MUONGOZO WA UFUGAJI NYUKI NA USALAMA Ufugaji nyuki ni kutoa matunzo sahihi na ungalifu ufaao kwa mizinga yako ili nyuki waliokwepo wasiiache mizinga yao na wewe uweze kuvuna asali ya kiwango cha juu kwa usalama.
Uvunaji wa asali unafaa ufanywe na watu wawili hadi watatu, na mara nyingi hufanyika usiku, pale nyuko wanapokuwa wamepumzika ili kuepusha watoto na mifugo kung’atwa na nyuki. Ukiwa unavuna asali usiku, tumia taa nyekundu kwani nyuki hawaitambuai rangi nyekundu na pia wanakuwa na fujo pale wanapoona mwanga mweupe.
Epuka kufungua nyuki wanaokaliwa kama mvua au upepo. Miundo iliyopendekezwa ya mzinga inaruhusu salama uvunaji wa asali, bila kusumbua nyuki.
Kutunza mizinga mara kwa mara ili iwe misafi ni muhimu kwani nyuki ni wasafi sana na wanahitaji nyumba iliyo safi.
Mzinga wa masanduku
Mzinga wa KTBH
Mzinga wa Gogo
Mavazi ya Kinga Ufugaji nyuki unahitaji seti nzima inayojumuisha:
Hawatahamia kwenye mzinga ulio mchafu au ambao wanaishi wadudu wengine kama vile nyigu, buibui, nondo, mijusi au hata nyoka. Wapatie nyuki maji safi kila wakati kwani wanahitaji maji ili kundi la nyuki lifanye kazi vizuri, na maji yaliyochanganya na sukari (shira) wakati wa kipindi cha kiangazi.
1.
Ovaroli na taji la uso
Glovu
Viatu vya mipira (kama vinapatikana)
Utunzaji wa Mizinga 1. Mavazi ya Kinga Hakikisha unafunika ngozi yote inayoonekana kwa mavazi sahihi, ili nyuki wasikung’ate.
2. Nyumba ya kuangulia mayai na Bumba la Nyuki Zalia linamaanisha mayai na watoto wa nyuki wa asali.
Bumba la nyuki huongezwa tu pale ambapo nyumba ya kuangulia mayai inapokuwa imekaliwa kikamilifu na kundi la nyuki lililo na afya, na wanajishughulisha kikamilifu na uanguaji mayai. Kisanduku cha asali
Wakati mwingine unaweza kuhisi kunga’twa ndani ya ovaroli lako endapo nyuki wamekosa udhibiti au ovaroli ni chafu. Angalia kama ovaroli lako halina sehemu ya wazi/ matundu. Kama kuna matundu, funika kwa gundi ya karatasi au tengeneza ovaroli.
Kizuia Nyuki
Malkia
Tumia muda wa kutosha kulivaa vizuri, kwa usahihi.
3. Epuka kuwaponda nyuki Nyuki wanapoanza kuzunguka kwa fujo, usighafirike kwani ovaroli itakulinda dhidi ya kung’atwa. Nyuki watakapoanza kuwa na fujo, tumia bomba la moshi na taratibu wapulizie moshi. Kama uking’atwa, kuwa mtulivu na taratibu ondoka mbali na mzinga.
Nyumba ya kuangulia mayai
Kizuia nyuki cha wavu kinawekwa baina ya visanduku viwili; ni kikubwa cha kutosha kwa nyuki vibarua kupita lakini malkia hawezi. Usipulizie marashi au kupaka mafuta yoyote yenye harufu kabla ya kuvuna kwani harufu hiyo inaweza kuwaghafirisha nyuki na kuwasababisha washambulie.
Hii inaweza kuchukua wiki 2 hadi miezi minne kujaza chumba cha uanguaji, kutegemea na upatikanaji wa maua. Makundi ya nyuki yanastawi vizuri kwenye maeneo yenye maua mengi na maji ya kutosha. Kuongeza bumba la nyuki mapema sana kutasababisha nafasi tupu ya kuwezesha wadudu kukaa na itakuwa ngumu kwa nyuki kuratibu hali ya hewa ya nje. Nyumba ya kuangulia haipaswi kuvunwa asali, ili kutokuwapa shida nyuki na malkia. Mayai na vifaranga vinapoharibiwa, nyuki huogopa na hutekeleza mzinga.
