Vizuio vya kelele

Page 1

Vizuio vya Kelele “Vizuio vya kele ni kelele zinazotumika kuwazuia ndovu, kwa mshtuko wa kelele ya juu isiyotarajiwa, au kwa kelele maalumu zinazojulikana kuwashtua ndovu” (Parker et al., 2007).

VIZUIO VYA JADI Hivi mara kwa mara huundwa kutoka kwa vifaa rahisi na vinavyopatikana kote. Wakulima wanaweza kutumia aina mbalimbali za kelele, kama kupiga ngoma na makopo, ‘kupasua’ viboko, kupiga mayowe na kupiga miluzi ili kufukuza ndovu.

Kelele za juu ni kizuio kinachofaa cha muda mfupi dhidi ya ndovu. Ndovu ni werevu sana na wanaweza kuzoea mbinu zilizorudiwa au tabia ya kujifunza. Kwa muda, ndovu wanaweza kupuuza vizuio, mara wanapogundua kuwa haviwadhuru. Hivi vinaweza kuwa rahisi kutumika, vya gharama ya chini na vinaweza kutumiwa pamoja na mipango ya kijamii.

Aina ya vizuio vya kelele:

Wakulima wanaweza kutumia vifaa vinavyopatikana kwa urahisi kupiga kelele ya juu (Mabati ya chuma, chungu, ngoma). Kupiga ngoma

Kupiga risasi hewani

1.

Kupasua viboko

Kugonganisha mapipa, makopo, mabati, miti n.k kwa sauti ya juu

Mbweko

Kelele, mayowe, na kupiga miluzi

Fataki

Pembe/Vuvuzela

Kucheza sauti za nyuki na za wanyama kama (simba na chui)

Hizi hutumika vyema zikitumiwa pamoja na njia zingine za vizuio na ulinzi wa usiku.

Jiepushe na pombe/ulevi wakati wa msimu wa uvamizi wa mimea, kuwa mwangalifu. Vizuio vya jadi vya kufukuza ndovu shambani huonekana kutofaa vinapoendelea kutumika.


1. Kupiga kelele, miluzi, kugonganisha Mabati na sufuria, kubweka kwa mbwa Karibu kila mkulima anaweza kujaribu kufanya hivi.

Inapaswa kutumiwa pamoja na mbinu zingine za ulinzi wa shamba.

Faida

+

Ikiwa watu wengi wanaweza kupatikana, hii inaweza ikawa njia inayofaa ya kuwafukuza ndovu.

hasara

-

Sio endelevu. Inaweza kuwa hatari watu na ndovu wanapokaribiana, ajali zinaweza kutokea. Wakulima hawawezi kulala vyema kwa kuwa uvamizi mwingi hufanyika usiku wa manane.

Mbwa wanaobweka wanaweza kukuamsha ndovu wanapokaribia shamba lako na kelele yao inaweza kusaidia kufukuza ndovu.

Ndovu wanaweza kuzoea kelele.

kishindo! Wasiwasi wa juu na huenda ikawa vigumu kufanya hivyo ukiwa peke yako.

2.

2. Bunduki za kelele za kujitengenezea Hivi vinaweza kuwa vifaa vilivyotengenezewa nyumbani, vilivyotengenezwa kwa vifaa vilivyotumiwa tena.

Ni kama bunduki ya kelele, ya kusaidia kutoa kelele zaidi. Wazo hili ni la kuunda mashine inayotumia makopo ya kale kuongeza sauti ya kutisha ya kukwaruza ya chuma zikikwaruzana.

ORODHA YA VIFAA

Makopo

Misumari

Vipande vya mbao

Hii hutumika bora kwa tochi kali. Kwa kuvuta misumari ndani na nje, kelele hii ya mkwaruzo hutoa sauti ya kutisha ambayo imethibitishwa kuwa inafaa kwa kuwafukuza ndovu.

faida

+

Inaweza kutumika popote na ni rahisi kutumia. Gharama ya chini na vifaa vilivyotumika tena vinaweza kutumika. Inaweza kuwa ya kufaa sana. Chanzo kwa: Jones Mwakima, Kajire, Taita Taveta.

Mipira


3. Pembe za hewa/vuvuzela

Tanzania

4. Mishumaa ya Kiroma

Hivi ni vifaa vilivyoundwa ili kusababisha kelele ya juu ili kukufahamisha.

Pembe huongeza sauti, na kuifanya kuwa ya juu zaidi.

