SS Gomag Swahili I

Page 1

Mahali Michezo na Imani Vinapokutana

Какá 10

2

Brad Guzan

6

Isaac Diaz

Juan Carlos Valerón

4

José Luís Vidigal Portugal

Lee Young-Pyo

8


BONYEZA HAPA KUSOMA MAGAZINE KATIKA: KIARABU BONYEZA HAPA KUSOMA MAGAZINE KATIKA: BAHASA MALAYSIA

BONYEZA HAPA KUSOMA MAGAZINE KATIKA: KIVIETINAMU BONYEZA HAPA KUSOMA MAGAZINE KATIKA: KIURDU

BONYEZA HAPA KUSOMA MAGAZINE KATIKA: KIBENGALI

BONYEZA HAPA KUSOMA MAGAZINE KATIKA: TAMIL

BONYEZA HAPA KUSOMA MAGAZINE KATIKA: KISWAHILI

BONYEZA HAPA KUSOMA MAGAZINE KATIKA: TAGALOG

BONYEZA HAPA KUSOMA MAGAZINE KATIKA: KIHOLANZI

BONYEZA HAPA KUSOMA MAGAZINE KATIKA: KIHISPANIA

BONYEZA HAPA KUSOMA MAGAZINE KATIKA: KIINGEREZA

(CHA UINGEREZA)

BONYEZA HAPA KUSOMA MAGAZINE KATIKA: RUSSIAN

BONYEZA HAPA KUSOMA MAGAZINE KATIKA: KIINGEREZA

BONYEZA HAPA KUSOMA MAGAZINE KATIKA:

(CHA KIMAREKANI - USA)

KIRENO (ULAYA)

BONYEZA HAPA KUSOMA MAGAZINE KATIKA: KIFARANSA

BONYEZA HAPA KUSOMA MAGAZINE KATIKA:

KIRENO (BRAZIL)

BONYEZA HAPA KUSOMA MAGAZINE KATIKA: KIJERUMANI

BONYEZA HAPA KUSOMA MAGAZINE KATIKA: POLISH

BONYEZA HAPA KUSOMA MAGAZINE KATIKA: KIGIRIKI

BONYEZA HAPA KUSOMA MAGAZINE KATIKA: NEPALESE

BONYEZA HAPA KUSOMA MAGAZINE KATIKA: KIINDONESIA BONYEZA HAPA KUSOMA MAGAZINE KATIKA: KIJAPANI BONYEZA HAPA KUSOMA MAGAZINE KATIKA: KIKOREA

BONYEZA HAPA KUSOMA MAGAZINE KATIKA: MANDARIN BONYEZA HAPA KUSOMA MAGAZINE KATIKA: MALAGASY

KUSOMA ZAIDI NENDA: SPORTS SPECTRUM


02

JUAN CARLOS VALERÓN:

Sandra Behne/Getty Images

Juan Carlos Valerón amepata utoshelevu katika Kristo ambayo uwanja wa soka hauwezi kutoa

04

10 BRAD GUZAN:

ISAAC DIAZ:

Majanga yalipokita katika maisha ya Chile Isaac Diaz, aliona jinsi Mungu alivyokuwa maishani mwake

KAKÁ:

Mchezaji nyota wa Brazili amekamata usikivu wa dunia, si tu kwa mchezo wake bali kwa jinsi anavyoiishi imani yake kila siku

Christopher Lee/Getty Images

Goli kipa wa U.S. Brad Guzan amebakia wa kutumainiwa katika michezo na katika imani yake

YOUNG-PYO LEE:

Mkorea apendwaye sana kwa jina Young Lee alijikuta moyo wake ukibadilishwa kabisa baada ya kumtafuta Mungu na kuzungumza nja marafiki

