Kipato mbadala kutokana na biashara zinazojali ndovu

Page 1

KIPATO MBADALA KUTOKANA NA BIASHARA zinazojali ndovu Shughuli mbadala za kupata kipato zinatoa fursa kwa kwa wakulima kupata pesa ya ziada kwa namna nyinginezo, kuliko kutegemea moja kwa moja katika kilimo. Bidhaa zinazojali ndovu hutengenezwa kutokana na malighafi ambazo hazitishii maisha ya ndovu au kuwanyonya.

Jamii zinazoishi pamoja na wanyama pori pia wanakuwa na faida zingine zinazohusiana na uhifadhi wanyama pori uzingatiao maadili. Hii hupelekea kuimarika kwa hali ya kuishi pamoja baina ya watu na wanyama pori. Kwa sababu ya mabadiliko ya tabia nchi, ukame umekuwa ukitokea mara kwa mara, hivyo kupelekea mazao kutofikia ubora unaohitajika sokoni au hayapandwi kutokana na kukosekana kwa mvua. Kuwa na vyanzo vingine vya mapato tofauti na kuvuna mazao pia inapunguza mzigo kwa familia endapo ndovu wanafanikiwa kuvamia shamba na kuharibu/kula mazao.

1.

Afya Moja: watu, wanyama, na mazingira, vyote vinahitaji kuwa na afya ili jamii na ikolojia yetu istawi.


1) Asali Inayojali Ndovu

Ndovu hawapendi nyuki watengenezao asali hivyo kutundika mizinga ya nyuki kwa kuzunguka shamba lako, itakuwa ni njia nzuri ya kuwafukuza ndovu.

Mafuta ya mdomo yanaweza kutengenezwa kwa kutumia nta ya nyuki na kuuzwa. Elephants & Bees Project (Sagalla, Tsavo) hununua asali mbichi kutoka kwa wakulima ambao wana uzio wa mizinga ya nyuki ili kulinda mazao yao dhidi ya ndovu. Elephants Alive (Limpopo, South Africa) wanakusanya asali kutoka kwenye mizinga iliyotundikwa kwenye Miti ya Marula ambayo inatumika kuilinda miti hiyo dhidi ya uharibifu wa ndovu. Mizinga ya nyuki iliyotundikwa pia inaweza kuwazuia watu wasikate miti kwa ajili ya mkaa.

Kenya, Sagalla

South Africa, Limpopo

Kama ndovu wakijaribu kulazimisha kuingia ndani ya uzio, nyuki watatoa ‘umeme asilia’ (yaani kuwang’ata) kitu ambacho huwafukuza ndovu.

Chupa za asali na mafuta ya mdomo yanayojali ndovu © Elephants & Bees Project

Pale masega yanapokuwa yamejaa, asali huvunwa na kusindikwa kwa usalama. Asali ina thamani katika mauzo kwa ajili ya kipato cha ziada au ikitumika kama mbadala wa sukari.

2.

Tazama uzio za za mizinga ya nyuki kwa taarifa zaidi

Mishumaa iliyotengenezwa na nta ya nyuki © Elephants & Bees Project


2) Mazao yasiyoliwa na ndovu yasiyowadhuru Miradi ya Tom Yum project (Thailand) na Elephants & Bees Project(Sagalla, Kenya) inawaunga mkono wakulima kupanda mazao yasiyoliwa na ndovu bila kutumia kemikali.

Mazao yasiyolika ni yale yasiyoliwa na ndovu. Ukipanda mazao haya itapunguza uvamizi wa ndovu, ambao utapunguza migongano. Angalia Chaguzi za Mazao kwa maelezo zaidi kuhusu mazao yasiyoliwa na ndovu.

Jamu ya matunda na ya Marula na Ubuyu © The Pepper Company

Kenya, Sagalla Thailand

Mazao haya yanatumiwa kwenye bidhaa mbalimbali za mikono kama vile sabuni na mishumaa.

Mazao kama vile alizeti, mchaichai na vitunguu swaumu, n.k. Mshumaa na sabuni ya asali © Elephants & Co

Tangawizi Alizeti

Mbegu za alizeti zikivunwa zinaweza kutengenezwa kuwa mafuta na kisha kuuzwa.