2.
Harakati zozote za ghafla na kelele kubwa zitawaghafirisha zaidi nyuki. Epuka kuwaponda nyuki unapokuwa unarudisha vyumba na mfuniko. Tumia brashi laini ya nyuki au majani kuwaondoa nyuki taratibu kutoka kwenye mzinga na kwenye kingo.
Makundi madogo hayatavunwa asali kwani yanazingatia zaidi ulezi wa vifaranga. Kwa taarifa zaidi: Mwongozo wa Ujenzi wa Uzio wa Mizinga ya Nyuki na Dr. Lucy King.
Uvunaji Asali
Vifaa vinavyohitajika Kisu/Chuma cha mzinga
Kitambaa cha pamba/marikeni
1. Kupulizia Mzinga Moshi huficha feromoni za hatari zinazotengenezwa na nyuki waliokerwa, hivyo itapunguza fujo wakati wa kufanya kazi. Moshi pia huwadanganya nyuki kuwa kuna moto na nyuki hujikuta wanakula asali yao, wakijiandaa kuondoka. Katika mchakato huu, hawawezi kung’ata haraka kama ambavyo matumbo yao yangekuwa hayana kitu.
Chujio lenye nyavu mbili
Vidokezo vya Tahadhari
Usiwapulizie moshi mwingi nyuki. Usiwashe moto wa moja kwa moja kwenye mzinga.
Ndoo
Chupa / vyombo vitupu vya kuhifadhia asali
2. Kutoa Usega
Rina asali mbali na mzinga wa nyuki. Hakikisha hakuna nyuki anayekufuata.
Wakati wa kutoa usega ili kuangalia asali, hakikisha unarudisha kwenye mzinga kwa mpangilio ule ule kama awali.
Hakikisha vifaa vyote na maeneo ya kazi ni masafi kabisa na pakavu bila matone ya maji. Zingatia kanuni za usafi. Kwa umakini kata (engua) sehemu nyembamba ya nta iliyotengenezwa juu ya masega kwa kutumia kisu, kisha ihifadhi.
Kuwa makini na moto/ moshi; usiuache bila uangalizi. Weka bomba la moshi mbali na wewe ili kuepuka kuungua. Liweke mbali na pua, macho na mdomo wako.
Kata masega kutoka kwenye usega na weka kwenye chombo kisafi.
Ingawa unavuna asali, mzinga bado ni makazi yao asilia, hivyo lazima ushugulike kwa umakini.
3.
3. Kurina Asali
Kwa umakini na taratibu nyanyua usega moja moja na angalia kama masega yamejaa asali.
Usiwashe moto kwenye uso wa mtu.
Unapokaribia mzinga, fukiza moshi kidogo pembeni na ndani ya uwazi, huku ukiwa unainua mfuniko.
Viberiti
Vifaa vya kupulizia moshi maranda, kinyesi cha ndovu, gunia, vijiti vidogo vikavu na majani makavu yaliyokandamizwa.
Usega wenye masega madogo madogo au kiasi kikubwa cha asali isiyofunikwa inafaa usiguswe/urudishwe na kuangaliwa tena kwenye msimu unaofuata.
Huku ukitumia jiwe safi laini au mwiko wa mbao mzito, ponda/saga masega kwenye chombo. Chuja asali iliyosagwa kwa kutumia chujio la nyavu mbili na ondoa mapande yoyote makubwa.
4. Bidhaa zilizoongezwa thamani Asali halisi inaweza kuwekwa kwenye chupa na kuuzwa kwenye masoko ya ndani, au mashirika yanayouza asali. Asali iliyosalia ni rasilimali muhimu inayoweza kutumika kutengeneza bidhaa za nta kama vile mishumaa au mafuta ya mdomo vinavyoweza kuuzwa kwa ajili ya kipato cha ziada. Baadhi huweza kutumika kutengeneza mikanda mipya ya nta kwa ajili ya mzinga wako. Angalia Shuguli za Kipato Zinazojali Ndovu.
