Nje ya mpaka wa shamba.
Kwa kawaida kichwa huelekezwa chini, na mkonga kukunjwa, ikionyesha pembe tayari kushambulia. Kwenye vituo vya maji unapowapeleka mifugo kunywa.
Kukimbia akielekea mbele, kimya bila kutoa sauti
Kukimbia
1.
Kwa kawaida ndovu hugeuka na kukimbia huku wakiinua mkia. Ndovu wanaweza kutoa sauti huku wakikimbia.
Kukimbia, mkia juu na kichwa juu
2.
4.
2. Tazama na unuse mavi ya sasa karibu na wewe.
3.
Ndovu wakivunja nyumba yako ili kuiba mahindi yako, au kunywa kutoka kwa tangi la maji.
KAA SALAMA KARIBU NA NDOVU Sikiza sauti ya ndovu na uvunjaji matawi.
Usifuate ndovu.
Ndovu wakiwa wamejificha kichakani.
Kaa kimya. Geuka na urudi polepole. Chunguza upande wa upepo. (Unaweza kurusha mchanga hewani ili kufanya hivi). Jaribu kuelekea upande unapoelekea upepo. Tazama ikiwa kuna matawi yaliyovunjika kwenye ardhi. Tazama ikiwa kuna nyayo zaidi za ndovu.
ISHARA ZA ONYO ZA KUANGALIA 1
KUSIMAMA NA KUWA MREFU
2
KUTIKIKA KWA KICHWA
3
KUPIGA MASIKIO
4
KUZUNGUSHA MKONGA
“Nimekuona, kwa hivyo ngoja uone!”
Kusimama na kuwa mrefu, kwa kutandaza masikio nje na kuelekeza pembe kwa adui.
5
Kupiga masikio dhidi ya upande wa mwili.
Ndovu anaweza kuonekana kuongezeka kwa urefu na anaweza kusimama kwenye kitu kama gogo la mti au kichugu ili kuongeza urefu.
Ndovu akitikisa kichwa haraka na kupiga masikio kwa kasi, amekasirika.
Mtazamo wa moja kwa moja akiwa ameinua kidevu, akiangalia chini juu ya pembe. Kwa kawaida hii ni onyo kwa tishio, kama wawindaji na watu.
Mtikiso kwa kawaida huanza kwa kupinda kichwa upande mmoja na kisha kukizungusha haraka kutoka upande hadi mwingine. Masikio hupida dhidi ya upande wa uso au shingo na kutoa sauti ya juu ya mpigo.
TISHIO LA KUSHAMBULIA Kuelekea mbele haraka kwa tishio la kushambulia. Ndovu hukimbia akielekea kwa adui au muwindaji huku akitandaza masikio yake.
Kuchezesha kichwa na kurusha kichwa pia ni onyesho la tishio.
6
7 KUNG’OA MIMEA BILA KUILA 8
Ndovu anaweza kuzungusha na kurusha mkonga wake upande wa adui, kwa kawaida akitoa sauti.
KURUSHA VITu
Ndovu huinua au kung’oa vitu na kuvirusha upande wa adui.
Tishio la shambulio uhusishwa na sauti ya juu.
3.
Ndovu pia wakati mwingine hutandaza masikio wanaposisimuka, kushangaa au kushtuka.
Kuzungusha mkonga sana akiuelekeza kwa adui.
MKONGA JUU
Ndovu anaweza kusimama karibu na anayemlenga, akizungusha mkonga wake mbele na kurusha vumbi. Usimwonyeshe mgongo ndovu anayetishia kushambulia.
Ndovu anaweza kukabiliana na adui moja kwa moja akiwa ametandaza masikio yake (digirii 90 kutoka kwa mwili), wakati mwingine kwa lengo la kuonekana kutishia zaidi.
Mkonga juu, akinusa hewa ili kusikia harufu.
Ndovu anaweza kung’oa mimea na kuipiganisha dhidi ya mwili wake badala ya kuila.
Ndovu anaweza kulenga kwa ufasaha sana, hata kwa mbali.
9
SAUTI YA ndovu
Ishara zingine za kutazama Kuzungusha nyuma na mbele mguu mmoja wa mbele.
