Ulinzi wa miti

Page 1

ulinzi wa miti Tatizo: Ndovu kuharibu miti Ndovu wanahitaji kula miti na majani ili wapate virutubisho, lakini pia wanaweza wakaharibu moja kwa moja miti mikubwa yenye umuhimu – wanabandua magome, wanavunja matawi na kung’oa kabisa miti.

Miti mikubwa ya kihistoria ni muhimu kwa uchumi, utamaduni na wakati mwingine hata sababu za kimatibabu. Inahusika moja kwa moja na maisha ya msituni, wanyama, na mimea. Kwa mfano, huko kusini mwa Afrika, tafiti zinaonyesha kuwa ndovu wanapenda kutumia miti kama ya Marula, Knob thorn na Red bushwillow kupata virutubisho.

1.

Kwa mfano miti ya Marula iliyopo Afrika Kusini ni miti muhimu inayozaa matunda na yana thamani kubwa ya kiuchumi. Uharibifu wa miti hii ni chanzo cha migogoro baina ya wanadamu na ndovu. Ndovu wanaweza kubandua magome. Kuvunja matawi au kusukuma miti wakiwa wanakula – ndovu dume wanaweza kusukuma miti mingi zaidi kuliko ndovu jike.

Miti ambayo imepunguzwa au kuvunjwa huweza kuwaathiri wadudu au kushika moto.

Kulinda miti dhidi ya uharibifu wa ndovu ni muhimu kwa mfumo mzima wa ikolojia. Kuharibu miti mikubwa hupelekea kupungua kwa anuai ya ndege, popo na mamalia wadogo.


Umuhimu wa ndovu kwenye mfumo wa ikolojia Njia mbili ambazo zimetumika kwa mafanikio kulinda miti kwenye Hifadhi Binafsi ya Umbabat karibu na Hifadhi ya Taifa ya Kruger ni uwekaji neti na mizinga ya nyuki (Elephants Alive). Chanzo: Makala ya Nyuki na Miti

Ndovu wanajulikana kama ‘wahandisi wa ikolojia’

1. ULINZI KUTUMIA WAVU Ndovu mara nyingi hubandua magome. Wanaweza kula magome, hasa katika kipindi cha kiangazi. Ubanduaji wa magome huweza kuathiri kiwango cha ustawi cha miti na huifanya iwe hatarini kuathiriwa na hali ya hewa na wadudu. Tumia wavu ili kulinda shina la mti.

Wanaweza kuweka mbegu katika madonge ya mbolea asilia (kinyesi) hadi umbali wa 65km kutoka kwenye mti mama. Mara nyingi mbegu zina nafasi kubwa ya kuota baada ya kukutana na asidi za kwenye mfumo wa umeng’enyaji wa ndovu. Ndovu wana uwezo wa kuzalisha hadi 150 kg za kinyesi kibichi kwa siku, hivyo kuongeza virutubisho katika mazingira na kuhamasisha bioanuai kwa ujumla.

Hii inasaidia kupunguza uwezekano wa shina kubanduliwa magome.

50 - 80sm

Ndovu pia ni wasambazaji na waoteshaji wazuri wa mbegu za miti.

Ndovu wanasaidia mifumo ya ikolojia kwa kuboresha anuai yake ya mimea. Kitendo cha kuangusha miti hufungua maeneo ya misitu na kufanya maeneo ya nyasi kuonekana.

Lengo: kulinda miti dhidi ya ubanduaji wa shina Kwa nini ubanduaji wa magome ni haribifu? Sababu inazuia mzunguko wa virutubisho kwenye mti. Mti unakuwa hatarini kushambuliwa na wadudu na kuharibiwa na moto. Mti unaweza kufanywa uwe mtupu kwa ndani.

Njia ya kuzungusha mara mbili Wavu wa 13 mm: wenye urefu wa 1.8m. Vipimo vya urefu unaotakiwa (Mzunguko wa mti x 2) + 50sm. Kunja wavu mara mbili kisha zungushia kwenye shina kuu la mti, ukianzia 50sm kutoka juu ya ardhi.

2.

Kinyesi cha ndovu na alama zake za miguu huwapa makazi wadudu, vyura na spishi za reptilia.

Fungia wavu kwenye mti kwa kutumia misumari au waya.


vidokezo vya usimamizi wa ulinzi wa wavu Hakikisha mti unakuwa na nafasi ya kutosha ya kukua. Usiubane mti! Ni muhimu kufuatilia na kuutunza wavu mara kwa mara. Kuzungusha wavu ndio njia nzuri Zaidi ya kuzuia ubanduaji wa magome na husaidia sana katika kulinda shina la mti. Kuzungushia wavu hakuzuii sana aina zingine za athari za ndovu kama vile kuvunja matawi au kung’oa miti.