FAIDA

+

Gharama yake inaweza kuwa ya chini na ni rahisi kupata. Huhitaji mafunzo madogo na ni rahisi kutumia, kwa hatari ndogo kwa binadamu au ndovu. Hutumika vyema ikitumiwa pamoja na mianga ya LED na mbinu zingine.

hasara

-

Uzoefu wa haraka. Ndovu wanaweza kuzoea mbinu hizi haraka. Kelele nyingi za juu za kila wakati zinaweza kusumbua.

Hii ni fataki ya mshumaa inayotoa mfuatano wa milipuko ya juu, na mianga mikali. Inapaswa kutumika tu kama suluhisho la mwisho. Mafunzo ya mara kwa mara na uzoefu unahitajika!

faida

+

Mbinu hizi zinaweza kuwa za kufaa sana kufukuza ndovu, ikiwa zitatumika ipasavyo.

hasara

-

Hizi zinaweza kuwa za hatari ya juu kwa ndovu au watu zisipotumiwa ipasavyo. Gharama yake ni ya juu kiasi (takribani. gharama ya $30 [3,631 kshs] kwa kila mlipuko). Chanzo kwa: www.honeyguide.org

Zinapaswa kutumika tu kama suluhu ya dakika ya mwisho na kwa uangalifu mkuu. Mbinu hii inaweza kusababisha mlipuko, hivyo haifai kutumika kwenye maeneo yaliyo na matatizo ya kiusalama. Inaweza kuwafukuza ndovu na kuwaelekeza kwenye mashamba yaliyo karibu. Ndovu wakifaulu kula wanaweza kuzoea mbinu hii. Kuwa mwangalifu unapotumia mbinu hizi, na uwasiliane na majirani wako na jamii.

Ikiwa kuna wasiwasi wa usalama, usitumie kifaa hiki!

Chanzo: Kijitabu cha Mgogoro wa Binadamu na Ndovu wa Honeyguide Chanzo: Kwa maelezo zaidi, tembelea Kijitabu cha Migogoro kati ya Binadamu na Ndovu, www.honeyguide.org

3.


6. Vishindo vya Pilipili

5. Mabomu ya bomba ya kelele

Vishindo vya pilipili hujumuisha vizuio vya sauti na mwonekano kwa kutumia ponda ya pilipili na vishindo vya moto.

bomba la chuma 1. Funga upande mmoja na uliweke maji hadi nusu.

Vinapowashwa, hurushwa hewani, kwenye upande wa ndovu.

bomba na uliwekelee 2. Ziba kwenye moto.

Tazama Vizuio vya Pilipili kwa njia zingine zinazotumia pilipili. Vyanzo: www.connectedconservation.com, www.honeyguide.org, www.wrcsindia.org, www.ecoexistproject.org, na www.maraelephantproject.org.

7. Kengele za ng’ombe/Mitego ya ving’ora

3.

Kengele ya ng’ombe au makopo ya bati yenye mawe na kutundikwa kwenye ua la kamba kwenye ukingo wa mashamba yaliyo hatarini.

Litakapopata joto, kizibo kitalipuka kutoka kwa bomba na kutoa sauti ya mlipuko wa risasi. Zimbabwe

FAIDA

+

Ni nafuu na upatikana kwa urahisi,hufanya kazi kwa ufanisi .

hasara

-

Sio suluhisho la muda mrefu. Ndovu wanaweza kuzoea haraka. Katika hali za mvua nyingi,ni vigumu kudumisha mtego wa ving’ora wenye mifumo ya umeme, na pia huwa katika hatari ya kuibiwa.

4.

Tazama Kengele Za Kushtua kwa maelezo zaidi.

Kenya

India

Ndovu wanapojaribu kuingia shambani, wanasukuma king’ora, kikipiga kengele na kuwatahadharisha wakulima kuhusu kuwepo kwa ndovu.


8. Milio ya Risasi Kizuio cha muda mrefu na kinachotumiwa barani kote.

kishindo!

Hii huhusisha kuwatumia wafanyakazi wa serikali au wa wanyamapori ambao hupiga risasi juu ya vichwa vya ndovu wavamizi ikielekea kwenye anga. Kumimina risasi kwa ndovu moja kwa moja kunapaswa kuepukwa kila wakati.

faida

+

Sauti ya karibu na ya juu sana, huwashtua na kufanikiwa kuwatawanya ndovu.

hasara

Matatizo ya kawaida ya vizuio vya kiasili vya sauti: Kutegemea zaidi mbinu chache, zikitumiwa mara kwa mara na kufanyiwa mabadiliko kidogo (Mabadiliko yanahitajika). Vizuio mara kwa mara uhusisha kuwakaribia ndovu, ikiongeza uwezekano wa hatari ya majeraha kwa watu na ndovu. Mbinu nyingi zinaweza kuchukuliwa kuwa ‘vitisho tupu’ kwa kuwa ndovu wanaweza kushtuliwa navyo, lakini haziwadhuru.