Robert Cianflone/Getty Images

06

08 Esteban Garay/STR /Getty Images

YALIYOMO

Claudio Villa /Getty Images

1


2


Juan Carlos Valerón JUAN CARLOS VALERÓN AMEPATA UTOSHELEVU KATIKA KRISTO AMBAYO UWANJA WA SOKA HAUWEZI KUTOA. afari ya imani kwa Juan Valeron ni kielelezo kizuri kwa waamini wapya ambao mara nyingi hukabiliana na majaribu mapema wanapoamua kutembea na Kristo. Akiwa miongoni mwa wachezaji wazuri sana na wataalam waliobobea katika soka kwa miaka 15 iliyopita Valeron ameiongoza timu ya taifa katika ushindi mkubwa ikiwa ni pamoja na Ubingwa mara mbili wa Klabu Bingwa za ulaya, Kombe la Hispania, na akichezea Kombe la Dunia. Lakini ushindi wake uwanjani umerudishwa nyuma kutokana na maumivu nje ya uwanja, kuanzia kifo cha kaka yake katika umri wa miaka 30. “Kidogo tulikuwa ni familia yenye mshikamano, na kumpoteza kaka kulikuwa ni mshtuko mkubwa.” Alisema. “Pia ilikuwa ngumu kuwaona familia yangu wakipata shida. Lakini Mungu mwema alitusaidia, na nadhibitisha kwamba pasipo msaada wake, wazazi wangu wasingeliweza kuchukuliana na hali hii. Kwa bahati mbaya zaidi, maumivu yalizidi sana pale ambapo muda mfupi baadaye, baba yangu alifariki pia.” Katika maumivu yake, Valerón alisumbuka na maswali kama, Kwanini hili limetokea? Na alipokosa kupata majibu mwenyewe, alimtazama Mungu. “Yeye alikuwa jibu,” alisema Valeron “Alinionesha kuwa mazuri yanaweza kuja kupitia maumivu.Wakati ule, mmoja kati ya kaka zangu aliokoka, na kuanzia hapo, taratibu imani ya familia yangu imeendelea kukua.” Wakati Valerón alipokuwa kijana mdogo, lengo lake katika tasnia ya soka ilikuwa ni kucheza katika madaraja ya juu na kufikia viwango vya juu huko Uhispania. Lakini hata baada ya kufikia mafanikio makubwa, pamoja na yale ya Kombe la Dunia, alitambua kwamba pasipo Mungu, ushindi haukuweza kumpa utoshelevu maishani.

Valerón alipitia vipindi vigumu alipojaribu kumuuliza Mungu kwanini. Dunia nzima wanamichezo wanasaidiana na kutiana moyo kila mtu na mwenzake katika maeneo yote. “Nilitambua kwamba mafanikio yale hayakuwa muhimu hasa,” alisema. “Kwa kweli, bila Mungu, hayakuwa na thamani yoyote. Lakini Yesu ni kila kitu. Kama ambavyo ilivyo kwa chakula tunachokihitaji kwa kuishi, Yesu ni wa muhimu sana maishani. Mara nilipoamua kuwa na mahusiano naye, nilitaka tu niwe naye daima. Ili wakati nitakapopitia nyakati ngumu, Najua Mungu yu pamoja nami, na hivyo kuikubali hali hiyo nikua na furaha. Nikijua kwamba siku moja, Nitakwenda nikaishi naye na kushuhudia Utukufu Wake. ” Sandra Behne. / Getty Images

3


4

Christopher Lee/AFP/Getty Images


Brad Guzan GOLI KIPA WA U.S. BRAD GUZAN AMEBAKIA WA KUTUMAINIWA KATIKA MICHEZO NA KATIKA IMANI YAKE.