2. MIZINGA YA NYUKI

Nyuki wa Kiafrika wamekuwa wakitumiwa kwa mafanikio makubwa katika kulinda mazao na miti dhidi ya ndovu. Chanzo: Cook, R. M., Parrini, F., King, L. E., Witkowski, E. T. F., & Henley, M. D. (2018). African honeybees as a mitigation method for elephant impact on trees; and King, L.E., Lala, F., Nzumu, H., Mwambingu, E., and Douglas-Hamilton, I. (2017) Beehive fences as a multidimensional conflict-mitigation tool for farmers coexisting with elephants.

Mizinga ya nyuki inaweza kutumiwa kama njia ya kulinda mti mzima. Kama ndovu hapatani na nyuki, basi kutundika mizinga kwenye miti inaweza kuwafanya ndovu waepuke miti hiyo. Nyuki wana faida ya ziada ya kutoa asali na hufanya kazi kama wachavuhaji muhimu.

Elephants Alive, www.elephantsalive.org

Vifaa vya Kutundikia Mizinga ya Nyuki (IMETOLEWA kutoka Kitabu cha Ndovu, Nyuki na Miti) Vifaa vifuatavyo vinahitajika ili kuweza kutundika mzinga mmoja wa nyuki kwenye tawi la mti:

Chanzo: Bees and Trees Manual

Je unajua kuwa ndovu wanawaogopa nyuki? Ndovu wamegundulika kuwa huwa wanaepuka mizinga asilia ya nyuki inayoning’inia kwenye miti.

Kamba ya manilaHesabu za urefu:

Waya

(200 mm x 5 mm) vipande 8-12

2 x urefu kutoka kwenye tawi hadi 2 m juu ya ardhi + 30 sm (Kamba 2 zitahitajika)

Pini au misumari x6

Gundi

Imekuwa ikitumika kama kizuizi rafiki kwa ikolojia ili kusaidia kulinda mazao na miti.

Ubao wa mbao www.elephantsandbees.com

3.

Ngazi

Nyundo

Futikamba


Njia: Maandalizi Kabla ya Kutundika

Kutundika mizinga kwenye miti Unaweza kutumia aina yoyote ya mzinga wa nyuki (kila moja ina changamoto zake) mzinga una 1. Kama nyuki, tumia tochi

1.

Kokotoa urefu wa Kamba ya manila utakayohitaji kwa kutumia hesabu zilizokwishaainishwa.

yenye mwangaza mwekundu unapokuwa unatundika mzinga usiku.

ncha mbili za kamba 2. Funga zote mbili za manila ili kila

ncha iwe na kitanzi, ambacho kitaunganishwa kwenye mzinga.

utenganishe kwa umbali wa 50sm.

4.

Kama itahitajika, pigilia nyundo pini au misumari mitatu ili kushikia kamba inayoning’inia kwenye matawi ya mti.

mzinga wenye 3. Beba nyuki kwenye mti

Hakikisha unatumia vifaa vya utunzaji nyuki!

5.

Watu wawili wanyanyue juu mzinga wenye nyuki ili waya ufungwe kwenye vitanzi. Mzinga wenye nyuki ndani unaweza kuwa na uzito wa hadi 15 kg!

hivi viwili 5. Vitanzi vinatakiwa viwe

sambamba na viwe 2 m juu ya ardhi.

4.

Weka gundi au grisi kwa juu 6. mwishoni mwa kamba kwa

kutumia ubao wa mbao. Hii ni kuepusha mchwa wasivamie mizinga.

Weka waya mmoja kwenye sehemu ya kuunganishia.

Tahadhari: mzinga wako utahitaji hivi vishikizo kwa ajili ya kuutundika.

ambapo mzinga utatundikwa.

kamba mbili za 3. Weka manila juu ya tawi na

2.

7.

ngazi karibu 4. Weka na vitanzi vinne.

Mtu mmoja atasaidia kuunganisha vitanzi kwenye mzinga unaoning’inia.

ya pembe zote 6. Baada nne kuunganishwa kwenye vitanzi vinne, ongeza waya wa pili katika kila kitanzi kwa ajili ya uimara zaidi na mzinga kutulia.