Hivyo, ndovu wanaweza kuzizoea na wanaweza kuzipuuza.

-

Ni suluhisho la muda mfupi kwa ndovu. Inaweza kuwa hatari kwa kuwa inaweza kuwashtua ndovu sana. Haifai katika maeneo yenye masuala nyeti ya usalama. Kutegemea vitengo vya utekelezaji vya kati vya wanyamapori kunaweza kuwa na changamoto za kiitifaki, kwa mfano kwa maeneo ya mbali na ufikiaji duni. Hii inaweza kuathiri nyakati za mwitikio na ni gharama kubwa kwa mashirika ya utekelezaji ya wanyamapori. “Kuna ushahidi mkubwa wa kimaandishi wa kupendekeza kuwa ndovu huzoea milio ya risasi ikiwa wataisikia kwa muda mrefu.” (Parker et al., 2007) Gharama ya juu.

5.

kishindo! Baadhi ya ndovu huendeleza uvamizi na inaweza kuwa vigumu hasa kuwafukuza wale wa kiume shambani. Upe usalama wako kipaumbele kila wakati na ujiepushe na kuwakasirisha ndovu kwa kuwa hii inaweza kusababisha fujo.


Uchesaji wa sauti unaweza kuwa mikakati ya muda mfupi.

VIZUIO VYA MAJARIBIO

Vifaa vya kielektroniki vinaweza kuwa katika hatari zaidi ya kuharibiwa na hali ya hewa na utunzaji unahitajika.

Kuna mawazo mengi ya ubunifu kwa sasa yanayojaribiwa shambani. Vizuio vingi vya sauti huzingatia utafiti katika matumizi ya kelele inayotolewa na wanyama, watu, au vitu ambavyo vinajulikana kumchukiza ndovu.

mifano 1. Mingurumo ya chui jike na chui ndume nchini India (Thuppil et al., 2012 & 2016) Mingurumo ya chui wa kike na wa kiume ilichezwa kwa kutumia mfumo wa spika unaotumia betri usioingiza maji kwa ndovu wa pori wa Kiasia katika mbuga ya wanyama ya Ananjera nchini India.

2. Sauti za ndovu na nyigu nchini Sri Lanka

(Wijayagunawardane et al., 2016)

Majaribio kwa ndovu wazima wa pori wa Kiume wa Kiasia katika mbuga ya wanyama ya Udewalawe, Sri Lanka. India

Ndovu walionekana kuweza kutofautisha kati ya sauti hizi mbili. Huku mngurumo wa chui wa kike “ukiwafanya ndovu kutoa sauti za kuchukizwa, mngurumo wa chui wa kiume ulisababisha ndovu kurudi nyuma kimya kabisa” (Hahn, 2015). Unaweza kuona walivyofanya baada ya mingurumo hapa: Mingurumo ya chui wa kume: https://www.youtube.com/watch?v=CSdcQp3BsPU&t=26s Mingurumo ya chui wa kike: https://www.youtube.com/watch?v=mlUkmEa3m50&t=49s Chanzo: Thuppil V. & Coss, R. (2012). Kutumia Sauti za Kutisha kama Kifaa cha Kuhifadhi: Misingi ya Mabadiliko ya Kudhibiti Mgogoro wa Binadamu na Ndovu Nchini India. Journal of International Wildlife Law & Policy, 15. 167-185. Thuppil, V., & Coss, R. (2016). Huchezajiwa Migurumo ya chui hupunguza huvamizi wa mazao na ndovu Elephas Maximus katika India ya Kusini. Oryx, 50(2), 329-335.)

6.

Sri Lanka

Walitumia sauti zilizorekodiwa za ndovu wa pori wa Kiasia na sauti za nyigu wa Sri Lanka waliochukizwa (Vespa affinis affinis). Kila sauti iliyorekodiwa ilichezwa kwa dakika moja katika eneo ambapo waliweka chakula wanachokipenda ndovu. Hizi hapa ni sauti nne tofauti na idadi ya ndovu waliotoroka baada ya kuzisikia: a) Sauti za kikundi cha familia kinachoongozwa na ndovu wa kike: b) Nyigu waliochukizwa wa Sri Lankan:

11/17 [65%] 2/12 [17%]

c) Sauti za ndovu wa kike:

1/8 [13%]

d) Sauti wa kudhibiti msumeno wa nyororo :

0/11 [0%]

Sauti zote nne zilichezwa kwa kila ndovu isipokuwa kulipokuwa na sauti ya ndege.


