VITUO VYA MAJI VYA PAMOJA/MBADALA Vituo vya maji mbadala vinatoa usalama kwa jamii za vijijini na mifugo yao ambayo inatumia vyanzo vimoja na ndovu. Hii inawawezesha ndovu na mifugo kunywa maji bila kufarakana.
Katika miaka yote iiyopita kumekuwa na ukame wa muda mrefu na uhaba wa maji.
1.
Ndovu wanavutiwa na harufu ya maji yaliyohifadhiwa kwenye vijijini na kuvunja mabomba, matangi ya maji na vifaa vya kupata maji.
Hii inasababisha hasara kubwa na inaweza kuwaacha watu na mifugo bila maji kwa siku kadhaa, hivyo kuongeza migongano na chuki dhidi ya ndovu. Wanawake na watoto wanaweza kuathiriwa vibaya kwani mara nyingi wao hukusanya maji kwa ajili ya familia.
Suluhu moja ni kutenga maeneo mbadala ya ndovu kunywa maji, na wakati huo huo kuweka mipaka ya vituo vya maji vya jamii ili mifugo inywe maji na wanawake kufua kwa usalama. Vituo vya maji kwa ajili ya ndovu havipaswi kuchafuliwa na kinyesi cha mifugo au harufu ya mwanadamu.
Hii inapunguza migongano kwenye eneo moja la maji na ndovu wanaweza kujifunza kuepuka maeneo yanayotumiwa na jamii.
Jamii zinaweza kuweka alama kwa milingoti/nguzo mahali walipoamua kuacha nafasi kwa ndovu kunywa maji.
Mifugo na wafugaji watajifunza haraka kwamba hii ni njia salama ya kunywesha mifugo pale ndovu wanapochangia nao eneo moja la kunywa maji.
visima Visima vinatoa nafasi ya kupata maji yaliyo chini zaidi ambayo hayachafuliwi/kuwekwa uchafu. Njia nzuri zaidi ni pampu zinazotumia umeme wa jua, hii inaondoa shinikizo la kifedha kwa wakulima tofauti na kama ingekuwa inatumia umeme. Pampu za mkono zinaweza kupandisha maji lakini zinahitaji nguvu za mwili. Ni muhimu sana kufanya utafiti wa ardhi kabla hujachimba kisima kwani matumizi makubwa ya maji yanaweza kupunguza kiasi cha maji ya ardhini hivyo kuathiri mazao ya shambani. Matumizi makubwa ya maji pia yanaweza kusababisha kupungua kwa kiwango cha maji kwenye vijito na vinamasi.
2.
Baadhi ya vijiji pia hutumia round abouts kuendesha pampu ya maji. Kadri watoto wanavyozunguka, ndivyo maji yanavyotoka ardhini na kwenda kwenye tangi lililo karibu. Maji ya ziada yanaelekezwa kutoka kwenye tenki kurudi tena ardhini.
Soma zaidi kwenye http://www.playpumps.co.za/index.php/how-it-works/
Mifano hai Haya mabwawa yanajazwa kwenye kisima kile kile kinachojaza matangi ya maji ili watu wayapate.
Eneo: Namibia
Angalia Ulinzi wa Matangi ya maji kwa taarifa zaidi
Mabwawa ya kunyweshea ndovu yanajengwa mita chache nje ya kijiji.
Mifugo inaweza kunyweshwa kwenye haya mabwawa. Vifaa vyote vya kuhifadhi maji vinapaswa kulindwa vizuri ili kuepusha migongano ya binadamu na ndovu. Kutumia ukuta wa mawe au mawe meupe yenye ncha kali ni njia nzuri ya kuwazuia ndovu kutokufikia na kuangusha matangi/ mabomba.
Mifumo ya sola ya kusukuma maji-jua ni mepesi kiasi, inahitaji matunzo kidogo, na kutoa miradi ya kupampu inayojitegemea. Inafaa zaidi kwa usambazaji maji wa vijijini na sehemu za mbali ambako umeme haupo.