Mahitaji Hamisha kwenye kitambaa cha marikeni kilichokaa juu ya chujio la nyavu mbili, kisha kamulia asali kwenye jagi. Kilichobaki baada ya urinaji ni mabaki ya kunata nata ambayo yakichemshwa hutengeneza nta ambayo inaweza kutumiwa kutengeneza mishumaa na mafuta ya mdomo.
4.
1.
Bidhaa zilizoongezwa thamani kutoka kwenye uzio wa mizinga © Elephants & Bees
Mishumaa
2.
Nta iliyosalia
Utambi wa mshumaa/ kamba ya pamba iliyokunjwa
Umbo kwa ajili ya kuumba mshumaa wako
Mabaki ya kunata nata
Soma zaidi: Bidhaa zilizoongezwa thamani za Kituo cha Utafiti cha Ndovu & Nyuki
Mafuta ya kupikia
Kwenye moto wa chini, taratibu yeyusha nta kwenye sufuria.
Umbo linaweza kuwa kitu chochote kitakachoupa umbo mshumaa wako, m.f, umbo la silinda au mraba. Sambaza mafuta ya kupikia ndani ya umbo.
3.
Kata utambi kulingana na ukubwa wa mshumaa (inatakiwa iwe ndefu kidogo kuliko mshumaa), idumbukize kwenye nta ya maji na ifungie chini ya umbo.
4.
Kwa umakini mimina nta iliyoyeyushwa na ruhusu ipoe kabisa kwa takribani saa 5 kabla ya kutumia.
Mafuta ya mdomo
Mahitaji
200mls Mafuta ya zaituni
50gm ya nta iliyosalia
1.
50gm mafuta ya nazi
2.
3.
Kwenye moto wa chini, taratibu yeyusha nta kwenye chombo.
Ongeza mafuta ya zaituni na nazi kisha koroga mpaka nta itakapoyeyuka tena halafu ondoa kutoka kwenye moto.
Mara zote hifadhi asali yako iliyovunwa kwenye chombo kilichofungwa. Nyuki wanavutiwa sana na asali yao wenyewe na wataitafuta hata nyumbani kwako.
Asali iliyovunwa inapaswa kuhifadhiwa kwenye chombo kilichobana kwa sababu inaathiriwa na unyevu unyevu.
10gm marashi (marashi yoyote ya mimea kama vile vanila, lavenda, nanaa, waridi, n.k)
4.
Ongeza asali na marashi. Changanya vizuri, hadi itakapoanza kuwa nzito.
KIDOKEZO
Kwa taarifa zaidi: Mwongozo wa Ujenzi wa Uzio wa Mizinga ya Nyuki na Dr. Lucy King.
5.
20gm asali
Taratibu mimina kwenye chupa/vikopo vidogo wakati ikiwa bado ni kimiminika. Kama ikiganda wakati unajaza makopo, pasha tena kidogo na endelea kumimina.
Kung’atwa na nyuki si hatari labda tu kama una mzio au umeng’atwa na nyuki wengi kwa wakati mmoja.
Mwongozo wa Usalama
Angalia Uzio wa Mzinga wa Nyuki
Kung’atwa na Nyuki
Ufanye nini uking’atwa? Ondoa mwiba wa nyuki haraka sana ili kupunguza kiasi cha kusambaa kwa sumu. Fanya hivi kwa umakini, ukiondoa na msumari au kisu/chuma cha mzinga. Usiondoe moja kwa moja na mkono kwani itasambaza sumu haraka zaidi.
Kitu gani kinaweza kusababisha ung’atwe na nyuki? Kutembea karibu sana na mzinga wenye nyuki (hasa nyakati za mchana). Kusimama karibu na njia ya nyuki au mlango wa mzinga. Kufanya kazi kwenye mzinga bila msaada wa bomba la moshi na ovaroli. Kupaka mafuta yenye marashi au marashi. Kuongea kwa sauti, kupiga kelele au kubamiza vitu karibu na mzinga wa nyuki. Kuusumbua/kuutikiza mzinga kwa nguvu.