Weka ubao chini ya mzinga ili mzinga ukae juu yake. Ubao utahitaji kuwa na tundu kwenye kila pembe. Unganisha ubao na mzinga kwa kuweka waya mmoja katika vitundu vinne vya ubao na mzinga. Unganisha hivi kwenye sehemu ya vishikizo kwenye mzinga.


Unapaswa kuifuatilia mizinga yako mara kwa mara kuhakikisha kuwa hali ya hewa na wadudu hawauathiri mzinga, na kuangalia shughuli ndani ya mzinga.

Vifaa vinavyohitajika kwa ajili ya ufugaji nyuki

Hali asilia kama vile mvua, upepo mkali, upepo, mchwa, wadudu wa mizinga, buibui, kakakuona na ndovu wanaweza wakaathiri mzinga na kupunguza nafasi yake ya kustawi.

Inafaa kwa kuongeza kipato cha ziada.

Kuna uwezekano mkubwa wa uzalishaji asali kama utaitunza mizinga na kuhamasisha ustawi bora wa nyuki. Chanzo: Elephants Alive (Rasilimali/Ripoti) Tree_Protection_Methods_Sept2021

Hivi vinafaa kwa ulinzi wa kiwango kidogo cha ulinzi. Wakati wa nyakati za ukame au mvua hafifu, inawezekana ukalazimika kusaidia kuwalisha nyuki. (Unaweza kutumia sukari au virutubishi vya nekta). Uwapa maji nyuki ni muhimu. Unaweza kutumia chombo chochote ulichonacho kuwawekea maji. Vyombo vya maji kwa kuku ni njia nyepesi ya kuwapa nyuki maji.

5.

Mavazi ya kurinia asali na glovu

Kifaa cha kurina

Gundi

Kitoa moshi

Grisi

(kuzuia uvamizi wa mchwa)

Kitabu cha ufugaji nyuki

vidokezo vya usimamizi Hatari ni pamoja na kung’atwa na nyuki. Kuwa makini sana hasa kama una mzio na hakikisha una dawa ya kupunguza mzio karibu yako. Matunzo au mabadiliko yoyote kwenye mzinga yanapaswa kufanyika mapema asubuhi au jioni au usiku ambapo hali ya hewa inakuwa imetulia. Miti yenye mizinga isiyo na nyuki ina uwezekano mkubwa wa kutembelewa na ndovu, hivyo jaribu kuhamasisha ustawi bora wa nyuki kwa ajili ya matokeo mazuri zaidi. Jaribu kuepuka dawa za kuuwa wadudu za kemikali kwani si nzuri kwa wachavushaji asilia kama nyuki.

Njia hii imefanyiwa majaribio huko Gabon, Afrika ya Kati. Utafiti umegundua kuwa mizinga ya nyuki inafaa sana kuwafukuza ndovu wa misituni nchi Gabon, 2016 : Chanzo: Ngama, S., Korte, L., Bindelle, J., Vermeulen, C. and Poulsen, J. R. (2016) How Bees Deter Elephants: Beehive Trials with Forest Elephants (Loxodonta africana cyclotis) in Gabon, PLOS ONE 11 (5) e0155690.


3. KIZUIZI CHA MAWE

Huu ni mzunguko wa mawe au piramidi yaliyozungushwa kwenye shina la mti. Hii inafaa kwa matumizi madogo katika miti kadhaa.

Kuwa makini na nge unaponyanyua mawe!

Inahitaji umbali kiasi baina ya shina kuu la mti na mwisho wa mawe. Athari za ndovu hupungua kama mzunguko wa piramidi kuzunguka mti ni mkubwa. (Kadri ambavyo kizuizi cha mawe kinavyokuwa kipana, ndivyo ambavyo njia hii hufaa).

Njia ya kukokotoa gharama:

FAIDA/HASARA

Jumla ya gharama = Piramidi moja inagharimu x Idadi ya piramidi kwenye eneo la mraba mita x ∏ ((Upana unaotakiwa)² Mawe ya piramidi ninahitaji kubananishwa ili kuzuia ndovu kupata upenyo kwenye uwazi.

Kuwa makini unapokuwa unahamisha mapande makubwa ya mawe ili usilete usumbufu kwenye mazingira asilia.

Mawe au piramidi yanatakiwa yawekwe umbali wa hadi 4-5 m kutoka kwenye shina kuu la mti.

Hii inaweza kuwa njia fanisi na isiyo na gharama endapo itafanywa ipasavyo.

Nguvu za mwili zinahitajika.