Matokeo “yanatoa ushahidi kuwa sauti… ziliwafukuza ndovu wa Kiasia kutoka kwa chanzo cha chakula, ikionyesha kuwa kuwepo kwa sauti rahisi zilizorekodiwa kunaweza kuwa njia inayofaa ya kupunguza HEC nchini Sri Lanka na Asia ya Kusini Mashariki.” (Wijayagunawardane et al., 2016).

3. Nyuki nchini Kenya na Afrika Kusini Kupitia ushahidi wa jadi, kibinafsi na kisayansi, Lucy King alijaribu kujua jinsi ndovu walipatwa na wasiwasi baada ya kusikia sauti ya kikundi cha nyuki wenye hasira.

Jibu la nyigu lilikuwa vuguvugu, huku ndovu wawili tu wakitoroka. Hata hivyo, wawili waliotoroka walifanya hivyo “haraka na kuonyesha wazi kusumbuliwa, kuonyesha kuwa mwitikio huo ulitokana na tukio walilojifunza.”

(King et al., 2007)

Kenya

Waandishi walitambua kuwa “jambo muhimu zaidi walilopata ni mwitikio wa kutoroka kwa ndovu wakubwa wa kiumekwa… sauti za kikundi cha familia kilichoongozwa na wa kike” (Wijayagunawardane et al., 2016).

Utafiti wa mwanzo ulionyesha kuwa baada ya kusikia sauti iliyorekodiwa ya nyuki ~“familia 16 za ndovu kutoka kwa 17 zilizochunguzwa, ziliondoka pale ambapo walikuwa chini ya mti sekunde 80 baada ya kuanzishwa kwa kelele, ambapo 8 kutoka kwa 16 ziliondoka kwenye mti ndani yasekunde 10” (King et al., 2007). Utafiti wa King pia ulitambua kwamba ndovu huzoea sauti zilizorekodiwa baada ya kujifunza kuwa ni sauti tu zisizo na madhara. Hivyo, ingawa hufaa kwa muda mfupi, baada ya muda mrefu mbinu zingine huhitajika. Utafiti huu ulionyesha kuwa ndovu wa kiume hutambua sauti za ndovu wa kike na kutofautisha kati ya mwito wa mmoja wa kike na kikundi kilichoongozwa na jike.

Vyanzo: Wijayagunawardane M., Short R., Samarakone T., Nishanyi K., Harrington H., Perera V., Rassool R., & Bittner E. (2016). Matumizi ya uchezaji sauti ili kuwazuia ndovu wa Kiasia wanaovamia mazao: Sauti ya kuzuia Ndovu Wanaovamia Mazao. Wildlife Society Bulletin, 40. 10.)

7.

Utafiti huu ulisababisha uanzishaji wa nyua za mizinga kama vizuizi vya ndovu.

Kijikaratasi cha kijisanduku cha vifaa cha nyua za mizinga kwa maelezo zaidi; www.elephantsandbees.com


4. Uchezaji wa sauti za makabila tofauti ya Kenya

(McComb et al., 2011 & 2014)

5. Uchezaji wa sauti za ng’ombe nchini kenya

(McComb et al., 2011 & 2014)

Ndovu wanaweza kugundua kabila, jinsia na umri kutoka kwa ishara katika sauti za binadamu (McComb et al., 2014). Karen McComb alicheza sauti ya mwanaume Mumaasai iliyorekodiwa na sauti za watoto kwa ndovu wa pori kule Amboseli, Kenya. Pia alicheza sauti zilizorekodiwa za sauti za wanaume wa Maasai zilizorekodiwa na za wanaume Wakamba.

Amboseli - Kenya

Aligundua kuwa...“ndovu walionyesha uwezekano mkuu zaidi wa kutoroka na kuchunguza sauti wanapotoa mwitiko kwa sauti za kiume ikilinganishwa na sauti za kike”

(McComb et al., 2014).

