ua wa ukanda wa chuma Ua wa ukanda wa chuma “Kasaine” uliowekwa ukizunguka nje ya shamba hutoa kelele ya chuma isiyo ya kawaida unapopeperushwa na upepo. Huakisi mwanga wa jua au tochi kwa ndovu wanaokaribia hivyo kuwa kizuio cha sauti na kelele.
Ua huu huundwa kwa vipande vyepesi vilivyokatwa kutoka kwa vipande vya mabati ya kuezekea vikiwa vimefungwa kwa waya. Kenya - Njia ya Wanyamapori ya Kasigau, Sasenyi
Kizuio bora kwa bajeti ya chini ambacho wakulima wanaweza kutengeneza wenyewe kutoka kwa vifaa vinavyopatikana kote.
Von Hagen, R. L., et.al. (2020).Nyua za vipande vya chuma za kuzuia Ndovu wa Kiafrika (Loxodonta africana) Ulaji wa mazao katika Njia ya Wanyamapori ya Kasigau , Kenya. Jarida la Kiafrika la Ikolojia, 59(1), 293–298. African Journal of Ecology, 59(1), 293–298.
VIFAA VINAVYOHITAJIKA VYA UA
Mabati ya chuma (mabati), misokoto ya chuma au chuma nyingine yoyote ya mabati (chuma)
1.
Brashi ya rangi
Kifaa cha kukata mabati
Nguzo/miti ya kutumia kama nguzo
Ili kujenga ua wa kamba wa mabati/chuma, utahitaji kukusanya vitu vifuatavyo:
Waya ya kufunga
Koleo
Nyundo
Sepetu/jembe
Kama ilivyobainishwa katika Mwongozo wa Ujenzi wa Wildlife Works, 2021
Viua waduddu/mafuta ya zamani ya injini/ karatasi ya nailoni ya kulinda nguzo kutokana na mchwa
Futikamba
Misumari
Glavu nene za kazi za kukukinga
MBINU YA KUJENGA KUTAYARISHA NGUZO Chimba mashimo ya nguzo yakizunguka shamba lako kwa umbali wa mita 8 kati ya kila nguzo.
Tumia brashi ya rangi kupaka nguzo viua wadudu au mafuta ya injini.
Kila nguzo inapaswa kuwa na urefu wa mita 2.5.
Kila nguzo iwe na urefu wa 60cm. Mita 2.5
60 sm
kidokezo
Hii huzuia mchwa kuharibu nguzo. Mita 8
Wacha nguzo zilizopakwa zikauke kwa saa 24. Baada ya kupaka, weka nguzo katika mashimo kwa uthabiti ili ziwe imara.
MATAYARISHO YA VIPANDE VYA MABATI: Kwa kutumia kifaa cha kukata, kata mabati kwa uangalifu kwa vipimo vya urefu wa 13cm hadi 18cm na upana wa 4cm hadi 5cm. KIDOKEZO CHA uSALAMA:
kidokezo
Unaweza kukuza nanaa shambani mwako ili kufukuza mchwa kutoka kwa nguzo.
kidokezo
kidokezo
Ukubwa tofauti husaidia kwa kutoa kelele zaidi vipande vya chuma vinapogongana.
13-18 sm
Unaweza pia kufunga kabisa karatasi ya nailoni karibu na sehemu ya chini ya nguzo.
Tumia msumari na nyundo kudunga shimo juu ya kila kipande cha chuma ili kuvitundika.
Chaguo linalopendelewa la nguzo ni kutumia miti ya asili kama Commiphora spp, ambayo humea tena kwa mizizi. Hamna haja ya kuifunika kwa mafuta au viua vijidudu.
kidokezo
3-4 sm
2.
Tumia glavu nene au za raba kuzuia majeraha.
Hakikisha kuwa shimo haiko karibu sana na mwisho wa kipande cha chuma, kwa kuwa inaweza kukata na kuanguka.
Kata waya ya kuunganisha kwa urefu wa mita 12. Huu utakuwa urefu kati ya nguzo 2, ikijumuisha mashimo na sehemu.
Kwa kutumia koleo, unda upindo kwenye waya iliyojipinda katikati ya kila kifurushi cha vipande vya chuma.