Miguel Tovar/STF / Getty Images

N

yakati za Kupenya kwetu kukubwa zaidi huja wakati tusipo ama tunapotarajia kwa kiasi kidogo sana. Mwaka 2005, golikipa wa Marekani Brad Guzan alidhani anacheza chini ya kiwango katika nafasi ya Chivas kipa wa Marekani aliyeumia. Kikosi kilimaliza wakiwa wameshinda 4 na kuingia katika rekodi ya kukosa mabao 22 katika mwakati wake wa kwanza, na Guzan aliamini kabisa kwamba ilikuwa ni wajibu wake. “Nilikuwa mdogo,” alisema. “Sikuwa na uhakika iwapo nilikuwa tayari kiakili na kimwili. Na sikuwa na uhakika iwapo nilistahili hayo. Hatukuwa tukishinda michezo…hivyo kwakweli pointi zile zilikuwa ndogo kwangu. Kulikuwa na alama nyingi za kujiuliza zilizokuwa zikizunguka kichwa changu.” Katika mwisho wa majira, hivyo, Guzan akapokea barua pepe ikimwalika aende kuchezea katika kambi ya timu ya taifa la Marekani. Ulikuwa ni mwaliko wa kuiwakilisha nchi yake. Kitu ambacho hakukitarajia hata kidogo. Ulikuwa ni ujasiri baaada ya mwaka wake wa kwanza ambao haukuwa umekwenda vibaya. Na miaka miwili baadaye, umaarufu wake kama nyota wa mchezo uliendelea kupanda, kisha 2007 kutawazwa kuwa golikipa bora wa mwaka katika ligi kubwa ya soka. Hii ilipelekea kupata fursa ya kuichezea Aston Villa katika moja ya ligi bora za soka duniani, Ligi kuu ya Uingereza mwaka 2008, mahali ambapo alidumu tangu (mbali na mkopo wa mwezi mmoja kwa timu ya Hull City). Kuwa katika ligi ngumu haikuwa rahisi, lakini ametoka mbali tangu mwaka wake wa kwanza akiwa na Chivas ya Marekeni. “Ulikuwa ni wakati wangu wa kujaribu kwa miaka minne, miaka yangu ya kwanza nikiwa Uingereza,” Guzan anasema. “Ilikuwa ngumu sababu ungeliweza kucheza mchezo, cheza vizuri na wiki inayofuata ungelijikuta mwenyewe ukisugua benchi” kwa hiyo ilikuwa ni soka isiyo na uhakika ambayo nilikuwa nikiipitia na nilikuwa nikitafuta uhakika… (Lakini) unapaswa kuwa mtaalamu. Unatakiwa kustahimili...unatakiwa kuendelea kupambana...Nilijua kwamba ningeendelea ningelipewa fursa wakati mwingine.”

Brad ana uzoefu kupitia timu alizozichezea akihudumu kama kiongozi na mshauri wa mambo yahusuyo imani na maisha. “Wakati mambo yanapokuendea vizuri, huwezi kuwa na ujasiri uliozidi, Guzan anasema. “Wakati mambo yanapokuendea kombo, huwezi huwezi kunyong’onyea…Nadhani kama mwanamichezo, kila mtu hupitia katika nyakati hizo, na hivyo hufanya mambo ambayo hujutia badaye. Kwangu, Sina tofauti. Si mkamilifu…Lakini Mungu humpenda kila mtu. Nilazima uwe tayari kuwa wazi kwake na mruhusu aingie maisha mwako. Na iwapo utafanya hivyo, msamaha, ule wepesi unaotoka mabegani mwako, ukijua kwamba unalo pendo la Mungu, utakuwa tayari kumfuata Mungu katika safari ya maisha yako.” Mnamo mwaka 2013, Guzan alianza kwa kushuka nafasi ya Tim Howard aliyejeruhiwa katika timu ya taifa ya wanaume mara mbili mwaka 2014 katika Kombe la Dunia la FIFA Brazil ilishinda na haikupoteza lengo wala kupoteza mechi. “Kwangu, jinsi maisha binafsi, maisha ya imani na maisha yangu mchezoni—yote yanakwenda pamoja,” Guzaan anasema. “Nadhani yanapaswa kuwa hivyo. Nadhani hiyo ni asili. Huwezi kuishi namna hii na kuwa namna nyingine na muhimu zaidi unapaswa kuwa na Yesu maishani mwako… Kama nilivyosema, njia ya mafanikio haikuwa rahisi. Na kupitia magumu yote hayo, Yesu ndiye alinisaidia kuvishinda vikwazo vyote.”