6.
Kuwa makini kama unatumia kisu/au kitu chenye ncha kali kuondoa mwiba. Taratibu ondoka mbali na mzinga au kundi la nyuki. Tumia bomba la moshi kwenye eneo ulilong’atwa ili kuficha feromoni na kupunguza kusambaa kwake la sivyo itawavutia nyuki wengi zaidi kung’ata. Kuwa na dawa za antihistamine nyumbani kwako. Hupunguza madhara ya kuwashwa na kuvimba. EpiPen inaweza kutumiwa endapo kutakuwa na madhara makubwa ya mzio kutokana na kung’atwa na nyuki.
Kidokezo cha Tahadhari Kama una mzio na miiba ya nyuki, tafuta msaada wa daktari haraka sana kama umeng’atwa.
Mifugo Kama ambavyo ndovu na watu hawapendi kung’atwa na nyuki, pia wanaweza kuikera mifugo.
Kuwaweka watoto salama
Kama una mifugo, hakikisha unaiweka kwenye uzio wa tofauti, katika umbali salama. Wataarifu watu kwenye eneo lako kuwa unafuga nyuki, ili waiweke mifugo yao mbali na shamba lako.
Watoto wako kwenye hatari zaidi ya kung’atwa na nyuki. Wafundishe watoto wako wakubwa namna ya kuenenda kwa usalama kwenye shamba lako, huku wakikaa mbali na mizinga yote ya nyuki. Usiwaache watoto wadogo bila usimamizi karibu na mizinga.
Nyegere Nyegere wanavutiwa sana na mizinga ya nyuki kwa ajili ya asali yao, na wanaweza kuwa na vurugu kwa wanyama wengine. Ni muhimu kwa mfumo wa ikolojia na mara nyingi hula panya na nyoka, hivyo kuwaondoa viumbe hawa kwenye jamii yako. Mara nyingi huwakimbia wanadamu, hivyo si hatarishi kwako na kwa familia yako. Usiwadhuru au kuwaua nyegere ili kulinda asali yako. Ukiwa umbali salama, wakimbize kwa kupiga kelele na kupiga piga vitu. Tumia banda la nyegere linalotengenezwa kutokana na chuma zilizokunjwa au waya mgumu na kisha weka pembezoni kwa kila mzinga ili kuilinda dhidi ya nyegere.
Vidokezo vya Tahadhari
Inashauriwa kuepuka kuvuna asali ukiwa peke yako. Lakini, kama unavuna ukiwa peke yako, hakikisha una simu/redio pamoja nawe, ili uweze kuwasiliana endapo ajali inatokea na unahitaji msaada wa kitabibu. Usivune ukiwa umelewa pombe au dawa za kulevya.
7.
Imetengenezwa Kenya 2022
Imeandaliwa na Save the Elephants
Banda la nyegere lililokamilika © Elephants & Bees
Sifa na Katao la haki: Tumekusanya taarifa hizi kutoka kwenye Mwongozo wa Kujenga Uzio wa Mizinga ya Nyuki; Toleo la 4 na Dr. Lucy King, Mradi wa Elephants & Bees, Save the Elephants. Mwongozo huu sio kamilifu,pitia mwongozo kwa taarifa zaidi kuhusu ufugaji nyuki. Ili kujifunza zaidi na kuchunguza kuhusu Ufugaji Nyuki na Usalama, angalia Marejeleo. Save the Elephants inashauri tahadhari kwa taarifa zote zilizokusanywa na kuwasilishwa kwenye kitabu hiki. Utafiti zaidi unaweza kuhitajika kabla ya utekelezaji wa mbinu husika. *Save the Elephants haihusiki na gharama, uharibifu au majeraha yoyote yatokanayo na matumizi ya njia hizi.
www.savetheelephants.org
Michoro na Nicola Heath