Vitunguu Swaumu

Biringanya

Mabaki yanayobakia baada ya mafuta kukamuliwa hutumiwa kama chakula cha mifugo. Majani na miti ya aizeti inaweza kukusanwa na kuuzwa kwa wakulima wa maziwa, au kulishwa kwa mifugo.

Binzari

Pilipili Hoho

Pilipili Manga

Bamia

Ufuta

Viungo k.m. nanaa, rosemeri na mwarobaini

Mpira

Mchaichai Matunda jamii ya ndimu kama vile malimao

The Pepper Company inapata malighafi (ubuyu, ulezi na pilipili) kutoka kwa wakulima wanaoishi maeneo yenye migogoro kati ya binadamu na ndovu ambao wamejikita katika jitihada za uhifadhi, na kutengeneza bidhaa kama vile kachumbari na chachandu za pilipili.

3.

Shamba la alizeti linalolindwa na uzio wa mzinga wa nyuki © Elephants & Bees Project

Sabuni pia zinaweza kutengenezwa kutokana na mafuta ya Mwarobaini na aloe vera.

Angalia zaidi: Upandaji mbadala wa mazao


3) Chai Inayojali Ndovu

4) Biashara Ndogondogo

Ndovu hawahitaji majani ya chai, lakini ardhi ya kilimo kwa ajili ya utengenezaji chai ina nafasi muhimu kama maeneo yanaowezesha uhamaji baina ya mazingira asili. Hii inaonekana sana huko Assam, India, ambapo mashamba ya chai yapo katika maeneo mengi ambayo wanyama huishi. Ndovu hawana budi kupita katikati ya mashamba hayo. Kulinda makazi ya ndovu na rasilimali za maji, hupunguza migogoro baina ya watu na ndovu kwani ndovu hawalazimiki kuingia kwenye mashamba ya chai.

Wanawake wanahimizwa kutengeneza bidhaa kama vile vito, vikapu, mikoba, bangili na vingine ili kuuza sokoni au kwa watalii, ili kupata pesa ya ziada kwa ajili ya familia zao.

a. vito Mlambeni Basket Weavers (Sagalla, Tsavo) na Wildlife Works (Voi, Kenya) wanatoa ajira kwa wanawake wanaotengeneza bidhaa za mikono.

India, Assam

Kila bidhaa inayonunuliwa inawapa wanawake kipato na kuwapa mbadala wa kupata kipato kupitia kilimo tu.

Makampuni ya chai yameungana katika jitihada za uhifadhi ili kuweza kuanzisha programu ya kwanza duniani inayolenga kutoa ahueni kwa uhifadhi wa ndovu porini © Wildlife Friendly Enterprise Network

Elephant Friendly Tea inawahimiza wakulima kupanda chai bila kutumia kemikali kama vile viuatilifu. Mashamba ni lazima yawe na mashimo-mlalo katikati ya chai ili kuwawezesha ndovu kupanda endapo wataanguka kwenye moja ya mashimo. Angalia mashimo kwa maelezo zaidi

Vikap vilivyotengenezwa kwa mkono © Elephants & Bees Project

Bangili za shanga zilizotengenezwa kwa mkono © Wildlife Works

Kemikali kutokana na uzalishaji wa chai unaweza kuchafua maji na kuwadhuru watu na ndovu kwa sumu. Soma zaidi kuhusu: Makampuni ya Chai Yaalikwa Kujiunga na Jitihada za Uhifadhi Kupitia Ubia wa Chai Inayojali Ndovu wenye Ithibati.

4.

It’s Wild! (COMACO, Zambia) inauza vito vya mitego vilivyotengenezwa kutokana na mitego iliyokamatwa na wakulima wa ndani ili kulinda wanyama pori na inapatikana kwa watumiaji duniani kote. Hii inahamasisha wanajamii kukusanya mitego yoyote. Tazama zaidi kuhusu: Hadithi Crafts- Utengenezaji wa Vikapu vya Kiafrika. Soma zaidi kuhusu: Bidhaa zinazopatikana kutoka kwa wakulima wadogo.


b. Ushonaji wa nguo Shuguli hii inahitaji kiwango kidogo cha mafunzo na inaweza ikawa shuguli yenye kulinda ndovu na chanzo kizuri cha kipato wafanyakazi wenye ujuzi na kipato kwa mwaka mzima.

c. Ufugaji wa kuku wa nyumbani Kwa kutumia muda na fedha kidogo katika utunzaji kuku na chanjo, wakulima wanaweza kukusanya mayai na wakawa na nyama ya kuuza. Kinyesi cha kuku pia ni chanzo kizuri cha mbolea ya kuongezea kwenye ardhi ya kilimo.

