NDOVU KAMA WAHANDISI WA MFUMO IKOLOJIA Wahandisi wa mfumo ikolojia ni wanyama ambao huunda, kubadilisha au kuharibu makazi. Ni muhimu kwa kudumisha afya na uthabiti wa mazingira wanapoishi.
WAHANDISI WA MFUMO IKOLOJIA 1. Kusukuma miti na mimea
SPISHI KUU Spishi kuu ni kiumbe anayesaidia kushikilia mfumo pamoja na ni muhimu katika mfumo ikolojia.
Ndovu ni spishi muhimu sana
Ndovu ni spishi wenye athari kuu kwa mazingira.
Spishi nyingine hutegemea spishi kuu. Kuondoa spishi kuu kutoka kwa mfumo ikolojia kutasababisha ukosefu hatari wa usawa katika mfumo mzima. Utafiti unaonyesha kuwa ndovu ni mkulima, kontrakta, barabara na msawazishaji wa jumla katika mfumo ikolojia!
1.
Usukumaji wa miti wa ndovu unaweza kusaidia kudumisha Mifumo ikolojia ya Savana. Hii pia husaidia kuunda njia mpya ili kuwaruhusu wanyama wandogo kusonga bila tatizo. Hii huruhusu mwanga mwingi kwenye sakafu, ikiisaidia mimea mingine kustawi. Kupogoa miti pia husaidia kuboresha ukuaji na kupeana chakula.
2. Kushimba mashimo ya maji Ndovu huwawezesha wanyama wengine kuishi katika makazi kavu. Ndovu wana uwezo wa ajabu wa kugundua maji. Wakati wa kiangazi na nyakati za ukame mkuu, ndovu hutumia mikonga yao kunusa maeneo ambayo yanaweza kuwa na maji chini.
Hutumia pembe na mikonga yake kuchimba ili kupata maji.
3. Kupeana makazi Nyayo hujaa maji na kuunda makazi ya viumbe wadogo, amfibia na wadudu. Wakati wa kiangazi, alama za nyayo za ndovu hujaa maji. Hii hupeana mazingira bora ya vyura kutaga mayai na viluwiluwi kukua. Nyayo za ndovu hupeana makazi ya kuzalishana yasiyo na wawindaji kwa vyura na kuwa kama sinki ya kuunganisha kwa vyura kujiunganisha.
4. Husaidia kusambaza mbegu Ndovu huzurura na kutawanya mbegu mbali, wakisaidia kuunda misitu inayostahimili na yenye afya. Hii husaidia kupunguza athari za mabadiliko ya hali ya hewa.
Hii huwaruhusu ndovu kuishi katika mazingira kavu na wakati kuna ukame.
Pia hupeana maji kwa wanyama wengine wanaoshiriki makazi nao.
Mifumo ya usagaji ya ndovu haiwezi kusiaga mbegu zote anazokula. Wanapoishi, ndovu huacha kinyesi chenye virutubisho vingi kilichojaa mbegu kutoka kwa mimea mingi wanayokula.
Ndovu anapokunyia mbegu hupandwa ardhini na kukua na kuwa nyasi, vichaka na miti mipya, ikiboresha afya ya mfumo ikolojia wa savana. Mbegu nyingi za miti huhitaji kupitia kwenye utumbo wa ndovu ili kuota. Bila ndovu huenda zisiote. Hii pia husaidia kulipa shamba rotuba, ikipeana virutubisho ikiwezesha uotaji na ukuaji. Ndovu wanapotembea kutoka mahali hadi pengine, husaidia mimea kunawiri na kumea kwenye maeneo mapya, ikipeana mimea mbalimbali na makazi zaidi ya wanyama.
2.
5. kinyesi cha ndovu
6. Kutafuta mwamba asili wa chumvi wa kulambwa
Ndovu hukunyia zaidi ya mara 15 kwa siku, kinyesi chake ni chakula kizuri kwa spishi zinazokitegemea.
Madini ni muhimu kwa ukuaji wa viumbe wengi, wakiwemo ndovu. Porini, ndovu hupata madini wanayohitaji kutoka kwa mimea.