5


6

Robert Cianflone/Getty Images


Young-Pyo Lee

Karim Jaafar / Getty Images

MKOREA APENDWAYE SANA KWA JINA YOUNG LEE ALIJIKUTA MOYO WAKE UKIBADILISHWA KABISA BAADA YA KUMTAFUTA MUNGU NA KUZUNGUMZA NJA MARAFIKI akati yote yalipokwisha—alama zenye kukumbukika, mchezo mzuri, unaoshawishi kuelekea mashindano makubwa—kulikuwa na kustahimili tu. Kama Young-Pyo Lee alitoka dimbani akiwa mchezaji mahili sana wa soka akicheza katika fainali za mwaka 2013 za Vancouver Whitecaps, umati katika BC Place ulisimama wakimshangilia difenda na mzuiaji wao kwa shangwe baada ya kuchezea misimu miwili kama mchezaji soka chipukizi na hodari mwenye miaka 14 wa Vancouver Whitecap. Mashabiki waliojiachia—wakipaza sauti wakiita “Y.P.Lee!” Wengine walibeba bendera kubwa sana za Korea zikiwa na picha ya Lee katikati. Wachezaji wenzake walimzunguka na kumwinua juu juu hewani sana. “Mungu ni wa muhimu kwangu, sio soka,” Lee anasema. “Mchezo wa soka ni mojawapo kati ya mingi ambayo naweza kumtukuza na kumtumikia Bwana wangu kwayo.” Lee, hata anapostafu, anabakia kuwa Muasia ambaye ni mcheza soka maarufu katika historia. Alizaliwa Hongcheon, taaluma yake inajumuisha kushinda mara 127 — zaidi ya awamu tatu miongoni mwa Korea Kusini — na alishindana mara tatu katika Makombe ya Dunia ya mwaka (2002, 2006, 2010), akiisaidia Taeguk Warriors kufikia nusu fainali za mwaka 2002. Baada ya kuanza taaluma yake na Ligi ya Wachezaji mahili wa Soka huko Korea Kusini, Lee aliruka hadi angaza za viwango vya Ulaya aliposajiliwa na PSV Eindhoven ya Dutch Eredivisie. Akifuatia miaka mitatu akiwa na Netherlands katika Ligi kuu ya Uingereza (Tottenham Hotspurs), Ligi ya Ujerumani ya Bundesliga (Borussia Dortmund) na ligi ya Saudi Arabian Professional League (Al-Hilal). Kwa vipindi vyake mawili vya mwisho, alichagua Ligi kuu ya soka ya Vancouver Whitecaps japokuwa alikaririwa kuwa alipokea kitita kikubwa cha fedha, pengine alidhani Vancouver ingeliweza kumpatia fursa nzuri ya kujifunza jinsi ya kuendesha biashara mbali na soka.

Maelfu ya wacheza soka kama Young-Pyo Lee wamejikita katika kuwatia moyo wachezaji wengine kuishi, wakilisha na shirikisha shuhuda juu ya imani zao katika Ulimwengu wa Soka. Kinachoshangaza zaidi kwa Lee, japokuwa, si taaluma yake kama mcheze soka, bali ni wokovu. Akiwa amekulia maisha ya imani nyingine, aliamua kuweka imani yake kwa Kristo baada ya rafiki zake kumshuhudia na kumpa changamoto ya kusoma Biblia. “Wakati kiukweli nilipo tafuta kupitia kusoma na kuzungumza na rafiki zangu wa karibu, nilistajabu,” Lee anasema. “Mungu alinionyesha kuwa yupo, na moyo wangu ulibadilishwa kabisa.” 7


8


Isaac Diaz MAJANGA YALIPOKITA KATIKA MAISHA YA CHILE ISAAC DIAZ, ALIONA JINSI MUNGU ALIVYOKUWA MAISHANI MWAKE angu Isaac Diaz alipokuwa mdogo alikuwa na mpira wa soka kitandani mwake, kucheza kama mwanamichezo mtaalamu katika viwanja vinavyojaa tele, soka imekuwa ni sehemu ya maisha yake. Na alifanikiwa japokuwa alitokea katika mji mdogo.