Soma zaidi kwenye: - EHRA Sturdy Stone Wall & Chanzo cha maji kinachosukumwa kwa sola kimesaidia kupunguza migongano ya binadamu na wanyama pori na kuipa jamii faida za ziada. WWF
Shirika la Maendeleo ya Jamii Nkolale huko Maasai Mara, Kenya, lilijenga tangi la chini ya ardhi la lita 100,000 ambalo linakusanya maji kutoka kwenye chemchem asilia. Maji hayo yanapandishwa kwenye tangi la nje, ambapo baadhi yanaelekezwa kwenye visima vya wazi mbali na kijiji ili wanyama waweze kuyatumia. Maji zaidi yanavutwa kwa gravity kwa zaidi ya 13km ili kusambaza maji kwenye vijiji vinavyozunguka, shule na vituo vya afya. Soma zaidi kuhusu Uhifadhi wa maji ya chemchem yapunguza migogoro baina ya binadamu na wanyama, Kenya
3.
faida Jamii hazihitaji kutembea umbali mrefu kukusanya maji, kupunguza uwezekano wa kukutana na ndovu njiani/ kwenye vituo vya maji.
+
Upatikanaji salama wa maji kwa watu, mifugo na ndovu. Watu hawatakuwa hatarini kuambukizwa magonjwa yanayosambazwa kwa maji ambayo mara nyingi huja kwa kutumia maji ambayo wanyama pori hutumia.
Kupungua kwa kesi za migogoro baina ya binadamu na ndovu kwani ndovu wanapata maji, bila kuvunja matangi ya maji na kulumbana na mifugo na binadamu. Kuongezeka kwa mtazamo chanya kwa ndovu. Upatikanaji wa maji masafi unaongeza uzalishaji wa mazao kwa wakulima ili waweze kuhudumia familia zao na pia kuuza sokoni.
hasara
-
Gharama ya kuchimba kisima au mfumo wa uhifadhi wa maji uliopo chini na kuutunza ni kubwa na unaweza kuhitaji msaada za ziada wa kifedha ili kuuweka na kuutunza mfumo.
Vidokezo vya tahadhari:
Ni muhimu kwa wanavijiji kukumbuka kujaza maji bwawa la ndovu, ili ndovu wanywe maji na waondoke kwa usalama eneo la jamii. Kama vituo vya maji vya mbadala havijatengwa, itafika wakati vitawavutia wote binadamu na wanyama pori, hivyo kuongeza migogoro. Hakikisha watoto wanaelimishwa kuhusu eneo gani la mto na mabwawa ni salama kwao kwenda, na kutokuvuka mipaka iliyotiwa alama. Weka umbali wa kutosha na ndovu ukiwa maeneo ya vituo vya maji.
Mita 50
4.
Imetengenezwa Kenya 2022
Imeandaliwa na Save the Elephants
Bajeti ya matunzo ni lazima ijumuishwe kwenye mipango ya fedha ili kuepusha mabomba ya chuma kulika na lazima yatunzwe ili kuzuia maji kuvuja. Kama bwawa la ndovu ni tupu na matangi yanalindwa, ndovu watajaribu kuvunja kuta ili kufikia matangi.
Sifa na Katao la haki:
Tumekusanya hizi taarifa kutoka vyanzo mbalimbali. Vyanzo vikuu ni pamoja na: Wazo la bwawa la ndovu liliundwa na Elephant Human Relations Aid (EHRA), Namibia. Kwa taarifa zaidi kuhusu vituo vya maji mbadala, fasihi na rasilimali zilizotumika, angalia Marejeleo. Utafiti zaidi unaweza kuhitajika kabla ya utekelezaji wa eneo husika. Usalama na tahadhari inashauriwa katika njia zote zilizowasilishwa kwenye kitabu hiki. *Save the Elephants haihusiki na gharama, uharibifu au majeraha yoyote yatakayopatikana katika matumizi ya njia hizi.
www.savetheelephants.org
Michoro na Nicola Heath