Ushonaji pia ni shughuli inayowafaa wanajamii wazee/walemavu ambao hawana nguvu ya kulinda mashamba yao au kujenga vizuizi dhidi ya ndovu.

Mwanamke wa Mlambeni akishona kwa kutumia cherehani ya umeme © Elephants & Bees Project

kidokezo

Mavazi ya ufugaji nyuki na ukulima kama vile glovu, barakoa, nguo za kurina asali na maovaroli yanaweza kushonwa na wakulima wa ndani.

Ufugaji kuku unawakilisha chanzo mbadala cha protini ya hali ya juu kwa jamii. Kuku wanaweza kuwa mbadala muafaka kwa jamii zinazojihusisha na ujangili wa wanyama pori. Kuku pia hula nge, kunguni, tunutu na wadudu wengine wanaotoka kwenye bustani ya jikoni.

hasara

-

Chakula cha kuku ni lazima kiwe kizuri, la sivyo kuku hawatakuwa na afya, hivyo kuathiri ukubwa na ubora wa mayai na nyama.

hasara

-

Vyerehani vingi huhitaji umeme.

Matunzo kiasi ya cherehani yanahitajika.

Wanawake Niger wapiga hatua kupitia vyama vya ushonaji

5.

Kuku wanahitaji matunzo na usafi kiasi. Kama hawatatunzwa vizuri, ni rahisi kwa magonjwa kusambaa na biashara kufa. Maarifa fulani yanahitajika ili kukuza kuku wenye afya, lakini maafisa kilimo wengi wanaweza kusaidia katika mafunzo yake. -Ufugaji kuku huongeza chanzo cha kipato na kuboresha maisha. -Kuku wanaweza kuongeza kipato.


5) Pombe Inayojali Ndovu Bia zinaweza kutengenezwa kutokana na ulezi ambao umepandwa mashambani kwa kuzingatia uendelevu. Ingawa ndovu wanaweza kula ulezi, sio zao wanalolipendelea, hivyo ukiweka vizuizi vya ulinzi kwenye uzio unaweza kuwaepusha ndovu kwenye mashamba yako. Taarifa zaidi kuhusu ulezi na ndovu: The Living Elephants.

Ulezi ni zao linalohimili ukame, hivyo linaweza kustawi vizuri kwenye maeneo makavu.

6) Bidhaa zinazotokana na kinyesi cha Ndovu Kinyesi cha ndovu hupatikana bure kabisa, tena kwa kiasi kikubwa na kimethibitka kuwa na matumizi mengi.

Kitamaduni kuvuta moshi wa kinyesi cha ndovu huweza kutibu kichwa kuuma na kupunguza maumivu ya jino. Kataara Women’s group (Rubiriizi, Uganda) wanafanya kazi ili kutokomeza kabisa ujangili kwa kutengeneza makaratasi yanayotokana na kinyesi cha ndovu.

Okavango Craft Brewery (Botswana) hununua ulezi kutoka kwa wakulima wadogo wanaozunguka bonde la Okavango kwa bei nzuri ili kuwanufaisha kwa jitihada zao za kuishi pamoja na ndovu.

Uganda Bidhaa zilizotengenezwa kutokana na kinyesi cha ndovu © Kataara Women’s group

Bidhaa hii inayojali mazingira inatumika kutengeneza zawadi na bidhaa za uandishi za kipekee na zilizotengenezwa kwa mikono, bidhaa kama vile fremu za picha, vitabu vya wageni, kadi, mifuko na kadi za mialiko. Soma Zaidi kuhusu: - Kutengeneza Karatasi kutokana na Kinyesi cha Ndovu ili kupambana na Ujangili. Tazama Karatasi Kutokana na Kinyesi cha Ndovu

Wanageuza ulezi kuwa bia za viwanda vidogo. Asali inayojali ndovu inaweza kutumika kutengeneza bia au pombe za kienyeji, na viwanda vya bia hutoa soko mbadala.