Katika ulimwengu wa akademi za soka zimekuwa zikiendelea kukua kwa utoaji mbinu, maendeleo kiroho na kuwashauri kuishi maisha mema. “Nilipozaliwa, nililala kitanda kimoja na mpira wa soka…na amekuwa akicheza tangu hapo,” anasema Diaz. “Mji wetu, Fresia, ni mdogo sana lakini una akademi ya soka ya vijana. Pamoja na kucheza kienyeji, baba yangu alinizungusha nchi nzima ili niongeze ujuzi katika ligi na mashindano mengine. Nilibahatika kupanda kiwango, na kuchezea katika viwanja vilivyofurika ni furaha makubwa sana.” Diaz aliichezea Universidad de Chile daraja la kwanza na mara mbili katika Copa Libertadores ya Chile. Pigo la majanga, pamoja, na kufiwa na kaka yake, imani ilikuwa muhimu sana kwa wazazi wake na kwamba walichukulia kwa uzito isingelikuwa muhimu kwa Diaz. Lakini baada ya kupata fursa ya kulitafakari, na baada ya Mungu kujidhihirisha mwenyewe kwa Diaz, akaikumbati na na kukabidhi maisha yake kwa Kristo. “Familia yangu wakati wote walikuwa wakienda kanisani, lakini kusema kweli, nilitangulia kwanza kwa sababu wazazi walinitegemea mimi,” Diaz anasema. “Bado naweza kukumbuka kabisa tulipoketi matanga Kwa kifo cha kaka yangu, Hatimaye nilitambua jinsi Mungu alivyo kwangu – na yote aliyonitendea maishani mwangu. Nina amini asilimia 100 kwamba hakuna anayeweza kuishi bila Mungu!” Japokuwa imani ya Diaz inamwezesha kushinda kila siku, anaelewa kwamba yeye si bingwa wa majaribu. Imani yake haizuii mambo mabaya yasitokee, bali humsaidia kushinda katika nyakati ngumu zinapojitokeza. “Wakati mwingine maisha kama mwanamichezo yanweza kuwa magumu sana,” anasema. “Mazingira yasiyosalama yanayoizunguka klabu na wakati wa kucheza na maamuzi ya makocha kuhusu wachezaji yanaweza mara nyingi mtu kutilia shaka na kuingiwa na wasiwasi. Na kasha ongeza tena makelela ya siyo koma toka kwa mashabiki ambayo haiwezekani kuyazuia. Lakini najua kwamba maadamu imani yangu ipo kwa Mungu, naweza kuwa katika amani na kuifuata njia aliyoitengeneza kwa ajili yangu.” Anasema.

Wanamichezo wanajifunza kuishi kwa kuitii Biblia. “Nimejifunza kwamba Mungu wakati wote atafanya yasiyowezekana. Ninachohitaji ni kumwamini na Neno lake.” “Mfalme Sulemani alikuwa mwenye hekima kubwa. Wakati alipokuwa mfalme akiwa katika umri mdogo, Bwana akamtokea na kamwambia, Omba lolote nikupe’ (Kutoka katika Biblia 1 Wafalme 3:5). Juu ya mambo yote ambayo Sulemani angeliweza kuyataka, aliomba apewe ‘unyofu wa moyo.’ Alijua kwamba kumtumainia kwake Mungu kumwongoza kulikuwa ni jibu kwa maisha ya mafanikio. Kutoka katika Biblia kitabu cha Mithali 3:5-6, Sulemani aliandika hivi kutokana na uzoefu wake, ‘Mtumaini Bwana kwa moyo wako wote, wala usizitegemee akili zako mwenyewe; Katika njia zako zote mkiri yeye, Naye atayanyoosha mapito yako.’ Nawe pia mwamini Mungu na mjue kwa moyo wako wote.” Esteban Garay/STR / Getty Images

9


Laurence Griffiths/Getty Images

MCHEZAJI NYOTA WA BRAZILI AMEKAMATA USIKIVU WA DUNIA, SI TU KWA MCHEZO WAKE BALI KWA JINSI ANAVYOIISHI IMANI YAKE KILA SIKU kiwa amelala kitandani kwa miezi miwili shingo yake ikiwa imevunika, akiwa na miaka 18 Ricardo Izecson dos Santos Leite alifanya orodha ya magoli binafsi 10. Wala hakujali hali yake ya kutocheza tena baada ya kuvunja kifupa cha sita cha uti wa mgongo alivyopigiza sakafu ya bwala la kuteleza na kuogelea. Na kusahau umakini na tumaini. Kulikuwa na ndoto zinyekuweka alama kwa kijana aliyekulia katika mazingira ya kupenda Soka ya Brazil - hasa kwa aliyehitaji mpango wa matibabu kusaidia ukuaji wake uliodumaa na aliyekuwa tayari kujiunga na kikosi cha kwanza cha timu ya vijana ya klabu ya soka ya São Paulo. Orodha ilianza na “Rudi katika soka” na kupanda juu kwa kumaliza katika “Kombe la Dunia” na “Kuhamia klabu kubwa za Italia au Ujerumani.” Mnamo Januari 2001 takribani majuma mawili baada ya kurudia soka aliitwa São Paulo kujiunga na timu ya wataalamu. Mnamo Machi 7, zikiwa zimesalia dakika 10, akiwa ameingia badala la mtu katika fainali za michuano muhimu ya kombe la Rio-São Paulo. São Paulo iliifunga Botafogo 1-0 pale kiungo alipopokea pasi ya juu, alipompiga kanzu beki na kufunga mpira mfupi huku kipa akijirusha pakavu. Dakika mbili baadaye alifunga bao jingine kwa kasi ya roketi kutangaza ubingwa huku watangazaji wa TV wakipiga kelele “Goooooooooooooooal!” Timu ya Brazil ilikutana na Kaká. (Jina la utani, likitamkwa Ka-kah’, lilikuja pale kaka yake mkubwa aliposhindwa kutamka.) Alidai mwanzo wake na São Paulo na ndani ya miaka miwili kutazidisha zaidi ya magoli yake 10, ikijumuisha kuichezea Brazili katika kombe la Dunia huko Japani. Ilipofikia mwaka 2007 Kaká alikuwa mchezaji bora wa soka wa dunia, akijizolea sifa kemkem: akijizolea sifa na heshima katika viwango vya juu: pamoja na mchezaji bora wa 10