Zaidi, “Sauti za wanaume wa Maasai zilitofautishwa wazi na zile za wanaume Wakamba, huku zile za Wamaasai zikichochea viwango vya juu vya kujihami na uchunguzi wa harufu, majibu ambayo yangefaa sana ikiwa wanaume Wamaasai walikuwepo” (McComb et al., 2014).

Ndovu wanaweza kutofautisha kati ya simba wa kiume na wa kike. McComb alicheza mfululizo wa sauti zilizorekodiwa za simba kwa vikundi kadhaa vya ndovu kule Amboseli mwaka wa 2008. Viongozi wa kike wa ndovu wanaweza kutofautisha kati ya sauti za kike na za kiume za simba (McComb et al., 2011) na kati ya sauti za binadamu (McComb et al.,

Kutumia sauti zilizorekodiwa za ng’ombe wa Maasai kuliwashtua ndovu kule Mbuga ya wanyama ya Amboseli, Kenya. Ndovu hawa wameishi pamoja na jamii za Maasai kwa vizazi na ni waangalifu kwa sababu ya visa vya hapo awali, na tabia ya kujifunza. Mbinu hii huhitaji mazingira maalumu Na muktadha wa kihistoria. Pia hutumia kifaa cha gharama ya juu cha kurekodi na kucheza.

2014).

Chanzo: McComb K., Shannon G., Durant S. M., Sayialel K., Slotow R., Poole J, & Moss C. (2011) Uongozi katika ndovu: thamani inayobadilika ya umri, Proc. R. Soc. B.2783270–3276; McComb, K., Shannon G., Sayialel K. N., & C. Moss (2014) Ndovu wanaweza kutambua kabila, jinsia, na umri kutoka kwa ishara za sauti katika sauti za binadamu. Proceedings of the National Academy of Sciences of the United States of America, 111:5433–5438.)

8.

Chanzo: Garstang, M. (2004) Mawasiliano ya mbali, ya ndovu ya masafa ya chini. Journal of Comparative Physiology A, Neuroethology, Sensory, Neural, and Behavioral Physiology, 190:791–805.)


6. Masanduku ya Mvumo Yana sensa za kuhisi mwendo zinazoweza kutambua hadi mita mbili, na hivyo ni lazima ziwekwe kwa maarifa. Hii itawashtua ndovu na kuwafanya waache uvamizi.

faida

Kifaa kilichoundwa hivi karibuni kutoka kwa walionusurika kutokana na wanyamapori kinachoweza kushikizwa kwenye kitu chochote kutoka nguzo za ua hadi kwa miti. Sensa inapoguswa na ndovu anayevamia mimea, kijisanduku kitacheza sauti za nyuki waliokasirika. Kila kijisanduku cha mvumo kina betri zinazochajiwa kutoka kwa sola ndogo ya jua.

7. Mifumo ya Ving’ora

Ving’ora vilivyowekwa kwenye mipaka vyenye mtego wa waya ambao hupiga kelele unapochochewa.

+

Hii husaidia kuwatahadharisha wakulima.

Ni ndogo, rahisi kusakinisha na inaweza kufanya kazi kwa muda mrefu kabla ya kuhitaji kubadilishwa. Sauti ni ya juu na inaweza kufukuza ndovu. Kuna uhakika wa kupiga kelele wakati nyuki halisi hawapatikani.

hasara

-

Kama ilivyo kwa kifaa chochote cha umeme, kina uwezekano wa kutofanya kazi baada ya muda. Masanduku ya mvumo mara nyingi huhitajika kutumika katika maeneo ya mashambani kabisa. Lazima wakulima wawe na ufikiaji wa haraka wa njia nyingine ya kuchaji betri ikiwa hakutakuwa na jua. Hakuna hakikisho kuwa masanduku yataguswa kila wakati, na kuna uwezekano kuwa ndovu atahitajika kupitia ndani ya futi chache za sanduku la mvumo ili kijisanduku kitoe sauti, ikipunguza uwezekano wake wa kufaa kufanya kazi. Kinaweza kuchochewa zaidi kutoa sauti na mwendo wa vifaa au wanyama wengine. Inaweza kusababisha usumbufu na kuhatarisha kuwafanya ndovu kukizoea. Chanzo: www.wildsurvivors.org

9.