Nampath Paper (Mwaluganje Elephant Sanctuary, Kenya) inatumia kinyesi cha ndovu kutengeneza karatasi. Mchakato wa utengenezaji karatasi huanza pale ndovu wanapokula nyasi na miti na kuitoa kwa namna ya kinyesi. Kutokana na 50kg za kinyesi cha ndovu, hupatikana karatasi 125. Mbinu hii ya utengenezaji karatasi inapunguza ukataji miti hivyo kupunguza kidokezo athari za mabadiliko ya tabia nchi.

Mradi huu unaendeshwa na Ecoexist. Tazama zaidi kuhusu uhifadhi wa viwanda vya pombe https://www.youtube.com/watch?v=xaR1DObmonw&t=1s

6.

Bia iliyotengenezwa kutokana na ulezi © Okavango Craft Brewery

Angalia Duka la Mtandaoni nchini Thailand, linalouza bidhaa zilizotengenezwa kutokana na kinyesi cha ndovu Karatasi ya Nampath iliyotengenezwa kwa kutumia kinyesi cha ndovu: Chanzo- Makala ya Gitonga Njeru


7) Mkaa Mbadala Kutumia nishati mbadala ya kupikia ili kuachana na mkaa ni muhimu sana kwani kukata miti kwa ajili ya mkaa kunataabisha mazingira, na kuathiri binadamu na wanyama pori. Eco-makaa Briquettes (Kencoco, South of Kenya) inatumia fursa ya kuwepo kwa taka nyingi za nazi (vifuu vya nazi na mabufuru) kwenye eneo ili kutengeneza mkaa kwa ajili ya kupika au kupasha joto.

faida

+

Mkaa mbadala unatumika kama mbadala wa gharama nafuu ukilinganisha na nishati nyingine zinazoharibu mazingira kama vile kuni, mafuta ya taa na mkaa wa miti unaotoa gesi nyingi. Una kiwango kikubwa cha joto, huwaka kwa muda mrefu, hivyo unafaa zaidi kuliko kuni au mkaa wa kawaida.

hasara

Kwa kiasi kikubwa hauna moshi, hivyo kutoa faida za kiafya kwa watumiaji wa ndani.

Kutumia taka za mazao ni mbadala wa nishati zingine kama vile makaa na mafuta.

vidokezo: 7.

Hakikisha kuna soko linalopatikana kwa ajili ya bidhaaa mtakazoamua kuzalisha/ kutengeneza endapo mtataka kuuza masalia kwa ajili ya biashara. Bidhaa ni lazima zikunufaishe wewe na zinufaishe mazingira ili kuweza kupunguza athari za mabadiliko ya tabia nchi na kutoa kipato mbadala tofauti na kilimo.

Imetengenezwa Kenya 2022

Imeandaliwa na Save the Elephants

-

Mkaa mbadala unaotokana na taka za mazao unaweza kuchukua muda kabla haujashika moto na kuwaka.

Green charcoal briquettes (Uganda) hutengenezwa kwa taka za mazao kama vile maganda ya ndizi yaliyokaushwa, maganda ya buni, mimea na majani ya miti ambayo yamekaushwa na kusagwa kuwa vipande vidogo vidogo. Mchanganyiko huo huchanganywa na udongo mfinyanzi/matope kisha kukandwa kuwa madonge au matofali na hutandazwa ardhini ili kukauka kwa siku 3.

Mkaa mbadala uliotengenezwa kutokana na taka za nazi © The Charcoal Project, Kencoco Ltd

Mkaa unaojali mazingira.Imetolewa kwenye Makala ya Godfrey Olukya, Anadolu Agency.

Tazama zaidi Kencoco

Sifa na Katao la haki:

Tumekusanya rasilimali kutoka vyanzo mbalimbali. Baadhi ya njia zilizowasilishwa hapa bado zipo katika hatua ya majaribio na utafiti zaidi unatakiwa kufanyika. Angalia Marejeleo kwa taarifa zaidi. Save the Elephants inashauri kuwa na tahadhari na njia na taarifa zote zilizowasilishwa kwenye kitabu hiki. Utafiti Zaidi unaweza ukahitajika kabla ya utekelezaji wa eneo husika. * Save the Elephants haihusiki na gharama, uharibifu au majeraha yoyote yatakayopatikana kwa kutumia njia hizi.

www.savetheelephants.org

Michoro na Nicola Heath


Turn static files into dynamic content formats.

Create a flipbook
Issuu converts static files into: digital portfolios, online yearbooks, online catalogs, digital photo albums and more. Sign up and create your flipbook.