Mitaro Mitaro ni nini?
Uchunguzi Kifani
Hii ni aina ya vizuizi vinavyoonekana vya ndovu na wanyama wengine wa pori. Vizuizi hivi hutumika kuzuia ndovu kutoka nje ya maeneo ya hifadhi ya misitu au kuingia katika mashamba yaliyolimwa au maeneo wanakoishi binadamu. Vinaweza kutumika kuwaongoza ndovu kupitia juu ya daraja au njia za chini. Huhitaji uzingatiaji, udumishaji na udhibiti mpana wa mazingira.
Kwa nini husaidia?
Karibu na Mbuga ya Kitaifa ya Wanyama ya Kibale (Uganda) mitaro imechimbwa ili kuzuia mwendo wa ndovu kwenye mashamba jirani. Chanzo: Gross, E. M., Lahkar, B. P., Subedi, N., Nyirenda, V. R., Lichtenfield, L.L., Jakoby, O. (2019) Je, ulinzi wa jadi na ulioboreshwa hupunguza hasara kutokana na wanyama wa pori? Uchanganuzi linganishi kutoka Afrika na Asia, Journal for Nature Conservation, Volume 50, August 2019, 125712.
Uganda
Mitaro huchimbwa mita mbili kwenda chini na upana wa mita mbili, na mchanga huwekwa pamoja ili kuunda ngome kando ya mitaro hiyo.
Ndovu hawawezi kuruka, hivyo mitaro iliyo pana sana na mirefu kwenda chini inaweza kufaa kuwa kizuizi kinachofaa. Hii inafaa kama mifumo ya kudumu ambapo mchanga ni imara vyakutosha kuruhusu uchimbaji na ambapo mmomonyoko wa udongo ni mdogo. Zinaweza kuchimbwa kwenye ardhi kavu na tambare. Haiwezi kuchimbwa kwenye maeneo yenye mwinamo au yanayokumbwa na mafuriko kwa kuwa mitaro itajaa maji, na kuwaruhusu ndovu kuvuka.
1.
Usijaribu kukata miti, vichaka au mimea ili kuunda mitaro. Hii itaathiri usawa wa eneo wa kiikolojia na kusababisha mmomonyoko zaidi wa udongo.
Mitaro mpya iliyochimbwa na iliyodumishwa vyema imethibitishwa kufanikiwa kufukuza ndovu. Kulingana na Gross (2019) Wakulima wanaoishi karibu na Mbuga ya Kitaifa ya Kibale huheshimu mitaro kuwa muhimu sana, ambayo mara nyingi ulipiwa na mapato ya Nationa Park. Chanzo: Gross, E. M. (2019) kufuatilia njia za kuishi pamoja kwa amani, Migogoro ya Binadamu na Ndovu Afrika kufuatilia mwa Jangwa la Sahara.
PROS
+
hasara
Vifaa–Inaweza kuundwa bila vifaa vingi. Huhitaji sana mtu wa kufanya hivyo na zana za kawaida. Gharama–inaweza kuwa gharama ya chini ya wastani.
-
Husababisha mmomonyoko zaidi wa udongo hasa wakati wa mvua. Kuta za mitaro huhitaji kukarabatiwa. Ukarabati - Ufanisi wa mitaro hutegemea ukarabati, inayoweza kuwa kazi ngumu na ya gharama ya juu, hasa baada ya mvua nzito.
Upunguzaji wa ziara za wavamiaji wengine wa mimea. Mitaro inaweza kupunguza ufikiaji kutokana na wavamizi wengine wa mimea.
Vizuizi – wakati topografia ya udongo hairuhusu uchimbaji wa mitaro (imeinuka sana) au pale ambapo maji yanapitia kati. Kizuizi kinachoonekana kwa watu na mifugo.
Kizuizi kinachoonekana kwa watu na mifugo.
Hatari – Ndovu au wanyama wengine na mifugo wanaweza kujeruhiwa au kutegwa na kuanguka katika mitaro.
Mkakati wa muda mrefu wa kusaidia kuzuia ndovu kuingia na kutoka.
Hasa watoto wa ndovu huwa katika hatari ya kuanguka na kukwama kwenye mitaro. Inaweza pia kuwa hatari kwa binadamu.
inapaswa kutumiwa na nini ingine?
Ufikiaji uliozuiwa–Ndovu bado wanaweza pata njia ya kuvuka–hadithi za ndovu kuangusha miti chini ili kutafuta njia ya kuvukia au kusukuma matope katika mitaro ili kupata njia au ndovu wanaweza kutembea kando ya mitaro wakitafuta mahali pa kuvukia. Wakipata mahali pa kuvukia na kuingia shambani, huenda ikawa vigumu kuwafukuza hadi kwa PA kwa kuwa njia imezibwa. Matokeo yake yamechanganyika na hii sio njia iliyo fanisi zaidi.
Tumia kwa mbinu za vizuio vya pamoja k.m ua wa mizinga au ua wa pilipili.