Mifumo fulani inayotumia ving’ora imekuwa na mafanikio kiasi. Hata hivyo, ni rahisi kuiba mifumo ya umeme na haitumiki sana katika maeneo yenye mvua nyingi. Wakulima nchini waligundua kuwa ni muhimu kwa ulinzi wa shamba: a) Walifahamu kila wakati ndovu walikuwa wanakaribia. b) Wakati mwingine kengele ziliwafukuza ndovu. Zimbabwe

Wakulima wengi walilalamika kuwa ilichosha kulinda shamba usiku kucha na ilikuwa haiwezekani kuendelea kuwa mwangalifu kila wakati. Kwa sababu hii, mifumo ya ving’ora ni nzuri kwa kuwa huwaruhusu wakulima kulala huku wakiendelea kulinda. Chanzo: Parker G.E., Osborn, F.V., Hoare R.E. & Niskanen, L.S. (eds.) (2007): Upunguzaji wa Mgogoro wa Binadamu na Ndovu: Kozi ya Mafunzo ya Mitazamo ya Kijamii Barani Afrika. Mwongozo wa Mashiriki. Elephant Pepper Development Trust, Livingstone, Zambia and IUCN/SSC AfESG, Nairobi, Kenya)


matatizo ya kawaida ya vizuio vya sauti Ndovu wana uwezo mkuu wa kubadilika na wanaweza kuzoea haraka mbinu za vizuio za ‘vitisho tupu’ - zile ambazo hushtua lakini hazisababishi madhara. Ufanisi wa njia yoyote ya jadi unaweza kupungua mara ndovu wanapokabiliana na mbinu hizi mara kwa mara: “vizuio vyote vya jadi … huonekana kutokuwa na ufanisi baada ya muda.” (Parker et al., 2007)

Vidokezo vya udhibiti/ Ushauri muhimu Utumiaji wa mbinu tofauti ndio ufunguo wa kupata mfumo fanisi wa kizuio. Vifaa vya vizuio vya majaribio na kiufundi vinaweza kuwa bei ghali au vigumu kupata: k.m risasi (vibali vya silaha za moto), sola, umeme, sauti zilizorekodiwa.

Njia zinazotumiwa zinapaswa kuwa za kuanzia sio za pekee. Baada ya muda, mbinu mpya zinapaswa kuanzishwa. Ubunifu wa mbinu mpya za uzuiaji unapaswa kuhimizwa sana miongoni mwa wakulima. Wakulima wanahitaji usaidizi ili kuanzisha mbinu na mikakati ya upunguzaji.

Vizuio hivi vya majaribio mara kwa mara hutegemea mashirika ya nje kwa pesa, rasilimali na taaluma.

Ni muhimu kutokuza tabia ya kutegemea uhisani au shirika linalowasaidia wakulima hawa. Wakulima wanapaswa kujiamini kuwa mbinu hizi mwishowe zinaweza kutekelezwa bila usaidizi wa nje.

Sifa na Katao la Haki: vidokezo vya tahadhari

Baadhi ya mbinu hizi hazifai katika maeneo yenye masuala nyeti ya kiusalama. Utafiti huu unaonyesha jinsi ndovu wanavyoweza kuwa werevu. Ndovu wanaweza kutofautisha sauti za spishi tofauti za wanyama walao nyama na jinsia yao. Wanaweza kutofautisha umri, jinsia na kabila la watu na viwango vya hatari inayosababishwa na kila kikundi. Werevu huu na uwezo wa kupima vitisho halisi na vitisho tupu ndio huifanya vigumu sana kupata suluhisho moja kuu ya kuwazuia.

Tumekusanya rasilimali kutoka kwa vyanzo tofauti. Baadhi ya mbinu zilizopeanwa ni majaribio na utafiti zaidi unahitajika. Baadhi ya maneno halisi yaliyotumika yamerahisishwa ili iwe rahisi kuyaelewa. Vyanzo vikuu vimejumuishwa katika Marejeleo. Ili kujifunza zaidi kuhusu vizuio vya kelele, soma yaliyoandikwa zaidi. Save the Elephants inashauri kuwepo kwa uangalifu kwa mbinu zote na maelezo yaliyokusanywa na kupeanwa katika kijisanduku hiki cha vifaa kilichofafanuliwa. Huenda utafiti zaidi ukahitajika kabla ya utekelezaji wowote kwenye eneo maalumu. * Save the Elephants haiwajibikii gharama yoyote, uharibifu au majeraha yanayotokana na matumizi ya mbinu hizi.

10. Imetengenezwa Kenya 2021

Imeandaliwa na Save the Elephants

www.savetheelephants.org

Michoro na Nicola Heath


Turn static files into dynamic content formats.

Create a flipbook
Issuu converts static files into: digital portfolios, online yearbooks, online catalogs, digital photo albums and more. Sign up and create your flipbook.