Pedro Armestre/Getty Images



mwaka wa dunia wa FIFPro, Ballon d’Or kwa ubora wa dunia na mchezaji bora wa FIFA wa mwaka. “Nimekuwa mwenye Baraka sana na mafanikio - Kombe la Dunia la 2002, zawadi ya FIFA ya Mpira wa dhahabu, mengi na tuzo nyingi nimepata. Yaweza dhaniwa kuwa nina kila kitu. Kutokana na utajiri wangu na umaarufu, wengine wameniuliza kwanini na iwapo bado ninamhitaji Yesu,” alisema. “Jibu ni rahisi: Nina mwitaji Yesu kila siku ya maisha yangu. Neno lake, Biblia, inaniambia kwamba bila yeye siwezi kufanya lolote. Kwa hakika nina amini hilo. Uwezo nilionao wa kucheza soka na yote yatokanayo na uwezo huo ni kipaji kutoka kwa Mungu. Amenipa kipaji ili nikitumie kumtukuza Yeye, na ninajitahidi kufanya vema kila siku.” “Pia nina amini kuwa kutenda kwa ufanisi na kwa ujuzi Alionipatia kunamletea utukufu Mungu. Mungu hataki wafuasi wake wame watu wa kawaida; Anataka tutende kwa viwango vya juu. Biblia inasema katika Wakoritho wa kwanza10:31 “Basi, mlapo, au mnywapo, au mtendapo neno lolote, fanyeni yote kwa utukufu wa Mungu” Msukumo wangu wa kushinda mechi ... umekua kwa kutaka nifanye vizuri zaidi kwajili ya Muumba wangu. “Ilikuwa ni ndoto kwangu kwa mimi kuichezea São Paulo na mchezo mmoja na Brazil, lakini Biblia inasema Mungu aweza kukupa zaidi ya uwezayo kuyaomba na hilo limenitokea maishani mwangu.”

IMANI NA FAMILIA

Nyota ya Kaká ilichomoza katika medani za soka la Brazil kufuatia mchezo usioweza kusahaulika. Vyombo vya habari havikumwelewa vizuri, na alikuwa kivutio kikubwa cha wasichana. Asingeliweza kutoka mbele za watu pasipo kuzongwa. Mwanzoni mama yake mzazi na Kaká aliweza kuzijibu takribani barua 50 kwa siku kutoka kwa mashabiki wake wa kike,

12

lakini mafuriko ya umakini ghafla yakazidi. Baada ya kushtuka mwanzoni, Kaká aliboresha ukarimu na upatikanaji kwa vyombo vya habari na mashabiki, lakini aliepuka majaribu ya kuingia klabu za usiku na kamera za mapaparazi. Kama ilivyokuwa siku zote, familia na imani ndivyo vilikuwa vitu vya kushikamana navyo. “Watu wengi wanadhani niliamua kuokoka baada ya ajali, lakini hiyo si kweli,” anasema Kaká. “Wazazi wangu wamekuwa wakinifundisha Biblia na umuhimu wake, na pia kumhusu Yesu Kristo na imani ” Kubatizwa akiwa na umri wa miaka 12 ilikuwa ni hatua muhimu sana kwa Kaká na ambayo ilileta matokeo mazuri sana katika maisha ya uchanga wake wa kiroho. “Kidogo kidogo taratibu, nilikata kusikia watu wakisema kuhusu habari za Yesu ambaye wazazi wangu walinifundisha,” alisema. “Hapo ulikuja wakati ambao nilitaka kuishi maisha binafsi na Mungu.”