Credit: Elephants Alive (Rasilimali/Ripoti) Tree_Protection_Methods_Sept2021

4. FEROMONI YA SHAMBULIO LA NYUKI

Feromoni ya shambulio la nyuki husaidia nyuki kutafuta nyuki wengine kutoka kwenye koloni lao ili waweze kuwamudu wanyama wakubwa zaidi.

Feromoni za mshtuko huachiliwa pale nyuki anampomshambulia mnyama mwingine. Hii huwavutia nyuki wengine kufika eneo hilo na kusababisha nyuki wengine kujihami.

Feromoni ya shambulio la nyuki inajumuisha kemikali ambazo zimetengenezwa katika mchanganyiko wa SPLAT. Tahadhari: hii bado ipo katika hatua ya majaribio na utafiti.

Chanzo: ilivyotajwa kwenye Elephants Alive (Rasilimali/Ripoti) Tree_Protection_Methods_Sept2021

vidokezo: 86% ya ndovu waliokutana na harufu ya feromoni kwenye Mbuga ya Wanyama, Jejane, Afrika Kusini, waliepuka eneo hilo. Matokeo yanaonyesha kuwa njia hii inaweza ikafaa kama ndovu wameshawahi kushambuliwa na nyuki (uzoefu kwa kujifunza). Hii bado ipo kwenye hatua za mwanzo za utafiti na bado haipatikani kwenye jamii. Inaweza ikadumu kwa hadi Miezi 2 pale inapopakwa (inategemea na hali ya hewa).

6.


5. MAFUTA YA MWAROBAINI

6. MAFUTA YA PILIPILI

Mafuta ya mwarobaini hukamuliwa moja kwa moja kutoka kwenye mbegu za mti wa Mwarobaini (Azadirachta indica), ambao ni mti usiopukutisha majani, wenye asili ya India. Mwarobaini ni kiuatilifu ambacho hudhibiti wadudu waharibifu kwenye kilimo, misitu na kilimo cha mboga mboga, na huweza kutumika kama mbadala wa viuatilifu vya kemikali.

Pilipili zimekuwa zikitumiwa kama kizuizi cha ndovu kwa njia ya vipulizi, mafuta yaliyowekwa pilipili na kupakwa kwenye uzio na madonge ya kinyesi.

Mwarobaini unaoweza kudhibiti zaidi ya wadudu 400. Tahadhari: hii bado ipo kwenye hatua ya majaribio na utafiti

Chanzo: Osborn FV, Rasmussen LEL. 1995. Evidence for the effectiveness of an oleoresin capsicum aerosol as a repellent against wild elephants in Zimbabwe. Pachyderm 20:55–64.

Chanzo: Riaan van Zyl (Consulting and contracting Arborist) as mentioned in Elephants Alive (Rasilimali/Ripoti) Tree_Protection_Methods_Sept2021

Paka mafuta ya pilipili kwenye shina la mti.

Mchakato:

Mafuta yaliyo na pilipili yanadumu zaidi kuliko majimaji yenye pilipilii.

Mafuta ya mwarobaini hupulizwa kwenye matawi na shina la mti ili kuwazuia ndovu. Lengo ni kwamba ndovu hawapendi harufu wala ladha ya mwarobaini na hivyo watauepuka mti huo.

FAIDA/HASARA Suala kwamba ni kiuatilifu inamaanisha kuwa wanyama wengine wanaweza wakaathirika. Pia inazuia wadudu wengine kula kutoka kwenye mti huo uliopuliziwa dawa.

vidokezo:

Data zaidi zinahitajika katika kiwango kinachoweza kusimamiwa.

Pia inasababisha kuvuruga hatua za ukuaji za wadudu. Wadudu hawafikii hatua ya kupevuka.

Tumia nguo za kulinda ukiwa unafanya kazi na bidhaa za pilipili.

Wadudu wanashindwa kutaga mayai yao kwenye miti iliyopuliwa mwarobaini.

Paka tena kila wiki 2-4. (kwa kulingana na hali ya hewa)

Nyuki wa asali na wachavushaji wengine wanaweza kuepuka mimea yenye mwarobaini. Muda mfupi wa kudumu kwa dawa inamaanisha miti itabidi iwe inapuliziwa mara kwa mara. Utafiti zaidi unahitajika kwenye bidhaa hii kabla haijatumiwa kwenye maeneo yanayolindwa.

7.