Ndovu anaweza kutoa sauti au kupuliza hewa na kutoa sauti ya kishindo.
10 KUCHIMBA CHINI KWA KUTUMIA MKONGA “Tazama nitakavyokufanyia!”
Hii hufanywa sana na ndovu wa kiume wanaotamani wa kike.
Ndovu anaweza kuinama au kupiga magoti, akichimba ardhi kwa meno na kuinua mimea kuonyesha “Tazama nitakavyokufanya.”
11
Kugusa uso wake. Kushika mkonga katika mdomo wake. Kufanya vurugu au kupiga kele ili kuonyesha nguvu. Kutikisa kichwa na mkonga wake nyuma na mbele kwa kichaka au mimea.
TISHIO HALISI Ndovu kuelekea upande wa adui haraka akitandaza masikio yake na kuinua au kuinamisha kichwa. Mkonga wake unawezakuwa umekunjwa ili pembe zake ziweze kugusa kwanza. Tishio halisi kwa kawaida huwa kimya na hatari kabisa. Jaribu kutoroka haraka iwezekanavyo, kimbia kwa mtindo wa zigizaga, au utafute kitu kikubwa cha kuwa katikati yako na ndovu (kwa mfano chanzo cha maji, kichuguu, jabali, n.k).
4.
WAKATI WA KUWA MWANGALIFU ZAIDI Ndovu wa kike walio na watoto Ndovu walio na watoto hujilinda sana, Hasa ikiwa watoto wao ni wachanga. Kuwa mwangalifu karibu na vikundi vya familia na usitembee katika njia ya ndovu wa kike walio na watoto. Wanapotishiwa na adui, ndovu wazima wanaweza kuunda kikundi cha ulinzi wakiwazunguka ndovu wadogo.
Ndovu wa kiume wanaotamani wa kike Hiki ni kipindi ambapo ndovu wa kiume huwa na ongezeko la homoni za uzazi. Hii husababisha tabia kali ya fujo. Ndovu wa kiume wanapokuwa katika hali hii ya kutamani wa kike, mara nyingi wanatafuta ndovu wa kike wa kujamiiana nao. Jinsi ya kutambua ndovu wa kiume anayemtamani wa kike? Mwenye hisia – atakuwa na hisia Na anaweza kukasirika haraka. Kutokwa na mkojo – atatokwa na mkojo huku anapotembea. Kutoa harufu – atakuwa na harufu sana.
Tezi za muda zitatoa unyaji-
Kiowevu cha mafuta na zinaweza kuvimba. (Ndovu huonekana ni kama analia)
Kuhisi njaa – Anaweza
kuonekana kuhisi njaa na kukonda, kwa kuwa hali sana anapotamani ndovu wa kike. Ndovu wa kiume anaweza kumtamani wa kike mara moja kwa mwaka kwa miezi 2-3 kila mara. Ndovu wa kiume anapomtamani wa kike, anaweza kuwa na fujo zaidi. Usimkaribie wala kumsumbua – tulia na unyamaze.
Usiku
Mimea
Unaweza kukutana na ndovu kibahati mbaya usiku ambapo ni vigumu kuona.
Mimea inapokomaa, kuwa mwangalifu kwani ndovu wana hisia kali sana za kunusa.
Ukiwa garini
Unapokaribia ndovu ukiwa garini, heshimu nafasi ya kibinafsi ya ndovu. Usitoke garini. Usiwapite, usiwafuate kwa karibu au kuwasukuma ndovu ukiwa garini. Waondokee ndovu kwenye njia. Kuwa mwangalifu wa ndovu wa kiume wanaotamani wa kike na uwape nafasi zaidi. Usiendeshe gari kati ya ndovu wanaozaana au kuendesha kwa mbio na kuwapita. Unapoendesha gari, punguza mwendo unapokaribia ndovu.
Wana uwezekano mkuu wa kuvamia shamba mimea inapokomaa.
Ndovu wanapokuwa katika shamba la jamii – jiepushe na kutembea usiku, jiepushe na pombe na uwe mwangalifu zaidi.