MFUMO WA KIULAYA

Kuna msemo maarufu usemao kuhusu soka: “Waingereza wanausadiki. Wa Brazil wameuthibitisha.” Mchezo wa Brazil ni wa kiustadi, wenye mtiririko wa aina yake unaoacha alama za kukokota ngoma kwa umahiri mkubwa na pasi zisizotarajiwa. Taifa likawa limeleta jogo bonito, mchezo mzuri, kwa dunia na kushikiria makombe mengi ya ubigwa, matano, zaidi ya nchi yoyote. Lakini Ulaya ni kitovu cha soka la kitaalamu. Fedha nyingi kutoka kila nchi zinazo endesha ligi kubwa zimeleta karibu vipaji vya hali ya juu duniani pamoja, na kimabara mashindani ya ligi ya mabingwa ya UEFA huthibitisha jinsi ushindani ulivyo mkubwa na vipaji. Hivyo haikuwa jambo la kustaajabisha ambapo kwa wakati ule kijana mwenye miaka 21 Kaká alipokwenda kuichezea AC Milan ya Italia iliyo kundi A. Soka la Ulaya kwa ujumla linadhaniwa kuwa ni soka la kutumia nguvu na mbinu kuliko mchezo wa Marekani ya Kusini, lakini kwa urefu na nguvu zake Kaká mara moja aliweza kuumudu. Katika msimu wake wa kwanza alijizolea sehemu yake ya kuanzia, alifunga mabao 10 na kuisaidia Milan kuishinda Scudetto, katika kundi A la ubingwa. Alitajwa kuwa ni ndiye mchezaji bora wa mwaka wa ligi hiyo. “[Kaká] ana mbinu za kimchezo za Kibrazil na viwango vya nguvu za mwili za Kiulaya,” Vanderlei Luxemburgo, kocha wa zamani wa timu ya taifa ya Brazil, aliiambia FIFA.com. “Huyu ni kipimo cha ubora wa viwango wa soka la kisasa” Mnamo 2005, Kaká akiwa na Milan waliweza kuzifikia fainali za ligi ya mabingwa ambapo walipoteza 3 - 0 kipindi cha pili na kufungwa na Liverpool ya Uingereza kwa mikwaju ya penati. Milan ilirudi mwaka 2007, hatimaye, kushinda ligi ya washindi kwa kucheza tena na Liverpool. Ndipo ush-

indi wa Kaká kuwa mchezaji bora ulifuatia, na alitajwa katika gazeti la Time akiwa ni miongoni mwa orodha ya watu 100 wenye ushawishi duniani. Baada ya uhamisho uliogharimu kiasi kikubwa cha fedha kutoka Manchester City ya Uingereza Kaká na Milan walikubaliana kwa kiasi sawa cha fedha kwa kumuuza kwa timu ya Real Madrid ya Uhispania. Dili la rekodi lililovunjwa baada ya kumsajili Cristiano Ronaldo. Hatimaye timu ilitumia kiasi kikubwa cha fedha kuwasaka wachezaji nyota ili kurejesha ubingwa wa ndani na Ulaya. Kaká alisumbuliwa na majeraha kadha, na mara timu nzima haikucheza kama ilivyokusudiwa. Matarajio kwa Los Blancos yalikuwa makubwa sana, na mashabiki walitaka kufukuzwa kwa kocha Manuel Pellegrini walipo upoteza mchezo wao na Lyon ya Ufaransa katika mchezo wa mzunguko wa kwanza wa mtoano wa ligi ya Mabigwa. Ndipo Real Madrid ikamaliza ya pili nyuma ya Barcelona kwa ubingwa wa Spaniola.