Chanzo: kama ilivyoshatajwa kwenye Elephants Alive (Rasilimali/ Ripoti) Tree_Protection_ Methods_Sept2021


7. MCHANGANYIKO WA KINYESi

Mfinyanzi

Sifa za uponyaji miti: Huu ni uasili wa njia ya kizamani ya kutibu miti kwa njia ya kinyesi na udongo mfinyanzi.

Kinyesi cha nyati/ng’ombe

Kinyesi cha ndovu

Maji

Pipa safi

Sukari

Rangi brashi

mchakato:

1.

Mchanganyiko wa kinyesi una chembechembe za kuzuia bakteria na pia hunata.

Kusanya kinyesi kibichi cha nyati au mbolea ya ng’ombe kwenye pipa kubwa.

2.

Weka 100kg za mbolea ya ndovu kwenye pipa la lita 200.

(Hakikisha pipa ni safi na halina kemikali).

Chanzo: Riaan van Zyl (Consulting and contracting Arborist) as mentioned in Elephants Alive (Rasilimali/ Ripoti) Tree_Protection_Methods_Sept2021

Ongeza mchanganyiko huu wa sukari kwenye kinyesi cha ndovu kilicho kwenye pipa.

vidokezo:

Idadi ya miti huathiriwa katika hatua mbalimbali za ukuaji.

3.

Kwenye chombo cha pembeni, yeyusha 2kg sukari kwenye maji ya moto.

Jaza maji hadi kiasi cha 3/4.

4.

Kimsingi hii ni njia ya kutibu miti lakini ndovu wa Botswana wamegundulika kuwa huepuka miti iliyopakwa kinyesi. Inasaidia kufunga majeraha ya mti na huzuia vijidudu katika mti. Mchanganyiko unaweza kuondoshwa na mvua, hivyo paka tena pale itakapohitajika. Jaribu kadri uwezavyo kutafuta udongo mfinyanzi usiokuwa na kemikali.

vidokezo vya tahadhari:

Mahitaji:

5.

Siku ya kutumia, changanya kinyesi kibichi cha nyati au mbolea ya ng’ombe na kisha ongeza ‘chai’ iliyochachushwa ya kinyesi cha ndovu kwenye huu mchanganyiko.

Iache ichahe kwa hadi siku 3.

6.

7. Hakikisha bidhaa ya mwisho haina majimaji sana.

Baadhi ya njia bado zipo kwenye majaribio na tahadhari inahitajika kabla ya matumizi ya kiwango kikubwa.

Tumia brashi kupaka shina kuu la mti, huku ukijitahidi kupaka nyingi iwezekanavyo.

Hakuna njia yenye uhakika asilimia zote katika ufanisi, lakini kiwango cha ustawi wa miti mikubwa kinaweza kuongezeka endapo njia hizi zitatumiwa vizuri. Tathmini ufanisi na usahihi wa njia kabla ya kutumia. Tumia mavazi yanayolinda na vifaa vya usalama. Matumizi ya glovu za mpira yanashauriwa kwenye kinyesi cha ndovu kilicho kwenye pipa. Baadhi ya njia zinaweza kuhitaji mafunzo ya kiufundi na utaalam. Hakikisha una uzoefu wa kimafunzo unaohitajika (k.m ufugaji nyuki). Mfano hai kutoka Afrika Kusini unaweza kuhitaji mabadiliko ya muundo kwenye maeneo mengine.

Marejeleo na Angalizo: Tumekusanya rasilimali kutoka kwa Elephants Alive (Dr. Michelle Henley and Robin Cook), and Elephants Alive (Rasilimali na Ripoti)_Tree Protection Methods_Sept 2021. Baadhi ya njia zilizowasilishwa hapa bado zipo kwenye hatua ya majaribio na utafiti zaidi unahitajika. Kujua zaidi kuhusu kutumia njia za kulinda miti, fanya uchunguzi zaidi wa fasihi husika, angalia Marejeleo. Save the Elephants inashauri tahadhari kwa njia zote zilizokusanywa na kuwasilishwa kwenye kitabu hiki. Utafiti Zaidi unaweza kuhitajika kabla ya utekelezaji wa eneo husika. * Save the Elephants haihusiki na gharama, uharibifu na majeraha yoyote yatakayosababishwa na matumizi ya hizi njia.

8. Imetengenezwa Kenya 2021

Imeandaliwa na Save the Elephants

www.savetheelephants.org

Michoro na Nicola Heath


Turn static files into dynamic content formats.

Create a flipbook
Issuu converts static files into: digital portfolios, online yearbooks, online catalogs, digital photo albums and more. Sign up and create your flipbook.