Hakikisha kuwa unaacha mita 1 ya waya tupu kwenye kila upande ya kufunga kabisa ikizunguka nguzo. Tumia msumari ikiwa ungependa kuunda muunganisho imara wa waya kwenye nguzo.
Waya inapaswa kuwa kwenye urefu wa mita 1.5 kutoka kwenye ardhi ambayo ni urefu wa kifua kwa ndovu.
0.4 mita mbali
Kusanya vipande 3 hadi 4 vya chuma pamoja na uweke waya ya kuunganisha katika mashimo.
kidokezo
Hii ni ili kuzuia vipande vyote vya chuma kuteleza pamoja kwenye waya ambayo inaweza kupunguza ufanisi wake. Endeleza utaratibu huu hadi utayarishe urefu kati ya nguzo 2.
VIDOKEZO VYA UDHIBITI
Ni muhimu kuwa na nguzo imara ili kustahimili uzito wa vipande vya chuma. Tunashauri kuondoa ua wa Vipande vya Chuma “Kasaine” baada ya msimu wa mavuno, na uuhifadhi. Jinsi ndovu wanavyotangamana na ua mara chache, ndivyo walivyo na uwezekano mchache wa kuuzoea. Muda unavyosonga, vipande vya chuma vinavyosonga vitaharibu shimo na kuanguka. Ung’avu wa chuma utapungua kwa wakati, lakini kelele inapaswa kubaki. Ongeza safu ya pili ya vipande vya chuma kwa ufanisi zaidi.
Funga kila mwisho wa waya ya kufunga kwenye nguzo.
Unaweza kupiga msumari kwenye nguzo na utundike waya juu yake ili kustahimili uzito wa vipande vya chuma. Endelea hadi uweke ua kwenye eneo lote la shamba lako.
Faida Gharama ya chini ya kuweka.
+
Angalia: Mwongozo wa Ujenzi wa Ua wa Vipande vya Chuma wa wa Kasaine
Vipande vya chuma vinapatikana kwa urahisi kwenye maduka yaliyo karibu. Ua unahitaji utunzaji wa kiwango cha chini kwa kuwa chuma hudumu kwa miaka. Kuunda ua ni uwekezaji wa muda mrefu. Ua mzuri unapaswa kudumu kw amiaka kadhaa. Kelele zisizo za kawaida zinazotokana na ua zinaweza kuifanya mbinu hii kutozoewa na ndovu.
Tumia pamoja na Ua wa Pilipili au mbinu zingine za kizuio cha kelele.
Sauti yoyote au uakisi unaweza kuwazuia ndovu kukaribia. Ndovu wakivunja ua, kelele na kukasirika kwa sababu ya chuma zenye makali kunaweza kuwafanya kutohisi wakiwa salama na kunaweza kumwamsha mkulima ambaye anaweza kuwafukuza ndovu.
VIDOKEZO VYA tahadhari:
Kuwa mwangali wa kona za mabati zenye makali zinazoweza kukata ngozi. Tumia kifaa cha kujikinga inapohitajika. Punguza matumizi ya viua vijidudu. Viwango vya juu vitaathiri mazingira vibaya. Kuna hatari ya kuzoea kwa ndovu. Ni bora kutumia pamoja na mbinu tofauti ili kuongeza ufanisi.
Sifa na Katao la Haki:
Wazo hili liliundwa nchini Kenya na Simon Kasaine na kuanzishwa na kujaribiwa na mradi wa Elephants and Sustainable Agriculture in Kenya (ESAK) project and its partners: Wildlife Works, Western Kentucky University, Jomo Kenyatta University of Agriculture & Technology, Auburn University, the Earthwatch Institute and the International Elephant Foundation. Kwa makala na rasilimali zilizotumika, angalia Marejeleo. Huenda utafiti zaidi ukahitajika kwa kila utekelezaji maalumu wa eneo. Kunashauriwa kuweko kwa usalama na tahadhari unapotumia mbinu zote zilizopeanwa kwenye kijisanduku hiki cha vifaa. *Save the Elephants haigharamii gharama, uharibifu au majeraha yyote yanayotokana na matumizi ya mbinu hizi.
3. Imetengenezwa Kenya 2022
Imeandaliwa na Save the Elephants
www.savetheelephants.org
Michoro na Nicola Heath