Kinyesi cha ndovu ni chakula kwa wanyama wengi (sanasana wadudu) kinyesi chao ni nyumbani kwa maelfu ya wanyama wadogo wasio na uti wa mgongo.
Rasilimali zinapokuwa chache, hata hivyo, wanaweza kupata madini mengine, hasa sodiamu, moja kwa moja kutoka kwa mchanga.
Wadudu hawa ni chanzo muhimu cha chakula kwa ndege, reptilia na mamalia wadogo. Vipepeo hupatikana katika kinyesi hiki ili kupata joto. Kinyesi hiki pia kinaweza kuwa na madini muhimu kwa uzaanaji wa vipepeo, yaliyoingizwa na wa kiume.
Ndovu wana hisia nzuri za kunusa na hutumia mikonga yao kugundua maeneo ardhini yaliyo na kiwango cha juu cha madini.
Mifumo mingi muhimu ya ikolojia ingeharibika kiasi ikiwa ndovu hawako karibu.
Hutumia mikonga yao kuchimba mchanga na kisha kuinama kula. Miamba hii ya chumvi haitumiwi na ndovu tu lakini pia wanyama wengine wanaokula nyasi wanaoweza kuhitaji kupata madini zaidi. Kupeana miamba ya chumvi huwahimiza ndovu kukaa ndani ya mbuga na nje ya maeneo ya jamii. Soma zaidi kuhusu: Uchaguaji wa chakula wa ndovu kutoka kwa ‘miombo’ biome, kuhusiana na kemia ya majani
3.
7. Njia za mimea
Ndovu wa msituni wanapokula, huunda nafasi katika mimea.
8. Nyasi Kwenye savana, ndovu wanaokula miche ya miti na vichaka husaidia uwanda kuwa wasi na kusaidia wanyama wa uwandani wanaoishi katika mifumo ikolojia hii ya nyasi. Hii hulisha wanyama wengi wanaokula majani kama swalapala na kongoni, ambao hulisha wawindaji muhimu na ndege walaji mizoga kama simba, fisi na mbweha.
Nafasi huruhusu mimea mipya kumea na kuunda njia za kutumiwa na wanyama wengine wadogo.
Ndovu wanapotafuta chakula, matawi ya miti, majani, matunda na vijiti huanguka chini.
Wao ni wakulima kamili wa msitu.
Hii husaidia kupogoa miti, ambayo ni nzuri kwa ukuaji wake.
Vidokezo vya tahadhari:
Kama ilivyo kuwa kuondoa spishi muhimu katika eneo kutaziharibu, hivyo ndivyo pia ilivyo kuwa na spishi nyingi sana za spishi hiyo. Ikiwa kuna ndovu wengi sana katika mbuga yenye uga au mbuga iliyogawanywa ambapo hawawezi kuhamia kwenye sehemu tofauti kutafuta chakula wanachotaka–kwa muda athari zake kwa mazingira walipofungiwa zinaweza kuwa za uharibifu, na mfumo ikolojia utahathirika pakubwa. Hii inaweza kusababisha kupoteza miti, kuhamishwa kwa spishi zingine, kupungua kwa wanyamapori wengine wasioweza kushindana.
Njia za wanyamapori na uunganishaji wa makazi ni muhimu kwa ndovu na wanadamu.
Sifa na Katao la haki: Tumekusanya habari iliyo hapa kutoka kwa vyanzo vingi. Kwa maelezo zaidi, angalia Marejeleo. Save the Elephants inashauri kuwepo kwa uangalifu kwa habari yote iliyokusanywa na kupeanwa katika kijisanduku hiki cha vifaa. Huenda utafiti zaidi ukahitajika kabla ya kila utekelezaji maalumu wa eneo. * Save the Elephants haigharamii gharama yoyote, uharibifu au majeraha yanayotokana na matumizi ya njia au maelezo haya.
4. Imetengenezewa Kenya 2021
Imeandaliwa na Save the Elephants
www.savetheelephants.org
Michoro na Nicola Heath