KIMSINGI

Kufanikiwa kwa Kaká katika soka bila shaka kumepelekea umaarufu wake dunia nzima, lakini msimamo wake pia umesambaa dunia nzima miongoni mwa nyota wa michezo. Mchukue mwanasoka wa kimataifa - au mwanamichezo mtaalamu - pengine asowa kawaida Kaká niwatofauti. Ni Mbrazil, ni kwamba alikulia mazingira ya kimasikini akiwa na mpira wa kutengeneza? Wazazi wote wa Kaká walisomea kitaalam masuala ya michezo ambao waliwalea watoto wao katika eneo tajiri la vipaji la São Paulo, na Kaká alijifunza katika akademi ya Klabu ya soka ya São Paulo. Wakati wote angeliweza kucheza kwa madaha na kuukokota mpira na kwa mtindo wa Kibrazil? Wakati ustadi wa kucheza na mpira kusiko kwa kawaida, staili ya Kaká ni ya aina yake, ya kupendeza na ya kiwango. Wakati wote angelijaribu kwenda juu na wala si sambamba,” kocha wa AC Milan Bwana Carlo Ancelotti ameliambia Observer, gazeti la Uingereza. “kamwe hata tenda tofauti, yaani pasi isiyoyalazima” Lakini vipi kuhusu maisha yake nje ya uwanja wa michezo - je ni mchezaji tofauti kama wachezaji wengine nyota wa kimataifa? Walaa! Kaká na mkewe, Caroline, akitambulika kuwa aliolewa akiwa bikira na amepata kulizungumzia waziwazi hili katika vyombo vya habari. “Ilikuwa ni moja kati ya changamoto

Shauku ya Kaká ni kuishi kama mtumishi akitii maagizo yote ya Biblia.


Laurence Griffiths/Getty Images

kubwa sana maisha mwangu kwa sababu tuliamua maamuzi magumu,” alisema Kaká. “Tulitumia muda wetu mwingi kuomba na kutembea karibu na Yesu na Roho Mtakatifu. Ilikuwa changamoto kubwa, lakini ilikuwa bora na tukasubiri. Kujamiana ni Baraka toka kwa Mungu kwajili ya furaha ya wote mume na mke baada ya kuoana, lakini si jambo dogo au la kulichukulia kawaida kama ilivyo siku za leo.” Je, ni kweli kwamba ni mbinafsi na mpenda vitu? Utoaji wa Kaká wa ukarimu kwa kanisa lake la Brazil unajulikana sana. Pia alitumika kama Balozi wa Umoja wa Mataifa akihamasisha na kutokomeza njaa. “Sasa napenda kutoa na kuleta tumaini kwa watoto waliokumbwa na balaa la njaa na maisha duni kuliko mimi,” alisema “Naamini hali niliyoipitia mimi inaweza kuwashawishi watoto waamini kwamba wanaweza kushinda hali hizo na kuishi maisha ya kawaida,” Kaká akiwa na Umoja wa Mataifa kazi yake ilikuwa kuongea na watoto kuhusu njaa. Anatarajia kuwa mchungaji baada ya kustafu soka. “Kaká kamwe hajabadilika,” alisema Marcelo Saragosa, rafiki yake mkubwa tangu wangali wadogo na mchezaji nyota wa soka.

“Siku zote amekuwa wa kawaida kama nilivyokutana naye miaka 10 au 12 iliyopita.” Vyombo vingi vya habari wameonyesha nidhamu kwa imani ya Kaká wakimsifia kama mwanamichezo. Umahiri na wema wake un-

Kwa kupitia wimbi la michezo kumesaidia makanisa kuwahudumia vijana waimarike katika ujuzi juu ya michezo, juu ya maisha halisi na mtazamo wa Kibiblia. Kama Kaká alivyosema, “Bila Yesu hatuwezi kufanya chochote.”

aendana na kiwango cha mchezo na kufanya iwe ngumu kufanya vinginevyo. Japo kuwa wengine wamesema kuwa maisha yake hayavutii, Kaká ameyahesabu kuwa msingi wa kumfuta Kristo. Kadri ambayo Kaká anavyoendelea kufika malengo mapya, hasiti hata kidogo kuwambia watu yupo kwa ajii ya Kristo. “Leo, nina huduma yangu kupitia michezo, lakini nacheza hivi kwasababu Mungu amenipa kipaji,” anasema. “Nacheza kwasababu Mungu amethibitisha zawadi aliyonipa maishani mwangu. Yesu alisema ‘pasipo mimi hamwezi kufanya lolote’ na nina amini hili.”

13



Turn static files into dynamic content formats.

Create a flipbook
Issuu converts static files into: digital portfolios, online yearbooks, online catalogs, digital photo albums and more. Sign up and create your flipbook.