Kuwa mtulivu. Kuwa mwangalifu na ufahamu lugha ya mwili ya ndovu. Kuwa mwangalifu unapotembea au kuendesha gari usiku pale ambapo ndovu hupitia.
HATUA ZA KUCHUKUA
Tumia mwanga wa tochi na simu ili kuwasiliana na majirani na jamii yako kuhusu pale amabapo ndovu wako.
Linda na ukinge
Wakati wa kiangazi
Wakati wa kiangazi, una uwezekano mkuu wa kukutana na ndovu kwenye vituo vya maji.
Chunguza tabia ya ndovu
Dumisha umbali ulio salama na uwe mwangalifu wa tabia ya ndovu.
Linda shamba lako, nyumba au boma lako kwa kutumia mbinu za uzuiaji za shambani (ua, minara, dawa ya kufukuza ndovu). Kinga shamba lako–Tumia kelele za juu, taa zinazowaka na ulinzi wa usiku. Unapotumia moto wa mpaka wa shamba kwa ulinzi wa usiku–kuwa mwangalifu sana na uhakikishe kuwa moto huu umedhibitiwa. Kwa maelezo zaidi Hifadhi-Hifadhi chakula na maji kwa angalia hifadhi na ulinzi wa chakula. njia salama iwezekanavyo. Ikiwezekana, kaa upande wa chini wa upepo utokao kwa ndovu ili wasihisi harufu yako. Wape ndovu njia wapite. Kuwa mwangalifu wa maeneo ya kibinafsi ya ndovu. Rusha begi, shati la ziada, n.k. kama mtego unapotoroka ndovu.
Kuwa mwangalifu wa anga na uwe na njia ya kutorokea.
Chunguza tabia ya ndovu anachofanya akikuona, kabla ya kukaribia.
Ikiwa mnapaswa kukaribia wakati mmoja, maji yawe kati yako na ndovu.
Ikiwa ndovu anaonyesha tabia ya kutisha au wasiwasi, rudi nyuma polepole na umuondokee.
Kuwa mtulivu
Ndovu pia wanaweza kusoma lugha yako ya mwili. Usishtuke. Kaa kimya na utulie. Usisonge kwa ghafla au kukimbia. Jaribu kila wakati ikiwezekana kuwa na njia ya kutorokea. Jaribu kupanda mti ikiwa unaweza.
Usiwachokoze ndovu Kwa maelezo zaidi tazama Ulinzi Wa Usiki Kwa Kutumia Taa na Moto.
Usikasirishe ndovu wakiwa karibu. (Hasa katika maeno ya onyo na hatari) Usiwarushie mawe–hii inaweza kuwakasirisha. Usiwarushie moto.
Sifa na katao la haki:
Vidokezo vya tahadhari Mgogoro wa ndovu na wanadamu ni tishio la pili kubwa la ndovu. Ndovu ni wanyama wa pori na wanaweza kuwa hatari sana na wa kutotabirika. Licha ya kutii ishara za onyo, wakati mwingine ndovu wanaweza kuonyesha tabia isiyo ya kawaida. Kuwa mwangalifu kila wakati na uupe kipaumbele usalama wako na ukae umbali ulio salama unapokutana na ndovu.
‘Kuwaelewa Ndovu’ na The Elephant Specialist Advisory Group, 2017, na Miongozo ya Usalama ya Ndovu kutoka kwa Elephant Human Relations Aid (EHRA, Namibia). Hati hii sio pana. Kwa maelezo zaidi kuhusu tabia ya ndovu na usalama karibu na ndovu, angalia Marejeleo kwa rasilimali zaidi. Save the Elephants hushauri kutahadhari kwa njia na maelezo yote yaliyokusanywa na kupeanwa kwenye kijisanduku hiki cha vifaa. Huenda utafiti zaidi ukahitajika kabla ya utekelezaji wowote maalumu. *Save the Elephants haitagharamia gharama, uharibifu au majeraha yoyote yanayotokana na matumizi ya njia au maelzo haya.
5. Imetengenezwa Kenya 2021
Imeandaliwa na Save the Elephants
www.savetheelephants.org
Michoro na Nicola Heath