Mazingatio Mazingatio ya Kimazingira na athari Hii haipendekezwi sana kwa uwezekano mkuu wa mabadiliko ya mandhari. Mitaro inaweza kuathiri au kuzuia njia asili za uhamaji za wanyama wengine.
USITUMIE misumari au vifaa vingine vyenye ncha kali. Hivi ni hatari sana kwa ndovu, wanyama wengine wa pori, mifugo na watu.
2.
Bora kwa jaribio la kwanza na kisha tumia mbinu zingine na vizuio vya shambani. Inaweza kuwa na matokeo yanayodumu kwa muda mrefu. Mbinu hii haipendekezwi kwenye miinuko, au maeneo yenye maji.
Kupanda miti au mimea Panda miti, mimea au mazao ili kuimarisha na kuzuia mmomonyoko wa udongo. Huwa katika hatari ya mmomonyoko wa udongo, hasa kwenye miinuko na maeneo ya mvua nyingi.
Hatua za Pamoja Changanya mitaro na ua wa umeme au ua wa mizinga lakini kwenye upande wa shamba ulio na umitaro kizuio cha ndovu kilichijumuishwa. Hakikisha kuwa upande mmoja wa umitaro umeinuka ili ndovu wasikwame na kuwa wanawez akupanda wakitoka.
Matengenezo na usimamizi
Kwa sababu ya mmomonyoko wa udongo, na hasa baada ya mvua nzito – kuta za umitaro zinaweza kudhoofika na kuwawezesha ndovu kuvuka.
Huenda Ruhusa ikahitajika kutoka kwa mamlaka husika.
Lazima itumiwe pamoja na mikakati mingine na muhimu zaidi huhitaji kutunzwa vyema.
Utafiti wa muda mrefu unahitajika.
Jiepushe na kukata miti na mimea.
Ushirikiano na majirani Fanya kazi na majirani na jamii yako ili kupata mbinu zinazofaa zaidi ili kuweza kuishi pamoja. Fanya kazi na serikali ya eneo na mamlaka ya wanyamapori kuhusu udhibiti wa mandhari.
Vidokezo vya Tahadhari:
Ruhusa na Utafiti
Mitaro inaweza kujumuisha marekebisho makubwa na mabadiliko makubwa kwa mazingira ya ndani. Tumia mbinu zingine au mawazo kabla ya kuamua kutumia mbinu hii. Chunguza zaidi kuhusu uendelevu wa mbinu hii katika mazingira yako na ni zipi zinazoweza kuwa athari za muda mrefu. Hii haifai kwa kila muktadha * utafiti zaidi wa eneo maalumu unahitajika! Lazima itumike pamoja na vizuio vingine. Ndovu ni werevu sana na huenda wakazoea au kutafuta njia ya kuvuka. Mitaro hii inaweza kudhoofika kwa muda kwa sababu ya mrudikano wa udongo na vifusi. Marekebisho yanahitajika. Kuwa mwangalifu wa mifugo na binadamu, karibu na mitaro. Uzingatiaji na usimamizi wa njia za uhamaji za ndovu unahitajika.
Mitaro kubwa huhitaji uwekezaji wa juu na ni ngumu kuitunza. Tengeneza mitaro kwa saruji, ikiwa kuna rasilimali. Ni bora kuwa na mpango wa udhibiti wa muda mrefu. Kwa udhibiti bora – uundaji na utunzaji wa mitaro ya kuzuia ndovu unapaswa kupeanwa kwa usimamizi wa wilaya au mamlaka ya eneo.
Kuchimba mitaro kunaweza kusababisha usumbufu wa usawa wa mazingira, hivyo kubadilisha mienendo katika mfumo ikolojia. Huenda ikaathiri spishi zinazoishi katika eneo hilo na pia, mimea, utiririkaji wa maji na utulivu.
Kidokezo/Katao la haki Hii imetumika, kwa ufanisi uliochanganyika barani Asia. Kutunza na kulinda njia za wanyamapori ni muhimu kwa mwendo wa ndovu.
Ufanisi au kufaa hutegemea vipengele tofauti. ** Mitaro huhitaji uzingatiaji mpana wa mazingira, utunzaji na udhibiti. Mitaro ya kuzuia ndovu zinapaswa kuwekwa kwa makini tu pale ambapo hali inadai.
Tumia tu ikiwa ni lazima.
Sifa na Katao la Haki: Maoni yaliyopeanwa hapa ni ya kutoka vyanzo mbalimbali na kulingana na utafiti. Mbinu hii imetumika kwa mchanganyiko wa ufanisi. Angalia Marejeleo. Save the Elephants hushauri kuwepo kwa uangalifu kwa mbinu zote zilizokusanywa na kupeanwa katika kijisanduku hiki cha vifaa. Huenda kwa uangalifu zaidi ukahitajika kabla ya utekelezaji katika eneo maalumu. *Save the Elephants haitagharamia gharama yoyote au uharibifu uliosababishwa na matumizi ya mbinu hizi.
Tazama hati kuhusu Tabia ya ndovu ya kutambua.
3. Imetengenezwa Kenya 2021
Imeandaliwa na Save the Elephants
www.savetheelephants.org
Michoro na Nicola Heath